Nimesikitishwa na kifo cha Prof. Benno Ndulu (Ex-Governor BOT). Pole kwa familia na wafiwa wote. Nitamkumbuka kwa ushauri wake wa kuimarisha uchumi wa nchi yetu hususani mageuzi ktk sekta ya fedha. Alikuwa mchapakazi na mnyenyekevu. Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi,Amina
John Magufuli
John Pombe Joseph Magufuli (29 October 1959 – 17 March 2021) was a Tanzanian politician who served as the country's fifth president, serving from 2015 until his death in 2021. He served as Minister of Works, Transport and Communications from 2000 to 2005 and 2010 to 2015 and was chairman of the Southern African Development Community from 2019 to 2020. More on Wikipedia
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar. Natoa pole kwa Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Mwinyi, Familia, Wazanzibari, wanachama wa ACT-Wazalendo na Watanzania wote. Mungu amweke mahali pema peponi,Amina
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Kwa miaka 44 chama cha CCM kimeendelea kuongoza mapambano ya kulinda heshima na uhuru wa Tanzania, kazi iliyoasisiwa na vyama vya TANU na ASP. Hongereni Watanzania; Hongereni Waafrika
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Nakupongeza Mhe. Yoweri Kaguta Museveni kwa kutangazwa na Tume ya Uchaguzi ya Uganda kuwa mshindi wa kiti cha Urais. Tanzania itaendeleza urafiki na udugu wetu kwa maslahi mapana ya wananchi. Hongereni Waganda kwa kukamilisha Uchaguzi Mkuu, endeleeni kudumisha amani na upendo.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Nimesikitishwa na kifo cha Ndg. Subhash Patel. Wakati wa uhai wake ametoa mchango mkubwa katika maendeleo ya viwanda, kukuza biashara na kuzalisha ajira kwa Watanzania wengi. Natoa pole kwa Familia, CTI, TPSF na TNBC ambako alishiriki vizuri.
Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un. -
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Nimesikitishwa na kifo cha Kamishna wa Maadili, Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Harold Nsekela. Poleni familia, watumishi wote wa Sekretarieti ya Maadili na Mahakama. Jaji Mstaafu Nsekela alikuwa mwadilifu, mzalendo, asiyejikweza na mchapakazi. Mungu amweke mahali pema, Amina.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
I am deeply saddened by the news about the passing on of the former President of Ghana, H.E. Jerry John Rawlings. My condolences to Your Excellency Nana Akufo-Addo and the brotherly people of Ghana for the loss of this Great-man of Africa. May his soul rest in peace, Amen.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
On behalf of the Government and the people of Tanzania, I congratulate President-elect @JoeBiden and Vice President-elect @KamalaHarris on your victory in the US General Election. Be assured that Tanzania will continue to cherish the relationship that exist between our countries.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Naitwa John Pombe Joseph Magufuli, mgombea kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM). Ewe Mtanzania mwenzangu, naomba kura yako ya ndio tarehe 28/10/2020. Chagua Magufuli kwa maendeleo ya kweli ili tuendelee kujenga Tanzania mpya. Asante.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Nawapongeza Walimu wenzangu wa madaraja yote kwa kuadhimisha siku ya Walimu Duniani. Serikali inatambua mchango wenu mkubwa kwa Taifa na itaendelea kuboresha maslahi na mazingira yenu ya kazi. Endeleeni kuchapa kazi. Tulianza pamoja, tutamaliza pamoja.
:
Mwl. John Pombe Magufuli. -
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Nawapa pole familia na wote walioguswa na kifo cha Jaji Mstaafu Mark Bomani. Nitamkumbuka kwa mchango wake mkubwa Serikalini katika masuala ya sheria na katika chama akiwa Mjumbe wa Baraza la Wadhamini wa CCM. Mwenyezi Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi, Amina.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Nawashukuru wana CCM wote na Watanzania wa vyama vyote kwa kujitokeza katika uzinduzi wa kampeni za CCM 2020 Jijini Dodoma. Pia nawashukuru wasanii, waandishi wa habari, viongozi wa Dini, n.k waliojitokeza kuniunga mkono katika uzinduzi huu. Maendeleo hayana chama. Tanzania Hoyee
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
The Government and the people of Tanzania convey their warmest congratulations to Dr.Akinwumi Adesina on his re-election as the President of the @AfDB_Group. In our joint work over the last 5 years, we have appreciated your consistent commitment to Africa.
HONGERA SANA 👏🏼👏🏼👏🏼 -
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Nimesikitishwa na taarifa za kifo cha ghafla cha Rais wa Chama cha Wanamuziki wa Injili Tanzania, Dkt. Donald Kisanga aliyefariki dunia kwa ajali ya gari Jijini Dodoma. Mungu amweke mahali pema peponi, Amina.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Nawatakia heri WAKULIMA, WAFUGAJI na WAVUVI katika sikukuu hii ya Nanenane. Serikali inatambua mchango wenu mkubwa katika ujenzi wa Taifa na ustawi wa Watanzania. Tunaahidi kuendelea kuwaunga mkono na kushughulikia changamoto zenu ili kuongeza tija katika kazi zenu. NANENANE JUU!
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Nimesikitishwa na kifo cha Mzee wetu Benjamin Mkapa (Rais Mstaafu wa Awamu ya 3). Nitamkumbuka kwa mapenzi yake makubwa kwa Taifa, ucha Mungu, uchapakazi na utendaji wake katika kujenga uchumi. Hakika Taifa limepoteza nguzo imara. Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi, Amina.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Nimesikitishwa na kifo cha Mzee wetu Balozi (Mst) Job Lusinde. Nawapa pole Familia, wana Dodoma na Watanzania. Nitaukumbuka mchango wake mkubwa kwa Taifa akiwa Waziri, Balozi, Mdhamini wa CCM na Kiongozi wa Wazee wa Dodoma. Pumzika salama Mtani wangu, kazi kubwa umeifanya vizuri.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Today, the World Bank has declared Tanzania Middle Income Country. In this regard, I congratulate all my compatriots for this historic achievement. We had envisaged to achieve this status by 2025 but,with strong determination, this has been possible in 2020. GOD BLESS TANZANIA.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Benki ya Dunia leo tarehe 01 Julai, 2020 imeitangaza Tanzania kuingia UCHUMI WA KATI.Nawapongeza Watanzania wenzangu kwa mafanikio haya.Huu ni ushindi mkubwa na kazi kubwa tumeifanya, tulipanga kuingia uchumi wa kati ifikapo 2025 lakini tumefanikiwa 2020.MUNGU IBARIKI TANZANIA
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Nakupongeza Dkt. Lazarus Chakwera kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Malawi. Kwa niaba ya Serikali na Watanzania wote naahidi kuendeleza uhusiano wetu wa kidugu, kirafiki na ujirani mwema hususani katika masuala ya uchumi na ustawi wa jamii.
Hongera sana Mhe. Rais. -
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Nimeshtushwa na taarifa za kifo cha Rais wa Burundi, Mhe. Pierre Nkurunziza. Nitamkumbuka kwa uongozi wake imara na juhudi zake za kupigania amani, maendeleo na kuruhusu demokrasia. Kwa niaba ya Serikali na Watanzania nawapa pole familia na Warundi wote. Mungu amweke mahali pema.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Nakupongeza Ndg. Evariste Ndayishimiye kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Burundi. Wananchi wa Burundi wameonesha imani kubwa kwako. Kwa niaba ya Serikali na Watanzania wote naahidi kuendeleza uhusiano mzuri kati yetu. Nawatakia Warundi wote amani na ujenzi bora wa Taifa lenu.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Ndugu zangu Watanzania, kutokana na ugonjwa wa Corona, nawaomba tutumie siku 3 za kuanzia tarehe 17- 19 Aprili, 2020 {Ijumaa, Jumamosi na Jumapili} KUMUOMBA MWENYEZI MUNGU aliye muweza wa yote atuepushe na janga la ugonjwa huu. Tusali kwa kila mmoja kwa imani yake, atatusikia.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Nawapongeza Wanawake wote kwa kuadhimisha siku hii muhimu. Mchango wenu kwa familia,jamii na Taifa hauna mfano.Serikali ninayoiongoza itaendelea kuwathamini,kuwaheshimu na kujenga mazingira bora yatakayowawezesha kutekeleza majukumu yenu ipasavyo.
#happyinternationalwomensday -
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Nawapongeza wanachama na wakereketwa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa chama chetu kutimiza miaka 43 tangu kuzaliwa. Tunaposherehekea siku hii muhimu kwa kazi tuendeleze misingi ya chama chetu, tusimamie utekelezaji wa Ilani na tudumishe amani, upendo na mshikamano.
CCM HOYEE! -
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Kwa niaba ya Serikali na Watanzania nakupa pole Mhe.Rais Uhuru Kenyatta na Wakenya wote kwa kuondokewa na Rais Mstaafu Daniel Toroitich arap Moi. Watanzania tutamkumbuka kwa uongozi wake mahiri, jitihada za kuimarisha uhusiano wetu na Kenya na kufufua Jumuiya ya Afrika Mashariki.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
It is with deep sorrow that I received the news about the demise of the Leader of Oman Sultanate, Sultan Qaboos bin Said Al Said. During his leadership, our two nations enjoyed strong and close bilateral relations. We convey our profound condolences to all the people of Oman.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Nimehuzunishwa na taarifa za kifo cha rafiki yangu Ali Mufuruki (Mwenyekiti na Mwanzilishi wa Jukwaa la Wakurugenzi Watendaji wa Kampuni - CEOrt) Nitamkumbuka kwa uzalendo na mchango wake katika kukuza sekta ya biashara na ushauri kwa Serikali.Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Hongera sana Mhe. Rais Hage Geingob. Your re-election is clear testimony of the trust and confidence that Namibians have bestowed on you. I wish to assure you of our continued support to further strengthen the historical ties between our two brotherly countries.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Mhe. Spika. Nakushukuru wewe na Wabunge kwa azimio la kunipongeza. Mmenitia moyo na kunipa nguvu zaidi ya kufanya kazi. Nami nawapongeza kwa kazi nzuri mnazofanya Bungeni na Majimboni kwenu. Mbarikiwe sana.Kwa niaba ya Serikali naahidi kuendelea kushirikiana na Bunge letu Tukufu.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
NAMSHUKURU Mungu kwa kunifikisha siku ya leo.
Pia NAWASHUKURU nyote mlionitakia heri katika siku yangu ya kuzaliwa. Mmenionesha upendo wa dhati na mmenitia nguvu katika kutekeleza majukumu yangu.
Nami nawatakia afya njema, maisha marefu na Mwenyezi Mungu awabariki sana. -
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Congratulations Your Excellency Mokgweetsi Masisi on your election as President of Botswana. On behalf of the Government and People of Tanzania, I wish to reiterate our commitment to further strengthen the excellent bilateral relations that exist between our two countries.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Congratulations to Your Excellency President Xi Jinping and the people of China on commemoration of the 70th anniversary of your great Nation. On this occasion, I pledge to further enhance our historic, friendly and fraternal ties.
祝贺习近平主席!祝贺全体中国人民!
China Hoyee! -
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Rais Mstaafu na Baba wa Taifa la Zimbabwe Mzee Robert Mugabe. Afrika imepoteza mmoja wa viongozi Jasiri, Shupavu, Mwanamajumui wa Afrika na aliyekataa ukoloni kwa vitendo. Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi, Amina.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
I congratulate Your Excellency and dear brother Prof. Mutharika on your re-election as President of Malawi. On behalf of the Government and the people of Tanzania, I pledge our commitment to further strengthening our friendly and fraternal relations, in bettering our economies.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
On behalf of the Government and the people of Tanzania, I congratulate Y'r Excellency Narendra Modi on y'r re-election as Prime Minister of India.This indicates the confidence that y'r compatriots have in you. Be assured of our commitment to strengthen our bilateral co-operation
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Nimesikitishwa na taarifa za kifo cha Mzee na Rafiki yangu Dkt. Reginald Mengi. Nitamkumbuka kwa mchango wake mkubwa ktk maendeleo ya Taifa letu na maono yake yaliyopo ktk kitabu chake cha I Can, I Will, I Must. Poleni wanafamilia, wafanyakazi wa IPP na Jumuiya ya Wafanyabiashara
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
I am deeply saddened to hear about the crash of the Ethiopian Airlines' Boeing 737 which occurred early today. I seize this occasion to express my profound condolences to all the bereaved families and to all Heads of State whose people's lives have been claimed by this accident.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Nimepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha kijana wangu Ruge Mutahaba. Daima nitamkumbuka kwa mchango wake mkubwa ktk tasnia ya habari, burudani, na juhudi za kujenga fikra za maendeleo kwa vijana. Poleni wanafamilia,ndugu,jamaa na marafiki. Mungu amweke mahali pema, Amina.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Following the judgement by the High Constitutional Court. I congratulate HE. Felix Tshisekedi on his election as President of the DRC. While congratulating all the Congolese, I beseech you to maintain peace and affirm my commitment to furthering our historic and brotherly ties.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Punde nimezungumza na Mhe. Kenyatta kuhusu shambulizi la Jijini Nairobi,zaidi ya watu 14 wamefariki dunia na wengine kujeruhiwa.Pole sana Mhe. Rais na pole sana wananchi wa Kenya.Tupo nanyi katika kipindi hiki cha majonzi. Nawaombea Marehemu wote walale mahali pema peponi, Amina.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Vijana wangu - TAIFA STARS🇹🇿
Muda mfupi ujao nitakuwa nikitazama mchezo kati yenu na Timu ya Taifa ya Lesotho 🇱🇸.
Mimi na Watanzania wenzangu tunawatakia mchezo mwema, mrudi na ushindi. -
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Nawashukuru wote mlionitakia heri katika siku yangu ya kuzaliwa. Mungu ni mwema. Nimepokea salamu nyingi japo sikuweza kuwajibu wote, lakini muamini kuwa nimezipata. Nawaomba Watanzania tuendelee kudumisha amani,upendo,mshikamano na tuchape kazi za kulijenga Taifa letu.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Nakupa pole Mhe. Rais Museveni na wananchi wote wa Uganda kwa kuwapoteza watu zaidi ya 40 katika ajali ya maporomoko ya udongo iliyotokea katika Wilayani Bududa. Watanzania tunaungana nanyi katika kipindi hiki cha majonzi na tunawaombea majeruhi wote wapone haraka @KagutaMuseveni
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya ajali ya basi iliyotokea Kericho nchini Kenya na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 50. Nakupa pole Mhe. Rais Uhuru Kenyatta, familia za marehemu na Wakenya wote. Mungu aziweke roho za marehemu mahali pema na majeruhi wapone haraka. @UKenyatta
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Nakupongeza Mhe. Rais Yoweri Museveni na wananchi wote wa Uganda kwa kuadhimisha miaka 56 ya Uhuru. Kwa niaba ya Watanzania nawaahidi kuundeleza na kuukuza uhusiano na ushirikiano wetu wa kihistoria. Kwa pamoja tudumishe ujirani mwema, udugu na urafiki kwa manufaa yetu sote.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Cde. Mnangagwa. On behalf of the Government and people of Tanzania,I convey my sincere congratulations on your victory in the Presidential Election of Zimbabwe.Your victory is a reflection of the confidence reposed in you by the people of Zimbabwe in leading them to prosperity.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Nimefurahishwa na ushindi wa Grace Products, lakini pia nimefurahishwa kwa kutumia kiswahili kukizungumza nchini Marekani, hongereni sana Grace Products.
www.youtube.com/watch?v=zsuLim6doMM&t=13s -
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
MAN OF GOD, Rev. TB JOSHUA
On behalf of my family, I extend my heartfelt wishes on your 55th Birthday. May the Almighty God bestow upon you exceeding divine inspiration so that you can bring deliverance to more people and spread his fragrance across nations. HAPPY BIRTHDAY TO YOU -
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Nimesikitishwa na kifo cha Maria na Consolata. Nilipokwenda hospitali waliliombea Taifa. Walikuwa na ndoto ya kulitumikia Taifa. Poleni familia, Masista wa Maria Consolata na wote walioguswa, pumzikeni mahali pema wanangu. BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Ninayo furaha kukupongeza Mzee wangu Alhaji Ali Hassan Mwinyi kwa kutimiza miaka 93. Busara zako, ushauri, upendo, unyenyekevu, ucha Mungu na ushirikiano kwa Watanzania ni jambo tunalojivunia sana. Nakutakia afya njema na maisha marefu yenye furaha na amani. HAPPY BIRTHDAY.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Marehem Sokoine hatasahaulika katika historia ya Tanzania, ni wito wangu kwa watanzania tumuige na kumuishi. Ni rai yangu pia tumuenzi kwa kujenga umoja wetu , kupiga vita rushwa na kuchapa kazi . Mungu aiweke roho ya marehemu Edward Moringe Sokoine mahala pema peponi 3/3
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Wakati tunapoazimisha siku kama hii ya kifo chake, watanzania tuige mfano wake kwani alikuwa msema kweli, asiyeogopa, mpiga vita rushwa,ufisadi, unyonyaji,mzalendo wa kweli na aliyechukia rasilimali za watanzania kuibwa 2/3
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Katika siku kama ya leo tarehe 12 Aprili 1984 nikiwa Mpwapwa JKT nikitumikia jeshi langu “Oparesheni Nguvukazi” tukatangaziwa kifo cha marehem Edward Moringe Sokoine, ilikuwa siku ya majonzi shujaa huyu niliyemjua na kumshabikia ikawa siku yake ya mwisho 1/3
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
I have learnt with deep sorrow the sad news of the demise of Winnie Mandela, a woman of an exceptional courage and strength.
She will always be remembered for the important role she played during the struggle against apartheid.
May the Almighty God rest her soul in eternal peace. -
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
I'm very glad that we have commenced the second lot of our central line standard gauge railway construction from Morogoro to Dodoma. As we celebrate this important milestone in our country's development lets steadfastly preserve our peace, unity and solidality.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Nawapongeza wanawake wote kwa kusherehekea siku yenu ya leo na hasa kwa mchango wenu mkubwa mnaoutoa kwa jamii. Daima tutaendelea kuwaheshimu, kuwapa ushirikiano na kutambua juhudi zenu katika kujenga ustawi wa jamii yetu.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Nimesikitishwa sana na kifo cha mwanafunzi Akwilina Akwilini wa Chuo cha Usafirishaji (NIT).Natoa pole kwa familia,ndugu,wanafunzi wa NIT na wote walioguswa na msiba huu.Nimeviagiza vyombo vya dola kufanya uchunguzi na kuwachukulia hatua za kisheria waliosababisha tukio hili.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
My heartfelt condolences to Morgan Tsvangirai’s family. Our thoughts and prayers are with the Zimbabwean people during this time of grief and inexpressible sorrow.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Nawapongeza viongozi, wanachama na wapenzi wote wa CCM kwa kutimiza miaka 41. Tunaposherehekea mafanikio yetu tuendelee kutunza Amani na umoja wetu, tuchape kazi kwa maslahi ya nchi yetu na Serikali inayoongozwa na CCM.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Wakati tukisubiri taarifa kamili kutoka DRC niwaombe Watanzania tuwe na subira, Mungu wetu yuko pamoja nasi 2/2
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Nimepokea kwa mshituko mkubwa taarifa za kuuwawa askari wetu kumi na wanne na wengine arobaini na wanne kujeruhiwa na wawili hawajapatikana huko DRC wakati wakitekeleza majukumu ya ulinzi wa amani, natoa pole sana kwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania na familia 1/2
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Aidha, vyombo vya dola viwasake wale wote waliohusika na tukio hili la kinyama na kuwafikisha ktk mikono ya sheria.2/2
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Nimepokea kwa masikitiko tukio la kupigwa risasi Mh.Tundu Lissu, namuombea kwa Mwenyezi Mungu aweze kupona haraka. 1/2
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Najivunia kuwa Amiri Jeshi Mkuu wa JWTZ. Mungu ibariki Tanzania, Mungu libariki Jeshi letu.4/4
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Kwa uzalendo,umahiri,ushupavu,uadilifu na nidhamu ya hali ya juu na hivyo kujijengea heshima ndani na nje ya nchi yetu. 3/4
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Kwa kipindi chote hiki Jeshi letu limeendelea kutimiza wajibu wake ikiwa ni pamoja na kulinda amani ya nchi yetu. 2/4
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Nalipongeza Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa kutimiza miaka 53 tangu kuanzishwa kwake. 1/4
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Tunaposherehekea sikukuu hii tuendelee kudumisha upendo,amani,umoja na mshikamano wetu. Eid Mubarak.2/2
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Nawatakia Waislamu na watanzania wote sikukuu njema ya Eid el-Hajj. 1/2
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Nakupongeza Ndg.Uhuru Kenyatta kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Kenya kwa kipindi kingine. Nakutakia mafanikio mema.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Tutaendeleza na kukuza zaidi ushirikiano na uhusiano kati ya nchi zetu hususani biashara na maisha ya wananchi wetu. Hongera Wanyarwanda.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Nakupongeza Mhe. Paul Kagame kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Rwanda kwa kipindi kingine. Kwa niaba ya Watanzania wote nakutakia mafanikio mema.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Wito wangu kwa watanzania wote ni kuchangamkia fursa hii kipindi cha ujenzi na uendeshaji wa mradi huu. Mungu Ibariki Tanzania. 3/3
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Mradi huu ni kielelezo tosha cha muendelezo wa ushirikiano wa nchi zetu mbili na hasa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki. 2/3
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Nchi yetu imepata mradi mkubwa wa bomba la mafuta ghafi kutoka Kabaale/Uganda hadi Tanga/Tanzania,ni fursa kubwa ktk kuujenga uchumi wetu1/3
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
We will, therefore, continue to count on your support but also on the support of other partners ~ World Bank, EU, USA, China, UK, India etc
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Is on the track of economic growth. Indeed, your statement has given us encouragement and a fillip to our efforts. 4/5
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
And I welcome your commitment to continue to support our country. Yet, I was particulary moved by your assertion that Tanzania 3/5
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Also I wish to thank the IMF for the various support extended to us.
During your visit we held a very fruitful bilateral discussion 2/5 -
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
I thank you, Mr. Tao Zhang, Deputy Managing Director of IMF for choosing Tanzania to be your first country to visit in Africa. 1/5
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Tunapoomboleza vifo vya wapendwa wetu tuendelee kuwa wamoja. Mungu ibariki Tanzania.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Tumewapoteza mashujaa wetu ktk elimu. Tuwaombee na tuendelee kuwa na subira, uvumilivu na ustahimilivu 2/2
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Nimepatwa na uchungu na majonzi makubwa ninapoyaona majeneza ya watoto na walezi wao waliopoteza maisha katika ajali ya basi huko Arusha 1/2
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
In this respect, We look forward to further strengthening this partnership and cooperation. 3/3
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Indeed this support has once again demostrated in no uncertain terms that the World Bank is a valuable & dependable partner of Tanzania. 2/3
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
We thank the President of the World Bank for visiting our country and for the support extended to us during the visit. 1/3
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Aidha ninawapongeza Wanawake wa Tanzania kwa kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali ktk maendeleo. Mungu awabariki Wanawake wote 2/2
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Nachukua nafasi hii kuwapongeza Wanawake wote ktk kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani 1/2
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Tuendelee kushikamana, kukijenga chama kwa kuisimamia Serikali ktk kuleta maendeleo kwa Watanzania.KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
HAPA KAZI TU! -
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Nawapongeza wanachama wa CCM wote na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi katika kutimiza miaka 40 ya CCM kesho tarehe 5 Februari 2017.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Ombi langu kwa Watanzania wote tuulinde,tuutunze na kuudumisha umoja wetu ktk mwaka 2017 kwa kufanya kazi kwa bidii. MUNGU IBARIKI TANZANIA.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Watanzania wenzangu,tukiwa tunakaribia kuumaliza mwaka 2016,naomba niwatakie heri ya Mwaka Mpya 2017.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
On Behalf of myself and the people of Tanzania, our deepest sympathies go out to the people of Cuba on the death of Fidel Castro.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Congratulation President-Elect Donald Trump and the People of America. Tanzanians and I assure you of continued friendship and cooperation.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Ninaahidi kuendelea kufanya kazi kwa moyo na nguvu zangu zote kwa ajili ya maendeleo ya Taifa. Mungu Ibariki Tanzania 2/2.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Ninamshukuru Mungu kufikia siku yangu ya kuzaliwa,ninawashukuru watanzania nyote kwa kuniombea.Nitafanya kazi kwa moyo&nguvu zangu zote 1/2.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Ugunduzi huu utuelekeze kujipanga hasa ktk eneo la mikataba yetu ili rasilimali hii adimu isaidie kuujenga uchumi wetu 2/2
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Tunamshukuru Mungu Tanzania tumegundua gesi aina ya Helium(He),wito wangu kwa wachumi,wanasheria na watanzania wote kwa ujumla tujipange1/2
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Ndugu zangu Waislamu tunaanza mwezi mtukufu wa Ramadhani ktk kutekeleza moja ya nguzo kuu za Uislamu,nawatakia Waislamu wote mfungo mwema.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Kesho ni siku yakupiga kura kwa ndg zetu wa Zanzibari, ninawatakia uchanguzi mwema na wenye amani na utulivu. Mungu ibariki Tanzania.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Natuma salaam zangu za pole kwa Rais Mstaafu Mh.Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kufuatia kifo cha kaka yake Mzee Selemani Mrisho Kikwete.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
I wish you a blessed holiday season. May this Christmas bring you comfort, joy, peace and happiness to last throughout the coming year!
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Tumeshiriki kwa wingi wetu siku hii muhimu kwa kufanya kazi ktk maeneo mbalimbali. Uhuru na Kazi, Hapa Kazi Tu. Mungu Ibariki Tanzania.2/2.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Watanzania wenzangu ninawapongeza kujumuika nami kwa kuadhimisha siku ya Uhuru na Jamhuri.Nimefurahi na nimeguswa sana mlivyojitokeza.1/2.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Napenda kutuma salaam zangu za pole kwa Dr Helen Kijo-Bisimba kwa ajali ya gari na kikubwa namuombea kwa Mwenyezi Mungu apone haraka.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Watanzania wenzangu, leo siku yangu ya kwanza Ofsini kama Rais wenu, nawaomba kwa pamoja tulijenge taifa letu,tofauti zetu tuziweke pembeni.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Tumushukuru Mungu, tumepata ugeni wa Nabii TB Joshua, atashiriki nasi ktk sherehe nitakapoapishwa kuwa Rais wa awamu ya Tano wa Tanzania.
-
Dr John Magufuli reposted
Narendra Modi
@narendramodi
Congratulations to President-elect of Tanzania Dr John P Magufuli on his election victory today. Also, a very happy birthday to him.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Nawashukuru watanzania kwa upendo mliouonyesha kwangu,wakati wa kampeni na kwa kura mulizonipa zimeniwezesha kuwa Rais,Mungu awabariki sana.
-
Dr John Magufuli reposted
Chama Cha Mapinduzi
@ccm_tanzania
Our next Commander-in-Chief, Dr John Pombe Magufuli, the President-elect of The United Republic of Tanzania.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Siku hii ni kubwa na muhimu ktk maisha yangu, sherehe yangu ya kuzaliwa na nimepata ridhaa ya kuwaongoza watanzania ktk nafasi ya RAIS.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Namshukuru Mwenyezi Mungu kunifikisha siku hii adhimu ya leo siku yangu ya kuzaliwa. Ombi langu,tuilinde Amani yetu. MUNGU IBARIKI TANZANIA.
-
Dr John Magufuli reposted
Chama Cha Mapinduzi
@ccm_tanzania
#taarifaoktoba26
Tunawaomba wana-CCM watulie, wasiwe na hofu, wawe na subira hadi Tume imalize kazi yake. -
Dr John Magufuli reposted
Chama Cha Mapinduzi
@ccm_tanzania
Uchaguzi ni siku 1. Tanzania ipo siku zote. Tutunze amani na tumtangulize Mungu. Yeye anajua yote. - Dkt @MagufuliJP
-
Dr John Magufuli reposted
Chama Cha Mapinduzi
@ccm_tanzania
Tumshukuru Mungu tumeifikia siku hii. Nimetimiza wajibu wangu, sote tupige kura, demokrasia iamue. - Dkt @MagufuliJP
-
Dr John Magufuli reposted
Chama Cha Mapinduzi
@ccm_tanzania
Dkt @MagufuliJP atapiga kura katika kituo cha Shule ya Msingi Magufuli, kijiji cha Rubambangwe, kata ya Muungano, jimbo la Chato.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Tutaiboresha Bandari ya Mwanza na kukipanua Kiwanja cha Ndege cha Mwanza hususan jengo la abiria ili lifikie kiwango cha kimataifa.
-
Dr John Magufuli reposted
Chama Cha Mapinduzi
@ccm_tanzania
Leo Oktoba 24 2015, Dkt @MagufuliJP anafanya mkutano kuhitimisha kampeni toka uwanja wa CCM Kirumba, Jijini Mwanza.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Ndugu wananchi ninawakaribisha nyote ktk Uwanja wa CCM Kirumba,Mwanza nitakapofanya mkutano wa kufunga kampeni leo Oktoba 24,saa 10 jioni.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Leo Oktoba 23, saa 10 jioni nitafanya mkutano wa kufunga kampeni kwa mkoa wa Dar Es Salaam katika Uwanja wa Jangwani. Nawakaribisha nyote.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Nitajenga uchumi utakaokua kwa kasi nzuri na utakaobadilisha maisha ya watu masikini. Utakuwa ni uchumi utakaoleta maisha bora ya watu.
-
Dr John Magufuli reposted
Chama Cha Mapinduzi
@ccm_tanzania
Ujumbe wa Mama Maria Nyerere kuhusu Jumapili, Oktoba 25, 2015: youtu.be/8cfcNscJ8yM #ujumbekutokabutiama #chaguolawananchi
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Tutaanza ujenzi wa reli ya Dar es Salaam – Tabora – Kigoma/Mwanza kwa kiwango cha kimataifa (standard gauge).
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Tutaijenga Barabara ya Pete "Dar Outer Ring Road": Pugu –Mbezi–Mpiji Magoe–Bunju (km 33.7) kupunguza msongamano Dsm.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Tutakamilisha ukarabati/ujenzi wa barabara zote unaoendelea/umekwishaanza kwa lami ktk barabara kuu na za mikoa.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Naomba kura yako ya ndiyo tarehe 25 Oktoba 2015 tuipeleke nchi yetu mbele. Nakuahidi sitakuangusha. Mungu akubariki.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Tutaweka mazingira yatakayowezesha Taasisi za Fedha kutoa fursa kwa wananchi kupata mikopo kwa riba nafuu.
-
Dr John Magufuli reposted
Chama Cha Mapinduzi
@ccm_tanzania
Dkt @MagufuliJP akifanya sala fupi kwenye makaburi ya Babu & Bibi yake kijijini Katoma,njiani kuendelea na mikutano.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Tutaboresha huduma ya upatikanaji wa Maji Mijini na Miji Mikuu ya Mikoa kutoka asilimia 86 (2015) hadi 95 (2020).
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Tutajenga viwanda vya pamba na vile vitokanavyo na mazao ya mifugo, ninajua Ngudu ni wafugaji na wakulima wa pamba.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Nakumbuka kuzijenga barabara za Jiji la Mwanza, wananchi waliguswa na kunizawadia chui aliyekaushwa. NINAWASHUKURU.
-
Dr John Magufuli reposted
Chama Cha Mapinduzi
@ccm_tanzania
Uwanja wa Furahisha, jimbo la Ilemela Mwanza. Dkt @MagufuliJP akizungumza na wananchi jioni ya leo. #umojaniushindi
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Sijawahi kupokelewa na umati mkubwa wa watu Jijini Mwanza kiasi hiki, nawashukuru kwa kukiamini Chama cha Mapinduzi.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Leo nitashiriki na watanzania kuuaga Miili ya Marehemu Deo Filikunjombe na wenzake. Mungu aziweke pema peponi roho za marehemu, Amen.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Kampeni zangu Jimboni Ludewa nililala nyumbani kwa Deo Filikunjombe, napata shida kuamini kama hatunaye tena. Tutakosa utumishi wake mahiri.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Natoa pole kwa Mh.Jerry Silaa kwa kuondokewa na baba yake mzazi Capt.William Silaa. Mungu awape familia moyo wa subira na uvumilivu.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Kwa masikitiko makubwa nimepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa za kifo cha Deo Filikunjombe.Mungu aipe familia yake moyo wa subira na uvumilivu
-
Dr John Magufuli reposted
Chama Cha Mapinduzi
@ccm_tanzania
Nitaunda Baraza la Mawaziri waadilifu, wawajibikaji, sio 'njoo kesho', 'tuko kwenye mkutano', tuko kwenye mchakato'.
-
Dr John Magufuli reposted
Chama Cha Mapinduzi
@ccm_tanzania
Sihitaji utajiri, siutafuti. Miaka yote nimekuwa muadilifu na kumtanguliza Mungu katika kuwatumikia. Nitabaki kuwa hivyo. - Dkt @MagufuliJP
-
Dr John Magufuli reposted
Chama Cha Mapinduzi
@ccm_tanzania
Leo saa 7 mchana Dkt @MagufuliJP ameshuhudia uwekaji sahihi wa ujenzi wa Flyover ya TAZARA. #hapakazitu
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Nimepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa za kifo cha Dkt.Emmanuel Makaidi. Mungu aipe familia yake moyo wa subira na uvumilivu wakati huu mgumu.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Nitaunda serikali ndogo ya watu makini,waadilifu,wachapakazi,werevu na walio tayari kushughulikia kero za wananchi.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Leo ni siku muhimu,tutafakari namna tunavyoziishi fikra za Mwl.Nyerere,alipinga Rushwa &Ufisadi,alikataa mali&utajiri kuwa sifa ya uongozi.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Tutaelekeza nguvu zetu ujenzi barabara ya Dar es Salaam – Chalinze (km128) njia sita kwa viwango vya “Expressway”.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Ndugu yetu Dkt Abdallah Kigoda hatunaye tena. Moyo na sala zangu viko pamoja na familia yake na wana Handeni katika kipindi hiki kigumu.
-
Dr John Magufuli reposted
Chama Cha Mapinduzi
@ccm_tanzania
Wataalamu hao wazalendo katika uchumi, biashara, utawala & sheria, wanatoka taasisi za elimu ya juu, asasi zisizo za kiraia & sekta binafsi.
-
Dr John Magufuli reposted
Chama Cha Mapinduzi
@ccm_tanzania
Dkt. Magufuli, ameunda jopo la wanataaluma na wataalamu huru magwiji kwa ajili ya maandalizi ya kufanya mabadiliko makubwa Serikalini.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Tutajenga Barabara za Juu (Flyovers) Dsm, kwenye makutano:
• Chang’ombe
• Uhasibu
• KAMATA
• Morocco
• Mwenge
• Magomeni
• Tabata
3/3. -
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Tutajenga makutano ya barabara ya Ubungo (Ubungo Interchange) & mradi wa BRT umekamilika.www.youtube.com/watch?v=7eTffANxShQ 2/3
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Tutapunguza msongamano wa magari katika Jiji la Dar Es Salaam kwa kujenga TAZARA Flyover. www.youtube.com/watch?v=eFIq5tneqKk 1/3
-
Dr John Magufuli reposted
Chama Cha Mapinduzi
@ccm_tanzania
Mjini Moshi, Dkt @MagufuliJP amewapokea wanachama wa upinzani waliohamia CCM, wakiongozwa na Katibu wa Chadema jimbo la Hai, Jubilant Lema.
-
Dr John Magufuli reposted
Chama Cha Mapinduzi
@ccm_tanzania
Mazungumzo ya Dkt @MagufuliJP na wananchi Moshi leo yamegusia ajira, viwanda, utalii, miundombinu, afya, elimu, ardhi na umoja wa kitaifa.
-
Dr John Magufuli reposted
Chama Cha Mapinduzi
@ccm_tanzania
Mafisadi hata ndani ya CCM wapo, na inahitaji mtu ambaye ni shujaa kulisema hili. Mmeona wameanza kutoka nilipochaguliwa. - Dkt @MagufuliJP
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Kuna viwanda vilibinafsishwa sasa wahusika wasipoviendeleza wajiandae kuvirudisha haraka,azma ya Serikali ni Viwanda viongeze ajira kwa 40%.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Nitahakikisha kasi ya ukuaji wa uchumi inamfikia kila mmoja, serikali yangu itawajibika kwa wananchi hasa wanyonge.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Mch. Christopher Mtikila. Mungu, Mwingi wa Rehema awape moyo wa uvumilivu Wanafamilia.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Ili kukata kiu ya watanzania ya kutaka mabadiliko,nitaleta maendeleo yenye sura ya Umoja wa Kitaifa bila kubagua dini,kabila,rangi &itikadi.
-
Dr John Magufuli reposted
Chama Cha Mapinduzi
@ccm_tanzania
Kondoa tuliahidi barabara ya lami 261km, Babati-Dodoma. Nyote mmeona kazi hiyo inaelekea kukamilika. Tukiahidi, tunatimiza. -Dkt @MagufuliJP
-
Dr John Magufuli reposted
Chama Cha Mapinduzi
@ccm_tanzania
Asilimia mbili ya Watanzania ni wazee. Kuanzia mwaka 2016 tutaanza kuwapa pensheni ya kujikimu.- Dkt @MagufuliJP #tukiahiditunatimiza
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Nitakuwa rafiki mkubwa wa mama ntilie, wafanyabiashara ndogondogo na wakulima. Tutaongeza Ajira kwa Vijana-Singida.
-
Dr John Magufuli reposted
Chama Cha Mapinduzi
@ccm_tanzania
Tusikabidhi nchi katika mikono ya mafisadi. Wataiuza. Watanzania bila kujali vyama nahitaji kura zenu, tuungane kwa maendeleo. - @MagufuliJP
-
Dr John Magufuli reposted
Chama Cha Mapinduzi
@ccm_tanzania
2003, Singida haikuwa na hata 1km ya lami. Katika kipindi cha miaka 10 zimejengwa 474km za lami. Tutafanya zaidi ya haya. - @MagufuliJP
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Kama serikali chini ya CCM mengi tumefanya na kutekeleza na tunaendelea. Mwezi jana Daraja la Kikwete limefunguliwa.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Nawashukuru wazee wangu, Joseph Warioba na John Malecela kwa kushiriki nami ktk kampeni za kuinadi Ilani ya CCM-2015.
-
Dr John Magufuli reposted
Chama Cha Mapinduzi
@ccm_tanzania
Sehemu ya wananchi wa Dodoma mjini waliojitokeza kumsikiliza Dkt @MagufuliJP, uwanja wa Jamhuri. #umojaniushindi
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Tutaongeza kasi kuwapatia wafanyabiashara wadogo maeneo ya kufanyia biashara,leseni na mikopo yenye masharti nafuu.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Wawekezaji Wakubwa & Kati wa ndani na nje ya nchi ktk viwanda tutaendelea kuwawekea mazingira bora"best practice"kama yalivyo duniani kote.
-
Dr John Magufuli reposted
Chama Cha Mapinduzi
@ccm_tanzania
Sehemu ya wananchi wa mji wa Iringa waliohudhuria mkutano wa Dkt @MagufuliJP katika uwanja wa CCM Samora. #hapakazitu
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Mafanikio ya Serikali: Kivuko cha Mv Malagarasi Kipya na cha Zamani. Vivuko vya Serikali vimeongezeka na kufikia 28.
-
Dr John Magufuli reposted
Chama Cha Mapinduzi
@ccm_tanzania
Walikuja kuomba udhamini wakawahonga. Mimi sikuwahonga hata senti tano. Aliyeona unafaa kununuliwa, hatashindwa kukuuza. Dkt - @MagufuliJP
-
Dr John Magufuli reposted
Chama Cha Mapinduzi
@ccm_tanzania
Hatuwezi kukaa Shinyanga yenye ng’ombe bila kuwa na kiwanda cha nyama. Kiwanda kitawezesha Watanzania wengi kupata ajira. - @MagufuliJP
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Kina mama wanaweza,mwaka 1995,mama Anna Abdallah alinipokea na kunifundisha kazi kama N/Waziri wake wizara ya Ujenzi.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Ili kila mtanzania mmojammoja afaidike na rasilimali ya madini,ni dhahili wachimbaji wakubwa, wakati na wadogowadogo wote wapewe fursa sawa.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Mhe Celina Ompeshi Kombani.MUNGU awape moyo wa uvumilivu na subira kipindi hiki kigumu.
-
Dr John Magufuli reposted
Chama Cha Mapinduzi
@ccm_tanzania
Sehemu ya mkutano wa Dkt @MagufuliJP na wananchi mjini Geita siku ya leo, Septemba 23, 2015. #hapakazitu
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Watanzania wenzangu,nawatakia mapumziko mema ya Sikukuu ya Eid el Hajj. Serikali yangu italinda uhuru wa kuabudu kwa dini na madhehebu yote.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Nimefurahi kukutana na kijana mwenye kipaji wa darasa la nne aliyenichora sura nilipofanya kampeni Muleba.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Wananchi wa Bukoba nimefarijika pasipo na wasiwasi kwa namna mlivyojitokeza kwa wingi kukiunga Chama Cha Mapinduzi.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Rais mstaafu Mkapa na Rais Kikwete kwa namna ya pekee nawashukuru kwa kunipa nafasi kama Waziri ktk Serikali zao.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Nawakaribisha nyote kujumuika nasi mchana wa kesho Septemba 20, katika muendelezo wa kampeni za Chama Cha Mapinduzi zitakazofanyika Chato.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Tutaboresha njia za kuongeza mapato - wawekazaji wakubwa wote walipe kodi inavyopasa na madini walipe mapato stahili.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Ulinzi na Usalama: Tutapambana na changamoto kubwa likiwemo jukumu la kudumisha amani na utulivu.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Tutajenga barabara za Nyahua-Chaya(km 85),Urambo – Kaliua(km 33) na Chagu – Kazilambwa(Kigoma/Tabora )(km 40) kuiunganisha Tabora na Kigoma.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Tutaunda Serikali yenye nidhamu na uwajibikaji na rafiki wa wafanyakazi sanjari na kuboresha mishahara/marupurupu.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Mwaka 1978 - nikiwa na umri wa miaka 19, Kidato cha Nne katika shule ya Sekondari ya Lake, Mwanza.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Shilingi milioni 50 kwa kila Kijiji - Kukopesha vikundi vya wajasiriamali kupitia Ushirika wa Kuweka na Kukopa.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Nimefikishiwa kero kwa mabango yenye ujumbe wa aina mbalimbali. Ilani ya CCM ni njia pekee yenye kutatua kero hizo.
-
Dr John Magufuli reposted
Chama Cha Mapinduzi
@ccm_tanzania
Pongezi kwa Sheikh Aboubakar Zuberi kwa kuchaguliwa kuwa Mufti Mkuu wa Tanzania. Mungu amjalie hekima na afya katika kutimiza majukumu yake.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Wananchi Mkoa wa Simiyu ni wafugaji na wakulima wakubwa wa zao la pamba- tutasimamia upya sekta hii ili iwe na tija.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Nakumbuka mwaka 1995, Mzee Mkapa alipita Chato kuniombea kura na ndiyo ukawa mwanzo wangu kuingia katika siasa.
-
Dr John Magufuli reposted
Chama Cha Mapinduzi
@ccm_tanzania
Jeshi la Kujenga Taifa, Makutopora mwaka 1983. @MagufuliJP akiwa na miaka 24, katika mafunzo ya kijeshi. #hapakazitu
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Hakika sitawasahau wananchi wa Mkoa wa Mara kwa namna walivyonipokea nilipopita kuinadi Ilani ya CCM. SITAWAANGUSHA!
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Nikiwa Butiama, nimepata heshima kubwa ya kupewa kifimbo na Chief Japhet Wanzagi kwa niaba ya Wazee wa Butiama.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Nitaitekeleza Ilani ya CCM "Ukurasa kwa Ukurasa"- nimefanya Mkutano Butiama na kutembelea kaburi la Baba wa Taifa.
-
Dr John Magufuli reposted
January Makamba
@JMakamba
Yesterday I had the pleasure of welcoming @MagufuliJP, the next President of Tanzania, in my constituency.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Nimehitimisha kampeni Mkoani Tanga, ahadi kubwa ni kuufanya tena Mji wa Tanga kuwa wa Viwanda ikiwemo kuvifufua vilivyokufa. ASANTENI TANGA.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Barabara ya Soni hadi Bumbuli (km 22) ina jiografia ngumu ya mawasiliano, tutaijenga kwa kiwango cha lami - Bumbuli.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Natambua Tanga ulikuwa Mji wa Viwanda, bahati mbaya viwanda hivyo vimebaki kuwa magofu - serikali yangu itavifufua.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Serikali ya Awamu ya Tano - Elimu ya bure kuanzia darasa la kwanza hadi Kidato cha Nne.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Wananchi wamekuwa wakinipokea na mabango wakinitaka niwatatulie kero zao, yote hayo nitayasimamia - Mvomero.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Morogoro - sitamuonea mtu, ila nitafuta mashamba pori yaliyotelekezwa au kutoendelezwa ili yagawiwe kwa wananchi.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Kampeni Ifakara, nimepata mapokezi makubwa. Nitatatua tatizo sugu la ugomvi kati ya wakulima na wafugaji.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Barabara ya Dodoma – Manyoni (km 127) na Manyoni – Singida (km 118) kabla na baada ya ujenzi kwa kiwango cha lami.
-
Dr John Magufuli reposted
Chama Cha Mapinduzi
@ccm_tanzania
1991 Chuo Kikuu - Dar, @MagufuliJP kushoto akifanya Shahada ya Uzamili - Kemia. Kulia ni rafikiye, Christopher Kadio.
-
Dr John Magufuli reposted
Chama Cha Mapinduzi
@ccm_tanzania
Dokta @MagufuliJP akiongea na Husna Mikidadi, binti mwenye ualbino wakati akimalizia mkutano wake Mtwara jana jioni.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Tangu nianze kampeni nimetembea kwa barabara takriban kilomita 4885 lengo nijumuike na wananchi ili nijue kero na changamoto zinazowakabiri.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Tutakamilisha ukarabati na ujenzi kwa kiwango cha lami unaoendelea/umekwishaanza barabara ya Mtwara hadi Mbamba Bay
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Serikali nitakayoingoza itaendelea kuwalinda na kuwatambua Walemavu wote nchini ikiwemo kukomesha kabisa mila potofu.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
"Halmashauri zitahakikisha wazee wanatambuliwa na kupewa matibabu bure katika hospitali za Serikali"ILANI YA CCM 2015
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Nimeendelea na kampeni mkoani Mbeya, tumepata mapokezi makubwa Jijini Mbeya. Wananchi wananiamini na kuiamini CCM.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Nimefanya kampeni Makongolosi na Chunya na nikafanikiwa kusafiri kupitia barabara ya Makongolosi hadi Chunya (km 36).
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Nawashukuru wananchi wa Mbalizi kwa kuniamini na kukiamini Chama cha Mapinduzi ili kiendelee kushika dola.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Nimefarijika kuona wananchi wa Halmashauri ya Mji wa Tunduma wameendelea kuniamini na kukiamini Chama cha Mapinduzi.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Nimepata mapokezi makubwa ya kihistoria Mkoani Rukwa, asanteni sana. Ahadi, tutamalizia ujenzi wa barabara kutoka Sumbawanga hadi Kigoma.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Nawashukuru wananchi wa Mpanda kwa kuniunga mkono nilipopita kuinadi Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Leo tarehe 23 Agosti 2015 , nitaongea na watanzania namna nitakavyoitekeleza Ilani ya CCM ya mwaka 2015-2020 kwa vitendo.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Mwaka 2004 niliwaahidi watanzania watasafiri kutoka Mtwara hadi Bukoba kwa taxi kwa barabara ya lami, ahadi hii nimeitimiza kikamilifu.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Nawakaribisha nyote kujumuika nasi mchana wa leo Agosti 23, katika uzinduzi wa kampeni za Chama Cha Mapinduzi kwenye viwanja vya Jangwani.
-
Dr John Magufuli reposted
Chama Cha Mapinduzi
@ccm_tanzania
Usikose kujumuika pamoja nasi kesho kwenye uzinduzi wa kampeni katika viwanja vya Jangwani.
#umojaniushindi
youtu.be/yfkdbS0yTPQ -
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Ukaguzi ujenzi wa Daraja - Kigamboni
Barabara: 6
Urefu: Mita 680
Upana: Mita 27.5
Muundo: Cable-Stayed
#tunatekeleza -
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Tumezindua kivuko cha MV Mafanikio kinachounganisha Semo-Msangamkuu, Mtwara. Mradi huu umegharimu TZS bilioni 3.3.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Tatizo la barabara ya Ndundu - Somanga mkoani Lindi sasa ni historia, jana Agosti 7 imekamilika na tumeizindua rasmi.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Watanzania wako makini na mustakabali wa nchi yao, wana imani kubwa na Chama Cha Mapinduzi, na watakipa ushindi ili kiendelee kuwatumikia.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Ndugu zangu, sitawaangusha, na nitawatumikia ipasavyo. Rekodi yangu katika hilo iko wazi na dhahiri. Nitaeleza mengi kampeni zitakapoanza.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
3. Mpango huu utatupa faida mbili; kwanza utapunguza msongamano Dar Es Salaam na pili utasaidia kuzuia uharibifu wa barabara zetu. - JPM
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
2. Badala ya magari ya mizigo kuingia Dar Es Salaam, utaratibu uwe kwamba yatachukua mizigo toka Ruvu itakapopelekwa kwa njia ya reli. - JPM
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
1. Kama Waziri wa Ujenzi ningependa tuboresha na kutumia reli kusafirisha mizigo toka Bandari ya Dar Es Salaam hadi eneo la Ruvu. - JPM
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Utumishi = Kujifunza + Kujitoa. Miaka 40 iliyopita, Machi 1975 nikiwa mwanafunzi, Kidato cha Kwanza Katoke Seminari.
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Ndugu zangu, mimi si mkali bali ninawachukia sana watendaji wa serikali wasiotimiza wajibu wao; watumishi wa namna hiyo hawavumiliki. - JPM
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Watanzania wote wanahitaji maendeleo. Watanzania hawapendi kulalamika, wanahitaji kiongozi atayechapa kazi sawa sawa kutatua kero zao. - JPM
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Tumeungana pamoja, Chama Cha Mapinduzi ni kundi moja lenye nia moja ya kutumikia Watanzania kwa umoja na uimara wake. #umojaniushindi - JPM
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Nasema haya kutoka moyoni, nasema haya kwa dhati kabisa. Nawahakikishia nitakuwa nanyi, nitakuwa mtumishi wenu kweli kweli. - JPM
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Sasa ni wakati wa ndugu zangu watia nia wote 37, kuungana kupeperusha bendera ya Chama, kushinda kwa kishindo & kuwatumikia wananchi. - JPM
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Idadi ya kura za Wajumbe katika kunipitisha kuwa Mgombea Urais ni uthibitisho wazi kwamba CCM ni moja, na wana CCM ni wamoja. - JPM
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Nitumeni, nami nitawatumikia. Nakishukuru Chama Cha Mapinduzi, kwamba kimekubali kunituma kuomba ridhaa ya kuwatumikia Watanzania. - JPM
-
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Nimepewa heshima kubwa sana na dhahiri. Naahidi kuilipa heshima hii kwa kuinadi na kuitekeleza Ilani ya CCM katika kujenga Taifa letu. - JPM














































































































