HABARI:
Rais wa Kenya, William Ruto, amemnyoshea kidole mtangulizi wake, Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta, akihusisha changamoto za ufisadi zilizoibuliwa katika ripoti ya Benki ya Dunia na masuala yaliyotokea wakati wa uongozi wa serikali zilizopita, ikiwemo utekelezaji wa Mradi wa Reli ya Kisasa (SGR).
Kauli hiyo ya Ruto imekuja wakati utawala wake ukikabiliwa na ukosoaji kuhusu hali ya rushwa nchini Kenya, kufuatia ripoti ya Benki ya Dunia iliyoiweka nchi hiyo miongoni mwa mataifa yanayokabiliwa na kiwango kikubwa cha ufisadi.
Akizungumza katika Kanisa la St. Mary’s, Kaunti ya Narok, Jumapili, Novemba 15, 2026, Ruto amepinga juhudi za kumhusisha na changamoto zinazohusishwa na mradi wa SGR, akisisitiza kuwa ujenzi wa reli hiyo ulifanyika kabla ya yeye kushika madaraka ya urais.
Ameeleza kuwa si sahihi kumtwisha lawama za mradi huo, huku akidokeza kuwa baadhi ya watu wanaomkosoa huenda wana maslahi binafsi katika fedha zilizotumika kuutekeleza.
“Ripoti pia inaeleza changamoto zilizohusiana na SGR huko nyuma. Wanaojaribu kunilaumu wanapaswa kuelewa kuwa si mimi niliyejenga SGR. Kuna mambo mengi yanayosemwa, na huenda baadhi ya wanaotoa tuhuma hizo wana maslahi yanayohusiana na fedha za SGR,” amesema Ruto.
Rais Ruto pia amesisitiza kuwa Serikali yake haikupinga kuchapishwa kwa ripoti hiyo, bali ilihimiza iwekwe wazi ili wananchi wapate fursa ya kuelewa changamoto mbalimbali zinazoikabili nchi kiuchumi na kiutawala.
Amesema kuwekwa wazi kwa ripoti hiyo kunalenga kuongeza uelewa wa umma kuhusu hali halisi ya nchi, lakini amewashutumu baadhi ya wakosoaji wake kwa kuchukua sehemu moja ya ripoti na kuitumia kutoa hitimisho kuhusu utendaji wa Serikali yake bila kuzingatia maudhui yake yote.
Kwa mujibu wa Ruto, ripoti hiyo inaibua masuala mbalimbali yanayopaswa kuchambuliwa kwa upana, badala ya kuangazia kipengele kimoja pekee na kukitumia kama msingi wa kuhukumu utawala wake.
Peter Msigwa
Peter Simon Msigwa (born 8 June 1965) is a Tanzanian politician and Member of Parliament for Iringa Town constituency for two consecutive terms since 2010. Although he was formerly a member of CHADEMA, he joined the ruling party CCM in June 2024. More on Wikipedia
-
Jambo TV
@Jambotv_
-
Jambo TV
@Jambotv_
Mwanamuziki na mfalme wa mashairi nchini Tanzania, Selemani Msindi maarufu kama Afande Sele amedai kuwekwa kando na kuzuiwa kuendelea kutumbuiza kwenye tamasha la Miaka 30 ya Bongo Fleva kutokana na hatua yake ya kuzungumzia na kuwakumbuka watu waliotangulia mbele za haki wakati wa matukio ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025.
Katika tamasha hilo la Miaka 30 ya Bongo Fleva lililofanyika tarehe 7 Novemba 2026 mkoani Mbeya, Afande Sele alipanda jukwaani na kuimba akiwasihi wananchi kuwaombea na kuwakumbuka waliotangulia mbele za haki, akisisitiza kuwa matukio ya Oktoba 29 hayasauliki. Hata hivyo, amedai waandaaji wa tamasha hilo wameelekezwa asiruhusiwe kuendelea kuwepo kwenye maonesho yanayofuata.
Akizungumza na Jambo TV, Afande Sele amedai kuwa alitakiwa kuueleza umma kwa kusema kuwa ana dharura au yuko ‘bize’ ili kuficha sababu halisi ya kuachwa kwake. Hata hivyo, amekataa katakata mpango huo akisisitiza kuwa muziki ndiyo kazi yake kuu inayomlisha na kuwa hawezi kuwahadaa wananchi
Afande Sele amebainisha kuwa kuongelea kwake matukio ya Oktoba 29 hakukuwa na nia ya kumtuhumu yeyote bali kulilenga kuiondoa taswira iliyokuwepo kuwa tamasha hilo lilikuwa la ‘machawa’ pamoja na kuitetea serikali ambayo nayo yenyewe imekiri kuwepo kwa matukio hayo na kuunda tume za uchunguzi.
“Niliongea ili kuhakikisha kwamba watu hawachukulii kama ni ‘show’ ya machawa. Naitetea show pia, lakini pia natetea nchi... Mimi sijasema kama nani kaua, sijasema hivyo... hata mimi nasubiri uchunguzi na tume zinaundwa kutafuta ukweli”, ameeleza Afande Sele.
Tamasha lijalo la Miaka 30 ya Bongo Fleva litafanyika wilayani Kahama mkoani Shinyanga tarehe 27 Novemba 2026 ambapo katika mabango ya matangazo ya orodha ya wasanii watakaotumbuiza picha ya Afande Sele haijaonekana. Hata hivyo, akizungumza na Jambo TV kwa njia ya simu, Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki na mmoja wa waratibu wa tamasha la Miaka 30 ya Bongo Fleva, Hamisi Taletale (Babu Tale), amesema kutokuwepo kwa Afande Sele kwenye orodha hiyo hakuhusiana na mambo aliyoyazungumza jukwaani katika tamasha lililopita, bali unatokana na utaratibu wa kawaida wa kubadilisha na kuwapunguza wasanii kulingana...soma zaidi jambo.co.tz -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Jumanne Sagini amewataka madereva wa bajaji na wafanyabiashara wadogo (machinga) jijini humo kuzingatia taratibu zilizowekwa na Serikali katika upangaji wa jiji, huku akiwaagiza wasimamizi wa sheria kutumia busara na ubinadamu wanapotekeleza maelekezo hayo kwa wananchi wanaotafuta riziki.
Sagini ametoa kauli hiyo leo, Novemba 15, 2026, alipokutana na kuzungumza na makundi hayo katika eneo la Kabwe jijini Mbeya, kufuatia kuanza kutekelezwa kwa agizo la kuwaondoa waendesha bajaji kwenye Barabara Kuu ya TANZAM pamoja na uhamishaji wa wafanyabiashara wadogo.
Katika mkutano huo, dereva wa bajaji, Hasani Kazia ameeleza kuwa madereva wamekubali agizo la kuondoka kwenye barabara kuu, lakini wanakabiliwa na changamoto katika maeneo ya Iyunga na Uyole ambako baadhi ya njia hazina barabara za pembeni. Alidai kuwa wanapoingia barabara kuu kwa lengo la kuvuka tu ili kuwafikisha abiria upande wa pili, hukamatwa na kudaiwa Shilingi 10,000 kwa madai kuwa wamekatazwa kabisa kuigusa barabara hiyo.
Akijibu malalamiko hayo, Sagini amekiri kuwa haiwezekani dereva aliyebeba abiria kutoka upande mmoja wa barabara kuu kwenda mwingine kuvuka bila kuitumia barabara hiyo, akitolea mfano wa abiria anayekwenda Hoteli ya Royal Mgwasi ambako dereva hulazimika kuvuka ili kuingia barabara ya pembeni. Amewaagiza askari na wasimamizi wa sheria kutumia busara na kuepuka matumizi ya nguvu au faini zisizo za haki zinazowaumiza watafutaji.
Katika hatua nyingine, Sagini amewataka machinga wanaofanya biashara eneo la Kabwe kutekeleza agizo la kuhamia katika Uwanja wa Ndege wa Zamani, akibainisha kuwa muda wa mwisho uliotangazwa ulimalizika jana, Novemba 14, 2026. Amesema hataki kutumia vyombo vya dola kuwaondoa kwa nguvu kwa kuwa anawachukulia kama ndugu na watoto wake.
Kwa upande wao, mmoja wa wafanyabiashara hao amesema hawapingi kuhamia katika eneo hilo jipya, lakini ameeleza wasiwasi wao kuwa Uwanja wa Ndege wa Zamani una changamoto ya mzunguko mdogo wa biashara ikilinganishwa na Kabwe ambako kuna mkusanyiko mkubwa wa wateja.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Wazazi na walezi wanaoishi na watu wenye ulemavu wametakiwa kutoigeuza misaada inayotolewa kwa ajili ya kuwasaidia watu hao kuwa fursa ya kufanya biashara, badala yake wanapaswa kuhakikisha misaada hiyo inatumika kulingana na mahitaji halisi ya walengwa.
Wito huo umetolewa leo Novemba 15, 2026, na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Regina Ndege Qwaray wakati akitoa msaada kwa watu zaidi ya 100 wenye mahitaji maalumu wilayani Babati mkoani Manyara.
Regina amesema kuwa misaada inayotolewa kwa watu wenye ulemavu inalenga kuboresha maisha yao na kuwasaidia kukabiliana na changamoto mbalimbali wanazokutana nazo katika shughuli zao za kila siku, hivyo ni wajibu wa wazazi na walezi kuhakikisha inawafikia walengwa na kutumika kwa malengo yaliyokusudiwa.
Aidha, amewataka wazazi na walezi kuwa na moyo wa kujali na kuwapa kipaumbele watu wenye mahitaji maalumu kwa kuhakikisha wanapata huduma na mahitaji muhimu badala ya kutumia fursa ya misaada hiyo kwa manufaa binafsi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi amesisitiza kuwa matumizi ya nishati safi ya kupikia yana faida kubwa kwa afya za wananchi, utunzaji wa mazingira, na uchumi wa kaya, akibainisha kuwa gesi ya kupikia huondoa athari za moshi wa kuni na mkaa pamoja na kupunguza gharama za maisha.
Ndejembi ametoa kauli hiyo leo Jumapili wakati akishiriki zoezi la ugawaji wa sehemu ya mitungi 750 ya gesi yenye ujazo wa kilo sita kwa wananchi wa Jimbo la Mchinga, mkoani Lindi. Mitungi hiyo imetolewa kupitia ushirikiano kati ya kampuni ya Lake Gas (chini ya Lake Group) na Mbunge wa jimbo hilo, Salma Kikwete.
Akizungumza na wananchi katika hafla hiyo, Makamu wa Rais ameeleza kuwa kuhamia kwenye matumizi ya gesi kutapunguza kwa kiasi kikubwa ukataji wa miti na uharibifu wa mazingira, huku kukiwakinga wananchi hususan wanawake dhidi ya magonjwa yatokanayo na kuvuta moshi mzito jikoni.
“Mitungi hii ya gesi na nishati safi ya kupikia inaenda kulinda afya zetu. Badala ya kupika kwa kutumia mkaa na kuvuta moshi wote unaotokana na upishi, sasa tunaenda kutumia nishati safi ambayo haitadhuru afya zetu,” amesema Ndejembi akiongeza kuwa gesi pia ni nafuu kiuchumi na husaidia familia kuokoa fedha ikilinganishwa na gharama za kununua mkaa kila siku.
Awali, Mbunge wa Jimbo la Mchinga, Salma Kikwete amebainisha kuwa ushirikiano wa karibu kati yake na kampuni ya Lake Gas ndio uliowezesha upatikanaji wa mitungi hiyo kwa wananchi wake, ambapo pande zote mbili zilichangia kufanikisha mpango huo. Amesema hatua hiyo inaunga mkono moja kwa moja juhudi na maono ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuhamasisha mapinduzi ya nishati safi nchini.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mauzo na Masoko wa Lake Gas Tanzania, Sadiq Sabri ameeleza kuwa mchango huo ni sehemu ya mkakati wa kampuni hiyo kusaidia Serikali kufikia lengo la kitaifa la kuhakikisha asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2034.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Viongozi wa Chama cha ACT Wazalendo katika Wilaya ya Makambako, mkoa wa Njombe, wameeleza wazi hofu na mashaka makubwa yanayowakabili wanachama na viongozi wa ngazi za chini katika kuendelea na shughuli za kisiasa, kufuatia matukio ya yaliyotokea tarehe Oktoba 29, 2025.
Hayo yamebainishwa katika kikao cha ndani cha chama hicho kilichofanyika leo Jumapili wilayani Makambako, ambapo mmoja wa viongozi wa eneo hilo alieleza kuwa wanachama wanajisi hatari kubwa na kuogopa kujihusisha na siasa kutokana na yale yaliyojiri siku hiyo, huku akihoji mikango na hatua zilizochukuliwa na uongozi wa juu kuwalinda wanachama wao.
Akijibu hoja hiyo, Kiongozi wa Chama hicho, Dorothy Semu amewatoa hofu wanachama na kusisitiza kuwa chama kipo pamoja nao na kinafuatilia kwa karibu ili kuhakikisha hakuna mwanachama anayeachwa peke yake anapokumbwa na madhila yatokanayo na shughuli za kisiasa.
Semu amekiri kuwa hali ya kisiasa nchini imekuwa ngumu, ambapo watu wengi wameumizwa, mali na biashara zimeharibiwa, familia zimetatizika kiuchumi, huku wengine wakipoteza maisha au kupotea katika mazingira ya kutatanisha. Ameongeza kuwa uhuru wa kutoa maoni na kujadili masuala ya kisiasa umegeuka kuwa jambo la hatari, na kwamba chama kinasimamia msimamo wa kudai ukweli, haki, na uwajibikaji, pamoja na kuachiliwa huru kwa wafungwa wote wa kisiasa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Maboresho yaliyofanyika katika Bandari ya Mtwara yameanza kuleta manufaa kwa wananchi, yakiongeza fursa za ajira, biashara na vipato kwa wajasiriamali wadogo, madereva na wafanyakazi wengine.
Akizungumza katika mahojiano maalumu yaliyofanyika hivi karibuni bandarini hapo, mfanyakazi wa Idara ya Zimamoto, Irine Nguli, amesema ongezeko la shughuli za bandari limeongeza ajira za kudumu na za msimu kwa vijana, huku biashara za baba na mama lishe pamoja na huduma za bodaboda zikinufaika.
Amesema pia ajira hizo zimechangia kupunguza uhalifu mitaani kwa kuwafanya vijana wengi kujishughulisha na kazi.
Kwa upande wake, dereva wa Kampuni ya Dangote, Rashidi Harouni, amesema maboresho ya Gati Namba Nne yamerahisisha usafirishaji wa saruji kwenda Msumbiji, Comoro na Zanzibar, huku yakifungua fursa kwa madereva kusafirisha magari kwenda nchi jirani.
Naye mfanyakazi wa shughuli za ubaharia bandarini hapo, Gabriel Jarome, amesema maboresho hayo yamemuwezesha kuongeza kipato, kujenga mahusiano na mawakala wa meli na kujifunza ujuzi mpya kupitia shughuli mbalimbali za bandari.
Amewahimiza vijana kuwa wabunifu, waaminifu na wenye bidii katika kutafuta fursa, akisisitiza kuwa fursa hazimfuati mtu nyumbani bali zinahitaji kutafutwa.
Maboresho hayo yaliyogharimu Shilingi bilioni 157.8 yameongeza uwezo wa Bandari ya Mtwara kuhudumia mizigo kutoka tani 400,000 hadi tani milioni 2.6 kwa mwaka.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Nishati, Juma Homera amebainisha kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inakwenda kuanzisha Mfuko Maalum wa Nishati Safi utakaowezesha vikundi vya vijana na akina mama katika kila halmashauri nchini kunufaika na fursa za ajira na mtaji kupitia uzalishaji wa majiko banifu na mkaa mbadala.
Hayo yameelezwa leo Jumapili Novemba 15, 2026 Ikulu, Dar es Salaam wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliolenga kutoa taarifa kuhusu ushiriki wa Tanzania katika Mkutano wa 31 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP31) jijini Antalya, Uturuki
Waziri Homera ameeleza kuwa mfuko huo utatoa uwezeshaji wa kifedha kwa vijana ili watengeneze nishati mbadala na majiko ya kisasa, hatua itakayowasaidia kujipatia kipato huku wakishiriki kikamilifu katika kuhifadhi mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Pia, ametoa wito kwa sekta binafsi kuchangamkia fursa za nishati safi akibainisha kuwa ni eneo lenye uwezo mkubwa wa kuzalisha ajira na kuleta ukuaji wa kiuchumi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Baadhi ya wananchi wa Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma wameeleza hofu ya kupoteza maeneo yao kufuatia zoezi la upimaji na umilikishaji wa ardhi katika kata sita, wakidai kuwa kuna sintofahamu kuhusu utaratibu unaotumiwa na Halmashauri ya Wilaya hiyo, hususan matumizi ya Fomu Na. 69 na Fomu Na. 92.
Wakizungumza Novemba 14, 2026, wananchi hao wamesema wamekuwa wakipewa Fomu Na. 69 inayohusishwa na taratibu za uthamini wa fidia, jambo ambalo wamelipinga wakitaka kwanza kuwepo kwa utaratibu wa wazi wa kutambua wamiliki na kuhakiki mipaka ya maeneo yao. Wameeleza kuwa wanahitaji Fomu Na. 92 kwa madai kuwa itasaidia katika utambuzi wa maeneo na wamiliki wake.
Wamesema wako tayari hata kampuni binafsi yenye sifa za kitaalamu kushirikishwa katika zoezi hilo ili maeneo yao yapimwe, yapangwe na kumilikishwa kwa mujibu wa sheria. Hata hivyo, wamefafanua kuwa hakuna mwananchi aliyelipa fedha kwa ajili ya upimaji huo.
Wananchi hao wameeleza kuwa walikutana na Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Janeth Mayanja, na kukubaliana kusitisha matumizi ya Fomu Na. 69, lakini wanadai bado wamekuwa wakipewa fomu hiyo, hali inayozua maswali kuhusu utekelezaji wa makubaliano hayo.
Akijibu malalamiko hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Tito Mganwa amesema Fomu Na. 92 ilishafutwa na haitumiki tena katika utaratibu wa upimaji wa ardhi, hivyo Halmashauri inaendelea kutumia Fomu Na. 69 kwa ajili ya kueleza na kutambua hali ya maeneo yanayohusika na zoezi hilo. Amesisitiza kuwa hakuna udanganyifu katika matumizi ya fomu hiyo na hakuna mwananchi atakayechukuliwa ardhi yake kinyume na matakwa yake.
Kauli hiyo inatofautiana na maelezo ya Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Janeth Mayanja, ambaye amesema alisimamisha zoezi la matumizi ya Fomu Na. 69 na kuelekeza kuanza kwa utaratibu wa kutumia Fomu Na. 92, akisisitiza kuwa fomu hiyo ipo. Aidha, amewataka viongozi waliochaguliwa na wananchi kufika ofisini kwake ili changamoto zao ziweze kushughulikiwa.
Zoezi hilo linahusisha takribani ekari 4,000 katika kata sita kwa ajili ya upimaji, upangaji na umilikishaji wa ardhi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Serikali ya Tanzania imebainisha kuwa uwekezaji katika mradi wa kimkakati wa Reli ya Kisasa (SGR) wenye urefu wa zaidi ya kilomita 2,000 si tu kwamba unalenga kukuza uchumi, bali pia ni kielelezo kikuu cha jitihada za nchi katika kupunguza utoaji wa hewa ukaa na kukabili mabadiliko ya tabianchi.
Hayo yameelezwa leo Jumapili Novemba 15, 2026 Ikulu, Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Dkt. Ng'waru Maghembe, na Waziri wa Fedha, Balozi Khamis Mussa Omar, wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliodhahania ushiriki wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika Mkutano wa 31 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP31) uliofanyika jijini Antalya, Uturuki.
“Uwekezaji wote ambao tunafanya kwenye reli tunapata malengo mawili matatu makubwa. Moja kuwa na mtandao wa reli ya kisasa, pili kuwa na uwezo mkubwa zaidi wa kushajisha ukuaji wa uchumi. Lakini tatu vilevile ni hili la kupunguza utoaji wa hewa ukaa”, imeelezwa katika mkutano huo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Wadau na watumiaji wa Bandari ya Mtwara wamesema maboresho yaliyofanywa na Serikali, ikiwamo ujenzi wa gati lenye urefu wa mita 300, ununuzi wa vifaa vya kisasa na kuongeza rasilimali watu, yameongeza ufanisi wa shughuli za bandari na kuchochea ukuaji wa uchumi.
Wakizungumza katika mahojiano maalumu yaliyofanyika hivi karibuni mkoani Mtwara, wamesema maboresho hayo yameongeza uwezo wa kuhudumia meli na mizigo mbalimbali, pamoja na kufungua fursa za ajira na biashara.
Msimamizi Mwandamizi wa Uendeshaji wa Bandari Kavu ya Kampuni ya Makanjiro Ltd, Abdallah Darusi, amesema idadi ya makontena wanayohudumia imeongezeka kutoka 3,900 mwaka 2024/2025 hadi 5,914 kufuatia maboresho hayo.
Ameongeza kuwa wamepanua maeneo ya kuhifadhi mizigo na wanatarajia kupata wateja wengi zaidi.
Kwa upande wake, Meneja Uendeshaji wa Kampuni ya Nahodha Maritime Promotion Ltd, Omari Hassan, amesema maboresho hayo yameongeza idadi ya meli zinazotia nanga bandarini hapo, zikiwamo meli kubwa zinazoshusha magari na mitambo.
Amesema pia Bandari ya Mtwara imekuwa chachu ya biashara katika ukanda wa kusini kupitia usafirishaji wa mazao kama korosho, ufuta na mbaazi, pamoja na saruji ya Kiwanda cha Dangote kwenda Zanzibar, Msumbiji na Comoro.
Ameongeza kuwa shughuli za upakiaji wa saruji kwenye meli moja zinaweza kutoa ajira kwa vijana takribani 300, hivyo kuongeza kipato kwa wananchi.
Naye Msimamizi wa Kampuni ya Maxima Clearing and Forwarding Ltd, Venance Mrema, amesema maboresho yaliyofanyika kuanzia mwaka 2025 yameongeza fursa kwa mawakala wa forodha na wafanyabiashara, huku mabadiliko ya mfumo wa upakiaji wa makasha ya korosho yakitarajiwa kuongeza mizigo inayohudumiwa bandarini hapo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Kiongozi wa Chama cha @ACTwazalendo Dorothy Semu, ameitaka Serikali kufuta matangazo yaliyobadilisha mipaka ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, akidai kuwa yamesababisha mgogoro wa ardhi kati ya wananchi wa Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya na mamlaka za hifadhi. Semu ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya kutembelea kata zenye madiwani wa chama hicho.
Amesema Tangazo la Serikali Na. 28 la mwaka 2008 liliongeza eneo la hifadhi kutoka kilomita za mraba 10,113 hadi 20,126, hatua iliyohusisha vijiji 33 vilivyozunguka hifadhi hiyo. Amesema wananchi waliathirika kwa kupoteza maeneo ya makazi na shughuli za kiuchumi, huku wakitakiwa kutafuta njia nyingine za kujipatia maisha.
Semu amesema licha ya Serikali kutoa tangazo jingine GN. 754 mwaka 2023 lililopunguza eneo la hifadhi hadi kilomita za mraba 19,184, wananchi bado hawajaridhika na marekebisho hayo. Ameeleza kuwa changamoto za matumizi ya ardhi zinaendelea, huku wananchi wakiendelea kudai haki yao kupitia Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki.
Mgogoro huo ulizungumziwa pia na aliyekuwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Januari 17, 2023, alipotembelea eneo la Kapunga na kutangaza kuwa Serikali imeacha nje ya hifadhi zaidi ya hekta 74,000 kwa ajili ya shughuli za kilimo na ufugaji. Wakati huo, Majaliwa alisema hatua hiyo ililenga kutatua mgogoro uliokuwa umedumu kwa takribani miaka 15.
Machi 20, 2025, aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Stephen Wasira, akiwa Mbarali, alisema marekebisho ya mwaka 2023 yaliacha vijiji 28 nje ya hifadhi na vitano vikiendelea kubaki ndani yake huku akitaka Wizara ya Ardhi na uongozi wa Mkoa wa Mbeya kuweka utaratibu wa kuwapatia wananchi maeneo ya kilimo ili kushughulikia changamoto zilizokuwa zikiendelea.
Semu amesisitiza ACT Wazalendo inakataa uporaji wa ardhi na uonevu dhidi ya wananchi wa vijiji hivyo, akiwataka kuendelea kushikamana kudai haki zao.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Ndoa ya Abednego Mgaya na Astelina Mlelwa iliyokuwa imeahirishwa mkoani Njombe kutokana na changamoto ya kukosekana kwa kitambulisho cha utambulisho wa taifa (NIDA) kwa bwana harusi, hatimaye imefungwa baada ya taratibu zote za kisheria kukamilika na ndoa hiyo kufanikiwa kusajiliwa katika mfumo wa RITA.
Ndoa hiyo imefungwa katika Kanisa la EAGT Mlevela lililopo Igima, Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe. Akizungumza baada ya kufungwa kwa ndoa hiyo, Abednego Mgaya amesema mchakato wa kufanikisha ndoa yake ulikumbwa na changamoto mbalimbali zilizohusiana na mifumo ya kiserikali, lakini amefurahishwa na hatua ya mwisho ya kufanikiwa kufunga ndoa hiyo.
“Changamoto zote nilizoweza kupitia kutokana na mifumo ya kiserikali, ninachoweza kushukuru ni kwamba hatimaye nimefanikiwa,” amesema Mgaya.
Kwa upande wake, Matrida Kaduma, ndugu wa bwana harusi amesema familia inashukuru kuona ndoa hiyo imefungwa baada ya kupitia kipindi kigumu kufuatia kuahirishwa kwa harusi hiyo wiki kadhaa zilizopita, licha ya shughuli ya send-off kuwa tayari imefanyika.
Naye Lameck Moto, Msajili Msaidizi wa Masuala ya Ndoa Njombe Mjini amesema ushirikiano na ofisi za NIDA umewezesha kupatikana kwa kitambulisho cha bwana harusi kwa haraka, hatua iliyofungua njia ya kukamilisha usajili wa ndoa hiyo katika mfumo wa RITA na hatimaye kufungwa rasmi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Elihuruma Mabelya amebainisha kuwa kukuza mbinu za Uchumi Mzunguko (Circular Economy) ni mojawapo ya mipango mikuu inayolenga kuleta mabadiliko makubwa katika kurejesha na kutumia tena thamani ya taka za chakula na taka ngumu jijini humo.
Akizungumzia hatua hiyo wakati wa mkutano wa pembezoni mwa Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi wa COP31 uliofanyika nchini Uturuki, Mabelya ameeleza kuwa badala ya kuzichukulia taka za kikaboni kama tatizo la utupaji, mamlaka za jiji zinaziona kama rasilimali zinazoweza kuleta manufaa ya kiuchumi, kijamii na kimazingira.
“Mojawapo ya mipango yenye kuleta mabadiliko makubwa katika Jiji letu ni kukuza mbinu za uchumi mzunguko (Circular Economy) zinazowezesha kurejesha na kutumia tena thamani ya taka za chakula na taka ngumu. Badala ya kuzichukulia taka za kikaboni kama tatizo la utupaji, tunaziona kama rasilimali zinazoweza kuleta manufaa ya kiuchumi, kijamii na kimazingira”, ameeleza.
Mabelya alitolea mfano Mfumo wa Bonyokwa wa Usimamizi wa Taka Sifuri (Bonyokwa Zero Waste Model), ambapo taka za asili hukusanywa na kuchakatwa ili kuzalisha bidhaa muhimu kama mboji, chakula cha mifugo na rasilimali nyingine zinazosaidia mifumo ya uzalishaji wa chakula katika jamii, huku zikipunguza uzalishaji wa gesi chafuzi.
Pia, Mkurugenzi huyo amebainisha kuwa mageuzi ya mifumo ya chakula mijini hayawezi kufikiwa na serikali za mitaa pekee, bali yanategemea ushirikiano imara kati ya miji, serikali za kitaifa, jamii, washirika wa maendeleo, taasisi za utafiti pamoja na sekta binafsi.
Ameeleza kuwa ushirikiano huo utasaidia kuhamasisha uwekezaji, kuimarisha uwezo na kujenga msingi imara katika kushughulikia changamoto za mifumo ya chakula ili hatimaye kufikia mafanikio endelevu.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Taifa (BAWACHA), Sharifa Suleiman, amesema baraza hilo linalaani kushikiliwa kwa baadhi ya viongozi wa Chama hicho, kwa maelezo kwamba kushikiliwa kwa baadhi yao kumefanyika kinyume na sheria.
Sharifa meeleza hayo Novemba 15, 2026 visiwani Zanzibar, kupitia taarifa aliyoiwasilisha kwa umma kupitia vyombo vya habari. Amesema kwamba, kumekuwa na wimbi la baadhi ya wanawake kukamatwa na "kubambikiziwa kesi" huku akihoji sababu za hatua hiyo.
Ameziomba mamlaka kuhakikisha kuwa wanawake wote wa Chama hicho ambao wanashikiliwa wanapatiwa haki ya kuonana na ndugu zao, mawakili ikiwa ni pamoja na kuwapatia huduma za msingi za kibinadamu.
Aidha amevisihi vyombo vya dola kufuatilia na kufichua taarifa za wanaodaiwa kutekwa na kupelekwa kusiko julikana, ikiwemo kukomesha vitendo vya vitisho dhidi ya wakosoaji.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Katiba na Sheria Abdallah Ulega amesema serikali ya Tanzania imeshikilia msimamo wake wa kukataa kuruhusu mahusiano ya jinsia moja pamoja na kukataa kuondoa adhabu dhidi ya makosa ya kujamiiana kinyume na maumbile.
Ulega amesema msimamo huo uliwasilishwa katika kikao cha Mapitio ya Hali ya Haki za Binadamu (UPR) chini ya Umoja wa Mataifa ambapo Tanzania ilipokea jumla ya mapendekezo 280 yanayohusu haki za kijamii, kiraia kisiasa na kijamii huku ikikubali mapendekezo 196 yalikubaliwa, mapendekezo 168 yalikataliwa.
Ulega ameeleza kuwa yaliyokubaliwa ni yale yanayoendana na Katiba, Sheria, Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050, Ilani ya CCM pamoja na tamaduni zetu huku yale yaliyokataliwa ni yale yanayopingana na mila, desturi, sheria, katiba na kanuni ikiwemo la ushoga.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Mwenyekiti wa Ngome ya Wanawake Taifa wa @ACTwazalendo na Waziri Kivuli wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Janeth Rite amesema fedha zilizotumika kuwakopesha wasanii na zingine ambazo zimekuwa zikiripotiwa kupotea kupitia ripoti za CAG ni zingekuwa zimetumika kwenye miradi ya maji tatizo hilo lingepungua kwa kiasi kikubwa nchini.
Akizungumza jana Novemba 14, 2026 katika mkutano wa hadhara uliofanyika Mbarali, Mbeya amesema fedha za serikali zinazotolewa kwa wasanii na sekta ya michezo kulingana na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), wasanii walipewa karibu milioni 700, lakini hatma ya fedha hizo haijulikani.
Akitolea mfano wa fedha za Jeshi la Polisi zilizokusudiwa kununua sare na vifaa vya askari, ambazo CAG ameonyesha hazijulikani zilipo.
Alisisitiza kuwa fedha hizo zingeweza kutumika kutatua changamoto za maji nchini, ambapo wanawake bado wanabeba ndoo kichwani na miradi mingi imebaki katika hatua ya upembuzi yakinifu huku akitaka watuhumiwa wa ufisadi waitwe wezi kwa majina yao badala ya kuwaheshimu, na kuwapa changamoto Watanzania kuhakikisha nchi haitendewi ufisadi wa namna hiyo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
"Binti ukiwekeza kwenye mwonekano unavutia wapenda ngono, ukiwekeza kwenye tabia unavutia waoaji sasa mabinti wengi wanawekeza kwenye kuvutia wapenda ngono na hawaambiwi, anaumizwa anaanza kulalamika"
Anasema Mwalimu Cosmas Madulu tulipofanya naye mahojiano yaliyo kwenye YouTube yetu ya Jambo TV
Unakubaliana na mtazamo wa Mwl. Madulu?This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi, ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na Jeshi la Polisi, kuchunguza matumizi ya fedha za mradi wa kuboresha miundombinu ya Manispaa ya Lindi, baada ya taarifa kuonesha kuwa mkandarasi amelipwa shilingi bilioni 4.22, lakini utekelezaji umefikia asilimia 24 pekee huku asilimia 80 ya muda wa mkataba ikiwa imetumika.
Akitoa maelekezo hayo wakati wa ziara yake mkoani Lindi. Makamu wa Rais ametaka kufahamishwa namna malipo yalivyofanyika, fedha zilivyotumika na sababu za kazi kutotekelezwa kwa kasi iliyotarajiwa. Pia ametaka taarifa ya uchunguzi imfikie yeye mwenyewe ili aiwasilishe kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amewataka wananchi na wafanyabiashara kuimarisha usafi na nidhamu katika maeneo ya biashara, hoteli na barabara, akisema maandalizi hayo ni muhimu kuelekea mashindano ya AFCON 2027 yatakayofanyika Tanzania.
Akizungumza Novemba 14, 2026, wakati wa uzinduzi wa kampeni ya usafi katika Viwanja vya Posta, Kijitonyama, Chalamila amesema wageni watakaokuja nchini wanapaswa kukuta mazingira safi na huduma zinazozingatia hadhi ya kimataifa.
Amesema, “Mwaka 2027 mashindano ya AFCON ambayo zamani tulizoea yanafanyika Morocco, yanafanyika kwenye dunia nyingine. Eti mwaka 2027 mashindano hayo yako Tanzania, Dar es Salaam. Ndiyo maana wageni watakuja hapa, wataingia kwenye hoteli na kupita kwenye barabara”.
Aidha, amewataka wazazi kuwafundisha watoto nidhamu na usafi wakiwa nyumbani ili kujenga jamii inayothamini usafi na kuwajibika.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Kilimo Daniel Chongolo, amesema Serikali itaanza kugawa salfa kwa wakulima wa korosho katika mikoa ya Lindi na Mtwara mwezi Machi 2027, hatua inayolenga kuongeza uzalishaji na tija ya zao hilo pamoja na kuinua kipato cha wakulima.
Akizungumza wakati wa ziara ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mkoani Lindi, Novemba 14, 2026, Chongolo amesema upatikanaji wa pembejeo hizo ni muhimu katika kuimarisha uzalishaji na kuongeza ushindani wa zao la korosho katika msimu ujao wa kilimo.
Amesema Serikali inaendelea kuweka mikakati ya kuhakikisha wakulima wanapata salfa kwa wakati na kwa kiwango kinachohitajika ili kudhibiti magonjwa na wadudu waharibifu wa mikorosho, kuongeza ubora wa korosho na kuimarisha uzalishaji wa zao hilo nchini.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo, amevitaka Vyama vya Akiba na Mikopo nchini (SACCOS) kupanua wigo wa shughuli zake kwa kuwekeza katika sekta za uzalishaji badala ya kutegemea zaidi utoaji wa mikopo kwa matumizi binafsi ya wanachama ili kutasaidia kukuza uchumi, kuongeza uzalishaji na kutengeneza fursa za ajira nchini.
Akizungumza katika ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Tano wa Mapinduzi Umoja SACCOS Tanzania Limited, uliofanyika leo Novemba 14, 2026 jijini Dodoma, Profesa Mkumbo amesema SACCOS zinapaswa kuwa taasisi za uwekezaji na uzalishaji mali, huku zikiendelea kutoa mikopo kwa wanachama wake.
Aidha, amesema uwekezaji katika miradi ya uzalishaji, ikiwemo viwanda, utasaidia kuongeza fursa za ajira na kuchochea ukuaji wa uchumi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo, amesema Tanzania imepiga hatua katika sekta ya Vyama vya Akiba na Mikopo (SACCOS), ambapo kwa sasa vipo vyama zaidi ya elfu kumi vyenye leseni nchini. Amesema mafanikio hayo yanaonesha umuhimu unaozidi kuongezeka wa SACCOS katika kukuza uchumi na kuwawezesha wananchi kupata huduma za kifedha.
Akizungumza leo, Novemba 14, 2026, jijini Dodoma wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Tano wa Chama cha Mapinduzi cha Akiba na Mikopo, Kitila amesema takwimu zinaonesha kuwa mali za SACCOS nchini zimefikia Shilingi trilioni 1.6, kiwango ambacho ni kikubwa kuliko mali za baadhi ya benki nchini.
Aidha Kitila amesema kwa sasa Vyama vya Akiba na Mikopo ni sehemu muhimu ya uchumi wa Tanzania, kutokana na mchango wake katika kuimarisha ujumuishaji wa huduma za kifedha, kukuza uwezo wa wananchi kiuchumi na kuwawezesha kupata mitaji kwa ajili ya shughuli mbalimbali za maendeleo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mbunge wa Tunduru Kaskazini, Ado Shaibu Ado, amewasilisha mbele ya Makamu wa Rais, Deogratius Ndejembi, mgogoro wa wakulima na wafugaji unaotajwa kusababisha uharibifu wa mazao, kupelekea vifo na uvunjifu wa amani wilayani humo.
Akizungumza Novemba 11, 2026, wakati wa ziara ya Makamu wa Rais mkoani Ruvuma, Ado ameeleza kuwa uvamizi wa wafugaji katika mashamba ya wakulima huko Tunduru umefikia hatua mbaya kiasi ambacho mazao yote yakiwemo korosho, bustani, na mpunga yanasombwa au kuharibiwa.
Ameongeza kuwa wananchi wa Tunduru kwa asili ni waungwana, lakini wanapotoa malalamiko yao huchapwa viboko na hukosa msaada wa kutosha kutoka kwa vyombo vinavyohusika, hali inayopelekea wananchi kuachwa vilema, kuuawa pamoja na vifo vya baadhi ya viongozi akiwemo Diwani mmoja na Askari mmoja wa Jeshi la Polisi hivi karibuni.
Kutokana na mateso hayo, mbunge huyo amehoji kwamba "Wananchi wa Tunduru hadi afe nani ili hatua zichukuliwe?". Aidha, Ado amesisitiza kuwa suluhisho la msingi la kumaliza mgogoro huo ni kuzingatia sheria na mpango wa matumizi bora ya ardhi kwa kuwaondoa mara moja wafugaji walioko katika vijiji ambavyo hawapaswi kuwepo kisheria.
Amebainisha kuwa Wilaya ya Tunduru tayari ina maeneo ya vitalu, yanayoweza kutumika kuwaweka wafugaji hao ili kuepusha mwingiliano na mashamba ya wakulima na kuleta amani ya kudumu.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na World Vision Tanzania zimesaini mkataba wa ushirikiano unaolenga kuimarisha mifumo ya kudhibiti vitendo vya rushwa katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo na shughuli za kibinadamu.
Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika leo Novemba 14, 2026, katika makao makuu ya World Vision Tanzania jijini Arusha, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Crispin Chalamila, amesema makubaliano hayo yatawezesha taasisi hizo kubadilishana utaalamu, kubaini viashiria vya rushwa mapema na kuweka mikakati ya kuzuia mianya inayoweza kujitokeza.
Chalamila amesema utekelezaji wa mkataba huo utahusisha utoaji wa elimu na mafunzo kwa watumishi, viongozi, wazabuni, washirika na wanufaika wa miradi, ili kuwaongezea uelewa kuhusu madhara ya rushwa na namna ya kutoa taarifa za vitendo hivyo.
Aidha, amesema TAKUKURU itashirikiana na World Vision kufanya tathmini ya viatarishi vya rushwa katika usimamizi wa fedha, manunuzi, mikataba na maeneo mengine ya kiutendaji, akisisitiza kuwa udhibiti wa rushwa unahitaji ushiriki wa taasisi mbalimbali katika jamii.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa World Vision Tanzania, James Anditi, amesema makubaliano hayo yanaakisi dhamira ya shirika hilo ya kuimarisha uadilifu, uwazi na uwajibikaji katika shughuli zake, huku akibainisha kuwa mazungumzo ya kuanzisha ushirikiano huo yalianza Aprili 29, 2026.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Takribani vijana 1,500 wamefikiwa na elimu kuhusu afya ya uzazi na uzazi wa mpango, magonjwa ya ngono, afya ya akili pamoja na elimu ya uchumi ili kuwawezesha kujitegemea na kufanya maamuzi sahihi wanapokuwa katika maisha ya chuo.
Akizungumza Novemba 14, 2026, katika majadiliano yaliyoratibiwa na Chama cha Uzazi na Malezi Bora Tanzania (UMATI) kwa wanavyuo wa mwaka wa kwanza wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU), Daktari Kiongozi wa Hospitali ya UMATI Moshi, Kilimanjaro, Francis Mollel, amesema vijana wengi wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya kujieleza kuhusu masuala ya afya zao.
Amesema elimu hiyo inalenga kuwajengea uelewa na kuondoa hofu ya kuzungumza na wataalamu wa afya ili waweze kupata ushauri na huduma za matibabu kwa wakati.
Kwa upande wake, Ellyn Lilunde, Daktari anayeshughulikia masuala ya afya ya akili amesema baadhi ya wanavyuo wa kike wanakabiliwa na changamoto za afya ya akili zinazohusiana na mahusiano na kushindwa kukabiliana na changamoto zinazotokana na mahusiano hayo.
Ameeleza umuhimu wa vijana kupata msaada wa kitaalamu wanapokabiliwa na changamoto hizo, badala ya kukaa kimya au kufanya maamuzi yanayoweza kuathiri ustawi wao.
Akizungumzia suala hilo,Lilunde pia ameeleza wasiwasi wake kuhusu baadhi ya maudhui yanayochapishwa na wasichana wadogo kwenye mitandao ya kijamii, akisisitiza umuhimu wa elimu, malezi na msaada wa kisaikolojia kwa vijana, hata hivyo, amesisitiza kuwa changamoto za afya ya akili zinahitaji uelewa na usaidizi badala ya kuwahukumu vijana wanaozipitia.
Kwa upande wao, wanavyuo Emmy Mshanga na Golam Nyanda wameishukuru UMATI kwa kuwapatia elimu hiyo, hususan wanafunzi wapya wanaoanza maisha ya kujitegemea chuoni.
Wamesema wazazi na walezi wanapaswa kuendelea kuwa karibu na vijana wao na kuwapa elimu ya afya ya uzazi tangu wakiwa nyumbani ili wawe na uwezo wa kufanya maamuzi sahihi wanapoanza maisha ya chuo.
Kwa mujibu wa UMATI, majadiliano na wanafunzi wapya katika vyuo mbalimbali hufanyika kila mwaka kwa lengo la kuwajengea uelewa kuhusu afya ya uzazi na uzazi wa mpango, magonjwa ya ngono, afya ya akili pamoja na masuala mengine yanayohusu ustawi wao, ili kuwawezesha kukabiliana na changamoto zinazoweza kujitokeza katika maisha yao ya kila siku.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
“Mimi ni Mkristo, nasali, lakini sitaki makanisa kila mahali bila utaratibu. Mtu anaamka asubuhi anakuta nyumba imebadilika, imekuwa kwaya, imekuwa kila kitu. Hayo nayo ni makelele ya uchafu. Kwa Mungu tunahitaji utaratibu,” amesema Chalamila.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila amesema hayo leo Novemba 14, 2026 alipokuwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya usafi na ugawaji wa vifaa vya usafi katika Viwanja vya Posta, Kijitonyama, Dar es Salaam, yenye kaulimbiu “Dar es Salaam Safi, Tushiriki Pamoja,” Chalamila amesema shughuli za ibada zinapaswa kuzingatia utaratibu na kuheshimu mazingira ya makazi ili kuepusha usumbufu kwa wananchi.
Ameongeza kuwa usafi wa jiji unahitaji ushiriki wa kila mwananchi, akiwataka wananchi kuzingatia nidhamu na sheria katika shughuli zao za kila siku, ikiwemo matumizi sahihi ya vyombo vya moto na usalama barabarani.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amekemea tabia ya baadhi ya watu kuendesha magari bila namba za usajili, akisema kitendo hicho kinafanana na ujambazi na kinapaswa kuchukuliwa hatua.
Akizungumza Novemba 14, 2026, wakati wa uzinduzi wa kampeni ya usafi katika Viwanja vya Posta, Kijitonyama, Dar es Salaam, Chalamila amesema baadhi ya magari katika maeneo ya Masaki huendeshwa bila namba za usajili na kwa mwendo hatarishi, hali inayoweza kuhatarisha maisha ya watu wasio na hatia.
Amesema, “Unaamka asubuhi unaona gari haina plate number. Huo ni uzushi, ni ujambazi kama majambazi wengine, vinginevyo awe na kibali maalumu kutoka mamlaka husika.”
Aidha, amesisitiza kuwa uzingatiaji wa sheria ni jukumu la kila mwananchi na haupaswi kuhusishwa na vyama vya siasa, bali ni suala la usalama na ustawi wa jamii.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mchambuzi wa masuala ya siasa na jamii, Ezekiel Kamwaga ametoa tathmini ya kina kuhusu mijadala inayoendelea kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari nchini kuhusu uwekezaji na uwepo wa wafanyabiashara kutoka nchini China.
Akizungumzia hoja za baadhi ya wananchi wanaotaka raia wa China wafukuzwe au wanaowatuhumu kwa kutoaminika na ukatili, Kamwaga amesisitiza kuwa mjadala huo unapaswa kuendeshwa kwa haki na bila ubaguzi wa kimbari au utaifa. Amebainisha kuwa ni kosa kisheria na kiubinadamu kuchukua makosa ya mtu mmoja mchina na kuwahukumu Wachina wote kama jamii.
Kamwaga amewakumbusha Watanzania historia ndefu ya ushirikiano wa dhati kati ya Tanzania na China, ikiwemo ujenzi wa Reli ya TAZARA na mchango wa China katika harakati za ukombozi wa nchi za Kusini mwa Afrika wakati mataifa mengine ya Magharibi yakipinga.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Wananchi wa Mtaa wa Kimara Baruti, eneo la Nguzo 800, jijini Dar es Salaam, wamelalamikia vitisho vya kubomolewa kwa nyumba zao kupisha mradi wa kusafirisha umeme wa kilovolti 220 (220kV) kutoka Kinyerezi hadi Mburahati, wakidai hatua hizo zinaendelea licha ya kuwepo kwa zuio la mahakama.
Wananchi hao wamesema awali walitembelewa na maofisa wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), kupitia Kitengo cha Ustawi wa Jamii, walio waelekeza kuwasilisha taarifa za mali zao kwa ajili ya mchakato wa fidia. Hata hivyo, wanadai hadi sasa hawajapokea mrejesho wowote licha ya kutekeleza maelekezo hayo.
Diwani wa Kata ya Kimara, Ismail Mvungi, amesema kwa mujibu wa maelezo ya wananchi na nyaraka walizonazo, wana msingi wa kisheria wa kuendelea kuishi katika maeneo hayo. Amesisitiza kuwa wananchi hawapingi utekelezaji wa mradi huo, bali wanataka haki zao na maslahi yao yazingatiwe.
“Hakuna mwanakimara yoyote ambaye hana akili sawasawa akakataa maendeleo. Hawa watu wanataka wapate haki, hata kama Serikali inaleta mradi, basi ilete mradi huo kwa kuzingatia mapambano ambayo wananchi wameyafanya katika maisha yao,” amesema Mvungi.
JAMBO TV ilipowasiliana na TANESCO kutafuta ufafanuzi kuhusu malalamiko hayo, ilielezwa kuwa Mkurugenzi amesafiri nje ya nchi na ufafanuzi zaidi utatolewa atakaporejea.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Timu ya soka ya Rhino Rangers inayoshiriki Ligi ya Championship Tanzania, ambayo awali ilikuwa inamilikiwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), imekabidhiwa rasmi kwa wananchi wa Mkoa wa Tabora na sasa itakuwa mali ya wakazi wa mkoa huo.
Katika makabidhiano hayo yaliyofanyika usiku wa Novemba 13, 2026, Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Dkt. Angeline Mabula, ametajwa kuwa mlezi wa timu hiyo.
Akizungumza baada ya makabidhiano, Dkt. Mabula amesema Rhino Rangers sasa ni timu ya wanaTabora na haitauzwa kwa mtu binafsi au taasisi nyingine, akisisitiza umuhimu wa wananchi kuungana kuisimamia na kuiendeleza ili iweze kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali.
Aidha, amesema Serikali ya Mkoa itaendelea kuweka mazingira rafiki kwa maendeleo ya michezo, ikiwemo kupanga ukarabati wa Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi ili timu mbalimbali ziweze kuutumia kwa michezo yao badala ya kulazimika kucheza nje ya Mkoa wa Tabora.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Wananchi wanaotegemea Mto Mvuha, uliopo katika Kijiji cha Bungu, Wilaya ya Morogoro, wanakabiliwa na hatari ya kuathirika kwa upatikanaji na ubora wa maji kufuatia shughuli za uchimbaji wa madini zinazotuhumiwa kuharibu chanzo hicho.
Kutokana na hali hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mussa Kilakala, ameliagiza Jeshi la Polisi kumshikilia mchimbaji wa madini, Omari Muhondogwa, kwa tuhuma za kufanya uchimbaji ndani ya mto huo na kuharibu mazingira yake.
Maelekezo hayo yametolewa Novemba 13, 2026 wakati Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ilipofanya ziara ya kukagua eneo hilo na kubaini shughuli za uchimbaji ndani ya hifadhi ya mita 60 kutoka kingo za mto, kinyume na matakwa ya Sheria ya Usimamizi wa Rasilimali za Maji, Sura ya 331.
Kilakala pia ameiagiza Tume ya Madini kusitisha leseni ya mchimbaji huyo na kumpa siku saba kurejesha mto katika hali na mwelekeo wake wa asili. Aidha, amewaagiza wananchi kuondoka katika eneo hilo ili kuruhusu hatua za kudhibiti uharibifu.
Uchimbaji huo umesababisha tope kujaa ndani ya mto, kuvuruga mtiririko wa asili wa maji na kuhatarisha ubora wa maji pamoja na makazi ya viumbe hai.
Hatua hizo zinaelekezwa katika kulinda chanzo hicho cha maji na mazingira yanayokizunguka kwa manufaa ya wananchi wanaokitegemea.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imezitaka taasisi zote za umma, vyama vya siasa, mashirika ya kiraia, vyombo vya habari na wananchi wa Tanzania kwa jumla kuhakikisha kuwa tofauti zote za maoni kuhusu maamuzi ya mahakama na masuala ya maslahi ya umma zinashughulikiwa kwa amani na kupitia njia za kisheria, kikatiba na kidemokrasia.
Wito huo umetolewa kupitia tamko rasmi la msimamo wa Tume hiyo lililotolewa Novemba 13, 2026, na Mwenyekiti wa THBUB, Dunford George Mpelumbe. Tamko hilo limetolewa kufuatia hukumu iliyotolewa na Mahakama Kuu ya Tanzania mnamo Novemba 6, 2026 katika shauri la Jinai Namba 000019605 la Mwaka 2025, ambapo Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Antiphas Lissu aliondolewa hatiani kwenye kosa la uhaini lakini akatiwa hatiani na kuhukumiwa kifungo cha miaka minne gerezani kwa kosa la uchochezi chini ya Kifungu cha 390 cha Kanuni ya Adhabu na Kifungu cha 319 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai.
“THBUB inatoa wito kwa wadau wote, ikiwa ni pamoja na taasisi za umma, vyama vya siasa, mashirika ya kiraia, mashirika ya kimataifa, vyombo vya kitaaluma, taasisi za dini, vyombo vya habari na wananchi kwa jumla, kukuza mazungumzo ya ujenzi, kuheshimiana na kushirikiana kwa amani. Tofauti za maoni kuhusu maamuzi ya mahakama na masuala ya maslahi ya umma zinapaswa kushughulikiwa kupitia njia za kisheria, kikatiba na za kidemokrasia," amesisitiza Mpelumbe
THBUB imebainisha kuwa imefuatilia kwa karibu maoni na hisia zilizotolewa na wadau mbalimbali wa ndani, kikanda na kimataifa ikiwa ni pamoja na Serikali ya Tanzania, CCM, CHADEMA, ACT Wazalendo, Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Amnesty International, Human Rights Watch, FIDH, LHRC, Kikundi Kazi cha UN (UNWGAD), na Idara ya Mambo ya Nje ya Uingereza (FCDO).
THBUB imesisitiza kuwa jukumu lake la usimamizi wa haki za binadamu liko tofauti na mamlaka ya kimahakama, na kwamba Tume haina mamlaka ya kirufaa au uwezo wa kupitia, kubadilisha au kufuta maamuzi yaliyofanywa na mahakama yenye mamlaka.
Ikieleza mipaka yake ya kisheria, Tume imekumbusha kuwa Ibara ya 130(5) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaizuia THBUB kuchunguza maamuzi ya majaji, makadhi au mahakama yaliyofanywa katika kutekeleza majukumu ya kimahakama. Pia, Ibara ya 131(2)(a) ya Katiba na Kifungu cha 17(2)(a) cha Sheria ya THBUB kinaizuia Tume kuchunguza masuala yaliyo mbele ya mahakama au yanayosubiri rufaa.
Kutokana na misingi hiyo ya kikatiba, THBUB imeweka wazi kuwa haijaunga mkono wala kupinga hukumu iliyotolewa dhidi ya Lissu, ikieleza kuwa maamuzi ya kisheria yanapaswa kushughulikiwa kupitia mchakato wa rufaa mahakamani.
"Uhuru wa Mahakama, kutopendelea na heshima kwa mamlaka ya mahakama ni misingi mikuu ya utawala wa sheria na ni muhimu katika utoaji haki unaostahili... Kwa msingi huo, THBUB haijaunga mkono wala kupinga kutiwa hatiani au adhabu iliyowekwa dhidi ya Mheshimiwa Tundu Antiphas Lissu," inasomeka sehemu ya tamko hilo.
THBUB imerejea uchunguzi wa kujitegemea iliofanya mnamo Juni 27, 2025 gerezani kukagua hali na usalama wa Lissu akiwa mahabusu. Katika uchunguzi huo, THBUB ilibaini kuwa haki zake za msingi ziliendelea kuheshimiwa kulingana na Katiba na sharia.
Ikieleza matokeo ya uchunguzi huo wa gerezani, CHRAGG imebainisha kuwa Lissu alikuwa akipata na kufurahia uhuru wa kuabudu chini ya Ibara ya 19 ya Katiba, haki ya faragha chini ya Ibara ya 16, haki ya kuwasiliana na mawakili au ndugu zake chini ya Ibara ya 13(6)(a) na (b), pamoja na fursa ya kufanya mazoezi ya viungo kulingana na Ibara ya 13(6)(e) ya Katiba na viwango vya kimataifa vya Nelson Mandela Rules. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mjumbe wa Baraza la Uongozi la Tanganyika Law Society (TLS), Stella Rweikiza, amesema matumizi ya akili bandia (AI) yanaweza kurahisisha na kuboresha utendaji wa kazi za mawakili, lakini yanapaswa kuzingatia maadili ya taaluma hiyo.
Rweikiza amesema hayo leo Novemba 13, 2026, jijini Arusha wakati akifungua Kongamano la Utofauti wa Kitaaluma lililoandaliwa na TLS, lililowakutanisha wataalamu kutoka taaluma mbalimbali.
Amesema kongamano hilo linalenga kuunganisha ujuzi wa taaluma mbalimbali ili kuongeza tija katika utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, ikiwemo kupitia uwekezaji katika teknolojia na miundombinu ya kidijitali.
Ameeleza kuwa uwekezaji katika teknolojia pekee hauwezi kuleta tija bila wataalamu kuzingatia maadili katika utekelezaji wa majukumu yao ya kitaaluma.
Kwa upande wake, Wakili Janet Joseph, mwanachama wa TLS, amesema AI inaweza kurahisisha kazi za mawakili, lakini si kila taarifa inayozalishwa na teknolojia hiyo huwa sahihi, hivyo ni muhimu kuichambua kabla ya kuitumia.
Amesisitiza kuwa mawakili vijana wanapaswa kujenga uzoefu kwa kufanya kazi na mawakili waliowatangulia kabla ya kutegemea teknolojia hiyo, huku wakiendana na mabadiliko ya kiteknolojia.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwanafunzi aliyejulikana kwa jina la Denis Steven mwenye umri wa miaka 13 anayesoma kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari Kihonda, Manispaa ya Morogoro, amenusurika kifo baada ya kudaiwa kushambuliwa kwa kisu na mwanafunzi mwenzake wa kidato cha pili katika shule hiyo. Hata hivyo, chanzo cha tukio hilo bado hakijafahamika.
Akizungumzia tukio hilo lililotokea majira ya saa tatu asubuhi Novemba 13, 2026, baba mzazi wa mwanafunzi aliyejeruhiwa, Steven Paulo, amesema kuwa taarifa alizozipata kutoka kwa walimu na wanafunzi zinaeleza kuwa mwanafunzi anayedaiwa kutekeleza shambulio hilo alikuwa katika hali ya ulevi wakati wa tukio hilo.
Jambo TV inaendelea na jitihada za kuwasiliana na Jeshi la Polisi ili kupata ufafanuzi zaidi kuhusu tukio hilo na hatua zilizochukuliwa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi, ameagiza TAKUKURU mkoani Mtwara kuchunguza mchakato wa utoaji wa tenda ya shilingi bilioni 27, namna mkandarasi alivyopatikana na walioidhinisha tenda hiyo, baada ya kutoridhishwa na kasi na kiwango cha utekelezaji wa miradi ya uboreshajiMiundombinu ya Miji ya Tanzania (TACTIC) Mkoa wa Mtwara, licha ya mkandarasi kulipwa bilioni 4 za awali.
Makamu wa Rais ametoa maagizo hayo leo Novemba 13, 2026 katika mwendelezo wa ziara yake mkoani humo. Tenda hiyo inahusisha ujenzi wa soko, barabara yenye urefu wa kilomita mbili, mtaro mkubwa wa maji na eneo la wajasiriamali.
Akijibu maswali ya Makamu wa Rais kuhusu mwenendo wa mradi, mshauri wa mradi kutoka Norplan (T) Ltd JV Typsa amesema tangu mwanzo mkandarasi kampuni ya Serengeti LTD alionyesha kutokuwa na uwezo wa kutekeleza kazi, huku akiwa na vifaa duni.
Mshauri huyo amekiri kuwa baadhi ya kazi hazijaanza kabisa na kwamba kiwango cha kazi zilizofanyika hakiendani na fedha.
Kufuatia hali hiyo, Makamu wa Rais ameagiza ujenzi wa miradi hiyo ukamilike ifikapo Machi Mosi, 2027, bila nyongeza ya muda. Ameelekeza kuwa mkandarasi akishindwa kukamilisha kazi kwa wakati, atozwe fidia ya ucheleweshaji (liquidated damages) na kuchukuliwa hatua nyingine za kisheria.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Deogratius Ndejembi, ameagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) pamoja na vyombo vya usalama kuchunguza matumizi ya fedha katika vyama vikuu vya ushirika vya MAMCU na TANECU mkoani Mtwara, kufuatia kuwepo kwa madai ya matumizi mabaya ya fedha katika vyama hivyo.
Aidha, ameitaka Bodi ya Korosho kuhakikisha inasimamia kwa karibu suala hilo ili kubaini mwenendo wa matumizi ya fedha na kuhakikisha usimamizi wa rasilimali za vyama hivyo unazingatiwa.
Agizo hilo amelitoa leo Novemba 13, 2026 wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa kongani ya viwanda katika Kijiji cha Malanje Halmashauri ya Mji Nanyamba mkoani Mtwara, ambapo amesisitiza umuhimu wa vyombo husika kufuatilia suala hilo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imemrejeshea gari lake msanii maarufu wa muziki wa Bongo Fleva, Omary Nyembo, anayefahamika kama Ommy Dimpoz, baada ya msanii huyo kukamilisha malipo ya kodi ya ziada kufuatia gari lake kukamatwa kutokana na dosari katika taratibu za forodha.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika hafla fupi ya makabidhiano hayo, Kaimu Mkurugenzi wa Elimu kwa Mlipakodi na Mawasiliano wa TRA, Paul John Walalaze, ameeleza kuwa gari hilo lilizuiliwa baada ya kubainika kuwa na taarifa zisizo sahihi kwenye nyaraka za uingizaji wake nchini.
Walalaze amekumbusha kuwa kwa sasa TRA inatoa msamaha maalum wa kuondoa riba na adhabu kwa wamiliki wote wa magari yaliyoingizwa nchini kinyume cha taratibu ikiwemo matumizi ya njia za usafirishaji wa mizigo inayopita nchi za nje (transit), vibali vya muda kasoro, au kuwasilisha taarifa potofu kuhusu namba ya chasi (chassis), modeli, na mwaka wa utengenezaji wa magari hayo.
Wamiliki wenye changamoto kama hizo wametakiwa kujitokeza kabla ya tarehe Desemba 31, 2026, kutumia fursa hiyo kulipa kodi stahiki bila riba wala adhabu. Takwimu zinaonesha kuwa hadi kufikia mwezi Oktoba pekee, tayari wamiliki wa magari 168 walikuwa wamejitokeza kutumia fursa hiyo.
Kwa upande wake, msanii Ommy Dimpoz amekiri kuwa hapo awali aliamini gari lake liliingizwa nchini kwa kufuata sheria zote, lakini baada ya wataalamu wa TRA kumfafanulia dosari zilizokuwepo kwenye nyaraka, aliamua kushirikiana kikamilifu na kulipa kodi iliyobainika kuwa haijalipwa.
Msanii huyo ameeleza kuwa uamuzi wake wa kuweka suala hilo wazi unalenga kutoa elimu kwa jamii na Watanzania wenzake kuhusu umuhimu wa kufuatilia na kuhakikisha taratibu zote za forodha zinazingatiwa wakati wa kununua au kuagiza magari kutoka nje ya nchi.
Ametoa wito kwa wananchi na wamiliki wengine wenye magari yenye dosari za kiforodha kutopoteza muda, bali watumie msamaha huo uliotolewa na Serikali huku akiahidi kusimama kama balozi mzuri wa kuhamasisha ulipaji kodi nchini.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwananchi mkoani Njombe, Sabinus Mtwe amewasilisha kilio chake mbele ya Waziri Mkuu wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, akieleza jinsi alivyodhulumiwa, kutozwa fedha na viongozi wa mtaa na kata, na hatimaye kutishiwa kufungwa baada ya shamba lake la parachichi kuchomwa moto na kuharibiwa miundombinu ya maji.
Mtwe amewasilisha kero hiyo leo, Novemba 13, 2026, wilayani Ludewa, alipopewa fursa ya kuzungumza na Dkt. Mwigulu wakati wa mkutano wa hadhara wa kusikiliza na kutatua kero za wananchi.
“Mheshimiwa natamani kulia hata kujinyonga kwa gharama nilizotumia malori yote, parachichi zimeharibika. Naomba msaada kwako nipate lori zile saba …kwa hali niliyokuwa nayo wenzangu wanapiga suti mimi nanyong'onyea, amesema Mtwe.
Akijibu kero hiyo, Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba alimfariji mwananchi huyo na kumtaka asichukue maamuzi magumu ya kujinyonga, huku akiagiza wasaidizi wake kumweka pembeni mwananchi huyo ili aweze kuonana naye na kushughulikia tatizo lake kabla ya kuondoka.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mratibu wa Mradi wa Usalama Wetu Kwanza, Wilaya ya Kariakoo na Kati, Inspector Martin Shilla amesema uwezo wa kiuchumi wa mzazi hauondoi nafasi wala majukumu ya baba au mama ndani ya familia, akisisitiza kuwa kila mmoja ana nafasi yake katika malezi ya watoto.
Inspector Shilla ameeleza hayo leo, Novemba 13, 2026, alipokuwa akizungumza katika kipindi cha Jambo Asubuhi kinachorushwa na Jambo TV.
Akifafanua kuhusu nafasi za wazazi, amesema kuwa kuwawezesha wanawake kiuchumi na kuwapa elimu hakumaanishi kuwaondolea nafasi yao kama mama, huku akisisitiza kuwa uwezo wa mwanamke kiuchumi haupaswi kuwa sababu ya kumdharau baba.
Ameeleza kuwa si sahihi kwa mzazi kutumia kauli ya “Mimi ndiye baba na mama” hata pale wazazi wanapotengana au mmoja anapofariki, kwa kuwa mzazi anaweza kutekeleza majukumu ya mwenzake bila kubadilika na kuwa yeye. Amesema kauli hiyo inaweza kuwafanya watoto kupoteza uelewa wa nafasi ya kila mzazi katika familia.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri Mkuu wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, amewatoa hofu na kuwahakikishia mashujaa na wapiganaji wa Vita vya Kagera nchini kuwa watalipwa stahiki zao na pensheni ndani ya mwaka huu wa fedha, kufuatia serikali kukamilisha mabadiliko ya sheria na kanuni zilizokuwa zikikwaza mchakato huo.
Dkt. Mwigulu ametoa kauli hiyo leo, Novemba 13, 2026, mkoani Njombe alipokuwa akisikiliza na kutatua kero pamoja na malalamiko ya wananchi wa Wilaya ya Ludewa.
Katika mkutano huo, lalamiko hilo limewasilishwa na Ernest Yohana, mmoja wa wazee wapiganaji wa Vita vya Kagera, aliyezungumza kwa niaba ya wenzake waliofika eneo hilo kutafuta suluhu ya madai yao. Ernest ameeleza kuwa ingawa wanashukuru Serikali ya Awamu ya Siku kwa kuwatambua na kuahidi kuwalipa pensheni, wamekabiliwa na ugumu mkubwa wa maisha kutokana na kuchelewa kwa malipo hayo tangu mwezi Juni mwaka jana.
“Tumesubiri tangu mwaka jana mwezi wa sita mpaka sasa kimya. Hilo linatupa shida kwa sababu sasa hivi ni wazee na tunaishi mazingira magumu sana”, ameeleza.
Akijibu hoja hiyo, Dkt. Mwigulu Nchemba amekiri uwepo wa madai hayo akifafanua kuwa chanzo kikuu kilichochelewesha malipo hayo kilikuwa ni tofauti zilizokuwepo kati ya sheria na kanuni za wakati walipoandikishwa na sheria za sasa za utoaji wa mafao.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Baraza la Maaskofu Katoliki Kenya (KCCB) limepiga marufuku hotuba zote za kisiasa katika makanisa ya Kanisa Katoliki kote nchini humo, wakati taifa likijiandaa kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka 2027.
Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa Novemba 13, 2026 na Vatican News, tamko hilo lililotolewa mjini Embu na kusainiwa na Mwenyekiti wa KCCB, Askofu Mkuu Maurice Muhatia Makumba wa Jimbo Kuu la Kisumu, limeelekeza mapadre wote kuhakikisha nyumba za ibada zinabaki kuwa maeneo ya sala, umoja, na ukarimu kwa waumini wote bila kujali itikadi zao za kisiasa.
“Watu kutoka katika makundi mbalimbali ya maisha huja katika nyumba za ibada kutafuta amani na kuwa kimya mbele ya Yesu. Kipindi cha kampeni za uchaguzi hakipaswi kuwa sababu ya kufanya nyumba za ibada kuwa majukwaa ya kisiasa,” wamesema Maaskofu, wakisisitiza kuwa wanasiasa wana majukwaa mengine kama vile mikutano ya hadhara na vyombo vya habari.
Tamko hilo lenye kaulimbiu “Wito wa Kuijenga Kenya Yenye Haki, Amani na Umoja”, limeongozwa na maandiko kutoka Mika 6:8 pamoja na rejea ya Waraka wa Kitume wa Papa Leo XIV (Magnifica humanitas), likikumbusha wajibu wa Kanisa kusimama upande wa wanyonge pale utu wa binadamu unapokiukwa.
Maaskofu hao wamewapelekea vijana ujumbe maalumu wakiwataka kuchukua hatua za kiuwajibikaji kwa kupata vitambulisho vya kitaifa na kujiandikisha kupiga kura. Hata hivyo, wamewaonya vikali dhidi ya kutumiwa na wanasiasa kuchochea vurugu kwa ushawishi wa fedha. Wamewahimiza vijana kuwa vielelezo vyema katika jamii na kutumia ubunifu wao kwenye mitandao ya kijamii kueneza amani, haki, na utunzaji wa mazingira badala ya chuki na migawanyiko.
Kuelekea uchaguzi wa 2027, KCCB iMEtaka Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kujenga imani kwa wananchi kwa kuhakikisha mchakato mzima kuanzia usajili wa wapiga kura hadi utangazaji wa matokeo unakuwa huru, wa wazi, na usioingiliwa na wenye mamlaka. Aidha, wameitaka Mahakama kutenda haki bila upendeleo katika migogoro yote ya uchaguzi.
Wakigeukia Bunge la Kitaifa, Maaskofu wameonya dhidi ya kupitisha sheria zinazoweza kufifisha imani ya wananchi, wakipinga vikali mapendekezo ya kuzuia matangazo ya moja kwa moja (live broadcast) ya kuhesabiwa kwa kura za urais. Pia, wameeleza wasiwasi wao kuhusu miswada sita ya elimu iliyo bungeni, wakidai baadhi ya vifungu vyake vinakiuka misingi ya ushirikishwaji na vinaweza kudhoofisha taasisi za elimu zilizoanzishwa na mashirika ya dini.
Katika eneo la ulinzi na usalama, KCCB imeeleza kusikitishwa na kuendelea kwa matukio ya utekaji nyara, watu kupotea katika mazingira ya kutatanisha, na unyanyasaji wa watetezi wa haki za binadamu baadhi ya matukio yakidaiwa kuhusisha watu wenye silaha wanaoshirikiana na vyombo vya dola. Maaskofu wamevitaka vyombo vya usalama kutekeleza sheria kwa usawa bila upendeleo, huku wakiwaasa wananchi kutumia uhuru wao wa kujieleza bila kutoa kauli za ukabila au uchochezi. -
Jambo TV
@Jambotv_
Waziri wa Madini, Anthony Mavunde ameelekeza kufutwa mara moja kwa leseni kubwa saba za madini mkoani Katavi zikiwemo Leseni za Uchimbaji wa Kati (ML) na Leseni za Utafiti (PL) ambazo wamiliki wake wameshindwa kuzifanyia kazi na kuyaendeleza maeneo hayo.
Maelekezo hayo yametolewa leo, Novemba 13, 2026, wakati Waziri Mavunde akikabidhi leseni kwa vikundi tisa (9) vya wachimbaji wadogo mkoani humo. Hatua hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa Programu ya Mining for a Brighter Tomorrow (MBT), inayolenga kufuta leseni zisizoendelezwa na kuyagawa maeneo hayo kwa vijana, wanawake, na watu wenye uhitaji maalum.
Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri Mavunde amebainisha kuwa zoezi hilo ni utekelezaji wa maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na maelekezo ya Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, aliyoyatoa alipofanya ziara mkoani humo.
“Wakati wa ziara ya Mhe. Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba mliwasilisha changamoto ya upatikanaji wa maeneo ya kuchimba, na Mhe. Waziri Mkuu alielekeza Wizara kuchukua hatua ili wale wote wasioendeleza maeneo yao yarejeshwe serikalini na kugawiwa kwa wachimbaji wadogo,” amesema Mavunde.
Waziri Mavunde amefafanua kuwa Mkoa wa Katavi umejaaliwa utajiri wa madini mbalimbali, hivyo lengo la Serikali ni kuondoa kabisa utaratibu wa watu wachache kuhodhi maeneo makubwa ya leseni bila kuyaendeleza. Hata hivyo, ameongeza kuwa pamoja na kuwawezesha wachimbaji wadogo, Serikali bado inawakaribisha na kuwatazama wawekezaji wakubwa wenye nia ya dhati ya kuendeleza sekta ya uchimbaji mkoani humo.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Jamila Kimaro ameishukuru Serikali kupitia Wizara ya Madini kwa kuwapatia leseni vijana, kinamama, na watu wenye uhitaji maalum, akieleza kuwa hatua hiyo itawasaidia kujiajiri na kujikwamua kiuchumi. Aidha, amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha kupelekwa zaidi ya Shilingi bilioni 296 kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo wilayani Mpanda.
Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM) ngazi ya Mkoa wa Katavi na Wilaya, pamoja na wataalamu kutoka Wizara ya Madini na Tume ya Madini. -
Jambo TV
@Jambotv_
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimekosoa vikali taarifa rasmi iliyotolewa na Serikali ya Tanzania kwenda kwa Serikali ya Uingereza kufuatia hukumu ya miaka minne gerezani iliyotolewa dhidi ya Mwenyekiti wake ngazi ya taifa, Tundu Lissu.
CHADEMA imedai kuwa taarifa hiyo ni ya serikali kujificha nyuma ya kisingizio cha uhuru wa mahakama, mamlaka ya nchi na kutokuingiliwa masuala ya ndani na kwamba taarifa hiyo haiwezi kufuta kile CHADEMA inachodai kuwa ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu na taratibu za kisheria uliojitokeza wakati wa shauri hilo.
Msimamo huo umetolewa Ijumaa, Novemba 13, 2026, kupitia taarifa rasmi kwa umma iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa CHADEMA, Brenda Rupia. Taarifa hiyo ya CHADEMA imekuja kufuatia majibu ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ya Tanzania ya Novemba 12, 2026, iliyozitaka nchi washirika ikiwamo Uingereza kuheshimu uhuru wa mahakama na michakato ya kisheria.
Majibu hayo ya Tanzania yalitolewa baada ya Waziri wa Afrika na Maendeleo ya Kimataifa wa Uingereza, Kirsty McNeill, kutoa tamko mnamo Novemba 10, 2026, akieleza wasiwasi mkubwa wa Uingereza juu ya kutiwa hatiani kwa Lissu katika kesi ya uchochezi kutoka kwenye kesi ya uhaini na kukumbusha maoni ya Kikundi Kazi cha Umoja wa Mataifa kuhusu Uzuiaji Holela wa Uhuru (UN Working Group on Arbitrary Detention, Opinion No. 74/2025).
CHADEMA imeeleza kuwa majibu ya Serikali ya Tanzania yanasikitisha sana na ni taswira ya kiburi cha kidiplomasia kinachokiuka misingi ya demokrasia ya katiba na utawala wa sheria. Chama hicho kimesema kuwa uhuru wa mahakama hautoi kinga dhidi ya ukaguzi halali pale inapobainika kuwa kuna tuhuma nzito za ukiukaji wa taratibu za utoaji haki.
Pia, CHADEMA imekumbusha kuwa Tanzania ni... soma zaidi kupitia tovuti ya jambo.co.tz -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI:
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimehoji kuendelea kushikiliwa kwa viongozi wake wawili, Grace Shio na Fadhili Benedict Mbeya, kikisema hatua hiyo inazua maswali kuhusu uzingatiaji wa Katiba, sheria na haki za msingi za raia.
Katika taarifa iliyotolewa Novemba 13, 2026, na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa chama hicho, Brenda Rupia, CHADEMA imesema maombi ya kisheria yanayohusu kushikiliwa kwa viongozi hao yalitajwa Novemba 12 katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, shauri la Shio lilitajwa mbele ya Jaji Salma Maghimbi, ambapo mawakili waliomba mahakama iliagize Jeshi la Polisi kueleza sababu za kuendelea kumshikilia bila kumfikisha mahakamani wala kumpatia dhamana tangu Oktoba 22, 2026. Maombi yanayomhusu Mbeya, ambaye chama hicho kimesema anashikiliwa tangu Oktoba 10, 2026, yalitajwa mbele ya Jaji Awamu Mbagwa.
CHADEMA imesema haikubaliani na mwenendo wa kuwashikilia viongozi na wanachama wake kwa muda mrefu bila kuwafikisha mahakamani. Pia imedai kuwa, wakati mawakili wake wakiendelea kupambana mahakamani kutetea haki za viongozi hao, polisi wanaendelea kuwatafuta na kuwakamata viongozi wengine wa chama hicho katika maeneo mbalimbali nchini.
“Tunataka majibu. Ni sheria gani inayoruhusu mtu kushikiliwa kwa siku nyingi bila kufikishwa mahakamani? Kwa nini haki ya mtu kupata msaada wa kisheria na kuwasiliana na familia yake inakiukwa?” chama hicho kimehoji katika taarifa yake.
Chama hicho kimelitaka Jeshi la Polisi kufanya kazi kwa mujibu wa Katiba na sheria, kuacha ukamataji holela na kuheshimu haki za kila raia bila kujali msimamo wake wa kisiasa. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Dkt. Dorothy Semu, ameihimiza Serikali kuhakikisha Mkulima wa Tanzania analindwa huku akilaani hali ya wakulima kusumbuliwa na wafugaji, akisema Serikali imeshindwa kuwapa ulinzi na mazingira bora ya kufanya kilimo kwa amani.
Semu ametoa kauli hiyo Novemba 12, 2026, alipozungumza na wananchi wa Kata ya Milepa, Jimbo la Kwela, na kusema kuwa mkulima anaangukia migogoro ya ardhi na wafugaji, jambo linalomzuia kulima kwa utulivu na kuzalisha kwa kiwango kinachostahili.
Kwa mujibu wa Semu, kilimo ni sekta inayowaajiri Watanzania wengi na inayoleta fursa za ajira kwa vijana. Amesema Serikali haijaweka uwekezaji wa kutosha kumlinda mkulima na kuwezesha ukuaji wa sekta hiyo.
Semu amewataka maafisa wa Serikali kuhakikisha migogoro kati ya wakulima na wafugaji inatatuliwa kwa njia ya haki, bila kumdhuru mkulima. Ameongeza kuwa mbali na migogoro ya ardhi, mkulima anakabiliwa na changamoto nyingine zinazomfanya aendelee kuishi katika shida badala ya kufaidika na kazi yake.
Amesema ni lazima Serikali iweke mazingira bora ya kilimo ili kitoe ajira kwa watu wengi, kuongeza uzalishaji na kuboresha maisha ya wananchi, badala ya kuacha wakulima wakabiliane na migogoro wao wenyewe.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI:
Wakili Abshir Ahmedsadak Abdi wa Nairobi nchini Kenya, amepatikana akiwa hai katika eneo la Sololo, Kaunti ya Marsabit, ikiwa ni siku 12 baada ya kuripotiwa kutekwa.
Taarifa hiyo ya kupatikana kwake imethibitishwa na Huduma ya Polisi ya Kitaifa nchini humo (NPS), huku Rais wa Chama cha Wanasheria Kenya (LSK), Charles Kanjama pia akithibitisha kupatikana kwake.
Abdi aliripotiwa kutekwa alfajiri ya Novemba 1, 2026, katika eneo la Muchai Road, Kilimani, Nairobi. Inaelezwa kwamba watu wenye silaha waliovaa mavazi ya kijeshi walidaiwa kumteka mwanasheria huyo ambapo kamera za usalama (CCTV) zilirekodi tukio hilo.
Baada ya kutekwa kwa Wakili huyo, Gari lake aina ya Toyota Premio lilipatikana likiwa limeachwa karibu na Kituo cha Polisi cha Kilimani. Tukio hilo liliibua wasiwasi na kupelekea wanasheria Nairobi kuandamana wakitaka kujua alipo mwanasheria huyo.
Abdi amepatikana na wananchi katika eneo la Rawana Shopping Centre, huku rafiki yake, Ayub Maalim, akipatikana katika eneo la Uran Shopping Centre katika eneo la Sololo, Marsabit.
Wananchi hao walitoa taarifa kwa polisi, na maafisa wa Kituo cha Polisi cha Sololo waliwapeleka kituoni baada ya kupatikana. Katika kituo hicho wote wawili walirekodi taarifa zao na NPS ilisema kuwa uchunguzi unaendelea ili kubaini mazingira ya kutoweka kwao. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI:
Kampuni ya teknolojia ya Microsoft imeshuhudia hitilafu ya huduma zake za Microsoft 365, iliyoanza Novemba 12, 2026, na kuathiri watumiaji katika nchi na maeneo mbalimbali duniani.
Kutokana na hitilafu hiyo, Huduma zake zimeripotiwa kuathirika ikiwa ni pamoja na huduma ya barua pepe za Outlook, mfumo wa mawasiliano wa Teams, hifadhi ya OneDrive, SharePoint na usaidizi wa akili bandia, Copilot.
Watumiaji wa huduma hiyo wameripoti shida katika kutuma na kupokea barua pepe, kufungua faili, kufanya mikutano na kutumia vipengele vya kalenda. Microsoft imesema tatizo hilo limetokana na seva kadhaa kukosekana ghafla, hali iliyoweka mzigo mkubwa kwenye mifumo mingine ya kampuni hiyo.
Kampuni hiyo imesema imeanza kurejesha huduma, ingawa baadhi ya hatua za urejeshaji taarifa za haraka hazikufanikiwa mara moja. Microsoft pia imesema hakuna udukuzi wowote ulio sababisha hitilafu hiyo. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwenyekiti wa Umoja wa Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Fadhil Maganya, ameeleza kuwa hakuna kikwazo chochote cha kisheria wala kikatiba kinachomzuia Mtanzania kutoka Zanzibar kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mara baada ya muhula wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kumalizika.
Maganya ametoa kauli hiyo leo, Ijumaa, Novemba 13, 2026, wakati akizungumza na viongozi wa chama hicho Kanda ya Arusha, ambapo amefafanua kuwa Katiba ya nchi na kanuni zake hazijaweka sharti linalozuia marais kutoka upande mmoja wa Muungano kufuatana madarakani.
Kwa mujibu wa Maganya, kama ambavyo hakuna kizuizi cha kisheria kwa viongozi kutoka Tanzania Bara kuongoza kwa vipindi vinavyofuatana, ndivyo ambavyo Mtanzania kutoka Zanzibar ana haki na nafasi ya kushika wadhifa huo wa juu baada ya Rais Dkt. Samia.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mara nyingi imezoeoeleka kusikika wanawake wakilalamika kuwa wamepigwa na waume zao huku sauti za wanaume kuwa wamepigwa zikiwa chache, hapa Mkuu wa Dawati la Jinsia Mkoa wa Kipolisi Ilala, Mrakibu wa Polisi (SP) Glory Urassa, anaeleza kuwa dhana hiyo si kweli kwani hata wanaume hupigwa lakini wanaogopa kusema wakidhani kufanya hivyo ni kujidhalilisha.
SP Urassa ameeleza hayo kupitia kipindi cha Jambo Asubuhi cha hapa hapa Jambo TV kinachoruka mubashara kuanzia saa tatu asubuhi mpaka saa tano asubuhi siku ya Jumatatu mpaka Ijumaa.
Huko ulipo ni kweli wanaume pia wanapigwa au wanafanyiwa ukatili wenye ndoa zao lakini hawasemi?This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Wizara ya Afya imeanzisha mpango wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele, sambamba na kuendesha kambi maalumu ya upasuaji wa mabusha katika Mkoa wa Tanga.
Akizungumza na waandishi wa habari Novemba 12, 2026, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Balozi Dkt. Batilda Burian, amewataka wananchi wenye changamoto ya ugonjwa wa mabusha kujitokeza kupata huduma ya upasuaji kupitia kambi hiyo, ambayo itatolewa bure bila malipo.
Kwa upande wao, Afisa Mipango kutoka Wizara ya Afya, Mohamed Nyaki, pamoja na Daktari Gulinja Antony, ambaye ni mratibu wa magonjwa ya matende na mabusha kutoka wizara hiyo, wameeleza sababu zinazosababisha magonjwa hayo, dalili zake pamoja na namna yanavyoweza kuzuilika na kutibika.
Kambi hiyo ya upasuaji wa mabusha mkoani Tanga itafanyika katika Wilaya za Muheza Korogwe na Handeni, kuanzia Novemba 16 hadi Novemba 30, 2026.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Madereva mkoani Arusha wametakiwa kuzingatia sheria za usalama barabarani na kuepuka vitendo hatarishi vinavyoweza kusababisha ajali, huku Jeshi la Polisi likiimarisha ukaguzi wa vyombo vya moto kuelekea mwisho wa mwaka.
Akizungumza wakati wa operesheni iliyofanyika usiku wa kuamkia Novemba 13, 2026, eneo la Duka Bovu wilayani Monduli, Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoani Arusha, ACP Zauda Mohamed, amesema hatua hiyo inalenga kudhibiti makosa yanayoweza kuhatarisha maisha ya watumiaji wa barabara.
Amesema ukaguzi huo umejikita katika kubaini mwendo kasi, uendeshaji wa magari ukiwa umelewa, ubovu wa magari pamoja na kuhakikisha mabasi ya safari ndefu yanakuwa na madereva wawili kama inavyotakiwa.
Aidha, amewataka wazazi na walezi kuwa karibu na watoto wao katika kipindi hiki cha likizo, huku wamiliki wa vyombo vya moto wakisisitizwa kutunza funguo sehemu salama ili kuzuia watoto kuviendesha bila ruhusa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo, Dorothy Semu, amehoji uwazi katika ugawaji wa mikopo ya vijana yenye thamani ya Sh bilioni 200, akitaka Serikali kueleza fedha hizo zimewanufaisha vijana wangapi na kwa utaratibu gani.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Milepa, Jimbo la Kwela, Semu amesema wananchi wa eneo hilo hawajaona manufaa ya fedha hizo, licha ya Serikali kutangaza ugawaji wa mikopo hiyo.
Amesema kwa mujibu wa takwimu alizotoa, ni asilimia 25 pekee ya fedha hizo zilizokuwa zimegawanywa, huku akisisitiza kuwa uwezeshaji wa vijana unahitaji mifumo ya haki, uwazi na uwajibikaji ili kuhakikisha hata vijana wa vijijini wanapata fursa hizo.
Amemtaka Waziri Mkuu, Mwigulu Nchemba, pamoja na Waziri mwenye dhamana ya vijana, kutoa ripoti ya kina kuhusu waliopatiwa mikopo hiyo, idadi yao na mfumo uliotumika katika ugawaji.
Aidha, Semu amedai mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri imekuwa ikikabiliwa na changamoto za upendeleo, ikiwemo madai ya kunufaisha vikundi vinavyohusishwa na chama tawala na vikundi hewa.
Akitolea mfano Halmashauri ya Manispaa ya Moshi, amesema kati ya Sh milioni 360 zilizotolewa kwa vijana, wanawake na watu wenye ulemavu, Sh milioni 160 zilitumika kwa ajili ya ufuatiliaji, tofauti na Sh milioni 48 alizodai ziliruhusiwa, akitaja hali hiyo kuwa matumizi yasiyofaa ya fedha za umma.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Baada ya Bandari ya Mtwara kuboreshwa kwa gharama ya Sh bilioni 157.8 na kuongeza uwezo wa kuhudumia mizigo na kufikia tani milioni 2.6 kwa mwaka kutoka tani 400,000, wadau wengine wanataja faida wanazozipata katika shughuli zao baada ya maboresho hayo kukamilika Desemba 31, 2020.
Akizungumza katika mahojiano maalumu yaliyofanyika hivi karibuni bandarini Mtwara, mbali na faida, Ofisa Lojistiki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote, Stephen Nhwagay, pia ameeleza ufanisi wa kazi zao baada ya maboresho hayo.
Amesema majukumu yake kila siku ni kusimamia malori yanayotoka kiwandani na kwenda bandarini kushusha saruji na kupakiwa melini kisha kusafirishwa kwenda maeneo mbalimbali.
Amesema baada ya bandari hiyo kuboreshwa, wateja wao wakubwa wako Msumbiji, Comoro na Zanzibar kwa kuhakikisha wanapata saruji kwa wakati mwafaka bila changamoto yoyote.
“Kilichoongezeka baada ya maboresho ni kwamba tumeweza kusafirisha tani nyingi za saruji kwa wakati mmoja, ukiangalia hapa hii gati tunaweza kupakia saruji katika meli mbili hadi tatu kwa wakati mmoja na nyingine zinatusubiri. Kama gati nyingine hazina meli za korosho au makaa ya mawe unaweza kuhudumia meli nne kwa wakati mmoja. Kwa wiki tunaweza kupakia kati ya meli tano, meli kubwa naweza kupakia malori 150, malori 148 au malori 54. Meli hii inaweza kubeba malori 54. Lori moja linabeba ni tani 30 za saruji sawa na mifuko 600,” amesema.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Baada ya Bandari ya Mtwara kuboreshwa kwa gharama ya Sh bilioni 157.8 na kuongeza uwezo wa kuhudumia mizigo na kufikia tani milioni 2.6 kwa mwaka kutoka tani 400,000, wadau wengine wanataja faida wanazozipata katika shughuli zao baada ya maboresho hayo kukamilika Desemba 31, 2020.
Akizungumza katika mahojiano maalumu yaliyofanyika hivi karibuni bandarini Mtwara, mbali na faida, Mwakilishi wa Kampuni ya Wakala wa Meli ya Joyous Shipping Services Ltd, Esthersia Malya, ameeleza ufanisi wa kazi zao baada ya maboresho hayo.
Amesema ameona kila hatua ya maboresho inayoendelea na anaipongeza serikali kwa kuzingitia hali ya ukuaji wa bandari hiyo kwa kuongeza gati na vifaa vya kisasa vya kushusha makontena na shehena za magari.
“Tumeona maboresho yakiendelea kwa maana vifaa na mifumo ambayo inasanifu kwa kuharakisha kazi na kwenda haraka. Lakini maboresho pia ya bandari kwa maana ya kuwa na uwezo wa kufanya kazi,” anasema na kuongeza:
“Kabla tulitegemea shehena chache lakini sasa hivi tunapokea shehena za mafuta, magari na general cargo, haya ni matunda yamefanyika. Ajira nazo zinaongezeka kwa mfano soko letu la ndani, mimi nahudumia meli kubwa za saruji zinazokwenda Zanzibar, Comoro, Madagascar na Msumbiji”.
8mThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI:
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi, ameridhishwa na hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa mradi wa ulazaji wa bomba la gesi asilia kutoka kitalu cha Ntorya hadi kiwanda cha kuchakata gesi cha Madimba, mkoani Mtwara, alipofanya ziara ya kikazi mkoani humo leo, Novemba 13, 2026.
Mradi huo, wenye thamani ya takribani Shilingi bilioni 119, umekamilisha kazi ya ulazaji wa mabomba, huku kazi ya uunganishaji wa mwisho ikiendelea.
Bomba hilo lenye urefu wa kilomita 34, linatarajiwa kusafirisha gesi asilia kutoka Ntorya hadi Madimba na hivyo kuongeza kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa nishati hiyo kwa ajili ya uzalishaji wa umeme, matumizi ya viwandani, sekta ya usafiri, pamoja na matumizi ya majumbani kama vile nishati safi ya kupikia.
Akiwa katika eneo la mradi huo, Makamu wa Rais amepongeza kasi na viwango vya utekelezaji, akisisitiza kuwa mradi huo utakuwa kichocheo kikubwa cha ukuaji wa uchumi kwa wananchi wa Mtwara na Taifa kwa ujumla. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala kupitia Dawati la Jinsia na Watoto limebainisha kuwa tatizo la wanandoa kunyimana unyumba ni miongoni mwa aina za ukatili wa kisaikolojia ambazo mara nyingi haziripotiwi moja kwa moja kama malalamiko ya kujitegemea, bali huibuka kama chanzo cha migogoro mikubwa zaidi ikiwemo ukatili wa kimwili ndani ya ndoa.
Mkuu wa Dawati la Jinsia Mkoa wa Kipolisi Ilala, Mrakibu wa Polisi (SP) Glory Urassa, ameeleza hayo leo, Novemba 13, 2026, alipokuwa akizungumza katika kipindi cha Jambo Asubuhi kinachorushwa na Jambo TV.
Akifafanua kuhusu malalamiko ya wanaume kunyimwa unyumba na wake zao, SP Urassa amebainisha kuwa ingawa Jeshi la Polisi lina takwimu za matukio ya ukatili, suala la kunyimwa unyumba huwa halijitokezi mara moja kwa mtindo wa mtu kuja na kulalamika moja kwa moja mezani
Ameeleza kuwa mara nyingi malalamiko hayo huibuka wakati wa uchunguzi wa ukatili mwingine, kama vile ukatili wa kimwili ambapo mwanamke anaporipoti kupigwa na mumewe, ufuatiliaji wa kina unapofanyika hubaini kuwa mume anafanya hivyo kwa sababu ananyimwa unyumba na mke wake.
NB: KIPINDI CHA JAMBO ASUBUHI KIPO MBASHARA MUDA HUU KUPITIA CHANELI YA YOUTUBE YA JAMBO TV NA KURASA ZAKE ZA MITANDAO YA KIJAMII.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkuu wa Dawati la Jinsia Mkoa wa Kipolisi Ilala, Mrakibu wa Polisi (SP) Glory Urassa, amebainisha kuwa umaskini na ukosefu wa kipato ni miongoni mwa vyanzo vikuu vinavyochochea migogoro na matukio ya ukatili ndani ya familia.
SP Urassa ameeleza hayo leo, Novemba 13, 2026, akizungumza katika kipindi cha Jambo Asubuhi kinachorushwa na kituo cha Jambo TV.
“Chanzo kikubwa kabisa cha ukatili ndani ya familia wakati mwingine tunasema ni umasikini kwamba huyu hana huyu anacho au wote hamna kabisa... basi hapo pana njia kubwa sana ya kutokea ukatili," amesema SP Urassa.
Aidha, SP Urassa amefafanua athari za kiuchumi kwa wanaume ndani ya familia, akibainisha kuwa ukatili unaoelekezwa kwa akina baba mara nyingi ni ukatili wa kisaikolojia ambao wakati mwingine unakuwa mkubwa sana.
Ameeleza kuwa kulingana na mfumo wa kifamilia uliotatizwa na ukosefu wa fedha, baba anapokuwa hana kitu anajikuta akipoteza mamlaka na nguvu kwasababu hawi mtoaji, hali inayomfanya adharaulike na kuathirika kisaikolojia.
NB: KIPINDI CHA JAMBO ASUBUHI KIPO MBASHARA MUDA HUU KUPITIA CHANELI YA YOUTUBE YA JAMBO TV NA KURASA ZAKE ZA MITANDAO YA KIJAMII.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Serikali imeweka mikakati ya kuwawezesha watu waliokuwa waraibu wa dawa za kulevya kujitegemea kiuchumi baada ya kukamilisha matibabu kwa kuwapatia elimu, mafunzo ya ujuzi na fursa mbalimbali za kujiajiri ili waweze kurejea katika jamii na kushiriki shughuli za uzalishaji mali.
Akizungumza na waraibu katika Kitengo cha Tiba Saidizi (MAT) kilichopo Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga, Bombo, Novemba 12, 2026 Kamishna Msaidizi wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Aretas Lyimo, amesema Serikali imeanzisha vituo vya ustawi wa jamii vitakavyotoa elimu kwa jamii kuhusu namna ya kuwasaidia waraibu baada ya kukamilisha matibabu.
Amesema kupitia mpango huo, waraibu watakaopata nafuu watapatiwa mafunzo mbalimbali ya ujuzi yatakayowawezesha kujiajiri na kushiriki katika shughuli za kiuchumi ili kujipatia kipato na kuondokana na utegemezi.
Aidha, Lyimo amesema Serikali inaendelea na ujenzi wa Kituo cha Taifa cha Utengemao mkoani Dodoma, kitakachokuwa na mabweni kwa ajili ya kuwahudumia waraibu pamoja na kuwapatia mafunzo yatakayowawezesha kujitegemea.
Ameeleza kuwa ujenzi wa kituo hicho umefikia asilimia 50, hatua itakayoongeza uwezo wa Serikali katika kuwasaidia watu wanaopambana na uraibu wa dawa za kulevya kurejea katika maisha ya kawaida.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia Kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi @ppp_centre_Tz David Kafulila @kafulila_david ameeleza kuwa mkoa wa Tanga kijiografia ni mkoa wa kimkakati kiuchumi kutokana na uwepo wa bandari ambayo ni tegemezi kwa nchi nyingi za jirani.
Akizungumza katika Kongamano la Fursa za Uwekezaji na Ushiriki wa Sekta Binafsi Katika Miradi ya Ubia(PPP) lililofanyika leo Novemba 12, 2026 mkoani Tanga Kafulila ameeleza kuwa ni muhimu fursa zilizopo zikatumika vyema katika kuwainua wananchi wa kiuchumi huku akimpongeza Mkuu wa Mkoa huo Dkt. Batilda Burian kwa hatua ambazo amekuwa akichukua kujenga uchumi wa mkoa huo.
"Tanga hapa ilipo hapa ni nafasi kubwa sana na kweli hamjakosea kusema Tanga ni mkoa wa kimkakati sio kisiasa tu ni mkoa wa kimkakati kiuchumi"
Ameeleza kuwa hifadhi kubwa za mafuta na gesi zimeanza kujengwa katika mkoa huo pamoja na kupita kwa mradi kama wa bomba la mafuta linaloenda Hoima nchini Uganda kunauweka mkoa huo katika nafasi nzuri kiuchumi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katika kuchochea maendeleo ya Jiji la Tanga Mkuu wa mkoa huo Dkt. Batilda Burian ametaka miradi ya ubia ambayo imeshafanyiwa upembuzi yakinifu isimimamiwe na kutekelezwa kwa usahihi ili kuleta manufaa yanayotarajiwa.
Akizungumza katika Kongamano la Fursa za Uwekezaji na Ushiriki wa Sekta Binafsi Katika Miradi ya Ubia PPP lililofanyika leo Novemba 12 katika Ofisi yake, Dkt. Buriani amesema mkoa huo umeanza utaratibu ambapo kila robo ya mwaka utakuwa ukifanya tathmini ya utekelezaji wa miradi hiyo ya ubia.
"Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri tuhakiksihe miradi ya PPP inaandaliwa kikamilifu upembuzi yakinifu na taarifa sahihi ili iweze kuandaliwa kwa ajili ya uwekezaji"
Amesema usimamizi huo pekee hautoshi bila ushirikiano wa taasisi za fedha huku akizisihi kuandaa bidhaa ambazo zitakuwa rafiki kwa miradi ya aina hiyo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linatekeleza Mradi wa Usafirishaji Umeme wa Tanzania na Zambia (TAZA), unaogharimu zaidi ya Shilingi trilioni 2, mradi ambapo baadhi ya maboresho yake yanatarajiwa kuathiri upatikanaji wa huduma ya umeme katika mikoa 11 ya Kanda ya Kaskazini, Magharibi na pamoja na Kanda ya Ziwa kwa siku mbili kuanzia Novemba 14 na 15, 2026.
Akizungumza Leo Novemba 12, 2026 jijini Dodoma, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Mhandisi Timothy Mgaya, amesema maboresho hayo yatafanyika katika kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Zuzu jijini Dodoma, yakilenga kukiwezesha kufanya kazi kwa msongo wa kilovolti 400 (kV 400), hatua itakayoongeza uwezo wa kusafirisha na kusambaza umeme pamoja na kuimarisha uhakika wa huduma hiyo nchini.
Aidha ameeleza kuwa mikoa itakayoathirika na zoezi hilo ni Singida, Manyara, Arusha, Kigoma, Kagera, Tabora, Shinyanga, Simiyu, Geita, Mwanza na Mara, ambapo huduma ya umeme itasitishwa kuanzia saa 12:30 asubuhi hadi saa 1:30 jioni katika siku hizo mbili, huku akiwataka wananchi kuvumilia usumbufu huo wa muda wakati TANESCO ikifanya maboresho hayo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Vijana wenye elimu na ujuzi katika fani mbalimbali nchini wametakiwa kutumia fursa ya kujiunga na Mafunzo ya Kujitolea ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa mwaka 2026/27.
Wito huo umetolewa leo, Novemba 12, 2026, jijini Dodoma na Mkuu wa Tawi la Utawala wa JKT, Brigedia Jenerali Hassan Mabena, kwa niaba ya Mkuu wa JKT, Meja Jenerali Rajabu Nduka Mabele, wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Makao Makuu ya Jeshi hilo.
Amesema nafasi hizo zimetolewa kwa wahitimu wa vyuo vya kati, vyuo vikuu pamoja na vijana wenye ujuzi wa fani mbalimbali za ufundi. Amesisitiza kuwa vijana wenye sifa wanapaswa kuwasilisha maombi yao kupitia Ofisi za Wakuu wa Mikoa na Wilaya wanakoishi, ambazo zitasimamia upokeaji wa maombi na uteuzi wa watakaopata nafasi.
Kwa upande wa wahitimu wa stashahada, taaluma zinazohitajika ni Teknolojia ya Habari, Mifumo ya Taarifa za Biashara, Sayansi ya Kompyuta, ICT, Usalama wa Mitandao na Uchunguzi wa Kitaalamu wa Makosa ya Kidijitali.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mwigulu Nchemba, amewataka washiriki wa mashindano ya Michezo ya Mashirika ya Umma, Taasisi na Makampuni Binafsi (SHIMMUTA) kutumia jukwaa hilo kukemea vitendo vya mmomonyoko wa maadili vinavyoweza kuharibu mustakabali wa vijana, vizazi vijavyo na taifa kwa ujumla.
Waziri Mkuu ameyasema hayo leo mkoani Morogoro wakati wa ufunguzi wa mashindano ya SHIMMUTA, ambapo amesisitiza kuwa ni wakati sasa kwa jamii kusimama pamoja na kukemea vikali vitendo visivyofaa vinavyoendelea kujitokeza katika jamii ili kulinda maadili ya Watanzania.
Aidha, amesisitiza kuwa michezo hiyo inapaswa kuweka mazingira rafiki na wezeshi yatakayohakikisha makundi maalum yanapata fursa ya kushiriki kikamilifu katika mashindano hayo bila vikwazo.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Hamisi Mwinjuma amesema wizara hiyo itaendelea kushirikiana kwa karibu na SHIMMUTA katika kuratibu na kuendeleza mashindano hayo.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Queen Sendiga, amesema mkoa huo utaendelea kuwakaribisha wanamichezo kutoka maeneo mbalimbali nchini, huku Mwenyekiti wa SHIMMUTA, Marcel Bituro, akieleza kuwa jumla ya taasisi 96 zimeshiriki katika mashindano ya mwaka huu.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (VVU), vijana rika balehe na watumiaji wa dawa za kulevya wanatarajiwa kunufaika na huduma za afya zinazozingatia utu na usawa, kufuatia juhudi za kupunguza unyanyapaa na ubaguzi katika vituo vya afya nchini.
Juhudi hizo zinatekelezwa kupitia Afua Jumuishi ya eTFA, kwa ushirikiano kati ya Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) na Wizara ya Afya, kwa kutoa mafunzo kwa watumishi wa afya na wanafunzi wa kada mbalimbali.
Akizungumza katika mkutano wa kujadili matokeo ya afua hiyo, Mganga Mkuu wa Serikali, Dkt. Bruno Sunguya, amesema kila mwananchi anapaswa kupata huduma bora za afya bila kubaguliwa kutokana na hali yake ya kiafya au mazingira yake ya kijamii.
Amesema matokeo ya tafiti zilizofanyika yatasaidia Serikali kufanya maamuzi na kuboresha utoaji wa huduma za afya nchini.
Kwa upande wake, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Dkt. Julieth Magandi, amesema hospitali hiyo itaendelea kuhakikisha wagonjwa wanapata huduma katika mazingira salama na yasiyo na unyanyapaa, huku akisisitiza kuwa bado kuna haja ya kuimarisha juhudi hizo.
Mtafiti Mkuu na Mhadhiri wa MUHAS, Dkt. Linda Mlunde, amesema utafiti ulibaini uwepo wa unyanyapaa na ubaguzi katika baadhi ya vituo vya afya, hali iliyochochea utoaji wa mafunzo kwa watumishi na wanafunzi.
Amesema jumla ya watumishi 1,367 wa MNH na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwananyamala wamepatiwa mafunzo, huku maudhui ya kupunguza unyanyapaa yakiingizwa katika mitaala tisa ya fani za afya.
Juhudi hizo zinalenga kuhakikisha wananchi wanapata huduma za afya kwa heshima, utu na usawa bila kujali hali zao za kiafya.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
TANZANIA YAITAKA UINGEREZA KUHESHIMU UHURU WA MAHAKAMA ZA TANZANIA jambo.co.tz/tanzania-yaitaka-uingereza-kuheshimu-uhuru-wa… via @jambotv_
-
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI:
Tanzania imesisitiza umuhimu wa kuongeza ufadhili na uwekezaji katika miradi ya kilimo himilivu ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi, kuimarisha usalama wa chakula na kuongeza kipato cha wakulima, hususan wanawake na vijana.
Msisitizo huo umetolewa Novemba 11, 2026, katika Mkutano wa Wadau wa Sekta ya Kilimo uliofanyika pembezoni mwa Mkutano wa 31 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP31), unaofanyika Antalya, Uturuki, kuanzia Novemba 9 hadi 20, 2026.
Mkutano huo uliwakutanisha wawakilishi wa Serikali, taasisi za fedha, sekta binafsi na washirika wa maendeleo duniani kujadili mikakati ya kuongeza upatikanaji wa fedha kwa ajili ya miradi ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi katika mifumo ya chakula.
Akizungumza katika mkutano huo, Mkurugenzi wa Kitengo cha Usimamizi wa Mazingira kutoka Wizara ya Kilimo, Zaninabu T. Sheuya, amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya Serikali, sekta binafsi na washirika wa maendeleo katika kuongeza uwekezaji kwenye kilimo himilivu.
Sheuya amesema Serikali ina dhamira ya kuhakikisha upatikanaji wa fedha za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi unaongezeka, huku kipaumbele kikitolewa kwa wakulima wanaokumbwa moja kwa moja na athari zake.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkazi wa CARE Tanzania, Prudence Masako, amewahimiza wadau kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuongeza uwekezaji wa miradi yenye matokeo chanya katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Amesema uwekezaji huo ni muhimu katika kuimarisha usalama wa chakula, kuongeza kipato cha wakulima wadogo na kuchochea maendeleo ya uchumi endelevu.
Ufadhili wa miradi hiyo unatarajiwa pia kuchochea utekelezaji wa vipaumbele vya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 katika sekta ya kilimo kwa kuelekeza rasilimali kwenye uwekezaji utakaoongeza tija, ushindani na uwezo wa sekta hiyo kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Wananchi wa Wilaya ya Nanyumbu Mkoani Mtwara wameeleza changamoto mbalimbali walizokuwa wakikabiliana nazo katika kutafuta maji kabla ya kuanza kwa mradi wa maji kutoka Mto Ruvuma hadi Mangaka, ikiwemo kutembea umbali mrefu kufuata maji pamoja na baadhi yao kushambuliwa na mamba na kupoteza maisha.
Serikali imetumia zaidi ya shilingi bilioni 38 kutekeleza mradi huo kwa lengo la kutatua changamoto ya muda mrefu ya upatikanaji wa maji katika wilaya hiyo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius John Ndejembi, ameweka jiwe la msingi la mradi huo huku akiwataka wananchi kutunza misitu na vyanzo vya maji ili kuhakikisha mradi huo unadumu kwa muda mrefu na kunufaisha vizazi hadi vizazi.
Wananchi hao wameonesha furaha na kutoa shukrani kwa Serikali kwa kutekeleza mradi huo utakaowasaidia kuondokana na adha ya upatikanaji wa maji safi na salama.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeitaka Serikali ya Uingereza na washirika wa kimataifa kuheshimu uhuru wa Mahakama na michakato ya kisheria ya Tanzania, ikisisitiza kuwa hukumu iliyotolewa dhidi ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu ilifuata misingi ya Katiba, sheria na haki zote za kisheria.
Msimamo huo umetolewa leo, Novemba 12, 2026, kupitia taarifa rasmi kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Kitengo cha Mawasiliano cha Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Taarifa hiyo imekuja kufuatia tamko lililotolewa Novemba 10, 2026 na Waziri wa Afrika na Maendeleo ya Kimataifa wa Uingereza, Kirsty McNeill, aliyeeleza kuwa Serikali ya Uingereza ina wasiwasi mkubwa kuhusu kutiwa hatiani kwa Lissu katika kesi ya uchochezi.
Katika tamko hilo, McNeill alikumbusha maoni ya Kikundi Kazi cha Umoja wa Mataifa kuhusu Uzuiaji Holela wa Uhuru (UN Working Group on Arbitrary Detention, namba 74/2025), kilichobaini kuwa Lissu alishikiliwa kiholela bila msingi wa kutosha wa kisheria na kwamba kulikuwa na dosari kubwa katika mwenendo wa haki wa kesi hiyo.
Serikali ya Uingereza iliongeza kuwa hatua hiyo inakiuka Tamko la Kimataifa la Haki za Binadamu na Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiraia na Kisiasa ambapo Tanzania ni mwanachama, huku ikiikumbusha Tanzania wajibu wake wa kulinda haki za binadamu, ikiwamo kupata haki katika mwenendo wa kesi, uhuru wa kujieleza, kushiriki katika shughuli za kisiasa, kutendewa kwa usawa mbele ya sheria na kuendeleza maridhiano ya kisiasa.
Ikijibu wasiwasi huo wa Uingereza, Wizara ya Mambo ya Nje imebainisha kuwa hukumu ya Lissu ilitolewa na mahakama yenye mamlaka kamili kisheria baada ya kukamilika kwa mchakato unaostahili wa kisheria uliompa Lissu fursa zote za haki.
Wizara imebainisha kuwa ilielezwa kuwa Lissu alipata haki zote za msingi kabla na wakati wa shauri hilo, ikiwa ni pamoja na kuwakilishwa na mawakili wa kisheria, kupewa fursa ya kusikilizwa kwa haki, pamoja na kupewa ufafanuzi kamili wa haki yake ya kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.
Serikali ya Tanzania imesisitiza kuwa uhuru wa vyombo vya utoaji haki ni nguzo kuu isiyotikisika ya mfumo wa katiba wa nchi hiyo, na kwa msingi huo ikawataka washirika wote wa kimataifa kuheshimu uhuru wa Mahakama na michakato ya kisheria ya Tanzania badala ya kuingilia maamuzi yake.
“Wizara inapenda kufafanua zaidi kuwa, uhuru wa mahakama ni nguzo kuu ya mfumo wa katiba wa Tanzania, na kwa hiyo Serikali inatoa wito kwa washirika wote kuheshimu uhuru wa mahakama na michakato ya kisheria ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasalia thabiti katika ahadi yake ya kutetea haki za binadamu na utawala wa sheria," imesistitiza taarifa hiyo.
Aidha, Tanzania imekumbusha kuwa inafurahia uhusiano wa kihistoria, wa karibu na wa kirafiki na Uingereza uliodumu kwa miongo mingi, ukizingatia misingi ya kuheshimiana, maadili ya pamoja, ushirikiano wa maendeleo, biashara, uwekezaji, elimu na uhusiano wa wananchi wa pande zote mbili. Hata hivyo, imeweka wazi kuwa masuala yote yanayohusu masilahi ya pande mbili yanapaswa kujadiliwa kupitia mashauriano ya kidiplomasia yanayoheshimu mipaka ya kila nchi na kutokuingilia masuala ya ndani ya nchi nyingine -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
"Penye uamuzi ambao adhabu yake ni ama kifungo, ama faini, ama vyote kwa pamoja, kwa mshtakiwa wa kwanza, na ukisoma hukumu Mahakama inakiri wazi kwamba huyu ni mshtakiwa wa kwanza, kwahiyo ilitakiwa mtu huyo apewe kipaumbele cha adhabu ya faini"...
Lakini licha ya mtuhumiwa kwamba aliieleza Mahakama juu ya hili kwamba mtuhumiwa ni mshtakiwa wa kwanza, kwahiyo toeni adhabu ya faini, bado Mahakama haikuweza kuzingatia hilo" amesema Wakili Maduhu.
Meneja wa Ufuatiliaji na Majibu wa Haki za Binadamu katika Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Wakili William Maduhu, amesema hayo leo Novemba 12, 2026 jijini Dar es Salaam alipokuwa akiwasilisha uchambuzi wa taarifa ya LHRC mbele ya vyombo vya habari, iliyohusu Uchambuzi wa Hukumu ya Lissu kutoka Uhaini mpaka Uchochezi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Haki za Binadamu (LHRC), Wakili Fulgance Massawe, amesema kesi za Uhaini na Ugaidi zinachafua sura ya nchi na kuonesha Serikali ni dhaifu na kwamba kesi hizo zinatumika ili kuwaumiza wakabiliwa kutokana na kutokuwa na dhamana.
Wakili Massawe amebainisha hayo alipomuwa akizungumza na Vyombo va Habari, leo Novemba 12, 2026, jijini Dar es Salaam katika Uchambuzi wa Hukumu ya Lissu kutoka Uhaini hadi Uchochezi, uchambuzi ulioratibiwa na LHRC.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katika hali isiyo ya kawaida, Mganga wa tiba za asili jijini Dodoma, ameweka bango kubwa linalotangaza huduma za mvuto wa mapenzi na huduma zingine katikati ya Makaburi ya Chang’ombe, akidai kuwa kufanya shughuli zake katika eneo hilo ni sehemu ya maelekezo aliyopewa na wazee wake pamoja na kudumisha mila.
Akizungumza leo, Novemba 12, 2026, jijini Dodoma, Mganga huyo anayetambulika kwa jina la Kasana Shabani amesema amekuwa akifanya shughuli zake katika eneo hilo kwa kutumia nguvu za mizimu, huku akisisitiza kuwa hataondoka hadi atakapopokea maelekezo mengine.
“Ninafanyia shughuli hapa makaburini kwa sababu ni maelekezo kutoka kwa wazee wangu. Mpaka pale nitakapopokea maelekezo mengine, ndipo nitaondoka,” amesema Kasana.
Kwa upande wao, baadhi ya wakazi wanaoishi maeneo ya jirani na makaburi hayo wamesema uwepo wa bango hilo umekuwa kero kwa jamii, hivyo wameiomba Serikali kuingilia kati na kuhakikisha linaondolewa, wakieleza kuwa eneo hilo si sehemu inayostahili kufanyiwa shughuli za aina hiyo.
Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Chang’ombe ambaye pia ni Naibu Meya wa Jiji la Dodoma, Bakari Samweli, amesema hawezi kutoa ufafanuzi kuhusu uwepo wa bango hilo kwa sasa, akieleza kuwa anahitaji kufuatilia kwanza ili kupata taarifa sahihi kuhusu iwapo limewekwa kwa kufuata taratibu zinazotakiwa. Amesema baadhi ya mabango huwekwa bila kushirikisha ofisi za uongozi wa mitaa.
Aidha, Jambo Tv imefanya jitihada za kuwatafuta mamlaka zinazohusika na usimamizi na udhibiti wa uwekaji wa mabango jijini Dodoma kwa siku tatu mfululizo, lakini haikufanikiwa kupata ufafanuzi kuhusu utaratibu uliofuatwa katika uwekaji wa bango hilo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI:
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi, ameagiza kuanza kwa operesheni maalumu ya kuwabaini na kuwakamata watu wanaochochea migogoro ya wakulima na wafugaji katika Wilaya ya Tunduru, Mkoa wa Ruvuma, huku akitaka kupatiwa taarifa ya hatua zilizochukuliwa akiwa bado katika ziara yake mkoani humo.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara na wananchi wa Tunduru, Leo Novemba 12, 2026, Makamu wa Rais amesema Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imesikia kilio cha wananchi kutokana na migogoro hiyo iliyosababisha vifo vya watu, wakiwemo wananchi, viongozi na askari, na kwamba wakati umefika wa kuchukua hatua madhubuti kurejesha amani.
Ameelekeza Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Mkuu wa Wilaya ya Tunduru na Kamati za Ulinzi na Usalama kuwachukulia hatua wote watakaobainika kuchochea migogoro hiyo, bila kujali nafasi zao, nyadhifa au itikadi zao za kisiasa.
Makamu wa Rais amesema baadhi ya viongozi wa vijiji wanadaiwa kushiriki katika uuzaji wa maeneo na kuwaingiza wafugaji katika maeneo yasiyoruhusiwa, hali inayochangia migogoro ya mara kwa mara kati ya wakulima na wafugaji.
Ndejembi ambaye bado anaendelea na ziara yake kwenye mikoa ya Kusini, ameelekeza kuwa matumizi ya ardhi ya vijiji lazima yazingatie sheria na ushirikishwaji wa wananchi badala ya maamuzi ya watu wachache wenye maslahi binafsi.
Aidha, ameeleza kuwa Serikali inaendelea kutafuta suluhu ya kudumu kupitia timu ya kitaifa na wizara zinazohusika, lakini juhudi hizo zinapaswa kwenda sambamba na hatua za haraka dhidi ya wanaochochea migogoro.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Ayoub Mahmoud, amesema serikali imepokea maelekezo hayo na kwamba Jeshi la Polisi litashirikiana na mamlaka nyingine kuhakikisha wote wanaobainika kuhusika wanachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Meneja wa Ufuatiliaji na Majibu wa Haki za Binadamu katika Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Wakili William Maduhu, amesema ili dhana ya kosa dogo itumike kama ilivyofanyika katika hukumu dhidi ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, ni lazima mambo mbalimbali yazingatiwe ikiwemo, ushahidi wa kosa kubwa uthibitishe kosa dogo, kosa dogo liwe linatokana na jamii moja au kundi moja la kosa kubwa pamoja na mshtakiwa kupewa taarifa ya kujiandaa dhidi ya hilo kosa dogo.
Wakili Maduhu amebainisha yaho leo Novemba 12, 2026 jijini Dar es Salaam alipokuwa akiwasilisha uchambuzi wa taarifa ya LHRC mbele ya vyombo vya habari, iliyohusu Uchambuzi wa Hukumu ya Lissu kutoka Uhaini mpaka Uchochezi.
Ameongeza kwamba, ili kosa dogo litumike ni lazima upande wa mashtaka uwe uliomba kwamba ikiwa mshtakiwa hatokutwa na hatia kwa kosa kubwa, basi liangaliwe kosa dogo, jambo ambalo Wakili maduhu amesema halikufanyika.
Aidha amesema kwamba, hata katika hukumu ya Mahakama dhidi ya Lissu, mshtakiwa alipinga mbele ya majaji kwamba hakuna kosa dogo dhidi ya uhaini. Amesema kutokana na hoja hiyo hata upande wa Mashtaka (Jamhuri) hawakupinga chochote.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dkt. Anna Aloys Henga amesema kituo hicho kimebaini ukiukwaji wa haki mbalimbali za binadamu ikiwemo haki ya kuabudu, faragha, sambamba na kukamatwa na kuteswa kwa baadhi ya waangalizi wa kimataifa katika kesi hiyo.
Henga amebainisha hayo leo Novemba 12, 2026 jijini Dar es Salaam, wakati akiwasilisha taarifa ya kituo hicho mbele ya vyombo vya habari, iliyohusu Uchambuzi wa Hukumu ya Lissu kutoka Uhaini mpaka Uchochezi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dkt. Anna Aloys Henga, amesema kituo hicho kimebaini kwamba, katika kipindi cha mwenendo wa shauri la uhaini dhidi ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, muda wa kukamilishwa kwa upelelezi haukuzingatiwa kwani muda huo unatakiwa kukamilika ndani ya siku 90, badala yake katika shauri hilo ilichukua miezi mitano.
Hayo yamebainishwa leo Novemba 12, 2026 jijini Dar es Salaam, na Mkurugenzi Mtendaji huyo alipokuwa akiwasilisha taarifa ya kituo hicho mbele ya vyombo vya habari, iliyohusu Uchambuzi wa Hukumu ya Lissu kutoka Uhaini mpaka Uchochezi.
"Suala la tatu, kutokuzingatiwa kwa muda wa kukamilisha upelelezi. Kwa mujibu wa aya ya 7(3) ya Mwongozo wa Mkurugenzi wa mashtaka namba moja wa mwaka 2022, kuhusu ufunguaji wa mashtaka na ukamilishaji wa upelelezi wa kesi za jinai wa tarehe 30 Septemba 2022, upelelezi wa kesi zinazoruhusiwa kufunguliwa kabla ya upelelezi unatakiwa kukamilishwa ndani ya siku zisizozidi 90, hata hivyo mwenendo wa shauri la ndugu Lissu ulichukua takribani miezi mitano" amesema.
Ameongeza kwamba, licha ya mwongozo huo kuruhusu upande wa mashtaka kuomba muda wa ziada pale inapohitajika lakini upande huo haukuwasilisha ombi hilo jambo lililochangia shauri kuchukuwa muda mrefu zaidi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Deogratius Ndejembi, alivyombana Mkandarasi wa mradi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa kilovolti 220 kutoka Songea–Tunduru–Masasi–Mahumbika, kutokana na kutoridhishwa na kasi ya utekelezaji wa mradi huo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwenyekiti wa Ngome ya Wanawake Taifa wa ACT Wazalendo na Waziri Kivuli wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Janeth Rite, amesema Jeshi la Polisi lina wajibu wa kulinda raia na mali zao badala ya kutumika kulinda maslahi ya chama chochote cha siasa.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Miombo, Kata ya Mashete, Wilaya ya Nkasi, mkoani Rukwa, Rite amesema polisi, akiwemo Mkuu wa Polisi wa Wilaya (OCD), wanapaswa kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia wajibu wa kisheria wa kulinda wananchi bila upendeleo wa kisiasa.
Aidha, Rite amedai kuwa ACT Wazalendo ndicho chama tawala katika Kata ya Mashete, huku CCM kikiwa chama cha upinzani, akieleza kuwa chama chake hakipaswi kuzuiwa kutekeleza wajibu wake wa kuisimamia serikali na kukagua miradi ya maendeleo.
Amesema kwa kuwa Diwani wa kata hiyo, Michael Katumbo, anatoka ACT Wazalendo, chama kina wajibu wa kufuatilia utekelezaji wa miradi na matumizi ya rasilimali za umma bila kuwekwa vikwazo vya kiutawala.
Akifafanua msimamo wake, Rite ametumia mfano wa paka mmoja anayeweza kuwafukuza panya wanaoharibu ghala la mahindi, akimaanisha kuwa hata diwani mmoja anaweza kuwa na mchango mkubwa katika kupambana na ufisadi na kulinda rasilimali za wananchi.
Amesisitiza kuwa chama hicho kitaendelea na juhudi za kuisimamia serikali na kupigania mabadiliko.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Afisa Ardhi Mteule wa Manispaa ya Kinondoni, Kelvin Kipeta amewataka wamiliki wa viwanja vilivyopimwa kuzingatia masharti yote yaliyoainishwa kwenye hati zao za umiliki, ikiwa ni pamoja na kuomba kibali cha ujenzi ndani ya miezi sita na kuanza ujenzi ndani ya miaka mitatu, la sivyo watakabiliwa na notisi za kufutiwa hati na kupoteza umiliki wa viwanja hivyo.
Kipeta amebainisha hayo leo, Novemba 12, 2026, alipokuwa akizungumza katika kipindi cha Jambo Asubuhi cha Jambo TV kilichowakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya ardhi na kufanyika katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni.
Akifafanua maana halisi ya kuendeleza kiwanja, Kipeta ameeleza kuwa mwananchi anaposaini hati ya umiliki anakuwa ameingia mkataba rasmi na serikali unaomtaka kulipa kodi ya ardhi na kuendeleza eneo hilo kulingana na matumizi yaliyopangwa. Amebainisha kuwa kufyeka majani au kuweka uzio wa waya pekee hakutafsiriwi kama kuendeleza kiwanja, bali mwananchi anapaswa kuwasilisha michoro na kuomba kibali cha ujenzi Halmashauri.
Hata hivyo, Kipeta ametoa ufafanuzi kuwa wananchi wanaoshindwa kuendeleza viwanja vyao kutokana na majanga ya kiafya au mkwamo wa kiuchumi hawapaswi kukaa kimya, bali wanatakiwa kuandika barua kwa Kamishna wa Ardhi wakiambatanisha ushahidi kama vyeti vya daktari au maelezo ya hali ya kiuchumi ili kuomba nyongeza ya muda.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Saad Mtambule amebainisha kuwa chanzo kikuu cha migogoro ya ardhi kwa sasa si kuwepo kwa hati mbili halali katika eneo moja, bali ni tabia ya matapeli kutumia nyaraka feki ikiwemo mikataba ya mauzo ya uongo na mihtasari ya mirathi ya kufoji ili kutengeneza hati na kuwadhulumu wamiliki halali.
Mtambule amebainisha hayo leo, Novemba 12, 2026, akizungumza katika kipindi cha Jambo Asubuhi cha Jambo TV kinachowakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya ardhi.
Mtambule ameeleza kuwa kutokana na mifumo ya kiserikali kuimarishwa, suala la eneo moja kutolewa hati mbili za kiserikali kwa sasa halipo na ni jambo lisilowezekana kabisa kwa hati zilizotolewa kuanzia miaka ya 2005 na 2010 kuja juu, tofauti na maeneo machache yenye hati za zamani za miaka 99 zilizotolewa miaka ya 1980 na mapema miaka ya 1990.
Amesisitiza kuwa hati inapotolewa na serikali, nakala inabaki wizarani na nyingine anakaa nayo mwananchi, jambo linalowezesha ufuatiliaji rasmi kufanyika kwa urahisi.
NB: KIPINDI CHA JAMBO ASUBUHI KIPO MBASHARA MUDA HUU KUPITIA CHANELI YA YOUTUBE YA JAMBO TV NA KURASA ZAKE ZA MITANDAO YA KIJAMII.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mchambuzi wa masuala ya siasa, Ezekiel Kamwaga amebainisha kuwa tafiti za kisayansi za kisiasa zinaonesha wazi kwamba inapotokea fujo au vurugu katika nchi, vyama vya upinzani havifaidiki bali chama kilichopo madarakani ndicho kinachopata faida na fursa ya kubaki madarakani.
Kamwaga ameeleza kuwa hali ya siasa za dunia kwa sasa iko katika kile alichokiita "kipindi cha mserereko", ambapo mambo ya kisiasa yanaweza kubadilika kwa kasi kubwa ndani ya muda mfupi.
Akifafanua sababu zinazofanya fujo na vurugu kukinufaisha chama kilichopo madarakani badala ya vyama vya upinzani, Kamwaga ametaja sababu ya kwanza kuwa ni saikolojia ya binadamu, ambapo mtu anapoona uhai wake uko hatarini husahau kuhusu haki za kisiasa au kiuchumi na kuweka kipaumbele katika kulinda salama ya maisha yake.
Sababu ya pili amebainisha kuwa ni kundi la wananchi wengi walio kimya ambao baada ya fujo kujitokeza, hujipanga kupitia kura au njia zingine kuonesha kutokubaliana na vurugu hizo. Sababu ya tatu ni wapigakura wasio na upande ambao mara zote hukimbilia upande wenye utulivu na amani badala ya upande unaosababisha ghasia. Sababu ya nne ni kwamba machafuko husababisha viongozi na vyombo vya dola kushikamana kwa pamoja kama adui mmoja, jambo linalofanya upinzani kukosa uungwaji mkono kutoka ndani ya mfumo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Rhimo Nyansaho amesisitiza dhamira thabiti ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuendeleza misingi ya Umoja wa Afrika, usalama wa pamoja, na ushirikiano wa kikanda ili kudumisha amani barani Afrika.
Dkt. Nyansaho ametoa kauli hiyo Novemba 11, 2026, jijini Arusha, wakati akifunga rasmi Mkutano wa 20 wa Makamanda wa Vyuo vya Ukamanda na Mafunzo ya Kijeshi barani Afrika (African Conference of Commandants- ACoC
Katika hotuba yake, Dkt. Nyansaho amewasilisha salamu za pongezi kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa washiriki wote wa mkutano huo.
Aidha, amewapongeza makamanda na wajumbe kwa ushiriki wao na michango yenye tija katika kuimarisha elimu ya kijeshi na kukuza ushirikiano baina ya taasisi za kijeshi barani Afrika.
Amesisitiza kuwa elimu na mafunzo ya kitaaluma ya kijeshi yana nafasi muhimu katika kuandaa viongozi wenye maarifa, maono na uwezo wa kukabiliana na changamoto za kiusalama zinazozikabili nchi za Afrika, zikiwemo ugaidi, uhalifu wa kupangwa unaovuka mipaka ya nchi na vitisho vya kimtandao.
Aidha, amehimiza kuimarishwa kwa ushirikiano baina ya vyuo vya kijeshi kupitia mafunzo ya pamoja, kubadilishana wanafunzi na wakufunzi pamoja na kuoanisha mitaala ya mafunzo ya kijeshi, hususan katika maeneo ya Operesheni za Kusaidia Amani, Sheria za Kimataifa za Kibinadamu na Ulinzi wa Raia.
Mkutano huo uliwakutanisha viongozi waandamizi wa kijeshi na wajumbe kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika, akiwemo Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Luteni Jenerali Salumu Haji Othman, Mkuu wa Chuo cha Ukamanda na Unadhimu Tanzania na Mwenyekiti wa Mkutano wa Makamanda wa Vyuo vya Kijeshi vya Afrika (ACoC), Meja Jenerali Stephen Justice Mnkande, Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, Meja Jenerali Rajabu Mabele, wawakilishi wa Umoja wa Afrika, makamanda wa vyuo vya kijeshi, wakufunzi wakuu na maafisa waandamizi wa kijeshi.
Mkutano huo umekuwa jukwaa muhimu la kubadilishana uzoefu, maarifa na mbinu bora za mafunzo ya kijeshi, kwa lengo la kuimarisha uwezo wa pamoja wa majeshi ya Afrika na kuendeleza ushirikiano katika kukabiliana na changamoto za kiusalama, hivyo kuchangia juhudi za kudumisha amani, usalama na utulivu wa kudumu barani Afrika. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Dorothy Semu, ameitaka Serikali kutoa maelezo ya kina kuhusu sababu alizosema zinazosababisha takriban asilimia 30 ya wanafunzi wanaoandikishwa shule nchini kutokamilisha masomo yao.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Miombo, Kata ya Mashete, Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa, Semu amesema pamoja na wanafunzi wengi kuandikishwa katika shule za msingi na sekondari, idadi kubwa imekuwa ikiishia njiani bila kuhitimu.
Akitoa takwimu za kielimu katika mkutano huo, Semu ameeleza kuwa kati ya wanafunzi zaidi ya milioni moja na laki saba walioanza darasa la kwanza mwaka 2020, ni wanafunzi zaidi la milioni moja na laki moja pekee ndio walioweza kufika na kuhitimu darasa la saba mwaka 2026, huku wengine zaidi ya laki tano wakikosa mtihani wa mwisho.
Aidha, kwa upande wa elimu ya sekondari, amesema kati ya wanafunzi 1,073,402 waliojiunga na kidato cha kwanza mwaka 2022, walioweza kuhitimu kidato cha nne mwaka 2026 ni 617,040 pekee, jambo lililoacha pengo la wanafunzi 456,362 ambao hawakufanya mtihani.
Kufuatia hali hiyo, kiongozi huyo amewataka Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Prof. Riziki Shemdoe, pamoja na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, kuwajibu Watanzania juu ya hatima ya watoto hao.
"Tunawauliza mawaziri Prof. Shemdoe na Prof. Mkenda, watoto hawa wako wapi? Na serikali imeweka mikakati gani ya kuhakikisha wote wanaoandikishwa shuleni wanamaliza masomo yao?" alihoji Semu.
Semu amesisitiza kuwa uwekezaji madhubuti katika elimu na kuhakikisha kila mtoto anahitimu masomo yake ndiyo silaha pekee ya kulikomboa taifa dhidi ya maadui watatu ambao ni ujinga, maradhi na umaskini.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Saad Mtambule, amebainisha kuwa serikali ya wilaya hiyo imeweka mfumo madhubuti wa timu jumuishi yenye "macho ya aina mengi" inayoshirikisha maafisa ardhi, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), pamoja na Jeshi la Polisi ili kubaini kiini cha migogoro ya ardhi na kutenda haki bila kuangalia hali ya kifedha au kijamii ya wahusika.
Mtambule amebainisha hayo leo, Novemba 12, 2026, alipokuwa akizungumza katika kipindi cha Jambo Asubuhi cha Jambo TV kinachowakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya ardhi.
Mtambule ameeleza kuwa timu hiyo inatathmini mifumo ya ardhi, nyaraka, historia ya umiliki kuanzia mwanzo, pamoja na kutuma maafisa kuratibu mifumo katika eneo la tukio. Ameongeza kuwa pale inapobainika kuwa kuna viashiria vya jinai kama vile utapeli au unyang'anyi, serikali inasimama na haki, akitolea mfano mtu anayedai kuuziwa ardhi na "kijiji" ndani ya Wilaya ya Kinondoni wakati wilaya hiyo haina kijiji hata kimoja.
NB: KIPINDI CHA JAMBO ASUBUHI KIPO MBASHARA MUDA HUU KUPITIA CHANELI YA YOUTUBE YA JAMBO TV NA KURASA ZAKE ZA MITANDAO YA KIJAMII.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Dorothy Semu, ameitaka serikali kutoa maelezo ya kina kuhusu sababu za mbolea ya ruzuku kutowafikia wakulima wa vijijini, licha ya madai ya Serikali kuwa imeongeza bajeti ili kupunguza gharama za pembejeo hiyo.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Miombo, Kata ya Mashete, Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa, Novemba 11, 2026, Semu amesema kuwa hakuna mkulima yeyote katika maeneo ya Mashete na Miombo ambaye amenufaika na mbolea hiyo ya ruzuku.
Amesema hali hiyo imesababisha bei ya mbolea kuwa mzigo na kikwazo kikubwa kwa wakulima, jambo alilosema linaathiri uzalishaji wa mazao.
"Bei ya mbolea imekuwa kichwa cha ugumu kwa wakulima. Huku taifa likitegemea kilimo kwa ajili ya ajira na kukuza uchumi, Serikali imeshindwa kumlinda mkulima na kumpa mazingira wezeshi," amesema Semu.
Kiongozi huyo ameitaka Serikali kuchukua hatua za haraka kuhakikisha mbolea inapatikana kwa bei rafiki na kuwafikia wakulima wote moja kwa moja, badala ya kuendelea kutoa ahadi na "hadithi za ruzuku" ambazo hazina uhalisia kwa wananchi wa chini.
Aidha, Semu alisisitiza kuwa uwekezaji wa dhati katika sekta ya kilimo ndiyo njia pekee ya uhakika ya kumkomboa Mtanzania wa kawaida kutoka kwenye lindi la umaskini, pamoja na kutengeneza fursa za ajira kwa vijana wengi wanaotegemea kilimo kuendesha maisha yao.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Saad Mtambule amewatahadharisha wananchi na wanunuzi wa ardhi kutokimbilia kulipia viwanja au nyumba kabla ya kufanya ufuatiliaji wa kina katika maeneo husika pamoja na kwenye mamlaka za serikali, akibainisha kuwa haraka na ukiukwaji wa taratibu ndivyo vinavyochochea utapeli na migogoro ya ardhi wilayani humo.
Mtambule amebainisha hayo leo, Novemba 12, 2026, alipokuwa akizungumza katika kipindi cha Jambo Asubuhi cha Jambo TV, kilichowakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya ardhi.
Akieleza makosa yanayofanywa na wanunuzi, Mtambule amebainisha kuwa wanunuzi na wauzaji wamekuwa wakikutana kwa harakaharaka katika maeneo ya hoteli au kupitia matangazo bila kwenda eneo husika (site) kufanya ufuatiliaji wa kutosha
“Isivyo bahati matapeli wa ardhi hawatoi hiyo nafasi ya wewe kufanya due diligence (Due diligence) ...watakuambia kuna mtu mwingine anakitaka hicho kiwanja, mtu anaenda benki analipa milioni 100 halafu jioni anaambiwa kiwanja sio cha yule bwana ni cha mtu mwingine... Tusikimbie kulipia ardhi kabla ya kufanya ufuatilaji huo na kujiridhisha kwenye mamlaka," amesisitiza Mtambule.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam, Saad Mtambule amebainisha kuwa migogoro ya ardhi ndiyo changamoto kuu inayoongoza kwa kulalamikiwa wilayani humo, ambapo kati ya wananchi 10 wanaofika katika ofisi yake kutafuta msaada, watu saba wanakuwa na kero za ardhi.
Mtambule amebainisha hayo leo, Novemba 12, 2026, alipokuwa akizungumza katika kipindi cha Jambo Asubuhi cha Jambo TV kinachowakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya ardhi na kufanyika katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni.
Ameeeleza kuwa ili kukabiliana na mawimbi ya migogoro hiyo, ofisi yake imeweka utaratibu wa kila siku ya Alhamisi kuwa siku ya kusikiliza kero hizo, ambapo Alhamisi moja wanawasikiliza wananchi ofisini na Alhamisi inayofuata wanaenda eneo la tukio (site) kujionea wenyewe msingi wa mgogoro.
NB: KIPINDI CHA JAMBO ASUBUHI KIPO MBASHARA MUDA HUU KUPITIA CHANELI YA YOUTUBE YA JAMBO TV NA KURASA ZA MITANDAO YAKE YA KIJAMII.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Tanzania inatumia jukwaa la Mkutano wa 31 wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP31) unaofanyika Antalya, Uturuki, kuimarisha ushirikiano na wadau wa kimataifa katika kufanikisha lengo la kuhakikisha asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2034.
Waziri wa Nishati, Juma Homera, amesema kupitia mkutano huo Tanzania imekutana na wadau mbalimbali walioonesha utayari wa kushirikiana na nchi katika kufanikisha azma hiyo, akiwemo taasisi ya Sustainable Energy for All, ili kuimarisha upatikanaji na matumizi ya nishati safi ya kupikia kuanzia vijijini hadi mijini.
Amesema ushirikiano huo utaongeza nguvu katika utekelezaji wa ajenda ya nishati safi ya kupikia inayohamasishwa na Rais Samia Suluhu Hassan, ambaye ni kinara wa Umoja wa Afrika (AU) katika kuendeleza matumizi ya nishati safi ya kupikia barani AfrikaThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Félix Tshisekedi, ametia saini sheria mpya namba 26/045 inayoweka misingi na masharti ya kuandaa kura ya maoni nchini humo. Hatua hiyo inafungua rasmi milango ya kisheria ya kufanya marekebisho katika Katiba ya sasa au kuandika Katiba mpya kabisa.
Taarifa zilizotolewa leo, Novemba 11, 2026, na vyanzo mbalimbali vya habari nchini humo zimebainisha kuwa sheria hiyo ilisainiwa rasmi Novemba 9, 2026, kufuatia kupitishwa kwake na Bunge mnamo Oktoba 2026. Sheria hiyo mpya inachukua nafasi ya sheria ya awali ya Juni 22, 2005, na inapanua wigo wa kura ya maoni kwa kuwapa wananchi fursa ya kupiga kura ya 'Ndiyo' au 'Hapana' kuhusu rasimu mpya ya Katiba au marekebisho ya vifungu fulani iwapo dharura itajitokeza.
Kwa mujibu wa mfumo huo mpya, kura ya maoni inaweza kuitishwa na Rais, Serikali kupitia uamuzi wa Baraza la Mawaziri, nusu ya wabunge kutoka kila nyumba ya Bunge, au kwa ombi rasmi la wananchi 100,000. Kabla ya kutiwa saini, muswada huo ulifanyiwa marekebisho katika vifungu 13 ili kuzingatia maelekezo ya Mahakama ya Katiba baada ya kurudishwa bungeni.
Hatua hiyo ya kisheria imeibua ghadhabu na mvutano mkubwa wa kisiasa kutoka kwa vyama vya upinzani nchini DRC, ambavyo vinapinga vikali sheria hiyo vikiiita "mapinduzi ya kikatiba." Wanasiasa wa upinzani wanadai kuwa lengo lililojificha la serikali ni kuondoa ukomo wa mihula miwili ya miaka mitano ya urais ili kumwezesha Rais Tshisekedi (63) kugombea tena baada ya muhula wake wa sasa kumalizika mwishoni mwa mwaka 2028.
Hata hivyo, Rais Tshisekedi amekanusha vikali tuhuma za kutafuta muhula wa tatu. Pamoja na kanusho hilo, katika mkutano na waandishi wa habari mwezi Mei 2026, alinukuliwa akieleza kuwa atakubali kuendelea kuongoza iwapo wananchi wa Kongo wenyewe watataka afanye hivyo. Wakati huo huo, wataalamu wa sheria nchini humo wanaendelea kujadili ushawishi wa Ibara ya 220 ya Katiba ya mwaka 2006, ambayo inapiga marufuku kabisa mabadiliko yoyote yanayogusa idadi na urefu wa mihula ya Rais.
Licha ya sheria hiyo kuanza kutumika rasmi mara tu baada ya kusainiwa, Serikali ya Kinshasa bado haijatangaza tarehe ya kufanyika kwa kura hiyo ya maoni wala kuchapisha rasimu ya Katiba inayopendekezwa.
Wachambuzi wa siasa za Kanda ya Maziwa Makuu wanaeleza kuwa mbali na mvutano wa kisiasa jijini Kinshasa, changamoto sugu za kiusalama na mzozo wa kivita unaoendelea Mashariki mwa DRC zitakuwa na mchango mkubwa katika kuathiri au kukwamisha mjadala huo wa kikatiba kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2028. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Mahusiano, Deus Clement Sangu, amesema Serikali imebaini utekelezaji wa agizo la kima cha chini cha mshahara katika sekta binafsi kufikia takribani asilimia 90.
Hata hivyo, amesema baadhi ya waajiri bado hawajatekeleza kikamilifu agizo hilo, hivyo Serikali inatarajia kuwaita waajiri wa sekta husika mwanzoni mwa mwezi Desemba ili kuhakikisha wanazingatia matakwa ya sheria.
Sangu ameyasema hayo leo Novemba 11, 2026, jijini Arusha, wakati akifungua semina ya waajiri na viongozi wa matawi ya Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania (TUGHE), akisisitiza kuwa waajiri watakaobainika kukiuka sheria watachukuliwa hatua stahiki.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa TUGHE Taifa, Rugemalila Rutatina, amesema miongoni mwa changamoto zinazotukabili vyama vya wafanyakazi ni kuanzishwa kwa vyama vidogo vinavyotokana na migogoro ya uongozi ndani ya vyama vikubwa, hali inayochangia migogoro na kudhoofisha utendaji wa taasisi.
Aidha, Rutatina ameitaka Serikali kutoa mwongozo kuhusu changamoto hizo, huku akibainisha kuwa baadhi ya taasisi hazitekelezi ipasavyo matakwa ya kisheria ya kuunda na kuendesha mabaraza ya afya na usalama kazini, jambo linalohitaji kupewa kipaumbele ili kulinda ustawi wa wafanyakazi
Ikumbukwe kuwa Serikali ilitoa Amri ya Kima cha Chini cha Mshahara kwa Sekta Binafsi ya mwaka 2025, iliyopandisha wastani wa kima hicho kwa asilimia 33.4 kutoka Shilingi 275,060 hadi Shilingi 358,322 kwa mwezi, huku viwango vikitegemea sekta husikaThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Kilimo, Daniel Chongolo ametoa onyo kali kwa wafanyabiashara, mawakala na wote wanaojihusisha na usambazaji wa pembejeo za kilimo wanaotumia vibaya ruzuku ya mbolea inayotolewa na Serikali kwa manufaa yao binafsi.
Akizungumza leo Novemba 11, 2026 wakati wa kuhitimisha ziara ya kikazi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi mkoani Ruvuma, Waziri Chongolo amesema kuwa Serikali haitamvumilia mtu yeyote atakayebainika kujinufaisha kwa njia zisizo halali kupitia ruzuku hiyo.
Amesisitiza kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wote watakaobainika kuongeza gharama za mbolea kwa wakulima au kutumia mpango wa ruzuku kinyume na malengo yake, huku akieleza kuwa dhamira ya Serikali ni kuhakikisha wakulima wanapata mbolea kwa bei nafuu ili kuongeza uzalishaji na tija katika Sekta ya Kilimo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Jumanne Sagini ametoa agizo la siku tatu kwa waendesha bajaji wote jijini Mbeya kuacha kabisa kutumia Barabara Kuu ya TANZAM na badala yake kuhamishia shughuli zao katika barabara za pembeni zitakazopangwa na mamlaka husika.
Sagini ametoa agizo hilo Novemba 11, 2026, mara baada ya kupokea ripoti rasmi kutoka kwa kamati maalum iliyoundwa kwa maelekezo ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa - TAMISEMI), Riziki Shemdoe iliyokuwa na jukumu la kutathmini hali ya upangaji wa jiji na kupendekeza maboresho ya miundombinu na usafirishaji.
Hatua hiyo ni sehemu ya mikakati ya Serikali ya Mkoa wa Mbeya ya kuboresha mpangilio wa matumizi ya barabara na huduma za usafiri jijini humo, ikilenga kupunguza msongamano mkubwa wa magari na kuimarisha usalama kwa watumiaji wote wa miundombinu hiyo.
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa ripoti hiyo, Sagini amesisitiza kuwa waendesha bajaji wanapaswa kuzingatia kikamilifu muda huo wa siku tatu waliopewa na kufuata miongozo ya barabara za pembeni zitakazoelekezwa na mamlaka za jiji.
Barabara ya TANZAM ni miongoni mwa njia kuu za kiuchumi na kimkakati jijini Mbeya, ikitumiwa na magari makubwa ya mizigo na mabasi ya abiria yanayoingia, kutoka, au kupita kuelekea mikoa jirani na nchi za nje. Hivyo, kuondoa mwingiliano wa bajaji katika barabara hiyo kuu kunatarajiwa kusaidia kwa kiasi kikubwa kurahisisha mtiririko wa magari na kuweka mazingira salama zaidi ya usafirishaji.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI:
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi, ameitaka Wizara ya Nishati na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kumsimamia kwa karibu Mkandarasi Kampuni ya Kalpataru ili kuhakikisha mradi wa kusafirisha umeme wa kilovolti 220 wa Songea–Tunduru–Masasi unakamilika kwa wakati.
Ndejembi ametoa agizo hilo leo Novemba 11, 2026, wakati akikagua maendeleo ya mradi huo, akieleza kutoridhishwa na kasi ya utekelezaji licha ya Serikali kutoa zaidi ya Shilingi bilioni 42 kwa ajili ya kuendeleza kazi hizo.
Amesema mradi huo ni muhimu kwa kuimarisha upatikanaji wa umeme wa uhakika katika Mikoa ya Ruvuma, Lindi na Mtwara, hususan Wilaya ya Tunduru ambayo kwa sasa hupata umeme kutoka umbali mrefu.
Naibu Waziri wa Nishati, Salome Makamba, amesema sehemu ya mradi wa Tunduru–Masasi imeongezeka kutoka asilimia sita hadi 35 baada ya Serikali kutoa fedha kwa Mkandarasi, huku sehemu ya Songea–Tunduru ikiwa imefikia asilimia 58.
Amesema Wizara itahakikisha Mkandarasi anasimamiwa ipasavyo ili mradi ukamilike ifikapo Septemba 30, 2027.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Lazaro Twange, amesema sehemu ya Songea–Tunduru yenye urefu wa kilomita 214.5 inatekelezwa kwa gharama ya Shilingi bilioni 151, huku Tunduru–Masasi yenye kilomita 177 ikigharimu Shilingi bilioni 158.
Amesema mradi huo ni sehemu ya miradi 27 ya Gridi Imara inayotekelezwa na Serikali, na kwa ujumla umefikia asilimia 58. Kituo cha kupokea na kupoza umeme cha Tunduru kitakuwa na transfoma mbili zenye uwezo wa MVA 60 kila moja.
Mradi huo unatarajiwa kuimarisha upatikanaji wa umeme wa uhakika na kuchochea shughuli za kiuchumi, ikiwemo kilimo, uchimbaji madini na uzalishaji viwandani katika Mikoa ya Kusini. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkuu wa Wilaya ya Pangani mkoani Tanga, Mwanaidi Rajabu, amepiga marufuku magari ya abiria kuvuka Daraja la Pangani yakiwa na abiria ndani, huku akiruhusu magari hayo kutumia daraja hilo linaloendelea na ujenzi baada ya kuwashusha abiria, ambao wanapaswa kuvuka mto kwa kutumia vivuko maalumu vilivyotengwa.
Akizungumza Novemba 11, 2026, wakati wa kikao kilichowakutanisha wananchi na wadau wa usafirishaji, akiwemo Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Mwanaidi amesema magari yatakayobainika kukiuka agizo hilo yatakabiliwa na hatua za kisheria, ikiwemo kutozwa faini.
Amesisitiza kuwa utaratibu huo unapaswa kuzingatiwa ili kuhakikisha usalama wa abiria wakati ujenzi wa daraja hilo ukiendelea.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa kivuko cha Mto Pangani, Jumaa Ali, amesema baadhi ya abiria wamekuwa wakikwepa kutumia vivuko maalumu kwa kujificha kwenye magari yanayopita katika daraja hilo, hali inayohatarisha usalama wao.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesisitiza kuwa Mwenyekiti wake, Tundu Lissu, hana hatia yoyote kufuatia hukumu ya miaka minne gerezani kwa kosa la uchochezi, kikieleza kuwa kudai katiba mpya, tume huru ya uchaguzi na haki si uchochezi bali ni kutimiza wajibu kwa nchi.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu chama hicho bara, Amani Golugwa hapo jana mkoani Singida katika msiba wa aliyekuwa Wakili, Mzee Alute Mughwai Lissu, ambaye ni kaka wa Tundu Lissu.
“Lissu ametimiza wajibu wake kusema kwamba nchi hii inahitaji mabadiliko ya katiba, nchi hii inahitaji tume huru ya uchaguzi... Tunalipenda taifa hili na sisi ni watu wema tu," ameeleza Golugwa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Mwekezaji wa Kiwanda cha Nyamagara Fishing Net LTD kilichopo Chanika Dar es Salaam, amelalamikia Jeshi la Polisi @tanpol Mkoa wa Kagera kukamata na kushikilia mzigo wake wa nyavu wenye thamani ya shilingi milioni 12 kwa miezi mitatu huku akilalamika kutopata majibu sahihi pindi anapohitaji maelezo ya kina na hatua zilizofikiwa baada ya kushikiliwa kwa mzigo.
Mkurugenzi wa kiwanda hicho Bw. Basil Kyando amesema Agosti 10, 2026 mzigo wa nyavu 47 ulikuwa ukisafirishwa kwenda Uganda kupitia mpaka wa Mtukula ambapo msafirishaji alipofika mpakani hapo alisafirisha nyavu 22 kati ya 47 huku 25 zilizobaki zikikamatwa na kushikiliwa sababu ikidaiwa kuwa ni nyavu haramu na hazitakiwi kutumika Ziwa Victoria.
Anaeleza kuwa mzigo huo ulikuwa unaenda kwa mteja nchini Uganda na ulikuwa na vibali vyote vinavyohitajika na kuwa baada ya kukamatwa nyavu zilipelekwa kituo cha Polisi Kikuu Bukoba na msafirishaji aitwaye Tamimu Paulo akitakiwa kuwa anaripoti kituoni kila ijumaa.
Anaeleza baadae alipofuatilia amedai kutopata maelezo yasiyoridhisha kutoka kwa Mkuu wa Upelelezi Makosa ya Jinai wa Mkoa(RCO) huo juu ya kinachoendelea ambapo wakati mwingine alielezwa jalada halijafika mezani na lilipofika anadai alimjibu kuwa ameshalifanyia kazi akisubiri taratibu zingine.
Jambo TV ilimtafuta Afisa Uvuvi wa Mkoa wa Kagera Efrazi Chuma Mkama juu ya nyavu hizo kama wanazishikilia ambapo alitueleza kuwa hawezi zungumzia jambo hilo kwa sababu lipo polisi.
"Hata huyo Nyamagara anafahamu alichokuwa amekiuka nini, hilo suala lipo kwenye sheria kwa hiyo taratibu za sheria zinafuatwa siwezi kulizungumzia"
Hata hivyo Oktoba 30, 2026 Jambo TV ilimtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera SACP Blassius Chatanda ambaye alitueleza kuwa jambo hilo halifahamu anahitaji kulifuatilia ili awe na majibu sahihi.
"Sina ninachokifahamu inawezekana tukio hilo likawepo au lisiwepo naomba nifuatilie"
Novemba 9 na Novemba 10, 2026 Jambo TV ilimrudia tena SACP Chatanda lakini simu yake haikupokelewa.
Nyamagara ameziomba mamlaka kusaidia kufika hatma ya sakata hilo kwani tayari ameingia kwenye madeni ya kulazimika kumlipa mfanyabiashara wa uganda. -
Jambo TV
@Jambotv_
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikilia na kumhoji kwa kina Peter Mmasi (32), mkazi wa Kimara, kwa tuhuma za kumzuia na kumshambulia askari polisi aliyekuwa akitekeleza wajibu wa kisheria wa kumkamata.
Tukio hilo limebainishwa kupitia taarifa rasmi kwa umma iliyotolewa leo, Novemba 11, 2026 na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Jumanne Muliro.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya Polisi, askari aliyefanyiwa shambulio hilo ni Sajenti Johnson Sylivery, ambaye alikuwa katika jitihada za kumkamata mtuhumiwa huyo kufuatia tuhuma za kutishia kumuua raia. Mwananchi aliyetishiwa kuuawa na mtuhumiwa huyo ametajwa kuwa ni Carisma Amedeus Kileo, ambaye pia ni mkazi wa Kimara jijini Dar es Salaam.
Jeshi la Polisi limeeleza kuwa taratibu zote za kisheria zinaendelea kukamilishwa dhidi ya mtuhumiwa huyo. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikilia na kumhoji kwa kina Halidi Seleman Kalaghe (45), mwendesha mtambo aina ya 'Excavator', kwa tuhuma za kuharibu mali mbalimbali za mwajiri wake kufuatia mzozo uliotokea kati yao.
Hatua hiyo imebainishwa katika taarifa rasmi kwa umma iliyotolewa leo, Novemba 11, 2026, na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Jumanne Muliro.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya Polisi, tukio hilo lilitokea mnamo tarehe 10 Novemba, 2026, majira ya saa 06:05 mchana katika Mtaa wa Mvumoni, Somangila, uliopo ndani ya Manispaa ya Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Inaelezwa kuwa mtuhumiwa huyo alifikia uamuzi wa kufanya uharibifu huo katika mazingira yaliyozua taharuki kubwa baada ya kutokea kwa kutoelewana kati yake na mwajiri wake, kampuni ya China Energy Engineering Group Guanxi Hydroelectric Construction Bureau co.ltd, inayotekeleza mradi wa ujenzi wa barabara katika Manispaa hiyo ya Kigamboni.
Baada ya kutoelewana huko, Kalaghe anadaiwa kuingia kwenye mtambo wa 'Excavator' na kuanza kubomoa na kuharibu mageti mawili pamoja na uzio wake, gari ndogo yenye namba za usajili T 282 DEM aina ya Toyota Sienta mali ya Brighton Abraham Mfangavo, gari la kubebea mafuta namba T 391 EUN aina ya Sinortrack mali ya kampuni hiyo, pamoja na nyumba za muda zenye vyumba vitano na vyoo.
"Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam imemkamata Halidi Seleman Kalaghe, miaka 45, Mwendesha mtambo ‘Excavator’ kwa tuhuma za kuharibu mali za mwajiri wake. Tukio hilo limetokea tarehe 10 Novemba, 2026 saa 06:05 mchana Mtaa wa Mvumoni Somangila Kigamboni Dar es Salaam katika mazingira yaliyozua taharuki baada ya kutoelewana na mwajiri wake kampuni ya China Energy Engineering Group Guanxi Hydroelectric Construction Bureau co.ltd inayofanya kazi za ujenzi wa barabara katika Manispaa ya Kigamboni alichukua uamuzi wa kuingia kwenye mtambo ‘Excavator’ na kuanza kuharibu mageti mawili na uzio wake, gari ndogo yenye namba T 282 DEM aina ya Toyota Sienta mali ya Brighton Abraham Mfangavo, gari la kubebea mafuta namba T 391 EUN aina ya Sinortrack mali ya kampuni, nyumba za muda zenye vyumba vitano na vyoo”, ameeleza Muliro.
Jeshi la Polisi limeeleza kuwa taratibu zaidi za kisheria zinaendelea kukamilishwa dhidi ya mtuhumiwa huyo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara limemkamata na linaendelea kumhoji Emmanuel Evance Simon (52), mkazi wa Kijiji cha Chisegu, Kata ya Chanikanguo, Wilaya ya Masasi, kwa tuhuma za kumuua mke wake, Clauda Yohana Bakari (54).
Tukio hilo limetokea mnamo tarehe 10 Novemba, 2026 majira ya saa nane mchana huko maeneo ya Chanikanguo, ambapo mtuhumiwa anadaiwa kumjeruhi mke wake kwa kumkata na jembe maeneo ya kisogoni na kumsababishia majeraha yaliyopelekea kifo chake
Taarifa rasmi iliyotolewa Novemba 11, 2026 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, SACP Issa Suleimani imeeleza kuwa chanzo cha mauaji hayo ni wivu wa kimapenzi, baada ya mtuhumiwa kumtuhumu marehemu mke wake kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanaume mwingine.
Jeshi la Polisi limebainisha kuwa uchunguzi wa shauri hilo unaendelea na pindi utakapokamilika, mtuhumiwa atafikishwa mahakamani
“Mtuhumiwa alitenda kosa hilo mnamo tarehe 10 Novemba 2026 majira ya saa nane mchana... Chanzo cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi," imeeleza taarifa hiyo.
Aidha, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara limetoa wito kwa jamii kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi wanapokabiliwa na migogoro ya kimaisha, na badala yake watumie njia sahihi na za kisheria kusuluhisha changamoto zao. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Kufuatia kuongezeka kwa maudhui mbalimbali mitandaoni yenye viashiria vya ushoga na usagaji Mchungaji mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Richard Hananja ameibuka na kukemea vitendo hivyo huku akitoa lawama kwa wazazi, viongozi wa dini na Serikali kushindwa kutimiza wajibu wao ambapo amehimiza watu kuilinda mioyo yao akisema kwa kufanya hivyo "Mgongo utapona"
Akizungumza Novemba 10, 2026 na Jambo TV mkoani Mwanza, Mchungaji Hananja amedai kuwa vitendo hivyo vimekuwa vikiongezeka katika jamii kutokana na watu kuwa wavivu na kupenda vitu rahisi visivyohitaji kutumia nguvu na akili.
"Tukatae, linda moyo na mgongo utapona. Kama moyo haupo vizuri hata mgongo uvae boksa ya chuma watu watachana tu na kukubanjua tu kwahiyo linda moyo wako kwanza na mgongo wako utalindwa," amesema.
Ameongeza kuwa "Kizazi hiki kinataka maisha rahisi hakina hata mashavu ya kupuliza moto wana mashavu ya bigijii, kizazi legelege kinataka kulala na kubeti,".This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Kinondoni imebaini mapungufu mbalimbali katika utekelezaji wa miradi 14 ya maendeleo yenye thamani ya Shilingi bilioni 81, ukiwamo mradi mkubwa wa ujenzi wa viwanja vitatu vya mazoezi vinavyoandaliwa kwa ajili ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2027) jijini Dar es Salaam.
Taarifa hiyo imetolewa leo, Jumatano, Novemba 11, 2026, na Naibu Mkuu wa TAKUKURU Kinondoni, Bi. Elizabeth Mokiwa, wakati akiwasilisha ripoti ya utendaji kazi na mafanikio ya taasisi hiyo kwa kipindi cha miezi sita (Aprili hadi Septemba 2026) mbele ya vyombo vya habari
Kwa mujibu wa Mwananchi, Bi. Mokiwa ameeleza kuwa mradi huo wa Sekta ya Michezo wenye thamani ya zaidi ya Shilingi bilioni 51.6 unajumuisha ujenzi na ukarabati wa viwanja vya Leaders Club, Gymkhana 2, na Uwanja wa Farasi.
“Katika kutekeleza jukumu letu tumebaini mapungufu kadhaa katika utekelezaji wa miradi hiyo na hivyo kufanya vikao kazi na watekelezaji wakiwemo wakandarasi, washauri, wasimamizi, na Ofisi ya Mthibiti Ubora ili kuhakikisha inakamilika kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa,” amesema Bi. Mokiwa, huku akibainisha kuwa baadhi ya mapungufu tayari yameshafanyiwa kazi na mengine yanaendelea kurekebishwa.
Katika hatua nyingine, TAKUKURU Kinondoni imeeleza kuwa katika kipindi hicho ilipokea jumla ya malalamiko 110, ambapo malalamiko 47 yalihusu makosa ya rushwa na yanaendelea kuchunguzwa katika hatua mbalimbali, huku walalamikaji wa mashauri 63 yasiyohusu rushwa wakipewa ushauri wa kisheria.
Aidha, katika eneo la uendeshaji wa mashtaka, kesi 14 zilikuwa zikiendelea mahakamani (ikiwemo kesi mpya 10 zilizofunguliwa). Katika mashauri 12 yaliyotolewa maamuzi na mahakama katika kipindi hicho, Jamhuri ilifanikiwa kushinda kesi 9.
Bi. Mokiwa ameongeza kuwa TAKUKURU ilifanikiwa kuokoa Shilingi milioni 37 za ushuru na adhabu zilizolipwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kufuatia oparesheni iliyofanyika katika Pwani ya Kunduchi, ambapo gari lililokuwa limesafirisha magendo ya madumu 510 ya mafuta ya kula (lita 20 kila moja) bila kulipa kodi lilinaswa.
Baada ya mamlaka husika kujiridhisha kuwa mafuta hayo ni salama kwa matumizi ya binadamu na hatua za kisheria kuchukuliwa dhidi ya mwagizaji na mmiliki wa gari, ushuru na faini vililipwa kabla ya bidhaa hizo kuruhusiwa. TAKUKURU imetoa wito kwa wafanyabiashara kufuata sheria za uingizaji wa bidhaa nchini ili kulinda afya za wananchi, ushindani wa haki, na uchumi wa Taifa. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
"Shida inayotukumba kwa sasa hivi Mwanaume ambaye anatakiwa awe kiongozi awe baba amepoteza hizo sifa sasa wamama kwa sababu wamekuwa empowered wanang'ang'ania kuchukua hizo sifa kwa hiyo kunakuwa na mgogoro, siyo kila mwanaume ni baba ila kila baba ni mwanaume kuwa baba ni mchakato mwanaume yoyote ambaye hahudumii umeshapoteza sifa za ubaba siku nyingi"
Anasema Mwalimu Cosmas Madulu kwenye mahojiano na Jambo TV leo Novemba 11, 2026.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
"Kazi ya mwanamke ni kutunza akili mwanaume, kazi ya mwanaume ni kutunza hisia za mwanamke mwanamke anaweza kuvuruga akili yako kuliko unavyoweza kudhani kwa sababu wao wamtengenezwa kutunza akili zetu wanaume wengi tunatembea njiani tuna shida ya akili kwa sababu ya wanawake"
Anaeleza Mwalimu Cosmas Madulu kwenye mahojiano aliyofanya na Jambo TV leo Novemba 11, 2026. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI:
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi, leo Novemba 11, 2026 amekagua mradi wa ujenzi wa Stendi ya Mabasi ya Namtumbo akiwa ziarani mkoani Ruvuma ambapo ametoa angalizo kwa wasimamizi wa mradi huo katika utekelezaji wake.
Mradi huo wa Stendi unatekelezwa kwa gharama ya Shilingi Bilioni 8.4 na unatarajiwa kuboresha huduma za usafiri kwa wananchi, kuongeza mapato ya Halmashauri na kufungua fursa za ajira na biashara kwa vijana na wajasiriamali.
Makamu wa Rais amepongeza jitihada za Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo katika kusimamia utekelezaji wa mradi huo, akishauri miradi inayotegemea fedha za maendeleo kutoka Serikalini itekelezwe kwa awamu ili kuongeza ufanisi na kutoa uhakika wa kukamilika kwa wakati.
Mradi huo ulioanza kutekelezwa Oktoba 2026 unatarajiwa kukamilika Septemba 2027, huku mkandarasi ambaye ni kampuni ya AMJ Contractors Ltd akiwa katika hatua za awali za uchimbaji wa msingi.
Kwa mujibu wa Mhandisi wa Mradi, Injinia Allen Mshiru, stendi hiyo itakuwa na maeneo ya kuegesha magari, fremu 197 za maduka, maeneo ya lami, jengo la utawala pamoja na Kituo cha Polisi.
Akizungumza baadaye katika mkutano wa hadhara, Makamu wa Rais amesema Serikali tayari imetoa takribani Sh bilioni moja kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa mradi huo, ambao unatarajiwa kuboresha huduma za usafiri, kuongeza mapato ya halmashauri na kufungua fursa za ajira na biashara kwa vijana, wajasiriamali na mama lishe.
Katika mkutano huo, Waziri mwenye dhamana ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Profesa Riziki Shemdoe, amesema Serikali pia inaendelea na ujenzi wa barabara ya lami yenye urefu wa kilomita 3.9 pamoja na daraja lenye thamani ya Sh bilioni 1.1 wilayani Namtumbo.
Makamu wa Rais ameelekeza barabara hizo ziwekwe taa baada ya kukamilika ili kuimarisha usalama na kuwezesha shughuli za kiuchumi kuendelea wakati wa usiku. Aidha, amesisitiza umuhimu wa kusimamia kwa karibu miradi yote ya maendeleo ili kuhakikisha fedha za umma zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa na wananchi wanapata huduma bora. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Serikali ya Iran imefungua kituo kipya cha mafunzo ya kijeshi kwa ajili ya wanawake katika Eneo la Azadi Square jijini Tehran, kikilenga kuwapa uraia na ujuzi wa kivita kupitia mazoezi ya vitendo ya kutumia silaha mbalimbali na mbinu za medani.
Picha na vidio zilizosambazwa kutoka kituoni hapo zinawaonesha wanawake wakifanya mazoezi ya kushuka kutoka kwenye majengo marefu kwa kamba, na kulenga shabaha kwa kutumia bunduki za kawaida na za mitambo, na matumizi ya mizinga.
Kituo hicho kipya ni sehemu ya mpango mkubwa unaojulikana kama kampeni ya 'Jan Fada', iliyoanzishwa kwa lengo la kuwaandaa wananchi wa kawaida na raia kukabiliana na vitisho vyovyote vya kijeshi au kiusalama vinavyoweza kuikabili nchi hiyo.
Kamanda mwandamizi wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran (IRGC) amedai kuwa zaidi ya raia milioni 33 kote nchini Iran wameshajisajili kushiriki katika programu hiyo ya mafunzo ya ulinzi wa taifa.
Baadhi ya wanawake waliojiunga na kituo hicho wameeleza kuwa wameamua kujitolea kupata mafunzo hayo ili kuwa tayari kuilinda nchi yao na kutetea misingi ya imani zao endapo dhoruba au tishio lolote litatokea.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
"Miaka michache ijayo watakaotawala dunia ni wale wanaolisha hisia za wanadamu wasanii wacheza mpira wale wenye vyakula vyenye hisia kwa sababu ndiyo watakuwa na wafuasi wengi katika ulimwengu wa demokrasia wengi wape wa wafuasi watakaotawala ni hao bila kujali wana akili au lah"
Anasema Mwalimu Cosmas Madulu kwenye mahojiano na Jambo TV leo Novemba 11, 2026.
Upi mtazamo wako?This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
"hatuna uwezo wa kuchambua vitu kwamba hiki tunahitaji hiki hatuhitaji na sasa tumemezwa kwenye teknolojia tulitakiwa hatuna namna ya kukwepa kuchambua hiki tunataka hiki hatutaki hata kama ni haki za binadamu hatutaki, sio kila haki za binadamu Marekani ni haki za binadamu Tanzania"
Anasema Mwalimu Cosmas Madulu kwenye mahojiano na Jambo TV leo Novemba 11, 2026.
Upi mtazamo wako?This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba ameshangazwa na video zilizoenea mtandaoni zikiwaonyesha wanaume waliovaa nguo kama wanawake huku wakicheza kama wanawake akisema kuwa ni vitendo vya ajabu vinavyotokana na ukosefu wa malezi mazuri.
Akizungumza Novemba 10, 2026 eneo la Usanda Wilaya ya Shinyanga Vijijini mkoani Shinyanga Mwigulu amesema vitendo hivyo hata wanyama kama ng'ombe hawafanyi.
"Niliona juzi wanaume wazima wanacheza na maumbo ya.. kwa sisi wafugaji ni kichefuchefu aibu kwa Tanzania hapa mambo ya kuiga hayo sisi wafugaji tunajiuliza hata ng'ombe hawakoseagi hawa watu vipi hawa ni malezi" -
Jambo TV
@Jambotv_
Tatizo la mmonyoko wa maadili linazidi kuwa mjadala mkubwa na kushamiri kwa vitendo vinavyoshabihiana na ushoga huku suluhu ikiwa na maswali ni nani achukue hatua kudhibiti.
Lipo swali linaloibuka ambalo ni wenye mamlaka wakiwemo wabunge ambao ndiyowatunga Sheria nao wakibaki kulalamika.
Je ni kwa nini wenye mamlaka nao wanalalamika?This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Jamii imetahadharishwa kujiepusha na vitendo vya uharibifu wa miundombinu ya reli, ambapo imeelezwa kuwa mtu yeyote atakayebainika kuirushia treni mawe anaweza kukabiliwa na adhabu kali ya kifungo cha maisha jela kulingana na sheria za nchi.
Tahadhari hiyo imetolewa Novemba 10, 2026, mkoani Morogoro na Mpelelezi wa Makosa ya Jinai wa Kikosi cha Reli kutoka Shirika la Reli Tanzania (TRC), Staff Sajenti Mageta Marwa, wakati akitoa elimu ya usalama kwa viongozi na wananchi wanaoshi katika maeneo yanayopitiwa na ushoroba wa reli. Sajenti Marwa amesisitiza kuwa mbali na kurushia treni mawe, hata kitendo cha kutembea au kucheza kwenye njia za reli ni kosa la kisheria linaloweza kumfanya mtu achukuliwe hatua kali.
Kwa upande wake, Afisa Usalama wa Uendeshaji wa Treni za Reli ya Kisasa (SGR) na Reli ya Kati (MGR), Bw. Winfrid Chawala, ameeleza kuwa lengo kuu la kampeni hiyo ni kuongeza uelewa wa jamii kuhusu umuhimu wa kulinda miundombinu ya reli na kuepuka madhara makubwa yanayoweza kutokea kufuatia uharibifu huo. Bw. Chawala amebainisha kuwa kulingana na takwimu na ufuatiliaji wao, kundi la watoto ndilo linaloongoza kwa kufanya vitendo hivyo vya hatari vya kuirushia treni mawe.
Nao baadhi ya wananchi na viongozi wa Mkoa wa Morogoro waliohudhuria mafunzo hayo wamepongeza juhudi za TRC, wakieleza kuwa elimu hiyo imekuja wakati mwafaka. Wameeleza kuwa kampeni hiyo itasaidia kwa kiasi kikubwa kutoa elimu kwa wazazi na walezi ili kuwasimamia watoto wao, kupunguza vitendo vya uharibifu, na kuhakikisha usalama wa abiria na miundombinu ya treni nchini.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI:
Wanasheria wa Chama cha Wanasheria nchini Kenya (LSK), wamefanya maandamano Nairobi Novemba 10, 2026 wakishinikiza vyombo vya usalama nchini humo kufafanua mahali alipo Wakili Abshir Ahmedsadak Abdi, anayedaiwa kutekwa nyara Novemba 1, 2026.
Maandamano hayo yameongozwa na Rais wa LSK, Charles Kanjama na yalianzia eneo la Mahakama ya Milimani hadi Jogoo House ambako ni Makao Makuu ya Huduma ya Polisi ya Kitaifa nchini humo.
Wakili Abshir Abdi aliripotiwa kutekwa nyara na watu wenye silaha katika eneo la Kilimani, Nairobi, na tangu wakati huo hakuonekana. Tukio hilo limetajwa na Mawakili hao kwamba limeibua wasiwasi miongoni mwa wanasheria na walinzi wa haki za binadamu kuhusu usalama wa wataalamu wa sheria nchini Kenya.
Rais wa LSK, Charles Kanjama, amesema wanasheria hawawezi kuendelea kutoa huduma kama kawaida wakati usalama wao na wa wananchi upo hatarini. Amesema tishio kwa wakili mmoja ni tishio kwa mfumo mzima wa haki nchini Kenya.
Mahakama Kuu nchini humo imewataka maafisa wa Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI), Huduma ya Ujasusi ya Kitaifa (NIS) na Jeshi la Polisi kufika mahakamani ili kujibu maswali kuhusu alipo Wakili Abshir Abdi.
LSK pia imewataka wanachama wake kuendelea na mshikamano hadi Wakili Abshir Abdi atakapopatikana na maelezo kamili ya tukio la kutoweka kwake yatakapopatikana. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Wakili Peter Kibatala @PKibatala_ alipoulizwa mtazamo wake kufuatia hukumu ya miaka minne gerezani kwa Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu kutokana na kosa la uchochezi na juu ya rufaa dhidi ya hukumu hiyo amesema kuwa yeye binafsi anaona yapo mambo lukuki ya kujadiliwa katika Mahakama ya Rufani juu ya hukumu hiyo.
"Mimi kama Wakili kama nitapata nafasi ya kuchakata rufaa kuna mambo 1,000 ya kusema lakini kuna mahali pake pa kuyasemea lakini hata niseme nini sasa hivi haitabadilisha kile ambacho tayari kimeamuliwa"
Amesema Wakili Kibatala jana Novemba 10, 2026 Mahambe, Wilaya ya Ikungi mkoani Singida aliposhiriki mazishi ya kaka wa Lissu Marehemu Alute Mughwai Lissu.
Hata hivyo ameongeza kuwa mwenye uamuzi wa nani atakuwa kwenye jopo la Mawakili watakaochakata rufaa hiyo ni Lissu pamoja na chama chake cha @ChademaTZ2 na kama akiwepo kwenye timu hiyo basi atashiriki.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Halmashauri ya Wilaya ya Karatu mkoani Arusha imedhamiria kwa dhati kuongeza kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kwa kuimarisha mazingira ya kujifunzia na kuhakikisha upatikanaji wa chakula na lishe bora shuleni, mambo yanayotajwa kuwa nguzo kuu za kuongeza uelewa na matokeo mazuri darasani.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu, Juma Hokororo amebainisha kuwa juhudi za pamoja zinahitajika kati ya walimu, wakuu wa shule, na wataalamu wa elimu ili kuondoa kabisa alama D katika matokeo ya wanafunzi na kuiwezesha Karatu kufanya vizuri zaidi katika takwimu za ufaulu kimkoa na kitaifa.
Akizungumza katika kikao kazi kilichowakutanisha Wakuu wa Shule za Sekondari na Walimu Wakuu wa Shule za Msingi katika Ukumbi wa Hoteli ya Kudu mjini Karatu, Bw. Hokororo alisisitiza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano na wazazi kupitia vikao vya mara kwa mara ili kujadili maendeleo ya wanafunzi, hususan waliopo katika madarasa ya mitihani.
Aidha, Mkurugenzi Hokororo alikazia kuwa upatikanaji wa chakula cha mchana shuleni ni jambo la lazima na wala si hiari. Kufuatia msimamo huo, amewataka watendaji wa kata kusimamia kikamilifu michango ya chakula kutoka kwa wazazi na kuhakikisha inaratibiwa kwa uwazi na utaratibu mzuri, akieleza kuwa njaa na upungufu wa chakula shuleni ni miongoni mwa sababu kuu zinazoshusha taaluma.
Ili kuimarisha lishe bora, Mkurugenzi Hokororo ameiagiza Idara ya Elimu Msingi na Sekondari kusimamia kwa karibu uanzishwaji wa bustani za mbogamboga, matunda, na vitalu vya miche katika kila shule. Pamoja na hayo, alielekeza kuanzishwa kwa vilabu vya lishe shuleni vitakavyowafundisha wanafunzi kuhusu ulaji unaofaa ili nao wakawa elimisho wazazi na jamii inayowazunguka.
Mbali na masuala ya taaluma na lishe, kikao hicho kilijadili pia uratibu na maandalizi ya mapokezi ya wanafunzi wapya wa Kidato cha Kwanza pamoja na maandalizi ya awali ya mfumo wa kuanza madarasa mawili ifikapo mwaka 2028.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini, Dkt. Damas Ndumbaro, amemuomba Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi, kushughulikia kilio cha wakulima wa zao la mahindi kuhusu bei ndogo ya kuuza mazao yao pamoja na Changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji mkoani humo.
Ameeleza hayo alipokuwa akiwasilisha changamoto za bei ya mahindi pamoja na upatikanaji wa maji katika Manispaa ya Songea mbele ya Makamu wa Rais, Deogratius Ndejembi, Novemba 10, 2026. Ndumbaro amesema gharama za kilimo na pembejeo hazilingani na bei ya kuuza mahindi. Hivyo, amemuomba Makamu wa Rais kuhakikisha wakulima wa zao hilo wanapata bei nzuri itakayowanufaisha.
Katika hatua nyingine, Dkt. Ndumbaro amesema kuwa kuna miradi mikubwa inayotekelezwa katika Manispaa ya Songea, ukiwemo mradi wa maji unaogharimu zaidi ya shilingi bilioni 140 ambapo amesema wananchi wanasubili maji
Wakijibu changamoto hizo, Waziri wa Kilimo, Daniel Chongolo, pamoja na Waziri wa Maji, Juma Aweso, wametoa ufafanuzi kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali. Waziri wa Kilimo amesema Serikali imeweka mipango mizuri ya kuhakikisha msimu ujao wakulima wanapata bei nzuri ya mahindi baada ya kuanzisha vituo vya kununua mahindi katika mikoa minne inayozalisha zao hilo kwa wingi.
Kwa upande wake, Waziri wa Maji, Juma Haweso, amesema idadi ya watu katika Mji wa Songea imeongezeka, hali inayosababisha mahitaji ya maji kuongezeka. Amesema mahitaji ya maji katika mji huo ni lita milioni 21 kwa siku, wakati Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Songea (SOUWASA) ina uwezo wa kuzalisha lita milioni 11 pekee, hivyo kuwepo kwa upungufu wa lita milioni 10 kwa siku.
Akizungumzia changamoto ya bei ya mahindi, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi, amesema ni jukumu la Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kumlinda mkulima kwa kuweka bei rafiki itakayomwezesha kupata manufaa ya kilimo chake na kuendelea kuzalisha.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi, amembana kwa maswali Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea, Wakili Bashir Muhoja, akitaka kufahamu sababu za mkandarasi katika eneo hilo kuongezewa muda wa utekelezaji hadi Machi 2027, wakati tayari imebainika kuwa anakabiliwa na udhaifu wa usimamizi na upungufu wa vifaa vya kazi.
Akizungumza na wananchi wa Songea, Novemba 10, 2026 wakati wa ziara yake mkoani Ruvuma, Makamu wa Rais pia amewataka viongozi wanaosimamia miradi ya maendeleo kuacha kubembelezana na wakandarasi wanaoshindwa kutimiza wajibu wao, akionesha kukerwa na ucheleweshaji wa ujenzi wa Soko la Manzese A na B, mjini Songea.
“Hebu tubadilike! Tuwe accountable na fedha za umma. High-level meeting inakusaidia nini?” amehoji Ndejembi, akipinga utaratibu wa viongozi kuendelea kufanya vikao vya kumbembeleza mkandarasi badala ya kuchukua hatua zinazohakikisha mradi unakamilika kwa wakati.
Mradi huo ambao mkataba wake ulianza mwaka 2025 kwa kipindi cha miezi 18, ulitarajiwa kukamilika Septemba 2026, umetajwa kuchelewa licha ya mkandarasi huyo kulipwa shilingi bilioni 3 kama malipo ya awali.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi amewataka wananchi wa Mkoa wa Ruvuma kuendelea kulima na kuzalisha mazao kwa wingi, akieleza kuwa Serikali itahakikisha kuwa wakulima wananufaika na mfumo bora wa soko na bei za mazao, hususan Mahindi.
Amesema hayo tarehe 10 Novemba 2026 akiwa katika ziara ya kikazi Wilaya ya Mbinga, mkoani Ruvuma ambapo amekagua na kuzindua ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Mbinga wenye gharama ya Shilingi Bilioni 3.62; kukagua ujenzi wa barabara ya kilometa 35 ya Amani Makoro-Ruanda; pamoja na mradi wa maji katika kijiji cha Mtyangimbole, Wilaya ya Madaba.
Akizungumza katika ziara hiyo, Makamu wa Rais Ndejembi amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea kuwekeza katika Sekta ya Kilimo ili kuongeza uzalishaji, kuboresha masoko na kuimarisha usalama wa chakula nchini. Amesisitiza kuwa pamoja na kuongeza uzalishaji, hatua mahsusi zinaendelea kuchukuliwa ili kuimarisha uhifadhi wa mazao, kuongeza thamani kupitia usindikaji wa ndani na kulinda wakulima dhidi ya kushuka kwa bei wakati wa mavuno mengi.
Kwa upande wake, Waziri wa Kilimo, Daniel Chongolo ameeleza kuwa Wizara itaendelea kuisimamia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) ili kuhakikisha unaendelea kuwa kichocheo cha bei nzuri za mazao na kutoa uhakika wa soko kwa wakulima. Kuhusu kauli ya Judith Kapinga, Waziri wa Viwanda na Biashara ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mbinga Vijijini kuhusu ujenzi wa maghala ya kuhifadhi mazao na kiwanda cha kusaga unga, Waziri Chongolo amesema kuwa ni nguzo muhimu ya kuhakikisha thamani ya mazao ya nafaka iyakiwemo Mahindi inaongezeka huku wakulima wakipata mapato bora na yenye tija zaidi.
Kuhusu upatikanaji wa pembejeo, Waziri Chongolo amewahakikishia wakulima wa Mbinga na Mkoa wa Ruvuma kwa ujumla kuwa Serikali imeendelea kutoa ruzuku ya mbolea kwa lengo la kupunguza gharama za uzalishaji. Amefafanua kuwa ruzuku hiyo imepunguza bei ya mbolea kwa wastani wa Shilingi 63,000 hadi 65,000 kwa mfuko, wakati bei ya soko ya mfuko wa DAP ni takribani Shilingi 158,000. -
Jambo TV
@Jambotv_
Shirikisho la Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) limeandaa Mjadala wa Sekta Binafsi kwa Sekta Binafsi (Private-to-Private Dialogue), uliowakutanisha wazalishaji wa bidhaa za chuma nchini na wadau wa sekta ya ujenzi kujadili changamoto na fursa za kuimarisha matumizi ya bidhaa zinazozalishwa nchini
Mjadala huo uliofanyika leo Novemba 10, 2026 uliongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Bw. Deogratius Massawe, na kujikita katika maeneo mawili muhimu: kuongeza ununuzi wa bidhaa za chuma zinazozalishwa nchini kwa kuzingatia viwango vya ubora, na kuimarisha ushindani wa haki sokoni kupitia mapitio ya sera na kanuni za uingizaji wa bidhaa za chuma
Washiriki walisisitiza umuhimu wa kulinda ushindani wa wazalishaji wa ndani dhidi ya vitendo vya udanganyifu wa thamani ya bidhaa zinazoingizwa kutoka nje, pamoja na kuchunguza hatua stahiki za kisera na kikodi
Kupitia majadiliano haya, TPSF itaratibu mapendekezo ya sekta na kuyawasilisha kwa Serikali na mamlaka husika kupitia mfumo wa Mjadala wa Sekta Binafsi na Serikali (Private-Public Dialogue – PPD), huku ikifuatilia utekelezaji wa hatua zitakazokubaliwa
Juhudi hizi zinalenga kuimarisha uhusiano wa kibiashara kati ya wazalishaji na watumiaji, kukuza viwanda vya ndani, kuongeza matumizi ya bidhaa zinazozalishwa nchini na kujenga mazingira bora ya biashara na uwekezaji Tanzania -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mfanyabiashara na Mwenyekiti wa Taifa Group, Rostam Aziz, ametoa wito kwa Serikali ya Tanzania na wadau wa uchumi kuhakikisha nchi haiwi na kampuni moja au mbili tu za Kitanzania, bali kuwa na kampuni nyingi imara zenye uwezo wa kushindana ndani na nje ya nchi.
Rostam amebainisha hayo hivi karibuni alipokuwa Mgeni Rasmi katika hafla ya kutoa Tuzo za Umahiri katika Sekta za Ujenzi na Madini (African Construction and Mining Excellence Awards - ACAMEA 2026) iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Ameeleza kuwa ukuaji wa kampuni yoyote unahitaji muda, nidhamu pamoja na fursa akisisitiza kuwa fursa moja kubwa inaweza kubadilisha mwelekeo wa kampuni kwa miaka mingi, hivyo nchi inapaswa kuweka msisitizo katika kuwajenga wakandarasi wengi wa kizawa ili waweze kushindana hata katika soko la kimataifa.
“Ninapozungumzia wakandarasi wa Kitanzania ninazungumzia jambo ambalo ninalifahamu. Ninajua ugumu wa kujenga kampuni, ninajua umuhimu wa kuaminiwa, na ninajua kwamba fursa moja kubwa inaweza kubadilisha mwelekeo wa kampuni kwa miaka mingi. Lakini lengo letu lisiwe kuwa na kampuni moja au mbili za Kitanzania, lengo liwe kujenga sekta yenye kampuni nyingi imara zenye uwezo wa kushindana ndani na nje ya nchi”, amesema Rostam.
Rostam amebainisha kuwa ili kufikia lengo hilo la kuwa na kampuni nyingi imara zinazoshindana kimataifa, nchi haina budi kuacha kigezo cha ukosefu wa uzoefu kama sababu ya kuzinyima kampuni za Kitanzania fursa za kuupata uzoefu huo. Ameeleza kuwa badala ya kuzitenga kampuni za kizawa kwenye miradi mikubwa, miradi ya ndani inapaswa kutumiwa kujenga uwezo wa kampuni hizo pale unapopungua.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mfanyabiashara na Mwenyekiti wa Taifa Group, Rostam Aziz ametoa wito wa kujenga mazingira yatakayowawezesha Watanzania na vijana kuwa wamiliki na viongozi wa kampuni kubwa zinazozalisha utajiri ili kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050 ya kufikia uchumi wa Dola trilioni moja.
Rostam amebainisha hayo hivi karibuni alipokuwa Mgeni Rasmi katika hafla ya kutoa Tuzo za Umahiri katika Sekta za Ujenzi na Madini (African Construction and Mining Excellence Awards - ACAMEA 2026) iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
“Ninaunga mkono matarajio hayo lakini ninapofikiria Dira 2050 siangalii ukubwa wa uchumi tu, ninajiuliza je, ni nani atakayemiliki kampuni zitakazozalisha utajiri huo? Je, ni nani atakayemiliki mitambo? Je, ni nani atakayekuwa na teknolojia... Je, ni vijana wangapi wa Kitanzania watakaokuwa waajiri, wamiliki na viongozi wa kampuni hizo?" amehoji Rostam.
Amesisitiza kuwa vijana hawapaswi kupewa fursa za ajira pekee, bali nafasi ya kujenga na kumiliki biashara zao. Amesema ikiwa nchi haitajenga kampuni zenye nguvu za Kitanzania kuanzia sasa, kizazi kijacho kitakosa umiliki wa miundombinu na utajiri wa nchi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mfanyabiashara na Mwenyekiti wa Taifa Group, Rostam Azizi, ametoa rai kwa Serikali, taasisi za fedha, na wadau wa sekta binafsi kuweka maslahi ya taifa mbele katika kuwajengea uwezo Watanzania ili waweze kumiliki uchumi wa nchi yao, badala ya kubaki kuwa watazamaji kwenye miradi mikubwa inayotekelezwa nchini.
Rostam amezungumza hayo hivi karibuni alipokuwa Mgeni Rasmi katika hafla ya kutoa Tuzo za Umahiri katika Sekta za Ujenzi na Madini (African Construction and Mining Excellence Awards- ACAMEA 2026) iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Amebainisha kuwa Tanzania ina fursa nyingi katika sekta hizo pamoja na idadi kubwa ya vijana wenye ari, lakini wasipowekewa mazingira na sera wezeshi, fursa hizo hazitawanufaisha wazalendo na nchi haitakuwa na makampuni imara.
Rostam ameipongeza Serikali kupitia Wizara ya Madini kwa kuchukua hatua za makusudi za kuwalinda na kuwawezesha Watanzania kupitia Sheria na Kanuni za Maudhui ya Ndani (Local Content), yakiwemo marekebisho ya mwaka 2025 yaliyoimarisha ushiriki wa kampuni za ndani katika mnyororo wa thamani wa madini. Amehoji sababu za sekta nyingine za uchumi, hususan sekta ya ujenzi wa miundombinu mikubwa kama barabara, reli, madaraja na mabwawa, kushindwa kutumia mfumo huo wa kimkakati.
Rostam amesisitiza haja ya kuondokana na dhana mbaya kwamba kampuni za Kitanzania hazina uwezo wa kutekeleza miradi mikubwa au kumdharau mkandarasi kwasababu anazungumza Kiswahili, huku akikosoa mtindo wa kuamini kampuni za kigeni pekee. Amefafanua kuwa hapingani na uwepo wa kampuni za kigeni kwani zinajenga ubia na kuleta teknolojia, bali anapinga mtazamo wa kuwanyima fursa wazalendo kwa kigezo cha kukosa uzoefu.
Ameongeza kuwa uzoefu haupatikani kwa kusubiri bali kwa kufanya kazi, na akazitaka taasisi za fedha kutoa mitaji, huku Serikali ikihakikisha inalinda kampuni za ndani dhidi ya changamoto za kucheleweshewa malipo zinazoweza kuzifilisisha.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Shirika la Uwezo Tanzania limetangaza kuanza kwa utafiti mpya wa ujifunzaji kwa watoto wa umri wa miaka mitano hadi 17, ambao kwa mara ya kwanza utahusisha visiwa vya Zanzibar (Unguja na Pemba) pamoja mikoa yote 31 ya Tanzania.
Akizungumza na wanahabari Novemba 10, 2026 mkoani Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Uwezo Tanzania Baraka Mgohamwende, ameeleza kuwa utafiti huo utafanyika kwenye kaya zisizopungua 23,000 katika vijiji 1,150 nchi nzima kwa lengo la kupima uwezo wa watoto walio shuleni na wale waliokosa fursa ya kudahiliwa. Mwende amebainisha kuwa safari hii utafiti utaenda mbali zaidi kwa kupima stadi za maisha na maadili badala ya kuishia kwenye kusoma na kuhesabu pekee.
"Kwa mara ya kwanza katika tafiti zetu tangu tulipoanza mwaka 2008 tumekuwa tukiwapima watoto kwenye hesabu na kusoma. Lakini safari hii tutawapima pia watoto kwenye stadi za maisha na maadili... Hatuna sababu ya kusubiri kushughulika na watoto wakiwa tayari wameshakuwa katika kipindi cha balehe, bali tuna uwezo wa kukuza stadi hizi watoto wakiwa bado wana umri mdogo," ameeleza.
Taarifa ya utafiti huo kwa Tanzania inatarajiwa kutoka kufikia Desemba 2026 au mwanzoni mwa Januari 2027, huku ripoti ya kanda ya Afrika Mashariki ikitarajiwa kutolewa katikati ya mwaka 2027.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Naibu Waziri Mkuu Kivuli wa Chama cha ACT Wazalendo, Luhaga Mpina ameipongeza familia ya Mzee Lissu kwa kuonesha umoja na kusimama imara katika kipindi hiki kigumu ambacho familia hiyo inapitia changamoto kubwa na za kipekee.
Mpina amebainisha hayo alipokuwa akizungumza mkoani Singida katika msiba wa aliyekuwa Wakili, marehemu Alute Simon Mughwai Lissu, ambaye ni kaka wa Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu
Mpina ameeleza kuwa Watanzania wengi wamewekeza matumaini makubwa katika familia hiyo na kwamba familia haijawaangusha katika kusimamia misingi hiyo licha ya matatizo makubwa inayoyapitia.
Amebainisha kuwa familia zingine zikifikwa na matatizo na mitihani mikubwa kama hiyo zingeweza kusambaratika au kugawanyika, lakini familia ya Lissu imeendelea kushikamana kwa umoja mkubwa hata pale mambo makubwa yanapotokea kwa wakati mmoja ambapo kaka anafariki huku mdogo wake akiwa gerezani.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI:
Serikali ya Uingereza imesema ina wasiwasi mkubwa kufuatia kutiwa hatiani kwa kiongozi wa upinzani nchini Tanzania, Tundu Lissu, katika kesi ya uchochezi, huku ikizitaka mamlaka za Tanzania kuzingatia misingi ya haki, utawala wa sheria na maridhiano ya kisiasa.
Katika taarifa ya tamko la Serikali ya Uingereza, iliyotolewa Novemba 10, 2026, Waziri wa Afrika na Maendeleo ya Kimataifa, Kirsty McNeill, amekumbusha maoni ya Kikundi Kazi cha Umoja wa Mataifa kuhusu Uzuiaji wa Uhuru Kiholela (UN Working Group on Arbitrary Detention), namba 74/2025, kilichobaini kuwa Lissu alishikiliwa kiholela na hakukuwa na msingi wa kutosha wa kisheria.
"Tuna wasiwasi mkubwa kufuatia kutiwa hatiani kwa kiongozi wa upinzani nchini Tanzania, Bw. Tundu Lissu, kwa makosa ya uchochezi", imesomeka sehemu ya taarifa hiyo
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Kikundi Kazi hicho pia kilibaini kuwepo kwa dosari kubwa zilizohusu haki ya kupata mwenendo wa haki wa kesi, kikieleza kuwa hatua hiyo ilikiuka misingi ya Tamko la Kimataifa la Haki za Binadamu na Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiraia na Kisiasa ambao Tanzania ni mwanachama.
Kupitia taarifa hiyo, Uingereza imekumbusha wajibu wa Tanzania katika kulinda haki za binadamu, ikiwemo kupata haki katika mwenendo wa kesi, uhuru wa kujieleza, kushiriki katika shughuli za kisiasa na kutendewa kwa usawa mbele ya sheria.
Aidha, Serikali hiyo imeunga mkono msimamo wa Tume ya Rais ya Uchunguzi kwamba maridhiano ya kisiasa ni hatua muhimu katika kuponya majeraha yaliyotokana na vurugu zilizohusishwa na Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, kurejesha amani, kujenga upya imani na kuimarisha mshikamano.
Katika hatua nyingine, Uingereza imezitaka mamlaka za Tanzania kuendelea kuzingatia dhamira ya maridhiano, demokrasia inayoheshimu uwepo wa mitazamo tofauti, pamoja na misingi ya haki katika kesi, kufuata taratibu za kisheria na utawala wa sheria. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Zoezi la ubomoaji wa nyumba na majengo linaloendelea katika eneo la Maili Mbili jijini Dodoma limelenga kupisha mradi wa upanuzi wa barabara ya njia nne kuelekea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Msalato.
Akizungumza kwa njia ya simu leo Novemba 10, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, ameeleza kuwa operesheni hiyo inatekelezwa na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) katika maeneo yaliyo ndani ya hifadhi ya barabara.
Mkuu huyo wa Wilaya amefafanua kuwa wananchi waliokuwa wakiishi au kufanya shughuli zao katika maeneo hayo walishapewa taarifa mapema za kuondoka, huku wale wote waliokuwa wanastahili kulipwa fidia wakiwa tayari wameshapata malipo yao. Kutokana na hatua hiyo, amewataka wananchi wenye malalamiko kuwasilisha hoja zao katika ofisi za TANROADS ili ziweze kusikilizwa na kufanyiwa kazi.
Aidha, amewahimiza wananchi kuacha kufanya shughuli za kiuchumi ndani ya hifadhi za barabara na badala yake watumie maeneo rasmi yaliyotengwa na Serikali kwa ajili ya biashara.
Wakati huo huo, jitihada za Jambo TV za kuwatafuta viongozi wa TANROADS Mkoa wa Dodoma ili kupata ufafanuzi zaidi kuhusu zoezi hilo hazikufanikiwa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Wakili Boniface Mwabukusi, ametoa wito kwa viongozi wa dini kuacha kuwapa sakramenti watu wanaojihusisha na ukandamizaji na badala yake waanze kuwafukuza kanisani na misikitini.
Mwabukusi ametoa wito huo leo mkoani Singida alipokuwa akitoa salamu za rambirambi katika msiba wa Alute Mughwai Lissu.
Ameeleza kuwa kanisa limekuwa mwepesi kuwahukumu watu wanaotenda dhambi zingine kama vile uzinzi, lakini wanaowakandamiza wenzao wamekuwa wakiachwa wakiendelea kupata huduma za kiroho bila kukemewa.
Katika hatua nyingine, Mwambukusi amesema chama hicho kinashirikiana na mawakili wa Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu kwa kuzingatia maelekezo ya Lissu mwenyewe ili kushughulikia kwa haraka maombi yake ya dhamana na usikilizaji wa rufaa dhidi ya hukumu yake.
"Sisi kama TLS tutaendelea kuwasiliana na familia yake kwenye hatua zingine zinazofuata lakini vilevile tutashirikiana na mawakili kwa kuzingatia maelekezo ya Tundu Lissu mwenyewe. Sisi Baraza la Uongozi na mawakili wake Tundu Lissu kushughulikia swala la rufaa kwa haraka lakini vilevile maombi yake ya dhamana huku tukisubiri usikilizwaji wa rufaa," ameeleza.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Godbless Lema, ametoa onyo kuhusu kile alichokiita kuongezeka kwa uchungu na chuki na changamoto nchini, akieleza kuwa hali hiyo inaharibu msingi wa taifa na kutishia ustawi wa kizazi kijacho.
Lema amebainisha hayo leo alipokuwa akizungumza mkoani Singida katika msiba wa Mzee Alute Mughwai Lissu, ambaye ni kaka wa Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu.
Lema ameeleza kuwa nchi kwa sasa inakabiliwa na uchungu mkubwa unaojidhihirisha wazi hata kwenye mitandao ya kijamii na majukwaa mengina yanayowakutanisha watu kutokana sababu mbalimbali ikiwano namna mfumo wa vyombo vya haki unavyofanya kazi na kueleza kuwa ukiukwaji wa misingi ya sheria unaacha majeraha makubwa miongoni mwa wananchi.
“Hatari kubwa inayokabili nchi hii sasa kwa kiwango kikubwa sana ni pale unapoweza kupelekwa mahakamani kwa kosa la wizi wa gari halafu ukafungwa kwa kosa la kubaka. Mahakama yetu imefika hapo. Sasa kuna uchungu na hofu kwenye jamii," amesema Lema.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
"Hakuna namna tutakuja kumfufua Mzee Alute halafu(Lissu) ashiriki katika zoezi la kumzika wote tunajua kiafrika maana ya zoezi la kumuaga na kumzika ndugu yako"
Ameeleza Makamu Mwenyekiti wa @ChademaTZ2 John Wegesa Heche @HecheJohn leo Novemba 10, 2026 akizungumza na waombolezaji Mahambe Wilaya ya Ikungi, Mkoa wa Singida katika msiba wa Alute Mughwai Lissu ambaye ni kaka wa Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu aliye gerezani kutokana na kosa la uchochezi alilohukumiwa kifungo cha miaka minne.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkurugenzi wa taasisi ya The Women Wakeup Foundation, Dkt. Veronica Alexander, ametoa ushuhuda mzito kuhusu jinsi alivyofukuzwa kazi baada ya kumpokea na kumpatia huduma ya kwanza mwanasiasa Tundu Lissu aliposhambuliwa kwa risasi mkoani Dodoma.
Dkt. Veronica amebainisha hayo leo alipokuwa akizungumza na kutoa ushuhuda wake katika msiba wa marehemu Mzee Alute Mughwai Lissu mkoani Singida.
“Lakini nilifungua hii NGO kwa ajili ya kusaidia watu wasiotendewa haki na nilisema kazi sio riziki, riziki inatoka kwa Mungu," amesema Dkt. Veronica
Dkt. Veronica amesisitiza kuwa haogopi vitisho kwasababu ya kusimamia ukweli na haki, huku akiwasihi wananchi na Wakristo kuendelea kusimamia haki bila woga wowote.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora limewakamata na kuwafikisha mahakamani watuhumiwa 15 kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya watu sita na kujeruhi wengine watano, katika tukio linalodaiwa kuchochewa na wafugaji waliokuwa wakijaribu kuwaokoa ng’ombe wao waliokuwa wamekamatwa na Askari wa Hifadhi ya Wanyamapori (TAWA) ndani ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Isawagala, wilayani Sikonge mkoani Tabora.
Akitoa taarifa hiyo Novemba 10,2026, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora, ACP. Twaha Lulengelule, amesema tukio hilo lilitokea usiku wa manane Septemba 18, 2026, kufuatia operesheni iliyokuwa ikiendeshwa na askari wa TAWA kwa kushirikiana na askari wa Shirika la ADAP, askari wa Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Ipole, walinzi wa vijiji (VGS) pamoja na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge.
Kamanda Lulengelule amewataka wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi wanapokumbana na changamoto au migogoro, akisisitiza umuhimu wa kutumia vyombo vya dola kutatua matatizo, huku akibainisha kuwa operesheni ya kuwatafuta na kuwakamata watuhumiwa wengine wanaodaiwa kuhusika na tukio hilo ikiendelea.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu Mwenyekiti wa @ChademaTZ2 John Heche @HecheJohn amesema chama hicho hakijawahi kukataa maridhiano na kipo tayari ila hakiwezi kuyafanya haliyakuwa Mwemyekiti wake Tundu Lissu akiwa gerezani.
Heche amesema leo Novemba 10, 2026 akizungumza na waombolezaji katika msiba wa Alute Mughwai Lissu ambaye ni kaka wa Lissu uliofanyika Mahambe, Wilaya ya Ikungi mkoani Singida.
"Tunataka maridhiano ya ukweli sio ya hila na uongo na hakuna mazungumzo yatafanyika Mwenyekiti wetu akiwa ndani na mimi namwambia Samia(Rais Samia Suluhu Hassan) mwenye majibu na matatizo ya nchi hii yupo Ukonga" amesema HecheThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Dorothy Semu, amesema mkoa wa Kigoma umebarikiwa na rasilimali nyingi ikiwemo ardhi yenye rutuba, vyanzo vya maji, Ziwa Tanganyika na watu wenye uwezo wa kufanya kazi, lakini bado wananchi wake wamegubikwa na umaskini mkubwa.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara na wananchi wa Rusohoko, Semu amesema Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeshindwa kuwatoa Watanzania kwenye lindi la umaskini licha ya rasilimali hizo kuwepo.
Ameeleza kuwa vijana wengi wanataka kujiajiri kwenye kilimo, lakini mazingira ni magumu kutokana na bei ya mbolea inayozidi kupanda, bei ndogo za mazao sokoni na kile alichosema ni Serikali kuzuia fursa za kuuza mazao nje ya nchi.
Semu amesisitiza kuwa mkulima wa Tanzania bado hajawekwa kwenye mifumo inayomfanya kilimo kiwe na tija, heshima na mapato yanayomwezesha kujikimu.
Kuhusu sekta ya uvuvi, Semu amemgeukia Waziri wa Mifugo na Uvuvi kwamba wameweka kodi na tozo kubwa kwa wavuvi na wachakataji wa samaki wa Ziwa Tanganyika, ambao ndiyo chanzo kikuu cha kipato kwa wananchi wengi wa Kigoma.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
“Vyama vya Kiarabu vimekuwa na nafasi kubwa katika mchakato huu kwa sababu vinaweza kuamua kushirikiana na upande wa Netanyahu au mpinzani wake Gadi Eisenkot ili kufikisha idadi ya wabunge inayohitajika kuunda serikali,” amesema Mchambuzi wa masuala ya kimataifa, Wakili Henry Mwinuka.
Akizungumza leo, Novemba 10, 2026, katika kipindi cha Jambo Asubuhi cha Jambo TV, Mwinuka amesema Bunge la Israel lina wabunge 120 na chama au muungano wa vyama unahitaji angalau viti 61 ili kuunda serikali.
Amesema Netanyahu, kupitia chama cha Likud na washirika wake, amepata viti 53, huku upande wa Gadi Eisenkot ukiwa na viti 48, hali inayofanya vyama vya Kiarabu vyenye viti 19 kuwa na nafasi muhimu katika mazungumzo ya kuunda serikali.
Ameeleza kuwa changamoto iliyopo ni tofauti za kiitikadi na misimamo kuhusu masuala ya Gaza na Palestina, ambazo zimekuwa kikwazo kwa vyama vya Kiarabu kushirikiana na vyama vya Kiyahudi kuunda serikali.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Vita vinavyoendelea Gaza na namna Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, anavyoshughulikia suala la Palestina vimechangia kupungua kwa imani ya baadhi ya wananchi wa Israel kwake, hiyo ni kwa mujibu wa mchambuzi wa masuala ya kimataifa, Wakili Henry Mwinuka.
Akizungumza leo, Novemba 10, 2026, katika kipindi cha Jambo Asubuhi cha Jambo TV, Mwinuka amesema wananchi wameanza kuhoji mafanikio ya vita hivyo, huku kukiwa na changamoto za maisha na usalama nchini humo.
Amesema baadhi ya Waisraeli wanaamini Netanyahu anaendeleza vita ili kuendelea kubaki madarakani na kuepuka kushughulikiwa kwa kesi za rushwa zinazomkabili.
Kuhusu mchakato wa kuunda serikali mpya, Mwinuka ameeleza kuwa Rais wa Israel, Isaac Herzog, amefanya mashauriano na wabunge wa Knesset ili kubaini mgombea mwenye uungwaji mkono mkubwa wa kuunda serikali.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Wakili Boniface Mwabukusi, amesema kuwa suala la Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, kuendelea kuwa gerezani linamkera, lakini ameshindwa kulizungumzia kwa sasa kwa kuhofia kuathiri shughuli za msiba.
Mwabukusi ameyasema hayo leo Novemba 10, 2026, Mahambe, Wilaya ya Ikungi mkoani Singida, wakati wa msiba wa kaka yake Tundu Lissu, marehemu Wakili Alute Lissu.
Wakili Mwabukusi amesema kuwa TLS haitakaa kimya kuhusu suala hilo na kwamba watazungumza kwa wakati muafaka, akieleza kuwa kwa sasa wameamua kutolizungumzia kwa kina ili kutoathiri shughuli za mazishi ya marehemu Alute Lissu.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mchambuzi wa masuala ya kimataifa, Wakili Henry Mwinuka amesema Israel inahitaji kubadili mwelekeo wa sera zake kutokana na mabadiliko ya mtazamo wa jumuiya ya kimataifa kuhusu vita vinavyoendelea Gaza.
Akizungumza leo, Novemba 10, 2026, katika kipindi cha Jambo Asubuhi cha Jambo TV, Mwinuka amesema matukio tangu Oktoba 7 yameathiri taswira ya Israel kimataifa na uhusiano wake na washirika muhimu.
Amesema, “Kama tutaendelea na mwelekeo uliopo, Israel itapoteza kabisa nguvu yake na itapoteza zaidi ushawishi wake kwa washirika wake muhimu.”
Ameongeza kuwa maandamano ya kupinga mashambulizi ya Gaza na matukio ya Ukingo wa Magharibi, pamoja na taarifa zinazosambazwa kupitia mitandao ya kijamii na wanahabari raia, vimechangia kubadilisha mtazamo wa dunia kuhusu Israel.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mchambuzi wa masuala ya kimataifa, Wakili Henry Mwinuka, amesema Rais wa Marekani, Donald Trump, na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu wanaweza kukabiliwa na changamoto za kurejea madarakani kutokana na mabadiliko ya kisiasa katika nchi zao.
Akizungumza leo, Novemba 10, 2026, katika kipindi cha Jambo Asubuhi cha Jambo TV, Mwinuka amesema pamoja na kuwepo kwa watu wanaomshawishi Trump kuwania tena urais, kurejea kwake kunaweza kuwa kugumu.
Amesema, “Don't mess with Trump,” akieleza changamoto zinazoweza kujitokeza katika safari ya kisiasa ya Trump, huku kwa upande wa Israel akitaja dalili za kuandaliwa kwa viongozi wengine kuchukua nafasi ya Netanyahu.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Baadhi ya wakazi na wafanyabiashara wa Mtaa wa Maili Mbili jijini Dodoma wameathirika na zoezi la ubomoaji wa nyumba na majengo yao yanayodaiwa kujengwa ndani ya eneo la hifadhi ya barabara kuu ya Dodoma–Arusha, huku wakiiomba Serikali kuangalia kwa huruma hali wanayopitia.
Wakizungumza leo, Novemba 10, 2026, jijini Dodoma, wananchi hao wamedai kuwa wamekuwa wakiishi na kuendesha shughuli zao za biashara katika eneo hilo kabla ya kukumbwa na ubomoaji huo.
Baadhi yao wameeleza kushangazwa na hatua hiyo, wakidai hawakupatiwa notisi ya awali wala taarifa za kutosha kuhusu muda na utaratibu wa kuondoka katika maeneo hayo.
Hata hivyo, baadhi ya maafisa wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS), Mkoa wa Dodoma, waliokuwepo eneo la tukio wamekataa kuzungumzia suala hilo.
Jambo TV inaendelea na jitihada za kumpata Mkurugenzi wa TANROADS Mkoa wa Dodoma ili kupata ufafanuzi kuhusu sababu za ubomoaji huo pamoja na utaratibu uliofuatwa kabla ya zoezi hilo kutekelezwa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi, ameuagiza uongozi wa Halmashauri Mbinga kutumia sehemu ya mapato yake ya ndani, yanayofikia wastani wa Shilingi bilioni 14.7 kwa mwaka, kuharakisha ukamilishaji wa baadhi ya majengo hasa nyumba za wafanyakazi badala ya kutegemea fedha za Serikali Kuu pekee.
Ndejembe ametoa maagizo hayo wakati akikagua ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya Mbinga yenye thamani ya Shilingi bilioni 3.7, ambapo majengo 15 kati ya 29 yamekamilika tangu mradi huo uanze mwaka 2021.
Amepongeza mafanikio katika kuboresha huduma za uzazi na kupunguza vifo vya mama na mtoto vilivyoripotiwa hospitalini hapo kutoka 550 Kabla ya ujenzi wa hospitali hiyo hadi 106 tangu hospitali ilipoanza kutoa huduma.
Akieleza sababu za idadi ya Vifo, Mganga Mkuu katika hospitali hiyo amesema idadi kubwa ya Vifo inatokana na wajawazito kujifungulia nyumbani.
Akifikisha salamu za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa wagonjwa, Makamu wa Rais amesisitiza dhamira ya Serikali ya kuendelea kuimarisha miundombinu na huduma za afya ili kulinda maisha ya mama na mtoto. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Kada wa CHADEMA, Mchungaji Peter Msigwa, amesema kuwa uamuzi wake wa kujitoa CHADEMA na kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM) haukumfurahisha Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, na hivyo walipatanishwa na Kaka yake, Marehemu Alute
Msigwa ameyasema hayo leo Novemba 10, 2026, Mahambe, Wilaya ya Ikungi mkoani Singida, wakati wa mazishi ya Marehemu Wakili Alute Lissu.
Amesema kuwa mahusiano yake na Tundu Lissu hayakuwa mazuri baada ya kuhamia CCM, hadi pale Marehemu Wakili Alute Lissu alipochukua jukumu la kuwapatanisha nyumbani kwake jijini Arusha.
Ameeleza kuwa Alute Lissu ndiye aliyekuwa daraja la kurejesha mahusiano yake na Tundu Lissu.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Godbless Lema, amesema wengi walitarajia kuwa Mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu, angeachiwa huru kutokana na mwenendo wa kesi inayomkabili, lakini hali imekuwa tofauti na matarajio yao.
Lema ameyasema hayo leo, Novemba 10, 2026, Mahambe, Wilaya ya Ikungi mkoani Singida, wakati wa mazishi ya marehemu Wakili Alute Mughwai Lissu.
Amesema inasikitisha kuona Tundu Lissu akikosekana katika mazishi ya kaka yake, lakini anaamini kuwa ana nguvu ya kutosha kukabiliana na hali hiyo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Kazi, Ajira na Mahusiano Mhe. Deus Sangu ameupongeza Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa kuwekeza katika mardi wa kimkakati wa jengo la kitega uchumi nchini Kenya ambalo litachagiza kukuza thamani ya uwekezaji wa Mfuko huo na shughuli za kiuchumi.
Sangu ametoa pongezi hizo Novemba 9, 2026 alipokuwa katika ziara ya kikazi jijini Nairobi iliyolenga kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa jengo la kitega uchumi unaotekelezwa kwa ubia kati ya Mfuko wa NSSF na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
“Mradi huu unaotekelezwa katika eneo la kimkakati la takribani ekari mbili ndani ya jijini Nairobi utakapokamilika utaongeza thamani ya uwekezaji kwa Mfuko wa NSSF, kukuza shughuli za kiuchumi na kuwezesha Tanzania kutangaza zaidi vivutio vyake vya utalii,” amesema
Aidha, amesisitiza kuwa uwekezaji huo ni sehemu ya utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhusu kuelekeza uwekezaji katika maeneo yenye tija na yanayokuza uchumi wa Taifa kwa ujumla.
Kadhalika, ameutaka Mfuko wa NSSF pamoja na mkandarasi wa mradi huo kuendeleza kasi ya ujenzi ili kukamilisha mradi kwa wakati uliopangwa mwezi Juni, 2028. Pia, amesisitiza suala la usimamizi na udhibiti wa ongezeko la gharama za utekelezaji ili kuhakikisha thamani halisi ya fedha za Serikali inafuatwa.
Akizungumza kwa naiba ya Balozi, Mtawala Mkuu Bi. Herieth Magogo amesema mradi huo ni uwekezaji mkubwa na ni sehemu ya utekelezaji wa diplomasia ya Tanzania inayolenga kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi, biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Kenya.
Ameongeza kuwa, Kenya ni miongoni mwa wadau wakubwa wa Tanzania katika sekta za biashara na uwekezaji, hivyo utekelezaji wa mradi huo ni hatua muhimu inayoonesha dhamira ya nchi hizo mbili kuendeleza ushirikiano wenye manufaa ya pamoja, pamoja na kuimarisha zaidi uhusiano wa kidiplomasia na kiuchumi.
Naye, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii, Bw. Masha Mshomba amesema kuwa uwekezaji huo ni wa kihistoria kwa kuwa ni mara ya kwanza mfuko huo umewekeza nje ya mipaka ya Tanzania.
Amesema uamuzi huo umetokana na ukuaji mkubwa wa NSSF katika miaka ya hivi karibuni, hivyo kuhitaji kupanua zaidi shughuli zake za uwekezaji ili kuendana na mahitaji na malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050 iliyozinduliwa hivi karibuni.
“Uwekezaji huo wa kimkakati nje ya Tanzania ni mpango muhimu utakaoiwezesha NSSF kuongeza wigo wa uwekezaji, kukuza mapato na kuchangia utekelezaji wa malengo ya maendeleo ya taifa,” amesema.
Kwa upande wake, Mbunifu wa Majengo na Msimamizi wa Mradi huo, Bw. Albert Mwambafu, amemhakikishia Waziri kuwa mradi huo utakamilika kwa ubora uliokusudiwa na kuwa alama muhimu ya mafanikio ya Watanzania katika sekta ya usanifu majengo na usimamizi wa miradi mikubwa nje ya mipaka ya Tanzania.
Kwa upande mwengine, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu- Kazi, Ajira na Mahusiano, Deus Sangu, mara baada ya kukagua mradi huo ametembelea ofisi za Ubalozi wa Tanzania zilizopo Jijini Nairobi, nchini Kenya.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Katibu wa Idara ya NEC Organaizesheni wa Chama cha Mapinduzi @ccm_tanzania Paul Chacha amesema aliyekuwa kada wa chaa hicho Mchungaji Peter Msigwa aache kudanganya watu kuwa anazo siri nyingi za chama hicho jambo ambalo amedai sio kweli.
Akizungumza jana Novemba 9, 2026 kwenye Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Mwanza Chacha amesema Msigwa hana siri alizonazo za chama hicho kwani jukumu lake kubwa ilikua ni kupeleka simu ikiita kwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi.
Ameeleza kuwa chama hicho ni chama kilicho makini katika kujisimamia huku akisisitiza "Sasa muulizeni yeye(Msigwa na yule baba(Dkt. Nchimbi) wako wapi?" amehoji ChachaThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katika tukio la heshima na majonzi, jopo la mawakili likiongozwa na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Wakili Boniface Mwabukusi, limebeba jeneza lenye mwili wa marehemu Wakili Alute Lissu kuelekea eneo la kufanyika kwa ibada ya kumuaga.
Tukio hilo limefanyika leo, Novemba 10, 2026, katika eneo la Mahambe, Wilaya ya Ikungi, mkoani Singida, ambapo ndugu, jamaa na waombolezaji wamekusanyika kutoa heshima za mwisho kwa marehemu kabla ya kuzikwa katika makaburi ya familia.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI:
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi, ameielekeza Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) kuongeza juhudi za kutafuta na kupanua masoko ya kimataifa kwa kubaini bidhaa zinazohitajika pamoja na viwango vya ubora vinavyotakiwa katika masoko hayo.
Amesema hatua hiyo itawasaidia wazalishaji nchini kuendana na mahitaji ya wanunuzi wa kimataifa, kuongeza ushindani wa bidhaa zao na kupanua mauzo nje ya nchi.
Makamu wa Rais ametoa maelekezo hayo wakati akitembelea mabanda ya Maonesho ya Kimataifa ya Biashara na Uwekezaji wa Mazao ya Bustani, HortiLogistica Africa 2026, katika viwanja vya TGT mkoani Arusha, kabla ya ufunguzi rasmi. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, akiagana na Makamu wa Rais, Deogratius Ndejembi, leo Novemba 10, 2026 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kabla ya kuanza safari kuelekea jijini Antalya, Uturuki, kushiriki Mkutano wa 31 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP31).
Mkutano huo wa COP31 unawakutanisha viongozi na wadau mbalimbali kutoka mataifa tofauti kujadili masuala yanayohusu mabadiliko ya tabianchi na hatua za kukabiliana na athari zake.
Akiwa nchini humo, Rais Dkt. Samia atashiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali (Antalya Leaders' Summit), pamoja na kikao cha ngazi ya juu kuhusu matumizi ya nishati safi ya kupikia barani Afrika (High-Level Event on Clean Cooking in Africa). -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Hivi ndivyo hali ilivyo asubuhi hii eneo la Mahambe, Wilaya ya Ikungi, mkoani Singida, ambako maandalizi ya mazishi ya marehemu Wakili Alute Mughwai Lissu yanaendelea.
Marehemu anatarajiwa kuzikwa leo, Novemba 10, 2026, katika makaburi ya familia ya Lissu yaliyopo Mahambe.
Jambo TV imeweka kambi Mahambe tangu jana, Novemba 9, kwa ajili ya kukuletea taarifa za moja kwa moja kuhusu msiba huo, maandalizi ya mazishi na matukio mbalimbali yanayohusiana na kuaga na kumzika marehemu.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA na Mbunge wa zamani wa Arusha, Godbless Lema, pamoja na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Wakili Boniface Mwabukusi, wamewasili nyumbani kwa marehemu Mzee Alute Mughwai Lissu, eneo la Mahambe, mkoani Singida, kwa ajili ya kushiriki mazishi yake yanayotarajiwa kufanyika leo, Novemba 10, 2026.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwanasheria Nathaniel Maseke akihojiwa juu ya mtazamo wa taaluma ya sheria kama kosa la uhaini lina kosa dogo.
Sikiliza majibu yake.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwenyekiti wa Ngome ya Wanawake Taifa wa ACT Wazalendo na Waziri Kivuli wa Wanawake, Watoto na Makundi Maalum, Janeth Rite, amesema wananchi wa kata ya Rusohoko, wilaya ya Kibondo, mkoa wa Kigoma, bado wanateseka na upungufu wa maji safi na salama, huku akimuomba Waziri wa Maji, Jumaa Awezo kushughulikia tatizo hilo.
Ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wananchi eneo hilo, ambapo amesisitiza kuwa huduma ya maji ni muhimu zaidi na inapaswa kufikia kaya zote badala ya kuishia kwenye vyanzo pekee.
Rite amedai kuwa licha ya maji kuwepo kwenye vyanzo, mabomba na matangi makubwa hayajawekwa ili kusambaza maji kwa wananchi, hivyo wanawake kuendelea kubeba ndoo kichwani kwa miaka mingi.
Ametoa wito kwa Waziri Aweso kutembelea eneo hilo ili aone mateso ya wanawake na kuchukua hatua za haraka za kutatua kero hiyo ambapo pia amesema ACT Wazalendo itamsaidia Diwani wa eneo hilo kuhakikisha wanawake wanaondolewa mzigo wa kubeba maji kichwani.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Msafara uliobeba jeneza lenye mwili wa marehemu Mzee Alute Mughwai Lissu umewasili Mahambe, mkoani Singida, kwa ajili ya mazishi yanayotarajiwa kufanyika leo, Novemba 10, 2026.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Wanu Hafidh Ameir, amesema Serikali itaendelea kutumia Sayansi, Teknolojia na ubunifu kama nyenzo muhimu za kutatua changamoto za jamii na kuchochea maendeleo ya taifa.
Wanu amesema hayo Novemba 9, 2026 mkoani Dar es Salaam, wakati wa kufungua Kongamano lililoandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, ambapo alimwakilisha Waziri wa wizara hiyo, Prof. Adolf Mkenda.
Ametoa wito kwa vyuo vikuu, taasisi za utafiti, wataalamu wa afya, waganga wa tiba asilia pamoja na mamlaka za udhibiti kuhakikisha wanajenga na kuimarisha ushirikiano wa kudumu katika kuendeleza tafiti na bunifu.
Naye Mwenyekiti wa Baraza la tiba asili nchini Prof. Joseph Otieno, amesema taifa limeanza kuweka heshima katika masuala ya tiba asili jambo ambalo ni hatua ya maendeleo kwa tiba hizo.
Aidha Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi ya Afya na Tiba Shirikishi (MUHAS), Prof. Appolinary Kamuhabwa, amesema katika eneo la Mloganzila wametenga eneo la ekari 200 kwaajili ya kuendeleza masuala ya dawa asili.
Aidha wanafunzi wa Udaktari wa maeneo mbalimbali ambao ni miongoni mwa washiriki wa Kongamano hilo, wamesema kushiriki kwao kumewapa nafasi ya kutambua umuhimu wa tiba asili ikiwa inatumika sambamba na Sayansi ya tiba za kisasa katika kuwasaidia jamii.
Mapendekezo yatakayotolewa yanatarajiwa kuwa msingi wa kuandaa mfumo wa kitaifa wa kutambua, kutafiti, kuendeleza na kufanya biashara ya dawa na vifaa tiba vinavyotokana na maarifa na rasilimali za ndani.
Kaulimbiu ya Kongamano hilo ilikuwa "Kutumia ubunifu, utafiti na maarifa asilia ya ndani kwaajili ya maendeleo ya tiba na bidhaa za afya".This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) imewahimiza wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuchangamkia fursa zilizopo katika sekta ya kilimo cha bustani na vikolezo (Horticulture), hususan uwekezaji katika uzalishaji, uhifadhi, usafirishaji na uongezaji thamani wa mazao.
Meneja Uhamasishaji na Uwekezaji wa nje kutoka TISEZA, Daudi Riganda, amesema sekta hiyo inayojumuisha maua, matunda, mbogamboga na viungo inaendelea kuwa na fursa za kiuchumi kupitia mauzo ya nje na kuvutia mitaji, huku akitaja uwekezaji katika umwagiliaji, maghala, vyumba vya ubaridi (Cold Rooms), vituo vya kuhifadhi mazao (Cold Stores) na viwanda vya kuongeza thamani.
Akizungumza katika Maonesho ya Hortilogistical Africa 2026, Riganda amesema TISEZA imeshiriki kutoa elimu na kuhamasisha uwekezaji, huku ikitumia kituo cha huduma za pamoja (One Stop Center) kinachojumuisha taasisi takribani 15 za Serikali kuwezesha wawekezaji kupata huduma sehemu moja badala ya kufuata taasisi mbalimbali, amesema mwekezaji anayekidhi vigezo na kukamilisha nyaraka zinazohitajika anaweza kupata cheti cha uwekezaji ndani ya saa 24.
Kwa upande wa Ofisi ya Mageuzi ya Kilimo, mwakilishi wake amesema moja ya malengo yanayohamasishwa kupitia maonesho hayo ni kupunguza upotevu wa mazao ya bustani baada ya mavuno kutoka asilimia 40 hadi asilimia 20, kupitia uwekezaji katika miundombinu ya uhifadhi na uongezaji thamani. Fursa hizo zinahusisha mazao ya kimkakati yakiwemo parachichi, ndizi, zabibu na viungo.
Naye Nasrul Salum Nasrul kutoka Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), amesema ushiriki wao katika kituo hicho unalenga kuwaunganisha wazalishaji na masoko ya ndani, kikanda na kimataifa, pamoja na kukuza wajasiriamali wadogo ili waweze kupanua biashara zao na kufikia masoko makubwa.
Kwa upande wake, Tulibako Minga kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA), amesema kituo hicho kinatoa huduma kwa wadau wa mnyororo wa thamani wa Horticulture, kuanzia uzalishaji, biashara ya ndani na nje ya nchi hadi usafirishaji wa mazao.
Naye Mdili Katemani kutoka Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA), amesema mamlaka hiyo inasaidia kufungua masoko mapya ya kimataifa, kukagua mazao yanayosafirishwa nje ya nchi na kutoa cheti cha afya ya mimea, huku ikiwawezesha wakulima kupata taarifa na kutimiza masharti ya masoko ya kimataifa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwananchi fulani alivyogeuka kivutio baada ya kumfanyia maombi Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, John Heche alindwe dhidi ya utekaji na madhila yoyote yatakayoelekezwa kwake.
Tukio limetokea mkoani Arusha Novemba 9, 2026, mara baada ya ibada ya kuuaga mwili wa marehemu Wakili Alute Mughwai Lissu.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mzee Muro Lissu, mdogo wa marehemu Wakili Alute Lissu, amesema anatamani Tundu Lissu angekuwepo ili aweze kushiriki maziko ya kaka yake, lakini isivyo bahati sheria haijamruhusu kufanya hivyo.
Mzee Muro ameyasema hayo leo Novemba 9, 2026, eneo la Mahambe, Wilaya ya Ikungi, Mkoa wa Singida, ambako mwili wa marehemu Wakili Alute Lissu unatarajiwa kuzikwa kesho katika makaburi ya familia.
Amesema hukumu ya kifungo cha miaka minne alichopewa Tundu Lissu imewaumiza na kuwahuzunisha, kwani walikuwa na matarajio ya kumuona kiongozi wao akishiriki mazishi ya kaka yake.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mbunge wa zamani wa Jimbo la Arusha Mjini, Mrisho Gambo, amesema misimamo ya familia ya Lissu katika kusimamia haki na ukweli imejengwa tangu ngazi ya familia, akieleza kuwa marehemu Wakili Alute Mughwai Lissu alikuwa mfano wa mtu aliyesimamia kile alichokiamini bila kujali tofauti za kisiasa.
Akizungumza leo Novemba 9, 2026, wakati wa ibada ya kuuaga mwili wa marehemu, Gambo amesema Alute alikuwa mwanachama wa CCM aliyeamini misingi ya chama hicho kwa mujibu wa falsafa ya Mwalimu Julius Nyerere.
Amesema somo kubwa alilolipata kutoka kwa marehemu ni umuhimu wa kuishi katika ukweli, kusimamia haki na kutetea kile mtu anachokiamini.
Aidha, amewataka Watanzania kujenga misingi ya haki na ukweli, akisisitiza kuwa mtu anayesimamia haki anaweza kuchukiwa na kununiwa, lakini mwisho wa siku ataandikwa katika vitabu vya historia.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, John Heche, amesema chama hicho kimejiandaa kukabiliana na kipindi kigumu kinachoweza kukikabili katika safari yake ya kisiasa, akisisitiza kuwa viongozi na wanachama wake hawatakata tamaa katika kutetea nchi na kujenga chama.
Akizungumza leo Novemba 9, 2026, wakati wa ibada ya kuuaga mwili wa marehemu Wakili Alute Mughwai Lissu, Heche amesema pamoja na changamoto zinazoweza kujitokeza, CHADEMA itaendelea kusimamia misimamo yake, akieleza kuwa kuna wakati wanapaswa kusema ukweli kwa kujiuliza, 'wasiposema wao, nani atasema, na kama si sasa, ni lini?'.
Heche amewashukuru viongozi na wadau mbalimbali walioonesha mshikamano kwa familia ya marehemu wakati wa kipindi hiki cha majonzi, huku akieleza kuwa familia hiyo inapitia wakati mgumu na kuwataka Watanzania kuendelea kuiombea.
Aidha, ametoa wito wa kuendelea kumuombea Tundu Lissu ili apate moyo wa subira na nguvu kutoka kwa Mwenyezi Mungu katika kipindi hiki kigumu, huku akitoa pole kwa waombolezaji na jumuiya ya mawakili kwa kumpoteza Wakili Alute Mughwai Lissu, ambaye amesema alikuwa msaada kwa watu wengiThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI:
Tanzania imeibuka mshindi na kupata tuzo nne kati ya sita katika Maonesho ya 26 ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati wa Afrika Mashariki, maarufu kama Jua Kali - Nguvu Kazi, yaliyofanyika katika Viwanja vya Gikondo, Kigali, Rwanda.
Katika maonesho hayo yaliyofungwa Novemba 08, 2026, wajasiriamali wa Tanzania wameibuka washindi katika makundi mbalimbali. Anne Crochet ameibuka mshindi wa kwanza katika kundi la bidhaa za nguo za batiki, Sima Candle akishinda kundi la ubunifu, sanaa, fenicha na madini, huku Pishon Honey na Makai Moringa wakishika nafasi ya pili na tatu katika kundi la mbogamboga. Tuzo ya nne imechukuliwa na Afritech katika kundi la bidhaa za ngozi.
Kufuatia ushindi huo, Tanzania imekuwa mshindi wa pili kwa ujumla kupitia mjasiriamali Anne Crochet, huku Kenya ikishika nafasi ya kwanza kupitia Thonge Leather na nafasi ya tatu pia ikienda Kenya kupitia Mamlo Foods.
Akizungumza katika ufungaji wa maonesho hayo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Rwanda, Juan Haguma, amesema Serikali ya Rwanda imefarijika kuona wajasiriamali zaidi ya 2,000 wakishiriki kuonyesha na kufanya biashara, hatua inayokuza uchumi na kuimarisha Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Haguma amewasihi wajasiriamali kuendeleza ubunifu na kutumia teknolojia rahisi ili kuongeza thamani ya bidhaa, hatua itakayosaidia kuongeza uhakika wa masoko ndani ya Afrika Mashariki na nje ya Bara la Afrika.
Mwenyekiti wa Shirikisho la Wajasiriamali Wadogo na wa Kati wa Afrika Mashariki, Josephat Rweyemamu, amesema anashukuru kuwa maonesho ya mwaka huu yamewezesha washiriki kupata masoko mapya ya bidhaa zao pamoja na kukuza ushirikiano baina ya nchi wanachama.
Rweyemamu ameongeza kuwa mafanikio ya maonesho hayo yamechangiwa na Serikali ya Rwanda kuimarisha amani na usalama muda wote, hatua iliyosaidia wajasiriamali kufanya biashara zao vizuri bila vizuizi.
Mwenyekiti huyo amewataka wajasiriamali kutoka nchi zote nane kujiandaa kwa maonesho ya mwaka ujao 2027 kwa kuzalisha bidhaa bora na zilizoongezwa thamani, hatua itakayokuza masoko.
Maonesho hayo yalifanyika kuanzia Oktoba 30 hadi Novemba 8, 2026, ambapo Tanzania iliwakilishwa na washiriki zaidi ya 374. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, John Heche amesema wajibu wa serikali si kukomoa wananchi kwa vitisho, kukamata au kuwafanyia vitendo vya ukandamizaji, bali ni kuhakikisha sheria na taratibu zinafuatwa katika kuendesha nchi.
Akizungumza leo Novemba 9, 2026, kanisani katika ibada ya kuuaga mwili wa mzee Alute Mughwai Lissu, Heche amesema anafahamu familia inapitia maumivu makubwa kutokana na hali inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, pamoja na msiba wa kuondokewa na Mzee Alute Mughwai Lissu.
Amesema pamoja na changamoto hizo, chama kitaendelea kusimamia na kusema kile kinachoamini ni sahihi, akisisitiza kuwa wajibu wa viongozi ni kuzungumza kwa maslahi ya wananchi na kuhakikisha nchi inaendeshwa kwa kufuata sheria na utaratibu.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Wilaya ya Ikungi, Mkoa wa Singida, ambako mwili wa marehemu Wakili Alute Lisu unatarajiwa kuzikwa kesho, Novemba 10, 2026.
Jambo TV tupo eneo hili kwa ajili ya kukuletea taarifa zote kuhusu msiba wa marehemu Wakili Alute Lissu.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Akisoma barua yenye ujumbe wa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Tundu Lissu juu ya kaka yake, marehemu mzee Alute Mughwai Lissu, mmoja wa wanafamilia amesema kuwa Alute enzi za uhai wake alikuwa mtu aliyesimamia haki, asiyependa rushwa, alikuwa mkweli na hakujipendekeza kwa watawala kwa lengo la kupata maslahi binafsi.
Ujumbe huo umeeleza kuwa Alute alikuwa jasiri katika kusimamia misingi aliyoamini, huku akisisitiza ukweli na haki bila kujali mazingira wala maslahi aliyoweza kuyapata.
Ujumbe huo umesomwa leo Novemba 9, 2026, katika ibada ya kuaga mwili wa Mzee Alute Mughwai Lissu inayoendelea katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Theresa jijini Arusha.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Wakati jamii ikiendelea kukabiliwa na changamoto mbalimbali za kijamii, zikiwemo vitendo vya ukatili na madai ya kuwepo kwa mahusiano ya jinsi moja, viongozi wa kimila pamoja na wawakilishi wa wananchi wilayani Nzega mkoani Tabora wamepaza sauti, wakitaka familia na serikali kuimarisha juhudi za kulinda maadili na misingi ya Kitanzania.
Wito huo umetolewa Novemba 9, 2026, katika hafla ya ufunguzi wa Ofisi ya Mtemi wa Jadi Mwakalundi, ambapo viongozi hao, akiwemo Mbunge wa Jimbo la Bukene, John Luhende na mkuu wa matambiko, Maganga Ngeleja wamewataka wazazi kutimiza wajibu wao katika malezi, huku wakiomba serikali kuendelea kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa sheria ili kukabiliana na vitendo vinavyokiuka maadili ya jamii.
Wamesisitiza kuwa ni muhimu changamoto hizo kudhibitiwa mapema kabla hazijaenea zaidi, wakieleza kuwa malezi bora na ushirikiano wa jamii ni nguzo muhimu katika kujenga kizazi chenye maadili mema, uzalendo na heshima kwa mila na desturi za Kitanzania.
Aidha, Mbunge wa Jimbo la Bukene, John Luhende ameahidi kuendelea kushirikiana na viongozi wa kimila katika kuhifadhi maeneo ya urithi wa jadi, akibainisha kuwa hatua hiyo itasaidia kulinda historia, kudumisha mila na desturi pamoja na kuhakikisha urithi huo unarithiwa na vizazi vijavyo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, CP Salum Hamduni, ameitaja imani potofu kuwa ni miongoni mwa changamoto inayokwamisha utekelezaji wa kampeni ya chanjo na utambuzi wa mifugo katika awamu ya kwanza mkoani humo.
Akizungumza leo na waandishi wa habari wakati akizindua awamu ya pili ya kampeni hiyo kimkoa, CP Hamduni amesema baadhi ya wafugaji wamekuwa wakihofia kuchanja mifugo yao wakiamini kuwa chanjo zinaweza kusababisha vifo vya mifugo hali inayochangia kutoshiriki kikamilifu katika zoezi hilo.
"Najua katika kutekeleza kampeni hii awamu ya kwanza zilijitokeza changamoto ikiwemo ya wafugaji kutokujitokeza kwa wakati, uwepo wa gharama na imani potofu kwamba ukichanja mifugo kunaweza kusababisha mifugo kufa," amesema
CP Hamduni amepiga marufuku kwa wataalamu au mtu yeyote kutoza wafugaji gharama zinazozidi viwango vilivyowekwa na Serikali isipokuwa kwa chanjo ambazo hazijajumuishwa katika ruzuku ya Serikali.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI PICHA:
Leo tarehe 9 Novemba, 2026 Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, John Heche akiwa nyumbani kwa marehemu Alute Simion Mugwai, ndugu wa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa mkoani Arusha ambako amesaini kitabu cha maombolezo na kuwapa pole familia ya Lissu. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
"Nenda kwenye point, usizungukezunguke. Usitume waraka kutuambia kitu ambacho kingeweza kusemwa kwa sentensi mbili"
Hayo ni baadhi ya maoni ya watangazaji wa kipindi cha Jambo Asubuhi kuhusu Gen Z. Lakini Gen Z wenyewe mnasemaje? Kwanini hampendi maelezo mengi? Fungukeni hapo chini Wakuu 😂🔥
Fuatilia kipindi cha Jambo Asubuhi kupitia Youtube channel yetu kila siku ya Jumatatu hadi Ijumaa, kuanzia saa 3 hadi 5 asubuhiThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Watu 21 wamefariki dunia na wengine watano kujeruhiwa katika ajali ya basi la abiria la kampuni ya 'Maokoto Bus Services' kugongana na lori la mizigo eneo la Masumbo, kwenye barabara kuu ya Iringa–Mbeya.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, SACP Allan Bukumbi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo akisema waliofariki ni wanaume 10, wanawake tisa na watoto wawili huku uzembe wa dereva ukitajwa kama chanzo cha ajali hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa za awali, ajali hiyo imetokea wakati basi hilo lilipokuwa likisafiri kutoka Kijiji cha Wasa, Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, kuelekea Iringa Mjini.
Jambo TV itaendelea kuwajulisha kadri taarifa rasmi zitakavyopatikana.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Msafara uliobeba jeneza lenye mwili wa marehemu Mzee Alute Mughwai Lissu umeondoka nyumbani kwake, eneo la Fire jijini Arusha, kuelekea Kanisa la Mtakatifu Theresa, ambako ibada ya kumuaga inatarajiwa kufanyika.
Baada ya ibada hiyo, mwili wa marehemu utasafirishwa kwenda Mahambe, mkoani Singida, kwa ajili ya mazishi yanayotarajiwa kufanyika kesho, Novemba 10, 2026.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Imeelezwa kuwa Dunia iko katika njia ya kuelekea kuwa na mwaka wenye joto kali zaidi kuwahi kurekodiwa, huku wanasayansi wakihusisha hali hiyo na mabadiliko ya tabianchi pamoja na athari za hali ya hewa ya El Niño.
Taasisi huru ya utafiti ya Marekani, Berkeley Earth imeeleza leo Novemba 9, 2026 kuwa ina uhakika kwa asilimia 95 kwamba mwaka 2026 utapita rekodi ya joto iliyowekwa mwaka 2024. Onyo hili linatolewa wakati viongozi wa dunia na wapatanishi wakikusanyika mjini Antalya, Uturuki, kwa ajili ya ufunguzi wa mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi (COP31).
Hata hivyo athari hizo zinazotajwa zimeshaanza kujidhihirisha kwa kasi katika miezi ya hivi karibuni sehemu mbalimbali za dunia. Nchi nyingi zimejikuta zikikabiliana na majanga makubwa ya asili, ikiwemo mioto mikubwa ya nyikani iliyoteketeza maeneo ya Ulaya Magharibi hadi Indonesia, pamoja na kuanguka ghafla kwa barafu nchini Nepal kulikosababisha vifo vya zaidi ya watu 1,000. Aidha, huduma ya hali ya hewa ya Umoja wa Ulaya (Copernicus) imethibitisha kuwa mwezi Oktoba 2026 ndio uliokuwa mwezi wenye joto kali zaidi kuwahi kushuhudiwa tangu rekodi zianze kuwekwa.
Kwa upande wake, Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) limetoa ripoti yake likitabiri kuwa mwaka 2026 utakuwa miongoni mwa miaka minne yenye joto zaidi kuwahi kurekodiwa. Katibu Mkuu wa WMO, Celeste Saulo, ameonya kuwa hakutakuwa na nafuu mwaka 2027 kwasababu hali ya El Niño yenye nguvu isiyo ya kawaida itaendelea kutoa joto lililofyonzwa baharini na kusukuma halijoto ya dunia juu zaidi.
Kichocheo kikuu cha kupanda huku kwa halijoto ni kuongezeka kwa mkusanyiko wa gesi ya kabonidioksidi angani kunakotokana na uchomaji wa mafuta ya visukuku (vyanzo vya nishati vinavyotokana na mabaki ya mimea, wanyama, bakteria, na viumbe vya baharini).
Wanasayansi wanaonya kuwa dunia kwa sasa inaelekea kufikia ongezeko la nyuzi joto 2.8 ifikapo mwisho wa karne hii, kiwango ambacho kinavuka kwa mbali lengo la nyuzi joto 1.5 lililowekwa chini ya Mkataba wa Paris. Hali hii tayari imesababisha viongozi, akiwemo waziri mmoja nchini Uingereza, kuwataka wananchi na wafanyabiashara kujiandaa kwa dharura za hali ya hewa na usumbufu wa upatikanaji wa chakula.
Katika mkutano huo wa wiki mbili wa COP31, mkuu wa hali ya hewa wa Umoja wa Mataifa, Simon Stiell, amezihimiza serikali kuchukua hatua za haraka kwani joto kali tayari linaigharimu dunia kiuchumi na kijamii. Ingawa mikutano iliyopita ilijikita zaidi katika kupunguza uzalishaji wa hewa chafu, mataifa mengi sasa yanalazimika kutafuta mbinu za kuzoea mabadiliko haya ya hali ya hewa ambayo hayaepukiki.
Msimamo huo wa Umoja wa Ulaya unatajwa kupingana na mataifa yanayozalisha mafuta na gesi kama Saudi Arabia na Urusi, ambayo yanapigania matumizi ya gesi kama nishati mbadala ya muda mfupi badala ya makaa ya mawe. Huku mivutano hiyo ikiendelea, Katibu Mkuu wa WMO amesisitiza kuwa ukosefu wa makubaliano ya haraka baina ya mataifa ndio unaozidisha ukubwa wa majanga ya hali ya hewa yanayoikumba dunia hivi sasa. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Heche, leo Novemba 9, 2026 akiwasili nyumbani kwa marehemu Alute Mughwai, kaka yake Tundu Lissu, aliyefariki Novemba 1, 2026This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mjadala umeibuka juu ya kauli ya Katibu wa Halmashauri Kuu(NEC) wa Chama cha Mapinduzi(CCM) Kenani Kihongosi ambaye amedai kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo @ChademaTZ2 Tundu Lissu amekuwa akiomba kufanya maridhiano mara kadhaa na kuwa amefika mbali na kuanza kuandika barua ambazo Makamu Mwenyekiti wa chama hicho John Heche amekuwa akizichana.
Kauli hii inakuja ikiwa mara kadhaa Lissu amekuwa akisisitiza msimamo wake kuww hatopiga magoti huku chama chake kikisema hakitakubali kufanya maridhiano kama Lissu hajaachiwa na aongoze mwenyewe hayo maridhiano.
Godwin Mawanja anasema kauli ya Kenani inaweza msababishia wakati mwingine asiaminike.
Upi mtazamo wako?This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
BREAKING NEWS:
Watu kadhaa wanahofiwa kufariki dunia na wengine kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha basi la abiria la kampuni ya Maokoto Bus Services na lori la mizigo katika eneo la Masumbo, kwenye barabara kuu ya Iringa–Mbeya.
Inadaiwa kuwa ajali hiyo imesababishwa na hitilafu katika mfumo wa breki wa basi hilo, hali iliyomfanya dereva kushindwa kulidhibiti na kusababisha kugongana na lori hilo.
Mashuhuda wanasema basi hilo lilikuwa likitoka Kijiji cha Wasa, Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, kuelekea Iringa Mjini wakati ajali hiyo ilipotokea.
Taarifa zaidi kuhusu ajali hiyo na hatua zinazochukuliwa na mamlaka husika zinatarajiwa kutolewa kadri uchunguzi na taarifa rasmi zitakavyokamilika.
Jambo TV inaendelea kufuatilia tukio hilo na itawaletea taarifa zaidi kadri zitakavyopatikana. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Hali ya hofu, taharuki, na sintofahamu imetawala miongoni mwa wananchi wa Kijiji cha Igongwe, kilichopo Kata ya Sitalike, Halmashauri ya Nsimbo Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi, kufuatia kile walichokieleza kuwa ni kuzorota kwa usalama na kutokea kwa mauaji ya kikatili ya mkulima Seni Kibiriti (58) yanayohusishwa na mgogoro wa muda mrefu wa kugombea mbuga za kilimo cha mpunga. Tukio hilo limetokea kufuatia migawanyiko ya makundi mawili ya wananchi wanaogombania umiliki wa eneo hilo kupitia vyombo vya sheria.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Igongwe, Bw. Mayala Nkuba Mandilindi, ameeleza kuwa hali ya usalama ni tete mno kwani yeye mwenyewe amelazimika kukimbilia porini kujificha baada ya kutishiwa maisha na kikundi cha wakulima wapatao 90 wanaopinga uamuzi wa mahakama uliorejesha umiliki wa eneo hilo kwa umma, licha ya maelekezo ya Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, ya kuwataka wananchi waendelee na kilimo huku ulinzi ukiimarishwa.
Kufuatia kifo cha Seni Kibiriti aliyevamiwa na kuuawa shambani kwake, wananchi walioghadhabishwa walichukua uamuzi wa kugoma kumzika na badala yake kuuchukua mwili wake ukiwa kwenye jeneza na kuuacha katikati ya barabara kuu, hatua iliyosababisha usafiri kusimama.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi lilichukua hatua za haraka za kutuliza ghasia hizo na kufanikiwa kuondoa vizuizi, ikiwemo jeneza hilo, katika eneo la Kijiji cha Sitalike. Katika operesheni hiyo iliyofanyika Novemba 6, 2026, Jeshi la Polisi limewakamata watu 15 wanaodaiwa kuhusika na kitendo cha kufunga barabara hiyo kuu ya Mpanda Sumbawanga, huku msako mkali ukiendelea kuwasaka wahusika wote walioshiriki katika mauaji ya marehemu Seni Kibiriti ili wafikishwe mbele ya vyombo vya sheria.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Aliyekuwa msaidizi wa Tundu Lissu, David Djumbe, amesema Lissu licha ya kuwa Kiongozi wa Chama Kikuu cha Upinzani nchini, CHADEMA, aliheshimu msimamo wa kisiasa wa Kaka yake, Marehemu Alute Mughwai, aliyekuwa Mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Djumbe amesema tofauti zao za kisiasa hazikuathiri uhusiano wao wao, akieleza kuwa ndugu hao hawakuwahi kutofautiana kutokana na misimamo yao ya kisiasa
Amesema Lissu alitambua na kuheshimu haki ya Kaka yake kuwa na msimamo tofauti wa kisiasa, licha ya wao kuwa katika vyama vinavyotofautiana.
Djumbe ameyasema hayo leo, Novemba 9, 2026, katika mahojiano ya simu kupitia kipindi cha Jambo Asubuhi kinachorushwa na Jambo TV kila Jumatatu hadi Ijumaa, kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 5:00 asubuhi.
Alute Mughwai alifariki dunia Novemba 1, 2026, katika Hospitali ya Selian mkoani Arusha, alipokuwa akipatiwa matibabu.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri Kivuli wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi katika Baraza la Mawaziri Kivuli la ACT Wazalendo, Hussein Kalyango amewashukia viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kile alichokieleza kuwa ni kuwatelekeza wananchi katika huduma za msingi za afya, pembejeo za kilimo, na masoko ya mazao yao.
Kalyango amebainisha hayo mwishoni mwa wiki alipokuwa akizungumza na wananchi katika Kijiji cha Kigogo, Kata ya Itaba, Jimbo la Muhambwe, Wilaya ya Kibondo, Mkoa wa Kigoma.
Akiwahutubia wananchi hao, Kalyango ameonesha kushangazwa na hatua ya Kata ya Itaba pamoja na Kata ya Kumsenga kukosa vituo vya afya kinyume na sera ya taifa inayotaka kila kata kuwa na kituo cha afya, licha ya kwamba mbunge wa jimbo hilo, Dkt. Florence George Samizi ni Naibu Waziri wa Afya.
Ameeleza kuwa hali hiyo inawatesa akina mama wajawazito wanaolazimika kutaabika kwa gharama na usafiri wa pikipiki kwenda kutafuta huduma katika vituo vya mbali kama Mabamba
Katika hatua nyingine, Kalyango amedai kuwa ingawa zao la mihogo linalolimwa eneo hilo lina fursa ya soko nje ya nchi, serikali imeshindwa kuwawezesha wakulima zana za kisasa wala kujenga barabara za kufikisha mazao masokoni, na kuziacha familia zikiendelea kulima kwa jembe la mkono na kubaki kwenye umaskini.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Bandari za Tanganyika zimevuka lengo la kuhudumia shehena katika kipindi cha robo ya kwanza ya Mwaka wa Fedha 2026/2027, baada ya kuhudumia jumla ya tani 236,000 kuanzia mwezi Julai hadi Septemba 2026, sawa na ongezeko la tani 19,000 au asilimia 8.76 ikilinganishwa na tani 217,000 zilizohudumiwa katika kipindi kama hicho mwaka wa fedha 2025/2026.
Akizungumza kuhusu mafanikio hayo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TPA Bw. Plasduce Mbossa, Meneja wa Bandari za Ziwa Tanganyika, Bi. Joyceline Sima amesema ongezeko hilo ni matokeo ya uwekezaji mkubwa unaotekelezwa na Serikali katika kuboresha na kuimarisha miundombinu ya Bandari za Ziwa Tanganyika.
Ameeleza kuwa maboresho hayo yamekuwa chachu ya kuongeza ufanisi katika shughuli za upokeaji na uhudumiaji wa shehena, huku yakiimarisha uwezo wa bandari kuhudumia wateja na wafanyabiashara kwa ufanisi zaidi.
Bi. Sima amesisitiza kuwa uwekezaji unaoendelea katika miundombinu ya bandari una mchango mkubwa katika kuongeza uwezo wa kiutendaji, kukuza shughuli za biashara na kuimarisha mchango wa Bandari ya Kigoma katika kukuza uchumi na biashara za ndani na nchi jirani.
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) inaendelea kuboresha miundombinu na huduma za bandari nchini kwa lengo la kuongeza ufanisi, ushindani na kuchochea ukuaji wa uchumi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI PICHA:
Kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo, Dorothy Semu, ametembelea miradi mbalimbali ya maendeleo katika Kata ya Kumsenga, ikiwemo miradi ya maji, elimu na afya, inayolenga kuboresha huduma za kijamii kwa wananchi wa eneo hilo.
Kabla ya kuanza ziara hiyo, Novemba 7, 2026 Semu alifanya kikao cha ndani na viongozi wa kata, kisha kuelekea kukagua miradi iliyotekelezwa chini ya uongozi wa Diwani wa Kata ya Kumsenga.
Miongoni mwa miradi aliyokagua ni mradi wa maji pamoja na ujenzi wa vyoo vya walimu na wanafunzi katika Shule ya Sekondari ya Kumsenga, unaolenga kuboresha upatikanaji wa maji, usafi na mazingira ya kujifunzia.
Aidha, alitembelea ujenzi wa Zahanati ya Kumsenga, ambao bado unaendelea na umefikia hatua za mwisho. Zahanati hiyo inatarajiwa kuongeza upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi wa kata hiyo itakapokamilika.
Katika ziara hiyo, Semu pia alikagua Skimu ya Maji Kumsenga–Kukinama pamoja na chanzo chake cha maji cha Mto Linda, ili kujionea hatua za utekelezaji na mchango wa mradi huo katika kukabiliana na changamoto ya upatikanaji wa maji safi kwa wananchi. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI PICHA:
Kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo, Dorothy Semu, ametembelea miradi mbalimbali ya maendeleo katika Kata ya Kumsenga, ikiwemo miradi ya maji, elimu na afya, inayolenga kuboresha huduma za kijamii kwa wananchi wa eneo hilo.
Kabla ya kuanza ziara hiyo, Novemba 7, 2026 Semu alifanya kikao cha ndani na viongozi wa kata, kisha kuelekea kukagua miradi iliyotekelezwa chini ya uongozi wa Diwani wa Kata ya Kumsenga.
Miongoni mwa miradi aliyokagua ni mradi wa maji pamoja na ujenzi wa vyoo vya walimu na wanafunzi katika Shule ya Sekondari ya Kumsenga, unaolenga kuboresha upatikanaji wa maji, usafi na mazingira ya kujifunzia.
Aidha, alitembelea ujenzi wa Zahanati ya Kumsenga, ambao bado unaendelea na umefikia hatua za mwisho. Zahanati hiyo inatarajiwa kuongeza upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi wa kata hiyo itakapokamilika.
Katika ziara hiyo, Semu pia alikagua Skimu ya Maji Kumsenga–Kukinama pamoja na chanzo chake cha maji cha Mto Linda, ili kujionea hatua za utekelezaji na mchango wa mradi huo katika kukabiliana na changamoto ya upatikanaji wa maji safi kwa wananchi. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo, Dorothy Semu, amesema hofu ya vitisho, utekaji na kupotea kwa watu imeendelea kuwafanya baadhi ya wananchi kuogopa kushiriki katika shughuli za kisiasa, kuzungumzia masuala ya uchaguzi na kuhoji wakihofia usalama wao
Akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Bitulana, Novemba 7, 2026, Semu alisema hali hiyo imejenga mazingira ya hofu miongoni mwa vijana, wazee na wanawake, ambao wamekuwa wakihofia usalama wao wanapotoa maoni kuhusu masuala ya kisiasa.
Alisema baadhi ya Wananchi wamekuwa wakishindwa kuzungumza kwa uhuru kwa sababu hawajui nani anaweza kuwafuata nyumbani nyakati za usiku
Katika hotuba yake, Semu alieleza kuwa viongozi wa upinzani, wanasiasa wanaopigania mabadiliko pamoja na wanaharakati wamekuwa wakikabiliwa na vitisho, huku baadhi yao wakidaiwa kutekwa na kupotea.
Alitolea mfano wa Mzee Kangue wa Muhambwe, ambaye alisema alitekwa na watu wasiojulikana miaka 7 iliyopita na hadi sasa hajulikani alipo.
Semu alisema hali hiyo ni ukandamizaji wa haki za wananchi na demokrasia, akisisitiza kuwa taifa linapaswa kujengwa katika misingi inayowapa wananchi uhuru wa kuhoji, kuuliza maswali na kutoa maoni yao bila hofu.
Aliongeza kuwa wananchi wa Bitulana wanapaswa kujisikia salama, kulindwa na kuwa na uhuru wa kushiriki katika shughuli za kisiasa pamoja na kushirikiana katika maendeleo ya nchi.
Kabla ya mkutano huo wa hadhara, Semu alikutana na viongozi wa chama ngazi ya kata na kufanya kikao cha ndani.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Padri Lawrance Lukumay wa Parokia ya Mtakatifu Theresia amesema katika kipindi cha msiba ni muhimu familia na waumini kumtegemea Mungu, huku wakishikilia haki, amani na uaminifu katika maisha yao.
Akizungumza leo Novemba 8, 2026, wakati wa ibada fupi ya kumuaga marehemu Mzee Alute Mughwai Lissu iliyofanyika nyumbani kwake jijini Arusha, Padri Lukumay amesema marehemu aliendelea kutamani kuona haki ikitendeka, amani ikiwepo na watu wakifuata taratibu hata wakati afya yake ilipokuwa ikidhoofika.
Amesema marehemu alitumia maisha yake kutumikia jamii kwa uaminifu, akiwataka waumini kutumia vizuri akili na uwezo waliyopewa na Mungu katika kulitumikia taifa na jamii kwa haki.
Padri Lukumay pia ametoa pole kwa familia ya marehemu, akieleza kwa namna ya pekee maumivu ya Tundu Lissu, mdogo wa marehemu, ambaye ameshindwa kushiriki mazishi ya ndugu yake kutokana na kuwa gerezani.
Amesema Tundu Lissu angependa kuwepo katika ibada hiyo na kumsindikiza ndugu yake, akimwomba Mungu ampe faraja, nguvu na kumlinda katika kipindi hiki kigumu, huku akiomba pia Mungu aifariji familia yote.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mawakili mbalimbali wameonekana wakiwa na nyuso za huzuni huku wakiubeba mwili wa Wakili Alute Mughwai Lissu ndani ya jeneza, aliyefariki dunia usiku wa Novemba 1, 2026.
Ibada fupi ya kumuaga marehemu Alute inaendelea nyumbani kwake jijini Arusha, ikihudhuriwa na viongozi mbalimbali, ndugu, jamaa na marafiki.
mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa kesho kwenda kijiji cha Mahambe, mkoani Singida, ambako anatarajiwa kuzikwa Novemba 10, 2026.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA) Taifa, Wakili Deogratius Mahinyila, amejibu kauli ya Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Kenani Kihongosi, kuhusu maridhiano ya kisiasa, akieleza kuwa madai kwamba Tundu Lissu amekuwa akiandika barua za kuomba maridhiano ni propaganda zinazokinzana na ukweli uliowekwa wazi na familia.
Mahinyila amebainisha hayo Novemba 8, 2026, alipofika nyumbani kwa kaka wa Tundu Lissu, marehemu Mzee Alute Mughwai Lissu jijini Arusha kutoa pole na kuzungumza na wanahabari.
Akijibu kauli iliyotolewa Novemba 7, 2026 mkoani Morogoro na Kihongosi aliyedai kuwa CCM inaumizwa na hukumu ya Lissu na kwamba Lissu amekuwa akiandika barua za maridhiano huku Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Heche ‘akizichoma moto’, Mahinyila amesema maelezo hayo yanapingana na ukweli uliowekwa wazi na Mzee Alute kabla ya kifo chake.
Ameeleza kuwa Mzee Alute alieleza jinsi kiongozi mmoja mkubwa alivyokutana na familia na kuwashawishi waandike barua, lakini familia na CHADEMA walikataa ushawishi huo.
Mahinyila amezidi kuhoji ni barua zipi zinazodaiwa kuandikwa na Lissu, akisisitiza kuwa kiongozi huyo alikuwa akieleza wazi mahakamani kuwa hana hatia na hataki kuomba huruma au kupiga magoti ili kupata haki.
Katika hatua nyingine, Mahinyila amesema kifo cha Mzee Alute kinapaswa kuwa fundisho kwa Watanzania na viongozi wa CCM kuwa ukweli hauna chama na kudai haki au demokrasia hakupaswi kuhusishwa na CHADEMA pekee. Amesisitiza kuwa BAVICHA itaendelea kuwa imara na kusimamia haki na demokrasia bila kutetereka.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Fedha, Balozi Khamis Mussa Omar, ameanza ziara ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa kimkakati wa Reli ya Kisasa ya SGR katika vipande cha tatu ambacho ni kutoka Makutupora–Tabora, cha nne Tabora–Isaka na cha tano Isaka–Mwanza, akiambatana na Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa, amesema ameridhishwa na maendeleo ya kazi katika kipande cha tano na kueleza kuwa Serikali itaongeza nguvu katika usimamizi wa vipande vya tatu na nne ili kuhakikisha mradi unakamilika kwa wakati.
Amesisitiza kuwa wakandarasi wanapaswa kufanya kazi usiku na mchana, wakati wa jua na mvua, huku akieleza kuwa changamoto zilizokuwa zikikwamisha utekelezaji wa mradi huo zinaendelea kutafutiwa ufumbuzi.
Kwa upande wake, Waziri wa Fedha, Balozi Khamis Mussa Omar, amesema Serikali itaendelea kuhakikisha upatikanaji wa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo na kulipa wakandarasi kwa wakati ili kuongeza kasi ya ujenzi.
Ameeleza kuwa uwekezaji wa SGR ni sehemu ya miradi mikubwa ya kimkakati inayolenga kuimarisha miundombinu ya usafiri na usafirishaji nchini.
Aidha, viongozi hao wameeleza umuhimu wa ushirikiano kati ya Wizara ya Fedha na Wizara ya Uchukuzi katika kuhakikisha mradi huo unakamilika.
Reli ya SGR inatarajiwa kuwa na mtandao wa takribani kilomita 2,300 nchini Tanzania, ikiwa ni sehemu ya uwekezaji mkubwa wa miundombinu ya usafiri unaolenga kuchochea shughuli za kiuchumi, biashara na usafirishaji wa abiria na mizigo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Wakili Paul Kisabo amesema hakuna msingi wa kumhukumu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, kwa kosa ambalo kwa maelezo yake hakushtakiwa nalo wala kupewa nafasi ya kujitetea, akisisitiza kuwa mahakama ilisema maneno aliyoyatoa yalikuwa ya kisiasa na hayakufikia kiwango cha uhaini na kwamba kosa la uhaini halina kosa dogo na wala halihusiani na uchochezi.
Akizungumza leo Novemba 8, 2026, alipofika msibani nyumbani kwa Mzee Alute Mughwai Lissu jijini Arusha.
Amesema hatua hiyo inaweza kuathiri imani ya wananchi kwa mahakama, akisisitiza kuwa kwa mtazamo wao, mwanasiasa anapaswa kuwa na uhuru wa kueleza misimamo na kauli za kisiasa bila kuhusishwa na kosa ambalo hakushtakiwa nalo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mmoja wa mawakili wanaomtetea Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, Wakili Paul Kisabo, amesema tayari wameanza mchakato wa kukata rufaa dhidi ya hukumu iliyomtia hatiani Lissu kwa kosa la uchochezi na kumhukumu kifungo cha miaka minne jela.
Akizungumza leo Novemba 8, 2026 alipofika msibani nyumbani kwa Mzee Alute Mughwai Lissu, Kisabo amesema kwa sasa wanatarajia kupata nakala ya hukumu pamoja na mwenendo wa shauri ili kuandaa sababu za rufaa.
Kisabo amesema Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Rugemeleza Nshala, tayari amewasilisha taarifa ya nia ya kukata rufaa, hatua ambayo imefungua mchakato wa kupeleka shauri hilo Mahakama ya Rufaa.
Amesema mawakili wanaamini kuna hoja za msingi za kupinga hukumu hiyo, akisisitiza kuwa Lissu alishtakiwa kwa uhaini lakini Mahakama ilimkuta hana hatia ya kosa hilo, huku akidai hakujitetea dhidi ya shtaka la uchochezi.
Kisabo ameongeza kuwa wanaamini mchakato wa rufaa utasaidia kupata haki kwa Lissu, huku wakitarajia kuwa ataendelea na mapambano yake ya kudai haki na Katiba mpya nchini. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mchambuzi wa masuala ya siasa, Ezekiel Kamwaga, ameeleza kuwa vyama vya siasa na Watanzania wana mengi ya kujifunza kutoka kwenye mabadiliko na matukio ya siasa za kimataifa ikiwemo uchaguzi wa Marekani na Brazil katika namna ya kuendesha siasa, kuhamasisha wananchi, na kujiandaa na mabadiliko ya kura za mbeleni.
Kamwaga, ambaye amekuwa akifuatilia na kuchambua siasa kwa takriban miaka 20, amebainisha kuwa tofauti kuu kati ya nchi zilizoendelea na nchi za Afrika ni kwamba katika nchi zilizoendelea kama Uingereza na Marekani, vyama vya siasa vimejengwa katika misingi na itikadi zilizowazi wakati barani Afrika tofauti kuu imebaki kuwa kati ya chama kilicho madarakani na vile vilivyopo nje ya madaraka. Aidha, ameeleza kuwa fujo na vurugu haziwasaidii wapinzani bali zinakisaidia chama tawala, kujiandaa na uchaguzi wa 2030 na mabadiliko ya idadi ya watu, na namna ya kuhamasisha watu.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Watanzania wakazi wa Mkoa wa Geita wametakiwa kuendelea kulinda na kudumisha amani na utulivu uliopo nchini kwa kujiepusha na vitendo vyote vinavyoweza kusababisha uvunjifu wa amani na kuhatarisha mshikamano wa kitaifa.
Wito huo umetolewa Novemba 7, 2026 na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa na Mlezi wa CCM Mkoa wa Geita, Rajab Abdallah, wakati akizungumza na wananchi katika Kata ya Senga mkoani humo. Amesema Watanzania wana kila sababu ya kujivunia amani iliyopo nchini.
Amesema amani ni msingi muhimu wa maendeleo ya taifa, hivyo kila mwananchi ana wajibu wa kuilinda kwa vitendo, akisisitiza kuwa tofauti za kimtazamo na kisiasa hazipaswi kuwa chanzo cha migogoro, chuki au vitendo vinavyoweza kuvuruga utulivu wa nchi.
Aidha, amewataka wananchi kuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha umoja, mshikamano na kuheshimiana ili kuhakikisha amani inaendelea kudumu kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijachoThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Takribani wananchi 1,000 wa Kitongoji cha Saburi, Kata ya Makuyuni, Wilaya ya Monduli mkoani Arusha, wameiomba Serikali kupitia Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuingilia kati mgogoro wa ardhi kati yao na mwekezaji, wakieleza hofu ya kupoteza makazi yao baada ya kutoridhishwa na uamuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Wakizungumza na waandishi wa habari Novemba 6, 2026, wananchi hao wamesema hawajaridhishwa na uamuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Amos Makalla, wa kuwapangia ekari 100 pekee, wakidai eneo hilo halitoshelezi mahitaji ya wananchi ambao wamekuwa wakiishi katika eneo hilo kwa zaidi ya miaka 30.
Akizungumza kwa niaba ya wananchi hao, Mariam Faustine amesema mgogoro huo ulifikia hatua kubwa Oktoba 2 mwaka huu, baada ya watu wanaodaiwa kutofahamika kufika katika eneo hilo wakiwa na magreda na silaha, wakidaiwa kuwa na nia ya kubomoa nyumba za wananchi.
Aidha, wananchi hao wameeleza kutoridhishwa na maelekezo ya kusitisha shughuli za maendeleo katika eneo hilo, wakisema wamekuwa wakiishi na kuendesha shughuli zao kwa muda mrefu na wanaamini wana haki ya kisheria ya kumiliki ardhi hiyo.
Kwa upande wake, Sara Alaisi amesema uamuzi wa kuwapangia ekari 100 haujakidhi matarajio yao, huku akimuomba Rais Samia kuingilia kati ili kuhakikisha wanapata suluhisho wanaloamini kuwa ni la haki.
Awali, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Amos Makalla, alimtaka Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Kamati ya Ulinzi na Usalama pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha maamuzi yaliyotolewa kuhusu mgogoro huo yanatekelezwa.
Kutokana na hali hiyo, wananchi hao wameitaka Serikali kupitia upya suala hilo, wakisisitiza umuhimu wa kulindwa kwa makazi yao na kupatikana kwa suluhisho la kudumu litakalozingatia haki za pande zote zinazohusika.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Vijana wanaojishughulisha na uchotaji na uuzaji wa maji katika chanzo cha maji cha Lwenge, Kata ya Kalangalala, Manispaa ya Geita, wameibua malalamiko dhidi ya mwekezaji wa uchotaji maji katika eneo hilo, wakimtuhumu kuhamishia shughuli zake katika sehemu inayotumiwa na wananchi baada ya kupungua kwa kiwango cha maji katika eneo alilotengewa.
Wakizungumza katika chanzo hicho cha maji, wananchi hao wamesema awali mwekezaji huyo alikuwa na eneo maalumu aliloruhusiwa kuchota maji, lakini baada ya maji kupungua katika eneo hilo, alianza kutumia chanzo kinachotegemewa na wananchi kwa matumizi yao ya kila siku.
Wamesema hatua hiyo imeongeza ushindani wa upatikanaji wa maji, hali inayowaathiri katika shughuli zao za uchotaji na uuzaji wa maji na kuibua hofu ya kuendelea kudhoofika kwa upatikanaji wa huduma hiyo kwa jamii.
Kwa upande wake, mwekezaji huyo, Shija Joseph, amekiri kuchota maji katika chanzo hicho, akieleza kuwa hatua hiyo imesababishwa na kupungua kwa kiwango cha maji katika eneo alilotengewa, hususan katika kipindi hiki ambacho mvua zimechelewa kunyesha.
Akizungumzia malalamiko hayo, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Lwenge, Dismas Joseph, amemtaka mwekezaji huyo kusitisha mara moja uchotaji maji katika eneo linalotumiwa na wananchi, akisisitiza umuhimu wa kulinda chanzo hicho ili wananchi waendelee kukipata kwa matumizi yao ya kila siku.
Wananchi hao wameiomba Serikali na mamlaka zinazohusika kuingilia kati mgogoro huo na kuweka utaratibu utakaosimamia matumizi ya chanzo hicho kwa kuzingatia maslahi ya jamii, huku ukihakikisha shughuli za uchotaji na uuzaji wa maji haziathiri upatikanaji wa huduma hiyo kwa wananchi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
"Naishukuru sana Mahakama imeonyesha ujasiri wa hali ya juu sana na imeonyesha kwamba iko huru katika kutoa uamuzi kama ule kwa sababu ingekuwa ni nchi nyingine uamuzi kama ule usingetolewa"
Ni mtazamo wa Wakili Peter Madeleka @PMadeleka kwenye mahojiano aliyofanya na Jambo TV leo Novemba 7, 2026.
Upi mtazamo wako?This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Wanafunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi (FDC) Sengerema mkoani Mwanza wameiomba Serikali kutatua changamoto ya upungufu wa mabweni, madarasa, uzio na watumishi wakieleza kuwa zimekuwa kikwazo katika ujifunzaji na utoaji mafunzo chuoni hapo.
Akisoma risala leo kwa niaba ya wahitimu kwenye mahafali ya 27 ya chuo hicho, leo Novemba 7, 2026, Enock Emmanuel amesema upungufu wa mabweni, uzio na madarasa umekuwa ukisababisha baadhi ya wanafunzi kukosa muda wa kutosha wa kujisomea huku wengine wakikabiliwa na hatari ya kujiingiza katika makundi yasiyofaa yanayohusishwa na vitendo vya wizi, uvutaji bangi na uhuni.
"Upungufu wa mabweni ya wasichana na wavulana hivyo kupelekea wana chuo kukosa muda wa kusoma wakati wa usiku na baadhi yao kushawishika na makundi mabaya kama vile wizi, uvutaji bangi, uhuni na kushindwa na kuendelea na masomo," amesema
Akiunga mkono hoja hizo Mkuu wa Chuo hicho, George Lubinza ameitaja changamoto ya upungufu wa watumishi wa kada mbalimbali kuwa inakwamisha ufanisi wa utoaji wa mafunzo.
Akisisitiza Katibu wa Wazazi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Sengerema, Jamary Twaibu amemtaka Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema kuzishughulikia changamoto hizo haraka iwezekanavyo.
Akijibu changamoto hizo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Sengerema, Agape Fue ameahidi kuzifanyia kazi huku akiomba ushirikiano katika kuzitatua.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Kenani Kihongosi, ameitaka serikali kuchukua hatua za kisheria dhidi ya mkandarasi anayetekeleza ujenzi wa daraja katika barabara kuu ya Morogoro–Dodoma, mkoani Morogoro, kutokana na kuchelewesha mradi huo unaogharimu zaidi ya shilingi bilioni tano.
Kihongosi ametoa agizo hilo leo Novemba 7, 2026 baada ya kueleza kutoridhishwa na kasi na utendaji wa mkandarasi huyo, kampuni ya Osaka, licha ya hatua mbalimbali zilizochukuliwa na TANROADS pamoja na viongozi wa mkoa na wilaya katika kuhakikisha mradi unakamilika kwa wakati.
Amesisitiza kuwa fedha za mradi huo ni mkopo kutoka Benki ya Dunia ambao serikali inapaswa kuurejesha, hivyo hakuna sababu ya kuruhusu utekelezaji wake kwenda taratibu na kusababisha gharama zaidi kwa taifa
Aidha, ameitaka mamlaka husika kuchunguza utekelezaji wa mkataba na kuchukua hatua zinazostahili, ikiwemo makato na adhabu za zaidi ya shilingi milioni 400 kutokana na kuchelewa kwa kazi, huku akisisitiza fedha za dharura za zaidi ya shilingi milioni 500 zitumike kwa malengo yaliyokusudiwa.
Ameelekeza pia mkandarasi huyo kuwasilisha ratiba ya maandishi inayoonesha muda wa kukamilisha ujenzi wa daraja hilo, akionya kuwa wakandarasi wanaoshindwa kutekeleza majukumu yao kwa viwango vinavyotakiwa hawapaswi kuendelea kupewa miradi mingine ya serikali.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwananchi mmoja aliyejitokeza mbele ya Waziri Mkuu wa Tanzania Dkt. Mwigulu Nchemba, ametoa kilio chake kuhusu kero za huduma za afya, ukosefu wa nidhamu kwa baadhi ya watumishi wa umma, pamoja na madhila mengine aliyoyapata katika maisha yake.
Tukio hilo limetokea leo, Novemba 7, 2026, wakati Dkt. Mwigulu akizungumza na wananchi katika Viwanja vya Polisi Mwandoya, vilivyopo Jimbo la Kisesa, akiwa kwenye ziara ya kikazi mkoani Simiyu.
Akieleza kero yake mbele ya Waziri Mkuu, mwananchi huyo amebainisha kuwa amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa henia kufuatia kupigwa, lakini alipokwenda hospitalini Bariadi kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji baada ya kupewa rufaa kutoka Mwandoya, alikutana na urasimu pamoja na usumbufu kutoka kwa daktari, hivyo kumuomba Waziri Mkuu kufikisha ujumbe kwa Rais ili kurejesha nidhamu miongoni mwa watumishi wa umma.
Mwananchi huyo ameongeza kuwa alivamiwa dukani kwake na kukatwa panga kichwani, na baada ya kufanya jitihada binafsi za kumkamata mtuhumiwa, mtuhumiwa huyo aliachiwa kwa dhamana.
“Baadaye mtuhumiwa akadhaminiwa akawa nje. Nilivyoenda kwa Mkuu wa Wilaya ananiuliza: 'dogo haujafa? Yaani kakesi kadogo unafuatilia?”, ameeleza mwananchi huyo.
Waziri Mkuu amebainisha kuwa ingawa vyombo vya ulinzi na usalama vinafanya kazi nzuri na kulinda amani ya nchi, makosa ya mtu mmojammoja hayapaswi kuchukuliwa kama taswira ya taasisi nzima. Amemwagiza Mkuu wa Mkoa na Jeshi la Polisi kufanya ufuatiliaji wa kina wa tuhuma hizo ili kubaini ukweli wa shambulio hilo na hatua zilizochukuliwa dhidi ya mtuhumiwa aliyeachiwa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
"Tundu Lissu kufungwa imempa heshima kubwa sana, faida kubwa sana kisiasa inamuongezea mtaji mkubwa sana kuaminika na watu, uzoefu wa kidunia unaonyesha kwamba watu ambao huwa wanatoka gerezani mara nyingi wanakuwa Marais, Rais wa Senegal(Bassirou Faye) alikuwa naye ni wakili Lissu pia ni Wakili kwa hiyo labda ni suala la muda"
Hayo amesema Wakili Peter Madeleka katika mahojiano maalumu na Jambo TV leo Jumamosi ya Novemba 7, 2026 alipokuwa akizungumza yaliyotokea kwenye Hukumu kesi ya Lissu kisheria.
Upo mtazamo wako?This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile ameeleza kuwa Mahakama Kuu ya Tanzania imetenda kwa mujibu wa sheria katika kumtia hatiani na kumhukumu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Tundu Antiphas Lissu, kifungo cha miaka minne jela kwa kosa la uchochezi.
Balile ameyasema hayo akizungumzia uamuzi huo wa Mahakama Kuu, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, uliomvua Lissu mashtaka ya uhaini na kumtia hatiani kwa kosa dogo la uchochezi, huku akisisitiza kuwa njia pekee ya kuijenga nchi ni kurejea kwenye meza ya mazungumzo.
“Bado ninaamini mlango wa kuzungumza upo kwamba mheshimiwa Rais anayo nafasi katika hili, hakuna kosa ambalo Rais hawezi kusamehe, hakuna hukumu ambayo rais hawezi kusamehe kwa mujibu wa sheria. Kwahiyo hapa mazungumzo yaendelee kwamba CHADEMA, CCM, Watanzania kwa ujumla tuangalie tunaijengaje nchi yetu, maana nimesema mara kadhaa hata tukipambana kwa kiwango gani mwisho wa siku tutarudi kwenye meza ya mazungumzo”, ameeleza Balile.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI:
Rais wa Paraguay, Santiago Peña, amezuiliwa nyumbani kwake (house arrest) baada ya kung’olewa madarakani na Seneti, kufuatia sakata la benki ya Ueno Bank kushindwa kuendelea na huduma na kusababisha takribani watu milioni tatu kushindwa kupata fedha zao, zikiwemo akiba na mafao ya pensheni.
Peña aliondolewa madarakani baada ya maseneta 44 kati ya 45, wakiwemo baadhi ya wabunge wa chama chake, kupiga kura kumuondoa, huku mbunge mmoja akiwa hayupo. Seneti ilimtuhumu kushindwa kutekeleza wajibu wake na kuhusika katika ukiukwaji wa maadili ya uongozi.
Miongoni mwa tuhuma zilizomkabili ni mgongano wa maslahi, kuingilia usimamizi wa mamlaka za udhibiti wa sekta ya benki, kutumia vibaya fedha za mifuko ya pensheni na kushiriki katika jaribio la kuficha ukweli kuhusu sakata hilo kupitia Benki Kuu.
Tuhuma hizo zinahusishwa pia na ukweli kwamba Peña alikuwa na hisa katika kampuni iliyokuwa inamiliki benki hiyo hadi mwaka 2025. Hata hivyo, amekanusha kuhusika na makosa yoyote.
Kabla ya kung’olewa madarakani, Peña alikuwa amependekeza kujiuzulu Alhamisi, Novemba 5, 2026, lakini Seneti iliamua kuendelea na mchakato wa kumuondoa madarakani.
Baada ya kuondolewa kwake, Makamu wa Rais Pedro Alliana aliapishwa kuwa rais wa mpito hadi mwaka 2028, akiahidi kuhakikisha wananchi walioathiriwa na mgogoro huo wanarejeshewa fedha zao.
Wakati huo huo, sakata hilo limeibua hasira za wananchi na kusababisha maandamano katika maeneo mbalimbali nchini humo, huku maelfu wakitaka kurejeshewa fedha zao. Baadhi ya maandamano yaligeuka kuwa vurugu, polisi wakitumia mabomu ya machozi na maji kuwatawanya waandamanaji.
Kwa mujibu wa mwendesha mashtaka Silvia Margarita Gonzalez Vester, Peña alitarajiwa kuhojiwa Novemba 7, 2026, kuhusu tuhuma za kuvunja uaminifu, kutumia vibaya ushawishi na ubadhirifu wa fedha.
Akizungumzia sakata hilo, Seneta Rafael Filizzola amelielezea kuwa kashfa kubwa zaidi ya rushwa katika historia ya demokrasia ya Paraguay, akisema limeathiri serikali, wananchi na taswira ya taifa. -
Jambo TV
@Jambotv_
Mbunge wa Jimbo la Mtama Nape Nnauye amewashukia wanaharakati na watu wasio wanasiasa kwa kukiingilia "benchi la ufundi" la siasa nchini, akieleza kuwa hatua hiyo imechangia kuharibu utamaduni wa siasa za uvumilivu na kusababisha uadui miongoni mwa wanasiasa.
Nape amebainisha hayo leo, Novemba 7, 2026, akizungumza na Clouds TV ambapo ameeleza kuwa changamoto kubwa iliyopo sasa ni kuwepo kwa watu ambao hawamo kwenye vyama vya siasa wala hawana taaluma hiyo, lakini wamekuwa wakiongoza mijadala na kuendesha siasa kupitia mitandao ya kijamii.
Amedai kuwa wengi wa wanaharakati hao wanatumia jukwaa hilo kutukana na kushinikiza ajenda zao bila kuwa na taarifa kamili au za kutosha kuhusu mambo wanayoyazungumzia.
"Wanaharakati si wanasiasa, hawako na wengi wao inawezekana hata vyama hawana, lakini wanaendesha siasa kwasababu ndio wametawala mitandaoni, wanamtukana huyu, wanamrudisha huyu, na hii ni kwa pande zote wala sio upande mmoja. Kwangu mimi ungeniambia, kama wanasiasa wangeweza…tusiwapuuze lakini tusiwafanye waendeshe siasa," amesema Nape.
Nape amesisitiza kuwa siasa inapaswa kubaki kuwa shughuli ya kijamii inayojengwa juu ya ushindani wa hoja na mitazamo, badala ya kugeuzwa kuwa ugomvi au uadui wa kibinafsi. Amefafanua kuwa kuingiliwa kwa siasa na watu wasio wanasiasa ndiko kulikofikisha nchi mahali ambapo hata wanasiasa waliokuwa wakishirikiana na pengine ‘kupeana lifti’ hapo awali wameanza kutopendana.
"Benchi la ufundi linaingiliwa sana…leo tunaweza kutetereka kwasababu tu kuna wanaharakati au kuna watu wanasema jambo fulani. Kwanza hawana taarifa za kutosha, lakini kwa sababu wana nguvu mahali wanasukuma ajenda, mnajikuta na nyie mmesukumwa na presha ile," ameongeza.
Ameeleza kuwa viongozi na wanasiasa wanapaswa kufanya maamuzi kwa utulivu na kwa kuzingatia taarifa sahihi badala ya kuendeshwa na presha ya wanaharakati.
“Mimi sisemi harakati ni mbaya, ninachosema ni kwamba inapofika kwenye kufanya maamuzi tufanye maamuzi bila hii shinikizo ili tufanye maamuzi sahihi. Mnaweza mkajikuta mmefanya maamuzi kwa sababu ya shinikizo, maamuzi yakatoa matokeo mabaya”, ameeleza Nape. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Wananchi wanaofanya manunuzi katika Soko Kuu la Manispaa ya Mtwara Mikindani wameeleza kukabiliwa na changamoto ya kupanda kwa bei za bidhaa mbalimbali, hali inayotajwa kuchangiwa na ongezeko la gharama za usafirishaji pamoja na upungufu wa baadhi ya mazao yanayozalishwa ndani ya mkoa huo.
Miongoni mwa bidhaa zilizoathiriwa na ongezeko hilo ni vyakula na mbogamboga, huku parachichi moja ikiuzwa kwa hadi Shilingi 4,000, hali inayoongeza mzigo wa gharama kwa wananchi wanaotegemea soko hilo kupata mahitaji yao ya kila siku.
Wafanyabiashara katika soko hilo wameeleza kuwa kupanda kwa bei za mafuta kumeongeza gharama za kusafirisha bidhaa kutoka maeneo ya uzalishaji hadi sokoni, jambo linalochangia kupanda kwa bei kwa walaji.
Wafanyabiashara Zamiru Salim, Salumu Mtungata na Mikidadi Likoti wameongeza kuwa hali hiyo inachangiwa pia na upungufu wa uzalishaji wa baadhi ya mazao ya ndani, yakiwemo maharage, mchele na mbogamboga.
Kwa upande wake, Mjumbe wa Bodi ya Wafanyabiashara Mkoa wa Mtwara, Abdallah Magomba, ameeleza kwa kina sababu zinazochangia mwenendo huo wa bei, akisisitiza umuhimu wa kubaini vyanzo vya changamoto hizo ili kupata suluhu ya kudumu.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Wakili Boniface Mwabukusi, amekosoa uamuzi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, wa kumtia hatiani Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Wakili Tundu Antiphas Lissu kwa kosa la uchochezi kutoka kwenye kosa la uhaini, akidai kuwa mahakama imejipachika majukumu ya ushitaki na upelelezi badala ya kubaki kwenye kiti cha utoaji haki.
Mwabukusi ameyasema hayo akizungumza na televisheni ya mtandao ya Focus News Tanzania Tv 1 mara baada ya hukumu hiyo kutolewa, ambapo amebainisha kuwa Tundu Lissu ameachiwa makosa yote yaliyompeleka mahakamani hapo na badala yake majaji wakatengeneza kosa jipya ambalo halikuwa sehemu ya mashitaka ya msingi.
“Hakuna kosa lolote la Mbinga (Ruvuma) lililohusika na Tundu Lissu mahakamani, hilo ni kosa la majaji watatu waliloliibua wenyewe walipoliibua, wakatafuta ushahidi wao, wakapeleleza wao, wakafanya uchambuzi wao, wakamkuta na hatia wao, wakamhukumu bila kuwa na ushahidi wowote”, ameeleza Mwabukusi. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo, Dorothy Semu, amesisitiza umuhimu wa kujenga demokrasia ya kweli nchini, akieleza kuwa licha ya Tanzania kuwa na mfumo wa vyama vingi, haki za wananchi za kuchagua na kuchaguliwa hazitekelezwi ipasavyo.
Akizungumza jana Novemba 6, 2026 katika Kata ya Heru Juu, Jimbo la Kasulu Mjini, mkoani Kigoma, wakati akiendelea na ziara ya chama hicho, Semu amesema Katiba inatambua haki ya wananchi kuchagua viongozi na kugombea nafasi za uongozi, hivyo ni muhimu kuhakikisha misingi hiyo inaheshimiwa na kutekelezwa.
Amesema ACT-Wazalendo inaendelea kudai mabadiliko ya kweli nchini, yakiwemo kupatikana kwa Katiba mpya inayotokana na maoni ya wananchi, mageuzi ya mifumo ya uchaguzi ili kuhakikisha chaguzi huru na za haki, pamoja na kulinda haki na utu wa Watanzania.
Akizungumzia masuala ya uchaguzi, Semu amesema uchaguzi unapaswa kuwa mchakato wa wananchi kutumia haki yao ya kidemokrasia badala ya kuambatana na vitisho, kukamatwa au kubambikiziwa kesi. Aidha, amedai kuwa zaidi ya Watanzania 500 walipoteza maisha katika uchaguzi mkuu uliopita.
Kuhusu matukio ya Oktoba 29 na yaliyofuata, ikiwemo vifo, madai ya kubambikiziwa kesi na kuibiwa kwa uchaguzi, Semu ametaka kuundwa kwa tume huru ya uchunguzi ya kimataifa ili kubaini ukweli, kutoa ripoti na kuweka msingi wa uwajibikaji.
Ameongeza kuwa maandamano ni haki ya kikatiba, akisisitiza umuhimu wa kujenga demokrasia inayowapa Watanzania nafasi ya kutoa maoni yao, kuwa na uhuru wa mawazo na kushiriki katika masuala yanayohusu mustakabali wa nchi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Wazazi na Walezi wametakiwa kutenga muda wa kukaa na kuzungumza na watoto wao ili kufahamu changamoto zinazowakabili na kuwasaidia kukua katika mazingira salama yanayowaandaa kukabiliana na changamoto mbalimbali za kijamii.
Wito huo umetolewa na Paroko Mteule wa Parokia Teule ya Ufukoni, Jimbo Katoliki la Mtwara, David Mwaibaza, jana Novemba 2026, wakati wa mahafali ya vituo vya kulelea watoto wadogo vya Montessori St. Lioba na St. Monica, ambapo watoto 39 wamehitimu na wanatarajiwa kujiunga na darasa la kwanza.
Amesisitiza umuhimu wa wazazi kujenga ukaribu na watoto wao kupitia mazungumzo ya mara kwa mara, akieleza kuwa kufanya hivyo kutawasaidia kutambua changamoto wanazopitia na kuchukua hatua za kuwasaidia mapema.
Kwa upande wake, Polisi Kata wa Shangani, Hansi Onai, amewataka wazazi na walezi kuongeza uangalizi kwa watoto wanapokuwa nyumbani na katika maeneo ya michezo, ikiwemo kufuatilia watu wanaoshirikiana nao katika michezo, ili kuwalinda dhidi ya vitendo vya ukatili wa kingono.
Naye Msimamizi wa vituo vya St. Monica na St. Lioba, Sister Paula Mbunda, amesema wazazi wamechangia jumla ya Shilingi 825,000 kwa ajili ya kuchimba kisima kitakachosaidia vituo hivyo kukabiliana na changamoto ya upatikanaji wa maji, hususan wakati wa kiangazi.
Ujumbe uliotolewa katika mahafali hayo umeelekeza umuhimu wa ushirikiano kati ya wazazi, walezi na jamii katika kuhakikisha watoto wanapata malezi bora, ulinzi na mazingira yanayowawezesha kukua na kukabiliana na changamoto za maisha.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umeeleza kutumia teknolojia ya Akili Mnemba (AI) na mifumo ya kidijitali katika kubaini na kudhibiti vitendo vya udanganyifu vinavyohusiana na uchakataji wa madai ya huduma za afya, hatua inayolenga kuimarisha usimamizi wa fedha na utoaji wa huduma bora kwa wanachama.
Akizungumza katika mkutano kati ya NHIF na Wahariri wa Vyombo vya Habari ulioratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina, jana Novemba 6, 2026, Mkurugenzi Mkuu, Dkt. Irene Charles Isaka amesema matumizi ya teknolojia hiyo yamesaidia kubaini madai yasiyoendana na huduma za kitabibu zinazostahili kutolewa kwa wagonjwa.
Amesema mfumo wa kidijitali una uwezo wa kubaini viashiria vya udanganyifu, ikiwemo madai ya matibabu yasiyolingana na jinsia au hali ya mgonjwa, huku hatua hiyo ikisaidia kupunguza mianya ya udanganyifu katika vituo vya kutolea huduma za afya.
Aidha, amesema NHIF imefanya jumla ya uchunguzi 747 tangu kuanza kwa udhibiti huo, ambapo fedha zilizobainika kurejeshwa ni Shilingi bilioni 47.8, huku mikataba ya vituo 53 vya kutolea huduma za afya ikisitishwa kwa muda maalumu kutokana na ukiukwaji wa taratibu. Pia, wataalamu 234 wa afya wameripotiwa kwenye mabaraza yao ya kitaaluma.
Katika hatua nyingine, Dkt. Isaka amesema NHIF imeendelea kutoa mikopo kwa vituo vya kutolea huduma za afya kwa ajili ya kuboresha miundombinu na huduma nyingine, akieleza kuwa hadi Juni 2025 mfuko ulikuwa umetoa mikopo yenye thamani ya Shilingi Bilioni 51.15 tangu kuanza kwa mpango huo, huku vituo vya serikali vikiwa vinanufaika zaidi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI:
Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Dkt. Ayub Rioba Chacha, amesema amefarijika kuona Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, hajaadhibiwa kwa hukumu ya kunyongwa, akimtakia kila la kheri katika maisha yake gerezani kufuatia hukumu iliyotolewa dhidi yake.
Dkt. Rioba amesema hayo Novemba 6, 2026 kupitia ukurasa wake wa Facebook ikiwa ni maoni yake kuhusu hukumu ya Lissu. Amesema licha ya kutofautiana naye kimtazamo, anaamini ni muhimu kuheshimu misingi ya sheria na utawala wa nchi.
Amesema awali alikuwa miongoni mwa Watanzania walioandika hadharani wakipendekeza Lissu aondolewe kwenye kesi kwa utaratibu wa kisheria ili kutoa nafasi ya kujenga maridhiano nchini.
"Pamoja na hatia aliyokutwa nayo, ninamtakia ndugu yangu Tundu Lissu kila la kheri katika maisha yake gerezani," amesema Dkt. Rioba.
Ameongeza kuwa Watanzania wanapaswa kujifunza kutokana na hukumu hiyo kwa kutanguliza maslahi ya Taifa kuliko tofauti za kisiasa, akisisitiza kuwa Tanzania ni kubwa na muhimu kuliko mtu mmoja mmoja, wakiwemo wanasiasa.
Dkt. Rioba ametoa wito kwa wananchi kuendelea kuheshimu Mahakama, sheria na misingi ya utawala wa nchi, huku akisisitiza umuhimu wa kujenga jamii inayozingatia majadiliano, utu na utangamano badala ya siasa za chuki na mihemuko. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katibu Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo ambaye pia ni Mbunge wa Tunduru Kaskazini, Ado Shaibu ameeleza kuwa uamuzi wa Mahakama Kuu ya Tanzania kumhukumu Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Antiphas Lissu, kifungo cha miaka minne jela ni kama siku ya giza kwa haki za binadamu, utawala wa sheria, pamoja na demokrasia nchini Tanzania.
Ado ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam mara baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, kumpa Lissu adhabu hiyo ya kifungo kwa kosa la uchochezi kufuatia mabadiliko ya mashtaka kutoka kosa la uhaini.
"Ninachoweza kusema ni kwamba leo ni siku ya giza kwa haki za binadamu, utawala wa sheria pamoja na demokrasia nchini Tanzania. Mahakama imepoteza fursa muhimu sana ya kufungua ukurasa mpya wa kisiasa na wa kijamii nchini Tanzania." Ameeleza AdoThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, CPA Amos Gabriel Makalla, leo Ijumaa, Novemba 6, 2026, ametatua mgogoro wa ardhi katika Kijiji cha Makuyuni, Wilaya ya Monduli, uliodumu kwa takribani miaka 20 baada ya wananchi kuvamia eneo la mwekezaji la ekari 200 na kufanya shughuli za uzalishaji na kuweka makazi.
Akizungumza na wananchi wa Kitongoji cha Zaburi, Makalla amebainisha kuwa kampuni ya Rhino Equipment & Transportation ndiyo mmiliki halali wa eneo hilo, huku Serikali ikipendekeza mwekezaji huyo aridhie kutenga ekari 100 kwa ajili ya kitongoji hicho ambacho tayari kimesajiliwa na kina miundombinu mbalimbali ya kijamii ikiwemo msikiti, kanisa, shule ya awali pamoja na huduma za maji na umeme.
Katika maelekezo yake, Makalla ameutaka uongozi wa Rhino Equipment & Transportation kukaa na kuzungumza na wananchi walioingia katika eneo lake lingine lenye ukubwa wa ekari 100 na kuweka makazi na kufanya shughuli mbalimbali ili kwa pamoja waweze kufikia makubaliano yatakayowezesha matumizi sahihi ya ardhi hiyo na kuondoa mgogoro.
Makalla, kadhalika amewataka wananchi wa kijiji hicho kuwa watulivu na kusitisha uvamizi na uendelezaji wa maeneo hayo hadi pale makubaliano yote yatakapokamilika suala ambalo limeungwa mkono na uongozi wa eneo hilo, huku akiiagiza Halmashauri ya Wilaya ya Monduli kusimamia utekelezaji wa maelekezo hayo na kuhakikisha kunakuwa na mpango mzuri wa matumizi ya ardhi itakayotengwa na mwekezaji kwa ajili ya wananchi hao.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Dorothy Semu, ametuma salamu za mshikamano kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) pamoja na familia ya Mwenyekiti wa CHADEMA taifa, Tundu Lissu akieleza kuwa siku ya hukumu dhidi ya Mwenyekiti huyo ni siku ya giza kubwa katika mwendelezo wa kuipigania demokrasia nchini Tanzania.
Semu ameyasema hayo leo akiwa katika Kata ya Heru Juu, Jimbo la Kasulu Mjini mkoani Kigoma wakati wa ziara yake mkoani humo, mara baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, kumhukumu Tundu Antiphas Lissu kifungo cha miaka minne jela kwa kosa la uchochezi.
Akizungumza mbele ya wananchi na wanachama wa ACT Wazalendo mkoani Kigoma, Semu amebainisha kuwa msimamo wa chama chake tangu Lissu alipokamatwa ulikuwa ni kwamba kiongozi huyo alikamatwa kwa uonevu wenye lengo la kumfifisha na kumkandamiza kisiasa.
Kiongozi huyo wa ACT Wazalendo amesisitiza haja ya kujenga demokrasia inayompa Mtanzania haki ya kujisimamia, haki ya uhuru wa mawazo na matendo, badala ya kuona haki hizo zikiendelea kukandamizwa. Ameongeza kuwa Lissu alikuwa anapigania uwepo wa demokrasia na haki ya kupata chaguzi huru na za haki.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Kiongozi wa Chama cha People's Liberation Party (PLP) nchini Kenya, Martha Karua amelaani vikali uamuzi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam wa kumfutia kosa la uhaini Tundu Lissu lakini kumtia hatiani kwa kosa dogo la uchochezi na kumhukumu kifungo cha miaka minne gerezani.
Karua amedai kuwa uamuzi huo unazua maswali mazito kuhusu kuendelea kushikiliwa kwa Lissu, ambaye amekuwa mahabusu tangu Aprili 2025, pamoja na matumizi ya mfumo wa haki jinai kukandamiza ushindani wa kisiasa.
Kupitia taarifa aliyoitoa kwa vyombo vya habari Novemba 6, 2026, Karua amesisitiza kuwa kufutwa kwa kosa la uhaini kunathibitisha wazi kuwa hakukuwa na sababu ya kisheria ya kumweka Lissu gerezani kwa zaidi ya mwaka mmoja.
Kadhalika, Karua amelaani adhabu na hukumu hiyo ya uchochezi akieleza kuwa ni dhihaka kwa mfumo wa haki na thibitisho la mwendelezo wa uonevu wa kisiasa, hivyo kutoa wito wa kuachiwa huru mara moja kwa Lissu.
“Hukumu ya uchochezi na adhabu iliyotolewa ni dhihaka kwa haki. Inathibitisha kuwa hii ni kesi ya uonevu wa kisiasa ambayo lengo lake ni kumweka Bwana Lissu jela, kuendelea kukitishia chama chake, na kufuta kabisa ushindani wa kisiasa nchini Tanzania," ameongeza Karua.
Karua amebainisha kuwa uamuzi huo unapaswa kutazamwa ndani ya muktadha mpana wa kubanwa kwa uwanja wa demokrasia nchini Tanzania, ikiwa ni pamoja na kuondolewa kwa CHADEMA katika Uchaguzi wa 2025. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mnyika, amewasihi Wanachadema na Watanzania wote kujitokeza kwa wingi kumwakilisha Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Tundu Antiphas Lissu, katika maziko ya kaka yake, marehemu Alute Lissu Mughwai.
Mnyika ametoa ombi hilo jijini Dar es Salaam mara baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, kumhukumu Tundu Lissu kifungo cha miaka minne jela kwa kosa la uchochezi.
“Katika hatua hii niombe tu mambo mawili. La kwanza niombe kile ambacho alikitamani mwenyekiti cha kumzika kaka yake Wanachadema na Watanzania tukamzike Alute Lissu Mughwai kwa kiwango ambacho Lissu mwenyewe angekuwepo kumzika, tumwakilishe Lissu sisi wafungwa wenzake, tumwakilishe kwenye kumzika kaka yake”, ameeleza Mnyika.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Stephen Wasira, amewataka wanachama wanaokusudia kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya chama hicho kujipima kwanza na kuhakikisha wana uwezo wa kutekeleza majukumu ya nafasi wanazoziomba.
Wasira ametoa kauli hiyo leo, Novemba 6, 2026, jijini Arusha, wakati akizungumza na wanachama wa CCM, akisisitiza kuwa uongozi unapaswa kutokana na ridhaa ya wanachama na si uwezo wa kifedha wa mgombea.
Amesema CCM ilianzishwa kwa dhamira ya kutetea wananchi wa kawaida na kupambana na dhuluma, hivyo chama hicho hakipaswi kushuhudia dhuluma bila kuchukua hatua, akieleza kuwa kufanya hivyo ni kwenda kinyume na misingi ya chama.
Amesisitiza kuwa wanachama wana wajibu wa kuwachagua viongozi wenye uwezo na wanaoielewa vizuri misingi ya CCM, akifananisha uongozi na udereva ambapo mtu asiyejua kuendesha gari hawezi kupewa jukumu la kuwa dereva bila kuhatarisha safari.
Aidha, amewataka wanaotaka kugombea nafasi za uongozi kuanzia ngazi ya tawi, kata, wilaya, mkoa hadi taifa kujiuliza kama wana uwezo wa kuongoza, huku akisisitiza kuwa hakuna mtu anayefaa kuendelea kuwa kiongozi milele.
Wasira amesisitiza kuwa mtu anayeamini hawezi kushinda uchaguzi bila kutumia fedha anapaswa kuachana na kugombea, akitaka viongozi wachaguliwe kwa hiari na ridhaa ya wanachamaThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Rugemeleza Nshala, ametoa msimamo wa chama hicho akieleza kuwa Tundu Antiphas Lissu bado anatambulika kikamilifu kama Mwenyekiti wa CHADEMA.
Kauli hiyo imetolewa Jijini Dar es Salaam mara baada ya Mahakama kumhukumu Lissu adhabu ya kifungo cha miaka minne jela. Dkt.Nshala amefafanua kuwa hukumu iliyotolewa na Mahakama haiondoi moja kwa moja nafasi ya uongozi ya Lissu.
Amesema kwa mujibu wa msimamo wa CHADEMA, Lissu anaendelea kushikilia nafasi hiyo kwa kuwa bado ana haki ya kisheria ya kukata rufaa na mchakato mzima wa kisheria haujakamilika. Kutokana na mazingira hayo, chama hicho kimebainisha kuwa hakuna sababu yoyote ya kumuondoa katika nafasi ya Uwenyekiti kwa sasa.
Aidha, Dkt. Nshala amesisitiza kuwa mamlaka ya kuwachagua na kuwaweka viongozi wa CHADEMA yako mikononi mwa wanachama wa chama hicho wenyewe na wala si watu walio nje ya chama. Akifafanua zaidi, ameeleza kuwa Lissu alichaguliwa na wanachama katika mchakato wa kidemokrasia uliofanyika mwaka jana, hivyo chama hakiwezi kumuondoa kwa maamuzi ya watu ambao si wanachama wake.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, John Heche, amewataka Watanzania na Wanachadema kutokubali mpango wowote wenye nia ya kukiua chama hicho kufuatia hukumu ya Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Tundu Antiphas Lissu.
Heche ameyasema hayo mkoani Dar es Salaam mara baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, kumhukumu Tundu Lissu kutumikia miaka minne jela kwa kosa la uchochezi.
Heche amebainisha kuna mkakati mkubwa unaoendelea unaolenga kufuta kile alichokiita sauti na kauli pekee ya Watanzania iliyobaki ambayo ni CHADEMA, akiiomba jamii yote kusimama imara na kukataa mpango huo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, amesema Serikali itaendelea kulipa uzito suala la marekebisho ya Katiba, akisisitiza kuwa ahadi iliyotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan kuhusu suala hilo itatekelezwa kwa kufuata taratibu zinazohitajika.
Dkt. Mwigulu ametoa kauli hiyo leo, Ijumaa, Novemba 6, 2026, bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha hoja ya kuahirisha Bunge.
Amesema katika kujenga mshikamano na kufikia mustakabali wa pamoja wa kitaifa, Rais Samia amekuwa akikutanana makundi mbalimbali ya kijamii, yakiwemo viongozi wa vyama vya siasa, viongozi wa dini, wazee na wadau wengine kujadili masuala ya mshikamano, maridhiano, amani na umoja wa Watanzania.
Aidha, amesema ahadi ya Rais kuhusu marekebisho ya Katiba, pamoja na ahadi iliyoainishwa katika Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020–2025, zitazingatiwa katika hatua za kushughulikia suala hilo. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, John Heche, amesema kuwa njia na jaribu ambalo chama hicho kinapitia sasa ni mpango wa Mungu na kwamba hatimaye watashinda.
Heche ameyasema hayo mkoani Dar es Salaam mara baada ya Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Tundu Antiphas Lissu, kuhukumiwa na Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, kutumikia miaka minne jela kwa kosa la uchochezi.
Heche amefananisha mtihani unaokikabili chama hicho na kisa cha Waisraeli walivyokabiliwa na jeshi la Farao wakiwa wamezingirwa na bahari pamoja na milima huku akiwashukuru kwa dhati wanachama wa CHADEMA kwa ustahimilivu waliouonesha kwa kipindi cha mwaka mmoja na miezi saba ambacho Mwenyekiti Tundu Lissu alikuwa mahabusu gerezani.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, John Heche, amewataka wanachama wa chama hicho na Watanzania kuendelea kusimama imara bila kumpigia magoti mtu, akisisitiza kuwa mapito wanayopitia ni njia ambayo Mungu mwenyewe amewachagulia na kwamba mwisho wake ni ushindi wa haraka.
Heche ameyasema hayo mkoani Dar es Salaam mara baada ya Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Tundu Antiphas Lissu, kuhukumiwa na Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, kutumikia miaka minne jela kwa kosa la uchochezi.
“Na mimi nawaambia Wanachadema, wale waliokuwa wanatuambia tupige magoti, Mwenyekiti wetu amesema hakuna kupiga magoti, na mimi nataka niwaambie, Kamati Kuu yetu na uongozi wetu chini ya Katibu Mkuu tuli naye, na mimi hakuna kupiga magoti kwenye uongo. Hakuna kupiga magoti!”, ameeleza Heche. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Baadhi ya wabunge wamepinga uamuzi wa Mahakama Kuu ya Tanzania wa kufuta sehemu ya kanuni zinazosimamia utoaji wa adhabu ya viboko shuleni, wakieleza kuwa adhabu hiyo bado ina nafasi katika kujenga nidhamu kwa wanafunzi.
Uamuzi huo, uliotolewa Novemba 3, 2026, umebatilisha Kanuni za 2, 3 na 6 za Kanuni za Elimu (Adhabu ya Viboko) za mwaka 2002, baada ya Mahakama kubaini kuwa zinakinzana na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika masuala ya kulinda utu na haki za binadamu.
Akizungumza Novemba 6, 2026, nje ya viunga vya Bunge jijini Dodoma, Mbunge wa Katavi, Thomas Kampala, ameitaka Wizara ya Elimu kulifikisha suala hilo Bungeni ili sheria husika zipitiwe upya na kuweka utaratibu utakaowezesha kurejeshwa kwa adhabu hiyo.
Kampala amesema adhabu ya viboko ina mchango katika kuwajengea wanafunzi nidhamu, hivyo ni muhimu suala hilo kujadiliwa na kupata mwafaka kuhusu namna ya kuendelea kuitumia.
Kwa upande wake, Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Njombe, Rebecca Nsemwa, amesema amesikitishwa na uamuzi huo, akipendekeza kuwekwa kwa mwongozo maalumu utakaosimamia utoaji wa adhabu ya viboko ili kuhakikisha haitolewi kwa namna inayoweza kusababisha madhara kwa wanafunzi, badala ya kuifuta kabisa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, John Heche, amesema kuwa mabadiliko ya shauri la Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Tundu Lissu, kutoka kesi ya uhaini aliyoiita ya kughushi hadi kesi ya uchochezi ni kiashiria cha siku ya ushindi kwa CHADEMA na Watanzania wote.
Heche ameyasema hayo mkoani Dar es Salaam mara baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, kumhukumu Tundu Lissu kutumikia miaka minne jela kwa kosa la uchochezi.
Heche ameongeza kuwa Lissu pamoja na viongozi wengine ni alama tu katika harakati hizo, na kwamba chama hicho kina viongozi wa kutosha kuendelea na mikakati yake bila kuyumbishwa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Spika wa Bunge, Mussa Zungu, ameitaka Serikali kuhakikisha vipimo vya mionzi kwa mizigo inayohitaji ukaguzi huo vinafanyika Dar es Salaam badala ya kupelekwa Arusha, akisema utaratibu wa sasa unasababisha ucheleweshaji na kuongeza gharama kwa wafanyabiashara na wawekezaji.
Zungu ametoa rai hiyo leo, Novemba 6, 2026, bungeni jijini Dodoma, akieleza kuwa sampuli za mizigo huchukuliwa Dar es Salaam na kupelekwa Arusha kwa uchunguzi, kabla ya majibu kurejeshwa Dar es Salaam, mchakato unaoweza kuchukua hadi wiki moja.
Amesema ucheleweshaji huo unasababisha mizigo kukaa bandarini kwa muda mrefu, kuongeza gharama za uondoshaji na kuathiri shughuli za biashara na uwekezaji.
Aidha, ameitaka Serikali kuongeza ufanisi katika utoaji wa mizigo bandarini kwa kuhakikisha taasisi zinazohusika na ukaguzi na utoaji wa vibali hazicheleweshi huduma kwa sababu ya madai ya malipo. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Samia imepongezwa na wajumbe wa kimataifa katika Kikao cha Nne cha Tathmini ya Hali ya Haki za Binadamu (UPR) ya Tanzania kinachoendelea Geneva, Uswisi, baada ya kufanikiwa kuwafikia watu milioni 7.9 katika kipindi cha miaka minne, wakiwemo wanawake milioni nne.
Akitoa tathmini ya wasilisho la Tanzania, Waziri wa Katiba na Sheria, Abdallah Ulega, amesema wajumbe wa UPR wameeleza kuvutiwa na kampeni hiyo kutokana na mchango wake katika kupanua upatikanaji wa huduma za msaada wa kisheria kwa wananchi.
Ulega amesema katika kipindi cha tathmini iliyopita, Tanzania ilipokea mapendekezo 252 kutoka Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa, ambapo 187 yalikubaliwa, yakiwemo 20 kwa sehemu, huku 65 yakikataliwa. Mapendekezo yaliyokubaliwa yamekuwa sehemu ya msingi wa maboresho yanayoendelea kutekelezwa nchini.
Ameeleza pia kuwa Serikali imetafsiri sheria 446 kwa Kiswahili ili kuwawezesha wananchi kuelewa haki na wajibu wao, huku ikiendelea na mageuzi katika sekta ya sheria, demokrasia, utawala bora na usawa wa kijinsia.
Katika kuboresha utoaji wa haki, mrundikano wa mashauri mahakamani Tanzania Bara umepungua kutoka asilimia 10 hadi tano, huku muda wa wastani wa kumaliza mashauri ukishuka kutoka siku 95 hadi 66.
Kwa upande wa Zanzibar, mrundikano wa mashauri umepungua kutoka asilimia 43 hadi 18.
Tathmini ya UPR ni utaratibu wa Umoja wa Mataifa unaozikagua nchi wanachama kuhusu utekelezaji wa haki za binadamu na kutoa mapendekezo ya maeneo yanayohitaji maboresho.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Serikali imeahidi kufanyia kazi hoja zote za ukaguzi zinazotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), huku ikisisitiza kuwa watumishi watakaobainika kufanya ubadhirifu wa fedha za umma watachukuliwa hatua kali.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri Mkuu wa Tanzania, Dk. Mwigulu Nchemba, leo Ijumaa Novemba 6, 2026, bungeni jijini Dodoma wakati akitoa hoja ya kuahirisha Bunge, akieleza kuwa Serikali itazingatia pia mapendekezo na maazimio yanayotolewa na Bunge kuhusu taarifa za ukaguzi.
Amesema Serikali itahakikisha hoja za ukaguzi zinajibiwa na mapendekezo ya CAG yanafanyiwa kazi, huku akisisitiza kuwa wale watakaobainika kufanya ubadhirifu watachukuliwa hatua kali kwa mujibu wa maelekezo ya Rais.
Nchemba amesema fedha za umma ni kodi zinazotolewa na wananchi, hivyo Serikali haitafumbia macho watumishi watakaobainika kuzitumia vibaya.
Aidha, amewataka maafisa masuuli na watendaji wote wa Serikali kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za matumizi ya fedha za umma kwa kuzingatia mipango na bajeti zilizoidhinishwa, ili kuzuia upotevu wa fedha na kujitokeza kwa hoja za ukaguzi. -
Jambo TV
@Jambotv_
"(Lissu) awe imara kesi imeamuliwa kwa jinsi ilivyoamuliwa lakini ana nafasi ya kukata rufaa" Dkt. Vincent Lissu Mughwai ambaye ni mdogo wa Tundu Lissu aliyehukumiwa miaka minne gerezani kwa kosa la uchochezi.
-
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mchungaji Rose Masesa, dada wa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Antiphas Lissu, amesema familia yake haijakata tamaa licha ya ndugu yake huyo kuhukumiwa kifungo cha miaka minne gerezani kwa kosa la uchochezi, huku akisisitiza kuwa uamuzi huo umelitia doa taifa la Tanzania.
Mchungaji Masesa ametoa kauli hiyo katika viunga vya Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, mara baada ya jopo la majaji watatu kukamilisha kusoma hukumu dhidi ya Lissu, akisisitiza kuwa walifika mahakamani hapo kwa ajili ya kuonesha mshikamano na mdogo wao na kumpa nguvu mke wa Lissu.
“Hatujakata tamaa. Hatujakata tamaa. That's what I can say. Kwamba umetupa nguvu, tumejua kwa kiasi fulani kwamba nchi yetu sasa hivi tuko katika hali gani. Tumejua tunapita katika kipindi gani na taifa letu kwamba sasa hivi likoje; tumejua kwamba kumbe inawezekana mtu akanyimwa haki tu bila sababu hata kama ana haki, mtu akafungwa hata kama hakustahili kufungwa”, ameeleza.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Samia imepongezwa na wajumbe wa kimataifa katika Kikao cha Nne cha Tathmini ya Hali ya Haki za Binadamu (UPR) ya Tanzania kinachoendelea Geneva, Uswisi, baada ya kufanikiwa kuwafikia watu milioni 7.9 katika kipindi cha miaka minne, wakiwemo wanawake milioni nne.
Akitoa tathmini ya wasilisho la Tanzania, Waziri wa Katiba na Sheria, Abdallah Ulega, amesema wajumbe wa UPR wameeleza kuvutiwa na kampeni hiyo kutokana na mchango wake katika kupanua upatikanaji wa huduma za msaada wa kisheria kwa wananchi.
Ulega amesema katika kipindi cha tathmini iliyopita, Tanzania ilipokea mapendekezo 252 kutoka Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa, ambapo 187 yalikubaliwa, yakiwemo 20 kwa sehemu, huku 65 yakikataliwa. Mapendekezo yaliyokubaliwa yamekuwa sehemu ya msingi wa maboresho yanayoendelea kutekelezwa nchini.
Ameeleza pia kuwa Serikali imetafsiri sheria 446 kwa Kiswahili ili kuwawezesha wananchi kuelewa haki na wajibu wao, huku ikiendelea na mageuzi katika sekta ya sheria, demokrasia, utawala bora na usawa wa kijinsia.
Katika kuboresha utoaji wa haki, mrundikano wa mashauri mahakamani Tanzania Bara umepungua kutoka asilimia 10 hadi tano, huku muda wa wastani wa kumaliza mashauri ukishuka kutoka siku 95 hadi 66.
Kwa upande wa Zanzibar, mrundikano wa mashauri umepungua kutoka asilimia 43 hadi 18.
Tathmini ya UPR ni utaratibu wa Umoja wa Mataifa unaozikagua nchi wanachama kuhusu utekelezaji wa haki za binadamu na kutoa mapendekezo ya maeneo yanayohitaji maboresho.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mchungaji Rose Masesa, dada wa Tundu Lissu, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) akiondoka katika viunga vya Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Dar es Salaam mara baada ya mdogo wake kuhukumiwa miaka minne jela kwa uchochezi. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) taifa, Tundu Antiphas Lissu akitolewa nje ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam tayari kwa ajili ya kupelekwa gerezani kutumikia kifungo cha miaka minne (4) baada ya mahakama kumtia hatiani kwa kosa la uchochezi kufuatia mabadiliko ya mashtaka kutoka kosa la uhaini.
Hukumu hiyo imetolewa leo Novemba 6, 2026 na jopo la majaji watatu wakiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru, ambapo mahakama imeeleza kuwa licha ya kuzingatia kuwa Lissu ni mkosaji wa mara ya kwanza, kitendo cha kuhamasisha kuzuia au kuvuruga uchaguzi mkuu kinalenga kuminya na kuzuia haki za kikatiba za wananchi wengine, hivyo kinastahili adhabu ya kifungo badala ya faini.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, imemhukumu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Antiphas Lissu, kutumikia kifungo cha miaka minne (4) gerezani baada ya kumtia hatiani kwa kosa la uchochezi kufuatia mabadiliko ya mashtaka kutoka kosa la uhaini.
Hukumu hiyo imetolewa leo Novemba 6, 2026 na jopo la majaji watatu wakiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru, ambapo mahakama imeeleza kuwa licha ya kuzingatia kuwa Lissu ni mkosaji wa mara ya kwanza, kitendo cha kuhamasisha kuzuia au kuvuruga uchaguzi mkuu kinalenga kuminya na kuzuia haki za kikatiba za wananchi wengine, hivyo kinastahili adhabu ya kifungo badala ya faini. -
Jambo TV
@Jambotv_
Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, imemhukumu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Antiphas Lissu, kutumikia kifungo cha miaka minne (4) gerezani baada ya kumtia hatiani kwa kosa la uchochezi kufuatia mabadiliko ya mashtaka kutoka kosa la uhaini.
Hukumu hiyo imetolewa leo Novemba 6, 2026 na jopo la majaji watatu wakiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru, ambapo mahakama imeeleza kuwa licha ya kuzingatia kuwa Lissu ni mkosaji wa mara ya kwanza, kitendo cha kuhamasisha kuzuia au kuvuruga uchaguzi mkuu kinalenga kuminya na kuzuia haki za kikatiba za wananchi wengine, hivyo kinastahili adhabu ya kifungo badala ya faini.
Akitoa uamuzi huo wa mwisho wa mahakama, Jaji Ndunguru amebainisha kuwa mahakama imezingatia mambo kadhaa, ikiwemo maombi ya dhamana na ukweli kwamba mshtakiwa ni mkosaji wa mara ya kwanza asiye na rekodi za nyuma za kuingia hatiani kisheria.
Mahakama imekiri kuwa kwa mujibu wa misingi na takwa la kisheria, pale ambapo sheria inatoa chaguo la faini na kifungo, faini huwa ndicho chaguo la kwanza linalopaswa kuzingatiwa kabla ya kutoa kifungo. Hata hivyo, majaji wamebainisha kuwa mazingira ya kosa hilo yameilazimu mahakama kutoa adhabu ya kifungo gerezani.
“Tunajua kwamba ni takwa la sheria pale ambapo faini na kifungu vinatolewa chaguo la kwanza ni faini. Mahakama inasema imepitia hukumu mbalimbali kwamba Mahakama itatoa hukumu kwanza pale inapobidi... Kuzuia uchaguzi ni kukiuka katiba ya nchi. Katiba inaeleza pale ambapo mtu unapokuwa unatafuta haki zako kuhakikisha huingilii haki ya mtu mwingine. Katika mazingira hayo, kuhamasisha kuzuia uchaguzi, kuvuruga uchaguzi ni kuzuia haki ya kikatiba”, imeeleza Mahakama.
Adhabu hii inahitimisha shauri hilo lililochukua miezi kadhaa mahakamani, ambapo Lissu alikaa mahabusu gerezani kwa takribani siku 577 tangu alipokamatwa mwezi Aprili 2025. -
Jambo TV
@Jambotv_
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Antiphas Lissu ameonesha kushangazwa na kusikitishwa kwa kuwekwa gerezani kwa siku 577 chini ya kosa la uhaini linalobeba adhabu ya kifo, kabla ya kubadilishwa ghafla na kuitwa "mchochezi" kwa kosa ambalo hakushtakiwa nalo.
Akiwasilisha maelezo yake baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Dar es Salaam kumtia hatiani kwa kosa la uchochezi kutoka kwenye kosa la uhaini, Lissu amesisitiza kuwa uamuzi huo unathibitisha wazi kuwa hakuwa na kosa lolote na kwamba kesi hiyo ilikuwa ya kisiasa iliyolenga kumkomesha.
Lissu ameanza maelezo yake kwa kutoa wito wa kusikilizwa kwa makini, akibainisha kuwa leo ni siku ya 577 tangu alipowekwa gerezani kwa tuhuma za uhaini kosa ambalo kwa Katiba ya Tanzania ndilo kosa kubwa kuliko yote na pekee lililotamkwa wazi kikatiba.
Amesema kuwa kwa siku hizo 577, wingu jeusi la adhabu ya kifo chini ya Kifungu cha 39(2)(d) cha Kanuni ya Adhabu lilikuwa likining’inia juu ya kichwa chake, lakini leo mahakama inamwita mchochezi kwa kosa ambalo hata wakili wa serikali anahangaika kutafuta adhabu yake.
"Mmeniita mchochezi na Wakili wa Serikali mkuu anahangaika kutafuta adhabu yake ni nini, maana yake ni nini? Kosa nililoshtakiwa nalo halikuwa kosa na nyie leo mmesema halikuwa kosa, nilikaa siku 577 bila kosa lolote”, ameeleza Lissu.
Lissu amesisitiza kuwa kubadilishwa kwa kosa hilo kunathibitisha msimamo wake wa siku zote kuwa shauri hilo lilikuwa la kisiasa lenye lengo la kugeuza mahakama kuwa uwanja wa mapambano ya kisiasa ili kumuadhibu mpinzani wa serikali.
Aidha, Lissu ametangaza kwa msimamo thabiti kuwa hatakaa aombe msamaha kwa kuwa hajatenda kosa lolote, "Wasiokuwa na hatia kama mimi huwa hawaombi msamaha, unaomba msamaha kama una hatia, kama umekosa. Huombi msamaha unapokuwa huna hatia, siombi msamaha kwa sababu sina hatia kabisa."
Akiangazia ombi la Jamhuri la kutaka apewe adhabu kali chini ya Kifungu cha 35 cha Kanuni ya Adhabu (kinachotoa adhabu ya hadi miaka mitano jela au faini), Lissu amekumbusha msimamo wa kisheria wa Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani kupitia kesi za Salum Shaban vs. Jamhuri, Alice Nyawira vs. Jamhuri (Shauri la Jinai Na. 40/2022), na Elias Ndikumana vs. Jamhuri (Shauri la Jinai Na. 39/2022). Amesema sheria inaelekeza kuwa pale ambapo kuna chaguo la faini au kifungo, mahakama inawajibika kutoa adhabu ya faini kwanza kama chaguo la msingi.
Halikadhalika, Lissu amebomoa hoja za Wakili wa Serikali Mkuu aliyerejea Ripoti ya Jaji Chande kuhusu machafuko ya Oktoba 29, akibainisha kuwa ripoti hiyo haikuwahi kuwasilishwa kama kielelezo wala Jaji Chande hakuja kutoa ushahidi mahakamani. Amehoji mantiki ya kutaka aadhibiwe kwa matukio yaliyotokea miezi sita baadaye akiwa tayari yuko mahabusu gerezani.
Amejea rekodi yake ya kisheria akibainisha kuwa licha ya kushtakiwa mara 24, hajawahi kukutwa na hatia yoyote katika maisha yake.
“Sijawahi kukutwa na hatia yoyote katika maisha yangu. Wamenishtaki kwa miaka 24, hawajawahi kunipata na hatia hata mara moja. Kwa hiyo mnapofikiria adhabu ya kutoa, msije mkatoa kwa mtu ambaye hajawahi kupatikana na hatia abadani”, ameeleza. -
Jambo TV
@Jambotv_
“Natumai mnafahamu nina msiba mkubwa sana wa mtu ambaye amenifanya mimi mwanasheria ambaye nimekuwa, amenifanya mtu ambaye nimekua, mtu aliyenilea, nilikuwa na matumaini kwamba kwasababu sikupata nafasi ya kumuuguza nilikuwa natumaini mahakama itaona ukweli kwamba hii kesi haina kitu iniache nikamzike Mzee Alute, nikamzike kaka yangu. Waheshimiwa majaji mfikirie na hilo, wajibu wa kifamilia ni wa kuzingatia kwenye kuamua adhabu, huyu mtu amefiwa, dunia nzima inafahamu, ninatumai mtazingatia hilo kwamba nahitaji kwenda kutimiza wajibu wa kumzika aliyenilea kwasababu sikuweza kumuuguza”, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Antiphas Lissu akiieleza Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Dar es Salaam kuhusu msiba wa kaka yake, Wakili Alute Lissu Mughwai aliyefariki dunia usiku wa kuamkia Jumapili, Novemba 1, 2026.
-
Jambo TV
@Jambotv_
Upande wa Mashtaka umeiomba Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, kumpa adhabu kali Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Antiphas Lissu, baada ya kukutwa na hatia ya kosa la uchochezi, ili iwe mfano na onyo kwa watu wengine wenye nia ya kuvuruga amani ya nchi.
Ombi hilo limewasilishwa mahakamani hapo na Wakili wa Serikali Mkuu, Nassoro Katuga, wakati akiwasilisha hoja za Jamhuri za kuomba adhabu mara baada ya mahakama hiyo kumtia hatiani Lissu kwa kosa la uchochezi badala ya kosa la uhaini lililokuwa likimkabili awali.
Akiwasilisha hoja zake mbele ya jopo la majaji watatu, Wakili wa Serikali Mkuu Nassoro Katuga ameeleza kuwa chini ya Kifungu cha 339 (pamoja na Kifungu cha 390) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA), mahakama inayo mamlaka ya kupokea ushahidi na hoja zitakazosaidia kutoa hukumu na adhabu sahihi kisheria.
Katuga amebainisha kuwa adhabu katika mfumo wa haki jinai ina lengo kuu la kutoa onyo na funzo. Amesisitiza kuwa adhabu inayotakiwa kutolewa lazima iwe onyo kwa mshtakiwa mwenyewe asirudie kosa hilo, lakini pia iwe mfano kwa mtu mwingine au kikundi chochote chenye nia ya kutenda vitendo vya aina hiyo vya uchochezi.
Katika kuchagiza ombi la adhabu kali, Katuga amesema kuwa mbali na kutokuwa na rekodi za nyuma za kutenda makosa ya jinai kwa Lissu, jambo hilo halipaswi kuwa sababu kwa Jamhuri kutoomba adhabu kali.
Amefafanua kuwa kwa mujibu wa rekodi na taarifa za hivi karibuni za Jeshi la Polisi, kumekuwepo na ongezeko kubwa la watu wanaotenda kosa la uchochezi na kuhamasisha umma wa Watanzania kutenda makosa, kuvunja sheria, au kuvuruga amani ya nchi kwa ajili ya maslahi binafsi. Katuga ameongeza kuwa vitendo hivyo vya uchochezi vinakuwa na athari mbaya sana kwani vinasababisha watu kupoteza maisha na kuathiri vibaya uchumi wa nchi.
Wakili huyo wa Serikali Mkuu amerejea hotuba na ripoti ya Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Chande Othman kuhusu matukio na machafuko ya Oktoba 29, akibainisha kuwa ripoti hiyo ilibainisha wazi madhara mbalimbali yaliyotokana na uchochezi, ikiwemo uharibifu wa mali pamoja na vifo vya raia.
Katuga ameiomba mahakama kuangalia kwa kina athari ambazo zimetokana na kauli ambazo Lissu ametiwa nazo hatiani kama vile "kuzuia uchaguzi", "kukinukisha", na "kuhamasisha uasi". Ameeleza kuwa taarifa ya Jaji Chande ilionesha kuwa matukio ya Oktoba 29 yalilenga kuzuia uchaguzi na yakasababisha athari kubwa za hasara za kiuchumi na vifo vya watu.
Akiangazia vifungu vya sheria vinavyotoa adhabu, Katuga amebainisha kuwa Kifungu cha 390 cha CPA kilichomkuta Lissu na hatia hakitoi adhabu moja kwa moja, lakini vipo vifungu vingine vinavyotoa adhabu, ikiwemo Kifungu cha 35 cha Kanuni ya Adhabu kinachotoa adhabu ya hadi kifungo cha miaka mitano gerezani.
"Ni faini kiasi gani itamfanya mshtakiwa iwe onyo kwa wengine kufanya kosa hilo... ni maombi yetu Mahakama izingatie vyote upande wetu... Mahakama haitoki mbinguni, inayajua hata mngekuwa mbinguni mngeyaona”, ameeleza Katuga. -
Jambo TV
@Jambotv_
Katika uamuzi uliotolewa leo Ijumaa, Novemba 6, 2026, Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, imemfutia kosa la uhaini Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Antiphas Lissu, na badala yake kumtia hatiani kwa kosa la uchochezi.
Hukumu hiyo imesomwa na jopo la majaji watatu wakiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru, akisaidiwa na Jaji James Karayemaha pamoja na Jaji Ferdinand Kiwonde, katika kesi ya uhaini iliyosajiliwa kwa Namba 19605/2025.
Akisoma sehemu hiyo ya hukumu, Jaji Dunstan Ndunguru ameeleza kuwa mahakama imeridhika kuwa ushahidi wote uliowasilishwa mahakamani hapo umejikita kwenye kosa la uchochezi badala ya kosa la uhaini linalobeba adhabu ya kifo.
.
Kwa kutumia mamlaka yake ya kisheria chini ya Kifungu cha 309 cha Kanuni ya Adhabu, mahakama imemtoa mshtakiwa kwenye kosa kubwa la uhaini na kumhamishia kwenye kosa la uchochezi. Mahakama imebainisha kuwa kauli zilizotolewa na Tundu Lissu wakati wa mkutano wake na watia nia zilitengeneza uchochezi na kuzalisha matendo yasiyo ya kisheria yaliyolenga kuzuia mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
Mahakama imetupilia mbali uwezekano wowote wa mshtakiwa kuathirika kisheria kutokana na mabadiliko hayo ya mashtaka, ikizingatia kuwa alikuwa na nafasi kamili ya kujitetea
"Mahakama inaamini mshtakiwa alikuwa na ufahamu na uwezo wa kujitetea mwenyewe, kwa muktadha huo mahakama haioni kama atakuwa amenyimwa haki yoyote kwa kutolewa kwenye kosa kubwa (uhaini) kupelekwa kwenye kosa dogo”, ameeleza Jaji Ndunguru na kuongeza, "Mahakama imesema inaridhika kwamba kwa mujibu wa Kifungu cha 309 cha Kanuni ya Adhabu, Lissu ametenda kosa la uchochezi na inamtia hatiani kwa kosa la uchochezi."
Taarifa kamili inakujia hivi punde -
Jambo TV
@Jambotv_
Katika hukumu ya kesi ya uhaini namba 19605/2025 inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Antiphas Lissu, inayosomwa leo Novemba 6, 2026, katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, Mahakama imebainisha kuwa hakuna ushahidi wowote thabiti unaothibitisha kuwa Lissu ndiye aliyeyachapisha au kuyasambaza maudhui ya video kwenye chaneli ya YouTube ya Jambo TV.
Hukumu hiyo iliyosomwa na jopo la majaji watatu wakiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru, akisaidiwa na Jaji James Karayemaha pamoja na Jaji Ferdinand Kiwonde, imekubaliana na hoja za upande wa utetezi kuwa lazima kutofautishwa wazi kati ya mtu aliyetoa hotuba na mtu aliyepandisha video hiyo mtandaoni.
Mahakama Kuu imeeleza kuwa ushahidi uliowasilishwa na pande zote mbili unaonesha wazi kuwa waandishi wa habari kutoka Jambo TV na vyombo vingine ndio waliohusika kurekodi na kurusha mkutano huo uliofanyika Aprili 3, 2025.
Majaji wamesisitiza kuwa ili kumtia mtu hatiani kwa kosa la kuchapisha maudhui mtandaoni, upande wa mashtaka ulikuwa na wajibu wa kuthibitisha kuwa mshtakiwa alikuwa na mamlaka au uwezo wa kiufundi wa kuingia kwenye mtandao huo.
Mahakama imeweka wazi kuwa kushindwa kwa upande wa mashtaka kuthibitisha kuwa Lissu ndiye aliyepandisha video hiyo kwenye mtandao wa Jambo TV ni pengo kubwa la kiushahidi upande wa Jamhuri.
Ingawa Mahakama imeona kuwa mazingira yanaonesha Lissu alitoa hotuba hiyo mbele ya wanahabari na kwamba hazikuwa kauli za siri, imesisitiza kuwa tendo la kuchapisha au kusambaza video kwenye mtandao wa kijamii linahitaji thibitisho la nani aliyeweka faili hilo mtandaoni na mwenye milki ya akaunti husika.
Mahakama imeeleza kuwa wakati wa usikilizaji wa shauri hilo, mshtakiwa Tundu Lissu aliendelea kuhoji kwanini upande wa mashtaka ulishindwa kuwasilisha video yenyewe mahakamani kama kielelezo cha msingi. Mahakama imebainisha kuwa kitendo cha kutokuwepo kwa picha mjongeo (video) hakifanyi ushahidi wa mdomo usiaminike kabisa lakini kimeacha ufa mkubwa katika kuthibitisha tuhuma za kwamba Lissu ndiye aliyekuwa mchapishaji wa maudhui hayo katika vyombo vya habari au mitandao ya kijamii. -
Jambo TV
@Jambotv_
Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, imeyatupa mbali mapingamizi na hoja zote zilizowasilishwa na Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA, Tundu Lissu, kuhusu uhalali wa hati ya mashtaka katika kesi ya uhaini inayomkabili, huku ikikubaliana na upande wa Jamhuri kuwa hati hiyo iko sahihi na inajitosheleza kisheria.
Katika hatua za mwisho za usikilizaji wa shauri hilo baada ya pande zote kufunga ushahidi, Lissu aliiomba mahakama imwachie huru akidai hana hatia, huku akiwasilisha hoja tatu kuu kupinga usahihi wa hati ya mashtaka. Alidai kuwa hati hiyo haikutoa taarifa zinazomwezesha kujiandaa kikamilifu, kutumia neno "umma" ambalo halipo moja kwa moja katika kifungu cha 39(2)(d) cha Sheria ya Kanuni za Adhabu kinachozungumzia "mtu au kikundi cha watu", na kwamba kulikuwa na utofauti wa malengo katika mashtaka hayo.
Akisoma uamuzi wa mahakama hiyo, kiongozi wa jopo la majaji watatu waliosikiliza kesi hiyo, Jaji Dunstan Ndunguru, alieleza kuwa mahakama imepitia hoja zote za upande wa mashtaka na za utetezi na kujiridhisha kuwa pingamizi hilo halina mashiko ya kisheria, hususan kwa kuwa suala hilo lilishawahi kutolewa uamuzi hapo awali.
Jaji Ndunguru alifafanua kuwa neno "umma" (public) lililotumika katika hati ya mashtaka linajumuisha mtu yeyote au idadi yoyote kulingana na muktadha wa sheria na linapata tafsiri sahihi chini ya kifungu cha 5 cha sheria husika. Alisisitiza kuwa hati hiyo ilitoa maelezo ya kutosha yaliyomwezesha mshtakiwa kuelewa wazi tuhuma zinazomkabili na kuandaa utetezi wake ipasavyo.
“Kwa hiyo, pingamizi hili halina mashiko na mahakama inalitupilia mbali,” alitamka Jaji Ndunguru wakati akitupilia mbali mapingamizi hayo -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Doroth Semu, amesema bajeti inayotengwa na Serikali kwa sekta ya kilimo haitoshi kukidhi mahitaji ya wakulima, hali inayochangia kuendelea kwa changamoto zinazowakabili licha ya sekta hiyo kuajiri sehemu kubwa ya Watanzania.
Akizungumza jana, Novemba 5, 2026, katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kazuramimba, Kigoma Kusini, akiwa katika ziara ya chama hicho, Semu amesema asilimia 65 ya nguvu kazi nchini inategemea mnyororo wa kilimo, lakini sekta hiyo haipati fedha zinazolingana na umuhimu wake.
Amesema katika bajeti ya mwaka 2025/2026, Serikali ilitenga Sh trilioni 1.06 kwa kilimo, kiasi alichokitaja kuwa kidogo ikilinganishwa na mahitaji ya sekta hiyo na lengo la kutenga angalau asilimia 10 ya bajeti kwa kilimo.
Ameeleza kuwa wakulima wanaendelea kukabiliwa na gharama kubwa za pembejeo, utegemezi wa mvua na upungufu wa zana za kilimo zinazozalishwa nchini, hali inayopunguza tija na kipato chao.
Semu ameitaka Serikali kuongeza bajeti ya kilimo na kuweka mikakati madhubuti ya kuboresha uzalishaji ili wakulima wanufaike na kazi wanayoifanya.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Naibu Waziri Mkuu Kivuli na Waziri Kivuli wa Nishati na Madini wa ACT-Wazalendo, Luhaga Mpina, amewataka madiwani wa chama hicho kuwa watetezi wa wananchi bila ubaguzi wa kisiasa, akisisitiza kuwa wajibu wao ni kusimamia haki za wananchi wote.
Akizungumza Novemba 5, 2026, katika mkutano wa hadhara Kata ya Kikomelo, Bukoba Vijijini, mkoani Kagera, Mpina amewataka madiwani wawili wa chama hicho waliochaguliwa katika jimbo hilo kujiona kama wabunge wa jimbo zima na kuwahudumia wananchi wote.
Amesema madiwani wanapaswa kufuatilia matukio ya wananchi kukamatwa, kunyanyaswa au kuzuiwa kufanya shughuli zao za kiuchumi kinyume cha sheria, na kuhakikisha mamlaka husika zinawajibika.
Aidha, ametoa agizo kwa madiwani wote 65 wa ACT-Wazalendo nchini kuwa wasimamizi wa wananchi, akisema chama kitafuatilia malalamiko yao na kutoa msaada wa kisheria ikiwemo kugharamia mawakili pale inapohitajika.
Mkutano huo ni sehemu ya ziara ya viongozi wa ACT-Wazalendo katika Kanda ya Ziwa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri Kivuli wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wa ACT-Wazalendo, Hussein Kaliyango, ameitaka Serikali kutekeleza agizo la aliyekuwa Rais wa Tanzania, John Magufuli, kuhusu utatuzi wa mgogoro wa ardhi katika Kata ya Muzye na maeneo mengine ya Kigoma Kusini.
Akizungumza jana Novemba 5, 2026 katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Muzye, Kaliyango amesema mwaka 2018 Rais Magufuli alitoa agizo la kutatua mgogoro wa ardhi wa Kagera Nkanda, baada ya kuunda kamati ya mawaziri tisa iliyohusika na kupima mipaka kati ya wakala na maeneo yanayomilikiwa na wananchi.
Amesema maazimio ya kamati hiyo yalijadiliwa Novemba 3, 2019, ambapo iliamuliwa wananchi warejeshewe maeneo yao, huku Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu ikipewa jukumu la kuhakikisha ugawaji wa maeneo hayo unatekelezwa.
Hata hivyo, Kaliyango amesema pamoja na maamuzi hayo, utekelezaji wake umekwama kwa miaka kadhaa, hali inayowafanya wananchi kuendelea kukabiliwa na mgogoro huo.
Amemtaka Rais Samia Suluhu Hassan kuhakikisha agizo hilo halifutwi na badala yake linatekelezwa, huku akimwomba Waziri wa Ardhi kufika katika maeneo ya Kagera Nkanda na Msesa kutatua migogoro hiyo ili wananchi waweze kurejeshewa haki yao ya kumiliki ardhi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Jeshi la Polisi limeweka ulinzi mkali nje ya Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Dar es Salaam wakati Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa @ChademaTZ2 ikitarajiwa kutolewa hukumu leo Novemba 6, 2026 kuanzia saa tatu asubuhi katika mahakama hiyo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Serikali ya Tanzania imefafanua kuwa hatua ya kutoweka wazi mara moja ripoti kamili ya uchunguzi wa matukio ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 inalenga kulinda ushahidi, usalama wa mashahidi, na mchakato wa uchunguzi wa jinai unaoendelea ili kuhakikisha haki inatendeka.
Maelezo hayo yametolewa leo, Novemba 5, 2026, na Waziri wa Katiba na Sheria, Abdallah Ulega, alipokuwa akiwasilisha taarifa ya mafanikio ya Ulinzi wa Haki za Binadamu mbele ya Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa, jijini Geneva nchini Uswisi, katika kikao cha Mapitio ya Hali ya Haki za Binadamu kwa Tanzania (UPR).
Akiwasilisha taarifa hiyo, Waziri Ulega amebainisha kuwa Serikali inatambua uwepo wa maslahi makubwa ya umma katika kuchapishwa kwa ripoti hiyo kamili. Hata hivyo, amesisitiza kuwa uamuzi wa kuweka wazi taarifa hiyo lazima upimwe kwa umakini dhidi ya uchunguzi unaoendelea na uwezekano wa kufungua mashtaka ya kisheria.
"Kuweka wazi ripoti hiyo kabla ya wakati kunaweza kuathiri ushahidi, kuweka mashahidi hatarini, au kuathiri haki za kesi ya haki na dhana ya kutokuwa na hatia hadi ithibitike vinginevyo. Mambo kama haya yanaweza pia kujitokeza katika mifumo mingine ya kisheria ambapo utoaji wa taarifa si wa moja kwa moja," amesema Ulega.
Aidha, Ulega ameeleza kuwa matukio yaliyotokea wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 yalikuwa ya kusikitisha mno, kwani vifo vilitokea, familia zilipata mateso, na jamii zilishuhudia ghasia na uharibifu. Amebainisha kuwa Serikali inabaki na dhamira ya kubaini ukweli, kuhakikisha uwajibikaji, na kulinda utu wa mwanadamu bila kujali ufuasi wa kisiasa.
Amekumbusha kuwa Tume ya Rais ya Uchunguzi iliundwa Novemba 18, 2025, na matokeo yake makuu yaliwasilishwa hadharani Aprili 23, 2026. Tume hiyo ilipendekeza kuundwa kwa tume tofauti ya uchunguzi wa makosa ya jinai ili kuchunguza makosa na kubaini uwajibikaji wa mtu mmoja mmoja. Ulega amefafanua kuwa tofauti hiyo ni muhimu kwasababu matokeo ya tume ya uchunguzi hayapaswi kuchukuliwa kama uthibitisho wa kosa la jinai au ushahidi wa kutosha wa mashtaka.
"Katika kutekeleza pendekezo la tume ya kwanza, tume ya uchunguzi wa makosa ya jinai iliundwa ili kufanya uchunguzi zaidi na kukusanya ushahidi kulingana na sheria, huku ikilinda haki za wote wanaohusika," amesema Ulega.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Serikali ya Tanzania imekanusha kikamilifu madai ya kulazimisha vipimo vya matibabu kwa watu wanaotuhumiwa au kujihusisha na vitendo vya mapenzi ya jinsi moja ikisisitiza kuwa haivumilii uwekaji ndani wa kiholela, vitendo vya udhalilishaji wala kunyimwa kwa huduma za msingi za afya.
Msimamo huo umeelezwa leo, Novemba 5, 2026, na Waziri wa Katiba na Sheria, Abdallah Ulega, alipokuwa akiwasilisha taarifa ya mafanikio ya Ulinzi wa Haki za Binadamu mbele ya Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa, jijini Geneva nchini Uswisi, katika kikao cha Mapitio ya Hali ya Haki za Binadamu kwa Tanzania (UPR), kinachofanyika chini ya Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa.
"Serikali inakanusha kikamilifu madai ya vipimo vya matibabu vya kulazimishwa na haivumilii uwekaji ndani wa kiholela, vitendo vya udhalilishaji au kunyimwa kwa huduma za msingi za afya. Vyombo vya usimamizi wa sheria lazima viheshimu mchakato halali wa kisheria na ulinzi wa kisheria," amesema Ulega.
Amebainisha kuwa Tanzania inashikilia msimamo wake ikizingatia maadili na misingi yake ya kijamii na kitamaduni. Ameeleza kuwa kama vile baadhi ya nchi zingine zinavyopata ugumu kutambua mfumo wa ndoa za mke zaidi ya mmoja au ndoa fulani za kidini na kimila, Tanzania pia inakabiliwa na hisia nzito za kitamaduni kuhusu uhusiano wa jinsi moja.
Waziri Ulega ameongeza kuwa, pamoja na msimamo wa nchi wa kuheshimu maadili na utamaduni wa jamii, masuala ya utu wa mwanadamu, usawa mbele ya sheria, uhuru wa mtu binafsi na ulinzi dhidi ya utesaji ni haki zinazowahusu watu wote bila ubaguzi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Serikali ya Tanzania imesisitiza kuwa heshima kwa maamuzi ya mahakama na uhuru wa vyombo vya sheria ndiyo nguzo kuu ya kuimarisha haki za binadamu, demokrasia na amani nchini, hata pale ambapo maamuzi hayo hayakubaliani na matakwa ya pande husika.
Msimamo huo umeelezwa leo, Novemba 5, 2026, na Waziri wa Katiba na Sheria, Abdalla Ulega, alipokuwa akiwasilisha taarifa ya mafanikio ya ulinzi wa haki za binadamu mbele ya Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa, jijini Geneva nchini Uswisi, katika kikao cha Mapitio ya Hali ya Haki za Binadamu kwa Tanzania (UPR).
Akiwasilisha taarifa hiyo, Ulega amesema kuwa Tanzania inatambua na kuheshimu kikamilifu mamlaka ya mahakama zake, ikiwa ni pamoja na maamuzi yanayotaka kufanyika kwa mabadiliko ya kisheria. Amesema heshima hiyo haipaswi kuoneshwa tu na wananchi, bali na viongozi, wanasiasa na washirika wa kimataifa.
"Haki za binadamu, demokrasia na amani huchanua tu pale ambapo utawala wa sheria na uhuru wa mahakama unaheshimiwa na kila mtu- viongozi, wanasiasa, wananchi na washirika wa kimataifa kwa pamoja. Heshima lazima ienee hata kwa maamuzi ya mahakama ambayo hatukubaliani nayo," amesema Ulega.
Akitolea mfano wa jinsi Tanzania inavyoheshimu na kutekeleza maamuzi ya vyombo vya sheria, Ulega amebainisha kanuni inayomtaka mgombea asiye na mpinzani kupata ridhaa ya wapigakura, akieleza kuwa ilifuatia uamuzi wa Mahakama Kuu kuhusu haki ya kikatiba ya kupiga kura. Amesisitiza kuwa mahakama nchini lazima ziendelee kufanya kazi kwa kujitegemea bila uingiliaji wowote.
"Tanzania inatambua mamlaka ya mahakama zake, ikiwa ni pamoja na maamuzi yanayotaka kufanyika kwa marekebisho ya kisheria. Mahakama zetu lazima ziamue mashauri kwa haki kulingana na ushahidi na sheria bila kuwepo kwa uingiliaji wowote," amesisitiza.
Mbali na kusisitiza heshima kwa mahakama, Ulega ameeleza kuwa Serikali inaendelea kuchukua hatua za kimkakati kuhakikisha haki inawafikia wananchi wote bila vikwazo. Ametaja matumizi ya mahakama tembezi, usikilizaji wa mashauri kwa njia ya mtandao (virtual hearings), pamoja na huduma za msaada wa kisheria kuwa zimesaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa vikwazo vya umbali na gharama kwa jamii.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 1.1 katika kipimo cha Richter Scale limetokea mchana wa leo, Novemba 5, 2026, majira ya saa 6:22 mchana katika eneo la Isungabula, Wilaya ya Mbogwe mkoani Geita, huku mtikisiko wake ukisikika wazi katika baadhi ya maeneo ya mikoa ya Geita na Mwanza.
Akizungumza kwa njia ya simu na kituo cha habari cha Jambo TV akiwa jijini Dodoma, Mtaalamu wa Miamba na Mjiolojia Mwandamizi kutoka Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST), Gabriel Mbogoni amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kubainisha kuwa hadi sasa hakuna vifo vilivyoripotiwa, ingawa tathmini ya kina inaendelea kufanyika ili kubaini ukubwa wa madhara yaliyotokea.
Licha ya kutokuwepo kwa maafa ya kibinadamu, Bw. Mbogoni ameeleza kuwa madhara ya awali yaliyoripotiwa ni pamoja na baadhi ya majengo ya madarasa katika Kijiji cha Bukene, kilichopo Wilaya ya Nzega, kupata nyufa kutokana na nguvu ya mtikisiko huo.
Akifafanua kuhusu chanzo chake, mtaalamu huyo ameeleza kuwa tetemeko hilo limetokana na nguvu za asili zinazochochewa na mikandamizo ya matabaka ya miamba yaliyopo chini ya ardhi. Aidha, ameondoa hofu kwa wananchi kwa kueleza kuwa eneo la Isungabula halipo ndani ya mkondo mkuu wa Bonde la Ufa, akisisitiza kuwa jamii inapaswa kufahamu kuwa matetemeko ya ardhi yanaweza kutokea hata katika maeneo yaliyo nje ya Bonde la Ufa kutokana na mabadiliko ya kijiolojia ya miamba ya chini.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Joto na shauku vinaonekana kutawala nchini Tanzania kuelekea hukumu ya kesi ya uhaini Namba 19065/2025 inayomkabili Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Tundu Antipas Lissu, inayotarajiwa kutolewa kesho, Ijumaa, Novemba 6, 2026, saa 3:00 asubuhi katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam.
Miongoni mwa matukio yaliyovuta hisia za wengi siku moja kabla ya hukumu hiyo ni kauli ya Balozi wa Marekani nchini Tanzania, William Trachman, aliyeandika leo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa X akieleza kufuatilia kwa karibu mchakato huo wa kisheria na matokeo yake kwa utawala wa sheria na haki za binadamu.
“Kama mwanasheria wa katiba kutoka Marekani, binafsi nimesimamia mashauri ya kutetea haki za uhuru wa kujieleza na kufuata misingi ya kisheria. Hii ni misingi mikuu ya uhuru wa binadamu. Kwa sababu hiyo, ninafuatilia kwa karibu matokeo ya shauri la Tundu Lissu na madhara yake kwa utawala wa sheria,” ameandika Balozi Trachman.
Wakati msukumo wa kimataifa ukiongezeka, Lissu ameeleza kuwa yuko tayari kukabili matokeo yoyote yatakayojitokeza katika hukumu hiyo.
Ujumbe huo uliwekwa wazi leo, Novemba 5, 2026, na Afisa wa Programu za Utetezi wa Kisheria, Msaada wa Dharura na Uokoaji (LESR) kutoka Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Wakili Paul Kisabo, mara baada ya kumtembelea Lissu katika Gereza la Ukonga jijini Dar es Salaam. Kisabo ameeleza kuwa Lissu yuko imara kiafya na mwenye ujasiri mkubwa, akisoma kitabu cha mwanaharakati wa Kenya Koigi wa Wamwere kiitwacho "I Refuse to Die" (Ninakataa Kufa) kinachompa nguvu katika kipindi hiki.
“Bado nina matumaini mema kuhusu kesho, lakini pia niko tayari kwa baya lolote litakalotokea. Hivyo, zuri likitokea, nitaelekea moja kwa moja Arusha kumrudisha ndugu yangu nyumbani. Baya likitokea, basi mapambano yataendelea. Haitakuwa mwisho wa dunia bali utakuwa ni ukurasa mpya katika mapambano ya haki na demokrasia nchini hapa,” amenukuliwa Lissu kupitia Wakili Kisabo.
Naye Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa CHADEMA, Brenda Rupia, kupitia taarifa rasmi iliyotolewa leo Alhamisi, amewataka viongozi, wanachama, na Watanzania kwa ujumla kujitokeza kwa wingi Mahakama Kuu kesho ili kushuhudia kile alichokiita kuwa ni kielelezo muhimu cha misingi ya haki na utawala wa sheria nchini.
Lissu anakabiliwa na shtaka la uhaini linalohusishwa na madai ya kuhamasisha wananchi kuzuia kuendeshwa kwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025. Baada ya kukamatwa Aprili 9, 2025, Mahakama Kuu mnamo Agosti 21, 2026 iliamua kuwa ana kesi ya kujibu. Hukumu hiyo ya kesho itatolewa na jopo la majaji watatu likiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru, akishirikiana na Majaji James Karayemaha na Ferdinand Kiwonde. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Taasisi zinazohusika na masuala ya kazi na ajira nchini zimewekewa mkazo wa kuimarisha ushirikiano wa karibu ili kutafuta suluhu ya kudumu kwa changamoto zinazoikabili sekta ya hifadhi ya jamii, hususan masuala yanayohusu utoaji wa fidia kwa wafanyakazi wanaopata ajali, magonjwa, au vifo vinavyotokana na mazingira ya kazi zao.
Wito huo ulitolewa leo, Novemba 5, 2026, mkoani Morogoro, wakati wa hafla rasmi ya uzinduzi wa Juzuu (Compendium) ya Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi. Juzuu hiyo imeandaliwa kwa lengo kuu la kurahisisha uelewa, kuimarisha upatikanaji wa huduma za fidia, na kuboresha utendaji kazi wa pamoja baina ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) na Mahakama ya Tanzania.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mustapher Siyani, amesisitiza kuwa mafanikio katika sekta ya hifadhi ya jamii na utoaji haki yanategemea ushirikiano thabiti baina ya taasisi za serikali na wadau wa pande tatu wakiwemo waajiri, vyama vya wafanyakazi, na wadau wa maendeleo kwa kila mmoja kutekeleza wajibu wake kwa ufanisi.
Kwa upande wake, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Ajira na Mahusiano, Deus Sangu, ameeleza kuwa hatua hiyo ya ushirikiano kati ya WCF na Mahakama ya Tanzania ni utekelezaji wa wazi wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan yanayozitaka taasisi za umma kushirikiana kwa karibu ili kutatua kero za wananchi. Ameongeza kuwa hatua hiyo inaonyesha dhamira ya dhati ya kuimarisha utawala wa sheria, kulinda haki za wafanyakazi, na kuongeza uwajibikaji.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma, amefafanua kuwa juzuu hiyo mpya ni matokeo ya ushirikiano wa kimkakati uliopo kati ya Mfuko huo na Mahakama Kuu ya Tanzania - Divisheni ya Kazi, ikilenga kuondoa migogoro ya tafsiri ya kisheria na kuhakikisha kuwa sheria ya fidia inatekelezwa kwa urahisi na kwa maslahi mapana ya wafanyakazi nchini.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI:
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, amesema yuko tayari kukabili matokeo yoyote yatakayojitokeza Novemba 6, 2026, siku ambayo mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Dar es Salaam itasoma hukumu ya kesi ya uhaini inayomkabili.
Hayo yameelezwa Novemba 5, 2026 na Afisa wa Programu za Utetezi wa Kisheria, Msaada wa Dharura na Uokoaji (LESR) katika Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Adv. Paul Kisabo, katika kurasa zake za mitandao ya kijamii, ikiwa ni baada ya kumtembelea Lissu katika Gereza la Ukonga, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Adv. Kisabo, Lissu yuko katika hali nzuri ya kiafya na anaendelea kuonesha ujasiri na matumaini. Katika ujumbe wake kutoka gerezani, Lissu ameeleza msimamo wake kuhusu mustakabali wa kesi yake na mapambano ya kisiasa nchini.
“Bado nina matumaini mema kuhusu kesho, lakini pia niko tayari kwa baya lolote litakalotokea. Hivyo, zuri likitokea, nitaelekea moja kwa moja Arusha kumrudisha ndugu yangu nyumbani. Baya likitokea, basi mapambano yataendelea. Haitakuwa mwisho wa dunia bali utakuwa ni ukurasa mpya katika mapambano ya haki na demokrasia nchini hapa,” amesema Lissu Kwa mujibu wa Kisabo.
Mbali na kueleza msimamo wake huo, Lissu amebainisha kuwa anaendelea kupata ujasiri na nguvu za kiroho kupitia maandiko ya mwanaharakati mashuhuri wa Kenya, Koigi wa Wamwere.
Kwa mujibu wa Adv. Kisabo, Lissu amesema anatiwa moyo na kitabu cha historia ya maisha ya mwanaharakati huyo kiitwacho "I Refuse to Die", kwa maana ya "Ninakataa Kufa".
Amesema kitabu hicho kinamkumbusha umuhimu wa kubaki na ujasiri hata katika mazingira magumu, ikiwemo kifungo, dhiki na uonevu wa kisiasa. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI:
Kufuatia madai yanayosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa kuingiza vidonge vya Cetirizine ukeni kunaweza kufanya uke ubane, Bodi ya Dawa na Sumu Kenya (PPB) imewaonya wananchi dhidi ya matumizi hayo, ikisema hayana uthibitisho wa kisayansi na yanaweza kusababisha madhara kiafya.
Katika taarifa yake, Bodi hiyo imeeleza kuwa Cetirizine ni dawa inayotumika kupunguza dalili za mzio, ikiwemo mafua na vipele vinavyosababisha muwasho mwilini. Imefafanua kuwa dawa hiyo imekusudiwa kumezwa na si kuingizwa ukeni.
Imeonya kuwa matumizi ya vidonge hivyo ukeni yanaweza kusababisha muwasho, hali ya kuungua na maumivu, pamoja na kuvuruga mazingira ya asili ya uke na kuongeza hatari ya kupata maambukizi.
Aidha, Bodi hiyo imesema kutumia Cetirizine kwa dozi inayozidi kiwango kinachopendekezwa kunaweza kusababisha usingizi mzito, kizunguzungu, uchovu, kuchanganyikiwa, kutetemeka na mapigo ya moyo kwenda kasi.
Kutokana na hali hiyo, bodi hiyo imewataka Wananchi kutumia dawa hiyo kwa matumizi yaliyoidhinishwa pekee na kufuata dozi wanazoelekezwa na wataalamu wa afya.
Aidha, Bodi imewashauri Wanawake wenye changamoto za ukavu wa uke au masuala mengine ya afya ya uzazi kutafuta ushauri wa wataalamu wa afya badala ya kutegemea madai yasiyothibitishwa yanayosambaa kwenye mitandao ya kijamii. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeridhia maazimio ya mikataba miwili ya kimataifa, ikiwemo Marekebisho ya Mkataba wa Kimataifa wa Sukari wa mwaka 1992 huku ikielezwa kuwa marekebisho hayo hayakinzani na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977 ya sheria na sera za nchi.
Akiwasilisha azimio la kuridhia marekebisho ya Mkataba huo bungeni jijini Dodoma leo Novemba 5, 2026, Waziri wa Kilimo, Daniel Chongolo amesema mkataba huo unatarajiwa kuchochea ukuaji wa uchumi na kuongeza fursa za ajira kupitia sekta ya sukari.
Ameongeza kuwa marekebisho hayo yataimarisha ushiriki wa Tanzania katika soko la kimataifa la sukari, hususan katika mijadala kuhusu bei, uagizaji, matumizi na akiba ya sukari, huku yakiongeza ushindani wa bidhaa za Tanzania katika soko la dunia na thamani ya bidhaa zinazotokana na sukari kwa manufaa ya wazalishaji, wakulima na taifa kwa ujumla.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, Amani Golugwa, amesema Chama hicho kinatambua kuwa suala la uanaharakati si jambo baya kwani ni kutetea, kudai pamoja na kushawishi mabadiliko, uwajibikaji pamoja na kutaka kusukuma mambo yaende kwa haraka, akisisitiza kuwa Chama hicho kinakazi na wajibu wa kutaka kuona mambo ya muhimu katika taifa yanakwenda kwa haraka.
Golugwa ameeleza hayo leo Novemba 5, 2026 alipokuwa akizungumza na wananchi kupitia chaneli ya youtube ya Chama hicho.
"Uanaharakati si jambo baya, uanaharakati katika lugha ya kawaida maana yake ni kutetea, uanaharakati maana yake ni kudai, ni kushawishi mabadiliko, ni kushawishi na kuleta uwajibikaji, ni kutaka kusukuma mambo yaende kwa haraka na bila shaka sisi kama Chama cha siasa tunakazi na wajibu wa kutaka kuona mambo ya muhimu katika taifa hili yanakwenda kwa haraka" amesema Golugwa.
Ameongeza kwamba katika Katiba ya Chama hicho imewekwa bayana kwamba ushupavu na uanaharakati wa kweli katika kutetea maslahi ya Chama na jamii kwa ujumla kwa kuzingatia madhumuni, itikadi na falsafa ya Chama ni mambo ambayo yamefafanuliwa na kutambuliwa kikamilifu.
Ameongeza kwamba, kuwa mwanaharakati katika Chama hicho ni takwa la kimaadili ambalo kila mwanachama anatakiwa kuwa nalo akisisitiza kuwa uanaharakati halijawahi kuwa neno baya.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
"Afande Muliro la kwanza anatakiwa kufanya ka tayari ana taarifa za kiintelijensia ambazo zinamwambia kwamba kuna watu baadhi wanapanga kuja kufanya fujo kesho nilitegemea mpaka leo au siku hiyo hiyo Press atuambie amewakamata wangapi"
Ni mtazamo wa Wakili William Maduhu akizungumza leo Novemba 5, 2026 kwenye kipindi chetu cha Jambo Asubuhi kinachoanza saa tatu asubuhi mpaka saa tano asubuhi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
"sababu ya @godbless_lema kutoka kuzungumza nje ni kujipinya na kuponya familia yake lakini kama hivyo vitu Lema amezungumza chama kingeamua kuvisema chenyewe inawezekana asingesema hadharani. lakini chama kiliamua kukaa kimya kiliamua kuwalinda wanaharakati dhidi ya Lema"
Anasema @officialskawajr leo kwenye kipindi cha Jambo Asubuhi
Upi mtazamo wako juu ya Press aliyofanya Mjumbe Godbless Lema wa Kamati Kuu ya CHADEMA Novemba 1, 2026 na ukimya wa chama chake.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI:
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimewataka viongozi, wanachama, wafuasi na Watanzania kwa ujumla kujitokeza kwa wingi Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, kushuhudia hukumu ya kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Tundu Antipas Lissu.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa CHADEMA, Brenda Rupia, kupitia taarifa iliyotolewa leo, Alhamisi, Novemba 5, 2026, akieleza kuwa shauri hilo lina umuhimu katika misingi ya haki, utawala wa sheria na demokrasia nchini.
Lissu anakabiliwa na shtaka la uhaini linalohusishwa na madai ya kuhamasisha wananchi kuzuia Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025. Alikamatwa Aprili 9, 2025 na kufunguliwa kesi hiyo katika Mahakama Kuu ya Tanzania.
Agosti 21, 2026, Mahakama iliamua kuwa Lissu ana kesi ya kujibu na kumtaka kuanza kujitetea baada ya upande wa mashtaka kuwasilisha ushahidi wake.
Hukumu hiyo inatarajiwa kutolewa kesho, Ijumaa, Novemba 6, 2026, saa 3:00 asubuhi, mbele ya jopo la majaji watatu likiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru, akishirikiana na Majaji James Karayemaha na Ferdinand Kiwonde.
CHADEMA pia imetoa wito kwa asasi za kiraia, watetezi wa haki za binadamu na demokrasia pamoja na Watanzania wote kujitokeza mahakamani kushuhudia utoaji wa hukumu hiyo. -
Jambo TV
@Jambotv_
Mbunge wa Tarime Vijijini, Mwita Mwikabe Waitara, amekosoa ufafanuzi uliotolewa na serikali kupitia Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, kuhusiana na gharama za ujenzi wa Uwanja wa Arusha, akisisitiza kuwa Serikali haijatoa majibu ya kuridhisha na mapendekezo ya Bunge kuhusu suala hilo yanasimama palepale.
Akizungumza na Jambo TV, Waitara ameeleza kuwa maelezo aliyoyatoa Waziri Makonda hayakuwa majibu ya hoja za ukaguzi zilizowasilishwa na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), kwani hakueleza jinsi Serikali ilivyoboresha au kujibu hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
Waitara amebainisha kuwa kisheria na kikatiba, CAG ndiye jicho la Bunge katika ukaguzi wa fedha za umma. Ameeleza kuwa baada ya CAG kukamilisha ukaguzi na kukabidhi taarifa kwa Rais, ilipelekwa Bungeni ambapo Kamati ya PAC iliwaita wataalamu wa wizarani kujieleza, ikafanya ziara ya ukaguzi eneo la mradi, na hatimaye ikakubaliana na hoja za CAG.
"Kwa mujibu wa Sheria jicho la Bunge kwenye ukaguzi wa PESA ni CAG... Kamati ikiwasilisha taarifa Bungeni hiyo inakuwa taarifa ya Bunge, Waziri akikataa taarifa ya Kamati anakuwa amekataa taarifa ya Bunge… ile siyo namna bora ya kujibu hoja za Bunge," amesema Waitara.
Waitara ameongeza kuwa Bunge bado halijapata ufafanuzi wa kutosha kuhusu jinsi gharama za mradi huo zilivyopanda kutoka zabuni ya awali iliyotangazwa kupitia mfumo wa NeST hadi kufikia mkataba wa Shilingi bilioni 338, huku akirejea ripoti ya CAG iliyoainisha kuwa kuna fedha zililipwa kwa kazi ambazo hazikufanyika.
Pia, Waitara amepinga maelezo yaliyotolewa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Gerson Msigwa, pamoja na Waziri Makonda kuwa ongezeko hilo lilisababishwa na maelekezo ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF).
Akiwa bungeni jijini Dodoma, Waitara alisema endapo Bunge lingekuwa linawajibika ipasavyo, Msigwa na wote waliohusika na mchakato wa matumizi hayo ya fedha kutoka Shilingi bilioni 187 hadi Shilingi bilioni 338 wangekuwa gerezani au kufikishwa mahakamani.
Hata hivyo, Waziri Paul Makonda alitetea ujenzi huo akieleza kuwa Uwanja wa Arusha hauwezi kulinganishwa na Uwanja wa Benjamin Mkapa ambao unakabiliwa na changamoto ya kushindwa kuchezwa mvua inaponyesha.
Makonda alieleza kuwa gharama za Shilingi bilioni 338 zinajumuisha takribani Shilingi bilioni 52 za kodi (kutoka makadirio ya awali ya Shilingi bilioni 107 yasiyo na kodi) na miundombinu ya kisasa kama vile Sky Boxes 21 na lifti sita, huku akisisitiza kuwa mfumo wa manunuzi wa 'Single Source' ni njia halali kisheria. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Amir wa Dola ya Qatar, Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani, asubuhi ya leo Alhamisi, Novemba 5, 2026, ameungana na maelfu ya waumini katika eneo la ibada la Lusail, mjini Lusail, kutekeleza Swala ya Istisqa.
Swala hiyo ya kitaifa imefanyika kufuatia wito uliotolewa na Amir mwenyewe akiwataka Waislamu nchini humo kujitokeza kuomba rehema ya mvua kutoka kwa Mwenyezi Mungu katika kipindi cha ukosefu wa mvua.
Baada ya kumalizika kwa swala hiyo, waumini wamekumbushwa kufanya toba, kuwa na unyenyekevu, kutoa sadaka, pamoja na kuhifadhi maji yanayopatikana.
Maombi hayo yamekuja kutokana na mvua kutonyesha licha ya kuwa tayari wameingia katika kipindi ambacho kwa miaka ya nyuma walizoea kuona mvua ikinyesha kipindi kama hiki.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Serikali imesema inaendelea na maandalizi ya kufufua mchakato wa Katiba Mpya, ikiwemo kukamilisha taratibu za kisheria na kufanya marekebisho ya sheria yatakayowezesha mchakato huo kutekelezwa kwa kuzingatia mwongozo uliotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan.
Akijibu swali la Mbunge wa Tunduru Kaskazini, Ado Shaibu, aliyetaka kujua lini mchakato huo utaanza na utakuwa na sura gani, Bungeni leo Novemba 5, 2026 Waziri Mkuu Mwigulu Nchemba amesema Serikali tayari imepokea mwongozo wa utekelezaji na inaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuuandaa.
Nchemba amesema Katiba Mpya ni suala lenye uzito na umuhimu mkubwa kwa Watanzania, ndiyo maana Serikali imelijumuisha katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM baada ya kujadiliwa na kukubaliwa katika vikao mbalimbali vya chama hicho.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
"Kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu za Bunge hawa wlaiokuwa wanalalamika jana Baba Levo, Waitara walikuwa na uwezo wa kulisukuma Bunge kuunda Kamati teule ya Bunge ikaenda Kuchunguza ikamletea taarifa spika"
Anaeleza Wakili William Maduhu kwenye kipindi chetu cha Jambo Asubuhi kinachoanza saa tatu asubuhi mpaka saa tano asubuhi kinachoruka kwenye YouTube yetu ya Jambo TV.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Ulikuwa unayafahamu majukumu na mamalaka ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG)?
Msikilize Wakili Kulwa William Maduhu akichambua kwenye kipindi chetu cha Jambo Asubuhi kinachoanza saa tatu asubuhi mpaka saa tano asubuhi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini, Clayton Revocatus Chipando maarufu kama Baba Levo, amekataa utetezi uliotolewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, kuhusu ujenzi wa Uwanja wa Arusha akisisitiza kuwa hoja ya ‘kuponda’ Uwanja wa Benjamin Mkapa haina mashiko kwa kuwa viwanja vyote vipo chini ya wizara moja.
Akiieleza Jambo TV kuhusu kama ameridhishwa na ufafanuzi wa Serikali bungeni juu ya ujenzi wa uwanja huo kwa thamani ya Shilingi za Kitanzania bilioni 338, Baba Levo amesisitiza kuwa lengo si kupinga ubora wa mradi huo wa Arusha, bali ni kutaka uwazi kuhusu matumizi sahihi ya fedha za umma, na ndiyo maana akaomba kuwasilishwa kwa nyaraka za mchanganuo wa gharama (BOQ).
“Huwezi kuutetea Uwanja wa Arusha kwa kuuponda wa Mkapa na viwanja vyote vipo kwenye Wizara yako. Sisi hatujakataa kiwanja cha Arusha siyo bora ila tumehoji kuhusu matumizi ya pesa, mwisho tumeomba BOQ,” ameeleza Baba Levo.
Akichangia bungeni jijini Dodoma, Novemba 4, 2026, Baba Levo alihoji uhalali wa ujenzi wa Uwanja wa Arusha unaochukua mashabiki 30,000 kugharimu bilioni 338, wakati Uwanja wa Benjamin Mkapa uliokamilishwa kati ya mwaka 2005 na 2007 kwa uwezo wa mashabiki 60,000 uligharimu kati ya Shilingi bilioni 40 na 63 pekee.
Pia, alirejelea ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), akidai kuwa mkandarasi wa mradi huo alipatikana bila ushindani (Single Source), jambo ambalo lilisababisha ongezeko la gharama za mradi.
Hata hivyo, akijibu hoja hizo bungeni hapo, Waziri Paul Makonda alieleza kuwa Uwanja wa Mkapa hauwezi kulinganishwa moja kwa moja na Uwanja wa Arusha, akitolea mfano changamoto ya uwanja wa zamani kushindwa kuchezeka wakati wa mvua kubwa.
Makonda alifafanua kuwa gharama za mwisho za Shilingi bilioni 338 zinajumuisha takribani Shilingi bilioni 52 za kodi, ambapo makadirio ya awali ya Shilingi bilioni 107 hayakujumuisha kodi hiyo. Aliongeza kuwa kuongezeka kwa gharama kumetokana na kubadilishwa kwa miundombinu kuwa ya kiwango cha kimataifa cha CAF, ikiwemo ujenzi wa Sky Boxes 21 na lifti sita. Aidha, alisisitiza kuwa mfumo wa manunuzi ya Single Source ni halali na unatambulika kisheria, akihitimisha kuwa hakuna fedha nyingine za ziada zitakazohitajika kumaliza mradi huo. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Tumaini jipya limechipuka kwa Angel Wariaeli, binti wa miaka 13 aliyekuwa kitandani kufuatia kupigwa risasi siku ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025 mkoani Dar es Salaam baada ya mfadhili kujitokeza na kuahidi kugharamia matibabu yake yote ndani au nje ya nchi mpaka atakapotembea tena na kutimiza ndoto zake za kuwa daktari.
Angel amechukuliwa kutoka nyumbani kwao Manzese na kupelekwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ambako amepokelewa katika kitengo cha dharura na kuanzishiwa matibabu na vipimo mara moja na madaktari bingwa.
Mfadhili huyo ameahidi kuihamisha familia ya Angel kutoka kwenye nyumba yao ya awali ya Manzese ambayo haikuwa rafiki kwa afya yake na ilikuwa hatarini kuvunjwa muda wowote kwenda kwenye makazi salama, pamoja na kuwagharamia chakula na mahitaji yote ya kila siku.
Madaktari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili wamethibitisha kuanza kutibu vidonda vyake na wameahidi kufanya vipimo zaidi ili kuchunguza uwezo wake wa kutembea tena.
Angel, ambaye alikuwa ametoka kuhitimu darasa la saba na akijiandaa kujiunga na kidato cha kwanza, alipigwa risasi ya bega Oktoba 29, 2025, majira ya saa tisa mchana. Tukio hilo lilitokea maeneo ya nyumbani kwao Manzese alipokwenda kumpelekea dada yake simu kwenye kibanda cha chakula cha familia, ambapo alisikia watu wakikimbia na kisha akapigwa risasi iliyomwangusha chini.
Risasi hiyo iliharibu uti wake wa mgongo na kumfanya ashindwe kutembea au kuendelea na masomo, huku akibaki kulala kitandani tu na kupata vidonda vilivyolazimu asafishwe hospitalini kila Ijumaa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Dorothy Semu ametoa wito wa kuachiliwa huru kwa kiongozi wa kisiasa Tundu Lissu, akieleza kuwa kesi inayomkabili ni ya kisiasa na inahitaji suluhisho la kisiasa.
Amebainisha hayo Novemba 4, 2026 alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika Kata ya Nyarubanda, Jimbo la Kigoma Kaskazini mkoani Kigoma.
“Kesi ya Tundu Antipas Lissu ni kesi ya kisiasa na inahitaji suluhisho la kisiasa na siyo vinginevyo. Iwe iwavyo, sisi tunajua demokrasia itaendelea kupiganiwa," amesema Semu.
Aidha, kuhusu matukio ya Oktoba 29 na siku zilizofuata, Semu amebainisha kuwa umepita mwaka mmoja bila kiongozi yeyote kuwajibika, huku Serikali ikiunda tume mbalimbali ambazo amedai kuwa ni za kujificha kwenye ukweli. Amesisitiza haja ya kuundwa kwa tume huru ya uchunguzi ya kimataifa isiyoegemea upande wowote ili kuweka wazi ukweli wa kilichotokea, kuwapa haki waliopoteza maisha na majeruhi, na kuwawajibisha waliohusika.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Alphaxard Kangi Lugola ameitaka Serikali kurekebisha sheria zinazompa mamlaka Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), ili aweze kuwa na mamlaka ya kiuchunguzi dhidi ya ubadhirifu na matumizi mabaya ya fedha za umma, akisema mamlaka alizonazo sasa hazitoshi.
Lugola ametoa kauli hiyo leo, Novemba 4, 2026, Bungeni jijini Dodoma, wakati akichangia taarifa za Kamati za Kudumu za Bunge za Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), Hesabu za Serikali (PAC) na Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), kuhusu ripoti za CAG, akieleza kuwa kwa sasa CAG anaishia kukagua na kubaini viashiria vya wizi, ubadhirifu na ufisadi, bila kuwa na mamlaka ya kufanya uchunguzi wa kina.
Amesema marekebisho hayo yanapaswa kumpa CAG mamlaka ya kufanya uchunguzi wa kifedha (Forensic Financial Investigation), ikiwemo uwezo wa kuwaita na kuwahoji watuhumiwa pamoja na kukusanya ushahidi wa kina ili kubaini kama kuna makosa ya jinai, akisisitiza kuwa hatua hiyo itaimarisha uwajibikaji katika usimamizi wa fedha za umma.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Tanzania kesho, tarehe 5 Novemba 2026, itawasilisha rasmi taarifa ya mafanikio ya ulinzi wa haki za binadamu mbele ya Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa (UN), jijini Geneva, nchini Uswisi, ikiwa ni sehemu ya Duru ya Nne ya Mapitio ya Hali ya Haki za Binadamu Duniani (Universal Periodic Review- UPR).
Akizungumza jijini Geneva leo, siku moja kabla ya uwasilishaji huo, Waziri wa Katiba na Sheria, Abdallah Hamis Ulega, ameeleza kuwa mapitio hayo yanatoa fursa ya kipekee kwa Tanzania kueleza mafanikio makubwa yaliyopatikana nchini, kuwasilisha utekelezaji wa mapendekezo ya miaka ya nyuma, pamoja na kuthibitisha dhamira ya Serikali ya kuendelea kuimarisha na kulinda haki za binadamu.
Waziri Ulega amebainisha kuwa chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, na kupitia falsafa yake ya Maridhiano, Ustahimilivu, Mageuzi, na Kujenga Upya (4Rs), nchi imepiga hatua kubwa katika kuimarisha misingi ya utawala bora na haki za binadamu.
Taarifa hiyo ya Nne inaainisha hatua zilizotekelezwa katika kipindi cha mwaka 2021/22 hadi 2026, hususan katika maeneo ya utawala wa sheria, upatikanaji wa haki, afya, elimu, majisafi, na miundombinu. Maandalizi ya taarifa hiyo yalihusisha ushirikiano wa karibu kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, yakishirikisha Wizara, Idara, Mahakama, Asasi za Kiraia (AZAKI), taasisi za kidini, na mashirika ya watu wenye ulemavu.
Ushiriki wa Tanzania katika mchakato huu unaendana moja kwa moja na malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, inayolenga kujenga taifa lenye ustawi, haki, ujumuishi, na uwezo wa kujitegemea, huku utu wa binadamu na usawa wa fursa vikiwa misingi mikuu.
Utaratibu wa UPR chini ya Baraza la Haki za Binadamu la UN hutoa fursa kwa nchi zote wanachama kupitia hali ya haki za binadamu kwa misingi ya usawa, kuwasilisha hatua zilizochukuliwa, na kupokea ushauri pamoja na mapendekezo kutoka mataifa mengine ili kuimarisha zaidi utekelezaji wa haki hizo duniani.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu Mwenyekiti wa chama cha ACT Wazalendo Bara, Isihaka Mchinjita amedai kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimefikia hatua ya mwisho kisiasa kutokana na kile alichokieleza kuwa ni kupotea kwa uaminifu, kuongezeka kwa hujuma za ndani, na kushindwa kutatua migogoro yake.
Mchinjita alibainisha hayo Novemba 4, 2026, alipokuwa akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika wilayani Kahama, mkoani Shinyanga akisisitiza kuwa chama tawala hakina tena uwezo wa kujitibu maradhi yake ya kisiasa na badala yake kiko kwenye mkondo wa kuondoka madarakani.
"Hapa walipofika leo CCM hawana dawa ya kutibu maradhi yao. Dawa pekee waliyo nayo ni kulisogelea kaburi... Hiyo ndio dalili ya chama kinachokufa," amesema MchinjitaThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Wananchi wa Kata ya Kidahwe, iliyopo katika Jimbo la Kigoma Kaskazini mkoani Kigoma wameeleza kusononeshwa na kushitushwa na kile wanachodai ni kitendo cha baadhi ya viongozi wa Serikali za Mitaa na watendaji kuwatoza kodi isiyo rasmi pale wanapotaka kuandaa sherehe au kufanya shughuli za kijamii.
Kwa mujibu wa malalamiko ya wananchi hao, kiongozi au mwananchi anapotaka kuandaa sherehe au hata kwenda kumtembelea na kumsalimia mzazi aliyejifungua mtoto, amekuwa akilazimishwa kulipia kiasi cha fedha kinachofikia hadi Shilingi 20,000, jambo ambalo wamelieleza kama kero kubwa inayokiuka haki zao za msingi za kijamii.
Akizungumza leo Novemba 4, 2026 katika mkutano wa hadhara wa Chama cha ACT Wazalendo, katika kata hiyo, Mwenyekiti wa Ngome ya Wanawake wa chama hicho Kitaifa, Janeth Rite, amelaani vitendo hivyo akieleza kuwa kutoza ada yoyote ambayo haijaidhinishwa kisheria au kupitishwa na vyombo halali ni ukiukaji mkubwa wa taratibu za kiutawala.
Rite amefafanua kuwa mamlaka ya maamuzi na usimamizi wa sheria ndogo za halmashauri yapo mikononi mwa madiwani na wabunge waliochaguliwa na wananchi, na wala si watendaji wa vijiji au kata kujitungia tozo zao. Amesisitiza kuwa mtendaji wa kijiji au kata anapaswa kupokea na kutekeleza maelekezo halali kutoka kwa diwani na baraza la madiwani.
Ameongeza kuwa chini ya misingi ya utawala wa ACT Wazalendo, vitendo vya kuwakandamiza wananchi kwa tozo zisizo na msingi wa kisheria havitatatokea wala kuvumiliwa, akisisitiza kuwa kila mwananchi ana haki ya kusherehekea, kutembeleana, na kushirikiana na familia yake bila kushinikizwa kutoa fedha.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Paul Makonda amesema Uwanja wa Benjamin Mkapa hauwezi kulinganishwa na uwanja mpya wa Arusha, akieleza kuwa licha ya gharama za ujenzi kufikia takribani shilingi bilioni 338, hakuna nyongeza nyingine ya fedha itakayohitajika kukamilisha mradi huo.
Makonda ameyasema hayo leo Novemba 4,Bungeni Jijini Dodoma ambapo amesema Uwanja wa Benjamin Mkapa una changamoto ya kushindwa kuchezwa mvua inaponyesha, akitumia hoja hiyo kueleza kuwa viwanja hivyo haviwezi kulinganishwa kwenye viwango.
Aidha, amesema utaratibu wa manunuzi wa 'Single Source' si wizi kama baadhi ya watu wanavyodai, bali ni mojawapo ya taratibu tatu zinazotambuliwa katika mfumo wa manunuzi, hivyo matumizi yake hayapaswi moja kwa moja kutafsiriwa kuwa kuna ubadhirifu. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mbunge wa Jimbo la Tunduru Kaskazini, Ado Shaibu, amesema ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) zimekuwa zikibainisha ubadhilifu na matumizi yasiyo sahihi ya fedha za umma, lakini wahusika hawachukuliwi hatua za kisheria, hali inayochangia kuendelea kwa upotevu wa fedha za Serikali.
Amesema Bunge lina wajibu wa kufuatilia na kuhakikisha watu wanaotajwa katika ripoti hizo wanawajibishwa kwa mujibu wa sheria, badala ya kuendelea kuzichukulia hoja za CAG kama jambo la kawaida (business as usual).
Ametoa kauli hiyo wakati akichangia hoja za kamati mbalimbali za Bunge la 13, Mkutano wa Tano, akieleza kuwa kutokuwapo kwa uwajibikaji kwa waliohusika na ubadhilifu wa fedha katika miradi mbalimbali ya Serikali kunatoa nafasi kwa vitendo hivyo kuendelea.
Ado ameshauri Bunge kutumia mamlaka yake kufuatilia utekelezaji wa mapendekezo ya CAG na kuhakikisha wahusika wanachukuliwa hatua, akirejelea sakata la ESCROW kama mfano unaoonesha umuhimu wa Bunge kusimamia uwajibikaji katika matumizi ya fedha za umma. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
"kuna zaidi ya bilioni 120.48 zimetolewa kwa mwaka fedha 2025 hazijarejeshwa ukisoma sababu wanakuambia vikundi hewa, zingine wanasema Maafisa Maendeleo ya Jamii wanashindwa kwenda kwa wakati wakienda wanakuta hamna vikundi, mnakuta hamna vikundi ambavyo vinatumia NIDA nashindwa kuwatafuta walipo"
Amehoji Mbunge wa Jimbo la Tarime Mjini(CCM) Esther Matiko leo Novemba 4, 2026 bungeni jijini Dodoma kutokana na taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(LAAC) ambayo imeeleza kuwa zaidi ya bilioni 120 zilizotolewa kwenye mikopo ya asilimia 10% hazikurudishwa.
Hata hivyo amesema mikopo hiyo wamekuwa watumishi wakiunda vikundi hewa na kujikopesha jambo lililopolekea kutorejeshwa kwayo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mwigulu Nchemba, ameielekeza Wizara ya Viwanda na Biashara kuhakikisha bidhaa zinazozalishwa nchini zinapewa kipaumbele katika matumizi ya Serikali, ikiwemo miradi ya ujenzi wa majengo, ununuzi wa samani na vifaa mbalimbali, badala ya kutegemea bidhaa kutoka nje.
Mwigulu ametoa maelekezo hayo leo Novemba 4, 2026, jijini Dodoma, wakati wa uzinduzi wa Sera ya Maendeleo Endelevu ya Viwanda ya mwaka 2025 na Sera ya Maendeleo ya Biashara Ndogo na za Kati ya mwaka 2003, toleo la mwaka 2025, ambapo pia ameielekeza Wizara hiyo kupitia sheria na taratibu zinazochochea uagizaji wa bidhaa kutoka nje wakati bidhaa zinazofanana zinazalishwa nchini.
Amesema uwekezaji katika ujenzi wa viwanda hautakuwa na tija iwapo bidhaa zinazozalishwa nchini hazitatumika, akibainisha kuwa matumizi ya bidhaa za ndani yatasaidia kuongeza ajira, mapato ya Serikali na kuimarisha uchumi wa taifa.
Kwa upande wake, Waziri wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga, amesema Serikali imejipanga kuongeza uzalishaji wa bidhaa za ndani, kuongeza thamani ya malighafi zinazopatikana nchini na kupunguza utegemezi wa bidhaa zinazoagizwa kutoka nje.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katibu Wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Kanda ya Pwani Benjamin Ntele, amesema Chama hicho hakina mpango wa kufanya vurugu siku ya kusomwa kwa hukumu ya kesi ya Mwenyekiti wa Chama hicho taifa, Tundu Lissu katika Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Dar es Salaam.
Ntele ameeleza hayo Novemba 4, 2026 alipokuwa akizungumza mbele ya vyombo vya habari jijini Dar es Salaam ikiwa ni taarifa yake baada ya Kamanda wa Polisi Kanda maalumu ya Dar es Salaam Jumanne Muliro Novemba 3, 2026 kuzungumza na umma kupitia vyombo vya habari kuhusu kuelekea siku hiyo ya kusomwa kwa hukumu.
Muliro alisema kwamba Jeshi la Polisi Kanda limepokea taarifa kuwa kuna watu wanahamasishana kutoka maeneo mbalimbali nchini kwenda jijini humo siku ya ijumaa ya Novemba 6, 2026 kwa lengo la ufanya vurugu.
"Wanahamasishana kuja Dar es Salaam baadhi yao wakiwa na malengo ya kufanya fujo au vurugu" Alisema Muliro huku akieleza kuwa mipaka na idadi ya watu wanaotakiwa kuingia mahakamani inafahamika.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
#update - Idadi ya watu waliofariki dunia katika ajali iliyohusisha lori, bajaj na pikipiki aina ya boda boda mkoani Mtwara imeongezeka kutoka watatu hadi saba, baada ya majeruhi wengine wanne kufariki dunia wakati wakipatiwa matibabu.
Ajali hiyo ilitokea jana Novemba 3, 2026, majira ya saa 3:00 asubuhi, katika eneo la Magomeni Kanisani, Manispaa ya Mtwara-Mikinda
Kaimu Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini, Aletas Haule, amesema leo Novemba 4, 2026, kuwa majeruhi wanne kati ya sita waliokuwa wakipatiwa matibabu katika hospitali hiyo wamefariki dunia.
Haule amesema kati ya watu saba waliofariki, wawili walifikishwa hospitalini hapo wakiwa tayari wamepoteza maisha katika eneo la ajali, huku wengine wanne wakitokea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara Ligula.
Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, SACP Issa Suleiman, amesema uchunguzi wa awali umebaini kuwa dereva wa lori anayetajwa kuhusika na ajali hiyo alikuwa ametumia kilevi wakati wa tukio.
Kutokana na ajali hiyo, Kamanda Suleiman amewataka madereva na watumiaji wengine wa barabara kuzingatia sheria za usalama barabarani na kutumia mbinu za udereva wa kujihami ili kupunguza ajali na vifo vinavyoweza kuzuilika.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwanahabari Habibu Mchange, amesisitiza kuwa hakuna taifa duniani linaloweza kufumbia macho masuala ya usalama wa wananchi wake, uvunjifu wa amani na vitendo vinavyohatarisha utulivu wa nchi.
Mchange ameyasema hayo leo, Novemba 4, 2026, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Akizungumzia umuhimu wa kulinda usalama wa taifa na utekelezaji wa sheria, Mchange amerejelea mifano ya Marekani na Hispania, akieleza kuwa hata mataifa yenye misingi imara ya demokrasia huchukua hatua za kisheria dhidi ya watu wanaohusika na vitendo vinavyokiuka sheria na kuhatarisha mifumo ya nchi.
Ametaja tukio la Januari 6, 2021, ambapo wafuasi wa aliyekuwa Rais wa Marekani, Donald Trump, walivamia jengo la Bunge la Congress (Capitol), kufuatia mzozo wa matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2020.
Ameeleza kuwa tukio hilo lilisababisha uchunguzi na mashauri mbalimbali ya kisheria, ambapo baadhi ya washiriki walihukumiwa vifungo vya jela, akiwemo Enrique Tarrio na Stewart Rhodes.
Aidha, amerejelea Hispania mwaka 2017, wakati viongozi wa Catalonia walipoendesha mchakato wa kutaka eneo hilo lijitenge na Hispania, hali iliyosababisha hatua za kikatiba na kisheria dhidi ya baadhi ya viongozi waliohusika.
Kwa mujibu wa Mchange, mifano hiyo inaonesha umuhimu wa kila taifa kulinda sheria, amani na usalama wa wananchi wake, akisisitiza kuwa hakuna nchi inayopaswa kufanya mzaha na masuala hayo.
Hata hivyo, amebainisha kuwa utekelezaji wa sheria unapaswa kuzingatia haki, katiba na misingi ya utawala bora, kwa kuwa amani na utulivu ni nguzo muhimu za nchi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini, Clayton Revocatus Chipando maarufu kama Baba Levo, amesema Sh bilioni 338 zinazotajwa kutumika katika ujenzi wa Uwanja wa Arusha zingeweza kujenga viwanja vingine vitano hadi sita vyenye hadhi na uwezo unaofanana na Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Akizungumza leo, Novemba 4, 2026, Bungeni jijini Dodoma, Chipando ameitaka Wizara husika kuwasilisha bungeni nyaraka za makadirio ya gharama za ujenzi (BOQ) ili wabunge wazichunguze na kubaini gharama halisi za vifaa vilivyotumika, ikiwemo ununuzi wa nyasi za uwanja huo, na kuzilinganisha na bei za soko.
Amesema Uwanja wa Benjamin Mkapa, uliojengwa kati ya mwaka 2005 na 2007 kwa gharama ya Sh bilioni 40 hadi 63, una uwezo wa kuchukua mashabiki 60,000, wakati Uwanja wa Arusha unaojengwa ukiwa na uwezo wa kuchukua mashabiki 30,000 pekee, licha ya gharama yake kutajwa kufikia Sh bilioni 338.
Aidha, amesema kwa mujibu wa taarifa za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), mkandarasi aliyepewa zabuni ya ujenzi wa Uwanja wa Arusha alipatikana bila kuwepo kwa ushindani, akieleza kuwa hali hiyo imechangia ongezeko la gharama za mradi kwa zaidi ya Sh bilioni 151.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
"Tuna pambana kuhakikisha mawakili wanapatikana kwaajili ya kuwapa msaada wa kisheria, jana kesi ya Colletha inakuwa kesi ya 21. Ni kesi ya 20 kwa maana ya kesi za wanachama ambao walipewa kesi za ugaidi hapa nchini" amesema Wakili Garubindi.
Mkurugenzi wa Sheria na Haki za Binadamu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wakili Gaston Shundo Garubindi, amesema hayo leo Novemba 4, 2026 kwa njia ya simu ndani ya kipindi Cha Jambo Asubuhi, kinachorushwa na Jambo Tv.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
-
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mbunge wa Tarime Vijijini, Mwita Waitara, amesema Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa, pamoja na wengine waliohusika katika mchakato wa ujenzi wa Uwanja wa Arusha, walipaswa kuchukuliwa hatua za kisheria, ikiwemo kufungwa jela, iwapo Bunge lingekuwa linawajibisha ipasavyo.
Waitara ameyasema hayo leo, Novemba 4, 2026, wakati akichangia mjadala wa Bunge jijini Dodoma, akizungumzia ongezeko la gharama za ujenzi wa uwanja huo kutoka Sh bilioni 187 hadi Sh bilioni 338.
Amehoji maelezo yanayohusisha ongezeko hilo la gharama na maelekezo ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF), akisisitiza kuwa waliohusika katika maamuzi ya matumizi ya fedha hizo wanapaswa kuwajibishwa.
Amesema nchi inapitia wakati mgumu kiuchumi, hivyo ni muhimu kuhakikisha kuwa wote watakaobainika kuhusika na ubadhirifu au matumizi yasiyo halali ya fedha za mradi huo wanafikishwa mahakamani na kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkurugenzi wa Sheria na Haki za Binadamu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wakili Gaston Shundo Garubindi, amesema wanaendelea kuamini kwamba watu wote wanaoshtakiwa kwa makosa mbalimbali ikiwemo ni kutokana na sababu za kisiasa.
Wakili Garubindi amesema hayo leo Novemba 4, 2026 kwa njia ya simu ndani ya kipindi Cha Jambo Asubuhi, kinachorushwa na Jambo Tv. Amesema kwamba hata lengo la kufunguliwa kwa kesi hizi ni kwaajili ya "kuwakomoa".
"Msimamo wa Chadema, Jambo la kwanza kabla hatujafanya hata hiyo misimamo sisi always tunachoamini ni kwamba watu wote wanaoshtakiwa kwa sababu tunawafahamu tunajua hawajafanya makosa hayo. Kwahiyo msimamo wetu sisi ni kwamba kesi hizi ni kesi za kisiasa na zimefunguliwa kwa msukumo wa kisiasa kwa lengo la kuwakomoa"
Amesema katika kesi hizo hakuna mwananchi wa kawaida anayekamatwa na "kupewe" kesi hizo bali wanaokamatwa na kupewa hizo kesi kwanini wawe ni wanachama wa Chama kimoja?.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
"Mahakama Kuu ilitoa uamuzi mdogo kwenye maombi ambayo mawakili wa Colletha waliwasilisha kwenye Mahakama Kuu ya Tanzania, wakiomba colletha apewe dhamana ya Jeshi la Polisi au afikishwe mahakamani kwa sababu anashikiliwa kinyume cha sheria, kwa sababu alikuwa anashikiliwa tangu tarehe 14, mwezi wa kumi".
Ameongeza kwamba "katika uamuzi wake Mahakama jana ilikubaliana na maombi ikasema anashikiliwa kinyume na utaratibu regadless upelelezi wa Jeshi la Polisi umekamilika au haujakamilika na Mahakama ikaelekeza aweze kufikishwa mahakamani au apewe dhamana ya Polisi..., sasa masaa machache jana baada ya uamuzi huo Jeshi la Polisi wakaamua kumpeleka mahakamani na wakamshtaki kwa makosa ya ugaidi" amesema Wakili Garubindi.
Mkurugenzi wa Sheria na Haki za Binadamu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wakili Gaston Shundo Garubindi, amesema hayo leo Novemba 4, 2026 kwa njia ya simu ndani ya kipindi Cha Jambo Asubuhi, kinachorushwa na Jambo Tv.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) imebaini kuwa Halmashauri za Majiji ya Mwanza na Dodoma zimetumia fedha nyingi zaidi ya bajeti zilizoidhinishwa kwa ajili ya kugharamia timu zao za mpira wa miguu, Pamba Jiji FC na Dodoma Jiji FC.
Akiwasilisha taarifa ya Kamati kuhusu ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) za miaka ya fedha 2023/2024 na 2024/2025, Bungeni, jana Novemba 3, 2026, Mwenyekiti wa LAAC, Ado Shaibu, alisema Halmashauri ya Jiji la Mwanza ilitumia Shilingi bilioni 1.48 kugharamia Pamba Jiji FC, licha ya kutokuwa na fungu la matumizi hayo katika bajeti ya mwaka iliyoidhinishwa.
Shaibu aliongeza kuwa hali kama hiyo imebainika pia katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, ambayo ilitenga Shilingi milioni 745 kwa ajili ya Dodoma Jiji FC, lakini matumizi halisi yalifikia Shilingi bilioni 1.17, sawa na ongezeko la Shilingi milioni 427.70 zaidi ya bajeti.
Alisema matumizi hayo yanakiuka Aya ya 21.9(b) ya Mwongozo wa Uhasibu wa Mamlaka za Serikali za Mitaa wa mwaka 2019, unaowataka Makatibu Hazina kuhakikisha matumizi ya fedha hayaendi zaidi ya kiwango kilichoidhinishwa.
Katika uchambuzi wake, Kamati imeeleza kuwa matumizi yanayozidi bajeti yanaashiria udhaifu katika mifumo ya Halmashauri ya kusimamia na kufuatilia matumizi ya fedha za umma, hali inayoweza kuathiri utekelezaji wa shughuli nyingine zilizopangwa.
Kutokana na hali hiyo, LAAC imezitaka Halmashauri husika kuimarisha mifumo ya udhibiti na ufuatiliaji wa matumizi ya fedha za umma ili kuhakikisha Maafisa Masuuli wanasimamia matumizi kwa kuzingatia bajeti zilizoidhinishwa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
"Leo wamachinga wanafukuzwa kila kona, ACT Wazalendo tunataka Serikali iachane na kucheza na maisha ya vijana, maisha ya wamachinga na isiwageuze raia wake kuwa ni takataka kwenye miji. Tunataka Serikali, lazima ihakikishe kwamba ukuaji wa miji unakuwa ni fursa kwa watu wote".
Ameongeza kwamba "hatuwezi kuwa na miji ambayo inapokuwa na kutengeneza fursa za ajira, Serikali inakuja inawagawanya watu, inafukuza vijana wafanyabiashara ndogondogo, inaleta wafanyabiashara wakubwa kwa maslahi ya wao wenyewe" amesema Mchinjita.
Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo, Isihaka Mchinjita, amesema hayo Novemba 3, 2026 alipokuwa akizungumza na wanachi wa Katoro mkoani Geita kupitia Mkutano wa hadhara uliofanywa eneo hilo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Naibu Katibu Mkuu wa Haki za Binadamu wa Chama cha ACT Wazalendo, Mbarala Abdallah Maharagande, ambaye pia ni Katibu wa Msafara wa ziara ya Kiongozi wa chama hicho, Dorothy Semu, amesema ACT Wazalendo ina kazi za kujivunia katika Manispaa ya Ujiji mkoani Kigoma kutokana na maendeleo yaliyopatikana wakati chama hicho kilipokuwa kikiiongoza Halmashauri hiyo.
Maharagande amebainisha hayoNovemba 3, 2026 alipokuwa akizungumza na wananchi wa Kata ya Kasimbu mkoani humo, kupitia mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa Mwembe Mmoja ambapo amesisitiza haja ya madiwani kuendeleza kasi ya maendeleo iliyowekwa awali.
Maharagande ametaja miongoni mwa mafanikio hayo ni ujenzi wa soko la Muanga, ujenzi wa barabara za lami, ujenzi wa bandari ya Ujiji pamoja na mualo wa Katuga. Aidha, ameeleza kuwa serikali ya manispaa iliyokuwa chini ya ACT Wazalendo ilitekeleza programu za bima kwa wakulima na wavuvi, pamoja na usomeshaji wa wanafunzi wa kidato cha tano na sita ndani ya manispaa hiyo chini ya uongozi wa Zitto Kabwe.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo @ChademaTZ2 John Mnyika @jjmnyika amefika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kufuatilia na kusikiliza kesi ya uhaini inayomkabili Mkurugenzi wa Organaizesheni na Mafunzo wa chama hicho John Pambalu. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI:
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Kigoma, Colletha Glavery Ntidyicha amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam na kusomewa mashtaka ya kushauri umma kushiriki katika vitendo vya kigaidi.
Colletha alifikishwa mahakamani hapo Novemba 3, 2026 akidaiwa kutenda kosa hilo katika tarehe mbalimbali kati ya Agosti 1 na Oktoba 23, 2026, ndani ya Jiji na Mkoa wa Dar es Salaam.
Hati hiyo inaeleza kuwa mshtakiwa anadaiwa kuushawishi umma katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kushiriki katika vitendo vya kigaidi, ikiwemo kufanya uharibifu mkubwa wa mali kwa lengo la kuyumbisha kwa kiasi kikubwa mifumo ya msingi ya kisiasa, kikatiba, kiuchumi na kijamii ya nchi.
Shtaka hilo limewasilishwa chini ya Sheria ya Kuzuia Ugaidi, Sura ya 19, Toleo la 2023, ikisomwa pamoja na Sheria ya Udhibiti wa Uhalifu wa Kiuchumi na Kupangwa, Sura ya 200, Toleo la 2023. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mbunge wa Mtwara Vijijini (CCM), Arif Suleiman Premji, ameonesha kusikitishwa na udhaifu pamoja na mianya ya upotevu wa fedha iliyobainika katika Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), akieleza kuwa ukichunguza kwa kina hoja na mapungufu yaliyoibuliwa katika vitabu vyote vitano vya ripoti hiyo, mtu anaweza kupata msongo wa mawazo.
Premji ameyasema hayo Novemba 3, 2026, bungeni jijini Dodoma wakati akichangia hoja na ripoti za Serikali kufuatia ukaguzi wa hesabu za umma. Ameeleza kuwa kuna hoja za miaka mingi ambazo hadi sasa hazijapatiwa ufumbuzi.
“Kuna msemo anasema ukishaonja asali huwezi kuiacha mpaka uwekewe tindikali. Moja ni kwenye ‘revenue management (usimamizi wa mapato); ripoti nzima inaonesha kwamba revenue management tuna shida kwenye usimamizi wa mapato”, ameeleza.
Mbunge huyo ameanika takwimu za upotevu wa fedha hizo akibainisha kuwa baadhi ya halmashauri zilikusanya shilingi bilioni 1.67 na kutozifikisha benki, huku shilingi bilioni 5.34 zikipotea kutokana na utaratibu mbovu wa ukusanyaji mapato, na shilingi bilioni 10.28 zikihusisha mawakala wa ukusanyaji mapato.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Arusha, Elisa Mungure, amesema Chama hicho kinahitaji maridhiano ya haki na si maridhiano ya ulaghai wala kitapeli, akisisitiza kuwa hadi sasa mazingira ya maridhiano hayo bado hayajapatikana na kwamba wasemaji kuhusu maridhiano kutoka katika Chama hicho ni Makamu Mwenyekiti Bara John Heche pamoja na Katibu Mkuu John Mnyika.
Akizungumza na Jambo TV Novemba 3, 2026, Mungure amesema kabla ya kuzungumzia maridhiano, kipaumbele cha kwanza ni Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, kuwa huru ili aweze kutoa maelekezo kuhusu utaratibu wa maridhiano hayo.
Aidha, amesisitiza kuwa viongozi wa CHADEMA katika ngazi za mikoa, wilaya na kata wanafuata maamuzi ya Kamati Kuu, akiwataja Katibu Mkuu John Mnyika na Makamu Mwenyekiti wa Bara John Heche kuwa miongoni mwa viongozi wenye mamlaka ya kueleza msimamo wa chama kuhusu suala hilo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, John Heche, amesisitiza kuwa kumbukumbu ya tarehe 29 Oktoba ni tukio muhimu la kihistoria linaloonesha thamani kubwa ya uhai wa binadamu, huku akiahidi kuwa chama hicho kitaendelea kuadhimisha siku hiyo kila mwaka.
Heche ameyasema hayo leo, Novemba 3, 2026, wakati akihutubia katika maadhimisho ya kumbukizi ya mwaka mmoja ya mauaji ya Oktoba 29, 2025, yaliyoandaliwa na CHADEMA.
Akiwasilisha maelezo yake kuhusu umuhimu wa kuwakumbuka waliopoteza maisha wakipigania demokrasia, Heche ametolea mfano mataifa yaliyoendelea ambako minara na nembo za heshima hutumiwa kuwakumbuka watu waliotangulia ili kujifunza na kutorudia makosa ya zamani.
Ameeleza kuwa kila mwanadamu ana mchango na uwezo mkubwa wa kubadilisha dunia, akibainisha kuwa miongoni mwa watu waliouawa huenda kulikuwa na wavumbuzi wenye uwezo wa kugundua vitu vikubwa kwa ajili ya kuokoa dunia.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Wakili Peter Madeleka @PMadeleka amesema kuwa @ChademaTZ2 hawajui wanaitwa kwenye meza ya maridhiano kuridhiana kuhusu nini, akisisitiza kuwa taifa linahitaji kwanza ukweli, haki na uwajibikaji kuhusu vifo vya watu vilivyotokea wakati na baada ya Oktoba 29, 2026.
Madeleka akizungumza kwenye kipindi cha Jambo Asubuhi cha Jambo TV Novemba 2, 2026, amesema kuwa CHADEMA haijakataa maridhiano, bali imeweka sharti la Tundu Lissu kuachiwa huru ili aweze kushiriki katika mchakato huo.
Upi mtazamo wako?This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Heche, amesema kuwa chama hicho hakitanyamaza wala kufutika licha ya kile alichokiita vitisho, ukamataji, na mateso dhidi ya viongozi wake, akisisitiza kuwa "CHADEMA ni ukweli, na huwezi kuua ukweli".
Heche amesema hayo usiku wa Novemba 3, 2026, jijini Dar es Salaam, alipokuwa akizungumza kwenye maadhimisho ya mwaka mmoja wa mauaji yaliyojitokeza wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, John Heche, amezitaka mamlaka zilizopo madarakani kutoka hadharani, kuomba radhi, na kulipa fidia kwa familia za waliouawa na majeruhi wa matukio ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.
Heche ameyasema hayo leo, Novemba 3, 2026, wakati akizungumza katika maadhimisho ya kumbukizi ya mwaka mmoja wa mauaji ya Oktoba 29, 2025, yaliyoandaliwa na chama hicho.
Akiwasilisha msimamo wake kuhusu haja ya kuwa na ukweli, haki, na uwajibikaji, Heche amezisihi mamlaka kurudi nyuma mapema na kuweka wazi kilichotokea pamoja na waliohusika na matukio hayo.
"Ni suala la muda tu kuendelea kuwakandamiza Watanzania, Watanzania hawatakubali kamwe. Na mimi natumia nafasi hii usiku wa leo kuwasihi warudi nyuma ingali mapema. Moja, watoke hadharani waombe radhi”, ameeleza Heche.
Heche ameeleza kuwa wananchi wamebaki na majeraha makubwa huku wengine wakiishi na risasi mwilini kutokana na matukio ya Oktoba 29, 2025.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mnyika, ameitaka Serikali kuruhusu uchunguzi huru wa kimataifa na wa kitaifa ufanyike kufuatia matukio ya mauaji ya Oktoba 29, 2025, huku akisisitiza kuwa familia za wahanga wa mauaji hayo pamoja na majeruhi wanapaswa kulipwa fidia.
Mnyika ameyasema hayo leo, Novemba 3, 2026, wakati wa maadhimisho ya kumbukizi ya mwaka mmoja wa mauaji ya Oktoba 29, 2025, yaliyoandaliwa na CHADEMA
“Tumeendelea kusisitiza wakati wote katika mambo haya ya mauaji ya Oktoba 29 na siku zilizofuatia tunataka ufanyike uchunguzi huru wenye kuhusisha vyombo huru vya kimataifa na wadau huru wa kitaifa ili ukweli ukijulikana na haki itendeke, na tumetaka wakati wote wahanga wa mauaji, familia zao zilipwe fidia na wale waliojeuriwa waweze vilevile kulipwa fidia”, ameeleza Mnyika.
Aidha, Mnyika ametoa rai kwa wanachama wa CHADEMA wa Dar es Salaam na nchi nzima kujitokeza kwa wingi mahakamani tarehe 6 Novemba, 2026 kusikiliza na kumuunga mkono mwenyekiti wa chama hicho Tundu Lissu, ambapo uamuzi wa shitaka lake la uhaini utafanyika siku hiyo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Dorothy Semu ameitaka serikali kuhakikisha uwajibikaji, haki na ukweli kuhusu matukio ya Oktoba 29, akisema watanzania wengi wamekata tamaa na siasa na wanaishi kwa hofu.
Semu ameyasema hayo jioni ya leo Novemba 3, 2026 katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kata ya Kasimbu, Uwanja wa Mwembe Mmoja mkoani Kigoma.
Amesisitiza kuwa uchaguzi haupaswi kuwa sababu ya kupoteza maisha, bali ni kitendo cha kujivunia cha kuchagua viongozi bila vitisho. Amedai kuwa mwaka mmoja baadaye hakuna mtu aliyewajibishwa, na badala yake serikali inawatafuta waandamanaji ambao walikuwa na haki ya kikatiba ya kuandamana.
Semu ametaka serikali iunde tume huru ya kimataifa kuchunguza matukio hayo, iwaachilie huru wafungwa wote wa kisiasa akiwemo Tundu Lissu, itoe ratiba wazi ya mchakato wa katiba mpya ya wananchi, na ifanye mapitio ya sheria zinazozuia demokrasia ili Watanzania wafurahie demokrasia na uhuru huo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Dorothy Semu ameitaka Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuumiza kichwa na kuchukua hatua za haraka za kuboresha maisha ya Watanzania wa hali ya chini, huku akikosoa mchakato wa ununuzi wa mafuta na kile alichokiita tozo nyingi zinazozidi kuwaumiza wananchi.
Semu ameyasema hayo jioni ya leo Novemba 3, 2026 katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kata ya Kasimbu, Uwanja wa Mwembe Mmoja mkoani Kigoma, ambapo amedai kuwa Serikali imemsahau Mtanzania wa kawaida ambaye kwa sasa anahaha na ugumu wa maisha na hatari ya kukosa hata mlo mmoja
"Upande wa mafuta ya nishati. Kisingizio cha vita sio kisingizio sahihi. Usahihi ni kwamba serikali imeachia ununuzi wa mafuta umekuwa ununuzi wa kiholela, ununuzi usiomzingatia mlaji wa mwisho, ununuzi unaokwenda kuwaneemesha watu wachache. Lakini serikali imeweka tozo kubwa inayoelemea bei ya mafuta, kuna tozo mbalimbali. Haya mafuta yanapotufikia tayari yameshaongezwa tozo mbalimbali zaidi ya tozo 19... Na mtu anayekwenda kubeba gharama ya hizi tozo ni mlaji wa mwisho ambaye ni mimi na wewe", ameeleza.
Aidha, Semu ameihimiza Serikali kuingilia kati udhibiti wa bidhaa muhimu za ujenzi na chakula, akiitaka isimamie kikamilifu uingizaji wa sukari na simenti ili kuhakikisha bei za bidhaa hizo zinashuka na kumwezesha mwananchi wa hali ya chini kumudu maisha.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Naibu Waziri Mkuu Kivuli wa Chama cha ACT Wazalendo, Luhaga Mpina ameshangazwa na baadhi ya hospitali nchini kuzuia miili ya marehemu kuchukuliwa na ndugu zao kutokana na madeni ya gharama za matibabu, akibainisha kuwa mwananchi anayefariki alikuwa mlipakodi mzuri aliyeichangia nchi mabilioni ya fedha za kodi.
Mpina ameyasema hayo leo, Novemba 3, 2026, alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara na wananchi wa Jimbo la Katoro, Wilayani Geita mkoani Geita, ikiwa ni sehemu ya ziara ya Chama cha ACT Wazalendo katika Kanda ya Ziwa ambapo ameeleza kuwa hali hiyo ni matokeo ya serikali iliyopo madarakani kushindwa kusimamia vizuri fedha za umma zinazokusanywa kutoka kwa wananchi.
“Mnakusanya kodi za wananchi mabilioni ya fedha, matrilioni ya fedha. Huyu mwananchi aliyefariki huyu alikuwa ni mlipa kodi mzuri tu... Waganga wa kienyeji hawatozi kodi kwa marehemu kwasababu wanajua kwamba huyu alikuja kutibiwa apone, amefariki alipe tena hela? Ni mambo ya kushindwa kusimamia fedha za umma", ameeleza Mpina.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Stephen Wasira, amewataka wanasiasa na wanaharakati nchini kuendesha mijadala ya kisiasa kwa kutumia hoja zenye tija badala ya kutegemea matusi na uchochezi, akisisitiza kuwa CCM haina uhasama na chama chochote cha upinzani nchini.
Wasira aliyasema hayo leo, Novemba 3, 2026, wakati akihutubia wananchi katika mkutano wa kufunga kampeni za mgombea ubunge wa CCM katika Jimbo la Chamwino, mkoani Dodoma. Ameeleza kuwa chama hicho tawala hakikatai kukosolewa, bali kinakaribisha ukosoaji wenye kujenga unaolenga kuonesha mapungufu ili yafanyiwe kazi, badala ya kutumia mitandao ya kijamii kutoa lugha za matusi dhidi ya viongozi.
Katika hotuba yake, Wasira amegusia suala la wanaharakati na kueleza kuwa amekubaliana na baadhi ya hoja zilizowahi kutolewa na mwanasiasa wa CHADEMA, Godbless Lema kuhusu uwepo wa baadhi ya wanaharakati walioko nje ya nchi. Amebainisha kuwa mnamo Januari 25, 2025, baadhi ya wanaharakati hao walishiriki katika uchaguzi wa CHADEMA kwa lengo la kumwondoa Freeman Mbowe na kumweka Tundu Lissu.
Ameongeza kuwa, kwa mujibu wa maelezo ya Lema, baada ya kufanikisha mabadiliko hayo, wanaharakati hao walianza kuingilia uendeshaji wa chama hicho kwa kutoa maelekezo, amri, na wakati mwingine kuvuka mipaka kwa kutoa matusi dhidi ya viongozi wa CHADEMA bila sababu za msingi.
“Tunataka wanaharakati wa hoja, si wanaharakati wa kutukana. Wanatusaidia pale wanapotuambia mmefanya makosa haya na haya, sisi hatukatai kukosolewa,” amesisitiza Wasira, akiongeza kuwa hata kama mtu ni mpinzani au mpinzani wa kisiasa, anapozungumza jambo la kweli anapaswa kusikilizwa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Ukombozi wa Umma ((CHAUMMA), Benson Kigaila amewataka mawakala wa chama hicho kuhakikisha hawatoki katika vituo vya kupigia kura ili kusimamia na kulinda kura zao hadi matokeo yatakapotangazwa.
Kigaila ameyasema hayo leo Novemba 3, 2026, katika Kata ya Dabalo, Jimbo la Chamwino jijini Dodoma, wakati wa kufunga kampeni za chama hicho, ambapo amewataka mawakala kujiandaa kwa siku ya uchaguzi kwa kula vyakula visivyowalazimu kwenda chooni mara kwa mara. Amesema, "Kesho tule vyakula vikavu ili tusiende chooni mara kwa mara, tuhakikishe kura zetu zinapigwa, zinalindwa na zinatangazwa."
Kwa upande wake, mgombea ubunge wa Jimbo la Chamwino kupitia CHAUMMA, Mathias Nyakapala, amesema endapo atachaguliwa atapigania uboreshaji wa miundombinu ya barabara pamoja na huduma za kijamii. Uchaguzi mdogo wa ubunge katika Jimbo la Chamwino unatarajiwa kufanyika kesho, Novemba 4, 2026.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Naibu Waziri Mkuu Kivuli wa Chama cha ACT Wazalendo, Luhaga Mpina ametoa wito kwa wananchi kuikataa na kuifuta Chama Cha Mapinduzi (CCM), akidai kuwa chama hicho kimepoteza uwezo wa kuisimamia Serikali na badala yake kimebaki na kazi ya kuipongeza tu.
Mpina ameyasema hayo leo, Novemba 3, 2026, alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara na wananchi wa Jimbo la Katoro, Wilayani Geita mkoani Geita ikiwa ni sehemu ya ziara ya Chama cha ACT Wazalendo katika Kanda ya Ziwa.
Akiwasilisha maelezo yake mbele ya wananchi, Mpina ameeleza kuwa vipimo vyote vinaonesha kuwa CCM haina tena uwezo wa kuisimamia Serikali iliyopo madarakani kwa sababu viongozi walioko serikalini ndio hao hao walioko ndani ya chama.
"Haya yote tuliyoyapitia ndugu zangu lazima tukubaliane mambo matatu yafanyike. Moja wananchi kuikataa CCM. Wananchi ikataeni CCM kwa vipimo hivi vyote tulivyovipima. Ina serikali ambayo haiwezi kuisimamia, kazi yake kuipongeza. Haina uwezo tena wa kuisimamia serikali kwasababu ni wale wale walioko serikalini ni haohao, walioko kwenye chama ni haohao", ameeleza Mpina.
Mpina amewakaribisha wananchi kujiunga na ACT Wazalendo au vyama vingine vya siasa ili kupata ukombozi wa kweli, akibainisha kuwa hata wasiotaka kujiunga na chama chochote ni heri kukaa bila chama kuliko kuendelea kubaki CCM.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mbunge wa Jimbo la Segerea Jijini Dar es Salaam kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Agnesta Lambart Kaiza amewataka wananchi wa Kata ya Dabalo jijini Dodoma kutokubali kushawishiwa kwa rushwa akisisitiza kuwa wanapaswa kuwa imara, kuepuka propaganda na kufanya maamuzi sahihi kwa maslahi ya maendeleo yao.
Agnesta ameyasema hayo leo Novemba 3, 2026, wakati wa kufunga kampeni za mgombea ubunge wa CHAUMMA katika Jimbo la Chamwino Kata ya Dabalo, Mathias Nyakapala, ambapo amewataka wananchi kutambua thamani ya kura zao na kutoruhusu fedha kidogo kuamua hatima ya maisha yao.
Aidha, amesema hatima ya ushindi na mabadiliko wanayoyahitaji iko mikononi mwa wananchi wenyewe, hivyo amewahimiza kutumia haki yao ya kidemokrasia kwa kuchagua viongozi wanaoamini wanaweza kuwaletea maendeleo katika uchaguzi mdogo wa Ubunge wa Jimbo hilo utakaofanyika kesho Novemba 4, 2026.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Stanslaus Nyongo, amesema atayafuatilia kwa karibu madai yanayotolewa na wananchi kuhusu baadhi ya viongozi wa serikali na askari polisi kuhongwa na wafugaji wanaohusika na migogoro ya ardhi wilayani Bagamoyo, huku akisisitiza kwa mkazo kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan hainunuliwi na mtu yeyote.
Nyongo ametoa kauli hiyo leo, Novemba 3, 2026, alipokuwa akizungumza na wakulima wa Kijiji cha Fukayosi, kilichopo katika Halmashauri ya Mji wa Bagamoyo, baada ya kusikiliza kero na malalamiko yao mazito kuhusu migogoro ya muda mrefu kati yao na wafugaji.
Katika mkutano huo, wakulima walieleza kuwa hali imefikia hatua mbaya ya kuhatarisha maisha yao baada ya mifugo ya wafugaji kulishwa kwenye mashamba yao na kuharibu mazao, huku wakidai kuwa wanapojaribu kufuatilia haki zao hukutana na vitisho na vipigo. Mmoja wa wakulima amedai kuwa baadhi ya wafugaji hutumia silaha za jadi kama mikuki, mapanga, na marungu kuwashambulia wakulima.
Aidha, wananchi hao wameeleza hofu yao kubwa wakidai kuwa licha ya kupeleka malalamiko yao katika mamlaka mbalimbali, baadhi ya kesi hazifanyiwi kazi ipasavyo kutokana na madai ya wafugaji kwamba wamewanunua viongozi kuanzia ngazi ya kitongoji, kijiji, hadi wilaya, pamoja na baadhi ya askari polisi.
Akijibu malalamiko hayo, Nyongo amethibitisha kupokea taarifa hizo na kuahidi kuzifuatilia moja baada ya nyingine ili kubaini ukweli, akionya kuwa hatasita kuwachukulia hatua kali za kisheria viongozi au watumishi wa umma watakaobainika kujihusisha na vitendo vya rushwa na kulinda wafugaji wanaokiuka sheria.
Katika hatua ya kuchukua suluhu ya kudumu, Nyongo amemuelekeza Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Shaibu Ndemanga, pamoja na mamlaka husika, kuunda mara moja kamati za kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji, ambazo zitaweka utaratibu mzuri na adhabu thabiti za kukabiliana na ukiukaji wa sheria.
Pamoja na hayo, aliwaonya wakulima na wafugaji dhidi ya kujichukulia sheria mkononi, akiwataka wakulima kutowajeruhi wafugaji wala mifugo yao, na kuwakumbusha wafugaji kuacha tabia ya kuvamia mashamba na kuwadhuru wamiliki wake.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila ameipongeza Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kwa kufanya matengenezo kinga katika bomba kuu la maji linalosafirisha maji kutoka Mtambo wa Uzalishaji Maji wa Ruvu Chini, hatua inayolenga kuimarisha upatikanaji wa huduma hiyo wakati wa mvua kubwa zinazotarajiwa kunyesha kutokana na El Niño.
Chalamila amesema hayo leo baada ya kutembelea na kukagua kazi za matengenezo katika bomba hilo lenye kipenyo cha inchi 72, lililopo eneo la Mpiji, Wilaya ya Bagamoyo, Mkoa wa Pwani.
Amesema huduma ya maji ni muhimu kwa maisha ya wananchi na shughuli za kiuchumi jijini Dar es Salaam, hivyo ni muhimu kuchukua hatua za mapema kuimarisha miundombinu ili iweze kuhimili changamoto zinazoweza kusababishwa na mvua kubwa.
Amesema DAWASA imechukua hatua sahihi kwa kufanya matengenezo hayo kabla ya mvua kubwa kuanza, kwani uharibifu wa bomba hilo au miundombinu inayolizunguka wakati wa mvua ungeweza kuathiri kwa kiwango kikubwa upatikanaji wa maji kwa wananchi.
“Niwapongeze DAWASA kwa kuchukua tahadhari za mapema. Inawezekana wakati wa mvua kubwa ukarabati huu usingewezekana kufanyika na hali hiyo ingeathiri upatikanaji wa huduma ya maji. Nitoe rai kwa wananchi wanaohudumiwa na bomba hili kuanzia ukanda wa Bagamoyo hadi Ilala kuwa wavumilivu kutokana na kupungua kwa kiwango cha upatikanaji wa maji,” amesema Chalamila.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya DAWASA, Mhandisi Romanus Mwangingo, amemshukuru Chalamila kwa kutembelea na kukagua maendeleo ya matengenezo hayo, akisema ni sehemu ya mikakati ya kuimarisha miundombinu na kuzuia madhara yanayoweza kujitokeza wakati wa mvua kubwa.
Amesema kazi ya matengenezo itaanza Jumanne, Novemba 3,2026 na inatarajiwa kukamilika ndani ya saa 96 ambayo ni Novemba 6,2026 ambapo huduma ya maji inatarajiwa kurejea katika hali yake ya kawaida ifikapo Ijumaa jioni.
Ameeleza kuwa matengenezo hayo ni muhimu katika kuhakikisha bomba kuu linaendelea kufanya kazi kwa ufanisi na kuwa na uwezo wa kuhimili changamoto zinazoweza kusababishwa na mvua kubwa.
DAWASA imewaomba wananchi wanaotegemea maji kutoka bomba hilo, hususan katika maeneo ya Bagamoyo hadi Ilala, kuwa wavumilivu wakati wa matengenezo hayo, huku Mamlaka ikiendelea kusimamia kazi hizo ili zikamilike kwa wakati na huduma irejee kama ilivyopangwa -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila ameipongeza Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kwa kufanya matengenezo kinga katika bomba kuu la maji linalosafirisha maji kutoka Mtambo wa Uzalishaji Maji wa Ruvu Chini, hatua inayolenga kuimarisha upatikanaji wa huduma hiyo wakati wa mvua kubwa zinazotarajiwa kunyesha kutokana na El Niño.
Chalamila amesema hayo leo baada ya kutembelea na kukagua kazi za matengenezo katika bomba hilo lenye kipenyo cha inchi 72, lililopo eneo la Mpiji, Wilaya ya Bagamoyo, Mkoa wa Pwani.
Amesema huduma ya maji ni muhimu kwa maisha ya wananchi na shughuli za kiuchumi jijini Dar es Salaam, hivyo ni muhimu kuchukua hatua za mapema kuimarisha miundombinu ili iweze kuhimili changamoto zinazoweza kusababishwa na mvua kubwa.
Amesema DAWASA imechukua hatua sahihi kwa kufanya matengenezo hayo kabla ya mvua kubwa kuanza, kwani uharibifu wa bomba hilo au miundombinu inayolizunguka wakati wa mvua ungeweza kuathiri kwa kiwango kikubwa upatikanaji wa maji kwa wananchi.
“Niwapongeze DAWASA kwa kuchukua tahadhari za mapema. Inawezekana wakati wa mvua kubwa ukarabati huu usingewezekana kufanyika na hali hiyo ingeathiri upatikanaji wa huduma ya maji. Nitoe rai kwa wananchi wanaohudumiwa na bomba hili kuanzia ukanda wa Bagamoyo hadi Ilala kuwa wavumilivu kutokana na kupungua kwa kiwango cha upatikanaji wa maji,” amesema Chalamila.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya DAWASA, Mhandisi Romanus Mwangingo, amemshukuru Chalamila kwa kutembelea na kukagua maendeleo ya matengenezo hayo, akisema ni sehemu ya mikakati ya kuimarisha miundombinu na kuzuia madhara yanayoweza kujitokeza wakati wa mvua kubwa.
Amesema kazi ya matengenezo itaanza Jumanne, Novemba 3,2026 na inatarajiwa kukamilika ndani ya saa 96 ambayo ni Novemba 6,2026 ambapo huduma ya maji inatarajiwa kurejea katika hali yake ya kawaida ifikapo Ijumaa jioni.
Ameeleza kuwa matengenezo hayo ni muhimu katika kuhakikisha bomba kuu linaendelea kufanya kazi kwa ufanisi na kuwa na uwezo wa kuhimili changamoto zinazoweza kusababishwa na mvua kubwa.
DAWASA imewaomba wananchi wanaotegemea maji kutoka bomba hilo, hususan katika maeneo ya Bagamoyo hadi Ilala, kuwa wavumilivu wakati wa matengenezo hayo, huku Mamlaka ikiendelea kusimamia kazi hizo ili zikamilike kwa wakati na huduma irejee kama ilivyopangwaThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Dkt. Angeline Mabula, amewataka watumishi wa umma katika ngazi zote za uongozi mkoani humo kuhakikisha wanasikiliza na kutatua changamoto zinazowakabili wananchi kwa wakati, akisisitiza kuwa hatosita kuchukua hatua kwa viongozi watakaoshindwa kutekeleza wajibu huo.
Dkt. Mabula ametoa kauli hiyo leo Novemba 3, 2026, wakati wa hafla ya makabidhiano ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora kati yake na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo, Beno Malisa, ambapo ameeleza kuwa kipaumbele chake ni kuhakikisha kero za wananchi zinapatiwa ufumbuzi ili kupunguza malalamiko na msongamano wa wananchi wanaofuatilia huduma katika ofisi za serikali.
Aidha, amewataka wananchi na viongozi wa ngazi mbalimbali kumpa ushirikiano katika kusimamia na kuimarisha shughuli za maendeleo, hususan kukuza sekta ya viwanda na sekta nyingine muhimu kwa ustawi wa Mkoa wa Tabora.
Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi wa Serikali, Chama cha Mapinduzi pamoja na taasisi mbalimbali, ambao wameahidi kumpa ushirikiano Mkuu huyo wa Mkoa katika kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kuhakikisha wananchi wananufaika na huduma zinazotolewa na Serikali.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Ujenzi, Masanja Kadogosa, amefafanua tofauti kati ya barabara za kulipia na utaratibu wa tozo, akieleza kuwa katika mfumo wa barabara za kulipia, mtumiaji mara nyingi anakuwa na njia mbadala ya kupita bila kutoa malipo.
Akizungumza Novemba 2, 2026, Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu hoja za wabunge kuhusu Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka wa fedha 2027/2028, Kadogosa ametolea mfano wa Daraja la Kigamboni na Barabara ya Tanzanite, huku akibainisha kuwa utaratibu huo unatumika pia katika nchi mbalimbali kama Kenya, Uganda, Zambia, Rwanda, Ghana, na Misri.
Aidha, ameeleza kuwa mtazamo wa Wizara ni kujenga barabara za njia sita au nne kulingana na mahitaji ya eneo, na kwamba Serikali imejipanga kufanya mabadiliko ya kisera na kuharakisha utekelezaji wa miradi hiyo kwa kuzingatia maelekezo ya Rais SamiaSuluhuHassan.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tabora kimeitaka Serikali ya Mkoa huo kuzisaidia timu za mpira wa miguu za Rhino Rangers na Tabora United zinazoshiriki Ligi Daraja la Kwanza, ili ziweze kufanya vizuri na hatimaye kupanda kucheza Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu ujao.
Wito huo umetolewa Novemba 03, 2026 na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tabora, Said Nkumba, wakati wa hafla ya makabidhiano ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, ambapo amemtaka Mkuu wa Mkoa huo, Dkt. Angeline Mabula, kuhakikisha timu hizo zinapata ushirikiano na sapoti inayostahili, akisisitiza kuwa michezo ni moja ya chachu muhimu ya maendeleo ya mkoa.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Dkt. Angeline Mabula, amesema yuko tayari kuziunga mkono timu hizo, akibainisha kuwa yeye ni mwanamichezo na anatambua umuhimu wa michezo katika kuleta maendeleo, kuitangaza Tabora na kutoa fursa kwa vijana, hivyo atashirikiana na wadau kuhakikisha timu hizo zinafikia malengo ya kupanda Ligi Kuu msimu ujao.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Familia ya marehemu Mzee Alute Mughwai Lissu imetangaza ratiba ya shughuli za kuuaga na kuzika mwili wa marehemu, ambapo ibada ya kuuaga itafanyika Jumatatu, Novemba 9, 2026, katika Kanisa la Mtakatifu Teresa jijini Arusha, kuanzia majira ya saa saba mchana.
Akizungumza na waandishi wa habari,hii leo Novemba 3, 2026 msemaji wa familia, Vincent Lissu Mughwai ambaye ni mdogo wa marehemu, amesema baada ya ibada hiyo mwili wa marehemu utasafirishwa kuelekea mkoani Singida kwa ajili ya mazishi.
Amesema mazishi yanatarajiwa kufanyika Jumanne, Novemba 10, 2026, katika Kijiji cha Mahambe, ambacho ni nyumbani kwa marehemu na familia yake.
Katika hatua nyingine, Vincent amesema ratiba ya familia kwenda mahakamani Ijumaa, Novemba 6, 2026, kusikiliza hukumu ya kesi inayomkabili Mwenyekiti wa @ChademaTZ2 Tundu Antipas Lissu, haijabadilika, na kwamba familia itashiriki shughuli hiyo kabla ya kuendelea na taratibu nyingine za mazishi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
#update - Wananchi wametoa wito kwa mamlaka husika kuimarisha usimamizi wa madereva, ikiwemo kutumia mfumo wa kukata pointi kwa madereva wanaokiuka sheria za usalama barabarani na kufanya uzembe unaohatarisha maisha ya wengine.
Wito huo umetolewa Novemba 3, 2026, kufuatia ajali iliyohusisha lori, bajaj na pikipiki ya bodaboda katika eneo la Magomeni Kanisani, Manispaa ya Mtwara Mikindani, mkoani Mtwara, iliyosababisha vifo vya watu watatu na wengine sita kujeruhiwa.
Aidha, wananchi hao wameitaka Serikali kutanua na kuboresha barabara hiyo, wakieleza kuwa hali ya miundombinu katika eneo hilo inahitaji kufanyiwa kazi ili kupunguza hatari ya ajali kwa watumiaji wa barabara.
Kwa mujibu wa mashuhuda, ajali hiyo imetokea baada ya dereva wa lori kupoteza uelekeo na kugonga vyombo vingine vya usafiri.
Akithibitisha vifo hivyo, Msimamizi wa Kitengo cha Dharura katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ligula, Dkt. Deogratius Makoti, amesema hospitali hiyo imepokea miili ya marehemu wote watatu, ambao ni wanawake.
Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, SACP Issa Suleiman, amesema polisi imemkamata dereva wa lori lenye namba za usajili T.495 EMX, aina ya Vasol, kwa tuhuma za kuendesha gari kwa uzembe na kusababisha ajali hiyo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), Ojambi Didas Masaburi, amesema sekta binafsi inapaswa kushirikishwa zaidi katika kugharamia na kutekeleza miradi ya maendeleo ya taasisi na mashirika ya umma kupitia mfumo wa ubia kati ya sekta ya umma na binafsi (PPP).
Masaburi amesema hayo leo Bungeni wakati akiwasilisha taarifa ya Kamati hiyo kuhusu uwekezaji wa mitaji ya umma kwa mwaka wa fedha 2024/2025.
Amesema Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2026/2027 umeweka msisitizo wa sekta binafsi kuwa mshirika muhimu wa maendeleo, kwa lengo la kupunguza utegemezi wa bajeti ya Serikali na mikopo na kuongeza mfumo wa kugharamia miradi kwa kushirikiana.
Taarifa ya Kamati hiyo imetolea mfano wa mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (BRT), ambapo Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) ulijenga miundombinu na baadaye kushirikisha wawekezaji binafsi, UDART na MOFAT, katika uendeshaji wa huduma hizo.
Kamati pia imeeleza kuwa Shirika la Meli Tanzania (TASHICO) linahitaji takribani shilingi trilioni 1.19 kwa ajili ya kujenga meli mpya na kukarabati zilizopo, huku Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO) likihitaji mtaji, utaalamu na teknolojia kutoka sekta binafsi. Aidha, Kituo cha Mbolea Tanzania (TFC) kinahitaji shilingi bilioni 5.6 kukamilisha mradi wa kiwanda cha kuchanganya mbolea.
Masaburi amesema ushiriki wa sekta binafsi unaweza kuongeza upatikanaji wa mitaji, teknolojia na utaalamu, hivyo kuharakisha utekelezaji wa miradi na kupunguza mzigo wa Serikali katika kugharamia uwekezaji wa mashirika ya umma.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mbunge wa zamani wa Iringa Mjini na kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Peter Msigwa, amewatetea wanaharakati kwa kusisitiza kuwa kundi hilo lina mchango mkubwa katika maendeleo ya taifa, hususan katika kuibua hoja zinazochochea uwajibikaji wa Serikali.
Akizungumza na Jambo TV leo Novemba 3, 2026 Msigwa amesema wanaharakati ni sehemu muhimu ya jamii inayopaswa kuthaminiwa na kupewa heshima kutokana na nafasi yao katika kuibua masuala mbalimbali yanayohusu maslahi ya umma na kuikumbusha Serikali wajibu wake.
Aidha, amesisitiza kuwa wanaharakati hawapaswi kubezwa, kudharauliwa au kuhukumiwa kwa kuzingatia changamoto au mwenendo wa mwanaharakati mmoja mmoja, bali wanapaswa kutambuliwa kwa mchango wa kundi hilo kwa ujumla katika maendeleo ya nchi.
Fuatilia mahojiano kamili kupitia YouTube Channel yetu ya Jambo TV.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mbunge wa zamani wa Iringa Mjini na kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo @ChademaTZ2 Peter Msigwa @MsigwaPeter amewatetea wanaharakati kwa kusisitiza kuwa kundi hilo lina mchango mkubwa katika maendeleo ya taifa, hususan katika kuibua hoja zinazochochea uwajibikaji wa Serikali.
Akizungumza na Jambo TV leo Novemba 3, 2026wanaharakati ni sehemu muhimu ya jamii inayopaswa kuthaminiwa na kupewa heshima kutokana na nafasi yao katika kuibua masuala mbalimbali yanayohusu maslahi ya umma na kuikumbusha Serikali wajibu wake.
Aidha, amesisitiza kuwa wanaharakati hawapaswi kubezwa, kudharauliwa au kuhukumiwa kwa kuzingatia changamoto au mwenendo wa mwanaharakati mmoja mmoja, bali wanapaswa kutambuliwa kwa mchango wa kundi hilo kwa ujumla katika maendeleo ya nchi.
Fuatilia mahojiano kamili kupitia YouTube Channel yetu ya Jambo TV.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Beno Malisa, amemuomba radhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kufuatia uamuzi wa Rais wa kumtengua katika nafasi hiyo baada ya kuitumikia kwa siku 62 pekee.
Malisa ametoa kauli hiyo leo, Novemba 3, 2026, wakati wa hafla ya makabidhiano ya ofisi kwa Mkuu mpya wa Mkoa wa Tabora, Dkt. Angeline Mabula, iliyofanyika mkoani humo.
Akizungumza katika hafla hiyo, Malisa amesema bado ni kijana mwenye nguvu na ari ya kulitumikia Taifa, hivyo anaamini kuwa bado ana nafasi ya kuendelea kulitumikia kupitia majukumu mengine atakayopangiwa.
Amesisitiza kuwa anaendelea kuheshimu uamuzi wa Rais huku akieleza matumaini yake ya kuendelea kutoa mchango wake katika maendeleo ya Taifa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), Ado Shaibu Ado, amesema kamati hiyo imebaini changamoto mbalimbali katika uwekezaji wa halmashauri nchini, ikiwemo kushuka kwa mapato, uwekezaji usio na tija na kutokukusanywa kwa mapato yanayotokana na usimamizi wa ardhi.
Akiwasilisha taarifa ya kamati hiyo leo Novemba 3, 2026 bungeni jijini Dodoma kuhusu ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa hesabu zilizokaguliwa za mamlaka za serikali za mitaa kwa miaka ya fedha 2023/2024 na 2024/2025, amesema Halmashauri ya Jiji la Dodoma ilipata Shilingi milioni 89.8 kutoka Soko la Job Ndugai katika mwaka wa fedha 2024/2025, kiasi ambacho ni pungufu kwa asilimia 80 ya makadirio ya mapato ya Shilingi milioni 443.2.
Amesema katika Manispaa ya Ubungo, mwaka wa fedha 2023/2024, mabasi 1,388 kati ya 1,595 yaliyopewa vibali vya kutumia stendi hiyo, sawa na asilimia 87, hayakuitumia kwa ajili ya kushusha na kupakia abiria, hali iliyosababisha Halmashauri kukosa mapato yaliyotarajiwa.
Aidha, amesema uwekezaji katika kampuni ya jengo la biashara la Rock City Mall jijini Mwanza haujatoa gawio kwa Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela tangu uwekezaji huo ulipoanza mwaka 2010.
Katika usimamizi wa ardhi, Ado amesema kamati imebaini Manispaa ya Kibaha ilifanya mauzo ya viwanja 168 vyenye thamani ya Shilingi bilioni 4.09 nje ya mfumo wa TAUSI, kinyume na taratibu. Vilevile, Halmashauri hiyo iligawa viwanja 189 bila kupokea malipo, hali iliyosababisha upotevu wa mapato ya Shilingi bilioni 7.8.
Ameongeza kuwa katika Jiji la Tanga, halmashauri ilipima viwanja 3,782 katika maeneo ya Kange, Kasera na Mkurumzi vyenye thamani ya Shilingi bilioni 3.5 kwa ajili ya kurasimisha umiliki wa maeneo ya Serikali yaliyovamiwa, lakini ilishindwa kutambua umiliki wa viwanja 2,268 vyenye thamani ya Sh bilioni 2.6, na hivyo kushindwa kukusanya mapato yaliyotokana na viwanja hivyo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Zaidi ya Wananchi elfu 20 Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha wanatarajiwa kunufaika na huduma ya maji safi na salama kupitia mradi wa maji unaotekelezwa na Serikali ambapo wananchi wa Kijiji cha Makuyuni wameanza kupata huduma hiyo kabla ya mradi kukamilika.
Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Kundo Mathew leo Novemba 3, 2026, bungeni jijini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Marirta Gido Kivunge, aliyetaka kujua ni lini Mradi huo utakamilika.
Amesema hadi kufikia sasa ujenzi wa mradi huo umefikia asilimia 30 na unatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi juni mwaka 2027. Amesema zaidi kwamba.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) umesema utaendelea kuhakikisha kwamba huduma ya mawasiliano inapatikana katika maeneo yote nchini ambayo yanakaliwa na wananchi ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kutaka hadi kufikia 2030 huduma ya mawasiliano iwe imewafika Watanzania wote.
Taarifa hiyo imetolewa leo, Novemba 3, 2026, jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Idara ya Uendeshaji, Utafiti na Maendeleo wa UCSAF, Mhandisi Albert Richard wakati wa kikao kazi kilichowakutanisha wahariri wa vyombo vya habari na mfuko huo kilichoratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina (OTR).
"Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, aliagiza kwamba anataka atakapoondoka nchi nzima ya Tanzania ipate huduma za mawasiliano. Hilo agizo limechukuliwa na viongozi wetu wa Wizara na wameamua kulitekeleza kwa wivu mkubwa..., itakapofika 2030, angalau kila mahali ambapo mwananchi anaishi kuwe na huduma za mawasiliano" amesema Mkurugenzi huyo.
Amesema zaidi kwamba ili kuhakikisha kufanikiwa kwa matarajio hayo upo mkakati ambao unaandaliwa unaokwenda sambamba na utafutaji wa fedha.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, amesema dhamira ya Serikali kuhusu suala la Katiba mpya bado ipo, akieleza kuwa jambo hilo limeingizwa katika Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kwamba Serikali itatoa kauli kuhusu hatua zitakazochukuliwa wakati mwafaka.
Akijibu hoja za wabunge kuhusu Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka wa fedha 2027/2028, Novemba 2,2026 Bungeni jijini Dodoma, Prof. Mkumbo alikuwa akijibu hoja ya Mbunge wa Tunduru Kaskazini, Ado Shaibu, aliyehoji kutokuwepo kwa masuala ya Katiba mpya na demokrasia katika mpango huo.
Amesema serikali inatambua umuhimu wa utawala bora, demokrasia, amani na usalama, akisisitiza kuwa mambo hayo ni msingi wa utekelezaji wa mipango mingine ya maendeleo na kwamba bila kuwa na mazingira hayo, utekelezaji wa shughuli za maendeleo unaweza kuwa mgumu.
Kuhusu suala la Katiba mpya, Prof. Mkumbo amesema kuingizwa kwake katika Ilani ya CCM ni ishara ya dhamira ya kulishughulikia, huku akieleza kuwa uongozi wa Serikali utatoa maelezo kuhusu hatua zitakazochukuliwa katika utekelezaji wa jambo hilo.
Katika hatua nyingine, amesema serikali inahitaji nguvu kubwa ya kifedha na ushirikiano wa sekta binafsi kutekeleza miradi minne ya korido za usafirishaji yenye urefu wa kilomita 3,417, ambayo inakadiriwa kugharimu Sh trilioni 40.3, akibainisha kuwa Wizara ya Mipango na Uwekezaji itaratibu taasisi mbalimbali ikiwemo Wizara ya Ujenzi, TANROADS, Kituo cha PPP, Wizara ya Fedha na Mamlaka ya Bandari Tanzania ili kuhakikisha miradi hiyo inatekelezwa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Kanda Maalum ya Dar es Salaam limetoa onyo kali kufuatia taarifa ambazo limesema linazo kuwa kuna watu wanahamasishana kutoka maeneo mbalimbali nchini kwenda jijini humo siku ya ijumaa ya Novemba 6, 2026 kwa lengo la ufanya vurugu
"Wanahamasishana kuja Dar es Salaam baadhi yao wakiwa na malengo ya kufanya fujo au vurugu"
Amesema hayo leo Novemba 3, 2026 akizungumza na waandishi wa habari huku akieleza kuwa mipaka na idadi ya watu wanaotakiwa kuingia mahakamani inafahamika hivyo kama yupo mtu mwenye nia ya kufanya vurugu.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwalimu Fixon Mtelesi ambaye ni Mkuu wa Idara ya Elimu ya Awali na Msingi anaeleza kuwa Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu imeanzishwa kwa lengo la kuongeza hamasa ya watu kusoma kupitia ubunifu.
Mwl. Mtelesi amesema hayo akihojiwa kwenye kipindi chetu cha Jambo Asubuhi akieleza kuwa miaka ya 1980 Tanzania ilikuwa nchi ambayo inafanya vizuri zaidi kwenye kuondoa ujinga kupitia kusoma ikiwa ni jitihada za Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
"Tuliwahi kuwa vizuri kwenye miaka ya 80 huko kwenye kusoma kuandika na hata kuhesabi kwa juhudi za Mwalimu Nyerere...ule usomaji umeanza kushuka sio kwa Tanzania karibu nchi nyingi za Afrika ule usomaji umepungua" amesema Mwl. Mtelesi
Jitihada za kuhamasisha watu kusoma kupitia ubunifu ndizo zilizosababisha Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kuanzisha tuzo hiyo.
@TIE_TanzaniaThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI PICHA:
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Kenya, Douglas Kanja, ameiambia Mahakama Kuu kuwa Kada wa CHADEMA na mwanaharakati wa Tanzania, Twaha Mwaipaya, hayupo chini ya ulinzi au mikononi mwa polisi popote nchini humo.
Kanja ametoa kauli hiyo leo, Novemba 3, 2026, alipofika mbele ya Jaji Alexander Muteti wa Mahakama Kuu kujibu wito wa mahakama kuhusu kupotea kwa Mwaipaya.
Akizungumza mahakamani hapo, Kanja amesema hafahamu kama Mwaipaya aliwahi kukamatwa na maafisa wa polisi nchini Kenya, akisisitiza kuwa hajawahi kuwa chini ya ulinzi wa jeshi hilo.
Hata hivyo, amethibitisha kuwa Polisi walipokea taarifa kuhusu tukio hilo katika Kituo cha Polisi cha Ruai na kwamba uchunguzi unaendelea, huku afisa anayesimamia uchunguzi huo akiwa mahakamani.
Kanja amekanusha madai ya Polisi kuhusika na vitendo vya utekaji na upotevu wa watu, akisema jeshi hilo halijihusishi na vitendo hivyo na kwamba tukio lolote la utekaji linapaswa kuchukuliwa kama kosa la jinai.
Kauli hiyo imekuja baada ya Mahakama Kuu, Oktoba 30, 2026, kutoa amri ya polisi kumfikisha Mwaipaya mahakamani akiwa hai au amefariki ifikapo Novemba 2, 2026, pamoja na kuwasilisha hati ya awali ya kumweka kizuizini na kueleza sababu za kuendelea kumshikilia.
Mwaipaya aliripotiwa 'kutekwa' Oktoba 25, 2026, eneo la Kamulu, Kaunti ya Machakos nchini Kenya. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Kutokana na matukio ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo @ChademaTZ2 mara nyingi kuchukua hatua kali dhidi ya baadhi ya viongozi wanaokikosoa chama kwa kuwasimamisha uanachama wakati mwingine kuwafukuza.
Skawa anasema "CHADEMA nafikiri kuna ile kutokuvumiliana"
Skawa amesema hayo kwenye kipindi chetu cha Jambo Asubuhi ambacho kipo kuanzia jumatatu mpaka ijumaa Saa tatu asubuhi mpaka saa tano asubuhi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwenezi wa Taifa wa Baraza la Vijana la CHADEMA (BAVICHA), Felius Festo, amesema Freeman Mbowe bado anahitajika ndani ya chama hicho kutokana na uzoefu wake wa miaka 24 akiwa Mwenyekiti.
Akizungumza Novemba 3, 2026, katika mahojiano na kipindi cha Jambo Asubuhi cha Jambo TV, Felius amesema ni vigumu kusema Mbowe amepoteza heshima ndani ya chama hicho, akieleza kuwa anapaswa kuwa mlezi na mshauri wa viongozi na vijana.
“Mbowe aliyekuwa Mwenyekiti wa chama kwa miaka 24, kuna namna angekuwa kama baba wa chama, angekuwa kama mlezi,” amesema Felius.
Ameongeza kuwa viongozi wamewahi kumwalika Mbowe kwenye vikao vya Kamati Kuu ili kupata busara na ushauri wake, lakini hajahudhuria, akihoji njia nyingine wanazopaswa kutumia kumfikia ili aendelee kutoa mchango wake kwa chama.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Dorothy Semu, amesema wananchi wanaelewa kuwa chama hicho kinasimamia na kupigania maslahi yao, akisisitiza umuhimu wa kuendelea kuwa karibu na wananchi, kusikiliza kero zao na kutafuta majibu ya changamoto zinazowakabili.
Kauli hiyo inakuja wakati Semu akianza ziara ya siku saba mkoani Kigoma, baada ya kuwasili leo, Novemba 3, 2026, na kupokelewa na viongozi wa kitaifa wa chama hicho pamoja na viongozi na wanachama wa mkoa huo.
Katika ziara hiyo itakayohitimishwa Novemba 9, Semu anatarajiwa kufanya mikutano ya hadhara na kukutana na wananchi katika maeneo mbalimbali ya Kigoma. Leo jioni anatarajiwa kuhutubia mkutano wa hadhara katika Kata ya Kasimbu, kwenye Uwanja wa Mwembe Mmoja, Jimbo la Kigoma Mjini.
Kupitia mikutano hiyo, ACT Wazalendo inalenga kusikiliza changamoto za wananchi, kujadili masuala yanayogusa maisha yao na kuimarisha uhusiano kati ya chama na wananchi.
Ziara ya Kigoma ni sehemu ya ziara kubwa ya kitaifa ya siku 20 inayofanyika katika mikoa minane ya Tanzania Bara, chini ya ujumbe wa “Taifa la Wote, Maslahi ya Wote.”
Baada ya Kigoma, Semu ataendelea na ziara katika mikoa mingine ya Magharibi, Nyanda za Juu Kusini na Morogoro.
Ziara hiyo inafuatia shughuli zake za kichama visiwani Pemba, ambako alishiriki Mkutano Mkuu wa Mkoa wa Wete na kukagua ujenzi wa ofisi za chama.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga ameitaka Mamlaka ya Viwango Tanzania (TBS) kuongeza kasi ya kuwahudumia wajasiriamali kwa kurahisisha upatikanaji wa ithibati za bidhaa na kuboresha vifungashio, ili bidhaa zinazozalishwa nchini ziweze kushindana katika masoko ya ndani na nje ya nchi.
Akizungumzia leo Novemba 2, 2026 jijini Dodoma wakati akifungua maonesho ya bidhaa za viwanda na wajasiriamali yaliyoandaliwa kuelekea Uzinduzi wa Sera ya Maendeleo ya Viwanda ya mwaka 2025 na Sera ya Maendeleo ya Wajasiriamali Ndogo ya mwaka 2023, toleo la mwaka 2025.
Amesema serikali itaendelea kuboresha mazingira ya biashara na kufungua fursa za masoko ya ndani na nje ya nchi, hatua inayolenga kuwawezesha wajasiriamali kukuza uzalishaji, kuongeza thamani ya bidhaa zao na kupanua wigo wa biashara katika ushindani wa kitaifa na kimataifa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Abdallah Mwaipaya, amesema maboresho yaliyofanyika katika Bandari ya Mtwara yameleta mabadiliko makubwa ya kibiashara na kiuchumi katika mkoa huo, ikiwemo kuongezeka kwa mizigo, magari na fursa za ajira kwa vijana.
Akizungumza Oktoba 1, 2026 wakati wa mahojiano maalumu yaliyofanyika ofisini kwake kuhusu maboresho hayo, Mwaipaya amesema kabla ya kufanywa kwa maboresho, Mtwara ulikuwa Mkoa uliokuwa na shughuli za kiuchumi zilizokuwa chini.
“Mkoa ulitulia na shughuli zilikuwa chini mno hata mzunguko wa fedha kabla ya bandari haijaboreshwa ulikuwa changamoto kubwa. Wananchi walitegemea msimu wa korosho tu na ukiondoka fedha zote zinaisha na bandari yenyewe ilikuwa inasubiri, haikuwa bize,” amesema.
Amesema vijana wa Mtwara wamepata fursa za kufanya kazi bandarini, huku vijana kutoka mikoa mingine pia wakija kuchangamkia fursa hizo.
“Kuna fursa nyingi bandarini na hata vijana wa maeneo mengine kutoka mikoa mingine nao sasa hivi wanakuja kuchangamkia fursa hii,” alisema.
Amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuboresha bandari nchini, akitaja bandari za Dar es Salaam na Tanga kama sehemu ya juhudi za Serikali katika kuboresha miundombinu ya maeneo hayo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Donald Msengi, amesema Mtwara ni lango kuu la uchumi kwa ukanda wa kusini kutokana na miradi mikubwa inayopatikana.
Kupitia mahojiano maalumu yaliyofanyika ofisini kwake Oktoba 1, 2026 kuhusu maboresho ya Bandari ya Mtwara, amesema bandari hiyo ni kichocheo kikubwa cha ukuaji wa biashara katika ushoroba wa kusini.
Pia amesema wana Mtwara wanaishukuru Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa maelekezo yake ya kuhakikisha korosho zote za ukanda wa kusini zinasafirishwa kupitia bandari hiyo.
Amewataka wananchi wa Mtwara hasa vijana na Watanzania kwa ujumla kuchangamkia fursa za maboresho ya Bandari ya Mtwara ili waweze kujipatia vipato.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Meneja wa Bandari ya Mtwara, Ferdinand Nyathi, amesema bandari hiyo ni miongoni mwa miundombinu ya kimkakati iliyopo mwambao wa Bahari ya Hindi, inayomilikiwa na kuendeshwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) chini ya Sheria ya Bandari Namba 17 ya Mwaka 2004.
Nyathi amebainisha hayo alipokuwa katika mahojiano maalumu yaliyofanyika ofisini kwake mkoani humo kuhusu maboresho ya bandari hiyo. Akizungumzia historia ya bandari hiyo, Nyathi amesema ilijengwa miaka ya 1950 ikiwa na uwezo wa kuhudumia tani laki nne za mizigo kwa mwaka.
“Bandari hii ilijengwa miaka ya 1950 ikiwa na gati lenye urefu wa mita 385 na kina cha mita 9.5. Lango lake la kuingilia lina upana wa mita 250 na kina cha mlango wa bahari cha mita 20, jambo lililoiwezesha kuhudumia meli zenye urefu wa hadi mita 240,” ameeleza.
Meneja huyo ameongeza kuwa, matumizi ya pamoja ya gati la zamani na gati jipya yamesaidia kuongeza kiwango cha mizigo inayohudumiwa bandarini hapo mwaka hadi mwaka.
Kuhusu mipango ya baadaye, Nyathi ameeleza kuwa Serikali kupitia TPA ipo kwenye mpango wa kuongeza kina cha gati la zamani ili kuziwezesha meli kubwa zaidi kutia nanga.
“Kwa kuwa gati la zamani lenye urefu wa mita 385 na kina cha mita 9.5 limehudumia kwa muda mrefu, kuna mpango wa kuongeza kina chake ili liweze kupokea na kuhudumia meli kubwa zaidi,” ameongeza.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Wakili Dunford Mpelumbe amesema tume hiyo itaendelea kupokea na kuchunguza malalamiko ya wananchi pamoja na kusimamia misingi ya haki za binadamu na utawala bora bila upendeleo.
Amesema hayo leo Jumatatu Novemba 2, 2026 jijini Dodoma mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Ikulu, Chamwino na kupokelewa na watumishi wa tume hiyo, akieleza kuwa wamejipanga kuimarisha utekelezaji wa majukumu yao kwa kuzingatia maelekezo na changamoto zilizopo katika sekta ya haki za binadamu.
Mpelumbe amesema tume itaendelea kushirikiana na serikali katika kuimarisha mifumo ya kisheria, kisera na kitaasisi ili kuhakikisha Watanzania wanapata haki zao za kiraia na kijamii, ikiwemo haki ya kupata huduma bora za afya na maji safi na salama.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Wakili anayemtetea Mkurugenzi wa Mafunzo na Oganaizesheni ya Uchaguzi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) @ChademaTZ2 , John Pambalu, Hekima Mwasipu amekanusha madai yaliyotolewa na Mjumbe wa Baraza Kuu la CHADEMA kupitia Baraza la Wanawake CHADEMA (BAWACHA), Hilda Newton @HildaNewton21 kwamba kurejea kwa mteja wake nchini na kutoa maelezo kwa Jeshi la Polisi kunahusiana na madai ya kutekwa kwa mwanaharakati na mwanachama wa chama hicho, Twaha Mwaipaya, jijini Nairobi nchini Kenya.
Sintofahamu hiyo imeibuka katikati ya madai ya kutekwa kwa Twaha Mwaipaya nchini Kenya na kushikiliwa kwa Pambalu nchini Tanzania kufuatia kufunguliwa kwa mashtaka ya uhaini yanayohusiana na matukio ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.
Mnamo Novemba 1, 2026, kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, Hilda Newton alichapisha maelezo akimshutumu Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Godbless Lema @godbless_lema , kwa kumshawishi Pambalu kurejea nchini Tanzania na kutoa ushirikiano kamili kwa Jeshi la Polisi. Katika chapisho hilo, Hilda alidai kuwa Lema alimhakikishia Pambalu usalama wake akisema alizungumza na afisa wa polisi na kwamba kila kitu kilikuwa sawa, jambo lililompa Pambalu ujasiri wa kurejea nchini.
“Pambalu kwa maelekezo yake wakati anazungumza na watu walioenda kumuona gerezani hivi karibuni anasema, wakati polisi wanamhoji alizungumza ukweli wake wote ambao anaujua kuhusu watu waliopo Nairobi. Siku kadhaa baada ya Pambalu kusema ukweli wake wote, Twaha Mwaipaya akatekwa na watu wasiojulikana mpaka leo imetimia siku nane hatujui Twaha yupo wapi”, aliandika Hilda katika sehemu ya chapisho lake.
Kufuatia chapisho la Hilda, Wakili Mwasipu alijibu kupitia mitandao yake ya kijamii ili kuweka wazi masuala yote ambayo mteja wake alihojiwa mbele yake wakati akiwa mikononi mwa Jeshi la Polisi.
Wakili Mwasipu alitaja mambo ambayo Pambalu alihojiwa mbele yake ikiwamo majukumu aliyopangiwa na Kamati Kuu ya CHADEMA katika Hoteli za Desderia na Bagamoyo, kama alihusika kuandaa filamu ya kumbukumbu ya mauaji ya tarehe 29 Oktoba 2025 kabla akiwa na John Kitoka, uhusika wake na Dkt. Slaa na Mchungaji Mwamakula kwenda nchini Uganda na Kenya kuhamasisha maandamano, kama yeye ni ‘Admin Msaidizi wa akaunti ya mtandao wa kijamii ya 'Chadema in Blood' akiwa na Twaha Mwaipaya na kazi za Idara ya Mafunzo ya CHADEMA.
Baada ya chapisho hilo la Wakili Mwasipu, Jambo TV leo Novemba 2, 2026 imemtafuta wakili huyo kwa njia ya simu ili kupata ufafanuzi wa kina wa alichokiandika. Katika ufafanuzi wake, Wakili Mwasipu ameeleza kuwa... soma zaidi hapa jambo.co.tz/wakili-akanusha-tuhuma-za-hilda-kuhusu-pambal… -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya uwekezaji na Maeneo Maalumu ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA), Gilead John Teri, amesema wanatarajia kuendelea kufanya Kampeni kwaajili ya kuhamasisha uwekezaji wa ndani, ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan la kutaka kuona wawekezaji wakubwa nchini wanakuwa Watanzania.
Teri ameeleza hayo leo Novemba 2, 2026 jijini Dar es Salaam, alipokuwa akizungumza katika Mkutano kati ya Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) na Wahariri, ulioratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina (OTR) kwa lengo la kujenga na kuimarisha mahusiano kati ya Ofisi ya Msajili wa Hazina, TISEZA na vyombo vya habari nchini.
Ameongeza kwamba kampeni hizo za kuhamasisha uwekezaji wa ndani pia zimefanyika mwaka 2026 katika maeneo mbalimbali ikiwemo Geita, Mwanza, Simiyu, Shinyanga, Mara, Kagera, Katavi, Rukwa, Mbeya, Songwe pamoja na Njombe.
Amesema zaidi kwamba katika maeneo hayo walikutana na wawekezaji kuanzia mmojammoja zaidi ya 1,402, ambapo walihakikisha miradi zaidi ya 24 ambayo iliwekezwa ndani ya Mwezi mmoja ambao waliufanyia kampeni.
Teri amesema mafanikio waliyoyapata ilikuwa ni kuongeza uelewa wa Watanzania kufahamu kwamba uwekezaji si tu unawahusu watu kutoka ughaibuni bali ni jambo linalowahusu Watanzania.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya uwekezaji na Maeneo Maalumu ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA), Gilead John Teri, amesema suala la uwekezaji nchini ni la muhimu kwani linasaidia katika upatikanaji wa mitaji, ajira, kuongeza mzunguko wa uchumi na kuchochea kupatikana kwa kodi pamoja na kuwezesha uzalishaji wa bidhaa ambazo awali zilikuwa ninaagizwa kutoka nje ya nchi.
Teri ameeleza hayo leo Novemba 2, 2026 alipokuwa akizungumza katika Mkutano wa Wahariri wa vyombo vya Habari nchini, uliofanyika jijini Dar es Salaam ambao ulikuwa ukijadilina hali ya uwekezaji nchini.
"Kwanini uwekezaji ni jambo muhimu?... kwa upana wake, uwekezaji unaleta mitaji, unaleta ajira, unaongeza mzunguko wa uchumi, mzunguko ule unaleta kodi, unazalisha bidhaa amazo mwanzoni ulikuwa unazitegemea kutoka nje unazizalisha wewe mwenyewe sasa" amesema Teri.
Ameongeza kuwa suala hilo la uwekezaji haliishii tu kwa nchi zilizoendelea badala yake uwekezaji huo huitajika pia kwa mataifa yanayoendelea.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI:
Wananchi wa Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki wanatarajiwa kupata huduma za uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo bila malipo kuanzia Novemba 10 hadi 20, 2026, kupitia kambi maalumu itakayoendeshwa na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Mbunge wa jimbo hilo, Hamis Taletale maarufu Babu Tale.
Kambi hiyo, inayotekelezwa chini ya kampeni ya Afya Bora na Samia, itatoa fursa kwa wananchi kupimwa, kupata ushauri na matibabu kutoka kwa madaktari bingwa na wabobezi wa magonjwa ya moyo. Waziri wa Afya, Mohamed Mchengerwa, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wake.
Mbali na huduma hizo, Babu Tale amesema atatoa bima za afya bure kwa wananchi 150 wasio na uwezo kiuchumi ndani ya jimbo hilo, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuongeza upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Novemba 2, 2026, mjini Morogoro, mbunge huyo amewahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi kutumia fursa hiyo ili kuchunguza afya zao na kupata huduma za kibingwa bila gharama.
Amesema hatua hiyo inalenga kusogeza huduma za afya karibu na wananchi na kuunga mkono jitihada za Serikali kuelekea utekelezaji wa mpango wa Bima ya Afya kwa Wote. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Wakili Peter Madeleka amesema ana matumaini na ahadi ya kupatikana kwa katiba mpya iliyotolewa na Chama cha Mapinduzi (CCM) kupitia aliyekuwa mgombea wake ambaye kwa sasa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Rais Samia Suluhu Hassan.
Madeleka akizungumza kwenye kipindi cha Jambo Asubuhi cha Jambo TV leo Novemba 2, 2026, amesema anaamini ahadi hiyo itatkelezeka kabla Dkt. Samia hajamaliza muda wake wa Urais.
"Rais Samia kama Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi ambaye alisimamia uundwaji wa Kamati ya Uandishi wa Ilani ambayo Mwenyekiti wake alikuwa Professa Kitila Mkumbo wakaiweka katiba mpya kwenye ilani...ndiyo maana mimi ninaamini Samia kabla hajaondoka bila kujali siku 100 zimeisha au hazijaisha atatuletea katiba" amesema Wakili Madeleka.
Hata hivyo kuhusu kutekelezwa kwa ahadi ya kuanza mchakato huo ndani ya siku 100, Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Stephen Wasira akizungumza katika mkutano wa Wadau wa siasa kuhusu hali ya kisiasa nchini alisema mchakato huo umechelewa kidogo kutokana na matukio yaliyotokea Oktoba 29, 2025 na kuendelea huku akisisitiza kuwa siku sio nyingi mara baada ya kuanza kwa kuundwa kwa tume za maridhiano basi mchakato wa katiba utaanza.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
"Makamu mwenyekiti hapa amezungumza suala la Nchimbi, yaani Makamu wa Rais eti anaweza akapotezwa tu, tukaambiwa tu amejiuzulu. Utaratibu haukufuatwa, Katiba haikufuatwa, kila kitu hakikufuatwa, mwana CCM mwenzao walikuwa naye kwenye sanduku la kupiga kura, Nchimbi alifukuzwa alipobadilisha tu maneno, alipokataa mambo ya hovyo akafukuzwa." amesema Mpina.
Aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Kisesa kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Luhaga Mpina ambaye kwa sasa ni Mwanachama wa Chama cha ACT Wazalendo, ameeleza hayo Novemba 1, 2026 alipokuwa akizungumza katika Mkutano wa hadhara uliofanyika na wananchi wa jimbo hilo, ikiwa ni sehemu ya ziara ya Chama chake cha ACT Wazalendo Kanda ya Ziwa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewataka viongozi wapya wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kufuatilia kwa karibu shutuma zinazoihusu Tanzania, hususan zinazotolewa kupitia mitandao ya kijamii, kuzichunguza na kuzitolea majibu kwa wakati.
Akizungumza leo, Novemba 2, 2026, wakati wa kuwaapisha viongozi hao katika hafla iliyofanyika Ikulu ya Chamwino, Dodoma, Rais Samia amesema ni muhimu kwa tume hiyo kufuatilia masuala ya haki za binadamu yanayotokea ndani na nje ya nchi, ili kuelewa mwenendo wa kimataifa na hali halisi ya Tanzania.
Amesisitiza kuwa viongozi hao wanapaswa kutumia mitandao ya kijamii na vyanzo mbalimbali vya habari kufuatilia taarifa na shutuma zinazotolewa dhidi ya nchi, kuzichunguza na kuzifanyia kazi kwa haraka, ili kuhakikisha ukweli kuhusu hali ya haki za binadamu nchini unafahamika ndani na nje ya Tanzania. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mbunge wa Tarime Vijijini, Mwita Mwikabe Waitara, amehoji kuhusu kufanyika kwa sherehe za wanaojihusisha na mahusiano ya jinsia moja nchini, akitaka Serikali kueleza iwapo ilitoa kibali cha kuruhusu shughuli hiyo kufanyika.
Akiuliza swali hilo Leo Novemba 2, 2026 Bungeni jijini Dodoma Waitara amesema iwapo Serikali haikutoa kibali cha kufanyika kwa sherehe hizo, inachukua hatua gani dhidi ya waliohusika katika maandalizi na utekelezaji wake?
Akijibu hoja hiyo, Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhandisi Maryprisca Winfrid Mahundi amesema Serikali haitoi uhalali kwa waliohusika na shughuli hiyo, huku akieleza kuwa Wizara inaendelea kusisitiza umuhimu wa malezi bora ndani ya familia. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Wakili Peter Madeleka @PMadeleka anaeleza kuwa kwa misingi ya kisheria kama Alute Mughwai Lissu(kaka wa Tundu Lissu) angetakiwa kuzikwa kabla ya Novemba 6, 2026 basi Lissu angeshindwa kuhudhuria mazishi hayo.
Madeleka akizungumza kwenye kipindi cha Jambo Asubuhi cha Jambo TV leo Novemba 2, 2026 ameeleza kuwa kesi inayomkabili Lissu ya uhaini haina dhamana hivyo pia anakosa nafuu zingine kama kuwa nje.
Hata hivyo ameeleza kuwa ndiyo sababu ya familia ya Lissu imepanga kufanya mazishi baada ya Novemba 6, 2026 siku ambayo hukumu ya kesi ya uhaini inayomkabili Lissu inatoka.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
"Mpina alipochukuwa fomu, wakahakikisha kwamba jina lake halionekani kwenye sanduku la kupiga kura. Poleni sana, najua wananchi wengine wengi walifika mpaka kwenye sanduku la kupiga kura wakatafuta sana jina la Luhaga Mpina hawakuliona, wakawa wanalalamikia wasimamizi wa uchaguzi mbona hatulioni jina la Mpina?. Na wengine mpaka wakaamua kuongeza, pale kwenye 17 wagombea wa Urais, wakaongeza 18 wakaandika Luhaga Mpina wakanitumia hizo kura walizoharibu" amesema Mpina.
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kisesa Luhaga Mpina ambaye kwa sasa ni Naibu Waziri Mkuu Kivuli wa Chama cha ACT-Wazalendo Luhaga Mpina, ameeleza hayo leo Novemba 1, 2026 alipokuwa akizungumza na wananchi wa Jimbo hilo kupitia ziara ya Chama hicho iliyolenga kutembelea mikoa ya kanda ya Ziwa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwandishi wa Habari Raidhan Namwadila amemuuliza Mjumbe wa Kamati Kuu ya @ChademaTZ2 Godbless Lema @godbless_lema juu ya chama hicho kuwa kama 'kimetekwa' na wanaharakati kutokana na mara kadhaa uongozi kushinikizwa kufanya maamuzi na wakati mwingine kutolewa maneno makali.
Akijibu swali hilo katika mkutano wake na waandishi wa habari leo Novemba 1, 2026 Lema amesema "nikubaliane na wewe kwamba walihamasisha kwa kiasi kikubwa wajumbe wa mkutano mkuu kufanya maamuzi(kuuchagua uongozi uliopo) lakini hiyo haiwapi uhalali wa kuingilia mambo ya chama kila wakati" alijibu LemaThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini kwa tiketi ya CCM, Mrisho Gambo, ni miongoni mwa waombolezaji waliofika nyumbani kwa familia ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, kutoa pole kufuatia kifo cha kaka yake, Alute Mughwai Lissu.
Akizungumza msibani hapo, Novemba 1,2026, Gambo amesema amepokea kwa masikitiko na mshangao mkubwa taarifa za kifo cha Alute, akieleza kuwa siku chache zilizopita alimuona akifanya mahojiano na vyombo vya habari.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo, Isihaka Mchinjita, amesema Demokrasia maana yake ni wananchi waamue ni nani wa kuwa kiongozi wao.
Mchinjita ameeleza hayo leo Novemba 1, 2026 alipokuwa akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Meatu Mkoa wa Simiyu, katika kata ya Mwandoya.
Amesema zaidi kwamba ikiwa katika taifa wananchi hawana uwezo wa kuchagua viongozi wao tafsiri yake nchi hiyo ni ya kimabavu au kikoloni.
Mchinjita yupo Kanda ya Ziwa pamoja na Luhaga Mpina ambaye aliwahi kuwa Mbunge wa kisesa katika ziara ya kichama ambayo imelenga kuwapa viongozi hao fursa ya kukutana na Watanzania wanaokabiliwa na changamoto za kijamii na wanaodai haki pamoja na uwajibikaji.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo, Isihaka Mchinjita, amesema kuondolewa kwa aliyekuwa Makamu wa Rais Dkt. Emmanuel Nchimbi katika Chama cha Mapinduzi (CCM), kulitokana na madai yake ya mabadiliko hasa Katiba, huku akiongeza kwamba pia aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kisesa kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Luhaga Mpina, kuondolewa katika Chama hicho kulitokana na hatua yake ya kuihoji Serikali bungeni katika maeneo mbalimbali ikiwemo masuala ya Sukari pamoja na Pamba.
Mchinjita ameeleza hayo leo Novemba 1, 2026 alipokuwa akizungumza na wananchi wa Jimbo hilo la Kisesa lilipo Mkoa wa Simiyu ambapo wamefika kwaajili ya kufanya ziara ya kichama iliyolenga kuzungumza na wananchi hao.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
"Nataka niwaambie wanaharakati wanaopigania mabadiliko nyie mlioko nje mna tofauti kubwa na sisi tuliopo hapa ardhini na ukitaka kujua Maria Sarungi @MariaSTsehai alifiwa na baba yake mimi nilienda kwenye msiba kusapoti mwanaharakati Maria Sarungi hakuja kama umefiwa baba anaogopa kuja kumzika baba yake wale wanaochukau tahadhari asiwaone waoga"
Hayo ameyasema Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Godbless Lema @godbless_lema akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 1, 2026 jijini Arusha. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
"Sisi ni Chama cha siasa, ni taasisi sio Chombo cha harakati, yaani siyo mwanaharakati mmoja hiki ni Chama cha siasa. Sasa imefika mahali hata engagement zinaopa kufanyika, engagement sio maridhiano yaani leo huyu akikamatwa akawekwa lokapu mimi nikampigia OCCID nikasema huyo kijana ninamjua usimweke ndani sija compromise, namtafutia uhuru" amesema Lema.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Godbless Lema, amesema hayo leo Novemba 1, 2026 jijini Arusha, katika mkutano wake maalumu na waandishi wa habari.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Godbless Lema, amemtuhumu mwanaharakati Mange Kimambi kuwa anatumika kuleta mgawanyiko ndani ya chama hicho, akipinga madai yanayotolewa dhidi yake kuwa yeye ni mradi wa kukigawa chama.
Lema amesema hayo leo Novemba 1, 2026 alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha. Amesema anasikitishwa na baadhi ya wanachama wa CHADEMA wanaosikiliza kauli za Mange Kimambi na kuanza kugawanyika kwa misingi ya madai kuwa yeye ni mradi, akisisitiza kuwa madai hayo si ya kweli.
Ameeleza kuwa hawezi kuwa sehemu ya mpango wa kukigawa chama na uongozi wake, wakati yeye mwenyewe ni sehemu ya uongozi wa CHADEMA, akisisitiza kuwa hana nia ya kukidhoofisha chama hicho.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo @ChademaTZ2 Godbless Lema @godbless_lema amewasili nyumbani kwa Marehemu Mzee Alute Mughwai Lissu kutoa pole kwa familia kufuatia kifo chake.
Akizungumza na Jambo TV leo Novemba 1, 2026 akiwa msibani hapo(jijini Arusha), Lema amesema amepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa za kifo cha Mzee Alute, ambaye ameeleza kuwa alikuwa mtu wake wa karibu.
Amesema hata hivi karibuni, kabla ya kifo chake, alimtembelea hospitalini kwa ajili ya kumjulia hali.
Aidha, Lema amesema licha ya tofauti zao za kiitikadi, ambapo marehemu alikuwa kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) huku yeye akiwa mwanachama wa CHADEMA, wamekuwa wakishirikiana mara kadhaa katika mambo mbalimbali.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI:
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kimetoa salamu za pole kwa wote walioguswa na msiba wa kaka wa Mwenyekiti wa Chama hicho, Tundu Lissu, kikieleza kupokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha kaka huyo ambaye ni Wakili Allute Mughwai Lissu.
Kulingana na taarifa iliyotolewa leo, Novemba 1, 2026, na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa CHADEMA, Brenda Rupia, Wakili Allute amefariki dunia usiku wa kuamkia leo akiwa anapata matibabu katika Hospitali ya Selian jijini Arusha, taarifa ambayo pia familia ilithibitisha awali.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa msiba huo umetokea katika kipindi kigumu kwa familia, ikiwa ni siku chache kabla ya hukumu ya kesi ya uhaini inayomkabili Tundu Lissu, kesi ambayo Chama hicho kimeendelea kuitaja kuwa ni ya kubambikizwa ambayo inayotarajiwa kutolewa uamuzi Ijumaa, Novemba 6, 2026.
CHADEMA imetoa salamu za rambirambi kwa Mwenyekiti wake (TunduLissu), mjane na watoto wa marehemu, ndugu, jamaa, marafiki, Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), pamoja na Watanzania wote walioguswa na msiba huo.
“CHADEMA inaungana na familia katika maombolezo haya na kuwaombea nguvu, faraja na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu,” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.
Aidha, Chama hicho kimewaomba viongozi na wanachama wake kote nchini kushiriki katika hatua mbalimbali za msiba huo kwa kuzingatia ratiba na utaratibu utakaotolewa na familia. CHADEMA imebainisha kuwa inaendelea kuwasiliana na familia kuhusu maandalizi ya mazishi na itatoa taarifa zaidi pindi taratibu zitakapokamilika.
Hata hivyo katika Mazungumzo na vyombo vya Habari leo Novemba 1, 2026, Familia ya Lissu imesema kuwa Marehemu Alute Mughwai Lissu atazikwa mara baada ya hukumu ya kesi ya ndugu yao Tundu Antiphas Lissu ambaye ni Mwenyekiti wa CHADEMA. -
Jambo TV
@Jambotv_
#ad
MAMILIONI YA WASAFIRI SASA WANAWEZA KUPANGA SAFARI ZAO KUPITIA DESTINATION TANZANIA APP!
Ni mwezi mmoja tu tangu kuzinduliwa kwake, tarehe 27 Septemba 2026, Destination Tanzania App inaendelea kuimarisha safari ya mabadiliko ya kidijitali katika sekta ya utalii nchini.
Kupitia App hii, Watanzania na watalii kutoka sehemu mbalimbali duniani wanaweza kugundua vivutio vya utalii vilivyopo Tanzania, kuunganishwa moja kwa moja na kampuni za utalii za Kitanzania, kupata huduma za malazi na taarifa nyingine muhimu za safari zao, yote kupitia simu zao za mkononi.
Destination Tanzania App inaweka fursa mpya kwa watoa huduma za utalii nchini kufikia masoko ya ndani na kimataifa, huku ikiwarahisishia wasafiri kupanga safari zao kwenda Tanzania.
Akizungumzia mafanikio ya mwezi mmoja tangu kuzinduliwa kwa App hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Dkt. Thereza Mugobi, amesema:
“Tulipoizindua Destination Tanzania App, lengo letu lilikuwa moja tu, kumuwekea mtalii Tanzania yote kiganjani mwake. Ndani ya mwezi mmoja, tumeona mwitikio mkubwa kutoka kwa Watanzania na wasafiri wa kimataifa. Hii inaonesha umuhimu wa teknolojia katika kurahisisha upatikanaji wa taarifa, kuunganisha watalii na watoa huduma na kukuza ushindani wa Tanzania katika soko la utalii duniani.”
Je, tayari umepakua Destination Tanzania App?
Pakua sasa, sajili biashara au huduma yako ya utalii na uwe sehemu ya safari hii ya mapinduzi ya utalii wa kidijitali.
📲 Inapatikana kupitia Google Play Store na Apple App Store.
Destination Tanzania, Tanzania Yote Kiganjani Mwako!
#destinationtanzaniaapp #tanzaniaunforgettable
@tanzania_unforgattabl @dktabbasi
@dr_thereza.mugobi
@ashatukijaji
@jamesmhilu
@paulinamkamaThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Familia ya Lissu imesema kuwa Marehemu Alute Mughwai Lissu atazikwa mara baada ya hukumu ya kesi ya ndugu yao Tundu Antiphas Lissu ambaye ni Mwenyekiti wa @ChademaTZ2
Hayo yameelezwa na Dkt. Vincent Lissu Mughwai leo Novemba 1, 2026 akitoa msimamo wa familia juu ya msiba wa kaka yao Alute ambaye amefariki usiku wa kuamkia leo.
"Tunategemea mazishi yatafanyika Singida...tutasukuma mbele mazishi ili ijumaa(Novemba 6, 2026) tuweze kuwepo Dar es Salaam kuhudhuria hukumu ya kesi ya ndugu yetu Tundu." amesema Dkt. Vincent.
Hata hivyo ameeleza kuwa Alute alikuwa akiugua kwa muda mrefu ambapo alilazwa katika Hospitali ya Selian jijini Arusha na kuanzia juzi alizidiwa.
Ikumbukwe Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Dar es Salaam imepanga kutoa hukumu katika kesi ya uhaini inayomkabili Lissu siku hiyo ya Novemba 6, 2026.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima, amewataka wahitimu wa kidato cha nne kutumia elimu na maarifa waliyoyapata kujikwamua kiuchumi na kushiriki kikamilifu katika kufanikisha Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2050.
Akizungumza Oktoba 31, 2026 katika mahafali ya 13 ya Shule ya Sekondari ya Wasichana Waja na mahafali ya 12 ya Shule ya Sekondari ya Waja ya Wavulana zilizopo mkoani Geita, Dkt. Gwajima amesema wahitimu hao wanapaswa kubadili fikra na mitazamo yao ili waweze kutumia elimu waliyoipata kutatua changamoto za jamii na kuchangia maendeleo ya taifa.
Amesisitiza kuwa badala ya kukata tamaa na kulalamika kuhusu changamoto zinazowakabili, wanapaswa kujitambua, kutafuta fursa za kiuchumi na kutumia maarifa yao kubuni suluhisho litakalowasaidia kujiletea maendeleo.
Kwa upande wao, Mkurugenzi wa Kampuni za Waja, Jackline Tesha, na Mbunge wa Jimbo la Geita Mjini, Mhandisi Chacha Wambura, wamewataka wahitimu hao kumtegemea Mungu, kuheshimu na kuwasikiliza wazazi wao pamoja na kuzingatia maadili mema katika maisha yao.
Akisoma risala ya shule, Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Waja, Glory Ottaru, amesema miongoni mwa mafanikio yaliyopatikana ni utoaji wa elimu bora na maandalizi ya wanafunzi wenye uwezo wa kukabiliana na changamoto za maisha.
Katika hatua nyingine, shule hiyo imetoa zawadi za pikipiki kwa walimu waliofanya vizuri katika ufundishaji wa masomo yao, ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wao katika kuinua kiwango cha taaluma shuleni hapo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Ruvuma, Oddo Mwisho, ametoa onyo kwa watumishi na viongozi wa chama hicho mkoani humo dhidi ya vitendo vya ubadhirifu, huku akisisitiza umuhimu wa kuwa waadilifu katika kusimamia miradi ya maendeleo ya chama.
Onyo hilo limetolewa Oktoba 31, 2026, wakati wa hafla ya kumuaga aliyekuwa Afisa Miradi wa CCM Mkoa wa Ruvuma, Thomas Mwaifunge, ambaye amehamishiwa Makao Makuu ya CCM.
Mwenyekiti Mwisho ameeleza kuwa Chama hicho hakitavumilia kuwa na viongozi au watendaji wasio waadilifu, akiwataka wanaopewa dhamana ya kuongoza kutumia nafasi zao kwa uwazi na kuhakikisha rasilimali za Chama hicho zinalindwa na kusimamiwa kwa ufanisi.
Akizungumza katika hafla hiyo, Katibu wa CCM Mkoa wa Ruvuma, Mohamed Aly, amewasilisha taarifa ya mafanikio ya Mkoa huo ambapo amesema kuwa hadi sasa chama kimefanikiwa kutekeleza miradi yenye thamani ya shilingi bilioni 1.8 katika ngazi ya mkoa pekee.
Aly ameongeza kuwa thamani hiyo haijumuishi miradi mingine inayotekelezwa katika ngazi za Wilaya, hatua ambayo amesema imewezesha Mkoa wa Ruvuma kujitokeza kuwa miongoni mwa mikoa inayoongoza kwa kujitegemea kiuchumi nchini kupitia vyanzo vyake vya ndani.
Kwa upande wake, Afisa Miradi aliyeondoka, Thomas Mwaifunge, ametumia nafasi hiyo kuwashukuru viongozi wenzake, wanachama, na wananchi wa Mkoa wa Ruvuma kwa ushirikiano alioupata wakati wote wa utekelezaji wa majukumu yake ya kusimamia miradi hiyo iliyofikisha mkoa huo hatua kubwa kiuchumi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
BREAKING NEWS:
Wakili Alute Mughwai Lissu ambaye ni kaka wa Mwenyekiti wa @ChademaTZ2 Tundu Lissu amefariki usiku wa kuamkia leo Novemba 1, 2026.
Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Dada yake aitwaye Rose Masesa pindi alipozungumza na Jambo TV.
Jambo TV ilipotaka kufahamu chanzo cha kifo chake Rose ametueleza kuwa kwa sasa hawezi kuzungumza lolote huku akitueleza kuwa msiba upo jijini Arusha.
"Ni taarifa za kweli msiba upo Arusha na mimi naelekea huko" alisema Rose kwa ufupi. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikimuonesha Rais wa Urusi, Vladimir Putin, akiwapatia aisikrimu viongozi wa ujumbe kutoka mataifa ya Afrika, imezua gumzo kuhusu heshima na hadhi ya viongozi wa Afrika katika majukwaa ya kimataifa na namna wanavyolinda maslahi ya bara hilo.
Tukio hilo lilitokea Oktoba 28, 2026, wakati Putin alipotembelea maonesho yaliyoandaliwa sambamba na Mkutano wa Tatu wa Urusi na Afrika jijini Moscow. Mkutano huo wa siku mbili uliwakutanisha wajumbe kutoka nchi 48 za Afrika, zikiwemo 22 zilizowakilishwa na viongozi wa nchi, ikiwa ni sehemu ya juhudi za Moscow kuimarisha uhusiano wake wa kisiasa na kiuchumi na bara hilo.
Baada ya video hiyo kusambaa, baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii wamehoji uwiano kati ya thamani ya rasilimali za Afrika na manufaa ambayo bara hilo hupata kupitia ushirikiano wake na mataifa ya nje.
Hoja hizo zimeibua maswali kuhusu nafasi ya viongozi wa Afrika katika diplomasia ya kimataifa na namna hukirimiwa na wenyeji wao pindi wanapokuwa ugenini, wengi wakidai kuwa mara nyingi viongozi hao hawapewi hadhi inayowastahili
Mkutano huo ulilenga kuimarisha uhusiano wa kisiasa, kiuchumi na kiusalama kati ya Urusi na mataifa ya Afrika. Putin aliitaja Urusi kuwa mshirika anayefaa kwa Afrika, huku akizikosoa nchi za Magharibi kwa kile alichodai kuwa ni kunyonya rasilimali za bara hilo na kutumia mikopo kuathiri maendeleo yake.
Aidha, alieleza utayari wa Urusi kupanua ushirikiano na nchi za Afrika katika sekta za biashara, kilimo, teknolojia na miundombinuThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI:
Raia wa Rwanda, Eric Nshimiye, mwenye umri wa miaka 54, amekutwa na hatia nchini Marekani kwa kutoa ushahidi wa uongo kuhusu ushiriki wake katika mauaji ya kimbari ya Rwanda ya mwaka 1994, baada ya miaka 30 ya kuficha ukweli
Mahakama ya shirikisho mjini Boston imemkuta na hatia ya makosa manne ya kutoa ushahidi wa uongo chini ya kiapo na kosa la kuzuia haki, wakati wa kesi ya aliyekuwa mwanafunzi mwenzake, Jean Leonard Teganya, mwaka 2019.
Ushahidi mahakamani ulionyesha kuwa Nshimiye alishiriki katika mashambulizi dhidi ya Watutsi alipokuwa mwanafunzi wa chuo kikuu mjini Butare, yakiwemo ya kuwapiga vichwani kwa marungu.
Nshimiye alikimbilia Kenya mwaka 1994 na kuhamia Marekani kama mkimbizi mwaka 1995. Waendesha mashtaka walisema alificha ushiriki wake katika mauaji hayo ili kupata nafasi ya kuingia Marekani na baadaye kutoa taarifa za uongo ili kupata uraia.
Mauaji ya kimbari ya Rwanda ya mwaka 1994 yalisababisha vifo vya takribani watu 800,000, wengi wao wakiwa Watutsi, ndani ya siku 100.
Nshimiye anakabiliwa na kifungo cha hadi miaka mitano kwa kila kosa la kutoa ushahidi wa uongo na hadi miaka 10 kwa kuzuia haki. Anatarajiwa kuhukumiwa Januari 26, 2027.
Wakati huo huo, Teganya alihukumiwa kifungo cha miaka 8 jela mwaka 2019 kwa udanganyifu wa uhamiaji baada ya kuficha taarifa kuhusu tuhuma za kuhusika katika mauaji ya kimbari. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita linamshikilia mwanafunzi Lameck Isack kwa tuhuma za kumuua mwanafunzi mwenzake, David Lucas, kwa kumchoma na kitu chenye ncha kali katika sehemu za shingo na ubavu wa kulia, kufuatia ugomvi unaodaiwa kuchochewa na wivu wa kimapenzi.
Tukio hilo limetokea Oktoba 29, 2026, majira ya saa 8 mchana, katika Kijiji cha Mhama, Kata ya Namonge, Wilaya ya Bukombe mkoani Geita, ambapo vijana hao wawili walikuwa wamekutana na wenzao watatu kwa mazungumzo katika eneo maarufu kama kijiwe.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 30, 2026, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, SACP Safia Jongo, amesema mtuhumiwa, marehemu na wanafunzi wengine watatu wote ni wahitimu wa Kidato cha Nne mwaka 2026 katika Shule ya Sekondari Said Nkumba.
Amesema muda mfupi baada ya kukutana, kulitokea mabishano kati ya mtuhumiwa na marehemu baada ya kila mmoja kudai kuwa na uhusiano wa kimapenzi na msichana mmoja ambaye pia ni mhitimu wa Kidato cha Nne katika shule hiyo.
Kamanda Jongo amesema mabishano hayo yaligeuka kuwa ugomvi, ambapo mtuhumiwa aliyekuwa amejihami kwa kitu chenye ncha kali alimchoma David sehemu za shingo na ubavu wa kulia, hali iliyosababisha kifo chake muda mfupi baadaye.
Amesema chanzo cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi, huku mwili wa marehemu ukiwa tayari umefanyiwa uchunguzi wa kitabibu na kukabidhiwa kwa ndugu zake kwa ajili ya mazishi.
Aidha, amesema mtuhumiwa anaendelea kushikiliwa na kuhojiwa na Jeshi la Polisi huku uchunguzi ukikamilishwa kwa ajili ya hatua za kisheria na kumfikisha mahakamani.
Katika hatua nyingine, Kamanda Jongo amewataka wazazi na walezi kuimarisha malezi, maadili na uangalizi kwa watoto wao, ikiwemo kufuatilia makundi wanayoshirikiana nayo pamoja na kuwapatia mwongozo na ushauri unaofaa ili kuepusha vitendo vya ukatili na uhalifu miongoni mwa vijana.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI PICHA:
Dodoma. Mkurugenzi wa Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi @ppp_centre_Tz David Kafulila @kafulila_david amehudhuria hafla ya uzinduzi rasmi wa Majengo ya Mji wa Serikali Mtumba, iliyofanyika leo, Oktoba 30, 2026, katika Viwanja vya Mashujaa, jijini Dodoma.
Hafla hiyo iliyoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh.Samia Suluhu Hassan, imeweka alama muhimu katika juhudi za Serikali za kukusanya taasisi zake katika eneo moja kwa lengo la kuimarisha uratibu na ufanisi wa utoaji huduma kwa wananchi.
Ushiriki wa Kafulila katika hafla hiyo unaonesha umuhimu wa ushiriki wa taasisi za umma katika matukio ya kitaifa yanayolenga kuimarisha utendaji wa Serikali na kuchochea maendeleo ya nchi. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Uongozi wa Kata ya Levolosi jijini Arusha umeiomba Serikali kupitia Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Baraza la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), pamoja na mamlaka nyingine husika kuchunguza kwa kina taratibu za umiliki wa kiwanja namba 428 na mchakato wa utoaji wa vibali vya ujenzi wa jengo la biashara la ghorofa namba 235.
Hatua hiyo inafuatia madai kuwa jengo hilo linajengwa katika eneo linalohifadhi miundombinu muhimu ya maji ya mvua na maji taka.
Wakizungumza na waandishi wa habari leo, Oktoba 30, 2026, Diwani wa Kata ya Levolosi, Abbasi Haji, Mwenyekiti wa Mtaa wa Levolosi, Evelin Shirima, pamoja na Balozi Edward Sumari, wamesema hawakushirikishwa kabisa katika hatua za ujenzi huo.
Viongozi hao wamedai kuwa jengo hilo limejengwa katikati ya mtaro wa maji ya mvua na juu ya chemba za maji taka, hali inayozua hofu kubwa ya kero za kiafya na mafuriko kuelekea msimu wa mvua.
Kufuatia hali hiyo, wameomba Serikali ichunguze uhalali wa taratibu zilizotumika kupata eneo hilo na vibali vya ujenzi, wakihofia kuwa kuwepo kwa jengo hilo kutaathiri mfumo wa upitishaji wa maji.
Kwa upande wake, msimamizi wa jengo hilo, aliyetambulika kwa jina la Jacob, amepinga vikali madai hayo na kueleza kuwa mtaro huo ndio uliojengwa kimakosa katika eneo hilo. Pia amesisitiza kuwa jengo hilo halijajengwa juu ya chemba za maji taka, huku akielekeza maswali zaidi kwa Mhandisi wa Jiji la Arusha.
Akifafanua kuhusu historia ya kiwanja hicho, Mhandisi wa Jiji la Arusha, Jacob Mwakyambiki, amebainisha kuwa eneo hilo awali lilikua mali ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kabla ya kuuzwa kwa mtu mwingine, na baadaye kununuliwa na Abdalla Mussa, ambaye ndiye mmiliki wa sasa mwenye hati miliki halali kisheria.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mbunge wa Jimbo la Bunda, Boniface Mwita Getere, ameitaka Serikali kuhakikisha mipango ya bajeti inalenga kutatua changamoto zinazowakabili Wananchi, ikiwemo upungufu wa madawati katika shule za msingi na sekondari, barabara na huduma ya maji, ili kuimarisha imani ya wananchi kwa viongozi wao.
Akichangia Mapendekezo ya Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2027/2028, leo Oktoba 30, 2026, Bungeni jijini Dodoma, Getere amesema kuna maeneo ambayo wanafunzi wanalazimika kukaa chini kutokana na ukosefu wa madawati, hali aliyosema inahitaji kushughulikiwa kupitia mipango ya Serikali.
Amesema ni muhimu mipango ya maendeleo iandaliwe kwa kuzingatia mahitaji halisi ya wananchi, akieleza kuwa viongozi wanapaswa kuhakikisha wanatimiza matarajio ya wananchi badala ya kutoa ahadi ambazo hazitekelezwi.
Aidha, Getere amesema changamoto kubwa katika utekelezaji wa miradi nchini ni usimamizi usioridhisha wa fedha, akitoa mfano wa miradi ambayo gharama zake huongezeka kutoka Sh milioni 300 hadi Sh milioni 700, huku akitaka kuwepo kwa usimamizi madhubuti wa rasilimali za umma.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) limetoa semina maalum kwa madereva teksi (maafisa usafirishaji) wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam, likiwalenga kama wadau wakuu katika kukuza utalii na kuiinua taswira ya nchi kwa kuwa ndio watu wa kwanza kukutana na watalii na wageni wanaoingia nchini.
Semina hiyo ya siku moja imefanyika leo, Oktoba 30, 2026, katika Uwanja wa Ndege wa JNIA Terminal 3, ikihusisha viongozi wa TANAPA, maafisa usafirishaji, pamoja na maofisa wa Jeshi la Polisi.
Akizungumza wakati wa semina hiyo, Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi na Mkuu wa Kanda ya Mashariki (TANAPA), Fredrick Malisa, anayesimamia uhifadhi na maendeleo ya biashara, ameeleza kuwa lengo kuu la mafunzo hayo ni kuwapa madereva uelewa wa kina kuhusu vivutio vya utalii nchini pamoja na umuhimu wa kutoa huduma bora na za usalama kwa wageni
"Sisi TANAPA tunaamini kwamba hawa ndio wadau wetu wakubwa kwa kuwa wanakutana na watalii au na wageni wao kwa mara ya kwanza na anakuwa naye kwa muda wakati anampeleka katika eneo lake la pili baada ya kushuka kutoka kwenye ndege aliyokuja nayo. Kwa hiyo tumewapa semina ya siku moja kujua wajibu wao ni nini, wanatakiwa watekeleze nini, umuhimu wao wa kuzingatia sheria mbalimbali za nchi", ameeleza.
Malisa ameongeza kuwa semina hiyo imezingatia pia nidhamu ya udereva, kuwa na leseni halali, afya njema, kauli nzuri kwa wateja (customer care), pamoja na elimu ya usalama barabarani kutoka Jeshi la Polisi ili kuhakikisha wageni wanatoka uwanjani salama na kuondoka na taswira chanya kuhusu Tanzania
Kwa upande wake, Kiongozi wa Madereva Teksi wa Uwanja wa Ndege wa JNIA, Patrick Joseph, amewashukuru TANAPA kwa kutoa elimu hiyo na kuomba mafunzo hayo yawe endelevu ili kuwajengea uwezo wa kutoa huduma za kiwango cha juu bila kuiangusha nchi
"Semina hii imetujenga na kutuongezea upana wa kuelewa ni namna gani tunatakiwa tuwakarimu wageni wetu wanapokuja Tanzania sababu sisi tukifanya makosa ya kutowakaribisha vizuri wageni na kuwapa huduma iliyo bora ina maana tunaiangusha nchi. Kwa hiyo semina hii tumeikubali na tunaomba TANAPA isiwe mwisho leo", ameeleza.
Kadhalika, Afisa Airport Tax Terminal 3, Sophia Omar, pamoja na maafisa wengine, wametoa shukrani zao kwa TANAPA na kuomba semina hizo zitolewe angalau mara moja au mbili kwa mwaka ili kuendelea kuwafunda madereva hao kuwa mabalozi wazuri wa utalii
"Semina hii tuliyoipata leo itaendelea kutujenga na inaendelea kutujenga na itaendelea kuwasaidia madereva teksi kuendelea kuwapokea wateja wetu vizuri kila wanapoingia na kwenda kutembelea mbuga zetu na utalii mbalimbali uliokuwepo nchini kwetu", ameeleza.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametambua na kupongeza mchango wa aliyekuwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, katika usimamizi na utekelezaji wa hatua mbalimbali za kuhamishia shughuli za Serikali jijini Dodoma na ujenzi wa Mji wa Serikali Mtumba.
Rais Samia ametoa pongezi hizo leo, Oktoba 30, 2026, wakati akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa majengo ya ofisi za Wizara na Taasisi za Serikali, barabara za lami pamoja na miundombinu muhimu na wezeshi katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.
Amesema mafanikio yaliyofikiwa katika ujenzi na kukamilisha miundombinu ya mji huo yametokana na usimamizi wa karibu wa viongozi na watendaji wakuu wa Serikali waliohusika katika hatua mbalimbali za utekelezaji wa mradi huo.
Katika kutambua mchango huo, Rais Samia amemtaja kwa namna ya pekee Majaliwa, aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na Hayati John Kijazi, aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, na Balozi Moses Kusiluka, Katibu Mkuu Kiongozi wa sasa, kwa mchango wao katika kufanikisha azma ya kuhamishia shughuli za Serikali Dodoma.
Pia amezitambua kamati za wataalamu kwa uratibu na usimamizi wao uliowezesha utekelezaji wa shughuli mbalimbali zilizohusiana na uhamisho wa Serikali na maendeleo ya Mji wa Serikali.
Rais Samia amesema kukamilika kwa majengo ya kudumu ya ghorofa, barabara za lami na miundombinu mingine ni sehemu ya kuendeleza maono ya Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, ya kuifanya Dodoma kuwa Makao Makuu ya nchi.
Amesisitiza kuwa mafanikio hayo ni matokeo ya juhudi za pamoja na yanapaswa kuendelezwa kwa kuhakikisha miundombinu hiyo inatumika kuongeza ufanisi wa utendaji wa Serikali na kuboresha huduma kwa wananchi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira, Hamad Masauni amezitaka nchi wanachama wa Mamlaka ya Ziwa Tanganyika (LTA) kuhakikisha kuwa juhudi za uhifadhi wa ziwa hilo zinaenda sambamba na kukuza fursa za uwekezaji rafiki kwa mazingira, ili kuchangia ajira na kipato cha jamii bila kuhatarisha mfumo wa ikolojia.
Waziri Masauni ametoa wito huo leo, Oktoba 30, 2026, mkoani Dar es Salaam wakati wa kikao cha 14 cha Mkutano wa Mawaziri wa Mamlaka ya Ziwa Tanganyika (LTA), kinachozikutanisha nchi wanachama za Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Tanzania na Zambia.
“Ni muhimu pia kuhakikisha kuwa uhifadhi wa ziwa unaenda sambamba na maendeleo ya kiuchumi... na fursa za uwekezaji rafiki kwa mazingira ili kuchangia ajira na kuongeza kipato cha jamii bila kuhatarisha uwezo wa ziwa wa kuendelea kutoa huduma muhimu za kiikolojia", ameeleza Masauni.
Waziri Masauni amebainisha kuwa Ziwa Tanganyika ni miongoni mwa rasilimali zenye thamani kubwa Afrika na duniani, na kwamba uamuzi wa nchi moja ndani ya bonde hilo una athari moja kwa moja kwa nchi jirani, akisisitiza kuwa Ziwa Tanganyika linahitaji utashi thabiti wa kisiasa na uwajibikaji wa pamoja kati ya nchi zote zinazolizunguka ili kulinda rasilimali hizo kwa uendelevu.
"Ziwa Tanganyika linahitaji utashi wa nchi husika katika kuhakikisha kwamba ulinzi wa rasilimali zetu kwa pamoja linakuwa ni endelevu na jukumu letu sote. Hivyo basi niwahimize nchi wanachama tuendelee kushughulikia ama kutathmini maamuzi ya pamoja", ameeleza.
Aidha, ameeleza kuwa katika mtazamo wa kidiplomasia ya kikanda, ziwa hilo ni mfano wa jinsi rasilimali za pamoja zinavyoweza kujenga ushirikiano wa kiuchumi na maendeleo endelevu, huku akisisitiza kuwa Mkataba wa Usimamizi Endelevu wa Ziwa Tanganyika una nafasi muhimu ya kuimarisha uratibu kati ya mataifa hayo manne.
Kwa upande wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchumi wa Kijani na Mazingira wa Jamhuri ya Zambia, Dkt. Douty Chibamba Akiwasilisha msimamo wa Jamhuri ya Zambia, mwakilishi wa nchi hiyo amethibitisha kuwa Zambia itaendelea kushirikiana bega kwa bega na serikali za Burundi, DRC, na Tanzania katika kulinda na kusimamia rasilimali za Ziwa Tanganyika.
Naye Waziri wa Uvuvi na Mifugo wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Jean-Pierre Tshimanga Buana amebainisha kuwa washiriki wa mkutano huo ndio watekelezaji wakuu wanaotegemewa katika kuleta matokeo na uendelevu wa ziwa hilo. Hivyo, ametoa wito ulitolewa kwa LTA kuwakusanya wadau wote wakubwa wanaozunguka ziwa hilo ili kuunganisha nguvu katika kutatua changamoto za kiikolojia zinazokabili ziwa hilo.
Katika kikao hicho, Tanzania imechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kikanda ya Mkataba wa Usimamizi Endelevu wa Mazingira ya Bonde la Ziwa Tanganyika, hatua inayoiweka katika nafasi ya kuongoza juhudi za kikanda za kukabiliana na changamoto za kimazingira. Tanzania inashika nafasi hiyo wakati takribani theluthi mbili ya bonde la ziwa hilo ikiwa ndani ya mipaka yake, huku kukiwa na changamoto za ongezeko la kina cha maji, kupungua kwa akiba ya samaki, na athari za mabadiliko ya tabianchi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewataka watumishi wa umma kuhakikisha wanaendelea kufanya kazi kwa bidii na ufanisi katika kutoa huduma kwa wananchi.
Rais samia ameeleza hayo leo Oktoba 30, 2026 Jijini Dodoma alipokuwa akihutubia katika Hafla ya uzinduzi wa majengo ya Wizara, Taasisi za Serikali, Barabara za lami katika Mji wa Serikali Mtumba.
Pia ameitaka Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji kwa kushirikiana na Sekta nyingine kuendeleza, kuhamasisha na kuweka mikakati madhubuti ya kuvutia wawekezaji mkoani humo ili kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuiendeleza Dodoma.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema majengo ya ofisi za Wizara na Taasisi za Serikali katika Mji wa Serikali Mtumba, Dodoma, yamejengwa kwa fedha za ndani bila mikopo kutoka taasisi yoyote.
Akizungumza leo, Oktoba 30, 2026, wakati wa uzinduzi wa majengo hayo na barabara za lami, Rais Samia amesema Watanzania wanapaswa kujivunia miundombinu hiyo ya kisasa iliyojengwa kwa rasilimali za nchi.
“Majengo na miundombinu mizuri, imara na ya kisasa tuliyojenga kwa fedha zetu wenyewe hapa, hamna mkopo kutoka taasisi yoyote,” amesema.
Amewataka watumishi wa umma kutumia mazingira hayo bora kuongeza uwajibikaji, uadilifu na ufanisi katika kutoa huduma kwa wananchi. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema Serikali inaendelea na utekelezaji wa mipango mbalimbali ya kuendeleza Jiji la Dodoma, ikiwemo kuimarisha miundombinu ya barabara, upatikanaji wa maji safi na salama, huduma za afya, elimu pamoja na usambazaji wa nishati ya umeme wa uhakika.
Rais samia ameeleza hayo leo Oktoba 30, 2026 Jijini Dodoma alipokuwa akihitubua katika Hafla ya uzinduzi wa majengo iliyofanyika Mkoani humo katika Mji wa Serikali Mtumba.
"Serikali inaendelea na utekelezaji wa mipango mbalimbali ya kuendeleza jiji la Dodoma, ikiwemo kuimarisha miundombinu ya barabara, upatikanaji wa maji safi na salama" amesema Rais Samia.
Amesisitiza utunzaji wa majengo hayo na miundombinu mingine pamoja na usafi wa mazingira katika eneo hilo akihimiza usimamizi mzuri ili mandhari ya ke yaendelee kuvutia.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema uamuzi wa kuhamishia makao makuu ya nchi mkoani Dodoma kulilenga kusogeza huduma karibu na wananchi pamoja na kuboresha utaratibu wa ufuatiliaji wa shughuli za Serikali kutoka maeneo mbalimbali ya nchi.
Rais samia ameeleza hayo leo Oktoba 30, 2026 Jijini Dodoma alipokuwa akihitubua katika Hafla ya uzinduzi wa majengo iliyofanyika Mkoani humo katika Mji wa Serikali Mtumba.
"Kuhamishia makao Makuu ya nchi Dodoma kulilenga kusogeza huduma za Serikali karibu na wanachi kwa kuboresha utaratibu wa ufuatiliaji na utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Serikali kutoka maeneo mbalimbali ya nchi" amesema Rais Samia.
Amesema kukamilika kwa majengo ya eneo hilo, barabara za lami na miundombinu mingine ya lazima kutaongeza tija na ufanisi kwa watendaji wa serikali na kupunguza gharama kwa wananchi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI:
Mahakama Kuu ya Kenya katika Kaunti ya Nairobi imewaamuru maafisa wa polisi kumfikisha Mwanaharakati na Kada wa CHADEMA, Twaha Mwaipaya mbele yake Jumatatu, Novemba 2, 2026, saa tano asubuhi, akiwa hai au amefariki, ili kueleza alipo na sababu za kukamatwa na kuzuiliwa kwake.
Amri hiyo imetolewa Oktoba 30, 2026, na Jaji Alexander M. Muteti, kufuatia maombi yaliyowasilishwa na shirika la VOCAL Africa kwa kushirikiana na wadau wake, likiitaka mahakama ichunguze kutoweka kwa Mwaipaya, raia wa Tanzania.
Kwa mujibu wa amri hiyo, Inspekta Jenerali wa Polisi Kenya, Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) na Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Ruai wanapaswa kuhakikisha Mwaipaya anafikishwa mahakamani pamoja na hati halisi ya kumweka kizuizini.
Maafisa hao pia wanatakiwa kueleza sababu za kukamatwa na kuzuiliwa kwake, pamoja na kwa nini asiachiliwe mara moja.
Katika taarifa yake, VOCAL Africa imesema imewasilisha maombi hayo pamoja na washirika wake kufuatia madai ya kutekwa kwa Mwaipaya. Shirika hilo limetaka kuwepo kwa uwajibikaji wa Serikali na kukomeshwa kwa vitendo vya utekaji na watu kupotezwa kinyume cha sheria.
Mahakama pia imewaagiza walalamikiwa na wahusika wengine katika shauri hilo kuwasilisha majibu yao kabla ya saa tatu asubuhi Jumatatu, Novemba 2, 2026.
Shauri hilo litatajwa tena siku hiyo hiyo saa tano asubuhi kwa maelekezo zaidi ya mahakama. Mahakama imeonya kuwa yeyote atakayekiuka au kushindwa kutekeleza amri hiyo anaweza kuchukuliwa hatua za kisheria.
Twaha Mwaipaya anadaiwa kutekwa na watu wenye silaha katika eneo la Kamulu, lililoko nje kidogo ya Jiji la Nairobi nchini Kenya, Oktoba 25, 2026
Taarifa kutoka shirika la Haki za Binadamu la Amnesty International zilieleza kuwa Mwaipaya alitekwa mnamo saa nne asubuhi wakati akiwa safarini kwa teksi kwenda kuwatembelea marafiki zake huko Kamulu, katika Kaunti ya Machakos, ambapo watu waliomteka walikuwa wakitumia magari matatu, likiwemo gari la aina ya Toyota Land Cruiser Hardtop. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Chama cha ACT Wazalendo kimetangaza ziara yake ya kwanza kitaifa inayolenga kukutana na wananchi maeneo mbalimbali nchini ili kusikiliza kero zao na kuhamasisha uwajibikaji.
Taarifa hiyo imetolewa leo Oktoba 30, 2026 na Naibu Katibu wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma wa Taifa wa chama hicho, Shangwe Ayo, ambaye ameeleza kuwa ziara hiyo itaongozwa na Kiongozi wa Chama, Dorothy Semu, akishirikiana na Makamu Mwenyekiti wa Bara, Isihaka Rashid Mchinjita.
Katika ziara hiyo, misafara ya viongozi hao amesema imegawanywa ambapo, Makamu Mwenyekiti Isihaka Mchinjita akishirikiana na Luhaga Mpina wataelekea Kanda ya Ziwa. Kwa upande mwingine, Kiongozi wa Chama Dorothy Semu ataongoza msafara katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini na Magharibi, ukiwemo mkoa wa Mbeya, Iringa, Njombe, Kigoma pamoja na Tanga.
Ayo amesisitiza kuwa ziara hiyo ni muhimu kwani inawapa viongozi wa ACT Wazalendo fursa ya kukutana na Watanzania wanaokabiliwa na maisha magumu na wanaodai haki pamoja na uwajibikaji.
Kufuatia hatua hiyo, chama hicho kimewaomba Watanzania kujitokeza kuunga mkono ziara hiyo na kuunganisha nguvu kwa pamoja katika mapambano ya kuleta mabadiliko nchini.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Rais Samia Suluhu Hasaan amepongezwa kwa jitihada zake za kukamilisha ujenzi Majengo ya Serikali katika mji wa Mtumba jijini Dodoma ikielezwa kuwa ametimiza ndoto za viongozi waliomtangulia.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Prof. Kitila Mkumbo akizungumza kwenye uzinduzi wa majengo hayo leo Oktoba 30, 2026
"Mheshimiwa Rais tunakushukuru na kukupongeza kwa kazi kubwa mliyoifanya katika kupokea na kuendeleza na kukamilisha utekelezaji wa maono ya Baba wa Taifa kuhamishia Makao Makuu ya Serikali hapa Dodoma" amesema Kitila
Ameeleza kuwa Rais Samia amekuwa na nafasi kubwa katika kushiriki utekelezaji wa ujenzi na uhamiaji wa mji huo toka alipokuwa Makamu Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania (TNMC), Agnes Yotamtawa amewasisitiza wauguzi watarajali kuzingatia miongozo, taratibu na kanuni za utoaji huduma za uuguzi na ukunga ili kuhakikisha wagonjwa wanapata huduma bora, salama na zenye kuzingatia weledi wa taaluma.
Msisitizo huo umetolewa leo Oktoba 30, 2026 Jijini Dodoma na Msajili huyo katika semina elekezi kwa wauguzi na wakunga wanafunzi (watarajali) kabla ya kuelekea katika hospitali mbalimbali hapa nchini kuanza mafunzo ya mwaka mmoja kwa vitendo baada ya kuhitimu shahada za kwanza za uuguzi na ukunga katika vyuo mablimbali vya ndani nanje ya nchi.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga, Saturini Manangwa, amewataka wauguzi hao kutumia kipindi hicho cha mafunzo kwa vitendo kujifunza kwa bidii, kushirikiana na wataalamu wenye uzoefu pamoja na kuzingatia maelekezo wanayopewa na wasimamizi wao.
Amesisitiza kuwa mafunzo kwa vitendo ni hatua muhimu katika kuwaandaa wauguzi watarajali kuwa wataalamu wenye ujuzi, uwezo na weledi unaohitajika katika kutoa huduma bora za uuguzi na ukunga.
Wauguzi watarajali ni wataalamu wa afya ambao wameshahitimu masomo yao ya nadharia katika vyuo vya uuguzi na ukunga, ambao wanapitia kipindi cha mafunzo ya vitendo kazini kabla ya kupewa leseni kamili ya kusajiliwa na kuanza kufanya kazi rasmi ya uuguzi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, akifuatana na Rais wa Angola, João Manuel Gonçalves Lourenço, rasmi amezindua barabara za lami uenye urefu wa kilomita 51.2 katika Mji wa Serikali Mtumba Mkoani Dodoma.
Uzinduzi huo umefanyika leo, Oktoba 30, 2026, kupitia hafla ya uzinduzi wa majengo ya ofisi na miundombinu hiyo, ikiwa ni hatua muhimu katika kukamilisha na kuanza kutumika kwa Mji wa Serikali Mtumba ili kuimarisha ufanisi wa shughuli za Serikali na kurahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mbunge wa Jimbo la Katavi, Thomas Kampala Maganga ameihoji Serikali ieleze Mipango na Mikakati yake katika kukabiliana vitendo vya mmomonyoko wa maadili hasa Ushoga ambao amesema umeendelea kuongezeka katika jamii
Mbunge huyo amehoji hayo leo, Oktoba 30, 2026 bungeni jijini Dodoma huku akisema licha ya Serikali kuendelea kuweka juhudi katika kukabiliana na masuala hayo lakini bado hali imeendelea kuwa mbaya.
Akijibu hoja ya Mbunge hiyo, Naibu Waziri wa maendeleo ya jamii, jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Maryprisca Mahundi, amesema Serikali itaendelea kushirikiana na viongozi wa mitaa, vijiji na kata, pamoja na maafisa maendeleo ya jamii katika kuimarisha malezi na kudhibiti changamoto za mmomonyoko wa maadili miongoni mwa vijana nchini.
Amesema mkakati wa Taifa wa kukabiliana na hali hiyo tayari umeanza kutekelezwa, huku akisisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya serikali na wananchi.
Ameongeza kuwa, jukumu la kulinda maadili halipaswi kuachwa kwa Serikali pekee, bali jamii kwa ujumla inapaswa kusimamia mila, desturi na tamaduni salama ili kuendeleza misingi bora ya malezi kwa kizazi kipya.
Aidha ameeleza kuwa familia inayo nafasi kubwa katika kujenga maadili ya watoto, hivyo amewataka wazazi kutotanguliza shughuli za kutafuta kipato na kusahau wajibu wao wa kuwalea watoto, kuzungumza nao mara kwa mara na kuwafuatilia katika makuzi yao.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
#ad
🏃♂️🐟 MUSOMA MARATHON 2026 🚴♂️✨
Kukimbia kwa ajili ya Uchumi, Elimu, Kilimo cha Samaki na Utalii!
Mkoa wa Mara unakwenda kusimama kwa matukio makubwa ya michezo, utamaduni na uwekezaji!
🗓️ Tarehe: 18–20 Desemba 2026
📍 Mahali: Wilaya ya Musoma, Mara
🚀 Uzinduzi Rasmi: 1 Novemba 2026 (Mgeni Rasmi: Mkuu wa Mkoa wa Mara)
🔥 Vivutio Vikubwa:
• Michezo: Marathon (5km, 10km, 21km), Mashindano ya Baskeli, Makasia na Kuogelea Ziwa Victoria.
• Tamasha: Kichuri Festival (Utamaduni) & Samaki Festival (Maonesho ya Uchumi wa Buluu na vyakula).
• Biashara: Business Round Table (Mazungumzo ya fursa za uwekezaji na masoko).
💼 Fursa za Udhamini:
Tunakaribisha Makampuni, Benki, Taasisi na Wafanyabiashara kuwa wadhamini ili kukuza chapa zenu na kuunga mkono uchumi wa mkoa wetu.
#musomamarathon2026 #uchumiwabuluu #utaliiwamara
Mawasiliano
0757 372138 -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Spika wa Bunge, Mussa Zungu, ameitaka Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha, Ofisi ya Waziri Mkuu na taasisi nyingine za Serikali, kuchunguza ununuzi na matumizi ya magari ya Serikali katika kipindi cha mwaka 2013 hadi 2026, kwa lengo la kubaini maeneo yanayoweza kupunguza gharama za uendeshaji.
Akitoa maelekezo hayo bungeni jijini Dodoma, leo Oktoba 30, 2026, Zungu amesema ni muhimu Serikali kudhibiti matumizi yasiyo ya lazima, ikiwemo ununuzi wa magari ya kifahari yanayohusisha gharama kubwa, akieleza kuwa fedha zinazotumika kununua gari moja la aina hiyo zinaweza kuelekezwa katika miradi ya kijamii, ikiwemo ujenzi wa nyumba za watumishi, vituo vya afya na madarasa.
Amesema uchunguzi huo unapaswa pia kujumuisha matumizi ya fedha za mafuta, gharama za matengenezo ya magari pamoja na uzingatiaji wa miongozo inayosimamia ununuzi wa magari ya watumishi wa umma.
Aidha, amesisitiza umuhimu wa kupitia utekelezaji wa Waraka Mkuu wa Utumishi wa Umma Na. 2 wa mwaka 2021, ili kubaini taasisi zinazokiuka taratibu zilizowekwa na kuweka mikakati ya kudhibiti matumizi yasiyo na tija.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Wakili Kulwa William Maduhu anaeleza kuwa mteja akipokea fedha kutoka benki au kwenye laini yake ya simu ana jukumu la msingi la kutoa taarifa kwenye benki au mtandao husika aliopokea fedha.
Anaeleza sababu ya kufanya hivyo ni kutokana na kuwa muamala huo unaweza msababishia matatizo kama atatumia fedha hiyo halafu ilitokana na miamala yenye mashaka
Una maoni gani mdau?.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) taifa, Mohammed Ali Kawaida ametoa wito kwa baadhi ya viongozi wa dini kuendelea kuhubiri malezi na maadili na siyo kufanya siasa katika nyumba za ibada.
Kawaida ametoa wito huo Oktoba 29, 2026 akiwa Chamwino mkoani Dodoma ambapo amesema karibuni kumekuwepo na mwelekeo wa wanafunzi kujirekodi wakiongea maneno yasiyo ya maadili.
"Leo ukienda msikitini unasikia siasa, ukienda kanisani siasa, sasa najiuliza nani atawakumbusha waumini kukumbuka kuwa kuna Mungu na siku ya mwisho, nitoe wito kwa viongozi wa dini kwanza kurudi katika maadili ya kazi yao," amesema Kawaida
Ameongeza kuwa baadhi ya viongozi hao wa dini kama wamechoka kufanya kazi ya dini waache kuwa huko na waingie katika ulingo wa siasa.
Amesema maadili yameshuka kwenye jamii kwasababu kundi la viongozi wa dini wa Kiislamu na Kikristo wamejikita kwenye siasa badala ya kuhubiri malezi na maadili kwa jamii.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Kuelekea uzinduzi rasmi wa majengo ya wizara na taasisi za Serikali katika Mji wa Serikali Mtumba unaotarajiwa kufanyika Oktoba 30, 2026, Serikali imeeleza kuwa ujenzi wa mji huo umeongeza tija katika utendaji kazi kwa kuwezesha watumishi kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi na kuharakisha utoaji wa huduma kwa wananchi.
Akiweka wazi faida za mradi huo leo Oktoba29, 2026, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Nsubili Joshua, amesema kuwa uwepo wa wizara na taasisi za Serikali katika eneo moja umesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza urasimu katika utoaji wa huduma, kurahisisha uratibu, pamoja na kuimarisha ushirikiano baina ya wizara mbalimbali.
Joshua amefafanua kuwa hatua hiyo imewezesha upatikanaji wa huduma jumuishi za Serikali katika eneo moja, hali inayochochea uwazi, uwajibikaji na ufuatiliaji wa karibu wa utekezingaji wa majukumu ya umma.
Aidha, ameongeza kuwa Mji wa Serikali Mtumba unasaidia kupunguza kwa kiasi kikubwa gharama za uendeshaji wa Serikali kwa kurahisisha matumizi ya pamoja ya rasilimali na kuboresha mifumo ya kiutendaji katika taasisi za umma, jambo linalotajwa kuwa hatua kubwa katika kuboresha utawala bora nchini.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Agrey Mwanri, amewataka watumishi wa Serikali wanaofanya kazi katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma, kuzingatia utumishi uliotukuka kwa kuhakikisha wanatoa huduma bora na zenye viwango vinavyolingana na ubora wa majengo na miundombinu iliyopo katika mji huo.
Mwanri ameyasema hayo leo, Oktoba 29, 2026, wakati wa ziara yake ya kutembelea baadhi ya majengo ya Serikali na taasisi zilizopo katika Mji wa Serikali Mtumba, ambapo amesisitiza umuhimu wa watumishi kuwahudumia wananchi kwa ufanisi, weledi na kuzingatia maadili ya utumishi wa umma.
Amesisitiza kuwa uwepo wa majengo ya kisasa unapaswa kwenda sambamba na utoaji wa huduma bora, ili wananchi wanaofika katika ofisi hizo waweze kupata huduma zinazokidhi matarajio yao.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametangaza uamuzi rasmi wa Serikali wa kufungua tena ubalozi wake nchini Angola, hatua inayolenga kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia, kukuza mawasiliano ya karibu, na kuongeza ushirikiano wa kimkakati kati ya nchi hizo mbili za kusini na mashariki mwa Afrika.
Rais Samia amesema hayo leo, Alhamisi, Oktoba 29, 2026, Ikulu jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza na waandishi wa habari kufuatia mazungumzo rasmi ya pande mbili na Rais wa Jamhuri ya Angola, João Manuel Gonçalves Lourenço, ambaye yuko nchini kwa ziara ya kitaifa. Rais Samia amebainisha kuwa tayari amemjulisha Rais Lourenço kuhusu uamuzi huo na kwamba katika kipindi kifupi kijacho atateua balozi atakayesimamia shughuli za ubalozi huo mjini Luanda.
Katika hotuba yake, Rais Samia amekumbushia kuwa uhusiano imara uliopo kati ya Tanzania na Angola ulitiliwa nanga na viongozi waasisi, Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere na Rais wa kwanza wa Angola Hayati Dkt. Agostinho Neto, wakati wa harakati za ukombozi wa nchi hiyo hadi ilipopata uhuru wake mwaka 1975.
Amesisitiza kuwa ziara ya Rais Lourenço ni ya kwanza ya kitaifa kufanywa na rais wa Angola nchini Tanzania kwa takriban miaka 47, tangu ziara ya mwisho iliyofanywa na Dkt. Agostinho Neto mwaka 1979. Ameongeza kuwa hatua ya hivi karibuni ya Angola kumwalika yeye binafsi kuzuru nchi hiyo mwaka jana, pamoja na kumweka mgeni maalum kwenye uzinduzi wa hospitali iliyopewa jina la Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mwezi Agosti mwaka huu, kunadhihirisha uthamani mkubwa ambao Rais Lourenço anaupa uhusiano na Tanzania.
Ubalozi wa Tanzania nchini Angola ulikuwa umefungwa mwanzoni mwa miaka ya 1990 kufuatia changamoto za kiuchumi na mkakati wa serikali wa kubana matumizi kwa kupunguza mtandao wa uwakilishi wa kidiplomasia kimataifa, ambapo tangu wakati huo shughuli za kidiplomasia zilianza kusimamiwa kupitia Ubalozi wa Tanzania ulioko Lusaka, Zambia.
Uamuzi huu wa sasa unatajwa kutoa msukumo mpya wa kiuchumi na kijamii, kurejesha mawasiliano ya moja kwa moja, na kusimamia kwa ufanisi makubaliano mbalimbali ya ushirikiano yaliyofikiwa kati ya nchi hizi mbili. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo amesema maandalizi ya hafla ya uzinduzi wa majengo ya ofisi za wizara na taasisi za serikali pamoja na barabara za lami katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma yamekamilika.
Kitila amesema hafla hiyo inaanza rasmi leo usiku kwa shughuli mbalimbali, ikiwemo upigaji wa fataki, huku kesho kukitarajiwa kufanyika shughuli kuu tatu zitakazohusisha uzinduzi wa barabara zinazounganisha maeneo mbalimbali ya Mji wa Serikali, uzinduzi wa jengo la Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa niaba ya majengo mengine, pamoja na hotuba ya Rais kwa Watanzania.
Aidha, Profesa Kitila amewataka wananchi wa Mkoa wa Dodoma kujitokeza kwa wingi kushiriki hafla hiyo ya uzinduzi, akieleza kuwa Mji wa Serikali ni alama muhimu katika maendeleo ya nchi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Baba wa mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 12, anayedaiwa kulawitiwa katika Kijiji cha Bulamba, Wilaya ya Bunda, mkoani Mara, amedai kuwa mtuhumiwa wa tukio hilo alikwenda kanisani na kukiri mbele ya waumini kuwa alitenda kosa hilo, huku familia ikiendelea kuhoji mwenendo wa shauri hilo.
Akizungumza na Jambo TV nyumbani kwa familia hiyo, baba wa mtoto huyo amesema wana wasiwasi kuhusu maendeleo ya shauri hilo, akidai kutopata taarifa za kutosha kuhusu hatua zinazochukuliwa na mamlaka husika. Amesema hali hiyo inawafanya waendelee kufuatilia suala hilo ili kufahamu hatua zilizofikiwa.
Amesema madai ya mtuhumiwa kwenda kanisani na kukiri kosa hilo mbele ya waumini ni miongoni mwa mambo yaliyowafanya waendelee kufuatilia shauri hilo.
Akieleza alichokifahamu kuhusu tukio hilo, baba huyo amesema: “Kitu ambacho sisi tulikithibitisha ni baada ya mtuhumiwa kufika kanisani na watu kanisani kuna watu wengi waliomthibitisha mtuhumiwa akatoa ushuhuda, akawaomba na kukiri kwamba jamani nimetenda kosa ambalo ni baya, nilimlawiti kijana. Hivyo mjue kwamba sasa hivi mimi nina kesi, ila kama waumini ninawaomba mniombee.”
Kwa mujibu wa baba huyo, tukio la madai ya kulawitiwa kwa mtoto huyo, ambaye jina lake limehifadhiwa kwa ajili ya kulinda utambulisho wake, linadaiwa kutokea Oktoba 3, 2026, katika Kijiji cha Bulamba, Wilaya ya Bunda, mkoani Mara, wakati mtoto huyo akiwa machungani
Tukio la madai ya kukiri kanisani linadaiwa kufanyika katika kanisa moja la kiroho lililopo Mwiseni, Bulamba.
Jambo TV inaendelea kufuatilia suala hilo ili kupata maelezo ya mamlaka zinazohusika kuhusu mwenendo wa shauri hilo.
Fuatilia mahojiano yote kupitia chaneli yetu ya YouTube ya Jambo TV.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mratibu wa Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) @THRDCOALITION , Wakili Onesmo Olengurumwa @OlengurumwaO amesisitiza kuwa taifa linapaswa kutibu majeraha, kuwajibika, na kukaa mezani kutafuta ukweli kuhusu matukio ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, badala ya kusahau yaliyotokea.
Wakili Olengurumwa ameyasema hayo leo, Oktoba 29, 2026, mkoani Dar es Salaam wakati wa Ibada maalum ya kuwakumbuka waliopoteza maisha, waliopotea, na majeruhi wa matukio ya wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania.
Akimulika haja ya kukabiliana na ukweli badala ya kupuuza changamoto zilizojitokeza, Wakili Olengurumwa amerejea methali za Kiswahili akionya kuwa kuweka kichwa chini kama mbuni hakutatui matatizo ya nchi.
“Waswahili wanasema taifa lisilokumbuka misiba yake ni taifa lisilokumbuka furaha zake. Maana yake tukijidanganya kana kwamba hatukupata msiba maana yake tunakuwa tuko tayari kuendelea kuwa katika eh changamoto... Sisi kama taifa hatupaswi kufikiri kwamba kwa kuweka kichwa chini kama anavyofanya mbuni basi kila kitu kinakuwa salama”, ameeleza Olengurumwa.
Olengurumwa amebainisha kuwa vitabu vitakatifu vya dini zote mbili za Uislamu na Ukristo kwa maana ya Qurani na Biblia vinafundisha kuwa haki, rehema, msamaha, amani, na ulinzi wa uhai ndio msingi mkuu wa jamii yenye mshikamano. Ameeleza kuwa Qurani inasisitiza kujibu uovu kwa namna iliyo bora zaidi ili uhasama ubadilishwe kuwa ukaribu, huku vitabu vya Kikristo vikihimiza kuondoa uchungu na hasira na badala yake kujenga huruma na msamaha.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Jumanne Muliro, amewatoa hofu wananchi na kutangaza kuwa hali ya usalama katika Jiji la Dar es Salaam ni shwari na njema, huku kila sekta ikiendelea na shughuli zake za kiuchumi kama kawaida.
Muliro ameyasema hayo leo, Oktoba 29, 2026, wakati akizungumzia hali ya usalama jijini humo, ambapo ameeleza kuwa wananchi katika maeneo mbalimbali pamoja na wafanyakazi wa ofisi za Serikali na sekta binafsi wameamka mapema na kuingia katika majukumu yao bila hofu wala taharuki.
Kamanda Muliro ameeleza kuwa miradi mikubwa ya kitaifa kama vile ujenzi wa barabara na madaraja inaendelea bila kikwazo chochote, na taasisi zote za kifedha zinafanya kazi vizuri.
Kamanda Muliro amewasifu wananchi wa Dar es Salaam kwa kutoa ushirikiano mkubwa kwa Jeshi la Polisi na mamlaka za kisheria, akibainisha kuwa wananchi wengi wanachukia uhalifu na wanatamani kuona utulivu na amani vikitawala.
"Wananchi wengi wanachukia uhalifu, wananchi wengi hawawapendi wahalifu, wananchi wengi hawataki vurugu. Wananchi wengi wanataka usalama. Usalama sio wangu. Usalama ni wetu... Tukizungumza suala la usalama sio langu, suala la usalama ni letu la kila mwananchi, mwananchi hasa mzalendo wa nchi hii, tushirikiane wote tuilinde nchi yetu. usalama ni wetu sio wangu", ameeleza.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI:
Jeshi la Polisi mkoani Mwanza linafanya uchunguzi wa miili ya vichanga wawili wa kiume wanaodaiwa kuwa mapacha iliyokutwa imetelekezwa katika jalala lililoko Mtaa wa Chamwenda Kata ya Nyasaka, wilayani Ilemela.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo, Oktoba 29, 2026 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, DCP Wilbrod Mutafungwa, amesema vichanga hivyo vinakadiriwa kuwa na umri wa miezi mitano hadi sita tangu kutungwa kwa mimba huku Polisi ikifanya uchunguzi kubaini chanzo cha kifo chao na mtu aliyehusika na kuvitupa.
"Tukio hilo limetokea Oktoba10, 2026, saa 12:45 jioni katika Mtaa wa Chamwenda Kata ya Nyasaka, Wilaya ya Ilemela, ambapo Jeshi la Polisi lilipokea taarifa kutoka kwa wananchi kuhusu kuonekana kwa miili ya vichanga hivyo vikiwa vimetelekezwa jalalani katika eneo hilo," amesema DCP Mutafungwa.
Kamanda Mutafungwa amesema baada ya Jeshi la Polisi kupata taarifa kutoka kwa wananchi kuhusu kuonekana kwa miili ya vichanga hivyo ikiwa imetelekezwa jalalani Askari walifika eneo la tukio na kufanya uchunguzi wa awali, kabla ya kuichukua miili hiyo na kuihifadhi katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Rufaa ya Sekou Toure.
Kamanda Mutafungwa amesema Jeshi la Polisi linaendelea na juhudi za kumtafuta mtu anayehusishwa na tukio hilo, pamoja na kubaini hali halisi iliyosababisha vichanga hivyo kupoteza maisha.
"Uchunguzi kuhusiana na tukio hili unaendelea na tunaomba mtu yeyote mwenye taarifa zinazoweza kusaidia katika uchunguzi aziwasilishe ili kusaidia
kukamatwa kwa mtuhumiwa aliyetenda tukio hili," amesema.
Katika tukio jingine Kamanda Mutafungwa amesema wameanzisha uchunguzi na kumsaka mwanamke mmoja ambaye bado hajafahamika jina wala makazi yake, anayetuhumiwa kuiba mtoto wa kiume mwenye umri wa miezi mitatu unaendelea.
"Tukio hilo limetokea tarehe 25.10.2026, majira ya saa 7:00 mchana, katika Kanisa la Living Water lililopo Mtaa wa Kiseke "A", Kata ya Kiseke, Wilaya ya Ilemela, ambapo mama wa mtoto huyo, Godliver Bahati Zilahenda, miaka 23na mkazi wa Galuma, Kawekamo, alikutana na mwanamke huyo kwa mara ya kwanza kanisani hapo tarehe 18.10.2026. Walikutana tena tarehe 25.10.2026 na kukaa pamoja ibadani," amesema Mutafungwa. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Ni zaidi ya siku saba tangu Jambo TV turipoti adha wanayopitia wananchi wa mtaa Yombo Dovya Temeke Dar es Salaam kutokana na ubovu wa daraja la kwa Muki.
Kwa mara ya kwanza tuliripoti kuanguka daraja hili Oktoba 21, 2026 ambapo wananchi wakieleza hata kushindwa kwenda kuzika mara nyingine hasa mvua zinaponyesha huku wakitaabika zaidi ya miaka mitano na wakieleza kuchoshwa na ahadi zisizotimia za viongozi.
Tumerudi Oktoba 28, 2026 kukagua je hatua zimechukuliwa baada ya kutoa taarifa hiyo.
Diwani wa Kata ya Makangarawe Fadhili Mboga na Mwenyekiti wa Mtaa wa Mbonde Rashid Mbanga wametueleza kuwa tayari umeanza mchakato ujenzi wa daraja la muda ili kuanza kutolewa kwa daraja lililoanguka.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mjumbe wa Shura ya Maimamu Tanzania, Sheikh Aboubakar Mgodo ametoa mwito wa kuwa wakweli, kuwajibika ili kuponya majeraha na maumivu yanayowakabili wananchi waliopoteza ndugu na waliotoweka wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu.
Sheikh Mgodo ameyasema hayo leo, Oktoba 29, 2026, mkoani Dar es Salaam wakati wa Ibada maalum ya kuwakumbuka waliopoteza maisha, waliopotea, pamoja na majeruhi wa matukio ya wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania wa Oktoba 29, 2025.
“Uongo hauwezi kutufikisha pazuri. Tunashauri vyombo vyetu, serikali yetu tuwe wakweli. Kosa linaweza kutokea iwe kwa bahati mbaya au makusudi, lakini baada ya kosa watu wanatakiwa wajirudi”, ameeleza Sheikh Mgodo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Katiba na Sheria, Abdallah Hamis Ulega amesisitiza kuwa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia Awamu ya Pili ni nguzo kuu katika kuwawezesha wananchi kupata haki bila kukumbana na vikwazo vya kiuchumi, akibainisha wazi kuwa haki haipaswi kuwa fursa ya watu wenye uwezo mkubwa wa kifedha pekee.
Amesema hayo jana, Oktoba 28, 2026, wakati akifungua rasmi utekelezaji wa kampeni hiyo katika Mkoa wa Pwani kwenye Viwanja vya Stendi ya Zamani ya Maili Moja, mjini Kibaha.
“Kampeni hii ya Mama Samia Legal Aid ni daraja, ni ukombozi kwa wananchi wengi wa hali ya chini, wasiojua wapi pa kwenda na hatua gani ya kuchukua,” amesisitiza Waziri Ulega, huku akiongeza kuwa shughuli hiyo inalenga kuwafikia moja kwa moja wajane, yatima, watu wenye ulemavu, na wananchi wa maeneo ya pembezoni.
Waziri Ulega amewahimiza wananchi wa Mkoa wa Pwani kujitokeza kwa wingi kutumia fursa hiyo ya siku 10 itakayoanza leo Oktoba 29 hadi Novemba 7, 2026, katika halmashauri zote za mkoa huo na kuwataka kuwa mabalozi wazuri kwa kuwahamasisha wengine wenye changamoto mbalimbali za kisheria. Pia amewapongeza viongozi wa dini na wataalamu wa sheria kwa mchango wao mkubwa katika kusogeza huduma hizo kwa wananchi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Askofu Wolfgang Pisa, ambaye pia ni Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Lindi, ameihimiza jamii kuomba huruma ya Mungu, kuliombea taifa na kuwaombea viongozi wa Serikali ili wawezeshe kupatikana kwa amani, haki, uhuru na ukweli katika jamii.
Askofu Pisa ameeleza hayo leo Oktoba 29, 2026 mkoani Lindi katika Adhimisho la Misa Takatifu ya kuwaombea watu walioumizwa, kupotea na kuuawa wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.
"Tuzidi kuomba huruma ya Mungu, tuliombee taifa letu, tuwaombee viongozi wote wa Serikali, ili Mungu bwana wetu aelekeze akili na mioyo yao kadiri ya mapenzi yake" amesema Askofu Pisa.
Amesisitiza kwamba ni muhimu kumilikiwa na ukweli, kuongozwa na ukweli hu, huku akikemea kuupotosha ukweli akisema kwamba ikiwa ukweli utapotoshwa bado utabaki kama ulivyo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Tume ya Taifa ya Mipango kwa kushirikiana na wizara za kisekta na taasisi za umma inaendelea na zoezi la kukusanya taarifa (fact-findings) za programu za kielelezo na miradi shikizi nchi nzima kwa lengo la kupata taarifa za kina na sahihi za programu hizo.
Akizungumza kuhusu zoezi hilo, Bw. Royal Lyanga ambaye ni Mkurugenzi anayesimamia Maeneo Muhimu yenye Matokeo Makubwa kwa Taifa kutoka Tume ya Taifa ya Mipango amesema lengo la zeozi hilo ni kuhakikisha kuna ufanisi katika utekelezaji wa Mpango wa Nne wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (FYDP IV) 2026/27 – 2030/31.
Bw. Lyanga amesema kuwa taarifa zinazokusanywa ni muhimu kwa kuwa zitasaidia kuhakikisha kuwa programu saba za kielelezo zilizobainishwa zinatekelezwa kwa kuzingatia malengo makubwa ya Dira 2050.
Aidha, ameeleza kuwa mbali na programu hizo za kielelezo, Tume ya Taifa ya Mipango inakusanya taarifa za miradi yote ya kimkakati ambayo ina mchango chanya katika kufikia matokeo makubwa kwa nchi, ikijumuisha miradi ya Barabara, nishati, maji, miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji, miradi ya mifumo ya teknolojia ya mawasiliano pamoja na miradi mingine ya kisekta.
Aidha, Bw. Lyanga amefafanua kuwa baada ya kukusanya taarifa hizo, miradi yote itaingizwa katika maabara (Labs) kwa kuwashirikisha wadau wote wa sekta kwenye kila mradi wa kielelezo ambapo itasaidia kupata matokeo chanya kwa kutatua changamoto mbalimbali ambazo zitabainika kwa kila mradi, kufungamanisha miradi hiyo na sekta nyingine, kuimarisha wigo wa ushirikishwaji wa sekta binafsi na kutambua uhalisia wa miradi hiyo kwa kuzingatia malengo ya Dira 2050 hususan katika kuzalisha ajira kwa vijana, kuboresha maisha ya watu na kuongeza mapato ya Serikali.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padre Dkt. Charles Kitima, amesema katika uchaguzi wa 2020 aliuliza kama kuiba kura ni dhambi au si dhambi huku akisisitiza kwamba utawala wa dunia kisiasa ni utumishi kwa watu wengine akirejea katika Katiba ya Tanzania ibara ya nane kwamba, maamuzi tayari yalisha fanyika hivyo ni lazima wananchi wasikilizwe.
Padre Dkt. Kitima amebainisha hayo leo Oktoba 29, 2026 Katika Misa ya kuwaombea marehemu na waathirika wa matukio ya Uchaguzi Mkuu wa 2025, iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
"Utawala wa dunia, utawala wa kisiasa ni utumishi kwa wenzako, kwenye katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya nane tulishafanya maamuzi, utawala ni dhamana unayopewa na wananchi na lazima uwasikilize wananchi... Uchaguzi wa 2020 hapa niliuliza swali mimi, wizi wa kura ni dhambi di dhambi?, niliuliza tu swali" amesema Padre Kitima.
Ameongeza kuwa suala la utawala kuwasikiliza wananchi pia lilisisitizwa na hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambaye ni mwasisi wa Tanzania.
Amesema kwamba licha ya ibara ya 3 ya katiba ya Tanzania i kwamba mfumo utakaotumika ni wa vyama vingi na mchakato wa kukabidhiana madaraka katika ibara ya tano kwa njia ya uchaguzi lakini bado wanaotoa ridhaa ya utawala ni wananchi.
Ameongeza kwamba hata katika ibara ya 21 wananchi ni lazima washiriki katika kuitawala nchi yao. Amesema zaidi kwamba pia wananchi ni lazima wawe huru kuzungumza ikiwemo kupitia midahalo mbalimbali.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI:
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, John Heche na aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, wametoa wito wa kutafuta ukweli, haki na uwajibikaji, mwaka mmoja baada ya matukio ya vurugu za baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.
Katika jumbe za kukumbuka matukio hayo kupitia kurasa za mitandao yao ya Kijamii, wamesisitiza umuhimu wa kuwakumbuka waliopoteza maisha, kuwajali majeruhi na familia zilizoathirika, wakieleza kuwa amani ya kudumu inahitaji ukweli, haki na uwajibikaji.
Katika andiko lake, Lema amesema Oktoba 29 inapaswa kuwa siku ya kutafakari kuhusu thamani ya maisha ya binadamu na kuchukua hatua za kuzuia matukio kama hayo yasijirudie. Amesema kuwakumbuka waathirika si kwa lengo la kulipiza kisasi, bali ni kusisitiza haki, utu na heshima kwa maisha ya kila Mtanzania. "
Kwa upande wake, Heche ameeleza matukio ya Oktoba 29, 2025 yangeweza kuepukika iwapo wito wa mabadiliko ya Katiba na sheria za uchaguzi uliotolewa na viongozi wa dini, vyama vya siasa na wadau wengine ungesikilizwa.
Amesema mwaka mmoja baadaye, bado kuna changamoto za kisiasa zinazohitaji kushughulikiwa, akieleza wasiwasi kuhusu madai ya utekaji na watu kupotezwa. Pia amedai kuwa baadhi ya wanaotaka maridhiano na uwajibikaji wanakabiliwa na vitisho na mashitaka ambayo anayataja kuwa hayana msingi.
Heche ameitaka Serikali kutanguliza mazungumzo na busara katika kutafuta suluhu ya changamoto hizo, akisisitiza umuhimu wa kujenga mazingira yanayowezesha pande zinazohusika kukutana na kujadili tofauti zao kwa amani.
Katika mapendekezo yake ya kutatua mkwamo wa kisiasa, Heche ametaka kuachiwa kwa Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, na wanachama wengine wanaokabiliwa na kesi anazodai hazina msingi, kuachiwa kwa watu wanaodaiwa kutekwa, pamoja na kuruhusu mazungumzo yatakayosimamiwa na msuluhishi huru.
Pia amesisitiza umuhimu wa kufanya uchunguzi huru kuhusu vifo vilivyotokea, kuwawajibisha waliohusika, kulipa fidia kwa familia za waathirika na majeruhi, kuandika Katiba mpya na kuboresha sheria za uchaguzi ili kuimarisha haki na kuzuia matukio kama hayo yasijirudie. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padre Dkt. Charles Hugo Kitima, amewataka Watanzania kutubu na kujirekebisha kutokana na matukio ya mauaji yaliyotokea wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, akisisitiza kuwa hatua hiyo ni muhimu ili kuzuia madhara kama hayo kujirudia.
Padre Kitima ametoa wito huo leo Oktoba 29, 2026 wakati wa adhimisho la Misa ya kuwaombea marehemu na waathirika wa matukio ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, akisisitiza umuhimu wa kujifunza kutokana na yaliyotokea badala ya kuangalia yajayo bila kukiri na kurekebisha makosa ya nyuma.
Amesema Kanisa lina wajibu wa kuwakumbusha waumini na jamii kwa ujumla umuhimu wa kutubu, kujirekebisha na kurejea katika misingi ya kutenda mema.
Akizungumzia athari za matukio hayo, Padre Kitima ameeleza maumivu yanayoendelea kuzikabili familia zilizopoteza wapendwa wao, akitoa mfano wa mtoto aliyeshiriki mahafali ya Kidato cha Nne bila wazazi wake, ambao alielezwa kuwa waliuawa nyumbani kwao Oktoba 29.
Amesisitiza kuwa Watoto na familia zilizoathirika wanahitaji kupewa matumaini, lakini matumaini hayo yanapaswa kwenda sambamba na toba na mabadiliko ya kweli katika jamii
Aidha, Padre Kitima amesema kuwa jamii inapaswa kujifunza kutokana na historia na makosa yaliyotokea ili kujenga mazingira yanayoheshimu uhai wa binadamu na kuzuia matukio ya mauaji kujirudia.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Askofu wa Jimbo Katoliki Kayanga, Mhashamu Almachius Vincent Rweyongeza, amesisitiza kuwa viongozi wa Kanisa hawawezi kukaa kimya wakati majeraha, huzuni, na masikitiko ya waliopotea au kuuawa bado vipo miongoni mwa wananchi, akiwataka waumini kujitokeza kwa wingi katika Misa Takatifu na Sala ya Rozari kwa ajili ya kuwaombea marehemu na waathirika wa matukio ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
Kauli hiyo ameitoa leo wakati wa Sala ya Rozari Takatifu katika Parokia ya Mtakatifu George, alipokuwa akifafanua barua ya wito uliotolewa na Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Askofu Wolfgang Pisa (Askofu wa Lindi), wa kuadhimisha Misa hizo tarehe 29 Oktoba 2026 katika parokia, vituo vya sala, na taasisi zote za kanisa.
Akijibu wanaotuhumu na kukejeli wito huo wa Maaskofu, Askofu Rweyongeza amebainisha kuwa jukumu la kinabii la viongozi wa dini ni kuwa sauti ya wanyonge na waliopatwa na msiba.
"Majeraha yapo, huzuni ipo, makaburi yapo, waliopotea hawajapatikana na hatuwezi kukaa kimya. Sisi maaskofu sisi ni sauti ya wanyonge, sauti ya bubu, sauti ya viziwi”, amesisitiza.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Askofu wa Jimbo Katoliki Kayanga, Mhashamu Almachius Vincent Rweyongeza, amekana madai ya baadhi ya watu wanaotafsiri wito wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) wa kuadhimisha Misa ya kuwaombea marehemu na waathiriwa wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 kama tamko la kisiasa la kuvuruga amani ya nchi, akisisitiza kuwa silaha pekee ya Wakatoliki ni sala na maombi.
Kauli hiyo ameitoa leo wakati wa Sala ya Rozari Takatifu katika Parokia ya Mtakatifu George, Kanisa Kuu la Kayanga mkoani Kagera, ambapo amewataka waumini kujitokeza kwa wingi katika Misa hizo bila woga wala wasiwasi wowote.
Akihoji nia ya watu wanaopotosha wito huo na kudai kuwa Maaskofu wanaangazia "kufukua makaburi" na kuvuruga amani ya taifa, Askofu Rweyongeza amebainisha kuwa kuombea amani, haki, na waliopoteza maisha au kuumizwa si utaratibu wa uchochezi wala uvunjifu wa amani.
“Kuwaalika kwa sala na maombi ni kuvuruga amani ya nchi? Nawauliza ninyi, ni kuvuruga amani ya nchi? Kuombea marehemu waliofariki siku hiyo ni kuvuruga amani ya nchi? Kuombea taifa amani, haki na amani ni kuvuruga amani ya nchi?", amehoji.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Askofu wa Jimbo Katoliki Kayanga, Mhashamu Almachius Vincent Rweyongeza, amewataka waumini na wananchi kujitokeza kwa wingi katika Misa Takatifu na Sala ya Rozari kwa ajili ya kuwaombea marehemu na waathirika wa matukio ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, huku akifafanua kuwa wito huo uliotolewa na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) si tamko la kisiasa wala wito wa kuhamasisha vurugu kama ambavyo baadhi ya watu wamekuwa wakipotosha.
Kauli hiyo ameitoa wakati wa Sala ya Rozari Takatifu katika Parokia ya Mtakatifu George, Kanisa Kuu la Kayanga mkoani Kagera, ambapo amefafanua barua ya wito uliotolewa na Rais wa TEC, Mhashamu Wolfgang Pisa (Askofu wa Lindi), wa kuadhimisha Misa hizo mnamo tarehe 29 Oktoba 2026 katika parokia, vituo vya sala, na taasisi zote za kanisa.
Askofu Rweyongeza amesoma barua rasmi ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) iliyoandikwa tarehe 23 Oktoba 2026 inayoeleza kuwa adhimisho hilo linatenga muda wa kuliombea taifa na kukumbuka waliopatwa na maumivu katika uchaguzi wa Oktoba 29, 2025.
"Katika kutimiza mwaka mmoja tangu uchaguzi wa mwaka jana, tunakumbuka baadhi ya watu wetu kuumizwa, kupotea na hata kuuawa. Hali hiyo ya maumivu na msiba bado ipo kati ya watu wetu. Katika mazingira haya tunaitwa kusimama pamoja kama jumuiya ya waamini tukimkabidhi Mwenyezi Mungu mwenye huruma taifa letu, viongozi wetu na watu wake, tukiomba umoja, upendo, ukweli, mshikamano ambavyo ni matunda ya haki na amani", ameeleza.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa @MsigwaGerson amesema ni jambo la ajabu kwa mtu kubeza ujenzi wa Mji wa Serikali jijini Dodoma, akieleza kuwa uwekezaji huo utarahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi na kuboresha utendaji wa taasisi za Serikali. Kauli hiyo ameitoa kuelekea hafla ya uzinduzi wa majengo ya wizara na taasisi za Serikali inayotarajiwa kufanyika Oktoba 30 jijini Dodoma.
Msigwa amesema kukamilika kwa majengo hayo kutasaidia kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wananchi wanaofika katika ofisi za Serikali, huku kukiwa na mazingira bora ya kuhifadhi kumbukumbu na nyaraka mbalimbali za Serikali. Ameongeza kuwa hatua hiyo pia itapunguza usumbufu unaoweza kujitokeza kwa wananchi wanapohitaji huduma kutoka katika taasisi tofauti za Serikali.
Aidha, Msigwa amesema watu wanaokosoa uwekezaji huo wana uhuru wa kutoa maoni yao, lakini amesisitiza umuhimu wa kuthamini na kuunga mkono maendeleo yanayotekelezwa nchini. Amesema ujenzi wa Mji wa Serikali ni sehemu ya jitihada za kuboresha mazingira ya kazi na utoaji wa huduma kwa umma.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
“TUSIRUHUSU WACHACHE KUBOMOA AMANI YETU”, KATAMBI AZITAKA JUMUIYA ZA KIRAIA NA VIONGOZI WA DINI KUMLINDA RAIS jambo.co.tz/tusiruhusu-wachache-kubomoa-amani-yetu-katamb… via @jambotv_
-
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, ametoa wito kwa viongozi wa dini na jumuiya za kiraia nchini kuchagua njia ya maridhiano, kufuata sheria na kulinda amani ya taifa, akionya kuwa machafuko na vurugu huumiza wananchi wasio na hatia na kurudisha nyuma maendeleo ya nchi.
Katambi ameyasema hayo leo, Oktoba 28, 2026, alipokuwa akizungumza wakati wa maadhimisho ya miaka 70 ya usajili wa jumuiya za kiraia nchini Tanzania.
Akirejea matukio yaliyotokea huko nyuma, Katambi ameeleza kuwa nchi iliingia katika madhila na vurugu zilizosababisha kupoteza maisha, majeraha, na uharibifu wa mali za Serikali na za watu binafsi kutokana na baadhi ya watu kuamini katika vurugu badala ya maridhiano na kufuata katiba na sheria.
"Nchi yetu iliingia katika madhila ya changamoto zilizojitokeza na vurugu mbalimbali ambazo zilipelekea kupatikana kwa changamoto aidha watu kupoteza maisha ama kujeruhika ama uharibifu wa mali za serikali na za watu binafsi. Lakini hii yote ilitokana na baadhi yetu kuchagua kuamini katika vita, machafuko na vurugu kuliko maridhiano. Kuamini katika njia ya kutafuta maslahi fulani au madaraka kwa njia isiyokuwa ya kikatiba au ya kisheria... Waheshimiwa viongozi wa dini, viongozi wa jumuiya, haya yote ni sisi Watanzania kuyatafakari. Hivi kweli tunapenda vita? Hivi kweli tunapenda machafuko? Na je tuko tayari na tumejiuliza nani atabaki salama?", amehoji Katambi.
Ameongeza kuwa pindi sheria na haki zisipofuatwa, makundi yaliyo hatarini kama vile wazee, wanawake, na watoto ndio wanaoteseka zaidi kwasababu hawawezi kukimbia pindi machafuko yanapotokea.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Nishati, Dkt. Juma Homera, amesema ugunduzi wa gesi asilia yenye futi za ujazo bilioni 223 katika Kitalu cha Mnazi Bay mkoani Mtwara unatarajiwa kuongeza akiba ya gesi nchini.
Dkt. Homera ameyasema hayo leo, Oktoba 28, 2026, katika hafla ya utiaji saini mikataba ya utafutaji wa mafuta na gesi katika vitalu vya Mnazi Bay North, West Songo Songo, Eyasi Wembere na Lindi–Mtwara.
Amesema uchimbaji wa visima vitatu katika Kitalu cha Mnazi Bay umekamilika, ambapo viwili ni vya uzalishaji na kimoja ni cha utafiti.
Aidha, amesema ujenzi wa bomba la kusafirisha gesi kutoka Ntorya hadi Madimba mkoani Mtwara umefikia asilimia 74, huku Serikali ikiendelea kupanua matumizi ya gesi asilia katika uzalishaji wa umeme, majumbani, viwandani na vyombo vya moto.
Dkt. Homera ameeleza kuwa hadi Septemba 2026, Tanzania ilikuwa na vituo 22 vya CNG, magari zaidi ya 20,000 yanayotumia gesi hiyo, viwanda 57, taasisi 21 na takribani kaya 3,000 zilizounganishwa na huduma ya gesi asilia.
Katika hatua nyingine, Dkt. Homera amesema Serikali inaendelea kupanua matumizi ya gesi asilia nchini kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) pamoja na makampuni binafsi.
Amesema matumizi ya gesi asilia yanajumuisha uzalishaji wa umeme, matumizi ya majumbani na viwandani, pamoja na vyombo vya moto kupitia mfumo wa gesi asilia iliyoshindiliwa (CNG).This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali wa Serikali na Taasisi za Umma, ikiwa ni pamoja na kumteua Bi. Angeline Lubala Mabula kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, pamoja na kuwateua Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wapya wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi kwa umma iliyotolewa leo, Oktoba 28, 2026, na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais (Ikulu), Shaaban Kissu, kufuatia taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka.
Rais Samia amemteua Mbunge wa Zamani wa Jimbo la Ilemela mkoani Mwanza Bi. Angeline Mabula kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, akichukua nafasi ya Bw. Beno Morris Malisa ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
Vilevile, Rais Samia amefanya uteuzi wa viongozi wakuu wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kwa kumteua Bw. Dunford George Mpelumbe kuwa Mwenyekiti wa Tume hiyo. Kabla ya uteuzi huo, Bw. Mpelumbe alikuwa Wakili wa Serikali katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Bw. Mpelumbe anachukua nafasi ya Jaji Mstaafu Mathew Pauwa Mwaimu ambaye amemaliza muda wake wa utumishi.
Pia, Rais amemteua Bw. Omar Ali Omar kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora. Kabla ya uteuzi huu, Bw. Omar alikuwa Mkuu wa Idara ya Utawala, Mipango na Fedha katika Taasisi ya Sayansi na Teknolojia Karume, Zanzibar, ambapo anachukua nafasi ya Bw. Mohamed Khamis Hamad ambaye naye amemaliza muda wake. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi, amesema sekta ya mafuta na gesi ina nafasi muhimu katika kufanikisha Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, akisisitiza umuhimu wa kusimamia rasilimali hizo kwa ufanisi ili ziweze kuchochea ukuaji wa uchumi na kuwanufaisha Watanzania.
Ndejembi ameyasema hayo leo, Oktoba 28, 2026, jijini Dar es Salaam, wakati wa hafla ya utiaji saini mikataba ya utafutaji wa mafuta na gesi asilia katika vitalu vya Mnazi Bay North, West Songo Songo, Eyasi Wembere na Lindi–Mtwara.
Amesema Serikali inalenga kujenga uchumi imara, jumuishi na shindani kupitia utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, Mpango wa Nne wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano pamoja na Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2025–2030.
Ameeleza kuwa sekta ya nishati ni miongoni mwa mihimili muhimu ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini, huku akibainisha kuwa mahitaji ya umeme yanatarajiwa kufikia zaidi ya megawati elfu sabini ifikapo mwaka 2050.
Akizungumzia utoaji wa leseni za utafutaji wa mafuta na gesi, Ndejembi amesema hatua hiyo ni muhimu katika kuimarisha uwezo wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kutekeleza majukumu yake na kushiriki kikamilifu katika mnyororo mzima wa thamani wa sekta hiyo.
Amesisitiza kuwa TPDC inapaswa kuhakikisha shughuli za utafutaji na uendelezaji wa rasilimali hizo zinafanyika kwa kuzingatia sheria, kanuni, masharti ya leseni, viwango vya kitaalamu na taratibu za usimamizi wa mazingira na usalama.
Vilevile, amelitaka shirika hilo kuimarisha uwezo wa wataalamu wazawa, kuboresha mifumo ya usimamizi wa miradi na kuhakikisha uwekezaji katika sekta hiyo unazingatia maslahi ya taifa kwa muda mfupi, wa kati na mrefu.
Ndejembi amesisitiza pia umuhimu wa kuhakikisha jamii zinazozunguka maeneo ya miradi ya mafuta na gesi zinanufaika na uwekezaji huo kupitia fursa mbalimbali za kiuchumi, ikiwemo ajira na shughuli za kibiashara.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Serikali imetangaza vipaumbele sita (6) kuu itakavyoweka mkazo katika kipindi cha robo mwaka ya pili ya mwaka wa fedha 2026/27 ikilenga kuimarisha ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo, uwekezaji wa sekta binafsi, na uwajibikaji katika taasisi za umma.
Vipaumbele hivyo vimebainishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Alexander Mkumbo, leo, Oktoba 28, 2026, bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2027/28.
Akiwasilisha hotuba hiyo, Prof. Kitila ameeleza kuwa kwa kuzingatia uzoefu uliopatikana katika robo mwaka ya kwanza, Serikali itaweka mkazo katika maeneo sita ya kipaumbele ili kuhakikisha utekelezaji wa mipango ya maendeleo unaleta matokeo yaliyokusudiwa.
"Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia uzoefu uliopatikana katika robo mwaka ya kwanza, Serikali itaweka mkazo katika vipaumbele sita (6) katika kipindi cha Oktoba–Desemba 2026. Kwanza, tutaendelea kuimarisha ulinganifu wa mipango na bajeti za taasisi na malengo ya Dira 2050. Pili, tutaboresha ukamilifu na uaminifu wa takwimu za msingi, viashiria vya utendaji na mifumo ya utoaji taarifa za robo mwaka. Tatu, tutaimarisha ufuatiliaji wa miradi ya kipaumbele ya maendeleo, kwa kuzingatia hatua za utekelezaji, matumizi ya bajeti na utatuzi wa changamoto kwa wakati", ameeleza.
Prof. Kitila ameeleza kuwa Serikali itaongeza juhudi za kuhamasisha na kutathmini uwekezaji wa sekta binafsi, pamoja na kuimarisha uratibu kati ya wizara, idara, wakala, mikoa na mamlaka za serikali za mitaa ili vipaumbele vya kitaifa vizae matokeo katika ngazi za maeneo.
Akielezea mwelekeo huo wa sekta binafsi na uratibu wa mikoani, Prof. Mkumbo amesema, "Nne, tutaongeza juhudi za kuhamasisha, kufuatilia na kufanya tathmini ya hali ya uwekezaji wa sekta binafsi na kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji, kwa kutambua kwamba shughuli za uzalishaji za sekta binafsi ni muhimu katika mabadiliko ya uchumi wetu. Tano, tutaongeza uratibu kati ya wizara, idara, wakala, mikoa na mamlaka za serikali za mitaa ili kuhakikisha kwamba vipaumbele vya maendeleo ya kitaifa vinazaa matokeo katika ngazi za maeneo".This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Serikali imebainisha maeneo sita ya kipaumbele cha kipekee katika kuimarisha mnyororo wa thamani kwenye sekta za uzalishaji, ikiwa ni sehemu ya ugharamiaji wa Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2027/28 ambapo sekta binafsi inatarajiwa kuchangia asilimia 70 ya gharama zote.
Hayo yamebainishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Alexander Mkumbo, leo, Oktoba 28, 2026, bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha mapendekezo hayo mbele ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Akiwasilisha hotuba hiyo, Prof. Kitila ameeleza kuwa Mpango wa Nne wa Maendeleo ya Taifa wa Miaka Mitano (FYDP4) umebainisha na kufungamanisha minyororo ya thamani katika programu za kielelezo ili kuhakikisha zinakuwa na manufaa ya kibiashara, uzalishaji, na kukuza ushindani wa kiuchumi.
"Katika mwaka 2027/28 maeneo ya mnyororo wa thamani yatapewa kipaumbele cha kipekee. Maeneo haya ni mosi, kilimo cha maua na mazao ya bustani. Pili, ufugaji wa viumbe hai. Tatu, utafiti uchimbaji na kuongeza thamani ya madini. Nne, uzalishaji wa mafuta ya kula. Tano, uzalishaji wa nguo na mavazi kwa kuimarisha mnyororo wa thamani wa pamba. Na sita kuimarisha uzalishaji wa mazao ya kilimo ikiwemo korosho, sukari, ngano, chai na kahawa na uongezaji wa thamani wa mazao hayo", ameeleza Prof. Kitila.
Vilevile, Prof. Kitila amebainisha kuwa mwelekeo wa ugharamiaji wa mpango huo wa maendeleo kwa mwaka 2027/28 utabaki katika mfumo uleule unaoipa sekta binafsi nafasi kubwa ya kuongoza uwekezaji.
"Mheshimiwa mwenyekiti, tumeeleza pia ugharamiaji wa mpango wa maendeleo ya taifa kwa mwaka 2027. ambayo kwa kiasi kikubwa itakuwa kama ilivyo kwa mwaka huu wa fedha na fomu wetu ni ile ile 30% sekta ya umma 70% sekta binafsi", ameeleza.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Ujenzi wa Bandari ya Mbamba Bay, iliyoko wilayani Nyasa mkoani Ruvuma, umezidi kuleta tija kubwa kwa jamii na uchumi wa taifa baada ya kufikia asilimia 78 ya utekelezaji wake, hukukiwanja hicho kikiwa tayari kimeanza kutoa fursa za ajira, ufundi, na kuimarika kwa biashara ndogo kwa wananchi.
Baadhi ya vijana wanaoshiriki moja kwa moja katika ujenzi wa mradi huo wameeleza kuwa ajira hiyo imewapatia kipato thabiti cha kuendesha familia zao, huku wengine wakipata nafasi adimu ya kujifunza stadi mbalimbali za ufundi ambazo zitawasaidia kujiajiri pindi mradi huo utakapokamilika. Mradi huo unatajwa kuwa na mchango mkubwa katika kuimarisha usafirishaji wa mizigo na kukuza biashara za mipakani kati ya Tanzania na nchi jirani za Malawi, Msumbiji, na Zambia.
Akizungumzia maendeleo ya mradi huo, Mhandisi Msimamizi kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), John Paul, ameeleza kuwa eneo la Mbamba Bay lilichaguliwa kufuatia upembuzi yakinifu uliofanyika mwaka 2023 uliothibitisha umuhimu wake wa kimkakati. Amesema kazi inaendelea kwa ufanisi mkubwa kutokana na usaidizi mkubwa kutoka Serikalini na upatikanaji wa fedha zilizomwezesha mkandarasi kulipwa kwa wakati.
“Tunaishukuru Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa maono yake na kutoa fedha kwa wakati,” amesema Paul, huku akimpongeza pia Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Plasduce Mbossa, kwa usimamizi thabiti unaochochea mafanikio ya bandari hiyo.
Kwa upande wake, Mhandisi Mkazi wa Kampuni ya Anova, Agathon Mwenda, alithibitisha kuwa kazi zinaendelea kwa kiwango kizuri na kwamba kampuni hiyo imejipanga kukamilisha mradi huo ifikapo Februari 26, 2027, ikiwa ni kwa mujibu wa ratiba ya mkataba.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
“Eneo hili (Kuimarisha Misingi ya Uendelevu wa Taifa) limelenga kuimarisha uwazi, uwajibikaji, maadili na tunu za kidemokrasia, pamoja na amani na utulivu, na kuimarisha utumishi wa umma unaoendana na mahitaji ya wananchi. Afua zitakazotekelezwa katika eneo hili ni kuendelea kuimarisha utawala bora, demokrasia, usalama na utulivu pamoja na kuongeza uwezo na ufanisi wa taasisi za Serikali, Kuimarisha uwezo wa Serikali za Mitaa ili kuwezesha mipango na utekelezaji wa maendeleo kwa kuzingatia mahitaji halisi ya wananchi na maeneo husika; Kuimarisha uwajibikaji na ushiriki wa wananchi katika utoaji wa huduma za umma; Kuboresha sheria ili kuendana na Dira 2050; Kuimarisha matumizi ya teknolojia za kidijitali na takwimu sahihi katika kupanga, kutekeleza na kufuatilia maendeleo; Kuweka msukumo katika mabadiliko ya mtazamo, fikra na utamaduni wa utendaji ili kujenga nidhamu, ubunifu, uwajibikaji na uzalendo katika utumishi wa umma na jamii; na Kusisitiza maadili ya uadilifu, uwajibikaji, ujumuishi, uendelevu na ubunifu kama msingi wa kuhakikisha mageuzi yanatekelezwa kwa ufanisi na manufaa yake yanafikia wananchi wote”, Prof. Kitila.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Alexander Mkumbo akizungumza leo Oktoba 28, 2026, bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2027/28. -
Jambo TV
@Jambotv_
“Uhifadhi wa Mazingira na Ustahimilivu wa Mabadiliko ya Tabianchi Mpango utaweka uhifadhi wa mazingira na ustahimilivu wa mabadiliko ya tabianchi kama sehemu muhimu ya maendeleo endelevu. Vipaumbele vimejielekeza katika kuendeleza miji iliyopangwa, matumizi endelevu ya ardhi na bahari, uhifadhi na urejeshaji wa misitu, mabonde ya maji na rasilimali za bahari; Kuimarisha mifumo ya kukabiliana na majanga na tahadhari za mapema. Lengo ni kupunguza athari za majanga na mabadiliko ya tabia nchi kama vile El-nino; Kuendeleza uchumi wa kijani kupitia uzalishaji wenye kiwango kidogo cha hewa ukaa, matumizi bora ya rasilimali na teknolojia rafiki kwa mazingira; na Kutumia fursa za uchumi wa buluu na biashara ya kaboni kama vyanzo vya ukuaji na mapato”, Prof. Kitila.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Alexander Mkumbo akizungumza leo Oktoba 28, 2026, bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2027/28. -
Jambo TV
@Jambotv_
“Mpango unatambua rasilimali watu kuwa msingi wa mageuzi na maendeleo ya Taifa. Kwa hiyo, juhudi zitaelekezwa katika kuboresha upatikanaji na ubora wa elimu, mafunzo ya ujuzi na elimu inayozingatia mahitaji ya soko la ajira, hususan katika sayansi, teknolojia, uhandisi na hisabati, kujenga nguvu kazi yenye ujuzi, tija na uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya teknolojia na mahitaji ya uchumi, kuendelea na maandalizi ya utekelezaji wa elimu ya sekondari kwa wote kuanzia mwaka 2028, kuimarisha upatikanaji wa ajira kwa vijana na maendeleo ya biashara ndogo na za kati ili kutumia fursa ya ongezeko la watu wenye umri wa kufanya kazi, kuendelea na utekelezaji wa programu ya bima ya afya kwa wote, kuimarisha uwekezaji wa viwanda vya uzalishaji dawa na vifaa tiba, kuimarisha malezi, makuzi na maendeleo ya mtoto, na kuanza kutekeleza afua mahsusi zinazolenga kuondoa umasikini uliokithiri miongoni mwa wananchi kwa kuzingatia kiwango cha umaskini katika maeneo ya kijiografia”, - Prof. Kitila.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Alexander Mkumbo akizungumza leo Oktoba 28, 2026, bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2027/28. -
Jambo TV
@Jambotv_
“Katika eneo hili (Uchumi Imara, Jumuishi na Shindani), Mpango (Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2027/28) utaweka kipaumbele katika kujenga uchumi imara, jumuishi na shindani kwa kuimarisha utulivu wa uchumi jumla, uhimilivu wa kifedha na ustahimilivu wa sekta ya nje. Msisitizo utawekwa katika kuongeza tija katika uzalishaji, kupanua minyororo ya thamani na kuongeza uwezo wa Tanzania kushiriki katika masoko ya kikanda na kimataifa, kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji ikiwemo kurahisisha mifumo ya udhibiti, na kurasimisha shughuli zisizo rasmi, kukuza ushiriki wa sekta binafsi kuwekeza katika sekta zenye tija kubwa, matumizi ya teknolojia na mitambo ya kisasa, kuimarisha uzalishaji wa bidhaa kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya soko la ndani na mauzo ya nje, kuongeza uwezo wa kukusanya mapato ya ndani, na kuimarisha masoko ya mitaji na kutumia vyanzo bunifu vya fedha”, - Prof. Kitila.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Alexander Mkumbo akizungumza leo Oktoba 28, 2026, bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2027/28. -
Jambo TV
@Jambotv_
Serikali imetangaza vipaumbele sita (6) kuu itakavyoweka mkazo katika kipindi cha robo mwaka ya pili ya mwaka wa fedha 2026/27 ikilenga kuimarisha ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo, uwekezaji wa sekta binafsi, na uwajibikaji katika taasisi za umma.
Vipaumbele hivyo vimebainishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Alexander Mkumbo, leo, Oktoba 28, 2026, bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2027/28.
Akiwasilisha hotuba hiyo, Prof. Kitila ameeleza kuwa kwa kuzingatia uzoefu uliopatikana katika robo mwaka ya kwanza, Serikali itaweka mkazo katika maeneo sita ya kipaumbele ili kuhakikisha utekelezaji wa mipango ya maendeleo unaleta matokeo yaliyokusudiwa.
"Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia uzoefu uliopatikana katika robo mwaka ya kwanza, Serikali itaweka mkazo katika vipaumbele sita (6) katika kipindi cha Oktoba–Desemba 2026. Kwanza, tutaendelea kuimarisha ulinganifu wa mipango na bajeti za taasisi na malengo ya Dira 2050. Pili, tutaboresha ukamilifu na uaminifu wa takwimu za msingi, viashiria vya utendaji na mifumo ya utoaji taarifa za robo mwaka. Tatu, tutaimarisha ufuatiliaji wa miradi ya kipaumbele ya maendeleo, kwa kuzingatia hatua za utekelezaji, matumizi ya bajeti na utatuzi wa changamoto kwa wakati", ameeleza.
Prof. Kitila ameeleza kuwa Serikali itaongeza juhudi za kuhamasisha na kutathmini uwekezaji wa sekta binafsi, pamoja na kuimarisha uratibu kati ya wizara, idara, wakala, mikoa na mamlaka za serikali za mitaa ili vipaumbele vya kitaifa vizae matokeo katika ngazi za maeneo.
Akielezea mwelekeo huo wa sekta binafsi na uratibu wa mikoani, Prof. Mkumbo amesema, "Nne, tutaongeza juhudi za kuhamasisha, kufuatilia na kufanya tathmini ya hali ya uwekezaji wa sekta binafsi na kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji, kwa kutambua kwamba shughuli za uzalishaji za sekta binafsi ni muhimu katika mabadiliko ya uchumi wetu. Tano, tutaongeza uratibu kati ya wizara, idara, wakala, mikoa na mamlaka za serikali za mitaa ili kuhakikisha kwamba vipaumbele vya maendeleo ya kitaifa vinazaa matokeo katika ngazi za maeneo".
Prof. Kitila amelieleza Bunge kuwa Serikali itaimarisha uwajibikaji kwa kutaka taasisi zinazotekeleza programu kueleza sababu za tofauti kati ya malengo na matokeo halisi na kuonyesha hatua za kurekebisha mapungufu. Ameongeza kuwa vipaumbele hivyo vitaungwa mkono na mapitio ya mara kwa mara ya utendaji ili mafunzo yanayopatikana yanaingizwa kwenye maamuzi katika mwaka wote wa fedha.
"Sita, tutaimarisha uwajibikaji kwa kutaka taasisi zinazotekeleza programu kueleza sababu za tofauti kubwa kati ya malengo na matokeo halisi, na kuonesha hatua zinazochukuliwa kurekebisha mapungufu yaliyobainika", ameeleza. -
Jambo TV
@Jambotv_
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Alexander Mkumbo, amebainisha kuwa miezi mitatu ya utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 (Dira 2050) imetoa matumaini makubwa kwamba malengo makubwa yaliyowekwa yanatekelezeka na yanafikika, huku akiainisha mambo matano ya msingi yanayothibitisha mwelekeo huo chanya.
Prof. Kitila ameyasema hayo leo, Oktoba 28, 2026, bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2027/28.
Prof. Kitila ame3leza kuwa nchi ina msingi imara wa ukuaji wa uchumi ambapo uchumi unakua kwa kasi nzuri na unatarajiwa kufikia ukuaji wa asilimia 6.6 kwa mwaka 2027, huku mfumko wa bei ukisalia chini ya asilimia 5.
Akinukuu tathmini hiyo ya miezi mitatu ya Dira 2050, Prof. Mkumbo amesema, "miezi mitatu ya utekelezaji wa Dira 2050 imetupa matumaini makubwa kwamba malengo makubwa tuliyojiwekea yanatekelezeka na yanafikika. Mambo matano ni bayana: Tuna msingi imara wa ukuaji wa uchumi. Uchumi unakua kwa kasi nzuri na unatarajiwa kukua kwa asilimia 6.6 kwa mwaka 2027. Mfumko wa bei umeendelea kuwa chini ya asilimia 5".
Vilevile, Prof. Kitila amebainisha kuwa sekta ya fedha ya umma imeendelea kufanya vizuri ambapo katika mwaka mmoja imefikiwa shabaha ya kutenga dola za Marekani bilioni 8.1 kwa ajili ya maendeleo, huku katika bajeti ya mwaka 2026/27 Serikali ikitenga bajeti ya TZS 20.82 bilioni (sawa na dola bilioni 8.2).
Pia ameongeza kuwa bajeti ya maendeleo imeendelea kuongezeka hadi kufikia asilimia 7.7 ya Pato la Taifa (GDP), ikionesha kuongezeka kwa uwekezaji wa sekta ya umma katika shughuli za maendeleo.
"Sekta ya fedha ya umma imeendelea kufanya vizuri ambapo katika mwaka mmoja tumefikia shabaha ya kutenga dola bilioni 8.1 kwa ajili ya maendeleo (ambapo katika bajeti ya mwaka 2026/27 serikali ilitenga bajeti ya TZS 20.82 bilioni sawa na dola bilioni 8.2)... Bajeti ya maendeleo imeendelea kuongezeka ambapo asilimia 7.7 ya GDP ikionesha kuongezeka kwa uwekezaji wa sekta ya umma katika shughuli za maendeleo", ameeleza.
Aidha, Prof. Kitila amebainisha kuwa umaskini wa mahitaji ya msingi umeendelea kupungua nchini kutoka asilimia 34.4 mwaka 2007 hadi kufikia asilimia 25.1 mwaka 2025.
Amesisitiza kuwa Dira 2050 inaeleweka na imepokelewa vizuri na umma wa Watanzania wa kada zote, huku kukiwa na nyenzo thabiti za utekelezaji na taasisi imara za usimamizi wake. -
Jambo TV
@Jambotv_
"Katika kuendelea kuimarisha ushiriki wa sekta binafsi, serikali imebaini na itasukuma utekelezaji wa miradi ya maendeleo 131 ya ubia inayostahili kutekelezwa kwa ubia kati ya sekta binafsi na sektaya umma. Miradi hii ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji na tutaitolea taarifa zaidi katika taarifa ya nusu mwaka. Aidha, Serikali inaandaa sera mpya ya uwekezaji wa sekta binafsi pamoja na muswada wa sheria wa maendeleo ya sekta binafsi. Ukuaji wa sekta ya uwekezaji nchini sio takwimu katika makaratasi tu. Ni ajira na maisha kwa watanzania halisi. Nazungumzia kwa mfano, vijana 10,000 watakaoajiriwa katika kongani za viwanda inayojengwa na Kampuni ya HWTZ Bagamoyo ifikapo mwaka 2030/31, vijana 2,000 walioajiriwa katika kiwanda cha Itracom- Nala Dodoma. Pia kuna vijana3,000 ambao wameajiriwa na kiwanda cha nguo cha Kampuni ya Sinovest Bagamoyo na vijana 10,000 watakaoajiriwa ifikapo mwaka 2030/31. Pia kuna vijana 6,000 watakaoajiriwa katika mradi wa Kongani za viwanda wa Kampuni ya HWTZ Songea, Vijana 12,640 walioajiriwa katika Kiwanda cha Sukari cha Kilombero. vijana 4,800 walioajiriwa katika Kiwanda cha Sukari.cha Mtibwa. Vijana 5,061walioajiriwa katika Kiwanda cha Mkulazi Holding Morogoro. Aidha, vijana 11,262 watakaoajiriwa katika mradi wa Kampuni ya Eagle Agrotech Morogoro na vijana 498 watakaoajiriwa katika mradi wa kuchakata mazao ya kilimo wa Kampuni ya Kom Food Products Company Limited Kahama", -Prof. Kitila.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Alexander Mkumbo akizungumza leo Oktoba 28, 2026, bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2027/28. -
Jambo TV
@Jambotv_
Serikali ya Tanzania imebainisha kuwa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 inaitambua na kuiweka sekta binafsi kama injini kuu ya mageuzi ya kiuchumi nchini, huku ikitarajiwa kuwa sekta hiyo itachangia asilimia 70 ya uwekezaji wote unaohitajika katika kufanikisha maendeleo ya muda mrefu.
Hayo yamebainishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Alexander Mkumbo, leo, Oktoba 28, 2026, bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2027/28.
Akiwasilisha hotuba hiyo, Prof. Kitila ameeleza kuwa Mpango wa Maendeleo wa Muda Mrefu (LTPP 2026/27 – 2050/51) umeimarisha mwelekeo wa kujenga sekta binafsi yenye ushindani, ustahimilivu, na inayowajibika, ikichagizwa na biashara ndogo na za kati (MSMEs) zilizorasimishwa
"Dira 2050 inaitambua na kuiweka sekta binafsi kama injini ya mageuzi ya kiuchumi. Dira 2050 inalenga kujenga sekta binafsi yenye ushindani, ustahimilivu, jumuishi na inayowajibika, ikichagizwa na sekta binafsi ndogo na za kati (MSMEs) inayoendeshwa kisasa na katika mfumo ulio rasmi wa uchumi. Mpango wa Maendeleo wa Muda Mrefu (LTPP 2026/27 – 2050/51) umeimarisha mwelekeo huu kwa kutambua mitaji ya uwekezaji kutoka ndani na nje ya nchi kutoka sekta binafsi kama chanzo kikuu cha kugharamia maendeleo ya muda mrefu, ikitarajiwa kuwa sekta binafsi itachangia asilimia 70 ya uwekezaji unaohitajika", ameeleza Prof. Kitila.
Prof. Kitila amebainisha kuwa msingi wa mwelekeo huo unatokana na ukweli kwamba sekta binafsi ndiyo inayochukua sehemu kubwa ya nguvu kazi nchini. Amerejea Taarifa ya Utafiti ya Ajira na Kipato ya mwaka 2024/25 (Employment and Earnings Survey of 2024/25) iliyobaini kuwa kati ya ajira 4,565,960 zilizobainishwa, ajira 3,220,452 (sawa na 70.5%) zilikuwa katika sekta binafsi, huku sekta ya umma ikichangia ajira 1,345,508 (29.5%).
"msingi wa mweleko huu upo katika ukweli kwamba sekta binafsi inaajiri sehemu kubwa ya nguvu kazi na kumiliki sehemu kubwa ya shughuli za uzalishaji. Kwa mfano, taarifa ya utafiti ya ajira na kipato ya mwaka 2024/25 (Employment and Earnings Survey of 2024/25) ilibaini kuwa kati ya ajira 4,565,960 zilizobainishwa, ajira 3,220,452 (70.5%) zilikuwa katika sekta binafsi na ajira 1,345,508 (29.5%) zilikuwa katika sekta ya umma", ameeleza Prof. Kitila.
Pia, ameongeza kuwa katika mwaka wa fedha 2025/26, miradi 934 ya wawekezaji yenye thamani ya Dola za Marekani bilioni 12.5 ilisajiliwa, ikitarajiwa kuzalisha ajira 307,743. Katika robo ya kwanza ya mwaka 2026/27, miradi 243 yenye thamani ya Dola za Marekani bilioni 3.44 ilisajiliwa, ambapo asilimia 57.2 ni miradi ya viwanda.
Prof. Kitila amebainisha kuwa miradi ya Ubia (PPP) iliyo katika utekelezaji imeongezeka hadi kufikia 10, ikijumuisha Kituo cha Biashara cha Kariakoo, Mfumo wa Mabasi Yaendayo Haraka (BRT), na Reli ya TAZARA. -
Jambo TV
@Jambotv_
“Mfumuko wa bei uliendelea kuwa katika kiwango cha chini na himilivu. Katika mwaka 2025/26, mfumuko wa bei ulifikia wastani wa asilimia 3.6, ikilinganishwa na asilimia 3.1 mwaka 2024/25. Mwenendo huo uliakisi utekelezaji wa sera makini za fedha na bajeti, pamoja na kupungua kwa kasi ya ongezeko la bei za bidhaa zisizo za chakula. Hata hivyo, kuanzia Aprili hadi Juni 2026, mfumuko wa bei ulivuka asilimia 4.0 kwa mara ya kwanza tangu Mei 2023 na kufikia asilimia 4.3 mwezi Septemba 2026. Ongezeko hilo lilichangiwa zaidi na kupanda kwa bei za nishati katika soko la dunia kufuatia kuongezeka kwa migogoro Mashariki ya Kati, hali iliyoathiri bei za mafuta nchini na kuongeza gharama za usafirishaji, bidhaa na huduma nyingine. Pamoja na shinikizo hilo, mfumuko wa bei uliendelea kuwa ndani ya lengo la kitaifa la asilimia 3.0 hadi 5.0, kigezo cha EAC kisichozidi asilimia 8.0 na wigo wa SADC wa asilimia 3.0 hadi 7.0”, - Prof. Kitila.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Alexander Mkumbo akizungumza leo Oktoba 28, 2026, bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2027/28. -
Jambo TV
@Jambotv_
“Kwa mujibu wa taarifa ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu ya mwezi Septemba 2026, katika robo ya kwanza na ya pili ya mwaka 2026, Pato Halisi la Taifa lilikua kwa asilimia 6.0 na asilimia 6.5, mtawalia. Kilimo kilitoa mchango mkubwa zaidi katika ukuaji huo wa asilimia 19.2, kikifuatiwa na huduma za fedha na bima kwa asilimia 16.7, utawala na ulinzi (asilimia 9.2), ujenzi (asilimia 9.0), na uzalishaji viwandani (asilimia 6.6). Huduma za fedha na bima ziliongoza kwa kasi ya ukuaji wa asilimia 22.5, zikifuatiwa na utawala na ulinzi (asilimia 12.8), umeme (asilimia 11.8), sanaa na burudani (asilimia 11.0), na habari na mawasiliano (asilimia 10.3). Kwa kuzingatia mwenendo huo, uchumi unatarajiwa kukua kwa asilimia 6.3 mwaka 2026 na asilimia 6.6 mwaka 2027, kulingana na mwelekeo wa Mpango wa Nne wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2026/27–2030/31”, - Prof. Kitila.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Alexander Mkumbo akizungumza leo Oktoba 28, 2026, bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2027/28. -
Jambo TV
@Jambotv_
Serikali imesema kuanzishwa Mfumo wa Kielektroniki wa Kitaifa wa Usimamizi wa Mipango na Miradi ya Maendeleo, unaojulikana kama 'e-Delivery', kutaimarisha ufuatiliaji, tathmini, na matumizi ya taarifa sahihi katika utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Alexander Mkumbo, ameyasema hayo leo, Oktoba 28, 2026, bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2027/28.
“Lengo la Serikali katika kuanzisha mfumo wa e-delivery ni kuhakikisha kwamba viongozi na wasimamizi wanaweza kubaini si tu kama mradi umeidhinishwa au umefadhiliwa, bali pia kama unaendelea kutekelezwa kulingana na ratiba, kama matumizi ya fedha yanazalisha matokeo yaliyokusudiwa na kama changamoto zinazojitokeza zinashughulikiwa”, ameeleza Prof. Kitila.
Prof. Kitila amesisitiza kuwa taarifa sahihi na ushahidi unaoaminika ndio msingi wa utekelezaji wenye ufanisi wa ajenda ya mabadiliko ya miaka 25 ya Dira 2050. Amebainisha kuwa pale ambapo utendaji wa taasisi utakuwa chini ya matarajio au taarifa hazijakamilika, Serikali itakiri mapungufu na kuzitaka taasisi husika kueleza sababu na kuweka ratiba ya kurekebisha hali hiyo
Akiweka msisitizo juu ya uwajibikaji na utendaji unaozingatia ushahidi, Prof. Mkumbo amesema, "taarifa sahihi ni msingi wa utekelezaji wenye ufanisi. Pale ambapo taarifa hazijakamilika, Serikali tutakiri mapungufu hayo na kuweka ratiba ya kuyatatua. Pale ambapo utendaji uko chini ya matarajio, taasisi husika lazima zieleze sababu na kubainisha hatua za kurekebisha hali hiyo. Hatuwezi kusimamia kwa ufanisi ajenda ya mabadiliko ya miaka 25 bila kuwa na ushahidi unaoaminika, taarifa zinazowasilishwa kwa utaratibu unaofanana na utayari wa kuchukua hatua kutokana na kile kinachooneshwa na ushahidi huo". -
Jambo TV
@Jambotv_
“Serikali pia inaendelea kuimarisha uratibu kati ya taasisi zinazohusika na mipango, bajeti, utekelezaji, ufuatiliaji na tathmini. Lengo letu ni kupunguza mgawanyiko wa utekelezaji, kuondoa urudufu usio wa lazima na kuhakikisha kwamba taasisi za Serikali zinafanya kazi kwa kuzingatia matokeo ya pamoja ya kitaifa. Hatua hii ni muhimu kwa sababu Dira 2050 si jukumu la wizara moja. Ni jukumu la Serikali nzima na taifa zima kwa ujumla. Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inatambua kwamba utekelezaji wenye ufanisi unahitaji pia mabadiliko ya utamaduni wa utendaji katika taasisi. Tunapaswa kuachana na hali ambayo mafanikio yanapimwa zaidi kwa shughuli zilizofanyika, mikutano iliyofanyika au taarifa zilizoandaliwa. Mwelekeo wetu ni kuona kuwa tunapima mafanikio kwa kuzingatia bidhaa na huduma zilizotolewa, matokeo yaliyopatikana, matumizi bora ya rasilimali na maboresho yaliyofanyika katika maisha ya wananchi. Hii ndiyo nidhamu ya utekelezaji inayotakiwa na Dira 2050. Hivyo basi, Serikali imeelekeza kila taasisi kujua kikamilifu inachotakiwa kutekeleza, muda wa kutekeleza, rasilimali ilizonazo na hatua zitakazochukuliwa pale inaposhindwa kufikia makubaliano ya utendaji. Jukumu letu sasa ni moja: kuhama kutoka kwenye Dira kwenda kwenye utekelezaji, na kutoka kwenye utekelezaji kwenda kwenye matokeo yanayopimika”, - Prof. Kitila.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Alexander Mkumbo akizungumza leo Oktoba 28, 2026, bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2027/28. -
Jambo TV
@Jambotv_
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Alexander Mkumbo, amezitaka Wizara, Sekretarieti za Mikoa, Mamlaka za Serikali za Mitaa, na taasisi zote za umma ambazo bado hazijaoanisha mipango mikakati yao na Mipango ya Maendeleo ya Kitaifa kufanya hivyo kabla ya Juni 2027.
Prof. Kitila ametoa agizo hilo leo, Oktoba 28, 2026, bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2027/28.
Prof. Kitila amebainisha kuwa Dira ya Taifa inaweza kutekelezwa kwa ufanisi pale tu kunapokuwa na uhusiano wa wazi na wa moja kwa moja kati ya kile ambacho nchi inalenga kufikia mwaka 2050 na utekelezaji wa kila siku wa taasisi za umma katika kila mwaka wa fedha.
Amefafanua kuwa ingawa tathmini ya awali inaonesha kuwa mipango ya maendeleo ya kitaifa imeshabihiana vyema na mipango mikakati ya sekta, taasisi za umma na mamlaka za mitaa, bado kuna haja kwa taasisi ambazo hazijakamilisha uoanishaji huo kuwasilisha mipango yao Tume ya Taifa ya Mipango ili ifanyiwe uchambuzi na kuidhinishwa
"Dira ya taifa inaweza kutekelezwa kwa ufanisi pale tu kunapokuwa na uhusiano wa wazi kati ya kile ambacho nchi inataka kufikia mwaka 2050 na kile ambacho kila taasisi ya umma inapaswa kutekeleza katika mwaka husika wa fedha... Nitoe wito kwa Wizara, Sekretarieti za Mikoa, Mamlaka za Serikali za Mitaa, na taasisi za umma ambazo bado hazijaoanisha mipango mikakati yao na mipango ya maendeleo ya kitaifa kufanya hivyo kabla ya Juni 2027. Mipango hii iwasilishwe Tume ya Taifa ya Mipango kwa uchambuzi na uidhinishaji", ameeleza Prof. Kitila. -
Jambo TV
@Jambotv_
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Alexander Mkumbo, amesisitiza kuwa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 si waraka mwingine wa kawaida wa Serikali tu, bali ni dhamira kuu ya kitaifa inayolenga kuubadilisha uchumi wa Tanzania, kuimarisha uwezo wa wananchi, na kuboresha maisha ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.
Prof. Kitila ameyasema hayo leo, Oktoba 28, 2026, bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2027/28, ambapo amebainisha kuwa utekelezaji wa Dira hiyo unahitaji ushirikiano wa wadau wote katika jamii na si Serikali pekee.
Akieleza umuhimu wa ushirikikaji wa kitaifa katika kufanikisha malengo ya muda mrefu ya nchi, Prof. Kitila amebainisha kuwa Dira 2050 inahitaji ushiriki wa Bunge, sekta binafsi, mamlaka za serikali za mitaa, mashirika ya umma, taasisi za elimu ya juu na utafiti, asasi za kiraia, washirika wa maendeleo, pamoja na Watanzania waishio nje ya nchi.
"kama ambavyo tumeeleza kila mara, Dira 2050 si waraka mwingine wa Serikali tu, bali ni dhamira yetu ya kitaifa ya kuubadilisha uchumi wa Tanzania, kuimarisha uwezo wa wananchi, kuboresha maisha yao na kuhakikisha kwamba tunajenga ustawi kwa kizazi cha sasa na vizazi vijavyo. Kwa hiyo, utekelezaji wake si jukumu la Serikali pekee. Unahitaji ushiriki wa Bunge, sekta binafsi, mamlaka za serikali za mitaa, mashirika ya umma, taasisi za elimu ya juu na utafiti, asasi za kiraia, washirika wa maendeleo, Watanzania waishio nje ya nchi na kila mwananchi", ameeleza Prof. Kitila.
Prof. Kitila ameeleza kuwa kipaumbele cha kwanza katika robo mwaka ya kwanza ya utekelezaji wa Dira 2050 kilikuwa kuweka msingi wa mfumo utakaounganisha matarajio ya muda mrefu na programu halisi za maendeleo. Amefafanua kuwa mfumo huo wa usimamizi unajumuisha Mpango Elekezi wa Maendeleo wa Muda Mrefu (LTPP) wa mwaka 2026/27 hadi 2050/51, Mpango wa Nne wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano wa mwaka 2026/27 hadi 2030/31, pamoja na mipango na bajeti za mwaka husika ili kutafsiri malengo ya nchi katika miradi inayopimika.
Akimulika matokeo ya tathmini ya awali, Prof. Kitila amesema kuwa kwa kiasi kikubwa mipango ya maendeleo ya kitaifa imeshabihiana vyema na mipango mikakati ya sekta na mamlaka za mitaa. Hata hivyo, ametoa maelekezo kwa taasisi zote ambazo hazijaoanisha mipango yao kufanya hivyo mapema.
Akiweka agizo kwa taasisi zote za umma na sekretarieti za mikoa, Prof. Kitila amesema, "Dira ya taifa inaweza kutekelezwa kwa ufanisi pale tu kunapokuwa na uhusiano wa wazi kati ya kile ambacho nchi inataka kufikia mwaka 2050 na kile ambacho kila taasisi ya umma inapaswa kutekeleza katika mwaka husika wa fedha... Nitoe wito kwa Wizara, Sekretarieti za Mikoa, Mamlaka za Serikali za Mitaa, na taasisi za umma ambazo bado hazijaoanisha mipango mikakati yao na mipango ya maendeleo ya kitaifa kufanya hivyo kabla ya Juni 2027. Mipango hii iwasilishwe Tume ya Taifa ya Mipango kwa uchambuzi na uidhinishaji" -
Jambo TV
@Jambotv_
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Alexander Mkumbo, amemwaga pongezi maalum kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, akieleza kuwa uongozi wake mahiri na wa kiwango cha juu ndio ulioiwezesha Tanzania kupata fursa ya kihistoria ya kuwa mwenyeji wa Mkutano wa 153 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU).
Prof. Kitila ameyasema hayo leo, Oktoba 28, 2026, bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2027/28.
Prof. Kitila amebainisha kuwa hatua ya dunia kuiamini Tanzania kuandaa Mkutano huo wa IPU ni kielelezo tosha cha diplomasia madhubuti, heshima, na uaminifu mkubwa ambao nchi imejijengea kimataifa chini ya uongozi wa Rais Samia
"Kwanza, ninampongeza Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa uongozi wake uliowezesha Tanzania kupata fursa ya kuwa mwenyeji wa Mkutano wa 153 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU). Mafanikio haya ni kielelezo cha heshima na imani ambayo Tanzania imejijengea katika medani za kimataifa, pamoja na uwezo wetu wa kuandaa na kuendesha mikutano mikubwa ya kimataifa", ameeleza Kitila.
Prof. Kitila ameeleza kuwa mafanikio hayo yote yaliyopatikana katika Mkutano wa IPU yanadhihirisha kuwa Tanzania ina viongozi wenye sifa za kimataifa wanaoweza kuiwakilisha na kuiongoza nchi vyema kwenye nyanja za diplomasia ya kibunge
Ameongeza kuwa pamoja na pongezi kwa Rais Samia, mafanikio hayo yaliwezeshwa pia na uongozi wa Spika wa Bunge la Tanzania, Mussa Azzan Zungu, mchango wa Rais wa 31 wa IPU (2023–2026), Dkt. Tulia Ackson, pamoja na kuchaguliwa kwa Dkt. Zeyana Abdallah Hamid kuwa mjumbe wa Kamati ya Afya ya IPU. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI:
Mkutano wa tatu unaozihusisha pande mbili ambazo ni Urusi na Afrika umeanza rasmi jijini Moscow, Urusi, leo Jumatano, Oktoba 28, 2026, na utaendelea hadi Alhamisi Oktoba 29, 2026 huku kuimarisha diplomasia kupitia nyanja mbalimbali kukiwa sehemu ya ajenda kuu.
Katika Mkutano huo, wawakilishi kutoka nchi 48 za Afrika wanahudhuria, wakiwemo viongozi 22 wa nchi mbalimbali na serikali.
Mkutano huo unaongozwa kwa na Rais wa Urusi, Vladimir Putin na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, Rais Evariste Ndayishimiye wa Burundi.
Hadi sasa, mikutano ya kiuchumi inaendelea huku Rais Putin akitarajiwa kutoa hotuba kuu na kufanya mfululizo wa mazungumzo na viongozi wa hao wa Afrika.
Katika mkutani huo karibu Nyaraka 33 za ushirikiano zinatarajiwa kusainiwa, zikiwemo za biashara, uwekezaji na maendeleo ambapo ajenda kuu inahusisha biashara, nishati, chakula, usalama, teknolojia na uhusiano wa kisiasa kati ya Urusi na bara la Afrika.
Kikao kikuu cha viongozi na tamko la mwisho la mkutano huo linatarajiwa Alhamisi, Oktoba 29, 2026 -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Wananchi wa Kata ya Msimbati, Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara, mkoani Mtwara, wameiomba Serikali kujenga barabara yenye urefu wa kilomita 35 kwa kiwango cha lami, wakieleza kuwa ubovu wa barabara hiyo umekuwa kikwazo cha usafiri na shughuli za kiuchumi katika eneo hilo kwa muda mrefu.
Wakizungumza Oktoba 27, 2026 katika mkutano wa hadhara uliofanyika mbele ya Waziri wa Nishati Juma Homera, wananchi hao wamesisitiza kuwa ujenzi wa barabara hiyo utasaidia kurahisisha usafiri na kupunguza changamoto zinazowakabili katika shughuli zao za kila siku.
Miongoni mwa wananchi walioeleza changamoto hizo ni Rabia Mwarabu na Juma Rashidi, ambao wamebainisha namna hali ya barabara hiyo inavyoathiri maisha ya wananchi na maendeleo ya uchumi wa eneo hilo. Ombi hilo pia limeungwa mkono na Mbunge wa Jimbo la Mtwara Vijijini, Arif Premji, akieleza kuwa barabara hiyo ni muhimu kwa wananchi wanaoishi karibu na wanaozunguka miundombinu ya gesi asilia.
Wananchi hao wametoa ombi hilo wakati wa mkutano uliofuatia ziara ya ukaguzi wa shughuli za gesi asilia katika Kitalu cha Mnazi Bay, ambako Waziri wa Nishati Juma Homera alitangaza ugunduzi mpya wa gesi asilia unaokadiriwa kuwa na futi za ujazo bilioni 223.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Viongozi wapya wa Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA) mkoani Ruvuma, wametakiwa kuhakikisha wanasimamia vizuri miradi ya maendeleo iliyo chini ya baraza hilo ikiwa ni pamoja na kubuni vyanzo vipya vya mapato ili kuinua uchumi wa taasisi hiyo.
Akizungumza baada ya kumalizika kwa uchaguzi uliofanyika mapema wiki hii, Katibu wa Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA) mkoani Ruvuma, Sheikh Rajabu Songambele, amesema kuwa kwa kiasi kikubwa shughuli za BAKWATA zinahitaji kujitolea.
Kwa upande wake Afisa kutoka Ofisi ya Katibu Mkuu wa Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Sheikh Buruan Mohamed Mlau, ambaye alikuwa msimamizi wa uchaguzi wa BAKWATA mkoani Ruvuma, amesema viongozi wapya wanapaswa kuzingatia kauli mbiu ya Mufti wa Tanzania inayowataka Waislamu kujitambua, kubadilika na kuacha mazoea.
Nao viongozi wapya wa BAKWATA mkoani humo wamesema watahakikisha kuwa katika kipindi chao cha uongozi wanafanya kazi ya kuwaunganisha Waislamu, huku wakisimamia vizuri miradi yote iliyo chini ya BAKWATA.
Viongozi waliochaguliwa katika uchaguzi huo ni mwenyekiti wa Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA)mkoa wa Ruvuma pamoja na wajumbe wa Baraza hilo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI:
Uchaguzi Mkuu nchini Israel umeingia katika hatua ya kuhesabu kura, siku moja baada ya Waisraeli kwenda vituoni kuchagua wabunge 120 wa Knesset jana Oktoba 27, 2026.
Uchaguzi huo umehusisha upande wa Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu na upande wa kiongozi wa upinzani Gadi Eisenkot.
Hadi asubuhi ya leo, Oktoba 28, 2026 takriban asilimia 32.5 ya masanduku ya kura yamehesabiwa na matokeo ya awali yameonesha kambi ya Netanyahu ikiwa na takribani viti 59, ikifuatiwa na upinzani wenye takribani viti 46.
Hata hivyo, hakuna mshindi rasmi kwa kuwa chama au muungano unahitaji viti 61 ili kupata kibali cha kuunda serikali.
Kura za askari na wapiga kura walio nje ya vituo vyao vya kawaida bado hazijahesabiwa jambo linalotajwa kwamba linaloweza kubadilisha matokeo.
Uchaguzi huo ni wa kwanza tangu shambulio la Hamas la Oktoba 7, 2023, na unatajwa kuendeshwa katika hali ya mgawany wa kisiasa, pamoja na masuala ya usalama na vita vya Gaza. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI PICHA:
Aliyekuwa Mgombea Urais kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2025 kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) Salum Mwalim, Oktoba 27, 2026 amefika nyumbani kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Inspekta Jenerali Camillius Wambura, Masaki, Dar es salaam kumpa pole kwa kufiwa na baba yake Mzee Deusdedit Daniel Mwita Wambura. -
Jambo TV
@Jambotv_
Mahakama ya Rufaa ya Tanzania imetupilia mbali rufaa ya Private Clinton Honest Damas(Nyundo) na wenzake watatu waliokuwa wamehukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kosa la kumbaka kwa kundi binti wa wa miaka 17 maarufu kama binti wa Yombo huku ikihibitisha hukumu hiyo iliyotolewa na Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma.
Kwa mujibu wa hukumu iliyotolewa leo Oktoba 27, 2026, tukio la kumbaka binti huyo lilitendwa na Nyundo akishirikiana na Amini Lord Lema(Kindamba), Nickson Idala Jackson na C.1693 WDR Praygod usiku wa Mei 25 na 26, 2024, katika eneo la Mpamaa, Dodoma ambapo msichana mwenye umri wa miaka 17 alidai kufanyiwa ukatili wa kingono na kundi la vijana.
Katika rufaa yao, Nyundo na wenzake kupitia wakili wao waliomba Mahakama ya Rufaa itengue hukumu ya hatia na adhabu ya kifungo cha maisha jela, wakipinga uhalali wa hati ya mashtaka, namna ushahidi wa video ulivyopatikana na kuhifadhiwa, utambuzi wao wakati wa tukio la usiku pamoja na matumizi ya taarifa ya maungamo ya Nyundo.
Pia walidai kuwa ushahidi haukuthibitisha kosa la kubaka kwa kundi pasipo kuacha mashaka yenye msingi na kwamba utetezi wao wa kutokuwepo eneo la tukio haukuzingatiwa ipasavyo.
Kuhusu utambuzi wa wahusika, hoja za Nyundo na wenzake zilikataliwa kutokana na ushahidi wa 'Binti wa Yombo' kueleza kuwa tukio hilo lilifanyika kwa muda wa saa mbili huku taa ikiwa inawaka pia umbali baina yake na watendaji wa tukio uliondoa mashaka juu ya utambuzi.
Katika uamuzi wake, Mahakama ya Rufaa ilisema ushahidi uliowasilishwa ulithibitisha kosa la kubaka kwa kundi bila kuacha mashaka yenye msingi, hivyo kutupilia mbali rufaa na kuthibitisha vifungo vya maisha jela.
Hata hivyo, mahakama ilisimamia uamuzi wa Mahakama Kuu wa kufuta hukumu ya kosa la pili la kufanya tendo lisilo la kawaida kwa pamoja(unnatural offences) kwa kuwa msingi wa kisheria wa kuwahukumu washitakiwa wote kwa kosa hilo haukuwepo katika mazingira ya kesi hiyo. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limesena limesajili bidhaa elfu 9,731 za chakula na vipodozi pamoja na maeneo zaidi ya elfu 80 ya uzalishaji, uuzaji, usambazaji na uhifadhi wa bidhaa hizo katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Sita, huku pombe ikitajwa kuongoza katika usajili huo.
Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dkt. Ashura Katunzi, ameeleza hayo leo, Jumanne, Oktoba 27, 2026, katika mkutano kati ya TBS na wahariri wa vyombo vya habari ulioandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina (OTR), katika makao makuu ya TBS, Ubungo, Dar es Salaam.
“Usajili wa bidhaa na maeneo ya uzalishaji, uuzaji, usambazaji na uhifadhi wa chakula na vipodozi unalenga kuhakikisha ubora na usalama wa bidhaa hizo ili kuendelea kulinda afya za walaji.” amesema Dkt Ashura.
Amongeza kwamba TBS inaendelea kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria ya Viwango, Sura ya 130, kwa kusimamia ubora na usalama wa bidhaa zinazozalishwa na kuuzwa nchini.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa, amelipongeza Shirika la Reli Tanzania (TRC) kwa kuanzisha teknolojia ya kisasa ya kufundishia madereva wa treni, hatua inayolenga kuimarisha ujuzi wa madereva hao na kuongeza usalama katika usafiri wa reli nchini.
Profesa Mbarawa ametoa pongezi hizo leo, Oktoba 27, 2026, alipokuwa katika ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) katika Kituo cha Fela, mkoani Mwanza. Katika ziara hiyo, alipata fursa ya kuona teknolojia hiyo inayotumika katika mafunzo ya madereva wa treni.
Teknolojia hiyo, inayojulikana kama Motion Platform Simulator, inatoa mazingira ya mafunzo yanayokaribiana na uendeshaji wa treni halisi. Mwanafunzi anaweza kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoweza kujitokeza wakati wa safari, ikiwemo vikwazo kwenye njia ya reli na hali mbaya ya hewa.
Mfumo huo pia una uwezo wa kufuatilia kasi ya treni na kutathmini namna dereva anavyofuata maelekezo ya uendeshaji, ikiwemo kuzingatia viwango vya kasi katika vituo na maeneo ya kubadilisha njia za reli. Teknolojia hiyo inaweza kutumika katika mafunzo ya madereva wa reli za SGR, Meter Gauge Railway (MGR) na Cape Gauge.
Akizungumzia maendeleo hayo, Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Machibya Shiwa, amesema Tanzania ni nchi ya pili barani Afrika kuwa na simulator hiyo. Amesema teknolojia hiyo inamfanya dereva aliye ndani ya chumba cha mafunzo kutokuwa na tofauti na aliye relini
Amesema zaidi kwamba kituo hicho kitajumuisha madarasa ya kisasa, karakana za vitendo na miundombinu ya mafunzo ya kitaalamu kwa ajili ya kuendeleza rasilimali watu katika sekta ya reli.
Hatua hiyo inatarajiwa kuimarisha ubora wa mafunzo, kuongeza usalama wa safari za treni na kuboresha uwezo wa wataalamu wa Kitanzania katika kuendesha na kusimamia mifumo ya kisasa ya usafiri wa reli.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Seif Shekalaghe pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ally Gugu, leo Oktoba 27, 2026 wamesaini Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano inayolenga kuimarisha upatikanaji wa huduma za msaada wa kisheria kwa wafungwa na mahabusu magerezani, kwa lengo la kulinda haki zao na kuboresha upatikanaji wa haki.
Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri wa Katiba na Sheria, Abdallah Hamis Ulega amesema ushirikiano huo utaimarisha uratibu wa utoaji wa huduma za msaada wa kisheria kwa wafungwa na mahabusu, huku akisisitiza umuhimu wa kuandaa mpango kazi utakaobainisha majukumu ya kila taasisi na matokeo yanayotarajiwa sambamba na kuimarisha matumizi ya mifumo ya kidijitali katika usimamizi wa taarifa za mashauri.
“Haki haipaswi kutolewa kutokana na hali ya kiuchumi ya mtu. wafungwa na mahabusu wana haki ya kupata msaada wa sheria bila kujali hali zao za kiuchumi. Hivyo, tuna wajibu wa kusimamia, kuratibu na kuwezesha upatikanaji wa huduma za msaada wa kisheria magerezani”, ameeleza.
Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi amesema makubaliano hayo yatawasaidia wafungwa na mahabusu kuelewa haki zao, taratibu za kisheria na hatua zinazopaswa kuchukuliwa katika mashauri yao.
Kwa upande wake Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Tanzania, Jeremiah Yoram Katungu, amesema kupitia Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia, wafungwa na mahabusu 19,511 katika mikoa ya Dodoma, Manyara, Shinyanga, Simiyu, Ruvuma, Singida na Njombe wamenufaika na Huduma za Msaada wa Kisheria.
Ameongeza kuwa watumishi zaidi ya 290, wakiwemo Maafisa Sheria, Maafisa Urekebu na Wasaidizi wa Kisheria, wamepatiwa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kutoa huduma hizo kwa ufanisi.
Sambamba utiaji saini wa hati hizo za makubaliano, Ulega na Katambi wamezindua rasmi mwongozo wa uanzishaji na uendeshaji wa Madawati ya Msaada wa Kisheria Magerezani wenye lengo la kuimarisha uratibu na usimamizi wa huduma hizo. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeagiza bendera zake kupepea nusu mlingoti kuanzia siku ya Oktoba 29, 2026 mpaka Novemba 4, 2026 ikiwa ni sehemu ya kuwakumbuka waliofariki kutokana na matukio ya Oktoba 29, 2025.
Mnyika amesema hayo leo Oktoba 27, 2026 akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam ikiwa anasoma maazimio ya kamati kuu ya chama hicho iliyoketi leo pia.
Pamoja na hayo ameeleza kuwa kamati kuu ya chama hicho imeendelea kuazimia juu ya uchunguzi huru wa mauaji yaliyotokana na matukio ya siku hiyo pamoja na ulipwaji wa fidia kwa wale walioathirika.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Kufuatia taarifa za kutekwa kwa Mwanaharakati na Mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo @ChademaTZ2 Twaha Mwaipaya, chama hicho kimesema kimeandila barua rasmi kwenda kwa Rais wa Kenya William Ruto kumtaka kuingilia kati sakata hilo.
Hayo ameyaeleza Katibu wa chama hicho John Mnyika akizungumza na waandishi wa hanari leo Oktoba 27, 2026 akieleza kuwa tayari barua hiyo imeshafikishwa Ubalozi wa Kenya uliopo hapa nchini.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mbunge wa Jimbo la Mtama mkoani Lindi, Nape Nnauye amebainisha kuwa fursa ya Tanzania kuwa mwenyeji wa Mkutano Mkuu wa 153 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) kwa mara ya kwanza ni matokeo ya kazi nzuri ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuimarisha misingi ya utawala bora na diplomasia ya kimataifa.
Nape ameyasema hayo leo, Oktoba 27, 2026, bungeni jijini Dodoma wakati akichangia azimio la Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania la kumpongeza, kumtia moyo Rais Dkt. Samia kwa kuridhia na kufanikisha kufanyika kwa mkutano huo mkubwa wa kimataifa nchini kuanzia Oktoba 5 hadi 9, 2026
Nape ameeleza kuwa mkutano huo uliofanyika Arusha umeonyesha uwezo mkubwa wa Tanzania katika kuandaa na kuendesha mikutano mikubwa ya kimataifa na kuwa jukwaa la majadiliano ya masuala yanayoigusa dunia.
Nape amebainisha kuwa katika kipindi ambacho dunia inakabiliwa na migogoro ya kivita, migawanyiko ya kisiasa na mabadiliko ya tabianchi, Mkutano wa Arusha umetoa jukwaa muhimu la kidiplomasia ya kibunge, utatuzi wa migogoro kwa njia za amani, na ulinzi wa haki za binadamu.
"Kwa kuwa Tanzania imeandika historia chini ya uongozi madhubuti wa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kuwa mwenyeji wa mkutano mkuu wa IPU kwa mara ya kwanza ambapo mafanikio ya maandalizi na uendeshaji wake yameonesha uwezo mkubwa wa Tanzania wa kuendesha mikutano mikubwa ya kimataifa na kuwa jukwaa la majadiliano kuhusu masuala yanayoigusa dunia", ameeleza Nape.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mbunge wa Jimbo la Mtama mkoani Lindi, Nape Nnauye amebainisha kuwa fursa ya Tanzania kuweka historia na kuwa mwenyeji wa Mkutano Mkuu wa 153 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) ni matokeo ya uongozi mahiri wa Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na kazi nzuri ya kuimarisha utawala bora na diplomasia ya kimataifa.
Nape ameyasema hayo leo, Oktoba 27, 2026, bungeni jijini Dodoma wakati akichangia azimio la Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania la kumpongeza, kumtia moyo Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia na kufanikisha kufanyika kwa mkutano huo mkubwa wa kimataifa nchini kuanzia Oktoba 5 hadi 9, 2026
Nape ameeleza kuwa kuaminiwa na kuheshimiwa kwa Tanzania na taasisi hiyo kuu ya mabunge duniani kunadhihirisha usimamizi thabiti wa diplomasia na utawala bora chini ya Serikali ya Awamu ya Sita
Vilevile, Nape amebainisha kuwa mkutano huo uliokusanya viongozi na wajumbe kutoka zaidi ya nchi 150 uliwawezesha wageni hao wa kimataifa kujionea wenyewe amani, usalama, na maendeleo yaliyopo nchini badala ya kutegemea taarifa za upotoshaji.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mbunge wa Jimbo la Mtama mkoani Lindi, Nape Nnauye, amewataka Watanzania na wabunge kusimama imara bila hofu wala uoga na kutokubali watu wachache wasiotakia mema taifa kuandika historia ya nchi, huku akisisitiza wajibu wa kumlinda na kumtia moyo Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kufuatia uongozi wake uliowesha dunia kuiamini Tanzania.
Nape ameyasema hayo leo, Oktoba 27, 2026, bungeni jijini Dodoma wakati akichangia azimio la Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania la kumpongeza, kumtia moyo na kumshika mkono Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia na kufanikisha kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa 153 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) nchini kuanzia Oktoba 5 hadi 9, 2026.
Nape ameeleza kuwa uongozi bora unadhihirika pale ambapo kiongozi anakabiliana na changamoto bila kukata tamaa na kuwavusha wananchi salama. Amebainisha kuwa imani iliyooneshwa na dunia kuileta mikutano mikubwa nchini inatokana na ujasiri na uongozi wa Rais Samia wa kuivusha nchi kwenye milima na mabonde.
Vilevile, Nape ametoa wito kwa Watanzania na wabunge kuendelea kuwa wamoja na kulinda mambo makubwa ambayo nchi inapaswa kujivunia, badala ya kuruhusu nia ovu za watu wachache ziharibu historia na mwelekeo wa taifa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Jeshi la Magereza Tanzania limesisitiza kuwa mawakili wanaomwakilisha Mahabusu Tundu Lissu wanaendelea kuruhusiwa kuonana na mteja wao gerezani kwa mujibu wa sheria mara baada ya kujiridhisha kuwa ni mawakili wake halali, likikanusha madai ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuwa mawakili wa kiongozi huyo wamekuwa wakizuiwa kuingia gerezani.
Akiwasilisha taarifa rasmi kwa umma leo, Oktoba 27, 2026, Msemaji wa Jeshi la Magereza, SACP Elizabeth Mbezi amefafanua kuwa taarifa zinazosambazwa na CHADEMA kuhusu kuzuiwa kwa mawakili si za kweli na zinalenga kuleta taharuki katika jamii.
"Kuhusu kutembelewa na mawakili wanaomwakilisha wameendelea kuruhusiwa kuonana na mteja wao kwa mujibu wa taratibu baada ya kujiridhisha kuwa ni mawakili wake na si vinginevyo. Jambo hili limekuwa likitekelezwa kwa mujibu wa Sheria na Taratibu zilizopo", ameeleza SACP Mbezi.
SACP Mbezi ameongeza kuwa Jeshi la Magereza linazingatia sheria, utu na misingi ya haki za binadamu katika kuwahifadhi mahabusu wote, huku akibainisha kuwa Mwenyekiti huyo wa CHADEMA yupo salama na wala hayupo kwenye mgomo wa kula kama ilivyodaiwa.
Ufafanuzi huo wa Jeshi la Magereza unakuja kufuatia taarifa iliyotolewa tarehe 26 Oktoba 2026 na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa CHADEMA, Brenda Rupia, aliyedai kuwa mawakili watatu wa Tundu Lissu walizuiwa kuingia gerezani kumuona mteja wao.
Kwa mujibu wa Rupia, mawakili hao, Dickson Matata, Doris Kafuku, na Neema Massame walifika gerezani tarehe 26 Oktoba 2026 kwa lengo la kumtembelea na kuwasiliana na Lissu, lakini walizuiwa kuingia ndani na mamlaka za gereza hilo, jambo linalohatarisha haki yake ya msingi ya kupata msaada wa kisheria. -
Jambo TV
@Jambotv_
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimedai kuwa Mwenyekiti wake, Tundu Lissu, ameanza mgomo wa kula chakula kuanzia tarehe 26 Oktoba 2026 akiwa gerezani, huku mawakili wake watatu wakizuiwa kuingia gerezani kumuona
Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa Oktoba 26, 2026 na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa CHADEMA, Brenda Rupia, chama hicho kilitangaza kuwa Lissu alifikia uamuzi wa kuanza mgomo wa kula kutokana na wasiwasi juu ya upatikanaji wa haki yake ya msaada wa kisheria na mawasiliano na mawakili wake.
Rupia ameeleza kuwa mawakili watatu wa Lissu, Dickson Matata, Doris Kafuku na Neema Massame walikwenda gerezani tarehe 26 Oktoba 2026 kwa lengo la kumuona na kuwasiliana naye, lakini walizuiwa kuingia ndani na mamlaka za gereza
"Leo, mawakili wake watatu, Dickson Matata, Doris Kafuku na Neema Massame, walikwenda gerezani kwa lengo la kumuona na kuwasiliana naye, lakini walizuiwa kuingia. CHADEMA inaeleza wasiwasi wake mkubwa kuhusu kuzuiwa kwa mawakili hao kumwona Mwenyekiti wa Chama, hasa wakati huu ambapo tayari ameanza mgomo wa kula. Hali hii inazua maswali mazito kuhusu kupatikanaji wa huduma za kisheria na namna haki za Mheshimiwa Tundu Lissu zinavyolindwa akiwa gerezani", ameeleza Rupia.
CHADEMA imezitaka mamlaka husika kuhakikisha mawakili hao wanaruhusiwa kumwona Lissu bila vikwazo visivyo na msingi wa kisheria na kuchukua hatua za haraka kulinda usalama na ustawi wake
Akijibu madai hayo kupitia taarifa kwa umma iliyotolewa Oktoba 27, 2026, Msemaji wa Jeshi la Magereza, SACP Elizabeth Mbezi ameeleza kuwa taarifa zilizosambazwa na CHADEMA si za kweli, ni za upotoshaji na zinalenga kuleta taharuki katika jamii.
Amefafanua kuwa mahabusu Tundu Lissu yupo salama gerezani na wala hayupo kwenye mgomo wa kula chakula kama ilivyoripotiwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa CHADEMA.
Kuhusu suala la mawakili, SACP Mbezi amebainisha kuwa mawakili wanaomwakilisha Lissu wameendelea kuruhusiwa kuonana na mteja wao kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizopo mara baada ya kujiridhisha kuwa ni mawakili wake halali
"Jeshi la Magereza linapenda kuujulisha umma kwamba, Mahabusu Tundu Lissu yupo salama na hayupo katika mgomo wa kula chakula kama ilivyorotiwa. Kuhusu kutembelewa na mawakili wanaomwakilisha wameendelea kuruhusiwa kuonana na mteja wao kwa mujibu wa taratibu baada ya kujiridhisha kuwa ni mawakili wake na si vinginevyo. Jambo hili limekuwa likitekelezwa kwa mujibu wa Sheria na Taratibu zilizopo", imeeleza taarifa hiyo.
SACP Mbezi ameongeza kuwa katika kutekeleza majukumu yake ya kuwapokea, kuwahifadhi na kuwarekebisha wanaoshikiliwa, Jeshi hilo limekuwa likizingatia usalama, sheria, kanuni, utu na misingi ya haki za binadamu. Amewataka wananchi kupuuza taarifa hizo zisizo na ukweli na kuacha kuzisambaza kwani kufanya hivyo ni kosa kisheria. -
Jambo TV
@Jambotv_
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeagiza bendera zake kupepea nusu mlingoti kuanzia siku ya Oktoba 29, 2026 mpaka Novemba 4, 2026 ikiwa ni sehemu ya kuwakumbuka waliofariki kutokana na matukio ya Oktoba 29, 2025.
Mnyika amesema hayo leo Oktoba 27, 2026 akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam ikiwa anasoma maazimio ya kamati kuu ya chama hicho iliyoketi leo pia.
"Bendera za chama zitapepea nusu mlingoti kuanzia Oktoba 29 mpaka Novemba 4" amesema Mnyika -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI PICHA:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, akimfariji Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Camillus Wambura, nyumbani kwake Masaki Jijini Dar es Salaam leo Oktoba 27, 2026 kufuatia kufiwa na Baba yake mzazi Deusdedit Mwita Wambura aliyefariki Oktoba 24, 2026 Jijini Dar es Salaam. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI:
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) umetoa wito kwa mamlaka nchini Kenya kufanya uchunguzi wa haraka ili kubaini mahali alipo mwanaharakati na raia wa Tanzania, Twaha Mwaipaya, anayedaiwa kutekwa nchini humo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mratibu wa Kitaifa wa THRDC, Onesmo Olengurumwa, Oktoba 26, 2026, tukio hilo lilitokea Jumapili, Oktoba 25, 2026, jijini Nairobi, Kenya. THRDC imesema watu wasiojulikana walikuwa wakimfuatilia Mwaipaya, kisha kuvamia gari alilokuwa nalo na kuondoka naye kusikojulikana.
Kutokana na mazingira hayo, THRDC imeeleza kushtushwa na kile imesema ni ukimya pamoja na ukosefu wa taarifa rasmi kutoka kwa vyombo vya usalama nchini Kenya hadi kufikia Jumatatu, Oktoba 26, 2026, ikiwa ni siku mbili tangu kuripotiwa kwa tukio hilo.
THRDC imeeleza kuwa, licha ya Ubalozi wa Tanzania nchini Kenya kufuatilia suala hilo, kutoonekana kwa taarifa rasmi za kiserikali kumezidi kuleta hofu kwa familia yake, jamii, na wanaharakati.
Zaidi THRDC imeeleza kwamba, Katiba ya Kenya ya mwaka 2010, Ibara za 21, 26, 29, 49 na 51 zinaweka wazi wajibu wa kulinda haki ya kuishi, uhuru, usalama, na haki za mtu anayeshikiliwa, ikiwemo kuonana na wakili na kufikishwa mahakamani.
Aidha imesema kupitia Sera ya Mambo ya Nje ya mwaka 2001 na mikataba ya kimataifa kama Mkataba wa Vienna wa Mahusiano ya Kidiplomasia wa 1961 na Mahusiano ya Kibalozi wa 1963, Tanzania ina wajibu wa kulinda maslahi na raia wake walioko nje ya nchi.
Katika taarifa hiyo, THRDC imetoa maazimio na ushauri, ikiiomba Serikali ya Kenya kufanya uchunguzi huru na wa wazi ili kubaini alipo Mwaipaya na kuchukua hatua za kisheria dhidi ya waliohusika.
Aidha imeisihi Wizara ya Mambo ya Nje ya Tanzania kupitia ubalozi wake jijini Nairobi kuongeza juhudi za kufuatilia suala hilo na kutoa taarifa sahihi kwa umma.
THRDC imesema zaidi kwamba, Iwapo Mwaipaya anashikiliwa na vyombo vya dola, sheria na taratibu zifuatwe ikiwemo kupata huduma za kisheria, matibabu, na haki ya kuwasiliana na ndugu zake na ubalozi. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mbunge wa Jimbo la Mtama mkoani Lindi, Nape Nnauye, amebainisha kuwa kuridhiwa na kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa 153 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) nchini ni ushahidi usiopingika kuwa Tanzania bado ni kisiwa cha amani duniani, huku akiwataka Watanzania kulinda amani na utulivu kama mtaji mkuu wa taifa.
Nape ameyasema hayo leo, Oktoba 27, 2026, bungeni jijini Dodoma wakati akichangia azimio la Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania la kumpongeza, kumtia moyo na kumshika mkono Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia na kufanikisha kufanyika kwa mkutano huo mkubwa wa kimataifa nchini kuanzia Oktoba 5 hadi 9, 2026.
Akizungumza bungeni, Nape ameeleza kuwa pamoja na maneno yote yanayoweza kusemwa, uamuzi wa dunia kuipenda na kuileta mikutano mikubwa nchini na wajumbe kuja na kuondoka salama unathibitisha kuwa Tanzania bado ni sehemu salama
"Ukiona vinaelea vimeundwa, azimio hili lina lengo la kumpongeza, kumtia moyo, kumshika mkono Rais wetu ambaye ameunda hivi ambavyo leo tunavisifia vinaelea... Ukweli kwamba Tanzania bado ni kisiwa cha amani, pamoja na maneno yote lakini sisi bado ni kisiwa cha amani ndio maana dunia iliridhia, ikaamini, ikaja Tanzania ikafanya mkutano huu mkubwa na wakaondoka salama. Hiki bado ni kisiwa cha amani, tunao wajibu wa kuendelea kukitunza kisiwa hichi cha amani", ameeleza Nape.
Nape amebainisha kuwa michango ya wabunge mbalimbali waliosema bungeni imedhihirisha kuwa amani na utulivu wa nchi si jambo la kuchukulia kawaida, bali ni mtaji mkuu ambao lazima uendelee kulindwa na kutunzwa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Oktoba 27, 2026, amefika Masaki, jijini Dar es Salaam, kutoa pole kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Camillus Wambura, kufuatia kifo cha baba yake mzazi, Deusdedit Mwita Wambura.
Mzee Deusdedit alifariki dunia Oktoba 24, 2026, jijini Dar es Salaam.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mahakama ya Rufani ya Tanzania, iliyoketi Dar es Salaam leo, Jumanne Oktoba 27, 2026, imeiondoa Rufaa ya Kamati ya Taifa Maadili ya Mawakili dhidi ya Peter Michael Madeleka baada ya rufaa hiyo kuonekana ina makosa ya kisheria na kufunguliwa nje ya muda wa kisheria.
Uamuzi huo mdogo umetolewa na jopo la Majaji watatu (3) waliokuwa wanasikiliza kesi hiyo wakiongozwa na Jaji Deo Nangela kwa niaba ya Majaji wenzake ambao ni Augustine Mwarija na Gerson Mdemu,
Kufuatia kuondolewa kwa Rufani hiyo Na. 1568/2024, kwa maana hiyo ushindi wa Michael Peter Madeleka ambaye pia ni Wakili, umebaki kama ulivyo.
Katika kesi hiyo Madeleka amejiwakilisha mwenyewe, wakati Kamati ya Taifa ya Maadili ya Mawakili imewakilishwa na Mawakili wa Serikali Edwin Webiro na Erigh Rumisha.
Msingi wa Rufaa hiyo ni uamuzi wa Mahakama Kuu katika kesi aliyofungua Madeleka dhidi ya Kamati hiyo na wengine kuwa mashtaka yaliyofunguliwa na DPP, Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Wakili wa Serikali Mkuu dhidi yake ni batili jambo ambalo lilipelekea upande ulioshindwa kukata rufaa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
📍MAREKANI - Je, kipaji cha mtoto kinaweza kugeuka kuwa sababu ya kutengwa badala ya kuungwa mkono? Hilo ni miongoni mwa maswali yaliyoibuka nchini Marekani baada ya mtoto wa miaka mitatu, anayejulikana kwa jina la Nevada, kujikuta katikati ya mzozo katika ligi ya soka la watoto uliofikia hatua ya polisi kuitwa uwanjani.
Tukio hilo lilitokea Oktoba 24, 2026, mjini Winter Park, Florida, wakati Nevada alipokuwa akishiriki ligi ya i9 Sports iliyohusisha watoto wenye umri wa miaka minne hadi sita. Video zilizosambaa mitandaoni zilimuonesha akiwapita wachezaji wenzake na kufunga mabao.
Mama yake, Martasia Griffin, anadai mwanawe aliondolewa kwenye ligi kutokana na uwezo wake mkubwa wa kucheza soka. Hata hivyo, mwakilishi wa ligi aliwaeleza polisi kuwa malalamiko yalihusu madai kwamba mtoto huyo alikuwa akisukuma wachezaji wengine wakati wa mchezo.
Polisi walifika uwanjani na kuzungumza na pande zilizohusika, lakini hakuna mtu aliyekamatwa wala kulazimishwa kuondoka. Familia iliondoka baada ya mazungumzo, huku ligi ikitoa ofa ya kurejesha ada ya usajili.
Tukio hilo limeibua mjadala kuhusu namna watoto wenye vipaji vya kipekee wanavyoshughulikiwa, huku baadhi ya watu wakiliangalia pia katika muktadha mpana wa ubaguzi wa rangi nchini Marekani.
Miongoni mwa walioonesha kumuunga mkono Nevada ni Rachel Griffin-Accurso, maarufu kama Ms. Rachel, mtayarishaji wa maudhui ya watoto, ambaye ametoa wito kwa wachezaji maarufu wa soka kumpa mtoto huyo nafasi ya kupata uzoefu na kuendeleza kipaji chake.
Ligi ya i9 Sports imesema inafanyia uchunguzi malalamiko kuhusu tukio hiloThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Serikali ya Kenya kupitia Ofisi ya Msemaji wake Charles Owino Wahong'o imesema bado haijapokea taarifa rasmi kutoka kwa taasisi yoyote kuhusu madai ya kutekwa kwa mwanaharakati na Mwanachama wa @ChademaTZ2 Twaha Mwaipaya, anayedaiwa kutekwa katika eneo la Kamulu, Kaunti ya Machakos nchini Kenya.
Kwa mujibu wa BBC Swahili, ofisi hiyo imesema bado inafuatilia suala hilo, “Bado hatujapata taarifa kuhusu tukio hilo, hivyo tunalifuatilia.” imesema taarifa hiyo.
Chombo cha habari nchini cha Mwananchi kiliripoti kuwa Ubalozi wa Tanzania nchini Kenya kupitia Balozi Dkt. Bernard Kibesse alisema anafuatilia taarifa za madai hayo.
"Bado taarifa ya tukio hilo hatujazipata, hivyo tunafuatilia" Dkt. Kibesse aliiambia Mwananchi
Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Amnesty International Kenya lilieleza kuwa Mwaipaya anadaiwa kutekwa Jumapili ya Oktoba 25, 2026 huku 'watekaji' wakitumia magari matatu, likiwamo Toyota Land Cruiser Hardtop. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI:
Mamia ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Gambia (UTG) jana Oktoba 26, 2026, waliandamana wakipinga kuzorota kwa mazingira ya masomo, changamoto za upatikanaji wa chakula na huduma duni za intaneti.
Waandamanaji hao walikusanyika katika chuo hicho kilichopo Banjul, mji mkuu wa Gambia, wakilalamikia changamoto mbalimbali zinazoathiri shughuli zao za kitaaluma, zikiwemo usafiri usiokidhi mahitaji, upatikanaji mdogo wa maji ya kunywa na kufungwa kwa mgahawa wa chuo.
Kwa mujibu wa taarifa ya Umoja wa Wanafunzi wa chuo hicho iliyotolewa Oktoba 25, 2026 Wanafunzi pia wanakabiliwa na huduma zisizoaminika za intaneti pamoja na kukwama kwa shughuli za masomo. Wakati wa maandamano hayo, wanafunzi walisikika wakipaza sauti wakisema, “Tumechoka.”
Maandamano hayo yamefanyika wiki chache baada ya maandamano mengine yaliyochochewa na kukatika mara kwa mara kwa umeme nchini humo.
Wizara ya Elimu ya Juu ya Gambia imesema imepokea malalamiko ya Wanafunzi na kusisitiza umuhimu wa mazungumzo ya kujenga, ikikiri kuwa madai hayo yanahitaji ufuatiliaji endelevu, uratibu mzuri na suluhisho la vitendo.
Oktoba 24, 2026, Serikali ilitangaza hatua kadhaa za kushughulikia malalamiko hayo, ikiwemo kurejesha huduma za chakula kuanzia Jumatatu, kuongeza sehemu za kupata maji ya kunywa, kuboresha usafiri na kuimarisha huduma za intaneti.
Hata hivyo, Umoja wa Wanafunzi uliendelea na wito wa kuhamasisha wanafunzi kushiriki kwa wingi katika maandamano hayo, huku ukiwataka washiriki kudumisha amani.
Maandamano hayo yanaibuka wakati Rais wa Gambia, Adama Barrow, akijiandaa kuwania muhula wa tatu katika uchaguzi uliopangwa kufanyika Desemba 5, 2026.
Wakati huo huo, katika wiki za hivi karibuni, Wanafunzi wa shule za sekondari nchini Ufaransa, Italia na Ubelgiji wameandamana wakitaka kuboreshwa kwa mazingira ya masomo, huku baadhi ya maandamano yakigeuka kuwa ya vurugu. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mtandao na Muungano wa Mashirika ya Kiraia, Watetezi wa Haki za Binadamu na Wanaharakati barani Afrika (The Pan-African Solidarity Network- PASNET) umelaani vikali kile ulichokieleza kuwa ni kutekwa kwa mwanaharakati wa Tanzania na mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Twaha Mwaipaya, huku ukitaka Mamlaka nchini Kenya kuchukua hatua za dharura kuokoa maisha yake.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 26, 2026, Mtetezi wa Haki za Binadamu, Alex Mukasa, amebainisha kuwa Mwaipaya alitekwa Oktoba 25, 2026 katika eneo la Kamulu, Kaunti ya Machakos nchini Kenya, nchi ambayo alikuwa amekimbilia kutafuta hifadhi na usalama.
Kwa mujibu wa taarifa za PASNET na mashirika ya haki za binadamu (ikiwemo Amnesty International), Mwaipaya alitekwa majira ya asubuhi akiwa safarini kwenye teksi kwenda kuwatembelea marafiki zake, ambapo watu waliomteka walikuwa wakitumia magari matatu, likiwemo gari la aina ya Toyota Land Cruiser Hardtop
“Kenya haiwezi kuendelea kuwa kitovu cha utekaji katika Afrika Mashariki. Mamlaka za Kenya zinapaswa kuingilia kati kwa dharura kuokoa maisha ya Twaha na kuhakikisha anaachiwa mara moja", ameeleza Mukasa.
Mukasa ameeleza kuwa uwepo wa taarifa za mashuhuda kuhusu magari yaliyotumika ni vidokezo madhubuti vya kiupelelezi vinavyopaswa kufanyiwa kazi mara moja na Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) pamoja na Idara ya Usalama wa Taifa nchini Kenya ili kubaini mahali alipo na kumpata akiwa salama.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Wakazi wa eneo la Luhanga, Kata ya Kisukuru katika Wilaya ya Ilala mkoani Dar es Salaam wamepokea mabomba kutoka kwa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kwa lengo la kuanza utekelezaji wa mradi wa usambazaji wa maji kwa wananchi takribani 6,500 wa eneo hilo ikiwa ni kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuboresha huduma za maji.
Semeni Adam ambaye ni mkazi wa Mtaa wa Luhanga ameipongeza DAWASA kufikisha na kukabidhi mabomba hayo kwa wananchi ikiwa ni ishara ya kuanza utekelezaji wa mradi wa maboresho ya huduma ya maji katika eneo hilo.
Kwa upande wa Meneja wa DAWASA mkoa wa kihuduma Tabata, Gilbert Massawe amesema mamlaka hiyo inakwenda kubadilisha miundombinu katika Mtaa wa Luhanga ili kuendana na mahitaji ya sasa na baadaye kuendelea kufanya utafiti wa maeneo yatakayoweza kuchimbwa visima kusaidia upatikanaji wa maji.
Naye, Mwenyekiti wa Mtaa wa Luhanga Kisukuru, Lukresia Msuya ameipongeza Serikali kupitia Mamlaka kwa juhudi za makusudi na haraka zilichokuliwa ili kuwasaidia wananchi kuondokana na changamoto ya majisafi.
"Nitoe wito kwa wananchi wa Luhanga kutoa ushirikiano katika utekelezaji wa mradi huu, awali Serikali ilidhamiria kuchimba visima kusaidia upatikanaji wa maji lakini kutokana na mazingira ya maeneo kutokuwa rafiki imeamua kuja na mradi mbadala hivyo wananchi tutunze mradi huu”, amesema Msuya.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) imetoa wito wa kitaifa kwa makanisa yote wanachama nchini kuungana katika maombi maalum ya toba, rehema, amani na haki, kuelekea kutimiza mwaka mmoja tangu kutokea kwa matukio ya mauaji na umwagaji damu wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa tarehe 29 Oktoba 2025.
Wito huo umetolewa katika taarifa rasmi iliyosainiwa na Mwenyekiti wa CCT, Askofu Dkt. Stanley Hotay ikielekezwa kwa Maaskofu, Viongozi Wakuu, na Wakuu wa Makanisa yote wanachama wa CCT nchini.
Katika taarifa hiyo, CCT imebainisha kuwa ni wajibu wa Kanisa kumwomba Mungu kulirehemu taifa na kuponya majeraha ya matukio yaliyopita, ili kuzuia kujirudia kwa umwagaji damu na kuvunjika kwa amani.
"Wote tunafahamu kuwa ni takribani mwaka mmoja tangu matukio ya mauaji, umwagaji damu na uvunjifu wa amani kutokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa tarehe 29 Oktoba 2025, hivyo kama Kanisa ni wajibu wetu na inafaa tumwombe Bwana, Mungu wetu; Aturehemu na kutusamehe kwa dhambi na makosa wetu kama taifa na kwa kumwaga damu isiyo na hatia katika Taifa". Imeeleza taarifa hiyo.
Dkt. Hotay ameongeza kuwa maombi hayo yanadhaniwa kuwafariji waliofiwa na kuleta uponyaji kwa waliojeruhiwa, akisisitiza"Tumwombe Mungu atulinde dhidi ya kurudia matukio kama hayo na atujalie amani, haki, umoja na maridhiano ya kweli katika Taifa letu la Tanzania".
Akinukuu Neno la Mungu kutoka 2 Mambo ya Nyakati 7:14, Dkt. Hotay ameitaka jamii kujinyenyekesha mbele ya Mungu, kuacha njia mbaya ili Mungu aisikie nchi na kuiponya.
Mbali na maombi ya amani na haki, taarifa hiyo ya CCT imegusia pia utabiri wa hali ya hewa uliotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) unaoonesha uwezekano wa mvua kubwa na maafa, ikihimiza waumini kuomba Mungu kuepusha mafuriko, uharibifu wa mali, mazao, miundombinu, magonjwa, na kupoteza maisha.
Dr. Hotay ameeleza kuwa waumini wanapaswa kuomba ili Mungu ajaalie mvua za wastani zitakazosaidia kilimo na ustawi wa taifa, pamoja na kupewa hekima ya kuchukua tahadhari zinazostahili.
Akinukuu Maandiko Matakatifu ya Isaya 43:2 na Zaburi 46:1, Dr. Hotay amesema, "Kitabu Cha Zaburi 46:1 kinatukumbusha kuwa: 'Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso.' Kwa hiyo, sisi kama Kanisa na viongozi tuendelee kumtegemea Mungu kwa imani, hata katika nyakati hizi za matetesho ya Maafa na majaribu ya amani na haki katika Taifa Letu, huku tukiendelea kutenda kwa upendo na kujenga amani katika jamii zetu".
CCT imewataka viongozi wote wa makanisa wanachama kuongoza maombi hayo katika ibada, mikutano ya maombi, na vikundi vya waumini kote nchini. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Jeshi la Polisi Tanzania limesema kuwa hali ya usalama nchini ni shwari, huku likitoa onyo kali kwa baadhi ya viongozi wa dini, siasa, na wanarakati wanaodaiwa kuhamasisha vurugu, fujo, na uharibifu wa miundombinu pamoja na mali za umma na binafsi kupitia vikao vya ndani na hadharani.
Akiwasilisha taarifa hiyo leo, Oktoba 26, 2026, kutoka Makao Makuu ya Polisi jijini Dodoma, Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, DCP David Misime, amesema Jeshi la Polisi limeeleza kuwa limebaini kuwepo kwa mipango, matamko, na uhamasishaji unaofanywa kisirisiri na wazi na makundi hayo kwa nia ya kuhamasisha wananchi kujiingiza kwenye vitendo vya uhalifu.
“Kumekuwepo na mipango, matamko na uhamasishaji unaofanywa na baadhi ya viongozi wa dini, siasa na wanaharakati kisirisiri kupitia vikao vya ndani na uhamasishaji wa wazi wenye nia/mwelekeo wa kutaka kuhamasisha watu kujiingiza kwenye vitendo vya uhalifu”, ameeleza Misime.
Misime amewahakikishia Watanzania kuwa Jeshi la Polisi, kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama, linafuatilia kwa karibu taarifa zote linazopokea na halitasita kuwakamata na kuwachukulia hatua kali za kisheria wote wanaojihusisha na mipango hiyo.
"Tunatoa onyo, kwa wanaojihusisha kwa namna moja ama nyingine katika vitendo hivyo vya uhalifu vyenye mwelekeo wa kufanya fujo na kuharibu mali kuacha kwani halitasita kuchukua hatua kali kwa mujibu wa sheria kwa yeyote atakayebainika kujihusisha na mipango hiyo ya kihalifu", imeelezwa.
Katika hatua nyingine, Jeshi la Polisi limetoa rai kwa wananchi wote nchini kuendelea kuwa watulivu na kutii sheria za nchi bila shuruti ili kudumisha amani na usalama wa taifa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI PICHA:
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo @ChademaTZ2 Bara, John Heche @HecheJohn ameitaka Serikali ya Kenya kushirikiana na wahusika wengine kuhakikisha mwanachama wa chama hicho Twaha Mwaipaya anapatikana akiwa salama, kufuatia taarifa za 'kutekwa kwake'.
Heche ameandika kwenye ukurasa wake wa Instagram leo Oktoba 26, 2026 akieleza kuwa wamejitahidi usiku kucha kuwasiliana na vyombo vinavyohusika nchini Kenya ili kupata taarifa kuhusu alipo Mwaipaya lakini hawakufanikiwa
Akieleza msimamo wake kuhusu suala hilo, Heche amesema hana sababu ya kuamini kuwa Serikali ya Kenya inahusika moja kwa moja na tukio hilo, lakini amesisitiza umuhimu wa mamlaka za nchi hiyo kusaidia uchunguzi na kuhakikisha Mwaipaya anapatikana.
“Tunajua serikali ya Kenya haina sababu ya kumteka Twaha.” ameandika Heche
Hata hivyo ameeleza wasiwasi wake kuhusu uwezekano wa watu kuvuka mipaka ya nchi na kutekeleza vitendo vya utekaji bila msaada wa watu wengine, huku akimwomba Rais wa Kenya, William Ruto, na serikali yake kuhakikisha suala hilo linashughulikiwa.
“Lakini pia tunajua sio rahisi hawa watekaji waingie Nchi nyingine wamchukue mtu bila kusaidiwa na watu wa serikali hiyo tunamsihi Rais @WilliamsRuto na serikali yake wasaidie kuhakikisha Twaha anapatikana akiwa mzima.”
Aidha, Heche amesema tukio hilo, endapo litathibitishwa kuwa limetokea ndani ya mipaka ya Kenya, linaweza kuibua maswali kuhusu usalama wa watu wanaoishi au kutafuta hifadhi nchini humo.
Twaha Mwaipaya ameripotiwa kutekwa jana Oktoba 25, 2026 ikielezwa kuwa watu wenye silaha walimteka akiwa kwenye taxi ambapo alikuwa anaelekea kwa rafiki zake huku Wadau wa Haki za Binadamu kama shirika la Amnesty International nchini Kenya zikilaani tukio hilo. -
Jambo TV
@Jambotv_
Mwanaharakati wa Tanzania na mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Twaha Mwaipaya anadaiwa kutekwa na watu wenye silaha katika eneo la Kamulu, lililoko nje kidogo ya Jiji la Nairobi nchini Kenya, tukio ambalo limezua hofu kubwa kuhusu usalama na mahali alipo.
Taarifa kutoka shirika la Haki za Binadamu la Amnesty International zinabainisha kuwa Mwaipaya alitekwa mnamo saa nne asubuhi wakati akiwa safarini kwa teksi kwenda kuwatembelea marafiki zake huko Kamulu, katika Kaunti ya Machakos. Watu waliomteka walikuwa wakitumia magari matatu, likiwemo gari la aina ya Toyota Land Cruiser Hardtop.
"Twaha Mwaipaya, raia wa Tanzania, aliripotiwa kutekwa... na watu waliokuwa wakisafiri kwa magari matatu, ikiwemo Toyota Land Cruiser hardtop wakati akisafiri kwa teksi kuwatembelea marafiki," imesema taarifa ya Amnesty International.
Habari za kupotea kwa mwanaharakati huyo zimeelezwa pia na mwanaharakati maarufu wa Tanzania, Maria Sarungi, ambaye ameeleza kuwa anashirikiana kwa karibu na taasisi za haki za binadamu ili kumtafuta.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Habari, Mawasiliano na Uenezi wa CHADEMA Taifa, Brenda Rupia, kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, ametoa wito kwa mamlaka husika nchini Kenya akisema, “Tunaziomba mamlaka husika kwa haraka kubaini alipo, kuhakikisha usalama wake wa mara moja, na kuwachukulia hatua wahusika. Yeyote mwenye taarifa anahimizwa kujitokeza mara moja kutoa taarifa. Usalama wa Twaha lazima uwe kipaumbele, familia yake na umma wanastahili majibu.”
Hadi kufikia sasa, hakuna taarifa rasmi au tamko lolote lililotolewa na mamlaka za usalama nchini Kenya kuhusiana na tukio hilo la kutekwa kwa Mwaipaya. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, ametoa ufafanuzi wa kisayansi kuhusu maana halisi ya El Niño na kutetea taarifa za wataalamu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), huku akifafanua ukweli kuhusu makadirio ya Shilingi bilioni 730 zilizotajwa kwa ajili ya utayari wa kukabiliana na majanga na athari za El Niño.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma, Msigwa ameeleza kuwa El Niño kimsingi ni ongezeko la joto linaloweza kuambatana na mvua za kupita kiasi au jua kali kulingana na eneo, huku akitaka wananchi kuacha kuwashambulia au kuwakosoa wataalamu wa hali ya hewa.
Msigwa amebainisha kuwa ingawa uhuru wa kujieleza na kukosoa upo, si vyema kwa watu wasio na utaalamu kupotosha umma au kumkosoa mtaalamu mbobezi wa sekta husika.
Kuhusu hofu na upotoshaji uliozuka kuhusiana na kiasi cha Shilingi bilioni 730, Msigwa amefafanua kuwa fedha hizo si taslimu zilizowekwa pembeni au kuliwa, bali ni makadirio ya gharama zitakazotumiwa na serikali pamoja na sekta binafsi katika kujiandaa na kujilinda dhidi ya majanga.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Serikali kupitia Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, imetoa wito kwa Watanzania wote, hasa vijana, kujiepusha na hamasa za uchochezi au kujihusisha na matukio yenye viashiria vya vurugu na uvunjifu wa amani, huku ikisisitiza kuwa sheria ni msumeno na hakuna aliye juu yake.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Oktoba 25, 2026, jijini Dodoma, Msigwa amebainisha kuwa nchi inahitaji amani na utulivu ili wananchi na Serikali waweze kujielekeza katika uzalishaji mali, biashara za ndani na za nje, utekelezaji wa miradi ya maendeleo, na kuinua ustawi wa jamii.
Akimulika kuhusu madai mbalimbali ya wananchi katika jamii, Msigwa ameeleza kuwa Serikali ina mifumo rasmi na sheria zilizowekwa kwa ajili ya kushughulikia changamoto zote, na kwamba njia ya vurugu au kuchocheana haijawahi kuwa suluhisho la matatizo
"Madai mbalimbali ya wananchi hayatatuliwi kwa vurugu, kwa kuchocheana kwa kutiana hasira na kuharibiana misingi na tunu ya nchi yetu. Naomba kutoa wito kwa Watanzania wote kuendelea kujiepusha kushiriki katika matukio yoyote yenye viashiria vya vurugu na uvunjifu wa amani", ameeleza Msigwa.
Ameongeza kuwa pindi amani inapovurugika, hakuna msaada wa nje utakaoweza kuirudisha nchi kwenye mstari badala ya juhudi za Watanzania wenyewe, hivyo wananchi wanapaswa kupuuza hamasa zote zinazolenga kuleta machafuko.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Serikali ya Tanzania kupitia kwa Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, imetoa ufafanuzi na kukanusha kile ilichokiita upotoshaji unaoendelea katika jamii kuhusiana na makadirio ya bajeti ya Shilingi Bilioni 730 zilizotajwa kwenye Mpango wa Taifa wa Dharura wa Kujiandaa na Kukabiliana na Madhara ya El Niño kwa mwaka 2026/27.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Oktoba 25, 2026, jijini Dodoma, Msigwa amebainisha kuwa kiasi hicho cha Sh730 bilioni si bajeti mpya iliyochukuliwa kutoka kwenye mifuko ya wananchi au iliyotengwa upya na Serikali kuu pekee kwa ajili ya kugawana, bali ni mjumuisho wa makadirio ya rasilimali zilizopo tayari katika taasisi za serikali, sekta binafsi, na mashirika ya kimataifa.
Ameongeza kuwa taasisi mbalimbali za umma pamoja na sekta binafsi kama vile viwanda vya wafanyabiashara binafsi au wananchi wanaojenga na kuimarisha makazi yao wanatumia bajeti zao za kawaida zilizoidhinishwa kuchukua tahadhari.
Msigwa ameeleza kuwa maandalizi hayo ya dharura yanazingatia utabiri rasmi uliotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) unaoonesha uwezekano wa kutokea kwa El Niño yenye nguvu kubwa inayoweza kusababisha mafuriko, maporomoko ya ardhi, na milipuko ya magonjwa
Aidha, amesema kuwa serikali imeendelea kuweka kipaumbele katika kulinda maisha, usalama, na mali za wananchi kwa kuchukua hatua za tahadhari na kuimarisha mifumo ya utayari dhidi ya majanga.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Wizara ya Maendeleo ya Vijana, Dkt. Kedmon Mapana amewataka vijana kuacha tabia ya kulalamika na kuingia barabarani badala yake watumie fursa ya kuchukua mikopo inayotolewa na Serikali ili kujikwamua kiuchumi.
Akizungumza leo Jijini Mwanza kwenye hafla ya uvunaji wa samaki wa vizimba waliofugwa na kikundi cha Kitwina Youth Group kilichopo katika Kata ya Luchelele, Dkt. Mapana amewasihi vijana wenye mawazo bunifu kuhakikisha wanajisajili katika mfuko wa vijana wa YES ili kunufaika ni mikopo itakayotolewa ya awamu ya pili.
"Uwezeshaji upo tupunguze kulalamika, tupunguze kuingia barabarani ila tujitambue serikali itawasaidia lakini nitumie muda huu kuwambia vijana kuwa mikopo dirisha la pili litafunguliwa hivi karibuni kupitia Ofisi ya Rais Maendeleo ya Vijana, hakikisheni mmejisajili kwenye mfumo wa vijana unaitwa YES (Youth empowerment System)," amesema.
Akisoma risala, Katibu Kikundi cha Kitwina Youth Group, Bung'e Nawe amesema mbali na kikundi hicho kutarajia kuvuna tani 15 za samaki kutoka kwenye vizimba sita katika kipindi cha ukuaji wakikabiliwa na changamoto ya vifo vya samaki, upungufu wa chakula na wizi.
Nao baadhi wa wachuzi wa samaki Jijini Mwanza wamesema ujio wa vizimba umesaidia kupunguza changamoto ya uhaba wa samaki sambamba na kupunguza changamoto ya ajira.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mbunge wa zamani wa Jimbo la Arusha Mjini, Mrisho Gambo, ameitaka Serikali kutoa ufafanuzi wa kina na kuharakisha ukamilishwaji wa mchakato wa kukabidhi eneo lililoko karibu na Msikiti Mkuu wa Bondeni jijini Arusha kwa jumuiya ya Waislamu ili litumike kwa shughuli za kidini.
Akizungumza katika mkutano wa waumini wa Kiislamu uliofanyika mkoani Arusha hivi karibuni, Gambo alikumbushia kuwa hapo awali kulikuwa na maelekezo rasmi ya Serikali kuwa eneo hilo lingekabidhiwa kwa Waislamu, hivyo anataka kufahamu ni kwa nini mchakato huo umepata kikwazo na umefikia hatua gani hadi sasa.
Alibainisha kuwa suala hilo liliwahi kufikishwa serikalini na kujadiliwa hata katika vikao vya baraza la madiwani huku akikumbusha kuwa aliyekuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Geophrey Mizengo Pinda aliwahi kufika katika eneo hilo miaka kadhaa iliyopita kushughulikia suala hilo kwa kushirikiana na viongozi wa halmashauri.
Akijibu ombi na hoja hiyo ya Gambo, Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Nicodemus Tambo, ameeleza kuwa serikali ipo tayari kulifanyia kazi ombi hilo kwa kushirikiana kwa karibu na Mkurugenzi wa Jiji la Arusha pamoja na maafisa wa ardhi ili kubaini ukweli wa mambo na hatua zilizofikiwa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Mkoa wa Mbeya umeanza kufungua maeneo na njia 106 za pembezoni mwa mradi wa ujenzi wa njia nne, kufuatia agizo lililotolewa na Makamu wa Rais wa Tanzania, Deogratius Ndejembi, wakati wa ziara yake jijini humo Oktoba 16 na 17, 2026.
Hatua hiyo inalenga kuondoa changamoto za foleni kwa watumiaji wa barabara na kuruhusu shughuli za kiuchumi za wananchi kuendelea bila vikwazo wakati ujenzi wa mradi huo ukisonga mbele. Mradi huo wa kimkakati wa njia nne zenye urefu wa kilomita 29 kutoka Nsalaga hadi Ifisi, unagharimu kiasi cha Shilingi bilioni 138.
Akieleza hatua za utekelezaji wa maagizo hayo, Meneja wa TANROADS Mkoa wa Mbeya, Mhandisi Suleman Bishanga, amebainisha kuwa tayari wamemuagiza mkandarasi kufanya kazi usiku na mchana ili kukamilisha mradi huo kwa wakati
"Hapa tulipo ni eneo la Stendi ya Kabwe, ambalo ni sehemu ya mradi wa ujenzi wa barabara ya njia nne, Makamu wa Rais alitoa maelekezo kwamba njia zote ambazo wananchi wanatumia zifunguliwe", ameeleza Mhandisi Bishanga na kuongeza,
“Tayari maeneo 106 yamefunguliwa yanaendelea kufanyiwa kazi katika hatua mbalimbali ikiwamo kuyajazia ili yaweze kupitika, tunaendelea kutekeleza vyema maagizo ili kuondoa adha kwa wananchi na kazi inaenda pamoja”.
Akifafanua mpango wa kuzuia ajali katika eneo la Inyala, Mhandisi wa TANROADS, Frank Kamara, ameeleza kuwa maboresho hayo yataleta suluhisho la kudumu la usalama akisema, “kwanza tunaboresha eneo hili tukijenga daraja kwa lengo la kutanua sehemu hii ambayo ilikuwa changamoto kwa ajali, tumefanya uamuzi wa kutenganisha njia kati ya magari makubwa, madogo na kwa watembea kwa miguu”.
Mhandisi mwingine wa TANROADS, Gerina Mhando, amethibitisha kasi ya ujenzi wa daraja hilo na mabadiliko yanayotarajiwa kabla ya msimu wa mvua kuanza
“Tunafanya kazi usiku na mchana, ujenzi kwa sasa wa daraja hili upo asilimia 75 na matarajio ya yetu ni kabla hizi mvua tuwe tumemaliza ili kuruhusu shughuli za wananchi kuendelea”, ameeleza Mhandisi Mhando.
Kwa upande wao, wananchi wa Mbeya wamepongeza hatua hizo, ambapo mkazi wa jiji hilo, Esau Msuya, ameeleza kuwa ziara ya Makamu wa Rais imetafuta majibu ya kero zao katika barabara za Ilomba na vivuko mbalimbali.
“Mfano, hizi barabara za Ilomba na vivuko vimefanyiwa kazi, tunashukuru serikali kwa utekelezaji huu na tunatarajia kuona ujenzi ukikamilika na kuondoa changamoto hizi”, ameeleza Esau. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI:
Kituo cha Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) kimependekeza Oktoba 29 ya kila mwaka iwe Siku ya Kitaifa ya Kumbukizi ya matukio ya Oktoba 2025, ili kuwakumbuka wahanga na kuweka mikakati ya kuzuia kujirudia kwa vifo, majeruhi na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.
Katika taarifa yake iliyotolewa Oktoba 23, 2026, THRDC imesema siku hiyo inapaswa kuwa zaidi ya maombolezo kwa kuwa fursa ya kutafuta ukweli, kutenda haki, kuimarisha uwajibikaji na kujenga mshikamano wa kitaifa.
Kituo hicho kimesisitiza kuwa kumbukizi hiyo inapaswa kuongozwa na falsafa ya “Yasijirudie Tena” (Never Again), huku juhudi za maridhiano zikienda sambamba na uchunguzi wa kuaminika na uwajibikaji pale makosa yatakapothibitishwa.
Aidha, THRDC imependekeza kutathminiwa kwa mifumo ya ulinzi wa raia na uwajibikaji wa vyombo vya usalama, pamoja na kuhifadhi kumbukumbu za matukio hayo kwa ajili ya vizazi vijavyo.
Kituo hicho kimetolea mfano Rwanda, ambayo huadhimisha kumbukizi ya mauaji ya kimbari kuanzia Aprili 7, na Afrika Kusini, ambayo huadhimisha Siku ya Haki za Binadamu Machi 21, inayohusishwa na mauaji ya Sharpeville ya mwaka 1960.
THRDC imependekeza kumbukizi ya kwanza kufanyika Oktoba 29, 2026, kwa kushirikisha familia za wahanga, taasisi za umma, viongozi wa dini, asasi za kiraia na wananchi katika ngazi za kitaifa, mikoa na wilaya.
Shughuli zinazopendekezwa ni pamoja na ibada na dakika za ukimya kuwaenzi waliofariki, ushuhuda wa hiari wa familia za wahanga, kongamano kuhusu ukweli na haki, pamoja na elimu kwa vijana kuhusu haki za binadamu na amani.
Pia, kituo hicho kinapendekeza kuanzishwa kwa utaratibu wa kuhifadhi kumbukumbu za matukio hayo na hatimaye kujenga makumbusho rasmi, huku tathmini ya kila mwaka ikifanyika kuhusu utekelezaji wa hatua za kuzuia kujirudia kwa matukio kama hayo.
Kaulimbiu iliyopendekezwa ni na kituo hicho ni "Kumbukizi, Ukweli, Haki, Uwajibikaji na Uponyaji, Kamwe Yasijirudie Tena.” -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imeweka kambi rasmi katika eneo la Makoka, lililoko katika Kata ya Kisukuru, Wilaya ya Ilala, ikiwa ni mkakati maalum wa kupata suluhisho la haraka la upatikanaji wa huduma ya majisafi kwa wakazi wa maeneo hayo.
Timu ya wataalamu wa mamlaka hiyo, ikiongozwa na Meneja wa Uendelezaji Miradi ya Majisafi wa DAWASA, Mhandisi Salum Nkinda, imekuwa ikifanya tathmini ya kina kuhusu njia mbalimbali za dharura ikiwemo uchimbaji wa visima vya kuzalisha maji. Hatua hii inalenga kuimarisha upatikanaji wa huduma katika maeneo yanayokua kwa kasi kubwa kimaendeleo na kiuchumi.
Akizungumza wakati wa ziara maalum iliyofanyika leo, Jumamosi, Oktoba 24, 2026, Meneja wa DAWASA Mkoa wa Tabata, Gilbert Massawe, ameeleza kuwa wametembelea maeneo ya Makoka na Luhanga ili kujiridhisha na ufaafu wake kabla ya kazi kuanza mara moja. Amebainisha kuwa wananchi kupitia uongozi wa serikali ya mtaa wameridhia kutoa maeneo yao ili yawekewe miundombinu ya kuchimba visima hivyo vya dharura.
"Sisi kama DAWASA tumejipanga kwa namna ya dharura kuanza uchimbaji huu wa kisima mara moja na hata kesho timu yetu ya survey itapita maeneo haya kwa ajili ya kuweza kuanza uchimbaji," ameeleza Massawe, huku akiwaomba wananchi kuwa na uvumulivu wakati mamlaka hiyo ikiendelea kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa changamoto hiyo.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Mtaa wa Luhanga, Lukresia Haika Msuya, ameeleza kuwa mtaa huo umefanikiwa kupata maeneo mawili yaliyotolewa kwa hiari na wananchi kwa ajili ya ufungaji wa miundombinu ya visima. Amefafanua kuwa ongezeko kubwa la idadi ya watu na kasi ya ujenzi wa makazi huko Kisukuru ndiyo yaliyosababisha mahitaji ya maji kuongezeka na kupunguza msukumo wa maji kwa wakazi wote, hivyo msaada huo wa DAWASA utapunguza kwa kiasi kikubwa kero iliyokuwepo.
Naye mmoja wa wananchi waliojitolea eneo lake, Janeth Mfuruki, ameelezea kufurahishwa kwake na hatua hiyo akiamini kuwa ni wakati wa kupata nafuu baada ya kukabiliwa na changamoto ya uhaba wa maji kwa muda mrefu.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa, ametaka Shirika la Reli Tanzania (TRC), Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) na Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) kushirikiana kuboresha mfumo wa usafirishaji na upokeaji wa mizigo nchini, kwa lengo la kupunguza msongamano katika Jiji la Dar es Salaam na Bandari yake.
Profesa Mbarawa ametoa maelekezo hayo, Oktoba 24, 2026, wakati wa ziara ya kukagua kituo cha mizigo cha Reli ya Kisasa (SGR) kilichopo Bahi, mkoani Dodoma, ambapo amesisitiza umuhimu wa taasisi hizo kuratibu mifumo yao na kujifunza kutoka nchi nyingine, ikiwemo Misri.
Amesema TASAC, kwa nafasi yake ya udhibiti, inapaswa kushiriki kikamilifu katika kuhakikisha kunakuwepo na mfumo jumuishi unaorahisisha taratibu za usafirishaji pamoja na malipo ya huduma na tozo zinazohusiana na matumizi ya bandari na reli.
Aidha, ameelekeza hati ya usafirishaji wa mizigo inayojulikana kama Bill of Lading (BL) kuonesha wazi kituo ambacho mteja atapokelea mzigo wake, badala ya kuelekeza mizigo yote katika Bandari ya Dar es Salaam.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Mhandisi Machibya Shiwa, amesema jumla ya abiria milioni 7.6 wamesafirishwa kupitia reli ya SGR kati ya Dar es Salaam na Dodoma tangu huduma hiyo ilipoanza Juni 2024 hadi Septemba 2026.
Ameeleza pia kuwa kituo cha Bahi kimeboreshwa na kuwa eneo la kuhamishia mizigo kutoka reli ya kisasa ya SGR kwenda reli ya zamani ya MGR inayoelekea Isaka, mkoani Shinyanga, hatua ambayo imewezesha muda wa uhamishaji wa makontena kupunguzwa hadi ndani ya saa 24.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Kufuatia taarifa za wafanyabiashara wadogo kudai kuwa Serikali imewapatia eneo la Jamatini, lililokuwa stendi ya zamani jijini Dodoma, Mwenyekiti wa Wamachinga Mkoa wa Dodoma Christian Msumali, amesema wafanyabiashara hao wamevamia eneo hilo bila kibali, huku wakianza kugawana maeneo kwa ajili ya kufanyia biashara.
Akizungumza katika eneo hilo leo Oktoba 24, 2026, Msumali amesema wafanyabiashara hao wameingia katika eneo hilo kinyume na taratibu, akieleza kuwa eneo hilo halimilikiwi na Halmashauri ya Jiji la Dodoma, bali ni mali ya Shirika la Reli Tanzania (TRC). Amesema wafanyabiashara hao hawataki kuhamia eneo jingine lolote, wakisisitiza kutaka kufanya biashara katika eneo hilo
Aidha, Msumali ameitaka Serikali kutafuta suluhu ya haraka kuhusu suala hilo ili kuepusha taharuki na sintofahamu zinazoweza kujitokeza kutokana na mgogoro huo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Wananchi wa vijiji vya Kondeni na Matala, Kata ya Mwika Kusini, Wilaya ya Moshi, Mkoa wa Kilimanjaro, wameiomba Serikali kuboresha miundombinu ya barabara na kujenga mitaro ya kupitisha maji ya mvua ili kuzuia maji kuingia katika makazi yao na kuhatarisha usalama wa wananchi.
Wakiwasilisha changamoto hiyo Oktoba 23, 2026, mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Godfrey Mnzava, aliyeambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama pamoja na wataalamu wa TARURA na TANROADS, wananchi kupitia Diwani wa Kata ya Mwika Kusini, John Tarimo, wamesema barabara inayounganisha vijiji hivyo kuelekea Kilacha imekuwa katika hali mbaya, hasa wakati wa masika.
Tarimo amesema kukosekana kwa mitaro ya kupitisha maji kunasababisha maji ya mvua kutiririka bila kuelekezwa maeneo salama, hali inayochangia uharibifu wa barabara hiyo na kuathiri usafiri na usafirishaji.
Akijibu changamoto hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Godfrey Mnzava, amemtaka Meneja wa TANROADS Mkoa wa Kilimanjaro kuhakikisha hatua za kutatua tatizo hilo zinachukuliwa ndani ya wiki mbili, akisisitiza kuwa usalama wa wananchi unapaswa kupewa kipaumbele.
“Tengenezeni huo mtaro na maji yakija nisione mwananchi anapata madhara hata mmoja. Atakayepata madhara kule chini mimi sitahusika na Kamati yangu ya Usalama; utabaki wewe ukinieleza imekuwaje wananchi wamepata madhara,” amesisitiza Mnzava.
Kwa upande wake, Meneja wa TANROADS Mkoa wa Kilimanjaro, Motta Kyando, amesema watashughulikia changamoto hiyo kwa kufungua mitaro ya kupitisha maji kwa kushirikiana na wananchi, hatua inayolenga kupunguza athari za mvua na kulinda miundombinu ya barabara pamoja na makazi ya wananchi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dkt. Rugemeleza Nshala amesema Mwenyekiti wa chama hicho Tundu Lissu amemtaka atoe taarifa kuwa kuanzia jumatatu ya Oktoba 26, 2026 hatokula wala kunywa dawa kutokana na Gereza la alilopo(Ukonga) kukiuka amri ya Mahakama Kuu ya Tanzania ya kuwepo kwa mazingira ya usiri wakati mfungwa au mahabusu wanazungumza.
"Mwenyekiti amesema kuanzia Jumatatu ya tarehe 26/10/2026 anaanza mgomo wa kutokula chakula kwa sababu amenyimwa haki yake ya kukutana na Mawakili kwa sababu anasimamia maamuzi ya Mahakama Kuu ya Tanzania huo ambao ulitolewa wiki iliyopita kuwa ana haki ya kukutana na mawakili."
Dkt. Nshala amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 24, 2026 jijini Dar es Salaam na kueleza kuwa Lissu amesema hatojali kuhusu afya yake mpaka amri halali za Mahakama zitakapotekelezwa
Jambo TV imefanya jitihada za kulitafuta Jeshi la Magereza ambapo Msemaji wake SACP Elizabeth Mbezi amejibu kuwa taarifa hizo zinafuatiliwa.
"Hiyo mimi sijaiskia nipo Dodoma ngoja nifuatilie" amesema SACP Mbezi kwa ufupi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Msemaji wa Jeshi la Magereza nchini SACP Elizabeth Mbezi amesema anafuatilia kupata majibu sahihi juu ya taarifa kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo @ChademaTZ2 Tundu Lissu kuwa atagoma kula kuanzia Jumatatu kutokana na kutotendewa kwa haki katika Gereza la Ukonga anaposhikiliwa.
SACP Mbezi akizungumza na Jambo TV leo Oktoba 24, 2026 amejibu kwa ufupi kuwa taarifa hizo bado hana hivyo anazifuatilia.
"Hiyo mimi sijaiskia ngoja nifuatilie kwa sababu nipo dodoma na yeye yupo Dar es Salaam kwa hiyo ngoja nifuatilie" amesema SACP Mbezi
Taarifa za mgomo wa kula wa Lissu zimetolewa na Mwanasheria Mkuu wa chama chake Dkt. Rugemeleza Nshala akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 24, 2026 ambapo amesema alielezwa nae moja kwa moja akisema sababu kuu ya mgomo huo ni viongozi wa gereza na maafisa kutaka kuwa sehemu anapozungumza na washauri wake wa kisheria jambo ambalo mahakama imeshatoa maagizo sio sahihi. -
Jambo TV
@Jambotv_
"Mwenyekiti(Tundu Lissu) amesema kuanzia Jumatatu ya tarehe 26/10/2026 anaanza mgomo wa kutokula chakula kwa sababu amenyimwa haki yake ya kukutana na Mawakili kwa sababu anasimamia maamuzi ya Mahakama Kuu ya Tanzania huo ambao ulitolewa wiki iliyopita kuwa ana haki ya kukutana na mawakili."
Hayo ameyaeleza Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dkt. Rugemeleza Nshala akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 24, 2026 jijini Dar es Salaam.
Dkt. Nshala amesema uamuzi wa Lissu umetokana na mawakili wake ambao ni Nashon Nkungu na Paul Kisabo kwenda gerezani kwa lengo la kumuona Lissu lakini uongozi wa Gereza la Ukonga uliwaambia kuwa utaratibu utatumika kama ule uliokataliwa na Mahakama kuwa Naibu Mkuu wa Gereza, Mwanasheria na Maafisa wengine watakuwepo katika chumba wanachozungumza na Lissu.
Dkt. Nshala amesema Lissu alikataa kuzungumza na mawakili wake akisema utaratibu ulioagizwa na Mahakama kuwa maafisa wakae umbali wanaoweza kuona na sio kusikia umekiukwa.
Baada ya hapo Dkt. Nshala anasema alienda gerezani mwenyewe ambapo aliambiwa kuwa hawezi kuonana na Lissu kwa sababu amesema hayupo tayari kuzungumza ndipo alipokataa ujumbe huo na kutaka kuonana na Lissu lakini hata alipofanikiwa kuonana nae msimamo ulikuwa ule ule kuwa hawezi kuzungumza mpaka amri ya Mahakama ifuatwe.
Jambo TV inaendelea na jitihada za kulitafuta Jeshi la Magereza ili kupata ufafanuzi wa tuhuma hizi. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwenyekiti wa UVCCM Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Mtwara, Elias Malekela, amekosoa vikali kauli ya Rais wa Shirikisho la Serikali za Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu Tanzania (TAHILISO), Geofrey Kiliba kuwa alipopata nafasi ya kukutana na Rais Samia Suluhu Hassan alienda kumuomba kuwatukana wapinzani badala ya kuwasilisha changamoto za wanavyuo.
Akizungumza na waandishi wa habari Oktoba 23, 2026, Malekela amemtaka kiongozi huyo kuacha kuwasilisha mawazo ambayo sio wanavyuo wote kwani wana matatizo lukuki ambayo inaonekana Rais wao hayafahamu hivyo ni vyema akawatembelea na kuyafahamu ili akikutana na viongozi wakuu aweze kuwaeleza.
Katika hatua nyingine amesema kama Kiliba anakiheshimu Chama cha Mapinduzi anafaa kuendana na falsafa za Rais Samia ambazo zinahimiza maridhiano lakini pia kufanya siasa kwa namna ambayo atajitofautisha na wapinzani huku wakimtaka kufuta machapisho yake yanayohusu kauli hizo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo @ChademaTZ2 Bara John Heche @HecheJohn amesema ataendelea kukagua na kuonyesha changamoto zilizopo katika miradi mbalimbali iliyotekelezwa na ambayo bado haijatekelezwa na serikali nchini.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram leo Oktoba 23, 2026 Heche amechapisha video akieleza ubovu wa barabara ya Katesh-Singida ambayo imekuwa na mashimo mengi yanayotokana na lami kumeguka jambo ambalo linaathiri muda wa usafiri na usafirishaji lakini kuharibu vyombo hivyo.
Amehoji serikali kutenga zaidi ya shilingi bilioni 700(zimetengwa Shilingi bilioni 730) kwa ajili ya kujiandaa na kuikabili El Niño, huku hatma ya barabara hiyo ikiwa bado na maswali pamoja na kuwa na umuhimu mkubwa katika uchumi wa Taifa letu kupitia usafirishaji wa bidhaa kuelekea nje ya nchi.
Oktoba 14, 2026 Msemaji Mkuu wa Serikali na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Gerson Msigwa alichapisha video ya Msikilize Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mhandisi Mohammed Besta akieleza kuwa ukarabati wa barabara hiyo unaendelea huku akionyesha vifaa vikiwa vinaendelea na uwekaji wa lami katika barabara hiyo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Njombe, Sigrada Mligo, ametoa wito kwa wananchi wa Kijiji cha Segala, Wilaya ya Chamwino, mkoani Dodoma kumchagua mgombea wa Ubunge wa CHAUMMA, Mathias Nyakapala akieleza kuwa ni wakati wa kuleta mabadiliko kupitia uongozi utakaowapa wananchi fursa ya kuboresha maisha yao.
Akizungumza Oktoba 22, 2026, wakati wa uzinduzi wa kampeni za CHAUMMA katika Kijiji cha Segala, Mligo amedai kuwa CCM imekuwa ikiwapa wananchi baiskeli zinazodaiwa kuathiri nguvu imekuwa ikitumia fursa ya hali duni za maisha ya wananchi kwa kuwapa vitu kama baiskeli, kofia na khanga wakati wa kampeni ili kuwarubuni wawape kura.
Anasema kuwa pamoja na CCM kutoa mara kadhaa viti hivyo lakini kwa sasa waliopewa baiskeli wamekuwa wakiona aibu kutembea nazo
Kwa upande wake, Mgombea wa ubunge wa CHAUMMA katika Jimbo la Chamwino, Mathias Nyakapala, amesema kuwa akichaguliwa, kipaumbele chake cha kwanza kitakuwa kupima ardhi na kuwawezesha wananchi kupata hati miliki, pamoja na kuhamasisha uanzishwaji wa viwanda na kuendeleza ufugaji wa ng’ombe wa maziwa ili kuongeza fursa za kiuchumi kwa wakazi wa jimbo hilo. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, John Heche, ameikosoa Serikali ya Tanzania kwa kile alichodai kuwa ni kushindwa kutengeneza ajira za kueleweka kwa vijana na kuporomoka kwa sekta ya viwanda, huku akiwataka madereva wa bodaboda na bajaji kuacha kutumiwa na wanasiasa wakati wa kampeni na badala yake wadai mabadiliko ya kiuchumi.
Akizungumza Oktoba 23, 2026 katika mkutano wa hadhara uliofanyika wilayani Nzega mkoani Tabora, Heche ameeleza kuwa ni jambo la kusikitisha kuona madereva bodaboda wakipewa jina la "maafisa usafirishaji", kutumiwa wakati wa kampeni za uchaguzi, lakini baada ya kampeni kuisha wanaachiwa mateso ya umasikini.
"Halafu nyie mnaambiwa muendeshe bodaboda na mnaongezewa ujinga mnaitwa maafisa usafirishaji, mnavimba vichwa, wanawatumia wakati wa kampeni kampeni ikiisha mnasema tusemeee bodaboda”, ameeleza Heche.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
“Bwana mmoja ambaye sijui ndiye ‘Mkurugenzi wa hali ya hewa’ anaulizwa El Niño itakuja lini anasema sasa hivi tuko katikati ya El Niño…au ni mimi nilimsikia vibaya? Mlimsikia au hamkumsikia? Kwamba unajua kwenye nchi nyingine El Niño ni jua…wewe! Sisi tunakuuliza India au tunakuuliza sisi?”, Heche.
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, John Heche akizungumza Oktoba 23, 2026, alipohutubia mkutano wa hadhara wilayani Nzega mkoani Tabora ambapo amehoji matumizi ya matumizi ya kiasi cha Shilingi bilioni 730 alizoeleza kuwa zimetengwa kwa ajili ya kukabiliana na athari za mvua za El Niño.
Hata hivyo mwanzoni mwa mwezi jana, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Watu Wenye Ulemavu), Prof. Palamagamba Kabudi, alisema shilingi bilioni 730 ni yaliyotajwa katika mpango wa kujiandaa na kukabiliana na El Niño, na hayahusu maandalizi pekee, bali yanajumuisha gharama za hatua zitakazochukuliwa endapo majanga yatatokea.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, John Heche, amedai kuwa chama chake hakiombi upendeleo wowote kutoka kwa serikali wala vyombo vya dola, bali kinataka haki sawa katika uwanja wa kisiasa na uchaguzi nchini.
Heche ameyasema hayo akizungumza Oktoba 23, 2026 katika mkutano wa hadhara uliofanyika wilayani Nzega mkoani Tabora ambapo pia amehoji wanaosema kuwa anatumia lugha ngumu katika uwasilishaji wa hoja zake majukwaani wanataka atumie lugha ya namna gani kwa mambo ambayo amedai CHADEMA na Watanzania hawaridhishwi nayo.
“Mnaniambia natumia lugha kali. Unataka nitumie lugha gani? …Wwanataka tutumie lugha gani? Mimi nimesema nitasema ukweli na sitaogopa mtu, hata uwe na mapembe yanayotoboa dunia hii”, ameeleza Heche.
Aidha, Heche amekosoa kauli za Serikali kuhusu mafanikio ya ujenzi wa Reli ya Mwendokasi (SGR), akilinganisha kasi hiyo na ujenzi wa reli ya Mjerumani aliyebuni na kujenga kilomita 1,200 za reli kutoka Dar es Salaam hadi Tabora kwa miaka tisa tu (1905- 1914) katikati ya mapori na bila mitambo ya kisasa. Ameeleza kuwa ni jambo la kushangaza kuona miaka 65 baada ya uhuru Serikali bado inajisifu kwa ujenzi wa reli iliyofika maeneo machache.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Wafugaji kutoka vijiji vya Ololosokwan na Kiritalo, Wilaya ya Ngorongoro, Mkoa wa Arusha, wamelalamikia uhaba wa maeneo ya malisho na maji kwa mifugo yao baada ya eneo kubwa walilokuwa wakilitegemea kutengwa na kuwa Pori la Akiba la Pololeti mwaka 2022.
Wakizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni, wafugaji hao walisema hali ya ukame imezidisha changamoto ya upatikanaji wa malisho na maji, hali wanayodai kusababisha vifo vya mifugo na kufanya maisha yao kuwa magumu wakisema ufugaji ni shughuli yao kuu ya kujipatia kipato na kukidhi mahitaji ya familia.
Wameiomba serikali kutafuta suluhisho la kudumu kwa kuwapatia maeneo ya kutosha ya malisho na kuhakikisha upatikanaji wa maji kwa mifugo, wakieleza kuwa hali hiyo ikiendelea inaweza kuhatarisha zaidi maisha yao na uchumi wa kaya zao.
Akizungumza kwa njia ya simu Oktoba 22, 2026, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro, Murtallah Sadiki Mbillu, alisema Serikali ilichukua sehemu ya eneo hilo na kuwaachia wafugaji maeneo mengine kwa ajili ya malisho.
Alieleza kuwa hatua hiyo ililenga kulinda wanyamapori na makazi yao dhidi ya usumbufu wa shughuli za binadamu na mifugo, pamoja na kuhifadhi vyanzo vya maji.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, John Heche amewataka vijana na wananchi kwa ujumla kujitokeza na kuongoza mapambano ya kudai mabadiliko pamoja na Katiba Mpya, akisisitiza kuwa kundi hilo ndilo lenye kila sababu ya kupigania mfumo bora wa nchi.
Akizungumza Oktoba 23, 2026 katika mkutano wa hadhara uliofanyika wilayani Nzega mkoani Tabora, Heche ameeleza kuwa mabadiliko mengi ya kihistoria duniani yamekuwa yakisukumwa na vijana na watu wa tabaka la chini kwasababu wao ndio wanaokumbana moja kwa moja na athari za kile alichokiita uongozi mbovu na huduma duni katika jamii.
“Ndugu zangu vijana mabadiliko duniani hapa yameletwa na vijana na watu masikini kwa sababu nyie hamna cha kupoteza…kijana na mtu maskini. Kijana mabadiliko yanakuhusu kwasababu utatoka kwenye hali ya umasikini utaenda kwenye hali bora zaidi”, ameeleza Heche na kuongeza,
“Wanaoogopa mabadiliko kama alivyosema Mwalimu Nyerere ni wanyonyaji. Sisi tuna kila kitu cha kupigania ili tupate mabadiliko”.
Heche amesisitiza kuwa mapambano ya kudai Katiba Mpya ni takwa la msingi la mfumo na wananchi wote ili kuinusuru nchi iliyobarikiwa na rasilimali nyingi kama dhahabu, bandari na madini lakini wananchi wake wakiendelea kuteseka na tozo pamoja na umasikini.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Baadhi ya madereva wa bodaboda wanaofanya shughuli zao katika Manispaa ya Mtwara, mkoani Mtwara, wamelalamikia utaratibu wa ukamataji unaofanywa na Jeshi la Polisi, Kikosi cha Usalama Barabarani, wakidai kutoridhishwa na namna wanavyokamatwa.
Malalamiko hayo yametolewa leo, Oktoba 23, 2026, baada ya askari wa usalama barabarani kumkamata dereva wa bodaboda aliyefanya kosa la kupakia abiria zaidi ya mmoja, hali iliyosababisha abiria mmoja kudondoka baada ya dereva huyo kukamatwa.
Saidi Yusufu amesema changamoto kubwa wanayokutana nayo ni kile alichodai kuwa ni ukamataji holela unaofanywa na askari wa usalama barabarani, hali inayowakatisha tamaa madereva hao. Amewataka askari kufuata sheria katika utekelezaji wa ukamataji.
Naye Amisi Ibrahim amesema wamekuwa wakitozwa faini kubwa zinazofikia hadi shilingi 70,000, akidai kuwa ni kinyume cha sheria, huku akieleza kuwa kwa mujibu wa kanuni, kosa moja linapaswa kutozwa faini ya shilingi 10,000.
Akijibu hoja hizo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, SACP Issa Suleiman, amesema baadhi ya madereva wa bodaboda wamekuwa hawafuati sheria za barabarani, hali inayosababisha wakamatwe. Amewataka kutii sheria bila shuruti ili kuepuka migongano baina yao.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Wazalishaji wa vyakula na vinywaji nchini wametakiwa kuzingatia viwango vilivyoidhinishwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kwa kutotumia ladha au viambato vingine tofauti na vilivyokubaliwa katika bidhaa zao, ili kulinda ubora wa bidhaa na afya za watumiaji.
Wito huo umetolewa Oktoba 23, 2026 na Mkurugenzi wa TBS, Dkt. Ashura Katunzi, wakati wa uzinduzi wa ofisi mpya za shirika hilo Kanda ya Magharibi, zinazohudumia Mikoa ya Kagera, Geita, Shinyanga na Kigoma.
Dkt. Katunzi amesema kwa kuzingatia viwango hivyo kutasaidia kulinda afya za watumiaji na kuhakikisha wanapata bidhaa zenye ubora unaotakiwa.
Kwa upande wake, Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita, Mohamed Gombati, amesisitiza umuhimu wa kuzingatia usalama wa bidhaa pamoja na utunzaji wa mazingira, hususan katika uzalishaji unaohusisha matumizi ya kemikali.
Nao baadhi ya wafanyabiashara waliopatiwa vyeti vya TBS wameeleza kuwa uthibitishaji wa bidhaa zao unawapa fursa ya kuongeza ushindani katika masoko ya ndani na nje ya nchi.
Uzinduzi wa ofisi hizo unatarajiwa kuimarisha upatikanaji wa huduma za viwango na udhibiti wa ubora wa bidhaa katika Kanda ya Magharibi, huku ukirahisisha huduma kwa wazalishaji na wafanyabiashara.
TBS imewahimiza wazalishaji na wafanyabiashara kutumia fursa hiyo kuboresha ubora wa bidhaa zao na kuongeza ushindani katika masoko ya ndani na nje ya nchi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Jengo la ghorofa 12 lililokuwa likiendelea kujengwa katika Jiji la Nairobi, nchini Kenya, limeporomoka siku ya Ijumaa, huku hofu ikitanda kuwa huenda kukiwa na watu waliofukiwa chini ya vifusi.
Taarifa kutoka ofisi ya Gavana wa Kaunti ya Nairobi, Johnson Sakaja, imethibitisha kuwepo kwa taarifa za watu wanaosadikiwa kukwama kwenye kifusi hicho, ikiongezwa kuwa sakafu ya chini ya jengo hilo lililoko katika mtaa wa Eastleigh ilikuwa inatumika.
Hadi sasa, bado haijafahamika mara moja nini kilichosababisha kuporomoka kwa jengo hilo lililopo kando ya Barabara ya Yusuf Haji, karibu na Supermarket ya Day to Day.
Vikosi vya kukabiliana na majanga vya Msalaba Mwekundu nchini Kenya pamoja na timu za dharura za Kaunti ya Nairobi ziliwasili haraka kwenye eneo la tukio na kuanza shughuli za uokoaji.
"Tunasihi umma kuweka eneo hilo wazi ili kuruhusu timu za dharura kufanya kazi kwa usalama," imeeleza taarifa ya Msalaba Mwekundu.
Ili kurahisisha kazi ya uokoaji, mashine nzito zimesambazwa eneo hilo ili kusaidia kuondoa vifusi na kupata njia ya kuwafikia wahanga. Wakati huo huo, Kamanda wa Polisi wa Nairobi, Issa Mohamed, ameeleza kuwa polisi walilazimika kurusha gesi ya machozi ili kuwatawanya watazamaji waliokuwa wakijazana eneo hilo na kuzuia wizi au uporaji wa maduka ya jirani, hususan baada ya baadhi ya vijana kuripotiwa kuanza kulenga vyuma chakavu kutoka kwenye vifusi hivyo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI PICHA:
Waziri wa Katiba na Sheria, Abdallah Ulega akikagua gwaride lililoandaliwa rasmi kwa maadhimisho ya Siku ya Umoja wa Mataifa iliyoadhimishwa katika Ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Viongozi wa dini nchini, wakiwemo Sheikh Khamis Said Mataka, Padri Daktari Joseph Matumaini, Modest Pesha, pamoja na Kanali Samuel Mkami, wamesisitiza kuwa viongozi wa kiroho wana wajibu wa kuikosoa na kuinasihi serikali kwa hekima na busara pale inapokosea, huku wakihimiza ujasiri wa kusema ukweli ili kulinda amani na haki nchini.
Wazungumzaji hao wamebainisha hayo wakati wa Kongamano la Kitaifa la Dini Mbalimbali Kuhusu Amani, Haki na Uwajibikaji Nchini Tanzania lililofanyika mkoani Dar es Salaam hivi karibuni ambapo pamoja na mambo mengine viongozi wa dini walihimizwa kutenda haki, kuwa wapatanishi, kupaza sauti dhidi ya dhuluma, kuelimisha jamii na kuimarisha umoja na uzalendo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mbunge wa Jimbo la Segerea, Mkoani Dar es Salaam, Agnesta Kaiza wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), amesema kuwa upinzani haimaanishi kupinga kila jambo, huku akisema Deogratius Ndejembi anazo sifa za kuwa Makamu wa Rais ndiyi ndiyo maana aliungwa mkono na wote ikiwemo wapinzani.
Agnesta ameyasema hayo Oktoba 22, 2026, Mkoani Dodoma, wakati wa uzinduzi wa kampeni za CHAUMMA katika Kijiji cha Segala, ambapo alikuwa akimnadi mgombea wa Chama hicho katika uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo la Chamwino, Mathias Nyakapala.
“Ukiwa upinzani haimaanishi kwamba unapinga kila kitu. Mimi mwenyewe, pamoja na kuwa Mbunge wa Upinzani, nakubaliana kwamba Deogratius Ndejembi ana sifa zote za kuwa Makamu wa Rais,” amesema Agnesta.
Aidha, amesema kuwa licha ya mambo mazuri yaliyofanywa na Ndejembi katika Jimbo la Chamwino, wakazi wa jimbo hilo wanapaswa kumpigia kura mgombea wa CHAUMMA, Mathias Nyakapala, akisisitiza kuwa nafasi ya ubunge si ya kurithishana, bali wananchi wana haki ya kuchagua kiongozi wanayemtaka.
Uchaguzi huo mdogo unafanyika kufuatia aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo, Deogratius Ndejembi, kuteuliwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo kwa mujibu wa ratiba iliyowekwa wazi na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), uchaguzi mdogo wa Ubunge katika Jimbo la Chamwino unatarajiwa kufanyika Novemba 4, 2026, sambamba na uchaguzi wa madiwani katika kata 11 Tanzania Bara.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limesema watuhumiwa wawili waliokuwa wakitafutwa kwa tuhuma za mauaji na uporaji wa pikipiki wamefariki dunia hospitalini baada ya kujeruhiwa katika mapambano na askari eneo la Kijenge, jijini Arusha.
Akizungumza Oktoba 22, 2026, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, SACP Justine Masejo, amesema tukio hilo lilitokea Oktoba 21, 2026, saa 3:30 usiku, akiwataja watuhumiwa hao kuwa ni Yusuph Hamis maarufu Yuzo na Dickson Livingstone maarufu Ndesaa.
Amesema watuhumiwa hao walikutwa na bastola, panga na pikipiki mpya isiyokuwa na namba za usajili, huku Yuzo akihusishwa na tuhuma za mauaji ya madereva bodaboda Erasto Losujaki na Adiel Thomas Spitari, waliouawa katika matukio tofauti mwaka 2026 na kuporwa pikipiki zao.
Kamanda Masejo amesema watuhumiwa hao waliwahi kufikishwa mahakamani kwa makosa mbalimbali ya uhalifu, huku Jeshi la Polisi likiendelea na uchunguzi na kuwatafuta watu wengine wanaodaiwa kushirikiana nao pamoja na kufuatilia pikipiki zilizoporwa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkulima Ezekiel Silvester Kinombo, mkazi wa Kijiji cha Mbesa, Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma, amemuomba Rais Samia Suluhu Hassan kuingilia kati malalamiko yake ya uharibifu wa mazao unaodaiwa kusababishwa na ng’ombe wa wafugaji, uliomsababishia hasara ya Sh milioni 3.168.
Kinombo amesema ng’ombe hao waliingia katika shamba lake lenye ukubwa wa ekari tano na nusu na kula mbaazi, hali aliyosema imeathiri kipato chake na uwezo wa kugharamia elimu ya watoto wake.
Amesema baada ya tukio hilo, alitoa taarifa kwa uongozi wa kijiji, akafuatilia suala hilo kwa validator na baadaye kufungua kesi polisi Agosti 12, 2026. Hata hivyo, kwa mujibu wake, hadi sasa hajapata suluhisho la malalamiko yake.
Akieleza changamoto alizokumbana nazo, Kinombo amedai kuwa mwanawe alipowapiga picha ng’ombe hao wakiwa shambani, alikaribia kushambuliwa na wafugaji waliokuwapo eneo hilo.
Amesema hasara hiyo imeathiri uwezo wake wa kulipia ada za mwanawe anayesoma chuoni pamoja na watoto wengine wanaosoma katika shule za binafsi.
Kutokana na hali hiyo, ameiomba Serikali, kupitia Rais Samia, kuingilia kati ili malalamiko yake yashughulikiwe na hatua stahiki zichukuliwe kwa mujibu wa sheria.
Kinombo amesema ni muhimu kuwepo kwa hatua madhubuti za kulinda mazao ya wakulima na kutatua migogoro kati ya wakulima na wafugaji kwa wakati, ili wananchi waendelee na shughuli zao za uzalishaji bila kuathiriwa na uharibifu wa mazao.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Profesa Riziki Shemdoe, amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Jumanne Sagini, kuunda timu itakayozunguka maeneo mbalimbali ya Jiji la Mbeya kwa lengo la kubaini maeneo yanayofaa kwa shughuli za bajaji na wafanyabiashara wadogo maarufu kama machinga.
Profesa Shemdoe ametoa maelekezo hayo leo Oktoba 22, 2026 alipokuwa akizungumza na wafanyabiashara wadogo, madereva na wamiliki wa bajaji katika Soko la Machinga la Old Airport, jijini Mbeya, baada ya kufanya ukaguzi wa soko hilo.
Hatua hiyo inafuatia sintofahamu iliyojitokeza siku za hivi karibuni kuhusu maeneo ya kufanyia shughuli za biashara kwa machinga na maeneo ya bajaji kufanya shughuli za usafirishaji jijini humo.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Mbunge wa Mbeya Mjini, Patrick Mwalunenge, amesema suala hilo lilikuwa limeleta changamoto, lakini kwa sasa limetatuliwa.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Jumanne Sagini, amesema amepokea maelekezo yaliyotolewa na Waziri wa TAMISEMI na atayafanyia kazi.
Kwa upande wake, Damas Mwakalinga, mwakilishi wa madereva na wamiliki wa bajaji Mkoa wa Mbeya, amesema wako tayari kushirikiana na Serikali katika utekelezaji wa maelekezo hayo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Viongozi wa dini mbalimbali nchini wamejadili kwa kina uhusiano uliopo kati ya amani na haki katika kuiletea nchi ustawi wa kweli, huku wakisisitiza kuwa viongozi wa dini wana jukumu kubwa la kujenga imani na uwajibikaji kuanzia kwenye nyumba za ibada kabla ya kuliponya taifa.
Hayo yamejiri wakati wa Kongamano la Kitaifa la Dini Mbalimbali Kuhusu Amani, Haki na Uwajibikaji Nchini Tanzania lililofanyika Oktoba 21, 2026 mkoani Dar es Salaam.
Akiwasilisha mtazamo wake kuhusu ushirikiano wa amani na haki, Sheikh Khamis Said Mataka amebainisha kuwa haki ni jambo mtambuka linalohitaji mazungumzo na majadiliano ya utulivu badala ya vita au mapambano.
Kwa upande wake, Padri Daktari Joseph Matumaini ameeleza kuwa ili haki iweze kushamiri, ni lazima kwanza kuwe na mazingira ya amani, huku akihoji kiwango cha imani walichonacho viongozi wa dini kwa sasa katika kuongoza jamii.
Naye, Askofu Dkt. George Mark Fihavango ameeleza kuwa katika muktadha wa haki za binadamu na siasa, haki inaweza kutangulia amani, lakini katika amani ya kweli ya kimaandiko, amani hubeba haki ndani yake.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Serikali imesitisha usajili wa bajaji mpya katika Jiji la Mbeya, huku bajaji zaidi ya 6,000 zilizopo zikiruhusiwa kuendelea kutumia barabara kuu kwa siku 14 wakati tathmini ya changamoto za miundombinu ikiendelea.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Profesa Riziki Shemdoe, amesema ameunda timu maalumu yenye wawakilishi wa wadau mbalimbali wa usafiri na usafirishaji ili kuchunguza hali ya barabara na kubaini maeneo yanayohitaji ukarabati.
Amesema timu hiyo itakuwa na siku 14 za kutathmini miundombinu na kupendekeza maboresho yatakayowezesha barabara kuwa rafiki kwa bajaji zinazofanya shughuli za usafiri jijini humo.
Kutokana na hatua hiyo, Profesa Shemdoe amemuagiza Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya, Justice Kijazi, kusitisha mara moja usajili wa bajaji mpya, akieleza kuwa idadi iliyopo imezidi 6,000 na miundombinu ya sasa imezidiwa.
Ameeleza kuwa uamuzi huo umefikiwa baada ya makubaliano kati ya Serikali ya Mkoa wa Mbeya na viongozi wa vyama vya siasa, ikiwemo Chama cha Mapinduzi (CCM), kwa lengo la kutafuta suluhisho la changamoto zinazowakabili waendesha bajaji.
Katika kipindi cha siku 14, timu hiyo inatarajiwa kubaini barabara zinazohitaji ukarabati mkubwa na kutoa mapendekezo ya kuboresha miundombinu, huku bajaji zikiendelea na shughuli zake katika barabara kuu.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Serikali ya Tanzania imeweka ahadi kwamba kuanzia sasa hakuna raia yeyote atakayekosa huduma za afya au kupoteza maisha kwa sababu tu ya ukosefu wa fedha au umaskini, kufuatia uzinduzi wa kitaifa wa Mfumo wa Bima ya Afya kwa Wote.
Akizungumza leo Oktoba 22, 2026 katika uzinduzi huo wa kitaifa uliofanyika mkoani Mtwara, Waziri wa Afya, Mohamed Mchengerwa, ameeleza kuwa uzinduzi huo ni tukio la kihistoria linaloleta usawa kwa Watanzania wote na kwamba unashuhudiwa kwa wakati mmoja katika mikoa yote nchini
Waziri Mchengerwa ameeleza kuwa uchaguzi wa Mtwara kuwa makao makuu ya uzinduzi wa kitaifa unalenga kufuta dhana ya zamani iliyokuwa ikiuchukulia mkoa huo kama eneo la pembezoni, na badala yake kuonesha kuwa mfumo huo mpya unamweka kila mwananchi katikati ya huduma za afya.
"Na si bahati mbaya kwamba uzinduzi wa kitaifa umefanyika hapa Mtwara. Kwa miaka mingi Mtwara iliitwa mkoa van pembezoni. Lakini leo tunasema katika bima ya afya kwa wote hakuna pembezoni. Kila Mtanzania yupo katikati", ameeleza Mchengerwa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Tunataka tarehe 6, Novemba 2026 wafike kwa wingi sana katika Mahakama, na tutaomba viongozi wa Mahakama waweze kurusha matangazo ya kusomwa kwa hukumu ya Tundu Lissu irushwe wazi, ni kesi ya Watanzania, waisikie wajue kwa sababu ni kiongozi wa Chama kikuu cha siasa katika nchi hii. Watanzania wana haki ya kujua, utake usitake ukweli ndiyo huo, CHADEMA ni Chama kikuu cha siasa katika nchi hii" amesema Dkt. Nshala
Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Lugemeleza Nshala, amesema hayo leo Oktoba 22, 2026 kupitia Mkutano alioufanya na vyombo vya habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Lugemeleza Nshala, amesema maombi ya Said Issa Mohammed ya kutaka Chama hicho kiwekewe zuio la kufanya shughuli za siasa yametupiliwa mbali kutokana na maombi yake kutothibitisha vigezo vinavyohitajika ili kuwekwa kwa amri ya zuio hilo.
Dkt. Nshala ameeleza hayo leo Oktoba 22, 2026 kupitia Mkutano alioufanya na vyombo vya habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam. Amesema kwamba Mahakama kuu imekataa vigezo hivyo na kwamba iliona Said Issa na wenzake walithibitisha kigenzo kimoja pekee lakini vingine viwili walishindwa kuvithibitisha.
"Mahakama kuu imekataa katika vile vigezo vitatu, vya kutoa amri ya zuio imeona wamethibitisha kimoja lakini vile viwili wameshindwa kuvithibitisha, na kwa maana hiyo jaji akaamua kwamba atupilie mbali maombi yao". Amesema Dkt. Nshala.
Hayo yanajiri ikiwa leo Oktoba 22, 2026 katika Mahakama kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam Maombi ya kutaka Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kiwekewe zuio la kufanya shughuli za kisiasa nchini yameshindikana ambapo Chama hicho kitaendele na Shughuli zake kama kawaida.
Katika uamuzi uliotolewa na Jaji Awamu Mbagwa, amesema Mahakama haioni sababu za msingi za kuzuia shughuli za kisiasa kwa Chama hicho.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Viongozi wa dini mbalimbali nchini Tanzania wametakiwa kuwa mstari wa mbele katika kuhubiri kuhusu haki, amani na uwajibikaji katika majukwaa yao ya kiroho badala ya kuiachia serikali pekee jukumu hilo.
Wito huo umetolewa katika Kongamano la Kitaifa la Dini Mbalimbali Kuhusu Amani, Haki na Uwajibikaji Nchini Tanzania lililofanyika Oktoba 21, 2026 mkoani Dar es Salaam.
Aidha, katika kongamano hilo viongozi wa dini wamehimizwa kutenda haki, kuwa wapatanishi, kupaza sauti dhidi ya dhuluma, kuelimisha jamii na kuimarisha umoja na uzalendo. Majadiliano yamesisitiza umuhimu wa kukubali makosa, kuwajibika, kutubu na kuendeleza mazungumzo ya kitaifa, maridhiano, uponyaji wa kijamii na kuzuia migogoro.
Wakizungumza katika kongamano hilo, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Mchungaji Dkt. Moses Matonya, Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Sheikh Khamis Said Mataka, na Mchungaji Dkt. Basilisa Ndonde wa Kanisa la Restoration Bible Church (RBC), wamesisitiza viongozi wa dini wanapaswa kutenda haki, kuwa wapatanishi, kupaza sauti dhidi ya dhuluma, kuelimisha jamii na kuimarisha umoja na uzalendo.
Wameeleza kuwa ukosefu wa fursa za kuzungumza pamoja unatoa mwanya wa kutuhumiana na kudhaniana vibaya, hivyo makongamano ya pamoja yana mchango mkubwa katika kuimarisha uhusiano na kuelewana.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Tanzania imepata sifa kubwa na kung'ara barani Afrika kutokana na utashi thabiti wa kisiasa na uwekezaji mkubwa uliofanywa katika sekta ya maji chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Serikali imetajwa kutoa kipaumbele cha kipekee kwa kutenga fedha za kutekeleza miradi na kusimamia kwa ufanisi upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi, huku ikipiga hatua za haraka katika maeneo yaliyokuwa yakikabiliwa na changamoto kubwa ya maji hapo awali.
Pongezi hizo zimetolewa na viongozi mbalimbali wa Afrika katika Mkutano wa Maraisi, Mawaziri wa Mambo ya Nje, na Mawaziri wa Maji unaofanyika jijini Luanda, nchini Angola, unaokwenda sambamba na kaulimbiu isemayayo “Kuimarisha Utawala wa Rasilimali Maji Inayovuka Mipaka barani Afrika kama Nyenzo ya Kuzuia na Kutatua Migogoro.”
Ujumbe wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unaoshiriki mkutano Mkutano huu tarehe 22 Oktoba 2026 unaongozwa na Balozi Dkt. Mahmoud Thabit Kombo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akimwakilisha Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na unamjumuisha Jumaa Hamidu Aweso, Waziri wa Maji na wataalam wengine.
Majadiliano yamehusisha diplomasia ya maji na usimamizi wa rasilimali za maji zinazovuka mipaka; ushiriki wa jamii, wanawake na vijana; athari za mabadiliko ya tabianchi, uhamaji na migogoro; pamoja na uwekezaji katika miundombinu ya maji na kujenga uwezo.
Pamoja na mambo mengine, ujumbe wa Tanzania imetatumia jukwaa hili kueleza mafanikio yake katika sekta ya maji, mchango wake katika kuimarisha ushirikiano wa kikanda na usimamizi wa pamoja wa mabonde, mito na maziwa. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Wivu uliopitiliza, kudhoofika kwa malezi ya familia na kushindwa kutatua migogoro kwa njia za amani ni miongoni mwa sababu zinazochangia mauaji yanayotokana na migogoro ya kimahusiano, amesema Dkt. Sylvia Ruambo, Mkurugenzi wa Support for Future Foundation na mwanachama wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC).
Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za THRDC jijini Dar es Salaam, Oktoba 22, 2026, Dkt. Sylvia amesema sababu nyingine ni ukosefu wa elimu kuhusu haki za binadamu na usawa wa kijinsia, pamoja na udhaifu wa mifumo ya kuzuia ukatili.
Amesema baadhi ya matukio ya mauaji hutanguliwa na viashiria vya hatari, ikiwemo vitisho vya kuua, kumdhibiti mwenza, unyanyasaji wa kisaikolojia na vipigo vya mara kwa mara.
Amesisitiza kuwa viashiria hivyo vinapaswa kuchukuliwa kwa uzito na jamii pamoja na mamlaka husika ili hatua za mapema zichukuliwe kuzuia ukatili usiozuilika na vifo.
Dkt. Sylvia amesema watoto pia ni miongoni mwa waathirika wa migogoro hiyo, kwani wanaweza kushuhudia ukatili, kufanyiwa vitendo vya ukatili au hata kupoteza maisha.
Ametaka jamii na taasisi zinazohusika kuimarisha huduma za ushauri nasaha na mifumo ya ulinzi kwa waathirika wa ukatili, ili kuwasaidia walio katika hatari kupata msaada kwa wakati na kuzuia matukio zaidi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Dkt. Rose Reuben, amesema wanawake ni miongoni mwa waathirika wakubwa wa mauaji yanayotokana na migogoro ya kimahusiano, akihimiza jamii kutafuta suluhu za amani badala ya kutumia ukatili.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Muungano wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), jijini Dar es Salaam, Oktoba 22, 2026, Dkt. Rose amesema takwimu za mauaji nchini zinaonesha umuhimu wa kuimarisha juhudi za kuzuia vifo vinavyotokana na migogoro hiyo.
Kwa mujibu wa takwimu alizowasilisha, mwaka 2024 yaliripotiwa matukio 2,193 ya mauaji, ambapo 422 yalihusishwa na migogoro ya kimahusiano. Mwaka 2025, matukio ya mauaji yalipungua hadi 1,977, lakini mauaji yaliyohusishwa na migogoro hiyo yaliongezeka hadi 725.
Aidha, kuanzia Januari hadi Juni 2026, matukio 941 ya mauaji yaliripotiwa, ikilinganishwa na matukio 926 katika kipindi kama hicho mwaka 2025.
Dkt. Rose amesisitiza umuhimu wa kutatua migogoro ya kimahusiano kwa njia za amani, ikiwemo mazungumzo, usuluhishi na ushauri nasaha, badala ya kutumia ukatili unaoweza kusababisha vifo.
Kauli hiyo imetolewa katika mkutano wa wanachama wa THRDC uliofanyika kwa lengo la kuhamasisha jamii kukomesha mauaji ya wenza na kutoa elimu kuhusu madhara ya ukatili katika mahusiano, kupitia kaulimbiu “Mapenzi Sio Vita, Usiue.”This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Licha ya kukabiliwa na vikwazo vizito kutoka nchini Marekani, Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) imetangazwa rasmi leo, Alhamisi, Oktoba 22, 2026, kuwa mshindi wa Tuzo ya Sakharov kwa mwaka 2026, hatua inayotajwa kuwa ishara thabiti ya uungwaji mkono kutoka Bunge la Ulaya, ingawa inaweza kuzua mtafaruko wa kidiplomasia na utawala wa Rais Donald Trump.
Rais wa Bunge la Ulaya, Roberta Metsola ameeleza kuwa uamuzi huo umelenga kutambua mchango wa ICC katika kusimamia sheria za kimataifa na haki za binadamu akisema, "Umoja wa Ulaya umejengwa juu ya misingi ya kuheshimu ushirikiano wa kimataifa na taasisi za kimataifa, na tuzo hii inatambua kazi kubwa inayofanywa na mahakama katika kusimamia sheria na haki za kimataifa”.
Uamuzi huu unajiri wiki chache tu baada ya Marekani kutangaza vikwazo vipya dhidi ya ICC kwa madhumuni ya kudhoofisha shughuli zake za kila siku, hatua iliyochochewa na ghadhabu za utawala wa Trump kufuatia mahakama hiyo kutoa hati ya kukamatwa kwa Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, kutokana na tuhuma za uhalifu huko Gaza. Hali hiyo inafuatia pia tuzo ya amani ya Nobel aliyopewa aliyekuwa jaji wa ICC, Navi Pillay, mwezi huu ambayo Trump aliikosoa vikali.
Umoja wa Ulaya umeweka wazi msimamo wake wa kusimama kidete na ICC, ukisema uko tayari kuchukua hatua zote zinazohitajika kuhakikisha mahakama hiyo inaendelea na majukumu yake bila kushinikizwa au kutishwa.
Tuzo hiyo ya kila mwaka, iliyoanzishwa mwaka 1988 kwa heshima ya mwanaharakati wa zamani wa Soviet, Andrei Sakharov, inatambua watu na mashirika yanayopigania haki za binadamu.
Katika kinyanyanyiro cha mwaka huu, ICC imewashinda washindani wengine wawili wa mwisho waliokuwa kwenye orodha ambao ni Tundu Lissu, kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, CHADEMA ambaye amekuwa kizuizini tangu Aprili 2025 akikabiliwa na mashitaka ya uhaini, na Taraneh na Romina Rahimi ambao ni dada pacha wenye umri wa miaka 21 kutoka Iran, waliohukumiwa kifo na miaka 36 jela kwa kushiriki maandamano ya kupinga serikali nchini humo. -
Jambo TV
@Jambotv_
Waziri Mkuu wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, amesisitiza kuwa mafanikio ya kweli ya mageuzi ya kilimo hayawezi kupimwa kwa wingi wa mavuno pekee, bali yanapaswa kuonekana kupitia ongezeko la kipato, ustawi wa maisha ya wakulima, na upatikanaji wa masoko ya uhakika, bei zenye tija, pamoja na miundombinu bora ya kuhifadhi na kuchakata mazao.
Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo Jumatano, Oktoba 21, 2026 alipokuwa akizungumza na vijana 75 wanaochipukia katika sekta ya kilimo kutoka mataifa mbalimbali, kando ya Mkutano wa Kimataifa wa Norman E. Borlaug (Borlaug Dialogue), unaofanyika jijini Des Moines, Jimbo la Iowa, nchini Marekani. Kiongozi huyo alihudhuria mkutano huo kwa kumwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
“Kwa familia za wakulima, kupata mavuno mengi pekee hakumaanishi kwamba wamefanikiwa kiuchumi. Mavuno mazuri yanapaswa kuleta maisha bora kwa mkulima,” amesisitiza Dkt. Mwigulu.
Akifafanua zaidi, Dkt. Mwigulu amebainisha kuwa wakulima wanaweza kuzalisha kwa wingi lakini bado wakapata hasara kutokana na gharama kubwa za usafirishaji, uhaba wa maghala, na bei duni zisizofidia gharama za uzalishaji. Amesema changamoto hizo zinashughulikiwa na Serikali kupitia uwekezaji mkubwa katika miradi ya umwagiliaji, uzalishaji wa mbegu bora, utafiti, huduma za ugani, na kuwawezesha vijana kupata ardhi, mikopo, na teknolojia za kisasa ili kilimo kiwe biashara inayovutia na yenye tija.
Aidha, amehimiza umuhimu wa nchi kuongeza uwezo wa ndani wa kuzalisha mbolea, mbegu, na mafuta ya kula ili kujikinga na misukosuko ya kiuchumi duniani na kupunguza utegemezi wa bidhaa kutoka nje.
Akielezea kuhusu kaulimbiu yao, Waziri Mkuu alisema: “Kaulimbiu yenu isemayo ‘Wakati Wakulima Wanafanikiwa, Afrika Inastawi,’ inatukumbusha kwamba ni lazima tupime mageuzi ya kilimo kwa kuangalia mabadiliko yanayotokea kwenye maisha ya wakulima. Uzalishaji mkubwa ni muhimu. Lakini muhimu ni mapato yanayopatikana, usalama unaopatikana na fursa zinazojitokeza kwa familia.”
Awali, akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na vijana hao, Rais wa Taasisi ya Mapinduzi ya Kijani Barani Afrika (AGRA), Alice Ruhweza, aliipongeza Tanzania kwa hatua kubwa inazochukua katika kilimo cha umwagiliaji na uwezeshaji vijana. Kipekee, alimpongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uongozi wake mahiri katika kuendesha programu ya kukuza vijana kwenye kilimo ya Jenga Kesho Bora (BBT).
Bi. Ruhweza alifichua kuwa AGRA, kwa kushirikiana na Mastercard Foundation, inaendesha programu ya kuwawezesha vijana katika kilimo yenye thamani ya Dola za Marekani milioni 350 katika nchi mbalimbali zikiwemo Tanzania, ambapo utekelezaji wake nchini unaunganishwa moja kwa moja na mpango wa BBT ili kuleta tija kubwa na kuepuka kurudia juhudi. Aliongeza kuwa uzoefu na mafanikio ya Tanzania sasa yanatumika kama mfano wa kuigwa na nchi nyingine za Afrika.
Katika ziara hiyo na mkutano huo, Waziri Mkuu ameambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Ngwaru Maghembe; Naibu Waziri wa Kilimo, David Silinde; Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Dkt. Elsie Kanza; pamoja na watendaji wengine wa Serikali. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Wafanyakazi zaidi ya 700 wanaoshiriki katika ujenzi wa ukumbi mkubwa wa mikutano wa Mount Kilimanjaro International Convention Centre (MKICC), jijini Arusha, wamegoma kufanya kazi leo, Oktoba 22, 2026 wakilalamikia kucheleweshewa malipo yao pamoja na kiwango kidogo cha fedha wanazolipwa.
Wakizungumza na waandishi wa habari, wafanyakazi hao wamedai kuwa hawajalipwa mishahara na stahiki zao kwa zaidi ya siku tano, hali iliyowalazimu kusitisha kazi wakishinikiza kulipwa fedha zao.
Wamesema kuchelewa kwa malipo hayo kunawaathiri katika kukidhi mahitaji yao ya kila siku, ikiwemo chakula na usafiri. Aidha, wamelalamikia kulipwa shilingi 15,500 kwa siku na kudai kutokuwa na mikataba rasmi ya ajira.
Akizungumzia malalamiko hayo, Meneja wa Mradi kutoka Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Salha Mohamed Kasimu, amesema serikali tayari imeshakamilisha malipo yote kwa mkandarasi anayetekeleza mradi huo.
Amesema mradi huo unatekelezwa kwa fedha za ndani na siyo mkopo, huku akieleza kuwa wanafuatilia kubaini chanzo cha kuchelewa kwa malipo ya wafanyakazi hao.
Ameahidi kuwa changamoto hiyo itashughulikiwa ili kuhakikisha wanalipwa mishahara yao na matatizo mengine yanapatiwa ufumbuzi.
Mradi wa MKICC unatekelezwa kwa ushirikiano kati ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) na Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC).This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Askofu Dkt. Stanley Hotay, amesisitiza kuwa amani ya kweli haiwezi kupatikana nchini bila kuwepo kwa haki, akionya kuwa kuhubiri amani huku ukosefu wa haki ukifumbiwa macho ni kuzalisha udhalimu uliojificha.
Akizungumza jana Oktoba 21, 2026 jijini Dar es Salaam wakati wa Kongamano la Kitaifa la Dini Mbalimbali Kuhusu Amani, Haki na Uwajibikaji Nchini Tanzania, Askofu Hotay ameeleza kuwa haki na amani ni mambo mawili yaliyoshikamana kwa karibu na yasiyoweza kutenganishwa.
Akiweka msisitizo juu ya uwajibikaji wa viongozi wa dini na jamii katika kusimamia mambo hayo mawili, Askofu Hotay amesema: "Haki na amani zimesongana, huwezi kuzitenganisha hizi mbili. Kuna wakati tunajaribiwa kufikiri tutangaze amani pekee yake huku hatutendeani haki, na kumbe haiwezekani".
Ameongeza kuwa kutenda haki ni takwa la msingi kwa kila mwananchi bila kujali historia au tabia yake, na viongozi wa kiroho wana wajibu wa kukemea uonevu badala ya kukaa kimya.
"Amani bila haki inageuka kuwa udhalimu uliojificha. Kama viongozi wa dini hatuwezi kuhubiri amani huku tukifumbia macho ukosefu wa haki. Haki ya mtu hata kama ana ubaya kiasi gani anayo haki, zile haki lazima zitazamwe kwa ukaribu", ameeleza.
Katika kongamano hilo, viongozi wa dini wamehimizwa kutenda haki, kuwa wapatanishi, kupaza sauti dhidi ya dhuluma, kuelimisha jamii na kuimarisha umoja na uzalendo. Majadiliano yamesisitiza umuhimu wa kukubali makosa, kuwajibika, kutubu na kuendeleza mazungumzo ya kitaifa, maridhiano, uponyaji wa kijamii na kuzuia migogoro.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Viongozi, wafuasi wa CHADEMA wakiwa katika Ukumbi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Dar es Salaam leo Oktoba 22, 2026 wakisubili kutolewa kwa Uamuzi kuhusu maombi ya zuio katika maombi madogo Na. 14864/26 ambayo yameletwa Mahakamani Makamu Mwenyekiti wa zamani wa CHADEMA Zanzibar Said Issa Mohammed na mwenzake Ahmed Rashid Khamis dhidi ya Bodi ya Wadhamini wa CHADEMA na Katibu Mkuu wa CHADEMA.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda ametoa mwito kwa Watanzania kujenga uzalendo wa kweli kwa kuwekeza katika kusoma na kuhifadhi historia na utamaduni wa nchi kupitia vitabu vya waandishi wa ndani.
Prof. Mkenda ameyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Mfumo Jumuishi wa Maktaba Mtandao wa Taifa (INDLS) uliokwenda sambamba na Kongamano la Nne la Kitaifa la Huduma za Maktaba lililoanza Oktoba 20 hadi 22.
"Kusema tuwe wazalendo ni maneno rahisi sana... lakini kujenga uzalendo ni pamoja na watu kujielewa na kujitambua. Sisi kama nchi lazima tujitambue kama Watanzania, tutambue utamaduni wetu na historia wetu. Huwezi kutamka 'tuwe wazalendo' ikawa basi... lazima tuwekeze katika vitabu, katika kuhifadhi historia yetu, kusambaza historia yetu na utamaduni wetu kwa kutumia vitabu na kuhimiza watu kusoma", ameeleza Prof. Mkenda.
Prof. Mkenda ameongeza kuwa Serikali itaendelea kuwahimiza na kuwasaidia waandishi wa ndani ili vitabu vyao vichapishwe, visambazwe na visomwe kote nchini na hata kimataifa.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania, Dkt. Mboni Ruzegea, ameeleza kuwa Mfumo huo wa Maktaba Mtandao wa Taifa umejengwa kwa ushirikiano na Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za maktaba kwa wananchi wote, wakiwemo walioko maeneo ya pembezoni.
Dkt. Ruzegea amebainisha kuwa mfumo huo mpya utamwezesha mwananchi yeyote mwenye simu au kompyuta kuingia kwenye mtandao, kutafuta, kuteua, na kuazima vitabu katika maktaba iliyo karibu naye.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana ya ACT Wazalendo Taifa, Abdul Nondo ametoa salamu za mshikamano kwa Mkurugenzi wa mafunzo, Oganaizesheni ya Uchaguzi ya CHADEMA, John Pambalu John Pambalu, kufuatia kukamatwa kwake na kufunguliwa mashtaka ya uhaini.
Akizungumza leo Oktoba 22, 2026 jijini Dar es Salaam, Nondo ameeleza kuwa Pambalu ni rafiki yake wa karibu waliyefanya naye kazi kwa pamoja, huku akisimulia namna alivyokutana naye mkoani Tanga akiwa chini ya ulinzi wa Jeshi la Polisi.
Nondo amesema alipata nafasi ya kukutana na Pambalu Oktoba 14, 2026, katika eneo la Mkata, wilayani Handeni, mkoani Tanga wakati Pambalu akiwa kwenye gari akisindikizwa na polisi waliokuwa wakimsafirisha kutoka eneo alikokamatwa kuelekea Dar es Salaam.
"Nilipomuana kwenye gari niliwaomba Polisi nipate nafasi ya kumsalimia, walikubali na kufungua dirisha la gari na kupata fursa ya kuzungumza naye, nilimpa moyo, na kumtia ujasiri awe imara huku yeye akimjibu kuwa anahitaji tumuombee" amesema Nondo.
Nondo ameitaka Serikali kutambua kuwa kipindi hiki kinahitaji utulivu wa hali ya juu wa kisiasa, na kwamba kukamata vijana pamoja na kuwafungulia kesi za uhaini kunaharibu mshikamano na umoja wa kitaifa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI:
Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, inatarajiwa leo Oktoba 22, 2026, kutoa uamuzi kuhusu maombi ya zuio katika maombi madogo namba 14864 ya mwaka 2026 yanayowahusu Said Issa Mohamed na wenzake dhidi ya CHADEMA.
Kwa mujibu wa taarifa ya chama hicho iliyosainiwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi, Brenda Rupia, uamuzi huo unatarajiwa kutolewa saa 8:00 mchana huu katika Mahakama hiyo.
Taarifa hiyo inaeleza zaidi kwamva maamuzi ya leo yanawahusisha Said Issa Mohamed na Ahmed Rashid Khamis dhidi ya Wadhamini Waliosajiliwa wa Chadema pamoja na Katibu Mkuu wa chama hicho.
Kufuatia hatua hiyo, CHADEMA imewaomba wanachama, viongozi na wafuasi wake kufika mahakamani kushuhudia na kufuatilia utoaji wa uamuzi huo, ikieleza kuwa shauri hilo lina umuhimu kwa chama na wanachama wake.
“Kwa umuhimu wa shauri hili na kwa kuzingatia maslahi ya chama na wanachama wake, wanachama, viongozi na wafuasi wa Chadema wanaombwa kufika kwa wingi mahakamani kushuhudia na kufuatilia mwenendo wa utoaji wa uamuzi huo,” imesema taarifa hiyo. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Ngome ya Vijana ya Chama cha ACT Wazalendo Taifa imetangaza azma ya kuandika barua yenye ushauri na mapendekezo kwenda Ofisi ya Makamu wa Rais pamoja na kuomba fursa ya kukutana naye, ili kuwasilisha ajenda ya kutaka wataalamu wa bioteknolojia nchini kutambulika rasmi, kutengenezewa bodi, kupewa leseni, na kuwekewa muundo wa utumishi.
Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana ya ACT Wazalendo Taifa, Abdul Nondo, akizungumza na wanahabari leo Oktoba 22, 2026 mkoani Dar es Salaam, ameeleza kuwa taaluma ya bioteknolojia inahusu moja kwa moja usalama wa nchi na ina uhusiano mkubwa na Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambapo kitengo kikuu cha kitaifa na kamati ya kusimamia matumizi bora ya bioteknolojia pamoja na udhibiti wa mbegu za GMO ziko chini ya ofisi hiyo.
Nondo amebainisha kuwa barua hiyo itakayowasilishwa Ofisi ya Makamu wa Rais pia itapelekwa nakala kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ikihitaji maamuzi ya kisera na uratibu wa serikali ili mabadiliko ya sayansi na teknolojia katika sekta za afya, kilimo, viwanda na mazingira yasiikute Tanzania ikiwa imesimama.
"Tunaomba sana Mheshimiwa Makamu wa Rais... beba hili suala kwa kumsaidia Mheshimiwa Rais kwa kuisaidia nchi yetu na taifa letu kuhakikisha wanataaluma wa teknolojia wanatambulika nchini kwetu, mawazo yao, fikra zao na elimu yao wanayoipata kwenye vyuo vyetu inatumika kwa mustakbali wa nchi yetu, wanatengenezewa bodi wapewe leseni na watengenezewe muundo wa utumishi", ameeleza Nondo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Rais mstaafu wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ameishauri Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kuangalia uwezekano wa kujenga Bwawa Dogo eneo la Wami, litakalosaidia kuongeza upatikanaji wa maji Chalinze ifikapo mwaka 2030 hadi 2050.
Akizungumza baada ya kutembelewa na Meneja wa DAWASA Chalinze, Mhandisi Boniface Ole Philemon, nyumbani kwake, Msoga- Chalinze, Dkt. Kikwete amesisitiza mahitaji ya maji yanaongezeka kutokana na ongezeko la watu na viwanda, hivyo maandalizi ya muda mrefu yanahitajika.
Pia, ameshauri mazungumzo yafanyike na mashamba ya Mtibwa mkoani Morogoro, kubaini kiasi cha maji wanachotumia ili kuwezesha maji mengi zaidi kufika mto Wami. Aidha, amependekeza matumizi ya maji kwa Bagamoyo Sugar yazingatiwe.
Dkt. Kikwete amefurahishwa na hali ya huduma ya maji Mji wa Chalinze na kupongeza kazi inayofanywa na Wizara na DAWASA, na kusema kazi kubwa imefanyika chini ya Waziri wa Maji, Jumaa Aweso na watumishi wote wa sekta ya maji nchini.
Dkt. Kikwete amesema kwa sasa hapokei malalamiko kuhusu huduma ya maji Chalinze na amesisitiza kazi nzuri inayoendelea iendelezwe, huku mapendekezo yake yakilenga kuimarisha upatikanaji wa maji kwa mahitaji yajayo. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, John Heche, amewataka Watanzania kuacha kutumia muda mwingi kwenye mazungumzo ya mpira wakiwa vijiweni na badala yake wazungumzie maisha yao na kudai mabadiliko ya kiuchumi yatakayowawezesha kujikwamua kutoka kwenye umasikini.
Akizungumza wakati wa Kongamano la Baraza la Wanawake la CHADEMA (BAWACHA) Mkoa wa Manyara lililofanyika Haydom, wilayani Mbulu, Heche amebainisha kuwa tofauti na nchi za Magharibi kama Uingereza ambako viwanja vya mpira vinajaa kwa sababu wananchi wana uchumi na fedha mifukoni, nchini Tanzania wananchi wengi wamefanywa maskini kiasi cha kuishia kuangalia mechi kwenye vibandaumiza.
"Tunataka tukutengenezee uchumi ili uwe unaruka hata kwenda Uingereza kuangalia mpira kwa sababu una uchumi mfukoni", ameeleza.
Heche amekosoa mtazamo uliopo katika jamii kwamba wazungu tu ndio walioumbwa kusafiri na kutalii Afrika, akibainisha kuwa umasikini na ukosefu wa elimu ndivyo vilivyowafanya wananchi kuamini hivyo. Ameeleza kuwa iwapo mwananchi atatengenezewa uchumi imara, atakuwa na uwezo wa kuchukua likizo ya mapumziko pamoja na familia yake kwenda nchi kama Uingereza au Ufaransa kama wanavyofanya wazungu.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Waziri Mkuu wa Tanzania Dkt. Mwigulu Nchemba, amewakaribisha wenye mitaji na wawekezaji wa kimataifa kuwekeza nchini Tanzania kwenye sekta ya kilimo, akibainisha kuwa nchi hiyo inatoa fursa kubwa ya kipekee inayowezesha kufikia soko la takribani watu milioni 170 katika ukanda mzima wa Afrika Mashariki na Kati.
Hayo aliyasema jana, Jumanne, Oktoba 20, 2026, wakati akiongoza mjadala mkubwa kuhusu uwekezaji kwenye kilimo biashara uliowakutanisha viongozi wa kampuni za utafiti, teknolojia, mbegu, na dawa za wadudu. Mkutano huo ulifanyika kando ya Mkutano wa Kimataifa wa Norman E. Borlaug (Borlaug Dialogue), mjini Des Moines, Jimbo la Iowa, nchini Marekani.
Katika kuwasilisha fursa za nchi, Dkt. Mwigulu alieleza kuwa Tanzania ina jumla ya hekta milioni 44 za ardhi inayofaa kwa kilimo, huku hekta milioni 10.8 pekee ndizo zinazotumika kwa sasa. Kuhusu kilimo cha umwagiliaji, alibainisha kuwa nchi ina uwezo wa kumwagilia hekta milioni 29.4, lakini kwa sasa zinazotumutumia ni hekta 727,282 pekee, hali inayotoa nafasi kubwa ya uwekezaji.
Alitaja maeneo mahususi ya uwekezaji kuwa ni pamoja na usindikaji na ufungashaji wa mazao, ujenzi wa maghala na miundombinu ya ubaridi, usafirishaji, huduma za kidijitali, na huduma za kifedha kwa wakulima, huku akisisitiza kuwa Serikali imeweka vivutio vya kikodi na visivyo vya kikodi ili kuvutia sekta binafsi.
Katika mjadala huo ulioangazia matumizi ya teknolojia, Mkurugenzi Mtendaji wa Utafiti na Viwanda wa Kampuni ya Microsoft, Dkt. Ranveer Chandra, alieleza kuwa kampuni hiyo imekuwa ikitekeleza miradi mbalimbali nchini Tanzania kwa miaka 10 iliyopita. Miradi hiyo inajumuisha ushirikiano na MADE Alliance kwenye mifumo ya malipo ya kidijitali kwa wakulima 50,000 wa alizeti, ushirikiano na kampuni ya Mawingu kupanua intaneti ya vijijini, pamoja na mafunzo ya Akili Unde kwa wanawake 5,000 kwa kupitia ABSA Tanzania na Women in Tech.
“Tanzania ina fursa ya kuwa kituo cha kikanda cha akili unde kwa ajili ya kilimo, ambacho nchi nyingine zinaweza kujifunza kutoka kwake,” alisisitiza Dkt. Chandra.
Kwa upande wake, Mwanzilishi na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya CeluNova kutoka Mexico, Bw. Adolfo Vidal Ruiz, alieleza ubunifu wa kampuni yake wa kutumia majani ya nanasi kuzalisha nyuzi zinazotumika kutengeneza karatasi za chooni na taulo za jikoni ambazo ni imara zaidi na zinazostahimili unyevu na kuvutwa bila kuchanika haraka. -
Jambo TV
@Jambotv_
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, John Heche, amekosoa vikali mfumo wa Stakabadhi Ghalani pamoja na tozo mbalimbali dhidi ya wakulima akidai kuwa serikali inawanyonya bila kuwapa msaada zaidi wa kuwezesha kilimo chao.
Akizungumza katika Kongamano la Baraza la Wanawake la CHADEMA (BAWACHA) Mkoa wa Manyara lililofanyika Haydom, wilayani Mbulu leo, Heche amebainisha kuwa wakulima wa vitunguu na dengu mkoani Manyara wanatumia mtaji wao wenyewe na kukabiliwa na ukame bila msaada wa serikali, lakini wanapovuna serikali inakimbilia kukusanya kodi na tozo.
Akiiponda hatua hiyo na mfumo wa Stakabadhi Ghalani, Heche amesema, "Serikali ya CCM ni kama kupe... Kupe anamnyonya ng'ombe, kwani kupe anamlisha ng'ombe? Yeye ananyonya tu. Serikali ya CCM inanyonya watu, inataka kula pale ambapo haijapanda".
Ameongeza kuwa mfumo wa Stakabadhi Ghalani kwenye mazao kama dengu umekuwa ukiwalaza wakulima na umaskini badala ya kuwasaidia kujikwamua kiuchumi, "Hiyo stakabadhi ghalani inafanyaje? Wanachukua mazao yako wanakulipa muda wanaotaka. Wewe umelima ili uuze upate hela, wao wanakupa karatasi"
Aidha, Heche ameeleza kuwa kilimo kinapaswa kuchukuliwa kama suala la usalama wa taifa akieleza kuwa nchi zilizopiga hatua kiuchumi zinawawezesha na kuwalipa wakulima ili kuhakikisha usalama wa chakula kwa raia wao, tofauti na hali ilivyo nchini
"Kilimo duniani ni suala la usalama wa nchi, kama ambavyo serikali inalipa wanajeshi ili walinde mipaka, serikali zingine zinalipa wakulima ili wazalishe chakula walinde nchi", ameeleza.
Katika hatua nyingine, Heche amewataka Watanzania kutafakari sababu za akina mama na watoto kuendelea kuteseka katika huduma za afya wakati nchi ikiwa na utajiri mkubwa wa rasilimali kama dhahabu, Tanzanite na hifadhi za wanyama. Amedai kuwa uongozi mbovu ndicho chanzo cha wananchi kuteseka kiasi hicho na zaidi kubaki kwenye umaskini uliokithiri. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, John Heche amesikitishwa na taarifa ya Mkurugenzi wa Mafunzo na Oganaizesheni ya Uchaguzi wa chama hicho Makao Makuu, John Pambalu kufunguliwa mashtaka ya uhaini sawa na yale yanayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Lissu huku akisisitiza kuwa hatakimbia nchi hata kama naye atafunguliwa mashtaka ya uhaini au ugaidi.
Heche ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumza katika Kongamano la Baraza la Wanawake la CHADEMA (BAWACHA) Mkoa wa Manyara lililofanyika Haydom, wilayani Mbulu.
Pambalu amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam akikabiliwa na shtaka la uhaini lililoainishwa chini ya Kifungu cha 39(2)(d) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu iliyorekebishwa mwaka 2023. Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, inadaiwa kuwa kati ya Septemba 1, 2025 na Oktoba 29, 2025, katika maeneo mbalimbali mkoani Dar es Salaam, Pambalu alidhamiria kuwashawishi wananchi kukwamisha Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025. Hati hiyo inaeleza kuwa alionesha nia hiyo kwa kuendesha na kuratibu maandamano yasiyo na kikomo kote nchini kwa lengo la kuitisha na kuishinikiza Serikali.
“Najua na mimi wakati wowote watanipa kesi ya aina hiyo hiyo au nyingine wanayotaka iwe ya ugaidi iwe ya uhaini lakini mimi nimesema sitakimbia nchi yangu. Hii ni nchi yetu. Tutaipambania tukiwa humu. Tutapambana tukiwa humuhumu... Uhakika kama jua linavyochomoza asubuhi... Kitu nilicho na uhakika nacho ni kwamba tutashinda, hilo nina uhakika nalo”, ameeleza heche akibainisha kuwa Pambalu alishikiliwa na Jeshi la Polisi kwa zaidi ya siku 10 kabla ya kufikishwa mahakamani na kusomewa mashtaka hayo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Waziri wa Madini, Anthony Peter Mavunde ameongoza kikao cha Mawaziri wa Afrika kilichojadili namna ya kuimarisha ufadhili wa Sekta ya Madini kuanzia hatua za utafiti hadi uchakataji na usafishaji, akizitaka nchi za Afrika kuimarisha uwezo wa kutumia rasilimali na mapato ya ndani kuendeleza miradi ya kimkakati ya madini.
Kikao hicho cha ngazi ya mawaziri, kilichofanyika Oktoba 20, 2026, katika Mkutano wa Mining in Motion 2026, jijini Accra, Ghana kilijadili mada isemayo “Financing Africa’s Mineral Future- From Exploration to Refining”, inayolenga kuchunguza namna taasisi za fedha za Afrika na kimataifa zinavyoweza kuwezesha upatikanaji wa mitaji katika mnyororo mzima wa thamani wa madini.
Akiongoza majadiliano hayo, Mavunde amesisitiza umuhimu wa nchi za Afrika kuanza kwa kutumia uwezo wake wa ndani kufadhili maendeleo ya Sekta ya Madini badala ya kutegemea zaidi ufadhili kutoka nje na kwamba utekelezaji wa mikakati ya ndani ya ufadhili unahitaji maamuzi madhubuti ya kisera, dhamira ya kisiasa na ushirikiano kati ya Serikali, taasisi za fedha na sekta binafsi.
Akitoa mfano wa Tanzania, Mavunde ameeleza kuwa Serikali imeweka utaratibu wa kutenga asilimia 10 ya makusanyo yatokanayo na Sekta ya Madini kwa ajili ya utafiti wa kina wa kijiolojia, hatua inayolenga kuongeza wigo wa maeneo yanayofanyiwa utafiti na kubaini rasilimali zilizopo nchini na kubaishisha kuwa Tanzania bado ina fursa kubwa ya kuendeleza utafiti huo, ikizingatiwa kuwa takribani asilimia 16 tu ya eneo la nchi limefanyiwa utafiti wa kina
“Utashi wa kisiasa uliooneshwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, wa kutenga asilimia 10 ya mapato yatokanayo na Sekta ya Madini kwa ajili ya utafiti wa kina ni hatua muhimu katika kupunguza utegemezi wa fedha za wahisani na kuwezesha Tanzania kufadhili utafiti wa rasilimali zake kwa kutumia mapato ya ndani” amesema Mavunde.
Aidha, Mavunde ameeleza kikao hicho kuwa ufadhili wa Sekta ya Madini haupaswi kuishia katika utafiti na uchimbaji pekee, bali unapaswa kujumuisha ujenzi wa viwanda vya uchakataji na usafishaji wa madini na kusisitiza kuwa uwekezaji katika hatua hizo unaweza kuongeza ajira, kukuza ujuzi wa kitaalamu, kupanua shughuli za kiuchumi na kuongeza mapato yatokanayo na mauzo ya bidhaa za madini zilizoongezwa thamani.
Ameongeza kuwa Tanzania inaendelea kuimarisha ushiriki wa Watanzania katika Sekta ya Madini kupitia mfumo wa maudhui ya ndani (Local Content), unaolenga kuwawezesha wazawa kushiriki katika utoaji wa bidhaa na huduma kwa migodi, ambako katika kueleza umuhimu wa mkakati huo, ametaja hatua za kukuza uzalishaji wa ndani wa bidhaa zinazotumika migodini na kuimarisha uwezo wa Kampuni za Kitanzania kunufaika na fursa za biashara zinazotokana na sekta hiyo.
Katika mjadala huo, umuhimu wa ubia kati ya sekta ya umma na binafsi, mifumo bunifu ya ufadhili na uwekezaji katika miundombinu ulijadiliwa kama sehemu ya kuwezesha maendeleo ya viwanda vya madini. Vilevile, ushirikiano wa kikanda na fursa zinazotokana na Eneo Huru la Biashara la Afrika (AfCFTA) zilitajwa kuwa muhimu katika kujenga masoko mapana na minyororo ya thamani inayounganisha nchi za Afrika.
Mavunde amesisitiza kuwa mafanikio ya Sekta ya Madini barani Afrika yanahitaji dhamira ya kisiasa, uvumilivu na utekelezaji wa mikakati inayowezesha nchi kufadhili miradi yake na kuongeza thamani ya rasilimali zake na kueleza kuwa kwa kuimarisha uwezo wa ndani, kuendeleza viwanda na kushirikiana kikanda, Sekta ya Madini inaweza kuwa mhimili wa uchumi wa viwanda, ajira na maendeleo endelevu kwa wananchi wa Afrika.
Kwa upande wake, Waziri wa Ardhi na Rasilimali Asili wa Ghana, Emmanuel Armah-Kofi Buah amezitaka nchi za Afrika kuimarisha ushirikiano katika kukabiliana na changamoto za Sekta ya Madini, ikiwemo upungufu wa mitaji, miundombinu na nishati, pamoja na kuongeza thamani ya madini na kusisitiza umuhimu wa kuwa na mkakati wa pamoja utakaowezesha nchi za Afrika kutumia nguvu zake katika majadiliano ya uwekezaji, kuendeleza viwanda vya uchakataji wa madini na kulinda maslahi ya jamii zinazozunguka maeneo ya migodi. -
Jambo TV
@Jambotv_
Waziri wa Madini, Anthony Peter Mavunde ameongoza kikao cha Mawaziri wa Afrika kilichojadili namna ya kuimarisha ufadhili wa Sekta ya Madini kuanzia hatua za utafiti hadi uchakataji na usafishaji, akizitaka nchi za Afrika kuimarisha uwezo wa kutumia rasilimali na mapato ya ndani kuendeleza miradi ya kimkakati ya madini.
Kikao hicho cha ngazi ya mawaziri, kilichofanyika Oktoba 20, 2026, katika Mkutano wa Mining in Motion 2026, jijini Accra, Ghana kilijadili mada isemayo “Financing Africa’s Mineral Future- From Exploration to Refining”, inayolenga kuchunguza namna taasisi za fedha za Afrika na kimataifa zinavyoweza kuwezesha upatikanaji wa mitaji katika mnyororo mzima wa thamani wa madini.
Akiongoza majadiliano hayo, Mavunde amesisitiza umuhimu wa nchi za Afrika kuanza kwa kutumia uwezo wake wa ndani kufadhili maendeleo ya Sekta ya Madini badala ya kutegemea zaidi ufadhili kutoka nje na kwamba utekelezaji wa mikakati ya ndani ya ufadhili unahitaji maamuzi madhubuti ya kisera, dhamira ya kisiasa na ushirikiano kati ya Serikali, taasisi za fedha na sekta binafsi.
Akitoa mfano wa Tanzania, Mavunde ameeleza kuwa Serikali imeweka utaratibu wa kutenga asilimia 10 ya makusanyo yatokanayo na Sekta ya Madini kwa ajili ya utafiti wa kina wa kijiolojia, hatua inayolenga kuongeza wigo wa maeneo yanayofanyiwa utafiti na kubaini rasilimali zilizopo nchini na kubaishisha kuwa Tanzania bado ina fursa kubwa ya kuendeleza utafiti huo, ikizingatiwa kuwa takribani asilimia 16 tu ya eneo la nchi limefanyiwa utafiti wa kina
“Utashi wa kisiasa uliooneshwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, wa kutenga asilimia 10 ya mapato yatokanayo na Sekta ya Madini kwa ajili ya utafiti wa kina ni hatua muhimu katika kupunguza utegemezi wa fedha za wahisani na kuwezesha Tanzania kufadhili utafiti wa rasilimali zake kwa kutumia mapato ya ndani” amesema Mavunde.
Aidha, Mavunde ameeleza kikao hicho kuwa ufadhili wa Sekta ya Madini haupaswi kuishia katika utafiti na uchimbaji pekee, bali unapaswa kujumuisha ujenzi wa viwanda vya uchakataji na usafishaji wa madini na kusisitiza kuwa uwekezaji katika hatua hizo unaweza kuongeza ajira, kukuza ujuzi wa kitaalamu, kupanua shughuli za kiuchumi na kuongeza mapato yatokanayo na mauzo ya bidhaa za madini zilizoongezwa thamani.
Ameongeza kuwa Tanzania inaendelea kuimarisha ushiriki wa Watanzania katika Sekta ya Madini kupitia mfumo wa maudhui ya ndani (Local Content), unaolenga kuwawezesha wazawa kushiriki katika utoaji wa bidhaa na huduma kwa migodi, ambako katika kueleza umuhimu wa mkakati huo, ametaja hatua za kukuza uzalishaji wa ndani wa bidhaa zinazotumika migodini na kuimarisha uwezo wa Kampuni za Kitanzania kunufaika na fursa za biashara zinazotokana na sekta hiyo.
Katika mjadala huo, umuhimu wa ubia kati ya sekta ya umma na binafsi, mifumo bunifu ya ufadhili na uwekezaji katika miundombinu ulijadiliwa kama sehemu ya kuwezesha maendeleo ya viwanda vya madini. Vilevile, ushirikiano wa kikanda na fursa zinazotokana na Eneo Huru la Biashara la Afrika (AfCFTA) zilitajwa kuwa muhimu katika kujenga masoko mapana na minyororo ya thamani inayounganisha nchi za Afrika.
Mavunde amesisitiza kuwa mafanikio ya Sekta ya Madini barani Afrika yanahitaji dhamira ya kisiasa, uvumilivu na utekelezaji wa mikakati inayowezesha nchi kufadhili miradi yake na kuongeza thamani ya rasilimali zake na kueleza kuwa kwa kuimarisha uwezo wa ndani, kuendeleza viwanda na kushirikiana kikanda, Sekta ya Madini inaweza kuwa mhimili wa uchumi wa viwanda, ajira na maendeleo endelevu kwa wananchi wa Afrika.
Kwa upande wake, Waziri wa Ardhi na Rasilimali Asili wa Ghana, Emmanuel Armah-Kofi Buah amezitaka nchi za Afrika kuimarisha ushirikiano katika kukabiliana na changamoto za Sekta ya Madini, ikiwemo upungufu wa mitaji, miundombinu na nishati, pamoja na kuongeza thamani ya madini na kusisitiza umuhimu wa kuwa na mkakati wa pamoja utakaowezesha nchi za Afrika kutumia nguvu zake katika majadiliano ya uwekezaji, kuendeleza viwanda vya uchakataji wa madini na kulinda maslahi ya jamii zinazozunguka maeneo ya migodi. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, John Heche, ameonesha kushangazwa na kusikitishwa na hatua ya Tanzania kuendelea kuwa nchi inayotegemea kuagiza bidhaa ndogondogo za kila siku kutoka nje ikiwamo njiti za meno, nguo za ndani pamoja na nepi za watoto.
Akizungumza wakati wa Kongamano la Baraza la Wanawake la CHADEMA (BAWACHA) Mkoa wa Manyara lililofanyika Haydom, wilayani Mbulu mkoani humo siku ya Jumatano Oktoba 21, 2026, Heche amebainisha kuwa ni jambo la kushangaza kuona serikali haina hata uwezo wa kujenga kiwanda cha kutengeneza njiti za meno, na kulazimika kuzisafirisha kwa meli kutoka nchini China.
"Mwalimu Nyerere alijenga viwanda hapa tulikuwa na viwanda 35 vya nguo, kanga ya Tanzania ndio ilikuwa bora na kitenge... Leo hata zile nguo za ndani tunazovaa tunatoa nje", amedai Heche.
Heche ameonya kuwa kuagiza kila kitu kutoka nje ikiwemo nguo za ndani na nepi za watoto kunaweka afya za wananchi katika hatari zisizojulikana.
Amesisitiza kuwa nchi zilizoendelea kama China, India na Marekani zimefanikiwa kwasababu ya kuwa na idadi kubwa ya watu kama mtaji wa kiuchumi, hivyo Tanzania inapaswa kuwa makini na bidhaa inazoingiza kwa wananchi wake
Aidha, amesema kuwa viongozi wa upinzani wanaofichua ukweli huo wamekuwa wakiwindwa lakini ukweli huo utaendelea kusemwa kwasababu Tanzania imebarikiwa na Mwenyezi Mungu lakini inakabiliwa na uongozi mbovu.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Waziri Mkuu wa Tanzania Dkt. Mwigulu Nchemba amekutana na Makamu wa Rais wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD), Dkt. Geraldine Mukeshimana na kujadiliana naye masuala ya kilimo, uvuvi na uchumi wa bluu.
Mazungumzo hayo yalifanyika Jumanne, Oktoba 20, 2026 kando ya Mkutano wa Kimataifa wa Norman E. Borlaug (Borlaug Dialogue) ulioanza Oktoba 20, 2026 katika Kituo cha Mikutano cha Iowa jijini Des Moines, Marekani.
Katika majadiliano yao, Waziri Mkuu alimshukuru Dkt. Mukeshimana kwa ufadhili unaotolewa na IFAD kwenye uvuvi wa bahari kuu chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi pamoja na uendelezaji wa uchumi wa buluu kupitia Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi ya Zanzibar.
“Hii miradi ni ya muhimu na inapewa kipaumbele zaidi kwani inasaidia kuzalisha ajira kwa wanawake na vijana,” amesema.
Kwa upande wake, Makamu wa Rais wa IFAD, Dkt. Mukeshimana ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuendelea kuwa kitovu cha upatikanaji wa chakula kwa maeneo yanayoizunguka akisema, “binafsi ninawapongeza kwasababu mmeendelea kuwa kitovu cha uzalishaji wa chakula cha uhakika barani Afrika. Mnafanya kazi kubwa na nzuri mno ya kulisha chakula kwenye maeneo ya jirani”.
Alisema taasisi hiyo itaendelea kufadhili miradi inayolenga kuondoa njaa na umasikini kwa kuwekeza kwa watu wa vijijini, kuwezesha ushiriki wao katika masoko na kuimarisha ustahimilivu wa hali ya hewa wa maisha yao.
Waziri Mkuu ameambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Ngwaru Maghembe; Naibu Waziri wa Kilimo, David Silinde; Balozi wa Tanzania Washington, Elsie Kanza; na watendaji wengine wa Serikali. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mtandao wa Wanafunzi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Vyuo Vikuu na Kati (CHASO) wameonesha kutokuridhishwa na utendaji kazi wa Raisi wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (TAHLISO), Geofrey Kiliba kwa kile walichodai hatimizi wajibu wake wa kuwatetea na kuwasemea wanafunzi.
Wakizungumza ikiwa imepita masaa machache tangu, Kiliba azungumze na waandishi wa habari, Katibu wa CHASO Mkoa wa Dar es Salaam, Katisho Segeredi amemtaka kuacha mara moja kuacha tabia ya kuigeuza jumuiya hiyo ya TAHLISO kuwa tawi la chama fulani.
"Napenda kumwambia Kiliba asiigeuze taasisi ya wasomi wa Vyuo Vikuu (TAHLISO) kuwa tawi la chama fulani ambacho anakijua yeye kama ambavyo amekuwa akifanya, TAHLISO ni taasisi inayosimamia wasomi na kuna mambo mengi ambayo wasomi wa vyuo vikuu tunakumbana nayo lakini hatujawai kumsikia aliyazungumzia," amesema.
Akiunga mkono hoja hiyo Katibu wa CHASO Mkoa wa Mwanza, Raphael Wangwe amesikitishwa na hatua ya Kiliba kuunda kampeni ya "Mama Asemewe" akidai kuwa wanafunzi wa vyuo vikuu wanakabiliwa na msululu wa changamoto ambazo zinatakiwa zisemewe.
Katibu wa CHASO katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agostino cha Tanzania (SAUT) Mwanza, Heka Nyanda amemuomba rais huyo wa TAHLISO kupigania changamoto ya ugumu wa maisha kwa wasomi wa vyuo vikuu kutokana na fedha inayotolewa ya kujikimu kutokidhi mahitaji.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria imepokea taarifa mbili za Wizara ya Katiba na Sheria kuhusu hatua za kulinda haki za watuhumiwa na marekebisho ya sheria 41 zilizobainika kukinzana, zilizowasilishwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Abdallah Hamis Ulega, leo tarehe 20 Oktoba, 2026, katika ukumbi wa Frank Mfundo, Bungeni, jijini Dodoma.
Taarifa ya kwanza iliyowasilishwa inahusu hatua zinazochukuliwa na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (OTM), kwa kushirikiana na taasisi nyingine zinazohusika na upelelezi, ukamataji na utaifishaji wa mali, kuhakikisha haki za watuhumiwa zinalindwa na mali zao zinatunzwa ipasavyo bila kupoteza thamani hadi mashauri yanayowahusu yanapohitimishwa mahakamani.
Taarifa ya pili inahusu hatua zilizochukuliwa katika kupitia na kufanya marekebisho ya sheria 41 zilizobainika kukinzana, ikiwemo kifungu cha 80(2) cha Sheria ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, Sura ya 263, kwa lengo la kuondoa mkanganyiko wa kisheria na changamoto za tafsiri wakati wa utekelezaji wa sheria hizo.
Akiwasilisha taarifa hizo mbele ya Kamati hiyo, inayoongozwa na Dkt. Damas Daniel Ndumbaro, Waziri Ulega amesema Wizara ya Katiba na Sheria imejipanga kuimarisha utawala wa sheria, kulinda haki za binadamu na kuhakikisha wananchi wanapata haki kwa wakati.
Waziri Ulega amesema, hatua hiyo inalenga kuhakikisha kuwa sheria zinazotungwa na kufanyiwa marekebisho nchini zinachochea maendeleo na ustawi wa wananchi.
Aidha, taarifa hizo zinalenga kuimarisha ubora wa sheria kwa kuhakikisha kuwa zinakuwa na ulinganifu, zinaondoa migongano ya kisheria na kupunguza changamoto za tafsiri zinazoweza kujitokeza wakati wa utekelezaji wake.
Wakizungumza katika nyakati tofauti tofauti Wajumbe wa Kamati hiyo wameshauri kuharakishwa kwa mapitio ya taarifa hizo na kufanya maboresho ya Sheria ikiwemo katika mashauri yanayohusu mali ili kuhakikisha haki inatolewa kwa wakati na kulinda haki za wahusika (Watuhumiwa).
Aidha, wameshauri kuwekwa kwa muda maalumu wa kukamilisha uchunguzi wa mashauri hayo, kama ilivyo katika mashauri ya kibiashara, pamoja na kuendeleza matumizi ya mifumo ya TEHAMA katika kuhifadhi kumbukumbu sahihi za mashauri na taarifa za watuhumiwa. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, John Heche, amerejesha majibu kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT), Sheikh Alhad Mussa Salum akipinga madai kuwa CHADEMA ina kiburi au haioni umuhimu wa maridhiano, na kueleza kuwa chama hicho kinataka haki na uwanja sawa wa kisiasa badala ya kuombewa upendeleo.
Akizungumza leo Oktoba 20, 2026 katika mkutano wa hadhara wilayani Karatu mkoani Arusha, Heche ameeleza kuwa CHADEMA ni chama kilichosajiliwa kisheria na kina haki kamili ya kushiriki siasa bila kuomba hisani au kuonekana kinataka kupendelewa.
Akizungumza na chombo cha habari cha Nijuze, Sheikh Alhad alitoa wito CHADEMA kutojiondoa katika mchakato wa maridhiano ya kisiasa, akisisitiza kuwa ushiriki wa chama hicho kikuu cha upinzani ni muhimu kwa amani na maslahi mapana ya taifa. Alisema viongozi wake wanapaswa kutumia busara na kuweka mbele utaifa badala ya maslahi mengine.
"CHADEMA ni chama kikubwa kuliko vingine, sasa chenyewe kuingia kwenye maridhiano ni muhimu, ila kama hakitataka chenyewe hakitaangalia masilahi mapana ya nchi utafanyaje? Lakini chenyewe kuingia kwenye maridhiano, chama hiki ni muhimu kutokana na ukubwa wake. Lakini kama wao hawakuona hawakutanguliza utaifa mbele ikawa wametanguliza vitu vingine unafanyaje?", alihoji Alhad.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, John Heche, amewataka wananchi wa Karatu na Watanzania wote kuungana kwa pamoja kumuombea Mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu, ili aweze kuibuka mshindi wa Tuzo ya Kimataifa ya Haki za Binadamu ya Sakharov (Sakharov Prize for Freedom of Thought).
Akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo Oktoba 20, 2026 wilayani Karatu mkoani Arusha, Heche ameeleza kuwa Bunge la Ulaya limemteua Lissu anayeshikiliwa kwa tuhuma za uhaini, kuwa miongoni mwa watu watatu wa mwisho (finalists) wanaovania tuzo hiyo kubwa duniani, inayotolewa kwa watu waliojitolea maisha yao na kuumia kwa ajili ya kutetea wengine.
Katika kinyang'anyiro hicho, Lissu anashindana na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) pamoja na watetezi wa haki kutoka nchini Iran, ambapo kura ya mwisho ya kuamua mshindi itapigwa tarehe 22 Oktoba.
Akiweka msisitizo juu ya ombi lake la maombi kwa Watanzania, Heche amesema, “Sisi na nyie tunamwombea Tundu Lissu ashinde kwasababu tunajua Lissu ameumizwa sana kwa ajili ya watu wa nchi... Na sisi watu wa Karatu na Watanzania ni mashahidi kwamba Lissu ameumizwa sana katika kupigania demokrasia"This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Waziri wa Madini, Anthony Peter Mavunde, amezitaka nchi za Afrika kuacha kufanya kazi kwa kujitenga na badala yake kuunganisha nguvu katika usimamizi na uendelezaji wa rasilimali za madini ili kukuza viwanda, ajira na uchumi wa bara hilo.
Ameyasema hayo Oktoba 19, 2026 wakati akizungumza katika mjadala wa jopo la Mawaziri kutoka nchi za Tanzania, Nigeria na Liberia uliokuwa na mada isemayo “From Vision to Delivery: Making the African Mining Vision Work for Member States”, katika mkutano wa Kimataifa wa Mining in Motion unaofanyika kwa siku tatu kuanzia Oktoba 19 hadi 21, 2026 jijini Accra Ghana.
Mavunde amesema wakati umefika kwa nchi za Afrika kuweka pembeni tofauti zao na kushirikiana kutekeleza mikakati ya pamoja ya maendeleo ya Sekta ya Madini.
Amesema Afrika ina zaidi ya asilimia 32 ya rasilimali za madini muhimu zinazojulikana duniani, lakini bado sehemu kubwa ya utajiri huo husafirishwa nje ya bara bila kuongezwa thamani ya kutosha na kuwa hali hiyo inanyima nchi za Afrika fursa za kujenga viwanda, kutengeneza ajira na kuongeza mapato.
Akifafanua hatua zinazochukuliwa na Tanzania, Mavunde amesema mageuzi ya kisheria yaliyofanyika mwaka 2017 yameimarisha usimamizi wa rasilimali za madini na ushiriki wa Serikali, huku hatua za kuzuia usafirishaji wa madini ghafi zikichochea uongezaji thamani nchini.
Ameeleza kuwa Tanzania sasa chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ina zaidi ya viwanda vinane vya kusafisha dhahabu na viwanda zaidi ya 16 vya uchakataji na usafishaji wa madini ya metali za msingi na kuwa Sekta ya Madini inachangia asilimia 10.3 ya Pato la Taifa, huku wachimbaji wadogo wakichangia takribani asilimia 40 ya uzalishaji wa sekta hiyo ikiwa ni matokeo ya hatua za dhati za Serikali kuimarisha sekta hiyo.
Katika kuimarisha ushirikiano wa kikanda, Mavunde amezitaja Tanzania, Madagascar na Msumbiji kuwa na fursa ya kuunganisha nguvu katika uendelezaji wa rasilimali za grafiti, uchakataji na uoanisha wa sera ili kujenga mnyororo wa thamani unaowanufaisha wananchi wa nchi hizo.
Amesisitiza kuwa Dira ya Madini ya Afrika haipaswi kubaki kwenye nyaraka na majadiliano, bali inapaswa kuambatana na utekelezaji wa vitendo huku akihimiza nchi wanachama kuimarisha mifumo ya mazungumzo na maamuzi ya pamoja ili kuharakisha utekelezaji wa mikakati iliyokubaliwa.
“Ni wakati sasa kwa Afrika kuanza kufanya kazi pamoja. Afrika ni moja, na tunapaswa kufanya kazi kama timu moja,” amesisitiza Mavunde, akieleza kuwa ushirikiano ni muhimu katika kuhakikisha rasilimali za madini zinachochea maendeleo ya viwanda na ukuaji wa uchumi.
Waziri Mavunde ametoa wito kwa nchi za Afrika kugeuza utajiri wa madini kuwa fursa za viwanda, ajira, teknolojia na mapato zaidi, badala ya kuendelea kuuza madini ghafi na kununua bidhaa zilizoongezwa thamani kutoka nje ya bara hilo.
Awali akifungua rasmi Mkutano huo, Rais wa Jamhuri ya Ghana, John Dramani Mahama amesema kuwa ni muda wa Afrika kugeukia soko la madini muhimu na mkakati kutokana na uhitaji mkubwa wa nishati safi ulimwenguni, lengo ni kuyaongezea thamani madini haya kabla hayajaenda katika soko la dunia. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, John Heche, amewataka Watanzania kuunganisha nguvu na kusimama imara katika kudai Katiba Mpya na mabadiliko ya nchi, akisisitiza kuwa hakuna mamlaka duniani inayotoa haki au mabadiliko bila kushinikizwa.
Akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika leo Oktoba 20, 2026 wilayani Karatu mkoani Arusha, Heche amerejelea nukuu ya mpigania haki za watu weusi kuhusu namna mamlaka zinavyotenda kazi kuweka msisitizo juu ya haja ya wananchi kujitambua na kuchukua hatua.
“Mamlaka haijawahi kuachia kitu chochote bila kushinikizwa. Haijawahi kutokea na haitaka ikatokea, mamlaka zote zinaachia mambo kwa kushinikizwa”, ameeleza Heche akieleza namna ambavyo amekuwa akipiga kelele kuhusu kero mbalimbali za wananchi ikiwamo ubovu wa barabara.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Godbless Lema, amebainisha kuwa lengo kuu la harakati za mabadiliko nchini halipaswi kuwa tu kuiondoa CCM madarakani, bali ni kuhakikisha kuwa chama cha upinzani na wananchi wanaonesha mfano wa uadilifu, tabia njema, na fikra bora kuliko chama tawala.
Akizungumza leo katika mkutano wa hadhara wilayani Karatu mkoani Arusha, Lema amesema kuwa wananchi wanapaswa kuwa makini na kuwachunguza viongozi wa upinzani, badala ya kuwaunga mkono kipofu, ili kuhakikisha kuwa chama kinakuwa baraka ya kweli kwa taifa.
"Lengo la mabadiliko ya nchi hii sio tu kutoa CCM madarakani, ni vilevile sisi tabia zetu, uadilifu wetu, kufikiri kwetu lazima kuwe bora kuliko Chama Cha Mapinduzi, kwasababu tunawakataa Chama Cha Mapinduzi kwasababu ya tabia zao na fikra zao na siyo rangi ya chama chao”, ameeleza Lema.
Aidha amedai kuwa mbinu na msisitizo wa chama hicho tawala wa kushikilia madaraka hautokani tu na kutaka kushinda uchaguzi, bali ni mikakati ya kujilinda dhidi ya mkono wa sheria na magereza.
Katika hatua nyingine, Lema amesisitiza kuwa viongozi wa chama hicho hawana nguvu yoyote kama wananchi hawako nyuma yao kwa vitendo. Ameitaka jamii kujitafakari na kuacha uoga ili kulinda utu na amani ya nchi.
“Hawa viongozi wenu hawana nguvu kama nyinyi hamko nyuma yao... Kaeni nyuma yake kwa vitendo ili siku moja chama hiki kikapate kwenda kuwa baraka”, ameeleza. -
Jambo TV
@Jambotv_
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Godbless Lema, amewataka Watanzania na vijana wanaoikimbilia Katiba Mpya kutambua kuwa mabadiliko ya sheria mama hayatakuwa na tija kama jamii haitabadilika kiutendaji, kiimani na katika kulinda utu wa binadamu.
Akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo Oktoba 20, 2026 wilayani Karatu mkoani Arusha, Lema amesisitiza kuwa wananchi hawapaswi kutarajia katiba pekee iondoe uoga na kutojali pale haki za wenzao au ndugu zao zinapokiukwa.
Akifafanua kuhusu Katiba Mpya, Lema amesema, “Sasa hii hali mbaya kila mtu anaongea katiba mpya. Nawaambia mimi katiba mpya haitakuwa na maana kama wewe hautabadilisha fikra na uwe na tabia mpya kuhusu maisha yako".
Katika mkutano huo, Lema pia amezungumzia uhusiano kati ya Jeshi la Polisi na raia, akibainisha kuwa mfumo na wanasiasa wametengeneza chuki kati ya raia na askari wa usalama waliokula kiapo cha kulinda amani. Amesisitiza kuwa msimamo wa CHADEMA unabaki kuwa kutolipa ubaya kwa ubaya.
"Sisi hatuwezi kulipa ubaya kwa ubaya... Tukifikiri kama wao tukatenda kama wao maanake ni kwamba wanachokifanya sasa ni sahihi. Tunawaambia wanachokifanya sasa siyo sahihi ndio sababu tumechagua kuwa wapinzani tubadilishe namna watu wanavyofikiri na wafikiri kwa upendo na siyo kwa chuki na mauaji", ameeleza Lema.
Aidha, amekosoa vikali mtazamo wa kuchukulia biashara ya bodaboda na bajaji kama ajira rasmi za kuwakomboa vijana kutoka kwenye umaskini, akitaja hatua hizo kama mbinu za kuwakandamiza zaidi.
Lema amesema kugawa pikipiki chache kwa kundi la vijana sio kuwainua kiuchumi bali ni kuendeleza mzunguko wa umaskini, huku akitolea mfano mgomo na maandamano ya madereva wa bajaji yaliyotokea jijini Mbeya kama ishara ya ugumu wa maisha.
"Nilisema hizi bajaji na hizi boda boda siyo ajira. Mnawakusanya huko vijana wanakutana kwa sababu ya ugumu wa maisha. Serikali lazima iwe na ubunifu wa kutosha kuwatoa vijana kwenye umaskini. Mbunge ananunua pikipiki anaita kundi la vijana anawapa pikipiki tano au 10... Pikipiki 10 kwa vijana 20 siyo kuinua vijana ni kuwafanya vijana kuwa maskini", ameeleza Lema.
Vilevile, Lema amewataka wananchi na wanachama kuacha kuchukulia mapambano ya haki na demokrasia kama ushabiki wa michezo ya Simba na Yanga, badala yake wajitokeze kwa vitendo kuunga mkono viongozi na kutetea haki mahakamani. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Serikali ya Tanzania imetangaza kuwa imefanya maboresho makubwa ya kisheria na mabadiliko ya kisera ili kuimarisha udhibiti wa uhalifu wa kupangwa unaovuka mipaka na kufanikisha utekelezaji madhubuti wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa.
Hayo yamebainishwa tarehe 19 Oktoba 2026 mjini Vienna, Austria, na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Zainab Katimba alipomwakilisha Waziri wa Katiba na Sheria katika Kikao cha 13 cha Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa Dhidi ya Uhalifu wa Kupangwa Unaovuka Mipaka (Conference of the Parties to the United Nations Convention against Transnational Organized Crime).
Katimba ameeleza kuwa miongoni mwa hatua madhubuti zilizochukuliwa ni pamoja na kuimarisha uwezo wa taasisi zinazosimamia utekelezaji wa mkataba huo hapa nchini. Taasisi hizo zinajumuisha Jeshi la Polisi, Idara ya Uhamiaji, Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (NPS), Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), pamoja na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (PCCB).
Amesema hatua hizo zimeleta mafanikio makubwa kupitia ushirikiano wa karibu na mashirika ya kikanda na kimataifa kama vile INTERPOL, UNODC, SADC, na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
Katika kikao hicho, ambacho hufanyika kila baada ya miaka miwili ili kutathmini utekelezaji wa mkataba huo, Tanzania iliwasilisha maeneo yake ya kipaumbele yanayohitaji mkazo wa pamoja, nayo ni ushirikiano wa kisheria na urejeshaji wa wahalifu au watuhumiwa, uchunguzi wa kifedha na urejeshaji wa mali zinazotokana na uhalifu, na msaada wa kitaalamu na ujenzi wa uwezo wa kiutendaji kwa watendaji.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Serikali ya Tanzania imetangaza kuwa imefanya maboresho makubwa ya kisheria na mabadiliko ya kisera ili kuimarisha udhibiti wa uhalifu wa kupangwa unaovuka mipaka na kufanikisha utekelezaji madhubuti wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa.
Hayo yamebainishwa tarehe 19 Oktoba 2026 mjini Vienna, Austria, na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Zainab Katimba alipomwakilisha Waziri wa Katiba na Sheria katika Kikao cha 13 cha Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa Dhidi ya Uhalifu wa Kupangwa Unaovuka Mipaka (Conference of the Parties to the United Nations Convention against Transnational Organized Crime).
Katimba ameeleza kuwa miongoni mwa hatua madhubuti zilizochukuliwa ni pamoja na kuimarisha uwezo wa taasisi zinazosimamia utekelezaji wa mkataba huo hapa nchini. Taasisi hizo zinajumuisha Jeshi la Polisi, Idara ya Uhamiaji, Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (NPS), Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), pamoja na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (PCCB).
Amesema hatua hizo zimeleta mafanikio makubwa kupitia ushirikiano wa karibu na mashirika ya kikanda na kimataifa kama vile INTERPOL, UNODC, SADC, na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
Katika kikao hicho, ambacho hufanyika kila baada ya miaka miwili ili kutathmini utekelezaji wa mkataba huo, Tanzania iliwasilisha maeneo yake ya kipaumbele yanayohitaji mkazo wa pamoja, nayo ni ushirikiano wa kisheria na urejeshaji wa wahalifu au watuhumiwa, uchunguzi wa kifedha na urejeshaji wa mali zinazotokana na uhalifu, na msaada wa kitaalamu na ujenzi wa uwezo wa kiutendaji kwa watendaji.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Godbless Lema, amewataka vijana wanaopigania mabadiliko nchini kujitafakari tabia zao na kuthamini maisha yao binafsi wakati wakiitaka Tanzania mpya.
Akizungumza leo Oktoba 20, 2026 katika mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika wilayani Karatu mkoani Arusha, Lema amesema kuwa mabadiliko ya kisiasa na Katiba Mpya hayatakuwa na tija kama wananchi na vijana hawatabadilisha fikra zao na kuwa na tabia mpya kuhusu maisha.
Kiongozi huyo pia ameonya kuhusu athari mbaya za matumizi ya pombe kwa afya ya vijana, akibainisha kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye wagonjwa wengi wa kisukari, wengi wao wakiwa ni vijana chini ya miaka 40, na pia matatizo ya figo yameendelea kuwakuba vijana.
Kuhusu suala la uchumi na ajira, Lema amekosoa mtazamo wa kuhesabu biashara za bodaboda na bajaji kama ajira rasmi za kuondoa umaskini. Amebainisha kuwa hatua ya wabunge au viongozi kutoa pikipiki kwa vijana si kuwainua kiuchumi bali ni kuwafanya waendelee kuwa maskini.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Jeshi la Polisi Tanzania limetoa wito kwa wananchi wanaomiliki silaha haramu kutumia siku 11 zilizobaki za msamaha wa Serikali kuzisalimisha kwa hiari kabla ya kuanza kwa msako mkali nchi nzima kuanzia tarehe 1 Novemba 2026.
Taarifa iliyotolewa leo Oktoba 20, 2026 na Msemaji wa Jeshi la Polisi, DCP David Misime, inaeleza kuwa tangu kuzinduliwa kwa kampeni hiyo ya Kitaifa tarehe 31 Agosti 2026 na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Paschal Katambi, jumla ya silaha 230 zimeshasalimishwa hadi kufikia tarehe 19 Oktoba 2026. Silaha hizo zinajumuisha AK 47 tano (05), Rifle 15, Shotgun 50, Mk IV mbili (02), Bastola nane (08) na Magobole 150
“Kuanzia tarehe 01/11/2026, Jeshi la Polisi litaendesha misako nchi nzima ili kuwakamata na kuwachukulia hatua za kisheria watu wote watakao kutwa wanamiliki silaha haramu na walishindwa kutumia miezi hii miwili ya msamaha”, ameeleza DCP Misime.
Akiikumbusha jamii kuhusu adhabu kali zinazowakabili wanaokiuka sheria hiyo, Msemaji wa Jeshi la Polisi ameongeza, “Kifungu cha 62 cha Sheria ya Udhibiti wa Silaha na Risasi, Sura ya 223 marejeo ya mwaka 2023, kinatoa adhabu ya kifungo cha miaka 10 jela au faini ya shilingi milioni 15 au vyote kwa pamoja kwa mtuhumiwa atakayekutwa na silaha kinyume cha sheria na kutiwa hatiani na mahakama”.
Jeshi la Polisi limesisitiza kuwa katika vipindi vya msamaha vya miaka ya nyuma (2023, 2024 na 2025), baadhi ya wananchi waliidharau fursa hiyo na baadaye kukamatwa na kufungwa miaka 10 jela baada ya muda wa msamaha kwisha. Kwa mfano, kati ya Novemba 2023 na Agosti 2024, jumla ya watuhumiwa 176 walihukumiwa kifungo hicho. Vilevile, watuhumiwa 161 walihukumiwa miaka 10 jela kati ya Novemba 2024 na Agosti 2025, huku watuhumiwa wengine 172 wakihukumiwa kifungo hicho kati ya Novemba 2025 na Agosti 2026.
Pia, Jeshi la Polisi limewasihi wamiliki halali wa silaha wanaokabiliwa na changamoto za umri mkubwa au afya kuzisalimisha ili zisiangukie mikononi mwa watu wasiostahili. Wamiliki halali wote pia wamehimizwa kufika katika Vituo vya Polisi vya Wilaya kufanya uhakiki wakiwa na silaha, leseni, na picha moja ya pasipoti.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Kaskazini kimelaani vikali kitendo cha uvamizi na uharibifu ulioelezwa na kuonekana kutokea katika ofisi ya chama hicho Jimbo la Hai, mkoani Kilimanjaro, usiku wa kuamkia tarehe 20 Oktoba 2026.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Idara ya Habari ya CHADEMA Kanda ya Kaskazini kupitia kwa Katibu wa CHADEMA Kanda ya Kaskazini, Yohana Kaunya, watu wasiojulikana wameivamia ofisi hiyo, wakafanya uharibifu, wakapaka rangi na kufuta maandishi yaliyokuwa katika jengo hilo yenye ofisi hiyo iliyozinduliwa rasmi hivi karibuni na Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Heche.
"Kitendo hiki ni cha kulaaniwa na hakipaswi kuvumiliwa katika jamii inayozingatia misingi ya amani, demokrasia, utawala wa sheria na kuheshimu haki za wengine", ameeleza Kaunga.
Ameongeza kuwa tofauti za kisiasa hazipaswi kuwa sababu ya mtu au kikundi chochote kujichukulia sheria mkononi, kuharibu mali za wengine, au kuzuia shughuli halali za vyama vya siasa.
CHADEMA Kanda ya Kaskazini imeliomba Jeshi la Polisi nchini kuchukua hatua za haraka ikiwemo kufanya uchunguzi wa kina ili kuwabaini na kuwakamata wahusika wote ili wafikishwe mbele ya vyombo vya sharia, kuimarisha ulinzi katika ofisi za vyama vya siasa na mali za raia na kuhakikisha ulinzi na haki sawa kwa kila raia na kila chama cha siasa chini ya sheria za nchi pamoja na kutoa taarifa kwa umma kuhusu hatua zinazochukuliwa katika uchunguzi wa tukio hilo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Bunge la Ulaya limetangaza wateule watatu wa mwisho (finalists) wanaowania Tuzo ya Sakharov Prize for Freedom of Thought. Orodha hiyo inajumuisha Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC), kiongozi wa upinzani nchini Tanzania Tundu Lissu, na wanawake wawili wa Iran waliohukumiwa adhabu ya kifo katika nchi yao.
Wateule hao wa mwisho wa Tuzo ya Andrei Sakharov ya Mwaka 2026 walichaguliwa na Wajumbe wa Bunge la Ulaya siku ya Jumatatu, Oktoba 19, mjini Strasbourg nchini Ufaransa. Rais wa Bunge la Ulaya, Roberta Metsola, atamtangaza mshindi rasmi tarehe 22 Oktoba.
Mahakama ya ICC, majaji wake, mawakili, na wafanyakazi wake walipendekezwa kuwania tuzo hiyo kutokana na uchunguzi wao kuhusu mauaji ya kimbari, makosa ya kivita, na makosa dhidi ya ubinadamu. Mahakama hiyo ipo chini ya shinikizo kubwa kutoka kwa Rais wa Marekani Donald Trump, ambaye aliweka vikwazo dhidi ya mahakama hiyo na wafanyakazi wake, na kuagiza kuzuiliwa kwa rasilimali zao na kadi zao za mikopo nchini Marekani.
Tundu Lissu, ambaye yupo gerezani tangu mwaka 2025 na anayeongoza chama cha upinzani nchini Tanzania, CHADEMA, yupo katika hatihati ya kukabiliwa na adhabu ya kifo kwa kosa la uhaini. Vyama vya European People's Party (EPP) na European Conservatives and Reformists (ECR), vilivyomteua, vilifafanua uamuzi wao kwa kutaja jitihada za Lissu katika kupigania uchaguzi huru, mahakama inayojitegemea, na kukomesha ghasia za kisiasa nchini Tanzania.
Zaidi ya hayo, mabinti wawili wa tumbo moja, Taraneh na Romina Rahimi, waliohukumiwa adhabu ya kifo nchini Iran, waliteuliwa kama wawakilishi wa maandamano ya mwaka huu nchini humo. Uteuzi wao ulipendekezwa na kundi la Patriots for Europe, linalojumuisha wanasiasa wa mrengo wa kulia wa Ufaransa.
David McAllister, Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la Ulaya na mwanachama wa EPP, amesema: "Kipindi hiki cha vita na ongezeko la ukandamizaji, wale wanaopaza sauti zao kwa ajili ya uhuru wanahitaji kujua kwamba wana washirika. Tuzo ya Sakharov inasaidia kufanya sauti zao zisikike. Ujasiri wao unatukumbusha kwamba haki za binadamu lazima ziongoze sera zetu za mambo ya nje, hasa pale ambapo ulinzi wake unapokuwa na changamoto za kisiasa."
Tuzo ya Andrei Sakharov ya Uhuru wa Mawazo itatolewa rasmi tarehe 16 Desemba mjini Strasbourg, Ufaransa. Tangu mwaka 1988, Bunge la Ulaya limekuwa likitoa tuzo hiyo kwa watu binafsi na mashirika yanayotetea haki za binadamu na uhuru wa kujieleza. Zawadi ya fedha taslimu ni Euro 50,000 (takriban Shilingi za Kitanzania Milioni 145). Mwaka jana, tuzo hiyo ilitolewa kwa waandishi wa habari kutoka nchi za Belarus na Georgia. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Kenani Kihongosi, ametoa wito kwa viongozi na wanachama wa chama hicho kuzingatia kwa dhati maadili ya CCM kupitia usomaji na uelewa wa kina wa katiba na misingi yake ya uongozi.
Akizungumza leo, Oktoba 19, 2026, wakati wa ufunguzi wa mafunzo maalum kwa ajili ya viongozi na wanachama wa CCM mkoani Arusha, Kihongosi amewakumbusha viongozi hao kujiepusha na tabia za kuiga mwenendo au kauli zinazotolewa na wanasiasa wa vyama vingine vya upinzani kwenye majukwaa ya kisiasa.
Aidha, Kihongosi amesisitiza kuwa viongozi wa CCM wanapaswa kulinda hadhi na heshima yao kila wanaposhiriki shughuli za starehe au za kijamii, akionya dhidi ya tabia au mwenendo wowote unaoweza kukidhalilisha chama au kuleta taswira hasi ya kimaadili mbele ya jamii.
Amesisitiza kuwa msingi wa kiongozi bora ni kuishi kwa kufuata maadili ya chama ama iwe kwenye siasa au katika maisha binafsi ili kuendelea kuwa kioo na mfano wa kuigwa na jamii nzima.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Wakati visa vya Ebola vikiongezeka nchini Kenya na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Tanzania imeimarisha uchunguzi wa afya katika viwanja vya ndege, bandari na vituo vya mipakani, katika hatua ya kuzuia kitisho cha virusi hivyo kuingia na kusambaa nchini.
Hatua hiyo inakuja baada ya Kenya kuthibitisha kisa kipya cha Ebola, kilichofikisha jumla ya watu wanane walioambukizwa kufikia Oktoba 18, 2026, huku mlipuko huo nchini DRC ukiripotiwa kuenea katika mikoa nane.
Kwa mujibu wa mamlaka za afya nchini Kenya, mgonjwa huyo mpya alipata maambukizi baada ya kukaribiana na kisa cha kwanza kilichoripotiwa nchini humo. Mgonjwa wa kwanza alikuwa raia wa Kenya aliyerejea kutoka DRC akiwa ameambukizwa Ebola na kufariki dunia muda mfupi baada ya kuwasili.
Tangu wakati huo, maambukizi mapya yameripotiwa miongoni mwa wahudumu wa afya na watu wengine waliokuwa na mawasiliano ya karibu na mgonjwa huyo.
Kwa upande wa DRC, mlipuko huo umefikia mikoa minane, ukiwemo Nord Ubangi, uliopo kaskazini magharibi mwa nchi hiyo na unaopakana na Jamhuri ya Afrika ya Kati. Nchini humo, visa viwili vimeripotiwa, huku kifo kimoja kikithibitishwa.
Kufuatia hali hiyo, Serikali ya Tanzania imechukua hatua za kuimarisha ufuatiliaji wa afya ya wasafiri wanaoingia nchini, kwa lengo la kubaini mapema watu wanaoweza kuwa na maambukizi na kuzuia kusambaa kwa ugonjwa huo.
Hatua hizo zimeainishwa katika Mwongozo wa Ushauri kwa Wasafiri Na. 18 wa Oktoba 17, 2026, uliosainiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Grace E. Magembe, ambao umeanza kutumika mara moja.
Kwa mujibu wa mwongozo huo, wasafiri wanatakiwa kujaza Fomu ya Ufuatiliaji wa Afya ya Msafiri kupitia tovuti maalumu kabla ya safari ya kuja Tanzania au wanapowasili. Pia wanapaswa kuhifadhi msimbo wa QR au namba ya kumbukumbu watakayopewa kwa ajili ya uhakiki katika vituo vya kuingilia nchini.
Katika maeneo hayo, wasafiri watafanyiwa uchunguzi wa afya, ikiwemo kupimwa joto la mwili. Wale watakaobainika kuwa na dalili za Ebola au magonjwa mengine ya kuambukiza watahudumiwa kwa kuzingatia miongozo ya kitaifa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Jeshi la Polisi nchini limewataka madereva wa magari ya abiria kuzingatia sheria za usalama barabarani, huku abiria wakihimizwa kutokukaa kimya wanapobaini mienendo hatarishi ya madereva, ikiwemo ukiukwaji wa sheria unaoweza kusababisha ajali zinazoweza kuzuilika.
Wito huo umetolewa na Afisa Mnadhimu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Makao Makuu, ACP Desdery Rugimbana, katika Kituo Kikuu cha Mabasi mkoani Tabora, wakati wa utoaji wa elimu ya usalama barabarani kwa madereva na abiria, akisisitiza kuwa abiria hawapaswi kukubali kusafiri wakiwa wamekaa chini kutokana na msongamano wa abiria ndani ya magari.
Kwa upande wake, Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Tabora, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi Peter Magayane, amewataka madereva na abiria kuchukua tahadhari zaidi barabarani, hususan katika kipindi kijacho kinachotarajiwa kuwa na mvua za El Niño, ambazo zinaweza kuongeza changamoto za usalama barabarani.
Baadhi ya abiria waliopatiwa elimu hiyo Elizabeth James , wameeleza utayari wao wa kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za madereva wanaokiuka sheria, huku wakiiomba serikali kuhakikisha hatua kali za kisheria zinachukuliwa dhidi ya madereva watakaobainika kufanya makosa hayo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Ufaransa inaendelea kushuhudia mojawapo ya ghasia kubwa zaidi katika miaka ya hivi karibuni. Maandamano yaliyoanza kama malalamiko madogo ya wanafunzi wa sekondari yamegeuka kuwa vurugu za kitaifa zenye athari kubwa kwa mali, usalama na siasa za nchi hiyo.
Vuguvugu hili lilianza katikati ya mwezi Septemba 2026 katika Shule ya Sekondari ya Saint-Exupéry, iliyopo kitongoji cha Créteil karibu na Jiji la Paris. Wanafunzi walitoka mitaani kuunga mkono walimu wao waliofanya mgomo kutokana na uchache wa walimu na ukosefu wa rasilimali za shule.
Malalamiko yao makuu yalihusu pia idadi kubwa ya wanafunzi madarasani, majengo yaliyochakaa, ratiba ndefu za masomo na mfumo mgumu wa kuomba nafasi za vyuo vikuu. Ndani ya siku kumi pekee, harakati hizo zilienea kwa kasi kutoka shule moja hadi shule kadhaa na miji zaidi ya arobaini nchini humo, huku wanafunzi wa vyuo vikuu, walimu na vyama vya wafanyakazi wakijiunga nazo.
Mnamo Oktoba 1, mgomo wa wanafunzi uliathiri zaidi ya shule 700, na kufikia Oktoba 13 walirejea tena mitaani wakisisitiza kuendelea na mapambano mpaka serikali itakapotimiza ahadi zote.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Serikali ya Tanzania imesisitiza dhamira yake ya kuendelea kushirikiana na madhehebu ya dini nchini, ikitambua mchango wake katika malezi ya kiroho, utoaji wa huduma za kijamii na kuimarisha amani na mshikamano wa kitaifa.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Mahusiano, Deus Sangu aliyemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika ibada takatifu ya kumweka wakfu Askofu John Jumanne Wambura wa Kanisa la Mennonite Tanzania (KMT), iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa juma.
Akizungumza katika ibada hiyo, Sangu amesema viongozi wa dini wameendelea kuwa nguzo muhimu katika kutoa mafundisho, ushauri na malezi bora, pamoja na kuwahudumia wananchi wenye mahitaji maalumu, wakiwemo yatima, wajane na watu wenye ulemavu.
Amesema Serikali inatambua mchango wa taasisi za dini katika sekta za afya, elimu na huduma nyingine za kijamii, hususan katika maeneo ya pembezoni, na kwamba ushirikiano huo ni muhimu katika kuharakisha maendeleo ya wananchi. Aidha, amewataka viongozi wa dini kuendelea kuliombea Taifa na kuhamasisha jamii kulinda amani iliyopo nchini, akisisitiza kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu iko tayari kushirikiana na wadau wote katika kuimarisha mshikamano na maendeleo ya Taifa.
Kwa upande wake, Askofu Mkuu wa Kanisa la Mennonite Tanzania, Nelson Kisare, amewataka viongozi kutumia nafasi walizopewa kwa manufaa ya watu wanaowaongoza na jamii kwa ujumla, badala ya kujinufaisha binafsi. Amesema viongozi wanapaswa kuwa vielelezo vya maadili mema na matendo yanayojenga jamii.
Naye, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo amelishukuru Kanisa la Mennonite kwa kuendelea kuliombea taifa na kuchangia juhudi za kudumisha amani nchini. -
Jambo TV
@Jambotv_
Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu Dodoma, imeamuru kusimamishwa kwa mwenendo wa shauri la nidhamu linalomkabili Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Wakili Boniface Anyisile Mwabukusi mbele ya Kamati ya Taifa ya Mawakili, hadi shauri la kikatiba alilofungua Mahakamani hapo litakaposikilizwa na kutolewa uamuzi wa mwisho.
Uamuzi huo umetolewa Oktoba 19, 2026, na jopo la majaji watatu, likiongozwa na A.R. Mruma, S.H. Hassan na Irene Musokwa, katika shauri la kikatiba namba 25918 la mwaka 2026, lililofunguliwa na Mwabukusi dhidi ya Kamati ya Taifa ya Mawakili, Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mwita Nashon.
Katika uamuzi wake, Mahakama imesema kusimamishwa kwa shauri hilo la nidhamu kunalenga kulinda hali iliyopo na kuzuia uwezekano wa taasisi hizo mbili zinazoshughulikia haki za wahusika kutoa maamuzi yanayoweza kukinzana, jambo ambalo lingeweza kuwa na athari kwa usimamizi wa haki nchini.
Mahakama imeeleza kuwa Kamati ya Taifa ya Mawakili ni chombo halali chenye mamlaka ya kutekeleza majukumu ya kimahakama, lakini shauri la kikatiba lililopo mbele ya Mahakama Kuu linapaswa kuamuliwa kwanza kabla mwenendo wa nidhamu haujaendelea, huku ikisisitiza kuwa kusimamishwa huko hakumaanishi upande wowote utanyimwa haki.
Wakati huohuo, Mahakama imekataa ombi la Mwita Nashon la kutaka majaji hao wajiondoe katika kusikiliza shauri hilo, ikieleza kuwa kutoridhishwa na maamuzi ya awali ya Mahakama hakutoshi kuwa sababu ya kisheria ya kuwataka majaji kujiondoa, bila kuwepo mazingira yanayoonesha uwezekano halisi wa upendeleo.
Aidha, Mahakama imekataa ombi la kutaka Mwenyekiti au mjumbe wa Kamati ya Taifa ya Mawakili aitwe Mahakamani kujieleza kuhusu madai ya kutokutii amri ya Mahakama, ikieleza kuwa madai ya dharau kwa Mahakama yaliyotokea nje ya Mahakama yanahitaji kufunguliwa kwa utaratibu rasmi, kupitia maombi yanayoambatana na hati ya kiapo inayoeleza madai hayo.
Mahakama imeahirisha shauri hilo hadi Novemba 10, 2026, saa nne asubuhi, kwa ajili ya kutajwa na kupokea maelekezo zaidi, huku amri ya kusimamisha mwenendo wa shauri la nidhamu dhidi ya Mwabukusi ikiendelea kutumika hadi shauri la kikatiba litakapoamuliwa kwa ukamilifu. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kagera linawashikilia askari 13, wakiwemo askari watatu wa Shirifisho la Hifadhi za Taifa (TANAPA), askari sita wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), na askari mgambo wanne, kwa tuhuma za kuhusika na vifo vya watu wane katika Kijiji cha Kanyamika, kilichoko wilayani Muleba.
Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Blasius Chatanda, aliyoitoa jana Jumapili, Oktoba 18, 2026, tukio hilo la kusikitisha lilitokea tarehe 17 Oktoba 2026, majira ya saa 4:00 asubuhi, wakati kikosi hicho kilipokuwa katika doria ya kikazi ndani ya Hifadhi ya Misitu ya Ruiga.
Taarifa za awali zinaeleza kuwa vurugu ziliibuka baada ya askari hao kuwazuia watu waliokuwa wakisafirisha mkaa kwa kutumia pikipiki zipatazo kumi, ambapo inadaiwa kuwa watuhumiwa waligoma kukamatwa na kujaribu kuwanyang'anya silaha ya kivita ya aina ya AK-47 askari waliokuwepo eneo la tukio.
Kufuatia mapambano hayo, shambulio lililofuata lilisababisha vifo vya watu watatu papo hapo, ambao ni Osward Yuster (38), Pius Charles (40), na Charles Michael (35), huku mtu wa nne, Edgar Elias Lukangula (44), akipoteza maisha tarehe 18 Oktoba 2026 akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera. Katika tukio hilo la ghasia, gari moja la Serikali mali ya TFS aina ya Toyota Landcruiser liliharibiwa vibaya.
Hadi kufikia sasa, Jeshi la Polisi limefanikiwa kukamata pikipiki 10, magunia 22 ya mkaa, mapanga matano, pamoja na silaha na risasi zilizotumiwa katika tukio hilo. Sambamba na uchunguzi unaoendelea, polisi limetoa wito mkubwa kwa wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi ama kupambana na vyombo vya ulinzi wakati wa utekelezaji wa sheria.
VIDEO CREDIT: AZAM TV.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Dar es Salaam, Nasra Mohamed @comrade_nasra_mohamed, amewasihi viongozi na makada wa chama hicho kuwakumbatia na kuwapa nafasi wanachama pamoja na vijana kutoa maoni yao kwa uhuru kamili, bila kuwa na hofu ya kutofautiana mitazamo kutokana na misimu ya uchaguzi.
Nasra ametoa rai hiyo mwishoni mwa wiki alipokuwa akizungumza na makada wa CCM na wajumbe wa mikutano mikuu ya kata za Miburani, Azimio, Tandika, Temeke 24, na Mtoni. Amesisitiza umuhimu mkubwa wa wanachama kushirikiana na kuheshimiana hata wanapokuwa na mitazamo au maoni tofauti kuhusu wagombea mbalimbali, akionya kuwa viongozi wanapaswa kuepuka tabia ya kuwabagua wanachama kwa misingi ya uchaguzi uliopita.
Aidha, amewakumbusha wote wenye malalamiko kutumia misingi na vikao halali vya chama kutafuta ufumbuzi, huku akihakikisha kila mwanachama anapata fursa ya kusikilizwa. Mwenyekiti huyo amewataka wanachama kuweka mbele umoja na ustawi wa chama badala ya migawanyiko ya uchaguzi, akisisitiza ukweli kwamba viongozi huja na kuondoka lakini mshikamano wa wanachama unabaki.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limethibitisha kutokea kwa tukio la mauaji ya Humphrey Elisamon Msoka (63), aliyejeruhiwa vibaya kichwani kwa panga na mtoto wa mdogo wake, kabla ya mtuhumiwa huyo naye kushambuliwa na wananchi na kufariki dunia akiwa njiani kupelekwa hospitali.
Tukio hilo limetokea tarehe 18 Oktoba, 2026, katika eneo la Mungu Mwema, Mtaa wa Hongoro, Kibamba Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam.
Kulingana na taarifa rasmi iliyotolewa leo Oktoba 19, 2026 na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Jumanne Muliro, marehemu Humphrey Elisamon alishambuliwa na kujeruhiwa kichwani na kijana aitwaye Dickson Elimringi Msoka (22), mkazi wa Hongoro, ambaye ni mtoto wa mdogo wa marehemu.
“Mtuhumiwa huyo baada ya tukio alishambuliwa na wananchi kabla ya Polisi kufika akiwa katika hali mbaya na baadaye alipoteza maisha akiwa anapelekwa hospitali”, ameeleza Kamanda Muliro akiongeza kuwa uchunguzi zaidi unaendelea kuhusiana na tukio hilo.
Kufuatia tukio hilo, Jeshi la Polisi limetoa wito kwa jamii kujiepusha na tabia ya kujichukulia sheria mkononi na badala yake kutumia vyombo na mamlaka halali za kisheria, kijamii, kiuchumi na kidini katika kutatua migogoro. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Wananchi wa vijiji vya Magomeni na Majimaji, Jimbo la Tunduru Kaskazini, wameiomba Serikali kuingilia kati migogoro kati yao na wafugaji, wakilalamikia kuendelea kwa vitendo vya vurugu vinavyohatarisha maisha na usalama wao.
Wakizungumza katika mkutano na Mbunge wa Tunduru Kaskazini, Ado Shaibu Ado, jana Oktoba 18, 2026 Wananchi hao wamedai kuwa baadhi ya wafugaji wamekuwa wakivamia mashamba na makazi yao, kuharibu mazao, kuwaibia mifugo na kuwashambulia, huku wengine wakidaiwa kuuawa na kujeruhiwa.
Wananchi hao wameeleza kutoridhishwa na hatua zinazochukuliwa na vyombo vya dola, wakidai kuwa mtu aliyemjeruhi mfugaji kidole alikamatwa na polisi, lakini watu wanaowatuhumu kuhusika na vifo vya ndugu zao bado hawajakamatwa.
Wamesema hali hiyo imezua hofu kubwa katika jamii, kiasi cha baadhi ya wakulima kushindwa kuendelea na shughuli zao za kilimo, huku wananchi wakihofia kutembea nyakati za usiku na wazazi wakiwa na wasiwasi kuhusu usalama wa watoto wao wanapokwenda shuleni.
Kutokana na hali hiyo, wananchi hao wamemsihi mbunge wao kufuatilia suala hilo ili Serikali ichukue hatua za kurejesha amani na usalama katika maeneo yao, wakisisitiza umuhimu wa vyombo vya dola na sungusungu kushirikiana kukabiliana na changamoto hiyo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu wa Rais wa Tanzania, Deogratius John Ndejembi, amekubali ombi la Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, la kuwa mlezi wa mchezo wa mpira wa kikapu nchini, akiahidi kushirikiana na wadau kuukuza mchezo huo.
Ndejembi ametoa kauli hiyo Jumapili, Oktoba 18, 2026, alipokuwa mgeni rasmi katika fainali ya mpira wa kikapu kati ya Dar City na Stein Warriors, iliyofanyika katika Uwanja wa International School of Tanganyika (IST), Masaki, Dar es Salaam.
Amesema anatamani kuona mpira wa kikapu ukifikia kiwango cha ushindani na umaarufu wa soka nchini, hususan ushindani unaozikutanisha timu za Simba, Yanga na Azam FC.
“Lengo langu ni kuona siku moja mpira wa kikapu unapiga hatua kubwa kama mpira wa miguu ulivyo kwa Yanga na Simba. Hili litawezekana ikiwa wadhamini watajitokeza kuwekeza na vijana wataonyesha utayari wao,” amesema Ndejembi.
Amesema amekubali jukumu hilo kutokana na upendo wake kwa mchezo huo na dhamira ya kuona unapiga hatua kubwa nchini.
Awali, Makonda alisema miongoni mwa malengo yake ni kuona kunajengwa viwanja vikubwa vitatu vya michezo (arenas) vitakavyowezesha Tanzania kuandaa mashindano mbalimbali na kukuza sekta ya michezo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Wananchi wa Kitongoji cha Songambele, Kata ya Masonya, Wilaya ya Tunduru, mkoani Ruvuma, wamelalamikia ukosefu wa shule katika eneo lao, wakisema watoto wanalazimika kutembea umbali mrefu kufuata elimu, hali inayochangia baadhi yao kukosa masomo.
Wakizungumza Oktoba 18, 2026, wananchi hao, wakiwemo wazazi na viongozi wa kitongoji, wamesema idadi ya watoto wanaohitaji elimu katika eneo hilo ni kubwa, hivyo wanahitaji shule yao badala ya kuelekezwa Magomeni, ambako wanasema idadi ya watoto ni ndogo.
Baadhi ya wazazi wameeleza hofu yao kuhusu mustakabali wa elimu ya watoto wao, wakiiomba Serikali na viongozi husika kuweka kipaumbele katika ujenzi wa shule Songambele ili kuwawezesha watoto kupata elimu bila vikwazo vya umbali.
Akijibu kero hizo, Mbunge wa Tunduru Kaskazini, Ado Shaibu, amesema wananchi hawazuiwi kushiriki katika ujenzi wa shule na kusisitiza kuwa haikubaliki kwa watoto kutembea umbali wa kilomita tano hadi saba kufuata elimu katika mazingira ya sasa.
Shaibu amesema atakuwa mstari wa mbele kuhakikisha wananchi wanapata shule katika eneo lao, akieleza kuwa iwapo Serikali itachelewa kutatua changamoto hiyo, wananchi wanaweza kushirikiana kujenga shule yao wenyewe.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Kongamano la Nne la Kitaifa la Uboreshaji wa Huduma za Maktaba litakalofanyika Oktoba 20 hadi 22, mwaka huu, katika viwanja vya Maktaba Kuu ya Taifa, jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania (TLSB), Dkt. Mboni Ruzegea, amesema kongamano hilo litajadili namna ya kuboresha huduma za maktaba kupitia mageuzi ya kidijitali, kwa lengo la kukuza maarifa na ujuzi kwa maendeleo endelevu. Amesema mkutano huo utawakutanisha wadau wa serikali na sekta binafsi, wachapishaji, waandishi, wasomaji na washirika wa maendeleo.
“Kaulimbiu yetu imejikita katika maboresho ya huduma za maktaba kupitia mageuzi ya kidijitali, kukuza maarifa na ujuzi kwa maendeleo endelevu,” alisema Dkt. Ruzegea wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya kongamano hilo.
Alisema moja ya matukio makubwa yatakayofanyika ni uzinduzi wa Mfumo Jumuishi wa Maktaba Mtandao ya Taifa (Integrated National Digital Library System), pamoja na programu tumishi itakayowawezesha wananchi kupata huduma za maktaba kupitia simu za mkononi. Hatua hiyo inalenga kurahisisha upatikanaji wa machapisho na taarifa kwa kutumia teknolojia, sambamba na mwelekeo wa taifa wa kuimarisha matumizi ya kidijitali.
Dkt. Ruzegea alifafanua kuwa mfumo huo hautamaanisha kila kitabu kitapatikana chote mtandaoni, akisema machapisho yanayolindwa na hakimiliki yatahitaji utaratibu maalumu wa makubaliano na wenye haki hizo. Aidha, kongamano hilo litatambulisha maboresho ya sheria ya huduma za maktaba na kanuni zake, zitakazowapa wadau nafasi ya kutoa maoni kuhusu utekelezaji wa huduma hizo katika mazingira ya kidijitali.
Alisema maktaba za ana kwa ana, zikiwemo za mikoa, wilaya na jamii, zitaendelea kutoa huduma kwa wananchi wasio na intaneti, huku kongamano likijadili namna ya kuziimarisha kwa kuzipatia vitabu, wataalamu na mazingira bora ya kujifunzia. Aliongeza kuwa taasisi zitaunganishwa kwenye mfumo wa kidijitali kwa awamu kulingana na utayari wake.
Kongamano hilo pia litaambatana na Tamasha la Vitabu na Usomaji, maonyesho ya machapisho na mijadala kuhusu maendeleo ya maktaba za jamii. Vilevile, litaadhimisha miaka 37 ya chuo cha mafunzo ya ukutubi kinachohusishwa na TLSB, pamoja na kuanzisha jukwaa la Partnership Marketplace litakalowakutanisha wadau na washirika kwa ajili ya kuendeleza miradi ya maktaba.
Dkt. Ruzegea alisema kongamano hilo litafuatia mkutano wa siku moja wa wakutubi wakuu kutoka taasisi za serikali na binafsi, utakaofanyika Oktoba 19 kujadili uendeshaji wa huduma za maktaba. Alisema baada ya kongamano, maazimio yatakayofikiwa yatawekewa vipimo na kufuatiliwa ili kuhakikisha yanatekelezwa. Kongamano hilo ni la nne baada ya yaliyofanyika mwaka 2021, 2022 na 2023, na ushiriki wake ni bure kwa wananchi na wadau wote. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Familia ya Yusuph Rashid Salumu, mkulima aliyeuawa kufuatia vurugu katika Kijiji cha Majimaji, Wilaya ya Tunduru, mkoani Ruvuma, imemuomba Rais Samia Suluhu Hassan kuingilia kati mgogoro kati ya wakulima na wafugaji unaodaiwa kuhatarisha usalama wa wananchi katika eneo hilo.
Familia hiyo imesema marehemu alishambuliwa na watu wanaodaiwa kuwa wafugaji alipokuwa akirejea nyumbani kutoka shambani, Oktoba 8, 2026 hali iliyosababisha kifo chake Oktoba 10, 2026 na kuwaacha watoto wake wawili katika mazingira magumu.
Mke wa marehemu, Zabibu Abasi Muhammedi, amesema mumewe alikuwa akitoka katika mashamba ya Angalinje kuelekea nyumbani alipovamiwa.
Alisema marehemu alijaribu kujiokoa kwa kukimbia na kuacha baiskeli pamoja na vifaa vyake, kabla ya familia kupata taarifa kuwa alikuwa hospitalini.
Kwa upande wake, ndugu wa marehemu, Muhidini Twalibu Amadi, ameiomba Serikali kuchukua hatua za haraka kutatua mgogoro wa wakulima na wafugaji ili kuzuia vifo vingine na kuwawezesha wakulima kuendelea na shughuli zao kwa amani.
Aidha, ameiomba Serikali kuwasaidia watoto wawili walioachwa na marehemu, mmoja anayesoma darasa la nne na mwingine ambaye bado ni mdogo, ili waweze kuendelea na masomo na kupata huduma muhimu.
Familia hiyo imesisitiza umuhimu wa hatua za haraka za Serikali katika kurejesha amani na usalama kwa wakulima na wafugaji wa eneo hilo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Kenani Kihongosi, amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kiongozi mwenye upendo ambaye ameamua kushughulika na matatizo mbalimbali yanayowakabili Watanzania.
Kihongosi amesema hayo Oktoba 18, 2026 alipokuwa akizungumza na wananchi kwenye Mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa mwandege eneo la mwandege Mkuranga mkoani Pwani.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Kenani Kihongosi, amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kiongozi mwenye upendo ambaye ameamua kushughulika na matatizo mbalimbali yanayowakabili Watanzania.
Kihongosi amesema hayo Oktoba 18, 2026 alipokuwa akizungumza na wananchi kwenye Mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa mwandege eneo la mwandege Mkuranga mkoani Pwani.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
"Msigwa anachotafuta kwa Heche, Heche ampigie pande aingie kuwa kiongozi wa kamati kuu ya CHADEMA. Sasa viongozi wa CHADEMA mkae mguu sawa, na pale wanataka wampige chini Godbless Lema ili msigwa aingie Kamati Kuu" amesema Kihongosi.
Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Kenani Kihongosi, amesema hayo Oktoba 18, 2026 alipokuwa akizungumza na wananchi kwenye Mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa mwandege eneo la mwandege Mkuranga mkoani Pwani.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI PICHA:
Juliana Michael Mbaga mkazi wa Kingereka B Kata ya Bondeni Wilayani Hai, mkoani Kilimanjaro amedai kulazimika kuwataka Chama Cha Demokrasi na Maendeleo (CHADEMA) kuondoka katika nyumba aliyowapangishia kwa madai ya kuogopa vitisho alivyovisikia kutoka kwa kundi la watu wenye pikipiki waliofika eneo hilo analomiliki.
Akizungumza na Jambo tv leo Oktoba 18,2026 amesema kuwa eneo hilo alilowapangishia CHADEMA ndipo na yeye anaishi hivyo vitisho alivyovisikia vilimpelekea kufanya maamuzi ya kutaka kusitisha mkataba nao.
"Nilikuwa nipo kwangu nikaona watu wengi wakija na pikipiki na makelele nilipo toka kwenda kuangalia nikawaona wako pale wakisema wao wakija tutawakomesha,sasa kumbuka pale ni eneo ambalo na mimi naishi nikaona hapa ni mwanzo tu itakuja kuleta shida" alisema Mbaga
Amesema kuwa licha CHADEMA kulipia nyumba hiyo kwa miezi mitatu (3) na kufanya ukarabati wao bado ataendelea na mchakato wa kuwataka kuondoka katika nyumba hiyo.
Awali akizungumza na Jambo Tv baada ya kuibuka kwa sintofahamu hiyo Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Hai John Munisi amekiri jaribio hilo kuibuka baada ya mwenyewe nyumba iliyopo Kingereka B Kata ya Bondeni Wilayani Hai kutaka kuzuia ratiba ya ufunguzi wa ofisi hizo kwa madai kuwa baadhi ya vitu havikuwa kwenye mkataba.
"Mimi sina hakika lakini hoja yake ni kwamba kuna baadhi ya vitu ambavyo tumevifanya ambavyo hatukuwa tumekubaliana, ambayo sasa siyo kweli kwasababu mambo yote tulikuwa tumekubaliana sasa kama ni hofu yake au ametishwa hayo ni yake mwenyewe" alisema Munisi.
Alidai kuwa baada ya mvutano huo Mkuu wa Kituo Cha Polisi Wilaya ya Hai alifika na wakaonyesha mkataba ambapo waliusoma na kuuelewa na kwamba jambo hilo limetatulika na ratiba itaendelea kama kawaida.
Haya yanajiri wakati Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara John Heche akiendelea na ziara yake Mkoani Kilimanjaro ya kuimarisha Chama kwa Wananchi na Operesheni Katiba mpya ambapo pamoja na mambo mengine walikusudia kufungua Ofisi za Chama hicho Wilaya katika eneo hilo. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha na Mbunge wa zamani wa jimbo la Arusha Mjini, Mrisho Mashaka Gambo, ameiomba Serikali kufuatilia suala la eneo lililo mtaa wa kati karibu na Msikiti Mkuu wa Arusha, ambalo Waislamu waliliomba kwa ajili ya shughuli za kidini.
Akizungumza leo Oktoba 18, 2026, katika sherehe za Maulid za kuadhimisha kuzaliwa kwa Mtume Muhammad jijini Arusha, Gambo amesema suala la eneo hilo liliwahi kuwasilishwa Serikalini na kujadiliwa katika vikao vya Baraza la Madiwani.
Gambo amesema alielezwa kuwa Serikali iliridhia eneo hilo kubaki kwa matumizi ya Waislamu, akitaka suala hilo lifuatiliwe ili kuhakikisha wanapata eneo hilo kwa ajili ya shughuli zao za kidini.
Amesisitiza kuwa Serikali inapaswa kuheshimu dini zote kwa usawa, akitolea mfano wa eneo lililotolewa kwa Kanisa Katoliki karibu na Kanisa Kuu la Jimbo Kuu la Arusha.
Akijibu hoja hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Nicodemus Tambo, amesema atashirikiana na Mkurugenzi wa Jiji la Arusha pamoja na maafisa wa ardhi kufuatilia suala hilo, huku akimwomba Gambo kufika ofisini kwake kwa maelezo zaidi na kuahidi kuwa Serikali italifanyia kazi ombi hilo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI:
Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linawashikilia watu watatu, akiwamo Vivian Jackson Salekwa, mkazi wa Majengo jijini Arusha, kwa tuhuma zinazohusiana na taarifa za uongo za kutekwa kwake zilizoripotiwa Oktoba 10, 2026.
Kupitia taarifa kwa umma ya Jeshi la Polisi ya leo Oktoba 18, 2026, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, SACP Justine Masejo, amesema uchunguzi uliofanyika hadi Oktoba 16 ulibaini kuwa madai ya kutekwa kwa Vivian hayakuwa ya kweli.
Kwa mujibu wa Kamanda Masejo, uchunguzi umebaini kuwa Vivian anadaiwa kupanga tukio hilo kwa lengo la kuficha tuhuma za kutishia kuua zinazomkabili mpenzi wake, Castus Bagambisa, mkoani Kilimanjaro.
Ameongeza kuwa Vivian anadaiwa kumtuma mfanyakazi wake wa ndani, Mariam Mwinjuma, kuwafikishia wazazi wake taarifa kuwa ametekwa na watu wasiojulikana, huku yeye akienda kujificha.
Wengine wanaoshikiliwa ni Mariam Mwinjuma na Castus Bagambisa, ambao kwa mujibu wa Jeshi la Polisi, wanachunguzwa kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria.
Awali, taarifa zilizosambaa zilidai kuwa Oktoba 10, 2026, Vivian akiwa maeneo ya Majengo jijini Arusha, alichukuliwa na watu wasiojulikana waliokuwa kwenye gari jeusi na kupelekwa kusikojulikana. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius John Ndejembi, ameipongeza Wizara ya Maji chini ya uongozi wa Waziri Jumaa Aweso kwa usimamizi thabiti na utekelezaji mzuri wa miradi ya kimkakati ya maji nchini, wakati akiweka jiwe la msingi la Mradi wa Maji wa Miji 28 ulioko Rujewa, mkoani Mbeya.
Mradi huo mkubwa, wenye thamani ya Shilingi bilioni 105.7, unatekelezwa kupitia ushirikiano wa Serikali ya Tanzania na Serikali ya India, ukiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya majisafi na salama, sambamba na azma endelevu ya kumtua mama ndoo kichwani.Mradi huo unatazamiwa kuwanufaisha wananchi zaidi ya laki tano katika miji ya Rujewa, Wanging’ombe, na Makambako.
Akizungumza katika hafla hiyo, Ndejembi amewataka wataalamu na watendaji wote wanaohusika kuendelea kufanya kazi kwa weledi, uadilifu, na uwajibikaji mkubwa ili kuhakikisha mradi unakamilika kwa wakati uliopangwa.
Aidha, amesisitiza umuhimu wa kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi yote ya maji nchini na kutatua changamoto za upatikanaji wa huduma hiyo bila kuchelewa, akielekeza kuchukuliwa kwa hatua za dharura kupunguza adha kwa wananchi.
Kwa upande wake, Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, amebainisha kuwa serikali imejipanga kikamilifu kuhakikisha miradi ya maji inakamilika kwa wakati uliowekwa, akisisitiza msimamo thabiti wa serikali kuwa wananchi wanahitaji kuona matokeo ya vitendo badala ya michakato mirefu inayochelewesha upatikanaji wa huduma za kijamii.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mbunge wa Jimbo la Tunduru Kaskazini, Ado Shaibu Ado ametoa wito kwa viongozi wa serikali kusimamia sheria kwa nguvu na bila woga ili kukomesha migogoro ya mara kwa mara kati ya wakulima na wafugaji ambayo inaendelea kuangamiza maisha ya wananchi wilayani humo.
Ado ameyasema hayo alipohudhuria mazishi ya Diwani wa Kata ya Misechele, Marehemu Zuberi Abas Binamu, aliyepoteza maisha baada ya kushambuliwa kwa kitu chenye ncha kali.
Akitoa salamu za rambirambi kwa familia, wanafamilia, na wananchi wote wa Tunduru, Mhe. Ado ameeleza kuwa msiba huo na vifo vingine vilivyotangulia ni ishara tosha kwamba wilaya hiyo inazama na kupoteza sifa yake ya kihistoria ya kuishi kwa amani.
Amefafanua kuwa migogoro mingi huanza pale wakulima wanaponyanyaswa, kupigwa, au kudharauliwa wanapokwenda mashambani, na wanapojaribu kujitetea hukumbana na mapigano makubwa yenye matokeo ya vifo.
Mbunge huyo amekumbusha kuwa aliwahi kulifikisha suala hilo bungeni mbele ya Waziri Mkuu kwamba damu inaendelea kutiririka Tunduru, na akasisitiza kuwa serikali ina uwezo mkubwa wa kusimamia sheria na kuwaondoa wote wanaochunga ng'ombe katika maeneo ambayo hayajatengwa kwa shughuli hizo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma linashikilia watuhumiwa 15 wa jamii ya wafugaji (Wamang'ati) kufuatia mauaji ya watu wawili, akiwemo Diwani wa Kata ya Misechela, Zuberi Abasi Binamu (51), na mfanyabiashara Omari Zuberi Yassini (45), huku watu wengine watatu wakijeruhiwa vibaya katika Kitongoji cha Mkambala, Kijiji cha Chiungo, Tarafa ya Namasakata, Wilaya ya Tunduru.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi ya Jeshi la Polisi iliyotolewa leo Jumamosi Oktoba 17, 2026, tukio hilo lilitokea mnamo tarehe 16 Oktoba 2026, majira ya saa tatu usiku, pale kundi la wafugaji lilipovamia eneo ambalo wanakijiji walikuwa kwenye msiba na kuwashambulia kwa fimbo na vitu vyenye ncha kali. Washiriki wengine watatu katika tukio hilo, ambao ni wakulima wakazi wa kijiji hicho, Abasi Makina (35), Daudi Ally Seleman (34), na Bakari Hamadi Mtamila (52), walijeruhiwa vibaya na sasa wanaendelea kupata matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Tunduru.
Chanzo cha vurugu hizo kinatajwa kuwa ni mfululizo wa migogoro kati ya wakulima na wafugaji, ambapo awali mkulima Jafari Hamad Hemed (56) alidaiwa kujeruhiwa kwa kuchomwa mkuki kwenye paja wakati wa mzozo. Hali hiyo iliwafanya wanakijiji kuungana na kuvamia makambi ya wafugaji katika Kijiji cha Mkotamo kulipiza kisasi, ambapo mtoto mwenye umri wa miaka 12 alijeruhiwa, jambo lililochochea shambulio la kulipiza kisasi lililofanywa na wafugaji usiku uliofuata na kugharimu maisha ya diwani huyo na mfanyabiashara huyo.
Miili ya marehemu imefanyiwa uchunguzi wa kitabibu na kukabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya taratibu za mazishi. Kufuatia tukio hilo, Jeshi la Polisi limeendesha operesheni kali iliyofanikiwa kuwanasa watuhumiwa 15, huku likitoa wito mkubwa kwa wananchi wa Wilaya ya Tunduru kuendelea kuwa watulivu, kuacha kujichukulia sheria mkononi, na kushirikiana na vyombo vya ulinzi kutoa taarifa wakati msako mkuki wa kuwasaka watuhumiwa wengine ukiendelea.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Kenani Kihongosi, ametoa msimamo mkali dhidi ya viongozi wa vyama vya upinzani, akisisitiza kuwa CCM haitishwi, haitaondoka madarakani kwa matamanio au maneno ya kisiasa, na ipo tayari kushindana kupitia sanduku la kura kulingana na kazi kubwa za maendeleo zilizofanyika.
Kihongosi ameyasema hayo leo, Jumamosi Oktoba 17, 2026, wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Wilaya ya Rufiji, Mkoa wa Pwani
"Leo ninadhibitisha hapa chama hiki hakitatoka madarakani. Kazi iliyofanyika ni kubwa kitaendelea kuongoza taifa hili. Chagua maendeleo sio maneno, na nchi yetu ina mifumo ya kidemokrasia, twende kwenye sanduku la kura tukapigiane kura watu waamue. Sio kusema CCM iondoke madarakani. Hiyo biashara haipo." Amesema Kihongosi.
Kihongosi amewasihi Watanzania kulinda amani na ardhi yao, akibainisha kuwa hakuna mgeni au mzungu kutoka duniani atakayeipenda na kuilinda Tanzania kuliko Watanzania wenyewe.
“Hiki chama hakitishwi... Tuna mambo mengi ya kusimamia ndani ya nchi hii: maendeleo ya vijana wetu, maendeleo ya kina mama, maendeleo ya wazee. Tunawaza kujenga hospitali, kuboresha huduma za afya, miundombinu ya barabara na reli, tunawaza uchumi upande. Kuna mtu anawaza kuchoma, haitawezekana na haitakubalika”, ameeleza.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Kenani Kihongosi, amemtaja Mbunge wa zamani wa Iringa Mjini, Mch. Peter Msigwa, kuwa ni "tapeli wa kisiasa" aliyeondoka CCM na kurejea CHADEMA baada ya kukataliwa matakwa yake ya kupewa cheo cha Ukuu wa Mkoa, Ukuu wa Wilaya, au Uwaziri.
Kihongosi ameyasema hayo leo, Jumamosi Oktoba 17, 2026, wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Wilaya ya Rufiji, Mkoa wa Pwani.
Akieleza mnyororo wa matukio yaliyomfanya Msigwa kujiunga na kisha kuondoka CCM, Kihongosi amebainisha kuwa Msigwa alijiunga na CCM baada ya kushindwa katika uchaguzi wa ndani wa CHADEMA ambapo CCM ilimpokea bila ubaguzi kwa mujibu wa katiba yake
“Akaamua kuja kuomba kujiunga na Chama Cha Mapinduzi... Kikampokea kikafungua milango akaja na amezunguka nchi nzima kuhubiri mabaya ya CHADEMA... baadaye anasema sasa ninyi CCM mimi naomba cheo... mnipe Ukuu wa Mkoa au Ukuu wa Wilaya au mnipe Uwaziri. CCM ikasema sisi tuna hazina kubwa ya makada wetu... tutachagua kwa utaratibu wetu.", ameeleza Kihongosi.
Kihongosi ameongeza kuwa baada ya CCM kukataa kumpa vyeo hivyo kwa masharti, Msigwa aliamua kuondoka na kurejea CHADEMA huku akianza kuishambulia CCM, jambo alilolieleza kuwa ni tabia ya wanasiasa wanaoweka maslahi binafsi na vyeo mbele badala ya kuwatumikia wananchi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Mipango na Uwekezaji, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Prof. Kitila Mkumbo, amekabidhi jumla ya vyerehani 66 vikiwemo 55 vya kawaida na 11 vya matumizi ya viwandani kwa kata nane ndani ya jimbo hilo, akiwataka wanufaika kuvitumia kama nyenzo madhubuti ya kukuza kipato chao na kuboresha maisha ya familia zao.
Akizungumza leo, Oktoba 17, 2026, katika hafla fupi iliyofanyika katika Ofisi ya Mbunge iliyoko Manzese, Prof. Kitila ameeleza kuwa mkakati wa kuwawezesha wananchi kiuchumi kupitia vitendea kazi ni njia sahihi na endelevu ya kupambana na umaskini, badala ya kuwapatia fedha taslimu ambazo mara nyingi huisha kwa matumizi ya siku moja bila kuacha tija ya kudumu.
Aidha, Prof. Kitila amesisitiza kuwa uwezeshaji wa wanawake una mchango mkubwa na wa moja kwa moja katika ustawi wa jamii, kwani mwanamke anapokuwa na uwezo wa kiuchumi, faida yake huonekana wazi katika kusimamia familia na maendeleo ya jamii kwa ujumla.
Amewataka wanufaika kuvitumia vyerehani hivyo kwa uaminifu na malengo yaliyokusudiwa ili kuongeza kipato, kujiwezesha kumudu mahitaji ya msingi kama vile elimu ya watoto, na kujiletea maendeleo ya kujitegemea.
Kwa upande wao, wanufaika wa msaada huo wamemshukuru sana Mbunge wao kwa uamuzi huo wa kizalendo na wa vitendo, wakieleza kuwa vyerehani hivyo vitakuwa chachu kubwa ya kuboresha shughuli zao za ushonaji na kuinua uchumi wao wa kila siku.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Mipango na Uwekezaji, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Prof. Kitila Mkumbo, amekabidhi jumla ya vyerehani 66 vikiwemo 55 vya kawaida na 11 vya matumizi ya viwandani kwa kata nane ndani ya jimbo hilo, akiwataka wanufaika kuvitumia kama nyenzo madhubuti ya kukuza kipato chao na kuboresha maisha ya familia zao.
Akizungumza leo, Oktoba 17, 2026, katika hafla fupi iliyofanyika katika Ofisi ya Mbunge iliyoko Manzese, Prof. Kitila ameeleza kuwa mkakati wa kuwawezesha wananchi kiuchumi kupitia vitendea kazi ni njia sahihi na endelevu ya kupambana na umaskini, badala ya kuwapatia fedha taslimu ambazo mara nyingi huisha kwa matumizi ya siku moja bila kuacha tija ya kudumu.
Aidha, Prof. Kitila amesisitiza kuwa uwezeshaji wa wanawake una mchango mkubwa na wa moja kwa moja katika ustawi wa jamii, kwani mwanamke anapokuwa na uwezo wa kiuchumi, faida yake huonekana wazi katika kusimamia familia na maendeleo ya jamii kwa ujumla.
Amewataka wanufaika kuvitumia vyerehani hivyo kwa uaminifu na malengo yaliyokusudiwa ili kuongeza kipato, kujiwezesha kumudu mahitaji ya msingi kama vile elimu ya watoto, na kujiletea maendeleo ya kujitegemea.
Kwa upande wao, wanufaika wa msaada huo wamemshukuru sana Mbunge wao kwa uamuzi huo wa kizalendo na wa vitendo, wakieleza kuwa vyerehani hivyo vitakuwa chachu kubwa ya kuboresha shughuli zao za ushonaji na kuinua uchumi wao wa kila siku.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Ruvuma, Mohamed Aly, ameweka wazi msimamo wa chama hicho mkoani humo na kueleza kuwa kimeumizwa sana na matukio ya uvunjifu wa amani na upotevu wa maisha yanayosababishwa na migogoro ya mara kwa mara kati ya wakulima na wafugaji wilayani Tunduru, huku akisisitiza kuwa chama hakijaridhishwa na kasi ya sasa ya hatua zinazochukuliwa na Serikali kukomesha tatizo hilo ambalo tayari limesababisha vifo vya watu zaidi ya saba.
Aly ametoa kauli hiyo leo, Oktoba 17, 2026, mara baada ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma, Oddo Mwisho, kuwasilisha taarifa rasmi ya Kamati ya Siasa Mkoa iliyojadili kwa kina hali ya kiusalama na changamoto zinazoendelea kuhatarisha maisha na mali za wananchi wilayani humo.
Katibu huyo amesisitiza kuwa ni wajibu wa Serikali kuchukua hatua za haraka, thabiti, na zenye tija ili kusuluhisha mivutano hiyo ya kimazingira na kiuchumi kabla haijazidi kuleta madhara makubwa kwa jamii na kuchafua misingi ya amani mkoani Ruvuma.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkuu wa Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma, Denis Masanja, ametoa ahadi ya kuchukua hatua za kisheria bila huruma dhidi ya wote wanaochochea na kujihusisha na migogoro ya wakulima na wafugaji mkoani humo, kufuatia tukio la kusikitisha la kifo cha aliyekuwa Diwani wa Kata ya Misechele, Marehemu Zuberi Abas Binamu, aliyeshambuliwa kwa kitu chenye ncha kali na kupoteza maisha. Marehemu amezikwa leo katika Kijiji cha Misechele.
Akizungumza mbele ya wananchi na viongozi waliokusanyika kwenye maziko hayo, Masanja alionesha masikitiko yake makubwa juu ya wimbi la vifo, majeruhi, na ulemavu unaosababishwa na migogoro hiyo ya mara kwa mara, akibainisha kuwa mzizi wa tatizo unachochewa na baadhi ya wafugaji wanaokaidi sheria za nchi.
Ameongeza kuwa serikali tayari imeanza kuchukua hatua madhubuti na itashirikiana kwa karibu na viongozi wa eneo hilo, wakiwemo mbunge, madiwani, pamoja na viongozi wa vijiji na kata, ili kumaliza hali ya hofu inayowakabili wananchi. Ametoa mfano wa vitendo vya kikatili ambapo wakulima wanaokenda mashambani kuvuna korosho zao wamekuwa wakifukuzwa na wafugaji, huku mazao yao yakiibwa au kuharibiwa.
Mkuu huyo wa wilaya amesisitiza wazi kuwa eneo la Misechele halijatengwa kwa shughuli za ufugaji, akiwataka wananchi kutoruhusu kuwakaribisha wafugaji hao huku akiwataka watoe taarifa za viongozi wa vijiji au kata wanaojihusisha na kuwakaribisha hata kama kukiwa na mianya ya rushwa au malipo yaliyofanyika.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Aliyekuwa Diwani wa Kata ya Misechele, Marehemu Zuberi Abas Binamu, amezikwa leo, Oktoba 17, 2026, katika kijiji chake cha asili cha Misechele kilichoko wilayani Tunduru, mkoani Ruvuma, kufuatia kifo chake cha ghafla kilichotokea baada ya kushambuliwa na watu wanaosadikika kuwa ni wafugaji.
Marehemu Binamu aliuawa usiku wa kuamkia leo ambapo alishambuliwa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali. Tukio hilo la kusikitisha limeacha simanzi nzito miongoni mwa wakazi wa wilaya hiyo na viongozi mbalimbali waliofika kuungana na familia katika mazishi hayo.
Viongozi wakuu walioongoza mamia ya wananchi kumpumzisha marehemu ni pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Denis Masanja, Mbunge wa Tunduru Kaskazini, Ado Shaibu, na mwakilishi wa Mbunge wa Tunduru Kusini, Mhandisi Fadhili Chilombe.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Kutokana na kuripotiwa mara kwa mara kwa matukio ya uvunjifu wa amani katika Wilaya ya Tunduru, kunakosababishwa na migogoro kati ya wakulima na wafugaji, Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Ruvuma kimesema hakijaridhishwa na taarifa ya Serikali ya Mkoa huo kuhusu hali ya usalama katika wilaya hiyo.
Akisoma taarifa ya Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Ruvuma Oktoba 17, 2026, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoani humo, Oddo Mwisho, amesema kamati hiyo ilikaa Oktoba 16, 2026 kujadili taarifa ya hali ya usalama katika wilaya ya Tunduru, inayohusisha migogoro kati ya wakulima na wafugaji, ambapo vifo kadhaa vimeripotiwa kutokana na migogoro hiyo.
Oddo Mwisho amesema kuwa hadi Oktoba 16, 2026, zaidi ya vifo saba vilikuwa vimeripotiwa kutokea katika wilaya ya Tunduru kutokana na migogoro kati ya wafugaji na wakulima. Hivyo, ameiomba Serikali ya Mkoa huo kuhakikisha inachukua hatua za kumaliza migogoro hiyo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Pwani, Samaha Seif Said, amekemea vikali kauli iliyotolewa hivi karibuni na Waziri wa Afya na Mbunge wa Jimbo la Rufiji, Mohamed Mchengerwa, akidai kuwa imewadhalilisha na kuwakatisha tamaa vijana wanaojitolea bila kuchoka kukitumikia chama hicho tawala.
Samaha ametoa kauli hiyo akijibu matamshi ya Mchengerwa yaliyotolewa wilayani Kibaha wakati akifungua kikao cha Baraza la Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Pwani, ambapo waziri huyo alidai kuwa vijana hawafanyi kazi bila kupewa hongo na kwamba wamechagua upande.
Akiongea kwa niaba ya vijana hao, Samaha ameeleza kuwa kauli hiyo imewaumiza na kuwakera sana, huku akisisitiza kuwa wako tayari hata kuomba radhi iwapo itabainika walimkosea, lakini kwa utaratibu wa kistaarabu unaolinda maslahi ya umoja huo.
Aidha, Mwenyekiti huyo wa UVCCM Mkoa wa Pwani amemtaka Mchengerwa ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), kuacha kutumia kauli za jumla zinazoweza kuchafua taswira na heshima ya jumuiya nzima, badala yake ataje wazi mtu au watu maalum anaowalenga ikiwa ana malalamiko binafsi, akisisitiza kuwa vijana wa UVCCM wanafanya kazi kwa kujitolea na hawapaswi kudharauliwa wala kuhusishwa na vitendo vya rushwa hasa ikizingatiwa kuwa si kipindi cha uchaguzi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Wafanyabiashara wadogo na wa kati wanatarajiwa kupata maarifa ya kupanua masoko, kutumia teknolojia na kukabiliana na changamoto za biashara kupitia Kongamano la Saba la Biashara na Maendeleo ya Uchumi litakalofanyika jijini Mwanza, Oktoba 22 na 23, 2026
Akizungumza na waandishi wa habari Oktoba 16, 2026, jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Prof. Edda Tandi Lwoga, amesema kongamano hilo litafanyika kwa mara ya kwanza Mwanza na linatarajiwa kushirikisha wadau takribani 300 kutoka ndani na nje ya Tanzania.
Amesema kongamano hilo litajadili namna ya kuimarisha biashara, kutumia ubunifu na teknolojia, kurasimisha shughuli za biashara na kutumia takwimu kufanya maamuzi sahihi, huku msisitizo ukiwekwa katika kutafuta suluhisho kwa changamoto zinazowakabili wajasiriamali wadogo na wa kati.
Washiriki kutoka nchi mbalimbali, zikiwemo Finland, China, Afrika Kusini, Indonesia na Malaysia, wanatarajiwa kushiriki kubadilishana uzoefu kuhusu masoko, uwekezaji na mikakati ya kukuza biashara.
Prof. Lwoga amesema CBE imekuwa ikifanya tafiti na kutoa mafunzo kwa wadau wa biashara kuhusu masuala ya masoko, biashara za mipakani, kilimo cha biashara na matumizi endelevu ya rasilimali.
Kongamano hilo linatarajiwa kuwa na mgeni rasmi Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Denis Londo.
Prof. Lwoga amewahimiza wafanyabiashara, wanafunzi na watafiti kushiriki ili kupata maarifa na kujenga mitandao itakayosaidia kukuza biashara na uwekezaji nchini.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Mawaziri na makatibu wakuu kutoka nchi za Afrika Mashariki, Kaskazini na Kusini (MOESNA) wameipongeza Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kwa maboresho ya miundombinu na kuimarika kwa ufanisi wa shughuli za upakuaji na upakiaji wa mizigo katika Bandari ya Dar es Salaam, hatua inayochangia kurahisisha biashara katika ukanda huo.
Akiongea kwa niaba ya ujumbe huo, Katibu Mtendaji wa MOESNA, Bw. Kassim Mpaata, alisema ujumbe huo umeridhishwa na maendeleo na kasi ya maboresho yanayoendelea bandarini hapo, akiahidi kuendelea kuunga mkono matumizi ya Bandari ya Dar es Salaam.
“Sisi Waganda tumekuwa tukitumia bandari hii kwa muda mrefu, lakini kwa sasa tumeshuhudia mabadiliko makubwa na kasi ya juu ya maboresho yanayofanyika hapa,” alisema Mpaata.
Bw Mpaata alisema kuwa mara zote wamekuwa wakihimiza nchi wanachama kuboresha miundimbinu yote ya usafirishaji hususani barabara, bandari na mipakani ili kufanya mazingira ya biashara kuwa rafiki kwa kila nchi mwanachama.
“Kwa mara nyingine tunaipongeza mamlaka hii kwa maboresho haya yote na kuwaomba kuyafanyia kazi changamoto ambazo zinabainishwa na wajumbe ili kuongeza utendaji kazi na ufanisi n akuendelea kuvutia wateja Zaidi”, alisisitiza Bw. Mpaata.
Alisema maboresho hayo yanaimarisha nafasi ya Bandari ya Dar es Salaam kama lango muhimu la biashara kwa Tanzania na nchi jirani zisizo na bandari, kwa kurahisisha usafirishaji wa bidhaa na kuchochea shughuli za kiuchumi katika ukanda huo.
Akiongea katika ziara hiyo kwa niaba ya Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Abdallah Mitawi, alisema ziara ya ujumbe huo ililenga kujionea maendeleo ya miundombinu na kutathmini utendaji wa bandari hiyo.
“Tulipokea ujumbe wa mawaziri na makatibu wakuu 22 waliokuja kushiriki mkutano wa wanachama. Tulijadili masuala mbalimbali ya kiuchumi, na wakaomba kutembelea bandari yetu ili kujionea wenyewe utendaji wake,” alisema Mitawi.
Alisema ujumbe huo uliridhishwa na maboresho yaliyofanyika na kuahidi kuendelea kuhamasisha wananchi na wafanyabiashara katika nchi zao kutumia Bandari ya Dar es Salaam kuingiza na kusafirisha bidhaa, ikiwemo mazao ya kilimo na madini, kwenda katika masoko mbalimbali, hususan ya Mashariki ya Mbali.
Katika ziara hiyo, wajumbe walitembelea gati namba sifuri hadi saba. Katika gati namba sifuri, walishuhudia meli kubwa ikipakua magari, huku katika magati mengine wakiona meli za makasha zikiendelea na shughuli za upakuaji wa mizigo.
Mitawi alisema wajumbe hao walipata fursa ya kushuhudia meli kubwa iliyowasili moja kwa moja kutoka Japan ikiwa na uwezo wa kubeba magari 5,272, ikiwa ni rekodi mpya katika bandari hiyo.
“Leo tumepata bahati ya kuishuhudia meli kubwa kama hii kutoka moja kwa moja nchini Japan, yenye urefu wa mita 199.8 na iliyoweka rekodi katika bandari hii kwa kubeba magari 5,272,” alisema.
Kwa upande wake, Meneja wa Huduma za Meli wa TPA, Nahodha Peter John, aliyemwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo, Bw. Plasduce Mbossa, alisema wajumbe hao walifurahishwa na mpangilio mzuri wa shughuli na ufanisi walioishuhudia bandarini hapo.
Alisema miongoni mwa maboresho makubwa yaliyofanyika ni kuongeza kina cha maji bandarini kutoka mita 12 hadi mita 14.5, hatua iliyowezesha bandari hiyo kupokea meli kubwa zaidi.
Aliongeza kuwa kina cha njia ya kuingilia meli na miundombinu mingine ya uongozaji wa meli vimeboreshwa, hivyo kuwezesha meli kubwa kuingia na kugeuka kwa urahisi zaidi.
Kwa mujibu wa Nahodha John, maboresho hayo yameongeza uwezo wa bandari kupokea meli zenye urefu wa hadi mita 305, ikilinganishwa na mita 234 hapo awali, huku kina cha maji kikiwa mita 14.
Aidha, alisema kiwango cha shehena inayohudumiwa na bandari hiyo kimeongezeka kutoka tani milioni 33.4 katika mwaka wa fedha 2024/2025 hadi tani milioni 33.7 katika mwaka wa fedha 2025/2026, jambo linaloashiria kuendelea kuimarika kwa shughuli za kibiashara. -
Jambo TV
@Jambotv_
Waziri Mkuu mstaafu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amezindua rasmi Kilimanjaro International Marathon 2027, kuelekea maadhimisho ya mwaka wa 25 tangu kuanzishwa kwa mashindano hayo.
Uzinduzi huo uliofanyika katika Hoteli ya Serena umehudhuriwa na wadau mbalimbali kutoka serikalini na sekta binafsi wakiwemo wadhamini wakuu wa mbio hizo, Kilimanjaro Premium Lager, kampuni ya Yas pamoja na Benki ya CRDB inayodhamini mbio za kilomita tano (KM 5).
Kilimanjaro International Marathon 2027 inatarajiwa kufanyika Februari 7, 2027, Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro, ikiwa ni sehemu ya kuendeleza utamaduni wa Marathon, kuhamasisha ushiriki wa wananchi katika michezo na kuitangaza Tanzania kupitia utalii wa michezo. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Baadhi ya waliokuwa wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na baadaye kuhamia vyama vingine vya siasa wameomba msamaha kwa wananchi na wafuasi wa chama hicho, wakieleza kuwa wameamua kurejea ili kushiriki katika kukijenga na kuendeleza harakati za kushika dola.
Wakizungumza jana, Oktoba 16, 2026, katika Viwanja vya Manyema, mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro, Mchungaji Peter Msigwa, aliyewahi kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kabla ya kurejea CHADEMA, pamoja na Patrick Assenga, aliyehamia Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) na baadaye kurejea CHADEMA, wamesema wamegundua kuwa walifanya makosa kuondoka katika chama hicho.
Wamesema uamuzi wao wa kurejea CHADEMA unatokana na kutambua umuhimu wa kuungana na wanachama wengine katika kukijenga chama hicho na kuendeleza harakati zake za kisiasa.
Aidha, wamewaomba Wananchi na wafuasi wa Chama hicho kuwasamehe na kuwapokea tena ili kwa pamoja waendelee na safari ya kukijenga chama na kufikia lengo la kushika dola.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Godbless Lema, amewakosoa wananchi kwa kile alichodai kuwa ni kushindwa kuwaunga mkono viongozi na wanachama wanaopambana kwa ajili ya mabadiliko ya kisiasa nchini.
Lema amedai kuwa wananchi wana mchango katika hali inayowakabili wapiganaji wa chama hicho, akieleza kuwa kukosekana kwa mshikamano na uungwaji mkono kumevunja moyo baadhi ya wanachama, huku wengine wakiamua kuondoka CHADEMA na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Ametoa kauli hiyo jana, Oktoba 16, 2026, katika viwanja vya Manyema, mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro, wakati wa ziara ya Mwenyekiti wa CHADEMA, John Heche.
Akizungumza katika mkutano huo, Lema amedai kuwa baadhi ya wananchi wamekuwa wakiwaita wasaliti wale walioondoka ndani ya chama na kujiunga na CCM, bila kujiuliza mchango wao wenyewe katika kuunga mkono harakati za chama hicho.
Ametoa mfano wa kesi ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, akiwahoji wananchi wa Moshi kuhusu hatua walizochukua kuhudhuria kesi hiyo katika Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam.
“Kabla hujawaita wasaliti, nataka nikuulizie wewe mtu wa Moshi, ni lini umepanda basi kuja Mahakama Kuu Dar es Salaam kusikiliza kesi ya mwenyekiti wako?” Alihoji Lema.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalumu ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA), Anna Lyimo, amesema mradi wa ujenzi wa Kongani ya Viwanda Bagamoyo ni eneo lenye fursa mbalimbali za uwekezaji kwa wawekezaji wa kawaida na wale wanaowekeza katika maeneo maalumu ya kiuchumi kutoka ndani na nje ya nchi.
Lyimo ameeleza hayo Oktoba 16, 2026 alipokuwa akiwasilisha taarifa ya mradi huo mbele ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mwigulu Nchemba, ambaye amefika eneo hilo kama mgeni rasmi kwaajili ya kufanya uzinduzi wa maendeleo ya ujenzi wa Kongani hiyo.
"Mradi huu wa kiuchumi maalumu Bagamoyo, unatoa fursa za uwekezaji kwa wawekeza wa kawaida lakini pia wawekezaji wa maeneo maalumu ya kiuchumi" amesema Kaimu huyo.
Amesema wawekezaji wa maeneo hayo maalumu ni watakaojikita kuwekeza katika maeneo ya kilimo, uchakataji ngozi na bidhaa za ngozi, uchakataji wa pamba sambamba na uzalishaji wa nguo, ikiwemo utengenezaji wa vyombo vya moto.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalumu ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA), Anna Lyimo, amesema mradi wa eneo la Ukanda Maalumu wa Kiuchumi Bagamoyo utakuwa na mchango mkubwa katika kufanikisha ufikiaji wa uchumi wa dola trilioni 1 katika pato la taifa.
Lyimo ameeleza hayo Oktoba 16, 2026 alipokuwa akiwasilisha taarifa ya mradi huo mbele ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mwigulu Nchemba, ambaye amefika eneo hilo kama mgeni rasmi kwaajili ya kufanya uzinduzi wa maendeleo ya ujenzi wa Kongani hiyo.
"Kama ilivyoainishwa katika mpango wa taifa wa maendeleo wa miaka mitano, mradi wa ukanda wa eneo maalumu la kiuchumi bagamoyo utakuwa na mchango mkubwa katika kufikia uchumi wa dola trilioni moja" amesema Lyimo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, amesema licha ya uwepo ya mvua za El Niño ni muhimi kuchukuwa tahadhari na wakati huhuo kazi zikiendelea.
Waziri Mkuu ameeleza hayo leo Oktoba 16, 2026 alipofika kufanya uzinduzi wa maendeleo ya ujenzi wa Kongani ya Viwanda ya HWTZ SEZ LIMITED iliyopo Bagamoyo Mkoani pwani.
"Hapa taarifa zote, jambo likiwa halijafanyika wanasema tulichukuwa tahadhari ya mvua za El Niño, tunasubiria kama harusi, hii siyo sawa. Tuchukuwe tahadhari huku tukiendelea na kazi" amesema Waziri Mkuu.
Amesisitiza kuendelea kwa zoezi la uthamini wa wananchi ambao wanatakiwa kupisha maeneo ya uwekezaji, zoezi ambalo limeelezwa kwamba lilisitishwa kutokana hofu ya mvua hizo, liendelee na likamilike kwa haraka ili maeneo ya shughuli za kiuchumi yapatikane.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, amewasihi wananchi wa Mkoa wa Pwani na Watanzania kwa ujumla kuepuka kuchukia uwekezaji kutokana na migogoro ya ardhi ambayo imekuwa ikijitokeza.
Waziri Mkuu ameeleza hayo leo Oktoba 16, 2026 alipofika kufanya uzinduzi wa maendeleo ya ujenzi wa Kongani ya Viwanda ya HWTZ SEZ LIMITED iliyopo Bagamoyo Mkoani pwani.
"Nitoe lai kwa wananchi wakiwemo wananchi wa pwani, kama ambavyo nimesema maeneo mengine, wala tusichukie uwekezaji, wala tusichukie wawekezaji, kwa sababu ya mizozo ya mambo ya ardhi", amesema Waziri Mkuu.
Amesema katika nchi yoyote inayopiga hatua za kimaendeleo kama Tanzania, bila kuwa na shughuli imara za uzalishaji, tatizo la umasikini, ukosefu wa ajira, pengo la wenye nacho na wasionacho haliwezi kumalizika.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Shirika la reli Tanzania (TRC) na kampuni ya Arab contractors ya Misri, zimetia saini hati ya makubaliano kuhusu mradi wa reli ya Mtwara–Songea–Mbamba bay, yenye matawi ya Mchuchuma na liganga, hafla iliyofanyika Oktoba 16, 2026 Jijini Dar Es Salaam, na kushuhudiwa na Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa.
Akizungumza muda mchache baada ya tukio la utaiji Prof. Mbarawa, alisema, mradi wa Reli ya Kusini una umuhimu wa kipekee katika kufungua fursa za kiuchumi katika Ukanda wa Kusini aidha aliongeza kusema kuwa Reli hiyo inatarajiwa kuunganisha Bandari ya Mtwara na maeneo ya uzalishaji wa kilimo, madini na viwanda, hususan miradi ya Mchuchuma na Liganga.
Waziri huyo wa Uchukuzi, Pamoja na mambo mengine, alisisitiza mambo matatu ambayo ni,
‘’Kwanza, TRC na Arab Contractors waandae mpango wa kazi wenye majukumu, na matokeo yanayotarajiwa na muda maalumu wa utekelezaji. Pili, tafiti zizingatie uhalisia wa kiuchumi, mahitaji ya mizigo na uwezekano wa kupata fedha za ujenzi na uendeshaji wa reli. Tatu, ushirikiano huu uhakikishe ushirikishwaji wa taasisi muhimu, ujenzi wa uwezo wa wataalamu wa Tanzania na uzingatiaji wa maslahi ya Taifa’’, alimalizia Prof. Mbarawa.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Mhandisi Machibya Shiwa, amesema hati hiyo ya Makubaliano iliyosainiwa inaweka msingi wa ushirikiano katika kufanya tafiti na kuandaa mapendekezo ya kitaalamu na kifedha kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo.
Mha. Machibya, ameeleza kuwa, kwa mujibu wa makubaliano hayo, Arab Contractors itafanya tafiti za awali na upembuzi yakinifu kwa gharama zake, ikitarajiwa kuwasilisha taarifa ya awali ndani ya miezi mitatu tangu kusainiwa kwa hati hiyo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Mahakama Kuu ya Tanzania imesisitiza Taasisi zinazohusika katika mnyororo wa haki kuzingatia misingi ya utoaji haki bila kuangalia upande kama ambavyo Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inavyotamka.
Hayo yametajwa na Jaji wa Mahakama Kuu Amiri Mruma wakati akisoma hukumu katika kesi ya kikatiba na 7300/2026 ambayo ilifunguliwa na mawakili wa Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu walilalamikia kushindwa kuonana na mteja wao pamoja na kukosa usiri wa kimazungumzo pindi wanapoonana naye.
"Taasisi zote Magereza, Upelelezi, Mashtaka wanapaswa kufata sheria na haki kama ambavyo katiba inaelekeza ni jambo ambalo linapotoshwa kwa baadhi ya taasisi ambazo zinahusika katika mnyororo wa haki, kwenye taasisi za haki wamepata upofu kudhani kuwatia watu hatiani basi hiyo ndiyo haki" amesema Jaji Mruma
Katika shauri hilo walalamikaji walikuwa ni Kulwa Maduhu, Paul Kisabo na Nashon Nkungu ambapo Mahakama imeagiza Magereza kuhakikisha Lissu anapata wakati wa usiri anapozungumza na mawakili wake au washauri wa kisheria.
Akizungumza hukumu hiyo Wakili Kisabo ameutaja uamuzi huo kama uamuzi wa kihistoria ambao utaweka misingi ya muda mrefu katika mifumo ya Magereza.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Mahakama Kuu ya Tanzania imesisitiza Taasisi zinazohusika katika mnyororo wa haki kuzingatia misingi ya utoaji haki bila kuangalia upande kama ambavyo Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inavyotamka.
Hayo yametajwa na Jaji wa Mahakama Kuu Amiri Mruma wakati akisoma hukumu katika kesi ya kikatiba na 7300/2026 ambayo ilifunguliwa na mawakili wa Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu walilalamikia kushindwa kuonana na mteja wao pamoja na kukosa usiri wa kimazungumzo pindi wanapoonana naye.
"Taasisi zote Magereza, Upelelezi, Mashtaka wanapaswa kufata sheria na haki kama ambavyo katiba inaelekeza ni jambo ambalo linapotoshwa kwa baadhi ya taasisi ambazo zinahusika katika mnyororo wa haki, kwenye taasisi za haki wamepata upofu kudhani kuwatia watu hatiani basi hiyo ndiyo haki" amesema Jaji Mruma
Katika shauri hilo walalamikaji walikuwa ni Kulwa Maduhu, Paul Kisabo na Nashon Nkungu ambapo Mahakama imeagiza Magereza kuhakikisha Lissu anapata wakati wa usiri anapozungumza na mawakili wake au washauri wa kisheria.
Akizungumza hukumu hiyo Wakili Kisabo ameutaja uamuzi huo kama uamuzi wa kihistoria ambao utaweka misingi ya muda mrefu katika mifumo ya Magereza.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Wachimbaji wadogo nchini wanatarajiwa kupata nafuu ya
upatikanaji wa mikopo kupitia mpango wa Serikali wa kuanzisha benki maalumu ya wachimbaji, kufuatia malalamiko ya kundi hilo kuhusu sharti la kuweka dhamana ya asilimia 20 wanapoomba mikopo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Dkt. Venance Mwasse, amesema mchakato wa kuanzishwa kwa benki hiyo unaendelea, huku akieleza inalenga kuwa suluhisho la changamoto za mikopo zinazowakabili wachimbaji wadogo.
"Niwashirikishe Mwarobaini, ambao hata jana nilisema kwenye Kamati ya Bunge, Mwarobaini wa kumkomboa mchimbaji mdogo hasa kwenye kukopeshwa ni Benki ya wachimbaji"
Mwasse ameyasema hayo leo, Oktoba 16, 2026, wakati wa Kikao Kazi cha STAMICO na Wahariri wa Vyombo vya Habari ijini Dar es Salaam.
Imeelezwa kuwa, benki hiyo inayopendekezwa kuitwa Tanzania Mineral Bank, itasimamiwa na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) na inalenga kupanua fursa za upatikanaji wa mitaji kwa wachimbaji ili kuwawezesha kuendeleza shughuli zao, kununua vifaa, kuboresha teknolojia na kuongeza uzalishaji.
Kwa mujibu wa Mwasse, makubaliano kuhusu uanzishwaji wa benki hiyo inayotarajiwa kuwa fursa kwa wachimbaji wadogo wanaokabiliwa na vikwazo vya kifedha, yalifikiwa Agosti 26, 2026, katika kikao kilichohusisha Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania na wadau wa sekta ya madini. -
Jambo TV
@Jambotv_
Wakili wa Serikali Mwandamizi Daniel Nyakiha akimpa mkono Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu mara baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania kutoa hukumu katika kesi ya Kikatiba juu ya haki za mawakili wa Lissu kumuona na kupata usiri wakati wa mazungumzo yao gerezani Ukonga.
Wakili Nyakiha leo alikuwa akimwakilisha mdaawa wa kwanza hadi wa tatu katika kesi hiyo ambao ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Kamishna Jenerali wa Magereza na Mkuu wa Gereza la Ukonga.
Soma zaidi kuhusu uamuzi katika page zetu.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mahakama Kuu ya Tanzania imeuagiza uongozi Gereza la Ukonga jijini Dar es Salaam kufuata taratibu za Kanuni za Uendeshaji wa Magereza kwa kutowanyima Mawakili na Washauri wa kisheria kuzungumza na mteja wao lakini pia maafisa magereza kusimamia maongezi hayo kwa kukaa umbali ambao wataweza kuona tu na sio kusikia mazungumzo.
Maagizo hayo yametolewa leo Oktoba 16, 2026 katika kikao cha Mahakama hiyo Masjala Kuu ya Dodoa kilichoketi Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Dar es Salaam katika shauri na 7300/2026 lililofunguliwa na Kulwa Maduhu na wenzake ambao ni Mawakili washauri wa Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu wakidai kuzuiwa kuonana na mteja wao na wakati mwingine walipoonana nae kukosa usiri wakati wa mazungumzo.
Akisoma uamuzi huo Jaji Amir Mruma ambaye ni kiongozi wa Jopo la Majaji watatu waliokuwa wakisikilzia kesi hiyo amesema"Mamlaka ya magereza ya Ukonga wafuate kanuni kuhakikisa maafisa Maafisa Magereza wanaangalia usalama lakini wawe umbali wa kutosikia."
Pamoja na maagizo mengine yaliyotolewa katika uamuzi huo mahakama hiyo imetamka kuwa kitendo cha Maafisa Magereza kusikiliza mazungumzo ya Lissu na Mawakili wake au washauri wake wa kisheria ambao ni Paul Kisabo na Nashon Nkungu ni uvunjifu wa Kanuni ya 13 ya Uendeshaji wa Magereza.
"Tunatamka Kanuni 13 ya Uendeshaji wa Magereza ya mwaka 1968 inataka mashauriano kati ya mfungwa na mshauri au wakili wake yafanyike mahali ambapo Magereza wanaweza kuona lakini hawawezi kusikia"
Pamoja na hayo hukumu hiyo imetamka kuwa kuzuiliwa kwa Wakili Maduhu Oktoba 28, 2025 kuingia gereza la ukonga licha ya kuonyesha vitambulisho vyake vya uwakili sababu ikitajwa kuwa hayupo kwenye orodha ya Lissu aliyowasilisha gerezani sio sahihi na sio sababu inayojitosheleza kwani kama Wakili na mshauri wa kisheria alikuwa ana sababu za kutosha kuonana na mteja wake.
Hata hivyo pamoja na uamuzi mwingine Mahakama hiyo Mahakama imeagiza Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Kamishna Jenerali wa Magereza na Mkuu wa Gereza la Ukonga kuhakikisha Mawakili wa Lissu watakapoenda gerezani hapo waweze kukutana na kufanya mazungumzo na mashauriano na mteja wao pasina kuingiliwa kwa vyovyote wala kusikilizwa.
Maelekezo mengine yaliyotolewa katika uamuzi huo ni kuwa Maafisa Magereza wanaruhusiwa kukagua nyaraka za kisheria kwa ajili ya usalama lakini sio kuangalia maudhui au kunukuu yaliyo katika nyaraka hizo.
Aidha Kamishna Jenerali wa Magereza ameagizwa ndani ya siku 60 atepewa na kusambaza waraka kwa kila Mkuu wa Magereza kutekelezwa kwa kanuni hiyo ya 13 kuwepo mazingira yanayowezesha na kuwepo kwa mazungumzo kati ya mteja na Wakili mahali panapoonekana bila kusikika.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Kampuni ya Kitanzania ya Amsons Group imefanya ununuzi mkubwa katika sekta ya nishati baada ya kuingia makubaliano rasmi ya kuinunua na kuchukua miundombinu yote ya kuchakata, kuzalisha, na kusambaza mafuta ghafi na gesi asilia ya Oryx Energies nchini Tanzania.
Ununuzi huo wa kimkakati unahamishia vituo muhimu vya kujaza mafuta (petrol stations), bohari za kuhifadhia mafuta, pamoja na mtandao mpana wa usambazaji na uzalishaji mikononi mwa kampuni hiyo. Hatua hii inadhihirisha ukuaji wa kampuni za wazawa katika kumiliki na kuendesha miundombinu mikuu ya uchumi na nishati katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
Amsons Group, ambayo ina uwepo thabiti na uwekezaji katika sekta mbalimbali, imeelezwa kuwa katika nafasi nzuri ya kuendeleza misingi iliyowekwa na Oryx Energies na kufungua fursa mpya za kibiashara nchini. Ununuzi huo ni sehemu ya tathmini ya kimkakati inayofanywa na Oryx Energies juu ya rasilimali zake za usambazaji mafuta barani Afrika.
Akizungumzia uamuzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Oryx Energies, Bw. Moussa Diao, amesema kuwa wanafurahi kufikia makubaliano hayo na Amsons Group kutokana na kampuni hiyo kuwa na misingi imara nchini Tanzania na nia ya kukua.
“Tunaamini kuwa Amsons Group ipo katika nafasi nzuri ya kuivusha biashara hii kwenda hatua inayofuata, ikijenga juu ya uwezo uliopo na kutengeneza fursa mpya kwa wafanyakazi, wateja, na washirika wake. Mkataba huu pia ni hatua muhimu katika muundo wa mkakati wa Oryx Energies, tukilenga kuelekeza mitaji na juhudi zetu katika kuendeleza miundombinu ya nishati kote barani Afrika na kuimarisha shughuli zetu za kibiashara. Afrika inabaki kuwa moyo wa biashara yetu na malengo yetu ya muda mrefu”, ameeleza Diao.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Amsons Group, Bw. Edha Nahdi, ameeleza kuwa ununuzi huo ni hatua kubwa katika azma yao ya kupanua biashara za nishati na usafirishaji.
“Kuunganishwa kwa mtandao mpana wa usambazaji wa Oryx na uwezo wake wa bohari za kuhifadhia mafuta kunatuwezesha kuimarisha usalama wa nishati nchini na kuifanya Tanzania kuwa kituo kikuu na cha kimkakati cha vifaa na usafirishaji kwa Afrika Mashariki na Kati”, ameeleza.
Kukamilika kikamilifu kwa uuzaji huu kunasubiri idhini kutoka kwa mamlaka za udhibiti za serikali. Wakati mchakato huo ukiendelea, huduma za Oryx Energies zitaendelea kutolewa kama kawaida bila usumbufu kwa wateja, wafanyakazi, na washirika wao. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu akiingia mahakamani kwa ajili ya kusikiliza hukumu ya kesi ya kikatiba juu ya haki za Mawakili wake kumuona na kuzungumza nae kwa usiri akiwa Gerezani.
Hukumu hiyo itatoelewa katika Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Dar es Salaam na Jopo la Majaji watatu wakiongozwa Jaji Amir Mruma.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu akiingia mahakamani kwa ajili ya kusikiliza hukumu ya kesi ya kikatiba juu ya haki za Mawakili wake kumuona na kuzungumza nae kwa usiri akiwa Gerezani.
Hukumu hiyo itatoelewa katika Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Dar es Salaam na Jopo la Majaji watatu wakiongozwa Jaji Amir Mruma.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Mahakama Kuu ya Tanzania Masijala Kuu ya Dodoma inatarajiwa kutoa hukumu katika kesi ya kikatiba Na. 7300 ya mwaka 2026, inayohusu haki ya Mawakili kuzuiwa na kukosa faragha pindi wanapotaka kukutana na mteja wao gerezani ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Tundu Antipas Lissu.
Shauri hilo ambalo limefunguliwa na Mawakili Nashon Nkung, Kulwa Maduhu na Paul Kisabo dhidi ya Mkuu wa Gereza la Ukonga na Wenzake, hukumu yake itasomwa leo saa tatu asubuhi katika Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Dar es Salaam ambapo kesi hiyo ipo mbele ya jopo la Majaji watatu Jaji Anir Mruma, Dkt. Angelo Rumisha na Dkt. Evaristo Longopa.
Wakati wa usikilizwaji wa shauri hilo walalamikaji hayo waliieleza mahakama kuwa kwa nyakati tofauti tofauti walipokuwa wakienda Gereza alipo Lissu ambaye anashtakiwa kwa uhaini, wamekuwa wakizuiwa kuingia kwa kile walichoelezwa kuwa hawapo katika 'list' ya mawakili ambao Lissu aliorodhesha kuwa wanaweza kumuona.
Mashahidi Kisabo na Nkung walieleza kuwa pindi walipoingia kuonana na mteja wao mara kadhaa walikaa kwenye chumba ambacho palikuwa na askari wawili wa magereza wakiskiliza maongezi na wakati mwingine waliwekwa katika Ofisi ya Mkuu wa Gereza hilo ambaye kuna nyakati alikuwepo au nyakati zingine walikuwa wasaidizi wake ambao walisikia maongezi hayo lakini pia kuna kamera ambazo huenda zilikuwa zikinasa maongezi hayo.
Hata hivyo katika ushahdi wake na dodoso Mkuu wa Gereza la Ukonga ACP Andrew Shabani alikana juu ya kusikiliza maongezi hayo na kuyaingilia lakini pia alikiri kuwa taratibu za kisheria zinataka askari magereza kuwa anasimamia maongezi ya Wakili na mteja wake katika umbali anaoweza kuona na asioweza kusikia.
Hata hivyo katika kutathmini umbali huo uliibuka utata wa kihoja kama chumba au maeneo lalamikiwa yalikuwa na ukubwa gani ambapo maafisa magereza waliokuwa mashahidi walikana kutojua umbali au ukubwa wa ofisi zao kwa vipimo kwani wao sio wataalamu wa ujenzi.
Walalamikaji katika shauri hili wanaiomba mahakama itamke kuwa kusikilizwa kwa maongezi yao na mteja wao ni kinyume cha Kanuni za Magereza lakini pia wapewe fursa hiyo na kuonana naye akiwa gerezani kwa ajili ya mashauriano. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Wananchi wa Mtaa wa Sindano, Kata ya Makumbusho jijini Dar es Salaam, wameeleza kushangazwa na ubomoaji wa nyumba zao bila taarifa ya mapema, wakidai kuwa hawakujulishwa kuhusu muda wa kuanza kwa zoezi hilo.
Wakizungumza na Jambo TV baada baada ya kufika eneo hilo, wananchi hao wamesema Oktoba 13, 2026, walipokuwa wakiendelea na shughuli zao za kila siku, walipata taarifa kuwa nyumba zao zimewekewa alama ya X, lakini waliporejea walikuta zoezi la ubomoaji likiendelea kwa kutumia tingatinga.
Wananchi hao wamedai kuwa hata kama nyumba zao zilijengwa karibu na mto katika eneo lisiloruhusiwa, walipaswa kupewa taarifa mapema kabla ya ubomoaji kuanza ili waweze kujiandaa.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa Mtaa wa Sindano, Suleiman Mohammed, amesema wananchi walipewa taarifa kuhusu zoezi hilo na kwamba wanafahamu sababu za kutakiwa kuondoka katika eneo hilo.
Amewashauri wananchi ambao hawajaridhishwa na hatua hiyo kufika katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ili kuwasilisha malalamiko yao.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba @mwigulunchemba1 anatarajiwa kutembelea Eneo Maalumu la Uwekezaji la Bagamoyo (Bagamoyo SEZ) kesho, Oktoba 16, 2026.
Eneo la Bagamoyo SEZ llinalosimamiwa na Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalumu ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) ni eneo maalum la uwekezaji ambalo lina ukubwa wa hekta 9,800 ndani yake pakiwa na maeneo yaliyotengwa viwanda vya aina mbalimbali ambavyo vimeanza kujengwa huku vingine vikiwa tayari vimeanza kufanya kazi na kuzalisha ajira. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika(TLS) Wakili Msomi Boniface Mwabukusi @Mwabuk2Boniface ametoa wito kwa Mawakili na wananchi wote nchini kutokuwa wanyonge wala kuwa na hofu kwani kufanya hivyo kutamfanya ajione kuwa amepewa jukumu ambalo watu wanaliogopa.
Ametoa wito huo leo Oktoba 15, 2026 akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuhojiwa na Jeshi la Polisi katika kituo Kuu cha Polisi(Central) jijini Dar es Salaam.
"Ni wakati wa kuunguruma kwa sauti ambayo haijawahi kusikika kwenye taifa hili, sio wakati wa unyonge, ni wakati wa kuthibitisha maana halisi ya utawala wa sheria na tutume ujumbe wa wote wanaofikiri wanatubabaisha kwamba hatubabaiki" amesema Mwabukusi
Mapema leo Mwabukusi akiambatana na mawakili wake alienda kuripoti Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Kanda Maalum ya Dar es Salaam(ZCO) ambapo inaelezwa kuwa huko alihojiwa juu ya masuala mbalimbali ikiwemo kuendesha TLS kiharakati na kuhusika kwa taasisi hiyo kufadhili maandamano ambapo inaelezwa kuwa alikataa tuhuma zote.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Imeelezwa kuwa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika(TLS) Wakili Msomi Boniface Mwabukusi amehojiwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo Baraza la Uongozi la TLS kupokea fedha za 'kufadhili' maandamano ya Oktoba 29, 2026.
Hayo yameelezwa na Wakili wa Mwabukusi Jebra Kambole leo Oktoba 15, 2026 mara baada ya mteja wao kuhojiwa na kuachiwa kwa dhamana.
"Hakuhojiwa kama mtuhumiwa amehojiwa kwa kifungu cha 36(2)(c) cha Sheria ya Ushahidi kwa hiyo amehojiwa kama shahidi...amehojiwa kwa tuhuma kwamba TLS imeacha kufanya shughuli zake kama Rais wa TLS anafanya shughuli za kiharakati akajibu kuwa TLS inafanya shughuli za kiharakati za kitaaluma"
Kwa mujibu wa Jebra mteja wao alionyeshwa video mbalimbali zenye matamko yake ikiwemo aliyowahi kuyatoa wakati wa sakata la bandari la DP World pamoja na hotuba zake alizozitoa kwa miaka kadhaa.
"Kulikuwa na tuhuma kwamba Baraza la Uongozi la TLS lilipokea fedha kwa ajili ya kufadhili maandamano ya tarehe 29 Oktoba mwaka 2026 ambayo hayajatokea alipohojiwa kuhusu tuhuma hizo alizikana tuhuma hizo kwamba baraza la uongozi halijawahi kukaa juu ya maandamano ya tarehe 29 Oktoba 2026"
Baada ya mahojiano Mwabukusi alidhaminiwa na Jebra Kambole pamoja na Ziada Mkwazu kwa masharti kuwa muda wowote atakaoitwa na Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Kanda Maalum ya Dar es Salaam(ZCO) atatakiwa kwenda.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Tukio la mauaji linalodaiwa kusababishwa na wivu wa kimapenzi limetikisa Kijiji cha Mapinduzi, Kata ya Kigwe, Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma, baada ya mwanamke mwenye umri wa miaka 58, Clementine Pius, kudaiwa kuuawa na mumewe, Raphael Ulanga, kwa kushambuliwa kwa shoka kichwani.
Tukio hilo limetokea Octoba 14 majira ya saa 4 usiku ambapo Kwa mujibu wa ndugu wa marehemu wamesema mtuhumiwa Raphael Ulanga baada ya kutekeleza shambulio hilo anadaiwa kujisalimisha mwenyewe katika kituo cha polisi.
Ndugu wamesema kifo cha Marehemu kimewaacha katika majonzi makubwa, huku wakihimiza wanandoa wenye migogoro kutafuta suluhu kupitia mazungumzo, usuluhishi na msaada wa kisheria badala ya kutumia nguvu.
Akizungumzia tukio hilo, Diwani wa Kata ya Kigwe, Adon Mabalwe, ameeleza kusikitishwa na mauaji hayo na kutoa wito kwa wanandoa na familia zinazokabiliwa na migogoro kutafuta msaada kutoka kwa viongozi na vyombo husika kabla tofauti zao hazijafikia hatua ya kusababisha madhara makubwa.
Aidha Jeshi la Polisi lilifika eneo la tukio na kuuchukua mwili wa marehemu kwa ajili ya uchunguzi na hatua nyingine za kisheria huku mtuhumiwa akishikiliwa kwa ajili ya hatua za kisheria.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Hati fungani ya Hatua Bond iliyotolewa na Benki ya I&M Tanzania imeweka rekodi mpya katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), baada ya kupokea maombi ya uwekezaji yenye thamani ya takribani Sh bilioni 161, sawa na asilimia 806.92 ya lengo la awali.
Mafanikio hayo yameifanya Hatua Bond kuvunja rekodi iliyokuwa imeshikiliwa na hati fungani ya iTrust, iliyoorodheshwa Julai 2026, na kuashiria mwitikio mkubwa wa wawekezaji katika soko la mitaji nchini.
Akizungumza katika hafla ya kuorodhesha hati fungani hiyo, leo Oktoba 15, 2026, Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji (CMSA), CPA Nicodemus Mkama, amesema mafanikio hayo yanaonesha uwezo wa masoko ya mitaji kukusanya fedha kwa ajili ya uwekezaji na kuchochea maendeleo ya uchumi.
Amesema matokeo hayo yanapaswa kuhamasisha taasisi za umma na binafsi kutumia fursa zinazotolewa na masoko ya mitaji kupata fedha za kupanua biashara na kutekeleza miradi ya maendeleo.
Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Hazina wa Benki ya I&M Tanzania, Patrick Kapella, amesema mwitikio huo unaonesha imani ya wawekezaji kwa benki hiyo na bidhaa zake za uwekezaji.
Kapella ameongeza kuwa kuorodheshwa kwa Hatua Bond katika DSE kutawawezesha wawekezaji kununua na kuuza hati fungani hiyo katika soko la sekondari, hatua inayowapa fursa ya kufanya biashara ya hati hiyo baada ya kuorodheshwa rasmi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI:
Mfanyabiashara na mkazi wa Bunju jijini Dar es Salaam, Laurence Paul Kweka (48), leo Oktoba 15, 2026 amefikishwa Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni akikabiliwa na shtaka la mauaji ya Jane Maloo Urassa.
Kesi hiyo ya mauaji namba 23407/2026, imesomwa na Wakili wa Serikali Harrison Lukosi, mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama hiyo, Kemilembe Josiah.
Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, mshtakiwa anakabiliwa na shtaka hilo chini ya Kifungu cha 196 na 197 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16, Marejeo ya Mwaka 2023.
Inadaiwa kuwa mnamo Oktoba 1, 2026, katika eneo la Bunju A, Wilaya ya Kinondoni, mkoani Dar es Salaam, Laurence Paul Kweka alimuua Jane Maloo Urassa.
Hata hivyo, kutokana na shtaka hilo la mauaji, mshtakiwa hakutakiwa kujibu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka kisheria ya kusikiliza mashauri ya mauaji.
Upande wa mashtaka umeeleza kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika. Kutokana na hali hiyo, kesi hiyo imeahirishwa na itatajwa tena Oktoba 29, 2026, mbele ya Hakimu Mkazi Josiah, huku mshtakiwa akirudishwa mahabusu kusubiri tarehe hiyo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Naibu Waziri Mkuu Kivuli na Waziri Kivuli wa Nishati na Madini wa ACT-Wazalendo, Luhaga Mpina, amesema anaamini haki itatendeka katika hukumu ya kesi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, inayotarajiwa kutolewa Novemba 6, 2026.
Akizungumza na waandishi wa habari Msimbazi Center jijini Dar es Salaam, Oktoba 15, 2026, Mpina amesema amekuwa akifuatilia mwenendo wa kesi hiyo hatua kwa hatua, akisisitiza kuwa ana matumaini ya haki kutendeka.
“Mungu atasimama na haki itatendeka. Mungu aliwaahidi watu wema na wanaomtegemea katika kitabu cha Isaya 54:17 kuwa silaha yoyote itakayotengenezwa juu yako haitafanikiwa, na kila ulimi utakaoinuka juu yako katika hukumu utauhukumu kuwa na hatia,” amesema Mpina. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Naibu Waziri Mkuu Kivuli na Waziri Kivuli wa Nishati na Madini wa ACT-Wazalendo, Luhaga Mpina, ameibua maswali kuhusu uhalali wa mchakato wa kujiuzulu kwa aliyekuwa Makamu wa Rais, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, akidai kuwa muda wa kujiuzulu kwake na uteuzi wa mrithi wake unazua utata wa kikatiba.
Akizungumza na waandishi wa habari katika Kituo cha Msimbazi, jijini Dar es Salaam, Oktoba 15, 2026, Mpina amesema hatua ya mrithi wa Nchimbi kuteuliwa na kuapishwa kabla ya tarehe iliyotajwa ya kujiuzulu kwake inahitaji ufafanuzi kwa kuzingatia Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
“Uamuzi huu umekwenda kinyume na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” amesema Mpina, akieleza kuwa utaratibu uliofuatwa unazua maswali kuhusu uhalali wa mabadiliko hayo katika nafasi ya Makamu wa Rais.
Aidha, Mpina amesema umma haujaelezwa kwa uwazi utaratibu uliotumika katika kuwasilisha na kushughulikia barua ya kujiuzulu kwa Nchimbi. Amesema ni muhimu kuwepo kwa ufafanuzi kuhusu taarifa rasmi za kujiuzulu na hatua zilizochukuliwa na mamlaka husika.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mtangazaji wa masuala ya siasa nchini, Chief Odemba, ameadhimisha siku yake ya kuzaliwa Oktoba 14 kwa kukata keki na watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu, akitumia siku hiyo muhimu katika maisha yake kuleta furaha na matumaini kwa watoto hao.
Katika maadhimisho hayo, Chief Odemba alitembelea watoto hao na kuwapatia msaada wa mahitaji mbalimbali, akiamini kuwa siku ya kuzaliwa si wakati wa kusherehekea maisha pekee, bali pia ni fursa ya kuwagusa wenye uhitaji na kushiriki nao kile ambacho Mwenyezi Mungu amemjaalia. Hatua hiyo imelenga kuwafariji watoto hao na kuwafanya wajisikie kupendwa, kuthaminiwa na kukumbukwa katika jamii.
Akizungumza kuhusu maadhimisho hayo, ujumbe wake ni kuhamasisha Watanzania kujenga utamaduni wa kusaidiana, hasa kwa watoto wanaokabiliwa na changamoto mbalimbali za maisha.
Chief Odemba amesisitiza umuhimu wa upendo, mshikamano na moyo wa kujitolea, akiamini kuwa zawadi yenye thamani kubwa katika siku ya kuzaliwa si mali wala sherehe kubwa, bali ni tabasamu unaloweza kulileta kwenye uso wa mtu mwingine mwenye uhitaji.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika, Wakili Boniface Mwabukusi akiongozana na timu ya Mawakili wake kuelekea kituo kikuu cha Polisi(Central) jijini Dar es Salaam.
Mwabukusi amedai kuwa alipata wito kutoka kwa Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai(ZCO) Kanda Maalum ya Dar es Salaam akitakiwa kufika kituoni hapo leo Oktoba 15, 2026.
Kwa mujibu wa Mawakili wake mpaka sasa hawajafahamu kile ambacho kimesababisha Mwabukusi kupokea wito huo hivyo watamsindikiza mteja wao na kusikiliza kile walichoitiwa.
Timu ya mawakili hao yupo Wakili Paul Kisabo kutoka Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania(THRDC), Wakili Jebra Kambole, Wakili Joseph Gideon ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa TLS-AYL na mawakili wengine.
Hata hivyo jitihada zinaendelea kupata taarifa za mamlaka husika juu ya wito huo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI:
Serikali ya Kenya inaandaa mkakati mpya wa mawasiliano ili kurejesha imani ya wananchi katika miradi ya mafuta na gesi, kufuatia malalamiko kuhusu fidia, ajira, mgawanyo wa mapato na upatikanaji wa maji katika maeneo yanayotekelezwa miradi hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa na vyombo vya habari nchini humo, Oktoba 14, 2026, wadau waliokutana katika warsha ya kupitia mkakati huo wameeleza umuhimu wa kuwashirikisha wananchi katika maamuzi yanayoathiri maisha yao, badala ya kuwapa taarifa baada ya maamuzi kufikiwa.
Mshauri mkuu wa mkakati huo, Dkt. Victoria Kutto, amesema ukosefu wa ushirikishwaji ni miongoni mwa mambo yanayochangia kutokuaminiana kati ya jamii na waendelezaji wa miradi ya mafuta na gesi.
Kwa upande wake, mshauri wa mikakati ya mawasiliano, Dkt. Enoch Warinda, ametaja taarifa potofu, kuingiliwa kwa masuala ya kisiasa na changamoto za kimazingira, ikiwemo kumwagika kwa mafuta, matumizi ya ardhi na fidia, kuwa miongoni mwa vikwazo vinavyoweza kuathiri utekelezaji wa miradi hiyo.
Ili kukabiliana na changamoto hizo, mkakati unapendekeza kuwepo kwa njia zilizo wazi za kupokea na kushughulikia malalamiko, utoaji wa taarifa kwa lugha rahisi na usimamizi bora wa majukwaa ya WhatsApp ili kudhibiti kuenea kwa taarifa potofu.
Pia, unalenga kuhakikisha wanawake, vijana na makundi mengine ya jamii yanapata taarifa zinazozingatia mahitaji yao, huku yakipewa nafasi ya kushiriki katika maamuzi.
Mkakati huo unatarajiwa kusaidia kuongeza uwazi na kuimarisha ushiriki wa wananchi katika miradi ambayo inaweza kuathiri moja kwa moja maisha yao na shughuli zao za kiuchumi. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Damas Mgaya (38), mkazi wa Mtaa wa Kambarage, Halmashauri ya Mji wa Njombe, amefariki dunia baada ya kukutwa amejinyonga ndani ya chumba chake kwa kutumia kamba ya kiatu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, ACP Mahamoud Banga, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo lililoripotiwa jana , Oktoba 13, 2026, majira ya saa 12 asubuhi.
Kwa mujibu wa Kamanda Banga, marehemu alikutwa akiwa amejinyonga kwa kutumia kamba iliyofungwa kwenye nondo ya dirisha.
RPC Banga amesema tukio hilo linadaiwa kuhusishwa na mgogoro wa kifamilia kati ya marehemu na mkewe, uliotokana na kutokubaliana kuhusu masuala ya ndoa na tendo la ndoa, ambapo inadaiwa kuwa mkewe alikataa kushiriki tendo hilo akieleza kuwa Mumewe hajaokoka.
"Sababu kuu ya tukio hili ni msongo wa mawazo ambao umetokana na kuto kuwa na maelewano na mke wake kwamba mgogolo wa kifamilia ambao upo,Marahemu huyu alikuwa hawezi kushiriki tendo la ndoa kwasababu mke wake alikuwa anadai ameokoka"amesema Kamanda Banda
Aidha, Kamanda huyo ametoa wito kwa viongozi wa dini kuzingatia mafundisho yanayojenga amani, maelewano na mshikamano katika familia na jamii, huku akieleza kuwa Jeshi la Polisi halitasita kuchukua hatua pale inapobainika kuwepo kwa vitendo vinavyokiuka sheria.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi, amesema amani na utulivu ni msingi muhimu wa maendeleo ya taifa, akisisitiza kuwa utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2050 unategemea uwepo wa amani nchini.
Akizungumza katika ziara ya Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2026, mkoani Rukwa, Makamu wa Rais amesema Baba wa Taifa, Mwalimu Kambarage Nyerere, alitetea utu, usawa na haki bila ubaguzi wa rangi, dini, kabila au tabaka, huku akipinga dhuluma, ufisadi, rushwa na chuki.
Amesema, “Pasipo amani na utulivu hakuna maendeleo,” akieleza kuwa rasilimali za nchi zinapaswa kutumika kupambana na umaskini, ujinga na maradhi, huku wananchi wakishiriki kikamilifu katika kuleta maendeleo yao.
Aidha, amewataka Watanzania kuendeleza umoja na mshikamano wa kitaifa licha ya tofauti za itikadi, imani na mitazamo, akisisitiza kuwa kila mwananchi ana wajibu wa kulinda amani na utulivu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi, amesema baada ya kutembelea Banda la Ofisi ya Rais, Maendeleo ya Vijana na Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Mahusiano, amebaini kuwa zipo changamoto katika suala la kuhakikisha mifumo ya Serikali inasomana, hasa katika kuwawezesha vijana kupata fursa mbalimbali ikiwemo ajira Serikalini.
Ameeleza hayo Oktoba 14, 2026 alipokuwa akihutubia katika Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa 2026, kilichofanyika Mkoani Rukwa, sambamba na maadhimisho ya wiki ya vijana kitaifa. Amesema amebaini uwepo wa mifumo mitatu tofauti ambayo yote ni ya Serikali moja, jambo ambalo amesema linaweka ugumu kwa vijana kupata nafasi hasa ajira.
"Maelekezo ya Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambayo amekuwa akiyatoa mara kwa mara ya kutaka mifumo isomane, bado tupo nyuma Waziri Mkuu. Huku kuna 'Yes', mfumo mzuri kabisa, huku kuna kazi portal, nayo kazi portal kijana huyu huyu anayejisajili Yes, anatakiwa na yeye aingie kazi Portal, lakini huyuhuyu kijana aliyehitimu wakati anatafuta ajira ya kuingia katika Public Service, tunamuambia tena ajisajili ajira portal. Serikali moja, mifumo mitatu". Amesema Makamu wa Rais Ndejembi.
Ameongeza kuwa, licha ya kwamba alitoa maelekezo ya kutaka kuratibiwa kwa utaratibu wa kuwatengeneza na kuwapa ujuzi vijana wa Tanzania katika kipindi cha wiki mbili na akaombwa muda zaidi ambao tayari umekwisha, sasa ametaka kupewa taarifa ya uratibu wa mifumo hiyo siku ya Jumatatu ili aweze kuwasilisha mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Baadhi ya wazee nchini wameeleza masikitiko yao kuhusu kile wanachokiona kuwa kupungua kwa uzingatiaji wa misingi na maadili aliyoiacha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, wakisema hali hiyo inatofautiana na taifa alilolikusudia.
Wakizungumza jijini Dodoma leo, Oktoba 14, 2026, wakati wa kuadhimisha miaka 27 tangu kifo cha Mwalimu Nyerere, wazee hao wamekumbuka mchango wake katika kupigania uhuru wa Tanganyika na kujenga taifa, wakitaja uadilifu, umoja na uzalendo kuwa miongoni mwa misingi wanayoona inaanza kupoteza nguvu katika jamii.
Mmoja wa wazee hao amesema licha ya changamoto zilizokuwepo wakati wa kupigania uhuru, Mwalimu Nyerere alipambana hadi Tanganyika ilipopata uhuru na taifa kuendelea kujengwa, akieleza kuwa hali ya sasa si ile aliyokuwa akiitarajia.
“Pamoja na kwamba tulipata uhuru katika shida, aliweza kupambana mpaka tukafikia sehemu hii. Angekuwepo leo, Nyerere angesema tumepotea; aliyokuwa anaiacha si hii,” amesema.
Wazee hao wamewataka Watanzania kuendelea kumuenzi Mwalimu Nyerere kwa vitendo, kwa kudumisha umoja, mshikamano na uzalendo, wakisisitiza kuwa maadili hayo ni muhimu katika kulinda amani na kuimarisha mshikamano wa kitaifa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Jumatatu, Oktoba 12, 2026, muungano mpya unaoitwa Front for the Refoundation of the Nation, kwa kifupi FRN kutoka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ulitangaza rasmi Joseph Kabila ambaye ni Rais wa zamani wa taifa hilo kuwa kiongozi wake.
Muungano huo umesema unalenga kuunganisha nguvu za makundi yanayopinga serikali ya Tshisekedi ili kukomesha kile unachokiita utawala wa kidikteta nchini humo.
Katika tamko lake, FRN imesema iko tayari kutumia njia zote kufikia lengo hilo, ikiwemo nguvu.
Tangazo hilo lilitolewa mjini Goma, mashariki mwa DRC, katika eneo ambalo limekuwa chini ya udhibiti wa M23 tangu Februari 2025.
Claude Ibalanky, mshauri wa muungano huo, ndiye aliyetangaza muundo wa uongozi wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika makazi ya Kabila.
Miongoni mwa viongozi waliotajwa ni Sultani Makenga, kiongozi wa M23, aliyeteuliwa kuwa mmoja wa manaibu wanne wa Kabila. Manaibu wengine watatu pia wanatoka katika muungano wa AFC-M23.
Jambo linalofanya tangazo hili kuwa muhimu ni kwamba halihusishi tu kuanzishwa kwa kundi jipya la kisiasa. Linaashiria pia kuunganishwa kwa sura ya zamani ya uongozi wa nchi na harakati za waasi wanaopigana na serikali iliyopo madarakani........
Tembelea YouTube chanel ya Jambo tv kupata makala kamiliThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Moto umezuka katika eneo la Shamsi jijini Arusha, mapema leo Oktoba 14, 2026, na kuteketeza sehemu kubwa ya jengo la Tarakea Baa pamoja na mali mbalimbali zilizokuwa ndani yake.
Kwa mujibu wa mashuhuda, moto huo ulianza majira ya saa 11 alfajiri baada ya kutokea kwa shoti ya umeme iliyosababisha mbao zilizokuwa pembezoni mwa jengo hilo kushika moto, kabla ya kusambaa katika jengo zima.
Mmoja wanafamilia wanaomiliki baa hiyo amesema amesikitishwa na tukio hilo, akieleza kuwa mzigo mpya wa vinywaji uliingizwa jana, lakini umeteketea kwa moto uliozuka leo.
Amesema uharibifu huo unaweza kuathiri shughuli za biashara hiyo na kusababisha baadhi ya wafanyakazi kukosa ajira kutokana na hasara iliyotokea.
Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani Arusha, Oswadi Mwanjejele, amesema shoti ya umeme ilisababisha mbao zilizokuwa pembezoni mwa jengo kushika moto na kusababisha moto kusambaa kwa kasi.
Amesema hakuna madhara yaliyowapata binadamu, hata hivyo, mali mbalimbali zimeteketea, zikiwemo vitanda na magodoro, pamoja na vyumba 14 vya kulala wageni vilivyokuwa ndani ya gesti hiyo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Shabiki wa Simba, Kay Mziwanda, akizungumzia uwezo wa mshambuliaji wa klabu hiyo, Ibrahim Doumbia, amesema uongozi wa Simba 'umepigwa', akipendekeza mchezaji huyo aitwe na kuhojiwa kwa upole ili huenda akafichua kazi yake halisi.
Kay ametoa kauli hiyo Oktoba 13, 2026, baada ya mchezo kati ya Simba na Mashujaa uliomalizika kwa Simba kuibuka na ushindi wa mabao 6-1.
Video kamili inapatikana YouTube channel ya Jambo TV.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, John Heche, amemjibu Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, kuhusu hali ya miundombinu ya barabara nchini, akisema bado kuna changamoto ya ubovu wa barabara katika maeneo mbalimbali.
Hoja hiyo imekuja baada ya Heche kulalamikia hali ya barabara kupitia mitandao ya kijamii, ambapo Msigwa alijibu kwenye maoni ya chapisho hilo, akieleza juhudi za serikali katika ujenzi wa barabara na kumtaka Heche azungumzie pia miradi inayoendelea kutekelezwa.
Akijibu hoja hiyo Oktoba 13,2026 jijini Arusha, Heche amesema ubovu wa barabara ni miongoni mwa mambo yanayopaswa kuzingatiwa katika kujadili sababu za ajali za barabarani, badala ya kuhusisha ajali hizo na uzembe wa madereva pekee.
Heche pia amelinganisha ujenzi wa reli wakati wa ukoloni na kipindi cha baada ya uhuru, akieleza kuwa wakoloni waliweza kujenga reli kwa muda mfupi, huku Tanzania ikiwa imetimiza miaka 65 ya uhuru, lakini urefu wa reli iliyojengwa katika kipindi hicho ni mdogo ikilinganishwa na reli zilizojengwa wakati wa ukoloni.
Hali hiyo imeibua mvutano wa hoja za kisiasa kati ya Heche na Msigwa kuhusu maendeleo ya miundombinu nchini. Wakati Msigwa akisisitiza juhudi za serikali katika ujenzi wa barabara na miradi mingine ya maendeleo, Heche amekuwa akiibua changamoto za ubovu wa barabara na kuhoji kasi ya maendeleo ya miundombinu nchini.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, John Heche, amewataka Watanzania kutambua kuwa nchi ni mali ya wananchi wote na siyo ya viongozi wachache au familia zao, hivyo kila raia ana wajibu wa kikatiba wa kulinda na kupigania haki za taifa.
Akizungumza na wakazi wa Mkoa wa Arusha muda mfupi baada ya kuzindua ofisi ya CHADEMA Kanda ya Kaskazini katika kata ya Ereri, Jumanne Oktoba 13, 2026, Heche ameeleza kuwa matatizo ya maji, umeme, na barabara yanayoikabili Arusha ndiyo yanayoikabili mikoa ya Mwanza, Mtwara, na Lindi, na kwamba chanzo kikuu ni uongozi mbovu unaodai kuwa unawakandamiza wananchi.
Heche amekemea tabia ya baadhi ya wananchi kubaki kimya wakati viongozi au watetezi wa haki wanapopitia changamoto au kujitoa mhanga kwa ajili ya maslahi ya umma. Ametolea mfano wa aliyekuwa Balozi wa Cuba, Humphrey Polepole aliyejiuzulu nafasi yake kuitetea nchi lakini jamii ikabaki kimya
“Tunastahili kuipenda nchi hii wote, tunastahili kuipigania nchi hii wote, na tunastahili kuilinda nchi hii sisi wote... Polepole alikuwa balozi, amejiuzulu kwasababu yenu... akasema sitaki ubalozi narudi kupigania nchi yangu inaenda shimoni... Mko kimya. Hivi mimi nikiamua kuacha hii kazi mtanilaumu kwamba nimekuwa msaliti au ninyi mmenisaliti?", ameeleza.
Heche amewataka wananchi kubadilika, kuacha mtazamo wa kudhani wanasiasa wanapigania maslahi binafsi, na badala yake kuungana mkono kupigania Katiba Mpya na maendeleo ya kizazi kijacho.
Katika hatua nyingine, Heche, ameeleza kuwa Tanzania ina hifadhi kubwa ya rasilimali za madini adimu ardhini akieleza kuwa matumizi bora ya rasilimali hizo yana uwezo wa kuondoa umaskini kwa Watanzania wote zaidi ya milioni 70. Amedai kuwa usimamizi mzuri wa rasilimali hizo ambazo hutumika duniani kote kutengeneza teknolojia za kisasa kama simu, kamera, magari ya umeme, na injini za ndege utawezesha Watanzania wote kuishi maisha yenye ufahari kiasi cha serikali kuweza kuwalipa mishahara pasina kufanya kazi kwa miaka 100. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Kada wa CHADEMA, Mchungaji Peter Msigwa, amewakosoa baadhi ya viongozi wa dini nchini, akiwatuhumu kushindwa kusimama katika nafasi zao na kukemea maovu yanayotokea katika jamii na taifa kwa ujumla.
Akizungumza jana Oktoba 13, 2026, jijini Arusha, wakati wa uzinduzi wa ofisi ya CHADEMA Kanda ya Kaskazini, Msigwa amesema baadhi ya viongozi hao wamekuwa wepesi kukemea mambo madogo, lakini wanashindwa kuzungumzia masuala mazito kama mauaji na ufisadi.
Msigwa amewataka Viongozi wa dini kuiga mifano ya viongozi wa kibiblia kama Nabii Nathani, Danieli na Amosi, ambao walisimama katika ukweli, kukemea dhuluma na kutetea haki za watu, wakiwemo maskini.
Aidha, ametoa mfano wa Martin Luther King, akisisitiza kuwa viongozi wa dini wanapaswa kusimama katika kweli na kukemea maovu bila kuogopa, ili kusaidia kujenga jamii yenye haki na uwajibikaji. -
Jambo TV
@Jambotv_
RAIS SAMIA MGENI RASMI KILELE CHA MAADHIMISHO MIAKA 70 YA TAASISI ZA KIRAIA OKTOBA 29 jambo.co.tz/samia-mgeni-rasmi-kilele-maadhimisho-miaka-70… via @jambotv_
-
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkandarasi anayetekeleza Mradi wa Maji wa Miji 28 katika Mji wa Korogwe, Mkoani Tanga, amefanikiwa kufanya majaribio ya kusafirisha maji kutoka kwenye chanzo cha maji na kuyafikisha katika eneo la mtambo wa kutibu maji (WTP) tarehe 12 Oktoba 2026, hatua inayoonesha maendeleo katika utekelezaji wa mradi huo.
Hatua hiyo inafuatia agizo la Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, alilolitoa Septemba 21, 2026, akimtaka mkandarasi kuhakikisha ndani ya siku tisa, ifikapo Septemba 30, anaanza majaribio ya kuyatoa maji mtoni na kuyapeleka kwenye mtambo wa kutibu maji.
Mafanikio hayo yanaonesha kuwa kazi ya majaribio imefikiwa, huku jitihada zikiendelea kuhakikisha mradi unakamilika na maji yanaanza kuingizwa kwenye mtandao wa usambazaji ifikapo mwishoni mwa Novemba, ili wananchi waanze kupata huduma ya maji.
Mradi huo unatarajiwa kunufaisha wananchi wa Wilaya za Korogwe, Handeni, Muheza na Pangani, huku Serikali ikiendelea kusimamia utekelezaji wa miradi ya maji ili kuboresha upatikanaji wa huduma hiyo kwa wananchi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Katiba na Sheria, Abdallah Hamis Ulega ametoa maagizo kwa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka akisisitiza umuhimu wa watendaji kufanya kazi kwa bidii, weledi, na ufanisi wa hali ya juu ili kuimarisha mfumo wa upatikanaji wa haki nchini.
Akizungumza leo Oktoba 13, 2026 katika kikao chake cha kujitambulisha kwenye ofisi hizo zilizoko Njedengwa jijini Dodoma, Waziri Ulega ameelekeza kuwa ni lazima maagizo ya viongozi wakuu wa serikali na mapendekezo ya Tume ya Jaji Chande yafanyiwe kazi kwa vitendo usiku na mchana.
Amesisitiza kuwa kesi lazima zifikishwe mahakamani kwa wakati na watuhumiwa wanaostahili wapatiwe dhamana kisheria ili kupunguza wimbi la msongamano mkubwa wa mahabusu gerezani.
Aidha, Waziri Ulega ameeleza kufurahishwa kwake na ongezeko la watendaji wa mashtaka kutoka 630 hadi kufikia 1,200, akabainisha kuwa ongezeko hilo linapaswa kuendana na kasi mpya ya utendaji kazi na kuleta matokeo chanya yanayoonekana. Sambamba na hayo, amevitaka vitengo vya elimu kwa umma kuongeza nguvu katika kutoa uelewa kwa wananchi kuhusu vigezo na taratibu za kisheria za dhamana, hatua itakayosaidia kupunguza malalamiko na kujenga imani kubwa ya umma kwenye vyombo vya utoaji haki.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Mkutano wa 11 wa Kitaifa wa Kilimo Misitu nchini Tanzania unatarajiwa kufanyika kuanzia Oktoba 19 hadi 21, 2026, katika Kituo cha Mafunzo ya Kilimo Misitu kilichopo Bweri, Musoma mkoani Mara, ukiwa na lengo la kufungua fursa za uwekezaji wa kijani unaoongozwa na vijana pamoja na kuimarisha mikakati ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Musoma, Meneja wa Vi Agroforestry nchini, Martha Olotu amesema mkutano huo utawakutanisha wawakilishi wa serikali, vijana, wakulima, wafanyabiashara, taasisi za fedha, watafiti na wadau wa maendeleo ili kujadili fursa za uwekezaji na kuimarisha ushirikiano katika mnyororo mzima wa thamani wa kilimo misitu.
Amesema mkutano huo wa kitaifa unalenga kubaini fursa za uwekezaji na biashara zinazoweza kutekelezeka katika sekta hiyo, huku ukichangia kuimarisha ustahimilivu dhidi ya mabadiliko ya tabianchi, usalama wa chakula na maendeleo endelevu vijijini.
Kwa mujibu wa Olotu, mkutano huo wenye kaulimbiu isemayo “Kilimo Misitu kwa Ajili ya Vijana na Uwekezaji wa Kijani,” unalenga kuwawezesha vijana kushiriki kikamilifu kama wakulima, wajasiriamali, wabunifu na viongozi katika kuijenga Tanzania yenye uchumi wa kijani unaostahimili changamoto za kimazingira.
“Majadiliano yatajikita katika upatikanaji wa mbegu na miche bora, uzalishaji endelevu, usindikaji, upatikanaji wa masoko, maendeleo ya biashara na upatikanaji wa fedha kwa ajili ya uwekezaji wa kijani, kwa lengo la kuifanya sekta ya kilimo misitu kuwa chanzo cha biashara endelevu na ajira zenye staha,” amesema.
Olotu amesema mkutano huo unafanyika wakati Tanzania ikiendelea kutekeleza dhamira yake ya kuhifadhi mazingira, kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kuimarisha usimamizi endelevu wa ardhi.
Ameeleza kuwa Programu ya Mageuzi ya Usimamizi wa Mazingira kuelekea Dira ya Maendeleo ya Tanzania 2050 inalenga kuunga mkono utekelezaji wa dira hiyo, ikiwamo azma ya kupanda miti bilioni mbili kila mwaka, huku Serikali ikiwa na lengo la kupanda miti bilioni 10 ifikapo mwaka 2030.
“Kilimo misitu kinaweza kugeuza malengo haya kuwa matokeo halisi kwa kuboresha rutuba ya udongo, kuimarisha upatikanaji wa maji, kurejesha bioanuwai, kuongeza kipato cha wananchi wa vijijini na kujenga mifumo ya chakula inayostahimili changamoto mbalimbali.Matokeo haya yanaendana pia na vipaumbele vya Afrika na dunia kwa ujumla katika kutafuta suluhisho zinazotekelezeka na zinazoongozwa na jamii husika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, uharibifu wa ardhi na ukosefu wa ajira kwa vijana”, amesema.
Amesisitiza kuwa ili kufikia manufaa hayo, ni muhimu kuachana na mtazamo wa kampeni za muda mfupi za upandaji miti na kuelekea katika mifumo endelevu ya uzalishaji inayohakikisha miti inastawi, inazalisha thamani ya kiuchumi na kusaidia kuimarisha mashamba, biashara na mazingira kwa muda mrefu.
Amesema vijana wana fursa ya kuanzisha na kuendeleza biashara zinazohusiana na ukusanyaji wa mbegu, uanzishaji wa vitalu vya miche, upandaji na utunzaji wa miti, utoaji wa huduma za kitaalamu, matumizi ya teknolojia za kidijitali, usindikaji na uuzaji wa mazao.
Hata hivyo, amesema ili vijana waweze kutumia fursa hizo kikamilifu, wanahitaji ujuzi wa vitendo, upatikanaji salama wa ardhi, mitaji, huduma za kuwaendeleza kibiashara, huduma za ugani pamoja na masoko ya uhakika.
Olotu amesema Mkakati wa Taifa wa Kilimo Misitu Awamu ya Pili (2024–2031) unaweka msingi wa kuratibu utekelezaji wa shughuli za sekta hiyo, akibainisha kuwa kipaumbele cha sasa ni kuhakikisha mkakati huo unatafsiriwa katika bajeti, huduma na uwekezaji katika ngazi za kitaifa na za maeneo husika. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Victoria Mwanziva akiambatana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi, Juma Mnwele, na Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Mchinga, Abdallah Mkokoi wameshiriki zoezi la uchimbaji wa msingi wa ujenzi wa Zahanati ya katika kijiji cha Mchinga 1.
Ushiriki wa viongozi hao ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za wananchi wa Kijiji cha Mchinga 1, ambao wameamua kuunganisha nguvu zao katika ujenzi wa zahanati hiyo kwa lengo la kusogeza huduma za afya karibu na wananchi, ambapo Serikali ya Kijiji imetanguliza kiasi cha Shilingi milioni 10 kufanikisha hatua hii ya ujenzi.
Aidha, ujenzi wa zahanati hiyo unatarajiwa kuwa na mchango mkubwa katika kuboresha upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi wa kijiji hicho na maeneo jirani, huku ukionesha umuhimu wa ushirikiano kati ya wananchi na viongozi katika kutekeleza miradi ya maendeleo.
Aidha katika hatua hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Lindi ametoa wito kwa wananchi na wadau kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali katika kuwaletea maendeleo wananchi wake na kusisitiza kuwa, serikali sikivu ya awamu ya sita chini ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan itahakikisha inaunga mkono juhudi hizi zilizowekwa na wananchi katika kumalizia ujenzi wa zahanati hiyo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa, Juma Mnwele naye kwa upande wake amewapongeza wananchi wa Kijiji cha Mchinga pamoja na uongozi wa kijiji kwa jitihada hizi kubwa walizochukua. Aidha ametumia nafasi hiyo kuahidi kumalizia hatua ya mwisho mara baada ya kukamilika boma.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA na aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, amesema yupo katika hali ya kukata tamaa kutokana na mwenendo wa baadhi ya vijana wanaotanguliza burudani badala ya masuala muhimu ya kisiasa na kijamii.
Akizungumza leo Oktoba 13,2026 jijini Arusha katika hafla ya uzinduzi wa ofisi ya CHADEMA Kanda ya Kaskazini, Lema amesema baadhi ya vijana wamekuwa wakijikita katika matamasha ya burudani, ikiwemo tamasha la kuadhimisha miaka 30 ya muziki wa Bongo Fleva na matamasha ya Nyama Choma, akidai kuwa hali hiyo inawafanya kusahau masuala ya msingi yanayohusu haki na mustakabali wa taifa.
Amesema inaumiza kuona baadhi ya wananchi hawatoi uzito unaostahili kwa mapambano ya kudai haki, akitolea mfano wa Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, ambaye anashikiliwa mahabusu ya magereza akikabiliwa na kesi ya uhaini.
Aidha, Lema amewataka vijana kuelekeza nguvu zao katika masuala muhimu ya kisiasa na kufuatilia mwenendo wa kesi ya Tundu Lissu, huku akieleza kuwa licha ya juhudi zake za muda mrefu katika kupigania haki za wananchi, mwenendo wa baadhi ya vijana umemvunja moyo na kumfanya ajikute katika hali ya kukata tamaa, akimuomba Mungu amsaidie.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi ametangaza kuwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia Ofisi ya Msajili wa Taasisi za Kiraia inatarajia kuadhimisha miaka 70 ya usajili, usimamizi, na udhibiti wa taasisi hizo nchini kuanzia tarehe 27 hadi 29 Oktoba, 2026, katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Akizungumza leo Oktoba 13, 2026 jijini Dar es Salaam, Katambi ameeleza kuwa usajili wa taasisi hizo unaofanyika chini ya Sheria ya Usajili wa Jumuiya za Kiraia (Sura namba 337) una lengo kuu la kulinda na kudumisha amani na usalama wa nchi, huku ikijumuisha taasisi za kidini, kimila, kibiashara, na kijamii.
Katambi amebainisha kuwa Mgeni Rasmi katika siku ya kilele cha maadhimisho hayo tarehe 29 Oktoba 2026 anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Ameongeza kuwa maadhimisho hayo yatatoa fursa na jukwaa maalum la kuimarisha amani na usalama, kuboresha ushirikiano wa kimkakati kati ya serikali na taasisi za kiraia, pamoja na kukusanya maoni, ushauri, na mijadala ya kuboresha sera, sheria, na mifumo ya utendaji wa taasisi hizo ili kuwahudumia Watanzania kwa ufasaha.
Maadhimisho hayo yatawakutanisha viongozi wa taasisi za dini, viongozi wa kijamii na kimila, wanazuoni, wageni kutoka ndani na nje ya nchi, viongozi wa serikali, pamoja na wawakilishi kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BOT) na benki za biashara.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkurugenzi wa Amsterdam Group, Joseph Sulle, ametangaza mwaliko kwa jamii ya wafugaji wa kuku na wadau wote wa sekta ya mifugo kushiriki katika tukio kubwa la Tanzania Poultry Show 2026 litakalofanyika tarehe 16 na 17 Oktoba, 2026, katika Ukumbi wa Kilimanjaro, Ubungo Plaza.
Akizungumza leo makao makuu ya Amsterdam Group, Sulle amesema tukio hilo, linaloandaliwa na Tanzania Poultry Association, linalenga kukutanisha wadau wote wa sekta ya kuku nchini ili kuonesha huduma zao, kutoa elimu bure na kushirikisha teknolojia mpya zinazotumika Tanzania, Afrika na duniani kwa ujumla.
“Elimu ni bure, hakuna kiingilio,” amesisitiza Sulle, huku akieleza kuwa shughuli zitaanza saa 2 asubuhi hadi saa 11 jioni kila siku kwa siku hizo mbili.
Aidha, tarehe 16 kutakuwa na tukio maalum la Tanzania Poultry Champions Award 2026, ambalo litawatambua na kuwapa tuzo wafugaji na watengenezaji wa vyakula vya mifugo bora ili kuwatia moyo katika kazi zao.
Aidha Mgeni Rasmi atatoa maelezo kuhusu mipango ya serikali ya kukuza sekta ya kuku, huku wadau kutoka nchini na nje watatoa elimu juu ya mbinu mbalimbali zenye tija kwa wafugaji.
Amsterdam Group, kama moja ya kampuni zinazotoa huduma za ufugaji wa kuku, itashiriki katika tukio hilo kwa kuonesha bidhaa na huduma zake. Mtaalamu wa mifugo kutoka kampuni hiyo amethibitisha kuwa watakuwa kwenye banda namba 27 na kuwaalika wafugaji na wadau kuwatembelea, kujifunza na kuona bidhaa zao.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT), Francis Alfred, amewataka wakulima wa korosho kuzingatia kanuni bora za ukaushaji ili kuhakikisha wanapata bei shindani sokoni.
Akizungumza baada ya mnada wa kwanza wa msimu wa 2026/2027 uliofanyika Oktoba 13, 2026, kupitia Chama Kikuu cha Ushirika cha MAMCU, katika Halmashauri ya Mji wa Masasi, mkoani Mtwara, amesema ubora wa korosho ni muhimu katika kuongeza ushindani wake sokoni.
Alfred amewataka wasimamizi wa maghala kuhakikisha hawapokei korosho ambazo hazijakauka ipasavyo, akisisitiza kuwa hatua hiyo italinda ubora wa zao na kuwawezesha wakulima kunufaika zaidi na mauzo yao.
Katika mnada huo, korosho zimeuzwa kwa bei ya juu ya Sh. 3,370 kwa kilo na bei ya chini ya Sh. 3,110 kwa kilo, huku jumla ya kilogramu milioni kumi, laki tisa na themanini na tisa elfu na mia tatu arobaini na mbili zikiuzwa.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa MAMCU, Azam Mfaume, amewataka viongozi wa vyama vya msingi vya ushirika (AMCOS) kuharakisha malipo kwa wakulima ili waweze kupata fedha zao kwa wakati na kuendelea na shughuli za uzalishaji bila changamoto za kifedha.
Baadhi ya wakulima walioshiriki mnada huo, akiwemo Rehema Dienga na Hamza Abdulkarim, wameeleza kuridhishwa na bei zilizopatikana na kutoa wito kwa wanunuzi kuendelea kununua korosho kwa bei nzuri bila kuzishusha. Wamesema matumaini yao ni kuona soko likiendelea kutoa bei zinazowapa motisha ya kuongeza uzalishaji.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Waziri Mkuu wa Tanzania Dkt. Mwigulu Nchemba, amesema kujenga ustahimilivu dhidi ya maafa ni wajibu wa pamoja unaohitaji ushiriki wa serikali, sekta binafsi na jamii, akisisitiza umuhimu wa maandalizi kuanzia katika ngazi ya kaya.
Dkt. Mwigulu amesema hayo leoOktoba 13, 2026, wakati akitoa tamko la kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kupunguza Hatari ya Maafa katika Uwanja wa Nelson Mandela, Sumbawanga mkoani Rukwa.
Amesema serikali itaendelea kuimarisha mifumo ya kuzuia na kupunguza athari za maafa katika ngazi ya taifa na jamii, kuboresha utoaji wa taarifa na kuongeza uhamasishaji wa umma kuhusu hatua za tahadhari na maandalizi.
Waziri Mkuu amesisitiza kuwa familia ndiyo msingi wa jamii, hivyo usalama na ustahimilivu wa kaya ni muhimu katika kuijengea jamii uwezo wa kujiandaa, kukabiliana na maafa na kurejesha hali ya kawaida baada ya kutokea.
Aidha, amehimiza mamlaka za serikali za mitaa, taasisi za utafiti, mashirika yasiyo ya kiserikali, vyombo vya habari, taasisi za dini na viongozi wa kimila kushiriki katika kuimarisha maandalizi na ustahimilivu wa jamii dhidi ya maafa.
Akizungumzia maandalizi ya msimu wa mvua za vuli wa Oktoba hadi Desemba, amewataka wananchi kuzingatia tahadhari zilizotolewa na kujiandaa mapema ili kupunguza hatari na athari za maafa. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Heche leo Oktoba 13, 2026, amezindua rasmi ofisi ya chama hicho Kanda ya Kaskazini, iliyopo Kata ya Elerai mkoani Arusha.
Ofisi hiyo inalenga kuratibu shughuli za chama katika Kanda ya Kaskazini inayojumuisha mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Tanga, pamoja na kurahisisha utekelezaji wa majukumu mbalimbali ya kichama.
Uzinduzi huo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa CHADEMA, akiwemo Godbless Lema, Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, pamoja na Amani Golugwa, Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Bara.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mfanyabiashara na mkazi wa Ilala ambaye ni Mshirazi, Luqman Issac, maarufu kama Luqman Albusayyid leo Oktoba 13, 2026, amefikishwa tena katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya usikilizwaji wa kesi inayomkabili.
Kesi hiyo iliyotajwa mbele ya Hakimu wa mahakama hiyo, Beda Nyaki, imepata mwelekeo mpya baada ya upande wa mashtaka kuiarifu Mahakama kuwa upelelezi wake umekamilika.
Kutokana na hatua hiyo, Jamhuri imeiomba Mahakama iwape muda ili waweze kuandaa na kukamilisha nyaraka zote za muhimu ambazo zitawezesha kuanza kwa hatua ya usikilizaji wa hoja za awali.
Akijibu ombi hilo, Hakimu Beda Nyaki, amekubali kutoa muda na kuahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 26, 2026, itakapofikishwa tena mahakamani hapo kwa ajili ya usikilizaji. Katika msisitizo wake, Hakimu Nyaki amewataka mawakili wa Jamhuri kuhakikisha wanarudi siku hiyo wakiwa na nyaraka zote zikiwa zimekamilika.
Akizungumza mbele ya Mahakama, mshtakiwa Luqman ameeleza kuwa yuko tayari kwa ajili ya tarehe hiyo mpya na kwamba anasubiri kwa hamu kuonana na mtu ambaye Jamhuri inadai alimsafirisha.
Vilevile, mshtakiwa amesisitiza kuwa hayuko tayari kubadilishiwa hakimu, akisisitiza kuwa angependa kesi yake iendelee kusikilizwa mbele ya Hakimu Nyaki
Kesi inayomkabili Luqman inahusisha mashtaka matatu, likiwemo la usafirishaji haramu wa binadamu. Alifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Septemba 4, 2026, na kusomewa mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Bilal Ahmed. Siku hiyo, Wakili wa Serikali Godfrey Olugwey alidai kuwa kati ya Julai 1 na Julai 29, 2026, katika eneo la Magomeni Fundikila, mshtakiwa alimsafirisha mwanamume mtu mzima kwenda nje ya nchi kwa ajili ya unyanyasaji wa kingono.
Katika shtaka la pili, alidaiwa kuwa mnamo Agosti 4, 2026, katika eneo la Msimbazi Center, alitumia laini ya simu iliyosajiliwa kwa jina la Nadil Hassan bila kumjulisha mtoa huduma.
Shtaka la tatu linahusu tukio la Machi 2025 ambapo anadaiwa kujipatia kitambulisho cha mpiga kura kwa kutoa maelezo ya uongo kuwa ni raia wa Tanzania huku akijua si kweli.
Baada ya mshtakiwa kukana mashtaka yote mwezi Septemba, kesi iliahirishwa kupisha upelelezi ambao leo umetangazwa kukamilika.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Serikali ya Wilaya ya Mbeya imetoa onyo kali dhidi ya vitendo vya uchafuzi wa mazingira, ikisisitiza kuwa wananchi wanaotema mate ovyo katika maeneo ya umma wanapaswa kuchukuliwa hatua za kisheria, ikiwa ni pamoja na kutozwa faini ya hadi shilingi milioni moja.
Msisitizo huo umetolewa Oktoba 12, 2026, na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Solomon Itunda, katika mkutano uliowakutanisha viongozi wa Serikali pamoja na viongozi wa madereva wa bajaji, bodaboda na daladala mkoani humo.
Katika mkutano huo, Itunda ameeleza kuwa vitendo vya kutema mate ovyo na kutupa taka katika maeneo ya umma vinachangia kwa kiasi kikubwa uchafuzi wa mazingira na kuhatarisha afya ya jamii.
Kwa mujibu wa Mkuu huyo wa Wilaya, faini kwa mtu yeyote atakayebainika kukiuka masharti hayo itaanzia shilingi laki mbili hadi shilingi milioni moja.
Kutokana na hatua hiyo, Mkuu huyo wa Wilaya amewataka wananchi wote pamoja na wadau wa usafirishaji kuzingatia taratibu za usafi na kushirikiana kwa karibu na Serikali ili kuhakikisha Jiji la Mbeya linakuwa safi na la kijani.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Heche, amewasili katika Uwanja wa Ndege wa Arusha akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali wa chama hicho kwa ajili ya kushiriki uzinduzi wa ofisi ya CHADEMA Kanda ya Kaskazini.
Baada ya kuwasili, msafara huo unatarajiwa kuelekea katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Arusha kwa shughuli za chama, ikiwemo uzinduzi wa vizimba vya matawi ya CHADEMA, kabla ya kuelekea kwenye uzinduzi wa ofisi ya kanda.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Waziri wa Katiba na Sheria, Abdallah Hamis Ulega amefanya ziara yake ya kwanza ya kujitambulisha katika Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma, ambapo alikutana na Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, George Masaju, kufuatia uteuzi wake wa hivi karibuni uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Katika mazungumzo hayo ya Oktoba 12, 2026 yaliyohudhuriwa pia na Mtendaji Mkuu wa Mahakama, Dkt. John Jingu, pamoja na viongozi wengine wa Mahakama, Waziri Ulega ameomba ushirikiano thabiti katika utekelezaji wa majukumu ya sekta ya haki nchini. Sambamba na hilo, ameonesha kuvutiwa kwake na kuipongeza Mahakama kwa kuwa na miundombinu bora ya majengo, uwekezaji mkubwa katika matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), pamoja na maandalizi madhubuti yaliyowekwa kuhakikisha wananchi wanaendelea kupata huduma za kimahakama bila kukatizwa hata wakati wa mvua za El Niño.
Kwa upande wake, Jaji Mkuu George Masaju amempongeza Waziri Ulega kwa kuendelea kuaminiwa na Rais Dkt. Samia, akimhakikishia ushirikiano wa dhati kutoka muhimili huo na kubainisha kuwa ushirikiano kati ya Mahakama na Wizara ya Katiba na Sheria ni takwa la kikatiba linalolenga kuboresha utoaji wa haki.
Aidha, Jaji Masaju ameipongeza wizara hiyo kwa kuendelea kutoa huduma mbalimbali kwa wananchi, zikiwemo huduma za msaada wa kisheria na mpango maalum wa "Sema na Waziri" unaowezesha wananchi kupiga simu katika Kituo cha Huduma kwa Wateja cha Wizara na kuwasilisha malalamiko yao.
Naye Mtendaji Mkuu wa Mahakama, Dkt. John Jingu amefafanua kuwa mikakati ya dharura imewekwa wazi kukabiliana na changamoto za hali ya hewa, ikiwemo matumizi ya mifumo ya kidijitali kuhakikisha haki inatolewa kwa wakati na kwa urahisi. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Wananchi mkoani Iringa wametakiwa kuepuka kujichukulia sheria mkononi wanapokumbana na migogoro ya mahusiano, huku wakihimizwa kuripoti vitendo vya jinai polisi badala ya kuvificha kwa sababu ya huruma.
Wito huo umetolewa Oktoba 12, 2026, na Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto Mkoa wa Iringa, ASP Elizabeth Swai, wakati akizungumza katika mkutano wa kampeni ya Ongea na Kamanda uliofanyika Kata ya Kitwiru, Manispaa ya Iringa.
Swai amesema wananchi wanapaswa kutoa taarifa mapema kuhusu matukio ya jinai yanayotokea katika mahusiano ili yaweze kushughulikiwa kwa mujibu wa sheria, badala ya kutumia nguvu au kuchukua hatua nje ya utaratibu wa kisheria.
Akifafanua majukumu ya Dawati la Jinsia na Watoto, amesema dawati hilo si chombo cha kusuluhisha migogoro ya kimahusiano, bali ni sehemu yenye usiri ndani ya Jeshi la Polisi inayopokea na kushughulikia masuala ya jinai yanayohusiana na mahusiano kwa mujibu wa sheria.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Joseph Kabila, ametajwa rasmi kuwa kiongozi wa muungano mpya wa kisiasa na kijeshi unaohusisha waasi wa M23, muungano ambao unafahamika kama Front pour la Refondation de la Nation (FRN), ambao umezinduliwa mjini Goma, mashariki mwa nchi hiyo, kwa lengo la kupinga utawala wa Rais Félix Tshisekedi na kuunganisha nguvu za makundi ya upinzani chini ya mfumo mmoja.
Katika tamko la kuanzishwa kwa muungano huo lililosomwa na Claude Ibalanky, aliyekuwa mshauri wa Rais Tshisekedi kabla ya kujiunga na FRN, ilielezwa kuwa muungano huo unachukua nafasi ya Alliance Fleuve Congo (AFC).
Katika muundo mpya wa uongozi, Bertrand Bisimwa na Corneille Nangaa wameteuliwa kuwa manaibu wa Kabila, huku Jenerali Sultani Makenga akishika nafasi ya mkuu wa jeshi na Dk. Freddy Kaniki akiteuliwa kuwa katibu mkuu.
Viongozi hao wamesisitiza kuwa FRN imejipanga kukabiliana na kile walichokiita utawala wa kimabavu, huku wakirejea Ibara ya 64 ya Katiba ya DRC inayowapa wananchi haki ya kupinga mamlaka yanayokiuka misingi ya kikatiba, na kuweka wazi kuwa wako tayari kutumia njia mbalimbali, ikiwemo nguvu, kufikia malengo yao.
Uzinduzi wa muungano huo unakuja siku chache tu baada ya Joseph Kabila, aliyeiongoza DRC kuanzia mwaka 2001 hadi 2019, kutoa hotuba yake ya hadhara tarehe 9 Oktoba. Katika hotuba hiyo, ameiangushia lawama kali serikali ya Tshisekedi kwa kushindwa kulinda usalama, kusimamia vibaya uchumi, kukiuka misingi ya kikatiba, na kuwakamata kiholela wanasiasa wa upinzani pamoja na wanajeshi. Hadi kufikia sasa, Serikali ya Kinshasa bado haijatoa tamko rasmi kujibu kuanzishwa kwa muungano huo mpya. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
“Katiba iliyopo si kwamba imefikia ubaya kiasi hicho, tatizo ni kwamba haina msingi wa kuilinda,” amesema Mwenyekiti wa Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC), Shabani Itutu, akisisitiza umuhimu wa kuanzishwa kwa Mahakama ya Katiba ili kuhakikisha Katiba inaheshimiwa na kulindwa dhidi ya ukiukwaji.
Itutu alisema hayo Oktoba 7, 2026, katika mahojiano na Jambo TV yaliyofanyika nje ya ukumbi wa Hyatt Regency Dar es Salaam, baada ya uzinduzi wa uongozi mpya na nembo ya Baraza la Vyama vya Siasa.
Itutu alisema kuandaa Katiba mpya bila kuweka mfumo madhubuti wa kuilinda ni sawa na kujenga nyumba juu ya mto, akieleza kuwa hata Katiba mpya inaweza kukiukwa ikiwa hakutakuwa na chombo cha kuwawajibisha wanaovunja masharti yake.
Amesisitiza kuwa maridhiano, mchakato wa Katiba mpya na kuanzishwa kwa Mahakama ya Katiba vinaweza kwenda sambamba, akitaka mahakama hiyo iwe na uwezo wa kuwawajibisha viongozi wote watakaokiuka Katiba bila kujali nyadhifa zao, wakiwemo Rais na Mawaziri. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana ya Chama cha ACT Wazalendo @NgomeyaVijana Taifa, Abdul Nondo amewataka vijana na wananchi wa Zanzibar kuunganisha nguvu kwa pamoja kupigania mabadiliko ya Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itakayorejesha muundo wa serikali tatu na kuipatia Zanzibar mamlaka yake kamili.
Nondo ameyasema hayo mwishoni mwa juma alipokuwa akizungumza na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Ngome ya Vijana wa ACT Wazalendo Mkoa wa Kaskazini A - Unguja, ambapo alieleza kuwa mfumo wa sasa wa muungano unahitaji kufanyiwa marekebisho makubwa kulingana na Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa na Tume ya Jaji Joseph Warioba.
Alibainisha kuwa Ibara ya 60 ya Rasimu ya Warioba ilieleza kwa uwazi uwepo wa mamlaka tatu- Serikali ya Zanzibar, Serikali ya Tanganyika, na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania muundo ambao amedai ulikataliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakati wa Bunge la Katiba.
Nondo ameongeza kuwa kazi ya pili kwa vijana ni kushirikiana kukiondoa Chama Cha Mapinduzi madarakani Bara na Zanzibar, akidai kuwa chama hicho kimeonesha wazi kutokuwa na uchungu na maendeleo ya Zanzibar wala kuunga mkono mamlaka yake kamili
"Kazi ya kwanza tushirikiane kwa pamoja kupigania mabadiliko ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kazi ya pili ni ya kukiondoa Chama Cha Mapinduzi madarakani... Na ili kuondoa Serikali ya Chama Cha Mapinduzi madarakani ni lazima tuwe na mifumo imara ya kiuchaguzi, tunakuwa na tume huru za kiuchaguzi, na mifumo imara ya kiutawala itakayofanya vijana kunufaika”, ameeleza Nondo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Ramadhani Nyagawa Said (32), maarufu kama Mwalimu Bravo Star, mkazi wa Sekei, Idara ya Maji, jijini Arusha, amekuwa kivutio kutokana na utaratibu wake wa kuwabeba watoto mgongoni na kuwapeleka katika kituo chake cha kulelea na kutoa elimu ya awali (daycare).
Akizungumza na Jambo TV, Oktoba 12, 2026, mwalimu huyo mwenye stashahada ya ualimu, amesema huanza kuwafuata watoto majumbani mwao kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa 3 asubuhi, kabla ya kuanza kuwafundisha.
Kwa sasa, anahudumia zaidi ya watoto 20, ambao huwafuata majumbani mwao na kuwapeleka kituoni kwa utaratibu huo, huku jioni akiwafikisha tena kwa wazazi au walezi wao.
Kwa Mwalimu Bravo Star, utaratibu huo si suala la usafiri pekee, bali pia ni sehemu ya kujitoa kwake katika kuwasaidia watoto kupata elimu ya awali.
Amesema upendo wake kwa watoto ndio unaomsukuma kuendelea na jukumu hilo licha ya kutokuwa na gari maalumu la usafiri wa wanafunzi.
Baadhi ya wazazi wamepongeza huduma hiyo, wakieleza kuwa imewarahisishia majukumu yao ya kila siku na kuwasaidia katika malezi ya watoto wao.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mjadala mkali umeibuka leo Oktoba 12, 2026 kati ya Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, John Heche, na Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania, Gerson Msigwa, kuhusu hali ya miundombinu ya barabara, kasi ya ujenzi, na uendeshaji wa uchumi wa nchi.
Mjadala huo umeanza baada ya Heche kuchapisha kipande cha video kwenye ukurasa wake wa Instagram kikionesha hali ya barabara inayounganisha Mbalizi, Iwiji, na Umalila mkoani Mbeya. Katika chapisho hilo, Heche alimuambatanisha (kum-tag) Msemaji Mkuu wa Serikali na kuhoji namna serikali inavyoweza kujenga uchumi shindani kupitia miundombinu inayokabiliwa na changamoto.
Akijibu mapigo kwenye sehemu ya maoni chini ya chapisho hilo, Msigwa ameeleza kuwa serikali inatambua changamoto hizo na inafanya kazi kwa awamu kulingana na uwezo wa kiuchumi na ukusanyaji wa kodi.
"Ni sahihi kwamba nchi yetu haijafikia uwezo wa kujenga barabara zote kwa kiwango cha lami kwa wakati mmoja. Kazi ya ujenzi wa barabara inaendelea na hivi sasa kuna kilometa 2,550 za lami wakandarasi wapo site ujenzi unaendelea. Tunakwenda kwa awamu, hata hii itafikiwa. Nchi wakati inapata uhuru mwaka 1961 ilikuwa na kilometa 1,300 za lami leo kuna zaidi ya kilometa 12,000 za lami na kilometa zaidi ya 25,000 za changarawe ambazo zinapitika vizuri na zipo katika hatua mbalimbali za kuwekewa lami.", ameeleza Msigwa.
Hata hivyo, takriban saa tatu baadaye, Heche alichapisha video nyingine ikionesha hali ya barabara kuu ikiwemo barabara ya kutoka Singida kwenda Babati na Arusha na kujibu hoja hizo za Msigwa. Heche amepinga takwimu za kilometa 12,000 za lami zilizotajwa na Msigwa, akidai kuwa barabara nyingi kuu zinakabiliwa na changamoto ya viraka na mashimo.
Aidha, Heche ameeleza kuwa ukuaji wa idadi ya watu na magari unahitaji miundombinu yenye viwango vya juu zaidi kama barabara za njia mbili-mbili (highways/bypasses). Pia amegusia historia ya ujenzi wa reli tangu enzi za wakoloni na kuhoji ongezeko la deni la taifa linalofikia zaidi ya trilioni 110, akisisitiza kuwa rasilimali nyingi kama madini, misitu, na ardhi zinapaswa kuleta maendeleo ya haraka kwa wananchi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mhandisi Hamad Masauni amesema yupo tayari kujiuzulu nafasi yake ya Uwaziri na Ubunge endapo Makanu Mwenyekiti wa @ChademaTZ2 John Wegesa Heche @HecheJohn atathibitisha taarifa alizowahi kusema kuwa serikali imeuza misitu kwa Saudi Arabia na Oman kupitia biashara ya Carbon Credit.
Masauni amesema hayo Oktoba 11, 2026 jijini Dar es Salaam akizungumza wakati wa kutembelea na kukagua shughuli za usafi na hatua zinazochukuliwa kutunza mazingira katika Mto Ng'ombe, uliopo Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam na kueleza kuwa hayo yaliyokuwa yakisemwa na Heche sio ya kweli na kuwa serikali haijafanya biashara hiyo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Hitilafu ya mfumo wa mtandao imesababisha kuahirishwa kwa mnada wa kwanza wa zao la korosho wa Chama Kikuu cha Ushirika cha (MAMCU) hadi Oktoba13, 2026, baada ya tani 8,620 za korosho kuingizwa sokoni, huku tani elfu 5 na 96 elfu zikiwa zimeuzwa kabla ya mnada huo kusitishwa.
Hayo yamesemwa Oktoba 12, 2026 na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT), Francis Alfred, ambapo amesema korosho zimeuzwa kwa bei ya juu ya shilingi 3,310 kwa kilo na bei ya chini ya shilingi 3,210 kwa kilo.
Kiongozi huyo amewataka wakulima kuendelea kuzingatia ubora wa korosho zao ili kuhakikisha zinapata bei shindani sokoni.
Awali, akifungua mnada huo, Mkuu wa Wilaya ya Masasi, Mwita Marwa, amewahimiza wanunuzi kuhakikisha wanafanya malipo kwa wakati.
Baadhi ya wakulima, akiwemo Bakari Rajabu, wameeleza kuridhishwa na bei zilizopatikana katika mnada huo, huku wakiomba bei hizo ziendelee kuwa nzuri ili kuwawezesha kunufaika na zao hilo.
Mnada huo unatarajiwa kuendelea kesho katika Ukumbi wa Masasi Mji, wilayani Masasi, mkoani Mtwara.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
HECHE NA MSIGWA WAVUTANA KWA HOJA UBOVU WA MIUNDOMBINU YA BARABARA NCHINI jambo.co.tz/heche-na-msigwa-wavutana-kwa-hoja-ubovu-wa-mi… via @jambotv_
-
Jambo TV
@Jambotv_
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imethibitisha kuwa bado inaendelea kufanya mapitio ya kina kuhusu mapendekezo mapya yaliyowasilishwa na Marekani kwa lengo la kurejea kwenye meza ya mazungumzo ya kidiplomasia, huku mawasiliano hayo yakiendelea kufanyika kwa njia ya siri kupitia nchi wapatanishi za Qatar na Pakistan.
Akizungumza mbele ya waandishi wa habari leo, Oktoba 12, 2026, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Esmaeil Baghaei, ameeleza kuwa nchi hizo mbili zinaendelea kubadilishana ujumbe usio wa moja kwa moja wakati huu kukiwa na mivutano ya kikanda inayohusu usalama wa njia kuu za nishati. Hata hivyo, Iran imeweka msimamo mkali ikitaka masharti yake ya awali yapewe kipaumbele, huku ikisistiza kuwa Marekani inapaswa kuonyesha nia thabiti kwa vitendo badala ya kutoa kauli zinazokwamisha mchakato wa kidiplomasia.
Mkwamo mkubwa katika mazungumzo hayo unatokana na utofauti wa vipaumbele; wakati Washington ikishinikiza suala la mpango wa nyuklia wa Iran liwekwe mbele tangu mwanzo, Tehran inataka mazungumzo yaanzie kwenye utatuzi wa mgogoro wa usalama wa Mlango-bahari wa Hormuz na kuondolewa kwa vikwazo vya kiuchumi.
Sambamba na hilo, Iran imewasilisha mpango wake wa "siku saba" unaolenga kufungua upya njia hiyo ya kimkakati ya biashara ya mafuta na gesi duniani, ikitaka Marekani iondoe vikwazo vya mafuta, iachie mali zilizozuiliwa nje ya nchi, na kusitisha mzingiro wa majini kabla ya kugusa masuala ya nyuklia.
Kwa upande wake, Katibu wa Baraza Kuu la Usalama la Taifa la Iran, Mohsen Rezaei, alibainisha kuwa ingawa majibu ya hivi karibuni kutoka Marekani yamegusia baadhi ya masharti yao, bado hayajajitosheleza kukidhi matakwa ya nchi hiyo. Wakati huo huo, Urusi inaendelea kupongezwa kwa mchango wake chanya kutokana na ushiriki wake wa kihistoria kwenye mkataba wa mwaka 2015, ingawa jukumu la uwasilishaji wa jumbe za sasa limebaki mikononi mwa Qatar na Pakistan.
Hali hii inajiri wakati Rais wa Marekani, Donald Trump, akiendelea kutoa kauli zinazoashiria kuwa mzozo huo unaweza kumalizika ama kwa njia ya shinikizo la kijeshi au makubaliano yanayozingatia masharti ya Marekani, huku akisisitiza kutoruhusu Iran kumiliki silaha za nyuklia. Wachambuzi wa mambo ya kikanda wanaeleza kuwa diplomasia hii isiyo ya moja kwa moja inasalia kuwa ngumu na yenye kusuasua, huku macho ya dunia yakiwa yamewekwa Tehran kusubiri uamuzi rasmi wa nchi hiyo dhidi ya ofa ya mwisho ya Marekani. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imewataka wanufaika wa mikopo hiyo hasa waliojiajiri, kurejesha madeni yao kwa wakati ili kuwawezesha wanafunzi wengine kupata mikopo
Akizungumza leo Jumatatu, Oktoba 12, 2026, jijini Dar es Salaam, katika mkutano na wahariri ulioandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina (OTR), Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Dkt. Bill Kiwia, amesema bodi inaendelea kuimarisha mikakati ya ukusanyaji wa marejesho ili fedha hizo ziendelee kunufaisha wanafunzi wengine, ikiwemo kupitia Kampeni ya kurejesha kidogo kidogo (Kiduchu)
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Urejeshaji na Urejeshwaji Mikopo wa HESLB, CPA George Mziray, amesema mikopo yenye thamani ya Sh bilioni 2.7 imefikia muda wa kurejeshwa, ambapo Sh bilioni 1.9 tayari zimekusanywa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Baadhi ya mawakili ambao ni wanachama wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) wamefungua shauri la kikatiba katika Mahakama Kuu kupinga mchakato wa kinidhamu unaoweza kusababisha Rais wa chama hicho, Boniface Mwabukusi kuvuliwa uwakili.
Mawakili hao wameeleza hayo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Jumapili, Oktoba 11, 2026, wakisema hatua ya kumfikisha Mwabukusi mbele ya Kamati ya Maadili ya Mawakili inazua maswali kuhusu uhuru wa TLS na utekelezaji wa maamuzi ya wanachama wake.
Wakili Paul Kisabo na Wakili Jebra Kambole kwa niaba ya mawakili hao wameeleza kuwa amesema msingi wa tuhuma zinazomkabili Mwabukusi unatokana na kauli alizotoa katika Mkutano Mkuu wa TLS wa mwaka 2026 kuhusu mwenendo wa kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu.
Wamesema kauli hizo ziliungwa mkono na wanachama wa TLS, ambao waliagiza uongozi wa chama hicho kutoa tamko rasmi kwa waandishi wa habari ndani ya saa 48 kuhusu mashtaka yanayomkabili Lissu, na Mwabukusi alikuwa akitekeleza wajibu wake kama Rais wa TLS kwa kufuata maelekezo yaliyotolewa na wanachama wa chama hicho.
Mawakili hao wanadai kuwa kumfikisha Mwabukusi mbele ya Kamati ya Maadili ya Mawakili si suala linalomhusu yeye binafsi pekee, bali pia linagusa uhuru wa TLS kama taasisi inayopaswa kusimamia na kushauri serikali pamoja na jamii kuhusu masuala ya kisheria.
Wamesisitiza kuwa hawatakubali kuona uhuru wa chama hicho ukiingiliwa, wakieleza kuwa hatua yao ya kisheria inalenga kulinda uhuru wa TLS na nafasi yake katika kusimamia masuala ya sheria nchini.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Semaji @ahmed__ally anasema ushahidi dhidi ya Yanga Sc moja ya faida zake ni kurejesha heshima ya viongozi wao ambapo walikuwa wakidharaulika na sasa heshima ya Mwenyekiti wa Klabu ya Simba Sc Murtaza Mangungu imeongezeka mara dufu.
Full video ipo kwenye YouTube yetu ya Jambo TVThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI:
Urusi imeshambulia miundombinu ya nishati nchini Ukraine usiku wa Jumapili, Oktoba 11, 2026, saa chache baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kutangaza kuwa Urusi na Ukraine zimekubali kusitisha mashambulizi dhidi ya miundombinu hiyo.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema kituo cha umeme cha CHPP-5 mjini Kharkiv kilishambuliwa. Pia aliripoti kuwa droni ilishambulia kituo cha umeme Kyiv, na kusababisha kukatika kwa umeme katika maeneo kadhaa ya mji huo.
Zelensky amesema Kyiv iko tayari kuunga mkono usitishaji huo iwapo Moscow itafanya hivyo pia. Hata hivyo, Urusi bado haijatoa tamko kuhusu tangazo la Trump, na ripoti za mashambulizi baada ya tangazo hilo zimeibua mashaka kuhusu utekelezaji wake.
Tangazo hilo limekuja wakati Trump akiishinikiza Ukraine kusitisha mashambulizi dhidi ya miundombinu ya mafuta ya Urusi.
Siku chache zilizopita, Trump alisema Urusi itasambaza zaidi ya tani laki 3 za dizeli mara moja, tani laki 5 mwezi Novemba na tani milioni moja nyingine baadaye, kwa ajili ya Marekani na soko la kimataifa. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI:
Serikali ya Kenya imewaweka karantini watu 108 waliokuwa na mawasiliano na mgonjwa wa kwanza kuthibitishwa kuwa na virusi vya Ebola nchini humo, huku ufuatiliaji wa watu wengine ukiendelea. Hakuna kati ya watu hao aliyeonesha dalili za ugonjwa huo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa na Citizen Digital, Oktoba 11, 2026, Wizara ya Afya ya Kenya imesema jumla ya watu 122 waliokuwa na mawasiliano na mgonjwa huyo wametambuliwa na kuthibitishwa.
Aidha, sampuli 293 zilizokusanywa kutokana na taarifa 289 za watu wanaoshukiwa kuwa na maambukizi zimefanyiwa uchunguzi. Wakati huo huo, wasafiri 667,675 wamefanyiwa uchunguzi wa afya katika vituo 26 vya kuingilia nchini humo, wakiwemo 2,345 ndani ya saa 24.
Wizara hiyo imesema Kenya ina maabara tano za uchunguzi wa Ebola na vitanda 241 vya kutenga wagonjwa katika hospitali tano zilizopo Nairobi, Eldoret na Mombasa. Pia, wahudumu wa afya 4,917 wamepatiwa mafunzo ya kukabiliana na ugonjwa huo, huku kikosi cha wataalamu 343 kikiwa tayari kutoa msaada.
Hata hivyo, serikali imesisitiza kuwa hakuna zuio la usafiri, biashara au mikusanyiko ya watu lililowekwa, huku ukaguzi wa afya ukiimarishwa katika viwanja vya ndege, bandari na vituo vya mipakani.
Katika hatua nyingine, Kenya imeimarisha ufuatiliaji wa safari za ndege kutoka nchi 10, zikiwemo Tanzania, Uganda, Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC). Ndege kutoka nchi hizo zinatakiwa kutumia kituo maalumu cha kuingilia katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA), jijini Nairobi.
Kenya iliripoti kisa chake cha kwanza cha Ebola kilichosababisha kifo Oktoba 6, 2026, baada ya mgonjwa aliyetoka DRC kufariki katika Hospitali ya Nairobi alipokuwa akipatiwa matibabu. -
Jambo TV
@Jambotv_
Aliyekuwa Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa, Said Goha, amefariki dunia kufuatia ajali ya gari iliyotokea Jumamosi, Oktoba 10, 2026, katika eneo la Mbezi Luis, jijini Dar es Salaam.
Taarifa ya kifo chake imetolewa na Katibu wa Siasa, Uenezi na Mafunzo wa CCM Mkoa wa Pwani, Dk. David Mramba, huku ikieleza kuwa mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Tumbi iliyopo Kibaha, mkoani Pwani.
Hadi mauti yanamkuta, Goha alikuwa amesimamishwa katika nafasi yake ya Ukatibu wa CCM Mkoa wa Iringa kufuatia tuhuma za ukiukwaji wa maadili zilizotangazwa mwezi Septemba na Katibu wa NEC, Idara ya Oganaizesheni, Paul Matiko Chacha, wakati wa Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM mkoani humo, ambapo hata hivyo ilielezwa kuwa angepangiwa majukumu mengine badala ya kuondolewa moja kwa moja kwenye safu ya chama.
Hata hivyo, taarifa iliyotolewa na uongozi wa chama haikufafanua kwa kina mazingira yaliyosababisha ajali hiyo wala kubainisha iwapo kulikuwa na watu wengine waliojeruhiwa, ikisisitiza kuwa taarifa rasmi zaidi kuhusiana na taratibu za msiba huo zitatolewa hapo baadaye. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma limethibitisha kutokea kwa ajali ya kusikitisha ya kuungua moto kwa meli ya mizigo ya MV Chambo, iliyosajiliwa nchini Msumbiji, iliyotokea alfajiri ya leo, Oktoba 11, 2026, katika Ziwa Nyasa na kusababisha vifo vya watu watatu huku wengine 41 wakiokolewa salama.
Akitoa taarifa rasmi kwa vyombo vya habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, SACP Marco Chilya, ameeleza kuwa tukio hilo lilitokea meli hiyo ilipokuwa ikisafiri ikitokea katika Bandari ya Mbamba Bay, wilayani Nyasa, mkoani Ruvuma, kuelekea katika Bandari ya Mitengula nchini Msumbiji, ikiwa na jumla ya abiria 44 waliokuwa ndani yake.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Nyasa, Peres Magiri, ametoa shukrani za dhati kwa wananchi wa wilaya hiyo kwa moyo wao wa ujasiri katika kushiriki kikamilifu kwenye zoezi la haraka la uokoaji. Sambamba na hilo, alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa uamuzi wake wa kuleta boti ya uokoaji katika Ziwa Nyasa, ambayo ilitoa msaada mkubwa na wa kipekee katika kuokoa maisha ya abiria wengi waliokumbwa na janga hilo.
Kufuatia tukio hilo, Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Ruvuma, (SSF) Melania Nyabwinyo, ametoa rai kwa wananchi na wadau wote wanaotumia Ziwa Nyasa kwa shughuli za usafiri na kiuchumi kuzingatia kikamilifu maelekezo ya wataalamu wa usalama, hasa umuhimu wa kuvaa maboya ya kujiokolea safarini ili kuepuka maafa zaidi wakati wa dharura.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi @CCMTanzania Taifa imemteua Faris Buruhani kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), akichukua nafasi iliyoachwa na Khalid Mwinyi ambaye ameteuliwa kuwa Kaimu Katibu wa CCM Mkoa wa Kigoma.
Taarifa iliyotolewa na Katibu wa NEC ya CCM Itikadi, Uenezi na Mafunzo Kenani Kihongosi imesema yUteuzi wa Faris umefanyika katika kikao maalum cha Kamati Kuu ya chama hicho kilichofanyika Oktoba 11, 2026, Kizimkazi, Zanzibar.
Kabla ya uteuzi huo, Buruhani alikuwa Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Kagera. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mfuko wa Udhamini wa Pembejeo za Kilimo (AGITF) umesaini makubaliano na Benki ya Azania kwa lengo la kuwawezesha wakulima wadogo, vijana na wanawake wasiokuwa na dhamana za kutosha kupata mikopo ya kununua zana za kilimo, pembejeo na kuwekeza katika miundombinu ya umwagiliaji.
Kupitia mpango huo, zaidi ya shilingi bilioni 10 zimetengwa kwa ajili ya kuwawezesha vijana na wanawake kujikwamua kiuchumi kupitia kilimo, huku mkakati huo ukilenga kuhamasisha mabadiliko kutoka kilimo cha mazoea kwenda kilimo cha kisasa chenye tija.
Akizungumza baada ya kusaini makubaliano hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa AGITF, Bi. Mwanahiba Mzee amesema ushirikiano huo ni sehemu ya juhudi za mfuko huo kupanua wigo wa upatikanaji wa mikopo kwa wakulima na kuwawezesha kuwekeza katika shughuli za kilimo.
Kwa upande wake, Meneja Mwandamizi wa Biashara za Kilimo na Biashara Ndogondogo wa Benki ya Azania, Bw. Augustino Matutu, amesema ushirikiano huo utawasaidia wakulima kukabiliana na changamoto za masoko na kuwawezesha kunufaika zaidi na shughuli zao za kilimo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Watu watatu wamefariki dunia baada ya meli ya MV Chambo kuteketea kwa moto alfajiri ya Jumapili ya leo, tarehe 11 Oktoba 2026, katika Ziwa Nyasa wilayani Nyasa mkoani Ruvuma.
Akitoa taarifa za awali kuhusu ajali hiyo kwa njia ya simu, Mkuu wa Wilaya ya Nyasa, Peres Magiri, amesema meli ya MV Chambo ilikuwa ikifanya safari zake kutoka Bandari ya Mbamba Bay, Tanzania, kuelekea Msumbiji. Meli hiyo ilikuwa imebeba abiria 44, na watu watatu wamefariki dunia akiwamo mtoto wa miezi mitatu.
Chanzo cha ajali hiyo bado hakijafahamika, huku uchunguzi ukiendelea.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mjadala mkali wa kisheria na kikatiba umeibuka kuhusu uhuru wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kutokana na aliyekuwa Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Balozi Omar Ramadhani Mapuri kuwa Kamishna wa Tume hiyo pamoja na hatua ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi, Dkt. Wilson Mahera Charles kugombea ubunge wa Jimbo la Butiama na kushida ubunge huo kupitia CCM.
Mjadala huo umejitokeza kwenye kipindi cha Medani Kuu kilichorushwa na kituo cha Star TV chini ya mtangazaji Edwin Odemba (Chief Odemba) @chiefodemba Jumamosi, tarehe 10 Oktoba 2026, ukimkutanisha Wakili Leonald Manyama, Wakili Maduhu William, Wakili Dickson Matata na Wakili Sweetbert Nkuba.
Katika mjadala huo, Wakili Maduhu William amehoji vigezo vya kisheria na usawa akionesha wasiwasi juu ya Mapuri kuteuliwa kuwa Kamishna wa INEC wakati amewahi kuwa Katibu Mwenezi wa CCM Taifa. Pia ameeleza mashaka juu ya mazingira ya Dkt. Wilson Mahera kujiunga na CCM na kugombea ubunge mara baada ya kustaafu nafasi ya Mkurugenzi wa Uchaguzi.
Akijibu hoja hizo, Wakili Leonald Manyama amebainisha kuwa Dkt. Mahera hakuwa mwanachama wa CCM wakati akitekeleza majukumu yake kama Mkurugenzi wa Uchaguzi, na kwamba katiba na sheria za nchi hazimzuii raia kujiunga na chama cha siasa au kugombea uongozi mara baada ya kustaafu.
Kuhusu Balozi Mapuri kuwa Mjumbe wa INEC, Wakili Manyama ameeleza kuwa wajumbe wote wanaoteuliwa na Rais hula kiapo cha kuwajibika kwa mujibu wa sheria na kulinda katiba, hatua inayowatua na kuweka kando ukada au nafasi zozote za kisiasa
Wakili Manyama alizidi kueleza kuwa kipimo kikuu cha mjumbe wa Tume ni utendaji wake kwa mujibu wa sheria na sio historia yake ya nyuma au vazi analovaa, huku akiwataka wakosaji kutoa ushahidi iwapo Balozi Mapuri ametenda jambo lolote kinyume cha sheria tangu ateuliwe.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Wakili Leonald Manyama na Wakili Maduhu William wameingia katika mchanganuo mkali wa kisheria na kisiasa kuhusu kauli ya Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Idara ya Oganaizesheni, Paul Chacha, aliyedai kuwa vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na viongozi wa serikali ni mali ya CCM.
Mjadala huo umejitokeza katika kipindi cha Medani Kuu kinachorushwa na kituo cha Star TV chini ya mtangazaji Edwin Odemba (Chief Odemba) Jumamosi, tarehe 10 Oktoba 2026, ambapo mawakili hao wawili wamekabiliana kuhusu iwapo kauli hiyo ni msimamo rasmi wa CCM au maoni binafsi ya kiongozi huyo.
Akizungumza kwenye mjadala huo, Wakili Manyama ameeleza kuwa kwa mujibu wa katiba na utaratibu wa CCM, msemaji rasmi wa chama ambaye tamko lake linaweza kuchukuliwa kama msimamo rasmi ni Mwenyekiti wa Taifa wa CCM au Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo kwa maelekezo ya Mwenyekiti. Amefafanua kuwa si kila kauli inayotolewa na kiongozi wa CCM kwenye mikutano ya ndani inawakilisha msimamo rasmi wa chama.
Wakili William amepinga vikali utetezi huo wa Manyama, akieleza kuwa ikiwa kweli kauli ya Chacha ilikuwa ni maoni yake binafsi na si msimamo wa chama, CCM kama taasisi ilipaswa kujitokeza hadharani kupitia Mwenyekiti au Msemaji wake kukanusha kauli hiyo na kuwataka wananchi waipuuze.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Kauli ya Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Idara ya Oganaizesheni, Paul Chacha, kusema vyombo vya ulinzi na usalama na viongozi wa serikali ni mali ya CCM, akidai kuwa chama hicho ndicho kilichowaweka katika nafasi hizo, imeendelea kuibua mjadala nchini Tanzania.
Wakati wa mjadala wa Utawala wa Sheria uliorushwa kupitia kipindi cha Medani Kuu cha Star TV chini ya mtangazaji Edwin Odemba (Chief Odemba) Jumamosi Oktoba 10, 2026, Wakili Leonald Manyama na Wakili Dickson Matata wamechambua kauli hiyo ambapo Manyama ameeleza kuwa vyombo vya ulinzi na usalama msingi wake ni mali ya wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lakini akasisitiza kuwa video ya kiongozi huyo wa CCM imesambazwa ikiwa imekatwa bila kuangalia muktadha halisi wa mazungumzo.
"Vyombo vya ulinzi na usalama havipokei maagizo kutoka Chama cha Mapinduzi. Vinapokea maagizo kutoka kwa Amiri Jeshi Mkuu ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye amepewa mamlaka hayo na wananchi kwa kura zao... Anapotoa maagizo kwa vyombo vya ulinzi na usalama hawi kama Mwenyekiti wa CCM, anatoa kama Amiri Jeshi Mkuu." Ameeleza Manyama.
Wakili Manyama ameongeza kuwa mawaziri wanaowasilisha bajeti za wizara za ulinzi na usalama bungeni wanatokana na CCM na wameteuliwa na Rais anayetokana na chama hicho, hivyo kutoa wajibu kwa CCM kuhakikisha vyombo hivyo ili kulinda taifa.
Kwa upande wake, Wakili Matata amepinga vikali utetezi huo, akisema kuwa maelezo ya Manyama yanaakisi kilekile alichokisema Chacha kwamba CCM inavichukulia vyombo vya ulinzi na usalama ama mali yake ya chama. Matata amebainisha kuwa mtazamo huo unapingana wazi na Katiba inayotaka vyombo hivyo kubaki huru bila kuunganishwa na chama chochote cha siasa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Wakili Sweetbert Nkuba ameeleza kuwa kudai Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 si ya haki ni upotoshaji, kwani Katiba hiyo ndiyo msingi mkuu wa sheria zote nchini na imeweka misingi thabiti ya utawala wa sheria na haki za msingi za raia.
Wakili Nkuba ameyasema hayo leo Jumamosi, tarehe 10 Oktoba 2026, wakati akichangia katika mjadala wa Utawala wa Sheria kwenye kipindi cha Medani Kuu kinachorushwa na kituo cha Star TV chini ya mtangazaji Edwin Odemba (Chief Odemba).
Akijibu hoja za wanaodai kuwa Katiba ya sasa haina haki na ni katiba ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wakili Nkuba amebainisha kuwa Ibara ya 13 ya Katiba ndiyo inayotoa msingi wa utawala wa sheria kwa kuhakikisha usawa mbele ya sheria, uhuru wa mtu, na haki ya kutohukumiwa kabla ya mahakama yenye mamlaka kujiridhisha.
Wakili Nkuba amekiri kuwa Katiba hiyo ilitungwa wakati nchi ikiwa chini ya mfumo wa chama kimoja ili kuendana na mazingira ya wakati huo, lakini alisisitiza kuwa hilo halifanyi Katiba hiyo kuitwa ya CCM au kukosa haki. Hata hivyo, amekiri kuwa kuna hoja ya msingi ya kuwa na Katiba mpya kutokana na Katiba ya sasa kudumu kwa muda mrefu.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mjadala mkali wa kisheria umeibuka kati ya mawakili kuhusu uhalali na uwezo wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 katika kulinda haki za binadamu na utawala wa sheria nchini.
Mjadala huo unaendeshwa katika kipindi cha Medani Kuu kinachorushwa na kituo cha Star TV chini ya mtangazaji Edwin Odemba (Chief Odemba), ukiwakutanisha Wakili Dickson Matata na Wakili Leonald Manyama, Wakili Sweetbert Nkuba na Wakili William Maduhu wakijadili kama Katiba iliyopo sasa ni ya haki au la.
Akizungumza kwenye mjadala huo, Wakili Dickson Matata ameeleza kuwa Katiba ya sasa ya mwaka 1977 haina haki kwa kuwa mchakato wa upatikanaji wake haukushirikisha wananchi wote. Amebainisha kuwa katiba bora duniani zinapatikana kwa maridhiano ya wananchi, tofauti na Katiba ya Tanzania aliyodai kuwa ilitengenezwa na kundi dogo la watu kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Kwa upande husika, Wakili Leonald Manyama amepinga mtazamo huo na kusisitiza kuwa Katiba ya Tanzania ni ya haki na inalinda kikamilifu misingi ya utawala bora, utawala wa sheria, pamoja na haki za binadamu. Ametolea mfano Ibara ya 12 hadi 24 za Katiba zinazoeleza na kulinda haki za msingi za binadamu na usawa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Kiongozi wa Chama mstaafu wa ACT Wazalendo, Zitto Zuberi Kabwe @zittokabwe , ameongoza harambee maalum ya kuchangisha Shilingi bilioni moja kwa lengo la kuboresha miundombinu mbalimbali katika Shule ya Sekondari Tosamaganga, ikiwemo ujenzi wa mabweni na utatuzi wa changamoto zingine zinazowakabili wanafunzi.
Katika mchakato huo, huku kukiwa na mafanikio ya awali ya kukusanya Shilingi milioni 500 kutoka kwa wadau na wanafunzi wa zamani waliopitia shuleni hapo, leo wameanzisha awamu mpya ya kukusanya kiasi kilichobaki cha milioni 500, ambapo zaidi ya Shilingi milioni 180 zimeshaahidiwa siku ya leo pekee.
Wakati wa harambee hiyo, wahitimu na wanafunzi wa zamani wa shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 1926 na wamisionari wa Consolata walihimizwa kuendelea kujitoa kwa dhati kuchangia maendeleo ya shule hiyo ili kuacha alama ya kudumu na kulinda historia adhimu ya taasisi hiyo iliyotoa viongozi wengi wakubwa nchini.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, CP Salum Hamduni, amewataka wanachama wa kikosi cha ulinzi shirikishi cha Sungusungu kuacha mara moja tabia ya kujichukulia sheria mkononi na kuanza kujigeuza kuwa mahakama kwa kutoa adhabu na faini kiholela pindi wanapowatia nguvuni watuhumiwa au wavunjifu wa sheria.
CP Hamduni ametoa maagizo hayo leo wakati akizungumza katika Sherehe za Sungusungu (Sanjo) za Kanda ya Ziwa na Magharibi zilizofanyika katika Kijiji cha Shirima, Kata ya Kikubiji, wilayani Kwimba, mkoani Mwanza. Amesisitiza kuwa kikosi hicho hakiruhusiwi kutoa hukumu, akishauri kutumika kwa viwango na taratibu za Polisi Kata na sheria za nchi kupitia mafunzo ya Jeshi la Polisi Wasaidizi na sheria za mwenendo wa makosa ya jinai.
Katika hafla hiyo, Mtemi wa Sungusungu Kanda ya Ziwa na Magharibi na Wilaya ya Kwimba, Shimbi Morgan, amewataka sungusungu hao kusimama kidete kudhibiti vitendo vya baadhi ya wazazi na walezi kuozesha watoto waliohitimu darasa la saba, akihakikisha wanaripoti shuleni ifikapo Januari 2027.
Kwa upande wake, Katibu wa Sungusungu Wilaya ya Kwimba, Paul Kahema, alipokuwa akisoma risala mbele ya Mkuu wa Mkoa, aliomba serikali kuwasaidia kupata ofisi maalum ya kanda pamoja na eneo la uwanja maalum kwa ajili ya kufanyia shughuli na sherehe mbalimbali za kikosi hicho.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Kiongozi wa Chama Mstaafu wa ACT Wazalendo, Zitto Zuberi Kabwe @zittokabwe , ameeleza kuwa Shule ya Sekondari Tosamaganga imekuwa na mchango mkubwa na wa pekee katika kujenga msingi imara wa safari yake ndefu ya uongozi na kisiasa.
Akizungumza katika maadhimisho ya kutimiza karne moja (miaka 100) tangu kuanzishwa kwa shule hiyo kongwe mwaka 1926, Zitto amekumbuka maisha yake ya uanafunzi na kufichua kumbukumbu ya kuwahi kuwa kiranja mkuu wa siku moja, jambo ambalo linaakisi mbegu za uongozi zilizopandwa ndani yake tangu enzi hizo.
Maadhimisho hayo ya miaka 100 ya Shule ya Sekondari Tosamaganga yametumika kama fursa ya kutambua na kuthamini mchango mkubwa uliotolewa na taasisi hiyo ya elimu katika kuandaa viongozi mbalimbali nchini, huku Zitto akisisitiza nafasi ya pekee iliyo nayo katika historia ya maisha yake binafsi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Miili ya askari watatu wa Jeshi la Polisi waliopoteza maisha katika ajali ya barabarani iliyotokea usiku wa kuamkia Oktoba 9, 2026 eneo la Mitibora kwenye barabara kuu ya Morogoro–Dodoma imeagwa leo Oktoba 10, 2026 mkoani Morogoro, huku viongozi wa Jeshi la Polisi wakitoa wito wa kuimarishwa kwa uzingatiaji na usimamizi wa sheria za usalama barabarani ili kupunguza ajali na kuokoa maisha ya wananchi.
Akitoa heshima za mwisho kwa marehemu, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Camillus Wambura, amewataka madereva kuzingatia sheria na kanuni za usalama barabarani, akisisitiza umuhimu wa kuwa makini wanapokuwa barabarani ili kuepusha ajali zinazoweza kusababisha vifo na majeraha.
Kwa upande wake Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi Kamishna Awadh Juma Haji, amewataka askari wa usalama barabarani kuongeza umakini katika kusimamia na kutekeleza sheria za barabarani, ili kuhakikisha madereva wanazifuata na hivyo kuimarisha usalama kwa watumiaji wote wa barabara.
Naye mwakilishi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Sebastian Masanja, amezifariji familia, ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu, akitoa pole kwa msiba huo mzito uliolipata Jeshi la Polisi na taifa kwa ujumla.
Askari hao watatu walipoteza maisha katika ajali hiyo wakati wakitekeleza majukumu yao ya kikazi ya kulitumikia taifa. Miili yao imeagwa katika viwanja vya Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) mkoani Morogoro, katika hafla iliyohudhuriwa na viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama, Serikali pamoja na waombolezaji kutoka maeneo mbalimbali.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI PICHA:
Miili ya Askari Polisi watatu waliofariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea Oktoba 8, 2026, eneo la Magole, Wilaya ya Kilosa, Mkoa wa Morogoro, imeagwa leo Oktoba 10, 2026 katika Viwanja vya Makao Makuu ya Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) ambapo wananchi mbalimbali wametoa heshima zao za mwisho kwao. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mtaalam wa Saikolojia @DeoSukambi anatueleza kuwa tatizo la afya ya akili lina dalili nyingi ikiwemo kuwa na hasira sana, wivu kupita kiasi, kukosa usingizi, kujichukia zinaweza kuwa dalili.
Leo Oktoba 10, 2026 ni siku ya afya ya akili duniani hivyo tumezungunza na Deo Sukambi akitueleza mambo mengi kuhusu Afya ya akili na Tatizo la Afya ya akili. Fuatilia kwenye youtube yetu ya Jambo TV.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Anaeleza mwanasaikolojia Deogratius Sukambi kuwa kutokana mwanamke kiumbe anayetumia hisia zaidi ni jinsia ambayo inasumbuliwa sana na matatizo ya afya ya akili japokuwa wanaume ndio wanaofanya matukio mabaya pindi wakipata tatizo la afya ya akili kutokana na kuwa na uwezo mdogo wa kudhibiti hisia na tabia hatarishi. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI PICHA:
Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amefanya kikao na Menejimenti Maalum ya Wizara ya Maji tarehe 09 Oktoba 2026 ofisi za Wizara ya Maji, Mtumba, Dodoma akiwa na lengo la kufanya tathmini ya ziara aliyofanya maeneo mbalimbali nchini.
Ujumbe muhimu uliobeba maudhui ya kikao ni kaulimbiu yenye msisitizo aliyotoa kwa wajumbe wa Menejimenti ya kwamba Sekta ya Maji Tuwaze Tofauti, Tutende Tofauti, Tupime Matokeo.
Aidha, akizungumza kwa msisitizo, ameeleza kubadili namba ya utendaji na amepokea taarifa ya utekelezaji wa maelekezo yake aliotoa katika maeneo hayo na kusisitiza kuwa kila jambo alilobaini na kutolea maagizo litekelezwe mara moja.
Halikadhalika, Waziri Aweso ameyabainisha maeneo sugu yenye changamoto ya maji kama majiji ya Dar es Salaam, Mwanza na Dodoma na kumuelekeza Katibu Mkuu kutengeneza mpango maalum wa suluhisho katika maeneo haya ikiwezekana kuwepo kwa mikakati ya dharura itakayotoa matokeo ya haraka wakati miradi ya utatuzi ya muda mrefu ikiendelea. -
Jambo TV
@Jambotv_
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (DAWASA) imehitimisha wiki ya huduma kwa Wateja kwa kutoa misaada kwa wahitaji wenye ulemavu kupitia shirika lao la Equal Right for All lenye makazi yake Mabibo katika Wilaya ya Ubungo mkoani Dar es salaam.
Msaada huo umekabidhiwa kwa Asasi ya Haki Sawa kwa Watu Wenye Ulemavu Tanzania na unajumuisha vitimwendo, baiskeli za magurudumu matatu, fimbo za kusaidia watu wenye ulemavu wa kuona, magongo ya kutembelea na mafuta maalumu kwa watu wenye ualbino.
Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo, Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja DAWASA, CPA (T) Ritamary Lwabulinda, amesema huduma bora kwa mteja haiishii katika upatikanaji wa majisafi na usafi wa mazingira pekee, bali pia inahusisha kujali na kuunga mkono makundi mbalimbali katika jamii.
“Natoa wito kwa jamii kuwashika mkono watu wenye uhitaji ili waweze kushiriki katika shughuli mbalimbali na kuchangia maendeleo ya taifa,” amesema Lwabulinda.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Asasi ya Haki Sawa kwa Watu Wenye Ulemavu Tanzania, Said Halili, ameishukuru DAWASA kwa msaada huo na kuzitaka taasisi na wadau wengine kuiga mfano huo wa kuwajali watu wenye ulemavu. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Jeshi la Polisi Kanda ya Kusini limetangaza mikakati ya kuimarisha usalama na kudhibiti migogoro ya wakulima na wafugaji katika Mikoa ya Mtwara, Lindi, Ruvuma na Njombe, kwa lengo la kulinda amani, maisha na mali za wananchi.
Hatua hiyo imekuja kufuatia kikao kazi cha Makamanda wa Polisi wa Kanda ya Kusini kilichofanyika mkoani Mtwara leo Oktoba 9, 2026.
Akitoa taarifa kuhusu kikao hicho kilichofanyika Mkoani Mtwara, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma ambae pia ni Mwenyekiti wa Mikoa ya Kanda ya Kusini SACP Marco Chilya, amesema hali ya usalama katika mikoa hiyo ni shwari, kutokana na ushirikiano mzuri kati ya wananchi na Jeshi la Polisi.
Amesema ushirikiano huo umeendelea kuwa nguzo muhimu katika kuzuia uhalifu na kuhakikisha wananchi wanaishi katika mazingira yenye amani na utulivu.
Katika kikao hicho, makamanda wamejadili tathmini ya hali ya usalama, changamoto za kiutendaji na mikakati ya kuboresha utendaji wa Jeshi la Polisi.
Vilevile, wameweka mikakati ya kukabiliana na matishio ya uhalifu unaovuka mipaka, ambao unahitaji ushirikiano wa karibu kati ya wananchi na vyombo vya ulinzi na usalama.
SACP Chilya amesema kikao hicho pia kimeweka kipaumbele katika maandalizi ya operesheni maalumu za kudhibiti migogoro ya wakulima na wafugaji katika mikoa hiyo.
Jeshi la Polisi limeeleza kuwa litaendesha operesheni hizo kwa lengo la kuimarisha amani na utulivu, huku likiwataka wananchi kuzingatia sheria na kuepuka vitendo vinavyoweza kuchochea migogoro.
Aidha, Jeshi la Polisi limewataka wananchi kuendelea kutoa taarifa sahihi kuhusu viashiria vya uhalifu unaovuka mipaka pamoja na migogoro inayoweza kujitokeza kati ya wakulima na wafugaji, ili hatua stahiki zichukuliwe kwa wakati.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI:
Makamu wa kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Masoud Othman Masoud, amezihimiza nchi wanachama wa Mkataba wa Nairobi kutekeleza maamuzi ya Mkutano wa 12 wa Nchi Wanachama (COP12) kwa vitendo, akisema mafanikio ya mkutano huo yatapimwa kwa maboresho katika afya ya bahari, mifumo ya ikolojia ya pwani na maisha ya wananchi.
Masoud ametoa wito huo leo, Oktoba 9, 2026, alipofunga mkutano huo uliofanyika Dar es Salaam kuanzia Oktoba 6 hadi 9, sambamba na maadhimisho ya miaka 40 ya Mkataba wa Nairobi.
Amesema maamuzi ya COP12 yanapaswa kutafsiriwa kuwa mipango kazi ya kitaifa, majukumu yaliyo wazi na bajeti za ndani ya nchi, akisisitiza kuwa malengo ya kikanda yatafikiwa pale yanapotekelezwa kikamilifu katika ngazi za kitaifa.
Katika wito wake, Masoud amesisitiza umuhimu wa ushirikiano wa kikanda kukabili changamoto zinazovuka mipaka, zikiwemo usimamizi wa rasilimali za bahari zinazoshirikishwa, uchafuzi wa mazingira, upotevu wa viumbe hai, mabadiliko ya tabianchi na maandalizi ya majanga ya baharini.
Amesema pia ni muhimu wadau kutafuta na kutenga ufadhili unaowajibika na unaopatikana kwa urahisi ili kuwekeza katika ulinzi wa mifumo ya ikolojia.
Amesema Mpango wa Masoko ya Uvuvi Endelevu na Ukulima wa Viumbe vya Majini wa Tanzania umekusanya zaidi ya dola milioni 41 kwa ajili ya Zanzibar, ndani ya mradi wa miaka mitano wa dola milioni 117 unaotarajiwa kunufaisha takriban watu laki mona na sitini elfu huku asilimia 80 wakiwa wanawake.
Masoud ametaka utekelezaji wa maamuzi uwe jumuishi na kuwashirikisha wanawake, vijana, watafiti, wafanyabiashara na jamii za mitaa. Amesema uchumi wa buluu unapaswa kuwanufaisha moja kwa moja watu wanaotegemea bahari kwa maisha yao.
Pia ametaja Mpango wa Pamoja wa Umoja wa Mataifa wa Kilimo cha Mwani uliozinduliwa Zanzibar mwaka 2025, unaolenga kaya elfu 15 na kuongeza wastani wa kipato kwa asilimia 40 ifikapo 2028.
Akizungumzia miaka 40 ijayo ya Mkataba wa Nairobi, Masoud amezitaka nchi wanachama kutumia mafanikio ya kipindi kilichopita kama msingi wa kuweka mwelekeo kabambe na bunifu. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetoa elimu ya udhibiti wa mifumo ya umeme kwa wenyeviti na watendaji wa mitaa na kata katika Manispaa ya Tabora, lengo likiwa ni kukabiliana na ongezeko la majanga ya moto katika maeneo ya makazi.
Mafunzo hayo yamefanyika kama sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja, ikizingatiwa kuwa matukio mengi ya moto yamekuwa yakisababisha vifo, majeraha, ulemavu na uharibifu mkubwa wa mali kutokana na hitilafu za umeme.
Akizungumza wakati wa kutoa elimu hiyo, Meneja wa EWURA Kanda ya Magharibi, Kalim Ally, amewataka wananchi kuacha tabia ya kutumia mafundi wasio na sifa au leseni wakati wa kufanya ufungaji na matengenezo ya mifumo ya umeme majumbani.
"Matumizi ya mafundi wasio na sifa husababisha ufungaji usio salama wa mifumo ya umeme, jambo linalohatarisha maisha na mali za wananchi. Tunawasihi wananchi kutumia mafundi walioidhinishwa ili kupunguza hitilafu zinazoweza kusababisha majanga ya moto," amesema Ally.
Kwa upande wao, baadhi ya viongozi na watendaji walioshiriki mafunzo hayo wameeleza kupata uelewa mkubwa kuhusu usalama wa umeme, na wameahidi kuwa mabalozi katika maeneo yao kwa kuhamasisha wananchi kuchukua tahadhari na kufuata kanuni za usalama.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Zaidi ya wanunuzi 50 wamepata leseni za kusafirisha korosho nje ya nchi, 72 wa korosho na karanga, na 14 wa soko la awali wamepatiwa leseni kuelekea msimu wa korosho wa 2026/2027.
Bodi ya Korosho Tanzania kupitia Kaimu Mkurugenzi wa bodi hiyo, Hamidu Mponda, imebainisha hayo Oktoba 9, 2026, katika kikao cha wadau kilichoandaliwa na Benki ya CRDB.
Ongezeko hili la wanunuzi kutoka 26 msimu uliopita hadi zaidi ya 50 msimu huu linatajwa kama kiashiria cha ushindani utakaoleta bei nzuri kwa wakulima.
Bodo hiyo imesema imewaelimisha wakulima zaidi ya elfu 95 kuhusu mbinu bora za kuokota, kukausha na kuhifadhi korosho ili kulinda ubora wake katika masoko ya ndani na nje.
Kwa upande wa vyama vya ushirika vya MAMCU na TANECU vimeahidi kusimamia ubora, huku Benki ya CRDB ikiahidi malipo ya haraka kwa wakulima kuanzia minada ya Oktoba 12, 2026.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Queen Sendiga, ametoa wito kwa wananchi ambao ndugu zao walikuwa safarini na hawajulikani walipo kujitokeza kwa ajili ya kusaidia zoezi la utambuzi wa mabaki ya miili ya watu waliofariki katika ajali iliyotokea eneo la Mkambarani mkoani humo, kupitia vipimo vya vinasaba.
Sendiga ametoa wito huo Oktoba 8, 2026 wakati akizungumza na waandishi wa habari. Ameeleza kuwa zoezi la utambuzi wa sehemu za miili hiyo linaendelea huku akisisitiza umuhimu wa ushirikiano wa wananchi ili kufanikisha utambuzi huo na kuiwezesha familia kupata taarifa sahihi kuhusu ndugu zao.
Kwa upande wake, Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko, amesema Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali itaendelea kushirikiana na Ofisi ya Mganga Mfawidhi pamoja na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro katika kuhakikisha zoezi la utambuzi wa mabaki ya miili hiyo linafanikiwa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwanamke mmoja anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 35 amefariki dunia baada ya kudaiwa kuchomwa kwa kisu shingoni na mume wake, katika tukio linalodaiwa kuhusishwa na wivu wa kimapenzi.
Tukio hilo limetokea katika Mtaa wa Maili Mbili jijini Dodoma, ambapo shemeji wa marehemu Mohamed Iddy, amesema tukio hilo lilitokea Oktoba 8, 2026 majira ya saa mbili usiku ambapo baada ya tukio hilo mtuhumiwa alibaki nyumbani hadi asubuhi, ndipo alipoelekea kituo cha polisi kutoa taarifa.
Baadhi ya majirani wamedai kuwa mtuhumiwa alikuwa na tabia ya kumpiga mke wake mara kwa mara. Kutokana na hali hiyo, wameiomba Serikali kuhakikisha hatua za kisheria zinachukuliwa dhidi yake.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Mtaa huo, Maximilian Jeremiah, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa linadaiwa kuchochewa na wivu wa kimapenzi.
Aidha, amesema mtuhumiwa tayari anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa ajili ya uchunguzi na hatua zaidi za kisheria.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mbunge wa Jimbo la Bukombe, Dkt. Doto Biteko, amepongeza juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kuimarisha sekta ya elimu nchini, akisema Serikali imefanya uwekezaji mkubwa unaochochea maendeleo ya elimu.
Dkt. Biteko ameyasema hayo leo, Oktoba 9, 2026, wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mwalimu Duniani yaliyofanyika wilayani Bukombe, mkoani Geita, huku akisisitiza umuhimu wa kuendelea kuwekeza katika elimu na kuthamini mchango wa walimu katika kujenga taifa lenye maarifa, ujuzi na maendeleo endelevu.
Aidha, amewahimiza walimu kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa weledi, bidii na uzalendo ili kuhakikisha uwekezaji unaofanywa katika sekta ya elimu unaleta matokeo chanya kwa wanafunzi na Taifa kwa ujumla.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Hatimaye mwili wa Jane Urassa (46) umezikwa leo Oktoba 9, 2026 katika makaburi ya Kanisa la KKKT Nkuu Kati, Kijiji cha Nkuu Sinde, Kata ya Machame Mashariki, Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro.
Maziko hayo yameongozwa na Mkuu wa KKKT, Dayosisi ya Kaskazini Dkt.Fredrick Shoo huku akiwaeleza waombolezaji kujifunza juu ya kifo cha Jane Urassa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini, Askofu Dkt. Fredrick Shoo, amewataka waumini na familia kuombea ndoa za vijana wao na kuwaandaa kiroho ili waweze kukabiliana na changamoto za maisha ya ndoa kwa upendo, uvumilivu na kusameheana.
Askofu Shoo ametoa rai hiyo Oktoba 9, 2026, wakati akihubiri katika Ibada ya mazishi ya Jane Urassa iliyofanyika katika Kanisa la KKKT Nkuu Kati, Kijiji cha Nkuu Sinde, Kata ya Machame Mashariki, Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro, iliyohudhuriwa na mamia ya waombolezaji.
Amesema ndoa za vijana zinakabiliwa na changamoto nyingi zinazohitaji maandalizi ya kutosha, maombi na uelewa wa majukumu ya mume na mke, akisisitiza kuwa wanandoa wanapaswa kujifunza kuvumiliana, kukubali wanapokosea na kuombana msamaha badala ya kutegemea uwezo wao pekee.
“Wanandoa wachanga wanapaswa kuombewa badala ya kusubiria mambo kama haya yatokee. Vijana wanahitajika kuandaliwa vema kujua wajibu wa kuishi vema kama mke na mume katika kuvumiliana katika hali yoyote. Hiyo ndiyo ahadi ya ndoa. Kuamua wenyewe hamtaweza; kwenye ndoa kuna kukoseana na kuombana msamaha. Someni Wakolosai 3,” amesema Askofu Shoo.
Aidha, amewataka waombolezaji kutafuta kwa bidii amani na watu wote, akisisitiza kuwa msiba huo haupaswi kuwa chanzo cha mafarakano na chuki ndani ya familia za wafiwa, bali uwe fursa ya kuimarisha upendo na maridhiano.
Amewashukuru familia za Urassa na Kweka kwa kudumisha amani na kukaa pamoja kujadiliana hadi kufikia mapatano kuhusu utaratibu wa kumuaga marehemu, akiwataka kuendelea kulinda mshikamano huo.
“Amani na upendo vipate kutawala katika mioyo yenu na shina la uchungu lisije likachipuka na kuwasumbua. Maana tukiendekeza uchungu na chuki na shina likachipuka, halitaishia tu hapa. Naomba tutafute kwa bidii amani na upendo,” amesema.
Katika hatua nyingine, Askofu Shoo amesema msiba huo umegusa watoto ambao wanahitaji kutunzwa na kupewa malezi yanayozingatia mahitaji yao ya kiroho, kimwili na kiakili, akizitaka familia husika kuendelea kushikamana na kutoruhusu mazingira ya msiba kuleta mgawanyiko.
Akisoma wasifu wa Marehemu Thame Urassa amesema kuwa familia itazidi kumkumbuka kwa mengi ikiwemo ukarimu na namna alivyoijali familia yake.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametuma salamu za rambirambi kufuatia ajali mbili tofauti za barabarani zilizotokea usiku wa kuamkia leo, Oktoba 9, 2026, mkoani Morogoro na kusababisha vifo vya watu 32, wakiwemo askari polisi watatu.
Salamu hizo za rambirambi zimetumwa kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Queen Cuthbert Sendiga, pamoja na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Camillus Mongoso Wambura.
Katika taarifa yake, Rais Dkt. Samia ametoa pole kwa familia zilizopoteza wapendwa wao, ndugu, jamaa na marafiki, huku akiwaombea nguvu, subira na faraja katika kipindi hiki kigumu cha majonzi. Pia, amewatakia majeruhi wote wa ajali hizo uponyaji wa haraka.
Aidha Rais Samia amelitaka Jeshi la Polisi kuendelea kusimamia kwa umakini sheria za usalama barabarani huku akiwasihi madereva na watumiaji wote wa barabara kuchukua tahadhari na kuzingatia sheria ili kuzuia ajali zinazoweza kuepukika.
Ajali ya kwanza ilitokea eneo la Mkambarani, Morogoro katika barabara kuu ya Dar es Salaam, baada ya basi la abiria lililokuwa likielekea Mbeya kugongana uso kwa uso na lori la mbao. Mgongano huo ulisababisha basi kulipuka na kuwaka moto.
Ajali ya pili ilihusisha maafisa wa Polisi katika Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro usiku wa kuamkia Oktoba 9, 2026, baada ya gari la Jeshi la Polisi lililokuwa kwenye doria kugongana uso kwa uso na lori la mizigo. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro imetoa taarifa ya awali kuhusu ajali mbili zilizotokea katika maeneo tofauti mkoani humo, na kusababisha vifo vya watu 31, wakiwemo askari polisi watatu, huku wengine wakijeruhiwa.
Ajali ya kwanza imehusisha lori aina ya Scania lililokuwa limebeba miti aina ya milunda na basi la abiria lililokuwa likitoka Dar es Salaam kuelekea Mbeya, Ajali hiyo imesababisha vifo vya watu 28 pamoja na majeruhi.
Ajali nyingine imetokea eneo la Dakawa, katika Barabara ya Morogoro–Dar es Salaam, ikihusisha magari matatu, likiwemo gari la Polisi, Ajali hiyo imesababisha vifo vya watu wanne, wakiwemo askari Polisi watatu, huku askari wengine saba wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) wakijeruhiwa.
Akizungumza na waandishi wa habari, Kaimu Ofisa Habari wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro Scholastica Ndunga, amesema kuwa kati ya miili 28 ya waliofariki katika ajali iliyohusisha basi na lori, miili 17 imetambuliwa, ikiwemo ya wanaume 10 na wanawake saba, huku miili mingine ikiendelea na taratibu za utambuzi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, anayeshughulikia Uwekezaji Dkt. Fred Msemwa, amesema wamekutana na wadau wa sekta binafsi kwaajili ya kupitia rasimu ya sera ya uwekezaji ambayo inakwenda sambamba na utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2050.
Msemwa amebainisha hayo Oktoba 9, 2026 jiji Dar es Salaam katika Mkutano wa kukusanya maoni ya wadau wa sekta binafsi kuhusu Rasimu ya Sera ya Taifa ya uwekezaji ya mwaka 2026 na mkakati wa utekelezaji wake.
"Tuko hapa kwaajili ya kufanya kazi ya kupitia Rasimu ya Sera ya Uwekezaji na kama mnavyokumbuka, mwaka jana mwezi julai Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan, alizindua dira mpya ya maendeleo ya taifa, inayoitwa Dira ya 2050 na dira hiyo iliweka malengo makubwa kwa taifa letu na malengo hayo yakijidhihirisha zaidi katika kuongeza uwekezaji pamoja na kuwezesha sekta binafsi kuwa na mchango mkubwa zaidi katika ukuaji wa uchumi wetu" amesema Dkt. Fred.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Bankers Association, Tusekelege Joune, amesema sekta ya Bank wao wanatamani kuona uwepo wa Sheria ya sekta binafsi ambayo itaweka bayana mazingira ya sekta hizo kuhusu haki na wajibu wake katika kuchangia maendeleo ya taifa.
Ameongeza kuwa kutokana na kukosekana kwa muongozo kamili hapo awali, wa kuelekeza sekta binafsi zitende vipi majukumu yake, ilikuwa inapelekea kukosekana kwa usimamizi kamili.
Kutoka Chemba ya Taifa ya Biashara (TNCC) ambayo awali ilikuwa TCCIA, Kervin Ogodo, amesema wanaangalia namna zaidi ya kuwawezesha wawekezaji wa ndani bila kuwaathiri wageni wanaofika kuwekeza lengo likiwa ni kuzinufaisha pande zote mbili.
Aidha, Kaimu Mkurugenzi wa Shirikisho la Sekta Binafsi (TPSF), Deogratius Masawe, amesema mkutano huo wa kukusanya maoni ya wadau wa sekta binafsi ni fursa ya kutoa mapendekezo na maeneo ambayo yanaweza kuwekewa nguvu zaidi katika utekelezaji wa rasimu hiyo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Askari wa Jeshi la Polisi wakiwa Msibani kwa Jane Urassa Kijiji cha Nkuu Sinde Kata ya Machame Mashariki Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro anayedaiwa kuuawa na Mume wake Laurent Kweka kwa kupingwa risasi Oktoba Mosi,2026 nyumbani kwao Bunju A Mtaa wa Mkoani Jijini Dar es salaam kwa kile kinachodaiwa ni mgogoro wa hati ya nyumba.
Jane Urassa atazikwa leo Oktoba 9,2026 katika makaburi ya Kanisa la Mkuu Kati ambapo Ukoo wa Kweka umeruhusiwa na familia ya Urassa kuhudhuria Ibada hiyo huku wakiwekewa zuio la kutofika nyumbani kwa Jane kipindi hiki cha msibaThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Rais wa Umoja wa Maaskofu, Wachungaji, Mitume, Manabii na Madhehebu ya Kikristo Tanzania ambaye pia ni Askofu Mkuu wa Makanisa ya SPCT, Askofu Musa Mlawi, amewataka vijana nchini kuwaheshimu wazazi wao, akieleza kuwa hiyo ni sehemu muhimu ya kujenga jamii yenye maadili.
Askofu Mlawi ametoa kauli hiyo wakati akizungumza katika ibada maalumu ya usimikaji na pongezi kwa Makamu wa Rais Deogratius Ndejembi, iliyofanyika katika Kanisa hilo Chamwino mkoani Dodoma, kufuatia uteuzi wake na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Amesema kila mmoja ana wajibu wa kuhakikisha matendo yake hayavunji sheria wala kuhatarisha usalama wa wengine na kuongeza kuwa viongozi wa dini wana wajibu wa kuiombea Serikali na viongozi wake ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa manufaa ya wananchi, pamoja na kuwaombea vijana ili wawe na mwelekeo mzuri katika maisha.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Kiwanda kikubwa cha nguo cha Sinovest kilichopo katika Eneo Maalum la Kiuchumi la Bagamoyo (Bagamoyo SEZ) mkoani Pwani kimejipanga kutoa ajira kwa vijana 10,000 na kukuza mnyororo mpana wa thamani katika sekta ya viwanda, huku kikichochea uwekezaji wa kimkakati na uhamisho wa ujuzi kwa Watanzania.
Uwekezaji huo unaomilikiwa na mwekezaji kutoka China unajumuisha eneo lenye ukubwa wa mita za mraba 210,080 na kuingiza mtaji wa takriban Dola za Kimarekani milioni 50 hadi 55. Kiwanda hicho tayari kimeshaanza uzalishaji wa bidhaa kama jezi na fulana kwa ajili ya masoko ya ndani na nje ya nchi huku kikiendelewa kupanuliwa zaidi.
Akizungumza hivi karibuni kiwandani hapo katika ziara yake ya kikazi ya ukaguzi wa miradi ya kipaumbele Bagamoyo SEZ, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo @kitilam amebainisha kuwa mradi huo ni chachu kuelekea Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2050 na kwamba tayari umeanza kutoa fursa za ajira kwa vijana wa eneo hilo la Bagamoyo.
Kwa upande wake, Meneja Mradi wa Sinovest, Vitus Mkinga ameeleza kuwa mradi huo utatengeneza mnyororo mpana wa thamani unaohusisha uzalishaji wa bidhaa na vifaa mbalimbali, huku ukitoa fursa kubwa ya uhamisho wa teknolojia na ujuzi kwa Watanzania ili kujenga uchumi shindani wa viwanda.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Vilio na simanzi vimetawala wakati Mwili wa Jane Maloo Urassa (46) ukiwasili nyumbani kwao Kijiji cha Nkuu Sinde Kata ya Machame Mashariki Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro kwaajili ya mazishi.
Msemaji wa familia ya Urassa, Judica Urassa, ameeleza kuwa Ukoo wa akina Kweka hawataruhusiwa kufika nyumbani hapo badala yake wataruhusiwa kuhudhuria Ibada ya kumuaga Kanisa la KKKT Nkuu Kati pekee, akisisitiza watu kutokuongea kitu wasicho kijua.
Jane Urassa, anadaiwa kuuawa kwa kupigwa risasi na mumewe, Laurent Kweka, chanzo kikitajwa ni mgogoro wa hati ya nyumba, tukio linalodaiwa kutokea alfajiri ya Oktoba Mosi, 2026, katika nyumba yao iliyopo Bunju A, Mtaa wa Mkoani Jijini Dar es salaam.
Watu mbalimbali tayari wamekusanyika nyumbani kwao baada ya kupokea mwili huo ikiwa ni maandalizi ya kuelekea Kanisani majira ya saa Saba Mchana kwaajili ya Ibada ya mazishi ambapo mwili wake unatarajiwa kupumzishwa katika makaburi ya Kanisa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu Wakili Amon Mpanju, amesema mchakato wa kufuta kifungu cha 13 na 17 vya Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971 vinavyoruhusu watoto wa kike kuolewa chini ya umri wa miaka 18 unaendelea, Serikali imesema.
Amesema hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa kuelekea maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike Duniani inayofanyika kila mwaka Oktoba 11.
Amesema vifungu hivyo vinaenda kinyume na Sheria ya Mtoto Namba 13 ya mwaka 2009 inayomtafsiri mtoto kuwa ni mtu yeyote mwenye umri chini ya miaka 18, pamoja na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Shirika la Plan International Tanzania, Janeth Mbucha amesema wanaendelea kushirikiana na Serikali na wadau wengine kupambana ili kuhakikisha Sheria ya Ndoa inarekebishwa na kuendana na Sheria ya Mtoto.
Naye mnufaika wa mradi wa Girls Takeover amesema kumekuwa na harakati mbalimbali zinazofanywa na wadau kwa pamoja ikiwa na lengo la kutokomeza ndoa za utotoni nchini.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limetangaza rasmi marekebisho ya kanuni yaliyopunguza kwa kiasi kikubwa utitiri wa tozo na ada ambazo zimekuwa zikitozwa wasanii na wadau wa sekta ya sanaa nchini kwa mwaka, ikiwa ni utekelezaji wa mabadiliko yaliyofanywa na Bunge ili kuimarisha usimamizi na kukuza uchumi wa wasanii.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kaimu Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Edward Buganga, ameeleza kuwa kanuni hizo mpya tayari zimeanza kutumika na zinalenga kulinda wasanii, hadhira, watoto, na urithi wa sanaa bila kuzuia ubunifu, huku zikiwahusisha makundi mbalimbali yakiwemo ya wasanii huru, vikundi vya sanaa, ma-DJs, washereheshaji, maproduza, mameneja, waandaaji wa matukio, studio, vyombo vya habari, na wamiliki wa kumbi.
Katika muundo huo mpya wa ada, msanii huru sasa atajisajili na kuhuisha kibali chake kila mwaka kwa kulipa Shilingi 10,000 pekee badala ya Shilingi 40,000 za awali, wakati usajili na uhuishaji wa vibali vya vikundi vya sanaa umepunguzwa kutoka Shilingi 60,000 hadi Shilingi 30,000 kwa mwaka.
Aidha, waandaaji wa matukio ya sanaa wametakiwa kuomba vibali kupitia mfumo wa kidijiti wa AMIS siku 30 kabla ya tukio, ambapo vibali hivyo sasa vitatolewa bure kabisa ili kuwezesha wataalamu wa baraza hilo kutoa mwongozo wa usalama na ufanisi.
“Hapa tunasisitiza waandaaji wa matukio ya sanaa wawe na vibali ili wataalamu wetu wawasaidie kuwapa mwongozo wa kwenda vizuri na kibali atapata bure, akikiuka tutamchukulia hatua,” alisema.
Buganga amesisitiza kuwa kanuni hizo mpya zimeweka misingi thabiti ya usimamizi katika mikoa na wilaya, ulinzi wa watoto, maadili, pamoja na udhibiti wa matumizi ya sanaa za jadi kwa madhumuni ya kibiashara ili kuhakikisha mapato yanayopatikana yanarejeshwa kwa jamii husika zinazomiliki urithi huo.
Pamoja na hayo, wasanii wanaotoka nje ya nchi au kwenda nje kwa ajili ya maonesho wametakiwa kufuata taratibu rasmi za kupata vibali vya BASATA, huku shughuli za mafunzo au ubadilishanaji ujuzi wa kidiplomasia zikiwekewa utaratibu maalum wa kutozwa ada.
Amesisitiza maadili kwenye kazi za sanaa akisema kazi za sanaa hazipaswi kuchochea vurugu, ubaguzi, unyanyasaji au kukiuka sheria na badala yake sanaa inaweza kuelimisha, kukosoa, kuonya na kuelekeza jamii na kwamba ukosoaji wa kijamii si kosa iwapo unazingatia sheria na maadili.
Akizungumzia ulinzi wa sanaa za jadi, amesema matumizi ya sanaa za jadi kwa madhumuni ya kibiashara nje ya muktadha wa jamii husika yatahitaji kibali cha BASATA.
Amesema hatua hiyo inalenga kulinda urithi, utamaduni na haki za jamii zinazomiliki na kurithisha sanaa hizo na kwamba mapato yatakayopatikana kupitia matumizi ya sanaa jadi yatarejeshwa kwa jamii husika kwenye eneo la sanaa. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Watu kadhaa wanahofiwa kufariki dunia baada ya basi la abiria kugongana uso kwa uso na lori la mizigo aina ya Scania na kuwaka moto katika eneo la Makambarani mkoani Morogoro usiku wa kuamkia leo Oktoba 9.2026
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Andrew Kantimbo amesema watu 30 wamejeruhiwa katika ajali hiyo, huku idadi kamili ya waliofariki bado haijafahamika kutokana na miili kuungua vibaya
Katika ajali nyingine aliyoyokea eneo la Mvomero watu wanne wakiwemo askari Polisi watatu wamefariki dunia baada ya gari la Polisi kugongana na Lori, taarifa zaidi kuhusu chanzo cha ajali hizo na utambulisho wa waliofariki zinatarajiwa kutolewa na Jeshi la Polisi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Machozi na majonzi vimetawala baada ya Rebeca Naffi, mwenye umri wa miaka 22, kupoteza maisha ndani ya nyumba ya wageni usiku wa Octoba 8, 2026 alipokuwa akifanya kazi ya usafi, katika Kitongoji cha Msorongo, Kata ya Ambureni, Arumeru mkoani Arusha.
Rebeca alikuja Arusha kwa dada yake, ambaye alichukua jukumu la kumpeleka chuoni na kumlipia ada.
Baada ya kumaliza masomo na kukaa muda bila ajira, Rebeca alipata kazi hiyo, jambo lililoifanya familia kupanga kwenda kanisani Jumapili hii kumshukuru Mungu.
Hata hivyo, kabla ya siku hiyo kufika, mipango ya furaha na shukrani ikageuka kuwa msiba mzito, baada ya Rebeca kukutwa amefariki dunia ndani ya nyumba hiyo ya wageni, akiwa na jeraha linalodaiwa kusababishwa na kitu chenye ncha kali katika eneo la kifua pamoja na majeraha katika eneo la macho.
Jeshi la Polisi mkoani Arusha limesema linamshikilia mtu mmoja kwa tuhuma za kuhusika na kifo cha Rebeca, huku likiendelea na uchunguzi kubaini mazingira ya tukio hilo na hatua zaidi za kisheria.2 media couldn't be displayed. See them on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, CP Salum Hamduni amewataka Viongozi wa Dini kushirikiana na Serikali katika kuimarisha uchumi wa waumini wa dini zao sambamba na kulinda amani na kukemea mmomonyoko wa maadili.
Akizungumza Oktoba 8, 2026, wakati akifungua Mkutano wa neno la Mungu na maombi uliondaliwa na 'A light to the nations' (ALN) unaofanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Buhongwa B jijini Mwanza, uliolenga kuliombea Taifa na kuomba lisiwe na madhara yatokanayo na El Nino.
CP Hamduni amesema Viongozi wa Dini wana nafasi kubwa katika kuboresha hali za kiuchumi za waumini na Watanzania kwa ujumla, akiwataka kuwawezesha waumini kuunda vikundi vya uzalishaji, kupata mitaji na elimu ya biashara.
Aidha CP Hamduni amewataka Viongozi wa Dini kuendelea kukemea vitendo vya mmomonyoko wa maadili ikiwemo dawa za kulevya, uasherati, wizi, ubadhirifu na rushwa ambavyo vinaendelea kuathiri jam.
Mhubiri wa Injili kutoka Marekani ambaye pia ni mwazilishi wa huduma ya ALN, Dk Dana Morey amefurahishwa na uhuru wa dini uliopo nchini huku akitoa wito wa kuendelea kuilinda amani nchini.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa, ameiagiza Shirika la Reli Tanzania (TRC) kuchukua hatua zote muhimu kulinda miundombinu ya Reli ya Kisasa (SGR) na Reli ya Kati (MGR) dhidi ya athari za mvua kubwa za El Niño zinazotarajiwa kunyesha hivi karibuni.
Profesa Mbarawa ametoa agizo hilo leo Alhamisi Oktoba 8, 2026, wakati wa ziara ya ukaguzi kutoka Kilosa hadi Gulwe/Mgodagoda mkoani Morogoro, ambapo amekagua kazi zinazoendelea za kuimarisha miundombinu ya reli, hususan maeneo yenye madaraja yanayoweza kuathiriwa na mafuriko na mmomonyoko wa udongo.
Profesa Mbarawa amesema, Serikali imewekeza zaidi ya Shilingi trilioni 8 katika ujenzi wa Loti ya Kwanza na ya Pili ya SGR, hivyo miundombinu hiyo inapaswa kulindwa kwa nguvu zote ili kuhakikisha uwekezaji huo unaendelea kuwa na manufaa kwa Watanzania.
Profesa Mbarawa amesisitiza kuwa, usalama wa abiria na mali zao ni kipaumbele cha kwanza katika usafirishaji, huku akiiagiza TRC kuhakikisha huduma za SGR kati ya Dar es Salaam, Morogoro na Dodoma zinaendelea kupatikana wakati wote, bila kujali changamoto za hali ya hewa.
Aidha, Waziri huyo wa Uchukuzi ameitaka TRC kuweka akiba ya kutosha ya mawe katika maeneo yenye madaraja ili yatumiwe kwa haraka endapo kutatokea changamoto ya mafuriko au mmomonyoko huku akisisitiza ulinzi wa pamoja wa SGR na MGR katika maeneo ambayo reli hizo zinapita sambamba.
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Ujenzi na Miundombinu wa TRC, Mhandisi Ismail Athuman Ismail, amesema shirika limepokea maelekezo hayo na limeanza kuyatekeleza, ikiwemo kuongeza uzalishaji wa mawe katika machimbo ya Kilosa na Godegode.
Sambamba na hilo ameeleza kuwa, TRC pia imeunda timu za wataalamu zinazofanya ufuatiliaji wa miundombinu saa 24, huku ikiendelea kushirikiana na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kupata taarifa za utabiri wa hali ya hewa.
Vilevile, TRC inakamilisha utafiti wa matumizi ya mifumo ya kidijitali ya ITS LED na GIS kwa ajili ya kudijitisha miundombinu ya reli na kuweka vitambuzi katika maeneo hatarishiThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Wafanyabiashara wa Soko la Kimataifa la Kariakoo, jijini Dar es Salaam, wameiomba Serikali kuondoa meza za machinga zinazowekwa mbele ya maduka na kwenye njia za kupita, wakisema hali hiyo inaathiri shughuli zao za biashara na usafirishaji wa mizigo.
Hoja hiyo imetolewa leo, Oktoba 8, 2026, katika kikao kati ya wafanyabiashara na Serikali kilichofanyika Kariakoo.
Akizungumza katika kikao hicho, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Kariakoo, Severine Mushi, amesema wafanyabiashara hawapingi uwepo wa machinga, bali wanataka shughuli zao zifanyike kwa utaratibu na bila kuzuia njia za kupita.
Mushi amesema kuachwa wazi kwa njia hizo kutarahisisha upatikanaji wa wateja pamoja na usafirishaji wa mizigo katika eneo hilo.
Katika kikao hicho, wafanyabiashara pia wameiomba Serikali kutatua changamoto ya kutozwa kodi ya taka kwa duka na stoo inayotumika kuhifadhi bidhaa za biashara hiyo hiyo.
Akijibu hoja hizo, Katibu Tawala wa Wilaya, Charangwa Selemani Makwiro, amesema Serikali itakutana na mkandarasi wa huduma ya taka ili kutatua suala hilo, huku akieleza kuwa wafanyabiashara watapatiwa majibu ndani ya wiki moja hadi mbili.
Makwiro amesema doria za usiku pia zinaendelea katika eneo la Kariakoo kwa ajili ya kuimarisha usalama na utaratibu wa shughuli za biashara.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Wabunge kutoka Kundi la Kijiografia-Kisiasa la Bara la Afrika kupitia Umoja wa Mabunge ya Duniani (IPU) wameunga mkono ajenda ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ya kuimarisha afya ya uzazi, mama, mtoto na vijana barani Afrika.
Kauli hiyo imetolewa leo Oktoba 8, 2026 jijini Arusha katika mkutano wa pembezoni wa Mkutano wa 153 wa IPU, ambapo viongozi hao pamoja na wadau wa maendeleo ya sekta ya afya duniani wamejadili umuhimu wa kuimarisha sera, mifumo ya utoaji huduma, uwekezaji na uwajibikaji katika sekta ya afya.
Kiongozi wa Kundi la Kijiografia-Kisiasa la Wabunge wa Bara la Afrika kupitia IPU, Ali Kolotou Tchaïmi, amesema wakati umefika kwa nchi za Afrika kuunganisha nguvu, kujifunza kutoka kwa kila mmoja na kuwa na ajenda ya pamoja ya kuboresha afya ya mama na mtoto.
Kwa upande wake Spika wa Bunge la Afrika Kusini, Angela Didiza amesema Afrika inaweza kujifunza kutokana na uzoefu wa Tanzania katika kuendeleza afya ya wanawake, watoto wachanga, watoto na vijana, akisisitiza kuwa uongozi wa kisiasa una nafasi muhimu katika kuweka mazingira ya utekelezaji wa hatua za kibunge.
Spika wa Bunge la Botswana, Dithapelo Keorapetse, amesisitiza umuhimu wa kuunganisha uwekezaji katika sekta ya afya na ufuatiliaji wa matumizi na matokeo yake.
“Uwekezaji pekee hautoshi, bado tunakabiliwa na changamoto katika matokeo ya afya, hali hii inaonesha umuhimu wa kuangalia ufanisi wa matumizi ya rasilimali” amefafanua Keorapetse.
Akizungumza, Rais wa Umoja wa Mabunge ya Duniani (IPU), Dkt. Tulia Ackson amesema juhudi za Rais Samia katika kuimarisha afya ya uzazi zinapaswa kuungwa mkono, huku akisisitiza kuwa bila utashi wa kisiasa na uwajibikaji wa viongozi, wataalamu wa afya na na mifumo ya afya haitoshi kuimarisha huduma za afya ya uzazi, mama na mtoto.
“IPU inajizatiti kuwa mshirika wa vitendo kwa mabunge katika kuhakikisha ahadi zinatafsiriwa kuwa hatua na matokeo chanya ya kuimarisha afya ya uzazi, mama na mtoto” amesema Dkt. Tulia.
Naye Spika wa Bunge la Tanzania, Mussa Azzan Zungu amesema afya ya mama na mtoto ni kipaumbele cha Serikali ya Tanzania na kwamba Bunge kwa niaba ya wananchi lina wajibu wa kusimamia rasilimali zinazotengwa kwa ajili ya huduma hizo.
Awali, Mshauri wa Rais kuhusu Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto, Ummy Mwalimu, amesema vifo vitokanavyo na uzazi barani Afrika vimepungua kwa asilimia 42 kati ya mwaka 2000 na 2023, lakini Afrika bado inachangia asilimia 70 ya vifo vya kina mama duniani.
Amesema kupitia Mpango Kazi wa Rais Samia wa Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto Barani Afrika 2026–2030, ajenda ya Rais Samia inalenga kufikia Sifuri Tatu: sifuri ya kujifungulia nyumbani, sifuri ya vifo vinavyoweza kuzuilika vya mama na mtoto, na sifuri ya watoto wasiochanjwa. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Imeelezwa kuwa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) si chuo cha kuchukua degree pekee, bali ni taasisi inayowaandaa wanafunzi kupata elimu, ujuzi na maarifa yanayoweza kutumika katika kutatua changamoto za maisha halisi.
Hayo yamebainishwa Oktoba 8, 2026 katika Mahafali ya 48 ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), ambapo Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Raphael Chibunda, pamoja na baadhi ya wahitimu wakiongozwa na Evaline Tarimo, wameeleza kuwa elimu inayotolewa chuoni hapo inalenga zaidi kuwajengea wahitimu uwezo wa kutumia taaluma.
Wamesema kuwa wahitimu wanapaswa kuondoka chuoni wakiwa na zaidi ya shahada, kwa kuwa ujuzi na maarifa waliyojengewa yanapaswa kuwa chachu ya mabadiliko katika jamii, hususan katika sekta ya kilimo.
Kwa upande wake, Jaji Mstaafu Joseph Warioba amewataka wahitimu hao kutumia elimu na ujuzi walioupata kuhakikisha wanatatua changamoto zinazowakabili wakulima nchini, ikiwemo kuwasaidia kuondokana na kilimo cha jembe na kuelekea katika matumizi ya teknolojia na mbinu za kisasa za kilimo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mahakama ya Rufani ya Tanzania, Kanda ya Arusha, imetengua uamuzi wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha uliokuwa umeamuru mwenendo wa shauri dhidi ya Peter Michael Madeleka kuanza upya, ikisema amri hiyo haikuwa sahihi kisheria kwa mazingira ya shauri hilo.
Uamuzi huo umetolewa leo, Oktoba 8, 2026, katika rufaa ya jinai namba 595/596 ya mwaka 2023 inayomuhusisha Peter Michael Madeleka dhidi ya Jamhuri, kufuatia Madeleka kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha uliotolewa Julai 17, 2023 na Jaji Bade.
Historia ya shauri hilo inaonesha kuwa kesi ilianza Mei 14, 2020, ambapo Madeleka na Jamila Augustino Ilomo walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha na kutakiwa kujibu mashtaka yaliyohusisha makosa ya jinai, ikiwemo kupata fedha kwa njia ya udanganyifu (obtaining money by false pretence).
Baadaye, kupitia utaratibu wa plea bargaining, makubaliano ya kukiri kosa yalifanyika na Madeleka akahukumiwa kwa adhabu iliyohusisha faini pamoja na utaratibu wa kurejesha fedha.
Hata hivyo, Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, katika uamuzi wake wa Julai 17, 2023, iliondoa makubaliano hayo ya plea bargaining, ikafuta mwenendo wa Mahakama ya Hakimu Mkazi na kuamuru shauri lisikilizwe upya, yaani 'trial de novo'.
Hatua hiyo ndiyo iliyomsukuma Madeleka kukata rufaa katika Mahakama ya Rufani, akipinga miongoni mwa mambo mengine uhalali wa kuamriwa kusikilizwa tena baada ya kuwa tayari alishughulikiwa na mahakama katika shauri hilo.
Katika uamuzi wake wa leo, Mahakama ya Rufani imekubaliana na hoja za msingi zilizowasilishwa na Madeleka, na hivyo imetengua na kufuta mwenendo pamoja na amri zilizotolewa na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, ikiwemo amri ya kuanza upya kwa shauri hilo.
Mahakama pia imeelekeza kurejeshwa kwa shilingi laki mbili ambazo Madeleka alilipa kama faini, pamoja na shilingi milioni mbili zilizolipwa kama sehemu ya fidia (compensation) katika utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa kupitia plea bargaining.
Kwa mujibu wa hoja zilizowasilishwa katika rufaa hiyo, msingi mkubwa wa pingamizi ulikuwa kwamba kumrudisha Madeleka katika mchakato mwingine wa jinai baada ya kuwa tayari amehukumiwa na kutekeleza adhabu kulizua suala la kutoadhibiwa au kuhukumiwa mara mbili kwa kosa lilelile (double jeopardy.)
Madeleka amesema uamuzi huo ni muhimu kwake kwa sababu, kwa maoni yake, umeweka msimamo wa kisheria kuhusu namna ambavyo utaratibu wa plea bargaining unapaswa kutekelezwa na mipaka ya mamlaka za vyombo vya haki jinai katika kushughulikia shauri ambalo tayari limefikia hatua ya hukumu na utekelezaji wa adhabu.
Amesema pia anaiamini Mahakama ya Rufani kwa kutafsiri sheria na kutoa uamuzi unaolinda misingi ya utawala wa sheria, huku akisisitiza kuwa hakuna mamlaka, ikiwemo Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), iliyo juu ya sheria.
Madeleka ameitaka taasisi na watu aliowataja katika mchakato huo kuwajibika kwa kuomba radhi kwa kile anachodai kuwa ni madhara aliyoyapata kutokana na mashtaka hayo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mchungaji Abraham Mchome ameitaka jamii kutafakari matendo yake dhidi ya misingi ya utu na imani, akisema mwanadamu ameumbwa kwa sura na mfano wa Mungu, lakini baadhi ya watu wanaendelea kufanya mambo yanayokwenda kinyume na maadili hayo.
Akizungumza wakati wa ibada ya kumuaga marehemu Jane Urassa katika Kanisa la KKKT Mbezi Beach jijini Dar es Salaam leo, Oktoba 8, 2026, Mchungaji Mchome amesema taifa limeguswa na tukio hilo, huku akitilia mkazo umuhimu wa kuheshimu uhai na utu wa mwanadamu.
Amesema hali hiyo inapaswa kuwa changamoto kwa jamii kujiuliza, “Sura ya Mungu iko wapi, mbona tunafanya yaliyo chukizo kwa Mungu?” huku akisisitiza kuwa hata katika ndoa na maeneo ya kazi, watu wanapaswa kuacha kuwaziana mabaya na badala yake kuheshimiana na kuthamini maisha ya wenzao.
Mchungaji Mchome amesema ni jambo la kusikitisha kuona baadhi ya watu wakionekana watakatifu wanapokuwa kanisani, lakini wanapokuwa katika mazingira mengine wanatenda kinyume na misingi ya utu na maadili.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH), Prof. Abel Makubi, amewahimiza wananchi kuwa na utamaduni wa kupima afya zao mara kwa mara, akisisitiza kuwa afya ni jambo muhimu zaidi kuliko mali na fedha.
Amesema hayo Oktoba 8, 2026 jijini Dodoma wakati Hospitali ya Benjamin Mkapa kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ilipozindua Kambi Maalumu ya Huduma za Ubingwa na Ubobezi kwa ajili ya uchunguzi na matibabu ya magonjwa.
Prof. Makubi amesema hakuna kitu kikubwa kwenye mwili wa binadamu kuliko afya, hivyo wananchi wanapaswa kuhakikisha wanafanya uchunguzi wa afya zao badala ya kuweka mbele suala la fedha na kusahau afya zao.
Kambi hiyo inafanyika katika Viwanja vya Soko la Machinga, Bahi Road, kuanzia Oktoba 8 hadi 12, 2026, huku walengwa wakiwa Mama Lishe na Baba Lishe, waendesha bodaboda na bajaji, madereva wa daladala na magari makubwa pamoja na wananchi wote kwa ujumla.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI:
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi, amefungua rasmi Mkutano wa 12 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Nairobi (COP12) huku akiainisha vipaumbele sita muhimu vikiwemo kuweka mifumo ya kisheria na kushirikisha sekta binafsi katika kulinda ikolojia ya Bahari ya Hindi.
Akitubia mkutano huo leo Oktoba 8, 2026 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam, Ndejembi amesema vipaumbele hivyo ni msingi wa kuingia katika sura mpya ya utekelezaji wa mkataba huo kwa miaka 40 ijayo.
Katika kipaumbele cha kwanza, Ndejembi amezitaka nchi wanachama kutafsiri mkataba, itifaki na maamuzi ya COP kuwa sheria za kitaifa, sera, bajeti na utekelezaji, akibainisha kuwa Tanzania tayari imesaini karibu itifaki zote nne zinazohusu maeneo yaliyohifadhiwa, usimamizi wa pwani, na kuzuia uchafuzi wa bahari.
Kuhusu mabadiliko ya tabianchi, amesisitiza haja ya kuharakisha hatua za kurejesha uoto wa mikoko, nyasi za baharini na miamba ya marijani, pamoja na kuboresha uwezo wa jamii za pwani kupata fedha za miradi kupitia biashara ya kaboni ili kukabiliana na ongezeko la tindikali baharini.
Makamu wa Rais pia amehimiza udhibiti wa uchafuzi wa mazingira kuanzia nchi kavu hadi baharini kwa kutumia uchumi duara kwenye taka za plastiki na kemikali, huku akizitaka nchi wanachama kulinda bioanuwai ili kufikia lengo la kimataifa la kuhifadhi asilimia 30 ya maeneo ya bahari na pwani ifikapo mwaka 2030.
Ili kufanya maamuzi sahihi, Ndejembi ameeleza umuhimu wa kuwekeza kwenye sayansi, matumizi ya Akili Mnemba (AI), na takwimu za pamoja, sambamba na kuvutia uwekezaji wa sekta binafsi katika uchumi wa bluu unaojali hifadhi ya mazingira.
Akimalizia hotuba yake, amesisitiza umuhimu wa kuwashirikisha wanawake, vijana na sekta binafsi katika safu ya mbele ya maamuzi ya uchumi wa buluu, huku akipongeza kuingizwa kwa Jukwaa la Biashara na Jukwaa la Vijana kwa mara ya kwanza katika COP12 na kutaka utaratibu huo uwe endelevu. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Familia ya marehemu Jane Urassa imewaomba waombolezaji kuendelea kuwaombea watoto wa marehemu ambao wamempoteza mama yao, huku ikisisitiza kuwa katika kipindi cha maisha yake marehemu aligusa maisha ya wengi.
Akizungumza kwa niaba ya familia wakati wa zoezi la kuaga mwili wa marehemu katika Kanisa la KKKT Mbezi Beach jijini Dar es Salaam, leo Oktoba 8, 2026.
Oswald amewashukuru watumishi wa Mungu pamoja na makanisa mbalimbali yaliyokuwa sehemu ya maisha ya marehemu, huku akiomba waombolezaji kuendelea kuiombea familia wakati ikiendelea na safari kuelekea Moshi, ambako mazishi yanatarajiwa kufanyika kesho, Oktoba 9, 2026.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwili wa marehemu Jane Urassa umeondolewa katika Kanisa la KKKT Mbezi Beach jijini Dar es Salaam na kuanza safari kuelekea mkoani Kilimanjaro, ambako mazishi yake yanatarajiwa kufanyika kesho, Oktoba 9, 2026.
Mwili huo umeondolewa baada ya kufanyika kwa zoezi la kuaga, lililowakutanisha ndugu, jamaa, marafiki na waombolezaji kwa ajili ya kutoa heshima zao za mwisho.
Kwa mujibu wa ratiba ya mazishi, mwili wa Jane Urassa unasafirishwa kuelekea Machame kwa ajili ya mazishi, huku familia ikiwaomba waombolezaji kuendelea kuwaombea watoto wa marehemu waliompoteza mama yao.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwili wa marehemu Jane Urassa umeondolewa katika Kanisa la KKKT Mbezi Beach jijini Dar es Salaam na kuanza safari kuelekea mkoani Kilimanjaro, ambako mazishi yake yanatarajiwa kufanyika kesho, Oktoba 9, 2026.
Mwili huo umeondolewa baada ya kufanyika kwa zoezi la kuaga, lililowakutanisha ndugu, jamaa, marafiki na waombolezaji kwa ajili ya kutoa heshima zao za mwisho.
Kwa mujibu wa ratiba ya mazishi, mwili wa Jane Urassa unasafirishwa kuelekea Machame kwa ajili ya mazishi, huku familia ikiwaomba waombolezaji kuendelea kuwaombea watoto wa marehemu waliompoteza mama yao.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Familia ya marehemu Jane Urassa ikiuaga mwili wa mpendwa wao, katika Kanisa la KKKT Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.
Baada ya familia, ndugu, jamaa na marafiki kutoa heshima zao za mwisho, mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa kuelekea Machame, mkoani Kilimanjaro, kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika kesho, Oktoba 9, 2026.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM, Idara ya Uchumi na Fedha, Ndugu Jamal Kassim Ali, amewataka viongozi wa chama hicho Mkoa wa Dar es Salaam kufanya mapitio ya kina ya mali na mikataba yote ya uwekezaji, akionya kuwa utaratibu uliopo umejenga mtazamo kuwa mali za CCM ni "shamba la bibi."
Ndugu Jamal Kassim ameyasema hayo leo, Oktoba 8, 2026, alipokuwa akizungumza kwenye kikao kazi na Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam kilichofanyika katika Ofisi Ndogo za CCM, Lumumba, jijini Dar es Salaam.
Akifafanua kuhusu hali ya mali za chama hicho, alieleza kuwa CCM inamiliki rasilimali na maeneo mengi ya kimkakati jijini humo ikiwemo eneo kubwa lililopo katikati ya mji eneo la Sinza lakini bado kuna changamoto kubwa ya usimamizi na matumizi bora ya rasilimali hizo ili kuleta tija inayostahili.
Akiweka msisitizo wa hatua za kuchukuliwa, Katibu huyo wa NEC ameagiza kila Kamati ya Siasa ya Wilaya kuainisha na kujumuisha maeneo yote ya kimkakati kwenye kanzi data (profile) zao ili kuwa na kumbukumbu sahihi na usimamizi madhubuti.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katibu Tawala Mkoa wa Manyara, Mariam Muhaji, amewataka wataalamu wa afya kutoka mikoa ya Manyara, Dodoma na Singida kuendelea kuimarisha huduma za afya ya mama na mtoto, hatua inayolenga kupunguza zaidi vifo vitokanavyo na uzazi pamoja na vifo vya watoto wachanga.
Mariam ameyasema hayo wakati akifungua kikao kazi cha wataalamu wa afya kutoka mikoa hiyo mitatu, kilicholenga kutathmini utekelezaji wa huduma za afya ya uzazi, mama na mtoto, pamoja na kuweka mikakati madhubuti ya kupunguza vifo hivyo.
Takwimu za kipindi cha mwaka 2024 hadi 2025 zinaonesha kuwa vifo vitokanavyo na uzazi katika mikoa hiyo vimepungua kutoka vifo 182 hadi 161, sawa na kupungua kwa vifo 21.
Aidha, vifo vya watoto wachanga vimepungua kutoka 1,872 hadi 1,503 katika kipindi hicho, ikiwa ni upungufu wa vifo 369. Wataalamu wa afya wametakiwa kuendeleza juhudi za kuboresha huduma na kuhakikisha mafanikio hayo yanaongezeka zaidi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Kundo Mathew, amegoma kuweka jiwe la msingi katika Mradi wa Maji Kinyamburi, Wilaya ya Hanang’ mkoani Manyara, baada ya kutoridhishwa na ubora wa utekelezaji wa mradi huo.
Mhandisi Kundo amechukua hatua hiyo Oktoba 7, 2026, wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Manyara, akisema Serikali haiwezi kuruhusu mradi unaotekelezwa kwa fedha za wananchi kukabidhiwa au kuzinduliwa wakati haujakidhi viwango vinavyotakiwa.
Kutokana na hali hiyo, Naibu Waziri amemuelekeza mkandarasi kurejea eneo la mradi na kufanya maboresho, ikiwemo kujenga upya sehemu ambazo hazijatekelezwa kwa kiwango kinachokubalika, ili kuhakikisha mradi huo unakuwa na ubora unaostahili.
Amesema dhamira ya Serikali ni kuhakikisha wananchi wa Kinyamburi wanapata huduma ya maji safi na salama kupitia miundombinu bora, imara na inayoweza kudumu kwa muda mrefu.
Mhandisi Kundo amesisitiza kuwa Wizara ya Maji itaendelea kusimamia kwa karibu miradi inayotekelezwa nchini na haitasita kuchukua hatua pale ambapo kazi hazifanywi kwa mujibu wa viwango na mikataba, akisisitiza kuwa fedha za Serikali lazima zitoe thamani halisi kwa wananchi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI:
Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, imeahirisha kutolewa kwa uamuzi wa maombi ya zuio katika kesi inayowahusisha Said Issa Mohamed na Ahmed Rashid Khamis dhidi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Mahakama imesema uamuzi huo umesogezwa mbele hadi tarehe 22 Oktoba 2026, saa 8 mchana, kutokana na Jaji aliyetarajiwa kutoa uamuzi huo kuwa na majukumu mengine nje ya kituo cha kazi.
Kesi hiyo ya Maombi Madogo Namba 14864 ya 2026, inatokana na mgogoro wa ndani ya CHADEMA ulioanza mwaka 2025, ambapo Said Issa Mohamed, aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Zanzibar, pamoja na Ahmed Rashid Khamis na marehemu Maulidah Anna Komu, walifungua kesi dhidi ya viongozi wa Chama hicho wakiwadai ubaguzi wa usambazaji wa rasilimali za chama kati ya Tanzania Bara na Zanzibar.
Mwezi Aprili 2026, Mahakama ya Rufaa ilifuta uamuzi wa Mahakama Kuu uliokuwa umekataza shughuli za siasa za CHADEMA kwa siku 309, na kurudisha haki ya Chama hicho kuendelea na shughuli zake za kisiasa.
Mei 28, 2026, Mahakama Kuu iliitupa kesi hiyo kuu (Namba 8323 ya 2025) kutokana na kasoro za kisheria katika maandishi ya malalamiko, hasa kutotaja tarehe husika za madai.
Kufuatia hatua hiyo, Juni 6, 2026, CHADEMA ilimuondoa Said Issa Mohamed kutoka Chama hicho, ikidai alikiuka katiba na kanuni za chama kwa kuchukua hatua ya kisheria dhidi ya viongozi wake. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Kaimu Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Faustine Mafwele, ametoa taarifa leo katika ukumbi wa Central Police akieleza kuwa hali ya usalama jijini ni shwari kabisa na kila mwananchi anaendelea na shughuli zake bila kuingiliwa.
Akizungumzia mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara utakaofanyika Jumamosi tarehe 10 Oktoba 2026 majira ya jioni katika Uwanja wa Uhuru, Temeke, ambao utakutanisha timu za Simba na Yanga, Kamanda huyo amesema ulinzi na usalama umeimarishwa kwa kushirikiana na wadau wote.
Aidha amewakumbusha mashabiki, wapenzi na wadau wote wa soka kujiepusha na vitendo vyote vinavyokwenda kinyume na sheria, kanuni za ligi na taratibu za mikusanyiko. Polisi imewataka timu zote mbili mchezo mzuri.
Katika taarifa nyingine, polisi imethibitisha kupatikana kwa binti mmoja aitwaye Enjo Abayo, mwenye umri wa miaka 19, ambaye alidaiwa kutoweka na mtoto mdogo wa miezi 10 eneo la Kibada, Kigamboni.
Katika uchunguzi, binti huyo alieleza kuwa aliondoka na mtoto huyo kwenda kumsalimia dada yake aliyepata ajali Kibaha baada ya waajiri wake kukataa kumruhusu. Polisi imewashukuru wananchi na wadau wa uchunguzi kwa kushirikiana ili tukio hilo litafutuliwe kwa muda mfupi.
Aidha, SACP Mafwele amewahimiza wananchi kushiriki katika kampeni mpya iitwayo “Ongea na Kamanda” inayolenga kuwawezesha wananchi kuzungumza na makamanda katika ngazi mbalimbali ili kutoa changamoto za kiusalama na kupata suluhisho pale inapohitajika.
“ukisikia Kamanda yuko eneo fulani, nenda pale uweze kupata taarifa na kutoa changamoto ili tusaidiane kutatua matatizo ya kiuhalifu,” amesema Kamanda huyo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI PICHA:
Baada ya kuzinduliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Bodi ya Utalii Tanzania, Destination Tanzania App inaendelea kuwasaidia wasafiri kupanga safari kwa urahisi zaidi.
Kupitia programu hii, mtalii anaweza kuona vivutio mbalimbali nchini, kuchagua vifurushi vya utalii na kupata watoa huduma wanaoaminika. Kupitia mfumo huu unaweza kutafuta hoteli na malazi, pamoja na huduma za kukodi magari. Kila kitu kinapatikana sehemu moja.
Je, Unapanga kuvunja kikoba kwa kutembelea vivutio vya Tanzania? Destination Tanzania App ni mshirika wako kukusaidia kupanga safari yako. Itakusaidia kuchagua unapotaka kwenda na huduma unazohitaji.
Teknolojia sasa inarahisisha zaidi kupanga na kufurahia safari. Je, tayari umeanza kutumia Destination Tanzania App? Usibaki nyuma. Pakua programu hiyo leo kupitia App Store au Google Play, au tembelea www.destinationtanzania.tz.
Anza kupanga safari yako.
Tanzania nzima sasa ipo kiganjani mwako.
@tanzania_unforgattable
@dktabbasi
@dr_thereza.mugobi
@ashatukijaji
@jamesmhilu
@paulinamkama -
Jambo TV
@Jambotv_
Mradi wa Sinovest Industry ni kiwanda cha nguo kilichopo katika eneo la Bagamoyo Special Economic Zone (BSEZ) linalosimamiwa na Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi (TISEZA)
Kiwanda hicho kwa sasa kinazalisha bidhaa mbalimbali za nguo ikiwemo jezi, T-shirt na boxers, huku mwekezaji akiwa amepangiwa eneo lenye ukubwa wa mita za mraba 210,080.
Mwekezaji anatarajia kuwekeza mtaji wa Dola za Marekani milioni 50 katika mradi huo, huku akilenga kuzalisha ajira 10,000 ambapo mpaka sasa, tayari amewekeza Shilingi bilioni 26 na ameanza kutoa ajira kwa awamu, huku awamu ya kwanza ilihusisha kuajiri mabinti 139 kwa ajili ya mafunzo ya 'Training of Trainers' ambao tayari wamehitimu na mchakato wa kuwapatia mikataba ya ajira umeanza.
Aidha, Sinovest Industry imepokea awamu ya pili ya wanafunzi 50 walioanza mafunzo mwezi Septemba 2026 na mwekezaji huyo pia amekamilisha ujenzi wa mabanda mawili ya viwanda (Two Industrial Sheds) yenye zaidi ya mashine 1,000 za kushonea, huku akiendelea na zoezi la kufunga mashine hizo kwa ajili ya kuongeza uzalishaji, kutoa mafunzo na kuajiri vijana zaidi wa Kitanzania.
Kwa upande wa masoko, Sinovest Industry inalenga kuuza bidhaa zake katika masoko ya Ghuba ya Uajemi, hususan Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Qatar, Oman na Saudi Arabia. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mahakama ya Rufani Tanzania imetupilia mbali rufaa iliyowasilishwa na Zitto Zuberi Kabwe dhidi ya uamuzi wa Mahakama Kuu kuhusu kuondolewa kwa aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Prof. Mussa Juma Assad, kutoka kwenye nafasi hiyo mwaka 2019.
Katika uamuzi wake uliotolewa Oktoba 6, 2026, Mahakama hiyo imekubaliana na Mahakama Kuu kwamba Kifungu cha 6(1) cha Sheria ya Ukaguzi wa Umma ya mwaka 2008, kilichoweka muda wa miaka mitano wa CAG kuhudumu na uwezekano wa kuongezwa mara moja, kinakinzana na Katiba kwa sababu kinaweka ukomo wa muda badala ya kuzingatia umri wa kustaafu uliowekwa kikatiba.
Mahakama pia imethibitisha kuwa kuondolewa kwa Prof. Assad katika nafasi hiyo hakukuwa kwa mujibu wa Katiba, kwa kuwa kulifanyika kwa kutegemea Kifungu hicho kilichobainika kuwa kinyume cha Katiba.
Mahakama imesema suala hilo halingeokolewa na kile kinachojulikana kisheria kama doctrine of operative fact, kwa kuwa kuondolewa kwake kulikuwa ni kuingilia moja kwa moja ulinzi wa kikatiba wa muda wa kuhudumu kwa CAG.
Hata hivyo, Mahakama ya Rufani imeamua kwamba uteuzi wa Charles Kichere kuwa CAG ulikuwa halali, kwa sababu uteuzi huo ulifanyika chini ya Kifungu cha 4 cha Sheria ya Ukaguzi wa Umma ambacho hakijawahi kutangazwa kuwa kinyume cha Katiba. Mahakama imesema kuonekana kwa dosari katika kuondolewa kwa Prof. Assad hakumaanishi moja kwa moja kuwa uteuzi wa Kichere nao ulikuwa batili.
Mahakama imekataa pia ombi la kurejeshwa Prof. Assad katika nafasi hiyo, ikisema kufanya hivyo kungeweza kusababisha kuwepo kwa watu wawili wanaodai kuwa CAG kwa wakati mmoja na hivyo kuleta hali isiyo ya kawaida kikatiba pamoja na kuathiri mwendelezo wa usimamizi wa fedha za umma.
Mahakama pia imekataa madai mengine kuhusu kauli iliyodaiwa kutolewa wakati wa kuapishwa kwa CAG, ikisema ushahidi uliowasilishwa, ukiwemo vipande vya magazeti, haukutosha kuthibitisha ukiukwaji wa Katiba.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwenyekiti wa Kitengo cha Wanawake Taifa kutoka CHAUMMA (KIWACHA) Verena Ghati, amesema anakubaliana na kauli ya Waziri wa Nchi, Prof. Palamagamba J.A. Kabudi, kwamba vyama vyote vya siasa vina hadhi sawa, lakini amesema usawa huo bado una changamoto kwenye suala la kifedha.
Ghati ameyasema hayo Oktoba 7, 2026 baada ya kushiriki Uzinduzi wa Uongozi mpya na Nembo ya Baraza la Vyama vya Siasa jijini Dar es Salaam.
Amesema vyama visivyo na wabunge havipati ruzuku, hali inayovifanya kushindwa kuendesha shughuli zao ipasavyo hivyo akipendekeza uwekwe utaratibu wa kuviwezesha kupata angalau shilingi milioni 20 kila mwezi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Serikali kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara imechukua hatua za kukabili changamoto ya upatikanaji wa miche ya kahawa katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga, baada ya kukabidhi tani moja ya mbegu bora za zao hilo kwa Vyama vya Msingi vya Ushirika (AMCOS) 20.
Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano hayo iliyofanyika Oktoba 7, 2026, Waziri wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga, amesema mbegu hizo zilizotolewa na Halmashauri zinalenga kuzalisha miche milioni 3.5 ili kuongeza uzalishaji na kukuza kipato cha mwananchi pamoja na Halmashauri.
Kilio cha muda mrefu cha wakulima wa Mbinga kimekuwa ni uhaba wa miche bora, licha ya kuwa kilimo cha kahawa ndicho uti wa mgongo wa uchumi wa wananchi mmoja mmoja na Halmashauri kwa ujumla.
Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Ruvuma, Oddo Mwisho, amebainisha kuwa zao hilo limekuwa nguzo kuu ya uchumi kwa vijana wa Mbinga.Pia Ametumia fursa hiyo kuwasihi vijana kubaki vijijini na kujikita kwenye kilimo badala ya kukimbilia mijini kufanya kazi za upigaji debe.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga, Desiderius Haule, ameagiza viongozi wote wa AMCOS waliopokea mbegu hizo kuhakikisha wanasimamia kwa umakini uzalishaji wa miche hiyo katika maeneo yao ili kutatua changamoto hiyo.
Wakizungumza mara baada ya kupokea msaada huo, viongozi wa AMCOS wamepongeza hatua iliyochukuliwa na Serikali na Halmashauri, wakieleza kuwa usambazaji wa mbegu hizo unakwenda kumaliza kero ya muda mrefu ya uhaba wa miche na kuchochea kasi ya maendeleo wilayani humo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Serikali imetakiwa kuanzisha mtaala wa muziki katika shule za msingi nchini ili kuwajengea watoto uwezo na kukuza vipaji vyao vya muziki tangu wakiwa wadogo.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Topshop Limited, Amin Mohamed Janmohamed, wakati wa uzinduzi wa keyboard mpya tatu za Yamaha nchini Tanzania, uliofanyika katika Hoteli ya Chelsea, Kariakoo, Dar es Salaam.
Janmohamed amesema elimu ya muziki inapaswa kupewa nafasi katika mfumo wa elimu ili watoto wapate fursa ya kutambua na kuendeleza vipaji vyao tangu wakiwa katika hatua za awali za elimu.
Uzinduzi huo umefanywa na Yamaha Music House kwa kushirikiana na Topshop Limited, huku keyboard zilizozinduliwa zikiwa ni PSR-SX620, PSR-E583 na PSR-E483.
Vifaa hivyo vimeelezwa kuwa na sauti na midundo inayozingatia muziki wa Afrika, ikiwemo Afrobeat na seben, na kulenga matumizi katika muziki, makanisa, shule pamoja na matukio mbalimbali.
Uzinduzi huo uliwakutanisha wadau wa muziki, wasanii na waandishi wa habari, waliopata fursa ya kuzijaribu keyboard hizo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Kamati ya Siasa ya Halmashuri Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Tabora, imempendekeza na kumteua Moses Emmanuel kuwa Mgombea Udiwani wa Kata ya Igalula wilaya ya Uyui Mkoa wa Tabora kwenye Uchaguzi Mdogo unaotarajiwa kufanyika Novemba 4, 2026.
Kupitia Katibu wa Siasa, Uenezi na Mafunzo wa Chama hicho mkoani humo Idd Moshi, akizungumza na waandishi wa habari amesema uchaguzi huo na uteuzi umefanyika kwa mujibu wa Chama hicho baada ya aliyekuwa Diwani wa Kata ya Igalula Mwishari Khalfan kufariki.
Aidha Idd, amebainisha kuwa kwa mujibu wa INEC zoezi la kuchukua fomu limeanza leo Oktoba 7, mpaka Oktoba 13, ambapo fomu hizo zitarejeshwa kisha kuanza kwa zoezi la kampeni na kwamba Chama hicho kimejipanga vyema kutetea nafasi hiyo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar Es Salaam (DAWASA) inashiriki Mkutano wa 12 wa Nchi wanachama wa Mkataba wa Nairobi (COP 12) kuhusu usimamizi wa Mazingira ya Pwani ya Bahari ya Hindi, unaofanyika Jijini Dar Es Salaam ukijumuisha zaidi ya wajumbe 500 kutoka nchi mbalimbali wanachama.
Mkutano huo ambao umeanza Oktoba 6, 2026 unakutanisha nchi wanachama wa Mkataba wa Nairobi ulio chini ya Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) huku ukilenga kujadili na kuweka mikakati ya pamoja ya ulinzi, usimamizi na uendelezaji wa mazingira ya bahari na ukanda wa Pwani katika kanda ya bahari ya Hindi ya Magharibi (WIO)
Miongozi mwa viongozi waliopita katika banda hilo ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Maendeleo ya Vijana, Joel Nanauka ambaye amepongeza ushiriki wa DAWASA katika mkutano huo muhimu na kusisitiza elimu ya mabadiliko ya tabianchi na athari zake kwenye sekta ya maji ipewe kipaumbele kwa jamii.
DAWASA ikiwa moja ya taasisi zilizopo chini ya Wizara ya Maji inaonesha shughuli zake sambamba na lengo la mkutano huku ikionesha utekelezaji wa miradi ya usafi wa mazingira ya kimkakati wa Mbezi Beach na Buguruni pamoja na mradi wa Bwawa la Kidunda unaolenga kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Wachimbaji wadogo wa madini wilayani Nachingwea mkoani Lindi wameiomba Serikali kuingilia kati changamoto wanazodai kukumbana nazo katika eneo lao la uchimbaji, wakisisitiza umuhimu wa kupatikana kwa mwekezaji atakayekuwa tayari kushirikiana nao kwa kuzingatia maslahi ya pande zote.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Mohamed Moyo, mmoja wa wachimbaji hao Mzee Ibrahim Ndolo amesema hawako tayari kuendelea kufanya kazi na mwekezaji wa sasa kutokana na kile alichodai kuwa ni kutokuwepo kwa mazingira rafiki ya kufanya shughuli zao za uchimbaji.
Amesema hali hiyo imewaathiri wachimbaji wadogo ambao kwa sasa wanakabiliwa na changamoto za kiuchumi huku baadhi yao wakishindwa kupata kipato cha uhakika kutokana na kusuasua kwa shughuli za uchimbaji.
Ameiomba Serikali, kupitia mamlaka husika, kusimamia suala hilo na kuhakikisha wachimbaji wadogo wanapata mwekezaji mwenye uwezo wa kuendesha shughuli kwa ufanisi, huku mikataba na makubaliano yote yakizingatia sheria na maslahi ya wachimbaji.
“Tunataka tupate mwekezaji mkubwa. Tunaomba Serikali isimamie jambo hili, itusimamie sisi wachimbaji wadogo. Tupate mwekezaji ambaye tutaweza kufanya naye kazi kwa makubaliano mazuri,” amesema.
Aidha, amesisitiza kuwa mchakato wa kumpata mwekezaji unapaswa kufanyika kwa uwazi na kwa kushirikisha Serikali pamoja na wataalamu wa sheria ili kuhakikisha mikataba inayosainiwa inalinda maslahi ya wachimbaji na wananchi wanaohusika.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mahakama ya Hakimu Mkazi Shinyanga imeahirisha kesi ya ugaidi inayomkabili Katibu wa CHADEMA Kanda ya Serengeti, Jackson Mnyawami, pamoja na wenzake 16 hadi tarehe 20 Oktoba 2026, kutokana na Upande wa Mashtaka kueleza kuwa upelelezi bado haujakamilika.
Kesi hiyo imeahirishwa baada ya Mahakama kutoa muda wa siku 14 zilizoombwa na Upande wa Mashtaka ili kukamilisha upelelezi huo au kuchukua hatua nyingine za kisheria iwapo watashindwa kukamilisha kabla ya tarehe hiyo.
Akizungumza mara baada ya kuahirishwa kwa shauri hilo leo Jumatano, Wakili wa Upande wa Utetezi, Alex Dotto Massaba, amebainisha kuwa mawakili wako tayari kupigania haki zao pindi upelelezi utakapokamilika pindi upelelezi utakapokamilika na shauri hilo kuhamishiwa Mahakama Kuu, jopo kubwa la mawakili litajitokeza kuwatetea wanachama hao.
“Lakini mnafahamu mmesikia mahakama imetoa siku 14 walizoomba ili waweze kukamilisha upelelezi... Na kama hawakamilishi kwa namna wanavyoongea ni kana kwamba wanataka kuiondoa hii kesi... Tuko imara, tumekunywa maji mengi hatutachoka”, ameeleza.
Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Bara, Amani Golugwa amekosoa kuendelea kuwekwa mahabusu kwa Mnyawami na wenzake kwa zaidi ya siku 100 bila upelelezi kukamilika, akibainisha kuwa hatua hiyo inaenda kinyume cha misingi ya Haki Jinai inayotaka upelelezi ukamilike kabla mtuhumiwa hajafikishwa mahakamani.
Golugwa amesisitiza kuwa chama hicho kitaendelea kuwasimamia na kuziunga mkono familia za mahabusu hao, huku akitoa wito kwa wanachama na wananchi kuendelea kuwa karibu na kutoa faraja kwa familia hizo katika kipindi hiki kigumu.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis S.K. Mutungi, amesema vyama 18 vya siasa vimeshiriki katika shughuli ya uzinduzi wa uongozi mpya na nembo ya Baraza la Vyama vya Siasa, huku akieleza kuwa kuna chama kimoja ambacho bado kinajitafuta ili kushiriki katika shughuli za Baraza.
Jaji Mutungi amesema ushiriki wa vyama hivyo unaonesha umuhimu wa Baraza kama jukwaa la kukutanisha vyama vyenye itikadi na mitazamo tofauti, kwa ajili ya kusikilizana, kujadiliana na kutafuta suluhu katika masuala yenye maslahi mapana ya taifa.
Amesema pamoja na ushindani unaojitokeza wakati wa uchaguzi wa viongozi wa Baraza, baada ya uchaguzi kukamilika wajumbe wanapaswa kurejea katika ari ya ushirikiano na mshikamano, huku maslahi ya taifa yakiwekwa mbele ya tofauti za kisiasa na kiitikadi.
“Vyama vina itikadi zao tofauti, lakini tunapokuja kwenye masuala ya kitaifa tunaweza kukaa pamoja, tukazungumza hata pale tunapopishana, lakini tukatafuta mwafaka wa kuibuka na hoja ambazo ni za kitaifa zaidi,” amesema Jaji Mutungi. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Wachimbaji wadogo wa madini ya nickel katika Kijiji cha Nditi wilayani Nachingwea mkoani Lindi kupitia Umoja wa Vikundi vya Wachimbaji wa Madini, wameiomba Serikali kuingilia kati changamoto ya utendaji wa wawezeshaji wanaofanya shughuli za uchimbaji katika maeneo yao ya leseni.
Mwenyekiti wa UVIWAMA, Abdallah Matayo Nkane amesema baada ya chama hicho kupewa leseni Julai mwaka jana, walipata wawezeshaji wanne katika maeneo manne ya leseni, lakini utendaji wao umekuwa wa kusuasua tangu Oktoba mwaka huo, hali iliyosababisha wanachama kutonufaika na shughuli za uchimbaji na mapato ya Serikali kutopatikana kwa kiwango kinachotarajiwa.
Nkane amesema awali chama hicho kilikuwa na mwekezaji mwingine, lakini baada ya Serikali kuelekeza watafute mwekezaji wa ndani, walipata wawezeshaji hao ambao, kwa mujibu wa chama, hawajawa na uwezo wa kutosha kifedha na kiteknolojia.
Mchimbaji mdogo wa nickel na mwanachama wa UVIWAMA, Said Mkindiga, amesema wawezeshaji waliopo wanakabiliwa na ukosefu wa mitaji, fedha na vifaa, hali inayosababisha uchimbaji kufanyika kwa kasi ndogo na kwa mbinu zisizokuwa na tija.
Naye mkazi wa Nditi, Atia Ali Chitumbi, amesema hali hiyo imeathiri uchumi wa wananchi ambao kwa kiasi kikubwa wanategemea mgodi huo kupata kipato cha kuendesha familia, kusomesha watoto na kukidhi mahitaji ya kila siku.
Kwa upande wake, Ismael Ndoro, mwanachama na mjumbe wa Bodi ya UVIWAMA, amesema wanachama wamekuwa wakikabiliwa na ukosefu wa kipato kutokana na uzalishaji mdogo.
Akijibu malalamiko hayo, Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Mohamed Moyo amesema tatizo kubwa ni kukosekana kwa mkataba kati ya wanakikundi na wawezeshaji ili kuweka makubaliano ya kazi.
Aidha, Moyo amewatupia lawama viongozi wa kikundi hicho kwa kutokuwa wakweli kwa wanachama wao hali iliyosababisha kuwa na mgogoro usiokwisha na wawezeshaji wao.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Kuelekea Tamasha la Muziki wa Injili linalojulikana kama 'SIFA Gospel' ambalo linatarajiwa kufanyika mkoani Arusha, imehimizwa kwamba haiwezekani kuchanganya injili ya Mungu na masuala ya kidunia.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya SIFA Gospel, Suma Mwaitenda, amesema hayo leo Oktoba 7, 2026 alipokuwa akizungumzia maandalizi ya tamasha hilo ambalo ni mwendelezo wa matamasha yanayofanyika katika mikoa mbalimbali nchini, huku Arusha ikiwa ni Mkoa wa nne baada ya Mbeya, Geita na Mwanza.
Amesema tamasha hilo litafanyika Jumamosi, Oktoba 10, kuanzia saa sita mchana hadi saa nne usiku katika viwanja vya Sinoni, Arusha, likiwa na lengo la kutoa jukwaa kubwa kwa muziki wa Injili na kufikisha ujumbe wa matumaini na ukombozi kwa jamii, hususan vijana.
Aidha, Mwaitenda amesema SIFA Gospel halihusiani na masuala ya kisiasa, akisisitiza kuwa waandaaji wanalenga muziki wa Injili na ujumbe wa kiroho pekee.
Tamasha hilo litawakutanisha wasanii mbalimbali wa muziki wa Injili, akiwemo Christina Shusho, Paul Clement, Eliya Mwantondo, Boaz Danken, Henrick Mruma na Agape Gospel Band, pamoja na wasanii wengine wa Injili kutoka mkoani Arusha.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu, Prof. Palamagamba Kabudi, amesema Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa akitoa nafasi sawa ya kuvisikiliza vyama vyote vya siasa nchini.
Prof. Kabudi amesema hayo leo Oktoba 7, 2026 katika Uzinduzi wa Uongozi Mpya na Nembo ya Baraza la Vyama vya Siasa uliofanyika hoteli ya Hyatt-Regency jijini Dar es Salaam.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu, Prof. Palamagamba Kabudi, amewataka viongozi na wanachama wa vyama vya siasa kuheshimiana katika kueleza tofauti zao za kisiasa, akisema matumizi ya lugha kama kumuita kiongozi mwenzake ambaye amechaguliwa “haramu” sio sahihi.
Prof. Kabudi amesema hayo leo Oktoba 7, 2026 katika Uzinduzi wa Uongozi Mpya na Nembo ya Baraza la Vyama vya Siasa uliofanyika hoteli ya Hyatt-Regency jijini Dar es Salaam ambapo yeye alikuwa mgeni rasmi
“Huwezi kumwita mwenzako kiongozi haramu, unaweza kusema hayupo hapo kihalali. Neno haramu katika Kiswahili lina maana ya ukakasi mkubwa sana,” amesema Prof. Kabudi.
Aidha, Prof. Kabudi amesisitiza umuhimu wa Baraza la Vyama vya Siasa kushirikisha wanawake na wadau wengine katika shughuli zake, akieleza kuwa heshima na ushirikiano ni sehemu muhimu ya kujenga mazingira mazuri ya kisiasa nchini.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga limepokea silaha aina ya gobore sitini na nane (68) kutoka kwa wananchi ambao wameitikia wito wa kusalimisha silaha hizo haramu katika kipindi cha msamaha, kabla ya zoezi hilo kuhitimishwa Oktoba 31, 2026.
Akizungumza na vyombo vya habari leo Jumatano Oktoba 7, 2026, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Almachius Mchunguzi, amesema wananchi wameonesha mwitikio mkubwa kutokana na elimu inayotolewa na Jeshi la Polisi kuhusu umuhimu wa kusalimisha silaha hizo.
Amesema wananchi wamekuwa wakizifikisha wenyewe katika vituo vya Polisi kwa ajili ya kuzisalimisha, hatua ambayo inawapa fursa ya kutekeleza wito huo ndani ya kipindi cha msamaha na kuepuka kuchukuliwa hatua za kisheria baada ya muda huo kumalizika.
Aidha, Kamanda Mchunguzi amewataka wananchi wa Mkoa wa Tanga kuepuka kujihusisha na utengenezaji wa silaha aina ya gobore, akisisitiza kuwa utengenezaji na umiliki wa silaha hizo ni kinyume cha sheria.
Amewataka pia wananchi wenye taarifa kuhusu watu wanaojihusisha na utengenezaji wa silaha hizo kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi ili hatua stahiki za kisheria ziweze kuchukuliwa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Wakili Boniface Anyisile Kajunjumele Mwabukusi, amependekeza kuanzishwa kwa kamati maalum chini ya sheria ya vyama vya siasa, itakayoshughulikia makosa na migogoro inayotokana na masuala ya kisiasa.
Mwabukusi amesema masuala ya kisiasa yana mazingira na lugha yake, hivyo yanapaswa kushughulikiwa kwa kuzingatia muktadha huo kabla ya kupelekwa katika mifumo mingine.
Amesema baadhi ya changamoto zinazojitokeza katika siasa zinaweza kuwa na muktadha tofauti na makosa ya kawaida, hivyo kuwepo kwa utaratibu maalum wa kuyachakata ndani ya mfumo wa kisiasa kunaweza kusaidia kupata suluhu zinazozingatia mazingira ya siasa na kupunguza migogoro.
Aidha, amesisitiza umuhimu wa vyama vya siasa kuvumiliana licha ya tofauti zao, akieleza kuwa siasa zinahitaji nafasi kwa watu wenye mitazamo tofauti kuishi, kujadiliana na kutafuta suluhu kwa njia ya mazungumzo.
Mwabukusi ameyasema hayo leo, Oktoba 7, 2026, katika uzinduzi wa Uongozi Mpya na Nembo ya Baraza la Vyama vya Siasa, unaofanyika jijini Dar es Salaam.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Kampuni ya Farvia Glo Industries inatarajiwa kuwekeza takriban Shilingi bilioni 15 za Kitanzania katika ujenzi wa kiwanda cha vinywaji baridi katika Eneo Maalum la Kiuchumi la Bagamoyo (BSEZ), mradi unaotarajiwa kutoa ajira takriban 300 na kuanza uzalishaji kabla ya mwisho wa mwaka huu.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi na mmoja wa wamiliki wa kiwanda hicho, William Stephen Kotta, wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, alipotembelea na kukagua utekelezaji na maendeleo ya miradi ya kipaumbele wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.
Akifafanua kuhusu hatua za ujenzi na mpango wa uzalishaji wa kiwanda hicho, Stephen alibainisha kuwa ujenzi wa ukuta ulishaanza na kwamba ndani ya siku 90 tangu tarehe 1 Oktoba, 2026 majengo ya kiwanda yaliyotengenezwa tayari viwandani yatakuwa yamekamilika na kupachikwa tayari kwa uzalishaji wa chupa ya kwanza ya maji.
“Tunatarajia kuajiri wafanyakazi wa kudumu na wa muda watakaofikia karibuni 300... Mtaji tunaotegemea kuwekeza hapa kwa sababu tunaenda hatua kwa hatua kwa ajili ya upanuzi, tutakapofika kamili tutatarajia kuwekeza karibu bilioni 15 za Kitanzania”, ameeleza.
Katika hatua nyingine, Mkurugenzi huyo ameipongeza Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) @InvestTanzania kwa ushirikiano mkubwa na mwongozo wa karibu wanaotoa kwa wawekezaji tangu hatua za awali za mradi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa, Mohamed Ally Ahmed, amesema uwepo wa viongozi wa vyama mbalimbali na wadau wa demokrasia katika uzinduzi wa Baraza la Vyama vya Siasa unaonyesha kuwa Watanzania wanaweza kukaa pamoja na kujadiliana licha ya tofauti za mitazamo ya kisiasa na kuwa hilo linaendana na dhana ya maridhiano na mazungumzo inayosisitizwa nchini.
Amesema hayo leo Oktoba 7, 2026 katika uzinduzi wa Uongozi Mpya na Nembo ya Baraza la Vyama vya Siasa unaofanyika jijini Dar es Salaam huku akisisitiza kuwa wadau wa vyama vya siasa pamoja na demokrasia wamezidi kuimarisha uhusiano wao wakibaki katika mstari wa mazungumzo.
"Mheshimiwa mgeni rasmi umeuona ukumbi ulivyojaa, Mheshimiwa Msajili ametueleza hapa kwamba vyama vyote 18 vipo pamoja na wadau wa demokrasia...salamu zetu zimfikie Mheshimiwa Rais kwamba wadau wa siasa na demokrasia nchi hii wanaunga mkono na kukubali dhana yako ya maridhiano na mazungumzo," amesema MohammedThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), Dorothy Semu, amesema taasisi hiyo itaendelea kuunga mkono majukwaa yanayowezesha mazungumzo, uvumilivu, ushirikishwaji, kuheshimu tofauti za kisiasa na utatuzi wa migogoro kwa njia za amani na kisheria.
Amesema TCD inaamini demokrasia imara inahitaji mifumo ya kudumu ya mazungumzo kati ya wadau wa kisiasa na kijamii, badala ya mazungumzo kufanyika wakati wa migogoro pekee, akisisitiza kuwa mazungumzo yanapaswa kuwa sehemu ya utamaduni wa kisiasa nchini.
“Maridhiano si kusahau tofauti, maridhiano si kuacha misimamo, wala si kushinikiza upande mmoja kukubali upande mwingine. Maridhiano ni kujenga mazingira ambayo tofauti zinaweza kujadiliwa, malalamiko yakasikilizwa, makosa yakatambuliwa na suluhisho likatafutwa bila kuvunja mshikamano wa kitaifa,” amesema Dorothy Semu.
Semu amesema hayo leo Oktoba 7, 2026 katika uzinduzi wa Uongozi Mpya na Nembo ya Baraza la Vyama vya Siasa, unaofanyika jijini Dar es Salaam -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI:
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imetangaza bei mpya kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli, dizeli na mafuta ya taa zitakazotumika nchini kuanzia Jumatano, Oktoba 7, 2026.
Kwa mujibu wa taarifa ya EWURA iliyotolewa leo Oktoba 7, 2026, katika Mkoa wa Dar es Salaam, lita moja ya petroli itauzwa kwa Sh4,057, dizeli Sh4,086 na mafuta ya taa Sh4,067. Mkoani Tanga, petroli itauzwa kwa Sh4,123, dizeli Sh4,152 na mafuta ya taa Sh4,133, huku Mtwara petroli ikiuzwa kwa Sh4,170, dizeli Sh4,199 na mafuta ya taa Sh4,180.
EWURA imesema ongezeko hilo limetokana na kuibuka upya kwa mgogoro wa kisiasa katika eneo la Mashariki ya Kati mwezi Septemba 2026 eneo ambalo imesema ni miongoni mwa vyanzo vikuu vya mafuta yanayotumiwa nchini Tanzania.
Kwa mujibu wa taarifa ya EWURA, kwa Mkoa wa Dodoma bei ya Petroli itakuwa Sh4,156, dizeli Sh4,185 na mafuta ya taa Sh4,166. Mbeya, petroli itauzwa kwa Sh4,219, dizeli Sh4,248 na mafuta ya taa Sh4,229. Mwanza, petroli itauzwa kwa Sh4,272, dizeli Sh4,301 na mafuta ya taa Sh4,282, huku Kigoma petroli ikiuzwa kwa Sh4,284, dizeli Sh4,313 na mafuta ya taa Sh4,294.
Kwa upande wa bei za jumla katika Bandari ya Dar es Salaam, EWURA imesema lita moja ya petroli itauzwa kwa Sh3,909.62, dizeli Sh3,937.91 na mafuta ya taa Sh3,920.05. Katika Bandari ya Tanga, bei ya jumla ya petroli itakuwa Sh3,906.19 na dizeli Sh3,934.06. Bandari ya Mtwara, petroli itauzwa kwa Sh3,905.70 na dizeli Sh3,932.94 kwa lita.
Aidha EWURA imewakumbusha wadau kuwa, kwa mujibu wa Sheria ya Mafuta ya mwaka 2015, hususan Kifungu cha 166, bei za mafuta zitaendelea kuamuliwa na ushindani wa soko. Na kwamba Kampuni za mafuta zinaruhusiwa kuuza bidhaa hizo kwa bei za ushindani, lakini hazipaswi kuuza kwa bei inayozidi bei kikomo. -
Jambo TV
@Jambotv_
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Alexander Mkumbo, amezikaribisha kampuni na wawekezaji kutoka nchini Uholanzi na Umoja wa Ulaya (EU) kuja kuwekeza nchini Tanzania katika maeneo ya kimkakati ya madini, kilimo, na ugavi wa bandari badala ya kuishia kufanya biashara ya kawaida tu.
Prof. Mkumbo ameyasema hayo tarehe 5 Oktoba 2026 mjini The Hague, Uholanzi, wakati wa Mkutano wa Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na EU, akieleza kuwa nafasi ya kimkakati ya Tanzania kijiografia, pamoja na miundombinu na masoko yanayozunguka nchi, vinaifanya Tanzania kuwa kitovu muhimu cha uzalishaji, biashara na usambazaji wa bidhaa katika masoko ya Afrika na kwingineko.
Ameeleza kuwa Tanzania imebarikiwa kuwa na rasilimali nyingi za madini ikiwemo dhahabu, kinywe, nikeli, shaba, na madini adimu yanayohitajika duniani kwa ajili ya nishati safi. Amesisitiza kuwa lengo la Serikali si kuuza madini ghafi nje ya nchi, bali ni kuongeza thamani, kuchakata, na kuyaunganisha katika mnyororo wa thamani wa kimataifa.
"Lengo letu si kuuza tu madini kama malighafi ghafi. Tunataka kukuza maendeleo ya madini yenye uwajibikaji, uongezaji thamani, uchakataji, viwanda na kuunganishwa kwenye mnyororo wa thamani wa kimataifa... Kwa upande wetu, mustakabali wa sekta ya madini lazima uwe kuhusu uongezaji thamani, uendelevu na ustawi wa pamoja”, ameeleza.
Katika sekta ya kilimo, Waziri Mkumbo alibainisha kuwa Tanzania inalenga kutoka kwenye uzalishaji wa mazao ya msingi pekee na kuelekea kwenye uchakataji, ufungashaji, na uuzaji wa bidhaa zenye thamani kubwa. Ameongeza kuwa sekta ya kilimo na lojistiki lazima zikue pamoja kwani bila miundombinu bora ya hifadhi, ubaridi na usafirishaji, thamani kubwa ya mazao ya wakulima inapotea.
Kuhusu lojistiki ya bandari na uunganishaji wa kikanda, Prof. Mkumbo ameeleza kuwa Bandari ya Dar es Salaam inahudumia takriban asilimia 95 ya biashara ya kimataifa ya Tanzania pamoja na nchi jirani zisizokuwa na bahari kama Zambia, Malawi, DRC, Burundi, Rwanda, Uganda, na Zimbabwe. Amebainisha kuwa Serikali inaendelea kuwekeza kwenye maboresho ya miundombinu ya bandari ikiwemo mradi wa Dar es Salaam Marine Gateway na Bandari ya Kina Kirefu ya Bagamoyo.
Prof. Mkumbo ameeleza pia kuwa Serikali inaendelea kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji, ikiwamo kurahisisha huduma kwa wawekezaji na kuweka mazingira yanayowezesha sekta binafsi kuwa injini muhimu ya maendeleo ya Taifa.
Mkutano huo ni sehemu ya ziara ya uhamasishaji wa uwekezaji barani Ulaya, iliyoanza Helsinki, Finland tarehe 28 Septemba 2026, na kuendelea nchini Italia kabla ya kufika Uholanzi. Ziara hiyo pia ni sehemu ya maandalizi kuelekea Jukwaa la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya, linalotarajiwa kufanyika Dar es Salaam mwaka 2027.
Kupitia ziara hiyo, Tanzania inalenga kuimarisha mahusiano na jumuiya ya wafanyabiashara wa Ulaya, kuvutia mitaji mipya na teknolojia, pamoja na kubadilisha majadiliano ya uwekezaji kuwa miradi halisi inayotekelezwa nchini. -
Jambo TV
@Jambotv_
Waziri wa Nishati, Dkt. Juma Homera, leo Oktoba 6, 2026 amezindua Mkataba wa Huduma kwa Wateja uliohuishwa pamoja na huduma mbalimbali za TANESCO zinazolenga kuboresha zaidi namna ya utoaji wa huduma kwa wateja kwa ufanisi na kwa wakati.
Katika uzinduzi huo uliofanyika jijini Dar es Salaam, Dkt. Homera amesema matumizi ya mifumo ya teknolojia za kisasa katika utoaji wa huduma kwa wateja yanazidi kuiwezesha TANESCO kupiga hatua kubwa katika kuboresha huduma zake kwa kuzingatia uwajibikaji, uwazi na weledi unaolenga kuleta matokeo chanya kiutendaji.
“Mwelekeo wa Serikali ni kujenga sekta ya nishati inayoweza kuunga mkono kasi ya ukuaji wa uchumi wa Tanzania. Tunataka kuona shughuli za uzalishaji zinaendelea bila vikwazo visivyo vya lazima na tunataka wananchi wapate huduma kwa urahisi zaidi,” ameeleza Waziri Homera.
Amesema Tanzania hivi sasa ina umeme wa kutosha, ambapo uwezo wa uzalishaji umefikia jumla ya Megawati 4,606 dhidi ya mahitaji ya juu ya Megawati 2,316, hatua inayotoa fursa zaidi za kukuza shughuli za kiuchumi kupitia uwekezaji katika viwanda, biashara na shughuli za kijamii.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Subira Mgalu, ameipongeza Wizara ya Nishati kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwa kuendelea kuja na ubunifu unaolenga kutatua changamoto zinazowakabili wananchi katika nyanja mbalimbali.
Naye Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TANESCO, Balozi Zuhura Bundala, amesema Bodi itaendelea kuisimamia TANESCO katika kuhakikisha utoaji wa huduma unaenda sambamba na matumizi ya teknolojia za kisasa, ili huduma zimfikie mteja moja kwa moja bila vikwazo.
“Bodi itaendelea kuishauri TANESCO katika utoaji wa huduma kwa ufanisi. Kwetu sisi, mteja ni mfalme, na huduma inayotolewa na Shirika inamgusa mwananchi moja kwa moja. Tumejipanga kuhakikisha jitihada hizi zinaendelea kupiga hatua,” amesisitiza Balozi Bundala
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Bw. Lazaro Twange, ametoa ufafanuzi kuhusu uzinduzi wa Twiga Assistant, mfumo unaolenga kuachana na utoaji wa huduma kwa njia za makaratasi na kuingia katika matumizi ya mifumo ya kielektroniki inayompunguzia mteja kutumia muda mrefu kusubiri huduma. -
Jambo TV
@Jambotv_
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Deogratius Ndejembi amesema matumizi ya mifumo ya kisasa ya teknolojia ni chachu katika ukusanyaji wa kodi hivyo yanapaswa kutiliwa mkazo ili kuongeza uwazi, kuimarisha usimamizi wa kodi na kurahisisha ulipaji kodi na kutaka mijadala ya mkutano wa 46 wa Chama cha Wasimamizi wa Kodi wa Jumuiya ya Madola (CATA) iangazie zaidi teknolojia.
Akizungumza Makamu jijini Arusha Oktoba 06, 2026 wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 46 wa CATA amesema teknolojia ni nyenzo muhimu katika kuboresha ukusanyaji wa mapato ya ndani na kuimarisha huduma kwa walipa kodi ndiyo maana mkutano huo umekuja na kaulimbiu inayogusa teknolojia.
Makamu wa Rais pia amesisitiza umuhimu wa ushirikiano wa kimataifa katika masuala ya kodi, akibainisha kuwa biashara zinazovuka mipaka, makampuni ya kimataifa, miamala ya kidijitali pamoja na mali za kifedha zinazohifadhiwa nje ya nchi zimefanya ushirikiano kati ya mamlaka za kodi kuwa muhimu zaidi.
Awali akizungumza katika mkutano huo Rais wa CATA, Abu Tariq Jamaluddin amesema matumizi ya teknolojia ya kisasa yamekuwa yakisaidia nchi wanachama wa CATA kurahisisha utawala wa kodi kwa kuweka mazingira rahisi ya ukusanyaji wa mapato na kuwasaidia walipakodi kufuata sheria za kodi.
Kwa upande wake Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambao ndiyo waandaaji wa mkutano huo, Yusuph Juma Mwenda amesema Mamlaka hiyo imepiga hatua kubwa katika matumizi ya teknolojia ambayo yameboresha zaidi huduma za usimamizi wa kodi kwa kuongeza uwazi na ufanisi.
Amesema kupitia matumizi ya teknolojia TRA imekuja na mfumo wa IDRAS unaosimamia kodi za ndani ambao unamuwezesha Mlipakodi kutoa risiti za kielektroniki kwa kutumia simu ya mkononi bila kuwa na mashine hali ambayo imeongeza uhiari katika kulipa kodi na kupunguza kuonana kwa walipakodi na maofisa wa TRA.
Mkutano huo utadumu mpaka Oktoba 09 mwaka huu. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI PICHA:
Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa, Saidi Othman Yakubu, akiwasilisha rasmi hati za utambulisho kwa Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron mjini Paris.
Katika mazungumzo yao, viongozi hao walijadili maendeleo ya ushirikiano baina ya Tanzania na Ufaransa, hususan katika sekta ya biashara inayoendelea kukua. Rais Macron pia alimpa Balozi Yakubu salamu za pole azifikishe kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kufuatia msiba wa mumewe, Marehemu Hafidh Ameir. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Wafanyabiashara katika eneo la Stendi Kuu ya Mabasi Karatu, mkoani Arusha, wamesema hali bado ni ngumu kutokana na maduka yao kuendelea kufungwa, licha ya Halmashauri ya Wilaya ya Karatu kutoa ufafanuzi kuhusu mgogoro wa kodi ya pango.
Oktoba 1, 2026, JAMBO TV iliripoti malalamiko ya wafanyabiashara hao kuhusu ongezeko la kodi ya pango kutoka Shilingi 50,000 hadi Shilingi 312,500 kwa mwezi, wakisema kiwango hicho ni mzigo kutokana na mzunguko wa biashara.
Oktoba 2, Halmashauri ilisema haikufunga vyumba vyote vya biashara, bali baadhi ya wapangaji hawajasaini mikataba mipya yenye viwango vya kodi vinavyotegemea ukubwa wa eneo kwa mita za mraba.
Halmashauri pia ilikanusha kuwepo kwa zuio la Mahakama, ikisema imepokea barua ya kusudio la kufungua shauri Mahakamani, huku ikiwahakikishia wafanyabiashara kuwa mazingira ya biashara ni salama na shwari.
Hata hivyo, wamiliki wa maeneo na majengo yanayozunguka stendi wamepinga ufafanuzi huo.
Katibu wa wamiliki hao, Paschal Joseph, amesema wao ni wamiliki halali wa maeneo hayo na hawajawahi kulipwa fidia, akitaja barua ya wadau ya mwaka 2001 pamoja na mkataba wa Januari 20, 2024 kati ya Halmashauri na wananchi wa eneo hilo.
Paschal amesema wamiliki hao hawahusiki na mkataba mpya unaotajwa na Halmashauri na kudai kuwa kuna zuio la Mahakama la Agosti 31 na Oktoba 1, 2026.
Ameiomba Halmashauri kuheshimu taratibu za kisheria na kufungua maduka hayo, ambayo wafanyabiashara wanadai bado yamefungwa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amezitaka nchi wanachama wa Baraza la Ushirikiano la Nchi za Ghuba (GCC) na Bara la Afrika kutoka kwenye kutoa ahadi pekee na kuelekea kwenye kuchukua hatua halisi zitakazosaidiwa na takwimu bora, uwazi wa taarifa, na ufuatiliaji wa utekelezaji ili kulinda haki za wafanyakazi.
Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo Jumanne, tarehe 6 Oktoba 2026, jijini Dar es Salaam alipokuwa akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kama mgeni rasmi katika ufunguzi wa Mkutano wa Pili wa Uhamaji wa Nguvu Kazi (Second Doha Dialogue on Labour Mobility). Mkutano huo umeandaliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Nchi ya Qatar, Tume ya Umoja wa Afrika (AUC), pamoja na nchi wanachama wa GCC, ukiratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Mahusiano) chini ya kaulimbiu "Kuendeleza Uhamaji wa Nguvu kazi yenye Haki na Endelevu kati ya Nchi za Afrika na Ghuba (GCC+)".
Akihutubia mkutano huo, Dkt. Mwinyi amesisitiza kuwa makubaliano ya pande mbili lazima yawe nyenzo kuu ya kuandaa mifumo inayotabirika ya ajira, ulinzi wa haki za wafanyakazi nyakati za ugonjwa, ajali na ujauzito, pamoja na njia za kutatua migogoro
Aidha, Dkt. Mwinyi ameeleza kuwa ili kuwe na mabadiliko ya kweli kutoka kwenye ahadi za maneno kwenda kwenye vitendo, kuna haja kubwa ya kuwa na takwimu sahihi zitakazowezesha nchi hizo kujua mahali wafanyakazi wanapokwenda, ujuzi unaohitajika, sekta husika, gharama za ajira, na masharti ya kazi ili kutengeneza sera zinazoendana na ushahidi badala ya dhana tu.
Halikadhalika, Dkt. Mwinyi ametoa wito kwa wajumbe wa mkutano huo kuhakikisha kuwa kipimo cha mafanikio ya majadiliano hayo hakitakuwa tu ahadi zinazotolewa leo, bali kitakuwa kile kitakachotokea baada ya mkutano kukamilika, hivyo kuhimiza kubainishwa kwa hatua halisi zenye muda mahususi wa utekelezaji na ufuatiliaji.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Msanii Mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva, Godfrey William maarufu kama Dudu Baya, leo Oktoba 6, 2026, ameshindwa kuonana na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima, jijini Dodoma kama ilivyokuwa imepangwa.
Dudu Baya amesema ameelezwa kuwa Waziri Gwajima amepata dharura, hivyo amepangiwa ratiba nyingine ya kuonana naye jijini Dar es Salaam, badala ya Dodoma kama ilivyopangwa awali. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ameainisha maeneo makuu yanayopaswa kuongoza ushirikiano mpya kati ya nchi za Afrika na za Baraza la Ushirikiano la Nchi za Ghuba (GCC) katika kusimamia uhamaji wa nguvu kazi, huku akisisitiza kuwa manufaa ya kiuchumi yasipatikane kwa kutojali haki na utu wa wafanyakazi.
Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo Jumanne, tarehe 6 Oktoba 2026, jijini Dar es Salaam alipokuwa akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kama mgeni rasmi katika ufunguzi wa Mkutano wa Pili wa Uhamaji wa Nguvu Kazi (Second Doha Dialogue on Labour Mobility). Mkutano huo umeandaliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Nchi ya Qatar, Tume ya Umoja wa Afrika (AUC), pamoja na nchi wanachama wa GCC, ukiratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Mahusiano) chini ya kaulimbiu "Kuendeleza Uhamaji wa Nguvu kazi yenye Haki na Endelevu kati ya Nchi za Afrika na Ghuba (GCC+)".
Akihutubia mkutano huo, Dkt. Mwinyi ametaja eneo la kwanza kuwa ni kuhakikisha uhamaji wa wafanyakazi unakuwa wa haki kuanzia katika nchi wanazotoka, kwa kuwapa taarifa sahihi za mikataba na haki zao, pamoja na kuweka uajiri wa wazi na kimaadili unaodhibitiwa vyema. Eneo la pili ni kuunganisha uhamaji huo na mahitaji halisi ya soko la ajira kupitia ubia wa kiujuzi, mafunzo endelevu, na utambuzi wa taaluma zao
Eneo la tatu la kulinda kazi zenye utu, akibainisha kuwa ni lazima wafanyakazi walindwe dhidi ya kutolipwa au kucheleweshewa mishahara, kupunguziwa kipato kinyume cha sheria, na kuhakikisha wanafanya kazi katika mazingira salama na yenye mifumo ya kutatua migogoro. Eneo la nne alitaja kuwa ni kuimarisha hifadhi ya jamii na afya, ili wafanyakazi walindwe nyakati za ugonjwa, ajali na wakati wa ujauzito.
Dkt. Mwinyi alihitimisha kwa kutaja eneo la tano kuwa ni kutumia makubaliano ya pande mbili (Bilateral Labour Agreements) kama nyenzo kuu ya kuweka vipaumbele hivyo vyote pamoja na kujenga mifumo inayotabirika ya ajira, ulinzi wa haki na utatuzi wa migogoro.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Sheikh Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Mkoa wa Mwanza, Hassan Kabeke, ameiomba jamii kuungana katika kupinga vitendo vya ushoga, ubasha na ulawiti, akisema hatua hiyo ni muhimu katika kujenga jamii na taifa bora.
Akizungumza leo na JAMBO TV ofisini kwake, Sheikh Kabeke amesema jamii haipaswi kujikita katika kuwalaumu watu wanaofanyiwa vitendo hivyo, bali inapaswa kuunganisha nguvu katika kukabiliana na watu wanaowafanyia vitendo hivyo.
“Hili ni jambo baya, Uislamu umelikataza kinaga ubaga mpaka Mtume Mohammad amefikia wakati wa kulikemea jambo hili, akasema amelaaniwa yule anayefanya matendo ya kuendeana kinyume na maumbile,” amesema.
Aidha, kuelekea msimu wa mvua kubwa zinazotarajiwa, Sheikh Kabeke amewaagiza viongozi wa dini hiyo kuanzia ngazi ya mkoa hadi misikiti kufanya dua ya Qunuti baada ya kila Swala, kwa ajili ya kumuomba Mwenyezi Mungu kuwalinda wananchi dhidi ya madhara yanayoweza kusababishwa na mvua hizo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika, amesema suala la kupigwa risasi kwa Mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu, mwaka 2017 lilipaswa kuwa miongoni mwa ajenda muhimu zinazofuatiliwa na kujadiliwa na Umoja wa Mabunge Duniani (IPU).
Mnyika amesema hayo leo Oktoba 6, 2026 akisema viongozi wa IPU walipomtembelea Lissu, Gerezani walipata fursa ya kuuliza kuhusu tukio hilo na hatua zilizochukuliwa katika uchunguzi, akidai kuwa uchunguzi huo haujatoa majibu ya kuridhisha hadi sasa.
Amesema pamoja na tukio la kupigwa risasi, Lissu aliieleza IPU kuhusu haki zake kama mbunge ambazo Mnyika anadai ziliondolewa wakati huo, akisisitiza kuwa suala hilo pamoja na uchunguzi wa tukio la kupigwa risasi linapaswa kupewa uzito ili kulinda haki na usalama wa wabunge.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Chama cha Demokrasia na Maendeleo @ChademaTZ2 kimetoa wito kwa wadau washiriki wa mkutano wa Umoja wa Mabunge Duniani(IPU) unaofanyika jijini Arusha kuhoji juu ya kushikiliwa kwa Mwenyekiti wa chama hicho Tundu Lissu ambaye yupo gerezani kutokana na kesi ya uhaini inayomkabili.
Hayo ameyasema Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika leo Oktoba 6, 2026 akizungumza na waandishi wa habari na kutoa wito kwa wakazi wa Arusha pindi watakapokutana na wajumbe wa mkutano huo kuwaeleza kile alichokiita hali halisi ya kisiasa nchini.
"Hivyo tunaomba msaada wa kuhoji juu ya mambo haya, moja kushikiliwa kinyume cha sheria kwa Tundu Lissu. Wahoji kwa nini Lissu anaendelea kishikiliwa pamoja na wito wa kuachiwa haraka uliotolewa na Umoja wa Mataifa, Bunge la Ulaya na Jumuiya ya Madola kutokana na kukamatwa kwake kukosa misingi ya kisheria" amesema Mnyika -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amezitaka serikali za nchi za Afrika na za Baraza la Ushirikiano la Nchi za Ghuba (GCC) kuweka ushirikiano madhubuti utakaohakikisha uhamaji wa wafanyakazi unakuwa wa haki, wa kimaadili, na unaoanzia kwa kutoa elimu na taarifa sahihi za mikataba tangu katika nchi wanakotoka.
Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo Jumanne, tarehe 6 Oktoba 2026, jijini Dar es Salaam alipokuwa akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kama mgeni rasmi katika Mkutano wa Pili wa Uhamaji wa Nguvu Kazi (Second Doha Dialogue on Labour Mobility). Mkutano huo umeandaliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Nchi ya Qatar, Tume ya Umoja wa Afrika (AUC), pamoja na nchi wanachama wa GCC, ukiratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Mahusiano) chini ya kaulimbiu "Kuendeleza Uhamaji wa Nguvu kazi yenye Haki na Endelevu kati ya Nchi za Afrika na Ghuba (GCC+)".
Akihutubia mkutano huo, Dkt. Mwinyi amesisitiza kuwa uhamaji wa wafanyakazi unapaswa kutazamwa kama ubia wa kimuundo unaoleta manufaa kwa pande zote ikiwamo wafanyakazi, waajiri na serikali, huku Tanzania ikibaki na dhamira ya dhati ya kuimarisha ushirikiano kati ya Afrika na nchi za Ghuba
Aidha, Dkt. Mwinyi ameweka wazi changamoto mbalimbali zinazowakabili wafanyakazi, waajiri pamoja na serikali, akibainisha kuwa utatuzi wake unategemea ushirikiano wa dhati kati ya serikali za nchi zinazotoa na kupokea wafanyakazi. Ametaja changamoto za wafanyakazi kuwa ni pamoja na gharama kubwa za kutafuta ajira, ukosefu wa taarifa za kutosha, kucheleweshewa malipo, mazingira yasiyo rafiki ya kazi, na ukosefu wa hifadhi ya jamii.
Kwa upande wa waajiri, ametaja changamoto ya kupata wafanyakazi wenye ujuzi stahiki, huku serikali nazo zikikabiliwa na ukosefu wa taarifa za kutosha za masoko ya ajira.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesisitiza kuwa uhamaji wa nguvu kazi kati ya nchi za Afrika na Ghuba unapaswa kutazamwa kama ubia wa kimuundo unaozalisha faida za pande zote mbili, badala ya kuutazama kama utaratibu wa kawaida wa watu kuvuka mipaka kutafuta ajira.
Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo Jumanne, tarehe 6 Oktoba 2026, jijini Dar es Salaam alipokuwa akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kama mgeni rasmi katika ufunguzi wa Mkutano wa Pili wa Uhamaji wa Nguvu Kazi (Second Doha Dialogue on Labour Mobility). Mkutano huo umeandaliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Nchi ya Qatar, Tume ya Umoja wa Afrika (AUC), pamoja na nchi wanachama wa Baraza la Ushirikiano la Nchi za Ghuba (GCC), ukiratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu- Kazi, Ajira na Mahusiano chini ya kaulimbiu "Kuendeleza Uhamaji wa Nguvu kazi yenye Haki na Endelevu kati ya Nchi za Afrika na Ghuba (GCC+)".
Akihutubia Mkutano huo, Dkt. Mwinyi amebainisha kuwa usimamizi mzuri wa uhamaji wa wafanyakazi ni fursa muhimu ya kushughulikia changamoto za upungufu wa ujuzi, kuimarisha mabadilishano ya maarifa, kutengeneza kipato, na kukuza ushirikiano madhubuti kati ya mataifa.
"Uhamaji wa wafanyakazi sio tu uhamaji wa wafanyakazi kupita kwenye mipaka. Inahusu watu, inahusu maisha ya watu, inahusu ujuzi, inahusu fursa na inahusu maendeleo, na ikisimamiwa vizuri, uhamaji wa wafanyakazi unaweza kutoa fursa na kushughulikia changamoto za upungufu wa ujuzi na kuhakikisha kwamba zinasaidia katika mabadilishano ya maarifa”, ameeleza Dkt. Mwinyi.
Dkt. Mwinyi ameongeza kuwa bara la Afrika lina utajiri mkubwa wa idadi ya vijana na nguvukazi yenye uwezo wa kufanya kazi, jambo linalotengeneza fursa ya kipekee ya kiuchumi inayopaswa kutumiwa kimkakati na kwa uwajibikaji ili kukuza ujuzi katika sekta mbalimbaliThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Shirika la Kazi Duniani (ILO) limepongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Pili wa Uhamaji wa Nguvu Kazi (Second Doha Dialogue on Labour Mobility), huku likisisitiza kuwa jukwaa hilo linapaswa kujikita katika utekelezaji wa mpango kazi endelevu unaoleta matokeo na kulinda haki za wafanyakazi wanaoenda kufanya kazi nchi za Ghuba na Kiarabu.
Hayo yameelezwa leo Jumanne, tarehe 6 Oktoba 2026, jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa ILO Kanda ya Nchi za Kiarabu, Dkt. Ruba Jaradat, wakati akihutubia ufunguzi wa mkutano huo wa siku mbili ulioandaliwa na Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Nchi ya Qatar, Tume ya Umoja wa Afrika (AUC), na nchi wanachama wa Baraza la Ushirikiano la Nchi za Ghuba (GCC).
Mkutano huo unaoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu- Kazi, Ajira na Mahusiano unaongozwa na kaulimbiu "Kuendeleza Uhamaji wa Nguvu kazi yenye Haki na Endelevu kati ya Nchi za Afrika na Ghuba (GCC+)".
Akizungumza kwenye mkutano huo, Dkt. Jaradat amebainisha kuwa Mjadala wa Kwanza wa Doha uliweka msingi wa ushirikiano katika kulinda wafanyakazi wahamiaji, na kwamba mkutano huu wa pili wa Dar es Salaam unalenga utekelezaji na upatikanaji wa matokeo ya pamoja kupitia mpango kazi wa vitendo.
Dkt. Jaradat ameeleza kuwa takwimu za mwaka 2022 zinaonesha kuwa wafanyakazi wahamiaji wa kimataifa walichukua asilimia 37.2 ya uhamiaji kwenda katika nchi za Kiarabu, ikilinganishwa na asilimia 27 barani Afrika. Hatua hiyo inathibitisha kuongezeka kwa fursa na soko la ajira, jambo linalotaka kuwepo kwa usimamizi madhubuti wa usawa katika uajiri na utambuzi wa viwango vya taaluma za wafanyakazi.
"Wahamiaji wa kimataifa waliwakilisha asilimia 37.2 ya uhamiaji kwenda kwenye nchi za Kiarabu ikilinganishwa na asilimia 27 Afrika, ambayo inaonyesha ongezeko la uhamiaji wa wafanyakazi... Hapa tunahitaji kuwa na kazi ya ufanisi ambayo itakuwa ni kitovu cha uongozi wa uhamiaji... Ili kuweza kupata mzunguko mzuri wa wahamiaji, tunahitaji kuangalia taaluma na uzoefu wa wahamiaji hawa na pia kuweza kutengeneza sera ambazo zinaweza kusaidia kufanya maamuzi na tathmini ya viwango vya uwezo vya wafanyakazi hawa.", ameeleza.
Aidha, Mkurugenzi huyo wa ILO amepongeza hatua na mabadiliko chanya ya kisheria yanayoendelea kushuhudiwa katika nchi za Kiarabu na za Ghuba zikiwemo Saudi Arabia, UAE, Bahrain, Oman, Jordan na Lebanon katika kuboresha sheria za kazi, usalama na mazingira ya afya kwa wafanyakazi wanaoenda kufanya kazi nchini humo.
Akihitimisha hotuba yake, Dkt. Jaradat alibainisha kuwa ILO ipo tayari kuzisaidia nchi wanachama katika maeneo matatu makuu ili kuhakikisha ulinzi na manufaa endelevu kwa pande zote.
"ILO imesimama tayari kuweza kuunga mkono nchi wanachama katika maeneo ya msingi matatu: ya kwanza ni kutengeneza mifumo ya usawa ya kuweza kutambua taaluma za wafanyakazi hao, kusimamia mzunguko wote wa uhamiaji huu ikiwemo hifadhi ya jamii, na mpango kazi wa vitendo wa kusaidia kufanya uendelevu wa manufaa tunayoyatarajia." Ameeleza. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetangaza mpango wa kutengeneza mfumo madhubuti wa kielektroniki wa kusimamia taarifa za wafanyakazi wanaoenda kufanya kazi ghaibuni, ili kuwa na takwimu sahihi na ushahidi wa kutosha kuhusu idadi ya wanaosafiri na wanaorejea nchini.
Hayo yameelezwa leo Jumanne, tarehe 6 Oktoba 2026, jijini Dar es Salaam na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu- Kazi, Ajira na Mahusiano, Deus Sangu wakati akihutubia Mkutano wa Pili wa Uhamaji wa Nguvu Kazi (Second Doha Dialogue on Labour Mobility).
Mkutano huo ulioratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu umeandaliwa kwa kushirikiana na Serikali ya Nchi ya Qatar, Tume ya Umoja wa Afrika (AUC), pamoja na nchi wanachama wa Baraza la Ushirikiano la Nchi za Ghuba (GCC) chini ya kaulimbiu "Kuendeleza Uhamaji wa Nguvu kazi yenye Haki na Endelevu kati ya Nchi za Afrika na Ghuba (GCC+)".
Akizungumza katika ufunguzi huo, Sangu amebainisha kuwa Tanzania imedhamiria kuimarisha ushirikiano kati ya nchi za Afrika na nchi za Ghuba (GCC) ili kukuza ujuzi, kutoa zana na vifaa vya kazi, pamoja na kuhakikisha ulinzi na hifadhi ya jamii kwa wafanyakazi wanaosafiri kwenda kufanya kazi katika nchi hizo
"Tunategemea kutengeneza mfumo wa kusimamia taarifa za wahamiaji iweze kuwa na ushahidi wa kutosha kati ya wanaotoka na wanaokurudi... Tanzania imelenga kuuboresha huu ushirikiano wa pamoja ambao utasimamia usimamizi wa wahamiaji ambao wanazunguka kutoka Afrika kwenda nchi za GCC. Tanzania bado imelenga kuboresha ushirikiano na Afrika pamoja na wadau wetu wa GCC kwa lengo la kuweza kuboresha ujuzi na kupata vifaa na kuleta ulinzi kwa watu wanaosafiri kwenda huko na ulinzi wao pamoja na hifadhi ya jamii.", ameeleza.
Aidha, Waziri Sangu ametumia fursa hiyo kuwakaribisha wajumbe na wageni wote wa kimataifa waliokusanyika jijini Dar es Salaam kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii nchini ikiwemo Mlima Kilimanjaro, Hifadhi za Taifa za Serengeti na Mikumi, pamoja na Zanzibar ili kujionea utajiri wa utamaduni, wanyamapori na ukarimu wa Watanzania.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeweka wazi hatua mbalimbali za kimfumo, kisheria na kifedha zilizochukuliwa ili kuweka ulinzi thabiti kwa Watanzania wanaokwenda kufanya kazi nje ya nchi, huku ikishukuru nchi za Baraza la Ushirikiano la Nchi za Ghuba (GCC) kwa ushirikiano endelevu.
Hayo yameelezwa leo Jumanne, tarehe 6 Oktoba 2026, jijini Dar es Salaam na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu- Kazi, Ajira na Mahusiano, Deus Sangu wakati akihutubia Mkutano wa Pili wa Uhamaji wa Nguvu Kazi (Second Doha Dialogue on Labour Mobility). Mkutano huo ulioratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu umeandaliwa kwa kushirikiana na Serikali ya Qatar, Tume ya Umoja wa Afrika (AUC) na nchi wanachama wa GCC chini ya kaulimbiu "Kuendeleza Uhamaji wa Nguvu kazi yenye Haki na Endelevu kati ya Nchi za Afrika na Ghuba (GCC+)".
Sangu amesema kuwa Tanzania inalenga kuhakikisha kuwa uhamiaji wa wafanyakazi kwenda nchi za nje unaimarishwa ili ujikite kwenye taaluma, kufikia malengo ya maendeleo endelevu, na kuleta manufaa ya kiuchumi yenye usawa kwa pande zote mbili
"Tanzania inategemea kuendelea kuhusika zaidi siku zijazo kuhakikisha kwamba uhamiaji wa wafanyakazi unajikita zaidi katika taaluma, malengo pamoja na maendeleo endelevu. Na katika mazingatio haya nchi ya Tanzania imechukua hatua kadhaa kuhakikisha kwamba haya mambo yanafikiwa ikiwemo kutengeneza mifumo sahihi ambayo inaweza kusimamia uhamiaji wa wafanyakazi kwa kutengeneza miongozo ambayo inaleta viwango vya wazi ambavyo vinasimamia mashirika binafsi ya kutoa ajira.", ameeleza.
Sangu amebainisha kuwa mbali na kuingia makubaliano ya pamoja na nchi mbalimbali, Serikali imeanzisha utaratibu wa kutoa mafunzo maalum kabla ya kuondoka ili kuwajengea uelewa wananchi kuhusu haki zao, majukumu yao, mikataba ya kazi, na mifumo ya kifedha katika nchi wanazokwenda.
Kadhalika, katika kutatua changamoto ya gharama za usafiri na mchakato wa kwenda kufanya kazi ghaibuni, Waziri Sangu ameeleza kuwa Serikali imeshirikiana na sekta binafsi pamoja na taasisi za kifedha kuweka Mfumo wa Mikopo ya Ghaibuni ili kuwapunguzia mzigo wananchi na kuzuia kutumiwa kwa njia zisizo rasmi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Kazi wa Nchi ya Qatar, Dkt. Ali bin Samikh Al Marri, amesisitiza kuwa juhudi za kuboresha mazingira ya kazi kwa wafanyakazi wanaohama hazipaswi kuishia tu katika nchi wanazokwenda kuajiriwa, bali zinapaswa kuangalia mahitaji ya kiuchumi na kuimarisha nyenzo za kukabiliana na changamoto mpya zinazoibuka maeneo ya kazi.
Hayo yameelezwa leo Jumanne, tarehe 6 Oktoba 2026, jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Pili wa Uhamaji wa Nguvu Kazi (Second Doha Dialogue on Labour Mobility). Mkutano huo umeandaliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Nchi ya Qatar, Tume ya Umoja wa Afrika (AUC), na nchi wanachama wa Baraza la Ushirikiano la Nchi za Ghuba (GCC), ukiratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Mahusiano) chini ya kaulimbiu "Kuendeleza Uhamaji wa Nguvu kazi yenye Haki na Endelevu kati ya Nchi za Afrika na Ghuba (GCC+)".
Akihutubia Mkutano huo ambao umehudhuriwa na Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi akimwakilisha Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassana kama mgeni rasmi, Dkt. Al Marri amebainisha kuwa nia kuu ya mazungumzo hayo ni kuhakikisha kuwa waajiri wanapata wafanyakazi walio bora na wafanyakazi pia wanapata huduma na mazingira mazuri, huku haki zao zikizingatiwa kwa usawa.
"Tunataka wafanyakazi na waajiri waweze kupata huduma zilizo nzuri na wao wapate wafanyakazi walio bora, na kwa pamoja tutapata mafanikio kwa kuhakikisha kwamba tunaleta huo ulinganifu uliosawia kwa kuhakikisha kwamba haki za wafanyakazi zinazingatiwa”, ameeleza.
Aidha, Waziri huyo wa Qatar ameeleza kuwa mkutano huo unatarajiwa kupitisha Azimio la Mjadala wa Pili wa Doha, ambalo litakuwa mwendelezo wa mkutano wa kwanza uliofanyika mwezi Machi 2024 mjini Doha, Qatar. Amebainisha kuwa hatua ya majadiliano hayo kuhamia Dar es Salaam ni ishara ya wazi ya wajibu wa pamoja na ushirikiano endelevu kati ya nchi za GCC na Afrika kama wadau muhimuThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Serikali ya Nchi ya Qatar imesifu ukarimu na uongozi wa Tanzania katika kuandaa Mkutano wa Pili wa Doha wa Uhamaji wa Nguvu Kazi (Second Doha Dialogue on Labour Mobility), huku ikisisitiza kuwa jukwaa hilo linalenga kutoka kwenye ahadi za maneno na kuvuka kuelekea kwenye vitendo ili kulinda haki za wafanyakazi na kuleta manufaa kwa pande zote.
Hayo yameelezwa leo Jumanne, tarehe 6 Oktoba 2026, jijini Dar es Salaam na Waziri wa Kazi wa Nchi ya Qatar, Dkt. Ali bin Samikh Al Marri, wakati akihutubia mkutano huo wa siku mbili ulioandaliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Qatar, Tume ya Umoja wa Afrika (AUC), na Baraza la Ushirikiano la Nchi za Ghuba (GCC), huku Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi akimwakilisha Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassana kama mgeni rasmi.
Akizungumza kwa niaba ya Serikali ya Qatar, Dkt. Al Marri ametoa shukrani za dhati kwa Serikali na wananchi wa Tanzania kwa kuwa wenyeji wa tukio hilo muhimu na kutoa ukaribisho mchangamfu, akibainisha kuwa hatua ya mkutano huo kuhamia Dar es Salaam kutoka Doha ni ishara ya wazi ya ubia wa usawa na umiliki wa pamoja wa majadiliano hayo baina ya nchi za Afrika na za Ghuba.
Dkt. Al Marri amebainisha kuwa misingi mikuu mitatu inayopaswa kuongoza majadiliano hayo na ushirikiano wa siku zijazo ni kukuza ujuzi, kuratibu uhamaji wa nguvu kazi, na kuhakikisha utumiaji wa wafanyakazi unazingatia haki na manufaa ya pande zote mbili yaani wafanyakazi, waajiri na serikali zote husika.
Mkutano huo unaoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Mahusiano) unaongozwa na kaulimbiu isemayo "Kuendeleza Uhamaji wa Nguvu kazi yenye Haki na Endelevu kati ya Nchi za Afrika na Ghuba (GCC+)".
Aidha, mkutano huo unakutanisha mawaziri wa kazi, viongozi waandamizi, na wataalamu kutoka zaidi ya nchi 33 za Afrika na nchi za Ghuba, ukiwa na lengo la kuweka mikakati ya pamoja ya kulinda haki za wafanyakazi wanaoenda kufanya kazi nchi za Ghuba, kuoanisha mifumo ya ajira, pamoja na kukuza ujuzi na maendeleo ya kiuchumi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI:
Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) imefunga kwa muda njia ya Rongai katika Hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro, kutokana na moto unaoendelea katika eneo hilo.
Katika taarifa iliyotolewa Oktoba 5, 2026, TANAPA imesema hatua hiyo imechukuliwa kwa ajili ya kuhakikisha usalama wa watalii na wadau wengine wanaofanya shughuli za utalii katika eneo hilo.
Kwa watalii waliokuwa wamepanga kutumia njia ya Rongai, TANAPA imewashauri kutumia njia nyingine za kupandia Mlima Kilimanjaro, ambazo ni Machame, Marangu na Umbwe, kwa kufuata taratibu zilizowekwa na mamlaka hiyo.
TANAPA imeeleza kuwa timu ya zimamoto inaendelea na shughuli za kukabiliana na moto huo, huku mamlaka ikiendelea kufuatilia hali hiyo kwa karibu na kuchukua hatua kuhakikisha usalama wa watalii, watumishi na wadau wengine wa utalii, pamoja na kulinda ikolojia ya Mlima Kilimanjaro. -
Jambo TV
@Jambotv_
Shirika la Vi Agroforestry limetangaza rasmi maandalizi ya Kongamano la 11 la Kitaifa la Kilimomisitu, ambalo linatarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 19 mwezi huu katika Kituo cha Mafunzo ya Kilimomisitu kilichopo Bweri, mjini Musoma mkoani Mara.
Akizungumza kuhusu kongamano hilo jana, Meneja Mkazi wa shirika hilo, Martha Olotu, alieleza kuwa tukio hilo limebeba kaulimbiu isemayo "Kilimomisitu kwa Vijana na Uwekezaji", likiwa na lengo la kuwakutanisha takribani washiriki 8,000 ana kwa ana na wengine kupitia mtandao ili kuharakisha upatikanaji wa fedha, kuimarisha ushirikiano wa kikanda na kitaifa, na kuchochea utekelezaji wa vitendo katika sekta hiyo.
Kongamano hilo linatajwa kuwa na lengo la kubadili fursa za kilimomisitu kuwa uwekezaji unaotekelezeka, kuchochea fursa za kiuchumi kwa vijana, kuimarisha usalama wa chakula, na kuchangia urejeshaji wa mandhari, huku likitoa wito kwa serikali, wawekezaji, wadau wa maendeleo, watafiti, na wakulima kujumuika pamoja kupanga utekelezaji wa pamoja baada ya miongo minne ya utekelezaji wa kilimomisitu nchini.
“Tunawaalika serikali, wawekezaji, wadau wa maendeleo, watafiti, wakulima na vijana kujadili na kupanga utekelezaji wa pamoja. Kwa kuzingatia zaidi ya miaka kumi ya majadiliano ya kitaifa na miongo minne ya utekelezaji wa kilimomisitu katika jamii, kongamano la 11 la kitaifa la kilimomisitu litaweka mkazo katika kuunganisha sera, uwekezaji na utekelezaji” alisema Martha.
Mpangokazi wa kongamano hilo la siku tatu umezingatia maeneo makuu matatu yanayokamilishana ambapo siku ya kwanza itajikita katika fursa za biashara na uwekezaji wa kijani kwa vijana katika sekta ya kilimomisitu, ikihusisha mdahalo maalum utakaowakutanisha vijana na taasisi za fedha na watunga sera ili kuondoa vikwazo vya kupata mitaji na ardhi. Siku ya pili itachambua mchango wa kilimomisitu katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, kuimarisha usalama wa chakula, na kurejesha mandhari, wakati siku ya tatu itajadili uimarishaji na uunganishaji wa sera za kilimomisitu na misingi ya uwekezaji.
Katika kongamano hilo, Shirika linatarajia kuzindua rasmi Jukwaa la Wadau wa Kilimomisitu Tanzania (Tanzania Agroforestry Stakeholders Platform - TASP), ambalo litaimarisha uratibu na kuhakikisha mapendekezo ya wadau yanaingizwa katika sera, mipango, na bajeti za serikali.
Shughuli nyingine zitakazofanyika zinajumuisha maonyesho ya ubunifu, mafunzo ya vitendo mashambani, mijadala ya uwekezaji, na simulizi za mafanikio kutoka kwa wakulima wenyewe ili kuwaunganisha wafanyabiashara na washirika wenye fursa za kibiashara. -
Jambo TV
@Jambotv_
#ad
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), Profesa Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi, anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika hafla ya uzinduzi wa Baraza la Sita la Vyama vya Siasa, itakayofanyika kesho Oktoba 7, 2026 katika Ukumbi wa Mikutano wa Mount Meru, Hoteli ya Hyatt Regency, jijini Dar es Salaam.
Hafla hiyo inatarajiwa kuwakutanisha wadau mbalimbali wa demokrasia ya vyama vingi katika kipindi ambacho Tanzania inaendelea kuimarisha mfumo wa siasa za vyama vingi na kuendeleza mazungumzo yanayojenga uelewano na ushirikiano miongoni mwa vyama vya siasa.
Tukio hili limeandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini @orpptanzania na litarushwa mubashara Jambo TV.
Usikose kufuatilia
@orpptanzania -
Jambo TV
@Jambotv_
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameyataka mabunge kuimarisha usimamizi wa rasilimali za umma na uwajibikaji wa serikali, akisisitiza kuwa wananchi wanatarajia wawakilishi wao kulinda maslahi yao na kuhakikisha mahitaji yao yanazingatiwa katika maamuzi.
Rais Dkt. Samia ametoa ujumbe huo kupitia picha mjongeo iliyooneshwa katika ufunguzi wa Mkutano wa 153 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), leo, Jumatatu, Oktoba 5, 2026, katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC). Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, amemwakilisha Rais Dkt. Samia katika ufunguzi rasmi wa mkutano huo unaofanyika Oktoba 5–9, 2026.
Amesema mamlaka ya mabunge yanatokana na wananchi, hivyo yana wajibu wa kutunga sheria kwa maslahi ya umma, kuchunguza mgawanyo na matumizi ya rasilimali na kuziwajibisha serikali. Ameeleza kuwa serikali yake inaheshimu jukumu la Bunge la kuisimamia na kuishauri, kwa kuwa linaimarisha utendaji na uwajibikaji kwa Watanzania.
Rais Dkt. Samia amesema kaulimbiu ya mkutano kuhusu kuimarisha utawala bora na kuziwezesha jamii kupitia ushirikishwaji, kuaminiana na fursa kwa wote inaendana na changamoto za sasa duniani. Amehimiza mabunge kutathmini makubaliano yanayofikiwa na serikali na kuendeleza ushirikiano unaovuka tofauti za kisiasa na mipaka ya nchi.
Akizungumza katika ufunguzi huo, Waziri Mkuu amesema mabunge yana nafasi muhimu katika kuhakikisha taasisi za umma zinaitikia mahitaji ya wananchi kupitia utungaji wa sheria, uidhinishaji wa matumizi ya fedha na usimamizi wa shughuli za serikali. Ametaja kuimarishwa kwa Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), iliyotengewa zaidi ya Sh. bilioni 132 katika mwaka wa fedha 2026/2027, kuwa sehemu ya juhudi za kuimarisha usimamizi wa rasilimali za umma.
Dkt. Mwigulu amesema Rais Dkt. Samia anaamini katika utawala wa kikatiba na mgawanyo wa madaraka, akisisitiza kuwa taasisi imara na huru ni muhimu katika kujenga jamii zenye ustawi, utulivu na ushirikishwaji.
Amesema changamoto za mabadiliko ya tabianchi, dharura za afya, misukosuko ya kiuchumi na maendeleo ya teknolojia zinahitaji majadiliano, ushirikiano na diplomasia ya kibunge. Amesisitiza kuwa utawala bora unahusu kulinda utu wa binadamu, kuhakikisha kila mwananchi anasikilizwa, jamii zinawezeshwa na kila kizazi kinapata fursa ya kustawi.
Aidha, ametaja maendeleo katika sekta za nishati, reli, elimu na afya kuwa miongoni mwa hatua za kuboresha maisha ya wananchi chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia. Pia, amempongeza Rais wa IPU, Dkt. Tulia Ackson, kwa uongozi wake katika taasisi hiyo, akisema ameiletea Tanzania heshima na kuonesha umuhimu wa fursa sawa katika uongozi wa kimataifa.
Awali, Rais wa IPU, Dkt. Tulia Ackson amesema mabunge yanapaswa kuhakikisha rasilimali za umma zinawafikia wanaozihitaji na kupima mafanikio ya sera kwa matokeo yake katika maisha ya wananchi. Amehimiza ushiriki wa wanawake, vijana, watu wenye ulemavu na makundi yanayotengwa katika maamuzi ya umma.
“Mti mmoja haujengi msitu,” amesema, akisisitiza umuhimu wa mshikamano na ushirikiano katika kukabiliana na changamoto za dunia. Ameeleza kuwa hiyo ni hotuba yake ya mwisho ya ufunguzi wa mkutano wa IPU akiwa Rais wa taasisi hiyo, baada ya kuhudumu kwa miaka mitatu.
Kwa upande wake, Spika wa Bunge la Tanzania, Mussa Azzan Zungu, amehimiza ushirikiano wa kimataifa unaozingatia usawa na manufaa ya pamoja. Amesema uwekezaji katika sekta za kimkakati unapaswa kuambatana na uhamishaji wa teknolojia na maarifa, mafunzo na ushiriki wa wananchi, huku mabunge yakiweka mifumo inayolinda maslahi ya umma.
Katika ujumbe uliowasilishwa kupitia picha mjongeo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameyataka mabunge kuimarisha uwajibikaji, ushirikishwaji na kuaminiana kati ya wananchi na taasisi za umma. Naye mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini amesisitiza kuwa ahadi za maendeleo zinahitaji kuungwa mkono na bajeti, sheria na usimamizi wa utekelezaji.
Katibu Mkuu wa IPU, Balozi Anda Filip, ameyataka mabunge kuipa kipaumbele mijadala kuhusu akili unde (AI), akisisitiza usimamizi wa kidemokrasia na ushirikiano wa kimataifa ili kuhakikisha teknolojia hiyo inatumika kwa usalama na kuendelea kuwa chini ya udhibiti wa binadamu. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Hali ya taharuki imeibuka hii leo Oktoba 5,2026 katika Mtaa wa Sanare, Kata ya Daraja mbili jijini Arusha baada ya binti mwenye umri wa miaka 22, anayefanya kazi ya kusajili laini za simu, kudai kubakwa na kuingiliwa kinyume na maumbile na vijana wanne katika moja ya vyumba vilivyopo eneo hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari akiwa katika Ofisi ya Mtaa wa eneo hilo, binti huyo (jina limehifadhiwa) amesema alifika katika eneo hilo kwa ajili ya kutoa huduma hiyo ya kusajili laini ndipo alipokutana na kijana aliyemwambia anahitaji kusajili laini, lakini baadaye alijikuta katika mazingira ya kutishiwa na kufanyiwa vitendo hivyo.
Mashuhuda wa tukio hilo wamesema wamesikitishwa sana na tukio hilo, huku wakiziomba mamlaka kufanya uchunguzi wa kina na kuwakamata wote watakaobainika kuhusika, ili hatua za kisheria zichukuliwe na iwe fundisho kwa wengine.
Wakazi hao pia wameeleza kuwa hali ya usalama katika eneo hilo si nzuri, wakidai kumekuwa na mwendelezo wa matukio mbalimbali ya uhalifu. Wameziomba mamlaka kuongeza ulinzi na kuchukua hatua za haraka kukabiliana na changamoto hiyo.
Jeshi la Polisi lilifika eneo la tukio na kuwakamata baadhi ya vijana wanaoshukiwa kuhusika, huku binti huyo akikimbizwa hospitalini kwa ajili ya kufanyiwa vipimo na kupata matibabu zaidi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Alexander Mnyeti amemtaka Mkuu mpya wa Wilaya ya Chato, Maiko Richard Kachoma kuanza kazi kwa kufuatilia na kusimamia madeni yanayodaiwa na wananchi dhidi ya Halmashauri, huku akisisitiza hatua kuchukuliwa kwa watumishi watakaobainika kukiuka sheria, kanuni na taratibu za nchi.
Mnyeti ametoa maelekezo hayo leo wakati wa shughuli ya kumuapisha Mkuu huyo wa Wilaya ya Chato, ambaye aliteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan Septemba 29, 2026.
Amesema Mkuu huyo wa Wilaya anatakiwa kuhakikisha Halmashauri inawalipa wananchi na wadau mbalimbali ambao wamekuwa wakidai malipo kutokana na huduma au kazi walizozifanya kwa ajili ya Halmashauri.
Aidha, Mnyeti amemtaka Kachoma kusimamia nidhamu na utendaji wa watumishi wa umma, huku akihakikisha watumishi wanaokiuka sheria, kanuni na taratibu za nchi wanachukuliwa hatua stahiki.
Amesema Wilaya ya Chato imekuwa na baadhi ya watumishi ambao, kwa mujibu wa malalamiko yaliyopo, wameshindwa kutimiza ipasavyo wajibu wao kwa wananchi, ikiwemo suala la kulipa madeni yanayodaiwa na wananchi waliofanya kazi au kutoa huduma kwa Halmashauri.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Chato, Maiko Richard Kachoma, ameahidi kushirikiana na watumishi pamoja na uongozi wa Halmashauri katika kubaini madeni yote yanayodaiwa na Halmashauri na kuweka utaratibu wa kuhakikisha yanalipwa.
Kachoma amesema pia atafuatilia madeni yanayodaiwa na taasisi nyingine ambazo si sehemu ya Halmashauri, kwa lengo la kuhakikisha wahusika wanatimiza wajibu wao na wananchi wanapata haki zao kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mahakama ya Rufani ya Tanzania, iliyoketi jijini Arusha mbele ya jopo la majaji Barke Sehel, Issa Maige na Immaculata Banza, leo Oktoba 5,2026 imesikiliza hoja katika rufaa ya jinai Rufaa ya Jinai Namba 595 ya Mwaka 2023 inayomhusu wakili Peter Michael Madeleka, huku Jamhuri ikiwasilishwa na mawakili Janeth Sekule na Rose Sule.
Msingi wa rufaa hiyo ni kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha uliotolewa tarehe 17 Julai 2023 na Jaji Bade, ambao uliweka pembeni makubaliano ya plea bargaining (makubaliano ya kukiri kosa), ukafuta mwenendo wa shauri la Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha uliotokana na makubaliano hayo na kuamuru shauri lisikilizwe upya (trial de novo).
Katika hoja zake, Madeleka ameiomba Mahakama ya Rufani kutengua amri hiyo, akisisitiza kwamba tayari alikuwa amehukumiwa na kutumikia adhabu iliyotokana na mchakato wa plea bargaining. Kwa mtazamo wa utetezi, kurejeshwa kwa shauri kwa ajili ya kusikilizwa upya kunaweza kumweka katika mazingira ya kuhukumiwa au kuadhibiwa mara mbili kwa kosa lilelile (double jeopardy).
Kwa upande wa Jamhuri, mawakili Janeth Sekule na Rose Sule wamepinga hoja hiyo, wakieleza kuwa baada ya Mahakama Kuu kuweka pembeni plea bargaining na hukumu iliyotokana nayo, msingi wa kutiwa hatiani kwa Madeleka nao uliondolewa. Kwa hiyo, kwa hoja ya Jamhuri, kusikilizwa upya kwa shauri si kumwadhibu Madeleka mara ya pili, bali ni matokeo ya kubatilishwa kwa mchakato wa awali.
Historia ya kesi hiyo inaanzia 14 Mei 2020, ambapo Madeleka na Jamila Augustino Ilomo walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha na kushtakiwa kwa makosa 10. Rekodi ya Mahakama Kuu inaonyesha kuwa mashitaka ya tisa na ya kumi yalihusu utakatishaji fedha (money laundering).
Baadaye, kupitia plea bargaining, hati ya awali ya mashtaka ilibadilishwa na kuwa shtaka moja la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu (Obtaining Money by False Pretence), chini ya kifungu cha 302 cha Kanuni ya Adhabu, na Madeleka pamoja na mshtakiwa mwenzake walikiri kosa hilo na kutiwa hatiani.
Hata hivyo, Madeleka alipinga uhalali wa mchakato huo, jambo lililopelekea shauri kufika Mahakama Kuu. Katika uamuzi wake wa tarehe 17 Julai 2023, Mahakama Kuu iliweka pembeni mchakato wa plea bargaining na hukumu iliyotokana nao, na kuamuru shauri kurejea katika hatua iliyokuwepo kabla ya makubaliano hayo kwa ajili ya kusikilizwa upya (trial de novo).
Uamuzi huo ndio uliosababisha Madeleka kufikisha malalamiko yake katika Mahakama ya Rufani, akiiomba Mahakama hiyo kutathmini uhalali wa amri ya kurejeshwa kwa shauri na iwapo utekelezaji wake unazingatia matakwa ya sheria.
Baada ya kusikiliza hoja za Mrufani na majibu ya Jamhuri, Mahakama ya Rufani haikutoa uamuzi leo, bali imeeleza kuwa itapanga tarehe ya kutolewa kwa uamuzi wa rufaa hiyo.
Kwa sasa, kinachosubiriwa ni uamuzi wa Mahakama ya Rufani, ambao utaamua mwelekeo wa hatua zinazofuata katika shauri hilo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imewataka watendaji na wafanyakazi wote wa mamlaka hiyo kuongeza ufanisi katika utendaji wao wa kazi za kila siku, ili kuendelea kujenga imani kwa watumiaji wa bandari na kuendana na ongezeko kubwa la shehena inayowasili nchini kufuatia maboresho ya miundombinu na utendaji kazi.
Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TPA Balozi Ernest Mangu leo Jumatatu, tarehe 5 Oktoba 2026, jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja.
Akiwasilisha msisitizo kuhusu haja ya watendaji kuongeza ufanisi ili kukabili ongezeko hilo la mzigo na kuondoa changamoto mbalimbali, mzungumzaji katika uzinduzi huo amesema, “Tunao mzigo mkubwa sasa hivi unakuja hapa kwetu ni kwa sababu ya maboresho ambayo yamefanyika katika utendaji na katika miundobinu. Sasa maboresho hayo au mzigo huu uliokuja mwingi unatutaka sisi watendaji wa TPA kuongeza ufanisi zaidi. Hilo ndilo jambo la msingi. Tuongeze ufanisi zaidi ili tuweze kusaidia kuendelea kujenga imani yetu kwa watumiaji wa bandari yetu."
Aidha, ameeleza kuwa utendaji mzuri wa bandari umevuta mzigo mkubwa ambao kwa nyakati fulani umesababisha kero ya msongamano wa malori kwenye barabara zinazoingia bandarini pamoja na Bandari Kavu (ICDs) jijini Dar es Salaam.
Kutokana na hali hiyo, uongozi wa TPA umewataka wasafirishaji na wadau wa lojistiki kushirikiana kikamilifu ili kutumia miundombinu iliyopo na kuondoa kero hizo mitaani, huku ukisisitiza kuwa kauli mbiu ya Wiki ya Huduma kwa Wateja inapaswa kuwa mwongozo endelevu wa utendaji wa kila siku badala ya kuishia kwenye wiki hiyo pekee.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Plasduce Mbossa ameeleza kuwa dhamira ya kutaka ufanisi zaidi inatokana na ukuaji mkubwa wa shughuli za kibandari katika kipindi cha miaka mitano (2021/2022 hadi 2025/2026), ambapo idadi ya meli zilizohudumiwa imeongezeka kutoka meli 4,686 hadi kufikia meli 6,000, huku mizigo ya nchi jirani ikiongezeka kutoka tani milioni 7.01 hadi tani milioni 15.499, na huduma za makasha zikipanda kutoka makasha 823,000 hadi makasha 1,381,598.
Naye, Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam, Abed Gallus Abed ameeleza kuwa katika Bandari ya Dar es Salaam pekee, ndani ya miaka miwili ya ushirikishwaji wa sekta binafsi, shehena iliyohudumiwa imeongezeka kwa tofauti ya tani milioni 10, ikitoka tani milioni 23.7 katika mwaka wa fedha 2023/2024 na kufikia tani milioni 33.7 katika mwaka 2025/2026.
Amebainisha kuwa matokeo hayo yamechagizwa na uwekezaji kwenye miundombinu, ushirikiano wa wadau, pamoja na mazingira wezeshi ya kibiashara yaliyowekwa na Serikali.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa CHADEMA Taifa (BAVICHA), Deogratius Mahinyila, amesema Vijana wa chama hicho hawatakubali kile alichokiita siasa za udalali na usaliti ndani ya chama, akiwataka wanachama kuwa na mshikamano katika kipindi hiki.
Mahinyila ameyasema hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika Nyamongo, akisema suala hilo ni miongoni mwa mambo yanayowakera vijana wa chama hicho.
“Sisi vijana wa CHADEMA kauli yetu ni kwamba yoyote anayefanya siasa za udalali, yoyote anayefanya mambo ya kumsaliti mwenyekiti wetu aliye gerezani bila hatia, yoyote anayewakwamisha, yoyote anayewasaliti Watanzania, yoyote anayewakera Watanzania kwenye mapambano tuliyonayo, sisi vijana wa CHADEMA, hata kama atakuwa na mapembe makubwa kwenye uongozi, tutampita juu,” alisema.
Mahinyila pia amewataka wanachama wa CHADEMA kutokubali matendo anayodai yanaweza kuvuruga mshikamano wa chama, akisema vijana wataendelea kusimamia masuala wanayoamini ni muhimu kwa chama na kwa wananchi.
“Hatutakubali vijana wenzetu wanapoteza maisha yao kwa sababu ya mambo haya ya CHADEMA na kupigania haki, halafu tuwe na mtu miongoni mwetu, hata kama aliwahi kuwa na nafasi ya uongozi huku CHADEMA, hatutaweza kuwaunga mkono watu hao. Tutawakataa usiku, tutawakataa sirini na tutawakataa hadharani", alisema Mahinyila -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa CHADEMA Taifa (BAVICHA), Deogratius Mahinyila, amesema anaamini Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Tundu Lissu, hatanyongwa katika kesi ya uhaini inayomkabili.
Mahinyila ameyasema hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika Nyamongo, akizungumzia kesi hiyo ambayo hukumu yake inatarajiwa kutolewa Novemba 6, 2026.
Amesema vijana wa CHADEMA wanaendelea kufuatilia mwenendo wa kesi hiyo, huku akieleza kuwa haamini Lissu atahukumiwa kunyongwa.
“Mwenyekiti wetu Lissu alisema hawatamninyonga kirahisi. Na mimi naomba kuwaambia vijana wa Tanzania nzima kwamba kama Mungu alisema mwenyekiti wetu Tundu Lissu asife, hata alipopigwa risasi kumi na sita, na nyingine moja bado anayo hadi leo, Lissu hatakufa,” amesema Mahinyila. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imewaaga rasmi wateja wake 14 wanaokwenda nchini Japan kushiriki maonesho ya J-AGRI Tokyo, yanayolenga kuwawezesha kujifunza teknolojia za kisasa na ubunifu katika sekta ya kilimo.
Akizungumza leo Oktoba 5, 2026 wakati wa kuwaaga, Mkurugenzi Mtendaji wa TADB @tadbtz Frank Nyabundege amesema ziara hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa kaulimbiu ya Wiki ya Huduma kwa Wateja 2026, “The Extra Mile”, inayolenga kwenda zaidi ya utoaji wa mikopo kwa kuwawezesha wateja kupata maarifa, teknolojia na fursa za kibiashara.
Nyabundege amesema kupitia J-AGRI Tokyo, wateja hao watapata fursa ya kukutana na wazalishaji wa mashine na teknolojia za kilimo, kujifunza kuhusu kilimo cha usahihi, umwagiliaji, usindikaji, uhifadhi na uongezaji thamani wa mazao, pamoja na kujenga mahusiano ya kibiashara.
Wateja hao 14, wanaojihusisha na shughuli mbalimbali katika mnyororo wa thamani wa kilimo, wamewezeshwa na TADB mikopo yenye thamani ya zaidi ya Shilingi bilioni 62. Ziara hiyo inatarajiwa kuwasaidia kupata teknolojia na uzoefu utakaoongeza tija, ufanisi na ushindani wa shughuli zao wanaporejea nchini.
Akizungumza kwa niaba ya wateja hao 14, Kamal Simba ameishukuru TADB kwa kuwapa fursa hiyo ya kwenda Japan kujifunza teknolojia za kisasa za kilimo, akisema wanatarajia kurejea nchini na maarifa na uzoefu utakaowasaidia kuboresha shughuli zao, kuongeza tija na kukuza biashara zao.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Kutokana na gharama kubwa ya matibabu ya magonjwa ya moyo nchini hasa kwa watoto kuwa kati ya Milioni 8 hadi 25 hali inayosababisha kushindwa kupata huduma hiyo, Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) inatarajia kuandaa chakula cha jioni (Gala dinner) kwa ajili ya kuchangisha fedha zaidi Bilioni 25 ili kusaidia matibabu ya moyo kwa watoto zaidi ya 1000.
Akizungumza Oktoba 5, 2026 baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, CP Salum Hamduni, Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Dk Peter Kisenge, amesema kati ya watoto milioni 2 wanaozaliwa nchini, watoto 16,000 wana matatizo mbalimbali ya moyo ambapo kati yao 4,000 wanahitaji upasuaji wa haraka.
"Magonjwa ya moyo kwa watoto yanazidi kuongezeka kati ya watoto 100 wanaozaliwa nchini, watatu wana matatizo ya moyo, takwimu zinaonyesha watoto milioni 2 wanaozaliwa kuna watoto zaidi ya 4000 wanakuwa na matatizo ya moyo na wanahitaji oparesheni za haraka sana," amesema Dkt. Kisenge
Dkt. Kisenge amesema katika watoto hao 4,000 wanaohitaji oparesheni ya haraka, asilimia 2/3 wanatoka mikoa ya Kanda ya Ziwa hali iliyowafanya kuandaa 'gala dinner' inayotarajiwa kufanyika Novemba mwaka huu mkoani Mwanza.
Naye Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kwa Watoto ambaye pia ni Mkurugenzi wa Tiba Shirikishi JKCI, Naizihijwa Majani, amesema kati ya watoto wanne wanaofika kupata huduma kwenye hospitali hiyo mmoja anatoka mikoa ya Kanda ya Ziwa.
"Katika Takwimu zetu JKCI, kila tunapowaona watoto wanne, mmoja anatoka Kanda ya Ziwa. Namba yao ni kubwa ukilinganisha na mikoa mingine kwa sababu hiyo tumeona tusogee hapa kuchangisha fedha lakini pia kuongea na madaktari wenzetu ambao wanatoa huduma Kanda ya Ziwa kuona namna ya kushirikiana," amesema Dkt. Majani.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva, Godfrey William maarufu kwa jina la Dudu Baya, amewasili jijini Dodoma kufuatia mwaliko rasmi wa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katika video iliyochapishwa na vyombo vya habari nchini Kenya, aliyekuwa Naibu Rais wa Kenya, Rigathi Gachagua, anaonekana akitoa madai kuhusu uhusiano wa Rais William Ruto na mfanyabiashara wa Zimbabwe, Wicknell Chivayo, aliyefariki katika ajali ya helikopta nchini Zimbabwe.
Katika video hiyo ya jana Oktoba 4, 2026, Gachagua akiwa huko Marekani, amedai kuwa Chivayo alikuwa akishikilia zaidi ya KSh1.5 trilioni, sawa na takribani TSh30.4 trilioni, za Ruto, akieleza kuwa Chivayo alikuwa akitumiwa na Ruto, kuhifadhi na kuhamisha fedha. Gachagua amedai Chivayo alikuwa akitumia uwanja wa ndege binafsi katika uhamishaji huo
Hata hivyo, madai hayo hayajathibitishwa, huku Gachagua akiwa hajatoa ushahidi wa nyaraka kuyaunga mkono. Hadi wakati wa kuripotiwa kwa madai hayo, Rais Ruto au wawakilishi wake hawakuwa wametoa majibu kuhusu tuhuma hizo. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI:
Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, amesema amefarijika na kujivunia heshima kubwa inayoletwa na wanafunzi 23 wa Kitanzania wanaosoma Chuo cha Kimataifa cha Arab Academy for Science, Technology and Maritime Transport (AASTMT) nchini Misri kutokana na nidhamu na ufaulu wao wa hali ya juu.
Waziri Mbarawa aliyasema hayo jana jijini Alexandria wakati alipofanya ziara rasmi chuoni hapo na kukutana na kundi la wanafunzi hao wanaosomea fani za Uhandisi wa Meli, unahodha na biashara ya kimataifa, logistiki ya usafiri wa majini .
Akizungumza mara baada ya kupokea taarifa ya maendeleo ya wanafunzi hao kutoka kwa uongozi wa chuo, Waziri Mbarawa amewapongeza wanafunzi hao na kuwataka kuendelea kuwa mabalozi wema wa taifa.
Kwa upande wake, Rais wa Chuo hicho Prof Ismail AbdelGhafar Farag amesema kuwa anaridhishwa na mwenendo wa wanafunzi wa Tanzania, ambao amewataja kuwa ni mfano wa kuigwa chuoni hapo.
"Wanafunzi hawa ni wenye nidhamu na Wanajituma kwa bidii masomoni na wanaheshimu miongozo yote ya chuo. Ndiyo maana matokeo yao ni mazuri kila wakati. Tunawapongeza sana," anesema Rais huyo.
Naye mmoja wa wanafunzi hao, Pasiano Nemes anayesomea fani ya Uhandisi wa Meli amesema wanafurahia mazingira ya masomo na namna wanavyotendewa vizuri na waalimu wao, jambo ambalo limekuwa chachu ya mafanikio yao.
"Tunatendewa vizuri hapa na tunapewa kipaumbele cha kutosha. Mazingira mazuri na upendo wa waalimu wetu ndio siri ya matokeo yetu mazuri. Tutaendelea kusoma kwa bidii ili tukareje nyumbani tukaitumikie nchi yetu," alisema mwanafunzi huyo.
Chuo cha AASTMT ni miongoni mwa vyuo vinavyoongoza duniani katika fani za baharini, na uwepo wa wanafunzi 23 wa Tanzania hapo ni sehemu ya mkakati wa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Wanafunzi hao 23 pamoja na wengine wawili kutimiza idadi ya wanafunzi 25, wote wanasomeshwa na TPA kwa niaba ya Serikali na wamepewa ajira ya kudumu na TPA. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mtumishi wa Mungu Apostle Boniface Mwamposa(Bulldozer) amesema bilionea wa Zimbabwe marehemu Wicknell Chivayo alipiga simu kwake akitaka kuhudhuria mkesha lakini alimkatalia.
Mwamposa amesema hayo katika ibada ya jumapili iliyofanyika kanisani kwake Kawe akieleza kuwa alimkatalia Chivayo kwa sababu aliona kuwa kama angekuja basi watu wangenasibisha jambo hilo na siasa lakini pia aliogopa kwamba watu wangedhani fedha zote za kanisa hilo zinatokana na tajiri huyo.
Ameeleza kuwa Chivayo aliendelea kupiga simu lakini alikataa kupokea simu zake kutokana na hofu aliyokuwa nayo.
Pamoja na hayo amedai kuwa tajiri huyo alikuwa akiishi maisha ya kifahari na gharama kiasi ambacho hakuna ambaye angedhani kwamba atakufa siku moja.
🎥 Arise and shine tanzaniaThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Kutokana na migogoro ya ardhi inayojitokeza kati ya wawekezaji na wananchi katika maeneo mbalimbali, inayotajwa kusababishwa na baadhi ya wawekezaji kushindwa kuendeleza ardhi zao, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Kaspar Muya, amewataka wawekezaji nchini kuendeleza ardhi wanazomiliki ili kuepusha migogoro hiyo.
Akizungumza Oktoba 4, 2026 katika Kata ya Muhukuru Lilahi, Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma, wakati akikabidhi hati ya umiliki wa ardhi yenye zaidi ya hekta 3,679 kwa kampuni ya SOAGRO, Muya amesema kutokana na hali hiyo inapelekea wananchi kuvamia maeneo hayo kwaajili ya matumizi mengine.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kampuni ya SOAGRO, Dkt. Joseph Kizito Mhagama, amesema kampuni hiyo inalenga kuongeza ajira za kudumu hadi 279 na zaidi ya ajira 400 za muda kwa mwaka ifikapo mwaka 2031, huku sehemu kubwa ya nafasi hizo ikilenga vijana na wanawake.
Kwa upande wao, wananchi wa Kata ya Muhukuru Lilahi wamesema uwepo wa mwekezaji SOAGRO katika maeneo yao utaongeza kwa kiasi kikubwa chachu ya maendeleo katika vijiji vya kata hiyo, ambayo ipo mpakani mwa Tanzania na Msumbiji.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwekezaji mkubwa barani Afrika, Aliko Dangote kupitia Kampuni ya Dangote ameonesha nia ya kufungua kiwanda kikubwa cha uzalishaji wa mbolea katika Eneo Maalum la Kiuchumi la Bagamoyo (Bagamoyo SEZ) mkoani Pwani, hatua inayolenga kuchochea ukuaji wa sekta ya kilimo na kuongeza fursa za kiuchumi nchini
Suala hilo limeelezwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo @kitilam , alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wilayani Bagamoyo mkoani Pwani wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji na maendeleo ya miradi ya kipaumbele katika eneo hilo la Bagamoyo SEZ.
Awali alipokuwa akioneshwa ramani ya Bagamoyo SEZ, Prof. Kitila alimuuliza Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) @InvestTanzania , Gilead John Teri iwapo Dangote ameshatengewa eneo lake la uwekezaji, na Teri akaeleza kuwa tayari hilo limeshafanyika.
Mradi huo wa kiwanda cha mbolea unakwenda kuongeza mnyororo wa thamani katika sekta ya kilimo na uwekezaji kwenye eneo hilo maalumu la Bagamoyo ambalo kiujumla limetengewa hekta 9,800.
Halikadhalika, eneo hilo limepangwa kuhusisha ujenzi wa bandari mpya, viwanda vya uchakataji wa mazao, madawa, nguo, pamoja na kongani za teknolojiaThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI:
Tanzania inatarajia kuwa mwenyeji wa Mkutano wa 12 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Nairobi (COP12), utakaofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 6 hadi 9, 2026, katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC).
Akizungumza kuhusu maandalizi ya mkutano huo leo Oktoba 4, 2026, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mhandisi Hamad Masauni, amesema Tanzania imepewa heshima hiyo kutokana na umuhimu wa kuimarisha usimamizi na uhifadhi wa mazingira ya bahari na pwani katika Bahari ya Hindi Magharibi.
Mkutano huo utaongozwa na kaulimbiu ya kitaifa isemayo, “Kuelekea Uchumi wa Buluu Endelevu katika Ukanda wa Magharibi wa Bahari ya Hindi kwa Manufaa ya Watu na Mazingira ya Asili: Safari ya Miaka 40".
Kwa mujibu wa Waziri Masauni, miongoni mwa masuala yatakayojadiliwa ni udhibiti wa uchafuzi wa bahari na pwani, uimarishaji wa ushirikiano wa kikanda, kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kuongeza ustahimilivu wa jamii, miundombinu na mifumo ya ikolojia ya pwani.
Aidha, mkutano huo utajadili uhifadhi wa bioanuai za bahari na pwani, ikiwemo mikoko, matumbawe, nyasi bahari na maeneo muhimu ya ikolojia. Pia, wajumbe wataangalia namna ya kuendeleza Uchumi wa Buluu kwa kuunganisha uhifadhi wa mazingira na uwekezaji, biashara, ajira pamoja na maendeleo ya jamii za pwani.
Mkutano wa COP12 pia unatarajiwa kuimarisha ushirikiano wa kisayansi na kiteknolojia, ikiwemo matumizi ya mpango wa matumizi ya maeneo ya bahari, unaojulikana kwa Kiingereza kama 'Marine Spatial Planning'. Hatua hiyo inalenga kuhakikisha maamuzi kuhusu rasilimali za bahari yanafanyika kwa kuzingatia taarifa na ushahidi wa kisayansi.
Waziri Masauni amesema kuwa Tanzania inatarajia kunufaika na mkutano huo kupitia kuimarika kwa diplomasia ya mazingira, kuongezeka kwa ushawishi katika masuala ya bahari na pwani, pamoja na kuvutia fedha, teknolojia na uwekezaji kwa ajili ya uhifadhi wa mazingira, udhibiti wa uchafuzi na miradi ya Uchumi wa Buluu.
Ameongeza kuwa mkutano huo unaweza kutoa Azimio la Dar es Salaam na kuongeza fursa kwa jamii za pwani kupitia uvuvi endelevu, ufugaji wa viumbe maji, utalii wa baharini, kilimo cha mwani, usafiri wa majini na shughuli nyingine za kiuchumi.
Aidha, Serikali imetoa wito kwa taasisi za umma, sekta binafsi, wanazuoni, watafiti, mashirika ya kiraia na wananchi kushiriki kikamilifu katika maandalizi na utekelezaji wa matokeo ya COP12.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri Mkuu wa Tanzania Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Jumapili, Oktoba 4, 2026, amesimikwa rasmi kuwa Kanoni Mlei (Lay Canon) wa Kanisa Anglikana Tanzania katika ibada iliyofanyika katika Kanisa Kuu Anglikana la Kristo Mfalme Chanika, Dayosisi ya Handeni, mkoani Tanga.
Dkt. Mwigulu amesimikwa katika wadhifa huo katika Ibada ya Misa Takatifu ya kuwekwa wakfu kwa Kasisi Canon Charles Mika Lundu kuwa Askofu wa Dayosisi ya Handeni. Dkt. Mwigulu alishiriki ibada hiyo kwa niaba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Waziri Mkuu alitunukiwa cheo cha Kanoni Mlei na Kanisa Anglikana Tanzania, chini ya Askofu Mkuu wa Kanisa hilo, Dkt. Maimbo Mndolwa, Juni 21, 2026, katika Harambee ya kukamilisha mradi wa jengo la Kitega Uchumi cha Kanisa Anglikana Tanzania iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Roho Mtakatifu, Jimbo la Dodoma.
Kanisa Anglikana Tanzania lilimtunuku Waziri Mkuu cheo hicho kwa kutambua mchango wake katika kuhamasisha na kufanikisha uchangishaji wa fedha kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo na vitega uchumi vya Kanisa hilo, tangu alipokuwa akitumikia nyadhifa mbalimbali za Serikali na kijamii.
Kutunukiwa cheo hicho na hatimaye kusimikwa rasmi leo katika ibada iliyoongozwa na Askofu Mkuu wa Kanisa Anglikana Tanzania, Dkt. Maimbo Mndolwa, kumemfanya Waziri Mkuu kuungana na viongozi wengine wa Serikali waliowahi kutunukiwa wadhifa huo, huku akiwa Kanoni Mlei wa kwanza kutoka nje ya dhehebu la Anglikana, kwa mujibu wa taarifa hiyo.
Viongozi wengine waliowahi kutunukiwa cheo cha Kanoni Mlei (Lay Canon) ni pamoja na Spika Mstaafu, Hayati Job Yustino Ndugai; Jaji Mkuu Mstaafu, Hayati Augustino Steven Lawrence Ramadhani; na Profesa Palamagamba John Kabudi, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu). Wengine ni Baraka Leonard, Katibu wa Bunge, pamoja na Gerald Mweli, Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo.
Kwa mujibu wa taratibu za Kanisa Anglikana, Kanoni Mlei ni cheo cha heshima katika Kanisa hilo, ambacho miongoni mwa majukumu yake ni kutoa ushauri na kuwa mlezi wa uongozi wa juu wa Kanisa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira, Mhandisi Hamad Yusuf Masauni, amewataka viongozi katika ngazi zote kusimamia kikamilifu utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, akisisitiza kuwa hakuna kiongozi anayepaswa kuwa na ubavu wa kuyapuuza au kutotekeleza maelekezo hayo.
Mhandisi Masauni ameyasema hayo Jumamosi wakati akishiriki zoezi la usafi katika eneo la Kariakoo, Wilaya ya Ilala, Mkoa wa Dar es Salaam, ambapo amewapongeza viongozi, wananchi na wadau mbalimbali kwa kushiriki katika kuhakikisha mazingira ya Jiji la Dar es Salaam yanakuwa safi na ya kuvutia. Amesema maelekezo ya kufanya usafi kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi yanapaswa kwenda sambamba na utaratibu wa kuhakikisha usafi unafanyika kila siku.
“Maelekezo ya Mhe. Rais lazima yasimamiwe na kutekelezwa. Hakuna kiongozi anayepaswa kuwa na ubavu wa kuyapuuza au kutotekeleza maelekezo hayo. Wajibu wetu ni kuhakikisha utekelezaji unafanyika kwa vitendo na matokeo yanaonekana kwa wananchi,” amesema Mhandisi Masauni.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Elihuruma Mabelya amebainisha kuwa tangu kuanza kwa zoezi hilo mwezi Septemba, hatua mbalimbali za kisheria na za kutoa elimu zimechukuliwa ili kuhakikisha jiji linakuwa safi.
"Tangu zoezi hili limeanza mwezi Septemba mpaka leo, watu waliokamatwa kwa kukiuka sheria hiyo ni 552. Watu 143 walikutwa na hatia na hivyo kupelekwa jela... lakini watu 404 walilipa faini kiasi cha Shilingi milioni 10,789,500. Wananchi ambao wameshafikiwa kwenye utoaji wa elimu ni 3,430.", ameeleza.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo aliahidi kuwa kampeni hizo za usafi zitakuwa endelevu usiku na mchana, huku akitangaza agizo la miezi mitatu kwa kampuni zote za ukandarasi wa taka kununua magari ya kisasa ili kufanya zoezi la usafi kuwa na ufanisi na uendelevu katika wilaya hiyo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu Mwenyekiti Taifa (Bara) wa ACT Wazalendo, Isihaka Mchinjita, amewataka wabunge wa chama hicho kuikataa Bungeni tozo mpya ya Sh250 kwa kila kilo ya korosho inayopendekezwa kuchangia Mfuko wa Maendeleo ya Taifa (National Development Fund).
Mchinjita alitoa kauli hiyo jana Octoba 2, 2026, katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Kitama, Jimbo la Tandahimba, mkoani Mtwara.
Amesema tozo hiyo itaongeza mzigo kwa wakulima wa korosho wa Kusini ambao, kwa mujibu wake, tayari wanakabiliwa na makato mbalimbali.
Mchinjita alidai mkulima anayezalisha na kupeleka tani moja ya korosho, sawa na kilo 1,000, huchangia hadi Sh1.5 milioni kwa mwaka kupitia tozo mbalimbali, ikiwemo za halmashauri na Sport Levy.
“Mfanyakazi wa sekta ya umma anayepata mshahara wa chini anakatwa Sh90,000 kwa mwezi, sawa na Sh1.08 milioni kwa mwaka. Yeye anapata bima ya afya inayomtibu yeye, mke au mume, wazazi na watoto, jumla watu wanane. Lakini mkulima wa korosho anayechangia milioni 1.5 hana bima yoyote. Anapoumwa, daktari anamlipa shilingi ngapi? Dawa anazipata wapi?” alihoji Mchinjita.
Alisema ACT Wazalendo ina mpango wa kuhakikisha wakulima wa korosho wanapata bima ya afya kama ilivyo kwa baadhi ya makundi ya wafanyakazi, akisisitiza kuwa wakulima wanapaswa kunufaika na huduma za kijamii kutokana na mchango wao katika uchumi.
“Tunataka mambo haya yakataliwe,” alihitimishaThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Wakulima wa tumbaku mkoani Tabora wamemlilia Waziri wa Kilimo, Daniel Chongolo, kuhusu mwenendo wa bei ya ununuzi wa zao hilo katika msimu wa kilimo wa 2025/2026, wakisema bado hawajapata taarifa za bei ya pembejeo kwa msimu mpya.
Hayo yamebainishwa Oktoba 3, 2026, wakati wa kikao maalum cha kusikiliza na kutatua changamoto za wakulima. Wakulima wamelalamika kuwa katika msimu uliopita walilazimika kuuza tumbaku yao kwa bei iliyokuwa chini ya bei elekezi ya Serikali ya dola 1.95 kwa kilo, hali waliyosema imeongeza mzigo wa gharama za uzalishaji na maisha.
Akijibu, Waziri Chongolo amesema ndani ya siku kumi atakutana na wataalamu wa sekta ya tumbaku na wadau wengine ili kupitia changamoto hizo na kutafuta majawabu yatakayosaidia kuboresha hali ya wakulima, huku akiwahakikishia upatikanaji wa pembejeo.
Kuhusu madai ya baadhi ya kampuni za ununuzi wa tumbaku kuwa na madeni kwa wakulima ambayo hayajalipwa tangu msimu uliopita, Waziri Chongolo amezitaka kampuni hizo kuhakikisha zinalipa ndani ya siku fedha wanazodaiwa wakulima ndani ya siku 30 ili kuwawezesha kuendelea na shughuli zao za kilimo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu, amesema Bunge la sasa halina kambi rasmi ya upinzani kwa sababu wabunge wa upande wa wachache ni 11 tu, sawa na asilimia tatu.
Alitoa kauli hiyo jana Oktoba 2, 2026 katika mkutano wa hadhara wilayani Tandahimba, kata ya Kitama, mkoani Mtwara.
Ado alisema mwaka 2015 upande wa wachache ulikuwa na wabunge zaidi ya 100, lakini sasa wamebaki 11. Kwa mujibu wake, ili kuwa na kambi rasmi ya upinzani inahitajika angalau asilimia 12 ya wabunge.
Alieleza kuwa waliwahi kuwa na mjadala mkali kama waende bungeni au la, baadhi wakisema CCM hawana haya na wakiwachwa peke yao hakutakuwa na mtu wa kupaza sauti kutetea wananchi, barabara, kuibua ufisadi n.k.
Hatimaye walikubaliana kwenda bungeni si kuuza sura wala kupiga meza, bali kupaza sauti kwa niaba ya raia wa Tanzania.
“Sisi wachache tutaunguruma kama mia. Pengine wataona haya japo kidogo. Bunge ni uwanja wa mapambano na ushindi wake ni kuibua madudu, kuzungumza mambo ambayo hawatarajii,” alisisitiza Ado.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Nicodemus Tambo Mwikazo, ametoa onyo kwa vijana wanaojihusisha na vitendo vya wizi na ukabaji wilayani humo, akisisitiza kuwa hawatavumiliwa na kwamba muda wao wa kufanya uhalifu umefika mwisho.
Akizungumza kwa mara ya kwanza Oktoba 3, 2026 wilayani humo, Mwikazo amesema jukumu lake kubwa kama Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ni kuhakikisha Arusha inaendelea kuwa sehemu salama kwa wananchi, wawekezaji na wageni.
Amesema atahakikisha anasimamia kikamilifu usalama wa wananchi kwa kusimamia sheria akisisitiza kuwa hatua stahiki dhidi ya watakaobainika kujihusisha na vitendo hivyo vya uhalifu zitachukuliwa.
Aidha amesema ataimarisha ukusanyaji wa mapato ya Serikali ili kuboresha huduma za kijamii.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Wanafunzi wa Dini ya Kiislamu wanao hitimu kidato cha nne mwaka huu, wametakiwa kutumia elimu na malezi waliyoyapata kujenga maisha yenye uwajibikaji, uzalendo na kuheshimu sheria, huku wakiepuka vitendo vya chuki, ubaguzi na vurugu vinavyoweza kugawanya jamii.
Rai hiyo imetolewa Oktoba 3, 2026, na Mbunge wa Moshi Mjini, Ibrahim Shayo, wakati wa mahafali yaliyofanyika katika Ofisi za Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Mkoa wa Kilimanjaro, yaliyowakutanisha wanafunzi wahitimu kutoka shule nne za Kiboriloni, Masoka, Mabogini na Korongoni.
Shayo amesema hatua ya kumaliza kidato cha nne ni mwanzo wa safari nyingine ya maisha kwa vijana hao, hivyo amewataka kutumia elimu waliyoipata kujitofautisha kwa matendo mema, kuheshimu sheria na taratibu na kuzingatia maadili ya Mtanzania.
Amesema vijana wanapokosa misingi ya uzalendo, uvumilivu na kuheshimu tofauti za wengine, wanaweza kushawishika kushiriki katika vitendo vinavyoweza kuvuruga amani na mshikamano wa jamii.
"Dini yetu inatufundisha kuheshimu watu na kuishi kwa amani pamoja na kuzungumzia amani hivyo epukeni chuki, ubaguzi na vurugu zinazo weza kuigawa jamii" amesema Shayo.
Kwa upande wake, Katibu wa Jumuiya ya Wanafunzi na Vijana wa Kiislamu (TAMSYA) Mkoa wa Kilimanjaro, Abdulkareem Nzogera, amesema jumuiya hiyo imeundwa kwa malengo ya kuwaunganisha na kuwaelimisha wanafunzi na vijana wa Kiislamu ili kuwaandaa kukabiliana na changamoto za maisha.
Amesema TAMSYA inalenga kuwajengea vijana uwezo katika nyanja za maendeleo ya kiroho, kijamii, kiuchumi na kimazingira, ili elimu wanayoipata darasani iambatane na uwezo wa kushiriki katika maendeleo ya jamii.
Naye Katibu wa BAKWATA Moshi Mjini, Sheikh Abdullah Mfaume, amewataka wahitimu hao kuendelea kuitumia elimu yao kwa kumtumikia Mwenyezi Mungu na jamii, wakizingatia maadili na wajibu wao katika shughuli mbalimbali watakazokutana nazo baada ya kumaliza elimu ya sekondari.
Amesema hatua ya kuhitimu kidato cha nne isiwe mwisho wa kujifunza, bali iwe mwanzo wa kutafuta maarifa zaidi na kujenga maisha yenye manufaa kwao, familia zao na jamii kwa ujumla.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Serikali imetangaza kuwa ipo katika hatua za mwisho za kukamilisha tathmini ili kuanza kulipa fidia ya awamu ya pili kwa wananchi wa Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani waliotwaliwa maeneo yao kupitia mradi wa Eneo Maalum la Kiuchumi la Bagamoyo (Bagamoyo SEZ).
Hatua hiyo imebainishwa leo Jumamosi Oktoba 3, 2026 wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo ya kukagua utekelezaji wa miradi ya kipaumbele katika eneo hilo.
Akiwasilisha maombi ya wananchi waliosubiri fidia kwa muda mrefu, Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, Subira Khamisi Mgalu ameeleza kuwa ingawa baadhi ya maeneo tayari yamelipiwa fidia na mengine bado, matunda ya mradi huo tayari yanaonekana kupitia fursa za ajira kwa vijana wa Bagamoyo, pamoja na kupelekwa kwa miundombinu ya barabara na umeme katika maeneo hayo ya uwekezaji.
Prof. Kitila amemhakikishia mbunge na wananchi wa Bagamoyo kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amelipa kipaumbele kikubwa eneo hilo na kwamba hakuna mwananchi atakayepoteza haki yake ya fidia
“Mheshimiwa mbunge nikuhakikishie serikali itaenda kulipa fidia na sasa tunakamilisha tathmini ili tuende kulipa fidia kwa awamu ya pili. Na mheshimiwa Rais hili ni eneo ambalo amelipa kipaumbele, lakini tumeweka utaratibu mpya kwanza TISEZA wenyewe kwenye mapato yao watatumika pia kulipa fidia. Lakini wawekezaji pia tunawashirikisha na serikali yenyewe. Kwahiyo wananchi wetu wa Bagamoyo wawe na uhakika haki zao haziwezi kupotea”, ameeleza Prof. Kitila.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu Ado, amesema eneo la Kusini mwa Tanzania limeachwa nyuma katika maendeleo licha ya kuwa na mchango mkubwa katika uchumi wa Taifa, akidai kuwa kwa miaka mingi eneo hilo limegeuzwa kuwa “shamba la bibi”.
Ado ameyasema hayo jana alipohutubia wananchi katika Kata ya Kitama, Jimbo la Tandahimba, mkoani Mtwara, ambapo alieleza changamoto zinazowakabili wananchi wa Kusini, ikiwemo hali ya barabara.
Amesema wakulima wa korosho katika mikoa ya Kusini wamekuwa miongoni mwa wachangiaji wakubwa wa fedha za kigeni kupitia zao hilo, lakini pamoja na mchango huo, miundombinu ya barabara imeendelea kuwa changamoto.
“Barabara zimegeuka andaki,” alisema Ado, akieleza kuwa hali hiyo inahitaji hatua za haraka, hususan wakati ambapo mvua zinatarajiwa kunyesha.
Ado alisema ACT Wazalendo itaendelea kutetea maslahi ya wananchi wa Kusini na kuahidi kurejea Kitama kwa ajili ya kuzungumza zaidi na wananchi kuhusu changamoto zinazowakabili.
Mbali na changamoto za maendeleo, Ado alisisitiza misimamo ya chama hicho kuhusu masuala ya kisiasa na utawala, akidai kuwa uchaguzi wa mwaka 2025 haukufanyika kwa usafi na kwamba kulikuwa na ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi.
Amesema ACT Wazalendo inataka Katiba mpya na kwamba mchakato wa kuipata uanze sasa, huku akitaka pia vyombo vya ulinzi na usalama kujitenga na siasa ili kutekeleza majukumu yao kwa weledi na haki.
Ado aliwataka wananchi kuendelea kueleza kero zinazowakabili, akisema ACT Wazalendo itaendelea kuwasemea na kutumia Bunge pale inapohitajika.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, amesema kuwa Serikali imedhamiria kulifanya Eneo Maalum la Kiuchumi la Bagamoyo (Bagamoyo SEZ) kuwa mji mpya wa kisasa wa kiuchumi na kitovu cha viwanda kama ulivyo mji maarufu wa Shenzhen nchini China.
Prof. Kitila ameyasema hayo leo Jumamosi Oktoba 3, 2026 alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji na maendeleo ya miradi ya kipaumbele katika eneo hilo lililopo wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.
Akibainisha dira ya eneo hilo, Prof. Kitila ameeleza kuwa Bagamoyo SEZ inajengwa kwa kuhusisha viwanda vya kila aina vikiwemo vya nguo vinavyozalisha ajira nyingi, viwanda vya dawa, na kemikali mbalimbali, pamoja na eneo la teknolojia litakalokuwa kielelezo cha Silicon Valley ya Tanzania.
Prof. Kitila ameongeza kuwa eneo hilo litabadilika na kuwa mji wa kisasa uliokamilika wenye hoteli za kifahari, makazi mazuri, bandari ya kisasa, na miundombinu ya reli inayounganisha hadi Bandari ya Kwala huku Serikali ikitazama uwezekano wa kujenga barabara mpya ya kuunganisha moja kwa moja hadi mkoani Tanga.
Kuhusu suala la fidia kwa wananchi wa Bagamoyo walioasisi maeneo yao kwa ajili ya mradi huo, Waziri Kitila amewatoa hofu wananchi hao kwa kueleza kuwa hakuna mwananchi atakayepoteza haki yake, kwani tathmini inakamilishwa ili kulipa fidia ya awamu ya pili kupitia mchanganyiko wa mapato ya TISEZA, mchango wa Serikali, na kushirikisha wawekezaji
Katika hatua nyingine, Prof. Kitila ametoa wito kwa wawekezaji na wamiliki wa viwanda eneo hilo kujihusisha kikamilifu na maendeleo ya jamii inayowazunguka (CSR) kwa kujenga shule na zahanati, akibainisha kuwa kuelekea mwaka 2028 Tanzania itahitaji shule nyingi za sekondari kufuatia uamuzi wa Serikali wa kufanya elimu ya sekondari kuwa ya lazima kwa watoto wote.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, amewataka wawekezaji na wamiliki wa viwanda katika Eneo Maalum la Kiuchumi la Bagamoyo (Bagamoyo SEZ) kujihusisha kikamilifu na maendeleo ya jamii inayowazunguka kwa kujenga shule, zahanati, vituo vya afya pamoja na miundombinu nyingine itakayonufaisha jamii inayozunguka miradi hiyo.
Prof. Kitila ametoa wito huo leo Jumamosi, Oktoba 3, 2026 wilayani Bagamoyo, mkoani Pwani wakati akizungumza na wanahabari kuhusu ziara yake ya kukagua utekelezaji na maendeleo ya miradi ya kipaumbele katika eneo hilo.
Waziri Kitila ameeleza kuwa wawekezaji hao tayari wameshakuwa sehemu ya jamii ya Bagamoyo, hivyo ni vyema wakahakikisha wanatoa mchango wa dhati katika ustawi wa kijamii na kiuchumi wa wananchi wa eneo hilo kupitia uwajibikaji wa kijamii wa kampuni (CSR).
Amesisitiza kuwa kuelekea mwaka 2028, Tanzania inahitaji shule nyingi za sekondari kutokana na uamuzi wa Serikali wa kufanya elimu ya sekondari kuwa ya lazima na kwa wote jambo ambalo Serikali pekee haitaweza kulitekeleza kwa kasi inayotakiwa bila ushirikiano na sekta binafsi.
“Kwahiyo, tunawakaribisha sana, itakuwa ni aibu kuwa na miundombinu mizuri namna hii halafu hapo pembeni kidogo mkawa na shule iliyochakaa sana. Lakini ninaamini mtashirikiana nasi katika shughuli za maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa manufaa ya watu wetu”, ameeleza Prof. Kitila akiongeza kuwa hatua hiyo pia itasaidia wawekezaji hao kujenga uhusiano wa karibu na wa amani na jamii inayowazunguka.
Katika ziara hiyo, Prof. Kitila ameeleza pia kuwa Serikali inalenga kuifanya Bagamoyo kuwa mji mpya wa kisasa wa kiuchumi, viwanda na teknolojia kama ulivyo mji wa Shenzhen nchini China huku ikipanga kuwekeza kwenye miundombinu ya barabara, maji, umeme, reli, na kupanua fursa za ajira kwa vijana wa Bagamoyo.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalumu ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA), Gilead Teri amebainisha kuwa mpaka sasa takriban viwanda 25 vimeshaanzishwa Bagamoyo SEZ, vikiwa vimevuta mitaji ya dola za Marekani bilioni 1.5 na kutoa fursa za ajira zaidi ya 15,600 kwa Watanzania.
Teri ameongeza kuwa TISEZA inaendelea kuwapongeza wawekezaji wa ndani kutoka Tanzania, kikanda kutoka Afrika Mashariki na SADC, pamoja na wawekezaji wa kimataifa waliowekeza ili kutoa fursa za ajira kwa vijana wa Kitanzania.
Naye Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, Subira Khamisi Mgalu, ameunga mkono wito wa Prof. Kitila kwa kuomba TISEZA iwaunganishe wananchi na wawekezaji hao ili wawe chachu ya kusaidia ujenzi wa miundombinu ya afya na elimu.
Ameeleza kuwa mradi wa Bagamoyo SEZ ulikuwa umekwama kwenye makabrasha kama ndoto kwa zaidi ya miaka 16 iliyopita, lakini sasa Serikali ya Awamu ya Sita imegeuza ndoto hiyo kuwa halisi kupitia ujenzi wa viwanda na uboreshaji wa miundombinu ya barabara, maji na umeme. Aidha, Subira amepongeza pia hatua ya TISEZA kuleta ofisi yake karibu na eneo la uwekezaji Bagamoyo ili kurahisisha mawasiliano na wananchi. -
Jambo TV
@Jambotv_
Picha mbalimbali za droni zikionesha mwonekano wa juu wa baadhi ya miradi ya Eneo Maalum la Kiuchumi la Bagamoyo (Bagamoyo SEZ) ambayo imetembelewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, leo Jumamosi, Oktoba 3, 2026 wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.
Katika ziara hiyo, Prof. Mkumbo ametembelea miradi sita (6), vikiwemo viwanda vilivyopo katika hatua mbalinbali za ujenzi huku vingine vikiwa tayari vinazalisha bidhaa.
Baadhi ya miradi hiyo ni kiwanda cha Aarsal Steel Mill Limited kilichopo kwenye eneo la hekta saba kwa ajili ya kuzalisha nondo, misumari, na vifaa vingine vya ujenzi kwa uwekezaji wa Dola za Kimarekani 250,000 ambapo tayari kimeajiri watu 50 kati ya 350 vinavyotarajiwa.
Aidha, kuna kiwanda cha Canaries Industrial Limited, mradi wa mwekezaji wa ndani Rishit Radia uliopo kwenye hekta moja unaohusika na uzalishaji wa vifungashio kwa mtaji wa Dola 400,000, kabla ya kutembelea kiwanda cha maji cha Farvio Glo Industries kinachomilikiwa na mwekezaji wa ndani Faraja Kotta, ambapo kimejengwa kwenye hekta mbili kwa uwekezaji wa Dola 700,000 kwa ajili ya kuzalisha vinywaji kama maji safi ya kunywa.
Eneo lingine muhimu ni Yintae Motorcycle Factory Tanzania, mradi mkubwa uliopangiwa ekari 50 unaojihusisha na uunganishaji na uzalishaji wa pikipiki, bajaji, na baiskeli za miguu mitatu zinazotumia umeme kwa mtaji wa Dola za Kimarekani milioni 55 uliopanga kutoa ajira 200.
Aidha, kuna kiwanda kikubwa cha nguo cha Sinovest kinachomilikiwa na mwekezaji kutoka China, ambacho kimeshaanza uzalishaji wa jezi na fulana katika eneo lenye mita za mraba 210,080 baada ya kuwekeza Dola za Kimarekani milioni 50, kikiwa kinalenga masoko ya ndani, nje, na nchi za Ghuba ya Uajemi huku kikitarajia kuajiri vijana 10,000 kufikia mwaka 2027.
Halikadhalika, kuna Kongani ya Viwanda ya Hongwang Tanzania (HWTZ SEZ) iliyopewa eneo la hekta 500 kwa ajili ya uwekezaji wa Dola za Kimarekani bilioni 1.5 unaojumuisha pia matumizi ya gesi inayozalishwa Mtwara. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI PICHA:
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, leo Jumamosi, Oktoba 3, 2026, amefanya ziara ya kikazi kukagua utekelezaji wa miradi ya kipaumbele katika Eneo Maalum la Kiuchumi la Bagamoyo (Bagamoyo SEZ) wilayani Bagamoyo, mkoani Pwani.
Ziara hiyo inajiri ikiwa ni takriban miezi tisa tangu kufanyika kwa makabidhiano ya hati kwa wawekezaji mnamo Desemba 30, 2025, katika eneo hilo lenye ukubwa wa hekta 9,800. Prof. Kitila amejionea mabadiliko makubwa kutoka eneo ambalo awali lilionekana kuwa tupu hadi kufikia hatua ya ujenzi na uendeshaji wa viwanda 25 vilivyopo kwa sasa, ambapo katika ziara ya leo ametembelea viwanda sita vikubwa vyenye thamani ya takriban Dola za Kimarekani bilioni 1.567 ambavyo vinatarajiwa kuzalisha ajira 15,675 kwa Watanzania.
Katika ziara hiyo, Prof. Kitila alianza kwa kutembelea kiwanda kinachojengwa cha Aarsal Steel Mill Limited kilichopo kwenye eneo la hekta saba kwa ajili ya kuzalisha nondo, misumari, na vifaa vingine vya ujenzi kwa uwekezaji wa Dola za Kimarekani 250,000 ambapo tayari kimeajiri watu 50 kati ya 350 vinavyotarajiwa.
Aliendelea na ukaguzi katika Canaries Industrial Limited, mradi wa mwekezaji wa ndani Rishit Radia uliopo kwenye hekta moja unaohusika na uzalishaji wa vifungashio kwa mtaji wa Dola 400,000, kabla ya kutembelea kiwanda cha maji cha Farvio Glo Industries kinachomilikiwa na mwekezaji wa ndani Faraja Kotta, ambapo kimejengwa kwenye hekta mbili kwa uwekezaji wa Dola 700,000 kwa ajili ya kuzalisha vinywaji kama maji safi ya kunywa.
Eneo lingine muhimu alilolikagua ni Yintae Motorcycle Factory Tanzania, mradi mkubwa uliopangiwa ekari 50 unaojihusisha na uunganishaji na uzalishaji wa pikipiki, bajaji, na baiskeli za miguu mitatu zinazotumia umeme kwa mtaji wa Dola za Kimarekani milioni 55 uliopanga kutoa ajira 200.
Pamoja na hayo, alitembelea kiwanda kikubwa cha nguo cha Sinovest kinachomilikiwa na mwekezaji kutoka China, ambacho kimeshaanza uzalishaji wa jezi na fulana katika eneo lenye mita za mraba 210,080 baada ya kuwekeza Dola za Kimarekani milioni 50, kikiwa kinalenga masoko ya ndani, nje, na nchi za Ghuba ya Uajemi huku kikitarajia kuajiri vijana 10,000 kufikia mwaka 2027.
Mwisho wa ziara hiyo, Prof. Kitila alitembelea Kongani ya Viwanda ya Hongwang Tanzania (HWTZ SEZ) iliyopewa eneo la hekta 500 kwa ajili ya uwekezaji wa Dola za Kimarekani bilioni 1.5 unaojumuisha pia matumizi ya gesi inayozalishwa Mtwara. Mpaka mwezi Septemba, 2026 mwekezaji huyu ameshatumia zaidi ya Dola za Marekani milioni 15. Kongani hiyo inatarajia kuwa na jumla ya viwanda 150, ambapo kwa sasa imeshaanza ujenzi wa kiwanda cha Rafiki Automobile cha kuunganisha magari makubwa na madogo yanayotumia gesi, na mpaka sasa mwekezaji huyo ameshaajiri Watanzania 147 na kupanga kuongeza idadi hiyo hadi kufikia 447 mwakani kabla ya kufikisha jumla ya ajira 5,000 hapo baadaye. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Kundo Mathew, ameipa siku 30 Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu kufanya tathmini ya mwenendo wa vyanzo vya maji, ili kubaini hali ya upatikanaji wa maji pamoja na muda ambao Bwawa la Kidunda linaweza kufikia ujazo unaohitajika.
Mhandisi Kundo ametoa maelekezo hayo Oktoba 3, 2026 alipofanya ziara katika Bwawa la Kidunda, mradi unaolenga kuongeza upatikanaji wa maji kwa mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Morogoro.
Amesisitiza umuhimu wa kudhibiti shughuli za kibinadamu zinazoweza kuathiri vyanzo hivyo, pamoja na kuhakikisha mazingira yanahifadhiwa kwa ajili ya usalama na uendelevu wa Bwawa la Kidunda.
Kwa upande wake Msimamizi wa Mradi wa Ujenzi wa Bwawa la Kidunda, Mhandisi Christian Gava, amesema ujenzi wa bwawa hilo umefikia asilimia 65, huku akieleza kuwa utekelezaji wa mradi unaendelea kwa kuzingatia hatua mbalimbali za ujenzi.
Amesema kukamilika kwa mradi huo kutasaidia kuongeza uwezo wa upatikanaji na uhifadhi wa maji kwa Mikoa inayolengwa, pamoja na kuimarisha upatikanaji wa maji kwa matumizi mbalimbali.
Naye Mkuu wa Sehemu ya Maji Juu ya Ardhi na Usalama wa Mabwawa kutoka Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu, Mhandisi Pascal Joseph, amesema bodi hiyo imeanza kuweka alama za mipaka kuzunguka eneo la bwawa hilo kwa lengo la kulinda eneo la mradi dhidi ya uvamizi na shughuli zinazoweza kuhatarisha usalama wa bwawa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
#ad
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Nchi ya Qatar, Tume ya Umoja wa Afrika na washiriki kutoka nchi wanachama wa Baraza la Ushirikiano la Nchi za Ghuba (Gulf Cooperation Council - GCC) imeandaa Mkutano wa Pili wa Uhamaji wa Nguvu Kazi (Second Doha Dialogue on Labour Mobility).
Mkutano huo unaratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira na Mahusiano na utafanyika kuanzia Oktoba 5 - 6, 2026 katika hoteli ya Hyatt Regency, Dar es Salaam ukiongozwa na kaulimbiu “Kuendeleza Uhamaji wa Nguvu kazi yenye Haki na endelevu katika ya Nchi za Afrika na Ghuba (GCC+). -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Angellah Kairuki, amesema Serikali imetenga shilingi bilioni 5 kwa ajili ya kuwawezesha mitaji kampuni changa za TEHAMA, ikilenga kukuza ubunifu, ujasiriamali na kuongeza fursa za ajira kwa vijana katika sekta ya teknolojia, akiwakumbusha wahusika wa fedha hizo kwamba ni “fedha za moto”.
Ameeleza hayo Oktoba 2, 2026 wakati wa hafla ya uzinduzi wa programu ya kuwawezesha mitaji kampuni changa za TEHAMA Jijini Dodoma.
"Kwa upande wa wanufaika ndugu zangu wabunifu, ni lazima fedha hizi, ni fedha za moto, mnazijua fedha za moto?, fedha za moto, mmeona jopo hilo watu kumi na tatu siyo wa mchezo, mkazielekeze kwa mtakaopata katika shughuli zilizokusudiwa" amesema Kairuki.
Aidha Waziri Kairuki amewataka vijana na kampuni zitakazonufaika na fedha hizo kuzitumia kwa malengo yaliyokusudiwa, akisisitiza kuwa ubunifu ni fursa muhimu ya kukuza biashara, uwekezaji, ajira na kuchochea ukuaji wa uchumi wa kidijitali.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Wanawake wametakiwa kujitokeza kushiriki katika mchezo wa mbio za magari kama ilivyo kwa michezo mingine, ili kuongeza ushiriki wa wanawake na kuchangia katika kukuza mchezo huo nchini.
Wito huo umetolewa Oktoba 2, 2026, mkoani Morogoro, katika uzinduzi wa mashindano ya Serengeti Rally of Tanzania, ambapo washiriki na waandaaji wa mashindano hayo wameeleza kuwa ni wakati sasa kwa wanawake kuutazama mchezo wa mbio za magari kama michezo mingine na kujitokeza kushiriki.
Mshiriki wa mashindano hayo kutoka Uganda, Susan Muwonge, amesema kujiamini ni miongoni mwa mambo muhimu yanayomsaidia mtu kufikia malengo yake, akieleza kufurahishwa na kuwa mwanamke pekee anayeshiriki katika mashindano hayo.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mussa Kilakala, amesema Serikali ipo tayari kuwaunga mkono wanawake wanaotaka kushiriki katika mchezo huo.
Naye Msimamizi Mkuu wa mashindano hayo, Mosi Makau, ameeleza kuwa mashindano hayo yanatarajiwa kutoa fursa mbalimbali za kiuchumi na kuchangia kukuza uchumi wa Mkoa wa Morogoro.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu- Kazi, Ajira na Mahusiano, Deus Sangu, amepongeza Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF @wcf_tz ) na Shirika la Reli Tanzania (TRC) kwa kushirikiana katika ujenzi wa miradi ya kimkakati ambayo imekuwa na tija katika kukuza uchumi kwa maendeleo ya Taifa.
Sangu ameyasema hayo leo, Oktoba 2, 2026, wakati akizungumza katika hafla ya utiaji saini wa Mkataba wa Makubaliano (MoU) kati ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) na Shirika la Reli Tanzania (TRC) kwa ajili ya kushirikiana katika uwekezaji wa ujenzi wa Ukumbi wa mikutano na hoteli katika eneo la Stesheni ya SGR ya Jakaya Kikwete mjini Morogoro.
Waziri sangu amesema uwekezaji huo ni sehemu ya utekelezaji wa azma ya Serikali ambayo imekuwa ikizitaka taasisi za umma kuzingatia matumizi yenye tija ya rasilimali za umma na uwekezaji unaozalisha thamani kwa Taifa.
“Kwa mantiki hiyo, ushirikiano kati ya WCF na TRC unaonesha namna Taasisi za Serikali zinavyoweza kutumia nguvu na uwezo wao kwa pamoja ili kuendeleza miradi yenye manufaa mapana kwa Taifa,” amesema Waziri Sangu.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile, amesema kuwa uamuzi wa WCF kukubali kujenga mradi huo katika eneo la SGR linalomilikiwa na TRC ni uthibitisho wa namna taasisi hizo zinavyoweza kuchangia katika ukuaji wa Uchumi wa Taifa pamoja na kutekeleza majukumu yao ya msingi.
Naye, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya WCF, Bi. Renatha Rugarabamu, amesema Mfuko huo umeamua kuwekeza katika mradi huo ikiwa ni utekelezaji wa sheria inayoyataka mashirika kuwa na vyanzo vya mapato vitakavyoyawezesha kujitegemea.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TRC, Jaffer Machano, amesema ujenzi wa kumbi za mikutano na hoteli ya nyota nne utakaofanywa na WCF umekuja wakati sahihi, ikizingatiwa kuwa kwa siku TRC inasafirisha abiria zaidi ya 2,800 kutoka Dar es Salaam na Morogoro.
Mradi huo unatarajiwa kuwa na kumbi za mikutano 26 zenye uwezo wa kuhudumia watu kuanzia 10 hadi 600, kulingana na mahitaji, pamoja na hoteli ya nyota nne yenye vyumba takribani 90 katika eneo la Stesheni ya SGR Jakaya Mrisho Kikwete.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, ameelekeza kuwa matokeo na mapendekezo ya Ripoti ya Hali ya Uchumi Tanzania (Tanzania Economic Update), Toleo la Septemba 2026 yatumike katika kuboresha sera, mipango na utekelezaji wa hatua za maendeleo, hususan katika kuongeza ajira zenye tija na kuboresha kipato cha Watanzania.
Prof. Mkumbo ameyasema hayo leo, Oktoba 2, 2026, wakati akizindua rasmi Ripoti ya Hali ya Uchumi Tanzania, yenye kaulimbiu Kufanya Ajira kuwa Zenye Kuleta Tija (Tanzania Economic Update: Making Jobs Work) katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam.
Ripoti hiyo ya Benki ya Dunia inaangazia namna Tanzania inavyoweza kuhakikisha ukuaji wa uchumi unazalisha ajira bora, zenye tija na zinazoboresha maisha ya wananchi. Amesema Tanzania haipaswi kupima maendeleo kwa kuangalia idadi ya sera, mipango, programu na bajeti zilizotekelezwa pekee, bali inapaswa kuangalia matokeo yanayopatikana, ikiwemo ongezeko la uzalishaji, ajira zenye tija, kipato, ushindani wa biashara na uboreshaji wa maisha ya wananchi.
“Ni lazima tuanze kupima maendeleo kwa matokeo, si michakato pekee. Tunapaswa kujiuliza kama uwekezaji tunaoufanya unaongeza uzalishaji, kama biashara zinaongezeka na kuwa na ushindani, kama Watanzania wanapata ujuzi unaotambuliwa na kama kipato na fursa za kiuchumi vinaongezeka,” amesema Prof. Mkumbo. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Jumla ya wananchi 819 kati ya 886 wa Mtaa wa Mgeo, Kata ya Buhanda, Kigoma Ujiji, Mkoa wa Kigoma, waliopangwa kufikiwa katika zoezi la uhakiki wa mali zao "disclosure" Mkoani Kigoma, tayari wamepata fursa ya kuhakiki taarifa za mali zao na kutoa maoni kuhusu uthamini na fidia katika mradi wa SGR.
Rashidi Mageta, ambaye ni mthamini mwandamizi kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi, amesema lengo la zoezi hilo shirikishi ni kuwawezesha wananchi kuona na kujiridhisha juu ya taarifa zilizokusanywa kuhusu mali zao na kutoa hoja endapo kuna taarifa zinazohitaji kufanyiwa marekebisho kabla ya mchakato wa uthamini kukamilika.
Amesema wananchi waliofikiwa ni sawa na asilimia 92.4 wanaotoka katika maeneo ya Masanga, Mungonya, Msufini na Butunga huku wananchi 67 waliosalia wakihimizwa kutumia fursa hiyo kuhakiki mali zao.
Mageta amesema, disclosure ni sehemu muhimu ya uthamini kwakuwa inampa mwananchi nafasi ya kushirikiana na mthamini kuhakikisha taarifa za mali na fidia zinaakisi hali halisi ya mali husika.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imetoa Waraka wa Elimu Na. 3 wa Mwaka 2026 unaoelekeza shule zote za awali, msingi na sekondari nchini Tanzania Bara kufungwa mapema tarehe 13 Novemba 2026 badala ya tarehe 4 Desemba 2026 kama ilivyokuwa imepangwa awali.
Umauzi huo umechukuliwa kama hatua ya tahadhari baada ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kutoa taarifa ya mwelekeo wa mvua za vuli kwa kipindi cha Oktoba hadi Desemba 2026, ikionya kuhusu uwezekano wa kuwepo kwa mvua kubwa za El Niño zinazoweza kusababisha mafuriko na athari nyingine katika baadhi ya maeneo.
Waraka huo rasmi uliotolewa tarehe 30 Septemba 2026 wenye Kumbukumbu Namba CA.128/191/01J/53 na kusainiwa na Kamishna wa Elimu, Dkt. Lyabwene M. Mtahabwa umeeleza kuwa, “Kwa kuwa madhara ya mvua za El Nino yanaweza kuathiri shughuli za uendeshaji wa shule kwa ujumla ikiwa ni pamoja na wanafunzi wasio katika madarasa ya Upimaji na Mitihani ya Kitaifa, ni muhimu kuchukua hatua za tahadhari kwa ajili ya usalama na ustawi wa wanafunzi wote, walimu na watumishi wengine katika shule”.
Mabadiliko haya ya tarehe za kufunga shule yamebadilisha maelekezo ya awali yaliyokuwa katika Waraka wa Elimu Namba 06 wa Mwaka 2025 kuhusu kalenda ya mihula ya masomo kwa shule za awali, msingi na sekondari kwa mwaka 2026, pamoja na Waraka wa Elimu Namba 01 wa Mwaka 2026 uliokuwa ukielekeza kufungwa kwa shule tarehe 4 Desemba 2026
Uamuzi huu unajiri kufuatia hatua ya awali iliyochukuliwa na Wizara tarehe 25 Septemba 2026 ya kubadili tarehe za Upimaji na Mitihani ya Kitaifa ili kuepuka usumbufu unaoweza kusababishwa na mafuriko hayo. Waraka huu mpya umeanza kutumika rasmi kuanzia tarehe 1 Oktoba 2026. -
Jambo TV
@Jambotv_
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imezidisha msako na udhibiti dhidi ya vitendo vya ukwepaji kodi, biashara za magendo na ukiukaji wa maadili, ambapo katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita imekamilisha uchunguzi wa mashauri 130 ya ukwepaji kodi yenye thamani ya Shilingi bilioni 331.15 na kukusanya Shilingi bilioni 44.74.
Katika taarifa yake ya utendaji kazi ya robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2026/2027 (Julai - Septemba 2026), Mamlaka hiyo imeweka wazi kuwa haitasita kuchukua hatua kali za kisheria na kinidhamu dhidi ya mianya yote inayoisababishia Serikali hasara, ikijumuisha wafanyabiashara wasio waaminifu na watumishi wa umma wanaokiuka misingi ya kazi.
Katika udhibiti wa mpakani, TRA imefanya operesheni 1,185 za kufuatilia uingizaji wa mizigo kwa njia zisizorasmi (magendo), ambapo ilikamata bidhaa za magendo zenye thamani ya Shilingi bilioni 12.72 na kufanikiwa kuokoa kodi ya Shilingi bilioni 5.34. Hali kadhalika, kuzuia mizigo na magari 47,773 yanayohusika na usafirishaji wa mizigo, kulibaini makosa 197 ya udanganyifu na kuiwezesha TRA kukusanya Shilingi bilioni 79.68
Akitangaza hatua zilizochukuliwa kuimarisha nidhamu na uwajibikaji ndani ya taasisi hiyo, Kamishna Mkuu wa TRA, Bw. Yusuph Juma Mwenda, kupitia taarifa rasmi amesema, “TRA imewapatia mafunzo watumishi 1,028 ili kuboresha ujuzi wao katika usimamizi wa sheria za kodi na ukusanyaji wa mapato ya Serikali. Aidha, imeimarisha maadili ya watumishi kwa kuwachukulia hatua za kinidhamu watumishi 09 waliobainika kuwa na changamoto mbalimbali za kimaadili katika kipindi husika”.
Mbali na hatua hizo za kinidhamu na udhibiti wa mpakani, Mamlaka hiyo imefanikiwa pia kutatua mashauri 10 ya migogoro ya kodi mahakamani yenye thamani ya Shilingi bilioni 7.78, hatua iliyotajwa kuongeza usawa na kuweka mazingira salama ya biashara na uwekezaji nchini
Kwa ujumla, TRA imefanikiwa kukusanya jumla ya Shilingi trilioni 10.65 kwa kipindi hicho sawa na ufanisi wa asilimia 107.49 ya lengo la kukusanya Shilingi trilioni 9.91. Makusanyo hayo ni sawa na ukuaji wa asilimia 18.81, ikilinganishwa na makusanyo ya Shilingi trilioni 8.96 yaliyokusanywa katika kipindi kama hicho katika mwaka wa fedha 2025/26.
Mwenda amesema TRA imeimarisha utoaji wa huduma kwa walipakodi kwa kuboresha mifumo, mazingira ya ufanyaji biashara nchini ili kurahisha na kuchochea ulipaji kodi wa hiyari.
Katika hatua nyingine, sehemu ya makusanyo kwenye Pato la Taifa kwa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2026/27 imefikia asilimia 15.80, ukilinganisha na asilimia 12.7 iliyofikiwa mwaka 2021/22 wakati Serikali ya Awamu ya Sita, chini ya uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilipoingia madarakani. Makusanyo haya ni wastani wa makusanyo ya Shilingi trilioni 3.55 kwa mwezi kutoka wastani wa Shilingi Trilioni 2.98.
Katika kipindi cha robo ya kwanza (Julai -Septemba) mwaka wa fedha 2026/27, TRA imesajili walipakodi wapya 447,611 na kupelekea idadi ya walipakodi kufikia 9,011,783, ukilinganisha na walipakodi 8,564,172 waliokuwa wamesajiliwa mpaka mwezi Juni 2026.
Mafanikio haya yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na kuongezeka kwa ufanisi wa watumishi wa TRA, matumizi ya ofisi inayotembea (mobile vehicle office), matumizi ya vishikwambi katika kuwatembelea wateja walioko maeneo ya pembezoni, pamoja na ufunguzi wa ofisi mpya katika maeneo mbalimbali nchini. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mwigulu Nchemba @mwigulunchemba1 amelitaka Jeshi la Polisi nchini kutofumbia macho watu wanaojichukulia sheria mkononi wakati mwingine hata dhidi ya vyombo vya dola.
Ametoa wito huo akiwa Mwibara mkoani Mara leo Oktoba 2, 2026 akieleza kuwa vitendo hivyo vikifumbiwa macho vitatengeneza madhara makubwa na kuathiri hali ya kiusalama nchini.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi, amesema umeme ni huduma inayofungamanishwa na maendeleo kwa ujumla kwa kuwa nishati ni msingi wa maendeleo ya taifa na kichocheo muhimu cha ukuaji wa uchumi.
Ndejembi amesema hayo leo Ijumaa Oktoba 2, 2026, jijini Dar es Salaam, wakati wa hafla ya utiaji saini mpango wa ufadhili wa uunganishwaji wa umeme kwa wananchi kati ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Benki ya CRDB.
Amesema Serikali imeendelea kuwekeza kwa kiwango kikubwa katika miundombinu ya uzalishaji, usafirishaji na usambazaji wa umeme, ikiwa ni sehemu ya kuhakikisha hakuna Mtanzania anayebaki nyuma katika safari ya maendeleo kutokana na kukosa huduma hiyo muhimu.
“Megawati 2,115 kutoka Mradi wa Kuzalisha Umeme wa Bwawa la Julius Nyerere zitakuwa na maana endapo hazitamfikia Mtanzania au mlaji wa mwisho wa umeme huo, awe hospitalini, kiwandani, majumbani au akifanya shughuli za kibiashara,” amesema Ndejembi.
Amesema Tanzania imeweka malengo ya kuongeza uzalishaji wa umeme hadi megawati 8,000 ifikapo mwaka 2030 na kufikia megawati 74,000 ifikapo mwaka 2050, huku akisisitiza umuhimu wa sekta ya nishati katika kufanikisha Dira ya Taifa 2050.
Vilevile Ndejembi amesema, Tanzania imepiga hatua katika kuwafikishia wananchi huduma ya umeme, ambapo vijiji vyote 12,318 nchini vimeunganishwa na huduma hiyo, huku vitongoji 33,657 kati ya 64,359 vikiwa tayari vimeunganishwa.
Ameendelea kwa kusema kuwa, vitongoji 30,702 vilivyosalia viko katika hatua za kuunganishiwa umeme ifikapo mwaka 2030, akieleza kuwa Serikali inaendelea kutekeleza maelekezo ya kuhakikisha huduma hiyo inawafikia wananchi wote.
Ndejembi pia ameipongeza TANESCO na Benki ya CRDB kwa ushirikiano huo, akisema unatoa fursa kwa taasisi za umma, taasisi za fedha na sekta binafsi kuunganisha nguvu katika kuondoa vikwazo vinavyomzuia mwananchi kupata huduma ya umeme.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mara baada ya Mbunge wa Jimbo la Mtwara Mjini, Dkt. Joel Nanauka, kutoa maelekezo kwa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) pamoja na Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara Mikindani, kuchukua hatua za dharura kukabiliana na changamoto ya ubovu wa daraja linalounganisha Mtaa wa Mbawala Chini, Kata ya Naliendele, Mkoani Mtwara, hatimaye ukarabati wa daraja hilo umefanyika.
Mara baada ya kukamilika kwa ukarabati huo, wakazi wa mtaa huo, akiwemo Fakihi Bushiri, wamewashukuru Mbunge wa Jimbo hilo pamoja na TARURA kwa jitihada zilizofanyika, wakieleza kuwa kukamilika kwa ukarabati huo kutawaondolea changamoto walizokuwa wakikabiliana nazo, hasa katika kupita kwa magari na kusafirisha mazao yao.
Zubeda Issa amesema licha ya daraja hilo kukarabatiwa, bado wanakabiliwa na changamoto katika baadhi ya maeneo, hivyo ameomba ukarabati huo usiishie hapo, badala yake waendelee kuboresha miundombinu ya barabara hiyo, kwani kuna maeneo ambayo bado barabara haipitiki vizuri.
Naye Kaimu Meneja wa TARURA, Ramadhan Abdala, amesema marekebisho yaliyofanyika ni ya awali, ambapo baadaye wanatarajia kufanya marekebisho zaidi ili kuhakikisha kuwa daraja hilo linapitika bila changamoto yoyote katika misimu yote.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, amewataka Watanzania, hususan watoa huduma katika sekta ya madini, kuachana na malalamiko yasiyo na tija, badala yake kutumia fursa zinazotokana na mfumo wa 'Local Content', akisisitiza kuwa Serikali imeweka mazingira yanayolenga kuwawezesha wazawa kushiriki kikamilifu katika shughuli za migodi mikubwa nchini.
Waziri huyo ameyasema hayo Oktoba 2, 2026, mkoani Geita wakati akizungumza katika Kongamano la 'Local Content', lililowakutanisha viongozi mbalimbali wa Serikali, wadau wa sekta ya madini pamoja na watoa huduma katika maeneo ya migodi.
Mavunde amesema Serikali imeendelea kuweka mifumo na mazingira bora yatakayowawezesha Watanzania wenye kampuni na uwezo mbalimbali kushiriki katika kutoa huduma kwenye migodi mikubwa iliyopo nchini.
Aidha, Mwenyekiti wa tume ya Madini Dkt. Janeth Lekashingo, amesema tume hiyo itaendelea kusimamia kwa haki fursa zote ambazo zinatokana na local Contect kwa kuhakikisha watanzania wanapata haki na ushiriki wa fursa mbalimbali zinazopatikana.
Kongamano hilo limekuwa sehemu ya kujadili namna ya kuongeza ushiriki wa Watanzania katika shughuli za madini kupitia mfumo wa Local Content, huku Serikali na wadau wakisisitiza umuhimu wa kampuni za ndani kujiimarisha kiuweledi, kuzingatia sheria na kutumia fursa zinazotokana na sekta ya madini kwa ajili ya kukuza ajira, biashara na uchumi wa Taifa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI:
Nchi ya Ethiopia na Eritrea zimevunja uhusiano wao kidiplomasia baada ya Ethiopia kuishutumu Eritrea kwamba inawaunga mkono wapiganaji wa TPLF, ambao kuanzia wiki iliyopita, wanaripotiwa kupigana na vikosi vya Serikali katika jimbo la Tigray, Kaskazini mwa Ethiopia.
Ikichukua hatua juu ya hilo, Addis Ababa imesema, imewafukuza wanadiplomasia 10 wa Eritrea, ikisema wanatishia usalama wa taifa la Ethiopia. Aidha, Ethiopia imesema imefunga ubalozi wake jijini Asmara huko Eritrea.
Baada ya hatua hiyo, Eritrea nayo imechukua hatua kama hiyo kwa kufunga ubalozi wake, jijini Addis Ababa.
Tangu kuanza tena kwa mapigano, raia wa kawaida wameripotiwa kuuawa na wengine kujeruhiwa kwenye vita hivyo vinavyoendelea.
Mapigano hayo yaliyoanzia katika jimbo la Tigray, yamesambaa hadi katika majimbo jirani ya Afar na Amhara.
Hata hivyo, ripoti za vyombo vya habari kimataifa zinasema kwamba, Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed, hajazungumzia kuanza tena kwa vita katika nchi yake. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI PICHA:
Tanzania imepewa kipaumbele katika mpango mpya wa Uturuki wa kushirikiana na nchi zinazoendelea katika ujenzi wa viwanda, kuongeza thamani ya bidhaa na kuunganisha viwanda.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Dennis Londo, amesema hayo Oktoba 1, 2026 nchini Uturuki, baada ya kufanya mazungumzo na Naibu Waziri wa Viwanda na Teknolojia wa nchi hiyo, Muhammet Kasım Gönüllü, kuhusu fursa za kuimarisha ushirikiano katika sekta ya viwanda na matumizi ya teknolojia katika uzalishaji.
Londo amesema mpango huo, ulioanzishwa na Uturuki mwezi huu, unalenga kuhusisha sekta binafsi, taasisi za fedha, wataalamu wa teknolojia na waendeshaji wa viwanda kutoka nchi zinazoshirikiana, huku Tanzania ikitarajiwa kuwa miongoni mwa nchi za kuanzia utekelezaji wa mpango huo.
Amesema wataalamu kutoka Tanzania na Uturuki watabaini maeneo ya kimkakati yatakayowezesha kuanza utekelezaji wa ushirikiano huo, hususan katika kuongeza uzalishaji na thamani ya bidhaa zinazozalishwa nchini.
Katika eneo la kilimo na mifugo, Londo amesema nchi hizo pia zimejadili kubadilishana uzoefu kupitia programu ya Uturuki inayofahamika kama TUME, ambayo amesema ina mfanano na mpango wa Tanzania wa Jenga Kesho Iliyo Bora (BBT).
Aidha, mazungumzo hayo yameangazia mabadiliko ya kidijitali, sayansi na teknolojia, biashara mtandao na serikali mtandao, maeneo ambayo Tanzania inayapa uzito katika utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
Londo pia amekutana na Naibu Meneja Mkuu wa kampuni ya teknolojia ya Uturuki ya HAVELSAN, Savaş Yanık, kujadili fursa za matumizi ya teknolojia na mifumo ya kisasa katika sekta mbalimbali.
Londo amesema mazungumzo hayo yanafungua fursa kwa Tanzania kujifunza kutoka Uturuki na kutumia uzoefu wake katika viwanda, teknolojia na ubunifu, kwa lengo la kuongeza uzalishaji na thamani ya bidhaa za ndani. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Polisi Kata ya Ngomeni wilayani Muheza mkoani Tanga, Inspekta Asifiwe Msahana, amewasihi wanafunzi kuepuka kuhudhuria Sherehe zinazofanyika nyakati za usiku (Vigodoro), akieleza kuwa kuhudhuria katika sherehe hizo kunaweza kuchangia mmomonyoko wa maadili na kuwaweka katika hatari ya kufanyiwa vitendo vya ukatili.
Ametoa wito huo wakati akizungumza na wanafunzi hao Oktoba 1, 2026 katika Shule ya Sekondari ya Kwemkambala mkoani humo, kuhusu umuhimu wa kujiepusha na vitendo vya ukatili, katika tukio lililoandaliwa na Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT).
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Muheza, Teresia Nikandi, amesema umoja huo uko tayari kushirikiana na jamii katika kukabiliana na vitendo vya ukatili, ikiwemo kuwaibua watu wanaojihusisha na vitendo hivyo ili hatua stahiki zichukuliwe.
Baadhi ya wanafunzi walioshiriki katika mafunzo hayo wameishukuru UWT kwa elimu waliyopewa, huku wakiahidi kufuata waliyofundishwa ili kujiepusha na vitendo vinavyoweza kuhatarisha usalama na maadili yao.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Wanawake wa Kikundi cha Amani Ligera kilichopo Kata ya Ligera, Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma, wameeleza kuondokana na utegemezi kiuchumi baada ya kupata mashine ya kukamua alizeti inayowawezesha kufanya biashara ya bidhaa ya mafuta inayowapatia kipato.
Wakizungumzia ufanisi wa kiwanda hicho kidogo cha kuzalisha mafuta ya kupikia, Oktoba 1, 2026, wanawake hao wamesema wanaweza kujikopesha fedha zinazowawezesha kununua pembejeo za kilimo kupitia mapato yanayotokana na mashine hiyo.
"Kabla ya kupata Mashine hii, wanachama tulikuwa kiwango cha chini sana katika mambo mengi, tulikuwa hatufanikishi kitu, baada ya kupata mashine hii kiwango chetu kimepanda" amesema mmoja wa wanakikundi.
Mbali na kuwanufaisha wanawake hao, pia Mashine hiyo imetajwa kutoa ajira kwa wananchi wengine ambao si wanachama wa kikundi hicho.
Mashine hiyo ilitolewa na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Ruvuma, Jacqueline Ngonyani Msongozi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu Ado, amehoji uteuzi wa baadhi ya wanajeshi kushika nafasi za uongozi wa kiutawala, akisema hatua hiyo inaweza kuibua maswali kuhusu utenganishaji wa vyombo vya ulinzi na usalama na shughuli za kisiasa.
Ado ameyasema hayo jana, Oktoba 1, 2026, katika mkutano wa hadhara uliofanyika Masasi Mjini, mkoani Mtwara, ambapo amesisitiza umuhimu wa vyombo vya ulinzi na usalama kujitenga na siasa ili viweze kutekeleza majukumu yake kwa weledi, haki na bila upendeleo.
Amesema moja ya ishara anayoiona ya kuhusishwa kwa wanajeshi na siasa ni kuwepo kwa baadhi yao wanaoteuliwa kuwa wakuu wa mikoa na wilaya, nafasi ambazo, kwa mujibu wa Ado, zinawahusisha na vikao na shughuli za kisiasa.
Kwa mujibu wa Ado, vyombo vya ulinzi na usalama vinahitaji mageuzi ya kimfumo yatakayowezesha kutekeleza majukumu yao kwa usawa na kuhakikisha wananchi wote wanapata haki bila kujali misimamo yao ya kisiasa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
#ad
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Nchi ya Qatar, Tume ya Umoja wa Afrika na washiriki kutoka nchi wanachama wa Baraza la Ushirikiano la Nchi za Ghuba (Gulf Cooperation Council - GCC) imeandaa Mkutano wa Pili wa Uhamaji wa Nguvu Kazi (Second Doha Dialogue on Labour Mobility).
Mkutano huo unaratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira na Mahusiano na utafanyika kuanzia Oktoba 5 - 6, 2026 katika hoteli ya Hyatt Regency, Dar es Salaam ukiongozwa na kaulimbiu “Kuendeleza Uhamaji wa Nguvu kazi yenye Haki na endelevu katika ya Nchi za Afrika na Ghuba (GCC+). -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu Ado, amesema uwepo wa wabunge wa upinzani katika Bunge lenye wabunge 11 pekee, sawa na takribani asilimia tatu ya wabunge wote, ni muhimu katika kuibua hoja na kuikosoa Serikali.
Ado ameyasema hayo jana, Oktoba 1, 2026, katika mikutano ya hadhara iliyofanyika Kata ya Mijelejele, Jimbo la Lulindi na Masasi Mjini, mkoani Mtwara.
Akizungumzia hoja ya baadhi ya watu kuhoji namna anavyoweza kufanya kazi katika kile walichokiita “Bunge la Makofi tu”, Ado amesema uwepo wa wabunge wa upinzani ni muhimu katika kutoa sauti mbadala ndani ya Bunge.
“Hawa jamaa hawana aibu, hawana aibu wakati wa kula, wapo tayari hata kula chakula cha mtoto hawa jamaa wa CCM. Hivyo ni lazima iwepo sauti inayopambana, inayokataa ili waone haya kidogo,” amesema Ado.
Katika hatua nyingine, Ado amedai kuwa mabadiliko ya makatibu wote wa mikoa wa CCM yanaashiria kuwepo kwa “minyukano ya ndani” kuelekea uchaguzi wa chama hicho na Uchaguzi Mkuu wa 2030.
Amesema, kwa mtazamo wake, mabadiliko hayo si ya kawaida ya kiuongozi, bali yanahusishwa na maandalizi ya kisiasa na mvutano wa ndani ya chama hicho.
Ado pia amedai kuwa CCM imepoteza udhibiti wa siasa za nchi, akisema kwa sasa siasa zinaendeshwa zaidi na vyombo vya dola.
Hata hivyo, Ado amesema yuko tayari kuendelea na kile alichokiita “mapambano” bila kujali vikwazo, akisema ukimya unaweza kuongeza kero zinazowakabili wananchi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) @ChademaTZ2 Tanzania Bara, John Heche @HecheJohn , amesema ni msimamo na sera rasmi ya chama hicho ya kuwalipa pensheni ya kila mwezi wananchi wote wanaofikisha umri wa miaka 60, kuwapatia huduma za matibabu ya daraja la kwanza (first class) bila malipo, pamoja na kuwekeza kwenye kilimo ili kulinda afya zao na usalama wa chakula nchini, pale chama hicho kitakapopewa nafasi ya kushika dola.
Heche ameyasema hayo tarehe 1 Oktoba 2026 wilayani Tarime, Mkoa wa Mara, wakati akizungumza kama mgeni rasmi katika maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani yaliyoandaliwa na Baraza la Wazee la CHADEMA (BAZECHA).
Akiwahutubia wazee hao, Heche ameeleza kuwa wazee ndio waliojenga uchumi wa Tanzania kwa kukulima, kujenga nyumba, na kuzalisha mali, hivyo wanastahili kupewa heshima na hifadhi ya jamii badala ya kutelekezwa.
"Kila mmoja anapotimiza miaka 60 anastahili kulipwa pension na serikali, na tunasema kila mtu anastahili pension kwa sababu... huyu mzee aliyetengeneza taifa hili kwa kulima, kwa kujenga nyumba na kuzalisha, anajenga uchumi wa nchi hii…Kwanini wazee wa Zanzibar wapewe pension alafu nyinyi hampewi hata 100? Huu ni ubaguzi wa wazi kama nchi. Ahadi ya chama chetu kwenu ni kwamba wazee mnastahili heshima ya kupata matibabu first class bure na kupata pension”, ameeleza Heche.
Aidha, Heche ameeleza kuwa mfumo wa CHADEMA utazijengea uwezo jumuiya za wazee kupitia mikopo ya kibenki, zana za uzalishaji, na masoko ya uhakika akitolea mfano wa mfumo wa Kibbutz unaotumiwa nchini Israel na mifumo ya kijamii nchini Ujerumani. Amebainisha kuwa hatua hiyo itawafanya wazee waishi uzee wenye heshima na kujitegemea badala ya kuonekana mzigo kwa familia zao.
Akiunganisha ustawi wa wazee na sekta ya kilimo, Heche amesisitiza kuwa nchi yenye akili inapaswa kuchukulia kilimo kama suala la usalama wa taifa na kuwalipa wakulima ruzuku. Alikosoa utawala wa CCM kwa namna unavyoisimamia sekta ya kilimo nchini kwa kuendelea kutumia fedha nyingi kwa kuagiza bidhaa kama ngano kutoka nje ya nchi kama Urusi, Ukraine, na Saudi Arabia akisema bidhaa hizo zinaweza kuzalishwa katika ubora nchini Tanzania.
Pia, ameonya kuhusu hatari ya afya inayowakabili Watanzania kutokana na matumizi ya mbegu zilizobadilishwa vinasaba (GMO) na mafunzo duni ya vyakula vinavyoingizwa kutoka nje, akidai kuwa vinasababisha vijana wa miaka 40 hadi 50 kupatwa na kiharusi, shinikizo la damu, na tezi dume.
Heche amesisitiza kuwa CHADEMA ndicho chama pekee nchini kilichoandaa sera mbalimbali mahususi ikiwemo sera ya wazee, sera ya wanawake, na sera ya vijana ili kuinua kiwango cha umri wa kuishi nchini kufikia viwango vya nchi zilizoendelea. -
Jambo TV
@Jambotv_
Rais wa Kamati ya Olimpiki Duniani (IOC), Kirsty Coventry, amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa uongozi wake alioutaja kuwa ni wenye kutukuka unaowatia moyo na kuwapa fahari wanawake kote duniani.
Pongezi hizo zimetolewa katika Makao Makuu ya Kimataifa ya Kamati ya Olimpiki (IOC) yaliyopo Lausanne, Uswisi, wakati wa ziara ya kikazi ya viongozi wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC).
Akiwasilisha ujumbe huo kutoka kwa Mkuu huyo wa IOC, Rais wa TOC, Anthony Mtaka, alibainisha kuwa Coventry alieleza kuvutiwa kwake na mchango pamoja na mfano wa kuigwa wa Rais Samia.
Katika nukuu ya moja kwa moja ya maneno ya pongezi, Coventry alisema, “Rais wenu Samia Suluhu Hassan anatufanya wanawake tuone fahari, kwa hakika anatupa hamasa kubwa”.
Katika ziara hiyo nchini Uswisi, Mtaka aliongozana na timu ya viongozi wa TOC ikijumuisha Makamu wa Rais wa TOC, Bi. Nasra Juma. Ujumbe huo ulipata fursa ya kukutana na kufanya mazungumzo na Rais wa IOC Kirsty Coventry, pamoja na Wakurugenzi na wakuu wa vitengo mbalimbali katika Ofisi Kuu ya IOC.
Mazungumzo kati ya ujumbe huo wa Tanzania na viongozi wa IOC yaliangazia kwa kina maendeleo ya michezo nchini, hususani utambuzi wa vipaji na fursa za udhamini wa masomo kwa wanamichezo ndani na nje ya nchi kwa ajili ya masomo na mafunzo. Aidha, pande hizo mbili zilijadili mipango ya ujenzi wa ofisi za TOC pamoja na ujenzi wa kituo cha umahiri wa michezo mbalimbali nchini.
Vilevile, mazungumzo hayo yalihusisha fursa za masomo na udhamini kwa Watanzania wanaotaka kujifunza fani za ukocha na uamuzi pamoja na kutoa mafunzo, masomo na ujuzi wa kujiandaa na maisha ya baada ya michezo kwa wanamichezo wanaojiandaa kustaafu.
Eneo jingine kubwa lililopewa kipaumbele katika mazungumzo hayo ni maandalizi ya wachezaji na timu za Tanzania kuelekea Mashindano ya Olimpiki ya mwaka 2028, yanayotajiwa kufanyika katika mji wa Los Angeles, California nchini Marekani.
Mtaka ameeleza kuwa Michezo ya Olimpiki ijayo itakuwa na jumla ya michezo 35, ikijumuisha kuogelea, riadha, mpira wa kikapu, judo, ngumi, mishale, baiskeli, mpira wa miguu, mpira wa wavu, na mpira wa mikono.
Akitangaza ahadi yake kwa vyama vya michezo na wachezaji wanaojiandaa na Olimpiki ya 2028, Mtaka ametoa wito wa kuanza maandalizi ya mapema ili kuijengea Tanzania fursa ya kuwa na uwakilishi katika michezo mingi zaidi.
Amesisitiza kuwa kila chama cha mchezo kinapaswa kuanza mapema mchakato wa kupata wachezaji wenye sifa na viwango vinavyohitajika, ili TOC iweze kuwaingiza kwenye programu za udhamini wa mafunzo ya muda mrefu na kuepuka maandalizi ya zimamoto na kutupiana lawama
“Watanzania wanataka medali kwenye Olimpic Ijayo, TOC inamkaribisha kila mdau kushirikiana kwa pamoja ili vipaji vya vijana wa taifa letu katika michezo vipeperushe bendera yetu huko duniani 2028”, ameeleza Mtaka. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI:
Walimu na wafanyakazi wa vyuo vikuu vya umma nchini Kenya wametangaza kuanza mgomo wa kitaifa leo Ijumaa, Oktoba 2, 2026, ikiwa ni baada ya mazungumzo ya mkataba wa ajira na kushughulikia madai yao kutofikia muafaka.
Vyama vitatu vya wafanyakazi vya UASU, KUSU, na KUDHEIHA vimetangaza mgomo huo, ukilenga kudai utekelezaji wa mkataba wa pamoja wa ajira (CBA) wa 2025-2029.
Madai makuu ya vyama hivyo ni pamoja na ahadi ya serikali ya kufadhili mkataba huo kupitia Hazina ya Taifa, marekebisho ya mishahara, posho, na huduma bora za matibabu kwa wafanyakazi wote.
Tume ya Mishahara na Sahu (SRC) nchini humo iliwajulisha vyama vya wafanyakazi tarehe 21 Septemba kuwa, Wizara ya Elimu na Wizara ya Hazina hazikupeana ahadi ya maandishi kwamba fedha za CBA zitatolewa kupitia Hazina ya Taifa.
Katika mahojiano na vyombo vya habari huko Mombasa Oktoba 1, 2026 Rais William Ruto alijibu kuhusu mgomo huo akisema kwamba watashughulikia madai yao.
"Kwa walimu wanaotishia kwenda mgomoni, tutawashirikisha kwa sababu kwa miaka minne iliyopita, umesikia walimu wakienda mgomoni? Walikuwa wakienda mgomo kila wakati. Tunajaribu kubadilisha mambo," alisema Ruto.
Hata hivyo, Waziri wa Elimu nchini humo Julius Ogamba alisema mbele ya Seneti kuwa serikali imelipa bilioni 7.2 kati ya bilioni 7.9 iliyodaiwa kwa walimu wa vyuo vikuu, na kuongeza kuwa kuna mkutano umepangwa Oktoba 9, 2026, kwa ajili ya kuthibitisha kiasi kilichobaki.
Mgomo huo unatarajiwa kuathiri shughuli za ufundishaji katika vyuo vya umma nchini humo, ambapo hadi sasa hakuna tangazo lolote la kufikiwa kwa makubaliano kati ya vyama vya wafanyakazi na serikali. -
Jambo TV
@Jambotv_
Serikali ya Tanzania imebainisha kuwa inalenga kuimarisha zaidi uhusiano wake wa kiuchumi na nchi ya Italia kwa kuupanua kutoka biashara ya kawaida na kuelekeza nguvu katika uwekezaji wa teknolojia, maarifa, ubunifu pamoja na mageuzi ya kidijiti.
Msimamo huo umeelezwa tarehe 1 Oktoba 2026 mjini Cesena, Italia, wakati ujumbe wa Tanzania uliposhiriki katika jukwaa la EU-Tanzania Investment and Business Forum Roadshow, ikiwa ni sehemu ya ziara ya uhamasishaji uwekezaji barani Ulaya.
Akizungumza katika jukwaa hilo, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Mipango na Uwekezaji, Dkt. Pius Stephen Chaya amebainisha kuwa Tanzania inatafuta ushirikiano utakaobadili mwelekeo wa kiuchumi kupitia teknolojia na ubunifu.
Dkt. Chaya ameongeza kuwa Serikali inalenga uwekezaji utakaotoa matokeo yanayoshikika katika uchumi kupitia uzalishaji, uongezaji thamani, mauzo ya bidhaa nje ya nchi, ajira, uhamishaji wa teknolojia na maendeleo ya ujuzi.
Katika sekta ya uchumi wa kidijiti na teknolojia, kampuni na wawekezaji kutoka Italia wamealikwa kuwekeza katika maeneo ya kimkakati ikiwemo miundombinu ya kidijiti, usambazaji wa intaneti, vituo vya kuhifadhia data, teknolojia ya fedha (fintech), mfumo wa serikali mtandao, akili unde, pamoja na ukuzaji wa ujuzi wa kidijiti.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA), Gilead Teri, aliwasilisha fursa mbalimbali za uwekezaji na kueleza utayari wa TISEZA katika kuwaunganisha wawekezaji wa Italia na fursa zilizopo.
Mbali na teknolojia na mageuzi ya kidijiti, majadiliano hayo pia yaliangazia uwekezaji katika sekta ya kilimo na usindikaji, nishati safi na jadidifu, pamoja na usafirishaji na lojistiki.
Ziara hiyo ya nchini Italia ni sehemu ya maandalizi ya kuelekea Jukwaa la Uwekezaji na Biashara la Tanzania na Umoja wa Ulaya (Tanzania–EU Investment and Business Forum 2027) linalotarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Baadhi ya wafanyabiashara katika eneo la Stendi Kuu ya Karatu, wilayani Karatu mkoani Arusha, wamelalamikia kufungiwa kwa maduka yao na Halmashauri ya Karatu leo, Oktoba 1, 2026, wakidai kuwa hatua hiyo imechukuliwa licha ya kuwa bado wana mikataba ya kuendelea kufanya biashara hadi mwaka 2032.
Wafanyabiashara hao wamesema awali walikubaliana na Halmashauri kulipa kodi ya shilingi 50,000 kwa mwezi, wakieleza kuwa baadhi ya maduka hayo walijenga kwa gharama zao wenyewe.
Hata hivyo, wanadai kuwa baadaye walipewa utaratibu mpya wa malipo uliowataka kulipa hadi shilingi 312,500 kwa mwezi, kiwango ambacho wanasema ni kikubwa ikilinganishwa na hali ya biashara na mzunguko wa fedha wanaoupata.
Wakieleza hatua walizochukua kupinga utaratibu huo, wafanyabiashara hao wamesema walifungua kesi mahakamani wakidai haki zao, huku wakidai kuwa mahakama ilitoa notisi ya pamoja ya siku 90 kuhusu kusitishwa kwa shughuli za kufunga maduka hayo.
Pamoja na hatua hiyo, wafanyabiashara hao wanadai kuwa zoezi la kufunga maduka liliendelea leo, hali waliyosema imewaathiri katika shughuli zao za biashara.
Jambo TV imemtafuta Mkurugenzi wa Halmashauri ya Karatu, Juma Okororo, kwa ajili ya kupata ufafanuzi kuhusu suala hilo. Amesema alikuwa nje ya Karatu leo, huku akiahidi kulifuatilia suala hilo.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Lameck Karanga, amesema hana taarifa kuhusu kufungwa kwa maduka hayo leo, akieleza kuwa kwa uelewa wake, suala hilo linahusisha maamuzi yaliyopitishwa na Baraza la Madiwani.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha mfanyabiashara maarufu na bilionea kutoka nchini Zimbabwe, Wicknell Chivayo, mkewe, na wengine waliopoteza maisha katika ajali mbaya ya helikopta iliyotokea Septemba 30, 2026, katika eneo la Marondera nchini humo.
Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, Rais Samia ameandika, ““Ni kwa masikitiko makubwa ninaomboleza kifo cha mfanyabiashara wa Zimbabwe Bw. Wicknell Chivayo, mke wake mpenzi, na wengine watatu waliopoteza maisha katika ajali ya helikopta huko Marondera. Zimbabwe na Afrika zimepoteza mjasiriamali kijana mwenye maono ambaye aligusa maisha ya wengi. Kwa niaba ya Serikali na wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, natoa salamu zangu za pole na rambirambi za dhati kwa Mheshimiwa Rais Emmerson Mnangagwa, Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe; familia ya Chivayo, familia zote zilizopoteza wapendwa wao, na wananchi wa Zimbabwe.”.
Wakati huo huo, Jeshi la Polisi nchini Zimbabwe limetoa taarifa rasmi leo, Oktoba 1, 2026, kufuatia uchunguzi uliofanywa na wataalamu wa sayansi ya uchunguzi na masuala ya anga katika eneo la tukio huko Shamba la Kudenga, Marondera.
Polisi wamethibitisha rasmi kuwa helikopta hiyo ilikuwa na jumla ya watu watano pekee waliokuwemo ndani ambao wote wamepoteza maisha, huku wakikanusha taarifa za awali zilizozagaa zilizodai kulikuwa na abiria sita wakiwemo watoto wa bilionea huyo. Waliofariki katika ajali hiyo wametajwa kuwa ni Wicknell Munodaani Chivayo (Mfanyabiashara), Lucy Rujeko Muteke (Mke wa Chivayo), Saneliswe Magagula, Calvin Tafirei Soda (Rubani Mkuu) na Courage Mutavirva (Rubani Msaidizi) -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Sekta za maji mkoani Morogoro ikiwemo Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu, Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Morogoro (MORUWASA) pamoja na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) zimeagizwa kufanya tathmini na ukaguzi wa miundombinu ya maji, pamoja na kubaini maeneo hatarishi yanayoweza kuathiriwa na mafuriko na mmomonyoko wa udongo kuelekea msimu wa mvua za El Niño.
Agizo hilo limetolewa Oktoba 1, 2026 na Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Kundo Mathew, wakati wa ziara yake mkoani Morogoro, ambapo amesema hatua hiyo ni muhimu katika kujiandaa na kukabiliana na madhara yanayoweza kusababishwa na mvua hizo.
Aidha, Mhandisi Kundo amekagua utekelezaji wa mradi wa kunyanyua tuta la Bwawa la Mindu kwa urefu wa mita 2.5, hatua inayotarajiwa kuongeza uwezo wa bwawa hilo kuhifadhi maji.
Katika hatua nyingine, Naibu Waziri huyo amewatoa hofu wananchi wanaotakiwa kulipwa fidia kwa ajili ya kupisha upanuzi wa tuta la Bwawa la Mindu, akieleza kuwa fedha kwa ajili ya malipo hayo tayari zipo Hazina.
Kwa upande wao, Mkurugenzi wa Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu, Mhandisi Elibariki Mmasy, pamoja na Mkurugenzi wa MORUWASA, CPA Sais Kyejo, wamesema miundombinu ya usambazaji wa maji ipo katika hali salama, huku vifaa vya dharura vikiwa tayari kutumika endapo changamoto zitajitokeza.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Sakata la aliyekuwa Mwalimu wa Shule ya Sekondari Karansi wilayani Siha mkoani Kilimanjaro, Omari Salimu Ally aliyeondolewa katika nyumba ya Shule Karansi kwa madai ya kukaidi agizo la kuhamia shule nyingine ya Dahani Sekondari amedai kuwa kwa sasa anaishi msikitini Karansi huku mke na watoto wakimkimbia.
Akizungumza na Jambo TV iliyotaka kufahamu ikiwa ameshahamia kituo kipya cha kazi, amedai kuwa hana pingamizi juu ya uhamisho wake ila sababu ya msingi anayotaka kujua ni juu ya uhamisho wake kudaiwa kuwa ulitolewa kwa sababu ya kiusalama hivyo anataka kufahamu ni usalama upi.
Ameongeza kuwa alipohamishwa aliripoti kituo cha kazi Shule ya Sekondari Dahani na wanafunzi wanamfahamu hivyo hivyo anashangaa taarifa za kutoripoti shuleni hapo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkuu wa Wilaya ya Ilala mkoani Dar es Salaam, Edward Mpogolo amesema wilaya hiyo itasimamia kikamilifu kuhakikisha wakandarasi wanafanya kazi usiku na mchana kukamilisha ujenzi wa Daraja la Bonyokwa linalojengwa kwa gharama ya Shilingi bilioni 24.
Mpogolo ameyasema hayo leo wakati Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ilala ilipofanya fanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo wilayani humo ambapo amesema daraja hilo linapaswa kukamilika na kuanza kutumika kabla ya mvua za El Niño kuanza kunyesha.
Kamati hiyo iliongozwa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala, Said Sidde, akiambatana na wajumbe wake, Mkuu wa wilaya hiyo Edward Mpogolo, Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Nurdeen Bilal 'Shetta', Mbunge wa Viti Maalumu Bonnah Kamori, wakuu wa idara wa halmashauri hiyo, Meneja wa Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini (TARURA) Wilaya ya Ilala Mhandisi John Magori, na mwakilishi wa Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) mkoani humo Allan Shura.
Mbali na mradi wa daraja la Bonyokwa, kamati hiyo ilitembelea ujenzi wa Barabara ya Upanga (Muhimbili-Msuta) kilometa 7 inayojengwa kwa gharama ya shilingi bilioni 26, ujenzi wa Barabara ya Vingunguti-Kijiwe Samli kilometa moja kwa kiwango cha zege kwa gharama ya shilingi bilioni 2.9, ujenzi wa Barabara ya Bonyokwa Zahanati na Segerea Bonyokwa kilometa 0.8 kwa gharama ya shilingi bilioni 1.3, na Kituo Atamizi cha Wajasiriamali Wadogo Pugu, kwa gharama ya shilingi milioni 990.0474.
Akizungumza baada ya kukagua miradi hiyo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Said Sidde, ameeleza kuwa kamati imeridhishwa na utekelezaji wa miradi hiyo na kuwataka wakandarasi kuikamilisha kwa wakati ili iwanufaishe wananchi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) imesema inaendelea kuhimiza uwekezaji nchini kwa kuwa ni miongoni mwa nguzo muhimu katika kukuza uchumi na kufikia malengo ya maendeleo yaliyowekwa na Serikali.
Mamlaka hiyo imesema inaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi, huku ikieleza kuwa sekta ya madini ni miongoni mwa maeneo yenye fursa kubwa ya kuchochea uwekezaji na kuongeza mchango wa sekta hiyo katika uchumi wa Taifa.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Oktoba 1, 2026, katika Maonesho ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea katika Viwanja vya Dkt. Samia Suluhu Hassan, mkoani Geita, Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa TISEZA, Absalom Kibanda, alisema uwekezaji ni sehemu muhimu ya mkakati wa kukuza uchumi wa nchi.
Kibanda alisema miongoni mwa sekta zenye uwezo mkubwa wa kuchangia katika kufikia malengo hayo ni sekta ya madini, ambayo imeendelea kukua kwa kasi na kuwa na mchango mkubwa katika uchumi, hususan mkoani Geita.
Kwa upande wake, Meneja wa Kanda ya Ziwa wa TISEZA, Venance Mashiba, alisema mamlaka hiyo imeendelea kuwahudumia wawekezaji wa aina mbalimbali, wakiwamo wawekezaji wakubwa na wadogo, kwa kuwa wote wana nafasi katika kukuza uchumi wa Taifa.
Mashiba alisema katika sekta ya madini, TISEZA imeendelea kushirikiana na taasisi mbalimbali zenye utaalamu wa masuala ya madini, hususan katika kuwasaidia wawekezaji kupata taarifa na kuelekezwa maeneo yenye uwezekano wa kuwa na madini.
Ameongeza kuwa kuendelea kuimarisha ushirikiano kati ya TISEZA na taasisi za sekta ya madini kutasaidia kuongeza ufanisi katika kuvutia uwekezaji, kupunguza changamoto zinazoweza kujitokeza kwa wawekezaji na kuhakikisha fursa zilizopo zinatumika kwa manufaa ya Taifa.
Maonesho hayo ya Teknolojia ya Madini yanaendelea mkoani Geita yakilenga kutoa fursa kwa wadau wa sekta ya madini, wakiwamo wachimbaji, wawekezaji, wazalishaji wa vifaa na teknolojia pamoja na taasisi za Serikali, kukutana, kubadilishana uzoefu na kutafuta fursa za uwekezaji.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Wachimbaji wadogo wa madini wameiomba Serikali na wadau wa sekta ya madini kuendelea kutoa elimu ya uchimbaji wa kisasa ili kuwasaidia kubaini maeneo sahihi yenye uwezekano mkubwa wa kuwa na madini na hivyo kuongeza tija na kipato katika shughuli zao.
Mwenyekiti wa Wanawake Wachimbaji Mkoa wa Geita, Asia Masimba, ametoa ombi hilo leo Oktoba 1, 2026 wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wachimbaji wadogo yaliyoratibiwa na HakiRasilimali.
Masimba amesema mafunzo hayo yamekuwa muhimu katika kuongeza uelewa na kuhamasisha wachimbaji kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu sekta ya madini, ikiwemo umuhimu wa Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) na matumizi ya teknolojia za kisasa katika shughuli za uchimbaji.
Naye Andrea Nicolaus, kutoka TEITI, amesema moja ya mambo yaliyojadiliwa katika mafunzo hayo ni namna ya kutambua na kuimarisha mchango wa wachimbaji wadogo katika uchumi wa Taifa, hususani kupitia mapato wanayozalisha kutokana na shughuli zao.
Amesema wachimbaji wadogo wana nafasi kubwa katika kuchangia maendeleo ya jamii na uchumi wa nchi, hivyo ni muhimu kutambua mchango wao na kuwapatia elimu na mazingira bora yatakayowawezesha kufanya shughuli zao kwa tija.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Watendaji wa uchaguzi watakaosimamia Uchaguzi Mdogo wa Ubunge katika Jimbo la Chamwino mkoani Dodoma pamoja na uchaguzi wa Udiwani katika Kata 11 za Tanzania Bara, unaotarajiwa kufanyika Novemba 4, 2026, wametakiwa kuzingatia Katiba, sheria, kanuni na maadili ya uchaguzi ili kuhakikisha zoezi hilo linafanyika kwa haki, uwazi na bila dosari.
Wito huo umetolewa Oktoba 1, 2026 na Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Dkt. Zakia Mohamed, wakati akifunga mafunzo kwa Watendaji wa Uchaguzi yaliyofanyika mkoani Tabora, ambapo amewataka watendaji hao kufanya marejeo ya mara kwa mara ya Katiba, sheria na kanuni za uchaguzi ili kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa usahihi wakati wa uchaguzi.
Kwa upande wao, baadhi ya Watendaji wa Uchaguzi walioshiriki mafunzo hayo wamesema mafunzo hayo yamewajengea uelewa zaidi wa taratibu na kanuni za uchaguzi, hivyo kuwawezesha kusimamia zoezi hilo kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Wanachama wa vyama vya ushirika mkoani Njombe, wameiomba Serikali kuendelea kuchukua hatua kali dhidi ya watumishi wa ushirika wabadhilifu, ili kuendelea kuimarisha vyama vyao.
Wameomba hayo leo Oktoba 1, 2026 walipozungumza na Jambo TV wakati wa Kliniki ya Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC), inayofanyika mjini Njombe kwa lengo la kutoa elimu kwa wanachama wa vyama vya ushirika na wananchi.
Miongoni mwa wanachama hao ni Anna Kitindi, ambaye amesema changamoto nyingi zinazowakabili ni pamoja ubadhilifu ambao amesema umekuwa ukidhoofisha ushirika.
Kwa upande wake Stiven Kalabo ambaye ni Afisa Ushirika wa Tume ya Maendeleo upande wa vyama vya kifedha, amesema wamelazimika kuwafikia wanachama ili kuwasikiliza na kutoa elimu, huku akiwataka viongozi kuepuka ubadhilifu hali itakayowaepusha na mkono wa sheria.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Njombe Juma Sweda amesema vyama vya ushirika vimekuwa vikikabiliwa na changamoto nyingi na kusababisha vingine kufa.
"Vyama vyetu vya ushirika vinachangamoto nyingi na vyama vingi vilivyopitia changamoto vilikufa, lakini kwa sasa tume ya ushirika imejipanga kuhakikisha inafufua vyama vya ushirika"amesema Sweda.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Askari sita wa Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro wamepata ajali katika eneo la Cooperative, mpakani mwa Wilaya za Siha na Hai, wakiwa njiani kwenda kuchukua mahabusu katika Gereza la Karanga wilayani Moshi.
Ajali hiyo imetokea baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupasuka tairi upande wa kulia, kugonga mti na kisha kupinduka.
Kwa mujibu wa taarifa ya TBC Digital kuhusu tukio hilo imesema Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa, amesema askari watatu kati yao wamepata majeraha na wanaendelea na matibabu.
Kamanda Maigwa amesema chanzo cha ajali hiyo ni kupasuka kwa tairi, huku akieleza kuwa uwepo wa ngao katika gari hilo umesaidia kupunguza madhara.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mbunge wa Jimbo la Mtwara Mjini ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Maendeleo ya Vijana, Dkt. Joel Arthur Nanauka, amesema ni sehemu ya majukumu yake kuhakikisha anakuwa daraja la kuwaunganisha wananchi na fursa kulingana na mahitaji yao.
Nanauka ameeleza hayo alipokuwa akizungumza wakati wa kukabidhi mashine ya kisasa ya kubangua korosho kwa Kikundi cha Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake jimboni humo. Mashine hiyo imetajwa kuwa na thamani ya shilingi milioni 6.5.
Amesema zaidi kwamba amefanikisha upatikanaji wa mitaji kwa wanawake kupitia mradi maalum unaolenga kuwapatia mafunzo na kuwaunganisha na mitaji yenye masharti nafuu ili kukuza biashara zao.
Hadi sasa, jumla ya shilingi milioni 95 zimetolewa kwa wanawake kupitia programu hiyo ya Uwezo, huku Dkt. Nanauka akieleza kuwa maono yake ni kuwafikia wanawake 5,000 ifikapo mwaka 2030.
Aidha, amevitaka vikundi vinavyokopeshwa kuhakikisha vinarejesha fedha kwa wakati ili kuwawezesha wananchi wengine kunufaika na fursa hiyo ya kupata mitaji.
Kwa upande wao, wanachama wa Kikundi cha Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi wamesema mashine hiyo itarahisisha shughuli za ubanguaji wa korosho kwani awali walitumia muda mrefu kubangua, huku baadhi yao wakitumia hadi shilingi 40,000 kwa ajili ya kubangua gunia moja.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mbunge wa Jimbo la Kondoa Mjini, Mariam Ditopile, ameungana na ujumbe wa Baraza la Madiwani na Wataalamu wa Halmashauri hiyo katika ziara ya kimkakati Jijini Tanga, yenye lengo la kujifunza utekelezaji na usimamizi wa miradi ya maendeleo ili kuboresha huduma kwa wananchi wa Kondoa.
Katika ziara hiyo, Ditopile ameweka wazi dhamira ya ujumbe huo, akisisitiza kuwa wao kama viongozi wana wajibu wa kuhakikisha fedha zinazoletwa na Serikali zinaleta tija na kubadilisha maisha ya wananchi.
"Sisi ni wapanga maendeleo, watekelezaji, na wasimamizi wa miradi ya maendeleo, hususani kusimamia fedha nyingi zinazoletwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye Halmashauri yetu. Kuja kwetu Tanga kutatuwezesha kuongeza ujuzi na kasi kuelekea Dira ya Taifa ya Maendeleo ya Mwaka 2025-2050, ambayo zaidi ya asilimia 70 itatekelezwa na sekta binafsi," amesema Ditopile.
Ujumbe huo umetembelea miradi mbalimbali jijini Tanga, ikiwemo Dampo la Kisasa la kukusanya taka ngumu lililopo Mtaa wa Mpirani, Kata ya Chongoleani, pamoja na mradi wa Maegesho ya Malori uliopo Kange, ujenzi wa shule za ghorofa na Bandari ya Tanga.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kondoa, Fatma Almas Nyangasa, amesema ameambatana na wataalamu ili kujifunza matumizi sahihi ya ardhi ndogo ili kujenga majengo yanayoleta faida kwa wananchi.
"Huu mradi wa kukusanya taka, tukienda kuutekeleza baada ya kujifunza hapa utaleta tija, utaongeza mapato ya Halmashauri, lakini pia utatoa ajira kwa watu wetu," amesema DC Nyangasa.
Pia, amempongeza Rais Samia kwa uboreshaji wa Bandari ya Tanga na kufungua barabara ya Handeni - Kondoa hadi Singida, hatua inayotajwa kwamba itachochea uchumi wa Wilaya hiyo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mtoto anayefahamika kwa jina la Edgar (7), mwanafunzi wa darasa la kwanza na mkazi wa Mtaa wa Mkangala, Kata ya Naliendele, Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara Mikindani mkoani Mtwara, amejeruhiwa kwa kuchomwa moto kwenye sehemu za mwili wake na mama yake mzazi huku sababu ya kufanya hivyo ni mtoto huyo kudaiwa kuiba Korosho shambani.
Kwa mujibu wa taarifa za Jeshi la Polisi mkoani humo Septemba 30, 2026, imesema tukio hilo lilitokea Septemba 29, 2026, ambapi wananchi wa Mtaa huo wameeleza kutopendezwa na adhabu hiyo, huku wakikemea vikali kitendo hicho na kutaja kwamba ni ukatili wa kijinsia.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mkangala, Zamda Hemedi, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa kwa mujibu wa mahojiano aliyomfanyia mtoto huyo pamoja na majirani, mtoto huyo hakuwa ameiba huku akitoa wito kwa wazazi kuacha kutoa adhabu kali kwa watoto.
Kwa upande wake, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara, SACP Issa Suleiman, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, akieleza kuwa mtoto huyo amejeruhiwa kwa kuchomwa moto kwa kutumia makuti, kitendo kilichomsababishia majeraha kwenye mwili wake.
Kamanda Suleiman ametoa wito kwa wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi na kuzingatia kiwango cha adhabu kwa watoto.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katika kuadhimisha Mwezi wa Maendeleo ya Jamii, Halmashauri ya Mji wa Nzega mkoani Tabora kupitia Idara ya Maendeleo ya Jamii, imeendelea kutoa elimu kwa makundi mbalimbali na wananchi kuhusu fursa za kiuchumi na kijamii.
Wakizungumza Septemba 30, 2026, baadhi ya wananchi wamesema miradi hiyo pamoja na mikopo inayotolewa na Halmashauri imekuwa chachu ya kuboresha maisha yao kiuchumi na kijamii, huku wakieleza kuwa ushirikiano kati ya wananchi na Serikali umewezesha utekelezaji wa miradi yenye manufaa kwa jamii.
Miongoni mwa miradi iliyotembelewa ni ujenzi wa Ofisi ya Mtendaji wa Kijiji cha Kitangili pamoja na Zahanati ya Nyasa, ambayo ilianza kujengwa kwa nguvu za wananchi kabla ya Serikali kuunga mkono juhudi hizo kupitia usimamizi wa Idara ya Maendeleo ya Jamii ya Halmashauri hiyo.
Kwa upande wake, Mkuu wa Divisheni ya Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Mji wa Nzega, Omary Mungi, amesema Idara hiyo imeendelea kuyaunganisha makundi mbalimbali na fursa zilizopo, ikiwemo mikopo ya Halmashauri, huku akisisitiza umuhimu wa malezi bora ya watoto katika kujenga jamii yenye ustawi.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Nzega, Recho Erasto, amewataka wananchi kuunda vikundi ili waweze kunufaika na mikopo inayotolewa na Halmashauri, huku akiwataka kuachana na dhana potofu kuhusu kuwepo kwa matabaka katika utoaji wa mikopo hiyo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkuu wa Mkoa wa Katavi ametoa siku 14 kwa viongozi wa Bodi na watendaji wa Chama cha Ushirika cha Mkombozi AMCOS, kufanya uchunguzi na kukusanya fedha kiasi cha shilingi milion 133 kupitia akaunti ya chama hicho ili kuwalipa fedha za mauzo ya tumbaku wakulima 56 kati ya 70 wanaodai kutolipwa fedha hizo kwa asilimia 100 ya mauzo yao.
Ametoa tamko hilo Septemba 30, 2026 alipotembelea Chama hicho katika Kitongoji cha Luhafwe kata ya Tongwe Wilaya ya Tanganyika, mkoani Katavi ikiwa ni baada ya wanachama wa Chama hicho kutoa malalamiko ya kutolipwa fedha zao za mauzo ya tumbaku kwa msimu wa 2024/2025.
“Nitoe siku 14, hizi fedha zote zirudishwe na zilipwe kwa wakulima. Wewe kama unajijua kwamba wakati hii Kamati yangu inafanya uchunguzi ulikuja kuhakikiwa na ikaonekana kabisa kwamba risiti uliyonayo na malipo uliyopewa havifanani, umezidishiwa fedha au umelipwa fedha ambazo hukustahili kulipwa anza kuzirudisha kuanzia leo,” amesema Mrindoko.
Mrindoko amesema viongozi wote wa bodi na watendaji waliohusika katika kuandaa taarifa ya malipo isiyo sahihi na kupelekea wakulima hao kulipwa asilimia 50 ya malipo yao badala ya asilimia 100 za malipo yao, wachukuliwe hatua za kisheria ili kukomesha tabia za wizi, ubabe na ubadhirifu wa fedha za wakulima hao.
Pia ameagiza viongozi ikiwemo Mrajisi Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa na Maafisa Ushirika katika ngazi ya Halmashauri kusimamia na kuhakikisha vyama vyote vilivyopo na vinavyotarajiwa kuanzishwa vinaajiri wataalamu wenye weledi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mahakama Kuu ya Tanzania, kupitia Jaji Dafina Ndumbaro, imetengua amri zote za kumkamata na kumrejesha nchini mwanaharakati wa mtandaoni, Edger Mwakabela (@Sativa), zilizotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mwaka 2025.
Mahakama Kuu imeamua kuwa amri ya kumkamata Sativa ilikuwa batili kisheria kwa sababu tatu kuu. Kwanza, hakukuwa na kesi iliyosajiliwa mahakamani kabla ya amri hiyo kutolewa.
Pili, Hakimu wa Kisutu hakuwa na mamlaka ya kutoa amri ya kumtafuta nchini Kenya, na jambo la tatu ikisema kiapo cha polisi kilichotumika kuomba amri hiyo kilikuwa na kasoro za kisheria.
Kesi hii ilianza Novemba 28, 2025, wakati Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) ilipowasilisha maombi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ikitegemea kiapo cha Afisa wa Polisi ACP Wilson Mlowola.
DPP alidai kuwa Edger alikuwa amechapisha taarifa za uongo mtandaoni chini ya Sheria ya Makosa ya Mtandao na kwamba alikuwa akiishi nchini Kenya ambapo siku hiyo hiyo, Hakimu wa Kisutu alitoa amri ya kukamatwa kwa Edger" mahali popote alipo" na kuelekeza zitumike mbinu zozote kumrejesha nchini kutoka Kenya.
Edger Mwakabela, kupitia wakili wake Jebra Kambole wa Law Guards Advocates, alikata rufaa Mahakama Kuu kupinga maamuzi hayo. Rufaa hiyo ilisikilizwa na Jaji Dafina Ndumbaro katika Rufaa ya Jinai Namba 000029293 ya Mwaka 2025.
Katika uamuzi wake wa Septemba 29, 2026, Jaji Ndumbaro alitupilia mbali pingamizi la DPP na kubaini makosa makubwa ya kisheria. Kosa la kwanza lilikuwa kutokuwepo kwa kesi ya msingi iliyosajiliwa mahakamani....This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
#ad
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Nchi ya Qatar, Tume ya Umoja wa Afrika na washiriki kutoka nchi wanachama wa Baraza la Ushirikiano la Nchi za Ghuba (Gulf Cooperation Council - GCC) imeandaa Mkutano wa Pili wa Uhamaji wa Nguvu Kazi (Second Doha Dialogue on Labour Mobility).
Mkutano huo utaratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira na Mahusiano na utafanyika kuanzia Oktoba 5 - 6, 2026 katika hoteli ya Hyatt Regency, Dar es Salaam ukiongozwa na kaulimbiu “Kuendeleza Uhamaji wa Nguvu kazi yenye Haki na endelevu katika ya Nchi za Afrika na Ghuba (GCC+). -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Donald Msengi, ameyataka mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) mkoani humo kuweka mikakati ya kujenga uwezo wa kujitegemea kiuchumi kwa kuwekeza katika shughuli za uzalishaji na vyanzo vya mapato vya ndani.
Ametoa wito huo Septemba 30 2026 wakati wa Jukwaa la Mwaka la Mashirika yasiyo ya kiserikali Mkoa wa Mtwara, lililofanyika katika Manispaa ya Mtwara Mikindani na kushirikisha wadau kutoka taasisi mbalimbali za umma na binafsi.
Kanali Msengi amesema hatua hiyo ni muhimu kutokana na mabadiliko ya ajenda za wafadhili wa kimataifa, hivyo mashirika hayo yanapaswa kuwa na vyanzo vya mapato vitakavyowawezesha kuendelea kutekeleza majukumu yao bila kutegemea ufadhili kutoka nje ya nchi.
Kwa upande wake, Mwakilishi wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali katika Baraza la Taifa la NGOs (NaCoNGo), Baltazar Komba, amesema mashirika hayo tayari yameanza kuweka mikakati ya kujenga vyanzo vya mapato na kutumia rasilimali zilizopo ili yaweze kuendelea kutoa huduma kwa jamii.
Naye Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali la MOCE mkoani Mtwara, Adam Malima, amesema NGOs zina nafasi kubwa katika kuiwezesha jamii kiuchumi na kuchangia utekelezaji wa Dira ya Taifa 2050, huku akisisitiza umuhimu wa mashirika hayo kujenga vyanzo vyao vya ndani vya mapato ili kusaidia jamii kuwa na uchumi imara.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Kutokana na changamoto ya kutembea umbali mrefu wa zaidi ya kilometa 64 kufuata huduma za kipolisi, wananchi wa kata za Lukumbule na Mchesi, wilayani Tunduru, mkoani Ruvuma, wamefanikiwa kukamilisha ujenzi wa kituo kipya cha polisi kwa gharama ya zaidi ya shilingi milioni 105.
Kwa mujibu wa madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru, waliozungumza kwa niaba ya wananchi hao, changamoto ya kukosekana kwa kituo hicho awali ilikuwa ikisababisha wananchi wengi kuachana na kufuata haki zao za kupata ulinzi na usalama kutoka kwa Jeshi la Polisi.
Wamesema kutokana na ukosefu wa kituo cha polisi hapo awali, walilazimika kutembea umbali mrefu kufuata kituo cha polisi kilichopo Tarafa ya Nalasi, ambacho wamesema kilikuwa ni kituo kimoja tu kilichokuwepo Jimbo la Tunduru Kusini.
Akizungumza wakati wa uzinduzi, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Marco Chilya, amewataka askari watakaofanya kazi katika kituo hicho kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa wananchi, wakitambua kuwa kituo hicho kipo kwa ajili ya kuwahudumia wananchi hao.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Denis Masanja, amesema kuwa ni muhimu kuwepo kwa ushirikiano thabiti kati ya Jeshi la Polisi na wananchi wa maeneo hayo ili kuhakikisha usalama na amani vinaendelea kuimarika.
"Kituo hiki ni cha wananchi, kwa hiyo tunapaswa kuendelea kushirikiana na polisi kuhakikisha eneo letu lina usalama wa kutosha," alisema Masanja.
Ujenzi wa kituo hicho cha polisi ulianza mwaka 2011, lakini ulikwama kwa muda mrefu baada ya kujengwa boma bila kukamilika. Hata hivyo, wananchi waliamua kuendeleza jitihada hizo kwa kujitolea fedha na nguvu kazi hadi Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru na Jeshi la Polisi walipounga mkono na kukamilisha ujenzi huo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Afya, Mohamed Mchengerwa, amepiga marufuku kali dhidi ya vitendo vya rushwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, huku akitaka uwekezaji mpya wa Kliniki ya VIP na ubunifu wa mapato usitumike kama sababu ya kumsahau mwananchi wa kijijini asiye na uwezo.
Waziri Mchengerwa ameyasema hayo Jumatano tarehe 30 Septemba 2026 jijini Dar es Salaam, wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Wadhamini ya Hospitali ya Taifa Muhimbili pamoja na uzinduzi wa miradi mbalimbali ya kimkakati katika hospitali hiyo.
Waziri Mchengerwa ameeleza kuwa Muhimbili ikiwa ni kioo cha huduma za afya nchini, vitendo hivyo vitendo vya rushwa havipaswi kusikika wala kuonekana kwenye mitandao. Mchengerwa amemwagiza Mkurugenzi wa hospitali hiyo kuweka matangazo na namba za simu kuanzia getini hadi kwenye wodi zote ili wananchi waweze kutoa taarifa pindi wanapoombwa rushwa. Pia amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya kuhakikisha utaratibu huo unatekelezwa katika vituo vyote vya afya nchini.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dkt. Delilah Kimambo, amebainisha kuwa uwekezaji katika jengo na miundombinu ya jengo la upasuaji (theater) umetumia kiasi cha shilingi bilioni 1.8 za Kitanzania. Ameeleza kuwa uwekezaji huo unaonesha dhamira ya dhati ya Serikali katika kulinda afya ya mama na mtoto, kupitia ushirikiano wa Serikali, hospitali na wadau wa maendeleo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Bandari ya Dar es Salaam imeendelea kuonesha maboresho makubwa katika ufanisi wa kuhudumia meli, baada ya kupanda kwa nafasi 105 katika Ripoti ya Utendaji wa Bandari katika kuhudumia Makasha (Container Port Performance Index -CPPI) 2025 ya Benki ya Dunia kwa kushirikiana na Taasisi inayotoa taarifa na uchambuzi wa masoko ya kimataifa (S&P Global Market Intelligence).
Kwa mujibu wa Ripoti hiyo ya CPPI 2025, Bandari ya Dar es Salaam imepanda kutoka nafasi ya 360 mwaka 2024 hadi nafasi ya 255 mwaka 2025, mabadiliko yanayoonesha kuimarika kwa ufanisi wa shughuli za meli bandarini. CPPI hupima hasa muda ambao meli za makasha hutumia bandarini, ukiwemo muda wa kusubiri na muda wa kuhudumiwa katika gati.
Katika ulinganisho na baadhi ya bandari za Afrika Mashariki na Kusini, Bandari ya Dar es Salaam imeorodheshwa mbele ya Mombasa (396), Beira (315), Nacala (356), Walvis Bay (372), Durban (398) na Cape Town (400). Aidha, Bandari ya Dar es Salaam imeorodheshwa nyuma ya Maputo, iliyopo nafasi ya 273, katika orodha ya bandari hizo.
Mabadiliko hayo yanaonesha mwenendo wa kuimarika kwa ufanisi wa Bandari ya Dar es Salaam katika kipindi ambacho biashara ya kimataifa ya usafirishaji imeendelea kukabiliwa na changamoto mbalimbali, ikiwemo mabadiliko ya njia za meli kutokana na hali ya usalama katika Bahari ya Shamu na athari zake kwenye mtiririko wa usafirishaji katika Bahari ya Hindi. Benki ya Dunia inaonya kwamba matokeo ya CPPI yanapaswa kutafsiriwa kwa kuzingatia mazingira mapana ya usafirishaji duniani, kwa kuwa mambo kama mabadiliko ya njia za meli, hali ya hewa na misukosuko ya minyororo ya ugavi yanaweza kuathiri muda wa meli bandarini.
Kwa upande wa Tanzania, kuimarika kwa utendaji wa Bandari ya Dar es Salaam kunaendana na hatua zinazoendelea kuchukuliwa katika kuboresha miundombinu, mifumo ya uendeshaji, matumizi ya teknolojia na uratibu wa shughuli za bandari, kwa lengo la kuongeza kasi ya kuhudumia meli na mizigo.
Bandari ya Dar es Salaam ina umuhimu wa kimkakati katika biashara ya kikanda kutokana na nafasi yake kama lango muhimu la Ushoroba wa Kati (Central Corridor), inayounganisha Tanzania na nchi jirani zisizo na bandari. Ufanisi katika kuhudumia meli na mizigo una umuhimu katika kuimarisha uaminifu wa huduma, kupunguza ucheleweshaji na kusaidia ushindani wa njia za biashara zinazopita katika ukanda huo.
Hata hivyo, ni muhimu kutambua kwamba CPPI si kipimo cha ukubwa wa bandari, kiasi cha mizigo inayohudumiwa au umuhimu wake wa kiuchumi. Ni kipimo kinacholenga ufanisi wa muda wa meli bandarini. Kwa hiyo, nafasi ya 255 inapaswa kutazamwa kama kiashiria cha ufanisi wa uendeshaji wa meli na kutumika pamoja na viashiria vingine vya utendaji wa bandari.
Kwa ujumla, CPPI 2025 inaonesha mabadiliko chanya katika utendaji wa Bandari ya Dar es Salaam, huku kupanda kwa nafasi 105 ndani ya mwaka mmoja kukitoa kiashiria muhimu cha maendeleo katika ufanisi wa huduma za meli. Matokeo hayo pia yanaweka msisitizo wa kuendelea kuboresha miundombinu, teknolojia, mifumo ya kidijitali na taratibu za uendeshaji ili kuimarisha zaidi ushindani wa Bandari ya Dar es Salaam katika biashara ya kikanda na kimataifa. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Picha na kanda za video zilizosambaa zikionesha eneo la tukio zimeweka wazi mabaki ya helikopta iliyoanguka katika Shamba la Kudenga, huko Marondera, nchini Zimbabwe, ajali iliyochukua maisha ya mfanyabiashara maarufu Wicknell Chivayo, mkewe Lucy Muteke, na abiria wengine wanne.
Miili ya marehemu hao pamoja na abiria wengine wanne ambao bado hawajatajwa rasmi kwa majina yao yote, ingawa bado iko katika eneo la ajali Shamba la Kudenga, inaendelea kulindwa huku vyombo vya dola vikiendelea na taratibu za uchunguzi.
Uchunguzi wa awali unaonesha kuwa helikopta hiyo ilianguka ikiwa imepita dakika 40 tangu ipae kutoka eneo la Gandami, wilayani Chikomba, ambako tajiri huyo na mkewe walikuwa wakijenga nyumba yao.
CREDIT: ZBC NEWSThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Mfanyabiashara maarufu na bilionea kutoka nchini Zimbabwe, Wicknell Chivayo, pamoja na mkewe, Lucy “Lulu” Muteke, wanaripotiwa kupoteza maisha kutokana na ajali mbaya ya helikopta iliyotokea katika eneo la Marondera nchini humo Jumatano hii, Septemba 30, 2026.
Taarifa kutoka vyombo vya habari vya Zimbabwe, ikiwemo ZimLive, zimethibitisha kuwa Chivayo na mkewe walikuwa miongoni mwa watu sita waliopoteza maisha kwenye ajali hiyo, ripoti iliyotoka muda mfupi baada ya Serikali kuthibitisha kutokea kwa ajali hiyo ya kifo bila kuacha manusura yoyote.
Msemaji wa Serikali, Nick Mangwana, alithibitisha tukio hilo kupitia taarifa rasmi jioni ya Jumatano, akieleza kuwa ndege hiyo ilikuwa imewabeba mfanyabiashara maarufu, abiria wengine, na marubani wawili.
“Serikali inatamani kuthibitisha kuwa ajali ya helikopta imetokea, ikihusisha mfanyabiashara mmoja maarufu, abiria wanne, na marubani wawili,” ilisema taarifa ya Serikali, huku ikiongeza kuwa hakuna manusura waliotangazwa na kwamba Jeshi la Polisi la Zimbabwe (ZRP) litatoa orodha rasmi ya majina ya wote waliokumbwa na mkasa huo baada ya taratibu kukamilika.
Awali, Jeshi la Polisi lilieleza kuwa ndege hiyo ilikuwa na abiria sita, hali iliyoleta utofauti mdogo na taarifa ya Serikali iliyotaja jumla ya watu saba, huku mamlaka zikiwa bado hazijatoa ufafanuzi wa kina kuhusu utofauti huo wakati taarifa hii inatolewa. Hata hivyo, ripoti za uchunguzi huru zimeendelea kuwataja Chivayo na mkewe kama wahanga wakuu wa ajali hiyo. -
Jambo TV
@Jambotv_
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, CPA Amos Makalla, amesema kuwa zaidi ya wajumbe 100 kutoka mataifa 48 wanatarajiwa kuwasili jijini Arusha kuhudhuria Mkutano wa 46 wa Wakuu wa Mamlaka za Kodi za Jumuiya ya Madola (CATA), utakaofanyika kuanzia Oktoba 5 hadi 9, 2026.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Septemba 30, 2026, jijini Arusha, CPA Makalla amesema mkutano huo utafunguliwa rasmi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi, mnamo Oktoba 6 katika Hoteli ya Grand Melia.
Amebainisha kuwa kaulimbiu ya mkutano huo inalenga matumizi ya teknolojia katika kuongeza ufanisi wa ukusanyaji mapato, jambo ambalo litatoa fursa kwa Tanzania kujifunza mbinu bora za kimataifa, kujenga uwezo kwa wataalamu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), na kukabiliana na changamoto za biashara zinazovuka mipaka.
Sambamba na hilo, CPA Makalla amewataka wananchi na watoa huduma Arusha kutumia fursa hiyo kuwahudumia wageni kwa ukarimu na upendo, akisema wajumbe hao watatumia hoteli, usafiri na huduma mbalimbali wakati wa kukaa jijini humo.
Kwa upande wake, Naibu Kamishna Mkuu wa TRA, Mcha Hassan Mcha, ameeleza kuwa mbali na teknolojia na uchumi wa kidijitali, mkutano huo utajadili masuala ya kuboresha huduma kwa walipakodi ili kufikia viwango vya kimataifa na kubadilishana uzoefu wa kukabiliana na mabadiliko ya teknolojia katika mifumo ya kodi. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi ametangaza kuwa wizara nne za serikali zinakwenda kukutana kwa pamoja ili kuchakata na kutatua kero zinazotokana na Mfumo wa Kufuatilia Magari (VTS), kufuatia mgongano wa kitakwimu kati ya mfumo huo na kamera za usalama barabarani.
Katambi ameyasema hayo leo tarehe 30 Septemba 2026 mara baada ya kufika tena kuzungumza na madereva na abiria wa mabasi ya masafa marefu katika Kituo Kikuu cha Mabasi cha Magufuli jijini Dar es Salaam, kufuatia mgomo wa madereva wa kupinga mfumo wa kukatwa pointi za leseni na kero nyinginezo zilizosimamisha usafirishaji kwa siku mbili tangu tarehe 29 Septemba 2026.
Akibainisha changamoto zinazowakabili madereva kutokana na mfumo huo wa VTS, Katambi ameeleza kuwa zipo maeneo ambapo kamera za usalama barabarani zinasoma spidi 100 lakini mfumo wa VTS unaonesha spidi 130, hali inayowasababishia madereva adhabu na kero zisizo na hakit.
“Kwa hiyo hizi changamoto kwa maelekezo ambayo tumeyapata pia kwa Ofisi ya Waziri Mkuu, tunakwenda kukaa Wizara ya Ujenzi, Wizara ya Uchukuzi, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi lakini pia Wizara ya Kazi, Ajira na Mahusiano ili kwenda kulichakata jambo hili na kuweka utaratibu mzuri zaidi”, ameeleza.
Katambi amesisitiza kuwa mfumo wa VTS ni wa muda katika kipindi hiki cha mpito, akiahidi kuwa nchi inaelekea kwenye mfumo wa kisasa wa kidijiti wa kudhibiti spidi barabarani unaofanana na mfumo wa 'VAR' unaotumiwa kwenye mchezo wa mpira wa miguu.
Amesema mfumo huo utafanya kazi kwa kutumia kamera huru zitakazorekodi makosa moja kwa moja bila kuendeshwa au kudhibitiwa na askari, ili kuhakikisha haki inatendeka kwa kila dereva.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, leo tarehe 30 Septemba 2026 ametangaza hatua zilizochukuliwa na Serikali kufuatia maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, yenye lengo la kumaliza kero za madereva na mgomo uliodumu kwa siku mbili tangu tarehe 29 Septemba 2026.
Akizungumza katika Kituo Kikuu cha Mabasi cha Magufuli (Mbezi) jijini Dar es Salaam, Katambi amebainisha kuwa Rais ametoa maelekezo kwa Waziri Mkuu, ambaye naye amemkabidhi maagizo hayo ili kuyatekeleza kwa haraka, ikiwa ni pamoja na kurudisha leseni za madereva, kuondoa vizuizi visivyo na sababu barabarani, pamoja na kufanya matengenezo ya miundombinu ya barabara ili kuondoa mashimo yanayosababisha ajali.
Kuhusu suala la leseni zilizokamatwa na kufungiwa, Waziri Katambi ametangaza kuwa madereva waliofungiwa leseni zao kwa makosa madogomadogo watarejeshewa leseni zao kisheria kupitia Mamlaka ya Rufaa iliyo chini ya Waziri wa Mambo ya Ndani, kasoro wale tu waliosababisha ajali mbaya za vifo zinazokabiliwa na ushahidi mahakamani.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, leo tarehe 30 Septemba 2026 amefika tena kuzungumza na madereva na abiria wa mabasi ya masafa marefu katika Kituo Kikuu cha Mabasi cha Magufuli jijini Dar es Salaam, kufuatia kumalizika kwa mgomo wa madereva uliodumu kwa siku mbili tangu tarehe 29 Septemba 2026.
Mgomo huo uliokuwa ukipinga mfumo wa kukatwa pointi kwenye leseni za udereva na kero nyinginezo, umehitimishwa baada ya Serikali kufanya mazungumzo na wadau wa sekta ya usafirishaji, ambapo abiria wameanza tena safari zao kuelekea mikoani.
Akiwa kituoni hapo akisikiliza abiria kwenye mabasi, mmoja wa abiria ameeleza kushukuru kwa uamuzi wa Serikali kuingilia kati na kumaliza mgogoro huo uliokuwa ukiwakera wananchi na kusababisha manung'uniko dhidi ya Serikali
Akizungumza mbele ya Waziri Katambi, msafiri huyo amesema, “Kwahiyo hili jambo kwa kweli lilitukera sisi na vile ulivyolifungua tulishukuru sana, lakini yote kwa yote tunakushukuru sana. Maanake hili jambo linasababisha watu kuitukana serikali yao lakini sisi wengine wazee tunaipenda serikali yetu”, ameeleza abiria huyo. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Leo tarehe 30 Septemba 2026, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi amefika tena kuzungumza na madereva na abiria wa mabasi ya masafa marefu katika Kituo Kikuu cha Mabasi cha Magufuli jijini Dar es Salaam, kufuatia mgomo wa madereva wa kupinga mfumo wa kukatwa pointi za leseni na mambo mengine yanayowahusu, mgomo uliochukua siku mbili tangu jana Septemba 29, 2026.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Septemba 30, 2026, amekutana na kufanya mazungumzo maalum na viongozi wa madereva wa mabasi na malori nchini katika Ofisi Ndogo ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Mkutano huo umefanyika kufuatia mkwamo uliotokana na mgomo wa madereva uliodumu kwa siku mbili mfululizo katika baadhi ya mikoa nchini, uliovuruga shughuli za usafiri wa umma na kuwaacha abiria wakiwa wamekwama vituoni.
Katika mazungumzo hayo yaliyolenga kutafuta suluhu ya kudumu, viongozi wa madereva wameafiki kusitisha mgomo huo ili kuruhusu huduma za usafiri na usafirishaji kurejea kama kawaida, huku Serikali ikisisitiza utayari wake wa kusikiliza, kuchambua, na kuzifanyia kazi changamoto zote zinazowakabili wadau hao wa sekta ya usafiri nchini. -
Jambo TV
@Jambotv_
Wakazi wa Wilaya ya Kigamboni mkoani Dar es Salaam wako hatua chache kupunguza kwa kiwango kikubwa gharama za uondoshaji na usimamizi wa majitaka, kufuatia Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kukamilisha ujenzi wa mitambo miwili midogo ya kisasa ya kuchakata majitaka katika Kata za Vijibweni na Gezaulole, inayohudumia wakazi zaidi ya 410,400.
Mitambo hiyo, iliyogharimu kiasi cha Shilingi bilioni 2.3, imejengwa maalum kwa ajili ya kuchakata majitaka yanayozalishwa katika maeneo hayo, pamoja na kutoa huduma kwa malori na magari yanayojihusisha na shughuli za uondoshaji majitaka ndani ya Wilaya ya Kigamboni.
Meneja wa Miradi ya Majitaka wa DAWASA, Mhandisi Eric Mutalemwa, amesema kuwa mitambo hiyo imekamilika kikamilifu, imefanyiwa ukaguzi wote wa kitaalamu, na sasa ipo tayari kuanza kutoa huduma kwa wananchi.
“Miradi hii ya Vijibweni na Gezaulole ni ya kisasa ya kuchakata majitaka. Tumekagua na kujiridhisha na ukamilishaji wake na sasa iko tayari kutumika kuhudumia wananchi na watumiaji wa magari ya uondoshaji majitaka katika Wilaya hii,” amesema Mhandisi Mutalemwa.
Ameongeza kuwa kukamilika kwa kituo hicho kutapunguza mzigo mkubwa wa gharama ambazo watoa huduma binafsi na wananchi walikuwa wakizipata wakati wa kusafirisha majitaka hadi kwenye mabwawa ya mbali.
Mtazamo huo umeidhinishwa na madereva wa malori ya majitaka eneo hilo, akiwemo Habibu Ally, aliyeeleza kuwa mradi huo utapunguza kwa kiasi kikubwa gharama za uendeshaji kwa kuwa hautalazimu tena kusafiri umbali mrefu hadi Vingunguti au Kurasini.
“Awali ilitulazimu kwenda hadi katika mabwawa ya majitaka Vingunguti na Kurasini. Umbali huo ulifanya tozo kuwa kubwa kwa wateja na kuongeza gharama za uendeshaji wa magari. Mitambo hii itatusaidia kumwaga majitaka hapa hapa Kigamboni na kutupunguzia gharama,” amesema Ally.
Hatua hii inaelezwa kuongeza tija kubwa katika uboreshaji wa usafi wa mazingira wilayani humo na kurahisisha huduma za kijamii kwa ufanisi zaidi. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI PICHA:
Leo, Jumatano ya Septemba 30, 2026, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, John Heche, amevuka maji kwa kutumia mtumbwi kutoka eneo la Kisorya kuelekea kisiwa cha Ukerewe wilayani Ukerewe mkoani Mwanza ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa operesheni ya chama hicho ya Free Tundu Lissu na Katiba Mpya.
Heche, ambaye yuko katika ziara hiyo ya kisiasa, anatazamia kufanya mkutano mkubwa wa hadhara leo katika mji wa Ukerewe ili kuzungumza na wananchi na wanachama wa chama hicho, huku akiendelea na harakati za kushinikiza masuala mbalimbali yanayobeba ajenda kuu za chama hicho kwa sasa. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Baada ya mgomo wa madereva wa mabasi uliotokea jana, Septemba 29, katika Kituo cha Mabasi cha Nane Nane jijini Dodoma na kusababisha usumbufu kwa baadhi ya wasafiri baadhi ya mabasi yameanza tena safari leo, huku madereva wakisema bado changamoto zao hazijapatiwa majibu ya msingi.
Wakizungumza baadhi ya madereva walioanza safari leo, wamesema kurejea kwao barabarani kumetokana na ugumu wa maisha pamoja na kile walichodai kuwa ni msukumo kutoka kwa baadhi ya waajiri wao. Hata hivyo, wameeleza kuwa kurejea kwao kazini hakumaanishi kuwa wameacha madai yao.
“Hatujasaliti mapambano. Ni kweli Dodoma watu wameondoka kwa mihemko na njaa, lakini je, majibu kamili yako wapi?” amesema mmoja wa madereva.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Tanzania inaendelea kupanua wigo wa kimkakati katika kuvutia uwekezaji wa moja kwa moja kutoka barani Ulaya, ikitumia ziara maalum ya uhamasishaji nchini Finland kuwasilisha fursa zake kubwa za kiuchumi, kujenga ushirikiano mpya wa kibiashara, na kuunganisha miradi ya ndani na mitaji, teknolojia, na utaalamu wa kisasa kutoka mataifa ya Nordic na Ulaya kwa ujumla.
Akizungumza mbele ya wawekezaji jijini Helsinki, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Mipango na Uwekezaji, Dkt. Pius Stephen Chaya anayeongoza ujumbe wa Tanzania katika ziara ya kuhamasisha mataifa ya Ulaya kuwekeza nchini Tanzania, amewakaribisha wafanyabiashara na wawekezaji wa Finland kuichagua Tanzania kama kitovu kikuu cha uwekezaji wao, akisisitiza kuwa nchi inaendelea kuboresha mazingira ya biashara na kuweka sekta binafsi mbele kama kichocheo cha ukuaji wa uchumi.
Dkt. Chaya amebainisha kuwa kupitia Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, Tanzania inalenga kujenga uchumi shindani na jumuishi unaotumia teknolojia na uvumbuzi kuongeza tija katika sekta za kilimo, viwanda, miundombinu, TEHAMA, na uchumi wa kidijitali.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA), Gilead Teri, amewasilisha fursa mbalimbali za miradi mikubwa, huku akigusia kwa kina sekta ya madini ya kimkakati kama vile graphite, nickel, cobalt, na niobium.
Ametaja miradi mikubwa inayotoa fursa za mitaji na ushiriki wa kimataifa kuwa ni pamoja na Epanko Graphite, Kabanga Nickel, Southern Rukwa Helium, na Panda Hill Niobium. Aidha, ametolea mfano Eneo Maalum la Kiuchumi la Buzwagi (Buzwagi Special Economic Zone), ambalo lilikuwa mgodi wa dhahabu na sasa linabadilishwa kuwa kitovu cha uchakataji na uongezaji thamani wa madini.
Upande wa Finland, kupitia Katibu wa Kisiasa Pasi Rajala, umesifu uhusiano wa miaka 60 kati ya nchi hizo mbili na kuonesha utayari wa kuimarisha ushirikiano katika nyanja za uchumi wa kidijiti na madini, huku taasisi za kifedha kama Finnvera na Finnfund zikitajwa kuangalia uwezekano wa kutoa mifumo ya ufadhili kwa miradi ya pamoja.
Katika hatua nyingine, Teri ameongeza kuwa TISEZA, kupitia Kituo cha Pamoja cha Huduma za Uwekezaji itaendelea kurahisisha safari ya mwekezaji kuanzia hatua ya awali hadi utekelezaji, ikihakikisha kuwa rasilimali na mazungumzo hayo yanageuka kuwa miradi thabiti itakayonufaisha pande zote mbili. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (TABOA) kimetangaza kumalizika kwa mgomo wa madereva wa mabasi ya masafa marefu na kuwataka abiria kujitokeza kusafiri kurejea kwenye shughuli zao, huku kikiisistiza Serikali kuzingatia na kuzifanyia kazi kwa dhati hoja za msingi za madereva ili kuzuia kujirudia kwa migogoro hiyo.
Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa TABOA, Mustafa Mwalongo, ameyasema hayo leo tarehe 30 Septemba 2026 alipokuwa akizungumza na wanahabari katika Kituo Kikuu cha Mabasi cha Magufuli (Mbezi) jijini Dar es Salaam, ikiwa ni siku moja tangu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, alipokutana na kuzungumza na madereva na abiria jioni ya tarehe 29 Septemba 2026 kufuatia mgomo huo.
Hata hivyo, Mwalongo ameeleza kuwa baada ya Waziri kuondoka jana, kundi la madereva halikukubaliana na majibu hayo na lilitaka mgomo uendelee. Mzozo huo uliwalazimu viongozi wa TABOA kukutana saa 5:00 usiku na kuanza kupiga simu kwa wamiliki wa mabasi ili wazungumze na madereva wao.
"Magufuli tuna idadi ya magari yanayotoka kwa siku yasiyopungua 400... time table nyingi watu wanachukua jioni kuanzia alasiri kwa maana ya saa 9:00, saa 10, 11 usiku wa saa 2:00, saa 3:00, saa 4:00 hapa ndio tunakuwa tuna ‘peak kubwa’ ya magari yanayoondoka. Hivyo tunatarajia leo hizo gari 400 zitaondoka na abiria wengi watasafiri. Kwa hiyo naomba niwatangazie abiria kwamba mgomo umekwisha.", ameeleza.
Wakati huo huo, TABOA imethibitisha kuwa ipo katika kituo hicho cha Magufuli ikisubiri ujio wa Waziri Mkuu wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, ambaye anatarajiwa kufika kituoni hapo kuzungumza na wadau na kutoa mwafaka wa mwisho.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Faustine Mafwele amefika katika Kituo cha Mabasi Magufuli akiwa na askari wengine wa Kamati ya Ulinzi na Usalama kushuhudia hali ya mgomo wa madereva wa mabasi unaoendelea.
Mgomo huo ulianza jana, Septemba 29, 2026 na leo umeingia siku ya pili, huku madereva wakishinikiza madai yao, ikiwemo kushughulikiwa kwa suala la kufungiwa leseni ili waweze kuendelea na shughuli zao kwa amani na kukidhi mahitaji yao.
Hii ni hali ya tarehe 30 Septemba 2026 inajiri siku moja tangu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi kuzungumza na madereva na abiria wa mabasi ya masafa marefu jioni ya Septemba 29, 2026 katika Kituo Kikuu cha Mabasi cha Magufuli jijini Dar es Salaam, kufuatia mgomo wa madereva wa kupinga mfumo wa kukatwa pointi za leseni.
Katika kile kinachoonekana kuwa mfupa mgumu, Waziri Mkuu wa Tanzania Dkt. Mwigulu Nchemba anatarajiwa kufika kituoni hapo kuzungumza na madereva na abiria juu ya malalamiko yao -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO: Siku moja tangu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, alipokutana na kuzungumza na madereva na abiria jioni ya tarehe 29 Septemba 2026 kufuatia mgomo wa kupinga mfumo wa kukatwa pointi za leseni, baadhi ya madereva katika Kituo Kikuu cha Mabasi cha Magufuli (Mbezi) jijini Dar es Salaam wameeleza kuendelea kuwa na wasiwasi na ahadi za Serikali kwa kudai kuwa hakuna utekelezaji wa dhati.
Hali hiyo inajiri asubuhi ya leo tarehe 30 Septemba 2026 katika Kituo cha Magufuli, wakati ikiwa inatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, atawasili kituoni hapo kuzungumza na madereva na abiria ili kutafuta muafaka wa mwisho kwenye suala hilo.
Akizungumza kituoni hapo asubuhi ya leo, dereva wa basi la kampuni ya Mbazi Trans aliyekuwa anaandaa basi lake kufanya safari ya kuelekea Arusha ikiwa ni gari la kwanza kuelekea mkoani humo tangu siku iliyopita amebainisha kuwa ingawa viongozi wameeleza kusitisha Mfumo wa Ukataji Pointi na kunyang'anya leseni, madereva wengi wanajikuta kwenye sintofahamu kwa sababu maelekezo yanayotolewa yanapingana na yanayotokea barabarani. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Tangazo rasmi limetolewa kupitia spika za Kituo Kikuu cha Mabasi cha Magufuli (Mbezi) jijini Dar es Salaam likitaka gari lolote ambalo haliko tayari kufanya safari liondolewe kituoni hapo na abiria warejeshewe nauli zao, huku ulinzi ukiimarishwa kikamilifu leo tarehe 30 Septemba 2026.
Hali hii inajiri ikiwa ni siku moja tangu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, alipozungumza na madereva pamoja na abiria wa mabasi ya masafa marefu jioni ya Septemba 29, 2026 kufuatia mgomo wa madereva wa kupinga mfumo wa kukatwa pointi za leseni. Katika kile kinachoonekana kuwa mfupa mgumu, Waziri Mkuu wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, anatarajiwa kufika kituoni hapo leo kuzungumza na madereva na abiria juu ya malalamiko yao ili kutoa mwafaka wa mwisho.
Jambo TV ipo 'live' muda huu kutoka Stendi ya Magufuli upande wa Youtube na itakuwa ikikuletea kila kinachojiri huko hapahapa katika kurasa zake za mitandao ya kijamii.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mvutano umeibuka katika Kituo Kikuu cha Mabasi cha Magufuli (Mbezi) jijini Dar es Salaam asubuhi ya leo tarehe 30 Septemba 2026, kufuatia kukamatwa na kushikiliwa na Jeshi la Polisi kwa dereva anayejulikana kwa jina la Said, kwa tuhuma za kuhamasisha wenzake kuendelea na mgomo wa kutosafirisha abiria.
Madereva waliopo kituoni hapo waliweka msimamo mkali kuwa hakuna gari litakalotoka wala kuanza safari mpaka pale dereva mwenzao Said atakapoachiwa huru na utatuzi wa msingi wa kero zao utakapopatikana. Hata hivyo haijajulikana kama Said ameshaachiwa au laa kwani baadhi ya mabasi yameonekana yakiondoka kituoni hapo.
Hali hii inajiri ikiwa ni siku moja tangu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, alipozungumza na madereva na abiria jioni ya Septemba 29, 2026 kufuatia mgomo wa kupinga mfumo wa kukatwa pointi za leseni. Katika kile kinachoonekana kuwa mfupa mgumu, Waziri Mkuu wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, anatarajiwa kufika kituoni hapo kuzungumza na madereva na abiria juu ya malalamiko yao.
Jambo TV ipo 'live' muda huu kutoka Stendi ya Magufuli upande wa Youtube na itakuwa ikikuletea kila kinachojiri huko hapahapa katika kurasa zake za mitandao ya kijamii.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Baadhi ya madereva wakijaribu kumzuia dereva wa gari la kampuni ya Burudani Tosha asitoe gari katika kituo cha Mbezi Magufuli.
Jambo TV ipo 'live' muda huu kutoka Stendi ya Magufuli upande wa Youtube na itakuwa ikikuletea kila kinachojiri huko hapahapa katika kurasa zake za mitandao ya kijamii. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Hali ya mvutano imeendelea kutanda katika Kituo Kikuu cha Mabasi cha Magufuli (Mbezi) jijini Dar es Salaam asubuhi ya leo tarehe 30 Septemba 2026, ambapo baadhi ya kampuni za mabasi zimeonekana zikianza michakato ya kuondoka na kuhudumia abiria, huku kundi jingine la madereva likiendelea kushinikiza kuwa msimamo wa kugoma uendelee hadi kero zao za miaka mingi na changamoto za barabarani zitakapopatiwa majibu ya msingi.
Mabadiliko haya ya asubuhi yanajiri ikiwa ni siku moja tangu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, alipofika na kuzungumza na madereva na abiria jioni ya tarehe 29 Septemba 2026 kufuatia mgomo wa kupinga mfumo wa kukatwa pointi za leseni. Katika kile kinachoonekana kuwa mfupa mgumu, Waziri Mkuu wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, anatarajiwa kufika kituoni hapo leo kuzungumza na madereva pamoja na abiria ili kupata suluhu ya kudumu.
Kufika kwa Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba kunatarajiwa kutoa mwelekeo rasmi wa Serikali na kumaliza mgogoro huo uliolemaza huduma za usafirishaji na kuathiri shughuli za wananchi katika maeneo mbalimbali nchini tangu siku ya jana.
Jambo TV ipo 'live' muda huu kutoka Stendi ya Magufuli upande wa Youtube na itakuwa ikikuletea kila kinachojiri huko hapahapa katika kurasa zake za mitandao ya kijamii.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkandarasi anaetekeleza Mradi wa Maji wa vijiji Nane Ngorongoro, ametakiwa kuhakikisha ndani ya miezi mitatu Mradi huo unakamilika na unaanza kutoa huduma ya maji safi na salama kwa wakazi wa vijiji vya Ng'arwa, Mageri, Tinanga, Olorieni, Magaiduru, Mgongo, Yasi na Mdito.
Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ametoa maagizo hayo wakati alipotembelea kukagua utekelezaji wa mradi huo katika Kijiji cha Yasi.
"Huu Mradi ninaujua vizuri sana, sasa miezi mitatu inawatosha kuhakikisha Mradi huu unakamilika na wananchi wanaanza kupata huduma ya maji". Amesema Waziri Aweso.
Mradi wa Maji wa vijiji Nane unaotekelezwa na RUWASA pamoja na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa mazingira Arusha (AUWSA) kutoka vyanzo vya Mto Orkanjor na chemchem ya Yasi unathamani ya shilingi bilioni 6.1 na umefikia asilimia 60 ya utekelezaji wake, ukikamilika unatarajiwa kuwanufaisha wananchi wapatao 32,000 na Mifugo 10,000 iliyopo katika vijiji hivyo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mmoja wa wasafiri wa mabasi ya masafa marefu aliyekuwa akisafiri kuelekea mkoani Mara katika Kituo Kikuu cha Mabasi cha Magufuli jijini Dar es Salaam, ameeleza kukata tamaa kabisa ya kuondoka na kubainisha kuwa yuko tayari kusalia hapo hadi afe na njaa kufuatia kukwama kwa safari zao.
Msafiri huyo, amebainisha kuwa pamoja na kulipia tiketi yake, kampuni husika imekuwa ikimzungusha bila kurejesha gharama zake huku wakiendelea kumwambia asubiri gari litaondoka. Ameeleza kuwa amepoteza kabisa imani ya kusafiri baada ya kuona viongozi mbalimbali wa serikali na Jeshi la Polisi wakishindwa kutatua mgogoro huo.
Kukwama huko kwa abiria kunaendelea leo tarehe 30 Septemba 2026, ikiwa ni siku moja tangu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, alipofika na kuzungumza na madereva na abiria jioni ya Septemba 29, 2026 kufuatia mgomo wa madereva wa kupinga mfumo wa kukatwa pointi za leseni. Katika kile kinachoonekana kuwa mfupa mgumu, Waziri Mkuu wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, anatarajiwa kufika kituoni hapo kuzungumza na madereva na abiria juu ya malalamiko yao.
Akizungumzia ujio wa Waziri Mkuu, msafiri huyo ametoa ushauri wa namna kikao hicho kinavyopaswa kuendeshwa ili kupata suluhu ya kudumu badala ya mikutano ya hadhara ambapo watu wengi ‘wanaropoka’ tu. Amependekeza kuwa Waziri Mkuu akae chemba na pande zinazohusika.
"Waziri anapokuja tunaomba atoe kauli kama Waziri Mkuu kwamba hiki kifanyike na watu watekeleze tu, ndicho tunachokiomba... Kinachotakiwa kifanyike, madereva waitwe na LATRA waitwe wakae pamoja na Waziri Mkuu uelewano utakuwepo, lakini sio Waziri Mkuu anakuja anakaa na watu wote, mwingine siyo dereva, mwingine ni dereva wanaropokaropoka pale.", ameeleza msafiri huyo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwananchi wa Kijiji cha Mkwajuni, Tunduru Kaskazini, amesema hajatosheka na majibu ya Serikali kuhusu namna ya kutatua changamoto ya mifugo kuingia kwenye mashamba ya wakulima, akisema bado ng’ombe wanaendelea kuharibu mazao na kuwaongezea wananchi hasara.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika Septemba 28, 2026 kijijini hapo, mwananchi huyo amemweleza Mbunge wa Tunduru Kaskazini, Ado Shaibu Ado, kuwa wananchi bado wanasubiri utekelezaji wa kauli iliyowahi kutolewa na Waziri Mkuu kuhusu kuchukuliwa hatua dhidi ya wafugaji wanaoingiza mifugo kwenye mashamba ya wakulima.
Amesema hali hiyo imeendelea kuwa kero kwa wakulima wa Mkwajuni, ambao mazao yao yakiwemo mahindi na korosho yamekuwa yakiharibiwa na mifugo, licha ya Serikali kueleza hatua inazochukua kukabiliana na migogoro ya wakulima na wafugaji.
Kauli hiyo imekuja baada ya Mbunge Ado Shaibu Ado kuibua suala hilo Bungeni Agosti 27, 2026, akiiomba Serikali kuchukua hatua madhubuti kutokana na migogoro ya wakulima na wafugaji ambayo, kwa mujibu wake, imekuwa ikisababisha uharibifu wa mazao, majeruhi na vifo katika Jimbo la Tunduru Kaskazini na maeneo mengine nchini.
Akijibu swali hilo, Waziri Mkuu Mwigulu Nchemba alisema Serikali inaendelea kuchukua hatua kadhaa, ikiwemo kusimamia matumizi bora ya ardhi na kuwachukulia hatua za kisheria wafugaji wanaoingiza mifugo kwenye mashamba ya wakulima.
Waziri Mkuu pia aliagiza Kamati za Ulinzi na Usalama za Mikoa na Wilaya kusimamia sheria katika kudhibiti migogoro hiyo.
Hata hivyo, kwa mwananchi huyo wa Mkwajuni, hatua hizo bado hazijatoa suluhu anayotarajia, akisema wananchi wanaendelea kukabiliwa na mifugo inayoharibu mashamba yao.
“Sijaridhishwa na majibu ya Waziri Mkuu. Bado tunateseka mashambani, ng’ombe wanaingia na kuharibu mahindi na korosho zetu,” amesema.
Ametaka Mbunge Ado Shaibu Ado kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa hatua zilizotajwa na Serikali ili changamoto hiyo ipate suluhu ya kudumu.
Kwa upande wake, Mbunge Ado Shaibu Ado ameitaka Serikali kuendelea kuchukua hatua madhubuti katika kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji, akisema suala hilo linaendelea kuwa changamoto kwa wananchi wa Tunduru Kaskazini na maeneo mengine nchini.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Asubuhi ya leo tarehe 30 Septemba 2026, simanzi imetawala katika Kituo Kikuu cha Mabasi cha Magufuli jijini Dar es Salaam baada ya Bwana Harusi aliyekuwa akisafiri kuelekea wilayani Kahama mkoani Shinyanga kwa ajili ya sherehe ya Send-off iliyopangwa kufanyika kesho, kukwama na kumwaga machozi kufuatia mgomo wa madereva wa mabasi ya masafa marefu.
Bwana Harusi huyo ameeleza kuwa alikata tiketi ya Shilingi 70,000 kutoka kwa wakala wa mabasi kwa ahadi kwamba gari lingeondoka saa 12:00 asubuhi, licha ya wakala huyo kujua fika kuwepo kwa mgomo huo.
Baada ya safari kukwama, msafiri huyo alimfuata wakala huyo ili arudishiwe fedha zake atafute usafiri mbadala, lakini wakala alikataa na kumtaka aende Polisi akidai kuwa hilo ni janga la kiserikali. Ameeleza kuwa ndugu na wageni kule Kahama tayari wameshajikusanya, hivyo kuchelewa kwake kunatishia kuvunja sherehe hiyo na kusababisha hasara kubwa.
Jambo TV ilipopiga simu kwa mwakilishi wa kampuni hiyo ya basi ili kuhoji sababu za kutosafirisha abiria wala kurejesha nauli, mwakilishi huyo alidai kuwa mgomo huo ni "janga la taifa" na kwamba kampuni pia imepata hasara kwani magari yapo tayari lakini madereva ndio waliogoma kuendesha.
Kukwama huko kwa abiria kunatokea ikiwa ni siku moja tangu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, alipofika na kuzungumza na madereva pamoja na abiria kituoni hapo jioni ya Septemba 29, 2026 kufuatia mgomo wa kupinga mfumo wa kukatwa pointi za leseni. Katika kile kinachoonekana kuwa mfupa mgumu, Waziri Mkuu wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, anatarajiwa kufika katika stendi hiyo leo kuzungumza na madereva na abiria ili kutafuta ufumbuzi wa malalamiko hayo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mmoja wa wasafiri wa mabasi ya masafa marefu katika Stendi Kuu ya Mabasi ya Magufuli jijini Dar es Salaam, Abdallah Shabani, akizungumza na Jambo TV asubuhi ya leo tarehe 30 Septemba 2026, ameeleza kukabiliwa na hofu kubwa ya kupoteza ajira na kuingia hasara kufuatia kukwama kwa safari yake kutokana na mgomo wa madereva.
Kukwama huko kwa abiria kunajiri ikiwa ni siku moja tangu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, alipofika na kuzungumza na madereva pamoja na abiria katika kituo hicho jioni ya Septemba 29, 2026 ili kusikiliza kero zao zilizosababishwa na mgogoro wa mfumo wa kukatwa pointi za leseni.
Bw. Abdallah, aliyekuwa akisafiri kuelekea Tanga, amebainisha kuwa alikata tiketi tangu jana lakini hadi asubuhi ya leo alikuwa hajapewa mwongozo wowote na wamiliki wa basi kuhusu muda wa kuondoka, huku juhudi zake za kupiga namba zilizopo kwenye tiketi na kutafuta watumishi katika ofisi zao zikiishia patupu.
Hata hivyo, tofauti na mabasi mengine yaliyoanza kuonesha matumaini kwa madereva kuwasha magari, Abdalla ameeleza kuwa basi alilokata tiketi halikuwa na mhudumu wala dereva tangu siku iliyopita, hali iliyomnyima matumaini yoyote ya kuondoka.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
#ad
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Nchi ya Qatar, Tume ya Umoja wa Afrika na washiriki kutoka nchi wanachama wa Baraza la Ushirikiano la Nchi za Ghuba (Gulf Cooperation Council - GCC) imeandaa Mkutano wa Pili wa Uhamaji wa Nguvu Kazi (Second Doha Dialogue on Labour Mobility).
Mkutano huo utaratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira na Mahusiano na utafanyika kuanzia Oktoba 5 - 6, 2026 katika hoteli ya Hyatt Regency, Dar es Salaam ukiongozwa na kaulimbiu “Kuendeleza Uhamaji wa Nguvu kazi yenye Haki na endelevu katika ya Nchi za Afrika na Ghuba (GCC+). -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI:
Upande wa mashtaka umesema kunyongwa si adhabu pekee inayoweza kutolewa endapo Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, atapatikana na hatia katika kesi ya uhaini inayomkabili.
Kauli hiyo imetolewa Septemba 29, 2026 na Wakili wa Serikali Mkuu, Nassoro Katuga, wakati akihitimisha uwasilishaji wa hoja za mwisho za Jamhuri mbele ya jopo la majaji watatu linaloongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru.
Katuga ameiambia Mahakama kuwa kifungu cha 39(2)(d) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu kinaipa Mahakama mamlaka ya kutumia busara katika kuamua adhabu inayofaa.
Katika hoja zake nyingine, Katuga amesema Jamhuri imeweza kuthibitisha viini vya kosa kupitia ushahidi wa mashahidi 17. Ameeleza kuwa Lissu, akiwa raia wa Tanzania, alikuwa na wajibu wa utii kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lakini alitoa na kusambaza kauli ambazo, kwa madai ya mashtaka, zililenga kuitishia Serikali.
Kuhusu madai ya Lissu kwamba baadhi ya maneno yaliondolewa katika hati ya mashtaka, Katuga amesema Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Jinai inahitaji hati hiyo kuwa na maelezo yenye maana na taarifa muhimu kuhusu kosa, si lazima ijumuishe kila neno lililotamkwa. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mtu mmoja ameuawa kwa risasi na polisi baada ya kumteka mwanamke na mtoto wake katika Kijiji cha Parakuyo, Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro, na kuwafungia ndani ya chumba huku akiwatumia kama kinga dhidi ya polisi.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, ACP Andrew Kantimbo, mwanaume huyo, aliyetajwa kwa jina la Kokan State, mwenye umri wa miaka 30, alikuwa akitafutwa na polisi kwa tuhuma zinazohusisha mauaji, ubakaji na wizi wa kutumia silaha.
Kantimbo amesema polisi walifanikiwa kubaini alikokuwa mtuhumiwa huyo na kufika eneo hilo kwa ajili ya kumkamata, ambapo Kokan alimshika mwanamke aliyekuwa akimhudumia kinywaji pamoja na mtoto wake mdogo na kuwafungia ndani ya chumba.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, ameingilia kati mgomo wa madereva na abiria wa mabasi ya masafa marefu katika Kituo Kikuu cha Mabasi cha Magufuli jijini Dar es Salaam, huku akiagiza kupatiwa orodha kamili ya leseni zote zilizofungiwa pamoja na sababu zake.
Akizungumza na madereva na abiria hao jioni ya leo Septemba 29, 2026, kufuatia mgomo wa kupinga mfumo wa kukatwa pointi za leseni na ufungaji wa leseni zao, Katambi ametoa wito wa kuwepo kwa utulivu na usikilizano ili kufikia suluhu ya pamoja.
"Hakuna jamii ambayo inaweza ikafanikiwa jambo kama hamsikilizani... Kwenye zile leseni zilizofungiwa kuna wengine wamefungiwa leseni lakini kuna wengine ambao wanazungumzia swala la ufungaji leseni wasifunge polisi ziwe na utaratibu mwingine," amesema Katambi.
Akiweka wazi kuhusu takwa la madereva la kutaka mfumo wa ufungaji leseni ufutwe mara moja, Katambi ameeleza ukweli kuwa maamuzi ya mfumo huo yalipitishwa na Bunge na vikao halali vya kiserikali, hivyo hayawezi kufutwa tu kwa tamko la kiongozi aliyesimama jukwaani.
Katambi amewahakikishia madereva na abiria hao kuwa serikali imechukua kero na maoni yao kwa uzito na kwamba suala hilo linakwenda kufanyiwa kazi kwa pamoja na wizara zote husika chini ya uratibu wa Ofisi ya Waziri Mkuu.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwanamke mkazi wa Kijiji cha Mkwajuni, Tunduru Kaskazini, amemweleza Mbunge wa eneo hilo, Ado Shaibu Ado, kwa uchungu na machozi namna mifugo inavyoharibu mashamba na kuathiri maisha ya familia yake.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara jana Septemba 28, 2026, mwanamke huyo aliyejitambulisha kuwa mzaliwa wa eneo hilo, alisema familia yake imekosa chakula baada ya mazao yao kuharibiwa na mifugo.
Alisema amewahi kumfuata mtendaji wa eneo hilo na kuomba suala hilo lifikishwe kwa Serikali, akieleza kuwa hali hiyo imekuwa ikiathiri wakulima wengi katika eneo hilo.
“Maombi yangu makubwa ni kupitia Mheshimiwa Rais ili aweze kuwaokoa binadamu walioko katika hali ngumu,” alisema.
Mwanamke huyo aliomba hatua zichukuliwe haraka kulinda mashamba ya wakulima na kuzuia hali hiyo kuendelea kuathiri maisha ya familia zinazotegemea kilimo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mvutano na mshikemshike umeibuka katika Stendi Kuu ya Mabasi Mkoa wa Kigoma (Stand Mpya), kufuatia madereva wa mabasi ya mikoani kukaidi agizo la Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma (RPC) aliyewataka kuanza safari, huku wao wakishikilia msimamo wa kusitisha huduma kuanzia leo mchana, Septemba 29, 2026. Mtafaruku huo umeacha mamia ya abiria kituoni hapo tangu karibu kutwa nzima ya licha ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, SACP Filemon Makungu kuingilia kati.
Wakizungumza eneo hilo, madereva kupitia Kassim, Thabiti Juma, na Hamisi Hamisi, wamesisitiza kuwa hatua hiyo si mgomo wa kukataa kuwahudumia wananchi, bali ni shinikizo la kutaka Serikali kubadili mfumo wa sasa.
Akiingilia kati mzozo huo, RPC Filemon Makungu, ameagiza magari yote yaondoke mara moja chini ya ulinzi wa polisi:
"Tumefika hapa kuhakikisha magari yote yaliyopangwa kwenda safari yanakwenda kwa usalama na hairuhusiwi kwa mtu kuzuia gari. Ninawahakikishia abiria tutatoa ulinzi wa kutosha. Kama madereva wana madai, yanashughulikiwa na ngazi husika na yasitatize safari za wananchi," amesema Kamanda Makungu.
Licha ya amri hiyo na ahadi ya ulinzi kutoka kwa RPC, madereva hao waliendelea kushikilia msimamo wao wa kutosafirisha magari, huku Jeshi la Polisi likiendelea kusimamia eneo hilo ili kurejesha huduma.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, ametoa wito kwa Watanzania na makundi mbalimbali ya kijamii kuondoa chuki, visasi na kujenga utamaduni wa kuvumiliana na kusikilizana ili kulinda amani na ustawi wa taifa.
Katambi ameyasema hayo leo jioni ya tarehe 29 Septemba 2026 wakati akizungumza na madereva na abiria wa mabasi ya masafa marefu katika Kituo Kikuu cha Mabasi cha Magufuli jijini Dar es Salaam, kufuatia vuguvugu la mgomo wa madereva wa kupinga mfumo wa kukatwa pointi za leseni.
Akiwasilisha ujumbe huo mbele ya madereva na abiria waliokusanyika kituoni hapo, Katambi ameeleza masikitiko yake kuhusu kuongezeka kwa chuki zisizo na sababu kwenye jamii na kusisitiza kuwa nchi haiwezi kujengwa kwa misingi ya kutokusikilizana.
Katika kuonesha jinsi makundi yote katika jamii yanavyotegemeana, Katambi ametoa mfano wa umuhimu wa ushirikiano kati ya madereva, abiria na Jeshi la Polisi. Ameeleza kuwa iwapo kundi moja litakosekana au kuacha kuwajibika, mnyororo wa uchumi na maisha ya kila siku yatasimama, kwani biashara na huduma mbalimbali zinategemea usafirishaji wa madereva.
Waziri Katambi ametoa ahadi kwamba atakuwa balozi wa madereva katika kufikisha na kushughulikia kero zao zilizofungamanishwa na sheria kwenye mamlaka husika, akisisitiza kuwa Serikali inatambua mchango mkubwa wa madereva katika ujenzi wa uchumi wa taifa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amemteua aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesera kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro.
Uteuzi huo umefanyika leo Septemba 29, 2026 kwa mujibu wa taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka iliyowasilishwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Bakari Machumu. -
Jambo TV
@Jambotv_
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua Mbunge wa zamani wa Jimbo la Nyamagana mkoani Mwanza, Stanslaus Shing' oma Mabula kuwa Mkuu wa Wilaya ya Rorya mkoani Mara.
Uteuzi huo umefanyika leo Septemba 29, 2026 kwa mujibu wa taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka iliyowasilishwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Bakari Machumu. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI PICHA:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amemhamisha Hassan Omary Bomboko kutoka Wilaya ya Hai kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro.
Uteuzi huo umefanyika leo Septemba 29, 2026 kwa mujibu wa taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka iliyowasilishwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Bakari Machumu. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI PICHA:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amemteua Neema Lugangira kuwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha.
Uteuzi huo umefanyika leo Septemba 29, 2026 kwa mujibu wa taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka iliyowasilishwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Bakari Machumu. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Maji, Jumaa Aweso akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Arusha, amewataka watumishi wa sekta ya maji wilayani Karatu kusimama imara na kukaa “mguu sawa” katika kuhakikisha wanatoa huduma ya maji ya uhakika kwa wananchi badala ya huduma za kusuasua au himilivu, huku akisisitiza kuwa watumishi watakaoshindwa kuendana na kasi hiyo wanapaswa kupisha wengine.
Akizungumza katika kikao kazi maalum kilichowakutanisha watumishi wa sekta ya maji kutoka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Karatu (KARUWASA), Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA), na Bodi ya Maji ya Bonde la Kati katika ukumbi wa Mkurugenzi wa Mji wa Karatu, Waziri Aweso amewasihi watumishi hao kuwaza na kutenda kwa namna itakayoleta tija ya haraka.
Amebainisha kuwa kwa vile Karatu ni mji wa kitalii unaotembelewa na wageni wengi kutoka ndani na nje ya nchi, unapaswa kuwa na miundombinu na huduma ya maji safi na salama isiyo na dosari wala usumbufu.
Waziri Aweso yupo mkoani Arusha kwa ziara maalum ya kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maji, akifuatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Mwajuma Waziri, pamoja na wataalamu wengine kutoka wizara hiyo na taasisi zake.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, amesema alishatoa maelekezo kwamba hakuna dereva anayepaswa kukatwa pointi kwenye leseni kwa sasa, akisema mfumo huo bado uko katika hatua ya majaribio.
Katambi amesema hayo leo, Septemba 29, 2026, wakati akizungumza na madereva wa mabasi ya masafa marefu katika Kituo Kikuu cha Mabasi cha Magufuli jijini Dar es Salaam, kufuatia mgomo wao kupinga mfumo wa pointi.
Amesema dereva yeyote ambaye tayari amekatwa pointi katika kipindi hiki ameonewa, huku akiwataka ambao wamefungiwa leseni kufika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa hatua zaidiThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Madereva wa mabasi ya masafa marefu wamewasilisha kero na changamoto mbalimbali zinazowakabili wakati wakitekeleza majukumu yao mbele ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, alipofika katika Kituo Kikuu cha Mabasi cha Magufuli mkoani Dar es Salaam.
Waziri Katambi amefika kituoni hapo kwa maelekezo ya Waziri Mkuu ili kusikiliza hoja za madereva na kutafuta ufumbuzi wa changamoto hizo kufuatia mgomo wa madereva wakipinga 'mfumo wa pointi' na usumbufu katika kazi zao.
Mmoja wa madereva, amebainisha kuwa chanzo kikuu cha usumbufu katika kazi zao kinatokana na mfumo wa ukataji wa pointi 15 kwenye leseni pamoja na utendaji wa askari wa usalama barabarani. . Ameeleza kuwa iwapo pointi hizo 15 zitagawanywa katika kipindi cha miaka mitano cha uhalali wa leseni, dereva anaweza kujikuta leseni yake imeisha ndani ya siku tatu tu za safari kutokana na makosa madogo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Hukumu katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, itasomwa Novemba 6, 2026 saa tatu asubuhi, ikiwa ni baada ya majaji kupitia ushahidi wa pande zote mbili na kufanya maamuzi.
Hayo yamesemwa leo Septemba 29, 2026 na Jaji Dunstan Ndunguru ambaye anaongoza jopo la majaji waliokuwa wanasikiliza shauri hilo la uhaini namba 19605/2025.
Jaji Dunstan Ndunguru amesema kwamba, kutokana na aina ya ushahidi uliowasilishwa na pande zote mbili, wao kama majaji pia watahitaji muda wa kutosha ili mwisho waje na maamuzi ambayo yameandaliwa vyema.
Kabla ya majaji kutoa uamuzi huo, upande wa mashtaka ulikuwa ukiendelea na mawasilisho ya hoja za mwisho ambapo baada ya kuhitimisha waliwasihi majaji kuja na uamuzi mzuri, wakisema wao wamehakikisha wamethibitisha mashtaka.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi amewasili Stendi Kuu ya Mabasi ya Mbezi Magufuli mkoani Dar es Salaam kufuatia mabasi kusitisha safari zake kwa kile kilichoelezwa kuwa mgomo wa madereva.
Katambi anatarajiwa kuzungumza na madereva na abiria mbele ya vyombo vya habari jioni hiiThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Chama cha ACT Wazalendo kimemtaka Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, kujiuzulu mara moja kufuatia mgogoro wa usafirishaji na mgomo wa madereva wa mabasi na malori unaotajwa kuathiri shughuli za kijamii na kiuchumi nchini.
Tamko hilo limetolewa leo Jumanne tarehe 29 Septemba 2026 kupitia kwa Waziri Kivuli wa Ofisi ya Waziri Mkuu- Sera, Bunge na Uratibu, Naggy Kaboyoka, kufuatia hatua ya madereva katika maeneo mbalimbali nchini kusitisha huduma za usafirishaji.
"Hivyo basi, ACT Wazalendo inamtaka Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Ndg. Patrobas Katambi, kujiuzulu mara moja kwa kushindwa kuchukua hatua kwa wakati za kusikiliza malalamiko ya madereva na kuzuia mgogoro huu usifikie hatua ya kuathiri maisha na shughuli za wananchi." , imeeleza taarifa hiyo.
Taarifa hiyo ya ACT Wazalendo inakuja saa chache baada ya Jeshi la Polisi nchini, kupitia Kamishna wa Operesheni na Mafunzo, CP Awadh Juma, kusisitiza wakati akizungumza na wanahabari mkoani Dar es Salaam kuwa mfumo mpya wa ukataji wa pointi 15 kwenye leseni za udereva bado haujaanza kutekelezwa rasmi kisheria na kwamba hadi sasa hakuna dereva aliyefutiwa leseni au kukatwa pointi. CP Awadh alieleza kuwa hatua iliyopo sasa ni ya kutoa uelimishaji kwa umma, huku akitoa onyo kali dhidi ya watu wanaohamasisha na kuzuia vyombo vya usafiri barabarani, akiahidi kuwa serikali imeweka ulinzi wa kutosha.
Hata hivyo, ACT Wazalendo imeeleza kuwa imepokea kwa uzito mkubwa kusitishwa kwa huduma za usafirishaji kulikoanza leo, ikibainisha kuwa malalamiko ya madereva kuhusu utekelezaji wa mfumo huo na ukosefu wa utaratibu wa haki wa kushughulikia kero zao yamepuuzwa na Serikali kwa muda mrefu.
"Madereva wamekuwa wakitoa malalamiko na kuomba Serikali iingilie kati changamoto zinazowakabili hasa utekelezaji wa mfumo wa kukata alama 15 katika leseni zao. Madereva walieleza mapungufu ya mfumo wenyewe na utekelezaji wake. Ni wazi kuwa ni mfumo kandamizi, unaweka mzigo usio wa haki kwa madereva, unaongeza hofu ya kupoteza ajira, na kufungua mianya ya rushwa na uonevu", ameeleza Naggy Kaboyoka.
Tamko hilo linaeleza kuwa ingawa Serikali kupitia Waziri imedai mfumo huo uko kwenye majaribio, madereva wameendelea kukumbana na changamoto, vitisho, faini na kufungiwa leseni zao, hatua iliyosababisha wananchi kuathirika vibaya kwa kukosa usafiri wa kwenda hospitalini, kwenye biashara na kusafirisha mizigo.
ACT Wazalendo imesisitiza kuwa Serikali ilikuwa na wajibu wa kutumia nafasi iliyokuwepo kufanya mazungumzo na madereva kabla mgogoro haujafikia hatua hiyo. Kutokana na hali hiyo, Kaboyoka amesema,
"Mwisho, tunasisitiza tena msimamo wetu kwamba utekelezaji wa mfumo wa pointi 15 katika leseni za madereva usimamishwe mara moja na Serikali ifanye mapitio ya kanuni hizo kwa kushirikisha madereva na wadau wengine wa sekta ya usafirishaji.", imeeleza taarifa ya ACT. -
Jambo TV
@Jambotv_
Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu limefanikiwa kumpata kijana Gatami Maduhu Martine (20), mkazi wa kijiji cha Mwauchumu Wilaya ya Bariadi, aliyekuwa anaripotiwa kutoweka katika mazingira ya kutatanisha kwa muda wa wiki moja na kuibua hofu kubwa kwa familia yake.
Kulingana na taarifa rasmi kwa umma iliyotolewa leo tarehe 29 Septemba 2026 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Edith Swebe, ufuatiliaji wa tukio hilo ulianza mnamo tarehe 25 Septemba 2026 baada ya babu wa kijana huyo, Gatami Maduhu Maltine (64), kuripoti kituo cha Polisi Bariadi kuhusu kutoweka kwa mjukuu wake tangu tarehe 19 Septemba 2026.
Kijana huyo alikuwa ameondoka kwenda mgodini Mwabasabi, Kata ya Gibeshi, kabla ya tarehe 23 Septemba 2026 kumpigia simu mdogo wake, Sayi Maduhu, na kudai kuwa amefungiwa ndani ya nyumba na watu wanaotaka afidiwe shilingi milioni tano (5,000,000) ili wamwachie.
Baada ya kupokea taarifa hizo, timu ya makachero wa Polisi ikishirikiana na ndugu wa kijana huyo ilifanya ufuatiliaji na kufanikiwa kumpata Gatami akiwa katika Kata ya Bwanga, Wilaya ya Chato mkoani Geita, akiwa mzima wa afya bila tatizo lolote.
Hata hivyo, uchunguzi wa kina wa Jeshi la Polisi ulibaini kuwa kijana huyo hakuwahi kutekwa na watu wowote, bali alipanga na kutekeleza mpango huo mwenyewe kwa lengo la kujipatia fedha kutoka kwa ndugu zake.
"Aidha, Jeshi la Polisi linaeleza kuwa, uchunguzi kuhusiana na tukio hilo umebaini kuwa Gatami Maduhu Martine alijiteka kwa nia ya kupata pesa toka kwa ndugu zake..." , limeeleza jeshi la polisi.
Jeshi la Polisi limekemea vikali kitendo hicho na kutoa wito kwa wananchi kuacha mbinu hizo za udanganyifu ambazo zinaleta taharuki isiyo ya lazima katika jamii. Polisi imesisitiza kuwa chombo cha dola hakitasita kuchukua hatua za kisheria dhidi ya mtu yeyote atakayejaribu kufanya udanganyifu wa aina hiyo. -
Jambo TV
@Jambotv_
#ad
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Nchi ya Qatar, Tume ya Umoja wa Afrika na washiriki kutoka nchi wanachama wa Baraza la Ushirikiano la Nchi za Ghuba (Gulf Cooperation Council - GCC) imeandaa Mkutano wa Pili wa Uhamaji wa Nguvu Kazi (Second Doha Dialogue on Labour Mobility).
Mkutano huo utaratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira na Mahusiano na utafanyika kuanzia Oktoba 5 - 6, 2026 katika hoteli ya Hyatt Regency, Dar es Salaam ukiongozwa na kaulimbiu “Kuendeleza Uhamaji wa Nguvu kazi yenye Haki na endelevu katika ya Nchi za Afrika na Ghuba (GCC+). -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Madereva wa mabasi ya masafa marefu katika vituo vya mabasi vya Arusha na Msamvu, Morogoro, wamegoma kuendelea na safari kuelekea mikoa mbalimbali nchini, wakipinga utaratibu wa kukatwa pointi kwenye leseni zao za udereva wanapobainika kufanya makosa ya barabarani.
Mgomo huo umeanza leo, Septemba 29, 2026, ambapo katika Stendi Kuu ya Mabasi Arusha, baadhi ya safari za kuelekea Tanga, Dar es Salaam na Mwanza zimesitishwa, huku abiria wakikwama stendi tangu asubuhi.
Hali kama hiyo pia imejitokeza katika Kituo Kikuu cha Mabasi cha Msamvu mkoani Morogoro, ambako abiria waliokuwa wamepanga kuanza safari tangu saa 12:00 alfajiri wamekwama wakisubiri hatma ya safari zao.
Madereva waliozungumza na Jambo TV wamesema wanapinga mfumo huo kwa sababu makosa ya barabarani yanaweza kusababisha pointi kukatwa kwenye leseni zao na hatimaye leseni kufungiwa, jambo wanaloeleza linaweza kuwaathiri kiuchumi kwa kuwa udereva ndiyo kazi wanayotegemea kwa ajili ya maisha yao na familia zao.
Madereva hao pia wameeleza kutokuamini kuwa mfumo huo bado uko katika hatua ya majaribio, wakiiomba Serikali kutoa ufafanuzi na kuangalia namna nyingine ya utekelezaji wake.
Akizungumza Septemba 19, 2026, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, alisema mfumo huo bado haujaanza kutekelezwa rasmi, bali Serikali inaendelea na majaribio pamoja na kutoa elimu kwa madereva.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Usafirishaji katika Kituo cha Mabasi cha Msamvu, Aziz Kapilima, ameiomba Serikali kuingilia kati suala hilo na kutafuta suluhisho la haraka ili kurejesha huduma za usafiri na kuwawezesha abiria kuendelea na safari zao.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ameanza rasmi ziara ya kikazi mkoa wa Arusha kwa kuwataka Watumishi wa sekta ya Maji Mkoani Arusha kuhakikisha wanasimamia utoaji wa huduma bora ya maji katika jiji la Arusha na Mkoa wa Arusha kwa ujumla kwani serikali imewekeza fedha nyingi kinachotakiwa kwasasa ni usimamizi na ufanisi wa kazi.
Akizungumzia Mamlaka ya Maji Arusha Waziri Aweso amezungumzia changamoto ya Upotevu wa Maji na kuzungumia ufanisi wa utendaji kazi hususana maeneo yenye upungufu wa Maji kama Murieti.
Akizungumza na watumishi wa sekta ya Maji katika kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa mazingira Arusha (AUWSA) na kuwakutanisha Watumishi kutoka AUWSA, RUWASA na Bodi ya maji ya bonde la Kati, nimesisitiza Watumishi kutozoea changamoto za wananchi, kufanya kazi kwa bidii na wazingatie kuwa jukumu lao kuu ni huduma Bora ya maji kwa wananchi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Jeshi la Polisi nchini limesisitiza kuwa mfumo mpya wa ukataji wa pointi kwenye leseni za udereva bado halijaanza kutekelezwa rasmi kisheria, na kwamba hadi sasa hakuna dereva yeyote nchini aliyefutiwa leseni au kukatwa pointi kufuatia mfumo huo.
Msisitizo huo umetolewa leo Jumanne tarehe 29 Septemba 2026 na Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi Tanzania, CP Awadh Juma, wakati akizungumza na wanahabari mkoani Dar es Salaam kufuatia taarifa na vuguvugu la mgomo wa madereva wa mabasi na malori.
CP Awadh ameeleza kuwa hatua iliyopo sasa ni ya kutoa uelimishaji kwa umma na kwamba wananchi watajulishwa rasmi wakati utakapowadia wa kuanza kutumika kwa mfumo huo.
CP Awadh ameongeza kuwa madereva wanaotii sheria hawapaswi kuwa na hofu yoyote. Amefafanua kuwa hata wakati utekelezaji utakapofika, serikali imeweka taratibu za wazi za kisheria za kushughulikia malalamiko kwa dereva yeyote atakayeona ameonewa au kufanyiwa kinyume cha utaratibu.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi Tanzania, CP Awadh Juma, akizungumza na wanahabari leo Jumanne tarehe 29 Septemba 2026 mkoani Dar es Salaam, ametoa onyo kali dhidi ya watu wanaohamasisha na kuzuia mabasi na malori kutembea barabarani kufuatia taarifa za vuguvugu la mgomo wa madereva.
CP Awadh amesisitiza kuwa kuzuia chombo chochote cha usafiri au kufanya vitendo vya hujuma na uvunjifu wa sheria ni kosa la jinai, na Jeshi la Polisi halitasita kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya mtu au kikundi chochote kitakachobainika. Ameongeza kuwa serikali imeweka ulinzi wa kutosha ili kuhakikisha usafirishaji wa abiria na mizigo unaendelea bila hofu.
Katika hatua nyingine, CP Awadh amefafanua kuhusu hofu inayotokana na taarifa za mfumo wa ukataji wa pointi kwenye leseni za udereva, akibainisha kuwa mfumo huo bado haujaanza kutekelezwa na kwamba kwa sasa serikali inaendelea na hatua ya kutoa uelimishaji kwa umma. Amekanusha uvumi kwamba kuna madereva ambao tayari wamenyang'anywa leseni au kukatwa pointi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Jeshi la Polisi Tanzania limetoa onyo kali kwa mtu yeyote au kikundi kinachojihusisha na vitendo vya kuzuia mabasi na malori kuendelea na safari zao barabarani, kufuatia kile kinachoelezwa kuwa ni vuguvugu la mgomo wa madereva katika baadhi ya mikoa nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne, Septemba 29, 2026, jijini Dar es Salaam, Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi Tanzania (CP), Awadh Juma, amesema ni kosa kisheria kumzuia dereva yeyote kutoa huduma au kufanya hujuma dhidi ya vyombo vya usafiri na abiria.
"Polisi wanaelekeza kuwa haitasita kuchukua hatua kali sana kwa mtu yeyote yule atakayebainika kuzuia gari... siyo kuzuia tu, hata kufanya kitu chochote ambacho ni kinyume cha sheria dhidi ya mabasi hayo au kufanya hujuma yeyote dhidi ya madereva," ameonya CP Awadh.
Aidha, aligusia taarifa zinazosambaa kuhusu mfumo wa alama (pointi) za leseni akisema bado haujaanza kutumika na kwamba wananchi na madereva wasiongozwe na propaganda mitandaoni, huku akiwahakikishia wamiliki na madereva kuwa usalama umeimarishwa na wawasilishe huduma zao bila hofu yoyote.
Hata hivyo, hali katika vituo mbalimbali vya mabasi nchini imeonesha kusuasua kwa usafiri. Katika Stendi ya Nanenane jijini Dodoma, mabasi ya kwenda mikoani yamesitisha safari asubuhi ya leo, huku madereva wakidai migomo hiyo imechochewa na kukamatwa kwa magari yao, kufungiwa leseni kinyume cha utaratibu, na malalamiko dhidi ya mfumo wa pointi. Abiria wamelalamikia usumbufu mkubwa uliotokea.
Hali kama hiyo imeripotiwa jijini Mwanza, ambapo madereva wamesitisha huduma na kusababisha mamia ya abiria kukwama vituoni wakishinikiza marekebisho ya mfumo wa pointi za leseni kabla ya kurejea kazini. Katika Kituo Kikuu cha Magufuli (Mbezi Luis) jijini Dar es Salaam, baadhi ya abiria wameshushwa nje ya stendi kutokana na kile kilichoelezwa kuwa madereva kusitisha safari zao wakigoma kwa sababu hiyohiyo.
Jeshi la Polisi limesisitiza kuwa linaendelea kufuatilia na kuchukua hatua za kisheria dhidi ya yeyote anayevunja amri na kuingilia shughuli za usafirishaji nchini. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Leo Septemba 29, ,2026 Mabasi yanayobeba abiria katika Stendi ya Nanenane jijini Dodoma kuelekea mikoa mbalimbali yamesitisha safari asubuhi ya leo, huku madereva wakidai kuwa watarejea kutoa huduma baada ya madai yao kufanyiwa kazi.
Wakizungumza jijini Dodoma, baadhi ya madereva hao wamesema mgomo huo umetokana na malalamiko mbalimbali, ikiwemo kukamatwa kwa magari yao kwa madai ya kukiuka sheria za barabarani, kufungiwa leseni zao kwa kile wanachodai kufanyika kinyume cha utaratibu, pamoja na madai kwamba baadhi ya askari wa usalama barabarani wamekuwa wakiweka mawakala katika shughuli za usafirishaji.
Aidha, baadhi ya abiria wamelalamikia hatua hiyo na kuiomba Serikali kuingilia kati ili kutatua mgogoro huo, wakidai kuwa mgomo huo umewasababishia usumbufu na kuvuruga mipango yao ya safari.
Hata hivyo, hadi sasa, Jambo TV inaendelea kuzitafuta mamlaka husika kwa ajili ya kupata ufafanuzi kuhusu madai hayo pamoja na kauli ya Serikali juu ya mgomo huo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Leo Septemba 29, 2026 katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu wanaanza kufanya uwasilishaji wa hoja za mwisho (Final Submission) ambazo zitakuwa zimelenga kuithibitishia Mahakama kwamba Tundu Lissu alifanya kosa la uhaini.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesema imebaini uwepo wa udanganyifu juu ya taarifa za forodha kwenye G-Wagon ya msanii Omary Nyembo (Ommy Dimpoz).
Taarifa iliyotolewa na TRA leo Septemba 28, 2026, imesema operesheni ya ufuatiliaji wa ukwepaji kodi za magari nchi nzima ilifanikiwa kulifikia gari aina ya Mercedes-Benz G-Wagon lililokutwa katika eneo la Palm Beach Casino jijini Dar es Salaam Septemba 26, 2026 ambalo lilikutwa likiwa limeegeshwa bila namba za usajili, na uchunguzi wa awali wa taarifa zake ulionesha tofauti kubwa kati ya taarifa zilizowasilishwa wakati wa taratibu za forodha na hali halisi ya gari hilo.
Imeeleza zaidi kuwa Namba ya utambulisho wa gari(VIN) ilibainishwa kuwa WDB4632762X322756, huku taarifa zilizowasilishwa wakati wa taratibu za forodha zikionesha gari hilo kuwa Mercedes-Benz G-Class G350, yenye mwaka wa kutengenezwa 2020.
Hata hivyo, TRA imeeleza baada ya kufanya uhakiki wa kisayansi na kutumia Forensic, taarifa za gari hilo zilionyesha kuwa modeli yake halisi ilikuwa Mercedes-Benz AMG G63, yenye mwaka wa kutengenezwa 2018, gari ambalo thamani yake ni kubwa kuliko ile iliyowasilishwa katika nyaraka za awali.
Kwa mujibu wa mamlaka hiyo, tofauti hiyo inaashiria uwezekano wa kuwepo kwa udanganyifu uliolenga kupunguza uthamini wa forodha na hivyo kupunguza kiwango cha kodi kilichopaswa kulipwa na baada uchunguzi wa tukio hilo pamoja na gari hilo mamlaka imesema imebaini kuwa limesajiliwa kwa jina la Omary Faraji Nyembo, anayefahamika kama Ommy Dimpoz.
Haya yanatokea siku chache baada ya kusambaa kwa video mtandaoni ikimuonyesha Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini Clayton Revicatus Chipando @babalevotz akizozana na Afisa wa TRA juu ya kukamatwa kwa gari hilo ambapo video hiyo ilijenga mjadala juu ya mipaka na mamlaka ya mbunge katika kujaribu kumzuia afisa huyo kutekeleza majukumu yake.
Hata hivyo jana Septemba 27, 2026 Ommy Dimpoz aliomba radhi juu ya tukio hilo akisema kuwa yeye hakuwazuia maafisa hao. Na baadae Baba Levo pia alionekana kuandika ujumbe wa kuomba radhi mtandaoni. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI:
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, amesema mbele ya Majaji kwamba kwa muda mrefu amekuwa akipigania haki na demokrasia ili kuwezesha uwepo wa nchi ya demokrasia.
Lissu ameeleza hayo Septemba 28, 2026, ikiwa ni sehemu ya maneno yake ya mwisho ambayo ameyatoa mbele ya majaji baada ya kumaliza kuwasilisha hoja zake za mwisho.
"Waheshimiwa Majaji, nimepigania haki na demokrasia kwa sehemu kubwa ya maisha yangu ili kuwe na nchi ya demokrasia". Amesema Lissu.
Ameongeza kwamba msimamo wake wa kupigania demokrasia umepelekea madhira kwake huku akisema katika kipindi chake chote cha maisha yaliyosalia hapa duniani ataendelea kuwa na msimamo huo wa kupigania demokrasia hata ikimbidi kupoteza uhai.
"Imekuwa ni ideal kwa nchi yangu, msimamo huo umenigharimu sana, umeniletea madhira mengi sana, msimamo huo kwa siku zilizobaki za maisha yangu ni msimamo ambao nitaendelea kuusimamia, na kama ikibidi kufa nipo tayari kufa". Ameongeza Lissu.
Lissu katika maneno yake hayo ya mwisho amewaambia majaji kwamba wanao mzigo wa kuamua baada ya ushahidi wote uliotolewa mbele yao kama uhaini upo au hakuna.
Amewasisitiza kutoa hukumu ikiwa watabaini uwepo wa uhaini na kusema kama wataona hakuna uhaini pia wasisite kusema kama hana makosa na aachiliwe huru.
"Waheshimiwa Majaji, mzigo wenu mabegani mwenu ni kuamua kama kwa ushahidi huu kuna uhaini. Kama mkiona kuna uhaini, msiogope kuniadhibu kwa hukumu inayostahili uhaini. Na kama mkaona hakuna uhaini, msiogope kusema hakuna uhaini hapa, mshtakiwa hana hatia." Amehitimisha Lissu. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu wa Rais wa Tanzania, Deogratius Ndejembi, akizungumza leo Jumatatu Septemba 28, 2026 katika Kikao Kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi na Mashirika ya Umma (C-CEOs Forum) 2026 kinachofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano Arusha (AICC) mkoani Arusha, amependekeza mpango mkakati wa kuwatengenezea mfumo wa mafunzo kwa vitendo vijana watarajali 30,000 kila mwaka.
Ndejembi amependekeza kuwa taasisi na mashirika ya umma yachukue walau vijana 10,000 kila mwaka kupitia taasisi kama TaESA na TRA, huku sekta binafsi ikitengenezewa vivutio ili kuchukua vijana 20,000 wengine kupata mafunzo ya mwaka mzima. Ameeleza kuwa hatua hiyo italenga kuwapa vijana ujuzi wa kibobezi katika taaluma mbalimbali kama uandishi wa mikataba na uhandisi.
“Tukasema tuwalipe milioni moja ya kuweza kuwawezesha kufika kazini na akafika kazini, akawa na mentor wake akampa kazi sio tena unampa mentorship halafu unamweka mapokezi, unampa mentorship unaanza kumtuma chai, unamweka na mtu ili ajifunze. Ndani ya mwaka tutakuwa tumetengeneza vijana ambao wako tayari kutufikisha katika malengo tuliyojiwekea kwenye dira yetu ya taifa”, ameeleza.
Mkutano huo unahudhuriwa na wawakilishi wa sekta binafsi, wawekezaji, ukilenga kujadili namna mashirika ya umma yanavyoweza kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Peter Msigwa, ameshangazwa na ukimya wa vyombo vya ulinzi na usalama kufuatia kauli ya Katibu wa NEC, Idara ya Oganaizesheni wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Paul Matiko Chacha, kuhusu umiliki wa vyombo vya dola.
Chacha alitoa kauli hiyo Septemba 26, 2026, mkoani Iringa, akizungumza katika mkutano maalum wa CCM Mkoa wa Iringa, ambapo alisema "Nani hajui Vyombo vya Ulinzi na Usalama ni mali ya CCM?"
Akizungumza leo Septemba 28, 2026, katika mahojiano maalum na Jambo TV, Msigwa amesema kutokuwepo kwa kauli ya kukemea kauli hiyo kutoka kwa vyombo vya ulinzi na usalama kuna ibua maswali -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, jioni ya leo Septemba 28, 2026 amemaliza rasmi kuwasilisha hoja zake za mwisho (Final Submission) katika utetezi.
Baada ya kuhitimisha, majaji wameahirisha shauri hilo hadi kesho Septemba 29, 2026 ambapo upande wa Jamhuri wataanza kuwasilisha hoja sao za mwisho (Final Submission). -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu wa Rais wa Tanzania, Deogratius Ndejembi, amezitaka bodi na taasisi za umma nchini kutumia fursa zao kuwaandaa na kuwanoa vijana wahitimu ili kupata ujuzi unaohitajika katika soko la ajira, akisisitiza kuwa utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 hautafanikiwa bila kuwekeza kikamilifu katika rasilimali watu.
Akizungumza leo Septemba 28, 2026, wakati akifungua Kikao Kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi na Mashirika ya Umma (C-CEOs Forum) 2026 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano Arusha (AICC), Ndejembi amekosoa utaratibu wa kimazoea wa kuwataka wahitimu wapya kuwa na uzoefu wa miaka mitatu hadi mitano kabla ya kuajiriwa.
"Graduate anaambiwa lazima awe na uzoefu wa miaka mitatu, miaka mitano. Uzoefu huo ataupata wapi kama sisi kwenye taasisi zetu za umma hatutumii taasisi zetu katika kuwaandaa vijana hawa ili waweze kuwa na uwezo wa kushindana katika soko la ajira za Tanzania, Afrika Mashariki, Afrika na duniani kwa ujumla?", amedokeza Makamu wa Rais.
Amebainisha kuwa mashirika ya umma yana nafasi ya kipekee katika kufikia malengo ya Dira 2050 kwa kuwa ndiyo yanayosimamia miundombinu ya kimkakati na kutoa huduma za msingi za nishati, usafirishaji, mawasiliano, fedha, afya, na maji. Amesisitiza kuwa mashirika hayo yanapaswa kutazamwa kama injini kuu ya mageuzi makubwa ya kiuchumi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu wa Rais wa Tanzania, Deogratius Ndejembi, akizungumza leo Jumatatu Septemba 28, 2026 katika Kikao Kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi na Mashirika ya Umma (C-CEOs Forum) 2026 kinachofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano Arusha (AICC) mkoani Arusha, ameagiza Ofisi ya Msajili wa Hazina kuimarisha mfumo wa tathmini ya utendaji wa taasisi hizo ili kuboresha ufanyaji kazi na kuacha kufanya kazi kwa mazoea.
Akiwasilisha maelekezo hayo, Deogratius Ndejembi amesisitiza kuwa tathmini za utendaji zinapaswa kujikita katika kuhakikisha kunapatikana matokeo na thamani halisi inayozalishwa badala ya kuangalia tu uthabiti wa hesabu za fedha. Amebainisha kuwa viongozi wanaposimamia taasisi hizo wanapaswa kukumbuka kuwa dhamana waliyopewa ni kwa ajili ya kuwatumikia Watanzania
Kuhusu namna ya kufanya tathmini hiyo, Ndejembi ameonya dhidi ya mfumo wa ndani wa kujitathmini pekee, akieleza kuwa mara nyingi taasisi zimekuwa zikifanya tathmini za ndani zisizotoa picha halisi. Amemtaka Msajili wa Hazina kushirikisha sekta binafsi na wataalamu huru ili kufanya ukaguzi na tathmini ya kweli itakayowasilishwa kwa Rais.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu wa Rais wa Tanzania, Deogratius Ndejembi, ameyataka mashirika ya umma, taasisi za serikali na wizara kupunguza matumizi yasiyo ya lazima ikiwemo ununuzi wa magari ya kifahari (V8) na safari za nje ya nchi ili kupata kiasi cha Shilingi bilioni 120 zitakazoelekezwa katika kuwanoa na kujenga uwezo wa rasilimali watu na vijana nchini.
Akizungumza leo Septemba 28, 2026, wakati akifungua Kikao Kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi na Mashirika ya Umma (C-CEOs Forum) 2026 kinachofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano Arusha (AICC), Ndejembi amehoji matumizi makubwa yanayofanywa na bodi na taasisi hizo kwenye vikao, posho, na safari za nje, akieleza kuwa kubana matumizi hayo kutawezesha taifa kupata fedha za kutosha kujenga nguvukazi imara itakayosukuma uchumi wa nchi.
Akiirejelea Dira ya Taifa ya Maendeleo na nguzo zake ikiwamo kujenga uchumi shindani na kuendeleza watu, Ndejembi amesisitiza kuwa maendeleo ya kweli yatafikiwa pale tu taifa linapowekeza kwenye utaalamu na ujuzi wa watu wake.
"Katika zile nguzo tatu za dira yetu ya maendeleo ya taifa tunasema tujenge uchumi shindani, nguzo ya pili tunasema kujenga watu, ya tatu mazingira. Sasa hizi zote ili tuweze kuziishi nguzo hizi na tukafanikiwa, lazima tuanze kuwekeza sasa kwenye rasilimali watu ili wawe na utaalam na ujuzi wa kuweza kutusaidia kufikia malengo yetu," amesisitiza.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, amebainisha kuwa katika kipindi cha miaka mitano ijayo (kuelekea mwaka 2030/31), uchumi wa Tanzania unahitaji kukua na kufikia Shilingi trilioni 477 kutoka Shilingi trilioni 238 za sasa, ambapo sekta binafsi inatarajiwa kuchangia asilimia 70 ya uwekezaji huo huku sekta ya umma ikichangia asilimia 30.
Akizungumza leo, Septemba 28, 2026, katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano Arusha (AICC) mkoani Arusha wakati wa Kikao Kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi na Mashirika ya Umma (C-CEOs Forum) 2026, ambapo mgeni rasmi ni Makamu wa Rais wa Tanzania, Deogratius Ndejembi, Prof. Kitila amefafanua kuhusu mgawanyo wa majukumu katika kufikia ukuaji huo wa uchumi, akibainisha kuwa sekta ya umma imegawanyika katika maeneo matatu: mashirika na taasisi za umma, mamlaka za serikali za mitaa, na serikali kuu inayoweka sera.
Amesisitiza kuwa ingawa serikali kuu inaweka sera, mashirika ya umma ndiyo yaliyobeba jukumu kuu la utekelezaji wa asilimia 30 ya sekta ya umma na kuifungulia milango sekta binafsi.
“Kuelekea mwaka 2030/31 miaka mitano ijayo tunahitaji uchumi wetu ukue ufikie Shilingi trilioni 477 kutoka Shilingi trilioni 238 za sasa hivi. Hiyo tumekubaliana baada ya utafiti wa kutosha kwamba watekelezaji ni watu wawili. Sekta binafsi tunatarajia watoe mchango katika uwekezaji huo wa 70% na sekta ya umma 30%... tunatarajia wenzetu wa sekta binafsi waweze kubadilisha fursa kuwa uzalishaji kuwa ajira. Lakini watengenezaji wa fursa ni sisi ambao tupo serikalini huku ikiwa mashirika yetu ya umma”, ameeleza Prof. Mkumbo.
Kikao kazi hicho kinachohudhuriwa pia na wawakilishi wa sekta binafsi, wasajili, na wawekezaji kinafanyika wakati Tanzania ikiendelea na utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, kikiwa na kaulimbiu isemayo "Mashirika ya Umma yenye Ufanisi wa Juu kwa Uchumi Shindani, Shirikishi na Imara katika Kutekeleza Dira 2050", inayolenga kujadili namna mashirika ya umma yanavyoweza kuongeza ufanisi na kuendana na malengo ya Dira 2050.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI:
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, ameiambia Mahakama kwamba kesi ya uhaini iliyofunguliwa dhidi yake ina mapungufu mengi akisema miongoni mwa hayo ni kwamba kesi hiyo imeamuliwa kufunguliwa na mtu mmoja kama siyo wawili huku akimtaja Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), ambaye anahudumu kama Naibu Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai George Bagyemu kufanya hivyo.
Lissu amesema hayo leo Septemba 28, 2026 alipokuwa akiendelea kutoa hoja zake za mwisho mbele ya jopo la majaji watatu wakiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru. Amesema kwamba mapungufu hayo siyo pekee yaliyopo katika kesi hiyo bali pia yapo mapungufu mengine ambayo amesema yanaibua "mashaka makubwa" ambayo ni ya msingi kuhusu kesi hiyo.
Kwa mujibu wa Lissu, Bagyemu ndiye aliyeamua kwamba maneno yaliyokuwa kwenye video yanaunda kosa la uhaini. Amesema rekodi ya mahakama katika ukurasa wa 145 hadi 146 inaeleza yaliyotokea Aprili 8, 2025, siku nne baada ya video hiyo kuonekana.
Lissu amesema baada ya Bagyemu kuipata video hiyo, aliamua kufungua faili la uhaini bila kuwashirikisha baadhi ya wakuu wake wa kazi, akiwamo Mkuu wa Polisi Kanda Maalum (ZPC) na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI).
Kwa mujibu wa Lissu, Bagyemu aliwafahamisha wakuu hao baada ya kufungua faili hilo. Amesema jambo lingine analodai linaibua mashaka ni kwamba Bagyemu hakutafuta ushauri wa kisheria kabla au baada ya kufungua faili la uhaini.
Akirejea ukurasa wa 159 wa rekodi ya ushahidi, Lissu amesema suala hilo limethibitishwa katika ushahidi wa Bagyemu. Amesema hata Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) hakujulishwa kuhusu kesi hiyo wakati huo.
Lissu amesema licha ya Bagyemu kuwajulisha baadhi ya watu kuhusu suala hilo, hakuna hata mmoja kati yao aliyefika mahakamani kutoa ushahidi. Ameongeza kuwa shahidi huyo pia hakuhusisha wala kutoa taarifa kwa mamlaka nyingine za uchunguzi au taasisi nyingine za Serikali kuhusu hatua alizochukua.
Lissu anaendelea na maelezo yake ya mwisho katika kesi hiyo, huku akisisitiza kuwa mzigo wa kuthibitisha mashtaka unabaki kwa upande wa mashtaka na kwamba ushahidi uliowasilishwa haujafikia kiwango cha uthibitisho kinachotakiwa na sheria. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu, amebainisha kuwa ili Tanzania iweze kufikia lengo la kuijenga nchi yenye uchumi wa Dola za Marekani trilioni moja ifikapo mwaka 2050, Pato la Taifa linatakiwa kukua kwa wastani wa asilimia 10.31 kila mwaka kwa kutegemea mchango wa sekta zote za uchumi zikiwamo taasisi na mashirika ya umma.
Akizungumza leo, Septemba 28, 2026, katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano Arusha (AICC) mkoani Arusha wakati wa Kikao Kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi na Mashirika ya Umma (C-CEOs Forum) 2026 ambapo mgeni rasmi ni Makamu wa Rais wa Tanzania, Deogratius Ndejembi, Mchechu ameeleza kuwa Ofisi ya Msajili wa Hazina na viongozi wa mashirika ya umma wanajipanga vyema kutimiza malengo na shabaha walizopewa kama sehemu ya uwekezaji wa umma katika kutimiza malengo ya Dira 2050.
“Dira 2050 inaweka lengo la kuijenga Tanzania yenye uchumi wa Dola za Marekani trilioni moja ifikapo mwaka 2050. Kufikia lengo hili tunahitaji pato la taifa kukua kwa wastani wa 10.31 na kwa mchango wa sekta zote za uchumi zikiwemo taasisi na mashirika ya umma. Kwa hiyo tutakuwa tunajipanga vizuri kuangalia ni jinsi gani tutaweza kutimiza malengo na tageti ambazo tumepewa kama sehemu ya uwekezaji wa umma katika kufikisha Dira 2050”, ameeleza Mchechu.
Akifafanua kuhusu ukubwa wa matarajio ya Serikali na wananchi katika kufikia malengo ya Dira 2050, Mchechu alieleza kuwa Ofisi ya Msajili wa Hazina inatambua kwa unyenyekevu mkubwa kuwa mchango wa taasisi na mashirika ya umma utakuwa nguzo kuu katika kufikia ukuaji huo wa uchumi.
Kikao kazi hicho kinachohudhuriwa na wenyeviti wa bodi, watendaji wakuu, wawakilishi wa sekta binafsi, wasajili, na wawekezaji kinasukumwa na kaulimbiu isemayo "Mashirika ya Umma Yenye Ufanisi wa Juu kwa Uchumi Shindani, Shirikishi na Imara katika Kutekeleza Dira 2050", inayolenga kujadili namna mashirika ya umma yanavyoweza kuongeza ufanisi na kuendana na malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
#ad
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Nchi ya Qatar, Tume ya Umoja wa Afrika na washiriki kutoka nchi wanachama wa Baraza la Ushirikiano la Nchi za Ghuba (Gulf Cooperation Council - GCC) imeandaa Mkutano wa Pili wa Uhamaji wa Nguvu Kazi (Second Doha Dialogue on Labour Mobility).
Mkutano huo utaratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira na Mahusiano na utafanyika kuanzia Oktoba 5 - 6, 2026 katika hoteli ya Hyatt Regency, Dar es Salaam ukiongozwa na kaulimbiu “Kuendeleza Uhamaji wa Nguvu kazi yenye Haki na endelevu katika ya Nchi za Afrika na Ghuba (GCC+). -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPC), David Kafulila, amebainisha kuwa ukosefu wa mtaji, ubunifu, na ufanisi wa kiutendaji ndizo sababu kuu zinazokwamisha mashirika na taasisi za umma kutoa mchango unaotakiwa kwenye uchumi wa taifa.
Akizungumza leo, Septemba 28, 2026, katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Arusha (AICC) mkoani Arusha wakati wa Kikao Kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi na Mashirika ya Umma (C-CEOs Forum) 2026, Kafulila amesisitiza kuwa changamoto hizo ndizo zilizosukuma kuanzishwa kwa utaratibu wa Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) ili kuunganisha nguvu za pamoja kuelekea utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050
Akieleza umuhimu wa kushirikisha sekta binafsi, Kafulila amesema kuwa Serikali haina uwezo wa kufadhili miradi yote mikubwa ya maendeleo kupitia makusanyo ya kodi na mikopo pekee. Ameongeza kuwa ushirikiano wa PPP unasaidia kupata mtaji wa sekta binafsi, kuleta ufanisi unaopunguza hasara kubwa zinazotengenezwa na baadhi ya mashirika ya umma, pamoja na kuleta ubunifu mpya.
Akimulika changamoto inayokabili sekta hiyo duniani na nchini, Kafulila ameeleza kuwa Tanzania inaonekana kuwa na uhaba wa miradi inayokopesheka na kuvutia wawekezaji kwasababu mashirika ya umma hayatengi bajeti ya kufanya tafiti za uwezekano wa kufanyika miradi hiyo. Ametahadharisha kuwa hali hiyo huilazimu nchi kutegemea zaidi mapendekezo binafsi kutoka kwa wawekezaji jambo linaloiweka Serikali na mashirika kwenye nafasi dhaifu ya majadiliano ukilinganisha na wawekezaji hao waliogharamia tafiti hizo
Mkurugenzi Mtendaji huyo wa PPPC ametoa wito kwa Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Mashirika ya Umma kuhakikisha wanatenga fedha maalum kwenye bajeti zao kwa ajili ya maandalizi na tafiti za miradi ya PPP, badala ya kutegemea mfuko wa PPP (PPP Fund) au ufadhili mdogo wa Benki ya Dunia.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI:
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, ameiomba Mahakama isitumie ushahidi wa mashahidi wa kificho kutoka upande wa mashtaka waliofika kutoa ushahidi wao, kwa maelezo kwamba ushahidi wao ulikuwa wenye uongo na maslahi.
Ombi hilo amelitoa leo Septemba 28, 2026 alipokuwa akiendelea kuwasilisha hoja zake za mwisho mbele ya jopo la majaji watatu wakiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru. Amesema mashahidi hao ni PW5, PW7, PW8, PW10, PW11, PW13 na PW14.
"Ushahidi wa mashahidi wa mafichoni hautakiwi kuguswa kwa sababu ulikuwa wa uongo na wenye maslahi". Amesema Lissu.
Lissu amesema kwamba, Shahidi PW5 alidanganya kuhusu dini yake kwani alikula kiapo mahakamani kama "Mkristo" na katika maelezo yake yaliyopo katika kielelezo D4 amesema yalieleza kuwa ni "Muislamu" ambapo pia amesema shahidi huyo alidanganya kwamba alikuwa mwanacha wa CHADEMA jambo alilosema halikuwa la kweli.
Shahidi mwingine ambaye Lissu amesema aliidanganya Mahakama ni PW7 ambaye Lissu amesema, alisema uongo kuhusu kupelekwa Kituo cha Polisi Songea na kwamba alidanganya pia kuhusu uanachama wake wa CHADEMA jambo ambalo Lissu amesema si kweli kwani hakuwa Mwanachadema.
Amesema pia, ushahidi wa PW8 ushahidi wake ulikuwa umejaa mikanganyiko na uongo, akiendelea kwamba ushahidi wa PW10 yeye alidanganya kuhusu maelezo yake ya Polisi aliyosema kwamba "mshtakiwa alisema tumejipanga kufanya fujo kuzuia uchaguzi" jambo ambalo Lissu amesema hakuwahi kulisema.
Amesema zaidi kwamba, Shahidi PW11 ushahidi wake ulijaa pia mkanganyiko na haukuwa wa kweli bali ulikuwa wa kutungwa, amesema pia PW13 yeye alidanganya juu ya uanachama wake wa CHADEMA kwamba, katika maelezo yake alisema ni mwanachama wa chama hicho wakati siyo mwanachama wa chama hicho.
Amesema shahidi wa mwisho katika hao alikuwa ni PW14 ambaye amasema alidanganya kuhusu kazi yake kwamba katika maelezo yake ya Polisi alisema yeye ni Mkulima wa Kata ya Mwakibete na kwenye maelezo ya mahakamani alisema yeye ni fundi umeme wa Jiji la Mbeya, amesema shahidi huyo alisema uongo mwingine kwamba "Mshtakiwa alisema "lazima tukichafue" jambo ambalo Lissu amesema hakuwahi kusema hivyo. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu, amebainisha kuwa Ofisi ya Msajili wa Hazina imefanya mageuzi makubwa katika usimamizi na uwajibikaji wa mashirika na taasisi za umma nchini, ikiwa ni pamoja na kupanua uwezo wa kufanya tathmini ya utendaji kutoka taasisi 70 pekee hapo awali hadi kufikia taasisi zote 252 kwa mwaka huu.
Akizungumza leo, Septemba 28, 2026, wakati wa Kikao Kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi na Mashirika ya Umma (C-CEOs Forum) 2026 kinachofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano Arusha (AICC) mkoani Arusha, Mchechu ameeleza kuwa hatua hizo zinalenga kuimarisha ufanisi wa mashirika hayo ili kuendana na malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
Akimulika mifumo na mbinu mpya za uwajibikaji zilizowekwa, Mchechu alibainisha kuanza kutumika rasmi kwa mfumo wa PIMS (Public Investment Management System) ambao utatumika kujaza na kuwekeana malengo pamoja na mikataba ya utendaji kidijitali badala ya njia za zamani za karatasi.
Akiwasilisha maendeleo ya kisekta na kifedha, Mchechu ameeleza kuwa vigezo vya utendaji kazi (KPIs) vimefanyiwa marekebisho ili viweze kugusa mahitaji maalum ya kila taasisi kulingana na sekta husika kulingana na vigezo vilivyowekwa. Amesema kupitia hatua hizo, kiwango cha utegemezi wa serikali kimeendelea kupungua, huku mapato ya ndani ya taasisi hizo yakiendelea kuongezeka sanjari na kuboreka kwa huduma kwa wateja na matumizi ya mifumo ya kidijiti.
Mkutano huo unaoangazia kaulimbiu ya "Mashirika ya Umma Yenye Ufanisi wa Juu kwa Uchumi Shindani, Shirikishi na Imara katika Kutekeleza Dira 2050", unajumuisha wenyeviti wa bodi, watendaji wakuu, wawakilishi wa sekta binafsi, wasajili, na wawekezaji wanaojadili mbinu za kimkakati za kuboresha mchango wa mashirika ya umma katika uchumi wa taifa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) imetajwa kuwa Taasisi Bora Zaidi ya Uhamasishaji Uwekezaji Barani Afrika kwa mwaka 2026, hatua inayoweka rekodi ya mwaka wa tatu mfululizo kwa mamlaka hiyo kupata utambuzi wa kimataifa katika Tuzo za Annual Investment Meeting (AIM) Global Foundation.
Tuzo hiyo ilitolewa katika hafla ya utoaji wa tuzo hizo jijini Dubai hivi karibuni, ambapo TISEZA ilitambuliwa kwa mchango wake mkubwa katika kuhamasisha na kuwezesha uwekezaji barani Afrika.
Tuzo hii inakuja wakati miradi ya uwekezaji iliyosajiliwa nchini Tanzania ikiongezeka zaidi ya mara tatu katika kipindi cha miaka mitano iliyopita ikitoka miradi 252 mwaka 2021 hadi miradi 915 mwaka 2025, kulingana na takwimu za TISEZA. Katika kipindi hicho, thamani ya mtaji wa uwekezaji ulioidhinishwa iliongezeka karibu mara tatu, ikipanda kutoka Dola za Marekani bilioni 3.7 mwaka 2021 hadi Dola za Marekani bilioni 10.95 mwaka 2025.
Akipokea tuzo hiyo, Mjumbe wa Bodi ya TISEZA, Felista Lelo, alisema tuzo hiyo ni heshima kubwa kwa Tanzania na taasisi hiyo, akieleza kuwa ni kiashiria cha uaminifu ambao jumuiya ya kimataifa inao juu ya mazingira ya uwekezaji nchini. Alieleza kuwa hatua hiyo inaonesha matokeo ya juhudi zinazofanywa na serikali na TISEZA katika kutengeneza mazingira wezeshi zaidi kwa wawekezaji, akibainisha kuwa mabadiliko ya kisera yamesaidia kuvutia uwekezaji wa ndani na wa kigeni.
"Tuzo hii ni heshima kubwa kwa taifa na pia kwa TISEZA. Inaonesha uaminifu ambao ulimwengu unao kwa Tanzania na inaakisi matokeo ya juhudi zinazofanywa na serikali na taasisi yetu kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji," alisema.
Lelo aliongeza kuwa Tanzania pia imeongeza juhudi za kutangaza fursa zake za uwekezaji kimataifa, huku ikiboresha sheria na sera ili kuoanisha na maendeleo ya dunia pamoja na utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Gilead Teri, alisema utambuzi huo unaweka rekodi ya mwaka wa tatu mfululizo kwa mamlaka hiyo kushinda tuzo za dunia katika vipengele tofauti. Alikumbusha kuwa mwaka 2025, mamlaka hiyo ilitwaa tuzo ya juu kwa matumizi bora ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kupitia Kituo chake cha Huduma za Pamoja kinachounganisha mifumo ya kidijiti kwa ajili ya kuwahudumia wawekezaji bila vikwazo.
Teri alihusisha mafanikio hayo moja kwa moja na mazingira rafiki ya kibiashara na kisheria yanayoongozwa na Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan tangu mwaka 2021.
“Naweza kusema kwa ujasiri kwamba ndani ya Afrika, hakuna nchi inayowajali wawekezaji zaidi au yenye mazingira wezeshi zaidi ya kibiashara kuliko Tanzania”, alisema.
Aliongeza kuwa uongozi wa Rais Samia unatoa kipaumbele katika kuongeza thamani ya bidhaa, maisha ya staha kwa wananchi, ujenzi wa viwanda vya ndani, na kutanua wigo wa kibiashara wa Tanzania katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) pamoja na bara zima la Afrika.
Aidha, alizungumzia uamuzi wa serikali wa tarehe 1 Julai 2025 wa kuunganisha kilichokuwa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na Mamlaka ya Maeneo ya Uzalishaji kwa Mauzo ya Nje (EPZA) ili kuunda TISEZA chini ya Sheria Namba 6 ya Mwaka 2025. Amesema mabadiliko haya ya kimfumo yanamwezesha mwekezaji kupata huduma zote za msingi kutoka usajili hadi upatikanaji wa ardhi chini ya paa moja. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, amepandishwa kizimbani leo Septemba 28, 2026 kwaajili ya kuendelea na uwasilishaji wa hoja zake za mwisho.
Katika kuendelea na uwasilishaji wa hoja hizo, leo anaendelea na hoja ya nane kati ya tisa, ambayo inahusu kama upande wa mashtaka umethibitisha mashtaka yake kwa kiwango cha uthibitisho kinachotakiwa na sheria.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkuu wa Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza, Ng’wilabuzu Ludigija, amemuamuru Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo pamoja na Wakuu wa Idara wote kuripoti kwa Mkuu wa Polisi wa Wilaya (OCD) kufuatia kukaidi kwao mara kadhaa agizo la kushiriki katika zoezi la kufanya usafi wa mazingira wilayani humo.
Ludigija ametoa maelekezo hayo makali Jumamosi, Septemba 26, 2026, wakati akiongoza Kamati ya Ulinzi na Usalama pamoja na wananchi wa Kwimba katika zoezi la kufanya usafi wa mazingira katika maeneo mbalimbali, akisisitiza kuwa anakusudia kuwaweka mahabusu watendaji hao kwa kitendo chao cha kupuuzia maagizo ya serikali ya kusafisha mazingira.
Amesema kuwa viongozi hao wameonesha dharau kwa zoezi hilo ambalo ni muhimu katika kujiandaa na tahadhari dhidi ya mvua za El Niño zinazotabiriwa kuanza kunyesha hivi karibuni, ili kuepusha athari na milipuko ya magonjwa ya milipuko.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amemteua Masanja Kungu Kadogosa kuwa Waziri wa Ujenzi..
Uteuzi huo umefanyika leo Septemba 27, 2026 kwa mujibu wa taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka iliyowasilishwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Bakari Machumu. -
Jambo TV
@Jambotv_
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amemteua Abdallah Hamis Ulega kuwa Waziri wa Katiba na Sheria. Kabla ya uteuzi huu, Ulega alikuwa Waziri wa Ujenzi nafasi ambayo imechukuliwa na Masanja Kadogosa.
Uteuzi huo umefanyika leo Septemba 27, 2026 kwa mujibu wa taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka iliyowasilishwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Bakari Machumu. -
Jambo TV
@Jambotv_
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amemteua Dkt. Juma Zuberi Homera kuwa Waziri wa Nishati. Kabla ya uteuzi huu, Dkt. Homera alikuwa Waziri wa Katiba na Sheria.
Uteuzi huo umefanyika leo Septemba 27, 2026 kwa mujibu wa taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka iliyowasilishwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Bakari Machumu. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Maelekezo yaliyotolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Kenani Laban Kihongosi, kuhusu kuimarisha usafi wa mazingira katika Jiji la Tanga yameanza kufanyiwa kazi kwa vitendo.
Wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Tanga, Kihongosi alitoa rai thabiti kwa viongozi wa halmashauri hiyo kusimamia kwa karibu usafi wa jiji na kuwahimiza wananchi kushirikiana kikamilifu katika utunzaji wa mazingira, hatua inayokwenda sambamba na maelekezo ya mara kwa mara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ya kuifanya Tanzania kuwa nchi safi na salama.
Kufuatia maagizo hayo, Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira, Reuben Kwagilwa, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa maagizo hayo, ameagiza kukamatwa na kuhojiwa mara moja kwa Kaimu Afisa Biashara wa Jiji la Tanga, Hussein Mbwana, Kaimu Mkurugenzi wa Jiji, Bahati Kahindi, na Meneja wa Soko la Mgandini, kutokana na kushindwa kusimamia kikamilifu usafi katika maeneo ya masoko.
Hatua hii inalenga kuwakumbusha viongozi wote nchini kuwa usafi sio tu suala la mwonekano, bali ni nguzo muhimu ya kulinda afya za wananchi, ustawi wa jamii, na kujenga mazingira bora ya kufanyia biashara na shughuli za kiuchumi kwa ufanisi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mbunge Ado Shaibu Ado amekutana uso kwa uso na wakulima na wafugaji katika Kata ya Chawisi, kwa lengo la kusikiliza kero zao na kutafuta suluhisho la mgogoro unaohusisha mifugo kuharibu mashamba.
Katika mkutano huo, uliofanyika jana Septemba 26, 2026, wakulima walilalamikia mifugo kuingia na kulisha kwenye mashamba yao, huku wakidai kuwa baadhi ya vijana wa wafugaji wamekuwa wakiwapiga wananchi na kusababisha fujo.
Kwa upande wao, wafugaji walieleza kuwa wanataka kuishi kwa amani na kuheshimu sheria, wakisisitiza umuhimu wa kupata utaratibu utakaowawezesha kuendelea na shughuli zao bila kuathiri wakulima.
Akizungumza katika mkutano huo, Ado alisisitiza kuwa sheria ya nchi inahitaji kuwepo kwa utaratibu maalum pale shughuli za kilimo na ufugaji zinapofanyika katika eneo moja.
“Bila utaratibu, leo mtagombana, kesho mtagombana,” alisema.
Ado aliahidi kukutana na viongozi wa wilaya, polisi pamoja na wadau wengine ili kutafuta suluhisho la kudumu litakalozingatia maslahi ya pande zote.
“Sauti yenu nimesikia kwa uzito. Sitawasaliiti,” alimalizia.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, amechagiza kuimarishwa kwa huduma ya maji safi na salama katika Mji wa Mkuranga mkoani Pwani, kwa kukabidhi pampu mpya ya maji yenye thamani ya zaidi ya Shilingi milioni 250 itakayoboresha huduma kwa wakazi 67,670.
Akikabidhi pampu hiyo kwa niaba ya Waziri wa Maji, Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), Mhandisi Mkama Bwire, ameeleza kuwa changamoto ya maji katika eneo la Mkuranga mjini inaenda kufika ukingoni kufuatia ununuzi wa pampu hiyo kubwa itakayofungwa kwenye kisima kinachohudumia eneo hilo na kumaliza kabisa migao ya maji.
Aidha, Mhandisi Bwire ameongeza kuwa katika Kata ya Mipeko, ambayo pia inakabiliwa na uhaba wa maji, wamepokea maagizo ya Waziri wa Maji kuanza uchimbaji wa kisima kipya mapema mwezi Oktoba ili kusaidiana na kisima cha sasa kuimarisha huduma katika eneo hilo. Pamoja na hayo, alibainisha mpango wa kuongeza mtandao wa majisafi katika maeneo ya Mipeko, Kiguza, na Hoyoyo, huku mpango wa muda mrefu ukiwa ni kuleta maji kutoka kwenye visima vya Kimbiji na Mpera hadi Mkuranga.
Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Mkuranga na Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega, ameipongeza Wizara ya Maji na DAWASA kwa hatua za haraka za ununuzi wa pampu hiyo, akisisitiza kuwa Mji wa Mkuranga unakua kwa kasi kubwa na mahitaji ya maji yanaongezeka kila siku.
"Ni ukweli kuwa mji huu wa Mkuranga unakua kwa kasi, mahitaji ya maji yanaongezeka kila siku. Tumeshuhudia pampu imefika kwenye kisima, na ni matumaini yangu ndani ya mwezi mmoja tutamaliza changamoto hii ya maji Mkuranga mjini," ameeleza Ulega.
Pia, Ulega ameshukuru kwa maagizo ya kuanzishwa kwa uchimbaji wa kisima kipya na upanuzi wa mtandao wa maji katika Kata ya Mipeko, akibainisha kuwa hatua hiyo itatoa suluhisho la kudumu kwa wananchi ambao kisima chao cha awali kilikuwa hakikidhi tena mahitaji kutokana na ongezeko kubwa la watu.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Hassan Bomboko, anadaiwa kuagiza kukamatwa na kuwekwa ndani kwa Mwenyekiti wa @CCMTanzania Kata ya Bomang’ombe, Agness Kimaro, huku sababu za kukamatwa kwake zikiwa hazijawekwa wazi.
Kimaro amedai alikamatwa Septemba 25, 2026 na kupelekwa Kituo cha Polisi Bomang’ombe, kabla ya kuachiwa kwa dhamana iliyowekwa na Mbunge wa Hai, Saashisha Mafuwe na kuwa alikamatwa akiwa njiani kwenda Gezaulole kushiriki maandalizi ya ujenzi wa shina la CCM linalotarajiwa kuzinduliwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Aggrey Mwanri.
Amesema baada ya kufikishwa kituoni aliwekwa ndani na baadaye kuambiwa kuwa hatua hiyo ilikuwa kwa amri ya Mkuu wa Wilaya, lakini hakuelezwa kosa alilodaiwa kufanya. Amesema alisubiri Mkuu wa Wilaya kufika kituoni kwa ajili ya kupata maelezo, lakini hakufika na hadi kuachiwa kwake hakujua sababu ya kukamatwa.
Alipotafutwa kwa simu kuhusu tukio hilo, Bomboko amekana kutokufahamu kuhusu taarifa hiyo.“Ni wewe nimekusikia hiyo taarifa kwako, sijamkamata mtu,” alisema kisha akakata simu.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Wenyeviti wa CCM Wilaya ya Hai, Nandumi Yobu, amesema viongozi wa chama walifika kituoni baada ya kupata taarifa za kukamatwa kwa mwenzao, akisisitiza kuwa kiongozi anapokuwa na changamoto anapaswa kuitwa na kupewa maelezo ya kosa analodaiwa kufanya.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
#ad
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Nchi ya Qatar, Tume ya Umoja wa Afrika na washiriki kutoka nchi wanachama wa Baraza la Ushirikiano la Nchi za Ghuba (Gulf Cooperation Council - GCC) imeandaa Mkutano wa Pili wa Uhamaji wa Nguvu Kazi (Second Doha Dialogue on Labour Mobility).
Mkutano huo utaratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira na Mahusiano na utafanyika kuanzia Oktoba 5 - 6, 2026 katika hoteli ya Hyatt Regency, Dar es Salaam ukiongozwa na kaulimbiu “Kuendeleza Uhamaji wa Nguvu kazi yenye Haki na endelevu katika ya Nchi za Afrika na Ghuba (GCC+). -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile, amejibu maswali na mijadala inayohusu kutoonekana hadharani kwa aliyekuwa Makamu wa Rais wa Tanzania kiongozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, akibainisha kuwa amezungumza na ndugu pamoja na watu wake wa karibu waliothibitisha kuwa yupo.
Akizungumza na mwanahabari Edwin Odemba kupitia kipindi cha Medani Kuu cha Star TV, Balile ameeleza kuwa baadhi ya watu katika jamii na kwenye mitandao ya kijamii wamekuwa wakipendelea kusikia taarifa za kwamba Nchimbi haonekani kwa sababu wanaona taarifa hizo zina "nyama" na mvuto wa hisia, ingawa ukweli uliothibitishwa na watu wake wa karibu unaonesha kuwa yupo.
Hata hivyo, ameeleza kuwa taarifa za ukweli mara nyingi hazipokelewi vizuri na makundi yanayotafuta hisia za udaku mtandaoni
Mbali na hayo, Balile alirejelea pia mjadala wa kauli ya awali ya Dkt. Nchimbi kuhusu Katiba Mpya, akieleza kuwa Katiba Mpya ni jambo la msingi linalotakiwa na wote na kwamba mchakato wake unapaswa kuanza na kuendelea kwa maslahi ya nchi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Idara ya Oganaizesheni, Paul Matiko Chacha, ametoa onyo kali na kukemea tabia ya baadhi ya viongozi wanaofanya makosa kisha kujaribu kujificha kwenye kivuli cha chama ili kukwepa uwajibikaji.
Chacha amesema kuwa chama hikitavumilia uvunjifu wa sheria, huku akisisitiza kuwa pindi kitakapobaini kiongozi au mwanachama yeyote anayekiuka katiba, kanuni, na taratibu za chama pamoja na jumuiya zake, hatua kali zitachukuliwa mara moja ili kukifanya chama kibaki salama na imara.
Akihutubia Mkutano Mkuu Maalum wa CCM Mkoa wa Iringa uliofanyika tarehe 26 Septemba, 2026, katika Chuo cha Umoja wa Vijana Ihemi, Chacha aligusia pia minong'ono inayouliza kuhusu alipo aliyekuwa Makamu wa Rais wa Tanzania, Dkt. Emmanuel Nchimbi, ambapo alihoji iwapo waliouuliza swali hilo walishawahi kwenda nyumbani kwake na kumkosa.
“Kama mlivyoona wapo viongozi na wanachama wamechukuliwa hatua na wanapambana na makosa yao wenyewe, na Chama kimebaki salama hadi sasa,” ameeleza Chacha.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Wakili wa Kujitegemea, Noelina Bippa, amesema mwanamke anayeishi na mwanaume bila ndoa halali hawezi kurithi kama mke, akieleza kuwa haki ya kurithi hutegemea sheria inayotumika na hadhi ya mtu kisheria katika uhusiano huo.
Amesema dhana ya ndoa inaweza kutumika katika mahakama kutambua na kulinda baadhi ya haki zinazotokana na maisha ya pamoja, lakini haimaanishi kwamba mwanamke huyo anakuwa mke halali kwa kila suala, ikiwemo mirathi. Aidha, mali zilizochumwa kwa pamoja zinaweza kuhitaji ushahidi ili kubainisha mchango na umiliki wa kila upande.
Bippa ameyasema hayo wakati wa mahojiano na Jambo TV, akisisitiza kuwa changamoto kubwa hujitokeza wakati wa mirathi pale familia inapomkataa mwanamke aliyekuwa akiishi na marehemu. Ameishauri jamii kuhalalisha ndoa na kupata cheti ili kupunguza migogoro na kulinda haki za wahusika.
@Missbippaofficial
@mckamenduThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Wakili wa Kujitegemea, Noelina Bippa, amesema dhana ya ndoa si ndoa yenyewe, bali ni hali inayoweza kutambuliwa na mahakama pale watu wawili wameishi pamoja na kujiona kama wanandoa, wakapata watoto au mali kwa pamoja bila kufunga ndoa rasmi.
Amesema chini ya Kifungu cha 160 cha Sheria ya Ndoa, mahakama inaweza kuangalia mazingira ya maisha yao na, endapo imebaini kuwa wameishi pamoja kwa kipindi cha miaka miwili au zaidi katika mazingira yanayoonesha kuwa ni wanandoa, inaweza kuweka dhana ya ndoa na kutumia sheria kulinda haki zao ikiwemo masuala ya mali.
Bippa ameyasema hayo wakati wa mahojiano na Jambo TV, akisisitiza kuwa dhana ya ndoa haimaanishi kwamba wahusika wamefunga ndoa, bali ni utambuzi wa kisheria unaoweza kutolewa na mahakama kwa ajili ya kulinda haki zinazotokana na maisha yao ya pamoja.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Wakili wa Kujitegemea, Noelina Bippa , amesema kuishi pamoja kwa mwanaume na mwanamke hakutoshi kisheria kuifanya hali hiyo kuwa ndoa, akieleza kuwa ndoa inahitaji wahusika kuwa na umri unaotakiwa na kutoa ridhaa yao kwa hiari.
Amesema mbali na ridhaa, wanandoa wanapaswa kufuata taratibu rasmi za kufunga ndoa kwa mujibu wa sheria, ikiwemo kufunga ndoa ya kidini kwa wanaofuata imani za Kikristo au Kiislamu, ndoa ya kimila kwa wanaofuata mila, au kufunga ndoa katika mamlaka husika kwa wanaohitaji ndoa ya kiraia.
Bippa ameyasema hayo wakati wa mahojiano na Jambo TV, akisisitiza kuwa baada ya taratibu hizo kukamilika na wahusika kupewa cheti cha ndoa, ndipo ndoa inapotambuliwa rasmi kisheria.
Mtangazaji: @mckamenduThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katibu wa NEC, Itikadi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Kenani Kihongosi, amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, ni kiongozi mwenye uwezo mkubwa, mvumilivu, anayejua kazi na ameithibitishia dunia kuwa akina mama wanaweza.
Kihongosi amebainisha hayo Mkoani Tanga ambako amehitimisha ziara yake ya kichama, iliyolenga kukagua uhai wa CCM mkoani humo na utekelezaji wa Ilani yake ya 2025/2030.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwandishi wa habari mwandamizi, Absalom Kibanda, ameeleza kuwa Tanzania inakabiliwa na jinamizi la kitaifa la hofu linalowaingiza wananchi, wanasiasa, viongozi wa dini, na waandishi wa habari kwenye hali ya kutokujua usalama na hatima ya kesho yao.
Akizungumza na mwanahabari Edwin Odemba kupitia kipindi cha Medani Kuu cha Star TV siku ya Jumamosi, Septemba 26, 2026, Kibanda amebainisha kuwa hali hiyo ya hofu inatokana na mfululizo wa matukio yasiyoeleweka yanayohusishwa na kundi la "watu wasiojulikana" bila kuwa na majibu ya wazi ya chanzo wala mwisho wake.
Amefafanua kuwa sintofahamu iliyopo inafanya watu washindwe kutambua nini kitakachowatokea kesho kuhusu usalama wao na hatima zao.
"Kwanza nikuambie kitu kimoja. Taifa zima lina hofu. Viongozi wana hofu, wanaharakati wana hofu, wanasiasa wana hofu. Viongozi wa dini wana hofu. Waandishi wa habari wana hofu. Hofu ni jinamizi la kitaifa... Wana hofu kwasababu kuna sintofahamu. Watu hawafahamu kesho yao. Watu hawafahamu usalama wao. Watu hawafahamu hatima zao", ameeleza Kibanda.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile, ametoa msimamo wa vyombo vya habari kuhusu kuripoti matukio ya utekaji na watu kupotea nchini, akisisitiza kuwa uandishi wa habari wa kitaaluma unazingatia uchunguzi na ushahidi badala ya kufuata msisimko wa harakati za mitandao ya kijamii.
Akizungumza na mwanahabari Edwin Odemba kupitia kipindi cha Medani Kuu cha Star TV siku ya Jumamosi, Septemba 26, 2026, Balile ameeleza kuwa vyombo vya habari vinaripoti matukio yaliyothibitishwa kisheria na kwamba kazi ya wanahabari ni kuonesha ukweli badala ya kukurupuka kuchapisha taarifa zisizothibitishwa.
Akimulika wajibu wa vyombo vya habari na thamani ya maisha ya binadamu, Balile amesisitiza kuwa maisha ya mtu yeyote hayapaswi kupotea na kwamba yeye kama binadamu anasikitishwa na matukio ya vifo au kupotea kwa raia.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mhariri wa habari wa The Chanzo, Khalifa Said, amekiri kuwa vyombo vya habari nchini vinawajibika zaidi kwa serikali na viongozi kuliko kwa umma au wananchi, huku akitaja hofu ya kukabiliana na mamlaka kuwa sababu kuu inayowafanya waandishi kuogopa kuwapa sauti wananchi.
Akizungumza na mwanahabari Edwin Odemba kupitia kipindi cha Medani Kuu cha Star TV Jumamosi, Septemba 26, 2026, Khalifa Said ameeleza kuwa tafiti mbalimbali zinaonesha kuwa habari nyingi zinazoandikwa zimejikita kwenye maagizo na kauli za viongozi badala ya kuibua kero, hofu, na matatizo ya wananchi wa kawaida.
Akifafanua kuhusu hali halisi ya uandishi wa habari nchini, Khalifa Said amebainisha kuwa magazeti na vyombo vingi vya habari vimekuwa vikipanga habari zao kulingana na kile kinachosemwa au kufanywa na viongozi wa serikali, asasi za kiraia, na sekta binafsi.
"Ni ukweli kwamba kwa kiwango kikubwa kwa mtazamo wangu mimi na sidhani kama ni mtazamo wangu binafsi kwa sababu kuna tafiti mbalimbali ambazo zimewahi kufanywa hapa Tanzania kuhusiana na namna ambavyo vyombo vya habari na waandishi wa habari wanafanya kazi zao... ripoti zimekuwa zikionesha kwamba habari nyingi zinazoandikwa na vyombo vya habari ni habari zinazohusu viongozi... Na kuna habari chache au hafifu sana zinazohusu wananchi... kuainisha matumaini, hofu, matatizo, harakati, michakato ambayo wananchi wanafanya huko chini", ameeleza Khalifa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwenyekiti wa Waandishi wa Habari za Vijijini, Neville Meena, amekiri kuwa umma wa Watanzania umepunguza imani na vyombo vya habari nchini kutokana na kushuka kwa habari za uchunguzi na athari za mazingira magumu ya kisheria.
Akizungumza na mwanahabari Edwin Odemba kupitia kipindi cha Medani Kuu cha Star TV Jumamosi, Septemba 26, 2026, Meena amebainisha kuwa vyombo vya habari na waandishi vinakabiliwa na kibarua kizito cha kufanya kazi ya ziada ili kurejesha kuungwa mkono na umma.
Meena ameeleza kuwa ingawa vituo vya redio, televisheni, na magazeti vinaendelea kufanya kazi kila siku, mtazamo wa wananchi na wasomaji umegubikwa na kutoridhishwa na kile kinachoripotiwa. Amebainisha kuwa wananchi wamekuwa wakihoji sababu za vyombo vya habari kuacha kuibua skendo kubwa na habari za uchunguzi kama ilivyokuwa zamani kwenye matukio kama vile sakata la Escrow.
Akijibu swali kuhusu waandishi kuacha misingi ya taaluma, Meena amekiri kuwa kwa sehemu fulani misingi imeachwa, lakini akasisitiza kuwa hali hiyo inasababishwa na mazingira magumu ya kisheria yanayowarudisha nyuma waandishi na wamiliki wa vyombo vya habari.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile, amewataka Watanzania na wajadili wa masuala ya habari kutofautisha kati ya uandishi wa habari wa kitaaluma na harakati za mitandao ya kijamii, huku akikanusha tuhuma za kuiacha misingi ya taaluma hiyo na kuwa "mpambe wa serikali".
Akizungumza na mwanahabari Edwin Odemba kupitia kipindi cha Medani Kuu cha Star TV siku ya Jumamosi, Septemba 26, 2026, Balile amebainisha kuwa uandishi wa habari wa kweli unapaswa kusimamia maslahi ya muda mrefu ya jamii badala ya kufuata matakwa mepesi ya muda mfupi.
Mjadala huo umechochewa na swali la mwanahabari Edwin Odemba aliyehoji sababu za jamii kumwona Balile na baadhi ya waandishi wa habari kama wapambe wa serikali badala ya kuwa sauti ya umma kama ilivyokuwa hapo awali.
Akifafanua kuhusu misingi ya taaluma ya habari, Balile amebainisha kuwa mfumo wa sasa wa habari umekabiliwa na changamoto ambapo kila mwenye simu ya mkononi anajichukulia kama mwandishi wa habari na kusambaza harakati zake badala ya kufuata misingi ya uandishi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mradi mkubwa wa maji wa Miji 28 unaotekelezwa katika Kijiji cha Mavuji, Kilwa Masoko, mkoani Lindi, umekamilika na wananchi wameanza kupata huduma safi ya maji, hatua inayowatoa kwenye lindi la changamoto za magonjwa ya milipuko kama kipindupindu yaliyokuwa yakiwakumba mara kwa mara kutokana na ukosefu wa maji salama.
Baada ya kufunguliwa kwa tone la kwanza la mradi huo wa kihistoria, wananchi wameupokea kwa shangwe na furaha kubwa, huku wazee wa eneo hilo wakimtumia salamu za shukrani na kumuombea dua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa uwekezaji huo mkubwa.
Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, ametembelea mradi huo kujionea utekelezaji wake na kuagiza kuwa maunganisho mapya ya maji kwa wananchi yasichukue zaidi ya siku saba.
Akizungumza na wananchi wa Mavuji mara baada ya ukaguzi, Waziri Aweso amezitaka mamlaka zote za maji nchini, kupitia Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Kilwa Masoko (KIMUWASA), kuondoa urasimu katika kuwahudumia wananchi wanaoomba kuunganishiwa maji majumbani mwao.
"Sasa niwasihi sana watendaji wa Wizara ya Maji. Mradi umekamilika na umeanza kutoa huduma, sasa maunganisho mapya yasizidi siku saba. Sio mwananchi anaomba kuunganishiwa maji unamwambia njoo kesho, njoo kesho... hizo zilipendwa," amesisitiza Waziri Aweso.
Mradi huo wa kimkakati wa Miji 28 umegarimu kiasi cha Shilingi bilioni 44 za Kitanzania, ukiwa umefikia asilimia 94.3 ya utekelezaji wake na unatarajiwa kuwanufaisha wakazi zaidi ya 59,983 huku ukizalisha lita milioni 5.5 za maji kwa siku kutoka katika chanzo cha Mto Mavuji.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Idara ya Oganaizesheni, Paul Chacha, amesema vyombo vya dola na viongozi wa serikali ni mali ya CCM, akidai kuwa chama hicho ndicho kilichowaweka katika nafasi hizo.
Chacha ameyasema hayo katika mkutano maalumu wa CCM Mkoa wa Iringa, uliojadili maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa CCM na Jumuiya zake mwaka 2027, pamoja na maandalizi ya maadhimisho ya miaka 50 ya chama hicho.
Kuhusu madai ya upinzani kwamba CCM huwasomba watu kwenye mikutano yake, Chacha amesema chama hicho kitaendelea kufanya hivyo, ikiwemo kutumia mabasi kuwapeleka wanachama wake kwenye mikutano na kuwapatia posho.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, ameipongeza Serikali ya Qatar kwa mafanikio makubwa ya matumizi ya teknolojia ya kisasa na nishati safi katika mifumo ya usafiri wa umma.
Dkt. Nchemba ametoa pongezi hizo leo, Jumamosi, Septemba 26, 2026, jijini Doha, Qatar, mara baada ya kupokea taarifa rasmi ya uendeshaji wa kampuni ya usafirishaji ya Mowasalat kutoka kwa Waziri wa Uchukuzi wa Qatar, Sheikh Mohammed bin Abdullah bin Mohammed Al Thani.
Waziri Mkuu, ambaye yuko nchini humo kwa ziara rasmi ya kikazi ya siku tatu, amesema ubunifu na mifumo ya usafiri wa umma ya Qatar imesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza msongamano wa magari barabarani kutokana na kuwa na usafiri wa uhakika.
“Nyumbani tunalo tatizo la msongamano wa magari na kupitia teknolojia mnazotumia, Tanzania inaweza kujifunza mbinu mlizotumia ili nasi tuweze kukabiliana nalo,” amesema Dkt. Nchemba.
Aidha, amebainisha kufurahishwa kwake na uamuzi wa kampuni hiyo kutumia nishati safi kwa sehemu kubwa, akihusisha hatua hiyo na ajenda ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye ni kinara wa nishati safi barani Afrika, jambo litakalosaidia maandalizi kuelekea michuano ya AFCON 2027.
Katika upande mwingine, Waziri Mkuu ameishukuru kampuni hiyo kwa kutoa ajira kwa Watanzania 722 katika nafasi mbalimbali, akisisitiza kuwa ni fursa nzuri kwa vijana wa Kitanzania kupata ujuzi na kujifunza teknolojia mpya.
Awali, Waziri wa Uchukuzi wa Qatar, Sheikh Mohammed bin Abdullah bin Mohammed Al Thani, alimweleza Waziri Mkuu kuwa Mowasalat inatoa huduma za usafiri wa abiria kwa kutumia mabasi, teksi, na usafiri wa wanafunzi au matukio maalumu. Alibainisha kuwa kwa mwaka 2025, kampuni hiyo ilihudumia watu milioni 42, huku asilimia 70 ya magari yake ikitumia umeme na yakiwa yamefungwa mifumo ya ukaguzi wa kielektroniki kubaini hitilafu kwa haraka. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Kenani Kihongosi, akizungumza leo Jumamosi Septemba 26, 2026 katika mkutano wa hadhara uliofanyika Tanga Mjini mkoani Tanga, amehoji mwenendo wa chama cha upinzani cha CHADEMA kuhusu namna kinavyowachukulia hatua viongozi wake wanaotoa tuhuma dhidi ya Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Heche.
Kihongosi amebainisha kuwa katika kipindi cha hivi karibuni, viongozi mbalimbali wa chama hicho wamekuwa wakisimamishwa na kufukuzwa uongozi pale tu wanapohoji matumizi ya fedha au kutoa tuhuma dhidi ya Heche. Ameeleza kuwa hatua hizo zinazua maswali iwapo taasisi hiyo inafaa kuendelea kuitwa chama cha siasa.
"Hicho chama kinafaa kuwa chama cha siasa? Kwamba kila anayetuhumiwa ni mwizi wao wanamfukuza uongozi...nini kila anayetuhumu Heche mwizi anafukuzwa chama?", amehoji Kihongosi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Kenani Kihongosi, amewataka wananchi wa Mkoa wa Tanga na Watanzania kwa ujumla kuheshimu, kuwapenda, na kuwapa ushirikiano askari wa vyombo vya ulinzi na usalama, huku akionya dhidi ya watu wanaowachochea wananchi kuvichukia vyombo hivyo.
Akizungumza leo Jumamosi, Septemba 26, 2026, katika mkutano wa hadhara uliofanyika Tanga Mjini mkoani Tanga, Kihongosi ameeleza kuwa chuki hiyo inasukumwa na ajenda mbaya ya kisiasa kutoka kwa watu walioshindwa na kukataliwa na wananchi .
Amepiga msisitizo kuwa askari wamekula kiapo cha kulinda nchi mpaka kifo chao, hivyo wanastahili kuungwa mkono na kutiwa moyo badala ya kudhalilishwa au kuvunjwa moyo.
"Sasa anatokea mtu mmoja amechanganyikiwa huko na stressi zake za kukataliwa na Watanzania anaamua kuwaambia nyinyi watu wa Tanga kwamba chukieni vyombo vyenu vya ulinzi na usalama. Leo nitawaambia hapa kati ya watu tunaopaswa kuwapenda na kuwatia moyo ni askari wetu ndani ya taifa letu. Wewe unapolala wao wanakesha, wewe uwe salama", ameeleza.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Kenani Kihongosi, akizungumza leo Jumamosi Septemba 26, 2026 katika mkutano wa hadhara uliofanyika Tanga Mjini mkoani Tanga, amemjibu Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, John Heche, kufuatia kauli zake za kutilia shaka mafanikio ya nchi.
Kihongosi amebainisha kuwa alimsikia Heche akiwa Bariadi mkoani Simiyu akidai kuwa haoni kilichofanyika nchini tangu kupatikana kwa Uhuru. Akijibu kauli hizo mbele ya wananchi wa Tanga, Kihongosi amesisitiza kuwa CCM iko tayari kumpa Heche data na takwimu sahihi ili kuondoa kile alichokiita upotoshaji kuhusu uelekeo wa nchi.
Kihongosi pia alijibu madai ya Heche kwamba anatajwa mara kwa mara na viongozi wa CCM au kwamba Kihongosi ni kijana mdogo asiye na hoja, akimfahamisha kuwa mwanasiasa wa kweli hupimwa kwa hoja za msingi na siyo kwa ‘makelele’ au umri.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Kenani Kihongosi, amewataka wananchi wa Mkoa wa Tanga na Watanzania kwa ujumla kuheshimu, kuwapenda, na kuwapa ushirikiano askari wa vyombo vya ulinzi na usalama, huku akionya dhidi ya watu wanaowachochea wananchi kuvichukia vyombo hivyo.
Akizungumza leo Jumamosi, Septemba 26, 2026, katika mkutano wa hadhara uliofanyika Tanga Mjini mkoani Tanga, Kihongosi ameeleza kuwa chuki hiyo inasukumwa na ajenda mbaya ya kisiasa kutoka kwa watu walioshindwa na kukataliwa na wananchi .
Amepiga msisitizo kuwa askari wamekula kiapo cha kulinda nchi mpaka kifo chao, hivyo wanastahili kuungwa mkono na kutiwa moyo badala ya kudhalilishwa au kuvunjwa moyo.
"Sasa anatokea mtu mmoja amechanganyikiwa huko na stressi zake za kukataliwa na Watanzania anaamua kuwaambia nyinyi watu wa Tanga kwamba chukieni vyombo vyenu vya ulinzi na usalama. Leo nitawaambia hapa kati ya watu tunaopaswa kuwapenda na kuwatia moyo ni askari wetu ndani ya taifa letu. Wewe unapolala wao wanakesha, wewe uwe salama", ameeleza.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Kenani Kihongosi, akizungumza leo Jumamosi Septemba 26, 2026 katika mkutano wa hadhara uliofanyika Tanga Mjini mkoani Tanga, amemjibu Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, John Heche, kufuatia kauli zake za kutilia shaka mafanikio ya nchi.
Kihongosi amebainisha kuwa alimsikia Heche akiwa Bariadi mkoani Simiyu akidai kuwa haoni kilichofanyika nchini tangu kupatikana kwa Uhuru. Akijibu kauli hizo mbele ya wananchi wa Tanga, Kihongosi amesisitiza kuwa CCM iko tayari kumpa Heche data na takwimu sahihi ili kuondoa kile alichokiita upotoshaji kuhusu uelekeo wa nchi.
Kihongosi pia alijibu madai ya Heche kwamba anatajwa mara kwa mara na viongozi wa CCM au kwamba Kihongosi ni kijana mdogo asiye na hoja, akimfahamisha kuwa mwanasiasa wa kweli hupimwa kwa hoja za msingi na siyo kwa ‘makelele’ au umri.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Wananchi wa Manispaa ya Mtwara Mikindani wameanza kuona urahisi wa huduma za ardhi baada ya mfumo wa kidijiti kuwawezesha kuwasilisha maombi ya hati miliki kwa njia ya mtandao bila kulazimika kufuatilia huduma hizo kwa njia za kawaida.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kliniki ya Ardhi Kidijiti katika Manispaa ya Mtwara Mikindani, Mkurugenzi wa Idara ya TEHAMA wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Fratern Hassan, amesema mfumo huo umeanzishwa ili kupunguza ulazima wa wananchi kufuatilia huduma za ardhi kwa njia za kawaida.
Hassan amesema kupitia mfumo huo wananchi wanaweza kupata huduma mbalimbali za ardhi, ikiwemo kuomba hati miliki kwa kutumia simu zao wakiwa nyumbani. Kwa mujibu wa maelezo yake, mfumo huo unalenga kuwasaidia wananchi kupata huduma kwa muda mfupi na kwa ufanisi zaidi.
Kwa upande wake, Waziri mwenye dhamana, Dk. Leonard Akwilapo, amesema huduma hizo za ardhi kidijiti kwa sasa zinapatikana katika mikoa 17 nchini ambayo ni Mtwara, Lindi, Pwani, Dodoma, Singida, Tabora, Kigoma, Shinyanga, Mwanza, Mbeya, Ruvuma, Njombe, Kagera, Arusha, Tanga, Kilimanjaro na Morogoro.
Akwilapo amesema Wizara inaendelea na maandalizi ya kuhakikisha mikoa tisa iliyosalia inaingizwa kwenye mfumo huo kabla ya kumalizika kwa mwaka wa fedha 2026/2027, hatua ambayo inalenga kupanua upatikanaji wa huduma za ardhi kidijiti kwa wananchi katika maeneo zaidi nchini.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema watu wengi wanaowazungumzia watoto wa Rais Samia Suluhu Hassan akiwemo Wanu Hafidh, Abdul na Ahmed hawajawahi kukutana nao ana kwa ana wakaujua uhalisia wao na kwamba ni watu wenye moyo wa upendo na huruma kwa Watanzania.
Akizungumza kwenye hitma ya marehemu Hafidh Ameir aliyekuwa mume wa Rais Samia, Chalamila amesema watoto wa marehemu Hafidh wanawapenda na kuwahurumia Watanzani na kwamba wamelelewa kwenye mazingira mazuri.
"Watanzania wengi ukiwasikiliza namna ambavyo wanayazungumzia maisha ya watu hawa, unakubali kwamba hawajawahi kuonana nao ana kwa ana lakini leo hii ukimsogelea vizuri dada Wanu, ukamsogelea vizuri Abdul , ukamsogelea vizuri ndugu yangu Ahmed ambaye amekaa pale, utauona moyo wa huruma pamoja na mioyo ya heshima kwa Watanzania kuliko vile ambavyo wachache wanaweza kusema" amesema Chalamila.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Chama cha ACT Wazalendo kupitia kwa Waziri Kivuli wa TAMISEMI na Maendeleo Vijijini, Kulthumu Jumanne Mchuchuli, kimeitaka Serikali kusitisha mara moja operesheni za kuwapanga na kuwaondoa wamachinga pamoja na wafanyabiashara wadogo katika maeneo yao ya biashara nchi nzima.
Akizungumza na waandishi wa habari tarehe 25 Septemba, 2026, Mchuchuli amebainisha kuwa badala ya kutumia nguvu na kubomoa meza za biashara, Serikali inapaswa kukaa na wafanyabiashara hao ili kutafuta suluhu ya pamoja bila kuharibu mitaji yao.
Mchuchuli ameeleza kuwa suala la wamachinga si ni la kijamii, hivyo linapaswa kushughulikiwa kwa hekima na maafisa maendeleo, maafisa biashara, pamoja na maafisa ustawi wa jamii waliopo kwenye halmashauri. Aidha, amebainisha kuwa kujenga masoko pembezoni mwa miji ambako hakuna mzunguko wa watu hakutaisaidia jamii hiyo, na badala yake akapendekeza kuanzishwa kwa masoko ya jioni kwa kufunga baadhi ya barabara kuu ili kuwaruhusu wamachinga kufanya biashara na kuwafikia wateja wanaotoka makazini.
Mbali na kusitishwa kwa operesheni hizo, ACT Wazalendo imewasilisha mapendekezo mengine makuu ikiwemo Bunge kupitia Kamati ya Kudumu ya Serikali za Mitaa liunde kamati maalum ya kuchunguza matukio ya kuungua kwa masoko nchini kama vile masoko ya Kariakoo, Karume, na Marangu Moshi ili kubaini vyanzo vya moto na waliohusika kuchukuliwa hatua za kisheria.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Chama cha Hisabati Tanzania (MAT/CHAHITA), kwa kushirikiana na Idara ya Hisabati ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), kimetangaza matokeo ya Mashindano ya Kitaifa ya Hisabati (Tanzania Mathematics Olympiads – TAMO) kwa mwaka 2026.
Mashindano hayo yalifanyika tarehe 8 Agosti 2026, yakishirikisha wanafunzi wa Sekondari ya Chini (O-Level) na Sekondari ya Juu (A-Level) kutoka Tanzania Bara na Zanzibar.
Akizungumza leo Septemba 26, 2026, Mwenyekiti wa Taifa wa MAT/CHAHITA, Dkt. Said Sima, amesema ameridhishwa na mwenendo wa mashindano hayo, akibainisha kuwa idadi ya washiriki imeongezeka kutoka wanafunzi 1,852 waliotoka shule 119 mwaka 2025 hadi wanafunzi 2,366 kutoka shule 118 mwaka 2026.
Amesema ongezeko hilo linaashiria kuongezeka kwa hamasa ya wanafunzi na shule katika kujifunza Hisabati, pamoja na juhudi zinazoendelea za kubaini na kukuza vipaji vya Hisabati nchini.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Mhandisi Peter, ameipongeza CHAHITA kwa juhudi zake za kuratibu ushiriki wa Tanzania katika mashindano ya Hisabati ya kimataifa.
Amesema juhudi hizo zimeendelea kuifanya Tanzania kupata matokeo mazuri katika mashindano hayo, ambapo mwaka huu Tanzania imefanikiwa kushika nafasi ya tano kati ya nchi 26 zilizoshiriki.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
#ad
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kushirikiana na Serikali ya Nchi ya Qatar, Tume ya Umoja wa Afrika na washiriki kutoka nchi wanachama wa Baraza la Ushirikiano la Nchi za Ghuba (Gulf Cooperation Council - GCC) imeandaa Mkutano wa Pili wa Uhamaji wa Nguvu Kazi (Second Doha Dialogue on Labour Mobility)
Mkutano huo wenye kauli mbiu "Kuendeleza Uhamaji wa Nguvu
Kazi yenye Haki na Endelevu kati ya Nchi za Afrika na Ghuba
(GCC+)" utafanyika kuanzia Oktoba 5 - 6, 2026, katika hoteli ya Hyatt Regency, Dares Salaam -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Wazazi na walezi mkoani Geita wametakiwa kuhakikisha wanawapa watoto wao malezi bora nyumbani na kutowalazimisha walimu kubeba jukumu la malezi pekee, kwa kuwa msingi wa maadili ya mtoto huanzia katika familia.
Wito huo umetolewa Septemba 26, 2026 na Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa Madini Mkoa wa Geita, Mussa Kasuku, wakati akiwa mgeni rasmi katika mahafali ya sita ya Shule ya Msingi Glory to God iliyopo Buselesele, Wilaya ya Chato mkoani Geita.
Amesema pamoja na wahitimu hao kuonesha uwezo wao katika masomo, wanapaswa pia kutumia muda wao vizuri, kujitunza na kuwasaidia wazazi wao katika majukumu mbalimbali ya nyumbani.
Akitoa taarifa ya shule, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Glory to God, Joseph Sililu, amesema shule hiyo imeendelea kufanya vizuri kitaaluma kila mwaka, huku ikiweka mkazo katika kuwajenga wanafunzi kimaadili ili kuwaandaa kuwa raia wema na wenye manufaa kwa jamii.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Shule ya Msingi Glory to God, Godfrey Miti, amesema shule hiyo inalenga kutoa huduma bora ya elimu kwa wanafunzi na si kuichukulia elimu kama biashara.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Balozi Simon Sirro, ameliagiza Jeshi la Polisi mkoani Kigoma kuweka nguvu ya ziada na kufuatilia kwa kina kisa cha kupotea kwa vijana wawili katika mazingira ya kutatanisha wilayani Uvinza, huku akikiri kuwa kutopatikana kwa majibu ya haraka kutoka kwa vyombo vya usalama kunazua hofu na maswali mengi miongoni mwa wananchi.
Mkuu huyo wa Mkoa ametoa kauli hiyo Septemba 25, 2026, alipokuwa akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Ilagala wilayani Uvinza, kufuatia kilio cha wazazi na wakazi wa eneo hilo walioeleza kuwa vijana hao walichukuliwa tangu Agosti 16, 2026, na watu wasiojulikana na mpaka sasa hawajulikani walipo, licha ya jitihada za kuwatafuta kufanyika.
Balozi Sirro amewahakikishia wananchi na wazazi wa vijana hao kuwa Serikali inalichukulia tukio hilo kwa uzito mkubwa, kwani nchi ipo huru na kazi kuu ya vyombo vya usalama ni kulinda maisha na mali za raia.
Kwa upande wa Jeshi la Polisi, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, SACP, Filemon Makungu, amethibitisha kuwa jeshi hilo lina taarifa za kupotea kwa vijana hao na kwamba upelelezi wa kina unaendelea, ingawa mpaka sasa bado hawajafanikiwa kuwapata au kubaini walipo.
Tukio hilo limeendelea kuzua taharuki katika Kijiji cha hicho na maeneo ya jirani, huku wananchi wakiomba serikali na Jeshi la Polisi chini ya Kamanda Makungu kuharakisha upelelezi huo ili kukata kiu ya familia zinazoteseka kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa bila kujua hatima ya watoto wao.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Fursa mbalimbali zinazopatikana nchini, ikiwemo uwekezaji katika sekta ya madini, zimetakiwa kuzingatia sheria, kanuni na mikataba inayosimamia shughuli hizo ili kuhakikisha fursa hizo zinawanufaisha wananchi na kuchangia katika maendeleo ya Taifa bila kuvuruga mfumo wa sheria uliopo.
Akizungumza katika Jukwaa la Fungua Fursa lililoandaliwa na Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) mkoani Geita, kwa niaba ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Wakili wa Serikali kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali mkoani Kagera, Richard Nkaina, amesema fursa mbalimbali zinazopatikana nchini zinapaswa kutekelezwa kwa kuzingatia sheria na mikataba iliyowekwa.
Nkaina amesema kuwa katika kutumia fursa hizo, wananchi na wawekezaji wanapaswa kuelewa sheria zinazowaongoza ili kuepuka migogoro na kuhakikisha shughuli za uwekezaji zinaendana na maslahi mapana ya Taifa.
Amesema kuwa Tanzania inaendelea kujenga Taifa lenye uchumi imara kwa kuzingatia mipango ya maendeleo, ikiwemo Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, hivyo kila fursa inayopatikana inapaswa kutumiwa kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa.
Ameongeza kuwa uelewa wa sheria ni muhimu kwa wananchi, wafanyabiashara na wawekezaji kwa kuwa unawasaidia kutambua haki na wajibu wao katika kutumia fursa mbalimbali zinazopatikana nchini.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI:
Mbunge wa Jimbo la Muheza ambaye pia ni Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Hamis Mwinjuma (MwanaFA), ameongoza mamia ya wananchi wa Mtaa wa Beach Boy, Kata ya Majengo, wilayani Muheza, katika zoezi la kusafisha mfereji mkuu wa eneo hilo kwa kuondoa taka na udongo ulioziba njia ya maji, ikiwa ni hatua ya kukabiliana na tishio la mvua za El-Nino.
Katika zoezi hilo la msalagambo, Mwinjuma ameshiriki moja kwa moja katika kuondoa udongo na taka zilizokuwa zimeziba mfereji huo ili kuruhusu maji kupita kwa urahisi na kupunguza hatari ya kutokea kwa mafuriko wakati wa mvua.
Akizungumza baada ya zoezi hilo, Mwinjuma amesema lengo la usafi huo ni kuhamasisha wananchi kuchukua jukumu la kusafisha mazingira yanayowazunguka na kujiandaa mapema kukabiliana na athari zinazoweza kusababishwa na mvua hizo.
“Kila mmoja afanye usafi katika eneo lake kwa sababu kuna tishio la mvua za El-Nino ambazo zinatarajiwa kuwa kubwa. Kila mmoja akichukua jukumu lake, uwezekano wa kutokea kwa maafa unakuwa mdogo sana,” alisema Mwinjuma.
Aidha, Mwinjuma aliuomba Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kutathmini uwezekano wa kufanya ukarabati wa haraka wa kalavati lililopo katika eneo hilo ili kurahisisha upitishaji wa maji na kuzuia maji kuzuiliwa njiani.
Vilevile, aliishauri Halmashauri ya Wilaya ya Muheza kuweka mkakati wa kuwahamisha wananchi wanaoishi katika maeneo ya mabondeni na kuwapeleka maeneo salama, huku akisisitiza umuhimu wa kusitisha utoaji wa vibali vya ujenzi katika maeneo hatarishi.
Akijibu maelekezo hayo, Kaimu Meneja wa TARURA Wilaya ya Muheza, Athanas Faris, alisema wakala huo umepanga kujenga kalavati la kisasa la zege (Box Culvert) katika eneo hilo ili kuongeza uwezo wa kupitisha maji na kupunguza tatizo la mafuriko.
Kwa upande wake, Katibu Tawala wa Wilaya ya Muheza (DAS), Mohamed Mfaki, aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya, aliwataka wananchi wanaoishi mabondeni na karibu na mifereji mikubwa kuchukua tahadhari mapema ili kujikinga na madhara yanayoweza kusababishwa na mvua hizo.
Naye Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Muheza, Simon Leng’ese, alisisitiza umuhimu wa kutoa elimu ya kutosha kwa wananchi wanaoishi katika maeneo hatarishi ili waweze kuchukua hatua za kujinusuru kabla ya maafa kutokea.
“Mvua zitakuwa kubwa, hivyo watu wote wanaokaa kwenye mabonde wachukue tahadhari za mvua hizo ili kuondoa uwezekano wa kutokea kwa mafuriko yatakayopoteza maisha na mali,” alisisitiza Leng’ese.
Zoezi hilo lilihitimishwa na Diwani wa Kata ya Majengo, aliyewashukuru wananchi wa kata hiyo na wa Kwamkabala kwa kujitokeza kwa wingi kushiriki katika msalagambo huo ulioongozwa na Mbunge wao. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makundi mbalimbali ya kijamii mkoani Tabora, wakiwemo Waganga wa tiba asili, Wajasiriamali, watu wenye mahitaji maalumu na wakulima, yamewasilisha changamoto zinazowakabili kwa Katibu wa NEC, Idara ya Mambo ya Siasa na Mahusiano ya Kimataifa, wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rabia Hamid, na kuomba hatua za haraka zichukuliwe kuzitatua.
Changamoto hizo zimetolewa katika ziara ya Kiongozi huyo ya kutembelea na kusikiliza kero za wananchi, ambapo miongoni mwa mambo yaliyolalamikiwa ni uwepo wa maegesho holela ya pikipiki, mahitaji ya waganga wa tiba asili ya kupata duka maalumu la kuuza nyara pamoja na gharama za pembejeo kwa wakulima wa tumbaku ambapo baadhi ya changamoto hizo zimepatiwa ufafanuzi na wataalamu wa sekta husika.
Akizungumza baada ya kusikiliza kero hizo, Rabia Hamid amemtaka Waziri wa Kilimo kufanya ziara maalumu mkoani Tabora kwa ajili ya kuwasikiliza na kutafuta ufumbuzi wa changamoto zinazowakabili wakulima wa tumbaku, huku akiwataka watumishi wa Serikali kuwa karibu na wananchi kwa kutenga muda maalumu wa kuwafikia, kusikiliza na kutatua changamoto zao.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Beno Malisa, amewataka watumishi wa Serikali kutenga siku maalumu kila wiki kwa ajili ya kusikiliza kero za wananchi, akisema hatua hiyo itasaidia kuwapa wananchi fursa ya kueleza changamoto zao na kupata majibu pamoja na hatua za utatuzi kwa wakati.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Wananchi katika Kijiji cha Kikubwa, Kata ya Butuguri, wilayani Butiama mkoani Mara, wameamua kuchangishana fedha pamoja na nguvu kazi, kwaajili ya kujenga Shule ya Sekondari katika Kijiji hicho kufutia kuchoshwa na vitendo vya watoto wao kutembea umbali mrefu jambo walilosema linachochea wasichana kupata mimba kutokana na vishawishi.
Wakizungumza katika zoezi la ukusanyaji wa mawe, wananchi hao wamesema kwamba, kwa muda mrefu watoto wao wamekuwa wakitembea Umbali kwenda katika shule ya kata ambayo inakadiliwa kuwa umbali wa kilomita 6-10 kutoka kijijini hapo, ambapo imekuwa ikipelekea watoto wengi kukatisha masomo.
Wamesema suala la kuchangishana fedha hawajashikizwa na mtu yeyeote, bali wao kwa umoja na wanafunzi walioko mikononi wa kijiji hicho watafanya zoezi hilo kwa ushirikiano wakati wakisubiri usaidizi wa Serikali.
“Ni mateso ambayo wanapitia watoto wetu, ndio maana tumeamua sasa kuanza kujenga shule karibu na makazi, na hapa tunaamini watafaulu vizuri na watasoma na kumaliza masomo yao kama kawaida” Amesema Boniphace Nyambulili, Mkazi wa kijiji cha Kibubwa Butiama.
Aidha, kwa upande wake Afisa Elimu Kata ya Butuguri Mgaya Mgisa amewapongeza wananchi hao kwa uamuzi huo na kusema kwamba Serikali itahakikisha inawasaidia kufikia malengo ya ukamilikaji wa Shule hiyo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Wadau mbalimbali kwa sasa wanaweza kuwekeza katika ujenzi wa vituo vya mafuta katika maeneo ya vijijini, baada ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kupunguza gharama za uwekezaji na masharti ya uombaji wa leseni, hatua inayolenga kuondoa uuzaji holela wa nishati hiyo katika maeneo hayo.
Hayo yamesemwa na Meneja wa EWURA Kanda ya Ziwa, Mhandisi Nyirabu Musira, wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye Maonesho ya Tisa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea katika Viwanja vya Dk. Samia Suluhu Hassan, mkoani Geita.
Musira amesema EWURA imetambua umuhimu wa upatikanaji wa nishati ya mafuta kwa wananchi wa vijijini, hivyo imechukua hatua za kupunguza masharti pamoja na gharama za uombaji wa leseni ili kuwavutia wawekezaji kuanzisha vituo vya mafuta katika maeneo hayo.
Amesema hatua hiyo inalenga kuhakikisha wananchi wa maeneo ya vijijini wanapata huduma ya mafuta kwa njia rasmi na salama, huku ikisaidia kupunguza utegemezi na uuzaji holela wa mafuta ambao unaweza kuhatarisha usalama wa wananchi na mazingira.
Kwa upande wake, Afisa wa Mahusiano kutoka EWURA, Thobietha Makafu, amesema mamlaka hiyo imejipanga kutoa elimu ya kutosha kwa wananchi kuhusu udhibiti wa huduma za maji na nishati, pamoja na kuwafahamisha wadau kuhusu taratibu na matakwa ya kisheria katika utoaji wa huduma hizo.
Makafu amesema elimu hiyo itasaidia wananchi na wawekezaji kuelewa wajibu wao, huku ikichangia upatikanaji wa huduma bora na salama za maji na nishati nchini.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Mwajuma Waziri, kutoa kiasi cha Shilingi milioni 500 ili kuanzia Jumatatu ijayo zianze kazi za uchimbaji wa visima saba katika eneo la Somanga, Kilwa Masoko, mkoani Lindi.
Hatua hiyo imekuja kufuatia ombi la Mbunge wa Kilwa Kusini, Kinje Kinjikitile, aliyemwomba Waziri Aweso kuchimba visima sita katika eneo hilo ili kuwapunguzia wananchi adha ya maji, wakati Waziri huyo alipokuwa akisimamishwa na wananchi usiku barabarani wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi ya maji.
Akijibu ombi hilo papo hapo mbele ya wananchi waliojitokeza kumlaki, Waziri Aweso ameongeza idadi ya visima vilivyoombwa na kuagiza fedha za kuanzia ziletwe mara moja.
“Mhe.Mbunge umeomba vichimbwe visima sita, sasa mimi nakuongezea vitachimbwa saba. Nikuagize Katibu Mkuu, kufikia Jumatatu hakikisha umeleta milioni 500 hapa Somanga na visima saba vianze kuchimbwa ili kuongezea nguvu visima vilivyopo na wananchi wa Somanga wapate huduma ya maji bila usumbufu wowote,” amesema Waziri Aweso.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, amesema kwamba, ikiwa Jamhuri ilitishika na maneno yaliyotumika kumshtaki ni yapi yalikuwa matokeo ya vitisho hivyo ambapo pia amesema suala hilo halijathibitishwa na upande wa Jamhuri kama kulikuwa matokeo yoyote.
Lissu amebainisha hayo Septemba 25, 2026 alipokuwa akiendelea kuwasilisha hoja zake za mwisho mbele ya jopo la majaji watatu wakiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Nyumba ni zaidi ya jengo. Kwa familia, ni mahali pa usalama, heshima na mwanzo wa maisha yenye uhakika. Kwa mwekezaji, ni mali yenye uwezo wa kuhifadhi na kuongeza thamani kadiri muda unavyopita. Kwa mji, miradi ya makazi na biashara iliyopangwa vizuri huleta ajira, huchochea biashara na kuboresha maisha ya watu.
Sekta ya milki nchini Tanzania inaendelea kukua, lakini ukuaji huo unaambatana na changamoto kadhaa. Miongoni mwazo ni upungufu wa nyumba unaokadiriwa kufikia nyumba milioni 3.8, huku mahitaji mapya yakiwa takribani nyumba 300,000 kila mwaka. Pia kuna ongezeko la gharama za ujenzi, ugumu wa kupata mikopo nafuu ya nyumba, shinikizo kwenye miundombinu na kasi kubwa ya ukuaji wa miji.
Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) linakabiliana na changamoto hizo kwa kuendeleza miradi ya makazi, biashara na matumizi mchanganyiko katika maeneo mbalimbali ya kimkakati.
Katika utekelezaji wake, NHC pia linazingatia dhana ya Mazingira, Jamii na Utawala Bora, inayojulikana kama ESG. Hii inahusisha matumizi bora ya ardhi, kujenga makazi yanayofikiwa na makundi tofauti, kuunganisha nyumba na huduma muhimu, kusimamia ubora wa ujenzi na kuhakikisha rasilimali za umma zinatumika kwa uwajibikaji.
Dhana ya ESG inasimamia masuala ya Environmental (Mazingira), Social (Jamii), na Governance (Utawala Bora). Huu ni mfumo au seti ya vigezo vinavyotumiwa na wawekezaji, mashirika, na taasisi za kifedha kutathmini jinsi kampuni inavyofanya kazi kwa uwajibikaji nje ya malengo yake ya kawaida ya kutengeneza faida ya kifedha tu.
Miradi hii 10 inaonyesha kwa vitendo namna NHC linavyogeuza changamoto za sekta ya nyumba kuwa fursa za makazi, biashara na uwekezaji.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Lugabela Patrick, ameibua kero ya baadhi ya wawekezaji wa kigeni kuingia nchini na kuwatumia Watanzania kusajili kampuni kwa majina yao kisha kuwadhulumu na kuwatupa mara baada ya kupata fursa za kibiashara na mitaji.
Suala hilo limeibuliwa leo, Ijumaa tarehe 25 Septemba, 2026, mkoani Pwani mbele ya Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPC), David Kafulila, wakati wa uzinduzi wa kongamano la fursa za uwekezaji na ushiriki wa sekta binafsi katika Miradi ya Ubia (PPP) lililoratibiwa na PPPC.
Patrick ameeleza kuwa ingawa kuingia ubia na mwekezaji mgeni kunarahisisha upatikanaji wa miradi, baadhi ya wawekezaji wa kigeni wamekuwa wakitumia mwanya huo kuwaingiza "kingi" Watanzania na kuwageuza vibarua na "mawinga" badala ya washirika halisi wa kibiashara.
Akijibu kero hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa PPPC, David Kafulila, amebainisha kuwa mwelekeo na msingi wa sera ya Tanzania unampa kipaumbele kikuu mwekezaji wa ndani, na kwamba uwekezaji wa kigeni unapaswa kuja kama msukumo wa kusaidia maeneo ambayo nchi haina uwezo nayo kikamilifu ili kuhamisha teknolojia, ueledi, na kujenga mtaji wa Watanzania. Hata hivyo, amekiri kuwa katika utekelezaji wa kila siku uwandani, baadhi ya Watanzania huingizwa kwenye mikataba ya ujanjaujanja kutokana na shida zao na kisha kutelekezwa.
Kafulila amesisitiza kuwa Serikali haitavumilia wawekezaji wageni kuja kuwadhulumu Watanzania, huku akiwataka vijana na wawekezaji wa ndani kuwa tayari kutetea haki zao na kutoa taarifa za malalamiko yao zikiwa na ushahidi kamili badala ya kuogopa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI:
Kuhusu madai kwamba Serikali ya Jamhuri ya Muungano ilitishika na maneno yaliyotumika na Jamhuri kumshitaki Tundu Lissu katika kesi ya uhaini, amekanusha jambo hilo kwa kusema kuwa kifungu cha 39 kilichotengeneza kosa la uhaini hakijazungumzia wala kuweka sharti la matokeo ya nia ya kutenda kitendo cha kihaini kwa kuitishia Jamhuri.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, leo Septemba 25, 2026 mbele ya jopo la majaji watatu wakiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru, ambapo ilikuwa ni sehemu ya hoja yake ya saba kati ya zile tisa alizozitaja katika utetezi wake wa mwisho.
Maneno ambayo Jamhuri waliyatumia kumshtaki Lissu na kwamba yaliitishia jamhuri ni pamoja na haya "Wanasema kitu kimoja sahihi hapa, wanasema hivi: Msimamo huu unaashiria uasi; ni kweli, ni kweli kwa sababu tunasema tutazuia uchaguzi, tutahamasisha uasi na hiyo ndio namna ya kupata mabadiliko kwahiyo tunaenda kukinukisha sana sana. Huu uchaguzi tutauvuruga, tutauvuruga kwasababu tunaenda kuuvuruga sana sana."
Lissu amesema kuwa matokeo ya nia hiyo ya kuitishia Jamhuri ya Muungano pia hayawezi kupatikana katika kesi mbili za uhaini zilizotangulia kesi yake, akitaja kesi ya Khatibu Ghandi na ile ya Bibi Titi Mohamed, ambayo amesema ndiyo ilikuwa kesi ya kwanza ya uhaini kwa mtu aliyekuwa akipigania uhuru.
Lissu amesema kuwa Mahakama haikuambiwa na mawakili juu ya matokeo ya nia ya kutenda kosa hilo, na sasa ina fursa ya kujielekeza kwenye masharti ya kifungu cha 10(2) cha Kanuni ya Adhabu. Amefafanua kuwa kama nia ni sehemu ya kosa, basi matokeo yake yanakuwa ya lazima na yalipaswa kuonyeshwa katika hati ya mashtaka na kuthibitishwa kwa ushahidi jambo ambalo amesema upande wa mashtaka haukulifanya, na kufanya hati hiyo kuwa batili au sawa na "sifuri".
Kuhusu ukosefu wa ushahidi wa Serikali kutishika, Lissu ameeleza kuwa upande wa mashtaka haukuleta shahidi yeyote wa kuthibitisha kuwa Serikali (inayoongozwa na Rais kama Mkuu wa Nchi na Amiri Jeshi Mkuu) ilitishiwa. Ameongeza kuwa aliomba viongozi mbalimbali wakiwemo aliyekuwa Makamu wa Rais, Philip Mpango, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, na wakuu wa vyombo vya ulinzi lakini hawakufika. -
Jambo TV
@Jambotv_
#ad
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kushirikiana na Serikali ya Nchi ya Qatar, Tume ya Umoja wa Afrika na washiriki kutoka nchi wanachama wa Baraza la Ushirikiano la Nchi za Ghuba (Gulf Cooperation Council - GCC) imeandaa Mkutano wa Pili wa Uhamaji wa Nguvu Kazi (Second Doha Dialogue on Labour Mobility)
Mkutano huo wenye kauli mbiu "Kuendeleza Uhamaji wa Nguvu
Kazi yenye Haki na Endelevu kati ya Nchi za Afrika na Ghuba
(GCC+)" utafanyika kuanzia Oktoba 5 - 6, 2026, katika hoteli ya Hyatt Regency, Dares Salaam -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI PICHA:
Waziri Mkuu wa Tanzania Dkt. Mwigulu Nchemba, jana Alhamisi Septemba 24, 2026, alitembelea Vatican City akiwa jijini Roma, Italia, katika ziara ya kando ya Mkutano wa Kimataifa wa Afya Moja na Mifumo ya Chakula na Kilimo, uliofanyika Makao Makuu ya Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO).
Akiwa Vatican City, Waziri Mkuu alikutana na Mkuu wa Itifaki wa Sekretarieti ya Nchi ya Vatican, Monsinyori Javier Domingo Fernández González.
Katika ziara hiyo, Dkt. Mwigulu pia alitembelea maeneo mbalimbali ya kihistoria na kiutamaduni ya Vatican City, yenye umuhimu mkubwa katika historia ya Kanisa Katoliki duniani. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, imeahirishwa mchana huu wa Septemba 25, 2026 hadi jumatatu Septemba 28, 2026, ambapo itakuja kuendelea katika usikilizaji wa uwasilishaji wa hoja za mwisho (Final Submission) kutoka kwa mshtakiwa.
Uamuzi huo umetolewa na Jaji Dunstan Ndunguru ambaye anaongoza Jopo la majaji watatu wanaosikiliza kesi hiyo.
Kabla ya majaji kuamua kesi kuendelea jumatatu, Lissu aliomba muda wa mapumziko kama ilivyo katika siku zingine baada ya kufika saa saba kamili, ndipo majaji wakaja na uamuzi huo.
Lissu alikuwa akiendelea kuwasilisha hoja zake tisa za mwisho, ambapo hadi uamuzi huo unapotolewa alikuwa amefika katika hoja ya saba inayosema "kama Jamhuri ya Muungano ilitishika" kwa maneno ambayo yametumika kumshtaki Lissu. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPC), David Kafulila ameeleza kuwa utaratibu wa Ubia (PPP) unawapa wafanyabiashara na wawekezaji fursa ya kuibua na kuwasilisha mapendekezo ya miradi binafsi (unsolicited proposals) bila kulazimika kusubiri Serikali itangaze zabuni au fursa za uwekezaji.
Akizungumza leo, Ijumaa tarehe 25 Septemba, 2026, mkoani Pwani wakati wa uzinduzi wa kongamano la fursa za uwekezaji na ushiriki wa sekta binafsi katika miradi ya PPP lililoratibiwa na PPPC, Kafulila amebainisha kuwa fursa hizo zinapaswa kutumiwa kikamilifu na wafanyabiashara wa Mkoa wa Pwani kutokana na eneo hilo kuwa la kimkakati
Akiwasilisha elimu ya namna ubia unavyofanyika, Mkurugenzi Mtendaji huyo amebainisha kuwa kuna njia kuu mbili za ushiriki wa sekta binafsi; Njia ya Kawaida (Solicited Projects) ambapo Serikali inatambua na kuandaa maeneo ya uwekezaji kisha kuyatangaza sokoni ili wawekezaji na wafanyabiashara washindane kupata fursa hizo, na Njia ya Mapendekezo Binafsi (Unsolicited Projects) ambapo mwekezaji au mfanyabiashara mwenyewe anaona fursa kwenye halmashauri au mkoa, kisha anaandaa na kuwasilisha barua ya kusudio la kuwekeza moja kwa moja Serikalini bila kusubiri zabuni.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkurugenzi Mtendaji wa Chemba ya Taifa ya Biashara Tanzania (TNCC), Oscar Kissanga, ameiomba Serikali kukiwezesha Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPC) kwa kukiongezea bajeti ya fedha pamoja na kukipa mamlaka kamili ya kutoa uamuzi, ili kuondoa ucheleweshaji wa miradi ya ubia nchini.
Akizungumza leo, Septemba 25, 2026, mkoani Pwani wakati wa uzinduzi wa kongamano la fursa za uwekezaji na ushiriki wa sekta binafsi katika miradi ya PPP lililoratibiwa na PPPC, Kissanga amebainisha kuwa taratibu ndefu zinazolazimisha maamuzi zimekuwa zikifanya baadhi ya miradi kuchelewa kwa muda wa mwaka mmoja hadi miaka mitatu.
Kissanga ameeleza kuwa licha ya changamoto ya bajeti finyu inayokabili kituo hicho, kumekuwa na maendeleo makubwa katika kueneza uelewa na fursa za miradi ya PPP nchini ambazo hapo awali zilikosa kuonekana au kusikika miongoni mwa wananchi na wafanyabiashara.
Mkurugenzi Mtendaji huyo wa TNCC ameongeza kuwa sekta binafsi kupitia TNCC imeona kongamano hilo kuwa ni fursa na wakati sahihi wa kushirikiana na PPPC ili kuijenga uelewa, kuweka uthubutu, na kuhakikisha wafanyabiashara wazawa wanakuwa washiriki wakuu katika miradi ya PPP badala ya kubaki wakilalamika.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkurugenzi Mtendaji wa Chemba ya Taifa ya Biashara Tanzania (TNCC), Oscar Kissanga, ametoa pongezi kwa Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPC) kwa kuendelea kuwa kiungo muhimu katika kuunganisha Serikali na sekta binafsi, akisisitiza kuwa mfumo wa Ubia (PPP) ndio utakaoifikisha Tanzania katika uchumi wa Dola za Marekani trilioni moja kulingana na Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050.
Akizungumza leo, Septemba 25, 2026, mkoani Pwani wakati wa uzinduzi wa kongamano la fursa za uwekezaji na ushiriki wa sekta binafsi katika miradi ya PPP, kongamano lililoratibiwa na PPPC, Kissanga amebainisha kuwa kuelekea utekelezaji wa Dira ya 2050, sekta binafsi imepewa jukumu kubwa la kubeba asilimia 70 ya uchumi wa nchi.
Akifafanua ukubwa wa maono ya kiuchumi ya miaka 25 ijayo, Kissanga ameeleza kuwa ili kufikia uchumi wa Dola za Marekani trilioni moja, Tanzania inatakiwa kuipita nchi ya Afrika Kusini ambayo kwa sasa ina uchumi wa takriban Dola bilioni 400 mara tatu zaidi kimaendeleo, miundombinu, na huduma za afya.
Amebainisha kuwa ingawa lengo hilo linaonekana kuwa kubwa, linawezekana kabisa iwapo Watanzania watathubutu, wakaelimishana kupitia makongamano ya uwekezaji, na kutumia fursa za miradi ya PPP inayojumuisha sekta zote za maendeleo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkurugenzi Mtendaji wa Chemba ya Taifa ya Biashara Tanzania (TNCC), Oscar Kissanga, ametoa wito kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi, pamoja na taasisi za fedha, kushirikiana kikamilifu katika kuchangamkia fursa za miradi ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) nchini.
Akizungumza leo Ijumaa, Septemba 25, 2026, mkoani Pwani wakati wa uzinduzi wa kongamano la fursa za uwekezaji na ushiriki wa sekta binafsi katika miradi ya PPP lililoratibiwa na Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPC), Kissanga amezitaka pande hizo tatu kuchukua hatua za makusudi ili kuitumia fursa hiyo kwa maendeleo yao na uchumi wa taifa.
Akiwahutubia wawekezaji wa ndani, Kissanga amewasihi kutowazia kutafuta fursa nje ya nchi wakati fursa nyingi zipo mezani hivi sasa nchini zikihitaji kujengewa uwezo na kutumiwa kikamilifu.
"Kwanza wawekezaji wa ndani tusisubiri fursa zitafutwe nje ya Tanzania. Fursa ziko hapa ziko mezani leo. Tuzichunguze tujenge uwezo na tuzitumie; tukisita sisi nani atatufanyia au nani atakuja kuwekeza?" amesema Kissanga.
Wakati huo huo, amewakaribisha wawekezaji kutoka nje ya nchi na kuwahakikishia kuwa hawatakuwa peke yao, kwani sekta binafsi ya Tanzania ipo tayari kuwa mshiriki wa kweli na wa kuaminika katika utekelezaji wa miradi mbalimbali na kwamba TNCC ipo tayari kushirikiana nao.
Katika hatua nyingine, Mkurugenzi Mtendaji huyo ameziomba taasisi za kifedha kubuni mifumo ya kifedha inayowezesha wajasiriamali wadogo, wa kati na wakubwa kufikiwa na kukopesheka ili wasiwe waangaliaji tu bali washiriki kikamilifu katika miradi mikubwa ya kimkakati ya PPP.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI:
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, ameiambia Mahakama kwamba, kihistoria katika sheria za Tanzania hadi sasa, hakuna uhaini wa maneno, akieleza kuwa hoja ya upande wa mashtaka lengo lake lilikuwa ni "kuingiza uhaini wa maneno" ambao amesema haukuwahi kuwa sehemu ya sheria.
Lissu ameeleza hayo leo Septemba 25, 2026 alipokuwa akiendelea kutoa hoja zake za mwisho (Final Submission) katika kesi ya uhaini inayomkabili mbele ya jopo la majaji watatu wakiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru.
"Uhaini wa maneno haujawahi kuwa sehemu ya sheria zetu milele" amesema Lissu.
Akifafanua jinsi Sheria ya kosa la uhaini ilivyoanza nchini, Lissu amesema kwamba sheria hiyo ilianzia katika utawala wa Waingereza kipindi cha ukoloni na kwamba hata katika kipindi hicho hakukuwahi kuwepo kwa uhaini wa maneno pekee, akisisitiza kuwa maneno hayatengenezi uhaini bali vitendo.
Amesema wakoloni walianzisha sheria ya uhaini tangu nyakati za 1929 ikizihusu nchi ya Tanzania, Kenya na Uganda lakini ni katika nchi ya Uganda pekee ndiko kulikuwa na sheria ya uhaini wa maneno ambao kwa Tanzania na Kenya haukuwepo.
Akirejea baadhi ya maamuzi ya kesi ambazo zimewahi kufanyiwa uamuzi na mahakama, Lissu amesema "Jaji Nyalali Katika Khatibu Ghandi alisema, maneno matupu hayatengenezi uhaini. Alisema hivyo, alikuwa anajua hii sheria imetoka wapi" amesema Lissu.
Tundu Lissu amesema kwamba upande wa mashtaka kwa kuleta hoja kwamba kauli yake au maneno yake yanatengeneza uhaini, ni kwamba "wanataka kuingiza kitu katika sheria za Tanzania ambacho waingereza wenyewe walioileta sheria ya uhaini waliachana nacho miaka 176 iliyopita". -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkurugenzi Mtendaji wa Chemba ya Taifa ya Biashara Tanzania (TNCC), Oscar Kissanga, ametoa wito wa kuachana na utaratibu wa "business as usual" katika makongamano ya uwekezaji, akisisitiza kuwa mikutano hiyo lazima ilete tija, ufanisi, pamoja na mikataba halisi ya biashara kati ya Serikali na wafanyabiashara wa ndani kupitia Miradi ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP).
Kauli hiyo imetolewa leo, Septemba 25, 2026, mkoani Pwani wakati wa uzinduzi wa kongamano la fursa za uwekezaji na ushiriki wa sekta binafsi katika miradi ya PPP, lililoratibiwa na Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPC).
"Tumezoea makongamano tunakuja tunasikiliza tunapiga picha tunapiga makofi tunaondoka na mambo yanabaki pale pale. Kwa hiyo tuondoke kwenye business as usual. Leo tunasema si hivyo. Tunataka makongamano kama haya yalete tija”, ameeleza Kissanga.
Akipitia takwimu za mahitaji ya uwekezaji nchini, Kissanga amebainisha kuwa zaidi ya theluthi mbili ya mahitaji ya Mpango wa Nne wa Maendeleo wa Miaka Mitano sawa na Shilingi trilioni 334 kati ya Shilingi trilioni 477 zinatarajiwa kutoka sekta binafsi. Katika mipango ya awali, Shilingi trilioni 21.03 zilipangwa kupatikana kupitia utaratibu wa PPP kutoka kwenye mchango wa sekta binafsi uliopangwa kufikia Shilingi trilioni 40.6.
Amesisitiza kuwa TNCC imejipanga kuwa daraja la kuwavusha wafanyabiashara wa Kitanzania ili wawe wadau wakuu katika utekelezaji wa miradi hiyo mikubwa badala ya kubaki watazamaji
Kissanga ameeleza kuwa uzinduzi huo mkoani Pwani ni mwanzo wa programu inayolenga kufikia mikoa yote ya Tanzania ili kubaini miradi ya kimkakati, kuandaa muhtasari wa miradi, maandiko ya biashara (business proposals), pamoja na tafiti za uwezekano wa miradi. Mkakati huo pia unahusisha kuendesha kliniki za uwekezaji na majukwaa ya biashara kati ya wafanyabiashara na Serikali (B2G).This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Leo Septemba 25, 2026 katika Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, inaendelea kusikilizwa katika hatua ya uwasilishaji wa hoja za mwisho (final submission).
Tundu Lissu anaendelea kuwasilisha hoja hizo mbele ya jopo la majaji watatu wakiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru, ambapo katika hoja 9 ambazo aliiambia mahakama kwamba atatamatisha nazo, jana aliwasilisha hoja ya 4 na 5 ambapo pia ataendelea na hoja nyingine. -
Jambo TV
@Jambotv_
“LEO WATOTO WANGU WALALE KWA AMANI”, LISSU AKIWASILISHA HOJA ZAKE ZA MWISHO jambo.co.tz/leo-watoto-wangu-walale-kwa-amani-lissu-akiwa… via @jambotv_
-
Jambo TV
@Jambotv_
WAZIRI MAKONDA APUUZA UVUMI WA MAANDAMANO KUELEKEA AFCON, ‘NI MANENO YA MITANDAO TU’ jambo.co.tz/waziri-makonda-apuuza-uvumi-wa-maandamano-kue… via @jambotv_
-
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, John Heche, amekosoa usimamizi wa sekta ya mifugo nchini, akidai kuwa wafugaji wa Kanda ya Ziwa wametelekezwa hali inayosababisha waendelee kufuga ng'ombe wa asili wenye uzito mdogo na mavuno duni ya maziwa badala ya kupata msaada wa mbinu za kisasa za ufugaji.
Akizungumza Septemba 24, 2026, katika mkutano wa hadhara uliofanyika wilayani Bariadi mkoani Simiyu, Heche amebainisha kuwa udhaifu wa mipango ya Serikali umesababisha nchi ndogo kama Rwanda yenye eneo dogo kuliko Mkoa wa Kagera kuipiku Tanzania na kuanza kuiuzia maziwa.
Heche amesema Serikali ya Rwanda imewawezesha wananchi kwa kuwagawia maeneo ya ekari mbili, mbegu za majani ya kisasa yaliyofanyiwa utafiti wa kitalaamu pamoja na ng'ombe wa maziwa wenye mimba. Ameeleza kuwa iwapo mfumo huo ungetumika Tanzania kwa kuunganisha akina mama na vyama vya ushirika vya maziwa, mama mmoja anayepata lita 30 za maziwa kwa siku kwa bei ya TZS 1,000 kwa lita angeingiza TZS 30,000 kwa siku na TZS 900,000 kwa mwezi fedha ambazo zingeboresha elimu na mzunguko wa uchumi wa kijiji.
Aidha, Makamu Mwenyekiti huyo wa CHADEMA amesikitishwa na jinsi umasikini unavyosababisha wananchi katika mikoa ya Singida, Dodoma, na Kanda ya Ziwa kuendelea kuishi kwenye nyumba za majani, wakati nchi kama Rwanda yenye eneo dogo kuliko Mkoa wa Kagera na idadi ya watu milioni 14 imeshapiga marufuku nyumba za majani na kuwawezesha wananchi wake wote kuishi kwenye nyumba za mabati.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, John Heche, amejibu mashambulizi ya maneno yaliyotolewa na Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, Kenani Laban Kihongosi, kuhusu shughuli zake za kilimo cha parachichi, akieleza kuwa anaweza kulima kwa mafanikio kwasababu ana mtaji wa kibinafsi uliomwezesha kuwekeza kwenye kilimo hicho.
Akizungumza leo, Septemba 24, 2026, katika mkutano wa hadhara uliofanyika wilayani Bariadi mkoani Simiyu, Heche amekiri kuwa ni kweli yeye ni mkulima mkubwa wa parachichi na mfugaji mzuri. Hata hivyo, ameeleza kuwa maendeleo yake kwenye kilimo na ufugaji yanasukumwa na fursa ya mtaji aliyoipata wakati alipokuwa mbunge, fursa ambayo kijana wa kawaida wa Kitanzania hana hadi Serikali itakapowajibika.
“Anasema ooh! anawaambia vijana wa Kitanzania sijui nini! Nini! yeye analima parachichi. Ni kweli, mimi ni mkulima mkubwa wa parachichi na ni mfugaji mzuri lakini mimi nafuga vizuri na nalima vizuri kwa sababu nina mtaji", ameeleza.
Heche amebainisha kuwa badala ya viongozi wa CCM kukejeli maendeleo ya kibinafsi, wanapaswa kutambua kuwa ni wajibu wa Serikali kuweka miundombinu kama maji, matrekta, na mbegu bora ili kuwawezesha vijana na wananchi wengi kushiriki kwenye kilimo cha tija.
"Nimekuwa mbunge, nimechimba kisima shambani kwangu, kisima kirefu nimepandisha maji kwenye matenki. Parachichi zangu wakati wa jua zinamwagiliwa hazifi. Sasa wewe utalimaje? Kisima chenyewe kuchimba milioni 25 unaweza? Hiyo ni kazi ya serikali", ameeleza.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, John Heche, amebainisha kuwa matatizo ya kiuchumi na maisha magumu yanayowakabili Watanzania yanatokana na kasoro za mfumo wa katiba ya sasa na aina ya viongozi wanaowekwa madarakani.
Akizungumza leo, Septemba 24, 2026, katika mkutano wa hadhara uliofanyika wilayani Bariadi mkoani Simiyu, Heche amesema kupatikana kwa Katiba Mpya yenye misingi ya Rasimu iliyoandikwa na Tume ya Jaji Joseph Warioba ndiyo njia pekee itakayorejesha mamlaka ya kweli kwa wananchi na kubadilisha mfumo wa uchumi unaotajirisha watu wachache huku wengi wakiumia.
Heche ameeleza kuwa Watanzania waliweka vifungu vilivyomtaka mbunge kuwa mwakilishi halisi wa wananchi anayekwenda bungeni kusimamia kero zao na sio matakwa ya serikali.
Amebainisha kuwa tofauti na katiba ya sasa ambapo mwananchi hana mamlaka ya kumuwajibisha mbunge mara baada ya kuchaguliwa, Rasimu ya Warioba ilitoa haki kwa wananchi kumvua ubunge mwakilishi wao kabla ya miaka mitano kuisha iwapo atashindwa kuwasilisha hoja zao au akitekeleza majukumu yake kwa kutelekeza jimbo.
"Leo iko hivi, unachagua mbunge... akienda bungeni kinachoweza kumuondoa bungeni labda afe au chama chake kimfukuze. Lakini mwananchi unayemweka huna mamlaka naye. Warioba akaona huo ni ujinga, akasema mbunge asiposimamia hoja za wananchi, wananchi mnayo haki ya kumuondoa bungeni kabla ya miaka mitano ya uchaguzi haijaisha... Kama mbunge mmemchagua anaishi Bariadi, akihama kutoka Bariadi akahamia Dar es Salaam ikapita miezi sita hajarudi kuzungumza na nyie, mnamfukuza ubunge mnachagua mbunge mwingine", ameeleza Heche.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, John Heche, amekosoa vikali taratibu za uchaguzi na demokrasia ya ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), akidai kuwa chama hicho kilivunja kanuni zake wenyewe wakati wa kupitisha viongozi na mgombea wake wa Urais wa Tanzania katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.
Akizungumza leo, Septemba 24, 2026, katika mkutano wa hadhara uliofanyika wilayani Bariadi mkoani Simiyu, Heche ameeleza kuwa CHADEMA iliweka msimamo wa kutoshiriki katika mchakato ambao hata ndani ya CCM yenyewe kanuni zake zilikiukwa
Heche amebainisha kuwa katika kikao cha mkutano mkuu wa chama hicho, ajenda ilibadilishwa ghafla bila kufuata taratibu za kuchukua fomu, kujaza fomu, wala kusaka wadhamini, na badala yake viongozi walipitishwa kwa kuinua tu mikono
"Wanataka kumpitisha Wasira kama Makamu Mwenyekiti kama mimi, eti Wasira naye wanamlinganisha na mimi, ndugu zangu hebu oneni hizi dharau wanazotuletea hawa jamaa. Sasa ajenda ya mkutano mkuu ilikuwa ni tofauti... Wakaigeuza, mtu akanyanyua mkono akasema mimi naomba tumpitishe Rais moja kwa moja".
Hata hivyo, viongozi wakuu wa chama hicho akiwamo aliyekuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla walijibu kuwa chama hicho hakikubadili gia angani kwa kuwateua wagombea urais mapema kuelekea uchaguzi wa mwaka huo kwani uamuzi uteuzi wao ulichochewa na shinikizo la wajumbe wa mkutano mkuu wa chama hicho, baada ya kuridhishwa na namna makada hao walivyotekeleza ilani.
Akisisitiza msimamo na madai makuu ya CHADEMA mbele ya wananchi wa Bariadi, Heche amebainisha kuwa chama hicho kina mambo mawili makuu kinachoyapigania kwa sasa, ikiwemo kutaka Mwenyekiti wake wa chama taifa, Tundu Lissu kuachiwa huru.
"Sisi CHADEMA tukasema hatuwezi kwenda kwenye huo uchaguzi ambao hata kuanzia ndani ya CCM yenyewe kanuni zao zimevunjwa... Ndio maana tunakuja kwenu sasa tunasema mambo mambo yetu ni mangapi? Mawili. Moja, tunataka mwenyekiti wetu aachiwe awe huru kwa sababu hana kosa kwa kudai katiba. Jambo la pili, tunataka Katiba Mpya", ameeleza Heche.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI:
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu ameiambia mahakama kwamba mawakili wa Jamhuri hawakumhoji nia ya maneno yake yaliyotumika kumshtaki wakati akiendelea kujitetea katika kesi ya uhaini inayomkabili.
Lissu ameeleza hayo leo Septemba 24, 2026 alipokuwa akiendelea kuwasilisha hoja za mwisho (final submission), kutokana na kesi ya uhaini inayomkabili, akibainisha kuwa ushahidi wa utetezi katika hoja hiyo ulikuwa mrahisi, ulionyooka na wenye mwendelezo mzuri tangu mwanzo hadi mwisho.
"Nilishughulikiwa kwelikweli kwenye kizimba cha ushahidi, nilikaliwa kooni kweli kweli lakini naomba muangalie kwenye rekodi kama ushahidi wangu juu ya kusema maneno hayo umehojiwa hata mara moja," amesema Lissu akisisitiza namna ambavyo upande wa mashtaka ulikwepa kugusa kiini cha nia yake.
Akizungumzia maneno yaliyoletwa mahakamani, amesema katika mjadala huo hakuirejea Serikali wala kusema walichodhamiria kufanya kwa Serikali, huku akiongeza kuwa hajaona hata eneo moja ambalo mawakili wa serikali walimhoji juu ya nia aliyokuwa nayo wakati anatoa kauli hizo.
Akirejea kesi kadhaa, Lissu amesema upande wa mashtaka kwa kushindwa kumhoji kuhusu nia ya mkutano na nia ya maneno yake hawawezi kusema nia hiyo wameikataa bali wameikubali, akidai kuwa kushindwa kudodosa juu ya jambo maana yake umelikubali kisheria.
"Sijaona hata eneo moja ambalo Mawakili wa Serikali walionihoji juu ya nia niliyokuwa nayo wameniuliza mambo elfu mia moja, lakini juu ya nia yangu hawakuhoji dodoso na kushindwa kudodosa jambo maana yake umelikubali," ameeleza Lissu mbele ya majaji.
Amesema katika mkutano huo walilenga kuwaeleza watia nia juu ya azimio la Chama lililoazimiwa Bagamoyo la "No reform no election" kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025.
Pia, ameeleza kuwa msimamo huo ulishikiliwa na DW3 Amani Golugwa, DW4 Brenda Jonas Rupia na DW5 John Wegesa Heche, na kwamba ushahidi huo wa mashahidi wa utetezi ulishambuliwa sana na Jeshi la mawakili wa Serikali, lakini kwenye swali la nia ushahidi wao uliachwa kama ulivyo.
"Hata walipowashambulia mashahidi wangu kama DW3 Amani Golugwa, DW4 Brenda Jonas Rupia na DW5 John Wegesa Heche, kwenye swali la nia ushahidi wao uliachwa kama ulivyo kwa sababu walishindwa kabisa kupinga ukweli huo," aliongeza Lissu. -
Jambo TV
@Jambotv_
Serikali ya Tanzania imelipa Dola za Marekani milioni 32 (sawa na takriban Shilingi bilioni 74 za Kitanzania) ili kuipatia nchi uhalali wa kuwa mwenyeji wa Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) kwa mwaka 2027.
Hatua hiyo imebainishwa leo, Septemba 24, 2026, na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Christian Makonda, wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu uwekezaji mkubwa unaofanywa na Serikali katika sekta ya michezo na usimamizi wa nembo za taifa.
Waziri Makonda ameeleza kuwa mbali na kitita hicho cha Dola milioni 32 cha uenyeji, Serikali pia ipo katika mazungumzo na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) ili kulipa Dola za Marekani milioni 12 (takriban Shilingi bilioni 30) kwa ajili ya kupata haki za matangazo ya televisheni (broadcast rights) ya mashindano hayo.
Amefafanua kuwa fedha hizo si za ujenzi wa viwanja au miundombinu ya barabara, bali ni uwekezaji wa kimkakati wa kuitangaza Tanzania duniani, kukuza utalii, na kutengeneza fursa za ajira kwa vijana
"Tumelipa sisi taifa kuwa wenyeji wa AFCON milioni 32... Sawa na bilioni takriban 74. Hii ni pesa ya kuwa tu mwenyeji. Lakini pia tunazungumza na CAF tunatakiwa tulipe dola milioni 12 ya kupata haki za matangazo. Hizi fedha sio za kujenga uwanja, sio za kununua maji, sio za kufanya kujenga barabara. Kama nchi tumelipa ili tupate uhalali wa kuhosti haya mashindano. Namba mbili tupate uhalali wa kuitangaza taifa letu kupitia mashindano ili watakaokuja waje wakiona Tanzania ni sehemu sahihi ya kuwekeza, vijana wengi wapate ajira”, ameeleza Makonda.
Waziri Makonda amesisitiza kuwa kutokana na Serikali kuwekeza mabilioni hayo ya fedha, jezi ya Timu ya Taifa (Taifa Stars) ni vazi kuu linalotambulisha nchi na nembo inayopaswa kuongezewa thamani kubwa ya kimasoko badala ya kuchukuliwa kwa wepesi au kutangazwa bila uratibu rasmi. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Wananchi wa Kijiji cha Machemba, Wilaya ya Tunduru, wameiomba Serikali kuwapatia vyanzo salama vya maji baada ya kueleza kuwa wanategemea kisima ambacho, kwa mujibu wao, hakikidhi viwango vya usalama kwa matumizi ya kila siku.
Ombi hilo limetolewa baada ya Mbunge wa Tunduru Kaskazini, Ado Shaibu Ado, kumaliza kuzungumza na wananchi hao katika ziara yake ya Kijiji kwa Kijiji, ambapo wananchi waliongozana naye hadi kwenye kisima wanachokitumia kwa shughuli zao za kila siku.
Wananchi hao wamemweleza Ado kuwa hali ya kisima hicho ni changamoto, huku wakidai kuwa matumizi ya maji hayo wakati mwingine yamekuwa yakisababisha matatizo ya kiafya.
“Hayo ndo maji tunayokunywa tuna visima vitatu hali yake ndo hiyo na tukinywa haya maji muda mwengine tunaharisha”
Akijibu kilio hicho, Mbunge Ado ameahidi kulifikisha suala hilo kwa Waziri mwenye dhamana ya Maji, Jumaa Aweso kwa lengo la kutafuta suluhisho la changamoto hiyo na kuwawezesha wananchi kupata maji safi na salama.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI:
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, ameiambia mahakama kwamba kesi ya uhaini dhidi yake imejengwa katika msingi wa hisia na haina ushahidi thabiti unaokubalika kisheria ili kuthibitisha kama kulikuwa na nia ya kutenda kosa la kihaini.
Lissu amesema hayo leo Septemba 24, 2026, alipokuwa akiendelea kufanya uwasilishaji wa hoja za mwisho (final submission) mbele ya jopo la majaji watatu wakiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru, ambo wanasikiliza kesi hiyo katika Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Dar es Salaam.
"Walionishtaki wanataka kunihukumu kifo kwa sababu ya hisia zao, kwa sababu wanahisi nilikuwa nataka kuitishia Serikali." Amesema Lissu.
Lissu ameongeza zaidi kwamba, upande wa mashtaka na mawakili wamerudia madai ya kosa la uhaini kwa kisingizio kuwa uchaguzi unafanywa kwa mujibu wa katiba na Serikali ndiyo inasimamia katiba, huku akihoji kama serikali ndiyo chombo pekee kinachosimamia katiba wakati zipo sheria zinazosimamiwa na mihimili mingine kama vile Mahakama na Bunge, na akihoji pia kama Tume ya Uchaguzi ni serikali.
Aidha, amesema kuwa kujenga kesi nzito kama ya uhaini ambayo ni kosa pekee lililotajwa katika Katiba ya Tanzania kwa kutumia hisia tupu hakuwezi kuwa msingi halali wa kumtia mtu hatiani.
"Hii si kesi ya mauaji ni kesi ya uhaini na ni kosa pekee ambalo limetajwa katika katiba ya Tanzania, na kuhisi tu huyu mtu anailenga serikali hata kama huyu mtu ana hisia hizo kiasi gani haziwezi kuwa msingi wa kumtia mtu hatiani." Ameongeza Lissu.
Akieleza zaidi kuhusu misingi ya kisheria, amesisitiza kuwa mahakama haiwezi ikawakubalia upande wa mashtaka na akawaomba majaji kutoitikia wito wa mashtaka hayo ambayo amesema yamejengwa kwa hisia za walioshtaki badala ya ushahidi thabiti wa kisheria. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Ndugu Aggrey Mwanri, amekemea vikali vitendo vya rushwa ndani ya chama, akisisitiza kuwa hakuna mwanachama au kiongozi atakayevumiliwa endapo atatumia fedha au njia nyingine zisizo halali katika kuwania nafasi za uongozi.
Mwanri ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na Wananchi na wanachama wa CCM katika mkutano wa hadhara uliofanyika Viwanja vya CCM Sanya Juu, Wilaya ya Siha, mkoani Kilimanjaro, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi mkoani humo.
Katika mkutano huo, Mwanri ameonya dhidi ya vitendo vya rushwa vinavyoweza kujitokeza kuelekea uchaguzi wa ndani wa CCM, akieleza kuwa chama hakitakubali mtu kutumia fedha au mbinu nyingine zisizo za kimaadili kujitengenezea mazingira ya ushindi.
Aidha, amesisitiza kuwa hatua zitachukuliwa dhidi ya mtu yeyote atakayeanza kuonyesha dalili za kutengeneza safu au makundi kwa lengo la kuathiri mchakato wa uchaguzi wa ndani wa chama.
Katika hatua nyingine, Mwanri amemuagiza Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, Ndugu Patrick Boiysafi, kuhakikisha anafanya vikao na viongozi na wanachama katika ngazi mbalimbali za chama ili kukemea kwa nguvu zote vitendo vya rushwa na mienendo inayoweza kuhatarisha uchaguzi wa ndani wa chama.
Kauli hiyo inaendana na msimamo wa CCM kuhusu mapambano dhidi ya rushwa katika uchaguzi wa ndani, ambapo nyaraka za chama zinaelekeza kuchukuliwa hatua dhidi ya wanaobainika kujihusisha na utoaji wa rushwa kwa mujibu wa kanuni za chama na sheria za nchi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Leo Septemba 24, 2026 Mwenyekiti wa @ChademaTZ2 Tundu Lissu ambaye anakabiliwa na kesi ya uhaini ataendelea kuwasilisha hoja zake za mwisho(Final Submissions) katika Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Dar es Salaam mbele ya Jopo la Majaji watatu wakiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru.
Jana Septemba 23, 2026 alianza kuwasilisha hoja hizo ambapo kufikia saa 11 jioni alikuwa ameeleza mahakama mambo matatu kati ya tisa ambayo anaona ni muhimu yakaamuliwa kutokana na mkanganyiko wake.
Katika hoja zake Lissu aliieleza Mahakama kuwa yeye hakuitisha mkutano alioongea na watia nia uliofanyika April 3, 2025, pia si yeye aliyeita waandishi wa habari na kuwa kesi hiyo ya uhaini inayomkabili haikufunguliwa kwa mujibu wa sheria akifafanua mkanganyiko huo ambao anaendelea kuufafanua asubuhi hii.
Akimaliza kuwasilisha hoja zake za mwisho upande wa jamhuri pia utapata nafasi ya kufanya hivyo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Wananchi wa Kijiji cha Kidodoma, Tunduru, wamemtaka Katibu wa ACT Wazalendo na Mbunge wa Tunduru Kaskazini, Ado Shaibu Ado, kuendeleza kasi ya kuwasemea Wananchi na makundi mbalimbali, hususan katika masuala ya haki, utekaji na changamoto zinazowakabili wananchi.
Wamesema hayo jana Septemba 23, 2026, wakati Ado Shaibu kiendelea na ziara yake ya kijiji kwa kijiji katika Jimbo la Tunduru Kaskazini, yenye lengo la kusikiliza changamoto za Wananchi na kuzifikisha katika maeneo husika, ikiwemo Bunge.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Watu 25 wamekamatwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma kwa tuhuma za kuhusika na mauaji na vurugu zinazodaiwa kuchochewa na mgogoro kati ya wakulima na wafugaji wilayani Tunduru.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, SACP Marco G. Chilya, amesema watu watatu wameuawa na wengine wawili kujeruhiwa, huku mali mbalimbali zikiharibiwa, ikiwemo kuchomwa kwa ofisi za Serikali na kuharibiwa kwa gari la Polisi.
Amesema kati ya waliokamatwa, wanane wanahusishwa na mauaji na 17 na vurugu, huku 15 wakiwa wakulima na 10 wafugaji. Polisi wanaendelea na operesheni kuwabaini na kuwakamata watuhumiwa wengine.
Matukio hayo yalianza Septemba 17, 2026, baada ya mfugaji Shimbi Upole Shimbi kudaiwa kupoteza ng’ombe 180. Baadaye ng’ombe 179 walipatikana, huku mchungaji wao, Msanja Shimbi Upole, akikutwa ameuawa na mwili wake kuzamishwa kwenye matope katika Mto Chermambo, Kijiji cha Chinunje.
Baada ya tukio hilo, wafugaji walivamia Vijiji vya Chikomo na Chinunje, ambako Mohamed Kasim Chabwela aliuawa na watu wawili, Yusuph Yasin Bakili na Rashid Ally Ahmad, kujeruhiwa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Leo Septemba 24, 2026, Kiongozi wa Chama Mstaafu wa ACT Wazalendo @ACTwazalendo , Zitto Kabwe @zittokabwe , ametimiza umri wa miaka 50 na kuweka wazi mambo makubwa matano anayojivunia katika maisha yake, huku pia akieleza ndoto zake ambazo hajafanikiwa kuzitimiza bado, ikiwemo nia yake ya zamani ya kuwa Rais wa Tanzania akiwa na umri mdogo pamoja na kuwa mwalimu wa chuo kikuu.
Zitto ameyabainisha hayo katika mahojiano maalum na Jambo TV, ambapo alitathmini safari yake ya maisha, familia, siasa, na uwakilishi wa wananchi.
Akizungumzia mafanikio anayojivunia zaidi, Zitto ameeleza kuwa jambo la kwanza ni kutoka katika familia ya kawaida mkoani Kigoma hadi kufikia alipo sasa na kupata familia yake mwenyewe. Pili, ametaja safari yake ndefu ya kisiasa ikiwamo kuhudumu kama Mbunge kwa miaka 15, kushiriki harakati za mwanzo za mageuzi kupitia CHADEMA, na baadaye kuasisi chama cha ACT Wazalendo. Jambo la tatu ni mchango wake bungeni katika kusimamia uwajibikaji, pamoja na mabadiliko ya sheria za madini na fedha zilizosaidia kuziba mianya ya ukwepaji kodi. Nne, ametaja uamuzi wa aliyekuwa Mwenyekiti wa ACT Wazalendo, Marehemu Maalim Seif Sharif Hamad, kujiunga na chama hicho mwaka 2019 na baraka za kushiriki kumzika kiongozi huyo. Jambo la tano ni kazi aliyoifanya mkoani Kigoma ya kurejesha ufahari na pride kwa wananchi wa eneo hilo kupitia uwakilishi na Sanaa.
Mbali na mafanikio hayo, Zitto ameanika mambo ambayo alitamani kuyatimiza kabla ya kufikisha umri wa miaka 50 lakini hakufanikiwa. Amebainisha kuwa alikuwa na ndoto ya kuwa Rais wa Tanzania akiwa na umri mdogo, kiasi cha kupambana kutaka katiba ibadilishwe ili umri wa kugombea uraisi ushuke kutoka miaka 40 hadi 35. Pia ameeleza hamu yake ya muda mrefu ya kuwa mwalimu wa chuo kikuu baada ya kustaafu siasa.
Jambo TV inamtakia umri mrefu, afya tele na kila lililo la heri Zitto katika maisha yake.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI:
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limemtoza msanii Rajab Abdul Kahali ‘Harmonize’ faini ya Sh milioni tano kwa tuhuma za kusambaza video ya wimbo wake wa Kudos, ambayo limeeleza kuwa inakiuka maadili ya Mtanzania.
Kwa mujibu wa BASATA, Harmonize hakuwasilisha utetezi wala maelezo mbadala kuhusu tuhuma hizo hadi wakati wa kutolewa kwa uamuzi.
Mbali na faini hiyo, BASATA imemuamuru kushusha video hiyo kwenye mitandao yake ya kijamii na kusitisha shughuli zote za sanaa hadi atakapotekeleza maamuzi hayo.
Muongoza video hiyo, Kennedy David Sanga ‘Dir. Kenny’, naye ameamriwa kulipa faini ya Sh milioni tano, kushusha video hiyo kwenye mitandao yake na kusitisha shughuli za sanaa hadi atakapotekeleza uamuzi huo.
Wakati huo huo, msanii Faustina Charles Mfinanga ‘Nandy’ ametozwa faini ya Sh milioni tatu baada ya kukiri kosa la kuvaa mavazi ambayo BASATA imesema hayakuwa na staha wakati akitumbuiza katika fainali ya Miss Universe Tanzania 2026.
BASATA imesema Nandy tayari ameshusha video hiyo kwenye mitandao yake na kulipa faini, hivyo ameruhusiwa kuendelea na shughuli zake za sanaa chini ya uangalizi.
Katika taarifa hiyo, BASATA imewataka Wasanii na wadau wa sanaa kuzingatia sheria, kanuni, miongozo na maadili ya Mtanzania wanapotekeleza shughuli zao. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katibu wa ACT Wazalendo na Mbunge wa Tunduru Kaskazini, Ado Shaibu Ado, ameitaka Serikali kuchukua hatua za haraka kutatua mgogoro kati ya wakulima na wafugaji katika maeneo ya jimbo hilo, akisema hali hiyo inaweza kuleta madhara makubwa ikiwa haitadhibitiwa.
Ado ametoa kauli hiyo leo, Septemba 23, 2026, katika Kijiji cha Machemba, alipokuwa akiendelea na ziara ya kutembelea vijiji mbalimbali na kusikiliza kero za wananchi.
Wananchi wa Machemba wamemtaka mbunge huyo kufikisha Bungeni kilio chao kuhusu mgogoro huo, huku Ado akisema amewahi kulifikisha suala hilo kwa Waziri Mkuu, Mwigulu Nchemba, mara kadhaa bila kuridhishwa na majibu aliyopata.
Ametaka Serikali kulivalia njuga suala hilo na kuchukua hatua mapema ili kuzuia mgogoro kati ya wakulima na wafugaji kuendelea kukua na kuhatarisha amani katika maeneo ya Tunduru.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga, amevitaka viwanda vinavyozalisha bidhaa kwa utoshelevu nchini kuhakikisha vinapewa kipaumbele katika soko la ndani, huku akiwataka wafanyabiashara wazawa kuamini na kutumia bidhaa zinazozalishwa na wazawa wenzao.
Kapinga ameyasema hayo leo, Septemba 23, 2026, jijini Dar es Salaam, wakati akizindua kiwanda cha kutengeneza vizibo vya chupa cha Simama Metal Crown, kilichopo Wilaya ya Kigamboni na kinachomilikiwa kwa asilimia 100 na mwekezaji mzawa.
Amesema matumizi ya bidhaa zinazozalishwa nchini ni sehemu muhimu ya kukuza viwanda vya ndani, kuongeza uzalishaji na kupunguza utegemezi wa bidhaa kutoka nje.
“Bilioni 14 zilizowekezwa kwenye kiwanda hiki ni sehemu ya juhudi za kuongeza uzalishaji wa bidhaa nchini na kupunguza utegemezi wa bidhaa kutoka nje,” amesema Kapinga.
Aidha, amezitaka taasisi za sekta binafsi, ikiwemo CTI, TPSF na TNBC, kuhakikisha zinaendelea kusimamia na kuwakumbusha wamiliki wa viwanda misingi ya uendelevu wa sekta hiyo.
Kapinga amesema Serikali itaendelea kuhimiza uwekezaji wa wazawa na kuweka mazingira wezeshi kwa wafanyabiashara na wawekezaji ili kuongeza uzalishaji wa bidhaa zinazokidhi mahitaji ya soko la ndani na nje.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Simama Tanzania, Norbert Simama, amesema kiwanda hicho kina uwezo wa kuzalisha vizibo milioni 130 kwa mwezi kwa ajili ya matumizi ya viwanda vya vinywaji, huku akisisitiza kuwa bidhaa hizo zinakidhi viwango vya ubora na zina uwezo wa kushindana katika soko la kimataifa.
Simama amevitaka viwanda vya vinywaji kushirikiana na kiwanda hicho kwa kutumia bidhaa zinazozalishwa nchini, akisema ubora wa bidhaa za ndani ni muhimu katika kuongeza ushindani na kuimarisha soko la ndani.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Tanzania imesema tafiti za bahari ni muhimu katika kubaini fursa zilizopo kwenye Uchumi wa Bluu, kuimarisha uvuvi endelevu na kulinda ikolojia ya bahari.
Kauli hiyo imetolewa leo, Septemba 23, 2026, jijini Dar es Salaam na Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Latifa Khamis, wakati wa ziara ya kukagua meli ya utafiti ya Dr. Fridtjof Nansen, inayofanya tafiti za rasilimali za bahari katika nchi mbalimbali za Afrika.
Akizungumza katika tukio hilo, Dkt. Latifa amesema Tanzania inaendelea kutambua umuhimu wa bahari na fursa zinazopatikana kupitia tafiti za kisayansi, ikiwemo katika uvuvi, mazingira na Uchumi wa Bluu.
Amesema ushiriki wa watafiti na wanafunzi wa Tanzania katika programu hiyo ni fursa ya kuongeza ujuzi, kubadilishana uzoefu na wataalamu kutoka nchi mbalimbali za Afrika na kutumia matokeo ya tafiti katika kupanga sera na mikakati ya maendeleo.
Kwa upande wake, Balozi wa Norway nchini Tanzania, Tone Tinnes, amesema meli ya Dr. Fridtjof Nansen imekuwa ikitumika kwa zaidi ya miaka 50 kufanya tafiti katika maeneo mbalimbali ya bahari, ikiwemo kukusanya sampuli na kuchunguza hali ya rasilimali za samaki.
Amesema kwa sasa tafiti hizo pia zinahusisha uchunguzi wa uchafuzi wa bahari, ikiwemo plastiki na microplastics, huku matokeo yakisaidia nchi kutumia sayansi katika kupanga sera zinazohusu rasilimali za bahari.
Naye Doreen Oromi kutoka Plan International Tanzania amehimiza Serikali na wadau wa maendeleo kuendelea kuwahusisha wasichana katika tafiti, ubunifu na fursa za kiuchumi zinazotokana na bahari.
Amesema bahari ina fursa nyingi ambazo wanawake na wasichana wanaweza kuzitumia katika ujasiriamali na maeneo mengine ya maendeleo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Wanafamilia watano wa familia ya Mushi na Mongi, akiwemo bibi mwenye umri wa miaka 86, wameachiwa huru leo, Jumanne, Septemba 23, 2026 saa 5 asubuhi baada ya kushikiliwa rumande kwa siku mbili katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay kutokana na agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila.
Wakizungumza na waandishi wa habari baada ya kuachiwa huru, mmoja wa wanafamilia hao, Mariamu Mongi (86), alikanusha taarifa zilizodai kuwa walikaidi wito wa Mkuu wa Mkoa wakati wa ziara yake kwenye eneo lenye mgogoro lililoko Madale Mtaa wa Scout, Wilaya ya Kinondoni, mnamo Septemba 19, 2026.
"Inadaiwa kwamba tulitaarifiwa kuhusu ziara ya Mhe. Mkuu wa Mkoa. Si kweli. Hatukupata taarifa yoyote rasmi, wito wa aina yoyote, wala kujulishwa kuwa Mkuu wa Mkoa angetembelea eneo letu ambalo tumerejeshewa na Mahakama," amesema Mariamu.
Aidha, familia hiyo imemwomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuingilia kati na kuliangalia suala hilo ili kuwasaidia kulinda haki yao ya ardhi, wakieleza kuwa waliinunua kihalali tangu mwaka 1994 na kushinda kesi ya miaka 16 mahakamani.
Kukamatwa kwa wanafamilia hao kulitokana na agizo la RC Chalamila, kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Mtatiro Kitinkwi, akidai kuwa familia hiyo ilikaidi wito wake wa kufika kwenye eneo hilo la mgogoro. RC Chalamila alieleza kuwa lengo la kuwaita lilikuwa ni kufanya nao mazungumzo baada ya familia hiyo kuchukua hatua mnamo Septemba 3, 2026, ya kuzitoa na kuzizuia kuingia ndani ya nyumba kaya zaidi ya 20 zilizokuwa zikiishi hapo, ambazo nazo zinadai kununua viwanja hivyo kupitia serikali ya mtaa. Hata hivyo, Chalamila alieleza kuwa kutopokea simu na kutosikiliza wito wake kuliashiria dharau kwa mamlaka.
Kwa upande wake, Mwanasheria wa familia hiyo, Wilson Ogunde hapo jana alieleza kuwa wanafamilia hawakukaidi kwa makusudi, bali walijitokeza kwa hiari kuripoti mara tu walipopata taarifa za agizo hilo kupitia mitandao ya kijamii, ndipo watano kati yao waliposhikiliwa hadi walipoachiwa huru leo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katika mwendelezo wa mawasilisho ya mwisho (final submissions) katika kesi ya uhaini namba 19605/2025 inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Antiphas Lissu, Lissu ameeleza jinsi upande wa mashtaka (Jamhuri) ulivyojichanganya na kuleta mashahidi wenye kauli zinazokinzana kuhusu nani aliyealika waandishi wa habari katika mkutano wa Aprili 3, 2025.
Akiwasilisha uchambuzi wake wa kisheria mbele ya jopo la majaji watatu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam wakiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru, Lissu amesisitiza kuwa mgongano huo mkubwa kati ya mashahidi wa serikali unayafanya maelezo yote ya Jamhuri juu ya suala hilo kuwa "ushahidi usiokuwa na thamani yoyote".
Katika taarifa ya ziada iliyowasilishwa na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) wakati wa usikilizaji wa awali (preliminary hearing - ukurasa wa 131 wa rekodi za mahakama), Jamhuri ilidai kuwa Tundu Lissu ndiye aliyealika waandishi wa habari kutoka vyombo vya habari kama Jambo TV, Clouds Media, na Mwananchi katika mkutano wa watia nia Makao Makuu ya CHADEMA Mikocheni.
Lissu amefafanua kuwa tuhuma hii haikuwa ya bahati mbaya, bali ilipangwa kimkakati ili kuthibitisha kile kinachoitwa "tendo la wazi" (overt act) la kisheria linalohitajika ili kuthibitisha kosa la uhaini. Amesema kisheria ikiwa mtuhumiwa ndiye aliyealika waandishi wa habari ili hotuba yake irushwe, kitendo hicho kingetumiwa kama thibitisho la nia ya kihaini. Zaidi ya hayo, kingewafanya waandishi wa habari waliohudhuria au kurusha matangazo hayo kuchukuliwa kama washirika walioingia kwenye kosa la kuchepusha, kuwezesha au kunyamazia uhaini (misprision of treason) linalobeba adhabu ya kifungo cha maisha gerezani.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu wa Rais wa Tanzania, Deogratius Ndejembi, akipita katika mitaa tofauti ya jiji la New York nchini Marekani wakati akielekea kwenye mkutano wa 81 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) unaoendelea nchini Marekani ambako amemuwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Wananchi wa Mkoa wa Rukwa wanatarajiwa kuanza kunufaika na huduma ya umeme wa uhakika pale Mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme wa Msongo wa Kilovoti 400 wa Iringa–Kisada–Mbeya–Tunduma–Sumbawanga (TAZA) utakapokamilika.
Hatua hiyo itakayochochea maendeleo ya kiuchumi, uwekezaji na utoaji wa huduma bora za kijamii katika mkoa huo na kuchochea kukua kwa shuguli za kiuchumi.
Akizungumza Septemba 23, 2026 wakati wa kikao na wakandarasi wa mradi huo, Bw. Twange amewataka wakandarasi hao kuhakikisha unakamilika ifikapo Novemba 15, 2026 ili wananchi waanze kupata manufaa yaliyokusudiwa.
“Huu ni mradi mkubwa wa kimkakati wenye urefu wa kilomita 616 na gharama ya takribani Shilingi trilioni 2. Tunamshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji huu mkubwa katika sekta ya nishati. Kukamilika kwa mradi huu kutawapatia wananchi wa Rukwa umeme wa uhakika na kufungua fursa mpya za maendeleo ya kiuchumi,” amesema Bw. Twange.
Amesema kuwa mpaka sasa mradi huo umefikia asilimia 96.57 ya utekelezaji wake na utakapokamilika utaongeza uwezo wa Gridi ya Taifa kusafirisha umeme, kupunguza changamoto za upatikanaji wa umeme katika maeneo ya Kusini Magharibi mwa Tanzania na kuweka mazingira bora ya uwekezaji katika sekta za viwanda, madini, biashara na kilimo.
Kwa wananchi wa Rukwa, mradi huo unatarajiwa kuongeza upatikanaji wa huduma bora katika hospitali, shule na taasisi nyingine za kijamii zinazotegemea umeme, huku ukiimarisha shughuli za uzalishaji mali na ajira kupitia uwekezaji unaotegemea nishati ya uhakika.
Aidha, Bw. Twange amesema mradi huo una umuhimu wa kikanda kwani utakamilisha maandalizi ya kuunganisha mifumo ya umeme ya Tanzania na Zambia, hatua itakayowezesha biashara ya umeme kati ya nchi hizo mbili na kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi ndani ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC). -
Jambo TV
@Jambotv_
MASHAHIDI WA JAMHURI KUPISHANA KAMA LISSU ALIALIKA WANAHABARI: “NI USHAHIDI USIOKUWA NA THAMANI YOYOTE” jambo.co.tz/mashahidi-wa-jamhuri-kupishana-kama-lissu-ali… via @jambotv_
-
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkuu wa Wilaya ya Serengeti mkoani Mara, Angelina Marco, ametoa wiki moja kwa kaya 100 za wakulima na wafugaji wanaoishi kando ya mto mara katika kijiji cha Iselesele kuondoka mara moja katika eneo hilo, huku wananchi wakiiomba Serikali kutumia nguvu itakapobidi kuwaondoa watakaokaidi ili kuepusha madhara ikiwemo vifo pindi mvua za El Nino zikapoanza kunyesha.
Marco ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wananchi hao Septemba 22, 2026 ambapo amesisitiza kuwa kwa muda mrefu maeneo hayo yamekuwa yakituama maji nyakati za mvua.
Pia amewatoa hofu wananchi hao kuwa hakuna mwananchi atanyang’anywa eneo lake badala yake pindi mvua hizo zitakaposimama watarejea na shughuli zao za kawaida kwenye maeneo hayo.
“Ninyi wenyewe nimashahidi hili eneo huwa nihatarishi ikinyesha mvua kidogo tu, shughuli mnaijuwa, niwatake sasa kaya 100 zilizoko katika bonde hil kupisha mara mmoja katika eneo hilo na kwenda katika maeneo salama. Hatutaki na wala hatutarajii kupoteza mwananchi katika eneo hilo hatuko tayari ondokeni”. Amsema DC Marco.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katika mwendelezo wa mawasilisho yake ya mwisho (final submissions) kwenye kesi ya uhaini namba 19605/2025 inayosikilizwa mbele jopo la majaji watatu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam., mshitakiwa Tundu Antiphas Lissu ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, ameiomba mahakama kuamua masuala tisa (9) makuu ya kisheria na kiushahidi ambayo kulingana naye, yanathibitisha kuwa kesi hiyo ya Jamhuri haina msingi wowote na inapaswa kutupiliwa mbali.
Masuala hayo ambayo Mahakama Kuu imetakiwa kuyatolea uamuzi katika hukumu yake ya mwisho ni ama mshtakiwa aliitisha mkutano wa Aprili 3, 2025 Makao Makuu ya CHADEMA Mikocheni kama inavyodaiwa na upande wa mashtaka, kama Lissu ndiye aliyealika waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari kuhudhuria mkutano huo, kama mshtakiwa amefanya au ametengeneza nia yoyote ya kumchochea mtu au kikundi cha watu kuzuia uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 kwa lengo la kuitishia Serikali, kama maneno yanayodaiwa kutolewa na mshtakiwa yanatengeneza kosa lolote linalojulikana na sheria za Tanzania, na kama jibu ni ndiyo, je kosa hilo ni la uhaini? Kama maneno yanayodaiwa kuzungumzwa na Lissu yanatengeneza matendo (overt acts), au ikiwa kutamka maneno pekee bila matendo halisi kunaweza kuwa uhaini.
Masuala mengine ni kama mshtakiwa ndiye aliyechapisha maneno hayo kwenye akaunti ya YouTube ya Jambo TV au mitandao mingine, kama Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilitishwa na maneno yanayodaiwa kuwa ya kihaini yaliyozungumzwa na mshtakiwa, kama upande wa mashtaka (Jamhuri) umethibitisha kesi hii katika kiwango kinachohitajika na sheria (beyond reasonable doubt) na ni hukumu au uamuzi gani sahihi ambao Mahakama inatakiwa kutoa kulingana na majibu ya masuala yote nane yaliyotangulia.
Akiingia kwenye uchambuzi wa kina wa masuala hayo, Lissu amekumbusha kuwa katika ukurasa wa 131 wa rekodi za mahakama, upande wa mashtaka ulidai kuwa mnamo Aprili 3, 2025, Lissu kwa nafasi yake kama Mwenyekiti wa CHADEMA aliitisha mkutano na kuzungumza na watia nia wa uchaguzi mkuu Makao Makuu ya chama Mikocheni.
Lissu amefafanua umuhimu mkubwa wa kisheria wa kubaini nani aliyeitisha mkutano huo kulingana na Kifungu cha 49 cha Kanuni ya Adhabu. Amesema kisheria, kila kitendo kinachofanywa kinahesabika kuwa ni tendo la wazi linalothibitisha nia. Ikiwa mshtakiwa aliitisha mkutano wenye lengo la kufanya uhaini, kuitisha huko kungehesabika kama kitendo cha wazi cha kisheria. Aidha, amesema kama mkutano ulikuwa wa kihaini, wote walioshiriki kuuandaa wangekuwa washirika kwenye kosa hilo la uhaini.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katibu wa ACT Wazalendo na Mbunge wa Tunduru Kaskazini, Ado Shaibu Ado, ameanza ziara ya kutembelea vijiji mbalimbali katika jimbo hilo, akianza rasmi leo Septemba 23, 2026, katika Kijiji cha Machemba.
Katika ziara hiyo, Ado Shaibu amepokelewa na mamia ya Wananchi wa Kijiji cha Machemba waliojitokeza kumlaki na kushiriki katika shughuli za ziara hiyo.
Ziara hiyo inalenga kumwezesha Mbunge huyo kufika katika maeneo mbalimbali ya jimbo hilo na kuzungumza na wananchi kuhusu masuala yanayowahusu pamoja na kusikiliza changamoto na mahitaji yao.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima, amewataka wanaume kutokukwepa wajibu wa malezi kwa kuwaachia jukumu hilo wanawake pekee, akisisitiza kuwa malezi ya watoto ni wajibu unaohitaji ushiriki wa wazazi.
Dkt. Gwajima ameyasema hayo leo Septemba 23, 2026, jijini Dodoma, wakati wa Mkutano wa nusu mwaka wa tathmini ya utekelezaji wa Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto, wenye kaulimbiu “Malezi Bora kwa Watoto, Msingi wa Kufikia Malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.”
Amesema baadhi ya watoto hawapati malezi yanayostahili wakiwa majumbani, huku wengine wakiwa mitaani bila malezi yanayofaa, jambo linalohitaji jamii kutafuta majawabu ya pamoja ya kuhakikisha watoto wanalelewa katika mazingira salama.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
LISSU AANIKA MASUALA MASUALA TISA MAKUU YATAKAYOAMUA KESI YAKE YA UHAINI jambo.co.tz/lissu-aanika-masuala-masuala-tisa-makuu-yatak… via @jambotv_
-
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Kesi ya uhaini namba 19605/2025 inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Tundu Antiphas Lissu, inaendelea leo Septemba 23, 2026, katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, ambapo Lissu ameanza kuwasilisha majumuisho yake ya mwisho mbele ya jopo la majaji watatu.
Akiwasilisha mahakamani, Lissu ameeleza kuwa kwa sheria za Tanzania na kwa ushahidi uliowasilishwa, haiwezekani kisheria kumhukumu adhabu ya kifo kiongozi wa kisiasa au mwananchi yeyote kwa kutoa maneno ya kisiasa katika mkutano wa kisiasa.
Lissu ameeleza kuhusu mashtaka ya uhaini yanayomkabili akisema kuwa imeelezwa akiwa na utiifu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mnamo tarehe 3 Aprili 2025 katika Wilaya ya Kinondoni, alitengeneza nia ya kuhamasisha umma kuzuia Uchaguzi Mkuu wa 2025 kwa lengo la kuitishia Serikali. Inadaiwa kuwa alidhihirisha nia hiyo kwa kutamka na kuchapisha maneno haya, "Wanasema kitu kimoja sahihi hapa... msimamo huu unaashiria uasi... tutazuia uchaguzi, tutahamasisha uasi... tunaenda kukinukisha... huu uchaguzi tutauvuruga... kwasababu tunaenda kukinukisha vibaya sana.".
Amesema kwa kuangalia namna maneno hayo yalivyowekwa, kuna mianyo (ellipsis) ambayo inaashiria kuna baadhi ya maneno yaliondolewa.
Wakati wa usikilizaji wa awali tarehe 22 Septemba 2025, Lissu amesema kuwa Jamhuri iliongeza madai kuwa yeye ndiye aliyeitisha mkutano wa watiania, akawaalika waandishi wa habari kutoka Mwananchi, Jambo TV, na Clouds Media, na kwamba kauli zake ziliwachochea baadhi ya wananchi.
Katika majumuisho yake, Lissu ameeleza kuwa hajawahi kukanusha au kuficha maneno yake. Amebainisha kuwa tangu alipokuwa Mahakama ya Kisutu (ukurasa wa 97 wa rekodi za mahakama), alikiri wazi kutamka maneno hayo katika mikutano ya wazi jijini Dar es Salaam, Mbeya, Iringa, Songwe, Njombe, Lindi, na Mtwara. Hoja ya msingi si kama alisema maneno hayo, bali ni kama maneno hayo yanatengeneza kosa la uhaini au kosa lolote la jinai kisheria.
Lissu amesisitiza kuwa hana haya wala aibu kwa kauli zake, kwani alichokisema si uhaini na wala si kosa la jinai chini ya sheria za Tanzania.
Ameongeza kuwa baada ya Mahakama kusikiliza mashahidi 17 wa Jamhuri, kupitia vielelezo 16 vya utetezi, na kutazama ukweli kuwa Jamhuri haikuleta kielelezo hata kimoja cha mashtaka (ikiwemo video yenyewe), kesi ya mashtaka imekuwa dhaifu mno kuliko siku ilipoletwa Mahakama Kuu.
Lissu ameyachambua matakwa ya Kifungu cha 39(2)(d) cha Kanuni ya Adhabu na Kifungu cha 10(2) cha sheria hiyo, akibainisha vigezo sita vinavyopaswa kuthibitishwa ili kosa la uhaini liweze kuwepo. Kwanza ni Utiifu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; Pili, ni tendo kufanyika ndani au nje ya Jamhuri ya Muungano; Tatu ni kutengenezwa kwa nia mahususi ya kutenda kosa la uhaini (si nia ya kufanya jambo jingine); Nne, ni ikiwa ni uchochezi, lazima ulenge mtu mmoja au kikundi cha watu waliotajwa, na si "umma" kwa ujumla; Tano, ni lazima idhihirishwe kwa kuchapisha maandishi au machapisho rasmi; Sita, ni sharti la Kifungu cha 10(2) ambacho ni matokeo halisi kwamba ni lazima kuwe na matokeo halisi yaliyojitokeza kutokana na nia hiyo au uchochezi huo.
Lissu amesisitiza kuwa ikiwa nia ilikuwepo lakini hakuna kosa au matokeo ya kiuhaini yaliyotokea, kosa la uhaini halipo kisheria.
Ameesema sehemu hii ya kwanza ya majumuisho yake kwa kuwakumbusha majaji watatu mzigo mzito wa kihistoria waliobebeshwa. Ameeza kuwa maamuzi watakayoyatoa katika kesi hii ya kwanza ya Kifungu cha 39(2)(d) hayatamhusu yeye pekee, bali yataweka msingi wa kisheria utakaoongoza mahakama za Tanzania na nchi kwa miaka mingi ijayo.
Ameiomba mahakama kubeba mzigo huo wa kihistoria kwa ujasiri, heshima, na bila upendeleo wowote kwa kuzingatia viapo vyao vya ujaji, ili kuweka mwongozo sahihi pindi kivumbi cha kesi hiyo kitakatapotulia.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa @ChademaTZ2 Tundu Lissu imeahirishwa kwa Lisaa limoja na nusu kuanzia (1:30PM-3:00PM) ambapo ataendelea na walisilisho lake la mwisho(Final Submission) aliloanza asubuhi ya leo Septemba 23, 2026 kabla ya majaji kutoa hukumu.
Saa nane na nusu Lissu atakutana na Mawakili kwa ajili ya kushauriana nao.
Simulizi ya submission ya Lissu ipo YouTube ya jambo TV na website yetu www.jambo.co.tz -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI:
Ubelgiji na Rwanda zimetangaza kukubaliana kurejesha tena uhusiano wa kidiplomasia, hii ikiwa ni hatua ya kuanza kurekebisha uhusiano ulionekana kuvunjika mwaka uliopita kutokana na mzozo wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Kwa mujibu wa taarifa yao ya pamoja ya Septemba 22, 2026, ikiwahusisha mawaziri wa mambo ya nje wa nchi hizo, mataifa hayo sasa yanatarajiwa kufungua tena balozi zake jijini Kigali na Brussels.
Uhusiano kati ya mataifa hayo uliingia dosari mwaka uliopita baada ya Ubelgiji kuikosoa Rwanda kwa kuwaunga mkono waasi wa M23 wakati wa uvamizi wao mashariki mwa DRC.
Kigali ilikatisha ushirikiano wake na Brussels mwezi Machi mwaka jana na kuwafukuza wanadiplomasia wa Ubelgiji, Kigali ikidai Brussels imekuwa ikiingilia masuala yake ya ndani mara kwa mara.
Katika taarifa yao ya pamoja, zimesema uamuzi wao unatokana na majadiliano na mawasiliano ya mara kwa mara kati ya mawaziri wa mambo ya nje, ambapo masuala tata na yaliyokuwa hayajaeleweka na pande hizo yalipatiwa ufumbuzi.
Wizara ya mambo ya nje ya Rwanda ilichapisha picha ya Waziri wake Olivier Nduhungirehe akisalimiana na mwenzake wa Ubelgiji Maxime Prevot nje ya makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Taarifa rasmi iliyotolewa tarehe 22 Septemba, 2026 na Mwanasheria wa Familia za David Mushi na Mariam Mongi, Wakili Wilson Ogunde, imeweka wazi ukweli wa kisheria na chanzo halisi cha mgogoro wa ardhi wa ekari 10 uliopo Madale (Mtaa wa Scout), Wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam.
Hatua hii inakuja kufuatia kadhia iliyowakuta wananchi wa kaya zilizopo eneo hilo waliotolewa katika nyumba zao tarehe 3 Septemba 2026 kufuatia madai ya wananchi hao kwamba waliuziwa ardhi hiyo kihalali na Bwana Abdallah Kitwanga kupitia usimamizi wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Mtaa huo, Gratian Mbelwa.
Kwa mujibu wa Mwanasheria Wilson Ogunde, familia za David Mushi na Mariam Mongi zilinunua eneo hilo la ekari 10 tangu mwaka 1994 na zinalimiliki kwa Hatimiliki halali namba 122566, 124794, 123549, 122557, 122528 na 123894 zilizotolewa mwaka 2009.
Ogunde amebainisha kuwa haki ya umiliki ya familia hizo imethibitishwa na Mahakama katika ngazi zote, ikiwemo Mahakama ya Rufani ya Tanzania katika Shauri Na. 286 la 2016 lililotoa hukumu ya ushindi kwa Familia ya David Mushi tarehe 2 Julai 2022.
Pia, tarehe 28 Oktoba 2022, Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi katika Shauri Na. 316 la 2010 iliitamka familia hiyo kuwa mmiliki halali, na baadaye mwaka 2023 Mahakama Kuu (Shauri Na. 261133 la 2023) ikaagiza familia irejeshwe eneo hilo na kulipwa fidia ya TZS milioni 80.
Amri ya kukaza hukumu ilitolewa tarehe 9 Mei 2025, ambapo Notisi za kuondoka zilianza kutolewa na Dalali wa Mahakama tangu Agosti 2025 kabla ya zoezi la kuwaondoa waliokuwepo kutekelezwa tarehe 3 Septemba 2026 chini ya usimamizi wa Jeshi la Polisi.
FUATILIA ZAIDI VIDEO HII KUPITIA CHANELI YA YOUTUBE YA JAMBO TV ILI KUJUA KWA UNDANI KUHUSU MGOGORO HUU.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwanasheria wa familia za David Mushi na Mariam Mongi, Wakili Wilson Ogunde, amesema kuwa baadhi ya wanafamilia wa familia hizo wanashikiliwa na Jeshi la Polisi katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay kufuatia mgogoro wa ardhi uliopo Madale Mtaa wa Scout, Wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam.
Hatua hiyo imekuja kufuatia agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, alilolitoa kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Mtatiro Kitinkwi, la kuagiza kukamatwa kwa wanafamilia hao kwa kile alichodai ni kukaidi wito wake wa Septemba 19, 2026.
Mkuu wa Mkoa Albert Chalamila alieleza kuwa alitoa wito kwa familia hiyo kufika katika eneo hilo ambalo wanalimiliki kwa mujibu wa hukumu ya Mahakama, ili kuzungumza nao baada ya familia hiyo kuchukua hatua mnamo Septemba 3, 2026, ya kuzitoa na kuzizuia kuingia ndani ya nyumba kaya zaidi ya 20 zilizokuwa zikiishi hapo. Chalamila alibainisha kuwa hakuiita familia hiyo kuvuruga amri ya Mahakama bali alitaka kufanya nayo mazungumzo, lakini kutosikiliza wito wake na kutopokea simu kuliingiza hisia za dharau kwa mamlaka yake. Kwa upande wao, kaya hizo zaidi ya 20 zimekuwa zikidai kuwa zilishanunua maeneo hayo halali kufuatia Serikali ya Mtaa kuwathibitishia kuwa eneo hilo halina mgogoro.
Hata hivyo akizungumza na wanahabari jioni ya siku ya Jumanne Septemba 22, 2026, Mwanasheria Wilson Ogunde amebainisha kuwa wanafamilia hao hawakukaidi kwa makusudi, bali walijitokeza kwa hiari kutoa maelezo mara tu walipopata taarifa za agizo hilo kupitia mitandao ya kijamii kisha kwenda polisi, ambapo watano kati yao walikamatwa na kuwekwa rumande. Miongoni mwa walioshikiliwa ni pamoja na bibi mwenye umri wa miaka 86.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Mtatiro Kitinkwi alipotafutwa na Jambo TV kwa njia ya simu kuzungumzia kukamatwa kwa wanafamilia hao alihoji kuwa kama tayari Wakili ameshalizungumzia suala hilo kuna haja ya kuwa na shaka nalo? Na baada ya hapo simu ikakatika.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Jeshi la Polisi nchini limewataka madereva wa vyombo vyote vya moto kuzingatia sheria za usalama barabarani na kutii sheria bila shuruti, likisisitiza kuwa ajali nyingi zinaratibiwa na makosa ya kibinadamu badala ya vyombo vyenyewe.
Wito huo umetolewa leo, Septemba 22, 2026, na Kamishna wa Intelijensia ya Jinai, CP Charles Mkumbo, aliyemwakilisha Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Camillus Wambura, wakati wa zoezi la kuaga miili ya askari watano wa Jeshi la Polisi waliofariki dunia katika ajali ya barabarani iliyotokea Septemba 21, 2026, eneo la Sekenke mkoani Singida, ajali iliyogharimu pia maisha ya mahabusu saba.
Akiwasilisha salamu za IGP Wambura, CP Mkumbo amesisitiza kuwa madereva wa pikipiki, bajaji, malori, na mabasi lazima wachukue tahadhari kubwa na kuacha kutegemea kushurutishwa na askari wa usalama barabarani.
“Tuchukue tahadhari wakati tunaviendesha hivi vyombo vya moto. Vyombo vya moto havina makossa, wenye makosa ni sisi binadamu tunaoviendesha. Ni lazima tuzingatie sheria zilizowekwa za usalama barabarani, hivyo ni lazima madereva kutii sheria bila shuruti. Tusisubiri kushurutishwa na askari wa usalama barabarani bali tuzingatie sheria tulizofundishwa wakati tunatafuta ujuzi wa kuendesha”, amesema CP Mkumbo.
Aidha, CP Mkumbo amekumbusha jamii na madereva wote nchini kuwa uhai wa binadamu hauna vipuri (spea) vya kununuliwa dukani pindi unapotoweka, hivyo kuna haja kubwa ya kuheshimu uhai na kuendesha vyombo vya moto kwa kuzingatia sheria na taratibu zote.
Zoezi hilo limefanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Shelui, Wilaya ya Iramba mkoani Singida, likiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego, na kuhudhuriwa na viongozi wa Polisi, Serikali, taasisi za kidini, vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na wananchi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, SACP Amon Kakwale, ameeleza kuwa kuondokewa kwa ghafla na askari watano wa Jeshi la Polisi katika ajali ya barabarani iliyotokea eneo la Sekenke ni pigo zito na kipindi kigumu mno kwa Jeshi la Polisi na Mkoa wa Singida kwa ujumla.
Kauli hiyo imeolewa leo, Septemba 22, 2026, katika Viwanja vya Shule ya Msingi Shelui, Wilaya ya Iramba mkoani Singida, wakati wa zoezi la kutoa salamu za heshima na heshima za mwisho kwa marehemu hao.
"Nitangulie nami kuwashukuru wote mliotukimbilia kuja kututia moyo na kututakia faraja katika kipindi hiki kigumu, ni kigumu kwelikweli ndani yetu ya jeshi la polisi lakini kipindi kigumu zaidi pia kupotelewa na ndugu zetu wengine waliokuwa bado tunawaita ni watuhumiwa kwani hatuwezi tukasema ni wafungwa. Hivyo basi tuungane pamoja kuziombea roho hizi za marehemu waliotangulia mbele za haki", ameeleza Kamanda Kakwale.
Akitoa salamu za pole kutoka Serikali ya Mkoa, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego, amempa pole Kamanda Kakwale na timu yake yote ya Jeshi la Polisi, akitambua maumivu makali ya kuondokewa na watendaji kazi wao kwa ghafla katika siku moja.
Aidha, RC Dendego ameongeza kuwa msiba huo mkubwa unaleta tafakuri nzito kwa jamii kwamba kila binadamu ni msafiri hapa duniani, hivyo wananchi wanapaswa kuendelea kuishi kwa upendo na kuyaenzi yale mema yote yaliyoachwa na askari hao waliokuwa wakijitoa usiku na mchana kulinda amani na usalama wa raia
Zoezi hilo la uagaji miili limeongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego, na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Jeshi la Polisi, viongozi wa serikali, taasisi za kidini, maafisa wa vyombo vya ulinzi na usalama, pamoja na wananchi waliojitokeza kutoa faraja na kuagana na waliotangulia.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mchambuzi wa Masuala ya Hali ya Hewa kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Ramadhan Omary, amesema mikoa mbalimbali nchini inatarajiwa kupata mvua za juu ya wastani katika msimu huu, huku baadhi ya maeneo yakitarajiwa kukumbwa na vipindi vya mvua kubwa.
Amesema mikoa inayozunguka Kanda ya Ziwa, ikiwemo Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga na Simiyu, inatarajiwa kupata mvua za juu ya wastani. Aidha, mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara, pamoja na Dar es Salaam, Tanga, Morogoro na Pwani, nayo inatarajiwa kupata mvua hizo.
Ameongeza kuwa hali hiyo inatarajiwa pia katika Kaskazini mwa Morogoro pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba, ambapo kiwango cha mvua kinatarajiwa kuwa juu zaidi ikilinganishwa na hali ya kawaida inayozoeleka.
Mahojiano kamili yapo youtube yetu ya Jambo TV.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Kampuni ya Tanzania International Tourism Festival (TITF) imeandaa tamasha kubwa la kitaifa la sanaa za ufundi litakalofanyika kuanzia tarehe 6 hadi 11 Oktoba, 2026, katika Viwanja vya General Tyre, Njiro, jijini Arusha.
Tamasha hilo limelenga kuunganisha sekta za sanaa, ufundi, utamaduni, utalii, na uchumi wa ubunifu, huku likitoa fursa pana za masoko, biashara, na uwekezaji kwa wazalishaji na wabunifu wa ndani.
Akizungumza na waandishi wa habari, Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Edward Buganga, amesema kuwa TITF imezishirikisha taasisi za BASATA, Bodi ya Filamu Tanzania, na COSOTA ili kuhakikisha malengo ya kuendeleza wasanii na kulinda miliki bunifu yanafikiwa. Buganga amebainisha kuwa BASATA itajikita katika kuendeleza wasanii na uchumi wa ubunifu, wakati Bodi ya Filamu itaonyesha namna filamu na sanaa zinavyoweza kukuza utalii na utamaduni.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa TITF, Ibrahim Othman, amesema tamasha hilo linatarajiwa kuwakutanisha washiriki zaidi ya 1,000, wakiwemo mafundi na waonyeshaji zaidi ya 200, viongozi wa Serikali, mabalozi, wanunuzi wa kimataifa, na wawekezaji.
Tamasha hilo linabeba kaulimbiu isemayo “Crafted in Tanzania. Desired by the World,” ikiwa na lengo la kuonesha ubora, thamani, na upekee wa bidhaa zinazotengenezwa Tanzania na kuhamasisha masoko ya ndani na nje ya mipaka ya nchi.
Mbali na maonyesho ya bidhaa, Othman ameeleza kuwa tamasha hilo litaonesha matumizi ya teknolojia katika uzalishaji, uongezaji thamani wa bidhaa, na ziara ya kujifunza katika Shirika la Uhandisi na Usanifu Mitambo Tanzania (TEMDO), kutakuwa na maonesho ya muziki, ngoma, na sanaa za maonesho kila jioni huku wageni na wananchi wakipata fursa ya kupata uzoefu wa vyakula mbalimbali vya asili vya Kitanzania. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Miaka minane baada ya kifo cha mfanyabiashara na mmiliki wa Kampuni ya Mabasi ya Super Sami, Josiah Methusela Mzuri(Super Sami) Mahakama ya Rufani ya Tanzania imefuta hukumu ya kifo iliyokuwa imewatia hatiani John Simon(Kadaso) na Paul Mashauri (Nchimika,Rubembeja, Jam Marshal) baada ya kubaini mapungufu katika ushahidi uliotumika kuwahukumu.
Uamuzi huo umetolewa Septemba 21, 2026 katika shauri la jinai la rufani namba 432/2024 lililokuwa mbele ya jopo la watatu Majaji watatu Kente, Kihwelo na Masabo ambapo mahakama hiyo ilikubaliana na hoja za upande wa waombaji ukiongozwa na Wakili Peter Kibatala @PKibatala_ kuifuta hukumu ya Mahakama Kuu na waliokuwa washtakiwa wakiachiwa huru.
Kifo cha Super Sami kilitikisa mwaka 2018, baada ya taarifa za kutoweka kwake kusambaa taarifa za vyombo vya habari za wakati huo zilieleza kuwa aliondoka Mwanza Februari 27, 2018 akielekea Simiyu kwa shughuli za biashara, lakini hakurejea nyumbani. Familia ilieleza kuwa kabla ya kutoweka, marehemu alimweleza mkewe kuwa angerudi akiwa na mgeni na baadaye, gari lake aina ya Nissan Patrol lenye namba T 323 BSF lilikutwa limeteketea kwa moto ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Mahakama ya Rufani ilikataa matumizi ya dhana ya “last seen together” dhidi ya John Simon, ikisema haikuthibitishwa bila shaka kwamba alikuwa mtu wa mwisho kuwa na marehemu kabla ya kifo chake.
Aidha, Mahakama iliona kuwa kulikuwa na mapungufu katika ushahidi wa gari, umiliki wake, tarehe ya mauaji na mlolongo wa ushahidi wa kimazingira. Kwa mtazamo wa Mahakama, katika kesi inayotegemea ushahidi wa kimazingira, kila kiungo muhimu lazima kiungane bila kuacha uwezekano mwingine wa kutokuwa na hatia.
Hivyo Mahakama hiyo ilikubaliana na hoja za upande wa waombaji na kuruhusu rufaa hiyo huku hukumu ya hatia dhidi ya John Simon na Paul Mashauri ikifutwa, adhabu ya kunyongwa ikaondolewa na Mahakama ikaamuru waachiwe huru mara moja iwapo hawakuwa wanashikiliwa kwa sababu nyingine halali.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amewataka Watanzania kutambua kuwa hatua ya maridhiano iliyofanyika visiwani humo siyo mwisho wa safari bali ndiyo mwanzo wa safari katika kujenga nchi, huku akimsihi Makamu wa Rais aliyeapishwa leo Masoud Othman Masoud kutambua kuwa dhamana aliyopewa ni kubwa na wananchi wanamatarajio makubwa kutoka kwa Serikali.
Rais Mwinyi ameeleza hayo leo Septemba 22, 2026 visiwani Zanzibar alipokuwa akihutubia baada ya zoezi la kumuapisha Makamu wake Othman Masoud kutamatika. Amesema kuapishwa kwa makamu huyo ni hatua muhimu katika utekelezaji wa matakwa ya katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 toleo la 2010.
Amesema kuapa kwa Makamu huyo ni ishara kwamba tayari wameingia katika hatua ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa, ambayo msingi wake ni umoja na inayotambua tofauti za kisiasa na kuweka mbele maslahi ya nchi.
Aidha, amesema Serikali hiyo inawataka viongozi na wananchi wote kuelekeza nguvu katika ujenzi wa nchi na kwamba kwa hatua hiyo kazi iendelee kufanyika ili kuipatia Zanzibar maendeleo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Moto ambao chanzo chake hakijafahamika unaodaiwa kuzuka saa saba usiku leo Septemba 22, 2026 katika Soko la mbao la Sabasaba lililopo wilayani Ilemela mkoani Mwanza umeteketeza vibanda na mbao za wafanyabiashara wa mbao hizo.
Akizungumza alfajiri mara baada ya kufika eneo la tukio, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, CP Salum Hamduni amesema ataunda kamati maalum ya kuchunguza chanzo cha tukio hilo sambamba na kupata mapendekezo ya namna ya kuimarisha usalama katika eneo hilo.
CP Hamduni amesema kamati hiyo itachunguza chanzo na mazingira ya tukio hilo, huku ikizingatiwa kuwa tukio kama hilo liliwahi kutokea katika eneo hilo mwaka jana.
Amesema kamati itawasilisha mapendekezo na hatua zinazopaswa kuchukuliwa, hususani katika masuala ya usalama, ili kuhakikisha matukio ya moto hayajirudii katika soko hilo.
Katika tukio hilo bado haijafahamika idadi ya vibanda vilivyoungua huku kukiwa hamna majeruhi wala vifo vilivyotokea kutokana na moto huo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Mama Fatma Karume, mjane wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Hayati Sheikh Abeid Amani Karume, amefariki dunia leo, Septemba 21, 2026, akiwa na umri wa miaka 97.
Taarifa rasmi ya kifo chake imetangazwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla, akieleza kuwa kimetokea leo Septemba 21, 2026 huko Mbweni, Zanzibar, alipokuwa nyumbani kwa mmoja wa watoto wake.
Mama Fatma alizaliwa Februari 2, 1929, huko Bumbwini Misufini, Mkoa wa Kaskazini Unguja, na baadaye kuolewa na Hayati Sheikh Abeid Amani Karume. Mbali na kuwa mke wa kiongozi huyo mkuu wa kihistoria kufuatia Mapinduzi ya Zanzibar ya Januari 12, 1964, Mama Fatma alikuwa mstari wa mbele na kushiriki kikamilifu katika harakati za kisiasa nchini. Yeye pia ni mama mzazi wa Rais wa zamani wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, aliyeiongoza nchi hiyo kuanzia mwaka 2000 hadi 2010.
Kufuatia msiba huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametoa salamu za pole akisema kuwa kifo chake kimeacha pengo kubwa kwa familia na Taifa kwa ujumla.
“Alikuwa sehemu muhimu ya historia adhimu ya Zanzibar kuanzia wakati wa harakati za kupigania uhuru, Mapinduzi Matufuku ya Zanzibar na kuasisiwa kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Daima tutaendelea kukumbuka, kuenzi na kuheshimu mchango wake katika kuhifadhi kumbukumbu na urithi wetu, pamoja na kuchochea maendeleo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii ya Taifa letu”, ameandika Dkt. Samia kupitia kurasa zake mitandao ya kijamii.
Aidha, Rais Samia ametoa pole maalum kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Rais Mstaafu Amani Abeid Karume, familia ya Hayati Sheikh Karume, ndugu, jamaa, na wananchi wote wa Tanzania. -
Jambo TV
@Jambotv_
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametuma salamu za rambirambi kufuatia vifo vya watu 12, wakiwemo askari polisi watano na mahabusu saba, waliopoteza maisha katika ajali mbaya ya barabarani iliyotokea Septemba 21, 2026, katika eneo la Mlima Sekenke, Wilaya ya Iramba mkoani Singida.
Katika ujumbe wake alioutoa kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, Rais Samia ameeleza kusikitishwa kwake na ajali hiyo iliyohusisha gari la Jeshi la Polisi na lori la mizigo.
“Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya vifo vya watu 12 (mahabusu saba na Askari Polisi watano), vilivyotokea leo katika Wilaya ya Iramba, Mkoa wa Singida, kufuatia ajali iliyohusisha gari la Jeshi la Polisi na lori,” amesema Rais Samia.
Aidha, ametoa pole kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP), Camillus Wambura, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Omary Dendego, familia za marehemu, ndugu, jamaa, na Watanzania wote kwa ujumla.
Katika salamu hizo, Rais Samia amewasisitiza madereva wote nchini kuendelea kuzingatia sheria za usalama barabarani na kuhakikisha vyombo vya moto viko katika hali nzuri kabla ya kusafiri, ili kulinda maisha ya wananchi.
“Ninaendelea kuwasisitiza madereva wote kuzingatia Sheria za Usalama Barabarani na kuhakikisha vyombo vya moto vinakuwa katika hali nzuri na salama kabla ya kutumika, ili kulinda maisha ya wananchi na watumiaji wengine wa barabara. Mwenyezi Mungu aziweke roho za marehemu mahala pema peponi, Amina”, ameeleza Dkt. Samia.
Ajali hiyo ilitokea majira ya asubuhi katika barabara kuu ya Singida-Nzega pale lori lililokuwa limetokea Kigali, Rwanda, lilipogongana na gari la Polisi aina ya Toyota Land Cruiser lililokuwa likitokea Kituo cha Polisi Shelui kuelekea Kiomboi kwa ajili ya kuwapeleka mahabusu mahakamani.
Askari waliopoteza maisha ni pamoja na Mkuu wa Kituo cha Polisi Shelui, SP Frank Lazima Mwasapili, S/SGT Ussi Hassan, SGT Paulo Silivin Gabriel, PC Ashraf Salumu Kheri, na PC Nangida Ramadhani Mushi. Kwa upande wa mahabusu, waliopoteza maisha ni Timotheo Lazaro Kimaro, Cassian Hassan, Fred Musuguli Mazoa, Wilfred Marko Amos, Mariam Hamis Kasijao, Vivian Saidi, na Hussen Hussen Kea, huku kukiwa na majeruhi wawili ambao ni mahabusu Petro Organes Nkana na dereva wa lori, Ndanarasa Christian Alfonce. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Hassan Kabeke amewataka wanaodai kuwa Tanzania kuna utulivu lakini hakuna amani kuangalia mazingira na vyanzo vya taarifa vinavyowafanya kutoa kauli hiyo.
Akizungumza leo na Jambo TV ofisini kwake jijini Mwanza katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Amani yanayofanyika kila mwaka Septemba 21, Sheikh Kabeke amesema baadhi ya kauli kuhusu hali ya amani nchini zinapaswa kuangaliwa kwa kuzingatia mtu anayezitoa na vyanzo vya taarifa anavyovitumia.
Amesema kauli zinazodai kuwa Tanzania haina amani ikiwemo zinazotolewa kwa kurejea madai ya watu kupotea zinahitaji kuangaliwa kwa kuzingatia mazingira na ushahidi unaotumika kufikia hitimisho hilo.
"Mimi nimesikia wanasema hakuna amani ila kuna utulivu, ukimsikiliza huyu mtu unatakiwa kwanza umtazame anayezungumza ni nani? kapitia kwenye maeneo gani? Vyanzo vyake vinavyomuonesha hii ni vipi? mfano anaposema watu wanapotea hiki kinampa kigezo kwamba Tanzania hamna amani?," amesema.
Sheikh Kabeke ameongeza kuwa "Huyu ukimtazama vizuri hajaona amani inapovurugika, mfano rahisi unao onesha kwamba Tanzania tuna amani ni Oktoba 29 na 30 na katika hili huwa sirudi nyuma katika kuelezea haya mambo,".This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Wananchi wa kata ya Mhandu Jijini Mwanza wameeleza kusikitishwa na changamoto ya upatikanaji wa maji sambamba na ubovu wa barabara hali wanayosema imekuwa ikiwapa ugumu katika shughuli zao za kila siku.
Wakizungumza leo kwenye mkutano wa hadhara wa mbunge wa Jimbo hilo la Nyamagana, John Nzilanyingi wamedai kuwa wakati mwingine hupata maji mara moja kwa wiki hadi wiki mbili hali inayo walazimu wakati mwingine kutumia maji kutoka vyanzo visivyo salama jambo linaloweza kuhatarisha afya zao.
Meneja Msaidizi Ufundi Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA) kanda ya Nyakato Jijini Mwanza, David Saranga amesema Serikali inaendelea kuboresha miundombinu ya maji ikiwa ni pamoja na kujenga matenki mapya katika kata hiyo ili kuwaondolea changamoto hiyo.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Meneja Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Wilaya ya Nyamagana, Mhandisi Daudi Mtalisi amesema mamlaka hiyo inakabiliwa na ufinyu wa bajeti ambao unapelekea kushindwa kurekebisha miundombinu hiyo ya barabara.
Akizungumzia changamoto ya maji mbunge wa Jimbo hilo la Nyamagana, John Nzilanyingi amesema miradi mitatu ya ujenzi wa matenki ya maji inayotarajiwa kukamilika Disemba mwaka huu itaenda kupunguza changamoto hiyo katika eneo hilo.
Kuhusu changamoto ya barabara, Nzilanyingi amesema tayari Halmashauri ya Jiji la Mwanza imenunua mitambo ya kutengeneza barabara ikiwemo greda ambayo inaenda kutatua changamoto hiyo katika mitaa yote katika jimbo hilo akidai kuwa zoezi hilo limeanza na linaendelea.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Hassan Kabeke amewapinga na kuwakosoa wanaochochea vurugu na fujo akidai kuwa vurugu na fujo nchini anaweza kuchangia vifo vya watu kwa kuwa hali hiyo inaweza kuwazuia madaktari na wauguzi kufika hospitalini kutoa huduma kwa wagonjwa.
Akizungumza leo na Jambo TV ofisini kwake kuhusu Siku ya Amani Duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka Septemba 21, Sheikh Kabeke amesema amani ni jambo la msingi katika jamii kwa kuwa bila amani shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo huduma za afya zinaweza kuathirika.
"Mtu anayeleta vurugu na fujo katika nchi huyo ni muuaji kwa sababu ni ukweli usiopingika itafika mahala madaktari na manesi watashindwa kwenda hospitalini na kutoa huduma matokeo yake kuna wagonjwa kadhaa watakufa bila kufika hospitalini," amesema.
Sheikh Kabeke amesisitiza kuwa amani ni wa kila kitu katika jamii huku akidai kuwa bila amani wananchi hawezi kupata haki na huduma mbalimbali za kijamii.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Watu 12, wakiwemo askari watano wa Jeshi la Polisi Tanzania na mahabusu saba, wamefariki dunia katika ajali mbaya ya barabarani iliyotokea Septemba 21, 2026, katika eneo la Mlima Sekenke, Kijiji cha Misigiri, Kata ya Ulemo, Wilaya ya Iramba mkoani Singida.
Ajali hiyo ilitokea majira ya saa moja na dakika 30 asubuhi katika barabara kuu ya Singida-Nzega, ikihusisha lori lililokuwa na namba za usajili RAF 243X/T-RL 4255, mali ya Kampuni ya YYUSSA ya Kigali, Rwanda, lililogongana na gari la Jeshi la Polisi aina ya Toyota Land Cruiser lenye namba PT 1982.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi kutoka Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida, gari hilo la polisi lilikuwa likitokea Kituo cha Polisi Shelui likielekea Kiomboi kwa lengo la kuwapeleka mahabusu mahakamani.
Askari waliopoteza maisha katika ajali hiyo ni pamoja na Mkuu wa Kituo cha Polisi Shelui, SP Frank Lazima Mwasapili, S/SGT Ussi Hassan, SGT Paulo Silivin Gabriel, PC Ashraf Salumu Kheri, na PC Nangida Ramadhani Mushi.
Kwa upande wa mahabusu, waliopoteza maisha ni Timotheo Lazaro Kimaro, Cassian Hassan, Fred Musuguli Mazoa, Wilfred Marko Amos, Mariam Hamis Kasijao, Vivian Saidi, na Hussen Hussen Kea. Aidha, watu wawili walipata majeruhi katika ajali hiyo, ambao ni mahabusu Petro Organes Nkana na dereva wa lori, Ndanarasa Christian Alfonce.
Kufuatia tukio hilo, Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida limetoa wito kwa madereva wote nchini kuzingatia sheria, alama, na michoro ya usalama barabarani, hususan katika maeneo yenye miteremko na miinuko mikali kama Mlima Sekenke, ili kuepuka ajali zinazoweza kuzuilika zinazogharimu maisha ya wananchi na mali. -
Jambo TV
@Jambotv_
Wananchi wa Mkoa wa Pwani wanaendelea kunufaika na ushirikiano madhubuti kati ya Serikali ya Mkoa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), unaolenga kuhakikisha upatikanaji wa maji safi na salama katika kipindi ambacho mkoa huo unakua kwa kasi kiuchumi na kiviwanda.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Stanslaus Nyongo, amesema Serikali ya Mkoa itaendelea kushirikiana kwa karibu na DAWASA pamoja na wadau wengine kuhakikisha huduma ya maji inakuwa endelevu, huku akisisitiza umuhimu mkubwa wa wananchi kushiriki katika kulinda miundombinu ya maji.
Nyongo ameyasema hayo leo, Septemba 21, 2026, alipokutana na kufanya mazungumzo rasmi na uongozi wa Bodi ya DAWASA ofisini kwake, ulioongozwa na Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Mhandisi Romanus Mwangingo.
Akitoa taarifa wakati wa kikao hicho, Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Mkama Bwire, ameeleza kuwa mamlaka hiyo inahudumia jumla ya watu zaidi ya milioni nane katika Mkoa wa Dar es Salaam na maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Pwani.
Kwa upande wa Mkoa wa Pwani pekee, Mhandisi Bwire amesema DAWASA inahudumia takribani watu milioni 1.4, ikiwa ni sawa na asilimia 68 ya wakazi wote wa mkoa huo, huku mahitaji ya maji yakiendelea kuongezeka kutokana na kasi kubwa ya ukuaji wa viwanda na shughuli za kiuchumi.
Pamoja na mafanikio hayo, Mhandisi Bwire amebainisha kuwa mamlaka hiyo inakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo kuongezeka kwa gharama za uendeshaji, uwepo wa madeni kutoka kwa baadhi ya taasisi, na tatizo la upotevu wa maji, mambo yanayohitaji ushirikiano wa karibu kutoka serikalini na kwa wananchi.
Akijibu changamoto hizo, Mkuu wa Mkoa Nyongo ameahidi kuwa Serikali ya Mkoa itasimama kidete kulinda mitambo na miundombinu mikubwa ya uzalishaji na usambazaji maji, ikiwemo maeneo ya Ruvu Juu, Ruvu Chini, na Wami, ili kuepusha uharibifu unaoweza kukwamisha upatikanaji wa huduma kwa wananchi na viwanda. -
Jambo TV
@Jambotv_
Mkurugenzi wa Shule ya Green Acres iliyopo Mbezi Beach Salasala jijini Dar es Salaam, Jackline Rushaigo, ameelezea mikakati ya shule hiyo ya kutoa elimu ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) tangu wakiwa wadogo ili kwenda sanjari na kasi ya ulimwengu wa kidijitali.
Akizungumza kwenye mahafali ya darasa la saba na shule ya awali yaliyoshuhudia wanafunzi 60 wakihitimu elimu ya msingi, Rushaigo alieleza kuwa shule inatambua umuhimu wa mbinu za kisasa za ufundishaji.
“Tumeongeza ubora na ufanisi kwenye TEHAMA, wanafunzi wetu wanajifunza masuala ya akili mnemba/akili unde (AI) wakiwa wadogo hapa shuleni na mambo yanayoendana na uhalisia wa utanzania wetu na dunia ya sasa. Tunawapa taaluma ambayo hata wakiwa nje ya shule wanaweza kufanya vitu mbalimbali vya kujiajiri na kujiingizia kipato,” alisema.
Aidha, aliwakumbusha wahitimu hao kuendelea kuwa na nidhamu, bidii, na kujituma wanapoelekea katika hatua nyingine za elimu, huku akiwakumbusha wazazi na walezi umuhimu wa ushirikiano wa karibu kati ya familia na shule katika kujenga maadili na mafanikio ya mtoto.
Alisema Green Acres itaendelea kuwekeza katika elimu inayolenga kumjenga mwanafunzi kitaaluma, kimalezi na katika nyanja mbalimbali za maisha, ili kuwaandaa vijana wenye uwezo wa kushindana katika dunia inayobadilika kwa kasi.
Kwa upande wake, mgeni rasmi katika mahafali hayo, Edwin Odemba, aliwapongeza wahitimu hao kwa kuhitimisha vyema elimu ya msingi na kuwataka kutumia maarifa waliyoyapata kuwa msingi wa kujenga maisha yao ya baadaye.
Odemba alisisitiza umuhimu wa wanafunzi kuwaheshimu wazazi, walezi na walimu, pamoja na kuitumia elimu hiyo kama nguzo ya kuwa mabalozi wema wa shule hiyo huku wakijiandaa kukabiliana na changamoto za dunia inayobadilika kwa kasi. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI:
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Masha Mshomba, amebainisha mafanikio ya miradi ya kijamii inayotekelezwa na kusimamiwa na mfuko huo ikiwemo mradi wa Daraja la Nyerere Kigamboni ambalo amesema usimamizi wake umeendelea kuonesha manufaa.
Akizungumza leo Septemba 21, 2026, katika kikao kazi kilicho andaliwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina pamoja na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), kikiwashirikisha Wahariri wa Vyombo vya Habari, Mshomba ameeleza kuwa Daraja la Nyerere Kigamboni limeingiza kiasi cha shilingi bilioni 150.04 kupitia tozo za matumizi tangu mwaka 2016.
Katika sekta ya uzalishaji, Mshomba amesema kuwa Kiwanda cha Sukari cha Mkulazi kilichopo mkoani Morogoro kimeleta tija kwa kupata faida ya shilingi bilioni 4.56 kwa mwaka 2025/2026 huku kikiendelea kuzalisha ajira kwa wananchi.
Aidha, amefafanua kuwa mpango wa maendeleo wa miaka mitano wa NSSF umejikita katika kutekeleza vipaumbele vya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 ili kuleta ustawi endelevu kwa wananchi.
Katika mpango wao mpya wa miaka mitano kuanzia Julai 2026 hadi Julai 2031, amesema mfuko huo unalenga kuandikisha wanachama wapya na kuongeza makusanyo ya michango kupitia utoaji wa elimu kwa vikundi mbalimbali vya kijamii ambavyo vinahaja ya kujiunga na mfuko huo.
Mshomba ameongeza kuwa kupitia mpango wa miaka sita uliopita, thamani ya mfuko imekua na kufikia zaidi ya shilingi trilioni nne, mafanikio yaliyotokana na ongezeko la wanachama na udhibiti madhubuti wa mianya ya upotevu wa fedha.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile, ameipongeza Ofisi ya Msajili wa Hazina kwa kurejesha mikutano na wahariri, huku akiahidi ushirikiano thabiti na NSSF katika kuelimisha jamii kuhusu miradi inayowagusa wananchi. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
📍DODOMA - Tukio la kushangaza limetokea katika eneo la Makole, baada ya dereva wa basi la kampuni ya SATCO lenye namba za usajili T308 EME kudaiwa kutishiwa kwa silaha ya moto na mtu ambaye hakufahamika, aliyekuwa akiendesha gari aina ya Land Cruiser lenye namba za usajili T881 ENZ.
Mashuhuda wa tukio hilo wameeleza kuwa basi hilo lilikuwa likitoka katika stendi ya mabasi jijini Dodoma kuelekea mkoani Geita, ambapo lilipofika eneo la Makole, dereva wa Land Cruiser alidaiwa kulipita basi hilo kwa upande, hali iliyosababisha magari hayo kugongana.
Baada ya tukio hilo, mashuhuda wanadai kuwa dereva wa Land Cruiser alishuka akiwa na silaha ya moto inayodaiwa kuwa ni bastola na kumfuata dereva wa basi, akimtaka ashuke kwenye basi hilo na kuingia katika gari aina ya Land Cruiser.
Tukio hilo limezua hofu miongoni mwa Wananchi waliokuwa eneo hilo, huku baadhi yao wakilaani tukio hilo na kuitaka Serikali pamoja na vyombo vya usalama kuchukua hatua za haraka ili kubaini ukweli wa tukio hilo na kuwachukulia hatua wahusika endapo madai hayo yatathibitishwa.
Hata hivyo mara baada ya tukio hilo Jeshi la Polisi lilifika eneo la tukio na kuchukua magari yaliyohusishwa (basi na land cruiser) kwa ajili ya uchunguzi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, George Masaju, amezitaka mahakama na wadau wa utoaji haki nchini kuacha kuendekeza uahirishwaji wa kesi usio na sababu za msingi, akisisitiza kuwa Katiba ya nchi inakataza kuchelewesha haki bila sababu ya kimsingi.
Akizungumza wakati wa kufunga mkutano wa wadau kuhusu ushirikiano na mahusiano katika utekelezaji wa majukumu ya utoaji haki mahakamani katika Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma, Jaji Mkuu alibainisha kuwa Ibara ya 107A(2)(b) ya Katiba inaelekeza wazi kutochelewesha haki.
Alieleza kuwa ingawa ni kweli kuwa kesi zitaendelea kuahirishwa kutokana na sababu halisi za kisheria, uahirishwaji unaotokana na sababu zisizo na tija unapaswa kukemewa na kuachwa mara moja.
Alitaja baadhi ya sababu hizo zisizo na tija kuwa ni pamoja na shahidi kutofika, jalada kutokuwa tayari, wakili kutokuwepo, mshtakiwa kutojumuishwa au kutoletwa mahakamani au vielelezo kutofikishwa.
Ili kukabiliana na changamoto hiyo, alipendekeza kuwepo kwa mfumo wa usimamizi wa uwajibikaji ili kuhakikisha kila uahirishwaji unakuwa na sababu halisi na kuwekwa wazi kwenye mfumo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI:
Waziri wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga, na Waziri wa Biashara wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Julien Paluku Kahongya, wamesaini makubaliano ya uwezeshaji na ushirikiano wa kibiashara, yakilenga kukuza biashara na uwekezaji baina ya nchi hizo mbili.
Makubaliano hayo yamesainiwa jijini Dar es Salaam kufuatia ziara ya Rais wa DRC nchini Tanzania, iliyolenga kujadili fursa za kibiashara na uwekezaji, huku DRC ikiendelea kutumia Bandari ya Dar es Salaam katika usafirishaji wa bidhaa kwenda nchini humo.
Akizungumza baada ya ujumbe wa DRC kutembelea Bandari ya Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Sempeho Manongi, amesema DRC ni mshirika muhimu wa Tanzania katika biashara kutokana na fursa zilizopo baina ya nchi hizo mbili.
Amesema maeneo yaliyopewa kipaumbele katika ushirikiano huo ni pamoja na usafirishaji, mauzo ya nje ya bidhaa, uwezeshaji wa biashara, miundombinu na biashara zinazovuka mipaka.
Manongi amesema bidhaa zinazozalishwa DRC, ikiwemo madini, zinaweza kusafirishwa kupitia Bandari ya Dar es Salaam na kutumia miundombinu ya Tanzania, huku bidhaa zinazozalishwa Tanzania zikipata fursa ya kufikia soko la DRC.
Amesema Tanzania na DRC pia zimekubaliana kuanzisha Kamati ya Pamoja ya Kibiashara itakayosaidia kuimarisha ushirikiano na kuboresha mazingira ya biashara baina ya nchi hizo mbili.
Aidha, amesema Tanzania inaendelea kuboresha miundombinu na mazingira ya biashara ili kuongeza biashara na nchi jirani, huku akiwahimiza wadau wa sekta binafsi kuchangamkia fursa zinazotokana na ushirikiano huo. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, George Masaju, ameeleza kuwa kesi za jinai hazianzi mahakamani wala polisi pekee, bali huanzia katika jamii ambako matukio ya kihalifu hutokea.
Akizungumza wakati wa kufunga mkutano wa wadau kuhusu ushirikiano na mahusiano katika utekelezaji wa majukumu ya utoaji haki mahakamani katika Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma, Jaji Mkuu alibainisha kuwa mhalifu anapotenda kosa, vyombo vya sheria kama polisi wakati mwingine huwa hawapo eneo la tukio, hivyo ni muhimu jamii kutoa taarifa.
"Kosa limetendeka kabisa mtu kauawa pale, watu wanajua hawataki kujitolea kutoa taarifa, nani amemuua huyu mtu, sasa polisi unamlaumuje? Kwa hiyo kesi ya jinai inaanza kwenye jamii tu huko tukio lilipotokea," alisema Jaji Mkuu Masaju.
Jaji Mkuu alieleza kuwa mnyororo wa haki jinai ni mpana na mrefu, ukianzia kwenye jamii, ukienda vyombo vya uchunguzi kama Polisi, Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), kisha Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, Mahakamani, na hatimaye gerezani kwa ajili ya marekebisho ya tabia.
Alisisitiza kuwa licha ya kuwa mnyororo huo ni imara, mahakama haiwezi kuwa na ufanisi peke yake ikiwa hatua za awali kabla ya kuingia mahakamani hazijafanya kazi mapema na kwa ufanisi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI:
Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Morogoro imeongeza ufuatiliaji wa hali ya barabara na madaraja katika mkoa huo ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kukabiliana na changamoto zinazoweza kujitokeza wakati wa mvua za El-Nino.
Meneja wa TANROADS Mkoa wa Morogoro, Mhandisi Baraka Mwambage, amesema wataalamu wa Wakala hiyo wamefanya tathmini ya mtandao wa barabara wenye urefu wa kilometa 2,071 pamoja na madaraja 1,032, ili kubaini maeneo yanayohitaji uangalizi wa karibu wakati wa msimu wa mvua.
Amesema tathmini hiyo imewezesha TANROADS kutambua maeneo 49 yanayohitaji ufuatiliaji maalumu na hivyo kuweka mkazo wa maandalizi kulingana na hali ya maeneo hayo.
“Baada ya Serikali kutoa tahadhari ya El-Nino, tulifanya tathmini katika mtandao wetu wote na kubaini maeneo yanayohitaji uangalizi maalumu. Hatua hii inatusaidia kuelekeza ufuatiliaji na maandalizi yetu kwa wakati,” amesema Mwambage.
Amesema TANROADS itaendelea kufuatilia hali ya barabara, madaraja na makalavati na kuchukua hatua za tahadhari pale inapohitajika, huku wananchi wakitakiwa kutoa taarifa mapema endapo wataona changamoto katika miundombinu ya barabara. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, George Masaju, amesisitiza kuwa imani ya wananchi kwa taasisi za haki jinai inapaswa kuwa kipimo kikuu cha mafanikio, huku akipinga vikali kauli za baadhi ya watu wanaodai kuwa mfumo wa haki nchini umeharibika au kuanguka.
Akizungumza wakati wa kufunga mkutano wa wadau kuhusu ushirikiano na mahusiano katika utekelezaji wa majukumu ya utoaji haki mahakamani uliofanyika katika Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma, Jaji Mkuu Masaju alieleza kuwa moja ya matokeo makuu ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 ni kujenga taasisi zinazoaminika na wananchi ili waweze kufanya shughuli zao za kisiasa, kiuchumi na kijamii kwa ufanisi.
Alibainisha kuwa imani hiyo haijengwi kwa maneno matupu, bali kwa wananchi kupata haki na huduma mapema na kwa uwajibikaji wa dhati kutoka kwa watumishi wa umma.
"Imani ya wananchi haijengwi kwa kauli pekee. Inajengwa pale ambapo wananchi wanapata huduma mapema ipasavyo na in this case haki pia ipasavyo... Wanalindwa na sheria. Wanaolalamika wanasikilizwa na wanaona kuna uwajibikaji wa dhati kwa sisi watumishi wao," alisema Jaji Mkuu Masaju.
Jaji Mkuu Masaju alijibu dhana zinazoenezwa na baadhi ya watu wanaojaribu kuaminisha umma kuwa mfumo wa haki jinai Tanzania haufanyi kazi au umeanguka, akisisitiza kuwa vyombo na mifumo hiyo iko imara na inaendelea kutimiza wajibu wake kwa mujibu wa Katiba na sharia.
"Liko kundi lingine linaloaminisha wananchi kwamba hivi vyombo vyote vya mifumo ya haki jinai vime-collapse. Hapana. Sisi lazima tuwe wa kweli kujipima na hata hii mikutano tunafanya kwa sababu hiyo... Hii mifumo iko vizuri na iko imara. Tusiendekeze mambo mengine haya yasiyokuwa na sababu," alisisitiza Jaji Mkuu.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Kikundi cha Mawaziri cha Jumuiya ya Madola (CMAG) kimeihimiza Serikali ya Tanzania kuongeza juhudi na kasi katika kulinda uhuru wa vyombo vya habari, kuendesha mashauri ya kisheria kwa uwazi, na kuweka mifumo inayowajibika ya kutoa fidia kwa walioathirika na migogoro ya kisiasa.
Wito huo umetolewa wakati wa Mkutano wa Dharura wa 74 wa CMAG (CMAG74) uliofanyika tarehe 20 Septemba 2026 jijini New York, Marekani, pembezoni mwa Mkutano Mkuu wa 81 wa Umoja wa Mataifa.
Ikiwasilisha msimamo wake rasmi, CMAG ilirejelea masharti manne yaliyowekwa katika Mkutano wake wa 71 wa Desemba 2025 na matarajio yenye muda maalum wa utekelezaji ya Mkutano wa 73 wa Julai 2026.
Ingawa kamati hiyo ilipongeza hatua zilizopigwa katika baadhi ya maeneo, ilibainisha kuwa mambo muhimu ya kikatiba, haki za binadamu, na demokrasia bado yanahitaji kufanyiwa kazi kwa kina zaidi
"Huku ikikiri maendeleo katika maeneo fulani, CMAG imesisitiza haja ya kazi zaidi ili kuendeleza mchakato jumuishi na unaoaminika wa vyama vya siasa; ulinzi wa uhuru wa kiraia, kisiasa na vyombo vya habari; taratibu za haki, za wakati na za uwazi za kisheria katika kesi zinazoendelea; pamoja na taratibu zinazoaminika za uwajibikaji, urekebishaji na fidia stahiki kwa walioadhirika", imeeleza CMAG.
Ikumbukwe kuwa Julai 10, 2026, Serikali ya Tanzania ilipewa siku 30 CMAG kutatua suala la kuzuiliwa kwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) taifa, Tundu Lissu kupitia njia za kisiasa na kisheria, na kuwaachia huru watu wengine wanaoshikiliwa kwa sababu ya kutumia kile kilichotajwa na Jumuiya hiyo kama haki zao kwa amani.
Aidha, CMAG ilitaka pia kufanyika kwa jukwaa la mashauriano linaloshirikisha vyama vyote vya siasa Tanzania ndani ya siku 90 ili kujadili mageuzi ya mfumo wa uchaguzi, ushindani wa kisiasa, masuala ya mahabusu na uwajibikaji, na ndani ya siku 60 irejeshe uhuru kamili wa matumizi ya mitandao ya kijamii.
CMAG ilitaka pia kuondolewa kwa vikwazo vinavyohusu uhuru wa kukusanyika, kujieleza, shughuli za asasi za kiraia na vyombo vya habari, kufanyika kwa mazungumzo ya kisiasa kati ya vyama, pamoja na kuwepo kwa uwajibikaji kwa wahusika wa matukio ya vurugu na fidia kwa waathirika pale inapostahili.
Mkutano wa karibuni wa CMAG uliongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ulaya wa Malta, Chris Fearne, ukihudhuriwa pia na Makamu wa Waziri Mkuu wa Samoa, Mulipola Anarosa Ale Molioʻo, pamoja na mawaziri na wawakilishi kutoka nchi za Antigua na Barbuda, Botswana, Canada, Grenada, Malaysia, Mauritius, na Zambia
Katika mkutano huo, CMAG ilikuwa na majadiliano na Ujumbe wa Tanzania uliowakilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Mahmoud Thabit Kombo, pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Profesa John Palamagaba Kabudi. CMAG ilitambua na kupongeza ushirikiano wa Tanzania na Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu, mashauriano ya hivi karibuni na vyama vya siasa, pamoja na hatua zinazochukuliwa kuelekea maridhiano ya kisiasa visiwani Zanzibar kama msingi mzuri wa ujenzi wa maendeleo zaidi.
Ili kuendeleza mchakato huo wa mashauriano, CMAG imeihimiza Serikali ya Tanzania kuweka tarehe ya mapema kwa ajili ya ziara ya Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola ili kukutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na wadau wengine wa kisiasa.
Kutokana na tathmini ya jumla, Kamati hiyo imekubaliana kuendelea kuibakiza Tanzania kwenye Agenda yake Rasmi. Hatua hiyo inamaanisha kuwa Tanzania itaendelea kufuatiliwa na CMAG, huku kundi hilo likitarajia maendeleo zaidi katika maeneo yaliyotajwa.
Kabla ya kuanza kwa ajenda za mkutano huo, wajumbe wa CMAG walikaa kimya kwa dakika moja ili kutoa heshima zao kufuatia kifo cha Hafidh Ameir Hassan, aliyekuwa mume wa Rais Samia Suluhu Hassan, aliyefariki dunia tarehe 7 Septemba 2026.
Kamati hiyo ilisisitiza tena utayari wake wa kulinda na kukuza misingi mikuu ya kisiasa ya Jumuiya ya Madola kama ilivyoainishwa kwenye Mkataba wa Jumuiya hiyo (Commonwealth Charter) kupitia Mfumo wa Huduma Njema wa Katibu Mkuu.
Kikao kijacho cha kawaida cha CMAG kinatarajiwa kufanyika Novemba 2026 nchini Antigua na Barbuda, pembeni ya Mkutano wa Wakuu wa Serikali wa Jumuiya ya Madola (CHOGM), ambapo kundi hilo pia litawasilisha taarifa yake ya kila baada ya miaka miwili kwa wakuu wa Serikali. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Moto mkubwa umetokea usiku wa kuamkia leo, Septemba 21, 2026 katika Soko la Machinga jijini Dodoma na kuteketeza vibanda pamoja na mali za wafanyabiashara, huku chanzo cha moto huo kikiwa bado hakijajulikana.
Baadhi ya wafanyabiashara katika soko hilo wamesema walianza kuona moshi kabla ya moto kuzuka, ndipo walipoanza juhudi za kuokoa baadhi ya bidhaa zilizokuwa katika vibanda vyao.
Mmoja wa wafanyabiashara walioathirika amesema amepoteza takribani asilimia 95 ya mali zake kutokana na moto huo, huku akiomba Serikali kuwasaidia wafanyabiashara waliopata hasara.
Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Dodoma, Rehema Menda, amesema chanzo cha moto huo bado hakijajulikana, huku Jeshi hilo kwa kushirikiana na vyombo vya usalama likiendelea na uchunguzi pamoja na hatua za kuhakikisha eneo hilo linakuwa salama.
Aidha Menda amesema Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limefanikiwa kuudhibiti moto huo kwa asilimia 99.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule, amesema hakuna mtu aliyefariki wala kujeruhiwa katika tukio hilo.
Senyamule amewataka wafanyabiashara kuondoka katika eneo hilo nyakati za usiku ili kutoa nafasi kwa vyombo vya usalama kuendelea na shughuli zao.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, George Masaju, amesisitiza kuwa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 inaweka msisitizo mkubwa katika utawala wa sheria, ulinzi wa haki, na uimara wa asasi za kiraia, huku akizitaka taasisi za utoaji haki kuweka mikakati madhubuti ya kutatua changamoto za kiutendaji ili wananchi wapate haki zao kwa wakati.
Jaji Mkuu amezungumza hayo hivi karibuni wakati akifunga mkutano wa wadau kuhusu ushirikiano na mahusiano katika utekelezaji wa majukumu ya utoaji haki mahakamani, uliofanyika katika Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania, jijini Dodoma
Akifafanua misingi iliyowekwa katika Dira 2050, Jaji Mkuu alieleza kuwa utawala wa sheria ni nguzo kuu ya utawala bora inayolenga kujenga jamii yenye usawa, uwajibikaji, haki, na kuaminiana miongoni mwa wadau na wananchi.
Alibainisha kuwa mikutano ya pamoja kati ya wadau wa Mahakama inafanya kazi kubwa ya kuimarisha kuaminiana katika mfumo wa utoaji haki.
"Na katika dira hiyo pamoja na mambo mengineyo inasema dira 2050 inasisitiza utawala wa sheria, ulinzi wa haki na uhuru wa msingi, usalama wa watu pamoja na uimara wa asasi za kiraia. Lakini pia hiyo inasisitizwa mbele zaidi na kusema utawala wa sheria ambao ni kipengele muhimu cha utawala bora unakusudia kujenga jamii yenye usawa, uwajibikaji haki na kuaminiana", alieleza.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyasa na Mbunge wa zamani wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi 'Sugu', ametoa wito kwa serikali kuwaachilia huru Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu, pamoja na vijana wanavyuo wafuasi wa chama hicho na wafungwa wote wa kisiasa kama hatua ya kuonesha nia njema ya mabadiliko na maridhiano nchini.
Akihutubia mkutano wa hadhara leo Septemba 20, 2026, katika Jimbo la Nkasi Kaskazini mkoani Rukwa, Mbilinyi amesema kuwa mfumo wa sasa wa chama tawala umeshindwa kuwaletea wananchi maendeleo na badala yake umejikita katika kukandamiza wanasiasa wa upinzani.
Amesisitiza kuwa changamoto inayoidhoofisha nchi sio mtu mmoja mmoja bali ni mfumo mzima wa chama tawala unaopaswa kuondolewa.
Katika hatua nyingine, kiongozi huyo amegusia uhusiano kati ya Jeshi la Polisi na wananchi, akiwataka askari wa polisi kutogonganishwa vichwa na raia. Amewahakikishia kuwa CHADEMA ikishika dola, itaboresha maslahi, mazingira ya kazi, na kurejesha heshima ya askari katika jamii,This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mtaalamu wa masuala ya ulinzi na usalama aliyewahi kuwa mwanachama wa CHADEMA na baadaye Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Prosper Makonya, ametangaza rasmi kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM), akieleza kuwa amechukua hatua hiyo kwa sababu CCM ni chama cha Watanzania wote.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara wa Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo Taifa, Kenani Kihongosi, uliofanyika Stendi ya Mbondole wilayani Ilala mkoani Dar es Salaam, Makonya amesema atawajibika kukilinda Chama Cha Mapinduzi, mali zake na viongozi wake.
"Na kama kuna mtu anasema hatuwezi, tukutane naye field ndio atajua tunaweza au hatuwezi. Field ndio inayokutambulisha kazi yako.", ameeleza Makonya ambaye pia aliwahi kuwa msaidizi wa aliyekuwa mjumbe wa sekretarieti kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Marehemu Ali Mohamed Kibao akifahamika zaidi kama K2.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Wananchi wa kitongoji cha Midabini katika Wilaya ya Karatu mkoani Arusha, wameiomba Serikali kuchukua hatua dhidi ya vitendo vya ubakaji na ulawiti wanavyodai vimekithiri katika eneo hilo.
Wananchi hao wamesema waathirika wanadaiwa kuwa wanawake, watoto na vijana wa kiume, hali ambayo imewafanya baadhi yao kuishi kwa hofu na hata kushindwa kutoka majumbani kwa shughuli za kawaida.
Wamedai kuwa uuzaji na unywaji wa pombe za kienyeji kuanzia asubuhi hadi usiku ni miongoni mwa changamoto zinazochangia kuongezeka kwa vitendo hivyo, huku uongozi wa kijiji ukikiri kufahamu hali hiyo na kuanza kuchukua hatua.
Mkuu wa Wilaya ya Karatu,Lameck Karanga amemuagiza Mkuu wa Polisi wa eneo hilo kuimarisha operesheni dhidi ya mirungi na uuzaji wa pombe kinyume cha utaratibu, pamoja na kuwachukulia hatua wanaokiuka sheria
Amesema Serikali kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama itaendelea kuchukua hatua kuhakikisha hali ya usalama inaimarishwa na wananchi wanakuwa huru kufanya shughuli zao bila hofu.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyasa, Joseph Mbilinyi (Sugu), amemtaka Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Kenani Kihongosi, kuacha kumzungumzia Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Heche, katika mikutano yake ya hadhara.
Kauli hiyo imetolewa leo, Septemba 20, 2026, wakati Sugu akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la Kilando, Jimbo la Nkasi Kaskazini mkoani Rukwa.
Sugu amesisitiza kuwa viongozi wa CCM wanapaswa kujikita katika kueleza utekelezaji wa ahadi zao kwa wananchi badala ya kutumia mikutano ya hadhara kuwashambulia na kuwazungumzia viongozi wa upinzani kama John Heche.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, Kenani Laban Kihongosi, amesema ujenzi wa Daraja la Majumba Sita katika Jimbo la Segerea wilayani Ilala mkoani Dar es Salaam, utakuwa mkombozi kwa wananchi wanaokabiliwa na changamoto ya mafuriko wakati wa mvua.
Kihongosi amesema ujenzi wa daraja hilo unagharimu zaidi ya Shilingi bilioni 10, huku mkandarasi akiwa tayari amelipwa zaidi ya Shilingi bilioni 5.
Akizungumza leo wakati wa ukaguzi wa mradi huo, Kihongosi amesema Serikali imetenga Shilingi bilioni 4 kwa ajili ya fidia kwa wananchi 483 wanaoathiriwa na mradi, ambapo zaidi ya wananchi 200 tayari wamelipwa. Amesema mradi huo unatarajiwa kukamilika mwezi Desemba, huku maboresho yakihusisha upanuzi wa barabara na ujenzi wa miundombinu ya kudhibiti maji.
Kihongosi amesema utekelezaji wa mradi huo unaonesha kuwa maendeleo yanapaswa kuwafikia wananchi bila kujali chama cha mbunge wa eneo husika.
Aidha, amewataka wananchi kulinda daraja na vifaa vya mradi, huku akizitaka TARURA na taasisi nyingine za Serikali kuendelea kusimamia mradi huo ili ukamilike kwa wakati na kwa thamani ya fedha iliyotolewa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma imekanusha taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu ununuzi wa basi dogo aina ya "Toyota Coaster" mali ya Ofisi hiyo, ikifafanua kuwa ununuzi huo wa Shilingi milioni 334 ulifuata taratibu zote za kisheria kupitia Wakala wa Huduma za Ununuzi Serikalini (GPSA) ili kupunguza matumizi ya fedha za umma
Taarifa kwa umma iliyotolewa leo, Septemba 20, 2026, mjini Songea na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini cha Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, imeeleza kusikitishwa na upotoshaji unaofanywa kwa makusudi kutilia mashaka uhalali na umuhimu wa gari hilo lenye usajili namba STN 7615.
Katika kufafanua dhumuni na mchanganuo wa ununuzi huo, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa imeeleza: “Ofisi ya Mkuu wa Mkoa inapenda kuujulisha Umma kuwa taarifa zinazosambazwa mitandaoni zimepotosha maudhui ya nia njema ya ununuzi wa gari hilo kwa makusudi kwa kuonesha na kutilia mashaka uhalali na umuhimu wa ununuzi wa gari hilo. Hivyo Ofisi inajulisha kuwa ununuzi wa gari hilo ulifuata taratibu za ununuzi wa magari ya Serikali kupitia Wakala wa Huduma za Ununuzi Serikalini (GPSA) ambapo gari hilo lenye usajili STN 7615 limenunuliwa jipya na la kisasa kwa gharama ya Shilingi za Kitanzania Milioni 334 likiwa halijatembea (kilometra sifuri - 0 km)".
Taarifa hiyo imebainisha kuwa basi hilo lenye uwezo wa kubeba abiria 30 limenunuliwa maalum kwa ajili ya kuboresha usafiri wa watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na wadau wa maendeleo wanapokwenda kutekeleza shughuli za maendeleo za wananchi wa Mkoa wa Ruvuma. Aidha, imeelezwa kuwa hatua hiyo inalenga kubana matumizi, kwani gari hilo litakuwa mbadala wa kutumia magari mawili hadi matano kwa safari moja, hivyo kupunguza matumizi ya mafuta na uchakavu wa magari madogo
"Ofisi ya Mkuu wa Mkoa inatoa wito kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii, wadau wa habari, Wanahabari na wananchi kwa ujumla kutumia uhuru wa kujieleza kwa kuzingatia ukweli, uhalisia wa jambo ili kuepuka kutoa taharuki kutokana na maneno yenye lengo la kupotosha lengo la ununuzi wa gari hilo", imeeleza taarifa hiyo.
Ofisi hiyo imewataka wananchi kupuuzwa kwa taarifa hizo zinazosambazwa mitandaoni zenye nia ya kupotosha ukweli, ikisisitiza kuwa itaendelea kusimamia rasilimali za umma kwa uadilifu mkubwa kwa ustawi wa wana-Ruvuma na taifa kwa ujumla -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, Kenani Laban Kihongosi, amesema Rais Samia Suluhu Hassan amethibitisha kuwa ana uwezo wa kuliongoza Taifa, akitaja utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika kipindi cha uongozi wake.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara unaofanyika katika Stendi ya Mbondole, wilayani Ilala mkoani Dar es Salaam, Kihongosi amesema miradi ya umeme, reli na madaraja ni miongoni mwa maeneo ambayo yanaonesha hatua zilizopigwa chini ya uongozi wa Rais Samia.
"Dkt. Samia amethibitisha kwamba uongozi sio jambo la kujaribiwa. Amethibitisha kwamba taifa hili analiweza kuliongoza kwa viwango vikubwa kabisa... Katika miaka yake minne aliyokaa madarakani rekodi za maendeleo alizoziweka ni rekodi ambazo hazijawahi kuwekwa ndani ya taifa hili. Ndio maana tunasema mnyonge mnyongeni haki yake mpeni. Alikuwa na uwezo wa kusema miradi hii mikubwa ya umeme, miradi ya reli, miradi ya madaraja, hii miradi mimi siiendelezi kwa sababu bado ninataka kufanya vitu vyangu. Lakini kwa mapenzi ya taifa hili na kwa mapenzi ya watangulizi wake akasema nitakamilisha iliyoanzishwa na nitaanzisha mipya", ameeleza Kihongosi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, Kenani Laban Kihongosi, amesema Tanzania ina vyama vya upinzani ambavyo havijaonesha uwezo wa kuongoza nchi.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara unaofanyika katika Stendi ya Mbondole, wilayani Ilala mkoani Dar es Salaam, Kihongosi amesema Tanzania inahitaji viongozi wenye weledi, uzalendo na uwezo wa kuelewa mahitaji ya wananchi, akisisitiza kuwa nchi si sehemu ya kufanyia majaribio ya uongozi.
Amesema CCM inaendelea kuwa chama kiongozi nchini, huku akivitaka vyama vya upinzani kuacha kulalamika pekee na badala yake kutoa hoja na suluhisho mbadala kwa changamoto zinazolikabili taifa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Kenani Kihongosi, amewataka wananchi kutokubali kushawishiwa kuwachukia askari na vyombo vya ulinzi na usalama nchini.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara unaofanyika katika Stendi ya Mbondole, wilayani Ilala mkoani Dar es Salaam, Kihongosi amesema askari wana jukumu la kulinda maisha na mali za wananchi, huku wengine wakilinda mipaka ya nchi na kutekeleza wajibu wao kwa mujibu wa kiapo walichokula.
Amesema wananchi wanapaswa kutambua mchango wa vyombo vya ulinzi na usalama katika kulinda amani na utulivu wa taifa, akiwataka kuviheshimu na kuendelea kushirikiana navyo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Akizungumza wilayani Ilala mkoani Dar es Salaam, Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, Kenani Laban Kihongosi, amewataka wananchi kutokubali kushawishiwa kushiriki maandamano kwa maslahi ya watu wengine.
Kihongosi amewataka wananchi kuendelea na shughuli zao za uzalishaji, ikiwemo biashara, ujasiriamali na usafirishaji, akisisitiza umuhimu wa kulinda maisha na shughuli zinazowaingizia kipato.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, Kenani Laban Kihongosi, amesema haiwezekani kuzungumzia maendeleo mbalimbali nchini bila kutaja mchango wa Chama Cha Mapinduzi.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara unaofanyika katika Stendi ya Mbondole, wilayani Ilala mkoani Dar es Salaam, Kihongosi amesema CCM imekuwa ikiongoza nchi tangu kabla ya uhuru, baada ya uhuru na hadi sasa, akitaja sekta mbalimbali ikiwemo elimu, mikopo ya wanafunzi, ujenzi wa barabara na usambazaji wa umeme kuwa sehemu ya maeneo ambayo Serikali imeendelea kuyatekeleza.
Kihongosi amesema hata baadhi ya watu wanaokosoa Serikali na CCM kupitia mitandao ya kijamii wanaendelea kutumia na kunufaika na miundombinu iliyojengwa na Serikali, ikiwemo barabara za lami.
“Hata hao wanaopiga makelele kina Heche wanatembea kwenye lami zilizojengwa na serikali ya Chama Cha Mapinduzi. Kule Tarime kule kwa Heche umeme upo, sasa hivi unawaka vizuri kwasababu ya serikali ya Chama Cha Mapinduzi", ameeleza.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, Kenani Laban Kihongosi, amesema kuwa na wazee ndani ya Chama Cha Mapinduzi si jambo la aibu, akisisitiza kuwa wazee wana nafasi muhimu katika jamii na ndani ya chama.
Akizungumza Ilala, Dar es Salaam, Kihongosi amesema hoja kwamba CCM ni chama cha wazee haipaswi kuchukuliwa kama kasoro, kwa kuwa kila mtu ni mzee mtarajiwa.
Amesema chama cha siasa kinahitaji wazee kwasababu wana uzoefu na busara zinazosaidia katika kusuluhisha changamoto na migogoro ndani ya jamii na chama.
Kihongosi amesema CCM inawaheshimu na kuwathamini wazee kutokana na mchango wao katika ujenzi wa taifa, akieleza kuwa wazee wa leo ndio vijana waliowahi kushiriki katika harakati za kupigania uhuru wa Tanzania.
Amesisitiza kuwa CCM itaendelea kuwaheshimu na kuwathamini wazee, akisema bila mchango wao taifa la Tanzania lisingekuwa lilivyo leo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, ametoa wito kwa vyama vyote vya siasa na wananchi kuungana kwa pamoja ili kulinda amani na mshikamano wa taifa, huku akionya kuwa serikali haitawavumilia wale wanaozembea maendeleo au kuvunja sheria mkoani humo.
Kauli hiyo imetolewa leo Jumapili wakati wa mkutano wa hadhara wa Chama Cha Mapinduzi unaofanyika katika Stendi ya Mbondole, Wilayani Ilala jijini Dar es Salaam, ukimshirikisha Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Kenani Kihongosi.
"Huu ni muda mwafaka wa kuwa pamoja kati ya Chama Cha Mapinduzi na wanavyama wote wa vyama vya siasa. Tukipendana kwa pamoja mnatusaidia sisi kulinda amani na mshikamano wa taifa letu", ameeleza.
Akitolea ufafanuzi masuala ya ulinzi na utendaji kazi, Mkuu huyo wa Mkoa amethibitisha kuwa Mkoa wa Dar es Salaam utazidi kuwa salama, huku akitoa onyo kali kwa watendaji wanaozembea kutekeleza wajibu wao wa kuletea wananchi maendeleo
Aidha, amesema serikali itaendelea kutoa elimu kwa wananchi na viongozi wanaokiuka sheria na taratibu, lakini mkono wa sheria utachukua mkondo wake kwa wale watakaogoma kuelimika.
"Mkoa huu utaendelea kuwa salama leo na hata baadaye. Lakini nataka nikuthibitishie kwamba wale wote ambao wanazembea kufanya maendeleo tutakula nao sahani moja vilevile. Lakini jambo la tatu, nataka nikuthibitishie kwamba wale wote ambao wamezoea kuvunja vunja kanuni, taratibu na sheria katika mkoa wetu kazi yetu sisi ni kumwelimisha. Atakapogoma kuelimika mkono wa sheria utachukua mkondo wake", amesisitiza RC Chalamila.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Gazeti la Washington Post limeripoti kuwa kuna uwezekano wanajeshi wengi zaidi wa Marekani wamepoteza maisha katika vita kati ya Marekani na Israel dhidi ya Iran, tofauti na takwimu rasmi zilizowekwa wazi na Wizara ya Ulinzi ya Marekani (Pentagon).
Hata hivyo, Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Pete Hegseth, kupitia mtandao wa X, amekanusha vikali ripoti hiyo na kuitaja kuwa ni "uongo."
Likinukuu maafisa watano ambao hawakutajwa majina, gazeti hilo lilieleza kuwa angalau wanajeshi 22 wa Marekani wamefariki, idadi ambayo ni kubwa kwa wanne ukilinganishwa na takwimu za Pentagon zinazoonesha vifo vya wanajeshi 18 pekee.
Wakati mzozo huo ukiendelea, Spika wa Bunge la Iran, Baqer Qalibaf, ametangaza kuwa nchi yake imewasilisha ujumbe na masharti yake kwa Marekani kupitia wapatanishi, akisisitiza kuwa Iran itapigana na kujadiliana kwa wakati mmoja kwa kuwa hakuna bado utaratibu thabiti wa kusitisha vita.
Qalibaf ameonya kuwa hakutakuwa na mazungumzo wala kufunguliwa tena kwa Mlango-bahari wa Hormuz hadi pale masharti ya Iran yatakapotimizwa kikamilifu. Kauli hiyo iliungwa mkono na Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran, Mohsen Rezaei, aliyeeleza kuwa Tehran inasubiri majibu ya Rais Donald Trump kupitia wapatanishi kutoka Qatar na Pakistan.
Miongoni mwa masharti makuu yanayotakiwa na Iran ni kuachiliwa kwa mali zake zilizozuiwa, kuondolewa kwa mzingiro dhidi ya bandari na meli zake, kusitishwa kwa mapigano katika maeneo yote, na Marekani kuacha kuingilia masuala ya ndani ya Iran. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Habari, Sanaa, Michezo na Utamaduni, Paul Makonda, amehitimisha ziara yake nchini Hispania kwa kutembelea klabu ya soka ya FC Barcelona, ambako amekutana na viongozi pamoja na baadhi ya wachezaji wa klabu hiyo.
Katika ziara hiyo, Makonda amepata fursa ya kubadilishana mawazo na viongozi na wachezaji wa FC Barcelona, huku akiwakaribisha kutembelea Tanzania na kujionea utamaduni, vivutio vya utalii pamoja na fursa mbalimbali zinazopatikana nchini.
Ziara hiyo imeelezwa kuwa sehemu ya juhudi za Tanzania kutumia michezo kama jukwaa la kukuza mahusiano na taasisi za kimataifa, pamoja na kuitangaza nchi katika nyanja za michezo, utalii na utamaduni.
Ziara hiyo inakuja wakati Tanzania ikijiandaa kuwa mwenyeji mwenza wa Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027, pamoja na Kenya na Uganda.
Kupitia maandalizi ya AFCON 2027, Tanzania inapata fursa ya kuongeza mwonekano wake kimataifa na kutumia mashindano hayo kukuza sekta za michezo, utalii na utamaduni, huku Afrika Mashariki ikiwa kitovu cha mashindano hayo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imetangaza kuanza kutoza faini ya hadi Shilingi milioni moja kwa mtu yeyote atakayekiuka taratibu za usafi na kutupa taka hovyo katika maeneo ya jiji.
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, katika zoezi la usafi lililofanyika katikati ya Jiji (City Centre) leo septemba 19, 2026 lililoambatana na uzinduzi wa kampeni ya usafi katika Kata ya Kisutu.
Hatua hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa sheria ndogo ya afya, usafi na usimamizi wa mazingira ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ya mwaka 2024, ambapo Kifungu cha 41 kinaainisha makosa yanayohusu ukiukaji wa matakwa ya sheria hiyo, huku kifungu cha 42 kikieleza adhabu kwa watakaobainika kutenda makosa hayo, ikiwemo faini ya kuanzia shilingi laki tatu hadi shilingi milioni moja.
Mpogolo amewataka wenyeviti wa mitaa, watendaji wa kata na madiwani kusimamia kikamilifu zoezi la usafi katika maeneo yao, akimtaja Diwani Bhojani kuwa mfano wa kuigwa katika kusimamia usafi.
Kwa upande wake, Diwani Tousif Bhojani amesema uzinduzi wa kampeni hiyo ni muendelezo wa kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, la kuhakikisha Jiji la Dar es Salaam linakuwa safi, huku akisema zoezi la usafi katika eneo hilo ni endelevu na hufanyika kila Jumamosi kwa kujumuika.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa @ccmtanzania Kenani Kihongosi, amewataka wananchi wa Temeke kupuuza kile alichokiita 'makelele' ya watu aliodai 'wamefilisika kisera' na kihoja huku akidai kuwa kuna chama kimepoteza mwelekeo wa kisiasa.
Kihongosi ametoa kauli hiyo leo Septemba 19, 2026 wakati akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika Toangoma Temeke, akidai kuwa yapo baadhi ya matukio na migogoro ndani ya chama hicho ambapo wajumbe wa kamati kuu wamekuwa wakifokewa na aliyemuita dada mmoja amabye yupo nje ya nchi.
Amemtaja Godbless Lema kama miongoni mwa wanaofokewa na huyo 'dada' huku akidai kuwa vitendo hivyo haviwezi kutokea kwa mtu kumfokea Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Kenani Kihongosi, amemjibu Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Heche, kuhusu hoja zake za maendeleo ya nchi akisema kiongozi huyo anapotosha umma kuhusu maendeleo ya nchi.
Akizungumza na wanachi wa Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam leo Septemba 19, 2026, Kihongosi amesema kwamba Heche amekuwa akisema katika muaka 60 ya Tanzania hakuna maendeleo yanayofanyika huku akisema kwamba Katika Kijiji Chao haukuwepo lakini sasa upo kwa sababu ya CCM.
"Anasimama mtu anasema miaka 60 hatuoni kilichofanyika, nchi ina rasilimali nyingi. Wewe wewe funga mdomo huo. Yeye anayezungumza kijijini kwake anapozaliwa, umeme kwakina Heche haukuwepo leo unawaka kwa sababu ya Serikali ya CCM" amesema Kihongosi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katibu wa NEC, Itikadi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Kenani Kihongosi, amewataka wananchi wa Temeke kutokubali kuchochewa katika vitendo vya vurugu, akisema baadhi ya wanaohamasisha vurughizo hozo wana vibali vya kuwawezesha kukimbilia nje pamoja na kuwa na familia zinazoishi nje ya Tanzania.
Kihongosi amesema hayo leo Septemba 19, 2026 jijini Dar es Salaam, ambapo amewasihi wananchi kutambua kuwa wakipoteza amani, wao na familia zao ndio watakaobaki kukabiliana na madhara yake, huku akisisitiza kuwa amani ni msingi wa maendeleo ya nchi.
Amesema Tanzania ni urithi wa Watanzania na kila mmoja ana wajibu wa kuilinda, akieleza kuwa kupoteza amani kunaweza kusababisha kusimama kwa shughuli za biashara, elimu, usafiri na miradi ya maendeleo.
Aidha, Kihongosi amewataka wananchi kudumisha upendo, umoja na mshikamano, akisisitiza kuwa amani ya nchi inapaswa kulindwa na Watanzania wenyewe.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Rajabu Mabele, amesema mitandao ya kijamii imekuwa ikitumika kuwapotosha vijana huku akibainisha kuwa suala la uzalendo na Uzalendo wa Kidijitali kwenye silabasi za mafunzo ya JKT litaendelea kuboreshwa zaidi ili kuelimisha vijana juu ya umuhimu wa kutumia vema mitandao hiyo.
Meja Jenerali Mabele ameyasema hayo wiki hii, wakati akifunga ukurasa wa zoezi la uhitimishaji wa mafunzo ya awali ya kijeshi kwa vijana wa Mujibu wa Sheria, Operesheni Linda Amani na Kujitolea katika Kikosi cha Kanembwa JKT kilichopo mkoani Kigoma.
Pia, Meja Jenerali Mabele ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuliwezesha Jeshi la Kujenga Taifa katika kuboresha miundombinu ya vikosi vyake ili liweze kutoa mafunzo kwa vijana wengi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Bodi mpya ya wakurugenzi ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira mjini Njombe (NJUWASA), imeagizwa kuanza kazi mara moja kwa kukagua vyanzo vya maji na miundombinu ili kujiandaa na athari zinazoweza kusababishwa na mvua za El Nino.
Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Wanging’ombe, Zakaria Mwansasu, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Anthony Mtaka, wakati wa uzinduzi wa Bodi hiyo yenye wajumbe 10. Amesema bodi inapaswa kutembelea vyanzo vya maji na kufanya tathmini ya miundombinu, ikiwamo maeneo ya kuchotea maji, ili kuzuia uharibifu unaoweza kusababishwa na mvua kubwa.
“Vyanzo vyetu vingi vya maji ni lazima bodi muende mkatembelee ili mkapange mikakati ya namna ya kuzuia mvua zisije zikabomoa intake zetu ambazo zimejengwa kwa ajili ya kuleta maji,” amesema.
Naye Mkurugenzi wa NJUWASA, Mhandisi Robert Lupoja, amesema mamlaka hiyo kwa sasa inakabiliwa na upungufu wa takribani lita milioni tano za maji kwa siku ambapo mamlaka inaendelea kutekeleza miradi ya kuongeza huduma ya maji, ikiwamo Mradi wa Miji 28.
Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Bodi iliyomaliza muda wake, Eunice Lwendo, amesema katika miaka mitatu ya uongozi wao walifanikiwa kusimamia mamlaka na kuongeza kiwango cha upatikanaji wa maji.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
"Kamati Kuu inasema kuwa, mnamo tarehe 3 mwezi novemba 2025, Kamati Kuu ilipinga uamuzi wa Samia wa kusema ataunda tume hiyo ya uchunguzi, alipoiunda kamati kuu ilitoa tamko la kupinga kuundwa kwa tume hiyo, Kamati Kuu ilisema na inaendelea kusisitiza kuwa tume hiyo ilikuwa imeundwa na mtu ambaye yeye mwenyewe ndiye anatakiwa kuchunguzwa, aidha, wajumbe wake wengi walikuwa na mgongano wa moja kwa moja wa maslahi na wasingetegemewa kuwa huru katika kazi hiyo" amesema Dkt. Nshala.
Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Rugemeleza Nshala ameeleza hayo Septemba 19, 2026 katika Mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Nshala ameongeza kwamba, " kamati kuu ilikumbusha msingi mkuu wa kisheria kuwa mtu hatakiwi kuwa hakimu au mwamuzi katika suala linalomuhusu yeye mwenyewe..., unapokuwa na tume ya aina hiyo, je unategemea kuupata na kuujua ukweli?, jibu ni hapana".This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo amewataka wajasiriamali vijana na wanawake na vijana Jimbo la Ubungo kutumia kwa usahihi mikopo ambayo watapatiwa kwa ajili ya uwezeshaji wa biashara zao.
Prof. Kitila ambaye ni mbunge wa jimbo hilo ametoa wito huo Septemba 18, 2026 alipokuwa akizungumza na wanufaika wa mikopo hiyo inayotolewa kwa ushirikiano wa Taasisi ya Kitila Mkumbo na CRDB Bank Foundation akiwaeleza kuwa amewadhamini wananchi hao kama sehemu ya jitihada za kuongeza nguvu katika mikopo ambayo serikali inatoa kupitia halmashauri
"Hii sio mbadala kwa yale ambayo serikali inayafanya hii ni jitihada ya kuongeza nguvu kwa ile ambayo serikali inafanya katika Halmashauri zetu," amesema Prof. Kitila.
Amewataka wanufaika wa mikopo hiyo kufahamu kuwa ni mikopo kama mikopo mingine ambayo inapaswa kutumika kibiashara na kukuza biashara zao wala si vinginevyo.
Aidha ameisisitiza CRDB kuhakikisha mikopo hiyo inatoka kabla mwezi huu haujaisha ili wafanyabiashara wanufaike na kukuza uchumi wa wanaUbungo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Rugemeleza Nshala, amesema Tume pekee inayoweza kuchunguza mauaji na makosa ya jinai katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 ni lazima itokane na wasimamaizi na wachunguzi huru kama ambavyo ilifanywa baada ya mauaji katika Uchaguzi Mkuu wa Kenya 2007 - 2008, chini ya usimamizi wa Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan.
Dkt. Nshala ameeleza hayo Septemba 19, 2026 jijini Dar es Salaam, alipokuwa akisoma Maazimio ya Kamati Kuu, yaliyotokana na kikao chake cha Agosti 29, 2026, yaliyohusu Tume iliyoundwa kuchunguza makosa ya jinai yaliyojitokeza wakati wa uchaguzi wa mwaka 2025.
"Kamati Kuu inasisitiza kuwa Tume pekee ambayo inaweza kuchunguza mauaji yaliyotokea lazima itokane na usimamizi wa wachunguzi huru wa mauaji hayo, kama ambavyo ilifanywa katika mauaji yaliyotokea wakati wa uchaguzi mkuu wa kenya wa mwaka 2007, 2008" amesema Dkt. Nshala.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI:
Waziri wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga, amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Biashara ya Kimataifa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Julien Paluku Kahongya, pamoja na ujumbe wake, uliopo nchini kwa ziara ya kiserikali.
Katika mazungumzo hayo, yaliyofanyika jana Septemba 18, 2026, Kapinga amesema Tanzania na DRC zina ushirikiano wa muda mrefu katika sekta mbalimbali, ikiwemo usafirishaji na miundombinu ya usafirishaji, hususan matumizi ya Bandari ya Dar es Salaam, akibainisha kuwa Tanzania ina nafasi kubwa ya kuimarisha ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji kati ya nchi hizo.
Amesema Tanzania imejipanga kukuza sekta ya viwanda na biashara kwa lengo la kuchangia kufikia uchumi wa Dola trilioni moja ifikapo mwaka 2050, huku ikiweka mkazo katika kuongeza uzalishaji na kuuza bidhaa zenye thamani iliyoongezwa badala ya kutegemea mauzo ya malighafi pekee.
Kwa upande wake, Waziri wa Biashara ya Kimataifa wa DRC, Julien Paluku Kahongya, amesema nchi hiyo inanufaika kwa kiasi kikubwa na Bandari ya Dar es Salaam, akieleza kuwa sehemu kubwa ya bidhaa zinazoingia DRC hupitia bandari hiyo.
Amesema hali hiyo inafanya mahusiano ya kibiashara kati ya Tanzania na DRC kuwa muhimu, hivyo kuna umuhimu wa kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya nchi hizo mbili.
Ujumbe wa Waziri Kahongya umeambatana na Balozi wa DRC nchini Tanzania pamoja na wawakilishi kutoka serikalini. Ziara hiyo ni mwendelezo wa ziara ya Rais wa DRC nchini Tanzania iliyofanyika Agosti mwaka huu -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI:
Rais wa Marekani Donald Trump, ametangaza kuvipiga marufuku vyombo vya habari CNN, MS NOW na Politico kuingia Ikulu, akivishutumu kuripoti habari za uongo na zenye upendeleo dhidi ya utawala wake.
Marufuku hiyo ameitoa wiki hii alipokuwa akifanya mahojiano katika Ofisi ya Oval akisema ni katika kukabiliana na kile alichokiita habari za uongo zinazochapishwa na vyombo hivyo.
CNN yenyewe imesema marufuku hiyo ni shambulizi lisilo halali dhidi ya uhuru unaolindwa na Katiba ya Marekani, ikisisitiza haki ya kufanya kazi bila kuingiliwa.
Politico nayo imeeleza kuwa itaendelea kuripoti kwa haki na kutetea kwa nguvu haki zake chini ya Marekebisho ya Kwanza ya Katiba yanayolinda uhuru wa habari nchini humo.
Hadi kufikia wakati tangazo hilo linatolewa, chombo cha MS NOW kilikuwa bado hakijatoa jibu rasmi kuhusu hatua hiyo iliyochukuliwa na utawala wa Trump. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkandarasi anayetekeleza Mradi wa Maji wa Miji 28 katika mji wa Kiomboi, wilayani Iramba mkoani Singida, amepewa maagizo makali ya kuhakikisha anakamilisha mradi huo ndani ya muda uliopangwa.
Rai hiyo imetolewa na Waziri wa Maji, Jumaa Aweso alipokuwa akizungumza na wananchi wa Kiomboi mara baada ya kufanya ukaguzi wa hatua zilizofikiwa katika utekelezaji wa mradi huo.
"Mkandarasi huna kisingizio, fedha zipo na vifaa vipo, kama kuna changamoto yoyote wasiliana na Katibu Mkuu wa wizara, ila rai yangu ni mradi ukamilike kwa wakati ili wananchi wapate maji safi na salama," amesema Waziri Aweso.
Aidha, Waziri huyo amewataka wataalamu wa Wizara ya Maji kusimamia kwa ukaribu mradi huo, huku wakizingatia tahadhari zote zinazotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kuhusu uwezekano wa kutokea kwa mvua za El Nino ili kuepusha athari zozote.
Mradi huo wa kimkakati wa Kiomboi unatazamiwa kuwa na uwezo wa kuzalisha lita za maji milioni 2.8 kwa siku, kiasi ambacho kitasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza upungufu ikilinganishwa na mahitaji halisi ya sasa ambayo ni lita milioni 3, wakati uzalishaji wa vyanzo vya sasa ukiwa ni lita milioni 1 tu kwa siku.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Chama cha Walimu na Wafanyakazi wa Shule zisizo za Serikali Tanzania (TPTU) kimedai kubaguliwa na kushindwa kunufaika na fursa mbalimbali zinazotolewa na Serikali ikiwemo ya mafunzo.
Akizungumza na Jambo TV, Katibu Mkuu wa chama hicho, Julius Mabula amedai kuwa mbali na walimu hao kuwa na mchango mkubwa katika taifa hili lakini linapokuja suala la kunufaika na fursa mbalimbali wamekuwa wakiachwa nyuma kwa kigezo cha kutokutambulika.
"Kumbuka hawa walimu wanafanyakazi ya nchi hii, unawanyima fursa ya kuwaendeleza kupitia mafunzo kazini ya mara kwa mara kwenda kuwanoa wakati wanafanyakazi yako, kwa sababu kazi ya kutoa elimu kwenye nchi hii ni ya kazi ya Serikali kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 11 imeelewa wazi," amesema
Kwa upande wa shule, Mabula ameeleza kusikitishwa na madai ya uwepo wa masharti magumu ya upatikanaji wa vibali vya ujenzi wa shule, ushirikishwaji mdogo kwenye maamuzi, sambamba na kukithiri utitiri wa tozo na kodi.
"Mazingira magumu yanayowapa shida, moja ni utaratibu mgumu wa kusajiri shule wanakiri kuwa utaratibu kusajili uliopo ni mgumu sana ikiwemo na masuala ya kibali cha ardhi ili ujenge shule lakini kubwa ni utitiri wa tozo, kodi na ada mbalimbali zinaathiri uwekezaji wao," amesema.
Mabula ameiomba Serikali kuzipa kipaumbele na kushughulikia changamoto hizo pamoja hoja zingine 27 zilizowasilishwa katika mamlaka husika.
Jambo Tv imemtafuta kwa njia ya simu Katibu Mkuu Wizara Ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Carolyne Nombo ambaye hata hivyo amejibu kwa ujumbe mfupi (SMS) kuwa tayari wameshafanya majadiliano na uongozi wa chama hicho na kuwaelekeza kuwa changamoto hizo ziwasilishwe Ofisi ya Waziri Mkuu, ajira na kazi.
"Tulishafanya naye majadiliano na kumjibu kwa barua kuwa masuala hayo awasilishe Ofisi ya Waziri Mkuu Ajira na Kazi ambao ndio wana mandates hizo," amesema Profesa NomboThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Wananchi wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma wameeleza kuridhishwa na kupongeza mafanikio ya Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia, wakieleza jinsi kampeni hiyo ilivyowarahisishia kupata ushauri na huduma za kisheria kwa urahisi katika kutatua changamoto zao mbalimbali.
Akitoa ushuhuda wake, mmoja wa wakazi wa Namtumbo, Amina Abedi Mbawala, amesema kuwa amefaidika moja kwa moja na kampeni hiyo baada ya kupata msaada wa kisheria na ushauri kuhusu mgogoro wa madai ya mirathi ya baba yake, ikiwemo kuandaliwa nyaraka muhimu bila gharama yoyote.
Akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa kampeni hiyo wilayani hapo, Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Juma Zuberi Homera, amewasihi wananchi wenye migogoro au changamoto za kisheria kujitokeza kwa wingi ili kunufaika na huduma hizo zinazotolewa karibu na makazi yao.
Dkt. Homera amefafanua kuwa huduma hizo zinajumuisha masuala mtambuka ya kisheria ikiwemo mirathi, ndoa, talaka, madai, migogoro ya ardhi, pamoja na urahisishwaji wa upatikanaji wa vyeti vya kuzaliwa na vifo.
Aidha, Waziri huyo amebainisha kuwa Wizara imeunda na kupeleka timu maalum ya wataalamu kutoka taasisi mbalimbali wilayani Namtumbo, hatua inayotajwa kuwa ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma za serikali kwa urahisi, kwa wakati, na kwa ufanisi mkubwa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Serikali kwa kushirikiana na wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nzega mkoani Tabora imepiga hatua kubwa katika kutatua kero za wananchi kwenye sekta za elimu, afya, na miundombinu, ambapo wananchi wameanzisha ujenzi wa shule mbili za sekondari kupitia nguvu zao na michango, huku shule nyingine mbili zikijengwa kwa kutumia mapato ya ndani ya Halmashauri.
Miradi hiyo ya kimkakati iliyopo katika Kata za Ndala na Utwigu imekemewa na kukaguliwa rasmi na Mwenge wa Uhuru ukiongozwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa, Wazo Michael, ambaye aliweka mawe ya msingi ili kusaidia kuwaondolea wanafunzi adha ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma za elimu.
Akizungumza kwa niaba ya wananchi, Mbunge wa Jimbo la Nzega Vijijini, Neto Kapalata, ameeleza kuwa changamoto ya wanafunzi kutembea umbali mrefu ndiyo iliyowasukuma wananchi kujichangisha ili kuanzisha shule hizo kwa lengo la kuboresha kiwango cha kitaaluma cha watoto wao.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Naitapwaki Tukai, amebainisha kuwa Serikali imekuwa ikitoa fedha na maelekezo ya utekelezaji, huku akiahidi kusimamia miradi yote kwa ufanisi mkubwa.
Baada ya ukaguzi na uwekaji wa mawe ya msingi, Mkimbiza Mwenge Kitaifa, Wazo Michael, alionyesha kuridhishwa kwake na hatua zilizofikiwa, huku akitoa maagizo maalum kwa Serikali ya Wilaya ya Nzega kusimamia kwa karibu miradi ambayo haijakamilika ili ikamilike kwa wakati na kuzingatia viwango vya ubora vinavyotakiwa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Vijana waliopatiwa mafunzo ya Kijeshi katika kambi ya Maramba wilayani Mkinga mkoani Tanga, wametakiwa kujiepusha na vitendo vya uhalifu na kutumia mafunzo hayo kwa manufaa ya jamii.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Mkinga, Gilbert Kalima, wakati akihitimisha mafunzo hayo yaliyodumu kwa miezi mitatu na kuwahusisha vikosi viwili, Kikosi cha Operesheni ya Kulinda Amani pamoja na Kikosi cha Operesheni ya Nishati Safi, yaliyohitimishwa Septemba 17, 2026.
Kwa upande wake, Kanali Projest Rutaihwa amewasisitiza vijana hao kuzingatia na kuishi kwa vitendo yale waliyofundishwa katika kipindi cha miezi mitatu ya mafunzo.
Aidha, wakisoma risala, Vijana waliopatiwa mafunzo hayo wameeleza changamoto mbalimbali walizokutana nazo wakati wa mafunzo, huku wakisema muda wa miezi mitatu uliotengwa kwa mafunzo hayo haukuwa wa kutosha.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Ramadhani Kingai, aliyetarajiwa kufika Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, leo Septemba 18, 2026, kutoa ushahidi kama shahidi wa sita wa upande wa utetezi katika kesi ya uhaini namba 19605/2025 inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, amekataa kuwa tayari kutoa ushahidi huo.
Akizungumza mbele ya jopo la majaji watatu wakiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru, Tundu Lissu ameeleza kuwa alikutana na DCI Kingai na kuzungumza naye kuhusu maeneo aliyotakiwa kuyatolea ushahidi, lakini afisa huyo alimueleza wazi kuwa hayuko tayari kutoa ushahidi kwa upande wa utetezi.
Lissu, ameongeza kuwa Kingai amedai kuwa hata mashahidi wengine wawili waliotakiwa kupewa wito wa mahakama Jenerali Jacob Mkunda na Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Camilius Wambura watakuwa na msimamo huo huo wakirejea nchini.
Kutokana na mazingira hayo, Lissu ameiomba mahakama kumruhusu kufunga ushahidi wa upande wa utetezi, kwani hawezi kuwalazimisha mashahidi hao, huku akiomba ipangwe tarehe maalum kwa ajili ya kusikiliza hoja za mwisho (Final Submissions) za pande zote mbili.
Kwa upande wake, upande wa mashtaka uliungana na ombi hilo huku ukihoji kama uwasilishaji wa hoja hizo utafanyika kwa njia ya mdomo au maandishi, ambapo Lissu alifafanua kuwa utakuwa wa mdomo kutokana na yeye kuwa gerezani na kukosa zana ambazo upande wa Jamhuri wanazo.
Mahakama imeahirisha shauri hilo na kupanga kusikiliza hoja za mwisho kwa njia ya mdomo siku ya Jumatano, Septemba 23, 2026.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Kampuni ya Sandaland Fashion Wear Limited imesema inakusudia kuchukua hatua za kisheria dhidi ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, kufuatia kauli yake kuhusu jezi mpya zinazotajwa kuwa za Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars.
Taarifa iliyotolewa na kampuni hiyo leo Septemba 18, 2026 imesema kauli ya Makonda imeathiri jina, hadhi na biashara ya kampuni hiyo, ambayo inadai kuwa inahusika katika uzalishaji na usambazaji wa jezi hizo kwa mujibu wa mkataba na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Hatua hiyo imekuja baada ya Makonda, Septemba 16, 2026, kuchapisha ujumbe kupitia akaunti yake ya Instagram, akieleza kutoridhishwa na jezi hizo na pia kuhoji matumizi ya picha ya Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma (Mwana FA), katika kuziwasilisha kwa umma ambapo kauli hiyo imeibua mjadala kuhusu jezi hizo pamoja na utaratibu uliotumika katika kuzitangaza.
Katika tamko lake, Sandaland imesema kauli hiyo si kauli ya kawaida kwa kuwa, kwa mtazamo wa kampuni, imehusisha moja kwa moja jina na bidhaa zake na inaweza kusababisha madhara ya kibiashara.
Aidha Kampuni hiyo imesema imepokea kwa masikitiko kauli hiyo na kwamba haitakaa kimya, huku ikisisitiza kuwa jezi hizo zimezalishwa na kusambazwa katika utekelezaji wa majukumu yake ya kimkataba na zimewahi kutumika na Timu za Taifa za wanaume na wanawake. "Sandaland inakusudia kuchukua hatua za kisheria juu ya kauli hiyo”, ikieleza kuwa tayari imeona madhara ya kiuchumi na ya kihadhi.
Chanzo cha mgogoro huo ni kauli iliyotolewa na Waziri Makonda kupitia Instagram, ambapo alikosoa ubora wa jezi hizo na kusema ofisi yake haikuwa na taarifa kuhusu matumizi ya picha ya Naibu Waziri. Waziri huyo alinukuliwa akisema: “Hii sio jezi ya Taifa Stars. Taifa Stars kwa ubora wake hatuwezi kuwa na jezi za kiwango cha chini hivi. Acheni kutumia picha za Naibu wangu huku ofisi yangu haina taarifa. Tuheshimiane.” -
Jambo TV
@Jambotv_
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Ramadhani Kingai, aliyetarajiwa kufika Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, leo Septemba 18, 2026, kutoa ushahidi kama shahidi wa sita wa upande wa utetezi katika kesi ya uhaini namba 19605/2025 inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, amekataa kuwa tayari kutoa ushahidi huo.
Akizungumza mbele ya jopo la majaji watatu wakiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru, Tundu Lissu ameeleza kuwa alikutana na DCI Kingai na kuzungumza naye kuhusu maeneo aliyotakiwa kuyatolea ushahidi, lakini afisa huyo alimueleza wazi kuwa hayuko tayari kutoa ushahidi kwa upande wa utetezi.
Lissu, ameongeza kuwa Kingai amedai kuwa hata mashahidi wengine wawili waliotakiwa kupewa wito wa mahakama Jenerali Jacob Mkunda na Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Camilius Wambura watakuwa na msimamo huo huo wakirejea nchini.
Kutokana na mazingira hayo, Lissu ameiomba mahakama kumruhusu kufunga ushahidi wa upande wa utetezi, kwani hawezi kuwalazimisha mashahidi hao, huku akiomba ipangwe tarehe maalum kwa ajili ya kusikiliza hoja za mwisho (Final Submissions) za pande zote mbili.
Kwa upande wake, upande wa mashtaka uliungana na ombi hilo huku ukihoji kama uwasilishaji wa hoja hizo utafanyika kwa njia ya mdomo au maandishi, ambapo Lissu alifafanua kuwa utakuwa wa mdomo kutokana na yeye kuwa gerezani na kukosa zana ambazo upande wa Jamhuri wanazo.
Mahakama imeahirisha shauri hilo na kupanga kusikiliza hoja za mwisho kwa njia ya mdomo siku ya Jumatano, Septemba 23, 2026. -
Jambo TV
@Jambotv_
BREAKING:
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amemteua tena Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo, Othman Masoud Othman (OMO) kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Septemba 18, 2026 na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi wa Zanzibar, Mansura Kassim, uteuzi huo umeanza rasmi leo.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais mteule ataapishwa Jumanne, Septemba 22, 2026, saa 4:00 asubuhi katika hafla itakayofanyika Ikulu, Zanzibar.
Othman Masoud Othman aliwahi kushika nafasi hiyo kuanzia Machi 2021, baada ya kuteuliwa na Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi kuchukua nafasi iliyoachwa na aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, aliyefariki Februari 2021. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Inaelezwa kiwa kanuni mpya za alama za leseni zinawahusu pia waendesha pikipiki, ambapo Jeshi la Polisi limesema madereva wanaweza kukatwa pointi kutokana na makosa ya usalama barabarani, ikiwemo kutovaa helmeti na kutokuzingatia taa za kuongozea magari.
Akizungumza na Jambo TV kuhusu mfumo huo, Mrakibu wa Polisi Mussa Manyama ambaye no Mkuu wa Kitengo cha Sheria kutoka Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, amesema dereva wa pikipiki anayefanya kosa kubwa linalohatarisha usalama ikiwemo kubeba mshikaki, kudharau taa nyekundu, pamoja na kupita magari sehemu isiyo sahihi atakatwa.
🎤@mckamendu
📸 @shabih_kassim291
🔴Tufuatilie kupitia YouTube yetu ya Jambo Tv, Subscribe, Like na Comment ili usipitwe na taarifa muhimu kutoka kila kona.
Kama una habari yoyote tutumie ujumbe DM au tupigie kwenye namba +255 767 252 999This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Tarehe 17 Septemba 2026 Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Masjala Ndogo ya Tabora, iliitishwa kwa ajili ya kutaja Shauri la Kikatiba Na. 000023438 la mwaka 2026 linalopinga uamuzi wa kuwazuia mawakili kuzungumza na vyombo vya habari wakiwa katika maeneo ya Mahakama.
Shauri hilo limefunguliwa na Mawakili Nyaronyo Kicheere, Sisty Massawe, Emmanuel Chengula, Paul Kisabo @Advocate_Kisabo , na Alphonce Lusako , huku Wajibu Maombi wakiwa ni Jaji Mkuu wa Tanzania, Jaji Kiongozi, na Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS). Shauri hilo linasikilizwa na jopo la majaji watatu ambao ni Mhe. M. Mnyukwa, Mhe. R.B. Massam, na Mhe. M.B. Mpaze
Katika kesi hiyo, waombaji wanapinga zuio hilo la jumla lililowekwa kupitia maelekezo ya kiutawala ya tarehe 5 Agosti 2026 na taarifa ya Msajili wa Mahakama Kuu ya tarehe 12 Agosti 2026. Wanadai kuwa zuio hilo linaathiri haki za kikatiba ikiwemo usawa mbele ya sheria, uhuru wa kutoa maoni, uhuru wa vyombo vya habari, na haki ya wananchi kupata taarifa za masuala muhimu kwa jamii
Wanadai kuwa mawakili ni maofisa wa mahakama na kwamba sheria zilizopo za maadili hazijaweka zuio la jumla kwa mawakili wote kuzungumza na vyombo vya habari katika maeneo ya Mahakama. Hoja yao ni kwamba, endapo wakili fulani atakiuka sheria au maadili ya taaluma, hatua zichukuliwe dhidi ya wakili huyo binafsi badala ya kuwazuia mawakili wote nchini.
Kutokana na hoja hizo, Waombaji wanaiomba Mahakama kutamka kuwa zuio hilo linakiuka Katiba na kurejesha haki ya mawakili kuzungumza na vyombo vya habari maeneo ya Mahakama kwa kuzingatia maadili ya taaluma zao.
Katika kutajwa kwa shauri hilo kwa njia ya mtandao Septemba 17, 2026, waombaji waliwakilishwa na Wakili Mwandamizi Mpale Kaba Mpoki pamoja na Wakili Jebra Kambole. Jaji Mkuu na Jaji Kiongozi waliwakilishwa na Wakili wa Serikali Jacqueline Kinyasi, huku TLS ikiwakilishwa na Mawakili Akram Magoti na Kelvin Kayaga.
Wakati wa kutajwa kwa shauri, Mahakama iliibua yenyewe hoja ya kutomjumuisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) kama Mjibu Maombi na kuwaamuru Waombaji kuwasilisha sababu zao ifikapo tarehe 01 Oktoba 2026. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI:
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Ramadhani Kingai, leo Septemba 18, 2026 anatarajiwa kupandishwa kizimbani kwaajili ya kuanza kumtetea Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, katika kesi ya uhaini namba 19605/2025 inayomkabili.
Kingai atapandishwa kizimbani akiwa ni shahidi wa sita wa upande wa utetezi ambapo ataongozwa na Tundu Lissu katika kutoa ushahidi wake.
Kama ilivyo kwa mashahidi wengine waliopita, Kingai baada ya kuhitimisha kutoa utetezi wake mbele ya jopo la majaji watatu wakiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru, upande wa Jamhuri wataruhusiwa na Mahakama kumuuliza shahidi huyo maswali ya dodoso (Cross-examination) na baadaye Lissu ataruhusiwa kuuliza maswali ya ufafanuzi (Re-examination) kwa shahidi huyo ikiwa Lissu atakuwa nayo.
Septemba 16, 2026 shahidi huyo alipaswa kuanza kutoa ushahidi wake lakini ilishindikana kutokana na yeye shahidi kuwa nje ya nchi. Mashaidi wengine ambao wanatarajiwa kufika mahakamani kwaajili ya kumtetea Lissu, ni pamoja na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Camillus Wambura na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF), Jenerali Jacob Mkunda.
Hata hivyo, Lissu aliieleza Mahakama kwamba mashahidi hao wawili wapo nje ya nchi kwa sasa na haifahamiki watarejea lini, huku akisema ikiwa atamalizana na DCI Kingai na mashshidi hao wakawa bado hawajarejea nchini ataieleza mahakama ikiwa anafunga zoezi la ushahidi wake au nini kifanyike kwa mwongozo wa Mahakama. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Dennis Londo, amewataka wafanyabiashara wa Tanzania kutumia fursa kupitia Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na Soko Huru la Afrika, kuuza bidhaa zao.
Londo ameyasema hayo jana Septemba 17, 2026 wakati alipokuwa akifunga hafla ya utoaji tuzo za jukwaa la 4 la biashara na uwekezaji kwa Watendaji Wakuu na Wakurugenzi wa makampuni 200, ambalo linawakutanisha wadau kujadili namna ya kufungua fursa
Kwa watanzania, wajasiriamali kufanya biashara nje ya Tanzania.
Londo amesema kuwa uwepo wa jukwaa hilo unasaidia kuwakutanisha Wakurugenzi wa Makampuni mbalimbali kubadilishana uzoefu na kuchangamkia fursa zilizopo.
Aliongeza kuwa Tanzania ni mwanachama wa EAC na SADC na sasa inaelekea kwenye Itifaki ya Soko Huru la Afrika, hivyo maandalizi ni sehemu muhimu ya kuhakikisha Watanzania wanashiriki na kunufaika na jumuiya hizo.
Amesema Wizara ya viwanda na Biashara itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa ajili ya wafanyabiashara kufungua fursa zaidi kwa kushirikiana na sekta binafsi ili kukuza uchumi wa nchi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Jeshi la Polisi limeeleza kuwa kuendesha gari kwa mwendo mdogo bila sababu ya msingi, hali inayoweza kuwasumbua au kuwazuia watumiaji wengine wa barabara, na ni kosa la usalama barabarani linaweza kusababisha dereva kukatwa alama moja kwenye leseni yake ya udereva.
Akizungumza na Jambo TV kuhusu mfumo wa alama za leseni, Mrakibu wa Polisi Mussa Manyama ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Sheria kutoka Jeshi la Polisi, Kikosi cha Usalama Barabarani, amesema sheria inaweka utaratibu wa matumizi sahihi ya barabara, ikiwemo kuzingatia viwango vya mwendo vinavyoelekezwa katika maeneo mbalimbali.
Manyama amesema dereva anapaswa kuendesha kwa mwendo unaoendana na mazingira ya barabara na watumiaji wengine, akieleza kuwa kuendesha mwendo mdogo kupita kiasi bila sababu za msingi na kusababisha kero au foleni kwa watumiaji wengine ni ukiukwaji wa sheria.
Mahojiano kamili yapo kwenye YouTube yetu ya Jambo TV
@GodwillKamendu -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mama mjamzito, Scholastika Mgimba, aliyepoteza shilingi 400,000 katika moto ulioteketeza nyumba yake eneo la Mtaa wa Kambarage, Njombe, amekabidhiwa shilingi 500,000 na Halmashauri ya Mji wa Njombe. Mgimba alipoteza fedha hizo baada ya nyumba hiyo kuteketea kwa moto usiku wa Septemba 10, 2026.
Fedha hizo zilikabidhiwa na Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Juma Sweda, kwa niaba ya Halmashauri, ikiwa ni sehemu ya msaada kwa waathirika wa tukio hilo. Mbali na fedha hizo, Halmashauri imekabidhi vitanda, magodoro na vifaa vingine kwa waathirika wa moto huo.
Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo, Sweda amemtaka Mgimba kuendelea kujiandaa kwa ajili ya kujifungua licha ya changamoto iliyomkuta, huku akimshauri kufika hospitalini kwa ajili ya uchunguzi endapo bado hajapata fursa ya kufanya hivyo.
“Uwe na furaha na usiende kumpa mtoto jina Moto au Matatizo. Sisi tunakuombea na kama hujapata fursa ya kwenda hospitali, basi baada ya zoezi hili uende wakakucheki,” amesema Sweda.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Njombe, Erasto Mpete, ameishukuru Halmashauri pamoja na uongozi wa Mtaa wa Kambarage kwa hatua za haraka walizochukua kuwasaidia waathirika.
Baadhi ya waathirika, akiwemo Erasto Mhagama, amesema tukio hilo limewaweka katika hali ngumu na kuwashukuru Watanzania kwa michango na msaada wanaoendelea kuwapatia.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI PICHA:
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, John Heche akiwa kwenye picha ya pamoja na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA Godbless Lema, Makamu Mwenyekiti CHADEMA upande wa Zanzibar, Said Mzee; na Mwanasheria Mkuu wa chama hicho Dkt.Rugemeleza Nshala baada ya kikao kilichofanyika leo Septemba 17, 2026 jijini Dar es Salaam.
Viongozi hao wamekutana katikati ya uwepo wa madai ya kutuhumiana na kurushiana maneno baina ya viongozi na wanachama wa chama hicho ambayo yamekuwa yakionekana katika majukwaa ya mitandao ya kijamii, madai ambayo yamewahusisha pia wanaharakati, hivyo kikao hicho kimetajwa kuwa sehemu ya jitihada za kuimarisha Umoja na mshikamano ndani ya chama hicho kikuu cha upinzani nchini Tanzania. -
Jambo TV
@Jambotv_
Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete, amewatoa hofu wanaume na kuwataka kujenga utamaduni wa kupima tezi dume mara kwa mara ili kugundua na kutibu ugonjwa huo mapema, akisisitiza kuwa teknolojia ya sasa imerahisisha vipimo kupitia damu (PSA) tofauti na ilivyokuwa zamani.
Kikwete ametoa wito huo jana jijini Dar es Salaam alipokuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya Mwezi wa Uelewa wa Saratani ya Tezi Dume yaliyofanyika katika Hospitali ya Kairuki, Mikocheni, ambapo pia alipata fursa ya kukagua mtambo wa kisasa wa High Intensity Focused Ultrasound (HIFU) unaoondoa vimbe mwilini bila kufanyiwa upasuaji kwa kutumia mwangwi wa sauti.
Aliwataka wanaume wasiogope kwenda kupima saratani ya tezi dume kwani teknolojia kwa sasa imekwenda mbali zaidi na ugonjwa unaweza kuonekana kwa kutumia kipimo cha damu cha PSA tofauti na njia ya zamani ya kutumia kidole.
Katika ushuhuda wake, Rais huyo mstaafu alifunguka kuwa yeye mwenyewe ni mwathiriwa aliyegundulika kuwa na dalili hizo mwaka 2014, hatua iliyomfanya kwenda Marekani kufanyiwa upasuaji na mpaka sasa anaendelea vizuri kabisa kiafya.
“Baada ya kufanyiwa upasuaji wakati ule nilianza kujenga utaratibu wa kupima afya yangu mara nyingi sana na kwa sasa afya yangu ni njema kabisa ndiyo maana mtu akisema naumwa nacheka tu kwasababu afya yangu naijua ni nzuri sana,” alisema Kikwete.
Aidha, aliipongeza Hospitali ya Kairuki kwa kuleta mtambo huo wa HIFU, akisema ungewepo wakati wa matibabu yake huenda asingehangaika kusafiri nje ya nchi, huku akisisitiza Serikali kuongeza mitambo mingi ya namna hiyo ili kuwapunguzia wananchi adha ya kutegemea kituo kimoja pekee.
Kwa upande wake, Mtaalamu wa mtambo wa HIFU hospitalini hapo, Fredy Felician, ameeleza kuwa tangu kusimikwa kwake, watu 444 wamehudumiwa kwa kuondolewa vimbe za aina mbali mbali, wakiwemo wanaume 95 waliotibiwa saratani ya tezi dume.
Naye Mkurugenzi wa Hospitali hiyo, Dk. Asser Mchomvu, amebainisha takwimu zinazoonyesha kuwa saratani ya tezi dume ndiyo inayoongoza kwa wanaume nchini Tanzania ikichangia kati ya asilimia 31.4 na 40 ya kesi zote za saratani kwa wanaume na kuwa chanzo cha tatu cha vifo vitokanavyo na saratani huku asilimia 43.6 ya wagonjwa wakichelewa kufika hospitalini na kugundulika wakiwa katika hatua ya ugonjwa uliosambaa. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
📍DODOMA - Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Deus Clement Sangu, ametoa wito kwa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) kuendesha uchaguzi wake kwa kuzingatia Katiba, demokrasia, uwazi, haki, usawa na amani.
Sangu ameyasema hayo, leo Septemba 17, 2026, wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa TALGWU, akisisitiza kuwa uchaguzi huo uwe fursa ya kuimarisha umoja na mshikamano badala ya kuwa chanzo cha mgawanyiko.
“Uchaguzi usiwe chanzo cha mgawanyiko, bali uwe fursa ya kuimarisha umoja na mshikamano, baada ya matokeo kutangazwa, viongozi na wanachama wote wanapaswa kuendelea kushirikiana, kwa kutambua kwamba TALGWU ni kubwa kuliko mtu mmoja,” amesema Sangu. -
Jambo TV
@Jambotv_
ACT YATEUA JINA LA ANAYEPENDEKEZWA KUWA MAKAMU WA RAIS WA ZANZIBAR jambo.co.tz/act-yateua-jina-la-anayependekezwa-kuwa-makam… via @jambotv_
-
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mzee Alute Mughwai Lissu, wakili mwandamizi na kaka wa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) @ChademaTZ2 , Tundu Lissu, amefunguka na kujibu tuhuma zilizotolewa na mwanaharakati Mange Kimambi, zinazomhusisha kulipiwa malazi katika hoteli ya kifahari jijini Dar es Salaam kwa zaidi ya miezi miwili.
Mange Kimambi @mangekimambi alitoa tuhuma hizo kupitia mitandao ya kijamii, akidai kuwa malipo hayo yalilenga kusaidia kufanikisha kuachiwa kwa Tundu Lissu, ambaye anakabiliwa na kesi ya uhaini.
Akizungumza leo, Septemba 17, 2026, jijini Arusha, Alute amekanusha madai hayo, akisema kwa muda mrefu amekuwa akisumbuliwa na matatizo ya kiafya yaliyomlazimu kulazwa hospitalini, na kwamba ameshangazwa na taarifa zinazodai amelipiwa malazi katika hoteli hiyo.
Alute amesema taarifa hizo si za kweli na ametoa wito zipuuzwe, akieleza kuwa mara ya mwisho kwenda Dar es Salaam ilikuwa Agosti 15, 2026, na tangu wakati huo hajarejea jijini humo.
“Mara ya mwisho kwenda Dar es Salaam ilikuwa ni mwezi wa nane, tarehe 15, na sijarudi tena. Kwa hiyo hiyo taarifa iliyotolewa na Mange Kimambi ni uongo. Taarifa hizo zinanisikitisha, mimi nipo kitandani, yeye anasema mimi nipo Seacliff?” amesema Alute.
....Tazama video hii kwa kirefu kupitia chaneli ya Youtube ya Jambo TV.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
ANAYETUHUMIWA KUMKATA SCOLA VIGANJA VYOTE VYA MIKONO AKAMATWA jambo.co.tz/anayetuhumiwa-kumkata-scola-viganja-vyote-vya… via @jambotv_
-
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Wakati kiwanda kipya cha kuchakata pamba mkoani Mwanza kikianza rasmi majaribio ya mitambo yake, hatua inayotajwa kumaliza kiu ya muda mrefu ya ukosefu wa viwanda vya uchakataji wa zao hilo mkoani humo, wasiwasi wa changamoto ya umeme imeibuka na kutajwa kuwa ni tishio kwa uzalishaji wake.
Akizungumza Septemba 17, 2026 wakati wa majaribio ya uwashaji wa mitambo hiyo, Meneja Viwanda Chama Kikuu cha Ushirika cha Nyanza (NCU), Elisha Midamo, amesema tangu Septemba 3, 2026 kiwanda hicho kilipoanza kufanyiwa majaribio kimekuwa kikikumbwa na tatizo la umeme jambo ambalo linasababisha mitambo kushindwa kufanya kazi ipasavyo na hivyo kuongeza muda wa uzalishaji.
"Katika kuanza kwetu tumepitia changamoto mbalimbali, ya kwanza ni kushuka kwa Voltage za umeme ambapo kiwanda hiki kinahitaji kuanzia Voltage 370 hadi 420 sisi tukawaza kwamba inawezekana tunatumia Transforma ya KVA 500 tunatakiwa tuibadilishe iwe Transforma ya KVA 750 na kuendelea," amesema.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Uongozi ya Chama Kikuu cha Ushirika cha Nyanza (NCU), Leonard Lyabalima amesema kuanza kwa kiwanda hicho ni hatua mkakati ya kurejesha heshima ya kilimo cha pamba Kanda ya Ziwa na kuhakikisha wakulima wanapata soko la uhakika la mazao yao badala ya kutegemea uuzaji wa pamba ghafi.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya NCU, Mariam Mashibe amesema baada ya kusubiri kwa muda mrefu, wamefurahi kuona kiwanda hicho kikianza kazi.
Kiwanda hicho kimegharimu bilioni 3.2 na kikianza kazi rasmi kitakuwa na uwezo wa kuzalisha kilo milioni 20 za pamba kwa msimu mmoja.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Waziri Mkuu wa Tanzania Dkt. Mwigulu Nchemba amewataka wanamipango na viongozi nchini kooanisha mipango na bajeti za serikali ili kuzuia ubadhirifu wa rasilimali kupitia miradi iliyotelekezwa, huku akiagiza ujenzi wa miundombinu ya elimu uzingatie mageuzi ya elimu ya lazima hadi kidato cha nne yanayoanza mwaka 2028.
Kauli hiyo imetolewa leo, Septemba 17, 2026, jijini Arusha wakati Dkt. Mwigulu akizungumza kama Mgeni Rasmi katika siku ya mwisho ya Kongamano la Kitaifa la Wanamipango 2026 linalofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Arusha (AICC) kujadili utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
Amewataka wanamipango na wanaopokea fedha za ujenzi kuanzia sasa kujenga shule zinazoshabihiana na mabadiliko hayo badala ya kuendelea na mifumo ya zamani iliyotenga shule za msingi na sekondari.
"2028 tutaanza utekelezaji wa mageuzi kwenye sekta ya elimu, elimu ya lazima mpaka kidato cha nne. Kwa maana hiyo, kwa lugha nyingine tunaongelea kila kijiji kitakuwa na sekondari yake. Naendelea kuwakumbushia kule, wanaopata fedha kuanzia sasa kujenga shule basi wazijenge shule zinazoakisi mabadiliko haya... Mambo ya mipango na bajeti zetu yaoanishwe", ameeleza Mwigulu.
Akifafanua kuhusu changamoto za miradi inayoanza kabla ya mipango kukamilika au kubadilishwa njiani, Dkt. Mwigulu amebainisha kuwa mabadiliko ya ramani na mipango isiyo na uoanishaji yamesababisha kuwepo kwa maboma ya vituo vya afya na madarasa yaliyokaa kwa miaka 15 hadi 20 bila kukamilika, huku yakiwa yametumia rasilimali nyingi za umma. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI PICHA:
Picha mbalimbali za Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, alipokuwa akizungumza na washiriki wa Kongamano la Kitaifa la Wanamipango 2026 linaloendelea katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Arusha (AICC), Arusha leo.
Kongamano hili limewakutanisha wataalamu, wadau na viongozi mbalimbali kujadili masuala ya mipango, maendeleo na utekelezaji wa mikakati ya kitaifa hasa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mjadala wa Katiba Mpya ulivyojadiliwa kati ya Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana wa ACT Wazalendo Taifa, Abdul Nondo, na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Wakili Boniface Mwabukusi hasa kuhusu mtindo, haraka, na mwelekeo wa kuipata na mfumo wa uwajibikaji nchini.
Katika mjadala huo wa hivi karibuni uliofanyika wakati wa maadhimisho ya Siku ya Demokrasia Duniani yaliyoratibiwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Abdul Nondo alizungumzia suala la muda katika mchakato wa Katiba, akipinga wazo la kuwa na Katiba ya Mpito. Nondo alieleza kuwa mifano ya nchi kama Uganda (1991–1993) na Kenya inaonesha kuwa mchakato wa katiba unaweza kukamilika ndani ya miaka miwili tu iwapo kuna utayari.
Alisisitiza kuwa nchi tayari ina Rasimu ya Warioba na Katiba Pendekezwa kama misingi mizuri ya kuanzia badala ya kuanza upya.
Akijibu na kutoa mtazamo wake, Rais wa TLS, Wakili Boniface Mwabukusi alihoji wanaodai muda hautoshi kwa kuuliza wanalinganisha na nini. Mwabukusi alibainisha kuwa maoni ya Katiba tayari yapo na wala hakuna haja ya kuvumbua gurudumu jipya bali kipaumbele kinapaswa kuwa kujua ukweli wa kilichotokea kwa wananchi waliopotea na sababu za mifumo ya nchi kupooza.
Akiweka msisitizo kwenye uadilifu na mfumo wa uwajibikaji, Mwabukusi alitahadharisha kuwa bila uwajibikaji, hata Katiba ikiwa nzuri kiasi gani inaweza kuangukia mikononi mwa viongozi wabaya.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Alexander Mnyeti, ameamuru gari la Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato aina ya Land Cruiser V8 lipelekwe Kituo cha Afya Muganza likatumike kama ambulance ya kubebea wagonjwa wanaohitaji rufaa kituoni hapo.
Mnyeti ametoa agizo hilo wakati wa mkutano wa hadhara na wananchi katika Soko la Kimataifa la Dagaa Kasenda, lililopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Chato, mkoani Geita, baada ya gari la wagonjwa kuharibika matairi.
"Lamwisho ni kuhusu ambulance, Dereva wa Mkurugenzi uko wapi?, njoo na funguo. Hamuwezi kuwa mnasubiri mkuu wa Mkoa ndiyo mnunue matairi, wewe Mkurugenzi unatakiwa kujua, kwahiyo watu wasiumwe wanasubiri michakato ya matairi?, leta hapa funguo, shika hapa, ambulance yangu hiyo hapo, pelekea gari kituoni" amesema Mnyeti.
Akizungumza katika mkutano huo, Mbunge wa Jimbo la Chato Kaskazini, Cornel Magembe, amemuomba Mkuu wa Mkoa kuhakikisha ambulance ya Kituo cha Afya Muganza inapatiwa matairi mapya ili kurejesha huduma ya usafirishaji wa wagonjwa, hususan wanaohitaji kupewa rufaa kwenda hospitali.
Kabla ya kuanza ziara yake ya kujitambulisha kwa wananchi wa Mkoa wa Geita, Mnyeti alianza kwa kutembelea kaburi la aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, lililopo Chato.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri Mkuu wa Tanzania Dkt. Mwigulu Nchemba ametoa wito wa kupanua wigo wa mapato ya ndani na kuiwezesha sekta binafsi kukuza uzalishaji, akitahadharisha kuwa kuongeza kodi bila kuongeza shughuli za uzalishaji kutawafanya walipakodi kuelemewa.
Kauli hiyo imetolewa leo, Septemba 17, 2026, jijini Arusha wakati Dkt. Mwigulu akizungumza kama Mgeni Rasmi katika siku ya mwisho ya Kongamano la Kitaifa la Wanamipango 2026 linalofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Arusha (AICC) kujadili utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
"Ndio inakuja ile hoja ya lazima tuiwezeshe sekta binafsi kukua. Lazima tuvutie uwekezaji. Lazima tuwe na uwekezaji mkubwa wa ndani na nje. Lazima tuongeze shughuli za uzalishaji. Ukidhania tutaongeza kodi tu bila kuongeza shughuli za uzalishaji itafika siku wataelemewa tu hao wanaotozwa hizo kodi", ameeleza.
Aidha, Waziri Mkuu amehimiza utekelezaji wa mapendekezo ya Tume ya Rais ya Kutathmini Maboresho ya Mfumo wa Kodi ili kuongeza mapato ya ndani, akibainisha kuwa mapato hayo hayawezi kuongezeka kupitia sekta ya umma pekee
Akieleza mabadiliko ya mfumo wa bajeti nchini, Dkt. Mwigulu amebainisha kuwa wakati zamani asilimia 80 ya bajeti za nchi nyingi za Afrika ilitegemea misaada na asilimia 10 hadi 20 pekee ikiwa ni makusanyo ya ndani, hivi sasa maeneo ya misaada kwenye bajeti hayapo tena. Amefafanua kuwa hali hiyo haikutokana na uzembe au diplomasia, bali ni hatua za kimaendeleo zinazoifanya nchi kupoteza vigezo vya kupewa misaada hiyo, jambo linalolazimisha taifa kupanga na kutekeleza mipango yake kwa kujitegemea.
"Sasa tunapopanga katika majira haya hiki tunachotaka kukifikia ni lazima kupanua wigo wa mapato ya ndani ya kodi, vyanzo vya mapato ya ndani. Kwa lugha nyingine tumepanga wenyewe tunatakiwa pia tupange kujitegemea. Tunatakiwa pia tujue tunatakiwa kutekeleza kwa kujitegemea", ameeleza.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri Mkuu wa Tanzania Dkt. Mwigulu Nchemba amesema kuanza kwa baadhi ya wizara kuomba mabadiliko ya bajeti muda mfupi baada ya bajeti ya Serikali kupitishwa kunaonesha mapungufu katika upangaji wa mipango ya utekelezaji.
Akizungumza katika Kongamano la Kitaifa la WanaMipango mkoani Arusha, Dkt. Nchemba amesema bajeti hupitishwa mwezi Juni na kuanza kutekelezwa mwezi Julai, lakini baadhi ya wizara huanza kuomba mabadiliko ya bajeti mara tu mwaka wa fedha unapoanza.
“Unapitisha bajeti mwezi wa sita, mwisho ni pale. Bajeti inaanza mwezi wa saba. Halafu mwezi wa saba huo huo kila wizara inaomba mabadiliko ya bajeti kwamba kile kilichopitishwa na bajeti si hicho wanachotaka kutekeleza, ni kingine wanachotaka kutekeleza na hakina bajeti,” amesema akiongeza kuwa hali hiyo inaonesha umuhimu wa kuimarisha mipango kabla ya bajeti kupitishwa, ili kile kinachopangwa kutekelezwa kiwe na fedha zilizotengwa.
Aidha, Waziri Mkuu amesema wakati mwingine mambo halisi katika jamii hutangulia mipango ya Serikali, hali inayosababisha Serikali kufuatilia baadaye ili kukabiliana na changamoto zilizokwishajitokeza. Ametoa mfano wa shule kujengwa katika eneo la hifadhi bila kuwa sehemu ya mipango, akisema hali hiyo huifanya Serikali kuanza kukimbizana na matukio badala ya kuyapanga mapema.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri Mkuu wa Tanzania Dkt. Mwigulu Nchemba amesema kuwa mtazamo wa kutegemea Serikali pekee katika shughuli za kiuchumi unaweza kuwa kikwazo kwa utekelezaji wa Dira ya 2050 huku akisisitiza umuhimu wa kuongeza ushiriki wa sekta binafsi.
Akizungumza katika leo Septemba 17, 2026 katika Kongamano la Kitaifa la Wanamipango, Dkt. Nchemba amesema Tanzania imeweka mkakati wa kuhakikisha sekta binafsi inashiriki kwa asilimia 70 katika utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, ikiwemo katika uwekezaji, uzalishaji na uanzishaji wa ajira.
Kadhalika, amesema bado kuna mtazamo miongoni mwa baadhi ya Watanzania kwamba shughuli zinazofanywa na Serikali ndizo zinazochukuliwa kuwa za kizalendo, hali ambayo inaweza kudhoofisha nafasi ya sekta binafsi katika uchumi.
“Hatuifelishi tu sekta binafsi, bali tunaifelisha nchi. Mawazo ya aina hiyo hayafelishi tu sekta binafsi, bali ni kufelisha dira yote na tutakuwa tunaifelisha nchi.”
Aidha, amesema Serikali na sekta binafsi zinapaswa kubadili mitazamo na namna ya kufanya kazi ili kuboresha mazingira ya biashara na kuongeza uwekezaji, akisisitiza kuwa utekelezaji wa Dira 2050 unahitaji ushiriki mpana wa sekta binafsi badala ya Serikali kubeba shughuli zote za kiuchumi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri Mkuu wa Tanzania Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Tanzania imefikia hatua ambayo utekelezaji wa mipango ya maendeleo haupaswi tena kufanywa kwa mtindo wa dharura, kutokana na uwepo wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 pamoja na nyenzo za kuiwezesha Serikali kutekeleza mipango hiyo.
Akizungumza akiwa Mgeni Rasmi leo Septemba 17, 2026 katika siku ya mwisho ya Kongamano la Kitaifa la Wanamipango 2026 linalofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Arusha (AICC) kujadili mipango ya maendeleo na utekelezaji wa Dira 2050, Dkt. Nchemba amesema uzoefu umeonesha kuwa Tanzania imekuwa na uwezo mkubwa wa kuandaa mipango, lakini changamoto imekuwa katika usimamizi na utekelezaji wa mipango hiyo.
Amesema Serikali inapaswa kutumia mipango iliyopo kama msingi wa utekelezaji wa shughuli za maendeleo badala ya kusubiri changamoto zitokee na kisha kuzishughulikia kwa dharura. Kwa mujibu wa Dkt. Nchemba, utekelezaji wa mipango kwa usimamizi madhubuti utawezesha Tanzania kufikia malengo yaliyoainishwa katika Dira ya Taifa ya Maendeleo.
"Lakini tunavyoenda sasa kwa mara ya kwanza tumepata dira na nyenzo zake zote. Kwa kweli hatuna sababu wala kisingizio cha kufanya mambo kwa dharura na kutekeleza mambo ambayo yamepangwa.” amesema MwiguluThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri Mkuu wa Tanzania Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Tanzania inahitaji sekta binafsi iliyo imara ili kukabiliana na changamoto za umaskini na ukosefu wa ajira kwa vijana, akisisitiza umuhimu wa kubadili mtazamo kuhusu sekta binafsi na uwekezaji nchini.
Kauli hiyo imetolewa leo, Septemba 17, 2026, jijini Arusha wakati Dkt. Mwigulu akizungumza kama Mgeni Rasmi katika siku ya mwisho ya Kongamano la Kitaifa la Wanamipango 2026 linalofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Arusha (AICC) kujadili mipango ya maendeleo na utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
Dkt. Mwigulu amesema heshima na imani vinavyotolewa kwa sekta ya umma vinapaswa pia kupewa sekta binafsi ili kujenga mazingira yatakayochochea uwekezaji na kukuza uchumi.
“Heshima ile ambayo tunaipa sekta ya umma, imani ile ambayo tunaipa sekta ya umma, tunatakiwa tufanye hivyo hivyo kwa sekta binafsi. Hapo ndipo tutakapoweza kufika hatua,” amesema Dkt. Mwigulu.
Aidha, amesema Tanzania inapaswa kuondokana na fikra zinazowafanya wananchi kuutilia shaka uwekezaji kila mara, akieleza kuwa tabia ya kufanya upigaji inaweza kutokea katika sekta yoyote, hivyo kinachopaswa kupingwa ni kitendo hicho na si sekta husika.
“Upigaji hauna sura. Unaweza ukafanyika upigaji kwenye sekta ya umma, unaweza ukafanyika upigaji kwenye sekta binafsi. Kwa hiyo si-condemn kwa sekta, lakini condemn kwa kitendo chenyewe,” amesema. Ameongeza kuwa uwekezaji unaofanywa kwa usahihi unapaswa kupewa heshima inayostahili.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri Mkuu wa Tanzania Dkt. Mwigulu Nchemba amewataka wataalamu na wanamipango nchini kutominyaminya wala kuficha utaalamu wao, bali kuwasilisha na kusimamia utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 na mipango ya kitaifa kwa ujasiri kwa kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anaheshimu sana taaluma na ushauri wa kitaalamu.
Kauli hiyo imetolewa leo, Septemba 17, 2026, jijini Arusha wakati Dkt. Mwigulu akizungumza kama Mgeni Rasmi katika siku ya mwisho ya Kongamano la Kitaifa la Wanamipango 2026 linalofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Arusha (AICC) kujadili mipango ya maendeleo na utekelezaji wa Dira 2050.
Akieleza ushuhuda wake wa kufanya kazi kwa karibu na Mkuu wa Nchi akiwa Waziri wa Fedha pamoja na aliyekuwa Waziri wa Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo, Dkt. Mwigulu amebainisha kuwa Rais Samia huweka msisitizo mkubwa kwenye ushauri wa kitaalamu na kwamba wizara zilizofanikiwa zimekuwa zikiandaa maandiko bora na ya kina yanayohusu sekta zao
“Mheshimiwa Rais anaheshimu sana taaluma, anaheshimu sana utaalam. Ukienda na blah blah zako atakuvumilia mara mbili tu. Baada ya hapo unaiona kalamu tu. Anaheshimu sana taaluma, anaheshimu sana ushauri wa kitaalamu sana. Ukiona wizara nyingi zimefanikiwa hivi ni kwamba walikuwa wanaandaa maandiko yao yanayohusu sekta zao", ameeleza.
Akiendelea kufafanua kuhusu namna Rais Samia anavyotoa nafasi kwa wataalamu kuwasilisha mada zao kwa kina bila kubanwa na muda pindi wanapofikisha hoja za msingi za kisekta, Waziri Mkuu amewasisitiza wanamipango na wataalamu waliokusanyika AICC kutumia fursa hiyo kikamilifu kwa maslahi ya taifa.
"Kwa hiyo mkienda huko msiminyeminye utaalamu wenu, msifichefiche utaalamu wenu tukasimamie, tukatekeleze dira, tukatekeleze mipango kwa ujasiri huku tukimtanguliza Mungu kwa maslahi mapana ya nchi yetu", ameeleza.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais–Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo, amesema Serikali imefikia hatua ya kuacha kuangalia zaidi uandaaji wa mipango na badala yake kuanza kupima utekelezaji wake kwa kuzingatia matokeo yanayopatikana.
Akizungumza mbele ya Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Septemba 17, 2026 katika Kongamano la Kitaifa la Wanamipango 2026, Profesa Mkumbo amesema washiriki 103 kutoka mikoa yote 26 ya Tanzania Bara, wizara, sekretarieti za mikoa na serikali za mitaa waliohudhuria mkutano huo wanahusika moja kwa moja katika usimamizi, upimaji na tathmini ya utekelezaji wa mipango ya maendeleo.
“Tumekubaliana jana Mheshimiwa Waziri Mkuu, sasa tukatekeleze, tuanze kupimana kwa kuzingatia matokeo,” amesema Profesa Mkumbo.
Amesema kuanzia mwaka huu, vikao vya mipango vitatumika zaidi kutoa taarifa kuhusu matokeo yaliyopatikana kutokana na utekelezaji wa mipango iliyowekwa, huku akisisitiza kuwa hatua hiyo inalenga kuifanya Serikali kuhamia kutoka katika hatua ya kupanga mara kwa mara kwenda katika utekelezaji wenye matokeo yanayopimika.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Amosi Makalla, amesema Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 inalenga kutoa mwelekeo wa maendeleo ya muda mrefu kwa kuweka kipaumbele katika ustawi wa wananchi na maendeleo ya uchumi.
Makalla ameyasema hayo leo Septemba 17, 2026, katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Arusha (AICC) wakati akizungumza katika siku ya mwisho ya Kongamano la Kitaifa la Wanamipango 2026 ambalo Mgeni Rasmi ni Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba.
Makalla ameeleza kuwa utekelezaji wa Dira 2050 unahitaji ushirikiano wa wananchi, taasisi za umma na sekta binafsi ili kuhakikisha malengo yaliyowekwa yanafikiwa kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo.
Amesisitiza kuwa Mkoa wa Arusha utaendelea kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa Dira 2050 kwa kuimarisha mipango ya maendeleo na kuhamasisha ushiriki wa wadau mbalimbali katika kujenga uchumi wenye tija na maendeleo endelevu.
“Na mimi nipongeze kwamba utekelezaji umekwisha kuanza hongereni sana, kwasababu wanamipango hawa wanaamini wao wateenda kuangalia mpango huu kuweka katika kila budget, kuweka katika kila mpango kuhakikisha kwamba yote yaliotajwa katika dira ya 2050 inakwenda kufanikiwa”, ameeleza.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mchakato wa uandaaji na utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 umefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutokana na utashi wa kisiasa wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, aliyeagiza kuandikwa kwa Dira mpya ya miaka 25 badala ya kufanyia marekebisho iliyokuwepo.
Kauli hiyo imetolewa leo, Septemba 17, 2026, katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Arusha (AICC) na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo, wakati akizungumza katika siku ya mwisho ya Kongamano la Kitaifa la Wanamipango 2026 ambalo Mgeni Rasmi ni Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba.
“Mheshimiwa Waziri Mkuu zoezi hili limesimamiwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia mwanzo mpaka mwisho na kikubwa sana ambacho ametupa ni utashi na utayari... kwasababu angeweza kufanya tu kwamba dira iliyekuwepo tungefanyia edit na tuka-extend lakini alielekeza kwamba tupate dira mpya itakayoongoza nchi kwa miaka mingine 25”, ameeleza.
Profesa Kitila amebainisha kuwa ni mara ya kwanza kwa Wizara hiyo na wataalamu wa mipango kupata nyenzo na rasilimali zote zinazohitajika kwa wakati muafaka, jambo linaloondoa kisingizio chochote cha kushindwa kufikia matokeo yaliyokusudiwa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Kongamano la Kitaifa la Wanamipango 2026 linatazamiwa kuwa chachu ya mageuzi makubwa katika mbinu za upangaji na utekelezaji wa mipango ya maendeleo nchini, huku likiweka msisitizo kwenye nidhamu ya hali ya juu ya utekelezaji ili kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
Kauli hiyo imetolewa leo, Septemba 17, 2026, katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Arusha (AICC), na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais - Mipango na Uwekezaji ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Dkt. Tausi Mbaga Kida, wakati akimkaribisha Mgeni Rasmi, Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba, katika siku ya mwisho ya kongamano hilo.
Akizungumza mbele ya Mgeni Rasmi Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba na wajumbe, Dkt. Kida amebainisha kuwa kongamano hilo ambalo ni la pili kufanyika tangu kuanzishwa kwa Tume ya Taifa ya Mipango mwaka 2023 limekutanisha takriban washiriki 1,300 kutoka kada mbalimbali, ikijumuisha wachumi, watakwimu, maafisa mipango, wataalamu wa fedha, watafiti, wawakilishi wa sekta binafsi, na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (AZAKI)
"Lengo la kongamano la kitaifa la wanamipango ni kutoa jukwaa na fursa kwa viongozi, watendaji na wataalamu na wadau wote muhimu katika kada na maswala ya mipango kujadili pamoja na kujifunza mbinu za kuimarisha mipango jumuishi ya maendeleo na kuwezesha majadiliano kuhusu utekelezaji madhubuti, ufuatiliaji na upatikanaji wa matokeo. Kongamano pia linatoa fursa ya kubadilishana uzoefu na maarifa kuhusu namna bora ya kusanifu na kutekeleza afua zenye kuleta matokeo chanya na kuboresha ustawi kwa maendeleo ya nchi yetu", ameeleza Dkt. Kida.
Akimulika kaulimbiu ya kongamano hilo isemayo "Kutekeleza Dira 2050: Kuimarisha Mipango Jumuishi, Utekelezaji na Matokeo", Dkt. Kida ameeleza kuwa imechaguliwa kwa dhumuni maalumu la Serikali la kuweka msisitizo katika kuimarisha upangaji fungamanishi na nidhamu ya utekelezaji, ikizingatiwa kuwa kongamano hilo linafanyika miezi miwili baada ya kuanza rasmi kwa utekelezaji wa Dira 2050.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Queen Sendiga, ametoa saa 24 kwa taasisi mbalimbali ndani ya Mkoa huo, ikiwemo Shirika la Reli Tanzania (TRC), Bodi ya Maji Bonde la Wami Ruvu, viongozi pamoja na wataalamu, kukaa pamoja na kuandaa mpango wa pamoja wa kutafuta ufumbuzi wa changamoto zinazowakabili wananchi, ikiwemo tatizo la mafuriko katika Mitaa ya Lukobe na Azimio.
Sendiga ametoa agizo hilo leo Septemba 16, 2026 wakati wa ziara ya kukagua maeneo yanayoweza kuathiriwa na mvua kubwa za El Nino zinazotarajiwa kunyesha, akisisitiza umuhimu wa taasisi hizo kuchukua hatua za haraka badala ya kusubiri madhara yatokee.
Amesema ni wakati sasa kwa taasisi zinazohusika kushirikiana na kuja na hatua madhubuti zitakazosaidia kupunguza athari za mafuriko na kulinda maisha pamoja na mali za wananchi.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Bodi ya Maji Bonde la Wami Ruvu Mhandisi Elibariki Mmasy, amesema bodi hiyo tayari imeanza zoezi la kufukua na kurekebisha maeneo yenye changamoto, hatua inayolenga kuboresha mtiririko wa maji na kupunguza uwezekano wa mafuriko.
Nao baadhi ya wananchi wakiongozwa na Swaum Ally, wameiomba Serikali kuendelea kuboresha maeneo yenye changamoto pamoja na kuchukua hatua za kudumu ili kuwawezesha wananchi kuondokana na tatizo la mafuriko ambalo limekuwa likiathiri maisha na shughuli zao.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI PICHA:
Washiriki mbalimbali kutoka sekta za serikali na binafsi wakiwamo wachumi, watafiti, wataalamu wa mipango pamoja na wadau wengine wa maendeleo wamekutana jijini Arusha katika Kongamano la Kitaifa la Wanamipango lililoandaliwa na Tume ya Taifa ya Mipango.
Kongamano hilo limefanyika leo, Septemba 16, 2026, katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Arusha (AICC), likiwa na lengo la kujadili masuala mbalimbali yanayohusu mipango ya maendeleo na utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
Mgeni rasmi katika kongamano hilo alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo, huku washiriki wakipata fursa ya kutoa maoni, uzoefu na mapendekezo kuhusu namna ya kuimarisha mipango na utekelezaji wa miradi ya maendeleo nchini.
Kongamano hilo la siku mbili linatarajiwa kuhitimishwa kesho, Septemba 17, 2026, ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkuu wa Shule ya Sekondari Joseph Mbeyela iliyopo Halmashauri ya mji wa Njombe, ameomba wadau kuendelea kujitokeza ili kusaidia ukarabati wa shule hiyo kutokana na uchakavu wa majengo baada ya kukaa muda mrefu bila kukarabatiwa.
Akizungumza na Jambo TV baada ya kupokea mifuko 200 ya safuji kutoka kwa mbunge wa viti Maalumu Mkoa wa Njombe kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Sigrada Mligo, Mkuu wa shule hiyo Jimmy Ngumbuke amesema mpaka sasa wanaendelea na ukarabati kupitia michango ya wadau mbali mbali.
"Wadau tunaendelea kuwaomba watusaidie na nikushukuru sana Mbunge kwa kuwa mwenyewe pia umepita na umejionea majengo yetu" amesema Ngumbuke.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Njombe mjini Deo Mazao, amesema atahakikisha hakuna fedha yoyote ya wadau itakayopotea wakati wakiendelea na ukarabati wa shule hiyo iliyoanza mwaka 2007.
Naye Mbunge huyo amesema ataendelea kuhakikisha anaunga mkono shughuli za maendeleo zinazoendelea Mkoani Njombe bila kujali itikadi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Madereva wa Serikali wametakiwa kuepuka matumizi ya vilevi badala yake wazingatie sheria za usalama barabarani na kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia weledi, huku wakisisitizwa kushirikiana na Serikali pamoja na Jeshi la Polisi katika kutoa taarifa kuhusu changamoto wanazokutana nazo kazini.
Hayo yamesemwa Septemba 16, 2026 jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya, wakati wa Kongamano la Kitaifa la Chama cha Madereva wa Serikali Tanzania, ambapo amewataka madereva hao kuzingatia sheria za usalama barabarani na kuhakikisha wanapata huduma pamoja na maelekezo muhimu kwa wakati.
Mhandisi Kasekenya amesema ushirikiano kati ya madereva, Serikali na Jeshi la Polisi ni muhimu katika kukabiliana na changamoto zinazowakabili madereva hao na kuimarisha usalama barabarani.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Madereva wa Serikali Tanzania, Said Kapande amesema kuna changamoto katika upatikanaji wa leseni ikiwemo mkanganyiko kati ya Jeshi la Polisi na Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kuhusu utambulisho wa vyeti vya madereva wanaohudumia viongozi na abiria.
Amesema baadhi ya madereva wamepata vyeti vilivyoandikwa “VIP and F Passengers Service”, lakini wanapokwenda kupata leseni hukutana na maelekezo tofauti kutoka Jeshi la Polisi kuhusu namna vyeti hivyo vinavyopaswa kuandikwa.
Kapande amesema hali hiyo imekuwa ikiwafanya baadhi ya madereva kushindwa kupata leseni zinazostahili kwa wakati, hivyo ameiomba Serikali kupitia mamlaka husika kutatua changamoto hiyo ili kurahisisha mchakato wa upatikanaji wa leseni kwa madereva hao.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga, amezindua Kongamano la Uwekezaji kati ya Tanzania na Ujerumani, linalolenga kukuza fursa za uwekezaji na biashara katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Akizungumza leo, Septemba 16, 2026, wakati wa uzinduzi wa kongamano hilo, Kapinga amesema Tanzania ina fursa kubwa za uwekezaji ambazo zinaweza kuongeza biashara na kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi kati ya nchi hizo mbili.
Amesema mauzo ya Tanzania nchini Ujerumani yamefikia asilimia 62, huku biashara kati ya Tanzania na Ujerumani ikifikia asilimia 56.
Kapinga ametaja sekta zenye fursa kubwa za uwekezaji nchini kuwa ni viwanda, uongezaji thamani wa mazao, teknolojia, madini na utalii.
Awali, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, James Ole Millya, amesema diplomasia ya uchumi kati ya Tanzania na Ujerumani imechangia kuvutia kampuni za Ujerumani kuwekeza nchini, hususan katika sekta ya viwanda.
Kongamano hilo limewakutanisha wawekezaji 30 kutoka kampuni mbalimbali za Ujerumani wanaoshiriki katika ziara ya ukanda wa Afrika Mashariki kwa ajili ya kutathmini fursa za uwekezaji.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Alexander Mkumbo @kitilam , amezitaka Mamlaka za Serikali za Mitaa kubadili mtazamo na kujikita katika kuwa vitovu vya uchumi badala ya kubaki katika jukumu la utawala, akisisitiza kuwa mafanikio ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 yatategemea uwezo wa Halmashauri kuzalisha shughuli mpya za kiuchumi na matokeo yanayoonekana.
Prof. Mkumbo ametoa kauli hiyo leo Jumatano, Septemba 16, 2026, wakati akizungumza katika siku ya kwanza ya Kongamano la Kitaifa la Wanamipango linalofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC), jijini Arusha, akisema kila Halmashauri inapaswa kujiuliza imebuni shughuli gani mpya za kiuchumi, biashara gani zimeongezeka na ni fursa zipi mpya zimezalishwa ndani ya mwaka.
Amesema suala la kuongeza mapato ya Halmashauri halipaswi kuishia katika kubuni vyanzo vipya vya mapato pekee, bali linapaswa kuanzia katika kujenga vyanzo vipya vya uchumi vitakavyoongeza shughuli za uzalishaji na biashara, hivyo kuongeza mapato kama matokeo ya ukuaji wa uchumi katika maeneo husika.
Akizungumzia misingi ya kufikia malengo ya Dira 2050, Prof. Mkumbo amesema nchi inahitaji uwekezaji mkubwa katika watu, hususan elimu na ujuzi wenye matokeo, akisisitiza kuwa mafanikio hayapaswi kupimwa kwa wingi wa vyeti bali uwezo wa wananchi kutumia elimu na ujuzi wao kuzalisha matokeo katika maendeleo.
Ameongeza kuwa uwekezaji huo unapaswa kuhusisha afya ya mwili na akili pamoja na kujenga maadili na uadilifu kwa watumishi wa umma, akisema watumishi wamepewa dhamana ya kulinda mali za umma na hivyo wanapaswa kutambua tofauti kati ya mali ya umma na mali binafsi. Aidha, amesema serikali inaendelea kuwekeza katika miundombinu ya kiuchumi ikiwemo reli ya SGR na usafiri wa anga, pamoja na uzalishaji na utekelezaji wa majukumu kwa weledi na uadilifu.
Aidha Prof. Mkumbo amesema wanamipango wanapaswa kuwa na mtazamo wa utekelezaji na matokeo katika kuifikia Dira 2050, akisisitiza kuwa katika mkutano wa mwaka ujao matarajio si kusikia tena mawasilisho kuhusu Dira hiyo, bali kuona na kusikia Halmashauri na taasisi zimefanya nini na zimepata matokeo gani katika utekelezaji wa malengo yaliyowekwa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais- Mipango na Uwekezaji ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Dkt. Tausi Mbaga Kida, amesema muda umefika wa kuimarisha uhusiano kati ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, mipango, bajeti, utekelezaji na matokeo ili kuhakikisha malengo yaliyowekwa yanafikiwa kwa ufanisi.
Dkt. Kida amesema changamoto katika utekelezaji wa mipango ya maendeleo si ukosefu wa mipango mizuri pekee bali ni kuhakikisha mipango hiyo inaunganishwa, inawekewa rasilimali, inatekelezwa kwa wakati na kufuatiliwa kwa karibu ili kuhakikisha matokeo yanapatikana.
Amesema Dira 2050 inapaswa kufungamanishwa na mipango ya kisekta, taasisi za umma na sekta binafsi, pamoja na mipango ya Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa, huku mipango na bajeti za mwaka zikiendana na mipango ya muda mrefu ya Taifa.
Akizungumza katika Kongamano la Kitaifa la Wanamipango linalofanyika jijini Arusha, Dkt. Kida amesema upangaji jumuishi ni hitaji muhimu katika utekelezaji wa Dira 2050, kwa kuwa kongamano hilo linalenga kuongeza uwezo wa Wanamipango kuunganisha mipango ya kitaifa na kisekta, mipango ya Serikali Kuu na Serikali za Mitaa, pamoja na mipango na bajeti.
Amesema kongamano hilo pia linalenga kujenga utamaduni wa kutumia takwimu, ushahidi na uchambuzi wa kitaalamu katika kufanya maamuzi, huku Wanamipango wakitakiwa kuondokana na mtazamo wa kuwa waandaaji wa nyaraka pekee na badala yake kuwa wasanifu wa mabadiliko, waunganishaji wa taasisi na rasilimali, walinzi wa vipaumbele vya Taifa na wasimamizi wa matokeo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, pamoja na Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Elihuruma Mabelya, wametangaza kujifunga kitanzi kuhakikisha ujenzi wa Soko la Gongolamboto unakamilika ndani ya miezi saba ili kuwawezesha zaidi ya wafanyabiashara 5,000, wakiwemo wamachinga, kufanyia shughuli zao kwenye mazingira rasmi na yenye staha.
Akitangaza hatua hiyo wakati wa ziara ya ukaguzi katika eneo la Gongolamboto, Mpogolo ameeleza kuwa Serikali imedhamiria kumaliza kero ya wafanyabiashara kufanya shughuli zao maeneo yasiyoruhusiwa, hususan barabarani na kwenye njia za watembea kwa miguu, kwa kuwahamishia maeneo rasmi.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Jiji, Elihuruma Mabelya, amebainisha kuwa ujenzi huo ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa wakati wa uzinduzi wa Soko la Kariakoo, akiagiza Halmashauri zote kutenga asilimia tano ya mapato ya ndani kwa ajili ya ujenzi wa masoko.
Mabelya amefafanua kuwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam tayari imetenga Shilingi bilioni 6.4 kwa ajili ya ujenzi wa masoko ya wamachinga katika maeneo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na Gongolamboto ambapo eneo limeainishwa, tathmini na usanifu vinaendelea, na fedha zipo tayari.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Wadau kutoka taasisi mbalimbali za haki jinai nchini wamekutana kwa lengo la kupitia na kuiboresha Rasimu ya Mwongozo wa Ufuatiliaji wa Majukumu ya taasisi hizo ili kuweza kuimarisha uwajibikaji na kuboresha upatikanaji wa haki kwa wananchi.
Akifungua rasmi kikao hicho tarehe 15 Septemba, 2026 Mtumba jijini Dodoma, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Katiba na Sheria, Balozi Baraka Luvanda amesema kuwa lengo kuu la kikao hicho ni kupitia kwa kina rasimu iliyopo ili kubaini maeneo yenye mapungufu na kuyafanyia maboresho, ambapo msisitizo mkubwa utawekwa katika Viashiria Muhimu vya Utendaji (KPIs) ili kuufanya kuwa wa vitendo, unaopimika, na unaotekelezeka kwa tija.
“Viashiria vinavyoeleweka na kupimika vitasaidia kuimarisha uwajibikaji, jambo ambalo hatimaye litaboresha mfumo mzima wa haki jinai na kuharakisha upatikanaji wa haki kwa wananchi” alisema Balozi Luvanda.
Aidha, Balozi Luvanda aliongeza kuwa mwongozo huo unakusudia kujenga ushirikiano, kubadilishana uzoefu, na kusaidiana kutatua changamoto za kiutendaji ikiwa ni pamoja na kuondoa mazingira ya taasisi kulaumiana.
Awali, Mkurugenzi wa Katiba na Ufuatiliaji Haki, Wizara ya Katiba na Sheria, Jane Lyimo, akimkaribisha Naibu Katibu Mkuu kufungua kikao hicho alitoa wito kwa wadau wote kushiriki kikamilifu ili kuhakikisha mwongozo utakaopatikana unakuwa na uhalisia na unatekelezeka kikamilifu. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makundi maalum, yakiwemo wanawake, watoto na watu wenye ulemavu, yametakiwa kushirikishwa katika mipango ya utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 ili kuhakikisha mahitaji na maslahi yao yanazingatiwa katika mipango ya maendeleo nchini.
Hayo yamesemwa Septemba 16, 2026, jijini Arusha, katika Kongamano la Kitaifa la Wanamipango, na Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango, Dkt. Mursali Milanzi.
Akizungumza katika kongamano hilo, Dkt. Milanzi amesema katika kutafsiri Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 kuwa mipango na hatua za utekelezaji, makundi hayo lazima yashirikishwe.
“Sasa mipango yetu tunapotafsiri Dira 2050, ni lazima watoto, wanawake na wenye ulemavu washirikishwe tunapoweka mipango yetu,” amesema Dkt. Milanzi.
Sambamba na hilo, Dkt. Milanzi amesema mafanikio katika utekelezaji wa Dira 2050 hayategemei pekee ubora wa nyaraka zilizopo, bali yanategemea uwezo wa kutafsiri yaliyomo katika nyaraka hizo kuwa mipango inayotekelezeka na kupata matokeo yanayopimika.
Amesema ubora wa utekelezaji ndio msingi wa kuhakikisha mipango inayowekwa inaleta matokeo yaliyokusudiwa kwa wananchi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO;
Serikali imeendelea kuimarisha matumizi ya mifumo ya kidijitali ikiwemo mfumo wa E-Delivery, kwa lengo la kuongeza ufanisi katika ufuatiliaji wa utekelezaji wa mipango na miradi ya maendeleo nchini, pamoja na kuhakikisha taarifa za utekelezaji zinapatikana kwa wakati na kwa usahihi.
Akizungumza Septemba 16, 2026, jijini Arusha katika Kongamano la Kitaifa la Wanamipango, Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais- Mipango na Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango, Dkt. Tausi Kida, amesema matumizi ya mifumo ya kidijitali ni muhimu katika kuhakikisha miradi inayotekelezwa inaendana na mipango iliyowekwa pamoja na upatikanaji wa fedha za maendeleo.
Amesema utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 unahitaji mifumo imara ya takwimu na teknolojia, sambamba na ushirikiano wa wadau mbalimbali katika kupanga, kutekeleza na kufuatilia miradi ya maendeleo.
Aidha, Dkt. Kida amesema matumizi ya mifumo hiyo yanatarajiwa kuongeza ufanisi katika kufuatilia hatua za utekelezaji wa miradi na kuhakikisha rasilimali zinazotengwa kwa maendeleo zinatumika kwa kuzingatia malengo yaliyowekwaThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Serikali ya Tanzania imesisitiza kuwa uwekezaji ndiyo njia kuu na ya uhakika itakayowezesha kutengeneza ajira nyingi kwa vijana pamoja na kuongeza idadi ya matajiri nchini, ikihimiza haja ya kuwa na mabadiliko na uboreshaji wa mifumo ya kisera, kisheria, kikanuni na kitaasisi.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Mipango na Uwekezaji, Dkt. Pius Stephen Chaya, wakati akizungumza leo Septemba 16, 2026 kama mgeni rasmi kando ya ufunguzi wa Jukwaa la 17 la Uwekezaji lililoandaliwa na Taasisi ya Kimataifa ya Maendeleo Endelevu (IISD) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalumu ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) jijini Dar es Salaam.
Kongamano hilo la siku mbili lililofunguliwa leo limekutanisha washiriki na wataalamu kutoka zaidi ya nchi 60 za Afrika, Amerika Kusini na Asia ili kujadili namna nchi hizo zinavyopaswa kujiandaa kimuundo, kisera na kisheria katika kuvutia mitaji ya uwekezaji kutoka nje (FDI) na mitaji ya ndani (DDI)
Akifafanua kuhusu kipaumbele cha Serikali chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Dkt. Chaya ameeleza kuwa serikali imefarijika kwa IISD kuichagua Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano huo wa kimataifa, kwani suala la uwekezaji ndio nguzo kuu ya ukuaji wa uchumi na utengenezaji wa fursa za ajira kwa vijana wanaohitimu kutoka vyuo vikuu
Dkt. Chaya ameongeza kuwa ili uwekezaji unaoingia nchini uwe wenye tija na usizorote, ni lazima kuweka mifumo madhubuti ya kisera, kisheria, kikanuni, kimuundo na kitaasisi
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uwekezaji Endelevu katika Taasisi ya IISD, Suzy Nikièma amesema jukwaa hilo limejikita katika kujadili namna ya kuwa na mtazamo unaoenda sambamba katika utungaji na mabadiliko ya sheria na sera za uwekezaji, lengo ni kuhakikisha ahadi na makubaliano ya kiuchumi yaliyowekwa katika ngazi ya bara (kama Mkataba wa Eneo la Biashara Huru Afrika - AfCFTA) yanashabihiana kikamilifu na makubaliano ya kieneo kama vile SADC, pamoja na sheria za kitaifa.
Naye, Katibu Mkuu Wizara ya Kazi na Uwekezaji Zanzibar, Khamis Shibu amebainisha kuwa Tanzania bado ina fursa na nafasi ya kuendelea kuboresha sheria, sera na miongozo yake ya uwekezaji kwa kujifunza kutoka kwa nchi mbalimbali za Afrika, Asia na Amerika Kusini zilizoshiriki katika kongamano hilo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katika kuendelea kwa maswali ya ufafanuzi ya Lissu kwa shahidi wake wa tano, John Heche, leo Septemba 16, 2026, Lissu amemtaka Heche afafanue majibu yake kuhusu ripoti za waangalizi na taasisi za kimataifa kama SADC na kueleza kile kilichosemwa mbele ya majaji kuhusu suala la utekaji.
Heche amefafanua kwamba katika ukurasa wa 6 wa ripoti hiyo ya SADC, ulizungumzia masuala ya utekaji. Kutokana na Jibu hilo, Wakili wa Serikali Mkuu Nassor Katuga, alisimama na kupinga na kueleza kuwa hicho ni kipengele cha Re examination na siyo Examination in Chief, akidai kuwa Heche anaanza kusema mambo mapya.
Tundu Lissu alijibu madai hayo ya Wakili wa Serikali Mkuu Nassor Katuga kuwa, kitu anachokubaliana na Wakili huyo ni kutajwa kwa ukurasa wa 6 pekee ambao awali shahidi hakuutaja, akisema mengine yote yaliyosemwa na shahidi yalikuwa sahihi.
Lissu aliendelea kumuuliza Heche amwonyeshe kwenye ripoti ya SADC kuhusu utekaji pale aliposoma ili afafanue, na Heche alithibitisha kuwa ni kweli kwenye ripoti hiyo ya SADC ilizungumzia pia suala la utekaji.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katibu Mtendaji Tume ya Taifa ya Mipango Dkt. Tausi Kida amesema lengo la Kongamano la Kitaifa la Wanamipango ni kutoa fursa ya kuwajengea uwezo wataalam hao kupanga mipango yenye matokeo kwa wananchi ya wanayoendana na malengo ya Dira 2050.
Kongamano hilo la siku mbili linawakutanisha zaidi ya wanamipango 1,000 kutoka sekta ya umma na binafsi.
Jambo TV itakuletea matangazo mbashara ya kongamano hilo tarehe 17/09/2026 ambapo mgeni rasmi atakuwa Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo, amewataka wanamipango nchini kubadili mtazamo wa utekelezaji wa mipango ya maendeleo kwa kuhakikisha mipango hiyo haibaki kwenye makaratasi, bali inazaa matokeo yanayoweza kupimika.
Profesa Mkumbo ameyasema hayo jijini Arusha leo, Septemba 16, 2026, wakati akizungumza katika Kongamano la Kitaifa la Wanamipango 2026, linalofanyika kwa siku mbili na linatarajiwa kufungwa kesho na Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba.
Amesema wanamipango wana nafasi muhimu katika kuhakikisha malengo yaliyoainishwa kwenye Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 yanatafsiriwa kuwa mipango inayotekelezeka na yenye matokeo kwa wananchi.
Aidha, Profesa Mkumbo amesema kazi ya mwanamipango haipaswi kuishia katika kuandaa mipango ya maendeleo, bali inapaswa kwenda hatua zaidi kwa kuratibu utekelezaji, kufuatilia maendeleo na kuhakikisha malengo yaliyowekwa yanafikiwa. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Tume ya Taifa ya Mipango inalenga kuimarisha weledi, ujuzi na uwezo wa watendaji katika kuandaa, kutekeleza na kufuatilia mipango ya maendeleo, hatua inayolenga kuongeza tija na kuhakikisha malengo ya maendeleo ya Taifa yanafikiwa.
Akizungumza hii leo Septemba 16, 2026, jijini Arusha katika kongamano la kitaifa la Wana Mipango, Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango, Dkt. Tausi Kida, amesema Tume hiyo kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge na taasisi nyingine za Serikali, imekuwa ikitekeleza taratibu mbalimbali za kujenga uwezo na ujuzi wa mipango katika ngazi mbalimbali.
Amesema hatua hiyo inalenga kuwawezesha watendaji kuwa na uwezo katika kuandaa, kutathmini, kutekeleza na kufuatilia mipango ya maendeleo, ili kuboresha tija na kuhakikisha mipango hiyo inatekelezwa ipasavyo na kufikia matokeo yaliyokusudiwa.
Aidha Dkt. Kida amesema Tume ya Taifa ya Mipango imepewa jukumu la kusimamia na kuratibu mipango ya maendeleo ya Taifa, pamoja na kuhakikisha mipango katika ngazi mbalimbali inazingatia mwelekeo wa Taifa na utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050
Ameongeza kuwa kujenga uwezo wa watendaji katika eneo la mipango ni muhimu katika kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa ufanisi na mipango ya maendeleo inaleta matokeo yaliyokusudiwa kwa wananchi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ester Bulaya, ametekeleza ombi la mwananchi wake kwa kumkabidhi bati tatu pamoja na kuweka utaratibu wa kumvutia umeme katika makazi yake, ikiwa ni sehemu ya utaratibu wake wa kupokea, kusikiliza, na kutatua kero za wananchi jimboni humo.
Bulaya ameeleza kuwa alikutana na bibi huyo ambaye ni mkazi wa Kata ya Kabalimu wakati wa ibada ya misa ya asubuhi siku ya Jumapili ambapo alimnong'oneza shida yake, kabla ya kufika rasmi ofisini kwake siku iliyofuata na kuwasilisha maombi hayo mawili ya bati na umeme.
Amebainisha kuwa bibi huyo ni mtu anayejituma sana kutafuta riziki licha ya umri wake, kwani anajishughulisha na uuzaji wa kahawa.
“Kwahiyo mimi na mkurugenzi wa TANESCO tukasema hebu na sisi sasa tukamilishe ndoto za bibi za kutaka nyumba yake iwe na umeme... mimi nitatuma pesa na yeye kidogo ili bibi apate kuwekewa umeme”, ameeleza Bulaya.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo, amezitaka Mamlaka za Serikali za Mitaa kubadilika kutoka kuwa mamlaka zinazojikita zaidi katika shughuli za kiutawala na kuelekea kuwa vitovu vya shughuli za kiuchumi.
Profesa Mkumbo amesema hayo leo Septemba 16, 2026 jijini Arusha, wakati wa Kongamano la Kitaifa la Wanamipango, akisisitiza umuhimu wa wanamipango kubuni shughuli mpya za kiuchumi zitakazoongeza uzalishaji, ajira na vyanzo vya mapato katika halmashauri.
Aidha, amesema Serikali za Mitaa zinapaswa kujenga mazingira wezeshi kwa sekta binafsi kwa kuondoa vikwazo vinavyowakabili wazalishaji na wafanyabiashara, ikiwemo changamoto za masoko, miundombinu na usafirishaji wa mazao.
Ameongeza kuwa maamuzi ya Serikali yanapaswa kujengwa katika ushahidi na matumizi sahihi ya takwimu na data, huku kila mpango na mradi ukilenga kuongeza uzalishaji, kuchochea shughuli za kiuchumi na kutengeneza ajira, hususan kwa vijana.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, amesema Tanzania inahitaji uwekezaji mkubwa katika maeneo mbalimbali ili kufikia malengo yaliyowekwa kupitia Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
Prof. Kitila amesema hayo leo, Septemba 16, 2026, jijini Arusha, wakati akizungumza katika Kongamano la Kitaifa la Wanamipango, akieleza kuwa uwekezaji huo unapaswa kuanza na rasilimali watu, hususan elimu na ujuzi unaomwezesha mtu kufanya kazi, badala ya kulenga vyeti pekee.
Amesema pamoja na elimu na ujuzi, taifa linahitaji kuwekeza katika afya ya watu, ikiwemo afya ya akili na mwili, sambamba na kujenga maadili na uadilifu, hususan kwa watumishi wa umma, ili kuongeza uwezo wa kufikiri na kutenda kwa tija.
Aidha, Prof. Kitila amesema uwekezaji katika uchumi na uzalishaji, ikiwemo ujenzi wa viwanda, ni sehemu nyingine muhimu itakayosaidia Tanzania kuongeza uzalishaji na kufikia malengo yake ya maendeleo yaliyowekwa katika Dira 2050.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
"Familia ya Tundu hatuwezi kununulika hiyo watu wajue hatuwezi kumsaliti ndugu yetu kwa misimamo yake sisi tunamuunga mkono tunamuombea ni mtu ambaye anaipenda nchi yake analipenda Taifa lake hayo mengine yanayoongelewa huko nje mimi nawaomba watanzania wasije wakaingia kwenye kuweza kutafakari tunaweza kununuliwa hamna kitu kama hicho"
Hayo ameyasema Rose Masesa ambaye ni dada wa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo @ChademaTZ2 Tundu Antiphas Lissu wakati akizungumza na Jambo TV leo Septemba 16, 2026.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI:
Rais wa Kenya William Ruto ameendeleza mashambulizi yake ya kisiasa dhidi ya mtangulizi wake, Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta, akimtaja kuwa “kiongozi wa uasi” na kumkosoa kwa kuendelea kujihusisha na siasa za upinzani.
Kauli hiyo ya Ruto ni mfululizo wa shutuma ambazo amekuwa akizitoa dhidi ya Kenyatta na Mwenyekiti wa KANU, Gideon Moi, akiwatuhumu kuunga mkono upinzani dhidi ya Serikali yake.
Akizungumza katika kampeni za kuwania muhula mwingine wa urais katika Kaunti ya Siaya, Ruto amepongeza uamuzi wa Mahakama Kuu uliomzuia Kenyatta kushikilia nafasi katika chama cha siasa.
“Nashangaa, mtu ambaye amekuwa Rais wa Kenya, unaacha kiti cha Rais, badala ya kwenda kuwa statesman, unaenda kuwa rebel leader, kiongozi wa upinzani. Mpaka sasa mahakama inamwambia atoke,” Ruto amesema.
Ruto pia amemtuhumu Kenyatta kwa kuendelea kuunga mkono viongozi wa upinzani kwa lengo la kudhoofisha Serikali yake, huku akiwataka Wakenya kutowaunga mkono viongozi anaowatuhumu kutokuwa na mipango na sera za wazi kwa ajili ya nchi.
Kauli hizo zimetolewa wakati Ruto akiendelea na kampeni zake za uchaguzi wa mwaka 2027, ambapo viongozi waliomsindikiza katika ziara hiyo pia wamekosoa upinzani na kuhamasisha wananchi kumuunga mkono. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Watoa huduma za usafiri wa daladala katika eneo la Mnadani jijini Dodoma leo Septemba 16, 2026, wamegoma kutoa huduma, wakilalamikia umbali wa stendi iliyotengwa kwa ajili yao kutoka barabarani.
Watoa huduma hao wamesema umbali huo unawalazimu abiria kutembea hadi stendi, huku wao wakiwa stendi wakiwasubiri, hali wanayodai inaathiri biashara zao.
Aidha, wamesema wanapojaribu kusogea barabarani ili kuwachukua abiria, hukamatwa na kutozwa faini, jambo wanalodai kuwaongezea gharama za uendeshaji.
Wameiomba Serikali kuwaruhusu kuchukua abiria barabarani, wakidai kuwa utaratibu huo unatumika kwa madereva wa bajaji.
Akizungumza kuhusu sakata hilo, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule, amesema kila chombo cha usafiri kinapaswa kuingia stendi na kutokuchukua abiria nje ya stendi.
Senyamule amesema Serikali inaendelea na ujenzi wa stendi mpya itakayotumiwa na watoa huduma hao.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Rose Masesa ambaye ni Dada wa Mwenyekiti wa @ChademaTZ2 Tundu Lissu amewataka watanzania kupuuza taarfa ambazo ameziita za uzushi zinazoenezwa na mwanaharakati Mange Kimambi🇺🇸 @mangekimambi kuwa dada huyo kuwa amekuwa akishirikiana na Godbless Lema @godbless_lema na sasa anaishi hoteli ya Sea Cliff kwa miezi miwili wakifadhiliwa na Abdul Ameir mtoto wa Rais Samia kwa ajili ya kumshawishi Tundu Lissu akubali Maridhiano
Akizungumza na Jambo TV leo Septemba 16, 2026 Rose amesema taarifa hizo si za kweli na wanaompa taarifa Mange wanamdanganya kwani yeye kwa sasa anaishi kwa watoto wake waliopo hapa jijini Dar es Salaam na hajawahi kuishi wala kufika Hotel ya SEACLIF HOTEL na hajawahi kukutana wala kuzungumza na mtu anayeitwa Abdul wala Rais Samia kwa kuhusu kesi ya kaka yake Tundu Lissu
"Sikutegemea sasa na sisi kama familia tutaanza kuingizwa kwenye tuhuma ambazo hazina ukweli kazitoa wapi hakuna anayejua" amesema Rose
Hata hivyo amesema ni msimamo wake yeye binafsi na wa familia yao kuwa hawatoweza kumsaliti Lissu kwa vyovyote.
"Tupo pamoja kuhakikisha tunamtia ndugu yetu moyo anapotuona mahakamani sio kwamba hatuna kazi" ameongeza
Haya yanatokea ikiwa kwa zaidi ya mara mbili Mange Kimambi amekuwa akizungumza na kuandika kwenye mtandao wa X tuhuma hizo.
"Dunia nzima inajua kuwa Lissu hana shilingi 100, sasa nani anailipia familia ya Lissu kuishi Sea Cliff kwa miezi mitatu?. aliandika Mange.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI:
Rais wa Kenya William Ruto ameendeleza mashambulizi yake ya kisiasa dhidi ya mtangulizi wake, Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta, akimtaja kuwa “kiongozi wa uasi” na kumkosoa kwa kuendelea kujihusisha na siasa za upinzani.
Kauli hiyo ya Ruto ni mfululizo wa shutuma ambazo amekuwa akizitoa dhidi ya Kenyatta na Mwenyekiti wa KANU, Gideon Moi, akiwatuhumu kuunga mkono upinzani dhidi ya Serikali yake.
Akizungumza katika kampeni za kuwania muhula mwingine wa urais katika Kaunti ya Siaya, jana Septemba 15, 2026, Ruto amepongeza uamuzi wa Mahakama Kuu uliomzuia Kenyatta kushikilia nafasi katika chama cha siasa.
“Nashangaa, mtu ambaye amekuwa Rais wa Kenya, unaacha kiti cha Rais, badala ya kwenda kuwa statesman, unaenda kuwa rebel leader, kiongozi wa upinzani. Mpaka sasa mahakama inamwambia atoke,” Ruto amesema.
Ruto pia amemtuhumu Kenyatta kwa kuendelea kuunga mkono viongozi wa upinzani kwa lengo la kudhoofisha Serikali yake, huku akiwataka Wakenya kutowaunga mkono viongozi anaowatuhumu kutokuwa na mipango na sera za wazi kwa ajili ya nchi.
Kauli hizo zimetolewa wakati Ruto akiendelea na kampeni zake za uchaguzi wa mwaka 2027, ambapo viongozi waliomsindikiza katika ziara hiyo pia wamekosoa upinzani na kuhamasisha wananchi kumuunga mkono. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
"Tupo timamu" anasema Wakili wa Serikali Mkuu, Nassoro Katuga kabla ya kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu kuanzaThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Kundi la EPP (The EPP Group), ambalo ni kundi kubwa na lenye nguvu zaidi la kisiasa ndani ya Bunge la Umoja wa Ulaya, limependekeza rasmi jina la mwanasiasa, wakili, na mwanaharakati wa haki za binadamu wa Tanzania, Tundu Antiphas Lissu, kuwania Tuzo ya Sakharov ya mwaka 2026 (Sakharov Prize for Freedom of Thought).
Tuzo hiyo ya Uhuru wa Kujieleza ndiyo heshima ya juu zaidi inayotolewa na Umoja wa Ulaya (EU) kwa ajili ya kutambua watu binafsi, vikundi, au mashirika yaliyojitolea maisha yao kutetea haki za binadamu, uhuru wa kujieleza, demokrasia, na utawala wa sheria.
Katika taarifa yake rasmi iliyotolewa kupitia mtandao wa X, kundi la EPP limeweka wazi sababu za kumteua Lissu likisema, “baada ya kunusurika katika jaribio la mauaji la mwaka 2017, Lissu alirejea Tanzania kuendelea kupigania mabadiliko ya kidemokrasia, lakini akakumbana na ukamataji, mashtaka ya uhaini na hakushiriki katika uchaguzi wa Urais wa mwaka 2025, huku chama chake kikizuiwa kushiriki. Kesi yake inaakisi mmomonyoko mpana wa mfumo wa vyama vingi vya kidemokrasia na ushindani wa kisiasa nchini Tanzania”.
Aidha, taarifa hiyo imeeleza kuwa Lissu anawakilisha muunganiko thabiti wa ujasiri binafsi, msimamo wa kidemokrasia na umuhimu wa siasa za dunia. Kuteuliwa kwake kunathibitisha kuwa Ulaya inasimama na wale wanaotetea demokrasia ya kikatiba na uhuru wa kisiasa barani Afrika na katika nchi zingine washirika wa EU. Bw. Lissu ni kielelezo halisi cha utetezi wa demokrasia, siasa za vyama vingi, utawala wa sheria na uhuru wa kimsingi kwa gharama kubwa sana za maisha yake binafsi.
Kutokana na taarifa hiyo, Mjumbe wa Bunge la Ulaya, David McAllister, ameeleza kuwa Lissu amekuwa kizuizini kwa zaidi ya siku 500 kwasababu ya kupigania uchaguzi huru na wa haki pamoja na mustakabali wa kidemokrasia wa nchi yake.
“Hakuna shaka yoyote kuhusu asili ya kisiasa ya kuzuiliwa kwake. Ni mfano wa wazi wa shinikizo linaloongezeka dhidi ya upinzani, maandamano ya amani na uhuru wa kisiasa nchini Tanzania”, ameeleza McAllister.
McAllister ameongeza kuwa licha ya kile alichokiita mateso na ukandamizaji, Lissu amesalia imara katika msimamo wake wa kidemokrasia na kwamba kuteuliwa kwake kuwania tuzo hiyo kunaheshimu ujasiri huo wa kipekee.
Baada ya kuteuliwa kuwania Tuzo ya Sakharov, uteuzi wa mtu husika hupitia hatua kadhaa za tathmini na mchujo ndani ya Bunge la Ulaya (European Parliament) ikiwamo kamati ya Mambo ya Nje na Kamati ya Maendeleo kuufanya kikao cha pamoja ili kufanya tathmini ya wagombea wote walioteuliwa. Kamati hizi mbili hupiga kura na kuchagua orodha fupi ya wateuliwa watatu walioingia hatua ya fainali. Baada ya hapo, Mkutano wa Marais ambao unajumuisha Rais wa Bunge la Ulaya na viongozi wa vikundi vya kisiasa hukutana na kumchagua mshindi wa mwisho (laureate).
Mshindi wa Tuzo ya Sakharov hukabidhiwa cheti cha heshima pamoja na zawadi ya fedha taslimu kiasi cha Euro 50,000 (sawa na zaidi ya Shilingi milioni 150 za Kitanzania). Hafla ya utoaji wa tuzo hii hufanyika mwezi Desemba kila mwaka katika ofisi za Bunge la Ulaya jijini Strasbourg, nchini Ufaransa.
Baada ya hapo mshindi hujiunga na Mtandao wa Tuzo ya Sakharov (Sakharov Prize Network) ambao huwasaidia kuwasiliana, kushirikiana, na kuwalinda washindi wanaokabiliwa na hatari au vitisho katika nchi zao. Washindi huendelea kufanya kazi kama mabalozi wa kutetea haki za binadamu na uhuru wa fikra duniani kote, wakishirikiana kwa karibu na Bunge la Ulaya.
Watu wengi waliowahi kushinda tuzo hii ni wale waliopitia mateso, vifungo, au hatari kubwa kwa ajili ya misimamo yao ya kutetea haki. Baadhi ya waliowahi kutunukiwa tuzo hii huko nyuma ni pamoja na Nelson Mandela, na mwanaharakati wa Urusi Anatoly Marchenko ambao ni washindi wa kwanza kabisa mwaka 1988. Kofi Annan na wafanyakazi wote wa Umoja wa Mataifa mwaka 2003), na Malala Yousafzai, mwanaharakati wa elimu kwa watoto wa kike kutoka Pakistan mwaka 2013. -
Jambo TV
@Jambotv_
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Godbless Lema ametangaza kughairi kuzungumza na waandishi wa habari kama alivyokuwa amepanga kufanya leo majira ya saa sita mchana.
Jana Septemba 15, 2026 Lema kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii alitangaza kuwa angefanya mkutano huo ambao ulilenga kufafanua tuhuma ambazo zimekuwa zikielekezwa kwake kwa siku kadhaa.
“Mkutano wangu na waandishi wa habari niliokuwa nifanye katika Hotel ya Golden Tulip nimeuahirisha. Nimesikiliza hotuba za Makamu Mwenyekiti na Katibu Mkuu. Wameeleza vizuri kuhusu uvumi na upotoshaji uliokuwa ukifanyika juu yangu na misimamo juu ya chama chetu. Nimedumu katika mapambano haya kwa zaidi ya miaka 22. Nimeenda lock-up zaidi ya mara 50. Nimezunguka nchi hii usiku na zaidi ya mara tatu. Nimewahi kuwa magerezani mara kadhaa, nimekoswa kuuawa zaidi ya mara tatu, na nimewahi kukimbia nchi. Katika yote haya, nimekuwa nikitoa sadaka kubwa kwa ajili ya mapambano haya, ikiwemo ku-sacrifice familia yangu mara zote. Kazi hii kwangu si ajira, si cheo, wala si njia ya kujitafutia maslahi. Ni huduma. Ni wito. Ni kama injili ninayoamini na kuitumikia. Kwa hiyo, siwezi kuruhusu uvumi, upotoshaji au tafsiri za watu kuniondoa kwenye misingi ambayo nimeisimamia kwa zaidi ya miongo miwili. Nitakuwa kwenye mapambano haya kwa imani, ujasiri na dhamira njema siku zote”.
Kuahirishwa kwa mkutano huu kunakuja katikati ya mjadala mzito ulioibuka nchini kufuatia kifo cha mume wa Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, Marehemu Hafidh Ameir Hassan, aliyefariki dunia Septemba 7, 2026, katika Hospitali ya Emilio Mzena na kuzikwa siku hiyo hiyo huko Kizimkazi, Zanzibar.
Wakati vyama vingine vya siasa vikienda msibani na kumfariji Rais Samia, viongozi wa CHADEMA hawakuonekana msibani wala chama kutoa taarifa rasmi ya rambirambi. Hata hivyo, Septemba 7, 2026, Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, anayekabiliwa na kesi ya uhaini na kukaa mahabusu kwa takribani mwaka mmoja na miezi sita, alisikika akiwaambia viongozi wake Mahakama Kuu Dar es Salaam: "Nasikia kuna msiba, wape pole... jamani pelekeni pole zangu kwa wafiwa".
Septemba 11, 2026, kabla ya kesi yake kuanza, Lissu alisikika akirejea salamu hizo na kuhoji kama zimefika alipomuuliza Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Zanzibar, Said Mzee: "Makamu umepeleka rambirambi zangu bwana?", na alipojibiwa kuwa zimefika, Lissu aliongeza: "Nimefurahi kama zimefika
Septemba 13, 2026, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Godbless Lema, alichapisha ujumbe kwenye mitandao ya kijamii kuwasilisha salamu alizozitaja kuwa ni za Lissu na zake mwenyewe, jambo ambalo liliwawasha baadhi ya wanaharakati na wafuasi wa mtandaoni waliomshambulia Lema kwa matusi na kumwita msaliti. Wapo waliohoji ni kwanini ampe pole Rais wakati kuna watu walikufa au kuumizwa bila kupewa pole huku wengine wakidai kuwa hakuna mahali Lissu alipoashiria salamu na pole zake zilimlenga Dkt. Samia. Hata hivyo, baadhi ya wananchi walimuunga mkono Lema na Lissu kwa kile walichokiita kuonesha ukomavu wa hali ya juu.
Akijibu mashambulizi hayo Septemba 14, 2026, Lema amesisitiza kuwa hatua ya Lissu kutoa rambirambi si unyonge bali ni hekima na ukomavu akiandika, "Nimeona matusi na sintofahamu nyingi mtandaoni baada ya kuchapisha ujumbe wa kutoa pole kwa Mama Samia, hasa niliponukuu salamu za pole za Mwenyekiti Lissu kutoka gerezani. Kwa sisi jamii tunaodai kupigania uhuru wa maoni na demokrasia, hili linapaswa kutufikirisha. Kutofautiana kwa hoja hakuhitaji matusi, dhihaka wala chuki".
Licha ya kujibu mashambulizi hayo, watumiaji mbalimbali wa mitandao ya kijamii ambao wengine ni wanaharakati waliendelea kumshambulia Lema wengine wakidai kuwa amenunuliwa na anatumika na kundi Fulani la watu kuididimiza na kuiharibu CHADEMA na viongozi wake waandamizi, na hivyo Lema akawa amedhamiria kuitisha mkutano na wanahabari. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu Mwenyekiti wa @CCMTanzania Bara, Stephen Wasira, amesema ni muhimu kwa wanachama wa chama hicho kulinda umoja, uhuru na amani ya Tanzania, akieleza kuwa hicho ni chama cha vizazi na si cha kizazi kimoja.
Wasira ameyasema hayo leo Septemba 15, 2026, wakati akifungua mafunzo ya Itikadi, Ujenzi wa Chama na Kuongeza Wanachama Wapya yaliyofanyika katika Chuo cha UVCCM Ihemi, Iringa.
Amesema kuwa pamoja na hayo chama hicho kimekuwa kikichukiwa na mabeberu kutokana na harakati za ukombozi ilizofanya barani Afrika huku baadhi ya watu walio nchini wakitumika kwa ajili ya kuharibu taswira ya taifa na chama hicho.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Chama Cha Mapinduzi @CCMTanzania kimesema kitaendelea kuwa mfano wa demokrasia nchini, kikisisitiza kuwa misingi hiyo inaanza ndani ya Chama chenyewe kwa kuzingatia misingi ya demokrasia katika uendeshaji wa shughuli zake, ikiwemo katika mchakato wa uchaguzi wa viongozi wake.
Hayo yameelezwa leo Septemba 15, 2026 na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Stephen Wasira alipokuwa akifungua mafunzo ya Iitikadi na uenezi kwa makada wa Chama yaliyofanyika katika Chuo cha CCM, mkoani Iringa.
Wasira amevitaka vyama vingine vya siasa nchini kuiga mfano huo kwa kuhakikisha vinazingatia demokrasia katika shughuli zake na uchaguzi wa viongozi wao.
Kwa upande mwingine, ameelexa CCM haiwezi kuingilia mihimili ya dola kwa kuwa kila mhimili una majukumu yake kwa mujibu wa Katiba na sheria unapaswa kutekeleza majukumu yake kwa uhuru na kwa kuzingatia sheria.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padre Dkt. Charles Kitima, amebainisha kuwa demokrasia halisi katika nchi yoyote inasimikwa kwenye utawala wa sheria, uhuru wa mahakama, uhuru wa kitaaluma wa wasomi, na uhuru wa vyombo vya habari
Akizungumza leo, Septemba 15, 2026, mkoani Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya Siku ya Demokrasia Duniani yaliyoratibiwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Padre Kitima ameeleza kusikitishwa kwake na kupungua kwa uhuru wa kitaaluma nchini, akibainisha kuwa tofauti na zamani ambapo jamii ilikuwa ikisikiliza na kupata miongozo kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, siku hizi maprofesa na wasomi wamekuwa wakiwekwa ndani.
Akitahadharisha kuhusu athari za maisha ya hofu kwa ukuaji wa uchumi na ubunifu, Padre Kitima ameongeza kuwa nchi haiwezi kufikia uchumi unaotegemea maarifa iwapo wananchi na wasomi wanaishi kwa hofu, huku akisisitiza kuwa uhuru wa vyombo vya habari vya kijamii na vya kawaida ni nguzo nyingine kuu.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linamshikilia mfanyabiashara na mkazi wa Kiseke wilayani Ilemela, Emmanuel Ntobi (41) kwa kosa la kusababisha ajali ya barabarani iliyosababisha kifo cha mtoto mmoja na kujeruhi watu wengine wawili.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, DCP Wilbrod Mutafungwa imesema ajali hiyo imetokea leo Septemba 15, 2026 saa 6:20 katika barabara ya Makongoro eneo la Nyamanoro wilayani ya Ilemela.
"Gari lenye namba za usajili T750 BPH, aina ya Toyota Mark II iliyokuwa ikiendeshwa na Emmanuel Julius Ntobi ikitokea Kona ya Bwiru kuelekea Pasiansi iliwagonga watembea kwa miguu watatu waliokuwa wakivuka barabara kutoka upande wa kulia kwenda kushoto,".
Aliyepoteza maisha katika ajali hiyo ni, Johnson Florence (7) mwanafunzi wa darasa la kwanza, Shule ya Msingi Ibungiro huku majeruhi wakiwa ni, Kodo Joel (30) mkulima na mkazi wa Pasiansi, pamoja na Janeth Nambile (3) mwanafunzi wa chekechea, Shule ya Msingi Pasiansi wote wakiwa wakiendelea na matibabu katika Hospitali ya Rufaa Sekou Toure.
"Chanzo cha ajali ni uzembe wa dereva kushindwa kuchukua tahadhari kwa watumiaji wengine wa barabara kwenye eneo hilo lenye mwingiliano wa shughuli za kijamii. Mtuhumiwa amekamatwa na taratibu za kisheria zinaendelea kufanyika ili afikishwe mahakamani," imesema taarifa hiyo. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mzee Azaveli Lwaitama, amebainisha kuwa hasira za wananchi na madai ya Katiba Mpya nchini zinachochewa na hulka ya asili ya mwanadamu ya kutopenda kutawaliwa wala kuswagwa, bali kutaka ugatuzi wa kweli wa mamlaka.
Kauli hiyo imetolewa leo, Septemba 15, 2026, mkoani Dar es Salaam na Mzee Lwaitama wakati akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Demokrasia Duniani yaliyofanywa na CHADEMA.
Akifafanua msingi wa matubwa ya mabadiliko nchini, ametahadharisha kuwa hasira zilizojitokeza mwaka jana hazitokani na chama fulani cha siasa kama baadhi ya watu wanavyofikiria, bali zinatokana na hamu ya wananchi kujitawala zaidi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Dodoso dhidi ya shahidi wa tano wa utetezi katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, John Heche, limefikia mwisho baada ya Wakili wa Serikali Mkuu, Nassor Katuga kumaliza kumuuliza maswali.
Katika sehemu ya mwisho ya dodoso, Wakili Katuga alimtaka Heche kuwaeleza majaji kwamba mtu anapotishia kuvunja amani, anakuwa anamtisha nani, ambapo Heche alijibu kuwa hajui.
Wakili Katuga alirejea kauli ya Heche kuhusu hotuba ya Jaji Chande kwamba haikuwa na majina ya waliouawa na waliowaua, akitaka kujua kama alikuwa akizungumzia Katiba au taarifa. Heche alisema ni taarifa, na alipoulizwa kama aliisoma au kuisikia, akasema aliisoma. Alipoulizwa kama ni taarifa au ripoti, Heche alisema hajui.
Wakili Katuga pia alimuuliza Heche kama anafahamu kuwa taarifa ya Jaji Chande ilikabidhiwa kwa Rais, ambapo Heche alisema anajua kwa sababu walisema kwamba wamemkabidhi.
Katika hoja nyingine, Wakili Katuga alirejea kauli ya Heche kwamba katika hotuba ya Jaji Chande hakukuwa na majina ya waliouawa na waliowaua, magari yaliyochomwa moto na mengineyo, na kumuuliza kama huo ni ushahidi aliousoma au kuusikia. Heche alisema unatokana na hotuba na mambo aliyosikia.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo @ChademaTZ2 Kanda ya Nyasa Joseph Mbilinyi(Sugu) @TheRealJongwe ametoa wito kwa wanachama wa chama hicho kuonyesha kukiunga mkono zaidi ya mitandaoni na kukiunga kwa kutokea kwenye matukio yanayokihusu chama ikiwemo kwenda mahakamani kufuatilia kesi ya uhaini inayomkabili Tundu Lissu.
Sugu ametoa wito huo leo kupitia Instagram yake akisisitiza kuwa kama kesi hiyo ingekuwa inasikilizwa kwenye Mahakama za Mbeya basi watu wangefurika kuliko ambavyo wanajitokeza kuifuatilia.
"Ni sawa na ni vizuri tunakipenda sana chama chetu @ChademaTZ2 and WE appreciate much for your support. Lakini sasa tuwe zaidi ya mitandaoni basi, tutoke ground/field ikiwemo kuja Mahakama Kuu kwenye kesi kubwa ya uhaini ya Mwenyekiti wetu LISSU. Hii kesi ingekuwa Mbeya hakika Mahakamani pasingetosha. Kesho saa tatu asubuhi tukutane mahakamani, kila siku hatuzidi hata watu 200 na wakati hii Dar ina watu 7 millioni sio poa," ameandika Sugu -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeweka msimamo mpya wa kukwamua mchakato wa Katiba Mpya nchini, kikitaka mchakato huo uanzie kwenye Rasimu ya Warioba na kutungwa kwa sheria ya kufuta yote yaliyofanywa na Bunge Maalumu la Katiba la mwaka 2014.
.
Wito huo umetolewa leo, Septemba 15, 2026, mkoani Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika, wakati akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Demokrasia Duniani yaliyofanywa na chama hicho
.
Akizungumzia uamuzi huo, Mnyika amebainisha kuwa CHADEMA imefanya tafakari ya kina kuhusu historia ya mchakato wa katiba nchini ikipitia maoni ya Tume ya Nyalali, Tume ya Warioba, mazungumzo kati ya CHADEMA, CCM na Serikali, pamoja na ripoti ya Kikosi Kazi na kuona kuwa njia pekee ya kupata katiba bora ya wananchi ni kurejea kwenye msingi wa maoni yao halisi.
"Mchakato wa mabadiliko ya katiba uhuishwe kwa kuanzia na rasimu ya pili ya wananchi yaani Rasimu ya Jaji Joseph Sinde Warioba kwa kutunga sheria ya kufuta kila kilichofanywa na bunge maalum la katiba. Msingi wa kuchagua njia hii ni kuwa rasimu ya pili ya Jaji Warioba ilikuwa ni matokeo halisi ya maoni ya wananchi. Hivyo mwafaka wa kitaifa ni lazima ubebe maoni hayo ya wananchi ambayo ndio msingi wa katiba mpya bora ya wananchi", ameeleza.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Zoezi la upande wa mashtaka kumuuliza maswali ya dodoso shahidi wa tano katika kesi ya uhaini dhidi ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, limeendelea leo Septemba 15, 2026, ambapo pamoja na mambo mengine, John Heche amekiri kwamba mshtakiwa alieleza kuwa hawakuwa tayari kushiriki uchaguzi wa namna ile ambayo alidai una kasoro na mapungufu, na kwamba kama uchaguzi huo ungesogezwa mbele, maafa yaliyojitokeza yasingetokea.
Wakili Katuga alimtaka Heche kuwaeleza majaji kama ni ushahidi wake kwamba mshtakiwa alisema, “hatuko tayari kushiriki uchaguzi wa namna hii,” walipokuwa wakipita kwa wadau, jambo ambalo Heche alikubali.
Katuga aliendelea kumuuliza kama angekuwa sahihi kusema kwamba msimamo ulikuwa kutoshiriki uchaguzi mpaka mabadiliko yafanyike, ambapo Heche alijibu kuwa ni sahihi.
Katuga pia alimtaka Heche kukumbuka kama aliieleza Mahakama kwamba Lissu alipokuwa akipita kwa wadau hakuna sehemu alitumia neno “kuhamasisha uasi,” jambo ambalo Heche alikubaliana nalo.
Katuga aliuliza kama iwapo kutakuwa na shahidi aliyesema kuwa hata kwa wadau Lissu alitumia neno “kuhamasisha uasi,” ushahidi huo utakuwa wa uongo au ukweli, ambapo Heche alisema inategemeana na muktadha.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Shahidi wa tano upande wa utetezi katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Bara, John Heche, amemaliza kujibu maswali ya ya dodoso kutoka upande wa mashtaka.
Baada ya kuhitimisha zoezi hilo, mshtakiwa aliruhusiwa na majaji kuanza zoezi la kuuliza maswali ya ufafanuzi (Re-examination) ambalo litatamatishwa kesho Septemba 16, 2026.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa mapendekezo ya kukwamua mchakato wa Katiba Mpya, kikitaka Mwenyekiti wake Tundu Lissu aachiwe huru na awepo msuluhishi wa kimataifa wa masuala yanayohusu matukio ya wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025.
Mapendekezo hayo yametolewa leo Septemba 15, 2026, mkoani Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika, wakati akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Demokrasia Duniani yaliyofanywa na chama hicho.
"La kwanza ni lazima mwenyekiti wetu…Tundu Lissu aachiwe huru na mashtaka ya wanomkabili ya uhaini yanapaswa kuondolewa ili yeye binafsi kama mwenyekiti wa chama kikuu cha siasa aongoze jopo na hatua ambazo tunazipendekeza kuchukuliwa kuwezesha nchi yetu kupatikana katika katiba mpya. Kwa hiyo tunamtaka Lissu awe huru. Na jambo hili hatulisemi tu kwa sababu sisi ni Chadema. Tunalisema kwa sababu tunaona umuhimu na nafasi yake siyo tu kama mwenyekiti wetu ila kama mdau muhimu katika kushiriki kuliunganisha taifa katika kazi ya kuandika katiba mpya", ameeleza Mnyika.
Kuhusu sharti la pili lililoelezwa na CHADEMA ni uwepo wa msuluhishi au wasuluhishi kutoka jumuiya ya kimataifa au wa ndani wenye kibali na baraka za kimataifa, ili kushughulikia matukio ya mauaji, utekwaji, na utaratibu wa kupatikana katiba mpya.
"Pili ni lazima na ni muhimu awepo msuluhishi au wasuluhishi watakaoteuliwa au kuchaguliwa na jumuia yoyote ya kimataifa ambao majukumu ya wasuluhishi hao yatakuwa ni kushughulikia mambo makuu yafuatayo. Mosi mchakato wa kushughulikia matendo na matukio ya mauaji ya kinyama yaliyotokea kabla wakati na baada ya kipindi cha tarehe 29 Oktoba pamoja na matendo ya kutekwa... Tunataka vilevile usuluhishi huo na upatanishi uhusishe mchakato wa upatikanaji, muda na utaratibu mzima wa kuukwamua mchakato wa katiba mpya uliokwama mwaka 2014", ameongeza Mnyika.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Naibu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo @ACTwazalendo Tanzania Bara, Ester Thomas, amewalalamikia watetezi wa haki na wadau wa demokrasia akidai kuwa wamekuwa wakionesha ubaguzi na upendekezeo wa chama kimoja pale vyama vya upinzani vinapokabiliwa na ukiukwaji wa misingi ya utawala wa sharia
Akizungumza leo, Septemba 15, 2026, mkoani Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya Siku ya Demokrasia Duniani yaliyoratibiwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Ester alitolea mfano wa kile alichoashiria kama dhuluma waliyoipata kwenye ugawaji wa viti maalum vya ubunge.
"Lakini leo hapa humu ndani hakuna hata mmoja aliyesema kwamba anasimama na ACT Wazalendo kupigania rule of law (utawala wa sharia). Ila leo utasikia watu wanasimama na chama fulani kupigania rule of law", ameeleza.
Ester ameongeza kuwa hata walipochukua hatua ya kwenda mahakamani kupigania haki hiyo, hakuna wadau wala wanaharakati waliojitokeza kuwasemea au kuwaunga mkono.
Akijibu malalamiko hayo na kuweka kumbukumbu sawa, Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Wakili Boniface Mwabukusi, amekanusha madai ya kuwepo kwa ubaguzi, akieleza kuwa ACT Wazalendo ni miongoni mwa wanufaika wakubwa wa jitihada na utetezi wa TLS. Wakili Mwabukusi amebainisha kuwa TLS imekuwa ikipata adhabu na madhara makubwa kutoka kwa mamlaka kwa sababu ya msimamo wake thabiti wa kuitetea ACT Wazalendo pale ilipoona imeonewa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imewataka wafanyabiashara wanaotegemea maji katika shughuli zao za kila siku wakiwamo waosha magari, wafyatua matofali, na watunza bustani kushiriki kikamilifu katika kudhibiti upotevu wa maji na kulinda miundombinu ya huduma hiyo.
Wito huo umetolewa wakati wa kikao maalum cha kutoa elimu kwa wafanyabiashara hao kilichojikita kwenye matumizi sahihi ya nishati hiyo ya maji, sheria na taratibu za huduma, pamoja na umuhimu wa kutoa taarifa mapema pindi uvujaji au uharibifu wa miundombinu unapojitokeza.
Akizungumza katika kikao hicho, Afisa Sheria wa DAWASA, Ezekiel Lwenge, amesisitiza kuwa upatikanaji endelevu wa maji unategemea sana nidhamu ya ufuataji sheria, huku akiwaonya wateja kujiepusha na maunganisho yasiyo halali, kuchezea mita, au kufungua na kuhamisha vifaa vya huduma bila kibali rasmi cha DAWASA.
Naye Meneja wa Mkoa wa Kihuduma DAWASA Kawe, Alex Ng'wandu, amebainisha kuwa wafanyabiashara hao wana nafasi kubwa ya kuwa walinzi wa rasilimali ya maji kutokana na kutumia huduma hiyo kwa kiasi kikubwa kwenye uzalishaji wao.
“Maji ni muhimu katika uzalishaji na shughuli za biashara. Bila maji, biashara nyingi haziwezi kuendelea, hivyo ni muhimu kila mmoja kushiriki kulinda rasilimali hii,” amesema Ng'wandu.
Wakisimamia uhalisia wa elimu hiyo, Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa Bustani kutoka Mbezi Beach Africana, Jafari Mohammed, pamoja na Juma Lazaro, mfanyabiashara wa kuosha magari kutoka Kinondoni Mkwajuni, wameishukuru DAWASA kwa kuwajengea uelewa wa sheria hizo na kuahidi kuwa sehemu ya suluhu ya kulinda miundombinu na kupunguza upotevu wa maji jijini Dar es Salaam. -
Jambo TV
@Jambotv_
Balozi wa Norway nchini Tanzania, Tone Tinnes, amesema kuwa demokrasia si lengo lililokamilika mara moja bali ni mchakato endelevu unaohitaji kufanywa upya na kudumishwa na kila kizazi.
Kauli hiyo imetolewa leo, Septemba 15, 2026, mkoani Dar es Salaam wakati Balozi Tinnes akizungumza kwenye maadhimisho ya Siku ya Demokrasia Duniani yaliyoratibiwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC).
Balozi Tinnes amebainisha kuwa ingawa demokrasia inakabiliwa na changamoto kubwa duniani kote, ikiwa ni pamoja na kupungua kwa uaminifu wa umma na kubana kwa nafasi za kiraia barani Ulaya na Afrika Mashariki, tafiti za kimataifa zinaonesha kuwa watu wengi barani Afrika bado wanapendelea demokrasia kuliko mifumo ya kiimla.
Ameongeza kuwa matukio ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025 na yaliyofuata nchini Tanzania yanakumbusha kuwa demokrasia haiwezi kuchukuliwa kama jambo lililojipata lenyewe bila kuilinda na kuiimarisha.
Akizungumzia misingi mikuu inayowezesha demokrasia kuwa imara, Balozi Tinnes amesema, “demokrasia imejengwa kwa muda na kudumishwa kupitia kujitolea kwa mwendelezo... Kwanza, taratibu za kidemokrasia lazima ziwe za wazi, zenye kuaminika na za haki. Pili, demokrasia inahitaji ushindani halisi wa kisiasa na ushiriki wenye maana. Watu lazima wawe huru kueleza mitazamo tofauti, kujipanga kwa amani na kushiriki katika mijadala ya umma bila hofu”.
Akiendelea kufafanua, mwanadiplomasia huyo ameeleza kuwa ustahimilivu wa demokrasia unategemea kuwepo kwa utawala wa sheria ambapo sheria inatendeka kwa usawa kwa wananchi wote bila ubaguzi. Amesisitiza kuwa utawala wa sheria ndio unaobadili misingi ya kidemokrasia kuwa vitendo vinavyolinda haki za raia na kuwezesha walio madarakani kuwajibishwa
"Demokrasia ni zaidi ya uchaguzi pekee. Inategemea taasisi imara, mgawanyo wa wazi wa madaraka na ulinzi unaodumisha uwazi, uwajibikaji na ushindani wa haki wa kisiasa. Utawala wa sheria unabadilisha misingi ya kidemokrasia kuwa vitendo, unalinda haki, na kuhakikisha wale wanaotekeleza madaraka wanaweza kuwajibishwa", ameongeza Balozi Tinnes.
Aidha, Balozi Tinnes ameeleza kuwa sheria na taasisi pekee hazitoshi bila kuwepo kwa mashirika huru ya kiraia yanayofanya kazi ya kusikiliza wananchi, kutetea haki, na kuhimiza uwajibikaji. Amepongeza jitihada za muda mrefu za LHRC nchini Tanzania katika kutetea haki za binadamu, upatikanaji wa haki, na mabadiliko ya kisheria, akibainisha kuwa Norway inajivunia ushirikiano wake wa muda mrefu na kituo hicho
"Katika kuadhimisha Siku ya Demokrasia Duniani, tukumbuke kwamba demokrasia haijawahi kukamilika mara moja na kwa wote. Sio lengo, ni mchakato... Kupitia mazungumzo ya wazi, kuheshimu haki za binadamu, taasisi imara na mashirika ya kiraia yanayofanya kazi, Tanzania na Norway zinaweza kuendelea kujenga demokrasia jumuishi, inayowajibika na yenye ustahimilivu", ameeleza. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI:
Jeshi la Polisi Mkoa wa Rukwa limetoa ufafanuzi juu ya picha mjongeo inayomwonesha Kijana mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Pilato, akilumbana na Askari Polisi katika ibada iliyofanyika katika Kanisa Katoliki la Mlima Itwelele, Sumbawanga.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa leo Septemba 15, 2026, tukio hilo lilitokea Septemba 13, 2026 wakati wa ibada maalum ya Hijja iliyofanyika kwa waumini wa dhehebu la Kanisa Katoliki, ambapo miongoni mwa ibada hizo kulikuwa na kuhubiri Msamaha na kutoa sadaka.
Taarifa hiyo inaeleza kuwa wakati ibada ikiendelea, kijana huyo alitaka kwenda kuubusu Msalaba huku akiwa amelewa pombe jambo lililoonekana kuwa kinyume na utaratibu wa ibada hiyo, viongozi walimzuia asiende eneo hilo.
Baada ya kukataliwa, Pilato alidaiwa kutoa maelekezo ya viongozi na kuanza kufanya vurugu huku akilumbana na Askari Polisi aliyekuwa akisimamia usalama, askari huyo alifanikiwa kumuondoa eneo hilo na ibada ikaendelea kwa amani na utulivu.
Jeshi la Polisi limesema linaendelea na uchunguzi kuhusu tukio hilo kwa ajili ya kuchukua hatua zaidi. -
Jambo TV
@Jambotv_
Baada ya shahidi wa tano katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, kuiambia Mahakama kwamba hakuwahi kuitwa na Tume ya Rais ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani Wakati na Baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 (Tume ya Jaji Chande), Wakili wa Serikali Mkuu Nassor Katuga amemuonesha nyaraka ambazo ni barua zilizomtaka kufika mbele ya tume hiyo.
Shahidi huyo ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Heche, amesisitiza msimamo wake wa awali akidai kuwa hakuwahi kupokea wito wowote rasmi kutoka kwa chombo hicho cha uchunguzi ingawa Wakili wa Serikali Mkuu, Nassor Katuga aliomba ridhaa ya Mahakama na kumkabidhi mfululizo wa nyaraka ambazo zilikuwa ni barua ili kuupima ukweli wa kauli yake, ambapo Heche alizipokea, kuzitazama na kuzisoma mbele ya jopo la majaji.
Katika uchunguzi huo wa vielelezo, Heche alithibitisha kuwa barua ya kwanza ilitaja sanduku la posta 31191 linalomilikiwa na chama hicho. Wakili Katuga aliendelea kumuuliza shahidi huyo kwa kumwonesha barua ya pili na ya tatu, ambapo Heche alilazimika kusoma vichwa vya habari vilivyothibitisha wito wa wazi wa kutakiwa kukutana na tume hiyo ya Rais kuzungumzia matukio hayo ya Oktoba 2025.
Licha ya kubanwa na vielelezo hivyo vya kimaandishi ambavyo amesema pia vilielekezwa pia kwa Katibu Mkuu wa CHADEMA, Heche alikataa katakata pale alipoulizwa kama angetaka barua hizo zipokelewe rasmi kama ushahidi wa kesi hiyo mahakamani hapo.
Katuga alimuuliza heche pia kama alikuwa na ufahamu kuwa Tume hiyo ilitoa tangazo kwa umma ikiruhusu kuwasilisha ushahidi kwa tume hiyo kuhusu matukio ya Oktoba 29, 2025 kupitia njia mbalimbali za kidijiti kama SMS, WhatsApp na barua pepe kwa wasiotaka kufika mbele ya Tume hiyo ambapo Heche akasema hakuwa na ufahamu huo.
Heche alihitimisha kwa kufafanua kuwa msimamo wao haukuwa kukataa kutoa ushirikiano kwa ujumla, bali walipinga wazi muundo uliotumika kuunda Tume hiyo ya Jaji Chande. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwasisi wa chama cha siasa kinachotafuta usajili cha Independent People's Party (IPP), Gregory Urima ametoa malalamiko mbele ya Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza, kuhusu mchakato wa usajili wa vyama vya siasa nchini akidai kuwa ofisi hiyo inasahau wajibu wao wa msingi wa kusajili na kulea vyama ili kujenga ushindani wa kisiasa.
Ametoa malalamiko hayo leo, Septemba 15, 2026, mkoani Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya Siku ya Demokrasia Duniani yaliyoratibiwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC).
Urima ameeleza kuwa yeye pamoja na mwenzake Andrew Bomani waliipeleka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa Mahakama Kuu kupigania usajili wa chama chao cha IPP. Licha ya kwenda mahakamani na kutokea kile alichokiita kuangushwa kwa makusudi, Urima amedai kuwa viongozi wa ofisi hiyo wanapaswa kuona aibu kwa mambo yanayotokea, huku akiwaomba wadau wa siasa nchini kutambua kilio chao kuhusu vikwazo vya usajili.
Akijibu na kutolea ufafanuzi malalamiko hayo, Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza, ameyataja madai hayo kuwa ya uongo na yasiyo na ukweli. Nyahoza amekanusha madai kwamba ofisi hiyo haijasajili vyama kwa karibu miaka 30, akitolea mfano chama cha ACT Wazalendo kilichopata usajili mwaka 2014.
Kuhusu shauri la mahakamani lililofunguliwa na Urima, Nyahoza amebainisha kuwa mwombaji huyo alishindwa mahakamani baada ya kuonekana kuwa mchakato wa usajili ulikuwa ukiendelea, akisisitiza kuwa usajili wa vyama unahitaji kutimiza masharti ya kisheria.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, imeahirishwa hadi saa nane na nusu mchana huu ambapo itakapo rejea, shahidi wa tano katika kesi hiyo, ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Bara, John Heche, ataendelea kuulizwa maswali ya dodoso na upande wa Jamhuri.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Chama cha ACT Wazalendo kimetoa wito kwa Watanzania wote kuungana na kudai kwa nguvu zote kuanzishwa mara moja kwa mchakato wa Katiba Mpya ya wananchi huku kikisema kuwa kinaamini kuwa mkwamo wa kisiasa unaoendelea nchini hauwezi kutatuliwa kwa viraka, marekebisho ya hapa na pale wala maboresho ya katiba iliyopo.
Akitoa wito huo leo, Septemba 15, 2026 kama sehemu ya ujumbe wa maadhimisho ya Siku ya Demokrasia Duniani, Kiongozi wa ACT Wazalendo, Dorothy Semu, ameeleza kuwa nchi bado inakabiliwa na mkwamo mkubwa wa kisiasa unaodhihirishwa na kubanwa kwa uhuru wa habari na kujieleza, kukandamizwa kwa vyama vya upinzani, pamoja na kukamatwa na kufunguliwa kesi kwa wakosoaji wa serikali
Aidha, amebainisha kuwa ubinywaji huo wa demokrasia umefikia kiwango cha kutisha ukidhihirishwa na kesi za uhaini, ugaidi, na matukio ya kutekwa, kupotea, na kuuawa kwa wananchi bila kuwepo kwa uwajibikaji wa kutosha.
Semu ameeleza kuwa Katiba Mpya ndiyo njia pekee itakayoweka misingi imara ya demokrasia, kulinda haki na uhuru wa raia, kuweka mipaka ya mamlaka ya dola, na kujenga taasisi huru zitakazohakikisha uwepo wa chaguzi huru na za haki.
"Tunaamini kuwa mkwamo wa kisiasa unaoendelea nchini hauwezi kutatuliwa kwa kuweka viraka katika katiba yetu kufanya marekebisho ya hapa na pale wala maboresho ya katiba iliyopo. Tunapoadhimisha siku hii ya kimataifa ya demokrasia mwaka huu wa 2026, Tanzania bado tuna mkwamo mkubwa wa kisiasa unaodhihirishwa na kubanwa kwa uhuru wa habari na kujieleza, kukandamizwa kwa vyama vya upinzani, kukamatwa na kufunguliwa kesi kwa wakosoaji wa serikali pamoja na matukio ya kutekwa, kupotea na kuuawa kwa wananchi bila uwajibikaji wa kutosha", ameeleza.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mjadala mkali na majibizano yamezuka kati ya mwanahabari mkongwe Jenerali Ulimwengu, Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padre Dkt. Charles Kitima, na mwanahabari Charles William kuhusu takwimu za uchaguzi, viti maalum vya ubunge, na uhalali wa taarifa za matokeo nchini.
Majibizano hayo yametokea leo, Septemba 15, 2026, mkoani Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya Siku ya Demokrasia Duniani yaliyoratibiwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC).
Katika majibizano hayo, Padre Kitima amebainisha kuwa taasisi za dini haziruhusiwi na sheria iliyotungwa na Watanzania kwenda kwenye vituo vya kura kuangalia jinsi watu wanavyopiga kura. Amefafanua kuwa taarifa za matokeo ya uchaguzi alizipata kupitia vyombo vya habari baada ya kutangazwa siku kabla ya kuapishwa kwa Rais na wabunge.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padre Dkt. Charles Kitima, amebainisha kuwa kuvurugwa na kuondolewa kwa dhana ya ushindani wa haki wa kisiasa ndicho chanzo kikuu kilichoharibu mfumo wa uchaguzi na misingi ya demokrasia nchini.
Kauli hiyo imetolewa leo, Septemba 15, 2026, mkoani Dar es Salaam wakati Padre Kitima akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Demokrasia Duniani yaliyoratibiwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC).
Akirejea msingi wa kihistoria wa taifa, Padre Kitima ameeleza kuwa Mwalimu Julius Nyerere aliweka msingi thabiti baada ya uhuru kwamba uhalali wa kiongozi kuongoza lazima utokane na ushindani wa haki na wa wazi kutoka kwa wananchi, kulingana na misingi ya Katiba inayoeleza kuwa uongozi ni dhamana na wananchi ndio wenye mamlaka ya utawala
"Mwaka 1962 Nyerere alisema siwezi kuwa rais wa nchi bila kuchaguliwa na wananchi baada ya kuwa tumepata uhuru tarehe 9 Disemba 1961, akasema lazima nichaguliwe nipate kile kitu kinaitwa legitimacy... ule uhalali wa kuongoza upatikane kwa ushindani ulio halali unaotoka kwa wapiga kura wananchi wenyewe. Kwa sababu tunaamini na Nyerere alijaribu kujitahidi sana kuaminisha Watanzania kwamba uongozi ni dhamana", ameeleza Padre Kitima.
Akifafanua kuhusu sababu zilizofanya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 kuwa na idadi kubwa ya wagombea urais waliofikia 17 ukilinganisha na chaguzi za nyuma, Padre Kitima amefafanua kuwa hali hiyo haikutokana na kukua kwa demokrasia, bali ilitokana na mbinu za makusudi za kuondoa ushindani halisi wa kisiasa ulioanza kubomolewa tangu mwaka 2019 na 2020.
Ameongeza kuwa michakato hiyo ya kisiasa ilianza kuvurugwa kuanzia ndani ya vyama vya siasa kabla hata ya kufika kwenye uchaguzi mkuu.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Wakili Boniface Mwabukusi, amepinga vikali madai ya kuwepo kwa maboresho katika mifumo ya uchaguzi na demokrasia nchini, akisisitiza kuwa Tanzania imerudi nyuma hadi kwenye hali mbaya zaidi kuliko hata wakati wa mfumo wa chama kimoja.
Kauli hiyo imetolewa leo, Septemba 15, 2026, mkoani Dar es Salaam wakati Mwabukusi akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Demokrasia Duniani yaliyoratibiwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC).
"Tuko nyuma zaidi ya pale tulipokuwa... 2015 tulifika mahala, sasa tumerudi nyuma sana. Mtu ukiniuliza siwezi, kwa sababu hata 95 kulikuwa na ushindani mkubwa, tuliuona watu hawakuondolewa ule uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi. Kwa sasa tumerudi kwenye hali ambayo ni mbaya kuliko ilivyokuwa wakati wa mfumo wa chama kimoja", ameeleza Mwabukusi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwenyekiti wa zamani wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Bahame Tom Nyanduga, amedai kuwa kuwa taifa la Tanzania limejeruhiwa na wananchi wanaishi kwa hofu kubwa kutokana na mwendelezo wa matukio ya mauaji, utekwaji, na upoteaji wa watu nchini.
Kauli hiyo imetolewa leo, Septemba 15, 2026, mkoani Dar es Salaam wakati Nyanduga akizungumza kama mgeni rasmi katika maadhimisho ya Siku ya Demokrasia Duniani yaliyoratibiwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC).
Nyanduga ameeleza kuwa jukumu kuu la serikali katika nchi yoyote ni kulinda usalama wa nchi na raia wake, na kwamba matendo ya ukatili si mambo yanayopaswa kushuhudiwa katika mfumo wa kidemokrasia. Amebainisha kuwa matatizo hayo ya utekwaji na unyanyasaji yamekuwa yakitokea katika kipindi cha miaka 10 iliyopita, yakiwepo kabla ya uchaguzi wa Oktoba 2025 na kuendelea mpaka sasa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega, ameanza ziara barani Asia ambayo mojawapo ya madhumuni ni kukutana na kuvutia wawekezaji kuja Tanzania ili kuwekeza katika ujenzi wa barabara za kimkakati nchini kupitia Ushirikiano baina ya Serikali na Sekta Binafsi (PPP).
Barabara za kimkakati ni zile zinazounganisha Tanzania na nchi jirani, bandari za Tanzania na maeneo yenye uzalishaji na masoko nchini na nje ya nchi na barabara zinazounganisha nchi na maeneo ya kibiashara kama mikoa inayokuza utalii.
Ziara hiyo itamfikisha katika nchi za China na Korea Kusini ambazo baadhi ya wawekezaji wake tayari wameonesha nia ya kutaka kuwekeza nchini. Nchini China, tayari Ulega amekutana na baadhi ya wawekezaji na kujionea baadhi ya miradi mikubwa ambayo inajengwa kwa kutumia njia ya PPP.
Kupitia PPP, kampuni binafsi zinaweza kujenga barabara, madaraja na miundombinu mingine katika nchi husika, kwa makubaliano maalumu na serikali kwamba baada ya kurejesha gharama za uwekezaji na faida yake, miundobinu husika itabaki kuwa mali ya serikali.
Nchini Korea Kusini, Ulega anatarajiwa kuwa mmoja wa wazungumzaji wakuu katika Kongamano la Kimataifa la Masuala ya Miundombinu Duniani linalotarajiwa kuanza leo jijini Seoul. Kongamano hilo hukutanisha wadau muhimu katika sekta ya ujenzi zikiwamo taasisi za kifedha, serikali, wawekezaji na wataalamu wa sekta hiyo. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, Padre Dkt. Charles Kitima akiteta na Katibu Mkuu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda pamoja na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika(TLS) Wakili Boniface Mwabukusi katika Mjadala wa Tathmini ya Demokrasia Uchaguzi na Katiba Hali ya Demokrasia Nchini katika kuadhimisha Siku ya Demokrasia Duniani ulioandaliwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu(LHRC) tukio linalofanyika hoteli ya Four Points by Sheraton.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwenyekiti wa zamani wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Bahame Tom Nyanduga, ameonya kuwa kutoheshimu ukuu wa katiba na kupuuzwa kwa taasisi za kidemokrasia kunasababisha kuingia kwa dalili za utawala wa mabavu na imla nchini.
Onyo hilo limetolewa leo, Septemba 15, 2026, mkoani Dar es Salaam na Nyanduga wakati akizungumza kama mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya Siku ya Demokrasia Duniani yaliyoratibiwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC).
Akifafanua kuhusu maana ya demokrasia, Nyanduga ameeleza kuwa demokrasia si tukio la muda mfupi bali ni mchakato endelevu unaoanza tangu huko nyuma. Amebainisha kuwa matukio ya vurugu na mauaji yaliyotokea Oktoba, 2025 yalikuwa ni mwendelezo wa changamoto za kidemokrasia zilizokuwa zikiendelea tangu huko nyuma
Akiingia kwa kina kwenye chanzo cha changamoto hizo, Nyanduga amebainisha kuwa tatizo kubwa ni kutoheshimu ukuu wa katiba jambo linalosababisha mmomonyoko wa utawala bora, kuheshimu haki za binadamu, na utawala wa sheria. Ametahadharisha kuwa mtazamo huo unasababisha viashiria vya utawala wa mabavu kuanza kuingia katika mfumo wa kisiasa wa Tanzania.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimebainisha kuwa njia kuu ya kupata suluhu ya changamoto za kidemokrasia nchini ni kupitia majadiliano ya wazi, kuimarisha utawala wa sheria, uwajibikaji, na kulinda uhuru wa vyombo vya habari.
Wito huo umetolewa leo, Septemba 15, 2026, mkoani Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Dkt. Anna Henga, wakati akizungumza kwenye maadhimisho ya Siku ya Demokrasia Duniani yaliyoratibiwa na kituo hicho kikitawala mijadala na wadau mbalimbali.
Akifafanua wigo wa demokrasia, Dkt. Henga ameeleza kuwa demokrasia inajumuisha haki za binadamu, ushiriki wa wananchi kwenye mikutano na masuala ya maendeleo, pamoja na uwepo wa katiba bora. Ameongeza kuwa lengo la maadhimisho hayo si kuangalia tu mambo yaliyopita kwa masikitiko, bali ni kutathmini yaliyotokea ili kujifunza nini kilikwenda vizuri na nini kilikwenda vibaya ili kuchukua hatua za kusonga mbele
"Masuala ya utawala wa sheria, masuala ya uwajibikaji, masuala ya ufikiwaji wa haki, masuala ya haki za binadamu, yote hayo ni utawala wa sharia, ni demokrasia, masuala ya uhuru wa vyombo vya habari yote hiyo ni demokrasia, masuala ya ushiriki wa wananchi kwenye mikutano, kwenye masuala mbalimbali ya maendeleo ya nchi, yote hiyo ni demokrasia, masuala ya katiba ni demokrasia, pia kwahiyo leo tutajadiliana kwa kina masuala haya lakini pia kwetu sio tu kuangalia mambo ya zamani yaliyopita mwaka jana kwa masikitiko pekee yake bali tunataka tujifunze kwamba yale yaliyotokea tumejifunza nini, nini kilikwenda vizuri, nini kilikwenda vibaya na tunachukua hatua gani kutoka hapa tulipo", ameeleza Dkt. Henga.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD) kimewataka Watanzania na wadau wa siasa kuheshimu tofauti za kifikra na kisiasa, kikisisitiza kuwa utofauti huo unapaswa kuchukuliwa kama nguvu ya kujenga taifa na wala sio udhaifu au uadui
Wito huo umetolewa leo, Septemba 15, 2026, mkoani Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa TCD, Bernadetha Kafuko, wakati akizungumza kwenye maadhimisho ya Siku ya Demokrasia Duniani yanayoratibiwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC).
Akizungumzia hali ya kisiasa na kidemokrasia nchini, Kafuko amebainisha kuwa mfumo umekuwa ukikabiliwa na changamoto ambapo kutofautiana kimawazo kumekuwa kukitafsiriwa vibaya kama uadui na kusaidia kuzaa chuki katika jamii. Ametahadharisha kuwa mtazamo huo unapingana na maana halisi ya demokrasia, ambayo msingi wake mkuu ni watu wenye mitazamo tofauti kushawishiana kwa hoja ili kufikia mwafaka.
"Lazima sana tuwe na mifumo madhubuti ya mazungumzo na pia tuheshimu kuwa fikra na mitizamo tofauti na tofauti ambazo tunazipitia za kimfumo za kifikra na za kisiasa tuzichukulie kama nguvu ya taifa na sio udhaifu wala uadui. Hapa Tanzania saa hizi kutokana na kwamba kumetikiswa sana na mifumo ya demokrasia, ukitofautiana kimawazo na mwenzio anakuona wewe adui, kunakuwa na chuki dhidi yetu, lakini hiyo sio maana halisi ya demokrasia. Maana halisi ni kwamba wote tuna mawazo tofauti tofauti tuweze kushawishiana kwa hoja ili tuweze kufikia mwafaka", ameeleza Kafuko.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI:
Katika maadhimisho ya Siku ya Demokrasia Duniani, leo Septemba 15, 2026, Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania, (THRDC) umetoa wito kwa Serikali, taasisi za umma, vyama vya siasa, wananchi na wadau wa demokrasia kuchukua hatua za kulinda na kuimarisha misingi ya demokrasia nchini.
Kupitia taarifa iliyotolewa na Mratibu wa Mtandao huo nchini, Onesmo Olengurumwa, THRDC imetaka kulindwa na kupanuliwa kwa nafasi ya kiraia ili wananchi, asasi za kiraia na Watetezi wa Haki za Binadamu waweze kutekeleza majukumu yao kwa uhuru na usalama, huku uhuru wa kujieleza, vyombo vya habari, kukusanyika, kujiunga na kupata taarifa ukilindwa kwa vitendo.
Mtandao huo pia umetoa wito wa kujengwa kwa uwanja sawa wa kisiasa, kuimarishwa kwa uhuru na uwajibikaji wa taasisi za kidemokrasia, pamoja na kufanyika kwa mapitio ya sheria zinazobana nafasi ya kiraia.
Aidha, THRDC imetaka madai ya ukiukwaji wa haki za binadamu kuchunguzwa kwa uhuru, uwazi na ufanisi, huku wahusika wakichukuliwa hatua na waathirika kupata haki na nafuu stahiki
Katika suala la ushiriki wa wananchi, THRDC imehimiza kuimarishwa kwa nafasi ya vijana, wanawake, watu wenye ulemavu na makundi mengine katika uundaji wa sera, sheria na maamuzi ya kitaifa.
THRDC pia imependekeza kuanzishwa na kuendelezwa kwa mazungumzo na maridhiano ya kitaifa yatakayosaidia kupunguza migawanyiko, kujenga umoja na kurejesha imani ya wananchi katika taasisi na michakato ya kidemokrasia.
Kuhusu Katiba, THRDC imetaka kukamilishwa kwa mchakato wa Katiba Mpya kwa njia ya wazi, jumuishi na shirikishi yenye umiliki wa wananchi, pamoja na kufanyiwa kazi kwa mapendekezo ya Tume za Nyalali, Warioba na Chande Othman.
Kwa upande wa vyama vya siasa, THRDC imevitaka kuimarisha demokrasia ndani ya vyama, hususan katika uchaguzi wa viongozi, uteuzi wa wagombea na maamuzi ya ndani, huku wanachama wenye maoni tofauti wakipewa nafasi ya kushiriki bila vitisho au ubaguzi.
Aidha, THRDC imewataka wananchi kujenga utamaduni wa kuvumiliana na kuheshimu tofauti za maoni, ikisisitiza kuwa kutofautiana kwa mawazo si uadui, bali ni sehemu muhimu ya jamii huru na ya kidemokrasia. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Dodoso dhidi ya shahidi wa tano wa upande wa utetezi katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, John Heche, limeendelea katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo Dar es Salaam, ambapo Wakili wa Serikali Mkuu, Nassor Katuga, ameendelea kumuuliza maswali kuhusu baadhi ya taarifa alizozitoa wakati wa ushahidi wake.
Katika moja ya maswali, Wakili Katuga amemuuliza Heche kuhusu thamani ya baadhi ya mali, ikiwemo gari aina ya Prado, trekta na Mitsubishi.
Heche amesema Prado hiyo ina thamani ya shilingi milioni 80, trekta pia milioni 80, huku Mitsubishi ikiwa na thamani ya shilingi milioni 60.
Alipoulizwa alinunua mali hizo akiwa katika nafasi gani, Heche amesema alinunua akiwa Makamu Mwenyekiti.
Wakili Katuga pia amemuuliza kama ni kweli kwamba katika kipindi chote ambacho amekuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA hajawahi kulipwa fedha yoyote kutokana na nafasi hiyo, huku Heche akitaka kufahamu ni nani anayelipia.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Wadau wa siasa nchini wamekitahadharisha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) @ChademaTZ2 kujitenga na mienendo ya wanaharakati wanayoitaja kuwa inadhibitiwa na hisia za mtandaoni, ili kulinda uwezekano wake wa kuaminiwa na wapiga kura na kushika dola.
Akimulika tofauti kati ya uanaharakati na siasa za chama cha dola, msanii Ibrahim Musa maarufu kama Roma Mkatoliki ameeleza kuwa wanaharakati mara nyingi hufuata mtazamo wa "jino kwa jino" ambapo adui anapofikwa na maafa huchukulia hatua hiyo kwa hisia na hata kushangilia maafa hayo.
Kupitia andiko lake kupitia mitandao ya kijamii, Roma ameonya kuwa CHADEMA kama chama chenye ajenda ya kupinga, kukosoa, na hatimaye kushika dola hakiwezi kufuata mkondo huo wa hisia.
Roma ametahadharisha kuwa chama cha upinzani kinapaswa kujiepusha na viashiria vya ukatili kabla hata hakijashika dola, kwani mpiga kura anaweza kuingiwa na hofu na kuamua kubaki na mtawala aliyepo sasa.
“Kama unamkosoa kiongozi wa Chadema kwenye maoni kisha aka-kublock means huyo siku akiwa tu DC ukakosoa atakuweka ‘ndichi’ (ndani) masaa 72!! Ni lazima anayempinga mtawala asiwe na characters za mtawala!!”
Tahadhari hiyo inakuja katikati ya mjadala mzito ulioibuka nchini kufuatia kifo cha mume wa Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, Marehemu Hafidh Ameir Hassan, aliyefariki dunia Septemba 7, 2026, katika Hospitali ya Emilio Mzena na kuzikwa siku hiyo hiyo huko Kizimkazi, Zanzibar.
Wakati vyama vingine vya siasa vikienda msibani na kumfariji Rais Samia, viongozi wa CHADEMA hawakuonekana msibani wala chama kutoa taarifa rasmi ya rambirambi. Hata hivyo, Septemba 7, 2026, Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, anayekabiliwa na kesi ya uhaini na kukaa mahabusu kwa takribani mwaka mmoja na miezi sita, alisikika akiwaambia viongozi wake Mahakama Kuu Dar es Salaam: "Nasikia kuna msiba, wape pole... jamani pelekeni pole zangu kwa wafiwa".
Septemba 11, 2026, kabla ya kesi yake kuanza, Lissu alisikika akirejea salamu hizo na kuhoji kama zimefika alipomuuliza Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Zanzibar, Said Mzee: "Makamu umepeleka rambirambi zangu bwana?", na alipojibiwa kuwa zimefika, Lissu aliongeza: "Nimefurahi kama zimefika".
Septemba 13, 2026, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Godbless Lema @godbless_lema , alichapisha ujumbe kwenye mitandao ya kijamii kuwasilisha salamu alizozitaja kuwa ni za Lissu na zake mwenyewe, jambo ambalo liliwawasha baadhi ya wanaharakati na wafuasi wa mtandaoni waliomshambulia Lema kwa matusi na kumwita msaliti. Wapo waliohoji ni kwanini ampe pole Rais wakati kuna watu walikufa au kuumizwa bila kupewa pole huku wengine wakidai kuwa hakuna mahali Lissu alipoashiria salamu na pole zake zilimlenga Dkt. Samia. Hata hivyo, baadhi ya wananchi walimuunga mkono Lema na Lissu kwa kile walichokiita kuonesha ukomavu wa hali ya juu.
Akijibu mashambulizi hayo Septemba 14, 2026, Lema amesisitiza kuwa hatua ya Lissu kutoa rambirambi si unyonge bali ni hekima na ukomavu akiandika, "Nimeona matusi na sintofahamu nyingi mtandaoni baada ya kuchapisha ujumbe wa kutoa pole kwa Mama Samia, hasa niliponukuu salamu za pole za Mwenyekiti Lissu kutoka gerezani. Kwa sisi jamii tunaodai kupigania uhuru wa maoni na demokrasia, hili linapaswa kutufikirisha. Kutofautiana kwa hoja hakuhitaji matusi, dhihaka wala chuki"
Naye mwanahabari Stanslaus Lambart ameeleza kuwa siasa lazima ziende na utu na kwamba Lissu na Lema walitumia nafasi hiyo kutuma ujumbe wa ubinadamu kwa washindani wao huku naye akitoa tahadhari kwa viongozi wa CHADEMA dhidi ya kutekwa na uanaharakati wa mtandaoni.
"Moja kitu kitakachoiumiza CHADEMA ni kuruhusu wanaharakati kuendesha siasa kwa shinikizo la mtandaoni (mob psychology) badala ya stadi za kisiasa zenye mikakati, diplomasia, na wakati mwingine lugha za staha hata kwa adui. Lakini mwanaharakati yeye anataka kila kitu kiwe cha ‘kupigana au kufa’ bila kuiachia akili nafasi”, ameandika Lambart na kuongeza,
"Ukiniambia niishauri CHADEMA, nitawaambia wajikite kwenye misingi ya siasa na wasikubali kuendeshwa kwa hofu ya nini kitasemwa X (Twitter) au Instagram na wanaharakati, otherwise itapoteza muelekeo". -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Dodoso dhidi ya shahidi wa tano wa upande wa utetezi katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, John Heche, limeendelea katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo Dar es Salaam, huku mawakili wa upande wa mashtaka wakijikita katika kuhoji baadhi ya taarifa alizozitoa wakati wa kutoa ushahidi wake.
Akijibu maswali ya Wakili Ignas Mwinuka, Heche amesema amewahi kushiriki katika chaguzi kuu tatu za ubunge kupitia CHADEMA, ambapo alishinda katika chaguzi mbili.
Heche amekana kwamba katika chaguzi hizo alishuhudia polisi wakijaza kura kwenye masanduku au mawakala wa chama chake kuzuiwa kufanya kazi zao. Pia amesema matokeo ya uchaguzi wa ubunge yanaweza kupingwa katika Mahakama Kuu, lakini amekiri kwamba hakuwahi kupinga matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2020.
Katika eneo lingine, Heche ameulizwa kuhusu taratibu za wagombea kujaza fomu za kugombea nafasi mbalimbali za kisiasa. Amesema kujaza fomu ni moja ya vigezo vinavyohitajika, lakini akafafanua kwamba hakujaza mwenyewe fomu ya aliyekuwa mgombea Susan Kiwango, ingawa alisema alihusika katika masuala ya malalamiko yaliyohusiana na uchaguzi huo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema kuundwa kwa Kamati ya Pamoja ya Majadiliano yenye wajumbe kutoka CCM na ACT Wazalendo ni hatua muhimu katika kuendeleza mchakato wa maridhiano na kuimarisha amani, umoja na utulivu wa kisiasa Zanzibar.
Dkt. Mwinyi amebainisha kuwa uteuzi wa wajumbe hao umezingatia mambo makuu manne ambayo ni uzoefu, taaluma, uwezo, na weledi, sifa ambazo ameeleza kuwa ni muhimu katika kuhakikisha dhamira iliyowekwa kwenye tamko la pamoja inafanyiwa kazi kwa muda mfupi na kwa ufanisi
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa kamati hiyo iliyofanyika Ikulu, Zanzibar, Dkt. Mwinyi amewakumbusha wajumbe wa kamati hiyo kuwa wananchi wa Zanzibar wana matarajio makubwa sana kuelekea mchakato huo, hivyo wanapaswa kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia maslahi ya taifa.
“Wanatarajia kuona siasa zinazojenga badala ya siasa zinazobomoa, siasa zinazounganisha badala ya siasa zinazogawa, siasa zinazotafuta suluhisho badala ya kuongeza migogoro. Hivyo na zaidi ya yote wanatarajia kuona maridhiano yakileta amani, utulivu na maendeleo katika nchi yao na katika maisha yao ya kila siku,” amesema Dkt. Mwinyi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Taifa, Othman Masoud Othman, amewataka wajumbe wa Kamati ya Pamoja ya Majadiliano kati ya CCM na ACT Wazalendo kutambua kuwa wamepewa jukumu la heshima kubwa la kuandika "hadithi mpya" ya maendeleo na amani ya kweli kisiwani Zanzibar, badala ya kuendelea kubaki kwenye historia na hadithi za kale
Othman ameyasema hayo leo wakati wa hafla ya uzinduzi wa kamati hiyo ya pamoja pamoja na sekretarieti yake iliyofanyika Ikulu ya Zanzibar, itakayosimamia utekelezaji wa Tamko la Pamoja la Maridhiano la Julai 9, 2026.
Akizungumza katika hafla hiyo, Othman amesisitiza kuwa amani na utulivu si masuala ya kisiasa pekee, bali ndio mhimili mkuu wa maisha na uchumi wa Zanzibar kutokana na kutegemea zaidi sekta ya huduma na uwekezaji
“Amani na utulivu sio tu masuala ya kisiasa lakini amani na utulivu kwa Zanzibar ndio uchumi wenyewe, ndio biashara yenyewe, ndio maisha yenyewe kutokana na ukweli kwamba Zanzibar inategemea uchumi wa huduma zaidi. Hapawezi kuwa na huduma bila ya kuwa na utulivu na amani endelevu,” amesema Othman.
Ameongeza kuwa uwekezaji unahitaji mazingira salama, kwani wawekezaji hawapeleki fedha zao kwenye maeneo yasiyo na utulivu.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI PICHA:
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi @CCMTanzania Bara, Stephen Wasira, leo Septemba 14, 2026, amewasili mkoani Iringa na kupokelewa na viongozi wa Chama na Serikali wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa, Daudi Yasin, katika Uwanja wa Ndege wa Nduli mkoani humo.
Wasira, akiwa mkoani hapo pamoja na mambo mengine, atafungua Mafunzo ya Wakufunzi wa chama hicho yatakayofanyika katika Chuo cha Mafunzo cha UVCCM. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI PICHA
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema kuundwa kwa Kamati ya Pamoja ya Majadiliano yenye wajumbe kutoka CCM na ACT Wazalendo ni hatua muhimu katika kuendeleza mchakato wa maridhiano na kuimarisha amani, umoja na utulivu wa kisiasa Zanzibar.
Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo tarehe 14, Septemba 2026 Ikulu Zanzibar, wakati wa uzinduzi rasmi wa Kamati hiyo, akiwataka wajumbe kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, kuheshimiana na kuweka mbele maslahi mapana ya Zanzibar na wananchi wake.
Kamati hiyo ni mwendelezo wa utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa baina ya CCM na ACT Wazalendo, huku akisisitiza umuhimu wa viongozi wa kisiasa na wadau wengine kuendelea kushirikiana katika kujenga Zanzibar yenye amani, utulivu na maendeleo.
Aidha, Dkt. Mwinyi amewapongeza viongozi wa CCM, ACT Wazalendo, viongozi wengine wa kisiasa, wazee na Marais Wastaafu wa Zanzibar, Dkt. Amani Abeid Karume na Dkt. Ali Mohamed Shein, kwa mchango wao katika kuendeleza mchakato wa maridhiano.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa ACT Wazalendo, Othman Masoud Othman, amesema chama hicho kiko tayari kuendelea kushirikiana katika kuijenga Zanzibar, akimpongeza Rais Dkt. Mwinyi kwa hatua mbalimbali alizochukua katika kusimamia mchakato wa maridhiano.
Katika hafla hiyo, Dkt. Mwinyi amekabidhi Hadidu Rejea za Kamati kwa Wenyeviti Wenza, Omar Ali Sheikh kutoka ACT Wazalendo na Abdi Mahmoud Abdi kutoka CCM Zanzibar. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI:
Mahakama Kuu nchini Kenya imetoa amri ya muda kuizuia Kampuni ya Standard Group kurudia, kuchapisha upya au kusambaza madai yanayomhusisha Charlene Ruto, binti wa Rais William Ruto, na zabuni ya ununuzi wa sare za Polisi nchini humo yenye thamani ya Shilingi Bilioni 2.8 za Kenya, sawa na takriban Bilioni 57.1 za Tanzania
Amri hiyo imefuatia maombi yaliyowasilishwa na Charlene akipinga taarifa iliyochapishwa na gazeti la The Standard Agosti 30, 2026, iliyodai kuwepo kwa uhusiano kati yake, kampuni ya Nalitex Limited na zabuni hiyo.
Kupitia mawakili wake, Charlene amesema taarifa hizo zilijenga taswira kwamba alishiriki katika mchakato wa zabuni, alisambaza bidhaa au alinufaika kutokana na ununuzi huo.
Hata hivyo, kwa mujibu wa nyaraka za mahakama, Jeshi la Polisi la Kenya lilifafanua kuwa Nalitex Limited haikushiriki katika mchakato wa zabuni, haikupewa kandarasi, haikuwa mkandarasi mdogo wala haikupokea oda au malipo yoyote kuhusiana na zabuni hiyo. Jeshi hilo lilimtaja Bedi Investments Limited kuwa mkandarasi wa zabuni hiyo.
Charlene pia amesema aliwasilisha kwa Standard Group barua ya madai na haki ya kujibu, akiomba taarifa hizo zisahihishwe, ziondolewe pamoja na kuombewa radhi, lakini machapisho hayo yaliendelea kupatikana mtandaoni.
Katika maombi yake, aliiomba Mahakama kuzuia usambazaji wa madai hayo hadi pale yatakapothibitishwa kwa ushahidi unaoonesha kuwa alishiriki au alinufaika na zabuni hiyo.
Mahakama imekubali ombi hilo la muda, na Standard Group imepewa siku saba kuwasilisha majibu yake. Kesi hiyo itatajwa tena Oktoba 19, 2026. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Kesi ya uhaini namba 19605/2025 inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, imeahirishwa kwa muda wa saa moja na nusu mchana huu hadi itakapofika saa nane na nusu mchana huu.
Kabla ya kuahirishwa, Wakili Mkuu wa Serikali, Nassor katuga, alikuwa akiendelea kumuhoji shahidi huyo maswali ya dodoso (Cross-examination) zoezi ambalo litaendelea hapo baadaye. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Leo Jumatatu, Septemba 14, 2026, rasmi zoezi la kumuuliza maswali ya dodoso (Cross-examination) shahidi wa tano katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) taifa Tundu Lissu, litaanza.
Hatua hiyo inaanza ikiwa ni baada ya shahidi huyo ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Bara, John Heche, kuhitimisha sehemu yake ya kwanza ya kumtetea Tundu Lissu ijumaa, Septemba 11, 2026.
Katika sehemu ya utetezi wake wiki iliyopita, shahidi huyo aliieleza Mahakama kwamba Mkutano wa Aprili 3, 2025, ambao kwa maelezo yake, uliwakutanisha viongozi wa Chama hicho pamoja na watia nia wa uchaguzi Mkuu wa 2025, kwamba kupitia huo inaelezwa kuwa Tundu Lissu alitoa maneno yaliyomuweka gerezani hadi sasa.
Heche aliieleza Mahakama kuwa, Tundu Lissu hakuhusika na maandalizi ya Mkutano huo bali alialikwa kama Mgeni rasmi ambaye alikuwa pia mzungumzaji mkuu. Alisema kuhusu Lissu Kutamka maneno kama tutauzuia uchaguzi, tutauvuruga uchaguzi ni ya kweli lakini iliwa ni kwa njia ya kidemokrasia.
Kuhusu maneno ya Lissu na kilichotokea Oktoba 29, 2025 siku ya Uchaguzi Mkuu, Heche alisema Lissu hakuhusika kwani hata kabla ya siku hiyo yeye (Lissu) alikuwa tayari amekamatwa na kuwekwa ambapo pia aliieleza Mahakama kwamba baada ya Lissu kukamatwa pia viongozi wa CHADEMA walianza kukamatwa ikiwemomo yeye mwenyewe (Heche) ambapo alikuwa chini ya polisi Dodoma, akisisitiza kwa Lissu hakuhusika na yaliyotokea siku ya uchaguzi.
Hata hivyo baada ya Heche kumaliza kumtetea Tundu Lissu, majaji waliwaruhusu upande wa mashtaka kuanza moja kwa moja maswali hayo ya (dodoso), lakini Wakili Mkuu wa Serikali, Wakili Nassor katuga alisimama na kuiomba Mahakama kuahirisha kesi hiyo hadi leo Jumatatu, akisema wao kama upande wa mashtaka wana maswali mengi kwa shshidi huo kutoana na aina ya ushahidi aliyoitoa mbele ya Majaji.
Kwa hamu kubwa, pande zote zinasubiri kuona namna ambavyo shahidi huyo atayakabili maswali hayo ya dodoso kutoka kwa mawakili wa Serikali kabla ya kwenda hatua ya maswali ya ufafanuzi (Re-examination).
Ikumbukwe kuwa, Tundu Lissu, anashtakiwa kwa kosa la uhaini chini ya Kifungu cha 39(2)(d) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu (Penal Code), Sura ya 16 ya Sheria za Tanzania, kama ilivyorekebishwa 2023.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Godbless Lema @godblessjlema1 amejibu maoni ya watu kufuatilia mjadala na mkali ulioibuka mitandaoni baada ya yeye kuchapisha ujumbe wa pole kwa Rais Samia Suluhu Hassan kufuatia kifo cha mume wake, huku ujumbe huo akiamnatanisha salamu za pole kutoka kwa Mwenyekiti wa @ChademaTZ2 Tundu Lissu, akiwa gerezani.
Leo Septemba 14, 2026 amechapisha andiko akieleza kuwa hatua Lissu ni mfano mzuri kwa jamii inayodai kupigania uhuru wa maoni na demokrasia, kuheshimu misingi ya utu na kuweza kutofautiana bila kuvuka mipaka ya heshima ni sehemu muhimu ya ukomavu wa kisiasa na kijamii.
Anaeleza kuwa Lissu, ambaye amekuwa mahabusu kwa takribani mwaka mmoja na miezi sita akikabiliwa na kesi ambayo wafuasi wake wanaiona kuwa ya kisiasa na isiyo na haki, alitoa salamu za pole kwa Rais Samia mara mbili, jambo analiona kuwa si unyonge bali ni ishara ya hekima, utu na ukomavu wa kisiasa.
Hata hivyo amesema hii si mara ya kwanza kwa Lissu kuonekana akisimamia kile anachoamini kuwa ni haki bila kuangalia upande wa kisiasa kwani aliwahi pia kumtetea aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya, katika kesi yake iliyofanyika Moshi, hatua iliyowashangaza wengi na baadaye, alipoulizwa kuhusu msimamo huo, alieleza kwa mantiki kwamba kwake haki haichagui upande.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Tanzania na Japan zimeendelea kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na uwekezaji, huku nchi hizo mbili zikieleza nia ya kushirikiana katika kuboresha mazingira ya uwekezaji na kuwezesha kampuni zaidi za Japan kuanzisha na kupanua shughuli zao nchini Tanzania.
Hayo yamebainika katika kikao kati ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila A. Mkumbo, na Naibu Waziri wa Uchumi, Biashara na Viwanda wa Japan anayeshughulikia masuala ya Bunge, Bw. Komori Takuo, kilichofanyika Tokyo tarehe 8 Septemba 2026.
Katika kikao hicho, viongozi hao walibadilishana mawazo kuhusu namna ya kuboresha mazingira ya uwekezaji na kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi kati ya Tanzania na Japan, kwa lengo la kuongeza shughuli za biashara na uwekezaji wa kampuni za Japan nchini Tanzania.
Pande hizo mbili pia zilieleza nia ya kuendelea kushirikiana katika kukuza uwekezaji baina ya Tanzania na Japan, hatua inayotarajiwa kufungua fursa zaidi za biashara, uwekezaji na ushirikiano wa sekta binafsi za nchi hizo mbili.
Kikao hicho kilikuwa sehemu ya Ziara ya Uwekezaji ya Tanzania nchini Japan, inayoongozwa na Waziri Mkumbo kwa lengo la kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo Tanzania, kuvutia wawekezaji wapya na kuimarisha mahusiano ya moja kwa moja kati ya sekta binafsi za Tanzania na Japan.
Ziara hiyo imeandaliwa na Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Japan, kwa kushirikiana na Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA), Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP), Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF).
Kupitia ziara hiyo, Tanzania inalenga kutumia uhusiano wake wa muda mrefu na Japan kujenga ushirikiano mpana zaidi wa kiuchumi unaoongozwa na biashara na uwekezaji, pamoja na kuvutia kampuni za Japan kuwekeza katika miradi yenye tija nchini.
Ushirikiano huo ni sehemu ya juhudi za Serikali za kuimarisha diplomasia ya uchumi, kuvutia uwekezaji wenye ubora na kuongeza mchango wa sekta binafsi katika ukuaji wa uchumi na maendeleo ya Tanzania. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu, jana Septemba 12, 2026, alikamilisha ziara yake ya siku kadhaa katika mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Ziara hiyo ilianza Mwanza, Geita, Mara, Simiyu, Shinyanga na kumalizia Kahama. Aliambatana na Naibu Mwenezi wa chama, Shangwe Ayo, aliyetokea makao makuu ya ACT Wazalendo.
Lengo kuu lilikuwa kukutana na wenyeviti na makatibu wa chama ngazi ya mikoa ili kuimarisha miundo ya chama, kisha kuzungumza moja kwa moja na wananchi na kuwapa nafasi ya kuuliza maswali.
Katika mikutano yote, Ado alisisitiza umuhimu wa kujenga chama chini na kushiriki kikamilifu katika siasa. Pia alizungumzia kwa kina suala la Katiba Mpya, akisisitiza hitaji la mchakato wa kweli unaohusisha wananchi wote. Aligusia pia masuala mengine ya kitaifa yakiwemo mageuzi ya kisiasa, haki za binadamu na changamoto za uchumi zinazowakabili Watanzania.
Wananchi walipata nafasi ya kutoa maoni na kuuliza maswali, na Ado alijibu kwa uwazi. Ziara hiyo imekamilika kwa mafanikio, ikiimarisha uhusiano kati ya viongozi wa chama na wananchi wa Kanda ya Ziwa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI:
Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linamshikilia Mwanamke mmoja kati ya watuhumiwa 7 wanaodaiwa kuhusika katika mtandao wa uhalifu unaohusisha unyang’anyi wa kutumia silaha, mauaji na wizi wa pikipiki.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, SACP Justine Masejo, mwanamke huyo anadaiwa kuwa na nafasi ya kuwavuta waendesha bodaboda kwa kujifanya abiria, kabla ya kuwaelekeza kwenye maeneo ambayo wahalifu wenzake walikuwa wakingojea kwa ajili ya kutekeleza matukio ya uhalifu.
Kamanda Masejo amesema uchunguzi wa Polisi umebaini kuwa watuhumiwa hao wanadaiwa kuhusika katika matukio mbalimbali ya uhalifu yaliyotokea Arusha, huku baadhi yao wakiwa tayari wamefikishwa mahakamani na mashauri yao yakiwa katika hatua mbalimbali za kisheria.
Miongoni mwa matukio yanayohusishwa na mtandao huo ni mauaji ya Anold Osward (28), mkazi wa Orolesho, Kata ya Olasiti jijini Arusha, yaliyotokea Juni 19, 2026, katika Mtaa wa Olteves, Kata ya Olmot.
Kamanda Masejo amesema baada ya mahojiano, watuhumiwa hao walikiri kuhusika katika tukio hilo pamoja na matukio mengine yaliyotokea katika Wilaya ya Arumeru.
Wakati huo huo, Jeshi la Polisi limesema linaendelea na uchunguzi wa mauaji ya Hamis Idd Masimba (22), dereva wa bodaboda na mkazi wa Olasiti, ambaye anadaiwa kupotea Septemba 9, 2026 baada ya kumchukua abiria. Mwili wa Masimba ulipatikana Septemba 12, 2026 ndani ya nyumba ambayo haijakamilika katika eneo la Stendi Mpya, Mtaa wa Bondeni City jijini Arusha.
Aidha, Jeshi hilo limewataka wananchi, hususan waendesha bodaboda na wamiliki wa pikipiki, kuwa makini wanapobeba abiria au kukodisha pikipiki zao, hasa nyakati za usiku, na kutoa taarifa mapema wanapobaini mienendo inayotia shaka, huku likiwasihi wananchi kutoa taarifa kuhusu uhalifu na wahalifu ili hatua za kisheria zichukuliwe. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Wakili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Omari Omari, amesema wazazi, ndugu au marafiki wanaomshawishi mmoja wa wanandoa kuachana na mwenza wake wanaweza kuwajibishwa kisheria endapo ushawishi wao utasababisha ndoa kuvunjika.
Akizungumza wakati wa mahojiano na Jambo TV, Wakili Omari amesema Kifungu cha 73 cha Sheria ya Ndoa kinaweka masharti kuhusu mtu anayemshawishi mume au mke kuondoka kwenye ndoa yake, akisisitiza kuwa sheria hiyo inaweza kumhusisha mtu yeyote, wakiwemo wazazi au marafiki.
Amesema pia mtu anayemshawishi mwenza wa mtu mwingine kuondoka kwenye ndoa na kisha kuishi naye, huku akijua kuwa bado yuko kwenye ndoa, anaweza kukabiliwa na madai yanayohusiana na kuingilia ndoa pamoja na uzinzi, kulingana na mazingira ya tukio.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Simu za mkononi zimekuwa miongoni mwa vyanzo vya migogoro katika ndoa, hasa pale wanandoa wanapofichiana simu kwa kuhisi kuna usaliti.
Akizungumza wakati wa mahojiano na Jambo TV, Wakili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Omari Omari, amesema kuingia kwenye ndoa hakumuondolei mtu haki yake ya faragha, kwa kuwa haki hiyo inalindwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Amesema hakuna anayepaswa kuingilia faragha ya mwingine kiholela, ikiwemo mawasiliano yake, isipokuwa pale ambapo sheria inaruhusu kufanya hivyo.
Wakili Omari amesisitiza kuwa kuwa katika ndoa hakumaanishi mtu amepoteza haki yake ya faragha, bali haki hiyo inaendelea kuwepo hata baada ya kufunga ndoa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Wakili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Omari Omari, amesema mume au mke ‘aliyesalitiwa’ anatakiwa kumtafuta mwanasheria kwa ajili ya kupata mwongozo wa namna ya kufungua shauri la kudai fidia kutokana na usaliti ndani ya ndoa.
Akizungumza wakati wa mahojiano na Jambo TV, Wakili Omari amesema Sheria ya Ndoa ya Tanzania inaweka utaratibu wa mtu aliyefunga ndoa kumdai mtu aliyefanya uzinzi, ambapo madai hayo yanaweza kuhusisha fidia.
Amesema fidia hiyo mara nyingi huwa katika mfumo wa malipo ya fedha, hivyo mtu aliyesalitiwa anaweza kufuata utaratibu wa kisheria kupitia mwanasheria wake ili kudai fidia hiyo.
Tembelea chaneli ya Youtube ya Jambo TV kutazama video hii kwa undani.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Wananchi wa Kata ya Shirimatunda na maeneo ya jirani katika Manispaa ya Moshi, mkoani Kilimanjaro, wanatarajia kuondokana na adha ya kukatikiwa na huduma za matibabu pindi umeme unapokatika, kufuatia hatua ya Serikali kununua jenereta kubwa la dharura kwa ajili ya Kituo cha Afya Shirimatunda.
Akimbelea kituo hicho tarehe 12 Septemba, 2026, Mbunge wa Jimbo la Moshi Mjini, Ibrahim Shayo, amebainisha kuwa ingawa jenereta hilo limeshanunuliwa na kufikishwa kituo hapo, bado halijafungwa na kuanza kufanya kazi, jambo alilodai linakwaza utoaji wa huduma za matibabu na operesheni licha ya kuwepo kwa madaktari na vifaa tiba vyote vinavyohitajika.
Akitolea ufafanuzi suala la kuchelewa kufungwa kwa mtambo huo, Mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi, Mwajuma Nasombe, ameeleza kuwa hatua za kiufundi za ufungaji zinaendelea na kwamba ununuzi wa jenereta hilo umefanyika kwa kutumia mapato ya ndani ya halmashauri na si fedha kutoka Serikali Kuu.
Aidha, Mkurugenzi Nasombe amebainisha kuwa Mbunge huyo hakutoa taarifa rasmi kwa Manispaa kuhusu ziara hiyo ya kagua miundombinu, huku akiahidi kuwa halmashauri itahakikisha jenereta hilo linaanza kufanya kazi mara moja ili kuokoa maisha ya wananchi na kuimarisha huduma za afya za saa 24.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katibu Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Tunduru Kaskazini, Ado Shaibu, ameipa Serikali pamoja na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi muda wa wiki moja kutoa maelezo rasmi kwa umma kuhusu aliko na usalama wa Aliyekuwa Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt. Emmanuel Nchimbi, akionya kuwa wakishindwa kufanya hivyo, chama hicho kitachukua hatua za kisheria kuiburuza serikali mahakamani.
Ado Shaibu ametoa msimamo huo jana, Septemba 12, 2026, wakati akihitimisha ziara yake katika Mkoa wa kichama wa Kahama baada ya kukutana na wenyeviti na makatibu wa chama hicho ngazi ya mikoa, pamoja na kuzungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliyofanyika Kata ya Kagongwa, Jimbo la Kahama Mjini mkoani Shinyanga.
Ado Shaibu ameeleza kuwa baada ya kutoa kauli siku chache zilizopita, alitoa fursa ya siku moja kuona kama Dkt. Nchimbi mwenyewe, familia yake, au serikali wangejitokeza kutoa taarifa. Hata hivyo, kutokana na kuendelea kwa ukimya huo, amebainisha kuwa kuna kila dalili za kutilia shaka usalama wake.
“Tunataka serikali itueleze Nchimbi yuko wapi, familia yake itueleze Nchimbi yuko wapi au na yeye mwenyewe Nchimbi atoke atuambie yuko wapi…angekuwa salama angejitokeza. Na usalama ninaosema mimi tunataka tujue hali yake ni salama. La pili tunataka tujue anao uhuru wa kutembea…la tatu tunataka kujua ana uhuru wa mawasiliano, atoke tu tumuone. Lasivyo kama hajitokezi tutajua hayuko salama,” amesema Ado Shaibu.
Katika hatua nyingine, Ado Shaibu amemshukia Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, akimtaka kutambua uzito wa dhamana aliyopewa inayohusu usalama wa raia na mali zao, na inayosimamia vyombo vikuu kama Jeshi la Polisi, Magereza, Zimamoto, na Idara ya Uhamiaji.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mbunge huyo wa Jimbo la Tunduru Kaskazini ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo @ACTwazalendo , Ado Shaibu amevitaka vyombo vya habari na vyama vyote vya upinzani kuweka tofauti zao kando na kuungana pamoja katika mapambano ya amani na ya kisheria ya kudai Katiba Mpya, akisisitiza kuwa mabadiliko hayo ni msingi wa kuleta haki, utawala wa sheria, na demokrasia ya kweli nchini.
Wito huo ameutoa jana Septemba 12, 2026 wakati akihitimisha ziara yake katika Mkoa wa Kahama baada ya kukutana na wenyeviti na makatibu wa chama hicho ngazi ya mikoa, pamoja na kuzungumza na wananchi wa Kata ya Kagongwa, Jimbo la Kahama Mjini mkoani Shinyanga.
Akihutubia mkutano wa hadhara, Shaibu amebainisha kuwa Katiba ya sasa ina mapungufu makubwa yanayozuia ushiriki kamili wa wananchi na uwajibikaji wa viongozi waliopo madarakani, hivyo mchakato wa kupata Katiba Mpya si kazi ya chama kimoja tu bali ni wajibu wa kitaifa wa Watanzania wote.
Amesisitiza kuwa vyombo vya habari vina jukumu la msingi la kutoa taarifa sahihi na kuhamasisha mjadala wa kitaifa kuhusu Katiba Mpya, huku akiwasihi viongozi wa vyama vyote vya upinzani kuweka mbele maslahi ya taifa badala ya tofauti zao za kisiasa.
Ziara hiyo ya Katibu Mkuu nchini Mkoa wa kichama wa ACT Wazalendo wa Kahama ilikuwa na lengo kuu la kutoa elimu ya kisiasa kwa wananchi pamoja na kuimarisha miundombinu na safu ya uongozi ya Chama cha ACT Wazalendo katika ngazi za msingi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Tanzania, Jaji Francis Mutungi, amesema kitendo cha wadau mbalimbali kukutana na kujadiliana hali ya siasa nchini, kimeonesha dhamira ya kuwa tayari kufikia muafaka wa siasa utakao saidia kulikwamua taifa.
Jaji Mutungi amesema hayo katika Mkutano wa Kitaifa wa Wadau wa Kutafakari Hali ya Siasa nchini, uliofanyika Dar es Salaam wiki hii. Ameongeza kwamba mikutano kama hiyo inatakiwa kutoa maelezo ambayo ni kwaajili ya kujenga.
"Kitendo cha kukutana hapa, ni dhamira namabari moja kuonesha tuna lengo madhubuti la kufikia muafaka fulani kwa maslahi mapana ya taifa letu" amesema Mutungi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katika mkutano wa hadhara wa Chama cha ACT Wazalendo wa Septemba 11, 2026, uliofanyika Kata ya Dutwa, Jimbo la Bariadi mkoani Simiyu, mwananchi Fulani amesimama na kumhoji Katibu Mkuu wa chama hicho ambaye pia ni Mbunge wa Tunduru Kaskazini, Ado Shaibu, kuhusu sababu za yeye kuendelea kubaki bungeni na kulipwa posho kupitia mfumo wa uchaguzi anaoukosoa.
Katika swali lake, mwananchi huyo amemhoji Ado Shaibu akihoji ni kwa namna gani anajisikia amani kuendelea kuhudumu kama mbunge na kupokea posho za bunge zilizotokana na uchaguzi ambao ndugu zao walipotea, wakati huohuo akiwaambia wananchi wa Dutwa wapiganie mifumo rafiki ya uchaguzi na Katiba Mpya
Akijibu hoja hiyo, Ado Shaibu ameeleza kuwa uamuzi wake wa kwenda bungeni haukutokana na kuridhika na mfumo uliopo, bali ulikuwa ni mkakati wa kuzuia chama tawala (CCM) kupitisha kile alichokiita sheria kandamizi bila kupingwa. Amedai kuwa iwapo wapinzani wangesusia bunge na kuwaacha CCM peke yao, chama hicho kisingepata uangalizi katika uamuzi wa nchi.
Amebainisha kuwa ataendelea kutumia nafasi hiyo kupigania haki za Watanzania waliopoteza maisha na kuuawa wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Sakata la wananchi wa Kijiji cha Oldean, wilayani Karatu mkoani Arusha, la kufyekwa kwa mazao yao ikiwemo migomba na miwa limeendelea kuchukua sura mpya, baada ya wananchi hao kueleza kilichotokea na kusisitiza kutoridhishwa na hatua hiyo.
Wananchi hao wanasema wameishi katika eneo hilo lenye ukubwa wa ekari 27 kwa zaidi ya miaka 12, wakifanya shughuli mbalimbali ikiwemo kilimo na kupanda mazao tofauti. Pamoja na kukiri kutokuwa na hati ya umiliki wa eneo hilo, wanasema hawakufurahishwa na kitendo cha mwekezaji raia wa kigeni kutuma watu waliokwenda kufyeka mazao yao.
Kwa upande wake, mwakilishi wa mwekezaji, Arshad Ally, amesema eneo hilo ni mali ya kampuni yao na kwamba kupitia wanasheria wao waliwaandikia wananchi hao notisi ya siku 14 ya kuondoka katika eneo hilo, lakini walikaidi. Amesema baada ya wananchi hao kutokutekeleza notisi hiyo, walichukua hatua ya kuwatuma watu ambao walienda kufyeka mazao yao.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Lameck Karanga, amekiri kuufahamu mgogoro huo na hatua zilizochukuliwa, huku akisema wananchi hao wamekuwa wakiishi na kufanya shughuli zao pembeni mwa vyanzo vya maji, jambo ambalo haliruhusiwi kisheria.
Karanga pia amekanusha kutoa maagizo ya kumpiga mtu viboko wala kumfukuza mtu, kama inavyodaiwa na baadhi ya wananchi, akisisitiza kuwa hajawahi kutoa maagizo hayo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Baraza la Watoto Tanzania limedai kuwa baadhi ya shule nchini zinakiuka Waraka wa Elimu Na. 24 wa mwaka 2002 kuhusu Adhabu ya Viboko shuleni hali wanayodai kuwa inaathiri kujiamini kwa wanafunzi na wengine kushindwa kutimiza ndoto zao.
Hayo yamebainishwa jijini Dodoma wakati wa Jukwaa la Baraza la Watoto Kitaifa, ambapo Mwenyekiti wa Baraza la Watoto Taifa, Daniel Magembe, amesema Serikali inapaswa kuimarisha usimamizi wa utekelezaji wa miongozo inayosimamia utoaji wa adhabu shuleni.
Magembe amesema waraka wa adhabu unaweka utaratibu wa utoaji wa adhabu ya viboko, ikiwemo kutotakiwa kuzidi viboko vinne kwa wakati mmoja, huku ikizingatiwa ukubwa wa kosa, umri, jinsia na afya ya mwanafunzi.
Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Amon Mpanju, amesema wakati umefika wa kuangalia upya matumizi ya viboko kama njia ya kumrekebisha mtoto, akisisitiza kuwa nyakati za kutegemea adhabu ya viboko zimepitwa na wakati.
Aidha, Mpanju ameiitaka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kuhakikisha walimu wanazingatia miongozo iliyowekwa kuhusu utoaji wa adhabu za viboko shuleni.
Amesema viboko havipaswi kuwa njia pekee ya kumkanya au kumrekebisha mtoto, bali kunahitajika kutumia njia zinazomjenga mtoto na kumsaidia kuelewa kosa lake bila kumjengea hofu.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Baadhi ya wafanyabiashara wameshiriki katika Hitma ya kumuombea marehemu Hafidh Ameir Hassan, aliyekuwa mume wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Hitma hiyo imefanyika Kizimkazi Mkunguni, Mkoa wa kusini Unguja Zanzibar na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali, ndugu, jamaa pamoja na waombolezaji waliokusanyika kumuombea marehemu.
Katika Hitma hiyo waombolezaji walimuombea marehemu kwa mwenyezi Mungu ampumzishe kwa amani na awape subira wafiwa "katika kipindi hiki cha majonzi" -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma imemwachia huru Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Melkisedek Kaijage, baada ya upande wa Jamhuri kueleza kuwa hauna nia ya kuendelea na mashtaka yaliyokuwa yakimkabili.
Kaijage ameachiwa huru leo, Alhamisi Septemba 10, 2026, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma, Denisi Mpelembwa.
Mwendesha Mashtaka Mwandamizi wa Serikali, Jonathan Chuwa aliiambia mahakama kuwa jamhuri haina nia ya kuendelea na mashtaka hayo na kuiomba mahakama kumwachia huru Kaijage, akieleza kuwa uamuzi huo unahusu mashtaka ya ugaidi na uhujumu uchumi yaliyokuwa yakimkabili, iwapo hana kosa lingine la jinali lilokuwa likimkabili.
Hata hivyo, kabla ya mahakama kutoa uamuzi wa kumwachia huru, Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Dodoma (RCO) aliwasilisha maombi yaliyoambatanishwa na kiapo, akiomba mahakama imuwekee Kaijage masharti ya mwenendo baada ya kuachiwa huru.
Kwa mujibu wa Wakili wa utetezi, Godfrey Wasonga, mahakama imemtaka Kaijage kuwa na wadhamini wawili ambao ni wakazi wa Mkoa wa Dodoma.
Wadhamini hao wanatakiwa kuwa na barua za utambulisho kutoka kwa mamlaka za Serikali zinazotambulika, kusaini dhamana ya maneno ya shilingi milioni tano kila mmoja, pamoja na kuwa na vitambulisho halali.
Aidha, mahakama imemtaka Kaijage kuripoti kwa Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Dodoma (RCO) kila Ijumaa ya mwisho wa mwezi kwa kipindi cha mwaka mmoja, saa 2:30 asubuhi, bila kukosa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI PICHA:
Mwenyekiti Mstaafu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo @ChademaTZ2 Taifa Freeman Aikaeli Mbowe amemtembelea na kumfariji Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, nyumbani kwake Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar, leo Septemba 10, 2026, kufuatia kufiwa na Mume wake Marehemu Maalim Hafidh Ameir Hassan aliyefariki dunia katika Hospitali ya Kumbukumbu ya Emilio Mzena Zanzibar, tarehe 07 Septemba, 2026. -
Jambo TV
@Jambotv_
MTOTO AMEPOTEA:
Mtoto Elia Dominic Mwinuka, mwenye umri wa miaka 13, Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Viwege, iliyopo Kata ya Majohe, Wilaya ya Ilala, Jijini Dar es Salaam amepotea tangu tarehe Septemba 05, 2026, majira ya saa moja jioni.
Mara ya mwisho alikuwa eneo la Viwege akiwa amevaa Tishet ya Lagut Bluu(blui mpauko).
Taarifa ya kupotea kwake imeripotiwa Polisi. Tafadhali ukifanikiwa kumuona au kupata taarifa zake unaombwa kutoa taarifa kwenye Kituo chochote cha Polisi au Ofisi yoyote ya Serikali iliyopo karibu,
Au unaweza kupiga simu moja kwa moja kwa familia kupitia Namba: 0652820150 au 0753366438.
Ahsante🙏🏼 -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwenyekiti wa Taifa wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania (JWT), Hamisi Abdallah Livembe, amewataka wamachinga kutowapanda wafanyabiashara kichwani, akisema wafanyabiashara wamekuwa wavumilivu kwa muda mrefu licha ya changamoto ya wamachinga kuweka meza mbele ya maduka yao.
Livembe ameyasema hayo Septemba 9, 2026, alipotembelea Soko la Tandika jijini Dar es Salaam kukagua utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa kati ya Serikali na wafanyabiashara, ambapo wafanyabiashara wamekubali kufungua maduka yao huku Serikali ikiahidi kuwaondoa wamachinga waliopo mbele ya maduka na kuwapatia maeneo rasmi ya kufanyia biashara.
Amesema viongozi wa wafanyabiashara wamekuwa wakiwazuia wafanyabiashara kuchukua hatua dhidi ya hali hiyo, badala yake wakatumia mazungumzo na Serikali kutafuta suluhu ya changamoto hiyo.
Makamu Mwenyekiti wa JWT Mkoa wa Dar es Salaam amesema suala hilo limefikishwa kwa Serikali kuanzia ngazi ya Wilaya, Mkoa hadi Serikali Kuu, huku akisema wafanyabiashara wataendelea kuipa serikali nafasi ya kutekeleza makubaliano yaliyofikiwa.
Mwenyekiti wa JWT Temeke amesema wafanyabiashara wa Tandika hawapingi wamachinga kufanya biashara, bali wanataka wapatiwe maeneo rasmi ili kila kundi lifanye biashara katika eneo lake bila kuingiliana.
Wafanyabiashara wa Tandika wameishukuru serikali kwa kusikiliza kilio chao na kuingilia kati suala hilo, wakitaka maelekezo yaliyotolewa yaheshimiwe na kila upande kupewa eneo lake la biashara.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katika muendelezo wa maswali ya dodoso kwa shahidi wa nne wa upande wa utetezi katika shauri la uhaini linalomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa CHADEMA, Brenda Jonas Rupia, leo Septemba 9, 2026, amekutana na maswali ya kina kutoka kwa mawakili wa Serikali, yaliyolenga zaidi ushahidi alioutoa mahakamani.
Wakili Mwandamizi wa Serikali, Nassor Katuga, alianza kwa kumuuliza Brenda kuhusu taarifa aliyoitoa kwamba Lissu alitaka kupewa sumu akiwa gerezani.
Brenda alikiri kuwa hakutoa taarifa polisi kabla ya kuchapisha taarifa hiyo. Alipoulizwa kama anajua kuwa kutoa taarifa za jinai bila uhakika kunaweza kuwa kosa, alisema hajui, huku akikiri kuwa anafahamu sheria za makosa ya mtandao zinahusu utoaji wa taarifa zisizo na uhakika.
Alipoulizwa kama katika uchunguzi wake alifanikiwa kumpata mtu aliyedaiwa kutoa taarifa kuhusu mpango wa kumpa Lissu sumu, Brenda alisema hakumpata. Hata hivyo, alisisitiza kuwa taarifa hiyo haikuwa ya uongo baada ya kufanya uchunguzi na kuzungumza na aliyempa taarifa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imetangaza kusitishwa kwa huduma ya maji kwa takribani saa 12 katika maeneo ya Dar es Salaam na Pwani, kesho Alhamisi, Septemba 10, 2026.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano DAWASA, Everlasting Lyaro amesema huduma itakatika kuanzia saa 12:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni, kutokana na matengenezo kinga ya miundombinu ya maji katika Mtambo wa Ruvu Juu uliopo Kibaha, yanayolenga kujiandaa kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza kutokana na mvua kubwa zinazotarajiwa.
Amesema maeneo yatakayoathirika kutokana na matengenezo haya ni pamoja na Ruvu Darajani, Ruvu JKT, Vigwaza, Mlandizi, Mbwawa, Soga, Mwendapole, Tanita, Kwa Mathias, Picha ya Ndege, Kibaha, Kiluvya, Kibamba, Malamba Mawili, Saranga, Mbezi, Ubungo, Kimara, Tabata, Segerea, Kinyerezi, Kisukuru, Bonyokwa, Ukonga, Uwanja wa Ndege, Kiwalani, Vingunguti, Gongo la Mboto, Pugu na Kisarawe.
Mamlaka imewataka wananchi wa maeneo hayo kuhifadhi maji ya kutosha kwa matumizi muhimu wakati wa matengenezo, huku ikiomba ushirikiano wao ili kazi hiyo ikamilike kwa ufanisi. -
Jambo TV
@Jambotv_
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na familia yake, wametoa shukrani za dhati kwa watu mbalimbali walioonyesha upendo, mshikamano, kutoa salamu za pole, dua na maombi kufuatia kifo cha mume wake Bw. Hafidh Ameir Hassan.
Hafidh alifariki dunia Zanzibar Septemba 7, 2026 katika hospitali ya Kumbukumbu ya Emilio Mzena alipokuwa akifanyiwa matibabu ambapo alizikwa siku hiyo hiyo.
Rais Samia amewashukuru pia Wakuu wa Nchi na Serikali, viongozi wa kitaifa, wanadiplomasia na jumuiya ya kimataifa, viongozi wa dini pamoja na Watanzania wote kwa faraja, salamu za pole, dua na maombi yao.
Taarifa hiyo iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Bakari S. Machumu imeeleza kiwa shukrani hizo zimetolewa wakati familia ikihitimisha siku tatu za maombolezo ya kuondokewa na mpendwa wao. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega ameagiza kufanyika kwa ukaguzi wa barabara na madaraja yote nchini kama sehemu ya maandalizi dhidi ya mvua kubwa za El Nino zinazotarajiwa kuanza hivi karibuni.
Ulega amesema ukaguzi huo ndiyo utakuwa msingi wa kufahamu ni wapi na wapi panahitaji kufanyiwa kazi ili mvua hizo zisiathiri mzunguko wa watu na biashara.
“Naagiza Wakala wa Barabara (TANROADS) kuhakikisha barabara na madaraja yote nchini yanakaguliwa na hatua za haraka kuchukuliwa ili miundombinu hiyo iendelea kutoa huduma hata wakati wa mvua kubwa zinazotarajiwa kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini," alisema Ulega.
Ulega ametoa maelekezo hayo jana akiwa mkoani Pwani katika ziara yake aliyoianza ya ukaguzi wa maandalizi ya kimiundombinu kufuatia maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa watendaji wa Serikali kuhakikisha nchi inakingwa na athari mbaya za mvua hizo.
Katika ziara yake hiyo, pamoja na mambo mengine, waziri Ulega alikagua pia vifaa mbalimbali vitakavyotumika kufanya matengenezo ya dharura katika miundombinu ya barabara na madaraja nchini kote.
Aidha, Ulega ameagiza Wizara ya Ujenzi kwa kushirikiana na TANROADS kufanya tathmini ya kila wiki katika mikoa yote nchini, ili kubaini maeneo yoyote yanayohitaji kuongezewa nguvu kwa wakati.
Kwa upande wake, Meneja wa TANROADS Mkoa wa Pwani, Mhandisi Joel Mwambungu, ameeleza kuwa Wakala huo umejipanga kukabiliana na athari za mvua hizo kwa ununuzi na usambazaji wa vifaa vya dharura katika maeneo mbalimbali nchini.
Mwambungu amesema TANROADS tayari ina kalavati za chuma zenye jumla ya mita 5,638 ambazo zitakazotumika katika maeneo ambayo barabara au madaraja yanaweza kupata athari kutokana na mvua kubwa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Hali ya kiafya ya Dkt. Conrad Agonza Kahyoza, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Ndani katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila ambaye anatuhumiwa kwa kumshambulia Askari wa Usalama Barabarani imeelezwa kuwa inaendelea vizuri huku kwa sasa akishikiliwa katika Kituo cha Polisi Oysterbay, Dar es Salaam.
Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dkt. Alex Elifuraha Msoka amesema viongozi wa chama hicho wameonana na Dkt. Conrad, wamezungumza naye na kufanya tathmini ya hali yake ya kiafya na kuthibitisha kuwa hali yake ni nzuri.
Dkt. Alex amesema MAT, kwa kushirikiana na wanasheria pamoja na familia ya Dkt. Conrad, inaendelea na taratibu za kisheria, ikiwemo juhudi za kuhakikisha anapata dhamana.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI PICHA:
Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania @InvestTanzania kwa kushirikiana na Uongozi wa Mkoa wa Ruvuma, inaendelea kuwezesha utekelezaji wa uwekezaji wa kimkakati unaolenga kuchochea uzalishaji wa viwandani, kuongeza ajira na kuimarisha uhamishaji wa teknolojia kwa Watanzania.
Miongoni mwa uwekezaji huo ni mradi wa HWTZ, unaotekelezwa ndani ya Ruvuma Special Economic Zone (SEZ) katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea, Mkoa wa Ruvuma. Mradi umetengewa eneo lenye ukubwa wa eka 1,056 kati ya eka 5,000 za eneo hilo maalum la kiuchumi.
Utekelezaji wa mradi ulianza Februari 2026, ukihusisha ujenzi wa kiwanda cha kuzalisha aluminium ingots, aluminium alloys na aluminium plates kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya soko la ndani na kuuza nje ya nchi.
Kwa sasa, mradi umefikia hatua ya ujenzi wa miundombinu ya barabara pamoja na ujenzi wa kiwanda cha kuzalisha nishati kwa kutumia makaa ya mawe. Aidha, ujenzi wa makazi ya wafanyakazi umekamilika, ikiwa ni sehemu ya maandalizi kuelekea hatua za uzalishaji.
Mradi unatarajiwa kutumia makaa ya mawe yanayopatikana Mkoa wa Ruvuma kama chanzo cha nishati, huku mahitaji yakitarajiwa kufikia hadi tani 20,000 kwa siku utakapofikia uzalishaji kamili. Hatua hii inatarajiwa pia kufungua fursa katika mnyororo wa thamani wa makaa ya mawe, usafirishaji na huduma nyingine zinazohusiana na shughuli za kiwanda.
Uwekezaji huo unatarajiwa kuzalisha takribani ajira 5,000 kwa Watanzania utakapofikia uzalishaji kamili. Sambamba na hilo, Watanzania 40 wamepelekwa nchini China kupata mafunzo ya uendeshaji wa mitambo ya kiwanda, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuhakikisha uhamishaji wa teknolojia, maarifa na ujuzi kwa nguvu kazi ya ndani.
Kupitia uwekezaji kama huu, Ruvuma SEZ inaendelea kujengwa kuwa kitovu cha uzalishaji wa viwandani, kinachounganisha rasilimali zinazopatikana katika mkoa huo na uwekezaji wenye uwezo wa kuzalisha ajira, kuongeza thamani, kuleta teknolojia na kufungua masoko ya ndani na nje ya nchi. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mtoto mwenye umri wa miaka 10, Juma Malanga, mkazi wa Mtaa wa Swaswa, Kata ya Ipagala jijini Dodoma, amefariki dunia baada ya kukutwa akiwa amejinyonga na shuka ndani ya chumba alichokuwa akilala na kaka yake. Tukio hilo limetokea Septemba 7, 2026 huku chanzo cha tukio hilo kikiwa bado hakijafahamika.
Akizungumza kuhusu tukio hilo baba mzazi wa mtoto huyo, Simon Mzengo, amesema Juma alijifungia ndani ya chumba hicho kabla ya familia kumkuta akiwa amefariki. Amesema familia haikujua kilichomsukuma mtoto huyo kuchukua hatua hiyo.
Mzengo amesema Juma alikuwa mtoto wa mwisho kati ya watoto saba na hakuwa na tatizo lolote la kiafya. Aidha, amesema familia haikuwahi kugombana wala kuwa na ugomvi na mtoto huyo ambao ungeweza kuashiria kuwepo kwa changamoto yoyote.
Amesema Juma alikuwa na tabia ya kumuomba simu ili kutazama video za katuni, na mara ya mwisho alichukua simu hiyo na kuingia uvunguni mwa kitanda kwa ajili ya kuangalia katuni hizo, kabla ya baadaye kukutwa akiwa amefariki.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Mtaa wa Swaswa, Henri Lazaro, amesema tukio hilo limewashtua wakazi wa eneo hilo, huku akiwataka wazazi kuwa karibu na watoto wao, kuzungumza nao mara kwa mara na kufuatilia mienendo yao ili kubaini mapema changamoto wanazoweza kuwa nazo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkutano wa Kitaifa wa Wadau wa Kutafakari Hali ya Siasa nchini wa Septemba 8, 2026, umegeuka uwanja wa mnyukano mkali wa hoja baada ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanataaluma ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDASA), Profesa Elgidius Ichumbaki, kukishutumu Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuendeshwa na "dude" lisilojulikana, huku Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Stephen Wasira, akijibu kwa kuwataka wasomi kuacha kulinganisha hoja zao na "mambo ya mitandao ya kijamii"
Profesa Ichumbaki amefunguka kumweleza mzee Wasira pamoja na viongozi wengine wa CCM kuwa wameshindwa kutekeleza wajibu wao wa kikatiba, kisheria, na kijamii wa kuisimamia serikali ipasavyo. Profesa Ichumbaki amekwenda mbali zaidi na kuhoji kama kweli CCM inayo mamlaka kamili ya maamuzi nchini, akidai kuwa kuna nguvu nyingine ya siri inayoratibu mambo.
Aidha, amegusia ahadi ya CCM ya kuanzisha mchakato wa Katiba Mpya ndani ya siku 100 za kwanza za uongozi wa Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, akidai kuwa wanachama wanaosimama kudai katiba hiyo, na wengine kutetea haki nyingine za wananchi wamekuwa ‘wakiadhibiwa’ na kufukuzwa uanachama wa CCM.
Akimjibu Ichumbaki, Wasira, amepinga vikali madai kuwa watu wanaoongea kwa niaba ya wananchi wanashughulikiwa akisema, “Yeye anasema mtu akisema kwa niaba ya mambo wanayotaka wananchi anashughulikiwa. Sio kweli. Na wewe kwa kuwa ni msomi, na wasomi wana sifa moja kubwa ya kufanya utafiti. Utafiti ni sehemu muhimu ya usomi. Usipotafiti utasema chochote tu. Utakuwa kama mitandao ya kijamii ambayo haina control”.
Wasira amekitetea chama chake akisema kuwa wanachama na viongozi wa CCM nao ni sehemu ya wananchi na sio malaika, hivyo nao wana haki na uwezo wa kutoa maoni yao huru.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira, amekataa katakata matumizi ya dhana ya "kesi za kisiasa" mahakamani, akisisitiza kuwa mahakama zinasimamia sheria na sio siasa, na kutoa onyo kuwa CCM haiwezi kuingilia uhuru wa mahakama kwa kufuta kesi zilizopo kwani kufanya hivyo ni kukigeuza chama tawala kuwa mahakama yenyewe.
Wasira amebainisha hayo leo Septemba 8, 2026, wakati akihutubia katika Mkutano wa Kitaifa wa Wadau wa Kutafakari Hali ya Siasa nchini unaofanyika mkoani Dar es Salaam.
“Mimi sielewi kesi za kisiasa zinavyofanana. Najua kesi ambayo iko mahakamani huwezi kuita ya kisiasa. Maana mahakama hizi hazikusomea siasa. Mahakama wamesomea sheria,” amesisitiza Wasira
Ameongeza kuwa mahakama ni chombo huru cha kutoa haki, na kwamba mtu yeyote anayefikishwa mbele ya sheria akiwa hana kosa, mahakama ikiridhika kuwa hana hatia itamwachia huru.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikilia mtu mmoja, Conrad Agonza Kayoza, mwenye umri wa miaka 35, kwa tuhuma za kumshambulia kwa ngumi na mateke askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani('traffic') katika eneo la Lugalo, Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Kanda hiyo SACP Muliro Jumanne Muliro imesema tukio hilo limetokea Septemba 8, 2026, majira ya saa 1:30 asubuhi katika Barabara ya Bagamoyo, wakati askari Polisi namba F.8886 SGT Andrew alipokuwa akitekeleza majukumu yake ya kikazi kwa kuwazuia kisheria madereva waliokuwa wakitumia pembezoni mwa barabara, maarufu kama ‘Service Road’, nje ya utaratibu.
Kwa mujibu wa taarifa ya Polisi, mtuhumiwa alishuka kwenye gari aina ya Toyota RunX lenye namba T 455 EER baada ya kusimamishwa na kuanza kumshambulia askari huyo kwa ngumi na mateke. Baadaye wananchi waliokuwa eneo hilo walimshambulia mtuhumiwa, ambaye alipelekwa hospitalini kwa matibabu.
Polisi imesema baada ya mtuhumiwa kupata nafuu atahojiwa kwa kina na hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake. Aidha, Jeshi hilo limetoa onyo kali kwa mtu yeyote au kundi lolote linalowashambulia askari wakati wakitekeleza majukumu yao ya kisheria, likisisitiza kuwa halitasita kuchukua hatua za kisheria.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
"Msemaji mmoja alisema huwezi ukaleta amani kwa bunduki, na mimi siamini kama amani inaweza ikaletwa kwa bunduki, haiwezekani hata kidogo amani ya nchi ikategemea bunduki na sidhani kama Tanzania amani yetu kwa miaka 60 imekuwa amani ya bunduki. Mimi naamini kinachofanya amani ni kufuata sheria, naamini watu wanafuata sheria wale ambao hawafuati ndiyo wanahitaji labda bunduki"
Hayo ameyasema Makamu Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania(TCD) Stephen Wasira katika Mkutano wa Kitaifa wa Wadau wa Kutafakari Hali ya Siasa nchini uliofanyika leo Septemba 8, 2026 mkoani Dar es SalaamThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania(TCD), Stephen Wasira ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa @CCMTanzania amesema mchakato wa kuandika katiba mpya kwa Tanzania hautakuwa mchakato mgumu kutokana na uwepo wa nyaraka ambazo tayari ni mwongozo ikiwemo Katiba ya sasa ya mwaka 1977 na Rasimu ya Katiba maarufu kama 'katiba ya Warioba'
Ameeleza hayo leo Septemba 8, 2026 akisisitiza kuwa pamoja na uwepo wa nyaraka hizo bado mchakato wa katiba sio jambo la siku moja linahitaji muda wa kutosha.
Akitumia jukwaa hilo katika utani alikosoa wale wanaosema Waziri Mkuu Mstaafu na Makamu wa Kwanza wa Rais Jaji Warioba ana katiba bali amesema ni nyaraka pekee anazo(Rasimu ya Katiba). -
Jambo TV
@Jambotv_
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeendelea na juhudi zake za kuongeza kiwango cha uwekezaji kutoka nje kwa kuishawishi Serikali ya Japan na sekta yake binafsi kuongeza uwekezaji nchini ili kusaidia kufikia lengo kubwa la kihistoria la kukuza uchumi wa nchi kufikia Dola za Kimarekani Trilioni moja ($1 trillion) ifikapo mwaka 2050.
Wito huo umetolewa Jumanne, Septemba 8, 2026, jijini Tokyo, Japan, na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Alexander Mkumbo, wakati wa mazungumzo yake maalum na Naibu Waziri wa Bunge wa Wizara ya Uchumi, Biashara na Viwanda ya Japan (METI), Komori Takuo.
Prof. Mkumbo ameeleza kuwa Tanzania imeanza awamu mpya ya mageuzi ya kiuchumi inayongozwa na Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050 pamoja na Mpango wa Nne wa Maendeleo wa Miaka Mitano (FYDP IV) wa mwaka 2026/27 hadi 2030/31. Amesisitiza kuwa kufikia malengo hayo makubwa kunahitaji washirika thabiti wa kimkakati kama Japan, nchi yenye teknolojia ya kisasa, ujuzi wa viwanda, na uwezo mkubwa wa usimamizi wa ubora
Akizungumzia mwelekeo mpya wa ushirikiano kati ya mataifa hayo mawili, Prof. Mkumbo amesema, "Ushahidi wetu ni rahisi: tunataka kuhama kutoka kwenye biashara kwenda kwenye uwekezaji, kutoka uwekezaji kwenda kwenye viwanda, na kutoka kwenye kusafirisha malighafi ghafi kwenda kwenye uzalishaji unaoongeza thamani”.
Waziri Mkumbo amebainisha sekta muhimu ambazo kampuni za Kijapan zinaweza kuwekeza ili kupata soko kubwa la Tanzania pamoja na masoko ya kikanda ya EAC, SADC, na soko huru la Afrika (AfCFTA). Sekta hizo ni pamoja na sekta ya magari hasa kuunganisha magari, pikipiki, zana za kilimo, vipuri, betri, na mifumo ya usafiri wa umeme.
Sekta nyingine ni uwekezaji katika uzalishaji wa dawa na vifaa tiba kupitia eneo maalum la uwekezaji wa dawa (Pharmaceutical Special Economic Zone) huko Bagamoyo, ushiriki katika mradi mkubwa wa chuma wa Liganga-Mchuchuma, pamoja na mifumo ya kisasa ya kilimo, umwagiliaji, usafirishaji, na uhifadhi wa baridi, uchakataji wa madini ya grafaiti, nikeli, kobalti na lithium ili kuongeza thamani yake kabla ya kusafirishwa nje, na uwekezaji katika miundombinu na usafirishaji hasa kwenye reli ya SGR, bandari, uchumi wa buluu, na ujenzi wa miji ya kisasa.
Prof. Mkumbo amesisitiza kuwa uwekezaji unaotafutwa na Tanzania ni ule unaosaidia kukuza uwezo wa ndani na kutengeneza fursa za kiuchumi kwa wananchi: "Kwa Tanzania, uwekezaji sio mwisho wa jambo lenyewe. Tunatafuta uwekezaji unaotengeneza kazi zenye tija, unaoendeleza ujuzi, unaohamisha teknolojia, unaoimarisha biashara za ndani na kuziingiza kampuni za Kitanzania kwenye minyororo ya thamani ya kikanda na kimataifa."
Waziri Mkumbo ameiomba METI kusaidia katika kuhamasisha wawekezaji na taasisi za kifedha za Japan kuchangamkia fursa zilizopo Tanzania, kusaidia katika uhamishaji wa teknolojia na ujuzi, pamoja na kuimarisha majukwaa ya majadiliano kati ya serikali na wafanyabiashara (G2B na B2B) ili kupata miradi thabiti inayoweza kufadhiliwa. -
Jambo TV
@Jambotv_
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetoa wito kwa Serikali ya Japan kuimarisha ushirikiano wao wa kihistoria kwa kuingia katika hatua mpya ya Ushirikiano wa Miundombinu ya Ubora kati ya Tanzania na Japan.
Wito huo umetolewa Septemba 8, 2026 na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo @kitilam , wakati wa mkutano wake maalum nchini Japan na Naibu Waziri wa Ardhi, Miundombinu, Usafiri na Utalii wa Japan (MLIT), Manabu Nagai.
Katika mazungumzo hayo, Prof. Mkumbo amesisitiza nia ya Tanzania ya kufanya Mpango wa Miundombinu ya Ubora wa Japan kuwa nguzo muhimu katika utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2050. Amebainisha kuwa mbinu inayotumiwa na Japan katika miradi ya miundombinu inathaminiwa sana nchini kutokana na kuzingatia viwango vya juu.
"Tunathamini sana kwamba mbinu ya Japan sio tu kuhusu kujenga miundombinu, bali ni kuwasilisha ubora, usalama, uimara, thamani ya kudumu ya mradi, uhamishaji wa teknolojia, na uendelezaji wa uwezo wa ndani," amesema Prof. Mkumbo.
Prof. Mkumbo amewasilisha vipaumbele vya Tanzania katika mageuzi makubwa ya miundombinu yanayoendelea hivi sasa, akieleza kuwa miradi hiyo ina tija kubwa si kwa Tanzania pekee bali kwa nchi jirani zisizo na bandari.
“Tanzania inapitia mageuzi makubwa zaidi ya miundombinu katika historia yake, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR), barabara kuu na madaraja ya kimkakati, pamoja na upanuzi na uboreshaji wa bandari na viwanja vya ndege," ameeleza Waziri huyo na kuongeza,
"Hii si tu miradi ya Tanzania, bali ni shoroba muhimu za usafirishaji zinazounganisha Bahari ya Hindi na nchi kadhaa zisizo na bandari za Afrika Mashariki, Kati na Kusini. Kwa hiyo, tunaiomba Japan kuiona Tanzania kama lango la kimkakati la ugavi na miundombinu kwa soko kubwa la Afrika."
Ili kufanikisha hili, serikali ya Tanzania imewakaribisha wawekezaji na kampuni za Kijapan kushiriki kupitia ushirikiano wa sekta ya umma na binafsi (PPPs), mikopo nafuu, uwekezaji wa moja kwa moja, na matumizi ya teknolojia za kisasa za Kijapan katika mifumo ya reli, usimamizi wa bandari, na mifumo ya kisasa ya usafirishaji
Katika hatua nyingine, Prof. Mkumbo amesisitiza umuhimu wa kuanza kutekeleza kwa vitendo Mkataba wa Ushirikiano wa Maendeleo ya Rasilimali Watu katika Sekta ya Ujenzi (MOC) uliosainiwa wakati wa mkutano wa TICAD 9 mjini Yokohama, mwezi Agosti 2025.
Tanzania imependekeza mpango wa mafunzo kwa wahandisi, mafundi, na wafanyakazi wa ujenzi wa Kitanzania ili kupata ujuzi na uzoefu wa kitaalamu nchini Japan, pamoja na kuanzisha viwango vya ujenzi vya Kijapani nchini.
Waziri ameonesha kufurahishwa na nia inayoongezeka ya kampuni kubwa za Japan kama vile Fujita Corporation inayojihusisha na miundombinu ya nyumba na barabara ya mzunguko ya Dodoma, Shimizu Corporation inayokarabati Bandari ya Kigoma kwa msaada wa ruzuku ya Japan.
"Tanzania ina fursa na eneo la kimkakati; Japan ina teknolojia inayoheshimika duniani kote, ufadhili, utaalamu wa kihandisi, na viwango vya ubora. Kuunganisha nguvu hizi pamoja kunaweza kuifanya Tanzania kuwa mfano wa kuigwa wa Miundombinu ya Ubora ya Japan barani Afrika," ameeleza Prof. Mkumbo. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira, amepinga madai kuwa mtu anayesimama na kusema kwa niaba ya mambo wanayotaka wananchi huwa anashughulikiwa akisema kuwa hakuna mtu aliyezungumza kwa niaba ya wananchi akaondolewa kwa sababu hiyo.
Wasira ametoa kauli hiyo leo Septemba 8, 2026, katika Mkutano wa Kitaifa wa Wadau wa Kutafakari Hali ya Siasa nchini unaofanyika mkoani Dar es Salaam
Kuhusu hoja ya kuandika Katiba Mpya, Wasira ameeleza kuwa ahadi ya siku 100 waliyoiweka ilikuwa kabla ya mwezi Oktoba mwaja jana na hawakutabiri jinsi hali ingekuwa katika mwezi huo. Amefafanua kuwa ilipofika Oktoba kulitokea changamoto ambazo zisingeruhusu Katiba kuandikika hata kama wangeanza mchakato huo mwezi Januari mwaka huu.
Amesisitiza kuwa ilikuwa lazima kwanza kutatua changamoto zilizojitokeza na kuwaleta watu pamoja ili waelewane kabla ya kuanza kuandika.
Aidha, Wasira amehoji mantiki ya wito wa kutaka wadau "kupambana" ili kupata katiba hiyo, akitaka kujua wanapambana na nani hasa. Amefafanua kuwa kwa jinsi CCM ilivyokwishaamua kuwa katiba itaandikwa, wito huo wa kupambana hauna tija na unaweza kusababisha wadau kupambana wao kwa wao badala ya kujenga nchi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katibu Mkuu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda, amewatuhumu wanasiasa nchini kwa ubinafsi, kupora haki za msingi za wananchi, na kutumia taasisi pamoja na sherehe za kidini kama daraja la kufikia maslahi yao binafsi ya kisiasa.
Sheikh Ponda, ambaye pia alikuwa mgombea ubunge wa Jimbo la Temeke kupitia Chama cha ACT Wazalendo katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, ameyasema hayo leo Jumanne, Septemba 8, 2026, wakati akihutubia katika Mkutano wa Kitaifa wa Wadau wa Kutafakari Hali ya Siasa nchini unaofanyika mkoani Dar es Salaam.
Sheikh Ponda amebainisha kuwa mataifa mengi duniani yamefanikiwa kujenga misingi mizuri ya umoja na utulivu kwa kuzingatia masuala ya dini katika mifumo yao ya kikatiba ili kuweka mazingira ambapo waumini na viongozi wa dini wanajua nafasi yao, wanaheshimiana, kuaminiana, na kupendana
Sheikh Ponda ameeleza kuwa wakati mataifa mengine yakitumia dini kama nyenzo ya kuunganisha watu na kupata maendeleo ya kitaifa, nchini Tanzania hazina hiyo inadhulumiwa kutokana na ubinafsi wa wanasiasa ambao wamepora haki za msingi na kujifanya wao ndio kila kitu.
“Tanzania tuna hazina kubwa kabisa ambayo inaweza kabisa kutumika kulifikisha taifa katika maendeleo, katika umoja na katika namna ambayo ilikuwa bora zaidi. Lakini wanasiasa wamekuwa binafsi wamepora haki za msingi kabisa na wanadhani kwamba wao sasa ndio kila kitu,” amesema Sheikh Ponda.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Naibu Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padri Dkt. Faustine Furaha, ametoa wito kwa viongozi na wananchi kurejea kwenye misingi ya kusema ukweli, kupiga vita rushwa, na kurejesha chaguzi zenye ushindani halisi ili kuponya taifa na kuwavutia vijana wanaozidi kukata tamaa na michakato ya kidemokrasia.
Akizungumza leo tarehe 8 Septemba, 2026, katika Mkutano wa Kitaifa wa Wadau wa Kutafakari Hali ya Siasa nchini unaofanyika mkoani Dar es Salaam, kiongozi huyo wa kiroho, amerejea hoja zilizowahi kuwasilishwa na Jaji Joseph Sinde Warioba kuhusu kukithiri kwa rushwa nchini akieleza kuwa rushwa bado ipo na imesambaa kiasi cha kuwa ya kimfumo na jambo linaloonekana kuzoeleka katika jamii.
Ameonya kuwa jambo hili la rushwa lisiposimamiwa na kukemewa kwa dhati kutoka mioyoni mwa watu, taifa litapotea, akibainisha kuwa rushwa imekuwa sababu ya baadhi ya watu kushindwa hata kushiriki katika chaguzi.
Kuhusu ushiriki wa kidemokrasia, Padri Furaha ameweka wazi wasiwasi wake juu ya kundi la vijana, ambao wanawakilisha takriban asilimia 60 ya idadi ya watu nchini na ambao kanisa hukutana nao kila siku katika maisha ya kawaida na ya kiroho. Amebainisha kuwa tofauti na zamani ambapo vijana walifurahia ushindani wa kisiasa na kwenda kupiga kura kwa shauku, sasa hivi hali ni tofauti kwani vijana wengi wamepoteza kabisa nia na ushawishi wa kushiriki.
Ametolea mfano wa uchaguzi mkuu uliopita ambapo vijana wengi walipoulizwa walionesha kutokuwa na nia kabisa ya kwenda kupiga kura.
“Tusifunge macho, tusiseme hakuna shida kwako wakati kuna tatizo pale. Lazima hilo suala tulifuatilie, tuliangalie linakwendaje,” amesisitiza kiongozi huyo, akiongeza kuwa suluhu ni kuhakikisha chaguzi zinakuwa za ushindani wa kweli ambapo anayeshinda kwa haki anatangazwa na asiyeshinda anakubali matokeo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Wakili Boniface Anyisile Mwabukusi amesema kutokana na hali ya kisiasa inayoendelea nchini haoni haja ya haraka ya kuandika Katiba Mpya hivi sasa na badala yake akasisitiza hitaji la dharura la kuundwa kwa Tume ya Ukweli ili kuiponya nchi kwanza.
Mwabukusi ameyabainisha hayo leo Septemba 8, 2026, katika Mkutano wa Kitaifa wa Wadau wa Kutafakari Hali ya Siasa nchini unaofanyika mkoani Dar es Salaam.
“Mimi niliwauliza watu... wengi wanaoliangalia katiba wanafikiri Tanzania inaisha mwaka 2030. Utaendaje kuandika katiba wakati bado hamuwezi kukaa kwa utulivu na kuelewana kwa pamoja? There is no national healing,” ameonya.
Rais huyo wa TLS amewataka wadau kutotazama changamoto za nchi kupitia mlango wa uchaguzi pekee, bali kuangalia mtazamo mpana wa kutoridhika uliopo mioyoni mwa wananchi.
Mwabukusi ameeleza kuwa TLS inaitazama tarehe 29 Oktoba, 2025 kama mkusanyiko wa mambo mengi yanayowasikitisha na kuwakosesha matumaini wananchi nchini, Ametaja mambo hayo kuwa ni pamoja na migogoro ya ardhi, utekaji na upotezwaji wa wakosoaji, na kudorora kwa hali ya kidemokrasia ya uchaguzi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Taifa, Othman Masoud Othman, ametoa kauli kuhusu mustakabali wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akisema kuwa katiba ya sasa ndiyo tishio kubwa zaidi kwa muungano huo kuliko kitu kingine chochote.
Akizungumza leo Septemba 8, 2026, katika Mkutano wa Kitaifa wa Wadau wa Kutafakari Hali ya Siasa nchini unaofanyika mkoani Dar es Salaam chini ya uratibu wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), Othman amesisitiza kuwa suala la mamlaka huru ni jambo la kukubaliana kwamba mamlaka hayo yanakwenda mpaka wapi, yanaishia wapi, yapi yatasimamiwa na mamlaka ya kati au mamlaka kuu na wanachama wa muungano watakuwa na mamlaka kwa kiasi gani.
Akitoa mfano, Othman amefafanua kuwa, ingawa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ni mwanachama wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) kama mwakilishi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kiuhalisia TFF haiwakilishi muungano bali inawakilisha ligi ya Tanzania Bara. Wakati huo huo, upande wa Zanzibar umezuiwa kupata uanachama wa FIFA, jambo linalofanya upande mmoja wa muungano kufurahia na kutumia mamlaka ya kimataifa kwa faida yake pekee kinyume na misingi ya usawa wa pande mbili
Mwanasiasa huyo ameonya kuwa kwa sasa muungano unaonekana kuwa shwari kwa sababu tu chama tawala cha CCM kinashika madaraka pande zote mbili, Tanzania Bara na Zanzibar. Hata hivyo, amesisitiza kuwa mfumo wa kikatiba lazima ujengwe kuhimili mabadiliko ya kisiasa pindi chama kingine kitakaposhika madaraka upande wowote.
Ametahadharisha kuwa, kutokana na migongano mikubwa iliyopo kwenye katiba ya sasa, akitokea kiongozi yeyote atakayeamua kusimama kidete na kuifuata katiba hiyo kama ilivyo sasa bila kuifanyia marekebisho, nchi itaingia kwenye vurugu kubwa sana.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Aliyekuwa mgombea Urais wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025, Salum Mwalimu, ametoa wito kwa vyama vya siasa na wadau nchini kupunguza kelele, hasa katika mitandao ya kijamii, and badala yake kujikita katika kutafuta tiba ya changamoto za kisiasa kwa njia ya mazungumzo kama wanavyofanya viongozi wa Zanzibar.
Mwalimu ameyabainisha hayo wakati akizungumza Septemba 8, 2026, kwenye Mkutano wa Kitaifa wa Wadau wa Kutafakari Hali ya Siasa nchini unaofanyika mkoani Dar es Salaam chini ya uratibu wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD).
Ingawa amekiri kuwa Zanzibar bado inakabiliwa na shida zake, amesisitiza kuwa kuna maendeleo makubwa yanayopatikana kwa sababu viongozi wapo tayari kukaa na kutafuta tiba.
Mwalimu ametoa rai kwa waandaaji wa mkutano huo, kwa kushirikiana na Msajili wa Vyama vya Siasa ambaye amevileta vyama vyote pamoja, kuhakikisha kunakuwa na mwendelezo wa vikao hivyo ili kupata mwelekeo wa pamoja wa jinsi ya kwenda mbele.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Zanzibar, Ismail Jussa, amepinga dhana kwamba ni lazima kuwepo na wasimamizi au wasuluhishi kutoka nje ili kufikia maridhiano ya kisiasa yenye tija nchini, akitolea mfano jinsi mwafaka uliosimamiwa na Jumuiya ya Madola (Commonwealth) ulivyofeli vibaya kuliko mikataba yote ya ndani.
Akizungumza Septemba 8, 2026, katika Mkutano wa Kitaifa wa Wadau wa Kutafakari Hali ya Siasa nchini unaofanyika mkoani Dar es Salaam, Jussa ameshirikisha uzoefu wa kihistoria wa Zanzibar katika kutafuta suluhu ya migogoro ya kisiasa, akichambua makubaliano mbalimbali tangu mwaka 1995 hadi sasa
Jussa ameeleza kuwa baada ya uchaguzi mkuu wa kwanza wa vyama vingi wa mwaka 1995, kulianzishwa mazungumzo yaliyochangiwa na utatuzi wa Jumuiya ya Madola (Commonwealth). Mchakato huo ulioanza mwezi Agosti 1996 ulichukua takriban miaka mitatu ya diplomasia kutokana na wasuluhishi kulazimika kwenda upande mmoja na kurudi kwa mwingine kuwasilisha ujumbe, hadi uliposainiwa rasmi mnamo Juni 9, 1999.
Hata hivyo, mwanasiasa huyo ameweka wazi kuwa mwafaka huo uligubikwa na mbwembwe nyingi na haukuwa mzuri zaidi katika utekelezaji. Ameongeza kuwa licha ya makubaliano kuainisha kuwa Jumuiya ya Madola ingekuwa dhamana ya kimaadili (moral guarantor) ya kusimamia utekelezaji, barua zote walizoandikiwa kulalamikia kutoendelea vizuri kwa mambo hazikupata majibu ya maana, na jumuiya hiyo ilionesha nia ndogo sana ya kufuatilia
Tofauti na uzoefu huo wa nje, Jussa ametoa mfano wa Mwafaka wa pili wa mwaka 2001, ambao ameuita kuwa ndio uliokuwa makubaliano madhubuti na yenye mnyororo mpana zaidi wa masuala katika historia ya nchi
Amesema mwafaka huo wa mwaka 2001, pamoja na mazungumzo ya mwafaka wa tatu yaliyojenga msingi wa Maridhiano ya kihistoria ya mwaka 2009 kuelekea 2010, yote yalifanywa na kusimamiwa na watendaji wa ndani pekee bila uwepo wa msimamizi yeyote wa nje au wa kati.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira, ameitaka jamii na wanasiasa kutafakari kwa kina dhana ya mabadiliko ya katiba, akionya kuwa mchakato huo unapaswa kuheshimu historia ya nchi badala ya kujaribu kuunda nchi mpya au kunakili katiba za nje.
Akizungumza Septemba 8, 2026, katika Mkutano wa Kitaifa wa Wadau wa Kutafakari Hali ya Siasa nchini unaofanyika mkoani Dar es Salaam, mwanasiasa huyo mkongwe amejibu hoja za viongozi wa upinzani kuhusu mabadiliko ya katiba huku akigusia uhusiano wa muungano na mustakabali wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (GNU/SUK).
Kuhusu hali ya kisiasa ya Zanzibar, Wasira ameeleza imani yake kuwa tofauti zilizopo katika kukamilisha na kuanza kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (GNU) zinaweza kutatuliwa na kuundwa kwa serikali madhubuti kwa ajili ya kuleta utulivu (stability), ambayo ndiyo msingi wa maendeleo ya nchi yoyote.
Pamoja na matumaini hayo, Wasira alirusha "swali la kichokozi" kwa chama cha ACT Wazalendo akitaka ufafanuzi wa kisera kuhusu msimamo wa ACT Wazalendo unaodai "Zanzibar yenye mamlaka kamili".
Amehoji maana halisi ya mamlaka hayo kamili kwa kusema kuwa kwa sasa Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano na inayo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) inayoshughulikia takriban mambo yote ya Zanzibar, isipokuwa mambo machache. Ameonya kuwa kutofafanuliwa vizuri kwa dhana ya "mamlaka kamili" kunaleta mkanganyiko mkubwa kwa wananchi na kunaweza kuamsha migogoro hadi Tanzania Bara
“Sasa unaposema Zanzibar yenye mamlaka kamili... inakuwa sehemu ya muungano au inakuwa sovereignty? Na kama inakuwa sovereignty, huo ndio mwisho wa United Republic of Tanzania au inakuwaje? Hili ni jambo kubwa ambalo nalo tusipolifanyia ufafanuzi linayumbisha watu,” amesema Wasira.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Taifa, Othman Masoud Othman, amefichua siri ya mkwamo wa kisiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, akieleza jinsi Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilivyokiuka makubaliano ya dhati ya mambo matatu yaliyofikiwa kabla ya uchaguzi huo na kusababisha nchi kuingia kwenye uchaguzi bila marekebisho yoyote.
Akizungumza Septemba 8, 2026, katika Mkutano wa Kitaifa wa Wadau wa Kutafakari Hali ya Siasa nchini unaofanyika mkoani Dar es Salaam, Othman amebainisha kuwa uzoefu uliopatikana katika chaguzi za miaka ya 2015 na 2020 ulichangia kwa kiasi kikubwa kuunda mchakato wa sasa, ikiwa ni pamoja na uamuzi wa kuingia kwenye Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK)
Hata hivyo, Othman ameweka wazi kuwa namna uchaguzi wa 2025 ulivyoendeshwa haukuwa tofauti sana na ule wa 2020. Ametaja changamoto zilizoanza tangu hatua ya uandikishaji, makubaliano ya ACT na CCM likiwamo la kuondoa kabisa utaratibu wa kura ya mapema, mpaka kukiukwa kwa baadhi ya makubaliano katika uchaguzi mkuu wa 2025.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Serikali ya Tanzania inalenga kuongeza mara mbili uwekezaji wa Japan nchini, kutoka miradi 24 iliyosajiliwa sasa yenye mtaji wa takribani dola milioni 42.7 za Marekani hadi kufikia miradi isiyopungua 48.
Hayo yamebainishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo @kitilam , akiwa nchini Japan anakoongoza ujumbe maalum wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Japan, Mkutano wa Kimataifa wa Tokyo kuhusu Maendeleo ya Afrika na Kazi Endelevu ya Kampuni za Japan nchini Tanzania.
Prof. Mkumbo ameeleza kuwa ziara hiyo inalenga kubadilisha sura ya ushirikiano wa nchi hizo mbili kutoka kwenye usaidizi wa maendeleo kwenda kwenye uwekezaji wa pamoja na ushirikiano wa kibiashara, ili kuchangia utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 inayolenga kujenga uchumi wa Dola trilioni moja.
Akiwasilisha fursa za kiuchumi mbele ya viongozi wa Shirika la Biashara la Nje la Japan (JETRO), Prof. Mkumbo amebainisha kuwa Tanzania ina uchumi unaokua kwa kasi wa kati ya asilimia 5 na 7, utulivu wa kisiasa, na ndiyo lango kuu la kibiashara kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na SADC kupitia Bandari ya Dar es Salaam na miundombinu ya treni na barabara.
“Ujumbe wetu kwa Japan ni rahisi; wekezeni Tanzania si kwa ajili ya kulitumikia soko la Tanzania pekee, bali kwa ajili ya kulitumikia soko pana la Afrika lenye mamia ya watumiaji,” amesema Prof. Mkumbo.
Katika kukuza sekta ya viwanda na teknolojia, Serikali imependekeza ushirikiano wa karibu kati ya JETRO na Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalumu ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) ili kuanzisha maeneo maalum ya viwanda vya kampuni za Japan, kuhamisha teknolojia, na kutatua changamoto za kibiashara.
Aidha, Prof. Mkumbo ameeleza kuwa Tanzania inaweka utaratibu wa kusaidia wazalishaji na wauzaji wa bidhaa wa Kitanzania kukidhi viwango vya soko la Japan ikiwemo ubora, ufungashaji, na uthibitishaji wa usalama wa chakula ili kuwaunganisha moja kwa moja na wanunuzi nchini humo. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Ofisi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA Kanda ya Kaskazini, kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi, imefanikiwa kulikamata gari aina ya Toyota Land Cruiser, lenye namba za usajili T523 EMK, linalodaiwa kuwa mali ya chama na lililokuwa likitumiwa na aliyekuwa Katibu wa chama hicho Kanda ya Kaskazini, Ndonde Totinan ambaye alijiondoa chamani Aprili Mosi, 2026.
Akizungumza na waandishi wa habari nje ya Kituo Kikuu cha Polisi Arusha, Katibu wa chama hicho Kanda ya Kaskazini, Yohana Kaunya amesema baada ya kushika nafasi hiyo alianza mkakati wa kutafuta na kurejesha mali za chama, ndipo alipobaini kuwa baadhi ya mali hizo zilikuwa zikishikiliwa na aliyekuwa Katibu wa Kanda hiyo.
Kaunya amesema walijaribu mara kadhaa kuzungumza na Ndonde kuhusu kurejeshwa kwa mali hizo, ikiwemo gari hilo, lakini juhudi hizo hazikufanikiwa na hivyo wakaamua kuchukua hatua za kisheria zilizowezesha kukamatwa kwa gari hilo.
Kuhusu madai kwamba Ndonde anadai CHADEMA ikiwemo mishahara yake na kwamba hilo ndilo lililomfanya aendelee kushikilia mali hizo, Kaunya amesema endapo kuna madai ya mishahara, alipaswa kufuata taratibu za kisheria kupitia mamlaka husika za kazi badala ya kushikilia mali za chama.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Arusha, Elisa Mungure, amesema kushikiliwa kwa mali za chama, ikiwemo gari hilo, kumeathiri shughuli za CHADEMA Mkoa wa Arusha na Kanda ya Kaskazini kwa ujumla, hali iliyosababisha baadhi ya shughuli za chama kudorora.
Jambo TV ikiendelea kufuatilia taarifa hii kwa karibu, ikiwemo kupata upande wa pili kutoka kwa Ndonde Totinan kuhusu tuhuma na madai haya.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Nyumba la Taifa nhctanzania imesisitiza kasi, ubora na ujenzi unaokwenda sambamba na mahitaji ya soko, ikieleza kuwa NHC ya sasa lazima iwe na uwezo wa kushindana kwa ubora na wawekezaji binafsi katika sekta ya nyumba.
Kauli hiyo imetolewa leo na Mwenyekiti wa bodi ya hiyo Dkt. Sophia Kongela, baada ya bodi kufanya ziara ya kukagua miradi ya Samia Housing Scheme Medeli, Njedengwa Valley View na Iyumbu Urban Apartments jijini Dodoma.
Ziara hiyo iliyohusisha wajumbe wa bodi pamoja na Menejimenti ya NHC imelenga kujionea hatua za utekelezaji wa miradi, ubora wa kazi na namna Shirika linavyotekeleza dhamira yake ya kuongeza nyumba za kisasa katika maeneo mbalimbali nchini.
Dkt. Kongela amesema bodi imeridhishwa na mabadiliko yanayoonekana katika utekelezaji wa miradi na juhudi kubwa zinazofanywa na wahandisi pamoja na Menejimenti ya Shirika.
“Ukipita kwenye miradi yetu sasa unaona kabisa nguvu kubwa iliyowekwa na kazi inayofanywa na wahandisi wetu. Tunachotaka sasa ni kuona kasi hii inaendelea na ile habari ya kuchelewa kuingiza nyumba zetu sokoni isiwepo tena,” amesema Dkt. Kongela.
Amesisitiza kuwa kasi pekee haitoshi, bali nyumba zinazojengwa na NHC lazima ziwe na ubora, usanifu wa kisasa na thamani inayolingana na matarajio ya wateja.
“Watu wa sasa wanataka vitu vizuri. Ukilinganisha nyumba zetu na za private developer mwingine, NHC lazima iwe kwenye viwango vya juu. Tunataka kutoa bidhaa zenye ubora wa hali ya juu na kuzifikisha sokoni kwa wakati,” amesema.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Hamad Abdallah, amesema Menejimenti imejipanga kutekeleza maelekezo ya Bodi, huku hatua mbalimbali zikiwa zimechukuliwa kuondoa sababu zilizokuwa zikichelewesha miradi hapo awali.
Amesema shirika sasa lina mikataba ya muda mrefu na wasambazaji wa vifaa vya ujenzi, hatua inayosaidia kuhakikisha maeneo ya miradi yanapata vifaa kwa wakati bila kusimamisha kazi.
“Katika sites zetu hakuna uhaba wa building materials. Timu zetu pia zinafanya kazi kwa kujituma sana; pale inapohitajika kazi zinaendelea hata nje ya muda wa kawaida ili kuhakikisha ratiba zetu hazirudi nyuma,” amesema Abdallah. -
Jambo TV
@Jambotv_
Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, imeendelea leo Septemba 7, 2026 katika Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, ambapo shahidi wa tatu wa upande wa utetezi, Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Amani Golugwa, amepandishwa kizimbani kuendelea kuhojiwa na mawakili wa Serikali, ambapo alianza kuhojiwa na Wakili Mkuu wa Serikali Nassor Katuga.
Katika kuanza kwa dodoso lake leo, Wakili Katuga alimhoji shahidi akitaka afafanue iwapo maudhui yaliyochukuliwa na mwandishi wa habari yanakuwa mali ya mwandishi huyo na kama anaamua kuyatumia atakavyo. Shahidi Golugwa alijibu kuwa ni kweli yanakuwa mali yake, na alipoulizwa kama maneno hayo ni kwa mujibu wa sheria au maoni yake, alidai ni kwa mujibu wa sheria na maoni yake pia, ingawa alipobanwa kama alitaja kifungu cha sheria, alikiri kuwa hakutaja kifungu chochote.
Wakili Katuga aliendelea kumhoji shahidi iwapo alikiri kuwa kuhamasisha uasi siyo kosa bali ni neno la kisiasa, ambapo Golugwa alithibitisha kukumbuka hilo. Wakili Katuga alihoji juu ya lugha ya Kiswahili na matumizi yake, shahidi alieleza kuwa wanatumia lugha hiyo kwenye shughuli zao za kisiasa na kwamba zipo lugha za kisiasa, ingawa hakutaja kuwepo kwa kamusi maalumu ya lugha ya kisiasa.
Katuga alimhoji tena kuhusu kauli ya "tunaenda kuuvuruga uchaguzi", huku shahidi akisisitiza kuwa kauli hiyo inatokana na ukweli wa shughuli za siasa na si maoni binafsi, akitambua kuwa uchaguzi upo kwa mujibu wa katiba. Shahidi alikana kusema kuwa kuvunja sheria hakupelekei kuwa kosa la uhaini na akaeleza kuwa kupinga siyo kosa, ingawa hakutaja sheria husika. Alipoulizwa kuhusu sentensi "tunaenda kuzuia uchaguzi" na "tunaenda kuvuruga uchaguzi", Golugwa alithibitisha kuwa zikisomwa mpaka mwisho zinakuwa sentensi kamilifu zenye kuleta maana.
Katika kuendeleza maswali yake, Wakili Katuga aliuliza kuhusu kauli za Lissu kuhusu kuwa majaji ni ma ccm, amapo alimuuliza kama alimsikia akisema majaji ni ma-CCM, mahakamani hakuendeki, au polisi wanaingiza kura feki. Golugwa alijibu kuwa hakukumbuka mambo hayo na kusisitiza kuwa maswali hayo yaulizwe kwa Mwenyekiti mwenyewe, akiongeza kuwa yeye alieleza yale tu aliyoyasikia kutoka katika hotuba iliyochukua saa moja na nusu hadi mawili, ambayo sehemu yake ndogo ya sekunde 26 ndiyo iliyoandikwa kwenye hati ya mashtaka.
Alipoulizwa Kuhusu vikao na maazimio, shahidi alikiri kuwa vikao vya chama vina maazimio na kwamba yeye ndiye mtunza kumbukumbu, akithibitisha kuwa uandishi wa maazimio huandikwa kwa sentensi fupi zinazoeleweka. Alipoulizwa kuhusu neno "kukinukisha", shahidi alikubali kuwa ni kitendo lakini akaeleza kuwa tafsiri yake ilikuwa ni kufanya kitu kitoe harufu, akiongeza kuwa katika hotuba ya Mwenyekiti hakukuwa na maelekezo ya jinsi ya kukinukisha au kuchoma vitu kama vile matairi. Golugwa alisisitiza kuwa si haki kwa yeyote kwenda kuvinukisha vituo vya kupigia kura kwa kuvichoma.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mashirika yanayopigania haki na maendeleo ya mtoto wa kike nchini Tanzania yametoa wito kwa Serikali na wadau wa maendeleo kuongeza uwekezaji katika ujuzi wa kidijiti na teknolojia kwa wasichana, ili kuwawezesha kushiriki kikamilifu katika uchumi wa kisasa, uongozi, na ajira.
Wito huo umetolewa leo, Septemba 7, 2026, jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa rasmi wa maandalizi ya jukwaa la Ajenda ya Msichana 2026, ambalo linalenga kuwapa wasichana nafasi ya kueleza changamoto, fursa, na mapendekezo yao kuhusu elimu, usalama, teknolojia, na uongozi.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Isabela Mushi, mwanafunzi wa Kidato cha Tatu katika Shule ya Sekondari Karanga, amesisitiza kuwa kuwajengea wasichana uwezo wa kutumia na kuunda teknolojia ni uwekezaji wa kimkakati kwa uchumi wa taifa.
“Kuandaa wasichana mapema na kuwajengea uwezo wa kutumia, kuunda na kuuza teknolojia si suala la kuwapa ujuzi wa ziada tu, bali ni uwekezaji wa kimkakati katika kuhakikisha kwamba wanawake na wasichana wanakuwa washiriki kamili wa uchumi wa kidijitali wa Tanzania ya 2050,” amesema Isabela.
Naye Expirence Kobelo, mwanafunzi wa Darasa la Sita katika Shule ya Msingi Msasani, ameeleza kuwa jukwaa hilo linatoa fursa ya kipekee kwa wasichana kujieleza badala ya kufanyiwa maamuzi na watu wengine.
“Ajenda ya Msichana 2026 ni nafasi ya kuhakikisha kwamba wasichana hawazungumziwi tu, bali wanazungumza wenyewe, wanasikilizwa na wanashiriki katika kujenga mustakabali wanaoutaka,” amesema Kobelo.
Kwa upande wake, Mjumbe wa Bodi ya Ushauri ya Wasichana ya Taasisi ya Msichana Initiative @MsichanaUwezo , Letisia Mswaki, ametoa wito kwa Serikali, wanahabari, na wadau wote kushirikiana ili kuweka mazingira wezeshi yatakayowaunganisha wasichana na kuwasaidia kufikia ndoto zao.
Jukwaa la Ajenda ya Msichana 2026 lenye kaulimbiu “Kuinua Sauti za Wasichana kwa Maendeleo Endelevu” linatarajiwa kufanyika Oktoba 8 na 9, 2026, katika viwanja vya Maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, likiwakutanisha takribani wasichana 200 kutoka mikoa mbalimbali pamoja na Serikali, mashirika ya kiraia, sekta binafsi, walimu na wadau wa maendeleo. Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Tanzania na Malawi zimeendelea kufungua fursa mpya za biashara na uwekezaji kupitia Jukwaa la Biashara na Uwekezaji la Tanzania na Malawi 2026, linalofanyika katika Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam kwa siku tatu.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Ephraim Balozi Mafuru amesema jukwaa hilo ni fursa kwa wafanyabiashara wa nchi hizo mbili kuunganishwa na kuongeza biashara, akibainisha kuwa Tanzania ilisafirisha bidhaa zenye thamani ya zaidi ya Dola milioni 86 kwenda Malawi mwaka uliopita.
Amesema Malawi ni miongoni mwa nchi zinazotumia miundombinu ya Tanzania, ikiwemo Bandari ya Dar es Salaam, katika kusafirisha na kuingiza bidhaa, huku wafanyabiashara wakihimizwa kutumia fursa hiyo kuingia katika soko la Malawi.
Kwa upande wake, Mgeni rasmi wa kongamano hilo ambaye pia ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Utalii wa Malawi, Simoni Itaye, amesema Tanzania na Malawi zina bidhaa na fursa mbalimbali za uwekezaji ambazo zinaweza kuongeza biashara na kukuza uchumi wa nchi hizo mbili.
Naye Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Agnes Richard Kayola, amesema ukaribu wa Tanzania na Malawi pamoja na uhusiano wao wa muda mrefu ni fursa muhimu ya kuongeza biashara na uwekezaji kati ya nchi hizo mbili.
Akizungumza katika kongamano hilo, Mkurugenzi wa Uhamasishaji na Uwekezaji wa Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalumu ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA), George Mukono, amesema Mamlaka hiyo inalenga kutumia fursa hiyo kuwahamasisha wawekezaji kutoka Malawi kuleta malighafi na kuwekeza katika uzalishaji na usindikaji nchini Tanzania.
Amesema pia Tanzania inalenga kutumia nafasi yake kama kiungo kati ya masoko ya Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika, ili kukuza biashara na uwekezaji kwa manufaa ya nchi zote mbili.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mbunge wa Jimbo la Tunduru Kaskazini ambaye ni Katibu Mkuu wa @ACTwazalendo Ado Shaibu Ado @AdoShaibu amemtaja Mwenyekiti wa @ChademaTZ2 Tundu Lissu kama Nelson Mandela wa Tanzania na mtu muhimu kuelekea kuanza na kukamilika kwa mchakato wa maridhiano.
Ado amesema hayo leo Septemba 7, katika Mkutano wa Kitaifa wa Wadau Kutafakari Hali ya Kisiasa Nchini kutafakari hali ya kisiasa uliofanyika Serena Hotel Jijini Dar es Salaam
Amesema ni muhimu wakati mchakato huo unaanza Lissu awe ameshaachiwa ili kushiriki katika mchakato huo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri Mkuu na Makamu wa Rais Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba alishindwa kumalizia hotuba yake ya ufunguzi katika mkutano wa kitaifa wa wadau kutafakari hali ya kisiasa ambapo yeye alikuwa mgeni rasmi, kutokana na kuanguka akiwa jukwaani.
Wadau waliokuwa katika ukumbini(Serena Hotel Dar es Salaam) walimpatia huduma ya kwanza na baadae aliweza kuondoka akitembea kwa msaada wa mlinzi wake na wadau wengine.
Hata hivyo Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Dorothy Semu aliwaeleza wadau kuwa hali ya Jaji Warioba iko vizuri kwa sasa.
Ikumbukwe tukio hilo lilitokea mara baada ya Warioba mwenye umri wa miaka 86 kuzungumza akiwa amesimama kwa takribani lisaa limoja.
Inaelezwa kuwa mara baada ya kupata ahueni inayodaiwa ilitokana na uchovu, alihitaji kuendelea na hotuba lakini alihusiwa kwenda kupumzika na kuangalia afya yake zaidi jambo ambalo alilikubalThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri Mkuu na Makamu wa Rais Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba amesema yapo mazingira kuwa ukabila, udini, ukanda na utaifa yameanza kuwepo na yanasababisha mpasuko
Amesema hayo leo Septemba 7, katika mkutano wa kitaifa wa wadau kutafakari hali ya kisiasa nchini unaofanyika Serena Hotel Jijini Dar es Salaam akieleza kuwa jitihada zinahitajika ili kudhibiti mambo hayo.
"Kuna mpasuko wa dini sasa hivi na umeanza kutugawa, kuna ukanda, kuna utaifa umezuka, Uzanzibari Utanganyika tunaanza kujiona sisi Wazanzibar sisi Watanganyika na tunadai haki zetu" amesema WariobaThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
"Amani haikuletwa na bunduki na hutalinda amani kwa bunduki lakini kwa sasa tunafikiri bunduki ndiyo inaweza kuleta amani inaweza kuleta utulivu lakini hailindi amani lazima turudi kwenye misingi na hii kazi kubwa ipo kwenye vyama vya siasa"
Hayo ameyasema Makamu wa Rais na Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba leo Septemba 7, 2026 katika mkutano wa kitaifa wa wadau kutafakari hali ya kisiasa nchini unaofanyika Serena Hotel Jijini Dar es SalaamThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
BREAKING NEWS: Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi ametangaza taarifa ya kifo cha Hafidh Ameir Hassan ambaye ni Mume wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kilichotokea leo Septemba 7, 2026 huko Zanzibar akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa moyo
Taarifa ya Makamu wa Rais imeeleza zaidi kuwa mipango ya mazishi inaendelea huko Kizimkazi, Zanzibar -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI:
Mjadala mkali umeibuka nchini Malawi baada ya mshindi wa Miss Malawi 2025, Thandi Chisi, kuondolewa katika nafasi ya kuiwakilisha nchi hiyo kwenye mashindano ya Urembo ya Dunia, 'Miss World' na nafasi yake kuchukuliwa na mshindi wa pili, Ireen Navicha, ambaye ni binti wa Waziri wa Jinsia, Watoto, Walemavu na Ustawi wa Jamii, Mary Navicha.
Chisi alitwaa taji la Miss Malawi Desemba 13, 2025, mjini Lilongwe na alitarajiwa kuiwakilisha Malawi katika mashindano ya 'Miss World', lakini waandaaji baadaye walimchagua Navicha, hatua iliyozua maswali kuhusu uwazi na usawa wa mchakato huo.
Awali, waandaaji walidai Chisi aliondolewa kwa sababu ya umri, wakisema alikuwa amevuka kikomo kinachoruhusiwa. Hata hivyo, maelezo hayo yalihojiwa kwa kuwa Chisi angekuwa na umri wa miaka 27 wakati wa mashindano hayo.
Shirika la Miss Malawi baadaye liliomba radhi na kukiri kuwa kulikuwa na mkanganyiko kuhusu sifa ya umri. Kwa upande mwingine, mfadhili mkuu wa mashindano hayo, Goshen City, ulitoa sababu tofauti, ukisema uamuzi huo ulilenga kutoa fursa kwa washiriki wengine wa fainali na kwamba Navicha alikuwa na uzoefu wa kimataifa.
Licha ya mjadala huo, Miss World ilithibitisha Navicha kuwa mwakilishi rasmi wa Malawi katika mashindano hayo yaliyofanyika Septemba 5, 2026 huko Vietnam.
Navicha alifikia hatua ya Top 40 kabla ya kuondolewa katika kinyang’anyiro cha kuingia Top 20. Hata hivyo, aliiandikia historia Malawi kwa kuwa mwakilishi wa kwanza wa nchi hiyo kufika Top 40 katika historia ya 'Miss World'.
Kwa upande wake, Chisi alionekana kutulia licha ya kuondolewa katika nafasi hiyo, akisema: “Taji halimfanyi mtu kuwa Malkia; tabia ndiyo humfanya. Na hakuna mazingira yanayoweza kuliondoa hilo.”
Tukio hilo limeacha maswali mazito nchini Malawi kuhusu uwazi na uadilifu wa mchakato wa Miss Malawi, huku mjadala ukitazama zaidi ya taji lenyewe na kuibua hoja pana kuhusu upendeleo na matumizi mabaya ya madaraka. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI:
Uchunguzi wa polisi umeanza nchini Kenya baada ya afisa mwandamizi wa Jeshi la Magereza, Senior Superintendent of Prisons Eric Kiarie Wainaina (40), kukutwa amefariki ndani ya gari lake katika eneo la wazi nyuma ya Spur Mall, Ruiru, asubuhi ya Septemba 6, 2026
Wainaina, aliyekuwa akihudumu katika Makao Makuu ya Kanda ya Kati ya Jeshi la Magereza mjini Nyeri, alikutwa akiwa kwenye kiti cha dereva wa gari aina ya Nissan Wingroad, huku mlango wa gari ukiwa wazi.
Imeelezwa, Polisi walifika eneo la tukio baada ya mwananchi kutoa taarifa na ndani ya gari kukutwa vitu binafsi vya marehemu, ikiwemo simu ya mkononi, pasipoti, leseni ya udereva na dawa za shinikizo la damu.
Pia, wachunguzi wanadai kuona chupa tupu za maji na pombe. Hata hivyo, chanzo cha kifo chake bado hakijathibitishwa, huku uchunguzi ukiendelea kubaini kilichotokea kabla ya kifo chake.
Taarifa kutoka kwa watu waliokuwa karibu na Wainaina zinaeleza kuwa alikuwa akipitia changamoto binafsi, ikiwemo msongo wa mawazo na utegemezi wa pombe. Inadaiwa pia alikuwa amewahi kupata matibabu na hivi karibuni alifika Hospitali ya Mathari kwa ajili ya kupata msaada wa afya ya akili.
Mwili wake umepelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kenyatta University kwa ajili ya uchunguzi wa kitabibu (postmortem), ambao unatarajiwa kusaidia kubaini chanzo halisi cha kifo.
Kamanda wa Polisi wa Jimbo la Juja, Isaac Kombo, amethibitisha tukio hilo na kusema maafisa wa Kurugenzi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) kutoka Juja wanaendelea na uchunguzi kuhusu mazingira ya kifo hicho. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
“Chumba kimoja nakaa na watoto wangu watano.” Haya ni maneno ya Bahati Rashidi, mama aliyeonekana kwenye video akiendesha baiskeli huku amembeba mtoto wake, akitafuta riziki
Baada ya taarifa yake kusambaa mitandaoni, Jambo TV tumefanikiwa kumpata Bahati katika Mtaa wa Milembe, Vingunguti jijini Dar es Salaam, ambako anaishi katika nyumba ya kupanga pamoja na watoto wake.
Bahati anajitafutia riziki kwa biashara ya matunda, akitumia baiskeli kama nyenzo ya kusafirisha bidhaa na kutafuta mahitaji ya familia.
Baada ya kumtembelea, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanahabari wa Mitandao ya Kijamii Tanzania (JUMIKITA) Shaban Matwebe, amemkabidhi Bahati Shilingi laki tano, pamoja na kumlipia kodi ya nyumba kwa miaka miwili.
Hata hivyo, msaada huu ni mwanzo. Mwenyekiti amesema lengo ni kukusanya kati ya shilingi milioni 5 hadi 10, fedha zitakazomsaidia Bahati kupata mtaji wa kuanzisha biashara ya kudumu na kuondokana na changamoto ya kutafuta riziki barabarani.
Wadau mbalimbali wameombwa kujitokeza kumuunga mkono Bahati ili lengo hilo lifikiwe na kumpa nafasi ya kuanza maisha mapya pamoja na watoto wake watano.
Kwa upande wake, Bahati ametoa shukrani kwa wote waliofanikisha kupatikana kwake na kuanza kwa safari hii ya msaada.
Kwa yeyote aliyeguswa na mama huyu anaweza kusaidia kumchangia chochote kupitia namba 0688706053- BAHATI ONYANGOThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Serikali ya Tanzania imeendelea kusisitiza kutekelezwa mkakati wa kubana matumizi ya rasilimali za umma ili kuelekeza fedha hizo katika kugharamia mpango mpya wa elimu ya lazima hadi kidato cha nne (darasa la 10), huku ikifichua jinsi safari za vikundi vya watendaji wa mikoa kwenda bungeni kupitisha bajeti zilivyokuwa zikitafuna zaidi ya Shilingi bilioni 20 kwa wiki moja pekee.
Akizungumza na wananchi wa Jimbo la Ilongero, Wilaya ya Singida, mkoani Singida leo Jumapili, Septemba 6, 2026, Waziri Mkuu wa Tanzania Dkt. Mwigulu Nchemba amesema kuwa mfumo huo mpya wa elimu ya lazima unamaanisha kuwa serikali lazima ihakikishe kila kijiji nchini kinakuwa na shule ya sekondari.
Ili kufanikisha azma hii ndani ya mwaka mmoja, Dkt. Nchemba amesema serikali inakabiliwa na mahitaji makubwa ya miundombinu ikiwemo ujenzi wa madarasa, maabara, maktaba, pamoja na mahitaji ya walimu, madawati, vitabu na vifaa vya kufundishia, na ili kupata fedha za kugharamia miradi hii mikubwa bila kuwaumiza wazazi, serikali lazima ibadili tamaduni na tabia zake za matumizi.
Amesema Rais tayari ameonesha mfano kwa kupunguza msafara wake na kuwabeba maafisa wengine kwenye gari moja. Kufuatia mfano huo, Dkt. Nchemba amepiga marufuku tabia ya watendaji wa mkoa mzima kukusanyika mahali pamoja wakati wa ziara zake akibainisha kuwa atakuwa anakutana na watendaji wilayani kwao ili kuokoa fedha za walipa kodi zinazopotea kwenye mafuta na matengenezo ya magari.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Uwekezaji wa Shilingi bilioni 16 uliofanywa na Serikali chini ya Wizara ya Maji kupitia Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) katika ununuzi wa pampu mpya nane umeanza kuonesha matokeo chanya ya uzalishaji na usafirishaji wa maji, hatua iliyolenga kuboresha upatikanaji wa huduma ya maji kwa wananchi wa Dar es Salaam na Pwani.
Kwa mwananchi, uwekezaji huo unalenga kuongeza uwezo wa maji yanayochukuliwa na kusafirishwa kutoka chanzo hadi mtamboni, hivyo kuwezesha DAWASA kuzalisha na kusambaza maji kwa ufanisi zaidi.
Maeneo yaliyokuwa na changamoto ya upatikanaji hafifu wa huduma ya maji katika mikoa ya Dar es salaam na Pwani sasa ni dhahiri kuwa mashuhuda wa upatikanaji wa maji ya uhakika.
Maeneo ambayo imeshuhudia maboresho makubwa ya kihuduma baada ya kufungwa kwa pampu hizi ni maeneo ya Kimara, Mbezi, Golan, Ukombozi, Saranga, Madale, Chasimba, Mbezi Juu, Baraza la Mitihani na maeneo mengine ndani ya eneo la kihuduma la DAWASA.
Afisa Mtendaji Mkuu DAWASA, Mhandisi Mkama Bwire, amesema uwekezaji wa pampu mpya nane kwa gharama ya Shilingi bilioni 16 unahusisha pampu sita ambazo tayari zimewasili, huku mbili zikiwa katika mchakato wa kuwasili.
Amesema pampu saba kati ya hizo zimepangwa kufungwa katika Mtambo wa Ruvu Juu, ambapo nne zitafungwa katika eneo la uchukuaji na usafirishaji wa maji ghafi, huku tatu zikiwa zimepangwa kufungwa katika eneo la mtambo.
Mhandisi Bwire amesema pampu zilizokuwa zikitumika awali zilikuwa na uwezo wa kusafirisha kati ya lita 900,000 hadi lita milioni moja za maji kwa saa. Pampu mpya zina uwezo wa kusafirisha kati ya lita milioni 1.5 hadi milioni mbili kwa saa.
Tofauti hiyo ina maana ya ongezeko kubwa la uwezo wa kusafirisha maji, jambo ambalo likiendana na uwezo wa mtambo na mtandao wa usambazaji, linaweza kuongeza kiasi cha maji kinachofikishwa kwa wananchi.
Kwa wananchi wa Dar es Salaam na Pwani, matokeo yanayotarajiwa ni kuimarika kwa upatikanaji wa maji, kupunguza changamoto zinazotokana na uwezo mdogo wa kusafirisha maji na kuongeza uwezo wa mamlaka kukidhi mahitaji yanayoongezeka ya huduma. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Chama cha ACT Wazalendo kimeonesha kutoridhishwa na mwenendo wa maandalizi ya serikali katika kukabiliana na tahadhari ya mvua kubwa za El Niño zinazotajwa na kutarajiwa kuanza Oktoba hadi Desemba 2026. Kutokana na hali hiyo, chama hicho kimeitaka serikali kuchukua hatua za dharura za kivitendo ili kuepusha maafa, vifo, na uharibifu wa miundombinu.
Akizungumza na wanahabari leo Jumapili, Septemba 6, 2026, jijini Dar es Salaam, Waziri Mkuu Kivuli wa ACT Wazalendo, Isihaka Mchinjita, ameeleza kuwa chama chake kimekuwa kikifuatilia kwa karibu kauli, matamko, na mipango ya serikali kuhusu tahadhari hiyo lakini hairidhishwi hata kidogo na kasi ya maandalizi ya sasa
Ili kulinusuru taifa na maafa yanayoweza kuepukika, Mchinjita ameweka hadharani mambo saba ambayo serikali inapaswa kuyatekeleza haraka sana. Mambo hayo ni kuunda timu maalum ya kitaifa ya kukabiliana na majanga, kuongeza fedha kwa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) ili kununua na kuhifadhi chakula cha kutosha kwa ajili ya dharura na kusaidia maeneo yatakayoathirika, kutangaza maeneo hatarishi na kuwahamisha wananchi, kuharakisha ujenzi na ukarabati wa miundombinu muhimu kama vile madaraja, makalavati, na barabara.
Mambo mengine ni kusafisha na kupanua mitaro na njia za maji ili kuzuia mafuriko, huku miradi yote iliyo hatarini ikitakiwa kukamilishwa haraka au kufikia viwango vya salama kabla ya mvua kuanza, shughuli za uchimbaji madini kusitishwa kwa muda katika maeneo hatarishi, wamiliki wa migodi wanapaswa kuimarisha kingo za machimbo na kutengeneza njia salama za maji ili kuzuia mafuriko na ajali ambazo zinaweza kupoteza maisha ya watu wengi.
Aidha, serikali imetakiwa kufanya maandalizi ya dharura ya kimatibabu na kiokoaji kwa kuongeza wataalamu wa afya, dawa, na vifaa tiba, kuhakikisha viongozi katika ngazi zote wanakuwa kazini kikamilifu na katika maeneo yenye vihatarishi vikubwa badala ya kusubiri majanga yatokee ndipo waanze kuchukua hatua.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Ukaguzi duni wa ubora wa mazao ya uvuvi umetajwa kuwa miongoni mwa changamoto zinazoweza kushusha thamani ya samaki na mazao mengine ya uvuvi ndani ya nchi na kimataifa.
Akizungumza leo wakati akihitimisha mafunzo ya kuwajengea uwezo maafisa uvuvi na wakaguzi wa mazao ya uvuvi nchini, Mratibu wa mafunzo hayo, Anold Mbunda amesema ukaguzi madhubuti ni muhimu katika kuhakikisha mazao yanayozalishwa nchini yanakuwa na ubora unaokubalika katika masoko ya ndani na nje ya nchi.
"Kwa sababu mazao yetu ya uvuvi yanauzwa ndani na nje ya nchi na ili upeleke kwenye hizo nchi za wenzetu lazima yaweze kukidhi viwango vya ubora vinavyohitajika katika hizo nchi ambazo tunapeleka mazao yetu," amesema Mbunda
Kwa upande wake Mkuu wa Maabara ya Taifa ya Uvuvi, Dkt. Ofred Mhongole amewataka maafisa walioshiriki mafunzo kutumia ujuzi walioupata katika kuboresha utekelezaji wa majukumu yao na kuhakikisha viwango vya ubora wa mazao ya uvuvi vinalindwa.
Nao baadhi ya washiriki wamesema mafunzo hayo yamewaongezea uelewa kuhusu namna ya kufanya ukaguzi na kutambua changamoto zinazoweza kuathiri ubora wa mazao ya uvuvi.
Mafunzo hayo yamewakutanisha maafisa uvuvi kutoka mikoa ya Mara, Mwanza, Geita na Kagera, huku zaidi ya maafisa 20 wakijengewa uwezo kuhusu ukaguzi na udhibiti wa ubora wa mazao ya uvuvi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri Mkuu Kivuli wa Chama cha ACT Wazalendo, Isihaka Mchinjita, ameeleza kuwa kwa sasa wananchi wa kawaida wanakabiliwa na kupanda kwa gharama za maisha na mfumuko wa bei za bidhaa huku kukiwa hakuna uwiano na mapato yao duni.
Akizungumza na wanahabari leo Jumapili mkoani Dar es Salaam, Mchinjita ameweka wazi kuwa miongoni mwa visababishi vya kupanda kwa gharama hizo ni bei ya nishati ya mafuta akidai kuwa bei hiyo imekuwa chanzo kikubwa cha maumivu ya wananchi tangu mwezi Aprili 2026.
Ameonya kuwa kupanda huku kwa bei ya mafuta kunasababisha athari katika mnyororo kwenye sekta zingine zote, ikiwemo kuongezeka kwa nauli za usafiri, gharama za vyakula, na kila huduma ya kijamii.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri Mkuu Kivuli wa Chama cha ACT Wazalendo, Isihaka Mchinjita, ametoa wito kwa wadau wote wanaopitia ukandamizaji nchini kuungana na kusitiza kuanza mara moja kwa mchakato wa kupata Katiba Mpya ya wananchi, akisisitiza kuwa nchi inahitaji katiba kamili na sio viraka au marekebisho ya muda mfupi.
Akizungumza na wanahabari leo Jumapili mkoani Dar es Salaam, Mchinjita ameweka wazi msimamo wa chama chake kuwa Tanzania ina uwezo wa kupata katiba mpya kabla ya mwaka 2028. Amebainisha kuwa madai ya kwamba muda uliobaki hautoshi kabla ya uchaguzi wa serikali za mitaa sio ya kweli, kwani mchakato wa kuwashirikisha wananchi tayari ulishaanza huko nyuma.
“Kinachotukwaza siyo muda. Kinachotukwaza ni kuwepo kwa watawala ambao hawataki mambo yabadilike,” amesema Mchinjita, akihimiza wananchi kutumia njia zote za kidemokrasia kudai haki hiyo.
Mchinjita amesisitiza kuwa katiba ya wananchi si kwa ajili ya uchaguzi pekee, bali ni msingi wa mabadiliko ya mifumo ya utawala, uchumi, na jamii. Amesema kuwa nchi hivi sasa imekwama, huku mijadala muhimu ya kitaifa kuhusu ukosefu wa ajira kwa vijana na changamoto za wakulima ikikosa masuluhisho ya kudumu.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri Mkuu Kivuli wa Chama cha ACT Wazalendo, Isihaka Mchinjita, amevishambulia vyombo vya ulinzi na usalama nchini kwa kudai kuwa vimeshindwa kuonesha nia thabiti ya kukabiliana na matukio ya utekaji, mauaji, na watu kupotea.
Akizungumza na wanahabari leo Jumapili mkoani Dar es Salaam, Mchinjita amesema kuwa nchi imekuwa ikikabiliwa na wimbi la matukio ya utekaji, mauaji, na kupotea kwa watu bila kujulikana waliko, lakini hakuna taswira yoyote kutoka kwa vyombo vya dola inayoonesha kuwa kuna tatizo kubwa linalopaswa kushughulikiwa kwa dharura.
“Ukirejea ripoti nyingi zinazoonesha kwamba mamia ya Watanzania wamepotea, watu wameuawa lakini huoni ukisikiliza viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama haupati taswira kwamba wanataka kukabiliana na jambo kubwa”, ameeleza Mchinjita ambaye pia Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Bara.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) Septemba 5, 2026 imeongeza nguvu katika ulinzi na usimamizi wa rasilimali za wanyamapori baada ya askari wapya 268 kuhitimu mafunzo ya kijeshi katika Chuo cha Mafunzo ya Jeshi la Uhifadhi Mlele mkoani Katavi.
Askari hao wamehitimu baada ya kukamilisha mafunzo ya miezi sita yaliyowajengea uwezo katika maeneo mbalimbali, ikiwemo matumizi sahihi ya silaha, mfumo wa taarifa za kijiografia (GIS), utimamu wa mwili, nidhamu, haki za binadamu, udhibiti wa wanyamapori wakali na waharibifu pamoja na maadili ya kijeshi.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Mlele, Majid Mwanga amesema Serikali imeendelea kuimarisha Jeshi la Uhifadhi kwa kuongeza nguvu kazi na kuboresha miundombinu mafunzoni.
Kwa upande wake, Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Bodi ya TAWA, Prof. Jafari Kidegesho ameishukuru Serikali chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuiwezesha TAWA kuongeza nguvu kazi, vitendea kazi na kuboresha mazingira ya mafunzo kwa ajili ya kuimarisha uhifadhi.
Naye, Kaimu Kamishna wa Uhifadhi, Mlage Yussuf Kabange amesema kuwa uwezeshaji unaotolewa na Serikali umeendelea kuimarisha shughuli za uhifadhi na utalii. TAWA inajukumu la kuhakikisha rasilimali za wanyamapori na maliasili zinalindwa kikamilifu ili ziendelee kuwa msingi wa shughuli za utalii, uwekezaji na maendeleo ya wananchi.
Kamishna Kabange amewataka askari hao wapya kuwa mstari wa mbele katika kudhibiti ujangili, kulinda mazingira na rasilimali za Taifa, huku akisisitiza umuhimu wa kushirikiana na jamii kwa kutoa elimu ya uhifadhi na kupunguza migogoro kati ya binadamu na wanyamapori ili kuendelea kulinda rasilimali za Taifa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Aliyewahi kuwa Mbunge wa Iringa Mjini na mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Peter Msigwa, amekosoa kitendo cha Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, kuwaita baadhi ya wasanii na watu mashuhuri katika kikao chake kwa tuhuma za makosa ya kijinai akisema hatua hiyo inakwenda kinyume cha sheria.
Msigwa amesema anashangazwa na kitendo hicho, hasa kwa kuzingatia kuwa Waziri Katambi ni mwanasheria kitaaluma, akimtaka kujitathmini na kuhakikisha anaongoza kwa kuzingatia misingi ya sheria.
Msigwa amelinganisha kuwa, wakati Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) anatumia nguvu zake za kisheria kusimamia na kutekeleza sheria, waziri anapaswa kuwa mafuta yanayolainisha mambo. Ameshauri kuwa, kama kulikuwa na changamoto yoyote, Katambi alipaswa kuwasiliana na IGP ili kufuata njia rasmi za kisheria, au kuwaita wasanii hao kirafiki ili kujadiliana nao na kuwashauri kwa ajili ya kujenga amani ya nchi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mbunge mstaafu wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa, amemjia juu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, akitaka atulie na kuacha kutoa matamko na maonyo akidai kuwa maonyo hao yanatengeneneza chuki kwa wananchi.
Msigwa ametoa kauli hiyo akizungumza na Jambo TV, kufuatia hatua ya Katambi kutoa onyo kwa msanii maarufu wa kizazi kipya kutoka Morogoro, Afande Sele, ambaye alikuwa ametoa maoni yake kumtetea msanii mwenzake, Godfrey Tumaini 'Dudubaya'.
Msigwa ameweka wazi kuwa onyo alilopewa msanii Afande Sele kwa kutoa maoni yake ni batili na liko kinyume kabisa cha sheria, akisisitiza kuwa nchi hii ni ya watu huru.
Akifafanua kuhusu utendaji wa Katambi, Msigwa amesema kuwa nchi haiwezi kuendeshwa kwa kiongozi mmoja kujitwika madaraka ya kuwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), mpelelezi, na mahakama kwa wakati mmoja.
Amemtaka kiongozi huyo kuonesha uwezo na kipaji chake cha uongozi kwa kufanya kazi kwa mujibu wa sheria badala ya kile alichokiita kutisha wananchi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kiliumizwa sana na tukio la kuvamiwa na kuchukuliwa kwa aliyekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Humphrey Polepole, huku kikieleza kuwa kinaendelea kufuatilia kwa karibu uchunguzi unaofanywa na vyombo vya ulinzi na usalama.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa, Kenani Kihongosi, wakati akizungumza kwenye mahojiano na mtangazaji Edwin Odemba wa kituo cha Startv.
“Chama Cha Mapinduzi kwanza kilisikitishwa sana na tukio hilo, na pia ndani ya chama tulielekeza vyombo vinavyohusika na masuala ya upelelezi na uchunguzi kulichunguza jambo hili kwa haraka ili kiongozi mwenzetu ajulikane yuko wapi,” alisisitiza Kihongosi huku akiongeza kuwa chama kiliomba mamlaka hizo zifanye kazi yake na hadi sasa zinaendelea nayo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Irene Mziray, mama mzazi wa kijana mwenye umri wa miaka 22, Junior Joyful Jonathan, ameiomba serikali kusaidia katika jitihada za kumpata mwanawe ambaye amepotea na kudaiwa kutekwa na watu wasiojulikana.
Irene amesema mwanawe hana ugomvi na mtu yeyote na familia haijawahi kusikia akiwa na tatizo na mtu mwingine kabla ya kutoweka kwake.
Akizungumza kuhusu mazingira ya tukio hilo, Irene amesema kabla ya Junior kutoweka alikuwa katika mahusiano na msichana ambaye mara kadhaa walikuwa wakigombana na kuachana, kabla ya kurudiana.
Amesema siku ya tukio alipata taarifa kutoka kwa mama mwenye nyumba kwamba wawili hao waligombana na msichana huyo akaondoka, huku baadhi ya vitu vyake, ikiwemo nguo na madaftari yenye jina lake na la baba yake, vikibaki ndani ya nyumba.
Irene amesema baada ya kupata taarifa hizo alifika kwa wazazi wa msichana huyo eneo la Mbweni, Dar es Salaam, na kuwaeleza kuhusu mahusiano ya watoto wao. Amesema pia alifika kituo cha Polisi na kueleza mashaka yake, akimtaja baba na binti yake kuwa miongoni mwa watu anaowashuku kuhusika na kutoweka kwa mwanawe.
Hata hivyo, Irene amesisitiza kuwa hayo ni mashaka yake na kwamba anaiomba Polisi kuyafanyia uchunguzi.
Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Salim Morcase amethibitisha kuwa taarifa ya tukio hilo ilipokelewa na polisi na kwamba uchunguzi umeanza kufanyika. Kamanda Morcase amesema Polisi hufanyia kazi taarifa zinazowasilishwa na huchukua hatua za kisheria pale uchunguzi unapobaini kuwepo kwa kosa.
Wakati huohuo, familia imeendelea kuomba msaada wa Serikali, viongozi na wananchi katika kumpata Junior Joyful Jonathan, huku ikieleza kuwa yeyote mwenye taarifa kuhusu alipo awasiliane na vyombo vya dola au kuwatafuta kwa mawasiliano ya simu.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Wananchi wa Mkuranga mkoani Pwani wanatarajia kupata ahueni kubwa ya maisha baada ya Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Ardhini (LATRA) kutangaza ruti mpya za usafiri wa mabasi kuiunganisha na jiji la Dar es Salaam.
Kwa sasa, wananchi wa Mkuranga walikuwa wakilazimika kutumia usafiri wa bodaboda na bajaji kwa gharama ya mpaka shilingi 20,000, lakini ruti hizi mpya zitapunguza gharama hizi.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mbunge wa Mkuranga ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega, ameishukuru LATRA kwa hatua hiyo aliyoiita ni ukombozi kwa wana Mkuranga na Dar es Salaam kwa jumla.
Amesema gharama kubwa za usafiri ni miongoni mwa sababu za kupanda kwa gharama za maisha na anaamini hatua hii itasaidia kurahisisha safari, kupunguza gharama na ukali wa maisha.
“Mkuranga ni mojawapo ya maeneo yenye ongezeko kubwa la watu. Kuna viwanda vingi ambavyo waajiriwa wake wanatoka sio Mkuranga peke yake bali maeneo tofauti ya Dar es Salaam. Ruti hizi mpya zitakuwa na faida kwa wa Mkuranga na wengine,” amesema.
Waziri huyo alitumia nafasi hiyo pia kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa Ujenzi wa barabara ambazo hazikuwepo awali za kuunganisha Mkuranga na maeneo ziliko ruti mpya.
“Hii yote isingewezekana bila kuwepo kwa barabara ambazo hazikuwepo kabla Rais Samia hajaingia madarakani. Ujenzi wa hizi barabara kwenye Urais wake ndiyo umefanya ruti hizi ziwezekane. Tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais,” alisema.
Kwa mujibu wa mbunge huyo, ruti hizo mpya zitahusu usafiri kutoka Mkuranga kwenda katika maeneo 10 tofauti ya Mkoa wa Dar es Salaam kama vile Mipeko, Mbande, Tandika na Chambani.
Hatua ya LATRA imetokana na ombi la Ulega alilofikisha kwao kama mbunge kutokana na mahitaji ya Mkuranga ambayo inakua kwa kasi kwa idadi ya watu na mji wenyewe.
Pamoja na ukuaji huo, bado kumekuwa na changamoto ya usafiri, huku wananchi katika baadhi ya maeneo wakilazimika kutumia pikipiki za bodaboda kusafiri kutoka vijijini kwenda mijini kwa gharama kubwa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI PICHA:
Waziri wa Viwanda na Biashara na Mbunge wa Mbinga Vijijini, Judith Salvio Kapinga, ameishirikisha Wizara ya Madini changamoto zinazowakabili wananchi wanaoathiriwa na shughuli za uchimbaji wa makaa ya mawe mkoani Ruvuma.
Kapinga amewasilisha changamoto hizo katika kikao na Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, Septemba 4, 2026, jijini Dodoma, akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Mbinga, Kisare Makori, pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga, Joseph Kashushura.
Katika kikao hicho, viongozi hao waliwasilisha kero mbalimbali zinazowakabili wananchi, ikiwemo kuchelewa kwa ulipaji wa fidia kwa wananchi wanaoathiriwa na shughuli za uchimbaji, kutotekelezwa kwa wakati kwa Wajibu wa Kampuni kwa Jamii (CSR), pamoja na baadhi ya kampuni kutotekeleza wajibu wao katika maeneo wanayofanyia shughuli.
Kapinga amesema changamoto hizo zimekuwa na athari kwa maisha ya wananchi, ikiwemo upatikanaji wa huduma za maji, barabara na afya, hivyo kuiomba Wizara ya Madini kuchukua hatua kuhakikisha kampuni za uchimbaji zinatimiza wajibu wao kwa jamii.
Akijibu hoja hizo, Mavunde ameahidi kuwa Wizara yake itashughulikia changamoto hizo ndani ya mwezi mmoja. Aidha, ameiagiza Tume ya Madini kufika mkoani Ruvuma na kukutana na wamiliki wa migodi pamoja na wananchi ili kutafuta suluhu ya changamoto hizo na kuhakikisha masuala yanayohusiana na shughuli za uchimbaji yanapatiwa ufumbuzi.
Kwa upande wao, Mkuu wa Wilaya ya Mbinga, Kisare Makori, na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga, Joseph Kashushura, wamependekeza kuwekwa kwa mikakati madhubuti ya ukusanyaji wa madeni ya mapato yanayokadiriwa kufikia takribani asilimia 70. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Mabala Mlolwa, amewataka wanachama wa chama hicho kupuuza kile alichokiita upotoshaji unaofanywa na baadhi ya wanaharakati kupitia mitandao ya kijamii, akimtaja mwanaharakati Mange Kimambi.
Amesema baadhi ya taarifa zinazosambazwa na wanaharakati kuhusu maamuzi yaliyofikiwa na vikao vya CCM zinaweza kuwachanganya wanachama na kuleta taswira kwamba chama hicho kimegawanyika.
Akizungumza na wanachama wa CCM wakiwemo madiwani, mabalozi na makatibu katika Wilaya ya Shinyanga Vijijini, Mlolwa amesema maamuzi yaliyofikiwa kuhusu masuala ya ndani ya chama yalizingatia katiba, kanuni na taratibu za CCM.
Amemtaja Mange Kimambi akidai kuwa yeye ni miongoni mwa wanaohusika katika kusambaza taarifa zinazopotosha kuhusu hali ya ndani ya CCM.
Kauli hiyo imekuja wakati kukiwa na mjadala katika mitandao ya kijamii kuhusu maamuzi yaliyofikiwa na CCM dhidi ya aliyekuwa Makamu wa Rais na mwanachama wa chama hicho Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Kheri James ameitaka Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Iringa kuhakikisha matengenezo ya daraja la Ipogolo kwenye barabara ya Iringa–Mbeya yanafanyika kwa haraka ili kuondoa changamoto ya eneo hilo kujaa maji wakati wa mvua.
Kheri James ametoa maagizo hayo mapema leo hii Septemba 4,2026 alipotembelea kuangalia maendeleo ya ujenzi wa mradi huo.
Kwa upande wake Kaimu Meneja wa TANROADS Mkoa wa Iringa, Mhandisi Mwanaisha Rajabu, amesema eneo hilo limekuwa likipata changamoto ya maji, hivyo limefungwa kwa muda kupisha maboresho yatakayosaidia kutatua tatizo hilo kabla ya msimu wa mvua kuanza.
Mhandisi Rajabu amesema matengenezo hayo yanatarajiwa kuchukua miezi miwili, huku Mhandisi wa TANROADS Mkoa wa Iringa, Alex Mgongolwa, akieleza kuwa watumiaji watatumia barabara mbadala wakati kazi hizo zikiendelea.
Barabara hiyo ya TANZAM ni muhimu kwa magari ya ndani na nje ya nchi pamoja na wakazi wa Iringa wanaoitumia kuingia na kutoka katikati ya mji, kwa sasa watembea kwa miguu, bajaji na bodaboda wameanza kutumia njia ndogo za mkato kupunguza umbali wa safari.
Wananchi wa Iringa wamesema wanatarajia matengenezo hayo yatakamilika kwa wakati na kuondoa kabisa changamoto ya kujaa maji katika eneo hilo, hasa wakati wa msimu wa mvua.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imewataka vijana kutumia fursa zinazotokana na ukuaji wa sekta mbalimbali za uchumi kwa kuongeza ujuzi unaohitajika katika soko la ajira.
Mkurugenzi Mkuu wa VETA, CPA Anthony Kasore, amesema sekta za ujenzi, madini, viwanda, kilimo, nishati, utalii na TEHAMA zimeendelea kufungua nafasi nyingi za ajira na kujiajiri, lakini upatikanaji wa wataalamu wenye ujuzi wa vitendo bado ni changamoto.
Kasore ameyasema hayo jijini Dodoma Septemba 4, 2026, wakati akieleza utekelezaji wa mipango ya VETA kwa mwaka wa fedha 2025/26 pamoja na mwelekeo wa mwaka 2026/27.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Serikali ya Tanzania imetoa agizo thabiti kwa Wizara ya Uchukuzi, Shirika la Reli Tanzania (TRC), na wakandarasi kuweka mikakati mahususi na kupambana usiku na mchana ili kuhakikisha ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) katika vipande vyote unakamilika kwa kasi.
Agizo hilo limetolewa leo Ijumaa, Septemba 4, 2026, bungeni jijini Dodoma na Waziri Mkuu wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, wakati akiwasilisha hoja ya kuahirisha Bunge la 13, Mkutano wa Nne. Dkt. Mwigulu ameeleza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, wakati akilihutubia Bunge, alibainisha wazi dhamira yake ya dhati ya kukamilisha miradi yote ya kimkakati nchini.
“Naziagiza Wizara ya Fedha na Wizara ya Uchukuzi, zikishirikiana na Shirika la Reli, wakandarasi waliopewa kazi ya kujenga vipande hivi vya miradi ya Reli ya Kisasa (SGR) pamoja na wale waliopewa jukumu la kuhamasisha fedha za miradi hiyo, kupambana usiku na mchana”, ameeleza.
Dkt. Mwigulu amefafanua kuwa dhamira ya Rais Samia imedhihirishwa kwa vitendo kupitia falsafa yake ya “continuity and change” (mwendelezo na mabadiliko) ambapo falsafa hii imeshuhudia kukamilika kwa baadhi ya miradi mikubwa ya kielelezo nchini, ikiwemo mradi wa Bwawa la kuzalisha umeme la Mwalimu Julius Nyerere.
Amesema chini ya falsafa hiyo hiyo, serikali imejikita katika kukamilisha ujenzi wa miradi ya kielelezo kama reli ya SGR kwa vipande vyote, huku mfano wa karibuni ukiwa ni uzinduzi wa kipande cha kutoka Tabora hadi Kigoma uliofanywa na Rais Samia.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Dodoma imeitaka CCM kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya viongozi wastaafu wanaokiuka sheria, kanuni, taratibu na miiko ya chama hicho, ikiwemo kuwafukuza uanachama pale inapobainika wamekiuka masharti hayo.
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Dodoma, Abdulhabib Mwanyemba, wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za jumuiya hiyo jijini Dodoma.
Amesema hatua hizo ni muhimu katika kulinda nidhamu, mshikamano na heshima ya chama, huku akisisitiza kuwa kila mwanachama anapaswa kuwajibika kwa mujibu wa sheria na kanuni za CCM bila kujali nafasi aliyowahi kushikilia.
Katika hatua nyingine, Mwenyekiti huyo amewataka vijana kuwa wavumilivu katika masuala ya kisiasa, kuendelea kukiunga mkono Chama Cha Mapinduzi na kulinda uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa uzalendo na mshikamano.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Serikali mkoani Tanga inatarajia kugawa jumla ya vyandarua 1,561,925 kwa wananchi ili kuimarisha mapambano dhidi ya ugonjwa wa malaria na kujikinga na maambukizi mapya.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo, Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Dadi Kolimba, amezitaja halmashauri tisa zinazokwenda kunufaika na zoezi hilo kuwa ni Handeni DC, Handeni TC, Kilindi, Korogwe DC, Korogwe TC, Mkinga, Muheza, Pangani, pamoja na Jiji la Tanga.
Akiangazia mchakato wa usambazaji, Mkurugenzi wa Ugavi na Uendeshaji wa Bohari ya Dawa (MSD), Hassan Ali, amebainisha kuwa mfumo imara wa vifaa na usafirishaji (logistics) umeandaliwa ili kuhakikisha vyandarua hivyo vinawafikia walengwa katika maeneo yote bila vikwazo.
Wananchi waliojitokeza katika uzinduzi huo, wakiwemo Mohamedi Kassim na Rukia Mbega, wameipongeza Serikali kwa hatua hiyo huku wakitoa wito kwa wakazi wenzao kutumia vyandarua hivyo kwa malengo yaliyokusudiwa badala ya kuvitelekeza au kuvitumia sivyo.
Kwa mujibu wa takwimu za kitaifa za viashiria vya malaria kwa watoto wa shule za msingi za mwaka 2025, Mkoa wa Tanga unashika nafasi ya 11 nchini ukiwa na kiwango cha maambukizi cha asilimia 3.9, kiwango ambacho kiko chini ya wastani wa kitaifa wa asilimia 5.5.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mfanyabiashara Luqman Issac maarufu kama Luqman Albusayyid, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la usafirishaji haramu wa binadamu.
Albusayyid ambaye ni mkazi wa Ilala, Mshirazi, alifikishwa mahakamani hapo leo Septemba 4, 2026, na kusomewa mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Bilal Ahmed.
Akisomewa mashtaka hayo na wakili wa serikali Godfrey Olugwey ilidaiwa, katika tarehe isiyofahamika kati ya Julai mosi hadi 29, 2026, eneo la Magomeni Fundikila, Wilaya ya Kinondoni Dar es Salaam, alimsafirisha mwanaume mtu mzima kwenda nje ya nchi kwa ajili ya unyanyasaji wa kingono.
Katika shtaka la pili, wakili huyo wa serikali alidai, Agosti 4, 2026 eneo la Msimbazi Center, Mivinjeni, Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam, mshtakiwa huyo alitumia laini ya simu yenye jila la mtu mwingine, Nadil Hassan, bila kumjulisha mtoa huduma.
Katika shtaka la tatu, ilidaiwa katika tarehe isiyofahamika Machi mwaka 2025, eneo la Msimbazi, Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam, mshtakiwa huyo alijipatia kitambulisho cha kupigia kura kutoka kwa afisa usajili, baada ya kutoa maelezo ya uongo kuwa yeye ni raia wa Tanzania akijua si kweli.
Baada ya kusomwa mashtaka hayo, mshtakiwa huyo alikana. Upande wa jamhuri ulidai, haujakamilisha upelelezi hivyo kesi iliahirishwa hadi Septemba 17 mwaka huu kwa ajili ya kutajwa. Mshtakiwa huyo alipelekwa mahabusu kwasababu shtaka la usafirishaji haramu wa binadamu halina dhamana.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Serikali ya Tanzania imetoa agizo zito kwa Kamati za Maafa katika ngazi zote kuanzia ngazi ya vijiji, mikoa, hadi taifa kujipanga kikamilifu na kuchukua hatua za dharura kukabiliana na changamoto zinazoweza kusababishwa na mvua kubwa za El Niño zinazotarajiwa kuanza katika wiki ya nne ya Septemba na wiki ya kwanza ya Oktoba 2026.
Wito huo umetolewa bungeni jijini Dodoma leo Ijumaa, Septemba 4, 2026, na Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, wakati akiwasilisha hoja ya kuahirisha Bunge la 13, Mkutano wa Nne, ambapo amewataka viongozi na watendaji wa maeneo yote hatarishi kuanza maandalizi mapema ili kuzuia na kupunguza maafa yanayoweza kujitokeza.
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa utabiri wa mwelekeo wa mvua za msimu wa vuli kwa mwaka 2026, unaoonesha uwepo wa hali ya El Niño itakayoambatana na mvua kubwa kuanzia mwishoni mwa Septemba, na kuendelea Oktoba hadi Desemba. Mvua hizo zinatarajiwa kuwa za juu ya wastani hadi wastani katika maeneo mengi ya ukanda wa pwani ya kaskazini, nyanda za juu kaskazini mashariki, ukanda wa Ziwa Victoria, pamoja na kaskazini mwa mkoa wa Kigoma
Serikali imetahadharisha kuwa vipindi vya mvua hizi kubwa vinaweza kuambatana na mafuriko na kusababisha madhara makubwa ya kiafya, kijamii, kiuchumi, uharibifu wa miundombinu, na upotevu wa mali za wananchi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Msanii wa muziki nchini, Godfrey Tumaini, maarufu kama Dudubaya, amejibu agizo la kukamatwa kwake lililotolewa na Serikali kwa kutangaza kuwa anaenda kujisalimisha mwenyewe katika Kituo Kikuu cha Polisi (Central Police Station) jijini Dar es Salaam
Hatua hiyo ya Dudubaya inakuja muda mfupi baada ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, kuzungumza na wanahabari leo Ijumaa, Septemba 4, 2026, na kuliagiza Jeshi la Polisi nchini kumtafuta na kumfikisha mbele ya vyombo vya sheria msanii huyo kwa madai ya kukaidi wito wa serikali.
Waziri Katambi alieleza kuwa Dudubaya alitakiwa kufika wizarani kujibu tuhuma za makosa ya jinai yanayomkabili lakini alishindwa kufanya hivyo kwa mara ya pili, na badala yake akaonekana kwenye mitandao ya kijamii akitoa kauli za kukaidi mamlaka.
Kupitia video aliyoichapisha kwenye ukurasa wake rasmi wa mtandao wa kijamii wa Instagram mara baada ya kupokea taarifa za kusakwa kwake, Dudubaya amekiri kulipata tamko la Waziri Katambi lililoagiza akamatwe
Hata hivyo, msanii huyo ameweka wazi kuwa yeye si mtu wa kukimbia mkono wa sheria. Amefafanua kuwa amekuwa na urafiki wa karibu na wa muda mrefu na Jeshi la Polisi tangu alipoanza tasnia ya muziki, akibainisha kuwa mwanamuziki yeyote hawezi kufanya tamasha la hadhara bila kupata ulinzi thabiti wa askari polisi.
“Mimi ni Mtanzania. Mimi siwezi kukimbia polisi,” amesema Dudubaya katika video hiyo akisisitiza uzalendo wakeThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwananchi wa Kijiji cha Lembapuli, Kata ya Loolera wilayani Kiteto mkoani Manyara, Saitabahu Mirakwa anadaiwa kumshambulia kwa fimbo Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Lembapuli baada ya kutoridhishwa na hatua ya mwalimu huyo kumuadhibu mtoto wake wa kiume anayesoma Darasa la Tatu.
Akizungumza na wananchi wa Lembapuli katika mkutano wa hadhara, Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Remidius Mwema ameagiza Serikali ya Kijiji kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi kuhakikisha mtuhumiwa anapatikana.
Mwema amesema atachukua hatua dhidi ya Kamati ya Usalama ya Serikali ya Kijiji endapo itabainika kuwa baadhi ya viongozi walihusika katika kumficha au kumtorosha mtuhumiwa huyo huku akieleza kuwa hakuna mtu aliye juu ya sheria na kwamba vitendo vya kuwashambulia walimu vinaweza kuwavunja moyo katika kutekeleza majukumu yao.
Kwa upande wao, Wazee wa Kimila (Malaigwenani) kutoka Kijiji cha Lembapuli wameahidi kushirikiana na Jeshi la Polisi kuhakikisha mtuhumiwa huyo anapatikana na kuchukuliwa hatua za kisheria. Wamesema wananchi wanapaswa kufuata taratibu na sheria badala ya kujichukulia sheria mkononi.
Aidha Diwani wa Kata ya Loolera, Sokoine Edward Oltus, amelaani tukio hilo na kuahidi kushirikiana na wananchi pamoja na vyombo vya dola kuhakikisha mtuhumiwa anapatikana ili sheria ichukue mkondo wake.
Katika hatua nyingine baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano huo wamemshukuru Mkuu wa Wilaya ya Kiteto kwa kuchukua hatua ya kukemea tukio hilo na kusisitiza umuhimu wa kuheshimu sheria, huku wakitoa wito kwa viongozi kuchukua hatua za haraka dhidi ya vitendo vinavyokiuka sheria na kuhatarisha usalama wa jamii.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, amesema kuanzisha makundi yenye sura ya kufanya kazi za ulinzi na usalama bila kutambuliwa na mamlaka ni kinyume cha sheria.
Katambi ameeleza hayo akizungumza na wanahabari leo mara baada ya mkutano uliomhusisha Sheikh Said Mwaipopo aliyekiri kuwa na kundi la Chui Mweusi na Mbwa Mwitu, akieleza kuwa makundi hayo yaliundwa kutokana na dhamira ya kukabiliana na watu waliokuwa wakipanga kuandamana
Waziri Katambi amesema Mwaipopo ameeleza kuwa alichukua hatua hiyo kutokana na uchungu aliokuwa nao kama Mtanzania kufuatia matukio yaliyotokea Oktoba 29,2025 lakini amesisitiza kuwa jukumu la kulinda usalama wa nchi na kuchukua hatua dhidi ya wanaokiuka sheria ni la vyombo vya ulinzi na usalama pekee.
Katambi amesema katika ufuatiliaji uliofanyika, hakuna rekodi iliyoonesha kuwa Mwaipopo au kundi lake walijeruhi au kumdhuru mtu, na kwamba Mwaipopo alieleza kuwa alikuwa na nia njema.
Hata hivyo, Waziri amesema nia njema haiwezi kuhalalisha njia isiyo sahihi, hivyo amemtaka Mwaipopo na makundi mengine yenye nia ya kushiriki katika masuala ya ulinzi na usalama kufanya hivyo kwa kufuata utaratibu unaotambuliwa na Jeshi la Polisi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, ameliagiza Jeshi la Polisi kumtafuta na kumfikisha mbele ya vyombo vya sheria msanii Godfrey Tumaini maarufu Dudubaya, baada ya kushindwa kuitikia wito wa Wizara hiyo.
Akizungumza na wanahabari leo Ijumaa, Katambi amesema Dudubaya alikuwa ametakiwa kufika Wizara ya Mambo ya Ndani baada ya kutajwa katika tuhuma za makosa ya jinai, lakini licha ya kuitwa kwa mara ya pili, bado hakufika.
Waziri amesema Dudubaya ameonekana kwenye mitandao ya kijamii akitoa kauli ambayo Waziri ameielezea kuwa ni kukaidi wito wa Serikali.
Kutokana na hali hiyo, Katambi ameliagiza Jeshi la Polisi kuhakikisha Dudubaya anapatikana kokote aliko na kufikishwa mbele ya Jeshi hilo ili achukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Leo Septemba 4, 2026, katika Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, zoezi la Jamhuri kuuliza maswali ya dodoso kwa shahidi wa tatu wa upande wa utetezi, ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, Amani Golugwa, katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu, limeanza.
Katika mchakato huo, Wakili wa Serikali, alianza kwa kumkumbusha shahidi kuwa maswali ya dodoso ni utaratibu wa kisheria na si uadui, ambapo Golugwa alijibu kuwa wapo mawakili wenye roho mbaya. Shahidi alikiri pia kufahamu kuwa mahakama si uwanja wa siasa na kwamba kesi ya jinai inategemea ushahidi, huku akibainisha kuwa baadhi ya taarifa zake zipo kwenye maeneo ya wazi akisema (Public domain).
Kuhusu uongozi na miundo ya chama, Golugwa alieleza kuwa nafasi yake na ile ya Katibu Mkuu, John Mnyika, huteuliwa na Mwenyekiti Tundu Lissu kwa mujibu wa Katiba ya CHADEMA. Alikiri kuwa mjumbe wa Kamati Kuu tangu Januari 22, 2025, na ndiye aliyetangaza maazimio ya hivi karibuni yaliyowaelekeza viongozi wakuu akiwemo yeye kuweka nguvu zao "kumtetea kwa nguvu zote" mwenyekiti wao.
Hata hivyo, mzozo ulitokea mahakamani kuhusu tafsiri ya katiba ya chama na aina za vikao, ambapo baada ya kutakiwa kusoma vipengele husika, shahidi alikiri kuwa majibu yake yalitofautiana na maandishi ya katiba, ingawa alikanusha madai ya kutoijua katiba hiyo.
Upande wa mashtaka ulihoji pia kuhusu ushiriki wa chama katika chaguzi mbalimbali, ambapo Golugwa alieleza kuwa CHADEMA ilishiriki uchaguzi wa 2015 na kupata wabunge, lakini hakugombea nafasi yoyote mwaka 2020. Ameongeza kuwa hakugombea pia katika chaguzi za 2024 na 2025 kutokana na msimamo wa chama chao wa kutoshiriki uchaguzi wa 2025 bila mabadiliko ya mifumo.
Alipoulizwa kuhusu wadhifa wake wa zamani wa Katibu wa Kanda ya Kaskazini, alikiri kuandaa taarifa kali kupinga ushiriki wa chama ili kushinikiza mabadiliko serikalini. Amethibitisha kuwa Mwenyekiti Mbowe alitoa tamko la kutokushiriki katika uchaguzi lakini alikanusha kuwa mwenyekiti huyo alitishia "kuuvuruga uchaguzi" au "kukinukisha".
Aidha, amekiri kuwa kuna haki ya kikatiba ya kushiriki au kutoshiriki uchaguzi, na si sahihi kumlazimisha au kumzuia mtu kufanya hiyo. Mbali na hayo, Golugwa alikiri kuwa hana uelewa mkubwa wa sheria, ingawa huwa anazisoma.
Alipoulizwa kuhusu ripoti za waangalizi wa uchaguzi wa 2025 zilizoandikwa kwa Kiingereza, alikiri kuwa yeye si mwandishi wa ripoti hizo na hajawahi kuitwa kuzitafsiri, licha ya kuzirejelea mahakamani kwa Kiswahili. Akijibu kuhusu ripoti za kimataifa za Jumuiya ya Madola, Thabo Mbeki Foundation, na SADC, amesema hana imani nazo kwa ujumla wake isipokuwa maeneo machache yanayoendana na uhalisia wa yaliyotokea Oktoba 29, 2025.
Kuhusu takwimu za matokeo ya uchaguzi wa uchaguzi wa 2025, shahidi awali alidai mshindi alipata asilimia 98.6 na wengine kugawana 2.4, lakini Wakili Katuga alimthibitishia kuwa alitoa takwimu za uongo mbele ya mahakama, na shahidi mwenyewe akakiri hilo.
Sehemu ya dodoso imegusia matukio ya uhalifu wakati wa maandamano ya oktoba 29, 2025, Golugwa amekiri kuwa kuchoma mali za umma, kukata vidole vya waliopiga kura, na kuua askari polisi ni vitendo vya uhalifu mkubwa. Pamoja na kukiri hayo, alifafanua kuwa yeye binafsi hakuwa na taarifa yoyote ya matukio hayo ya uhalifu yaliyotokea tarehe 29 Oktoba 2025, huku akikanusha kabisa kushiriki au kupanga maandamano yaliyosababisha vurugu hizo.
Kutokana na muda wa mapumziko kuwa tayari umewadia, mshtakiwa Tundu Lissu aliwaomba majaji kukumbusha kuwa mawakili wa serikali huenda wamejisahau kama muda wa kupunzika umefika hatua ambayo ilikubwaliwa na pande zote. Majaji wakaahirisha kesi kwa muda wa saa moja na nusu na kutangaza kuwa ingerejea te saa nane na nusu mchana ili kuendelea na zoezi la dodosoThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Kampuni ya Taifa Group imetoa tahadhari kwa umma ikionya dhidi ya mpango mkubwa wa utapeli wa uwekezaji unaosambazwa kwenye mitandao ya kijamii ukitumia jina la ‘TaifaAI’ na utambulisho wa mfanyabiashara, Rostam Azizi.
Kupitia taarifa maalum kwa umma iliyotolewa tarehe 4 Septemba, 2026, kampuni hiyo imeweka wazi kuwa jukwaa hilo linalojiita "TaifaAI" ni la kitapeli na halina uhusiano wowote nao au na Rostam Azizi.
Taifa Group imeeleza kuwa matangazo na maudhui yanayohusu mpango huo yamekuwa yakisambazwa kwa kasi kupitia mitandao ya kijamii kama vile Facebook na Instagram yakitumia udanganyifu wa jina, picha, na utambulisho wa Rostam Azizi pamoja na nembo ya Taifa Group ili kuaminisha umma uwepo wa jukwaa la uwekezaji linalotumia teknolojia ya Akili Unde (Artificial Intelligence - AI)
Mpango huo wa kitapeli unalenga kushawishi wananchi kujiunga kwa kuahidi faida kubwa sana za kifedha zisizo za kawaida. Aidha, Taifa Group imefafanua kuwa nukuu na taarifa zote zinazodaiwa kurejea kauli za Bw. Rostam Azizi katika matangazo hayo zimetengenezwa kwa uongo na zina nia ovu ya kupotosha umma
Katika taarifa hiyo, kampuni imetoa mwongozo kwa wananchi ili kujilinda dhidi ya kupoteza rasilimali zao, ikihimiza wananchi kutojiandikisha kabisa katika jukwaa hilo la utapeli, kutotoa taarifa zao binafsi, za kibenki, au za kifedha kwa mtu yeyote, kutotuma wala kuweka fedha zozote kwenye akaunti zinazohusishwa na jukwaa hilo na kuepuka mawasiliano au kufanya miamala na mtu yeyote anayedai kuiwakilisha "TaifaAI" au Taifa Group kuhusiana na mpango huo.
Taifa Group imesisitiza kuwa Rostam Azizi hatumii kamwe jina lake au nafasi yake ya kijamii na kibiashara kuhamasisha wananchi kujiunga na miradi ya uwekezaji mtandaoni, mifumo ya biashara ya kidijitali, au mipango yoyote inayowaahidi wananchi kupata faida za haraka za kifedha
“Taifa Group inachukua hatua stahiki kutoa taarifa kuhusu maudhui haya ya kitapeli kwa mamlaka husika pamoja na watoa huduma wa majukwaa ambako maudhui hayo yanasambazwa. Tunawasihi wananchi kuwa waangalifu na kusambaza tahadhari hii kwa wengine, hususan kwa mtu yeyote ambaye amepokea au kuona tangazo hili la kitapeli. Taifa Group haitawajibika kwa hasara yoyote itakayotokana na mtu kujihusisha na mpango huu wa kitapeli”, imeeleza taarifa hiyo.
Kwa taarifa rasmi kuhusu Taifa Group na shughuli zake, wananchi wameshauriwa kutegemea taarifa zinazotolewa kupitia njia rasmi za mawasiliano za Taifa Group pekee. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Imani ya mataifa jirani yanayozunguka Tanzania kutumia huduma zinazotolewa na Bandari ya Dar es Salaam imeendelea kuimarika kwa kasi, baada ya kurekodiwa kwa ongezeko kubwa la shehena inayopitishwa kwenda katika nchi hizo.
Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam, Abed Gallus Abed, ameyabainisha hayo Alhamisi, Septemba 3, 2026, alipokuwa akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari wakati wa ziara maalum ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa matanki ya kuhifadhia mafuta katika bandari hiyo.
Abed ameeleza kuwa, katika jumla ya tani milioni 33.7 za shehena zilizohudumiwa na Bandari ya Dar es Salaam mwaka jana, takriban tani milioni 14.7 zilikuwa ni shehena zilizokuwa zikielekezwa katika nchi jirani zisizo na bandari. Kiwango hiki kinawakilisha hatua kubwa ya ukuaji ikilinganishwa na mwaka wa fedha wa 2024/25, ambapo shehena iliyosafirishwa kwenda nchi jirani ilikuwa ni tani milioni 12.6
Mkurugenzi huyo amesisitiza kuwa ukuaji huo wa shehena ni kielelezo tosha cha imani kubwa ambayo mataifa yanayozunguka nchi ya Tanzania wanayo dhidi ya huduma zinazotolewa katika Bandari ya Dar es Salaam, jambo linalowafanya waendelee kupitisha mizigo yao hapa.
Katika hatua nyingine, Abed amegusia mwelekeo wa soko la madini katika nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), akieleza kuwa kumekuwa na ongezeko kubwa sana la shughuli za uchimbaji wa madini nchini humo. Kutokana na uwekezaji huo wa kimkakati, mamlaka ya bandari inatarajia kushuhudia ongezeko kubwa zaidi la usafirishaji wa madini ya shaba (kopa) kwenda nje ya nchi kupitia Bandari ya Dar es Salaam katika siku za usoni.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Sheikh Said Mwaipopo kile alichokuwa akikiita kikosi chake hatari cha 'Chui weusi' hawakuwa askari wala hakutumwa na serikali bali walikuwa ni raia na aliyokuwa anayafanya alifanya kwa ajili ya uzalendo
Amesema hayo leo Septemba 4, 2026 mara baada ya kukaa kikao alichoitwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Patrobas Katambi huku akiomba msamaha kwa yale ambayo amekosea.
Hata hivyo amesisitiza kuwa ataendelea kuwa mzalendo kwa nchi yake.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Sheikh Said Mwaipopo kile alichokuwa akikiita kikosi chake hatari cha 'Chui weusi' hawakuwa askari wala hakutumwa na serikali bali walikuwa ni raia na aliyokuwa anayafanya alifanya kwa ajili ya uzalendo
Amesema hayo leo Septemba 4, 2026 mara baada ya kukaa kikao alichoitwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Patrobas Katambi huku akiomba msamaha kwa yale ambayo amekosea.
Hata hivyo amesisitiza kuwa ataendelea kuwa mzalendo kwa nchi yake.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mama na mtoto wake mwenye umri wa miaka mitatu wamefariki dunia baada ya nyumba waliyokuwa wakiishi kuteketea kwa moto wakati wakiwa ndani, huku chanzo cha moto huo kikitajwa kuwa bado hakijafahamika.
Tukio hilo limetokea jana majira ya saa 9 mchana katika Mtaa wa Kizota, Jijini Dodoma, ambapo mume wa marehemu na baba wa mtoto, Joshua Mawona, amesema alipigiwa simu na kupewa taarifa kuwa nyumba yake ilikuwa ikiteketea kwa moto. Alipofika eneo la tukio, alikuta moto mkubwa ukiwaka katika nyumba hiyo na kusababisha vifo vya familia yake.
Mashuhuda wa tukio hilo wamesema marehemu alikuwa amelala ndani ya nyumba hiyo kabla ya kusikia kelele na kutoka nje, lakini baada ya kuona moto ukiwaka katika dirisha, alirejea ndani kumfuata mtoto wake aliyekuwa bado amelala. Inadaiwa wakati akijaribu kutoka, mlango ulijifunga huku moto ukiwa umeenea, na hivyo kushindwa kutoka pamoja na mtoto wake hadi walipopoteza maisha.
Aidha Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Dodoma, Mrakibu (SF) Rehema Menda, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema uchunguzi wa kubaini chanzo cha moto bado unaendelea, huku akiwataka wananchi kutoa taarifa haraka pindi wanapobaini kutokea kwa majanga ya moto ili hatua za uokoaji zichukuliwe kwa wakati.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Mhariri, Mwandishi wa habari mahiri na Mtangazaji wa Millardayo, Bakari Chijumba (@BecaTZA ) ameweka rekodi ya aina yake kwa kuchaguliwa kuwania vipengele sita tofauti kwenye msimu wa pili wa Samia Kalamu Awards 2026.
Tuzo hizo zilizoandaliwa na TCRA na TAMWA ni za habari za maendeleo zinazolenga kutambua, kuthamini na kuhamasisha uzalishaji wa maudhui ya ndani yenye ubora ambapo majina ya waliochujwa na jopo la Majaji na kuchaguliwa kwenye vipengele mbalimbali yametangazwa jana na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Peter Mwasalyanda na Mkurugenzi Mkuu wa TAMWA, Dkt. Rose Reuben.
Vipengele ambavyo Chijumba amechaguliwa kupigiwa kura ni Sekta ya Ardhi na Makazi, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Kazi na Ajira, Uchukuzi, Ujenzi na Usalama wa Raia.
Kumpigia kura Bakari Chijumba tembelea www.samiaawards.tz kisha nenda kwenye kundi la tuzo chagua tuzo za kisekta kisha chagua category hizo 6 na ukiona jina na picha yake bonyeza kitufye cha piga kura Au tuma SMS yenye neno SKA ikifuatiwa na namba yake yoyote ya ushiriki kati ya namba sita ambazo ni 260203, 260104, 260124, 260196, 260249, 260135 kisha tuma kwenda namba 15200, au mpigie kupitia link www.samiaawards.tz/mshiriki/260203 , www.samiaawards.tz/mshiriki/260104 , www.samiaawards.tz/mshiriki/260196 .. unaweza kumpigia kura kila baada ya saa 24. -
Jambo TV
@Jambotv_
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Rhimo Nyansaho, amezindua rasmi Jengo la Ramani la Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) lililopo katika Mji wa Serikali, Mtumba, jijini Dodoma.
Akizungumza Septemba 3, 2026, katika hafla ya uzinduzi wa jengo hilo ambalo ni sehemu ya miundombinu ya kimkakati ya ulinzi, Dkt. Nyansaho amelipongeza JWTZ kwa kukamilisha mradi huo kwa viwango vya juu na kuweka vifaa pamoja na teknolojia za kisasa zitakazowezesha utoaji wa huduma kwa ufanisi na weledi mkubwa.
Waziri Nyansaho amebainisha kuwa kukamilika kwa jengo hilo ni kielelezo tosha cha dhamira ya dhati ya Serikali ya Awamu ya Sita ya kuendelea kuliwezesha JWTZ kiutendaji na kimiundombinu, ili kutekeleza majukumu yake ya msingi ya kulinda mipaka, mamlaka, na usalama wa nchi. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Halmashauri ya Wilaya ya Karatu mkoani Arusha imepanga kuongeza kiasi cha fedha kinachotengwa kwa ajili ya mikopo ya asilimia 10 kwa makundi ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kutoka Shilingi milioni 500 zilizotolewa mwaka wa fedha 2025 hadi Shilingi milioni 600 katika mwaka huu wa fedha, huku ikieleza kuwa mikopo hiyo imeendelea kuwa chachu ya uwezeshaji wananchi kiuchumi.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelea shughuli mbalimbali za Maafisa Maendeleo ya Jamii ikiwa ni muendelezo wa shamrashamra za Wiki ya Maafisa hao Wilayani Karatu, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Juma Hokororo, amesema usimamizi wa mikopo hiyo umeleta mafanikio makubwa kwa wanufaika, ikiwemo kuwaimarisha kiuchumi na kuwapa fursa ya kujiajiri na kujitegemea kiuchumi.
Hokororo amesema uwezeshaji huo pia umesaidia kuwapa vijana shughuli za kufanya na hivyo kuwaepusha na baadhi ya tabia hatarishi, ikiwemo matumizi ya dawa za kulevya na kujihusisha na vitendo vya uhalifu, akiongeza kuwa halmashauri hiyo imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha makundi yanayonufaika na mikopo hiyo yanapata fursa za kiuchumi, ikiwemo utoaji wa tenda mbalimbali kwa wanufaika.
Aidha, Mkurugenzi huyo amesisitiza umuhimu wa halmashauri kuendelea kusimamia matumizi ya mikopo hiyo pamoja na kutoa elimu kwa makundi lengwa ili fedha hizo zitumike katika shughuli zenye tija na zinazoweza kuongeza kipato, akiwapongeza Wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kwa kuendelea kurejesha mikopo kwa uaminifu hatua ambayo imewezesha fedha hizo kuzunguka na kuwafikia wanufaika wengi zaidi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Wananchi zaidi ya kaya 15 zilizopo Mtaa wa Nyakasangwe, Kata ya Wazo, Wilaya Kinondoni jijini Dar es Salaam wamejikuta katika hali ya taharuki baada ya mabaunsa na watu wenye silaha kufika katika nyumba zao wakiwa na polisi wakiwalazimisha kutoa vitu ndani huku wakiwazuia kurudi katika nyumba hizo.
Tukio limetokea leo Septemba 3, 2026 ambapo wamedai chanzo cha kadhia hiyo ni mgogoro uliopo baina ya wale waliowauzia eneo hilo huku wananchi hao wakidai kumiliki ardhi hizo kihalali kwani waliuziwa mbele ya viongozi wa mtaa huo ambao wamemaliza muda wao.
Kwa mujibu wa wananchi hao waliwauliza viongozi kama kuna mgogoro wowote na viongozi walikiri kuwa haupo hivyo mauziano yakafanyika kihalali.
Aliyekuwa mwenyekiti wa mtaa huo Bw. Regration Mbelwq amesema wananchi hao yeye alihusika wakati wanauziwa kutoka kwa aliyekuwa mmiliki Abdallah Kitwanga ambaye aliwauzia wananachi eneo hilo lakini baadae aliingia kwenye mgogoro na mtu aitwaye David Mushi na wakaenda mahakamani lakini ushindi ukawa kwa Kitwanga.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Saad Mtambule ameeleza kuufahamu mgogoro huo na kuwa kwa nyakati tofauti pamekuwa na kesi juu ya umiliki wa eneo hilo lakini baadae ikatafutwa suluhu kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu na tayari pande zote zilishakutana kwa mara ya kwanza na hivi karibuni(Septemba 10, 2026) pande hizo zilikuwa zinakutana tena kwa ajili ya kutatua jambo hilo kwa kulipana.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Chama cha ACT Wazalendo @ACTwazalendo Mkoa wa Dar es Salaam kimeshtushwa na kupinga vikali mpango unaodaiwa kuwepo wa kuhamisha wakazi na kufuta kata 10 katika Wilaya ya Temeke kwa ajili ya kupisha ujenzi na upanuzi wa mradi wa bandari kavu.
Akizungumza leo Alhamisi, Septemba 3, 2026, Katibu wa chama hicho Mkoa wa Dar es Salaam, Felix Kamugisha, ameeleza kuwa chama hicho kimepokea kwa mshtuko mkubwa kauli iliyotolewa hivi karibuni na Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sixtus Mapunda, kuhusu mpango huo. Kamugisha amemtaka Mkuu huyo wa Wilaya kusitisha mara moja mpango wowote wa kuwahamisha wakazi au kufuta kata za Temeke kwa kisingizio cha kupisha mradi huo wa bandari kavu.
Katibu huyo ametoa onyo kwa serikali kuwa iwapo itaendelea kusukuma mbele mpango huo wa kuwaondoa wakazi wa Temeke katika maeneo yao, ACT Wazalendo itahamasisha wananchi kutumia haki yao ya kikatiba ya kuandamana kwa amani na kupaza sauti
Kamugisha amefafanua kuwa maandamano hayo hayatabaki Temeke pekee, bali yatahusisha kata zote 102 za mkoa wa Dar es Salaam. Amebainisha kuwa kwa sasa wanazungumza kwa kutumia maneno, lakini kama serikali haitasikia, watachukua hatua ya kufanya matembezi na maandamano ya amani ili sauti zao zisikike.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Queen Sendiga amesema hatomvumilia kiongozi yeyote atakayebainika kuchochea migogoro ya ardhi katika mkoa huo, akisisitiza kuwa viongozi wanaohusika watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.
Sendiga ametoa kauli hiyo leo, Septemba 3, 2026, mkoani Morogoro wakati wa makabidhiano ya ofisi kati yake na Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Adam Malima ambapo amesisitiza kuwa umefika wakati viongozi na wananchi kushirikiana kutafuta suluhu za kudumu za migogoro ya ardhi badala ya kuchochea hali hiyo.
Amesema hataruhusu mtu yeyote, ikiwemo viongozi, kutumia nafasi zao kuchochea migogoro kati ya wakulima na wafugaji, akieleza kuwa hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya watakaobainika kufanya hivyo.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Morogoro, Mhandisi Joseph Masunga, amesema si wakati wa viongozi kuleana kuhusu migogoro ya ardhi, bali wanapaswa kutumia nafasi zao kuhakikisha changamoto hizo zinapatiwa ufumbuzi.
Masunga amesema viongozi wanapaswa kuwa sehemu ya suluhu na si chanzo cha migogoro, akiwataka kushirikiana na mamlaka husika katika kutafuta njia zitakazosaidia kudhibiti migogoro hiyo.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Adam Malima amesema Mkoa wa Morogoro una mifugo zaidi ya milioni mbili, hali inayohitaji kuwepo kwa utaratibu mzuri wa kuitambua na kuisimamia ili kupunguza migogoro kati ya wafugaji na wakulima.
Malima amesema wakati akiwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, serikali ilianza mkakati wa kutambua mifugo hiyo ili kujua idadi na maeneo ilipo, hatua ambayo alisema inaweza kusaidia katika kupanga matumizi bora ya ardhi na kupunguza migogoro.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Vijana nchini Tanzania wamefunguliwa fursa mpya za kushiriki katika uwekezaji wa viwanda kupitia maeneo maalumu yaliyotengwa na serikali kwa ajili ya uwekezaji wao, hatua iliyotajwa kuwa sehemu ya kutekeleza maelekezo ya Rais ya kuwawezesha vijana kiuchumi.
Hayo yamebainishwa wakati wa ukaguzi maalum wa utekelezaji wa programu ya uwekezaji wa viwanda kwa vijana uliofanywa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Maendeleo ya Vijana, Joel Nanauka, katika eneo la Benjamin William Mkapa SEZ jijini Dar es Salaam, Septemba 1, 2026.
Waziri Nanauka ameeleza kuwa hekari hizo 520 zimetengwa katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo Mabibo (Dar es Salaam), Bagamoyo, Kwala (Pwani), Nala (Dodoma), Tanga, na Songea, ambapo kila eneo lina lengo maalum la kuwekeza kwa ajili ya vijana
Amesema katika maeneo haya, vijana wanapatiwa ardhi bila kuhitaji kuigharamia kiasi chochote, huku kukiwa na miundombinu tayari kama umeme, maji, na barabara, pamoja na miundombinu ya kutumia pamoja kwa ajili ya uzalishaji wa pamoja.
Kwa upande wake Meneja wa Uhamasishaji Uwekezaji wa Ndani wa Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA), Felix Michael amefafanua kuwa TISEZA inakwenda kujenga mabanda ya kisasa ya viwanda (industrial sheds) ili kumpatia kijana unafuu wa kuanza uzalishaji mara moja bila gharama kubwa za ujenzi
Aidha, serikali imeweka vivutio maalum vya kikodi (tax incentives) vinavyoweza kupunguza mahitaji ya mtaji wa kuanzisha mradi kwa hadi asilimia 50.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Tanga kwa kushirikiana na vyombo vya dola imekamata lita 20,950 za mafuta yaliyoingizwa nchini kwa njia ya magendo katika kijiji cha Kwale wilayani Mkinga yakiwa yamehifadhiwa kwenye vifaa visivyo rasmi.
Akizungumza leo na waandishi wa habari, Kaimu Meneja Msaidizi wa Forodha wa TRA Mkoa wa Tanga, Joseph Raymond, amesema mafuta hayo yalibainika kupitia operesheni maalum iliyofanywa na kikosi cha kuzuia magendo kwa ushirikiano na vyombo vya ulinzi na usalama vya mkoa.
Meneja huyo ametoa mchanganuo wa mafuta yaliyokamatwa akieleza kuwa lita 15,990 ni mafuta ya dizeli wakati lita 4,960 zikiwa ni petrol yenye thamani ya Shilingi milioni 79.5 na ukwepaji wa kodi uliokadiriwa kufikia Shilingi milioni 19.
Mbali na hayo, Meneja huyo amewataka wananchi mkoani Tanga kushirikiana na mamlaka ya ukusanyaji wa mapato kwa kutoa taarifa pindi wanapobaini viashiria vya uingizwaji wa bidhaa za magendo nchini, ili kusaidia kudhibiti biashara hiyo na kulinda mapato ya serikali.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Chama cha ACT Wazalendo @ACTwazalendo Mkoa wa Dar es Salaam kimepinga vikali mpango unaodaiwa kuwepo wa kuhamisha wakazi na kufuta kata 10 katika Wilaya ya Temeke kwa ajili ya kupisha ujenzi na upanuzi wa mradi wa bandari kavu.
Akizungumza leo Septemba 3, 2026, Katibu wa chama hicho Mkoa wa Dar es Salaam, Felix Kamugisha, ameeleza kuwa wameshtushwa na kauli iliyotolewa hivi karibuni na Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sixtus Mapunda, kuhusu mpango huo, huku akiitaka Serikali kutoa ufafanuzi wa kina na wa haraka kuhusu hatima ya wananchi watakaoathirika.
Kamugisha amebainisha kuwa Wilaya ya Temeke ina jumla ya kata 23 na zaidi ya wakazi milioni 1.3 kwa mujibu wa Takwimu za Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022, hivyo hatua ya kufuta kata 10 itagusa na kuathiri maisha ya idadi kubwa ya wananchi wa kipato cha chini.
“Wanawapeleka wapi wananchi hao? Kwa ajili ya nini na kwa faida ya nani?” amehoji Kamugisha, huku akisisitiza kuwa wananchi wanastahili kupewa taarifa sahihi na maelezo ya kutosha kabla ya hatua yoyote kuchukuliwa.
Ameeleza kuwa ingawa ACT Wazalendo inatambua na kuunga mkono umuhimu wa maendeleo ya sekta ya uwekezaji na ukuaji wa huduma za bandari nchini, hatua hizo hazipaswi kutekelezwa kwa gharama ya kuwaondoa wananchi kwa nguvu au bila kuwepo kwa utaratibu unaoeleweka wa fidia na makazi mbadala.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI PICHA:
Mradi wa kwanza wa kisasa na usafi wa Mazingira Afrika Mashariki wa kuchakata majitaka Mbezi Beach mkoani Dar es Salaam unaotekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) umefikia asilimia 88 ya utekelezaji wake huku ukitajwa kunufaisha kaya takribani 11,000 katika Wilaya ya Kinondoni.
Mradi huu unaotekelezwa kwa gharama ya Shilingi bilioni 124 unahusisha ulazaji wa mtandao wa bomba za majitaka kilomita 101, ujenzi wa vituo viwili vya kusukuma majitaka, ujenzi wa chemba zaidi ya 2,300 pamoja na ujenzi wa mtambo wa kisasa wa uchakataji majitaka.
Mradi huu unategemea kukamilika mwishoni mwa mwezi Oktoba 2026 na utanufaisha zaidi ya kaya 11,000 katika kata nne za Kawe, Kunduchi, Mbezi Juu na Wazo wilayani Kinondoni, huku ukitegemewa kutoa bidhaa nyingine muhimu kama vile mbolea na gesi. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Ujenzi wa matanki maalumu ya kupokea na kuhifadhi mafuta katika Bandari ya Dar es Salaam umefikia asilimia 52, huku mradi huo ukitarajiwa kukamilika Februari 2027.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam, Abed Gallus Abed, alipokuwa akitoa ufafanuzi kwa wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari waliotembelea eneo la mrad huo leo.
Amesema ujenzi wa mradi huo ulianza Agosti 2024, na hadi kukamilika kwake unatarajiwa kugharimu Sh678.6 bilioni. Mradi huo unahusisha ujenzi wa matanki 15 yenye uwezo wa kuhifadhi mafuta, ukiwa na lengo la kuongeza uwezo wa Bandari ya Dar es Salaam kupokea na kuhifadhi shehena ya mafuta pamoja na kupunguza muda wa meli kukaa nangani ikisubiri kushusha mzigo.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Abed, kukamilika kwa matanki hayo kutasaidia kupunguza muda wa meli kushusha shehena ya mafuta na kukaa nangani kutoka siku 22 za awali hadi siku saba.
Kwa muda mrefu, Bandari ya Dar es Salaam haikuwa na eneo lake maalumu la kuhifadhia mafuta, hivyo shehena iliyopokelewa ililazimika kuondolewa bandarini na kupelekwa kwenye matanki yanayomilikiwa na watu binafsi.
Mkurugenzi Abed amesema uwepo wa matanki hayo ni muhimu kwakuwa mafuta ni uti wa mgongo wa taifa, huku mradi huo ukitarajiwa kuongeza ufanisi wa Bandari ya Dar es Salaam na uwezo wake wa kuihudumia Tanzania pamoja na nchi jirani.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mbunge wa Bariadi Vijijini, Masanja Kadogosa, ameunga mkono marekebisho ya sheria yanayolenga kuondoa utaifishaji wa mifugo, akisema hatua hiyo ni muhimu kwa kuwa mifugo ni mali na chanzo cha maisha kwa wafugaji.
Kadogosa amebainisha hayo bungeni jijini Dodoma wakati akichangia Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali wa Mwaka 2026 (The Written Laws (Miscellaneous Amendments) Bill, 2026).
Amesema yeye anatoka katika familia ya wafugaji na jimbo lake lina wananchi wengi wanaojishughulisha na ufugaji na kilimo kwa pamoja, hivyo suala hilo linamhusu moja kwa moja.
Ameeleza kuwa tangu sheria hiyo ilipotungwa mwaka 2009, wafugaji wamekuwa wakipitia changamoto mbalimbali na hata kuanzisha chama kwa ajili ya kuimarisha sauti yao na mahusiano na Serikali.
Kadogosa amesema yeye pamoja na wabunge kutoka maeneo yenye wafugaji wamekuwa wakisubiri kwa muda mrefu mabadiliko hayo, akimpongeza Waziri mwenye dhamana, Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na uongozi wa Serikali kwa kusikiliza kilio cha wafugaji.
Amesema hatua hiyo inapaswa kufuatiwa na marekebisho ya sheria nyingine zinazohusiana na mifugo ili kuondoa kabisa utaratibu wa kutaifisha mifugo, akisisitiza kuwa kwa wafugaji, “mifugo ni maisha, kutaifisha mifugo ni kutaifisha maisha.”This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Leo Septemba 3, 2026, katika mwendelezo wa kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Tundu Lissu, shahidi wa tatu ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Amani Golugwa, ameendelea kutoa utetezi wake mahakamani hapo huku akiongozwa na Lissu katika kutoa ushahidi huo.
Katika ushahidi wake, Golugwa ameanza kwa kuwasilisha mbele ya majaji tathmini na kauli zilizotolewa na watazamaji wa uchaguzi wa mwaka 2025 kutoka mataifa mbalimbali na jumuiya za kimataifa na kikanda.
Ameeleza kuwa taarifa ya watazamaji wa uchaguzi kutoka SADC ilihitimisha kuwa uchaguzi wa Tanzania ulishindwa kukidhi vigezo vya viwango vya kidemokrasia, ulikuwa na vitisho kwa viongozi wa upinzani, ukakosa ushindani sawa na uwazi, na ulikumbwa na udanganyifu pamoja na vurugu siku ya uchaguzi, jambo lililoufanya kukosa uhalali wa kuitwa uchaguzi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
SHAHIDI GOLUGWA: KAULI ZA LISSU HAZIKUTAJA KIONGOZI WALA CHOMBO CHOCHOTE CHA DOLA jambo.co.tz/shahidi-golugwa-kauli-lissu-hazikutaja-kiongo… via @jambotv_
-
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Vyama vya siasa nchini vimehimizwa kuepuka matumizi ya lugha kali katika uwasilishaji wa hoja na badala yake kutumia lugha ya staha ili kudumisha amani na utulivu nchini.
Wito huo umetolewa leo na Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa Tanzania, Mohamed Ally Ahmed, wakati wa uchaguzi wa Kamati za Kisekta wa Baraza la Vyama vya Siasa Nchini uliofanyika mkoani Morogoro.
Amesema viongozi waliochaguliwa katika kamati hizo wanapaswa kuwa mfano wa uwajibikaji na kutoa mwelekeo sahihi utakaosaidia kuimarisha umoja, mshikamano na amani nchini.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa Tanzania, Juma Ali Khatibu, amesisitiza umuhimu wa viongozi wa vyama vya siasa kushirikiana katika kulinda amani na utulivu wa taifa.
Baadhi ya viongozi waliochaguliwa, akiwemo Majaliwa Kyara aliyechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, wameahidi kusimamia umoja na uwajibikaji kwa maslahi ya amani na maendeleo ya Watanzania.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi, ametoa agizo kwa Wizara ya Viwanda na Biashara pamoja na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuhakikisha wanamaliza haraka mkwamo wa uzalishaji unaosababisha bei ya saruji kupanda na kumuumiza mwananchi wa kawaida.
Akizungumza jana Jumatano, Septemba 2, 2026, alipomwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika msimu wa 19 wa Tuzo za Rais za Wazalishaji Bora wa Mwaka (PMAYA) jijini Dar es Salaam, Ndejembi alionesha kusikitishwa na gharama kubwa ya mfuko wa saruji inayomkabili Mtanzania hivi sasa.
Alifafanua kuwa changamoto kubwa inasababishwa na kutokuwa na uwiano katika mnyororo mzima wa uzalishaji kati ya viwanda vinavyozalisha klinka (clinker) na vile vinavyosaga saruji (grinders).
Makamu wa Rais alieleza kuwa kukosekana kwa uwiano huo kunasababisha baadhi ya wasagaji kukosa klinka ya kutosha kwa sababu mzalishaji mkubwa wa malighafi hiyo hazalishi ipasavyo, jambo linalopelekea uhifadhi au ukandamizaji wa bidhaa sokoni (holding of goods), na hatimaye mwananchi wa kawaida kuumia.
“Sisi kama serikali tunafanya nini katika kuhakikisha tunasynchronize production katika viwanda vyetu kwenye ile value chain yote?... Leo hii Mtanzania anapata gharama kubwa ya mfuko wa sementi. Ni kwa sababu hatuja-synchronize production yetu,” alisema Ndejembi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Shughuli za kijamii, uwepo wa miundombinu mingine pamoja na changamoto za ulipaji wa fidia kwa wananchi zimetajwa kuwa miongoni mwa sababu zinazochangia kuchelewesha utekelezaji wa baadhi ya maeneo ya Mradi wa Reli ya Kisasa (SGR) hususan katika maeneo ya mijini.
Akizungumza Septemba 2, 2026 kwenye ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa SGR kipande cha Makutopora hadi Mwanza, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Machibya Shiwa akitoa mfano amesema katika kipande cha tano cha mradi huo kutoka Fera kuelekea Mwanza mjini cha takribani kilomita 20 bado kinakabiliwa na changamoto zinazohusiana na fidia na uondoshaji wa wananchi kutoka katika maeneo yanayohitajika kwa ajili ya ujenzi.
"Tuliruka tukaja kuanzia Mwanza kuelekea Isaka, kwanini? Changamoto za kuingia kwenye miji mikuu zimekuwa ni tatizo kutokana na mwingiliano wa shughuli za kijamii lakini ndani ya hiyo miji tumekuta kuna miundombinu mingine ambayo inabidi tuhamishe ili kuwezs kuunganisha na mradi huu," amesema Shiwa
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TRC, Jaffer Machano amesema bodi hiyo imemtaka Mkandarasi kuhakikisha unaongeza kasi kwa kufanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha mradi huo unakamilika hadi ifikapo mwishoni mwa mwaka 2028.
Meneja Mawasiliano wa Mradi huo kutoka Kampuni ya ujenzi na uhandisi ya CCECC, You Can amesema kwa upande wa mhandisi wa mradi huo wamejipanga vizuri kuhakikisha mradi huo unakamilika ndani ya muda ulipangwa kwenye mkataba.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Siku chache baada ya kuibuka kwa tuhuma za uporaji wa mirathi ndani ya familia ya marehemu Askofu Dkt. Gertrude Pangalile Rwakatare, mambo yamechukua sura mpya kufuatia mawakili wa familia hiyo kujitokeza hadharani kukanusha vikali madai hayo na kutoa tishio la kudai fidia ya mabilioni ya shilingi.
Mawakili wa familia ya Marehemu Askofu Rwakatare wakiongozwa na Wakili Derick Paschal Kahigi, Wakili Fredrick Massawe Augusti, na Wakili Justin Justus Rweyongeza wamefanya mkutano na waandishi wa habari Septemba 1, 2026, kukanusha madai yaliyotolewa na mmoja wa watoto wa marehemu, Tibe Kenneth Rwakatare
Wakili Kahigi, akizungumza kwa niaba ya mawakili wenzake, ameeleza kuwa tuhuma zote zilizotolewa na Tibe na mawakili wake dhidi ya dada yake, Kellen Rose Rwakatare ambaye ni Mbunge wa Mlimba (CCM), na familia kwa ujumla ni za uongo, potofu, na zenye nia ovu ya kudhalilisha na kuharibu heshima ya familia hiyo.
Mawakili hao wamefafanua kuwa hakuna mgogoro wowote unaoendelea kuhusu mirathi ya marehemu Askofu Dkt. Gertrude Rwakatare. Wamebainisha kuwa katika shauri la mirathi namba 32 la mwaka 2020 lililopo Kituo Jumuishi cha Temeke mkoani Dar es Salaam, warithi wote akiwemo Tibe Kenneth Rwakatare waligawiwa mirathi hiyo kwa mujibu wa sheria. Aidha, wameeleza kuwa Tibe mwenyewe aliridhika na mgao huo na ndiye aliyekuwa mstari wa mbele kusaini nyaraka zote za orodha ya mali na mgao husika
Kuhusu tuhuma kuwa Mbunge Kellen Rose Rwakatare alighushi saini na kuchukua mkopo wa shilingi bilioni 8 kutoka benki kwa kutumia mali za marehemu mama yao, mawakili hao wamekanusha vikali na kuzitaja tuhuma hizo kama uzushi mtupu. Wamesisitiza kuwa hakuna uamuzi wowote wa Mahakama ya Rufani uliomnyang'anya Tibe majengo ya shule au kumwachia viwanja vitupu vilivyowekwa rehani kwa ajili ya mkopo huo.
Tazama video hii kwa ukubwa kupitia chaneli ya Youtube ya Jambo TVThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Spika wa Bunge la Tanzania, Mussa Zungu, ametoa onyo kwa watendaji wa serikali, hususan wale wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), akitaka wabadilishe haraka fikra zao na kuacha kuchelewesha miradi ya ubia kati ya sekta ya umma na binafsi (PPP).
Akizungumza bungeni jijini Dodoma leo Alhamisi, Septemba 3, 2026, Zungu amekumbusha kuwa hivi karibuni Rais alitoa maelekezo, kulalamika, na kukemea vikali hali ya uchafu katika jiji la Dar es Salaam. Hata hivyo, amefichua kuwa changamoto kubwa ipo kwa watendaji wa TAMISEMI ambao wamekuwa kikwazo cha utatuzi wa kero hiyo
Amebainisha kuwa pale halmashauri za Dar es Salaam na miji mingine mikubwa nchini zinapobuni miradi ya PPP kwa ajili ya usafi na kuiwasilisha TAMISEMI ili ishughulikiwe, majibu yamekuwa yakichelewa au hayaji kabisa. Amesema kutokana na watendaji hao kushindwa kutoa majibu ya kuwatia moyo wawekezaji, matokeo yake miji hiyo imeendelea kubaki katika hali ya uchafu.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Makamu wa Rais wa Tanzania, Deogratius Ndejembi, ameitaka Wizara ya Viwanda na Biashara kukaa meza moja na wazalishaji wa saruji nchini ili kuweka mikakati ya haraka itakayohakikisha bidhaa hiyo inapatikana kwa wingi na kurejea katika bei nafuu ya awali.
Ndejembi ametoa agizo hilo jana jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya utoaji wa Tuzo za Rais kwa Mzalishaji Bora Viwandani (President’s Manufacturer of the Year Awards - PMAYA), zinazoratibiwa na Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI).
Katika tuzo hizo, Kampuni ya SILAFRICA Tanzania Limited imeibuka mshindi wa kwanza wa jumla, ikifuatiwa na Alliance One kama mshindi wa pili, huku Tanzania Cigarette PLC ikitwaa ushindi wa tatu.
Akieleza kero ya wananchi kuhusu gharama za ujenzi, Makamu wa Rais amebainisha kuwa Watanzania wanalazimika kununua saruji kwa bei kubwa kutokana na usimamizi na uratibu dhaifu wa uzalishaji viwandani, jambo ambalo linaenda kinyume na maelekezo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
“Sasa nakuagiza Waziri wa Viwanda na Biashara namwona hapa Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kaeni pamoja mmalize hili suala ili Mtanzania apate saruji kwa bei iliyokuwepo. Nataka kupata ripoti ya suala hilo baada ya kikao hiki, mjadili na mwandike ripoti tumkabidhi Rais,” amesisitiza Ndejembi.
Akiangazia mwenendo wa uchumi, Makamu wa Rais ameeleza kuwa sekta ya viwanda imeendelea kukua, ambapo mwaka 2025 ilikua kwa asilimia 5.2 ikilinganishwa na asilimia 4.2 ya mwaka 2024, huku mchango wake katika Pato la Taifa ukifikia asilimia 5.9 na kuchangia takribani asilimia 12 ya ajira rasmi nchini.
Hata hivyo, ametoa rai kwa wamiliki wa viwanda kutojiridhisha na soko la ndani pekee, bali kuongeza ubora na tija ili bidhaa za Tanzania ziweze kushindana katika masoko ya Afrika Mashariki na duniani kote.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa CTI, Leodegar Tenga, ameeleza kuwa tuzo za PMAYA zinalenga kutambua mchango wa sekta ya viwanda na kuchochea ubunifu. Pia amesisitiza utekelezaji wa misingi ya uzalishaji endelevu unaozingatia mazingira, jamii na utawala bora (ESG), akitangaza kuanzishwa kwa Mabalozi 10 wa ESG watakaopimwa kwa mwaka mmoja. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga @CCMTanzania Mabala Mlolwa amesema tukio la aliyekuwa Makamu wa Rais Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi kuzungumza hadharani akiwasihi Watanzania kupambana kupata Katiba Mpya hakikuwa sahihi kwani tayari ilani imeshasema kuwa kutakuwa na marekebisho ya katiba na yalikubaliwa.
Mlolwa amesema hayo alipokuwa akizungumza na wanachama hao eneo la Kishapu mkoani Shinyanga ambapo amedai kuwa pamoja na kuwa ilani imeshasema juu ya hilo na Nchimbi alishiriki kuinadi, tayari alikuwa ni mshauri namba moja wa Rais na angeweza kuzungumza na Rais Dkt. Samia moja kwa moja juu ya jambo hilo.
Amesisitiza kuwa kitendo hicho kiikuwa ni usaliti kosa ambalo listahili adhabu ya kuvuliwa uanachama kama ambavyo imefanyika.
Ikumbukwe Julai 24, 2026 Dkt. Nchimbi akizungumza na watetezi wa haki za binadamu Mlimani City alisema kama angekuwa na nafasi moja ya mwisho kuzungumza na watanzania angewataka kupambania mpya huku akidai kuwa Rais tayari ana nia ya dhati ya kuipata katiba hiyo hivyo watanzania washikilie jambo hilo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
“MGOMBEA WA CCM HAJAWAHI KUENGULIWA KWENYE UCHAGUZI”, SHAHIDI GOLUGWA AKIMTETEA LISSU LEO jambo.co.tz/mgombea-wa-ccm-hajawahi-kuenguliwa-kwenye-uch…
-
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Serikali imetoa tahadhari kuhusu uwezekano wa kutokea kwa hali ya hewa ya El Niño kuanzia Oktoba 2026, ambayo inaweza kusababisha mvua kubwa, mafuriko, maporomoko ya ardhi na uharibifu wa makazi, huku ikieleza kuwa athari zake zinaweza kuwa kubwa.
Hayo yamebainishwa leo Septemba 2, 2026 jijini Dodoma na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Profesa Palamagamba Kabudi, akisema Serikali imejiandaa kwa kuweka mipango ya dharura na kutenga Shilingi Bilioni 730 kwa ajili ya kukabiliana na madhara yanayoweza kujitokeza.
Profesa Kabudi ametoa wito kwa Wananchi kuepuka kusambaza taarifa zisizo sahihi zinazoweza kusababisha taharuki, badala yake wafuatilie taarifa rasmi kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) na kutoa taarifa kwa mamlaka husika endapo maafa yatatokea.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDASA), Prof. Eligidius Ichumbaki, amesisitiza kuwa jumuiya hiyo itaendelea kutoa karipio, matamko na ushauri pale itakapoona inafaa kufanya hivyo.
Prof. Ichumbaki ameyasema hayo hivi karibuni katika mahojiano maalum na Jambo TV, akijibu swali kuhusu ukinzani wa matamko kati ya UDASA na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Akirejea tamko lililotolewa na UDASA Oktoba 23, 2025, kuhusu yanayoendelea nchini, ambalo baadaye lilifuatiwa na taarifa ya UDSM kujitenga nalo, Prof. Ichumbaki amesema taratibu za uongozi zinawalazimu Viongozi Wakuu wa Chuo kufuata maelekezo ya Serikali.
Amesema hali hiyo inaweza kuifanya UDSM kuonekana kama inapinga misimamo ya UDASA, jambo ambalo amesema si sahihi.
“Mkutano Mkuu ulikubaliana kwamba yeye anafanya hivyo katika kutimiza majukumu ya Serikali, lakini sisi kama Jumuiya huru tutaendelea kutoa karipio, tamko na ushauri pale ambapo tutaona inafaa kufanya hivyo”, amesema Prof. Ichumbaki akifafanua taarifa iliyotolewa na Makamu Mkuu wa chuo kikuu Cha Dar es Salaam, ya kujitenga na tamko la UDASA la Oktoba 23, 2025This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDASA), Prof. Eligidius Ichumbaki, amesema baadhi ya viongozi waliopo Serikalini ambao waliwahi kupita UDASA, wamekuwa wakiwasiliana nao na kuwapongeza baada ya kutoa matamko na maoni kuhusu masuala mbalimbali ya kitaifa yanayotolewa na UDASA.
Akizungumza hivi karibuni katika mahojiano maalum na Jambo TV, Prof.Ichumbaki amesema baadhi yao hushindwa kujitokeza hadharani kutokana na nafasi zao na viapo walivyowahi kula, lakini wanapoyaona matamko ya UDASA hujisikia kuwa bado wasomj wanaendelea kutekeleza wajibu wao kwa jamii.
"Kuna baadhi ya watu ambao pengine sitawataja majina, tukisimama tukatoa kauli juu ya kitu fulani wanarudi kwetu na kutupigia simu na kutupongeza kwamba angalau sasa tumeona wasomi wakifanya kazi", ameeleza Prof. Ichumbaki
Prof. Ichumbaki amesema UDASA itaendelea kutoa maoni na kufanya yale yanayostahili, bila kuvunja sheria wala kuhatarisha amani ya nchi. -
Jambo TV
@Jambotv_
Mamia ya wananchi wamejitokeza kupata huduma katika Kambi Maalum ya Matibabu ya Macho inayoendeshwa na madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Qatar Charity ambapo Septemba 01, 2026 huduma hizo zimeanza kutolewa rasmi katika Kituo cha Afya Sebuleni, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Akizindua huduma hizo, Mkuu wa Wilaya ya Mjini, Hassan Khamis Hafidh, amepongeza ushirikiano kati ya Muhimbili, Qatar Charity na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, akisema umewezesha wananchi kusogezewa huduma za kibingwa za macho na kuongeza fursa ya kupata matibabu ya kisasa karibu na maeneo yao.
"Ushirikiano kati ya Hospitali ya Taifa Muhimbili, Qatar Charity na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar umeleta huduma za kibingwa karibu na wananchi wetu. Hii ni hatua muhimu ya kuboresha upatikanaji wa huduma za afya na kuwafikia wananchi wanaohitaji matibabu ya macho kwa wakati, nawaombeni wananchi wote wa Zanzibar tuitumie fursa hii” amesema Hafidh.
Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Macho kutoka Muhimbili, Dkt. Joachim Kilemile, amesema hospitali imejipanga kuhakikisha kila mwananchi anayefika kambini anapata huduma, na kuwataka wananchi kutokata tamaa licha ya idadi kubwa ya watu waliojitokeza kwani wote watahudumiwa.
“Tunawaomba wananchi wasikate tamaa kutokana na idadi kubwa ya waliojitokeza. Muhimbili imejipanga kwa wataalamu na vifaa vya kutosha kuhakikisha kila mgonjwa anayefika kambini anapata huduma stahiki, ikiwemo upasuaji wa mtoto wa jicho kwa njia ya tundu dogo.” ameeleza Dkt. Kilemile.
Kambi hiyo imeanza Agosti 29 na itahitimishwa Septemba 4, 2026, ikitoa huduma za uchunguzi wa macho, dawa, miwani kwa wenye uhitaji pamoja na upasuaji wa mtoto wa jicho kwa njia ya tundu dogo, upasuaji unaofanyika kwa kutumia gari maalum la upasuaji, ikiwa ni mara ya kwanza nchini Tanzania kutekelezwa kwa mfumo huo wa kisasa.
Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi 2022, kiwango cha ulemavu kwa watu wenye umri wa miaka 7 na kuendelea Zanzibar kimeongezeka kutoka 7.5% mwaka 2012 hadi 11.4% mwaka 2022, sawa na ongezeko la asilimia 3.9 ambapo katika makundi hayo, ulemavu wa kuona ni miongoni mwa aina zilizoongoza, ikiashiria ongezeko la mahitaji ya huduma za afya ya macho Zanzibar. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mhariri Msaidizi wa Chombo cha habari cha Standard Group cha nchini Kenya, Alex Kiprotich ametekwa usiku wa kuamkia leo na watu wenye silaha wasiojulikana.
Taarifa iliyochapishwa na ukurasa wa chombo hicho cha nchini Kenya imesema kuwa Mhariri huyo ametekwa akiwa kwenye gari lake katika barabara ya Gilgil-Nakuru.
Viongozi hasa wa upinzani, wananchi na wanahabari nchini humo wameanza kupaza sauti wakitaka kuachiwa haraka kwa mwandishi huyo kwani 'Uandishi wa habari sio uhalifu'.
Hii inakuwa tukio la pili kwa mhariri wa chombo hicho kosoaji kwa serikali ya Rais William Ruto kutekwa, mara baada ya jaribio la kwanza lililokwama ambalo lilimlenga mhariri huyo ambapo watu waliokuwa katika gari aina ya probox kujaribu lakini hawakufanikiwa.
Haya yanatokea miezi kadhaa mara baada ya chombo hicho kulalamikiwa na Rais Ruto katika mtandao wa X akidai kuwa kimekuwa kikitumika kumchafua na kimeacha kufanya kazi za kihabari huku kikitumika kuchapisha habari mbaya tu dhidi yake.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Chama cha Demokrasia Maendeleo @ChademaTZ2 Mkoa wa Mara kimemkataa Katibu wa mkoa huo Donald Felix Mwembe aliyesema kuwa chama hicho kikiongozwa na Makamu Mwenyekiti wake John Heche kinatakiwa kuzungumza na watawala ili kufikiwa kwa muafaka wa kesi ya uhaini inayomkabili Tundu Lissu.
Akizungumza leo Septemba 1, 2026 kwenye kikao Cha Baraza la mashauriano la CHADEMA Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Mara Chacha Heche amesema yeye kama msemaji wa chama mkoa anasimamia msimamo wa chama hicho kuwa hakuna maridhiano.
"hatutambui, hatupokei, hatuna mpango wa kuridhiana na Chama cha Mapinduzi kwenye hatua yoyote," amesema Chacha.
Hata hivyo amesisitiza wanachama wa chama hicho kutoyumbishwa na baadhi ya wanachama ambao wamekuwa wakitumika huku akimtaka Katibu Mwembe kujitafakari juu ya kauli alizotoa kwenye vyombo vya habari.
Ikumbukwe siku mbili zilizopita Mwembe alieleza kuwa viongozi wa chama hicho wakae na kuzungumza na serikali ili kutoka kwenye mtanziko na kupatikana kwa suluhu itakayowezesha Lissu kuweza kuachiwa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Chama cha Demokrasia Maendeleo @ChademaTZ2 Mkoa wa Mara kimemkataa Katibu wa mkoa huo Donald Felix Mwembe aliyesema kuwa chama hicho kikiongozwa na Makamu Mwenyekiti wake John Heche kinatakiwa kuzungumza na watawala ili kufikiwa kwa muafaka wa kesi ya uhaini inayomkabili Tundu Lissu.
Akizungumza leo Septemba 1, 2026 kwenye kikao Cha Baraza la mashauriano la CHADEMA Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Mara Chacha Heche amesema yeye kama msemaji wa chama mkoa anasimamia msimamo wa chama hicho kuwa hakuna maridhiano.
"hatutambui, hatupokei, hatuna mpango wa kuridhiana na Chama cha Mapinduzi kwenye hatua yoyote," amesema Chacha.
Hata hivyo amesisitiza wanachama wa chama hicho kutoyumbishwa na baadhi ya wanachama ambao wamekuwa wakitumika huku akimtaka Katibu Mwembe kujitafakari juu ya kauli alizotoa kwenye vyombo vya habari.
Ikumbukwe siku mbili zilizopita Mwembe alieleza kuwa viongozi wa chama hicho wakae na kuzungumza na serikali ili kutoka kwenye mtanziko na kupatikana kwa suluhu itakayowezesha Lissu kuweza kuachiwa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu wa Rais wa Deogratius Ndejembi ametoa wito kwa wananchi wa Moshi mkoani Kilimanjaro kumuombea yeye ili aweze kufanya kazi akimsaidia Rais Samia Suluhu Hassan huku akiahidi kuwa 'hatomzingua'.
Ndejembi amesema hayo leo Septemba 1, 2026 alipokuwa kwenye ziara yake binafsi mkoani humo ambapo pamoja na mambo mengine ameahidi kutowaangusha watu wa eneo hilo kwani ni 'Wajomba' zake.
"Ni imani yangu kwa maombi yenu nitamsaidia kwa hekima na utii Rais wa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzanai Dkt. SAMIA Suluhu Hassan sina maneno mengi narudia niliyoyasema kwa wanaChamwino sitazingua na wala sitamzingua Mama" amesema NdejembiThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
MWANACHADEMA ISHENGOMA, SAKATA LA TONETONE LILIVYOTIKISA MAHAKAMA MNYIKA AKIHOJIWA.
jambo.co.tz/mwanachadema-ishengoma-sakata-la-tonetone-lil… -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Wakili wa Godlisten Malisa, Dickson Matata amesema mteja wake alikamatwa jana bila kufuata utaratibu, huku Polisi wakishindwa kueleza kosa alilokuwa akishikiliwa nalo.
Amesema leo asubuhi alifika kituo cha Polisi cha utalii na Diplomasia Arusha ,baada ya kupata taarifa kuwa Malisa alikuwa amepelekwa hapo, lakini alipofika alikuta tayari amesafirishwa hadi nje ya eneo la ofisi za TANAPA ambapo aliachiwa huru bila kupewa dhamana wala kutakiwa kusaini nyaraka yoyote.
Aidha, Wakili Matat amesema Polisi hawajaeleza kosa wala kifungu cha sheria ambacho Malisa alikiuka, akidai hali hiyo inaonyesha kuwa alikamatwa bila sababu na bila kufuata utaratibu wa kisheria.
Mapema leo, taarifa ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha ilisema Godlisten liliwakamata Malisa na mwenzake, jana Agosti 31, 2026, majira ya usiku, kwa tuhuma za jinai zilizokuwa zikichunguzwa dhidi yake, ambapo baada ya kuhojiwa waliachiwa kwa dhamana wakisubiri kukamilishwa kwa taratibu nyingine za kisheria. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Godlisten Malisa amewashukuru Watanzania kwa kupaza sauti na toka alipokamatwa hadi kuachiwa, akisema anaamini msukumo huo huenda ulichangia kuachiwa kwake.
Malisa amesema wakati wote walipokuwa wakishikiliwa, hawakusomewa mashitaka au tuhuma zozote na hivyo wameachiwa bila masharti yoyote
Mapema leo, taarifa ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha ilisema Godlisten iliwakamata Malisa na mwenzake, jana Agosti 31, 2026, majira ya usiku, kwa tuhuma za jinai zilizokuwa zikichunguzwa dhidi yake, ambapo baada ya kuhojiwa waliachiwa kwa dhamana wakisubiri kukamilishwa kwa taratibu nyingine za kisheria. -
Jambo TV
@Jambotv_
JAMHURI YAMBANA MNYIKA KUHUSU AJENDA ZA SIRI NA “MKAKATI WA KUZUIA UCHAGUZI”, MWENYEWE ATETEA HAKI YA “UASI WA KIDEMOKRASIA” jambo.co.tz/jamhuri-yambana-mnyika-kuhusu-ajenda-za-siri-…
-
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Muda mfupi baada ya kuachiwa na Polisi, Godlisten Malisa amezungumza na Jambo TV, ambapo amedai kuwa ameachiwa huru bila masharti yoyote, na si kwa dhamana kama ambavyo taarifa ya Polisi ilieleza
Jeshi la Polisi mkoani Arusha lilitoa taarifa mapema leo, Septemba 1, 2026, likisema kuwa lilimkamata Malisa na mwenzake kwa tuhuma za kijinai na baadaye kuachiwa kwa dhamana.
Malisa amekanusha taarifa hiyo ya Jeshi la Polisi, akidai kuwa hakuachiwa kwa dhamana kama ilivyoelezwa, bali aliachiwa huru bila masharti yoyote, licha ya Polisi kubaki na hati yake ya kusafiriaThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Jaji Mkuu wa Tanzania George Mcheche Masaju amesema kuwa vitendo vya kuidharau Mahakama havitavumiliwa wala kupewa nafasi huku akionya kuwa yale yale yatakayofanya taifa lisitawalike pia hayatopewa nafasi.
Jaji Masaju ameeleza hayo Agosti 31, 2026 alipokuwa akifungua semina elekezi kwa Naibu Wasajili wa Mahakama Kuu ambapo amewasititza kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia misingi ya katiba na viapo vyao.
"Hatutaruhusu watu kuidharau Mahakama, kuitisha hii Mahakama nchi itatawalikaje tunahitaji amani kwa hiyo mtakuwa macho kwenye hili hatutaendekeza kitendo ambacho kitafanya taifa hili ilisitawalike kwa kile kinachoitwa kutetea haki za binadamu" amesema MasajuThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Wiki ya Ubunifu imeelezwa kuwa si tukio la kawaida, bali ni jukwaa la kimkakati linalowakutanisha wadau mbalimbali kujadili na kukubaliana hatua za kuimarisha mchango wa ubunifu katika maendeleo ya taifa.
Akizungumza leo Agosti 31, 2026 katika ufunguzi wa Wiki ya Ubunifu, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Dkt. Tausi Mbaga Kida amesema tukio hilo linafanyika katika kipindi muhimu cha utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, ambayo inalenga kuweka msingi wa Tanzania yenye maendeleo jumuishi na endelevu.
Dkt. Tausi amesema wiki hiyo imeandaliwa kwa ushirikiano kati ya Tume ya Taifa ya Mipango, UNDP, COSTECH na wadau wengine, kwa lengo la kujenga uelewa na kuimarisha jitihada za pamoja za kuunganisha ubunifu na mipango ya maendeleo ya Taifa.
“Mawazo bunifu yanahitaji kuunganishwa na vipaumbele vya kitaifa, rasilimali, utekelezaji na upimaji wa matokeo ili yaweze kuleta mabadiliko.” amesema Dkt. Kida
Hata hivyo Wiki ya Ubunifu inatarajiwa kuwa sehemu muhimu ya kuibua mawazo mapya na kuimarisha ushirikiano kati ya serikali, sekta binafsi, wataalamu, wabunifu na wadau wengine, ili kuhakikisha ubunifu unatumika kama nyenzo ya kutatua changamoto na kuchochea maendeleo kuelekea Tanzania tuitakayo ifikapo mwaka 2050.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Ruvuma, Oddo Mwisho, amesema chama hicho hakijakurupuka kufanya maamuzi ya kumfukuza uanachama aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi huku akieleza kuwa walimuomba msamaha mwenyekiti wa chama hicho Rais Samia Suluhu Hassan kutokana na kadhia.
Akizungumza na wananchi wa kata za Langiro, Kipapa na Maguu zilizopo Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma katika ziara ya kuimarisha uhai wa chama Agosti 31, 2026, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma, Oddo Mwisho amesema Mkoa wa Ruvuma ulikuwa unamtegemea Nchimbi kutokana na nafasi aliyokuwa nayo lakini amewaangusha wananchi wa mkoa huo.
Amesema yaliyofanywa na Dkt.Nchimbi ni ya kwake binafsi na si ya wananchi wa Ruvuma, kwani wananchi wa mkoa huo wana imani na Rais Dkt. Samia ambaye bado anawaamini vijana mbalimbali walioko ndani ya Mkoa huo ambao wanafanya kazi vyema katika chama na serikali.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI:
Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limesema limemkamata Godlisten Elisante Malisa pamoja na mtu mwingine, kufuatia tuhuma za jinai zilizokuwa zikichunguzwa dhidi yake.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Septemba 1, 2026, na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, watu hao wawili walikamatwa jana Agosti 31, 2026, majira ya usiku na kuhojiwa kuhusiana na tuhuma hizo.
“Baada ya mahojiano wameachiwa kwa dhamana wakisubiri taratibu nyingine za kisheria kukamilishwa,” imeeleza taarifa hiyo -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Baada ya mapumziko mafupi mchana wa leo, kesi ya uhaini namba 19605/2025 inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Antiphas Lissu, ilirejea huku Katibu Mkuu wa chama hicho, John John Mnyika, akipanda kizimbani kukabiliana na maswali ya dodoso kutoka kwa Wakili wa Serikali Mkuu, Nassor Katuga.
Moja ya maeneo yaliyozua mjadala ni pale Katuga alipohoji kama raia yeyote, ikiwa ni pamoja na Mwenyekiti wa CHADEMA, ana haki ya kuzuia uchaguzi mkuu uliowekwa kwa mujibu wa Katiba ya nchi.
Mnyika alitoa jibu akisema, "Ni haki kwa uchaguzi usio huru na wa haki, ni haki kuuzuia kwa njia za kidemokrasia. Ni haki kabisa". Amesisitiza kuwa wananchi wana haki ya kushiriki uchaguzi ukiwa huru, wa haki na halali tu.
Katuga alimtaka Mnyika kufafanua kile alichokisikia wakati wa hotuba ya Tundu Lissu katika mkutano wa watia nia wa Aprili 3, 2025. Mnyika alikiri kusikia kauli za ‘Polisi kukimbia na mabegi ya kura’, ‘tunaenda kuzuia uchaguzi’ na ‘tunaenda kukinukisha’ akisema kuwa Lissu alifafanua kauli hizo.
Katuga alipohoji kama Mnyika ameleta mahakamani hotuba hiyo inayofafanua maneno hayo, Mnyika alijibu: "Nimeileta kwa maelezo ya mdomo kwasababu si wajibu wangu kuthibitisha mashtaka".
Katuga alijaribu kumjenga Mnyika kama shahidi mwenye masilahi binafsi (interested witness) katika kesi hiyo, kwa kuwa uteuzi wake kama Katibu Mkuu ulipendekezwa na mshitakiwa (Tundu Lissu), na kwamba yeye ndiye aliyeratibu kikao cha Kamati Kuu cha tarehe 29 Agosti 2026 kilichoazimia kumtetea Lissu kwa nguvu zote.
Mnyika alikataa vikali madai hayo akieleza kuwa masilahi yake katika kesi hiyo yanawakilisha masilahi ya chama (party interest) na masilahi ya umma (public interest), na siyo masilahi yake binafsi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
“MASILAHI YA CHAMA SI BINAFSI”, MNYIKA ACHARUKA BAADA YA UPANDE WA JAMHURI KUMTAJA KAMA SHAHIDI WA MASILAHI jambo.co.tz/masilahi-ya-chama-si-binafsi-mnyika-acharuka-… via @jambotv_
-
Jambo TV
@Jambotv_
Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, amezindua rasmi Programu ya Mining for a Brighter Tomorrow (MBT)maarufu kama “Kesho Iliyo Njema, inayolenga kufungua fursa za kiuchumi kwa vijana, wanawake, na watu wenye mahitaji maalum katika Sekta ya Madini nchini.
Akizungumza leo, Agosti 31, 2026, katika eneo la Nyamongo, Wilaya ya Tarime, Mkoani Mara, Waziri Mavunde ameeleza kuwa programu hiyo ni mkakati wa Serikali wa kuondoa uchimbaji wa kubahatisha na kuelekea kwenye uchimbaji wa kisasa unaotumia sayansi, teknolojia, na data sahihi za kijiolojia. Hafla hiyo imeenda sambamba na uzinduzi wa utafiti wa kina wa madini unaofanywa na Kampuni ya Barrick Gold Corporation.
Waziri Mavunde amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa maelekezo yake ya kutenga asilimia 10 ya mapato ya Sekta ya Madini kwa ajili ya tafiti za kina, hatua inayowewezesha maeneo mapya kubainishwa na kutengwa kwa ajili ya wananchi.
Pamoja na pongezi hizo, Waziri Mavunde ameishukuru kampuni ya Barrick kwa kurudisha leseni na kukubali kufanya utafiti katika eneo la kilomita za mraba 6,000 Nyamongo kwa ajili ya wachimbaji wadogo. Amemwelekeza Kamishna wa Madini, akishirikiana na Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), kuhakikisha mitambo ya uchorongaji inafika eneo hilo mara baada ya utafiti wa awali kukamilika.
Akiweka msisitizo kwa watendaji wa serikali, Waziri Mavunde amebainisha kuwa atawapima Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa ya Kimadini kwa kigezo cha utoaji wa haraka wa leseni na utengaji wa maeneo ya uchimbaji kwa ajili ya makundi ya vijana na wanawake. Pia amewataka viongozi wa wachimbaji kuweka pembeni tofauti zao ili migogoro isiwe kikwazo cha programu hiyo.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Mara, Brigedia Jenerali Evans Mtambi, ameeleza kuwa kukosekana kwa taarifa sahihi za kijiolojia ndiyo iliyokuwa changamoto kubwa kwa wachimbaji wadogo, na kwamba programu hiyo na tafiti zinazoendelea zitasaidia kupunguza hasara na kuongeza tija.
Naye Meneja Mkazi wa Barrick Gold nchini, Dkt. Melkiory Ngido, amebainisha kuwa kampuni hiyo inajivunia kushirikiana na Serikali kwa kurudisha eneo hilo ili liwe chanzo cha ajira na fursa za kiuchumi kwa jamii inayozunguka mgodi.
Akimshukuru Waziri na Serikali, Makamu wa Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Madini Tanzania (FEMATA), Victor Tesha, ameeleza kuwa wachimbaji wadogo wana imani kubwa na programu hiyo ya MBT na wanaisubiri kama mkombozi wa maisha yao na familia zao. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI:
Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga limetoa taarifa ya kifo cha askari wake mwenye namba H.1796 Koplo Mwita, aliyefariki dunia akiwa anashikiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Wilaya ya Tanga kwa ajili ya uchunguzi
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Almachius Mchunguzi, tukio hilo lilitokea Agosti 27, 2026 majira ya saa 1:03 usiku, ambapo askari huyo alikutwa amefariki ndani ya chumba cha mahabusu.
Taarifa hiyo imesema kabla ya kifo chake, Koplo Mwita pamoja na Afisa mmoja na askari watano wa Jeshi la Polisi wa vyeo mbalimbali walikuwa wakishikiliwa kwa tuhuma za kijinai, na baada ya uchunguzi wa kisayansi kufanyika pamoja na ndugu zake kushuhudia, ulibaini kuwa chanzo cha kifo ni kukosa hewa kutokana na kujinyonga, huku mwili wake ukikabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya taratibu za mazishi.
"Jeshi la polisi mkoa wa Tanga linaendelea kusisitiza dhamira yake ya kuhakikisha kuwa uchunguzi wa tukio hili unaendelea kukamilishwa kwa kuzingatia taratibu zote za kiuchunguzi kwa mujibu wa Sheria, kanuni na taratibu", imesema sehemu ya taarifa hiyo
Katika hatua nyingine, Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga limewataka Wananchi, vyombo vya habari na watumiaji wa mitandao ya kijamii kuepuka kusambaza taarifa ambazo hazijathibitishwa kuhusu tukio hilo, likisisitiza kuwa kufanya hivyo ni kinyume cha sheria. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Prof. Kitila Mkumbo @kitilam amesema Serikali inalenga kuhakikisha ukuaji wa uchumi wa Tanzania unaenda sambamba na ongezeko la ajira na kipato kwa wananchi.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Wiki ya Ubunifu Tanzania 2026 uliofanyika leo Agosti 31, 2026 jijini Dar es Salaam, Prof. Mkumbo amesema utekelezaji wa Dira 2050 hautapimwa kwa takwimu za ukuaji wa uchumi pekee, bali pia kwa uwezo wa uchumi huo kuzalisha ajira na kuboresha maisha ya wananchi.
“Uchumi hauwezi kukua kwenye takwimu pekee, lazima ukue kwenye mifuko ya wananchi wetu. Ukuaji wa uchumi unaonekana pale ambapo wananchi wanapata kipato zaidi kupitia ajira au biashara.”
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH, Dkt. Amos Nungu, amesema katika kujenga mfumo imara wa ubunifu nchini, ni muhimu kuanzia kwenye maono makubwa yaliyowekwa katika Dira ya Taifa 2050, ikiwemo lengo la kujenga uchumi wa Tanzania unaofikia thamani ya dola trilioni moja za Marekani ifikapo mwaka 2050
“Tunapofikiria mfumo wa ubunifu tunaohitaji, ni muhimu kuanzia kwenye maono makubwa yanayoendesha Dira ya Taifa 2050. Dira yetu inatutaka kujenga uchumi wa dola trilioni moja za Marekani, na ubunifu ni miongoni mwa nyenzo muhimu za kufikia lengo hilo.” amesema Dkt. NunguThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwekezaji raia wa Marekani Timothy Cook Draper(Tim Draper) ametangaza kuwa anauza kisiwa chake cha Lupita kilichopo Ziwa Tanganyika nchini Tanzania kwa dola milioni 7.9(Zaidi ya bilioni 20 za kitanzania) akieleza kuwa ni mahali pazuri lakini hawapatumii vizuri.
Tim alitoa taarifa hiyo kupitia ukurasa wake wa X Agosti 28, 2026 akieleza kuwa anayehitaji kununua kisiwa hicho awasilane naye kwa mawasiliano yake binafsi.
Taarifa hii ya Tim imetengeneza mjadala mkubwa na maswali mengi juu ya umiliki huo ambapo kwenye cha ukurasa wa 154 wa kitabu chake How to Be the Startup Hero: A Guide and Textbook for Entrepreneurs and Aspiring Entrepreneurs Tim alieleza kuwa hakuna bima wala umiliki wa karatasi kutoka kwa serikali ya Tanzania kwenye kisiwa hicho bali walipewa tu OK kutoka kwa mji wa jirani.
Leo Agosti 31, 2026 Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi imetolea ufafanuzi umiliki wa Tim Draper ikieleza kuwa ardhi ya kisiwa hicho kinamilikiwa na Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi (TISEZA) na imeipangishia kampuni ya Firelight Safaris Ltd ambayo Tim ni mmoja wa wanahisa wa kampuni hiyo lakini sio wamiliki wa asili wa ardhi hiyo.
"Hivyo kampuni ya Firelight Safaris Ltd ni mwekezaji halali katika eneo hilo na anaweza kuhamisha uwekezaji wake kwenda kwa mwekezaji mwingine kwa kuzingatia sheria na taratibu za Nchi." Imesema taarifa hiyo ya WizaraThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, amesema katika kutekeleza majukumu yake hatarajii kupendwa na kila mtu, akisisitiza kuwa kipaumbele chake ni usalama wa Taifa na kuhakikisha Wananchi wanapata haki zao kwa mujibu wa sheria.
“Sitegemei kupendwa kwa sababu mimi sio hela wala ice cream, na sitegemei kupendwa na wahalifu, ilimradi Taifa letu linabaki salama na watu wanapata haki zao kwa mujibu wa sheria,” alisema.
Aidha, Katambi amesema kila mtu ana haki ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akisisitiza umuhimu wa mamlaka za Serikali kutumika kwa mujibu wa sheria bila kumpa mtu yeyote hadhi ya kuwa juu ya sheria.
Waziri Katambi amesema hayo leo, Agosti 31, 2026, mkoani Dodoma, wakati wa uzinduzi wa kampeni ya msamaha wa usalimishaji wa silaha haramu kwa hiari. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Agosti 31, 2026 John Mnyika ambaye ni Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ameendelea kutoa ushahidi wake kama shahidi wa pili wa upande wa utetezi katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa chama hicho ngazi ya taifa, Tundu Lissu na kumaliza ushahidi huo.
Kesi hiyo imeahirishwa mpaka saa 8 na nusu mchana ambapo shahidi Mnyika atakabiliana na maswali ya dodoso kutoka upande wa mashtaka.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, ameagiza Jeshi la Polisi kuwanyang'anya silaha watu wanaozitumia kama mapambo au kujionyesha hadharani, akisema kitendo hicho kinaweza kuhatarisha usalama wao na jamii kwa ujumla.
Katambi ametoa agizo hilo leo, Agosti 31, 2026, jijini Dodoma, wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Msamaha wa Usalimishaji wa Silaha Haramu kwa Hiari 2026, ambapo amesisitiza kuwa silaha hazipaswi kumilikiwa kwa ajili ya kutafuta sifa au kuonyesha uwezo katika jamii.
Waziri Katambi amesema baadhi ya vijana wamekuwa na tabia ya kuonyesha silaha zao katika maeneo ya starehe, ikiwemo kuzitoa na kuziweka mezani wanapokuwa baa, hali ambayo amesema inaweza kuwavutia watu wenye nia ya kuzichukua na kuzitumia kwa madhara. "Sasa hatumiliki silaha kwa fashion.
Tunamiliki silaha palipo na matishio ya usalama," amesema.
Akizungumzia kauli ya Dotto Magari kuhusu umiliki wa silaha, ya kusema "na hapa ipo", Katambi amesema kauli hiyo inaweza kuwapotosha watu na kuwaingiza katika mazingira hatarishi, akisisitiza kuwa kumiliki silaha si jambo la kujivunia wala njia ya kutafuta umaarufu katika jamii.
"Kumekuwa na wimbi fulanj la vijana hata yule ambaye hana matishio, ule msemo wa Dotto Magari wa kusema na hapa ipo, kitendo cha kusema na hapa ipo, Kamanda wa jeshi la polisi IGP utawapa maelekezo", Amesema Waziri katambi
Katambi amesema raia wanaomiliki silaha wanapaswa kuzingatia masharti na taratibu zilizowekwa kwa mujibu wa sheria, huku akieleza kuwa wanaoruhusiwa kubaki na silaha ni wale wanaokidhi matakwa ya kisheria. Amesema serikali haitaruhusu silaha kutumiwa kwa mtindo wa 'fashion' au kama nyenzo ya kujionyesha mbele ya jamii. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP), Camillius Wambura, amezindua kampeni ya msamaha wa usalimishaji wa silaha haramu kwa hiari, 2026 jijini Dodoma, akiwahimiza Wananchi kutumia fursa hiyo kusalimisha silaha walizonazo kinyume cha sheria bila hofu.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, leo Agosti 31, 2026, IGP Wambura amesema kampeni hiyo inalenga kuimarisha usalama wa wananchi na kuzuia matumizi ya silaha haramu katika vitendo vya uhalifu, akieleza kuwa ushirikiano wa Wananchi na vyombo vya ulinzi na usalama ni nguzo muhimu ya kudumisha amani nchini.
“Tunawaomba wananchi wajitokeze kusalimisha silaha haramu walizonazo kwa hiari. Lengo letu ni kuimarisha usalama na kulinda amani ya nchi yetu,” amesema IGP Camillius Wambura.
Aidha, IGP Wambura amesema Jeshi la Polisi litaendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa kumiliki silaha kwa kufuata sheria na taratibu zilizowekwa, huku akisisitiza kuwa kampeni hiyo ni sehemu ya jitihada za kuondoa silaha haramu katika jamii. -
Jambo TV
@Jambotv_
Katibu wa NEC Organaizesheni wa Chama cha Mapinduzi CCM Paul Matiko Chacha @PaulMchacha_ amesema kuwa chama hicho sio chama cha maneno pekee bali ni chama cha matendo.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram leo Agosti 31, Chacha ameeleza kuwa watanzania wana imani na chama hicho na imani hiyo imejengwa kwenye misingi ya kazi, matokeo na dhamira ya kuwatumikia.
"Imani ya Watanzania kwa Chama chetu (CCM) ina msingi katika kazi, matokeo na dhamira ya kuwatumikia wananchi...CCM si chama cha maneno pekee ni chama cha vitendo, uwajibikaji na kuendelea kujenga Tanzania bora." ameandika Chacha.
Yapi maoni yako? -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI PICHA
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo jana jumapili tarehe 30 Agosti 2026 aliongoza harambee ya kuchangia ujenzi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Turiani mkoani Morogoro ambapo zaidi ya Shilingi milioni 80 zilikusanywa huku yeye binafsi akichangia Shilingi milioni 10 na marafiki zake wakichangia Shilingi million 20.
Katika harambee hiyo Prof.Kitila aliongozana na Mbunge wa Mikumi ambaye pia ni Naibu Waziri wa Viwanja na Biashara, Denis Londo pamoja na Mbunge wa Mvomero, Sarah Msafiri. -
Jambo TV
@Jambotv_
Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita linamshikilia Jackline Peter, mkazi wa Mji Mdogo wa Katoro, Wilaya ya Geita, kwa tuhuma za kumshambulia kwa fimbo Rahel Jumanne, akimtuhumu kumuibia Shilingi 60,000.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Sophia Jongo, tukio hilo lilitokea Agosti 26, 2026, majira ya saa 5:00 asubuhi, katika nyumba ya mtuhumiwa iliyopo Katoro.
Kamanda Jongo amesema kabla ya tukio hilo, Jackline alidai kupoteza fedha hizo zilizokuwa kwenye pochi yake iliyokuwa chumbani, ndipo akaanza kumtilia shaka Rahel, ambaye alikuwa amemtembelea nyumbani kwake.
Amesema baada ya kubaini fedha hizo hazikuwepo, mtuhumiwa alimkamata Rahel na kuanza kumpiga kwa kutumia fimbo.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, wakati tukio hilo likiendelea, mtuhumiwa alimtaka mfanyakazi wake wa ndani kurekodi tukio hilo kwa kutumia simu yake, kabla ya baadaye kusambaza video hiyo kwenye mitandao ya kijamii.
Kamanda Jongo amesema Jeshi la Polisi lilipobaini video hiyo kwenye mitandao ya kijamii, lilianza ufuatiliaji na kufanikiwa kubaini eneo lilipotokea tukio, kumtambua mtuhumiwa na kumkamata.
Amesema mtuhumiwa anaendelea kuhojiwa wakati Jeshi la Polisi likikamilisha uchunguzi wa tukio hilo, na kwamba baada ya uchunguzi kukamilika atafikishwa katika mamlaka husika za kisheria kwa hatua zaidi.
Jeshi la Polisi limetoa wito kwa wananchi kuacha vitendo vya kujichukulia sheria mkononi na badala yake kutoa taarifa kwa mamlaka husika pale wanapodhani mtu amehusika na uhalifu.
“Tuhuma za uhalifu hazimruhusu mtu mwingine kutoa adhabu mwenyewe, bali anapaswa kutoa taarifa kwa mamlaka za kisheria kwa hatua zaidi,” imeeleza taarifa hiyo. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Hali ya sintofahamu imeibuka ndani ya Chama Cha Wafugaji Tanzania (CCWT), baada ya baadhi ya viongozi na wajumbe wa chama hicho kutuhumiana matumizi mabaya ya madaraka ikiwamo ubadhirifu wa fedha na mali za chama, hali inayodaiwa kuchangia kushuka kwa kasi ya usajili wa wanachama.
Madai hayo yameibuka siku chache baada ya taarifa za kudaiwa kukamatwa kwa Katibu Mkuu wa chama hicho, kwa tuhuma zinazohusishwa na matumizi mabaya ya ofisi.
Baadhi ya wajumbe na wanachama wa CCWT wameeleza kutoridhishwa na namna fedha zinazotokana na usajili wa wanachama zinavyosimamiwa, wakidai kuwa viongozi wamekuwa wakilaumu vyombo vya dola huku wakitafuta huruma ya wafugaji, wakati fedha hizo ambazo zilipaswa kugawanywa na kurejeshwa katika maeneo ya wanachama kwa ajili ya kutatua changamoto zao wilayani na vijijini, hazijulikani zilipo.
Akizungumzia hali hiyo, Samweli Nyarandu, mwanachama wa CCWT na Katibu wa Chama hicho Wilaya ya Maswa, Kanda ya Nyanza, amesema katika wilaya yake alifanikiwa kusajili zaidi ya wanachama 300 ambapo kwa kila mwanachama aliyesajiliwa, Shilingi 9,000 zilitakiwa kurejea wilayani kwa ajili ya kuendesha shughuli za chama, lakini fedha hizo hazijarejea kama ilivyotarajiwa. Amesema kila wanapojaribu kupata ufafanuzi kutoka kwa viongozi wa juu, hawapati majibu ya kueleweka.
Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa CCWT, Kusundwa Wamalwa, amekiri kuwepo kwa malalamiko kutoka kwa baadhi ya wafugaji, akisema baadhi yao wamefikia hatua ya kuwasilisha malalamiko kwa Msajili wa Vyama vya Kiraia.
Wamalwa amesema moja ya malalamiko hayo yanahusu fedha zinazolipwa wakati wa usajili wa mwanachama, ambapo mwanachama hulipa Shilingi 22,000. Amesema katika kiasi hicho, Shilingi 10,000 ni kwa ajili ya kadi, huku Shilingi 9,000 zikitarajiwa kurejea katika wilaya husika kwa ajili ya kusaidia uongozi wa chini kuendesha shughuli za chama.
Amesema utaratibu huo umeingia dosari na kusababisha kushuka kwa kasi ya usajili wa wanachama. Aidha, amedai kuwa manunuzi ya gari la chama hayakufuata utaratibu unaotakiwa.
Akijibu tuhuma hizo kwa njia ya simu, Mwenyekiti wa CCWT, Mrida Mshota, amewapuuza Makamu Mwenyekiti wake pamoja na wajumbe wanaotoa malalamiko hayo, akiwataja kuwa ni wahuni na wanaharakati ambao, kwa madai yake, hawana hata mifugo.
Kuhusu madai ya kurejeshwa kwa Shilingi 9,000 kwa kila mwanachama wilayani, Mshota amesema hakuna utaratibu huo ndani ya chama. Aidha, amesema endapo Makamu Mwenyekiti wake alikuwa na taarifa au malalamiko ambayo anaona hayako sawa, alipaswa kuyawasilisha katika vikao vya chama badala ya kuyazungumza nje ya vikao.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Chama cha ACT Wazalendo kimeitaka Serikali kuangalia upya tozo ya uendelezaji wa miundombinu ya bandari (Port Infrastructure Development Fee – PID), kikionya kuwa tozo hiyo imeanza kupandisha bei za bidhaa na inahatarisha kuwakimbiza watu kwenda kutumia bandari shindani za nchi nyingine.
Msimamo huo umetolewa leo Jumapili, Agosti 30, 2026, na Waziri Kivuli wa Ujenzi, Uchukuzi na Miundombinu wa ACT Wazalendo, Mtutura Abdallah Mtutura, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tozo hiyo ya asilimia 4.5 ambayo Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) ilianza kuitekeleza rasmi Julai 1, 2026.
Mtutura ameeleza kuwa kuna mkinzano mkubwa katika maamuzi ya serikali. Wakati serikali ikijinasibu kuongezeka kwa mapato na ufanisi wa kiutendaji katika Bandari ya Dar es Salaam, inashangaza kuona bado inarudi kuwatoza wafanyabiashara tozo kwa ajili ya kujenga miundombinu hiyo. Ameongeza kuwa, ingawa serikali inaweza kuamini kuwa ‘inayemkamua’ ni mfanyabiashara, ukweli ni kwamba mwananchi wa kawaida ndiye anayeumia zaidi.
Vilevile, ameonya kuwa tozo hiyo haibagui na inawakandamiza hata wateja kutoka nchi jirani kama Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Zambia, na Malawi. Ameonya kuwa nchi jirani zinaweza kuamua kutumia bandari mbadala kama Beira (Msumbiji) au Lobito (Angola) na hivyo kuifanya Tanzania ‘ijikaange’ yenyewe kiushindani.
Hata hivyo, tofauti na msimamo wa ACT Wazalendo, baadhi ya wadau wakubwa wa bandari nchini wamekuwa wakijitokeza kuitetea tozo hiyo. Chama cha Mawakala wa Forodha Tanzania (TACAS) na Baraza la Wasafirishaji Shehena Tanzania (TSC) wanasisitiza kuwa ujenzi wa miundombinu ya kisasa kupitia rasilimali za ndani ni jambo lisiloepukika ili kukabiliana na kasi kubwa ya ukuaji wa mizigo na kuongeza ufanisi.
Wamebainisha kuwa tofauti na kodi zingine, makusanyo ya PID yanasimamiwa kwa misingi thabiti ya kisheria ili yaende moja kwa moja kwenye ujenzi wa miundombinu mipya ya bandari, na hakuna fedha itakayopotea au kutumika katika matumizi ya kawaida ya kiutawala.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Serikali itaendelea kushirikiana kwa karibu na Kanisa Katoliki katika masuala mbalimbali ya kijamii na kiroho, kutokana na kutambua na kuthamini mchango wake mkubwa katika maendeleo ya taifa.
Dkt. Nchemba ameyasema hayo Agosti 30, 2026, mkoani Katavi, aliposhiriki maadhimisho ya Jubilei ya miaka 25 tangu kuanzishwa kwa Jimbo Katoliki la Mpanda, kufuatia mwaliko maalum wa Askofu wa Jimbo hilo, Mhashamu Eusebius Alfred Nzigilwa.
Amebainisha kuwa Serikali ya Awamu ya Sita, chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, itaendelea kuheshimu uhuru wa kuabudu na kupokea ushauri kutoka kwa viongozi wa dini, ili kuhakikisha Tanzania inaendelea kubaki kuwa nchi ya amani, utulivu, na inayolinda haki za binadamu.
Maadhimisho hayo ya miaka 25 ya Jimbo Katoliki la Mpanda yamelenga kutambua safari ya robo karne ya jimbo hilo katika kutoa huduma za kiroho, elimu, afya, na ustawi wa jamii mkoani Katavi na maeneo ya jirani.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Serikali imesema itaendelea kuhakikisha uwekezaji mkubwa unaofanyika katika sekta ya maji unawafikia wananchi kwa kuwapatia huduma ya maji safi na salama.
Akizungumza wakati wa ziara ya Kamati ya Bunge ya Maji na Mazingira iliyokagua mradi wa maji Kigamboni jijini Dar es Salaam, Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema Serikali imetenga zaidi ya Shilingi bilioni 23 kwa ajili ya mradi huo.
“Mheshimiwa Rais alitupatia zaidi ya bilioni 23 za fedha za ndani kujenga mradi huu, kuhakikisha Wanakigamboni wanapata huduma ya maji safi na salama… sasa jukumu letu ni kuhakikisha maji haya yanawafikia wananchi.”
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maji na Mazingira Jackson Kiswaga amesema kamati hiyo imeridhishwa na maendeleo ya mradi, ikiwemo uzalishaji wa maji kutoka katika visima 11 unaofikia takribani lita milioni 37 kwa siku, wakati mahitaji ya Kigamboni yakiwa takribani lita milioni 7 kwa siku.
“Kwa kweli tumejionea maendeleo makubwa. Uzalishaji wa maji kutoka katika visima 11 hapa Kigamboni ni mkubwa… ombi letu kwa Wizara ni kuhakikisha maji haya yanawafikia wananchi mpaka kwenye majumba yao.”, ameeleza.
Kamati hiyo pia imeitaka Serikali kuendelea kulinda vyanzo vya maji ili uwekezaji huo uwe endelevu, huku wananchi wa Kigamboni wakihimizwa kutumia fursa ya kuunganishiwa huduma ya maji kwa shilingi 80,000 iliyotolewa na Wizara.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Chama cha ACT Wazalendo @ACTwazalendo kimeitaka Serikali kusitisha mara moja utoaji wa vibali vipya vya ujenzi wa Bandari Kavu (ICDs) katikati ya jiji la Dar es Salaam, huku kikipendekeza kuondolewa kwa utaratibu maalum kwa zile zilizopo ili kupunguza msongamano wa mizigo na maroli jijini.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumapili, Agosti 30, 2026, Waziri Kivuli wa Ujenzi, Uchukuzi na Miundombinu wa chama hicho, Mtutura Abdallah Mtutura, ameeleza kuwa si vyema kuzifunga bandari hizo kwa ghafla kwani haiwezekani, bali wamiliki wapewe muda wa mpito wa kati ya miezi mitatu hadi miezi sita ili kuondoa mizigo iliyopo bila kuruhusiwa kupokea mizigo mipya.
Mtutura amesisitiza kuwa mizigo yote mipya inapaswa kuelekezwa katika bandari kavu ya Kwala mkoani Pwani.Sambamba na hilo, ACT Wazalendo inapendekeza wamiliki wa bandari kavu wapewe maeneo yaliyopangwa nje ya jiji la Dar es Salaam kulingana na uelekeo wa mizigo husika
Katika kuondoa msongamano wa maroli jijini, chama hicho kimeainisha maeneo mapya matatu ya kimkakati kulingana na mwelekeo wa nchi na mikoa. Kwa mfano, mizigo inayokwenda mikoa ya kusini inapaswa kuelekezwa katika wilaya ya Mkuranga ambapo kuna maeneo makubwa. ACT imependekeza kuwa wananchi wa maeneo hayo wapewe fidia ili serikali ichukue ardhi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Kundi jingine la mamia ya wanafunzi wa Kitanzania limeondoka nchini kuelekea katika vyuo vikuu mbalimbali duniani kuanza masomo ya elimu ya juu, kupitia uratibu wa Taasisi ya Global Education Link (GEL).
Wanafunzi hao walioondoka nchini kupitia Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Terminal 3, jijini Dar es Salaam, wamechagua zaidi fani za kimkakati za sayansi na teknolojia zinazohitajika katika soko la sasa la ajira. Fani hizo ni pamoja na Computer Engineering, Cyber Security, Artificial Intelligence (AI), Civil Engineering, taaluma za afya, sheria, pamoja na biashara.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa GEL, Meneja wa Tawi la Dar es Salaam, Micky Musa, ameeleza kuwa kuondoka kwa wanafunzi hao ni muendelezo wa mpango kabambe wa kuwaunganisha vijana wa Kitanzania na fursa za elimu zenye viwango vya kimataifa.
Musa amebainisha kuwa mbali na kundi hilo lililoelekea nchini India, GEL inaendelea kukamilisha maandalizi ya wanafunzi wengine wanaotarajiwa kwenda masomoni nchini China, Malaysia, Marekani, na Uingereza.
“Kadiri muda unavyokwenda Watanzania wataendelea kuona makundi mengine ya wanafunzi yakiondoka. Tunawaomba vijana wenye ndoto ya kusoma nje ya nchi wafike katika ofisi zetu zilizopo Dar es Salaam, Dodoma, Zanzibar, Mwanza, na Arusha. Muda bado upo; njoo na matokeo yako, nasi tutakusaidia kufanya ndoto yako kuwa uhalisia,” amesema Musa.
Pamoja na kutoa wito kwa vijana, amewahimiza wazazi na walezi kutumia ofisi za GEL kupata ushauri wa kitaalamu kuhusu uchaguzi sahihi wa vyuo, kozi zenye tija, michakato ya udahili, utafutaji wa visa, na maandalizi yote ya safari.
Kwa upande wao, baadhi ya wanafunzi walioondoka wameeleza kuwa uamuzi wao wa kusomea masuala ya kompyuta, usalama wa mtandao, na akili bandia (Artificial Intelligence) unatokana na kasi kubwa ya mabadiliko ya kiteknolojia na mchango wake katika kukuza uchumi wa kisasa. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Hali ya maji katika Mto Ruvu unaosimamiwa na Bodi ya Maji Bonde la Wami Ruvu imeelezwa kuwa ni himilivu, licha ya kuwepo kwa changamoto ya ukame katika maeneo mbalimbali.
Akizungumza Agosti 29, 2026, Mkurugenzi wa Bodi ya Maji Bonde la Wami Ruvu, Mhandisi Elibariki Mmassy amesema kiwango cha maji kilichopo mtoni kwa sasa ni takribani mita za ujazo 11,200, wakati mahitaji ni mita za ujazo 6,000, huku kiasi cha maji kinachoelekea baharini kikiwa takribani mita za ujazo
“Hali ya mto kwa sasa ni himilivu. Bado kuna maji ya kutosha na shughuli kubwa zinazofanywa na Wami Ruvu pamoja na Wizara na Serikali katika kulinda vyanzo vya maji ndiyo maana Jiji la Dar es Salaam, Pwani na Morogoro yanaendelea kupata maji mpaka hivi sasa.” Ameeleza.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) imeazimia kwamba viongozi wakuu wa Chama hicho watawekeza nguvu zao zote katika kumsaidia Mwenyekiti wa Chama, Tundu Lissu, katika utetezi wa kesi ya uhaini inayomkabili, baada ya baadhi yao kuitwa kuwa mashahidi wa utetezi.
Hayo yamebainishwa na Naibu Katibu Mkuu Bara wa Chama hicho, Amani Golugwa leo Agosti 29, alipokuwa akizungumza na Waandishi wa habari Dar es Salaam.
"Kamati Kuu imezingatia kuwa baadhi ya viongozi wakuu wa chama wanashiriki kama mashahidi wa utetezi katika hatua hii ya kesi ya Mwenyekiti na hivyo Kamati Kuu imeazimia kwamba viongozi hawa wakuu wa Chama wawekeze nguvu zao zote katika suala hili la kumsaidia Mwenyekiti kama mashahidi wake wa upande wa utetezi.”
Golugwa amesema hatua hiyo ni muhimu kwa kuzingatia hatua iliyofikiwa katika kesi hiyo, ambapo Lissu ameanza kutoa utetezi wake, huku akisisitiza kuwa hana hatia.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) imeazimia kusogeza mbele kikao cha Baraza Kuu la chama hicho hadi tarehe nyingine, ili kutoa nafasi kwa viongozi wakuu wa Chama kushiriki kikamilifu katika kesi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA.
Akizungumza na waandishi wa habari, Naibu Katibu Mkuu Bara wa Chama hicho Amani Golugwa, amesema uamuzi huo umetolewa leo, Agosti 29, 2026, katika kikao cha Kamati Kuu kilichofanyika jijini Dar es Salaam, ambapo pamoja na mambo mengine, wajumbe wamejadili maandalizi ya Baraza Kuu na mwenendo wa kesi hiyo.
Kabla ya kuahirishwa, kikao hicho lilitarajiwa kufanyika Septemba 15, 2026 ambapo tarehe ya kufanyika haijatajwa ambapo Golugwa amesema itapangwa
Kuhusu kesi ya uhaini, Kamati Kuu imewaelekeza viongozi wakuu wa chama kuelekeza nguvu katika kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika mchakato wa kesi hiyo.
Aidha, Kamati Kuu imeeleza kuwa CHADEMA itaendelea kuongeza nguvu katika kudai Katiba Mpya, huku ikisisitiza umuhimu wa kuongeza nguvu katika kuhakikisha Mwenyekiti wa Chama anaachiwa, kwa msimamo wa chama kwamba hana hatia.
Katika kikao hicho pia, Kamati Kuu imepokea taarifa kuhusu michango ya “Tone kwa Tone” kuelekea Baraza Kuu la chama, ambapo jumla ya shilingi milioni 302 zimekusanywa.
Kamati Kuu imewapongeza na kuwashukuru wanachama wote walioshiriki katika zoezi hilo la uchangishaji.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo Zanzibar, Ismail Jussa Ladhu, amesema baadhi ya watu wamekuwa wakilalamikia ushirikiano na mikutano kati ya viongozi wa Zanzibar na Serikali ya Muungano, akidai kuwa hali hiyo inatokana na ukweli kwamba Rais Samia Suluhu Hassan anatoka Zanzibar.
Jussa amesema Wazanzibari wamekuwa wakipigania maslahi na mamlaka ya Zanzibar kwa muda mrefu, kupitia hoja za kikatiba, kisheria, kiutawala na kimfumo, akisisitiza kuwa misingi hiyo haipaswi kuachwa kwa sababu ya tofauti binafsi.
Ameongeza kuwa, harakati hizo zimekuwa zikisimamiwa na viongozi mbalimbali, akiwemo Marehemu Maalim Seif Sharif Hamad, pamoja na viongozi waliopo sasa, akiwataja Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo, Othman Masoud Othman, na viongozi wengine wanaoendelea kusimamia maslahi ya Zanzibar.
Jussa amesisitiza kuwa haoni sababu ya baadhi ya watu kulalamikia viongozi wa Zanzibar kukutana na kushirikiana na viongozi wa Serikali ya Muungano, akisema kukutana huko hakumaanishi kuachana na misingi ya kupigania mamlaka na maslahi ya Zanzibar.
Jussa amesema hayo leo Agosti 29, 2026, akiwa katika ziara ya ACT Wazalendo, katika ukumbi wa Majid Hall, Mjini Magharibi, Unguja.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwanahabari nguli nchini, Jenerali Ulimwengu, amesema Tanzania inapaswa kujipa muda katika kujenga mifumo bora ya kidemokrasia, akitolea mfano uchaguzi wa ndani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wa mapema Januari 2025, kama miongoni mwa chaguzi za mfano zilizofanyika kwa uwazi.
Akizungumza katika Jukwaa la Demokrasia, jana Agosti 28, 2026, Ulimwengu amesema Tanzania itaendelea kuwepo kwa miaka mingi, hivyo hatua zinazochukuliwa sasa zinapaswa kuzingatia pia vizazi vijavyo.
“Tujipe muda, tusiwe na haraka. Tunakwenda wapi? Nchi hii itakuwepo miaka mia tatu, mia tano ijayo. Tunatengeneza si tu kwa ajili yetu sisi, ni hao wanaokuja baada yetu.”
Amesema suala la uchaguzi linapaswa kuangaliwa kwa umakini, akitaja malalamiko ya madai ya Wananchi kunyimwa uhuru wa kuchagua viongozi wanaowataka.
Ulimwengu amesema katika kipindi cha miaka kadhaa iliyopita, uchaguzi wa ndani wa CHADEMA umeonyesha kiwango cha uwazi na ushindani ambacho, kwa mtazamo wake, kinaweza kulinganishwa na mifumo ya uchaguzi inayosifiwa katika baadhi ya nchi za Afrika.
Ametaja Botswana, Ghana, Cape Verde na Mauritius kuwa miongoni mwa nchi ambazo zimekuwa zikisifiwa kwa namna chaguzi zao zinavyoendeshwa.
Kwa mujibu wa Ulimwengu, tofauti kubwa ni namna mchakato wa kupiga na kuhesabu kura unavyosimamiwa kwa uwazi, akisema uchaguzi wa ndani wa CHADEMA uliwahi kuonesha mfano wa utaratibu huo.
“Kura zinapigwa na hakuna ile ya kusema "ukishapiga kura, ondoka nenda nyumbani kajenge nchi". Nakwenda kujenga nchi gani? Najenga nchi kwa kuangalia uchaguzi inakwendaje hapa. Na wakati wa kuhesabu, zinachukuliwa kura moja moja na wananchi wanaona. Kila kura inasopolewa moja moja, inawekwa hapa, nyingine hapa mpaka mwisho, ndivyo wanavyofanya nchi zilizostaharabika"
Ulimwengu amesisitiza kuwa Tanzania inapaswa kutumia muda kujenga mifumo inayowapa Wananchi uhuru wa kuchagua viongozi wanaowataka, badala ya kufanya mabadiliko kwa haraka bila kujenga msingi imara.
“Tujipe raha ya kupumzika, tufanye kazi tukiwa tumetulia.”, amesisitiza UlimwenguThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Wakilj Boniface Mwabukusi, amesema Tanzania inahitaji umakini, kusikilizana na kukubali makosa ili kujenga maridhiano na kuanza mchakato wa uponyaji wa taifa.
Mwabukusi amesema hayo jana, Agosti 28, 2026, katika Jukwaa la Demokrasia, akisisitiza kuwa taifa halihitaji vitisho wala kutukanana katika kipindi hiki, bali linahitaji kukabiliana na changamoto zilizopo na kutafuta suluhisho la pamoja.
“Hatuhitaji vitisho. Hatuhitaji kutukanana. Lazima tukubali tumekosea. Na wote tuwe tayari kusikilizana. Sisi wanaharakati tuwe tayari kusikilizana, Serikali iwe tayari kutusikiliza na vyama viwe tayari kusikilizwa.”
Amesema changamoto inayolikabili taifa si ya kisiasa pekee, bali ni ya kijamii, hivyo inahitaji mchakato wa uponyaji na haki ya mpito unaozingatia waathirika.
Mwabukusi amesema haki ya mpito haipaswi kuangalia tu upande wa makosa ya jinai, bali pia kuangalia waathirika waliopoteza mali na ndugu zao, akisisitiza umuhimu wa marejesho ya haki (reparations).
Aidha, Mwabukusi amesema Tanzania inahitaji kwanza kujenga mazingira ya uponyaji na utulivu wa fikra kabla ya kuingia katika mjadala mpana wa Katiba.
“Sasa unataka tuanze kuingia kwenye hii Katiba toka article 1 hadi mia thelathini na ngapi, wakati article 3 tu tumenyofoana roho? Sasa tukianza kujadili hii Katiba nzima kabla hatujatengeneza na kuleta ile healing process na utulivu wa fikra, huko ni kuruka kwenye tanki la petroli na sigara mdomoni, hatutanusurika,” amesema Mwabukusi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Karibu katika fursa nyingine kubwa ya uwekezaji. Hapa ni Eneo Maalum la Kiuchumi Bagamoyo, chini ya Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania @InvestTanzania lenye takribani hekta 9,800 zilizotengwa kwa ajili ya shughuli mbalimbali za uwekezaji. Eneo hili sasa linazidi kubeba sura mpya ya Tanzania ya viwanda, likivutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.
Miongoni mwa wawekezaji ni kampuni ya HWTZ kutoka China, inayotekeleza mpango wa kujenga kongani ya viwanda itakayojumuisha zaidi ya viwanda 150.
Mkurugenzi wa Bagamoyo SEZ Felix Michael anaeleza kuwa kampuni hii ni moja kati ya wawekezaji makubwa ya uzalishaji wa viwanda 500 kutoka nchini China wapo Bagamoyo wakiwa wamekabidhiwa hekta 500 kwa ajili ya utekelezaji wa kongani hiyo kubwa kuliko zote barani Afrika ambayo inatarajiwa kujumuisha viwanda zaidi ya 150 huku ikizalisha ajira zaidi ya 5,000.
Mradi huo utakapokamilika, ukiwa na viwanda vya kuunganisha magari madogo na makubwa, pamoja na kiwanda cha bidhaa za chuma kitakachozalisha coil, nondo na bidhaa za galvanized iron. Hii ina maana ya kuongeza uzalishaji wa bidhaa ndani ya nchi, kupanua fursa za ajira na kutoa nafasi kwa Watanzania kupata ujuzi na teknolojia katika sekta ya viwanda.
Kwa TISEZA, uwekezaji huu ni zaidi ya kujenga viwanda. Ni sehemu ya jitihada za kujenga uchumi unaotegemea uzalishaji, kuongeza ajira na kuimarisha ushiriki wa sekta binafsi. Kupitia kurahisisha usajili wa miradi, vibali na huduma mbalimbali za uwekezaji, TISEZA inalenga kupunguza urasimu na kuweka mazingira yanayomwezesha mwekezaji kuanzisha na kukuza biashara kwa ufanisi.
Na nyuma ya hatua hizi kuna mwelekeo mpana wa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambao umeweka msisitizo katika kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji, kuvutia mitaji na kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na sekta binafsi. Kuanzishwa kwa TISEZA na msukumo wa kurahisisha huduma kwa wawekezaji ni sehemu ya mwelekeo huo. Bagamoyo sasa si eneo la uwekezaji pekee, bali ni taswira ya Tanzania inayojenga mazingira bora kwa mitaji, viwanda, ajira na uchumi unaozalisha ndani ya nchi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) imesema inapongeza na kuunga mkono uamuzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kumfuta uanachama Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, ikidai kuwa kiongozi huyo alikosa maadili na kushindwa kufuata taratibu, kanuni na Katiba ya CCM.
Hayo yamebainishwa leo Agosti 28, 2026 na Mwenyekiti wa UWT, Mary Chatanda jijini Dodoma ambaye amesema taratibu na miongozo yote ya chama imefuatwa katika kufikia uamuzi huo, hivyo hatua hiyo haikuchukuliwa kwa bahati mbaya bali imezingatia misingi na kanuni za chama.
Aidha, Chatanda amesema uamuzi huo unaakisi wazi kuwa ndani ya CCM hakuna mtu aliye juu ya chama, hakuna mwenye umaarufu unaozidi chama, wala hakuna anayeweza 'kukibagaza au kukidhalilisha' chama hicho kisha akanyamaziwa. Amesisitiza kuwa kila mwanachama, bila kujali cheo au nafasi yake, anapaswa kuheshimu taratibu, kanuni na misingi ya CCM.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
MNYIKA AINGIA KIZIMBANI, ASEMA YEYE NDIYE ALIYEANDAA MKUTANO WA APRILI 3, SI LISSU jambo.co.tz/mnyika-aingia-kizimbani-asema-yeye-ndiye-aliy… via @jambotv_
-
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
John Mnyika ambaye ni Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), amepandishwa kizimbani mchana huu wa Agosti 28, 2026, kama shahidi wa pili wa upande wa utetezi katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa chama hicho ngazi ya taifa, Tundu Lissu.
Kesi hiyo imeahirishwa mpaka Jumatatu Agosti 31, 2026 ambapo Mnyika ataendelea kutoa ushahidi wake baada ya muda wa mahakama siku ya leo kuisha.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Profesa Anna Kajumulo Tibaijuka, amesema Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimekuwa katika mapambano ya kuleta mabadiliko nchini kwa muda mrefu, akilinganisha juhudi hizo na mapambano ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.
Akizungumza leo katika Jukwaa la Demokrasia, Profesa Tibaijuka amesema mapambano ya Mwalimu Nyerere ya kudai uhuru wa Tanganyika yalidumu kwa takribani miaka 7, kuanzia mwaka 1954 hadi 1961, wakati CHADEMA imekuwa ikiendelea na mapambano yake kwa muda mrefu zaidi.
“Hawa wenzetu juhudi inaendelea, tuwape nguvu, lakini kazi ni ngumu kwa sababu kubadili 'establishment' ya ndani, mjue ni ngumu kuliko kuwabadilisha 'external establishment',” amesema Profesa Tibaijuka.
Aidha, Profesa Tibaijuka amesema Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inaweza kufanyiwa mabadiliko ili kutoa nafasi zaidi kwa demokrasia, ikiwemo suala la usajili wa vyama vya siasa akitoa mfano kupitia vijana wanaojaribu kusajili chama cha siasa lakini wamekumbana na vikwazo, huku akieleza kuwa suala hilo sasa liko mahakamani.
“Sasa ngoja niwaambie nyie Wanasheria, wameshindwa hawa vijana, wanataka kuandikisha chama cha Siasa, wamewekewa mizingwi, sasa hivi wako Mahakamani wanapambana,” amesema.
Miongoni mwa mabadiliko aliyopendekeza Prof. Tibajuka kwenye katiba ya 1977 ni pamoja na mabadiliko ya uandikishaji wa Vyama vya siasa pamoja na suala la uraia pacha.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Rais wa Tanganyika Law Society, (TLS), Wakili Boniface Mwabukusi, amesema Tanzania ina watu wenye uwezo, uadilifu na wanaokubalika na jamii wanaoweza kusaidia kuunganisha taifa na kutatua changamoto zinazolikabili, endapo watapewa nafasi bila kujali nani aliwateua.
Akichangia mjadala katika Jukwaa la Demokrasia Tanzania, Mwabukusi ametaja viongozi na wasomi mbalimbali akiwemo Jaji Joseph Warioba,Prof. Issa Shivji, akisisitiza kuwa Tanzania ina hazina ya watu wenye uzoefu ndani ya nchi.
“Tuna watu humu ndani, ambao bado wana uadilifu na wanakubalika na wananchi; hawa ndio watumike kulileta taifa pamoja.”
Mwabukusi amesema mchakato huo unaweza kuanza kwa uwakilishi mpana, huku akipendekeza pia kutumia wataalamu na waangalizi kutoka nje pale inapohitajika, ili kusaidia kuondoa vikwazo vilivyowahi kukwamisha michakato ya mazungumzo ya kitaifa, ikiwemo mchakato wa Katiba.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Jaji Mstaafu, Joseph Sinde Warioba amesema licha ya kuwepo kwa matarajio ya Tanzania kupata Katiba mpya, haoni uwezekano wa mchakato huo kukamilika kufikia mwaka 2029.
Akizungumza katika Jukwaa la Demokrasia leo Agosti 28, 2026, Jaji Warioba amesema Serikali inapaswa kuangalia njia mbadala za kushughulikia changamoto zilizopo, akionya kuwa kuendelea na uchaguzi bila kushughulikia hoja hizo kunaweza kulisababishia taifa madhara makubwa.
“Kuhusu kupata Katiba nilisema mimi sioni uwezekano wakupata Katiba kufika mwaka 2029 sioni uwezekano wa hiyo”, amesema Jaji Warioba
Amesisitiza kuwa wananchi bado wanaomboleza kutokana na yaliyotokea Oktoba 29, 2025 akieleza kuwa hali hiyo haiwezi kupuuzwa.
“Bado tunaomboleza Wananchi wanaomboleza lakini ukiangalia kama serikali naona hakuna kikubwa”
Jaji Warioba ameongeza kuwa madhara na majeraha yaliyotokea ni makubwa na haipaswi kuonekana kana kwamba yatasahaulika na taifa kuendelea na maisha ya kawaida.
"Madhara tuliyopata majeraha tuliyopaya ni makubwa na inaonekana ni kama tunakwenda kwa mwendo wa kusema, twende hivi yatasahaulika tutaendelea kama kawaida”, amesema Jaji Warioba -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Profesa Issa Shivji amesisitiza umuhimu wa uwazi katika utendaji wa Serikali, akisema Wananchi wana haki ya kujua maamuzi yanayofanywa kwa niaba yao, hususan katika mikataba na masuala ya uwekezaji.
Profesa Shivji amesema Katika Kongamano la Jukwaa la Demokrasia Tanzania ambapo amesema mara nyingi wananchi wanapouliza kuhusu mikataba huambiwa kuwa taarifa hizo ni siri, licha ya kuwa rasilimali zinazohusika ni za wananchi.
“Serikali inapofanya mambo kwa niaba yetu, kwa nini sisi tusijue? Tunaambiwa mikataba ni siri, hakuna transparency. Ndiyo maana ni muhimu kusisitiza uwazi, kwa sababu jambo mnalolifanya kwa niaba yetu, lazima tujue.” Ameeleza Shivji
Prof. Shivji amesema hayo leo Agosti 28, 2026 katika Jukwaa la Demokrasia linaloendelea sasa Jijini Dar es Salaam -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Jaji Mstaafu Joseph Sinde Warioba amesema hatua ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kumvua uanachama Dkt. Emmanuel Nchimbi, imeibua maswali kuhusu nafasi ya ukweli na uhuru wa kutoa maoni ndani ya chama hicho.
Warioba ametoa kauli hiyo wakati akizungumza katika Jukwaa la Demokrasia Tanzania, akirejelea taarifa za CCM kumchukulia hatua Nchimbi kwa tuhuma mbalimbali, baada ya aliyekuwa Makamu wa Rais kujiuzulu nafasi hiyo.
Amesema jambo hilo linampa wasiwasi kuhusu utashi wa kisiasa, hususan pale ambapo kusema ukweli au kutoa mtazamo unaotofautiana na msimamo wa chama kunatafsiriwa kama kuchochea fitina.
“Ukiangalia ahadi zetu wana CCM, moja inasema ‘nitasema kweli daima’, ipo kwenye ahadi zetu lakini siku hizi ukisema ukweli unaanzisha fitina.”
Akizungumzia zaidi tuhuma zinazohusishwa na hatua hiyo dhidi ya Nchimbi, Warioba amesema hali hiyo inapaswa kuibua tafakari pana kuhusu mwelekeo wa siasa nchini na iwapo kuna utashi wa kisiasa wa kuendelea na mjadala wa masuala muhimu badala ya kuyasahau.
“Katika tuhuma ambazo inasemekana amepewa ni kusema hivyo na hiyo ndiyo inanipa wasiwasi, kweli tuna utashi wa siasa? Ama tunatia tuendelee hivi tusahau?”, Amesema Jaji Warioba -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Heche, amesema Tanzania ipo katika kipindi kinachohitaji viongozi na Wananchi kusema ukweli ili kulinda mustakabali wa Taifa.
Heche amesema ameguswa na kauli za Jaji Joseph Sinde Warioba kuhusu hali ya nchi, akisema hoja zilizotolewa zinapaswa kuchukuliwa kwa uzito, ikiwemo suala la Katiba Mpya na uwajibikaji kutokana na matukio ya Oktoba 29, 2025 na siku zilizofuata
Amesema suluhisho la kupata uwajibikaji ni kuzidisha mashinikizo kutoka ndani na nje ya nchi, huku akisisitiza kuwa chanzo cha matatizo mengi ni mfumo wa uchaguzi na matumizi ya mamlaka kubaki madarakani.
“Kwa maoni yangu, hoja iliyopo hapa lazima tuongeze pressure from within. Watu waliopo madarakani wajue, na pia pressure from outside. Tusipolitatua hilo, kama alivyosema Mzee Warioba, nchi hii itatoa wakimbizi.” Amesema Heche
Heche amesema hayo akichangia hoja katika Jukwaa la Demokrasia Nchini, linalofanyika leo Agosti 28, 2026 Jijini Dar es SalaamThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha NCCR - Mageuzi, James Mbatia amesema Tanzania inahitaji Katiba Mpya ili kutatua changamoto zinazowakabili Wananchi na kujenga misingi ya haki, usawa na utawala bora, akisemaa mabadiliko ya Kikatiba yanaweza kuwa mwanzo wa kuponya migawanyiko na maumivu ambayo Wananchi wamekuwa wakiyapitia.
Akizungumza katika jukwaa la demokrasia, leo Agosti 2026, Mbatia amesema "Tuone hali ya msingi itakayoponya kwa kiasi kikubwa madonda ya wale ambao wameumizwa miaka yote hiyo kupata katiba ambayo inajenga mfumo wenye kukuza uhai wa mwanadamu”
Mbatia ameongeza kuwa Katiba Mpya itatoa nafasi kwa wananchi kushiriki kikamilifu katika maamuzi yanayohusu mustakabali wa nchi, akisisitiza mchakato huo unapaswa kuwa wa wazi na jumuishi ili kuakisi matakwa ya Watanzania wote.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwanataaluma Prof. Issa Shivji amesema taifa lipo katika kipindi cha maombolezo kutokana na kukosekana kwa uwajibikaji kuhusu yaliyotokea Oktoba 29, akisisitiza kuwa hali hiyo inahitaji wananchi kuendelea kushikamana na kutafakari njia za kujenga haki, amani na utawala bora.
Akizungumza leo, Agosti 28, 2026, katika Jukwaa la Demokrasia Tanzania (Tanzania Democracy Forum), Prof. Shivji amesema ni muhimu mazungumzo kuhusu haki ya mpito na mustakabali wa taifa kuendelea, ili kusaidia kupata suluhisho la changamoto zinazolikabili taifa.
“Tuko kwenye maombolezo, lakini tunapaswa kuendelea kusimama pamoja na kutafuta haki na mwelekeo bora wa nchi yetu,” alisema Prof. Shivji -
Jambo TV
@Jambotv_
Kesi ya uhaini namba 19605/2025 inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Antiphas Lissu, inafikia hatua nyingine muhimu leo Ijumaa, Agosti 28, 2026, ambapo shauri litarejea mchana huu ikitazamiwa shahidi wa pili wa upande wa utetezi kuanza kutoa ushahidi wake kizimbani.
Hatua hiyo imekuja mara baada ya shahidi wa kwanza, ambaye pia ni mshitakiwa katika kesi hiyo, Tundu Lissu, kumaliza kutoa maswali ya ufafanuzi (Re-examination) kufuatia kukamilika kwa maswali ya dodoso (Cross-examination) kutoka kwa upande wa mashtaka.
Ingawa haijabainika ni kiongozi gani wa CHADEMA atakayesimama kuanza kutoa ushahidi baada ya mapumziko ya mchana, rekodi za mahakama zinaonesha kuwa viongozi waandamizi waliokuwa wamebaki kwenye orodha iliyoruhusiwa na mahakama kutoa ushahidi ni pamoja na Katibu Mkuu wa CHADEMA John Mnyika, Naibu Katibu Mkuu Bara Amani Golugwa, na Makamu Mwenyekiti Bara John Heche, na Brenda Rupia, ambaye ni Mkurugenzi wa Habari, Mawasiliano na Uenezi CHADEMA.
Macho na masikio ya wengi sasa yameelekezwa katika kipindi cha mchana huu kuona jinsi gani shahidi huyo wa pili atakavyoendelea kushusha ushahidi wa kuusambaratisha ushahidi wa uhaini uliowasilishwa na upande wa serikali. -
Jambo TV
@Jambotv_
Baada ya upande wa mashtaka (Jamhuri) kuhitimisha zoezi la maswali ya dodoso kwa shahidi wa kwanza ambaye pia ni mshtakiwa katika kesi ya uhaini, Tundu Lissu leo asubuhi Agosti 28, 2026, Lissu alisimama na kuiomba Mahakama kufanya Maswali ya ufafanuzi (Re-Examination) ambapo aliruhusiwa baada ya mjadala wa dakika kadhaa za hoja za upande wa jamhuri za kutaka kufahamu atafanyaje hivyo ikiwa Lissu anajiwakilisha mwenyewe kisheria.
Lissu alieleza kuwa haki ya kufanyiwa maswali ya ufafanuzi ni ya kisheria chini ya Kifungu cha 156(1) cha Sheria ya Ushahidi na kwamba kujiwakilisha mwenyewe hakuwezi kumnyima haki hiyo. Ameongeza kuwa hofu ya Serikali kuhusu yeye kuibua mambo mapya haina msingi, kwani Serikali inayo haki ya kuweka mapingamizi wakati wowote atakapovuka mipaka.
Baada ya jopo la majaji kuruhusu mchakato huo uendelee, Lissu alisimama kizimbani na kuanza kushusha ufafanuzi mzito wa kisheria juu ya masuala mbalimbali yaliyoibuliwa wakati wa mahojiano ya dodoso, akijikita katika kubomoa hoja za serikali na kuweka kumbukumbu sawa.
Lissu alianza kwa kufafanua jibu lake la "siyo kweli" alilolitoa asubuhi ya leo kuhusu kama nia ya kutenda kosa inathibitishwa na tendo husika. Alieleza kuwa siyo makosa yote ambayo nia yake inathibitishwa na matendo, kwani kuna makosa mengine ambayo nia yake inathibitishwa tofauti na matendo yenyewe, na hasa katika kesi za uhaini, tafsiri ya nia ina umuhimu wa kipekee wa kisheria.
Wakati wa dodoso, Lissu alibanwa kuhusu sababu za kutokuleta mahakamani tuzo zake za kimataifa alizozitaja. Akifafanua jambo hilo, Lissu alirejea kanuni kuu za ushahidi wa jinai zinazobainisha kuwa mshtakiwa hana wajibu wowote wa kuthibitisha kuwa hana hatia; badala yake, mzigo mzima wa uthibitishaji wa mashtaka na hatia upo mikononi mwa upande wa mashtaka pekee.
Lissu aligusia pia suala la "Constructive Publication" lililoibuliwa na upande wa serikali kuhusu video ya Jambo TV. Alieleza kuwa kisheria, uchapishaji wa namna hiyo unaweza tu kutokea ikiwa mshitakiwa ana mamlaka au udhibiti (control) juu ya uchapishaji husika. Lissu alifafanua kuwa yeye hakuwa na udhibiti wowote juu ya waandishi wa habari waliokuwa wanarusha matukio hayo live.
Lissu alielezea mashahidi wa siri (wa kificho) kama P1, P2, na P3. Alifafanua kuwa mashahidi hao hawajulikani na mtu yeyote ikiwemo mahakama yenyewe na upande wa utetezi isipokuwa na mawakili wa serikali waliowaleta, jambo linalofanya ushahidi wao kutoaminika. Lissu aliwaita mashahidi hao kuwa ni "wahalifu" kwa sababu walikiri kwa maandishi na kwa mdomo mahakamani kuwa walipanga njama za kufanya vurugu, na sheria inawachukulia kama wahalifu pindi wanapokiri wenyewe vitendo hivyo vya jinai mbele ya mahakama.
Mwishoni mwa utetezi wake, Lissu alitumia vielelezo vya maandishi D1, D2, D5, D15, na D14 kuonesha jinsi maafisa wa polisi walivyokiuka sheria kwa "kujishuhudia wenyewe". Kielelezo D1 (John Kaaya) alisema kina sehemu ya saini ya mtoa maelezo na afisa aliyeandika lakini iliandikwa na Kaaya na kujishuhudia mwenyewe badala ya kuandikwa na askari mwingine.
Amesema kielelezo D2 cha Shahidi PW3 kilisainiwa na mtu mmoja kama mtoa maelezo na shuhuda. Kielelezo D5 (PW6), saini ya mtoa maelezo na ya afisa zimepigwa saini moja iliyogusa pande zote. Kielelezo D15 (Amini Mahamba): Kila ukurasa una saini ya mtoa maelezo lakini saini ya afisa aliyeshuhudia utoaji maelezo haijajazwa kabisa.
Aidha ameeleza kuhusu kielelezo D14 (PW15 Koplo Amani Michael). Amesema huyu ndiye shahidi pekee wa polisi ambaye kielelezo chake kipo sahihi kisheria kwasababu kina saini mbili tofauti zilizothibitishwa vyema.
Baada ya kumalizika kwa maswali ya ufafanuzi (Re-examination), jopo la majaji liliafiki kukamilika kwa ushahidi wa Tundu Lissu na kuahirisha shauri hilo hadi saa nane kamili mchana wa leo ili kuruhusu shahidi wa pili wa upande wa utetezi kupanda kizimbani kuanza kutoa ushahidi wake. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwanataaluma Prof. Issa Shivji amesema taifa lipo katika kipindi cha maombolezo kutokana na kukosekana kwa uwajibikaji kuhusu yaliyotokea Oktoba 29, 2025, akisisitiza kuwa hali hiyo inahitaji wananchi kuendelea kushikamana na kutafakari njia za kujenga haki, amani na utawala bora.
Akizungumza leo, Agosti 28, 2026, katika Jukwaa la Demokrasia Tanzania (Tanzania Democracy Forum), Prof. Shivji amesema ni muhimu mazungumzo kuhusu haki ya mpito na mustakabali wa taifa kuendelea, ili kusaidia kupata suluhisho la changamoto zinazolikabili taifa.
“Tuko kwenye maombolezo, lakini tunapaswa kuendelea kusimama pamoja na kutafuta haki na mwelekeo bora wa nchi yetu,” alisema Prof. Shivji -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mjadala kuhusu hali ya demokrasia nchini Tanzania umeendelea kuibua hoja mbalimbali, huku Prof. Issa Shivji akisisitiza umuhimu wa kulinda misingi ya msingi ya demokrasia, hususan uhuru wa kujieleza na uhuru wa kujumuika.
Akieleza sababu ya kusisitiza mambo hayo, Prof. Shivji amesema uhuru wa kujieleza una uhusiano wa moja kwa moja na utu wa binadamu, akieleza kuwa utu ndio msingi wa haki na uhuru mwingine unaozungumziwa katika demokrasia.
Akizungumza katika Jukwaa la Demokrasia Tanzania, leo Agosti 28, Prof. Shivji amesema suala la utu wa binadamu halijapewa uzito unaostahili katika mijadala ya kitaifa, akisisitiza kuwa kila mwanadamu anastahili kuheshimiwa bila kujali hadhi yake katika jamii.
Akizungumzia hali halisi katika jamii, Prof. Shivji amesema kuna mazingira mbalimbali yanayoweza kudhalilisha utu wa binadamu, ikiwemo vitendo vya kumteka au kumpoteza mtu, umaskini na ukosefu wa ajira.
“Ukiteka binadamu umedhalilisha utu wake, ukimpoteza binadamu umedhalilisha utu wake. Umaskini unadhalilisha utu wa binadamu, kutokuwa na ajira kunadhalilisha utu wa binadamu.”This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Ilivyokuwa Hatua ya maswali ya dodoso (Cross Examination) kwa Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, alipokuwa akiulizwa na upande wa Jamhuri jana Agosti 27, 2026.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) imetakiwa kujiweka katika nafasi ya kuwa taasisi kiongozi katika utafiti wa madini na jiosayansi nchini na katika ukanda wa Kusini mwa Jangwa la Sahara, kupitia uwekezaji mkubwa katika teknolojia, wataalamu, miundombinu, na uandaaji wa taarifa sahihi za kijiolojia.
Rai hiyo imetolewa Agosti 27, 2026, jijini Dodoma na Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, wakati wa uzinduzi wa Bodi mpya ya GST. Waziri amebainisha kuwa mkakati huo unaenda sambamba na azma ya Serikali ya kuongeza kiwango cha tafiti za kina ili kubaini maeneo mapya yenye rasilimali, kuongeza uwekezaji, na kuondoa uchimbaji wa kubahatisha.
Waziri Mavunde ameeleza kuwa katika kuelekea lengo la kuifikisha Tanzania katika uchumi wa dola trilioni moja, GST inatakiwa kufanya utafiti wa jiolojia katika eneo la kilomita za mraba 50,000 ndani ya Quarter Degree Sheet (QDS) 20, sawa na asilimia 5 ya eneo lote la nchi.
Pamoja na hilo, ameitaka Bodi hiyo mpya kufanya utafiti wa kina katika QDS 23 ili kuongeza kiwango cha taarifa za rasilimali za madini kutoka asilimia 16 za sasa hadi kufikia asilimia 21 ifikapo mwaka 2030, huku akisisitiza matumizi ya mifumo ya kisasa ya kiteknolojia katika utunzaji na usambazaji wa data hizo.
Akizungumza katika hafla hiyo, Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa, ameitaka GST kufanya shughuli zake kwa ushirikiano wa karibu na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) ili kutambua na kuendeleza maeneo yenye uwezekano mkubwa wa upatikanaji wa madini.
Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Msafiri Mbibo, amebainisha kuwa katika miaka 100 ya kuwepo kwake, GST imemudu kufanya mambo makubwa, na kwamba Bodi hiyo mpya inatarajiwa kutatua changamoto zinazowakabili wachimbaji wadogo na kuvutia wawekezaji wakubwa.
Naye Mwenyekiti wa Bodi mpya ya GST, Bi. Yokobeth Myumbilwa, ameishukuru Serikali kwa kuridhia kutengwa kwa asilimia 10 ya makusanyo ya sekta ya madini kwa ajili ya kufanya tafiti, akiahidi kuwa fedha hizo zitatumika kikamilifu kukuza uchumi wa taifa.
Mtendaji Mkuu wa GST, Mhandisi Ally Samaje, amehitimisha kwa kuhakikisha kuwa watumishi na menejimenti ya taasisi hiyo wako tayari kushirikiana na Bodi mpya ili kutimiza malengo yote ya kimkakati yaliyowekwa na Serikali. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwanasheria na Mkurugenzi wa Everlasting Legal Aid Foundation amesema kufutwa uanachama wa CCM kwa aliyekuwa Makamu wa Rais, Dkt. Emmanuel Nchimbi, hakufuti hadhi wala historia yake iliyowekwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Amesema kuna tofauti kati ya mamlaka ya chama na mamlaka ya dola, akieleza kuwa chama kinaweza kuchukua hatua dhidi ya mwanachama wake kwa mujibu wa taratibu zake, lakini suala la mafao na stahiki za aliyekuwa Makamu wa Rais linaongozwa na sheria za nchi.
“Lazima watu watofautishe vitu viwili. Chama kina mamlaka ya kudhibiti masuala yanayomhusu mwanachama wake, lakini hata kama wamemfukuza mwanachama, hakiwezi kumuondolea mtu hadhi au historia iliyowekwa kwa mujibu wa sheria au Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.”
Kwa mujibu wa mwanasheria huyo, kwa kuwa Dkt. Nchimbi alijiuzulu na kujiuzulu kwake kuridhiwa, hadhi yake inabaki kuwa ya aliyewahi kuwa Makamu wa Rais, hivyo historia yake haiwezi kufutwa kwa sababu ya kufukuzwa uanachama.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwanasheria na Mkurugenzi wa Everlasting Legal Aid Foundation, Dkt. Khamis Masoud akizungumzia taarifa ya kujiuzulu kwa Makamu wa Rais, Dkt. Emmanuel Nchimbi, amesema kujiuzulu si udhaifu, bali kunaweza kuwa ishara ya uwajibikaji, heshima na ukomavu wa kimaamuzi kwa maslahi ya umma.
Akitumia mfano wa watu wawili wanaojenga nyumba moja, amesema viongozi wanapokuwa katika nafasi zinazohitaji ushirikiano, kutokubaliana kunaweza kuathiri ufanisi wa shughuli za umma.
“Kujiuzulu ni heshima, ni uwajibikaji, ni jambo linaloleta ukomavu wa kiakili, ukomavu wa kimaamuzi na ukomavu wa kidemokrasia.”
Amesema iwapo Dkt. Emmanuel Nchimbi aliona kuwa katika mazingira yaliyopo ingekuwa vyema Rais kuwa na Makamu wa Rais mwingine, basi uamuzi wa kujiuzulu unaweza kutazamwa kama hatua ya kulinda maslahi ya umma. -
Jambo TV
@Jambotv_
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua Jumanne Abdallah Sagini kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, hiyo ni kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka, na kusainiwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Bakari Machumu leo Agosti 27, 2026.
Beno Moris Malisa ambaye amekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kabla ya uteuzi wa hivi punde, yeye amehamishwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora. Malisa anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Paul Matiko Chacha, ambaye aliteuliwa hivi karibuni kuwa Katibu wa NEC - Idara ya Organizesheni ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). -
Jambo TV
@Jambotv_
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amemteua CP. Salum Rashid Hamduni kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka, na kusainiwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Bakari Machumu leo Agosti 27, 2026.
Kabla ya uteuzi huu, CP. Hamduni alikuwa akihudumu kama Katibu Tawala wa Mkoa (RAS) wa Shinyanga. Uapisho wake utafanyika kwa tarehe itakayopangwa baadaye na Ikulu. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Serikali ya Tanzania na wawakilishi wa sekta binafsi pamoja na mabalozi kutoka Jumuiya ya Ulaya (EU) wamekubaliana kuimarisha mshikamano wa kibiashara na uwekezaji kwa kujikita katika uwekezaji unaolenga uzalishaji wa viwandani na uongezaji thamani wa rasilimali za ndani.
Mkakati huo umewekwa wazi mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa mashauriano wa mazingira ya biashara na uwekezaji uliofanyika katika ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam leo Alhamisi, Agosti 27, 2026.
Akizungumza kwa niaba ya serikali, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo @kitilam , amebainisha kuwa serikali imewapitisha washirika hao katika mageuzi makubwa yaliyofanywa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita katika kuboresha mifumo ya kisheria, kodi, na ardhi nchini.
Profesa Mkumbo ameeleza kuwa wawekezaji hao wamepongeza juhudi zilizochukuliwa na pande zote mbili zimejadili hatua za ziada zinazotakiwa kuchukuliwa ili kuhakikisha wawekezaji wa Ulaya waliopo nchini wanaendelea kubaki na wengine wapya wanakuja kwa wingi.
Naye Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Nicola Brennan, ameonesha nia thabiti ya nchi yake na wawekezaji wa Ulaya katika kuunga mkono utekelezaji wa Dira ya Tanzania ya 2050. Balozi Brennan ameeleza kuwa dira hiyo inatoa mfumo madhubuti wa kukuza uchumi wa nchi, uzalishaji, pamoja na kutengeneza fursa mpya za ajira kwa wananchi
Kwa upande wake, Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Anne Sophie Avé, ameshukuru kwa majadiliano hayo na kuonesha kukubaliana kikamilifu na maelezo yote yaliyowasilishwa na kujadiliwa katika mkutano huo, akiahidi ushirikiano wa dhati na serikali ya Tanzania katika lengo la kuvutia wawekezaji wengi kutoka Ulaya.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Serikali ya Tanzania na wawakilishi wa sekta binafsi pamoja na mabalozi kutoka Jumuiya ya Ulaya (EU) wamekubaliana kuimarisha mshikamano wa kibiashara na uwekezaji kwa kujikita katika uwekezaji unaolenga uzalishaji wa viwandani na uongezaji thamani wa rasilimali za ndani.
Mkakati huo umewekwa wazi mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa mashauriano wa mazingira ya biashara na uwekezaji uliofanyika katika ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam leo Alhamisi, Agosti 27, 2026.
Akizungumza kwa niaba ya serikali, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo @kitilam , amebainisha kuwa serikali imewapitisha washirika hao katika mageuzi makubwa yaliyofanywa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita katika kuboresha mifumo ya kisheria, kodi, na ardhi nchini.
Profesa Mkumbo ameeleza kuwa wawekezaji hao wamepongeza juhudi zilizochukuliwa na pande zote mbili zimejadili hatua za ziada zinazotakiwa kuchukuliwa ili kuhakikisha wawekezaji wa Ulaya waliopo nchini wanaendelea kubaki na wengine wapya wanakuja kwa wingi.
Amesisitiza kuwa msisitizo mkubwa wa Serikali ya Tanzania na Rais wake ni kujikita katika uzalishaji wa viwandani kwa kuongeza thamani ya mazao yanayozalishwa hapa nchini, hususan katika sekta za kilimo na madini ili kukuza uchumi wa viwanda.
Ili kuhakikisha uendelevu wa mikakati hiyo, pande zote zimekubaliana kufanya vikao hivyo kila baada ya miezi sita, ambapo mkutano ujao umepangwa kufanyika mwezi Februari mwaka 2027 chini ya uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, ukishirikisha pia wizara za uwekezaji, fedha, na biashara.
Naye Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Nicola Brennan, ameonesha nia thabiti ya nchi yake na wawekezaji wa Ulaya katika kuunga mkono utekelezaji wa Dira ya Tanzania ya 2050. Balozi Brennan ameeleza kuwa dira hiyo inatoa mfumo madhubuti wa kukuza uchumi wa nchi, uzalishaji, pamoja na kutengeneza fursa mpya za ajira kwa wananchi
“Tanzania ni eneo zuri sana la kuwekeza... lina fursa nzuri sana kwa ajili ya biashara, na kwa kushughulikia changamoto hizi, tutahakikisha kuwa kuna uwekezaji mwingine mkubwa zaidi wa baadaye utakaoifanya Tanzania kuwa nguvu kubwa ya kiuchumi katika ukanda wa Afrika Mashariki na kwingineko,” amesema Balozi Brennan.
Kwa upande wake, Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Anne Sophie Avé, ameshukuru kwa majadiliano hayo na kuonesha kukubaliana kikamilifu na maelezo yote yaliyowasilishwa na kujadiliwa katika mkutano huo, akiahidi ushirikiano wa dhati na serikali ya Tanzania katika lengo la kuvutia wawekezaji wengi kutoka Ulaya. -
Jambo TV
@Jambotv_
Kesi inayomkabili Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Melkisedeki Kitunzi Kaijage, imeahirishwa tena katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma, huku mshtakiwa akiendelea kusota rumande akisubiri shauri lake kuendelea.
Wakili anayesimama upande wa mshtakiwa, Meshack Ngamando, amesema kesi hiyo iliyopangwa kuendelea leo, Agosti 27, 2026, haikuweza kusikilizwa baada ya Hakimu aliyepangwa kusikiliza shauri hilo kutokuwepo Mahakamani. Kwa sababu hiyo, kesi imeahirishwa hadi Septemba 10, 2026, ambapo inatarajiwa kuendelea katika Mahakama hiyo.
Kaijage anakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi yenye namba 16278, inayohusisha tuhuma za makosa chini ya sheria ya kuzuia ugaidi.
Kaijage anatuhumiwa kuwa Julai 3, 2026 akiwa katika maeneo ya UDOM alikuwa na nia ya kuchoma majengo ya umma pamoja na makazi ya askari Polisi katika maeneo mbalimbali nchini, ikiwemo Zanzibar.
Awali, kesi hiyo ilipangwa kuendelea Agosti 19, 2026, lakini haikuendelea baada ya Hakimu Mkazi anayesikiliza shauri hilo, Zabibu Mpangule, kutokuwepo Mahakamani.
Kesi hiyo ilitajwa mbele ya Hakimu Kombe na kuahirishwa hadi leo, Agosti 27, ambapo sasa imeahirishwa tena hadi Septemba 10.
Kwa sasa, Kaijage anaendelea kuwa rumande wakati akisubiri hatua inayofuata ya kesi hiyo, inahusisha uchunguzi wa awali (Preliminary Inquiry) kabla ya shauri hilo kupelekwa Mahakama Kuu kwa ajili ya kusikilizwa. -
Jambo TV
@Jambotv_
Mwandishi wa habari Luqman Maloto amesema historia inaweza kumweka huru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kutokana na matokeo ya miradi mikubwa ya maendeleo iliyotekelezwa na kukamilishwa katika kipindi cha uongozi wake. Maloto ametumia kauli ya mwanazuoni Peter Drucker kwamba uongozi madhubuti hupimwa kwa matokeo, si hotuba wala sifa.
Maloto ametumia kukamilika kwa Mradi wa Kufua Umeme wa Maji wa Julius Nyerere (JNHPP) kama mfano mkuu, akisema Rais Samia alipokula kiapo Machi 19, 2021, mradi huo ulikuwa umefikia asilimia 37, lakini hadi Agosti 22, 2026 ulikamilika kwa asilimia 100. Kwa mtazamo wake, Rais Samia alisimamia asilimia 63 iliyobaki ya utekelezaji wa mradi huo.
Amesema wakati wa utekelezaji wa JNHPP kulikuwa na mashaka kuhusu uwezo wa Rais Samia kukamilisha miradi mikubwa iliyoanzishwa na mtangulizi wake, Hayati Dkt. John Magufuli, huku baadhi ya wakosoaji wakitoa kauli za wazi kwamba asingeweza. Hata hivyo, amesema Rais Samia hakujikita kujibu kwa maneno, bali aliruhusu kazi na matokeo kuzungumza.
Maloto amesema kukamilika kwa JNHPP kunapaswa kutazamwa pia katika historia ya muda mrefu ya wazo la kuzalisha umeme mkubwa katika Mto Rufiji, akibainisha kuwa utekelezaji wa mradi ulianza mwaka 2017 na jiwe la msingi likawekwa mwaka 2019. Ameongeza kuwa katika kipindi cha Rais Samia kulikuwa na mabadiliko kadhaa ya mawaziri wa Nishati, viongozi wa TANESCO na wahandisi wakazi wa mradi, jambo analoliona kama sehemu ya jitihada za kuhakikisha mradi unakamilika.
Akitumia falsafa ya Niccolò Machiavelli kwamba matokeo ya mwisho yanaweza kutoa hukumu kuhusu maamuzi yaliyofanyika, Maloto amesema muda umeanza kutoa majibu kuhusu mjadala wa JNHPP. Ameunganisha hoja hiyo na kauli maarufu ya Fidel Castro, “History Will Absolve Me” — “Historia Itaniweka Huru”, akisema historia mara nyingi hutoa hukumu tofauti na mijadala ya kisiasa ya wakati husika.
Mbali na JNHPP, Maloto ametaja miradi mingine kama upanuzi wa miundombinu ya mabasi ya mwendokasi Dar es Salaam, maendeleo ya reli ya Standard Gauge, kuanza kwa treni za umeme kati ya Dar es Salaam na Dodoma, pamoja na kukamilika kwa Daraja la Kigongo–Busisi, akisema yote yanaweza kuwa sehemu ya kumbukumbu ya utawala wa Rais Samia.
Kwa Maloto, presha za kisiasa na lawama zinazomkabili kiongozi akiwa madarakani si lazima ziwe hukumu ya mwisho ya historia. Amesema baada ya Rais Samia kuondoka madarakani, Watanzania watapata nafasi ya kuangalia nyuma na kutathmini matokeo ya utawala wake kwa upana zaidi, ndipo kazi iliyofanyika katika kipindi chake inaweza kutoa msingi wa historia kumtetea na kumweka huru. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDASA), Prof. Elgidius Ichumbaki, amesema changamoto ya baadhi ya Wanataaluma kushindwa kujenga hoja na kutoa mawazo mbadala, inatokana kwa kiasi kikubwa na hofu ya madhara yanayoweza kujitokeza.
Amesema hayo katika mahojiano maalum na Jambo TV, akieleza kuwa katika mazingira ambayo viongozi wa kisiasa hawapokei kwa urahisi mawazo yanayopingana na misimamo yao, mwanataaluma anayechagua kusema anahitaji moyo na ujasiri, huku akitambua changamoto zinazoweza kujitokeza.
"Kuna Mwanafalsafa mmoja aliwahi kusema, kuwa mjuaji wakati ambapo viongozi wa kisiasa wana changamoto ya kusikia maoni na mawazo mbadala ni kuhatarisha maisha yako. Kwa hiyo Wanataaluma walio wengi tayari wameliona hilo na kwa hiyo wanaweza wakawa wanajitokeza kwa kuandika, kwa kuzungumza, lakini kwa kutoka wazi, kidogo inaleta changamoto. Inahitaji moyo na ujasiri wa kusema nipo tayari kwa lolote litakaloweza kutokea", amesema Prof. Ichumbaki
Kauli hiyo inakuja wakati UDASA ikiwa imewahi kutoa tamko kuhusu hali ya nchi kufuatia matukio ya Oktoba 29, 2025, likigusa masuala ya demokrasia na haki za binadamu, jambo lililoibua mjadala kuhusu nafasi ya Wanataaluma katika masuala ya Kitaifa.
Prof. Ichumbaki amesema jamii haipaswi kuishia kuzungumza tu, bali kila mmoja kwa nafasi yake anapaswa kuwa sehemu ya kuleta mabadiliko na kujenga kesho bora kwa Watoto na Vizazi vijavyo. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
NJOMBE: Wakazi wa kijiji cha Ihanga, Kata ya Ukwama, Wilaya ya Makete wameingiwa na hofu ya miradi yao ikiwemo majengo ya shule kubaki tupu, kutokana na upungufu wa Wanafunzi wanaofikia 83 kwa shule nzima ya msingi Ihanga.
Wakizungumza na Jambo TV, wakazi wa kijiji hicho akiwemo Askabernad Sanga, Lea Sanga pamoja na John Sanga wanasema huenda sababu kubwa iliyopelekea upungufu wa wanafunzi ni kutokana na vijana wengi kukimbia Kijiji chao kwasababu ya changamoto za kimazingira kama ubovu wa miundombinu ya barabara.
Wanasema sababu nyingine iliyopelekea upungufu huo ni kutokana na matumizi ya njia za uzazi wa mpango, kwa kuwa zimepelekea watu wengi kuishia kuzaa Watoto Wawili mpaka watatu, huku pia taarifa zisizo rasmi zikibainisha kuwa ni takribani Watoto watatu wanaozaliwa kwa mwaka katika kijiji hicho
Hata hivyo Serikali haijawatupa wakazi wa Kijiji hicho, wanaofikia 439 huku nguvu kazi ikiwa ni 153 ambapo imefanikisha kusogeza huduma zote za msingi ikiwemo Shule yenye majengo mapya ya kisasa, umeme, maji pamoja na kuimarisha kilimo hususani cha viazi na kupelekea waliohama kijiji kuanza kurejea taratibu pamoja na wageni kuingia.
Dkt. Jonathan Kitundu, Kaimu Mganga Mkuu wa halmashauri ya Makete anasema suala la uzazi wa mpango ni la hiari hivyo hakuna sababu ya Wananchi kujizuia kuzaa.
Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Njombe imefika katika kijiji hicho kukagua miundombinu ya shule, ambapo katibu wa Chama Julius Peter akitoa wito kuendelea kuzaa kwa kuwa takwimu bado zinaonyesha Mkoa wa Njombe una idadi ndogo ya watu wanaofikia 889,946 kulingana na takwimu za Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022
"Jitihada zinahitajika ili madarasa haya yapate wanafunzi maana Serikali imeleta Madarasa halafu walimu wanakaa na wanafunzi wawili,hapa Dkt.Samia Suluhu Hassan anawadai" amesema Julius PeterThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi @CCMTanzania imepokea na kupitisha jina la Deogratius Ndejembi(Waziri wa Nishati) kushika nafasi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Taarifa hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa chama hicho Balozi Dkt Asha-Rose Migiro leo Agosti 26, 2026 akieleza kuwa uamuzi huo umeamuliwa na Halmashauri Kuu ya chama hicho kilichokaa leo jijini Dar es Salaam.
Dkt. Migiro ameeleza uamuzi huo umefikiwa mara baada ya kujiuzulu na kuvuliwa uanachama kwa Makamu wa Rais Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi.
Aidha Dkt. Migiro ameeleza kuwa baada ya kupendekeza na kupitishwa jina hilo mchakato wa kikatiba utaendelea ikiwemo jina hilo kwenda kupigiwa kura bungeniThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Chama cha Mapinduzi CCM kimetangaza kumvua uanachama Makamu wa Rais Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi
Taarifa hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Chama hicho Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro leo Agosti 26, 2026 akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba.
Dkt. Migiro ameeleza kuwa uamuzi huo umefikiwa mara baada ya kukaliwa kwa vikao vya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya chama hicho ambavyo vilijadili suala la maadili ya Dkt. Nchimbi na vikaazimia kwa pamoja kumfuta uanachama mwanachama huyo.
Ikumbukwe jana Agosti 25, 2026 Dkt. Nchimbi alitangaza kujiuzulu nafasi yake ya Makamu wa Rais kwa kile alichoeleza kuwa amejidhihirisha pasina shaka kuwa Rais Samia Suluhu Hassan anahitaji Makamu mwingine wa RaisThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimetangaza kumvua uanachama Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi.
Uamuzi huo umetangazwa usiku wa leo na Katibu Mkuu wa CCM Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro akizungumza na wanahabari juu ya maazimio ya vikao vya kamati kuu na halmashauri kuu vya chama hicho vilivyoketi leo mkoani Dar es Salaam -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Nchini (LHRC) kimekutana na wadau wa masuala ya 'Haki Ardhi' kutoka Asasi na Mashirika mbalimbali, kwaajili ya kuwasilisha ripoti ya utafiti ilioufanya kwenye Mikoa saba (7) ya Tanzania Bara kuhusu uvunjifu wa Haki za Binadamu unaotokana na migogoro ya Ardhi Nchini
Akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya kumalizika kwa kikao kazi hicho, Wakili Maduhu Williams kutoka LHRC ametaja Mikoa hiyo kuwa ni pamoja na Pwani, Tanga, Morogoro, Tabora, Kigoma, Mara na Katavi
Amesema katika utafiti wake, LHRC imebaini matukio mengi ikiwemo migogoro inayohusisha wananchi na wananchi kama vile migogoro ya wakulima na wafugaji, wananchi na wawekezaji, wananchi na Hifadhi za Taifa zilizopo chini ya TAWA, TFS nk, lakini pia wamebaini uwepo wa migogoro inayohusisha wananchi na mamlaka/ taasisi mbalimbali za serikali
"Baada ya kupata taarifa ile LHRC, tumeona ni muhimu tukakutana na wadau nao tuwasikilize wanasemaje na wana maoni gani kwenye taarifa hii, tumekuwa na kikao kizuri karibu siku nzima, tumewasilisha matokeo ya utafiti ule na wadau wametoa maoni yao, na maboresho kuhusiana na taarifa ile, baada ya hapa tunaenda kuandaa taarifa fupi ya kisera ambayo tubatarajia kuiwasilisha kati ya mwezi wa tisa au wa kumi kwenye management za Wizara mbalimbali serikalini" -Wakili Maduhu
Akizungumza baada ya kumalizika kwa kikao hicho kilichofanyika Morogoro Mjini, mmoja wa washiriki ambaye ni Mtaalamu wa masuala ya Ardhi -Landesa Wakili Masawe Luhula amesema ni vyema kama Nchi tukatazama upya mfumo wa usimamizi wa ardhi kwa ujumla wake katika kutazama ushiriki wa moja kwa moja kwenye uamuzi wa masuala ardhi, sambamba na kutazama taasisi za Kitaifa zenye uwezo wa kuwakilisha kikamilifu mawazo ya wananchi kwenye maeneo ya usimamizi ikiwemo Tume ya Ardhi NchiniThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
#bungeni - Serikali imewataka Wazazi kuwa makini na kushiriki kikamilifu katika ulinzi wa watoto, kufuatia taarifa za upotevu wa watoto ambazo zimekuwa zikiripotiwa kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.
Kauli hiyo imetolewa leo Agosti 26 , 2026 Bungeni jijini Dodoma na Waziri wa mambo ya ndani ya nchi, Patrobass Katambi, wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Kaskazini Unguja, Shadia Haji Omar, aliyehoji kuhusu upotevu wa watoto na hatua zinazochukuliwa na Jeshi la Polisi katika kuwatafuta, pamoja na upatikanaji wa taarifa zitakazosaidia kuwabaini na kuwapata.
Waziri Katambi amesema wazazi wanapaswa kuwa sehemu muhimu ya ulinzi wa watoto katika maeneo mbalimbali, ikiwemo maeneo ya elimu na michezo, ili kusaidia kuimarisha usalama wao.
Aidha, amesema Serikali iko katika hatua za kuwa na mifumo maalumu ya kiusalama kwa ajili ya kufuatilia matukio mbalimbali, ikiwemo matumizi ya kamera katika maeneo tofauti.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mchana wa Agosti 26, 2026, katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar Es Salaam, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu, ameanza kukabiliana na maswali ya dodoso kama shahidi wa kwanza wa utetezi, kutoka kwa mawakili wa serikali wakiongozwa na Nassor Katuga mbele ya jopo la Majaji watatu wakiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru katika kesi ya uhaini inayomkabili.
Hata hivyo, Mawakili wa Serikali hawajamaliza maswali yao kutokana na muda wa mahakama kuisha, hivyo mahakama imeahirisha kesi hiyo mpaka kesho Agosti 27, 2026 saa 3 kamili asubuhi. -
Jambo TV
@Jambotv_
Kesi ya uhaini namba 19605/2025 inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Antiphas Lissu, imeshika kasi kubwa mchana wa Agosti 26, 2026, baada ya kurejea kwa ajili ya maswali ya dodoso (cross-examination) ambapo Lissu kama shahidi wa kwanza amedodoswa na Wakili wa Serikali Mkuu, Nassor Katuga, ambapo mwanasiasa huyo amekiri kuwa kauli za ‘tutakinukisha’ ni zake lakini akasisitiza kuwa hazina shida yoyote kisheria wala hazitengenezi kosa la uhaini.
Joto la maswali hayo ya dodoso lilianza pale Wakili wa Serikali Mkuu alipotaka Lissu athibitishe kama anatambua kuwa Tanzania ni nchi huru iliyopata uhuru Desemba 9, 1961, na kama Mahakama ndicho chombo cha mwisho cha maamuzi ya kisheria. Lissu amekiri kuwa Mahakama hailazimishwi na mamlaka yoyote ya ndani au nje inapotoa uamuzi yake.
Alipoulizwa kama wadhifa wake kama Mwenyekiti wa CHADEMA unampa kinga ya kutoshtakiwa, Lissu alijibu: "Sijaiambia mahakama hiyo, na sina hakika na hilo.
Upande wa serikali ulihoji sababu za Lissu kutoleta tuzo zake za kimataifa (kama vile Bush-Thatcher Award ya IDU) mahakamani kama thibitisho la sifa alizojigambia nazo kizimbani. Lissu alijibu kuwa hana wajibu huo kisheria, “Mimi sina wajibu wa kuthibitisha chochote”.
Katika hatua nyingine, Wakili wa Serikali alimuuliza Lissu kama anakataa maneno yaliyo kwenye hati ya mashtaka yanayosema " Wanasema msimamo huu unaashiria uasi, ni kweli..., kwa sababu tunasema tutazuia uchaguzi, tutahamasisha uasi, hivyo ndivyo namna ya kupata mabadiliko..., kwa hiyo tunaenda kukinukisha..., sana sana huu uchaguzi tutaenda kuuvuruga kwelikweli". Lissu alijibu kuwa ili kuelewa maneno hayo, ni lazima mtu aelewe hotuba nzima. Wakili aliendelea kumuuliza kama maneno hayo ni yake au la, Lissu alijibu "Maneno ni ya kwangu, na hayana shida".
Wakili wa Serikali alimuuliza Lissu kama ana chuki binafsi dhidi ya serikali kutokana na mfululizo wa mapambano yake ya kisiasa. Lissu hakumung'unya maneno bali alijibu thabiti, "Nina chuki dhidi ya uonevu, nina chuki na serikali inayoonea watu".
Aidha, Wakili wa serikali aliunganisha kauli ya Lissu na fujo za uchaguzi zilizodaiwa kupangwa na baadhi ya watu...soma zaidi kupitia jambo.co.tz kwa kiungo hiki
jambo.co.tz/lissu-wakili-wa-serikali-mkuu-walivyovutana-m… -
Jambo TV
@Jambotv_
Kesi ya uhaini namba 19605/2025 inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Tundu Antiphas Lissu, Jumatano Agosti 26, 2026 imefikia hatua ya kusisimua baada ya mwanasiasa huyo kushusha utetezi wake wa mwisho.
Katika ushahidi wake uliodumu kwa masaa kadhaa mbele ya jopo la majaji watatu linaloongozwa na Jaji Dastan Ndunguru, Lissu ameeleza kuwa upelelezi wa kesi inayomkabili umefanyika "kienyeji" na kwa hila za kisiasa, huku akiwananga baadhi ya mashahidi wa upande wa mashtaka (mashahidi wa siri) akisema kuwa waligeuzwa kutoka kuwa wahalifu na kuwa mashahidi wa serikali.
Katika utetezi wake, Lissu aliwachambua mashahidi 17 walioletwa na upande wa mashtaka, kati ya 30 waliokuwa wameorodheshwa hapo awali. Lissu amebainisha kuwa upande wa mashtaka ulishindwa kuwaleta mashahidi 13, jambo ambalo alisema si la bahati mbaya bali lilikusudia kuficha ukweli wa ukamataji wake.
Amesema katika mashahidi 17 waliofika mahakamani mashahidi 8 walikuwa ni maafisa wa polisi wanaofanya kazi chini ya IGP Camilius Wambura na DCI Ramadhan Kingai, watu ambao Lissu ameeleza kuwa ana migogoro na chuki nao ya binafsi kwa takribani miaka 24 kutokana na harakati zake za kupinga ukandamizaji.
Amesema mashahidi 9 waliobaki walikuwa ni "mashahidi wa siri au kificho" ambao hawajulikani majina yao, makazi yao, wala kazi zao na mahakama au upande wa utetezi, isipokuwa na waendesha mashtaka pekee. Walipewa majina ya kificho kama PW1, PW2, nk.
Lissu amesema kuwa kupitia maelezo ya maandishi ya mashahidi hawa wa kificho (isipokuwa PW4), mashahidi 7 wa kificho walikiri kwa maandishi na kwa mdomo mahakamani kuwa walipanga njama za kufanya uhalifu wa kupiga watu na kuchoma moto majengo wakati wa Uchaguzi Mkuu wa tarehe 29 Oktoba 2025. Polisi waliwatambua na kuwakamata kati ya tarehe 4 na 8 Aprili 2025. Hata hivyo, badala ya kuwashtaki kwa makosa hayo mazito ya jinai na vurugu zilizosababisha vifo vya mamia ya raia, polisi waliwaachia huru kwa maelekezo ya PW16 (ACP Amini Mahamba). Baadaye, polisi waliwapa sharti: "Kubalini kuwa mashahidi dhidi ya Lissu, na tukifanya hivyo tutafuta mashtaka yenu." Mashtaka yao yote yalifutwa baada ya kukubali mpango huo.
"Huu ndio ushahidi wa serikali dhidi yangu... ushahidi wa wahalifu waliokiri kwa maandishi, wakaachiwa huru wakati watu waliuawa kwenye uchaguzi. Ushahidi wa aina hii hauwezi kuwa...Soma zaidi katika tovuti ya jambo.co.tz -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Leo Agosti 26, 2026, katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar Es Salaam, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu, amemaliza kujitetea kama shahidi wa kwanza mbele ya jopo la Majaji watatu wakiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru katika kesi ya uhaini inayomkabili.
Baada ya kumaliza utetezi wake, kesi imeahirishwa kwa saa moja na nusu ikitarajiwa kurejea tena saa 8 na nusu mchana ambapo Lissu atakabiliana na maswali ya dodoso na kama muda utatosha basi mashahidi wengine upande wa utetezi watatoa ushahidi wao. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Madereva wa malori na magari yanayotumia barabara ya Mlima Kitonga mkoani Iringa, wamempongeza Askari wa Usalama Barabarani, Marcus Mongo, kwa juhudi zake za kusimamia mtiririko wa magari katika eneo hilo, hatua ambayo imekuwa ikisaidia kupunguza msongamano na kuepusha ajali.
Kwa kutambua mchango wake, Afande Mongo ametunukiwa Tuzo ya Heshima, cheti pamoja na fedha taslimu Tsh. Milioni 1.5 kama pongezi kwa kazi yake.
Zawadi hizo zimepokelewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, SACP Allan Bukumbi, ambaye amewapongeza madereva hao kwa kutambua na kuthamini mchango wa Jeshi la Polisi kupitia askari huyo.
Aidha, Kamanda Bukumbi amewasisitiza madereva kuendelea kuzingatia sheria za usalama barabarani na kuimarisha ushirikiano na Jeshi la Polisi ili kuongeza usalama kwa watumiaji wote wa barabara.
Hatua hiyo imekuja baada ya Jambo TV, Agosti 5, 2026, kuripoti namna baadhi ya madereva wanaotumia Barabara ya Mlima Kitonga walivyompongeza SSGT Marcus Mongo kwa usimamizi wake wa magari, uliosaidia kupunguza foleni na kuimarisha usalama katika eneo hilo.
Wakizungumza na Jambo TV wakati huo, madereva hao walisema uwepo wa askari huyo uliwarahisishia safari zao na kuongeza usalama, huku wakitoa wito wa juhudi hizo kuendelea ili kupunguza msongamano na ajali katika barabara hiyo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinachokutana leo, Agosti 26, 2026, kinafanyika wakati mjadala kuhusu hatma ya Dk. Emmanuel Nchimbi ukiwa umechukua sura mpya, baada ya jana, Agosti 25, kutangaza kujiuzulu nafasi ya Makamu wa Rais pamoja na kustaafu siasa na utumishi wa umma.
Uamuzi huo unakuja wakati ambapo historia yake ndani ya CCM imewahi kuhusishwa na hatua za kinidhamu.
Mwaka 2017, Nchimbi ambaye wakati huo alikuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Balozi wa Tanzania nchini Brazil, alipewa onyo kali na NEC baada ya chama kumtuhumu kwa makosa yaliyohusishwa na mwenendo wake katika mgogoro wa uteuzi wa mgombea urais wa CCM mwaka 2015. Aliagizwa pia kuomba radhi kwa wanachama na uongozi wa CCM, jambo ambalo Katibu wa Itikadi na Uenezi wakati huo, Humphrey Polepole, alisema alipaswa kulifanya akiwa Brazil.
Katika hatua hiyo ya kinidhamu, Nchimbi pia alifungiwa kwa kipindi cha miezi 12, hali iliyomfanya kukosa sifa za kuwania uongozi ndani ya CCM kwa kipindi hicho. Polepole alieleza wakati huo kuwa adhabu hiyo ni kutokana na mwanachama huyo kurudia kosa lilelile bila ya kujirekebisha.
Jina la Nchimbi pia liliingia kwenye mjadala huo pamoja na la Sophia Simba baada ya wote kuhusishwa na kutoridhishwa na uamuzi wa Kamati Kuu wa kumuondoa Edward Lowassa katika mchakato wa uteuzi wa mgombea urais wa CCM mwaka 2015. NEC ya Machi 2017 ilimvua Simba uanachama, huku Nchimbi akipewa onyo kali.
Historia hiyo inarejea pia katika mazingira ya taarifa zilizozagaa siku chache zilizopita kwamba Nchimbi aliitwa mbele ya Kamati ya Maadili ya CCM. Hata hivyo, si mara ya kwanza jina la Nchimbi kuhusishwa na vikao vya maadili, kwani hata mwaka 2017 mjadala wa hatua za kinidhamu ulihusisha vikao vya juu vya chama na tuhuma za kukiuka maamuzi ya chama.
Sasa, wakati NEC ikikaa leo, kujiuzulu kwa Nchimbi kunafungua ukurasa mpya katika safari yake ya kisiasa na kuibua maswali kuhusu hatua zitakazofuata ndani ya CCM. Kinachosubiriwa ni iwapo kikao hicho kitajadili moja kwa moja uamuzi wake wa kujiuzulu na mustakabali wake ndani ya chama, huku historia ya adhabu aliyowahi kupewa, ikiwemo kufungiwa kwa kipindi cha miezi 12, ikifanya suala hilo kuwa moja ya masuala yanayofuatiliwa kwa karibu katika kikao cha leo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amepokea na kuridhia ombi la kujiuzulu kwa Makamu wa Rais, Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo, Agosti 25, 2026, na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses M. Kusiluka, Nchimbi ameiomba nafasi hiyo kuanzia Septemba 4, 2026.
Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi imeeleza kuwa taratibu za kikatiba za kumpata Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwingine zitachukuliwa kwa mujibu wa Katiba.
Taarifa hii imekuja mara baada ya leo kupitia ukurasa wake binafsi wa Instagram wa Nchimbi kuchapisha taarifa kwa umma juu ya barua aliyomuandikia Rais Samia akiomba kujiuzulu.
"Tarehe 27 Agosti 2025, nilimuahidi Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa nitamsaidia yeye na Nchi yetu kwa uwezo wangu wote na kwa uaminifu. Pia, nilimuhakikishia kuwa siku yoyote akiona anahitaji Makamu mwingine wa Rais, nitaachia nafasi hii. Nimejiridhisha pasipo shaka kuwa Mhe. Rais anatamani mabadiliko, hivyo nimeamua kutimiza ahadi yangu." ilisema taarifa aliyotoa Dkt. Nchimbi leo -
Jambo TV
@Jambotv_
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, ametangaza kujiuzulu nafasi yake ya Umakamu wa Rais kuanzia tarehe 4 Septemba 2026, huku akitangaza pia kustaafu rasmi siasa na utumishi wa umma
Uamuzi huo umewekwa wazi kupitia taarifa yake kwa umma aliyoitoa leo tarehe 25 Agosti 2026 kwenye ukurasa wake wa Instagram ambapo amebainisha kuwa tayari amemwandikia barua ya kujiuzulu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan. Vyanzo kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais vimeithibitishia Jambo TV juu ya taarifa iliyochapishwa kwenye ukurasa wa Dkt. Nchimbi.
Kwa mujibu wa taarifa ya Nchimbi, kujiuzulu kwake kumezingatia Ibara ya 50(2)(c) ikisomwa kwa pamoja na Ibara ya 149(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Balozi Nchimbi amefunguka sababu iliyomfanya kuchukua hatua hiyo akirejea ahadi aliyompa Rais Samia tarehe 27 Agosti 2025. Katika ahadi hiyo, Nchimbi alimhakikishia Rais kuwa angemtumikia kwa uaminifu na uwezo wake wote, lakini pia akamwahidi kuwa siku yoyote ambayo Rais ataona anahitaji Makamu mwingine wa Rais, yeye angeachia nafasi hiyo bila kusita.
Dkt. Nchimbi amebainisha kuwa amechukua uamuzi huo baada ya kujiridhisha kuwa Rais anatamani kufanya mabadiliko katika safu yake ya uongozi.
“Nimejiridhisha pasipo shaka kuwa Mhe. Rais anatamani mabadiliko, hivyo nimeamua kutimiza ahadi yangu,” imeeleza sehemu ya barua hiyo ya kujiuzulu
Kupitia taarifa hiyo, Balozi Nchimbi ametoa shukrani za pekee kwa Rais Samia na Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa imani kubwa waliyoonesha kwake wakati wa utumishi wake. Kadhalika, amewashukuru Watanzania wote kwa ushirikiano mkubwa waliompa katika kipindi chote cha utumishi wake wa umma na kuwahakikishia kuwa ataendelea kuwa raia mwema wa Tanzania. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katika Maadhimisho ya Maulid ya Mtume Muhammad (S.A.W) Kitaifa ya mwaka 2026 yaliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, Mufti wa Tanzania, Dkt. Abubakar Zubeir Ally, ametoa kwa masheikh na viongozi wa dini nchini kutonyamaza kimya mbele ya mmomonyoko mkubwa wa maadili unaolikabili taifa ikiwamo kuwatukana viongozi wakuu wa nchi, akisisitiza kuwa jukumu lao kuu ni kusema na kutoa mawaidha bila uoga wowote
Dkt. Zubeir amebainisha kuwa ni wajibu wa masheikh kusema na kueneza mafundisho yao kupitia hotuba zao, nyadhi zao mbalimbali, na katika hafla zote. Ametahadharisha kuwa endapo viongozi hao watasalia kimya, umma utakabiliwa na hatari ya kupotea na kuangamia kabisa
“Mseme katika hafla mbalimbali, Mashekhe mseme. Msiposema umma utapotea, utaangamia, huu utakuwa hakuna jambo hapa. Nyinyi mkisema, kila siku mkisema, mambo yataeleweka siku moja hata kama siyo leo au kesho,” amesema.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katika Maadhimisho ya Maulid ya Mtume Muhammad (S.A.W) Kitaifa ya mwaka 2026 yaliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, viongozi wakuu wa dini ya Kiislamu nchini wametoa onyo kali dhidi ya kile walichokitaja kuwa mmomonyoko wa maadili, utamaduni wa kutukana viongozi, na fikra potofu kuwa vurugu zinaweza kuleta maendeleo nchini
Katika maadhimisho hayo, imeelezwa kuwa kwa sasa kuna wimbi la vijana wanaodai kutaka maendeleo kwa kutumia vurugu na fujo huku wakiamini kuwa kuwatukana viongozi wa serikali na wa dini ndiyo siri ya kupata mafanikio
Akikemea mtazamo huo, Sheikh Muharram Rashid Mziwanda akizungumza kwa niaba ya Taasisi za Kiislamu ameeleza kuwa tabia hiyo ni “akili ya mgando” na kuhoji: “Uliona wapi fujo zikaleta maendeleo?”
Ameonya kuwa kuwatukana na kuwadhalilisha viongozi ni dalili ya wazi kuwa taifa linakwenda kuharibikiwa na kusisitiza kuwa viongozi wanapaswa kuombewa dua badala ya kulaaniwa ili nchi isipoteze baraka na amani yake
Akijibu hoja hizo na kutilia nguvu mada iliyowasilishwa, Mufti wa Tanzania, Dkt. Abubakar Zubeir Ally, amesisitiza kuwa uhai na uimara wa taifa lolote unategemea sana kubakiwa na tabia njema, maadili, na malezi mema kwa vijana na vizazi vya sasa.
Mufti ameonya kuwa kama jamii itapoteza maadili na kila mtu akaamua kujifanyia mambo anavyotaka, basi taifa hilo litakuwa limekwisha kabisa.
Kufuatia ombi maalum alilopewa na Sheikh Muharram Rashid Mziwanda, Mufti Zubeir ametoa agizo kwa Masheikh wa mikoa, wilaya, kata, maimamu, na viongozi wa taasisi mbalimbali za Kiislamu nchini kusimama imara na kukemea maovu kila wanapoona mambo hayajakaa sawa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Serikali imekutana na wamiliki wa viwanda vya kuzalisha pombe kali nchini ikiwa ni hatua ya kuendelea kupambana na bidhaa bandia na duni.
Hatua hiyo imefikiwa baada ya Waziri wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga kukutana na kufanya mazungumzo na wamiliki wa viwanda vya pombe kali Agosti 24, 2026 jijini Dar es Salaam, katika kikao kilicholenga kutafuta suluhu ya changamoto hiyo.
Akizungumza katika kikao hicho, Kapinga amesisitiza umuhimu wa mzalishaji wa pombe kali kuendelea kuzingatia sheria, taratibu na kanununi za uanzishwaji wa viwanda hivyo, kwa kuzingatia ubora, usafi na afya ya mtumiaji.
Hatua hiyo inatajwa kuwa sehemu ya jitihada za serikali za kuhakikisha mazingira ya biashara yanakuwa rafiki huku wananchi wakipata bidhaa muhimu na halali kwa bei inayokubalika.
Kikao hicho pia kimeweka mkakati wa pamoja wa kila mzalishaji wa pombe kali kuendelea kutoa elimu kwa wadau na wananchi ili kutofautisha bidhaa bandia na halali. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Kesi ya uhaini namba 19605/2025 inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Antiphas Lissu, iliendelea jana mchana katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam. Shauri hilo lilirejea saa nane na dakika 50 mchana kufuatia mapumziko mafupi, ambapo mshitakiwa Tundu Lissu, akisimama kama shahidi wa kwanza wa utetezi kwenye kesi yake, aliendelea kutoa ushahidi wake mbele ya jopo la majaji watatu wakiongozwa na Jaji Dastan Ndunguru.
Katika utetezi wake wa Agosti 24, 2026, Lissu ameeleza siri ya mazungumzo yake na Rais Samia Suluhu Hassan akiwa uhamishoni Ubelgiji, mazingira yaliyosababisha kufa kwa "maridhiano" kati ya CHADEMA na CCM, chimbuko la kampeni ya "No Reforms No Election", na jinsi alivyoshtakiwa kwa uhaini kwa kutumia maneno aliyodai kuwa yalichukuliwa nje ya muktadha.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Serikali kupitia Wizara ya Madini imeanza kuchukua hatua madhubuti za kuboresha mfumo wa biashara na uchimbaji wa madini ya Tanzanite nchini, ikiwa ni utekelezaji wa maamuzi yaliyotokana na taarifa za Tume na Kamati zilizoundwa kuchunguza changamoto za sekta hiyo ili kuimarisha usimamizi na kuongeza thamani ya rasilimali hizo adimu.
Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, ametoa maelekezo hayo leo, Agosti 24, 2026, wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua shughuli za uchimbaji na biashara ya Tanzanite mkoani Manyara, ambapo ametembelea migodi ya Franone Mining & Gems Co. Ltd. na Chusa Mining Limited, soko dogo la madini, eneo la uthaminishaji, pamoja na jengo rasmi la biashara Mirerani.
Katika ziara hiyo, Waziri Mavunde ametoa agizo la wiki mbili kwa wachimbaji wa kati wa Tanzanite kuwasilisha taarifa ya hatua wanazochukua katika kuwekeza kwenye teknolojia za kisasa za utafiti ili kubaini mashapo na kuacha uchimbaji wa kubahatisha.
“Wekezeni kwenye teknolojia ya kisasa ya utafiti, wekezeni kwenye sayansi ili kubaini mashapo yaliyopo. Ndani ya wiki mbili kuanzia leo nataka kupata taarifa ya juhudi zenu za uwekezaji katika teknolojia ya kisasa ya utafiti,” amesisitiza Mavunde.
Pamoja na maelekezo hayo, Mavunde amempongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uamuzi wa kutenga asilimia 10 ya mapato ya Sekta ya Madini kwa ajili ya utafiti wa kina, akibainisha kuwa Mirerani na Mkoa wa Manyara ni miongoni mwa maeneo ya kipaumbele katika mpango huo.
Akiangazia masuala ya mitaji, ameeleza kuwa Shirika la Mfuko wa Dhamana za Mikopo (Credit Guarantee Scheme Corporation) chini ya Benki Kuu ya Tanzania limeundwa na kusajiliwa rasmi ili kuwezesha wachimbaji kupata mikopo nafuu kupitia taasisi za fedha.
Katika kuimarisha ulinzi na ufuatiliaji, Waziri Mavunde ametangaza kuanza kutumika kwa kofia ngumu yenye kamera kuanzia Mgodi wa Franone Mining, teknolojia inayoruhusu ufuatiliaji wa shughuli za uchimbaji hata chini ya ardhi.
Waziri Mavunde pia amepiga marufuku wafanyabiashara wa madini (dealers) kutumia raia wa kigeni kufanya biashara kinyume na sheria, huku akimuelekeza Afisa Madini Mkazi wa Mirerani kukutana na makampuni ya uwekezaji na wadau kuboresha mazingira ya kazi kwa 'wanaapolo' na masoko ya ndani ya migodi.
Halikadhalika amekiagiza Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC) kutembelea na kuwawezesha wanawake wanaojihusisha na shughuli za magonga, huku akiiagiza Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro kuangazia fursa ya kutoa mikopo ya asilimia 10 kwa wananchi wanaojihusisha na mnyororo wa thamani wa uchimbaji madini. -
Jambo TV
@Jambotv_
Kesi ya uhaini namba 19605/2025 inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Antiphas Lissu, imeendelea leo mchana katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam. Shauri hilo lilirejea saa nane na dakika 50 mchana kufuatia mapumziko mafupi, ambapo mshitakiwa Tundu Lissu, akisimama kama shahidi wa kwanza wa utetezi kwenye kesi yake, aliendelea kutoa ushahidi wake mbele ya jopo la majaji watatu wakiongozwa na Jaji Dastan Ndunguru.
Katika utetezi wake vya leo Agosti 24, 2026, Lissu ameeleza siri ya mazungumzo yake na Rais Samia Suluhu Hassan akiwa uhamishoni Ubelgiji, mazingira yaliyosababisha kufa kwa "maridhiano" kati ya CHADEMA na CCM, chimbuko la kampeni ya "No Reforms No Election", na jinsi alivyoshtakiwa kwa uhaini kwa kutumia maneno aliyodai kuwa yalichukuliwa nje ya muktadha.
Akianza ushahidi wake baada ya mapumziko, Lissu alionya kuwa masuala ya uchaguzi na katiba yasipowekwa sawasawa na kutatuliwa kwa amani, huwa yanaleta maafa makubwa na umwagaji wa damu. Alitolea mfano wa kihistoria wa Zanzibar, akieleza kuwa Muungano wa Tanzania ulitokana na Mapinduzi ya Zanzibar yaliyosababishwa na uonevu na dhuluma za uchaguzi, kama ilivyochambuliwa na Ripoti ya Tume ya Nyalali ya mwaka 1992.
Lissu amedai kuwa baada ya kufariki kwa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano, John Pombe Magufuli, na kuingia madarakani kwa Rais Samia Suluhu Hassan, yeye (Lissu) alikuwa bado anaishi uhamishoni nchini Ubelgiji. Mnamo tarehe 17 Februari 2022, wakati wa Mkutano wa Kilele wa Umoja wa Afrika na Umoja wa Ulaya (AU-EU Summit) huko Ulaya, Rais Samia alimtumia ujumbe akieleza kuwa anataka waonane. Wakati huo, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, alikuwa bado gerezani akikabiliwa na tuhuma za kigaidi.
Katika mazungumzo yao, Rais Samia alimweleza Lissu kuwa alikuwa anatamani "kusafisha na kusawazisha matatizo yote yaliyoachwa na mtangulizi wake". Lissu ameeleza kuwa alimjibu Rais Samia kuwa kama kweli ana nia hiyo, basi jambo la kwanza la kufanya ni kumtoa Mwenyekiti Mbowe gerezani, na kisha kuanzisha mazungumzo ya kitaifa kuhusu Katiba Mpya, mfumo huru wa uchaguzi, na kupata Tume Huru ya Uchaguzi.
Aidha....Soma zaidi jambo.co.tz kupitia kiungo hiki jambo.co.tz/lissu-adai-kukinukisha-si-uhaini-aanika-jinsi… -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Sakata la kiwanja namba 212, Njedengwa West, Kata ya Makulu jijini Dodoma, limechukua sura mpya baada ya familia inayodai kuwa mmiliki wa eneo hilo kujitokeza na nyaraka za umiliki, ikimtaka Katibu wa CCM Tawi la Njedengwa West, Maulid Juma, kuacha eneo hilo ili waweze kuendelea na ujenzi.
Familia ya Simon Silau, ambayo inadai kuwa mmiliki halali wa kiwanja hicho, imesema ilipatiwa kiwanja namba 212, Kitalu DD baada ya nyumba yao kuathiriwa na mradi wa Ndugai, huku ikidai kuwa Maulid alipewa viwanja vitatu na baadaye kuviuza.
Kwa mujibu wa familia hiyo, baada ya Maulid kuanza ujenzi kwenye kiwanja hicho, walitoa taarifa kwa Mwenyekiti wa Mtaa ambaye alimsihi asitishe ujenzi.
Hata hivyo, familia hiyo imesema baada ya ujenzi kuendelea, ilifika Halmashauri ya Jiji la Dodoma ambako eneo hilo liliwekewa alama ya X na kuamriwa kubomolewa, lakini ujenzi ukaendelea.
Hatua hiyo inakuja siku chache baada ya Maulid Juma na mkewe, Fridaus Matuliani, kulalamika kubomolewa nyumba yao wakidai kuwa walifanyiwa uonevu na kwamba ubomoaji huo ulihusishwa na Diwani wa Kata ya Makulu, Samson Mkopi.
Akizungumzia sakata hilo, Diwani Samson Mkopi amesema cheo cha Maulid kama kiongozi wa CCM hakiwezi kuwafanya wananchi wengine kunyimwa haki zao.
Mkopi pia amekanusha madai kwamba mgogoro huo unatokana na masuala ya kisiasa, akisema maelekezo ya kusitisha ujenzi wa eneo hilo yalitolewa kabla hajaingia madarakani mwaka 2025.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Kesi ya uhaini namba 19605/2025 inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Antiphas Lissu, inaendelea leo Jumatatu, Agosti 24, 2026, katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam.
Lissu ameendelea kushusha utetezi wake mbele ya jopo la majaji watatu wakiongozwa na Jaji Dastan Ndunguru, akieleza kwa kina historia ya harakati zake, mfululizo wa kesi alizofunguliwa wakati wa tawala tofauti, na uchambuzi wa kihistoria kuhusu kile alichokiita "uchafu" wa mfumo wa uchaguzi nchini.
Katika kuanza kwa ushahidi wake leo, Lissu ameiambia mahakama kuwa mara baada ya kesi hiyo kufunguliwa mwaka jana (2025), taasisi mbalimbali za kikanda na kimataifa zilitoa matamko makali ya kulaani mashtaka hayo. Taasisi hizo ziliziita tuhuma hizo kuwa ni za uonevu na matumizi mabaya ya mifumo ya mahakama na uendeshaji wa mashtaka ya jinai.
Miongoni mwa taasisi zilizotoa matamko hayo ni pamoja na Chama cha Mawakili wa Afrika Mashariki (EALS), Chama cha Wanasheria cha Nchi Wanachama wa SADC (SADCLA), Muungano wa Wanasheria Afrika (Pan African Lawyers Union - PALU), Chama cha Mawakili wa Tanganyika (TLS), pamoja na vyama vya mawakili vya Kenya na Zambia, Tume ya Wanasheria Duniani (ICJ) – Kenya Chapter, Ofisi ya Kikanda ya Amnesty International ya Afrika Mashariki na Kusini, Uganda Law Society (ULS), Democrats Union of Africa (DUA) na Platform of African Democrats (jukwaa linalounganisha vyama vya kidemokrasia vya nchi 17 barani Afrika).
Lissu amefafanua kuwa mnamo Julai 30, 2025, Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu na Haki za Wananchi (ACHPR) yenye makao makuu yake Arusha, ilifanya kikao cha dharura na kupitisha azimio rasmi lililoitaka Serikali ya Tanzania kuheshimu na kufuata mkataba wa Afrika wa haki za binadamu ulioridhiwa mwaka 1984.
Lissu ameeleza kuwa utetezi wake unathibitisha kwamba kesi hii si kwa sababu yeye ni mhaini, bali inatokana na msimamo wake wa miaka mingi wa kupigania haki na utawala bora. Alibainisha kuwa alianza harakati zake tangu akiwa shule ya sekondari mwaka 1988, ambapo alikaribia kufukuzwa shule kwa kuwatetea wanafunzi wa kidato cha nne wakati yeye akiwa kidato cha sita.
Soma zaidi jambo.co.tz hapa
jambo.co.tz/lissu-aanika-miaka-38-ya-harakati-ukandamizaj… -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Shauri la uhaini namba 19605/2025 dhidi ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa Tundu Lissu, leo Agosti 24, 2026 linaendelea kusikilizwa siku ya leo katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar Es Salaam, ikiwa katika hatua ya uwasilishaji wa ushahidi wa mshtakiwa mbele ya jopo la Majaji watatu wakiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru.
Kwasasa shauri limeahirishwa kwa saa 1 na nusu, na litaendelea saa 8 na nusu mchana na mshtakiwa Lissu kuendelea kutoa ushahidi wake kama shahidi ambao kwa siku ya leo umegusia sana masuala ya uchaguzi na mfumo wa uchaguzi tangu Uhuru mpaka mfumo wa vyama vingi ulipoanzishwa miaka ya 90This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwenyekiti wa Tume ya Uchunguzi wa Wahusika wa Ghasia na Ukiukwaji wa Sheria wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani, Shaban Ally Lila, amesema tume hiyo ina jukumu tofauti na Tume ya Rais iliyokuwa ikiongozwa na Jaji Mstaafu Othman Chande.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 24, 2026, Jaji Lila amesema Tume ya awali ilijikita katika kuchunguza matukio ya ghasia yaliyotokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, ikiwemo kubaini aina ya vurugu, ghasia na uvunjifu wa amani uliojitokeza.
Amesema tofauti na tume hiyo, Tume anayoiongoza imepewa jukumu la kwenda hatua zaidi kwa kuchunguza na kubaini watu waliohusika katika kupanga, kufadhili, kuratibu na kutekeleza matukio hayo ya ghasia.
Kwa mujibu wa Jaji Lila, tume pia itachunguza aina na kiwango cha nguvu iliyotumika katika kudhibiti ghasia hizo, ili kubaini kama hatua zilizochukuliwa zilizingatia sheria na taratibu zilizowekwa.
“Sisi tumepewa jukumu la kwenda kuangalia wahusika ni kina nani, waliopanga, walioratibu, waliofadhili, waliotekeleza. Halafu pia tuangalie masuala ya madhara kwa maana ya watu wameumia, watu wamefariki kutokana na ghasia zile nani wahusika, na aina na kiasi cha nguvu kilichotumika kwenye kudhibiti zile ghasia. Thamani ya mtu hailinganishwi na kitu kingine chochote", amesema Jaji Lila
Tume hiyo, maarufu kama Tume ya Jaji Lila, iliundwa na Rais Samia Suluhu Hassan na kuzinduliwa rasmi Agosti 7, 2026. Ina jukumu la kuchunguza wahusika wa ghasia na ukiukwaji wa sheria katika matukio yaliyotokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.
Tume hiyo inaongozwa na Jaji Shaban Ally Lila na inahusisha pia majaji wastaafu pamoja na majaji kutoka nje ya Tanzania na imepewa siku 150 kukamilisha majukumu yake -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI:
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Agosti 24, 2026, Mwenyekiti wa Tume ya Kuchunguza wahusika wa Ghasia na Ukiukwaji wa Sheria Wakati na Baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani, Shaban Ally Lila, amesema Tume hiyo imepewa hadidu tano za rejea ambazo zinaainisha mawanda na mipaka ya mamlaka yake katika kutekeleza majukumu yake.
Amesema hadidu ya kwanza ni kuchunguza na kubainisha wahusika wa ghasia na namna kila mmoja alivyoshiriki katika kupanga, kufadhili, kuratibu au kutekeleza shughuli zilizohusiana na ghasia wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
Jaji Lila amefafanua kuwa hadidu hiyo inatokana na maelezo yaliyotolewa katika ripoti ya Tume iliyotangulia, iliyoongozwa na Jaji Chande, ambayo ilibainisha kuwa ghasia na fujo zilizotokea hazikuwa za bahati mbaya, bali zilidaiwa kuwa zilipangwa, kuratibiwa, kufadhiliwa na kutekelezwa kwa mpango maalum.
Hadidu ya pili ni kuchunguza matukio mahsusi yaliyotokea wakati na baada ya uchaguzi, ikiwemo suala la vifo visivyokuwa vya kawaida vya watoto na watu wa makundi maalum.
Hadidu ya tatu ni kuchunguza matukio ya watu kupotea katika maeneo yaliyokumbwa na ghasia na uvunjifu wa amani tangu kipindi cha uchaguzi na baada
Aidha, Jaji Lila ameeleza hadidu ya nne ni kuchunguza madai ya matumizi ya nguvu kupita kiasi pamoja na iwapo taratibu na miongozo iliyowekwa ilizingatiwa wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
Hadidu ya tano ni kuchunguza suala lolote ambalo Tume itaona ni muhimu na linalohusiana na majukumu yake.
Jaji Lila amesema hizo ndizo hadidu tano za rejea ambazo Tume imepewa, na ndizo zitakazoainisha upana wa kazi na mipaka ya mamlaka yake katika kufanya uchunguzi. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI:
Mwenyekiti wa Tume ya Kuchunguza wahusika wa Ghasia na Ukiukwaji wa Sheria Wakati na Baada ya Uchaguzi Mkuu, Jaji Mstaafu Shaban Ally Lila, amesema lengo kuu la Tume hiyo ni kuchunguza na kubainisha wahusika wa ghasia na ukiukwaji wa sheria katika matukio yaliyotokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
Jaji Lila amesema Tume hiyo pia ina jukumu la kuchunguza chanzo cha madhara mbalimbali yaliyotokea kutokana na ghasia na uvunjifu wa amani, ikiwemo vifo, majeruhi na watu waliopotea.
Akizungumza na Waandishi wa Habari, Jaji Lila amegusia kuwa Tume iliyokuwa chini ya Mwenyekiti Jaji Chande ilibainisha kuwa watu 518 walifariki katika matukio hayo, huku ikieleza kuwa huenda idadi hiyo ilikuwa kubwa zaidi kutokana na baadhi ya waathirika kutokufikiwa na utaratibu wa utambuzi.
"Tume ya Mheshimiwa Jaji Chande ilibainisha kuwa kulitokea vifo na ikataja kwa mujibu wa uchunguzi wao kwamba walibainisha vifo vya watu 518, lakini pia tume ile ilisema inawezekana idadi ni zaidi ya hapo kwa sababu si wote walipita kwenye utaratibu ambao wangeweza kutambuliwa", amesema Jaji Lila
Aidha, Jaji Lila amesema katika kutekeleza majukumu yake, Tume imepewa hadidu tano za rejea ambazo zinaainisha maeneo na mipaka ya mamlaka yake katika kufanya uchunguzi.
Amesema hadidu hizo ndizo zitakazoongoza Tume katika kutekeleza jukumu lake la kuchunguza matukio yaliyotokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI:
Tume ya Kuchunguza Wahusika, Ghasia na Ukiukwaji wa Sheria Wakati na Baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025 imeanza rasmi kazi, huku Mwenyekiti wake, Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani, Shaban Ally Lila, akieleza kuwa Tume hiyo imeundwa kuchunguza matukio ya ghasia, uvunjifu wa amani na madhara yaliyotokea wakati na baada ya uchaguzi huo.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Agosti 24, 2026, Jaji Lila amesema Tume hiyo imeundwa na Rais kwa lengo la kuwafahamisha Watanzania kuhusu mchakato wa uchunguzi wa matukio hayo na kubaini wahusika, chanzo cha ghasia pamoja na ukiukwaji wa sheria uliojitokeza.
Amesema uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025, ambao ulifanyika kwa mujibu wa matakwa ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, haukwenda kwa amani katika baadhi ya maeneo kutokana na kutokea kwa ghasia na uvunjifu wa amani.
Jaji Lila amefafanua kuwa kutokana na matukio hayo na madhara yaliyotokea, Rais aliunda Tume hiyo mpya kwa ajili ya kufanya uchunguzi kuhusu matukio yaliyosababisha madhara wakati na baada ya uchaguzi, akibainisha zaidi kuwa Tume hiyo inaongozwa na naye, ambaye ni Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania
Wajumbe wa ndani wa Tume hiyo ni Majaji Wastaafu wa Mahakama Kuu, Jaji Gad Mjemmas, Jaji Awadh Bawazir na Jaji Aishieli Sumari, Petrus Tileinge Damaseb, pamoja na wajumbe wa Nje ambao ni Naibu Jaji Mkuu wa Namibia, na Jaji Cheborion Barishaki kutoka Uganda -
Jambo TV
@Jambotv_
Zaidi ya wanafunzi 95 wa Kitanzania wameondoka nchini kuelekea India kuanza masomo ya elimu ya juu katika vyuo mbalimbali, ikiwa ni kundi la kwanza kati ya wanafunzi 198 wanaotarajiwa kwenda kusoma nchini humo kupitia Global Education Link katika mwaka 2026.
Wanafunzi hao walioondoka kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Terminal 3, jijini Dar es Salaam, wengi wao wamechagua programu zinazohusiana na sayansi, teknolojia na taaluma zinazohitajika katika dunia ya sasa, zikiwemo Computer Engineering, Cyber Security, Artificial Intelligence, Civil Engineering, programu mbalimbali za afya, sheria na biashara.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Global Education Link, Meneja wa Tawi la Dar es Salaam, Micky Musa, amesema kuondoka kwa wanafunzi hao ni sehemu ya mpango mpana wa kuwaunganisha vijana wa Tanzania na fursa za elimu ya kimataifa.
“Zaidi ya wanafunzi 95 wanaondoka katika kundi hili la kwanza kuelekea India, lakini kwa mwaka huu tunatarajia wanafunzi 198 kwenda kusoma nchini India. Hili si kundi la mwisho kwa sababu bado tuna wanafunzi wengine wanaoendelea kukamilisha taratibu zao,” amesema Musa.
Amesema mbali na India, Global Education Link inaendelea kuwaandaa wanafunzi wengine wapatao 185 wanaotarajiwa kuelekea nchini China, huku wengine wakiwa katika hatua mbalimbali za maandalizi ya kwenda kusoma Malaysia, Marekani na Uingereza.
“Kadiri muda unavyokwenda Watanzania wataendelea kuona makundi mengine ya wanafunzi yakiondoka. Tunawaomba vijana wenye ndoto ya kusoma nje ya nchi wafike katika ofisi zetu zilizopo Dar es Salaam, Dodoma, Zanzibar, Mwanza na Arusha. Muda bado upo. Njoo na matokeo yako, nasi Global Education Link tupo tayari kukusaidia kuifanya ndoto yako kuwa uhalisia,” amesema.
Musa pia amewataka wazazi na walezi wenye vijana wanaotamani kupata elimu nje ya nchi kutumia ofisi za Global Education Link kupata ushauri kuhusu uchaguzi wa vyuo, programu za masomo, udahili, visa na maandalizi ya safari.
Miongoni mwa wanafunzi walioondoka ni vijana wanaokwenda kusomea Computer Science Engineering, Artificial Intelligence na Cyber Security, wakisema wamechagua taaluma hizo kutokana na kasi ya mabadiliko ya teknolojia na umuhimu wake katika maendeleo ya uchumi wa kisasa.
Alvin Andrew Munda, mwenye umri wa miaka 17, anayeelekea Lovely Professional University nchini India, amesema amechagua Computer Science kwa sababu anataka kujenga ujuzi wa vitendo katika teknolojia na baadaye kujikita zaidi katika Cyber Security.
Amesema mfumo wa masomo wenye nafasi kubwa ya mafunzo ya vitendo na matumizi ya maabara ulimvutia kuchagua chuo hicho.
“Napenda mfumo wenye practical zaidi kuliko kusoma theory na kuandika mitihani pekee. Nataka nitumie elimu nitakayoipata kutengeneza suluhisho na baadaye nijikite katika Cyber Security kwa sababu usalama wa mtandao ni muhimu sana katika dunia ya sasa,” amesema.
Akimshukuru Global Education Link, Munda amesema taasisi hiyo imeisaidia familia yake katika mchakato mzima, kuanzia kupata chuo hadi kukamilisha maandalizi ya safari.
“Global imenisaidia katika process nzima kabisa. Wametuelekeza hatua moja hadi nyingine na wamekuwa kiungo kati yetu, wazazi wetu na chuo mpaka tumefikia hapa airport tayari kuondoka,” amesema.
Mwanafunzi mwingine anayekwenda kusomea masomo yanayohusiana na Computer Science na Artificial Intelligence amesema anatarajia kuwa mtaalamu wa data na teknolojia katika miaka ijayo.
Amesema AI imeanza kuwa sehemu muhimu katika benki, hospitali, biashara, serikali na sekta nyingine, na hivyo anaamini elimu katika eneo hilo itamwezesha kuwa sehemu ya maendeleo ya kiteknolojia nchini Tanzania.
Naye mwanafunzi anayekwenda kusomea programu jumuishi ya Bachelor of Business Administration na Bachelor of Laws amesema ana ndoto ya kuwa mwanasheria na mfanyabiashara mwenye mafanikio baada ya kumaliza masomo yake.
Amesema Global Education Link imechangia kwa kiasi kikubwa kumfikisha katika hatua ya kuondoka kwenda masomoni. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Serikali imetoa wito kwa wananchi kudumisha utulivu na mshikamano huku ikiwataka kupuuza kampeni hasi zinazoendeshwa mtandaoni na kurejesha nyuma juhudi za maendeleo nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Morogoro, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, amesisitiza kuwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii hayawezi kupatikana katika mazingira ya vurugu na uharibifu wa miundombinu
“Hatuwezi tukawa tunazungumza kupeleka umeme huku watu wanapanga maandamano. Hatuwezi kuwa tunazungumza kuendeleza kilimo huku watu wanapanga kuchoma miundobinu ya serikali,” ameonya Msigwa huku akitaka Watanzania kuwa wamoja na kuzungumza lugha moja.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Serikali inatarajia kujenga Kituo Kikubwa cha Urithi wa Ukombozi wa Afrika katika eneo la Kongwa mkoani Dodoma, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kutunza na kuhifadhi historia ya Tanzania pamoja na mchango wake katika harakati za ukombozi wa Bara la Afrika.
Hayo yamebainishwa leo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa, mkoani Morogoro wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya Tamasha la Kitaifa la Utamaduni msimu wa nne.
Msigwa amesema Serikali tayari imetenga shilingi bilioni moja kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho, akisisitiza kuwa ni wakati muafaka wa kuendelea kujenga na kuimarisha maeneo ya urithi wa taifa yatakayosaidia kuhifadhi historia ya nchi.
Amesema kituo hicho kitakuwa sehemu muhimu ya kutunza historia kwa ajili ya vizazi vya sasa na vijavyo, pamoja na kutoa fursa kwa wananchi na watalii kujifunza kuhusu historia ya Tanzania na mchango wake katika harakati za ukombozi wa Bara la Afrika.
Aidha, Msigwa amesema Tamasha la Kitaifa la Utamaduni linatarajiwa kuimarisha umoja na utaifa, kukuza uchumi wa wananchi pamoja na kuitangaza Tanzania kupitia utamaduni na utalii.
Ameongeza kuwa tamasha hilo linatarajiwa kufanyika kuanzia Agosti 25 hadi 29 mwaka huu, likishirikisha mikoa 26 ya Tanzania katika kuonesha na kuendeleza utajiri wa tamaduni mbalimbali nchini.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Dkt. Festo Dugange, amewapongeza viongozi wa Mkoa wa Songwe wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo, Jabiri Makame, kwa kuwa wa kwanza kuanzisha Jukwaa la Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, lililowaleta pamoja wadau wa sekta binafsi na sekta ya umma ili kujenga uelewa wa pamoja na mikakati ya utekelezaji wake.
Dkt. Dugange ametoa pongezi hizo wakati akihitimisha Jukwaa la Siku Mbili la Songwe Dira 2050 Forum kwa niaba ya Waziri wa TAMISEMI, Prof. Riziki Shemdoe. Jukwaa hilo limekutanisha watendaji, watumishi, viongozi, na wadau mbalimbali kwa lengo la kuweka dira ya maendeleo ya mkoa huo kuelekea mwaka 2050.
Katika maelekezo yake, Dkt. Dugange amewataka wadau wote kutambua kuwa Dira 2050 si mali ya Serikali pekee, bali ni mwongozo wa taifa zima unaompa kila mwananchi na mdau wajibu wa kuitekeleza kwa nafasi yake.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Jabiri Makame, ameeleza kuwa Dira 2050 imeandaliwa kimkakati, hivyo ni jukumu la wadau wa sekta ya umma na binafsi mkoani humo kubadili mtazamo na kufanya maamuzi yenye tija.
Amesisitiza kuwa ili kufikia malengo yaliyowekwa na Mkoa wa Songwe na taifa kwa ujumla, wadau wote wanapaswa kufikiri, kupanga, kufanya maamuzi, na kutekeleza mipango yao kimkakati.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Taharuki imeibuka katika Mtaa wa Njedengwa jijini Dodoma baada ya Katibu wa CCM wa Tawi la Njedengwa, Maulid Juma, kudai kuwa nyumba yake imebomolewa bila kufuata utaratibu, licha ya kueleza kuwa yeye ndiye mmiliki halali wa eneo hilo.
Maulid amesema mgogoro huo ulianza baada ya mtu mwingine kudai umiliki wa eneo alilonunua na kuliandikisha kwa jina la mtoto wake. Kutokana na mvutano huo, amesema suala hilo lilipelekwa katika Baraza la Kata na baadaye katika ngazi ya Serikali ya Mtaa kwa ajili ya kutafuta suluhu, lakini hakupata majibu aliyotarajia.
Amesema baadaye aliitwa pamoja na upande wa pili wa mgogoro huo katika kikao alichodai kuitishwa na Diwani wa Kata ya Makulu, Samson Mkopi, kwa lengo la kujadili suala hilo. Hata hivyo, amesema wakati majadiliano yakiendelea, Diwani pamoja na baadhi ya viongozi waliondoka huku wakimueleza yeye asiondoke na kuendelea kusubiri.
Kwa mujibu wa Maulid, muda mfupi baadaye alipokea simu kutoka kwa mkewe, Fridaus Matuliani, akimjulisha kuwa msafara uliokuwa umeambatana na kikosi cha ubomoaji ulikuwa umefika katika eneo hilo na kuanza kubomoa nyumba yao.
Maulid amesema tukio hilo limemshtua na kumsababishia hasara kubwa, akidai kuwa ubomoaji huo umefanyika bila yeye kupewa nafasi ya kutosha ya kusikilizwa au kuonyeshwa utaratibu wa kisheria uliotumika. Aidha, amesema kitendo hicho kinamuweka katika mazingira magumu yeye na familia yake.
Aidha amesema anachokitaka si kingine bali ni haki na ufafanuzi kuhusu nani alitoa agizo la ubomoaji huo, kwa mamlaka gani na kwa kuzingatia utaratibu gani. Pia amedai kuwa tukio hilo linajenga taswira mbaya kwa CCM na kuhoji namna viongozi wanavyopaswa kushughulikia migogoro ya wananchi.
Kwa upande wake, Fridaus Matuliani, ambaye ni mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Njedengwa na pia mke wa Maulid, amelia kwa uchungu kufuatia kubomolewa kwa nyumba hiyo, akisema familia yao imeathirika kutokana na tukio hilo. Ameitaka mamlaka husika kuingilia kati na kuhakikisha haki inapatikana kwa mujibu wa sheria.
Naye Mwenyekiti wa Mtaa wa Njedengwa West, Daimu Haji, amekana kuhusika na ubomoaji huo, akisema Serikali ya Mtaa haikuwa na taarifa kuhusu hatua hiyo. Amesema hana taarifa za kutosha kuhusu nani aliyeongoza zoezi hilo na kwa mamlaka gani.
Akizungumza kwa njia ya simu, Diwani wa Kata ya Makulu, Samson Mkopi, amewapa pole wananchi hao na kusema hana mamlaka ya kubomoa nyumba ya mwananchi wala hakuhusika kwa namna yoyote katika tukio hilo. Amesema yeye pia alipata taarifa kuhusu tukio hilo kwa kusikia, akisisitiza kuwa madai ya kuhusishwa moja kwa moja na ubomoaji huo si ya kweli.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Pwani, Boniface Jacob (Boniyai), amemtolea uvivu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo, akisema kuwa madai yake kwamba nchi imejitosheleza na haihitaji misaada ya wahisani ni ujanja wa kisiasa unaolenga kuficha ukweli wa umaskini wa wananchi.
Akizungumza jana, Agosti 22, 2026, katika Mkutano Mkuu Maalumu wa CHADEMA Wilaya ya Temeke mkoani Dar es Salaam, Boniyai alijibu ripoti iliyotolewa na Profesa Kitila mnamo Agosti 3, 2026. Katika ripoti hiyo, Waziri huyo alijinasibu kuwa kiwango cha misaada katika bajeti ya serikali kimeshuka kwa kasi kutoka asilimia 7.1 (mwaka 2020/21) hadi kufikia asilimia 0.9 pekee katika bajeti ya mwaka wa fedha 2026/27.
Hata hivyo, Boniyai amepinga maelezo hayo akimtaja Profesa Kitila kama “mjanjamjanja tu” ambaye si mchumi wala mpangaji. Ameeleza kuwa masuala makubwa ya kiuchumi na bajeti yanapaswa kujadiliwa na wasomi wa uchumi, na akashutumu mfumo wa CCM wa kushindwa kutumia rasilimali watu kwa usahihi kwa kuwapa watu wasio na utaalamu kusimamia sekta nyeti, ikiwemo kumkabidhi Profesa Kitila jukumu la kusimamia Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
Boniyai amefafanua kuwa ujitoshelezaji wa nchi hauamuliwi na namna serikali inavyoandika bajeti yake kwenye makaratasi, bali unaonekana kupitia utatuzi wa changamoto halisi za wananchi katika maisha ya kila siku.
“Sisi hatuangalii kwa wao walivyoandika bajeti yao; tunaangalia mahitaji ya kijamii yameisha? Tuna hospitali? Tuna madawa? Tuna barabara? Tuna shule, watoto hawakai chini tena? Halafu ukiwa umemaliza hizi shida zote ndio tunakuita wewe ni nchi iliyojitosheleza,” amesema Boniyai.
Mwenyekiti huyo wa Kanda ya Pwani amesisitiza kuwa mazingira ya bajeti ya sasa yametengenezwa kisanii ili ionekane haitegemei wahisani, lakini ukweli ni kwamba nchi bado ina uhitaji mkubwa wa misaada hiyo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake mkoani Pemba Kusini visiwani Zanzibar ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya hiyo, Zuhura Mgeni Othman, amefanya uvamizi katika nyumba inayodaiwa kutumika kama danguro katika eneo la Chanjamjawiri.
Katika uvamizi huo, DC Zuhura amebaini uwepo wa kondomu ndani ya nyumba hiyo, jambo lililoibua tuhuma nzito za kuwepo kwa biashara ya kuuza mwili na shughuli zisizo za kimaadili.
Mwanamke mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Mariam Joseph anadaiwa kuhusishwa na uendeshaji wa shughuli hizo, huku vyombo vya dola vikitazamiwa kufanya uchunguzi wa kina ili kuchukua hatua za kisheria.
DC Zuhura ameeleza kuwa hali hiyo inatia wasiwasi mkubwa kufuatia taarifa kuwa nyumba hiyo imekuwa ikifikiwa na vijana pamoja na watoto, hatua inayoweka maadili na ustawi wao katika hatari kubwa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katibu wa Umoja wa Wanafunzi wa CHADEMA (CHASO) tawi la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na Chuo cha Maji, Katisho Raphael Segeredi, amewasihi wazee wa Tanzania kuacha kutoa maneno yanayowakatisha tamaa Watanzania na badala yake wawe hazina ya busara na watetezi wa haki.
Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Dar es Salaam Agosti 22, 2026, Segeredi amewalenga moja kwa moja baadhi ya wazee waliopo serikalini kwa muda mrefu, akieleza kuwa wazee hawa wamekuwa wakipotosha umma kwa kudai kuwa katiba mpya haitawaletea wananchi chakula.
"Mzee kama huyo amekuwepo serikalini muda mrefu, unadhani anajua ni matatizo gani sasa hivi yanawakumba vijana na jamii kwa ujumla? Maana yake ni mtu ambaye hazifahamu shida," amesema Segeredi.
Ameongeza kuwa, badala ya kutetea maslahi yao binafsi ya sasa, wazee wanapaswa kusimama upande wa haki kwa manufaa ya vizazi vijavyo, ikiwa ni pamoja na wajukuu na vitukuu vyao.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) taifa, Freeman Mbowe ametoa rai kwa wanasiasa na wananchi kutoishia kukosoa na kuponda tu kila jambo, bali kuwa na ujasiri wa kupongeza mafanikio makubwa ya kitaifa yanapotokea.
Mbowe ametoa kauli hiyo Agosti 22, 2026, mara baada ya kushuhudia uzinduzi wa kihistoria wa Kituo cha Kuzalisha Umeme cha Julius Nyerere (JNHPP) kilichopo Rufiji, mkoani Pwani. Ameeleza kuwa uamuzi wake wa kukubali mwaliko na kufika eneo la mradi ni kielelezo tosha cha kusimamia kile anachokiamini.
"Mambo ya umeme tumepiga kelele kwa muda mrefu. Kilio chetu kimejibiwa kwa kitendo (action). Ni jambo jema. Tunapoona jambo jema limetekelezwa tusiponde tu; maadamu tunaponda, tuwe na ujasiri wa kupongeza vilevile pale jambo jema linapokuwa limefanikiwa," amesema Mbowe.
Mbowe amefafanua kuwa mradi huo wenye uwezo wa kuzalisha megawati 2,115 si mafanikio ya serikali wala ya chama chochote cha siasa, bali ni ushindi mkubwa kwa taifa zima la Tanzania.
Ameongeza kuwa nishati hiyo si kwa ajili ya kizazi cha sasa cha viongozi waliouanzisha mradi huo, bali ni kwa ajili ya watoto na vizazi vijavyo vya Watanzania, hivyo miradi mikubwa kama hiyo ya kimkakati inapaswa kutazamwa kwa jicho pana la kitaifa na kuungwa mkono.
Pamoja na pongezi hizo, kiongozi huyo hakusita kuweka wazi changamoto zinazouzunguka mradi huo, akibainisha kuwa kuzalisha umeme ni hatua moja, lakini usambazaji wake ni kazi kubwa ambayo hata Rais amekiri.
Mbowe ameitaka serikali kutumia nguvu na rasilimali zilezile zilizowekwa kukamilisha ujenzi wa bwawa hilo kuelekezwa sasa katika kujenga miundombinu ya kusambaza umeme huo kwa kasi hadi vijijini.
Aidha, ametoa wito kwa serikali kuangalia namna ya kupunguza gharama za uunganishaji nishati hiyo ili wananchi wa kawaida wanufaike
“Wananchi wengi umeme umepita juu ya mapaa ya nyumba zao lakini wanashindwa kuunganisha kwa ajili ya gharama zake. Vyote hivyo vikaangaliwe ili ile nia njema ya kujenga bwawa hili iweze kutimilika kwa ukamilifu,” amesisitiza.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, John Heche, amesema kuwa chama chake kinaendelea kukabiliwa na vita kali ya kisiasa kwasababu kimekataa katakata kushiriki katika "siasa za udalali".
Akizungumza jana, Agosti 22, 2026, katika Mkutano Mkuu Maalumu wa CHADEMA Wilaya ya Temeke mkoani Dar es Salaam, Heche ameeleza kuwa vita inayoelekezwa kwake binafsi na kwa chama chake inatokana na msimamo wao thabiti wa kukataa kuwa mawakala wa unyonyaji.
“Hii serikali haipaswi kuwa madarakani siyo leo. Jana ilipaswa iwe imeondoka madarakani. Na ndio maana wanapoona watu hatutaki kufanya siasa za udalali tunapigwa vita kweli kweli,” ameongea Heche huku akiwataka wananchi kusimama imara na kukataa kuyumbishwa.
Heche ameeleza kuwa kukataa kwao "udalali" kumezua hofu kubwa kwa watu ambao amewataja kuwa wamekuwa wakimshambulia kwa maneno kila wanapopata fursa akisema, “Ukisikia kila siku waziri akitokea huku, ‘Heche tu, Heche, Heche!’... Kwa nini? Kwasababu tumekataa udalali. Sema kataa udalali!”.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro linawashikilia watu wawili, Sharif Abdallah Mabishi (20) na Boniface Machila (22), raia wa nchi jirani (ambazo hazikutajwa jina kwasababu za kiuchunguzi) kwa tuhuma za wizi wa mita 14 za maji zinazomilikiwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Moshi (MUWSA).
Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia tarehe 22 Agosti, 2026, katika Kitongoji cha Miembeni, Kata ya Makuyuni, Mamlaka ya Mji Mdogo wa Himo, ambapo Askari Polisi kwa ushirikiano na Wananchi pamoja na Vikundi vya Ulinzi Shirikishi (Sungusungu) walibaini uwepo wa wanaume watatu majira ya saa 8:00 usiku wakiwa na mita hizo kwenye pikipiki yenye namba za usajili KMGW 960 aina ya TVS.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa, amethibitisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao wawili, huku akieleza kuwa mtuhumiwa wa tatu alifanikiwa kukimbia na msako mkali unaendelea ili kumkamata.
“Uchunguzi wa tukio hilo unaendelea na baada ya kukamilika, hatua nyingine za kisheria zitachukuliwa kwa mujibu wa sheria. Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro linatoa wito kwa Wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa zitakazosaidia kuwakata wahusika wa wizi wa mali za Serikali na uhalifu mwingine ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao”, imeeleza polisi.
Akimzungumzia tukio hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa MUWSA, Mhandisi Kija Limbe, amebainisha kuwa mamlaka hiyo imekuwa ikipata hasara kubwa kutokana na wizi wa mita za maji.
Amesema kuwa kuanzia mwezi Januari hadi Agosti 2026, jumla ya mita 641 zenye thamani ya Shilingi 97,175,600 zimeibiwa katika maeneo mbalimbali yanayohudumiwa na mamlaka hiyo.
Mhandisi Limbe amelishukuru Jeshi la Polisi na kikundi cha ulinzi shirikishi cha Himo kwa kufanikisha ukamataji huo, huku akikumbusha kuwa MUWSA bado inatoa zawadi ya hadi Shilingi Milioni 2 kwa mwananchi yeyote atakayetoa taarifa zitakazowezesha kufichua na kukamatwa kwa mtandao wa wezi wa mita hizo. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Wakili wa kujitegemea, Godfrey Wasonga, amependekeza Serikali kuangalia upya mfumo wa upelelezi na uendeshaji wa kesi za ugaidi na uhaini, akisema makosa hayo ni makubwa na yanahitaji viashiria vya kutosha kabla mtu hajafikishwa mahakamani.
Akizungumza na Jambo TV jijini Dodoma, Wasonga amesema Serikali inapaswa kuweka sheria itakayoruhusu private investigation, ili uchunguzi usibaki mikononi mwa Serikali pekee, bali kuwe na nafasi ya uchunguzi huru ambao unaweza kusaidia Mahakama kupima ushahidi wa pande zote.
Pia amependekeza kuwepo kwa mwongozo wa Jaji Mkuu kuhusu kesi za ugaidi na uhaini, ukiweka viashiria vinavyopaswa kuonekana kabla mtu hajafunguliwa mashtaka hayo.
“Sio kila mtu tu ameiba kuku, mhaini. Amefanyaje uhaini? Haitakiwi kwenda hivyo.”
Wasonga amesema mifumo hiyo inapaswa kuangaliwa upya ili iendane na mabadiliko ya teknolojia na mfumo wa maisha, akisisitiza umuhimu wa kuweka utaratibu unaohakikisha mashtaka ya ugaidi au uhaini yanafunguliwa pale ambapo viashiria na ushahidi wa awali vinajitosheleza.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Wakili wa kujitegemea, Godfrey Wasonga, ametoa ufafanuzi kuhusu utaratibu wa kisheria unaotumika kumuita Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mahakamani, akirejea sheria inayojulikana kama Presidential Affairs Act.
Wasonga amesema
sheria hiyo inaweka utaratibu maalum kuhusu namna Rais anavyoweza kuombwa kufika mahakamani, ikiwemo masharti yanayohusu utoaji wa summons au amri za Mahakama.
Kwa mujibu wa Wasonga, chini ya vifungu vya sheria hiyo anavyovitaja, Mahakama haiwezi kupeleka moja kwa moja summons au order kwenye makazi ya Rais, ikiwemo sehemu yoyote ambayo Rais anaishi au anatarajia kuishi.
Amesema badala yake, mtu anayehitaji Rais kutoa ushahidi anatakiwa kuwasilisha maombi, ambayo hupitia kwa viongozi waliotajwa kwenye sheria hiyo, akiwemo Katibu Mkuu Kiongozi, Katibu Mkuu wa Ikulu au Katibu binafsi wa Rais.
Wasonga amesema utaratibu huo haujaweka sharti la Rais kulazimishwa kufika mahakamani baada ya maombi hayo kupokelewa, akisema sheria hiyo haijaainisha adhabu kwa Rais endapo hatakwenda mahakamani.
Aidha, amesema Presidential Affairs Act pia inaweka kinga dhidi ya kukamatwa kwa Rais akiwa madarakani.
Kwa hiyo, kwa tafsiri ya Wasonga, suala la Rais kutoa ushahidi mahakamani linahitaji kufuata utaratibu huo maalum wa kisheria, badala ya kutumia utaratibu wa kawaida wa kumlazimisha shahidi mwingine kufika mahakamani.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Kituo cha Kuzalisha Umeme cha Bwawa la Mwalimu Nyerere (JNHPP) kimetajwa kuwa alama ya kipekee ya jinsi ushirikiano, udugu, na utashi wa kisiasa wa mataifa ya Afrika unavyoweza kuleta maendeleo makubwa na kuunganisha bara zima la Afrika.
Kauli hiyo imetolewa leo Jumamosi, Agosti 22, 2026, na Waziri Mkuu wa Misri, Mostafa Madbouly, wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa mradi huo uliyofanywa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika eneo la Rufiji, mkoani Pwani
Madbouly alihudhuria hafla hiyo kwa maelekezo ya moja kwa moja kutoka kwa Rais wa Misri, Abdel Fattah El-Sisi, kuwasilisha pongezi za dhati kwa serikali na wananchi wa Tanzania.
Katika hotuba yake, Waziri Mkuu Madbouly amefafanua kuwa kukamilika kwa mradi huu mkubwa ni thibitisho la kile ambacho Waafrika wanaweza kukifanikisha pindi wanapoungana kwa pamoja.
“Mradi huu mkubwa uliokamilika na kuanza kufanya kazi leo unasimama mbele ya macho yetu kama ushuhuda wa utashi imara wa Tanzania na uwezo mkubwa wa kitaalamu na kihandisi wa Misri. Unaimarisha uelewa wa kisiasa wa pamoja wa kile ambacho watu wetu wanaweza kukifanikisha katika maendeleo endelevu pindi roho ya udugu, kuelewana, na ushirikiano inapotawala,” amesema Waziri Mkuu Madbouly.
Madbouly ameongeza kuwa mafanikio ya ujenzi wa bwawa hili, ambalo ni miongoni mwa mabwawa matatu makubwa zaidi barani Afrika, ni mfano hai wa uwezo wa kampuni za ndani za Afrika kutekeleza miradi mikubwa yenye viwango vya kimataifa.
Mradi huo umejengwa kwa miezi 42 ukizalisha megawati 2,115 za umeme kupitia ushirikiano wa kampuni za Misri za Arab Contractors na El Sewedy Electric. Suala hili linatajwa kufungua milango ya ushirikiano mpana zaidi wa kikanda. Madbouly amesisitiza kuwa Misri iko tayari kuendeleza ushirikiano huu sio tu na Tanzania, bali na nchi zote za Afrika ili kuunganisha nguvu kazi na rasilimali za bara hili. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesisitiza kuendelea na ujenzi wa miradi ya kuimarisha Gridi ya Taifa ili kuhakikisha umeme unaozalishwa katika Bwawa la Mwalimu Julius Nyerere unawafikia wananchi kote nchini.
Rais Samia ametoa maelekezo hayo leo Jumamosi, Agosti 22, 2026, Mkoani Pwani, wakati akizungumza na wananchi mara baada ya kuzindua Mradi wa Kuzalisha Umeme wa Megawati 2,115 wa Bwawa la Mwalimu Julius Nyerere.
Amesema miongoni mwa miradi hiyo ni ujenzi wa njia ya umeme ya Kilovoti 400 kutoka Chalinze hadi Dodoma yenye urefu wa kilomita 345, pamoja na upanuzi wa kituo cha kupokea na kupooza umeme cha Zuzu Mkoani Dodoma. Amesema njia hiyo imekamilika na kuwashwa Agosti 20, 2026, hali ambayo imewezesha Dodoma kupata umeme wa uhakika bila kukatika mara kwa mara.
Rais Samia amesema kukamilika kwa njia hiyo pia kunaiwezesha SGR ya Dodoma kuwa na umeme wake wa uhakika na kuondokana na changamoto ya kuingiliwa kwa umeme unaotumika kuendesha huduma hiyo. Amesema njia hiyo ina umuhimu mkubwa katika kusafirisha umeme kutoka Bwawa la Mwalimu Julius Nyerere kwenda Nyanda za Juu Kusini, Kanda ya Kati, Ziwa, Magharibi na Kaskazini.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewataka Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, na Wakuu wa Taasisi mbalimbali za Serikali kujiandaa mapema kukabiliana na mvua kubwa zinazotabiriwa kunyesha nchini, ili kuzuia maafa na kulinda maisha na mali za wananchi.
Rais Samia amebainisha kuwa taarifa rasmi zinazotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) zinaonesha uwezekano mkubwa wa kuwepo kwa mvua hizo kubwa zinazohusishwa na mfumo wa hali ya hewa wa El Niño, jambo linalohitaji hatua za haraka na za kimkakati kabla ya athari kujitokeza.
“Niwaombe nendeni mkajitayarishe, mkaweke mazingira sawa ili mvua hizo zitakapoanza zisilete maafa makubwa kwa wananchi wetu,” amesisitiza Rais Samia.
Amehimiza kuwa tahadhari na mrejesho kutoka TMA vinapaswa kuchukuliwa kwa uzito wa hali ya juu na viongozi katika ngazi zote, kwa kusafisha mifereji, kuandaa mifumo ya uokoaji, na kuondoa wananchi waliopo katika maeneo hatarishi.
“Kwa hiyo niwaombe sana, tahadhari zimeanza kutolewa, hatua zichukuliwe ili mvua hizi zisilete madhara kwa wananchi wetu,” amesisitiza.
Rais Samia ametoa maelekezo hayo leo Jumamosi, Agosti 22, 2026, wakati akizungumza na wananchi mkoani Pwani mara baada ya kukamilisha uzinduzi rasmi wa Mradi wa Kimkakati wa Kufua Umeme wa Bwawa la Mwalimu Julius Nyerere (JNHPP) wenye uwezo wa Megawati 2,115. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amebainisha kuwa kukamilika kwa Mradi wa Kufua Umeme wa Bwawa la Mwalimu Julius Nyerere (JNHPP) kutoa somo kubwa kuhusu umuhimu wa nidhamu ya ufuatiliaji, ustahimilivu wa changamoto, na uimara katika kusimamia malengo ya miradi ya kimkakati nchini.
Akizungumza leo Jumamosi, Agosti 22, 2026, wakati akizindua rasmi mradi huo mkoani Pwani, Rais Samia ameeleza kuwa uamuzi wa kuanzisha mradi pekee hautoshi, bali matokeo chanya hutegemea namna Serikali inavyofuatilia utekelezaji wake hatua kwa hatua hadi kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Rais Samia amewashukuru viongozi wa Awamu zilizotangulia kwa kuendeleza maono ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, ya kutumia rasilimali za Mto Rufiji kuzalisha umeme, akiwataja Hayati Ali Hassan Mwinyi, Hayati Benjamin Mkapa, na Rais wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete, kwa mchango wao mkubwa katika kuendeleza dira hiyo.
Akiangazia ujasiri uliotumika kuanza kwa ujenzi huo, Rais Samia amemkumbuka na kumshukuru Hayati Dkt. John Pombe Magufuli kwa msimamo wake wa kuhakikisha fedha zinapatikana na kazi inaanza bila kuyumbishwa na upinzani wa ndani au nje ya nchi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema kukamilika kwa Mradi wa Bwawa la Kuzalisha Umeme la Julius Nyerere (JNHPP) ni utekelezaji wa ndoto ya muda mrefu ya nchi wa kuwa na nishati ya uhakika kwa ajili ya kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Akizungumza leo Jumamosi, Agosti 22, 2026, wakati akizindua rasmi mradi huo mkoani Pwani, Rais Samia ameeleza kuwa Serikali ilitekeleza mradi huo kwa uzito unaostahili kutokana na umuhimu wake mkubwa kwa maendeleo ya Taifa, akisisitiza kuwa hakukuwa na namna ya kuuacha kutokana na mchango wake katika Gridi ya Taifa.
Rais Samia amekumbusha kuwa mnamo Desemba 22, 2022 alifika eneo hilo kushuhudia hatua ya kufungwa kwa njia ya kuchepusha maji ya Mto Rufiji na kuanza kujazwa kwa bwawa, ambapo awali ilitarajiwa kuchukua miaka mitatu lakini kwa neema ya Mungu bwawa hilo lilijaa ndani ya mwaka mmoja na nusu na kuwezesha majaribio ya uzalishaji kuanza mapema.
Katika hafla hiyo ya kihistoria, Rais Samia amezindua rasmi kituo cha kuzalisha umeme, pamoja na kutembelea na kukagua mitambo ya uzalishaji, tuta kuu, na kituo cha kupokea na kusafirisha umeme kwenda kwenye Gridi ya Taifa, huku akibainisha kuwa maeneo yote yanafanya kazi kwa ufanisi mkubwa na kuleta fahari kwa taifa.
Mradi wa JNHPP una uwezo wa kuzalisha megawati 2,115 za umeme, hatua inayoongeza kwa kiasi kikubwa uwezo wa nchi katika kuhudumia shughuli za uzalishaji, viwanda, uwekezaji, na maendeleo ya mwananchi mmoja mmoja.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewakosoa watu wanaodai kuwa Mradi wa Kuzalisha Umeme wa Bwawa la Mwalimu Julius Nyerere (JNHPP) ni mradi usio na tija ama "tembo mweupe" (white elephant), akisisitiza kuwa Serikali inaendelea na ujenzi wa njia kuu za kusafirisha umeme huo kwa kasi kubwa ili kufikia wananchi na maeneo ya uzalishaji nchi nzima.
Akizungumza leo Jumamosi, Agosti 22, 2026, mkoani Pwani mara baada ya kuzindua rasmi mradi huo wa kimkakati, Rais Samia ameeleza kuwa kasi ya ukuaji wa uwekezaji na viwanda nchini inaongeza mahitaji ya nishati kwa kiwango kikubwa, kiasi kwamba akiba ya umeme iliyopo hivi sasa huenda isitoshe katika miaka michache ijayo.
Amesisitiza kuwa madai ya mradi huo kukosa manufaa hayana msingi wa kitalaamu wala kiyakinifu, kwani changamoto ya miundombinu ya usafirishaji iliyokuwepo inashughulikiwa kikamilifu.
“Ujenzi wa njia za kusafirisha umeme unaendelea kwa kasi kubwa na mradi huu ni mradi wa manufaa makubwa kwa Taifa na si kama wanavyosema,” amesema Rais Samia.
Ameongeza kuwa kutokana na kasi hiyo ya ukuaji wa uchumi, Serikali haitasimama hapo bali itaendelea kuwekeza katika vyanzo vingine vya nishati mseto vikiwemo umeme wa jua na upepo ili kujenga usalama wa nishati wa muda mrefu.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Mkurugenzi mstaafu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Akinwumi Adesina, amekitaja Kituo cha Kuzalisha Umeme cha Bwawa la Mwalimu Nyerere (JNHPP) kama kielelezo thabiti cha maono ya maendeleo ya nchi ya Tanzania na safari yake ya utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050
Akizungumza leo Jumamosi, Agosti 22, 2026, katika hafla ya uzinduzi rasmi wa kituo hicho uliofanywa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan huko Rufiji mkoani Pwani, Adesina ameeleza kuwa Tanzania haisherehekei tu mafanikio makubwa ya kihandisi, bali pia inatoa tamko zito la kujiamini katika mustakabali wake wa baadaye.
“Tanzania inapotazama mbele kuelekea Dira yake ya 2050 chini yako Mheshimiwa Rais... somo hapa liko wazi kabisa: kusanya nguvu za ndani, karibisha nguvu kutoka nje, jenga Tanzania imara zaidi,” amesema Adesina.
Adesina amebainisha kuwa ujenzi wa mradi huo mkubwa zaidi wa kufua umeme nchini, uliogharimu shilingi trilioni 7.45 (sawa na takriban dola bilioni 3 za Kimarekani) zilizofadhiliwa kikamilifu na Serikali ya Tanzania, unaonesha kile kinachowezekana pale ambapo malengo ya kitaifa yanapokutana na nia thabiti pamoja na vitendo.
Adesina ameongeza kuwa ni jambo la heshima mradi huo kubeba jina la Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, ambaye aliwafundisha Watanzania kuamini katika uwezo wao wenyewe wa kuunda kesho yao
Akitaja faida za kiuchumi za mradi huo, Adesina amesisitiza kuwa umuhimu wa JNHPP haupo tu kwenye megawati 2,150 zitakazozalishwa, bali upo kwenye kile ambacho nishati hiyo inakiwezesha katika kubadili maisha ya jamii na uchumi. Umeme wa uhakika utasaidia kupanua viwanda, kukuza biashara, kutengeneza ajira, kuimarisha sekta za elimu na afya, kukuza kilimo cha kisasa, na kuendeleza teknolojia za kidijitali
Amesema nishati hiyo pia itawezesha uongezaji wa thamani ya madini ya Tanzania kupitia usindikaji wa ndani, pamoja na kubadilisha mazao ya kilimo kuwa bidhaa za thamani kubwa zinazoweza kushindana katika masoko ya Afrika na duniani.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Nishati, Deogratius Ndejembi, amesema kuwa kuanza kufanya kazi na kuzinduliwa rasmi kwa Mradi wa Kuzalisha Umeme wa Bwawa la Mwalimu Julius Nyerere (JNHPP) ni matokeo ya juhudi na maono makubwa ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa asilimia 100 na kuimarisha uchumi wa taifa.
Ndejembi ameyasema hayo leo Jumamosi, Agosti 22, 2026, wakati akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mradi huo mkoani Pwani mbele ya Rais Samia, akieleza kuwa kituo hicho kina jumla ya mitambo tisa, ambapo kila mtambo una uwezo wa kuzalisha megawati 235 na kufikisha jumla ya megawati 2,115.
Amesema kuwa kukamilika kwa JNHPP kumeongeza uwezo wa jumla wa Tanzania wa kuzalisha umeme kufikia megawati 4,646, huku mahitaji ya juu ya Gridi ya Taifa yakiwa ni megawati 2,271, hali inayofanya nchi kuwa na ziada kubwa ya umeme wa megawati 2,375.
Akitaja mwelekeo wa ziada hiyo, Ndejembi amebainisha kuwa Serikali chini ya uongozi wa Rais Samia imeelekeza kuanza kutumika kwa fursa hiyo kufanya biashara ya nishati na nchi jirani, ambapo tayari Tanzania imeingia makubaliano rasmi na Zambia kwa ajili ya kuiuzia umeme.
Pamoja na Zambia, Ndejembi ameeleza kuwa Tanzania pia ina makubaliano na Serikali ya Kenya ya kuuziana umeme kulingana na mahitaji ya kila nchi, huku mazungumzo na nchi nyingine jirani yakiendelea ili kukuza biashara ya nishati kikanda.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Nishati, Deogratius Ndejembi, amesema Serikali inaendelea kuimarisha miundombinu ya usafirishaji na usambazaji wa umeme nchini ili kuhakikisha ongezeko la uzalishaji linaendana na upatikanaji wa umeme wa uhakika kwa wananchi na shughuli za kiuchumi, akisisitiza kuwa hatua hiyo ni sehemu ya kutekeleza maelekezo na maono ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Mradi wa Kufua Umeme wa Bwawa la Mwalimu Nyerere (JNHPP) mkoani Pwani, Ndejembi amesema Serikali imekamilisha kwa asilimia 98 ujenzi wa njia ya umeme yenye urefu wa zaidi ya kilomita 617 ya msongo wa kilovolti 400 kutoka Iringa kupitia Mbeya hadi Songwe, ambayo pia itaunganisha Mkoa wa Rukwa kwenye Gridi ya Taifa. Pamoja na hayo, ujenzi wa njia ya Songea–Tunduru–Masasi–Maumbika unaendelea ili kuimarisha upatikanaji wa umeme katika mikoa ya Lindi na Mtwara.
Ameongeza kuwa Serikali inaendelea kuwekeza katika Kituo cha Kupokea Umeme cha Ibadakuli mkoani Shinyanga, kituo kinachoboreshwa kutoka msongo wa kilovolti 220 hadi 400 ili kuongeza uwezo wa kusafirisha umeme kutoka Dodoma kupitia Singida na Tabora hadi Shinyanga. Boreshaji hilo linaenda sambamba na uanzishwaji wa mradi wa Tanzania–Uganda Interconnector, utakaosaidia kusafirisha umeme kuelekea Geita na Kanda ya Ziwa kwa ajili ya shughuli za madini na kiuchumi.
Waziri Ndejembi amesema kuwa pamoja na kuongezeka kwa uzalishaji wa umeme, Wizara inajikita katika kuboresha miundombinu ya usambazaji ili kuondoa changamoto za kukatika kwa umeme kunakotokana na uchakavu, na kuhakikisha ziada ya umeme inawafikia wananchi kwa ufanisi na uhakika mkubwa.
Akizungumzia malengo ya siku za usoni, Ndejembi amebainisha kuwa mahitaji ya nishati yanapoongezeka kutokana na kasi ya shughuli za kiuchumi na kijamii, Wizara itaendelea kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 kwa kulenga kufikisha uzalishaji wa umeme hadi megawati 8,000 ifikapo mwaka 2030 kupitia vyanzo mbalimbali vikiwemo maji, gesi asilia, jua, upepo, na makaa ya mawe.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Lazaro Jacob Twange, amebainisha kuwa ujenzi wa Kituo cha Umeme cha Bwawa la Mwalimu Nyerere (JNHPP) umewajengea wataalamu na wafanyakazi wa Kitanzania uzoefu na ujuzi wa hali ya juu, utakao waongezea uwezo wa kushindana katika soko la ajira la ndani na nje ya nchi.
Twange ameyasema hayo leo Jumamosi, Agosti 22, 2026, wakati akitoa taarifa rasmi ya mradi huo mbele ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wa hafla ya uzinduzi wa bwawa hilo mkoani Pwani.
Amesema zaidi ya asilimia 95 ya nguvu kazi iliyoshiriki kikamilifu katika utekelezaji wa mradi huo ilikuwa ya Watanzania, hatua iliyotoa mafunzo kwa vitendo na ujuzi wa kimkakati katika kusimamia miundombinu mikubwa ya nishati.
Pamoja na nguvu kazi hiyo, Twange amefichua kuwa hata Mhandisi Mshauri wa mradi huo alikuwa Mtanzania, jambo linalothibitisha kuwa wataalamu wa ndani wana uwezo mkubwa wa kusimamia miradi ya kimkakati na kuikamilisha kwa wakati na viwango vinavyotakiwa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI PICHA:
Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega na mwenzake, Waziri wa Maji, Juma Aweso wakimpokea aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA. Freeman Mbowe alipowasili kuhudhuria uzinduzi wa Bwawa la Kuzalisha umeme la Julius Nyerere unaofanyika Rufiji, mkoani Pwani -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Kituo cha Umeme cha Bwawa la Mwalimu Nyerere (JNHPP) kimetajwa kuwa mhimili mkuu wa nishati nchini Tanzania, ukifungua fursa mpya za ukuaji wa viwanda, uwekezaji, biashara, pamoja na kuboresha maisha ya mwananchi mmoja mmoja.
Akiwasilisha maelezo hayo mkoani Pwani wakati wa uzinduzi rasmi wa mradi huo ulioongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Lazaro Jacob Twange, amebainisha kuwa kituo hicho ni miongoni mwa uwekezaji mkubwa zaidi kuwahi kufanywa katika sekta ya umeme nchini.
Twange ameeleza kuwa uwekezaji huo haukidhi tu ongezeko la mahitaji ya ndani na kuimarisha Gridi ya Taifa, bali pia unaiweka Tanzania katika nafasi nzuri ya kuwa kitovu cha biashara ya umeme kwa nchi za Afrika Mashariki na Kusini.
Kituo hicho kilichopo kwenye Mto Rufiji kina mitambo tisa ya kisasa, kila mmoja ukiwa na uwezo wa kuzalisha megawati 235 na kufanya jumla ya uwezo kufikia megawati 2,115, pamoja na miundombinu ya kupokea na kusafirisha umeme yenye ukubwa wa zaidi ya mita za mraba 58,075.
Ametaja kuwa mradi huo umegharamiwa na Serikali kupitia mapato ya ndani kwa Shilingi trilioni 7.45, ambapo hadi kufikia Juni 2026 mkandarasi alikuwa amelipwa Shilingi trilioni 7.11 (sawa na asilimia 96), huku ukiendeshwa na watumishi 161 wa Kitanzania bila msaada wa wataalamu wa kigeni.
Akiweka wazi takwimu za uzalishaji, Twange amebainisha kuwa tangu mtambo wa kwanza uanze kazi Februari 2024, kituo kilichangia asilimia 43.5 ya umeme wote wa gridi katika mwaka wa fedha 2024/25, na kufikia mwaka 2026 kimechangia asilimia 50 ya umeme wote unaoingizwa kwenye Gridi ya Taifa.
Pamoja na uzalishaji wa nishati, mradi huo umewezesha kupatikana kwa miundombinu mingine ya kijamii, ikiwemo nyumba 84 za watumishi, zahanati, maeneo ya michezo, pamoja na daraja la kudumu lenye urefu wa mita 250 linaloweza kubeba hadi tani 250.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Kituo cha Kuzalisha Umeme cha Bwawa la Mwalimu Nyerere (JNHPP) kimezinduliwa rasmi leo Jumamosi, tarehe 22 Agosti, 2026, na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika eneo la Rufiji mkoani Pwani.
Hatua hii inadhihirisha mabadiliko makubwa na ya kihistoria katika sekta ya nishati nchini, kupitia mradi huo wa kimkakati wenye uwezo wa kuzalisha megawati 2,115 kupitia mitambo tisa, ambapo kila mtambo una uwezo wa Megawati 235.
Mradi huo umegharimu takribani Shilingi trilioni 7.452 za fedha za ndani za Serikali ya Tanzania, ambapo ujenzi wake ulianza rasmi Juni 2019 na kukamilika kikamilifu Machi 2025.
Uzinduzi huo unaashiria dhamira ya dhati ya Serikali ya kuimarisha upatikanaji wa umeme wa uhakika, kuchochea uwekezaji wa viwanda, na kukuza uchumi wa taifa kwa ujumla.
Kwa mujibu wa takwimu za Wizara ya Nishati, hadi kufikia Mei 31, 2026, JNHPP ilikuwa imechangia takriban asilimia 44.9 ya umeme wote unaozalishwa na kuingizwa kwenye Gridi ya Taifa, hatua iliyosaidia kufikisha jumla ya uwezo wa uzalishaji umeme nchini kuwa megawati 4,646 na kupunguza changamoto za mgao.
Pamoja na kutumia teknolojia ya kisasa katika uendeshaji wake, kituo hicho kimekuwa kielelezo cha utaalamu wa ndani kwani kinaendeshwa na kusimamiwa na Watanzania kwa asilimia 100.
Mbali na kutoa nishati ya umeme, mradi wa JNHPP unatarajiwa kuleta faida mseto kijamii na kiuchumi, ikiwemo kudhibiti mafuriko katika Bonde la Rufiji, kuendeleza kilimo cha umwagiliaji, pamoja na kuchochea fursa mpya za utalii.
Kutokana na ukubwa wake, Kituo cha JNHPP kinashika nafasi ya tano kwa ukubwa barani Afrika, hatua inayoweka jina la Tanzania kwenye ramani ya dunia katika miundombinu mikubwa na endelevu ya nishati.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) taifa, Freeman Mbowe ni miongoni wa waliohudhuria tukio la uzinduzi wa Kituo cha Kuzalisha Umeme cha Julius Nyerere (JNHPP) chenye uwezo wa kuzalisha Megawati 2,115 leo tarehe 22 Agosti 2026, katika eneo la mradi lililopo Rufiji, Mkoa wa Pwani.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI PICHA:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Waziri wa Nishati, Deogratius Ndejembi na viongozi wengine wakati alipowasili katika eneo la Mradi Kituo cha Kuzalisha Umeme cha Julius Nyerere (JNHPP).
Rais Samia atazindua rasmi Kituo cha Kuzalisha Umeme cha Julius Nyerere (JNHPP) chenye uwezo wa kuzalisha Megawati 2,115 leo tarehe 22 Agosti 2026, katika eneo la mradi lililopo Rufiji, Mkoa wa Pwani. -
Jambo TV
@Jambotv_
Mbunge wa Tunduru Kaskazini, Ado Shaibu Ado, amesema amewasilisha Bungeni mapendekezo ya masuala mawili muhimu akitaka yapangiwe muda na kushughulikiwa katika Mkutano wa Nne wa Bunge unaotarajiwa kuanza Agosti 26, 2026.
Hoja ya kwanza inahusu mchakato wa upatikanaji wa Katiba Mpya, ambapo Ado amesema amewasilisha hoja kwa mujibu wa Kanuni ya 64(1) ikisomwa pamoja na Kanuni ya 65(1) za Kanuni za Kudumu za Bunge.
Mbunge huyo anataka Bunge liazimie Serikali kuwasilisha ramani kamili ya mchakato wa Katiba Mpya, ikieleza hatua zitakazopitiwa, ratiba ya utekelezaji, muda wa kukamilisha mchakato pamoja na bajeti inayohitajika.
Ado amesema ramani hiyo inapaswa pia kuainisha mapitio ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, kuundwa kwa Kamati ya Wataalam, matumizi ya maoni na kazi zilizofanyika katika mchakato uliopita, Mkutano wa Kitaifa wa Wadau, ushirikishwaji wa wananchi pamoja na Kura ya Maoni.
Hoja ya pili inahusu vijana 436 wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) walioshiriki katika ujenzi wa Ikulu ya Chamwino na miradi mingine ya kimkakati ya Serikali.
Ado amesema vijana hao wamewasilisha kwake ombi la kuifikisha hoja yao Bungeni, wakieleza kuwa baada ya kushiriki katika kazi hizo walipewa matarajio na ahadi ya kupatiwa ajira, lakini hadi sasa sehemu kubwa yao haijapata ajira wala kuwezeshwa kwa namna itakayowasaidia kujenga maisha yao.
Kupitia ombi hilo, Ado amesema vijana hao wanataka Bunge liishauri au kuitaka Serikali kuchunguza hali ya vijana wote 436, kutekeleza ahadi ya ajira kwa wale wanaokidhi vigezo na ambao bado hawajapata ajira, au kuweka utaratibu maalum wa kuwawezesha kiuchumi pale ajira ya moja kwa moja inaposhindikana.
Pia wameomba Serikali izingatie changamoto za maisha wanazokabiliana nazo baada ya kumaliza utumishi wao, pamoja na wale waliopata athari za kiafya kutokana na kazi nzito walizofanya.
Ado amesema kupitia hoja hizo mbili, anatarajia Uongozi wa Bunge utazipatia nafasi ili ziweze kushughulikiwa katika Mkutano wa Nne wa Bunge. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI PICHA:
Waziri wa Nishati, Deogratius Ndejembi akiwa na Naibu Waziri wa Nishati, Salome Makamba na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati anayeshughulikia Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Felchesmi Mramba wakiwa tayari kwa uzinduzi rasmi wa Kituo cha Kuzalisha Umeme cha Julius Nyerere (JNHPP) chenye uwezo wa kuzalisha Megawati 2,115 utakaofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 22 Agosti 2026. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkuu wa Mkoa wa Songwe ndugu Jabiri Makame, amesema Mkoa wa Songwe upo tayari kuilea, kuiwezesha na kukuza Sekta Binafsi ili kuiwezesha kuchangia utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 kwa kuweka mazingira wezesheshi ya kuvutia uwekezaji, kuondoa vikwazo vinavyokabili Sekta Binafsi.
RC Makame ameyasema hayo katika Jukwaa la siku 2 la Dira 2050 Mkoani Songwe (Songwe Dira Forum) lililowakutanisha Wadau wa Sekta ya Umma na Sekta Binafsi kuanzia ngazi ya Kata hadi Mkoa kwa lengo la kuwajengea uwezo kuhusu maudhui ya dira na utekelezaji wake, wajibu wa Mamlaka za Serikali za Mitaa katika utekelezaji wa dira, uwezeshaji wa Sekta Binafsi ili kuchangia 70% ya utekelezaji wa dira, fursa za miradi ya ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi sambamba na uongozi wa kimkakati katika utekelezaji wa dira.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Mameneja wa Kanda na Mikoa wa Taasisi za Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Tume ya Ushindani (FCC) pamoja na Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA) wameagizwa kuhakikisha hakuna bidhaa bandia na duni katika maeneo yao wanayoyasimamia kiutendaji.
Maelekezo hayo yametolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Balozi Waziri Rajab Salum, wakati wa kikao cha menejimenti za Tume ya Ushindani (FCC), Shirika la Viwango Tanzania (TBS) pamoja na Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA), Agosti 21, 2026 jijini Dodoma, kwa lengo la kujadili na kupanga mikakati ya kuimarisha udhibiti wa bidhaa bandia nchini.
Katika kikao hicho, Balozi Salum amesisitiza umuhimu wa taasisi hizo kufanya kazi kwa ushirikiano, weledi, haki na uwajibikaji, akieleza kuwa uratibu mzuri ni muhimu katika kuhakikisha bidhaa zisizokidhi viwango na bidhaa bandia hazitawali soko.
Amesema udhibiti wa bidhaa bandia ni suala muhimu katika kulinda mlaji, wafanyabiashara wanaofuata sheria pamoja na uchumi wa nchi, hivyo taasisi zenye dhamana ya kusimamia soko zinapaswa kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa.
Balozi Salum amezitaka FCC, TBS na WMA kuongeza ushirikiano katika kubadilishana taarifa, kufanya ukaguzi na kuchukua hatua stahiki dhidi ya wanaojihusisha na uzalishaji, uingizaji au usambazaji wa bidhaa bandia na zisizokidhi viwango.
Aidha, amesisitiza umuhimu wa watumishi wa taasisi hizo kuwa waadilifu na kutekeleza majukumu yao kwa haki, ili kuhakikisha wafanyabiashara wanafuata sheria wanapata mazingira sawa ya ushindani na walaji wanapata bidhaa salama na zenye ubora.
Amesema matumizi ya teknolojia na taarifa sahihi yanapaswa kupewa kipaumbele katika kuimarisha mifumo ya udhibiti, kutokana na mabadiliko ya mbinu zinazotumiwa na baadhi ya watu katika kusambaza bidhaa bandia katika masoko.
Kwa upande mwingine, kikao hicho kimekuwa fursa kwa viongozi wa FCC, TBS na WMA kueleza changamoto zinazowakabili katika utekelezaji wa majukumu yao, pamoja na kuweka mikakati ya pamoja ya kuongeza ufanisi katika usimamizi wa soko.
Balozi Salum amesisitiza kuwa Serikali itaendelea kuimarisha ushirikiano kati ya taasisi zake ili kujenga mazingira ya biashara yenye ushindani wa haki, kulinda walaji na kuhakikisha wafanyabiashara wanaofuata sheria wanaendelea kufanya shughuli zao katika mazingira salama na yenye tija.
Kikao hicho ni sehemu ya jitihada za Wizara ya Viwanda na Biashara kuimarisha uratibu wa taasisi zake na kuhakikisha majukumu ya udhibiti wa soko yanatekelezwa kwa weledi, haki, uwajibikaji na kwa kuzingatia maslahi mapana ya Taifa. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) John Heche ameeleza kusikitishwa na kilichotokea leo Mahakamani, akibainisha kuwa Chama hicho kinapitia misukosuko mikubwa ambayo hakijawahi kupitia tangu kuanzishwa kwake Mwaka 1992
Heche amesema hayo akizungumza na Wanahabari, akieleza katika kipindi cha siku 576 tangu yeye na Lissu wachaguliwe kuongoza Chama, uongozi wao umekumbwa na changamoto ambapo CHADEMA imefanya Siasa kwa siku 267, huku Lissu akikaa Ofisini 78 pekeeThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Baada ya jopo la majaji watatu wa Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Dar es Salaam kukataa maombi yake ya kuachiwa huru na kumkuta na kesi ya kujibu, kesi ya uhaini namba 19605/2025 inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Antiphas Lissu, ilirejea tena mahakamani mchana wa leo Agosti 21, 2026 kwa ajili ya kuanza rasmi kwa utetezi wake
Kesi hiyo iliendelea mchana wa leo saa 9:48 mchana baada ya mapumziko mafupi yaliyotolewa na mahakama. Mara baada ya jopo la majaji kuingia ukumbini, upande wa mashtaka ulitangaza kuwa upo tayari kuendelea kusikiliza utetezi wa mshitakiwa kama shahidi wa kwanza, na Lissu pia alithibitisha utayari wake.
Hata hivyo, kabla ya kuanza utetezi wake, Lissu aliomba maelekezo ya mahakama kuhusu utaratibu wa mashahidi wake ambao tayari walikuwa wameruhusiwa kutoa ushahidi, akitaka kujua kama wanapaswa kuwepo ukumbini au watoke nje kwanza. Majaji walitoa maelekezo kuwa mashahidi wengine hawapaswi kuwepo ndani ya ukumbi wakati shahidi mwingine akiwa kizimbani
Kufuatia amri hiyo, viongozi waandamizi wa CHADEMA ambao walipangwa kuwa mashahidi wakiwemo John Mnyika, Amani Golugwa, na John Heche waliondoka ukumbuni ili kusubiri kuitwa kutoa ushahidi wao
Baada ya hapo, Lissu alisimama kama shahidi wa kwanza na kula kiapo kizimbani
Akianza kutoa ushahidi wake, Lissu alieleza kuwa sehemu ya kwanza ya utetezi wake inahusu maisha yake binafsi ili kuisaidia mahakama kuelewa yeye ni mtu wa namna gani. Alijitambulisha kama kiongozi wa chama cha kisiasa kilichosajiliwa kisheria, akishikilia nafasi ya Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa tangu tarehe 22 Januari 2025, nafasi ambayo alidumu nayo kwa takriban wiki tano au sita tu kabla ya kukamatwa na kufunguliwa mashtaka ya uhaini
Lissu alieleza kwa kina historia ya uongozi wake ndani ya CHADEMA, akibainisha kuwa alishikilia nafasi ya Umakamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara kwa miaka mitano tangu Desemba 2019 hadi Januari 22, 2025. Alikuwa Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA na Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama kuanzia mwaka 2010 hadi Septemba 7, 2017.
Kabla ya hapo, alihudumu kama Mkurugenzi wa Sheria, Katiba na Haki za Binadamu wa CHADEMA kuanzia...soma zaidi jambo.co.tz kupitia kiungo hiki
jambo.co.tz/sio-uhaini-ni-vita-ya-kisiasa-lissu-aanza-kuj… -
Jambo TV
@Jambotv_
MVUTANO MKALI RAIS KUITWA MAHAKAMANI, JAMHURI YAPINGA/ KESI ‘YASIMAMA’ KWA MUDA jambo.co.tz/mvutano-mkali-rais-kuitwa-mahakamani-jamhuri-… via @jambotv_
-
Jambo TV
@Jambotv_
Jopo la majaji watatu wa Mahakama Kuu, likiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru, leo Agosti 21, 2026, limetoa uamuzi katika shauri la uhaini namba 19605/2025 linalomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu.
Katika uamuzi huo uliokuwa unasubiriwa kwa hamu, mahakama imetangaza kuwa Lissu ana kesi ya kujibu na hivyo anapaswa kuanza kutoa utetezi wake .
Uamuzi huu unakuja kufuatia kikao cha Ijumaa ya Agosti 17, 2026, ambapo majaji walisikiliza hoja za pande zote mbili baada ya upande wa mashtaka kufunga ushahidi wake wa mashahidi.
Katika hatua hiyo, Lissu aliiomba mahakama imwachie huru akitumia kifungu cha 312(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA), akidai kuwa upande wa Jamhuri umeshindwa kuthibitisha ushahidi wa awali (Prima facie case). Lissu alijenga hoja kuwa ushahidi uliowasilishwa haukufikia kiwango cha kumtia hatiani hata kama hangejibu lolote.
Hata hivyo, katika uamuzi wao wa leo, majaji wameeleza kuwa baada ya kupitia hati ya mashtaka, ushahidi wa mashahidi, na kanuni za kisheria, wamebaini kuwepo kwa kesi iliyojengwa dhidi ya mshitakiwa .
Mahakama imebainisha kuwa upande wa mashtaka umewasilisha viini vinavyoashiria mshitakiwa alitengeneza nia ya kuhamasisha umma kuvuruga uchaguzi kwa lengo la kuitisha serikali.
Miongoni mwa mambo yaliyochukuliwa kama uthibitisho wa nia hiyo ni maneno yaliyodaiwa kutamkwa na kuchapishwa na Lissu yakisema, "...msimamo huu unaashiria uasi... kwahiyo tunaenda kukinukisha sana sana" . Mahakama imehitimisha kuwa kutokana na ushahidi huo na mashauri mbalimbali ya kisheria yaliyorejewa, Lissu ana wajibu wa kujitetea.
Hatua inayofuata sasa ni kwa mshitakiwa kuanza kutoa utetezi wake dhidi ya tuhuma hizo nzito za uhaini. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara John Heche akiwasili Mahakamani Dar es Salaam leo kufuatilia kesi ya uhaini ya Tundu Lissu.
Jopo la majaji watatu, wanaoongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru, ambao ndiyo wanasikiliza Shauri la uhaini namba 19605/2025 dhidi ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu, leo Agosti 21, 2026 wanatarajiwa kuja na uamuzi utakaobainisha kama Tundu Lissu anayo kesi ya kujibu au hana katika shauri hilo.
Ijumaa ya Agosti 17, 2026 Majaji hao walieleza kuwa mara baada ya kusikiliza hoja za Lissu kuwa hana kesi ya kujibu na zile za jamhuri kuwa ana kesi ya kujibu pamoja na ushahidi wa mashahidi 17 wa jamhuri, jopo hilo lilihitaji muda kuandaa uamuzi ambao utatolewa leo.
Ijumaa hiyo Lissu aliiomba mahakama kutamka kuwa hana hatia na itamke kuwa anatakiwa kulipwa fidia. Akitumia kifungu cha 312(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA), Lissu alisema upande wa Jamhuri umeshindwa kuthibitisha kile alichoita "Prima facie case" (kutokuwa na kesi ya kujibu).
Alieleza kwamba Prima facie evidence/case ni ushahidi wa upande wa mashtaka peke yake kama haujafikia kiwango cha kumtia mtuhumiwa hatiani usipojibiwa hakuna hatia na Mahakama inatakiwa kurekodi mtuhumiwa kutokua na hatia.
Hata hivyo, macho na masikio ya wengi yanasubiri kuona na kusikia kama kiongozi huyo wa upinzani atakuwa na kesi ya kujibu au hatakuwa na kesi hiyo ambapo baada ya uamuzi wa majaji leo utaratibu mwingine utaendelea.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) imekataa kuendelea na mahojiano na Halmashauri ya Wilaya ya Same, ikisema haijaridhishwa na kiwango cha utekelezaji wa hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) pamoja na maagizo iliyoyatoa kwa Halmashauri hiyo.
Kamati hiyo imefikia uamuzi huo leo baada ya kupitia na kuchambua Taarifa ya Hesabu zilizokaguliwa za Halmashauri ya Wilaya ya Same kwa miaka ya fedha 2023/2024 na 2024/2025.
Katika uchambuzi huo, Kamati imesema haijaridhishwa na utendaji wa Halmashauri hiyo chini ya Afisa Masuuli, ikieleza kuwa kumekuwa na uzembe na kukosekana kwa utayari wa kushughulikia hoja za CAG pamoja na maagizo ya Kamati.
Kamati imesema kati ya maagizo saba iliyoyatoa katika kikao cha Oktoba 27, 2024, ni maagizo mawili pekee, sawa na asilimia 28, yaliyotekelezwa kikamilifu.
Aidha, katika Hesabu za mwaka wa fedha 2024/2025, CAG alitoa hoja na mapendekezo 18, lakini Halmashauri imetekeleza hoja nne pekee, sawa na asilimia 22.
Kamati pia imebaini kuwa Halmashauri hiyo haijatekeleza kikamilifu hoja zilizotolewa na CAG katika miaka iliyopita, ambapo kati ya hoja tisa zilizotolewa, ni hoja tatu pekee zilizotekelezwa.
Kutokana na hali hiyo, LAAC imesema mwenendo huo ni dharau kwa Bunge pamoja na CAG, ambaye kwa mujibu wa Kamati ni “jicho la Bunge”.
“Kutokana na hali hii, Kamati haiwezi kuendelea na mahojiano na Halmashauri ya Same, na hivyo wakatekeleze hoja zote.”
Kamati imeitahadharisha Halmashauri ya Same kutekeleza hoja zote za CAG na maagizo ya Kamati, huku ikitoa onyo kwa Halmashauri nyingine nchini ambazo zimekuwa zikishindwa kutekeleza maagizo ya Kamati na hoja za CAG.
Taarifa hiyo imesomwa na Mwenyekiti wa LAAC na Mbunge wa Tunduru Kaskazini, Ado Shaibu Ado, kwa niaba ya Kamati hiyo. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi imemhukumu kifungo cha maisha gerezani Alli Hamisi Mbelenje (30), mkazi wa Kijiji cha Makonde, Kata ya Mtama, Wilaya ya Lindi Mkoani Lindi baada ya kupatikana na hatia ya kosa la kumlawiti mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka nane.
Mtoto huyo, ambaye ni mwanafunzi wa darasa la nne, alidaiwa kufanyiwa kitendo hicho na mshtakiwa, ambaye hatimaye alipatikana na hatia katika Kesi Na. 15000 ya mwaka 2025.
Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi, Subira Mwakarobo, baada ya mahakama kuridhika na ushahidi uliotolewa dhidi ya mshtakiwa.
Upande wa Jamhuri uliwasilisha mashahidi sita (6) pamoja na vielelezo vitatu (3) ili kuthibitisha shtaka hilo. Upande huo wa mashtaka uliongozwa na Mofati Seti.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Stephen Wasira, amesisitiza umuhimu wa kuzingatia haki na uadilifu bila kuegemea maslahi binafsi, huku akikemea vikali tabia ya kuwa na viongozi wasio na msimamo madhubuti ndani ya chama hicho.
Wasira ametoa msisitizo huo leo, Agosti 20, 2026, alipokuwa akizungumza na viongozi pamoja na wanachama wa CCM wilayani Iramba mkoani Singida, ambapo amewataka wanachama wote kufuata misingi ya haki wakati wa mchakato wa uchaguzi wa viongozi.
Amebainisha kuwa CCM inahitaji viongozi thabiti wanaosimamia ukweli na misingi ya chama bila kuyumba au kubadilishwa na mazingira pamoja na tamaa za binafsi.
"CCM inahitaji viongozi wenye msimamo katika mambo ya msingi na wasiobadilika kutokana na mazingira au maslahi binafsi. Tunataka uongozi ambao hauyumbi. Tunataka mtu ambaye ana msimamo kwa mambo ya msingi. Huyo ndiye kiongozi wetu,” amesisitiza Wasira.
Katika wito wake kwa wanachama, Wasira ameonya dhidi ya kupatikana kwa viongozi kupitia njia za rushwa, vitisho, au ujanja wa aina yoyote, akieleza kuwa kiongozi anayechaguliwa ndiye kielelezo kuu cha taswira ya chama mbele ya jamii.
"Wanachama ndiyo wenye jukumu la kuhakikisha watu wanaopewa dhamana ya kuongoza Chama wana sifa na uwezo unaohitajika. Sisi ndiyo tunateua wanachama. Msije mkakubali Chama chetu kikapata uongozi unaotokana na rushwa bila uwezo wa kuongoza,” amesema.
Ametumia fursa hiyo kuwakumbusha viongozi wa ngazi mbalimbali ikiwemo Wenyeviti wa Wilaya wanaohusika na uteuzi wa viongozi wa matawi na Wenyeviti wa Mikoa wanaosimamia ngazi ya kata kuchukua tahadhari kubwa na kuwa waangalifu wanapotekeleza majukumu yao ya uteuzi.
Ametamatisha kwa kutoa onyo kali kuwa kiongozi yeyote atakayebainika kutumia nafasi yake vibaya kwa kupokea rushwa au kuteua viongozi wasio na sifa, hatavumiliwa bali atawajibishwa mara moja kulingana na kanuni na katiba ya chama. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) umetoa mapendekezo kuhusu kesi ya uhaini inayomkabili Wakili Tundu Lissu, baada ya kufuatilia mwenendo wa shauri hilo kuanzia Aprili 9, 2025 hadi Agosti 19, 2026.
Mratibu Kitaifa wa Mtandao huo, Wakili Onesmo Olengurumwa ameitaka Mahakama kuhakikisha kesi inasikilizwa na kuamuliwa kwa haraka, kudhibiti maombi ya kuahirisha kesi, kulinda mawasiliano ya siri kati ya mshtakiwa na mawakili wake, pamoja na kuhakikisha ushiriki wa umma na vyombo vya habari.
Kwa upande wa DPP, THRDC imependekeza tathmini ya mara kwa mara ya ushahidi unaotumika katika mashtaka na kupunguza ucheleweshaji usio wa lazima. Pia imeitaka Jeshi la Magereza kuhakikisha mahabusu wanapata huduma muhimu, mawasiliano na familia pamoja na mashauriano ya siri na mawakili.
Kwa Serikali, THRDC imeitaka kulinda uhuru wa waangalizi, waandishi wa habari na wafuatiliaji wa haki za binadamu, kuchunguza tuhuma za ukiukwaji wa haki na kutumia mifumo halali ya kisheria kutafuta suluhu ya shauri la Lissu.
THRDC pia imewasihi wanasiasa na vyama vya siasa, ikiwemo CHADEMA, kukaa kwenye meza ya mazungumzo ili kutafuta suluhu ya kudumu ya changamoto zilizopo, huku ikiendelea kusisitiza umuhimu wa Tanzania kupata Katiba mpya.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Baada ya kusambaa kwa picha na video mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii zikimuonesha Mama Veronica Mwachali Bilingi akilalamikia kubomolewa kwa nyumba ya familia yake bila kulipwa fidia, sakata hilo limechukua sura mpya.
Diwani wa Kata ya Makulu, Samson Mkopi, amekanusha madai ya kuwa ubomoaji huo una uhusiano na masuala ya kisiasa, akisema hatua hiyo imefanyika kwa kuzingatia utaratibu uliowekwa.
Mkopi amesema hana ajenda ya kisiasa dhidi ya familia hiyo, akisisitiza kuwa ubomoaji huo haukulenga familia hiyo kwa sababu za kisiasa.
Kwa upande mwingine, Halmashauri ya Jiji la Dodoma imetupatia nyaraka mbalimbali zinazohusiana na eneo hilo, ikiwemo nyaraka zinazoonesha mpango wa kupanua barabara katika eneo husika.
Kwa mujibu wa nyaraka hizo, maeneo yaliyofikiwa na hatua hiyo yalikuwa maeneo ya wazi yaliyotengwa kwa ajili ya matumizi hayo kabla ya baadhi ya wananchi kujenga katika maeneo hayo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Aliyekuwa Naibu Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Zanzibar, Abdi Mahmoud Abdi, amepokelewa rasmi katika Ofisi za CCM Pemba kufuatia uteuzi wake mpya wa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Zanzibar.
Katika mapokezi yaliyofanyika leo Pemba, Naibu Katibu Mkuu Abdi amewashukuru viongozi na wanachama waliojitokeza na kuahidi kuwa utumishi wake utajikita katika kukifanya chama kuwa imara zaidi na kimbilio la wanyonge
Akizungumzia mjadala ulioibuka kwenye mitandao ya kijamii na maeneo mbalimbali kuhusu umri wake tangu kuteuliwa kwake, Abdi ameweka wazi kuwa ukomavu wa uongozi na utumishi serikalini au ndani ya chama haupimwi kwa miaka ya mtu
Kuelekea uchaguzi wa ndani wa chama unaotarajiwa kufanyika mwakani kuanzia ngazi ya shina hadi taifa, Abdi amewahimiza wanachama wote wenye nia na uthubutu wa kugombea kujitokeza kwa ujasiri. Amefafanua kuwa ndani ya CCM uongozi unapatikana kwa misingi ya demokrasia na hakuna mwanachama mwenye umiliki wa kudumu wa nafasi hizo
“Msiogope, hakuna mtu mwenye hatimiliki ya nafasi ya uongozi kwenye chama chetu. Na wanachama na viongozi wanapimwa kwa utumishi wao katika chama chetu. Ni nini wamekifanyia chama katika utumishi wao katika nafasi za miaka mitano iliyopita”, ameeleza.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Serikali kupitia Wizara ya Nishati imetangaza mkakati thabiti wa kuhakikisha nchi inaondokana kabisa na changamoto ya kukatika kwa umeme nchi nzima, ikieleza kuwa lengo la sasa la wataalamu ni kuhakikisha nishati hiyo inakuwepo wakati wote bila adha ya nchi nzima kuingia gizani.
Mkakati huo umewekwa wazi leo Agosti 20, 2026, na Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati, Mhandisi Innocent Luoga, wakati wa mahojiano maalum kuelekea uzinduzi wa kihistoria wa Bwawa la Julius Nyerere (JNHPP) utakaofanywa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Jumamosi hii ya Agosti 22, 2026.
Akifafanua kuhusu hitilafu ya kiufundi iliyotokea mwezi Juni na kusababisha nchi nzima kukosa nishati hiyo, Mhandisi Luoga amesema kuwa changamoto hiyo ilikuwa ya kiufundi na imetafsiriwa kama fursa ya kuimarisha mifumo ya dharura ili kuzuia matukio ya aina hiyo kujirudia
“Kwa hiyo suala la kukatika umeme kwa nchi nzima, halitakiwi, halitakiwi. Kwahiyo imekuwa changamoto na fursa... huko tunakoelekea sasa tunataka tuondokane na hali ya kukatika kwa umeme kwa nchi nzima,” amesisitiza Mhandisi Luoga.
Ili kufikia azma hiyo, Wizara imeanza kutekeleza mipango madhubuti ikiwa ni pamoja na ujenzi wa njia huru na maalum ya kusafirisha umeme kwa ajili ya treni za mwendokasi (SGR) kuanzia Dar es Salaam hadi Makutopora, na tayari imeshafika Isaka na Mwanza. Hatua hii inalinda usafiri huo wa kimkakati na mtikisiko wowote wa gridi ya taifa
Pia, serikali imetenga kituo maalum cha kuzalisha umeme kwa kutumia gesi kilichopo Ubungo mkoani Dar es Salaam chenye uwezo wa takriban megawati 385 kama mbadala na 'jenereta' la dharura nchi nzima inapokabiliwa na changamoto ya nishati
“Endapo kutatokea na tatizo lolote pale bado tuna nafasi ya kuipatia umeme SGR, Na pamoja na mikakati tuliyokuwa nayo, mpango uliopo mwingine ni kuhakikisha kwamba kituo hicho hicho kinaweza kutumika kama jenereta hapo baadaye inapotokea tatizo lolote la umeme kwa nchi nzima basi baadhi ya maeneo yatakuwa yanapata umeme na SGR itakuwa inapata umeme,” amebainisha Kamishna Luoga -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati, Mhandisi Innocent Luoga, amesema kukamilika kwa miundombinu ya usafirishaji wa umeme kumewezesha mitambo yote tisa ya Bwawa la Julius Nyerere yenye uwezo wa MW 2,115 kufanya kazi na kusafirisha umeme katika maeneo mbalimbali nchini.
Luoga amesema njia ya KV 400 kutoka JNHPP hadi Chalinze, yenye urefu wa takribani kilomita 160, imekamilika, huku njia ya Chalinze hadi Dodoma, yenye kilomita 354, ikiwa imefikia asilimia 99.
Amesema mtandao huo utawezesha umeme kusafirishwa kuelekea Iringa, Mbeya, Tunduma, Rukwa na Zambia, pamoja na Singida, Tabora, Shinyanga, Mwanza na Ukanda wa Kaskazini hadi Kenya. Pia utaunganisha Kinyerezi na Mkuranga kwa ajili ya mahitaji ya umeme katika maeneo ya viwanda.
Mhandisi Luoga ameeleza hayo siku ya Alhamisi akizungumza katika mahojiano maalum na mwandishi Salehe Mohamed, kuhusu mradi huo utakaozinduliwa rasmi na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Jumamosi hii ya Agosti 22, 2026.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Kituo cha kuzalisha umeme kwa maji cha Bwawa la Mwalimu Nyerere (JNHPP), chenye uwezo wa kuzalisha megawati 2,115, kimekamilika kwa asilimia 100 na kuanza kufanya kazi kikamilifu ili kukidhi mahitaji ya umeme nchini.
Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati, Mhandisi Innocent Luoga, amebainisha kuwa mafanikio hayo yanatokana na kukamilika kwa ufungaji wa mitambo yote tisa, ambapo kila mtambo una uwezo wa kuzalisha megawati 235.
Akizungumza katika mahojiano maalum na mwanahabari Saleh Mohamed, Mhandisi Luoga ameeleza kuwa kukamilika kwa mradi huo kumesababisha Serikali kuanza maandalizi ya uzinduzi rasmi, ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, tayari ameridhia kuongoza uzinduzi huo.
Amesisitiza kuwa pamoja na kukamilika kwa JNHPP, Serikali haina mpango wa kusimama hapo bali inaendelea kutekeleza mkakati kabambe wa kuongeza vyanzo mseto vya nishati ili kuondoa utegemezi wa chanzo kimoja cha umeme.
Katika kuelekea huko, Mhandisi Luoga amefichua kuwa mnamo mwezi Juni Serikali ilikamilisha ujenzi wa mtambo wa umeme wa jua wa megawati 50 wilayani Kishapu, na kwamba mwezi uliopita (Julai) Waziri wa Nishati alisaini mkataba mwingine wa megawati 100 za sola ili kufikisha jumla ya megawati 150 za nishati hiyo.
“Tunataka tuwe na vyanzo mseto. Zamani tulikuwa na vyanzo viwili tu—maji na gesi, na wakati fulani mafuta, jambo ambalo lilitusababishia changamoto pindi chanzo kimoja kilipopata hitilafu,” amesema Mhandisi Luoga, akiongeza kuwa nchi sasa inawekeza kwenye maji, gesi, upepo, jua, na joto ardhi.
Ili kuimarisha zaidi gridi ya taifa dhidi ya athari za mabadiliko ya tabianchi, Serikali imeanza kuweka mkazo kwenye nishati ya joto ardhi (mvuke kutoka ardhini), ambapo maeneo 52 tayari yamebainishwa nchi nzima kwa ajili ya uzalishaji huo.
Kukamilika kwa JNHPP na utekelezaji wa mikakati hiyo ya nishati mseto kunatarajiwa kuwa mhimili mkuu wa kuimarisha upatikanaji wa umeme wa uhakika, pamoja na kuchochea ukuaji wa viwanda, biashara, na uwekezaji nchini. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Kuelekea uzinduzi wa Bwawa la Kuzalisha Umeme la Julius Nyerere (JNHPP) uliopangwa kufanyika Jumamosi hii, Agosti 22, 2026, Serikali imeweka wazi kuwa haitasimama hapo, bali inaendelea kutekeleza mkakati kabambe wa kuongeza vyanzo mseto vya nishati ili nchi isiwe na utegemezi wa chanzo kimoja tu cha umeme
Akizungumza katika mahojiano maalum leo Agosti 20, 2026, Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati, Mhandisi Innocent Luoga, amebainisha kuwa uzinduzi huo utakaofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, utaingiza megawati 2,015 za umeme wa maji kwenye gridi ya taifa. Hata hivyo, amesisitiza kuwa wizara inaendelea kupanua vyanzo vingine vya uzalishaji ili kuhakikisha usalama na uhakika wa nishati nchini
Mhandisi Luoga alieleza kuwa serikali tayari imepiga hatua kubwa katika nishati mbadala, ambapo mnamo mwezi Juni, ilikamilisha ujenzi wa mtambo wa kuzalisha umeme kwa kutumia nishati ya jua wa megawati 50 uliopo Kishapu. Mbali na mradi huo, Kamishna amefichua kuwa mwezi uliopita (Julai), Waziri wa Nishati alisaini mkataba mwingine wa kuzalisha megawati 100 za nishati ya jua, hatua inayolenga kufikisha jumla ya megawati 150 za uzalishaji wa sola
"Tunataka tuwe na vyanzo mseto. Zamani tulikuwa na vyanzo viwili tu- maji na gesi, na wakati fulani mafuta, jambo ambalo lilitusababishia changamoto pindi chanzo kimoja kilipopata hitilafu," amesema Mhandisi Luoga akiongeza kuwa hivi sasa nchi inaelekea kuzalisha umeme kwa kutumia maji, gesi, upepo, jua, na nishati ya joto ardhi ili kupata umeme wa uhakikaThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati, Mhandisi Innocent Luoga, amesema Tanzania kwa sasa ina umeme wa kutosha, hali anayosema imechangiwa kwa kiasi kikubwa na kukamilika kwa Mradi wa Bwawa la Kuzalisha Umeme la Julius Nyerere (JNHPP).
Akizungumza katika mahojiano maalum na mwandishi Salehe Mohamed, Luoga amesema tofauti na mwaka 2023 ambapo Tanzania ilipitia kipindi kigumu cha mgawo wa umeme na jenereta kuonekana katika maeneo mbalimbali, tangu kuanza kwa uzalishaji wa JNHPP hakujawa na matangazo ya mgawo wa umeme hadi mwaka 2026.
Amesema baada ya uzinduzi rasmi wa bwawa hilo utakaofanywa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Jumamosi hii ya Agosti 22, 2026, Tanzania inatarajia kuwa na umeme wa uhakika zaidi, huku akieleza kuwa taarifa za kukatika kwa umeme zitakazotolewa na TANESCO kwa sasa zinahusu zaidi matengenezo na ukarabati wa miundombinu, si mgawo wa umeme.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Kituo cha kuzalisha umeme cha Julius Nyerere (JNHPP) chenye uwezo wa kuzalisha megawati 2,115, kimekamilika kwa asilimia 100 na tayari kinaendelea kufanya kazi kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya umeme nchini.
Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati, Mhandisi Innocent Luoga, amesema uwezo huo unatokana na kufungwa kwa mitambo tisa, ambapo kila mtambo una uwezo wa kuzalisha megawati 235.
Akizungumza katika mahojiano maalum na Saleh Mohamed, Mhandisi Luoga amesema mitambo hiyo imeundwa kufanya kazi kulingana na mahitaji ya umeme nchini, huku kukamilika kwa mradi huo kukitoa sababu ya serikali kuuandaa kwa ajili ya uzinduzi rasmi ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameridhia kuzindua mradi huo.
Kwa mujibu wa Mhandisi Luoga, kukamilika na kuanza kufanya kazi kwa JNHPP kunatarajiwa kuwa hatua muhimu katika kuimarisha upatikanaji wa umeme nchini, huku kukiwa na matarajio ya kuchochea zaidi ukuaji wa viwanda, biashara na uwekezaji.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati, Mhandisi Innocent Luoga, amesema Mradi wa Bwawa la Kuzalisha Umeme la Julius Nyerere (JNHPP) ulianzishwa ili kuondokana na tatizo la upungufu wa umeme nchini, huku akisema tangu bwawa hilo lianze kufanya kazi hakujawa na mgawo wa umeme na ni matokeo ya bwawa hilo katika uzalishaji.
Akizungumza katika mahojiano maalumu na Mtangazaji Saleh Mohamed Agosti 20, 2026, kuhusu "Bwawa la Julius Nyerere litafungua vipi fursa mpya Tanzania", Luoga amesema kwamba kwa umeme uliopo sasa hivi unatosheleza mahitaji ya kijamii na kiuchumi.
"Tangu mwaka 2024 bwawa hili lilipoanza kufanya kazi hatujakuwa na mgao wa umeme, 25 hatujakuwa na mgao wa umeme, 26 tu hapa hatukuwa na mgawo wa umeme, kwahiyo tayari umeshaanza kuona hili bwawa limeanza kuonesha matokeo yake kwamba, namna gani linaweza kusaidia nchi yetu" amesema Luoga.
Mahojiano hayo yamekuja ikiwa Agosti 22, 2026, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan atakwenda kuzindua mradi huo ulipo mkoani Pwani unaotajwa kuzalisha megawati 2115 za umeme.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Kuelekea uzinduzi wa kihistoria wa Bwawa la Kuzalisha Umeme la Julius Nyerere (JNHPP) unaotarajiwa kufanywa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Jumamosi hii ya Agosti 22, 2026, Wizara ya Nishati imekata mzizi wa fitina kuhusu gharama halisi zilizotumika kukamilisha mradi huo mkubwa wa nishati nchini.
Akizungumza katika mahojiano maalum leo Agosti 20, 2026, Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga, amefafanua kuwa utofauti wa tarakimu uliokuwa ukitajwa awali na wananchi ulitokana na ukweli kwamba hesabu hizo zilitolewa kabla ya mradi kukamilika kikamilifu. Hata hivyo, baada ya kazi zote kukamilika, gharama halisi sasa imewekwa wazi kisheria na kitaalamu.
“Ghalama halisi ya bwawa hili ni shilingi trilioni 7.452. Hiyo ndio gharama halisi ya bwawa hili,” amethibitisha Mhandisi Luoga ili kuondoa mkanganyiko wa takwimu za awali zilizokuwa zikitofautiana kati ya shilingi trilioni 6.5, trilioni 7.2, na trilioni 7.4
Mhandisi Luoga amefafanua kuwa gharama hiyo kubwa imeenda kwenye maeneo makuu mawili ya kimkakati. Eneo la kwanza ni ujenzi wa bwawa kuu (main dam) ambalo lina ukubwa wa kustaajabisha unaolingana na umbali wa mikoa miwili.
“Kwanza katika hili bwawa sehemu ya kwanza kabisa ni ujenzi wa lile bwawa lenyewe eh ambayo tunaita main dam kwa ukubwa wake ni kilomita takribani 100 yaani kutoka hapa Dar es Salaam mpaka Chalinze,” ameeleza Kamishna Luoga.
Mbali na ujenzi wa bwawa hilo kubwa la kilomita 100, sehemu ya pili ya gharama hiyo imehusisha ununuzi, usafirishaji, na ufungaji wa mitambo tisa (9) ya kisasa ya kuzalisha umeme ambayo sasa ipo tayari kuwasha taifaThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Jengo la Kanisa la Victory Gospel Assembly lililopo chini ya Askofu Paulo Shemsanga limebomolewa kufuatia mgogoro wa muda mrefu wa uwanja kati ya familia ya Mzee Wilfred Mwankuga Mwanjala na Askofu Shemsanga, katika Kiwanja Namba TMK/KEKOMAGURUMBASI A2/122 kilichopo Mtaa wa Magurumbasi A, Kata ya Keko, Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.
Familia ya Mzee Wilfred Mwankuga Mwanjala inadai kumiliki hati halali ya makazi ya eneo hilo yenye namba TMK002389, ikisisitiza kuwa ubomoaji huo umeendeshwa kwa mujibu wa sheria kufuatia kushindikana kwa mashauriano na makubaliano ya awali kati yao na uongozi wa kanisa hilo.
Akifafanua chanzo cha mgogoro huo, Elisha Wilfred, ambaye ni mtoto wa kwanza wa Mzee Wilfred, ameeleza kuwa familia yao ilinunua eneo hilo mwaka 1991 na baadaye baba yake alimkaribisha Mchungaji Paul Shemsanga kutumia kiwanja hicho kwa ajili ya ibada kukiwa na makubaliano maalum kufuatia kanisa kukosa eneo.
Hata hivyo, Elisha amebainisha kuwa mwaka 2002 Mzee Wilfred alisitisha makubaliano hayo kwa barua rasmi na kumtaka Askofu Shemsanga kurejesha eneo hilo lakini halikurejeshwa. Ameongeza kuwa hata jitihada za maridhiano zilizofanyika tena mwaka 2019 hazikufanikiwa kutokana na upande wa kanisa kukiuka masharti, hatua iliyomfanya baba yake kuchukua mkondo wa kisheria ili kurudishiwa eneo lake.
Kwa upande wake, mchungaji wa kanisa hilo, Mch. Flora V. Shemsanga, ameeleza kuwa walipata taarifa za watu kufika katika eneo la kanisa usiku wa kuamkia Agosti 18, 2026 wakiwa na zana za ubomoaji, wakisindikizwa na walinzi wa kampuni binafsi.
Amesikitishwa na hatua hiyo huku akidai kuwa upande wa kanisa haukuoneshwa kibali chochote cha Mahakama wala wakili wao kushirikishwa kwenye shauri lolote lililoamuru kuondolewa kwao.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Rais wa Marekani, Donald Trump, ametangaza kuanzisha vikwazo vipya na vikali vya kiuchumi dhidi ya Iran, huku akitoa onyo kali kwa nchi yoyote au taasisi itakayojihusisha na biashara au kutoa usaidizi kwa taifa hilo la Mashariki ya Kati.
Akitumia mtandao wake wa kijamii wa Truth Social, Rais Trump ameeleza kuwa amechukua hatua hiyo kufuatia Iran kushindwa kufikia makubaliano ya kuzuia mzozo unaoendelea, baada ya muda wa makubaliano ya kusitisha vita kwa siku 60 kukamilika rasmi Jumatatu ya wiki hii bila kuwepo kwa dalili za amani.
Trump, ambaye mara kwa mara ametishia kuichukulia hatua kali zaidi Iran, amesema kuwa kuanzia sasa anatangaza operesheni kali zaidi ya kiuchumi kuwahi kuchukuliwa dhidi ya taifa lolote duniani, akifafanua kuwa yatakuwa ni "vita vya kiuchumi na kutengwa kiasi ambacho hakijawahi kushuhudiwa."
Akiweka msimamo huo dhidi ya washirika wa Iran, Trump ametangaza kuwa nchi yoyote itakayoruhusu benki, taasisi za kifedha, kampuni za biashara, viwanja vya ndege, au asasi za kiserikali kuisaidia Iran, nayo itakabiliwa na adhabu na athari mbaya za kiuchumi kutoka Marekani.
"Marekani inatangaza vita vya kiuchumi visivyowahi kutokea. Nchi yoyote, benki, au chombo kitakachoamua kuisaidia au kufanya biashara na Iran, kitakutana na vipigo na athari mbaya sana za kiuchumi," amesema Rais Trump.
Hata hivyo, Rais Trump hakutoa maelezo ya kina ya kiufundi kuhusu vikwazo hivyo vipya au kutaja majina ya mataifa yatakayolengwa mara moja. Kauli hii inakuja wiki moja tu baada ya Waziri wake wa Fedha, Scott Bessent, kusema kuwa Marekani inajipanga kuiwekea Iran vikwazo vya kiuchumi visivyo na mfano.
Shinikizo hili jipya linalolenga uchumi wa Iran linakuja wakati vita hivyo vilivyoanzishwa mwishoni mwa mwezi Februari 2026 na Marekani ikishirikiana na Israel vikielekea kutimiza miezi sita bila uwepo wa jitihada thabiti za kidiplomasia.
Hatua hii ya Trump inatazamwa pia kupitia jicho la kisiasa la ndani ya Marekani, ambapo anachunguzwa kwa karibu kuelekea Uchaguzi wa Katikati ya Muhula (Midterm Elections) unaotarajiwa kufanyika mwezi Novemba 2026.
Naye mshirika wake, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, anakabiliwa na shinikizo kubwa la kisiasa kuhusu anavyomudu mzozo huo wa Iran na ule wa Gaza kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Israel uliopangwa kufanyika mwezi Oktoba 2026.
Licha ya mashambulizi ya makombora kupungua katika siku za hivi karibuni kati ya pande hizo, Iran imeendelea kuzuia usafiri wa meli katika Mlango-Bahari wa Hormuz (Strait of Hormuz), ikiwa ni ishara ya mgogoro huo kuendelea kuathiri sekta ya nishati duniani. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Kesi inayomkabili Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Melkisedeki Kitunzi Kaijage, imeahirishwa hadi Agosti 27, 2026, baada ya Hakimu Mkazi anayesikiliza shauri hilo kutokuwepo mahakamani.
Kaijage anakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi yenye namba 16278 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma, ambapo kwa mujibu wa Wakili wake, Godfrey Wasonga, anatuhumiwa kwa makosa yanayohusiana na sheria ya kuzuia ugaidi.
Akizungumza Agosti 19, 2026 jijini Dodoma, Wakili Wasonga amesema mteja wake anatuhumiwa kuwa Julai 3, 2026 akiwa katika maeneo ya UDOM, alikuwa na nia ya kuchoma majengo ya umma pamoja na makazi ya askari Polisi katika maeneo mbalimbali nchini, ikiwemo Zanzibar.
“Si majengo ya umma tu, pia anatuhumiwa kwamba anataka kuchoma makazi ya askari Polisi Tanzania nzima ikiwepo na Zanzibar,” amesema Wakili Wasonga.
Amesema tuhuma hizo zinahusisha majengo mbalimbali ya umma, ikiwemo shule, zahanati, mahakama na majengo mengine ya Serikali, huku akieleza kuwa suala hilo liko chini ya vifungu vya sheria ya kuzuia ugaidi.
Kwa sasa, Wakili Wasonga amesema hatua inayofuata katika kesi hiyo ni uchunguzi wa awali (Preliminary Inquiry), ambao unalenga kuwezesha shauri hilo kupelekwa Mahakama Kuu kwa ajili ya kusikilizwa.
Hata hivyo, kikao cha kesi hiyo kilichopangwa kufanyika Agosti 19 hakikuendelea baada ya Hakimu Mkazi anayesikiliza shauri hilo, Zabibu Mpangule, kutokuwepo.
Kwa mujibu wa Wasonga, shauri hilo lilitajwa mbele ya Hakimu Kombe na sasa limepangwa kutajwa tena Agosti 27, 2026, ambapo pande zote zinatarajiwa kufahamisha mahakama hatua inayofuata.
Wakili huyo amesema siku hiyo itatoa mwelekeo wa namna shauri hilo litakavyoendelea.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo imeipongeza Wizara ya Viwanda na Biashara pamoja na taasisi zake ikiwemo Tume ya Ushindani (FCC) na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) kwa hatua kubwa zinazochukuliwa katika kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini.
Pongezi hizo zimetolewa leo, Agosti 19, 2026, na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Deodatus Mwanyika, wakati wa kikao cha tathmini ya utekelezaji wa shughuli za Wizara hiyo kilichofanyika Bungeni jijini Dodoma.
Mwanyika amebainisha kuwa juhudi za Wizara zimeanza kuonesha matokeo chanya, lakini akasisitiza kuwa Serikali inapaswa kuongeza nguvu katika mapambano dhidi ya bidhaa bandia na hafifu zinazoingizwa sokoni, kwani zinaumiza wazalishaji wa ndani na kuhatarisha afya za walaji.
Ameitaka Wizara na taasisi zake kuimarisha mifumo ya ukaguzi na kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya watu wote wanaojihusisha na uingizaji au uzalishaji wa bidhaa zisizokidhi viwango.
Akijibu maelekezo hayo, Waziri wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga, amesema Wizara imepokea ushauri huo na itaufanyia kazi kikamilifu ili kuimarisha mazingira ya biashara na kulinda maslahi ya wazalishaji na wateja.
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa FCC, Bi. Khadija Ngasongwa, ameeleza kuwa taasisi hiyo itaendelea kusimamia ushindani wa haki sokoni, huku Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA, Bw. Godfrey Nyaisa, akisisitiza kuwa wataendelea kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wafanyabiashara wanaokiuka sheria na kuboresha huduma zao kwa umma. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Serikali ya Tanzania, kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, imesisitiza kuwa itaendelea kuhakikisha kunakuwepo na mfumo wa uhamiaji salama unaolinda usalama wa nchi, raia, mali zao, pamoja na amani ya kikanda na kimataifa.
Katika kufanikisha azma hiyo, Serikali imebainisha kuwa fursa za maendeleo ya kiuchumi, ajira, ukuaji wa utamaduni, na masuala ya kisiasa zitaendelea kutekelezwa bila kuathiri usalama wa taifa wala kuingilia tunu ya amani na haki za binadamu.
Yakiwa ni matokeo ya msimamo huo, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, ameyasema hayo wakati akizindua rasmi Mfumo wa Uratibu wa Kitaifa kuhusu Uhamiaji Nchini Tanzania, tukio lililoshuhudiwa pia na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji (IOM), Amy Pope.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Waziri Katambi ameeleza kuwa masuala ya uhamiaji yanalenga kuweka uratibu mzuri kati ya fursa za kiuchumi na ulinzi wa taifa.
“Uhamiaji ni masuala ya usalama wa raia na mali zao, usalama wa nchi, usalama wa kikanda na kimataifa na ndio maana Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ina dhamana katika hili. Lakini majukumu ya kiuchumi yanalazimu mtu aweze kwenda maeneo mbalimbali kutafuta ajira na fursa, lakini haya yote yafanyike bila kuathiri usalama wa nchi husika, uchumi wa nchi husika, na bila kuathiri raia wa nchi husika,” amesema Waziri Katambi.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa IOM, Amy Pope, aiishukuru na kuipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuchukua hatua za kimkakati katika kutafuta suluhisho sahihi la changamoto za uhamiaji, hatua inayowezesha uwepo wa mgerereko wa watu unaofuata sheria, kanuni, na taratibu zilizowekwa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Stephen Wasira, amewataka wanachama wa chama hicho nchi nzima kukutana mara kwa mara katika vikao rasmi vya kikatiba, ili kujadili masuala muhimu na kuepuka kupotoshwa na taarifa zisizo na ukweli zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii.
Wasira ametoa wito huo leo, tarehe 19 Agosti, 2026, Wilaya ya Ikungi mkoani Singida, wakati akianza ziara rasmi ya kikazi ya kukagua uhai wa chama hicho na utekelezaji wa Ilani yake, ambapo amebainisha kuwa vikao hivyo vinawapa wanachama fursa ya kupata taarifa sahihi na kuambizana ukweli.
“Wanachama wetu nchi nzima, kwa mujibu wa Katiba mna vikao vya wanachama. Mkutane muambizane. Siku hizi kwenye mitandao kuna uongo mwingi sana. Usipoangalia unaweza hata wewe kushirikishwa kusema uongo,” amesema Wasira.
Amesisitiza kuwa pindi wanachama wanapokutana na kubaini kuwepo kwa madai au taarifa zinazotatiza zinazosambazwa mitandaoni, ni vyema wakawaalika watu wenye ujuzi na uelewa mpana ili wawasaidie kutoa ufafanuzi wa kina na sahihi wa kisheria au kiserikali.
“Kwa hiyo ni vizuri kukutana mkasema hili jambo limesemwa sana, maana yake ni nini? Mkamwita mtu anayejua akawasaidia kufafanua,” ameeleza.
Kuhusu misingi ya Taifa, Wasira amebainisha kuwa CCM itaendelea kulinda na kutetea urithi wa amani, uhuru, na umoja wa nchi uliopatikana kwa kazi kubwa na waasisi, akionya kuwa jitihada zote za kujaribu kubomoa msingi huo hazitafanikiwa.
“Hii ndiyo CCM. Kazi ya kwanza tulipewa ni uhuru na tunalinda. Ya pili ni umoja na tunahakikisha unabaki. Yeyote anayetaka kuubomoa anabomoa msingi ambao hawezi. Anaweza kutikisa matawi lakini mizizi itabaki chini,” amesema.
Ametamatisha kwa kurejelea wanaokosoa utendaji wa chama hicho kwa kudai kuwa hakijafanya chochote tangu kupatikana kwa uhuru, akieleza kuwa madai hayo ni ya kinyume cha ukweli na kwamba hata uhuru wa kujieleza unaotumiwa na wakosoaji hao ni matunda ya uongozi wa CCM.
“Wanasema hatujafanya chochote tangu uhuru. Lakini uhuru wa kusema ndio huo walionao. Mdomo una kazi mbili: kusema na kula. Mtu akisema hakuna chochote tangu uhuru, muache tu. Huyo ana matatizo anahitaji msaada,” amehitimisha Wasira. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, amesema Mkoa wa Songwe unapaswa kuwa mfano wa utekelezaji wa Dira ya Taifa 2050 kwa kujenga uchumi unaozalisha fursa, ajira na kuongeza thamani ya bidhaa, badala ya kutegemea kupokea shughuli za kiuchumi kutoka nje ya mkoa.
Akizungumza leo, Agosti 19, 2026, katika siku ya kwanza ya Jukwaa la Dira 2050 – Songwe, linalofanyika kwa siku mbili, Prof. Kitila amesema lengo ni kuubadilisha mkoa kutoka kuwa wa kiutawala na kuwa mkoa wa kiuchumi, kwa kuanzia kwenye fursa, kwenda kwenye uwekezaji, uzalishaji, kuongeza thamani na hatimaye mauzo ya nje.
“Dhamira yetu kama Serikali si kuwa na Mikoa inayosimamiwa vizuri tu, hiyo haitoshi. Dhamira yetu ni kuwa na Mikoa yenye uzalishaji mkubwa zaidi, ushindani, viwanda, miunganiko bora na ustawi mkubwa kwa Wananchi ikiwemo kipato kwa Wananchi. Tunataka mikoa ambayo haipokei shughuli za kuichumi tu bali inazalisha shughuli hizo”. Amesema Prof. Kitila
Amesema Songwe inapaswa kujipima si kwa kiasi cha fedha na miradi inayopokea kutoka Serikalini pekee, bali kwa ukubwa wa shughuli za kiuchumi inazozalisha, wawekezaji inayowavutia, ajira zinazotengenezwa na thamani inayoongezwa kwenye mazao na malighafi zinazozalishwa mkoani humo.
Aidha, Prof. Kitila amewataka viongozi kuweka mazingira yatakayowawezesha Vijana kupata fursa za ajira na biashara ndani ya Songwe, badala ya kulazimika kuondoka kwenda kutafuta fursa katika Mikoa mingine.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI PICHA:
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, amezitaka mamlaka za Serikali kuendelea kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji ili kuiwezesha sekta binafsi kuwa injini ya ukuaji wa uchumi, uzalishaji na ajira nchini.
Akizungumza leo, Agosti 19, 2026, katika siku ya kwanza ya Jukwaa la Dira 2050 na Uwekezaji mkoani Songwe, Prof. Kitila amesema utekelezaji wa Dira ya Taifa 2050 unahitaji mabadiliko ya namna Mikoa inavyoendesha shughuli zake za kiuchumi, ikiwemo kuacha kutegemea fedha na miradi kutoka Serikali pekee na badala yake kujenga uwezo wa kuzalisha shughuli mpya za kiuchumi, kuvutia uwekezaji na kuongeza thamani ya bidhaa.
Katika hilo, Prof. Kitila amesisitiza umuhimu wa kuweka mazingira rafiki ya biashara kwa kuondoa vikwazo na usumbufu usio wa lazima unaoweza kuongeza gharama za uendeshaji wa biashara. Ametolea mfano malori yanayosafirisha mizigo kutoka Bandari ya Dar es Salaam, ambayo licha ya kukamilisha taratibu za ukaguzi bandarini, yamekuwa yakisimamishwa mara kwa mara barabarani, hali inayochelewesha mizigo na kuongeza gharama kwa wafanyabiashara.
“Hili tulifanyie kazi kwa sababu uchumi wa usafiri na usafirishaji ni eneo kubwa lazima tuliweke vizuri ili Wananchi wetu wafanye biashara kwa uhuru na sisi tukikusanya kodi tukusanye kwa furaha” amesema Kitila.
Sambamba na hilo, Prof. Kitila amezitaka Halmashauri Nchini kubadili mtazamo kutoka kuwa wakusanyaji wa tozo na ushuru kwenda kuwa injini za uchumi, kwa kubuni shughuli mpya za uzalishaji, kuvutia uwekezaji na kutengeneza fursa zaidi kwa Wananchi, badala ya kuongeza mzigo kwa wafanyabiashara waliopo.
Kwa upande mwingine, Prof. Kitila ameeleza kuwa sekta binafsi yenye nguvu ni muhimu katika kuongeza ajira, uzalishaji na mapato ya Serikali kupitia kodi. Hivyo, akasisitiza kuwa mazingira ya biashara yanapaswa kumwezesha mfanyabiashara kufanya kazi kwa uhuru na utulivu, huku Serikali ikisimamia uchumi na kukusanya mapato kwa ufanisi. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Rais wa Chemba ya Taifa ya Wafanyabiashara Tanzania (TNCC), Vicent Minja, amebainisha kuwa sekta binafsi imejipanga kutekeleza asilimia 70 ya Dira ya Taifa 2050, huku asilimia 30 ikitekelezwa na sekta ya umma kupitia Serikali Kuu na taasisi zake.
Akizungumza leo, Agosti 19, 2026, katika siku ya kwanza ya Jukwaa la Dira 2050 na Uwekezaji mkoani Songwe, Minja amesema dhamira hiyo ni sehemu ya ahadi iliyotolewa mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hivyo utekelezaji wake unahitaji ushirikiano wa karibu kati ya sekta binafsi na Serikali, hususan katika ngazi za mikoa na wilaya.
Kwa niaba ya wadau wa sekta binafsi, Minja ameiomba Serikali kuweka mazingira rafiki ya biashara na uwekezaji yatakayowezesha wafanyabiashara na wawekezaji kutekeleza wajibu wao katika Dira hiyo kwa ufanisi.
Minja ameeleza kuwa mazingira bora ya biashara katika ngazi za Mikoa na Wilaya yatawezesha sekta binafsi kuongeza uwekezaji, uzalishaji na ajira, na hivyo kuongeza mchango wake katika ukuaji wa uchumi na utekelezaji wa Dira ya Taifa 2050.
Aidha, amewataka Madiwani na Viongozi wanaohusika na utungaji wa kanuni na sheria ndogo kuwashirikisha wadau wa sekta binafsi kabla ya kutunga taratibu zinazoweza kuathiri shughuli za biashara na uwekezaji.
Kwa upande mwingine, Minja amesema utekelezaji wa Dira ya Taifa 2050 si jukumu la Serikali pekee, bali ni wajibu wa kila mdau, huku sekta binafsi ikiwa mshirika muhimu katika utekelezaji wa dira hiyo
Amesema sekta binafsi ipo tayari kuanza ukurasa mpya wa ushirikiano na Serikali, kwa lengo la kuongeza uwekezaji, uzalishaji, ajira na kuhakikisha Tanzania inafikia malengo yaliyowekwa katika Dira ya Taifa 2050.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limetangaza operesheni kali dhidi ya kundi la waendesha pikipiki “bodaboda” wanaojihusisha na vitendo vya kihalifu baada ya kutokea kwa ajali za barabarani. Hatua hiyo imekuja kufuatia tukio la ajali iliyosababisha vifo vya watu wawili na kufuatiwa na kitendo cha baadhi ya waendesha pikipiki kuchoma moto gari la mizigo.
Ajali hiyo ilitokea leo, tarehe 19 Agosti, 2026, majira ya saa 03:45 asubuhi katika barabara ya Kilwa, eneo la Mivinjeni Temeke. Gari aina ya DAF lenye namba T 945 CBG likitokea Uhasibu kuelekea Bendera Tatu liligongana na pikipiki yenye namba MC 851 FJP aina ya Boxer.
Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, SACP Jumanne Muliro, chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa pikipiki, Msichoke Mohamed @Mnyige, ambaye alihama kutoka barabara ya mchepuko na kuingia barabara kuu bila tahadhari akiwa amebeba abiria wawili. Ajali hiyo ilisababisha vifo vya dereva huyo (Msichoke Mohamed) na abiria wake, George Luis Nyantora, mfanyabiashara wa Mbagala Zakhem, huku mjasiriamali mmoja, William Ashery @tumbo, akijeruhiwa
Hata hivyo, baada ya ajali hiyo, kundi la waendesha pikipiki wengine walijikusanya kinyume cha sheria na kuchoma moto sehemu ya mbele (horse) ya gari hilo la mizigo Jeshi la Polisi limelaani kitendo hicho likiwaita wahusika kuwa ni wahalifu.
“Vitendo vya baadhi ya waendesha pikipiki kuchoma au kupiga magari na kupora vitu vilivyo kwenye vyombo hivyo vya moto mara baada ya ajali ni vya kihalifu, havivumiliki na ni kinyume na sheria za Nchi,” imesisitiza taarifa hiyo.
Katika hatua ya haraka, Polisi wamekwishawakamata watuhumiwa 18 na pikipiki 23 zikiwemo zilizotelekezwa katika maeneo mbalimbali kama Mbopo, Bunju B, Tegeta, Kunduchi, na Kimara kufuatia mfululizo wa matukio ya aina hiyo. Miongoni mwa waliokamatwa ni Ally Abdallah (44), anayedaiwa kuhusika katika tukio la tarehe 15 Agosti, 2026, ambapo kundi la bodaboda lilishambulia gari aina ya Harrier kwa mawe baada ya ajali Magomeni Kanisani.
Jeshi la Polisi limetoa onyo kali kwa waendesha pikipiki kuacha mtindo wa kujichukulia sheria mkononi hata pale wanapokuwa chanzo cha ajali, likionya kuwa hatua kali sana za kisheria zitaendelea kuchukuliwa dhidi yao.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) pamoja na Taasisi ya ELLA Foundation, leo Agosti 19, 2026, zimeingia katika ushirikiano wa kuwawezesha watu wenye uziwi kupitia mafunzo na ujuzi mbalimbali katika tukio la utekelezaji wa wajibu kwa jamii (CSR).
Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi Mkuu wa TISEZA, Gilead Teri, amesema ushirikiano huu unaakisi dhamira ya TISEZA @InvestTanzania ya kuhakikisha kuwa juhudi za kukuza na kuvutia uwekezaji nchini pia zinachangia katika ukuaji wa uchumi jumuishi, uwezeshaji wa jamii na ujenzi wa maisha endelevu.
Kwa upande wake Muasisi wa ELLA FOUNDATION, Esther Jaswant amesema kwamba ulemavu ya mtu si sababu ya kumfanya akose fursa zitakazomuwezesha kuwa huru kiuchumi.
Ameongeza kwamba taasisi hiyo ina miradi mbalimbali ikiwemo ELLA Workshop inayozalishwa bidhaa mbalimbali zinazoashiria viziwi kushiriki katika uchumi. Amesema fursa ya kushirikiana na TISEZA imetoa nafasi ya watu wenye changamoto ya kusikia kuonesha ubunifu wao.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Mwanzilishi na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya SpaceX, Elon Musk, ametangaza mabadiliko ya kimkakati kwa kuelekeza nguvu mpya katika ujenzi wa mji wa kudumu kwenye Mwezi, akibainisha kuwa mradi huo unaweza kuanza kutekelezeka ndani ya kipindi cha chini ya miaka 10.
Mwelekeo huo mpya unaonesha kuupa Mwezi kipaumbele cha kwanza badala ya Sayari ya Mars, ambayo kwa muda mrefu imekuwa nguzo kuu ya maono ya Musk na SpaceX kuhusu upanuzi wa maisha ya binadamu nje ya Dunia.
Musk ameeleza kuwa lengo kuu ni kuanzisha makazi ya kudumu Mwezini yanayoweza kupanuka hatua kwa hatua, kwa kutumia rasilimali zilizopo huko na kuungwa mkono na safari za mara kwa mara za vyombo vya anga kutoka duniani.
Akitofautisha miradi hiyo miwili kupitia mtandao wa kijamii wa X, Musk amebainisha kuwa ujenzi wa mji mwezini unaweza kufikiwa kwa haraka ndani ya miaka 10, wakati safari na ujenzi wa makazi katika Sayari ya Mars unaweza kuchukua zaidi ya miaka 20.
Amesisitiza kuwa safari za kwenda Mars zina changamoto kubwa za kiufundi na kimfumo, kwani Dunia na Mars hukaribiana katika mpangilio unaofaa kwa usafiri wa anga mara moja tu kila baada ya miezi 26, huku safari moja pekee ikichukua takribani miezi sita.
Licha ya kubadili kipaumbele cha muda mfupi, Musk amesisitiza kuwa dhamira ya msingi ya SpaceX haijabadilika, ambayo ni kuongeza uwezo wa binadamu wa kuishi katika sayari mbalimbali na hatimaye kufikia maeneo ya mbali zaidi angani.
Hata hivyo, hadi sasa mpango huo wa ujenzi wa mji mwezini bado uko katika hatua ya kidhana, huku kukiwa hakuna michoro rasmi ya kiufundi au maelezo ya kina kuhusu ukubwa wa mji, idadi ya wakazi, miundombinu, na namna utakavyojitegemea. -
Jambo TV
@Jambotv_
Chama cha ACT Wazalendo kimelaani uamuzi wa Idara ya Huduma za Habari (MAELEZO) wa kusitisha leseni ya uchapishaji na usambazaji wa gazeti MwanaHALISI kwa muda wa miezi sita, kuanzia tarehe 19 Agosti 2026.
Hatua hiyo ya Serikali imetokana na kile kilichodaiwa kuwa ni ukiukaji wa viwango vya usahihi na mizania katika toleo namba 571, ambapo gazeti hilo lilichapisha habari yenye kichwa "Nchimbi agoma kujiuzulu." MAELEZO ilibaini makosa ya kiuhariri ikiwemo kuweka picha ya Waziri Paul Makonda na kumtaja kimakosa kama Makamu wa Rais wa Tanzania, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, pamoja na kukosa uthibitisho kutoka kwa wahusika.
Kupitia taarifa rasmi kwa umma leo Agosti 19, 2026, Waziri Kivuli wa Mawasiliano, Habari na Teknolojia ya Habari wa ACT Wazalendo, Shangwe Ayo amesema kuwa ingawa wanatambua wajibu wa weledi, adhabu hiyo ni tishio kwa demokrasia.
“Serikali imejipa mamlaka ya kumchunguza, kumsikiliza na kumuadhibu mtoa huduma wa habari. Hii inakinzana na kanuni za haki na utawala bora,” amesisitiza Ayo.
ACT Wazalendo imetoa rai kuwa makosa ya kitaaluma yanapaswa kushughulikiwa kwa njia inayolinda uhuru wa habari na si kwa kufungia vyombo vya habari, jambo ambalo linagusa haki ya jamii kupata taarifa.
Kufuatia adhabu hiyo ambayo inajumuisha pia kuzuiliwa kwa maudhui ya gazeti hilo ya kielektroniki na mtandao, ACT Wazalendo imeitaka serikali isimamishe mara moja adhabu dhidi ya MwanaHALISI na kurejesha leseni yake, imetaka kufutwa kwa Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari ya mwaka 2016 na vifungu vyote inavyodai kuwa vinakandamiza uhuru wa habari na Kuundwa kwa chombo huru cha kitaaluma cha wanahabari cha kushughulikia malalamiko badala ya Serikali kuwa mlalamikaji na mwamuzi.
“Uhuru wa habari na haki ya kupata, kutoa na kupokea taarifa ni nguzo za Katiba, demokrasia na uwajibikaji wa Serikali. Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari ya mwaka 2016 na sheria nyingine zinazoweka mamlaka makubwa Mkurugenzi wa Habari juu ya vyombo vya habari zinapaswa kufutwa”, ameeleza Ayo.
Licha ya adhabu hiyo kufuatia maonyo ya awali ya mdomo na maandishi yaliyotolewa mwezi Februari na Mei, gazeti MwanaHALISI limepewa siku 30 kukata rufaa. -
Jambo TV
@Jambotv_
Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) imeingia katika ushirikiano wa kimkakati na taasisi ya ELLA Foundation, wenye lengo la kuwawezesha watu wenye changamoto ya usikivu (uziwi) kupitia mafunzo ya ujuzi na kuwatafutia soko la bidhaa zao kwa wawekezaji wa ndani na wa kimataifa.
Katika kuitafsiri dhana ya utekelezaji wa wajibu wa taasisi kwa jamii (CSR), TISEZA @InvestTanzania itaanza kununua mifuko yenye ubunifu wa hali ya juu inayotengenezwa na wanufaika wenye uziwi na kuitumia kama sehemu ya vifaa rasmi na zawadi kwa wawekezaji na wadau mbalimbali wanaokuja nchini. Hatua hii inalenga kuwapa vijana hao soko endelevu na kuonesha uwezo wa Watanzania wenye mahitaji maalum katika kuzalisha bidhaa bora.
Akizungumza mkoani Dar es Salaam katika hafla ya utiaji saini na makabidhiano ya awali leo Agosti 19, 2026, Mkurugenzi Mkuu wa TISEZA, Gilead Teri, amesema ushirikiano huo ni sehemu ya dhamira ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuleta uchumi jumuishi.
“Tumekuwa na taratibu ya kutumia bidhaa za Kitanzania zikiwa sehemu ya kuonesha uwezekaji unaofanyika Tanzania... Lakini sasa pia tutaongeza bidhaa hizi ambazo zimetengenezwa na wadau ambao ni wa kwenye makundi maalum. Hatua hii itawasaidia kuwapatia wanufaika soko endelevu la bidhaa zao na kuongeza fursa za kiuchumi kwa watu wenye makundi maalum,” amebainisha Teri.
Kwa upande wake, Muasisi wa ELLA Foundation, Esther Jaswant ameeleza kuwa ushirikiano huo unatuma ujumbe mzito kwa jamii na wawekezaji kuwa ulemavu si kizuizi cha tija katika uchumi
“Mtu ambaye ana ulemavu hiyo sio kikwazo chake kupata fursa na pia kupata kujikimu kimaisha ama kupata uhuru wa kiuchumi. Mojawapo ya miradi yetu mikubwa ni ELLA workshop ambapo tunazalisha bidhaa zenye ubora... na kuwasaidia hawa viziwi kushiriki kwenye uchumi na kujitegemea kifedha,” amesema Jaswant.
Ushirikiano huu unatarajiwa kuwa wa muda mrefu, ambapo TISEZA imejipanga pia kuwashawishi wawekezaji wanaokuja nchini kutoa kipaumbele cha ajira kwa watu wenye ulemavu katika viwanda vyao, ikizingatiwa kuwa kazi nyingi za viwandani ni zile zinazoweza kufundishika kwa urahisi
Hadi sasa, karakana ya ELLA Foundation inahudumia vijana 10 ambao wamebobea katika ufundi na ujuzi wa ubunifu. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, amesema Tanzania inahitaji kuboresha mazingira ya biashara kwa kuondoa usumbufu usio wa lazima kwa wafanyabiashara, hususan katika usafirishaji wa mizigo kutoka bandarini kwenda maeneo mbalimbali nchini.
Akizungumza leo Agosti 19, 2026 katika Jukwaa la Dira 2050 lililofanyika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Prof. Kitila ametolea mfano malori yakitoka Bandari ya Dar es Salaam, baada ya kukaguliwa na taratibu zote kukamilishwa bandarini, yamekuwa yakisimamishwa mara kwa mara barabarani jambo ambalo limekuwa likileta usumbufu na wakati mwingine kutoa mianya ya rushwa.
Amesema baada ya mizigo kutoka bandarini, ni muhimu miundombinu na mifumo ya usafirishaji iwe na ufanisi ili mizigo ifike kwa wakati na kwa gharama nafuu.
"Hili tulifanyie kazi kwa sababu uchumi wa usafiri na usafirishaji ni eneo kubwa lazima tuliweke vizuri ili wananchi wetu wafanye biashara kwa uhuru na sisi tukikusanya kodi tukusanye kwa furaha" amesema Kitila.
Amesisitiza kuwa lengo ni kujenga mazingira ambayo mfanyabiashara anafanya biashara kwa utulivu, serikali kwani serikali ikikusanya kodi kwa ufanisi na uchumi wa nchi unaendelea kukua. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, amempa siku 14 mkandarasi wa kampuni ya China Wu Yi Construction kuhakikisha anaanza kumwaga lami katika barabara muhimu inayopita eneo la Hospitali ya Taifa Muhimbili, huku akiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Wilaya ya Ilala kufuatilia kwa karibu uwajibikaji wa kila mhusika katika mradi huo.
Mpogolo ametoa maagizo hayo Agosti 18, 2026 wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa Mradi wa DMDP II Package IV wenye thamani ya Shilingi bilioni 26.06 unaohusisha ujenzi wa barabara 16 zenye urefu wa kilomita 7.38, ambapo alisisitiza kuwa barabara ya Muhimbili ni kiungo muhimu kwa wagonjwa na wananchi hivyo haipaswi kuendelea kucheleweshwa.
“Nataka ndani ya siku 14 barabara hii iwe imeanza kumwagwa lami. Meneja wa TARURA Wilaya ya Ilala simamia hili. Pia nataka TAKUKURU Wilaya ya Ilala ifuatilie commitment hii na kuhakikisha kila mmoja anawajibika kwa nafasi yake. Baada ya siku 14 tutarudi hapa kuona kazi iliyofanyika,” amesema Mpogolo.
Ameeleza kuwa ingawa mradi huo uliotakiwa kukamilika Agosti 14, 2026 umeongezewa muda hadi Desemba 16, 2026, kuongezwa kwa muda hakupaswi kuwa sababu ya kufanya kazi kwa kasi ndogo, hasa ikizingatiwa kuwa mradi umefikia asilimia 55 pekee huku Serikali ikiwa imeshalipa zaidi ya Shilingi bilioni 5.
Ili kuongeza kasi ya kazi, DC Mpogolo amemtaka mkandarasi kuongeza mara moja mitambo, wataalamu, na nguvu kazi pamoja na kufanya kazi usiku na mchana, huku akibainisha kuwa kati ya barabara zote 16 ni barabara tatu pekee zinazoonyesha maendeleo ya kuridhisha.
“Serikali imelipa fedha. Tunachotaka sasa si maelezo, tunataka matokeo. Ongezeni vifaa, ongezeni watu, ongezeni zamu na mfanye kazi usiku na mchana. Mradi huu ni wa wananchi na lazima tuone thamani ya fedha zao,” amesisitiza.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, amezitaka halmashauri nchini kubadili mtazamo wa ukusanyaji wa mapato na kuanza kubuni shughuli mpya za kiuchumi na uwekezaji badala ya kuongeza tozo na ushuru kwa wafanyabiashara wale wale.
Prof. Kitila amesema halmashauri nyingi zimekuwa zikielekeza nguvu kubwa katika kubuni tozo na ushuru mpya kila zinapokutana na changamoto ya mapato, hali ambayo inaweza kuwabebesha mzigo wafanyabiashara na kudhoofisha shughuli za kiuchumi.
Amesema mamlaka ya ukusanyaji wa kodi nchini ni Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), huku halmashauri zikitakiwa kujenga mazingira yatakayowezesha shughuli za uzalishaji na biashara kukua.
Amesema badala ya kuongeza mzigo kwa wafanyabiashara waliopo, halmashauri zinapaswa kujiuliza zimebuni miradi gani mipya ya uzalishaji, imevutia uwekezaji gani na imewezesha biashara ngapi mpya kuanzishwa.
Ameeleza kuwa kuongeza wigo wa mapato kunapaswa kwenda sambamba na kuongezeka kwa shughuli za kiuchumi, ikiwemo kufunguliwa kwa maduka makubwa, viwanda vidogo na biashara mpya.
Prof. Kitila amesema Serikali inalenga kupunguza mzigo wa tozo na ushuru ili kutoa nafasi kwa wafanyabiashara kufanya biashara zaidi na kukuza shughuli zao.
Amesisitiza kuwa halmashauri zinapaswa kubadilika kutoka kuwa vituo vya kukusanya ushuru na tozo na kuwa injini za ukuaji wa uchumi, kwa kubuni na kuwezesha shughuli mpya za uzalishaji na uwekezaji.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, amesema Tanzania inalenga kutumia uwezo wake mkubwa wa uzalishaji wa chakula kuwa kikapu cha chakula cha Afrika, kama sehemu ya utekelezaji wa malengo ya maendeleo ya taifa.
Prof. Kitila amesema Tanzania kwa sasa inajitosheleza kwa chakula kwa asilimia 130, huku ukanda wa Nyanda za Juu Kusini ukiongoza kwa kiwango cha kujitosheleza kwa chakula kwa asilimia 219.
Amesema kuanzia mwezi Oktoba, ukanda wa Afrika Mashariki unatarajiwa kukumbwa na mvua za El Niño, ambazo zinaweza kuleta changamoto katika usalama wa chakula kwa baadhi ya nchi.
Kwa mujibu wa Prof. Kitila, Tanzania iko katika nafasi nzuri ya kukabiliana na changamoto hiyo kutokana na kuwa na chakula cha kutosha, huku ikielezwa kuwa ni nchi pekee katika ukanda huo yenye kiwango hicho cha kujitosheleza.
Prof. Kitila amesema hayo katika Jukwaa la Dira 2050 - Songwe, ambapo ameeleza dira ya maendeleo ya Tanzania inaweka msukumo wa kuitumia fursa hiyo kuifanya nchi kuwa chanzo muhimu cha chakula kwa bara la Afrika.
“Tunataka Tanzania iwe kikapu cha chakula cha Afrika.”
Amesema hatua hiyo itahitaji kuongeza uzalishaji, tija na uwekezaji katika sekta ya kilimo ili Tanzania isiishie kujitosheleza kwa chakula, bali iweze pia kuzalisha ziada kwa ajili ya masoko ya kikanda na bara la Afrika.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Jabiri Makame amesema Serikali inalenga kujenga taifa jumuishi lenye ustawi, haki na linalojitegemea kupitia utekelezaji wa Dira ya Taifa 2050.
Amesema Dira hiyo inalenga kuweka msingi wa maendeleo jumuishi na endelevu, huku kila Mtanzania akipata fursa ya kushiriki na kunufaika na maendeleo ya taifa.
"Tunataka kujenga taifa jumuishi lenye ustawi, haki na linalojitegemea" amesema RC Makame
Kauli hiyo imetolewa katika Jukwaa la Dira 2050 Songwe, linalofanyika kwa siku mbili, Agosti 19 na 20, 2026.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Songwe, Radwell Mwampashe, amesema Dira ya Taifa inapaswa kujikita katika kuwajengea vijana uzalendo, ili kuwa na kizazi kinachofahamu mwelekeo wa nchi na kinachothamini amani, mshikamano na maendeleo.
Akitoa salamu za Chama katika Jukwaa la Dira 2050 - Songwe, Mwampashe amesisitiza umuhimu wa kuwaandaa vijana, hususan kizazi cha Gen Z na Gen Alpha kuwa wazalendo na washiriki muhimu katika kulinda na kuendeleza misingi ya taifa. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Wananchi na mawakala wa meli wamezungumzia fursa mbalimbali zinazotokana na uwekezaji mkubwa wa miundombinu uliofanywa na Serikali kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) katika Bandari ya Mtwara, wakieleza kuwa umeleta tija kubwa na kufungua fursa mpya za kiuchumi mkoani humo.
Maboresho hayo yameongeza kwa kiasi kikubwa kiasi cha shehena ya mizigo inayopakiwa na kushushwa kwenda maeneo mbalimbali ya ndani na nje ya nchi ikijumuisha mataifa jirani ya Malawi, Zambia, Zimbabwe, Rwanda, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), pamoja na Msumbiji.
Wakizungumza na waandishi wa habari wananchi, mawakala na uongozi wa bandari hiyo wamepongeza uwekezaji huo uliofanywa na Serikali jinsi ulivyofungua fursa kwa kila mmoja.
Mama lishe wa eneo la bandarini, Rehema Mputa, amesema maboresho ya bandari yamebadili biashara yake na kuongeza kipato huku kiongozi wa madereva bodaboda, Issa Mchika akisema shughuli za bandari zimeongeza abiria na kipato kwa madereva.
Wakala wa Meli wa Joyous Shipping Service Ltd, Esthersia Mallya ameeleza mazingira yalivyo rafiki katika bandari hiyo na Kaimu Meneja wa Bandari Mtwara, Hekima Ngeze akielezea maboresho yalivyofanyika na yanayoendelea ili kuifanya kuwa bora zaidi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
📍SONGWE - Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, tayari amewasili kushiriki Jukwaa la Dira 2050 na Uwekezaji linalofanyika kwa siku mbili, Agosti 19 na 20, 2026, mkoani Songwe.
Jukwaa hilo linafanyika katika Ukumbi Mkuu wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, likilenga kujadili utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 na fursa za uwekezaji.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio, ametangaza vikwazo rasmi dhidi ya Rais wa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC), Tomoko Akane, pamoja na viongozi wengine wa chombo hicho cha sheria cha kimataifa.
Hatua hiyo inatajwa kuwa muendelezo wa msimamo mkali wa utawala wa Rais Donald Trump katika kampeni yake inayolenga kuikabili na kuidhoofisha mahakama hiyo, ambayo imepewa mamlaka na zaidi ya nchi wanachama 120 kuchunguza na kushtaki uhalifu wa kivita pamoja na uhalifu dhidi ya ubinadamu.
Rubio amebainisha kuwa Marekani imeweka vikwazo hivyo dhidi ya Rais wa ICC, Tomoko Akane kutoka nchini Japan, pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Mashtaka wa Mahakama hiyo, Abdoulaye Seye kutoka nchini Senegal.
Ameeleza kuwa hatua hiyo imechukuliwa kufuatia viongozi hao kushiriki katika jitihada za ICC za kuwafungulia mashtaka maafisa kutoka nchi ambazo serikali zao hazijaridhia mkataba wa kuwa wanachama wa mahakama hiyo.
Kufuatia tangazo hilo, Mamlaka ya ICC imetoa taarifa ikisisitiza kuwa inaendelea kuwaunga mkono kikamilifu wafanyakazi na viongozi wake wote waliolengwa.
ICC imeeleza kuwa inaamini kwa dhati kwamba hatua kama hizo zilizotangazwa na Rubio hazisaidii ustawi wa haki za binadamu, bali zinadhoofisha misingi mikuu ya utawala wa sheria na haki duniani. -
Jambo TV
@Jambotv_
Serikali ya Ghana imetoa wito wa kutaka kukomeshwa mara moja kwa kitendo cha raia wa mataifa ya Afrika kusajiliwa na kushiriki katika vita vinavyoendelea kati ya Urusi na Ukraine, kufuatia vifo vya raia wake nchini humo.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ghana, Samuel Okudzeto Ablakwa, amethibitisha kuwa hadi sasa jumla ya raia 62 wa Ghana wameuawa wakiipigania Urusi katika vita hivyo vya Ukraine, huku raia wengine 15 wakiwa bado hawajulikani waliko.
Bwana Ablakwa ameyasema hayo jijini Moscow alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara yake nchini Urusi kwa ajili ya kufanya mazungumzo ya kidiplomasia na mwenzake wa Urusi, Sergei Lavrov.
Amebainisha kuwa matumizi ya raia wa Kiafrika katika uwanja wa mapambano ni jambo linalopaswa kusitishwa mara moja ili kulinda maisha ya raia hao na usalama wa mataifa yao.
Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na maafisa wa Ukraine, zaidi ya raia 272 wa Ghana wamesajiliwa na kujiunga na jeshi la Urusi tangu kuibuka kwa vita hivyo mwaka 2022.
Tathmini za Serikali ya Ukraine zinaonesha kuwa takribani raia 2,000 kutoka nchi 36 tofauti za Afrika wanapigana katika uwanja wa vita kwa niaba ya Urusi.
Hata hivyo, kwa upande wao, maafisa wa Serikali ya Urusi wamekuwa wakikanusha tuhuma hizo wakisisitiza kuwa hawawasajili raia kutoka mataifa ya Afrika kinyume na sheria za kimataifa au bila ridhaa yao. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkurugenzi wa Huduma za Wawekezaji kutoka Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalumu ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA), James Maziku, amesema Jukwaa la Pili la Uwekezaji kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya linalenga kufungua fursa za kibiashara kati ya wafanyabiashara wa sekta binafsi wa Tanzania na wale wa Ulaya.
Maziku ameeleza hayo Agosti 18, 2026, Jijini Dar es Salaam, wakati wa uzinduzi rasmi wa toleo la pili la Jukwaa la Uwekezaji na Biashara kati ya Umoja wa Ulaya (EU) na Tanzania, unaofanyika kwa kushirikiana na sekta binafsi.
Amebainisha kuwa jukwaa hilo, ambalo pia linahusisha majadiliano ya kibiashara, linalenga kuibua maeneo ya kimkakati yatakayovutia wawekezaji wa mitaji kutoka Bara la Ulaya. Akatolea mfano sekta ya kilimo hapa nchini, akisema ni sekta kubwa lakini uwekezaji wake bado upo chini. "Lengo ni kuunganisha mitaji ya sekta binafsi kutoka Ulaya ili kufungamanisha kilimo chetu na ongezeko la thamani." Amesema.
Naye, Balozi John Ulanga kutoka Idara ya Diplomasia ya Uchumi ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, amesema Wizara hiyo kwa kushirikiana na TISEZA na Ujumbe wa EU, itahakikisha miradi inayohitaji uwekezaji wa sekta binafsi inachangamkia na kutumia kikamilifu fursa hiyo.
Kwa upande wake, Mkuu wa Ushirikiano wa Ujumbe wa Umoja wa Ulaya Tanzania na EAC, Marc Stalmans, amesema ushirikiano uliopo kati ya pande hizo mbili utazinufaisha pande zote, ikiwemo fursa ya EU kuleta teknolojia na ujuzi kwa Watanzania.
Ameongeza kuwa kuanza kwa ushirikiano huo mpya wa kiuchumi ni hatua muhimu kwa sababu kutaziweka pamoja sekta binafsi za Tanzania na Ulaya, pamoja na serikali, katika kuendeleza biashara na kuimarisha uhusiano wa pande zote mbili.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Serikali imewapa siku saba wamiliki wa viwanda vya kuzalisha saruji nchini kuwasilisha mapendekezo ya namna ya kutatua changamoto ya bei kubwa ya saruji sokoni pamoja na kero ya kuadimika kwa bidhaa hiyo.
Msimamo huo umefikiwa kufuatia kikao cha pamoja kilichoongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Balozi Waziri Salum, alipokutana na kufanya mazungumzo na wamiliki wa viwanda vya saruji, Agosti 18, 2026, jijini Dodoma.
Kikao hicho kimehudhuriwa pia na viongozi wa taasisi mbalimbali za udhibiti, viwango na masoko nchini ikiwemo Tume ya Ushindani (FCC), Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), pamoja na Wakurugenzi kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara.
Akizungumza katika kikao hicho kilichokutanisha wadau wote muhimu wa sekta hiyo, Balozi Waziri Salum amesisitiza kuwa lengo kuu la Serikali ni kupata suluhu ya kudumu itakayohakikisha saruji inapatikana kwa urahisi na kwa bei inayozingatia maslahi ya wazalishaji, wafanyabiashara, na wananchi wa kawaida.
"Serikali imewataka wazalishaji kutumia muda huo wa siku saba kufanya tathmini ya changamoto zinazoathiri bei ya saruji na upatikanaji wake sokoni na kuwasilisha mapendekezo yanayoweza kusaidia kupunguza au kudhibiti ongezeko la bei ya bidhaa hiyo na upatikanaji wake," amesema Balozi Salum.
Hatua hiyo imetajwa kuwa sehemu ya jitihada za Serikali za kuweka mazingira rafiki ya biashara nchini huku ikilinda walaji na kuhakikisha bidhaa zote muhimu za ujenzi zinapatikana bila usumbufu katika maeneo yote ya nchi.
Baada ya kukamilika kwa muda huo wa siku saba, Serikali inatarajiwa kupitia na kufanya tathmini ya mapendekezo yatakayowasilishwa na wazalishaji hao ili kuchukua hatua za mwisho zitakazohitimisha changamoto hiyo ya bei na upatikanaji wa saruji. -
Jambo TV
@Jambotv_
Serikali ya Tanzania, kwa kushirikiana na Umoja wa Ulaya (EU), imezindua rasmi maandalizi ya ziara maalum ya kibiashara na uwekezaji (European Roadshows) itakayofanyika katika nchi nne za Ulaya, ikiwa na lengo la kuvutia mitaji mikubwa na kuimarisha ongezeko la thamani kwa bidhaa za Tanzania
Ziara hiyo, ambayo ni sehemu ya awamu ya kwanza ya Jukwaa la Uwekezaji na Biashara kati ya Umoja wa Ulaya na Tanzania (2026-2027), itafanyika kuanzia tarehe 28 Septemba hadi 6 Oktoba 2026 katika nchi za Finland, Italia, Uholanzi, na Ubelgiji. Maeneo yaliyopewa kipaumbele ni pamoja na kilimo, madini ya kimkakati, uchumi wa kidijiti, nishati mbadala, na miundombinu ya usafirishaji.
Akizungumzia umuhimu wa ziara hiyo wakati wa Jukwaa la Uwekezaji na Biashara kati ya Umoja wa Ulaya na Tanzania Agosti 18, 2026, Mkurugenzi wa Huduma kwa Wawekezaji kutoka Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalumu ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA), James Maziku, ameeleza kuwa lengo ni kuunganisha sekta binafsi ya Tanzania na ya Ulaya.
“Tunataka kufika mahala tuunganishe mitaji ya sekta binafsi kutoka bara la Ulaya kuja kuwekeza kwenye sekta ya kilimo ili kuweza kufungamanisha kilimo na ongezeko la thamani,” amesema Maziku
Ameongeza kuwa katika sekta ya madini, Tanzania inalenga kuvutia mitaji kwa ajili ya madini ya kisasa kama kinywa, lithium, na cobalt ili kupunguza uuzaji wa madini ghafi.
Naye Balozi John Ulanga kutoka Idara ya Diplomasia ya Uchumi (Wizara ya Mambo ya Nje), amebainisha kuwa ziara hiyo ni ishara ya imani ya kimataifa kwa uchumi wa Tanzania, akieeleza pia kuwa nchi kama Italia zina hamu kubwa ya kuwekeza katika kilimo cha mpunga, kahawa, na korosho, kwa msisitizo wa ufungashaji na usindikaji nchini.
“Hii ni dalili ya ushirikiano mzuri na dalili ya imani ambayo wamekuwa nayo kwenye mazingira ya uwekezaji na mazingira ya uchumi kwa ujumla kwa nchi yetu,” amesema Balozi Ulanga
Kwa upande wake, Mkuu wa Ushirikiano wa Ujumbe wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania na EAC, Marc Stalmans, amesisitiza kuwa ushirikiano huu mpya unalenga kuleta manufaa ya pande zote kwa kuhakikisha kuwa usindikaji wa bidhaa unafanyika hapa nchini badala ya kuuza malighafi nje.
“Manufaa ya mabadiliko hayo yanapaswa kubaki katika mifuko ya Watanzania... Soko la Ulaya litapata bei nzuri na ubora ule ule huku likijua bidhaa inatoka Tanzania, na mkulima mdogo pamoja na serikali ya Tanzania watanufaika,” amesema Stalmans
Ziara hizi zitahusisha mikutano ya ana kwa ana kati ya wafanyabiashara (B2B) na kati ya serikali na wafanyabiashara (B2G), na zinatarajiwa kuhitimishwa na Jukwaa kubwa la Uwekezaji jijini Dar es Salaam mapema mwaka 2027. -
Jambo TV
@Jambotv_
Tanzania imeingia katika hatua mpya ya uendelezaji wa Madini Tembo (Heavy Mineral Sands), huku Serikali ikisisitiza kuharakishwa kwa ujenzi wa kiwanda cha uchakataji wa madini hayo katika eneo la Tajiri Tanga, ili kuongeza thamani ya madini nchini kabla ya kusafirishwa nje.
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa, ametoa agizo hilo leo, Agosti 18, 2026, wakati akikagua shughuli za uchimbaji katika Mradi wa Fungoni wilayani Kigamboni mkoani Dar es Salaam unaotekelezwa na Nyati Mineral Sands Limited, pamoja na kupata taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa kiwanda cha Tajiri Tanga. Serikali inamiliki asilimia 16 ya hisa katika kampuni hiyo.
Dkt. Kiruswa amesema Serikali imetoa kibali cha miaka miwili kwa kampuni hiyo kusafirisha madini ghafi nje ya nchi ili kuiwezesha kukamilisha ujenzi wa kiwanda, huku akisisitiza kuongezwa kwa ajira kwa Watanzania, uhamishaji wa teknolojia na ujuzi pamoja na utekelezaji wa mipango ya uwajibikaji kwa jamii na urejeshaji wa maeneo baada ya uchimbaji.
Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa Nyati Mineral Sands Limited, Wei Huang, amesema kampuni mama ya Shenghe Resources Holding Co. Ltd imeichagua Tanzania kuwa kitovu cha uchakataji wa Madini Tembo, ambapo madini yatakayozalishwa katika miradi yake mbalimbali ikiwamo Madagascar, yatachakatwa nchini.
Amesema tangu mwaka 2024, jumla ya tani 85,000 za Madini Tembo zimezalishwa kupitia Mradi wa Kigamboni, huku tani 14,793.35 zikiwa tayari zimesafirishwa.
Miradi ya Kigamboni na Tajiri ina uwekezaji wa zaidi ya Dola milioni 30, wakati uwekezaji wa Shenghe nchini Tanzania ukifikia takribani Dola milioni 600.
Wei amesema zaidi ya asilimia 90 ya wafanyakazi katika miradi hiyo ni Watanzania, huku wakazi wa Kigamboni wapatao 284 tayari wamenufaika na ajira. Mradi wa Kigamboni unakadiriwa kuwa na uhai wa miaka minne, wakati Mradi wa Tajiri, Tanga ukitarajiwa kuendelea kwa miaka 23.
Akizungumzia mapato, Dkt. Kiruswa amesema Mkoa wa Kimadini wa Dar es Salaam na Pwani ulikusanya Shilingi bilioni 27.07 katika mwaka wa fedha 2025/26 dhidi ya lengo la Shilingi bilioni 24. Kwa mwaka 2026/27, mkoa umepewa lengo la Shilingi bilioni 33 na tayari mwezi Julai pekee umekusanya Shilingi bilioni 4.06, sawa na asilimia 147.50 ya lengo la mwezi.
Madini Tembo hutumika katika utengenezaji wa bidhaa mbalimbali ikiwamo rangi, vigae na vipuri vya ndege, hivyo uwekezaji huo unatajwa kuwa fursa kubwa kwa Tanzania kujenga mnyororo wa thamani wa madini na kuongeza mapato na ajira nchini. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imesema haijaridhishwa na utekelezaji wa baadhi ya manunuzi yaliyofanywa na Chuo Kikuu cha Mzumbe, baada ya kubaini ukiukwaji wa sheria na taratibu za manunuzi katika hoja zilizowasilishwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2024/2025.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Agosti 18, 2026, Bungeni jijini Dodoma, Mwenyekiti wa PAC, Mheshimiwa Devotha Minja, amesema Kamati haijaridhishwa na majibu yaliyotolewa na Chuo hicho kuhusu hoja hizo, ikiwemo manunuzi yenye thamani ya shilingi bilioni 29.77 yaliyofanywa kutoka kwa wazabuni ambao hawakukidhi vigezo vilivyowekwa.
Kwa mujibu wa taarifa ya CAG, pia kuna shilingi bilioni 1.54 zilizolipwa kwa watu ambao hawakukidhi viwango vilivyotakiwa. Kamati imeeleza kuwa hoja hiyo inahitaji maelezo na hatua stahiki ili kuhakikisha matumizi ya fedha za umma yanafuata sheria na taratibu.
Aidha, PAC imeeleza kutoridhishwa na ujenzi wa barabara chini ya kiwango wenye thamani ya shilingi milioni 523, pamoja na madai ya ziada ya shilingi milioni 718 ambayo Kamati imesema hayakustahili na hayakuzingatia masharti ya mkataba.
Minja amesema kutokana na uzito wa hoja hizo, Kamati inaendelea kutafakari hatua zaidi za kuchukua ili kulishauri Bunge ipasavyo kuhusu namna ya kushughulikia kasoro hizo na kuimarisha uwajibikaji katika matumizi ya fedha za umma.
Hoja hizo zimeibuliwa wakati PAC ikijadili Taarifa ya Hesabu zilizokaguliwa za Chuo Kikuu cha Mzumbe kwa mwaka wa fedha 2024/2025.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo, amepongeza ubunifu mkubwa uliooneshwa na wanafunzi wa Chuo cha Mtakatifu Joseph (St. Joseph) cha jijini Dar es Salaam, huku akitangaza kuwa Serikali itashirikiana kwa karibu na vyuo binafsi kuhakikisha masomo ya sayansi yanapewa kipaumbele ili kupata wahandisi wengi na kuondoa utegemezi wa wataalamu kutoka nje.
Profesa Mkumbo ameyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati akizungumza kwenye maonesho ya Wiki ya Tafiti na Ubunifu katika chuo hicho, ambapo wanafunzi walionesha teknolojia mbalimbali za uhandisi na sayansi.
Ameeleza kuwa chuo hicho kimekuwa kikiongoza kwa muda mrefu katika kutoa wataalamu wa fani hiyo, hivyo anakitaka kuendelea kushikilia nafasi yake ya ukinara nchini.
Pamoja na pongezi hizo, Profesa Mkumbo ametoa changamoto kwa uongozi wa chuo hicho kuhakikisha kazi za ubunifu za wanafunzi hazibakii vyuoni kama mawazo pekee, bali ziunganishwe na sekta ya viwanda ili kuleta matokeo halisi na kusaidia ajira.
“Nimejionea ubunifu mkubwa sana kwa wanafunzi wenu lakini kinachosikitisha ni kuwa ubunifu huo unaishia kuwa wazo tu haufikii mwisho kwa hiyo nawapa changamoto mhakikishe ubunifu wa wanafunzi wenu unaunganishwa na viwanda na kuwa halisi,” alisema Profesa Mkumbo.
Amesisitiza kuwa ili mwanafunzi ajiajiri au kuajiriwa kwa urahisi lazima aoneshe matokeo ya kile alichobuni badala ya kuacha mawazo hayo kuishia kwenye majengo ya chuo, huku akiwataka wanafunzi kuendelea kubuni vifaa nafuu vinavyotatua kero za kijamii.
Katika hatua nyingine, Waziri Mkumbo ameeleza kufurahishwa kwake na ubunifu wa wanafunzi hao katika matumizi ya nishati safi ya kupikia majumbani, akibainisha kuwa hatua hiyo inaunga mkono kwa vitendo jitihada za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuhamasisha matumizi ya nishati safi nchini.
“Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa akifanya jitihada kubwa kuhakikisha wananchi wake wanatumia nishati safi ya kupikia kwa hiyo nilipoona na nyinyi mmebuni matumizi ya nishati safi nilifurahi sana, nawapongeza sana,” alisema Waziri Mkumbo.
Akiipongeza menejimenti na Makamu Mkuu wa chuo hicho kwa kuanzisha vituo vitano vya uhamiri vinavyofundisha masuala ya sayansi, Profesa Mkumbo ameeleza kuwa jitihada zao kwenye maeneo ya roboti na akili mnemba (Artificial Intelligence) zinakwenda sambamba na mwelekeo wa dunia na maandalizi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 inayolenga kuimarisha matumizi ya teknolojia.
Aidha, amempongeza mwanzilishi wa chuo hicho kwa uamuzi wake wa kijasiri wa kuwekeza katika elimu ya sayansi kupitia sekta binafsi wakati ambapo sekta hiyo ilikuwa haijapata mapokeo makubwa kama ilivyo sasa. -
Jambo TV
@Jambotv_
Ushindani katika soko la mafuta nchini Tanzania umeongezeka katika mwaka wa fedha wa 2024/25, huku kampuni ya Camel Oil ikiibuka kama iliyopiga hatua kubwa zaidi wakati baadhi ya wachezaji wa zamani wakipoteza sehemu kubwa ya soko, kulingana na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura).
Kwa mujibu wa habari ya mwandishi Gadiosa Lamtey iliyochapishwa na The Citizen, ripoti ya Utendaji wa Sekta Ndogo ya Mafuta ya Ewura kwa mwaka 2024/25 inaonesha kuwa makampuni matano makubwa ya usambazaji wa mafuta (OMCs) yalidhibiti asilimia 48.7 ya soko la mafuta, ikiiachia asilimia 51.3 kwa wachezaji wengine.
Puma Energy iliendelea kuwa kinara wa soko ikiwa na hisa ya asilimia 15.5, ikifuatiwa na Camel Oil yenye asilimia 11.4, Mansoor Industries Limited (MOIL) ikiwa na asilimia 10, Oilcom Tanzania yenye asilimia 6.4, na Mount Meru Petroleum ikiwa na asilimia 5.3.
Takwimu hizo zinaonesha mabadiliko makubwa miongoni mwa wachezaji wakuu, hasa Camel Oil, ambayo ilipanda kutoka nafasi ya walio shika nafasi ya nane mwaka 2023/24 hadi nafasi ya pili mwaka 2024/25. Hisa yake ya soko iliongezeka zaidi ya mara mbili kutoka asilimia 5.54 hadi asilimia 11.4.
"Puma Energy imeweka msimamo wa kushikilia nafasi ya kwanza kwa kipindi cha miaka ane, wakati Camel Oil imetoka nafasi ya nane ikiwa na hisa ya soko ya asilimia 5.54 katika Mwaka wa Fedha 2023/24 hadi nafasi ya pili ikiwa na hisa ya asilimia 11.4," inasema ripoti hiyo.
Mabadiliko hayo hayakugusa Camel Oil pekee. MOIL, ambayo iliyokuwa ya pili kwa ukubwa, ilishuka hadi nafasi ya tatu baada ya hisa yake ya soko kupungua kutoka asilimia 11.12 mwaka 2023/24 hadi asilimia 10 mwaka 2024/25.
Acer Petroleum nayo ilikutana na mporomoko mkubwa, ambapo hisa yake ilishuka kutoka asilimia 7.96 hadi asilimia 4.8, hatua iliyoisukuma kutoka nafasi ya nne hadi ya nane. Oryx Oil ilirekodi anguko jingine kubwa, hisa yake ikishuka kutoka asilimia 5.99 hadi asilimia 2.8, na kuporomoka kutoka nafasi ya sita hadi ya 11. Mount Meru Petroleum, kwa upande wake, iliongeza hisa yake hadi asilimia 5.3 na kujitwalia nafasi ya tano.
Kipi Kinachotawala Ukuaji wa Hisa ya Soko?
Ewura ilisema hisa ya soko inaathiriwa na mambo kadhaa badala ya idadi tu ya makampuni yanayofanya kazi katika sekta hiyo. Mambo haya ni pamoja na idadi ya vituo vya mafuta vinavyomilikiwa na kampuni (retail outlets), uaminifu wa wateja kwa chapa fulani (brand loyalty), ubora wa huduma zinazotolewa kwa vituo vya mafuta vinavyojitegemea na mikataba ya usambazaji na wateja wakubwa (viwanda, shughuli za uchimbaji madini, na biashara za kilimo).
Mkurugenzi wa Sekta ya Mafuta wa Ewura, Gerald Maganga, ameeleza kuwa takwimu hizi zinaonesha sekta hiyo ina ushindani wa kweli na uwepo wa wachezaji wengi unalinda soko dhidi ya uhaba wa mafuta pindi kampuni moja inapojitoa.
Hata hivyo, Ewura imesisitiza kuwa makampuni yanazuiwa kujihusisha na vitendo vinavyovunja ushindani wa haki, ikiwa ni pamoja na kuchafua au kushusha viwango vya ubora wa mafuta, kuuza bidhaa za mafuta juu ya bei kikomo zilizoainishwa na serikali, kukiuka masharti ya afya, usalama, na mazingira (HSE).
Naye, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirikisho la Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Deogratius Massawe, amesema ukuaji wa makampuni ya ndani ni hatua chanya inayoongeza ustahimilivu wa kiuchumi. Ameonya kuwa kutegemea zaidi makampuni ya kigeni kunaweza kuingiza nchi kwenye mshtuko wa kiuchumi pale makampuni hayo yanapokabiliwa na vikwazo vya kimataifa.
Kupaa kwa Camel Oil kutoka nafasi ya 8 hadi ya 2, na kuendelea kushikilia nafasi za juu kwa makampuni kama MOIL na Oilcom, ni ishara ya wazi kuwa makampuni ya ndani ya Kitanzania yameongeza uwezo wa kimitaji, usimamizi, na mtandao wa kibiashara. Mwelekeo huu unajibu moja kwa moja mijadala yetu iliyopita kuhusu Local Content na sheria za uwezeshaji wazawa-w azawa sasa hawapo tena kwenye karatasi tu, bali wanamiliki sekta za kimkakati.
Soma zaidi hapa jambo.co.tz/waliopata-waliokosa-ushindani-wa-soko-la-mafu… -
Jambo TV
@Jambotv_
Tume ya Uchaguzi ya Zambia (ECZ) imemtangaza rasmi Rais aliyepo madarakani, Hakainde Hichilema, kuwa mshindi wa Uchaguzi Mkuu wa Urais nchini humo kwa kuibuka na asilimia 60 ya kura zote zilizopigwa.
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Mwangala Zaloumis, ametangaza matokeo hayo leo Jumanne, tarehe 18 Agosti 2026, akibainisha kuwa ingawa matokeo ya majimbo matano (5) kati ya 226 yalikuwa bado hayajakamilika, takwimu hizo hazina uwezo wa kubadilisha matokeo ya mwisho ya kinyang'anyiro hicho.
Kwenye uchaguzi huo uliokuwa na wagombea 13, Hichilema (64) anayeongoza tangu mwaka 2021 kupitia chama cha UPND, alifuatiwa na mpinzani wake mkuu, Brian Mundubile (55) wa chama cha NRPUP, aliyepata takribani asilimia 38 ya kura.
Akizungumza mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa kiti cha Urais, Rais Hichilema ameeleza kuguswa na ushindi huo huku akiahidi kuwatumikia hata wale waliowapigia kura wapinzani wake:
"Tunyenyekevu mkubwa kwa uaminifu mliouweka mikononi mwetu. Kwa wale wananchi waliopendelea mawazo yaliyowasilishwa na wapinzani wetu, tunawasikia na tutaendelea kuwatumikia na kuwafanyia kazi," amesema Hichilema.
Mara baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo, mamia ya wafuasi wa chama cha UPND wakiwa wamevalia mavazi ya rangi nyekundu walifika katika mitaa ya mji mkuu wa Lusaka, wakiimba, kucheza na kulipua fataki kusherehekea ushindi huo.
Ushindi huo unakuja katikati ya vuguvugu zito la kisiasa kufuatia upinzani kulalamikia vitendo vya vitisho na matumizi mabaya ya vyombo vya dola kabla na baada ya siku ya upigaji kura.
Siku ya Jumatatu, Mundubile alichapisha ujumbe wa video akidai kuwa nyaraka za matokeo zilibadilishwa, hasa katika Mkoa wa Kusini (Southern Province), ili kumpendelea mgombea wa chama tawala.
Mvutano huo uliingia dosari zaidi kufuatia tangazo la serikali siku ya Jumapili kuwa polisi waliwakamata watu 11, wakiwemo viongozi sita wa upinzani, katika msako dhidi ya kile walichokiita "shughuli za kigaidi na kundi la waasi." Serikali ilidai watuhumiwa hao walikutwa na silaha nzito za kijeshi na risasi.
Hata hivyo, chama cha NRPUP kilikanusha vikali madai hayo kikieleza kuwa operesheni hiyo ya polisi ilifanyika nyumbani kwa Mundubile ambapo risasi zilipigwa na kusababisha mbunge mmoja kujeruhiwa.
"NRPUP inakataa kwa dharau kubwa madai yote ya uongo yaliyotolewa na Serikali ya Zambia kwamba uongozi au wanachama wetu wanahusika na uasi au makundi ya kigaidi," ilieleza taarifa ya chama hicho. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
📍KAGERA - Mkazi wa Mtaa wa Rwamishenye katika Manispaa ya Bukoba, Frank Stanley, amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando jijini Mwanza, huku familia yake ikiomba uchunguzi kufanyika kubaini mazingira yaliyosababisha kulazwa kwake akiwa katika hali mbaya kiafya.
Taarifa zinaeleza kuwa Frank amelazwa katika Wodi Namba 6 tangu Agosti 8, 2026, huku ndugu zake wakisema hali yake bado ni mbaya.
Baba mzazi wa Frank, Stanley Ndibalema, amedai kuwa mwanawe alikamatwa na Polisi Julai 30, 2026, na tangu wakati huo familia imekuwa ikifuatilia taarifa kuhusu hali na mahali alipo, huku wakieleza kuwa wamekuwa wakipata majibu ambayo hawajayaelewa kikamilifu.
Akizungumza kuhusu hali hiyo, Ndibalema amesema familia inaomba uchunguzi wa kina kufanyika ili kubaini kilichotokea na hatua zinazofaa kuchukuliwa.
“Kitu kinachotuumiza sana kama familia ni namna kijana alivyokamatwa na kufikishwa hospitali ha Bugando kwahiyo sisi tunacho kiomba sana tupate kijana wangu akiwa hai kama ni adhabu ya kisheria apewe sio kutaka kumdhurumu uhai wake, namuomba Rais, Waziri Mkuu, Waziri wa Mambo ya Ndani na IGP waingilie kati haki ipatikane watu wote walio husika wawajibishwe,” amesema.
Mama mwenye nyumba aliyokuwa akiishi Frank, Leticia Josephat, amesema mara ya mwisho kijana huyo aliondoka nyumbani akiwa katika hali nzuri, lakini aliporejea akiwa ameambatana na polisi kwa ajili ya upekuzi, alionekana akiwa na alama mwilini na akiwa amedhoofika.
“Sisi tunaomba polisi watuelezee Frank aliuguaje wakati alitoka hapa akiwa mzima, walipomleta alikuwa amepigwa nguvu zake zilikuwa hazipo vizuri na walivyomrudisha ndo wanadai alizimia sasa tunataka kujua walimfanya nini mpaka akafikia kuzimia mpaka sasa haongei, haamki, hasimami wala kutembea,” amesema.
Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Blasius Chatanda, amethibitisha kuwa Frank alikamatwa na makachero wa polisi kufuatia tuhuma za kuhusika na matukio ya wizi.
Kuhusu madai ya Frank kuteswa au kujeruhiwa akiwa mikononi mwa polisi, Chatanda amesema suala hilo linashughulikiwa na mamlaka husika ambazo zinaendelea na uchunguzi ili kubaini ukweli wa jambo hilo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo (WMA), Alban Kihulla amekutana na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Salum Mnuna, jijini Dodoma tarehe 17 Agosti 2026, kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wa kimkakati kati ya taasisi hizo mbili katika sekta za mafuta, gesi, maji na umeme.
Mazungumzo hayo yalilenga kuimarisha ushirikiano na uratibu wa kiutendaji, kubadilishana taarifa za kimkakati, pamoja na kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya taasisi hizo mbili katika sekta za mafuta, gesi, maji na umeme, kwa lengo la kuimarisha usimamizi, kulinda maslahi ya walaji na kuhakikisha utoaji wa huduma wenye tija na unaozingatia haki.
Viongozi hao wamesisitiza umuhimu wa kuhakikisha kuwa vifaa vyote vya kupimia vinavyotumika katika utoaji wa huduma na biashara vinatoa vipimo sahihi na vinavyoaminika, hatua ambayo ni muhimu katika kulinda maslahi ya walaji, wafanyabiashara na watoa huduma.
WMA, ikiwa na jukumu la kuhakikisha usahihi wa vipimo vinavyotumika katika biashara, itaendelea kushirikiana kwa karibu na EWURA ili kuimarisha haki katika miamala, uwazi, uwajibikaji na thamani ya fedha kwa mlaji.
Ushirikiano huo ni sehemu ya juhudi za Serikali za kujenga mazingira ya biashara yenye haki na kuimarisha imani ya wananchi katika mifumo ya vipimo na huduma zinazotolewa nchini. -
Jambo TV
@Jambotv_
-
Jambo TV
@Jambotv_
Wakili wa Kujitegemea, Peter Madeleka, ameachiwa kwa dhamana leo Agosti 17, 2026, baada ya kushikiliwa kwa takriban siku tatu katika Kituo Kikuu cha Polisi (Central) Dar es Salaam.
Upatikanaji wa dhamana hiyo umethibitishwa na Wakili Paul Kisabo kutoka Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), ambaye amekuwa akifuatilia mchakato huo tangu asubuhi ya leo. Akizungumza na Jambo TV kwa njia ya simu, Kisabo ameeleza kuwa licha ya Wakili Madeleka kutofikishwa mahakamani ndani ya saa 24 kama sheria inavyoelekeza, Jeshi la Polisi limeridhia kumpa dhamana.
Akielezea mchakato wa kuachiliwa kwake, Wakili Kisabo amesema: “Asubuhi niliamkia Central Policy Station Dar es Salaam kwa ajili ya kufuatilia dhamana yake. Na baada ya kufika nilikutana na ZCO na kuzungumza naye kuomba dhamana ya wakili Madeleka lakini yeye ZCO aliniambia nirudi mchana saa 8”
Baada ya kurejea kituoni hapo majira ya mchana, taratibu za dhamana zilikamilika kwa Madeleka kudhaminiwa na watu watatu. “Amekubali kwamba Madeleka adhaminiwe na watu watatu tumemdhamini kwa maana ya mimi Paul Kisabo nimemdhamini pamoja na ndugu zake wengine wawili... dhamana iko wazi na tumemdhamini,” ameongeza Wakili Kisabo.
Kuhusu utaratibu wa kumfikisha mahakamani, Wakili Kisabo amebainisha kuwa msisitizo wao kwa sasa ulikuwa ni kupata dhamana ya polisi ili mteja wao aweze kuwa nje wakati taratibu zingine zikiendelea.
Wakili Peter Madeleka alikamatwa Agosti 14, 2026, majira ya saa 9:30 alasiri akiwa katika viunga vya Mahakama ya Uhujumu Uchumi (Mikocheni B) wakati akitekeleza majukumu yake ya kitaaluma. Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi, Madeleka alishikiliwa kwa tuhuma za kudharau amri za Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi zilizotolewa tarehe 27 Julai na 13 Agosti, 2026.
Ukamataji huo ulitokea saa chache baada ya Madeleka kutangaza nia ya kufungua kesi kupinga zuio la Msajili wa Mahakama Kuu linalowazuia mawakili kufanya mahojiano na vyombo vya habari ndani ya maeneo ya mahakama. -
Jambo TV
@Jambotv_
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imewakumbusha wananchi na jamii kwa ujumla kuhusu umuhimu wa kulinda miundombinu ya maji, ili kujenga jamii inayothamini na kulinda huduma hiyo kwa ajili ya vizazi vya sasa na vijavyo.
Ujumbe huo umetolewa wakati wa tukio la Bonyokwa Women Gala 2026 lililoandaliwa na Diwani wa Kata ya Bonyokwa, Tumike Malilo, wilayani Ilala mkoani Dar es Salaam, likiwa na kauli mbiu isemayo “Mwanamke Imara, Jamii Imara, Maendeleo Endelevu” kwa azma ya kuwawezesha wanawake kiuchumi.
Akishiriki kama Mgeni Rasmi katika tamasha hilo, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mussa Azzan Zungu, amewahimiza wanawake kutumia elimu na fursa walizopata kuboresha shughuli zao za kibiashara, huku akiwataka pia kuchangamkia fursa za kiuchumi zitakazojitokeza wakati wa mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).
Kwa upande wa DAWASA, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano, Everlasting Lyaro, amewaomba wanawake wa Bonyokwa kuwa mabalozi wema wa huduma za maji kwa kutoa taarifa mapema pindi wanapobaini changamoto za kihuduma ikiwemo mivujo ya maji katika maeneo yao.
Lyaro amebainisha kuwa utoaji wa taarifa kwa wakati unaiwezesha DAWASA kuchukua hatua za haraka, huku akiwakumbusha wananchi kutumia kituo chao cha huduma kwa wateja kupitia namba 181 inayopatikana bure saa 24.
Ameongeza kuwa DAWASA itaendelea kushirikiana kwa karibu na wanawake pamoja na jamii kwa ujumla katika kuboresha miundombinu na kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya majisafi na salama bila kikwazo.
Naye mmoja wa wakazi wa eneo hilo, Swaumu Kinindi, ameishukuru DAWASA kwa kuwafikia wananchi na kuwapatia elimu, akieleza kuwa elimu hiyo imemsaidia kupata ufafanuzi wa kutosha kuhusu mfumo wa bili za maji na namna ya kuhifadhi rasilimali hiyo. -
Jambo TV
@Jambotv_
MASHAHIDI WANASEMA ULIKUSUDIA KUITISHA SERIKALI/ JAMHURI YATAJA SABABU ZA LISSU… jambo.co.tz/mashahidi-wanasema-ulikusudia-kuitisha-serika… via @jambotv_
-
Jambo TV
@Jambotv_
SINA KESI YA KUJIBU SABABU NI HIZI/ LISSU ASISITIZA FIDIA jambo.co.tz/sina-kesi-ya-kujibu-sababu-ni-hizi-lissu-asis… via @jambotv_
-
Jambo TV
@Jambotv_
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Tundu Lissu ameieleza Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo Dar es Salaam kuwa hana kesi ya kujibu katika shauri la uhaini linalomkabili huku akiiomba mahakama kutamka kuwa hana hatia na itamke kuwa anatakiwa kulipwa fidia.
Akiwasilisha hoja zake leo Agosti 17, 2026 mbele ya jopo la Majaji watatu wakiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru Lissu akitumia kifungu cha 312(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai(CPA) amesema upande wa Jamhuri umeshindwa kuthibitisha ile aliyoiita Prima facie case (kutokuwa na kesi ya kujibu).
Lissu ameieleza Mahakama kuwa kuwa Prima facie evidence/case ni ushahidi wa upande wa mashtaka pekee yake kama haujafikia kiwango cha kumtia mtuhumiwa hatiani usipojibiwa hakuna hatia na Mahakama inatakiwa kurekodi mtuhumiwa kutokua na hatia.
Akitumia kifungu cha 312(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai na maamuzi ya Mahakama katika kesi kadhaa ikiwemo ya kesi ya Rambaklal Trambaklal Bhatt dhidi ya Jamhuri amesema zimetengeneza misingi ya kisheria juu ya kitu gani mahakama inatakiwa kufanya kuhusiana na hoja ya kutokuwa na kesi ya kujibu.
Sababu ziliaoainishwa na mahakama hizo ni kuwa ni utiifu wa Jamhuri ya Muungano, lazima kuwe na uthibitisho wa nia ya kufanya kitendo cha uhaini na hiyo nia lazima ithibitishwe kwa maandishi au matendo ya wazi.
Anaeleza kuwa suala la utiifu kwa Jamhuri ya Muungano halina mjadala na suala lenye shida ni je kulikuwa na nia ya dhati ya kufanya uhaini akieleza kuwa katika maneno yaliyoandikwa kwenye hati ya mashtaka ambayo aliyatoa April 3, 2025 na pia kupitia ushahidi wa mashahidi 17 wa jamhuri hakuna sehemu alipoonyesha nia ya kuitisha serikali kwani hakuna sehemu ilipotamkwa.
Lissu anasema kwa mujibu wa Sheria ya Uchaguzi wa Rais Wabunge na Madiwani ya mwaka 2023, Sheria ya Kanuni ya Adhabu na sheria zingine hazithibitishi kosa la uhaini analodaiwa kulifanya.
Soma zaidi kwenye website yetu ya www.jambo.co.tz -
Jambo TV
@Jambotv_
Ushahidi upande wa Jamhuri kwenye kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Tundu Lissu umefungwa rasmi leo Agosti 17, 2026.
Majira ya saa nne kamili katika Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo Dar es Salaam kesi hiyo ilianza ambapo upande wa Jamhuri kupitia Wakili wa Serikali Mkuu Nassoro Katuga aliwasilisha taatifa ya maombi ya kuufunga ushahidi huo akieleza kuwa wanaona mashahidi ambao mpaka sasa wametoa ushahidi kwa upande wao wanatosha.
Akiwasilisha maombi hayo mbele ya Jopo la Majaji watatu wakiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru Wakili Katuga amesema “Waheshimiwa Majaji wa Mahakama Kuu kuwa upande wa Jamhuri baada ya kupitia ushahidi ambao tayari umewasilisha mahakamani na kuangalia ushahidi uliobakiwa kwa maana mashahidi waliobaki tumeuchambua na kuangalia hoja zilizokubaliwa upande wa jamhuri ukajikuta kwamba unaona ushahidi ambao tayari umeshautoa ni ushahidi toshelezi na kuleta ushahidi zaidi kuthibitisha hoja ambazo zilikubaliwa wakati wa hoja za awali(Preliminary hearing)ni kinyume cha sheria.” Amesema Katuga
“Hivyo basi tunafurahishwa kuitaarifu mahakama hii tukufu kwamba upande wa jamhuri umefunga ushahidi wake kwa mashahidi hao 17.” aliongeza Katuga
Lissu alieleza mahakama kuwa hana shida na hoja hiyo huku Majaji wakikubaliana na hoja hiyo, kwa sasa kesi inaendelea tutakuletea habari kamili za mwenendo wa leo utaipata baadae.
Ikumbukwe katika kesi hii Jamhuri ilikuwa na jumla ya mashahidi 30 lakini hata hivyo ilishaeleza haitalazimika kutumia mashahidi wote bali itatumia wale ambao itaona wanatosha kukamilisha ushahidi wao. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Wananchi wa Kata ya Msingi, Wilaya ya Mkalama mkoani Singida, wamepata matumaini ya kupata ufumbuzi wa changamoto ya maji baada ya Mbunge wa Iramba Mashariki, Jesca David Kishoa, kuwasiliana moja kwa moja na Waziri wa Maji, Juma Aweso, wakati wa mkutano wa hadhara jimboni humo.
Wananchi walimweleza Mbunge huyo adha wanayoipata kutokana na ukosefu wa maji na kumuomba achukue hatua za haraka ili changamoto hiyo iweze kutatuliwa.
Akizungumza kwa njia ya simu, Agosti 16, 2026 Waziri Aweso amepokea malalamiko hayo na kuahidi kutuma wataalamu wa maji wilayani Mkalama kesho, kwa ajili ya kufuatilia hali hiyo, kubaini chanzo cha changamoto na kuangalia hatua zinazopaswa kuchukuliwa.
Hatua hiyo imewapa wananchi matumaini ya kuona changamoto hiyo ikianza kushughulikiwa, huku wakisubiri ujio wa wataalamu hao na matokeo ya uchunguzi wao.
Katika mkutano huo, Mbunge Kishoa pia ametoa mifuko 200 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya cha Msingi, hatua inayolenga kusaidia kuboresha huduma za afya kwa wananchi wa eneo hilo.
Kwa sasa, macho ya wananchi yako kwa ujio wa wataalamu wa maji, huku wakitarajia uchunguzi huo utakaofanyika kesho utoe majibu na hatua za kupata suluhisho la kudumu la changamoto ya maji.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI PICHA:
Wafanyakazi wa Wakala wa Vipimo (WMA) kutoka Makao Makuu jijini Dodoma na Mkoa wa Dar es Salaam, wameshiriki katika mbio za CRDB Bank Marathon 2026 zilizofanyika jijini Dar es Salaam, wakijumuika na maelfu ya washiriki wengine katika kuhamasisha mtindo bora wa maisha na afya.
Mbio hizo kubwa zilihudhuriwa na Mgeni Rasmi, Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla, zikiwa na azma kuu ya kuhamasisha jamii kujenga utamaduni wa kufanya mazoezi na kulinda afya.
Ushiriki huo wa WMA unalenga kuunga mkono kwa vitendo jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, anayeendelea kuhamasisha wananchi kufanya mazoezi mara kwa mara ili kujikinga na magonjwa yasiyo ya kuambukiza, kuimarisha afya za miili na akili, pamoja na kuongeza ufanisi na uchangamfu katika majukumu ya kila siku.
Kufuatia ushirikiano huo, watumishi walioshiriki mbio hizo wametoa shukrani za dhati kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa WMA, Bw. Alban Kihulla, kwa kuwajali na kuwawezesha kushiriki kikamilifu katika CRDB Bank Marathon 2026.
Watumishi hao wamebainisha kuwa fursa hiyo imewapa hamasa kubwa ya kuendeleza utamaduni wa mazoezi katika maisha yao ya kila siku ili kuongeza tija na ufanisi wanapotekeleza majukumu yao ya kiutendaji. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, amesema ajenda ya Katiba Mpya si ya vyama vya upinzani bali ni ajenda ya msingi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), iliyoanzishwa tangu awamu ya nne ya Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na kuendelezwa kwa kasi katika awamu ya sita ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Akizungumza jana katika Kijiji cha Kangagani, Mkoa wa Kaskazini Pemba, alipomwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika hafla ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Shule ya Amali inayogharimu Shilingi bilioni 4, Katambi amebainisha kuwa mchakato huo wa mabadiliko ya Katiba tayari umejumuishwa rasmi katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM na hatua za utekelezaji wake zimeshaanza.
Waziri Katambi amekosoa vyama vya upinzani kwa kudai kuwa ndivyo vilivyokwamisha mchakato huo wa Katiba katika awamu za nyuma kwa kuweka mbele maslahi binafsi ya kisiasa.
Amesisitiza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan itaendelea kutekeleza kwa dhati ahadi zote zilizomo katika ilani ya CCM, ikiwemo kukamilisha mchakato wa Katiba Mpya kwa maslahi mapana ya wananchi na Taifa kwa ujumla.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Wakili kutoka Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Paul Kisabo, ametoa wito wa mshikamano kwa mawakili wote nchini kufuatia kuendelea kushikiliwa kwa Wakili Peter Madeleka, akisisitiza kuwa hatua hiyo ni shambulio la moja kwa moja dhidi ya taaluma ya sheria.
Kisabo ameyasema hayo Agosti 16, 2026, wakati akizungumza na Jambo TV mara baada ya kumtembelea Madeleka katika Kituo Kikuu cha Polisi (Central) jijini Dar es Salaam. Madeleka alikamatwa Agosti 14, 2026, majira ya saa 9:30 alasiri katika viunga vya Mahakama ya Uhujumu Uchumi iliyopo Mikocheni akiwa anatekeleza majukumu yake ya kitaaluma.
Ingawa Jeshi la Polisi linadai Madeleka anashikiliwa kwa tuhuma za kudharau amri za Mahakama Kuu zilizotolewa tarehe 27 Julai na 13 Agosti 2026, Kisabo amebainisha kuwa mteja wake hatambui amri yoyote ya aina hiyo anayotuhumiwa kuikiuka.
Katika maelezo yake, Kisabo amehoji utaratibu uliotumika kumkamata wakili huyo akiwa katika viunga vya mahakama akitekeleza majukumu yake badala ya kumtumia wito wa kawaida wa polisi, huku pia akiibua hoja nzito ya kisheria kuhusu uwezekano wa mgongano wa kimaslahi.
Pamoja na Polisi kuahidi kutoa dhamana kesho Jumatatu saa 3:00 asubuhi, Kisabo amekosoa kitendo cha kuendelea kumshikilia Madeleka kwa zaidi ya saa 24 bila dhamana, akibainisha kuwa hatua hiyo inakiuka kanuni ya msingi ya kisheria inayotaka kila mtu kuonekana hana hatia mpaka ithibitike vinginevyo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Kwa miaka mingi, wakazi wa Bangulo na Pugu Stesheni wilayani Ilala mkoani Dar es Salaam wamekuwa wakiishi kwa hofu na wasiwasi wa kuitwa "wavamizi" kwenye ardhi wanayoishi, hali iliyowafanya washindwe kupata hati miliki za maeneo yao kutokana na eneo hilo kutambuliwa kisheria kama Shamba la Mifugo la Kabimita (Hati Na. 4873) la Wizara ya Mifugo.
Katika mkutano wa hadhara uliofanyika Jumapili Agosti 16, 2026, wananchi wamdeleza kiu yao ya kutaka kutambuliwa kihalali ili waweze kuendeleza maisha yao bila ukakasi wa kisheria. Mmoja wa wakazi hao alitumia mfano wa ndoa kuelezea hali hiyo akisema: “Unajua unapoenda kuoa, unaenda kufunga ndoa halafu unaambiwa kwamba huyu mwanamke ni wa John halafu nawe unaitwa Luka, lazima kuwe na ukakasi. Ila mimi nilikuwa naomba kwa mkuu wa wilaya na Rais kwa ujumla angetutolea tamko la kutufutia hii hati... ikaingizwa hati ya Watanzania ya wananchi wa Bangulo”.
Akijibu ombi hilo, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo amethibitisha kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesikia kilio chao na ameridhia kufutwa kwa hati hiyo ya wizara ili kuwapa wananchi haki ya kumiliki ardhi
“Kwa dhati kabisa, tunamshukuru Rais wetu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan. Uamuzi wake wa kufuta Hati Na. 4873 ya Wizara ya Mifugo, iliyokuwa ikifahamika kama Shamba la Mifugo la Kabimita, ni uamuzi mkubwa kwa wananchi wa Bangulo. Tunauona kama ishara ya upendo wake kwa wananchi na dhamira yake ya kuhakikisha wananchi wanapata fursa ya kumiliki ardhi yao kihalali,” amesema Mpogolo.
Amesema hatua hiyo imeondoa kikwazo kikubwa na sasa wananchi wanapaswa kutumia fursa hiyo kwa kukamilisha taratibu za upimaji, urasimishaji na upatikanaji wa hati miliki ili waweze kuwa wamiliki halali wa ardhi wanayoishi.
Mpogolo amesema eneo hilo, linalohusisha Bangulo na Pugu Stesheni, lina maelfu ya wananchi na zaidi ya kaya 10,000, ambao wamekuwa wakihitaji maeneo yao kupimwa na kurasimishwa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekanusha vikali tuhuma zilizotolewa na mgombea urais nchini Zambia kupitia chama cha upinzani cha National Reconciliation Party for Unity and Prosperity (NRPUP), Brian Mundubile, aliyedai kuwa Tanzania imetuma raia wake kuingilia na kuvuruga Uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo uliofanyika Agosti 13, 2026.
Taarifa rasmi iliyotolewa leo, Jumapili Agosti 16, 2026, na Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania, Gerson Msigwa imeeleza kuwa Serikali imechukulia kwa uzito mkubwa tuhuma hizo na tayari kupitia Ubalozi wa Tanzania nchini Zambia imeiandikia barua Serikali ya Zambia kutaka maelezo ya kwa nini mgombea huyo amezusha tuhuma zisizo na ukweli.
Msigwa amesisitiza kuwa Serikali ya Tanzania inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inawahakikishia Watanzania na Jumuiya ya Kimataifa kuwa haijatuma mtu yeyote kuingilia mchakato wa uchaguzi nchini Zambia, kwani kufanya hivyo ni kinyume kabisa na misingi na utamaduni wa diplomasia ya nchi.
“Serikali ya Tanzania haijamtuma mtu yeyote kwenda Zambia kuingilia uchaguzi wa nchini humo na hiyo si desturi yetu,” amesema Msigwa.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa, kama ilivyo kwa nchi nyingine wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), uwepo wa Watanzania nchini Zambia katika kipindi hiki unahusu waangalizi wa uchaguzi pekee wanaotekeleza majukumu yao kwa mujibu wa miongozo rasmi ya SADC na si vinginevyo.
Tuhuma za Mundubile ziliibuka hivi karibuni wakati akizungumza na vyombo vya habari nchini Zambia, ambapo alikilaumu chama tawala cha United Party for National Development (UPND) akidai kuwa kimekodi raia kutoka Tanzania na kutumia mbinu alizoziita "Tanzania formula" ili kupata ushindi katika uchaguzi huo mkuu unaomhusisha pia Rais wa sasa, Hakainde Hichilema.
"UPND hawawezi kushinda uchaguzi huu, hakuna muujiza. Sasa wameamua kutumia Tanzania formula. Zambia si Tanzania. Zambia si Tanzania. Hii ni Zambia," alisema Mundubile wakati akitoa kauli hiyo iliyosambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii.
Katika maelezo yake, Mundubile alidai pia kuwa kuna raia wa Tanzania walioajiriwa kuingilia mchakato huo na kuwataka waondoke nchini humo, ingawa hakutaja majina ya watu hao wala kutoa ushahidi wowote wa kuonesha ni kazi gani wanazofanya au nani aliyewaajiri.
Kauli hiyo ya Mundubile imekuja kufuatia mvutano wa kisiasa unaoendelea nchini Zambia baada ya Uchaguzi Mkuu wa Agosti 13, 2026, ambapo Tume ya Uchaguzi nchini humo (ECZ) ililazimika kusitisha kwa muda zoezi la kuhesabu kura kufuatia matukio ya ghasia yaliyowalenga baadhi ya maofisa wa uchaguzi katika baadhi ya maeneo. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Meli kongwe na ya kihistoria ya MV Liemba iko tayari kuhudumu kwa zaidi ya miaka 60 ijayo kufuatia kukamilika kwa ukarabati wake mkubwa uliogharimu zaidi ya Shilingi bilioni 34, uliohusisha kubadilishwa kwa mitambo yote ya ndani na injini.
Kukamilika kwa mradi huo kutawezesha meli hiyo kuanza rasmi safari zake za kibiashara kuanzia Septemba 1, 2026, hatua inayotarajiwa kufungua fursa kubwa za kiuchumi kwa wakazi wa mikoa ya Kigoma, Katavi, Rukwa, pamoja na nchi jirani ya Zambia.
Akizungumza mkoani Kigoma Agosti 15, 2026, wakati wa shughuli ya safari ya kwanza ya majaribio ya kiufundi, Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa, amebainisha kuwa ujasiri na maamuzi ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ndivyo vilivyofanikisha kukamilika kwa mradi huo kufuatia kukwama kwa jitihada za ukarabati mara kadhaa tangu mwaka 2016.
"Kila kitu ndani ya meli hii kimebadilishwa kuanzia mitambo, injini na majenereta. Tunaamini ukarabati huu sasa utaifanya meli hii ya kihistoria iliyojengwa mwaka 1913 kudumu tena kwa zaidi ya miaka 60. Mheshimiwa Rais anaenda kuacha tabasamu kubwa kwa wananchi," amesema Profesa Mbarawa.
Naye Mkurugenzi wa kampuni ya Dar es Salaam Merchants Group (DMG) iliyopewa dhamana ya kufanya ukarabati huo, Rayton Kwembe, amefafanua kuwa pamoja na kuweka injini mpya, mitambo ya kisasa ya uongozaji, na kuboresha sehemu za abiria, wamefanikiwa kulinda na kuhifadhi kikamilifu muundo na historia ya asili ya meli hiyo iliyojengwa tangu zama za mkoloni.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa, amesema hatishwi na watu wanaojihusisha na kuhamasisha uvuvi usiofuata sheria, akisisitiza kuwa ataendelea kusimamia rasilimali za uvuvi kwa maslahi ya taifa.
Dkt. Bashiru ameyasema hayo Agosti 15, 2026, baada ya kutembelea wawekezaji wa viwanda vya kuchakata samaki jijini Mwanza, ambapo alielezwa changamoto ya upungufu wa malighafi unaotokana na kupungua kwa samaki katika Ziwa Victoria.
Amesema moja ya sababu za changamoto hiyo ni uvuvi usiofuata sheria, huku akieleza kuwa Wizara imeunda kikosi maalum kinachotoa elimu kwa vitendo na kufanya utafiti kubaini chanzo na mizizi ya tatizo hilo.
Kwa mujibu wa Dkt. Bashiru, hatua za awali za utafiti zimebaini kuwa baadhi ya watu wanaendelea na uvuvi haramu kwa kupata kinga kutoka kwa baadhi ya wanasiasa.
“Tumekubaliana na mwekezaji tutatue tatizo la malighafi na hali ni mbaya sana. Nilivyojaribisha kidogo kutengeneza kikosi kwa msaada wa Mheshimiwa Rais ambacho kitapita kutoa elimu kwa vitendo na kufanya utafiti wa vyanzo na mizizi ya tatizo hili, kwa hiyo niwatahadharishe waliozoea na ninawajua wote kwa majina. Wengine wanajifanya wanauswahiba na viongozi wa kisiasa, sitishwi, niacheni nifanye kazi ya Mheshimiwa Rais,” amesema Dkt. Bashiru.
Amesema pamoja na juhudi zinazoendelea za kukabiliana na uvuvi haramu, bado baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakitetea vitendo hivyo.
Aidha, amesema Wizara ipo katika hatua za kukamilisha kanuni zitakazodhibiti uvuvi wa samaki walio chini ya kiwango, huku akisisitiza kuwa Wizara itasimamia utekelezaji wa hatua hizo ili kukomesha tatizo hilo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, ametoa onyo kwa watu waliohusika na vurugu za Oktoba 29, 2025 akisisitiza kuwa serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan haitampendelea mtu yeyote katika kutoa haki.
Akizungumza jana katika Kijiji cha Kangagani, Kaskazini Pemba, alipomwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuweka jiwe la msingi la Skuli ya Amali inayojengwa kwa gharama ya Shilingi bilioni 4, Waziri Katambi ametolea ufafanuzi juu ya tume zilizoundwa na Rais kuchunguza vurugu zilizotokea baada ya uchaguzi wa Oktoba 29. Amebainisha kuwa kuundwa kwa tume hizo ni hitaji la sheria za kitaifa na kimataifa ili nchi ianze kuchukua hatua yenyewe
Waziri Katambi ameeleza kuwa baada ya Tume ya Jaji Chande kukamilisha kazi ya kutafuta ukweli, sasa Tume ya Jaji Lila imeanza kazi ya kushughulikia masuala ya kijinai. Katika kusisitiza msimamo wa serikali kuhusu usawa mbele ya sheria, Waziri Katambi amesema,
“Ndugu zangu Watanzania niwaambie na niwahakikishie serikali iko very serious na jambo hili. Hatutapendelea mtu, hata kama ni Katambi anahusika atawajibika. Sheria ni msumeno. Yeyote ambaye anahusika... awe kiongozi wa serikali, awe ni kiongozi mtu binafsi, awe yoyote, awe ni raia aliyehusika katika changamoto hizo tulizokwenda kuzipata, atawajibika kwa mujibu wa sheria”This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Waangalizi wa kimataifa wa Uchaguzi Mkuu nchini Zambia, wakiwamo kutoka Umoja wa Ulaya (EU) na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), wameonyesha wasiwasi mkubwa kufuatia taarifa za matukio ya vurugu, utekaji, na kusimamishwa kwa muda kwa zoezi la kuhesabu kura.
Hatua hiyo inakuja baada ya Tume ya Uchaguzi ya Zambia (ECZ) kusitisha kwa saa kadhaa zoezi la kuhesabu kura siku ya Ijumaa kufuatia mashambulizi dhidi ya makatibu wa vituo na madai ya kuibiwa kwa karatasi za kura, kabla ya kurejesha tena zoezi hilo baada ya kueleza kuwa ulinzi umeimarishwa.
Kinyang'anyiro hicho kinamkutanisha Rais aliyepo madarakani, Hakainde Hichilema (64) wa chama tawala cha United Party for National Development (UPND), anayewania muhula wa pili, dhidi ya mpinzani wake mkuu, Brian Mundubile (55), aliyekuwa waziri wa zamani kupitia chama cha Patriotic Front (PF) na sasa anagombea kupitia muungano wa National Reconciliation Party for Unity and Prosperity (NRPUP).
Mundubile amekosoa vikali uamuzi wa kusimamisha kuhesabu kura akisema unaleta shaka ya kuwepo kwa "mchezo mchafu wa kubadili matokeo." Hata hivyo, Mkurugenzi wa Habari wa Kampeni za Hichilema, Mark Simuuwe, ameyakataa madai hayo na kusema upinzani unateswa na hofu kwasababu matokeo ni halali.
Kiongozi wa Timu ya Waangalizi wa SADC, Samuel Tembenu (aliyekuwa Waziri wa Sheria wa Malawi), ameeleza kuwa timu yake haikuweza kushuhudia uhesabuji wa kura wakati wa sitisho hilo, huku akibainisha kupokea ripoti za kujeruhiwa kwa watu, uharibifu wa mali, utekaji, na kifo cha msimamizi mmoja wa kura:
"Kusitishwa kwa zoezi hilo kumeleta taharuki na wasiwasi mkubwa. Tumepokea taarifa za vitendo vya vitisho, utekaji na angalau kifo cha mtu mmoja katika mikoa mitano, ingawa bado tunajiridhisha kwa kina. Tunasihi pande zote zitulie," aMEsema Tembenu.
Naye Mkuu wa Waangalizi wa Umoja wa Ulaya (EU), Michael McNamara, na Mkuu wa Ujumbe wa Bunge la Ulaya, Reinhold Lopatka, wametoa wito kwa serikali kutoa maelezo ya kina kuhusu uamuzi huo wa kusimamisha kura ambao wameutaja kama "usio na uwiano" kwa kuwa ni vituo vichache tu kati ya zaidi ya 13,000 vilivyoathirika na vurugu.
Jeshi la Polisi nchini Zambia limethibitisha kuwakamata watu 9 wakituhumiwa kuhusika na mauaji ya msimamizi wa kura mwenye umri wa miaka 57 katika mji mmoja karibu na Lusaka.
Hadi kufikia mwishoni mwa Jumamosi, Tume ya Uchaguzi (ECZ) ilikuwa imetangaza matokeo ya awali kutoka majimbo 49 kati ya 226, ambapo matokeo hayo yasiyo ya mwisho yanaonesha kuwa Hakainde Hichilema (UPND) alikuwa na kura 438,708 (Sawa na 52.6%), Brian Mundubile (NRPUP): Kura 351,281 (Sawa na 42.1%), na Kelvin Bwalya (ZMBP): Kura 3,965.
Mundubile tayari ametangaza ushindi akitaja matokeo ya kituo chake cha majumuisho na kudai jeshi limeingilia vituo vya majumuisho vya Mufulira. Hichilema hajaandika ushindi lakini amesema takwimu za mwanzo "zinatoa matumaini makubwa."
Hali ya usalama imezidi kuimarishwa katika mji mkuu wa Lusaka, ambapo askari wa jeshi na polisi wakiwa na magari ya kivita wametanda mtaani, huku Tume ya Uchaguzi ikitarajiwa kutoa taarifa zaidi kuhusu muda rasmi wa kutangaza matokeo ya mwisho. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Aggrey Mwanri, ameweka wazi kuwa sifa anazopewa Mbunge wa Ubungo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, si za upendeleo bali zinatokana na uwezo wake mkubwa wa kiutendaji na kifikra.
Akizungumza leo katika mkutano wa hadhara wa kuelezea utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM (Novemba 2025- Julai 2026) jimboni humo, Mwanri amebainisha kuwa Prof. Kitila amepewa heshima kubwa ya kuratibu mipango ya maendeleo ya taifa zima kabla ya mambo mengine kufuata
Mwanri amefafanua kuwa dunia haiongozwi na watu tu, bali inaongozwa na mawazo yanayotoka kwa watu wenye uwezo. Ametumia mfano wa ‘vyombo’ kuelezea kwa nini Ubungo inapata maendeleo makubwa, akilinganisha uwezo wa Prof. Kitila na chombo kikubwa cha kuhifadhia maji (Simtank).
Aidha, Mwanri alionya kuwa familia au jamii isiyo na mawazo na mipango madhubuti hukumbwa na vurugu na kukosa mwelekeo, akisisitiza kuwa Prof. Kitila amekuwa chanzo cha ‘mabubujiko ya mawazo’ yanayoliletea taifa na jimbo la Ubungo tija.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) anayeshughulikia Oganaizesheni, Paulo Chacha, amesema CCM imejijengea msingi imara wa kisiasa unaoiwezesha kuendelea kushinda uchaguzi katika ngazi mbalimbali za uongozi nchini, huku ikijiwekea lengo la kuendelea kuongoza dola kwa miaka 100 ijayo.
Chacha ametoa kauli hiyo mkoani Tabora wakati wa hafla ya kumuaga na kumpongeza kwa kuanza majukumu yake mapya ya uongozi, ambapo amesema hadi sasa hakuna Chama cha siasa chenye uwezo wa kuiondoa CCM madarakani.
"Bado chama cha kuitoa CCM madarakani hakijazaliwa. Hivi vilivyopo tayari vimeshindwa, vingine vinaendelea kuanzishwa," amesema Chacha.
Aidha, amesema hata baada ya CCM kutimiza miaka 100 ya uongozi, chama hicho kitaendelea kujiwekea malengo ya kuongoza kwa kipindi kingine cha miaka 100, akieleza kuwa mafanikio hayo yanatokana na misingi imara ya chama, ikiwemo kuwa na wanachama wengi na wenye ushiriki hai katika shughuli za kisiasa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Aggrey Mwanri, amemmwagia sifa kedekede Mbunge wa Ubungo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, kwa namna anavyotekeleza ahadi za chama hicho kwa vitendo.
Akizungumza leo wilayani Ubungo mkoani Dar es Salaam katika mkutano wa hadhara wa kuelezea utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa kipindi cha Novemba 2025 hadi Julai 2026 jimboni humo, Mwanri amesema Prof. Kitila ni miongoni mwa wabunge mfano wanaotafsiri kwa uhalisia kile kilichoahidiwa wakati wa kutafuta kura
Mwanri ametumia mfano wa ‘mpishi’ kuelezea nafasi ya Prof. Kitila katika maendeleo ya Ubungo, akibainisha kuwa mbunge huyo alishiriki kikamilifu katika uandaaji wa ilani ya chama.
Mwanri ameeleza kuwa amevutiwa sana na kiwango cha mafanikio yaliyowasilishwa na Prof. Mkumbo kiasi cha kuandika maelezo mengi ya kumbukumbu. Amesisitiza kuwa utendaji wa namna hiyo ndio unaofanya wananchi waendelee kukiamini na kukiashiria Chama Cha Mapinduzi kuwa ni chama cha watu wanaotekeleza ahadi zao.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mbunge wa Jimbo la Ubungo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, ameeleza kuwa uhai na ukuaji wa bandari unaratibiwa na takwimu za kisayansi za utendaji wala sio maneno ya kisiasa, ikiwa ni majibu ya moja kwa moja kwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Heche, aliyedai kuwa Bandari ya Dar es Salaam inaelekea kufa.
Akizungumza leo katika mkutano wa hadhara wa kuelezea utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa kipindi cha kuanzia Novemba 2025 hadi Julai 2026 jimboni humo, Prof. Kitila amesisitiza kuwa kazi kuu ya bandari ni kupakia na kupakua mizigo na hapo ndipo kipimo cha utendaji wake kinapofanyika.
“Nataka nimuoneshe kwamba kipimo cha bandari kukua ama kufa ni sayansi. Na unaangalia vitu vingi lakini vitu vikubwa sana viwili. Unaangalia je bandari yako inaendelea kutumika? Kazi ya bandari ni kupakia na kupakua mizigo,” amesema Prof. Kitila
Katika kufafanua ukuaji huo kwa takwimu, Prof. Kitila amebainisha ongezeko kubwa la shehena ya mizigo inayopita katika bandari za Tanzania, ambapo katika mwaka wa fedha wa 2021/22 uwezo wa kuhudumia mizigo ulikuwa tani milioni 20.78, lakini kufikia Machi mwaka huu kiwango hicho kimeongezeka maradufu na kufikia tani milioni 39.90.
Prof. Kitila ameeleza kuwa kuingia kwa mwekezaji DP World kumeongeza ufanisi mkubwa katika uendeshaji na kushusha muda wa kushusha mizigo kutoka kwenye meli kwa kiwango cha juu mno.
Ufanisi huo umeiwezesha Bandari ya Dar es Salaam kuingia katika orodha ya bandari 10 bora Barani Afrika kwa kushika nafasi ya saba, huku Prof. Kitila akiwahakikishia wananchi kuwa kuimarika huko kumesababisha kuongezeka kwa mapato ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kupunguza utegemezi wa misaada, na kuilazimu Serikali kujipanga kupanua barabara ili kukidhi ongezeko la malori yanayosafirisha mizigo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI PICHA
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mussa Azzan Zungu (Mb), amekutana na kufanya Mazungumzo na Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) ikiwa na lengo la kupokea na kujadili mipango ya uboreshaji huduma za Maji katika Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani inayosimamiwa na DAWASA.
Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi Ndogo ya Bunge, Jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe Edward Mpogolo na Mbunge wa Kinononi, Mhe Abbasi Tarimba.
Katika mazungumzo hayo Zungu ameitaka DAWASA kuongeza kasi ya ukamilishaji wa miradi ya kimkakati itakayosaidia kupunguza changamoto za kihuduma na kuimarisha huduma.
“DAWASA ni Taasisi muhimu katika ustawi wa Jamii, najua uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali katika sekta ya Maji Mkoani Dar es salaam na Pwani na hata sasa kiasi kikubwa cha fedha zaidi ya Bilioni 335 zinawekezwa katika Bwawa la Kidunda ili kuongeza upatikanaji wa Maji. Hivyo niwatake bodi kuendelea kuisimamia vyema Managementi ili malengo ya Serikali yafikiwe” alisisitiza Zungu
Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi DAWASA, Mhandisi Romanus Mwangingo amemshukuru Mheshimiwa Zungu kwa kuendelea kutoa mawazo chanya kwa Mamlaka ambayo yataboresha ufanisi na kuimarisha huduma za Maji ndani ya eneo la kihuduma DAWASA. -
Jambo TV
@Jambotv_
Zaidi ya Watanzania 600 wanatarajiwa kupata ajira za moja kwa moja kupitia mradi mkubwa wa uchimbaji na uchakataji wa madini ya kinywe mkoani Morogoro, kufuatia uwekezaji wa Dola za Marekani milioni 100 (takribani Shilingi bilioni 265) uliofanywa na Kampuni ya Henan Yudi Mining kutoka nchini China.
Makubaliano ya mradi huo yamefikiwa leo Agosti 15, 2026, mkoani Morogoro wakati wa hafla ya utiaji saini wa Mkataba wa Ubia wa Uchimbaji wa Madini ya Kinywe kati ya Serikali na kampuni hiyo, ambapo mradi huo utakuwa na uwezo wa kuchakata tani milioni moja za kinywe kwa mwaka na kuzalisha tani 50,000 kwa mwaka mara uzalishaji kamili utakapokamilika.
Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde, ameeleza kuwa mradi huo una mashapo yaliyothibitishwa ya takribani tani milioni 104.28 za kinywe, huku akibainisha kuwa ndani ya miaka minne Sekta ya Madini imefanikiwa kuvutia uwekezaji wa Shilingi trilioni 9 na kuifanya Tanzania kuwa kinara wa uwekezaji wa madini Barani Afrika.
“Mradi huu ni mradi wa shilingi bilioni 265, ni mradi mkubwa ambao utakwenda kuchochea maendeleo katika eneo letu. Mradi huu utazalisha madini kinywe ambayo ndio graphite ya tani 50 kwa mwaka na utakuwa una uwezo wa kuchakata zaidi ya tani milioni moja kwa mwaka”, ameeleza Mavunde.
Mavunde amesema kupitia mkataba huo wa 14 wa msingi kusainiwa nchini, Serikali inamiliki asilimia 17 ya hisa ili kuhakikisha inakuwa mshiriki wa moja kwa moja wa thamani inayozalishwa badala ya kuwa mwenyeji pekee, hatua inayosaidia Tanzania kushiriki kikamilifu katika mnyororo wa thamani wa kinywe duniani kinachotumika kutengeneza anode za betri za teknolojia za kisasa.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Timu ya Majadiliano ya Serikali (GNT), Profesa Sifuni Mchome, amesema Serikali itaendelea kusimamia kwa karibu utekelezaji wa mradi huo ili kuhakikisha Watanzania wanapata manufaa yote stahiki yaliyokusudiwa kupitia umiliki huo wa hisa na fursa za ajira.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mussa Kilakala, ameishukuru Serikali kwa kufanikisha mradi huo utakaofungua fursa nyingi za kiuchumi, huku akiahidi kuwa mkoa utaweka mazingira rafiki kwa wawekezaji, kuzingatia sheria, na kuhakikisha wananchi wanaozunguka mradi huo wananufaika kikamilifu.
Aidha, Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe. Chen Mingjian, amezipongeza pande zote zilizoshiriki katika majadiliano hayo, akibainisha kuwa China itaendelea kuwa miongoni mwa nchi zinazoongoza kwa uwekezaji wa moja kwa moja nchini Tanzania, na mradi huo utazidi kuimarisha ushirikiano wa muda mrefu na wa kibiashara kati ya mataifa hayo miwili. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mbunge wa Jimbo la Ubungo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, amemjibu Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Heche, akisisitiza kuwa uongozi wa nchi unahitaji mipango na kura za wananchi badala ya maombi ya ‘kupewa’ nchi ili kuijaribu.
Akizungumza leo katika mkutano wa hadhara wa kuelezea utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) jimboni Ubungo mkoani Dar es Salaam kwa kipindi cha Novemba 2025 hadi Julai 2026, Prof. Kitila amerejea kauli ya Heche aliyoitoa hivi karibuni akidai kuwa upinzani ukipewa nchi kwa miaka miwili tu mabadiliko yataonekana.
Prof. Kitila amefafanua kuwa katika mifumo ya kidemokrasia, uongozi haugawiwi kama zawadi bali unatafutwa kupitia ridhaa ya wananchi kwenye sanduku la kura.
“Sasa kuna kiongozi mmoja wa upinzani nimemsikiliza juzi akiongea na vijana wa chama chao... anasema hivi sisi watupe nchi miaka miwili tu waone... Sasa unafikiri nchi unapewa? Huwa inapewa hivyo? Hii nchi uongozi unapatikana kwa kura sio kwa kupewa,” amesema Prof. Kitila kwa msisitizo
Prof. Kitila amebainisha kuwa uongozi ni dhamana nzito inayohitaji mikakati na siyo majaribio. Amesema kuwa CCM kimejikita katika mipango ya maendeleo wakati wapinzani wamebobea katika "kuzodoa".
“Uongozi wa nchi sio uji kwamba kila mtu anataka apewa kuonja... uongozi wa nchi ni mipango, uongozi wa nchi ni mikakati. Uongozi wa nchi ni utawala bora... uongozi kuongoza sio kubobea kwenye kuzodoa. Wewe ukibobea kuzodoa, my friend, kuzodoa kupiga kelele nyingi hiyo inafurahisha,” ameeleza Prof. Kitila
Katika kulinganisha utendaji wa serikali ya CCM na nchi jirani, Prof. Kitila amebainisha kuwa Tanzania inatumia mikopo yake kwa ajili ya miradi ya kimkakati kama SGR, barabara na bandari, tofauti na mataifa mengine yanayokopa ili kulipa mishahara ya watumishi. Amesema hatua hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa mipango ya maendeleo iliyoandaliwa na timu imara ya serikali.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri Mkuu na Jaji mstaafu, Joseph Sinde Warioba, ameelezea kushangazwa na kuumizwa na wimbi jipya la ukamataji wa raia, wakiwemo wasomi, ambao wengine hufunguliwa mashtaka ya ugaidi mara tu wanapopata dhamana katika makosa ya awali.
Akizungumza katika mahojiano maalumu na tovuti ya The Jenerali Ulimwengu Post kuhusu hali ya kisiasa nchini, Jaji Warioba amebainisha kuwa kuna mwelekeo wa mamlaka kutumia sheria za makosa yasiyo na dhamana kama nyenzo ya kutisha wananchi na kuwakosesha haki yao ya uhuru.
Jaji Warioba ametoa mfano wa kesi ya hivi karibuni mkoani Dodoma inayomhusu mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Melkisedeki Kaijage ambaye awali alishtakiwa kwa kosa la uchochezi ambalo kisheria lina dhamana. Alieleza kuwa baada ya mahakama kuridhia kumpa dhamana, mashtaka yalibadilishwa ghafla na kuwa ya ugaidi
Kuhusu mchakato wa maridhiano ya kitaifa, Jaji Warioba ameonya kuwa matumizi ya mashtaka mazito kama ugaidi yanaweza kukwamisha juhudi za kuiponya nchi kufuatia yaliyotokea Oktoba 2025.
Amesema kuwa maridhiano si kazi rahisi na yanahitaji mazingira ya kuaminiana, huku akionesha shaka kama ratiba ya kupata Katiba Mpya ifikapo mwaka 2028 itafikiwa ikiwa hali ya hofu itaendelea kutawala.
CHANZO CHA VIDEO: @the_jenerali_ulimwengu_postThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Jaji mstaafu Joseph Sinde Warioba ameeleza kuwa kwa saa bado anaona kuna mgongano mkubwa wa makundi, hasa vyama vya siasa, ambapo baadhi wanashikilia msimamo wa kutoshiriki kwenye mchakato wa sasa wa maridhiano kwa sababu ya masharti na mazingira yaliyopo.
Akizungumza katika mahojiano maalumu na tovuti ya The Jenerali Ulimwengu Post, Jaji Warioba, amesema kuwa bila kuwekwa kwa mazingira rafiki, hakutakuwa na maridhiano ya kweli.
“Ukiona malumbano yanayotokea hivi hujawa na hakika kwamba wote wale wanaohusika watashiriki na kama kutakuwa na watu ambao hawashiriki hutakuwa na maridhiano tutaendelea na hali kama hii... kwa hiyo unasema kwamba inachofanyika sasa hivi ni kutwanga maji ndani ya kinu,” amesisitiza Jaji Warioba.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI:
Chama cha ACT Wazalendo kimekemea vikali kukamatwa kwa Wakili Peter Madeleka jioni ya Agosti 14, 2026, nje ya Mahakama Kuu, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, akidaiwa kukamatwa kwa kosa la kudharau amri ya Mahakama Kuu.
Katika taarifa iliyotolewa leo, Agosti 15, 2026, na Waziri Mkuu Kivuli wa ACT Wazalendo, Isihaka R. Mchinjita, chama hicho kimesema kukamatwa kwa Wakili Madeleka akiwa katika utekelezaji wa majukumu yake ni tishio kwa uhuru wa kitaaluma wa mawakili na uhuru wa kujieleza.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa mapema jana, baada ya kutoka mahakamani, Madeleka alizungumza na waandishi wa habari kuhusu zuio la Mawakili kuzungumza na Vyombo vya Habari wakiwa nje ya eneo la Mahakama, akidai kuwa halina msingi wa kisheria na kutaka itajwe sheria inayokataza Mawakili kuzungumza na Waandishi wa habari.
Aidha, Chama hicho kimesema Madeleka alihoji mantiki ya Mahakama kuwazuia Mawakili kuzungumza na Vyombo vya Habari wakati Mahakama yenyewe ina chombo cha habari kinachorusha matukio yanayotokea Mahakamani.
ACT Wazalendo imedai tukio hilo ni mwendelezo wa kile ilichokiita mwelekeo wa mihimili ya dola kubana uhuru wa kujieleza na kupata habari.
“ACT Wazalendo tunaona huu ni mwendelezo wa mihimili ya dola kuchukua mwelekeo wa ukandamizaji. Tumeona Serikali ikidhibiti uhuru wa habari, Bunge likidhibiti wabunge, na sasa mahakama ikidhibiti mawakili wanapouhabarisha umma,” taarifa hiyo imesema.
Kupitia taarifa hiyo, Chama cha ACT Wazalendo kimetoa wito kwa Jeshi la Polisi kumwachia huru bila masharti yoyote Wakili Peter Madeleka ili aweze kuendelea kutekeleza majukumu yake. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Jaji mstaafu na aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Joseph Sinde Warioba, ametoa onyo kali kuhusu hali ya usalama na uhuru wa kutoa maoni nchini, akibainisha kuwa sasa hivi Watanzania wanaishi katika hali ya uoga inayozuia ushiriki wao katika masuala muhimu ya kitaifa.
Akizungumza katika mahojiano maalumu na tovuti ya The Jenerali Ulimwengu Post, Jaji Warioba ameeleza kuwa mazingira ya hofu ya kutekwa na kupotea yanazuia wananchi kutoa maoni yao ya kweli juu ya mustakabali wa taifa
Jaji Warioba ameeleza kuwa tofauti na nyakati za nyuma, hivi sasa kuna wasiwasi mkubwa miongoni mwa wananchi wa kawaida kuhusu usalama wao binafsi. Amebainisha kuwa matukio ya watu kupotea yameacha kovu kubwa ambalo linaathiri hata michakato ya kiserikali inayohitaji maoni ya umma.
“Ukichukua wananchi kwa sasa hivi hawana uhuru kama ilivyokuwa, kwamba sasa hivi Watanzania wanaishi kwa uoga, sio kama ilivyokuwa wakati ule, wanaishi kwa uoga wanaishi kwa uoga, wanaogopa kutekwa, kupotea. Kwahiyo unakuta hata haya tunayoyafanya yote hupati maoni ya wananchi wanavyoona kwa sababu wanaogopa,” amesema Jaji Warioba
Kuhusu kuundwa kwa Tume ya Maridhiano, Jaji Warioba ametoa ushauri kuwa suala hilo ni mtambuko na halipaswi kushughulikiwa kama tume za kawaida za Rais ambazo hupewa hadidu za rejea na kuanza kazi bila ushirikishwaji mpana. Amesema ili tume hiyo iaminiwe, ni lazima Rais apate ushauri na mawazo kutoka kwa makundi mbalimbali kabla ya kuiteua.
Amesisitiza kuwa maridhiano ya kweli yanahitaji ushiriki wa watu wengi zaidi, wakiwemo wanasiasa, taasisi za dini, asasi za kiraia na kundi muhimu la vijana, ambao mara nyingi wamekuwa wakionesha hasira zao kupitia maandamano yanayokabiliwa na nguvu ya dola.
Jaji Warioba amesisitiza kwa kusema kuwa bila kutafuta njia ya kuwafanya vijana na raia wengine wajihisi kuwa sehemu ya mazungumzo, itakuwa vigumu kuiponya nchi kufuatia yaliyotokea Oktoba 2025. Amebainisha kuwa mchakato huo unapaswa kuwa kama Tume ya Mabadiliko ya Katiba ili kuleta mwafaka unaokubalika na pande zote.
CHANZO CHA VIDEO: @the_jenerali_ulimwengu_postThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Jaji mstaafu, Joseph Sinde Warioba, amesema kutokana na hali ya sasa nchini kwanini Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu asiachilwe, akisisitiza haja ya kutumia busara za kisiasa ili kumuachilia huru kiongozi huyo wa upinzani ambaye hadi sasa yupo gerezani kwa kesi ya uhaini.
Akizungumza katika mahojiano na Mwandishi wa habari Mwandamizi, Jenerali Ulimwengu, Jaji Warioba ameeleza kuwa changamoto za kisiasa na kisheria mara nyingi zinahitaji maamuzi yenye kuweka mbele maslahi mapana ya umma.
Katika maelezo yake, Mzee Warioba ametolea mfano hatua zilizochukuliwa wakati wa kuzuiliwa kwa Mwenyekiti mstaafu wa CHADEMA, Freeman Mbowe, akibainisha kuwa iliwezekana kufanya mazungumzo na kumtoa ili kuweka uwanja sawa wa majadiliano akisema kwamba hatua kama hizo zinaweza kuchukuliwa dhidi ya Lissu.
Aidha, Jaji Mstaafu Warioba amekumbusha baada ya matukio ya Oktoba 29, 2025, akisema Rais alitumia mamlaka yake kuwaachia huru vijana na watuhumiwa wengine waliokuwa wakikabiliwa na mashtaka ya uhaini mahakamani akisema anaweza kufanya hivyo kwa Lissu.
Amebainisha kuwa maamuzi ya aina hiyo yanachukuliwa kutokana na kutambua hali halisi iliyopo nchini, ambapo nia kuu inakuwa ni kuzuia mivutano zaidi na kutoa fursa kwa taifa kupona majeraha ya kisiasa na kijamii.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Jaji mstaafu na aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Joseph Sinde Warioba, ametoa mtazamo wake wa kitaalamu na kisheria kuhusu hali ya kisiasa nchini, akionya kuwa ratiba ya Serikali ya kupata Katiba Mpya ifikapo mwaka 2028 inaweza isiwe na tija kutokana na uchache wa muda wa utekelezaji.
Akizungumza katika mahojiano maalumu na tovuti ya The Jenerali Ulimwengu Post, Jaji Warioba ameeleza kuwa ingawa Serikali inaonekana kukubali mapendekezo ya Tume ya Jaji Chande ikiwemo kuundwa kwa Tume ya Maridhiano, bado kuna wasiwasi mkubwa ikiwa mchakato huo utahusisha wananchi kikamilifu kulingana na misingi ya kidemokrasia.
Mapendekezo hayo ya Serikali yanalenga kukamilisha mchakato wa Katiba Mpya ifikapo mwaka 2028 ili iweze kutumika katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka 2029 pamoja na Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2030. Hata hivyo, Jaji Warioba amesisitiza kuwa mnyororo wa matukio ya kisheria na kijamii yanayopaswa kufuatwa ili kupata Katiba hiyo ni mrefu na mgumu.
Jaji Warioba amebainisha kuwa mchakato huo unahitaji hatua kadhaa nyeti, ikijumuisha kazi ya kamati ya wataalamu ya kulinganisha rasimu zilizopo, na muhimu zaidi, zoezi la kukusanya maoni ya wananchi nchi nzima.
CHANZO CHA VIDEO: the_jenerali_ulimwengu_postThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkurugenzi wa Taasisi ya Everlasting Legal Aid Foundation (ELAF), Wakili Dkt. Khamis Masoud, ametoa ufafanuzi kufuatia baadhi ya kurasa za mitandao ya kijamii kuchukua vipande vya mahojiano yake na vyombo vya habari na kuyaambatanisha na maneno ya uongo ambayo hakuyatamka.
Dkt. Masoud amebainisha kuwa maudhui hayo ya awali yalichapishwa kwa usahihi na vyombo vya habari, lakini baadaye baadhi ya watu wakayachukua na kuyawekea maelezo yanayodai kimakosa kuwa yeye ni kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kwamba amemshambulia Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, jambo aliloeleza kuwa linapotosha kabisa ukweli.
Akifafanua msimamo wake wa kitaaluma na kiutendaji, Dkt. Masoud amesisitiza kuwa yeye si kada wala mwanachama wa chama chochote cha siasa nchini, na kwamba mahojiano yake yalilenga kutoa mtazamo wa kisheria kuhusu tukio lililokuwa likijadiliwa, pamoja na kukumbusha wajibu wa vyombo vyenye mamlaka kufanya uchunguzi na kutoa majibu kwa wananchi.
Ameeleza kuwa jukumu lake kuu kupitia taasisi ya ELAF ni kushughulikia masuala ya sheria na haki za wananchi, huku akisisitiza kuwa taasisi hiyo haina vita au uadui wowote na Serikali, Jeshi la Polisi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wala chombo kingine chochote cha Dola.
Dkt. Masoud amebainisha kuwa hoja zote wanazozitoa siku zote ni za kitaaluma, kisheria, na kifalsafa, zikiwa na azma ya kujenga amani, umoja, mshikamano wa kitaifa, na kuhakikisha haki za wananchi zinapatikana kulingana na misingi ya sheria za nchi.
Aidha, amekemea tabia ya baadhi ya watu kutumia vipande vya habari au mahojiano kwa kuviongezea maneno yasiyo ya kweli, akieleza kuwa kitendo hicho kinapotosha umma na kutengeneza taswira mbaya tofauti na dhamira halisi ya mhojiwa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imetenga takribani Shilingi bilioni 1.2 kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo kusaidia matibabu ya watoto 300 wenye magonjwa ya moyo nchini, hatua inayolenga kuongeza upatikanaji wa huduma za kibingwa kwa watoto kutoka familia zisizomudu gharama za matibabu.
Mpango huo umehalalishwa kupitia makubaliano rasmi yaliyosainiwa katika makao makuu ya GGML mkoani Geita, kati ya kampuni hiyo na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), kwa uratibu wa taasisi ya Global Medicare ya jijini Dar es Salaam. Katika mkataba huo, GGML itakuwa ikitoa Shilingi milioni 400 kila mwaka kigharimia matibabu ya watoto 100 wenye matatizo ya moyo.
Akizungumza katika hafla ya utiaji saini, Mkurugenzi Mtendaji wa GGML, Ashraf Suryaningrat, ameeleza kuwa uamuzi huo uliafikiwa baada ya tathmini ya kina kuhusu matokeo chanya yaliyopatikana huko nyuma katika kuokoa maisha ya watoto na kuimarisha huduma za afya.
“Tunatazamia ushirikiano wa miaka mitatu. Ni watoto 100 kwa mwaka na takribani Shilingi milioni 400 kwa mwaka. Tunatarajia ushirikiano huu kuwa wa mafanikio na tunatumaini utaendelea hata katika siku zijazo,” amesema Suryaningrat.
Suryaningrat ameongeza kuwa mafanikio hayo ni matokeo ya kazi ya pamoja kati ya GGML, JKCI, na Global Medicare, huku akibainisha kuwa msaada huo utasaidia kwa kiasi kikubwa kurejesha afya za watoto na kuleta matumaini mapya katika familia zao.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo, Dkt. Peter Richard Kisenge, ameishukuru GGML kwa niaba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Wizara ya Afya, akisisitiza kuwa mchango huo utagusa moja kwa moja maisha ya watoto wanaohitaji upasuaji na matibabu ya dharura ya moyo.
“Huu si msaada wa pesa tu. Huu ni msaada unaokwenda kuokoa maisha. Mmeenda kutimiza matumaini ya watoto ambao wanakwenda kujenga Taifa la Tanzania la kesho,” amesema Dkt. Kisenge.
Dkt. Kisenge amebainisha kuwa magonjwa ya moyo kwa watoto yanaendelea kuwa changamoto kubwa nchini, ambapo watoto wengi kutoka Kanda ya Ziwa na maeneo mengine hufika JKCI wakiwa wanahitaji upasuaji au kurekebishwa matundu ya moyo, hivyo msaada huo utakuwa mkombozi mkubwa kwa wazazi wao.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Global Medicare, Abdulmalik Mollel, amesema JKCI imejenga jina kubwa si tu nchini bali pia katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, ambapo imekuwa ikipokea na kutibu wagonjwa kutoka nchi za Zambia, Malawi, Kenya, na Uganda.
Mollel ameipongeza GGML kwa kuonesha mfano bora wa namna sekta binafsi inavyoweza kushirikiana na taasisi za umma katika kuimarisha sekta ya afya, kutoa elimu ya kinga, na kuokoa maisha ya Watanzania. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katika maziko ya kijana Sefu Mussa yaliyofanyika leo Agosti 14,2026 katika eneo la Mrombo jijini Arusha, Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Kipolisi Muriet (OCD) SSP Daudi Mwakalobo amewataka wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa kuhusiana na matukio mbalimbali ya kihalifu.
Akizungumza msibani kwa niaba ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Justin Masejo, Mwakalobo amesema Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa kina kuhusu mazingira ya kifo cha Sefu, kinachodaiwa kuhusisha askari wa Hifadhi ya Ngorongoro, huku akisisitiza kuwa tukio hilo halipaswi kutafsiriwa kama kosa la askari wote.
Amesema Jeshi la Polisi linaendelea kufuatilia kwa karibu taarifa na ushahidi unaohusiana na tukio hilo, na kwamba wote watakaobainika kuhusika watafikishwa katika vyombo vya sheria kwa hatua zaidi.
Aidha, amewataka wananchi, hususan vijana, kuendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi, akisisitiza kuwa ushirikiano huo ni muhimu katika kuhakikisha ukweli unapatikana na haki inatendeka.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, leo tarehe 14 Agosti, 2026, saa 9.30 alasiri, limemkamata Wakili wa Kujitegemea, Peter Madeleka, akiwa katika eneo la Mikocheni B, Kinondoni. Madeleka amekamatwa akiwa katika viunga vya Mahakama ya Uhujumu Uchumi (maarufu kama Mahakama ya Mafisadi) wakati akitekeleza majukumu yake ya kitaaluma.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi ya Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, SACP Jumanne Muliro, Madeleka anashikiliwa na kuhojiwa kwa tuhuma za kudharau amri ya Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi iliyotolewa tarehe 27 Julai, 2026 na tarehe 13 Agosti, 2026.
“Lilimkamata na linamuhoji Peter Madeleka, kwa tuhuma za kudharau amri ya Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi “Mahakama ya Mafisadi” iliyotolewa tarehe 27 Julai, 2026 na 13 Agosti, 2026. Taratibu za kisheria zinatekelezwa ili kumfikisha kwenye mamlaka nyingine za kisheria kwa hatua zaidi”, imeeleza polisi.
Kukamatwa huku kumetokea saa chache baada ya Wakili Madeleka kufanya mkutano na waandishi wa habari akitangaza nia yake ya kufungua kesi kupinga zuio la Msajili wa Mahakama Kuu linalowazuia mawakili kufanya mahojiano na vyombo vya habari mahakamani. Taarifa za awali kutoka kwa Wakili Gideon Mathew zilieleza kuwa wakati wa ukamataji huo, watu waliojitambulisha kama polisi walichukua pia gari la Madeleka, fedha, na nyaraka mbalimbali alizokuwa nazo.
Aidha, Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kilieleza kupokea taarifa hizo kwa masikitiko makubwa kikitoa wito kwa mawakili waliopo Dar es Salaam na maeneo ya jirani kufika Kituo Kikuu cha Polisi (Central Police) ili kutoa msaada wa kisheria na kuhakikisha Wakili Madeleka anapata usaidizi unaostahili
“Chama cha Wanasheria Tanganyika kinaendelea kusimamia na kutetea haki, utu na uhuru wa mawakili katika utekelezaji wa majukumu yao ya kitaaluma kwa mujibu wa sheria,” imeeleza taarifa ya TLS iliyotolewa na Baraza la Uongozi. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Wananchi wa mtaa wa Kiembeni, Kata ya Msangani wilayani Kibaha mkoani Pwani, wameanza kupata matumaini mapya baada ya Serikali leo Agosti 14, 2026, kuanza rasmi utekelezaji wa mpango wa kuchimba kisima kirefu cha maji katika eneo hilo ili kutatua changamoto ya huduma hiyo ya msingi.
Mchakato huo wa uchimbaji wa kisima unalenga kupunguza kero ya muda mrefu ya ukosefu wa maji safi na salama inayowakabili wananchi wa eneo hilo, ambao wamekuwa wakilazimika kusafiri umbali mrefu na kukesha usiku kucha wakitafuta maji.
Akizungumza kwa furaha mara baada ya kushuhudia kuwasili kwa mtambo wa kuchimba kisima katika eneo hilo, mkazi wa Msangani, Neema Rutumo, ameishukuru Serikali kwa hatua hiyo na kueleza kuwa ni mwanzo mzuri wa kurejesha amani na matumaini kwa wananchi, hususan wanawake.
“Mungu awabariki sana, tumechoka kukesha usiku tukitafuta maji, tunaacha vitanda na watoto wamelala, tunakuja kulinda maji. Leo kuona mtambo umefika na tunaanza kuchimbiwa kisima ni jambo la kumshukuru Mungu,” amesema Neema Rutumo.
Kwa upande wa uongozi wa eneo hilo, Diwani wa Kata ya Msangani, Frank Emilian Msimbe, ameishukuru Serikali kwa kuitikia kilio cha wananchi na kuanza kuchukua hatua za haraka za kutatua kero hiyo iliyodumu kwa muda mrefu.
Msimbe amebainisha kuwa ingawa Serikali ina mpango mpana zaidi wa kufikisha miundombinu ya maji katika kata hiyo, hatua ya dharura ya kuchimba kisima kirefu imechukuliwa ili kutoa afua ya haraka na kuwawezesha wananchi wa Kiembeni kuanza kunufaika na huduma hiyo karibu na makazi yao.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
📍ARUSHA - Leo, familia, ndugu, marafiki na Wananchi wengine wameuaga mwili wa kijana Sefu Musa, aliyefariki dunia kufuatia tukio linalodaiwa kutokea Agosti 12, 2026, wakati yeye na wenzake watatu wakielekea Babati, mkoani Manyara, kuhudhuria mazishi ya rafiki yao. Safari hiyo iligeuka kuwa ya kusikitisha baada ya Vijana hao kudaiwa kupotea njia na kujikuta ndani ya eneo la Hifadhi ya Ngorongoro.
Kwa mujibu wa Abdullah Nuru, mmoja wa Vijana walionusurika katika tukio hilo, walipokuwa ndani ya hifadhi walikumbana na adhabu mbalimbali, ikiwemo kulazwa kwenye miiba na kupigwa. Anadai vitendo hivyo vilisababisha hali ya Sefu kuwa mbaya na hatimaye kupoteza maisha.
Leo, Sefu ameagwa na kuzikwa katika Makaburi ya Msikiti yaliyopo Mrombo, jijini Arusha. Jambo TV imezungumza na baadhi ya vijana waliomfahamu Sefu, ambao wamemuelezea kama kijana mwema, mwenye mahusiano mazuri na jamii na aliyefahamika katika mtaa wao.
Wamesema wamepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo chake, huku wakitaka haki itendeke na hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya wote watakaobainika kuhusika na kifo chake.
Hata hivyo, Agosti 13, 2026, Jeshi la Polisi lilieleza kuwa limewashikilia askari watatu kwa ajili ya uchunguzi na mahojiano ya kina kuhusu tukio hilo. Uchunguzi huo unatarajiwa kubaini kwa kina kilichotokea na, iwapo kutabainika makosa, hatua zaidi kuchukuliwa kwa mujibu wa sheria.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limesema kukatika kwa umeme nchini hakusababishwi na hitilafu za kiufundi pekee, bali pia vitendo vya uhalifu vinavyolenga miundombinu ya umeme, hususan ukataji na wizi wa nyaya kwa ajili ya biashara ya chuma chakavu.
Akizungumza jijini Dodoma, Lenin Kiobya, Meneja wa huduma za usalama TANESCO Makao Makuu amesema hujuma hizo huathiri moja kwa moja huduma kwa wananchi na kulilazimu shirika kutumia muda na gharama kubwa kurejesha miundombinu iliyoharibiwa, hali inayochangia wananchi kulilaumu shirika kwa kukatika kwa umeme.
"Unakuta umeme umekatika sio tumepanga sisi ni kwa sababu ya matukio ya uhalifu wananchi wanasema TANESCO wamekata umeme na wanatumia maneno yao mabayambaya" amesema Kiobya
Katika kukabiliana na changamoto hiyo, TANESCO imetoa elimu kwa kamati ya ulinzi na usalama kuanzia ngazi ya kata hadi mkoa kwa lengo la kuhamasisha utunzaji wa miundombinu kwa wananchi pamoja na kuzuia vitendo hivyo vya uhalifu.
Kwa upande wake Kamishna msaidizi wa Polisi (ASP) Fikiri Bakari amemtaka kila polisi kata atoe elimu kwa wananchi ili kupunguza athari ya miundombinu ya umeme.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri Kivuli wa Maliasili, Utalii, Utamaduni na Michezo, wa Chama cha ACT Wazalendo, Emmanuel Ntobi, ametoa wito wa kujiuzulu kwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Ashatu Kijaji na Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Abdul Razaq Badru, kufuatia kifo cha kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Seif Mussa (25), kilichodaiwa kusababishwa na askari wa hifadhi hiyo Agosti 12, 2026.
Ametoa wito huo Agosti 14, 2026 kupitia taarifa rasmi iliyobeba ujumbe kuhusu kulaani vikali ukatili uliokithiri unadaiwa kufanywa na askari wa hifadhi nchini dhidi ya raia.
Hatua hiyo inakuja kufuatia tukio lilitokea Agosti 12, 2026 katika Hifadhi ya Ngorongoro, ambapo vijana watatu walieleza kuwa walipotea njia na kujikuta ndani ya hifadhi hiyo jambo lililopelekea kukamatwa na kupewa adhabu iliyopelea kifo cha mmoja wao.
Hata hiyo kupitia taarifa ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha chini ya Kamanda wake SACP Justine Masejo Agosti 13, 2026, Jeshi hilo lilikiri kupokea taarifa kuwa, kuna watu wawili wanaume wamefikishwa katika Hospitali ya Lutheran Wilayani Karatu na kati ya hao wawili mmoja alikuwa ameshafariki.
Kwa mujibu wa SACP Masejo, uchunguzi wa awali ulibaini aliyekuwa amefikishwa hospitalini akiwa amefariki anaitwa Sefu Mussa (25) Fundi Gereji, Mkazi wa Matejo Jijini Arusha huku mtu wa pili ambaye alikuwa anaendelea kupatiwa matibabu alitambulika kwa jina la Salimu Haji maarufu Chambega, Fundi Gereji na Mkazi wa Makao Mapya Jijini Arusha.
Katika taarifa ya Polisi Arusha ilisema kwamba Jeshi hilo linaendelea na Uchunguzi zaidi wa kuthibitisha taarifa hizo za awali, kwani limeshapata maelezo ya baadhi ya watu ili kusaidia kupata ukweli wa nini kilitokea baada ya kukamatwa na Askari hadi mmoja kufariki dunia na mwingine kuendelea kupatiwa matatibu hospitalini na wa tatu kufanikiwa kurejea Jijini ArushaThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Maafisa wa Jeshi la Polisi mapema leo wamefika katika msiba wa Sefu Mussa, mkazi wa Matejoo jijini Arusha, aliyefariki dunia baada ya kudaiwa kupewa adhabu na askari watatu wa Hifadhi ya Ngorongoro.
Sefu alidaiwa kufariki baada ya yeye na wenzake kupotea njia Aprili 12, 2026, walipokuwa wakielekea Babati kuhudhuria mazishi ya rafiki yao. Inadaiwa walijikuta wakiingia katika eneo la Hifadhi ya Ngorongoro, ambako walikutana na askari hao.
Imeelezwa, kufika kwa maafisa hao msibani kunalenga kutoa pole kwa familia, pamoja na kuimarisha ulinzi na usalama wakati wa mazishi ya Sefu, yanayotarajiwa kufanyika leo, Agosti 14, majira ya saa 10 jioni katika eneo la Mrombo.
Akizungumza kwa uchungu kuhusu kifo cha mwanawe, baba mzazi wa Sefu amesema taarifa hizo zimemuumiza sana, huku akiitaka Serikali kuhakikisha haki inatendeka na wote waliohusika wanachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Wakili wa Kujitegemea, Peter Madeleka, ametangaza nia ya kufungua kesi Mahakamani kupinga zuio lililotolewa na Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, linalowazuia Mawakili kufanya mahojiano na Vyombo vya Habari katika viunga vya Mahakama au kuzungumzia mwenendo wa kesi zinazoendelea.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo, Ijumaa, Agosti 14, 2026, jijini Dar es Salaam, Madeleka ameeleza kuwa anafikia hatua hiyo ya kisheria ili kupata tafsiri rasmi ya Mahakama, akisisitiza kuwa zuio hilo linakiuka wazi Ibara ya 18(b) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayotambua haki ya kupata, kutafuta na kutoa habari.
Msimamo huo wa Madeleka unakuja kufuatia taarifa rasmi iliyotolewa na Msajili wa Mahakama mnamo Agosti 12, 2026, iliyowakumbusha Mawakili wote nchini kuzingatia maelekezo ya Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) na Mahakama Kuu.
Sehemu ya taarifa hiyo ya Msajili wa Mahakama inasema, “Mahakama Kuu ya Tanzania inapenda kuwakumbusha na kuwasisitizia mawakili wote wanaohudhuria mashauri mahakamani, kuzingatia na kuheshimu maelekezo hayo ya TLS na Mahakama, kwa kutofanya mahojiano na vyombo vya habari katika viunga vya Mahakama na kutokuzungumzia mwenendo wa mashauri yanayoendelea mahakamani kwa namna inayoweza kuathiri mwenendo wa mashauri”.
Kwa mujibu wa Madeleka, zuio hilo linapaswa kuangaliwa kwa kuzingatia haki ya kikatiba ya kupata, kutafuta na kutoa habari, jambo analotarajia kulifikisha Mahakamani ili kupata tafsiri kuhusu uhalali wake.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa Watanzania kulinda amani, usalama, na utulivu kama nyenzo kuu ya kuchochea maendeleo ya kiuchumi nchini.
Akizungumza wakati akihitimisha Tamasha la Kizimkazi Festival leo Ijumaa, Agosti 14, 2026 visiwani Zanzibar, Dkt. Samia amesisitiza kuwa mafanikio yanayoonekana katika sekta za uwekezaji na huduma za jamii yanategemea uwepo wa hali ya utulivu. Amewataka wananchi kutochukulia tunu hizo kama jambo la kawaida, bali wazitunze kwa nguvu zote.
Mkuu huyo wa nchi amebainisha kuwa mipango mikubwa ya serikali katika kuvutia utalii, biashara, na kutengeneza ajira haiwezi kufanikiwa ikiwa nchi itaingia katika machafuko. Ameeleza kuwa amani ni kila kitu katika maisha ya binadamu na ndiyo roho ya maendeleo yoyote.
“Uwekezaji, maendeleo tunayoyaona hapa; uwekezaji, utalii, biashara, ajira na huduma za jamii hayawezi kustawi katika mazingira ya vurugu na uvunjifu wa amani. Niwaombe Watanzania wenzangu hususan vijana msikubali kuharibu amani ya nchi yenu. Amani ndio kila kitu katika maisha yetu,” amesisitiza Dkt. Samia.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
📍IRINGA - Mbwa katika Kijiji cha Ihomasa, Kata ya Wasa, Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, wameibua kero kwa Wananchi baada ya kulalamikiwa kuvamia mashamba na kula mahindi mabichi, hali inayowaongezea wakulima hasara.
Kero hiyo iliwasilishwa kwa Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Benjamin Sitta, Agosti 12, 2026, wakati wa ziara yake iliyohusisha mkutano maalum wa kusikiliza na kutatua changamoto na kero za wananchi katika Kata ya Wasa, Tarafa ya Kiponzelo.
Mwananchi aliyeibua suala hilo alisema mbwa hao huachiliwa kutoka kwenye makazi ya wamiliki wao na kuingia mashambani, ambako huharibu na kula mahindi mabichi, hatua inayosababisha wakulima kupata hasara.
Akijibu kero hiyo, Sitta aliwataka wamiliki wa mbwa kuhakikisha wanawafuga kwa utaratibu unaozingatia usalama wa Wananchi na mali zao, ikiwemo mazao ya Wakulima.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padre Dkt. Charles Kitima, ametoa wito kwa serikali na viongozi wa umma kuimarisha utamaduni wa kuwasikiliza wananchi, akisisitiza kuwa Watanzania ni watu wavumilivu ambao hawajazoea kutumia silaha wala kufanya vurugu katika kudai haki zao.
Akizungumza na waandishi wa habari Agosti 13, 2026, kufuatia mkutano kati ya Maaskofu wa TEC na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan uliofanyika Agosti 10, Padre Kitima amebainisha kuwa msingi wa utawala bora ni kutambua kuwa mamlaka yote yanatoka kwa wananchi.
Padre Kitima amekumbusha masharti ya Ibara ya 8 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inayoeleza kuwa utawala wa nchi uko chini ya wananchi na viongozi wamepewa dhamana tu ya kusimamia.
“Ukiwa kiongozi... lazima ukubali kuwasikiliza wananchi. Eh wananchi wanachosema kizuri kitamu lazima usikilize. Na huo ndio uwajibikaji... Sasa unapopora yale mamlaka kuwafanyia chochote unachotaka kwa kweli inakuwa ni kukosea utu wa Mtanzania na kukosea ubinadamu,” amesisitiza Padre Kitima.
CHANZO CHA VIDEO: Breez Online TvThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padre Dkt. Charles Kitima, ameelezea wasiwasi wake kuhusu kuibuka kwa vikundi na watu binafsi wanaojianzishia "vikosi" na wengine kutumia lugha za matusi na kashfa mitandaoni bila kukemewa.
Akizungumza na waandishi wa habari Agosti 13, 2026, Padre Kitima amesema kuwa vitendo hivyo vinavuruga utamaduni wa Watanzania wa kupenda ukweli akisisitiza kuwa nchi tayari ina vyombo imara na vinavyofahamika kisheria kwa ajili ya ulinzi na usalama, vikiwemo Jeshi la Wananchi (JWTZ) na Jeshi la Polisi, hivyo hakuna haja ya kuruhusu "vikosi" visivyo rasmi kuchukua nafasi hiyo.
“Nchi hii tunajua sisi tuna vikosi vya kuleta ulinzi na usalama. Tuna vyombo maalum... Sasa mtu mmoja anaamka tu huoni akikemewa huoni mwingine anaamua yaani kumtukana fulani tu. Mwingine anaamua yaani kutukana watu tu na anaachwa,” amesema Padre Kitima.
Amehoji kuhusu watu wanaofadhili vikundi hivyo ambavyo kazi yake ni kushambulia watu, viongozi, na taasisi akisema, “Ni wazi tunaona wapambe wa kwenye mitandao…tusipoangalia wanaweza wakavuruga zaidi utamaduni wa kuwa watu wa kweli. Eh kwasababu uongo mwingi unapita kwenye mitandao na tunajiuliza anayevigharamia hivyo ni nani?” amehoji kiongozi huyo.
Padre Kitima ametoa wito kwa serikali kujali sauti za wananchi na kukemea vikundi hivyo vinavyoonekana vimepangwa kwa malengo ya kisiasa. Amehimiza Watanzania washikamane na serikali yao wakiongozwa na misingi ya ukweli na uadilifu ili kuliponya taifa kufuatia mivutano iliyojitokeza baada ya uchaguzi wa mwaka 2025.
CHANZO CHA VIDEO: Breez Online TvThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) limeonya kuwa taifa haliwezi kupata amani ya kweli ikiwa litafumbia macho uovu uliotokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, likisisitiza kuwa uovu usipokemewa una tabia ya kujirudia.
Akizungumza na waandishi wa habari Agosti 13, 2026, Katibu Mkuu wa TEC, Padre Dkt. Charles Kitima, amebainisha kuwa msimamo wa kanisa Katoliki ni kuhakikisha kuwa matukio ya mauaji na ukatili yaliyojitokeza yanalaaniwa na kurekebishwa ili kulinda heshima ya binadamu.
Padre Kitima amesisitiza kuwa kanisa halijaanza leo kulaani mauaji, akirejea historia tangu mwaka 1887 kule Pugu, vita vya Maji Maji, na mauaji ya Pemba ya mwaka 2001 ambapo kanisa liliungana na taasisi nyingine kukemea umwagaji damu.
“Ovu kama hili limefanyika lazima likemewe na lilaaniwe. Hili ni ovu. Tusitoke kwenye mstari wa uovu, msipolikemea na kulilaani litakuja kurudia... uovu huu haupaswi kufumbiwa macho lazima ulaaniwe na ukataliwe na urekebishwe,” amesema Padre Kitima kwa msisitizo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Kila tofali lina hadithi yake. Kuna linalobeba ndoto ya familia iliyokuwa ikitafuta mahali salama pa kuita nyumbani. Kuna linalofungua mlango wa mfanyabiashara anayeanzisha safari ya ukuaji wa biashara yake. Kuna linalowapa ajira mafundi, wahandisi na mamia ya vijana wanaoshiriki katika ujenzi.
Lakini yapo pia matofali ambayo hadithi yake haisikiki kirahisi—matofali yanayogeuka kuwa mapato ya Serikali, yanayoongeza thamani ya mali za umma na yanayochangia ukuaji wa uchumi wa Taifa.
Mara nyingi tunapoona jengo jipya likiinuka katikati ya jiji, macho yetu huvutiwa na uzuri wake. Tunaliona kama alama ya maendeleo ya mji. Hata hivyo, nyuma ya kuta hizo kuna mzunguko mpana wa uchumi.
Kuna viwanda vilivyozalisha saruji na nondo, wakandarasi waliotekeleza kazi, taasisi za fedha zilizowezesha uwekezaji, wafanyabiashara watakaofungua milango yao na familia zitakazoishi humo. Mwishoni mwa mnyororo huo, kuna Serikali inayopata mapato ya kuendelea kugharamia huduma za elimu, afya, miundombinu na maendeleo ya wananchi.
Fuatilia simulizi hii kufahamu mazuri ya NHCThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padre Dkt. Charles Kitima, amesisitiza kuwa mkwamo wa kisiasa nchini utatatuliwa tu ikiwa kutakuwa na utayari wa kukiri makosa, kusimamia ukweli, na kuombana msamaha kufuatia matukio yaliyogubika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025
Akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 13, 2026, kufuatia mkutano kati ya TEC na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan uliofanyika Ikulu ya Chamwino tarehe 10 Agosti, Padre Kitima amebainisha kuwa msingi wa andiko walilomkabidhi Rais ni kuhakikisha nchi inapata uponyaji wa kweli.
Padre Kitima ameeleza kuwa viongozi wa kiroho wanaona kuna haja ya kuwa na ujasiri wa kutaja kile kilichokwenda mrama ili kurejesha mahusiano yaliyovunjika kati ya serikali na wananchi. Amebainisha kuwa bila kukiri ukweli wa yaliyotokea, mchakato wa maridhiano hautakuwa na tija
“Kutokana pia na kwamba waliweka bayana kwamba ili tutoke katika hali hii inabidi kwenda katika kusimamia ukweli na vile vile kutakana msamaha kusameheana na hata kuponya nchi. Kwa hiyo kwa kiingereza tunasema ‘to admit the truth then reconciliation healing the nation’,” amesisitiza Padre Kitima
Katibu Mkuu huyo amekiri kuwa matukio ya tarehe 29 Oktoba 2025 yameacha sononeko kubwa kwa Watanzania wengi na kuharibu imani ya raia kwa mamlaka zao. Amesisitiza kuwa maaskofu wameweka wazi masikitiko yao kuhusu mauaji na uharibifu wa mali uliotokea na kwamba sasa ni wakati wa kutatua mambo hayo yaliyosababisha watu kuingia katika hali ya maandamano
CHANZO CHA VIDEO: Breez Online TvThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
📍MTWARA - Serikali imesema itaendelea kutengeneza mazingira wezeshi ya biashara nchini, ikiwa ni pamoja na kuboresha mfumo wa kodi na tozo, kwa kujiweka kama wawezeshaji wa sekta binafsi badala ya kuwa wadhibiti pekee.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga, jana Agosti 12, 2026 kwenye mkutano na wafanyabiashara wa Mkoa wa Mtwara, wakati akihitimisha ziara yake ya kikazi ya siku tatu Mkoani humo.
Waziri Kapinga amesisitiza kuwa zama za viongozi kuwasikiliza wafanyabiashara bila kutoa majibu au mrejesho wa kero zao zimepitwa na wakati, na sasa viongozi wana wajibu wa kisheria na kiutendaji wa kutoa majibu ya haraka.
“Tumeshasema kuwa takribani asilimia 70 ya maendeleo ya nchi yetu yanategemea sekta binafsi. Lengo letu ni kuhakikisha tunakuwa na taasisi na Sera zinazowezesha sekta hii kukua na siyo kuikandamiza,” amesema Waziri Kapinga.
Ameongeza kuwa kazi kuu ya Serikali ni kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji na biashara, huku akiwataka wafanyabiashara nao kutimiza wajibu wao kikamilifu kama ambavyo Serikali inatekeleza majukumu yake.
Katika hatua nyingine, Waziri Kapinga ametoa onyo kwa mtu au kikundi chochote kitakachojaribu kuhujumu Mfumo wa Stakabadhi za Ghala, akieleza kuwa mfumo huo una faida kubwa kwa wakulima pamoja na Serikali na umewekewa msisitizo mkubwa ndani ya Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Kuhusu maendeleo ya viwanda mkoani Mtwara, Kapinga ameeleza kuwa Serikali inaendelea kuwekeza kwa kiasi kikubwa kwenye miundombinu mbalimbali na hivi karibuni wananchi na wawekezaji wataanza kushuhudia mabadiliko na maendeleo makubwa katika sekta ya viwanda mkoani humo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) limeweka wazi kuwa lengo kuu la kukutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kutoa mtazamo wao kuhusu hali ya kisiasa nchini na kushauri njia bora ya kuiponya nchi kufuatia matukio ya Uchaguzi Mkuu uliopita.
Akizungumza na waandishi wa habari leo kufuatia kikao hicho kilichofanyika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma, Agosti 10, 2026, Katibu Mkuu wa TEC, Padre Dkt. Charles Kitima, amebainisha kuwa mkutano huo ulitokana na ombi la maaskofu wenyewe waliotaka kumshirikisha Rais maoni yao.
Padre Kitima ameeleza kuwa maaskofu wamewasilisha andiko rasmi lenye kurasa nne ambalo linasisitiza umuhimu wa kusimamia ukweli na msamaha ili kurejesha utulivu wa kweli nchini.
“Kutokana pia na kwamba waliweka eh bayana kwamba ili tutoke katika hali hii inabidi kwenda katika kusimamia ukweli na vile vile kutakana msamaha, kusameheana na hata kuponya nchi. Kwa hiyo kwa kiingereza tunasema ‘to admit the truth then reconciliation healing the nation’,” amesema Padre Kitima.
Padre Kitima amewataka Watanzania kuwa na imani na ujumbe uliowasilishwa na maaskofu na kuwa na utulivu wakati serikali ikielekea katika kutatua mkwamo wa kisiasa uliopo nchini.
CHANZO CHA VIDEO: Breez Online TvThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Kifo cha kijana Sefu Mussa, mkazi wa Matejoo jijini Arusha, kinazidi kuzua maswali baada ya kudaiwa kufariki dunia Agosti 12, 2026, katika tukio linalodaiwa kuhusisha askari wa Hifadhi ya Ngorongoro. Sefu alikuwa pamoja na vijana wenzake wawili, Salimu Haji na Abdillah Nuru, wakielekea Babati kwa ajili ya mazishi kabla ya kupotea njia na kukutana na askari hao.
Kwa mujibu wa Abdillah, vijana hao walidaiwa kuamriwa kuvua nguo na kulazwa kwenye miba, hali iliyosababisha kuvimba sehemu mbalimbali za miili yao. Sefu alizidiwa na kufariki dunia wakati akikimbizwa hospitalini.
Jeshi la Polisi limethibitisha kuwashikilia askari watatu waliokuwa zamu wakati wa tukio hilo kwa ajili ya uchunguzi. Hata hivyo, wananchi na vijana waliomfahamu Sefu wameendelea kutaka uchunguzi wa kina ufanyike na hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya wote watakaobainika kuhusika.
Akizungumza na Jambo TV, Balozi wa mtaa huo, Hawa Ramadhani, amekemea vikali tukio hilo na kuhoji, “Mnaua watoto wasio na hatia?”, huku akisema kama vijana hao walikuwa na makosa, walipaswa kufikishwa kwenye vyombo vya sheria badala ya kufanyiwa ukatili, huku akiomba haki itendekeThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Kijana anayefahamika kwa jina la Sefu Musa amefariki dunia baada ya kudaiwa kupigwa na askari watatu katika eneo la Ngorongoro mkoani Arusha, kufuatia tuhuma za kuhusishwa na ujangili.
Tukio hilo limetokea Agosti 12, 2026, majira ya saa nne na nusu asubuhi, wakati Sefu akiwa pamoja na wenzake wawili, Abdallah Nuru na Salim Hamisi, wakisafiri kuelekea Babati mkoani Manyara kwa ajili ya kuhudhuria mazishi ya rafiki yao. Hata hivyo, walielezwa kupotea njia na kuingia katika eneo la Ngorongoro.
Kwa mujibu wa maelezo ya Abdallah Nuru, mmoja wa walionusurika, walipofika katika lango la kwanza la Hifadhi ya Ngorongoro walikamatwa na askari hao na kuhojiwa kuhusu sababu ya kuwepo kwao katika eneo hilo. Abdallah anadai kuwa baada ya mahojiano, waliamriwa kuvua nguo na kulala kwenye miba, kabla ya kudaiwa kupigwa na askari hao.
Baada ya hali kuwa mbaya, Abdallah alifanikiwa kuwapeleka wenzake katika Hospitali ya Lutheran Karatu kwa ajili ya matibabu. Hata hivyo, kutokana na majeraha aliyoyapata Sefu Musa alifariki dunia njiani akiwa anapelekwa hospitali, huku Salim Hamisi akiendelea kupatiwa matibabu.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limesema askari hao watatu waliokuwa zamu wakati wa tukio wanashikiliwa kwa ajili ya mahojiano, huku uchunguzi ukiendelea kubaini ukweli wa kilichotokea na hatua stahiki kuchukuliwa endapo itathibitika kuwa walikiuka sheria na taratibu za kazi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Naibu Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Bukombe, Dkt. Doto Mashaka Biteko, amesema mashindano ya Ngalawa Race ni miongoni mwa matukio yaliyoongeza burudani, mvuto na hamasa katika Tamasha la Kizimkazi Festival 2026.
Mashindano hayo yaliyofanyika Agosti 12, 2026, Kizimkazi, Kusini Unguja, yamewakutanisha vijana na washiriki mbalimbali katika ushindani wa kuvutia, huku Nassor Pandu kutoka Mkunguni akiibuka mshindi wa mashindano hayo.
Akizungumza wakati wa tukio hilo, Dkt. Biteko amesema mashindano ya ngalawa yameendelea kuwa sehemu muhimu ya tamasha hilo kwa kuwa yanatoa burudani huku yakifungua fursa kwa vijana kushiriki katika shughuli za michezo na kiuchumi.
“Ni dhahiri kwamba mashindano haya yamekuwa muhimu kwa vijana na jamii kwa ujumla. Tukio hili limewaleta pamoja wadau mbalimbali na kuchangia kwa kiasi kikubwa juhudi za kuboresha mazingira ya michezo na burudani,” amesema Dkt. Biteko.
Ameongeza kuwa Ngalawa Race imeendelea kuwa sehemu muhimu ya Kizimkazi Festival, ikitoa fursa kwa vijana kuonesha vipaji, uwezo na ushindani katika mchezo huo wa asili, sambamba na kuchochea shughuli za kiuchumi katika eneo hilo.
Katika mashindano hayo, timu mbili bora kutoka Mchangamle na Mkunguni zilishiriki katika hatua za mwisho, huku kila timu ikiwa na manahodha 10 waliopambana kuwania ushindi.
Dkt. Biteko amesema matukio kama hayo yana umuhimu mkubwa katika kuendeleza michezo, burudani na utalii, huku yakitoa nafasi kwa jamii kunufaika kiuchumi na kuitangaza Kizimkazi kama sehemu yenye vivutio mbalimbali. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Wananchi Mkoani Mtwara wameeleza kuwa ujenzi na uboreshaji wa Kituo cha Afya Msangamkuu umewapunguzia changamoto ya kusafiri umbali mrefu kufuata huduma za matibabu, huku wakisema uwepo wa huduma hiyo karibu na makazi yao utawawezesha kupata matibabu kwa wakati.
Wananchi hao wamesema awali baadhi yao walilazimika kutumia muda na gharama zaidi kufuata huduma za afya katika maeneo ya mbali kama Mtwara Mjini, hali iliyokuwa changamoto hasa kwa wagonjwa wanaohitaji huduma za haraka.
Kituo hicho kimezinduliwa Agosti 12, 2026, na Waziri wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi mkoani Mtwara ya kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Waziri Kapinga amesema Serikali inaendelea kusogeza huduma za afya karibu na Wananchi ili kuwawezesha kupata matibabu kwa urahisi na kwa wakati, badala ya kutumia muda mwingi kusafiri kutafuta huduma hizo.
Amesema upatikanaji wa huduma za afya karibu na Wananchi una nafasi muhimu katika kuwawezesha kuendelea na shughuli zao za uzalishaji, jambo linalochangia ustawi wa familia na uchumi wa Taifa.
Waziri Kapinga pia amewataka Wananchi kushirikiana na Serikali katika kulinda na kutunza miundombinu hiyo ili iendelee kuwahudumia kwa muda mrefu.
Uzinduzi wa Kituo cha Afya Msangamkuu umefanyika katika siku ya tatu ya ziara ya Waziri Kapinga mkoani Mtwara, ambapo pia ametembelea miradi mbalimbali katika Majimbo ya Nanyamba, Mtwara Mjini na Mtwara Vijijini.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Wakili William Maduhu kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) ametoa wito kwa Vijana wa Chama cha ACT Wazalendo kuwaelimisha Wananchi kuhusu dhamira ya chama hicho katika mchakato wa mazungumzo ya maridhiano Zanzibar, akisema baadhi ya Wananchi wanaamini kusainiwa kwa mazungumzo ni ishara kwamba Chama hicho kinakwenda kuingia Serikalini kupitia Serikali ya Umoja wa Kitaifa
"Ni kama Wananchi walikuwa wanajua kwamba mkishasaini yale makubaliano tayari mnaingia Serikalini. Lakini Wananchi wakaona mmesaini makubaliano, mkapiga picha pale, lakini Serikali ya Umoja wa kitaifa bado haiundwi. Nikampigia simu kiongozi mmoja wa Chama kutaka ufafanuzi. Nyie si mmesaini makubaliano, kwanini hamuingii serikalini?", alieleza Maduhu
Maduhu amesema ni jukumu la Vijana wa Chama ACT Wazalendo kueleza na kuelimisha umma kwamba “ACT haipo Zanzibar ili kuingia madarakani, bali ipo kwa ajili ya maslahi ya Wananchi kwa ujumla.”
Amesema kutokuwepo kwa uelewa wa kutosha kuhusu maana ya makubaliano hayo kumeendelea kuwafanya baadhi ya Wananchi kuyatafsiri kama makubaliano ya kugawana madaraka, badala ya kuyaona kama hatua ya kuanzisha mazungumzo rasmi kuhusu masuala yanayogusa mustakabali wa Zanzibar.
Maduhu amesisitiza kuwa ushiriki wa ACT Wazalendo katika mazungumzo hayo haupaswi kutafsiriwa moja kwa moja kama nia ya kuingia Serikalini, bali ni sehemu ya juhudi za kutafuta maridhiano na kujadili masuala ya uchaguzi, Utawala wa Sheria, haki za binadamu na maslahi mapana ya Wananchi.
Maduhu alizungumza hayo jana Agosti 12, 2026 katika maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani yaliyoandaliwa na Ngome ya Vijana ya ACT Wazalendo, huku akiwataka Vijana hao pia kujiuliza iwapo Serikali inayoongozwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) ina utashi wa kisiasa wa kufanya mazungumzo ya kweli, yenye uwazi na ushirikishwaji wa wananchi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Anthony Mtaka, amewaagiza viongozi wa halmashauri zote mkoani humo kuanzisha kambi maalum za kuwafundisha wanafunzi 3,001 wa darasa la kwanza hadi la tatu ambao bado hawajamudu stadi za msingi za kusoma, kuandika na kuhesabu.
Mtaka ametoa agizo hilo wakati akifungua kikao kazi cha maandalizi ya utekelezaji wa Mradi wa Jifunze Kijiji Changu unaofadhiliwa na Taasisi ya Uwezo Tanzania, kilichofanyika mkoani Njombe.
Amesema kila kiongozi katika halmashauri ana wajibu wa kuhakikisha madarasa maalum yanaanzishwa kwa ajili ya wanafunzi hao, yakiwemo madarasa ya muda wa jioni, ili kuwapa fursa ya kujengewa uwezo katika stadi hizo muhimu.
Mtaka ameeleza kuwa mfumo huo unaweza kuendeshwa kwa utaratibu unaofanana na madarasa yanayoandaliwa kwa ajili ya mitihani, akisisitiza kuwa suala la wanafunzi kushindwa kusoma, kuandika na kuhesabu linahitaji hatua za haraka na za pamoja.
Kwa upande wake, Ofisa Elimu Mkoa wa Njombe, Nelas Mulungu, amesema Mradi wa Jifunze Kijiji Changu hautawahusu wanafunzi wa darasa la kwanza hadi la tatu pekee, bali pia utawajumuisha watoto ambao hawajawahi kwenda shule lakini wanaishi katika vijiji vinavyotekeleza mradi huo.
Naye Ofisa kutoka Uwezo Tanzania, Judith Kimambo, amesema wamefika mkoani Njombe kwa ajili ya kuuzindua mradi huo ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za Serikali chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuhakikisha Watanzania wanapata stadi za msingi za kusoma, kuandika na kuhesabu.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Dorothy Semu, amesema mchakato wa kupata Katiba Mpya ya Wananchi unapaswa kuanza sasa, akisisitiza kuwa Chama hicho tayari kina msimamo wa namna mchakato huo unavyopaswa kuendeshwa.
Semu amesema hayo leo katika maadhimisho ya Siku ya Vijana yaliyoandaliwa na Ngome ya Vijana ya ACT Wazalendo, ambapo amewataka Vijana kushiriki kikamilifu katika kudai na kuwezesha mchakato wa upatikanaji wa Katiba Mpya.
Amesema msimamo wa ACT Wazalendo kuhusu Katiba Mpya ulipitishwa na Kamati Kuu ya chama mwaka 2021 na uliwasilishwa katika kikosi kazi kilichoundwa na Rais
Kwa mujibu wa Semu, ACT Wazalendo inapendekeza kuanza kwa mabadiliko ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na Sheria ya Kura ya Maoni, akisema sheria hizo ndizo zitakazoweka utaratibu na njia ya kuendesha mchakato wa kupata Katiba Mpya.
Baada ya hatua hiyo, amesema Chama kinataka kuitishwa kwa Mkutano wa Kitaifa wa Makubaliano, utakaowezesha Watanzania kujadili masuala muhimu na kufikia makubaliano kuhusu aina ya Katiba wanayoitaka.
Semu amesema hatua inayofuata inapaswa kuwa kuundwa kwa Kamati ya Wataalamu, itakayokusanya na kuunganisha maoni yaliyotolewa katika michakato mbalimbali ya Katiba, ikiwemo maoni ya Tume ya Jaji Joseph Warioba na Rasimu ya Katiba ya mwaka 2014, ili kuandaa Rasimu ya Katiba Mpya ya Wananchi.
Amesema baada ya rasimu hiyo kukamilika, inapaswa kupelekwa kwa wananchi kupitia kura ya maoni ili kutoa uamuzi wa mwisho kuhusu Katiba wanayoitaka.
"Tunatamani mchakato huu uanze sasa, tuache bla bla, tuache kona kona", alisema Semu
Aidha, Semu amewataka Vijana wa ACT Wazalendo kutokuwa watazamaji katika mjadala huo, bali kujifunza Katiba iliyopo, rasimu mbalimbali zilizowahi kuandaliwa na kushiriki katika kutoa maoni, kukosoa na kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa Katiba Mpya.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Februari 27, 2026 kupitia mitandao ya kijamii ilionekana video ya Mzee Ramesh Ramji Ramesh mwenye umri wa miaka 72 akilalamika kunyanyaswa katika nyumba yake na mwanae huku akidai sababu kuu ni yeye kumuoa mwanamke wa kiswahili.
Agosti 10, 2026 Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Ardhi ilitamka kuwa Mzee Ramesh ndiye mmiliki halali wa nyumba hiyo, hapaswi kubugudhiwa katika umiliki wake, na pia Mahakama hiyo ya Ardhi imetamka kwamba Jayprakash Ramesh, ambaye ni mtoto wa huyo Ramesh, kuondoka katika nyumba ya baba yake, huku ikiamuru kuwa hatakiwi kumsumbua katika makazi hayo.
Amri hiyo ya Mahakama imekuja mara baada ya Mzee Ramesh kufungua kesi na 000005357/2026 akiomba mahakama kutambua umiliki wake wa Flat No. B1, Block B4, Phase 5, Plot No. 1064 mtaa wa Olympio, wilaya ya Ilala, Dar es Salaam ambayo mwanae amekuwa akidai umiliki wa apartment iliyopo.
Katika kuwasilisha hoja zake mtoto wa Mzee Ramesh aliiomba mahakama kuwa alipwe fidia na baba yake shilingi 320,900,000/= kama fidia kwa kufanya maboresho katika nyumba hiyo huku akidai kuwa yeye ana haki za mirathi ya nyumba hiyo kwani mama yake aliyefariki alikuwa mke wa mzee huyo.
Hata hivyo, madai hayo ya mtoto wa Mzee huyo yameondolewa Mahakamani kwani Mahakama hiyo haina mamlaka kisheria kushughulikia Madai hayo.
Jambo TV imezungumza Wakili wa Mzee Ramesh Peter Kibatala @PKibatala_ na hapa anaeleza kilichotokea mahakamani.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA na Mlezi wa CHADEMA Kanda ya Kati, Salma Kasanzu, amedai kuwa uhuru wa kutoa maoni kwa vijana umeminywa kiasi cha kugeuka kuwa chanzo cha watu "kupotezwa" au kubambikiwa kesi nzito za jinai.
Akizungumza leo Agosti 12, 2026, katika Kongamano la BAVICHA lililofanyika jijini Dodoma kuadhimisha Siku ya Vijana Duniani, Kasanzu ameeleza kuwa licha ya takwimu kuonesha kuwa vijana ndio kundi kubwa zaidi nchini, bado hawana sauti katika maamuzi na uongozi wa sekta muhimu kutokana na misingi mibovu ya kidemokrasia.
“Ndugu zangu vijana takwimu za Tanzania hivi sasa zinasema vijana ndio wengi kuliko wote... Kwa mantiki hiyo tungekuwa tunaenda kisawasawa na mambo ya demokrasia tungetawala sekta zote. Uongo? Kweli,” amesema Kasanzu huku akiwataka vijana kutokubali wengine wawapangie hatima yao.
Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ameweka wazi kuwa mazingira ya kisiasa kwa sasa yanatisha, ambapo kijana anapojaribu kudai haki au kutoa maoni yake, anakabiliwa na vitisho vya usalama wa maisha yake au kufunguliwa mashtaka ya ugaidi na uhaini, jambo ambalo ameliita kuwa halikubaliki katika nchi inayojinasibu kwa demokrasia.
Ametoa wito wa dhati kwa vijana kushikamana na kupambana ili kupata Katiba Mpya sasa, akisema hiyo ndiyo itakuwa dawa ya kudumu ya changamoto zinazowakabili.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, John Heche, ametoa wito kwa vijana nchini kuacha hofu na kutambua nguvu yao ya kitakwimu kama kundi kubwa zaidi linaloweza kuleta mabadiliko ya kiutawala na kiuchumi nchini Tanzania.
Akihutubia katika Kongamano la BAVICHA lililofanyika leo Agosti 12, 2026, jijini Dodoma kuadhimisha Siku ya Vijana Duniani, Heche amesema kuwa mfumo wa sasa wa mamlaka hautoi haki kwa njia ya kubembeleza, bali utarekebika tu pale utakapoona kuwa wananchi wamekataa kuogopa.
“Lazima mjue hatutapewa mabadiliko kwa kupigia watu magoti na kuwabembeleza. Tutapewa mabadiliko pale ambapo watakapoona tukiendelea na mchezo huu wote tutakuwa kwenye hatari... lazima mfike sehemu muweke uoga”, amesisitiza Heche.
Kiongozi huyo amechambua changamoto zinazowakabili vijana, akibainisha kuwa licha ya kuwa na elimu, nguvu, na ubunifu, wengi wanakwama kutokana na ukosefu wa mitaji na mazingira wezeshi ya kiuchumi yanayosababishwa na uongozi mbovuThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo Zanzibar, Ismail Jussa Ladhu, amesema baadhi ya watu wamejimilikisha ajenda ya mabadiliko, akisisitiza kuwa Chama hicho hakiwezi kuwa mfuasi wa ajenda za kisiasa zinazoanzishwa na wengine.
Jussa amesema ACT-Wazalendo kimejijenga kwa misingi na misimamo yake, huku ajenda za Chama hicho zikifahamika kwa Wananchi.
“Chama chetu kimenyooka sawa sawa na ajenda zetu zinafahamika,” amesema Jussa.
Amesema kauli hiyo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Vijana yaliyofanyika leo, Agosti 12, 2026, akisisitiza kuwa ACT-Wazalendo itaendelea kusimamia ajenda zake badala ya kuwa mkia kwa kufuata ajenda za Vyama vingineThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mbunge wa Tunduru kupitia ACT-Wazalendo, Ado Shaibu Ado amesema Tanzania inaweza kufika mwaka 2029 bila kuwa na Katiba mpya iwapo wananchi na wadau wa mabadiliko hawatasimamia kwa nguvu mchakato wa kupata Katiba hiyo.
Ado amedai dalili za kutokuwepo kwa dhamira ya dhati ya Serikali kuendelea na mchakato huo zinaonekana kwenye Bajeti ya Serikali ya mwaka wa fedha 2026/27, akidai kuwa hakuna fedha zilizotengwa kwa ajili ya kuendesha mchakato wa Katiba mpya.
“Ukitazama bajeti ya mwaka wa fedha 2026/27, utaona katika bajeti ile hakuna fedha, hata shilingi moja, ambayo Bunge limepanga ili kugharamia mchakato wa Katiba mpya,” amesema Ado
Amedai hali hiyo, pamoja na Serikali kutoweka wazi mpango wake wa namna itakavyotekeleza ahadi ya Katiba mpya, inatoa ujumbe kuwa mchakato huo haupewi kipaumbele.
Ado amewataka vijana wa ACT-Wazalendo na wadau wengine kushinikiza Serikali kutekeleza matakwa ya wananchi ya kupata Katiba mpya, akionya dhidi ya kutegemea kauli pekee kwamba mchakato huo upo kwenye mipango ya Serikali.
“Tusidanganyike na maneno yao kwamba Katiba mpya ipo kwenye ilani yao. Tusidanganyike na hotuba zao. Haya ni maneno ya kupoteza muda tu,” amesema.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Aliyekuwa Mgombea Urais 2025 na Naibu Waziri Mkuu Kivuli wa ACT Wazalendo, Luhaga Mpina, amedai aliyekuwa nyuma ya vikwazo alivyokutana navyo katika mchakato wa uchaguzi ndiye
"aliyeishiwa pawa", akisisitiza kuwa yeye hajawahi kuogopa mapambano ya aina yoyote.
"Nilimsikia mtawala kule Zanzibar akisema eti Lissu na mwenzake Mpina waliishiwa Pawa, nataka niseme na nirudie tena, aliyeishiwa pawa ni yeye, sijawahi kuogopa mapambano"
Akizungumza na Vijana wa Chama cha ACT Wazalendo katika maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani, leo Agosti 12, 2026, Mpina amesema historia yake ya kukabiliana na changamoto mbalimbali imemjengea ujasiri wa kuendelea na mapambano,
akisisitiza kuwa hajawahi kuogopa mazingira yoyote, iwe mchana au usiku.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katibu wa ACT-Wazalendo Bara, Isihaka Mchinjita, ametoa wito wa Serikali kukubali kuundwa kwa chombo huru cha uchunguzi kitakachoweka hadharani ukweli kuhusu matukio yaliyotokea Oktoba 29, 2025.
Mchinjita amesema chombo hicho kinapaswa kuwa huru na kuwa na uwezo wa kubaini waliohusika na matukio hayo, akisema kuna maswali ambayo bado hayajajibiwa kuhusu vifo na majeruhi vilivyoripotiwa.
Aidha, ametoa wito kwa jumuiya za kimataifa kushiriki katika mchakato wa kutafuta suluhisho la changamoto hiyo, huku akiitaka Serikali kuwa tayari kuunda tume huru ya kuchunguza yaliyotokea ili haki, ukweli na uwajibikaji viweze kupatikana.
Amesema ACT-Wazalendo itaendelea kusimamia wito huo, akisisitiza kuwa ukweli kuhusu yaliyotokea Oktoba 29, 2025 hauwezi kufichwa na kwamba nchi inahitaji hatua zitakazoweka msingi wa kusonga mbele. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana ya Chama cha ACT Wazalendo, Abdul Nondo amesema licha ya kutangazwa kuwa miongoni mwa wanufaika wa Mikopo ya Vijana inayotolewa na Serikali chini ya Wizara ya Vijana, sasa ni mwezi wa tatu hajapokea mkopo huo
Nondo ameyasema hayo leo Agosti 12, 2026, katika maadhimisho ya Siku ya Vijana, iliyoandaliwa na Ngome ya Vijana ya Chama cha ACT Wazalendo na kufanyika Manzese Dar es Salaam -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mratibu wa Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Wakili Onesmo Olengurumwa, amesema Vijana ni msingi muhimu katika upatikanaji wa Katiba Mpya nchini, hivyo wanapaswa kuiweka ajenda hiyo katika vipaumbele vyao na kuendelea kuipambania kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2030.
Olengurumwa ameyasema hayo leo, Agosti 12, 2026, katika maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani yaliyoandaliwa na Ngome ya Vijana ya ACT Wazalendo katika Ukumbi wa Mrina Hall, Manzese, jijini Dar es Salaam
Akiwasilisha hotuba yake, Olengurumwa amenukuu kauli ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, akisisitiza umuhimu wa vijana kuwa jasiri, kujiamini na kuwa na uwezo wa kuhoji mifumo inayokwenda kinyume na matakwa ya jamii.
“Nyerere alisema tunataka kuona katika Taifa hili vijana jeuri na wenye kujiamini; si vijana waoga, akina ‘ndiyo bwana mkubwa’; vijana wenye ujasiri wa kuhoji na kupiga vita mifumo ya jamii isiyoshabihiana na matakwa na matarajio ya jamii ya Kitanzania,” amesema.
Ameongeza kuwa kauli hiyo inapaswa kuwa sehemu ya hamasa kwa vijana katika kudai mifumo bora ya uongozi na Katiba inayozingatia maslahi ya Wananchi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, John Heche, ametoa ahadi ya kuhakikisha vijana wa chama hicho wakiwemo wanafunzi wa vyuo waliokamatwa wanaachiwa huru na kugharamikiwa masomo yao ya elimu ya juu.
Akizungumza leo Agosti 12, 2026, katika Kongamano la BAVICHA jijini Dodoma lililofanyika kuadhimisha Siku ya Vijana Duniani, Heche amesema kuwa CHADEMA haitawatelekeza vijana wa hao walioingia kwenye mkono wa sheria kutokana na harakati za kisiasa.
“Na kwa maana hiyo wale vijana wa BAVICHA na CHASO waliokamatwa Mbeya, chama chetu mimi binafsi na uongozi wa chama chetu wote tutawapigania mpaka tone letu la mwisho kuhakikisha wanatoka gerezani. Lakini cha pili tutahakikisha wanapotoka ndani wanaendelea na masomo yao, iwe ndani ya nchi au nje ya nchi kwa kuhakikisha wanalipiwa na wanasoma mpaka wamalize shahada zao. Kwa hili kwangu ni muhimu sana ili mtu asije akafikiri tutawatelekeza”, ameeleza Heche.
Aidha, Heche amewataka vijana kutokubali kutishwa na hali zao za sasa, akieleza kuwa chama kitahakikisha mazingira ya haki yanapatikana ili kila mwenye uwezo apate fursa anayostahili.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, amewahakikishia wananchi wa kijiji cha Endumeti, kata ya Ngarenairobi wilayani Siha, kuwa serikali haina mpango wa kuwaondoa wakulima wazawa katika mashamba ya serikali ili kuwapisha wawekezaji wa nje
Akizungumza wakati wa ziara yake ya kukagua mashamba manne yanayomilikiwa na serikali chini ya Msajili wa Hazina, Prof. Kitila amefafanua upya dhana ya uwekezaji, akisisitiza kuwa mkulima wa Kitanzania mwenye nyenzo zake ni mwekezaji kamili anayepaswa kulindwa.
Waziri huyo ameweka wazi kuwa serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inatokana na kura za wananchi, hivyo haiwezi kufanya uamuzi wa kuumiza waliotoa mamlaka. Amewataka wananchi kuacha kuwa na wasiwasi wa kupoteza maeneo yao ya kujipatia riziki
Prof. Kitila amesisitiza kwa kusema kuwa uamuzi wote utakaofanywa na Rais Samia utakuwa ni kwa ajili ya kunufaisha uchumi wa wananchi kwanza ili serikali nayo iweze kukua.
Katika hatua ya kuondoa dhana potofu kuhusu wawekezaji, Prof. Kitila amebainisha kuwa uwekezaji haupimwi kwa rangi ya mtu au ukubwa wa mtaji wa nje pekee.
“Nani aliwaambia uwekezaji maanake wawe watu kutoka nje? Nani aliwaambia hivi hawa wenye matrecta hapa sio wawekezaji hao? ...wawekezaji ndugu wananchi wenzangu haimaanishi mwekezaji awe na ngozi nyeupe awe tajiri awe na kitambi. Ahah. Ni nyie,” amesisitiza Prof. Kitila.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Wakili Boniface Mwabukusi, ameishauri Serikali kutumia njia za kiutu katika kutafuta mwafaka kuhusu mchakato wa Katiba Mpya.
Mwabukusi ametoa ushauri huo alipokuwa akitoa mada katika Kongamano la BAVICHA la Maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani jijini Dodoma.
Amesema moja ya hatua zinazoweza kuchukuliwa na Serikali ni kuachiliwa huru kwa Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu, ambaye anakabiliwa na mashtaka ya uhaini.
“Hatusemi Serikali iingilie Mahakama. Mahakama haijamshtaki Tundu Lissu, Tundu Lissu ameshtakiwa na Serikali. Kwa hiyo Serikali ikiamua lile shauri liishe leo, litaisha.”
Mwabukusi amesema hatua za kiutu kutoka upande wa Serikali zinaweza kusaidia kujenga mazingira ya mazungumzo na kufikia mwafaka kuhusu suala la Katiba Mpya.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI PICHA:
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo ametembelea na kukagua mashamba manne yanayomilikiwa na Serikali na kusimamiwa na Msajili wa Hazina Wilayani Siha, Mkoani Kilimanjaro, ili kuangalia tija ya matumizi ya rasilimali hizo kwa faida ya Taifa na wananchi.
Katika ziara hiyo ya kikazi, Prof. Mkumbo aliambatana na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais (Uwekezaji) Dkt. Fred Msemwa, Msajili wa Hazina Nehemiah Msechu, Mkuu wa Wilaya ya Siha Dkt. Christopher Timbuka, pamoja na Mbunge wa Jimbo la Siha, Dkt. Godwin Mollel. Mashamba yaliyokaguliwa katika eneo la West Kilimanjaro ni Harlington, Journey’s End, Fosters, na Kanamodo.
Akizungumza na umati wa wananchi wa Kijiji cha Endumeti, Kata ya Ngarenairobi, Prof. Kitila amesisitiza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inalenga kuhakikisha uwekezaji wowote unaofanyika unaleta manufaa ya moja kwa moja kwa jamii inayozunguka miradi hiyo.
Ofisi ya Msajili wa Hazina inasimamia jumla ya mashamba 10 ya Serikali kote nchini kwa ajili ya kilimo cha kibiashara, yaliyogawanyika katika makundi makuu mawili. Kundi la kwanza ni mashamba sita (6) ya iliyokuwa Shirika la NAFCO ambayo yaliyosalia baada ya Serikali kusitisha ubinafsishaji wake ili kuyaendeleza kwa tija ya umma. Mashamba hayo ni Basotu (Hanang), Namtumbo (Ruvuma), pamoja na mashamba manne ya West Kilimanjaro (Harlington, Journey’s End, Fosters, na Kanamodo).
Kundi la pili ni mashamba manne (4) yaliyonunuliwa na serikali kwa maslahi mapana ya Taifa. Mashamba hayo ni KPL Mng’eta- Morogoro, Shamba la Maua la Malalua- Arusha, Kiliflora Usa River- Arusha na Kiliflora Chekereni- Arusha. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema (BAVICHA) taifa, Wakili Deogratius Mahinyila, amesema vijana wa chama hicho hawatamvumilia mwanasiasa yeyote atakayejaribu kukidhoofisha au kukichezea chama.
Mahinyila amesema hayo wakati akiwahutubia vijana katika Kongamano la BAVICHA jijini Dodoma, lililofanyika katika kuadhimisha Siku ya Vijana Duniani.
Amesema BAVICHA haitamuunga mkono wala kumruhusu mtu yeyote kuichezea Chadema, huku akiwataka wanasiasa wanaokikosoa na kuwatukana viongozi wa chama hicho kutotarajia kurejea na kupokelewa kwa shangwe.
“BAVICHA hatutounga mkono wala kuruhusu mtu yeyote atakayecheza na chama chetu. Hatutowavumilia wanasiasa ambao kwa siku za karibuni wamekuwa wakikitukana chama chetu, wanatukana viongozi wetu, halafu wanategemea kesho watarudi tutawapigia vigelegele.”
Mahinyila amesema BAVICHA itaendelea kusimamia msimamo wake na haitakubali watu wanaokidhoofisha chama kurejea bila kuwajibika kwa kauli na matendo yao.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mchambuzi wa masuala ya Siasa nchini, Deus Kibamba akizungumza kwenye mjadala mezani kuhusu Katiba mpya, kwenye Kongamano la Bavicha jijini Dodoma.
Kongamano hilo linafanyika leo Agosti 12, 2026 kwenye maadhimisho ya siku ya vijana Duniani.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkurugenzi wa Jukwaa la Katiba Tanzania (JUKATA), Thobias Messanga, amesema makundi ya kisiasa yanayopinga mabadiliko ya Katiba hutumia propaganda kama moja ya mbinu za kuwashawishi wananchi kuamini kuwa hakuna umuhimu wa kufanya mabadiliko ya Katiba.
Messanga amesema hayo wakati akizungumza katika mjadala wa mezani kwenye Kongamano la Bavicha la Maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani jijini Dodoma.
Amesema propaganda hizo zinalenga kupotosha umma, kubadili fikra na mitazamo ya wananchi kuhusu Katiba, pamoja na kuhamisha mjadala kutoka kwenye masuala ya msingi yanayohusu mabadiliko ya Katiba.
“Makundi ya kisiasa ambayo hayataki mabadiliko ya Katiba, moja ya mbinu wanayoitumia ni propaganda za Katiba. Maana yake ni mbinu au taarifa inayolenga kupotosha umma ambayo inatumiwa na makundi ya watu ambayo yanapinga Katiba ili kuwashawishi wananchi waamini hakuna umuhimu wa mabadiliko ya Katiba", , ameeleza.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkurugenzi wa Jukwaa la Katiba Tanzania (JUKATA), Thobias Messanga, amesema makundi ya kisiasa yanayopinga mabadiliko ya Katiba hutumia propaganda kama moja ya mbinu za kuwashawishi wananchi kuamini kuwa hakuna umuhimu wa kufanya mabadiliko ya Katiba.
Misanga amesema hayo wakati akizungumza katika mjadala wa mezani kwenye Kongamano la Bavicha la Maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani jijini Dodoma.
Amesema propaganda hizo zinalenga kupotosha umma, kubadili fikra na mitazamo ya wananchi kuhusu Katiba, pamoja na kuhamisha mjadala kutoka kwenye masuala ya msingi yanayohusu mabadiliko ya Katiba.
“Makundi ya kisiasa ambayo hayataki mabadiliko ya Katiba, moja ya mbinu wanayoitumia ni propaganda za Katiba. Maana yake ni mbinu au taarifa inayolenga kupotosha umma ambayo inatumiwa na makundi ya watu ambayo yanapinga Katiba ili kuwashawishi wananchi waamini hakuna umuhimu wa mabadiliko ya Katiba", , ameeleza.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mchambuzi wa masuala ya siasa, Deus Kibamba, amesema Katiba ya sasa imekusanya mamlaka makubwa ya utawala na maamuzi ya nchi kwa Rais, hali anayosema imekuwa miongoni mwa mambo yanayolikwamisha Taifa.
Kibamba amesema hayo wakati akizungumza katika mjadala wa mezani kwenye Kongamano la Bavicha la Maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani jijini Dodoma.
Amesema pamoja na Ibara ya 8 ya Katiba kueleza kuwa wananchi ndio msingi wa mamlaka yote, michakato inayopaswa kuwawezesha wananchi kutumia mamlaka hayo imekuwa ikichezewa.
“Jambo ambalo limetukwamisha hivi sasa, Katiba hii imepindua mamlaka yote juu ya utawala wa nchi yetu na maamuzi ya nchi yetu.”
Kibamba amesema kuna haja ya kutekeleza mabadiliko yatakayogawa mamlaka katika vyombo mbalimbali ili kuhakikisha mamlaka hayajikiti sehemu moja.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Rais wa Chama cha Sheria Tanganyika (TLS), Wakili Boniface Mwabukusi amehoji kauli ya Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt. Emmanuel Nchimbi iliyowataka Watanzania kupambania Katiba Mpya, akisema serikali ndiyo yenye wajibu wa kuanzisha mchakato huo kwa mujibu wa sheria.
Mwabukusi ameyasema hayo wakati akizungumza katika mjadala wa mezani kwenye Kongamano la Bavicha, lililofanyika jijini Dodoma katika kuadhimisha Siku ya Vijana Duniani.
Amesema kauli ya kuwataka Watanzania “wapambane” haikuwatendea haki, kwa kuwa Serikali inafahamu taratibu za kisheria zinazopaswa kufuatwa ili kuanza mchakato wa Katiba Mpya.
“Mimi sidhani kama ile kauli ya Makamu wa Rais ilitutendea haki kutuambia tupambanie Katiba Mpya, kwa sababu yeye ni Serikali, na ili tuanze utaratibu wa Katiba Mpya wanajua utaratibu wa kisheria wa nini cha kufanya.”This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Rosemary Mwakitwange amewataka vijana kushiriki kikamilifu katika mchakato wa kujenga Katiba bora, akisisitiza kuwa Katiba hiyo inapaswa kuzingatia maisha na maslahi ya kizazi cha vijana.
Mwakitwange ameyasema hayo wakati wa majadiliano kwenye Kongamano la BAVICHA katika maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani jijini Dodoma.
Amesema vijana wanapaswa kuwa na ushiriki wa moja kwa moja katika mijadala na maamuzi yanayohusu mustakabali wa nchi, badala ya kutegemea kuwakilishwaThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Wakili Boniface Mwabukusi, amesema Katiba inapaswa kuanzisha taasisi imara za uwajibikaji zitakazolazimisha Serikali kupanga na kutekeleza mipango inayoakisi mahitaji ya jamii.
Mwabukusi ameyasema hayo wakati wa majadiliano kwenye Kongamano la BAVICHA katika maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani jijini Dodoma.
Amesema utekelezaji wa uwajibikaji utawezekana ikiwa kutakuwa na Bunge huru lisilodhibitiwa na chama, pamoja na taasisi za ukaguzi zitakazokuwa na mamlaka madhubuti ya kuwawajibisha wahusika wa makosa ya matumizi ya rasilimali za umma.
“Katiba ndiyo ingeleta taasisi za uwajibikaji ambazo zingeilazimisha Serikali kupanga mipango inayoakisi hitaji la jamii. Hilo litawezekana tukiwa na Bunge huru lisilodhibitiwa na chama,” amesema.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Wakili Boniface Mwabukusi, amesema Katiba inapaswa kuhakikisha mwananchi anakuwa na haki zaidi juu ya ardhi, akieleza kuwa sehemu kubwa ya Watanzania wanategemea ardhi kama chanzo cha ajira na kipato.
Mwabukusi ameyasema hayo wakati wa majadiliano kwenye Kongamano la BAVICHA katika maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani jijini Dodoma, akizungumzia umuhimu wa Katiba katika kulinda haki za wananchi.
Amesema Katiba ndiyo inayoweka msingi wa nani anamiliki ardhi, huku akieleza kuwa takribani asilimia 80 ya Watanzania wanategemea ardhi katika shughuli zao za ajira na uzalishaji.
“Katiba ndiyo inayosema nani ni mmiliki wa ardhi, ambayo Tanzania asilimia 80 ya watu ajira yao ipo kwenye ardhi. Kama huwezi ukamiliki njia kuu ya uchumi ambayo ni ardhi, utakuwaje na uhakika wa ajira yako?” amesema.
Mwabukusi amesema hakubaliani na kifungu kinachosema Rais anamiliki ardhi kwa niaba ya wananchi kama mdhamini, akisisitiza umuhimu wa mwananchi kuwa na haki ya moja kwThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Naibu Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Bukombe, Dkt. Doto Biteko, amesema Tanzania imepiga hatua kubwa katika utekelezaji wa Ajenda ya Nishati Safi ya Kupikia, huku akisisitiza kuwa ni wajibu wa kila Mtanzania kuhakikisha mafanikio yaliyopatikana yanaendelea kuwa endelevu.
Dkt. Biteko amesema hayo wakati akishiriki mjadala kuhusu “Uongozi wa Kimkakati wa Tanzania katika Kuharakisha Mabadiliko ya Nishati Endelevu na Jumuishi”, uliofanyika katika Mdahalo wa Nishati Safi ulioandaliwa na Taasisi ya Mwanamke Initiative Foundation (MIF), Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar.
Amesema uwepo wa Mkakati wa Taifa wa Nishati Safi ya Kupikia ni sehemu ya jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye ameendelea kuipa msukumo ajenda hiyo katika ngazi mbalimbali za uongozi wake na kuifikisha hadi katika majukwaa ya kimataifa.
Dkt. Biteko amesema umuhimu wa kuendelea kuipa kipaumbele ajenda hiyo unatokana na ukubwa wa athari za matumizi ya nishati isiyo safi ya kupikia, ikiwemo uharibifu wa mazingira unaosababishwa na matumizi ya kuni na mkaa, ambapo takribani hekta 470,000 za misitu hupotea kila mwaka nchini.
Aidha, amesema zaidi ya watu 33,000 hupoteza maisha kila mwaka kutokana na magonjwa yanayohusishwa na uchafuzi wa hewa wakati wa kupika, hali inayoonesha umuhimu wa kuongeza kasi ya mpito kuelekea matumizi ya nishati safi.
Ameongeza kuwa matumizi ya nishati isiyo safi yana athari za kijinsia, hususan kwa wanawake ambao hutumia muda mwingi kutafuta kuni badala ya kushiriki kikamilifu katika shughuli za uzalishaji na maendeleo ya kiuchumi.
Amesema athari hizo pia zinawagusa watoto, ambapo baadhi yao hukosa muda wa kutosha wa kuhudhuria masomo kutokana na kulazimika kusaidia familia zao kutafuta kuni kwa ajili ya kupikia.
Katika mjadala huo, Dkt. Biteko amesisitiza umuhimu wa kufanya tathmini za mara kwa mara ili kubaini kiwango cha uendelevu wa matumizi ya nishati safi ya kupikia, hususan baada ya wananchi kuwezeshwa kupata teknolojia na miundombinu husika.
Amesema tathmini hizo zitasaidia Serikali na wadau kubaini changamoto zilizopo, kupima matokeo yaliyofikiwa na kuweka mikakati madhubuti zaidi ya kuendeleza matumizi ya nishati safi ya kupikia nchini.
Pia, Dkt. Biteko ameipongeza Taasisi ya Mwanamke Initiative Foundation (MIF) kwa kuwa miongoni mwa taasisi zinazochangia utekelezaji wa Ajenda ya Nishati Safi ya Kupikia kupitia shughuli mbalimbali, ikiwemo kusaidia upatikanaji wa miundombinu pamoja na kuendesha midahalo inayowakutanisha wadau kujadili namna bora ya kuharakisha matumizi ya nishati safi, salama na endelevu nchini. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mchambuzi wa masuala ya siasa, Deus Kibamba, amesema Tanzania haiwezi kupata Katiba Mpya kwa kusubiri mabadiliko yatokee yenyewe, akisisitiza kuwa kutahitajika msukumo wa ubunifu kutoka kwa wananchi.
Akizungumza wakati wa majadiliano ya mada kwenye Kongamano la BAVICHA katika maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani jijini Dodoma, Kibamba amesema hali iliyopo haiwezi kubadilika kwa “kilele mama”
Amesema kila mara Tanzania inapokaribia kupata Katiba Mpya, watu wanaonufaika na mfumo uliopo huingiwa na hofu kwamba maslahi yao yanaweza kubadilika.
“Lakini kila mara tunapokaribia kupata Katiba Mpya, wale wanaokula unono wana wasiwasi kama unono ule utaendelea,” amesema.
Kibamba amesema hatua ya kwanza katika kufikia mabadiliko hayo ni kutuliza presha iliyopo nchini kufuatia matukio ya Oktoba 29, akieleza kuwa hali hiyo imeleta hofu kwa watawala na wananchi, hususan kutokana na kupoteza ndugu.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mchambuzi wa masuala ya siasa, Deus Kibamba, amesema Tanzania imekuwa ikikabiliwa na changamoto ya watu waliokuwepo kwenye utawala tangu wakati wa uhuru ambao hawataki mabadiliko ya kweli, akisema hali hiyo imekuwa miongoni mwa sababu za kushindwa kupatikana kwa Katiba Mpya.
Kibamba ameyasema hayo wakati wa majadiliano ya mada kwenye Kongamano la BAVICHA katika maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani yanayofanyika jijini Dodoma.
Amesema madai ya Katiba Mpya yalianza tangu mwaka 1961, akieleza kuwa wakati huo kulikuwa na watu ambao hawakukubaliana na wazo la Tanzania kukabidhiwa Katiba na wakoloni.
“Madai ya mwanzo ya Katiba Mpya ilikuwa ni mwaka 1961, wako ambao hawakukubaliana kwamba tukabidhiwe Katiba na mkoloni,” amesema Kibamba.
Aidha, amedai kuna dalili za kufutwa kwa baadhi ya historia ya Tanzania, akitoa mfano wa kitabu alichodai kimeandikwa hivi karibuni na kinachotaka kuaminisha vijana kuwa historia ya Zanzibar inaanza mwaka 1964, badala ya kutambua historia yake ya uhuru wa mwaka 1963.
“Kuna dalili za kufuta historia, kuna kitabu kimeandikwa hivi karibuni ambacho kinataka kufuta kwamba Zanzibar haikupata uhuru mwaka 1963, kinataka kuaminisha nyie vijana kwamba historia ya Zanzibar inaanza mwaka 1964,” amesema.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA bara, John Heche akiwasili katika Maadhimisho ya siku ya Vijana Duniani katika ukumbi wa vijana jijini DodomaThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA na Mlezi wa chama hicho Kanda ya Kati, Godbless Lema, amewataka vijana wa chama hicho kuwa makini katika kauli na matendo yao, akisisitiza umuhimu wa mshikamano na tabia njema katika harakati za kisiasa.
Lema amesema vijana wengi ni miongoni mwa watu waliopotea na waliopo magerezani, akieleza kuwa taifa limepoteza vijana wengi.
Akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani yanayoandaliwa na Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) jijini Dodoma, Lema amesema tofauti kati ya vijana wa CHADEMA na CCM inapaswa kuonekana katika tabia na mienendo yao.
Amesema lengo la CHADEMA kuwaondoa CCM madarakani halipaswi kujengwa katika chuki, bali katika kutofautiana na mienendo ya uongozi wa chama hicho.
Lema ameonya kuwa vijana wa CHADEMA wanapaswa kujifunza kutokana na makosa ya wengine ili wasije wakaingia madarakani na kuanzisha utawala ambao utakuwa mbaya kuliko waliowatoa.
Amesema vijana wanapaswa kuwa na mshikamano na kuwa makini kabla ya kuanza kuwashambulia viongozi wenzao, akiwataka kutofanya vitendo ambavyo vinaweza kuwafanya “wacheze ngoma ya Serikali.”This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Katika mwendelezo wa maswali ya Dodoso ya Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu kwenye shauri la uhaini linalomkabili ambalo linaendelea Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam mbele ya majaji watatu wakiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru Lissu amehoji kwa nini hakutafutwa kuulizwa maana ya maneno ambayo ameshtakiwa kwayo.
Lissu amemhoji shahidi wa 16 kwa mashahidi wa Jamhuri ACP Amini Mahamba ambaye alikuwa kiongozi wa timu ya upelelezi iliyopeleleza jalada la uhaini la Lissu lakini pia akiwa mpelelezi kwenye matukio ya Oktoba 29, 2025.
Lissu: Waeleze Majaji baada ya kutoa hotuba yangu April 3, 2025 kama wewe na Jeshi la Polisi mlichukua hatua yoyote ya kunitafuta kuniuliza haya maneno kukinukisha kuuvuruga uchaguzi yana maana gami
Shahidi: Sio kweli
Lissu: Hamkutafuta ufafanuzi wa hayo maneno yangu…nitakuwa sahihi au si sahihi nikisema kwamba kwa miaka yote 35 'no reform no election' ilikuwa ni msimamo sahihi katika mazingira ya aina hii
Shahidi: Haukua sahihi
Lissu: (Akirejea ripoti ya Jaji Chande Ukurasa wa 11 juu ya katiba mpya akidai kuwa hata Tume ya Jaji Chande iliafiki vichochezi vya vurugu za Oktoba 29, ilikuwa katiba mpya hivyo msimamo wa CHADEMA ni sahihi)
Shahidi: Sifahamu
Katika mwendelezo wa maswali hayo pia alihoji juu ya uwepo wa ripoti mbalimbali za taasisi za kimataifa kushiniliza kutaka kuachiwa kwa kwake iwapo ACP Mahamba anafahamu.
Lissu alihoji kuachiwa kwa watu waliowahi kukamatwa na kushtakiwa ambao walidai kuhamasika na hotuba yake ya April 3, 2025 ambapo watu hao katika ushahidi wao mahakamani walieleza kuwa walikuwa wanakwenda kuzuia uchaguzi kwa kufanya vurugu ambazo zikitokea.
Shahidi ACP Mahamba alieleza kuwa watu hao walishtakiwa lakini waliachiwa kwa mujibu wa sheria.
Lissu: Ushahidi wako kuhusiana na wale mashahidi waliofichwa mliowatoa mikoani unakumbuka ulisema kwamba hao mashahidi waliofichwa ni watu ambao walikamatwa na Polisi kweli si kweli
Shahidi: Kweli
Lissu: Waeleze majaji kama wale waliosema wataenda kufanya vurugu na wakafanya kama kuna hata mmoja aliyechukuliwa hatua mpaka sasa.
Shahidi: Ni matukio mawili tofauti
Soma zaidi kwenye website yetu ya www.jambo.co.tz -
Jambo TV
@Jambotv_
Shahidi wa 16 wa Jamhuri katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu ACP Amini Mahamba amemaliza kutoa ushahidi wake leo Agosti 12, 2026 mbele ya Jopo la Majaji watatu wakiongozwa Jaji Dunstan Ndunguru na shauri limeahirishwa mpaka kesho Agosti 13, 2026 saa tatu asubuhi.
Shauri hilo lililopo Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam leo liliendelea kwa Lissu kumaliza maswali ya dodoso kwa shahidi kisha upande wa Jamhuri kuhoji maswali ya kusawazisha (Re-examination) kwa shahidi huyo.
Simulizi ya ushahidi kwa leo utaipata kwenye website yetu ya www.jambo.co.tz na Youtube yetu ya Jambo TV -
Jambo TV
@Jambotv_
Wakazi wa Mji wa Idlib kaskazini-magharibi mwa Syria wamejitokeza mitaani kusherehekea kufuatia uamuzi wa Mahakama nchini humo kumhukumu adhabu ya kifo aliyekuwa Rais wa nchi hiyo, Bashar al-Assad, pamoja na Maafisa wa ngazi ya juu wa utawala wake.
Picha na video zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii zinaonesha umati wa watu ukishangilia katika mitaa ya Idlib, huku wengine wakipanda juu ya magari, kuimba na kupiga vigelegele mara baada ya hukumu hiyo kusomwa.
Mahakama ya Syria imemhukumu kifo Assad bila yeye kuwepo mahakamani, baada ya kumpata na hatia ya makosa ya kivita na uhalifu dhidi ya binadamu wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoidhoofisha nchi hiyo kwa miaka mingi.
Assad alikimbilia nchini Urusi pamoja na familia yake kufuatia kupinduliwa kwa serikali yake mwezi Desemba 2024, hatua iliyohitimisha utawala wa familia yake uliodumu kwa miongo mitano.
Katika shauri hilo hilo, Mahakama pia imemhukumu adhabu ya kifo binamu wa Assad, Atef Najib, aliyekuwa Mkuu wa Usalama wa Kisiasa katika Jimbo la Deraa. Tofauti na Assad, Najib alionekana akiwa ndani ya kizimba cha mahakama wakati jaji akisoma hukumu yake, akiwa miongoni mwa maafisa wa ngazi ya juu kabisa wa utawala huo kufikishwa mahakamani na Serikali ya Mpito ya Syria.
Jimbo la Deraa ambalo Najib alikuwa akiliongoza kisiasa na kiusalama linatazamwa kama chimbuko la vuguvugu la mapinduzi nchini Syria.
Mnamo Machi 2011, kukamatwa na kuteswa kwa kundi la vijana walioandika ujumbe wa kupinga serikali kwenye kuta za mji huo kuliamsha hasira za wananchi. Ukandamizaji mkali uliotumiwa na vikosi vya usalama vya Najib na Assad dhidi ya waandamanaji hao uliwasha moto wa maandamano nchi nzima, kabla ya kugeuka kuwa vita kamili vya wenyewe kwa wenyewe vilivyosababisha vifo vya mamia ya maelfu ya raia.
Serikali ya Mpito ya Syria, iliyoingia madarakani baada ya kuanguka kwa utawala huo, ilianza rasmi mchakato wa kuwashtaki maafisa wote waliohusika na uhalifu chini ya utawala wa familia ya Assad mapema mwaka huu. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Meneja wa Wakala wa Vipimo (WMA) Mkoa wa Dodoma, Said Ibrahim ameendelea na ziara ya kutoa elimu kwa wafanyabiashara pamoja na kukagua vipimo vinavyotumika katika biashara ya kuuza maji ya kunywa mtaani na vile vinavyotumika kwenye kumbi za mazoezi (Gym) jijini Dodoma tarehe 11 Agosti, 2026.
Katika ziara hiyo, Said ametembelea maeneo mbalimbali yanayofanya biashara hizo, ikiwemo Makole, Makulu, Hazina, Wajenzi, Maili Mbili, Nkuhungu na Nyerere Square, kwa lengo la kujiridhisha kuwa vipimo vinavyotumika maeneo hayo vimehakikiwa na WMA.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Said amesema ukaguzi huo unaenda sambamba na utoaji wa elimu kwa wafanyabiashara kuhusu umuhimu wa kutumia vipimo sahihi na vinavyokidhi vigezo.
Amesema WMA imejiridhisha kuwa mashine za kuuza maji ya kunywa zilizotembelewa zinatoa vipimo sahihi kulingana na thamani ya fedha aliyotoa na ujazo wa maji ambao anauhitaji.
Aidha, katika kumbi za mazoezi, WMA imekagua vifaa mbalimbali vinavyohusiana na uzito na kujiridhisha kuwa vifaa hivyo viko sahihi, hatua inayolenga kuhakikisha usalama wa watu wanaotumia huduma hiyo ya mazoezi.
Bw. Said amesisitiza umuhimu wa wafanyabiashara kuhakikisha vifaa vyao vinaendelea kuwa katika hali inayokidhi matakwa ya sheria, huku wananchi wakihimizwa kuwa makini na kuuliza pale wanapokuwa na mashaka kuhusu usahihi wa vipimo wanavyotumia.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
-
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia Jumuiya yake ya Wazazi kimeomba viongozi na Maaskofu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) kuingilia kati na kutumia nafasi yao ya kidini kuwaombea na kuwashawishi viongozi wa CHADEMA ili waweze kuweka pembeni kile walichokiita ukaidi na kuitikia wito wa kurejea kwenye meza ya maridhiano ya kisiasa.
Wito huo umetolewa Agosti 11, 2026 na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa, Ally Hapi, wakati akizungumza na wanachama wa CCM na wakazi wa Kilosa Mjini, mkoani Morogoro, kufuatia mkutano uliofanyika Agosti 10, 2026, Ikulu ya Chamwino Dodoma, kati ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Maaskofu wa TEC.
Akipongeza hatua ya Rais Samia na Maaskofu wa Katoliki kukutana na kujadili masuala ya kitaifa, Hapi alisisitiza kuwa TEC imeonyesha mfano wa kuigwa wa ukomavu wa kidemokrasia unaopaswa kufuatwa na vyama vya upinzani:
“Maaskofu TEC, waombeeni CHADEMA. Mungu awasaidie pepo ya ukaidi iwatoke, waende kwenye meza ya maridhiano,” amesema Hapi.
Pamoja na ombi hilo la CCM, msimamo wa sasa wa CHADEMA kupitia viongozi wake wakuu umekuwa ukisisitiza kuwa hawatashiriki katika mchakato wowote wa maridhiano na Serikali au CCM bila kuwepo kwa mpatanishi huru wa kimataifa asiyefungamana na upande wowote, kuachiliwa Mwenyekiti wa chama hicho taifa Tundu Lissu na kuwepo kwa ukweli na uwajibikaji kutokana na matukio ya Oktoba 29, 2026.
Hata hivyo hivi karibuni, Katibu Mkuu wa CHADEMA John Mnyika alisema kuwa viongozi wa dini nchini wanaweza kuongoza mchakato huo kama wapatanishi rasmi wa ndani endapo pande zote zitakubaliana.
Kauli ya Hapi imesukumwa na kikao cha Agosti 10, 2026, ambapo Rais Samia alikutana na Maaskofu wa TEC Ikulu ya Chamwino. Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Bakari Machumu, mazungumzo hayo yalilenga kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na Kanisa Katoliki, kujadili amani, mshikamano, na masuala yanayogusa siasa, imani, na maendeleo ya jamii na kukumbusha nafasi ya madhehebu ya dini katika kulea jamii yenye maadili na uwajibikaji.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwenyekiti wa Makatibu wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Basil Lema, amesema chuki na migogoro ya kisiasa imekuwa ikitawala siasa za Tanzania, hali inayowafanya Wananchi kushindwa kutambua adui wa kweli.
Akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Vijana yaliyofanyika Jimbo la Segerea, Lema amesema tofauti za Vyama zimekuwa chanzo cha migawanyiko miongoni mwa Watanzania, huku akisisitiza kuwa “adui si CCM, bali ni kikundi kidogo cha watu” wanaonufaika wakati Wananchi wakiwa katika migogoro.
Amesema wakati Wananchi na Vyama vya Siasa wakiendelea kuzozana na kugawanyika, kundi hilo linaendelea kutumia nafasi hiyo kujinufaisha na kupora rasilimali za nchi.
Maadhimisho hayo yaliyobeba kaulimbiu “Vijana na Demokrasia Kidigitali,” yamekuwa pia fursa kwa Lema kuwataka Vijana kuendelea kuhubiri haki, upendo na mshikamanoThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwenyekiti wa @ChademaTZ2 Tundu Lissu akikusanya nyaraka zake ajili ya kutoka Mahakamani na kurejeshwa gerezani baada ya kesi yake ya uhaini kuahirishwa kwa leo.
Leo Lissu ametumia siku nzima kuanzia majira ya saa tatu mpaka saa kumi na moja jioni(pakiwa na mapumziko ya lisaa limoja pekee) kwa kumhoji shahidi maswali ya dodoso shahidi wa 16 ACP Amini Mahamba ambaye alikuwa kiongozi wa upelelezi katika shauri la uhaini la Lissu.
Shauri hilo lililopo mbele ya Jopo la Majaji watatu wakiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru litaendelea kesho saa tatu asubuhi tena mahakamani hapo.
Soma zaidi kuhusu maswali ya dodoso na ushahidi katika website yetu ya www.jambo.co.tz au sikiliza katika YouTube yetu ya Jambo TV.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Global Education Link (GEL) imewakabidhi nyaraka rasmi za safari wanafunzi 387 wa Kitanzania wanaotarajia kwenda kuendelea na masomo ya elimu ya juu nchini China na India, huku wakihimizwa kutumia fursa hiyo kupata zaidi ya shahada kwa kujenga maarifa, ujuzi, teknolojia, mitandao ya kimataifa na uwezo wa kujitengenezea fursa za maisha.
Ukabidhi huo umefanyika kupitia mikutano miwili maalumu iliyofanyika Agosti 10 na 11, 2026 katika Ukumbi Mkuu wa Makao Makuu ya Global Education Link, Dar es Salaam, na kuhudhuriwa pia na wazazi na walezi wa wanafunzi hao.
Kati ya wanafunzi hao, 198 wanaelekea nchini China na 189 wanaelekea nchini India kwa ajili ya kuanza masomo katika vyuo mbalimbali vya elimu ya juu.
Wazazi na walezi waliohudhuria mikutano hiyo kwa ajili ya kushuhudia ukabidhi wa nyaraka na kupata maelekezo kuhusu safari na maisha ya watoto wao watakapokuwa nje ya nchi.
Lengo kuu la mikutano hiyo lilikuwa kuwakabidhi wanafunzi nyaraka muhimu za safari ambazo zimekamilishwa na GEL kama sehemu ya huduma inayofanywa na taasisi hiyo katika hatua mbalimbali za maandalizi yao, zikiwemo pasipoti, visa, tiketi za ndege, NOC (No Objection Certificate), cheti au kijitabu cha chanjo ya homa ya manjano (Yellow Fever Certificate) pamoja na nyaraka nyingine zinazohitajika na mamlaka husika kulingana na nchi, chuo na masharti ya safari ya mwanafunzi katika chuo husika.
Mbali na kukabidhiwa nyaraka hizo, wanafunzi pamoja na wazazi na walezi wao walipata maelekezo ya mwisho kuhusu taratibu za safari, uhamiaji, mazingira ya vyuo, makazi, bima ya afya, usalama, matumizi ya fedha, nidhamu na namna ya kukabiliana na mazingira mapya watakapofika katika nchi wanazokwenda.
Mtoa mada mkuu katika mikutano hiyo alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Global Education Link, Bw. Abdulmalik Mollel, akishirikiana na wawakilishi wa vyuo kutoka China na India waliotoa ufafanuzi kuhusu masomo, huduma za vyuo na maisha ya mwanafunzi wa kimataifa.
Global Education Link ni wakala wa vyuo vikuu vya nje ya nchi mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 19 katika kusaidia wanafunzi wa Kitanzania pamoja na wazazi na walezi wenye watoto wenye ndoto ya kupata elimu ya juu nje ya nchi.
Katika kipindi hicho, taasisi hiyo imekuwa ikitoa mwongozo katika hatua mbalimbali kuanzia ushauri wa kielimu, uchaguzi wa programu na chuo, maombi ya udahili, maandalizi ya nyaraka, visa, safari na maandalizi ya mwanafunzi kabla ya kuondoka nchini.
Akizungumza katika mikutano hiyo, Mollel aliwataka wanafunzi kutokwenda China na India kwa lengo la kupata cheti au shahada pekee, bali kutumia mazingira ya vyuo watakavyosoma kujenga uwezo mpana utakaowasaidia baada ya kuhitimu.
Alisema kwenda kusoma nje ya nchi kunamfungulia mwanafunzi mazingira mapya yenye teknolojia, maabara, warsha, vituo vya ubunifu, wataalamu pamoja na wanafunzi kutoka mataifa mbalimbali, hivyo ni jukumu la mwanafunzi mwenyewe kutumia fursa hizo kwa manufaa yake na Taifa.
Aliwataka vijana hao kwenda zaidi ya masomo yao ya darasani kwa kutembelea maabara, warsha na vituo vya ubunifu na kujifunza kwa vitendo namna teknolojia na bidhaa mbalimbali zinavyozalishwa na kutumika katika kutatua changamoto za jamii.
Akitolea mfano mwanafunzi anayesomea Business Administration, alisema haipaswi kutosha kujifunza nadharia za usimamizi wa biashara pekee, bali mwanafunzi huyo anapaswa kutafuta maarifa kuhusu bidhaa, teknolojia, uzalishaji na mifumo mbalimbali ya viwanda ili aweze kuelewa kile anachoweza kukisimamia au kukigeuza kuwa biashara. -
Jambo TV
@Jambotv_
Katika mwendelezo wa maswali ya dodoso kwa ACP Amini Mahamba katika shauri la uhaini linalomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo @ChademaTZ2 Tundu Lissu, shahidi amedai kuwa mshtakiwa ndiye aliyechapisha video katika YouTube ya Jambo TV.
Shahidi huyo wa 16 katika kesi hii ya uhaini wakati akitoa ushahidi wake wa awali jana Agosti 10 aliieleza Mahakama kuwa alipewa jukumu la kusimamia na kuratibu upelelezi wa jalada la uhaini lililokuwa katika ofisi ya Naibu Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Kanda Maalum Dar es Salaam.
Leo akihojiwa maswali hayo ya Dodoso ACP Mahamba amekiri kuwa katika maelezo ya mashahidi wengine katika kesi hiyo akiwemo P na P1 walirusha mbashara maudhui hayo.
Lissu: Wewe si ndiye uliyesema nimechapisha hiyo video mtandaoni?
Shahidi: Ni mimi.
Lissu: Unafahamu maana ya neno kuchapisha mtandaoni?
Shahidi: Naifahamu.
Lissu: (Akisoma tafsiri hiyo kwenye sheria ya makosa ya mtandao) kuchapisha maana yake ni kusambaza, waeleze majaji kama mimi ndiye niliyesambaza video kwenye Youtube ya Jambo TV.
Shahidi: Ni wewe.
Lissu: Kuchapisha maana yake ni ‘transmitting’ waeleze majaji kama ni ushahidi wako kwamba mimi ndiye ‘niliyetransmitt’ hiyo video kwenye mtandao wa Jambo TV.
Shahidi: ndiyo, ni wewe.
Lissu: Waeleze majaji mama mimi nili-disseminate (kuitoa) hiyo video na ku-circulate na ku-deliver.
Shahidi: Ni wewe.
Lissu: Waeleze majaji kama mimi ni mfanyakazi wa au Mkurugenzi au Mtumishi wa Jambo TV.
Shahidi: Sina uhakika
Lissu: Waeleze majaji kama mimi ni mpiga picha au mtangazaji wa Jambo TV.
Shahidi: Sina uhakika
Lissu: Waeleze majaji kama mimi nina access kwa maana ya kuwa na password (nywila) ya kuingia kwenye mtandao wa Jambo TV, Youtube.
Shahidi: Sina uhakika -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Agosti 11, 2026, amewapongeza wananchi wa Zanzibar kwa kuonesha ukomavu mkubwa wa kisiasa na kudumisha amani wakati wa mchakato wa uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka 2025.
Akizungumza na wananchi na wanaCCM katika eneo la Kisonge visiwani humo, Dkt. Samia amesema kuwa Zanzibar imepiga hatua kubwa kwani uchaguzi wa mwaka huo ulifanyika bila kuwepo kwa vitendo vya uvunjifu wa amani au raia kuumizwa.
Katika hali ya kuonesha kuwa ushindani wa kisiasa haupaswi kuwa chanzo cha uhasama, Dkt. Samia amefananisha siasa na ushindani wa klabu kongwe za soka nchini, Simba na Yanga. Amebainisha kuwa baada ya ushindani, jambo la msingi ni kukaa pamoja na kujenga nchi.
“Nawapongeza na saluti Wazanzibari mwaka huu. Tumefanya uchaguzi hakuna aliyenyukuliwa... Tumekwenda tumefanya kwa amani na utulivu... sisi wote ni wa nchi hii wa visiwa hivi na lazima tuishi pamoja kwa maendeleo yetu kwa hiyo kushindana kumo hata Simba na Yanga si wanashindana,” amesema Dkt. Samia
Aidha, Dkt. Samia amewataka wananchi kutumia fursa na mazingira wezeshi ya biashara na uwekezaji yanayowekwa na serikali ili kujiletea maendeleo binafsi na ya jamii kwa ujumla. Amesisitiza kuwa kulinda Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar siyo tu kupiga kura, bali ni kushiriki kikamilifu katika miradi ya maendeleo.
Halikadhalika, ametoa wito kwa Wazanzibari kuendelea kuishi kwa upendo na mshikamano ili kuvutia watalii na wawekezaji zaidi, jambo ambalo litachochea ukuaji wa uchumi wa visiwa hivyo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katika jitihada za kuimarisha mazingira ya uwekezaji na kuvutia mitaji zaidi nchini, Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) na kampuni ya Vodacom Tanzania PLC, leo Agosti 11, 2026, zimesaini Mkataba wa Makubaliano (MoU) wa miaka miwili kwa ajili ya kuunganisha huduma za uwekezaji na masuluhisho ya kisasa ya kiteknolojia.
Ushirikiano huo unalenga kutoa huduma bora kwa wawekezaji kupitia miundombinu ya kidijitali kama vile teknolojia ya mtandao wa vifaa (Internet of Things - IoT), internet isiyohamishika, na mifumo ya malipo ya kielektroniki ili kurahisisha uwekezaji.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa TISEZA, Gilead Teri, ameeleza kuwa ushirikiano huo unalenga kuifanya Tanzania kuwa nchi yenye muitikio rafiki kwa wawekezaji kwa kutumia utaalamu wa Vodacom katika sekta ya mawasiliano.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Vodacom Business, Nguvu Kamando, amewahakikishia wawekezaji kuwa kupitia ushirikiano huu, wataweza kupata huduma zilezile za kiteknolojia zinazopatikana katika mataifa yaliyoendelea kwasababu Vodacom ni sehemu ya familia ya kimataifa ya Vodafone.
Aidha, Kamando amebainisha kuwa Vodacom itatoa huduma za ulinzi dhidi ya udukuzi wa mitandaoni na mifumo ya malipo isiyotumia fedha taslimu kwa wawekezaji wakubwa na wadogo ili kuongeza ufanisi na usalama wa miamala.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Katika jitihada za kuimarisha mazingira ya uwekezaji na kuvutia mitaji zaidi nchini, Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) @InvestTanzania na kampuni ya Vodacom Tanzania PLC, leo Agosti 11, 2026, zimesaini Mkataba wa Makubaliano (MoU) wa miaka miwili kwa ajili ya kuunganisha huduma za uwekezaji na masuluhisho ya kisasa ya kiteknolojia.
Ushirikiano huo unalenga kutoa huduma bora kwa wawekezaji kupitia miundombinu ya kidijitali kama vile teknolojia ya mtandao wa vifaa (Internet of Things - IoT), internet isiyohamishika, na mifumo ya malipo ya kielektroniki ili kurahisisha uwekezaji.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa TISEZA, Gilead Teri, ameeleza kuwa ushirikiano huo unalenga kuifanya Tanzania kuwa nchi yenye muitikio rafiki kwa wawekezaji kwa kutumia utaalamu wa Vodacom katika sekta ya mawasiliano.
“Lengo la ushirikiano wetu ni kuendelea kuimarisha mazingira ya uwekezaji nchini lakini pia kuunganisha dhamana ambayo sisi tunayo ya kukuza, kuratibu na kuwezesha uwekezaji pamoja na utaalam ambao wenzetu wanao kwenye masuala ya teknolojia na masuluhisho ya kidijiti,” amesema Teri
Ameongeza kuwa ushirikiano huu ni utekelezaji wa maono ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa tarehe 3 Agosti, 2026, akisisitiza kuwa sekta binafsi ndiyo ufunguo wa kufikia uchumi wa dola trilioni moja ifikapo mwaka 2050.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Vodacom Business, Nguvu Kamando, amewahakikishia wawekezaji kuwa kupitia ushirikiano huu, wataweza kupata huduma zilezile za kiteknolojia zinazopatikana katika mataifa yaliyoendelea kwasababu Vodacom ni sehemu ya familia ya kimataifa ya Vodafone.
“Wawekezaji wanatakiwa wajue chochote walichoweza kukifanya wakiwa Ureno basi kinaweza kufanyika Tanzania. Chochote alichoweza kukifanya kwenye kiwanda chake kilichopo Ujerumani basi kinaweza kufanyika Tanzania kwa sababu sisi ni familia moja,” amesisitiza Kamando.
Aidha, Kamando amebainisha kuwa Vodacom itatoa huduma za ulinzi dhidi ya udukuzi wa mitandaoni na mifumo ya malipo isiyotumia fedha taslimu kwa wawekezaji wakubwa na wadogo ili kuongeza ufanisi na usalama wa miamala. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga, amewataka watendaji wa Serikali na taasisi za udhibiti kuwa wawezeshaji wa biashara badala ya kuzifungia, akisema hatua hiyo ni muhimu katika kulinda mitaji na maslahi ya Wananchi.
Kapinga ametoa agizo hilo leo Agosti 10, 2026, wakati akizindua ghala la kuhifadhia mazao la Halmashauri ya Mji wa Masasi, lililopo Kata ya Mtandi lililo gharimu takribani Shilingi Milioni 921.
“Ukikuta kiwanda hakina mifumo mizuri usikifungie, kisaidie kiweze kurudi kwenye ramani; ukikuta mtu hana leseni ya biashara, msaidie apate leseni badala ya kumfungia biashara.”
Amesema mfanyabiashara anayekosa leseni asaidiwe kuipata, huku viwanda vyenye changamoto vikielekezwa kurekebisha kasoro badala ya kufungiwa, na ameagiza TBS kuwasaidia wajasiriamali wanaohitaji nembo na viwango vya bidhaa ili waendelee kuzalisha na kuuza.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Kenani Kihongosi, amesisitiza kuwa vijana ndio walinzi wa nchi, hivyo wanapaswa kulinda amani na utulivu ili waweze kushiriki katika shughuli za uzalishaji kwa maendeleo ya Taifa na familia zao.
Kihongosi ameyasema hayo leo Agosti 10, 2026, wakati akitoa mada katika Mafunzo ya Uongozi wa Seneti za Vyuo vya Kati na Vyuo Vikuu yanayofanyika katika Chuo cha Mafunzo Ihemi, mkoani Iringa.
Aidha, Kihongosi ametumia jukwaa hilo kukemea lugha chafu zinazotolewa dhidi ya Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika mitandao ya kijamii, huku akiwataka vijana kuwa mstari wa mbele kumtetea Rais na kutokaa kimya wanapoona kauli hizo.
Vilevile, amewataka vijana wa CCM ndani na nje ya Tanzania kulipa ada za uanachama, akieleza kuwa uhai na uimara wa Chama cha Mapinduzi unatokana na wanachama kutekeleza wajibu wao wa kulipa ada. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amekutana na kufanya mazungumzo na Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini Tanzania kupitia Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), katika Ikulu ya Chamwino, mkoani Dodoma.
Kwa mujibu wa taarifa ya Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Bakari S. Machumu, mazungumzo hayo yalilenga kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na TEC na kujadili masuala mbalimbali ya kitaifa yanayogusa jamii, ikiwemo siasa, imani na maendeleo, pamoja na umuhimu wa kuendelea kuimarisha amani, mshikamano na kujenga mustakabali mwema wa Taifa.
Aidha, mazungumzo hayo yaligusia nafasi ya madhehebu na viongozi wa dini katika kulea jamii yenye maadili mema, uwajibikaji na mshikamano, sambamba na mchango wao katika ustawi na maendeleo endelevu ya Taifa.
Taarifa hiyo imeeleza zaidi kuwa, Rais Samia amewashukuru Maaskofu hao kwa kuona umuhimu wa kukutana na kujadiliana naye masuala yenye tija kwa Taifa, huku akiwahakikishia dhamira yake ya kuendeleza utamaduni wa kushauriana na kuwashirikisha viongozi wa dini pamoja na makundi mbalimbali katika jamii kuhusu masuala muhimu ya kitaifa kila inapohitajika.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Agosti 10, 2026 amekutana na kufanya mazungumzo na Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini Tanzania kupitia Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), katika Ikulu ya Chamwino, mkoani Dodoma.
Kwa mujibu wa taarifa ya Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Bakari S. Machumu, mazungumzo hayo yalilenga kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na TEC na kujadili masuala mbalimbali ya kitaifa yanayogusa jamii, ikiwemo siasa, imani na maendeleo, pamoja na umuhimu wa kuendelea kuimarisha amani, mshikamano na kujenga mustakabali mwema wa Taifa.
Aidha, mazungumzo hayo yaligusia nafasi ya madhehebu na viongozi wa dini katika kulea jamii yenye maadili mema, uwajibikaji na mshikamano, sambamba na mchango wao katika ustawi na maendeleo endelevu ya Taifa.
Taarifa hiyo imeeleza zaidi kuwa, Rais Samia amewashukuru Maaskofu hao kwa kuona umuhimu wa kukutana na kujadiliana naye masuala yenye tija kwa Taifa, huku akiwahakikishia dhamira yake ya kuendeleza utamaduni wa kushauriana na kuwashirikisha viongozi wa dini pamoja na makundi mbalimbali katika jamii kuhusu masuala muhimu ya kitaifa kila inapohitajika. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Ally Hapi, ameeleza kuwa maendeleo ya nchi na usalama wake haviwezi kujengwa kwa malalamiko ya majukwaani, bali kwa viongozi kukaa pamoja kwenye vikao na kujenga maridhiano ya kifikra.
Hapi ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na wanachama wa CCM pamoja na wakazi wa Manispaa ya Morogoro, ambapo alisisitiza umuhimu wa viongozi wa vyama vya siasa nchini kutumia meza ya majadiliano kutafuta suluhu ya changamoto zinazolikabili Taifa.
Akifafanua dira ya Serikali ya Awamu ya Sita, Hapi alikumbusha kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amekuwa mstari wa mbele kuhamasisha viongozi wa vyama vyote vya siasa kushiriki katika mazungumzo ya wazi na maridhiano ya kitaifa.
Akizungumzia kauli iliyotolewa hivi karibuni na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Lissu, aliyewataka wanachama wake "asiwakute alipowaacha," Hapi amedai kuwa kauli hiyo iliashiria kushiriki maridhiano kwa maana ya kwamba njia sahihi ya kutatua kasoro za kisiasa au kiutawala ni kukaa mezani badala ya kuendelea kuibua taharuki kwenye majukwaa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Watanzania wameanza kunufaika na upatikanaji wa huduma za matibabu ya kibingwa na teknolojia za kisasa za afya nchini, hali inayopunguza kwa kiasi kikubwa gharama za usafiri, malazi, na visa za kufuata matibabu hayo nje ya nchi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Universal Medical Tourism, Dk. Sharif Mollel, amebainisha kuwa huduma hizo zinapatikana katika Hospitali ya SINO iliyopo Mikocheni, Jijini Dar es Salaam hospitali inayomilikiwa na wawekezaji kutoka nchini China.
Dk. Mollel ameeleza kuwa uwepo wa huduma hizo umeifanya Tanzania kuanza kupokea pia wagonjwa kutoka nchi za Afrika Mashariki na Ukanda wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), hatua inayojenga msingi wa nchi kuwa kitovu kuu cha utalii wa tiba (Medical Tourism) Barani Afrika.
Hospitali ya SINO inatoa huduma za uchunguzi na matibabu ya kibingwa kwa kutumia mitambo na teknolojia za kisasa ikiwemo CT Scan, MRI, na Ultrasound, ikijikita katika uchunguzi na matibabu ya matatizo ya mifupa, usimamizi wa changamoto za neva na uti wa mgongo, tiba za mfumo wa mkojo na mazoezi ya viungo na tiba za jadi za China ikiwemo huduma ya sindano maalumu (Acupuncture) kwa ajili ya usimamizi wa maumivu na misuli.
“Lengo letu ni kuona Watanzania wanapata huduma nyingi zaidi hapa nchini. Kama huduma inayohitajika inapatikana Tanzania, hakuna sababu ya mgonjwa kuanza na safari ya kwenda nje ya nchi,” amesema.
Dk. Mollel amesema kampuni hiyo pia inalenga kuendeleza ushirikiano kati ya madaktari wa Tanzania na wataalamu kutoka China kupitia kambi za matibabu na programu mbalimbali za kubadilishana ujuzi.
Amesema hatua hiyo inaweza kusaidia teknolojia na maarifa yanayoletwa nchini kubaki na kutumika kwa muda mrefu badala ya huduma kutegemea wataalamu wa nje pekee. -
Jambo TV
@Jambotv_
Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa @ChademaTZ2 Tundu Lissu itaendelea kesho Agosti 11, 2026 saa tatu asubuhi katika Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam ambapo ndipo shauri hilo linaposikilizwa.
Leo Agosti 10, 2026 Shahidi wa Jamhuri ACP Amini Mahamba alitoa ushahidi wake wa awali na baadae Lissu alianza kumhoji maswali ya dodoso(Cross Examination) kwa uchache huku akieleza kuwa atamhoji shahidi huyo katika maeneo 54 ambayo yeye anaona yana utata katika ushahidi uliotolewa na shahidi huyo ukilinganisha na maelezo yake aliyoandika.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Katika maelezo ya ushahidi wake ACP Amini Mahamba katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu, amedai kuwa mashahidi wa kesi hiyo walitishwa na wafuasi na wanachama wa CHADEMA katika mitandao ya kijamii wakiwaambia kuwa ‘watawasalimia’.
Leo Agosti 10, 2026 ACP Mahamba ametoa ushahidi wake mbele ya Jopo la Majaji watatu wakiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru ambapo ameieleza mahakama kuwa mashahidi hao walifikisha malalamiko hayo kwa Wakuu wa Upelelezi wa Mikoa mbalimbali nchini ambapo ndipo walipoandikia ushahidi huo.
Anaeleza anakumbuka mara baada ya Lissu kusomewa mashtaka April 10, 2025 na jalada la upelelezi lilirudishwa kwao kwa ajili ya kukamilisha upelelezi ambapo wakiendelea na zoezi hilo walipokea malalamiko kutoka kwa baadhi ya mashahidi kupitia Wakuu wa Upelelezi wa Mkoa kwamba wanaweza kupata madhara endapo watakuja kutoa ushahid mbele ya mshtakiwa.
Anaeleza kuwa matishio hayo wahusika waliyaona kupitia mitandao ya kijamii na wengi wao walikuwa wafuasi wa CHADEMA wakitamka maneno kwamba ‘watawadhuru mashahidi endapo wakienda kutoa ushahidi’ wakisema ‘watawasalimia endapo wakienda kutoa ushahidi wengine wakasema ‘watawaombea mabaya’.
Anaeleza kuwa walifanya upelelezi wakajiridhisha kama hayo malalamiko yana ukweli wakajaribu kupitia baadhi ya mitandao kwenye comments kulikuwa na vitisho kupitia Instagram, Facebook, tiktok.
Baada ya kuthibitisha yeye kama mpelelezi mkuu aliwasiliana na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kuhusu matishio lengo ikiwa ni kama kuna uwezekano wa kuombea ulinzi waombe na ofisi hiyo iliweka kiapo(alichoapa yeye ACP Mahamba) maalum cha maombi ya kinga kwa mashahidi ambao wanapitia hali ya matishio. -
Jambo TV
@Jambotv_
Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa @ChademaTZ2 Tundu Lissu inaendelea katika Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Dar es Salaam ambapo shahidi wa Jamhuri Kamishna Msaidizi wa Polisi(ACP), Amin Mahamba ametoa ushahidi wake mbele ya mahakama hiyo.
ACP Mahamba amesema anafanya kazi Makao Makuu Ndogo ya Jeshi la Polisi Ofisi ya Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai nchini( DCI), ofisi ambayo ipo Dar es Salaam katika Kitengo X kinashughulikia makosa ya mtandao na migogoro inayotishia usalama wa nchi huku akiwa na uzoefu wa miaka 26 kwani ameajiriwa mwaka 2000.
Akiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu Nassoro Katuga ameieleza mahakama namna alivyoweza kuongoza timu ya upelelezi juu ya jalada la uhaini la Tundu Lissu.
Shahidi ACP Mahamba mbele ya jopo la Majaji watatu wakiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru ameeleza kuwa kauli alizotoa Lissu katika video iliyochapishwa Youtube na Jambo TV ni kauli ambazo zilikuwa zinaitisha serikali.
Anaeleza kuwa April 8, 2025 baada ya kupewa maelekezo na ‘bosi’ wake DCP Ramadhan Ng’azi kuwa aende Ofisi ya Upelelezi Kanda Maalum Dar es Salaam kukutana na Naibu Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya jinai(Deputy ZCO) wa Kanda hiyo ACP George Bagyemu ambae alimkutanisha na timu ya upelelezi iliyomuonyesha video hiyo ya Lissu.
Anadai kuwa katika video hiyo Lissu alitamka akisema “wanasema kitu kimoja sahihi hapa msimamo huu unaashiria uasi ni kweli kwa sababu tutazuia uchaguzi, tutahamasisha uasi hiyo ndiyo namna ya kupata mabadiliko kwa sababu tunaenda kukinukisha sana sana. Huu uchaguzi tutauvuruga kwa sababu tunaenda kukinukisha vibaya sana“
Anaendelea kueleza kuwa yeye pamoja na timu yake waliona kwamba mshtakiwa Lissu alikuwa na nia ya kuitisha serikali ili itende kile anachotaka, kitendo cha kuitisha serikali kwa kuzuia uchaguzi kwa kuhamasisha uasi ndio uhaini wenyewe.
Soma zaidi kwenye website yetu ya www.jambo.co.tz -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Angellah Kairuki, leo Agosti 10, 2026, amewasilisha Ripoti ya Utendaji ya Robo ya Nne ya Mwaka wa Fedha 2025/26 ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), ikionesha mafanikio makubwa katika mapambano dhidi ya uhalifu wa mitandaoni.
Katika ripoti hiyo iliyochakata kipindi cha kuanzia Aprili hadi Juni 2026, takwimu zinaonesha kuwa matukio ya ulaghai yaliyoripotiwa yamepungua kwa asilimia 25.29 ikilinganishwa na robo iliyopita.
Waziri Kairuki amebainisha kuwa kupungua kwa matukio hayo kumetokana na upekuzi na ukaguzi wa kina uliofanywa na TCRA kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Mbeya, na Mara
Pamoja na mafanikio hayo, Waziri amewasihi wananchi kuendelea kuwa waangalifu na kutotoa namba zao za siri (PIN), OTP, au kubofya kiungo (link) kisichojulikana.
Aidha, amesema TCRA inaendelea na uhakiki wa usajili wa laini za simu (SIM card verification) ili kuhakikisha usalama wa watumiaji wote katika mazingira ya kidijitali yanayokua kwa kasi nchini TanzaniaThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
USHAHIDI WA ACP MAHAMBA: KAULI ZA LISSU ZILILENGA KUITISHA SERIKALI jambo.co.tz/ushahidi-wa-acp-mahakamba-kauli-za-lissu-alii… via @jambotv_
-
Jambo TV
@Jambotv_
Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu inayoendelea Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam imeahirishwa kwa lisaa limoja mpaka saa nane kwa ajili ya mapumziko.
Leo shahidi ACP Amini Mahamba ameanza kutoa ushahidi wake ambao bado hajamaliza kuutoa hivyo utaendelea baadae ushahidi wake.
Tutakuletea baadae simulizi nzima ushahidi. -
Jambo TV
@Jambotv_
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Tundu Lissu amelalamikia upande wa Jamhuri akidai kuwa umechelewesha mwenendo wa kesi ya uhaini inayomkabili kwa kutumia kufungua maombi ya marejeo katika Mahakama ya Rufani.
Leo Agosti 10, 2026 mara baada ya kuanza kwa kesi ya uhaini inayomkabili katika Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam mbele ya Jopo la Majaji watatu wakiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru, ambapo Lissu amedai kuwa kwa ucheleweshwaji huo kuna mtu atalipa.
“leo majaji ni siku ya 166 tangu tarehe 24 Februari(2026) wamekewenda Mahakama ya rufaa nimewashinda lakini tumerudi baada ya kupotezeana siku 166. Twendelee lakini itapofika siku itabidi tuzungumze hii kesi ya bure na huu ucheleweshaji wa bure uliofanywa na Mawakili na anayewatuma someone has to pay for this.” amesema Lissu
Kwa upande wa Jamhuri Wakili wa Serikali Mkuu Nassoro Katuga amejibu maelezo ya Lissu akisema kuwa sio sahihi na Mkurugenzi wa Mashtaka hana nia ya kuchelewesha kesi bali kilichotokea ni upande huo ulikuwa unatekeleza haki yake ya kisheria ya kuomba marejeo ya shauri Mahakama ya Rufani baada ya kuhisi kuna sehemu Majaji hawakuamua kwa usahihi.
“Haikuwa nia ya upande wa Jamhuri kuchelewesha kesi.Kuhusu kushinda na kushindwa, kushindwa kwa Wakili mwenye weledi ni jambo la kawaida” amesema Katuga
Baada ya hayo Jaji Dunstan Ndunguru alitaka kesi iendelee na sasa shahidi ambaye ni ACP Amini Mahamba anaendelea kutoa ushahidi wake. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Kufuatia kusambaa kwa picha mjongeo zikimuonesha kijana mmoja akiwa amenasa kwenye kibanda cha biashara katika eneo la Chadulu jijini Dodoma, Jambo TV imefika eneo la tukio na kuzungumza na baadhi ya mashuhuda ili kupata undani wa tukio hilo.
Kijana huyo anayetambulika kwa jina la Festo, anadaiwa kunasa kwenye kibanda hicho kwa tuhuma za kujaribu kufanya wizi.
Mama mwenye nyumba, anayefahamika kwa jina la Jesca Hennry, amesema baada ya kupata taarifa za tukio hilo alimpigia simu mpangaji wake na kumueleza kuhusu kijana huyo, ambapo alijibiwa kuwa huenda mtuhumiwa huyo alikuwa mwizi na kumshauri asihusike naye.
Jesca amesema baadaye waliwasiliana na polisi ili mtuhumiwa huyo aweze kutolewa katika kibanda hicho, lakini juhudi hizo zilishindikana hadi pale mmiliki wa kibanda hicho alipomtuma mdogo wake kufika eneo la tukio na kumtoa kijana huyo, ambaye baadaye aliondoka akiwa ameambatana na jeshi la polisi.
Aidha, Jesca amewataka vijana kuachana na vitendo vya wizi na badala yake kufanya kazi halali zitakazowasaidia kujikwamua kiuchumi na kujenga maisha yao.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Mtaa huo, Nobert Pangaselo, amesema mtuhumiwa huyo amepelekwa kituo cha polisi kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria, huku akiwataka vijana kuachana na tabia za udokozi na vitendo vingine vya uhalifu.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Viongozi waandamizi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo @ChademaTZ2 wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti Bara wa chama hicho @HecheJohn wapo ndani ya chumba cha Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam kwa ajili ya kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa chama hicho Tundu Lissu.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwenyekiti wa @ChademaTZ2 Tundu Lissu amefikishwa tayari Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam kwa ajili ya kesi ya uhaini inayomkabili ambayo itaendelea leo mara baada ya kusimama kwa siku 167.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Kada wa Chama cha ACT Wazalendo, Luhaga Mpina, ametoa wito kwa Watanzania na vyama vya upinzani kushikamana zaidi katika kipindi hiki, akiwataka wapinzani kuacha tofauti zinazoweza kuwagawa na kuwatoa kwenye jukumu lao la msingi.
Akizungumza jana Agosti 9, 2026 na Wanahabari jijini Dar es salaam, Mpina amesema vyama vya upinzani vinapaswa kuzingatia masuala muhimu yanayowahusu Watanzania badala ya kujibizana na kutengenezeana maneno.
“Ni lazima Watanzania tuendelee kushikamana kuliko wakati wowote. Hata vyama vya upinzani, wapinzani wenzangu nawaomba waache mambo hayo ya kutengenezeana maneno maneno. Mnaondoka kwenye jukumu la msingi, mnacheza ngoma ya mtawala. Acheni,” amesema Mpina.
Amesema Watanzania wana matarajio makubwa kwa vyama vya upinzani katika kutafuta suluhisho la changamoto zinazolikabili taifa.
“Watanzania wanatutegemea, wanategemea vyama vya upinzani kuwatoa hapa walipo,” amesema.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Kada wa chama cha ACT Wazalendo @ACTwazalendo Luhaga Joelson Mpina ni miongoni mwa waliofika Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam kufuatilia kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa @ChademaTZ2 Tundu Lissu ambayo leo itaendelea mahakamani hapo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Jumla ya wanafunzi 85 wanatarajiwa kuondoka nchini kuanzia tarehe 21 hadi 23 Agosti, 2026, kuelekea kwenye vyuo vikuu mbalimbali nchini India kupitia Wakala wa Elimu Nje ya Nchi wa Global Education Link (GEL).
Wanafunzi hao pamoja na wazazi wao walihudhuria mkutano wa maandalizi uliofanyika katika ofisi za GEL mwishoni mwa wiki, ambapo walipewa elimu kuhusu sheria za kuelimika nchini humo, ikiwemo masuala ya vibali, bima, na makazi, pamoja na kukabidhiwa visa, tiketi za ndege, na nyaraka rasmi za kupokelewa vyuoni.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa GEL, Abdulmalik Mollel, aliwataka wanafunzi hao kutambua kuwa soko la ajira duniani linahitaji zaidi ya ufaulu wa madarasani (GPA), akiwahimiza kujenga mtandao na wanafunzi kutoka mataifa mbalimbali ili kubaini fursa za kiuchumi.
Mollel alibainisha kuwa India ni mfano wa kuigwa katika sekta ya viwanda vidogo vidogo na teknolojia, na kwamba fursa hiyo inapaswa kutumiwa kuleta maarifa hayo nchini Tanzania.
“Tunahitaji GPA nzuri lakini pia huko kuna fursa nyingi sana, mtasoma na watoto wa matajiri wenye viwanda, tunataka muwe karibu na watu kama hao kutambua fursa ya wewe kupata kazi, siyo unamaliza halafu unakuja kuhangaika kutafuta kazi wakati huko kulikuwa na fursa,” alisema
Aidha, Mollel alieleza kuwa nchi za Ulaya zinalikabiliwa na uhaba mkubwa wa rasilimali watu kutokana na umri wa kustaafu, hivyo aliwashauri wanafunzi hao kujifunza lugha za ziada kama Kifaransa au Kijerumani ili kupanua wigo wa kupata ajira za kimataifa baada ya kuhitimu.
Mollel aliongeza kuwa GEL inapeleka zaidi ya wanafunzi 800 kila mwaka kusoma vyuo vya nje ya nchi, na kuanzia mwaka ujao, wakala huo utafungua rasmi kitengo cha kuunganisha wahitimu na fursa za ajira kupitia kampuni kubwa zinazotafuta wataalamu wa ndani na nje ya nchi. -
Jambo TV
@Jambotv_
Baada ya kusimama kwa muda wa siku 167 kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo @ChademaTZ2 Tundu Lissu itaendelea leo Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Dar es Salaam.
Kesi hii ilisimama kuanzia Februari 24, 2026 kutokana na Jamhuri kupitia Mkurugenzi wa Mashtaka nchini(DPP) kuwasilisha notisi ya rufaa juu ya mwenendo na maamuzi yaliyotolewa na Mahakama ya kukubaliana na mapingamizi ya Lissu kuhusu kutokukubaliwa kwa ushahidi wa ziada wa ACP Amini Mahamba ambaye alikuwa kiongozi wa timu iliyopeleleza matukio ya wakati wa uchaguzi mkuu 2025.
Lissu anashikiliwa gerezani toka alipokamatwa april 9, 2025 na kushtakiwa kwa uhaini April 10, 2025 pamoja na kosa la uchochezi.
Kesi hii ipo chini ya Jopo la Majaji watatu wakiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru ambapo tayari vikao vya namna ya kuendesha kesi hii vimeshakaliwa Agosti 5,2026 kati ya Mahakama, Jamhuri, Lissu na mawakili Watafiti) wa Lissu.
Ikumbukwe kesi hii kwa sasa ipo katika hatua ya ushahidi ambapo tayari mashahidi ambao ni Askari Polisi na wasio askari(mashahidi wanaolindwa) wamekwishakutoa ushahidi wao. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkazi wa Kata ya Mtawanya, Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara Mikindani mkoani Mtwara, Furaha Chilambo amejifungua watoto watano kwa wakati mmoja katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini iliyopo mkoani humo.
Furaha amejifungua kwa njia ya upasuaji chini ya uangalizi wa jopo la madaktari bingwa, baada ya hospitali hiyo kumpa uangalizi maalumu tangu alipokuwa na ujauzito wa wiki 18 hadi wiki 31 alipofanyiwa upasuaji.
Daktari Bingwa wa Afya ya Uzazi wa Kanda ya Kusini, Dkt. Herry Mwambe amesema kujifungua watoto watano kwa wakati mmoja ni tukio nadra, akieleza kuwa kati ya vizazi laki tano, kimoja pekee kinaweza kuwa cha watoto watano.
Baba mzazi wa watoto hao, Saidi Hamisi, ameonesha furaha kubwa baada ya kupata watoto hao watano, ambao wameifanya familia yake kuwa na jumla ya watoto saba.
Wauguzi waliokuwa wakimhudumia Furaha tangu alipowasili hospitalini akiwa na ujauzito wa wiki 18 wamesema alipewa uangalizi wa kipekee na ufuatiliaji wa karibu, tofauti na wajawazito wengine, hadi alipofikia hatua ya kujifungua.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Kada mashuhuri wa chama cha ACT Wazalendo, Luhaga Mpina ametoa pendekezo la kutafutwa kwa msuluhishi huru wa kimataifa na ndani ya nchi ili kulinusuru taifa kutokana na madhila yaliyotokea wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa Tanzania wa Oktoba 2025.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumapili, Agosti 09, 2026, Mpina ameonya kuwa taifa haliwezi kuendelea kuchezewa na migogoro ya ndani inayoharibu sifa ya Tanzania duniani. Ameitaka jamii kushinikiza misingi mitatu ya ukweli, haki, na uwajibikaji kama njia pekee ya kuliponya taifa kufuatia mivutano ya kisiasa iliyopo sasa.
Katika hatua inayolenga kuleta suluhu ya kudumu, Mpina amependekeza mchanganyiko wa watu mashuhuri kutoka nje na ndani ya nchi ambao wako upande wa kati na wanaoweza kusimamia haki bila kujali itikadi za vyama.
Kwa upande wa kimataifa, amewataja viongozi kama Thabo Mbeki (Afrika Kusini), Abiy Ahmed (Ethiopia), Lazarus Chakwera (Malawi), na Olusegun Obasanjo (Nigeria), huku akizitaka jumuia za AU, SADC, na EAC kushiriki. Kwa upande wa ndani ya nchi, Mpina amependekeza viongozi na wanazuoni wanaoheshimika wakiwamo Jaji Joseph Sinde Warioba, Profesa Anna Tibaijuka, Mzee Juma Duni Haji, Profesa Issa Shivji, Dkt. Helen Kijo-Bisimba na Mzee Jenerali Ulimwengu.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Kada wa Chama cha ACT Wazalendo, Luhaga Mpina, leo Jumapili Agosti 09, 2026, amepinga kauli ya serikali kuwa imeshafikia makubaliano na vyama vyote vya siasa isipokuwa kimoja.
Mpina amerejea kauli ya Rais Samia Suluhu Hassan aliyoitoa tarehe 30 Julai 2026, alipokutana na viongozi wa vyama vya siasa Ikulu, ambapo alidai kuwa vyama vyote viko vizuri isipokuwa chama kimoja ambacho kimeelezwa na wadau siasa kuwa CHADEMA.
Mpina amebainisha kuwa msimamo wa ACT Wazalendo kuhusu maridhiano bado upo vile vile kama ulivyotangazwa kwenye matamko ya kamati kuu ya chama hicho. Mpina amesema kuwa hakuna maridhiano yoyote yanayoweza kufanyika bila kuzingatia misingi mitatu mikuu: Ukweli, Haki, na Uwajibikaji kufuatia matukio ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.
Amesema kuwa CHADEMA pia ilishatoa taarifa tarehe 3 Agosti 2026 kuwa haijawahi kukutana kwa siri na CCM au serikali kwa mazungumzo yoyote.
“Sasa haya maneno ambayo anayazungumza mtawala kwamba ameshaelewana na vyama vya siasa isipokuwa chama kimoja ina maana gani? Ina maana gani?” amehoji Mpina.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Madini, Antony Mavunde, leo Agosti 9, 2026, jijini Dar es Salaam, amefichua kufanyika kwa operesheni kali iliyofanikiwa kuvunja mtandao na soko lisilo rasmi la biashara ya madini lililokuwa likiendeshwa kwa siri katika Mtaa wa Jamhuri.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mavunde ameeleza kuwa mnamo Agosti 7, 2026, Kikosi Kazi cha Kupambana na Utoroshaji wa Madini Nchini kilifanya msako maalum ghorofa ya tano katika jengo moja lililopo Mtaa wa Jamhuri, ambapo walibaini uwepo wa soko hilo lililokuwa likinunua na kuuza madini nje ya mfumo rasmi wa Serikali.
Katika operesheni hiyo, eneo hilo limefungwa na kuwekwa chini ya ulinzi mkali wa vyombo vya usalama, huku watuhumiwa 14 wakitiwa baroni. Kati yao, watano ni waajiriwa wa soko hilo haramu na tisa ni wauzaji waliokutwa wakiwa na madini wakisubiri kupata huduma au kulipwa.
Aidha, kikosi kazi kilifanikiwa kukamata gramu 78 za dhahabu, pamoja na vifaa mbalimbali vya uthaminishaji na uchakataji wa madini. Vifaa hivyo ni pamoja na mashine mbili za XRF aina ya Nitro DXL 800, mizani ya kupimia uzito, mitungi ya gesi, vifaa vya kuyeyusha dhahabu, kemikali za kusafisha dhahabu, pamoja na mashine ya POS iliyokuwa ikitumika kufanya malipo kwa wachimbaji. Pia, fedha taslimu kiasi cha Shilingi milioni 54, laki saba na elfu tano zilikutwa eneo hilo.
Uchunguzi wa awali unaonesha kuwa kulikuwa na mzunguko mkubwa wa fedha katika soko hilo, na kuna mtuhumiwa mmoja aliyekimbia na sehemu ya madini kabla ya operesheni kufanyika, tayari maagizo yametolewa kwa vyombo vya ulinzi kuhakikisha mtuhumiwa huyo anazuiwa kuvuka mipaka ya nchi na kukamatwa popote atakapopatikana ndani ya Tanzania.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Serikali ya Iran imetangaza kuwa ipo "karibu sana" kufikia makubaliano na Oman kuhusu mwelekeo mpya wa usafirishaji wa meli katika Njia ya Bahari ya Hormuz, lakini ikatahadharisha kuwa mkataba huo pekee hautatosha kufungua kikamilifu njia hiyo muhimu ya nishati duniani bila Marekani kukubali masharti yake.
Vita hivyo vilivyoanza mnamo Februari 28 kufuatia mashambulizi ya kijeshi ya Marekani na Israel dhidi ya Iranvim efanya Tehran kuweka udhibiti mkali katika njia hiyo inayopitisha takribani robo tano (1/5) ya mafuta na gesi duniani, hatua iliyosababisha mfumuko mkubwa wa bei za nishati na bidhaa duniani.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araqchi, ameeleza kuwa mfumo wa zamani wa usafirishaji wa meli kupitia njia hiyo haukubaliki tena kwa Tehran. Araqchi amebainisha kuwa Iran inazungumza na Oman kuhusu njia ya muda mfupi wakati masuala ya kisheria na kiufundi kuhusu njia ya kudumu yakitafutiwa ufumbuzi.
Hata hivyo, Katibu wa Baraza Kuu la Usalama la Taifa la Iran, Mohammad Baqer Zolqadr, pamoja na Msemaji wa Jeshi la Mapinduzi la Iran (IRGC), Hossein Mohebbi, wameweka wazi kuwa kufunguliwa kwa njia hiyo kunategemea Washington kukubali kupunguzwa au kuondolewa kabisa kwa vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Iran na kuachiwa kwa rasilimali zake zilizoshikiliwa nje ya nchi, Marekani kulipa fidia kwa uharibifu uliotokana na mashambulizi yake nchini Iran, kukomesha vitisho vya kijeshi na kuacha mashambulizi dhidi ya Iran na washirika wake nchini Lebanon, Palestina, Yemen, na Iraq.
"Wakati wowote ambapo Marekani itakubali masharti ya Iran, Njia ya Bahari ya Hormuz itafunguliwa. Hilo halihusiani moja kwa moja na mazungumzo yanayoendelea kati ya Iran na Oman," amesema Mohebbi.
Wakati mazungumzo hayo yakielezwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Oman kuwa ni ya "mwelekeo chanya na wa kujenga," Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) umeripoti kuwa kombora la Iran limepiga meli ya mafuta inayomilikiwa na kampuni ya serikali ya UAE wakati ikipita katika Njia ya Hormuz.
Kituo cha Usimamizi wa Biashara ya Baharini cha Uingereza (UKMTO) kimesema meli hiyo ilipata moto baada ya kushambuliwa, lakini moto huo ulizimwa bila kuleta madhara kwa wafanyakazi au mazingira.
Afisa mmoja wa Serikali ya Marekani ameeleza kuwa Washington inatarajia mkataba kati ya Iran na Oman utafikiwa hivi karibuni, na kwamba pale usafirishaji wa kibiashara utakapofunguliwa bila vizuizi, Marekani nayo itaondoa vikwazo kwenye bandari za Iran.
Kamandi Kuu ya Jeshi la Marekani (CENTCOM) imeeleza kuwa tangu iweke vikwazo hivyo, imeruhusu zaidi ya meli 30 zenye misaada ya kibinadamu kupita, huku ikiwa imezuia meli 53 na kuzikamata nyingine.
Kwa upande wake, Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian ameeleza kuwa hii ndiyo fursa nzuri zaidi ya kufikia makubaliano, akisisitiza kuwa nchi yake ipo kwenye mshikamano mkubwa na kwamba inatoka ikiwa na nguvu katika mzozo huo, ingawa amelaumu vikwazo vya Marekani kwa kupandisha bei za chakula na mahitaji ya msingi nchini humo. -
Jambo TV
@Jambotv_
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, ametoa ufafanuzi kuhusu matukio ya ghasia yaliyotokea nchini mnamo Oktoba 29,2025 akidai kuwa yalikuwa na ajenda maalum ya siri na hayakufanyika kwa utashi wa hiari wa Watanzania wengi.
Katika mahojiano maalum na DW, Katambi amebainisha kuwa ushahidi upo wazi kuwa machafuko hayo yalipangwa na kuratibiwa kwa malengo ya kisiasa. Waziri Katambi amewataka Watanzania na jumuiya ya kimataifa kujiuliza maswali ya msingi kuhusu uhalali wa kile kilichoitwa maandamano siku hiyo. Amehoji ni nchi gani duniani inayoruhusu maandamano siku ya uchaguzi mkuu, na ni sheria gani inayoruhusu maandamano yasiyokuwa na taarifa, viongozi wanaojulikana, wala ruti maalumu.
“Nchi gani duniani imewahi kuruhusu maandamano kama yangekuwa ya halali, halafu waandamanaji wakaenda kwenye duka la simu la mtu wakachoma moto... wakaenda kwenye sheli wakachoma sheli moto... wakaenda kuchoma vituo vya polisi?” amehoji Katambi akionesha kusikitishwa na uharibifu wa miundombinu muhimu ya taifa
Katambi ametoa hoja ya kitakwimu akijiuliza kwanini ghasia hizo zilitokea katika mikoa minne au mitano tu, wakati taifa lina watu zaidi milioni 61. Amebainisha kuwa ikiwa hasira ingekuwa ya wananchi wote, ghasia hizo zingejitokeza pia vijijini ambako asilimia 70 ya Watanzania wanaishi, lakini hali huko ilikuwa ya utulivu
Aidha, amewashutumu aliowaita viongozi wa maandamano hayo kwa kushindwa kujitokeza tarehe 30 au 31 Oktoba kuomba radhi kwa mali zilizopotea, badala yake wakaendelea na uchochezi.
“Wakati haya yanatokea na kama kweli…si ilikuwa siku tarehe 29 Oktoba, tarehe 30 kwanini hawakujitokeza viongozi wa kusema kwamba sasa sisi tulikuwa tuna maandamano halali lakini imetokea bahati mbaya labda kuna wahuni waliingilia, tunaomba radhi kwa mali zilizopotea kwa wale waliofanyiwa uhalifu, kwanini, tarehe 30. Kwanini hawakujitokeza hao viongozi? Tarehe 31 sijui tarehe moja, kwanini badala ya kusikia watu wakitoa kauli za pole kwa mamlaka mbalimbali na walioathirika badala yake tulisikia uchochezi wa aina nyingine, na baadhi ya watu kujilaumu kwamba tumefeli tungefanya hivi…tarehe moja, kwanini hatukuona hata baadhi ya viongozi wa dini...
NB: Soma zaidi jambo.co.tz
jambo.co.tz/mlitaka-watanzania-wafe-wangapi-katambi-awash… -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) amevitaka vyama vya ushirika nchini kuendelea kuboresha utendaji kazi wake ili kujijengea sifa nzuri ya uwepo wa hati safi ambao umeonekana kuongezeka.
CPA Mugeta amesema hayo jijini Dodoma kwenye maonesho ya Nane Nane akieleza kuwa kwa mwaka 2025/26 kuna ongezeko la asimilia 4% kutoka asilimia 16% mpaka 20% kwa vyama vinavyopata hati safi.
Amesisitiza kuwa mafunzo yanayotolewa na COASCO kwa viongozi na watendaji wa vyama vya ushirika yamechangia kuboresha matokeo ya ukaguzi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, amepuuzilia mbali madai ya kuwepo kwa uhusiano mbaya kati ya jeshi la polisi na wananchi, akieleza kuwa jeshi hilo ni sehemu ya jamii na dhana ya watu kuliogopa imepandikizwa kwa malengo ya kisiasa
Akizungumza katika mahojiano maalum na DW Kiswahili, Katambi amesisitiza kuwa askari polisi na wanajeshi nchini Tanzania si watu kutoka "dunia ya tatu," bali ni ndugu, jamaa, na majirani wa Watanzania wenyewe. Amebainisha kuwa askari hawa ndio watu ambao wananchi wanasali nao makanisani, misikitini, na wamesoma nao mashuleni.
“Mazuri sana, mimi nikitaka kuwauliza kwa mfano, lini yaliharibika? Yaani lini yaliharibika mahusiano kati ya wananchi na jeshi kwa sababu wanajeshi wote wa vyombo vyote vya ulinzi na usalama hapa Tanzania nzima aidha ni kaka zetu, ni watoto wa shangazi, wa mjomba, kama sio wa mjomba, ni wa jirani zako. Kwani polisi hao wanatoka dunia ya tatu? Wanajeshi wanatoka dunia ya tatu. Vyote, vyombo vya ulinzi na usalama ni wanatokana na sisi, si wanatokana na jamii, ndio hao tulikuwa tunasali nao kanisani au tunaenda nao madrasa au sio? Au Sunday school au tumesoma nao shuleni. Ni sehemu ya jamii, na kama ni sehemu ya jamii tafsiri yake ni kwamba ni ndugu zetu”, ameeleza.
Akijibu hoja kuhusu hofu iliyopo miongoni mwa wananchi dhidi ya vyombo vya ulinzi, Waziri Katambi ameweka wazi kuwa hakuna sababu ya raia mwema kuwa na hofu.
“Mhalifu pekee ndio ataogopa... ni ile tu dhana potofu ambayo imekuwepo kwa muda mrefu sana kutaka tu kuonesha kwamba hawa watu ni hivi wakati labda nini hapana,” amesema Katambi akirejea utaratibu wa wananchi kuomba lifti kwenye magari ya askari kama ishara ya ukaribu
Katambi amedai kuwa chuki inayozungumzwa dhidi ya polisi ni matokeo ya "propaganda" na "mapandikizi ya kisiasa" yenye lengo la kuaminisha umma kuwa nchi ina matatizo ili baadhi ya taasisi au watu waweze kunufaika.
“Kwa sehemu kubwa sana ni mapandikizi ya kisiasa... ni wakati mwingine kutaka kuaminisha watu kwamba always we have a problem. Hakuna taasisi yoyote ambayo inaweza ika-operate kama hakuna matatizo,” amesisitiza Waziri huyo
SOMA ZAIDI jambo.co.tz -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, ametoa wito kwa jamii kurejea katika misingi imara ya malezi ya vijana inayozingatia kumjua Mungu, kufanya kazi kwa bidii, na kupenda masomo ili kujenga taifa lenye uadilifu na ujuzi
.
Akizungumza katika Ibada ya Misa Takatifu Maalum ya Wanajumuiya wa Uru Seminari iliyofanyika jana katika Kanisa Katoliki Parokia ya Kristo Mchungaji Mwema, Tabata Kimanga mkoani Dar es Salaam, Dkt. Nchimbi amekumbusha wajibu wa kila mbatizwa kuwa ‘mmishionari’ anayeleta mabadiliko chanya katika jamii
Dkt. Nchimbi amesisitiza kuwa waumini wanapaswa kutumia nafasi zao mahali walipo ili kuleta tofauti kwa kutenda haki na kueneza upendo.
“Tukumbuke wito wetu muhimu wa kwenda kutakatifuza malimwengu mahali ulipo pawe na tofauti... uwepo wako mahali pale ulete matumaini kwa watu, ulete upendo, ulete haki, ulete matumaini ambayo yanamfanya mtu aone leo ni bora kuliko jana,” amesema Makamu wa Rais
Aidha, amewataka vijana kuweka juhudi katika masomo na kuepuka kutamani mafanikio ya haraka bila kufanya kazi. “Kusoma kunaleta ujuzi, kutosoma kunazalisha tabia ya kupenda njia za mkato,” ameonya Makamu wa Rais
Katika hatua nyingine, Dkt. Nchimbi amewahakikishia waumini kuwa serikali inathamini na itaendelea kudhamini mchango wa taasisi za dini katika kutoa huduma za kijamii. Amesema kuwa taasisi hizo zimekuwa washirika wakubwa wa serikali, hususan katika sekta za elimu na afya nchini kote
.
Makamu wa Rais amehitimisha kwa kutoa wito kwa Watanzania kuendeleza umoja, kufanya kazi kwa juhudi, na kuendelea kuiombea nchi ili iendelee kuwa na amani na ustawiThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
WAZIRI KATAMBI AFICHUA SIRI: ADAI CHUKI DHIDI YA POLISI NI ‘MAPANDIKIZI YA KISIASA’ jambo.co.tz/waziri-katambi-afichua-siri-adai-chuki-dhidi-… via @jambotv_
-
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI PICHA:
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, John Heche alivyopokewa wilayani Musoma mkoani Mara kwa ajili ya Mkutano Maalum wa chama hicho mkoani humo. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega amesema uwekezaji mkubwa ambao Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan inaufanya katika sekta mbalimbali nchini siyo tu unachochea maendeleo, bali unaiheshimisha nchi na kujali utu wa Watanzania.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Ulega alisema mifano ya uwekezaji huo ni ujenzi wa barabara za Mwendo Kasi (BRT) jijini Dar es Salaam ambao umepunguza muda wa safari za watu kwenda na kurudi kusaka riziki na pia kuwa na safari zenye kujali utu.
Waziri huyo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mkuranga alitumia mifano halisi ya kueleza hilo, ikiwemo kadhia aliyokuwa akipitia yeye mwenyewe katika siku zake za uanafunzi na baada ya kumaliza masomo ya chuo kikuu.
Ulega alikuwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa awamu ya pili ya Mradi wa BRT unaohusisha safari za kutoka Mjini (Kivukoni na Kariakoo) na kwenda Mbagala Rangi Tatu.
Mbunge huyo wa Mkuranga, alitumia pia nafasi hiyo kumpongeza Rais Samia kwa hatua kubwa ya serikali yake na ile ya Rais Yoweri Museveni wa Uganda kuingia makubaliano ya kujenga mradi wa kusafisha mafuta mkoani Tanga, hatua aliyosema faida zake ni kubwa kwa mataifa hayo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Jaji Mstaaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Robert Makaramba, amedai kuwa kuna ukosefu wa "adabu" na nidhamu ya kisheria kati ya mihili ya dola- Serikali (Executive), Bunge, na Mahakam kufuatia kile alichokiita ucheleweshaji wa makusudi wa mabadiliko ya Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971 yanayolenga kumlinda mtoto wa kike dhidi ya ndoa za utotoni
Akizungumza katika kongamano la wadau lililoandaliwa na shirika la Msichana Initiative, likilenga kujadili mabadiliko ya sheria hiyo jijini Dar es Salaam siku ya Ijumaa, Jaji Makaramba alibainisha kuwa nchi imeingia katika mchezo wa “paka na panya” ambapo serikali imekuwa ikijiridhisha kwa kukaidi amri za mahakama kwa kisingizio cha kukusanya maoni, jambo ambalo ameliita ni kupoteza muda.
Jaji Makaramba alikosoa vikali namna hukumu ya kesi ya kihistoria ya Rebecca Gyumi ilivyoandikwa, akisema kuwa mahakama zenyewe (Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani) ‘zilijichanganya’. Amesema kuwa badala ya mahakama kutamka moja kwa moja kuwa vifungu vya 13 na 17 ni batili (null and void), zilitumia lugha ya kuwa vifungu hivyo “vinastahili kutamkwa kuwa ni batili”.
“Hiyo ndio ilitupa shida mpaka sasa hivi... mahakama haikutamka mara moja hivi ni batili na vifutwe. Nashangaa kwa nini haikufanyika hivyo,” alisema Jaji Makaramba huku akiongeza kuwa kutokana na makosa hayo ya kisheria, wadau sasa hawana “ubavu” wa kisheria wa kuibana serikali.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Mohammed Ali Kawaida, amewakosoa vikali baadhi ya vijana hasa wale wa CHADEMA kwa kile alichokiita kejeli na kubeza hotuba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wa uzinduzi wa Tume ya Rais ya Uchunguzi wa Ghasia na Ukiukaji wa Sheria Wakati na Baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya viongozi wa Seneti za Vyuo na Vyuo Vikuu, Kawaida ameeleza kuwa kejeli hizo hazina afya kwa taifa na zinalenga kuvunja moyo na kudhoofisha jitihada za Rais Samia za kuleta maridhiano ya kisiasa, haki, na ukweli nchini.
Kawaida amesisitiza kuwa UVCCM na vijana wa CCM wanaunga mkono kwa 100% kuundwa na kuanza kazi kwa Tume hiyo. Katika hatua ya kuonesha msisitizo wa uwazi na haki, Kawaida amewataka makamishna na watendaji wa Tume hiyo kufanya kazi yao kwa weledi mkubwa bila kumwogopa au kumwonea mtu yeyote muhali.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Saa chache baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuzindua Tume Rais ya Uchunguzi wa Wahusika wa Ghasia na Ukiukwaji wa Sheria wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 2025, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) @ChademaTZ2 Bara, John Heche @HecheJohn ametoa msimamo mkali wa kuikataa tume hiyo, akiitaja kuwa ni mbinu ya kutaka kutengeneza picha isiyo halisi mbele ya jumuiya ya kimataifa.
Akihutubia mkutano wa hadhara katika wilaya ya Rorya mkoani Mara leo Agosti 07, 2026, Heche amesema kuwa CHADEMA haitambui tume hiyo na matokeo yake yoyote yatakayotolewa yatakuwa ni "feki". Heche ametumia mfano wa ujenzi wa ghorofa juu ya tope kuelezea kutokuwa na imani na tume hiyo, akisema kuwa haiwezi kupata ukweli ikiwa inaongozwa na ripoti ya tume iliyopita.
Heche amekosoa vikali uamuzi wa kumjumuisha jaji kutoka Namibia, na Jaji kutoka nchini Uganda akidai kuwa nchi hiyo ina rekodi mbovu ya haki za binadamu na uhuru wa mahakama. Heche amesisitiza kuwa msimamo wa chama chake ni kuendelea kudai Katiba Mpya na msuluhishi wa kimataifa anayekubalika na pande zote.
Hata hivyo, Rais Samia ameelezea imani yake kuwa majaji wote waliopo kwenye Tume hiyo, watatumia uzoefu wao wa miaka mingi kutekeleza majukumu yao ndani ya miezi mitano ijayo kwa kwa “weledi, umakini, na uadilifu mkubwa”.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila MKumbo pamoja na ujumbe anaouongoza katika safari ya kutembelea viwanda na miradi mbalimbali ya Dangote, jijjni Lagos, Nigeria, leo amekutana na uongozi wa Dangote Group na kujadiliana masuala mbalimbali ya biadhara na uwekezaji nchini Tanzania.
Katika kikao hicho mambo yaliyojadiliwa ni fursa zilizopo nchini katika masuala ya biashara na uwekezaji yakiwemo, mradi wa Bandari ya Bagamoyo na Kongani ya viwanda, uzalishaji wa mbolea, pamoja na kuvua umeme kwa kutumia makaa ya mawe.
Akizungumza katika Mkutano huo Makamu wa Rais wa Dangote Group, DVG Edwin alitaka kufahamu mifumo na haki zilizopo kwa wawekezaji hususani kwenye ardhi, madini na masuala ya uzalishaji umeme, ambapo Prof. Kitila alimuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka za Uwekezaji na Maeneo Maalumu Tanzania (TISEZA) pamoja na Wakuu wa Taasisi walioshiriki ziara hiyo chini ya sekta husika na timu ya kiufundi kukutana na uongozi wa Dangote na kutoa ufafanuzi wa kina kwenye masuala hayo. -
Jambo TV
@Jambotv_
Mahakama ya Wilaya ya Ilala imemhukumu kifungo cha maisha jela Amoni Amandusi Mtwanga, miaka 72, mkazi wa Pugu kwa kosa la kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka 10. Hukumu hiyo ilitolewa katika Kesi namba CC 3920/2026 iliyosikilizwa mbele ya Hakimu Mohamed Burhani.
Kwa mujibu wa mashtaka, tukio hilo lilitokea tarehe 16/11/2025. Mhanga ambaye ni mwanafunzi wa Darasa la III Shule ya Msingi Kigogo, makazi Pugu Kigogo, alidaiwa kufanya ngono na mtuhumiwa njiani alipokuwa akitoka shuleni. Njia ya mtoto ilikuwa karibu na geti la nyumba ya mtuhumiwa ambaye anaishi peke yake bila familia.
Mahakama iliambiwa kuwa siku ya tukio mtuhumiwa alimwita mtoto huyo, akamuingiza ndani hadi chumbani na kumfanyia kitendo hicho kwa kumlazimisha kuvua nguo huku akimziba mdomo ili asipige kelele. Pia ilidaiwa kuwa mzee huyo alikuwa amemfanyia kitendo hicho zaidi ya mara moja na baada ya kila tukio alikuwa akimpa mtoto shilingi 1000 ili asimweleze mzazi wake.
Uhalifu huo ulibainika baada ya mama wa mtoto, Aisha Salum, kugundua mabadiliko kwa binti yake na kumuuliza. Mtoto ndipo alimtaja mzee huyo kuwa ndiye anayemfanyia kitendo hicho. Mama alitoa taarifa na kesi ikafunguliwa mahakamani.
Baada ya kusikiliza ushahidi wote, Hakimu Mohamed Burhani alimkuta mtuhumiwa na hatia na kumhukumu kifungo cha maisha jela. Mahakama imesema hukumu hiyo ni fundisho kwa wengine wanaofanya vitendo vya ukatili kwa watoto. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Naibu Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Bukombe, Dkt. Doto Biteko, amewataka Watanzania kuendelea kuuenzi na kuudumisha utamaduni wa amani, upendo na mshikamano, akisisitiza kuwa misingi hiyo ndiyo nguzo kuu ya maendeleo endelevu ya Taifa.
Akizungumza wakati wa ibada na mazishi ya aliyekuwa Diwani wa Kata ya Ilolangulu, Kabula Ndabacha, yaliyofanyika wilayani Mbogwe, Dkt. Biteko alisema nyakati za mafanikio na changamoto zinahitaji wananchi kuendelea kuthaminiana, kusaidiana na kuishi kwa upendo bila kujali tofauti zao.
“Amani ni urithi wetu mkubwa na ndiyo msingi wa maendeleo tunayoyashuhudia leo. Tuilinde kwa kuendelea kuishi kwa upendo, umoja na kuheshimiana, kwani maendeleo ya Taifa letu yanategemea mshikamano wa wananchi wake,” alisema Dkt. Biteko.
Aidha, alitoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa, marafiki na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), akieleza kuwa kifo cha Mhe. Kabula Ndabacha ni pigo kwa familia, wananchi wa Kata ya Ilolangulu na Chama Cha Mapinduzi kutokana na mchango wake katika kuwatumikia wananchi.
Dkt. Biteko aliwahimiza wananchi kuendeleza mema yaliyoachwa na marehemu kwa kushiriki katika shughuli za maendeleo, kuimarisha mshikamano wa jamii na kuendelea kuilinda amani ambayo imeendelea kuwa tunu na fahari ya Tanzania.
MwishoThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO
Leo Agosti 7, 2026 Kesi ya Uhujumu uchumi Na. 4521/2026 inayomkabili Wendy William Ishengoma na wenzake wanne imeendelea Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Rushwa na Uhujumu uchumi, Dar es Salaam ambapo shahidi wa pili wa jamhuri Inspekta Michael Mwakalikamo(40) ameendelea kutoa ushahidi wake mbele ya Jaji Dkt. Dafina Ndumbaro anayesikiliza kesi hiyo.
Akiongozwa na Mawakili wa Jamhuri Inspekta Michael alimalizia mahojiano ya awali ya ushahidi(examination in chief) kisha baadae upande wa utetezi kupitia Wakili Peter Madeleka na Wakili Grey Godifrey Dedan walipata kumuuliza shahidi maswali ya dodoso(Cross-examination).
Shahidi alidai mahakamani kuwa kampuni ya Atlantic Microcredit Ltd. ambayo ni mshtakiwa wa tano ilikuwa ikifanya ulaghai kwa wateja wao kwa kuwaambia wanawekeza huku wakipewa faida ya 40% ndani ya siku 25 hata hivyo amedai kuwa pindi walopohojiwa washtakiwa kuaw wanawekeza fedha hizo kwenye nini walisema ni kwenye biashara ya kubadilishana fedha(Forex trading) na sarafu mtandao(cryptocurrency) jambo ambalo anasema walishindwa kulithibitisha pindi walipopewa kompyuta na intaneti.
Alipohojiwa na Wakili Madeleka juu ya kama watu waliowekeza kwenye kampuni hiyo walilalamika kuhusu kulaghaiwa shahidi alisema taarifa walizipata kwa Benki Kuu ya Tanzania(BOT) hata hivyo wapo waliolalamika lakini hawajui na hakuwaweka kweye ushahidi kwa sababu si sehemu ya ushahidi wake.
Kuhusu utunzaji wa vielelezo shahidi alieleza kuwa vielelezo hivyo alikabidhiwa Mahakamani na Wakili wa Serikali Mkuu Mwahija jambo ambalo Madeleka alisema ataiomba mahakama apate nafasi ya kumdodosa aliyeleta vielelezo mahakamani.
Wakili: Mweleze jaji mara baada ya kukamilisha upelelezi vielelezo ulipeleka waoi
Shahidi: Nilikabidhi kwa inchaji wangu wa upelelezi na baadhi nilikuwa na access navyo, sehemu ya vielelezo vilikuwa vinakaaa jaladani hasamwa documentary evidence.
Wakili: Unakubaliana na mimi kwamba jalada la vielelezo lilikabidhiwa kwa waendesha mashtaka
Shahidi: Katika ushahidi wangu hakuna sehemu nikitaka
Wakili: Leo unajua ulitoa vielelezo kutoka kwa waendesha mashtaka
Shahidi: Sahihi
Wakili: Tutaiomba mahakama itoe amri kwa huyi mwendesha mashtaka kwa huyu alieyeleta vielelezo.
Pamoja na hayo alihojiwa juu ya kurekodi maelezo ya washtakiwa aliowahoji ambapo alikiri kurekodi baadhi ya maelezo na yapo ambayo hakurekodi na mengine alirekodi kwenye notebook yake ambayo aimesahau ilipo.
Wakili: Ni sahihi uliwahoji washtakiwa ulirekodi
Shahidi: Kuna mahojiano ya mdomo na ya kuandika
Wakili: Unataka kusema polisi anaruhusiwa kwa mdomo
Shahidi: Professionally
Wakili: Mahakama inathibitishaje
Shahidi: Kwa ushahidi niliotoa
Wakili: Haya ya Forex hukuona haja ya kuandika
Shahidi: Niliandika kwenye notebook ambayo sikumbuki iko wapi
Aidha juu ya kama kampuni ya kama kampuni hiyo imewahi kushtakiwa kwa kosa lolote alieleza kuwa hapana ndiyo mara ya kwanza huku akikiri kuwa BOT haijawahi kuharamisha shughuli inayofanywa na kampuni hiyo.
Wakili: Kama hawajakubaliana inakuwa ni kosa chini ya kifungu gani
Shahidi: Mheshimiwa jaji sijasema kwamba kukata bima ni kosa nimesemaregulatory authority(malaka ya uthibiti) ambayo ni BOT iinataka taasisi za kifedha kuwa na bima
Wakili: Kuna mahakama imewahi kuthibitisha Atlantic kufanya shughuli za kihalifu
Shahidi: Hapana
Wakili: Ni mara ya kwanza Atlantic inaletwa hapa
Shahidi: Ndio
Wakili: Kwa hiyi si wahalifu
Shahidi: Ndio maana nipo hapa kuthibitisha
Hata hivyo maswali ya dodoso hayakufika mwisho kutokana na muda kuwa hafifu(shauri liliisha saa kumi na mbili jioni kasoro) na shauri hilo liliahirishwa mpaka Agosti 13-14, 2026 ambapo litaendelea tena mahakamani hapo huku vielelezo vingine vikibaki chini ya Mahakama na magari mawili Toyota Alphard yakirudi kuhifadhiwa Ofisi ya Mashtaka.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Wadau wa haki za binadamu, viongozi wa dini, na wanasheria wameitaka serikali kuharakisha mchakato wa mabadiliko ya Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971 wakidai kuwa ucheleweshaji unaoendelea unazidi kuwaumiza watoto wa kike nchini.
Akizungumza Ijumaa Agosti 7, 2026 katika kongamano lililofanyika jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Msichana Initiative, Consolata Chikoti, ameeleza kuwa ni takribani miaka mitano sasa imepita tangu Mahakama ya Rufaa itoe uamuzi wa mwisho mwaka 2019 kuitaka serikali kufanya mabadiliko ya vifungu vya 13 na 17 vinavyoruhusu mtoto wa kike kuolewa. Chikoti amebainisha kuwa licha ya ushindi wa kisheria uliopatikana tangu mwaka 2016 katika Mahakama Kuu, muswada wa mabadiliko hayo bado haujafikishwa bungeni kwa ajili ya kupitishwa.
Kwa upande wake, Irene Nambuo ameweka wazi kutoridhishwa kwake na mchakato wa kukusanya maoni upya, akitaja hali hiyo kama “danadana” kwenye maisha ya mtoto wa kike. Amesisitiza kuwa serikali tayari inazo ripoti za tume tangu mwaka 1994 na kesi za kisheria zilizokamilika, hivyo hakuna haja ya kuendelea kutafuta maoni mapya badala ya kubadilisha sheria mara moja
Akijibu hoja hizo, Wakili wa Serikali kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Innocent Magesa amesema serikali haijakaa kimya na inaendelea kutoa elimu kwa jamii kupitia Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia. Hata hivyo, Magesa amekumbusha kuwa ziko sheria nyingine kama Sheria ya Mtoto, Sheria ya Elimu, na Kanuni ya Adhabu (Sura ya 16) ambazo zinaendelea kutoa ulinzi na adhabu kali, ikiwemo kifungo cha miaka 30 kwa makosa ya kijinsia, wakati mchakato wa Sheria ya Ndoa ukiendelea.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI PICHA:
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, John Heche akihutubia wananchi wa wilaya ya Rorya mkoani Mara Agosti 07, 2026 katika mwendelezo wa mikutano ya hadhara anayoifanya mkoani humo. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma linamshikilia Michael Hinju (58), mkazi wa kijiji cha Liuli wilayani Nyasa, kwa tuhuma za kujihusisha na utapeli kwa kuwalaghai wananchi kwa kuwaahidi nyadhifa serikalini na ajira katika majeshi.
Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, SACP Marco Chilya, amesema mtuhumiwa huyo alikuwa akijitambulisha kuwa Afisa wa Sheria wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma, wakati mwingine akidai ni Kamishna wa Jeshi la Polisi kutoka Makao Makuu Dodoma au kiongozi mwandamizi serikalini.
Kamanda Chilya amesema kupitia mbinu hizo, mtuhumiwa aliwalaghai watu kwa kuwaahidi kuwasaidia kupata nafasi mbalimbali ikiwemo ukuu wa wilaya (DC), ukatibu tawala wa wilaya (DAS), ukurugenzi wa halmashauri pamoja na ajira kwa watoto wao katika majeshi.
Katika tukio jingine, Kamanda Chilya amesema mwanaume mmoja aitwaye Enock Komba (40), mkazi wa kijiji cha Langandondo, anashikiliwa kwa tuhuma za kuwaua mke wake, Maria Sylverus (32), na mama mkwe wake, Astela Mapunda (69), baada ya kuwashambulia kichwani kwa kitu kizito na butu, na kusababisha vifo vyao.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katika hatua ya kuimarisha ukomavu na maridhiano ya kisiasa na ushirikishaji nchini, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amekubali ombi la viongozi wa vyama vya upinzani la kuambatana naye katika safari zake za nje ya nchi. Hatua hiyo imepokelewa kwa furaha na wadau wa siasa kama kielelezo cha nia ya dhati ya serikali katika kujenga maridhiano.
Uamuzi huu unatokana na kikao maalum kilichofanyika Ikulu, Dar es Salaam tarehe 30 Julai, 2026, ambapo Rais Samia alizungumza na viongozi wa vyama vya siasa nchini. Katika kikao hicho, viongozi wa vyama na taasisi za kisiasa walimuomba Rais kukubali utaratibu huo ili kuimarisha mshikamano wa kitaifa na kuwapa fursa viongozi wa vyama hivyo kujifunza mengi nje ya nchi kwa mustakabali wa taifa la Tanzania.
Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa, Juma Ali Khatibu, ameithibitishia Jambo TV kuwa utekelezaji wa uamuzi huo ulianza katika safari ya hivi karibuni ya kwenda nchini Angola. Viongozi walioteuliwa kuandamana na Rais katika safari hiyo walikuwa ni Juma Ali Khatibu mwenyewe (kutoka chama cha ADA-TADEA) na Dorothy Semu ambaye ni Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo.
Hata hivyo, wakati Juma Ali Khatibu akishiriki safari hiyo, Dorothy Semu hakufanikiwa kwenda. Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake wa Chama cha Wakulima (AAFP) Taifa, Shani Ally Kitumbua amedai kuwa Semu alitafutwa sana kwa njia ya simu bila mafanikio licha ya kuwa vigezo vya safari hiyo vilikuwa vimekamilika.
Akizungumza na wanahabari Agosti 5, 2026, Kitumbua alionya kuwa kitendo hicho kinaweza kumvunja nguvu Rais ambaye ameonesha nia ya kuwashirikisha wapinzani.
Hata hivyo, katika mahojiano na Jambo TV kuhusu tukio hilo, Dorothy Semu amegoma kutoa maelezo ya kina au sababu za yeye kutoshiriki safari hiyo akisema "no comment".
Pamoja na changamoto hiyo iliyojitokeza katika safari hiyo, Baraza la Vyama vya Siasa limempongeza Rais Samia kwa utaratibu wa kukutana na vyama vya siasa mara tatu kwa mwaka na kuwashirikisha katika safari za nje. Linaamini kuwa utaratibu huu utasaidia kutoa fursa kwa viongozi wa upinzani kujifunza na kutoa mchango wao katika diplomasia ya nchi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Serikali imepiga marufuku uchimbaji holela wa Visima vya maji nchini, ikionya kuwa shughuli hizo zikifanyika bila kuzingatia utaalamu na taratibu zinaweza kuhatarisha ubora wa maji, kuharibu mazingira na kuchangia kupungua kwa rasilimali za maji chini ya ardhi.
Akizungumza katika Mkutano wa Rasilimali za Maji Chini ya Ardhi Jijini Dodoma, Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, amezitaka kampuni zote zinazojihusisha na utafiti na uchimbaji wa maji chini ya ardhi pamoja na waendeshaji wa mitambo, kuhakikisha wanakuwa na leseni na vibali halali kabla ya kuanza shughuli zozote.
Aidha, Aweso amesema Serikali imeanza kutumia mifumo ya kidijitali katika utoaji wa leseni na vibali ili kupunguza urasimu, kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wadau na kuondoa ulazima wa Wananchi kusafiri umbali mrefu kufuata huduma hizo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mtaalamu wa Saikolojia, Dkt. Leonard Mgina, amesema Wanaume wengi hufariki dunia mapema kutokana na kubeba majukumu mengi ya kifamilia, huku wakiachwa kuyasimamia peke yao hali ambayo ameleza kuwa inachangia ongezeko la Wanawake wengi kubaki Wajane.
Akizungumza katika mahojiano maalum na Jambo TV, Dkt. Mgina aliwashauri Wanawake kushiriki kikamilifu katika majukumu ya familia badala ya kumuachia kila kitu Mume, akisisitiza kuwa ushirikiano ndani ya ndoa unaweza kupunguza msongo wa mawazo na kuboresha ustawi wa familia.
"Ukitaka Mumeo aishi muda mrefu, msaidie baadhi ya majukumu, usimuachie kila kitu," amesema Dkt. Mgina.
Mahojiano kamili yanapatikana kwenye chaneli yetu YouTube ya Jambo TV.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mtaalamu wa Saikolojia, Dkt. Leonard Mgina, amesema Wanaume wengi hufariki dunia mapema kutokana na kubeba majukumu mengi ya kifamilia, huku wakiachwa kuyasimamia peke yao hali ambayo ameleza kuwa inachangia ongezeko la Wanawake wengi kubaki Wajane.
Akizungumza katika mahojiano maalum na Jambo TV, Dkt. Mgina aliwashauri Wanawake kushiriki kikamilifu katika majukumu ya familia badala ya kumuachia kila kitu Mume, akisisitiza kuwa ushirikiano ndani ya ndoa unaweza kupunguza msongo wa mawazo na kuboresha ustawi wa familia.
"Ukitaka Mumeo aishi muda mrefu, msaidie baadhi ya majukumu, usimuachie kila kitu," amesema Dkt. Mgina.
Mahojiano kamili yanapatikana kwenye chaneli yetu YouTube ya Jambo TV.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Serengeti, Lucas Ngoto ameonya dhidi ya kile alichokiita kuwa ni mipango ya kumfuatilia na kumtishia usalama wake Makamu Mwenyekiti wa chama hicho bara, John Heche.
.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika Sirari wilayani Tarime mkoani Mara tarehe 6 Agosti, 2026, Ngoto ameeleza kuwa kuna mazingira ya kutatanisha yanayomzunguka kiongozi huyo, akidai kuwa gari moja limekuwa likionekana likifanya ufuatiliaji katika mazingira ya kutatanisha
Madai hayo yanaungwa mkono na maelezo ya John Heche mwenyewe, ambaye alibainisha kuwa gari aina ya Toyota Land Cruiser (hardtop) nyeupe yenye namba za usajili T 318 EQJ lilifika nyumbani kwake asubuhi siku chache zilizopita.
Akizungumza Julai 29, 2026 kwenye Mkutano Mkuu Maalumu wa CHADEMA Mkoa wa Mwanza uliofanyika katika soko la Mbao, Kata ya Igoma Jijini Mwanza, Heche alieleza kuwa baada ya kufanya uchunguzi na kupiga picha, ilibainika kuwa namba hizo ni za kughushi kwani katika mfumo wa usajili, namba hizo ni za katapila la kutengenezea barabara na siyo za gari hilo.
Lucas Ngoto amesisitiza kuwa hali hiyo haiwezi kuwa ya bahati mbaya. "Haiwezekani kwamba kuna gari itabadilishwa namba asubuhi ipite belia (barriers) zote isijulikane ni nani," alisema Ngoto, akibainisha kuwa hakuna mwananchi wa kawaida anayeweza kufanya hivyo bila kukamatwaThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katika kile kinachoonekana kama hatua ya kutafuta ukweli na haki kufuatia matukio ya ghasia yaliyogubika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Agosti 07, 2026, amezindua rasmi Tume ya Rais ya Uchunguzi wa Wahusika wa Ghasia na Ukiukwaji wa Sheria katika hafla iliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam.
Tume hiyo, iliyoundwa chini ya Sheria ya Tume ya Uchunguzi (Sura ya 32), inalenga kuingia kwa undani kubaini waliochochea, waliohusika, na hata waliotoa fedha kufanikisha ghasia hizo zilizotokea ndani ya nchi wakati na baada ya uchaguzi mkuu uliopita
Katika hali ya kuongeza uaminifu na upeo wa uchunguzi huo, Rais Samia amewajumuisha majaji waandamizi kutoka nje ya nchi. Tume hiyo inayoongozwa na Mwenyekiti Shaban Aliila, inajumuisha makamishna sita, ambapo wawili kati yao wanatoka katika kanda za Afrika Mashariki na SADC. Makamishna hao wa kimataifa ni Jaji Barishaki Cheborion kutoka Uganda na Jaji Petrus T. Damaseb kutoka Namibia
Rais Samia ameeleza kuwa ushiriki wa majaji hao unalenga kupata "muono mpana" wa matukio hayo na amewashukuru Rais Yoweri Museveni wa Uganda na Rais Netumbo Nandi-Ndwaitwa wa Namibia kwa kuridhia kuleta majaji hao kusaidiana na majaji wa Tanzania
Rais Samia amebainisha kuwa tume hiyo imepewa hadidu za rejea zitakazoongoza majukumu yake na inatarajiwa kuwasilisha ripoti rasmi pamoja na mapendekezo ndani ya miezi mitano. Hata hivyo, Rais ameweka wazi kuwa muda huo unaweza kuongezwa ikiwa kutakuwa na uhitaji wa kufanya kazi hiyo kwa upeo mpana zaidi
.
"Ni imani yangu kwamba majaji hawa watakwenda kutumia taaluma, uzoefu, na viapo vyao kutekeleza kazi hii kwa weledi, umakini, na uadilifu mkubwa," amesisitiza Rais Samia wakati wa uzinduzi huo uliofanyika Ikulu jijini Dar es SalaamThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Katika kile kinachoonekana kama hatua ya kutafuta ukweli na haki kufuatia matukio ya ghasia yaliyogubika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Agosti 07, 2026, amezindua rasmi Tume ya Rais ya Uchunguzi wa Wahusika wa Ghasia na Ukiukwaji wa Sheria katika hafla iliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam.
Tume hiyo, iliyoundwa chini ya Sheria ya Tume ya Uchunguzi (Sura ya 32), inalenga kuingia kwa undani kubaini waliochochea, waliohusika, na hata waliotoa fedha kufanikisha ghasia hizo zilizotokea ndani ya nchi wakati na baada ya uchaguzi mkuu uliopita
Katika hali ya kuongeza uaminifu na upeo wa uchunguzi huo, Rais Samia amewajumuisha majaji waandamizi kutoka nje ya nchi. Tume hiyo inayoongozwa na Mwenyekiti Shaban Aliila, inajumuisha makamishna sita, ambapo wawili kati yao wanatoka katika kanda za Afrika Mashariki na SADC. Makamishna hao wa kimataifa ni Jaji Barishaki Cheborion kutoka Uganda na Jaji Petrus T. Damaseb kutoka Namibia
Rais Samia ameeleza kuwa ushiriki wa majaji hao unalenga kupata "muono mpana" wa matukio hayo na amewashukuru Rais Yoweri Museveni wa Uganda na Rais Netumbo Nandi-Ndwaitwa wa Namibia kwa kuridhia kuleta majaji hao kusaidiana na majaji wa Tanzania
Rais Samia amebainisha kuwa tume hiyo imepewa hadidu za rejea zitakazoongoza majukumu yake na inatarajiwa kuwasilisha ripoti rasmi pamoja na mapendekezo ndani ya miezi mitano. Hata hivyo, Rais ameweka wazi kuwa muda huo unaweza kuongezwa ikiwa kutakuwa na uhitaji wa kufanya kazi hiyo kwa upeo mpana zaidi
.
"Ni imani yangu kwamba majaji hawa watakwenda kutumia taaluma, uzoefu, na viapo vyao kutekeleza kazi hii kwa weledi, umakini, na uadilifu mkubwa," amesisitiza Rais Samia wakati wa uzinduzi huo uliofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam -
Jambo TV
@Jambotv_
Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Namibia, Peter S. Shivute, amemteua Naibu Jaji Mkuu wa nchi hiyo, Jaji Petrus T. Damaseb, kuwa mjumbe wa Tume ya Uchunguzi wa Makosa ya Jinai (maarufu kama Tume ya Jaji Lila) iliyoanzishwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuchunguza viashiria vya jinai kutokana na matukio yaliyotokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.
Kupitia taarifa rasmi iliyotolewa na Tume ya Utumishi wa Mahakama ya Namibia (JSC) mnamo Agosti 5, 2026, imeelezwa kuwa uteuzi huo umefanywa kufuatia ombi rasmi lililowasilishwa na mamlaka za Tanzania likiomba kuteuliwa kwa Jaji anayehudumu au aliyestaafu kutoka Mahakama Kuu ya Namibia ili kushiriki katika Tume hiyo.
“Baada ya majadiliano ya kina, JSC iliunga mkono uteuzi wa Jaji Damaseb, ikiridhika kwamba kutokana na unyeti na uwezekano wa ugumu wa masuala yatakayochunguzwa, ilikuwa sahihi kumteua kiongozi mwandamizi wa Mahakama ya Namibia mwenye uzoefu mkubwa wa kazi za kimahakama na kiutawala.” Imesema taarifa hiyo
Kwa sasa, Jaji Damaseb anahudumu kama Naibu Jaji Mkuu wa Namibia na Rais wa Mahakama Kuu ya Namibia, na kwa mujibu wa nafasi yake, pia ni mjumbe wa moja kwa moja (ex officio) wa Mahakama ya Juu ya Namibia.
Mnamo Mei 18, 2026, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, aliteua Tume hiyo ya Uchunguzi wa Jinai kufuatia mapendekezo yaliyowasilishwa katika ripoti ya Tume ya uchunguzi wa matukio ya Oktoba 29 iliyokuwa ikiongozwa na Jaji Mkuu Mstaafu, Mohamed Othman Chande.
Julai 30, 2026 Rais Samia alieleza kuwa tume aliyoiteua ya jinai itaazinduliwa baadaye katika tarehe itakayotangazwa ambapo wajumbe wa tume hiyo ni pamoja na Jaji Lila, ambaye ni Jaji wa Mahakama ya Rufani na atakuwa kamishna na mwenyekiti wake pamoja na makamishna wa tume hiyo ambao ni Jaji mstaafu Gad Mjemmas, Jaji mstaafu Awadh Bawazir na Jaji mstaafu Aishieli Sumari. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Serikali ya Tanzania imeweka mkakati kabambe wa kuvutia uwekezaji mpya na mkubwa kutoka kwa kampuni za Dangote katika sekta za uzalishaji wa mbolea na nishati, ikiwa ni hatua ya kufuatilia kwa vitendo utekelezaji wa mazungumzo ya ngazi ya juu kati ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Mwenyekiti na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hizo, Alhaj Aliko Dangote.
Mkakati huo umeanza kushika kasi kufuatia ziara ya kikazi ya ujumbe wa Serikali ya Tanzania nchini Nigeria tarehe 6 Agosti, 2026, ulioongozwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo. Ujumbe huo ulitembelea na kukagua viwanda vikubwa vya Dangote ikiwamo kiwanda cha kusafisha mafuta cha Dangote Petroleum Refinery & Petrochemicals pamoja na kiwanda cha mbolea cha Dangote Fertiliser Limited.
Akizungumza Agosti 6, 2026 mara baada ya kutembelea viwanda hivyo, Prof. Kitila Mkumbo ameeleza kuwa mbali na Dangote kuwekeza kwenye kiwanda kikubwa cha saruji mkoani Mtwara, Lengo kuu la ziara hiyo ni kufungua na kukubaliana maeneo mapya ya uwekezaji ikiwamo sekta za mbolea na nishati.
Mkakati huu wa kuvutia uwekezaji kiwanda cha mbolea kutoka kwenye kampuni za Dangote unakuja wakati ambapo matumizi ya mbolea nchini Tanzania yameshuhudia ukuaji mkubwa. Takwimu rasmi zinaonesha kuwa matumizi ya mbolea yamepanda kwa asilimia 211, kutoka tani 363,599 katika msimu wa 2021/22 hadi kufikia tani 1,132,799 katika msimu wa 2025/26.
Aidha, mahitaji ya mbolea aina ya Urea yameongezeka kutoka tani 76,895 hadi tani 272,103 katika kipindi hicho, huku kukiwa na viwanda 48 vya ndani vinavyotumia Urea kama malighafi kuu.
Kufanikiwa kwa uwekezaji huu nchini kutaiwezesha Tanzania kuzalisha mbolea ya kutosha si tu kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya ndani yanayokadiriwa kufikia tani milioni 2.1 ifikapo mwaka 2030, bali pia kuifanya nchi kuwa kitovu cha kuuza mbolea katika masoko ya kikanda ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), SADC, na Soko Huru la Afrika (AfCFTA).
Katika ziara hiyo, Prof. Kitila aliambatana na mawaziri na viongozi wengine akiwamo Waziri wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga; Naibu Waziri wa Nishati, Salome Makamba; Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile, Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa; Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya; Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais- Uwekezaji, Dkt. Fred Msemwa, Mwenyekiti wa Bodi ya TISEZA, Balozi Dkt. Aziz Mlima, pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa TISEZA, Gilead Teri, na watendaji wa sekta za bandari, usafirishaji na miundombinu.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Namna wananchi wa Sirari, wilayani Tarime mkoani Mara walivyohusika kukichangia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia kampeni yake ya Tonetone katika mkutano wa hadhara wa chama hicho ulioongozwa na Makamu Mwenyekiti wake bara, John Heche, leo Agosti 6, 2026.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tanzania Bara, John Heche, ameendelea kuweka wazi msimamo mkali wa chama hicho kuelekea kile kinachoitwa maridhiano ya kitaifa, akisisitiza kuwa kuna mambo ya msingi lazima yatekelezwe ili nchi iweze kuanza upya
Akihutubia mkutano mkubwa wa hadhara leo, Sirari wilayani Tarime mkoani Mara, Heche ameeleza kuwa CHADEMA imemtumia ujumbe Rais Samia Suluhu Hassan ikibainisha kuwa hitaji lao la kwanza na la lazima ni kuachiwa huru kwa Mwenyekiti wa chama hicho ngazi ya taifa, Tundu Lissu. Heche amesisitiza kuwa ulimwengu unajua kuwa Lissu anaonewa, hivyo ni lazima awe nje kama sehemu ya kutenda haki
Aidha, Heche ameweka msimamo wa chama hicho kutaka kuwepo kwa msuluhishi wa kimataifa atakayekuja nchini kusimamia utatuzi wa matatizo ya kisiasa. Amesema msuluhishi huyo atasaidia kupitia nyaraka mbalimbali ili kuhakikisha watu wote waliohusika na matendo ya kuua na kuteka watu wanawajibishwa kwa mujibu wa sharia.
Msimamo mwingine uliotolewa na Heche ni hitaji la serikali kutoa fidia kwa familia za watu waliouawa kwa kupigwa risasi mnamo tarehe 29 na 30 Oktoba.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) @ChademaTZ2 Bara, John Heche @HecheJohn amekemea vikali wimbi la utekaji na kupotea kwa watu nchini wakati akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika leo katika mji wa mpakani wa Sirari, wilayani Tarime mkoani Mara.
Katika hotuba yake, Heche amehoji mantiki ya serikali kujinasibu kwa miradi ya maendeleo kama ujenzi wa barabara, hospitali, na miradi ya maji wakati raia wanaotegemewa kutumia huduma hizo wanapotea au kutekwa.
Amesisitiza kuwa kila kitu duniani kipo kwa ajili ya binadamu, hivyo ni vigumu kuelewa ununuzi wa ‘Ambulance’ au ujenzi wa hospitali ikiwa binadamu hawapo, akisema kuwa hospitali haziwezi kujengwa kwa ajili ya mbwa bali kwa watu.
Heche amebainisha kuwa thamani ya binadamu ni kuu kuliko mali yoyote, akitolea mfano kuwa nyumba hujengwa ili kumkinga binadamu na baridi, na hivyo nyumba haiwezi kuwa bora kuliko mtu.
Amewashambulia viongozi na Wabunge wa Tarime kwa kushindwa kuwasilisha hoja binafsi bungeni kuuliza walipo wananchi wao wanaopotea, akisema kuwa kiongozi hawezi kuwa kiongozi wa mawe, mijusi, au ng'ombe, bali lazima aongoze watu.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan na Yoweri Museveni wa Uganda wameshuhudia utiaji saini wa Hati ya Makubaliano (MoU) ya kuendeleza ujenzi wa kiwanda cha kusafisha mafuta na Kitovu cha Nishati cha Kikanda Jijini Tanga, mradi unaotarajiwa kubadili taswira ya sekta ya nishati Afrika Mashariki.
Makubaliano hayo yaliyosainiwa na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Kampuni ya Taifa ya Mafuta ya Uganda (UNOC) na kampuni ya VTTO Bahrain, yanafungua njia kwa hatua za awali za kitaalamu na uwekezaji katika ujenzi wa miundombinu hiyo muhimu.
Akizungumza katika hafla hiyo leo Ikulu jijini Dar es Salaam Waziri wa Nishati Deogratias Ndejembi amesema makubaliano hayo ni hatua muhimu katika kuimarisha ushirikiano wa Tanzania na Uganda kwenye sekta ya nishati.
Ndejembi amesema kuwa mradi huo unatarajiwa kujumuisha kiwanda cha kusafisha mafuta, miundombinu ya kuhifadhi bidhaa za petroli, huduma za usafirishaji pamoja na bomba la kusafirisha bidhaa za mafuta linaloweza kufanya kazi kwa pande zote mbili kati ya Tanzania na Uganda.
Amesema kuwa utekelezaji wa mradi huo unalenga kuifanya Tanga kuwa kituo muhimu cha usambazaji wa bidhaa za mafuta kwa nchi za Afrika Mashariki na ukanda mpana wa Afrika.
"Utiaji saini wa leo siyo tu makubaliano, bali ni msingi mwingine wa mageuzi ya kiuchumi katika Afrika Mashariki," amesema.
Amesema mradi huo unaendeleza ushirikiano ulioanza kupitia Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP), wenye thamani ya takribani dola za Marekani bilioni sita, unaolenga kusafirisha mafuta ghafi kutoka maeneo ya uzalishaji nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga.
Ndejembi amesema tofauti na EACOP ambayo inalenga kusafirisha mafuta ghafi, Kitovu cha Nishati cha Tanga kitasaidia kuongeza thamani ya rasilimali hiyo kupitia usafishaji wa mafuta, uhifadhi, usafirishaji na biashara ya bidhaa za petroli.
"Mradi huu ukikamilika una uwezo wa kuvutia uwekezaji unaozidi dola za Marekani bilioni 20, kuunda ajira, kuchochea ukuaji wa viwanda na kuimarisha usalama wa nishati katika ukanda huu," amesema.
Ndejembi ameongeza kuwa mradi huo unaendana na maono ya Rais Samia ya kuifanya Tanga kuwa kitovu cha biashara ya mafuta Afrika Mashariki kutokana na nafasi yake ya kimkakati, ikiwemo kuwa lango la Bahari ya Hindi na eneo la kupokea bomba la EACOP.
Kwa upande wake, Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini wa Uganda, Dkt. Ruth Nankabirwa Ssentamu amesema makubaliano hayo yanaonesha dhamira ya nchi hizo mbili ya kushirikiana katika kuongeza thamani ya rasilimali na kukuza uchumi wa kikanda.
"Hatupaswi kuuza malighafi pekee. Tunapaswa kujenga viwanda, kuunda ajira zenye ujuzi na kuhakikisha wananchi wetu wanapata manufaa makubwa kutokana na rasilimali hizi," amesema.
Dkt. Nankabirwa amesema kiwanda cha kusafisha mafuta kinachopangwa kujengwa Kabaale nchini Uganda na Kitovu cha Nishati cha Tanga havitashindana, bali vitakamilishana kwa kuongeza uwezo wa usafishaji wa mafuta na kuimarisha upatikanaji wa nishati katika Afrika Mashariki.
Ameongeza kuwa Tanzania na Uganda zinaendelea na utekelezaji wa miradi mingine ya pamoja, ikiwemo bomba la kusafirisha bidhaa za mafuta, bomba la gesi asilia kati ya nchi hizo mbili na mradi wa njia ya kusafirisha umeme wa kilovolti 400.
Utiaji saini wa makubaliano hayo ni hatua nyingine katika ushirikiano wa muda mrefu wa Tanzania na Uganda kwenye sekta ya nishati ulioimarishwa kupitia EACOP mwaka 2017. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Maji, Jumaa Hamidu Aweso amekagua ujenzi wa Kituo cha Afya Masieda kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, mkoani Manyara, na kusisitiza kuwa awamu ya pili ya mradi huo ikamilike kwa wakati ili wananchi waanze kunufaika na huduma bora za afya. Kituo hicho kinatarajiwa kuhudumia wakazi 7,865 wa Kata ya Masieda na maeneo ya jirani, ambao kwa muda mrefu walikuwa wakisafiri umbali mrefu kufuata huduma za afya.
Mradi huo wenye thamani ya Shilingi 586,032,142, unaotekelezwa kwa fedha za Serikali Kuu, unahusisha ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje (OPD), jengo la maabara, jengo la mama na mtoto, jengo la upasuaji, jengo la kufulia pamoja na kichomea taka. Hadi sasa, Shilingi 546,032,000 zimetumika katika utekelezaji wa mradi huo, huku Shilingi 40,000,142 zikitengwa kukamilisha kazi zilizobaki.
Akizungumza wakati wa ukaguzi wa mradi huo, Aweso amesema awamu ya pili ya utekelezaji itahusisha ununuzi wa vifaa tiba na vifaa vingine muhimu ili kituo hicho kianze kutoa huduma kwa wakati. Aidha, ameeleza kuwa changamoto ya upatikanaji wa nguzo za umeme itatatuliwa ili kuwezesha kufikishwa kwa umeme na huduma ya maji katika kituo hicho, akisisitiza kuwa Serikali haitaruhusu changamoto hizo kuchelewesha utoaji wa huduma kwa wananchi.
Aweso pia amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan itaendelea kuwekeza katika kuboresha huduma za kijamii kupitia sekta za afya, maji na elimu. Amesema pamoja na ujenzi wa vituo vya afya na miradi ya maji, Serikali inaendelea kujenga shule na kuimarisha miundombinu mingine ya maendeleo ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na maendeleo yanafika katika kila kona ya nchi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo @ChademaTZ2 John Heche @HecheJohn amepokewa na wananchi na wanachama wa chama hiyo Sirari, wilayani Tarime mkoani Mara leo kwa ajili ya mkutano wa hadhara wa chama hicho, mkutano ambao ni wa kwanza kufanyika tangu utaratibu wa kufanyika kwa mikutano hiyo utangazwe na Jeshi la Polisi Julai 29, 2026 baada ya mikutano hiyo kupigwa marufuku Juni 26, 2026 kutokana na vitisho vya kiusalama.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO
Kesi ya Uhujumu uchumi Na. 4521/2026 inayomkabili Wendy William Ishengoma na wenzake wanne imeendelea leo Agosti 6, 2026 Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Rushwa na Uhujumu uchumi, Dar es Salaam ambapo shahidi wa pili wa jamhuri Inspekta Michael Mwakalikamo(40) ameanza kutoa ushahidi wake mbele ya Jaji Dkt. Dafina Ndumbaro anayesikiliza kesi hiyo.
Awali shauri hilo lilianza kwa aliyekuwa shahidi wa kwanza Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Polisi (ASP) Democracy Hussein Nivako (51) kumalizia ushahidi wake kwa maswali ya kusawazisha (Re-examination) huku akifafanua kuwa hesabu ya zaidi ya bilioni tano ambazo Wendy na wenzake wanadaiwa kutakatisha zimetokana na hesabu walizopata kwenye fedha taslimu, nyaraka na vitabu vya mahesabu vya kampuni ya Atlantic Microcredit LTD, ambayo Wendy ni Mkurugenzi wake
Shahidi wa pili akiongozwa na Mawakili wa Jamhuri aliieleza Mahakama kuwa yeye anafanya kazi katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Kitengo cha Fedha(FCU) kuanzia mwaka 2016 na yeye ndiye aliyeongoza timu ya askari wanne na Afisa wa Benki Kuu ya Tanzania(BOT) mmoja katika upelelezi na ukamataji wa washtakiwa pamoja na nyaraka zao.
Inspketa Michael ameieleza mahakama alivyopokea maelekezo ya viongozi wake mpaka kuwakamata washtakiwa wa kesi hiyo kati ya Oktoba 8-10, 2024 ambapo pamoja na kuwakamata watuhumiwa pia alizikamata fedha, nyaraka zenye hesabu za kampuni ya Atlantic Microcredit LTD, bahasha, Leseni pamoja na magari mawili aina ya Alphard jeupe na jeusi yaliyokuwa yakimilikiwa na kampuni hiyo.
Aliieleza mahakama kuwa vitu vyote alivyovikamata alivipeleka na kuvikabidhi katika Ofisi ya taifa ya mashtaka.
Wakili wa Utetezi Peter Madeleka @PMadeleka nje ya mahakama hiyo ameeleza ju ya yaliyotokea kwenye kesi hiyo akieleza kuwa katika maswali ya dodoso ataiomba Mahakama kumhoji Mkurugenzi wa Mashtaka huku akitoa wito kutokucheleweshwa kwa usikilizwaji wa shauri hilo kwani wateja wake wamekaa gerezani kwa muda mrefu kuanzia 2024.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Wakala wa huduma za miamala ya fedha, Jijini Dodoma, Hilda Bryson, ameporwa fedha taslimu Shilingi Milioni 4 pamoja na vifaa vya kazi baada ya kuvamiwa na kundi la watu takriban 7 usiku wa Agosti 5, 2026
Kwa mujibu wa Hilda, alikuwa akirejea nyumbani akitokea kazini akiwa ameambatana na jirani yake, ndipo walipovamiwa na watu hao waliokuwa na mapanga na marungu, ambao walianza kuwashambulia na kuwajeruhi katika sehemu mbalimbali za miili yao.
Baada ya kuwazidi nguvu, wahalifu hao walifanikiwa kuondoka na mkoba uliokuwa na fedha taslimu Shilingi Milioni 4, mashine za benki za NMB na NBC, simu 8 za wakala pamoja na kadi binafsi za Wakala huyo kabla ya kutoweka kusikojulikana.
Wahanga hao wamesema walipiga kelele kuomba msaada wakati wa shambulio hilo, lakini hakuna aliyefika kuwaokoa.
Jambo TV imemtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gellus Hyera, kwa njia ya simu ili kupata ufafanuzi kuhusu tukio hilo, ambaye amesema Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi, na litatoa taarifa rasmi mara uchunguzi utakapokamilika.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Saad Mtambule, ameitaka jamii kuwafichua watu wanaowatilia shaka kuwa ni wahamiaji haramu ili vyombo vya ulinzi na usalama viweze kuwachunguza na kuchukua hatua za kisheria dhidi ya watu wanaokaa nchini kinyemela.
DC Mtambule ametoa wito huo jana wakati akizindua rasmi Klabu ya Uhamiaji katika Shule ya Green Acres jijini Dar es Salaam, tukio lililohudhuriwa na Afisa Uhamiaji wa Mkoa wa Dar es Salaam, Vicent Haule, pamoja na Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Songoro Mnyonge.
Akieleza mkakati wa Wilaya hiyo, DC Mtambule alibainisha kuwa Kinondoni ina zaidi ya shule 200, hivyo wataingia shule kwa shule kuhamasisha uanzishwaji wa klabu hizo ili kuwajenga watoto kutambua na kupinga uhamiaji haramu tangu wakiwa wadogo:
"Tutapita kuhamasisha shule zianzishe utaratibu huo ili wanafunzi wote wajue masuala ya uhamiaji wakiwa wadogo. Tunawapenda wahamiaji wanaofuata sheria na taratibu za nchi yetu, lakini lazima tuwajenge watoto wetu kuchukia na kupinga uhamiaji haramu tangu ngazi ya chini."
DC Mtambule alitoa onyo kali kwa wananchi wanaorubuniwa au kuwakingia kifua wahamiaji haramu katika maeneo yao ya makazi akisema, "Kuna watu wanarubuniwa na vitu vidogo ili wawafiche hawa wahamiaji haramu. Natoa wito tusithubutu kuwapa nafasi kwenye maeneo wetu, maana tukikubaini umemficha mhamiaji haramu, nawe pia utakamatwa na kuchukuliwa hatua kali za kisheria."
Aidha, alipongeza Jeshi la Uhamiaji nchini chini ya Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Makakala, kwa jitihada kubwa za usiku na mchana za kudhibiti uhamiaji haramu.
Kwa upande wa Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Songoro Mnyonge alisema kuanzishwa kwa klabu hiyo ni hatua kubwa ya kimkakati itakayorithisha vijana uelewa wa madhara ya uhamiaji kinyume cha sheria.
Meya Mnyonge aliipongeza Shule ya Green Acres kwa kuwa ya kwanza Mkoani Dar es Salaam kuzindua klabu hiyo, huku akimkumbuka mwanzilishi wa shule hiyo, aliyekuwa Diwani wa Magomeni, Marehemu Bujugo, na kumpongeza Mkurugenzi wa sasa, Jackline Rushaigo, kwa kuendeleza maono ya shule hiyo kitaaluma na kimaadili.
Naye Mkurugenzi wa Green Acres, Jackline Rushaigo, alilishukuru Jeshi la Uhamiaji kwa kuichagua shule yao kuwa vinara wa klabu hiyo na kuahidi kuwa klabu hiyo itakuwa chombo muhimu cha kulea maadili mema na usalama wa taifa. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Wanachama na Viongozi 23 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya Nyamagana, wamefikishwa tena mahakamani leo Agosti 6, 2026 mbele ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanza, Erick Marley kwa ajili ya kutajwa katika kesi mbili tofauti zinazowakabili zenye kosa moja la kujihusisha na vikao au mazungumzo yanayolenga kufanya ugaidi.
Katika kesi ya kwanza namba 16379/ 2026 inawahusisha washtakiwa 13 kutoka Wilaya ya Ilemela ambao wanatuhumiwa kufanya kosa hilo kati ya Juni 25 hadi Julai 7, 2026.
Washtakiwa hao ni Alphaxadi Nyamwaga, Fantson Mpango, Abely Mwesa, Hassan Said, Emanuel Wambura, Adam Idd, Damas Sadock, Petro Mabula, Abdul Kagwidi, Devid Mashaka, Philipo Masatu, Edward Mikindo na Emmanuel Doto.
Katika kesi ya pili namba 16375/2026 inawahusisha washtakiwa 10 kutoka Wilaya ya Nyamagana ambapo wanatuhumiwa kufanya vikao hivyo kati ya Julai 4 na Julai 7 mwaka huu katika eneo la Igoma.
Washtakiwa hao ni Deus Masalago, Mohamed Tosha, Fabian Nguvumali, Samweli Mtani, Samweli Kobell, Julius Makonga, Fanuel Lutana, Philipp Kulwa, Philipp Shipuluko na Hamis Mnyimvua.
Upande wa Jamhuri umewakilishwa na jopo la Mawakili wakiongozwa na Emmanuel Kimey ambaye aliiomba Mahakama isogeze mbele kesi hizo ili kukamilisha upelelezi. Hoja iliyopingwa vikali na Mawakili wa Utetezi wakiongozwa na Gaston Garubindi, Sijaona Revocatus, Alfred Sotoka na Girson Ishengoma.
Wakili wa Utetezi, Gaston Garubindi aliiomba Mahakama itoe amri upande wa Jamhuri katika tarehe ijayo, walete majibu ya hatua gani wamefikia katika upelelezi ili kesi hizo zisichukue muda mrefu kwa kisingizio cha ushahidi.
Akijibu hoja hiyo Wakili wa Jamhuri, Kimey amesema wamepokea maombi hayo na watajitahidi kuyafanyia kazi.
Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanza, Erick Marley baada ya kusikiliza hoja zote za pande mbili ameahirisha kesi hizo mpaka Agosti 17, huku akitaka hoja zilizoibuliwa na upande wa utetezi zifanyiwe kazi.
Akizungumza nje ya Mahakama, Mkurugenzi wa Sheria na Haki za Binadamu wa CHADEMA, Gaston Garubindi amekosoa vikali hatua ya upande wa mashtaka kudai kuwa upelelezi haujakamilikaThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila ameagiza kukamatwa kwa mmiliki na mjenzi wa jengo moja lililopo Masaki, baada ya kubainika kuwa walijenga ghorofa 13 badala ya ghorofa sita zilizoidhinishwa kwenye kibali cha ujenzi.
Akizungumza leo Agosti 6, 2026, wakati wa ziara ya ukaguzi wa utekelezaji wa sheria na taratibu za ujenzi, Chalamila amesema hatua hiyo inalenga kuruhusu uchunguzi wa kitaalamu kubaini iwapo msingi wa jengo hilo uliundwa kuhimili idadi hiyo ya ghorofa.
Amesema wataalamu wanapaswa kufanya tathmini ya haraka ya usalama wa jengo hilo, huku mmiliki na mjenzi wakishikiliwa kwa hatua za kisheria kutokana na tuhuma za kukiuka masharti ya kibali cha ujenzi.
Chalamila amesisitiza kuwa Serikali haitamvumilia mtu yeyote anayekiuka sheria za ujenzi, akieleza kuwa hatua kali zitachukuliwa dhidi ya wote watakaobainika kuhatarisha usalama wa wananchi kwa kujenga kinyume na vibali walivyopewa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, ameongoza ujumbe wa ngazi ya juu wa Serikali ya Tanzania katika ziara ya kimkakati jijini Lagos, Nigeria, kutembelea Kampuni za Dangote.
Katika ziara hiyo, Prof. Kitila amefanya mazungumzo ya kimkakati na Rais na Mtendaji Mkuu wa Dangote Group, Alhaj. Aliko Dangote kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wa uwekezaji kati ya Tanzania na kampuni hiyo kubwa zaidi ya viwanda barani Afrika.
Ziara hiyo ni mwendelezo wa kutafsiri maono ya Dira 2050 ambayo imesema Sekta Binafsi ndiyo iwe injini ya kujenga uchumi katika safari ya kulifikia taifa lanye uchumi wa Dola za Marekani Trilioni moja ifikapo mwaka 2050.
Pia ziara hiyo ni mwendelezo wa ushirikiano unaozidi kuimarika kati ya Serikali ya Tanzania na Dangote Group, kutokana na ziara ya hivi karibuni ya Alhaj Dangote nchini Tanzania ambapo alikutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, na kufanya mazungumzo kuhusu kupanua uwekezaji katika sekta mbalimbali za kimkakati za uchumi.
Mazungumzo hayo yaliweka msingi wa kuendeleza ushirikiano wa kiuchumi na kuharakisha maendeleo ya viwanda nchini Tanzania huku ziara ya Lagos ikiwa ni hatua inayofuata ya kutekeleza makubaliano yaliyofikiwa Dar es Salaam kupitia miradi ya uwekezaji na ushirikiano wa muda mrefu.
Mbali na Prof. Kitila Mkumbo, ujumbe huo unajumuisha Waziri wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga; Naibu Waziri wa Nishati, Salome Makamba; Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile; Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa, na Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya.
Wengine ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Uwekezaji, Dkt. Fred Msemwa; Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA), Balozi Dkt. Aziz Mlima; Mkurugenzi Mkuu wa TISEZA, Gillard Teri; viongozi wandamizi serikalini na watengaji wakuu wa mashirika mbalimbali ya kwenye sekta za uchukuzi, usafirishaji, ugavi, bandari na miundombinu
Akizungumza wakati wa kikao hicho Alhaji Dangote amempongeza Rais Dkt. Samia kwa uongozi wake wenye maono na jitihada za kuendelea kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini.
Amesema mageuzi yanayoendelea kutekelezwa chini ya uongozi wake yameongeza imani ya wawekezaji, kuboresha urahisi wa kufanya biashara na kuiweka Tanzania miongoni mwa nchi zinazovutia zaidi uwekezaji wa kimkakati barani Afrika.
Alhaji Dangote amesema kuwa mazungumzo aliyofanya na Rais Samia wakati wa ziara yake nchini Tanzania yameimarisha zaidi imani ya Dangote Group katika mwelekeo wa maendeleo ya uchumi wa Tanzania.
Ameeleza kuwa Tanzania ina fursa kubwa za uwekezaji na kusisitiza dhamira ya kampuni yake kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuharakisha ajenda ya maendeleo ya viwanda kupitia ubia wa kimkakati.
Aidha, amempongeza Prof. Kitila kwa kuongoza ujumbe wenye nguvu na ulioratibiwa kwa ufanisi, akisema muundo wa ujumbe huo unaonesha dhamira ya Serikali ya Tanzania ya kutafsiri sera na maono ya uwekezaji kuwa miradi halisi yenye manufaa kwa Taifa.
Amebainisha kuwa uwepo wa viongozi waandamizi na wataalamu kutoka taasisi muhimu unaonesha utayari wa Tanzania kujenga ushirikiano endelevu utakaochochea maendeleo ya viwanda na ukuaji wa uchumi.
Miongoni mwa mambo muhimu yaliyojadiliwa ni mpango wa muda mrefu wa Dangote Group wa kuwekeza hadi dola za Marekani bilioni 46 ifikapo mwaka 2030 katika sekta mbalimbali za kimkakati barani Afrika, ikiwamo Tanzania.
Mazungumzo yalijikita katika kupanua ushirikiano kwenye sekta za viwanda, nishati, madini, uchukuzi, usafirishaji na ugavi (logistics), bandari, miundombinu pamoja na sekta nyingine zenye kipaumbele katika ajenda ya maendeleo ya Tanzania.
Akizungumza kwa niaba ya Serikali ya Tanzania, Prof. Kitila alisisitiza dhamira ya Rais Dkt. Samia ya kuendelea kujenga mazingira ya biashara na uwekezaji yaliyo thabiti, shindani na rafiki kwa wawekezaji. Alieleza kuwa Serikali inaendelea kutekeleza mageuzi yanayolenga kuboresha miundombinu, kuimarisha mazingira ya uwekezaji na kuunda fursa zaidi za ukuaji wa uchumi endelevu, ajira na uhamishaji wa teknolojia.
Katika ziara hiyo, ujumbe wa Tanzania pia unatarajiwa kutembelea viwanda vya kisasa vya Dangote Group vilivyopo Lagos ili kujionea mifumo ya uzalishaji wa kisasa na usimamizi wa shughuli za ugavi. Ziara hiyo itatoa uzoefu na maarifa yatakayosaidia Tanzania katika azma yake ya kuwa kitovu cha viwanda na uwekezaji katika ukanda wa Afrika Mashariki. Ziara ya Lagos ni hatua nyingine muhimu katika utekelezaji wa diplomasia ya uchumi ya Rais Dkt. Samia -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Uchungu wa mwana aujuaye mzazi, ndivyo unavyoweza kusema unapokutana na Sharifa Kassim, mkazi wa Masantula, Chanika, mkoani Dar es Salaam ambaye kwa sasa anaishi katika hali ya huzuni na majonzi mazito kutokana na kupotea kwa mwanaye, Amaira. Ni takribani siku 31 sasa tangu mwanaye aibiwe akiwa na umri wa siku 42 tu, tukio ambalo limeacha kidonda kisichopona moyoni mwa mzazi huyu.
Mnamo tarehe 6 Julai, 2026, Sharifa alimpeleka mwanaye katika Hospitali ya Nguvu Kazi, Chanika, kwa ajili ya kliniki na kupata chanjo. Akiwa hospitalini hapo, Sharifa anasimulia kuwa alikutana na mwanamke mmoja aliyekuwa amevalia koti la udaktari ambaye alianza kuzungumza naye kwa urafiki kuhusu hali ya mtoto
"Ghafla nikajisikia haja ndogo, nikamwambia (yule dada) nishikie (mtoto). Nilivyompa, nikaenda uani, narudi sijamkuta; nikakuta mkoba wangu tu pembeni, yeye sijamkuta na mtoto," anasimulia Sharifa kwa uchungu.
Sharifa anabainisha kuwa aliamini mwanamke huyo ni mhudumu wa afya kutokana na mavazi yake na mazingira ya hospitali ambapo hata yeye mwenyewe alijifungulia hapo
Familia ya mtoto Amaira imeeleza kutoridhishwa na kasi ya kusaka ukweli wa tukio hilo ambalo kwa sasa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam linaendelea kulichunguza. Kutokana na hilo, imewaombaWaziri Mkuu wa Tanzania Dkt. Mwigulu Nchemba na Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kuingilia kati suala hilo.
"Mamangu Rais Samia, naomba unisaidie kumpata mtoto wangu. Mwezi sasa sijui mtoto wangu anakula nini, ananyonya nini, yupo hai ama hayupo? Naomba utumie jeshi lako ili mtoto wangu apatikane," amelalamika Sharifa.
KUFAHAMU UNDANI WA MKASA HUU, TEMBELEA CHANELI YETU YA YOUTUBE YA JAMBO TV KUPITIA KIUNGO HIKI youtu.be/SHQDT3IUdXwThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
📍IRINGA -Baadhi ya madereva wanaotumia Barabara ya Mlima Kitonga wamempongeza askari wa Jeshi la Polisi, Staff Sajenti (SSGT) Marcus Mongo, kwa usimamizi wa mtiririko wa magari jambo lililosaidia kupunguza foleni na kuimarisha usalama barabarani.
Wakizungumza na Jambo TV, madereva hao wamesema uwepo wa askari huyo umerahisisha safari zao na kuongeza usalama, huku wakiomba juhudi hizo ziendelee ili kupunguza ajali.
Akizungumzia siri ya mafanikio yake, SSGT Marcus Mongo amesema amekuwa akitoa elimu na maelekezo kwa madereva kuhusu usalama barabarani, jambo linalochochea ushirikiano na kurahisisha usafiri.
Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, SACP Allan Bukumbi, amesema utendaji wa askari huyo unatokana na mafunzo ya mara kwa mara pamoja na nidhamu yake kazini huku akiwataka madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani wakati wote, si wanapowaona askari pekee.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo @ChademaTZ2 Bara John Heche @HecheJohn amesema Mama yake mzazi amekuwa na hofu kutokana na taarifa anazozisikia na kuziona kwenye mitandao ya kijamii juu ya usalama wake.
Heche ameeleza akiwa mkoani Shinyanga na kufafanua kuwa kutokana hofu hiyo mama yake amekuwa akimpigia simu kila wakati na amekuwa akisumbuliwa mara kwa mara na presha.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Jeshi la Polisi Tanzania, limesema Dereva wa Pikipiki aliyeonekana kwenye picha mjongeo(video) akizozana na Askari Polisi alizuiwa kuingia barabarani wakati Mwenge wa Uhuru unatakiwa kupita lakini akakaidi ndipo askari wakamzuia.
Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi hilo DCP David Misime imeeleza kuwa tukio hilo lilitokea Julai 30,2026 Wilaya ya Bariadi Mkoa wa Simiyu ambapo dereva huyo alisimamishwa kwa ajili ya usalama wake na wa watu wengine lakini alikaidi ndipo ikabidi Askari wamzuie na matokeo yake pikipiki ikadondoka.
Pamoja na hayo taarifa imesema tukio hilo lilianza kushughulikiwa na kuchukuwa hatua kuanzia hiyo Julai 30, 2026 ikiwa ni pamoja na kupata maelezo sahihi ya walioshuhudia kilichotokea toka mwanzo.
Ikumbukwe leo ilionekana video mtandaoni ya mwanaume mmoja akizozana na askari watatu na mgambo wawili ambapo palikuwa na pikipiki chini huku magunia yaliyokuwa yamebebwa kwenye pikipiki yake yake moja likisukumwa mtaroni na jingine likisogezwa pembeni kidogo ya barabara jambo ambalo lilitengeneza mjadala mkubwa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake wa Chama cha Wakulima (AAFP) Taifa, Shani Ally Kitumbua, amemkosoa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, John Heche kutokana na kauli yake ya kukiita AAFP kuwa "chama cha mfukoni" na kudai kuwa kina watu wachache.
Akizungumza na waandishi wa habari Agosti 5, 2026 katika Makao Makuu ya AAFP mkoani Dar es Salaam, Shani amesema kauli hiyo inakidhalilisha chama hicho na wanachama wake.
Amesema AAFP ni chama halali kilichosajiliwa, kilishiriki uchaguzi mkuu na kinastahili kuheshimiwa kama vyama vingine vya siasa. Aidha, amesema chama hicho kilikubali kushiriki kikao kilichoandaliwa na Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa viongozi wa vyama vya siasa kwa hiari, kwa lengo la kuchangia maridhiano na kuimarisha amani nchini.
Kauli ya Shani inajibu matamshi ya Heche aliyoyatoa Agosti 3, 2026, wakati akizungumza na viongozi wa CHADEMA Wilaya ya Tarime. Katika hotuba hiyo, Heche alisema kuwa mazungumzo yoyote ya kisiasa yasiyohusisha CHADEMA hayawezi kuwa na uzito, akidai kuwa kukialika AAFP badala ya CHADEMA hakuwakilishi uhalisia wa kisiasa nchini.
"Mazungumzo ya aina yoyote yakiacha CHADEMA nje, hakuna mazungumzo hapo. Tusidanganyane, unachukua chama kinaitwa AAFP, chama chenye watu wawili unachukua AAFP, chama ambacho hata mke wa mwenyekiti wake ni mwanachama wa CHADEMA. Chama cha mfukoni 'briefcase', ukiacha CHADEMA nje umeacha robo tatu ya wananchi wa nchi hii”, alisikika Heche.
Akijibu kauli hiyo, Shani amesema viongozi wa kisiasa wanapaswa kutumia lugha za kuheshimiana na kuepuka kauli zinazoweza kudhalilisha vyama vingine, akisisitiza kuwa tofauti za kisiasa hazipaswi kuathiri juhudi za kujenga maridhiano na kudumisha amani nchini.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Dkt. Rugemeleza Nshala ametoa wito kwa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika TLS Wakili Boniface Mwabukusi kuchukua hatua za makusudi kutokana na mawakili kuzuiwa kutoa muhtasari wa kesi kwa waandishi wa habari(Press) ndani ya viunga mahakama
Dkt. Nshala ametoa wito huo leo Agosti 5, 2026 ofisini kwake jijini Dar es Salaam mara baada ya kushindwa kuzungumza na waandishi wa habari Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam baada ya kesi inayoihusu CHADEMA kuahirishwa.
Dkt. Nshala ameeleza kuwa kama mawakili watachukua hatua kwenda kwa uongozi wa Mahakama na baadae kufungua kesi mahakamani ikibdi juu ya jambo hilo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Agosti 28, 2026 saa tisa alasiri Mahakama Kuu inatarajiwa kutoa uamuzi juu ya maombi madogo ya zuio la kufanya shughuli za kisiasa kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo yaliyowasilishwa mahakamani hapo na Said Issa Mohammed na Ahmed Rashid.
Maombi hayo yametolewa na wadai hao katika kesi ya msingi ya mgawanyo wa rasilimali iliyofunguliwa na Said na mwenzake dhidi ya Bodi ya Wadhamini wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo na Katibu Mkuu wa chama hicho.
Uamuzi wa maombi hayo ulipangwa kutolewa leo na Jaji Mbagwa baada ya kukamilika kwa majibizano ya hoja kwa mawakili wa pande zote lakini Wakili anayeiwakilisha CHADEMA Dkt. Rugemeleza Nshala aliieleza mahakama kuwa hakuweza kukamilisha kuwasilisha majibu ya hoja za waleta maombi kutokana na kuwa na msiba wa kaka yake.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Shauri la ugaidi linalomkabili mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Dkt. Melikisedeki Kaijage, limeahirishwa hadi Agosti 19, 2026 baada ya kutajwa leo Agosti 05, 2026 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma.
Shauri hilo lilitajwa mbele ya Hakimu Mfawidhi, Zabibu Mpangule, ambapo ilielezwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kulisikiliza, bali jukumu lake ni kuhakikisha faili la shauri linakamilika kabla ya kupelekwa katika mahakama yenye mamlaka ya kulisikiliza.
Mahakama imeiagiza Jamhuri kuharakisha uchunguzi wa shauri hilo, ikieleza kuwa kutokana na mtuhumiwa kuwa mtumishi wa umma, ni vyema uchunguzi ukakamilika mapema ili endapo hana hatia aweze kurejea kutekeleza majukumu yake.
Dkt. Kaijage alifikishwa mahakamani huku akiendelea kushikiliwa rumande, ambapo uchunguzi wa shauri hilo bado unaendelea.
Dkt. Kaijage alikamatwa Julai 8, 2026 na anakabiliwa na tuhuma za kuhamasisha maandamano.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini mkoani Mara, Esther Bulaya ameanza rasmi utekelezaji wa mpango wa kugawa mashine za ‘fotokopi’ katika shule mbalimbali za jimbo hilo, akigawa mashine tatu za kwanza zenye thamani ya jumla ya Shilingi Milioni 9.
Mashine hizo ambazo kila moja ina thamani ya Shilingi Milioni 3, zimekabidhiwa kwa Shule ya Msingi Ligamba (Kata ya Sazira), Shule ya Sekondari Manyamanyama (Kata ya Manyamanyama) na Shule ya Msingi Nyasana (Kata ya Kabasa).
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Bulaya amesema lengo la mpango huo ni kuhakikisha shule zinapata vifaa vitakavyorahisisha uchapishaji wa mitihani, majaribio, nyaraka za kiutawala na vifaa vingine vya kujifunzia, hivyo kuongeza ufanisi katika utoaji wa elimu.
Bulaya amesema mpango huo unakusudia kugawa jumla ya mashine 10 za ‘fotokopi’ zenye thamani ya Shilingi milioni 30, ambapo awamu ya kwanza imeanza kwa kugawa mashine tatu zenye thamani ya Shilingi milioni 9.
Hatua hiyo imepokelewa kwa furaha na walimu pamoja na viongozi wa maeneo husika, wakieleza kuwa mashine hizo zitapunguza gharama na changamoto zilizokuwa zikijitokeza katika uchapishaji wa nyaraka muhimu za shule. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ameagiza kuongeza kasi ya utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Mabasi cha Mkoa wa Manyara wenye thamani ya Shilingi bilioni 19.996 baada ya kubainika kuwa maendeleo ya mradi huo yamefikia asilimia 17 badala ya asilimia 40 zilizokuwa zimepangwa kufikiwa kwa kipindi hiki.
Aweso ametoa maelekezo hayo jana wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Manyara ambapo alikagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo.
Amesema Serikali haitavumilia ucheleweshaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa fedha za umma na kumtaka mkandarasi kuongeza rasilimali watu, vifaa na muda wa kazi ili kuhakikisha mradi unakamilika kwa wakati na kwa ubora unaotarajiwa. Aidha, amesisitiza kuwa Wizara itaendelea kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa mradi huo ili kuhakikisha unakidhi malengo yaliyokusudiwa ya kuboresha huduma za usafiri na kuchochea maendeleo ya Mkoa wa Manyara.
Kwa upande wake, Mkandarasi Mshauri wa mradi huo, William Matemu, amesema tayari wameweka mikakati ya kuongeza kasi ya utekelezaji ili kufidia muda uliopotea.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI PICHA:
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), Prof. Palamagamba John Kabudi, ameipongeza Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam @dawasatz kwa hatua zinazochukuliwa katika kuboresha huduma za usafi wa mazingira, hususan sekta ya majitaka.
Prof. Kabudi ametoa pongezi hizo baada ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Mradi wa Kuchakata Majitaka Buguruni wenye thamani ya shilingi Bilioni 190 ambao utekelezaji wake umefikia asilimia 33.
Katika ziara hiyo, Prof. Kabudi alipokea taarifa ya kina kuhusu maendeleo ya mradi huo, hatua zilizofikiwa katika ujenzi, teknolojia inayotumika pamoja na manufaa yanayotarajiwa kupatikana baada ya kukamilika kwake.
Akizungumza baada ya ukaguzi huo, Prof. Kabudi amesema Serikali itaendelea kusimamia kwa karibu utekelezaji wa miradi ya kimkakati inayolenga kuboresha huduma za usafi wa mazingira na kulinda afya za wananchi.
“Utekelezaji wa mradi huu ni ishara ya jitihada za Serikali za kuboresha huduma za jamii kwa wananchi. Kukamilika kwake kutaongeza uwezo wa ukusanyaji na uchakataji wa majitaka, kupunguza uchafuzi wa mazingira na kuboresha maisha ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam,” amesema Prof. Kabudi.
Ametoa rai kwa wasimamizi na watekelezaji wa mradi kuhakikisha unakamilika kwa wakati, huku wakizingatia ubora wa kazi na usanifu ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na mradi unakuwa na tija iliyokusudiwa.
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Miradi DAWASA, Mhandisi Christian Gava, amesema mradi huo unatekelezwa kwa ushirikiano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Korea, na kwa sasa umefikia asilimia 33 ya utekelezaji, ikiwa ni hatua iliyo mbele ya muda uliopangwa.
Amesema kazi zinazoendelea kwa sasa zinahusisha ujenzi wa miundombinu muhimu ya mtambo, ikiwemo majengo ya mitambo, mifumo ya kusafirisha majitaka pamoja na maandalizi ya kufunga vifaa vya kisasa vya uchakataji. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Karagwe, Dkt. Benson Bagonza, amesema wanaokwamisha kupatikana kwa Katiba Mpya ni makundi mawili ambayo ni wana CCM wanaomchukia mwana CCM mwenzao anayetoa matumaini ya katiba, pamoja na wapinzani wanaokimbilia katiba kabla ya kufanya maridhiano ya kweli.
Dkt. Bagonza ameeleza hayo Agosti 4, 2026, kupitia ukurasa wake wa Facebook, akibainisha kuwa majibu hayo yanatokana na maswali aliyojiuliza kuhusu hotuba ya Katiba Mpya, na kusisitiza kuwa mchakato huo unahitaji maridhiano ya dhati badala ya mihemko ya kisiasa.
"Maswali niliyouliza kuhusu hotuba ya katiba mpya yamejibiwa. Wanaozuia katiba mpya ni makundi mawili. kwanza, ni wana CCM wanaomchukia mwana CCM anayewapa watu matumaini ya katiba mpya. Pili, ni wapinzani wanaokimbilia katiba mpya kabla ya maridhiano ya kweli." Ameandika Askofu Bagonza.
Kiongozi huyo ametoa wito kwa wana CCM kuweka akiba ya maneno, kufuatia mijadala iliyoibuka kabla na baada ya vikao vya chama hicho vilivyofanyika Zanzibar tarehe 28 na 29 Julai, 2026, akionya kuwa baadhi ya kauli zimevuka mipaka ya heshima kwa viongozi wakuu.
Askofu Bagonza ameeleza kuwa ni hatari kwa wanachama kujifanya wanahisi kuzorota kwa mahusiano kati ya Rais, Makamu wa Rais, Rais wa Zanzibar na Waziri Mkuu, na akawasihi kuacha tabia ya kuleta hoja za kutaka kujua mambo zaidi ya viongozi hao wanavyojuana.
Amesisitiza kuwa mfumo wa Urais na Umakamu hautenganishwi, hivyo kumkashifu Makamu wa Rais ni sawa na kumkashifu Rais mwenyewe, huku akiwakumbusha wana CCM kutotumia kauli zitakazowakosesha ushawishi au pa kuweka uso baada ya migogoro hiyo kumalizika.
Ameongeza kuwa Rais na Makamu wa Rais wakiishaapishwa wanakuwa mali ya Watanzania wote na si ya CCM pekee, akimweleza Makamu kama msaidizi na sauti ya Rais, na kusema ni Rais pekee mwenye haki isiyohojiwa ya kutilia mashaka jinsi anavyosaidiwa.
Dkt. Bagonza amewasihi viongozi hao wawili kutambua kuwa wanaongoza nchi iliyojeruhiwa inayohitaji kutunzwa, akizitaka chokochoko za ndani ya chama kurudi nyuma na kujielimisha kutokana na hekima iliyotumika wakati wa kuingiza mfumo wa mgombea mwenza.
Ametahadharisha kuhusu ajenda ya vijana wa rika la Gen Z akisema suala lao ni zito na halipaswi kuishia kwenye kuunda wizara au kutoa mikopo, bali linahitaji kusikilizwa kwa dhati badala ya kuwatumia.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Dominick Pius, mkazi wa Kijiji cha Moivo wilayani Arumeru, anayedaiwa kuuawa kwa kuchomwa kisu shingoni na mke wake, Fatuma Juma, Julai 29, 2026 anatarajiwa kuzikwa Agosti 6, 2026, katika Makaburi ya Serikali ya Njiro baada ya ndugu zake kushindwa kujitokeza kuuchukua mwili wake.
Akizungumza na Jambo TV, Mwenyekiti wa Kitongoji cha Moivo, Johnson Abrahaman amesema juhudi za kuwatafuta ndugu wa marehemu kupitia mitandao ya kijamii na maeneo mbalimbali hazijafanikiwa, hivyo marafiki wa marehemu waliokuwa wakifanya naye kazi ya udereva wameamua kugharamia mazishi yake.
Amesema watoto walioachwa na marehemu kwa sasa wapo chini ya uangalizi wa Idara ya Ustawi wa Jamii, ambapo wanaendelea kupatiwa huduma za usaidizi wa kisaikolojia na ufuatiliaji wa kitaalamu kufuatia athari za tukio hilo.
Marehemu alidaiwa kuuawa na mke wake aliyekuwa akiishi naye, huku Jeshi la Polisi likiendelea kumshikilia mtuhumiwa kwa uchunguzi zaidi wa tukio hilo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais- Mipango na Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango Dkt. Tausi Kida ameongoza kikao cha Makatibu Wakuu kwa niaba ya Mwenyekiti wa Kikao hicho ambaye ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) Dkt. Jim Yonazi kilicholenga kujadili utendaji wa Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka-BRT leo tarehe 04 Agosti, 2026 kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu Jijini Dar es Salaam.
Dkt. Tausi ameongoza kikao hicho kilichoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa lengo la kupokea na kujadili taarifa ya timu ya wataalam kuhusu utendaji wa mradi huo ambapo imeelezwa kuwa lengo lake ni kutatua changamoto ya msongamano wa magari katika Mkoa wa Dar es salaam kwa kuboresha huduma ya usafiri kwa jamii.
Kikao hicho kilijumuisha wataalam kutoka Ofisi ya Rais- Mipango na Uwekezaji, Tume ya Taifa ya Mipango, Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI, Wizara ya Fedha, Wizara ya Ujenzi, Wizara ya Uchukuzi, Msajili wa Hazina, Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART), Kampuni ya Mabasi Yaendayo Haraka Dar es Salaam (UDART) na Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP Centre), Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), na Kituo cha Taifa cha Kuhifadhi Data Kimtandao (NIDC).
Aidha, Dkt. Tausi ametumia kikao hicho kuwakumbusha watendaji kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa weledi huku akieleza lengo la Serikali la kuendelea kuwapatia wakazi wa jiji la Dar es salaam usafiri bora, wa haraka na salama na kuendelea kupunguza msongamano wa magari ili kuokoa muda wa safari na kuboresha usalama barabarani.
“Mradi huu utumike kama ilivyokusudiwa na kuendelea kujiratibu vyema ili kuendelea kutoa huduma bora za usafiri kwa wananchi,” amesema Dkt. Tausi. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Rajabu Mabele, amesema Watanzania hawapaswi kuogopa wanapoona wanajeshi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiwa katika maeneo mbalimbali akisisitiza kuwa majeshi hayo ni rafiki wa wananchi na sehemu salama ya kukimbilia pale panapohitajika msaada.
Meja Jenerali Mabele ametoa kauli hiyo alipotembelea banda la JKT katika Maonesho ya Nanenane, ambapo alipata fursa ya kujionea shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na jeshi hilo, ikiwemo uzalishaji wa mazao ya kilimo, ufugaji na teknolojia zinazotumika kuongeza tija katika sekta ya kilimo.
Aidha, amesema ushiriki wa JKT katika Maonesho ya Nanenane ni sehemu ya juhudi za kuendelea kuwaelimisha Watanzania kuhusu mbinu bora za kilimo na ufugaji, pamoja na kuwajengea vijana ujuzi na mafunzo yatakayowasaidia kujiajiri na kuchangia maendeleo ya sekta ya kilimo nchini.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Jumla ya wanachama 17 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), akiwamo Katibu wa chama hicho Kanda ya Serengeti, Jackson Mnyawami, wamefikishwa leo Jumanne, Agosti 4, 2026, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Shinyanga kwa ajili ya kutajwa kwa kesi inayowakabili ya kupanga na kula njama za kufanya matendo ya ugaidi.
Katika mfululizo wa mashauri hayo, watuhumiwa watatu wanakabiliwa na shtaka la kupanga kufanya kosa la ugaidi, huku wengine 14 wakishtakiwa kwa kosa la kula njama za kufanikisha kosa hilo. Kesi hiyo, ambayo ilitajwa kwa mara ya kwanza tarehe 24 Julai, 2026, imesikilizwa mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Glory Mwakihaba.
Upande wa Jamhuri umewakilishwa na jopo la mawakili watatu wakiongozwa na Leonard Kiwango, huku upande wa utetezi ukiongozwa na mawakili wane ambao ni Peter Kibatala, Gaston Garubindi, Alex Masaba, na Gloria Ulomy.
Akizungumza nje ya mahakama, Mkurugenzi wa Sheria na Haki za Binadamu wa CHADEMA, Gaston Garubindi, amekosoa vikali hatua ya upande wa mashtaka kudai kuwa upelelezi haujakamilika. Garubindi amehoji mantiki ya kumkamata raia na kumshtaki kwa kosa zito kama ugaidi kabla ya kupata ushahidi kamili.
Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tanzania Bara, John Heche, amelaani mazingira ya mahakama ya Shinyanga akidai yamejawa na askari wengi jambo linalotishia wananchi. Aidha, Heche amedai kuwa kesi hizo ni za "kubumba" na zinalenga kuwazuia Watanzania kupinga ufisadi na kudai katiba mpya.
Shauri hilo limeahirishwa na kupangwa kutajwa tena tarehe 17 Agosti, 2026.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Shirika la Reli Tanzania @tzrailways limepokea vipande 17,600 vya reli ya MGR kupitia Bandari ya Tanga mahususi kwaajili ya ukarabati wa njia ya reli hiyo kutoka Ruvu Junction hadi Mruazi yenye urefu wa Km 188.
Akizungumza kwenye hafla fupi ya kupokea shehena hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Balozi Dkt. Batilda Salha Burian, amesema maboresho ya reli hiyo yatafungua fursa mpya za kiuchumi kwa Mkoa wa Tanga na Taifa kwa ujumla.
Balozi Burian, amesema kukamilika kwa ukarabati wa reli hiyo kutarejesha hadhi ya kihistoria ya Mkoa wa Tanga kama kitovu cha usafiri na biashara, huku ikitarajiwa kutumika pia katika usafirishaji wa mafuta, jambo litakaloimarisha nafasi ya Tanga kuwa kitovu cha biashara ya mafuta nchini na hata kwenye ukanda wa Afrika Mashariki.
Awali akitoa taarifa kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Meneja wa TRC Kanda ya Tanga, Mhandisi Christopher Kalisti, alisema pamoja na reli hizo zilizopokelewa, TRC inatarajia kupokea shehena nyingine ya mataruma pamoja na vifungashio kupitia Bandari ya Dar es Salaam.
Aidha alifafanua kuwa kila kipande cha reli kilichowasili kina urefu wa mita 24 na ni cha ratili 80, tofauti na reli za awali zilizokuwa na ratili 60, hatua itakayoongeza uimara wa miundombinu hiyo ya reli na kuongeza usalama wa safari za reli, uwezo wa kubeba mizigo pamoja na kuongeza kasi ya usafirishaji.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu Mwenyekiti wa @ChademaTZ2 John Heche @HecheJohn akiwasili Mahakama Kuu ta Tanzania Kanda Shinyanga kwa ajili ya kufuatilia mwenendo wa mashauri mbalimbali yanayowakabili wanachama wa chama hicho.
Akiwasili mahakamani leo Agosti 4, 2026 hapo amesalimiana na Wakili Peter Kibatala @PKibatala_ ambaye ni miongoni mwa mawakili wanaowawakilisha wanachama hao.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, ameielekeza Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC) kufanya ukaguzi wa mara kwa mara katika vyama vya ushirika ili kudhibiti ubadhirifu wa mali, kuimarisha uwajibikaji na kulinda maslahi ya wanachama.
Akizungumza jijini Dodoma wakati wa Maonesho ya Kimataifa ya Nane Nane, Dkt. Nchimbi amesema Serikali imejipanga kuhakikisha vyama vya ushirika vinatoa huduma bora kwa wakulima huku mali zake zikisimamiwa kwa uwazi na kutumika kwa manufaa ya wanachama. Amesema ukaguzi wa mara kwa mara utasaidia kubaini mapema changamoto zinazovikabili vyama hivyo na kuchukua hatua stahiki dhidi ya matumizi mabaya ya rasilimali.
Kwa upande wake, Msajili na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC), Dkt. Benson Ndiege, amesema kumekuwa na changamoto za usimamizi wa mali za ushirika ambapo baadhi ya mali ziliuzwa isivyo halali. Amesema TCDC imeanzisha mfumo rasmi wa kutambua na kusajili mali za ushirika ili kuimarisha ulinzi wake, kudhibiti ubadhirifu na kuongeza thamani ya mali hizo kwa manufaa ya wanachama.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi ameielekeza Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC) kufanya ukaguzi wa mara kwa mara katika vyama vya ushirika ili kudhibiti ubadhirifu wa mali, kuimarisha uwajibikaji na kulinda maslahi ya wanachama.
Akizungumza jijini Dodoma leo wakati wa Maonesho ya Kimataifa ya Nane Nane, Dkt. Nchimbi amesema serikali imejipanga kuhakikisha vyama vya ushirika vinatoa huduma bora kwa wakulima huku mali zake zikisimamiwa kwa uwazi na kutumika kwa manufaa ya wanachama. Amesema ukaguzi wa mara kwa mara utasaidia kubaini mapema changamoto zinazovikabili vyama hivyo na kuchukua hatua stahiki dhidi ya matumizi mabaya ya rasilimali.
Kwa upande wake, Msajili na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC), Dkt. Benson Ndiege, amesema kumekuwa na changamoto za usimamizi wa mali za ushirika ambapo baadhi ya mali ziliuzwa isivyo halali. Amesema TCDC imeanzisha mfumo rasmi wa kutambua na kusajili mali za ushirika ili kuimarisha ulinzi wake, kudhibiti ubadhirifu na kuongeza thamani ya mali hizo kwa manufaa ya wanachama.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameweka wazi kuwa Serikali haitatoA ruzuku kwa sekta ya madini kwa sasa, akieleza kuwa wadau wa sekta hiyo wana uwezo mkubwa wa kujiendesha wenyewe bila kuhitaji usaidizi wa kifedha kutoka serikalini.
Dkt. Samia ametoa msimamo huo leo Agosti 3, 2026, Ikulu jijini Dar es Salaam, wakati wa hafla ya uzinduzi wa nyenzo za utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
Akizungumza mbele ya wadau wa sekta hiyo, Dkt. Samia amebainisha kuwa baadhi ya wafanyabiashara na wachimbaji wa madini wana ukwasi mkubwa wa kifedha, kiasi cha kugharamia sherehe kubwa za kifahari kama harusi zinazotumia helikopta. Hivyo, amesisitiza kuwa haitakuwa na mantiki kwa Serikali kurejesha fedha kidogo za kodi zinazokusanywa kwa njia ya ruzuku.
Aidha, Dkt. Samia amewahakikishia wadau wa madini kuwa Serikali itaendelea kuwekeza kwenye miundombinu na mazingira wezeshi ya kimkakati ili kuikuza sekta hiyo.
Ametaja miongoni mwa miradi mikubwa inayofanyiwa kazi hivi sasa kuwa ni ujenzi wa Soko la Kimataifa la Madini, ambalo litasaidia kuongeza thamani ya madini nchini na kupanua wigo wa biashara ya kikanda na kimataifa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Prof. Kitila Mkumbo, amesema safari ya kulifanya taifa la Tanzania lijitegemee kiuchumi imeanza muda mrefu uliopita, huku utegemezi wa misaada kutoka nje ukiendelea kupungua katika kila awamu ya serikali, akisema kwa sasa vikwazo vya misaada haviwezi kufanya kazi.
Prof. Mkumbo ameeleza hayo Agosti 3, 2026 jijini Dar es Salaam, katika uzinduzi wa nyenzo za utekelezaji wa Dira 2050, pamoja na kushiriki katika mkutano wa mazungumzo maalumu na Sekta binafsi kuhusu utekelezaji wa Dira 2050.
"Masharti ya misaada hayana tena athari ya kimkakati katika maamuzi ya serikali, kwani serikali tayari imejumuisha hatari ya kupungua au kusitishwa kwa misaada hiyo katika mfumo wake wa usimamizi wa fedha za umma, kwahiyo itabidi watafute vikwazo vingine, vikwazo vya misaada haviwezi kufanya kazi tena", amesema Prof. Kitila.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amewataka Watanzania wote kulinda na kuweka mbele amani na utulivu wa nchi, akisisitiza kuwa bila amani, utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 hautafanikiwa.
Rais Samia ametoa wito huo leo Jumatatu, Agosti 03, 2026, Ikulu jijini Dar es Salaam, wakati wa hafla ya uzinduzi wa nyenzo za utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 na Mkutano wa Mazungumzo Maalum kati ya Serikali na Sekta Binafsi.
Akifungua mkutano huo na kueleza umuhimu wa amani katika ukuaji wa uchumi, Rais Samia amesema: "Niendelee kusisitiza kuwa amani na utulivu ni mtaji mkubwa kuliko mitaji mingine yote. Kama hakuna amani na utulivu, Dira ya Taifa 2050 haitatekelezeka na hatutaweza kufanya chochote. Niwaombe Watanzania wote, sekta ya umma na sekta binafsi, tuweke amani mbele- lolote unalohisi litavunja amani, usiliunge mkono."This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Rais wa Shirikisho la Taasisi za Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Angelina Ngalula, amesema ipo haja kama taifa kuwa na mkakati wa kitaifa unaounganisha akili bandia, data na teknolojia zinazoibukia ili kuifanya Tanzania kuwa mbunifu na msuluhishaji wa masuala ya teknolojia.
Ngalula ameeleza hayo Agosti 3, 2026 jijini Dar es Salaam Katika uzinduzi wa nyenzo za utekelezaji wa Dira 2050, pamoja na kushiriki katika Mkutano wa mazungumzo maalumu na Sekta binafsi kuhusu utekelezaji wa Dira 2050.
"Tunapendekeza mkakati wa kitaifa unaounganisha akili bandia, data na teknolojia zinazoibukia, tukiweka msisitizo katika elimu, ujuzi wa vijana, miundombinu na usalama wa mitandao", amesema Ngalula.
Ameongeza kwamba ipo haja pia ya kuwa na mfumo wa kitaifa wa kutabiri mahitaji ya ujuzi ya baadaye utakaoainisha aina ya ujuzi, taaluma ambazo uchumi utahitaji katika kipindi husika.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Agosti 3, 2026, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na sekta binafsi nchini zimetoa tamko la pamoja kwa ajili ya kuharakisha utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, likilenga kuimarisha ushirikiano katika mageuzi ya uchumi na ujenzi wa uchumi shindani.
Akiwasilisha tamko hilo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Nyenzo za Utekelezaji wa Dira 2050 inayofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan atazizindua leo, na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais- Uwekezaji Dkt. Fred Msemwa ameeleza kuwa serikali imeahidi kudumisha utulivu wa uchumi, kuboresha mazingira ya biashara, kuharakisha uwekezaji katika miundombinu ya kimkakati, na kukuza maendeleo ya viwanda. Kwa upande wake, sekta binafsi imeahidi kuongeza uwekezaji, kuzalisha ajira zenye staha, kukuza ubunifu, na kuzingatia maadili mema na utawala bora katika uendeshaji wa kampuni.
Dkt.Msemwa ameeleza kuwa pande zote mbili zimekubaliana kushirikiana katika kufanikisha Dira 2050, kujenga mazingira ya kuaminiana na uwazi, na kuhakikisha ukuaji wa uchumi unawanufaisha Watanzania wote kwa usawa. Aidha, zimeahidi kuimarisha uwezo wa taifa kukabiliana na mishtuko ya kiuchumi duniani na mabadiliko ya tabia nchi
Amesema kuwa kupitia makubaliano haya, taifa linatarajia kuona ukuaji wa kasi wa uchumi, kuongezeka kwa tija, na kuimarika kwa ushindani wa uchumi wa Tanzania kimataifa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameeleza kuwa siasa na uchumi wa dunia vinabadilika kila siku, na mabadiliko hayo yanaathiri nchi zote duniani ikiwamo Tanzania na hivyo kusababisha kupungua kwa misaada na mikopo nafuu.
Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Nyenzo za Utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 na Mkutano wa Mazungumzo Maalum na Sekta Binafsi kuhusu Utekelezaji wa Dira 2050 uliofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam Agosti 3, 2026, Dkt. Samia ameeleza kuwa sababu ya kupungua kwa mikopo nafuu ni kutokana na takwimu kuonesha kuwa Tanzania imeingia katika uchumi wa kati, hali inayoilazimisha kuanza kuchukua mikopo mikubwa yenye riba kubwa, badala ya ile ya awali yenye masharti nafuu.
Kutokana na hali hiyo, Dkt. Samia ametoa wito kwa Watanzania "kukaza buti na kufunga mikanda" kwa kuongeza juhudi katika kuzalisha bidhaa kwa ajili ya mahitaji ya ndani na ziada kwa ajili ya kuuza nje na kupunguza kuagiza bidhaa nje kwa yale mambo ambayo yanaweza kuzalishwa hapa nchini ili kupata fedha zaidi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Mwenyekiti wa Chama cha Waendeshaji wa Utalii Tanzania (TATO), Wilbard Chambulo, amesema Tanzania inaweza kuongeza ushindani wake katika sekta ya utalii kwa kuondoa vikwazo vinavyochelewesha safari za watalii, hususan kupitia uwekezaji katika miundombinu na kurahisisha huduma za uhamiaji.
Akizungumza katika uzinduzi wa nyenzo za utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, Chambulo alisema sekta ya utalii inategemea zaidi urahisi wa safari na uzoefu wa mgeni kuliko taratibu ndefu zinazoweza kumkatisha tamaa kabla hajafika katika vivutio vya utalii.
Alitolea mfano watalii wanaotembelea Maasai Mara nchini Kenya na baadaye kutaka kuingia Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, akisema wengi wao hulazimika kupitia Nairobi, kisha Kilimanjaro na Arusha kwaajili ya taratibu za uhamiaji kabla ya kufika Serengeti. Alisema mlolongo huo huongeza gharama na muda wa safari, hali inayoweza kuwafanya baadhi ya wageni kuahirisha au kuacha kabisa safari yao ya Tanzania.
Kwa maoni yake, kujengwa kwa Kiwanja cha ndege katika eneo la Mugumu, Mkoani Mara pamoja na kuweka huduma huduma za uhamiaji kutawezesha watalii hao kuingia moja kwa moja Serengeti kutoka Maasai Mara, hatua ambayo itapunguza usumbufu na kuongeza ushindani wa Tanzania katika soko la utalii la Afrika Mashariki.
Akihitimisha, Chambulo alisema Tanzania tayari ina vivutio vinavyotambulika kimataifa, ikiwemo Serengeti na Zanzibar, na kwamba kuboresha miundombinu pamoja na kurahisisha taratibu za kuingia nchini kutasaidia kuongeza idadi ya Watalii na mapato yatokanayo na sekta hiyo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI:
Rais wa Marekani, Donald Trump, ametangaza kuwa mazungumzo mapya ya amani kati ya nchi yake na Iran yanatarajiwa kuanza rasmi Jumatatu hii alasiri.
Kiongozi huyo ametoa kauli hiyo usiku wa tarehe 2 Agosti 2026, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari akiwa ndani ya ndege ya Rais inayojulikana kama "Air Force One".
Hata hivyo, hadi sasa upande wa Iran bado haujatoa tamko lolote rasmi kujibu kauli hizo, ingawa Rais Trump amekuwa akisisitiza mara kwa mara kuwa suluhu ya kudumu iko karibu kabla ya mivutano na mashambulizi ya kulipiza kisasi kuibuka tena.
Kwa muda sasa, Iran na Marekani zimekuwa zikiingia katika Mazungumzo ya kutafuta suluhu ya vita vinavyoendelea kati yao, licha ya mazungumzo hayo kutofanikiwa na vita kuendelea. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI:
Watu 35 wameripotiwa kuuawa na wengine kujeruhiwa, kufuatia shambulizi lililotekelezwa na ndege zisizokuwa na rubani za jeshi la Sudan katika jimbo la Darfur Magharibi.
Shambulizi hilo limetokea mwishoni mwa wiki iliyopita katika kijiji cha Garra al-Zawaya, huku likithibitishwa na Mawakili wa Dharura na watetezi wa haki za binadamu nchini Sudan.
Wakati wa shambulizi hilo, raia wa kawaida walikuwa wamekusanyika kusikiliza kesi za kijamii katika kijiji hicho, ambacho kwa sasa kinadhibitiwa na wanamgambo wa Rapid Support Forces (RSF).
Miongoni mwa waliouawa ni viongozi wanne wa kikabila na makamanda wawili wa RSF.
Umoja wa Mataifa umeonya kuwa vita vinavyoendelea Darfur, hasa katika Mji wa El-Fasher unaozingirwa, vina viashiria vikubwa vya mauaji ya kimbari dhidi ya raia.
Matumizi ya ndege zisizo na rubani yanatajwa kuongezeka , yakisababisha vifo vya zaidi ya raia elfu moja katika miezi mitano ya kwanza ya mwaka 2026 pekee.
Tangu kuanza kwa mapigano kati ya jeshi la serikali na RSF mwezi Aprili 2023, maelfu ya watu wamepoteza maisha. Mgogoro huo umesababisha mamilioni ya raia kukimbia makazi yao, huku wengine wakivuka mpaka kutafuta hifadhi katika nchi jirani ya Chad. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katibu Mkuu wa @ChademaTZ2 John Mnyika ametoa wito kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) kutumia hekima na utaratibu uliotumika kufuta kesi ya ugaidi iliyokuwa inamkabili aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe utumike kwa Mwenyekiti wa sasa wa chama hicho Tundu Lissu ambaye anashtakiwa kwa uhaini.
Mnyika amesema hayo leo Agosti 3, 2026 akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam huku akitoa wito kwa wananchi kwenda kuhudhuria kesi ya Lissu itakayoendelea Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam kuanzia Agosti 10 mwaka huu.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo John Mnyika amesema kuwa chama hicho na Mwenyekiti wake Tundu Lissu mpaka hivi sasa hakijafanya mazungumzo yoyote na serikali huku akiipinga kauli iliyotolewa na Rais Samia Julai 30, 2026.
Kupitia mkutano wake na waandishi wa habari leo Agosti 3, 2026 ameeleza kauli ya Rais Samia alipokuwa akizungumza na vyama vya siasa kuwa yupo mwenzao mmoja ambaye anaendelea kutafakari masharti haikihusu CHADEMA.
Mnyika amesisitiza kuwa walipomtafuta Lissu kufahamu kama amezungumza na serikali alikataa akisema mara baada ya kuzungumza na Rais Mstaafu wa Malawi Lazarus Chakwera hajazungumza na mtu yoyote hivyo amewataka viongozi wa CHADEMA kuendelea kubaki kwenye msimamo wao.
Ikumbukwe Julai 30, 2026 Rais Samia alikutana na viongozi wa vyama 18 vya siasa vyenye usajili wa kudumu na CHADEMA pekee ndiyo haikushiriki na moja ya kauli aliyotoa alisema "Mwenzetu mmoja bado anaendelea kutafakari bado tunaendelea kupokea misukumo yake conditions zake matakwa yake ndiyo."This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais- Mipango na Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango, Dkt. Tausi Kida ameeleza kuwa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 imelenga kujenga uchumi shindani na jumuishi unaowanufaisha Watanzania wote akisisitiza kuwa dira hii si waraka wa sera tu, bali inaanza kutekelezwa mara moja kupitia mfumo ulioratibiwa wa uwajibikaji na ufuatiliaji wa matokeo.
Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Nyenzo za Utekelezaji wa Dira 2050 inayofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan atazizindua leo, Dkt. Kida ameelezea nyenzo hizo.
Amesema nyenzo hizo ni Mpango Elekezi wa Maendeleo wa Muda Mrefu, Mpango wa Nne wa Maendeleo ya Taifa wa Miaka Mitano (FYDP IV), Mwongozo wa Kitaifa wa Upimaji Matokeo na Utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo na Mkakati wa Mawasiliano wa Dira 2050 ambao unalenga kutafsiri lugha ya kisera kwenda katika lugha rahisi ili kuongeza uelewa na ushiriki wa wananchi na wadau wote.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo @ChademaTZ2 John Mnyika ametoa wito kwa watanzania kuendelea kuchangia chama hicho huku akiwashukuru kwa kuwachangia shilingi milioni 266 kama sehemu ya mchango wa milioni 334 kwa ajili ya kuendesha Baraza Kuu la chama hicho linalotarajiwa kufanyika septemba 15, 2026.
Amesema hayo akizungumza na waandishi habari leo Agosti 3, 2026 jijini Dar es Salaam.
"Mazingira tunayopitia ni magumu lakini tuna ujasiri wa kuyavuka kwa sababu nyinyi watanzania mnatuunah mkono ahsanteni kwa kutuchangia fedha," amesema MnyikaThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) limetangaza kuwa Tuzo za Rais za Wazalishaji Bora wa Mwaka (PMAYA) kwa mara ya 19, jukwaa kubwa zaidi nchini Tanzania kwa kutambua mafanikio ya Viwanda, litafanyika Agosti 24 mwaka huu.
Akizungumza hivi karibuni jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa CTI, Hussein Sufian alisema Kaulimbiu ya mwaka huu, ‘Green Elegance- Celebrating Sustainable Manufacturing Practices’, inaonesha mabadiliko katika kile ambacho PMAYA inatambua: si tu uzalishaji wa viwanda, bali pia uendelevu, uwajibikaji, na ustahimilivu unaosimamia uzalishaji huo.
Amesema jioni hiyo itashuhudia zulia la kwanza la kijani (Green Carpet) nchini Tanzania, likichukua nafasi ya zulia la kawaida la rangi nyekundu, ikiashiria dhamira ya pamoja ya sekta katika kuelekea ukuaji endelevu wa viwanda.
“Kwa miaka kumi na tisa, PMAYA imekuwa ikieleza hadithi ya viwanda vya Tanzania katika hali yake bora zaidi. Mwaka huu, tunaeleza hadithi kamili zaidi, moja inayotambua si tu kile wazalishaji wetu wanachozalisha, bali pia jinsi wanavyozalisha kwa uwajibikaji. Green Elegance si kaulimbiu tuliyoikopa; ni mwelekeo ambao sekta hii tayari inaufuata, na PMAYA ipo kutambua uongozi huo”,
Kwa mara ya kwanza katika historia ya miaka 19 ya PMAYA, mbali na washindi wa kategoria za Tuzo, PMAYA itatangaza Mabalozi sita wa ESG (ESG Ambassadors), wazalishaji walioainishwa kupitia kazi ya tathmini ya ESG inayoendelezwa na CTI kama viongozi katika utekelezaji wa masuala ya mazingira, jamii, na utawala bora. Alisema mabalozi hao wameainishwa kupitia tathmini ya moja kwa moja ya utendaji wao Viwandani.
Alisema kundi la mwaka 2026 litatumika kama mabalozi wa sekta kwa muda wa miezi 12 na litakuwa msingi wa kundi ambalo kutoka humo, tuzo mpya ya kudumu ya Mzalishaji Bora wa Mazingira wa Mwaka (Green Manufacturer of the Year), itaongezwa katika PMAYA ya 20.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa CTI, Mhandisi Leodegar Tenga amesema "kupitia mradi wetu wa ESG, timu yetu ilitembelea viwanda mbalimbali nchini na kushuhudia moja kwa moja jinsi utekelezaji halisi unavyoonekana kivitendo, si kwenye karatasi tu. Mabalozi sita wa ESG tutakaowatangaza waliainishwa kupitia mchakato huo. Huu ni mwanzo wa njia ya kudumu ya kutambua uzalishaji endelevu viwandani hapa Tanzania, na tunatarajia kushiriki hadithi zao tarehe 24 Agosti”.
Amesema PMAYA ya 19 inaungwa mkono na wazalishaji na kampuni mashuhuri za Tanzania, ikiwamo Tanzania Cigarette Company (TCC), Tanzania Breweries Limited (TBL), Chemi Cotex limited, na Africab Group (Kilimanjaro Cables). CTI inakaribisha kampuni nyingine zenye nia ya kushirikiana katika PMAYA ya 19; zinaweza kuwasiliana na Sekretarieti ya CTI kwa maelezo zaidi kuhusu udhamini.
Tenga amesema tuzo hiyo inatokana na mashindano kati ya wazalishaji, yaliyoanzishwa mwaka 2005 na kuandaliwa na Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) kwa lengo la kutambua, kutathimini na kuenzi umuhimu na mchango wa Sekta ya Viwanda katika maendeleo nchini.
“Siku hii ni ya muhimu sana kwetu kwa sababu ni fursa ya pekee tunayoipata mara moja kwa mwaka, kwa pamoja, ili kutambua, kutathimini na kuenzi umuhimu na mchango wa Sekta ya Viwanda katika maendeleo ya uchumi wa Taifa letu,” amesema na kuongeza,
“Katika miaka kumi na tisa tangu kuanzishwa utaratibu huu, maboresho mbalimbali yamefanyika ikiwemo kuongeza wigo wa washiriki, kwa kuhusisha sekta za uzalishaji 26 ili kujumuisha viwanda vidogo, vya kati na vikubwa”.
Aidha, alisema washindi wa tuzo hizi hupatikana kwa kuzingatia: mchango wa mzalishaji katika uchumi, maendeleo na uwekezaji kwenye teknolojia ya kisasa inayojali na kutunza mazingira, mauzo nje ya nchi, afya na usalama wa mazingira ya kazi, mchango katika kuendeleza jamii inayomzunguka (Corporate Social Responsibility) na mengineyo.
Tuzo hizi zinabaki kuwa jukwaa kuu la Tanzania katika utambuzi wa viwanda, uhamasishaji wa uwekezaji, na majadiliano baina ya sekta binafsi na serikali. -
Jambo TV
@Jambotv_
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tanzania Bara, John Heche, ametetea kauli yake aliyomtaka Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Stephen Wasira, kustaafu uongozi na kupisha vijana kwasababu “anasinzia kwenye vikao na mambo ya msingi yanampita”, akisisitiza kuwa ujumbe huo haukuwa tusi wala haukukiuka maadili.
Majibizano hayo yameibuka kutokana na taarifa ya Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC) Organizesheni ya CCM, Paul Chacha, iliyotolewa Agosti 1, 2026, iliyomtaka Heche kumwomba radhi Wasira kwa kile alichokiita kutoa kauli za udhalilishaji dhidi ya mzee huyo.
Akizungumzia suala hilo, Chacha alieleza kuwa kulingana na mila na desturi za Kabila la Wakurya, ni mwiko na kitendo kisichokubalika kumtukana au kumvunjia heshima mzee yeyote.
"Sisi Wakurya tumefundishwa kutokutukana wazee; tunaheshimiana kwa rika. Tunaweza tukatukanana mimi na yeye, lakini si kumtukana mzee au mtu mzima wowote, sisi ndivyo tulivyolelewa. Nimemshauri Heche, akiwa rafiki na ndugu yangu, amtafute Mzee Wasira amwombe radhi. Bado ana nguvu na imara, atakusamehe na kukushika mkono; vinginevyo utatembea lakini hutafika mbali," alisema Chacha.
Akijibu ushauri huo kupitia ukurasa wake wa Instagram, Heche amehoji uhalali wa kukiita kitendo cha kumtaka kiongozi mstaafu kuachia ngazi kuwa ni "tusi", huku akikosoa kimya cha viongozi wa chama tawala juu ya matukio makubwa ya kisiasa na kiusalama nchini.
"Nimemsikia kijana wa CCM akisema mimi kumwambia Mzee wetu Wasira astaafu kwa sababu ya umri mkubwa ni matusi. Je, amewahi kukemea matukio ya watu kutekwa, akiwemo aliyekuwa Katibu Mwenezi wa CCM, Bwana (Humphrey) Polepole? Je, ni vibaya kumwambia mtu astaafu na kuachia kizazi kipya kuliko matukio ya mauaji ya Oktoba 29? Huyu kijana amewahi kusema nini kuhusu mauaji hayo, au hajui kuwa wapo wazee pia waliouawa kwenye matukio hayo?" amehoji Heche. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA) umezindua Mpango Mkakati wa miaka mitano unaolenga kuimarisha ulinzi wa walaji kwa kuhakikisha usahihi wa vipimo, ubora wa bidhaa zilizofungashwa na kuimarisha utekelezaji wa sheria za vipimo nchini.
Akizindua mpango huo leo Agosti 2,2026 jijini Arusha, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Dennis Lazaro Londo amesema watumishi wa WMA wanapaswa kuzingatia maadili ya kazi, kupambana na udanganyifu wa vipimo na kuhakikisha kila mwananchi anapata haki anaponunua bidhaa na huduma.
Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa WMA, Alban Kihulla amesema mpango huo unalenga kuhakikisha bidhaa zote zinazozalishwa na zinazoingizwa nchini zinakidhi viwango vya vipimo vinavyotakiwa, hatua itakayoongeza ushindani wa bidhaa za Tanzania katika masoko ya ndani na kimataifa pamoja na kujenga imani ya wananchi.
Kihulla amesema utekelezaji wa mpango huo pia utaimarisha ushirikiano kati ya WMA na sekta binafsi, kuboresha huduma za ukaguzi wa vipimo na kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya wakala.
Wakala wa Vipimo Tanzania ni taasisi ya Serikali iliyo chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara yenye jukumu la kuhakikisha vipimo vya uzito, ujazo, urefu na vingine vinavyotumika nchini ni sahihi na vya kuaminika, kwa lengo la kulinda maslahi ya walaji na wafanyabiashara pamoja na kuhakikisha biashara zinafanyika kwa haki.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma limesema idadi ya watu waliofariki dunia kutokana na ajali iliyohusisha mabasi mawili ya abiria imeongezeka kutoka watu wanane hadi tisa. Ajali hiyo ilihusisha basi la Isamilo lenye namba za usajili T 428 EPX na basi la Libanika lenye namba za usajili T 897 DUR.
Akizungumza na Jambo TV jijini Dodoma, Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ASP) Asifiwe Ulime, amesema uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa basi la Isamilo, ambaye alijaribu kuyapita magari yaliyokuwa mbele yake bila kuchukua tahadhari na kusababisha kugongana uso kwa uso na basi la Libanika. Amesema dereva huyo amekamatwa na taratibu za kisheria zinaendelea dhidi yake.
Aidha, Ulime amewataka madereva kote nchini kuzingatia sheria na kanuni za usalama barabarani, ikiwemo kuendesha kwa tahadhari na kuepuka kuyapita magari bila kujiridhisha kuwa mazingira ni salama, akisisitiza kuwa kufanya hivyo kutasaidia kupunguza ajali na kulinda maisha ya watumiaji wa barabara.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Chama cha ACT Wazalendo kimetoa ushauri wa mambo matatu makuu kwa Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan ili kufikia maridhiano ya kweli na ya kudumu nchini, kikisisitiza kuwa nchi haiwezi kuwa na utulivu bila misingi ya ukweli, haki na uwajibikaji.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Naibu Katibu wa Habari, Uenezi na Uhusiano kwa Umma wa ACT Wazalendo, Shangwe Ayo, Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Dorothy Semu ameeleza hayo Agosti 1, 2026, jijini Dar es Salaam wakati akifungua mafunzo ya siku tatu ya Madiwani wa chama hicho kutoka kata mbalimbali nchini.
Semu ameeleza kuwa ili mchakato wa maridhiano uwe na tija na maana kwa wananchi, Serikali inapaswa kuwaachia huru wafungwa wote wa kisiasa nchini, kuruhusu uchunguzi huru wa kimataifa kuhusu matukio ya mauaji yaliyotokea tarehe 29 Oktoba 2025 na kutoa ramani ya wazi ya kupatikana kwa Katiba Mpya ya wananchi na kuanza mchakato wa kupatikana kwake.
Semu amebainisha kuwa mambo hayo matatu tayari yameshawasilishwa rasmi kwa Rais Samia Suluhu Hassan wakati wa mkutano wake na viongozi wa vyama vya siasa, na kwamba msimamo huo uliridhiwa na Kamati Kuu ya chama hicho katika vikao vyake vya Januari na Aprili 2026.
"Sisi tumetekeleza wajibu wetu wa kuyawasilisha. Wajibu wa Rais Samia na Serikali yake ni kuyatekeleza. Tutaendelea kusimama imara iwapo hatutaona nia ya dhati ya kuyatekeleza," alisema Semu.
Katika hatua nyingine, Kiongozi huyo wa ACT Wazalendo amewataka madiwani wa chama hicho kuwa mstari wa mbele kutetea msimamo huo wa uwajibikaji, huku wakiweka maslahi ya wananchi mbele. Aliwaagiza kusimamia kwa umakini matumizi ya rasilimali za umma na kulinda haki za wananchi katika kata wanazoziongoza. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Magharibi, Wakili Dickson Matata amedai kuwa kiongozi wa dini na mwanaharakati, Sheikh Said Mwaipopo, amekuwa akijihusisha na mpango wa kurubuni watu ambao si wanachama wala viongozi wa CHADEMA ili wajivike uongozi wa chama hicho na kutoa matamko ya kukichafua chama na viongozi wake.
Akizungumza leo Jumapili Agosti 02, 2026, Makao Makuu ya chama hicho mkoani Dar es Salaam, Wakili Matata amedai kuwa Sheikh Mwaipopo amefanya mipango hiyo katika Kanda ya Magharibi.
Hata hivyo akizungumza na Jambo TV kwa njia ya simu, Sheikh ameziita tuhuma hizo kuwa ni maneno ya uongo na ameshangazwa na madai ya Matata. Amesema yeye si mwanasiasa na kazi yake ni kushughulika na watu wa vyama vyote na dini zote, huku akikanusha kutoa fedha kwa watu, akidai kuwa yeye mwenyewe anasafiri kwa ufadhili wa Waislamu misikitini, akihoji, "Hiyo pesa ya kuwapa CHADEMA nimeitoa wapi?"
Mwaipopo ameahidi kuitisha mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam ili kuelezea ukweli na kile anachokiita uhuni unaofanywa na CHADEMA.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katika hatua ya kuboresha miundombinu ya elimu na kutatua changamoto ya nafasi za masomo, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imeanza rasmi ujenzi wa shule mpya ya Sekondari ya Ghorofa katika Kata ya Vingunguti, mradi utakaogharimu Shilingi bilioni 4.
Mradi huo unalenga kutatua kero ya umbali na msongamano kwa wanafunzi wa Vingunguti na kata za jirani, pamoja na kujiandaa na mapokezi ya wanafunzi wanaotarajiwa kumaliza elimu ya msingi kwa mkupuo (Double Cohort) ifikapo mwaka 2028.
Taarifa hizo zimebainishwa na Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Elihuruma Mabelya, mbele ya Mstahiki Meya wa Jiji hilo, Nurdin Bilal (Shetta), wakati wa ziara ya ukaguzi wa utekelezaji wa mradi huo uliogharamiwa kwa 100% kutokana na mapato ya ndani ya Halmashauri. Mradi huo unatarajiwa kukamilika rasmi mwaka 2027.
Shule hiyo ya ghorofa nne (4) itakuwa na uwezo wa kuchukua zaidi ya wanafunzi 800 kwa wakati mmoja mara itakapokamilika. Miundombinu inayojengwa inajumuisha vyumba 16 vya madarasa ya kisasa, maabara 4 za Sayansi na Maabara 1 ya kisasa ya TEHAMA na ofisi 10 za walimu pamoja na matundu 37 ya vyoo (ikiwa ni pamoja na miundombinu maalum kwa ajili ya watu wenye ulemavu).This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Magharibi, Wakili Dickson Matata ametangaza nia ya chama hicho kuchukua hatua za kisheria dhidi ya watu wanaojifanya kuwa viongozi au wanachama wa CHADEMA wakati si kweli, kwa kuwashitaki mahakamani watu hao.
Akizungumza leo Jumapili Agosti 02, 2026, Makao Makuu ya chama hicho mkoani Dar es Salaam, Wakili Matata amesema kuwa watu hao wamekuwa wakikidhalilisha chama na kukishushia hadhi kwa kutoa maneno ya uongo na kujifanya viongozi wa CHADEMA kupitia mikutano na wanahabari ambayo wamekuwa wakiifanya katika maeneo mbalimbali nchini.
Aidha, Wakili Matata amesema atamshauri Makamu Mwenyekiti wa chama hicho bara, John Heche, kuwafungulia watu hao kesi za madai ili waweze kudaiwa fidia kubwa kwa kumchafulia jina na kumdhalilisha kwani mashambulizi na shutuma nyingi alizodai kuwa hazina ushahidi zimekuwa zikielekezwa kwake.
Wakili Matata ameoa onyo kali kwa mtu yeyote kutorudia tabia hiyo ya kujifanya ni kiongozi wa CHADEMA kwa malengo ya kisiasa, akisisitiza kuwa lazima tabia hiyo ifike mwisho kwa wahusika kuwajibishwa mahakamani.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Watu nane wamepoteza maisha huku wengine 66 wakijeruhiwa kutokana na ajali iliyohusisha mabasi mawili ya abiria yaliyokuwa yakisafiri kwenda mikoani, yaliyogongana uso kwa uso katika Kijiji cha Ibiwa, Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma, majira ya saa 12:00 asubuhi, Agosti 2, 2026.
Ajali hiyo imehusisha basi la kampuni ya Isamilo lenye namba za usajili T 428 EPX na basi la kampuni ya Libanika lenye namba za usajili T 897. Kati ya majeruhi 66, watu tisa wameripotiwa kuwa katika hali mbaya na wanaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.
Wakizungumza wakiwa hospitalini, baadhi ya majeruhi wamedai kuwa chanzo cha ajali hiyo kilikuwa ni mwendo kasi wa moja ya mabasi hayo. Wamedai kuwa dereva wa basi moja alijaribu kulipita lori lililokuwa mbele yake, lakini katika jitihada za kulikwepa alijikuta akigongana uso kwa uso na basi lililokuwa likitokea upande wa pili wa barabara.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule amewataka madereva wote kuzingatia sheria za usalama barabarani na kuacha uzembe pamoja na mwendo kasi, akisisitiza kuwa hatua hiyo itasaidia kupunguza ajali zisizo za lazima zinazogharimu maisha ya wananchi na kusababisha majeraha makubwa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Magharibi, Wakili Dickson Matata ametoa wito na rai kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), Sylvester Mwakitalu kutumia mamlaka yake ya kikatiba kufuta kesi za ugaidi zinazowakabili wanachama na viongozi wa CHADEMA pamoja na Watanzania wengine katika maeneo mbalimbali nchini.
Akizungumza leo Jumapili Agosti 02, 2026, Makao Makuu ya chama hicho mkoani Dar es Salaam, Wakili Matata amesisitiza kuwa katika kukamilisha hilo kwa mujibu wa Ibara ya 59B ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, DPP anapaswa kuwa na nia ya kutenda haki, kuzuia matumizi mabaya ya taratibu, miongoni mwa mwambo mengine.
Akitolea ufafanuzi taarifa za kukamatwa kwa watuhumiwa wa makosa mbalimbali ikiwamo ugaidi hivi karibuni, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, alikanusha vikali kuwa kuna mkakati wa kiserikali wa kulenga kundi fulani, wanataaluma, au taasisi ya kisiasa.
Aliwataka wananchi na watumiaji wa mitandao ya kijamii kuacha kupotosha umma na badala yake kuziachia mahakama zifanye kazi yake kwa mujibu wa misingi ya kisheria na Ibara ya 13 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayomtambua mtu kuwa hana hatia hadi mahakama itakapothibitisha vinginevyo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Serikali ya Tanzania imeiomba Marekani kuondoa vikwazo vya viza kwa Watanzania wanaosafiri kwenda nchini humo, pamoja na vikwazo vingine vya kiuchumi na kiusafiri vilivyowekwa dhidi ya Tanzania, ili kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na wananchi wa nchi hizo mbili.
Ombi hilo limewasilishwa wakati wa mazungumzo baina ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Mahmoud Thabit Kombo, na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Rhimo Nyansaho, pamoja na ujumbe maalum wa wajumbe 11 wa Baraza la Wawakilishi la Marekani (Congress) kutoka vyama vyote viwili vikuu nchini humo.
Kikao hicho cha ngazi ya juu kilichofanyika Julai 27, 2026, katika Ofisi za zamani za Makao Makuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (Ngome), Upanga jijini Dar es Salaam, kiliongozwa na Mwenyekiti wa Kamati Ndogo ya Huduma za Kijeshi, Ulinzi na Usalama ya Baraza la Wawakilishi la Marekani, Ronny Jackson.
Pamoja na kuwasilisha ombi hilo la kuondoa vikwazo, pande hizo mbili zilijadili maeneo ya kipaumbele ikiwemo fursa za biashara, uwekezaji, ulinzi na usalama, pamoja na amani katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
Ujumbe wa Marekani uliipongeza sana Tanzania kwa mchango wake katika kudumisha amani na usalama wa kikanda, ikiwemo juhudi za kupambana na ugaidi na ushiriki katika operesheni za kulinda amani barani Afrika.
Aidha, pande hizo mbili zilikubaliana kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kimkakati katika maeneo yenye maslahi ya pamoja na pia kukubali kupitia tena maombi yote ya vikwazo yaliyowasilishwa rasmi na Tanzania na kukubaliana kukutana tena katika vikao vijavyo vitakavyofuata kwa lengo la ufuatiliaji kati ya nchi mbili. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi amekagua Mradi wa Ukarabati wa Miundombinu ya Maji katika Miji ya Vwawa na Mlowo wilayani Mbozi, Mkoa wa Songwe ambapo gharama ya mradi huo ni Shilingi milioni 752. 8, fedha kutoka katika Mfuko wa Taifa wa Maji.
Waziri Katambi yuko mkoani Songwe kwa ziara ya ufuatiliaji wa ahadi zilizotolewa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa wananchi wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
Mradi huo ambao unatarajiwa kukamilika mwezi Septemba mwaka huu unajumuisha ukarabati wa matenki nane ya maji, kulaza bomba, ujenzi wa chemba 94, ujenzi wa uzio sambamba na mahitaji mengine ambapo kukamilika kwake kutawezesha kupunguza upotevu wa maji lita laki tano kwa siku na kupunguza malalamiko ya kubambikiwa bili za maji kwa wananchi kwa kufunga mita janja.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Rais wa Marekani, Donald Trump ametangaza kusitisha kwa muda mpango wa kufanya mashambulizi mapya ya kijeshi dhidi ya Iran, kutokana na kile alichokieleza kuwa ombi kutoka serikali ya Tehran na mataifa mengine ya Mashariki ya Kati yaliyoomba muda wa kukamilisha mkataba wa amani.
Katika taarifa aliyoitoa kupitia mtandao wake wa Truth Social, Rais Trump ameweka masharti kuwa makubaliano hayo lazima yahusishe kufunguliwa mara moja kwa Mlangobahari wa Hormuz pamoja na kukomesha kabisa tishio la nyuklia la Iran.
Trump ameonya kuwa hatua hiyo ya kusitisha mashambulizi inategemea kasi na ufanisi wa kufikiwa kwa mkataba huo kwa haraka, huku akisisitiza kuwa jeshi la Marekani lipo tayari kwa hatua kali zaidi iwapo maongezi hayo yatagonga mwamba.
"Marekani ipo tayari na imejipanga kikamilifu kuchukua hatua dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, kwa nguvu za kijeshi na uwezo ambao haujawahi kushuhudiwa tangu Vita Kuu ya Pili ya Dunia. Pamoja na hayo, tumeombwa na Iran pamoja na nchi za Mashariki ya Kati kusitisha shambulio lolote kwa kuwa misingi ya makubaliano imeshafikiwa," ameandika Rais Trump.
Rais Trump ameongeza kuwa uamuzi huo wa kutoa nafasi ya diplomasia unalenga manufaa ya dunia nzima pamoja na ustawi wa baadaye wa taifa la Iran, huku akibainisha kuwa taifa la Israel pia linaunga mkono mchakato huo.
"Kulingana na ombi hili, nimekubali kughairi shambulio hilo kwa faida ya baadaye ya dunia na pia kwa ajili ya kupona na kustawi kwa Iran, ikitegemea uwezo wa kufikia makubaliano kwa haraka. Taifa la Israel linaungana nami katika ahadi hii. Kila mmoja aingie kazini na tukamilishe hili," amehitimisha Trump. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkuu wa Wilaya ya Songea, Wilman Kapenjama Ndile, ameiagiza Serikali ya Kijiji cha Lutukira kilichopo Halmashauri ya Madaba mkoani Ruvuma kumsimamia kikamilifu mfugaji mmoja aliyeingiza mifugo kwenye mashamba ya wakulima ili alipe fidia ya mazao yote yaliyoharibiwa.
Agizo hilo linakuja kufuatia oparesheni iliyofanikisha kukamatwa kwa mifugo (ng’ombe) iliyokuwa ikilishwa kwenye mashamba ya wananchi na kusababisha hasara kubwa ya mazao kijijini hapo.
Wakulima wa Kijiji cha Lutukira wamewasilisha masikitiko yao makubwa mbele ya Mkuu huyo wa Wilaya, wakieleza kuwa baadhi ya wafugaji wamekuwa wakitumia ubabe kwa kuingiza mifugo kwa nguvu kwenye mashamba yao na kuharibu mazao. Wananchi hao wameiomba Serikali kuchukua hatua dhabiti za kuwadhibiti wafugaji hao ili kuondoa kikwazo hicho katika shughuli za kilimo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA) umesema umefikia utekelezaji wa asilimia 92% wa mpango wake wa kazi katika mwaka wa fedha uliopita, mafanikio yanayotokana na matumizi ya mifumo ya kidijitali pamoja na ongezeko la mapato lililosaidia kuboresha huduma za vipimo nchini.
Akizungumza Agosti 1, 2026 jijini Arusha, Mtendaji Mkuu wa WMA, Alban Mark Kihula, amesema mafanikio hayo yatajadiliwa katika Kikao cha 38 cha Baraza la Wafanyakazi kinachotarajiwa kufanyika kesho, Agosti 2, 2026.
Amesema kikao hicho kitawakutanisha viongozi na watumishi kutathmini utekelezaji wa mpango na bajeti ya mwaka uliopita, kujadili changamoto zilizojitokeza na kuweka vipaumbele vya mwaka mpya wa fedha.
Kihula amesema kabla ya kikao hicho, wajumbe wapya wa Baraza la Wafanyakazi walipatiwa mafunzo kuhusu majukumu yao, maadili na taratibu za utumishi wa umma, hatua inayolenga kuongeza ufanisi na uwajibikaji katika utekelezaji wa majukumu ya taasisi.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Denis Lazaro Londo, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kikao hicho na kuzindua Mpango Mkakati mpya wa WMA wa miaka mitano, utakaolenga kuimarisha usimamizi wa vipimo nchini, kuongeza uwazi katika biashara na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Kufuatia kauli iliyotolewa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuundwa kwa Tume ya Maridhiano ili kuharakisha mchakato wa Katiba Mpya unaanza, Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Benson Kigaila amesema chama hicho kimepokea kwa mikono miwili taarifa hiyo huku akiahidi kuhakikisha wanapata Katiba Mpya bora itakayokidhi matarajio ya wananchi.
Akizungumza Agosti 1, 2026 Wilayani Ilemela mkoani Mwanza katika kikao cha ndani cha uzinduzi wa Operesheni "Tujenge Pamoja", Kigaila amesema CHAUMMA itaendelea kushiriki katika mijadala na kutoa mapendekezo ili kuhakikisha Katiba Mpya itakayopatikana inalinda maslahi ya wananchi, kuimarisha demokrasia, utawala wa sheria na haki za msingi.
"Sisi kama Chama, tangazo au uamuzi huo tume upokea kwa mikono miwili kwa sababu kubwa moja tu madai ya Katiba Mpya yamekuwa madai ya Watanzania toka mwaka 1980, tumedai kwa namna mbalimbali na utawala mbalimbali hatukupata, Rais Kikwete alijaribu kidogo ikakwama na kuishia pale sasa wametangaza," amesema Kigaila
Kigaila amesema Chama hicho kinaamini kuwa ushiriki mpana wa wananchi katika hatua zote za mchakato wa Katiba Mpya utasaidia kupatikana kwa katiba yenye kukubalika na Watanzania wengi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Itikadi Uenezi na Mafunzo Kenani Laban Kihongosi amesema baada ya kuruhusiwa kwa mikutano ya hadhara chama hicho kitaendelea na programu zake nchini huku akiwataka wafuasi wa chama hicho kujitenga na wanasiasa ambao siasa 'zimewashinda' na wakaamua kugeukia kwenye vurugu.
Kenani amesema hayo leo Agosti 1, 2026 katika hafla ya kuwapokea wajumbe wa Sekretarieti ya CCM ambao wameteuliwa hivi karibuni. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma, Ngollo Malenya, amemsimamisha kazi Mwenyekiti wa Kijiji cha Chengena, Valence Ndenje, kutokana na ripoti ya Tume ya Uchunguzi kubaini tuhuma za ubadhilifu wa fedha, kuuza maeneo ya Serikali ya kijiji bila kushirikisha wananchi, pamoja na kuuza viwanja na ardhi za wananchi kinyume cha sheria na taratibu.
Uamuzi huo umetangazwa na DC Ngollo wakati wa mkutano wa hadhara wa wananchi uliofanyika jana kijijini hapo. Hatua hiyo imekuja baada ya kusikiliza kero na hoja za wananchi, kumpa nafasi Mwenyekiti huyo kujitetea, na hatimaye kusoma maazimio ya Tume aliyoiunda wiki mbili zilizopita kuchunguza sakata hilo.
Akitangaza uamuzi huo wa Serikali ya Wilaya mbele ya mkutano huo, DC Ngollo alisema: "Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan alishaagiza kwamba tuhakikishe tunawapa wananchi tabasamu. Baada ya kuja hapa na kuunda Tume, nimejiridhisha pasipo shaka kwamba Mwenyekiti wetu hatoshi. Serikali haiwezi kusita kutekeleza majukumu yake; nimefika hapa kutamka rasmi kuwa kuanzia leo Mwenyekiti huyu anasimamishwa kazi."
Baada ya kutangazwa kwa uamuzi huo, DC Ngollo aliwapa wananchi fursa ya kidemokrasia ya kumchagua mmoja wa Wenyeviti wa Vitongoji anayeaminika ili kukaimu nafasi ya Uenyekiti wa Kijiji cha Chengena wakati wakisubiri mchakato wa uchaguzi mdogo kufuata taratibu.
Wanakijiji hao kwa pamoja walimchagua Thobias Komba kukaimu nafasi hiyo hadi uchaguzi mwingine utakapofanyika.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi @ccmtanzania Bara Aggrey Mwanri amewataka wanachama wa chama hicho kufanya kazi kwa uaminifu wakizingatia kuwa na tabia njema kwani zitawasaidia.
Amesema hayo leo Agosti 1, 2026 alipopokelewa jijini Dar es Salaam mara baada ya kuteuliwa na Halmashauri Kuu ya CCM Julai 29, 2026.
Mwanri amesisitiza kuwa makada wa chama hicho hawapaswi kukata tamaa na pia wanapaswa kujipenyeza kwa tabia na mwenendo mzuri. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katibu wa NEC Organaizesheni ya Chama cha Mapinduzi CCM Paul Matiko Chacha amesema kwa sasa nchini hakuna upinzani wenye nguvu kama ilivyokuwa miaka ya nyuma akitolea mfano wa upinzani wa Agustino Lyatonga Mrema(aliyewahi kuwa mgombea Urais kupitia NCCR Mageuzi) Freeman Mbowe, Dkt. Wilbroad Slaa na Maalim Seif Shariff Hamad.
Kauli hiyo ya Chacha ameitoa leo Agosti 1, 2026 alipopokelewa jijini Dar es Salaam mara baada ya kuteuliwa na Halmashauri Kuu ya CCM Julai 29, 2026. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katibu wa NEC Oganaizesheni ya Chama cha Mapinduzi CCM Paul Matiko Chacha amemshauri Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) John Heche kumuomba msamaha Makamu Mwenyekiti wa CCM Stephen Wasira kutokana na kile alichodai kuwa ni kauli alizotoa kutokuwa sawa kwa miiko na maadili ya Kikurya
Kauli hiyo ya Chacha ameitoa leo Agosti 1, 2026 alipopokelewa jijini Dar es Salaam mara baada ya kuteuliwa na Halmashauri Kuu ya CCM Julai 29, 2026. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Zaidi ya shilingi bilioni 33 zitatumika katika mradi wa kupanua kingo za Bwawa la Mindu kwa mita 2.5, hatua itakayoongeza uwezo wa bwawa kuhifadhi maji kutoka lita bilioni 12.6 za sasa hadi lita bilioni 22.06 ili kukidhi ongezeko la mahitaji ya maji kutokana na ukuaji wa idadi ya watu mkoani Morogoro.
Hayo yameelezwa wakati wa kusainiwa kwa mkataba wa utekelezaji wa mradi huo kati ya MORUWASA na mkandarasi Sinohydro Corporation Limited, Mkurugenzi Mtendaji wa MORUWASA, CPA Sais Kyejo, amesema mradi huo utatekelezwa kwa kipindi cha miezi 18.
Akishuhudia utiaji saini wa mkataba huo, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Adam Malima, amewataka wananchi wanaoishi karibu na Bwawa la Mindu kutunza vyanzo vya maji na amesema Serikali itahakikisha wote watakaopisha upanuzi wa bwawa wanalipwa fidia stahiki kwa wakati.
Serikali inalenga kuhakikisha ifikapo mwaka 2030 changamoto ya upatikanaji wa maji katika Manispaa ya Morogoro inakuwa historia, huku Bwawa la Mindu likiendelea kuwa chanzo kikuu cha maji kwa wakazi wa manispaa hiyo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Serikali imewataka vijana kujiajiri kupitia sekta ya kilimo ili kujijengea uchumi imara na kuwa na uhakika wa maisha yao ya baadaye, ikisisitiza kuwa itaendelea kuwaunga mkono wale wote watakaoamua kuwekeza katika shughuli za kilimo.
Akizungumza leo Ijumaa Jijini Dodoma kuelekea Maadhimisho ya Nanenane 2026, Waziri wa Kilimo, Daniel Chongolo amesema Serikali imeweka mikakati ya kuwasaidia na kuwafuatilia vijana wanaotaka kuingia kwenye sekta hiyo ili wanufaike moja kwa moja na fursa zilizopo na kuongeza uzalishaji wa kilimo.
Aidha amesema ushiriki wa vijana katika kilimo ni muhimu kwa maendeleo ya uchumi wa taifa na kuimarisha usalama wa chakula, huku akiwahimiza kutumia fursa mbalimbali zinazotolewa na Serikali kupitia programu na miradi ya maendeleo ya kilimo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Camillus Wambura, amesema kuwa kazi inayofanywa na Madawati ya Jinsia na Ulinzi wa Mtoto ni moja ya maeneo nyeti zaidi ndani ya jeshi hilo, kwani inahusu moja kwa moja wananchi waliopitia maumivu makali na hofu.
IGP Wambura ametoa kauli hiyo leo Ijumaa, Julai 31, 2026, jijini Dodoma wakati akifunga rasmi Mkutano Mkuu wa Dawati la Jinsia na Ulinzi wa Mtoto wa Mwaka 2025/2026 ambapo amesisitiza kuwa kulinda wanawake na watoto ni kujenga msingi imara wa amani na maendeleo endelevu.
Kwa upande wake, Kamishna wa Kamisheni ya Polisi Jamii, CP Alex Mkama amewasilisha ripoti ya utekelezaji wa shughuli za dawati kwa kipindi cha Julai 2025 hadi Juni 2026, akibainisha mafanikio makubwa katika utoaji wa elimu kwa jamii. Amesema jumla ya wanufaika 1,933,380 walifikiwa na elimu moja kwa moja kupitia mikutano 192, nyumba za ibada 648 (makanisa na misikiti), shule za msingi na sekondari zaidi ya 1,900, pamoja na vyuo 180.
CP Mkama amesisitiza umuhimu wa kampeni ya “Tuwaambie Kabla Hawajaharibiwa” inayolenga wanafunzi na wanavyuo, akitumia methali ya “samaki mkunje angali mbichi” kuhamasisha malezi bora na maadili mema kuanzia umri mdogo.
Katika kilele cha mkutano huo, IGP Wambura amezindua rasmi Kituo cha Huduma kwa Simu (Call Centre) cha Dawati la Jinsia, mfumo wa kisasa ulioundwa kuboresha upokeaji, ufuatiliaji, na ushughulikiaji wa taarifa na malalamiko ya ukatili nchini kote kwa haraka na ufanisi mkubwa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amepokea uenyekiti wa Kamisheni ya Bonde la Mto Ruvuma utakaodumu kwa kipindi cha mwaka mmoja ambapo Serikali ya Jamhuri ya Malawi itakuwa Makamu Mwenyekiti.
Aweso amepokea uenyekiti huo Julai 31, 2026 huko Pemba Msumbiji, ambapo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Serikali ya Msumbiji na Malawi zimesaini Mkataba wa kuanzisha Kamisheni ya Bonde la Mto Ruvuma.
Washiriki wengine katika hafla hiyo ni Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji Khamis Hamad, Balozi Mdogo wa Serikali ya Ujerumani nchini Msumbiji, Gavana wa Jimbo la Pemba Msumbiji, pamoja na Wadau wa Maendeleo (IUCN, GWPSA, GIZ, na WI).
Mkataba huo uliosainiwa unatarajiwa kuongeza chachu ya usimamizi wa rasilimali maji kwa njia shirikishi baina ya nchi wanachama na wadau wote wa Bonde la Mto Ruvuma. Imebainishwa kuwa Serikali ya Tanzania itanufaika kwa kuwa Mto Ruvuma ni moja ya vyanzo vitakavyotumika katika Gridi ya Taifa ya Maji. -
Jambo TV
@Jambotv_
Watu sita wamefariki dunia na wengine watatu kujeruhiwa kutokana na ajali iliyohusisha basi la abiria aina ya Higher na lori lenye tela katika eneo la Naiti, kata ya Makuyuni wilayani Monduli mkoani Arusha.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha, ajali hiyo ilitokea Julai 30, 2026 majira ya saa 12:40 jioni katika barabara ya Arusha–Dodoma. Watu watano walifariki papo hapo, huku mmoja akifariki akiwa anapatiwa matibabu hospitalini. Waliofariki ni wanaume watatu na wanawake watatu.
Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa chanzo cha ajali hiyo unaendelea, huku majeruhi wakiendelea kupatiwa matibabu na miili ya marehemu ikihifadhiwa katika Kituo cha Afya Makuyuni kwa taratibu zaidi. -
Jambo TV
@Jambotv_
Kesi ya Uhaini na 19605/2025 inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo @ChademaTZ2 Tundu Lissu itaendelea kuanzia Agosti 10, 2026 mpaka Septemba 7,2026 katika Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Mawakili Wanaomfanyia Utafiti Lissu, Wakili Hekima Mwasipu amethibitisha kupokea barua kutoka mahakamani hapo ambayo imeeleza kuwa kabla ya shauri kuendelea kitafanyika kikao cha awali cha maandalizi ya usikilizwaji wa shauri hilo agosti 5, 2026.
Lissu ambaye alikamatwa April 9, 2025 na kufunguliwa mashtaka ya uhaini, kesi yake ilisimama kwa muda kuanzia Februari 24, 2026 kutokana na kufunguliwa shauri la marejeo katika Mahakama ya Rufani juu ya mwenendo na uamuzi uliotolewa na majaji kukataa ushahidi wa nyongeza wa ACP Amini Mahamba.
Ikumbukwe jana Julai 30, 2026 Mahakama ya Rufani iliyatupilia mbali maombi ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini(DPP) juu ya kupitiwa kwa maamuzi hayo yaliyotolewa na Mahakama Kuu.
Shauri hili lipo mbele ya Jopo la Majaji watatu wakiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru ambapo kabla ya kuahirishwa tayari mashahidi 15 walikuwa wameshatoa ushahidi wao ambapo miongoni mwao wapo Askari wa Jeshi la Polisi, madereva pikipiki(bodaboda). -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda, amemwagiza Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Mkuu wa Polisi wa Wilaya (OCD), pamoja na watendaji wa kata na vijiji kuendesha oparesheni maalumu ya wiki mbili kuhakikisha wanafunzi wote waliopangiwa kujiunga na Kidato cha Tano wanaripoti shuleni mara moja.
RC Mtanda ametoa maagizo hayo akiwa kwenye ziara ya kikazi wilayani Ukerewe, kufuatia kusikitishwa kwake na idadi kubwa ya wanafunzi ambao bado hawajaripoti mashuleni licha ya muhula kuanza.
Kati ya wanafunzi 1,109 waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano wilayani humo, ni wanafunzi 569 pekee ndio walioripoti hadi kufikia Julai 24, 2026 sawa na asilimia 51.3 huku wanafunzi 540 (asilimia 48.7) wakiwa bado hawajaripoti.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, RC Mtanda amesisitiza kuwa Mkoa wa Mwanza hautavumilia uzembe au utoro wa wanafunzi wanaotakiwa kuendelea na masomo.
"Mkuu wa Wilaya, Kamanda wa Jeshi la Polisi, Watendaji wa Kata na Vijiji, ninataka mfanye oparesheni kubwa kabisa hapa Ukerewe. Wale wote wanaostahili kwenda shule, tunataka ndani ya wiki mbili wawe wamefika shuleni. Hatutaki watutie aibu Mkoa wa Mwanza," amesema Mtanda.
Aidha, RC Mtanda ametoa onyo kwa wazazi na walezi wanaojaribu kuwakatisha masomo wanafunzi hao, hususan wale wanaopanga kuwaozesha watoto wao badala ya kuwapeleka shuleni, akibainisha kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mtu yeyote atakayebainika kukwamisha elimu ya mtoto.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwanaharakati na Kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Godilisten Malisa @MalisaGJ_ amesema siasa za Chama cha Ukombozi wa Umma zinategemea uwepo wa CHADEMA.
Akizungumza katika mahojiano aliyofanya na Jambo TV Malisa amesema CHAUMMA inatumia muda mwingi kupambana na CHADEMA badala ya chama tawala (CCM).
Mahojiano kamili yapo YouTube yetu ya Jambo TVThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, leo tarehe 31 Julai, 2026, amezindua boti mbili mpya za doria kwa ajili ya kuimarisha ulinzi na usalama katika bahari na maziwa makuu, huku akitoa agizo kwa Wizara ya Uchukuzi na taasisi zake kutenga fedha kwa ajili ya mafuta na matengenezo ili doria hizo zisikwame.
Akizungumza katika viwanja vya Bandari ya Dar es Salaam, Dkt. Nchemba amesisitiza kuwa vitendea kazi hivyo lazima viwe tayari wakati wote akiwatahadharisha watendaji kwa kutumia mifano aliyokutana nayo mikoani, ambapo gari za wagonjwa za kisasa zinanunuliwa lakini zinashindwa kuokoa maisha kwa kukosa mafuta.
Naye, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), Prof. Palamagamba Kabudi ameelezea uratibu wa kiserikali uliohakikisha mradi huu unakidhi vigezo akisema boti hizo zimejengwa nchini Japan na kampuni ya Yamaha kwa kuzingatia vipimo na viwango vya kimataifa vilivyokubaliwa na wataalamu wa serikali. Amesema kabla ya kukamilika kwake, wataalamu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), na Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini (IRDP) walifanya ziara za ukaguzi nchini Japan ili kujiridhisha na ubora wa utekelezaji.
Akielezea sifa za boti hizo, Profesa Providence Dimoso, Mwakilishi wa Mkuu wa IRDP amesema boti hizo zina mwendokasi wa zaidi ya noti 52 (takribani kilomita 96.3 kwa saa), zikizidi kiwango cha noti 50 kilichokuwa kwenye mkataba na zikiwa na uwezo kutumia takribani dakika 30 tu kutoka Dar es Salaam hadi Zanzibar. Aidha, kila boti inaweza kubeba hadi watu 12 na imewekwa mifumo ya kisasa ya urambazaji (navigation systems) na vifaa vya uokoaji vinavyokidhi viwango vya kimataifa.
Mradi huu umetekelezwa kwa gharama ya dola za Kimarekani milioni 2 (Takriban Shilingi za Kitanzania bilioni 5) ukiwa ni ufadhili kutoka kwa Serikali ya watu wa Japan kupitia UNDP. Mradi huu uliodumu kwa mwaka mmoja tangu Machi 2025, haukuishia kwenye ununuzi wa boti pekee, bali ulihusisha pia mafunzo ya kuwajengea uwezo wakulima wa zao la mwani na ujenzi wa kikaushio cha mwani na usimikaji wa mashine za kusagisha mwani katika Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga, ili kuongeza thamani ya zao hilo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI PICHA:
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imetoa elimu kwa wanafunzi wa Klabu ya Mazingira na Maji katika Shule ya Msingi Osterbay, Wilaya ya Kinondoni, mkoani Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya kampeni ya kudhibiti upotevu wa maji. Lengo la elimu hiyo ni kujenga uelewa kuhusu umuhimu wa jamii kushiriki katika kudhibiti upotevu wa maji.
Katika mafunzo hayo, wanafunzi walihimizwa kuwa mabalozi wa kampeni hiyo kwa kutoa taarifa za uvujaji wa maji na kushiriki katika kulinda miundombinu ya maji, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuhakikisha huduma ya maji inaendelea kuwa endelevu kwa jamii.
Akizungumza wakati wa utoaji elimu hiyo, Afisa Mawasiliano DAWASA, Prisca Makenya alisema wanafunzi wamefundishwa aina mbalimbali za upotevu wa maji, ikiwemo upotevu unaotokana na mabomba kupasuka, maji yasiyopitia kwenye mita pamoja na matumizi halali ya maji yasiyopitia kwenye mita, kama yale yanayotumiwa na zimamoto.
"Tunaamini elimu hii itawasaidia wanafunzi kuwa mabalozi wazuri wa kampeni ya kudhibiti upotevu wa maji katika jamii zao," alisema Makenya.
Kwa upande wake, mwalimu anayesimamia Klabu ya Mazingira, Ninah Jeremia, aliishukuru DAWASA kwa kuendelea kutoa elimu ya udhibiti wa upotevu wa maji kwa jamii.
"DAWASA imekuwa mshirika muhimu katika kutoa elimu ya utunzaji wa miundombinu ya maji, jambo linalochangia kuongeza uelewa kwa wanafunzi na jamii kwa ujumla," alisema Jeremia.
Naye mwanafunzi Raiyat Mwarami alisema elimu aliyopata imemwezesha kuelewa aina za upotevu wa maji pamoja na namna ya kutoa taarifa za uvujaji kupitia kwa njia mbalimbali
"Kwa elimu hii, naahidi nitakuwa balozi mzuri wa kutoa taarifa za uvujaji wa maji kwa DAWASA," alisema Raiyat. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI PICHA:
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, leo tarehe 31 Julai, 2026, amezindua boti mbili mpya na za kisasa za doria katika viwanja vya Bandari ya Dar es Salaam. Boti hizo, zilizopewa majina ya PB Sailfish 02 na PB Sailfish 03, zinaongeza nguvu katika ulinzi wa rasilimali na mipaka ya bahari pamoja na maziwa makuu, zikifuatia uzinduzi wa boti ya kwanza (PB Sailfish) uliofanyika Machi 2, 2024.
Boti hizi zimejengwa nchini Japan kwa teknolojia ya hali ya juu inayozikubali kufanya kazi katika mazingira magumu ya baharini. Sifa zake kuu ni pamoja na mwendokasi wenye kufikia kasi ya zaidi ya noti 52 (takribani kilomita 96.3 kwa saa), jambo linalozifanya kuwa miongoni mwa boti za kisasa zenye mwendo wa kasi zaidi duniani. Kasi hii inaziwezesha kutumia takribani dakika 30 tu kutoka Dar es Salaam hadi Zanzibar. Aidha, kila boti ina uwezo wa kubeba hadi watu 12 kwa wakati mmoja na zimefungwa mifumo ya kisasa ya urambazaji (navigation systems), mawasiliano ya haraka, na vifaa vya uokoaji vinavyokidhi viwango vya kimataifa vya usalama.
Mradi huu umetekelezwa kwa gharama ya dola za Kimarekani milioni 2 (Takriban Shilingi za Kitanzania bilioni 5) ukiwa ni ufadhili kutoka kwa Serikali ya watu wa Japan kupitia UNDP. Mradi huu uliodumu kwa mwaka mmoja tangu Machi 2025, haukuishia kwenye ununuzi wa boti pekee, bali ulihusisha pia mafunzo ya kuwajengea uwezo wakulima wa zao la mwani na ujenzi wa kikaushio cha mwani na usimikaji wa mashine za kusagisha mwani katika Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga, ili kuongeza thamani ya zao hilo.
Uzinduzi huu umetajwa kuwa hatua kubwa katika kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa na uwezo wa kufanya doria, ufuatiliaji, na uokoaji wa haraka katika maeneo yake ya maji, huku ikisaidia kukuza uchumi wa buluu kupitia zao la mwani. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Wazee wa ambao ni wanachama na wafuasi Chama cha Demokrasia na Maendeleo Mkoa wa Simiyu wameeleza kuridhishwa na kiongozi wao Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Bara John Heche huku wakimtaka aendelee kukipigania chama hicho ili kuleta mabadiliko.
Akizungumza kwa niaba ya wazee hao Mjumbe wa Baraza la Wazee CHADEMA(BAZECHA) Mkoa wa Simiyu, Kenedy Onyangi kwenye Mkutano Mkuu Maalumu wa CHADEMA mkoa huo uliohudhuriwa na Heche @HecheJohn amesema pamoja na kusikia shutma mbalimbali ambazo zinaelekezwa kwa kiongozi huyo bado wana imani naye na wapo tayari kuchangia chama.
"Tunayaona yote wanayoyaongea kuhusu kwamba umekula hela sijui umefanya nini yote tunayaona sio kwamba hatuyaoni lakini sisi tunaimani na wewe lakini ukipata nafasi ya kumuona Mandela wa Tanzania, Tundu Lissu mwambie sisi wazee wa Simiyu tupo na yeye," amesema
Mbali na kutoa pongezi hizo, wazee hao pia walimpatia Heche zawadi ya fedha na mbuzi ikiwa ni ishara ya kumtia moyo katika mapambano ya uongozi ndani ya chama hicho.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema Serikali itaendeleza maridhiano ya kisiasa kuelekea hatua za maboresho ya Katiba kwa kuzingatia sheria na taratibu za nchi.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Bakari Machumu, Rais Dkt. Samia ameyasema hayo Julai 30, 2026, alipokutana na viongozi wa vyama 18 vya siasa nchini, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mazungumzo hayo yalihusu maridhiano, mageuzi ya kisiasa, uchumi, huduma za jamii, ajira, uwekezaji na ulinzi wa amani ya nchi. Akirejea hatua ya mchakato wa maridhiano visiwani Zanzibar, Rais Dkt. Samia amewaeleza viongozi hao hatua zilizofikiwa za maandalizi ya mchakato wa maridhiano kuelekea hatua zinazofuata za mapitio ya Katiba.
Amesisitiza kuwa hatua zote za mchakato huo zitafanyika kwa kuzingatia sheria, kanuni, na taratibu zilizowekwa, kwa maslahi mapana ya Taifa, na kwamba Serikali itaendelea kukutana na viongozi wa vyama vya siasa kwa mazungumzo katika kipindi cha angalau mara tatu kwa kila mwaka.
Mkutano huo, uliowaleta pamoja wenyeviti, makamu wenyeviti, makatibu wakuu na viongozi wa jumuiya za vyama vya siasa nchini, ni wa pili wa aina hiyo kuitishwa na Rais Dkt. Samia tangu kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.
Mkutano wa awali ulifanyika tarehe 31 Machi, 2026, Ikulu jijini Dar es Salaam, ukiwakutanisha wagombea wa nafasi ya Rais na wagombea wenza kutoka vyama vya siasa vilivyoshiriki uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.
Aidha, Rais amevitaka vyama vya siasa nchini kulinda amani, uhuru na maslahi ya nchi, akisisitiza kuwa ulinzi wa Tanzania ni wajibu wa pamoja baina ya Serikali, vyama vya siasa na wananchi wote.
Katika hatua nyingine, viongozi hao waliwasilisha maoni yao kuhusu masuala mbalimbali ya maendeleo na ustawi wa wananchi katika nyanja za siasa, maendeleo ya jamii na uchumi. Serikali iliahidi kuendelea kuyapokea na kuyafanyia kazi mapendekezo hayo kupitia majukwaa stahiki ya majadiliano na mifumo rasmi ya maamuzi. -
Jambo TV
@Jambotv_
Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), kimesisitiza kufanyika kwa mazungumzo ya pamoja, kikisema hatua hiyo itasaidia kujenga nchi kwa utulivu.
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Habari, Mawasiliano na Uenezi wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), John Mrema, alipokuwa akiwahutubia wanachama na wananchi katika kikao cha ndani kilichofanyika Kamachumu Wilaya ya Muleba mkoani Kagera.
Mrema amesema kutokana na baadhi ya masuala kutokuwa sawa nchini hususani utulivu wa kisiasa, ni vyema jitihada zikafanyika watu wakaacha kiburi, jeuri na ubinafsi badala yake wakubali kukaa pamoja na kuungana ili kufanya mazungumzo yenye kuleta tija kwa masilahi ya nchi.
Amesema wao CHAUMMA wanaunga mkono juhudi za mazunguzo kwa nguvu moja, kwani Chama hicho kina malengo ya kujenga na siyo kubomoa.
Hata hivyo hakusita kugusia changamoto za wananchi wa Muleba na Kagera kwa ujumla ikiwemo changamoto za uhaba wa masoko ya mazao ya kahawa, ndizi na mengineyo yanayozalishwa Kagera. Ametoa wito kwa serikali akiishauri kutafuta masoko ya uhakika na yenye kumuinua mwananchi wa mkoa huo.
Katika kikao hicho pia amegusia suala la Katiba Mpya akisema kuwa upatikanaji wake ni jukumu na haki ya kila mwananchi, hivyo inapaswa kutiliwa maanani na viongozi walioko madarakani na kuanza mchakato mapema na si vinginevyo.
John Mrema, akiongozana na Susan Kiwanga ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Katiba ya CHAUMMA, Elia Mahwa Mkurugenzi wa utafiti Operasheni ya TUJENGE PAMOJA na Rahman Rungwe, kwa pamoja wameelezea mipango inayoendelea kusukwa na Chama hicho kwa ajili ya maandalizi yatakayowawezesha kufanya vizuri katika chaguzi zijazo.
Viongozi hao wamewasihi wananchi kukiunga mkono CHAUMMA ambacho wamesema kimejizatiti kuwakomboa wananchi na wimbi la umaskini linalokabili Mkoa wa Kagera na maeneo mengine nchini. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali itaendeleza maridhiano ya kisiasa kuelekea hatua za maboresho ya Katiba kwa kuzingatia sheria na taratibu za nchi.
Dkt. Samia ameyasema hayo leo tarehe 30 Julai, 2026, alipokutana na viongozi wa vyama 18 vya siasa nchini, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mazungumzo hayo yalihusu maridhiano, mageuzi ya kisiasa, uchumi, huduma za jamii, ajira, uwekezaji na ulinzi wa amani ya nchi.
Halikadhalika, Rais Dkt. Samia amevitaka vyama vya siasa nchini kulinda amani, uhuru na maslahi ya nchi, akisisitiza kuwa ulinzi wa Tanzania ni wajibu wa pamoja baina ya Serikali, vyama vya siasa na wananchi wote.
Akirejea hatua ya mchakato wa maridhiano visiwani Zanzibar, Rais Dkt. Samia amewaeleza viongozi hao hatua zilizofikiwa za maandalizi ya mchakato wa maridhiano kuelekea hatua zinazofuata za mapitio ya Katiba.
Amesisitiza kuwa hatua zote za mchakato huo zitafanyika kwa kuzingatia sheria, kanuni, na taratibu zilizowekwa, kwa maslahi mapana ya Taifa, na kwamba Serikali itaendelea kukutana na viongozi wa vyama vya siasa kwa mazungumzo katika kipindi cha angalau mara tatu kwa kila mwaka.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, John Heche, amesema wanachama waliopoteza nafasi katika uchaguzi wa ndani wa chama hicho hawakutoa ushirikiano kwa uongozi mpya, badala yake waliwasaliti na wengine kugeuka miradi ya watu.
Akizungumza Julai 30, 2026 katika Mkutano Mkuu maalumu wa CHADEMA, uliofanyika Bariadi Mjini Mkoa wa Simiyu, Heche amesema yeye pamoja na Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu baada ya kushinda uongozi walitarajia kupata ushirikiano kutoka kwa wanachama wote bila kujali matokeo ya uchaguzi.
"Tukaenda kwenye uchaguzi wa ndani ya chama yaliyotokea wote mnayajua. Tundu Lissu akasimama, na mimi nikasimama tukashinda uchaguzi, tuliposhinda uchaguzi unategemea watu waliokuwa CHADEMA, wanajifanya Wanachadema, wameongoza sisi tukiwa tunawaunga mkono miaka yote hiyo waliposhindwa, wakageuka kuwa ‘project’ za watu," amesema Heche.
Aidha, Heche amesema msimamo wa Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu ni kuwa chama anachokiongoza hakiko tayari kufanya siasa za mzaha bali kinataka kusukuma mbele mabadiliko ya kweli.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, John Heche, amesimulia jinsi alivyokuwa akituhumiwa kumpindua aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe akisema tuhuma hizo zilikuja kila alipotoa msimamo wake kuhusu masuala ya chama na taifa.
Akizungumza leo kwenye Mkutano Mkuu Maalumu wa CHADEMA Mkoa wa Simiyu uliofanyika Bariadi Mjini, Heche amesema kuna kipindi chama hicho kilikaa kimya licha ya kuwepo kwa matukio mbalimbali yaliyohitaji msimamo wa viongozi, huku akidai kuwa kila mwanachama aliyekuwa akijitokeza kuzungumzia masuala hayo alitafsiriwa vibaya ikiwamo yeye, hivyo hata tuhuma ambazo zinaelekezwa hivi sasa ikiwamo kutafuna fedha za chama na kukwamisha maridhiano si jambo geni kwake.
"Kuna kipindi mliona chama kina watu, matukio yanatokea hakuna kinachozungumzwa mtu akitaka kunyenyuka kusema wanasema huyu ohooo anataka..., mimi tuhuma za kusema nataka kumpindua Mbowe na kujenga chuki hazijaanza leo, chama kipo kimya hakuna kinachoendelea, nchi inashambuliwa," amesema Heche.
FUATILIA HOTUBA HII KWA UREFU KUPITIA CHANELI YA YOUTUBE YA JAMBO TV.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI PICHA:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amekutana na kuzungumza na viongozi wa vyama vya siasa nchini, Ikulu Dar es Salaam tarehe 30 Julai, 2026. Hata hivyo, Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu-Tanzania haijatoa maelezo ya kina ya lengo la mkutano huo ni kipi hasa kimezungumzwa. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI PICHA:
Mahakama ya Rufani ya Tanzania imetupilia mbali shauri la marejeo na 720316/2026 lililofunguliwa Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini(DPP) dhidi ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) Tundu Lissu ambalo lilitaka kupitiwa mwenendo na uamuzi wa Februari 24, 2026 katika kesi ya uhaini iliyopo Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam.
Maombi hayo yalifunguliwa baada ya uamuzi mdogo kutolewa na Mahakama Kuu kukataa kuongezwa kwa ushahidi wa ziada wa ACP Amini Mahamba ambaye alikuwa Mpelelezi Mkuu wa matukio yaliyotokea Oktoba 29, 2025.
Uamuzi huo wa Rufani uliotolewa Julai 30, 2026 na Majaji wa Rufani Mwarija, Muruke na Khamis umeeleza kuwa mahakama kuu ilikuwa sahihi katika uamuzi huo kwani kifungu cha 308 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai(CPA) kinaeleza juu ya ushahidi wa shahidi ambaye ushahidi wake haukusomwa kabisa katika Mahakama ya Ukabidhi na sio ushahidi mpya wa shahidi ambaye ushahidi wake ulisomwa katika mahakama hiyo.
“Katika mazingira hayo, tunakubaliana na mahakama ya awali kwamba Kifungu cha 308 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA) kinamhusu shahidi ambaye hakutajwa wala ushahidi wake kusomwa kwa mshtakiwa wakati wa mwenendo wa awali wa kupeleka shauri Mahakama Kuu (committal proceedings).” umeeleza uamuzi
Uamuzi huo umeongeza “Kwa kuzingatia sababu zilizotangulia, tunaona kuwa notisi hiyo ilikuwa imewasilishwa kwa msingi usio sahihi wa kisheria (misconceived), na hivyo mahakama ya awali ilikuwa sahihi na ilijielekeza ipasavyo kuifuta (strike out).”
Ikumbukwe Februari 22, 2026 upande wa Jamhuri uliwasilisha mahakamani notisi ya ushahidi wa ziada wa ACP Mahamba juu ya ripoti ya matukio yaliyotokea wakati na baada ya uchaguzi ambapo Lissu alipinga vikali kupokelewa kwa notisi hiyo akieleza ni kinyume na sheria hoja ambayo Mahakama iliikubali.
Aidha uamuzi huo umeyakataa maombi ya Lissu juu ya kutaka kulipwa fidia na DPP kwa kile alichoeleza kuwa ni kusababishiwa usumbufu kwa siku 139 huku ikielezwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kutoa uamuzi huo kwa sasa haliyakuwa kesi bado haijafika mwisho. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katibu Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Ado Shaibu Ado amesema siasa za sasa zimewasaliti Wananchi, akisisitiza kuwa Wananchi hawaoni kama wanasiasa wanawahangaika kutatua kero zao.
Ado alieleza hayo jana Julai 29, 2026 alipokuwa akizungumza na Kamati ya Uongozi ya ACT Wazalendo Mkoa, Kamati za Uongozi za Majimbo pamoja na Kamati za Ngome ya Vijana.
"Siasa yenyewe imemsaliti mwananchi, ndiyo ukweli wenyewe. Kwa Mama lishe Mbagala, Kariakoo, akifungulia televisheni, akifungulia Redio, akisikia habari za wanasiasa hajioni yeye kwenye siasa, hatuoni wanasiasa kama tunahangaika na yeye" amesema Shaibu.
Amesema Wananchi katika jamii watakapoona wanasiasa wanapambana kwaajili ya yao, wananchi wenyewe watakuwa tayari kuungana na Waasiasa hao kwaajili ya kuipambania jamii.
Ameongeza kwamba, Wanasiasa wengi hawayazungumzi kwa kina maswala ya Wananchi badala yake wanayazungumza kwa uchache bila kuyapa kipaumbele, amesema hatua hiyo ndiyo inawafanya Wananchi waone wameachwa na Wanasiasa.
"Sisemi hatuyazungumzi kabisa mambo ya Wananchi, tunayagusa gusa. Unagusa leo hiki, kesho kile, unazungumza kwa juu juu, hatujayapa kipaumbele, Mwananchi ana akili ukiyazungumza mambo kijuu juu anaona, lakini ukiyazungumza mambo kwa utayari anaona pia" ameongeza Shaibu.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) umetoa tamko kulaani mfululizo wa matukio ya kukamatwa, kushikiliwa, na kufunguliwa mashtaka ya ugaidi kwa wahadhiri wa vyuo vikuu mkoani Dodoma. Mtandao huo umeelezea wasiwasi wake kuwa sheria za jinai zinatumika kugeuza ufundishaji, utafiti, na ukosoaji wa kitaaluma kuwa makosa ya jinai, jambo linalotishia uhuru wa kitaaluma nchini.
Akizungumza na wanahabari mkoani Dar es Salaam tarehe 30 Julai 2026, Mratibu wa Kitaifa wa THRDC, Wakili Onesmo Olengurumwa ameeleza kuwa miongoni mwa matukio yaliyopigiwa kelele ni kukamatwa na kufunguliwa mashtaka ya ugaidi kwa Melkisedeki Kitunzi Kaijage, Mhadhiri Msaidizi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).
Mbali na Kaijage, wahadhiri wengine wawili wa Chuo Kikuu cha St. John, Johaiven Revelian Bikongolo na Titus Joseph Kituli, wanaripotiwa kuendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Dodoma tangu mwezi Julai 2026 bila tuhuma zao kuwekwa wazi kwa umma.
THRDC imesisitiza kuwa matumizi ya mashtaka mazito kama ya ugaidi dhidi ya wanazuoni yanazalisha hofu na kujidhibiti miongoni mwa wanataaluma.
Kutokana na hali hiyo, THRDC imetoa wito wa kufutwa kwa kesi ya ugaidi dhidi ya Kaijage kwa upande wa mashtaka kuifanyia mapitio ya haraka kwani haina maslahi kwa umma na inaumiza uhuru wa kitaaluma. Aidha, polisi waweke wazi tuhuma dhidi ya wahadhiri wa St. John's na kuhakikisha wanapata haki zao za kisheria.
Aidha THRDC imeitaka Wizara ya Elimu na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) ziweke sera madhubuti za kulinda uhuru wa kitaaluma na usalama wa ajira kwa wanazuoni na imezitaka mamlaka kuacha tabia ya kukamata raia kabla ya kukamilisha upelelezi katika makosa makubwa yasiyo na dhamana.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tanzania Bara, John Heche amehoji kuhusu nguvu ya Baraza la Mawaziri katika kuamua mambo ya msingi ya nchi kwa ajili ya ustawi wa wananchi.
Akizungumza siku ya Jumatano Julai 29, 2026 kwenye Mkutano Mkuu Maalumu wa CHADEMA Mkoa wa Mwanza uliofanyika katika soko la Mbao, Kata ya Igoma Jijini Mwanza, Heche amechambua kauli ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Emmanuel Nchimbi, inayowataka Watanzania "kupambana" ili kupata katiba mpya kwa sababu katiba ya sasa inampa mtu mmoja ambaye ni Rais mamlaka makubwa.
Heche amelichambua Baraza la Mawaziri akisema kuwa Rais hatajwi kama mjumbe wa baraza hilo, lakini ndiye anayehudhuria na kuongoza mikutano yote kama mwenyekiti na kuwa na maamuzi ya mwisho. Heche amehoji mantiki ya mtu kuwa mwenyekiti wa kikao ambacho yeye si mjumbe na kusema hali hii inatengeneza “Mungu mtu".
Ameendelea kusema kuwa Baraza la Mawaziri ni chombo cha juu cha uamuzi kuhusu rasilimali za nchi, lakini mawaziri wana jukumu la kumshauri tu Rais, na Rais halazimiki kuchukua ushauri wao jambo ambalo amesema ni hatari kwa nchi, hivyo akawataka Watanzania waendelee kudai kupatikana kwa Katiba Mpya mapema iwezekanavyo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Ikiwa imepita siku moja tangu Jeshi la Polisi lifungue milango ya kupokea taarifa za nia ya kufanya mikutano ya hadhara kutoka kwa vyama vya siasa na wadau wengine kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zilizopo kutokanana hali ya usalama kuelezwa kuendelea kuwa shwari, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, John Heche amewataka viongozi wa chama hicho mkoa wa Simiyu kuandaa mkutano mkubwa wa hadhara ndani ya siku chache zijazo.
Akizungumza leo kwenye Mkutano Mkuu Maalumu wa CHADEMA Mkoa wa Simiyu uliofanyika Bariadi Mjini, Heche amedai kuwa kurejeshwa kwa ruhusa ya kufanya mikutano hiyo siyo kwasababu ya matakwa ya Jeshi la Polisi bali ni kwa mujibu wa sheria na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kauli ya Heche na Jeshi la Polisi zinakuja mwezi mmoja tangu serikali kupitia Waziri wa Mambo ya Ndani, Patrobas Katambi kutangaza kusitisha kwa muda mikutano yote ya hadhara ya vyama vya siasa nchini, bila kujali chama husika, ikieleza kuwa hatua hiyo inalenga kuimarisha usalama wa wananchi.
Taarifa iliyotolewa Julai 29, 2026 na Jeshi la Polisi na kusainiwa na msemaji wake, David Misime imesema kipindi ambacho kulikuwa na taarifa za mipango ya vitendo vya kihalifu, lilikuwa likipokea taarifa kutoka vyama mbalimbali vya siasa na baadhi ya wabunge kuhusu nia ya kufanya mikutano katika maeneo yao.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa kutokana na mazingira ya kiusalama yaliyokuwepo wakati huo, viongozi hao waliitwa na kufanya nao mazungumzo ili kuwashauri kuahirisha baadhi ya mikutano hiyo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Katika andiko lake lililochapishwa kwenye wavuti ya taasisi ya kiuchunguzi ya CODESRIA, mwanasheria nguli na msomi mashuhuri wa sheria nchini Tanzania, Prof. Issa Shivji ameonesha wasiwasi mkubwa juu ya kile alichokiita msururu wa ukandamizaji na ukiukaji wa uhuru wa kifikra, akitolea mfano kukamatwa na kushitakiwa kwa mhadhiri msaidizi wa Sayansi ya Siasa na Utawala wa Umma wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Melkisedeki Kitunzi Kaijage.
Prof. Shivji anafafanua kuwa Kaijage aliripoti kituo cha polisi Julai 8, 2026, akiambatana na mwanasheria wa Chama cha Wanataaluma UDOM (UDOMASA), kufuatia tuhuma za kuchochea maandamano ya siku ya mapumziko ya Saba Saba (Julai 7). Hata hivyo, baada ya kukaa mahabusu kwa siku 17 kinyume cha sharia na kufuatia amri ya Mahakama Kuu ya Julai 21 iliyoagiza apewe dhamana, Polisi tarehe 23 Julai walimfikisha Mhadhiri huyo Mahakama ya Hakimu Mkazi akituhumiwa kwa kosa la Ugaidi, kosa ambalo halina dhamana.
Hati ya mashtaka inamdai Kaijage kutishia kuchoma moto majengo ya umma na nyumba za polisi Julai 3, 2026. Prof. Shivji amekosoa hati hiyo akisema imekosa maelezo ya msingi kama vile eneo halisi vitisho vilipotolewa, chombo kilichotumika, na hadhira iliyokuwepo jambo linaloonesha matumizi ya mfumo wa mashtaka wa "kuchukua na kubandika" (cut-and-paste template) wenye lengo la kutisha wanataaluma na kupunguza uwezo wa vyuo vikuu kuwa vituo vya fikra tunduizi.
"Maelezo ya kosa katika hati ya mashtaka yanasomeka hivi: Melkisedek Kitunzi Kaijage, mnamo tarehe 03 mwezi Julai 2026 katika eneo la Chuo Kikuu cha Dodoma ndani ya Mkoa wa Dodoma, alitenda kitendo cha kigaidi, yaani; kutishia kuchoma moto majengo ya umma na makazi ya askari polisi ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiwa na nia ya kuwatisha kwa kiasi kikubwa wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mashtaka hayo yana tarehe ya Julai 22 yaani, siku moja baada ya uamuzi wa Mahakama Kuu. Maelezo ya kosa hilo yanasomeka kana kwamba yamenukuliwa na kubandikwa tu (cut and pasted) kutoka kwenye muundo uleule wa siku zote. Yanakosa....soma zaidi katika tovuti ya jambo.co.tz kupitia kiungo jambo.co.tz/prof-shivji-aonesha-wasiwasi-mashitaka-kwa-wa… -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katibu Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Ado Shaibu, amesema kuwa maridhiano ya kweli hayawezi kupatikana bila kuwepo kwa ukweli na uwajibikaji kuhusu matukio ya kisiasa yaliyotokea kabla, wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.
Ado ametoa kauli hiyo leo, Julai 29, 2026, alipokuwa akizungumza na Kamati ya Uongozi ya ACT Wazalendo Mkoa, Kamati za Uongozi za Majimbo pamoja na Kamati za Ngome ya Vijana.
Ado amedai kuwa uchaguzi wa mwaka 2025 umeacha idadi kubwa ya wafungwa wa kisiasa, huku akieleza kuwa uwajibikaji unapaswa kufuata kwa kuwaachia huru wote wanaokabiliwa na kesi hizo za kisiasa, akisema kuwa kuzungumzia maridhiano wakati watu bado wanashikiliwa kwa kesi hizo hakutaweza kuleta maridhiano ya dhati.
Ado amesema ACT Wazalendo inataka maridhiano yanayojengwa juu ya ukweli na uwajibikaji badala ya maneno matupu.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tanzania Bara, John Heche amewatolea uvivu watu wanaomtukana au kumchafua kwenye mitandao ya kijamii akisema kuwa yeye ni kama dhahabu isiyopoteza thamani yake hata ikitupwa kwenye kinyesi.
Akizungumza siku ya Jumatano kwenye Mkutano Mkuu Maalumu wa CHADEMA Mkoa wa Mwanza uliofanyika katika soko la Mbao, Kata ya Igoma Jijini Mwanza, Heche amebainisha kuwa CHADEMA na yeye binafsi hawawezi kuchafuliwa thamani yao kwa maneno ya kashfa kwani wako imara na wamevuka kiwango cha kuuawa na mtu yeyote.
Badala ya kujibizana nao, Heche ameanza kuchukua hatua za kisheria kwa kufungua kesi za kuchafuliwa jina, akitolea mfano wa kijana mmoja aliyekuwa akimtukana ambaye sasa analia na kumwita "baba" baada ya kuanza mchakato wa kisheriaThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeendelea na msimamo wake wa kupinga vikali wito wa maridhiano unaotolewa na serikali na baadhi ya wadaku kikieleza kuwa maridhiano yatakubalika ikiwa tu serikali itakiri makosa kutokana na yale yaliyotokea Oktoba 29, 2025 na kumuachia Mwenyekiti wa chama hicho taifa, Tundu Lissu.
Akizungumza siku ya Jumatano Julai 29, 2026 kwenye Mkutano Mkuu Maalumu wa CHADEMA Mkoa wa Mwanza uliofanyika katika soko la Mbao, Kata ya Igoma Jijini Mwanza, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tanzania Bara, John Heche amesema,
“Sisi hatutakubali, na wala tukisema hivi, mtu asiseme kwamba sisi sio watu tunaotaka majadiliano, kuna watu wameomba majadiliano kwenye nchi hii kuliko CHADEMA? ‘We were the first’ tangu zama za Magufuli kuwaambia tunaenda njia mbaya, mkishafika huko mtashindwa kurudi, tuokoe hii gari kabla haijadumbukia mtoni wakasema na iende mtoni, Sasa gari iko mtoni wanatuambia CHADEMA tuitoe humu”.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tanzania Bara, John Heche ameeleza kuwa ana taarifa za ndani za uhakika kuwa kuna mpango wa wa yeye kukamatwa.
Akizungumza siku ya Jumatano kwenye Mkutano Mkuu Maalumu wa CHADEMA Mkoa wa Mwanza uliofanyika katika soko la Mbao, Kata ya Igoma Jijini Mwanza, Heche amesisitiza kuwa yeye ni mtu huru anayefanya kazi kwa mujibu wa sheria na hatishiki na hatua hizo, akisema, "Mimi nimezaliwa mara moja, nitaishi mara moja na nitakufa mara moja"
Aidha ameeleza kuwa kuna gari aina ya Toyota Land Cruiser (hardtop) nyeupe iliyofika nyumbani kwake asubuhi ikiwa na namba za usajili T 318 EQJ. Baada ya kufanya uchunguzi na kupiga picha, imebainika kuwa namba hizo ni za kughushi kwani zimesajiliwa kwa ajili ya katapila la kutengenezea barabara na siyo gari hilo
Heche anawataka Watanzania wasikubali kunyimwa amani wala kutekwa katika mazingira yasiyoeleweka, huku yeye mwenyewe akisisitiza kuwa hawezi kukimbia na kuwasihi raia wasikubali kumuacha achukuliwe katika mazingira ya kutatanisha, akisema kuwa ni lazima kukataa kuishi kwa hofu katika nchi yao.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katika kuboresha mazingira na kurahisisha kutoa huduma kwa wawekezaji Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi nchini @InvestTanzania imeingia makubaliano ya kushirikiana na Umoja wa Mawakili Vijana Ndani ya Chama cha Wanasheria Tanganyika @TLSAYL kwa lengo la kushirikiana kutoa huduma.
Akizungumza leo Julai 29, 2026 mara baada ya kusaini makubaliano hayo Mkurugenzi Mkuu wa TISEZA Gilead Teri amesema hatua hiyo muhimu inalenga kuwawezesha Mawakili vijana kutambuliwa kama watoa huduma katika mamlaka hiyo.
Teri ameeleza kuwa ni dhamira ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwainua vijana kupitia fursa mbalimbali za kiuchumi kwa kuwafanya kuwa sehemu ya maendeleo ya taifa kuelekea kutekeleza Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050.
Naye Mwenyekiti wa TLS-AYL Wakili Emmanuel Ukashu amesema makubaliano ni ya miaka mitatu na yameweka unafuu kwa Mawakili Vijana kwani kwa sasa hawatohitajika kulipia gharama yoyote ili kuwa watoa huduma kupitia TISEZA.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (NEC), imefanya mabadiliko makubwa katika safu yake ya uongozi kwa kumteua aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora na Mbunge wa zamani wa Siha, Aggrey Mwanri, kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Tanzania Bara. Katika nafasi hiyo, Mwanri anachukua nafasi ya John Mongella.
Mabadiliko hayo yamefanyika Julai 29, 2026, katika kikao cha NEC kilichoketi visiwani Zanzibar chini ya Uwenyekiti wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Katika kikao hicho, NEC pia imemteua Abdi Mohamed Abdi kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM- Zanzibar, akichukua nafasi ya Dkt. Mohammed Said Mohammed (maarufu kama Dimwa). Kabla ya uteuzi huo, Abdi alikuwa akihudumu kama Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Zanzibar.
Katika safu ya Wakuu wa Idara za Halmashauri Kuu ya Taifa, mabadiliko yaliyofanyika ni pamoja na Idara ya Oganaizesheni ambapo Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paul Chacha, ameteuliwa kuwa Katibu wa Oganaizesheni wa CCM Taifa, akichukua nafasi ya Issa Haji Gavu, ambaye pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Chwaka, Zanzibar.
Katika Idara ya Uchumi na Fedha, aliyewahi kuwa Waziri wa Fedha na Mipango katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Jamal Kassim Ali, ameteuliwa kuwa Katibu wa NEC (Uchumi na Fedha), akichukua nafasi ya Joshua Mirumbe.
Taarifa kamili ya mabadiliko hayo ya uongozi imetangazwa rasmi kwa umma na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Kenani Kihongosi. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Jeshi la Polisi Tanzania limesema hali ya usalama nchini ni shwari na litaendelea kupokea taarifa za nia ya kufanya mikutano ya hadhara pamoja na vikao kutoka kwa vyama vya siasa na wadau wengine, huku likiwataka waandaaji kuwasilisha taarifa hizo kwa Wakuu wa Polisi wa Wilaya (OCD) kwa mujibu wa sheria.
Katika taarifa kwa umma aliyoitoa Julai 29, 2026, Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) David Misime, ameeleza kuwa uamuzi huo umechukuliwa baada ya usalama kurejea kikamilifu kutokana na hatua madhubuti zilizochukuliwa na vyombo vya ulinzi na usalama kudhibiti mipango ya watu waliokuwa wakihamasisha vitendo vya kihalifu.
DCP Misime amefafanua kuwa katika kipindi cha nyuma, Jeshi la Polisi lilikuwa likiwashauri waandaaji kuahirisha mikutano hiyo kutokana na viashiria vya kiusalama vilivyokuwepo wakati huo.
Msemaji huyo wa Polisi amewashukuru Watanzania kwa ushirikiano waliouonesha kwa kuzingatia maelekezo ya vyombo vya ulinzi na usalama, pamoja na kukataa kujiingiza kwenye vitendo vya kihalifu vilivyokuwa vikipangwa na kuhamasishwa na baadhi ya watu.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Rais wa Marekani Donald Trump, amesema kwamba Marekani itaishambulia Iran kwa nguvu ili kulipiza kisasi kufuatia mashambulizi ya hivi karibuni ya Tehran dhidi ya majeshi ya Marekani nchini Jordan.
Trump ametoa kauli hiyo Julai 29, 2026 alipokuwa akizungumza na kituo cha habari cha Fox News nchini Marekani. Pia Rais huyo amesema mashambulizi ya Marekani ya usiku kucha dhidi ya wanamgambo wanaoungwa mkono na Iran nchini Iraq yalikuwa yamefanyika kwa uratibu na serikali ya Iraq.
"Tutaendelea kuwapiga kwa nguvu, watapokea kipigo." Amesema Trump katika mazungumzo hayo.
Kuhusu mazungumzo na Iran kwa ajili ya makubaliano ya amani, Trump amesema "tutawaacha waendelee kuzungumza."
Mapema wiki hii, Trump alisema Marekani ilikuwa na mazungumzo mazuri na Iran na kwamba kuna nafasi nzuri ya kufikia makubaliano, lakini alionya kuwa operesheni ya kijeshi inaweza kuanza tena ikiwa mazungumzo hayo yatashindikana. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
📍MWANZA - Viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya za Magu na Kwimba wamekanusha taarifa zilizotolewa na baadhi ya watu waliojitambulisha kuwa wanachama na viongozi wa chama hicho kutoka Jimbo la Sumve, Kwimba, waliodai kuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Heche anapaswa kupisha uchunguzi kuhusu tuhuma zinazosambaa mitandaoni.
Akizungumza Julai 29, 2026 katika Mkutano Mkuu Maalumu wa CHADEMA Mkoa wa Mwanza unaofanyika katika Soko la Mbao, Kata ya Igoma, Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Magu, Peter Malima amesema watu hao si viongozi wa chama hicho kama walivyojitambulisha, hivyo wananchi wanapaswa kupuuza taarifa zao.
Kauli hiyo imeungwa mkono na Katibu wa CHADEMA Wilaya ya Kwimba, Samson Masalu, ambaye amesema baadhi ya watu hao hawana nafasi yoyote ya uongozi ndani ya chama hicho, huku wengine wakidaiwa kuondolewa kutokana na utovu wa nidhamu.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam leo, Jumatano tarehe 29/07/2026 imewaachia huru wanafunzi 18 wa Vyuo Vikuu mbalimbali Nchini wakiongozwa na Frank Benjamin Kayamba waliokuwa wanatuhumiwa kughushi nyaraka mbalimbali ili wanufaike na mikopo inayotolewa na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu, kinyume na tararibu
Mahakama kupitia Hakimu Mkazi Mkuu Romuli Mbuya, imefikia uamuzi huo baada ya kukubaliana na mapingamizi yaliyowekwa na Wakili wa utetezi Peter Madeleka aliyeieleza Mahakama kuwa hati ya mashaka inakosa nguvu za kisheria za kuendelea kubaki Mahakamani kutokana na kwamba upande wa Jamhuri haujaambatanisha maelezo ya mashahidi kwenye hati hiyo kama kanuni za msingi zinavyoelekeza
Awali akiwa Mahakamani hapo, Wakili wa Serikali Cuthbert Mbilinyi aliieleza Mahakama kuwa kesi hiyo Na. 13088/2026 ambayo upelelezi wake ulikuwa umekamilika imekuja kwaajili ya usikilizwaji wa hoja za awali, na kwamba upande wa Jamhuri ulikuwa umeshakamilisha kuweka kwenye mtandao wa Mahakama taarifa zote hitajika.
Hata hivyo, muda mfupi baada ya Mahakama kuwaachia huru wanafunzi hao, wakiwa wanatoka Mahakamani hapo walikamatwa tena na maafisa wa Jeshi la Polisi, na taarifa tulizonazo ni kwamba wanafunzi hao watapelekwa Kituo cha Polisi cha Kati (Central Police Station) kwaajili ya taratibu nyingine za kisheria, kwa sasa wakiwa wamehifadhiwa kwa muda kwenye mahabusu ya Mahakama
Akizungumzia hilo, Wakili Madeleka @PMadeleka amesema kwa sasa anafuatilia kujuwa wateja wake (yaani wanafunzi hao) wamekamatwa kwa kosa lipi, ili ajuwe hatua za kuchukua.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Uchambuzi wa kisiasa kutoka kwa mchambuzi wa masuala ya siasa nchini, Luqman Maloto, umeibua maswali mazito kuhusu dhamira na mbinu za kiuchambuzi zilizotumiwa na Makamu wa Rais wa Tanzania, Dkt. Emmanuel Nchimbi, kufuatia hotuba yake iliyotolewa Julai 24, 2026, kwenye Mkutano Mkuu wa 15 wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC).
Katika hotuba hiyo, Dkt. Nchimbi aliwataka Watanzania, hususan wanaharakati, "kukomaa" na "kupambana" ili kupata Katiba Mpya kabla ya fursa iliyopo kumpoteza Rais Samia Suluhu Hassan ambaye kwa mujibu wa Dkt. Nchimbi, ana utashi wa dhati wa kukamilisha mchakato huo.
Hata hivyo, Maloto katika andiko lake lenye kichwa "Kumwelewa Nchimbi inatakiwa ung’amue alikoficha nukta," anabainisha kuwa Makamu wa Rais amechagua mtindo wa "kuangusha hoja mojamoja" kama bendi maarufu ya African Stars (Twanga Pepeta), huku akitumia mbinu ya kisaikolojia na kisiasa inayojulikana kama "Manipulative Underspecification" yaani kuzungumza kwa namna inayoiacha hadhira kwenye njia panda na kila mtu akitafsiri ujumbe kulingana na hisia na maslahi yake.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Taasisi ya Flaviana Matata @FMFound imeendelea kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuboresha sekta za elimu na afya, kutokana na hatua yake ya kukamilisha na kukabidhi mradi wa miundombinu ya usafi na afya ya uzazi katika Shule ya Sekondari Busulwa mkoani Shinyanga. Mradi huo uliotekelezwa na taasisi hiyo kwa ufadhili wa shirika la Diamonds Do Good ulikabidhiwa rasmi Julai 28, 2026 na Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Bi. Flaviana Matata.
Akizungumza katika hafla hiyo iliyohudhuriwa na viongozi wa Serikali, walimu, wazazi na wanafunzi, Naibu Mkurugenzi wa Taasisi ya Flaviana Matata, Lineth Masala ameeleza kuwa lengo kuu la mradi huo ni kuondoa vikwazo vinavyowakabili watoto wa kike shuleni, ikiwamo changamoto za afya ya uzazi na hedhi salama.
“Katika shule 14 ambazo tunafanya nazo kazi mkoani hapa shule yenu ni moja ya shule ambayo tulianza kufanya nao kazi mwaka 2024, tulianza na kuelimisha wanafunzi si tunakumbuka mada tulizojifunza? lakini pia tuliweza kufanya mafunzo au maongezi na wazazi? Kutokana na hilo tulibaini ya kwamba kuna changamoto ya vyoo kwa hiyo tukaona kati ya shule ambazo tunatamani kuja kufanya nazo kazi hapo mbeleni ni shule ya Busulwa”, amesema Masala.
Akipokea mradi huo, Afisa Elimu Sekondari wa Manispaa ya Shinyanga, Richard Makoye ameishukuru taasisi hiyo na kueleza kuwa vyoo vya zamani vilivyokuwa vikitumiwa na wasichana sasa vitatumiwa na wanafunzi wa kiume ili kupunguza msongamano na kuzuia mlipuko wa magonjwa.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo, Flaviana Matata @FlavianaMatata amesisitiza umuhimu wa kuweka miundombinu jumuishi inayozingatia wanafunzi wenye ulemavu au mahitaji maalum.
"Ujenzi wa vyoo shuleni lazima uzingatie usawa na ujumuishi. Huwezi kujua mwaka unaofuata anaweza kupatikana mwanafunzi mwenye mahitaji maalum”, amesema Matata akitoa mfano alivyowezesha kupatikana kwa kitimwendo cha mwanafunzi mlemavu shuleni hapo ambacho kinamsaidia hata kwenda chooni pasina kutegemea msaada wa wanafunzi wengine.
Nao wanafunzi wa Shule ya Sekondari Busulwa wameeleza kuwa mradi huo utasaidia kupunguza utoro shuleni. Wameeleza kuwa awali, baadhi ya wasichana walilazimika kukosa masomo kwa siku 3 hadi 5 kila mwezi wakati wa hedhi kwa kukosa sehemu salama na rafiki ya kujisitiri, lakini uwepo wa vyoo hivyo na maji safi utawawezesha kuhudhuria masomo bila kukosa vipindi.
Miundombinu iliyokabidhiwa shuleni hapo inajumuisha matundu 13 ya vyoo vya wanafunzi wa kike, eneo la kunawia mikono, chumba maalum kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalum, chumba cha wasichana kujisitiri wakati wa hedhi, pamoja na tanuri la kuchomea taka (incinerator) hasa taulo za kike zilizotumika.
Kupitia mradi huo, zaidi ya wanafunzi wa kike 502 wa shule hiyo watanufaika kila mwaka na huduma ya maji safi na salama pamoja na mazingira bora ya usafi hatua inayotarajiwa kuongeza mahudhurio darasani na kuboresha kiwango cha ufaulu.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, ametoa ufafanuzi kutokana na kile alichokieleza kuwa ni upotoshaji unaoendelea kwenye mitandao ya kijamii, huku akikumbusha kuhusu Sheria ya Kuzuia Ugaidi inayokataza mtu yeyote kujishughulisha, kutishia, au kutenda jambo linalokiuka sheria na kuvunja haki za wengine.
Akizungumza leo, Julai 29, 2026, visiwani Zanzibar, Waziri Katambi amewahakikishia wananchi kuwa nchi ipo salama na kuwataka waendelee na shughuli zao za maendeleo, akisisitiza kuwa Serikali kupitia vyombo vya ulinzi na usalama inaendelea na wajibu wake wa kulinda raia na mali zao.
"Serikali kupitia vyombo vya ulinzi na usalama inao wajibu wa msingi wa kulinda haki za raia na mali zao kwa mujibu wa Katiba na sheria mbalimbali. Tunaheshimu utawala wa sheria; sisi ni nchi inayoheshimu demokrasia pamoja na uhuru wa mahakama," amesema Waziri Katambi.
Waziri Katambi ameongeza kuwa hakuna mtu aliyetukuka au aliye juu ya sheria, wala hakuna kinga dhidi ya makosa ya jinai, hivyo mtuhumiwa yeyote atakayekamatwa atafikishwa kwenye vyombo vya usalama na hatimaye kufikishwa mahakamani pamoja na ushahidi au vielelezo vilivyokamatwa.
Akiweka ufafanuzi kuhusu viashiria vya ugaidi, Waziri Katambi ameeleza, “Tanzania hatuna ugaidi kwa maana ya matukio makubwa, lakini vinaweza kuwepo viashiria vya matendo ya kigaidi. Ugaidi una vipengele mbalimbali vya makosa (elements of offense), na unajumuisha kila aina ya tendo ikiwemo kutishia, kupanga, kuratibu, kula njama, kutekeleza, au kuandaa zana zinazoweza kuleta madhara na kuzuia shughuli za kiuchumi”.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mratibu wa Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Wakili, Onesmo Olengurumwa, amesema kupitia andiko lake kwamba, aliwasilisha hoja muhimu tano kwa makamu wa Rais, Dkt. Emmanuel Nchimbi, zinazosisitiza umuhimu wa kuimarisha ulinzi wa Watetezi wa Haki za Binadamu, kushughulikia masuala ya usalama na matukio ya utekaji na kutoweka kwa watu, kuendeleza maridhiano ya kitaifa, kufufua mchakato wa Katiba Mpya na kuimarisha uhimilivu wa kifedha wa sekta ya haki za binadamu kupitia uhamasishaji wa rasilimali za ndani.
Olengurumwa amebainisha hayo Julai 28, 2026 kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Facebook, ikiwa ni hoja alizowasilisha Julai 24, 2026 wakati wa Mkutano Mkuu wa 15 wa THRDC pamoja na uzinduzi wa Tanzania Human Rights Grant Project uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Mlimani City, Dar es Salaam.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Dkt. Ayub Rioba Chacha, amesema ili kujenga utamaduni wa jamii kufuata mifumo iliyowekwa kikatiba ni lazima kuwepo na udikteta ambao utasimamia misingi ya katiba badala ya kuruhusu demokrasia ya vyama kubadilishana madaraka.
Dkt. Rioba ameeleza hayo katika kipindi cha One on One cha Wasafi TV, akisisitiza kuwa namna hiyo hujenga watu wenye nidhamu ya kuhakikisha mifumo iloyopo kikatiba haichezewi.
"Unajengaje utamaduni wa kuhakikisha watu wanaheshimu ile mifumo, lazima uwe na 'diktetaship', sio demokrasia hii ya chama hiki kiingie, chagua hiki kiingie, hapana" amesema Dkt. Rioba.
Ametoa mfano akirejea nchini Rwanda akisema licha ya kiongozi wa taifa hilo la Afrika Mashariki kukaa madarakani kwa muda mrefu, hali iliyosababisha baadhi kumtazama kama dikteta, lakini jamii ya taifa hilo inafuata misingi iliyowekwa.
"Nitakupa mfano, jirani zetu hapa kuna mtu anaitwa Kagame, wao wanaita dikteta lakini sisi hatuwezi kuwa na jina kama hilo kwa sababu watawala wetu wa Afrika kabla hawajakuja wakoloni na kukaa madarakani...ninachosema kwa pointi yangu, tangu alivyoshika madaraka Kagame, aliingia serikalini tokea 94 hiyo hiyo, baadaye akaja akawa Rais, ni miaka mingapi imepita? 32, sasa fikiria leo umezaliwa Rwanda haujawahi kuona mtu anatupa uchafu barabarani wewe unafikiri utatupa?" ameeleza Dkt. Rioba. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
“Hakuna mtu ambaye anaweza kulengwa wala hakuna kusudio lolote linalokusudia kumlenga mtu au taasisi na kama ingekua kuna lengo maalumu mbona kuna wanataaluma wengi wako huru, kwahiyo tusitetee vitu ambavyo hatuvijui na hasa kwenye mashauri ambayo yako mahakamani kwa sasa hatuna ujasiri wa kuyahoji”, - Katambi
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi akitoa ufafanuzi Julai 29, 2026 Visiwani Zanzibar baada ya kuwepo kwa malalamiko ya kukamatwa kwa watuhumiwa 130 wa makosa mbalimbali nchini.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katibu wa Siasa na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Arusha, Saipulan Ramsey amesema moja ya maamuzi yaliyomuumiza zaidi ni marufuku ya mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa, akidai hatua hiyo imekiathiri hata chama tawala kushindwa kuendelea kuwaeleza wananchi utekelezaji wa ilani na sera zake.
Akizungumza na waandishi wa habari Julai 28, 2026 jijini Arusha, Saipulan amesema CCM pia ilikuwa imekumbuka utaratibu wa mikutano ya hadhara na haikupaswa kunyimwa fursa hiyo kutokana na makosa yanayodaiwa kufanywa na baadhi ya watu au makundi mengine.
Akisisitiza msimamo wake, amesema, "Hakuna kitu ambacho mimi binafsi kimeniumiza kama kuzuiliwa kwa mikutano ya hadhara. Kuzuiliwa kwa mikutano ya hadhara kunakinyanyasa Chama Cha Mapinduzi, kwa sababu kunatuzuia kuwafikia wananchi na kuendelea kuwaeleza yale tuliyowaahidi na namna yanavyotekelezwa."
Ikumbukwe Juni 26, 2026 Serikali kupitia Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi ilitangaza kusitishwa kwa mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa, ikieleza ni kwa sababu za kiusalama kufuatia kuwepo kwa viashiria vya maandamano yaliyokuwa yamepangwa kufanyika Julai 7, 2026. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, John Heche, ameihoji Serikali ya Tanzania akitaka itaje wazi ni nani anayekwamisha mchakato wa Katiba Mpya, kutokana na kauli ya Makamu wa Rais, Dkt. Emmanuel Nchimbi, iliyowataka Watanzania ‘kupambana’ ili kuipata.
Akizungumza Julai 28, 2026, alipowatembelea na kuzungumza na wafanyabiashara katika Soko la Samaki la Kimataifa la Kirumba Mwaloni mkoani Mwanza, Heche amehoji mantiki ya kauli hiyo iwapo viongozi wakuu wa nchi tayari wanaunga mkono mchakato huo.
"Kutaka Katiba Mpya siyo kosa. Mmemsikia hata Nchimbi alisema tukomae Katiba ije, lakini anatumia lugha ya kutuchanganya; anasema Rais anataka Katiba na yeye pia anataka Katiba. Sasa inakwamia wapi ambapo anataka sisi tukomae?" amesema Heche.
Kauli hiyo ya Heche inakuja kutokana na hotuba iliyotolewa na Dkt. Nchimbi mnamo Julai 24, 2026, wakati akifungua Mkutano Mkuu wa 15 wa Mwaka wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC).
Katika mkutano huo, Dkt. Nchimbi alisikika akisema: "Nikiambiwa kuna jambo kama Makamu wa Rais niwaambie Watanzania, nitasema pambaneni mpate Katiba Mpya- Katiba ambayo ina makubaliano ya wadau wote, Katiba yenye muafaka katika taifa, Katiba ambayo kila Mtanzania popote alipo atajisikia fahari kujitambulisha, na Katiba inayojali maisha."This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) kupitia kwa Kaimu Katibu Mkuu wake, Benson Kigaila kimesema kitaendelea kudai haki na katiba mpya kwa kukaa kwenye mezani ya maridhiano.
Kigaila amesema hayo Julai 28, 2026 wilayani Uvinza mkoani Kigoma wakati akizungumza na wanachama na wananchi wa Jimbo la Kigoma Kusini ikiwa ni mwendelezo wa operesheni ya chama hicho ya Tujenge Pamoja Tanzania.
Ameeleza kuwa kupitia maridhiano kutakuwa na fursa kubwa kwa Watanzania kujadili na kutoa maoni kwa pamoja juu ya matatizo yao ambayo wanatamani kufanyiwa marekebisho kwenye katiba mpya, akisisitiza kuwa katiba ya mwaka 1977 imepitwa na wakati na haiwezi tena kubeba hali halisi ya maisha ya Watanzania wa sasa.
"Sisi CHAUMMA tutasema Katiba ya mwaka 1977 haifai tena leo kwa sababu imepitwa na wakati. Ni sawa na suruali ya 'Pepo' ya miaka ya nyuma leo huwezi kuivaa! Tunahitaji Katiba mpya iliyoandikwa kwa maoni ya leo ya Watanzania, itakayoweka muafaka wa kitaifa na kumaliza migogoro ya ardhi, matatizo ya kisiasa na ukosefu wa ajira kwa vijana," amesema Kigaila.
Ziara hiyo mkoani Kigoma pia inahusisha kuimarisha miundombinu ya chama hicho mashinani pamoja na kukusanya maoni ya wanachama kuhusu marekebisho ya Katiba ya CHAUMMA. -
Jambo TV
@Jambotv_
Viongozi wawili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoani Shinyanga wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Shinyanga, Jumanne ya tarehe 28 Julai, 2026, na kusomewa mashtaka yanayohusiana na matendo ya kigaidi.
Viongozi hao ni Alfred Masanja, ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la CHADEMA (BAVICHA) Wilaya ya Shinyanga, pamoja na Hamisi Ngunila, Mwenyekiti wa CHADEMA Jimbo la Shinyanga Mjini.
Katika Shauri Namba 16506 la Mwaka 2026, Jamhuri imewafungulia mashtaka Masanja na Ngunila ya kula njama za kutenda kosa la kigaidi, wakishitakiwa pamoja na Godwine Laurent, Johnson Paul Michael, na Joseph Isack Ongoro.
Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, washtakiwa hao wanatuhumiwa kuwa, kati ya tarehe 15 Juni, 2026 na tarehe 10 Julai, 2026, katika maeneo mbalimbali mkoani Shinyanga walikula njama za kufanya kitendo cha kigaidi kwa kupanga na kuhamasisha maandamano yasiyo halali jambo ambalo upande wa Jamhuri unadai lilikuwa na lengo la kuhatarisha usalama wa nchi.
Mashtaka hayo yamefunguliwa chini ya Vifungu vya 4(1), 3(d), na 31(c) vya Sheria ya Kuzuia Ugaidi (Sura ya 19, Mapitio ya Mwaka 2023), vikisomwa pamoja na Aya ya 24 ya Jedwali la Kwanza na Vifungu vya 58(1) na 61(2) vya Sheria ya Uhujumu Uchumi na Uhalifu wa Kupangwa (Sura ya 200, Mapitio ya Mwaka 2023).
Akizungumzia hatua hiyo, Katibu wa Kamati ya Sheria na Haki za Binadamu wa CHADEMA Kanda ya Serengeti, Frank Joshua, ameeleza kuwa kufikishwa mahakamani kwa viongozi hao wawili kunakamilisha idadi ya viongozi na wanachama 17 wa chama hicho mkoani Shinyanga wanaoshikiliwa gerezani wakikabiliwa na tuhuma hizo.
Mnamo Ijumaa ya tarehe 24 Julai, 2026, washtakiwa wengine walisomewa mashtaka yao, lakini Alfred Masanja alirudishwa mahabusu baada ya kubainika kuwa hati yake ya mashtaka ilikuwa na makosa ya kiufundi.
Kwa upande wa Hamisi Ngunila, jina lake lilikuwepo kwenye hati ya mashtaka siku hiyo lakini hakuwepo mahakamani, kabla ya kujisalimisha kituo cha polisi tarehe 27 Julai, 2026, ambapo alishikiliwa hadi alipofikishwa kizimbani leo.
Baada ya kusomewa mashtaka yao, washtakiwa wote wamerudishwa katika Gereza la Wilaya ya Shinyanga kusubiri taratibu na hatua nyingine za kisheria. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI:
Tetemeko la ardhi la ukubwa wa 7.1 kwa kipimo cha Richter limekumba eneo la Kyushu nchini Japan na kuzua tahadhari ya kiusalama iliyosababisha kusitishwa kwa huduma zote za usafiri wa reli katika eneo hilo.
Tetemeko hilo limetokea leo Jumanne, Julai 28, 2026. Idara ya hali ya hewa ya Japan imeripoti kuwa mtikisiko wa tetemeko hilo umefikia Kiwango cha 7 katika kipimo cha nguvu ya mtikisiko wa ardhi nchini humo.
Kufuatia tukio hilo, idara hiyo imetoa tahadhari ya tsunami kwa maeneo ya pwani, lakini imesema itaondoa tahadhari hiyo ifikapo jioni ya leo baada ya hali ya bahari kuonekana kutulia.
Takribani watu 50 wameripotiwa kujeruhiwa, huku moto ukionekana katika baadhi ya nyumba za makazi katika Mji wa Uki. -
Jambo TV
@Jambotv_
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, John Heche, leo Julai 28, 2026 ametembelea Mwalo wa Kirumba uliopo Wilaya ya Ilemela, Mkoa wa Mwanza, na kuwahamasisha wananchi pamoja na wanachama kuendelea kuchangia Kampeni ya "Tonetone".
Kuelekea Mkutano wa Baraza Kuu la CHADEMA uliopangwa kufanyika Septemba 15, 2026, kampeni hiyo ya Tonetone imegeuka kuwa mwelekeo wa marathoni yenye lengo la kukusanya Shilingi Milioni 334 ili kugharamia kikao hicho kikubwa cha kimaamuzi cha kitaifa.
Chama hicho kimelenga kukusanya kiasi hicho cha Shilingi Milioni 334, ambapo hadi kufikia asubuhi ya leo, Julai 28, 2026, jumla ya Shilingi Milioni 239.5 tayari zimeshakusanywa. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkoa wa Tanga umetajwa kuwa miongoni mwa mikoa inayoongoza nchini kwa kuwa na idadi kubwa ya wagonjwa wa homa ya ini, hali inayozua wasiwasi na kuibua wito kwa wananchi kujitokeza kupima afya zao mapema pamoja na kuchukua hatua za kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huo.
Hayo yamesemwa na Dkt. Penina Sikira, kutoka Hospitali ya Siha Polyclinic, leo Julai 28, wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Homa ya Ini Duniani.
Amesema Mkoa wa Tanga ni miongoni mwa mikoa inayoongoza nchini kwa kuwa na idadi kubwa ya wagonjwa wa homa ya ini, huku akiwahimiza wananchi kujitokeza kupima afya zao mapema, kupata chanjo pale inapohitajika na kuchukua hatua stahiki za kujikinga dhidi ya ugonjwa huo.
Mbali na hayo, Dkt. Penina amesema miongoni mwa njia zinazochangia maambukizi ya ugonjwa wa homa ya ini ni kujamiiana bila kutumia kinga, kushindwa kunawa mikono kwa usahihi, pamoja na kutofuata kanuni za usafi na afya.
Baadhi ya wananchi waliojitokeza katika maadhimisho hayo na kupatiwa huduma za upimaji pamoja na chanjo dhidi ya ugonjwa wa homa ya ini wameishukuru huduma hiyo, wakisema imewasaidia kutambua hali zao za afya na kuongeza uelewa kuhusu namna ya kujikinga na ugonjwa huo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara ni miongoni mwa maeneo yanayozalisha kwa wingi zao la korosho nchini na ambayo imeendelea kutafuta njia za kutumia zao hilo kuchochea maendeleo kupitia mapato ya ndani.
Hatua hiyo imejidhihirisha baada ya Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba kuazimia kurejesha makato ya shilingi 20 kwa kila kilo moja ya korosho kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali katika vijiji, vitongoji, kata na Halmashauri kwa ujumla.
Akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani cha robo ya nne kilichofanyika Julai 27, 2026, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Azizi Selemani, amesema kutokana na Tandahimba kuwa miongoni mwa wilaya zinazozalisha kwa wingi korosho, wameona kuna umuhimu wa kurejesha utaratibu huo ambao hapo awali ulikuwa ukichangia maendeleo.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Kanali Mstaafu Michael Mtenjele, amesema maelekezo tayari yalishatolewa ili wakulima wajadili pendekezo hilo kupitia mikutano ya vijiji na vyama vyao vya ushirika na kufikia makubaliano kwa hiari, ili kuepusha mkanganyiko.
Kutokana na hilo, Mwenyekiti wa Halmashauri amewaagiza Watendaji wa Kata kuandaa mikutano ya kuwaelimisha wananchi kuhusu makato hayo na faida zake kwa maendeleo ya maeneo yao.
Baadhi ya madiwani akiwemo Diwani wa Kata ya Kwanyama Hamza Salumu, wamesema fedha zitakazopatikana zitaendelea kusaidia kukamilisha miradi ya maendeleo badala ya kusubiri fedha kutoka serikalini ambazo wakati mwingine huchelewa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Kamishna wa Huduma za Urekebu wa Jeshi la Magereza Tanzania, CP Amina Kavirondo, amesema ingawa kushiriki tendo la ndoa ni haki ya msingi ya kibinadamu, utekelezaji wa haki hiyo kwa wafungwa unakwamishwa na changamoto za miundombinu, usimamizi na uthibitishaji wa wahusika.
Akizungumza na Jambo TV jijini Dodoma, Kavirondo amesema magereza yaliyopo hayajajengwa kwa kuzingatia utaratibu wa kuwapa wafungwa nafasi ya faragha kwa ajili ya kutekeleza haki hiyo, huku akieleza kuwa usimamizi wake nao unazua maswali.
"Wakati wanafanya hilo tendo la ndoa, tuwe na askari ambao tutawapanga nje ya vyumba? Jaribu kufikiria hata yule askari ambaye amesimama pale atasikiliza lile tendo linalofanyika," amesema.
Ameongeza kuwa changamoto nyingine ni kuthibitisha uhalali wa wanaotembelea wafungwa, ikiwemo kubaini kama anayefika ni mke halali wa mfungwa, pamoja na changamoto za kuthibitisha uhusiano wa mtoto endapo atazaliwa baada ya ziara hizo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, Mhashamu Wolfgang Pisa ameeleza kuwa hali ngumu ya kiuchumi imesababisha vijana kukumbwa na msongo wa mawazo, kutumiwa vibaya na wanasiasa kwa ajili ya malengo yao, na shinikizo la kuhama nchi kutafuta fursa, jambo ambalo ni hatari ikiwa hawatatayarishwa vizuri.
Akizungumza hivi karibuni kando ya Mkutano Mkuu wa 21 wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Afrika Mashariki na Kati (AMECEA) ulifanyika jijini Nairobi, Kenya, Pisa ambaye pia ni Askofu wa Jimbo Katoliki Lindi, amesisitiza kuwa kuna haja ya kuongea na vijana mara kwa mara kupitia njia tofautitofauti ikiwamo mitandao ya kijamii na kuwahamasisha kutumia mitandao hiyo vyema.
“Wengine wahanga wa mazingira kwasababu ya uchumi, na moja ya matatizo makubwa ni mambo mawili ambapo kutokana na hizo changamoto, moja ni wanasiasa, wanasiasa wanaotumia vijana kufikisha malengo yao, lakini vijana kwasababu hawana uchaguzi mkubwa katika uchumi wakati mwingine ni aidha nijiunge au nitakufa njaa”, ameeleza Pisa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Kamishna wa Huduma za Urekebu wa Jeshi la Magereza Tanzania, CP Amina Kavirondo, amesema si kweli kwamba wafungwa wote hutumikia kifungo chote walichohukumiwa, akieleza kuwa sheria inatoa msamaha wa theluthi moja ya kifungo kwa wafungwa wanaostahili.
Akizungumza na Jambo TV jijini Dodoma, Kavirondo amesema mfungwa anapopokelewa gerezani hufanyiwa hesabu maalum za kifungo chake kwa kuzingatia sheria, ili kubaini muda halisi atakaotumikia.
"Mfungwa anapohukumiwa kuja gerezani, miaka ile aliyohukumiwa anapata msamaha wa 1 ya 3 ya kifungo chake. Hiyo ni kwa wafungwa wote ambao si wa kunyongwa na si wa kifungo cha maisha. Iwapo mtu amefungwa miaka 30, moja ya tatu ni miaka 10, hivyo atatumikia miaka 20 badala ya miaka 30," amesema Kavirondo.
Amebainisha kuwa utaratibu huo unafanyika kwa mujibu wa sheria na unaonyesha kuwa mfumo wa magereza unatambua uzito wa kifungo lakini pia unalenga urekebu, si kuwaweka wafungwa katika mateso.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile amewataka Watanzania kuibeba ajenda ya katiba mpya iliyohimizwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Emmanuel Nchimbi, akisema ajenda hiyo inapaswa kuungwa mkono kwa dhati.
Balile ameeleza hayo kupitia makala iliyochapishwa na tovuti ya Jamhuri Media Julai, 28, 2026, akitilia mkazo kwamba katika wakati huu Watanzania wanapaswa kuchukua hatua kwa njia ya nguvu ya hoja, ili hatimaye katiba ipatikane.
Pia baada ya kauli ya Dkt. Nchimbi juu ya Katiba Mpya, Balile amesema alimsikiliza Askofu Benson Bagonza wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Karagwe, akimtaka asimamie ukweli kwa yale aliyoyasema akihimiza kupongeza au kukosoa panapostahili.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katibu wa Siasa, Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma, Jawadu Mohammed amesema mtaji wa chama hicho ni uwezo wake wa kujiongoza kiasi cha kupendwa na watanzania kuliko chama kingine cha siasa nchini
Akizungumza jijini Dodoma Julai 27, 2026 Jawadu amekanusha vikali chama hicho kutegemea msaada wa vyombo vya dola ikiwemo polisi akidai kuwa tuhuma hizo sio za kweli na zinatolewa na watu ambao hawana hoja.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Kesi ya Uhujumu uchumi Na. 4521/2026 inayomkabili Wendy William Ishengoma na wenzake wanne (4), imeitwa leo, Jumatatu Julai, 27 2026 Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Dar es Salaam mbele ya Jaji Dkt. Dafina Ndumbaro
Kesi hiyo imekuja Mahakamani hapo leo kwaajili ya Jamhuri kuanza kuita mashahidi wao na kutoa vielelezo ili kuithibitishia Mahakama hoja wanazowatuhumu washtakiwa ambapo leo, shahidi mmoja ametoa ameanza kutoa ushahidi wake Mahakamani hapo
Shahidi aliyeanza kutoa ushahidi wake leo ni Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Democracy Hussein Nivako (51), ambaye akiwa chini ya kiapo Mahakamani hapo shahidi huyo amejitambulisha kuwa yeye ni Afisa upelelezI, kutoka Makao Makuu ya upelelezI, kitengo cha udhibiti wa makosa yanayohusu fedha,
Baada ya kukamilika kwa ratiba ya leo, Wakili wa utetezi Peter Madeleka akafafanua kilichojitokeza Mahakamani hapo kwa siku ya leo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI:
Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa, Marekani ipo kwenye mazungumzo ya kina na mazuri na Iran, ili kumaliza vita vilivyoanza tangu mwezi Februari 2026.
Trump ametoa kauli hiyo usiku wa kuamkia Julai 28, 2026 kwa saa za Afrika Mashariki akiwa kwenye ziara ya kikazi huko Milford, Michigan, wakati wa mahojiano na mtandao wa habari wa Axios.
Trump ameonya kuwa iwapo mazungumzo hayo hayatakuwa na mafanikio, Marekani itarejea kufanya kile ilichokuwa ikifanya kabla ya kusitishwa kwa mashambulizi.
Licha ya madai hayo ya Trump, awali Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran pamoja na Spika wa Bunge, Mohammad Bagher Ghalibaf, wamekanusha vikali kuwepo kwa mazungumzo yoyote ya moja kwa moja na Marekani.
Iran imetaja kauli za Trump kama habari za uongo na njama za kisiasa zenye lengo la kushusha bei ya mafuta duniani na kujitafutia muda wa kujipanga kijeshi.
Kwa sasa kuna utulivu wa muda wa siku tatu ambapo pande zote mbili zimesitisha mashambulizi ya anga huku kukiwa na hofu kubwa iwapo utulivu huo utadumu. -
Jambo TV
@Jambotv_
Wafanyabiashara wa maduka katika eneo la Mbagala Rangi Tatu, Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam, wameiomba Serikali kuingilia kati changamoto ya wafanyabiashara wadogo (Machinga) wanaofanya biashara katika maeneo ya barabara na mbele ya maduka yao, wakisema hali hiyo imekuwa ikiwazibia njia wateja, na kuziba biashara zao na kusababisha kushuka kwa mauzo.
Akizungumza na Jambo Tv, kuhusu changamoto hiyo, Anafi Mohamed Selemani maarufu kama Kitonga, amesema uwepo wa wafanyabiashara hao katika maeneo ya barabarani umesababisha msongamano mkubwa wa magari na kuathiri biashara za wafanyabiashara wenye maduka, akisisitiza kuwa Serikali inapaswa kuwatafutia maeneo maalum badala ya kuwarasimisha katika maeneo ya barabara.
Amesema iwapo Wafanyabiashara hao wataruhusiwa kuendelea kufanya biashara katika maeneo hayo, hasa mbele ya maduka, wafanyabiashara wanaolipa kodi na gharama mbalimbali za uendeshaji wa biashara wataendelea kupata hasara na hatimaye kulazimika kufunga biashara zao.
Kwa upande wake, Erasto Jacob Chalser, mfanyabiashara wa nguo za Watoto, amesema wafanyabiashara wa maduka wamekuwa wakikabiliwa na gharama kubwa za uendeshaji, ikiwemo kodi, leseni, TRA na gharama nyingine, huku wafanyabiashara wadogo wanaofanya biashara mbele ya maduka yao wakiathiri biashara zao.
Amesema Wafanyabiashara hao wanapoziba maeneo ya mbele ya maduka, wateja hushindwa kuona bidhaa zinazouzwa ndani ya maduka, hali ambayo imekuwa ikisababisha biashara zao kudorora.
Wafanyabiashara hao wameiomba Serikali kuangalia upya utaratibu wa upangaji wa machinga, wakitaka maeneo ya mbele ya maduka yaachwe wazi ili wateja waweze kupita na kuingia kwenye maduka yao.
Wamesema licha ya kuwasilisha malalamiko yao kwa uongozi wa wafanyabiashara, bado hawajapata suluhisho la kudumu, huku wakidai kuwa machinga wamekuwa wakiondolewa na kurejea tena katika maeneo hayo.
Wafanyabiashara hao wameitaka Serikali kuhakikisha wafanyabiashara wote wanapata maeneo sahihi ya kufanyia biashara, bila kundi moja kuathiri biashara na kipato cha kundi lingine.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkuu wa Wilaya ya Ludewa, Mkoa wa Njombe Olivanus Thomas, amefunga mradi wa kikundi cha Ludewa Miller's kinachofanya shughuli za kusaga unga katika Kijiji cha Shaurimoyo, baada ya kubaini kikundi hicho kimetelekeza mradi huo uliodhaminiwa kupitia mpango wa Halmashauri wa kuwawezesha vijana kiuchumi.
Uamuzi huo umefikiwa baada ya kutembelea eneo la mradi na kukuta mashine zikiwa hazifanyi kazi huku wanakikundi wakiwa wamesambaratika, hali iliyosababisha mradi huo kusimama licha ya uwekezaji uliofanywa.
Olivanus amesema rasilimali zinazotolewa na Serikali zinapaswa kutumika kwa manufaa ya wananchi badala ya kuachwa zikipotea kutokana na uzembe.
Aidha ameelekeza Halmashauri kupitia Idara ya Maendeleo ya Jamii pamoja na Kitengo cha Sheria kuchukua hatua za kisheria dhidi ya kikundi hicho, huku mashine hizo zikichukuliwa na kukabidhiwa kwa vijana wengine watakaokuwa tayari kuziendesha.
"Kuanzia sasa hivi hili jengo lifungwe na maendeleo ya jamii endeleeni na utaratibu wa kisheria" ameagiza Olivanus
Awali akitoa ufafanuzi wa mradi huo,Mkuu wa Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi wa Halmashauri hiyo Dkt.Festo Mkomba, amesema kikundi cha Ludewa Miller's kilipewa mkopo wa shilingi Milioni 45 kwa ajili ya ununuzi wa mashine pamoja na kugharamia shughuli nyingine za kikundi mwaka 2019 lakini lakini mashine zilizofungwa zilifanya kazi mwezi mmoja.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo @ChademaTZ2 Dkt. Rugemeleza Nshala ametoa tahadhari juu ya kesi ya ugaidi ya Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma(UDOM) Melkisedeki Kaijage akieleza kuwa inachafua taswira ya nchi.
Dkt. Nshala amesema hayo leo Julai 27, 2026 akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam huku akieleza kuwa chama hicho kitatoa wanasheria kwa ajili ya kuwasaidia wote walioshtakiwa kwa mashtaka mbalimbali ikiwemo ya ugaidi.
Pamoja na hayo ameeleza kuwa wanasheria watahoji juu ya ukatiba wa mashauri mbalimbali yaliyofunguliwa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Simanzi na majonzi vimetanda katika familia ya Caren Remi mwenye umri wa miaka 22, baada ya kupoteza watoto wake watano waliozaliwa njiti na kupoteza maisha muda mfupi baada ya kuzaliwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Arusha, Mount Meru.
Watoto hao, ambao ni mapacha watano, walizaliwa usiku wa kuamkia Julai 26, 2026 baada ya ujauzito kufikia miezi sita.
Akizungumza na waandishi wa habari, Caren ameeleza kuwa alijifungua watoto wanne wakiwa hai, lakini walifariki muda mfupi baadaye, huku mtoto wa tano akizaliwa tayari akiwa amefariki.
Amesema tukio hilo limemuachia maumivu makubwa kwani ulikuwa uzao wake wa kwanza, na hakutarajia kupoteza watoto wake kwa kuwa kipindi chote cha ujauzito hakuwahi kupata changamoto yoyote ya kiafya. Watoto hao walikuwa watatu wa kike na wawili wa kiume.
Kwa upande wake, Baba wa watoto hao ameeleza kuwa tayari alikuwa ameanza kujiandaa kuwapokea na kuwalea watoto wake, lakini ndoto na matumaini hayo yamekatishwa baada ya vifo hivyo.
Akizungumzia tukio hilo, Muuguzi Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Arusha Mount Meru amesema vifo hivyo vilitokana na mama huyo kuanza kupata uchungu kabla ya wakati kutokana na kutanuka kwa mlango wa kizazi, hali iliyosababisha kujifungua watoto hao kabla ya kufikisha umri unaotakiwa wa ujauzito.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
"Kama watanzania lazima tujiulize je mtu kutoa maoni yake au kukutana na wenzake imegeuka kuwa tendo la ugaidi. CHADEMA haiungi mkono ugaidi kwa namna yoyote na CHADEMA inaamini katika matumizi ya njia za amani za kufikisha ujumbe wake na ndivyo katiba inavyosema ibara ya 20(2) na ndivyo sheria ya vyama vya siasa kifungu cha 19 kinavyosema na sisi tunakiamini"
Hayo ameyasema Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo @ChademaTZ2 Wakili Dkt. Rugemeleza Nshala @rugemeleza akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 27, 2026 juu ya wanachama wa chama hicho waliokamatwa maeneo mbalimbali nchini na kufunguliwa mashtaka ikiwemo ya ugaidi. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Karagwe, Dkt. Benson Bagonza amedai kuwa kuna tafsiri mbili zinazopingana za hotuba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Emmanuel Nchimbi aliyoitoa hivi karibuni ya kuwataka Watanzania wapambane kupata katiba mpya.
Amesema tafsiri ya kwanza ni ya baadhi ya wafuasi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanaompinga Nchimbi wakidai kuwa anajitafutia sifa, na pili ni wale wanaona kauli hiyo kama himizo la heri la kuongeza juhudi za kupata katiba hiyo.
Akizungumza na televisheni mtandao ya Pekuzi, Bagonza anaona upinzani dhidi ya Dkt. Nchimbi ndani ya CCM unaonesha kuwa hakuna nia ya dhati ya kuleta katiba mpya. Aidha Bagonza ameendelea kuhoji mantiki ya kuambiwa ‘pambaneni’ ikiwa Rais anaitaka katiba na ilani ya CCM imeshaahidi jambo hilo akisema kuwa ikiwa itabidi kupambana, basi watu watapambana na CCM yenyewe ambayo baadhi ya watu wake wanatafsiriwa kuzuia mchakato huo.
Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa 15 wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) Julai 24, 2025 jijini Dar es Salaam, Dkt. Nchimbi aliwataka watanzania kuongeza juhudi kupambania katiba mpya wakati huu ambapo Rais Samia Suluhu Hassan ameonesha nia ya dhati ya kuitaka katiba hiyo mpya.
"Nikiambiwa kuna jambo tu kama Makamu wa Rais waambie watanzania, nitasema pambaneni mpate katiba mpya, katiba ambayo ina makubaliano ya wadau wote, katiba yenye muafaka katika taifa, katiba ambayo kila Mtanzania popote alipo atajiskia fahari kujitambulisha mimi natoka Tanzania, katiba inayojali maisha", alisema Dkt. Nchimbi.
Aidha, Dkt. Nchimbi alieleza kwamba, kwa mujibu wa tafiti iliyofanywa na Kamati ya kuandika ilani ya Chama cha Mapinduzi(CCM) 2025, Tume ya Haki Jinai aliyounda Rais Samia pamoja na ripoti ya Tume ya uchunguzi ya Matukio ya Uvunjifu wa Amani yaliyotokea wakati na baada ya uchaguzi (2025), moja ya mambo wananchi wanayataka ni Katiba Mpya huku ikipendekezwa kupatikana kufikia mwaka 2028 ili itumike mwaka 2029.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI PICHA:
Tanzania imeandika historia nmuhimu katika sekta ya fedha na uwekezaji kufuatia kufanikisha uorodheshaji wa hati fungani yake ya kwanza ya kimataifa inayotolewa kwa Shilingi ya Tanzania (Offshore Tanzanian Shilling-denominated Bond) katika Soko la Hisa la London (London Stock Exchange).
Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA), ikiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wake Gilead Teri ambaye ameshiriki pamoja na Waziri wa Fedha wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi Khamis Mussa Omar, pamoja na viongozi waandamizi wa Serikali, Shirika la Fedha la Kimataifa (IFC), Kundi la Benki ya Dunia (World Bank Group), Benki ya NMB na wawekezaji kutoka mataifa mbalimbali kushuhudia na kuadhimisha mafanikio hayo ya kihistoria.
Hati fungani hiyo yenye thamani ya Shilingi bilioni 265.2 (sawa na Dola za Marekani milioni 100), iliyotolewa na Shirika la Fedha la Kimataifa (IFC), mwanachama wa Kundi la Benki ya Dunia, ndiyo hati fungani kubwa zaidi kuwahi kutolewa katika masoko ya kimataifa ikiwa imeainishwa kwa Shilingi ya Tanzania. Fedha zitakazopatikana zitatumika kutoa mikopo ya muda mrefu kupitia Benki ya NMB, hatua itakayoongeza upatikanaji wa mitaji nafuu kwa biashara ndogo, za kati na zinazokua (MSMEs), ikiwemo zinazomilikiwa na wanawake.
Mbali na umuhimu wake katika maendeleo ya masoko ya mitaji, hatua hii ya kihistoria inatuma ujumbe wenye nguvu kuhusu kuongezeka kwa imani ya wawekezaji wa kimataifa katika uthabiti wa uchumi wa Tanzania, mageuzi ya kiuchumi yanayoendelea pamoja na mazingira bora ya uwekezaji.
Kwa upande wa TISEZA, mafanikio haya yanaimarisha dhamira ya Mamlaka ya kuvutia, kurahisisha na kuwezesha uwekezaji wenye tija kwa kuendelea kujenga mazingira rafiki ya biashara yanayowawezesha wawekezaji kupata mitaji ya muda mrefu, kupanua shughuli zao kwa ufanisi na kuchangia maendeleo endelevu ya uchumi wa Taifa.
Mafanikio haya pia ni kielelezo cha matokeo chanya ya ajenda ya mageuzi inayotekelezwa na Serikali chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan. Kupitia falsafa ya 4Rs, hususan nguzo za Mageuzi (Reforms) na Kujenga Upya (Rebuilding), Serikali imeendelea kuimarisha utawala wa kiuchumi, kuongeza uwazi na uhakika wa sera, pamoja na kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI:
Shule ya Sekondari Bigwa Sister iliyopo mkoani Morogoro, inayomilikiwa na Kanisa Katoliki imekumbwa na tukio la moto ulioripotiwa kutokea katika eneo la mabweni ya shule hiyo,Taarifa za awali zinaeleza kuwa moto huo umeibuka katika eneo hilo na kusababisha hofu miongoni mwa wanafunzi na watu waliokuwa jirani na shule hiyo.
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji pamoja na wananchi wameendelea na juhudi za kuudhibiti na kuuzima moto huo, huku chanzo cha tukio hilo hakihafahamika,Wakati huo huo wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo wamewekwa katika eneo la uwanja wa shule kwa ajili ya usalama wao wakati zoezi la kuzima moto likiendelea.
Kwa mujibu wa taarifa za awali, hakuna majeruhi wala vifo vilivyoripotiwa kutokana na tukio hilo. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Jeshi la Polisi Tanzania limetangaza kuwa watuhumiwa 36 kati ya 130 waliokamatwa kwa tuhuma mbalimbali za uhalifu wamefikishwa mahakamani.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi Tanzania, watuhumiwa hao walikamatwa kutokana na tuhuma za kupanga na kuhamasisha vitendo vya kihalifu vilivyohusisha vurugu, uharibifu wa mali na uvunjifu wa amani.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa baadhi ya watuhumiwa walihusishwa na matumizi ya mitandao ya kijamii na njia nyingine za mawasiliano katika kuhamasisha mikusanyiko isiyofuata sheria, kusambaza jumbe za uchochezi pamoja na kuandaa mipango ya vitendo vya uhalifu.
Aidha, Jeshi la Polisi limesema ushahidi uliokusanywa unaonyesha kuwepo kwa tuhuma za kupanga na kushiriki vitendo kama vile kuchochea vurugu, kushambulia watu, kuharibu mali za umma na binafsi, pamoja na kuzuia utekelezaji wa majukumu ya vyombo vya dola.
Kati ya waliokamatwa, baadhi walifikishwa mahakamani katika mikoa mbalimbali, huku wengine wakiendelea kufanyiwa uchunguzi kutokana na ushahidi unaoendelea kukusanywa.
Jeshi la Polisi limewataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama ili kuhakikisha amani na utulivu vinaendelea kulindwa nchini.
Taarifa hiyo imetolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, DCP David Misime leo Jumapili Julai 26, 2026.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Mbunge wa Tunduru Kaskazini, Ado Shaibu, ameishauri Serikali kuharakisha mchakato wa kuwalipa posho mashujaa walioshiriki katika Vita vya Kagera, akisema ni sehemu ya kuwaenzi kwa mchango wao kwa taifa.
Katika andiko lake alilolisambaza kwenye mitandao ya kijamii, Ikiwa ni wakati wa kuadhimisha Siku ya Mashujaa, Ado amesema Tanzania ina mashujaa wengi waliolitumikia taifa, huku akitaja umuhimu wa kuwakumbuka waliopigana katika Vita vya Kagera.
Amesema Serikali katika mwaka wa fedha 2025/2026 iliahidi kuanza kuwalipa posho mashujaa hao, lakini utekelezaji huo haukufanyika kama ilivyopangwa.
“Leo ni Siku ya Mashujaa. Nchi yetu ina mashujaa wengi. Leo naomba niwaongelee mashujaa wa Vita ya Kagera. Ninatoa rai kwa Serikali kuharakisha mchakato wa kuwaenzi mashujaa hawa kwa kuwalipa posho,” amesema Ado.
Ameongeza kuwa katika mwaka wa fedha 2026/2027 Serikali imeeleza kuwa malipo hayo yataanza baada ya kukamilika kwa zoezi la uhakiki, hivyo ameitaka kuhakikisha ahadi hiyo inatekelezwa mapema.
“Mwaka uliopita Serikali iliahidi wataanza kulipwa posho, hawakulipwa. Mwaka huu imeahidi wataanza kulipwa mapema kwa sababu uhakiki umekamilika. Ni muhimu Serikali iwakumbuke mashujaa hawa kwa kuwalipa mapema iwezekanavyo,” amesema Ado Shaibu.
Ado ambaye pia ni Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, amesema hatua hiyo itakuwa ishara ya kutambua mchango wa mashujaa hao katika kulinda uhuru na usalama wa nchi. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI:
Wanawake sita wametunukiwa Tuzo za Malkia wa Nguvu Kanda ya Ziwa, ikiwa ni mwaka wa 10 wa tuzo hizo toka zianzishwe zilizofanyika jijini Mwanza, zikilenga kutambua na kuenzi mchango wa wanawake katika kuchangia maendeleo ya kiuchumi, uongozi na ustawi wa jamii.
Hafla hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Kwatunza, jijini Mwanza na kuhudhuriwa na zaidi ya wanawake 800, huku Mgeni Rasmi akiwa Waziri wa Madini, Antony Mavunde.
Miongoni mwa viongozi wengine waliohudhuria hafla hiyo ni Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Amir Mkalipa akimwakilisha Mkuu wa Mkoa, Mbunge wa Jimbo la Ngara, Dotto Bahemu pamoja na Mbunge wa Jimbo la Ilemela, Kafiti William Kafiti.
Katika hafla hiyo, wanawake sita wamepewa tuzo katika maeneo mbalimbali kutokana na mchango wao na mafanikio waliyoyapata katika sekta zao.
Waliopewa tuzo hizo ni Stella Tilya, aliyeshinda Tuzo ya Ustahimilivu na Uwezeshaji; Doroth Baltazari, aliyeshinda Tuzo ya Uongezaji Thamani wa Mazao ya Kilimo; Rose Rulangwa, aliyeshinda Tuzo ya Ubunifu na Utayarishaji wa Matukio; Ummy Tofiki, aliyeshinda Tuzo ya Uanzishaji na Usimamizi wa Biashara; Happiness John, aliyeshinda Tuzo ya Uvumbuzi wa Fursa; pamoja na Mwanabure Ihunya, aliyeshinda Tuzo ya Sekta ya Ufugaji. -
Jambo TV
@Jambotv_
Ofisi ya Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) baada ya kupitia rufaa ya Katibu wa chama hicho Mkoa wa Morogoro, Barnabas Okola, na kwa kuwa haki ya kusikilizwa ni haki ya msingi, imeeleza kuwa maamuzi ya kumsimamisha uongozi Barnabas Okola yaliyofanywa na Kanda ya Kati kupitia barua ya tarehe 09/07/2026, anafutwa rasmi na hivyo Okola anaendelea na majukumu yake.
Barua iliyosainiwa na Mkurugenzi wa Sheria na Haki za Binadamu wa CHADEMA Wakili Gaston Garubindi kwa niaba ya Katibu Mkuu wa chama hicho John Mnyika kwenda kwa Okola imesema “Katibu wa Kanda aliwasilisha maelezo yake Ofisi ya Katibu Mkuu, kupitia barua yake ya tarehe 19/07/2026, Ofisi ya Katibu Mkuu imepitia maelezo hayo na kujiridhisha kwamba, mlalamikaji hakusikilizwa kabla ya hatua ya kusimamishwa uongozi kwa nafasi ya Katibu Mkoa wa Morogoro kuchukuliwa"
"Kwa kuwa haki ya kusikilizwa ni haki ya msingi, maamuzi ya kumsimamisha uongozi Barnabas Okola yaliyofanywa na Kanda ya Kati kupitia barua ya tarehe 09/07/2026, yanafutwa rasmi kuanzia tarehe ya barua hii, ikiwa Kanda ya kati bado wana malalamiko dhidi ya Katibu wa Mkoa wa Morogoro wafuate utaratibu wa Kikatiba kama unavyoelekezwa kwenye kanuni ya 6.5.5 ikisomwa pamoja na kanuni ya 6.5.6 ya kanuni za chama”
Itakumbukwa kuwa, Okola alisimamishwa uongozi tarehe 09/07/2026 na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Kati, Ashura Mashaka Masoud, baada ya Okola kuibua tuhuma za kwamba Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tanzania Bara John Heche amefanya ubadhilifu wa pesa za chama, na akaitaka CHADEMA iunde kamati ya uchunguzi huku Heche akiachia ngazi na kupisha uchunguzi.
Akizungumzia barua hiyo, Wakili Garubindi licha ya kuthibitisha uhalali wake, lakini pia amesema baada ya kuona hatua zilizochukuliwa na uongozi wa Kanda tofauti kwa kuwasimamisha uongozi baadhi ya maafisa wake wa chini, Ofisi ya Katibu Mkuu imefanya maamuzi ya kufuta maamuzi yao lakini pia kuwaelekeza Makatibu wa Kanda kufuata utaratibu wa Kikatiba ikiwemo kupewa muda wa siku 14 wa kujieleza kabla ya hatua stahiki kuchukiliwa. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI:
Naibu Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Dkt. Pius Chaya, amefanya ziara katika maeneo ya Uwekezaji jijini Arusha kwa lengo la kujionea hali ya uwekezaji
Akiwa katika ziara yake, leo Julai 25, 2026 amesisitiza kuwa Serikali inaendelea kuimarisha mazingira ya uwekezaji katika sekta ya afya ili kuongeza uzalishaji wa vifaa tiba nchini na kupunguza utegemezi wa bidhaa zinazoagizwa kutoka nje.
ameyasema hayo alipotembelea kiwanda cha A - Z Health Care Ltd kilichopo Arumeru, Mkoani Arusha, akieleza kuwa Serikali inalenga kupunguza uagizaji wa vifaa tiba kutoka asilimia 85 hadi kufikia asilimia 20 na 30 kupitia uwekezaji wa viwanda vya ndani.
"Nitoe wito kwa wawekezaji wengine waige mfano wa A - Z, Serikali imejipanga kuendelea kuboresha miundombinu kama barabara, umeme na maji katika maeneo ya uwekezaji ili viwanda viweze kufanya kazi kwa ufanisi," amesema Dkt. Chaya.
Amesema uwekezaji huo unaunga mkono Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 na Mpango wa Nne wa Taifa wa Maendeleo, huku ukisaidia kupunguza gharama ambazo Serikali imekuwa ikitumia kuagiza vifaa tiba kutoka nje ya nchi.
Aidha, akiwa katika eneo la Uwekezaji la Dekker Bruns, inayojishughulisha na uzalishaji wa vipandikizi vya maua kwa ajili ya masoko ya nje, akieleza kuwa Serikali inalenga kuhakikisha wawekezaji wanafanya shughuli zao katika mazingira rafiki ili waongeze uzalishaji, ajira na mchango wao katika uchumi wa taifa.
Mbali na maeneo hayo pia ametembelea wazalishaji wa maua, Arusha Blooms Limited na kuhitimisha ziara yake katika Shamba la Kiliflora Usa River – Loliondo Farm -
Jambo TV
@Jambotv_
Shirika la Kikanda la Uhifadhi wa Uhuru wa Taaluma Afrika (Africa Coalition for Academic Freedom - ACAF) limemwandikia barua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, likieleza wasiwasi wake kuhusu kuendelea kushikiliwa kwa wahadhiri watatu wa vyuo vikuu waliokamatwa mapema mwezi Julai 2026.
Katika barua hiyo iliyosainiwa na Mkurugenzi wa Kanda wa ACAF, Profesa Kwadwo Appiagyei-Atua, shirika hilo limewataja wahadhiri hao kuwa ni Johaiven Revelian Bikongolo na Titus Joseph Kituli kutoka Chuo Kikuu cha St. John’s Tanzania (SJUT), pamoja na Melkisedeki Kaijage wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).
ACAF imeeleza kuwa kukamatwa kwao kunazua hofu kuhusu hali ya uhuru wa taaluma na kujieleza nchini, kutokana na taarifa kuwa walikamatwa kwa tuhuma za kuhamasisha maandamano ya Julai 7, 2026. Shirika hilo limesikitishwa zaidi na taarifa kuwa mmoja wa wahadhiri hao alikamatwa baada ya kufundisha somo la Maadili na Utawala Bora kwa kutumia mifano ya kashfa za kihistoria za ufisadi nchini kuelezea uwajibikaji hatua inayoweza kutafsiriwa kama adhabu dhidi ya ufundishaji na mijadala halali ya kitaaluma.
Aidha, ACAF imeeleza wasiwasi wake kuwa miongoni mwa wahadhiri hao wameendelea kushikiliwa kwa zaidi ya siku 17 bila kufikishwa mahakamani wala kupewa dhamana, huku familia na waajiri wao wakidaiwa kutoarifiwa kwa wakati, jambo linalokwenda kinyume cha utawala wa sheria.
"Vyuo vikuu vipo kwa ajili ya kuchochea fikra pevu, mijadala yenye ushahidi, na ubadilishanaji huru wa mawazo. Wanataaluma lazima waweze kufundisha, kufanya tafiti, na kushiriki katika mijadala ya umma bila hofu ya kutishwa, kukamatwa, au kuingiliwa kisiasa. Kugeuza mijadala ya darasani au uchambuzi wa kisomi kuwa makosa ya jinai hakudhoofishi tu uhuru wa taaluma, bali pia mfumo wa elimu ya juu na utawala wa kidemokrasia," imeeleza taarifa hiyo ya ACAF.
Kutokana na hali hiyo, ACAF imeiomba Serikali kuwaachia huru mara moja na bila masharti wahadhiri hao, isipokuwa kama kuna mashtaka ya jinai yenye ushahidi yatakayowasilishwa mahakamani kwa haraka. Pia imetaka kuheshimiwa kwa haki zao za kisheria na kulindwa kwa uhuru wa taasisi za elimu ya juu kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania na mikataba ya kimataifa.
Barua hiyo ya ACAF pia imenakiliwa kwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Mwanasheria Mkuu wa Serikali, pamoja na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola.
Kwa mujibu wa taarifa ya Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (THTU), Dkt. Paul Loisulie, mmoja wa wahadhiri wa SJUT alikamatwa kufuatia mada hiyo ya utawala bora (akitumia mifano kama Richmond na Escrow), huku mwingine ambaye ni Mkurugenzi wa Huduma za Wanafunzi akihusishwa na masuala ya uchaguzi wa wanafunzi chuoni hapo.
Wakati huohuo, Mhadhiri wa UDOM, Melkisedeki Kaijage, alibadilishiwa mashtaka yake kuwa ya ugaidi kutoka uchochezi. Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanataaluma UDOM (UDOMASA), Dkt. Gerald Shija, alithibitisha kuwa Kaijage ambaye amekuwa mikononi mwa polisi tangu Julai 8, 2026 alikuwa katika mchakato wa kukamilisha vigezo vya dhamana vilivyotolewa na Mahakama tarehe 21 Julai, kabla ya hati yake ya mashtaka kubadilishwa na kusomewa mashtaka hayo mapya ya ugaidi ambayo hayana dhamana. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Sakata la mgogoro wa ardhi linalowahusisha wakazi wa Kitongoji cha Udindivu, Kata ya Mapinga, Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani limeendelea kuchukua sura mpya kila siku. Leo, Jumamosi tarehe 25/07/2026 wakazi hao wamejitokeza kwa mara nyingine na kulaumu kile walichokiita kuwa ni uonevu kutoka kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani.
Wakizungumza na Jambo TV, wananchi hao wamedai kuwa hivi karibuni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani SACP Salim Morcase akiwa ameambatana na maafisa na askari wengine wenye silaha walifika kwenye eneo hilo ambalo mgogoro wake uko mahakamani kwa sasa, ambapo kufika kwao kuliibua sintofahamu baina ya wananchi na polisi, huku wananchi wakihoji kile walichokiita kuwa ni nguvu aliyokuwa nayo mtu waliyekuwa nae kwenye mgogoro hadi kufikia hatua ya kuongozana na askari kila anapoenda kwenye eneo hilo.
Hata hivyo, madai hayo ya wananchi yanapingana na kile kilichoelezwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani kuhusiana na sintofahamu hiyo. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani ACP Salim Morcase siku chache zilizopita akizungumzia sakata hilo alisema yeye na askari wake walifika hapo kwaajili ya kufuatilia taarifa waliyokuwa wameipokea kutoka kwa mmoja wa wananchi wanaomiliki maeneo sehemu hiyo aliyelalamikia kuvunjiwa ukuta wake na kuibiwa tofali zake, hata hivyo alidai kwamba baadhi ya wananchi walijaribu kuzuia ukaguzi huo wa Jeshi la Polisi.
Kamanda Morcase alienda mbali zaidi na kueleza kuwa eneo lililovunjwa ukuta na kuibiwa tofali, si sehemu ya eneo linalobishaniwa mahakamani kama inavyodaiwa na wananchi hao.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, John Heche, amehoji maana ya kauli ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Emmanuel Nchimbi, iliyowataka Watanzania ‘kupambana’ ili kupata Katiba Mpya, akihoji iwapo kuna kikundi kinachokwamisha mchakato huo.
Heche ametoa kauli hiyo Jumamosi, Julai 25, 2026, jijini Mwanza wakati akizungumza na waandishi wa habari. Amehoji kuwa, ikiwa viongozi wakuu wa serikali wanatamani Katiba Mpya, ni nini kinachozuia kupatikana kwake hadi wananchi walazimike kupambana.
"Nchimbi anasema Samia anataka Katiba lakini wakati huohuo anatuambia tukomae tupate katiba, sasa maana yake ni nini? Kama hakuna anayezuia si inatakiwa iwe yenyewe tu bila kukomaa!" amesema Heche.
Kauli hiyo ya Heche inakuja kutokana na hotuba ya Dkt. Nchimbi aliyoitoa Julai 24, 2026, wakati akifungua Mkutano Mkuu wa 15 wa Mwaka wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC). Katika mkutano huo, Dkt. Nchimbi alisema: "Nikiambiwa kuna jambo kama Makamu wa Rais waambie Watanzania, nitasema pambaneni mpate Katiba Mpya- Katiba ambayo ina makubaliano ya wadau wote, Katiba yenye muafaka katika taifa, Katiba ambayo kila Mtanzania popote alipo atajisikia fahari kujitambulisha, na Katiba inayojali maisha."
Mbali na hilo, Heche amewataka wanachama wa CHADEMA na Watanzania kwa ujumla kutokuwa waoga na kuungana katika kudai haki, ikiwemo Katiba Mpya, akisisitiza kuwa shinikizo na mashambulizi dhidi yao ni ishara ya udhaifu wa ‘wapinzani wao’ wa kisiasa. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Kassim Majaliwa, amemtembelea na kumjulia hali mdau wa muziki na mlezi wa vipaji, Said Fella maarufu kama Mkubwa Fella, nyumbani kwake, ambapo alimkabidhi msaada wa Shilingi milioni 20.
Majaliwa pia alifanya naye mazoezi mepesi ya viungo na kupata fursa ya kufanya mazungumzo marefu kuhusu mchango mkubwa wa Mkubwa Fella katika kukuza na kuendeleza muziki wa Tanzania pamoja na masuala mbalimbali yanayohusu tasnia ya sanaa.
Aidha, Majaliwa ameahidi kuendelea kumtembelea Mkubwa Fella mara kwa mara ili kufuatilia maendeleo ya afya yake na kumpa faraja.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
“Si walisema wanamweka Lissu ndani chama kitakufa, kimekufa? Ndiyo kinakuwa cha moto zaidi kabisa, wakimweka Heche…atakuja Chagulani, atakuja Obadi atakuja nani…yaani huu moto umeshawaka hakuna namna ya kuuzima, watamwachia kama walivyomkamata”, - Heche.
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) bara, John Heche ameeleza hayo Jumamosi, Julai 25, 2026, akizungumza na waandishi wa habari mkoani Mwanza kuhusu viongozi na wanachama kadhaa wa chama hicho wanaoshikiliwa maeneo mbalimbali nchini kwa tuhuma za ugaidi ambapo pia amedai kuwa kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa chama hicho taifa, Tundu Lissu ina msukumo wa kisiasa, akishangaa namna kesi hiyo inavyochukua muda mrefu kumalizika.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) bara, John Heche ameeleza kuwa chama hicho kinaandaa barua ambazo zimepangwa kupelekwa kwa mashirika mbalimbali ya kimataifa ikiwamo Amnesty International, Tume ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya (EU), pamoja na mashirika mengine ya kutetea haki za binadamu, lengo ni kuijulisha dunia kuwa kuna wanachama wao 51 ambao wameshtakiwa kwa kesi za ugaidi.
Heche ameeleza hayo Jumamosi, Julai 25, 2026, akizungumza na waandishi wa habari mkoani Mwanza ambapo amesisitiza kuna ulazima wa kupiga kelele jumuiya ya kimataifa ili kupata msaada badala ya kukaa kimya, jambo ambalo linaweza kugharimu maisha.
Aidha, CHADEMA imekiomba Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) na mashirika mengine nchini kusaidia kuongeza nguvu ya mawakili na rasilimali ili kuwapigania waliokamatwa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) bara, John Heche, amewaagiza Mawakili wa chama hicho pamoja na Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA kuandaa timu maalumu itakayohakikisha viongozi wa chama hicho na wanachama wengine wanaoshikiliwa maeneo mbalimbali nchini wanarudi katika shughuli zao.
Heche ameeleza hayo Jumamosi, Julai 25, 2026, akizungumza na waandishi wa habari mkoani Mwanza. Amewasihi wanachama wa CHADEMA nchini kote kuonana na ndugu wa watu waliokamatwa kama sehemu ya faraja.
"Natumia nafasi hii kuwaagiza viongozi wetu wa chama, mawakili wetu, viongozi wote wa chama na mawakili wengine wote waandae timu maalumu ya kuendelea kupambana kuhakikisha viongozi wetu wanaachiliwa wanarudi kwenye shughuli zao" amesema Heche.
Maagizo ya Heche yanakuja kutokana na viongozi mbalimbali na wanachama wa chama hicho kufikishwa katika mahakama mbalimbali nchini wakikabiliwa na mashitaka yanayohusu ugaidi ambayo hayana dhamana.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
📍NJOMBE: Wakazi wa Kijiji cha Mikongo, Halmashauri ya Mji wa Njombe, wamemhoji Mhandisi wa Maji kutoka Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA), wakitaka maelezo kuhusu kuchelewa kupatikana kwa huduma ya maji licha ya mradi wa maji kujengwa kwa zaidi ya miezi mitano.
Akizungumza mbele ya Mbunge wa Jimbo la Njombe Mjini, Deodatus Mwanyika, mmoja wa wakazi wa kijiji hicho, Sabinus Mhogofela, alisema ni jambo la kushangaza kuona mradi umefika kijijini lakini Wananchi wanaendelea kukosa huduma ya maji.
“Maji hapa ni mtihani hayapo mpaka sasa,sisi tunatekeleza Ilani gani kama hamjatendea haki watu wa Mikongo na raha yetu sisi ni nini?” amehoji Mhogofela.
Akijibu malalamiko hayo, Mhandisi wa Maji wa RUWASA Wilaya ya Njombe, Bakari Kitogota, alisema mradi huo uliwahi kuanza kutoa huduma ya maji, lakini ulipata hitilafu ya pampu ya kisima, na kwamba jitihada za matengenezo zinaendelea ili kurejesha huduma kwa Wananchi.
Naye Mbunge wa Jimbo la Njombe Mjini, Deodatus Mwanyika, alikiri kuwa pampu ya kisima hicho imekuwa imeharibika kwa muda mrefu, hali iliyowavunja moyo Wananchi, na kuahidi kufuatilia kwa karibu ili changamoto hiyo ipatiwe ufumbuzi haraka.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Mjadala wa kitaifa kuhusu mchakato wa kupatikana kwa Katiba Mpya nchini Tanzania umeingia katika hatua mpya na kuibua hisia mseto miongoni mwa wanasiasa, wasomi, mashirika ya kiraia na wananchi wa kawaida, kutokana na mfululizo wa kauli zilizotolewa na viongozi wa juu wa serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Mchakato huo ambao umekuwa ukifuatiliwa kwa karibu na pande zote za kisiasa, umeshika kasi zaidi kutokana na hotuba iliyotolewa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Emmanuel Nchimbi, tarehe 24 Julai, 2026. Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) uliofanyika katika ukumbi wa Mlimani City, Dkt. Nchimbi alitoa wito wa wazi na wa kimkakati akiwataka Watanzania kutolala wala kurudi nyuma katika harakati za kudai Katiba Mpya.
"Nikiambiwa kuna jambo tu kama Makamu wa Rais waambie watanzania, nitasema pambaneni mpate katiba mpya, katiba ambayo ina makubaliano ya wadau wote, katiba yenye muafaka katika taifa, katiba ambayo kila Mtanzania popote alipo atajiskia fahari kujitambulisha mimi natoka Tanzania, katiba inayojali maisha", alisema Dkt. Nchimbi.
Katika ufafanuzi wake, Dkt. Nchimbi alieleza kuwa nia na utashi wa Rais aliyeko madarakani ni nguzo kuu katika kukamilisha mchakato huo. Alibainisha kuwa Katiba ya sasa inampa Rais mamlaka makubwa mno, na kwamba pasipo utashi wa dhati kutoka kwa Mkuu wa Nchi, mchakato wa Katiba unaweza kukwama kwa miaka mingi. Dkt. Nchimbi alisisitiza kuwa Rais Samia Suluhu Hassan ana utashi na nia thabiti ya kuruhusu mchakato huo utekelezwe.
Hata hivyo, saa chache tu baada ya hotuba hiyo, Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Taifa, Mohamed Kawaida alichapisha ujumbe kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram ambao umetafsiriwa kuwa jibu la kuzuia kile kilichotafsiriwa kama ukiukaji wa nidhamu ya chama na wafuasi wake kwenye ukurasa huo na wachambuzi wa siasa, na jibu kwa Dkt. Nchimbi.
Andiko hilo liliambatana na kipande cha video kikimwonesha Prof. Kitila Mkumbo, alipokuwa akieleza wakati wa Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM jijini Dodoma Mei 30, 2025 kuwa ajenda ya Katiba Mpya ni ahadi rasmi na ya kisera ya CCM. Prof. Kitila ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2025- 2030 alibainisha kuwa mchakato huo tayari umeingizwa kwenye Ilani hiyo na kwamba Serikali inatenda kazi chini ya maelekezo hayo ya chama.
Katika ujumbe wake, Mohamed Kawaida alikazia umuhimu wa taasisi kusimamia misingi yake na kuzuia hali ya viongozi kujitengenezea umaarufu binafsi kupitia ajenda za chama.
“Chama cha siasa ni taasisi inayojengwa juu ya misingi ya utaratibu wa ndani, uwajibikaji wa pamoja, nidhamu ya chama, na uongozi wa pamoja. Uimara wa taasisi haupimwi kwa umaarufu wa mtu mmoja isipokuwa kwa uwezo wake wa kulinda taratibu, utamaduni na maamuzi ya pamoja. Pale ambapo viongozi au makada huanza kutanguliza malengo binafsi kuliko maamuzi ya taasisi hujitokeza kile kinachoitwa ‘personalisation of power’…hali ambayo maslahi ya mtu binafsi hupewa uzito kuliko uhalali wa taasisi”, ameandika Kawaida.
Kawaida ameongeza kuwa, kwa mtazamo wa kiongozi wa taasisi, michakato ya kumpima au kumchambua kiongozi si adhabu bali ni sehemu ya uwajibikaji wa kitaasisi na utawala bora wa ndani. Amehitimisha kwa kusema kuwa taasisi imara hudumu milele wakati viongozi ni watu wa kupita, na kwamba CCM itaendelea kuongozwa na utamaduni wake wa nidhamu na uwajibikaji wa pamoja kuliko matakwa ya mtu mmoja.
“Hatimaye, wanaoendana na maadili na misingi ya taasisi huendelea kubeba dhamana ya uongozi huku wale wanaotanguliza maslahi binafsi wakijitenga wenyewe na misingi waliyopewa kuisimamia. Kwa msingi huo uimara wa chama hauko katika uwezo wa kiongozi mmoja kujijengea taswira mbele ya umma bali katika uwezo wa taasisi kusimamia nidhamu, kulinda maamuzi yake ya pamoja na kuhakikisha kuwa uongozi unabaki kuwa wa taasisi badala ya kuwa wa mtu mmoja”, ameeleza Kawaida.
Mjadala huu unakuja kukiwa na muendelezo wa kauli kutoka kwa viongozi wengine wa CCM kuhusu Katiba Mpya. Hivi karibuni, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa, Ally Hapi, alipokuwa akizungumza mkoani Shinyanga, alitoa wito kwa Watanzania kutokubali ajenda ya Katiba Mpya ihodhiwe na vyama vya upinzani kama CHADEMA. Hapi alieleza kuwa Katiba Mpya ni takwa pana la kitaifa linalohusu maslahi ya wananchi wote, na kwamba CCM imeshaweka mwelekeo wa wazi wa namna ya kuitekeleza kupitia serikali yake. Naye, Prof. Mkumbo ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Ubungo (CCM) na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Mipango na Uwekezaji akizungumza hivi karibuni bungeni jijini Dodoma alieleza kuwa ajenda ya Katiba Mpya ni ‘mali ya CCM’ kwa kuwa tayari imeingizwa rasmi katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2025–2030 katika kile kilichoelezwa pia kama jibu kwa vyama vya upinzani ambavyo vilikuwa vikieleza kuhusu kuharakisha mchakato wa katiba mpya kupitia yao mikutano mbalimbali ya hadhara. -
Jambo TV
@Jambotv_
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Karagwe, Dkt. Benson Bagonza, amehoji kauli ya Julai 24, 2026 kutoka kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Emmanuel Nchimbi ya kuwataka Watanzania wapambane kupata katiba mpya akisema, ikiwa hitaji la katiba mpya ni takwa la Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kama alivyosema Dkt. Nchimbi, kuna haja gani ya wananchi kupambana ili waipate katiba hiyo mpya na ni nani wanapaswa kupambana naye ili waipate.
Askofu Bagonza ameeleza hayo alipofanya mahojiano na Saut Digital, Ijumaa Julai 24, 2026. Amesema kwa kuhoji kwamba, hatua ya Makamu wa Rais kusema Rais anahitaji katiba mpya ni jambo zuri lakini kwanini Rais hasemi mwenyewe maneno hayo badala ya kusemewa.
"Amesema Rais anaitaka kwa sababu iliwekwa kwenye ilani, swali langu ni, kama Rais anaitaka kwanini tuipambanie? Makamu amesema tuipambanie, tukomae, kama Rais anaitaka kwanini tuipambanie. Swali la pili, tunapambana na nani ili kuipata? Swali la tatu, Makamu kusema ni jambo zuri, lakini anaposema Rais anaitaka, kwanini Rais mwenyewe hasemi mwenyewe moja kwa moja?" Amehoji Askofu Bagonza.
Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa 15 wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) Julai 24, 2025 jijini Dar es Salaam, Dkt. Nchimbi aliwataka watanzania kuongeza juhudi kupambania katiba mpya wakati huu ambapo Rais Samia Suluhu Hassan ameonesha nia ya dhati ya kuitaka katiba hiyo mpya.
"Nikiambiwa kuna jambo tu kama Makamu wa Rais waambie watanzania, nitasema pambaneni mpate katiba mpya, katiba ambayo ina makubaliano ya wadau wote, katiba yenye muafaka katika taifa, katiba ambayo kila Mtanzania popote alipo atajiskia fahari kujitambulisha mimi natoka Tanzania, katiba inayojali maisha", alisema Dkt. Nchimbi.
Aidha, Dkt. Nchimbi alieleza kwamba, kwa mujibu wa tafiti iliyofanywa na Kamati ya kuandika ilani ya Chama cha Mapinduzi(CCM) 2025, Tume ya Haki Jinai aliyounda Rais Samia pamoja na ripoti ya Tume ya uchunguzi ya Matukio ya Uvunjifu wa Amani yaliyotokea wakati na baada ya uchaguzi (2025), moja ya mambo wananchi wanayataka ni Katiba Mpya huku ikipendekezwa kupatikana kufikia mwaka 2028 ili itumike mwaka 2029 na 2030 ambayo ni miaka ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu. -
Jambo TV
@Jambotv_
Sakata la kisheria linalomkabili mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Melkisedeki Kaijage, limeendelea kuibua mijadala mipana nchini baada ya aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Dkt. Ayub Rioba Chacha, kuibuka na kutoa tahadhari kuhusu usalama wa uhuru wa mawazo na fikra huru katika taasisi za elimu ya juu.
Kauli ya Dkt. Rioba inakuja kutokana na hatua ya mhadhiri huyo kutuhumiwa kufanya kosa la ugaidi, hatua inayowafanya wadau wa haki za binadamu na wanazuoni kufuatilia kwa karibu mwenendo wa shauri hilo.
Katika andiko lake alilolitoa kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii, Dkt. Rioba amefafanua kuwa ingawa hana uhakika wa kina kuhusu maudhui ya tuhuma zinazomkabili mhadhiri huyo wa UDOM, taifa halipaswi kuruhusu hali hiyo ya kujenga hofu inayoweza kuminya fikra huru.
"Sina uhakika na aina ya maudhui ya mhadhiri wa UDOM anayetuhumiwa kwa 'ugaidi', lakini ninashawishika kusema, kama Taifa, tusijiruhusu kufika huko! Tutakuwa Taifa la watu wajinga sana tukifika pahala tukadhani uhuru wa kufikiri, kuhoji na kukosoa unamilikiwa na watu fulani!" ameandika Dkt. Rioba.
Mwanahabari huyo mkongwe na msomi amesisitiza kuwa jukumu kuu la elimu ya chuo kikuu ni kuwajengea uwezo wa kutafakari kwa kina wale wanaosoma. Ameongeza kuwa, mchakato huo wa kitaaluma lazima ufanyike kwa misingi ya kisomi na siyo vinginevyo.
Hata hivyo, Dkt. Rioba amenyoosha kidole pia kwa upande wa wanazuoni akieleza kuwa endapo uchambuzi au utoaji wa taarifa unafanyika kwa mfumo wa harakati zisizo na tafakuri sahihi, nayo inakuwa ni changamoto nyingine.
Akihitimisha hoja yake, Dkt. Rioba ameeleza msimamo wake wa kutosimamia au kuunga mkono hatua yoyote inayolenga kudidimiza uhuru wa kutoa maoni, akitaja kuwa uhuru huo ndio nguzo kuu ya mfumo wa kidemokrasia.
"Siamini kabisa katika jitihada zozote za kufifisha uhuru wa mawazo au maoni katika demokrasia na haswa katika vyuo vikuu," ameandika.
Ikumbukwe kuwa Kaijage alikamatwa 8 Julai 2026 kwa tuhuma za uchochezi wa maandamano ya umma ya tarehe 7 Julai, kosa ambalo awali alinyimwa dhamana. Kutokana na hatua hiyo, Chama cha Wanataaluma cha Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOMASA) kiliwasilisha maombi mahakamani kuomba apewe dhamana, ambapo shauri hilo lilisikilizwa Jumanne, tarehe 21 Julai 2026. Baada ya usikilizwaji huo, Mahakama ilitoa miongozo iliyomwezesha Mhadhiri Kaijage kukidhi vigezo vya kupata dhamana.
Hata hivyo, wakati mawakili wa utetezi na viongozi wa UDOMASA wakiwa katika mchakato wa kutekeleza amri hiyo ya mahakama ili kumtoa nje kwa dhamana, hati yake ya mashtaka ilibadilishwa na kusomewa mashtaka mapya ya ugaidi ambayo hayana dhamana. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) @InvestTanzania imewahimiza wawekezaji kutumia fursa zilizopo Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya, ikisema eneo hilo lina uwezo mkubwa wa kuendeleza viwanda vya kuongeza thamani ya mazao ya kilimo yanayozalishwa kwa wingi.
Akizungumza wilayani humo, Meneja wa TISEZA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Fidelis Obanga amesema mamlaka hiyo imeanza kutoa elimu kwa wawekezaji wanaojihusisha na uzalishaji na usafirishaji wa bidhaa nje ya nchi ili wajisajili rasmi na kunufaika na vivutio vinavyotolewa na Serikali.
Obanga amesema Rungwe ni miongoni mwa wilaya zenye fursa nyingi za uwekezaji kutokana na uzalishaji mkubwa wa mazao ya biashara na chakula, huku akitaja parachichi, kakao, chai, ndizi na tangawizi kuwa mazao yenye uwezo mkubwa wa kuongeza thamani kupitia viwanda vya uchakataji.
Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya Kilimo na Uvuvi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe, Adam Salumu, amesema pamoja na wilaya hiyo kuwa miongoni mwa wazalishaji wakubwa wa parachichi nchini, bado kuna upungufu wa viwanda vya kuchakata mazao hayo pamoja na mazao mengine ya kilimo.
Amesema Serikali ya Wilaya imetenga maeneo kwa ajili ya uwekezaji na inaendelea kuwakaribisha wawekezaji watakaowekeza katika viwanda vya uchakataji ili kuongeza thamani ya mazao na kuwainua wakulima kiuchumi.
Naye Meneja wa Kampuni ya Kuza African Limited, Noel Kabuje, amesema kampuni hiyo imeendelea kutoa soko la uhakika kwa wakulima wa parachichi kwa kununua mazao yao na kuchangia maendeleo ya uchumi wa eneo hilo.
Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo wamesema uwekezaji huo umesaidia kuongeza ajira na kuwapatia vijana ujuzi wa kutumia mashine za kisasa za uchakataji wa mazao, jambo linalowajengea uwezo wa kujiajiri na kuongeza kipato.
Aidha, Afisa Kilimo kutoka COPRA, Majaliwa Mwalembe, amesema taasisi hiyo inaendelea kujenga vituo vya kukusanyia na kuuzia parachichi katika Halmashauri za Rungwe na Busokelo ili kurahisisha upatikanaji wa mazao kwa wawekezaji na kuboresha masoko kwa wakulima.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tabora, kimeitaka Serikali kutoa majibu juu ya mustakabali ya bei ya Tumbaku kushuka, hali ambayo imekua ikisababisha wakulima wa zao hilo kutokuona tija ya Kilimo kutokana na gharama za uzalishaji kuwa ni kubwa, tofauti na bei wanayoikuta sokoni.
Maagizo hayo ya Chama yametolewa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tabora, Said Nkumba, jana Julai 24, 2026 akiongozana na Kamati ya siasa CCM Mkoa, wakati wa ukaguzi wa miradi ya maendeleo Wilayani Kaliua ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Chama hicho kwa kipindi cha Miezi 6 .
Nkumba, ameitaka Serikali kuona namna bora ya kuhakikisha Wakulima kujua bei ya zao hilo kabla ya kuanza kwa masoko, ili kumpa urahisi mkulima wa kujiandaa vyema na msimu mpya wa kilimo
"Tumeelekeza kwamba Serikali lazima ije na majibu na baadhi ya maelekezo tunataka sasa utaratibu ubadilike, badala ya wakulima wetu kwenda sokoni wakiwa hawajui bei ya Tumbaku tunataka wajue bei " Nkumba alisemaThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi ya CCM na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), Rajabu Maganya, amesema mchakato wa Katiba Mpya ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2030.
Maganya amesema mchakato huo hauwezi kukamilika ndani ya mwaka mmoja, lakini ameeleza kushangazwa na baadhi ya vyama vya siasa na watu wanaohamasisha wananchi kupigania Katiba Mpya kana kwamba imezuiwa.
"Ni nani aliyezuia Katiba Mpya? Ni nani amesema hakutakuwa na Katiba Mpya?" amehoji Maganya, akisisitiza kuwa Serikali na CCM hazijawahi kutangaza kuwa mchakato huo hautafanyika.
Maganya ametoa kauli hiyo leo, Julai 24, 2026, jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika eneo la Sinza, Wilaya ya Ubungo.
Kauli yake imeibua mjadala miongoni mwa Watanzania, ikitolewa siku ambayo Makamu wa Rais Dkt. Emmanuel Nchimbi, pia alizungumzia suala la Katiba Mpya wakati wa Mkutano Mkuu wa 15 wa wanachama wa watetezi wa haki za binadamu uliofanyika leo, Julai 24, 2026.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Jumla ya watu 17 wakiwamo viongozi 7 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) @ChademaTZ2 Kanda ya Serengeti pamoja na wanachama wengine wa chama hicho, wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Shinyanga wakikabiliwa na mashitaka yanayohusu ugaidi, siku ya Ijumaa, Julai 24, 2026.
Miongoni mwa viongozi waliopandishwa kizimbani ni pamoja na Jackson Mnyawami (Katibu wa CHADEMA Kanda ya Serengeti), Hamis Ngunila (Mwenyekiti wa CHADEMA Jimbo la Shinyanga Mjini), na Salum Mwinyi (Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa CHADEMA - BAZECHA Wilaya ya Kahama), huku wengine wanne wakiwa ni viongozi wa chama hicho ngazi ya kata mkoani humo.
Washitakiwa hao wamegawanywa katika makundi mawili ambapo kundi la kwanza linamjumuisha Jackson Mnyawami, Daniel Emmanuel Athumani, na Jackson Venant Kabyeseleza. Hawa wanatuhumiwa kupanga kutenda kosa la ugaidi kwa kuuchochea umma kufanya maandamano mnamo Julai 7, 2026.
Kundi la pili lina watu 14 wanaotuhumiwa kwa kosa la kula njama za kutenda ugaidi. Wanaoshitakiwa katika kundi hili ni Godwine Laurent, Johnson Paul Michael, Joseph Isack Ongoro, Edwin Otieno Ongito, Jabari Abdul Sharifu, Sengiyumba Sadiki, Boniphace Kwini Kasuluba, Hussein Marijani Hamidu, Mohamed Shaban Nkimani, Mwinyi Salum Kulyengana, Omary Ally Ng'haniga, Maulid Ramadhan, Hamisi Ngunila, pamoja na Mhebi Charles Yoyo.
Kiini cha mashitaka hayo kinatokana na madai ya upande wa Jamhuri kuwa washitakiwa walihamasisha na kupanga maandamano yasiyo halali mnamo tarehe 7 Julai, 2026, kitendo kinachodaiwa kilihatarisha usalama wa nchi.
Akizungumza na Jambo TV, Wakili Alex Massaba ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria na Haki za Binadamu wa CHADEMA Kanda ya Serengeti, ameelezea mazingira ya kukamatwa kwa baadhi ya washitakiwa kuwa ni ya kusikitisha. Alitolea mfano wa Mzee Salum Mwinyi aliyekamatwa akiwa njiani kwenda kumdhamini mfanyabiashara mwenzake, na Mnyawami ambaye alikamatwa alipokwenda kuripoti kwa Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa (RCO) Shinyanga kwa jambo lingine. Aidha, Wakili Masaba amedai kuwa mashitaka hayo yana lengo la kuwakomoa viongozi wa kisiasa wa chama hicho badala ya kutafuta haki.
Kwa kuwa Mahakama ya Wilaya haina mamlaka ya kusikiliza kesi za aina hiyo, washitakiwa wote wamepelekwa katika Gereza la Shinyanga hadi tarehe 4 Agosti, 2026, kesi itakapotajwa tena.
Wakati huo huo, mtuhumiwa mwingine ambaye ni Fredy Masanja, Mwenyekiti wa Baraza la Vijana CHADEMA (BAVICHA) Wilaya ya Shinyanga, naye alirejeshwa mahabusu bila kusomewa mashitaka baada ya kubainika kuwa Hati yake ya Mashitaka ilikuwa na makosa ya kiufundi. -
Jambo TV
@Jambotv_
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uhispania Fernando Grande-Marlaska ametangaza hali ya dharura ya kitaifa katika mji wa Madrid na mkoa wa Avila, kufuatia kusambaa kwa kasi kwa moto wa nyika unaotishia maisha na makazi ya wananchi.
Kulingana na taarifa ya shirika la utangazaji la RTVE ya Julai 24, 2026, dharura hiyo inahusisha maeneo ya Villa del Prado na San Martin de Valdeiglesias huko Madrid, pamoja na Burgohondo katika mkoa wa Castilla na Leon.
Wizara ya Mambo ya Ndani nchini humo imeeleza kuwa uamuzi huo umetokana na mambo matatu ambayo ni kuwaka kwa moto kwa wakati mmoja katika maeneo tofauti tofauti, hali mbaya ya hewa, na uhitaji wa dharura wa nguvu ya uokoaji kutoka idara mbalimbali za serikali.
Mamlaka zimebainisha kuwa hali hiyo ni mbaya zaidi kutokana na kwamba moto uliowaka maeneo tofauti tofauti haujadhibitiwa na moto huo unatajwa kuchochewa na upepo mkali.
Taarifa zinaeleza kwamba zaidi ya watu elfu kumi wameondolewa kutoka miji ya Villa del Prado, San Martin de Valdeiglesias, Pelayos de la Presa, na Aldea del Fresno. Viongozi wa mikoa hiyo wameonya kuwa moto huo unaweza kuendelea kusambaa kwa kasi bila kuzimika.
Hata hivyo Uhispania inapitia msimu mgumu wa moto wa nyika unaochochewa na ukame, upepo mkali, na viwango vikubwa vya joto. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Afya, Mohammed Mchengerwa amesema Watanzania watamkumbuka Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa mambo mengi baada ya kutoka madarakani.
Amesema hayo Julai 23, 2026 alipokuwa kwenye ziara ya kikazi mkoani Kilimanjaro ambapo ameeleza kuwa kutokana na kazi kubwa anayoifanya Dkt. Samia, uzalendo wake na mazingira wezeshi ya biashara hayo yatawafanya watu wamkumbuke.
Amekumbusha kuwa baada ya Marais waliopita kutoka madarakani watu wamekuwa wakiwakumbuka na ndivyo itakavyotokea baada ya Dkt. Samia kumaliza muda wake.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Andrew, amesema uzinduzi wa mfumo mpya wa utambuzi wa wafanyabiashara wilayani Temeke utasaidia kutatua changamoto ambazo wafanyabiashara wamekuwa wakizipitia, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha udhibiti katika upotevu wa mapato.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Julai 24, 2026, amesema kutokana na kukosekana kwa mfumo huo, imepelekea wafanyabiashara wengi wa Wilaya ya Temeke kufilisika na kutokujua fursa mbalimbali ambazo zipo.
"Sisi kama jumuiya ya wafanyabiashara, leo tunatambulisha rasmi mfumo wetu mpya wa Jumuiya mpya ya Wafanyabiashara wa Temeke, ambao wafanyabiashara wengi tunashauri wajiunge nao ili kuepukana na changamoto ambazo tumeziona," amesema Andrew.
Ameongeza kuwa mfumo huo utasaidia kuimarisha ukusanyaji wa mapato, kudhibiti utapeli, pamoja na kuwawezesha wafanyabiashara kukuza mitaji yao.
Kwa upande wake, Afisa Viwanda na Biashara wa Manispaa ya Temeke, Ramadhan Gurumukwa, amesema mfumo huo utarahisisha Serikali kuwafikia wafanyabiashara na kuwapatia huduma mbalimbali muhimu kwa ajili ya maendeleo ya biashara zao na uchumi wa taifa kwa ujumla.
Naye Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Wilaya ya Kinondoni, Godfrey Mtei, amesisitiza kuwa mfumo huo utakuwa muhimu katika kuimarisha ushirikiano kati ya serikali na sekta binafsi, kwa lengo la kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wafanyabiashara nchini.
Aidha, uzinduzi rasmi wa mfumo huo unatarajiwa kufanyika Julai 27 mwaka huu, ambapo Waziri wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega amesema kazi ya ujenzi wa barabara inayoendelea nchini kote ina lengo la kuifungua Tanzania kwa kuiunganisha na jirani zake.
Akizungumza katika maeneo tofauti mkoani Kagera wakati wa ziara ya ukaguzi wa miradi ya ujenzi wa miundombinu ya barabara inayoendelea mkoani humo, Ulega amesema lengo la Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha kwamba hakuna eneo linaloachwa nyuma kimaendeleo kwa sababu ya kutofikika.
“Naomba niwaeleze leo kwamba tunajenga barabara hizi ili kuhakikisha kwamba hakuna mkoa au eneo linaachwa nyuma kwa sababu halijaunganishwa na wengine. Na tunaposema wengine hatumaanishi Watanzania tu bali na majirani zetu pia,” amesema.
Waziri huyo ameyasema hayo wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Rusahunga – Rusumo ambayo inaunganisha Tanzania na nchi za Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).
Ujenzi wa barabara hiyo ulioanza Julai 2023, umeigharimu serikali kiasi cha shilingi bilioni 210 na ujenzi wake sasa umefikia asilimia 73. 9.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika tukio hilo, baadhi ya wananchi na viongozi mkoani Kagera walisema ujenzi wa barabara hiyo utapunguza kero, usumbufu na muda wa kusafiri uliokuwa ukitumika katika siku za nyuma.
Kwa mfano, Mbunge wa Ngara, Doto Bahemu, alikumbusha namna alivyowahi kulala barabarani baada ya gari lake kupasuka matairi usiku wakati akielekea kijijini kwake kutokana na ubovu wa barabara.
“Binafsi sina maneno ya kutosha kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa barabara hii. Zamani mtu ukitoka Dar kuja Ngara ulikuwa ukifika hapa Rusahunga ndiyo inakuwa kama umeanza safari upya. Tunaishuru sana serikali kwa barabara hii,” alisema.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu wa Rais wa Tanzania Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amewataka watanzania kuongeza juhudi kupambania katiba mpya katika wakati huu ambapo Rais Samia Suluhu Hassan ameonesha nia ya dhati ya kuitaka.
Dkt. Nchimbi ameeleza kuwa huu ni wakati sahihi kwani Rais anayefuata huenda asiitake katiba mpya(kama haijapatikana) kutokana na hii iliyopo kuwa inampa mamlaka makubwa.
Dkt. Emmanuel Nchimbi amesema hayo leo Julai 24, 2026 akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania @thrdcoalition unaofanyika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi ameeleza kuwa anatamani kumtambua mwanaharakati yeyote kwa uwezo wake wa kufikiri na kushawishi akisisitiza kuwa anatamani pia kujenga taifa ambalo watu wenye mitazamo tofauti wanaweza kukaa pamoja na kuzungumza mambo ya nchi yao kwa amani, bila kuwepo kwa uhasama au uadui.
Dkt. Nchimbi ameeleza matamanio hayo akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) unaofanyika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, leo Julai 24, 2026, Dkt. Nchimbi
Aidha, ametoa wito kwa kila Mtanzania kutumia nafasi aliyonayo kurudisha umoja na mshikamano, pamoja na kusimamia haki kama msingi wa amani.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
"Nikiambiwa kuna jambo tu kama Makamu wa Rais waambie Watanzania, nitasema pambaneni mpate katiba mpya, katiba ambayo ina makubaliano ya wadau wote, katiba yenye muafaka katika taifa, katiba ambayo kila Mtanzania popote alipo atajiskia fahari kujitambulisha mimi natoka Tanzania, katiba inayojali maisha", - Dkt. Nchimbi.
Hayo ameyasema Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi leo Julai 24, 2026 akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania @thrdcoalition unaofanyika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amebainisha kuwa ni vigumu kwa mtetezi wa amani kuwa adui wa haki, au mtetezi wa haki kuwa adui wa amani, kwani mambo haya mawili yanategemeana.
Akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania @thrdcoalition unaofanyika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, leo Julai 24, 2026, Dkt. Nchimbi amewahimiza Watanzania kuacha kuogopa kutamka neno haki kwa sababu maneno yanazaa matendo ya kuitekeleza haki hiyo
Dkt. Nchimbi ameeleza kuwa anatamani kuona Tanzania ambapo kila mwananchi anajisikia fahari ya Utanzania wake, amani, na usalama akiwa ndani ya nchi yake. Amesema ingawa kuna utofauti wa itikadi za kisiasa, dini, na makabila, ni muhimu Watanzania watambuane kwa utaifa wao kwanza ili kila mmoja awe na hamu ya kuchangia maendeleo ya nchi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mbunge wa Jimbo la Ngara mkoani Kagera, Dotto Bahemu, ameelezea maumivu na changamoto kubwa ambazo wananchi wa jimbo hilo wamekuwa wakipitia kutokana na ubovu wa barabara ya Lusahunga–Rusumo.
Bahemu ameyasema hayo wakati wa ziara ya Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega aliyoifanya wilayani Ngara kwa ajili ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 92.
Ameeleza kuwa ubovu wa miundombinu hiyo umekuwa kero na shubiri kubwa kwa wananchi wa Ngara na wasafiri wengine wanaotumia njia hiyo, ambapo mara kadhaa umesababisha vifo, uharibifu wa vyombo vya usafiri, pamoja na wasafiri kulazimika kulala njiani.
Kwa upande wake, Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega amesema ujenzi wa barabara hiyo unaoendelea ni sehemu ya juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuendelea kuwekeza katika maboresho ya miundombinu ili kuhakikisha maeneo yote nchini yanafikika kwa urahisi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania (MISA-TAN), Edwin Soko, amesema mabadiliko yoyote katika nchi hayachochewi kwa nguvu ya watetezi wa haki za binadamu pekee bali hutokana na nguvu ya umma.
Ameeleza hayo Julai 24, 2026 jijini Dar es Salaam wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) ambapo amesema nguvu ya umma si kwa maana ya kuandamana tu bali katika kujenga hoja. Amesema ipo haja ya kujikita zaidi kuwekeza kwa jamii ili ielewe kwa kina kuhusu haki za binadamu.
Amesema ikiwa uwekezaji utafanyika katika kuwawezesha watu kujua haki za binadamu, kazi ya watetezi wa haki za binadamu itakuwa ndogo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Victoria, Zakaria Obad amesema uwepo wa kesi za ugaidi nchini unachafua taswira ya taifa kimataifa hivyo kuitaka Serikali kuziangalia upya uwepo wa kesi za ugaidi zinazofunguliwa.
Akizungumza leo mara baada ya kutoka kusikiliza kesi ya washtakiwa 23 wakiwemo wanachama na viongozi wa Chadema ngazi ya kata na shina kutoka Wilaya ya Ilemela na Nyamagana mkoani Mwanza waliosomewa kosa la kufanya vikao au mazungumzo yanayolenga kufanya ugaidi.
Obad amesema kesi hizo kesi za ugaidi hazina afya kwa taifa hali ambayo inaweza kusababisha watu kutoka nje ya nchi kuona Tanzania siyo sehemu salama ya kuishi.
Akizungumzia viongozi wao waliokamatwa, Obad amesema viongozi ngazi ya kata na shina waliokamatwa kutoka Wilaya ya Ilemela ni wanne na Wilaya ya Nyamagana wanne.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Wananchi wa Kata ya Naalarami, Wilaya ya Monduli mkoani Arusha wameendelea kukabiliwa na changamoto kubwa ya uhaba wa maji, hali inayowaathiri katika shughuli za kila siku na huduma muhimu za kijamii. Wakati wa ziara ya Mbunge wa Jimbo la Monduli, Isack Joseph, wanawake walimpokea wakiwa na ndoo tupu kuashiria ukubwa wa tatizo hilo.
Uhaba huo wa maji umeathiri pia sekta ya afya, ambapo zahanati iliyokamilika katika eneo hilo imeshindwa kuanza kutoa huduma kutokana na kukosekana kwa maji.
Akizungumza na wananchi, Mbunge Isack Joseph ameahidi kuwa Kata ya Naalarami itaunganishwa kwenye mradi wa maji wa vijiji 13 na kusisitiza kuwa atafuatilia utekelezaji wake hadi ukamilike.
Kwa mujibu wa mbunge huyo, mabomba ya mradi wa maji wenye thamani ya Shilingi bilioni 21 yanatarajiwa kuanza kupokelewa Julai 27 katika chanzo cha maji cha Ngaramtoni, Wilaya ya Arumeru, hatua inayotarajiwa kuharakisha utekelezaji wa mradi huoThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Wananchi wa Mtaa wa Bomba la Bure, Kata ya Magomeni Manispaa ya Mtwara Mikindani mkoani Mtwara, wamelalamikia changamoto ya kuziba kwa mfereji uliopo katika mtaa huo huku wakisema hali hiyo imekuwa ikihatarisha afya zao na mazingira ya makazi.
Baadhi ya wananchi, akiwemo Mwajuma Rashid na Maria Thomas wamesema mfereji huo umekuwa umeziba kwa muda mrefu na kusababisha maji kutuama, hali inayozalisha harufu mbaya na wadudu. Aidha, wameeleza kuwa kipindi cha masika maji huingia kwenye makazi yao na kusababisha usumbufu mkubwa.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Bomba la Bure Athumani Jumbe, amesema chanzo kikuu cha kuziba kwa mfereji huo ni baadhi ya wananchi kutupa taka ovyo, jambo linalosababisha mitalo kuziba na kuongeza kuwa Serikali tayari imetenga Shilingi milioni tatu kwa ajili ya kukarabati miundombinu hiyo.
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara Mikindani, Gwakisa Mwasyeba amesema mfereji huo hupitisha maji kutoka maeneo mbalimbali, hivyo ukarabati wake ni muhimu ili kupunguza changamoto hiyo.
Ameongeza kuwa mbali na Shilingi milioni tatu zilizotolewa kwa ukarabati wa mfereji huo, Serikali kupitia Mwaka wa Fedha 2026/2027 imetenga zaidi ya Shilingi milioni 150 kwa ajili ya kukarabati mifereji iliyoharibika katika maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Mtwara Mikindani.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, ametangaza msako mkali dhidi ya madanguro na vitendo vya ukiukwaji wa maadili, akisisitiza kuwa Serikali haitavumilia mtu yeyote anayehusika na biashara hizo au kuwatumia watoto katika vitendo vya unyanyasaji.
Mpogolo aliyasema hayo jana Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na wananchi, ambapo pia alilipongeza Jeshi la Polisi kwa hatua za haraka walizochukua kuwakamata watuhumiwa wa vitendo hivyo.
Alisema taarifa zilizopo zinaonesha kuwa katika Kata ya Zingiziwa kulikuwa na mtu anayeshukiwa kuwatumia watoto wa kike kuwachezesha wakiwa uchi kwa malipo ya kati ya Shilingi 3,000 na 5,000, jambo alilosema ni ukatili mkubwa na ukiukwaji wa maadili ya jamii.
Kwa mujibu wa Mpogolo, mtuhumiwa huyo tayari amekamatwa na Jeshi la Polisi, huku uchunguzi ukiendelea. Amewataka wananchi kutoshawishiwa kumtetea mtu yeyote anayekabiliwa na tuhuma hizo kabla ya sheria kuchukua mkondo wake.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Beno Malisa amesema Mkoa wa Mbeya unaendelea kuimarika kiuchumi, ukiwa na fursa nyingi za uwekezaji katika sekta mbalimbali, na kuwakaribisha wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kutumia mazingira mazuri yaliyopo kuwekeza.
Akizungumza mkoani humo 23 Julai 2026 katika kikao maalumu na waandishi wa habari kilichoandaliwa na Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) kwa lengo la kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo mkoani Mbeya, Malisa amesema shughuli za uzalishaji zinazofanywa na wananchi hazitakuwa kikwazo kwa uwekezaji, bali zitaenda sambamba na maendeleo ya uwekezaji.
Alibainisha kuwa Mkoa wa Mbeya una fursa nyingi katika sekta za kilimo, madini, mifugo, uvuvi, viwanda na maendeleo ya miundombinu, ambazo zinaweza kuchochea ukuaji wa uchumi na kuongeza ajira kwa wananchi.
Malisa pia ametaja maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya uwekezaji, ikiwemo Tanganyika Packers, Halmashauri ya Wilaya ya Chunya, Halmashauri ya Jiji la Mbeya, Mbeya University of Science and Technology (MUST) pamoja na College of Business Education (CBE) – Kampasi ya Mbeya, akisisitiza kuwa Serikali ya Mkoa itaendelea kushirikiana na TISEZA kuhakikisha wawekezaji wanapata mazingira rafiki ya kuanzisha na kuendeleza miradi yao.
Kwa upande wake, Mkuu wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini wa TISEZA, Bw. Fedilis Obanga amesema ofisi ya TISEZA katika kanda hiyo imekuwa kiungo muhimu katika kuhamasisha uwekezaji, kutoa huduma za ushauri na kuwezesha wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kutekeleza miradi yao kwa ufanisi.
Amesema TISEZA imeendelea kushirikiana kwa karibu na Serikali, sekta binafsi na wadau mbalimbali katika kutambua, kuendeleza na kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo, sambamba na kuwasaidia wawekezaji katika hatua zote za uwekezaji kuanzia utoaji wa taarifa, usajili wa miradi hadi utekelezaji wake.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Washtakiwa 23 wakiwemo viongozi wa ngazi ya chini wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wamefikishwa mahakamani na kushtakiwa katika kesi mbili tofauti zenye kosa moja la kujihusisha na vikao au mazungumzo yanayolenga kufanya ugaidi.
Kesi hizo mbili zimesikilizwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanza, Naibu Msajili Erick Marley ambapo katika kesi ya kwanza namba 16379/ 2026 imewahusisha washtakiwa 13 kutoka Wilaya ya Ilemela ambao wanatuhumiwa kufanya kosa hilo kati ya Juni 25 hadi Julai 7, 2026.
Washtakiwa hao ni Alphaxadi Nyamwaga, Fantson Mpango, Abely Mwesa, Hassan Said, Emanuel Wambura, Adam Idd, Damas Sadock, Petro Mabula, Abdul Kagwidi, Devid Mashaka, Philipo Masatu, Edward Mikindo na Emmanuel Doto.
Katika kesi ya pili namba 16375/2026 imewahusisha washtakiwa 10 kutoka Wilaya ya Nyamagana ambapo wanatuhumiwa kufanya vikao hivyo kati ya Julai 4 na Julai 7 mwaka huu katika eneo la Igoma.
Washtakiwa hao ni Deus Masalago, Mohamed Tosha, Fabian Nguvumali, Samweli Mtani, Samweli Kobell, Julius Makonga, Fanuel Lutana, Philipp Kulwa, Philipp Shipuluko na Hamis Mnyimvua.
Kwa pamoja washtakiwa hao 23 wanatuhumiwa kufanya vikao hivyo vyenye lengo la kufanya ugaidi vikiwa na lengo la kupanga kuchoma majengo ya binafsi na Serikali Julai 7, 2026 ili kuleta hofu kwa wananchi.
Akizungumza mara baada ya kutoka mahakamani Wakili wa Upande wa Utetezi, Erick Mutta amesema kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na uwezo wa kusikiliza kesi hiyo, washtakiwa wamerudishwa rumande mpaka Agosti 6, itakaposikilizwa tena.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Watu watatu wa jinsi ya kiume wamefariki dunia kwa kujinyonga katika matukio tofauti yaliyotokea wilayani Moshi, mkoani Kilimanjaro, akiwamo Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kotela Mashariki, Lamecky Matowo (57).
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, SACP Simon Maigwa, amethibitisha kutokea kwa matukio hayo leo tarehe 23 Julai 2026, akibainisha kuwa uchunguzi wa awali unaonesha matukio hayo yameshochewa na changamoto za afya ya akili na msongo wa mawazo.
Kamanda Maigwa ameeleza kuwa Mwenyekiti Matowo alikutwa amejinyonga kwa kutumia kamba ya manila aliyofunga kwenye mti uliopo shambani kwake.
Mbali na kiongozi huyo, wengine waliofariki ni Frank Makundi (54); fundi ujenzi na mkazi wa Kijiji cha Komakundi, Kata ya Mamba Kaskazini, na Januari Hussein (30); dereva wa pikipiki za abiria (bodaboda) na mkazi wa Kimaroroni.
Akifafanua kuhusu nyakati na visababishi vya vifo hivyo, Kamanda Maigwa amesema matukio mawili yalitokea tarehe 22 Julai na jingine lilitokea tarehe 21 Julai 2026 na kwamba uchunguzi wa awali umebaini kuwa Matowo alichukua uamuzi huo kutokana na changamoto ya afya ya akili. Kwa upande wa Makundi, naye alijinyonga kutokana na msongo mkubwa wa mawazo uliotokana na msiba wa mtoto wake aliyefariki miezi miwili iliyopita.
Jeshi la Polisi limeeleza kuwa uchunguzi bado unaendelea kubaini chanzo kamili cha kifo cha Januari Hussein, huku likitoa rai kwa jamii kutafuta msaada wa kisaikolojia wanapokabiliwa na changamoto za afya ya akili badala ya kuchukua maamuzi yanayogharimu maisha yao. -
Jambo TV
@Jambotv_
Sakata linalomkabili mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Melkisedeki Kaijage, limechukua mwelekeo mpya baada ya Upande wa Mashtaka kubadilisha mashtaka yake na kumpa mashtaka ya ugaidi, chombo cha habari cha The Citizen kimeripoti.
Kaijage amekuwa mikononi mwa Jeshi la Polisi tangu tarehe 8 Julai 2026, alipokamatwa kwa mara ya kwanza kwa tuhuma za uchochezi wa maandamano ya umma ya tarehe 7 Julai, kosa ambalo awali alinyimwa dhamana.
Kutokana na hatua hiyo, Chama cha Wanataaluma cha Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOMASA) kiliwasilisha maombi mahakamani kuomba apewe dhamana, ambapo shauri hilo lilisikilizwa Jumanne, tarehe 21 Julai 2026. Baada ya usikilizwaji huo, Mahakama ilitoa miongozo iliyomwezesha Mhadhiri Kaijage kukidhi vigezo vya kupata dhamana.
Hata hivyo, wakati mawakili wa utetezi na viongozi wa UDOMASA wakiwa katika mchakato wa kutekeleza amri hiyo ya mahakama ili kumtoa nje kwa dhamana, hati yake ya mashtaka ilibadilishwa na kusomewa mashtaka mapya.
Mwenyekiti wa UDOMASA, Dkt. Gerald Shija, amethibitisha kuwa mhadhiri huyo sasa anakabiliwa na kosa la ugaidi ambalo halina dhamana kisheria na tayari amehamishwa kutoka mahabusu ya polisi na kupelekwa katika Gereza Kuu la Isanga mjini Dodoma. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) @THRDCOALITION umeendesha mafunzo ya kujenga uwezo kwa Asasi za Kiraia na watetezi wa haki za watoto juu ya namna bora ya ufuatiliaji, uandishi wa ripoti na utoaji wa taarifa za ukiukwaji wa haki za watoto na uendelezaji wa haki kwa watoto katika mfumo wa haki jinai nchini Tanzania.
Akizungumza na wanahabari mkoani Dar es Salaam leo Alhamisi Julai 23, 2026, Mratibu Kitaifa wa THRDC, Wakili Onesmo Olengurumwa @OlengurumwaO , amebainisha kuwa nusu ya idadi ya watu nchini ni watoto ambao ndio msingi wa familia na taifa, akisisitiza kuwa uwekezaji kwa watoto unatazamwa kama njia ya kuhakikisha taifa linakuwa na watu wenye tija na nidhamu ambao watalipa kodi na kukuza uchumi hapo baadaye.
Kwa upande wake, Veronica Buchumi, mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) amesema kuwa Tanzania ina sheria nyingi za ulinzi wa mtoto, lakini kuna haja ya kuzipa uhai kwa kuzingatia mazingira tofauti ya jamii ambazo sheria hizo zinafanya kazi. Amesisitiza kuwa kila mtu mwenye wajibu wa kusimamia haki za watoto anapaswa kujua nafasi yake ili hatua stahiki zichukuliwe pindi ukiukwaji unapotokea.
Naye, Zachayo Shigongo, mhadhiri kutoka Taasisi ya Ustawi wa Jamii, ameelezea kuwa masuala ya haki za mtoto yanagusa maeneo yote ya maisha ya mwanadamu (kijamii, kiuchumi, na kisiasa). Kwa sababu hiyo, utetezi wa haki za watoto haupaswi kuwa jukumu la mtu mmoja au taasisi moja, bali unahitaji ushirikiano wa wadau wote, taaluma mbalimbali, na serikali.
Mafunzo haya yamewakutanisha takribani washiriki 100 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar, yakilenga kuimarisha ujuzi wa vitendo katika ufuatiliaji na uandishi wa nyaraka za ukiukwaji wa haki za binadamu, ukusanyaji, uhakiki na utunzaji salama wa ushahidi, utoaji wa taarifa kwa kuzingatia maadili na maslahi bora ya mtoto, mifumo ya rufaa na upelekaji wa mashauri kwenye mamlaka husika, pamoja na utetezi unaotegemea ushahidi. Washiriki pia wataimarisha uelewa wao kuhusu mifumo ya kitaifa, kikanda na kimataifa ya ulinzi wa haki za watoto na misingi ya haki kwa watoto katika mfumo wa haki jinai.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio, amesema gharama ya kijeshi na kiuchumi inayolipwa na Iran kwa sasa itazidi kuongezeka kila usiku hadi viongozi wa nchi hiyo watakapozinduka na kurudi kwenye fahamu zao.
Rubio ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Julai 23, 2026 alipokuwa akizungumza pembezoni mwa Mkutano wa kilele wa mawaziri wa nchi za ASEAN mjini Manila nchini Ufilipino.
Kionngozi huyo amedai kwamba Serikali ya Tehran imekuwa ikituma maombi ya siri ya kutaka mazungumzo ya kusitisha mapigano kupitia mataifa washirika. Hata hivyo, mwanadiplomasia huyo mkuu wa Marekani amesisitiza kuwa serikali ya Iran haiko tayari kufikia makubaliano thabiti kwa sasa.
Waziri huyo amehitimisha kwa kuonya kuwa operesheni na mashambulizi ya anga ya jeshi la Marekani (CENTCOM) yataendelea kulenga miundombinu ya makombora na rada za Iran hadi pale taifa hilo litakapobadili msimamo wake wa kijeshi. -
Jambo TV
@Jambotv_
Shauri la Kikatiba Na. 7300/2026 lililofunguliwa na Mawakili Kulwa William Maduhu, Nashon Nkung na Paul Kisabo dhidi ya Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini (CGP), Mkuu wa Gereza Ukonga, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na Tundu Lissu limeendelea leo, Alhamisi tarehe 23/07/2026, Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu Dodoma inayoketi vikao vyake kwenye Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam
Shauri hilo linalosikilizwa na jopo la Majaji watatu (3) wakiongozwa na Jaji Amir Mruma limekuja Mahakamani hapo leo mahsusi kwaajili ya shahidi pekee wa Jamhuri, Mkuu wa Gereza Ukonga ACP Andrew Shaban N'tamamiro kuendelea kuhojiwa maswali ya dodoso (cross examination) kutoka kwa wadaawa wengine, baada ya mjibu maombi wa Nne (4) kwenye shauri hilo Tundu Lissu kumaliza kuhoji maswali yake jana, tarehe 22/07/2026
Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) ambao ni wadaawa wenye maslahi kwenye shauri hilo jopo lao uwakilishi limeongozwa na Wakili Emmanuel Ukashu, ambapo katika maswali yake ya dodoso alianza kwa kumuuliza shahidi huyo ambaye kimsingi ni mjibu maombi wa pili (2) kwenye shauri hilo kwamba katika utumishi wake wa miaka 31 ndani ya Jeshi la Magereza anafahamu kitu gani kuhusu TLS?, shahidi huyo alijibu kuwa amekuwa akisia tu
Alipoulizwa endapo anafahamu au hafahamu kama waleta maombi wote watatu (3) kuwa ni Mawakili, shahidi huyo alijibu kuwa ni sahihi, hata hivyo alipoulizwa swali kama hilo kuhusu mjibu maombi wa Nne (4) ambaye ni Tundu Lissu, shahidi alisema hajuwi
Wakili Emmanuel Ukashu alienda mbali zaidi na kumuuliza shahidi huyo endapo anafahamu au hafahamu kuwa mjibu maombi wa Nne (4) Tundu Lissu amewahi kuwa Rais wa TLS kwa kipindi cha mwaka mmoja (2017/18), na kwamba hata hivyo alishindwa kukamilisha kipindi chake cha uongozi kufuatia kushambuliwa kwa risasi mwaka 2017, majibu ya shahidi kwenye eneo hilo yalikuwa ni kwamba hafahamu
ACP Andrew Shaban N'tamamiro, Mkuu wa Gereza Ukonga ambaye kwa ujumla wake ni shahidi wa Nne (4) katika orodha ya mashahidi waliopanda kuzimbani kuhusiana na shauri hilo, aliulizwa pia anaelewa nini anaposikia maneno 'maagizo kutoka juu', na katika majibu yake alieleza kuwa tafsiri ya uelewa wake ni maagizo ya kiutendaji
Hata hivyo alipoulizwa endapo, anaweza kupokea au kukataa maelekezo yanayotoka kwa mabosi zake wa juu ikiwemo Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini (CGP), shahidi huyo alijibu kuwa hawezi kumbishia, hata hivyo alikanusha madai kwamba endapo akibishia anaweza kufukuzwa kazi moja kwa moja kutokana na kile alichoeleza kuwa zipo taratibu za kufuatwa kabla ya maamuzi hayo,
Mapema leo, Mawakili wa waleta maombi John Seka na Edson Kilatu, kwa nyakati tofauti nao walimuohoji maswali ya dodoso shahidi huyo, ambao miongoni mwa maswali waliyomuuliza ni yale yanayohusu maelezo yaliyotolewa na mashahidi waliomtangulia Mahakamani hapo kuhusu sehemu walizofanyia mazungumzo na mteja wao pindi walipoenda kumtembelea gerezani, hoja ambazo hakuzikanusha
Hata hivyo, alipoulizwa mazingira ya namna ya ukaaji kwamba zilikuwa meza tatu za watu wanaoandika, na kwamba Mawakili walilazimika kukaa hapo pia shahidi huyo alijibu 'ndio', hata hivyo alivyotakiwa kukadiria ukubwa wa meza hizo shahidi alisema hajuwi
Alipoulizwa endapo aliwahi kumuona au kumfahamu mleta maombi wa kwanza (1) Kulwa William Maduhu, shahidi alijibu hapana, lakini kuhusu waleta maombi wengine yaani Nashon Nkung na Paul Kisabo aliieleza Mahakama kuwa hao anawafahamu
Alipotakiwa kueleza namna alivyowafahamu watu hao, alijibu kuwa amekuwa akiwaona mara kwa mara wanapokwenda gerezani kumuona mteja wao Tundu Lissu, hata hivyo madai ya kuwahi kukutana na Mawakili hao Ofisini kwake, lakini amekiri kuwa amewahi kukutananao Ofisi ya Bwana Recha na admission office
Alipoulizwa endapo amewahi kuhudhuria mazungumzo baina ya Mawakili hao na mteja wao Tundu Lissu, shahidi huyo alikana, badala yake alikiri kuwa amewahi kuchungulia wanapokuwa wamekaa
Kuhusu suala la maafisa wa Jeshi la Magereza kuwazunguka na kuwasikiliza Lissu na Mawakili wake wakiwa kwenye mazungumzo ya faragha, shahidi huyo alikanusha madai hayo na kuieleza Mahakama kuwa wakati wao wanazungumza askari na wahusika wengine wa Ofisi wanakuwa nje lakini mlango wa chumba wanachotumia kwa mazungumzo unakuwa wazi ili waweze kuwaona, na si kuwasikia
Baada ya kukamilika kwa maswali ya dodoso (cross examination), Mahakama ilitoa nafasi kwa Mawakili wa Jamhuri kumuhoji shahidi Re-Examination, zoezi ambalo halikuchukua muda mrefu hadi kukamilika kwake, na kesi hiyo sasa imeahirishwa hadi tarehe 16/09/2026 itakapotajwa tena Mahakamani, huku kipindi cha kati kabla ya tarehe husika pande zote zikiwasiliana kwa maandishi kufuatia mapingamizi yaliyowekwa na waleta maombi
Ikumbukwe kuwa, msingi wa shauri hilo ni waleta maombi ambao wamejitambulisha kuwa ni Mawakili wa Tundu Lissu kulalamikia kuzuiwa na/au kunyimwa faragha ya kuzungumza na mteja wao pindi wanapomtembelea Gerezani jambo ambalo wamedai kuwa ni kinyume cha taratibu, sheria, kanuni na uvunjifu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Msemaji Mkuu wa Serikali ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa, amewataka vijana kuacha kulalamika na badala yake kutumia fursa zilizopo kujikwamua kiuchumi, huku akieleza kusikitishwa na baadhi ya watu wanaowahamasisha vijana kutoa fedha walizonazo kuwapatia wao.
Msigwa amesema hayo jana jijini Dodoma wakati alipotembelea Soko la Machinga Complex na kukutana na wafanyabiashara, ambapo alisisitiza kuwa Tanzania ina fursa nyingi zinazoweza kuwainua vijana kiuchumi ikiwa wataamua kuzitumia ipasavyo badala ya kupoteza muda katika mambo yasiyo na manufaa.
"Tuwasikilize wanaotuelekeza kupata pesa, tusiwasikilize wanaotuelekeza kufanya fujo, mambo ambayo mwisho wa siku hayakupi pesa," amesema Msigwa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Karagwe, Dkt. Benson Bagonza, ametoa tahadhari kwa viongozi na jamii akieleza kuwa taifa linaelekea kuchelewa kupata maridhiano ya kweli.
Kiongozi huyo wa kiroho, ambaye sasa anatimiza mwaka mmoja kama mhadhiri wa somo la Falsafa ya Siasa (Political Philosophy) chuo kikuu, amesisitiza kuwa mbinu za kijanja hazitakiwi katika kuponya nchi. Akifafanua msingi wa uchambuzi wake, Askofu Dkt. Bagonza amebainisha kuwa mezani kwake anazo nyaraka za maridhiano kutoka mataifa yaliyopitia migogoro mbalimbali yakiwemo Afrika Kusini, Rwanda, Kenya, Sierra Leone, Gambia, na Cyprus.
Amesema maridhiano yanakuwa hitaji la lazima pale ambapo "jambo kubwa lisilo la kawaida" linapotokea na kuigawa nchi kwa vitendo vyenye sura ya jinai kubwa, ambavyo visiposuluhishwa kikamilifu vinakwamisha ustawi wa taifa.
Katika uchambuzi wake huo wa kitaalamu na kitaifa, Askofu Bagonza amebainisha faida nne kuu za maridhiano ambapo ya kwanza ni kuwa njia ya kuanza upya baada ya kukosea, ambapo pande husika zinakiri makosa na kuomba kuanza ukurasa mpya. Faida ya pili ni kujifunza "kushindwa" na kukubali sauti inayodai uwajibikaji wa kijamii, hatua inayomfanya kiongozi akubali matokeo hata kama anaamini ameshinda.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Leo Julai 23, 2026 shahidi wa nne (4) katika shauri la Kikatiba Na. 7300/2026 ambaye ni Mkuu wa Gereza la Ukonga ACP Andrew Shaban N'tamamiro ataendelea kuulizwa maswali ya dodoso (cross examination) katika shauri hilo ambalo linaendelea kwenye Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu Dodoma, inayoketi vikao vyake kwenye Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam mbele ya jopo la Majaji watatu watatu (3) wakiongozwa na Jaji Amir Mruma.
Wafunguaji wa shauri hilo ni Mawakili watatu (3) ambao ni Kulwa William Maduhu, Nashon Nkungu na Paul Kisabo ambao wanalalamika juu ya kukosa faragha pindi wanapomtembelea mteja wao gerezani ambaye ni Mwenyekiti wa @chadematzofficial Taifa Tundu Lissu.
Shauri limefunguliwa dhidi ya Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini (CGP) na wenzake wanne (4) na leo ACP Ntamamiro atahojiwa maswali ya dodoso na mawakili wa walalamikaji pamoja na Mawakili wa Chama cha Wanasheria Tanganyika(TLS) muda utakaporuhusu atahojiwa maswali ya kusawazisha(Re-examination)This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Dkt. Mustapher Mohamed Siyani, amesema kuwa Utatuzi wa Migogoro kwa Njia ya usuluhishi na upatanishi, unapaswa kutambuliwa kama sehemu muhimu ya mfumo wa utoaji haki nchini.
Siyani ameyasema hayo tarehe 22 Julai, 2026, katika hotuba aliyoisoma kwa niaba ya Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, George Masaju wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Nane wa Mwaka wa Taasisi ya Wasuluhishi Tanzania (TIArb) na Wiki ya Usuluhishi ya Dar es Salaam (DAR Arbitration Week) ya mwaka 2026 uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Ameeleza kuwa, Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inaielekeza Mahakama kukuza na kuimarisha utatuzi wa migogoro miongoni mwa wahusika wa migogoro kama ilivyofafanuliwa katika Ibara ya 107A(2)(d) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hivyo usuluhishi na upatanishi unapaswa kutazamwa kama mwendelezo wa jukumu la Mahakama katika utoaji wa haki ndani ya mfumo wa utawala wa sheria.
"Utoaji wa haki katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania umepewa Mahakama. Hata hivyo, mamlaka hiyo haiwazuii wahusika wa mgogoro kutafuta haki kwa njia nyingine walizokubaliana, kama inavyoainishwa katika Ibara ya 107A(2)(d) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambayo inaielekeza Mahakama kukuza na kuimarisha utatuzi wa migogoro miongoni mwa watu wanaohusika katika migogoro hiyo,” amesisitiza Mhe. Siyani.
Amesema mifumo ya jadi ya utatuzi wa migogoro iliyokuwepo kabla ya ukoloni, iliyojengwa katika misingi ya maridhiano na maelewano, bado ina mchango mkubwa katika maendeleo ya mifumo ya kisasa ya utatuzi wa migogoro kwa njia ya Usuluhishi, huku akisisitiza umuhimu wa kuhakikisha mifumo hiyo inaendana na mazingira ya Tanzania na inayokidhi viwango vya kimataifa.
"Uhalali wa mfumo wowote wa utatuzi wa migogoro hautegemei tu uhalali wake wa kisheria, bali pia kukubalika kwake na jamii pamoja na kuendana kwake na mila na utamaduni wa wananchi. Kwa hiyo, mustakabali wa mifumo ya Usuluhishi/upatanishi nchini Tanzania unapaswa kuwa shirikishi, ukichota mema kutoka katika mila na desturi mbalimbali huku ukizingatia misingi ya haki, kutopendelea upande wowote na utawala wa sheria,” amesema Jaji Kiongozi.
Kwa upande wake Rais wa Taasisi ya Wasuluhishi Tanzania (TIArb) Wakili Aderickson Njunwa, ameeleza kuwa, Taasisi hiyo iliyoanzishwa mwaka 1997, imebeba dhima kubwa ya kuisaidia jamii kutatua migogoro kwa njia ya upatanishi, kadhalika kukuza uwekezaji na kuimarisha uchumi endelevu.
Wakili Njunwa amefafanua kuwa miongoni mwa majukumu mengine ya (TIArb) ni kuhakikisha kuwa jamii ya Tanzania inapata elimu kuhusu maana ya usuluhishi na umuhimu wake kwa maendeleo endelevu pamoja na kuendeleza uwajibikaji kwa kujengeana uwezo na majukumu ya kitaasisi. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Wananchi wa Igominyi katika Halmashauri ya Mji wa Njombe mkoani Njombe wamemuomba Mbunge wa Jimbo la Njombe Mjini kushirikiana na Serikali ili kudhibiti wauzaji wa pembejeo za kilimo wanaouza mbolea kwa masharti yanayokiuka miongozo ya Serikali.
Wakizungumza mbele ya Mbunge wa Jimbo hilo, Deodatus Mwanyika, wananchi hao wakiongozwa na Daniel Mdendemi pamoja na Exavery Mtega, wameeleza kuwa baadhi ya wafanyabiashara wanapowauzia mbolea huwalazimisha pia kununua bidhaa nyingine ambazo hawazihitaji, jambo linalowaumiza sana wakulima kiuchumi.
“Ni kwanini Serikali imeshindwa kusimamia pembejeo kwa wakulima? Wengine tumekuwa tukipewa masharti ya kubandikizwa mbolea, yaani unalazimishwa uchukue NPS na TSP kwa pamoja,” amehoji Mdendemi.
Akijibu kero hiyo, Afisa Kilimo wa Halmashauri ya Mji wa Njombe, Nicas Rusahila, amesema changamoto hiyo imejitokeza hivi karibuni kutokana na baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu wanaokiuka utaratibu wa Serikali, na kusisitiza kuwa idara yake inakwenda kuifanyia kazi mara moja.
Kwa upande wake, Mbunge Deodatus Mwanyika amesema Serikali haiwezi kukubali mchezo huo wa kuwanyonya wakulima na kwamba anakwenda kushirikiana na mamlaka husika kutafuta ufumbuzi wa haraka ili kuwalinda wananchi wa jimbo hilo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Katika jitihada za kupunguza utegemezi wa mahakama na taasisi za kimataifa, Serikali ya Tanzania haina budi kuimarisha taasisi zake za ndani za usuluhishi wa migogoro ili iwe kituo kikuu na kinachopendekezwa kwa usuluhishi katika ukanda wa Afrika Mashariki na bara zima la Afrika.
Hayo yamebainishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Hamza Johari alipokuwa akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Nane wa Mwaka wa Taasisi ya Wasuluhishi Tanzania (TIArb) na Wiki ya Usuluhishi ya Dar es Salaam (DAR Arbitration Week) ya mwaka 2026 uliofanyika Julai 22, 2026. Amesisitiza kuwa ni wakati sasa kwa Tanzania kujenga uaminifu katika mifumo yake ya usuluhishi, badala ya kuendelea kupeleka migogoro kwenye mamlaka za kigeni.
"Badala ya kusafirisha migogoro nje ya nchi, tunapaswa kuendelea kuimarisha taasisi zetu za ndani ili Tanzania iwe chaguo la kwanza katika usuluhishi. Tunapaswa kujenga uaminifu huu siyo tu kwa migogoro yetu ya ndani, bali pia kwa migogoro inayoibuka Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla," ameeleza Mwanasheria Mkuu huyo.
Aidha, amebainisha kuwa mabadiliko hayo yatajumuishwa katika zoezi linaloendelea sasa la kupitia na kuoanisha sheria za nchi ili ziendane na Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050.
Kwa upande wake, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Dkt. Mustapher Mohamed Siyani amesema kuwa utatuzi wa migogoro kwa njia ya usuluhishi na upatanishi unapaswa kutambuliwa kama sehemu muhimu ya mfumo wa utoaji haki nchini.
Katika hotuba aliyoisoma kwa niaba ya Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, George Masaju, Siyani ameeleza kuwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inaielekeza Mahakama kukuza na kuimarisha utatuzi wa migogoro miongoni mwa wahusika wa migogoro kama ilivyofafanuliwa katika Ibara ya 107A(2)(d) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hivyo usuluhishi na upatanishi unapaswa kutazamwa kama mwendelezo wa jukumu la Mahakama katika utoaji wa haki ndani ya mfumo wa utawala wa sheria.
"Utoaji wa haki katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania umepewa Mahakama. Hata hivyo, mamlaka hiyo haiwazuii wahusika wa mgogoro kutafuta haki kwa njia nyingine walizokubaliana, kama inavyoainishwa katika Ibara ya 107A(2)(d) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambayo inaielekeza Mahakama kukuza na kuimarisha utatuzi wa migogoro miongoni mwa watu wanaohusika katika migogoro hiyo,” amesisitiza Siyani. -
Jambo TV
@Jambotv_
Marekani imeendeleza mashambulizi ya anga kwa usiku wa 12 mfululizo dhidi ya Iran ikisema imelenga kulinda meli za kibiashara zinazopita katika Mlango Bahari wa Hormuz.
Kamandi Kuu ya Marekani imesisitiza kuwa mashambulizi hayo yatapunguza uwezo wa kijeshi wa Iran. Imesema Lengo kuu ni kurejesha usalama wa njia hiyo muhimu ya nishati duniani.
Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, Rais Donald Trump ametishia kuongeza makali ya mashambulizi. Ameonya kuwa Marekani itaharibu miundombinu au madaraja ya Iran kama italipiza kisasi.
Hata hivyo Iran imejibu kwa kufanya mashambulizi katika nchi za Bahrain, Jordan na Saudi Arabia ambazo ni nchi washirika wa Marekani. Kupitia Waziri wake wa mambo ya nje, Abbas Araghchi, ametangaza mkakati wa "jicho kwa jicho" unaolenga kujibu kila shambulizi litakalotoka kwa malekani.
Juhudi za kidiplomasia za kuleta suluhu zimekwama baada ya mazungumzo nchini Pakistan kutofikia malengo. Maafisa wa pande zote mbili wameendelea kushikilia misimamo yao mikali ya kijeshi. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Wananchi ambao ni wamiliki wa shamba lenye ukubwa wa zaidi ya ekari 2,000 lililopo katika vitongoji vya Relini na Mariton, Kata ya Malula, Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha, wamemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kuingilia kati, wakidai Halmashauri ya Wilaya ya Meru imevamia ardhi yao licha ya familia ya Ahmed Okash kushinda shauri la umiliki katika Mahakama ya Rufani.
Wananchi hao wamedai kuwa maafisa wa halmashauri wameendelea na shughuli za upimaji wa eneo hilo na kuweka alama za mipaka (beacons), wakisema hatua hizo zinakiuka uamuzi wa mahakama na zimezua hofu kwa wakulima wanaotegemea ardhi hiyo kwa shughuli za uzalishaji.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru, Mwanasheria wa halmashauri hiyo, Jonathan Kiama, amekiri kuwa familia ya Ahmed Okash ilishinda shauri hilo, lakini amedai halmashauri inaendelea kulitambua eneo hilo kuwa mali yake. Hata hivyo, Wakili wa familia hiyo, Fridolin Gwemelo, ameipinga kauli hiyo na kuitaka halmashauri kuheshimu uamuzi wa Mahakama ya Rufani na kusitisha shughuli zozote katika eneo hilo.
Hadi jana, zoezi la upimaji lilikuwa linaendelea chini ya ulinzi wa askari, huku wananchi wakisisitiza kuwa wanachotaka si mgogoro, bali utekelezaji wa sheria na kuheshimiwa kwa uamuzi wa mahakama.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, John Heche amesema kuwa chama chao hakifanyi siasa za maigizo bali kinafanya siasa makini kwa ajili ya ukombozi wa nchi ya Tanzania.
Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Dar es Salaam leo Jumatano Julai 22, 2026, Heche amefafanua kuwa lengo la siasa zao ni kufanya mabadiliko makubwa ya mfumo wa Tanzania licha ya kile alichokiita madhara kwa wanachama wao ikiwamo kukamatwa na kuwekwa gerezani.
“Kwahiyo nataka nisisitize kwa viongozi na wanachama wa CHADEMA, chama chetu kama chama kikuu cha siasa cha nchi hii siasa tunazofanya ni za kwenda kubadilisha nchi hii, na zina ‘consequences’, zina madhara kwetu”, ameeleza Heche.
Heche amewataka viongozi na wanachama wa CHADEMA kuelewa kuwa siasa wanazofanya ni za mabadiliko ya kweli na anawaomba Watanzania wawaunge mkono.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, John Heche ameendelea kusisitiza kuwa hakuna maridhiano yatakayokubalika kuanza isipokuwa tu pale Mwenyekiti wa chama hicho ngazi ya taifa, Tundu Lissu atakapoachiwa huru, na vikao vya CHADEMA kutoa uamuzi.
Heche ametoa msimamo huo leo Jumatano Julai 22, 2026 akizungumza na waandishi wa habari mkoani Dar es Salaam ambapo amesisitiza kuwa CHADEMA haitahusika katika meza ya mazungumzo yatakayofanyika bila kuwa na mpatanishi wa nje atakayekuwa katikati ya pande zinazozungumza.
“Hakuna mazungumzo yatakayofanyika bila mwenyekiti kuwa nje, hakuna mazungumzo yatakayofanyika bila watu kuwajibika, hakuna mazungumzo yatakayofanyika bila ‘mediator’ ambaye atakuwa kati… ndiyo mazungumzo ya maana ambayo yametokea”, ameeleza Heche.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Tundu Lissu leo, tarehe 22/07/2026 amemuhoji maswali ya dodoso (cross examination) shahidi wa Nne (4) katika shauri la Kikatiba Na. 7300/2026 linaloendelea kwenye Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu Dodoma, inayoketi vikao vyake kwenye Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam mbele ya jopo la Majaji watatu watatu (3) wakiongozwa na Jaji Amir Mruma.
Shahidi huyo ambaye kimsingi ni shahidi wa kwanza na pekee wa Jamhuri katika shauri hilo lililofunguliwa na Mawakili watatu (3) ambao ni Kulwa William Maduhu, Nashon Nkung na Paul Kisabo dhidi ya Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini (CGP) na wenzake wanne (4), ni Mkuu wa Gereza la Ukonga, Dar es Salaam ACP Andrew Shaban N'tamamiro
Katika maswali yake ya dodoso, pamoja na mambo mengine Lissu ambaye anajiwakilisha mwenyewe amemuhoji shahidi huyo endapo ni kweli au si kweli kwamba kwenye masuala yanayomuhusu yeye (Lissu) amekuwa akiendesha 'kwa rimoti' na Mlalamikiwa wa pili (2) kwenye shauri hilo ambaye ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini (CGP) na wanasiasa walioko Serikalini, hata hivyo shahidi huyo alijibu kuwa si kweli
Baada ya kujibiwa hivyo, Lissu ambaye kitaaluma ni Mwanasheria na Wakili mbobevu alitoa mifano aliyodai kuwa inahusiana moja kwa moja na kile alichozungumza Mahakamani hapo kwamba Mkuu huyo wa Gereza Ukonga amekuwa akiendeshwa kwa 'rimoti' na CGP na wanasiasa walioko Serikalini hasa kwenye mambo yanayomuhusu yeye (Lissu)
Amedai kuwa siku moja aliitwa kwenye Ofisi ya shahidi huyo na kuelezwa kuwa kuna ujumbe muhimu umetumwa gerezani kwamba Lissu anatakiwa kwenda mjini kukutana na Mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola, ambaye ni Rais Mstaafu wa Malawi Dkt. Lazarus Chakwera, na ilikuwa hivyo
Anasema mara nyingine, ni pale alipomuita tena Ofisini kwake na kumueleza kuwa anatakiwa kwenda mjini kukutana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) Martin Chungong, na ilikuwa hivyo Lisuu alienda Mjini akiwa anasindikizwa na mmoja wa maafisa wa Magereza
Soma zaidi jambo.co.tz/lissu-amuhoji-mkuu-wa-gereza-unaendeshwa-na-w… -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania, Gerson Msigwa, amesema Serikali imepokea tamko la Jumuiya ya Madola linalohusu mwenendo wa kesi ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu na namna ya kuitatua kesi hiyo, na inalifanyia tathmini tamko hilo kisha itatoa majibu rasmi baada ya kupitia hoja zote zilizowasilishwa.
Akizungumza jijini Dodoma leo mara baada ya kuulizwa swali hilo, Msigwa amesema Tanzania ni nchi huru inayojitawala na kuongozwa kwa misingi ya Katiba na sheria zake, hivyo Serikali itaendelea kushughulikia masuala yote kwa kuzingatia utaratibu wa kikatiba na wa kisheria bila kuathiri mamlaka ya taasisi husika.
"Tutayaangalia maeneo yote ambayo Jumuiya ya Madola wametuandikia, tutawasiliana nao na tutawapa majibu ya Serikali," amesema Msigwa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, amesema suala la kufanyika kwa mikutano ya kisiasa linaongozwa na taratibu na sheria, akieleza kuwa uamuzi wa kuruhusu mikutano hiyo unategemea tathmini ya vyombo vya ulinzi na usalama.
Akijibu swali aliloulizwa na Mwandishi wa Habari, Msigwa amesema Serikali itaendelea kuweka mbele ulinzi wa amani na usalama wa Wananchi, akisisitiza kuwa demokrasia haiwezi kuwa juu ya usalama wa watu, hivyo vyombo vya ulinzi na usalama vinaendelea kutekeleza wajibu wake kwa kuzingatia hali halisi ya nchi.
"Tuviache vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vifanye kazi yao. Vikituelekeza hapa tusifanye, tusifanye. Vikisema sasa ni salama kufanya, tutafanya. Mikutano imezuiwa, na vyombo vyetu vitakapojiridhisha kuwa hali ni shwari, vitaruhusu iendelee," amesema Msigwa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI PICHA:
Kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mchungaji Peter Msigwa alifika Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam kwa ajili ya shauri la kikatiba lililofunguliwa katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu ya Dodoma, na Mawakili wa Mwenyekiti wa Chama hicho, Tundu Lissu wakilalamikia kunyimwa kumuona Lissu gerezani na kukosa faragha pindi wanapomuona mara baada ya kesi iliyofunguliwa na mawakili wawili kuahirishwa kwa muda, leo Julai 22,2026.
Mch. Msigwa alipata nafasi ya kuonana na kukumbatiana na kada wa chama hicho na Mbunge wa zamani wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa mara baada ya kesi iliyofunguliwa na mawakili wawili kuahirishwa kwa muda leo. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO
Mmoja wa wafanyabiashara katika Soko la Machinga Complex jijini Dodoma ameibua kilio kuhusu kudorora kwa biashara, akieleza kuwa ukosefu wa wateja pamoja na mzunguko mdogo wa fedha umeendelea kuathiri shughuli za wafanyabiashara wengi ndani ya soko hilo.
Akizungumza mbele ya Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, wakati wa ziara yake ya kutembelea soko hilo leo Julai 22, 2026, mfanyabiashara huyo amesema hali ya biashara imekuwa ngumu kwa kiwango cha kuathiri mapato ya wafanyabiashara, huku baadhi yao wakilazimika kukaa muda mrefu madukani bila kupata wateja.
“Mheshimiwa, hela ziko wapi? Hela hamna. Unakaa dukani unasinzia kwasababu hakuna wateja. Mzunguko wa fedha hamna, soko limeelemewa,” amesema mfanyabiashara huyo.
Akijibu hoja hiyo, Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, amesema wakati Serikali ilipojenga Soko la Machinga Complex haikutarajia ongezeko kubwa la wafanyabiashara waliokuja kufanya biashara katika eneo hilo. Amesema Serikali inaendelea na mpango wa kujenga masoko mengine katika maeneo mbalimbali ili kupanua fursa za biashara, kupunguza msongamano wa wafanyabiashara na kuweka mazingira bora zaidi ya kufanyia biashara nchini.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy, amemteua Mykhailo Drapatyi kuwa mkuu mpya wa majeshi ya nchi hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa ya Rais huyo kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, uteuzi wa Drapatyi umechukua nafasi ya aliyekuwa Mkuu wa Majeshi hayo Oleksandr Syrskyi.
Hatua hiyo imekuja ikiwa ni baada ya kuwepo kwa shinikizo la maandamano ya wananchi pamoja na wanajeshi kipindi kifupi kilichopita, waliotaka kufanyika kwa mabadiliko ya kiuongozi katika jeshi.
Aidha inatajwa kuwa uteuzi huo umechangiwa na mgogoro wa kimkakati kati ya aliyekuwa Mkuu wa Majeshi, Oleksandr Syrskyi, na Waziri wa Ulinzi, Mykhailo Fedorov.
Lengo kuu la mabadiliko hayo linatajwa kuwa ni kuongeza nguvu katika vita vinavyoendelea dhidi ya Urusi, huku ikitarajia kuishinikiza Urusi kuingia katika makubaliano ya amani. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, John Heche akiingia Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam kwa ajili ya shauri la kikatiba lililofunguliwa katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu ya Dodoma, na Mawakili wa Mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu wakilalamikia kunyimwa kumuona Lissu gerezani na kukosa faragha pindi wanapomuona.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Muungano mkuu wa upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), C64, umeahirisha maandamano yaliyopangwa kufanyika leo tarehe 22 Julai 2026 mjini Kinshasa.
Hatua hiyo imechukuliwa baada ya mikutano ya dharura iliyosababisha viongozi wa Muungano huo kukubali wito wa viongozi wa kidini kutoa nafasi kwa mazungumzo ya kitaifa. Lengo la maandamano hayo lilikuwa kupinga mpango wa Rais Felix Tshisekedi wa kubadilisha katiba ili kurefusha muda wake madarakani.
Muungano huo umekubali kusitisha harakati hizo ili kujaribu njia ya diplomasia ingawa baadhi ya viongozi wake wameonyesha upinzani juu ya uamuzi huo akiwemo Dominique Munongo kutoka chama cha Ensemble pour la Republique cha Moise Katumbi.
Munongo amesisitiza kuwa maandamano yalipaswa kuendelea mitaani ili kuweka shinikizo la moja kwa moja dhidi ya Rais Tshisekedi. Naye Seth Kikuni, kiongozi wa muungano wa "Sauvons la DRC" unayemuunga mkono Joseph Kabila, amekosoa uamuzi huo kama kosa kubwa la kimkakati. Kikuni anaamini hatua hiyo inarudisha nyuma nguvu ya umma iliyokuwa imejipanga kupaza sauti dhidi ya ukiukwaji wa sheria. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Miaka mitano ya utawala wa Rais Samia Suluhu Hassan imeufungua Mkoa wa Kigoma kwa kufanya ufikike kwa urahisi, kupunguza gharama za safari na kufungua fursa za kiuchumi kwa wakazi wake.
Akizungumza kwenye mikutano aliyofanya kwenye maeneo tofauti kukagua maendeleo ya ujenzi wa miradi inayoendelea, Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega, amesema Kigoma ya sasa ni tofauti kabisa na ile ilivyokuwa wakati Rais Samia akiingia madarakani mwaka 2021.
Akizungumza kwa kutumia takwimu, Ulega ametoa mfano wa mtandao wa barabara za lami ambao alisema kwa miaka takribani 60 ya Uhuru, Kigoma ilikuwa na kilomita za 259 za lami, lakini serikali ya Rais Samia imejenga kilomita 335.
Ulega ambaye yuko katika ziara ya kikazi mkoani Kigoma, jana alifanya ukaguzi wa takribani wilaya nne tofauti za mkoa wa Kigoma ambapo viongozi, wabunge na wananchi wa mkoa huo walieleza tofauti zilizoanza baada ya mabadiliko hayo.
Akihutubia Kasulu, Ulega alisema kwa ujumla serikali imetumia zaidi ya shilingi bilioni 600 kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya kimkakati tisa katika Mkoa wa Kigoma peke yake.
Waziri huyo alisema kinachoendelea Kigoma ndiyo taswira pia ya maendeleo makubwa ya ujenzi yanayoendelea katika mikoa tofauti nchini Tanzania kwasababu Rais Samia anaamini barabara ni mlango wa fursa kwa walio wengi.
Kwa mfano, Mbunge wa Kigoma Mjini, Clayton Chiponda, alisema zamani nauli ya kutoka Kigoma kwenda Dar es Salaam ilikuwa shilingi 120,000 lakini baada ya barabara kuimarika, hivi sasa nauli imekuwa shilingi 70,000.
Akiwa Kigoma Vijijini, Ulega alipita katika barabara ya urefu wa km 65 ya Mkongoro – Chankere – Mwamgongo – Kagunga ya Chankere ambayo inapita kwenye njia ya Bonde la Ufa la Afrika Mashariki na iliyohitaji utaalamu na gharama kubwa kuijenga. Barabara hiyo imejengwa kwa kutumia fedha za Mfuko wa Barabara.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini kupitia Chama cha ACT Wazalendo, Kiza Mayeye, alisema kazi ya kuufungua mkoa wa Kigoma inapaswa kuendelea kwasababu mkoa huo ni miongoni mwa milango muhimu ya uchumi wa Tanzania.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Wachimbaji wadogo wa madini wilayani Nyang'hwale mkoani Geita, wameishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuendelea kuwekeza katika upatikanaji wa nishati ya umeme kwenye maeneo ya migodi, hatua inayopunguza gharama za uzalishaji na kuongeza tija katika shughuli za uchimbaji.
Shukrani hizo zimetolewa wakati Waziri wa Madini, Anthony Mavunde alipozindua mradi wa kuzalisha nishati ya umeme wenye uwezo wa KVA 500 kwenye Mgodi wa wachimbaji wadogo katika eneo la Igalula, wilayani Nyang'hwale. Mradi huo umetekelezwa kwa gharama ya zaidi ya Shilingi milioni 426 na ni sehemu ya juhudi za serikali za kuboresha miundombinu ya nishati katika maeneo ya uchimbaji wa madini.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Mavunde amesema Serikali imeendelea kutekeleza kwa vitendo dhamira ya kuboresha mazingira ya uwekezaji na uzalishaji katika sekta ya madini kwa kusambaza umeme kwenye migodi ya wachimbaji wadogo na wa kati.
Amesema Serikali tayari imetumia zaidi ya Shilingi bilioni 7 kusambaza umeme katika maeneo mbalimbali ya migodi nchini, hatua iliyowezesha wachimbaji kupunguza utegemezi wa mitambo inayotumia mafuta na hivyo kushusha gharama za uzalishaji huku ikiongeza ufanisi wa shughuli za uchimbaji.
Katika kuendelea na ziara yake, Waziri Mavunde amekagua mradi wa maji safi na salama unaotekelezwa katika Kijiji cha Kakola, ambao unatarajiwa kuwanufaisha zaidi ya wananchi 24,801
Amesema mradi huo unatekeleza maelekezo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha wananchi, hususan wanawake, wanaondokana na adha ya kutembea umbali mrefu kutafuta maji.
"Ahadi ya Mheshimiwa Rais ya kumtua mama ndoo kichwani inaendelea kutekelezwa kwa vitendo kupitia miradi ya maji kama huu wa Kakola ambao utaboresha afya, ustawi na shughuli za kiuchumi za wananchi," amesema.
Katika sekta ya elimu, Waziri Mavunde amezindua Shule ya Msingi Imara Baruti iliyojengwa ili kuondoa changamoto ya wanafunzi kutembea umbali wa takribani kilomita nne kwenda kusoma katika Shule ya Msingi Shabaka.
Amesema ujenzi wa shule hiyo unatekeleza Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), inayosisitiza ujenzi wa shule karibu na makazi ya wananchi ili watoto wapate elimu katika mazingira bora.
"Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea kuthibitisha kuwa ahadi zinazotolewa kwa wananchi si maneno ya kampeni pekee, bali ni mipango inayotekelezwa kwa vitendo kwa manufaa ya Watanzania," amesema.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martin Shigella, amempongeza Waziri Mavunde kwa kufanya ziara ya kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo mkoani humo, akisema hatua hiyo imeongeza kasi ya utekelezaji wa miradi na kuimarisha ufuatiliaji wa huduma zinazowagusa wananchi moja kwa moja.
Shigella amebainisha kuwa uwekezaji unaoendelea katika sekta za madini, elimu, maji na nishati unaendelea kuifanya Geita kuwa kitovu muhimu cha uzalishaji wa madini na maendeleo ya kijamii nchini. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Shauri la kikatiba lililofunguliwa katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu ya Dodoma, na Mawakili wa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo @ChademaTZ2 Tundu Lissu wakilalamikia kunyimwa kumuona gerezani na kukosa faragha pindi wanapomuona linaendelea muda huu katika kikao kinachoketi katika Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo Dar es Salaam.
Leo Julai 22, 2026 Mkuu wa Gereza la Ukonga atahojiwa maswali ya dodoso kama shahidi upande wa wajibu maombi ambapo shauri hili la kikatiba na 7300/2026 limefunguliwa na Mawakili Kulwa Maduhu, Nashon Nkungu na Paul Kisabo na lipo mbele ya Jopo la Majaji watatu Amir Mruma, Dkt. Angelo Rumisha na Dkt. Evaristo Longopa.
Wajibu maombi katika shauri hili ni Afisa Inchaji wa Gereza Ukonga (Mkuu wa Gereza), Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Tundu Lissu na chama cha Wanasheria Tanganyika(TLS).This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Waziri Mkuu mpya wa Uingereza, Andy Burnham, ameidhinisha Jeshi la Marekani kuendelea kutumia vituo vya kijeshi vya nchi hiyo kwa ajili ya operesheni za kijeshi dhidi ya Iran, huku Serikali yake ikisisitiza kuwa ruhusa hiyo ni kwa ajili ya usalama na ulinzi pekee.
Uamuzi huo unaiwezesha ndege za kivita za Marekani kuendelea kutumia kituo cha RAF Fairford kilichopo Gloucestershire, pamoja na kituo cha pamoja cha kijeshi cha Uingereza na Marekani cha Diego Garcia kilichopo Visiwa vya Chagos, bila kuhitaji mabadiliko ya sera za sasa za Uingereza.
Hata hivyo, Ofisi ya Waziri Mkuu imebainisha kuwa ruhusa hiyo imewekewa mipaka thabiti, ikieleza kuwa operesheni hizo zinapaswa kulenga tu kulinda usafirishaji wa meli za kimataifa katika Njia ya Bahari ya Hormuz (Strait of Hormuz), na lazima zizingatie sheria za kimataifa pamoja na haki ya kujilinda.
Hatua hiyo, inayokuja siku chache tu tangu Burnham achukue mikoba ya uongozi wa nchi, imekuwa mtihani wake wa kwanza wa kidiplomasia na kisiasa, akijaribu kuweka urari kati ya ushirika wa kihistoria wa Uingereza na Marekani na masharti ya kisheria yanayohusu mgogoro unaoendelea kupanuka nchini Iran na Mashariki ya Kati.
Kabla ya uamuzi huo, kukiwa na vikao vilivyoongozwa na Sir Keir Starmer kabla ya kuondoka madarakani, maafisa wa ngazi ya juu wa usalama na mawaziri walipitia kwa kina maombi ya Washington ili kujiridhisha kama matumizi ya vituo hivyo yanakidhi masharti ya sheria za kimataifa.
Katika vikao hivyo, Uingereza ilikuwa tayari imekataa maombi ya Marekani ya kutumia ndege zake za kisasa za B-2 Stealth Bombers kurusha mashambulizi kutoka Diego Garcia, kwa hofu kuwa mashambulizi hayo yanaweza kukiuka sheria za kimataifa na kuvuka mipaka ya haki ya kujilinda.
Badala ya kuleta sera mpya, Burnham amechagua kuendeleza masharti yaliyowekwa na mrithi wake, Sir Keir Starmer. Hatua hii inalenga kuepusha mtafaruku mpya wa kidiplomasia kati ya London na Washington, kufuatia kutoridhishwa kwa Rais wa Marekani, Donald Trump, mapema mwaka huu baada ya Uingereza kugoma kutoa fursa ya mashambulizi ya moja kwa moja kutoka Diego Garcia. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Serikali kupitia Wizara ya Nishati imeahidi kutafuta fedha kuhakikisha vitongoji vyote mkoani Mtwara vinafikishiwa umeme.
Ahadi hiyo, imetolewa siku ya Jumanne na Waziri wa Nishati, Deogratius Ndejembi wakati wa hafla ya kuwasha umeme katika Kitongoji cha Maendeleo iliyofanyika katika Shule ya Sekondari ya Mtiniko iliyopo katika Kijiji cha Mtiniko, Wilaya ya Mtwara mkoani Mtwara.
“Mkoa wa Mtwara pekee umeletewa zaidi ya Shilingi Bilioni 203 kwa ajili ya kukamilisha upelekaji wa umeme kwenye vijiji na vitongoji vyake. Nanyamba hapa kuna vijiji 87 na vijiji vyote vimepata umeme. Lakini pia, hapa kuna vitongoji 324, na vitongoji 306 tayari vina umeme. Vitongoji 8 tayari Wakandarasi wanaendelea na kazi. Tunakwenda kutafuta fedha za vitongoji 10 vilivyosalia,” amesema Waziri Ndejembi.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba amesema kuwa Wizara ya Nishati itaendelea kuhakikisha wananchi wanapata umeme ulio bora.
Awali akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi ya kupeleka umeme kwenye vijiji pamoja na vitongoji kwa Mkoa wa Mtwara, Mkurugenzi wa Umeme Vijijini kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Jones Olotu amesema kuwa Mkoa wa Mtwara una jumla ya vijiji 785 ambavyo vyote tayari vina umeme.
Kwa upande wa vitongoji, Mhandisi Olotu amesema kuwa, Mkoa wa Mtwara una jumla ya vitongoji 3421 ambapo Serikali kupitia REA imefanikiwa kufikisha umeme katika vitongoji 2839 huku jitihada mbalimbali za kuhakikisha vitongoji vyote vinapatiwa umeme.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi amedai kuwa Tanzania inawindwa sana kutokana na rasilimali zake na madaraka, akilinganisha hali hiyo na ukoloni mamboleo na kuonya kuwa machafuko yanayosababishwa na rasilimali na madaraka duniani kote huathiri zaidi watu wasio na hatia kama akina mama, watoto, na walemavu.
Ametoa kauli hiyo siku ya Jumanne wakati akimwakilisha Makamu wa Rais, Dkt. Emmanuel Nchimbi katika maadhimisho ya miaka 40 tangu kuanzishwa kwa Kanisa la Elim Pentekoste katika hafla iliyofanyika wilayani Karatu mkoani Arusha ambapo pia iliadhimishwa miaka 40 ya Askofu Mkuu wa Kanisa hilo la Elim Pentekoste Tanzania, Peter Konki.
“Taifa letu kama ilivyo kwingine duniani linawindwa sana, linawindwa siyo kwa bahati mbaya, ni kwa sababu zilezile, sababu zilizowaleta wakoloni hapa ndizo hizohizo zinawarudisha kwa staili nyingine, rasilimali zinaua watu, uongo kweli? Leo watu wanapigana, wanauana kwasababu ya mali, uongo kweli? Madaraka yanaua watu, uongo kweli? Leo nchi duniani huko kote kila mtu anataka kuwa mbabe, nani nani! Wanapigana, wanaathiri watu wa kawaida- akina mama, watoto, watu wenye ulemavu, wazee na watu wenye umri mkubwa ambao hawawezi kukimbia hata kilomita tano”, ameeleza Katambi.
Katambi amewaomba maaskofu, masheikh, na wachungaji kuombea nchi ili kulinda amani na kutoichukulia amani hiyo kama mzaha, akionya kuwa machafuko yanaweza kuifanya nchi kuwa na wakimbizi.
“Nchi yetu hii tuna historia nzuri ya amani, tuna historia nzuri ya kuwalea wenzetu waliopata machafuko, wenye busara hujifunza kutokana na makosa ya wengine siyo tufanye makosa yetu tuseme tumejifunza kutokana na makosa, makosa ya wengine yalitupa mafunzo kwamba kumbe mnaweza mkachafua taifa mkawa wakimbizi kwenye taifa jingine na mkapoteza haki zenu zote. Kwahiyo hata leo ukiangalia waliobaki na vyeo vyao nadhani ni Mababa Askofu na Wachungaji lakini bado wanaitwa wakimbizi kwenye maeneo mbalimbali”, amesisitiza Katambi.
Ameongeza kuwa Watanzania wanapaswa kuwa na umoja, uzalendo na mshikamano ili kulinda maslahi ya taifa dhidi ya changamoto na ushawishi unaoweza kuhatarisha maendeleo na usalama wa nchi. -
Jambo TV
@Jambotv_
youtu.be/PNwVU5jgaoc
WAKILI WA LISSU AKIHOJIWA NA MAWAKILI WATATU MAHAKAMANI/ KESHO MKUU WA GEREZA LA UKONGA -
Jambo TV
@Jambotv_
WAKILI WA LISSU AKIHOJIWA NA MAWAKILI WATATU MAHAKAMANI/ KESHO MKUU WA GEREZA LA UKONGA jambo.co.tz/wakili-wa-lissu-akihojiwa-na-mawakili-watatu-…
-
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Chama cha ACT Wazalendo @ACTwazalendo kimetaka wahadhiri waliokamatwa katika vyuo vikuu mbalimbali nchini waachiwe huru mara moja bila masharti, kikisema hatua za kuwakamata wanataaluma hao zinaibua maswali mazito kuhusu uhuru wa taaluma na mamlaka ya vyuo vikuu.
Katika taarifa iliyotolewa siku ya Jumanne Julai 21, 2026 na Waziri Kivuli wa Elimu, Sayansi na Teknolojia wa chama hicho, Riziki Shari Mngwali, wamewataja wahadhiri hao kuwa ni Melkisedeki Kitunzi Kaijage kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), pamoja na Johaiven Revelian Bikongolo na Titus Joseph Kituli kutoka Chuo Kikuu cha St. John Tanzania (SJUT). ACT Wazalendo imesisitiza kuwa endapo kuna tuhuma za kitaaluma au kinidhamu, zinapaswa kushughulikiwa kupitia taratibu za vyuo husika na si vyombo vya dola.
Kwa mujibu wa taarifa ya Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (THTU), Dkt. Paul Loisulie, kupitia taarifa yake yenye kurasa 14, ameeleza kuwa mmoja wa wahadhiri wa SJUT alikamatwa baada ya kufundisha mada ya maadili na utawala bora kwa kutumia mifano ya kashfa za kihistoria nchini kama vile Richmond na Escrow, ili kuwaelewesha wanafunzi umuhimu wa kuzingatia sheria. Mhadhiri mwingine wa SJUT, ambaye ni Mkurugenzi wa Huduma za Wanafunzi, alihusishwa na masuala ya uchaguzi wa wanafunzi chuoni hapo, huku wote wakituhumiwa kuhamasisha maandamano ya Julai 7, 2026.
Naye, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanataaluma wa UDOM (UDOMASA), Dkt. Gerald Shija katika taarifa ya hivi karibuni ya UDOMASA ameeleza kuwa Mhadhiri Kaijage alikamatwa baada ya kuitikia wito wa Jeshi la Polisi. Dkt. Loisulie aliongeza kuwa hii ni mara ya pili kwa Kaijage kukamatwa, baada ya tukio la kwanza kutokea wakati wa vuguvugu la maandamano ya Desemba 9, 2025.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gallus Hyera kupitia tovuti ya Mwananchi alithibitisha kumshikilia Kaijage kwa tuhuma za kuhamasisha maandamano kupitia machapisho ya mitandao ya kijamii na kueleza kuwa suala hilo kwa sasa lipo katika uchunguzi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Arusha, Saipulan Ramsey, amesema utamaduni wa 'uchawa' na kuteteana bila kuzingatia ukweli ni miongoni mwa mambo yanayoweza kukwamisha maendeleo na hata kuliangamiza taifa.
Akizungumza leo Julai 21, 2026, ofisini kwake jijini Arusha, amesema kumekuwa na tabia ya baadhi ya watu kuwashambulia wanaohoji au kukosoa mambo mbalimbali, hususan kupitia mitandao ya kijamii, badala ya kujadili hoja zinazotolewa.
Ramsey amewataka viongozi kujifunza kuzungukwa na vijana wenye uwezo wa kutoa ushauri na ukosoaji wa kujenga, badala ya watu wanaosifia kila jambo. Amesema viongozi wanaokubali kukosolewa hupata fursa ya kujirekebisha na kufanya maamuzi bora zaidi kwa manufaa ya taifa.
Katika miaka ya hivi karibuni, neno "uchawa" limekuwa likitumika kuelezea tabia ya kujipendekeza, kumsifia kupita kiasi au kumtetea mtu mwenye mamlaka au ushawishi kwa lengo la kupata maslahi binafsi kama fedha, nafasi au upendeleo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Chama cha Wanasheria Afrika Mashariki (EALS), kwa kushirikiana na Taasisi ya Uongozi wa Mahakama (IJA), kinaendesha mafunzo ya siku mbili kwa Majaji na Mahakimu jijini Dar es Salaam. Mafunzo hayo yanawakutanisha maafisa wa mahakama kutoka Tanzania Bara na Zanzibar ili kutafakari nafasi ya mahakama katika kuendeleza haki katika ukanda unaozidi kuunganishwa.
Mafunzo hayo yameandaliwa chini ya kaulimbiu: "Nafasi ya Mifumo ya Mahakama ya Tanzania katika Kutekeleza Wajibu wa Nchi Chini ya Mikataba na Kuendeleza Misingi ya Kisheria ya Kikanda."
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, Mheshimiwa Jaji Salma Mussa Maghimbi, alisisitiza kuwa Tanzania ni nchi huru, lakini haijatengwa na mifumo ya kisheria ya kikanda na ya bara ambayo ni sehemu yake. Alibainisha kuwa wajibu unaotokana na mikataba ya kimataifa haupunguzi mamlaka ya nchi, bali unaakisi ahadi ambazo Serikali imezikubali kwa hiari kuzitekeleza kupitia taasisi zake kwa mujibu wa Katiba na sheria za nchi.
Naye Mkurugenzi Mtendaji (CEO) wa East Africa Law Society (EALS)- chama cha wanasheria kinachowakilisha nchi za Afrika Mashariki, David Mongosi Sigano, alihudhuria semina hiyo na kusisitiza umuhimu wa kuwajengea uwezo wanataaluma wa sheria ili kuimarisha mifumo ya kisheria na ushirikiano katika ukanda huo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
"Wazo hili kwa CHAUMMA la kuchangia ni geni, je, hii sio tonetone? Hii sio tonetone, huu ni mchango kwaajili ya CHAUMMA, wa tonetone wapo lakini hii ni operesheni kwaajili ya kuichangia CHAUMMA, na huwezi kusema kuchangia kumeigwa mahali fulani kwani Tanzania anayechangisha fedha ni chama kimoja tu? Mbona harusi watu wanachangia, nayo ni tonetone?”, Kigaila.
Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Ukombozi wa Umma ((CHAUMMA), Benson Kigaila ameeleza hayo leo Julai 21, 2026 Jijini Dar es Salaam alipofanya mkutano na waandishi wa habari, uliolenga kuzindua kampeni mpya ya chama hicho ya "Tujenge Pamoja,Tanzania ni Sisi".This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Zoezi la maswali ya dodoso(cross examination) kwa mashahidi watatu wa upande wa waleta maombi katika shauri la kikatiba lililofunguliwa na mawakili wa Tundu Lissu wakidai kukosa faragha ya mazungumzo wanapomuona na kuzuiwa kumuona akiwa gerezani Ukonga anakoshikiliwa kwa mashtaka ya uhaini.
Kesho Julai 22, 2026 shauri hilo litaendelea kwa kuhojiwa kwa maswali ya dodoso kwa shahidi wa upande wa walalamikiwa ambaye ni Mkuu wa Gereza la Ukonga pamoja na maafisa magereza wengine waliokula kiapo katika shauri hili.
Sababu za kuahirishwa kwa shauri hilo leo ni kutokana na muda kuwa finyu hivyo upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili Stanley Kalokola uliiomba mahakama kuahirisha shauri hilo mpaka kesho.
Walalamikaji kwenye kesi hii ambao pia ndio waliokuwa mashahidi ni Mawakili watatu ambao ni Kulwa Maduhu, Nashon Nkungu na Paul Kisabo ambao ni mawakili wa Lissu huku wajibu maombi wakiwa ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Kamishna Jenerali wa Magereza, Mkuu wa Gereza la Ukonga, Tundu Lissu na Chama cha Wanasheria Tanganyika(TLS).
Simulizi ya ushahidi utaipata kwenye Youtube yetu ya JAMBO TVThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam imeifuta kesi ya Uhujumu uchumi Na. 13647/2026 iliyokuwa imefunguliwa Mahakamani hapo na Jamhuri dhidi ya wanafamilia wawili (2) ambao ni Adam Caiser Poppe na Caiser Hans Poppe
Maamuzi hayo ya Mahakama yamekuja kufuatia mapingamizi mawili (2) ya kisheria yaliyokuwa yamewekwa awali na Wakili wa utetezi Peter Kibatala chini ya kifungu cha 134, kifungu kidogo cha kwanza (1), na kifungu cha Nne (4), kifungu kidogo cha Tatu (3) cha Sheria ya mwenendo wa mashauri ya jinai sura ya 20, marejeo ya 2023, ambapo mapingamizi hayo yalikuja baada ya upande wa Jamhuri kuieleza Mahakama kuwa upelelezi wa kesi inayowakabili wateja wake haujakamilika
Katika maelezo yake Mahakamani, Wakili Kibata alisema kufunguliwa kwa kesi hiyo ikiwa bado upelelezi haujakamilika kumevunja maelekezo ya msingi yaliyitolewa na Bunge, yanayotokana na kifungu tajwa cha 134, ambapo licha ya Jamhuri kupitia kwa Wakili wa Serikali Mwandamizi Thawabu Issa kupinga hoja hizo lakini haikushawishi Mahakama kuifuta kesi hiyo,
Akiwa kwenye viunga vya Mahakama hiyo, Wakili Kibatala akawaeleza Waandishi wa Habari kile kilichoisukuma Mahakama leo, Jumanne tarehe 21/07/2026 kuifuta kesi hiyo na kuwaachia huru wateja wake
Wanafamilia hao walikuwa wanakabiliwa na makosa 22 Mahakama hapo, ambapo kati ya hayo makosa 20 yalikuwa ya jinai ya kawaida na makosa mawili (2) yalikuwa ya Uhujumu uchumi yakigawanyika katika mafungu mann (4) tofautiThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
"changieni chama nisiwakute nilipowaacha, tutagombana"
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu akimwambia Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) Wakili Deogratius Mahinyila leo mahakamani.
Lissu ameupongeza uongozi wa chama hicho kwa kuendelea kufanya kazi bila ya uwepo wake huku akiwataka kuongeza juhudi bila kumsubiri yeye atoke gerezani.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Ukombozi wa Umma ((CHAUMMA), Benson Kigaila amesema ili operesheni mpya ya chama hicho ya "Tujenge Pamoja#Tanzania ni Sisi" ikamilike, ni lazima wana CHAUMMA wajisajili na kulipa ada na viingilio na viongozi kuhakikisha wanachangia chama hicho ili kiendeshe shughuli zake ikiwemo oparesheni hiyo.
Kigaila ameeleza hayo leo Julai 21, 2026 Jijini Dar es Salaam alipofanya mkutano na waandishi wa habari, uliolenga kuzindua operesheni hiyo ambayo imelenga kupigania masuala ya msingi kama Katiba Mpya na matatizo mengine ya Watanzania.
"CHAUMMA itajengwa na Wanachaumma pamoja na wapenzi wa CHAUMMA, tunakokwenda tunakwenda na kadi, tunategemea tutasajili wanachama, wanachama watalipa ada zao. Watalipa viingilio kwa kadi na watalipa ada za uanachama za mwaka..., lazima viongozi na wanachama tuchangie chama, tutaomba wadau wachangie lakini lazima tuanze na viongozi", amesema Kigaila.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma, imeamuru Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Melkisedeki Kaijage, aachiwe kwa dhamana kuanzia Julai 21, 2026, wakati upelelezi wa tuhuma za uchochezi zinazomkabili ukiendelea.
Uamuzi huo umetolewa na Jaji Joachim Tiganga wakati wa usikilizwaji wa Shauri Na. 15653/2026.
Kaijage amekuwa akishikiliwa katika Kituo cha Polisi Chang'ombe kwa tuhuma za kuhamasisha maandamano yaliyojulikana kama "Sabasaba".
Upande wa Serikali ulieleza mahakamani kuwa haukuwa na pingamizi kwa maombi ya kumwachia kwa dhamana, na kwamba taratibu za dhamana zinaweza kuendelea kwa mujibu wa sheria.
Wakili wa mwombaji, Prosper Malangalila, alidai kuwa mteja wake alikaa mahabusu kwa siku 12 bila kufikishwa mahakamani, licha ya kosa analotuhumiwa kuwa linadhaminika.
Malangalila aliiomba Mahakama iamuru Kaijage aachiwe kwa dhamana, alipwe fidia kwa kuzuiliwa kwa muda huo na Serikali pia ilipe gharama za maombi hayo.
Baada ya kusikiliza hoja za pande zote, Mahakama iliamuru Kaijage aachiwe kwa dhamana, lakini ikakataa ombi la kulipwa fidia.
Mahakama imeeleza kuwa baada ya upelelezi kukamilika, Kaijage atafikishwa mahakamani kujibu rasmi tuhuma zinazomkabili
Nje ya Mahakama hiyo, tumezungumza kwa ufupi na Wakili Prosper Malangalila ambaye ni Wakili wa mleta maombi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Shauri la kikatiba lililofunguliwa na Mawakili wa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo @ChademaTZ2 Tundu Lissu wakilalamikia kunyimwa kumuona gerezani na kukosa faragha pindi wanapomuona limeahirishwa kwa muda wa lisaa limoja (saa saba na nusu mpaka saa nane na nusu mchana) kutoa mapumziko.
Leo ilikuwa ni zoezi la kuhoji maswali ya dodoso ambapo tayari Lissu amemhoji shahidi wa pili katika kesi ambaye ni Nashon Nkungu na shahidi wa tatu Paul Kisabo.
Wakili Nashon Nkungu alihojiwa maswali ya dodoso (Cross Examination) na Lissu baadae akaulizwa na upande wa mjibu maombi wa kwanza mpaka wa tatu kisha maswali ya kusawazisha na wakili wao Edson Kilatu hivyo zoezi la ushahdi wake limekamilika ambapo kwa upande wa Kisabo ameulizwa maswali ya dodoso na Lissu pekee baada ya mapumziko zoezi litaendelea.
Shauri hili la kikatiba na 7300/2026 limefunguliwa Mawakili Kulwa Maduhu, Nashon Nkungu na Paul Kisabo na linasilkilizwa Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam mbele ya Jopo la Majaji watatu Amir Mruma, Dkt. Angelo Rumisha na Dkt. LongopaThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Shauri la Kikatiba Na.7300/2026 lililofunguliwa na Mawakili Kulwa William Maduhu, Nashon Nkung na Paul Kisabo dhidi ya Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP) na wenzake linaendelea kwenye Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu Dodoma mbele ya jopo la Majaji watatu (3) wakiongozwa na Jaji Amir Mruma.
Katika shauri hilo, ambalo vikao vyake vya usikilizwaji vinafanyika kwenye Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam waleta maombi waliojitambulisha kwenye kesi hiyo kuwa ni Mawakili wa Tundu Lissu wanalalamikia kuzuiliwa na/au kukosa haki ya faragha wanapokwenda kumuona mteja wao gerezani Ukonga.
Wakati akihoji maswali ya dodoso (cross examination) kwa shahidi wa pili (2) wa waleta maombi Nashon Nkung, Tundu Lissu ambaye ni mjibu maombi wa nne (4) shauri hilo licha ya kueleza kuunga mkono hoja zote zilizoletwa Mahakamani hapo na waleta maombi, amegusia namna maafisa wa magereza walivyokataa kumpatia nakala ya hotuba ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume Huru ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani yaliyotokea Nchini Oktoba 29.2025 (Siku ya Uchaguzi Mkuu) na siku zilizofuata Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Chande Othman aliyowasilisha wakati anakabidhi ripoti ya tume hiyo
Lissu ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa amesema aliwaagiza Mawakili wake wamletee nakala hiyo, kutokana na kwamba katika kesi ya uhaini inayomkabili upande wa Jamhuri umefungua maombi madogo ya kumuongeza shahidi ambaye kwa namna moja au nyingine endapo maombi hayo yatakubaliwa yeye (Lissu) atajumuishwa moja kwa moja na matukio ya vurugu za Oktoba 29.2025 na siku zilizofuata.
Anasema licha ya kwamba vurugu hizo zilitokea ikiwa miezi sita (6) tangu awe gerezani, lakini analazimika kujiandaa na utetezi, na kwamba aliwaagiza Mawakili wake kumpelekea nyaraka hiyo kama sehemu ya maandalizi ya utetezi wake, lakini licha ya Mawakili kufanya hivyo maafisa wa Magereza wameizuia na hawajamkabidhi hadi leo,
Kwa upande wake, Nkung ambaye alikuwa shahidi wa kwanza leo, Jumanne tarehe 21/07/2026 ameieleza Mahakama namna maafisa wa Magereza Ukonga wanavyo...soma zaidi hapa jambo.co.tz/lissu-aibua-madai-ya-kunyimwa-nakala-ya-hotub… -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Deus Sangu amewataka Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga kusimamia kwa uadilifu fedha zinazotolewa na Serikali kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili ilete tija na kuwanufaisha Wananchi.
Sangu ametoa kauli hiyo Julai 20, 2026, wakati akikagua eneo litakalojengwa Shule mpya ya Sekondari Uzia katika Kijiji cha Usangwa, Kata ya Muze, ambapo alisema usimamizi madhubuti wa fedha za umma ni msingi wa kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati na kwa ubora unaotarajiwa.
Amesema Serikali ya awamu ya 6 chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imetoa Shilingi Milioni 580 kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo, akisisitiza kuwa fedha hizo zitumike kwa malengo yaliyokusudiwa bila kuwepo ubadhirifu au matumizi yasiyoidhinishwa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mbunge wa Jimbo la Chato Kusini, Paschal Lutandula, amemuomba Waziri wa Madini, Antony Mavunde, kushirikiana na wawekezaji wa sekta ya madini kufanikisha ujenzi wa mabweni katika Shule za Sekondari Makurugusi na Buziba ili kupunguza changamoto zinazowakabili wanafunzi wa kike, hususan kusitisha masomo kutokana na umbali wa kutoka nyumbani hadi shuleni.
Lutandula ametoa ombi hilo wakati wa ziara ya Waziri Mavunde katika Jimbo la Chato Kusini mkoani Geita, ambapo alifika kukagua shughuli za uchimbaji wa madini pamoja na kujionea maendeleo ya miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa katika eneo hilo.
Amesema ujenzi wa mabweni hayo utatoa mazingira salama na rafiki kwa wanafunzi wa kike, kuongeza mahudhurio shuleni na kuchangia kuboresha kiwango cha ufaulu huku ukiwaondolea adha ya kutembea umbali mrefu kila siku.
Akijibu ombi hilo, Waziri wa Madini Antony Mavunde amesema Serikali itaendelea kuhimiza ushiriki wa sekta binafsi katika kuchangia maendeleo ya jamii kupitia uwajibikaji wa kampuni na wawekezaji wa madini.
Aidha, Waziri Mavunde amemuelekeza Mbunge Lutandula kushirikiana na wawekezaji wa sekta ya madini kuandaa harambee maalumu itakayowezesha kupatikana kwa fedha za ujenzi wa mabweni hayo, akieleza kuwa hatua hiyo itasaidia kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa wanafunzi na kuongeza fursa za watoto wa kike kuendelea na elimu bila vikwazo vinavyotokana na umbali.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Senegal imetangaza rasmi kuunga mkono nia ya Rais wake wa zamani, Macky Sall ya kuwania nafasi ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa. Hatua hii imefikiwa kufuatia kurejea kwake jijini Dakar wiki iliyopita, ambapo alifanya mazungumzo ya ana kwa ana na Rais wa sasa, Bassirou Diomaye Faye.
Uamuzi huu unatajwa kuwa unaashiria mabadiliko ya msimamo wa Senegal, kwani hapo awali nchi hiyo ilikataa kumuunga mkono kiongozi huyo aliyetawala kuanzia mwaka 2012 hadi 2024.
Serikali ya Senegal haikutaka kumuunga mkono Sall kutokana na tuhuma za utawala wake kutekeleza mateso na unyanyasaji wa kisiasa dhidi ya wapinzani wake alipokuwa madarakani.
Taarifa za vyombo vya Habari zinasema hatua ya Rais Faye kubadili msimamo na kumuunga mkono Sall inachochewa zaidi na sababu za kisiasa. Tangu alipoondoka madarakani mwaka 2024, Sall amekuwa akiishi uhamishoni nchini Morocco.
Hapo awali, mapendekezo ya Sall kuwania nafasi hiyo ya kimataifa yalitolewa na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, Rais Evariste Ndayishimiye wa Burundi. Hata hivyo, mpango huo ulikwama baada ya mataifa zaidi ya 20, ikiwemo Senegal yenyewe, kukataa kumuunga mkono. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
"Changieni Baraza Kuu, changieni chama cha ukombozi"
Ni maneno ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo @ChademaTZ2 Tundu Lissu baada ya kuingia mahakamani ambapo leo anatarajiwa kuendelea kuuliza maswali ya dodoso kwa mashahidi kwenye shauri la kikatiba na 7300/2026 lililofunguliwa Mawakili Kulwa Maduhu, Nashon Nkung na Paul Kisabo ambao wanalalamikia kuzuiwa kuingia gereza la Ukonga na kushindwa kupata faragha ya mazungumzo na mteja wao(Lissu) walipofanikiwa kuingia.
Baada ya kumaliza dodoso la jana kwa kwa shahidi wa kwanza ambaye ni Maduhu, leo shauri hilo lililopo mbele ya jopo la Majaji watatu (3) ambao ni Amir Mruma, Dkt. Angelo Rumisha na Dkt. Evaristo Longopa litaendelea kwa maswali ya dodoso pande zote.
Tofauti na siku zingine, leo Lissu hatokaa kwenye kizimba badala yake ametengewa kiti na meza kutokana na maelekezo ya Mahakama yaliyotolewa na mahakama jana kuwa asikae kwenye kizimba kutokana na kuwa shauri lililopo mahakamani ni la kikatiba sio la jinai.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Jimbo la Geita, Neema Chozaire, ameachiwa kwa dhamana na Mahakama ya Wilaya ya Geita baada ya kutimiza masharti ya dhamana yaliyowekwa na mahakama.
Akizungumza siku ya Jumatatu mara baada ya uamuzi huo, Katibu wa CHADEMA Kanda ya Victoria, Zacharia Obadi, amesema awali walifika katika Mahakama Kuu, Masijala Ndogo ya Geita, ambapo waliwasilisha maombi ya kutaka mtuhumiwa afikishwe mahakamani pamoja na kuomba apewe fidia kwa kile walichodai kuwa ni ukiukwaji wa haki zake.
Obadi amesema baada ya maombi hayo kusikilizwa, upande wa Jamhuri uliieleza Mahakama Kuu kuwa tayari shauri hilo lilikuwa limefunguliwa katika Mahakama ya Wilaya ya Geita, hivyo kesi ikaendelea kusikilizwa katika mahakama hiyo.
Katika Mahakama ya Wilaya ya Geita, Wakili wa Serikali, Liberatus John, alidai kuwa Neema Chozaire anakabiliwa na shtaka la kula njama ya kutaka kuwaua askari wa Jeshi la Polisi.
Kwa upande wa utetezi, Wakili Beatus Emanueli aliiomba mahakama imwachie mteja wake kwa dhamana akieleza kuwa alitimiza vigezo vinavyohitajika kisheria.
Baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Geita, Mujuni Mchunguzi, alikubali ombi hilo na kuamuru Neema Chozaire aachiwe kwa dhamana baada ya kukidhi masharti yaliyowekwa na mahakama.
Kesi hiyo inatarajiwa kuendelea katika tarehe itakayopangwa na mahakama kwa ajili ya hatua nyingine za kisheria.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mvutano unaohusu mgogoro wa ardhi kati ya Taasisi ya Imam Taqwa na wananchi wa Mtaa wa Mpamaa, Kata ya Miyuji jijini Dodoma umechukua sura mpya baada ya wananchi kuwazuia maafisa wa Jiji la Dodoma waliofika kwa ajili ya kuhakiki mipaka ya eneo hilo, wakidai zoezi hilo haliwezi kuendelea kabla haki haijatendeka.
Mgogoro huo, ambao tayari umesababisha kubomolewa kwa zaidi ya nyumba 17, umewaacha baadhi ya familia bila makazi ya kudumu. Wananchi hao wanasema hawako tayari kuondoka katika eneo hilo licha ya nyumba zao kubomolewa, wakisisitiza kuwa wataendelea kubaki hadi pale watakapopata haki wanayoidai.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Mtaa wa Mpamaa, Bi. Happy Joshua, amesema serikali ya mtaa haikupata taarifa yoyote kuhusu utekelezaji wa zoezi la ubomoaji wa nyumba hizo, jambo ambalo limezua maswali kuhusu utaratibu uliotumika.
Wakati huo huo, baadhi ya maafisa wa Jiji la Dodoma waliofika kwa ajili ya uhakiki wa mipaka walikataa kuzungumza na waandishi wa habari kuhusu sakata hilo licha ya kuombwa kutoa ufafanuzi.
Akizungumza na Jambo TV kwa njia ya simu, Mwenyekiti wa Taasisi ya Imam Taqwa, Yusuph Hussein, amesema taasisi hiyo ilinunua eneo husika mwaka 2016 likiwa halina nyumba yoyote kwa lengo la kujenga msikiti na shule. Amedai kuwa baadaye wananchi walivamia eneo hilo na kuanza kujenga makazi, huku akisisitiza kuwa taasisi hiyo inamiliki hati halali ya eneo hilo na kwamba inasubiri kuanza utekelezaji wa mradi wake wa ujenzi.
Jambo TV inaendelea kufuatilia kwa karibu mgogoro huo wa ardhi kati ya Taasisi ya Imam Taqwa na wananchi wa Mtaa wa Mpamaa na itaendelea kuwaletea taarifa zaidi, ikiwemo majibu ya mamlaka husika pamoja na hatua zitakazochukuliwa kutafuta suluhu ya mgogoro huo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mkazi wa Kijiji cha Itipula, Halmashauri ya Mji wa Njombe, Lenard Zabron, amemtaka Mbunge wa Jimbo la Njombe Mjini, Deodatus Mwanyika, kushirikiana na wabunge wengine kuhakikisha mabaraza ya ardhi yanafutwa, akidai yamekuwa yakichochea migogoro badala ya kuitatua.
Zabron ametoa ombi hilo wakati wa mkutano wa kusikiliza kero za wananchi uliofanyika kijijini hapo.
"Ninaomba mabaraza ya ardhi ya Wilaya yafutwe, siyo yarekebishwe, yafutwe kwa sababu yanarefusha kesi na mwisho wa siku mtu anakufa anaiacha kesi," amesema.
Akijibu hoja hiyo, Mbunge wa Jimbo la Njombe Mjini, Deodatus Mwanyika, amekiri kuwepo kwa changamoto katika baadhi ya mabaraza ya ardhi na kuahidi kuzifanyia kazi kwa kushirikiana na mamlaka husika.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Wananchi wa Kata ya Mchichira wilayani Tandahimba wameamua kuunganisha nguvu na rasilimali zao kujenga Kituo cha Afya baada ya mradi huo kusuasua kwa zaidi ya miaka 10 tangu uwekwe jiwe la msingi na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2008.
Hatua hiyo imekuja kufuatia changamoto ya muda mrefu ya ukosefu wa huduma za afya, huku wakazi zaidi ya 7,905 wa kata hiyo wakilazimika kusafiri umbali mrefu kupata matibabu katika maeneo mengine.
Mwananchi wa eneo hilo, Mariamu Mangamba, amesema wanawake wajawazito ndio wanaoathirika zaidi kutokana na kukosekana kwa kituo hicho, kwani hulazimika kufuata huduma za kujifungua mbali na makazi yao.
Diwani wa Kata ya Mchichira, Azizi Muhibu, amesema mwitikio wa wananchi umekuwa mkubwa, ambapo wamechangishana fedha, wamenunua eneo la ujenzi na tayari wameanza kujenga jengo la wagonjwa wa nje (OPD).
Muhibu ameiomba Serikali kuunga mkono jitihada hizo kwa kutoa fedha na vifaa vitakavyowezesha kukamilika kwa ujenzi wa kituo hicho ili wananchi waanze kupata huduma za afya karibu na makazi yao.
Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Tandahimba, Katani Ahmed Katani, ameahidi kuchangia shilingi milioni 50 kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa kituo hicho na kuitaka Serikali kushirikiana na wananchi kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati na kuanza kutoa huduma.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mwigulu Nchemba amesema maendeleo ya kweli ya Taifa yanategemea kujenga wananchi wenye maadili, uzalendo, uwajibikaji na mshikamano, huku akisisitiza umuhimu wa kuendelea kuimarisha utawala wa sheria na taasisi za umma.
Waziri Mkuu amesema hayo leo Julai 20, 2026 alipokutana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Mzee Joseph Butiku, katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Oysterbay, jijini Dar es Salaam.
"Hakuna maendeleo ya kudumu bila kujenga watu wenye maadili, uzalendo na uwajibikaji. Kama Taifa tuna kila sababu ya kuendelea kuwekeza katika kujenga tabia ya wananchi pamoja na kuimarisha taasisi zetu," amesema Waziri Mkuu.
Katika mazungumzo hayo, Mzee Butiku amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa uongozi wake na juhudi anazoendelea kuzifanya katika kuiongoza nchi. Pia, amempongeza Waziri Mkuu kwa mchango wake katika kumsaidia Rais kusimamia Serikali na kuhakikisha utekelezaji wa majukumu ya Serikali unaendelea kwa ufanisi.
Aidha, ameishukuru Serikali kwa kuendelea kushirikiana na Taasisi ya Mwalimu Nyerere na kuipatia mazingira ya kutekeleza majukumu yake, ikiwemo kupata eneo la ujenzi wa Mwalimu Nyerere World Leadership Institute, pamoja na kuitambua Taasisi hiyo kama mshirika wa maendeleo ya Taifa.
Mzee Butiku pia amesisitiza umuhimu wa kuendelea kujenga jamii inayoheshimiana, inayovumiliana na inayozingatia maadili, uzalendo, utawala wa sheria, haki za watu na misingi ya demokrasia. Amesema kumekuwepo na mwenendo wa baadhi ya watu kuwavunjia heshima viongozi, wazee, viongozi wastaafu na viongozi wa dini, jambo ambalo halijengi utaifa wala haliendani na misingi ya Taifa.
Ameongeza kuwa ni muhimu Watanzania kuendelea kukosoana kwa hoja na kwa kuzingatia sheria, huku kila mmoja akitimiza wajibu wake kwa lengo la kulinda amani, usalama, umoja na mshikamano wa Taifa. Amesema Taasisi ya Mwalimu Nyerere itaendelea kutoa elimu ya amani, maadili na uzalendo kwa manufaa ya Taifa.
Aidha ameipongeza Serikali kwa hatua inazoendelea kuchukua katika kuimarisha amani, utulivu, haki za watu, Serikali za Mitaa na misingi ya demokrasia. Amesema hatua hizo zimeendelea kuimarisha mshikamano wa Taifa na kurejesha hali ya utulivu nchini. Pia amepongeza hatua ya kuendelea kutoa kipaumbele suala la Katiba Mpya kupitia Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2025–2030. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
"Yataisha"
Hilo amesema Mwenyekiti wa @ChademaTZ2 baada ya kukamilika zoezi za maswali ya dodoso kwa shahidi William Maduhu katika kesi iliyofunguliwa juu ya mawakili kunyimwa kupata haki ya faragha wanapomtembelea gerezani.
Kesi hiyo namba 7300/2026 imefunguliwa Mahakama Kuu Masjala Kuu ya Dodoma na Nashon Nkung, William Maduhu na Paul Kisabo dhidi ya Kamishna Jenerali wa Magereza nchini na wengine ambapo leo Mahakama Kuu imeketi jijini Dar es Salaam.
Shauri limeahirishwa na litaendelea kesho kwa ajili ya maswali ya dodoso kwa mashahidi wengine.
NB:Tutakuletea simulizi kamili ya dodoso la leo. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kutoka Tabora hadi Kigoma utakapokamilika, utawawezesha wajasiriamali na wakulima mkoani Kigoma kupata pembejeo za kilimo kwa haraka na uhakika.
Akizungumza baada ya hafla ya uzinduzi wa meli nne za mizigo na uwekaji wa Jiwe la Msingi la Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kipande cha Tabora hadi Kigoma leo Julai 20, 2026 mkoani Kigoma, Dkt. Samia amesema reli hiyo itawasaidia wafanyabiashara kupunguza gharama pamoja na muda wa usafirishaji.
"Kwa wakulima wa Kigoma maana yake ni kwamba pembejeo zitawafikia kwa gharama nafuu na mazao yanayozalishwa yatapata masoko makubwa. Kwa ndugu zetu wanaoendesha maisha yao kwa kutegemea shuguli za uvuvi watasafirisha kwa urahisi mazao ya uvuvi kwenda kwenye masoko ya uhakika, vilevile wafanyabiashara na wajasiriamali reli hii itakapokamilika itawapunguzia muda na gharama za usafirishaji" amesema Dkt. SamiaThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema serikali itaendelea kuimarisha, kuendeleza na kuboresha miundombinu ya usafiri na usafirishaji kwa manufaa ya wananchi na taifa kwa ujumla.
Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa meli nne za mizigo na uwekaji wa Jiwe la Msingi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kipande cha Tabora hadi Kigoma leo Julai 20, 2026 mkoani Kigoma, Dkt. Samia amesema utekelezaji huo unalenga kukuza biashara, ajira na kipato kwaajili ya wananchi.
"Tunafanya hayo ili kukuza biashara, kipato na ajira kwa wananchi wetu na ustawi wa taifa letu kwa ujumla. Kwa muktadha huo, Kigoma haitokuwa tena mwisho wa reli kama ambavyo imekuwa ikifahamika bali itakuwa ni mwanzo wa kufunguka kwa fursa za kibiashara na uwekezaji", amesema Dkt. Samia.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa amesema Serikali ya Awamu ya Sita inaendelea kutekeleza uwekezaji mkubwa katika sekta ya uchukuzi unaolenga kuifanya Kigoma kuwa kitovu cha usafirishaji na biashara kinachounganisha Tanzania na nchi za Afrika Mashariki na Kati.
Prof. Mbarawa amesema hayo leo Jumatatu Julai 20, 2026 katika hafla iliyohudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, wakati wa uzinduzi wa meli nne za mizigo, uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa gati la abiria na mizigo Bandari ya Kigoma pamoja na uzinduzi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kipande cha Tabora–Kigoma.
Amesema chini ya uongozi wa Rais Samia, Serikali imewekeza kwa kiwango kikubwa katika reli ya kisasa, bandari, viwanja vya ndege na usafiri wa majini kwa lengo la kuunganisha mikoa yote ya Tanzania pamoja na nchi jirani kupitia mfumo jumuishi wa uchukuzi.
Kwa mujibu wa Profesa Mbarawa, meli nne mpya za mizigo zitaongeza usalama wa usafirishaji katika Ziwa Tanganyika, kupunguza gharama za usafirishaji wa mizigo, kukuza biashara kati ya Tanzania, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Burundi, pamoja na kufungua fursa mpya za ajira na uwekezaji.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi wa Kigoma na Watanzania kwa ujumla kudumisha amani na usalama ili kuchochea maendeleo, huku akivielekeza vyombo vya ulinzi na usalama, kwa kushirikiana na Wizara ya Uchukuzi kuweka mikakati madhubuti na shirikishi ya ulinzi wa miundombinu inayojengwa mkoani humo.
Dkt. Samia ametoa wito huo leo Julai 20, 2026 mkoani Kigoma mara baada ya hafla ya uwekaji jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa Reli ya kisasa (SGR) kutoka Tabora hadi Kigoma, akibainisha kuwa serikali imewekeza fedha nyingi katika miradi ya maendeleo, ikiwemo reli ya kisasa (SGR), pamoja na miradi ya meli na maboresho ya bandari ya Kigoma. Amesisitiza kuwa ni wajibu wa kikatiba na kizalendo kwa kila Mtanzania kulinda miundombinu hii dhidi ya hujuma.
Aidha, Dkt. Samia amewataka wananchi kuepuka kushawishiwa au kutumika na watu (wa ndani au nje) wasioitakia mema nchi akitoa mfano wa nchi jirani ambazo hukosa fursa ya kuzalisha ndani na kulazimika kuagiza kila kitu kutoka nje kwa sababu ya ukosefu wa amani.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Uchaguzi mdogo wa ubunge katika Jimbo la Ol Kalou, Kaunti ya Nyandarua nchini Kenya, uliofanyika Julai 16, 2026, umeibua mjadala mpana wa kisiasa huku ukitajwa kuwa kipimo muhimu cha kuelewa mwelekeo wa ushindani kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2027.
Uchaguzi huo ulilenga kumpata mrithi wa aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo, David Njuguna Kiaraho, aliyefariki dunia, lakini uligeuka kuwa uwanja wa ushindani mkubwa kati ya Chama cha Democracy for Citizens Party (DCP) cha aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua na United Democratic Alliance (UDA) cha Rais William Ruto.
Katika mchakato huo, vyombo mbalimbali vya habari nchini Kenya viliripoti kuwa Wananchi walijitokeza kwa wingi ambapo 57% walipiga kura, huku baadhi wakikuchukua hatua za ziada walizodai zililenga kulinda uadilifu wa kura zao
Video na picha mbalimbali zilizosambaa mtandaoni zilionesha Wananchi wakiweka vizuizi katika barabara zinazoingia eneo la uchaguzi na kusimamisha magari, kuyakagua pamoja na mizigo iliyokuwamo wakidai kuhakikisha hakuna jaribio la kuvuruga mchakato wa uchaguzi.
Hatimaye, mgombea wa DCP, Sammy Douglas Kamau Waweru, aliibuka mshindi kwa kupata kura 35,440 dhidi ya Samuel Muchina Nyagah wa UDA aliyepata kura 5,450.
Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanasema hatua za Wananchi kujitokeza kulinda kura kunaibua mjadala kuhusu nafasi yao kama nguzo muhimu katika kuhakikisha uwajibikaji na uaminifu wa chaguzi zijazo nchini humoThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini, Clayton Revocatus Chipando (Baba Levo) amewakosoa wale anaowaita "wenye midomomidomo" ambao hawasemi mazuri yanayofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, bali wanapiga kelele pale serikali inapokopa fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
Akizungumza leo Julai 20, 2026 mkoani Kigoma mara baada ya hafla ya uwekaji jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa Reli ya kisasa (SGR) kutoka Tabora hadi Kigoma uliofanywa na Dkt. Samia, Baba Levo amejitanabaisha kama mtetezi wa Rais Samia akijitambulisha kuwa ‘Cha mdomo’ wake kwa kutetea kazi zinazofanywa na Rais.
Kuhusu uwepo wa makundi, mbunge huyo ameweka wazi kuwa yeye yuko kwenye "kundi la mama" (Rais Samia) na yuko tayari kupambana na mbunge yeyote bungeni atakayejaribu kuipinga dhamira ya serikali ya awamu ya sita.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Leo Jumatatu Julai 20, 2026 mkoani Kigoma, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) la kipande cha kutoka mkoa wa Tabora hadi Kigoma.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amezindua ujenzi wa meli nne za mizigo katika bandari ya Kigoma leo Julai 20, 2026, zinazotarajiwa kurahisisha usafiri wa mizigo katika Ziwa Tanganyika.
Akizungumza kuhusu meli hizo, Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa amesema mwekezaji anayeitwa Golden Logistic Company Limited ndiye anayejenga meli hizo mizigo kwa lengo la kuboresha usafiri katika Ziwa Tanganyika na maeneo ya jirani.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Plasduce Mbossa ameeleza kuwa maboresho yanayoendelea katika Bandari ya Kigoma ikiwamo mradi mkubwa wa kurekebisha gati lenye urefu wa mita 310 katika eneo la mizigo, yana lengo la kuongeza uwezo wa kuhudumia mizigo kutoka tani 8,000 kwa mwaka hadi kufikia tani milioni mbili.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Mjadala kuhusu dhana ya uanaharakati na nafasi yake katika historia na ustawi wa taifa la Tanzania unazidi kutawala katika majukwaa mbalimbali ikiwamo yale ya mitandao ya kijamii, kutokana na kauli iliyotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan Julai 9, 2026, visiwani Zanzibar, wakati wa hafla ya utiaji saini mkataba wa maridhiano ya kisiasa kati ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na ACT Wazalendo.
Katika hotuba hiyo, Dkt. Samia ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM Taifa aliwaonya ‘watu wanaojivika mwavuli wa uanaharakati’ ili kupata umaarufu wa kimataifa, huku nyuma ya pazia wakisukumwa na maslahi binafsi na vitendo vyenye viashiria vya kigaidi vilivyojificha kwenye sura ya uzalendo. Rais alisisitiza kuwa serikali haitafanya mzaha na vitendo vyote vya kigaidi na akawataka Watanzania kushikamana kwa ajili ya maendeleo badala ya kufuata makundi yenye ajenda zilizofichika.
Katika kile ambacho kimeelezwa kuwa mwendelezo wa utoaji maoni juu ya kauli ya Dkt. Samia, Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Karagwe, Dkt. Benson Bagonza kupitia ukurasa wa Facebook amekumbusha kuwa herufi “M” katika jina la CCM inasimama badala ya "Mapinduzi," ambayo amesema kimsingi ndiyo kilele cha juu kabisa cha uanaharakati. Askofu Bagonza amefafanua kuwa chama tawala ndicho chimbuko kuu la harakati nchini, akitolea mfano hatua ya TANU kujitenga na starehe za chama cha kijamii cha TAA ili kupigania uhuru, pamoja na Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya mwaka 1964 chini ya ASP yaliyoleta ukombozi wa kweli.
“Mwaka 1967, TANU ilizindua Azimio la Arusha baada ya kukiri kuwa “tumenyonywa vya kutosha na sasa tunataka mapinduzi ili tusinyonywe tena”. Azimio la Arusha lilipindua meza na kuwafanya watwana kuwa mabwana. Hizo ni harakati. Mwaka 1977, TANU na ASP viliungana na kuunda CCM. Chama chenye historia ya kumwaga damu (ASP) kikaungana na chama chenye historia ya kudai haki kwa fikra kali na pevu (TANU). “Mapinduzi” ilikuwa ni alama wazi iliyowakilishwa na jembe na nyundo katika utambulisho wake. Ni harakati bado”, ameandika Dkt. Bagonza.
Kiongozi huyo wa kiroho amesisitiza kuwa chini ya mifumo ya asili ya TANU na CCM, ulinzi wa taifa ulikuwa mikononi mwa wananchi wenyewe, na vyombo vya dola vilitazamwa kama watumishi wa umma na sio zana za kukandamiza wanyonge kama inavyotazamwa sasa na baadhi ya Watanzania.
“Kimsingi, CCM ndiye baba wa harakati, nguzo ya haki na mpinga dhuluma popote duniani. Isimame ihesabiwe na isiwaache wapinzani kujitwalia utukufu kwa tunu za CCM. Yaliyotupata yote ni kwasababu tumeacha na kubeza harakati. Taifa lisilo na harakati ni sawa na pango la wanyang’anyi. Wanyonge ni kitoweo cha wenye nguvu. Taifa linajengwa na wenye moyo na kuliwa na wenye meno. Shangingi la Kijaluo linaimba, “Ukitoka na mume wangu, napita na baba yako ili uniite mama yako na mimi nikuite mke mwenza. Mama mkwe akikuzingua, mzingue binti yake mtaheshimiana””, amehitimisha Dkt. Bagonza. -
Jambo TV
@Jambotv_
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Jeshi la Polisi nchini Burundi limethibitisha kufariki kwa watu wasiopungua nane na wengine tisa kujeruhiwa katika tukio la mkanyagano uliotokea jijini Bujumbura, usiku wa kuamkia Jumapili ya Julai 19, 2026.
Maafa hayo yametokea baada ya maelfu ya waumini wa dini ya Kikristo kukusanyika katika uwanja wa Shule ya Ufundi ya Kamenge (ETS Kamenge) kuhudhuria mkutano mkubwa wa kidini wa mhubiri maarufu Chris Ndikumana, ambaye anajulikana kikanda.
Kulingana na mashuhuda na mamlaka za usalama, mkanyagano huo ulitokea wakati ibada ilipomalizika na umati huo mkubwa kujaribu kuondoka uwanjani hapo kwa wakati mmoja kupitia milango midogo ya kutokea. Hadi sasa, waandaaji wa mkutano huo hawajatoa tamko lolote rasmi kuhusu vifo na majeruhi hao.
Maafa haya yanakumbusha tukio lingine lililotokea katika taifa la Tanzania mnamo Februari mwaka 2020, ambapo watu takriban 20 walifariki dunia na wengine 12 kujeruhiwa mjini Moshi, wakati wakigombea kukanyaga "mafuta ya upako" kwenye mkutano wa kidini kama huo. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Patrobas Katambi amesema serikali itaendelea kupambana na viashiria vya uvunjifu wa amani huku ikidhibiti wale ambao wanapanga kufanya matukio yoyote yatakayohatarisha usalama wa nchi.
Ametoa kauli hiyo akizungumza na Makundi ya Walinzi wa amani katika jamii, Polisi jamii, Wazee, Sungusungu, Wenyeviti wa Mitaa,Mabalozi na Wenyeviti wa Vitongoji Vitongoji, Shinyanga Mjini.
Pamoja na hayo ameeleza kuwa mpaka sasa hajapokea wito wowote kutoka mahakamani kutokana na uwepo wa taarifa za kuwa kuna imefunguliwa dhidi yake.
“timu hiyo inayosema inanipeleka mahakamani ndiyo hiyo hiyo ilikua inapinga Mkataba wa Uwekezaji wa bandari...wameshindwa kuwapeleka mahakamani ambao wanachochea kuangamiza Taifa letu kwa kuchoma moto. Kama wana uchungu kweli na haki za Binadamu ni lini na wapi mliwasikia wanakemea vitendo hivyo hatarishi kwa uhai wa watu na Taifa?” amehoji Katambi
Kauli ya Katambi inakuja ikiwa zimepita siku chache tangu Mwanasiasa Dkt. Wilbroad Slaa, Chama cha Wanasheria Tanganyika(TLS) na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu(LHRC) kutoa taarifa kwa umma kuwa wamefungua kesi dhidi ya Waziri wa Mambo ya Ndani kuhoji juu ya katazo la mikutano ya hadhara lililotolewa na Patrobas Katambi bungeni Juni 26, 2026. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Misri zimekubaliana kuimarisha ushirikiano katika sekta ya usafirishaji kwa kuunganisha bandari za nchi hizo, hatua inayotarajiwa kurahisisha biashara, kuongeza uwekezaji na kufungua masoko mapya barani Afrika na eneo la Ghuba.
Akizungumza Ikulu jijini Dar es Salaam leo Julai 18, 2026 mara baada ya kumpokea Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, Abdel Fattah El-Sisi, Dkt. Samia amesema makubaliano hayo yanahusisha maendeleo ya Bandari ya Dar es Salaam pamoja na ujenzi wa eneo maalumu katika Bandari ya Bagamoyo litakalounganishwa na reli hadi Kwala kwa ajili ya kuhifadhi bidhaa na makontena ya Misri.
Amesema nchi hizo pia zimehimiza kuendelea kwa majadiliano ya kuunganisha Bandari za Dar es Salaam, Bagamoyo, Safaga na bandari nyingine za Misri ili kurahisisha usafirishaji wa bidhaa, kuongeza ushindani wa biashara na kufungua fursa kwa bidhaa za Tanzania kuingia katika masoko ya Ghuba huku bidhaa za Misri zikifikia nchi za Kusini mwa Afrika.
Rais Samia amesisitiza kuwa ushirikiano huo utaifanya Tanzania kuwa lango muhimu la biashara kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini, huku ukiimarisha uhusiano wa kiuchumi kati ya mataifa hayo mawili.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) @InvestTanzania imewaeleza wawekezaji na wafanyabiashara kutoka Misri sababu za kwanini Tanzania ni mahali salama kwa uwekezaji wa mitaji yao.
Akizungumza Jumamosi Julai 18, 2026 wakati wa Jukwaa la Uwekezaji na Biashara la Tanzania na Misri lililofanyika mkoani Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa TISEZA, Gilead Teri @GileadTeri amesema mwekezaji anapoweka fedha zake Tanzania, zinalindwa na mifumo ya kimataifa hivyo hakuna hofu ya kupoteza mtaji.
Aidha, Teri amesema Tanzania si tu soko la ndani, ni lango la kufika Ulaya, China, na India kupitia mikataba ya biashara huria, akitoa mfano wa kampuni ya Elsewedy ambayo inatumia ardhi ya Tanzania kuzalisha na kuuza bidhaa zake katika kanda nzima ya Afrika
Kwa upande mwingine, Teri ameeleza kuwa tangu tarehe 1 Julai mwaka huu, Tanzania imeanza kutekeleza Dira ya 2050, ambayo ni mpango wa kimkakati wa miaka 25 ijayo, akisisitiza kuwa serikali ina azma kubwa ya kukuza uchumi wa nchi kufikia thamani ya dola trilioni 1 (USD 1 trillion) ndani ya kipindi hicho cha miaka 25. Ili kufikia lengo hili, nchi inafanya mageuzi makubwa ya kiuchumi na kufungua fursa za ushirikiano na kampuni za kigeni zikiwamo zile zinazotoka Misri.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Leo Julai 3, 2026 Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo @ChademaTZ2 Tundu Lissu tayari amefikishwa Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Dar es Salaam kwa ajili ya maombi ya marejeo Na. 7440840/2026 kati ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) dhidi yake.
Maombi hayo yatasikilizwa na jopo la Majaji watatu wa Mahakama ya Rufani ambao ni Shimiwa Mwarija, Muruke na Khamis ambapo kumbi za Mahakama Kuu ndizo zitatumika kwa ajili ya shauri hilo.
Ikumbukwe msingi wa maombi haya ni uamuzi uliotolewa na Mahakama Kuu Februari 24, 2026 ambapo ilikubali maombi ya Lissu juu ya kuiomba Mahakama isipokee hati ya ushahidi wa ziada wa ACP Amini Mahamba unaohusu upelelezi wa matukio ya Oktoba 29, 2025.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
TUMERUDI HEWANI
-
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwanahabari mkongwe nchini, Jenerali Ulimwengu, amesema marehemu Mzee Edwin Mtei, muasisi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), alikuwa kiongozi aliyekataa vikali vitendo alivyoviita “Uswahili” katika uongozi, hususan tabia ya viongozi kukiuka ahadi walizozitoa kwa wananchi.
Ulimwengu ametoa kauli hiyo wakati wa shughuli za mazishi ya marehemu Mzee Mtei, akieleza kuwa marehemu aliamini katika uadilifu, uwajibikaji na uaminifu kwa wananchi kama misingi muhimu ya uongozi wa kweli.
Kwa mujibu wa Ulimwengu, Mzee Mtei hakuwa tayari kuvumilia unafiki wala siasa za maneno matamu zisizoendana na vitendo, akisisitiza kuwa kiongozi bora ni yule anayesimama na kutekeleza alichoahidi bila visingizio.
Mazishi ya Mzee Mtei yamehudhuriwa na viongozi wa kisiasa, wanachama wa CHADEMA, ndugu, jamaa na wananchi mbalimbali waliokuja kutoa heshima zao za mwisho, huku wengi wakimtaja marehemu kama kiongozi aliyethamini misingi ya haki, ukweli na demokrasia ya kweli.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mgombea wa nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Iramba Magharibi Mkoani Singida kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, amesema katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Serikali ya Awamu ya Sita imeweka rekodi ya kuajiri vijana wengi zaidi na kutengeneza fursa nyingi za ajira kwa Watanzania katika sekta mbalimbali kuliko kipindi chochote kilichopita.
Akizungumza leo Jumapili Oktoba 19, 2025, katika Mkutano wa Kampeni za Mgombea wa Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Samia Suluhu Hassan uliofanyika Viwanja vya Kizwite, Sumbawanga Mjini mkoani Rukwa, Dkt. Mwigulu amesema hatua hiyo inaonesha dhamira ya Rais Samia katika kujenga uchumi jumuishi unaowanufaisha wananchi wa makundi yote.
Amesema Dkt. Samia ni kiongozi mwenye upendo, anayeguswa na matatizo ya wananchi wake na anayechukua hatua za vitendo katika kuyatatua. Ametolea mfano namna alivyosikia malalamiko kuhusu tozo, kodi nyingi na ukosefu wa urasimu rafiki kati ya wafanyabiashara na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), na kuchukua hatua ya kuondoa zaidi ya kodi na tozo 250 zilizokuwa kero kwa wananchi.
Aidha, Dkt. Mwigulu amesema Rais Samia alihakikisha madeni makubwa yaliyokuwa yakidaiwa na Serikali yanalipwa, hatua iliyopunguza mzigo kwa wananchi na kuongeza ufanisi wa taasisi za umma, huku akiboresha huduma za afya kwa kujenga hospitali na kununua vifaa tiba vya kisasa ikiwemo mashine za CT-Scan katika hospitali mbalimbali nchini.
Ameongeza kuwa mafanikio hayo yameendelea kutambuliwa kimataifa na taasisi kubwa kama Benki ya Dunia, ambazo zimeitaja Tanzania kuwa miongoni mwa nchi kinara katika sekta za maji, elimu na afya kwa kutimiza malengo ya maendeleo endelevu (SDGs).
Dkt. Mwigulu amewataka Watanzania kuendelea kumuamini Dkt. Samia, akisema wanaoikosoa Serikali ya Awamu ya Sita hawana nia njema, bali wanataka kudhoofisha maendeleo yanayowanufaisha wananchi wengi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Na Fredrizzo Samson
Watu saba(7) wamefariki baada ya gari walilokuwa wakisafiria kugonga lori lililokuwa limeharibika na kusimama barabarani katika Kijiji cha Kongo kata ya Bukwe wilayani Rorya, mkoani Mara.
Ajali hiyo imetokea alfajiri ya leo Septemba 11, ambapo watu hao saba walikuwa kwenye gari dogo aina ya Probox yenye namba za usajili T.625 DYV ambayo iliyogonga lori lililokuwa limeharibikia barabarani.
Inaelezwa kuwa watu hao jana Septemba 10, walitokea Kijiji cha Utegi kwenda Tarime Mjini kufurahia 'Simba Day 'na Usiku walianza safari yao kutoka Tarime mjini kurudi Utegi walipofika katikati ya Kijiji cha Kongo kata ya Bukwe wilayani Rorya ndipo walipolivaa lori hilo.
Jambo TV imezungumza na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Tarime, Yonah Charles amethibitisha vifo vya watu hao akieleza kuwa alfajiri yaleo wamepokea miili ya watu saba watatu wakiwa wanawake na wanne wanaume wakiwa wamefariki kutokana na ajali. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Tanga Mjini, Ummy Mwalimu, ametoa wito kwa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika jimbo hilo kumuunga mkono Kassim Amari Mbaraka, aliyepitishwa na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kuwa mgombea wa ubunge wa Tanga Mjini, huku akisisitiza umuhimu wa kuvunja makundi ndani ya chama.
Ummy ametoa kauli hiyo Jumatatu, Agosti 25, 2025, akizungumza na wanahabari mkoani Dar es Salaam, akisema maamuzi ya chama yanapaswa kuheshimiwa na kila mwanachama.
"Kwa sisi WanaCCM pale ambapo chama tayari kimefanya maamuzi ya kumteua mtu kuwa mgombea wa CCM katika uchaguzi wa vyombo vya dola, wajibu wetu sisi sote ni kuheshimu uamuzi huo. Ninawaomba sana ndugu zangu kumuunga mkono ndugu yetu Kassim Amari Mbaraka ambaye ameteuliwa na chama chetu kuwa mgombea wetu wa Jimbo la Tanga Mjini," amesema Ummy.
Kauli hiyo ya Ummy inakuja siku moja tu baada ya makundi ya wanachama wa CCM Tanga kuandamana na kutangaza kurejesha kadi zao za uanachama wakipinga uamuzi wa Halmashauri Kuu kumteua Mbaraka, licha ya Ummy kuongoza kwa kura nyingi kwenye kura za maoni.
Wanachama hao, wakiongozwa na Mwinyi Zahoro Bakari, Mwenyekiti wa Tawi la CCM Chungurira, walifika katika ofisi za CCM Wilaya ya Tanga kuwasilisha malalamiko yao. Walisema hatua ya chama kumpitisha Mbaraka, aliyepata kura 80 pekee kwenye kura za maoni, badala ya mshindi Ummy aliyepata kura 5,750, ni dharau kwa wanachama wa ngazi za chini.
Aidha, walionya kuwa endapo chama hakitafanya marekebisho kwa kumrejesha Ummy, hawatakuwa tayari kumuunga mkono mgombea aliyeletwa na badala yake watampigia kura mpinzani.
Katika kura za maoni zilizofanyika Agosti 4, 2025, Ummy Mwalimu aliongoza kwa kura 5,750, akifuatiwa na Omary Ahmed Ayoub mwenye kura 4,146, huku Kassim Amari Mbaraka akishika nafasi ya nne kwa kura 80 pekee, lakini baadaye akatangazwa kuwa mgombea rasmi wa CCM.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, imepitisha rasmi majina ya wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi, ikiwemo ubunge na uwakilishi kwaajili ya kwenda kupigiwa kura na wajumbe watakaochagua mgombea mmoja ambaye atasimama kukiwakilisha Chama katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika tarehe 29 Oktoba mwaka huu.
Taarifa rasmi iliyotolewa Jumanne Julai 29,2025 katika Ofisi za Chama hicho Jijini Dodoma na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM CPA Amos Makalla imeeleza kuwa katika Jimbo la Tanga, walioteuliwa uteuzi wa awali ni watano, miongoni mwao akiwamo Ummy Mwalimu.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kampeni za uchaguzi zitaanza rasmi Agosti 28 na kumalizika tarehe 28 Oktoba 2025. -
Jambo TV
@Jambotv_
Akisisitiza kuwa hakuna kutetereka wala kuogopa, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema John Heche akiambatana na Katibu Mkuu wa Chama hicho John Mnyika, ameeleza kuwa Mwenyekiti wa Chama hicho Mhe. Tundu Lissu, amefurahia sana wingi wa wananchi waliojitokeza leo Mei 19, 2025 kusikiliza shauri la Lissu lililotajwa kwenye Mahakama ya Kisutu Dar Es salaam.
Heche katika maelezo yake, amehimiza pia wanachama wa Chama hicho kujitokeza kwa wingi Juni 02, 2025 kwenye Mahakama ya Kisutu, kwenye muendelezo wa usikilizwaji wa shauri la Lissu.
Heche pia amebainisha kuwa Wiki hii wataketi kama Kamati kuu na baada ya hapo watendelea na ziara za No Reforms, No election, akibainisha kuwa bado msimamo wa chama hicho ni kwamba hawakatai uchaguzi bali watashiriki uchaguzi pale tu ambapo yatafanyika mabadiliko ya sheria na mifumo ya uchaguzi, itakayoweka mizania sawa kwa vyama vya siasa n wanasiasa wanaoshiriki chaguzi.
Wakati akimaliza kuzungumza, wanachama na wananchi waliokuwa wakimsikiliza kando ya kuandamana naye wakilisindikiza gari lake, wamechanga fedha kadhaa kama sehemu ya utamaduni wao wa siku za karibuni kupitia kampeni ya Tone tone.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mapokezi ya Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) John Mnyika @jjmnyika mapema asubuhi ya siku ya Alhamisi eneo la Lamadi, Jimbo la Busega mkoani Simiyu ambapo yupo mkoani humo kupigia chapuo kampeni ya No Reforms No Election.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Chama Cha Demokrasia na na Maendeleo @ChademaTZ2 kupitia kwa Katibu Mkuu wake John Mnyika @jjmnyika kimesema aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho Mhe.Freeman Mbowe @freemanmbowetz hahusiki na hayuko nyuma ya kundi la wanachama na baadhi ya Viongozi wa chama hicho wanaojiondoa kwenye chama hicho kwa madai mbalimbali ikiwemo kubaguliwa ndani ya chama na kupinga chama hicho kutoshiriki uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huuThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Wakili Boniface Mwabukusi, ametoa kauli kali akiitaka Serikali kuwajibika na kuhakikisha mwanaharakati Mdude Nyagali anarejeshwa salama
Akizungumza na waandishi wa habari Mei 8, 2025 jijini Arusha, Mwabukusi alisema taifa haliwezi kuendelea kuishi kwa hofu huku matukio ya utekaji yakiendelea bila hatua za kisheria kuchukuliwa.
"Take it from me, hatuwezi kukaa hapa kwa hofu. Hili taifa ni letu – kwa nini hatulindwi? Hao watekaji ni kina nani wanaotekwa kila siku? Subirini vitendo… it will never happen again!" alisema @Mwabuk2Boniface
Amesema anafahamu kuwa Mdude alichukuliwa nyumbani kwake na watu waliokuwa wakimfuatilia kwa muda mrefu.
"Tunamtaka Mdude akiwa mzima. Warudishe – na hili si ombi, ni agizo la wananchi!" alisisitiza Mwabukusi.
Mwabukusi ametoa wito kwa Serikali na vyombo vya dola kuwachukulia hatua wote waliohusika katika matukio hayo ya kihalifu.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam leo, Jumatatu Mei 05.2025 imelezimika kuhairisha shauri la uchochezi linalomkabili Godlisten Malisa @MalisaGJ_ na Boniface Jacob (Boni Yai) @ExMayorUbungo kutokana na kile kilichoelezwa kuwa Jamhuri imekata rufaa Mahakama Kuu kutoka na mwenendo wa shauri hilo
Inaelezwa kuwa awali kesi ilitajwa leo kwa ajili ya kushuhudia shahidi wa sita (6) wa Jamhuri akitoa ushahidi wake Mahakamani, lakini msingi wa rufaa unakuja kufuatia Jamhuri kuitaariu Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa baadhi ya mashahidi wake wanapaswa kutoa ushahidi 'wa siri' jambo ambalo limegonga mwamba, hali iliyopelekea Jamhuri kukata rufaa Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam
Akizungumza na wanahabari kwenye viunga vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Wakili wa utetezi Dickson Matata @AdvMatata amesema kilichotokea Mahakamani hapo kimewashangaza kwakuwa walipohudhuria mara ya mwisho kusikiliza ushahidi wa shahidi wa tano (5) jambo hilo halikujitokeza hivyo kulisikia leo ni kama suala jipya kwao, hivyo kutumia fursa hiyo kuhoji msingi wakeThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud, amesema suala la kutafuta amani ya nchi linahitaji dhamira ya kweli, inayojali misingi ya utu, haki na uadilifu, wala si jambo la msimu kwa ajili ya kupata shukrani na fadhila za kisiasa.
Amesema kwa maoni yake, Kamati ya Amani Zanzibar inayohusisha viongozi mbalimbali wa dini bado haijafanikiwa, kwa sababu chanzo kinacholeta migogoro ni kutokuwepo haki kwa watu kunyimwa haki zao.
Amesema ili kustawisha amani kabla na baada ya uchaguzi, ni lazima kamati hiyo ijikite kwa kuyaeleza bayana na wazi wazi yale yanayochangia kuvunjika kwa amani pindi unapofika uchaguzi.
Othman amesema hayo leo Jumamosi, Mei 3, 2025, alipokutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa Kamati ya Amani inayojumuisha viongozi mbalimbali wa dini, wakiongozwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Saleh Omar Kaabi.
“Ni wajibu kwa kamati na mamlaka yoyote inayohubiri amani ya kweli, kuzingatia misingi muhimu ya haki, uadilifu, ambayo hatimaye yatabakiza nchi ikiwa salama na yenye utulivu,” amesema.
Hivyo, ameitaka kamati hiyo kushughulikia changamoto na malalamiko yanayojitokeza kila mara, akisema kuanzishwa kwa kamati hiyo ni jambo jema lakini kinachohitajika ni kuwepo nia thabiti na dhamira ya kweli ya kuyakabili mambo yote yanayoleta mkanganyiko wa amani kwa watu wa Zanzibar katika miongo mitatu ya uchaguzi uliopita.
Othman ameieleza kamati hiyo kuwa iwapo ina dhamira ya kupigania amani ya kweli katika visiwa hivyo, lazima isimame imara na kuwakabili wenye mamlaka wote waliopo madarakani, na itoke hadharani kuyakemea pindi yakitokea yasiyokubalika.
“Hata ukiwa kwenye mashindano ya mpira, kama refarii hatendi haki, amani hiyo ambayo ni tunu ya kila mtu, itapatikanaje iwapo patakosekana uadilifu na mwamuzi wake dhahiri hatendi haki,” amesema, huku akihimiza haja ya kuhusisha amani ya taifa na uchaguzi huru na wa haki.
Pia, ametumia fursa hiyo kuhimiza haja ya kulinda mshikamano wa wananchi katika jamii, maridhiano, umoja wa kitaifa, huku akisema wafuasi na wapenzi wa chama chake na hata waasisi wake, akiwemo Maalim Seif Sharif Hamad ambaye hadi anafariki dunia aliwausia juu ya kulinda amani, na wamekuwa mfano wa kwanza kutekeleza hilo.
Hata hivyo, Othman ameipongeza na kueleza kuunga mkono juhudi za kamati, huku akiahidi kuipa ushirikiano, na kwamba anaifungulia milango wakati wowote watakapohitaji msaada wake kwa ajili ya amani ya taifa.
Kwa upande wake, Mufti Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Kaabi, amemshukuru Othman kwa ukarimu wake, huku akiahidi kuyatendea kazi maoni, mapendekezo na miongozo aliyotoa kwa ajili ya maslahi mapana ya nchi.
Mufti Kaabi ambaye ni mwenyekiti wa kamati hiyo, pia amemuombea dua na kumtakia kila la kheri katika utekelezaji wa majukumu yake, wakati huu ambao nchi inaelekea katika uchaguzi mkuu. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
"Linapokuja suala la kuendesha kesi kwa njia ya mtandao siyo mbadala wa mahakama ya wazi, mbadala wa mahakama ya wazi ni chamber court ile ambayo mnaingia ofisini kwa hakimu mko wawili watatu",-- Wakili Jebra.
Wakili Jebra Kambole akizungumza na wanahabari siku ya Jumamosi mkoani Dar es Salaam wakati jopo la mawakili linalomwakilisha Mwenyekiti wa CHADEMA taifa Tundu Lissu katika kesi zinazomkabili, likizungumza na wanahabari hao.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Warioba amesema mara zote Jeshi la Polisi @tanpol nchini lonafanya kazi zake vyema, isipokuwa maafisa wa Jeshi hilo wanaanza kuingia 'doa' pale wanapojihusisha na masuala ya siasaThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Karagwe, Dkt. Benson Bagonza, ameibua mjadala mzito kuhusu hali ya usalama nchini, akieleza wasiwasi wake juu ya kundi la watu wanaofahamika kwa jina la “Wasiojulikana” ambao wamehusishwa na matukio mbalimbali ya ukiukwaji wa haki za binadamu.
Kupitia waraka wake kwa umma uliopewa kichwa cha “Wasiojulikana Wana Nguvu,” Askofu Bagonza amesema kuwa kushindwa kwa vyombo vya dola kuwabaini watu hao ni dalili ya udhaifu katika mfumo wa usalama wa nchi.
“Polisi hawawajui na wameshindwa kuwabaini. Idara nyingine nyeti, zimeshindwa na zimegwaya mbele yao,” alisema.
Askofu Bagonza ameongeza kuwa hali hiyo inaweka hatarini usalama wa viongozi wa serikali na raia wa kawaida, hususan wale wanaojitokeza wazi kutoa maoni au kuikosoa serikali.
“Raia wote hasa wenye mdomomdomo wako hatarini… Simba akikosa nyama hula majani. Mabubu mjiandae,” aliandika kwa lugha ya mafumbo.
Katika waraka huo ulioja uchungu, Askofu Bagonza ametumia ulinganisho wa kisiasa kuonesha namna “Wasiojulikana” walivyo na nguvu kuliko viongozi waliopo, na hata kupendekeza kwa dhihaka kuwa wachaguliwe kuwa viongozi wa taifa kwa sababu ya “uwezo wao mkubwa.”
“Ujuzi walioonesha katika kuteka, kutesa, kujeruhi, kuua, na kupoteza watu ni wa hali ya juu,” alisema, akitaka jamii ifikirie upya namna mfumo wa haki unavyofanya kazi." alihitimisha -
Jambo TV
@Jambotv_
Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) limekanusha vikali waraka unaosambazwa kwenye mitandao ya kijamii unaodaiwa kuwa wa kichungaji na unaotakiwa kusomwa katika parokia, vigango na jumuiya ndogondogo zote nchini kwa kipindi cha wiki 10 mfululizo.
Katika taarifa kwa umma iliyotolewa na Naibu Katibu Mkuu wa TEC, Padre Chesco Msaga, Baraza hilo limeeleza kuwa waraka huo ni wa kughushi na haujatolewa na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania.
TEC imesisitiza kuwa waraka huo hauna uhalali wowote na hauna maslahi kwa Kanisa wala taifa kwa ujumla.
“Tunapenda kuwatangazia Waamini na Watanzania wote kupuuza kabisa waraka huo, kwani si rasmi na si wa Baraza,” imesema sehemu ya taarifa hiyo.
Aidha, TEC imewaasa waamini na wananchi kutojihusisha na vitendo vyovyote vinavyoweza kuhatarisha amani na mshikamano wa taifa, ikisisitiza dhamira yake ya kuendeleza maadili mema na mshikamano miongoni mwa Watanzania.
Taarifa hiyo imekuja baada ya waraka huo kusambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii, huku ukiibua taharuki na maswali miongoni mwa waumini na wananchi. -
Jambo TV
@Jambotv_
Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) imelaani vikali tukio la kushambuliwa kwa Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padri Dkt. Charles Kitima, na kuitaka Serikali kuhakikisha wahusika wanakamatwa na kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria.
Taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa CCT, Askofu Dkt. Fredrick Shoo, imeeleza kuwa tukio hilo ni la kinyama na limelipokelewa kwa mshtuko na masikitiko makubwa na waumini wa madhehebu mbalimbali nchini.
“Tunatoa pole kwa Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki, Maaskofu, Mapadri, Watawa na waumini wote, lakini kipekee kabisa tunatoa pole kwa Fr. Kitima na kumuombea apone haraka,” alisema Askofu Shoo.
Aidha, CCT imeonya kuhusu mfululizo wa matukio ya aina hiyo ambayo yameanza kushuhudiwa nchini, hasa katika vipindi vya kuelekea uchaguzi, na kutaka hatua za haraka zichukuliwe ili kuzuia hali hiyo isiendelee.
“Ni wakati muafaka wa kuhakikisha matukio ya ukatili kama haya yanakomeshwa. Vitendo hivi vinawatia hofu wananchi, vinaharibu taswira ya Taifa na vinaumiza jamii kwa ujumla,” ilieleza taarifa hiyo.
Jumuiya hiyo pia imetoa wito kwa jamii nzima kuwa walinzi wa amani, hasa katika mwaka huu wa uchaguzi, na kuhimiza kutumia njia za majadiliano na maridhiano badala ya nguvu na machafuko.
“Tunahimiza upendo, haki, uadilifu na amani vitawale ili taifa liendelee kuwa na mshikamano. Ni wajibu wa kila mmoja kuhakikisha anapinga na anakataa kutumika katika kusababisha vurugu,” amesema Askofu Shoo.
Taarifa hiyo imehitimishwa kwa kauli ya kusisitiza mshikamano wa kitaifa: “Tudumishe upendo, haki, uadilifu na amani." -
Jambo TV
@Jambotv_
Katika hali inayotia simanzi, Jambo TV imeinasa video inayoonesha kundi kubwa la wanafunzi wa Shule ya Msingi Kinangali, Kata ya Kibaigwa, Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma wakisoma wakiwa wamekaa chini bila madawati – mazingira ambayo ni kinyume na mazingira bora ya ujifunzaji hususan kwa kasi ya elimu inayoendelea kukua hivi sasa.
Picha hizo zinazoonesha watoto wakiwa wamerundikana sakafuni darasani, zimeibua maswali mazito kuhusu usalama wao, hadhi ya ujifunzaji na mustakabali wa elimu vijijini.
Jambo TV ilifanya jitihada za kupata maelezo kutoka kwa uongozi wa shule na halmashauri. Mwalimu Mkuu alipoulizwa kuhusu hali hiyo, alijibu kuwa hawezi kutoa taarifa yoyote bila kibali cha Mkurugenzi wa Halmashauri.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa, Dkt. Omary Nkullo, alipohojiwa, alikiri kuwapo kwa changamoto hiyo, akieleza kuwa shule hiyo inakumbwa na ongezeko kubwa la wanafunzi kila mwaka, hali inayozidi uwezo wa miundombinu iliyopo.
Hata hivyo, alipoulizwa kuhusu uwezekano wa kuruhusu waandishi kutembelea shule hiyo kwa ajili ya kufuatilia undani wa tatizo, Dkt. Nkullo alishauri jambo hilo lisiripotiwe kwa sasa, akieleza kuwa ni mwaka wa kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu, hivyo linaweza kuibua tafsiri tofauti.
"Kwa sababu juhudi zinaendelea sidhani kama kuna haja ya kulipublish sana, huu ni mwaka wa kisiasa ujue... kuna wengine watachukulia kama ni masuala ya kisiasa," amesema Dkt. Nkullo.
Kwa kuzingatia picha halisi iliyojitokeza katika Shule ya Msingi Kinangali, ni wazi kuwa changamoto ya miundombinu ya elimu bado ni jambo linalohitaji kushughulikiwa kwa umakini na kasi. Watoto wa Kitanzania, popote walipo, wanastahili mazingira salama na rafiki ya kujifunzia kama sehemu ya haki yao ya msingi.
Majibu na hatua za wadau wote, ikiwemo serikali za mitaa, yanabaki kuwa na nafasi kubwa katika kuamua kama kesho ya mtoto wa kijijini itakuwa na matumaini au itaendelea kuwa hadithi ya kusubiri.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Katibu wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini Tanzania (TEC) Padri Dkt. Charles Kitima ameripotiwa na Vyanzo mbalimbali vya habari kuwa amevamiwa na kushambuliwa na watu wasiofahamika, akiwa kwenye makazi yake, zilipo Ofisi za baraza hilo Kurasini Jijini Dar Es salaam majira ya saa tatu na nusu usiku wa Aprili 30, 2025.
Baadhi ya mashuhuda na waumini wa Kanisa hilo waliokuwepo kwenye mgahawa mmoja ndani ya Viunga vya TEC, Kurasini wameieleza JamboTv kuwa Padri Kitima akiwa kwenye mazungumzo na baadhi ya watu, alinyanyuka na kuelekea msalani na ghafla kwa dakika chache walitokea watu waliomshambulia kwa sekunde chache na kisha kuondoka, na baadaye ndipo Padri Kitima alipoonekana akiomba msaada akiwa anavuja damu katika sehemu mbalimbali za mwili wake.
Mara baada ya shambulizi hilo, Padri Kitima amepatiwa matibabu ya awali kwenye Kituo kidogo cha afya cha TEC kilichopo eneo hilo na baadaye kusaidiwa na baadhi ya watu kupandishwa kwenye gari tayari kupelekwa kwenye Hospitali ambayo mpaka taarifa hii inaandaliwa bado haikuwa imefahamika ni Hospitali gani alipoenda kupatiwa matibabu.
Padri Kitima kando ya utumishi wake na nafasi aliyonayo ndani ya Kanisa, amejipatia umaarufu mkubwa nchini Tanzania kwa miaka ya hivi karibuni kwa namna ambavyo amekuwa mkosoaji mkubwa wa mienendo isiyofaa kwenye jamii na akiwa mstari wa mbele katika kuhubiri utawala wa sheria na haki za binadamu pamoja na Demokrasia. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Innocent Bashungwa ametoa wito kwa Watanzania kuelewa kuwa matumizi ya 'Mahakama Mtandao' wakati mwingine yanafanyika kama sehemu ya mkakati wa vyombo vya ulinzi na usalama kuzuia matukio ya uhalifu na uvunjifu wa amani katika nchi
Akizungumza wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge, Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) ilipofanya ziara ya kukagua makasha ya kisasa ya 'Mahakama Mtandao' yanayowezesha usikilizaji wa mashuhuri kwa njia ya kiteknolojia katika Gereza la Isanga -Dodoma, Waziri Bashungwa ametolea mfano wa shauri linalomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa Tundu Lissu kuwa ililazimika kuendeshwa kwa njia ya mtandao kufuatia kauli za viongozi wa chama hicho zilizokuwa zinaashiria uvunjifu wa amani
Katika ziara hiyo iliyofanyika leo, Jumatano Aprili 30.2025 Waziri Bashungwa amenukuliwa akisema:
"Jeshi la Polisi linapokuwa na taarifa za kiiterejensia za wazi na zisizo wazi, kwa mfano maandamano ya CHADEMA, na Watanzania ni mashahidi, viongozi wa CHADEMA walisema waziwazi kwamba wataandamana wakakinukishe, Jeshi linapokuwa na taarifa za kiusalama likashirikiana na Mahakama kutoa haki ile ile kwa kutumia teknolojia ya 'Mahakama Mtandao' ili kuzuia fujo mtaani, naomba Watanzania watuelewe"This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Karagwe, Dkt. Benson Bagonza, ametikisa mitandao ya kijamii baada ya kuandika ujumbe wenye tafakari nzito kuhusu namna kesi ya uhaini inavyoshughulikiwa nchini.
Kupitia ujumbe wake wenye kichwa kinachosema “UJINGA WANGU SASA UMEKOMAA”, Askofu Bagonza amehoji kwa nini kesi ya uhaini dhidi ya mtuhumiwa mmoja haifanywi wazi kwa wananchi wote, ilhali inahusisha jambo kubwa la usalama wa taifa.
Ameeleza kuwa awali aliamini uhaini ni kosa kubwa linalopaswa kusikilizwa hadharani kwa uwazi na kwa maslahi ya umma.
Katika tafakari hiyo, ameorodhesha mambo ambayo alitarajia yangefanyika ikiwa kweli kesi hiyo ni ya uhaini — ikiwemo kusikilizwa kwenye Uwanja wa Taifa, kurushwa mubashara na vyombo vya habari, na wananchi kupelekwa kwa makarandinga ili kushuhudia haki ikitendeka. Kwa maoni yake, hatua hiyo ingekuwa fundisho la uraia na utii wa sheria kwa vitendo.
Hata hivyo, amebaini kuwa mambo ni tofauti. Kesi hiyo haiwezi kusikilizwa wazi kwa madai ya “umuhimu na unyeti” wake.
Askofu Bagonza ameonesha masikitiko kuwa wananchi, ambao wanapaswa kuwa wahusika wakuu katika kuilinda serikali dhidi ya maadui wa taifa, hawaruhusiwi kushuhudia mwenendo wa kesi hiyo.
Katika sehemu ya mwisho ya ujumbe wake, Dkt. Bagonza ametoa pole kwa wote walioumizwa katika harakati mbalimbali, akionya kuwa “giza la kuona haki ikitendeka” linaweza kuwa hatari zaidi kwa jamii. -
Jambo TV
@Jambotv_
Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Boniface Mwabukusi, amelaani vikali hatua ya baadhi ya wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuonekana wakiwa wametupwa porini na wakiwa wamejeruhiwa, huku wanachama wengine wa chama hicho, raia na wanahabari kukamatwa ama kuzuiwa na Jeshi la Polisi wakiwa wanaelekea au tayari wamefika katika Mahakama ya Kisutu kushuhudia kesi ya mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, akitaja tukio hilo kuwa "shambulio dhidi ya utawala wa sheria."
Kupitia chapisho aliloliweka katika ukurasa wake wa mtandao wa X (zamani Twitter), Mwabukusi amesema kuwa hatua ya kuwazuia wananchi kuhudhuria mahakamani bila msingi wa kisheria ni ukiukaji wa wazi wa haki ya kikatiba ya kuona haki ikitendeka na kushiriki mchakato wa utoaji haki kwa uwazi.
“Mahakama ni chombo huru kinachopaswa kufanya kazi bila mashinikizo, vitisho au uingiliaji kutoka kwa vyombo vingine vya dola,” amesema Mwabukusi. “Polisi kuzuia wananchi kuhudhuria kesi ni sawa na kudhibiti mazingira ya kimahakama, kinyume cha katiba.”
Ameongeza kuwa wananchi wanayo haki ya kikatiba ya kukusanyika kwa amani na kushuhudia mwenendo wa mashauri mahakamani, hivyo kuwazuia au kuwatendea ukatili ni kuvunja haki hiyo.
TLS imesema tayari imeielekeza Kamati yake kufuatilia suala hilo kwa kina ili kuona hatua stahiki za kuchukua, ikiwa ni pamoja na kushirikiana na wahanga katika hatua za kisheria dhidi ya taasisi au watu binafsi waliokiuka haki hizo.
Aidha, TLS imetoa wito kwa wahanga wa vitendo hivyo kuwasiliana na Polisi mara moja kupata PF3, ambayo ni haki yao ya kisheria, kukusanya ushahidi kama picha, video, na maelezo ya maandishi kuthibitisha madhila waliyoyapata.
Mwabukusi ameongeza kuwa matukio haya yamekuwa yakijirudia na kuanza kuzoeleka, jambo ambalo TLS inaliona ni hatari kwa mustakabali wa haki, demokrasia na utawala wa sheria nchini.
Hata hivyo, taarifa iliyotolewa kwa umma, na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam inaeleza kuwa jeshi hilo liliimarisha ulinzi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kufuatia taarifa za kiintelijensia kuhusu vitisho vinavyohusiana na kesi inayomkabili Lissu, iliyotarajiwa kusikilizwa Aprili 24, 2025.
Kamanda Muliro amesema kuwa hatua kali za kiusalama zilichukuliwa ili kuhakikisha hali ya utulivu katika eneo la mahakama, kufuatia wasiwasi uliokuwepo kuhusu usalama wa mashabiki na viongozi wa kisiasa waliokuwa wakikusanyika mahakamani. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Kiongozi wa ACT Wazalendo @ACTwazalendo Dorothy Semu @SemuDorothy amezuiliwa kuingia kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam alipofika Mahakamani hapo kwa ajili ya kusikiliza kesi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Tundu Lissu @TunduALissu
Jambo TV imeshuhudia kiongozi huyo ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) akiwa kwenye majibizano na maafisa wa Jeshi la Polisi kwenye viunga vya Mahakama hiyo -
Jambo TV
@Jambotv_
"Mimi sio mwanasheria lakini niseme Tume inaongozwa na Jaji yaani mabingwa wa kutafsiri sheria na Katiba zetu zinasema nini na ndiyo maana hawakuniweka mimi wakamuweka Jaji.
Matumaini yangu ni kwamba maamuzi ya Tume ambayo sasa yanabishaniwa na wale wanaobishana na Tume mmoja wapo kwa mujibu wa Katiba na sheria atakuwa anasema kweli zaidi kuliko mwingine, hili ndilo tatizo.
Katika ubishi huu wa kwenda kusaini Kanuni, mimi nimewasikiliza, kikubwa ni kwamba wale wanaotuendeshea siasa, kimoja ya Chama na hata kilichoko madarakani nao wana ubishi kuhusu hili na hawa hawajasaini kwasababu wanaamini kwamba yapo mambo yamekosewa na hawawezi kusaini kwasababu ya masharti waliyonayo kwamba hawawezi kusaini mpaka imekuwa hivi.
Sasa mimi nasema hayo ni sehemu ya mazungumzo ya kabla ya uchaguzi na mimi matumaini yangu ni kuwa mazungumzo hayo yataruhusu kupata majibu na wahusika wote watashiriki uchaguzi na sisi wananchi tusiambiwe kwamba tusiende kupigakura.
Mimi binafsi nangoja kwenda kupiga kura haya mengine naamini vyama vya siasa na Jaji wa Tume na watumishi wake watatoa tafsiri inayozingatia katiba na sheria kuwawezesha vyama vya siasa kushiriki na sisi kwenda kupiga kura." Mzee Joseph Butiku, Mwenyekiti Taasisi ya Mwalimu Nyerere kwenye Dakika45 -
Jambo TV
@Jambotv_
Waziri wa Kilimo Hussein Bashe ameliambia Bunge la Tanzania kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, Aprili 28, 2025, anatarajiwa kuzindua Benki ya ushirika Tanzania ambayo Makao yake makuu yatakuwa Jijini Dodoma, Benki ambayo itaanza kufanya kazi ikiwa na Mtaji wa Bilioni 55 za Kitanzania.
Waziri Bashe ameeleza hayo leo Aprili 15, 2025 wakati akitoa maelezo ya hoja mbalimbali zilizowasilishwa wakati wa Mjadala wa hotuba ya bajeti ya Waziri Mkuu kwa mwaka 2025/26 akieleza kuwa Benki hiyo pia itaaanza na matawi manne yatakayokuwa kwenye Mikoa ya Kilimanjaro, Mtwara na Tabora.
Aidha Kulingana na Waziri Bashe, Vyama vyote vikuu vya ushirika nchini vitakuwa mawakala wa Benki hiyo ambao watakuwa na majukumu ya kufungua Akaunti za wakulima na kutoa huduma ya kuweka na kutoa fedha kwenye benki hiyo ya ushirika.
Katika hatua nyingine, Bashe amemshukuru Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwa ushirikiano wake na uratibu mkubwa katika Wizara hiyo ya Kilimo. Akimshukuru binafsi pia kwa namna ambavyo amekuwa karibu yake tangu wakati Waziri Bashe akiwa Naibu Waziri, akieleza kuwa utashi wa kisiasa wa serikali ya awamu ya sita umefanikisha kutimiza malengo ya Ilani ya Uchaguzi na matamanio ya Rais Samia Suluhu Hassan.
Kulingana na Waziri Bashe ukuaji wa sekta ya kilimo kwa mwaka 2021 wakati Rais Samia anaingia madarakani ulikuwa asilimia 2.7 na bajeti ikiwa ikiwa Milioni 290 na kufikia 2024, ukuaji wa sekta hiyo umefikia asilimia 4.2 kukishuhudiwa pia ongezeko la bajeti kutoka Milioni 290 mwaka 2021 hadi kufikia Shilingi Trilioni 1.2.
@HusseinBashe pia ameliambia bunge kuwa mauzo ya nje kwenye sekta ya mazao ya kilimo yamekuwa kufikia Dola za Marekani Bilioni 3.5 kutoka Dola za Marekani Bilioni 1.2 zilizokuwepo mwaka 2021.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Na Josea Sinkala, Mbeya.
Wakili wa kujitegemea Ezekiel Mwampaka amesema anakubaliana na mpango wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wa kutaka kutofanyika kwa uchaguzi mkuu baadaye Oktoba 2025 kutokana na kudai kugubikwa na kasoro mbalimbali na ukosefu wa tume huru ya uchaguzi.
Wakili Mwampaka amesema hayo kwenye mahojiano yake maalumu na kituo hiki ofisini kwake jijini Mbeya akieleza pia masikitiko yake juu ya ukamatwaji wa mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Tundu Antipas Lissu unaodaiwa kutokuwa wa staha na bila kosa linaloeleweka.
Wakili huyo wa kujitegemea nchini Tanzania, amesema pamoja na kuwa hajui mbinu ambazo CHADEMA itazitumia kuzuia uchaguzi jambo ambalo ni takwa la kikatiba kwa wananchi lakini mpango huo anaona CHADEMA iko sahihi kutokana na kushamiri kwa kasoro mbalimbali kwenye chaguzi za Tanzania hususani kuminywa kwa uhuru wa vyama vya upinzani, jeshi la Polisi kuingilia masuala ya kiuchaguzi na tume ya uchaguzi kutokuwa huru kutokana na kuwa na mfumo wa chama tawala (CCM) mambo anayosema ni wazi kuwa ndiyo yamewashawishi CHADEMA kuishinikiza jamii kuungana nao kuzuia kufanyika kwa uchaguzi mkuu mwaka huu hadi sheria za uchaguzi zitakaporekebishwa.
Kuhusu kukamatwa kwa Lissu na tuhuma zinazomkabili wakili huyo amesema "Hapa majuzi kuna kiongozi mmoja wa CHADEMA (Tundu Lissu) amekamatwa eti kwa uhaini na makosa mengine, sasa unafikiria kwa akili ya kawaida tu Polisi kutoka Dar es Salaam hadi Mbinga mkoani Ruvuma na msafara wa magari ambao ni kodi za wananchi kulikuwa na haja gani, walishindwa nini kutafuta namba ya simu wakampigia au wakamwamwambia bwana tunakuhitaji kituo cha Polisi Dar es Salaam siku fulani tarehe fulani wanadhani Lissu angekataa hadi watumie nguvu kiasi kile?", amehoji wakili Mwampaka na kuongeza.
"Ukiangalia ni mpango uleule kama walivyofanya kwa Mbowe (aliyekuwa mwenyekiti wa CHADEMA Taifa) walimkamata hivi hivi na baadaye wakamuachia. Utashangaa hili suala la Lissu linapigwa kalenda mpaka uchaguzi halafu baada ya hapo mtu anaamua anajisikia kumwachia anasema muachieni, sasa muda aliopoteza utamlipa nini na haya yote ni mfumo tulio nao kikatiba. Mimi nikisoma sioni mahali kusema utawaambia watu wagomee uchaguzi au uchaguzi uzuiwe kwamba ni uhaini sijaona", ameeleza wakili Ezekiel Mwampaka.
Pamoja na hayo ameeleza chaguzi za Tanzania kugubikwa na wizi wa kura ikiwemo maeneo ambayo kura feki na za wizi huingizwa na mara nyingine idadi ya kura kuzidi idadi ya wapiga kura jambo linalomsukuma kueleza umuhimu wa upatikanaji wa tume huru ya uchaguzi akisema tume iliyopo sasa kiongozi wake anayeteua viongozi wa tume ni mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa. -
Jambo TV
@Jambotv_
Msajili wa vyama vya Siasa Tanzania, Jaji Francis Mutungi amesema kauli ya ‘No reform, no Election’ bado haijavunja sheria ya vyama vya siasa, huku akisisitiza kuwa uchaguzi mkuu 2025 uko palepale.
Jaji, Mutungi amesema wakati anazungumza na waandishi wa habari baada ya kushiriki warsha ya wadau wa kujadili namna ya kuzuia na kupambana na rushwa katika uchaguzi mkuu 2025.
Tangu kumalizika kwa uchaguzi wa ndani, CHADEMA wamekuwa wakieleza kuwa, bila mabadiliko katika mifumo ya uchaguzi hakutakuwa na uchaguzi mkuu mwaka 2025 na kwamba watauzuia kwa kuandamana nchi nzima kauli ambayo inapingwa na vyama vingine vya siasa ikiwemo CCM.
Msajili huyo amesema hakuna anayeweza kuzuia uchaguzi wa mwaka huu, kwakuwa kinachosemwa ni matamshi ya wanasiasa majukwaani ambayo kila chama kinaweza kuwa na maana yake.
“Hakuna awezaye kuzuia uchaguzi kwa kutamka tu kwenye majukwaa, CHADEMA hawajavunja sheria na nilipokutana nao hivi karibuni walisema hawatakuwa tayari kuvunja sheria za uchaguzi,” amesema Jaji Mutungi.
Aidha, amesema chombo kinachoweza kuzuia uchaguzi ni mahakama na hadi sasa hakuna aliyekwenda huko isipokuwa kinachoendelea ni matamshi ya midomoni mwa wanasiasa.
Amesema hajasikia kuwa CHADEMA wamekwenda mahakamani kupinga uchaguzi licha ya kuwa wanao wanasheria wanaojua utaratibu mzima wa nini kifanyike hivyo kinachoonekana ni kama wanafanya propaganda za kisiasa ambazo haziwezi kuwatia hatiani isipokuwa kama kutakuwa na maneno mengine ndani ya kauli zao.
“Mimi nitatafuta muda wa kuwaiteni kuzungumza kirefu zaidi kuhusu mambo haya, lakini kama ulivyosema mimi ndiye baba wa vyama vya siasa ni kweli, na kila chama kina haki ya kusikilizwa lakini siyo kuvunja sheria, sisi hatutegemei kama wanaweza kuvunja sheria,” amesema. -
Jambo TV
@Jambotv_
"Tuache kuchezea neno “uhaini”. Maneno yanaumba. Tusilizoee maana halizoeleki. Tafsiri zake zinatisha:
Kupindua serikali ni uhaini lakini tuna wahaini wengi wanaongoza serikali Afrika na wanalaani uhaini.
Kuiba kura ni uhaini kwa sababu unapindua madaraka ya wananchi. Tunazo serikali nyingiiii barani Afrika zilizoiba kura na zinalaani wizi wa kura.
Kukalia kimya wizi wa kura, kuwezesha wizi wa kura, kukubali matokeo ya wizi wa kura ni uhaini. Uwiiiii, hata mimi ni mhaini maana nami nimo humu." Askofu Dkt. Benson Bagonza, Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Karagwe -
Jambo TV
@Jambotv_
Ni majira ya usiku katika mtaa wa Oleresho, kata ya Olasiti jijini Arusha ambapo wananchi wamefunga barabara inayoelekea Kisongo, wakilalamikia ajali za mara kwa mara eneo hilo.
Hatua hiyo imechukuliwa kufuatia ajali iliyotokea usiku huu na kupelekea kifo cha mtu mmoja.
Wakizungumza na waandishi wa habari, wananchi hao wameiomba serikali kuchukua hatua za haraka ikiwemo kuweka "bumps" ili kudhibiti kasi ya magari na kuokoa maisha.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katika muendelezo wa kudai haki yake, mzee Flavian Methew Nyendikuu (83) na familia yake leo, Ijumaa Aprili 04.2025 wamefika kwenye ofisi ya Kamishna Msaidizi wa Ardhi mkoa wa Dar es Salaam kwa ajili ya kufuatilia viwanja vyao viwili vilivyopo block L, Kilongawimba, Mbezi Beach, Dar es Salaam ambavyo vimemilikishwa kwa watu wengine
Msingi wa suala hilo ambalo Jambo TV imekuwa ikifuatilia kwa karibu unatokana na kesi namba 87 ya mwaka 2019 ambayo maamuzi yake yalitolewa na Mahakama Kuu ya Tanzania, Division ya Ardhi Aprili 29.2020, maamuzi ambayo yalikuja kufuatia rufaa ya Chacha Mantage ambaye hapo awali hakuridhika na maamuzi ya chini (Baraza la Ardhi na Nyumba la wilaya)
Maamuzi hayo yaliyotolewa na Jaji Opio yaliweka msisitizo kuwa mzee Nyendikuu ndiye mmiliki halali wa viwanja namba 2107 na 2120, pia Mahakama ilitupilia mbali kwa pingamizi lililowekwa, ambapo maamuzi hayo yalipelekea mmiliki kuweka zuio la kwamba viwanja vyake visiendelezwe kwa namna yoyote ile, zuio hilo lilifanyika Oktoba 06.2023 kwa kiwanja cha kwanza na Agosti 25.2023 kwa kiwanja cha pili
Hata hivyo, katika hali isiyokuwa ya kawaida kuanzia Machi 01.2024 viwanja hivyo wamemilkishwa Fatma Yusuph Suleiman (kiwanja namba 2107) na Irene Wankyo Maganga (kiwanja namba 2120), jambo ambalo mzee Nyendikuu hakubalianinalo kwa kile anachodai kuwa kumilikishwa kwao ni kinyume na taratibu hivyo anapigania kuziomba mamlaka husika kumrejeshea viwanja vyake kama ilivyoamuliwa na Mahakama
Katika kufuatilia suala hilo, Msajili wa Ardhi mkoa wa Dar es Salaam Apollo Laizer alimjibu mlalamikaji kuwa wamiliki wapya wa viwanja hivyo (Fatma na Irene) hawakuhusishwa kwenye kesi namba 872019, ambapo kwa mujibu wa mdai anasema ukiangalia tarehe ambayo watu hao wamemilikishwa viwanja hivyo utaona kuwa ilikuwa ni baada ya kesi ya msingi kumalizika na zuio lilikuwa limeshawekwa tayari hivyo ni dhihiri isingewezekana wao kuhusika kwa namba yoyote ile kwenye shauri hilo
Inaelezwa kuwa, awali mdai aliandika barua ya kulalamikia sintofahamu hiyo kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania a, ambapo maombi yake yalijibiwa Desemba 13.2024 kupitia barua yenye kumb.na.bd 214/320/02/52
Barua hiyo kutoka ofisi ya Waziri Mkuu iliyosainiwa na Senso M. Kisyeri kwa niaba ya Katibu wa Waziri Mkuu ilielekeza kuwa mdai awasilishe nakala za hukumu za viwanja husika kwa Kamishna Msaidizi wa Ardhi mkoa wa Dar es Salaam kwa ajili ya ufahamu na hatua stahiki.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
"Tumeenda Ikulu baada ya uchaguzi wa mwaka 2019 na 2020, kwa kauli ya Rais mwenyewe amesema yaliyojitokeza 2019 na 2020 hayatajirudia tena. Tumeshiriki kikao, Mwenyekiti Mbowe anatuongoza, tulikuwa na Mnyika na Kinana alikuwa anaongoza timu ya CCM na nyaraka tunazo, wakasema yaliyojitokeza hayatajitokeza tena, hiyo ni kauli ya Kinana na ipo kwenye maandishi. Nini kilichojitokeza 2024? Tumesimamisha wagombea 88 Tarime wamekata karibia asilimia 60 kabla hatujaingia kwenye uchaguzi, vitongoji 500 wamekata asilimia 60.
Kwa mujibu wa waziri wa Tamisemi alisema wagombea 12600 wa upinzani wamekatwa kwasababu mbalimbali ikiwemo kukosea kujaza fomu, kugonga miuri vibaya na kadhalika, maana yake tunaenda kwenye uchaguzi CCM ikiwa tayari imeshinda viti zaidi ya 2000 na kwa mujibu wa takwimu zetu wagombea zaidi ya 60,000 waliondolewa.
Kuna wanachadema wanaweza kusimama na kusema kwamba tukienda kwenye uchaguzi kwa mazingira haya tunaweza kushinda? Yupo?anyooshe mkono hapa aseme mimi mkiniacha hivi na jimbo langu nitashinda.
Tusidanganyane, tumekaa vikao tukathibitisha bila kuwa kuacha shaka kuwa mazingira ya sasa hatuwezi kushinda lazima tutafute mbinu za kukabiliana na hawa watu ili tuende kwenye uchaguzi ambao ni huru na haki. Sasa mtu anasimama anasema ooh sijui msipoenda kwenye uchaguzi chama kitashindwa, hii si sehemu ya biashara, kama unataka kufanya biashara kafungue duka ufanye biashara. Hii ni taasisi ya kisiasa ya mapambano na tutashinda."- John Heche, Makamu mwenyekiti wa Chadema bara, akizungumza na watia nia ya ubunge 2025This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Leo, Jumatano Aprili 02.2025 Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) Tundu Lissu @TunduALissu ameongoza kikao cha 'summit' ya kituo hicho, ambapo pamoja na mambo mengine kikao hicho kimejadili kuhusu umuhimu wa kufanyika kwa 'reforms' kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu (2025)
Akihojiwa na Jambo TV muda mfupi baada ya kumalizika kwa kikao hicho, Lissu amesema viongozi wa vyama vinavyounda TCD (CCM, NCCR-Mageuzi, CHADEMA, CUF na ACT Wazalendo) watakutana tena wenye kikao kingine siku chache zijazo, kabla ya kutoka na maazimio ya pamoja yatakayopelekwa kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan
NB: YouTube ya Jambo TV ina undani wa taarifa hiiThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
"Tanzania hatujawahi kuwa na Tume Huru. Lakini angalau wananchi walikuwa wana imani kuwa kura zao zitahesabiwa. Tujiulize, hivi sasa mawakala wanaingia vituoni? Wakiruhusiwa wana uhuru vituoni? Wanapewa karatasi za matokeo? Huu ni uchaguzi gani? Ndio maana ACT Wazalendo tunapigania kurejesha thamani ya kura"
"Tunapigania thamani ya kuratasi ya kupigia kura. Karatasi za kupigia kura zisiwe kwenye mikono ya mabalozi, polisi au Maofisa wa Usalama wa Taifa. Mpiga kura aikute kwenye kituo na aiche kwenye kituo, isitoke nyumbani kwa mtu"
"Sheria ya sasa ya Tume Huru ya Uchaguzi imeweka utaratibu kuwa angalau wajumbe wa Tume ya Uchaguzi wapatikane kwa ushindani. Watu waombe na wafanyiwe usaili. Serikali ya CCM haitaki kutekeleza jambo ambalo wamelitunga wenyewe"
"Tunataka wajumbe wa sasa wa Tume ya Uchaguzi waondoke. Nafasi zao zitangazwe, watu waombe, tupate wajumbe wapya. Huu umekuwa wimbo wetu tangu mwaka jana. Muda wa kufanya hilo bado upo. Tunataka Tume Huru ya Uchaguzi ambayo ndani yake haina makada kama Mapuri ambaye alikuwa Mwenezi wa CCM"
"Tumeona uchaguzi wa Serikali za Mitaa na chaguzi zilizopita, Wakurugenzi wa Halmashauri na Watendaji wa Kata ambao wengi ni makada wa CCM ndio wanasimamia uchaguzi. ACT Wazalendo tunataka Tume iajiri kwa muda watu huru wasimamie uchaguzi ili haki itendeke"
"Jana kuna rafiki yangu alikuja kwangu kupata naye futari. Akawa ananihadithia kuwa kuna jamaa amemuambia anishawishi nisigombee Ubunge Kigoma Mjini kwa sababu CCM hawatanipa. Nikasema ebo! kwani ni CCM au wananchi wanaotoa mbunge? Hapo ndipo tulipofika. Watu wa CCM wamefika pahala ambapo wanaweza kusema fulani hatutakupa"- @zittokabwe, kwenye operesheni linda demokrasia. -
Jambo TV
@Jambotv_
"Kwa chaguzi tatu mfululizo thamani ya kura imepotea. Uchaguzi wa Serikali za Mitaa hakukuwa na kura, takribani wagombea wote wa upinzani walienguliwa. Mwaka 2020 tuliona kwa mara ya kwanza kura feki zikizagaa hovyo barabarani. Mwaka 2024 wakafanya kama mwaka 2020"
"Matumaini yote tuliyokuwa nayo ya mageuzi kwenye uchaguzi na matarajio yetu yote kuwa mageuzi hayo yataaanza kutekelezwa kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024, yameyeyuka, tumechapwa kibao kikali sana cha uso"
"Tumewaona Polisi wanaolipwa kwa kodi zetu na Maofisa wa Idara ya Usalama wa Taifa ambao wajibu wao ni kutulinda sote wakitumbukiza kura feki ili CCM ishinde kitongoji, kijiji au mtaa. Tujiulize, kama wanafanya kwa hao ambao hawatungi sheria yeyote itakuwaje kwa wabunge ambao wana madaraka ya kupiga kura ya kutokuwa na imani na Rais?"
"Halmashauri Kuu imetuagiza viongozi wa @ACTwazalendo tuwaandae wanachama wetu kuwa tayari kuipigania demokrasia yetu"- @zittokabwe Kiongozi mstaafu wa ACT Wazalendo,kwenye ufunguzi wa operesheni linda demokrasia. -
Jambo TV
@Jambotv_
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na wenye Mahitaji Maalum, Dk Dorothy Gwajima amewasihi wanaozungumza vibaya kuhusu wanawake waolea watoto wao wenyewe maarufu kama 'Single Mothers' kuacha tabia hiyo kwani hao ni wazazi kama wengine hivyo wanahitaji kuheshimiwa.
Gwajima ameyasema hayo jijini Dar es Salaam katika hafla iliyoandaliwa na Taasisi ya Her Initiative na kukutanisha wadau mbalimbali kuzungumzia masuala ya wanawake na uongozi.
Gwajima amesema kutoa kauli mbaya dhidi yao ni kuwanyanyasa wanawake ambao wameamua kusimama na kulea watoto wao wenyewe kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kufiwa au kutokea migogoro kati yake na mwenza wake.
"Anayehamasisha hayo hana maadili na wala hajui ukuu wa mama katika dunia, cha kushangaza baadhi ya watu katika jamii wanashabikia lazima tujitafakari," amesema.
Hivyo amesema ajenda ya 'single mothers' hawafai haina tija kwani wapo kati yao ambao ni mifano ya kuigwa katika malezi ya watoto. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) @ChademaTz Mkoa wa Mara kimewasilisha ripoti maalum kwa Kanisa Katoliki, ikielezea matukio ya watu waliouawa au kupotea katika mkoa huo. Sambamba na hilo, chama hicho kimetumia nafasi hiyo kueleza msimamo wake wa No Reform No Election, ukimaanisha kwamba kitazuia uchaguzi wowote iwapo mabadiliko ya sheria na mfumo wa uchaguzi hayatatekelezwa.
Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Mara, Chacha Heche, amesema wamechukua hatua hiyo kwa sababu wamedanganywa mara nyingi kuhusu maridhiano ya kisiasa, huku wakihisi kuwa mfumo wa uchaguzi bado hauna usawa. Heche amewataka viongozi wa dini kuunga mkono juhudi za kupigania haki za wananchi, hususan katika kuimarisha demokrasia.
Diwani wa Kata ya Mbogi, Jimbo la Tarime Vijijini, Steven Nyahiri, ameainisha changamoto mbalimbali zilizojitokeza katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Novemba 2024, akisema uchaguzi huo ulikumbwa na mapungufu makubwa. Ameeleza kuwa viongozi wa dini wana nafasi muhimu katika kupaza sauti na kusaidia kuleta mabadiliko ya kweli ya kisiasa na kijamii.
Kwa upande wake, Veronica Sando, Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa CHADEMA (BAWACHA) @BawachaTaifa Mkoa wa Mara, amesema kuwa licha ya mkoa huo kuwa na rasilimali nyingi kama mbuga za wanyama, badala ya kuwa baraka kwa wananchi, rasilimali hizo zimekuwa chanzo cha madhila, huku baadhi ya watu wakijeruhiwa au hata kuuawa.
Katibu wa Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Musoma, Cleophas Sabure, amethibitisha kupokea ripoti hiyo na kuahidi kuiwasilisha kwa Askofu wa Jimbo. Amesema baada ya Askofu kupitia ripoti hiyo, CHADEMA itaitwa kwa majadiliano zaidi ili kufanyia kazi malalamiko yao.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) @ChademaTz Brenda Rupia @BrendaRupia ametoa rai kwa wanahabari na wadau wote wa habari kwa ujumla wake popote pale walipo kumpatia ushirikiano katika majukumu yake ya kila siku, kwa kuwa majukumu ya nafasi hiyo yanategemea wanahabari na vyombo vya habari kwa kiasi kikubwa
Brenda Rupia aliyeteuliwa na Kamati Kuu ya CHADEMA kushika nafasi hiyo hivi karibuni, ametoa rai hiyo muda mfupi kabla ya kumkaribisha Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Tanzania Bara Amani Golugwa @amanigolugwa aliyekuwa na mazungumzo na wanahabari mapema leo, Jumatano Machi 19.2025
Katika maelezo yake Brenda amesema atahakikisha anatoa ushirikiano kwa wanahabari na vyombo vya habari kwa ujumla huku yeye akiahidi kuendeleza yote mema yaliyofanywa na mtangulizi wake kwenye idara hiyo
"Mbele yenu (wanahabari) amesimama Brenda Rupia (Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi), lakini pia niwaombe tuwe na ushirikiano, nawahaidi kutoa ushirikiano wangu wote kama ambavyo mtangulizi wangu alifanya (John Mrema, aliyekuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano, Itifaki na Mambo ya nje CHADEMA) hapo awali lakini nategemea kuendeleza zaidi huo ushirikiano" -Brenda -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo @ChademaTz John Mnyika @jjmnyika ametoa wito kwa watanzania na wasio watanzania kuweza kujiunga na mkakati wa Tone Tone wa kukichangia chama hicho kwani wakijiunga watakuwa wamejiunga na kuchangia mabadiliko.
Mnyika akizungumza leo Februari 27 katika uzinduzi wa mkakati huo amesema michango hiyo itatumika katika kazi mbalimbali za kichama ikiwemo kuwawezesha viongozi wa chama hicho kusafiri maeneo mbalimbali nchini kuweza kuwaelimisha watanzania kuhusu sera za chama na kufanya mikutano ya hadhara.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
Waziri wa Kilimo, Mheshimiwa @HusseinBashe, leo Jumatatu Februari 24, 2025, ametoa taarifa rasmi kuhusu mradi wa ujenzi wa Bwawa la Mkomazi na skimu za umwagiliaji mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. @SuluhuSamia, ambaye ameweka jiwe la msingi la mradi huo.
Waziri Bashe amesema kuwa Bwawa la Mkomazi lilifikiriwa tangu enzi za serikali ya awamu ya kwanza lakini kutokana na changamoto mbalimbali halikuwahi kutekelezwa. Hata hivyo, serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia imeamua kulifanikisha kwa vitendo, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kitaifa wa ujenzi wa mabwawa makubwa 100 ya kuvuna maji kwa kilimo na matumizi mengine.
"Mkomazi ni miongoni mwa mabwawa 100 ambayo tumeanza kuyatekeleza. Kati ya hayo, 17 tayari yana wakandarasi na hili ni mojawapo. Hii ni hatua kubwa katika kuimarisha sekta ya kilimo na kuhakikisha nchi yetu inazidi kuwa ghala la chakula barani Afrika," alisema Waziri Bashe.
Mradi wa umwagiliaji wa Mkomazi unajumuisha skimu mbili kuu: Skimu ya Mkomazi, inayohusisha ekari 24,000, na Skimu ya Chekelei, yenye ekari 3,000.
Jumla ya vijiji 29 vitanufaika moja kwa moja na mradi huu, jambo linaloashiria mapinduzi makubwa katika kilimo cha umwagiliaji.
Akihitimisha amesema, mradi huo unagharimu shilingi bilioni 97, ambapo ujenzi wa Bwawa la Mkomazi umegharimu shilingi bilioni 18, Skimu ya Mkomazi bilioni 48, na Skimu ya Chekelei bilioni 31. -
Jambo TV
@Jambotv_
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) @ChademaTz Kanda ya Kati, kimekemea vikali kitendo kinachodaiwa kufanywa na Maafisa Elimu cha kuwalazimisha walimu kwenda kushiriki sherehe ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) @ccm_tanzania , mkoani Dodoma tarehe 05 Februari 2025.
Kwa mujibu wa taarifa kwa umma iliyotolewa na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Kati, Masonga Emmanuel, Maafisa hao wamewafuata watumishi hao wa umma kwa magari na kuwapa fedha za malazi.
“Haya ni matumizi mabaya ya madaraka, kuwalazimisha watumishi wa umma kuwa na mlengo wa kisiasa na kutumia kodi za Watanzania na uhuru binafsi wa wafanyakazi kushiriki matukio ya chama kimoja kwa kutumia ushawishi wa madaraka na fedha za walipa kodi wa nchi hii”, imeeleza taarifa hiyo.
CHADEMA imetoa wito kwa Serikali kuwachukulia hatua Maafisa Elimu wote wanaodaiwa kuhusika katika tukio hilo. Halikadhalika imetoa wito kwa umma kukikataa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ikidai kuwa chama hicho kinatumia kodi za wananchi kwa maslahi binafsi. -
Jambo TV
@Jambotv_
Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba @mwigulunchemba1 , amesema Serikali imechukua hatua madhubuti kudhibiti mianya ya ukwepaji kodi unaosababishwa na mabadiliko ya majina ya kampuni za kigeni kwa kuhakikisha Namba ya Utambulisho wa Kodi (TIN) inabaki ile ile hata kama kampuni itabadilisha jina.
Hayo ameyasema bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Tarime Mjini, Michael Mwita Kembaki, aliyetaka kujua hatua zinazochukuliwa na Serikali kwa wawekezaji wa nje ambao kila baada ya miaka kadhaa hubadili majina ya kampuni kwa lengo la kukwepa kodi.
Dkt. Nchemba amesema kuwa Serikali imechukua hatua mbalimbali ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa Sheria ya Kampuni, Sura 212, ambayo inawataka wawekezaji kutoa taarifa kwa Msajili wa Kampuni (BRELA) wanapobadilisha jina la kampuni.
“Historia ya mabadiliko yote ya majina ya kampuni huhifadhiwa kwenye kumbukumbu rasmi ili kuhakikisha majina mapya hayawezi kutumika kuficha madeni ya kodi au kushiriki katika shughuli zisizo halali”, amesema Dkt. Nchemba.
Amesema kuwa kupitia Sheria ya Usimamizi wa Kodi, Sura 438, Serikali pia imeweka sharti kwamba Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuhakikisha Namba ya Utambulisho wa Kodi (TIN) inabaki ileile hata kama kampuni itabadilisha jina kwa kuwa TIN hutumika kufuatilia historia ya ulipaji kodi wa kampuni, hivyo mabadiliko ya jina hayaondoi wala kufuta wajibu wa kodi.
Aidha, akieleza kuhusu kodi zinazotozwa wakati wa kubadili jina la kampuni kwa Watanzania na wageni, Dkt. Nchemba amesema kuwa kubadili jina la Kampuni haiathiri wala haihusiani na masuala ya kikodi.
Amesema kuwa kinachosababisha kuwepo na kodi au ukwepaji wa kodi ni mabadiliko ya umiliki kwa kuuza hisa ambazo zitaleta kipato cha ziada ambacho kinatakiwa kulipiwa kodi kutokana na faida iliyopatikana.
“Kama mmiliki ni yuleyule ameamua kubadilisha jina la kampuni kwa ajili ya matangazo ya kibiashara na Namba ya Mlipa Kodi ni ileile, haileti badiliko lolote kwenye kodi”, amefafanua Dkt. Nchemba.
Amesema kuna kampuni za nje ambazo zinamiliki sehemu ya kampuni nchini na hazina shughuli zaidi ya zinazofanyika Tanzania, ikitokea wamebadilishana umiliki unaozidi asilimia 50, hapo kuna kodi ambayo ni lazima ikusanywe.
Amesema Serikali imefanyia kazi kwa kiasi kikubwa suala hilo lililokuwa likijitokeza katika maeneo ya mawasiliano, madini na mengine na amewatoa hofu wabunge kuwa Serikali imeweka kwenye Sheria na inafuatilia kwa umakini panapotokea jambo hilo na kodi stahiki ya Serikali inakusanywa. -
Jambo TV
@Jambotv_
Mbunge wa Jimbo la Nzega Vijijini, Dk. @HKigwangalla, ameonya kuwa kupungua kwa fedha za wafadhili katika sekta ya afya barani Afrika ni changamoto kubwa inayohitaji hatua za dharura kutoka kwa serikali za Afrika.
Kupitia ujumbe wake aliouchapisha katika ukurasa wake wa mtandao wa X (zamani Twitter), Dk. Kigwangalla amesisitiza kuwa nchi za Afrika zinapaswa kuwekeza zaidi katika sekta ya afya ili kuhakikisha huduma bora kwa wananchi wote.
“Muda wa kutegemea wafadhili umepita. Ni lazima tubuni mbinu mpya na za kisasa za kugharamia afya za watu wetu,” aliandika.
Ameeleza kuwa ni muhimu kuwa na mikakati madhubuti kama vile bima ya afya kwa wote, kodi maalum za kulipia bima kwa watu wasio na uwezo, pamoja na kuhakikisha kila mtu anakuwa na bima ya afya.
Dk. Kigwangalla, ambaye ni mtaalamu wa afya ya jamii mwenye shahada ya udaktari wa binadamu na shahada ya uzamili ya afya ya jamii (MPH), ametoa wito wa matumizi ya raslimali kwa uwazi, ubunifu, na uwajibikaji ili kuboresha mfumo wa afya na kupunguza utegemezi wa misaada ya nje.
Kauli yake inakuja wakati ambapo mataifa mengi ya Afrika yanakabiliwa na changamoto za kifedha katika sekta ya afya, huku huduma za msingi zikihitaji uwekezaji mkubwa wa ndani. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) @ChademaTz John Mnyika @jjmnyika ameeleza sababu ya Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Freeman Mbowe @freemanmbowetz kutokumkabidhi ofisi Mwenyekiti wa sasa wa chama hicho Tundu Lissu @TunduALissu ni kuwa Katibu mkuu ndiye Mwenyekiti mtendaji wa chama na hata nyaraka za chama yeye zipo chini yake hivyo ndiye atahusika kukabidhi ofisi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
"Juzi (Jumatatu Januari 27, 2025) ilikuwa nizungumze kama mtendaji mkuu nieleze katika kuingia huku upya katika uongozi kama Katibu Mkuu ni mambo gani ningeyapa kipaumbele kama Katibu Mkuu lakini vilevile ilikuwa niwatangazie watanzania juu ya ujio wa Mwenyekiti, sasa watawala wakaingiwa hofu kwamba pengine hotuba zetu zinaweza kufunika mkutano ulikuwa unaendelea (Mkutano wa Nishati Afrika) na wakatuma polisi kuzuia Press Conference."
"Kitu ambacho kilitokea na wanahabari mkazuiwa kufanya kazi yenu ya habari. Katika mazingira yoyote katika taifa lolote hata katikati ya vita wanahabari wanatimiza wajibu wao wa habari lakini katika Tanzania ya leo vyombo vya habari vilizuiwa hapa na mlizuiwa kufanya kazi yenu"
John Mnyika @jjmnyika, Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) @ChademaTz akizungumza kwenye mapokezi ya Mwenyekiti wa chama hicho Tundu Lissu, Makao Mkuu ya CHADEMA Mikocheni Dar Es Salaam. -
Jambo TV
@Jambotv_
Baraza la Wanawake CHADEMA (BAWACHA) taifa limeeleza masikitiko yake makubwa juu ya kauli iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, aliyesema kuwa, “Wajawazito wasiotaka kununua glavu wakajifungulie nyumbani.”
Kauli hiyo iliyotolewa wakati wa mkutano na wananchi wa Temeke imeelezwa kuwa ya udhalilishaji, isiyo na staha, na inayokinzana na haki za afya ya mama na mtoto.
Kwa mujibu wa taarifa ya BAWACHA iliyotolewa siku ya Jumanne Januari 28, 2025 na Sigrada Wilhem Mligo, Mratibu wa Uenezi BAWACHA Taifa, kauli ya Chalamila inaenda kinyume na Sera ya Afya ya Taifa na Mpango Mkakati wa Sekta ya Afya (HSSP-V) wa mwaka 2021-2026 unaolenga kuboresha huduma za afya ya uzazi.
“Kujifungulia nyumbani ni hatari kwa afya ya mama na mtoto, kwani kunaongeza uwezekano wa maambukizi ya vimelea vya magonjwa (sepsis) na kukosa huduma ya dharura endapo matatizo yatatokea”, imesisitiza BAWACHA.
Baraza hilo limeeleza wasiwasi kwamba kauli ya Chalamila inaweza kufungua mianya ya rushwa kwa watoa huduma wasiokuwa waaminifu, ambao wanaweza kuwataka wajawazito kulipia huduma ambazo zinapaswa kuwa bure.
BAWACHA imesema, “Kauli hii inahamasisha vitendo vya rushwa na inaweza kuchochea ukosefu wa uwajibikaji miongoni mwa watoa huduma za afya.”
BAWACHA pia imetaka Wizara ya Afya kutoa ufafanuzi wa wazi juu ya huduma za afya ya mama na mtoto. Baraza hilo limesema kwamba kuna mkanganyiko mkubwa kuhusu iwapo huduma hizi ni bure kama inavyodaiwa na sera, au kama zinahitaji gharama ambazo wananchi hawajui waziwazi.
Katika taarifa yake, BAWACHA imetoa wito kwa Rais Samia Suluhu Hassan, kuchukua hatua dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa kauli hiyo, ikisema, “Ni muhimu viongozi wa umma wawe na staha wanapozungumza na wananchi, hasa wanaposhughulikia masuala nyeti kama afya ya mama na mtoto.”
Baraza hilo limewasihi watoa huduma wa sekta ya afya kuendelea kufanya kazi kwa kuzingatia maadili yao ya taaluma na utu, bila kujali changamoto zinazotokana na kauli au matendo ya baadhi ya wanasiasa.
BAWACHA imeonya kwamba, iwapo hatua hazitachukuliwa dhidi ya RC Chalamila, watatoa wito kwa wananchi kumkataa.
“Hatuwezi kukaa kimya wakati viongozi wa umma wanatoa kauli zinazochochea maumivu kwa wanawake wa kawaida ambao wanakosa uwezo wa kumudu gharama za afya,” wamesisitiza. -
Jambo TV
@Jambotv_
Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba, amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa miongozo yake madhubuti katika ukusanyaji wa kodi bila kutumia mabavu, akisisitiza kuwa mbinu hiyo imezaa matunda makubwa katika kuongeza mapato ya nchi.
Pongezi hizo zimetolewa Januari 23, 2025, wakati wa kilele cha Siku ya Mlipakodi, ambapo Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imewatunuku walipakodi 1,228 kutoka sekta mbalimbali nchini kwa mchango wao wa kikodi ambapo Rais Samia anakabidhi tuzo hizo, ikiwa ni ishara ya shukrani kwa walipakodi.
Dkt. Mwigulu amesema kauli ya Rais Samia ya kuhimiza ukusanyaji wa kodi kwa hiari imechangia kwa kiasi kikubwa kufanikisha makusanyo makubwa ya kodi. Pia ameeleza kuwa Rais amekuwa akifanya mapitio ya sheria za kodi kupitia tume maalum na kuwezesha TRA kujenga mifumo ya kisasa ya ukusanyaji wa kodi.
“Katika kipindi cha uongozi wa Mhe. Rais Samia, fedha nyingi zimeongezwa kwenye sekta za kilimo, huduma za jamii, afya, na miundombinu, ambapo barabara nyingi zimejengwa mijini na vijijini,” amesema Dkt. Mwigulu.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amesema mkoa huo utaimarisha biashara za usiku na mchana ili kuchochea maendeleo. Amebainisha kuwa hatua za kufunga taa na kamera za CCTV zinaendelea kufanyika ili kuboresha usalama, huku vyombo vya dola vikiwa tayari kulinda mazingira ya kibiashara.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya TRA, Bw. Mussa Uledi, amesisitiza umuhimu wa uwepo wa Rais Samia katika utoaji wa tuzo hizo, akisema kuwa uwepo huo unatoa motisha kwa walipakodi.
Bw. Uledi ameongeza kuwa TRA imeanza kutumia mfumo wa TANCIS, ambao unarahisisha shughuli za forodha bandarini, mipakani, na viwanja vya ndege, sambamba na kuhakikisha mifumo ya taasisi nyingine inasomana ili kuongeza ufanisi. -
Jambo TV
@Jambotv_
Hii ndiyo Safu ya uongozi wa Tundu Lissu.
Kuanzia kushoto ni Makamu Mwenyekiti Bara John Heche, Makamu Mwenyekiti Zanzibar Said Mzee Said, Mwenyekiti wa chama Taifa Tundu Lissu, Katibu Mkuu John Mnyika, Naibu Katibu Mkuu Bara Amani Golugwa na Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Ali Ibrahim Juma. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Hivi ndivyo wajumbe wa Baraza Kuu la CHADEMA walivyompitisha Katibu Mkuu mpya John Mnyika @jjmnyika baada ya Mwenyekiti wa chama hicho Tundu Lissu @TunduALissu kupendekeza jina lake. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) taifa, wamefanya matembezi katika Jiji la Dodoma kwa lengo la kumpongeza Mwenyekiti wa chama hicho ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan @SuluhuSamia pamoja na Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa kuteuliwa na Wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum wa CCM Taifa kuwania kiti cha Urais kwa mwaka 2025.
Matembezi hayo yamefanyika Jijini Dodoma ambayo yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa umoja huo akiwamo Mwenyekiti wake Taifa, Mohamed Ali Mohamed Kawaida, Makamu Mwenyekiti UVCCM Rehema Sombi Omary, pamoja na Katibu Mkuu wa UVCCM Jokate Mwegelo.
Akihutubia mamia ya vijana hao, Kawaida amesema matembezi hayo ni ishara ya kutuma salamu kwa watu wengine kuwa umoja huo uko tayari kwa mapambano kuhakikisha mwaka 2025 kura zote zinaenda CCM.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Hivi ndivyo aliyekuwa Mwenyekiti wa @ChademaTz Freeman Mbowe @freemanmbowetz alivyoondoka ukumbini baada ya matokeo ya uchaguzi kutangazwa na Tundu Lissu @TunduALissu kuibuka mshindi dhidi ya Freeman MboweThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
“Kuna jambo ambalo limeendelea ambalo limefunikwa kwa kiwango fulani na mjadala mkubwa juu ya uchaguzi wa ndani ya CHADEMA, lazima nilitolee kauli kwa ufupi sana leo, juu ya mchakato unaoendelea kufanywa na Tume ya taifa ya uchaguzi kutunga kanuni za uchaguzi wa Ubunge, Rais na Madiwani wa mwaka 2025. Na sisi walitupa rasimu hizo kanuni na walitupa mpaka tarehe 30 Disemba tuwe tumepeleka maoni kwao.”
“Katibu Mkuu nimemuandikia Mkurugenzi wa Tume huru ya taifa ya uchaguzi, kumtaarifu kwamba sisi hatukubaliani na huu utaratibu wa kuanza kuandika kanuni kutoa hii kanuni na kutaka maoni ya wadau kabla kwanza hayajafanyika marekebisho ya kikatiba na kisheria.” – Mnyika.
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mnyika akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari, Makao Makuu ya Chama hicho Mikocheni jijini Dar es Salaam, tarehe 7 Januari, 2025.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Makamu mwenyekiti wa CHADEMA @ChademaTz Tundu Lissu @TunduALissu amechukua rasmi fomu ya kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa chama hicho Taifa katika ofisi za makao makuu ya CHADEMA zilizopo Mikocheni, jijini Dar es Salaam leo, Jumanne Desemba 17.2024
Lissu amekabidhiwa fomu hiyo na Katibu mkuu wa CHADEMA John Mnyika @jjmnyika ambapo Lissu anatarajia kuirudisha fomu hiyo hapo kesho
Katika hatua nyingine Lissu ameweka wazi kuwa fomu hiyo amelipiwa na Sativa @Sativa255 -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Fedha, na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM @ccm_tanzania Taifa, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba @mwigulunchemba1 , amewahimiza wananchi wa Mkoa wa Singida kushiriki kikamilifu katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika, Novemba 27, 2024.
Akizungumza katika Mkutano wa kufunga kampeni za uchaguzi uliofanyika, Novemba 26, 2024, katika Kata ya Puma, Wilaya ya Ikungi, Dkt. Nchemba amewasihi wananchi kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani na utulivu, huku akisisitiza umuhimu wa kuchagua viongozi wa vitongoji, mitaa na vijiji wanaotokana na CCM kwa maendeleo ya jamii.
Amewahimiza wananchi kutunza mshikamano na kudumisha umoja kwa kuhakikisha uchaguzi unakuwa wa haki na usio na migogoro, kwa maslahi ya taifa zima.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) John Mnyika amefanya kampeni katika kata za Ulaya na Tindiga Jimbo la Mikumi Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro akiungana na Mwenyekiti wa Chama hicho Wilaya ya Kilosa Joseph Haule kuwanadi wagombea wa chama hicho
Mnyika amewataka wanachama wa chama hicho kuungana kwa pamoja kuweza kuhakikisha wanawachagua viongozi wa chama hicho ambao wameteuliwa na watakaowaletea maendeleo katika maeneo yao.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Maji Jumaa Aweso amesema kuwa jitihada kubwa zimefanyika kuboresha huduma ya maji safi na salama mkoani Tanga ikiwamo wananchi kufungiwa mita za luku za maji (Mita za malipo ya kabla) ili kuondokana na changamoto ya ubambikiziaji wa bili za maji.
Waziri Aweso ameyasema hayo siku ya Jumanne Novemba 19, 2024 wakati wa ziara yake katika Mradi wa Kuboresha Upatikanaji wa Huduma ya Maji Tanga Kupitia Hatifungani ya Kijani (Kijanibond) unaotekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Tanga (TangaUWASA)
Aidha amesema kuwa changamoto ya majitaka Tanga jiji litabaki kuwa historia kwakuwa tayari kuna kiasi cha fedha kimetengwa kuhakikisha miundombinu ya majitaka inakwenda kuboreshwa.
Waziri Aweso amesema kuwa mkoa wa Tanga umekuwa mfano Tanzania na duniani kote kwa kuwa na taasisi ya umma kujiendesha kibiashara akiashiria taasisi ya TangaUWASA kutekeleza mradi wa maji wa hatifungani.
Amesema kwa kuwa fedha za mradi huu zipo basi nguvu inahitajika ili ukamilike kwa asilimia 100.
Aidha ameiomba taasisi hiyo kuendeleza uaminifu wa kulipa gawio stahiki kwa wawekezaji katika hatifungani ya maji kwani ni mradi unaotekelezwa kwa kutumia fedha za wananchi.
Mradi wa Kuboresha Upatikanaji wa Huduma ya Maji Tanga Kupitia Hatifungani umetoa fursa kwa jamii kushiriki katika uwekezaji kupitia ununuzi wa hisa (bonds) hivyo kufanikisha upatikanaji wa fedha zitakazotumika katika utekelezaji wake.
Utekelezaji wa mradi huu unatarajiwa kuanza mapema mwaka huu ukilenga kuboresha miundombinu katika kituo cha kuzalisha na kusambaza maji cha Mowe, kuboresha miundombinu ya mabomba ya kusambazia maji katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Tanga, Mji wa Muheza, Pangani na Mkinga, kufunga Mita za Malipo ya Kabla (Smart Prepaid Water meters) kwa wateja 10,000 na kuendeleza jitihada za utunzaji wa vyanzo vya maji.
Mapema mwezi Februari, 2024 Makamu wa Rais, Dkt. Philip Isdor Mpango alizundua rasmi Dirisha la uuzaji wa Hatifungani ya Kijani ya TANGA UWASA, ambapo makusanyo ya mauzo hayo yalizidi lengo kwa asilimia 103 ambapo TANGA UWASA ilifanikiwa kukusanya Shilingi za Kitanzania Bilioni 54.72 ambapo lengo halisia lilikuwa ni kukusanya Shilingi Bilioni 53.12.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mbunge wa Tanga Mjini Ummy Mwalimu ametambua na kupongeza jitihada zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan na Wizara ya Maji chini ya Waziri Jumaa Aweso katika kuhakikisha upatikanaji wa maji mkoani Tanga unakuwa wa ufanisi mkubwa.
Ummy ametoa pongezi hizo siku ya Jumanne Novemba 19, 2024 wakati wa ziara ya Waziri Aweso katika Mradi wa Kuboresha Upatikanaji wa Huduma ya Maji Tanga Kupitia Hatifungani ya Kijani (Kijanibond) unaotekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Tanga (TangaUWASA).
Ummy amesema kuwa mkoa wa Tanga kuliahidiwa kutatuliwa changamoto tatu za maji ambazo ni kukatikakatika maji, bili kubwa za maji, na majitaka hasa kwenye barabara za namba, hata hivyo ameridhishwa na mambo hayo matatu kuanza kutekelezwa.
Aidha Waziri Ummy ameisifu TANGAUWASA kwa mradi wa hatifungani wa thamani ya Shilingi bilioni 53. 12 ambao umewezesha kuimarika miundombinu ya maji kwa kutumia pesa za wawekezaji wananchi akiwamo yeye mwenyewe.
Mradi wa Kuboresha Upatikanaji wa Huduma ya Maji Tanga Kupitia Hatifungani umetoa fursa kwa jamii kushiriki katika uwekezaji kupitia ununuzi wa hisa (bonds) hivyo kufanikisha upatikanaji wa fedha zitakazotumika katika utekelezaji wake.
Utekelezaji wa mradi huu unatarajiwa kuanza mapema mwaka huu ukilenga kuboresha miundombinu katika kituo cha kuzalisha na kusambaza maji cha Mowe, kuboresha miundombinu ya mabomba ya kusambazia maji katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Tanga, Mji wa Muheza, Pangani na Mkinga, kufunga Mita za Malipo ya Kabla (Smart Prepaid Water meters) kwa wateja 10,000 na kuendeleza jitihada za utunzaji wa vyanzo vya maji.
Mapema mwezi Februari, 2024 Makamu wa Rais, Dkt. Philip Isdor Mpango alizundua rasmi Dirisha la uuzaji wa Hatifungani ya Kijani ya TANGA UWASA, ambapo makusanyo ya mauzo hayo yalizidi lengo kwa asilimia 103 ambapo TANGA UWASA ilifanikiwa kukusanya Shilingi za Kitanzania Bilioni 54.72 ambapo lengo halisia lilikuwa ni kukusanya Shilingi Bilioni 53.12.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
"Katika mazungumzo ya maridhiano ajenda yetu kubwa ilikuwa ni kutaka kupatikana kwa Katiba Mpya, Tume Huru ya Uchaguzi na marekebisho ya kutaka uchaguzi uwe huru na wa haki nchini, pamoja na viambatanisho vingine vya kukwamua mchakato wa Katiba tuliwasilisha (kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa) mapendekezo mahsusi ya marekebisho ya Katiba na sheria ili kuhakikisha uchaguzi wa serikali za mitaa unakuwa huru na haki, mapendekezo haya hayakufanyiwa kazi na serikali kabisa pamoja na kukumbusha kwa nja mbalimbali" -Mnyika
"Hatimae serikali ikapeleka Bungeni miswada mitatu ya sheria, ambao ni muswada wa Tume Huru ilyoitwa 'Tume Huru ya Uchaguzi', muswada wa sheria mpya ya uchaguzi wa Udiwani, Ubunge na Urais na muswada wa sheria ya vyama vya siasa, lakini tukaipinga vilevile ile miswada mitatu, tukaenda Bungeni tukatoa maoni lakini maoni hayo yakapuuzwa, sheria mbovu zikapitishwa na Rais akasaini, tukapinga zile sheria wakaendeleanazo" -Mnyika
Katibu Mkuu wa CHADEMA John Mnyika amezungumza hayo mbele ya wanahabari leo, Jumanne Novemba 19.2024, Dar es Salaam -
Jambo TV
@Jambotv_
📍Windhoek - Namibia
Tanzania yapigiwa mfano kwenye kampeni ya matumizi ya nishati safi ya kupikia. -
Jambo TV
@Jambotv_
Benki ya Dunia, imemchagua Mtanzania, Dkt. Zarau Wendeline Kibwe, kuwa Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Benki ya Dunia atakayesimamia Kanda Namba Moja ya Afrika inayojumuisha nchi 22 ikiwemo Tanzania, nafasi ambayo Tanzania imewahi kuihudumu miaka 54 iliyopita.
Uamuzi wa Dkt. Kibwe kuikwaa nafasi hiyo nyeti katika taasisi hiyo kubwa ya Fedha Duniani, umetangazwa katika Mkutano wa Mwaka wa Kundi la Kwanza la Nchi za Afrika wa Benki ya Dunia, uliofanyika Jijini Washington D.C, nchini Marekani ambapo Mikutano ya Mwaka ya Shirika la Fedha Duniani (IMF) na Benki ya Dunia inafanyika.
Kabla ya kuchaguliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Benki hiyo atakayesimamia Kanda Namba Moja ya Afrika, Dkt. Kibwe alihudumu katika ofisi hiyo ya bodi kama Naibu Mkurugenzi Mtendaji, Mshauri na Mshauri Mwandamizi kwa zaidi ya miaka saba, tangu mwaka 2017.
Akizungumza Jijini Washington D.C, baada ya kutangazwa kuchukua nafasi hiyo, Dkt. Zarau Wendeline Kibwe amesema kuwa ataitumia nafasi hiyo kusimamia uendeshaji wa benki na taasisi zake pamoja na kutetea maslahi ya nchi katika Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Dunia pamoja na maslahi ya Kanda ya Afrika anayoisimamia ili kukuza maendeleo na uchumi wa nchi hizo.
Akizungumza kwa niaba ya Serikali katika Mkutano huo uliomtangaza Dk. Kibwe kuchukua nafasi hiyo, Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, anayeongoza Ujumbe wa Tanzania katika mikutano hiyo ya mwaka ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia, amesema kuwa hayo ni matokeo ya juhudi za Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, anavyoifungua nchi na kukuza Diplomasia ya Kimataifa.
Dkt. Nchemba amempongeza Dkt. Kibwe kwa kupata nafasi hiyo na kwamba kutokana na umahiri wake katika masuala ya uchumi na fedha, pamoja na uzoefu wake wa muda mrefu katika ofisi hiyo, anaamini kuwa maslahi ya nchi yataendelea kulindwa ipasavyo kwa manufaa ya Watanzania.
Dkt. Zarau Wendeline Kibwe ni mchumi wa Kitanzania ambaye hivi karibuni amechaguliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia kwa Kanda Namba Moja ya Afrika inayojumuisha nchi za Botswana, Burundi, Eritrea, Eswatini, Ethiopia, Gambia, Kenya, Lesotho, Liberia, Malawi, Msumbiji, Namibia, Rwanda, Shelisheli, Sierra Leone, Somalia, Sudan Kusini, Sudan, Tanzania, Uganda, Zambia, na Zimbabwe.
Kabla ya kujiunga na Ofisi ya Bodi, Dkt Kibwe alihudumu kama Mchumi wa Benki ya Dunia kwa Tanzania ambapo katika kipindi cha miaka 15 ya kazi yake, Dkt. Kibwe amehudumu katika Serikali ya Jamhuri wa Muungano katika nafasi mbalimbali ikiwemo ya Mchambuzi Mwanadamizi wa Sera (Ofisi ya Rais – Tume ya Mipango), Mhadhiri Msaidizi (Chuo Kikuu Dodoma), Afisa Forodha Msaidizi (Mamlaka ya Mapato Tanzania), na Mhadhiri Msaidizi (Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere).
Dkt. Kibwe ana Shahada ya Uzamivu (Ph.D.) katika Uchumi wa Maendeleo, Shahada ya Uzamili (MA) katika Uchumi wa Maendeleo, na Shahada ya Umahiri katika Sera za Umma, zote kutoka Taasisi ya Taifa ya Mafunzo ya Sera (GRIPS) huko Tokyo, Japan.
Alipata Shahada yake ya Kwanza ya Sayansi katika Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe kilichopo Morogoro, Tanzania. -
Jambo TV
@Jambotv_
Licha ya changamoto kubwa zinazokumba uchumi wa dunia, Tanzania imefanikiwa kujiimarisha kiuchumi na kuingia kwenye orodha ya nchi kumi bora barani Afrika kwa Pato la Taifa (GDP) kwa mwaka 2024 ikishika nafasi ya 10, hiyo ni kulingana na ripoti mpya ya Mtazamo wa Uchumi wa Dunia (WEO) iliyotolewa na Shirika la Fedha Duniani (IMF) mwezi Oktoba, 2024.
Katika mkutano wa mwaka wa IMF uliofanyika Washington, Marekani, uchumi wa Tanzania unatarajiwa kufikia dola za Kimarekani bilioni 79.87 ifikapo mwisho wa mwaka 2024.
Ukuaji huu umeelezwa kuwa ishara ya mafanikio ya sera bora na uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, ambaye ameendelea kusisitiza umuhimu wa maendeleo shirikishi katika sekta muhimu za kilimo, utalii, na viwanda.
Ukuaji wa uchumi wa Tanzania umeonekana kuwa endelevu na unaonyesha matumaini makubwa kwa miaka ijayo. Kulingana na makadirio ya IMF, ukuaji wa Pato la Taifa (GDP) wa Tanzania ulifikia asilimia 5.1 mwaka 2023 na unatarajiwa kuongezeka hadi asilimia 5.4 mwaka 2024, huku ikikadiriwa kufikia asilimia 6.0 mwaka 2025. Ukuaji huu unadhihirisha kuwa Tanzania inaimarisha misingi ya uchumi imara, licha ya changamoto za kimataifa kama vile mabadiliko ya tabianchi, bei za mafuta, na migogoro ya kikanda.
Kulingana na taarifa hiyo, Afrika Kusini inaongoza ikiwa na ukuaji wa uchumi wa Dola bilioni 403, ikifuatiwa na Misri (Dola Bil. 380). Kwa mataifa ya Afrika Mashariki katika orodha hiyo ukiachana na Tanzania, ni nchi ya Kenya ambayo ipo nafasi ya saba ikiwa na Dola bil. 116.3.
Kiujumla, Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) kupitia kwa Mkurugenzi mkuu wa shirika hilo, Kristalina Georgieva linatabiri ukuaji wa asilimia 4.2 kwa Afrika ifikapo mwaka 2025, huku likiona ukuaji thabiti lakini wa polepole barani humo.
“Eneo la Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara linaonyesha viwango vya ukuaji ambavyo viko thabiti mwaka huu ikilinganishwa na mwaka uliopita, takriban asilimia 3.6, na tunatarajia kuongezeka hadi takriban asilimia 4.2 mwakani,” alisema Pierre-Olivier Gourinchas, Mchumi Mkuu wa IMF.
Kulingana na takwimu za IMF kuhusu uchumi wa nchi zinazoendelea na masoko yanayokua, Tanzania imeweza kudhibiti viwango vya mfumuko wa bei ukilinganisha na baadhi ya nchi jirani. Kwa mfano, mwaka 2024, nchi nyingi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara zinatarajia mfumuko wa bei wa juu zaidi, kama vile Angola (asilimia 18.1) na Ghana (asilimia 19.5), wakati Tanzania inaendelea kusimama imara na viwango vya wastani vya mfumuko wa bei.
“Mfumuko wa bei unadhibitiwa katika baadhi ya nchi... na kufikia viwango karibu na malengo, lakini nusu ya nchi bado ziko mbali sana na malengo hayo, na theluthi moja bado zinakabiliwa na mfumuko wa bei wa tarakimu mbili,” alisema Jean-Marc Natal, Mkuu wa Idara ya Utafiti, IMF.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo ya IMF, ukuaji wa uchumi katika nchi za Afrika hasa Kusini mwa Jangwa la Sahara umekuwa wa polepole lakini endelevu. Ukuaji huo unakadiriwa kufikia asilimia 4.2 ifikapo mwaka 2025, kutoka asilimia 3.6 mwaka 2024. Ripoti hiyo inaeleza kuwa ukanda huu umekumbwa na changamoto mbalimbali kama vile mabadiliko ya tabianchi na migogoro, hali inayofanya ukuaji wa uchumi kuwa wa kusuasua katika baadhi ya nchi. Hata hivyo, Tanzania imeweza kuvuka vikwazo hivyo na kuendelea kujenga uchumi wa kisasa unaojumuisha sekta mbalimbali muhimu kama kilimo, viwanda, na utalii. -
Jambo TV
@Jambotv_
Waziri wa Fedha wa Tanzania Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu ameshiriki Mkutano wa Mawaziri wa Fedha na Magavana wa Benki Kuu za nchi za Afrika (African Caucus - WB) uliomshirikisha Rais wa Benki ya Dunia, Bw. Ajay Banga, Jijini Washington D.C, nchini Marekani, ambako Dkt. Nchemba, anaongoza Ujumbe wa Tanzania katika Mikutano ya Mwaka ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia.
Mkutano huo uliwapa fursa Mawaziri wa Fedha na Magavana wa Benki Kuu za Afrika kuwasilisha vipaumbele na changamoto zinazoathiri maendeleo barani Afrika kwa Rais wa Benki ya Dunia Bw. Ajay Banga, ili kuzingatiwa katika mipango na mikakati ya ushirikiano kati ya Benki ya Dunia na nchi za Afrika.
Baadhi ya changamoto zilizoainishwa ni pamoja na fursa chache za ajira kwa vijana, miundombinu hafifu ya umeme, barabara na tehama, uzalishaji mdogo wa chakula, tishio katika uhimilivu wa madeni, na ongezeko la gharama za upatikanaji wa mikopo.
Bw. Banga alikubaliana na umuhimu wa upatikanaji wa umeme wa uhakika na wa kutosha katika kuchochea shughuli za uchumi na namna unavyoweza kuathiri uzalishaji wa mbolea na chakula.
Amebainisha kuwa Benki ya Dunia ipo tayari kusaidia utekelezaji wa miradi ya umeme ambayo inahusisha matumizi ya nishati rafiki kwa mazingira na kuhimiza matumizi ya TEHAMA hususan kwa kundi kubwa la vijana kwa kuwa ni chanzo moja wapo kikubwa cha ajira. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Tamko la @humanrightstz lililotolewa na Mkurugenzi wake @HengaAnna mbele ya wanahabari leo, Jumatatu Oktoba 21.2024 ambapo pamoja na mambo mengine tamko hilo limelaani madai ya kutekwa, kupigwa na kutupwa porini Katibu Mwenezi wa @BawachaTaifa Aisha MachanoThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoani Simiyu kimekanusha taarifa zinazosambaa mitandaoni zikidai kuwa Mwenyekiti wa chama hicho Wilaya ya Itilima amefunga ofisi za chama na kuhamia Chama cha Mapinduzi (CCM). Taarifa hizo zimetajwa kuwa si za kweli na zinapaswa kupuuzwa.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza, Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Simiyu, Mussa Onesmo, amesema kuwa Katibu Mkuu wa CCM, Emmanuel Nchimbi, alisikika akitoa taarifa hizo wakati wa ziara yake kijijini Luguru, Simiyu. Hata hivyo, Onesmo amesisitiza kuwa taarifa hizo ni za uongo kwani CHADEMA haina mwenyekiti wa Wilaya ya Itilima anayeitwa Telly Maduhu wala katibu anayeitwa Ngasa Mipawa, majina yaliyotajwa na CCM.
Kwa upande wake, Jackson Luyombya, ambaye ni Mwenyekiti halali wa CHADEMA Wilaya ya Itilima, amesema amesikitishwa na taarifa zilizotolewa kwenye mkutano huo, akieleza kuwa Mwenezi wa CCM alidanganywa ili kutoa mvuto kwenye ziara yake.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Katibu Mkuu Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) John Mnyika ametoa wito kwa watanzania kujiandikisha kwenye Daftari la Mkazi ili kuweza kushiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa,Vijiji na Vitongoji unaotarajiwa kufanyika tarehe 27 Novemba 2024.
Akizungumza leo Oktoba 8, 2024 na Wanahabari Makao Makuu ya CHADEMA Dar Es Salaam Mnyika amesema “tarehe 11 mpaka 20 Oktoba kote nchini mnapaswa na tunawaomba sana mjitokeze kwenda kujiandikisha kwa wingi”This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI PICHA:
Matukio katika picha wakati Waziri wa Fedha na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Dkt Mwigulu Lameck Nchemba Madeluakihutubia maelfu ya wananchi wa wilaya ya Misungwi katika Viwanja vya Amani, katika mkutano ulioandaliwa na Mbunge wa jimbo hilo ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Alexandar Pastory Mnyeti.
Akizungumza katika mkutano huo, Dkt. Nchemba amewaomba Watanzania kuendelea kumwombea kwa Mwenyezimungu, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili awe na afya njema anapotekeleza majukumu yake ya kuwahudumia Watanzania kwa upendo na ari kubwa.
Amesema serikali imeendelea kutoa fedha nyingi wakati huu kuliko wakati wowote ule ambapo kila mahali nchini, inatekelezwa miradi ya maendeleo inayogharimu fedha nyingi, ikiwamo miradi ya kimkakati kama SGR, umeme wa Bwawa la Julius Nyerere, Ujenzi wa Daraja la Kigongo-Busisi na mingine mingi katika sekta za uzalishaji, afya, maji, elimu na miundombinu. -
Jambo TV
@Jambotv_
Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu amewasili wilayani Misungwi, mkoani Mwanza kwa ziara rasmi ya kikazi na kupokelewa na viongozi na wananchi wa wilaya hiyo.
Katika ziara hiyo Dkt. Nchemba atakagua maendeleo ya ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Tanzania (TIA) Kampasi ya Mwanza na kisha atazungumza na wananchi wa Misungwi katika mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Mbunge wa Jimbo hilo ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Alexander Mnyeti katika uwanja wa Amani, Misungwi Mjini.
Dkt. Nchemba yuko mkoani Mwanza kwa ziara ya kikazi ambayo imelenga kutembelea na kukagua, kuzindua na kuweka mawe ya msingi katika miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali mkoani humo. -
Jambo TV
@Jambotv_
📍VIDEO:
"Tumefungua kesi ya kupinga TAMISEMI kusimamia uchaguzi wa Serikali za Mitaa, naomba nitoe wito kwa wananchi na vyombo Habari kuhudhuria Mahakama Kuu ya Tanzania, Masijala ya Dar es Salaam kesho, Jumatano Agosti 28.2024 saa nane kamili mchana" Dkt. Ananilea Nkya. Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania (JUKATA)This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
📍VIDEO:
"Sisi tulipokuwa wadogo walikuwa wanasema anayepigwa ni punda lakini siku hizi hata punda hapigwi, niseme tu kazi ya vyombo vya Ulinzi ni kulinda watu sio kupiga, Binadamu huwa hapigwi" Mhashamu Wolfgang Pisa. Rais wa Baraza la Maaskofu (TEC). -
Jambo TV
@Jambotv_
Waziri wa Fedha Dkt. @mwigulunchemba1 ameungana na abiria wengine kutumia usafiri wa treni ya mwendo kasi (SGR), kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma na kuonja ladha ya usafiri huo ambao umekuwa ukifanyiwa kila jitihada ili ufike nchini kote na kuchochea biashara katika ukanda wa Maziwa Makuu.
Aliyekaa pembeni yake ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Mhandisi Ismail Hassan Rumatila. -
Jambo TV
@Jambotv_
Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba ameihakikishia Jumuiya ya Kimataifa na Watanzania kwa ujumla kwamba Serikali inaendelea kuweka na kuboresha mazingira ya uwekezaji ikiwamo kuboresha mifumo yake ya kodi.
Dkt. Nchemba ameyasema hayo katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha Jijini Dar es Salaam wakati akiagana na Balozi wa Uswizi aliyemaliza muda wake wa ubalozi nchini Tanzania Didier Chassot.
Amesema kuwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameunda timu ya wataalamu ya kupitia na kuja na mapendekezo yatakayosaidia kuboresha mifumo yake ya kodi ili kuvutia zaidi biashara na uwekezaji nchini.
Dkt. Nchemba amefafanua kuwa pamoja na kuundwa kwa timu hiyo, Serikali pia imechukua hatua kadhaa za kuboresha ya kielektroniki ya ukusanyaji kodi inayosaidia kukusanya mapato yake kwa ufanisi na kuondoa usumbufu kwa walipakodi.
Amesema kuwa lengo la kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji pamoja na kuimarisha mifumo ya kodi ni kuhakikisha kuwa idadi ya walipakodi inaongezeka hatua itakayosaidia pia kuiwezesha serikali kupunguza viwango vya kodi ya ongezeko la thamani siku za usoni kwa sababu walipakodi watakuwa wengi.
Kwa upande wake Balozi wa Uswizi aliyemaliza muda wake nchini Didier Chassot, ameipongeza Serikali kwa uamuzi huo wa kupitia mifumo ya kodi na kwamba anaamini mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao nchini watapata pia nafasi ya kuzungumza na kujadiliana na serikali kuhusu masuala hayo kama walivyoomba.
Balozi Chassot ametumia fursa hiyo ya kuagana na Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba kuipongeza Serikali ya Awamu ya Sita kwa hatua kubwa iliyopiga kimaendeleo katika kipindi kifupi.
Ameahidi kuwa Uswisi inaandaa mpango mpya wa ushirikiano wa kimaendeleo na Tanzania, utakaojielekeza katika kufanikisha ajenda mbalimbali za maendeleo ya nchi kupitia programu zake mbalimbali ikiwamo kusaidia mfuko wa maendeleo ya jamii-TASAF, usimamizi wa fedha za umma, biashara na uwekezaji kupitia asasi za kiraia na sekta binafsi.
Didier Chassot ameitumikia nafasi hiyo ya ubalozi akiwa nchini kwa kipindi cha miaka minne na ameahidi kuendelea kuwa Balozi mzuri wa Tanzania atakaporejea nchini kwake kuendelea na majukumu yake mengine. -
Jambo TV
@Jambotv_
Rais Wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) @Mwabuk2Boniface amesema pamoja na tamko walilolitoa hivi karibuni la kulaani vitendo vilivyofanywa na Jeshi la Polisi dhidi ya viongozi na wanachama wa @ChademaTz lakini chama hicho (TLS( kitafungua kesi kwa wahusika kupitia majina yao
Wakili Mwabukusi amesema, mnamo agosti 12.2024 tulitoa tamko la kulaani vitendo vya kuvunja sheria na kuvunja Katiba vilivyofanywa na Jeshi la Polisi kupitia Mkuu wa Oparesheni wa Jeshi hilo (Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi CP Awadh Juma Haji) vitendo viliyoonekana kwenye vyombo vya habari na magazeti”
Ameongeza kuwa, "kwa kuzingatia uzito na changamoto hii Baraza la Uongozi la TLS liliammua na kuazimia kwamba wahusika wote waliohusika kwenye kadhia hii wanafunguliwa mashtaka kwa majina yao, na timu ya Mawakili kwa ajili ya kufanya kazi hii inaongozwa na Wakili Nyalusi akisaidiana na Wakili Emmanuel Chengula na Wakili Kilato ambao watafungua kesi na tutaziendesha kwa ajili ya kuvindicate (kusimamia) sheria ambao ni wajibu wetu chini ya kifungu cha nne” -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Leo, Jumanne Julai 30.2024 kesi inayomkabili kada wa @ChademaTz Kombo Mbwana imetajwa katika Mahakama ya wilaya ya Tanga baada ya kusomewa mashtaka Julai 16.2024 mbele ya Hakimu Moses Malowa, lakini licha ya siku za nyuma Mahakama kuruhusu mtuhumiwa huyo apatiwe dhamana lakini leo upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili Paul Kusekwa umewasilisha Mahakamani kiapo cha Mkuu wa Upelelezi mkoa (RCO) wa Tanga Manyama Wambura wakiiomba Mahakama kutompatia dhamana mtuhumiwa huyo kwa kile kilichoelezwa kuwa upelelezi wa jambo hilo bado haujakamilika.
Wakili @AdvMahinyila ambaye ni miongoni mwa Mawakili wanaomtetea Kombo Mbwana kwenye kesi hiyo wakiongozwa na Wakili @PMadeleka ameeleza kwa kina kilichojitokeza Mahakamani hapo leo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Kikao kazi kilichohusisha Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na viongozi wa wafanyabiashara chini ya uratibu wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) kilichofanyika leo, Alhamisi Julai 18.2024 Johari Rotana Hotel, jijini Dar es Salaam pamoja na mambo mengine kimeadhimia pande hizo mbili kukutana kila baada ya miezi mitatu (3) ili kujadili changamoto za kikodi zinazowakwamisha wafanyabishara na kutafuta majawabu ya pamoja ili waweze kufanya biashara zao na walipe kodi stahiki
Hayo yameelezwa na Kamishna Mkuu wa TRA Yusuph Mwenda mbele ya wanahabari ikiwa ni muda mfupi baada ya kukamilika kwa kikao kazi hichoThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Nyasa Joseph Mbilinyi 'Sugu' amesema Serikali imetenga shilingi bilioni 890 kwa ajili ya kununua magari ya kifahari wakati ambao wananchi bado hawana huduma muhimu kama huduma za afya.
Akiongea wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya uongozi yaliyofanyika wilaya ya Mufindi mkoani Iringa, Sugu amesema kuwa fedha zilizotengwa kwa ajili ya kununua magari zinapanda kila mwaka na mwaka huu zimetengwa billioni 890 kutoka billioni 500 mwaka jana.
"Mwaka Jana walitumia zaidi ya Billion 500 mwaka huu wametenga billion 890 Kwa ajili ya anasa ya kununua magari ya kifahari" Amesema Sugu. -
Jambo TV
@Jambotv_
Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba @mwigulunchemba1 amemwagiza Kamishna Mkuu mpya wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Yusuph Juma Mwenda kuwachukulia hatua kali za kisheria na kinidhamu ikiwamo kuwafukuza kazi baadhi ya watumishi wa mamlaka hiyo wanaokiuka maadili ya kazi zao kama kudai na kupokea rushwa, kwa kuwa vitendo hivyo vinaitia doa TRA na kuikosesha Serikali mapato.
Dkt. Nchemba amesema hayo wakati akihitimisha Kikao cha Tathmini ya Utendaji Kazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 kilichofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano Arusha (AICC).
Aidha Dkt. Nchemba amemwagiza Kamishna huyo kuwachukulia hatua kali wafanyabiashara wasiowasilisha ritani za Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwa kuwa fedha hizo zinatakiwa kuwasilishwa serikalini kupitia TRA ikizingatiwa kuwa wafanyabiashara ni Mawakala wa Serikali wa kukusanya kodi hiyo, na hazitakiwi kufanywa kama sehemu ya mapato yao.
Halikadhalika Dkt. Nchemba amewataka watumishi wa TRA kuongeza ubunifu, umahiri na kuhakikisha wanatenda haki wakati wa kukusanya mapato ya Serikali ili kutimiza matarajio ya Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuwaletea Watanzania maendeleo ya uhakika.
Pia Dkt. Nchemba ametumia fursa hiyo kuwapongeza TRA kwa utendaji kazi mahiri kwa mwaka wa fedha ulioisha wa 2023/24, ambapo walikusanya kiasi cha Shilingi trilioni 27.64, ambayo ni sawa na ufanisi wa asilimia 97.67 ya lengo la kukusanya Shilingi trilioni 28.30 ambayo ni sawa na ongezeko la asilimia 14.50, ikilinganishwa na makusanyo ya Shilingi trilioni 24.14 katika mwaka wa fedha uliopita 2022/23.
Katika hafla hiyo Dkt. Nchemba aliambatana na Naibu Waziri wa Fedha Hamad Hassan Chande, Kamishna Msaidizi wa Idara ya Sera Wizara ya Fedha William Mhoja, na maafisa wengine waandamizi wa Wizara ya Fedha. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete Dkt. Peter Kisenge amesema wagonjwa zaidi ya asilimia 40 wamebainika mkoani Arusha kuwa na matatizo ya kupanuka kwa misuli ya moyo na moyo kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi unaohitajika.
Dkt. Kisenge amewaambia wanahabari takwimu hizo wakati akitoa tathimini ya siku mbili za kambi ya Matibabu ya kibingwa yanayofanyika mkoani Arusha kwenye viwanja vya Sheikh Amri Abeid yakiratibiwa na kuendeshwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Christian Makonda.
Dkt. Kisenge amesema kati ya wagonjwa wote 200 waliowahudumia tangu Jumatatu, asilimia 35 ya wagonjwa hao wamepata rufaa na kuandaliwa utaratibu wa kupelekwa Dar es Salaam kwenye Taasisi ya Moyo ili kupata huduma za ziada na matibabu.
Dkt. Peter Kisenge amesema wakazi wengi wa mkoa wa Arusha wanakabiliwa na changamoto ya mishipa ya damu kupanuka kutokana na shinikizo la juu la damu, shida ya umeme wa moyo pamoja na changamoto ya moyo kutofanya kazi kwa ufanisi.
Dkt. Kisenge amewataka pia wananchi wa Arusha kuendelea kujitokeza kwa wingi kwenye kambi hiyo ya matibabu akiwataka wananchi kupima ili kujitambua na kuchukua hatua za matibabu mapema.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Boniface Jacob na Godlisten Malisa wamepatiwa dhamana kwa mashtaka yanayowakabili baada ya leo Jumatatu Mei 06, 2024 kufikishwa mahakamani.
Wamepatiwa dhamana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa masharti ya kila mdhamini kusaini bondi ya Shilingi milioni 2 huku kesi yao ikielezwa kutajwa tena Juni 06, 2024.
"Tunafurahi fursa hii imepatikana, tunasubiri sasa mambo yote yajadiliwe hadharani, tupo tayari kufanya kazi ya kisheria." Wakili Peter Kibatala amezungumza.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI PICHA:
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara Tundu Antipas Lissu akiongoza maandamano ya amani wilaya ya Babati Mkoa wa Manyara leo Ijumaa tarehe 26 Aprili, 2024 ikiwa ni mwendelezo wa wiki ya maandamano nchi nzima kama ilivyotangazwa na chama hicho. -
Jambo TV
@Jambotv_
“.... Sisi kwa tathmini yetu tunaona idadi ya wapiga kura inapungua kwa sababu watu wamepoteza imani na mifumo ya uchaguzi”
“Kupelekwa miswada bungeni kungeweza kujenga imani lakini bahati mbaya kumepelekwa miswada mibovu tena karibu na uchaguzi wa serikali za mitaa”
“Tukitaka kuongeza idadi ya wapiga kura lazima tuongeze imani katika mifumo ya uchaguzi, lazima tudai Katiba mpya, marekebisho ya kisheria, tutengeneze uwanja sawa wa uchaguzi”
@jjmnyika
Katibu mkuu @ChademaTz -
Jambo TV
@Jambotv_
Katibu Mkuu wa CHADEMA John Mnyika ametoa wito kwa vijana kufahamu kwamba ujana wao ni hatua ya mpito hivyo wanapaswa kuwa na maono ya mbali zaidi kwa sababu mawazo ya kupigania harakati za vijana haitakuwa ya kudumu kwenye safari zao za kisiasa
Mnyika amezungumza hayo leo, Jumatatu Machi 11.2024 alipokuwa kwenye kongamano la majadiliano rika ya viongozi wa vyama vya siasa kubadilishana maarifa katika uongozi, kongamano linalofanyika katika ukumbi wa Confucious uliopo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo amesema wakati uliopo sasa Tanzania na Dunia inaamini kwenye nafasi ya vijana katika uongozi tofauti na ilivyokuwa hapo awali ambapo vijana walikuwa hawajadiliwi kwenye mazingira ya aina hiyo
Aidha, amewataka vijana walioingia au wanaowaza kuingia kwenye siasa kuwa wavumilivu kwa kuwa mapito ya kisiasa mara zote huwa ni magumu na yenye mambo mengi -
Jambo TV
@Jambotv_
"Wabunge wote 16 wa Dar es Salaam wale wa Majimbo na wa Viti maalum tumepambana sana kuhakikisha mradi wa DMDP unaendelea ili kwa Mimi na Ndugulile tuhakikishe mradi huu inakuja kutatua changamoto za Wilaya za Kigamboni na Ubungo, hizi ndo Wilaya mbili ambazo mradi huu ulikuwa haujapita hilo nalo limefanikiwa, tumekaa na Mawaziri, tumezungumza, tukaenda kwa Mama tukalia hatimaye tukakubaliwa hatua inayofuata na sasa habari njema ni kwamba wiki mbili zilizopita Mjini Zanzibar walikuja Watu wa Benki ya Dunia wakakaa na Watu wetu wa Serikali wakiongozwa na Waziri wetu wa Fedha Mheshimiwa Mwigulu Nchemba mradi umeidhinishwa rasmi na Benki ya Dunia" -Prof. Kitila
Mbunge wa Ubungo Prof. Kitila Mkumbo amezungumza hayo wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM leo, Jumapili Desemba 31.2023 -
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Haya ndio Mapinduzi makubwa yaliyofanyika kwenye Bandari ya Mtwara, Waziri wa Uchukuzi Mhe. @MbarawaM amwaga takwimuThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Jambo TV
@Jambotv_
#habaripicha
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - TAMISEMI Mhe. @AngellahKairuki, akikabidhi ngao ya ushindi wa kwanza kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Abubakar Kunenge (katikati) leo Agosti 29, 2023 kwa Mkoa wa Pwani kuibuka mshindi katika utekelezaji wa mkataba wa lishe kwa mwaka 2022/2023.
Mwingine ni Katibu Tawala Mkoa huo na Skauti Mkuu wa Tanzania Rashid Mchata. -
Jambo TV
@Jambotv_
*PLEASE MAKE A DIFFERENCE: TUNDU LISSU NEEDS US*
www.gofundme.com/Lissumedicalcare -
Jambo TV
@Jambotv_
Hujitangazi kuwa Mzalendo bali watu wanaona uzalendo wako, you don't say it, show it!
-
Jambo TV
@Jambotv_
Sioni kama serikali hii ina uwezo wa kuzuia ajali za barabarani, Magari NI mengi kuliko uwezo wa wabarabara zetu na hasa uduni wa highways!
-
Jambo TV
@Jambotv_
Viongozi Wazuri husifia hadharani, hukemea faragha (you praise in public, you rebuke in private) Katibu Mkuu wa ccm anatia aibu Bwana kinana
-
Jambo TV
@Jambotv_
Pamoja na madhaifu anayoweza kuwa nayo Nyarandu,kuhusu ujangili tumeshirikiana vizuri. UJANGILI umepungua sana ,ndio maana KINANA anamchukia



























































































































































































































































































































































































































































































































































































