Mwenyekit Tundu Lissu amehukumiwa kifungo cha miaka minne kwa kosa la uchochezi ambalo, kwa mtazamo wangu, ni la kutengenezwa. Safari sasa ni kwenda Mahakama ya Rufaa, lakini tusisahau kwamba hata Mahakama ya Rufaa haiwezi kuwa mbadala wa dhamiri ya umma katika kutetea haki na kupinga matumizi mabaya ya mifumo ya dola.
Mahakama ya rufaa ya Lissu haipaswi kuwa Mahakama ya Rufaa pekee. Inapaswa kuwa umma wote tunaohofia kwamba kesi hizi zinatumika kama njia ya kuwanyamazisha na kuwadhibiti wanasiasa wakosoaji.
Hatari kubwa zaidi si kifungo cha Lissu pekee. Ni uwezekano wa kifungo kutengeneza mazoea hatimaye kuwa sehemu ya mfumo wa kawaida wa kudhibiti upinzani. Hapo ndipo tunapopaswa kuwa na wasiwasi.
Leo hukumu imetolewa, lakini nchi inaendelea na shughuli zake kana kwamba hakuna jambo kubwa lililotokea. Kana kwamba ni mtu mwingine wa kawaida tu aliyefungwa. Hii ni ishara inayopaswa kutufanya tutafakari kwa kina kuhusu hali ya dhamiri ya jamii yetu.
Watu wengi, wakiwemo wanachama wetu, tayari wako mahabusu. Tusipojiuliza kwa pamoja tunakoelekea, tunaweza kuamka siku moja na kukuta magereza yamekuwa sehemu ya kawaida ya maisha ya kisiasa ya nchi yetu.
Uonevu hauzuiliwi na nguvu ya waliouonewa pekee, bali pia na dhamiri ya jamii inayokataa kuuzoea.
Kukaa kimya mbele ya jambo linalogusa haki za msingi za binadamu kunaweza kuifanya jamii izoeane na hali ambayo kesho inaweza kumkuta yeyote kati yetu.
Godbless Lema
Godbless Jonathan Lema (born 26 October 1976) is a Tanzanian Chadema politician and Member of Parliament for Arusha City constituency from 2010 to 2015. He was also a candidate for the same constituency in the 2015 general election which was conducted on 25 October 2015. However, the parliamentary election for Arusha Constituency had to be postponed following the death of Estomoh Malya who was the parliamentary candidate for the Alliance for Change and Transparency, a newly established opposition political party in Tanzania. More on Wikipedia
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
🔴#live: GODBLESS LEMA ANAFUNGUKA MAZITO MUDA HUU HAPA ARUSHA.... www.youtube.com/live/FY5m3_OEpqQ via @YouTube
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Kulinda taasisi ni wajibu, kulinda ukweli ni dhamana. Si kila anayezungumza anataka vita, na si kila anayenyamaza analinda amani.
YOHANA 8:32
“Nanyi mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru.”
Kesho Kibo Palace Hotel Saa Nane Mchana. -
Godbless E.J. Lema reposted
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mjumbe wa Shura ya Maimamu Tanzania, Sheikh Aboubakar Mgodo ametoa mwito wa kuwa wakweli, kuwajibika ili kuponya majeraha na maumivu yanayowakabili wananchi waliopoteza ndugu na waliotoweka wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu.
Sheikh Mgodo ameyasema hayo leo, Oktoba 29, 2026, mkoani Dar es Salaam wakati wa Ibada maalum ya kuwakumbuka waliopoteza maisha, waliopotea, pamoja na majeruhi wa matukio ya wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania wa Oktoba 29, 2025.
“Uongo hauwezi kutufikisha pazuri. Tunashauri vyombo vyetu, serikali yetu tuwe wakweli. Kosa linaweza kutokea iwe kwa bahati mbaya au makusudi, lakini baada ya kosa watu wanatakiwa wajirudi”, ameeleza Sheikh Mgodo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema reposted
U.S. Ambassador to Tanzania
@USAmbTanzania
Today, the U.S. Embassy community joined me to honor the memory of all those who lost their lives in the violence surrounding Tanzania’s October 2025 general elections. We remember them, and the families who still grieve and seek answers. As I said to the U.S. Senate during my confirmation hearing, this will not be swept under the rug.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
OCTOBER 29 - MWAKA MMOJA BAADA YA MAUAJI HATUWEZI KUSAHAU, HATUPASWI KUZOEA.
Leo, mwaka mmoja umetimia tangu matukio ya umwagaji damu ya Oktoba 29. Mwaka mmoja wa majonzi, maswali, majeraha ya mioyo na kumbukumbu za maisha yaliyopotea.
Tunawakumbuka waliopoteza maisha, tunazifikiria familia zilizopoteza wapendwa wao, na tunaitaka dhamiri ya taifa kutafakari kwa kina kuhusu thamani ya uhai wa binadamu.
Hatari kubwa kwa jamii si maovu yanapotokea pekee, bali ni pale jamii inapofikia hatua ya kuyazoea. Siku tunapoacha kushtushwa na kupotea kwa maisha ya watu, tunakuwa tumepoteza sehemu muhimu ya ubinadamu wetu.
Oktoba 29 isiwe tarehe ya kumbukumbu pekee. Iwe siku ya kutafakari, kutafuta ukweli, kudai haki na kuhakikisha kwamba misiba ya namna hii haijirudii.
Taifa haliwezi kujenga amani ya kudumu kwa kusahau maumivu ya wananchi wake. Amani ya kweli hujengwa juu ya ukweli, haki, uwajibikaji na heshima kwa uhai wa kila mtu.
Hatukumbuki kwa sababu tunataka kulipiza kisasi. Tunakumbuka kwa sababu tunataka haki, utu na taifa ambalo maisha ya kila Mtanzania yana thamani.
Oktoba 29. Hatutasahau. Hatutazoea. Haki na utu lazima vitangulie. -
Godbless E.J. Lema reposted
Brenda Rupia Jonas
@BrendaRupia
Leo, tarehe 28 Oktoba 2026, ujumbe wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ukiongozwa na Katibu Mkuu wa Chama, Mhe. John Mnyika, akiongozana na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi, Brenda Rupia, umekutana na kufanya mazungumzo na wabunge wa Bunge la Ujerumani kuhusu masuala ya Haki za binadamu, Demokrasia,Hali ya kisiasa na utawala bora.
Katika mazungumzo hayo, ujumbe wa CHADEMA umekutana na wabunge wafuatao:
1.Mhe. Ulle Schauws – Green Party.
2.Mhe. Derya Türk-Nachbaur – Social Democratic Party (SPD).
3.Mhe. Clara Bünger – DIE LINKE.
4.Mhe. Dr. Carsten Brodesser – Christian Democratic Union (CDU). -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema reposted
Chadema Tanzania
@ChademaTZ2
TAARIFA KWA UMMA
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Vijana na wananchi wengi wameikimbia nchi yao wakitafuta amani na kulinda uhai wao. Kwa kusikitisha, hata maeneo waliyokimbilia kutafuta usalama yanaanza kuonekana kuwa hatari.
Lakini hatari kubwa inayotukabili sasa siyo tu watu kutekwa au kuuawa, hata wanapokimbilia nchi jirani. Hatari kubwa zaidi ni the revenge of the tipping point, pale mateso yanapofika kiwango ambacho baadhi ya watu wanaweza kuanza kuamini kuwa kupambana kwa nguvu na kulipiza kisasi ndiyo njia pekee iliyobaki, maana hata kulimbia hakulindi uhai wako. Hii ni hatari sana.
Mtu anapofikiri kwamba nyumbani ni hatari na ugenini nako ni hatari, anaweza kuanza kujiuliza, je, suluhisho ni kupambana kwa nguvu? Hapo ndipo jamii inapoanza kusogea kwenye eneo hatari zaidi, ambako kukata tamaa kunaweza kuzaa fikra za kulipiza kisasi.
Huu haupaswi kuwa mwelekeo wa fikra za umma katika taifa letu. Ni wajibu wa mamlaka kutumia maarifa, busara na hekima katika kulinda maisha ya watu na kuzuia hali hii isifikie hatua isiyoweza kudhibitiwa. Usalama wa raia haupaswi kutegemea walipo, bali haki yao ya kuishi bila hofu.
Tukio la kutekwa kwa Twaha Mwaipaya nchini Kenya ni jambo la kusikitisha na linalopaswa kuchunguzwa kwa uzito. Serikali ya Kenya inapaswa kuchukua hatua za haraka na za dhati kubaini alipo, kuhakikisha usalama wake na kumrejesha akiwa hai na mwenye afya.
Tunapaswa kuelewa jambo moja, jamii inapopoteza imani kwamba haki inaweza kupatikana kwa njia za amani, hatari huwa kubwa zaidi kuliko tukio moja la utekaji. Kulinda maisha, kutafuta ukweli na kuhakikisha haki si udhaifu, ndiyo njia ya kuzuia kukata tamaa kusigeuke kuwa chuki na kisasi. -
Godbless E.J. Lema reposted
Amnesty Kenya
@AmnestyKenya
Twaha Mwaipaya, a Tanzanian national, was reportedly abducted at around 2pm today in Kamulu, Machakos County, by individuals travelling in three vehicles, including a Toyota Land Cruiser hardtop.
He was travelling by taxi to visit friends. Anyone with information on his whereabouts is urged to reach out immediately. Authorities must urgently establish his whereabouts and ensure his safety.
Please share widely. #freetwahamwaipaya -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
TWENDENI OFISINI KWA JAJI MKUU KWA UMOJA NA WINGI WETU, KUDAI HESHIMA YA MAHAKAMA
HUNGER STRIKE YA LISSU NI KILIO CHA JAMII NZIMA
Kitendo cha Mwenyekiti Tundu Lissu kugoma kula si suala lake binafsi pekee. Ni ujumbe mzito kwa jamii yetu na kwa kila mmoja wetu kwamba tumeshindwa kutekeleza wajibu wetu ipasavyo katika kusimamia haki. Ndiyo maana amefikia hatua ya kupigania haki yake mwenyewe kwa njia ya hunger strike.
Hii ni fedheha kwa jamii nzima. Tunapofika mahali ambapo mtu analazimika kuhatarisha afya na maisha yake ili haki isikike, tunapaswa kujiuliza, tumeshindwa wapi kama jamii ?
Kilio cha Lissu ni mwaliko kwetu sote kutafakari upya wajibu wetu na kutafuta njia sahihi, za pamoja na zenye uzito, za kupinga uonevu na kudai haki.
Katika mkutano wa leo Morogoro, nimewaeleza wananchi kwamba nitamuomba Katibu Mkuu na Makamu Mwenyekiti wa chama kufikiria kuitisha Kikao cha Dharura cha Kamati Kuu, ili tujadili hatua za pamoja za kuitikia kilio hiki.
Miongoni mwa hatua nitakazopendekeza ni kuandaa maandamano yatakayoongozwa na viongozi wakuu wa chama, kuelekea moja kwa moja katika Ofisi ya Jaji Mkuu, kuonyesha mshikamano wetu na kudai haki pamoja na heshima ya Mahakama.
Huu si wakati wa kutazama Lissu akipambana peke yake. Ni wakati wa kujiuliza sisi sote tunapaswa kufanya nini ili haki isitafutwe kwa gharama ya maisha ya mtu.
Tuna wajibu wa kuchukua hatua za pamoja ili kumuepusha Tundu Lissu na mateso na kuhakikisha kilio chake kinasikilizwa.
Haki ya mtu mmoja ni wajibu wa jamii nzima. Kilio cha Lissu kisiishie kuwa kilio chake, kiwe mwamko wa dhamiri ya taifa.
TWENDE KWA UMOJA. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Mh. Tundu Lissu kuanza mgomo wa kula (Hunger Strike) kuanzia Jumatatu.
Inasikitisha pale ambapo mtu anapolazimika kuhatarisha afya yake ili kudai haki ambayo ilipaswa kulindwa na mfumo wenyewe.
Haki si hisani ya serikali, ni wajibu wa mfumo wa sheria.
Jamii inayomlazimisha mtu kutumia mwili wake kama silaha ya mwisho ya kupigania haki inapaswa kujiuliza maswali mazito kuhusu hali ya utawala wa sheria na haki za binadamu nchini.
🔴#live: MAWAKILI WA TUNDU LISSU WANAZUNGUMZA MUDA HUU www.youtube.com/live/z1YRvjCEndU via @YouTube -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Highway ya Dodoma–Dar es Salaam… sorry, road strip! 😂
Nimepita hapa Mitumba, nimeona haya majengo yanayojengwa pembezoni mwa barabara hii. Nikajiuliza moyoni. Population inaongezeka kwa kasi Tanzania, miji inapanuka, na mahitaji ya usafiri yanaongezeka. Sasa hawa wanaopanga miji mipya, bado wanafikiria single-lane roads ? Hawaioni kesho ya miji hii ?
Ghafla nikajijibu mwenyewe. Labda hawana shida na kubomoa na kujenga upya. Planning ya leo haizingatii gharama za kesho, kwa sababu kesho wakivunja, tutaita maendeleo!
Dodoma ni mfano wa very organized squatters. Majengo yanaweza kupangwa kwa mistari, lakini kama mipango haizingatii ukuaji wa watu, upanuzi wa barabara na mahitaji ya miaka 30/50 ijayo, huo siyo mji uliopangwa vizuri, ni msongamano uliopewa ramani.
The real cost of poor planning is not what we build today, but what we must destroy tomorrow. -
Godbless E.J. Lema reposted
Chadema Tanzania
@ChademaTZ2
"Kama kuna janga kubwa katika nchi hii ambalo linaenda kwa kasi ni ukweli, haki na busara kupoteza heshima na chuki kuwa kiongozi." Mhe. @godbless_lema
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
MOROGORO, TUKUTANE KESHO!
Jumamosi, tarehe 24 October 2026, Uwanja wa K Ndege saa 8:00 mchana. Karibuni wote, tushiriki kwa wingi! Umoja wetu ni nguvu yetu. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Leo nilikuwa Kijiji cha Makiungu, Ikungi. Mwenyekiti wa Wilaya katika hotuba yake alizungumzia watu ambao wametekwa na kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa hawajulikani walipo.
Nafikiri tatizo kubwa la jamii yetu si mateso na uhuni pekee tunayopitia, bali ni jinsi tulivyojifunza kuishi navyo kana kwamba ni sehemu ya kawaida ya maisha.
Tumefika mahali ambapo ukatili hautushangazi tena, dhuluma haitunyimi usingizi, na mambo ambayo yalipaswa kututikisa kama jamii yanapita mbele yetu kama habari za kawaida.
The most dangerous stage of social decay is not when evil happens, but when society loses the ability to be shocked by it.
Jamii inapofikia hatua ya kuzoea maumivu ya wengine, inakuwa imeanza kupoteza utu wake. Na pale tunapozoea uovu, ukimya wetu huanza kuupa uovu uhalali.
Tatizo si kwamba hatuoni kinachoendelea. Tatizo ni kwamba tumeanza kukiona bila kuhisi wajibu wa kufanya chochote.
Mateso yanapokuwa kawaida, haki huonekana kama ombi, na uovu unapokuwa utamaduni, utu hugeuka kuwa jambo la hiari. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
TUKO LIVE JIMBONI KWA MWENYEKITI TUNDU LISSU - MAKIUNGU.
🅻🅸🆅🅴:LEMA ANAKIWASHA MUDA HUU IKUNGI SINGIDA www.youtube.com/live/tedoYBoiO1s via @YouTube -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Barabara ya kutoka Babati kwenda Singida ni mbaya sana, mbaya kweli kweli! Naomba mnielewe, wajameni!!! Mbaya sana , mbaya sana!!! Mbaya sana.
-
Godbless E.J. Lema reposted
Farah Omar
@FarahOm91196252
Majaji wa Zamani walikuwa wanaheshimika sana kwa Wananchi. Mwananchi akishindwa Mahakama za chini anasema haki yangu nitapata Mahakama kuu kwa Jaji.Sasa hivi utasikia matusi makali kwa majaji na maneno ya kukata tamaa ya wananchi kwa majaji hii ni janga kwa nchi.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
HUKUMU YA CHADEMA RIPOTI NZITO/ WAKILI ASHINDWA KUJIZUIA ATEMA CHECHE youtu.be/ub3tYQj45E8 via @YouTube
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
John Pambalu kashitakiwa kwa UHAINI.
-
Godbless E.J. Lema reposted
Freddie
@frediejustine
..... Kuna siku watu wengi watainamisha vichwa vyao kwa aibu na fedheha,
Pale watakapogundua ukubwa wa uovu walioutetea na thamani ya mashujaa waliowadhihaki.
Pindi ukweli utakapofunua yale waliyoyafumbia macho, wengi watajuta kwa kusimama upande usio sahihi wa historia. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Tunalaani vikali kukamatwa kwa kiongozi wetu Zakaria Obadi huko Kahama.
Serikali na CCM wanapaswa kuelewa kuwa demokrasia haiwezi kufungwa pingu, na mawazo hayawezi kushindwa kwa vitisho.
Mnaweza kuwakamata watu, lakini hamwezi kukamata dhamiri za wananchi. Mnaweza kulazimisha ukimya, lakini ukimya wa hofu si ridhaa, na ukandamizaji si ushindi.
Historia imethibitisha, nguvu inaweza kuchelewesha mabadiliko, lakini haiwezi kuua kiu ya uhuru na haki.
Nguvu ya uongozi si kunyamazisha upinzani, bali ni kuwa na ujasiri wa kukabiliana na hoja. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
ASANTE KARATU.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
WOMEN ON THE BOOTS | IFAKARA – MOROGORO, KANDA YA KATI
Huu ni wakati wa wanawake kusimama imara, kuhamasisha jamii na kuwa sehemu ya mapambano ya kujenga Tanzania yenye haki, uhuru na usawa. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
MWABUKUSI
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
UMMA UNAPASWA KUAMUA NA SIO VINGINEVYO.
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Tarehe 7 Oktoba 2026, Mahakama Kuu katika Shauri la Kikatiba Na. 25918/2026; Jopo la Majaji watatu Mh. A.R. Mruma, Mh. Suleiman Hassan na Mh. Irene Musokwa, Majaji ,waliamuru kusimamishwa kwa mwenendo wa shauri la kinidhamu Namba 4/2026 dhidi ya Wakili Boniphace Mwabukusi lenye lengo la kumfuta uwakili.
Licha ya Kamati ya Maadili kupewa taarifa ya maandishi kuhusu amri hiyo, iliendelea kutoa uamuzi mdogo wa mapingamizi ya kisheria na imesema itaendelea na shauri na imepanga kulisikiliza tena tarehe 19 Oktoba 2026.
Iwapo amri hiyo bado iko halali, kuendelea na shauri kunazua maswali mazito kuhusu utii wa amri za Mahakama, mipaka ya mamlaka na uwajibikaji wa taasisi. Hakuna chombo kilicho juu ya sheria, na amri za Mahakama si za kuchagua kutekeleza.
Kamati inayosimamia maadili inapaswa kuwa mfano wa kuheshimu sheria na Katiba. Hili si suala la kumtetea mtu binafsi, bali ni kulinda mamlaka ya Mahakama, haki za wananchi na imani katika mfumo wa haki.
Kamati inapaswa kutoa ufafanuzi wa wazi kuhusu msingi wa kuendelea na shauri hilo licha ya amri ya Mahakama.
Sheria lazima itawale kila mtu, hakuna mtu wala taasisi iliyo juu ya sheria. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
THANK YOU MOSHI.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Wonders shall never end! Dunia kweli ina mambo. Na kuna wafungwa wako uraiani, na wana ujasiri wa kuwakosoa Maaskofu. 🤔
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Huu sasa ndio UHAINI.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
IGP, jana saa nane mchana, John Pambalu alisafirishwa kutoka Arusha kwenda Dar es Salaam. Hadi sasa, mawakili wetu wako Kituo cha Polisi Kati wakijaribu kufahamu alipo, lakini bila mafanikio.
IGP, ni sababu gani inayofanya Jeshi la Polisi kuwa kimya kuhusu mahali alipo John Pambalu?
Kama amesafirishwa chini ya uangalizi wa Jeshi la Polisi, ni kwa nini taarifa za mahali alipo zinakuwa ngumu kupatikana hata kwa mawakili wake?
Ukimya huu unazua maswali mengi yasiyo ya lazima, unaongeza wasiwasi na kuleta taharuki ambayo ingeweza kuepukwa kwa kutoa taarifa zilizo wazi.
Very unnecessary tension and noise. Why ? -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Wizara ambayo nafikiri haijapewa uzito na uangalizi unaostahili kutoka kwa umma ni Wizara ya Maji.
Ninaamini kuna mambo yanayoendelea ndani ya wizara hii ambayo yanahitaji kufuatiliwa kwa umakini mkubwa. Hii ni sekta inayogusa maisha ya kila Mtanzania, uchumi, afya ya umma na maendeleo ya taifa kwa ujumla.
Ni muhimu kujiuliza, Je, fedha zinazotengwa kwa ajili ya miradi ya maji zinatumika kwa ufanisi ? Je, miradi inayotekelezwa inatoa thamani halisi ya fedha zilizotumika ? Je, kuna uwazi na uwajibikaji wa kutosha katika usimamizi wa miradi hiyo ?
Kuna siku nchi inaweza kushtuka kutokana na mambo yanayoendelea katika sekta hii ambayo hayajapewa uangalizi unaostahili. Ndiyo maana ni wakati wa kuanza kuifuatilia Wizara ya Maji kwa jicho kali zaidi, tukitaka majibu, uwazi na uwajibikaji.
Maji ni uhai. Usimamizi wa sekta hii haupaswi kuchukuliwa kama jambo la kawaida, wala kuachwa bila uchunguzi wa kina. Wananchi wanastahili kujua kinachoendelea, fedha za umma zinavyotumika na matokeo yanayopatikana.
Kwa mtazamo wangu, hali si nzuri zaidi. Ni wakati wa kuipa sekta hii uangalizi mkubwa unaostahili kabla hatujalazimika kujiuliza kwa nini tulipuuza ishara zilizokuwepo.
Kila shilingi inayotengwa kwa ajili ya maji lazima iwe na matokeo yanayoonekana katika maisha ya wananchi. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Tumetoka Kituo cha Polisi cha Mjini Arusha, nikiwa na Naibu Katibu Mkuu Bara, Mwenezi wa Vijana Taifa na Katibu wa Mkoa wa Arusha. Kwa sasa, John Pambalu anapelekwa Dar es Salaam.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema reposted
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA na aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, amesema yupo katika hali ya kukata tamaa kutokana na mwenendo wa baadhi ya vijana wanaotanguliza burudani badala ya masuala muhimu ya kisiasa na kijamii.
Akizungumza leo Oktoba 13,2026 jijini Arusha katika hafla ya uzinduzi wa ofisi ya CHADEMA Kanda ya Kaskazini, Lema amesema baadhi ya vijana wamekuwa wakijikita katika matamasha ya burudani, ikiwemo tamasha la kuadhimisha miaka 30 ya muziki wa Bongo Fleva na matamasha ya Nyama Choma, akidai kuwa hali hiyo inawafanya kusahau masuala ya msingi yanayohusu haki na mustakabali wa taifa.
Amesema inaumiza kuona baadhi ya wananchi hawatoi uzito unaostahili kwa mapambano ya kudai haki, akitolea mfano wa Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, ambaye anashikiliwa mahabusu ya magereza akikabiliwa na kesi ya uhaini.
Aidha, Lema amewataka vijana kuelekeza nguvu zao katika masuala muhimu ya kisiasa na kufuatilia mwenendo wa kesi ya Tundu Lissu, huku akieleza kuwa licha ya juhudi zake za muda mrefu katika kupigania haki za wananchi, mwenendo wa baadhi ya vijana umemvunja moyo na kumfanya ajikute katika hali ya kukata tamaa, akimuomba Mungu amsaidie.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
WANANCHI TUNAPASWA KUWA SERIOUS !! Mbele ni pagumu kuliko wakati huu.
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Brain power ni zaidi ya raslimali. Nchi inaweza kuwa na dhahabu, almasi, gesi, uranium na madini mengine mengi, lakini bila mipango madhubuti, ubunifu, maono, taasisi imara na usimamizi bora, utajiri huo unaweza usilete maendeleo yanayotarajiwa. Vivyo hivyo, nchi yenye rasilimali chache inaweza kupiga hatua ikiwa itawekeza katika elimu, teknolojia, ujuzi na ubunifu.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Kwa mujibu wa International Diabetes Federation (IDF) Diabetes Atlas 2025, Tanzania ilikuwa na takribani watu wazima milioni 2.93 wenye kisukari mwaka 2024. Kinachotia wasiwasi zaidi ni kwamba takribani asilimia 60.2 ya watu wenye kisukari wanakadiriwa kuwa hawajagunduliwa.
Hii ina maana kuwa watu wengi wanaweza kuishi na kisukari bila kujua hali zao, huku wakijiweka katika hatari ya kupata madhara makubwa kiafya.
Kisukari kisipodhibitiwa kinaweza kuharibu figo taratibu bila dalili za wazi katika hatua za mwanzo. Tatizo linapogunduliwa kwa kuchelewa, mgonjwa anaweza kuhitaji matibabu ya gharama kubwa, yakiwemo kusafishwa damu kwa mashine (dialysis).
Madhara haya hayaishii kwa mgonjwa pekee. Yanaweza kuathiri uchumi wa familia, kuongeza mzigo kwa jamii, kupunguza nguvu kazi na kuongeza gharama za huduma za afya, hivyo kuathiri maendeleo na uchumi wa taifa kwa ujumla.
Swali ni hili, Je, tunaelewa kweli ukubwa wa tatizo hili na madhara yake kwa taifa ? -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Soko la hisa ni kioo cha imani ya wawekezaji katika uchumi. Kupotea kwa karibu Shilingi bilioni 738 ndani ya wiki mbili katika thamani ya soko la DSE si jambo la kupuuzwa. Hili linapaswa kuibua mjadala mpana kuhusu hali ya uchumi, imani ya wawekezaji na mvuto wa Tanzania kama sehemu ya uwekezaji. Uchumi haupimwi kwa kauli za viongozi pekee, bali pia kwa mwenendo wa mitaji, uwekezaji na imani ya wanaoweka fedha zao nchini.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Amani si deni ambalo wananchi wanapaswa kulipa kwa kunyamaza mbele ya dhuluma. Mamlaka ni ya muda, lakini madhara ya chuki mnayoikuza yanaweza kulitesa taifa kwa vizazi. Acheni kuichezea nchi hii kwa ajili ya maslahi yenu ya kisiasa. Siku mbegu hii itakapokomaa, hakuna atakayekuwa na uwezo wa kuchagua matunda atakayovuna.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Bwana Paulo, inawezekana kujenga minara mipya, lakini huwezi kujenga upya historia iliyobomolewa. London wana Big Ben, Paris wana Eiffel Tower, Roma wana Colosseum, na Tokyo wana Tokyo Tower. Miji hii inaendelea kuwa ya kisasa huku ikitunza alama zake za kihistoria, ambazo zimekuwa sehemu ya utambulisho wake na vivutio vya utalii.
Mnara wa Eiffel huvutia mamilioni ya wageni na kuchochea biashara na shughuli za kiuchumi zinazouzunguka. Vivyo hivyo, Colosseum ya Roma na alama nyingine za kihistoria duniani zinaonyesha kuwa urithi wa zamani unaweza kuwa hazina kubwa ya utalii na uchumi. Miji hii haikufuta historia ili ionekane ya kisasa; imejifunza kuitunza na kuitumia kama fursa ya uchumi.
Kwa nini Arusha iwe tofauti ? Mnara wa Saa, unaohusishwa na historia ya enzi za Wajerumani, na Mnara wa Mwenge ni sehemu ya utambulisho wa Arusha na historia yetu. Badala ya kuibomoa historia, tunapaswa kuitunza, kuiboresha na kuitangaza ili kuvutia watalii na kunufaisha uchumi wa jiji.
Ushamba hauondolewi kwa kuiba na kushika mamlaka, mamlaka yanaweza tu kuufichua zaidi. Minara hii si samani za nyumbani kwako unazoweza kubadilisha kwa matakwa yako au kulingana na jinsi unavyojisikia siku hiyo. Minara hii ni alama za kihistoria zinazobeba utambulisho na urithi unaopaswa kuhifadhiwa kwa vizazi vijavyo.
Arusha inaweza kuwa ya kisasa bila kupoteza utambulisho wake. Usasa bila historia ni majivuno yasiyo na mizizi. Historia ikibomolewa, haiwezi kujengwa upya kwa saruji na nondo!
Kwa maoni yangu, ungeendelea na kazi zilezile za nyama choma, angalau huko unaonekana kuwa na kipaji kizuri cha uhamasishaji. Si kila jambo linahitaji kubomoa kilichopo ili kuonyesha kwamba umefanya jambo jipya!
#arusha #hifadhihistoria #urithiwetu -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Hizi ni sehemu chache tu za mitaro ya Jiji la Arusha. Mingine imejaa taka, mingine imeziba, na mingine inatumika kuhifadhi nguzo za TANESCO. Huu ni upuuzi wa kiutendaji unaohitaji maelezo na hatua za haraka kutoka kwa mamlaka zinazohusika.
Wakati TMA ikitoa tahadhari kuhusu uwezekano wa mvua kubwa zinazohusishwa na El Niño, Halmashauri ya Jiji la Arusha na taasisi nyingine zinazohusika zinafanya nini ?Mnasubiri mvua zianze kuharibu nyumba, biashara na mali za wananchi ndipo muanze kuamka?
Mitaro ni miundombinu ya kuzuia maji ya mvua yasilete maafa, si dampo la taka wala ghala la kuhifadhi nguzo. TANESCO nayo inapaswa kueleza kwa nini nguzo zake zimehifadhiwa kwenye mitaro hiyo na kuhakikisha hazizuii mtiririko wa maji.
Inasikitisha kuona maandalizi ya kuzuia maafa yakionekana kupuuzwa, ilhali gharama za uzembe huu zitalipwa na wananchi wasio na hatia.
Ninakemea vikali hali hii na kuzitaka mamlaka zinazohusika ziamke kutoka kwenye usingizi wa kiutendaji. Safisheni mitaro, ondoeni vizuizi, kagueni mifumo yote ya kupitisha maji na wekeni wazi hatua mnazochukua.
Wananchi hawahitaji visingizio baada ya maafa, wanahitaji hatua kabla ya maafa.
ARUSHA HAIHITAJI MATAMKO YA BAADA YA MAFURIKO. INAHITAJI UWAJIBIKAJI SASA!2 media couldn't be displayed. See them on the original post. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Huwezi kujenga Taifa bora na salama bila kuwa na familia imara, ndoa zenye afya na mazingira salama ya kulea watoto. Kwa bahati mbaya, msingi huu muhimu wa ustawi wa jamii haupewi uzito unaostahili.
Nilipokuwa Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani, nilishawahi kulizungumzia suala hili katika hotuba yangu, lakini ninaamini ujumbe wangu haukueleweka ipasavyo.
Leo, tunashuhudia dalili nyingi za kuvunjika kwa mifumo ya familia, migogoro ya ndoa, ukatili wa majumbani na madhara yake kwa watoto na jamii kwa ujumla. Haya si mambo ya kuyatazama kama matatizo ya watu binafsi pekee, ni changamoto zinazohitaji tafakari na hatua za kitaifa.
Lazima tufanye jambo sasa. Tuwekeze katika elimu ya ndoa na malezi, ushauri nasaha, ulinzi dhidi ya ukatili wa majumbani na mifumo ya kuwasaidia wanandoa na familia zilizo kwenye migogoro.
Taifa salama hujengwa kuanzia nyumbani. Tukipuuzia afya ya familia leo, tutalipa gharama kubwa kesho. Ni wakati wa kulitazama suala hili kama sehemu muhimu ya ajenda ya usalama na maendeleo ya Taifa.
Katika wakati huu mgumu, poleni sana familia ya Urassa kwa msiba huu mzito. Hata hivyo, ni muhimu kutofautisha kitendo cha mtu mmoja na ukoo mzima. Ukoo wa Kweka haujafanya kitendo hiki, Laurent Kweka ndiye anayepaswa kuwajibika kwa matendo yake binafsi. Tusihukumu ukoo mzima kwa kosa la mtu mmoja. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Nafikiri huyu muuaji si Mchaga, sivyo? Matatizo ya afya ya akili hayana kabila wala dini.
Wiki hii pekee, nimesikia na kuona taarifa za matukio zaidi ya matatu ya ukatili wa kutisha dhidi ya wanawake, yaliyosababisha vifo. Hata hivyo, matukio hayo hayajapewa uzito mkubwa katika mjadala wa umma, pengine kwa sababu wahusika si WACHAGA na hawakutumia bastola.
Ukatili hauna kabila. Mauaji hayana dini. Na uovu hauna kabila la kuuchukulia kama alama yake ya utambulisho.
Tusitumie kabila la mtuhumiwa mmoja kuwahukumu watu wote wa kabila lake, huku tukiyafumbia macho matukio yanayofanana yanapofanywa na watu wa makabila mengine. Kila maisha yaliyopotea yana thamani sawa, na kila muuaji anapaswa kuwajibishwa kwa matendo yake binafsi.
Haki isiwe na kabila, huruma isiwe na ubaguzi, na ukatili dhidi ya wanawake usiwe habari kubwa tu pale unapofanywa na mtu wa kabila fulani. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Natoa pole kwa familia zote zilizopoteza wapendwa wao katika ajali za Morogoro. Ni maumivu makubwa yasiyoweza kufutwa kwa maneno.
Lakini lazima tuseme ukweli, uzembe barabarani ni sawa na kuchezea maisha ya watu. Kupuuzia sheria, mwendo kasi na kutowajibika kwa madereva kunaweza kugeuza safari ya kawaida kuwa msiba wa taifa.
Tunahitaji hatua kali dhidi ya wanaokiuka sheria, usimamizi madhubuti na uwajibikaji bila upendeleo. Barabara si uwanja wa majaribio, na maisha ya watu si ya kubahatisha.
Uhai kwanza. Sheria zifuatwe. Uzembe usivumiliwe. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Bwana Msajili,
Biashara ya kuuza vinyonga ni ngumu sana! Mteja anataka kinyonga mweusi, unamkamata akiwa mweusi, lakini unapomfikisha kwa mteja, anabadilika na kuwa wa kijani! Mwishowe, mteja anamkataa kwa sababu si rangi aliyokuwa anaitaka.
CHADEMA si kinyonga wa kubadilisha rangi ili kukidhi matakwa ya CCM. Vivyo hivyo, kuwa na vyama vingi vya siasa hakumaanishi kuwa demokrasia imeimarika, hasa pale ambapo baadhi ya vyama vinatuhumiwa kuwa na misimamo inayolingana na matakwa ya CCM. Vyama vinavyodaiwa kuwa miradi ya CCM haviwezi kutumika kama kipimo pekee cha demokrasia nchini.
Bwana Msajili, ukiwa msajili wa vyama vingi vya siasa, jukumu lako si kuamua chama gani kinastahili kusifiwa kwa sababu kinakupendeza, bali kuhakikisha kila chama kinatendewa kwa haki sawa mbele ya sheria.
Msajili wa vyama vingi hapaswi kuwa dalali wa rangi za kisiasa.
Kukosa aibu ni jaribu baya sana katika maisha, hasa pale ambapo mtu anapopewa dhamana ya kusimamia haki, lakini kauli na matendo yake yanazua maswali ya heshima yake. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
It was also a pleasure meeting you, Mr Speaker.
House of Commons Speaker
@CommonsSpeaker
Great to meet @godbless_lema, @ChademaTZ2 former MP for Arusha, in the margins of @IPUparliament 153rd Assembly.
These parliamentary summits are a fantastic opportunity to hear perspectives from across the political spectrum and exchange views on representative democracy. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Bei ya mafuta inapanda Tanzania wakati soko la kimataifa bado liko kwenye mazingira yenye mabadiliko makubwa. Ni kweli gharama za kimataifa, usafirishaji na bima zinaathiri bei, lakini Serikali ina nafasi ya kutumia sera za kodi, tozo na ruzuku kwa muda maalum kupunguza mzigo wa dizeli bila kuvuruga mfumo wa bei.
Dizeli ni input muhimu katika usafirishaji, kilimo na uzalishaji. Kuipunguza bei kwa hatua iliyolengwa kunaweza kupunguza gharama za uzalishaji na usafirishaji, kupunguza pressure ya mfumuko wa bei na kusaidia uchumi kwa ujumla. Suluhisho si kupuuza bei ya dunia, bali kusimamia vizuri gharama zinazoweza kudhibitiwa ndani ya mfumo wetu. -
Godbless E.J. Lema reposted
Chadema Tanzania
@ChademaTZ2
Tanzania’s Political Crisis and a Call for @IPUparliament Action.
Hon. John Mnyika, Secretary General of CHADEMAThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema reposted
#NIPENI_MAUA_YANGU💐
@Roma_Mkatoliki
Mtu anateuliwa kuwa DC
Vyombo vya habari vinaandika na kutangaza kwa kusema
flani AULA uDC Meatu
flani AULA uDC Arumeru
Hapo kwenye mindset ya AULA ndipo panaposababisha matatizo yote haya!!
Jamii inayochukulia uteuzi wa uongozi ni kuula,kutoboa,kupewa shavu,kupiga mshindo….tunatengeneza wapigaji wa miamala na sio wawajibikaji wa raia!! -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Thamani ya maisha yako haipimwi kwa maua yatakayowekwa kaburini, bali kwa hisia za watu utakapoondoka, ikiwa watalia kwa maumivu au kushangilia kwa furaha. Upendo, unyenyekevu na huruma ktk maisha ni msingi bora ktk maisha. Hapa Duniani hakuna makazi ya mtu yoyote, ni mbwembwe tu bila ufahamu sahihi. Kugundua hill sio elimu bali ni neema.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Wewe Chalamila, kuna wakati ninapokusikia ukizungumza sana kuhusu usafi, huwa najiuliza moyoni, labda tatizo si uchafu ulioko mitaani tu; labda kuna “uchafu” mwingine wa kiuongozi unaohitaji kusafishwa.
Wewe ni RC wa Dar es Salaam ambaye haonekani kuelewa kwa kina changamoto za msingi za jiji. Hili ni jambo la hatari. Dar es Salaam haihitaji RC anayejua kuzungumzia usafi pekee, inahitaji kiongozi anayeelewa mipango miji, drainage system, sewage system, maji, barabara na miundombinu inayokwenda sambamba na kasi ya ukuaji wa jiji.
Kwa mfano, angalia Masaki na Oysterbay. Maeneo haya yanakua kwa kasi kubwa, yanajengwa majengo ya ghorofa nyingi na yanaendelea kuhudumia watu wengi zaidi, lakini miundombinu ya msingi haijakua kutoka kwenye mipango miji kabla ya uhuru. Mabomba ya inch mbili yaliyowahi kuhudumia nyumba ndogo leo yanatarajiwa kuhudumia majengo ya ghorofa yenye mamia ya wakazi. Hii ni changamoto kubwa ya mipango na uongozi.
Kwa hiyo, unapozungumzia usafi, ni muhimu pia ujiulize, ni nani anayesafisha mfumo wa mipango miji unaoruhusu jiji kukua bila miundombinu inayolingana na ukuaji huo?
Dar es Salaam haiwezi kuwa jiji bora kwa kusafisha mitaa pekee. Linahitaji uongozi wenye maono, unaoweza kuona miaka 100–200 ijayo na kuandaa miundombinu kabla matatizo hayajawa makubwa.
Pengine uchafu wa Dar ni wewe na uongozi wako, na sio chupa za plastiki barabarani. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Mahakama inapopuuzia haki, madhara yake hayabaki ndani ya ukumbi wa mahakama, huenea katika jamii na kuharibu imani ya watu kwa mfumo wa sheria, kwani ni afadhali wenye hatia elfu moja waachiwe huru kuliko mtu mmoja asiye na hatia aadhibiwe.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
*MANENO YA MWISHO YA TUNDU LISU, leo:*
“Waheshimiwa Majaji miaka 60 iliyopita, kuna mhaini mwingine alifungwa kifungo cha maisha nchini Afrika Kusini, kabla hajahukumiwa alisema maneno yafuatayo ambayo naomba kuyafanya yawe maneno yangu leo, "I have fought against white domination and I have fought against blood domination, and my Lords, it is an ideal I am prepared to die for"
Nimepigania haki na demokrasia kwa sehemu kubwa, kuwa na nchi ya demokrasia, imekuwa ni ideal kwa nchi yangu, msimamo huo umenigharimu sana, umeniletea madhira mengi sana, msimamo huo kwa siku zilizobaki kwa maisha yangu ni msimamo ambao nitaendelea kuusimamia, na kama ikibidi kufa ni msimamo ambao nipo tayari kufa.
Namalziia kwa neno moja:
waheshimiwa majaji, kosa la uhaini halina kosa dogo, halina kosa ambalo ukishindwa kuthibitisha uhaini unahukumu kwa kosa dogo, it is either death sentence or acquittal, hakuna kakosa kadogo kwenye uhaini, waheshimiwa majaji, mzigo ambao mmekabidhiwa mabegani mwenu ni
kuamua kama kwa ushahdii huu kuna uhaini, kama mkiona kuna uhaini you should not hesitate to convict and punish me appropriately, do not hesitate, msiogope, kama mtaona kuna uhaini msiogope kunihukumu, kama mkiona hamna uhaini
msiogope kuniachia huru.
You have God before you, msije mkaletewa maneno kuna kosa dogo, hakuna kosa dogo kwenye uhaini, if the evidence doesn't fit— acquit, huo ni mzigo ambao ni wa kwenu peke yenu waheshimiwa majaji. Nimemaliza”
Tundu Antiphas Lissu, September 28, 2026. Mahakama Kuu, Dar. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
-
Godbless E.J. Lema reposted
Kenya Ports Authority PLC
@Kenya_Ports
As the country prepares for the development of the Ksh 2 trillion Dangote East Africa Refinery project, the Port of Lamu welcomed MV Da Yang carrying heavy construction materials that will be utilized in the project.
Laden with 2,930 metric tons of heavy machinery, the arrival of MV Da Yang sets the stage for the anticipated groundbreaking ceremony for the construction of the first ever oil refinery north of Kenya planned for next week.
The refinery will process crude oil from Lokichar in Turkana County, and other parts of East and southern Africa and beyond, before supplying refined petroleum products to regional markets.
The port of Lamu will play a central role through supporting marine operations and handling petroleum tankers thereby boosting the Port’s operations.
Kenya Ports Authority PLC Chief Executive Officer Captain William Ruto welcomed the maiden vessel and successfully brought it alongside before presenting a certificate of first call and a plaque to the vessel’s master Captain Wang Shengli.
Captain Ruto said the vessel’s arrival was significant to the refinery project and demonstrated the Government’s commitment to ensuring its success.
“The arrival of this vessel is very critical and shows the Government’s commitment to ensuring this project succeeds. It will be a game changer for the entire region,” said Captain Ruto.
He assured shipping partners and customers that the Port of Lamu is fully prepared to handle current and future cargo volumes, with KPA committed to efficient vessel turnaround, seamless cargo operations and customer-focused services that meet international standards. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Masela sikilizeni 😂😂. Pia kumbukeni, huyu ndiye yule jamaa aliyetongozwa na demu, akaenda Polisi 😭. So kusema ukweli kwake si breaking news. Hapa kasema ukweli kabisa.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Nafikiri kasema ukweli, kwani sisi sote ni mashuhuda wa jinsi vyombo vya ulinzi na usalama vinavyotumika vibaya na CCM. Apongezwe kwa kuwa mkweli.
Hatari ninayoiona ni hii, tusipoamka na kusimama kwa umoja kama Taifa, siku moja hata wake zetu wanaweza kuwa “mali ya CCM”au kubinafsishwa kwa WAWEKEZAJI. Impunity ya sasa ni ya kiwango cha juu sana. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Kushindana na ubaya kuna maana zaidi pale wema unapohubiriwa kwa sauti kubwa kuliko ubaya. Tusiupe ubaya jukwaa kubwa kwa kana kwamba una nguvu kuliko wema au kuna mashindano kati ya wema na ubaya. Wema unapoongezeka, ubaya hupoteza nafasi kabisa.
Niliwahi kuombwa kusimamia harusi ya rafiki yangu. Nikampa sharti moja, sherehe ifanyike mchana na watoto wadogo waruhusiwe kuhudhuria. Anyway, mpaka leo hii , ukinikaribisha harusini kama wanangu wapo nitakuja nao hata kama kadi imeandikwa “
watoto tunawapenda lakini wabaki nyumbani”
Mchungaji aliniuliza, “Lema, umefikiria nini?”
Nilimweleza kuwa watoto wanahitaji kuona process ya ndoa na familia nzuri ili wajenge taswira chanya na kuzitamani tangu wakiwa wadogo. Mtoto akiona heshima, upendo na furaha ndani ya familia, hujifunza kuwa hayo ni maisha yenye thamani ktk siku za usoni.
Hapo ndipo tunapopaswa kutafakari kuhusu “normalization.” Tunapousema ubaya kwa kuutangaza, kuujadili na kuuonyesha mara kwa mara, bila kukusudia tunaweza kuufanya uanze kuonekana wa kawaida.
Ndiyo maana si kila ushindi dhidi ya ubaya unahitaji kelele zaidi. Wakati mwingine tunahitaji kuupa wema jukwaa kubwa zaidi.
Kama tunataka watoto wapende maisha yenye thamani, tuwaonyeshe maisha hayo. Kama tunataka waheshimu maisha ya adabu na familia, tuwaonyeshe familia zenye heshima. Kama tunataka wachague wema, waone wema ukiishi kupitia sisi.
Tusifanye ubaya kuwa maarufu kwa kuutangaza, tufanye wema kuwa maarufu kwa kuuishi. Wema usibaki kuwa hoja, uwe mfano.
Usibaki kuwa mahubiri, uwe maisha.
Mindset Matters. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Kuna tofauti kubwa kati ya viongozi wa dini na watumishi wa Mungu. Katika hali ambayo Lissu anauliza, “Nchimbi yuko wapi?” wakati mahali alipo Nchimbi hakujulikani, ni muhimu sasa sehemu kubwa ya viongozi wa dini wageuke kuwa watumishi wa Mungu.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Nafikiri, au labda naota, kwamba hata MAJAJI wanaweza kuwa wanafurahia kusikiliza hoja na mawasilisho ya M/kiti Lissu. Natamani kesi hii ingekuwa ikirushwa moja kwa moja, kwa sababu kile kinachoendelea hapa ni somo kubwa sana kuhusu sheria, ujenzi wa hoja, ujasiri, na namna ya kusimamia kile unachokiamini.
Kuwepo hapa mwenyewe ni somo kubwa. Kuna mambo ambayo huwezi kuyaelewa kikamilifu kwa kuyasikia au kuyasoma tu, wakati mwingine ni lazima uwepo, uyaone na uyasikie mwenyewe.
Kwa Mahakama, wito wangu ni mmoja tu, HAKI ITENDEKE.
Kila hoja isikilizwe kwa umakini na kwa haki, kila ushahidi upimwe kwa usawa na kwa mujibu wa sheria, na hatimaye, uamuzi utolewe kwa kuzingatia sheria, ushahidi na misingi ya haki. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Ktk submission inayoendelea kwenye kesi ya Uhaini ya Mhe. Lissu, kwa ninavyoona na kufikiri, Serikali haina njia ya kushinda kesi hii kwa hoja na ushahidi uliowasilishwa. Haiwezekani Majaji wafumbe macho mbele ya mapungufu makubwa sana ya kisheria na hoja zinazowekwa sana wazi katika hoja za majumuisho upande wa Utetezi.
Sio aibu hata kidogo haki kushinda. Aibu na fedheha itakuwa pale ambapo dhuluma na uonevu vitaendelea kuwa na nafasi katika Taifa letu. Hili si jaribu kubwa, litakuwa kubwa tu kama uoga utapewa nafasi mbele ya haki na kweli.
Sasa ni wakati wa Mahakama kusimama upande wa sheria, haki na kweli. Heshima ya Mahakama inalindwa si kwa maneno, bali kwa uamuzi unaosimamia haki bila hofu wala upendeleo.
Taifa linaitazama Mahakama na historia itaandika uamuzi huu. -
Godbless E.J. Lema reposted
Chadema Tanzania
@ChademaTZ2
TAARIFA KWA UMMA
-
Godbless E.J. Lema reposted
The Chanzo
@TheChanzo
Waziri Mkuu: Ili watu watabasamu, haki na uwajibikaji lazima zisisitizwe
Akizungumza katika mkutano wa kufunga makambi ya ulezi ya kanisa la Adventista-Kinyerezi leo Septemba 19, 2026, Waziri Mkuu Mwigulu Nchemba amesisitiza ili Watanzania watabasamu, haki na uwajibikaji vinabidi kuwa kipaumbele.
"Leo hii Mheshimiwa Rais aliposema anahitaji kuwaachia Watanzania anapomaliza awamu yake hii ya pili kwamba anataka aondoke asiwaachie tu miundombinu, majengo na barabara, anataka awaachie na tabasamu, mimi kama msimamizi wa shughuli za serikali na ambaye katiba inanielekeza jambo lolote ambalo Mheshimiwa Rais anataka lielekezwe, Waziri Mkuu atatekeleza ama atasababisha litekelezwe, nikajua ili watu wapate tabasamu kuna mambo mawili lazima yasisitizwe: haki na uwajibikaji, haki na uwajibikaji."This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
#live: MWANASHERIA MKUU WA CHADEMA ANAFUNGUKA MAZITO MUDA HUU www.youtube.com/live/gyJWwTV01JU via @YouTube
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Mkutano wangu na waandishi wa habari niliokuwa nifanye katika Hotel ya Golden Tulip nimeuahirisha.
Nimesikiliza hotuba za Makamu Mwenyekiti na Katibu Mkuu. Wameeleza vizuri kuhusu uvumi na upotoshaji uliokuwa ukifanyika juu yangu na misimamo juu ya chama chetu.
Nimedumu katika mapambano haya kwa zaidi ya miaka 22. Nimeenda lock-up zaidi ya mara 50. Nimezunguka nchi hii usiku na zaidi ya mara tatu. Nimewahi kuwa magerezani mara kadhaa, nimekoswa kuuawa zaidi ya mara tatu, na nimewahi kukimbia nchi.
Katika yote haya, nimekuwa nikitoa sadaka kubwa kwa ajili ya mapambano haya, ikiwemo ku-sacrifice familia yangu mara zote.
Kazi hii kwangu si ajira, si cheo, wala si njia ya kujitafutia maslahi. Ni huduma. Ni wito. Ni kama injili ninayoamini na kuitumikia.
Kwa hiyo, siwezi kuruhusu uvumi, upotoshaji au tafsiri za watu kuniondoa kwenye misingi ambayo nimeisimamia kwa zaidi ya miongo miwili.
Nitakuwa kwenye mapambano haya kwa imani, ujasiri na dhamira njema siku zote. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Kesho saa sita mchana nitakuwa na mkutano na waandishi wa habari katika Hotel ya Golden Tulip.
Waandishi wa habari wote mnakaribishwa.
Karibuni sana. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
NINAENDELEA KUTAZAMA BILA HOFU.
Kwanza, Kamati Kuu ya CHADEMA, mahali popote, haijawahi kujadili AJENDA ya Maridhiano tangu Oktoba 29 mpaka sasa.
Pili, hakuna watu wawili, watatu au kikundi cha watu ambao wamewahi kwenda kwa Makamu Wenyeviti, Katibu Mkuu au Manaibu Katibu Wakuu kuwaomba tufanye maridhiano.
Tatu, azimio la kukataa maridhiano lililosomwa na MMB , John Heche, pamoja na kutaka msuluhishi huru wa kimataifa, lilifanywa na KAMATI NDOGO YA KAMATI KUU, iliyokuwa na wajumbe wafuatao , Heche, Mnyika, Manaibu Katibu Wakuu wote wawili, Sugu, Boni Yai, Lema na Susan Lyimo.
Kwa hiyo, mtu au kikundi chochote kinachotaka kuugawa msimamo huu wa CHAMA na kuuweka kwenye makundi ya watu fulani, ni mzushi na mwongo. Msimamo huu si wa mtu mmoja. Ni msimamo wa CHAMA.
Na mtu au kikundi chochote kinachotaka kuaminisha umma kwamba wajumbe hao wamegeuka au kwamba msimamo huu ni wa baadhi ya watu na si wengine, kinafanya kazi ya kutugawa kwa uongo.
Ukweli unabaki kuwa ukweli, hata kama kuna watu wanaotaka kuupindisha.
Kuhusu familia yangu, watoto wangu wawili pamoja na mke wangu walikuja Tanzania baada ya takribani miaka sita wakiwa nje ya nchi, kwa ajili ya kusalimia kwa mwezi mmoja. Walifika tarehe 28/7/2026 na tayari walirudi nchini kwao Canada tarehe 3/9/2026.
Wito , wote wanaopigana na mimi vita vya uongo , wataanza kuadhibiwa na Mungu siku sio nyingi, kwani ninamjua Mungu ninayemuamini.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Nimeona matusi na sintofahamu nyingi mtandaoni baada ya kuchapisha ujumbe wa kutoa pole kwa Mama Samia, hasa niliponukuu salamu za pole za Mwenyekiti Lissu kutoka gerezani.
Kwa sisi jamii tunaodai kupigania uhuru wa maoni na demokrasia, hili linapaswa kutufikirisha. Kutofautiana kwa hoja hakuhitaji matusi, dhihaka wala chuki.
Lissu amekaa gerezani takribani mwaka mmoja na miezi sita, akikabiliwa na kesi ambayo sisi tunaamini ni ya kisiasa na isiyo na haki. Anafahamu yaliyompata na serikali iliyomweka mahabusu. Lakini alipofahamishwa kuhusu msiba wa mume wa Mama Samia, akiwa mbele ya mahakama, alitoa salamu zake za pole kwa wafiwa mara mbili.
Huu si unyonge. Hii ni hekima, utu na ukomavu wa kiwango cha juu.
Na si mara ya kwanza. Aliwahi pia kumtetea Sabaya katika kesi yake Moshi. Wengi tulishangaa, nami nilishangaa. Lakini nilipomuuliza baadaye, nilielewa kwamba kwake haki haichagui upande.
Hilo ndilo fundisho kubwa tunalopaswa kulibeba. Tunaweza kupinga serikali, kudai haki na kupigania demokrasia bila kujenga harakati zetu juu ya chuki na kisasi.
Lakini kama tunasema tunampenda Lissu, basi pale anaposema ana pumzi ya kuvumilia mateso na kukaa gerezani, sisi tunapaswa kuchukua kauli hiyo kama mwito wa ujasiri, si ruhusa ya kukaa kimya.
Kama tunaamini kesi hii si ya haki, basi viongozi tunanapaswa kuwaongoza wananchi katika hatua za amani, kisheria na kidemokrasia za kudai haki, pengine kwa njia ya maandamano. Sio kwenye keyboard tu na microphone.
Demokrasia inahitaji wananchi wanaothubutu kusimama kwa kile wanachoamini. Na kama siku moja tutapata nafasi ya kuongoza nchi hii, tusije tukarudia makosa tunayoyapinga leo. Lazima tutawala kwa haki, utu na dhamira njema.
Mimi nitasimama kwenye upendo, utu na haki siku zote ktk kazi hii. Anyway , hekima ya Lissu kutoa pole kwa Mama Samia was a top-class thinking. Inaonyesha kwamba hata unapoteseka, unaweza kuchagua utu, hata unapopinga, unaweza kukataa kisasi.
Wakati mwingine Mungu hataki umshinde adui yako kwa chuki, bali kwa upendo, hekima na maisha yenye ushuhuda kwamba uovu wake haukukushinda.
Mimi niko tayari kusimama kwa amani na kwa ujasiri. Katika hatua ya kupigania uhuru wa Lissu kuwa nje ya kuta za gereza na sio kusema ana pumzi ya kukaa jela hata maisha. Tuna watu wengi sana Chama hiki , pumzi yetu itoke mtandaoni , fikeni tu hata mahakamani kwa sasa na huku viongozi wakuu watusaidie kutafakari jambo muhimu la haki , sheria na amani.
“You don’t have to hate those who hurt you. Sometimes the greatest revenge is to rise above them with peace, dignity, and success.”
Thank you !! -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Kumpenda adui yako hakumaanishi kukubaliana na uovu wake, wala kusahau maumivu aliyokusababishia. Maana yake ni kukataa kuacha chuki ibadilishe moyo wako. Unaweza kusimamia ukweli, kudai haki na kupinga uovu, bila kugeuka kuwa mtu wa chuki. Huo ndio ushindi mkubwa. kumshinda adui bila kupoteza utu wako.
Thank you Mwenyekiti. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
M/kiti Lissu anakupa pole sana kwa kufiwa na mume wako kipenzi. Tukiwa mahakamani takribani mara mbili, amesisitiza salamu zake zikufikie pamoja na pole zake kwako, watoto na ndugu zako wote.
Lissu ni mtu mwenye upendo mkubwa kwa watu na anayesimamia haki. Ninaamini kama angekuwa nje ya gereza, angefika Unguja mwenyewe kutoa pole na faraja. Kwa bahati mbaya, akiwa bado yuko gerezani, hawezi kutoka na kufika mwenyewe kukupa pole katika kipindi hiki kigumu.
Nami nikupe pole sana kwa kumpoteza mume wako mpendwa. Jipe moyo na uimarishe imani yako katika tumaini la Mungu. Mungu awape nguvu, faraja na uvumilivu wewe, watoto na familia nzima.
Let’s Love Lead, Mama! Get Lissu out of the prison walls! -
Godbless E.J. Lema reposted
BBC News Swahili
@bbcswahili
Fuatilia hapa moja kwa moja kuhusu kinachoendelea Mahakamani kesi ya Lissu
www.bbc.com/swahili/live/cvn0n8gl61e5t -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Huyu Arifu vipi ? Nyie mnamuelewa kweli wajameni !!!
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
-
Godbless E.J. Lema reposted
BBC News Swahili
@bbcswahili
Brenda: Nguvu na mamlaka ni ya watu, hivyo ndio wanaofanya mabadiliko
www.bbc.com/swahili/live/cvn0n8gl61e5t?post=asset%3A84ec2… -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Pamoja na umuhimu mkubwa wa IBADA katika jamii, ni muhimu sana ujenzi wa nyumba za ibada katika maeneo ya makazi uzingatie usalama, mipango miji, faragha na utulivu wa maisha ya watu.
Si jambo la baraka, wala si kumpenda Mungu kujenga nyumba ya ibada kwa namna inayowasumbua, kuvuruga faragha au kuharibu utulivu wa majirani.
Ujenzi holela usiozingatia mipango miji ni hatari, na haupaswi kuhalalishwa kwa kisingizio cha dini au ibada.
Kumpenda Mungu ni pamoja na kuwajali na kuwaheshimu wengine. Haki ya mtu kuabudu haiwezi kuwa ruhusa ya kumnyang’anya mwingine haki ya kuishi kwa amani na utulivu.
Kwa hiyo, ni muhimu mamlaka husika kuhakikisha kila nyumba ya ibada inajengwa na kuendeshwa kwa kufuata sheria, mipango miji na viwango vya usalama.
Na jambo moja liwe la lazima, kila nyumba ya ibada inayotumia mifumo ya sauti iwe na SOUNDPROOF, ili ibada ifanyike kwa heshima bila kugeuka kuwa usumbufu kwa jamii inayozunguka.
IBADA ILETE AMANI, SI KUONDOA AMANI.
KUMPENDA MUNGU NI KUWAJALI WENGINE. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Nitakuwa na ziara ya mikutano katika mikoa ya Morogoro, Dodoma na Singida katika siku chache zijazo, nikitembelea maeneo ya majimbo yote yaliyokuwa yamebaki, kama ilivyokuwa imekusudiwa hapo mwanzo kabla ya mikutano kuzuiwa.
Kazi ya kukemea mapepo, upumbavu na kila aina ya uovu unaoendelea itafanyika kwa bidii, ujasiri na shauku kubwa.
CCM -Thank you for your attention.
GJL -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Kazi ya CCM ni ya Kipumbavu sana. Hakuna namna kwa upumbavu wa aina hii Nchi inaweza kuwa na ustawi na salama. Muda utaongea kwa sauti kubwa sana. Na kila mtu atajuta.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Unayeitwa Waziri mwenye dhamana ya kulinda raia na mali zao, unaweza kweli kuongea upumbavu kwa kiwango hiki na bado ukawa ofisini ? So sad.
Kwa kauli kama hii, hukupaswa kuwa ofisini hata kwa dakika moja. Dhamana ya kulinda maisha ya watu si mahali pa uzembe, dharau wala kauli zisizo na weledi. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Kuna usanii mkubwa unaendelea nao. Watu wasiojua kusoma alama za siasa wanaweza wasikuelewe. Acha mara moja. Nakuonya. Acha mara moja.
-
Godbless E.J. Lema reposted
Adv Omari Omari
@omari_manyama
LISSU: KITENDO CHA KUPINGA SERIKALI NI KOSA KISHERIA?
GOLUGWA: KUPINGA SERIKALI AU TAASISI SIO KOSA KISHERIA.
LISSU: WAELEZE MAJAJI MAANA YA NENO KUKINUKISHA.
GOLUGWA: KUKINUKISHA NI KUKIFANYA KITU KITOE HARUFU, HARUFU YA MARASHI, YAANI UNYUNYU, KUSABABISHA HARUFU ITOLEKE. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Kazi ya mawakili wa Serikali si kuhakikisha wanayemshitaki anafungwa kwa gharama yoyote. Kazi yao ni kuisaidia Mahakama kutenda haki kwa kiwango cha juu kabisa.
Kwa sababu nyuma ya kila kesi kuna maisha ya mtu, familia yake, watoto wake, kazi yake, heshima yake na kesho yake. Uamuzi usio wa haki hauishii kwenye karatasi ya Mahakama, unaweza kuvunja familia, na kuharibu maisha.
Ndiyo maana mkakati wa uonevu, chuki au kulazimisha ushindi si weledi wa sheria. Ni kugeuza mfumo wa haki kuwa chombo cha kuumiza watu.
Mawakili wa Serikali wanapaswa kuwa na uadilifu na kiu ya haki kuliko hata mawakili wa kujitegemea, kwa sababu hawasimamii mtu binafsi, wanasimamia Serikali na dhamana ya umma.
Haki si maneno ya kisheria. Haki ni maisha ya watu. Na Serikali inaposhindwa kulinda haki, inaweza kuharibu maisha ambayo ilipaswa kuyahifadhi. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Sijui kama Serikali inaona hatari hii. Mimi naiona. Tunapofanya “easy jobs” kama boda boda kuwa suluhisho kuu la ajira, tunaanza kupoteza skills muhimu zinazojenga taifa na uchumi.
Binafsi nina experience uhaba wa mafundi wazuri wa magari, plumbers, electricians, welders na mafundi ujenzi sana siku hizi. Tukiacha trend hii iendelee, kesho tunaweza kulazimika kuagiza mafundi kutoka nchi jirani kufanya kazi ambazo vijana wetu walipaswa kuwa wamefundishwa.
Wakati huo huo, boda boda zina gharama kubwa kwa taifa kupitia ajali, ulemavu, vifo na kupoteza nguvu kazi.
Tatizo si kijana kuendesha boda boda. Tatizo ni pale “easy option & cheap option” inapogeuzwa kuwa mfumo wa maisha, huku technical skills zikiachwa nyuma.
Serikali ibadili mwelekeo sasa, iwekeze kwa nguvu kwenye vocational training, apprenticeships na technical skills zenye tija na kipato.
Tusije tukawa na vijana wengi wanaotafuta ku-survive leo, lakini kesho tukakosa watu wa kujenga, kutengeneza na kuendesha uchumi wa nchi. -
Godbless E.J. Lema reposted
Adv Omari Omari
@omari_manyama
KATUGA: ULIsEMA UNA AKILI NYINGI, SASA NIKUULIZE SWALI...
MNYIKA: NILICHOSEMA NI KWAMBA NINA AKILI NYINGI KULIKO WEWE NA MABOSS ZAKO. SIO KWAMBA NINA AKILI KULIKO WATU WOTE DUNIANI. NI MUHIMU UELEWE: NINA AKILI NYINGI KULIKO WEWE, KATUGA, NA MABOSS ZAKO. -
Godbless E.J. Lema reposted
John Pambalu
@John_Pambalu
Mwambieni Katuga tulipokuwa Bavicha, tulipokuwa ofisini kwetu pale ufipa tukiona gari yake tu tunaambiana "The Moving encyclopedia" amefika. 😅😅😅 Katuga atakasirika mpaka atafurahi, huyo ndiyo J.J
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Kwani kuna nini Mangi ? mbona kama hii kitu mna push sana, au kuna kitu unataka ku justify ? Easy Bro!!
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
IGP, mantiki gani hii ? Mnamkamata mtu, hamtoi taarifa ya wazi alipo wala sababu ya kumshikilia, mnaacha hofu na tension isambae kila kona, halafu baadaye mnatokea kusema, “Ndiyo, sisi tunamshikilia.”
Hii ni calculus gani? Inasaidia nini kwa Nchi zaidi ya kuongeza taharuki, kuvuruga imani ya wananchi na kulitia aibu Jeshi la Polisi ?
Jeshi la Polisi linapaswa kutuliza hofu, si kuizalisha. Linapaswa kujenga imani, si kuacha wananchi wabahatisha hatma ya mtu aliyekamatwa.
Kama mtu amekamatwa kihalali, semeni yuko wapi, kwa kosa gani na hatua gani za kisheria zinaendelea. Usiri usio na sababu huzaa mashaka, na mashaka yakiachwa yakue, gharama yake ni kubwa sana kwa Taifa. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Tunaishi katika zama ambazo watu wanajivunia mambo ambayo walipaswa kuyaonea aibu.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Leo, Godlisten Malisa alikuwa akiingia nchini kupitia mpaka wa Namanga. Alishikiliwa na Uhamiaji kwa saa kadhaa, na kisha baadaye akachukuliwa na Polisi. Mpaka sasa, hata Wakili wake, Dickson Matata, hajui alikopelekwa. Akiwa Namanga, Godlisten alinipigia simu mara kadhaa na kunieleza mambo aliyokuwa akikabiliana nayo. Baada ya kuchukuliwa na Polisi, mawasiliano yakakatika.
Hili si jambo la kawaida, wala si jambo la kuchukuliwa kirahisi. Serikali haiwezi kumkamata mtu, ikamchukua mahali pasipojulikana, halafu ikanyamaza kuhusu alipo. Hata kama kuna tuhuma au uchunguzi wowote unaomhusu, sheria inamtaka mtu huyo ashughulikiwe kwa taratibu zinazotambulika na haki zake zilindwe. Godlisten Malisa yuko wapi? Amepelekwa kituo gani cha Polisi? Kwa kosa gani? Na kwa nini wakili wake hajui alipo?
Haki za msingi za mtu haziwezi kusimamishwa kwa sababu tu ameshikwa na vyombo vya dola. Mamlaka si ruhusa ya kutowesha watu. Serikali iwajibike na itoe majibu sasa. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Usichimbe shimo la dhambi kwa ajili ya mwingine, kwa sababu unaweza kulichimba kwa kina kiasi kwamba siku likikumeza, hakuna wa kukuokoa.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Kauli ya Jaji Mkuu kwamba watumishi wasiwe wanaharakati wa haki ni fedheha kubwa kwa Mahakama na Taifa.
Haki si uanaharakati. Haki ni msingi wa utumishi. Mtumishi wa anapopaswa kuisimamia haki, hawezi kuambiwa asiwe na msimamo juu ya haki.
Tatizo si mtumishi kuwa mwanaharakati wa haki, tatizo ni pale haki inapogeuzwa kuwa jambo la kisiasa au tishio kwa mfumo.
Mahakama yenye nguvu haiogopi watu wanaotetea na kupigania haki, bali inapaswa kuwa mstari wa kwanza kuilinda. -
Godbless E.J. Lema reposted
Zacharia Thomas Obad
@ZachariaObad
Lissu: matendo hayo ya ugaidi yalitokea na kesi ikaishaje ?
Mnyika : matendo ya ugaidi hayakutokea na mwendesha mashitaka alifuta kesi mwaka 2022. Mtuhumiwa wa ugaidi akaonekana Ikulu na Rais siku hiyo hiyo. Kutoka kuwa mtuhumiwa wa ugaidi hadi kuonekana mapokezi ya Ikulu. 🤣 -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
-
Godbless E.J. Lema reposted
John Pambalu
@John_Pambalu
"Niliwahi kumsikia Mwalimu Nyerere akisema vijana wanapaswa kuwa waasi dhidi ya mifumo kandamizi lakini sikuwahi kusikia amekamatwa kwa kauli hiyo" John Mnyika mahakamani leo.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Nilikuwa nateketea kwa moto wa ukandamizaji, lakini Serikali ikaja kunilaumu kwa harufu ya majivu, kana kwamba mimi ndiye niliyeanzisha moto.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Albert Einstein alifariki mwaka 1955 akiwa na miaka 76, lakini maneno yake bado yanaumiza kwa ukweli wake,
“Kuwa na akili wakati mwingine ni laana. Unaielewa mchezo, unaona uongo, na unatambua mienendo inavyoendelea, lakini bado unalazimika kujifanya mjinga ili uweze kuishi.” -
Godbless E.J. Lema reposted
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Wewe umeomba kuombewa ? Wanasema haufiki July ukiwa hapo. Wana mgombea urais 2030 na PM. Wanasema timu yote iliyokuwa kule kwa kina Ronaldino lazima ipanguliwe. Wanasema kwanza hauna hela na hujui deal!! uwezo wako mkubwa kifedha ni kumchangia mtu laki moja ya msiba au send off 😂😂😂Bado siko nyumbani, msalimie sana,Madilu na Mkwe. Kesheni Mkiomba. Usiogope ni ndoto tu.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Demokrasia ya kweli haipimwi kwa namna serikali inavyowatendea watu wanaoiunga mkono, bali kwa namna inavyowatendea wale wanaoikosoa. Ukandamizaji wa kisiasa unaweza kuonekana kama njia ya kulinda usalama wa taifa kwa muda mfupi, lakini ukizalisha kukata tamaa na kutokuamini taasisi, unaweza kuwa unatengeneza hatari kubwa zaidi kwa taifa lenyewe.
That is dangerous. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Nyakati ngumu katika maisha zitakufundisha tofauti kubwa kati ya “kuwajua watu” na “kuwa na watu.” Kwa sababu si kila unayemjua ni wako, na si kila anayesema yuko nawe atasimama nawe wakati wa dhoruba.
Hili ni somo muhimu sana katika maisha, watu wengi watakujua wakati wa raha, lakini ni wachache watakaobaki nawe wakati wa majaribu. Nyakati ngumu hazibadilishi watu, bali zinakufunulia watu. -
Godbless E.J. Lema reposted
Martin Maranja Masese
@IAMartin_
Job Mrema: turudi kuhusu kupigwa risasi. Ulishawahi Kulalamika Polisi
Tundu Lissu anasimama kwa hasira sana..
Tundu Lissu: nililalamika nimepigwa risasi nikiwa mbunge mchana kweupe katika makazi ya viongozi ikiwemo spika unataka kusema hawajui?
Job Mrema; mbona unakuwa mkali sasa?
Tundu Lissu; kwa sababu unanigusa katika jambo ambalo nina maumivu nalo makali sana ya kupigwa risasi 16
Job Mrema; basi sawa.. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Ukweli una gharama kubwa kuliko uongo, na haki mara nyingi huchukiwa kuliko dhuluma. Taifa haliwezi kwenda mbele kwa utamaduni unaomlinda mwongo, kumwadhibu mkweli, na kumfanya mwenye kudai haki aonekane kuwa tatizo. Huwezi kujenga maendeleo ya kweli juu ya msingi wa namna hii. Kila mtu atalipa gharama za kukaa kimya. Ni habari ya muda tu.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
MUNGU yuko kazini katika kiwango cha hali ya juu sana kuhusu Tanzania. Msiogope.
-
Godbless E.J. Lema reposted
Tito Magoti
@TitoMagoti
Katuga: Nakuheshimu kuna jambo sitaki kukwambia
Mhe Lissu: Unaniheshimu wapi? Acha umbea! Unataka kuninyonga unasema unaniheshimu? Msingenishtaki kwa uhaini kama unaniheshimu! -
Godbless E.J. Lema reposted
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Ukifikiri CCM hawawezi kufanya ujinga, ndipo wanapokuthibitishia kwamba bado hujui uwezo wao wa kufanya ujinga mkubwa zaidi.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
“ Nimejiuzulu kwa sababu naona Rais anataka mabadiliko “
DR EMMANUEL NCHIMBI. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Katika kesi inayomkabili Mheshimiwa Tundu Lissu, historia yake ya maisha, struggle yake, alikotoka na safari yake hadi alipofika si hadithi ya pembeni. Ni sehemu ya narrative ya utetezi inayolenga kuonesha character yake, misimamo yake, commitment yake kwa nchi na gharama kubwa alizolipa katika kusimamia demokrasia, haki na utawala wa sheria.
Hii si kesi ya kawaida. Ni kesi ambayo, ikiwa itamalizika kwa hukumu ya hatia, inaweza kuwa na adhabu ya kifo. Kwa mazingira hayo, kumtaka mshtakiwa aharakishe utetezi wake ni jambo linalopaswa kutazamwa kwa umakini mkubwa.
Hata kama utetezi wa Lissu utachukua mwaka mzima, huo si muda mrefu ukilinganisha na adhabu inayoweza kumpotezea mtu maisha yake milele.
Mahakama inapaswa kuwa na uvumilivu wa kutosha kuhakikisha kwamba kila jambo la msingi katika utetezi linasikilizwa. Ufanisi wa mahakama ni muhimu, lakini haki ni muhimu zaidi.
Kwa kesi yenye matokeo yasiyoweza kurekebishwa, hakuna muda unaoweza kuwa mrefu kuliko thamani ya maisha ya mtu.
Hakuna haraka inayopaswa kuwa kubwa kuliko haki. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Ni bahati mbaya sana , lakini wakati mwingine unamtazama mtu na kuwaza, pengine hapa, uzazi wa mpango ungekuwa msaada kwa taifa.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Haki inapopimwa kwa jina la mtu anayeshtakiwa badala ya ukweli wa jambo lenyewe, haki huwa imepoteza maana.
Muachieni Tundu Lissu, si kwa sababu ni Tundu Lissu, bali kwa sababu Tanzania haiwezi kujenga amani ya kudumu juu ya msingi wa dhuluma.
Serikali haionyeshi nguvu kwa kumshikilia mkosoaji wake, inaonyesha nguvu kwa kuwa na ujasiri wa kuiruhusu haki itawale. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Ukifikiri CCM hawawezi kufanya ujinga, ndipo wanapokuthibitishia kwamba bado hujui uwezo wao wa kufanya ujinga mkubwa zaidi.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Naogopa kutokuwa na imani, lakini kutokuwa na imani dhidi ya Serikali ya Tanzania kuhusu uwajibikaji wake juu ya haki si hofu wala kukosa matumaini, bali ni uelewa mzuri wa hali halisi na, kwa namna fulani, ni imani ya kweli. Msingi wa kutokujali haki unaojengwa leo ni tabia ambayo, siku moja, itamuangamiza kila mtu. Hakuna aliye salama, hata wale wanaoona ni sawa kuhukumu vibaya wengine leo.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Jamii inapovuka kiwango fulani cha mgawanyiko na chuki, uwezekano wa kutokea kwa jambo kama vita vya wenyewe kwa wenyewe huwa halisi.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Mahakama haipaswi kuhitaji ujasiri wa ajabu kusema kwamba Mkti Tundu Lissu hana kesi ya kujibu. Kwa ushahidi uliowasilishwa mahakamani, hakuna msingi wa kimantiki na kisheria wa kusema kwamba ushahidi huo umejenga kesi ya kujibu. Kilichoshuhudiwa mara nyingi ndani ya Mahakama kilionekana zaidi kama vituko kuliko ushahidi wenye mashiko unaoweza kumfanya mtu awe na kesi ya kujibu.
Katika mazingira kama haya, kusema kwamba Mkti Tundu Lissu hana kesi ya kujibu hakupaswi kuonekana kama ujasiri wa Mahakama. Inapaswa kuwa matokeo ya kawaida ya kutenda haki kwa kuzingatia sheria, ushahidi na dhamira njema.
Mahakama inapaswa kushinda jaribu hili, si kwa ajili ya CHADEMA, si kwa ajili ya Serikali, wala si kwa ajili ya Tundu Lissu. Ni kwa ajili ya Tanzania na mustakabali wake.
Haki inapowekwa mbele ya maslahi ya kisiasa, Taifa hushinda na Mahakama inayoaminika ni nuru ya Taifa. Na nuru hiyo haipaswi kuongozwa na hofu, shinikizo au maslahi ya upande wowote, bali na sheria, ushahidi na dhamira ya haki.
Kwa sababu mwisho wa yote, Mahakama inapolinda haki, hailindi mtu mmoja bali inalilinda Taifa. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Kuna watu wengi, hasa vijana, walioko katika magereza mbalimbali nchini kwa mashitaka ya ugaidi. Ni rahisi sana kuwasahau tunapokosa huruma na uelewa kama jamii. Majina yao si makubwa. Wengine ni wanafunzi ambao leo hawajui hata hatma ya elimu na maisha yao itakuwaje.
Lakini nyuma ya kila jina kuna mwanadamu, familia, ndoto na maisha yanayosubiri kuendelea.Tusiruhusu muda na ukimya viwafute kwenye fikra zetu. Tuendelee kuwakumbuka, kuwauliza, na kudai kwamba haki itendeke kwa kila mmoja wao.
Kwa sababu tukiwasaau wale walioko nyuma ya magereza ,tutakuwa tunapoteza kitu muhimu sana ndani yetu kama jamii.
Na tukiwasaau kabisa, tofauti yetu na wale tuliowapinga kwa kuwanyima wengine haki itakuwa nini?
FIKRA zetu zinapaswa kuwa juu yao. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Hivi viwanja vidogo vidogo vinavyojengwa hapa Arusha kwa ajili ya ku support AFCON vina sura ya deal deal hivi!
Hakuna eneo ambalo mara nyingi linahitaji uangalizi mkubwa wa fedha za umma kama sekta ya ujenzi. Ndiyo maana najiuliza, kama hitaji lilikuwa ni kuongeza viwanja, kwa nini Serikali isingewekeza na kuviimarisha viwanja vya shule vilivyopo hapa Jijini Arusha na maeneo ya nje ya mji ?
Badala yake, tunaona ujenzi mpya kila kona. Swali ni, hii ni mipango mizuri ya miundombinu au kuna maswali mazito ya matumizi ya fedha za umma yanayohitaji majibu?
Kuna mambo mengi yanayohitaji uwazi hapa. Na kama kuna uchafu wowote unaoendelea, si ajabu siku moja baadhi ya watu wakajikuta wanatoa maelezo mbele ya vyombo vya sheria.
AFCON iache legacy ya maendeleo, si legacy ya deals. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Kutafuta haki si kiburi. Ujasiri wa kuitafuta haki si uadui.
Na kumwachia Mkt. Lissu si kushindwa. Kinyume chake, huenda ukawa ni ushindi mkubwa wa Taifa na hasa kwenu ninyi Serikali.
Wakati mwingine, busara si kushikilia mtu kwa nguvu. Busara ni kutambua wakati wa kumwachia. Nchi haiwezi kujengwa kwa visasi au kwa kutafuta nani ameshinda na nani ameshindwa.
Msilifanye suala hili kuwa personal. Kesi hii ni kubwa kuliko mtu mmoja, chama kimoja au Serikali ya wakati mmoja. Inahusu haki, utawala wa sheria, amani na mustakabali wa nchi yetu.
Kataeni ushauri wa wahafidhina wanaowaambia kuwa kumwachia Lissu ni udhaifu. Wakati mwingine, uamuzi wa busara unaohitaji ujasiri zaidi ni ule wa kuachilia kuliko kushikilia.
Muwe wakubwa kuliko hasira, wakubwa kuliko visasi, na wakubwa kuliko ushindani wa kisiasa. Mumwachie Mkt. Lissu. Msiogope, kwa sababu tu mtatafsiriwa kama mmelegea. Kuna nyakati ambazo kumwachia mmoja ni kuifungua nchi nzima. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Check out Ndambo's video! #tiktok vt.tiktok.com/ZS4vrnkr5/
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Nimeshituka - Tufanye UTAFITI ZAIDI.
Source: JamiiForums Tanzania share.google/JWc9CzmjQIX7aNpIP -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Shahidi Amini Mahamba ameanza kwa kukana maelezo yake ya Shahidi, lakini baada ya kudodoswa ameamua kuyakubali, na Lissu a-impeach credit yake kwa kumuomba maelezo yake mwenyewe aliyokataa kuwa hakuwahi kuandika.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Tanzania kushuka nafasi 20 kwenye Global Peace Index si takwimu ya kupuuzwa. Hii si suala la sifa tu, ni suala la hadhi ya nchi, imani ya wawekezaji na gharama ya mtaji. Country risk ikipanda, risk premium hupanda na mwisho wake mwananchi analipa kupitia riba kubwa, mikopo ghali na fursa chache. Uchumi kukua bila amani, utulivu na taasisi imara si ushindi wa kudumu.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Nchi hii karibu kila kiongozi ana motorcade! Huu sasa siyo tena utaratibu wa kawaida, ni uhuni wa hali ya juu katika uvunjaji wa sheria za nchi. Barabara za wananchi zinageuzwa njia za misafara binafsi, sheria zinawekwa pembeni, na mamlaka zinaonekana kushangilia.
Kama kila mtu anahitaji motorcade ili ajione muhimu, basi tunahitaji kuuliza, nani anailinda sheria dhidi ya wanaoivunja kwa jina la mamlaka? -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Hakustahili huu unyama hata kidogo. Ukosoaji wake na utoaji wa maoni ni wa kawaida. Lakini kapigwa na kudhalilishwa kwa kiwango hiki.
Kuna hasira kali sana ndani yake. Amekubali na kuridhia kupigwa picha na kuirusha huku sehemu zake za siri (matako) zikiwa uchi? Tipping point.
Hii hasira ni pando linalopanda kisasi kwa jamii yote katika siku si nyingi? Kila mtu atapoteza amani na furaha. Wakati utasema.
Nani kafanya unyama huu? Kundi gani? Kwa manufaa gani? Na nani anafuata? Na maumivu haya yanaweza kuvumiliwa mpaka lini?
Haya ni maswali ya msingi ya kujiuliza, hasa zaidi wana CCM. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Jana nilitoka Moshi saa 12:00 jioni kuelekea Arusha. Safari ambayo ilipaswa kuwa ya kawaida ikageuka kuwa ya kuvumilia. Nilifika Arusha saa 3:30 usiku.
Kinachokatisha tamaa si hata ukarabati wenyewe, bali diversion road. TANROADS wameshindwa kabisa kuandaa njia mbadala inayofaa wakati ujenzi unaendelea. Foleni, vumbi na usumbufu ni wa kiwango cha juu, huku kasi ya ukarabati ikiwa ya kusuasua.
Ukiona mwendo wa mradi huu, unaweza kudhani fedha zake zinatolewa kwenye VICOBA badala ya bajeti ya maendeleo. Wananchi wanastahili barabara bora na utekelezaji wenye kasi inayoendana na umuhimu wa mradi wa ukarabati. SHAME !!! -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Bwana Kitila Mkumbo!!
Taifa halifi kwanza kwa kukosa rasilimali, hufa pale watu wake wanapoanza kuogopa kutumia akili zao.
Kuna tofauti kubwa kati ya elimu na akili. Elimu ni zao la akili. Kabla ya kuwepo shule, vitabu na vyuo, kulikuwepo akili iliyouliza maswali, ikafanya uchunguzi na kuumba maarifa. Ndiyo maana jamii inayoheshimu elimu lakini inaadhibu fikra huru, hujenga wasomi lakini si wenye hekima.
Hatari kubwa ya wakati wetu si ukosefu wa elimu, bali ni pale kufikiri kwa kina kunapoonekana kuwa kosa, na ujinga unapoonekana kuwa salama. Siku ambayo watu wataogopa kusema ukweli wanaouona kwa sababu ya hofu, siku hiyo taifa litakuwa limeanza kupoteza uhuru wake wa ndani, hata kama bendera yake bado inapepea.
Na taifa haliishi peke yake. Heshima ya taifa mbele ya mataifa mengine ni mtaji usioonekana, lakini wenye thamani kubwa kuliko mali nyingi zinazoonekana. Ndiyo maana mataifa huwekeza katika diplomasia, hujenga uaminifu na hulinda taswira yao kwa uangalifu mkubwa. Ni rahisi kubomoa sifa ya taifa kwa kauli moja, lakini inaweza kuchukua miaka mingi kuijenga upya.
Mahusiano ya kimataifa si mali ya serikali pekee, ni urithi wa kila raia. Ndani yake kuna biashara, uwekezaji, elimu, utalii, ajira na ndoto za mamilioni ya watu. Kauli inayodhoofisha hadhi ya taifa haimuumizi mtawala pekee, humuumiza mfanyabiashara, mwanafunzi, mkulima, mwekezaji na kijana anayesubiri nafasi yake duniani.
Pia , tunapaswa kukumbuka kuwa sehemu kubwa ya fedha za kigeni zinazoingia nchini hutegemea imani ya dunia kwa Tanzania. Wageni wengi wanaotembelea nchi yetu wanatoka Marekani, Ulaya na mataifa mengine yanayotuangalia kupitia taswira tunayoiunda kila siku kwa maneno na matendo yetu.
Hekima ya kweli si kusema kila unachoweza kusema, ni kujua athari ya kila neno kabla halijatamkwa. Kwa sababu mwisho wa yote, maneno hujenga historia, na historia ndiyo huamua hatima ya vizazi.
Bwana Kitila , tafadhali usikatishe watu tamaa kusomesha watoto.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
-
Godbless E.J. Lema reposted
Baba Mwita
@BabaMwita
Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) kilikaa Julai 29. Siku hiyo hiyo Jeshi la Polisi linatoa taarifa 'KURUHUSU' mikutano! Julai 30, mahakama ya Rufani inatoa 'ushindi' kwa Lissu dhidi ya DPP, huku mama Kizimkazi akikutana na wanasiasa Ikulu. Julai 31, kesi ya uhaini ya Lissu inapangiwa tarehe.
Bado unataka ushahidi gani kuona kuwa DPP, Jeshi & mahakama wote wanapokea maelekezo & kuwa kesi ya TAL ni ya KISIASA! Bado unataka ushahidi wa chama KUSHIKA HATAMU! -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Mnaweza kuwafunga vijana, kuwapa watoto wa shule kesi za ugaidi na kueneza hofu, lakini historia haijawahi kushuhudia wazo la haki likishindwa na minyororo.
Mamlaka hupimwa si kwa uwezo wake wa kuadhibu, bali kwa hekima yake ya kusikiliza. Taifa lolote linapoanza kuogopa sauti za watoto wake, huanza vita na kesho yake yenyewe.
Nina wasiwasi kwamba siku wananchi watakapoacha kuogopa, hakuna ukuta, cheo wala mamlaka yatakayokuwa na kinga dhidi ya matokeo ya hasira iliyocheleweshwa.
Haki inaweza kuchelewa, lakini hofu haijawahi kuwa msingi wa amani ya kudumu. -
Godbless E.J. Lema reposted
Zacharia Thomas Obad
@ZachariaObad
Rafiki yangu @jacksonmnyawam2 yupo gerezani na ametengwa na watoto wake kwa sababu tu , yupo upande wa kupigania HAKI.
Watoto wake wanamuuliza mama yao, “Mummy, where is our lovely daddy?"
Mama replies, "Your daddy is on safari.He will be coming back soon."
No hate No Fear -
Godbless E.J. Lema reposted
Jebra Kambole
@Advocate_Jebra
Watu wanapiga kelele wanasema watanzania tumuunge mkono Nchimbi kwenye kudai katiba mpya, kwanini wasimwambie Nchimbi atuunge mkono sisi?
Maana yeye ametukuta tuko kwenye mapambano kitambo! -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
TUENDELEENI NA TONE TONE WAJAMENI. MPESA 0744446969
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Gaidi ? Kweli ?
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
WATUMISHI WA SERIKALI, SEKTA BINAFSI NA UMMA.
Nafahamu tupo mwisho wa mwezi, kipindi ambacho wengi hupokea mishahara na mapato yao. Tunaomba kwa unyenyekevu muwe sehemu ya mabadiliko ya Taifa letu.
Mchango wako wa Tone Tone kwa CHADEMA ni muhimu sana. Hakuna mchango mdogo unapolenga kujenga mustakabali bora wa nchi yetu. Tumia njia yoyote iliyo salama na rahisi kutuma mchango wako. Pamoja, tunaweza kufanya makubwa.
Mungu awabariki sana. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Huyu mtoto ni Team Nchimbi naona kete inapangwa vizuri. maana kampiga shoti kali sana Mkti wake Taifa Mama Samia. Nchimbi anasema ameongea na Mama
Samia na yuko tiyari kwa Katiba Mpya , hawa watoto wanatoka wanasema
Emma muongo ? unafikiri ni mkakati wa bahati mbaya ? -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Mpaka sasa tumefanikiwa kukusanya TSh. Milioni 223.5, hatua kubwa inayotupeleka karibu zaidi na lengo la TSh. Milioni 334.
CHANGIA
M-Pesa
Namba: 0744446969
Jina: CHADEMA HQ
NMB Bank
Namba ya Akaunti: 22606600140
Jina la Akaunti: Chama cha Demokrasia na Maendeleo -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Wapendwa,
Nafikiri tumebakiwa na hatua moja tu kufikia lengo letu. Hebu fikirieni, kama kila mmoja ambaye tayari ameshachangia ataamua kutoa tena mchango wa kiwango kilekile alichotoa mwanzo, basi kufikia kesho tutakuwa tumekamilisha asilimia 100 ya mahitaji ya fedha za Baraza Kuu.
Hii ndiyo roho ya Tone Tone haswa Weekend hii, hatuhitaji mzigo mkubwa kutoka kwa mtu mmoja, bali moyo wa pamoja kutoka kwa wengi.
Tukiamua, tunaweza. Tukisimama pamoja, tunafika.
Asanteni sana kwa kujitoa, mshikamano wenu, na kuendelea kuamini katika wajibu huu mwema.
TONE TONE WEEKEND MISSION
“Kila tone lina thamani; pamoja tunatimiza kusudi.” -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Hii ni hatari inayoendeleza uonevu na unyanyasi kwa vijana wanachama wetu takribani 22 kupewa kesi ya ugaidi. Nchi yenye majeraha haiwezi kuponywa kwa njia ya uonevu na vitisho. Hiki sio kiburi tu pekee, bali ni uonevu ukaokatisha tamaa ya kuishi ambayo ni iahara mbaya sana kwa ustawi na utulivu wa Nchi. Naogopa sana watu wanavyoendelea kukinai hofu.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Mhe. Brenda: Mwenyekiti Tonetone imefika Milioni 174.5 mpaka jana usiku
Mhe. @TunduALissu: Waambie waongeze bidii, Baraza Kuu lifanyike
CHANGIA BARAZA KUU LA UMMA
M-Pesa
Namba: 0744446969
Jina: CHADEMA HQ
NMB Bank
Namba: 22606600140
Jina: Chama cha Demokrasia na Maendeleo -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Patrobas , mnataka kukamatwa ? wasiwasi wangu ukute wakamataji na watoa amri nao ni clients, hapo nani anakuwa referee wa mchezo? Udhibiti ni muhimu, lakini haki kwa wote muhimu zaidi.
TONE TONE MPESA 0744446969 -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
The deal sounds too good to be true. I think there’s something fishy going on.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Piga U turn haraka sana.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
"Changieni Baraza Kuu, changieni chama cha ukombozi.
TUENDELEE KUCHANGIA
M-Pesa
Namba: 0744446969
Jina: CHADEMA HQ
NMB Bank
Namba ya Akaunti: 22606600140
Jina la Akaunti: Chama cha Demokrasia na Maendeleo -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
ASANTENI sana kwa Tone Tone.
Lakini ni muhimu tuambiane ukweli. Bado sana. Kasi yetu ni ndogo mno kulinganisha na ukubwa wa CHADEMA, idadi ya watu wanaotamani mabadiliko na ukubwa wa jukumu lililo mbele yetu.
Mabadiliko hayaji kwa maneno mazuri, likes, shares au shangwe za mikutano. Mabadiliko yanahitaji sacrifice. Yanahitaji commitment. Yanahitaji kila mmoja wetu kubeba sehemu yake ya mzigo.
Tunaweza kuzungumza kwa saa nyingi kuhusu demokrasia, haki na mustakabali wa nchi yetu. Lakini ukweli mmoja unabaki palepale, hakuna chama cha siasa kinachoweza kufanya kazi bila fedha za kutosha. Na hatuwezi kuwa na fedha za kutosha kama utamaduni wetu wa kuchangia utabaki kuwa wa kusubiri wengine wafanye.
CHADEMA ina uwezo wa kukusanya hata bilioni moja kwa siku. Kinachotukwamisha siyo umaskini wetu, bali mtazamo wetu. Kila mmoja wetu anamfikiria mtu fulani atachanga. Naye huyo mtu fulani anamfikiria mtu mwingine atachanga. Mwisho wa siku, hakuna anayechanga vya kutosha kwa sababu kila mtu alikuwa anamngoja mtu fulani. Nina habari moja kwako. Huyo mtu fulani ni wewe.
Usisubiri mwanasiasa. Usisubiri mfanyabiashara. Usisubiri tajiri. Usisubiri rafiki yako. CHADEMA ni jukumu letu sote. Kiasi unachotoa siyo muhimu kuliko uamuzi wako wa kutoa. Tone Tone ya watu milioni moja ni kubwa kuliko mchango wa mtu mmoja wa milioni mia moja.
Tusijenge utamaduni wa kushangilia wanaochanga. Tujenge utamaduni wa kuchanga. Tafadhali, kuwa sehemu ya suluhisho. Kuwa huyo mtu fulani anayechanga, na siyo yule anayefikiri mtu fulani atachanga.
Mabadiliko tunayoyataka hayatakuja siku moja. Lakini yanaweza kuanza leo, kwa Tone Tone yako.
Pls, be concerned.
Much Love ! -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Kukosa akili ni gereza ambalo mfungwa wake huamini yuko huru.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Yeah Bro , Thank you so much. Let,s go 5 B .
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
I love blues music so much!
This is the Tone Tone Blues.
Changia Tone Tone
Mpesa 0744446969
CHADEMA HQ
Thank you Clara -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Kwenu Gen Z,
Oyaa! Mzigo umepanda. Target imehama, sasa tunaelekea Bilioni 5.
Msiache hii iwe kazi ya watu wachache. Kizazi chenu kimeonyesha mara nyingi kuwa kikiamua, hakuna kisichowezekana.
Mmebadilisha mijadala, mmeamsha matumaini, mmefanya sauti ya mabadiliko isikike kila kona ya nchi. Sasa ni wakati wa kuipa sauti hiyo nguvu ya mchango.
Tusibaki kwenye likes, reposts na hashtags pekee. Tuweke pia alama zetu kwenye Tone Tone.
Usichangie kwa sababu umeombwa. Changia kwa sababu unaamini. Hata elfu mbili yako ni sehemu ya Bilioni 5 tunayoiandika pamoja. Hakuna mchango mdogo unapokuwa wa watu wengi wenye imani moja.
Tonesheni Tone Tone. Tufanye historia pamoja, ili kesho tukisimulia ushindi huu, kila mmoja aweze kusema, “Nilikuwepo.”
CHADEMA MPESA- 0744446969
Wenu katika Struggle,
G. J. L -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Utasikia, “Mheshimiwa, tuko pamoja” Kama maneno haya yangekuwa vitendo, CHADEMA ingekusanya Bilioni 1 ndani ya masaa 12.
Bilioni 1 ni watu 500,000 wakitoa Sh 2,000 kila mmoja; watu 100,000 wakitoa Sh 10,000 kila mmoja; au watu 100 tu wakitoa Sh Milioni 1 kila mmoja. Tusiruhusu maadui zetu watucheke. Tusimame kwa vitendo, si kwa maneno pekee.
Tukiamua, tunaweza kukusanya hata Bilioni 10 ndani ya wiki moja. Impossible is Nothing.
M-PESA: CHADEMA HQ – 0744 446 969
CHADEMA NMB: 22606600140 -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Kwa wafuasi wote wa CHADEMA na mageuzi, wapenda haki, ukweli na demokrasia nchini.
Baada ya Katibu Mkuu wetu, John Mnyika, kutangaza maazimio ya Chama chetu, ikiwa ni pamoja na kikao cha Baraza Kuu kinachotarajiwa kufanyika siku sio nyingi , vilevile alizindua mpango maalumu wa uchangiaji wa fedha kupitia Tone Tone.
Kwa siku kadhaa sasa, kampeni hii imeendelea kwa nguvu kubwa mitandaoni, ikibebwa na viongozi wetu, wanachama, wananchi pamoja na wana harakati mbalimbali. Nawashukuru kwa dhati kabisa wote mlioamua kubeba jukumu hili; kuanzia anayehamasisha michango hadi anayetoa mchango wake. Kila mmoja wenu ni sehemu ya historia inayoandikwa.
Hata hivyo, pamoja na shukrani hizi, kuna ukweli ambao hatupaswi kuogopa kuusema. Wakati mwingine ukweli huwa ni sehemu muhimu ya kujitathmini kama taasisi na kama watu wenye maono ya pamoja.
CHADEMA ni Chama chenye wafuasi wengi kuliko Chama chochote cha siasa nchini. Wakati wa operesheni ya CHADEMA ni Msingi tulikuwa na kanzidata ya wanachama zaidi ya milioni saba. Kwa tafiti na tathmini zetu za sasa, si jambo la kupindukia kusema kuwa wapenzi wa demokrasia, haki na mabadiliko nchini wanafikia au hata kuzidi asilimia 65 ya Watanzania wazima. Kama tunakubaliana na ukweli huo, basi ni lazima tukubaliane pia na wajibu unaoambatana nao.
CHADEMA haipaswi kuwa na upungufu wa fedha za kuendesha shughuli zake. Kama watu milioni moja tu wataamua kuchanga shilingi 1,000 kila mwezi, Chama chetu kitakuwa kinapata zaidi ya shilingi bilioni moja kila mwezi. Katika kampeni hii ya kuhakikisha kikao cha Baraza Kuu kinafanyika, watu laki tano pekee wakichanga shilingi 2,000 kila mmoja, tayari watakuwa wamechangia takribani shilingi bilioni moja kwa Chama chao.
Hii ina maana kuwa changamoto yetu siyo idadi ya watu, bali ni kiwango cha dhamira yetu (commitment) katika kuwekeza kwenye kile tunachokiamini. Ni lazima tujifunze kwamba mapambano ya demokrasia yana gharama zake. Haki ina gharama yake. Mageuzi yana gharama yake. Hakuna taasisi inayoweza kuwa huru kama utegemezi wake unatoka mahali pengine isipokuwa kwa watu wake wenyewe. Vyama vikubwa vya siasa duniani vimejengwa kwa michango midogo lakini ya kudumu kutoka kwa wananchi wanaoviamini. Nasi tunapaswa kujenga utamaduni huo.
Tusifanye uchangiaji kuwa jambo la misimu au la kusubiri vikao maalumu. Uchaguzi wa mwaka 2025 ulipita na Chama chetu hakikushiriki. Hivyo, hatuna ruzuku tunayoitegemea. Tunachokitegemea ni imani, mshikamano na mchango wa wananchi wenyewe. Huo ndio mtaji mkubwa wa CHADEMA.
Ni jambo lisilo na mantiki kusema tuna mamilioni ya wafuasi huku tukishindwa kukusanya fedha za kuendesha shughuli zetu za msingi. Tukitaka kuwa Chama kikubwa, imara na huru, ni lazima tukubali kubeba gharama za ukubwa huo. Tusitarajie wachache wabebe jukumu ambalo mamilioni yetu yanaweza kulifanya kwa wepesi kabisa.
Ni rai yangu kwa kila mwanachama, mfuasi na mpenda mageuzi popote alipo, afanye jukumu hili kuwa sehemu ya maisha yake ya kisiasa. Elfu moja yako inaweza kuonekana ni ndogo, lakini inapoungana na elfu moja za wengine, hujenga taasisi kubwa. Michango yetu midogo ndiyo itakayolinda uhuru wa maamuzi yetu na uimara wa Chama chetu.
Tusichangie kwa sababu tunaombwa kuchangia. Tuchangie kwa sababu tunaamini katika Tanzania yenye haki, demokrasia na utawala wa sheria. Tuchangie kwa sababu tunaamini kuwa mageuzi tunayoyatamani hayawezi kujengwa kwa maneno pekee, bali kwa kujitoa kwetu kwa vitendo.
Your small donation can make a very big change.
Nawashukuru sana kwa upendo wenu, mshikamano wenu na imani yenu katika mapambano haya. Historia ya mageuzi huandikwa na watu wanaoamua kufanya zaidi ya kushangilia. Naamini tutafanya zaidi ya tuliyoyafanya jana.
Mungu akubariki , asanteni kwa wale wote mliochanga na mnaoendelea kuchanga na ni wito wangu kwa kila mtu kujali kwa vitendo jukumu hili muhimu , tena sio mara moja bali kila wakati. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Kutokuaminika kwa baadhi ya taasisi za utoaji haki kumechangia kwa kiasi kikubwa kukua kwa utamaduni wa watu kupeleka malalamiko yao kwa umma kupitia mitandao ya kijamii. Hali hii inanitia wasiwasi mkubwa. Kuna uwezekano wa watu wengi kuonewa au kuhukumiwa na umma bila kupata fursa ya kujitetea, huku mazingira ya nafasi zao za kazi, familia au kijamii yakiwalazimisha kubaki kimya.
Trend hii inakua kwa kasi na inaweza kuwa na madhara makubwa kwa jamii yetu. Ni muhimu elimu zaidi itolewe kuhusu matumizi yenye uwajibikaji ya mitandao ya kijamii, umuhimu wa kuheshimu haki ya kila mtu kusikilizwa, pamoja na nafasi ya taasisi zetu katika kuhakikisha haki inatendeka kwa wote.
Ninaweza kuwaza kuwa kuna watu wanaweza kupoteza mali, heshima na hata furaha ktk maisha yao , kwa sababu kukaa kwao kimya ni kulinda heshima zaidi huku maisha yao yakiwaka moto ndani.
Habari hii haina mahusiano na andiko langu. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Wewe Chalii , fungua mikutano ya hadhara haraka iwezekanvyo na pia punguza wenge.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
From Kigoma to Dar es Salaam — Tone Tone rally . The Chevy Pickup will be there. Endelea kuchangia CHADEMA Baraza Kuu kupitia M- Pesa CHADEMA HQ: 0744 446 969.
You got a G-Wagon. We got a seriously powerful machine. 😎 Respect your elder, bro!! 😉 -
Godbless E.J. Lema reposted
BBC News Swahili
@bbcswahili
Mke wa Lissu aelezea gharama ya mapambano ya kisiasa ya Tanzania kwa familia
www.bbc.com/swahili/articles/c77ypx04xv5o -
Godbless E.J. Lema reposted
Zitto MwamiRuyagwa Kabwe
@zittokabwe
Kwa makosa ya ukweli. Yule Mwaipopo aliyeunda kundi la kijeshi kinyume cha katiba na sheria hatujaona hatua yeyote dhidi yake! Yupo juu ya sheria? Kwanini hajakamatwa? Ndugu Rais @SuluhuSamia iponye nchi yetu. Turudishe 2021-2023. Hatua ya kwanza ni Tundu Lissu kuwa huru
BBC News Swahili
@bbcswahili
Rais Samia: Hakuna mtu aliye juu ya sheria
www.bbc.com/swahili/live/cly8wdj524vt?post=asset%3A0b3c09… -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Big failure, ni aibu hata kutangaza. Yaani , mauzo yote ya SABASABA sawa na zawadi ya sendoff KATORO. Uchumi hauko sawa hata kidogo. Rekebisheni siasa za Nchi zinavyoendelea kabla majuto hayajawa makubwa zaidi. Mitaani kuko vibaya sana.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
-
Godbless E.J. Lema reposted
John Pambalu
@John_Pambalu
Jana wame sainishana Makubaliano ya Maridhiano. Leo Mwenyekiti wao (Makamu wa kwanza wa Rais), anamlalamikia Katambi. Msituvuruge bana
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Habibu, acha uduanzi aisee! Umefanya mpaka Machame wameitisha kikao cha dharura. 😄
Milioni mbili, bro? Ungepandisha hata useme bilioni mbili ili hadithi iwe na uzito kidogo.
Anyway, kwa sababu wife wangu Neema amecheka sana baada ya kuisikia hii stori, leo nimeamua kukupotezea. Ila next time ongeza ubunifu kidogo. 😂 -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Nilitaka kusema, “Tazama huyu mtoto wa Rais Mstaafu Kikwete anavyojipotezea heshima waziwazi.” Lakini nikasita, ndipo nikagundua kuwa mtu hawezi kupoteza kitu ambacho hana.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Viongozi na wanachama wetu wengi wanaendelea kushikiliwa katika vituo vya polisi nchini,wakibambikiwa mashitaka mazito yasiyo na dhamana. Haki inapogeuzwa kuwa chombo cha hofu,haki hupoteza maana yake. Nchi hujengwa kwa haki, si kwa woga. Bado kuna nafasi ya kuchagua busara kuliko nguvu. Maamuzi ya leo ndiyo yataamua utulivu wa kesho. Waachieni huru mara moja. Nchi imevimba sana hii.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Kama kuna utamaduni hatari uliokita mizizi Tanzania leo, basi ni uchawa. Ni janga kubwa kuliko saratani kwa ustawi wa taifa. Unaua ukweli, unahalalisha uongo, unazika uwajibikaji, na kuwafanya wanaosema kweli waonekane maadui. Hakuna taifa linaloweza kujengwa kwa sifa za kupangwa na kuabudiwa kwa viongozi. Taifa hujengwa na ukweli, uwajibikaji, na ujasiri wa kukosoa pale panapokuwa na makosa. Uchawa si uzalendo; ni adui wa maendeleo na kikwazo cha haki.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
MAAZIMIO YA KAMATI KUU.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
LIVE: JOHN MNYIKA ANASOMA MAAZIMIO YA KAMATI KUU www.youtube.com/live/wH3LpSKjNjU via @YouTube
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Msipange kuumiza watu bila sababu za msingi. Haki ina nguvu kuliko hila.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Maazimio ya kikao cha Kamati Kuu kilichofanyika Kigoma yatatangazwa hivi karibuni na viongozi wakuu wa chama. Nina matumaini kwamba yatatoa majibu kwa kelele na mijadala mingi iliyoibuka hivi karibuni. Hata hivyo, iwapo italazimu kutetea heshima yangu binafsi dhidi ya kauli mbalimbali za dharau na upotoshaji, nitafanya hivyo kwa ufasaha. Nasikitika kwamba naweza kujikuta katika jaribu hilo, lakini heshima ya mtu si jambo la kupuuzwa.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Yohana 8:32
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
TAARIFA ZA MAHAKAMA!
Leo tarehe 8/7/2026 Viongozi na Wanachama wa Chadema SABA (7) wa Wilaya ya Kishapu ambao ni DAUD JOHN, SHIJA MISHAMO, JOSEPH MILEKWA, KENEDI BUNDALA, SUSANA JAMES, DANIEL DAUDI na MALALE MANDALU wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kishapi na kusomewa shitaka moja la Kusanyiko kinyume cha Sheria kifungu cha 74 na 75 cha Sheria ya Kanuni za adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marejeo 2023.
Kesi wanayoshitakiwa nayo ni Jinai Na.15286/2026 iko mbele ya Mheshimiwa Hakimu Michael Turuka. Kosa wanaloshitakiwa nalo linadhamana lakini Jamhuri kupitia Wakili wao wa Serikali ameweka pingamizi mahakama isitoe dhamana kwa Washitakiwa kwa sababu upelelezi unaonyesha wakipewa dhamana wataenda kusababisha uvunjifu wa amani kwenye jamii. Baada ya pingamizi hilo washitakiwa wote wamepelekwa Gerezani, Gereza la Shinyanga lililoko Ng'humbu.
Kesi imepangwa kutajwa tena tarehe 14/7/2026. Kamati ya Sheria na Haki za Binadamu Kanda ya Serengeti kuanzia kesho tutanyia kazi pingamizi hilo la Jamhuri kwa kupeleka kiapo kinzani ili trh 14/7/2026 Mahakama itusikilize swala la dhamana.
Na. Alex Massaba, Wakili via Mwenyekiti wa Chadema (W) Kishapu.
8.7.2026 -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Mkti Jimbo la Geita Neema Chozaile. Mpaka sasa bado anashikiliwa Polisi na hakuna ndugu,wakili,wanachama au viongozi wenzake walioruhusiwa kumuoana. Leo ni siku ya 10. Kuna tetesi kuwa kuna mpango wa Neema kupewa kesi mbaya isiyo na dhamana.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Africa ni Bara la ajabu sana.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
TAFAKARI !!!! 😭😭😭😭😭😭😭
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Dr Nshala ameandika mahali , “ Nchi yetu haifuati mfumo wowote wa kiuchumi bali "kula kwa urefu wa kamba yako" kwa Kiingereza Kleptocracy.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Inasikitisha sana kama kweli deal hii imeondoka Tanzania. Shame, shame, shame! Tumepoteza fursa ya kipekee na smart deal ambayo ingeweza kuleta manufaa makubwa kwa Nchi. Nimeumia sana.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Nchi haipaswi kuwa hivi hata kidogo. Uchungu na visasi vikikomaa zaidi hakuna mtu yoyote atakayekuwa salama.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Kigoma to Dar es Salaam… Ready? 😎
Tone Tone Vintage Cars Rally is coming!
Who said old cars can’t steal the show? Buckle up the legends are rolling!! -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Huu MZAHA na UPUMBAVU utadumbikiza Nchi shimoni.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
I think this guy is one of the best. He’s doing an amazing job and working really hard.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Hukustaili kuwa hata Mwenyekiti wa KITONGOJI.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Nakupa wiki mbili tu kutoka sasa, uwe umetoa pesa yote ya CHADEMA. Sio ombi ni amri kutoka kwa Mungu.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Nguvu ya nchi haipimwi kwa ukimya wa wananchi, bali kwa uwezo wake wa kusikiliza sauti tofauti na kutafuta suluhisho kupitia haki, uwajibikaji. Ondoeni hao Polisi barabarani , uncertainty kills innovation and ambience. Ondoeni sababu za watu kutaka kuandamana. Kila kona Polisi ? Nchi imekuwa ya mashaka na wasiwasi sana hii.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
“Nendeni ulimwenguni kote mkawafanye watu kuwa wanafunzi wangu,” ndicho Yesu alichowaagiza wanafunzi wake, lakini leo, changamoto ni kwamba wengi hutafuta wafuasi zaidi kuliko kujenga wanafunzi wa kweli wa Kristo. Wafuasi huongezeka kwa idadi, lakini wanafunzi hujengwa kwa mabadiliko ya moyo, utiifu, na maisha yanayomwiga Yesu Kristo. Kuna tatizo kubwa haswa na hizi Tik Tok.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Bwashee vipi ? unahitaji msaada wowote. Wewe siku hizi ni Bwashee wangu bhanaa.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Siku hizi ukiingia club unahisi kama umefika Parents’ Day. Kila kona unaona mabinti wadogo wadogo na Mababa Mababa hivii.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Baba Askofu nakusalimu. Hili jambo huwa linanitafakarisha sana. Kanisa linapomchagua mwanasiasa kuwa mgeni rasmi kwa kuamini kwamba kupitia kwake litapata fedha nyingi.
Msingi huu wa fikra unawajengea wanasiasa dhana kwamba ili wakubalike na kuheshimiwa, ni lazima wawe na uwezo wa kutoa fedha, haijalishi zimepatikanaje. Kwa namna hiyo, tunachangia kulea utamaduni wa ubadhirifu na ufisadi katika uongozi.
Cha kusikitisha zaidi ni kwamba, bila kukusudia, Kanisa linaweza kujikuta likihalalisha mfumo unaodhoofisha uadilifu. Nafikiri waumini wanahitaji fikra mpya zitakazotanguliza maadili kuliko fedha. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Au ni KOMKIZA imekata umeme ?
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Imani yangu kwenye mambo mengi imekuwa haba. Mna hujumiana sana sasa hivi , au usikute hii deal ni kama ya KATAMBI. Inaitwa “ Koroga mpake kinyesi zaidi” Kifupi KOMKIZA
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Nchi inahitaji Mindset Revolution kabla ya kitu chochote kingine. Huu
ni wajibu wa kila mtu kuanzia alipo. Mabadiliko ya taifa hayaanzi juu, yanaanzia kwenye namna kila mtu anavyofikiri, anavyozungumza, na anavyoishi na wengine kila siku. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Hamuwezi kuzuia kazi za siasa na mikutano ya hadhara, labda mikutano ya ndoa zenu. Tanzania haiwezi kuongozwa kwa hisia na hofu. Tanzania sio ghetto.
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Hii njia itachukua muda mrefu na sio salama sana. Tunapaswa aidha kushauriana.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Real estate Masaki na Oyster Bay zina price illusion kubwa. Bei zimepandishwa zaidi na matarajio kuliko msingi halisi wa soko. Soko likijirekebisha, ( market correction) wengi watashangaa kuona thamani halisi ilipo.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Umeshwahi kujiuliza kwa kina ni kwa nini viongozi wa CHADEMA hawaruhusiwi kwenda magereza kumsalimia Mkti Lissu ? Hofu na kuuziana uoga imekuwa biashara kubwa sana Nchini !! Bungeni kuna pandisha PRESHA mtaani kuna TINGISHA. Mkti Lissu sio threat kwa usalama wa Nchi bali ni ufunguo wa haki , amani na utulivu Nchini.
-
Godbless E.J. Lema reposted
Rose Mayemba
@rose_mayemba
Mimi nina roho ndogo sana,
Hii video nimeitazama jana nikashindwa kuimaliza, nimerudia leo asubuhi, mchana leo nikapata ujasiri nikasikiliza yote.
Huyu ni mwanamke kama mimi, amejaliwa mtoto mmoja wa kipekee kama ilivyo kwangu.
Lakini mwenzangu mtoto wake hajawahi kurudi nyumbani yeye wala mwili wake tangu October 29.
Mama anamuomba Samia awaonyeshe Makaburi angalau wawe wanaenda kuwaangalia watoto wao.
Anakumbuka vile alimsomesha kwa kuuza uji mpaka anakua, kwamba mapito yote aliyopitia kumlea alikuwa akimlea ili Samia aje kumuua.
Huyu ni mmoja tu, niambie ni akina mama wangapi wanapitia haya anayopitia huyu mama aliyebebeshwa mateso ya kudumu kwa kutokuanua matanga ya mwanae mpaka siku ya kufa kwake.
Ila Samia, iko siku yako.😭This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Ethiopia cuts Turkey cargo transit time from 40 days to nine, easing costs for manufacturers - Businessfront businessfront.com/finance/news/esl-turkey-transit-cut/
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Hapa ni MBEYA - Wale wa CHADEMA ITAKUFA !!! Bado mpo na kauli hii ??
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Bwashee vipi ?
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
SINGIDA, jiandaeni! Baada ya Kamati Kuu tunamalizia majimbo mawili ya Mkoa wa Morogoro, halafu tunahamia kwenu, kijiji kwa kijiji, mkoa mzima. Mood iko Top Class! Walisema CHADEMA itakufa, lakini muda unaendelea kuthibitisha tofauti. We are here to stay, and to conquer.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Uhuru wako huko karibu sana Bro. Utakuwa nje soon.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Asante MVOMERO
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Mungu anaipenda sana CHADEMA. Fikiria, mtu kama huyu aliwahi kuwa CHADEMA. Wakati mwingine kuondoka kwa baadhi ya watu ni baraka kuliko hasara.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Wanadeka!!! Maana wanajua nani yuko nyuma yao.
-
Godbless E.J. Lema reposted
Tausi Likokola
@tausilikokola
After listening to the testimonies of Tundu Lissu’s wife and Ambassador Humphrey Polepole’s sister before the European Parliament, my heart broke.
How can you watch others suffer as a human being and remain silent?
How can other human beings cause such pain to others, then go home, spend time with their own families, hug their children, sit around the dinner table, and carry on as if nothing happened?
How?
A wife is pleading for her husband.
A sister is pleading for her brother.
Mothers are grieving.
Children are asking where their fathers are.
Families are searching for answers that never come.
And then an illegitimate government still denies all of this.
They might even send officials and spokespersons to stand before the world and deny the truth.
How can some people deny even other people’s pain?
Yaani watu wanaleta ushahidi, familia zinatoa ushuhuda, dunia inasikiliza, lakini bado mnasukuma simulizi za propaganda ili kukwepa uwajibikaji?
People present evidence, testimonies, reports, and firsthand accounts, and still the response is denial, denial, denial and narrative management instead of truth and accountability.
Some of us speak because looking away was no longer an option.
Some of us speak because our humanity would not allow us to remain silent.
Free Tundu Lissu.
Free Humphrey Polepole.
Bring back Soka.
Bring back Mdude.
And for the many others who have disappeared, tell their families where they are.
Dead or alive-tell the truth.
Where are they?
Where are the bodies of many of those killed on October 29 and in the violent aftermath that followed?
Where are the answers that families deserve?
How can a state fail its people in this way and still stand before the world and claim legitimacy while denying the pain of its own citizens?
No government can build lasting peace on denial.
No nation can heal by hiding the truth.
No society can move forward while families are still searching for their loved ones and graves remain unknown.
Truth. Accountability. Justice.
That is all these families are asking for.
And that is why some of us refuse to be silent.
@StateDept @RepMcCormick @RepJoeWilson @SenatorRisch @SenTedCruz @SenatorShaheen @SenRickScott @SenRandPaul @LeaderMcConnell @SenOssoff @SenatorWarnock @SFRCdems @SFRCgop @Europarl_EN @EP_President @amnesty @hrw @UNHumanRights @BBCWorld @Reuters @CNN @nytimes @washingtonpostThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Mwenyezi Mungu husamehe mengi, lakini kiburi humfanya mwanadamu ashindane na Muumba wake. Unyenyekevu huinua, kiburi huangusha.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
IGP Wambura, baadhi ya askari wa Polisi katika maeneo ya Mkoa wa Morogoro wanaendelea kukandamiza shughuli halali za kisiasa. Gairo, chama chetu kilizuiwa kufanya mkutano katikati ya mji na OCD akatulazimisha kuhamishia mkutano nje ya mji, kinyume na ratiba na matangazo yaliyokuwa yametolewa. Kilosa, katika Kijiji cha Rudewa, gari la matangazo lililazimika kusitisha kazi baada ya wamiliki wa vifaa kupokea vitisho. Hata gari la pili lilipopatikana, vitisho hivyo viliendelea hadi wakalazimika kurejesha fedha na kujiondoa.
Demokrasia inaendelea kukabwa kwa njia zisizokubalika. Haipaswi kuwa hivi. Jeshi la Polisi lina wajibu wa kuhakikisha vyama vyote vinafanya shughuli zao za kisiasa kwa usawa, kwa mujibu wa sheria na Katiba. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
GEN. MUGISHA MUNTU ON GEN. MUHOOZI | Erias Lukwago | Muhoozi | Museveni ... youtu.be/V6WnXLFTPj0 via @YouTube
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Kijiji Cha Rudewa Jimbo la Kilosa. Kabudi hatakiwi kabisa.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Safari ya kuelekea Kilosa katika Operesheni Katiba Mpya na Free Tundu Lissu ilitupitisha Dumila. Huko, wananchi walituomba tumtembelee mzee huyu shupavu. Wanasema bendera kwenye baiskeli yake haijawahi kushuka, ishara ya msimamo na imani yake. Ilikuwa ni heshima kubwa kukutana naye. Kila siku huzunguka na spika hii niliyoibeba, akiendelea kueneza sauti ya kile anachoamini.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Bwana TUTUBA. Gavana bora wa benki kuu huonekana kidogo wakati mambo ni shwari, lakini hujidhihirisha zaidi wakati wa pressure za KISIASA, kwa maamuzi thabiti na ya busara. Uhuru wa taasisi ya fedha ni msingi wa uchumi imara, si kufuata shinikizo za kisiasa.
-
Godbless E.J. Lema reposted
Boniface Mwabukusi
@Mwabuk2Boniface
EXENOPHOBIA kama inayoendelea Afrika ya Kusini ni hofu dhidi ya wageni na msingi wake unaeleweka lakini hapa Tanzania kuna TL-Phobia ni hofu dhidi ya Tundu Lisu.Uadilifu wake ,Ukweli wake na Uzalendo wake.
Ya kwanza ina weza kueleweka au kuzungumzika hii ya pili ni zao la Ujinga na Kutofikiri sawasawa. Ni aibu kwa Taifa.
BAK MWABUKUSI. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
HII NI HATARI.
Naionya nchi kuwa tukilegeza mipaka ya Serikali kukopa kutoka Benki Kuu, tunaweza kufungua mlango wa mfumuko wa bei, kuporomoka kwa thamani ya shilingi, na kuongezeka kwa gharama za maisha kwa wananchi.”This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Ndiyo
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
🔵LEMA AWAPA MBINU POLISI ZA KUKABILIANA NA VUGUVUGU LA MAANDAMANO JULY 7 youtu.be/9phe-kfpGok via @YouTube
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Ukiwa mdogo huenda usione kila alichopitia baba yako. Lakini siku moja utaelewa kuwa alibeba mizigo mingi kimya kimya ili familia yenu isimame. Hata kama nyumbani hamkuwa wakamilifu.
Happy Father’s Day kwa baba wote. 🙏 -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Yeah
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Polisi TAFAKARINI.
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Moshi MUNGU AWABARIKI SANA.
-
Godbless E.J. Lema reposted
Josephine Marealle-Ulimwengu
@UlimwenguJm
Diplomasia siyo lelemama!!!!! Ukiwageuza wapiga porojo kuwa washauri na watetezi wako katika masuala nyeti ya taifa, hususan diplomasia na mahusiano ya kimataifa, ukidhani wataweza kuficha makosa au kuhalalisha uovu, unajidanganya. Garbage in, garbage out!
Mahusiano ya kimataifa hayajengwi kwa propaganda, makelele ya mitandaoni, wala simulizi za kujifariji. Hujengwa kwa uaminifu, uadilifu, haki, heshima, uwajibikaji na maslahi ya pamoja.
Acheni bla bla. Mahusiano hayadumishwi kwa uongo, na miujiza haiandaliwi mezani mwa diplomasia. Mataifa yenye mifumo thabiti huendesha mambo kwa misingi ya ukweli, si kwa matamanio au propaganda. Mwishowe, ukweli hujitokeza, na dunia hujibu kulingana na matendo, si maneno. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Lupiro- MAHENGE
🅻🅸🆅🅴:CHADEMA KUISIMAMISHA ULANGA MKUTANO WA HADHARA www.youtube.com/live/nlErpE83dWQ?is=fyXfEvHKBNGNiT2G via @YouTube -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
CCM Ina vijana wapumbavu sana. Sijui wanawaokota wapi ? Ohhh sorry , hata wakubwa zao ni ovyo kabisa. So ni DNA.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema reposted
Peter Msigwa
@MsigwaPeter
KUHUSU BUNGE LA ULAYA
kura hiyo si ya mwisho” ni kujibu athari, badala ya kujibu chanzo cha tatizo. Msemaji wa serkali jibu hoja za msingi.
Anaandika Rev Peter Simon Msigwa
1. Serikali inasema kura ya Bunge la Ulaya si ya mwisho, lakini haijibu uzito wa ujumbe wa kisiasa
Ni kweli kwamba Bunge la Ulaya halipeleki fedha moja kwa moja na kwamba Tume ya Ulaya ndiyo yenye jukumu la mwisho. Lakini swali kubwa si kama fedha zimekatwa tayari, bali ni kwa nini wabunge wa Ulaya walifikia hatua ya kupitisha azimio hilo kwa wingi mkubwa?
Hata kama ni pendekezo, linaonyesha kuporomoka kwa imani ya kisiasa kwa washirika muhimu wa Tanzania. Serikali imejibu utaratibu, lakini haijajibu sababu zilizosababisha azimio hilo.
2. Serikali imejikita kwenye “utaratibu”, si kwenye hoja za haki za binadamu
Taarifa inasisitiza kuwa mchakato wa fedha haujakamilika, lakini haijajibu madai yaliyotolewa na Bunge la Ulaya kuhusu:
Ukiukwaji wa haki za binadamu.
Ukandamizaji wa wapinzani.
Kesi dhidi ya viongozi wa upinzani.
Hali ya uchaguzi wa 2025.
Vifo na matumizi ya nguvu dhidi ya raia.
Kwa maneno mengine, serikali imejibu “fedha zipo salama”, lakini haijajibu “kwa nini dunia ina wasiwasi juu ya demokrasia na utawala wa sheria”.
3. Kudai kwamba fedha nyingi haziendi serikalini hakupunguzi uzito wa azimio
Serikali inasema euro milioni 139 zilikuwa zinaenda kupitia taasisi za Umoja wa Ulaya na asasi za kiraia.
Lakini hoja ya Bunge la Ulaya ilikuwa kwamba fedha hizo zielekezwe zaidi kwa wananchi na zisisaidie mifumo inayoweza kuhusishwa na ukiukwaji wa haki.
Kwa hiyo kusema “fedha hazikuwa zinaingia moja kwa moja serikalini” hakukanushi sababu za msingi zilizozua mgogoro.
4. Serikali inasema baadhi ya hoja za Bunge la Ulaya si za kweli, lakini haijataja zipi
Taarifa inasema baadhi ya hoja “hazina ukweli”, lakini haijaeleza:
Ni hoja gani hasa ni za uongo?
Ni ushahidi gani unaozikanusha?
Ni taarifa zipi mbadala zinazotolewa?
Kwa kawaida, kukataa tu bila kutoa ushahidi wa kina hakuondoi tuhuma.
5. Kama mahusiano ni mazuri sana, kwa nini hali imefika hapa?
Serikali inasema mahusiano kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya ni imara.
Lakini swali la msingi ni:
Kama mahusiano ni imara na hakuna tatizo kubwa, kwa nini Bunge la Ulaya limefikia hatua ya kupiga kura dhidi ya mpango wa msaada wa euro milioni 156?
Marafiki wa karibu pia huonyesha kutoridhishwa pale wanapoona misingi ya pamoja ya demokrasia na haki za binadamu imeanza kutetereka.
6. Hoja ya “hii ni maoni tu ya Bunge la Ulaya” inaweza kupunguza uzito wa tukio
Katika mifumo ya kidemokrasia, Bunge la Ulaya ni taasisi muhimu yenye ushawishi mkubwa.
Kwa hiyo, hata kama azimio lake si uamuzi wa mwisho, kisiasa lina uzito mkubwa na mara nyingi huathiri maamuzi ya Tume ya Ulaya.
Hitimisho
Utetezi wa serikali umejikita zaidi katika kueleza utaratibu wa utoaji wa fedha kuliko kujibu kiini cha wasiwasi wa Bunge la Ulaya.
Swali ambalo taarifa hiyo haijalijibu kikamilifu ni:
Kwa nini washirika wakubwa wa Tanzania wamefikia hatua ya kuonyesha kutokuwa na imani na mwenendo wa haki za binadamu, demokrasia na utawala wa sheria nchini?
Bila kujibu swali hilo la msingi, maelezo ya kwamba “kura hiyo si ya mwisho” ni kuonekana kujibu athari, badala ya kujibu chanzo cha tatizo. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Waliokuzunguka wanaweza kuwa wanakuzunguka, umeelewa mama? Wengine wanasema tu slow down juu yao maana wanakujua na kuijua familia yako vizuri. Siwapendi ndio maana na sanua deal.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Hivi waziri wako wa Mambo ya Nje Thabit Kombo anakuambia ukweli ? Nafikiri anakutia moyo zaidi ili ujisikie vizuri kuliko hali halisi. Mambo hayako kawaida kabisa. Amekuambia alichoambiwa na USA hivi karibuni ? Nafikiri is a nice guy zaidi for cookies and coffee especially anapokuwa kwenye diplomat corridor.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Mahakama inapopoteza taswira ya kuwa taasisi huru na kuanza kuonekana kama tawi lenye mwelekeo wa kisiasa, athari zake huwa pana na za muda mrefu. Imani ya wananchi kwa mfumo wa haki hupungua, na msingi wa utawala wa sheria unadhoofika. Hivyo, uhuru na uadilifu wa mahakama ni nguzo muhimu inayopaswa kulindwa kwa uangalifu mkubwa ili kuhakikisha haki na imani ya umma vinabaki imara.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Maazimio ya Brussels na Washington kuhusu utawala na haki za binadamu Tanzania yanaweza kuwa na athari zaidi ya misaada au fedha zinazoweza kupungua. Athari kubwa zaidi ni mabadiliko ya taswira ya nchi katika macho ya kimataifa.
Kitaalamu, hii huathiri impression ya hatari ya nchi (country risk perception), ambapo wawekezaji na taasisi za kifedha huanza kuwa waangalifu zaidi. Matokeo yake ni kuongezeka kwa gharama za mikopo, kupungua kwa kasi ya uwekezaji, na kuchelewa kwa baadhi ya miradi ya maendeleo.
Kwa ujumla, changamoto kubwa si fedha zilizozuiwa, bali ni imani na jina la Tanzania katika mfumo wa kimataifa, ambalo likidorora huathiri uchumi wa muda mrefu. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
ASANTE MLIMBA.
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
🅻🅸🆅🅴:LEMA ATIA TIMU MKUTANO WA HADHARA JIMBO LA MLIMBA ,KILOMBERO www.youtube.com/live/N65O-tQlTLc via @YouTube
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Much thanks to my Toyota Land Cruiser. We call you AKS. You’ve crossed this nation more than four times, carrying us through every road and every condition. You are more than a vehicle, you’re a legacy. No price tag could ever define your worth. I❤️ you.
-
Godbless E.J. Lema reposted
Tausi Likokola
@tausilikokola
🚨 BREAKING: WE WON TODAY! 🚨
We did not give up. We did not stay silent. Today, we moved one step closer to justice.
The Reassessing the United States–Tanzania Bilateral Relationship Act has passed the Senate Foreign Relations Committee and now advances forward.
This moment belongs to every mother who buried a child, every family still searching for answers, every victim of violence, every religious leader who stood firm, every journalist who spoke the truth, every activist who refused to be intimidated, and every Tanzanian who never stopped believing that accountability matters.
This is not the finish line.
But today, the world heard Tanzania.
Today, truth prevailed over propaganda.
Today, hope prevailed over fear.
Today, we moved one step closer to justice and accountability.
To everyone who prayed, advocated, testified, contacted congressional offices, shared evidence, and refused to look away-thank you.
The journey continues, but today we pause to thank God.
Justice delayed is not justice denied.
Safari bado inaendelea- ila leo haki imeshinda💪🏽
Thank you also to all senates and their staffers that heard our cries.
🇹🇿🙏🏾🇺🇸
🚨 HABARI NJEMA: TUMEPATA USHINDI LEO!
Hatukukata tamaa. Hatukukaa kimya.
Leo tumepiga hatua moja muhimu kuelekea haki.
Muswada wa Reassessing the United States–Tanzania Bilateral Relationship Act umepitishwa na Kamati ya Mahusiano ya Nje ya Seneti ya Marekani (Senate Foreign Relations Committee) na sasa unasonga mbele katika hatua zinazofuata.
Ushindi huu ni wa kila mama aliyempoteza mwanae, kila familia ambayo bado inatafuta majibu, kila mwathirika wa ukatili, kila kiongozi wa dini aliyesimama imara, kila mwanahabari aliyesema ukweli, kila mwanaharakati aliyekataa kutishwa, na kila Mtanzania ambaye hakuwahi kuacha kuamini kwamba uwajibikaji ni muhimu.
Huu si mwisho wa safari.
Lakini leo, dunia imeisikia Tanzania.
Leo, ukweli umeshinda propaganda. (Niliwaambia ile picha ya mkono wa bendera ya Tanzania ikishikana na ya marekani yaliyochapishwa na hayo magazeti yaliyonunuliwa ni propaganda- leo si kimewaka?)
Leo, matumaini yameshinda hofu.
Leo, tumesogea hatua moja karibu zaidi na haki na uwajibikaji.
Kwa kila aliyeomba, aliyehamasisha, aliyetoa ushuhuda, aliyewasiliana na viongozi wa Marekani, aliyeshiriki ushahidi, na aliyekataa kugeuza macho yake pembeni -asanteni sana.
Safari bado inaendelea, lakini leo tunasimama na kumshukuru Mungu.
Haki iliyocheleweshwa si haki iliyonyimwa.
Now muachieni na Lissu
🇹🇿🙏🏾🇺🇸
#justicefortanzania -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
🅻🅸🆅🅴:CHADEMA INAKIWASHA MUDA HUU JIMBO LA MIKUMI WILAYA YA KILOSA MOROGORO www.youtube.com/live/C_75KSvh8O8 via @YouTube
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Asante IFAKARA.
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
🅻🅸🆅🅴:LEMA KUISIMAMISHA IFAKARA MOROGORO MKUTANO WA HADHARA www.youtube.com/live/ebaUPIBcJho via @YouTube
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Unaitafuta nafasi ya KIHONGOSI kwa nguvu sana. Halafu na yeye alivyo boya wala hajui.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Watu wengine huona ni kama kukosa heshima unapokataa kuwapa nafasi ya kukudharau.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Mama Samia, pengine wanaokuzunguka wanakudanganya sana. Na msingi wa uongo huo kwao unaweza kuwa biashara kubwa sana. Wanaweza kuwa wanatumia intimidation kama strategy muhimu kwa maslahi yao. Lakini ukweli ni kwamba siasa za aina hii za kuongeza presha na taharuki hazileti faida ya muda mrefu kwa nchi, bali kwa watu wachache tu wanaonufaika na hali hiyo.
Kuhusu Mh Tundu Lissu, kumuweka mahabusu au kumdhibiti kisiasa hakutaondoa changamoto za kisiasa, bali kunaendelea kuongeza taharuki zaidi ndani na nje ya nchi. Hasara kubwa si yeye kufanya siasa akiwa nje, bali ni kuendelea kumuweka mahabusu.
Kwa mtazamo huu, hii sio faida , bali inaweza kuwa faida kwa watu wanaonufaika na mvutano huu. Ndiyo maana wakati mwingine huonekana kuna mkakati wa kupandisha presha ili maslahi fulani yaendelee kunufaika. Hofu nayo ni biashara , tena Tax free. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
IGP, mara nyingi uoga huwa na gharama kubwa zaidi kuliko hata ukatili. Polisi inapofanya maamuzi kwa msingi wa hofu badala ya ushahidi, madhara yake hayaishii kwa watu binafsi pekee bali huenea hadi kwenye uchumi wa nchi.
Mnaendelea kukamata viongozi wa CHADEMA kwa mtindo unaozua maswali mengi kuhusu msingi wa hatua hizo. Kama hakuna ushahidi wa tishio halisi kwa usalama wa taifa, hatua kama hizi hujenga taswira ya kutokuwa na utulivu wa kisiasa kuliko kutatua tatizo lolote.
Kwa mtazamo wa kiuchumi, perception matters. Wawekezaji, watalii, mashirika ya bima na serikali za kigeni hufanya maamuzi yao kwa kuzingatia taswira ya utulivu wa nchi. Hali ya sintofahamu ya kisiasa inaweza kusababisha travel advisories, kuongeza gharama za bima za safari na biashara, na kuathiri maamuzi ya watalii pamoja na wawekezaji.
Utalii ni moja ya vyanzo vikubwa vya fedha za kigeni nchini. Sekta hii inapopata mshtuko kutokana na hofu zinazoweza kuepukika, athari zake huonekana kwenye mapato ya forex, ajira, biashara zinazotegemea wageni na hata uwezo wa nchi kuhimili shinikizo la sarafu za kigeni. Ikiwa mapato ya utalii yatashuka kwa kiasi kikubwa, gharama zake kwa uchumi zinaweza kuwa kubwa zaidi kuliko faida yoyote inayodhaniwa kupatikana kutokana na hatua za ukandamizaji.
Ndiyo maana ni muhimu sana kwa vyombo vya dola kutenda kwa ushahidi, uwiano na busara. Hofu isiyo na msingi inaweza kuzalisha tatizo kubwa zaidi kuliko lile linaloogopwa. Mnatengeneza mashaka yasiyo ya lazima katika kipindi ambacho nchi inahitaji kuonekana kuwa salama, thabiti na inayoheshimu utawala wa sheria.
Anyway, ngoja tunywe mtori; nyama tutazikuta chini. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Kazi yetu sio rahisi hata kidogo, lakini ni lazima tuifanye. Tusipoifanya sisi, watoto na wajukuu wa Tanzania watakuja kukojolea makaburi yetu. Lazima tuikwepe hii aibu. Ni jambo la kumshukuru Mungu kuwa hata kama kuna uonevu , lakini umeitwa Polisi. Maana siku hizi, “bring back” imekuwa “forever lost.”
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Sisi ndio chanzo.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
IFAKARA ni Kesho Jumanne Tarehe 16/6/2026.
-
Godbless E.J. Lema reposted
Boniface Mwabukusi
@Mwabuk2Boniface
Tusimamie Ukweli kwa gharama yeyote hata ikilazimu wote kuondoka na kulazimika kubaki 12 kama ilivyo anza awali . Papa Leo XIV.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Baraza la Mashauriano Mkoa wa Morogoro limekutana leo Jumapili tarehe 14 Juni 2026 kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali yanayohusu chama na maendeleo ya mkoa. Kikao kimefanyika kwa mafanikio makubwa na wajumbe wamejadili pamoja na kutoa maelekezo kuhusu utekelezaji wa majukumu mbalimbali ya chama katika ngazi ya mkoa.
Tunawashukuru wajumbe wote kwa ushiriki wao na mchango wao katika kikao hiki. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Wewe endelea ku enjoy sasa , maana tukichukua mamlaka ya Nchi , utaenda makumbusho mapema sana. Trust me.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Hakuna miaka mingi mbele kutoka leo. Pombe inatengeneza janga ambalo wengi hawalioni. Ikiwa mwenendo wa sasa utaendelea, itaua watu wengi zaidi, kuvunja familia nyingi zaidi, na kuchochea kuporomoka kwa maadili ya jamii kwa kiwango ambacho kitakuwa tishio kubwa kwa mustakabali wa taifa letu. Inatisha sana.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Katika mabadiliko yanayotarajiwa ndani ya CCM, nina taarifa kwamba nafasi ya huyu bwana si salama. Ndiyo maana siku hizi amegeuza CHADEMA kuwa ajenda yake ya kila siku. Anatafuta relevance kwa kuwataja viongozi wa upinzani na CHADEMA akiamini kelele zinaweza kuziba upungufu wa upumbavu alionao. Yuko kwenye kampeni ya kupigania nafasi yake.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Sisi sio wauawaji kama nyie. Funga mdomo wako. Uongo , uongo tu umewajaa moyoni na vinywani.
-
Godbless E.J. Lema reposted
Shruti
@heyshrutimishra
Elon just created 4,400 millionaires in a single day.
400 of them are now worth over $100 million.
These aren't VCs. They're SpaceX employees, and the list includes welders, technicians, and cafeteria staff, because for two decades the company paid every level of the workforce in stock instead of higher salaries.
Juan Hernandez immigrated from Mexico and took a $28 an hour contractor welding job in 2015. He says he didn't even know what SpaceX was. The company gave him a $10,000 equity grant and let him buy more shares through payroll deductions. That stake is now worth $880,000.
Trevor Hise's parents wanted him to take a stable job at General Electric. He picked SpaceX instead, stayed 12 years, and accumulated over 100,000 shares. At the $135 listing price that's $13.5 million. He's 37 and semiretired. His words: "The magnitude of this has been ridiculous."
The most telling detail came before the listing. Over 100 employees quietly banded together and negotiated a group wealth management deal covering up to $5 billion, because none of them had ever needed a wealth manager before.
Software IPOs have minted millionaires for 30 years. This is the first one where the money went to the factory floor.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
God bless you.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Acha UPUMBAVU wewe. Unatuona sisi ni watoto.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Fimbo ya Mwenyezi Mungu itatua juu yako siku sio nyingi.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
How To Become An Influential Leader: Best Strategy By Myles Munroe For S... youtu.be/YLZ0Tkpls94 via @YouTube
-
Godbless E.J. Lema reposted
Lubasha Jr
@MarekaMalili
Zaburi 30:5
"Kilio chaweza kukaa usiku kucha, lakini furaha huja asubuhi." -
Godbless E.J. Lema reposted
Rugemeleza Nshala
@rugemeleza
Kesi ya Mwenyekiti Tundu Lissu Sasa itakuwa tarehe 3 Julai 2026 na si kesho tarehe 11 Juni 2026.
Tundu Lissu's revision case at the Court of Appeal of Tanzania has been rescheduled to the 3rd of July 2026 instead of June 11 2026. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
My Bro , Husein Mwinyi.
Ninakuandikia kwa masikitiko makubwa kufuatia kauli zinazoendelea kutolewa na baadhi ya viongozi kutoka Zanzibar ambazo, kwa mtazamo wangu, zinaonesha ubaguzi wa wazi dhidi ya Watanganyika. Kwa muda mrefu nimekuwa na imani kwamba fikra za namna hiyo haziwezi kupata nafasi katika uongozi wako. Ikiwa nimekosea katika tathmini hiyo, basi nitakuwa nimekosea kwa kiasi kikubwa sana.
Kauli hizi si hatari kwa mshikamano wa Muungano pekee, bali pia ni mbegu ya mgawanyiko wa kijamii na kisiasa ambayo inaweza kuzaa matokeo mabaya kwa Taifa letu. Kinachonisikitisha zaidi ni ukimya wako. Katika mazingira ya sasa, ukimya huo unaweza kutafsiriwa kama ridhaa au baraka kutoka mamlaka za juu, jambo ambalo linaweza kueleza kwa nini kauli hizi zinaendelea kutolewa kwa mfululizo, zikiwa na simulizi moja na bila hofu yoyote.
Kwa kweli, naogopa hata kuingia katika mjadala wa nafasi na fursa ambazo Wazanzibari wamewahi kushika au wanazoendelea kushika katika Muungano huu. Kufanya hivyo kungekuwa ni kuushusha mjadala kwenye kiwango ambacho siamini kinafaa kwa Taifa letu. Historia inaonesha wazi kuwa Wazanzibari wamepewa na wameendelea kupata nafasi kubwa za uongozi katika Jamhuri ya Muungano, ikiwemo nafasi ya Rais wa Tanzania. Hivyo, hoja za kuwatenga au kuwadharau Watanganyika hazina msingi wa haki wala busara.
Ninaamini kwamba maneno yana nguvu. Yanajenga, lakini pia yanaweza kubomoa. Kauli za ubaguzi zikipewa nafasi ya kukua bila kukemewa, zitajenga chuki, zitaongeza mgawanyiko, na hatimaye kila upande utajikuta umepoteza. Taifa lolote linaloruhusu ukweli kunyimwa nafasi huku upendeleo na ubaguzi vikipewa sauti, hujenga mazingira ya migogoro ambayo baadaye huwa vigumu kuyarekebisha.
Sioni mustakabali mwema ikiwa mwenendo huu utaendelea. Wakati wa kukemea na kusimama upande wa haki ni sasa. Kesho inaweza kuwa imechelewa. -
Godbless E.J. Lema reposted
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Mahakama popote duniani inapokubali ku-compromise, ni suala la muda tu kabla ya taifa kulipa gharama kubwa zaidi. Hata kama si leo, historia huja kutoa hukumu yake.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Mahakama popote duniani inapokubali ku-compromise, ni suala la muda tu kabla ya taifa kulipa gharama kubwa zaidi. Hata kama si leo, historia huja kutoa hukumu yake.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Msingi wa madai ya katiba mpya ni jambo muhimu katika siasa za nchi yetu sasa kuliko wakati mwingine wowote. Katiba mpya inaonekana kama chombo cha kuleta mageuzi katika utawala, haki, na uwajibikaji wa viongozi pamoja na wananchi kwa ujumla. Hata hivyo, pamoja na umuhimu huo, kuna jambo la msingi linalonipa wasiwasi mkubwa, nalo ni “mindset” tuliyonayo kama jamii juu ya haki, huruma na utu.
Katiba inaweza kuwa nzuri na yenye misingi imara ya kisheria, lakini bado ikashindwa kufanya kazi ipasavyo kama jamii yenyewe haina utamaduni wa kusimamia haki. Haki, utu na ukweli vinahitaji watu wenye ujasiri wa kuvisimamia bila woga. Pale jamii inapokosa ujasiri huo, hata sheria nzuri zinaweza kupuuzwa au kupindishwa kwa manufaa ya wachache.
Wasiwasi wangu mkubwa ni kwamba katiba mpya inaweza kuburuzwa vile vile na tabia mbaya zilizojengeka ndani ya jamii ambazo hazijali utu. Msingi wake mkuu wa tatizo ni uoga wa kusimamia haki, utu na ukweli. Watu wengi huona ni bora kunyamaza kuliko kusimama dhidi ya dhuluma au upotovu. Hali hii inafanya hata mifumo iliyopo kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi.
Swali la msingi ni kwamba, kama jamii haiwezi kujisimamia katika mambo ya kawaida yanayohusu haki na utu, hata katika katiba ya sasa tunayotaka mabadiliko juu yake, je, katiba mpya ikipuuzwa wakati mtazamo wetu juu ya haki bado ni duni, tutapaswa kufanya nini zaidi? Hili ni swali linalohitaji tafakari ya kina zaidi kuliko mjadala wa kisheria pekee.
Ni dhahiri kwamba tuna tatizo kubwa sana la “mindset”, na bila kulitatua, katiba mpya inaweza kuvunjwa mbele ya watu wale wale na bila hatua kuchukuliwa. Hivyo basi, pamoja na harakati za katiba mpya, ni lazima pia tuweke mkazo katika kuamsha fikra za jamii, kujenga ujasiri wa kusimamia haki, na kurejesha thamani ya utu na ukweli katika maisha ya kila siku.
Kwa ujumla, katiba mpya ni muhimu, lakini haitoshi pekee. Mabadiliko ya kweli ya taifa yatategemea pia mabadiliko ya fikra za wananchi. Tuamshe fikra, tujenge ujasiri, na turudishe utu katika msingi wa maisha ya jamii yetu. -
Godbless E.J. Lema reposted
Eng.Simon J.Msenga
@SimonMsenga
Last week, I married my missing rib and found my peace......
Now we are Mr&Mrs Simon Msenga, God is good always! -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Namshukuru Mungu wewe si baba yangu. Kwani ningekuwa natembea na mfuko wa kuficha uso kila ninapotoka nyumbani.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
KARATU ASANTENI
-
Godbless E.J. Lema reposted
Adv. Dickson Matata
@AdvMatata
Mkutano wa leo Karatu CDM tunaomba jeshi la zimamoto na uokoaji waje haraka na vifaa vya Oxygen. Watu ni wengi sana hewa inazidi kupingua kadri muda unavyosonga mbele tafadhari!!.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Karibuni wote , rudini nyumbani.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Masele anaweza kuwa yuko sahihi.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Jana nimepata fursa ya kutembelea KILIFAIR, moja ya maonyesho yenye mchango mkubwa katika uchumi wa utalii wa Tanzania. Ni wazi kwamba sekta binafsi imewekeza kwa kiwango kikubwa, si tu katika fedha bali pia katika ubunifu na juhudi za kuitangaza Tanzania ktk utalii.
Hata hivyo, kuna changamoto za msingi ambazo zinapunguza thamani ya uwekezaji huo. Vumbi kubwa katika eneo la maonyesho, pamoja na udhaifu wa huduma za mawasiliano na internet, vinaathiri uzoefu wa washiriki na wageni, lakini pia vinaathiri ufanisi wa biashara zinazokusudiwa kufanyika katika maonyesho hayo.
Katika uchumi wa kisasa, mawasiliano ni miundombinu muhimu sawa na barabara au umeme. Pale ambapo mfanyabiashara hawezi kuwasiliana kwa urahisi, kufanya malipo, kutuma taarifa au kuwasiliana na wateja, gharama za biashara huongezeka na fursa hupotea.
KILIFAIR imejijengea hadhi ya kuwa jukwaa muhimu la kuitangaza Tanzania kama kitovu cha utalii Afrika Mashariki. Hadhi hiyo inastahili kuungwa mkono na miundombinu inayolingana nayo. Kuboresha mazingira ya maonyesho na huduma za mawasiliano si suala la anasa, ni uwekezaji unaoongeza thamani ya tukio lenyewe na ushindani wa Tanzania katika soko la kimataifa la utalii.
KILIFAIR deserves better, kwa sababu mchango wake kwa uchumi wa Tanzania unastahili mazingira bora zaidi. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Fall seven times, stand up eight.” (Japanese proverb)
Come back home, darling. It’s time to rise again. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Watoto wa Mwenyekiti Tundu Lissu wamekua wakisikia simulizi za baba yao akiteswa na hata kushambuliwa kwa risasi kwa ajili ya kupigania haki za watu wengine. Leo, mtoto wake yuko barabarani akidai uhuru wa baba yake. Ni hadithi ya kutia moyo, lakini pia ya kuhuzunisha sana.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Naona mnataka kuivunja Kamati Kuu yenu. Hamtapata utulivu juu ya damu zilizomwagika mpaka KISASI cha Mungu kimekamilika juu yenu na familia zenu. Nilikuwemo kwenye kundi la hao mnaowaita wabunge kwa zaidi ya miezi 4, kwa kweli vita ni kali sana, na wengi wao wanajuta sana hadi leo juu ya October 29.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Kafanye MDAHALO na SIMAI na MWIGULU. Title ya MDAHALO iwe , NAMNA YA KU DEAL NA YUDA NDANI YA BUNGE.
-
Godbless E.J. Lema reposted
Liberatus Mwang'ombe
@Liberatus80
Kutoka Washington, DC, Marekani: Tupo na maGen—Z, mtoto wa Tundu Lissu, Tino, na mtoto wa dada @tausilikokola tukipigania Uhuru wa baba yake Tino na Watanzania kwa ujumla. Nipo na begi langu la maamuzi magumu. #hakihuinuataifa
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
-
Godbless E.J. Lema reposted
Josephine Marealle-Ulimwengu
@UlimwenguJm
Nashangaa mkuu wa mjengo wao anawaona watoro wa mahudhurio tu, hawaoni wale waliopo mjengoni lakini kazi yao kubwa ni kupiga meza kwa nguvu (Noise pollution!) kila baada ya koma kana kwamba ndiyo kipimo cha utendaji. Tofauti kati ya hawa wawili ni kwamba mmoja ni mtoro wa mahudhurio, mwingine ni mtoro wa mawazo na mijadala ya msingi. Wote ni watoro!!
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Simai , huko wapi Bro , kuna Chalii ananiparamia huku !!!
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema reposted
Hilda Newton
@HildaNewton21
Mhe. Lissu alikuwa mbele ya muda
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Uhuru wa maoni ni wazo (principle) linaloongoza msingi wa haki za binadamu katika jamii ya kisasa. Ni haki ya mtu kufikiri, kukosoa, kuhoji na kueleza mawazo yake bila hofu ya kuadhibiwa kiholela. Haki hii ni ya msingi kwa kila binadamu kwani humwezesha kuishi kama kiumbe mwenye akili, anayefikiri na anayejieleza kwa uhuru ndani ya mipaka ya sheria.
Uhuru wa maoni hauishii katika mazingira maalum au majukwaa ya hadhara pekee. Upo hata mtu akiwa nyumbani, kazini, kwenye mtandao, au katika mazungumzo binafsi. Hii inaonyesha kuwa uhuru wa maoni ni hali ya kudumu ya kiakili na kisheria, si tukio la muda au tukio linalotokea mara kwa mara.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Yes , it’s me.
-
Godbless E.J. Lema reposted
Joseph Mbilinyi
@TheRealJongwe
Shida ya Putin kinaponuka huwa hana msaada kwa wanaomtegemea…Maduro wa Venezuela alinyakuliwa na Trump kama kifaranga, Asad wa Syria zilimuokoa mbio kule Damascus!
#freelissu -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
KANDA YA KATI STAND UP!
Morogoro, Dodoma na Singida, jiandaeni!
Katika siku za hivi karibuni tutakuwa na ziara za vikao na mikutano ya hadhara.
Morogoro Stand Up!
Dodoma Stand Up!
Singida Stand Up!
Ratiba kamili itatolewa hivi karibuni.
Kanda ya Kati Stand Up! -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Yeah !
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Yeah !
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Dada MSHAURI , mambo !!! 😂 Miss you sometimes!
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Watajali kitu gani tena kama waliingia Bungeni bila ridhaa ya wananchi ? Wewe imagine una Mbunge yuko Bungeni halafu hajui alipata kura ngapi ? Sasa itakuwa kwenda Morroco bila kibali ? Stori gani za aibu hizi mnaleta ?
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Katika mazishi ya Baba Askofu Mungure. Askofu Mungure ni baba mzazi wa Elisa Mungure , Mwenyekiti wetu wa Mkoa CHADEMA Mkoa wa Arusha.
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Ukiharibu mifumo ya utawala wa haki, sheria , utawala bora na demokrasia huwezi kuwa na sifa yoyote nyingine ktk uongozi. Maana ktk msingi huu ndio Unaweza kuwa na kipimo halisi cha maana ya mafanikio. Barabara au madaraja hayawezi kuchukua nafasi ya haki , utu , utawala bora na demokrasia. Kanuni ya msingi ya mafanikio ni haki na utu.
-
Godbless E.J. Lema reposted
Liberatus Mwang'ombe
@Liberatus80
Wajumbe.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
God bless you guys !!
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Mwenyekiti wa Kata wa CHADEMA kwa sasa akiitiisha mkutano wa hadhara. Mkutano unakuwa mkubwa kuliko Mkutano wa CCM unaokutanisha Wasira, Kenan Kihongosi na Wabunge 50 wa CCM, pamoja na malori 30 na matrekta 33 yakusomba watu.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Mnakumbuka mnavyo tutesa, ndivyo mtakavyo teseka, mnaona mlivyo tudharau , ndivyo mtakavyo dharauliana, mnakumbuka mnavyo tuweka jela kwa ushahidi na kesi za uongo , ndivyo mtakavyo pelekana magereza, mnajua tunavyoishi kwa hofu ? sasa ni zamu yenu.
Mnakumbuka mlivyoteka na kuua watu , sasa ile mbegu imeota kwenu. Hali yenu itakuwa mbaya sana, kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti. Bahati mbaya Nchi pia inaharibika. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Nani ajuaye? Labda Yuda hakuwa na nia mbaya sana dhidi ya Yesu. Huenda alifikiri anawapiga changa la macho Wayahudi. Alijua Yesu ni mtu wa miujiza, mwenye uwezo wa kujinasua katika hali yoyote. Pengine aliamini atachukua vipande vyake 30 vya fedha, huku Yesu akiwashangaza tena waliokuja kumkamata.
Anyway , CCM haipo tena. TUBU na karibu CHADEMA. Umetukanwa sana. Dhihaka hiyo hapaswi kufanyiwa hata Mwenyekiti wa TAWI. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Siku zote kumbuka msemo huu, ukikuta kifaranga kiko juu ya mtungi, ujue mama yake yuko jirani.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Mwenyekiti Kanda ya Magharibi Wakili Dickson Matata akikemea mapepo Mjini Kasulu.
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Puuzeni huu uzushi. Mimi ni mzima wa afya.Naendelea kukemea Serikali, mapepo na washirika wao bila woga wala kupumzika.
Zaburi 118:17. “ Sitakufa bali nitaishi, nami nitayasimulia matendo ya BWANA.” -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Acha YADA YADA wewe Sisty. Historia itawahukumu kwa ukatili mkubwa kwa kushindwa kusimama upande wa haki na demokrasia. Mnajenga nchi mbaya kwa watoto wenu wenyewe, nchi ambayo kesho itahitaji ujasiri mkubwa kurekebisha makosa mnayo yahalalisha leo.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Wanawake wa nguvu wakiwasha Moto Mpanda Mjini leo. Mh. Rhoda Kunchela - Mwenyekiti CHADEMA Mkoa wa Katavi na Mh Aida Khenani - Mwenyekiti Bawacha Mkoa wa Rukwa
Wanawake wa nguvu. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Bwana Msajili Shikamoo. Huyu Chalii katuita wahuni, mwandikie barua pls.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Mimi si mshabiki wa mpira, lakini baada ya PSG kuichapa Arsenal, nimegundua noise pollution si tatizo la viwanda pekee. PSG walifanya usafi wa mazingira hadi mtandaoni.
Jana kuna mahali nilipita nikawakuta dada fulani wamevaa jezi za Arsenal. Walikuwa na kelele na kujiamini kuliko hata zile za “Oktoba tunatiki”. Kila dakika walikuwa wanatoa uchambuzi, utabiri na walikuwa wamepiga pamba kwa kiwango cha juu kabisa. Bado kidogo ningejifanya na mimi ni mshabiki wa mpira tena Arsenal. Naamini PSG hawakushinda mechi tu… walishusha pia decibel za mijadala ya mitaani. 😄 Sasa turudi kwenye FREE TUNDU LISSU na KATIBA MPYA ni SASA. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Katika mazishi ya Baba Askofu Mungure. Askofu Mungure ni baba mzazi wa Elisa Mungure , Mwenyekiti wetu wa Mkoa CHADEMA Mkoa wa Arusha.
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Bwana Msajili, kama hamtaki tuongee na kuikosoa Serikali hamieni BURUNDI. Hapa vipi ?
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Hili nalo ni kosa ambalo natuhumiwa kulifanya kwa mujibu wa Msajili. Sasa narudia tena kusisitiza, ofisi za Serikali si duka la wazazi wenu wala mali ya familia zenu. Mkipewa mamlaka ya umma, mnapaswa kuvumilia kukosolewa, kuulizwa maswali na kuwajibika kwa maamuzi yenu. Kama hamtaki kusemwa, kuhojiwa au kuwajibika, acheni hizo ofisi mrudi mkakae na wake zenu, waume zenu na familia zenu. Mamlaka si kinga dhidi ya uwajibikaji. Na hili linamhusu kila mmoja wenu, hususani pia na wewe Msajili
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Abdul,
Pengine mengi yanayosemwa mitandaoni na mitaani dhidi yako si ya kweli. Lakini ikiwa hata asilimia ndogo tu ya yanayosemwa yana ukweli ndani yake, nakusihi uyatafakari kwa makini na kuchukua hatua mapema.
Historia inatufundisha kuwa wale wanaoshangilia na kupiga makofi juu yetu leo wanaweza kuwa mashahidi wa kwanza kesho mambo yanapobadilika. Nguvu, umaarufu na ushawishi ni vitu vya muda, havidumu milele.
Kumbuka pia kwamba nafasi na mamlaka ya wazazi wetu si ya milele, na wewe bado una safari ndefu sana mbele yako kama kijana. Hekima kubwa ni kujenga heshima, uadilifu na jina jema mapema kabla ya mazingira kubadilika.
Mungu huchelewa wakati mwingine, lakini haki yake haipotei. Ikiwa kuna jambo lolote lisilo sahihi, kurekebisha njia mapema ni busara kuliko kusubiri wakati ambao marekebisho yatakuwa magumu zaidi.
Huu ni ukumbusho wa KIMUNGU, kwa nia njema. Sijui hata kwa nini nimeandika. Lakini kesho huwa inafika. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Mahakama haziwi huru kwa kusahihisha madhara yaliyokwisha kutokea, uhuru wa kweli wa mahakama hupimwa kwa uwezo wake wa kuzuia dhulma kabla haijavaa sura ya sheria. Haki inayochelewa baada ya uharibifu kutokea si ushindi wa sheria, bali ni ukumbusho wa udhaifu wa taasisi zilizopaswa kulinda haki tangu mwanzo.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
-
Godbless E.J. Lema reposted
Richard Mabala
@MabalaMakengeza
Risasi kwa jiwe si itikio sahihi hata kidogo. Halafu walioulia many manyumbani kwao walikuwa wanatupa mawe?
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Kuna dhambi unaweza kufanya mpaka badala ya kutubu, ukajikuta unampa Mwenyezi Mungu pole.
Kwa sababu ndipo unapogundua kuwa maonyo aliyokuwa anakutumia ulikuwa huyasikii. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Yeah
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema reposted
Peter Msigwa
@MsigwaPeter
“Uovu hauwi haki
kwa sababu tu umeamriwa na mamlaka.
Unaweza kutii au ukafuata amri…
lakini bado ukawa unadhulumu na kusaliti utu wa mwanadamu.” -
Godbless E.J. Lema reposted
Josephine Marealle-Ulimwengu
@UlimwenguJm
Sikulala vizuri nikitafuta majibu! Najiuliza: baadhi ya Wa-Tanganyika hawana hata visa ya kuishi na kutembea kwa uhuru nchini kwao; wananyimwa haki ya msingi ya kutembea bila hofu ya kutekwa, kupotezwa au kuuawa, lakini hilo haliwapi hamasa ya kuwatetea. Badala yake, wanalilia visa ya Marekani 😢
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Asante sana Mwenyezi Mungu. Jina lako libarikiwe.
-
Godbless E.J. Lema reposted
Boniface Mwabukusi
@Mwabuk2Boniface
TUACHE PROPAGANDA JUU YA UHAI WA WATANGANYIKA.
Hakuna Taifa linalotuonea wala kutuingilia mambo yetu ya ndani kinyume na Sheria za Kimataifa.
Yanayotupata leo yanatokana zaidi na ujinga wetu wenyewe, ukatili wetu wenyewe, na kushindwa kuwajibika kwa mujibu wa Sheria na Katiba ya nchi.
Tumeacha misingi ya utawala wa sheria na kujigeuza kuwa miungu watu wasioguswa na uwajibikaji.
Hatuwezi kuua, kutesa, kushambulia na kupoteza maelfu ya watu halafu tukajificha nyuma ya neno “sovereignty.” Huo siyo ulinzi wa mamlaka ya Taifa; huo ni upotoshaji wa dhana ya sovereignty chini ya Sheria za Kimataifa.
Kwa mujibu wa Katiba ya Umoja wa Mataifa (UN Charter), Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiraia na Kisiasa (ICCPR), Azimio la Kimataifa la Haki za Binadamu (UDHR), Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu (African Charter on Human and Peoples’ Rights), pamoja na kanuni ya Responsibility to Protect (R2P), Mataifa yana wajibu wa kulinda uhai, utu, uhuru na usalama wa wananchi wake.
Sovereignty katika sheria za kimataifa siyo leseni ya Serikali kufanya ukatili dhidi ya watu wake bila kuwajibishwa. Sovereignty ina mipaka ya kisheria na kiutu iliyowekwa na mikataba ya kimataifa, sheria za haki za binadamu, na wajibu wa Mataifa kulinda wananchi dhidi ya mauaji, mateso, upotezwaji wa watu na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.
Pale ambapo Taifa linashindwa au linakataa kulinda haki za msingi za wananchi wake, jumuiya ya kimataifa kupitia taasisi zake halali inaweza kuchukua hatua kwa mujibu wa sheria za kimataifa ili kuzuia ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.
Ndiyo maana hatua mbalimbali zinazochukuliwa na baadhi ya Mataifa ya Ulaya, Marekani, na taasisi za kimataifa kuhusu maafa ya Oktoba 29 dhidi ya Watanganyika ikiwemo mauaji, upotezwaji wa watu, mateso, na vitendo vinavyokiuka misingi ya haki za binadamu zinaweza kuwa na msingi ndani ya mfumo wa sheria za kimataifa na wajibu wa kimataifa wa kulinda utu wa binadamu.
Tusipokuwa tayari kujiwajibisha wenyewe, tutajikuta tunawajibishwa na jumuiya ya kimataifa.
Ukweli, Haki, Utawala wa Sheria na Uwajibikaji ndiyo msingi pekee wa kulinasua Taifa letu kutoka katika mkwamo huu.
BAK MWABUKUSI
SHAMBANI BUSOKELO -
Godbless E.J. Lema reposted
Peter Msigwa
@MsigwaPeter
“Msimamo wa mwanadamu haupaswi kuwa gereza la dhamira yake.
Kuna nyakati ambapo ukimya huwa mzigo kuliko maneno.
Sidai kuwa mimi ni mkamilifu, lakini nimeamua kutii dhamira yangu kuliko kuigiza consistency isiyo na ukweli. Si busara kushinikizwa kuonyesha “uanaume wa kisiasa” kwa kubaki sehemu ambayo dhamira yako haiwezi tena kutulia” -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Ujasiri ni kusema ukweli hata pale ambapo ukimya ungekuwa salama zaidi.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Tishio la usalama wa Nchi ni maono duni na UPUMBAVU wa CCM , just imagine wewe ni Waziri wa Mambo ya Ndani.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
-
Godbless E.J. Lema reposted
Chadema Tanzania
@ChademaTZ2
#peoplespower Dodoma Mjini.
-
Godbless E.J. Lema reposted
Twaha Mwaipaya
Tayari Peter Msigwa amewasili Dodoma na atakuwepo kwenye mkutano wa leo Bonyeza link Tupo Live www.youtube.com/live/qq6j-e_xwGA
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema reposted
Peter Msigwa
@MsigwaPeter
Nimefikiri na kutafakari kwa muda mrefu baada ya matukio ya ukiukwaji wa haki, utu na dhuluma dhidi ya uhai wa binadamu yaliyotokea tarehe 29 Oktoba 2025. Siwezi kuendelea kuishi katika huzuni na ukimya tena.
Kwa dhamira yangu binafsi, leo nimejiondoa rasmi kutoka CCM na kurejea CHADEMA kwa kufuata taratibu zote za CHADEMA.
Kwa Watanzania wote, na wanachama wa CHADEMA wale walioumizwa au kukatishwa tamaa na msimamo wangu wa awali, naomba radhi kwa dhati pale nilipokuwa kinyume na matarajio yetu ya pamoja katika safari ya kutafuta haki, utu na demokrasia ya kweli.
Naam, binadamu hukosea, lakini dhamira inapozinduka ni wajibu kusimama upande unaouona kuwa wa kweli na wa haki.
Asanteni Sana. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Wow !!!
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Utasikia wakisema Dodoma imepangwa vizuri, lakini ukiitazama kwa undani, ni organized squatter tu iliyovaa hadhi ya mji mkuu.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Nitakuabudu kwa kila pumzi niliyo nayo Mwenyezi Mungu , kwa maana wewe ni MWAMINIFU sana.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
ARUSHA ASANTE SANA. Much ❤️ Always.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Blood laundry haiwezi kufuta kumbukumbu za waathirika.
Huwezi kusafisha damu mbwembwe na mitikasi. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
-
Godbless E.J. Lema reposted
Human Rights Watch
@hrw
Do you have a video or photo of someone being killed or who died during the October 29 Tanzanian election?
Upload it to this secure platform and answer the questions, and help Human Rights Watch document what happened: hrw-tanzania-evidence-uploader.portal.massive.io -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Tume ilifika KAHAMA , KATORO na GEITA ? Ile namba uliyosema inaweza kuwa sio ya mwisho pengine unaweza kuipata huko. Hakuna mbinu, mateso wala vitisho yatakayo funika damu iliyomwagika. Hakuna. Ni habari ya muda tu.
-
Godbless E.J. Lema reposted
Boniface Mwabukusi
@Mwabuk2Boniface
NADHANI SASA NI DHAHIRI NANI ANAHUSIMA NA UTEKAJI.
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Siku inakuja ambako kila ubaya utalipwa.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
David Jumbe
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Hofu haiui mwili pekee, huua pia uvumilivu wa moyo. Mwanadamu akiona ukimya haumwokoi na woga haumzuii mauti, huanza kuamini kuwa ujasiri ni afadhali kuliko kuishi kwa kutetemeka. Ndipo jamii huingia katika hatari kubwa zaidi, pale watu wanapoacha kuogopa kupoteza maisha kwa sababu tayari wamepoteza matumaini. David Jumbe hastahili hofu, mateso wala maumivu yoyote mengine.
-
Godbless E.J. Lema reposted
Peter Msigwa
@MsigwaPeter
01 one of two
“Dhamiri ni mahakama ambayo haifungwi milele.” na hatia haina kaburi,
Kuna wakati ni hatari sana kwa taifa lolote…
Pale ambapo ukimya unaanza kuwa salama kuliko ukweli.
watu wanapoanza kunong’ona gizani
mambo ambayo walipaswa kuyasema hadharani.
Na historia imetufundisha jambo moja la kuogopesha sana ,
Serikali zinaweza kuficha mafaili,
zinaweza kuficha ripoti,
zinaweza kunyamazisha mashahidi,
zinaweza kuwaogopesha wakosoaji
lakini hatia haina kaburi.
Hata kama uhalifu, kosa, au tendo ovu limefichwa, limezikwa, limefunikwa, au limesahaulika na jamii — hatia yenyewe haifi kirahisi.
Mtu anaweza kuficha ushahidi.
Serikali inaweza kuwanyamazisha mashahidi.
Historia inaweza kupindishwa.
Lakini ndani ya dhamiri ya mwanadamu, hatia inaweza kuendelea kuishi kwa miaka mingi.
Huendelea “kumsumbua” mtu kupitia kumbukumbu, ndoto, hisia, na mateso ya ndani ya nafsi kutokana na uovu alioutenda kinyume na ubinadamu.
Kwa sababu dhamiri ya mwanadamu ni mahakama ambayo haifungwi milele.”
Mtu anaweza kuukwepa mkono wa sheria…anaweza kuficha ushahidi…anaweza kunyamazisha mashahidi…anaweza kutumia mamlaka, pesa, propaganda, au nguvu kufunika ukweli…
Lakini ndani ya nafsi yake mwenyewe, bado kuna mahakama nyingine inayobaki wazi:Dhamiri.
Na tofauti na mahakama za dunia:• dhamiri haihitaji polisi,• haihitaji jaji wa nje,• haihitaji ushahidi wote hadharani.
Inajua ukweli hata pale dunia nzima inapodanganywa.
Ndiyo maana watu wengi wanaonekana kuwa na nguvu nje —lakini ndani wanaishi na hofu, hasira, usingizi mbaya, au amani iliyopotea.
Historia ina mifano mingi sana.
Mfano wa kwanza:
Baadhi ya wanajeshi waliowahi kushiriki vita vya mauaji ya raia duniani walinusurika kisheria, lakini miaka baadaye walikiri kuwa walikuwa hawawezi kulala usiku.Walikuwa wakisikia sauti za waliouawa kichwani mwao.Sheria iliwaacha huru.Lakini dhamiri iliendelea kuwafunga.
Mfano mwingine:
Katika tawala nyingi za kiimla duniani, viongozi waliotesa wananchi waliweza kuzima vyombo vya habari, kufunga wapinzani, na kuogopesha taifa lote kwa miaka mingi.Lakini wengi wao waliishi maisha ya mashaka makubwa:• waliwaogopa hata marafiki zao,• waliwaogopa walinzi wao,• waliishi wakihamisha walinzi kila mara,• wengine walikufa wakiwa na paranoia na upweke mkubwa.
Kwa nini?Kwa sababu ndani yao walijua ukweli ambao propaganda haiwezi kuufuta.
Hata katika maisha ya kawaida:Mfanyabiashara anaweza kudanganya watu na kupata pesa.Mwanasiasa anaweza kusema uongo na kushangiliwa.Kiongozi wa dini anaweza kuhubiri haki huku akiishi kinyume chake.Mtu anaweza kuonekana “amefanikiwa” mbele ya jamii.
Lakini kuna tofauti kubwa kati ya:kuwa huru nje…na kuwa huru ndani.
Ndiyo maana baadhi ya watu wana kila kitu:• pesa,• mamlaka,• ulinzi,• umaarufu…
Lakini hawana amani.
Kwa sababu dhamiri inapofungua kesi dhidi ya mtu,hakuna usingizi wa kutosha,hakuna pombe ya kutosha,hakuna sifa za kutosha,na hakuna propaganda ya kutosha inayoweza kuifunga kabisa.
Biblia pia inaonyesha hili.
Baada ya Kaini kumuua Abeli, Mungu alimwambia:“Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka ardhini.” -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Sawa bhana 😄 Dhambi zako zote zimekuwa cleared. Sasa Ijumaa 22/5 fika Releni utoe ushuhuda live 😅. Na usiwe na wasi wasi… huku hakuna nyama za matambiko 😂
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Kuna tetesi kuwa Asha Rose Migiro atastaafu kuwa KM CCM. Nafikiri nafasi hiyo inaweza kukufaa wewe zaidi na Sisty Nyahoza kuchukua nafasi ya Kiongosi. Maombi yangu yako nawe Bwashee.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Nepotism
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
A-Town nimerudi home 😎🔥
Nimetua ARUSHA leo kutokea KAHAMA, nimekutana fresh na Mkti wa Kanda pamoja na viongozi wengine pale Relini.
Tarehe 22/05/2026 Mkutano hapa A Town , yaani Makaksi wote tupo yaani😂
Kahama, Katoro na Geita wasijipe hopes sana 😅… safari hii A-Town tunataka ku-set standard nyingine kabisa.
Tutawaonyesha difference ya “mlima na kichuguu” politely tu 😂🔥 -
Godbless E.J. Lema reposted
Peter Msigwa
@MsigwaPeter
“History whispers before it screams.”
Historia ya dunia ina mifano mingi ya serikali au tawala zilizohusika katika mauaji ya halaiki dhidi ya raia wao au makundi fulani ya watu. Mara nyingi matokeo yake yalikuwa:
• kuporomoka kwa tawala,
• majeraha ya kizazi kwa kizazi,
• migawanyiko ya kitaifa,
• hukumu za kimataifa,
• au viongozi kuishi maisha ya hofu, uhamisho, au aibu ya kihistoria.
Baadhi ya mifano mikubwa ni hii:
1. The Holocaust — Ujerumani ya Nazi
Chini ya Adolf Hitler, serikali ya Nazi iliua takribani Wayahudi milioni 6 pamoja na:
• Waroma (Gypsies),
• walemavu,
• wapinzani wa kisiasa,
• na makundi mengine
2. Rwandan Genocide
Rwanda (1994)
Ndani ya siku karibu 100 tu, zaidi ya watu 800,000 waliuawa — hasa Watutsi na Wahutu.
Vyombo vya serikali, wanamgambo, na propaganda za redio vilitumika kuchochea mauaji.
Majirani waliuana.
Marafiki waliuana.
Jamii ilipasuka vibaya sana.
3. Cambodian genocide Cambodia 1975- 1979
Utawala wa Pol Pot uliua takribani watu milioni 1.5–2.
Wasomi, walimu, watu waliovaa miwani, viongozi wa dini, na yeyote aliyedhaniwa kuwa “adui wa mapinduzi” waliuawa.
Katika Cambodian genocide chini ya Pol Pot, utawala wa Khmer Rouge ulikuwa na mtazamo mkali sana dhidi ya “wasomi” na kile walichokiita ushawishi wa dunia ya kisasa au elimu ya Magharibi.
Ndiyo maana hata kitu kidogo kama kuvaa miwani wakati mwingine kilitafsiriwa kama “dalili ya usomi.”
Mantiki yao ilikuwa ya kikatili na ya kipumbavu:
* mtu anayesoma sana anaweza kuvaa miwani,
* mtu anayesoma anaweza kuuliza maswali,
* mtu anayefikiri kwa uhuru anaweza kuipinga serikali.
Kwa hiyo katika paranoia ya mapinduzi yao, hata:
• walimu,
• madaktari,
• maprofesa,
• watu wanaozungumza lugha za kigeni,
• watu waliokuwa na elimu,
• au waliokuwa wanaonekana “wa mjini”
walionekana kama maadui wa mfumo mpya.
Katika baadhi ya maeneo, watu waliuawa kwa sababu tu:
* walikuwa na vitabu,
* walijua lugha ya kigeni,
* walikuwa na taaluma,
* au walionekana “wenye akili nyingi.”
Miwani ikawa kama “alama ya kushukiwa.”
Hii inaonyesha hatari kubwa sana ya:
• siasa inayochukia elimu,
• mapinduzi yasiyo na mipaka ya sheria,
• propaganda inayogeuza kundi fulani kuwa “adui wa wananchi,”
• na mfumo unaoona kufikiri tofauti kama tishio.
Ni moja ya mifano ya kihistoria inayoonyesha jinsi hofu, chuki, na itikadi kali zinavyoweza kuondoa kabisa ubinadamu wa kawaida.
Cha kusikitisha ni kwamba wengi waliouawa hawakuwa wanajeshi wala wahalifu.
Walikuwa raia wa kawaida tu waliokuwa wamewekewa “label” ya kuwa hatari kwa mfumo.
Na baada ya miaka mingi, Cambodia iliendelea kubeba majeraha makubwa:
• upungufu wa wasomi,
• trauma ya kizazi,
• hofu ya kisiasa,
• na kumbukumbu nzito ya taifa lililowahi kugeuza wananchi wake wenyewe kuwa maadui.
4. Bosnian genocide
Katika vita vya Balkan miaka ya 1990, maelfu waliuawa kwa misingi ya ukabila na dini.
Mauaji ya Srebrenica massacre yalikuwa moja ya matukio mabaya zaidi Ulaya baada ya Vita Kuu ya Pili.
5. Stalinist purges
Soviet Union
Chini ya Joseph Stalin:
• mamilioni walifungwa,
• kuuawa,
• au kutoweka kwenye kambi za mateso (Gulag).
Watu waliishi kwa hofu kubwa.
Kukosoa serikali kulikuwa hatari.
Hoja kubwa ya kihistoria
Karibu kila mahali ambapo serikali au tawala zilifanya mauaji makubwa dhidi ya wananchi:
• ukweli ulijaribu kufichwa mwanzoni,
• propaganda ilitumiwa,
• watu waliogopa kusema,
• taasisi zilinyamaza,
• baadhi ya wananchi walitetea ukatili huo kwa sababu ya siasa au hofu.
Lakini baadaye:
• ushahidi ulitoka,
• historia ilizungumza,
• dunia ilihukumu,
• na majina ya viongozi wengi yakabeba doa la kihistoria milele.
Ndiyo maana mataifa yenye hekima hujenga:
• taasisi huru,
• mahakama imara,
• vyombo vya habari huru,
• na uwezo wa serikali kukosolewa bila kuiona jamii kama adui.
Kwa sababu damu ya wananchi inapomwagika bila haki,
athari zake zinaweza kulitesa taifa kwa vizazi. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Thank you
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
KAHAMA ASANTE SANA.
Tone Tone 0744446969 -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
“ Nilipewa chungwa , embe na nanasi , baada ya kula , tumbo langu liliuma sana, maumivu ambayo sijawahi kuyapata toka nizaliwe”
Tundu Lissu atuma ujumbe kutoka magereza. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Sugu - KAHAMA.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
UZINDUZI WA OPERESHENI KATIBA MPYA, FREE TUNDU LISSU KANDA YA SERENGETI ... www.youtube.com/live/B1Ygb_BQNMc via @YouTube
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Tuko serious sana.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Huyu mtoto niaje niaje sana 😭 anafikiri kujenga nchi ni watoto wa maboss zake kujaa serikalini na bungeni. Nepotism imekuwa ideology kwao sasa.
Tusisahau Tone Tone wajameni wananchi namba ni CHADEMA HQ 0744446969 -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Hapa ni KIWIRA leo Tarehe 17/05/2026 , hakuna kiongozi yoyote wa KITAIFA.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
GEITA ASANTE SANA. Barabara ya lami si maendeleo ya kweli. Maendeleo ya msingi na yenye maana huanza kwa kuheshimu utu wa watu, haki zao, uhuru wao na usawa wao. Mambo mengine kama lami, majengo na miundombinu yanapaswa kuwa huduma za kawaida za dola, si mbadala wa haki za wananchi
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
🔴#live: CHADEMA WANAKIWASHA GEITA MJINI MUDA HUU, WANANCHI WAJITOKEZA KW... www.youtube.com/live/LIn-qi-WIkM via @YouTube
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Kazi
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Mtungi na wale watoto wake waione.
-
Godbless E.J. Lema reposted
Martin Maranja Masese
@IAMartin_
KATORO – GEITA. Viwanja vya SATELİTE. CHADEMA tumekusanya #tonetone kiasi cha TZS 2,071,000. MSAJILI USITUTISHE. Huwezi kamwe kutupangia namna gani tushughulike na MaCCM. RUZUKU ya kiwaki HATUTAKI. Angusha TONE lako hapo kupitia 0744446969; Jina - CHADEMA HQ. #peoplespower. 👊🏾
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema reposted
ROYAL TELEVISION PLUS
@Royaltv_plus
Rais wa Chama cha wanasheria wa Tanganyika TLS Wakili Boniface Mwabukusi amesema kufanyika kwa kongamano la Jumuiya ya wanafunzi wa elimu ya Vyuo na Vyuo Vikuu Nchini (TAHLISO) likiwa na kaulimbiu ya "Never Again" bila ya kupaza sauti kuhusu uwajibikaji, haki na ukweli ni kama wimbo mrefu usiokuwa na kibwagizo na wenye kukera masikio mwa wengi.
Mwabukusi ametoa kauli hiyo leo Jumamosi Mei 16, 2026 kupitia mtandao wake wa X, siku ambayo Jumuiya ya TAHLISO inakutana Jijini Dar Es Salaam kwaajili ya kongamano hilo lenye kuzungumza na kuonyana kuhusu athari za uvunjifu wa amani Nchini, wakirejea matukio ya ghasia za wakati na baada ya uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2026 likiwa na kaulimbiu ya "Never Again".
"Kusema " Never again" bila kujua waliko wenzetu ambao baadhi ni wa hapa hapa chini ni kufuru kwa uumbaji wa Mungu, never again bila Ukweli, haki na Uwajibikaji kwa masaibu na Uuwaji wa watanganyika wa Oktoba 29 ,2025 ni Wimbo mrefu usio na Kibwagizo unaokifu na kuchosha Masikioni."
"Ukweli, haki na uwajibikaji ndiyo utakaotupa suluhisho la kudumu na suluhisho hilo ndiyo kwa mantiki yake lisema "never again otherwise (vinginevyo) ni kukebehi na kupuuza hisia za Wahanga na Uhai wa Ndugu zetu." Amesema Mwabukusi.
Mwabukusi amesisitiza kuwa ukweli, haki na uwajibikaji ndiyo dira ya kwenda kwenye muafaka na maridhiano ya kitaifa na si vinginevyo kama ambavyo wengine wamekuwa wakisema. -
Godbless E.J. Lema reposted
Twaha Mwaipaya
TWENDENI YOUTUBE HUKO KATORO GEITA NI BALAA TUKUTANE MO 29 TV MUDA HUU. LINK www.youtube.com/live/-hAbW7YlMIg
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
KATORO - GEITA.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
It looks like wana-expand, lakini pia wanatafuta mazingira yenye utulivu na usalama wa muda mrefu kwa biashara zao. Wawekezaji wakubwa huwa hawaangalii soko pekee, wanaangalia pia stability ya kisiasa, policy consistency, na uhakika wa kesho.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
“ Big dream with a bad team is a nightmare”
Nice book from John C Maxwell. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Msajili aione hii.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Epuka MATAPELI NA MAJAMBAZI sina akaunti yoyote Facebook. Hawa ni Washenzi na Matapeli.
-
Godbless E.J. Lema reposted
Peter Msigwa
@MsigwaPeter
Tanzania haihitaji hofu zaidi.
Inahitaji uponyaji.
Kwa sababu taifa lililojeruhiwa, mwishowe huanza kujijeruhi lenyewe.
Leo tunapaswa kusema ukweli
si kwa chuki,si kwa kisasi,bali kwa hofu ya kweli kuhusu mustakabali wa nchi yetu.
Kama Michael Jackson alivyowahi kusema:
“Tunapaswa kuponya dunia yetu iliyojeruhiwa. Machafuko, kukata tamaa, na uharibifu usio na maana tunaouona leo ni matokeo ya watu kujisikia wametengwa kutoka kwa wenzao na mazingira yao.”
Kauli hii kwa sasa
Inakuwa onyo hata kwetu sisi Watanzania, kama sehemu ya dunia
Wananchi wanapoanza kujisikia:
hawasikilizwi, wametengwa, wananyamazishwa, wanadhalilishwa,
au wanachukuliwa kama maadui kwa sababu tu wana mawazo tofauti.
umbali wa hatari huanza kujengwa kati ya wananchi na dola.
Na historia inatufundisha jambo moja la kuogopesha:
Mataifa mengi hayaanguki kwanza kwa sababu ya adui wa nje.
Huanzia kudhoofika ndani
wakati imani ya wananchi inapokufa.
Nchi haiwezi kujenga amani ya kudumu:
kama hofu inakuwa kubwa kuliko uhuru, kama utii unakuwa muhimu kuliko ukweli, kama taasisi zinaonekana kuwa za upande mmoja, au kama ukosoaji unatafsiriwa kama usaliti.
Kwa sababu jamii iliyojeruhiwa huzalisha wananchi walioumia.
Na wananchi walioumia mwishowe huzalisha:
hasira, mgawanyiko, msimamo mkali, kukata tamaa,au chuki ya kimya kimya.
Viongozi wanapaswa kuelewa:
si kila ukimya ni amani.
Wakati mwingine watu wananyamaza kwa sababu:
wamechoka,wanaogopa,au wamekata tamaa.
Na kukata tamaa ni hatari kwa taifa lolote.
Tanzania ilijengwa juu ya msingi imara ya : utu,umoja,mazungumzo,
uvumilivu,na hisia ya kuwa taifa ni la wote.
Julius Nyerere alielewa jambo kubwa sana,taifa haliishi kwa nguvu pekee (power)
linaishi pia kwa uhalali wa kimaadili.
Wananchi wakianza kuhisi kwamba:
haki inategemea upande wa kisiasa, ambao mtu yupo, taasisi si huru tena,
au demokrasia ipo kwenye maneno lakini si kwenye vitendo,
ule mkataba wa kihisia kati ya taifa na wananchi huanza kupasuka.
Kwa hiyo haya si mashambulizi.
Hili ni onyo.
Onyo kwamba:
siasa zinapokuwa za uhasama kupita kiasi,
mamlaka zinapoanza kuogopa ukosoaji,
wapinzani wanapoonekana maadui,
na wananchi wanapopoteza imani kwa mifumo ya taifa
taifa lenyewe huanza kujeruhiwa kihisia.
Na taifa lililojeruhiwa huwa taifa lisilo tulivu.
Hatuhitaji kulewa kisiasa zaidi.
Tunahitaji hekima.
Hatuhitaji viongozi wanaotaka kusifiwa tu.
Tunahitaji viongozi wenye uwezo wa kusikiliza ukweli usiofurahisha.
Kwa sababu uzalendo si ukimya.
Wakati mwingine uzalendo ni ujasiri wa kusema:
“Kuna jambo linaenda vibaya kabla hatujachelewa.”
Kama Tanzania inataka kubaki imara,
basi uponyaji lazima uwe sera ya taifa.
Uponyaji:
kati ya viongozi na wananchi,kati ya dola na upinzani,kati ya mamlaka na uwajibikaji,kati ya sheria na haki.
Kwa sababu hakuna taifa linaloweza kuishi milele kwa:
hofu, propaganda,au mgawanyiko wa kihisia.
Mwisho wa yote,
taifa huwa imara zaidi pale wananchi wake wanapoamini kwamba:
wao ni sehemu ya taifa,wanalindwa,
wanasikilizwa,na utu wao una thamani.
Mungu ailinde Tanzania isije kuwa nchi ambayo wananchi wanaogopana kuliko kuaminiana.
Na viongozi wetu wakumbuke:
historia haitawahukumu viongozi kwa barabara, madarasa , vituo vya afya walivyojenga pekee,
bali pia watahukumiwa kwa hali ya kihisia walizoliachia taifa.
Usisahau:
“Jamii iliyojeruhiwa huzaa watu waliojeruhiwa…
na watu waliojeruhiwa huongeza machafuko zaidi.”
Rev Petet simon Msigwa!
Iringa -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Ungekuwa baba yangu, mimi ningekuwa ni mtoto mwenye huzuni sana.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Niliona meseji hii TikTok, “Mume wangu alinicheat na msichana aliyekuwa mdogo kwangu kwa miaka mingi. Mara tu nilipogundua na tukaanza kuzungumza kuhusu hilo, alipata kiharusi na kulazwa hospitalini. Nilihisi hasira zaidi kwa sababu hata hatukuwa tumemaliza kuzungumza.”
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Harakati na siasa
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Picha kama hizi zinaonesha changamoto mbili kwa wakati mmoja: usalama wa jamii na ukosefu wa ajira. Vijana wengi wanaingia kwenye biashara za kuuza visu, mapanga na majambia barabarani si kwa sababu wanapenda, bali kwa sababu mfumo umeshindwa kuwapa fursa salama na zenye heshima za kujipatia kipato.
Lakini pia hatuwezi kupuuza hatari yake. Vifaa vyenye ncha kali kuuzwa kiholela kwenye foleni na maeneo yenye msongamano mkubwa ni tishio kwa usalama wa wananchi. Suluhisho si kukimbizana na machinga pekee, bali kujenga uchumi unaotoa ajira za kweli, mafunzo ya ujuzi, mikopo yenye tija, na mazingira rasmi ya biashara. Vijana wakikosa matumaini ya kazi na mfumo ukikaa kimya, barabara ndiyo hugeuka soko la kila kitu, hata vitu vinavyoweza kuhatarisha maisha ya watu. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Tumefika mahali ambapo kuokota maiti imekuwa jambo la kawaida kuliko kuokota pesa. Hii si dalili ya umaskini wa uchumi pekee, bali ni umaskini wa utu. Jamii isiyoguswa tena na maumivu ya watu wake hupoteza hata asilimia ndogo ya huruma. Tunaishi karibu na watu wengi, lakini mbali sana na utu.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Dini inapogeuzwa kuwa chombo cha kutawala akili za watu badala ya kuongoza roho zao kuelekea kwenye ukweli na utu, hugeuka biashara ya hofu. Watu huanza kuishi kwa woga badala ya imani, wakiamini kuwa sauti kubwa za madhabahuni ndizo kipimo cha ukweli. Lakini ukweli haupimwi kwa kelele za mahubiri, wala kwa ukubwa wa mikusanyiko, unapimwa kwa matendo ya maisha.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Ukichelewa, mwingine atachukua nafasi yako.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Siasa zina gharama. lakini gharama ya kukaa kimya ni kubwa zaidi. Mabadiliko hayafadhiliwi na maneno pekee. Yanahitaji kujitoa, uthubutu, na support ya wananchi wenye IMANI na nchi yao.Changia leo kusaidia operation za chama nchi nzima. Tafadhali usiupite ujumbe huu bila kufanya chochote. Just be concerned.
TAFAKARI, gharama wanazolipa walioko mbele ya mapambano haya kwa ajili ya nchi yetu. Fikiria sacrifices, muda, mateso, na jinsi walivyoweka maisha yao rehani kwenye haya mapambano kwa ajili ya Watanzania wote. Je, wewe kweli unashindwa kuchanga chochote kwa ajili ya kazi hii muhimu na bora sana kwa kizazi cha sasa na hapo baadae.
Tafadhali tunakuomba ujali , kwani mchango mdogo unaweza kufanya tofauti kubwa. Pls do something. We need your support. Hatuna ruzuku, lakini tuna IMANI pamoja na wewe. Usiseme mtu fulani atafanya , huyo mtu fulani ni wewe.
Mungu akubariki sana. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Zina harufu ya damu pengine.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Free TUNDU LISSU Now.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Kadri ninavyozidi kukua na kuona mengi ya maisha, ndivyo ninavyozidi kuelewa kwa nini baadhi ya watu huchagua kuishi mbali na kelele za dunia , maisha ya utulivu, faragha, na amani ya moyo.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
“Kumekuwa na majaribio na vitisho kutoka kwa watawala kunizuia nisiongee. Kuna wakati niliambiwa nizime simu yangu, nisiitumie mpaka (wao) watakapo niambia. Nikawauliza, kwa sheria gani? Kuna wakati nilikaribishwa mahali fulani, nikapigiwa simu na watawala, wakasemam mzee usiendee kwenye huo mkutano. Kwanini? Hauna manufaa. Nikawauliza, nani anaamua hayo manufaa? Nikakataa. Wakawafuata watu walio karibu na mimi ili wanishawishi nisiende, nikakataa pia. Mnakumbuka nilifanya mahojiano hapa na Jamhuri? Wakatoa summary, wakasema watachapisha mahojiano yote, neno kwa neno. Baadae Jamhuri wakanieleza wamezuiwa wasitoe yale mahojiano. Kuna viongozi wanaogopa kuzungumza na mimi, wanatuma ujumbe kupitia mbali huko. Marafiki zangu wanaogopa wakisema nitatekwa au kupewa sumu. Nawaeleza mimi ni mali ya Mungu, ndiye atakayeamua lini ananihitaji.”
— Jaji Mstaafu Joseph Sinde Warioba, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais Tanzania. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Watoto wako wana baba mwema na mzuri sana. Mungu akubariki sana Mzee Warioba.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Nakubaliana na wewe, lakini zaidi kwa wauawaji na wezi wa utawala na mali za umma , maana imeandikwa kutoka katika Kitabu cha Isaya 57:20–21 “ Lakini waovu wanafanana na bahari iliyochafuka, isiyoweza kutulia… Kwa waovu hakuna amani.”
-
Godbless E.J. Lema reposted
Tito Magoti
@TitoMagoti
"Uchaguzi uliopita, tulipata rekodi ile [98%] kwa sababu Tume ilipiga kura." - Jaji Joe Warioba.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Ni muhimu wananchi na wanachama wa vyama vya siasa, ikiwemo vyama vyenye wafuasi wengi kama CHADEMA, kuelewa kuwa nguvu ya mabadiliko pia inategemea uwezo wetu wa kuchangia na kujitolea kifedha kwa shughuli za pamoja. Kwa uhalisia, tuna uwezo mkubwa wa kuchangisha fedha ikiwa tutakuwa na nidhamu ktk wajibu huu.
Tatizo kubwa tulilonalo si ukosefu wa fedha pekee, bali ni changamoto ya mtazamo (mindset) na vipaumbele vyetu. Tunaweza kuchangisha mamilioni ya shilingi kwa sherehe na shughuli za kifahari, lakini tunashindwa kuchangia kiasi kidogo kwa ajili ya kusaidia wakati mwingine wagonjwa au kuimarisha harakati za haki na maendeleo.
Hili linaonyesha wazi kuwa changamoto yetu kubwa ni fikra zetu zaidi kuliko hata masuala ya kikatiba. Tukibadilisha mtazamo wetu, tutaweza kujenga nguvu ya pamoja inayoweza kuleta mabadiliko ya kweli.
Tunaomba kuwe na moyo wa kujitolea kifedha kwa wote wanaotaka kuona haki, maendeleo na demokrasia ya kweli nchini. Inaumiza na kutesa nafsi sana kuomba pesa kwa jamii ambayo inapaswa kujua kuwa kuendesha vyama vya siasa kama CHADEMA ni wajibu wao. Hapa , usiandike Mh tuko pamoja. Changa pesa Mangi !! -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Kupanda kwa gharama za mafuta nchini kumeendelea kuongeza ugumu wa maisha kwa wananchi wengi. Angalau basi, punguzeni tozo na kodi kwenye mafuta ya dizeli, kwani dizeli inapopanda bei, gharama za usafiri wa umma, usafirishaji wa bidhaa na huduma mbalimbali hupanda pia. Hii ni kwa sababu dizeli ndiyo mafuta yanayotumika zaidi katika sekta ya logistics, mabasi, malori na shughuli za uzalishaji.
Mojawapo ya njia nzuri ni kupunguza au kuondoa baadhi ya kodi na tozo kwenye mafuta ya dizeli ili kushusha gharama za usafiri na bidhaa muhimu sokoni. Hatua hiyo itasaidia kudhibiti mfumuko wa bei na kuimarisha shughuli za biashara na uchumi kwa ujumla.
Uchumi imara huanza na maisha nafuu kwa wananchi wake. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
AI 😂😂😂😂😂😂😂
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Uyole Mbeya.
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Anaandika Askofu Bagonza
Kutumia sovereignity kama njia ya kutoruhusu maoni ya nje ni sawa na:
1. Baba anayempiga mkewe kwa madai kuwa alitoa mahari na ni mke wake siyo mke jamii. Baba huyu anaweza sema “mtoto ni jamii lakini mke siyo wa jamii”.
2. Baba mkatili anayembaka mtoto wake kwa madai ya kuwa ni mtoto wake na hakuna mwenye ubia naye.
3. Mtu anayekula kinyesi chake kwa madai kuwa ni chake kimetoka tumboni mwake.
UKWELI ni kwamba mipaka ya bandia baina ya mataifa imeondolewa na utandawazi. Ni rahisi kumzuia mtu asivuke mpaka lakini ugonjwa wake hauhitaji visa kuvuka.
Dhana ya sovereignity imehama toka mipaka ya ardhi kwenda kwenye sovereignity ya mtu, kundi au hata maslahi.
Uhuru wa taifa haupimwi tena kwa bendera, wimbo wa taifa wala nembo ya taifa. Uhuru unapimwa kwa kigezo cha mchakato wa kupunguza vipunguza uhuru katika maisha ya watu. Kwa vidhibiti vichache maana yake ni HURU ZAIDI, na vidhibiti vikiwa vingi ni UHURU KIDOGO hata kama bendera inapepea mlingoti mzima na nusu.
Wajaluo husema, “Tabia ya bibi kizee wa kijaluo kupenda kula sana chakula kwa kisingizio cha kuwa alilima mwenyewe, ilimfanya awe na kitambi ndipo akasingiziwa kuwa ni mja mzito”.
Sovereignity and accountability are friends like Wajaluo na kamongo. -
Godbless E.J. Lema reposted
Reuters Africa
@ReutersAfrica
Nigerian billionaire Aliko Dangote is looking at Kenya as the site of a 650,000-barrel-a-day oil refinery that he intends to build in East Africa, the Financial Times reported on Sunday, citing an interview with him. www.reuters.com/world/africa/africas-richest-man-dangote-…
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Inafikirisha sana.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Mateso mnayopata ni halali yenu.
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema reposted
Joseph Mbilinyi
@TheRealJongwe
Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyasa nitakuwa Uyole Jumapili hii pamoja na Viongozi wengine wa ngazi mbalimbali za chama…Ni mkutano wa hadhara na Wananchi wote wa Mbeya Mjini njooni tuendelee tulipoishia…✌🏾✌🏾
#limwenyekiti #nyasampya #freelissu -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Kuishi maisha ya haki si jambo gumu kuelewa, ingawa linaweza kuwa gumu kulitenda. Mara nyingi tunajua kilicho sahihi uaminifu, nidhamu, wema, uwajibikaji na kujitawala. Changamoto si kukijua kilicho sahihi, bali ni kuishi hivyo kwa uthabiti, hasa wakati maisha yanakuwa magumu au majaribu yanapotokea. Maisha ya kweli na haki yanahitaji nguvu, uvumilivu na wakati mwingine kujitoa sadaka. Ndiyo maana yanaweza kuwa magumu, lakini msingi wake unabaki kuwa rahisi.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Pia tuliongea kuhusu Tume ya Jaji Chande Mwananchi.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Nipashe nawasalimu. Tume ya Chande pia tumeongelea. Nawakumbusha tu, wala hakuna ugomvi. Good night Nipashe.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Arusha, asanteni sana. Baada ya muda mrefu bila kukutana, leo mmekuwa mashuhuda wa upendo wa demokrasia na haki katika nchi yetu. Pamoja na hofu iliyojengwa juu ya maumivu makali, mateso na mauaji, bado mmejitokeza kwa matumaini makubwa.
Mungu awabariki . Love you sana. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Asante Mwenyezi Mungu sana.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Tunaendelea kukemea MAPEPO . LIVE: SOKO KUU ARUSHA, LEMA ANAFUNGUKA MAZITO! www.youtube.com/live/KnjaBOjJjBI via @YouTube
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Human rights MEPs mission to Tanzania cancelled after authorities decline visit | News | European Parliament www.europarl.europa.eu/news/en/press-room/20260507IPR4290…
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Ukosoaji ni kinga ya taifa dhidi ya makosa yanayoweza kuwa kawaida.
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Kesho IJumaa Soko Kuu Arusha.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Nina wasiwasi. Huyu mtuhumiwa anaonekana very smart, strategic na sharp. Lakini namna anavyoomba msamaha mbele ya RC… mmmh. Naguna kabisa.
Pengine hakuna sinema yoyote; labda tu nimeathiriwa na movies za CIA na Mossad ambazo nimekuwa nikiziangalia sana. Maana mara nyingine unaanza kuona patterns, narratives na hidden motives kila mahali.
Lakini bado, kuna kitu hakikai sawa. Mtu ambaye anaonekana composed na calculated, ghafla awe mnyenyekevu kiasi hicho mbele ya mamlaka , naturally inafanya watu waulize maswali,
Je, ni hofu ya kawaida?
Ni pressure?
Ni survival instinct?
Au kuna narrative fulani inatengenezwa?
Sina majibu. Nauliza tu. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Kesho haitatusamehe!!
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema reposted
Chadema Tanzania
@ChademaTZ2
TAARIFA KWA UMMA
-
Godbless E.J. Lema reposted
Chadema Tanzania
@ChademaTZ2
"Mpaka leo hii, agizo hilo la Mahakama Kuu halijatekelezwa na Jeshi la Polisi linalojigamba kuwa linatenda kazi zake kwa uweledi na umahiri mkubwa. Lakini kwa Tume ya Chande ukiukwaji huu wa makusudi wa amri ya Mahakama Kuu kwake si tatizo kwa kuwa umefanywa na Jeshi la Polisi! Sasa inashangazaje kuona wananchi ambao wamekosa haki zao za msingi, ambazo kwa kweli hazihitaji hata kubishaniwa au kujadiliwa kwa sababu katika nchi ya kidemokrasia lazima ziheshimiwe na kuenziwa, wanapoamua kuandamana kuzidai na huku wakitambua kuwa uchaguzi hutokea mara moja tu katika kipindi cha miaka mitano na kuwa haki hiyo ikipotea itabidi wasubiri miaka mingine mitano! Je hiyo inahitaji mtu awe mtaalamu wa sayansi ya roketi (rocket scientist)?." Dkt. Rugemeleza A.K. Nshala Mwanasheria Mkuu-Chadema
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
-
Godbless E.J. Lema reposted
Chadema Tanzania
@ChademaTZ2
"Kauli za ajabu na kutisha." Dkt. Rugemeleza A.K. Nshala Mwanasheria Mkuu-Chadema
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema reposted
David Maraga
@dkmaraga
As Chief Justice, I cherished the brotherly bonds within our East African Jumuiya and worked closely with my colleagues in the Tanzanian judiciary in the shared pursuit of justice and the rule of law.
I am therefore deeply disturbed by the remarks attributed to Her Excellency President Samia Suluhu during President Ruto's address to Tanzania's National Assembly.
It is regrettable that the two presidents are reported to have discussed coordinating efforts to "chapa mikwajo" the Gen Z across Kenya and Tanzania.
These remarks are abhorrent.
They come barely a week after President Suluhu received the report of the Commission of Inquiry into killings during and after Tanzania's 29 October 2025 general elections, in which more than 518 people lost their lives, primarily from gunshot wounds.
To date, not a single person has been held accountable.
We must also not forget that our compatriot Boniface Mwangi, and Agather Atuhaire of Uganda, were tortured on Tanzanian soil. The perpetrators remain free.
Citizens of East Africa must speak up. The axis of tyranny that Presidents Suluhu and Ruto are constructing threatens to return our region to autocracy.
As I demonstrated through my solidarity appearance in Dar-es-Salaam on 19 May 2025, standing with opposition leader Tundu Lissu, our East African Jumuiya cannot advance while leaders suppress dissent and trample on the basic rights of our people.
#ukatibamovement #ukatibandiotiba -
Godbless E.J. Lema reposted
Deogratias #FreeTunduLissu🇹🇿 Munishi
@DeoMunishi
On Tundu Lissu, the @idualliance
calls for his immediate & unconditional release.
The #idu also demands that all politically motivated charges against him be dropped and that his fundamental rights be fully respected.
#freetundulissu
#standwithtundu
idu.org/idu-resolution-on-tundu-lissus-detention-and-tanz… -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
MUHIMU.
LIVE: Dr. NSHALA ANAFANYA UCHAMBUZI WA HOTUBA YA TUME CHANDE www.youtube.com/live/_CHwFVdSmlA via @YouTube -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
“ Sikiliza Albart , hili ni tukio la kumpa heshima Prof Jay na ni starehe kwa watu wote , nikiingiza siasa hapa , nyie CCM mpo na CHADEMA wapo, itabidi na Mnyika au Heche aje kuongea hapa , kitakachotokea hapa, kesho utafukuzwa kazi, halafu uanze kulilia. Matako yako”
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Ukatili hauanzi kwa tendo kubwa la mwisho, huanza kwa ukimya mdogo unaorudiwa. Jamii inaposhuhudia maumivu ya mwingine na kugeuza macho, si kwamba imekubaliana waziwazi, bali imeanza kuzoea. Na mazoea ndiyo hatari zaidi, kwa sababu huondoa mshangao, huua huruma, na polepole hubadilisha kilichokuwa kisichokubalika kuwa cha kawaida.
Kuna mvutano wa kimaadili kati ya hofu na wajibu. Mwanadamu ana haki ya kujilinda, lakini pia ana wajibu kwa wengine. Tunapochagua kimya kwa sababu ya hofu, tunakuwa tumelinda nafsi zetu kwa muda mfupi, lakini tumeweka hatarini utu wa pamoja kwa muda mrefu. Hapo ndipo jamii huanza kupoteza mwelekeo, si kwa sababu watu waovu ni wengi, bali kwa sababu wema umechagua kukaa pembeni.
Hata hivyo, si sahihi kuwalaumu wote kwa uzito mmoja. Wapo wanaopaza sauti, wanaotafuta haki, na wanaobeba gharama ya kusema ukweli. Hawa ndio chembe za dhamiri ya jamii, ukumbusho kwamba utu haujafa, umejeruhiwa tu. Swali la msingi si nani alaumiwe zaidi, bali ni kwa kiwango gani kila mmoja yuko tayari kubeba sehemu yake ya wajibu.
Haki si tukio, ni mchakato unaohitaji ujasiri wa kudumu. Ikiwa ukimya ndio ulioruhusu ukatili kuota mizizi, basi sauti hata ndogo ndiyo itakayouondoa. Na pengine hapo ndipo tumaini linapoanzia, katika uamuzi wa mtu mmoja mmoja kukataa kuzoea kile ambacho hakipaswi kuwa kawaida. Kifo hiki kinasikitisha sana, lakini imekuwa kawaida kwa Nchi yetu. -
Godbless E.J. Lema reposted
Tito Magoti
@TitoMagoti
James Temba ameuwawa kikatili sana. Alitekwa - ndugu wametafuta bila mafanikio. Jana mwili umekutwa mtoni Tabata hauna kichwa. Haya mambo yanaogopesha, yanaudhi sana.. nani yuko salama? Nani atahakikisha usalama wetu. RIP James Temba.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Pengine kichwa cha habari kilipaswa kuwa “ VICOBA 13 ndani vya CCM vyapinga uundwaji wa tume kutoka nje ya Nchi.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Maazimio ya KAMATI KUU
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Katibu Mkuu CHADEMA akisoma maazimio.
-
Godbless E.J. Lema reposted
Peter H. Diamandis, MD
@PeterDiamandis
Sundar Pichai just said data centers in space will be "the new normal" within a decade. @elonmusk has been saying this for years. When the CEO of Google starts agreeing with Elon, pay attention. The orbital compute era is closer than you think.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Trump nominee takes hard line on Tanzania as Congress tees up penalties www.theafricareport.com/416737/trump-nominee-takes-hard-l…
-
Godbless E.J. Lema reposted
Rugemeleza Nshala
@rugemeleza
The killings carried out in Tanzania were and are shocking to the human conscience. They were not ethnic violence pitting one ethnic group against another rather state security forces firing live bullets on peaceful protesters. Yet the illegal and power grabbing government of Samia wants them to be forgotten as if those killed were ants.
Julian Pecquet
@JulianPecquet
Trump's pick for Ambo. to #tanzania vowed that electoral violence "won't be swept under the rug" if he's confirmed
Meanwhile top @SFRCdems @SenatorShaheen announced that she's teeing up legislation mandating a review of ties
My latest @TheAfricaReport:
www.theafricareport.com/416737/trump-nominee-takes-hard-l… -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Nitakuwepo ku support your coming back Prof Jay. God is so good kukuona tena kazini. Praise God Always.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Takribani mwaka mzima Chama chetu hakijakutana, na leo Kamati Kuu imekutana Dar es Salaam. Majadiliano ya msingi ni muhimu kila wakati, hasa katika kipindi hiki ambacho nchi inapitia huzuni kubwa kufuatia matokeo ya Tume ya Jaji Chande.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Just imagine , matusi tu yanawaumiza kwa kiwango hiki mpaka unatoka hadharani kupiga ukunga. Imagine mke , baba , mtoto , ndugu wa yule aliyetekwa au kuuwawa atakuwa anaumia kwa kiwango gani ? Pole sana.
-
Godbless E.J. Lema reposted
MCHAMBUZI MEDIA
@Mchambuzi5
No reform No Election ilipangwa tangu 2023 Kabla Lisu hajawa Mwenyekiti,walipoona yupo siriaz wakakimbia chama
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Nilitoa mawazo haya Bungeni, lakini yakapuuzwa. Ninaamini ni wazo jema kubadili matumizi ya eneo hilo, kwa sababu kwa hali ya sasa haiwezekani tena pale kuwa kiwanda cha matairi. Hata hivyo, jambo hili linapaswa kushughulikiwa kwa uwazi, uadilifu wa hali ya juu na weledi, la sivyo scandal haiwezi kuepukika.
Ni idea nzuri, na nitakuwa nafuatilia kwa makini na kwa ukuda mpango huu. Hofu yangu pia msije mkajenga frame za maduka kama nyumba za njiwa. Kwa kuwa mara nyingi standards zenu kwenye quality zimekuwa za kushangaza, ni muhimu safari hii mkazingatia classy kwenye eneo hilo katikati ya Jiji la Arusha lenye ukubwa takribani wa heka 77. Lakini pia , naogopa isije kuwa pia ni mkakati wa kupewa mtu mmoja kwa njia za hila. -
Godbless E.J. Lema reposted
Joseph Mbilinyi
@TheRealJongwe
Hii ni Nkasi jana kikao cha ndani, tena Kirando huko! Najivunia sana kuwa Mwenyekiti wa Kanda ya Nyasa, pia najivunia tuna mtu imara kabisa my sister Mh. Aidah mkoa wa Rukwa!
#strongertogether -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Katika hili la kuwaita wananchi Nguchiro, umepatia kabisa. Fikiria Taifa ambalo maelfu wameuawa, lakini hakuna hatua. Taifa ambalo uongo na uhuni vimegeuzwa sifa, hata baadhi ya viongozi wa dini wakivisujudia kwa sababu vinatoka serikalini.
Taifa ambalo watu wanatekwa, wanapotezwa na kuuwawa, lakini kelele za ushabiki wa Simba na Yanga zinafunika vilio vya damu za wasio na hatia. Taifa ambalo ripoti za CAG zinaanika wizi wa mabilioni, lakini jamii haina hasira, haina msimamo, haina maamuzi.
Tumefikia mahali maovu yanakuwa habari za kawaida, ukatili unakuwa jambo la kupita, na unafiki unaitwa uzalendo. Hapa si wananchi tena, hapa ni kundi lililozoea minyororo yake.
Kwa hiyo ndiyo, kwenye hili umefikiri vyema, sisi ni NGUCHIRO, tunatazamishwa, tunanyamazishwa, na bado tunashangilia. Kuna wakati kumbe unaweza kuwaza vyema. Hapa umewaza vyema. NGUCHIRO tukuache. Thx Bro!! -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
VICOBA 12
-
Godbless E.J. Lema reposted
Rose Mayemba
@rose_mayemba
Yaani wameua, halafu wanaagizana kuchunguzana wenyewe.
Haya ni maumivu juu ya maumivu kwa watanzania.
@godbless_lemaThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Hii ni sauti ya wananchi
Thank you Clara.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema reposted
Tausi Likokola
@tausilikokola
www.reuters.com/world/africa/tanzania-inquiry-says-over-5…
I took a day to collect my thoughts after reading Justice Chande’s report on the events of October 29.🇹🇿
Haven’t read it all than what has been shared publicly. Not because I expected the full truth to emerge-given that the commission itself was appointed by the very government widely viewed as the primary suspect-but because I still held on to a small expectation of basic humanity. At the very least, this report could have acknowledged the pain of grieving families. Instead, it has deepened that pain. What was presented as a national effort to establish truth, instead, deliver the opposite- in narrative control. The report is being referred to as Samia report, rather than a people’s report. That alone tells about ownership, objectivity, and purpose.
Under international human rights law-particularly standards outlined in the UN’s Protocol on the Investigation of Potentially Unlawful Death-any investigation into state-related killings must be independent, impartial, thorough, and transparent. A government effectively investigating itself, through a body it appoints and influences, creates a clear conflict of interest. Yaani-haikubaliki kujichunguza.
No entity can be both the subject of an investigation and the authority controlling that investigation without compromising its legitimacy. This is a widely recognized principle across legal systems globally. The composition of the committee only reinforces these concerns. When individuals connected-directly to the current administration are tasked with examining allegations against that same administration, the outcome appears predetermined.
Even more troubling is the emotional tone-or lack thereof. Previous official statements already failed to give families space to mourn. Wengine wamekosa miili ya wapendwa wao kuzika-sad. This report goes further, adding frustration to grief.
Reports from some of those present during Chande report reading, especially members of the diplomatic community, suggest visible dissatisfaction. Some reportedly left early, declining even symbolic gestures like group photos. Conversations circulating among embassies point to disappointment and concern. That signals that international community is dissatisfied-well, as they should.
One notable shift, however, is the acknowledgment that hundreds of people were killed. That admission alone raises urgent and unavoidable questions:
Who are these individuals?
Where are they buried?
Who authorized the use of such force against civilians?
These questions-go to the heart of accountability for violations of the right to life, which is protected under both Tanzania’s Constitution and international frameworks such as the International Covenant on Civil and Political Rights (ICCPR), to which Tanzania is a party. Time will demand answers. We will demand answers and justice.
Inside the country, the space to question these narratives are limited. Many are forced into silence or exile to speak openly. In such an environment, expecting a fully independent domestic process is unrealistic.
That is why calls for an independent, internationally supported investigation are important- necessary steps toward credibility and justice. History has shown that where domestic systems are compromised or perceived to be so, international mechanisms can help restore trust and ensure accountability. This is a painful moment for Tanzania. Truth delayed is painful-but truth denied is dangerous.
This is not over. We demand justice for the lives lost, the full truth of what happened, and real accountability for those responsible.
@SenateForeign @HouseForeign @StateDept @USAmbUN
@SenatorMenendez @SenatorRisch @RepMcCaul @RepGregoryMeeks @ChrisCoons @SenatorCardin @SenatorBooker @RepSaraJacobs @RepIlhan @RepBarbaraLee
@hrw @amnesty @fidh_en @freedomhouse @CIVICUSalliance @RSF_inter @ICJ_org @UNHumanRights
@Reuters @AP @BBCWorld @BBCAfrica @CNN @cnni @AJEnglish @France24_en @nytimes @guardian @NPR -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
“ Msiogope, maana mimi nipo pamoja nanyi.”
Isaya 41:10 -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
TAARIFA FUPI YA CHAMA.
-
Godbless E.J. Lema reposted
Mpale Mpoki
@MpaleMpoki
Ushahidi wowote unaotolewa bila madodoso (cross examination) hauna thamani ya kiushahidi (of no probative value)
Hao watu wanaotuhumiwa hawakuitwa kujieleza mbele ya tume (right to hearing)
Nashangaa tume yenye Majaji Wakuu wawili iliwezaje kuendelea pasi kuzingatia hayo
millardayo
@millardayo
Mwenyekiti wa Tume iliyoundwa na Rais Dkt. Samia kuchunguza matukio yaliyojitokeza wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu October 29,2025, Jaji Mstaafu Mohamed Chande Othman amesema kwa mujibu wa ushahidi uliowasilishwa kwenye Tume matukio ya ghasia za October 29, yalikuwa na lengo la kuzuia na kuvuruga Uchaguzi Mkuu wa October 29 ambapo lengo hili linadhihirishwa kupitia vitendo vya Wafanya ghasia ikiwemo kuharibu vituo vya kura.
Jaji Mstaafu Chande amesema hayo wakati akiwasilisha Ripoti ya Tume hiyo mbele ya Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan leo April 23,2026 Ikulu Jijini Dar es salaam.
“Kwa mujibu wa ushahidi uliowasilishwa kwenye Tume matukio ya ghasia za October 29 yalikuwa na lengo la kuzuia na kuvuruga Uchaguzi Mkuu wa October 29, lengo hili linadhihirishwa kupitia vitendo vya Wafanya ghasia ikiwemo kuharibu vituo vya kura, kuwashambulia Polisi na Wasimamizi na Wananchi, kupora mali, na waliopiga kura wakawa na alama za wino walikatwa vidole na wengi walilipwa fedha ili wajinusuru kufanyiwa hivyo”
“Pili ghasia hizo zilifanywa ili kufikisha ujumbe kwa Serikali kuwa Vijana wanataka kusikilizwa na kutatuliwa changamoto zao, ilibainika kuwa Waratibu wa ghasia walitumia malalamiko ya Wananchi dhidi ya Serikali wakati wanawashawishi kufanya ghasia”
#millardayoupdates -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Ndiyo
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
ANAANDIKA MWANASHERIA MKUU WA CHADEMA
DR. @rugemeleza
Kwa vyovyote itakavyotolewa na kusema Tume ya Jaji Chande Othmani Juu ya Vurugu na Mauaji ya October 29, 2025 ni batili na haramu tokea ilipoundwa. Kwa sababu zifuatazo:
1. Imeundwa na Samia Suluhu Hassani ambaye ndiye mtuhumiwa namba Moja kwani ndiye alitoa amri ya kuwapiga risasi waandamanaji na watu ambao hawakuwa waandamanaji.
2. Samia alisema wakati wa Kampeni haramu za Udanganyifu Mkuu kuwa wanaosema hakutakuwa na uchaguzi wakumbuke kuwa yeye ndiye Amiri Jeshi Mkuu na kuwa hakutakuwa na nywinywi wala nywinywinywi.
3. Waandamanaji hawakuwa na silaha za moto ajabu yake walipigwa risasi kinyume kabisa na taratibu za kimataifa na nchi yetu za kukabiliana na waandamanaji ambazo ni matumizi ya mabomu ya machozi, maji ya kuwashawasha, hewa ya pilipili na ikilazimika risasi za plastiki.
4. Kuwekwa kwa zuio la kutoka nje na kutembea lililotangazwa na IGP Camillius Wambura ilikuwa kinyume Cha Sheria kwani hana mamlaka hayo.
5. Kuzimwa Kwa mtandao wa intaneti kwa siku sita ilikuwa kinyume Cha Sheria. Kwa kuzimwa kwake mauaji mengi yalitokea na yalisababisha watu kutokupata taarifa za kiwakati juu ya maovu makubwa yaliyofanywa na vyombo hivyo vya dola.
6. Kuzimwa kwa mtandao na zuio la kutoka nje sehemu nyingi za nchi yetu ilimaanisha hata wafanyakazi na mawakala wa Tume ya Udanganyifu Mkuu ya Jacobs Mwambegele haikuwa na uwezo wa kupata matokeo ya uchaguzi huo haramu. Ajabu yake Mdanganyifu huyo Mkuu asiyeheshimu kazi na maadili ya ujaji akatangaza matokeo kama kwamba uchaguzi ulifanyika na kura kuhesabiwa na matokeo kutangazwa katika Kila kituo na hatimaye kutumwa kwa Tume hiyo haramu!
7. Stargomena Tax ambaye alikuwa Waziri wa Ulinzi katika serikali ya Samia wakati wa udanganyifu huo ni mjumbe katika Tume hiyo ya Chande! Ni kanuni ya kisheria na haki kuwa huyu ana mgogoro wa kimaslahi na ni sehemu ya waliopaswa kuchunguza imekuwaje akageuka kuwa mchunguzi.
8. Jaji Othmani Chande na Jaji Ibrahimu Juma wanajua, kama wajuavyo wanasheria na wasomi wote, kuwa huwezi ukawa hakimu au muamuzi katika kesi yako mwenyewe(Nemo judex in causa sua) sasa imekuwaje wawe katika Tume ambayo ina kasoro hii kubwa? Je, si inafahamika kuwa pale Tume inapokuwa na kasoro hiyo yote iliyoyafanya hata kama ni mazuri, kisheria Huwa batili?
9. Wakati Tume inaanza kazi Samia ametoa matamshi ya kuingilia kati au kutoa majibu kwa Time ikiwa ni pamoja na kusema "nguvu iliyotumika ilikuwa sahihi" na kuwa "kwa nini wazazi hamkuwazuia watoto wenu kutoka nje?". Sasa hapo nini kinachunguzwa?
10. Tume ilizuia uwazi wa watu waliotoa maelezo yao kwa kuvikataza vyombo vya habari kuendelea kutoa maelezo ya waathirika wa mauaji hayo ya kinyama yaliyofanywa na vyombo vya dola. Kukosekana kwa uwazi ulikuwa mkakati wa kuleta giza na kuzuia ukweli wa mauaji hayo kufahamika na hivyo kile kitakachosemwa na Tume kuwa eti ndicho kilichosemwa na waathirika kichukuliwe kuwa ni cha ukweli.
11. Tume yenyewe imeanza kampeni ya kuuandaa umma kupokea ripoti yake na imekuwa na wasemaji wake. Hiyo inaashiria nia mbaya ya Tume hiyo.
Ni kwa msingi na sababu hizo nasema kuwa Tume hiyo ni batili na chote kitakochotolewa nayo ni batili. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Nimeona watu kadhaa ambao ni hatari sana kwa heshima ya Mh Lissu, wengine ambao walikuwa wanasiasa mashuhuri na wanaishi Dar, na hawajawahi hata kukanyaga mahakamani, ghafla wamekuwa “mashabiki” wa uhuru wake kwa spinning ya hoja ambayo inatengenezwa kumshushia heshima yake.
Mh Lissu ana heshima kubwa sana kisiasa nchini kuliko mwanasiasa yoyote. Kama risasi na jela zilitumika kummaliza zikashindwa, mkakati mpya sasa ni kujaribu ku–scale down heshima yake iliyojengwa juu ya misimamo inayobeba haki. Kazi hii inafanyika kwa bidii sana. Hata hivyo, mkakati umekosewa mpaka sasa, maadui zake hawakupaswa kutoka kuwa wapambe wake ghafla. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Kuna tofauti kubwa sana kati ya “ Tufanye Sex kwanza ndio tuowane na Tuowane kwanza ndipo Tufanye Sex .
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Tone Tone IMERUDI.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola, Mheshimiwa Dkt. Lazarus McCarthy Chakwera, Rais wa zamani wa Jamhuri ya Malawi, amekamilisha ziara yake katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Akiungwa mkono na wafanyakazi wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Madola, ziara hii ilifanyika kufuatia ombi la Mkutano wa 71 wa Kundi la Hatua za Mawaziri wa Jumuiya ya Madola (CMAG), ulioweka Tanzania katika ajenda rasmi ya CMAG.
Mjumbe Maalum alipewa jukumu la kushirikiana na wadau wote ili kuimarisha maadili na misingi ya Jumuiya ya Madola, ikiwemo uhuru wa kukusanyika, kujieleza na vyombo vya habari; kubaini mbinu zinazowezekana za kuanzisha jukwaa la mashauriano kati ya vyama vya siasa kuhusu mageuzi ya uchaguzi; na kuchunguza njia za wazi na shirikishi za mazungumzo ya kitaifa na uwajibikaji kufuatia maandamano, vurugu na matukio yaliyozunguka Uchaguzi Mkuu wa tarehe 29 Oktoba 2025.
Wakati wa ziara hiyo, Mjumbe Maalum alikutana na wadau mbalimbali katika Dar es Salaam, Dodoma na Zanzibar, akiwemo Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi; Mheshimiwa Othman Masoud Othman, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, pamoja na viongozi wengine waandamizi wa serikali.
Aidha, alikutana na Spika wa Bunge la Taifa, Jaji Mkuu, Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Msajili wa Vyama vya Siasa, pamoja na Tume ya Rais ya Uchunguzi kuhusu matukio ya Oktoba 2025.
Pia, Mjumbe Maalum alifanya mazungumzo na viongozi wa vyama vyote 19 vya siasa nchini, akiwemo mwenyekiti aliyeko kizuizini wa chama cha upinzani CHADEMA, Mheshimiwa Tundu Lissu, pamoja na viongozi wa zamani wa serikali, wabunge, wanadiplomasia na jumuiya ya kimataifa, asasi za kiraia, makundi ya haki za binadamu, viongozi wa dini, na wawakilishi wa vyombo vya habari, vijana na wanawake.
Dkt. Chakwera alitoa shukrani kwa ukarimu aliopewa na kufurahishwa na ushiriki endelevu wa Tanzania ndani ya Jumuiya ya Madola. Aliwahimiza wadau wote kufanya kazi pamoja kwa ajili ya uponyaji wa taifa na mazungumzo jumuishi. Pia alipongeza dhamira ya wadau wote kushirikiana katika kuleta maridhiano na uwajibikaji kwa waathirika na familia zao. Alisisitiza umuhimu wa kuimarisha imani ya wananchi kwa taasisi za umma, na kuendeleza mchakato wa maridhiano, ustahimilivu na utulivu wa muda mrefu.
Akizungumza mwishoni mwa ziara hiyo, Dkt. Chakwera alisema:
“Ninatiwa moyo na uzalendo wa wadau wote. Ingawa ninatarajia matokeo ya Tume Huru ya Uchunguzi katika siku zijazo, ninaungana na Watanzania katika imani kwamba kujenga amani ya kudumu na ustawi kunahitaji msingi wa nia njema, kuheshimiana, kujitolea kwa ukweli na uwajibikaji, mazungumzo ya wazi na yenye kujenga, haki na maridhiano, pamoja na michakato ya kidemokrasia iliyo wazi na jumuishi kwa ajili ya mageuzi.
Huu ni msingi ambao wakati mwingine huhitaji msaada na ushirikiano wa marafiki na majirani wema, na ninaishukuru Tanzania kwa kukubali msaada wetu.”
Ripoti ya Dkt. Chakwera itawasilishwa kwa Katibu Mkuu na itasaidia kuandaa taarifa yake kwa CMAG. Jumuiya ya Madola inaendelea kujitolea kushirikiana na Tanzania kama mwanachama muhimu, kwa roho ya ushirikiano na heshima, ili kusaidia juhudi za maridhiano na mageuzi, kuimarisha taasisi, utawala shirikishi na maendeleo. -
Godbless E.J. Lema reposted
Rugemeleza Nshala
@rugemeleza
Msimamo wa chama juu ya mauaji uloliofanywa na serikali haramu na dhalimu ya Samia na Chama Cha Mamumiani u wazi.
Bahati nzuri Kamati Kuu ya Chadema itakaa tarehe 28-29 Aprili 2026 na kupokea ripoti ya Wajumbe wa Chadema waliokutana na Mjumbe wa Umoja wa Mataifa na wale waliokutana na Raisi Mstaafu wa Malawi Lazarus Chakwera na kutoa msimamo wake rasmi.
Msimamo wa chama kikuu cha siasa katika Jamhuri ya Muungano ya Tanzania unatokana na vikao rasmi. Hivyo sote tutulie na kusubiri kauli ya Kamati Kuu ya Chadema.
Cha uhakika ni kuwa hiki si chama cha walamba asali au walishwa peremende bali hiki ni chama cha Ukombozi wa Pili wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Wakili Kisabo,
Nina wasiwasi na baadhi ya maneno uliyoandika mtandaoni kuhusu kauli ya Lissu baada ya wewe kutoka mahabusu. Msimamo wa Mkti Lissu mara zote kuhusu uhuru wake umekuwa wazi, kwamba kesi inayomkabili ni ya uongo na anapaswa kuachiwa huru bila masharti yoyote.
Hajawahi, wakati wowote, kuweka sharti la kuuza uhuru wake kwa njia ya mazungumzo, hata hivyo kama cha siasa tunaelewa kuwa mazungumzo ni sehemu ya utawala katika siasa. Lakini uhuru wa Lissu haupaswi kuwa ktk sharti ili.
Kisabo, labda kwenda kwako mahabusu kulikuwa ni sehemu ya mpango, na hata kauli hiyo inaweza kuwa imepangwa. Ndiyo maana viongozi, familia, na mawakili wa chama hawakupewa taarifa wala kushirikishwa wala hukuwashirikisha. Ndiyo maana pia ulipotoka mahabusu moja kwa moja uligeuka kuwa msemaji wa chama.
Nawasihi Watanzania tusubiri kauli ya Lissu mwenyewe. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Nyie WAPAMBE WA TUME, sikilizeni hii stori !!
Kuna jamaa yangu mmoja, kitambo alijifanya Mr. “Respectful Relationship”
Kumbe nyuma ya pazia… aka-save mchepuko kama “sister”
Plot twist ikachapa fast,
Wife akam-add huyo huyo kwenye family group 😭
System ikasema: Error 404, maisha yameanguka.
Ni kama hii serikali tu , kujaribu kutengeneza vibes , lakini zero legitimacy
Ina-run kwa propaganda, lakini hearts za watu haziko convinced.
Lesson iko simple,
ukishikwa na ukweli… hakuna spin, hakuna PR, hakuna comeback.
Tuendelee na Tone Tone
CHADEMA MPESA 0744446969 -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
CHADEMA iko ktk mioyo ya watu. Trust me , wewe Chaliii , ipo siku unaweza kuja kushtuka… hata wife wako anachangia TONE TONE.
Mwambie asikae nje ya game.
Mpe namba hii shemeji 👇MPESA: CHADEMA HQ 0744446969
Mwambie pia kila tone lina maana. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Hata mimi, kama ningekuwa sehemu ya mfumo wa utawala, ningelazimika kufanya “spinning” ili kubadilisha mwelekeo wa mjadala kuhusu mazungumzo ya Chakwera na Mwenyekiti Lissu. Ambayo ni heshima kwa Mwenyekiti Lissu.
Kitendo cha Commonwealth kuamua kwenda kumuona Mwenyekiti Lissu gerezani ni ishara yenye uzito mkubwa. Kinaonyesha wazi kuwa Lissu haonekani kama mhalifu wa makosa ya jinai ya kawaida, bali suala lake lina sura ya kisiasa zaidi. Kwa kawaida, si rahisi kwa taasisi ya kimataifa kama Commonwealth kuingia kwenye mazungumzo ya aina hiyo kama mhusika angechukuliwa kama mtuhumiwa wa makosa ya jinai ya moja kwa moja.
Katika muktadha huo, hili lilikuwa pigo kubwa kwa Serikali. Ili kupunguza athari na kulinda taswira yao, ilikuwa lazima kutafuta ajenda mbadala ya kushika mjadala wa umma na kubadili mwelekeo wa mazungumzo.
Ndipo tunaona juhudi za ku-highlight zaidi kauli tata za Project ya Kisabo kupitia vyombo vya habari vinavyoegemea upande wa serikali pamoja na wapambe wao mitandaoni. Lengo likiwa ni “kubalance” presha ya kisiasa na kufifisha mjadala mkuu uliokuwa unaibuka wa, “ Commonwealth yamfuata Lissu gerezani” -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Wakili Kisabo,
Nina wasiwasi na baadhi ya maneno uliyoandika mtandaoni kuhusu kauli ya Lissu baada ya wewe kutoka mahabusu. Msimamo wa Mkti Lissu mara zote kuhusu uhuru wake umekuwa wazi, kwamba kesi inayomkabili ni ya uongo na anapaswa kuachiwa huru bila masharti yoyote.
Hajawahi, wakati wowote, kuweka sharti la kuuza uhuru wake kwa njia ya mazungumzo, hata hivyo kama cha siasa tunaelewa kuwa mazungumzo ni sehemu ya utawala katika siasa. Lakini uhuru wa Lissu haupaswi kuwa ktk sharti ili.
Kisabo, labda kwenda kwako mahabusu kulikuwa ni sehemu ya mpango, na hata kauli hiyo inaweza kuwa imepangwa. Ndiyo maana viongozi, familia, na mawakili wa chama hawakupewa taarifa wala kushirikishwa wala hukuwashirikisha. Ndiyo maana pia ulipotoka mahabusu moja kwa moja uligeuka kuwa msemaji wa chama.
Nawasihi Watanzania tusubiri kauli ya Lissu mwenyewe. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
budi kuchukua jukumu.
Hatuna budi kusimama.
Hatuna budi kuchangia.
Kila Mwanachama na kila mpenda Demokrasia ana wajibu wa moja kwa moja, kuchangia CHADEMA.
Usione mchango wako ni mdogo.
Usisubiri mwingine achukue nafasi yako. Kila senti unayotoa ni nguzo ya kusimama kwa chama hiki. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Kama hamtaki kukosolewa, kaeni pembeni, ofisi ya umma si mali ya familia. Kauli na matendo yenu yanapokera, mtakosolewa usiku na mchana. Huo ndio uwajibikaji, si kero, ni haki ya wananchi. Kama hilo linawakera, hamieni Burundi.
Wananchi, ili kuendelea kupiga KERO za Msingi , Tafadhali Tuendelee na TONE TONE CHADEMA kupitia MPESA: 0744446969. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Imerudi Tone Tone.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Ndugu wanachama wa CHADEMA na Wapenzi wa Demokrasia Nchini.
Chama chetu kimefunguliwa rasmi kufanya shughuli za siasa. Hii ni fursa muhimu katika kuendelea na mapambano ya haki, uhuru na uwajibikaji katika Taifa letu.
Lakini ukweli usioepukika ni huu
hatuna ruzuku hata ya SENTI MOJA.
Hii ina maana kwamba uhai, nguvu na uendelevu wa CHADEMA uko mikononi mwetu sisi wenyewe.
Hatuna budi kuchukua jukumu.
Hatuna budi kusimama.
Hatuna budi kuchangia.
Kila Mwanachama na kila mpenda Demokrasia ana wajibu wa moja kwa moja, kuchangia CHADEMA.
Usione mchango wako ni mdogo.
Usisubiri mwingine achukue nafasi yako. Kila senti unayotoa ni nguzo ya kusimama kwa chama hiki.
Tujenge utamaduni wa kuchangia bila kusukumwa. Tujenge tabia ya kusaidia chama kila wakati. Hapo ndipo tutakapopata uhuru wa kweli wa kisiasa na kiutendaji.
Mimi nipo, na nimeanza.
Na wewe pia ni wakati wako sasa.
Chukua hatua.
Anza kuchangia.
Simama na CHADEMA.
Kwa pamoja, tutakijenga chama imara na Yaifa lenye HAKI.
Tuchange tu kwa namba maalumu za CHAMA na Akaunti za Benki ili kujenga uadilifu wa Taasisi Imara.
Mikakati zaidi inakuja baada ya vikao kuanza.
Asanteni.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema reposted
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Hapa anasema ukweli kabisa , msibishie huyu Chalii kwenye hili, kwa lugha nyepesi anawaambia kwamba Majaji na Mahakimu wanasikiliza wanachotaka wao.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Ndugu wanachama wa CHADEMA na Wapenzi wa Demokrasia Nchini.
Chama chetu kimefunguliwa rasmi kufanya shughuli za siasa. Hii ni fursa muhimu katika kuendelea na mapambano ya haki, uhuru na uwajibikaji katika Taifa letu.
Lakini ukweli usioepukika ni huu
hatuna ruzuku hata ya SENTI MOJA.
Hii ina maana kwamba uhai, nguvu na uendelevu wa CHADEMA uko mikononi mwetu sisi wenyewe.
Hatuna budi kuchukua jukumu.
Hatuna budi kusimama.
Hatuna budi kuchangia.
Kila Mwanachama na kila mpenda Demokrasia ana wajibu wa moja kwa moja, kuchangia CHADEMA.
Usione mchango wako ni mdogo.
Usisubiri mwingine achukue nafasi yako. Kila senti unayotoa ni nguzo ya kusimama kwa chama hiki.
Tujenge utamaduni wa kuchangia bila kusukumwa. Tujenge tabia ya kusaidia chama kila wakati. Hapo ndipo tutakapopata uhuru wa kweli wa kisiasa na kiutendaji.
Mimi nipo, na nimeanza.
Na wewe pia ni wakati wako sasa.
Chukua hatua.
Anza kuchangia.
Simama na CHADEMA.
Kwa pamoja, tutakijenga chama imara na Yaifa lenye HAKI.
Tuchange tu kwa namba maalumu za CHAMA na Akaunti za Benki ili kujenga uadilifu wa Taasisi Imara.
Mikakati zaidi inakuja baada ya vikao kuanza.
Asanteni.
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Asante Sana
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Nimetoka Ukonga kumtembelea Tundu Lissu.
Tumepata nafasi ya kujadili kwa kina mwenendo wa kesi zote zinazoendelea na zile zilizo pending. Amenieleza pia kuwa jana, tarehe 15 Aprili 2026, alikutana na Mhe. Lazarus Chakwera na kuwasilisha kwake masuala muhimu yafuatayo:
Kesi ya Uhaini inayomkabili ni kwasababu ya msimamo wa No Reforms No Election, Kesi zote zinazomkabili yeye na chama zifutwe, na kwamba yuko tayari kwa mazungumzo akiwa mtu huru yeye pamoja na chama.
Matukio yote ya Oktoba 2025 yafanyiwe uchunguzi huru kupitia chombo cha kimataifa, mfano SADC.
Kuwepo kwa mazingira wezeshi ya mazungumzo ya kweli pamoja na utekelezaji wake.
Uwajibikaji wa kitaasisi kwa yaliyotokea Oktoba 2025, mfano, Ofisi ya Msajili, INEC na TCRA, alisisitiza umuhimu wa kurejea Ripoti ya Jaji Nyalali (1992).
Mabadiliko katika vyombo vya ulinzi na usalama, alisisitiza kurejea Ripoti ya Jaji Chande (2023).
Mabadiliko ya mfumo mzima wa uchaguzi, ikiwemo kufutwa kwa INEC na kuundwa kwa chombo kipya huru, akisisitiza kurejea ripoti za waangalizi wa uchaguzi (1995-2025), pamoja na Ripoti za Jaji Warioba na Jaji Nyalali.
Katiba Mpya
Nimempatia pia uamuzi wa Mahakama ya Rufani uliotolewa jana kuhusu chama kuendelea kufanya kazi amesema "watu wajiandae, muhimu nijue mkutano utafanyika wapi a day after Ukonga"
Paul Kisabo
Wakili -
Godbless E.J. Lema reposted
Chadema Tanzania
@ChademaTZ2
"Ngazi zote za Chama zifanye vikao kutafakari mambo ya msingi na kuanza kutekeleza matakwa ya Katiba na kuendelea na uendeshaji wa Chama." Mhe. @jjmnyika
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Kenya wamepunguza VAT Kutoka 16% mpaka 8% ili kukabiliana na kupanda kwa bei ya mafuta.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Mathayo 16:23
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Uhuru wa mahakama si kipimo cha nani ameshinda au kushindwa kesi hasa pale ambapo msingi wa kesi wenyewe una dosari za kisheria au kiutendaji. Ni dhana ya kamili inayogusa zaidi uadilifu wa mfumo mzima wa utoaji haki kuliko matokeo ya kesi moja moja.
Mahakama huru ni ile inayojisimamia kwa misingi ya uadilifu sheria ukweli na dhamira ya haki bila kuyumba mbele ya shinikizo la nje wala kufuata hisia za wakati. Thamani yake haipo katika kutoa maamuzi ya haraka au yanayopendwa bali katika kuhakikisha kila uamuzi umejengwa juu ya haki uadilifu ujasiri mantiki na usawa.
Kwa hiyo uhuru wa mahakama hupimwa kwa kina cha uadilifu wake si tu katika kutoa hukumu bali katika kulinda ukweli na haki. Hivyo basi bado tuna wajibu wa kutafuta uhuru wa kweli wa mahakama si mahakama inayotawaliwa na hisia bali inayosimama imara juu ya misingi ya haki isiyoyumba.
Hivyo basi ushindi wa CHADEMA katika kesi ambayo kimsingi haikupaswa hata kufikishwa mahakamani si uthibitisho kamili wa uhuru wa mahakama bali ni ishara ya marekebisho ya kosa lililokuwepo ndani ya mfumo wa haki. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Africa ??? Kavu sana.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Nyie watu wabaya CCM. Leo CHADEMA imefunguliwa kufanya kazi zake za siasa na mahakama ya rufaa. Hili si jambo la furaha kwa CHADEMA tu, bali hata kwa CCM pia, maana CHADEMA kuwa kazini kutawafanya mfikiri kwa makini kila jambo.
Sasa ili mpate faida zaidi, Mh. Lissu anapaswa kuwa huru mapema. Msingi huu utapunguza sana namna baadhi ya viongozi wenu wanavyofanya mambo, kwani kwa sasa wanaonekana kama wanafikiri kuna chama kimoja tu haswa kule Dodoma.
Ndio maana hata akili, maarifa na ubunifu unakosekana kwa sababu hakuna accountability. Ndio maana mmeanza hata fujo za urais mapema sana. Kuna watu hawakupaswa hata kuwa madiwani lakini wameweza kufikia ofisi za juu za Nchi na wengine wakawa hata wabunge kwa sababu ya hila na fujo.
Kwa mfano Arusha ikianza Operation “ CHAPA NYAMA CHOMA “mnafikiri huyo chalii wenu ataonekana barabarani kwa kisabengo na maigizo.
CHADEMA huru ni fikra njema kwa taifa. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Habari zinazodai kuwa aliyekuwa rais wa Malawi, Lazarus Chakwera, anakabiliwa na uwezekano wa kukamatwa kwa tuhuma zinahusishwa na skandali za “Greenbelt” na “Fertilizergate,” ambazo zinadaiwa kuhusisha matumizi mabaya ya fedha za umma. Takribani K 39 Bilioni ambazo ni sawa na US $22.9 million USD.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Kuanzia Aprili 15, CHADEMA kipo huru kufanya shughuli zake nchi nzima baada ya mahakama kufuta zuio lililotolewa awali. Mahakama imebaini kuwa amri hiyo ilikiuka haki ya msingi ya kusikilizwa. Kwa sasa, polisi hawana tena msingi wa kisheria kuzuia chama, na yeyote atakayefanya hivyo atakuwa anavunja sheria.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Asante Wakili Jebra. Uamuzi wako wa siku ile wa kujiondoa kuendelea kusikiliza kesi, baada ya Jaji Mwanga kupuuza sababu zako za kuomba hairisho la muda mfupi ili kuhudhuria mazishi, haukuwa wa kawaida. Ilikuwa ni mpango wa Mungu. Kwani usingechukua hatua hiyo, ungehalalisha zuio batili na leo lingeonekana halali.
God bless you Bro!! -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Naandika kwenu MAWAKILI wetu. Hakuna anayewalipa. Hakuna anayewaahidi kesho iliyo salama. Lakini bado mnaamka kila siku na kuchagua kusimama upande wa haki kimya kimya bila kelele bila makofi.
Mnakesha mkisoma, mkitafiti mkisafiri mbali mkibeba mzigo wa wasiwasi ambao wengi hawawezi kuuelewa. Wakati wengine wanatafuta raha nyie mnachagua wajibu. Wkt wengine wananyamaza nyie mnabeba sauti za haki.
Hii si kazi hii ni wito. Demokrasia haifi kwa siku moja hufa taratibu pale watu wema wanapochoka kusimama. Na nyie mmeamua kutochoka. Historia haiandikwi na waliokuwa na nguvu bali na wale waliokuwa na ujasiri wa kusimama pale ilipokuwa ngumu.
Mnaweka misingi ambayo hata kama haitatambulika leo itasimama kesho kama nguzo ya taifa lenye haki. Mnaumizwa, mnapuuzwa wakati mwingine mnaogopwa lakini bado mnasimama. Huo ndio ujasiri wa kweli. Huo ndio uzalendo usio na matangazo.
God bless you na wengine wote wenye hari kama zenu kote Nchini.
Much Love MAWAKILI WETU -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Ushauri wangu. Jaji maana yake ni muamuzi wa haki, si mjasiriamali wa haki. Jaji hapaswi kupuuza haki na ukweli kwa maamuzi yake, anapaswa kuitetea kwa uadilifu wake. Mahakama si soko la maamuzi, bali ni madhabahu ya haki. Kwa sababu mwisho wa yote, haki haihitaji ubunifu wa kibiashara, haki inahitajika kusimamiwa kwa ukweli na utu.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Uamuzi wa Mahakama ya Rufaa kufuta zuio dhidi ya CHADEMA ni ukumbusho muhimu kwamba haki haiwezi kucheleweshwa bila madhara. Haki si matokeo tu, bali ni mchakato unaopaswa kuwa wa haraka, wazi na wa haki.
Haki ikichelewa, hugeuka kuwa aina ya dhuluma. Jaji asiye na utu anaweza kusoma sheria vizuri, lakini akashindwa kusimamia haki.
Hatua ya Mahakama ya Rufaa inaonyesha kuwa mfumo unaweza kujirekebisha, lakini pia ni onyo, kuchelewesha au kupotosha haki kunadhoofisha imani ya wananchi. Imani ya wananchi hujengwa na haki ya haraka, na hubomolewa na haki inayocheleweshwa. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Mama Samia, unapswa kuwa na mashaka na makini sana kwa hao unaowaamini na waliokuzunguka kwa karibu, kuliko hata uhuru wa CHADEMA na Mkt Tundu Lissu. Uimara wa uongozi hupimwa pia kwa uwezo wa kuchuja ushauri na watu unaowategemea. Naona ambacho huenda hauoni kabisa, ungekuwa mama yangu labda ungenisikiliza na kunielewa kuwa hao unaowapa sikio lako kwa karibu ni hatari kwako kuliko kelele/hoja za CHADEMA. Mwachie Tundu Lissu, na acha CHADEMA wafanye kazi zao. Amani yako iko katika kutafuta HAKI na TOBA, siyo kuzima UKWELI.
Mwambie Abdul, mtoto wako, atunze ujumbe huu kama hautanielewa. -
Godbless E.J. Lema reposted
Dr Calipso
@nulphin
Kuna namna aisee yaan umeme wa Elfu 10 units 28 siku tatu zimeisha duh apo nakuja tu usiku asubuhi nakua job. Apa tunapigwa sana siku izi na hii serikali
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Baba Askofu, Bwana Yesu asifiwe.
Nimekuwa nikiona mijadala mingi katika mitandao ya kijamii kuhusu madai ya kuhusishwa kwa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania na mikakati ya kisiasa kuelekea uchaguzi wa mwaka 2030. Ingawa si rahisi kuthibitisha kwa uhakika, kelele hizi zinaibua wasiwasi unaostahili kutafakariwa kwa kina.
Ni imani yangu kwamba kiongozi bora hatokani na dhehebu au dini, bali na sifa za msingi kama utu, haki na uadilifu. Taifa linahitaji uongozi unaojengwa juu ya kweli, si juu ya utambulisho wa DHEHEBU.
Kwa unyenyekevu mkubwa, naomba Kanisa liendelee kusimama katika nafasi yake ya kiroho na kimaadili, na lisikubali kuingizwa katika mkakati wa Kisiasa. Kanisa linapaswa kuwa mwanga wa jamii.
Ninafahamu pia kuna mengi yanayoendelea nchini ambayo yanahitaji hekima na uangalifu mkubwa. Siandiki bila kufuatilia mambo. Pengine siku moja nitaweza kukuona na kushauri mawazo na mitazamo yangu kwa kina zaidi ktk jambo hili.
Mungu aendelee kulilinda na kuliongoza Kanisa lake. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Wamekusikia , wamekuona. Wanasema wanashukuru sana.
-
Godbless E.J. Lema reposted
Victor Glover
@AstroVicGlover
Home, again! Mission complete. I hope we glorified God, humanity, our families and our terrific teams a @NASA and @csa_asc. Time to share the good news!
-
Godbless E.J. Lema reposted
Collin Rugg
@CollinRugg
NEW: Astronaut Victor Glover shares the gospel to a crowd who welcomed him back home to Houston, Texas.
People were seen lining the streets to welcome Glover back home.
“Some of us have never met before. And you know whose fault that is? Ours. So let's choose to do this. Let's be this more. Let's be neighbors.”
“I don't know if you heard me say it, but God told us to love Him with all that we are and love our neighbors as ourselves.”
What a remarkable person.
Video: sp00kycut1e / tt. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Amazing !!
-
Godbless E.J. Lema reposted
Bloomberg
@business
Aliko Dangote plans to offer shares in his oil-refining company on multiple African stock exchanges — a first for the continent. Read more: www.bloomberg.com/news/articles/2026-04-13/dangote-plans-…
📷️: Victor J. Blue/Bloomber -
Godbless E.J. Lema reposted
Liberatus Mwang'ombe
@Liberatus80
Halafu pesa za kuwalipa ma—homeless wa DC ili waandamane kupambana na wanaharakati wanazo.
#samiamustgo #tanzaniamassacre #freetundulissu -
Godbless E.J. Lema reposted
kharry_de_prince
@kharryson95
I think @LAZARUSCHAKWERA should have provided his WhatsApp number so people could send him videos. That way, even those who cannot meet him in person would still be able to reach him, making his report more balanced.
-
Godbless E.J. Lema reposted
kharry_de_prince
@kharryson95
The Chande Commission has already visited the community, but its report has not yet been released. We would like to understand the procedure for @LAZARUSCHAKWERA to meet with the public.
We expect this process to be conducted freely and with stronger protection for witnesses. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Swali la wasiwasi ni hili, nani anamuandalia audience Dr Lazarus Chakwera katika vikao vyake Dar kuhusu October 29 ? Kama wapambe wao wanaojiita wagombea Urais walipelekwa kwenye kikao kukutana na Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa wakiongozwa na Sisty Nyahoza, je, wadau na makundi mengine ya kijamii muhimu nani anawatambua na anaandaa ratiba zao na logistic ? Serikali ? Conflict of INTEREST.
Kama Tume yao ya Jaji CHANDE imetumia zaidi ya miezi kadhaa na bado wameomba siku nyingine, je, Chakwera atastahili muda na mkakati wa aina gani ili kuikabili hofu na manipulation ya Serikali ktk jambo hili gumu kwaon? Nina wasiwasi mkubwa kwamba hakuna jema litakalozaliwa kwa mfumo wa aina hii. Unafikiri mama au ndugu yule ambaye mtoto wake aliuwawa kule Mkoani atapata nafasi ya kutoa maoni mbele ya Chakwera ? Kama watoa maoni na ushuhuda ni watu wanaochaguliwa au kupendekezwa,unategemea ripoti ya aina gani ? -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Sikutilia maanani sana hizi video mwanzoni. Lakini nilianza kuziangalia kwa uzito zaidi pale nilipogundua kuwa maudhui ktk video hii yaliwekwa kwenye ukurasa wa Instagram wa gazeti la Habari Leo, gazeti la serikali, na baadaye yakaondolewa. Na haya ni maneno ya Makamu wenu wa Rais.
Kinachonishangaza ni kwamba maudhui yaliyomo yanalenga kukemea ufisadi wa fedha za umma na viongozi kuacha kujinufaisha. Swali la msingi linaanzia hapa, kama maneno ya aina hii yanaweza kuonekana mabaya kiasi cha kuondolewa, basi wale wananchi wote wenye akili na mapenzi ya nchi wanapaswa kujiuliza kwa kina mwelekeo wa zaidi tunaokwenda.
Je, ni rahisi kwa mhariri kuamua kuondoa maudhui yanayomhusu kiongozi wenu wa juu namna hiyo bila maelekezo kutoka juu? Na huko juu ni wapi ? Kuna hadithi moja huko Italia , askari wa barabarani alisimamisha gari , alipokuwa anakagua, akagundua kuwa aliyekuwa anaendesha alikuwa PAPA , ghafla alianza kukimbia kwa speed kali huku akitokwa jasho !! Wenzake walimuona na kumfuata na kumuuliza , nini kimekupata ? Alijibu , nimesimamisha gari nikakuta PAPA anaendesha akiwa na abiria mmoja , akaendelea kusema , nafikiri huyo abiria lazima atakuwa YESU !! Tafakari.
Huyu ni Makamu wa Rais wa serikali yenu mliyopata kupitia uchaguzi uliokuwa na maumivu makubwa kwa taifa. Mnaondoa video kama hii ktk kurasa zenu, meseji kwa umma ni moja , Amkeni sasa na sio baadae, maana Cartels wako RADA.
Nina hofu kuhusu kesho ya Tanzania. Si kwa sababu hakuna watu wenye uwezo, bali kwa sababu ukimya unapokuwa kawaida, hata mambo yasiyostahili yanaendelea kuonekana ya kawaida. Hapo ndipo hatari kubwa.
CCM, mnapaswa kutafakari kwa kina. Historia ina tabia ya kurudia matokeo yake pale pale makosa yanapopuuzwa. Hii si wakati wa kiburi, bali ni wakati wa kurekebisha mwelekeo kwa ajili ya taifa. Kila maumivu mliyowapatia wa Tanzania , mtalipa na Nchi itaharibika sana. Maisha ya Nchi sio ushabiki wa michezo. -
Godbless E.J. Lema reposted
Rugemeleza Nshala
@rugemeleza
Huo ndiyo ukweli halisi. Bei ya mafuta kwa lita moja nchini Marekani ipo chini ya hapa Tanzania kwa zaidi ya shilingi 1020. Hiyo ni mbali na ukweli kuwa sisi ni Taifa masikini kweli kweli. Hivyo Serikali hii haramu inawakamua na kuwafukarisha Watanzania kupitia kodi lukuki kwenye mafuta
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Mama Samia , naomba kukupa taarifa kuwa, mazungumzo kati ya Marekani na Iran yamefeli huko Pakistan. Hii inaashiria hatari ya hali kurudi katika mvutano mkali zaidi, hata kuzidi ilivyokuwa mwanzo. Dalili zake zinaonekana wazi, ushindani mkubwa wa kununua mafuta utaongezeka, hasa katika nchi zenye mafuta ambazo bado zina utulivu. Katika hali kama hii, Afrika itaendelea kuathirika zaidi, ikiwemo Tanzania.
Athari zake hazitaishia kwenye nishati pekee. Mfumuko wa bei , kuanguka kwa uchumi na sekta ya usafiri wa anga navyo vitapata pigo kubwa. Mashaka ya usalama yataongezeka, gharama za mafuta na bima zitapanda, na baadhi ya njia za ndege, hasa zile zinazopita Middle East, zitaanza kuepukwa. Hii itaathiri moja kwa moja utalii, biashara na uchumi kwa ujumla.
Katika kipindi hiki cha misukosuko ya kiuchumi duniani, Tanzania inapaswa kuwa makini zaidi. Ni wakati wa kusafisha hali ya kisiasa na kurekebisha mwelekeo wa diplomasia yake. Dunia inapokuwa katika hali ya taharuki, nchi zinahitaji kuonyesha utulivu wa ndani ili kujenga imani ya nje.
Kuendelea kumshikilia Tundu Lissu katika mazingira kama haya kunazidi kuongeza hali ya sintofahamu. Inachochea hisia za migogoro, inaongeza presha ya kisiasa, na inaleta picha ya nchi isiyo na uthabiti, hasa inapounganishwa na kumbukumbu za migogoro ya uchaguzi na matukio ya vurugu na mauaji Octoba 29. Ukizingatia kuwa ktk kila corridor za Kimataifa na ndani ya taasisi za kimataifa ni mjadala, anzia UN , ICC , COMMON WEALTH na Mataifa yote makubwa Duniani.
Hili si suala la mtu mmoja tu, bali ni taswira ya taifa. Wakati huu unahitaji hekima, si kiburi. Kwa sababu historia inaonyesha wazi, mataifa yanayoendelea kufanya maamuzi kwa misingi ya ubabe wakati wa nyakati ngumu, huishia kukutana na anguko kubwa kuliko walivyotarajia. Naona downfall yenu kubwa sana na ya aibu kama mkiendelea kukaza fuvu. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Wakati huku TANZANIA inasemekana kwamba Polisi wameanza uchunguzi wa taarifa zinazosambaa kuwa ukishikwa bega sehemu za siri zinatoweka, ambazo jina la kisayansi zimeitwa NYETI.
-
Godbless E.J. Lema reposted
Maria Sarungi Tsehai
@MariaSTsehai
The deputy Chair of CCM Stephen Wasira went on camera and declared that there was no peaceful protest because they burnt public buildings - failing to point out that initially it was a peaceful protest until the police and mask wielding mercenaries backed by the state started killing and shooting people including innocent bystanders which led to some youth reacting with anger and burning down symbols of repression like CCM offices
But worse, Wasira emphasized that the Commission of Inquiry was not formed to investigate or question the government - that is not their mandate!
So the unspoken truth has been spoken! This Commission of Inquiry has one job 👉🏽 to blame the innocent victims and to create a non existent conspiracy!
This fails to mention that majority of the people killed from the thousands were shot at home, in shops and bars and on the streets going about their business!
Whether Othman Chande likes it or not - this is what he signed up for and that is why he and his fellow commissioners have ZERO trust from the citizens!
The biggest disaster that would come out of this is for the international community to try and accept this Commission’r report as some form of “accountability”. This will really indicate to Tanzanians that the donors, international human rights and justice bodies do not really care about African lives and are more eager to whitewash the murderous cabal! The ensuing bitterness could transform to an even greater crisis!
So the solution - disregard Chande’s commission whether they finish the job or not and seek through other international means the Truth and Accountability necessary to bring back Sanity and Justice to a once peaceful nation!This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema reposted
Maria Sarungi Tsehai
@MariaSTsehai
📌Bookmark this
‼️🚨WHY CHANDE’S COMMISSION IS. NOT INDEPENDENT‼️
The Commission of Inquiry that was formed by Samia Suluhu (the main culprit in #tanzaniamassacre) does not meet the minimum threshold of an independent inquiry body nor is it legally armed to deal with the gross violations of human rights that occurred
I will break it down here for @UN_HRC @IntlCrimCourt @eucommission @Europarl_EN @WorldBankAfrica @IMFAfrica @SweAmbTZ @FCDOGovUK @commonwealthsec @_AfricanUnion and anyone who is still waiting for the report and hoping it can resolve the unprecedented stand off in #tanzania
The commission is about blaming the victims and not looking for the real perpetrators and killers. This was evident on November 20, 2025, when the Commissioners were being sworn in. Samia Suluhu Hassan issued directives that fundamentally shape the direction of the Commission of Inquiry into the October 29 killings.
Rather than establishing accountability for the killing of unarmed civilians, the framework of the inquiry appears to shift responsibility away from the state and toward the victims and civil society.
The directives emphasize:
👉🏽Why youth protested, instead of who used lethal force
👉🏽Opposition rhetoric, instead of state actions
👉🏽NGOs and alleged funding networks
👉🏽Political relationships and narratives
What is absent is decisive and central:
👉🏽No explicit focus on security forces
👉🏽No clear demand for command-chain accountability
👉🏽No prioritization of identifying those responsible for killings and injuries
This approach risks transforming an accountability process into a political narrative investigation, where the behavior of victims is scrutinized more intensely than the conduct of armed actors! A genuine inquiry into mass killings must begin with one non-negotiable question:
Who authorized and carried out the violence against unarmed civilians?
Without that, the process cannot credibly be called justice.
(👇🏾 continues below) -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Kumuita jina lake huko juu si kumbukumbu tu, ni uthibitisho kwamba upendo haujawahi kufa. Kuna majina huandikwa kwenye mioyo na hili limefika mwezini. Walitaja jiwe la mwezi, lakini kwa kufanya hivyo walihifadhi hadithi ya upendo isiyofutika. Sio tu crater, ni alama ya mapenzi yaliyoshinda muda, maumivu, na kifo.
Such a beautiful ❤️ -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Uwezo wako ni mkubwa kuliko hofu zako, chagua kuamini hilo. Kile unachokiona hakiwezekani leo, huanza kuwa kweli siku unapoacha kuogopa kujaribu. Nguvu ya binadamu haipo kwenye mwili tu, ipo kwenye maamuzi yake. Imani huanzisha safari, uamuzi huifikisha mwisho.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Jakaya Kikwete anasaka amani Sudan? Wakati huo huo, katika nchi aliyowahi kuiongoza, Tanzania, kuna kelele za matukio ya utekaji na vilio vya Oktoba 29.
Vilevile, kiongozi wa upinzani Tundu Lissu anaendelea kusota gerezani kwa zaidi ya mwaka sasa. Maajabu makubwa haya.
Kama hausomi maandiko vizuri, unaweza kudhani,siku ile ya saba, Mungu alipokuwa mapumzikoni, labda Shetani alipata nafasi ya kuwaumba viongozi wa Afrika. -
Godbless E.J. Lema reposted
Barack Obama
@BarackObama
What the Artemis II astronauts did over the last 10 days was a testament to their bravery. And the fact that they traveled farther from Earth than anyone ever has, re-entered our atmosphere at more than 24,000 mph, and splashed down safely was a testament to human ingenuity. Thanks to everyone at @NASA for making this mission possible, and for taking us along for the ride.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Mnatupanga ??? Mtumieni CAG😂😂😂
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Kauli za Jaji Mkuu zinahitaji kuendana na uzito wa nafasi yake ya kikatiba. Wananchi hawatarajii malalamiko ya kawaida, bali uongozi wa kitaasisi unaotoa suluhisho na hatua madhubuti.
Taasisi ya Mahakama inapaswa kuonyesha uimara na ufanisi, si kutoa hisia zinazofanana na mijadala ya kisiasa au ya kawaida ya kijamii.
Ni muhimu hatua zichukuliwe ndani ya mfumo, badala ya kuishia kwenye maneno yanayoacha maswali zaidi kuliko majibu. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Nimeona hatua ya kupunguza msafara wa Samia, ikielezwa kama sehemu ya kubana matumizi. Kwa juu juu inaonekana sahihi, lakini ukiangalia kwa kina, mantiki yake inatia shaka na sanaa.
Katika kipindi ambacho bei ya mafuta imepanda hadi kufikia takribani shilingi 4500 kwa lita katika baadhi ya maeneo, bado serikali inaruhusu watendaji wa mikoa kusafiri kwenda Dodoma kwa vikao kwa siku 14, jumlisha siku 2 za safari. Hawa ni pamoja na RC, RAS, Wahasibu, Planning Officer na madereva wao wote, kutoka mikoa yote 26 ya Tanzania Bara, kwa lengo la kufuatilia hotuba za Mtia nia Mwigulu Nchemba pamoja na michango ya watu wanaojiita wabunge waliotokana na October 29 .
Kwa makadirio ya kawaida, kama kila mkoa unakisiwa pengine unaweza kutumia takribani shilingi 23,680,000 kwa posho tu, basi jumla yake inaweza kuwa zaidi ya shilingi milioni 615. Hii haijumuishi gharama za mafuta na blah blah nyingine.
Swali la msingi linabaki kuwa ili , Je, huu ndio uelewa wa kubana matumizi? Kwa nini watu hawa washindwe kufuatilia shughuli hizo wakiwa kwenye maeneo yao ya kazi kwa njia ya mtandao na kuokoa fedha za umma?
Kupunguza msafara wa Samia na huku ukiruhusu matumizi makubwa ya aina hii hakujengi picha ya nidhamu ya kweli ya matumizi. Kunatoa taswira ya hatua za juu juu zisizogusa kiini cha tatizo.
Kubana matumizi si suala la kupunguza msafara pekee, bali ni uwajibikaji wa mfumo mzima. Bila hilo, jitihada hizi hubaki kuwa maonyesho na usanii badala ya suluhisho halisi. Kwa kifupi, watendaji wanapaswa kuwezeshwa kufanya kazi zao kwa ufanisi wakiwa vituoni, huku mikutano mingi ikihamishiwa kwenye mifumo ya kidigitali hii ndiyo njia ya kisasa na ya kweli ya kubana matumizi.
“ Tutawasadia kuwaza ili mpate muda wa kula kuku Chako ni Chako” -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Mboga za majani ni uhai wetu, lakini zimeanza kubeba hatari isiyoonekana. Matumizi mabaya ya kemikali yanaacha mabaki ya sumu yanayoingia moja kwa moja kwenye sahani zetu. Kimya kimya, sumu hizi zinachangia magonjwa sugu ikiwemo saratani, zikiathiri hata watoto na wajawazito.
Hili si tatizo dogo ni janga linalokua taratibu ndani ya jamii. Na inawezakana kuwa hatari yake ni kubwa kuliko hata uvutaji sigara kwa sasa. Ni wajibu wa wenye nafasi kuchagua kilimo salama na kupunguza matumizi ya kemikali hatari. Mwisho wa siku, chakula kinapaswa kutulisha si kutuadhibu. Wasiwasi wangu ni huu, sidhani kama serikali inayo pambana na kampeni ya “ Nyeti na Bega” inaweza kuona hili. -
Godbless E.J. Lema reposted
Tausi Likokola
@tausilikokola
Kwa wale walalamikaji ukitumia English, unajua ninapoishi tunatumia kiingereza? Post zangu zinasomwa na senate offices🇺🇸na wengineo kuelekea kukomboa Tanganyika. Pale post inapokuwa siyo ndefu na najua itamsaidia mtanzania, najitahidi kuweka kiingereza na kiswahili ila kama unaona post ni ya kiingereza tu, simple siku hizi unacopy na kumuomba ChatGPT au Google Translate wanakupa kiswahili bure. Mjifunze kujiongeza lugha pia….mimi nne naongea, wewe unataka kubaki na kiswahili tu-jielimishe- if you want to go places, inabidi ujiongeze kifikra, matendo, lugha, elimu etc…let’s be better, let’s grow⬆️
-
Godbless E.J. Lema reposted
Senate Foreign Relations Committee
@SFRCdems
"@TunduALissu's remains imprisoned for his advocacy for electoral reforms and civic freedoms in Tanzania. I call on Tanzanian authorities to drop their charges against Tundu and release him from detention immediately." -@SenatorShaheen
Tundu Antiphas Lissu
@TunduALissu
Today marks one year since Tundu Lissu was arbitrarily detained and denied his fundamental rights. Please share this and visit www.freetundulissu365.com for more information.
#freetundulissu
—Admin -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Bora nyie , Kassim Majaliwa ali-drop ahadi ya barabara.
Sisi tuliuziwa “maisha bora kwa kila Mtanzania” enzi za Jakaya Kikwete ( Mumeo) … hadi leo ni trailer tu, movie haijatoka. Na miaka 10 ulikuwa First Lady.
Kama ningekuwa advisor wa Kassim Majaliwa, ningemwambia, awe makini na kupigiwa makofi 🔥 -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Mkienda huko, watonyeni kwa akili hao wanaharakati waache mashambulizi dhidi yangu. Kelele zao nazielewa, Mimi ninaijua kwa karibu hii familia, hasa kwenye masuala ya finance ” Unajua kwa sasa, kuna wkt mwingine ninalazimika kuimba wimbo wao ili tufikie malengo.Lakini hilo halibadilishi ukweli kuwa hii Nchi inachezewa. Hivi, hawajui hadithi ya José dos Santos na João Lourenço wa Angola? Semeni nao kwa
akili, isije kuonekana kama mimi ndiye nimewatuma, hawa wengine wa huku kwa home boy niachieni mimi “
Mwisho wa nukuu wa ndoto niliyoota jana. -
Godbless E.J. Lema reposted
International Democracy Union
@idualliance
The International Democracy Union (IDU) expresses its grave concern on the occasion of the first anniversary of the arbitrary arrest on April 9th, 2025 and the continued detention of Tanzanian opposition leader and IDU Bush–Thatcher Award for Freedom recipient Tundu Lissu.
Mr. Lissu’s arrest following a peaceful political rally, and the subsequent charges brought against him, lack a credible legal foundation and reflect a troubling pattern of political persecution aimed at silencing democratic opposition. Read more here:
idu.org/idu-statement-on-the-detention-of-tundu-lissu/
#freetundulissu #standwithtundu #tanzania -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema reposted
Tausi Likokola
@tausilikokola
#freetundulissu #freelissunow
@UNHumanRights
@UN
@amnesty
@hrw
@FIDH
@Int_IDEA
@freedomhouse
@CarnegieEndow
@CIVICUSalliance
@Article19org
@Europarl_EN
@eu_eeas
@EUCouncil
@EUCourtPress
@coe
@OSCE
@StateDept
@StateDRL
@SFRCdems
@SenateForeign
@BBCWorld
@BBCNews
@Reuters
@AP
@CNN
@AlJazeera
@dwnews
@France24_en
@guardian
@washingtonpost
@nytimes
@FinancialTimes
@amnestyusa
@hrw_us
@freedomhouse -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Tundu LISSU.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Hello Mum Samia, Just a polite reminder kwamba Mkti Tundu Lissu bado yuko mahabusu na leo ametimiza mwaka mmoja. Hongera kwa hotuba yako ya jana kuhusu bei za mafuta duniani. Haikuwa mbaya sana. Nimewapenda zaidi wale walioirekebisha.
Anyway, siku zote kumbuka , hakuna kitu kibaya ktk maisha kama kuzungukwa na watu wanao kuogopa. Kwani, unaweza ukanywa sumu, wakakuacha wakajua unafanya mazingaombwe. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Kitu pekee kinachohitajika ili uovu ushinde ni watu wema kukaa kimya na kutochukua hatua.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Kuna wakati mamlaka huogopa zaidi wazo kuliko mtu. Na hofu hiyo hujificha nyuma ya nguvu, sheria, na vifungo lakini kiini chake ni kile kile woga wa ukweli usiodhibitika. Wanasema wanaogopa misimamo yako. Labda si wewe binafsi wanayeogopa bali kile unachowakilisha uhuru wa fikra, ujasiri wa kusema, na kukataa kuishi kwa masharti ya hofu.
Hata kupona kwako baada ya kupigwa risasi kwao lilikuwa kosa kwa sababu uliikataa simulizi ya mwisho waliyoitaka. Ukaendelea kuwa ushahidi hai kwamba si kila nguvu hushinda haki.
Sasa mwaka mmoja jela. Na ndani ya ukimya huo kuna kelele kubwa kuliko hotuba nyingi kelele ya dhamira isiyouzwa.
Ktk siasa nimejifunza kwamba wakati mwingine kuna biashara kubwa ya kuuza maneno. Lakini mara chache unakutana na mtu anayechagua gharama ya ukweli kuliko faida ya uongo.
Wewe ni mmoja wa wachache hao.Kwa sababu uhuru si kutoka gerezani tu bali ni uwezo wa kukataa kuusaliti ukweli hata unapouzwa kwa bei ya kuachiliwa. Basi jipe moyo mkuu. Historia huwa na kumbukumbu ndefu kuliko hofu za leo.
Na siku zote haki inapochelewa haifi.
God bless you. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Hii ni kadi ya babu yangu ya mwaka 1952, alipokuwa mpinzani wa serikali ya wakoloni kupitia Kilimanjaro Chaga Citizens. Leo nimejisikia kuwa na nguvu sana baada ya kuiona. Najua babu yangu alikuwa mcha Mungu sana, lakini kadi hii imenipa fahari zaidi na kunikumbusha misingi imara aliyosimamia. Inaonyesha ujasiri, mshikamano na hekima ya WACHAGA, huku pia ikibeba ujumbe unaomgusa kila mtu.
Shabaha na amri zao zilikuwa ,
Kuungana
Kupendana
Kuaminiana
Kushirikiana mawazo na mali
Huu ni urithi wa thamani unaoonyesha fahari ya Kichaga, lakini pia ni mwongozo wa maisha kwa yeyote anayetamani umoja, heshima na maendeleo. Kwa kweli inanipa motisha ya kuendeleza alichoanza babu yangu kwa vitendo.
Mmeona hapo , Mawazo na Mali ?? 😂 -
Godbless E.J. Lema reposted
Twaha Mwaipaya
Huyo aliyebebwa anaitwa Wilfred Elisha Mgonela ni diwani haramu wa ccm kata ya Pwaga iliyopo Jimbo la Kibakwe Wilayani Mpwapwa.
Huyu Wilfred Elisha Mgonela ni shemeji wa Mbunge wa Kibakwe George Boniface Simbachawene yaani dada wa Simbachawene kaolewa na huyu Wilfred.
Amekuwa akifanya vitendo vingi vya unyanyasaji Kwa Kinga ya Simbachawene. Ni mtu katili sana.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema reposted
Chadema Tanzania
@ChademaTZ2
Takwimu za kikanda za mwezi Aprili 2026;
Kenya
Petrol: Tsh 3,700
Diesel: Tsh 3,680
Kodi: 28%
Uganda
Petrol: TSh 3,600
Diesel: TSh 3,550
Kodi: 27%
Rwanda
Petrol: TSh 3,750
Diesel: TSh 3,720
Kodi: 30%
Zambia
Petrol: TSh 3,800
Diesel: TSh 3,770
Kodi: 30%
Mhe. @HecheJohnThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Africa kuna shida sana. Kama mavi yangekuwa na miguu na macho , bila shaka yangeweza kutawala Africa bila wasiwasi.
-
Godbless E.J. Lema reposted
Gunther Eagleman™
@GuntherEagleman
🚨 BOOM: US pulls off the MOST COMPLEX airman rescue in HISTORY, deep inside Iran.
Griff Jenkins: “Nothing short of extraordinary.” They’ll be studying this one for years.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Kabisa, some one can agree with you, kwamba hata UBONGO unaweza kuwa hauna. Wakati mwingine mimi nakuelewa sana. Sema tu , wale wenzangu tu ndio wana shida na wewe sometimes, tena kama wale wakina Bon Yai na Sugu.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Ukisema ukweli halafu ukapingwa, usiyumbe. Chukua muda, relax. Kwani ukweli una nguvu na mamlaka ya kujitetea wenyewe, na hauwezi kushindwa.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Donald Trump alitoa kafara ndege za kivita na vifaa vingine vyenye thamani ya zaidi ya dola milioni 600 (takriban shilingi trilioni 1.5 za Kitanzania) ili kumuokoa mwanajeshi mmoja wa anga. Hili ni jambo la KIPUMBAVU sana kueleweka kwa viongozi wa Afrika.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Mwenye akili humtukuza Mungu, lakini mpumbavu humkufuru bila kujua anajidhuru mwenyewe. Kumkufuru Mwenyezi Mungu ni ishara ya moyo uliojaa kiburi na akili iliyopotea.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Tunapofanya hukumu juu ya wengine mara nyingine, si kwa sababu ya dhambi au udhaifu wao, bali kutokana na level ya ufahamu tulio nao na circle zetu za maisha. Ushamba hauokoki, na hata mtu aliye na elimu ya juu anaweza kuwa mshamba kwa kukosa maarifa ya kweli. Jitihada zako na common sense katika kutafakari na kujifunza ndizo zinazojenga uelewa wa kweli.
Baadhi ya mahubiri ya ndoa leo yanaonyesha ukweli mgumu: wanawake bado wanakandamizwa, mara nyingi kupitia baadhi ya madhabahu au mafundisho yenye shinikizo. Kuhubiri neno la Mungu kwa wakati huu kunapaswa kuunganishwa na kusoma vitabu mbalimbali, kuelewa generation ya leo, na changamoto za multi-cultural, ili kuelimisha badala ya kuwachanganya au kuumiza watoto wa kike.
Kwa mfano, nilimsikia muhubiri mmoja akisema: “Kama mchumba wako anaenda saluni halafu anatumia shilingi elfu hamsini, huyo ni shetani!!” Usimuoe! Hii ni ajabu kabisa. Unaona huyu mhubiri hana uelewa wa pesa, hadhi, au mwanamke wa leo, kimsingi ana poverty mentality ya hali ya juu na ushamba.
Siku moja nilikuwa na wadogo zangu, wakaniambia wasichana wa leo hawawezi kumpelekea mume maji bafuni. Nikacheka 😂 nikawajibu: pengine kwa sababu wamewaona wazazi wao wakitumia shower head, na kama nyie hamna mpango wa kuoga ndani, atajifunza kupeleka maji na ndoo na kopo la blue band bafuni 😂. Mwingine akasema, “Hata ugali hawajui kupika ukute!” Nikawajibu, labda wanajua kutengeneza salad na sandwich, na wewe bado umekariri ugali 😂. Hii inaonyesha mtazamo wa hofu na shinikizo usio na maana unaochanganya vijana, na mara nyingine unyenyekevu na ukakamavu umefafanuliwa vibaya.
Shinikizo la jamii mara nyingine linafanya vijana kuingia kwenye mahusiano mabaya, kwa sababu familia zinatafuta impression ya nje badala ya adabu na maadili ya kweli. Mahusiano bora leo mara nyingi yanapimwa kwa financial status na prestige, na si kwa character na nidhamu. Hii ni changamoto kubwa, kwa sababu msingi huu ukiharibika, taifa haliwezi kuwa salama, na familia ndiyo msingi wa taifa.
Hivyo basi, sasa wewe Lema, kwani hii ni siasa? Ndiyo, ni siasa, lakini pia msingi wa utawala unaopaswa kuona mbali zaidi: jinsi maarifa ya leo yanavyoweza kuharibu nafasi ya familia kesho, na kwa hivyo kuathiri mustakabali wa taifa. Kuhubiri leo ni kuelimisha kwa hekima, kuelewa vizazi vya sasa, na kulinda msingi wa familia, kwani familia ndiyo msingi wa taifa salama.
Na nyie watoto wa kike, ushindi katika mahusiano unaanza na watu wawili wanaokubaliane, hata kama mwanzo ni mgumu na kutisha, lakini ndoto inaweza kugeuka kuwa maisha bora, salama, mazuri na yenye test.
Pls do not judge a man by the size of is wallet, but by dreams, character, and discipline. Na matavuka kila kizuizi.
Never Say Never !! Heri ya Pasaka. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Teknolojia inavyoendelea kwa kasi, ndivyo baadhi ya vitu tulivyoviita raslimali za Taifa vinavyoanza kupoteza msingi wake wa thamani. Hili si jambo la kubahatisha bali ni mwelekeo wa dunia ya leo. Ndiyo maana inahitaji maarifa, maono na uadilifu wa hali ya juu katika kufanya maamuzi ya rasilimali mapema kabla hatujapitwa na wakati.
Mfano halisi ni soko la almasi. Leo hii bei ya almasi imedondoka kwa takribani asilimia 27 hadi 60. Sababu kubwa ni kuibuka kwa almasi za maabara (lab-grown diamonds) ambazo zimechukua hadi karibu nusu ya soko la ndoa Marekani. Zaidi ya hapo, almasi hizi zinauzwa kwa bei ya chini kwa asilimia 30 hadi 70 ukilinganisha na zile za asili. Huu ni ushahidi wazi kwamba teknolojia inaweza kubadilisha thamani ya rasilimali kwa muda mfupi sana, kile kilichoonekana kuwa adimu jana, leo kinaweza kuzalishwa maabara kwa wingi.
Lakini wakati dunia inabadilika kwa kasi hiyo, sisi bado tunabaki kwenye mambo ya ajabu na ya aibu hadi kufikia hatua ya kuwa na mijadala ya “nyeti kupotea” kana kwamba hilo ndilo ajenda kuu ya Taifa. Ufara ufara mwingi, kelele zisizo na mwelekeo, wakati dunia inaenda kwa kasi ya mwanga.
Hali hii inaonekana pia katika usimamizi wa miradi mikubwa ya kimkakati. Mradi wa gesi nchini Tanzania umechukua zaidi ya miaka 25 katika hatua za majadiliano, mipango na maandalizi bila kufikia utekelezaji kamili. Huu si ukosefu wa rasilimali, bali ni dalili ya ukosefu wa maamuzi thabiti, kasi ya utekelezaji, na uwajibikaji wa kweli. Wakati huo huo, dunia inaelekea kwenye mabadiliko ya nishati (energy transition), jambo linaloweza kupunguza thamani ya rasilimali kama gesi kabla hata hatujainufaika kikamilifu.
Ukweli unabaki kuwa rasilimali peke yake haitoshi. Taifa linaweza kuwa na utajiri mkubwa chini ya ardhi, lakini bila maarifa, maono na uongozi wenye uadilifu, utajiri huo unaweza kubaki kuwa hadithi isiyo na matokeo.
Ni wakati wa kutambua kwamba dunia haisubiri mtu. Tukichelewa kufanya maamuzi sahihi leo, kesho tutakuta thamani ya tulichokuwa tukikitegemea imeshapotea. -
Godbless E.J. Lema reposted
Dr. Keroche Moro.🔬🔬
@NchiAhadi
Akaniambia twende pembeni kidogo maana tulikuwa kwa watu akaniambia nilipokuona tu nikamkumbuka mwanangu ilibidi nimuulize mwao yupi? Akaniambia Boniface, unajua Boniface hutanaye tena, Rafiki yako aliuliwa Mwaka jana yaani October 29! Ilibidi nimuulize Mara mbili mbili....
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Katika siku hii takatifu ya Pasaka, tafadhali pokeeni baraka tele kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Pasaka ni sikukuu muhimu sana katika imani yetu ya Kikristo, ni siku iliyotimiza kusudi la kuzaliwa kwa Yesu Kristo. Ni siku ya ushindi mkubwa dhidi ya mauti na dhambi.
Ukiielewa kwa kina maana ya Pasaka, hofu ya maisha hupoteza nafasi ndani yako. Kwa sababu ndani yako ipo ile nguvu iliyomfufua Kristo Yesu. Hivyo basi, wewe ni mshindi dhidi ya magonjwa, umasikini, roho mbaya, na hata kifo chenyewe.
Mimi na familia yangu tunawatakia nyote Pasaka njema, yenye amani, imani, na matumaini mapya.
Wewe ni mshindi na heri ya Pasaka. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Ikiwa mtatubu na kuziacha njia mbaya,rehema itawafikia na mwanzo mpya utaonekana. Msipoigeuza mioyo yenu, mtaendelea kubeba mizigo ambayo haikukusudiwa kuwa yenu. Moyo unaonyenyekea hupata neema, lakini moyo mgumu hujifungia mlango wa rehema. Rudini katika kweli, nanyi mtauona uhuru wa Mwenyezi Mungu.Maana haki huinua, lakini uovu huangusha hata aliye juu. Chagueni njia ya nuru, maana giza halina ahadi ya kesho. Ninakuombea Ujasiri wa Mungu.
Tubu,badilika na heri ya Pasaka. -
Godbless E.J. Lema reposted
Mario Nawfal
@MarioNawfal
🚨🇺🇸🇮🇷 BREAKING: Alleged pictures of U.S. C-130 that got stuck at a refueling point inside Iran during the rescue operation and was destroyed by Delta Force to prevent capture.
Source: @officialrnintel -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Pasaka si simulizi la ushindi mwepesi, bali ni fumbo la mateso yanayozalisha ukombozi. Ukweli hauuawi na kifungo, wala haki haifungwi na minyororo ya muda.
Katika ukimya wa dhiki, dhamiri hujifunua. Katika maumivu, historia huanza kuandika upya maana ya uhuru. Moyo mkuu kwako na kwa wote wanaobeba mzigo wa kuitafuta haki. Nuru ya kweli haizimwi na giza; hulifanya giza lijulikane. Heri ya Pasaka Bro. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Hii inaitwa Red Herring , mkakati wa kuingiza hoja ya pembeni ili watu waache mada kuu na jambo la msingi katika jamii. Wakati mwingine huitwa pia manufacturing consent , kutengeneza jambo kwa umma kwa njia ya udhibiti wa taarifa muhimu.
Kwa lugha rahisi, ni mkakati wa kuhamisha umakini wa watu kutoka kwenye suala nyeti kwenda kwenye jambo lingine (mara nyingi la hisia, burudani au mgogoro) ili kupunguza shinikizo, uchunguzi na mjadala.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Usafiri wa boda boda(Pikipiki) haukupaswa kuwa usafiri wa umma. Boda boda imegeuka njia ya kupeleka vijana na watu wengi kwenye vifo, ulemavu na umasikini. Ukosefu wa sera za uchumi, usalama barabarani, na ujinga wa kisiasa ni msingi mkuu wa janga hili. Kutega kura kwa gharama ya damu ni dhambi na ujinga wa kiwango cha juu. Kukaa kimya ni kushiriki kwenye mauaji na mateso haya. Vijana hawa siku moja, watashituka kuwa hawakuongozwa vyema na hali itakuwa mbaya sana kwenu.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Wapumbavu wakipeana sifa, upumbavu hugeuka huduma. Wasio na utambuzi hupiga makofi wakidhani ni baraka. Kelele zinapozidi bila maana, ujue si hekima inayoongea, ni ujinga uliopata jukwaa. Tatizo si mavazi wala vipaza sauti, bali ujumbe usio na maarifa unaopotosha jamii. Kikao hiki kimekutanisha upumbavu na ushamba. Kundi la wapumbavu likiongozwa na upumbavu, mwisho wake ni aibu. Angalia na sikiliza huu UPUMBAVU wa huyu content creator.
-
Godbless E.J. Lema reposted
Tausi Likokola
@tausilikokola
Justice Mohamed Chande 🇹🇿: I’ve read of the pending Oct 29 report under your leadership. I had the honor of meeting you through the late George Kristos (RIP), a man of integrity-so I held your name to that same standard.
I have not read the alleged initial report that existed, and I do not speak on what I haven’t seen or verified. But truth does not disappear, and justice cannot be rewritten.
Too many innocent lives were lost on Oct 29, 2025. No altered narrative or blame-shifting will cleanse that blood-only truth and accountability will.
The international community is watching & aware. What is done in darkness will come to light-it always does at some point-international community already know and have seen what happened with evidences. No one who demonstrated had guns, neither bystanders nor those who were killed in their own homes hawakumiliki silaha; those who had guns, and those who gave the orders to kill, are the ones responsible.
I am writing this publicly because shared writings have saved a few in the past and have also brought accountability at times . I urge wisdom: do not let your name be tied to injustice.
Kiswahili:
Jaji Mohamed Chande 🇹🇿: Nimesoma kwamba kuna ripoti ya Oktoba 29 inayosubiri kutolewa chini ya uongozi wako. Nilipata heshima ya kukutana nawe kupitia marehemu George Kristos (RIP), mtu wa uadilifu-hivyo nilishikilia jina lako kwa kiwango hicho hicho.
Sijasoma ile ripoti ya awali inayodaiwa ilikuwepo Ila ilirudishwa irekebishwe, na sizungumzii mambo ambayo sijayaona au kuthibitisha. Lakini ukweli haupotei, na haki haiwezi kuandikwa upya.
Maisha mengi ya watu wasio na hatia yalipotea Oktoba 29, 2025. Hakuna simulizi iliyobadilishwa wala kuhamisha lawama kutakakosafisha damu zilizopotea-ni ukweli na uwajibikaji pekee vitakavyoweza.
Jumuiya ya kimataifa inaangalia na ina ufahamu. Yaliyofanyika gizani yatawekwa wazi siku moja-Mataifa mangi tayari wanajua na wameona kilichotokea na evidences. Hakuna aliyekuwa anaandamana alikuwa na bunduki; wala watazamaji waliopigwa risasi au waliouawa majumbani mwao hawakuwa na bunduki. Wale waliokuwa na bunduki, na waliotoa amri za kuua, ndio wawajibishwe.
Ninaandika haya hadharani kwa sababu maandishi yanayowekwa wazi, yamewahi kusaidia hapo awali na pia kuleta uwajibikaji nyakati fulani maana hata kama mtu anatarajia kufanya kitu, wakati mwingine anajitafakari yakiongelewa hadharani. Nasisitiza hekima: usiruhusu jina lako kuhusishwa na dhuluma na ukuwikwaji wa haki za binadamu.
Mark this post.🙏🇹🇿 -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Kauli hii ya KIPUMBAVU inashusha hadhi ya Ndoa na Mwanamke. Mapenzi si “show” ya kununuliwa kwa iPhone, ni wajibu wa kiungu unaojengwa kwa upendo na heshima. Ukianza kujenga ndoa kwa zawadi, ujue umeiweka rehani.
Leo iPhone, kesho akipewa G Wagon nje anakuuza bila hata huruma. Ndoa si biashara, ni agano. Ukilifanya soko, usishangae bei ikipanda na wewe ukauzwa. Achaneni na hizi INJILI za Tik Tok. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Mara nyingi watu huchanganya serikali na nchi, kana kwamba ni kitu kimoja. Ukweli ni kwamba nchi ni watu, ardhi, utamaduni na mustakabali wa pamoja, ilhali serikali ni chombo cha uongozi cha muda. Hivyo inawezekana kuipenda nchi kwa dhati huku ukiikosoa au kuipinga serikali inapokwenda kinyume na haki na maadili.
Biblia katika Warumi 13:1 inasema, “kila mtu na aitii mamlaka iliyo juu yake, kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu, na ile iliyopo imewekwa na Mungu.” Hata hivyo mamlaka iliyowekwa na Mungu inapaswa kutenda haki, huruma na ukweli, yaani kufanya mambo ya Mungu. Pale mamlaka inapogeuka na kuanza kukandamiza, kueneza ufisadi au kumwaga damu isiyo na hatia, inakuwa imeacha nuru na kuanza kutumikia giza.
Kwa hali hiyo, kuikosoa au kupinga uovu wa serikali si kuichukia nchi, bali ni kuipenda kwa kutamani iongozwe kwa haki. Mwananchi anapokataa dhuluma na kusimama upande wa kweli, anatimiza wajibu wa kimaadili na kiroho.
Kwa hitimisho, utii kwa mamlaka ni sahihi pale inapofuata haki. Lakini mamlaka inapogeuka kuwa chombo cha giza, wananchi wana wajibu wa kusema hapana ili kulinda haki, amani na uadilifu katika jamii. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Kuna mtu kaandika hivi kule Jamii Forum !!
“ Huu msemo wa Africa bado tuna safari ndefu, sio sahihi. Sisi hatuna safari ndefu na wala fupi. Hatuna kabisa safari yoyote” -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
imani ya Kikristo utagundua kwamba kama shetani angekuwa na akili asingefikiria kabisa kumuua na kumsulubisha Yesu Kristo. Kwani katika hiyo dhana ndipo Ukristo na wokovu ulipozaliwa. Kwa hiyo hata Yuda Iskariote hakufanya kazi mbaya, ukimtafakari kama wewe ni Mkristo utamshukuru sana.
Katika siasa na harakati za kupigania haki,wasaliti wa mapambano ya kweli wanaogeuka bidhaa wana maana na faida kubwa sana kwetu kuliko wangebaki nasi. Wanatufundisha hata kujua tabia zetu na maadili yetu. Kama mtu anaweza kupewa pesa kusaliti haki na maumivu, vipi akiwa Waziri au Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, ataacha pesa za miradi zipite salama ? Kama Nchi tuna tatizo kubwa la Fikra, Uadilifu na Maadili kuliko siasa na katiba. Nafikiri ni baraka sana Yuda aendelee kubusu na kukumbatia watu CHADEMA. Ni funzo kubwa sana. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Ni bora kusali na kuomba usijibiwe kuliko kutokuomba na usijibiwe.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Mke wangu hata kama mimba Ina miezi tisa usizae sasa hivi, maana mimi bado sijapata pesa ya kutunza mtoto.
Huko ndiko tunakoekea. Trust me , nyie, hayo magari yanatumia maji ? Punguzeni kodi na tozo za mafuta. Igeni Zambia. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Nikiwa mdogo hivi, karibu na duka la Ma Bro wangu Mwanza (Sheikh Amin Street) kulikuwa na washikaji wanauza mitumba.
Mimi nikawa napiga nao stori, nikavutiwa… nikasema hii deal naweza.
Wakanipa idea, wewe Godiii , Ma Bro wako wana mpunga, nenda kaombe mtaji, tupige mchongo wa viatu vya Kampala.’ Nikaenda , kila nikienda kuomba pesa, naonekana kama bado nyoka yaani … sina credibility, bado kidogoo😅
Mpaka siku moja mshikaji mmoja Dula, akanipa trick, Godii, Ava kama mtu mzima, utaonekana serious.’ Punguza Jeans na Jordan!!
Basi nikapiga shati la Nino + suruali ya mchele mchele imepigwa pasi piriiii !! Nikawavizia Ma Bro wote wakiwa pamoja, siku hiyo kulikuwa na kama ka family party, nikaingia na confidence ya CEO wa mtaa . 😂. Nikapiga presentation full kunja kunja mikono kama Diwani anaongea na Mkuu wa Mkoa😂😂
Bro wangu mmoja akawa ananipiga chabo kwa undani , yaani deep😂, akaniambia,
‘umevaa kama unajua unachokisema… na umekuwa… lakini bado kidogoo😂
Nimeikumbuka hii story leo , ni kweli unaweza kuwa umevaa suti na tai na full confidence , lakini kumbe maarifa, akili na uelewa , bado kidogoo!!!
Huyu Chalii kuwa msemaji wa Serikali ni uduansi mkubwa sana, nami nasema kwa sauti ya Bro , Msigwaaa wewe ktk kazi hii , bado kidogooo😂😂😂😂😂 -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Serikali inayochaguliwa na watu, hupaswa kuishi kwa ajili ya watu, kulinda maisha yao si chaguo, ni wajibu.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Mungu anaipenda sana CHADEMA. Huyu chalii kachomoka? Honestly, si loss. Alikuwa full liability, yeye kuwa CHADEMA ilikuwa risk zaidi, kama meli za mafuta kupita Strait of Hormuz. Mara tatu nilishataka kumfukuza nikiwa Mkti wa Kanda ya Kaskazini, lakini waliomhitaji wakam-hold. Sasa hivi? POA. He is nothing, buddy.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Mungu akubariki sana.
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Son: Dad, I’m considering a career in organised crime!!
Dad: Government or private sector? -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Ninawaza. Ripoti ya CAG iliyowasilishwa jana haikuwa ngeni kwa Rais wala vyombo vya dola. Ni taarifa inayopitia mifumo ya utawala kabla ya kufika kwa umma. Swali la msingi linabaki, kama kulikuwa na uwezo wa kuchuja yaliyomo, kwa nini baadhi ya mambo yameruhusiwa yasomwe hadharani?
Kwa mtazamo wangu, hii inaweza kuwa sehemu ya mkakati. Yaliyotolewa yanaweza kuwa si makubwa zaidi bali ni sehemu ndogo ikilinganishwa na ambayo hayajawekwa wazi. Inawezekana mjadala wa umma umeelekezwa kwenye haya ili kuficha makubwa zaidi.
Mara nyingi baada ya taarifa kama hizi hufuata ufafanuzi wa kimkakati, kupunguza uzito wa hoja au kuelekeza simulizi upande fulani. Hapo ndipo umma huanza kuamini kuwa kila kitu kiko wazi ilhali ukweli kamili haujafikiwa.
Kwa hiyo siioni tu kama ripoti bali namna ilivyowasilishwa. Inawezekana tunasikia tulichopaswa kusikia na tulichopaswa kujua hakitafika kirahisi. Hii inaashiria uwepo wa fikra za kimkakati nyuma ya uwasilishaji wake.
Mwisho, si kila kinacholetwa hadharani ni picha nzima ya ukweli. Ukweli unahitaji uchambuzi wa kina zaidi ya kile kinachoonekana juu juu. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Some people leave marks on hearts, not just memories. He was a good guy.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Kuna msemo unasema “ Upendo ni kulinda utu wa mwingine, si kumfanyia mzaha wa hadharani”
-
Godbless E.J. Lema reposted
Martin Maranja Masese
@IAMartin_
UFISADI ujenzi wa uwanja wa michezo Arusha.
Uwanja huo wa michezo unaojengwa Jiji la Arusha unajengwa na Kampuni ya China Railway Construction Engineering Group Limited (CRCEG) kutoka China.
Makadirio ya ujenzi TZS bilioni 187. Gharama ya Mkataba Serikali na mkandarasi TZS bilioni 338.54. Ongezeko ni TZS bilioni 151.54. Ongezeko ni 81%.
Gharama zisizo halali ikiwemo TZS 3.27 bilioni za gharama za zabuni zilijumuishwa katika mkataba kati ya Serikali na Mkandarasi na kubebwa na serikali
Kuna tofauti kubwa kati ya makadirio (estimates) na thamani ya mkataba (contract value). Ongezeko la gharama (variations) ni ½ ya makadirio ya ujenzi.
Mchakato wa zabuni (procurement) haukuzingatiwa. Mkandarasi alipatikana kwa njia ya mzabuni mmoja kwa kisingizio cha dharura bila kuwepo ushahidi wa hilo.
Hii iliondoa ushindani ambapo ungeweza kuhakikisha upatikanaji bei nafuu kulinda maslahi ya serikali. Huu ni upigaji au upangaji wa bei usio na tija (over-pricing).
Huo ni ubadhirifu wa fedha za umma; hizo ni kodi za watanzania. Ni jasho halali la watanzania. Hayo ni matumizi mabaya ya ofisi za umma; huu ni UFISADI.
Unategemea wezi waliofanya ufisadi na ubadhirifu wa mali za umma kama huu waone aibu? Wezi wakamatwe, washtakiwe, wakipatikana na hatia WANYONGWE.
Mwizi hana aibu. Mwizi anastahili kupewa adhabu kali sana. Mwizi akipewa adhabu kali inakuwa fundisho kwa wezi wengine. You can’t shame the shameless.. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Kutaka kuonekana tajiri kumewafilisi watu wengi zaidi kuliko umaskini wenyewe. Kuishi kwa ajili ya macho ya watu ni biashara ya hasara.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Siku 34 zimepita tangu kesi ya Uhaini inayomkabili Mhe.
@TunduALissu isimame, hii ni baada ya ombi la mapitio lililofunguliwa na Jamhuri katika mahakama ya rufaa, ambayo halijapangiwa tarehe hadi leo. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Au tutengeneze !!!
TAAKUTA.
Taasisi ya Aibu na Kusuta Tanzania
Kaulimbiu:
Aibu Kwanza, Uwajibikaji Baadaye
Dhamira:
Kuwataja hadharani wale wote wanaosababisha hasara ya fedha za umma ili waone aibu ya taifa.
Majukumu Makuu:
•Kushirikiana na Public Procurement Regulatory Authority na Prevention and Combating of Corruption Bureau kupata orodha ya wahusika
•Kutangaza majina ya “Wasutwe” kila mwaka
•Kuendesha kampeni za VIBE ya AIBU kwenye mitandao ya kijamii
Huduma Maalum:
•Aibu Index: Kipimo cha kitaifa cha nani kaaibisha zaidi
•Wall of Shame: Orodha ya wazi ya waliotajwa
•Badge ya Aibu: Cheti rasmi cha kusutwa kinachoweza kusambazwa online .
Hitimisho:
Kwa sababu wakati mwingine sheria zipo kimya…TAAKUTA inasema kwa sauti kubwa, INATOSHA. 🔥 -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Kuna tukio kama hili kweli ? Ujinga ni mzigo sana. Kuna haja gani ya kutokuwa wazi kwenye mambo kama haya ? Maisha yetu yamekuwa na thamani ndogo kuliko mende. Jambo la huzuni na hatari sana.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Nafikiri sasa labda tutunge sheria-
AIBU & WASUTWE ACT 2026
Section 1: Definitions
•Aibu: kitendo cha mtu kuonekana hadharani akiwa amefanya makosa makubwa, hasa kuharibu fedha za umma.
•Wasutwe, wale wote wanaotajwa katika ripoti za PPRA na TAKUKURU.
Section 2: Punishment
•Kununiwa hadharani na wanajamii ni adhabu ya kwanza.
•Hakuna haja ya pesa kurudishwa; vibe ya aibu inatosha.
Section 3: Implementation
•PPRA na TAKUKURU watahakikisha orodha ya “wasutwe” inatolewa kila mwaka.
•Majina yatawekwa kwenye billboard, Instagram, TikTok na Twitter.
Section 4: Bonus Clause
•Ukiwa “wasutwe” unapata badge ya aibu: inaweza kusharewa kwa reels na memes.
•“Likes” nyingi hazirudishi fedha lakini zinachoma ego 🔥😂 -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Tazama tofauti ya mifumo, CANADA, CEO wa Air Canada ameingia kwenye shinikizo kubwa na kuondoka kazini baada ya kufanya mawasiliano ya umma kwa lugha ya Kiingereza pekee huku akisahau Kifaransa. Lugha zote mbili ni rasmi nchini Canada. Hilo lilionekana kukiuka misingi ya uongozi. Na sasa amejiuzulu. Sasa linganisha na Tanzania. Mabilioni yanapotea na utendaji mbaya unaendelea kuimarika lakini adhabu zinabaki kuwa aibu labda kusutwa.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Natoa pole kwa ndugu, rafiki na jamaa wa Bwege. Nilikuwa naye Bungeni, alikuwa mbunge anayechukizwa na mateso ya watu na mauaji.
Niliongea naye hivi karibuni na kuahidi kumuona siku za karibu, lakini haitowezekana tena sasa. Pumzika kwa amani.
“Kila nafsi itaonja mauti.” Qur’an (3:185)
Kifo kina ukimya unaozidi maneno. Hutufundisha kuwa muda si mali yetu bali ni mkopo. Kinaondoa kiburi cha kesho na kutuacha na ukweli wa leo. Mwisho wa pumzi si mwisho wa maana, bali ni mwanzo wa kupimwa kwa yale tuliyoishi. Tunapomlilia aliyeondoka, tunakumbushwa kuwa safari yetu ina mwelekeo ule ule, na thamani ya maisha ipo katika athari tunazoacha nyuma, si muda tunaokaa duniani. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Kauli ya Samia Suluhu Hassan ya kutaja taasis kuwa ni aibu kama adhabu ni udhaifu mkubwa mbele ya uzito wa tatizo. Hasara ya mabilioni ya fedha za umma si kosa la kuoneana aibu ni kosa la kuwajibika kisheria.
Tazama tofauti ya mifumo, CANADA, CEO wa Air Canada ameingia kwenye shinikizo kubwa na kuondoka kazini baada ya kufanya mawasiliano ya umma kwa lugha ya Kiingereza pekee huku akisahau Kifaransa. Lugha zote mbili ni rasmi nchini Canada. Hilo lilionekana kukiuka misingi ya uongozi. Na sasa amejiuzulu. Sasa linganisha na Tanzania. Mabilioni yanapotea na utendaji mbaya unaendelea kuimarika lakini adhabu zinabaki kuwa aibu.
Hapa ndipo tatizo lilipo. Taasisi kama Public Procurement Regulatory Authority PPRA na Prevention and Combating of Corruption Bureau TAKUKURU hazikuundwa kutengeneza orodha ya wanaoaibika. Zipo kulinda fedha za umma kwa hatua uchunguzi kesi na adhabu.
Ukiharibu mali ya umma adhabu haiwezi kuwa jina lako kusomwa kwenye ripoti. Lazima iwe hatua inayoonekana.
Bila hivyo aibu inabaki mzaha na mfumo unaendelea kuzalisha uzembe ule ule.
Aibu kubwa ndio hii hapa sasa. Tanzania inaumizwa sana. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
hawa washikaji leo. 😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Jambo la msingi ni kwamba COCO Beach ibaki kuwa ufukwe wa umma, unaopatikana kwa kila mwananchi. Hata hivyo, ni lazima tuingize ubora, hadhi (class), na viwango vya juu katika uendeshaji wake. Ubora na standards haviwezi kuwekwa pembeni kwa sababu ya wingi wa watu, badala yake, viwe juu ya populism. Watu wanapaswa kujengwa ktk hadhi na standard. Ni mkakati mzuri wa kuinua FIKRA na UBUNIFU.
Kwa hiyo, COCO Beach inapaswa kuwa ufukwe wa umma wenye hadhi, nidhamu, na viwango vya kimataifa mahali ambapo kila mtu anapata huduma bora, si tu kwa wingi wa watu, bali kwa ubora wa hali ya juu. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Huu sio uwekezaji hata kidogo. Nilisema hapo nyuma na ninarudia tena hapa Coco Beach panahitaji brain power. Ni ufukwe bora kabisa katika Jiji la Dar es Salaam na mipango yake haiwezi kuendeshwa kwa mjadala uliobeba poverty mentality.
Jitihada yoyote ya kurekebisha Coco Beach ili kubeba quality standard mimi nitakuwa mshirika wake ktk jitihada hizo. Nafurahi kwamba ukweli ktk eneo hili umeanza kusikika. Mindset transformation is bigger than voting collection.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema reposted
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
This is Lack of quality THINKING. Hata kama mlikuwa mmekusudia eneo hili la COCO Beach kufanyike biashara basi ni dhahiri kwamba standard ya biashara yenyewe hazikupaswa kuwa za aina hii.Huu ni ufukwe mrefu kabisa ktk eneo Posh la Jiji,lakini mmeshindwa ku regulate quality na standard.Mmeua ajira nyingi zaidi kwa kushindwa ku apply tu a proper THINKING ktk eneo hili.Kama fikra zako hazijali ktk kuzingatia ubora na classy basi uwezi kuwa na utamaduni wa raia wako kuwa na quality Thinking.Hii ni hatari maana maisha bora yanajengwa na mawazo na sio rasilimali.
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Kabla mtu hajawa mzazi, ni vigumu kuelewa kwa undani sacrifice (sadaka) ambazo wazazi wake walichukua ili kumfikisha hapo alipo. Mara nyingi tunaona malezi kama jambo la kawaida, bila kutambua kuwa nyuma yake kulikuwa na kujinyima, machozi, maamuzi magumu, na upendo wa kimya usiohitaji kuthibitishwa kwa maneno.
Kadri vizazi vinavyobadilika, imekuwa kawaida kuona wazazi wakitengwa taratibu wanapozeeka. Tunajipa sababu ya “struggle” za maisha, lakini ukweli huo hauondoi ukweli mwingine kuwa wanatuhitaji zaidi kadri wanavyozidi kuzeeka. Sio kwa uwepo wa kila wakati, bali kwa ukaribu unaoonekana na kuhisiwa.
Kadri ninavyozidi kukua, ndivyo ninavyotambua kuwa wazazi wengi wanaishi na upweke wa ukimya. Ni hali ambayo huenda hata wao waliirithi, wakaiishi, na sasa inaendelea bila wengi kutambua. Hapa ndipo tunapopaswa kubadilisha mwelekeo kwa vitendo vidogo vya kujali, kusikiliza, na kuwa karibu.
Tulipokuwa wadogo tuliwahitaji wazazi wetu kuishi, wanapozeeka wanatuhitaji sisi ili kuhisi kuwa bado wanaishi. Kuishi sio kuwa na pesa, ni upendo wenye hisia na kutambua. Ukitafakari kwa makini unaweza kutambua kuwa wazazi wako walionekana masikini mtaani, kwa sababu mitaji yao ya kujinufaisha wao waliwekwa katika maisha yako.
Inawezekana wewe na mzazi / wazazi wako kuna wakati hamkuelewana vizuri wakati wa malezi, lakini Kumbuka wakati wewe huko kwao unakua na wao bado walikuwa wanaendelea kukua na kukomaa vizuri. Hivyo likuwa ni watu wawili wote mnajifunza. Kwa hiyo some flaws does not mean walikuwa wakatili kwako. -
Godbless E.J. Lema reposted
Kenny Mmari Snr.
@KennedyMmari
Hii dhana kwamba viongozi wa serikali wanasafiri sana na kupata exposure ya kutosha wala siyo rahisi kama watu wanavyodhani na hata wakisafiri ni kwa kujibana sana na kuwa na predestinated itinerary😬
Pia, kama jamii, hatuna utamaduni mpana wa kusafiri na kujifunza kutoka nje.
Lakini hata hivyo, hoja yangu ya msingi haikuwa “kusafiri” pekee. Kusafiri hakumpi mtu exposure. Exposure inakuja pale ambapo kuna intentional learning.
Unaweza kusafiri mara nyingi na usibadilike chochote. Na unaweza kusafiri mara chache lakini ukarudi na mabadiliko makubwa ya fikra na utekelezaji.
Ndiyo maana katika kujenga taifa, exposure haiwezi kuachwa kwenye bahati, lazima ipangwe kwa makusudi.
Utawala wa Nyerere (mnisamehe ninamzungumzia sana) ulielewa hili kwa kiwango fulani. Kulikuwa na jitihada za makusudi za kupeleka Watanzania kusoma katika vyuo bora duniani kwa lengo la kurudi kujenga nchi. Hii si nadharia, ni historia hai maana hata kwenye familia yetu kuna mtu alisomeshwa Harvard. Wapo watu wengi walipelekwa nje kwa dhamira hiyo.
Hicho ndicho kinachoitwa closing the exposure gap through design.
Ukichunguza nchi nyingi za Asia, hasa China, utaona consistency ya mkakati huu. Kwa zaidi ya nusu karne, wamekuwa wakipeleka vipaji bora kusoma nje, kujifunza mifumo bora, na kurudi nyumbani kutekeleza na wanapewa uwanja wa kutekeleza, pamoja na rasilimali. Hii siyo ajali, ni mfumo wa makusudi mno!
Sasa, hata kama hatuwezi kufanya kwa scale hiyo, angalau tunahitaji kuwa na intentionality. Basi tupeleke watu kujifunza kwa muda mfupi, tujenge mifumo thabit ya knowledge transfer na tuhakikishe wanaorudi wana nafasi ya kutekeleza wanachojifunza
Bila hilo, exposure inabaki kuwa individual benefit, si national asset. Tukirudi kwenye uhalisia wa Tanzania leo, swali linabaki, kwa nini bado hatuna miji iliyopangiliwa vizuri, safi, na yenye ustaarabu wa hali ya juu? Jibu la swali hili haliwezi kuwa rasilimali pekee.
Ni ukosefu wa utamaduni wa learning and benchmarking. Na utamaduni hauji kwa bahati mbaya. Unajengwa kwa makusudi. Kupitia kuona mifumo mingine, kujifunza, na kuamua kuitekeleza kwa mazingira yako.
Bila kufanya hivyo, tutazidi kuboresha ndani ya kile tulichokizoea, badala ya kufikia kile kinachowezekana.
David Magundu
@Magundujunior
Moja katu ya andiko bora kabisa toka kwako kulisoma tangu mwaka uanze, lakini... Kweli viongozi wetu hawana exposure? Wao si ndo wanaongoza kwa kutembea huko nje na wanaona kabisa wenzetu wanachofanya...
Mi nadhani cha kubadilisha hapa ni uongozi wenyewe. CCM imechoka... -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Polisi nchini Nepal wamemkamata aliyekuwa
Waziri Mkuu wa nchi hiyo KP Sharma Oli na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchi hiyo Ramesh Lekhak kutokana na tuhuma zinazowakabili za kuhusika katika ukandamizaji wa maandamano
uliosababisha vifo vya watu kadhaa mwaka jana.
Oli alikamatwa jumamosi katika makazi yake yaliyopo kitongoji cha Bhaktapur katika mji wa Kathmandu na kuwekwa kizuizini.
Msemaji wa Polisi wa mji wa Kathmandu Om Adhikari amesema "Wamekamatwa leo asubuhi na taratibu zinaendelea kwa mujibu wa sheria"
Kufuatia maandamano makubwa yaliyotokea nchini humo Septemba 8-9, 2025 ambayo yalikuwa yanapinga kukithiri ufisadi angalau watu 77 waliuawa.
Ambapo yaliyoanza kutokana na marufuku fupi ya mitandao ya kijamii lakini yakagusa hasira zilizokuwa zimechukuliwa kwa muda mrefu kutokana na changamoto za kiuchumi. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
-
Godbless E.J. Lema reposted
ROYAL TELEVISION PLUS
@Royaltv_plus
Katika hali ya majonzi na tafakari nzito, Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Yosefu, Padre Denis Wigira, ametoa fundisho kali kuhusu asili ya mwanadamu, akibainisha kuwa migogoro na chuki zinazoikabili jamii hivi sasa zinatokana na binadamu kupoteza uwezo wa kutambua thamani ya mwenzake.
Akizungumza leo, Machi 28, 2026, katika viwanja vya Karimjee wakati wa ibada ya kuaga mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Hayati William Vangimembe Lukuvi, Padre Wigira amesisitiza kuwa mwanadamu ana thamani ya asili ambayo haitolewi, haiuzwi, wala haiwezi kuchukuliwa na kiumbe mwingine yeyote chini ya jua.
Padre Wigira amefafanua kuwa, kwa sababu ya kutotambua thamani hiyo ya kipekee, watu wamejikuta wakiishi katika tofauti, hasira, na mafarakano yasiyokuwa na tija. Alibainisha kuwa thamani ya mwanadamu ni ya kiungu na haipaswi kupimwa kwa vigezo vya kidunia au vyeo, bali kwa utu na udugu wa kibinadamu ambao ni zawadi ya kudumu.
Aidha, kiongozi huyo wa kiroho amegusia kile alichokiita "Upofu wa Baada ya Kifo," ambapo jamii huchelewa kutambua fahari na mchango wa mtu mpaka anapofariki. Alisema ni jambo la kuhuzunisha kuona sifa, heshima, na utukufu wa mwanadamu vikipamba anga wakati mhusika akiwa tayari amepoteza uhai, jambo linaloonyesha mapungufu makubwa ya kifikra na kimaadili katika jamii yetu.
Huku akitoa wito kwa waombolezaji waliojitokeza kutoa heshima zao za mwisho kwa Hayati Lukuvi, Padre Wigira amewataka Watanzania kujitathmini na kurejea kwenye misingi ya kuthaminiana wakati wa uhai. Amehitimisha kwa kusema kuwa maombolezo haya yanapaswa kuwa shule ya upendo, ambapo kila mmoja anapaswa kujifunza kuona thamani ya mwenzake kabla ya safari ya mwisho haijawadia. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Wewe wanakuondoa hapo wanasema huku mitaani tukikutana nao huku kwenye nyama choma, halafu wanaweka mtu wao. Pia wanakusema vibaya sana Baba huku mitaani. Mimi nakwambia kwa sababu wewe ni mtu wangu. Tumejuana zamani.😂😂😂😂
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Siku moja niliona umeandika mtandaoni kuwa unachukizwa sana na watu wanaoisema familia yako vibaya, hususani ulivyokuwa uki-post picha ya mtoto wako huku watu wakikejeli kuwa mtoto wako ameshiba kodi zetu.
Sasa, Mwigulu, ulishawahi ku-imagine namna, mke au watoto wa Ally Kibao huwa wanajisikia baada ya baba yao kuuwawa kikatili ? Au Ben Saanane au familia ya Msafiri Mbwambo aliyeuwawa kwa kuchinjwa kwa chain saw wkt ule wa uchaguzi mdogo Arumeru Mashariki wewe ulipokuwa unaratibu kampeni za CCM ? Mna mchapa mtu halafu akilia, mna mchapa tena kwa nini analia ? Very Narcissist personality.
Chama chenu kimejenga chuki kubwa sana ktk jamii. Hata tofauti ya watu safi na wabaya ndani yenu haionekani tena hata kama wamo. Na hatari yake kila mtu anavuna kejeli ya collective responsibility. Pigeni U Turn Acheni Kiburi !
Mnashangaa watu kufurahia matatizo yenu lakini hamhuzunishwi na watu wanaopotea na kufa bila miili hata miili yao kupatikana ? Mnafikiri nyie mnapaswa kuishi kwa starehe tu lakini the rest waishi maisha ya wasiwasi ?
Anyway, unakumbuka mjadala wangu Mimi na wewe wkt ule ukiwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Mimi Waziri Kivuli kuhusu mawuaji na utekaji ? Leo nitaishia hapa.
Pigeni U Turn Acheni Kiburi. Mmeumiza sana watu na Nchi , mateso yamegeuka hasira na hasira imeumba chuki. Kuna njia mbele ya kutoka hapa , nayo ni HAKI. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Utajiri wa Binadamu ni Haki , Utu , Huruma , Upendo na Afya.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
“Bwana akasema, Tazama, watu hawa ni taifa moja, na lugha yao ni moja; na haya ndiyo waanzayo kuyafanya; wala sasa hawatazuiliwa neno lolote walilokusudia kulifanya. Haya, na tushuke huko, tukachanganye lugha yao, ili wasisikilizane maneno yao kwa wao.” (Mwanzo 11:6–7)
Falsafa inayotokana na mstari huu ni dhahiri kuwa imani yenye mshikamano, pamoja na malengo thabiti, hata ikiwa inapatikana miongoni mwa wapumbavu, ina uwezo wa kuvunja vizuizi vya busara na akili isiyo na nguvu ya kushirikiana na kuamini.
Katika nchi yetu, mifumo ya utawala inayoonyesha udhaifu mara nyingi husababishwa na wajinga na watu wabaya wenye imani na mshikamano katika masuala ya siasa, huku watu wema na werevu wakibaki nyuma kwa sababu ya kushindwa kushirikiana na kuinua imani ktk mapambano.
Fikiria kuhusu mnara wa Babeli , hata Mwenyezi Mungu mwenyewe aliogopa mshikamano wa watu wa Babeli, na ikabidi awatengenezee confusion ili malengo yao yasifanikiwe.
Ubaya hauna nguvu kuliko wema Ila watu wema wametoa kibali kwa ubaya kutawala kwa sababu ya kukosa maarifa , imani na ushirika muhimu ktk kujali wema. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
CCM haijawahi kuwaza future generations hata siku moja , isipokuwa uchaguzi tu, mambo mengi yanayotokea ktk utawala wao ni basic issue tu. Umetumika vibaya ktk kila nyakati za utawala wa CCM , kudhalilisha, kuumiza na mabaya mengine mengi kama ambayo USA waliyatolea tamko.
Anayekutumia wewe hawezi kuwa na maarifa ya kutosha kwa sababu wewe ni liability. Kuanzia wakati wa JK, Magufuli, na sasa Samia. Ulimgeuka yoyote mwenye heshima yoyote kutokana na interest na sio integrity na haki. Nafikiri wanaokutumia wanafurahishwa na uzembe wa fikra za aina hii. Hata hivyo mambo yatakuwa tofauti sana ktk siku za usoni. Nafikiri siku zote huko nje ya kuta za jela kwa bahati mbaya. Unapaswa kuwa jela. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Nilikutana na hii video leo. I think was very nice UJUMBE.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
AU ni kundi la WASELA linalokutana mara kwa mara Addis Ababa, Ethiopia, wakijikita zaidi kwenye table manners na executive dressing code kuliko kushughulikia matatizo halisi ya Waafrika.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Jamii inapofikia hatua ambapo kusema haki kunachukuliwa kama kitu cha ajabu, si kwamba wanaosema wamebadilika bali mizani ya maadili imepindishwa. Haki inapogeuka kuwa nadra, ndipo ubaya hujipenyeza kimya kimya na kujifanya kawaida. Hatari kubwa si ukatili wenyewe, bali ni ule ukimya unaouhalalisha. Pale ambapo watu wanaanza kuogopa hata kutaja mema, ndipo dhamiri ya jamii huanza kufa polepole. Na mwisho wake, si kwamba watu hawajui lililo sahihi bali wamezoea kuishi kinyume nacho. Eti kusema ukweli ni trending issue na kusema uongo na hila ni connection. Sad society
-
Godbless E.J. Lema reposted
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
KATAA DHARAU - Unaweza kuishi bila kazi ya Serikali,una umri wa kutetea principle kuliko chakula. Kwanza kwa umri wako ni lazima utakuwa na masharti ya kula.Kwa hiyo mboga za majani na matango huwezi shindwa.Mtazame Jenerali Ulimwengu/Prof Assad.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Tunazaliwa bila kitu, na tunaondoka bila kitu, kifo hutukumbusha unyenyekevu wa maisha. Ukiyatafakari maisha kwa kina, utajifunza mengi, lakini zaidi ya yote utajifunza upendo, huruma, haki na utu wema ndio vitu vya msingi ktk kuishi. Maana hapa duniani tunapita kwa kasi kubwa sana, haijalishi tunamiliki nini au sisi ni nani. Kifo ni kumbusho kuwa kesho yetu haipaswi kuwa chanzo cha maumivu kwa wengine hata kidogo. Nafikri hii ndiyo maana halisi ya kuishi , kuacha alama ya wema na upendo si majeraha mioyoni mwa watu. Maumivu ya kuondokewa ni makubwa, lakini kumbukumbu nzuri ni tiba ya moyo.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Kujiona unajua kila kitu ndiyo kizuizi kikubwa cha kujifunza. Mpumbavu hujaza pengo la maarifa kwa majivuno na tatizo la mpumbavu si ujinga wake, bali kuamini anajua kila kitu. UPUMBAVU huu hapa tena.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Dr. Nshala: Tumeanika Jinsi Amri za Mahakama Kuu zilivyolenga Kuidhalili... youtu.be/N3N4XyvjqYk via @YouTube
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Wakili bora si yule anayeshinda kila kesi, bali yule asiyokata tamaa hadi haki ionekane.Katika giza la dhuluma, wakili jasiri huwa mwanga wa matumaini.
Thank you guys. -
Godbless E.J. Lema reposted
Jebra Kambole
@Advocate_Jebra
All the best Team!!
Japo haki ni bidhaa adimu sana maeneo yetu haya, lakini kwa uwezo wa Mungu haki ikatawale.
Ningekuwepo lakini ndo hivyo tena, nimeweka kiapo changu maana mimi ni shahidi wa kilichotokea mahakama kuu!
Kiwakeeee wakubwa wa kazi!!! -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Katika zama za mitandao ya kijamii, taarifa imekuwa silaha na uaminifu umekuwa uwanja wa mapambano. Sio kila kinachoonekana ni cha bahati mbaya, wakati mwingine kuna dalili za mikakati ya makusudi ya kupotosha, kuchafua, na hatimaye kudhoofisha sauti za watu wenye ushawishi.
Njia yake ni ya hila, uzushi unatengenezwa, unasambazwa kwa kasi kupitia mitandao, kisha watu wenye ushawishi wanauchukua bila uthibitisho. Baadaye ukweli unapojitokeza, walioueneza hubeba lawama na polepole huanza kupoteza credibility. Mwisho wake si mtu mmoja, bali ni jamii nzima kupoteza imani kwa taarifa na kwa mitandao yenyewe. Hii ni hatari kubwa. Jamii isiyoamini taarifa haiwezi kufanya maamuzi sahihi. Na pale ukweli unapochanganywa na uongo, hata ukweli wenyewe hupoteza nguvu.
Tahadhari ni moja, tusiwe wasafirishaji wa kila taarifa. Tuulize, tuthibitishe, na tuchambue kabla ya kusambaza. Kwa sababu katika vita hii ya taarifa, silaha kubwa si sauti kubwa peke bali taarifa zenye dalili za ukweli.Tukipoteza uaminifu, tumepoteza mwelekeo. Na jamii isiyo na mwelekeo ni rahisi kuongozwa popote. Na kuna mkakati kabisa wa makusudi ktk msingi huu. Mtafakari kila mtoa taarifa na tambua Disinformation campaigns (taarifa za kupotosha kwa makusudi) , pia huu huwa ni mkakati wa ujasusi ktk kulinda dola yoyote dhalimu. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Mahakama si jengo tu, bali ni dhamira ya nchi. Pale haki inapocheleweshwa, inapochaguliwa, au kuonekana kuwa ya upande, wananchi huanza kuuliza , je, bado kuna kimbilio? Swali hilo likiachwa bila majibu ya vitendo, hubadilika kuwa hasira, na hasira ikikomaa hugeuka kuwa kutotii, si kwa sababu wananchi hawapendi sheria, bali kwa sababu hawaioni tena.
Watawala wanapaswa kutambua, mamlaka si kinga dhidi ya ukweli. Heshima ya dola haitokani na nguvu, bali na uhalali unaotokana na haki inayoonekana na kugusika. Kila uamuzi unaotia doa taswira ya haki hujenga kizazi kisichoamini, na kizazi kisichoamini hakiogopi.
Tahadhari iko wazi, lindeni uhuru wa mahakama, achieni sheria ifanye kazi bila upendeleo, na wekeni mbele uwajibikaji kuliko maslahi ya muda mfupi. Kwa sababu siku wananchi wakiamini kuwa hawana pa kukimbilia, wataanza kujitafutia njia zao. Na historia inaonyesha, njia hizo mara nyingi si tulivu.
Haki ikisimama, taifa linasimama. Haki ikiyumba, hakuna atakayesalia salama wala mtawala, wala mwananchi. -
Godbless E.J. Lema reposted
Brenda Rupia Jonas
@BrendaRupia
Jamani hawa watu, Mwenyezi Mungu aendelee kuwapa afya njema na kuwatimizia mahitaji ya mioyo yao.
Mawakili wa @ChademaTZ2 , mbarikiwe sana. Wakati wengine wanatamani chama kife, nyinyi mmeonesha uthabiti na weledi hata kushuka kwenye SGR mmeshuka in style na hadhi na kujiamini.
CHADEMA bado tupo imara. Watajaribu kutuchosha kwa kesi nyingi, lakini tutaendelea kujitokeza na hatutakata tamaa.
Tupo rada. Dodoma tumeshafika, na tupo tayari kukabiliana na Jaji Mkuu.
#freelissu
#katibampyanisasa -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Wewe Chalii , acha maneno ya KIJINGA JINGA Mtandaoni. Nimekwambia TUBU.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Kwani Kaka yake mkubwa kabisa na CHAWA ana jina ? Kama analo, basi TAFAKARI hilo angalau, linaweza kuwa bora zaidi kwako. Nafikiri tu.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Watu wengi sana waliotabiri CHADEMA kufa wao ndio waliokufa. Kwani na wewe una mpango wa kufa hivi karibuni ? TUBU. Tena mwambie na wife akusaidie kufunga na kuomba na KUTUBU. La sivyo !!!! Mungu anakuchapa.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Katika mitandao ya kijamii na majukwaa ya burudani hata kwenye baadhi ya mahubiri kumejitokeza tabia inayotia wasiwasi , kuwafanya wanawake kuwa chanzo cha mzaha na lawama kwa jina la vichekesho na maonyo. Mara nyingi wanawake wanabezwa kwa mwonekano wao, maamuzi yao ya maisha, na hata kuonekana kama sababu ya kushindikana kwa baadhi ya ndoa nyingi. Hali hii imeanza kuzoeleka, ilhali kwa uhalisia ni udhalilishaji unaojificha nyuma ya kicheko.
Kinachoumiza zaidi ni ile hali ya mizani isiyo sawa. Kwa mfano Mwanamke akinunua wigi la gharama huonekana kama mfujaji asiye na sifa za kuwa mke bora, lakini mwanaume anayetumia fedha kila siku kwenye ulevi huonekana wa kawaida, na wakati mwingine hata kuonekana “anajua maisha.” Hii si haki, ni dalili ya fikra zilizopinda ndani ya jamii.
Zaidi ya hapo, baadhi ya vichekesho vimevuka mipaka kwa kudhalilisha miili ya wanawake na kutoa kauli za jumla zinazowahusisha wanawake wote au hata makabila yao kwa mtazamo hasi. Hii si burudani tena, bali ni sumu inayopandikizwa taratibu katika akili za watu, ikijenga picha potofu juu ya mwanamke.
Athari zake ni kubwa na za ndani zaidi kuliko inavyoonekana. Inaua kujiamini kwa wanawake kimya kimya, inapunguza heshima yao katika jamii, na inajenga mazingira ambayo dharau inaonekana kuwa ya kawaida. Mbaya zaidi, wengine wanaanza kuamini kuwa mwanamke ni chanzo cha matatizo mengi, jambo ambalo si kweli wala si haki.
Kama jamii, hatupaswi kunyamaza. Ni wajibu wetu kukemea hali hii kwa busara, kuhimiza burudani yenye mipaka, na kuunga mkono maudhui yanayojenga heshima badala ya kudhalilisha. Si kila utani ni mbaya, lakini utani unaovunja utu wa mwanamke haupaswi kuvumiliwa.
Ni muhimu pia tukumbuke kwamba mwanamke si mtu wa mbali, kwani ni mama, ni dada, ni mke, ni binti, na ni rafiki. Kumdharau mwanamke ni kudharau misingi ya jamii yenyewe.
Kwa hitimisho, heshima ya mwanamke si jambo la mzaha. Jamii inayomdharau mwanamke, hata kwa kisingizio cha burudani, inajidharau yenyewe. Ni wakati wa kubadilika, kusimama kwa haki, na kulinda heshima ya mwanamke kwa nguvu zote. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Barua ya Tundu Antiphas Lissu si maandishi ya kawaida, ni kengele ya hatari. Inatukumbusha kuwa haki inapocheleweshwa, si tu inaumiza, bali hugeuka mateso ya wazi. Wananchi, tusijidanganye. Ukimya wetu si neutral Bali ni upande ktk kukumbatia dhuluma. Kila tunaponyamaza, tunatoa nafasi kwa dhuluma kuendelea. Kila tunaposita, tunadhoofisha nguvu ya haki.
Je, tutakubali kuwa watazamaji wa historia, au washiriki wa mabadiliko? Kama mbinu zetu hazifanyi kazi, zibadilishwe. Kama sauti yetu haisikiki, ipazwe zaidi. Haki haiombwi kwa sauti ya chini , hudaiwa kwa msimamo thabiti. Huu si wakati wa hofu wala kusubiri wengine wachukue hatua. Ni wakati wa kila mmoja kusimama na kusema inatosha.Kwa sababu ukweli uko wazi, haki ya mmoja inapovunjwa, msingi wa haki ya wote unatetereka. Na jamii inayokubali hilo, hujijengea hatari yake yenyewe. Simama. Ongea. Chukua nafasi yako. Wakati wa haki ni sasa. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Ni kawaida kabisa sasa.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Waarabu wamekataa kuwa nyuma kabisa na kila aina ya movement ambayo ni tech na uchumi endelevu. Ktk miaka michache sana inayokuja uchumi wao hautategemea sana mafuta tu. Sisi tuendelee kuimarisha CHAWA.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Kila tukio la mauaji si mwisho wa maisha ya mtu mmoja tu, bali ni kipimo cha dhamiri ya jamii nzima. Yanapotokea matukio kama haya ikiwa ni Arusha au popote pale ndani ya Tanzania, swali si nani ameuawa pekee, bali nani amenyamaza.
Hatari haianzi pale mtu anapouawa , huanza pale jamii inapojifunza kuendelea kana kwamba hakuna kilichotokea. Kimya kinapokuwa cha kawaida, uovu hupata uhalali. Na kila mmoja anapochagua kutojali, anachangia kidogo katika kuifanya dunia kuwa sehemu isiyo salama hata kwake mwenyewe.
Hakuna aliye mbali na matokeo ya jamii aliyonayo. Leo ni mwingine, kesho inaweza kuwa karibu zaidi kuliko tunavyodhani. Hivyo basi, kulinda uhai ni wajibu wa kila nafsi kwa sauti, kwa msimamo, na kwa kukataa kuzoea maovu.
Mwisho wa yote, jamii haifi kwa sababu ya waovu wachache, bali kwa sababu ya wema wa wengi ulionyamaza.
Pole sana mama na watoto wako wote.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema reposted
U.S. Marines
@USMC
Chuck Norris didn't join the Marine Corps...the Marine Corps applied to him.
Heaven’s streets have always been guarded by Marines. Today, Chuck Norris reported for duty.
We mourn the passing of Chuck Norris, a @usairforce veteran, who also became an honorary Marine in 2007 when awarded the title by then Commandant of the Marine Corps, Gen. James T. Conway.
Chuck Norris is one of just over 100 individuals to be awarded the title of Honorary Marine in the entire 250-year history of the Corps.
Some missions may require a battalion, but this one just requires an Honorary Marine.
#usmchistory #usmc #semperfidelis -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Eid ni zaidi ya sherehe, ni kumbusho la uadilifu, ukweli, na haki. Ni wakati wa kujenga uaminifu, na kuanza maisha mapya yenye furaha na baraka.
Eid Mubarak! Furaha, amani, na baraka ziwe nanyi siku hii na siku zote. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Ikiwemo TANZANIA. Very Sad !!
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Nasisitiza tena kuwa hatua ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora kuzuia mahubiri ya Injili haikuwa sahihi, hasa kwa kigezo cha kuwepo kwa kitabu chenye rangi hizo bila hata kuzingatia maudhui yake. Rangi hizo si za LGBTQ+ moja kwa moja; ni rangi za kawaida zinazotumika katika maisha ya kila siku. Hivyo basi, jambo hili halipaswi kuonekana kama vita dhidi ya ushoga, bali linaashiria mwelekeo wa vita ya kiroho na udhalilishaji wa imani.
Kuwa sensitive kupita kiasi na kuongozwa na hisia kali katika suala hili kunachochea kile kile kinachopingwa au kukatazwa na maadili yetu na Mungu mwenyewe. Hatuwezi kumpa shetani mamlaka ya kiwango hicho kwa misingi ya hofu, wakati hofu hiyo inapaswa kushindwa kwa tabia njema na kumcha Mungu.
Kwa mantiki hiyo, kuzuia mahubiri haya ni sawa na kudai kwamba Injili ya Kristo iliyohubiriwa hadharani Tabora ilikuwa inalenga ku-promote LGBTQ+, jambo ambalo ni hatari kubwa kwa imani ya Kikristo na heshima yake.
Aidha, pale mtu anapokosa umakini wa kufikiri kwa kina, hushindwa kuona namna vita ya kiroho na imani inavyoendelea kudhoofisha heshima ya Ukristo katika jamii kupitia maamuzi ya kukurupuka. Kama kweli kulikuwa na mahubiri yaliyohamasisha ushoga hadharani, basi ni wajibu wa vyombo husika kuwachukulia hatua wote waliohusika wakamatwe, washitakiwe na wawajibishwe kwa mujibu wa sheria za nchi.
Vinginevyo, hatua kama hizi hubaki kuwa ni mbwembwe zisizo na msingi. Hatari kubwa ninayoiona ni kwamba, siku zijazo, kuhubiri Injili hadharani kunaweza kuanza kuchukuliwa kama jambo gumu au lenye vikwazo vingi, sawa na changamoto zinazoonekana katika shughuli za kisiasa leo. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Mungu akubariki sana.
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Huu ni upotoshaji. Hakuna ushahidi wa moja kwa moja kwamba rangi hizi zinawakilisha LGBTQ+. Hizi ni rangi za kawaida zinazotumika kila siku katika elimu, sanaa na ubunifu. Kuzihusisha moja kwa moja na ajenda fulani bila msingi ni uoga usio na sababu na tafsiri ya haraka isiyo na uthibitisho.
Rangi za LGBTQ+ zina utambulisho wake maalum kupitia rainbow flag yenye mpangilio unaojulikana: red, orange, yellow, green, blue na purple. Kama nilivyoonyesha ktk picha hapa. Hizi unazoona ni ubunifu wa kawaida kabisa kama rangi za watoto au michoro ya kijamii.
Kinachokera zaidi ni kuona imani ya Kikristo ikidhalilishwa kwa maamuzi ya haraka yasiyo na mantiki. Kuzuia mkutano wa injili kwa sababu ya rangi ni kuonesha udhaifu wa kufikiri na kuipa hofu nafasi ya kuongoza badala ya ukweli.
Tuache kudhoofisha na kudhalilisha imani yetu kwa maamuzi ya papara. Imani ya Kikristo haihitaji kulindwa kwa hofu wala kwa kuchanganya mambo yasiyo na uhusiano. Inahitaji kusimamiwa kwa ukweli, ujasiri na hekima.
Serikali imefanya udhalilishaji mkubwa dhidi ya imani ya KIKRISTO , na kwa viongozi wa dini maamuzi ya kuomba radhi bila kuchambua kwa kina yanaweza kuleta picha ya kukosa msimamo na kuendelea zaidi kudhalilisha Kanisa. Kanisa lina wajibu wa kusimama imara katika ukweli, si kuyumbishwa na tafsiri zisizo na msingi.
Kazi ya Kanisa si kuogopa vivuli, bali kusimama katika nuru ya kweli. Kupambana na uovu hakumaanishi kupoteza mantiki.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Huu ni upotoshaji. Hakuna ushahidi wa moja kwa moja kwamba rangi hizi zinawakilisha LGBTQ+. Hizi ni rangi za kawaida zinazotumika kila siku katika elimu, sanaa na ubunifu. Kuzihusisha moja kwa moja na ajenda fulani bila msingi ni uoga usio na sababu na tafsiri ya haraka isiyo na uthibitisho.
Rangi za LGBTQ+ zina utambulisho wake maalum kupitia rainbow flag yenye mpangilio unaojulikana: red, orange, yellow, green, blue na purple. Kama nilivyoonyesha ktk picha hapa. Hizi unazoona ni ubunifu wa kawaida kabisa kama rangi za watoto au michoro ya kijamii.
Kinachokera zaidi ni kuona imani ya Kikristo ikidhalilishwa kwa maamuzi ya haraka yasiyo na mantiki. Kuzuia mkutano wa injili kwa sababu ya rangi ni kuonesha udhaifu wa kufikiri na kuipa hofu nafasi ya kuongoza badala ya ukweli.
Tuache kudhoofisha na kudhalilisha imani yetu kwa maamuzi ya papara. Imani ya Kikristo haihitaji kulindwa kwa hofu wala kwa kuchanganya mambo yasiyo na uhusiano. Inahitaji kusimamiwa kwa ukweli, ujasiri na hekima.
Serikali imefanya udhalilishaji mkubwa dhidi ya imani ya KIKRISTO , na kwa viongozi wa dini maamuzi ya kuomba radhi bila kuchambua kwa kina yanaweza kuleta picha ya kukosa msimamo na kuendelea zaidi kudhalilisha Kanisa. Kanisa lina wajibu wa kusimama imara katika ukweli, si kuyumbishwa na tafsiri zisizo na msingi.
Kazi ya Kanisa si kuogopa vivuli, bali kusimama katika nuru ya kweli. Kupambana na uovu hakumaanishi kupoteza mantiki.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema reposted
QatarEnergy
@qatarenergy
Providing an update on the damage from the missile attacks on Ras Laffan Industrial City
H.E. Minister Saad Sherida Al-Kaabi: The missile attacks reduced Qatar’s LNG export capacity by 17% and caused an estimated loss of $20 billion in annual revenue
- Extensive damage to our production facilities will take up to five years to repair and will compel us to declare long-term force majeure
QatarEnergy expects the damage to its Ras Laffan Industrial City caused by missile strikes, which occurred on Wednesday 18 March 2026, and in the early hours of Thursday 19 March 2026, to cost about $20 billion a year in lost revenue and to take up to five years to repair, impacting supply to markets in Europe and Asia.
Providing an update on the damage to the facilities at Ras Laffan Industrial City, His Excellency Mr. Saad Sherida Al-Kaabi, the Minister of State for Energy Affairs, the President and CEO of QatarEnergy, said “I am relieved to confirm that no one was injured by these unjustified and senseless attacks, which weren’t just an attack on the State of Qatar but attacks on global energy security and stability. This was an attack on all of us who stand for development and human progress that is sustained by a fair, reliable, and secure access to energy.”
The attacks damaged two liquefied natural gas (LNG) producing Trains 4 and 6 totaling 12.8 million tons per annum (MTPA) of production, representing approximately 17% of Qatar’s exports. Train 4 is a joint venture between QatarEnergy (66%) and ExxonMobil (34%), and Train 6 is a joint venture between QatarEnergy (70%) and ExxonMobil (30%).
His Excellency Minister Al-Kaabi said: “The damage sustained by the LNG facilities will take between three to five years to repair. The impact is on China, South Korea, Italy and Belgium. This means that we will be compelled to declare force majeure for up to five years on some long-term LNG contracts.”
The attacks also targeted the Pearl GTL (Gas-to-Liquids) facility, a production sharing agreement operated by Shell, that converts natural gas into high-quality cleaner burning drop-in fuels and produces base oils used to make premium engine oils and lubricants, and paraffins and waxes.
“The damage caused to one of the two trains at Pearl GTL is being assessed and is expected to be offline for a minimum of one year” His Excellency Minister Al-Kaabi added.
It should be noted that there will be a loss of associated product production due to this outage as follows:
· Condensates: 18.6 million barrels which is around 24% of Qatar’s exports
· LPG: 1.281 MT which is around 13% of Qatar’s exports
· Naphtha: 0.594 MT which is around 6% of Qatar’s exports
· Sulfur: 0.18 MT which is around 6% of Qatar’s exports
· Helium: 309.54 MCFA which is around 14% of Qatar’s exports
His Excellency the Minister of State for Energy Affairs, the President and CEO of QatarEnergy paid tribute to the Qatari military and security forces and to the energy sector emergency response teams whose courage and extraordinary professionalism ensured the situation was contained quickly and safely.
#qatar -
Godbless E.J. Lema reposted
Stephen Mutoro
@smutoro
KEY PHONE HIGH COURT RULING!
⭕️ Your mobile number is now constitutionally protected data
⭕️ The High Court has declared that a registered phone number falls under Article 31(c) & (d)—meaning your private affairs cannot be exposed via “number recycling”
⭕️ The AG has 6 months to fix this as to new rules for reassigning numbers:
1️⃣ Requires VERIFIABLE consent of the original owner
2️⃣ Must exhaust documented verification & public notice before deactivation
3️⃣ Technical safeguards MUST prevent transfer of old personal data to new owners
⭕️ No more exposing your private life to a stranger who inherits your old number
#digitalrights #privacy #article31 #dataprotection #consumerrights -
Godbless E.J. Lema reposted
Julians Amboko
@AmbokoJH
UPDATE: Kenya's High Court declares that registered
mobile phone number constitutes a digital identifier linking personal data that relates to an individual’s private affairs hence qualifies for protection under Article 31 (c) & (d) of the Constitution to safeguard the right not have information relating to private affairs
unnecessarily required or disclosed.
This declaration by the High Court follows a petition challenging the reassignment &/or recycling of the deactivated but previously registered mobile telephone numbers owing to extended period of inactivity or non-use.
The High Court has now given the Office of the Attorney General 6 months to take all necessary and appropriate measures to safeguard digital identity associated with the registered mobile telephone number against unfettered deactivation, and subsequent arbitrary reassignment or recycling.
The High Court rules that reassignment of cell phone numbers should happen only when/if:
1. There is the previous registered owner’s informed & verifiable consent
2. After expiry of reasonable period following issuance of public notice which must be preceded by through documented verification process aimed at confirming the original registered owner cannot be located or has unequivocally revoked the rights to the number
3. Technical safeguards be put in place and implemented to prevent unauthorized exposure or transfer of personal data linked to previous registered owner to 3rd Parties upon reassignment or recycling of the number
Julians Amboko
@AmbokoJH
A petition has been filed at the High Court challenging the reassignment &/or recycling of the deactivated but previously registered mobile telephone numbers owing to extended period of inactivity or non-use.
The petitioner argues that those numbers constitute an individual’s digital identity that provides linkage to delicate personal information of which substantial risk of exposure to 3rd Parties is created by their unfettered reassignment.
The petitioner wants a declaration that there exists a personal digital identity & a person's registered phone number forms part of his/her digital identity just like the physical national ID., Passport or Driving license. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Tanzania tunaendelea ku perform vizuri sana kwa kuwa Nchi yenye watu wasio na furaha Duniani. Tuko hata mbele ya Congo na Lebanon
-
Godbless E.J. Lema reposted
Dr. Eli David
@DrEliDavid
How good is Israel's intelligence?
The regime's former president Ahmadinejad: “Iran's Secret Service had established a unit to target Mossad agents within Iran. However, the head of this unit turned out to be a Mossad operative himself, along with 20 other agents.” 🤣 -
Godbless E.J. Lema reposted
Hilda Newton
@HildaNewton21
HABARI MBAYA
Huyu kijana anayeonekana kwenye hii picha akiwa amewashika Polisi mabega akijaribu kujikongoja anaitwa Emmanuel Bernard Msele,
Mara ya mwisho alionekana katika video hii iliyopostiwa na BBC 29 October majira ya asubuhi maeneo ya ubungo Maji.
Huyu ni kati ya watu Waliokamatwa siku hiyo asubuhi kabisa wakati maandamano yanaanza na kupakiwa kwenye gari hilo la Polisi tangu siku hiyo hajaonekana tena.
November 6, 2025 Mwezi wa 11 familia yake ilipata taarifa kwamba ndugu yao yupo Hospital ya Mzena anatibiwa, walifika hapo na kuambiwa ni kweli alitibiwa hapo lakin baada ya kupata nafuu Polisi walimchukua na kuondoka nae.
Ndugu zake wametafuta vituo vyote vya Polisi bila mafanikio.
#freeemanuelmsele -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Uchumi wa nchi yoyote hutegemea sana imani ya wananchi na wawekezaji. Pale ambapo kuna hofu ya kisiasa, ukosefu wa haki, na kutokuwepo kwa uhakika wa usalama wa mali, wawekezaji hupoteza imani na kuanza kuhamisha mitaji yao kwenda nchi nyingine zenye utulivu zaidi. Hali hii husababisha kupungua kwa uwekezaji na kudhoofisha uchumi wa ndani.
Aidha, mazingira ya hofu husababisha pia kupungua kwa misaada ya kimataifa, kwani washirika wa maendeleo hupunguza au kusitisha msaada wanapoona changamoto katika utawala na uwazi. Vilevile, taasisi za kifedha huanza kuona nchi kuwa na hatari kubwa, jambo linalopelekea kuongezeka kwa riba za mikopo kutokana na mashaka yaliyopo.
Pia, jitihada za kukusanya kodi ya ndani huwa hazifanikiwi ipasavyo ikiwa zitafanywa kwa nguvu bila kuzingatia hali halisi ya uchumi. Hatua kama hizi huweza kunyonga uwezo wa wananchi wa kununua (purchasing power) na kupunguza matumizi (spending), jambo ambalo ni hatari zaidi kwa makusanyo ya kodi kwa muda mrefu. Uchumi unapopungua mzunguko wa fedha, hata mapato ya serikali hupungua licha ya juhudi kubwa za ukusanyaji.
Kwa ujumla, bila kuwepo kwa utawala unaoaminika, haki, na utulivu wa kisiasa, uchumi huendelea kudorora kutokana na kupungua kwa uwekezaji, misaada, pamoja na kuongezeka kwa gharama za mikopo na kudhoofika kwa uwezo wa wananchi kushiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi. -
Godbless E.J. Lema reposted
🦅 Eagle Wings 🦅
@CRRJA5
.@elonmusk 🔴BREAKING: Elon Musk just dropped this mind-blowing update on Neuralink…
“In the next 6 to 12 months, we’ll be doing our first implants for vision — even if somebody is completely blind, we can write directly to the visual cortex.”
Blindness? Cured.
Sight? Restored.
Humanity? Upgraded. 👀⚡
From zero vision → potential superhuman sight (infrared, UV, radar… like a real-life superhero).
This is no longer sci-fi. It’s happening NOW.
What do you think — game-changer or too wild? 🔥 Drop your thoughts below! -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Hatuwezi kufunika UKATILI wa Viongozi waliopita kwa sababu hawa waliopo wanaendelea kufanya mambo mabaya zaidi. Tukifanya hivyo utakuwa ni udhaifu na dhambi kubwa sana. Hatuwezi kumkumbuka mtu kwa kujenga madaraja dhidi ya roho za watu zilizopotea kikatili wakati wa uhai wake bila majibu hadi leo. Hisia za msiba haziwezi kuwa na nguvu kuliko wema , haki , huruma na upendo. Tukipoteza kumbukumbu za ukatili wao tutakuwa tunaimarisha ukatili kwa kila
utawala na haswa vizizi vinavyokuja.
Mimi namkumbuka Magufuli katika sura hii ma sio hisia na kelele za ngojera. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Thank you
-
Godbless E.J. Lema reposted
Deogratias #FreeTunduLissu🇹🇿 Munishi
@DeoMunishi
For those assembling today for tyrant #magufuli, just remember this testimony from the former Interior Cabinet Secretary of the Republic of Kenya🇰🇪 which explains how evil was your fella!
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Leo tunakumbuka miaka mitano tangu kuondoka kwa John Magufuli. Lakini kumbukumbu ya kweli haiwezi kufutwa wala kupambwa lazima iseme ukweli. Kipindi chake cha uongozi kiliacha alama nzito , hofu ya kisiasa, kubanwa kwa uhuru wa kujieleza, na maswali makubwa juu ya haki katika chaguzi na ukatili mwingi. Haya si maneno ya chuki, ni kumbukumbu ya waliopitia mazingira hayo na waliolazimika kunyamaza.
Tuseme wazi bila kupepesa macho, mifumo ya ukandamizaji na hofu iliyojengwa kipindi hicho bado inaathiri namna siasa na uchaguzi vinavyoendeshwa hata leo. Hii si historia iliyopita tu ni sehemu ya changamoto tunazokabiliana nazo sasa. Kumkumbuka leo si kuhalalisha yaliyopita, bali ni kusisitiza wajibu wetu wa kuyakataa. Hatutaki taifa linaloongozwa kwa hofu, tunataka taifa linalojengwa juu ya haki, uhuru, na uwajibikaji. Kumbukumbu hii iwe wito. Tusinyamaze. Tusisahau. Tusirudie na kuendelea na makosa yale yale. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Si mlisema kwa sauti kubwa kabisa: “wake zenu wanatosha kuwashangilia, hamuhitaji watu wengine.”
Sisi tukasema sawa boss, no cap. Leo tunaamka tunaona operation , vijana wote Chato kushangilia.
Sasa swali dogo tu ,
Wake zenu wameenda likizo ? au hesabu zimebadilika ghafla? 😅. Vijana wa CDM mkiona mnaitwa na bahasha ili muende kushangilia, tafadhali msikubali kuwa extras kwenye movie ya propaganda. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Kupigania haki na demokrasia kunahitaji kuheshimu na kupenda dhamira yako zaidi kuliko kuangalia watu unao wapigania, vinginevyo sababu za kukata tamaa zinaweza kuwa wazi. Imagine mtu anajivunia kwa ufasaha uhalifu ndani ya chama chake, halafu watu walioko mbele yake wanashangalia.
Ni muhimu sana kama jamii, kuwa wakati tunaongea kuhusu uhitaji wa katiba mpya na tume huru ya uchaguzi ni muhimu pia kuelewa tunahitaji mindset transformation ya hali ya juu, haswa kuanzia ktk level ya familia. Hakuna kinachoweza kujenga ustawi wa nchi bila kubadilisha fikra hasi na mbaya zilizoishika jamii na bahati mbaya zimekuwa normalized kama kanuni za kawaida za maisha. Tuna hatari kubwa sana. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Baada ya kutatua migogoro ya ndoa, hatua inayofuata kwa Chama Cha Mapinduzi ni kusuluhisha ugomvi wa watoto kugombea remote ya TV nyumbani. Kazi na UTU.
-
Godbless E.J. Lema reposted
Rugemeleza Nshala
@rugemeleza
We categorically told the UN Secretary General 's Envoy, Parfait Onanga-Anyanga, that CCM and its government, under Samia, are behind the 29th of October 2025 Massacre. They used the Police and other armed outfits to kill unarmed protesters demanding free and fair elections.
But that was not an accident because CCM from 1992 has refused to allow Tanzania to have a truly multiparty democracy. They have rigged the elections from 1995 to 2015. Then from 2019, 2020,2024 and 2025 no elections at all but sham elections.
Samia is on record enlisting the army to supervise elections when she met the TPDF bosses early 2024. Then came her no "nywinywi and nywinywinywi" warning against those campaigning for free and fair elections. She even said people should remember that even though she is the presidential candidate of CCM, she is still the Commander in Chief of the Armed Forces. Then should we now wonder of what happened on the 29th of October? The answer is apparent for everyone who is able to listen and see.
In sum, we have unelected cabal masquerading as a government. Chadema demandstotal accountability of these people and not accomodation or appeasement. We know the plot on the vogue is to frame Chadema to be behind the protests but the entire world knows that the State organs worked to silence if not annihilate Chadema through arresting and charging it's Chairperson, Tundu Lissu, with treason, refuse to recognize the Secretary General of the party and five other members of the Central Committee, freeze the disbursement of subsidies to Chadema, and obtain an injunction against Chadema thus preventing it from conducting political activities. Then when protesters emerged the Police massacred them but still embark in a campaign to frame Chadema as the force behind the massacre, via the so called Commission of Enquiry!
We also demanded for unconditional release of Tundu Lissu and let Chadema operate freely. We also demand that an independent and impartial commission of enquiry led by trusted international eminent persons like the one formed after the 2007-08 Massacre in Kenya led by the late Koffi Annan be formed and conduct the investigation in Tanzania. Those found by it should be held accountable and prosecuted without exception.
Deogratias #FreeTunduLissu🇹🇿 Munishi
@DeoMunishi
SG John Mnyika along with the party's AG @rugemeleza met the @UN SG's special envoy @parfait_onanga to discuss the October #tanzaniamassacre by tyrant @SuluhuSamia.
The unambiguous party's position to the envoy was as issued to public in December, 2025 by the Central Committee. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
“Wanaotupa watoto hawajui wanalolifanya. Kuliko kumtupa mtoto ni afadhali ukamkabidhi katika mamlaka za kisheria au kituo cha kulelea watoto. Kila mtoto aliyezaliwa ni hazina, na hatuijui kesho yake,” amesema Samia.
Baada ya kauli hiyo, napenda kusema kuwa viongozi wanapaswa kuonyesha uadilifu, haki, utu na ukweli katika maisha yao. Uongozi wa kweli haujengwi kwa matukio ya mbele ya kamera pekee, bali kwa matendo na maamuzi yanayolinda haki, usalama na ustawi wa jamii nzima. Kujitakasa kwa nafsi hakutokani na matendo ya kuonekana hadharani, bali kwa toba ya kweli na kuacha njia mbaya. Neno la Mungu linatukumbusha kuwa damu isiyo na hatia hunena, na ukweli hauwezi kufichwa milele.
Ni vyema kuonyesha huruma kwa mtoto aliyetelekezwa, lakini pia tusisahau maumivu ya wazazi wanaopoteza watoto wao na kuendelea kuwatafuta bila majibu. Jamii inahitaji haki, uwazi na uwajibikaji wa kweli, si matendo yanayoweza kuonekana kama mkakati wa kisiasa wa kutafuta huruma na kupendwa.
Hata hivyo hili sio jambo baya, pia nilikuona mama Samia ukimpa mama Kanumba zawadi ya gari siku ya Women’s Day. Kwa mwelekeo huu nafikiri tunaweza pia kujua watu wote waliopotea kama wakina Humprey PolePole, Soka, Mdude na wengine wengi wako wapi. Mungu akubariki. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Mwisho wa UOVU umekaribia sana.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
*Hekima za Baba Askofu Bagonza*
MAADUI WAKIISHA, MARAFIKI WATAGEUKA MAADUI.
Ajabu ya Wajaluo: Ukizoea kumsingizia adui kwa kila tatizo lako, siku ukimmaliza huyo adui, utawageuza marafiki zako wawe maadui ili upate wa kusingizia kila tatizo lako.
Nimesikia viongozi wetu wakidai wanaliunganisha taifa. Wengine wamesema taifa ni tulivu. Na wengine wameajiri mawakala wa kutafuta maridhiano. Sasa najiuliza:
1. Mawaziri wako London, New York, Addis Ababa na Brussels kueleza jinsi nchi ilivyotulia, LAKINI huku nyuma polisi wanakataa kwamba ndani ya Chadema hakuna wanawake na chama chote ni wanaume! Tulisitisha maadhimisho ya Uhuru; tunazuia hata siku ya wanawake wa dunia? Je, Tuna mashaka kama hao ni wanawake sawasawa?!
2. Mikutano ya hadhara inaonyesha kuna kero nyingi kuliko watatuaji, LAKINI kuna watu mitandaoni wanapongeza jinsi nchi ilivyo tulivu na maendeleo yanapaa! Tunaficha uchi, tutazaaje?
3. Janga la utekaji linaendelea na mamia wako mafichoni, LAKINI viongozi wetu hata kwenye mikutano ya hadhara hilo halizungumzwi! Kama serikali haihusiki na utekaji basi inahujumiwa na watekaji. Kauli ya serikali ilitakiwa toka juzi ileee.
4. Tunakodisha watu kwenda kuteka na kudhuru nje ya nchi BADALA ya kukodisha wapatanishi na mabalozi wa kurejesha nyumbani wakosoaji. Tunasubiri tukalishwe meza moja na Rachel Dangwa mbele ya Katibu Mkuu wa UN?
5. Polisi wanavuruga uwezekano wa maridhiano na kuizika serikali ikiwa hai. Tukumbuke: Polisi walioipigia saluti UNION JACK ndiyo walioipigia bendera ya Tanganyika huru. Serikali inawadanganya polisi na polisi inawadanganya serikali. Mchezo wa kitoto huu.
6. CCM haiko kimya. Ina historia ya kuibuka na kukataa dhuluma. Kuteka, kutesa na kuua si sera yake. Kuiba kura yaweza kuwa sera ya muda lakini si wote wanaipenda. Ukimya wa CCM ni kuchimba kaburi kwa meno yake. Itaamka, na kwa sasa adui wake si CHADEMA ambayo ni “marehemu”. Adui wa CCM anajijua na CCM inamjua. Mkumbukeni John Komba na “Jogoo limewika Dodoma”. Amkeni muokoe nchi na chama.
7. Tumekodisha mawakala wa maridhiano wakati tunavuruga maridhiano. Sasa watatuambia nini wakati hila tunaziona wenyewe? Mnawavunjia heshima hata kama wamejivunjia kwa kudokoa wali kabla haujawiva.
8. Mgonjwa wa kusahau hawezi kukumbuka tatizo lilianza lini. Serikali isiyokosolewa ni ile isiyokuwapo. Serikali isiyokosea na ile isiyofanya chochote. Serikali ipo; haina chanjo ya kutokosea. Inatakiwa kukiri makosa na kuwajibika ili tusonge mbele. Inapoteza muda na fedha kupiga propoganda. Ndevu waweza kuzificha kwa kunyoa; matiti je?
Vituko vyetu vimezidi mpaka Mjaluo amecheka na kutuonyesha mapengo anayoyaita mwanya.
Kwaresima Njema
Ramadhani Kareem -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Katika simulizi ya uumbaji ndani ya Kitabu cha Mwanzo kuna tafakari ya kina sana. Baada ya kila kitu kuumbwa, Mungu aliangalia akaona ni chema. Lakini alipotazama dunia ambayo ndani yake hakukuwa na mwanamke, akasema kwa mara ya kwanza: “Si vyema huyo mtu awe peke yake.” (Mwanzo 2:18).
Hapo tunajifunza jambo la kifalsafa na la moyo, dunia inaweza kuwa na milima, bahari na nguvu zote za maisha, lakini bado ikabaki na upungufu bila uwepo wa mwanamke. Ndani ya mwanamke kuna hekima tulivu, nguvu ya kuumba maisha, na akili ya ndani isiyoonekana kirahisi lakini inayobadilisha dunia kimya kimya.
Mwanamke hubeba upendo unaojenga familia, uvumilivu unaolinda jamii, na tumaini linaloifanya dunia iendelee kuwa na maana hata katika nyakati ngumu. Ndiyo maana leo tunaposema Happy Women’s Day, hatusemi tu maneno ya salamu , bali tunatoa shukrani ya kina kwa uwepo wenu ambao unaifanya dunia ikamilike zaidi.
Happy Women’s Day ❤️ -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Wanawake wa BAWACHA, msikate tamaa. Mabomu yanaweza kuvunja kusanyiko lenu, lakini hayawezi kuvunja fikra za haki na demokrasia. Ujasiri wenu ni sehemu ya historia ya mabadiliko.
Mungu awabariki wanawake wote majasiri.
Happy Women’s DayThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
BAWACHA nyinyi ni watu wa maana sana katika nchi yetu. Jipeni moyo mkuu mkijua kwamba hata katika giza refu zaidi, alfajiri huwa haikosekani. Historia ya jamii yoyote ina vipindi vya majaribu, mateso, kadhia na hata udhalilishwaji, lakini yote hayo huwa ya muda tu mbele ya nguvu ya dhamira na imani ya watu wake. Kutakuwa na siku mtatazama nyuma na kujiuliza, “Tulifikaje hapa?” Na katika mshangao huo mtatambua kuwa hatua zenu za leo, uvumilivu, ujasiri na mshikamano, ndizo zilizojenga kesho bora. Hapo ndipo mtakapokuwa na simulizi la heshima la kuwaeleza watoto na wajukuu zenu. Simulizi litakalowafundisha kwamba kukata tamaa si tabia ya wanaotafuta haki na mabadiliko.
Tambueni kuwa thamani ya juhudi zenu si ndogo. Mmekuwa baraka kubwa kwa chama chetu na kwa jamii inayotazama mbele kwa matumaini. Ni mtu mpumbavu tu asiyeweza kuona mchango wenu na mwanga mnaouleta katika safari hii.
Basi endeleeni kusimama imara. Busara iwape mwanga wa maamuzi na ujasiri uwe nguvu ya hatua zenu. Kwa sababu katika falsafa ya maisha ushindi wa kweli haupatikani kwa kukosa majaribu bali kwa kuyavuka kwa heshima, uvumilivu na imani thabiti. -
Godbless E.J. Lema reposted
Joseph Mbilinyi
@TheRealJongwe
Sasa hiyo tume ya nini?! Na ndio maana watu wanaikataa, wanaiona ni ya MCHONGO.
-
Godbless E.J. Lema reposted
George Tibaijuka
@GeorgeTibaijuka
Kwa taarifa iliyotolewa na serikali ktk vikao vya umoja wa mataifa ni wazi watu wa serikali hii hawajutii walichokifanya Oct 29 na kuna uwezekano mkubwa kikajirudia kwa siku za usoni! Hatuko salama !
-
Godbless E.J. Lema reposted
Deogratias #FreeTunduLissu🇹🇿 Munishi
@DeoMunishi
#tanzaniamasscre
"The EU🇪🇺 is concerned with the widespread human right violations in Tanzania🇹🇿 in the context of the general elections, including allegations of excessive use of force, of extrajudicial killings, enforced disappearances,...." www.eeas.europa.eu/delegations/un-geneva/hrc61-eu-stateme… -
Godbless E.J. Lema reposted
Teslaconomics
@Teslaconomics
I don’t think people truly understand what’s about to happen with 𝕏 Money.
This is Elon going back to his roots - back to x.com - and building what he always wanted in the first place: one place that runs your entire financial life.
When he rebranded Twitter to 𝕏 in 2023, he said straight up that we’re adding the ability to conduct your entire financial world. He even said you may not even need a traditional bank account.
Most people brushed that off. And now it’s becoming real.
𝕏 Money has already been live in closed beta internally within the company. A limited external beta is expected soon, and they’ve already secured money transmitter licenses in over 40 states plus DC. 𝕏 Payments is registered with FinCEN. Visa is officially partnered. You’ll be able to fund your wallet instantly, send peer-to-peer payments, move money to your bank, and eventually use a debit card.
And I think this is just the beginning.
This will probably start as a simple wallet where you can send money as easily as sending a DM. With this technology, you can pay creators, pay subscriptions, pay whatever bills, shop inside the app, get paid inside the app, and much more.
Then, there will be high-yield savings, you can invest, you can get loans, have money market accounts, maybe even treasury access, cool smart cashtags that let you see live stock prices in your timeline and execute trades seamlessly, crypto integration, potentially full asset management… the list goes on and on… Elon literally said this is meant to be the central source of ALL monetary transactions.
Bro… think about that for a sec.
Your 𝕏 profile becomes your financial identity.
Everyone you follow is already there. Everyone you interact with is already there. That social graph becomes your distribution engine. Like, you won’t need a separate banking app, no need for a separate investing app, no need for a separate payment app… this all lives where you already spend your time. Right here on 𝕏.
Look at WeChat in China, which Elon always alluded to. Payments, messaging, shopping, investing - all integrated in one app. It handles $ trillions in volume and became deeply embedded in everyone’s daily life. Now 𝕏 is building the Western version of that, but with a more global reach, and xAI’s AI layered on top of all this.
Before you call me crazy, you have to understand how big this opportunity is.
Digital payments globally are measured in the tens of $ trillions of dollars annually. Even just capturing a small slice of that across hundreds of millions, and eventually a billion, users can change everything. 𝕏 already has the audience. That lowers customer acquisition costs significantly. Add fintech revenue on top of ads, plus float, plus lending, plus investing tools, and we’re talking about a completely different valuation profile.
Now, $44B for this company looks like the bargain of the decade… this was one of the main reasons I invested in 𝕏.
And if they execute the way they’ve executed at Tesla and SpaceX, this could truly fundamentally redefine how people handle $ .
Most people today still see 𝕏 as just a social media app. I see it as the foundation of a financial system layered on top of a global network. Ultimately becoming the “everything” app.
And this I believe is a once-in-a-generation opportunity.
Elon is calling this a game-changer.
I believe him. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Maendeleo ya miji hayawezi kupatikana kwa kutoza kodi maji ya kuogelea. Bali kwa kuimarisha miundombinu na upangaji bora wa makazi. Serikali za mitaa zinapaswa kuwekeza katika barabara za kiwango cha lami, umeme wa uhakika, maji safi na salama, pamoja na upangaji miji wa kitaalamu na huduma bora zaidi za jamii. Miundombinu bora huongeza thamani ya ardhi na majengo. Na hivyo kuvutia uwekezaji wa nyumba za kisasa na bora.
Kadri thamani ya mali inavyoongezeka, ndivyo mapato yatokanayo na kodi ya majengo ( property tax) yanavyoongezeka bila kulazimisha viwango vipya vya kodi. Nyumba zenye ubora wa juu, zikiwemo zenye huduma za ziada kama swimming pool, huwa na thamani kubwa zaidi sokoni na hivyo kulipa kodi kubwa ( property tax) kulingana na tathmini ya mali na hata bima. Hii ni njia endelevu ya kuongeza mapato ya halmashauri kwa misingi ya ukuaji wa uchumi badala ya kutoza kodi maji ya kuogelea.
Hata hivyo , huyu msela amenikumbusha mbali, kwani DC mmoja kwenye mkutano fulani Arusha ktk siku za nyuma, alishawahi kutoa mawazo ya Kiwanja cha Gofu Gymkhana kikatwe katikati ili machinga waweze kupata eneo la kufanya biashara, yeye alikuwa anajua kuwa kiwanja cha gofu ni eneo la wazi ambalo wazee huwa wanatembembea tu , ni bahati nilikuwepo 😂 vinginevyo walikuwa wana rengeta Gymkhana Shaaaaa. -
Godbless E.J. Lema reposted
Amsterdam & Partners
@amsterdamllp
Press Release: Amsterdam & Partners LLP Files Applications on Behalf of Uganda’s NUP and Tanzania’s CHADEMA, Respectively, Calls for Immediate Commonwealth Suspensions
amsterdamandpartners.com/press-release-amsterdam-partners… -
Godbless E.J. Lema reposted
George Tibaijuka
@GeorgeTibaijuka
Wanakufa wanajeshi 3 wamarekani na taifa zima linaomboleza. Wako wazi na wanatoa taarifa za vifo! Uku kwetu wanakufa makumi ktk uwanja wa mapambano ila huwezi jua hata kusikia taarifa yoyote na bado mnategemea tuwe wazalendo! Kwa usiri huo mtabkia nyie kuwa wazalendo!
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Karma Says !!
A time will come in your life when some people will regret why they treated you wrong,
Trust me, it will definitely come. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Hakuna jambo la kufurahisha zaidi kuliko kuona adui yako akifanikiwa ktk maisha yake kwa namna hii . Kwa hakika, wanatimiza ndoto yao kwa ustadi mkubwa. Mungu ni mwema sana. Niko proud nao sana. Sisi ni Watanzania lazima tupendane.❤️❤️
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Na tatizo hilo limesabishwa na Kim Kardashian.
-
Godbless E.J. Lema reposted
Al Jazeera Breaking News
@AJENews
BREAKING: Iran's Supreme Leader Ali Khamenei killed, Reuters and Israeli media report citing unnamed senior Israeli officials
🔴 LIVE updates: www.aljazeera.com/news/liveblog/2026/2/28/live-israel-lau… -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Ohhh real ? God bless you mum!!
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Nina wasiwasi mkubwa kuwa hakuna muda mrefu video hii itakuwa haionekani ktk kurasa mbali mbali za Online TV. Sijui itakuwa ni kwa amri ya nani ? Lakini just watch.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Kuwatendea watu kwa haki , huruma , upendo na wema ni bora zaidi kuliko ku post aya za kidini ambazo hata huzifuati.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Usidanganyike na wingi wa maombi,sala na kufunga.
Kipimo cha kweli cha imani si maneno yako mbele za Mungu, bali matendo yako kwa watu. Unawezaje kumpenda Mungu usiyemuona, huku ukimchukia ndugu na jamii yako? Upendo wa kweli huonekana katika huruma, heshima na matendo mema, hapo ndipo roho yako inajidhihirisha mbele za Mungu. Kufunga na kusali kusiko tafuta upendo,haki, wema,uadilifu na huruma ni mgomo wa kula. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Usidanganyike na wingi wa maombi,sala na kufunga.
Kipimo cha kweli cha imani si maneno yako mbele za Mungu, bali matendo yako kwa watu. Unawezaje kumpenda Mungu usiyemuona, huku ukimchukia ndugu na jamii yako? Upendo wa kweli huonekana katika huruma, heshima na matendo mema, hapo ndipo roho yako inajidhihirisha mbele za Mungu. Kufunga na kusali kusiko tafuta upendo,haki, wema,uadilifu na huruma ni mgomo wa kula. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Ninatazama kwa makini nguvu ya AI na mitandao ya kijamii, hasa reels za Instagram na namna algorithimu zake zinavyofanya kazi. Ni kweli teknolojia imeleta manufaa makubwa, maarifa yanapatikana kwa urahisi, mawasiliano ni mepesi, na watu wanaweza kujifunza mambo mengi kwa muda mfupi. Hata hivyo, pamoja na faida hizo, kuna athari ambazo hazionekani kirahisi lakini ni za kina sana katika familia na ndoa. Leo hii, watu wengi wanategemea mitandao ya kijamii kama chanzo kikuu cha ushauri kuhusu malezi, mahusiano na ndoa. Tatizo ni kwamba algorithimu hazilengi kukuza hekima, zinakusukumia zaidi kile unachopenda kusikia au kile kinachochochea hisia zako. Ukianza kutazama maudhui ya kulaumu au kujitetea, utaendelea kuonyeshwa hayo hayo. Polepole, mtu anajikuta akiishi ndani ya mtazamo mmoja tu, bila kujitathmini au kusikiliza upande mwingine.
Kwa namna hii, maadili muhimu kama uvumilivu, heshima, adabu na mazungumzo ya ana kwa ana vinaanza kufifia katika maisha halisi. Migogoro midogo inakuwa mikubwa kwa sababu kila mmoja anapata uthibitisho wa mtazamo wake mtandaoni badala ya kutafuta suluhu ndani ya familia. Hili ni tatizo kubwa, lakini si rahisi kuliona isipokuwa uwe na mazoea ya kufikiri kwa kina na kuhoji unachokula kila siku kupitia skrini. Teknolojia si adui , tatizo ni pale inapochukua nafasi ya busara, maadili na mwongozo wa kweli katika maisha na familia. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Naogopa sana jamii ikichoka kusema….
“ TUNAMWACHIA MUNGU”
Kauli hii ichukuliwe kama kengele ya tahadhari. Kwa sababu jamii ikichoka kabisa, madhara yake si kwa wananchi pekee, bali kwa taifa zima. Uongozi makini husikia hata sauti iliyosemwa kwa upole na hasira kabla haijageuka ukimya wa maumivu na fujo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Haya, maisha yanapita kwa kasi sana. Miaka 50 inayokuja, takribani watu wote ulionao kwenye contacts zako hautakuwa nao kabisa, na pengine wengi hawatakuwepo. Na vitu kama magari na mali nyingine vilivyo tufanya tuwe wakatili, vingi havitakuwepo. Hakuna atakayekukumbuka sana, zaidi pengine wajukuu zetu , na wao hatuna uhakika.
Kwa hiyo, haya maisha ukiyatafakari sana, utagundua utajiri mkubwa unabaki kuwa upendo na uhuruma tu. Hakuna kitu kina thamani kwa binadamu kama unyenyekevu na upendo. Thamani yake ni kubwa kuliko kumiliki New York nzima na London. Tukijua hili, maisha hayapotezi thamani bali yanaongeza thamani. Nakuombea, kwa Mungu, uishi nafasi yako ya sasa kwa matendo. Vinginevyo ni UBATILI MTUPU.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Sawa. Tumepishana kwa 2% tu. 😂
-
Godbless E.J. Lema reposted
Twaha Mwaipaya
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUKAMATWA NA BAADAYE KUPOTEA MIKONONI MWA POLISI KWA MWENYEKITI WA BAVICHA MKOA WA IRINGA, NDUGU Ibrahim Myovella
Tarehe 10 Februari 2026, Ndugu Ibrahim Myovella pamoja na wenzake Suleiman Fyumagwa na Ally Kalolo walikamatwa na Jeshi la Polisi na kushikiliwa katika Kituo cha Polisi Iringa Mjini hadi tarehe 17 Februari 2026 walipoachiwa kwa dhamana.
Hata hivyo, tarehe 18 Februari 2026 walirejea katika Kituo cha Polisi Iringa Mjini kwa ajili ya kuripoti kama ilivyo masharti ya dhamana yao. Cha kusikitisha na kushangaza ni kwamba tangu walipoingia kituoni hapo kuripoti, hawajaonekana tena.
Jeshi la Polisi linadai kutofahamu walipo, licha ya ukweli kwamba mara ya mwisho walionekana wakiingia katika kituo hicho kwa ajili ya kutekeleza masharti ya dhamana.
Tunaliitaka Jeshi la Polisi kutoa taarifa ya haraka kwa ndugu, jamaa na marafiki kuhusu mahali walipo ndugu zetu hawa pamoja na sababu za kushikiliwa kwao, iwapo wanashikiliwa.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Unasubiria !! Woiiiiii, 😂. Acha UDUANSI Chalii. Tubu.Rudi. Wanasema wewe ni TIMU AFRO . Etii umekuja kwenye Press umevaa Ki Rich Dad 😂 Na hako Ka Koti Kako!! 😂bado unako ?? kamedumu sana, toka tukiwa Bungeni!!
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Kuna AMANI kweli ? Mnatazamana KIMACHALE MACHALE sana.😂😂😂😂😂Mmenifanya nikumbe CC yetu wakati ule tunamtimua Kitila Mkumbo kwa u snitch wake!!
Hapo hata chafya inaweza kutiliwa mashaka😂😂😂😂 Sisi tunashinda Mahakamani lakini nyie mnashinda na UCHUNGU na HATIA wakati wote. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Huwezi kutarajia fikra za standard ya juu kwa gharama za kiwango cha chini. Huwezi kuokoa mabilioni kwa kuogopa kuwekeza kiasi chenye uzito wa kimkakati katika kutafuta washauri wa kimataifa. Tatizo hapa si fedha ni upeo wa kufikiri.
Milioni kumi si bajeti ya kuunda dira ya usafiri wa jiji, hiyo ni pesa ya ushauri wa masuala ya “wikiendi wapi Dar kuna bamba?” Siyo ramani ya mageuzi ya mfumo wa usafiri wa jiji lenye mamilioni ya watu na linalobeba uchumi wa taifa.
Tatizo la foleni katika Dar es Salaam linachoma mabilioni ya shilingi kila siku. Linateketeza muda wa uzalishaji, linachafua mazingira na kuongeza athari za mabadiliko ya tabianchi, na linadhoofisha mahusiano ya familia. Ni jeraha la uchumi na mzigo mzito kwa maisha ya jamii.
Kama milioni kumi zinaonekana kuwa “pesa kubwa ya ushauri” kwenye meza ya maamuzi kwa ajili ya kutafuta suluhisho la foleni Dar, basi changamoto si foleni pekee bali ni kiwango cha fikra za uongozi na upana wa maono.
Huenda kabla ya kuondoa msongamano barabarani, tunapaswa kuondoa msongamano wa fikra finyu vichwani. Changamoto kubwa zinahitaji mawazo makubwa. Think big.
NB : Watu watembee kwa miguu Dar es salaam. Foleni zote zitakwisha kabisa. Pls naombeni Milioni kumi zangu. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Kesi ya Tundu Lissu inaendelea kuonyesha zaidi jinsi mfumo wa kisheria unavyoweza kukumbana na shinikizo la kisiasa. Ubakaji wa haki si tishio tu kwa Tundu Lissu au CHADEMA, bali kwa Watanzania wote wa kizazi hiki, na vizazi vya kesho. Uharibifu na ukosefu wa haki ndani ya Taifa ni mzizi wa uharibifu mkubwa katika kila kipengele cha maisha. Kuna majuto kwa kila mtu kesho.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
MSIMAMO WA HECHE BAADA YA LISSU KUKWAMA/ "HATUTARUDI NYUMA KAMWE" youtu.be/qkD7SnkWkXI via @YouTube
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Wapenzi waliooana hawajali sana kuombana radhi baada ya ugomvi na mabishano!! Badala yake, huwa wanaweza sema maneno ya kipumbavu pumbavu tu ili kurudisha amani!.. Utasikia , Ney , hivi umelikuta bafu bafuni ilivyoenda kuoga ? 😂😂😂. Anyway hii Tume inanipa andasi mingi kabisa na inanikumbusha issue mingi mingi mpaka za getoni😂
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Mimi siku nimepunguza sana kushangaa vioja vingi, kwani nimegundua hii Dunia ina mambo sana, jaribu kufikiria tu, watu wote wanaopigania haki ya utoaji mimba tayari wameshazaliwa. Kukosa huruma ni mkosi mkubwa kuliko kuwa masikini.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
During your downfall, keep a proper record of people's behavior so that when you rise again, you don't mix animals with humans
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Pole Mshabaha. Namshukuru sana Mungu kuwa watekaji hawakufanikiwa kuondoka na wewe. Haki ITASHINDA siku sio nyingi na kila uovu utalipwa.
-
Godbless E.J. Lema reposted
Tito Magoti
@TitoMagoti
Vibaka wa Mafwele & co wamekamatwa Nairobi Kenya wakijaribu kumteka Mshabaha. Si mlisema Nairobi sio mbali na mnaweza kuingia mkafanya uhalifu? Well, enjoy the ride in NBO. Na bado!
Amnesty Kenya
@AmnestyKenya
Yesterday, swift action by the Law Society of Kenya and Amnesty International Kenya, alongside security agencies, saved Tanzanian human rights defender Mshabaha Mshabaha Hamza from being illegally taken across the border.
Kenya must never be a corridor for transnational repression.
We demand full investigations, cross-border accountability, and protection for ALL human rights defenders. Read the full statement: www.amnestykenya.org/law-society-of-kenya-and-amnesty-int… -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Mungu aliwasamehe makahaba, lakini ulipofika wakati wa kumchagulia Mwanawe mama, alimchagua bikira. Jifunze kutoka kwa Mungu. Bado unasubiri kuwa DC ? Sababu ya kurudi ni mauaji 29/10/2025 kwani ina nguvu na heshima zaidi ya ile sababu iliyokuondoa kwenye wajibu mwema.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Siyo kila jambo linaweza kubadilika unapolikabili, lakini hakuna jambo linaloweza kubadilika bila kulikabili kwanza.Ujasiri wako sio tu kwa ajili ya kuitoa CCM madarakani bali ni mindset transformation juu ya thamani ya utu na haki kwa vizazi na vizazi. Haupaswi kuwa jela hata kidogo. Nafikiri we are not doing enough kama wananchi.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Thank you. This is real helpful advice.
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Poleni sana Serikali.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
This job can be done in less than 24 hrs. Easy , easy , easy , easy. Lakini haipaswi kufanywa na nyie Polisi.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Mbaya SANA.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Banjoo hakuwa rafiki yangu wa karibu, nilimjua tu wakati wa kampeni za CCM 2010. Lakini jinsi alivyouwawa kunanileta karibu naye kwa huruma na hofu. Nikijiuliza, ni nani mwingine, Mwana Arusha au Mtanzania, atakayefuata baada ya ujasiri wa aina hii ya wauwaji ?
Ni wazi kwamba kumjua nani aliyefanya kitendo hiki sio kazi ngumu, na bajeti ya uchunguzi wa tukio hili haihitaji kuzidi shilingi Milioni moja. Easy, easy, easy, easy 😭😭😭😭.
Nilimwona kijana wake akiongea, anaonekana ni kijana mwerevu, jasiri, na mwenye utulivu wa akili. Ni matumaini yangu kwamba yeye, familia yake, marafiki zake, na wananchi wote watasimama kidete dhidi ya maadui wa utekaji na hukumu ya kifo.
Nawaombea kwa Mungu awapatie nguvu na ujasiri wa kusimama imara, wakilinda heshima na maisha ya kila Binadamu na sasa Banjoo. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Hili JENGO la Ngorongoro Conservation Office lina KAMERA kila kona, liko karibu na ofisi ya RC Arusha na pembeni ni Benki kuu na ofisi ya DC Arusha na mita kama 300 ni Makao Makuu ya Polisi Mkoa wa Arusha. Maeneo yote haya na biashara zinazozunguka maeneo haya kuna KAMERA. Naambiwa Banjoo ametekwa akiwa hapa. Hata mjinga ataelewa kama ninavyofikiri. Sasa nasema, kelele ipigwe na kila mwenye Akili na Maarifa.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Ohhh , Banjoo umeuwawa ? Nakukumbuka sana , ulikuwa mstari wa mbele sana ktk kumsadia Batlida Burihani kushinda uchaguzi Arusha 2010. Msatari wa mbele sana.
Tumefika pabaya. Maisha ya mwanadamu yamekuwa na thamani ndogo kuliko maisha ya panya. Tumezoea ukatili na mauaji kama sehemu ya maisha. Tumehalalisha hofu na ubaya. Hakuna aliye salama katika nchi inayodharau uhai. Leo ni yeye, kesho ni mimi, kesho kutwa ni wewe. Taifa hufa pale watu wake wanapokubali maovu kuwa kawaida. Naogopa sana TAIFA LA VISASI. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Kauli hiyo inapotosha. Idadi haikuwa ndogo, na hata kama ingekuwa, maisha ya binadamu hayapimwi kwa mizani ya kulinganisha na maafa ya wengine. Kila kifo ni hasara kubwa kwa familia na taifa. Badala ya kupunguza uzito wa tukio, jamii inapaswa kuonyesha masikitiko, kuwajibika, na kuhakikisha haki na usalama vinatangulizwa. Maisha ya Mtanzania hayapaswi kupunguzwa kwa takwimu.Taifa hujengwa juu ya kulinda uhai, si kulinganisha maumivu yake na ya wengine. Ni muhimu jamii kuendelea kujua ukweli na kutambua uzito wa kila tukio na huchukua hatua za kuhakikisha halijirudii tena.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Taifa imara halijengwi kwa kufunga midomo ya wakosoaji, bali kwa kujenga mifumo inayoweza kuvumilia ukosoaji na kujibu kwa hoja. Hapo ndipo haki na utulivu hukutana. Mnaharibu Nchi kwa kasi kubwa sana.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Pumbavu zenu. Aliyewatuma PUMBAVU na aliyefikiri kuwatuma PUMBAVU zake. Mna kesi ICC nyie , jipangeni na USHAHIDI. Acheni UPUMBAVU.
-
Godbless E.J. Lema reposted
Joseph Mbilinyi
@TheRealJongwe
Always tunasema huyu mtu ni mshamba na mjinga. Serikali haijawahi kununua Bentleys wala Maybachs kwa ajili ya Mawaziri…Why usiyatumie kwa matumizi binafsi mpaka uweke Namba za Serikali?
NB: Huwezi kutuvimbia na hela za UFISADI,na wala wewe sio Daimondi. MATAKO YAKO!😎 -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Jana tulikuwa na mazungumzo kuhusu Siku ya historia ya VALANTINE DAY.
Mke wangu aliniuliza, Hivi Godbless , ungependa Brilliant (Binti yetu) aolewe na mume mwenye tabia kama zako ?
Nikajibu faster , aolewe na mtu kama Yesu !!
Akacheka 😂😂😂Bro, acha kurukaruka, Yesu hakuoa!!’ Nakuuliza wewe !!
Mbona jibu rahisi sana ?
Nikajibu, nahitaji marekebisho kidogo na maombi kwa sasa kwanza!!
Akasema, Awake your spirit Godbless, ikiwa wewe ni baba na hauwezi ku recommend mtoto wako aolewe na mwanaume mwenye tabia kama zako basi iko shida!! Bahati nzuri wakati stori zinaendela , Bon Yai alipiga simu , nikaenda pembeni nikasema naona kuna simu ya kikao, nikawa nimepita hivii , nikamwambia Ney , unajua Lissu kanyimwa chakula huku nikiwa nimekunja uso !! Ney , hawa CCM ni sadist sana!! Nikajiongelesha !!
Okay !! Sasa na wewe mwanaume mwenzangu nakuuliza kama nilivyo ulizwa? Je , ungependa binti yako aolewe na jamaa mwenye tabia kama zako ?
Kama jibu ni hapana !! Badilika !! Tubadilike!!
Unajua sisi wanaume tunapenda sana kulaumu wanawake kwa kuchagua mwanaume asiye sahihi, lakini kamwe hatumlaumu mwanaume aliyeficha utu wake wa kweli na kujifanya mtu mwingine ili ampate mwanamke mwema. Hatari kubwa sana hii.
Nawatakia Siku Njema ya Wapendanao. -
Godbless E.J. Lema reposted
The Economist
@TheEconomist
Samia Suluhu Hassan has caused Tanzania’s most dangerous crisis since independence www.economist.com/middle-east-and-africa/2026/02/12/dont-…
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Magereza wako sahihi kabisa kwa mtazamo wao kutompa Lissu access ya chakula, wanaona Lissu anastahili aina hii ya treatment. Walisikia na kuona alivyopigwa risasi, lakini hadi leo uchunguzi haujafanyika. Wanajua baada ya shambulio la risasi alikuwa mahututi, lakini hakupatiwa matibabu stahiki kupitia Bunge.
Sasa hivi yuko Magereza na haruhusiwi kutembelewa hata na viongozi wenzake. Kwa hiyo, wanafanya wanavyoona kutoka juu wanafuata mwelekeo wanaouona. Hata majaji kushangaa ni kama sanaa tu. Kama kweli wangekuwa serious na haki za binadamu, kesi yenyewe wangeshaifuta siku nyingi. Imagine una Majaji ambao walikubali Mashahidi wahojiwe bila hata wao wenyewe kuwaona ? -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Kinachoogopesha zaidi sio mashahidi wa kubumba ktk kesi ya Mchongo ya Mkti Lissu iliyoko Mahakamani, bali ni uwezo wa Serikali kuwa na aina hii ya mipango ya aibu bila kuona fedheha. Hii inatia hofu zaidi. Inawezekana huko mbele kukafanywa utafiti utakaoonyesha kwamba kulikuwa na wakati sisi wote tulikuwa vichaa, ilipaswa tufungwe pingu na kupewa dawa za usingizi masaa yote, tena Nchi yote , mpaka baba yako. Lakini tuliamka. Tukala. Tukapanga mipango ya Nchi, na kufanya maisha kawaida.
Huu utafiti utakuja, hakika. Trust me. AMA hata sisi hatupo hapa Duniani ni just illusion tu ? Na ukute hata hakuna kitu kinaitwa Tanzania ? Inatisha sana. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Naona vikao na posho vinatafutwa kwa bidii kabisa. Janja Janja.
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Utafikiri Polisi Africa Mashariki wote ni Mapacha. Angalau kidogo Kenya kuna tofauti.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Nimefurahi tena kumbe mnajua kuna future katika maisha. Hilo jambo linanipa faraja na amani kubwa sana. Imagine, umemlea Waziri Rajabu, amekua Katibu wa Rais, na sasa unam-expose kwenye sectors. Moyo mzuri sana. Sasa fikiria kuna mzazi anamtafuta mtoto wake ili amzike si kum-expose hata kijiweni , bali kumzika kaburini, na hamuoni. Mnafikiri haya mambo yatapita kawaida? Future zenu ni ngumu sana. Muda wa Mwenyezi Mungu utaongea kwa sauti kubwa .” Watu wote wanapenda better future pia , wawe tu exposed kwenye haki na utu wala sio sector na utajiri.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Kama Afrika ingekuwa na silaha za nyuklia, viongozi wa wake wangekuwa wanazitumia dhidi ya watu wake wenyewe!
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
*Hekima za Baba Askofu Bagonza*
IKIBAKI NI SIRI TUTANUFAIKA WOTE
Siku moja akaja mke wa “Mjaluo” mmoja aliyekuwa Waziri. Kaniomba nimuombee mmewe ambaye ni Waziri na ni “Mjaluo”. Baada ya sala, akaleta la pili.
Akasema watoto wao wanapata shida kumwona Baba yao anatukanwa mbele ya televisheni. Imefika mahali wanaogopa kuifungua kwa kuhofia watakuta baba yao anatukanwa na boss wake. Nikamjibu, “Boss wa mmeo, ndiye boss wa Taifa japo sisi huwa ni maboss wake wakati wa uchaguzi”. Nikamuahidi kuwa siku nikikutana naye nitamwambia. Ningeshauri:
1. Boss ana uhuru wa kuteua na kutengua. Asitokee anayehoji mpaka tubadili mkataba.
2. Sababu za kuteua na kutengua, zingebaki siri ya mteuaji. Kumsifia mtu wakati anateuliwa halafu “akabwatukiwa” wakati anatenguliwa, inauguza wengi wakiwamo watoto, michepuko mpaka wapishi wa nyumbani.
3. Sifa kemkem wakati wa uteuzi zikifuatwa na kimya wakati wa kutenguliwa nako ni shida. Bora kote kuwe kimya.
4. Watanzania hatuna dogo. Akisema, tunazua. Asiposema, tunabuni, LAKINI bora kimya. Na kiwe kimya kweli hata kwa washauri na Machawa. Tukumbuke, kuna watu wanalizwa pochi zao ili wateuliwe! Hakuna risiti, msinifuate kama Shabiby.
5. Kuna aliyeanzisha huu utamaduni wa kusema kwa nini. Natamani uachwe. Sema tu, dira yetu inadai mabadiliko. ITATOSHA na kubaki. Ukichokonoa sababu, kuna watu watanyimwa unyumba. Walidhaniwa wa maana kumbe wa ovyo tu. Kambarage alikuwa haongei siku ya kuapisha watu “uwongo”. Alipolazimika, aliongea siku anateua.
6. Unajua bhana! Uhusiano wa mteuaji na mteuliwa/mtenguliwa umejengwa katika usiri mkubwa sawa na ule wa wana ndoa. Mkiachana huwezi kusema alikuwa ananuka kikwapa. Akijibu?! Kujibu kushindwe na kulegea.
7. Kazi ya serikali si ya mtu mmoja. Kwa hiyo kutueleza kazi ya mmoja hakutupatii picha ya kutosha. Wapo wanaokwamishwa na wasiowajua. Ziko wizara zinaingiliana. Watoto wa shule (Elimu) wakicheza mpira (Michezo). Wasipocheza vizuri atumbuliwe nani?
8. Hili ni GUMU. Wazembe na wasiotosha, wabadilishwe tu. LAKINI tujue, mabadiliko yakiwa meeeengi na ya mara kwa mara, wazushi watasema tatizo ni la MTEUAJI. Watabwata, “hatoshi”, “ashindwe” nk. Hakuna chuo cha uwaziri. Semina elekezi moja haitoshi. Mkataba wetu ni mbovu. Eti sharti awe mbunge! Kweli? Mnaochelewesha mkataba mpya mnasababisha boss ajiadhibu.
9. Niliota siku moja naenda kutekeleza ahadi niliyompa mke wa Waziri Mjaluo. Nikajibiwa, “Nenda kawaambie, sihitaji kura zao ili niwe boss wao”! Sikumuita mke wa Mjaluo kumpa jibu. Nilisahau hata mlango ulioniingiza ofisi ya boss, nikaingia washroom. Akabaki ananicheka. Nami nikajifanya nilikuwa na haja wakati nimekosea njia.
10. Nina mpango wa kustaafu kuwatania Wajaluo. Nahitaji maoni yao inbox ili nifanye maamuzi.
Narudia tena
IKIBAKI NI SIRI TUNANUFAIKA WOTE. -
Godbless E.J. Lema reposted
Boniface Jacob
@ExMayorUbungo
Happy new year Chairman Lissu..!
Asanteni kanda ya pwani kwa kuja. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Pamoja na maumivu na changamoto zote unazopitia, bado tabasamu lako halijawahi kupotea, ni ishara ya moyo safi, wenye uvumilivu na wema wa dhati kwa Nchi yako. Heshima yako ni kubwa japo kuwa inapita ktk bonde la uvuli wa mauti.
Always on SmileThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema reposted
Hilda Newton
@HildaNewton21
Ujinga umefikisha Taifa kubaya, Viongozi wanatetea uwongo, ufisadi na upuuzi.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Siungi mkono hata kidogo uhalifu wa aina yoyote. Jamii salama hujengwa kwa kuheshimu sheria, si kwa kuvunja sheria kwa kisingizio cha kuilinda. Hata hivyo, kwa muda sasa kumekuwepo na mwelekeo hatari unaojengwa taratibu, kunormalize mauaji kupitia lugha na taarifa rasmi, hasa zile zinazotolewa mara kwa mara na Jeshi la Polisi zikihitimishwa kwa kauli rahisi ya “WAUWAWA”.
Kauli hii, inayotamkwa bila maelezo ya kina, bila uchunguzi wa wazi, na bila uwajibikaji unaoonekana, imeanza kuonekana kama jambo la kawaida. Ndipo hatari ilipo. Pale mauaji yanapoelezwa kwa sentensi moja kana kwamba ni hitimisho la kawaida la operesheni, dhamira ya utawala wa sheria inaanza kupotea. Mtuhumiwa anageuzwa kuwa mkosaji aliyekwisha hukumiwa, na risasi inachukua nafasi ya mahakama.
Swali la msingi ni hili, ni nani anayetoa mamlaka ya kuamua uhai na mauti? Sheria inatambua matumizi ya nguvu pale inapolazimu, lakini matumizi hayo hayaondoi wajibu wa uwazi, uchunguzi huru, na uwajibikaji. Taifa haliwezi kujenga haki kwa kuzoea vifo visivyohojiwa. Tunapokubali leo kwamba “WAUWAWA ” ni maelezo ya kutosha, tunafungua mlango wa kesho ambapo haki ya kila raia iko hatarini.
Hatari ya normalization hii si kwa wahalifu pekee, bali kwa jamii nzima. Leo ni “mtuhumiwa wa uhalifu,” kesho anaweza kuwa mpinzani wa kisiasa, mwanaharakati, au raia wa kawaida aliyekutwa mahali pasipo sahihi. Nchi inayojivunia utawala wa sheria haiwezi kuishi kwa hofu, wala kwa ukimya unaohalalisha kifo.
Kupinga mwelekeo huu hakumaanishi kuunga mkono uhalifu. Kinyume chake, ni kusimamia msingi wa haki, utu wa binadamu, na mustakabali wa taifa. Usalama wa kweli haujengwi kwa kuua bila maswali, bali kwa kuimarisha taasisi, kuheshimu sheria, na kuhakikisha kwamba hakuna aliye juu ya sheria iwe ni mtuhumiwa au mwenye mamlaka. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Kama wangekuwa na maarifa na busara, Kesho 9/2 utalala nyumbani. Ukweli ni kwamba wana hofu isiyo kifani na uwepo wako ukiwa nje, na bado wana sintofahamu kubwa uwepo wako gerezani. Uwepo wako ni tishio kwao katika hali yoyote. Pengine wangetamani ufe, kwa sababu historia inaonyesha tayari waliwahi kujaribu kukatiza uhai wako. Hata hivyo, kila njama, kila mpango mchafu watakaoupanga dhidi yako na CHADEMA, bila kujali giza lake, hatimaye utageuka kuwa ushindi wa Taifa na urithi wa haki kwa vizazi vinavyokuja. GIZA lao leo ndilo nuru ya kesho ya nchi hii.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Wewe umeomba kuombewa ? Wanasema haufiki July ukiwa hapo. Wana mgombea urais 2030 na PM. Wanasema timu yote iliyokuwa kule kwa kina Ronaldino lazima ipanguliwe. Wanasema kwanza hauna hela na hujui deal!! uwezo wako mkubwa kifedha ni kumchangia mtu laki moja ya msiba au send off 😂😂😂Bado siko nyumbani, msalimie sana,Madilu na Mkwe. Kesheni Mkiomba. Usiogope ni ndoto tu.
-
Godbless E.J. Lema reposted
Maria Sarungi Tsehai
@MariaSTsehai
‼️BUSINESS PARTNER WA MCHENGERWA AWEKWA WIZARA YA AFYA KUSIMAMIA MANUNUZI NA UPIGAJI VIFAA NA MADAWA‼️🚨
Kumbe ndugu Emmanuel Tayari ni business partner wa Mchengerwa kuanzia Crown Media - leo kamweka kupitia Mama mkwe kwenye wizara yake kama naibu katibu mkuu!
Talk about conflict of interest! Haya bana hongera zenu kwa ujanja huu!
Eniwei Crown Media ni ya Mchengerwa na Tayari ana 10% hapo!
Rufiji Media Holdings ambayo ndo kitovu cha Crown ni ya Mchengerwa na Ndugu yake! @Salym na @OfficialAliKiba ni front tu 😅
Watu wanamwaga data! Wamechoka!
Haya nadhani tumeelewana tunaposema serikali haramu hii ya upigaji?
Eniwei #tutaelewanatu -
Godbless E.J. Lema reposted
Hilda Newton
@HildaNewton21
Report ya DW kuhusu matukio ya mauaji ya Watanganyika Oktoba 29.😭
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Yeah !!!😭😭😭😭
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Nilikuwa napita mtandaoni nikasoma habari hii na maoni ya watu, kisha nilikumbuka maneno ya Bon Yai siku aliniambia siku moja !!
“Mangi, CHUKI is so real, duh!! So real, Mangi.”
Nakubaliana naye. Kwa kweli, kuna chuki kubwa sana katikati ya jamii, inatisha, na inanifanya kuogopa kesho ya Tanzania. CCM wameharibu sana nchi, wakitengeneza dalili zote na kurutubisha ugomvi katika jamii. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Usiogope wala kuyumba moyo, kwa maana waliokuweka jela wana mashaka makubwa kuliko wewe. Wewe una dhamira, wao wana hofu, wewe una msimamo wa haki wao wana wasiwasi. Ukweli haufungwi kwa minyororo, na haki haizimiwi kwa kuta za gereza. Endelea kusimama imara, kwa sababu unachokisimamia ni kikubwa kuliko hofu zao. Unapaswa kuwa na familia yako lakini huko jela kwa ajili ya watu na Nchi. Kusudi jema sana hili. Hauoni ujumbe huu lakini angalau ndugu na watoto wako wataona na kupata nguvu wakati wakitafakari.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
If you can see the invisible , you can do the impossible.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Watu watakuja na kuondoka maishani mwako, lakini mtu unayemuona kwenye kioo unapojitazama atakuwepo siku zote na wewe. Mtendee huyo mtu wema. Mpende huyo mtu.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Nimekuta hii inazunguka mitandaoni na maneno haya hapa chini 😭😭😭😭😭😭
“Kaka umepost video tumemuona ndugu yetu, Jina lake anaitwa Agrey Chazi alitoweka tangu Tarehe 29 OCTOBER, ubarikiwe sasa familia tunaweka MSIBA japo hatuna MWILI” -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Calm down chief, tunaongelea dhahabu sio matikiti maji. Ebu muone huyu Niaje Niaje !!
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Ndani ya nchi yao, rushwa ni kosa kubwa. Nje ya mipaka yao, ni mkakati wa kupata miradi na biashara. Wanahubiri maadili kwao, lakini huweka bei ya dhamira kwa asilimia na rushwa wanapokuja kwetu. Rushwa inakuwa daraja la biashara na miradi. Huu si mfumo uliovunjika, bali ni unafiki uliopangwa, uliofanikishwa kwa kiwango kikubwa na upumbavu wetu wenyewe.
-
Godbless E.J. Lema reposted
BBC News Swahili
@bbcswahili
BBC Africa Eye yachunguza matukio ya watu kutekwaa
www.bbc.com/swahili/live/cd0y8ynyegvt?post=asset%3A5eb400… -
Godbless E.J. Lema reposted
Larry Madowo
@LarryMadowo
"Tanzania now leads East African countries in press freedom" 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
-
Godbless E.J. Lema reposted
Twaha Mwaipaya
"Ninaishi katika nchi ya kigeni lakini hiyo haimaanishi kama niko salama, ni garama kubwa, ni upweke, inatisha". Edson Mwakalebela (SATIVA) mhanga wa tukio la utekaji na jaribio la mauaji Tanzania.
::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::
#bbc
"I live in a foreign country but that doesn't mean I'm safe, it's expensive, it's lonely, it's scary". Edson Mwakalebela (SATIVA) victim of kidnapping and attempted murder in Tanzania.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Kama watoto wenu wangekuwa miongoni mwa waliouawa na kama miili yao ingekuwa ikitafutwa kama mizigo isiyo na mwenyewe,
kauli zenu zisingekosa maarifa na utu kwa kiwango hiki. Hata hivyo nafikiri nitakuwa mpumbavu kudhani ungeweza kuzungumza tofauti. Maana, wewe ni Makamu wa Rais unayetokana na uchaguzi ule. Naona nataka kuwa Mpumbavu Mimi. Woiiii. Muda una nguvu sana. Na historia ina kumbukumbu ndefu kuliko vyeo. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Kila mwenye kufikiri vyema aliona hili litakuja tu.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Hapa Simba na Mamba wote walijua msingi na maana ya Maridhiano.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
India imetangaza sera ya kodi sifuri hadi mwaka 2047 kwa makampuni ya teknolojia ya wingu (cloud computing) yanayoanzisha vituo vya kuhifadhi data (data centers).
Je, Afrika ingeweza kufika katika fikra na hatua kama hii? Jibu la kuumiza ni kwamba ingeweza, lakini haijafanya. Sio kwa sababu ya ukosefu wa rasilimali, bali kwa sababu ya ukosefu wa maono, ujasiri wa maamuzi, na vipaumbele sahihi. Katika dunia ya leo, data ni mafuta mapya. Teknolojia ya wingu ndiyo uti wa mgongo wa uchumi wa kidijitali, benki, afya, elimu, usalama, biashara na hata kilimo cha kisasa hutegemea data. India imetambua hili mapema na ikaamua kujitoa kafara ya kodi leo ili kuvuna ajira, teknolojia, maarifa, na nguvu ya kiuchumi kesho. Huu ni uwekezaji wa kizazi, si wa muhula wa kisiasa.
Kwa upande wa Afrika, mara nyingi viongozi wetu huonekana kujishughulisha zaidi na mijadala midogo, isiyo na mwelekeo wa kimkakati. Badala ya kuzungumzia sera za kuvutia makampuni ya teknolojia, kuwekeza kwenye miundombinu ya kidijitali, au kulinda mazingira ya ubunifu, tunajikuta tukizungumza mambo madogo yasiyoleta mapinduzi ya kiuchumi. Ndiyo maana mtu anaweza kumweleza Waziri kuhusu fikra kama hizi, lakini mazungumzo yakahamia kwenye kilimo cha matikiti maji kana kwamba ndicho kitakachobeba uchumi wa karne ya 21. Tatizo si kilimo, kilimo ni muhimu. Tatizo ni kukosa uwiano wa fikra. Dunia inaenda kasi ya teknolojia, akili bandia, data, na uchumi wa maarifa, wakati sisi bado tunahangaika na siasa za kujikimu kisiasa na fikra za muda mfupi. Bila sera thabiti, zenye uthubutu na ulinzi wa maslahi ya kizazi kijacho, Afrika itaendelea kuwa soko la teknolojia za wengine badala ya kuwa kitovu cha uzalishaji. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Someni hii
Source: TICGL | Tanzania Investment and Consultant Group Ltd - Your Strategic Partner for Business, Investment and Economic Transformation in Tanzania share.google/S6da6FIGFyox9Jhat -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Sio kwenda kujenga vyoo na mabafu na %. This is called exchanging value.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Inaonekana kama TAKUKURU wako kazini, lakini huku ni kutishia watu kimkakakati, maana yake, mtu mwingine asifungue mdomo tena.
-
Godbless E.J. Lema reposted
BOBI WINE
@HEBobiwine
This video, recorded in Lagot, Kitgum District exemplifies the criminality of Museveni's regime of blood and national shame. UPDF soldiers under the command of a GISO are severely beating up a man who they accuse of stealing a motorcycle. Despite his pleas that he is innocent, they do not stop beating him. They simply want him to accept that he stole the motorcycle or they will continue the torture!
The way they tied him with ropes before beating him is similar to the many stories we have heard from our people who have been lucky to get out of those torture chambers. Imagine if there was no video. Regime apologists would be all over the place denying that this happened, and claiming that we want to make them look bad! Wangadya and her 'Human Rights Commission' would be shamelessly calling it a lie and covering up for the regime.
This is why the world must isolate the criminal regime. This is why we call for more sanctions against perpetrators of this criminality- beginning with their commander in chief. This is why Ugandan deserves better. This is why we are struggling for change! #bringbackourpeopleThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Mama Salma Kikwete, ulikuwa First Lady kwa miaka kumi. Hiyo ilikuwa heshima kubwa na ya kutosha kubaki nayo. Kuamua kutafuta nafasi ya Ubunge kumepunguza heshima badala ya kuiongeza. Kinachoonekana si huduma mpya kwa Taifa, bali ni kushuka daraja lisilo la lazima. Kama ungekuwa mzazi wangu, ningehisi maumivu makubwa. Wakati mwingine hekima ya kweli si kuongeza vyeo, bali kujua wapi pa kusimama na lini pa kuondoka kwa heshima.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Gavana wetu wa Benki Kuu . Ningependekeza usome vitabu kama The Changing World Order na Principles cha Ray Dalio, pamoja na The Sovereign Individual kama bado haujavisoma. Vitabu hivi vinafundisha jinsi taasisi kubwa na mataifa yanavyofikiri kimkakati kuhusu dhahabu, deni, sarafu, na nguvu ya uchumi wa muda mrefu.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Hakuna jambo baya kama Taifa kukosa maono. Kuwa na hifadhi ya dhahabu ya dola bilioni 1.3 halafu kujisifu kuwa umevuka lengo ? Aibu kubwa sana. Lengo dogo kwa kiasi hiki ? Dhahabu si pambo ni silaha ya kiuchumi.
Huzuni zaidi ni kwamba kile kinachoitwa lengo la Taifa ktk hifadhi ya dhahabu kinazidiwa na utajiri wa mtu mmoja kama Kim Kardashian. Hapa tatizo si rasilimali, bali ni fikra ndogo na maono duni.
Kama alivyosema Mfalme Suleiman, “Without vision, people perish.” Taifa lisilo na maono makubwa, hata likiwa na raslimali , bado litaendelea kuwa maskini, si kwa sababu hawana mali, bali hawana maarifa na dira. Imagine hii ni statement inatoka kwa wachumi wa Benki Kuu ? -
Godbless E.J. Lema reposted
Mpale Mpoki
@MpaleMpoki
Heri ya kumbukizi ya kuzaliwa kwako @Mwabuk2Boniface. Mtetezi wa ukuu wa katiba na utawala wa sheria. Dhana yako ya seksheni foo na kuitekeleza kama sheria itakavyo imefanya chama (TLS) kitambulike na kujulikana kwa maelfu ya watanzania. @Advocate_Jebra @TitoMagoti @MariaSTsehai
-
Godbless E.J. Lema reposted
Liberatus Mwang'ombe
@Liberatus80
I was listening to @TheCitizenTz interview with the @usembassytz Acting Ambassador, Lintz. CCM can’t even close an LNG deal worth half of Tanzania’s GDP—how incompetent can you be?
And now, in a masterstroke of “brilliance,” they’ve decided to sell off our gold reserves and our ports to the UAE. Truly inspiring leadership… if your goal is national embarrassment. -
Godbless E.J. Lema reposted
Martin Maranja Masese
@IAMartin_
BBC, BLOOMBERG na BUSINESS INSIDER AFRICA wamemnukuu Waziri wenu wa Nchi, Ofisi ya Rais – Mipango, KITILA MKUMBI akisema “Governments are no longer interested in providing aid to Africa so we are reorganizing ourselves,” mnatuona hatuelewi kitasha?
Kitila MKUMBO amewaeleza watasha kwamba wanauza akiba ya dhahabu iliyopo Benki Kuu ya Tanzania Serikali kutoka mchi wahisani na washirika hazina tena nia ya kutoa misaada kwa Afrika, kwa hivyo wanajipanga upya wenyewe. Huyu ni Waziri katika ofisi ya Rais.
Mkurugenzi wa Idara ya Masoko ya Fedha wa BoT, Emmanuel Akaro, amesema madai hayo si ya kweli na kwamba kuna upotoshaji. Sasa nani ametupotosha? Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais – Mipango, Bwana Kitila Mkumbo? Ametoa maneno hayo wapi?
Kitila Mkumbo anasema “Misaada ya nje imepungua, tunahitaji njia mbadala za kupata fedha”. Halafu Mkurugenzi wa Idara ya Masoko ya Fedha wa BoT anasema madai hayo siyo ya kweli. Kwani kuna serikali mbili za MaCCM? Nani ambaye anasema uongo?
Tunamsikiliza KITILA MKUMBO aliyezunguma akiwa London, United Kingdom na kusema kwamba Serikali imepanga kuuza sehemu ya akiba yake ya dhahabu ili kupata fedha za kusaidia kufadhili miradi mbalimbali ya miundombinu. Porojo nyingine hatusikilizi. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Yeah , wanaijua kesho vizuri.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Mood ya BOT & Serikali kwa sasa 😂😂😂
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Oyaaa Vibonge kuweni makini 😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Benki Kuu na Serikali, sikilizeni. Niko na nyie mpaka niwe WINGA wa hii deal ya dhahabu. Imekaa poa sana. Niwape email address yangu ?? 😂😂😂
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Kauli ya BoT inachochea maswali zaidi kuliko majibu. Dhahabu “imezidi kiwango” si tatizo, kwani dunia nzima inaongeza hifadhi yake kama ngao dhidi ya hatari za dola, siasa za kimataifa, na mishtuko ya kifedha. Dhahabu si asset ni akiba ya taifa yenye uthabiti. Kuuza kwa sababu thamani imepanda ni sawa na kuuza insurance kabla hatari haijatokea. Central banks makini huongeza dhahabu inapopanda bei, si kuuza
Fedha zinazotokana na mauzo ya dhahabu kwenda masoko ya fedha ya kimataifa ni hatari. Masoko hayo yana currency risk, interest rate risk, na counterparty risk, wakati dhahabu haina issuer risk. Hivyo, central banks hazifukuzi yield, bali zinalinda uthabiti wa taifa. Tatizo si mauzo yenyewe, bali mindset, kuangalia dhahabu kama trading asset badala ya ngao ya taifa. Uchumi wa kweli ni kwa watu wanaoelewa mishtuko ya dunia na dhahabu ni kinga, si mzigo. -
Godbless E.J. Lema reposted
Jeffrey Smith
@Smith_JeffreyT
#tanzania stages a brutal election crackdown with mass graves still being discovered, then hires a MAGA-connected consulting firm to spin the carnage as progress. Who needs accountability and justice when you can buy a rebrand. These people have no shame.
www.theafricareport.com/406867/the-45000-spin-can-trumps-… -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Mwaka 2012–2013 niliishauri Serikali kuwekeza dola milioni 2 tu kwenye Bitcoin. Kwa bei ya wastani ya $15/BTC, kiasi hicho kingewezesha kununua takriban 133,000 Bitcoin. Mnamo Oktoba 2025, Bitcoin ilifikia all‑time high ya $125,000/ kwa one BTC, ambayo ingelifanya thamani ya akiba hiyo kufikia takriban 41 trilioni TZS, mtaji wa awali ulikuwa shilingi bilioni 3 tu.
Tunapaswa kuwa na wachumi wenye hustler mentality, wanyenyekevu, wabunifu, na wanaoweza kutambua kwamba ideas za leo huzalishwa kutoka basement na mitaani.
Anyway, mteja wa dhahabu mmeshampata? Yaani 10% ya deal ya dhahabu ya 1.3 bilioni USD ni karibu USD milioni 130. Nawaza tu!! Pia, naweza hata kuwatafutia mteja mzuri. Pigeni deal na wapinzani mpunguze maneno😂 Niwatafutie mteja ? 😂 Niingie mtaani ?? -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Dhahabu ni mali muhimu sana kwa uchumi wa Taifa, hasa katika kipindi cha sintofahamu ya kiuchumi na kijamii duniani. Mwaka 2020, bei ya dhahabu ilikuwa takribani USD 1,500 kwa ounce moja, lakini kufikia Januari 2026 imepanda hadi takribani USD 5,400 kwa ounce moja. Hii ni sawa na ongezeko la asilimia 260 ndani ya kipindi cha miaka mitano.
Ongezeko hili linaonesha wazi kuwa dhahabu ni hifadhi salama ya thamani wakati sarafu na masoko ya fedha yanapoyumba. Katika mazingira haya, kuuza dhahabu ili kupata fedha za haraka si uamuzi wa busara wa muda mrefu. Ingawa serikali zinaweza kukabiliwa na uhaba wa fedha, kuuza mali yenye thamani inayoongezeka kwa kasi ni kupoteza fursa ya kiuchumi.
Njia mbadala iliyo salama zaidi ni kukopa kwa kutumia dhahabu kama dhamana (collateral). Njia hii huiwezesha serikali kupata fedha bila kupoteza umiliki wa dhahabu, huku ikiendelea kunufaika na ongezeko la thamani yake baadaye.
Kwa hitimisho, katika dunia yenye misukosuko ya kiuchumi, dhahabu inapaswa kuhifadhiwa na kutumiwa kwa hekima, kwani ni nguzo muhimu ya usalama wa uchumi wa Taifa. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Dhahabu ya taifa si “pesa iliyoko mezani,” bali kinga ya taifa, inadumisha thamani ya sarafu, inakabiliana na mfumuko wa bei, na inavutia uwekezaji. Kuiondoa kutoka hazina au kuuza zote mara moja ni kujipiga makofi. Ni hatari isiyo na kifani. Hatari hii si ya nadharia tu, bali ni kielelezo cha kupoteza hifadhi ya taifa, kushuka kwa imani ya wawekezaji, na kuathirika kwa uchumi kwa muda mrefu.
Dhahabu ni kinga, si suluhisho la haraka. Kulinda hazina hii ni kulinda uchumi wa taifa na mustakabali wake. Tukipuuza hili, hatari ya kuanguka kwa uchumi ni kubwa na madhara yake yatadumu vizazi.
Mtakumbuka huu UJUMBE , tunaelekea kuwa kama ZIMBABWE. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Blood LEGACY!!
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Happy Birthday Mama Samia.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Zawadi yangu ya wimbo kwa siku ya kuzaliwa kwa Mama Samia. ❤️❤️❤️
Happy birthday to you Mama Samia. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Leo unasherehekea siku yako ya kuzaliwa, na ninafurahi kwa sababu ninajua inakupa kujua thamani ya uhai na maisha. Bila uhai, sherehe hii haiwezi kuwepo. Kuna watu wengi sana wangependa kufurahia siku kama yako, lakini wapo waliokatishwa maisha wengine wakiwa bado wadogo sana.
Wakati unakata keki yako, kumbuka kwamba kuna wazazi na ndugu wanatafuta watoto wao bila matumaini ya kuwapata. Sio kwa ajili ya sherehe ya birthday, bali wanatamani angalau kupata miili ya ndugu zao hata kama wamekufa. Just imagine tu!!!
Happy birthday. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
It’s chess, not checkers.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Mara nyingi changamoto zinazoikumba taasisi za dini huonekana kama kosa la viongozi pekee, wakati waumini nao wana nafasi kubwa katika kuleta mabadiliko. Waumini ndiyo mhimili wa taasisi za dini kwa kuwa wanatoa ushiriki, rasilimali, na uhalali wa uongozi. Waumini wanaponyamaza au kuvumilia bila kuhoji, wanachangia kuendelea kwa matatizo yaliyopo. Kuwawajibisha viongozi si uasi, bali ni njia ya kulinda maadili na misingi ya taasisi za dini.
Ni wajibu wa waumini kuacha kuwalaumu watu au mifumo isiyofikiwa kwa urahisi, na badala yake wawajibishe viongozi walioko karibu nao. Kupitia umoja, mashinikizo ya busara, uwazi, na hata kususa shughuli fulani inapolazimu, waumini wanaweza kuhimiza uongozi unaowajibika. Taasisi imara za dini hujengwa na waumini wanaofikiri, wanaouliza maswali, na walio tayari kusimama kwa haki na ukweli. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Kama safari ikifika siku ya mwisho wa Dunia, tukawa sasa tuko foleni, aidha kwenda Jehanamu (motoni) au Peponi kwa Mwenyezi Mungu.
Mimi nitakuwa naangalia mbele kwa bidii sana. Nikiona baadhi ya viongozi wa dini wakielekea, kwa mfano, upande wa kushoto, mimi moja kwa moja nitaenda kulia.
Kwa maana huko kushoto hakuwezi kuwa mbinguni kabisa. Nimefikiria tu. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Kupiga kelele za haki ni burudani, kuisimamia ni mzigo ambao wengi hawataki kuubeba. Ndiyo maana jamii imejaa mahubiri matamu lakini imekauka kwa vitendo vya haki. Ukweli ni huu , haki haifi kwa kukosa watu wa kuizungumza, hufa kwa kukosa watu wa kuilinda. Taasisi za dini zimefeli vibaya. Zinaona wazi uchafuzi wa uchaguzi, uporaji wa sauti za wananchi, mateso na dhuluma za waziwazi lakini bado zinajipanga mstari wa mbele kuwabariki viongozi waliotokana na uhalifu huo. Hapa dini haitumiki kumtukuza Mwenyezi Mungu, bali kulainisha nyuso za uovu. Kimya chao si busara, ni ushirikiano. Baraka zao si ibada, ni usaliti wa maadili wanayodai kuyasimamia.
Kama kweli taasisi hizi zingemcha Mungu kuliko mamlaka, zingekataa waziwazi uongozi uliotokana na dhuluma kuanzia chini hadi juu. Lakini zimechagua usalama wa viti vyao badala ya damu ya haki. Kwa kufanya hivyo, zimegeuka kuwa nguzo za kuimarisha mfumo unaowakandamiza wale waliowapa uhalali wa kuzungumza kwa niaba yao.
Kinachofanyika sasa ni sawa na kumbaka mtoto wa miaka sita halafu uovu huo kujaribiwa kuoshwa kwa ahadi ya ndoa ya baadaye. Hakuna dini, hakuna sala, hakuna baraka inayoweza kuhalalisha hilo. Vivyo hivyo, hakuna maombi yatakayofuta dhambi ya uongozi uliopatikana kwa wizi wa haki za watu. Pale haki inapokanyagwa, baraka hugeuka kuwa laana, na dini inapogeuka kuwa mzaha mbele ya jamii.
Haki haitaki maneno mengi, inataka ujasiri. Na pale ujasiri unapokosekana, hata jina la Mungu hutumiwa vibaya kufunika uovu. Huo ndiyo moto unaoteketeza dhamiri ya taifa. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Ameandika Askofu Bagonza
MZEE MTEI AMEZIKWA MWILI; FIKRA ZAKE ZIMEBAKI
Jana 24/1/2026, taifa limeuzika mwili wa Mzee Edwin Mtei (94). Ana historia inayogusa sekta nyingi hapa nchini. Watu wa namna hiyo huwa ni kama moto ambao hufa/kuzimika na kuacha majivu badala ya kuacha moto. Yeye ameacha fikra. Ebu tudadavue umbeya kidogo:
1. Amewakusanya na kuwaunganisha watanzania. Hata waliohujumu fikra zake wakashika vipaza sauti kumsifia. Duh! Hata shetani anatamani kama wangekuwa wanamaanisha walichokuwa wanaongea bila kupepesa macho! Misiba ni darasa la uongozi.
2. Kanda zote za Chadema zikatoa salamu. Nikajifunza. Kama hatuko tayari kubadilika, basi tupanue mahabusu na magereza. Hakuna hela inayotosha kuwanunua wote, na hakuna risasi za kutosha kuwaua wote. Tunahitaji uongozi, siyo utawala.
3. Freeman Mbowe; Mkwe, mmoja wa waasisi, Mhanga wa maridhiano-hila, M/Kiti Mstaafu na mfungwa wa zamani, “akaiba show” kama alivyoiiba Monduli Februari 2024. Aliongea vizuri. Tunasubiri vitendo. Tomaso ni wengi sana. Ajue: Mkandamizaji wake wa jana hawezi kuwa mkombozi wake wa kweli leo. Awe moto siyo vuguvugu.
4. Madaraka makubwa hayaachani na upofu na ukiziwi. Mwenye madaraka akiona na kusikia, madaraka hupungua na usalama wake kuongezeka. Wananchi huchukua madaraka na kuyatumia kumlinda kiongozi wao. Bunduki haiongezi madaraka bali ni “Kausha madaraka”. Watawala wetu zindukeni, bunduki zinakausha madaraka yenu.
5. Upofu na ukiziwi ukimpata mtawala, mahabusu na magereza hugeuka vyuo vikuu vya mabadiliko katika nchi. Uhuru wa Afrika Kusini uliandaliwa Roben Island. Uhuru wa Kenya uliandaliwa Lokitang Prison na Lodwar Prison. Hapajawahi kutokea mfungwa wa kisiasa aliyerudi toka gerezani akamnyenyekea mtawala aliyemuweka. Hata Mandela alisamehe lakini hakuabudu aliyotendewa gerezani. Nipe ushahidi wa mfungwa wa kisiasa mnyenyekevu?
6. Katika nchi huru “zisizo huru”, mabadiliko huandaliwa katika vyuo vinavyoitwa House Arrests, mazuio ya maandamano, sheria za uchochezi, doria mitandaoni, na Safe Houses. Mahabusu maalum (solitary confinement) huwa ni madhabahu ya kuyeyusha dhahabu iwe bora zaidi. Hakuna barua nyepesi itokayo gerezani. Tunajikaanga.
7. Uhuru ni panga likatalo kuwili. Ukimweka huru mfungwa, mnufaika wa kwanza ni Askari Jela. Alipo mfungwa, yupo Askari. Wote wananyeshewa na wote wanakesha. Mkandamizaji na mkandamizwaji, wote hunufaika na uhuru. Kuwafungulia wafungwa wa kisiasa, ni kuwaweka huru watawala wetu. Mnataka nani aseme ndipo mjue hili ni kwa faida yenu?
8. Nimetoka ibadani. Leo tumehitimisha Ufunuo. Tumekumbushwa kubadilika kwa Bwana Yesu mbele ya wanafunzi wake kule mlimani. Wakatamani kubaki huko utukufuni. Yesu akasisitiza washuke ili kuhudumia wahitaji. Tunaalikwa kushuka ili kuwahudumia watu. Hitaji kuu la watu wetu ni UHURU na THAMANI YA UTU wao. Miradi bila uhuru ni sawa na chakula kizuri kwa mfungwa.
Ngoja niende kula. Kuna Mjaluo hapa kaazima suruali la kwenda kuposea mke wa pili, anasunbua sana hapa mtaani.😅😅 -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Ni jambo la kushangaza na la kusikitisha kuona Tanzania ikiendelea kukataa uraia wa pacha (dual citizenship) kana kwamba ni tishio kwa uhai wa taifa. Cha kuumiza zaidi ni ukweli kwamba sera hii inawaondolea Watanzania haki yao ya kuzaliwa haki ya msingi ya utaifa kwa sababu tu wamekuwa raia wa nchi nyingine. Huu si uzalendo , huu ni ushamba wa kisheria unaochochewa na hofu isiyo na msingi. Kisiasa, kukataa dual citizenship ni dalili ya uongozi unaokosa kujiamini. Taifa linalojiamini haliwaogopi raia wake, bali huwatumia kama rasilimali ya maendeleo. Serikali inapochagua kuwafukuza watu wake wenye elimu, mitaji, mitandao ya kimataifa na uzoefu wa dunia, inafanya maamuzi ya kisiasa yanayojidhuru yenyewe kwa makusudi. Watanzania wa diaspora si maadui wa taifa. Ni matokeo ya mfumo wa dunia ya leo walioondoka kutafuta elimu, ajira, au mazingira bora, wakarudi wakiwa na ujuzi, biashara, na uwezo wa kuwekeza. Badala ya kuwatengenezea mazingira ya kurudi na kuchangia, sera ya uraia wa pacha inawatisha, inawanyima haki, na inawasukuma wachangie maendeleo ya mataifa mengine.
Hoja ya “usalama wa taifa” inayotumika kupinga dual citizenship haina mashiko katika dunia ya sasa. Mataifa mengi imara kisiasa na kiusalama barani Afrika na kwingineko yanaruhusu uraia wa pacha bila kuyumba. Tanzania si ya kipekee kiasi cha kudhani raia wake wa nje ni hatari kuliko faida zao. Kiuchumi, gharama ya kisiasa ya sera hii ni kubwa , tunazuia mtiririko wa mitaji, tunapoteza maarifa , tunapunguza ubunifu, na tunajinyima fursa za ajira na ukuaji. Halafu tunajiuliza kwa nini uwekezaji wa ndani ni mdogo na kwa nini vijana wanakimbia nchi. Uzalendo wa kweli haujengwi kwa kuwavua watu wako utaifa, bali kwa kuwapa sababu ya kuamini na kushiriki katika mustakabali wa taifa. Mtanzania anabaki kuwa Mtanzania, hata akiwa na pasipoti ya nchi nyingine. Uraia wa pili hauondoi mapenzi ya kwanza. Ni wakati wa Tanzania kuachana na siasa za woga, kuachana na sera za kizamani, na kukumbatia uhalisia wa dunia ya leo. Dual citizenship si tishio kwa taifa ni fursa ya kisiasa, kiuchumi na kijamii. Kuendelea kuikataa ni kuendelea kujiumiza wenyewe kwa hiari. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Afya ya binadamu ina uhusiano wa moja kwa moja na chakula anachokula. Pamoja na hilo, mfumo wa afya duniani umejikita zaidi kwenye tiba ya magonjwa kwa kutumia dawa badala ya kuzuia magonjwa kupitia lishe sahihi. Hali hii imechangia kuongezeka kwa magonjwa sugu kama kisukari, shinikizo la damu na magonjwa ya moyo.
Lishe ni msingi wa afya ya mwili. Mwili hujijenga, hujirekebisha na kujilinda dhidi ya magonjwa kwa kutumia virutubisho vinavyopatikana kwenye chakula. Daktari asiye na uelewa wa kina kuhusu lishe humtibu mgonjwa kwa dawa bila kushughulikia chanzo halisi cha tatizo.
Kuwajengea madaktari elimu ya lishe kutasaidia kuzuia magonjwa kabla hayajatokea, kupunguza utegemezi wa dawa, na kuboresha maisha ya wagonjwa kwa muda mrefu. Aidha, gharama za huduma za afya zingepungua kwa kiasi kikubwa iwapo kinga ingekuwa kipaumbele kuliko tiba.
Kwa hiyo, elimu ya lishe kwa madaktari si hiari bali ni hitaji la msingi. Daktari anayeelewa lishe hutibu mwili mzima, si dalili pekee, na hilo ndilo lengo halisi la tiba.
Kwa hiyo, Tanzania pia inapaswa kufikiria kwa kina kujumuisha elimu ya lishe kama sehemu ya msingi katika mafunzo ya udaktari. Hatua hii itasaidia kujenga taifa lenye afya bora, tija kazini na maendeleo endelevu. -
Godbless E.J. Lema reposted
John Pambalu
@John_Pambalu
“Mkifautiana, mzungumze bila haya, bila unafiki, katika kweli na haki. Mungu atawapa uongozi bora na mtaendelea mbele kama familia, kama Taifa na kama serikali. Lazima kuzungumza mnapotofautiana,”. Askofu Simon Makundi wa kanisa la Anglikana.
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Mungu akutie nguvu sana Mama. Mume wako kaporwa uhai wake bila sababu yoyoye ile. Siku ya malipo inakuja.
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Tume huru haitaki uhuru na mwanga,sasa imekuwa Tume ya faragha. Wataanguka kwa kilio kikubwa sana. Kwani imeandikwa , Mshahara wa dhambi ni mauti.
-
Godbless E.J. Lema reposted
John Pambalu
@John_Pambalu
"Wanyama hufa Binadamu hufariki ili kujitofautisha na wanyama Binadamu lazima aache Historia ambayo itakumbukwa Ndivyo alivyifanya Mzee wetu Mtei"Amesema Mwenyekiti wa Bavicha Taifa @AdvMahinyila kwenye Ibada ya kumuaga Babu yetu na Muasisi wa CHADEMA Hayati Edwin Mtei.
-
Godbless E.J. Lema reposted
Mpale Mpoki
@MpaleMpoki
Asante sana Jenerali Ulimwengu, Mwanasheria, Mwandishi Mahiri, Mwanasiasa, Mwana Diplomasia, Mpigania Uhuru na Mtumishi wa Umma mwandamizi
UMETUPA MSAMIATI MPYA AMBAO UNAAKISI UHALISIA WA WATANZANIA WENGI
USWAHILI
@Advocate_Jebra @AdvMahinyila @Mwabuk2Boniface @MariaSTsehai
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mwanahabari mkongwe nchini, Jenerali Ulimwengu, amesema marehemu Mzee Edwin Mtei, muasisi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), alikuwa kiongozi aliyekataa vikali vitendo alivyoviita “Uswahili” katika uongozi, hususan tabia ya viongozi kukiuka ahadi walizozitoa kwa wananchi.
Ulimwengu ametoa kauli hiyo wakati wa shughuli za mazishi ya marehemu Mzee Mtei, akieleza kuwa marehemu aliamini katika uadilifu, uwajibikaji na uaminifu kwa wananchi kama misingi muhimu ya uongozi wa kweli.
Kwa mujibu wa Ulimwengu, Mzee Mtei hakuwa tayari kuvumilia unafiki wala siasa za maneno matamu zisizoendana na vitendo, akisisitiza kuwa kiongozi bora ni yule anayesimama na kutekeleza alichoahidi bila visingizio.
Mazishi ya Mzee Mtei yamehudhuriwa na viongozi wa kisiasa, wanachama wa CHADEMA, ndugu, jamaa na wananchi mbalimbali waliokuja kutoa heshima zao za mwisho, huku wengi wakimtaja marehemu kama kiongozi aliyethamini misingi ya haki, ukweli na demokrasia ya kweli.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
This is very big. Huyu Jennifer sasa ndiye mgeni maalumu na muhimu ktk tukio hili la kumpumzisha Mzee Mtei. Much ❤️❤️❤️❤️
Much Thanks To The Family.
NB: Kuna yule jamaa alisema ametumwa , mmmhh , yule hapana. Jennifer ni sawa sawa. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Nawakumbusha wajumbe wa TUME kuwa mshahara wa dhambi ni mauti.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Magic , yeah !!!
So it goes | @BlackSherifMusic Gospel Version #shorts youtube.com/shorts/_jGgeKT0jaw via @YouTube -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Pia swali lingine la msingi la kujiuliza ni hili ? Hivi huyu Mwigulu alishawahi kumiliki heshima mpaka na awe na ya kutoa ? Na eti nimesikia kuwa yeye ndiye kapewa maelekezo na Mwenyekiti wake wa CCM juu ya kuunganisha watu na Nchi. Dhihaka kubwa hii. Nimemsikiliza mara nyingi kila mara akiongea huwa anaongeza mpasuko mkubwa sana ktk jamii ambayo tiyari ina majeraha makubwa.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Hizi sio HESHIMA za mwisho. Huu ni UNAFIKI wa mwisho.
Angalia alivyoinama utafikiri ana uhalali hata wa kuitwa Waziri Mkuu. Mkti wetu yuko jela , Chama alicho kianzisha Mzee Mtei kimezuiwa kufanya kazi zake za siasa, ni juzi tu huko Mbeya viongozi wetu wamekamatwa kwa sababu tu ya kupandisha bendera ya Chama ktk maazimisho ya miaka 33 ya CHADEMA.Lakini hata kauli zake huyu Mwingulu huko barabarani anako zurura ni mbaya na za dhihaka kubwa ktk msingi wa kutafuta na kuimarisha haki. Africa unafiki ungekuwa unazalisha umeme ,Tanzania tungekuwa na umeme mwingi kuliko Marekani. -
Godbless E.J. Lema reposted
Jebra Kambole
@Advocate_Jebra
Salim Msemo Wakili wa Serikali akiwa kwenye Tume, sijui alikuwa anafanya nini? !
Hapa unategemea Tume iwe huru?, au na yeye ameenda kulalamika?
Kwanini amuangalie hivyo bibi? -
Godbless E.J. Lema reposted
Maria Sarungi Tsehai
@MariaSTsehai
Imependeza! Ingependeza zaidi angekuwepo na @TunduALissu but all is well 🙏🏽
Poleni wanafamilia ikiwemo @ChademaTZ2 family! -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
CHADEMA Arusha. Kuna nyakati historia huwaita watu wake si kwa maneno, bali kwa dhamira. Jumamosi tarehe 24/01/2026, Tengeru Arusha haitakuwa tu mahali pa mazishi ya Mzee Edwin Mtei, itakuwa mahali pa kuhoji dhamiri zetu kama wanachama wa CHADEMA.
Mzee Mtei na wenzake hawakuanzisha CHADEMA kwa ajili ya madaraka, bali kwa ajili ya haki na heshima ya utu wa Mtanzania. Pamoja kuwa niko nje ya nchi kwa masuala ya kifamilia, lakini dhamira yangu hainipi nafasi ya kunyamaza. Natoa wito kwa wanachama wote wa CHADEMA hususani Mkoa wa Arusha na Kanda ya Kaskazini kusimama upande wa historia kwa kujitokeza kwa wingi sana Tengeru kutoa heshima ya mwisho kwa Mzee Edwin Mtei, muasisi wa CHADEMA. Mzee Edwin Mtei anastahili heshima kubwa, si kwa maneno, bali kwa matendo.
Mungu awabariki sana. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Walitufunga minyororo.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Iende ?
-
Godbless E.J. Lema reposted
Boniface Jacob
@ExMayorUbungo
Baada ya kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA kanda ya Pwani, Oktoba 2024 nikiwa ndani ya kuta za gereza la Segerea.
Nilifika eneo la ujenzi wa ofisi ya CHADEMA, Mkoa wa pwani, Wilaya ya Kibaha na kuona ujenzi wa ofisi uliokwama kwa muda mrefu.
Niliomba wanikabidhi eneo hili la ujenzi lililokuwa na msingi niliendeleze kwa ujenzi wa ofisi ya CHADEMA Mkoa na Wilaya yenye ukumbi wa watu 150 ndani yake.
Ndani ya mwaka mmoja nimefanikiwa kulinyanyua Jengo lote na jana nimekabidhi vifaa vya ujenzi ili kukamilisha awamu ya kwanza ya ujenzi kwa kupiga renta na tofali za juu, jumla ya gharama kwa awamu hii ni Tsh. milioni 10.
Muda si mrefu nitaingia awamu ya pili ya upauaji wa jengo, madirisha na kupiga plasta jengo lote.
Nimefurahi jana kutembelea ujenzi kama sehemu ya kuadhimisha miaka 33 ya kuzaliwa kwa CHADEMA.
Zawadi yangu ya pekee kwa CHADEMA nikujenga taasisi imara na ya kudumu na kutumiwa na vizazi vijavyo. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Happy Birthday Bro.
Unaongeza mwaka mwingine wa maisha ukiwa gerezani si kwa sababu uliisaliti nchi, bali kwa sababu ulikataa kuisaliti dhamiri yako. Katika Tanzania ambako ukweli umegeuzwa kosa na ukimya umepewa heshima, wewe ulichagua kusema. Na kwa kusema, ukaadhibiwa.
Gereza si kipimo cha hatia, bali mara nyingi ni ushahidi wa uoga wa watawala. Minyororo haiwezi kufunga wazo, na kuta haziwezi kuzima ukweli. Mwili wako unaweza kuwa nyuma ya vizuizi, lakini fikra zako ziko huru, na historia daima huwa upande wa wanaothubutu kupinga uongo.
Nafahamu moyo wako , umejengwa kwa subira, umeumizwa lakini haukuvunjika. Falsafa ya haki ni hii, mateso ya mtu mmoja yanaweza kuwa mbegu ya ukombozi wa wengi.
Heri ya siku ya kuzaliwa TAL. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Chukua hii.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Miaka 33 iliyopita uliamini kwa dhati kabisa kuwa Tanzania inahitaji mabadiliko. Zilikuwa ni nyakati za giza, si zama za teknolojia wala urahisi. Ulijitoa kwa akili, mali, na ujuzi, ukawaita marafiki zako mkajadili hatma ya Taifa. Haikuwa kazi nyepesi hata kidogo. Kwani uli sacrifice urafiki wako, status yako na mahusiano yako na viongozi wa Serikali waandamizi siku zile, ambao mlifanya nao kazi ktk nafasi za juu.Hili si jaribu dogo hata kidogo.
Leo, maono yale yamekua na kuwa makubwa. CHADEMA imekuwa kimbilio la wanyonge kote nchini. Kuishi kwako kumeipa nchi yetu maana ya kipekee. Ibarikiwe siku uliyotolewa tumboni kwa mama yako. Tunamshukuru Mungu kwa maisha yako yenye kusudi. Watoto wako na familia ya Mtei wamebarikiwa kuwa na baba, ndugu, na kiongozi kama wewe. Umeacha alama kubwa isiyolinganishwa na chochote, na umeondoka ukiwa na heshima ya juu kabisa.
Hata wale wanaoizuia CHADEMA kufanya majukumu yake, na kuumiza,kutesa watu wengi wenye imani kama yako juu ya wema kwa Nchi yetu, na sasa wanamshikilia Mwenyekiti wa sasa Tundu Lissu, gerezani hata hataweza kukuzika, watasimama na kutoa salamu. Watasema kuwa ulikuwa mtu mwema na mpenda nchi yako. Na watakaposema hivi, watakuwa wakisema ukweli pamoja na ukatili wao mkubwa ktk maono yako ya Tanzania bora na yenye demokrasia safi.
Mauti yako hayana uchungu, kwa sababu uliishi kwa kusudi jema na ukautimiza wito wako kikamilifu.
Lala salama Mzee Mtei. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Kila chama kinachotaka kuongoza lazima kiwe mstari wa mbele katika kuhakikisha uwazi, uwajibikaji, na demokrasia. ACT, ni kielelezo cha chama kilichopoteza heshima kutokana na uwongo wake na ushirika ktk uchaguzi October 29 ,2025. ACT hawawezi kujitengana dhuluma na athari za uchaguzi. Na wanapaswa kuwajibishwa sawa na CCM mbele ya uso wa umma.Kauli yao sasa haina adabu hata kidogo. Wanasema uchaguzi urudiwe wakati wana Wabunge Zanzibar na Tanganyika ? Kuna mambo mawili wanatafuta wanapandisha presha ili watafutwe na vile vile kutumia hadaa ili waone kama wanaweza kurudisha uhalali wao. Nimemuona na Mzee Butiku anakuja kwa style hii.
-
Godbless E.J. Lema reposted
Think Different
@lifeofmshaba
HAYA NI MAAJABU MAKBUWA SANA
Mkurugenzi wa Fedha na Utawala (Director of Finance and Administration) wa Mamlaka ya vitambulisho vya taifa (NIDA), CPA George Mahigu Seni, amesimamishwa kazi kwa kupinga mauaji ya watu wasio na hatia Oktoba 29.
CPA Seni anatuhumiwa kuchapisha maneno ya uchochezi kwenye WhatsApp group ya marafiki zake aliosoma nao SHYCOM. Mmoja kati ya classmates zake alichukua maneno hayo na kuyatuma ofisi ya Waziri Mkuu, na ndipo ikatolewa order ya Seni kukamatwa.
Maneno ya George Mahigu Seni kwenye group hilo ni kama ifuatavyo:
"Siasa ndiyo kila kitu Mtani. Kinacho sababisha yote haya hata kama hatutaki ni ukosefu wa Siasa Bora, Uongozi Bora na Demokrasia thabiti. Je ni sawa mwanamke anayekimbia kupigwa risasi mgongoni? Ni sawa kijana asiyekuwa na chochote mkononi kupigwa risasi? Kwamba ni sawa kufanya mauaji ya halaiki kinyama namna ile?
Je ni sawa kuwatoa vijana ndani wakiangalia mpira na kuwalaza chini na kuwapiga mmoja baada ya mwingine? Siungi mkono watu kuharibu mali za umma na mali binafsi. Siungi mkono hata kufanya fujo tu, lakini kwa picha ambazo zilionekana siku ya tarehe 30 kabla hata zileza CNN si sawa nguvu iliyotumika.
Mtani usilete siasa ktk issue serious. Mnakuwaje na shida ya maji kama mna mto, Rufiji, Ruvuma, Kagera, ziwa Rukwa, Victoria, Tanganyika, Nyasa, Eyas, nk. Mna mvua ya wastani kwa mwaka, baadhi ya maeneo maji yapo chini lakini bado nchi inakosa maji safi? Justify hapo mtan??"
Hoja hizo mbili za CPA Seni za kupinga mauaji ya Oktoba 29 na kukosoa nchi kukosa maji licha ya kuwa na vyanzo vingi, zilitosha kabisa kumuweka matatani. Polisi walimvamia Seni akiwa Arusha kikazi tarehe 15 Desemba 2025 na kumkamata, kisha kumsafirisha hadi Dodoma kwa mahojiano. Alishikiliwa mahabusu kwa siku kadhaa akanyang'anywa simu, computer na kulazimishwa kutoa password zake za social media. Alipigwa sana akilazimishwa amtaje anayemtuma. Hata hivyo alishikilia msimamo wake kuwa hajatumwa na yeyote bali alotoa mawazo yake tu.
Baada ya kuhojiwa aliachiliwa na aliporudi ofisini, aliambiwa na boss wake kwamba amepokea maelekezo kutoka juu kuwa asiende tena kazini hadi hapo atakapopewa maelekezo mengine. CPA Seni alipoomba barua ya kusimamishwa kazi hakupewa barua yoyote rasmi, bali alijibiwa "kihuni" kwamba akihitajika ataitwa.
Hapa ndipo tulipofika kama taifa. Serikali imeua watoto wetu na sasa inafukuza kazi yeyote anayekemea mauaji hayo. Lakini wale waliofanya mauaji ya kinyama wanapandishwa vyeo na kupongezwa.
------------- ========+++++++-----------------
Fikiria mtu kuandika maswali kama haya anafukuzwa kazi na kukamatwa, ameweka maswali muhimu tu kuhusu namna tukio lilivyotokea
Kuna utashi wa kila mtu, yeye anaona haikuwa sasa kufanyika kwa siasa kwenye tukio kama lile
Wamechukua message yake na kutuma kwa Mwigulu amefukuzwa kazi na kukamatwa, Haya makosa Magufuli alifanya kwa Masamaki aliyekuwa Kamishina forodha iliisha je? Samia akafanya kwa mkurugenzi wa TPA ikaishia wapi?
Mwigulu anafikiria huu uonevu ataufanya mpaka lini? kwamba leo mtu kuhoja zile risasi ilikuwa sawa anafukuzwa kazi?
Ni wangapi wasihoji au kuandika wana hasira kuliko hata huyu? wangapi mmeua ndugu zao wamejikausha tu wanafanyia mipango ya kuwalipizia kimya kimya, Unakwenda hospital kumbe dokta hapo au nesi mmeua ndugu yake, anajua wewe ni li CCM anakufanyia kajambo unakwenda huko unakufa au unakuwa mlemavu, au mwanao anakutana na mtu ndugu zake wameuwawa
Mnafikiria mko salama kwa kuficha haya mauaji lakini hali ni mbaya kuliko mnavyofikiria, watu 10,000 ni wengi, wasira mwenyewe mmeua ndugu zake
mmshajua ndugu wa kila mliyeua? -
Godbless E.J. Lema reposted
Yoko
@Kibet_bull
Museveni boys who were secretly recorded marking ballot papers in favor of Museveni.
Bobi Wine should be declared the winner.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Miaka 33 ya CHADEMA imejazwa na uvumilivu wa mateso, changamoto, na majaribu, lakini roho zetu haizikuzimika. Tumesoma kuwa haki, ukweli, na huruma haziuziki kwa urahisi, lakini ndoto ya taifa lenye uwazi, mshikamano, na fursa sawa daima ni thamani isiyopotea.
Wacha tuendelee kusimama imara, tukijenga mustakabali kwa matumaini na ujasiri, tukithamini waliopoteza uhai na kuimarishana wanaoendelea na waliopo kwa vizazi vijavyo. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Thank you Muhammad Ali
-
Godbless E.J. Lema reposted
BOBI WINE
@HEBobiwine
Video showing Electoral Commission officials ticking all ballot papers in favor of Museveni at a polling station in western Uganda. This is what Museveni and his criminal system call an election! We campaigned. We voted. We tried to protect our vote but the criminals arrested or abducted many of our agents and officials. The only recourse is for the PEOPLE OF UGANDA to reclaim their voice. That is why we called this a PROTEST VOTE.
Please keep those videos coming in - and all other evidence of the theft that took place on the 15th.
#freeugandanow -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Seni , Nimekujua toka ukiwa Mhasibu Mkuu Bungeni , you are very nice and humble guy. Usiogope juu ya majaribu unayopitia. Mimi ningekuwa wewe nisingerudi hapo kazini. Ningeandika barua ya kuacha kazi. Fanya hivi uone ukuu wa Mwenyezi Mungu juu yako.
Zaburi 37:25, Nilikuwa kijana na sasa ni mzee; kamwe sijaona mwadilifu ameachwa na Mungu, au watoto wake wakiombaomba chakula.
Seni , iko njia kubwa na bora mbele yako. Usiogope.
Una baraka nyingi angalau unaumizwa na mateso ya wengine. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
George Mahigu Seni, Mkurugenzi wa Fedha na Utawala (Director of Finance and Administration) NIDA, alikamatwa na Polisi tarehe 15 Desemba 2025 akiwa Arusha kikazi, na kusafirishwa Dodoma kwa mahojiano. Baada ya tukio hili, kuhojiwa sasa ameambiwa na mkuu wake wa kazi asiende kazini bila hata kupewa barua yoyote rasmi. Sababu, alichapisha maneno yafuatayo kwenye WhatsApp group ya marafiki SHYCOM.
Maneno ya George Mahigu:
1.Siasa ndiyo kila kitu Mtani. Kinacho sababisha yote haya hata kama hatutaki ni ukosefu wa Siasa Bora, Uongozi Bora na Demokrasia thabiti. Huko kwingine kote maji kwenye kinu.
2.Kwamba ni sawa mwanamke aliyeogopa anapigwa risasi mgongoni?
Kwamba ni sawa kijana asiyekuwa na chochote mkononi kupigwa risasi?
Kwamba ni sawa kufanya mauaji ya halaiki kinyama namna ile?
Kwamba ni sawa kuwatoa vijana ndani wakiangalia mpira na kuwalaza chini na kuwapiga mmoja baada ya mwingine?
Siungi mkono watu kuharibu mali za umma na za binafsi na hata kufanya fujo tu.
Lakini kwa picha ambazo zilionekana siku ya tarehe 30 kabla hata hii ya CNN si sawa nguvu iliyotumika.”
3.Kaka!!!
Mtan usilete siasa ktk issue serious… mnakuwaje na shida ya maji km mna mto, Rufiji, Ruvuma,Kagera,Ruvua,Rukwa. Ziwe Victoria,Tanganyika,nyasa,eyas,nk..mna mvua ya wastan kwa mwaka, baadhi ya maeneo maji yapo chini…justify hapo mtan?? 😭😭😭” -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Wahuni wakiongea ? Wapige ignore. Hakuna cha kuthibitisha. Endelea na zako.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Usipokuwa makini katika maisha na kutafakari kwa kina, unaweza kujikuta unaishi bila kusudi. Ukizaliwa, unaishi kwa ajili ya kula, kunywa, mapenzi, kuzaa, kuzeeka na hatimaye kufa. Kukosa purpose ya maisha ni tatizo kubwa sana, na ndilo chimbuko la ujinga na upumbavu kutawala duniani.
Bila kusudi la kweli, haki na utu hakuna kitu chochote kinachoweza kuwa na maana. CCM ni mfano halisi wa andiko hili. Ni Chama kinacho haribu sana Taifa. Wana bidii ya kuficha uovu , mateso, mauaji kuliko kulinda na kutetea ukweli na utu. Hii ni hasara kwa Taifa lote na vizazi vijavyo. Wakati sadism inakua culture ya Nchi hakuna mtu anayeweza kuwa salama. Hata wao wenyewe. Muda utapiga kelele kubwa sana siku sio nyingi. -
Godbless E.J. Lema reposted
Chadema Tanzania
@ChademaTZ2
Live; John Mnyika anazungumza juu ya uundwaji wa Bavicha na safari yake ya kisiasa x.com/i/broadcasts/1BRKjgnzWkdGw
-
Godbless E.J. Lema reposted
John Heche
@HecheJohn
Tanzania: Ushahidi mpya juu ya mauaji ya Oktoba 2025 youtu.be/qyJUphOmnBw via @YouTube
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Tumetoka mbali na tumekaribia kufika.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Mimi nakushukuru sana kwa pole zako. Kwani nilipata shida kubwa sana kuwasiliana na Neema pamoja na watoto wangu katika siku zile, kutokana na kukatika kwa mtandao wa intaneti. Ilikuwa hali ngumu sana kwangu.
Mungu akulipe katika kila hatua ya mawazo yako na matendo yako yote uliyoyafanya na unayoendelea kuyafanya, hasa katika siku zile, kwa kadri ya uwezo wake. Uwezo wa Mungu na nguvu zake ziwe juu yako siku zote.
Na neno hili la Mungu likupe mwanga na nguvu ,
Wagalatia 6:7–8
Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna. Maana yeye apandaye kwa mwili wake, katika mwili wake atavuna uharibifu; bali yeye apandaye kwa Roho, katika Roho atavuna uzima wa milele.
Na pia nikukumbushe hekima hii,
Mithali 18:12
Kabla ya anguko moyo wa mtu hujaa kiburi, bali unyenyekevu hutangulia heshima. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Tumekaribia kufika siku zile muhimu sana ktk ukombozi wa taifa letu. Mateso uliyopitia kuanzia kupigwa risasi hata kufanywa mlemavu hadi sasa kuishi jela , huku yastahili kabisa. Lakini umethibitisha upendo mkubwa kwa nchi yako.Jambo muhimu sana kwetu sote ni kuendelea kuwa na ujasiri ktk mapambano yetu.
Ushindi wetu haupatikani pale tutakaposhinda tu uchaguzi; ushindi wetu wa kweli ni pale jamii nzima itakapoelewa thamani ya jirani yake, haki, upendo, na huruma. Hili ndilo jambo muhimu sana kwetu na ndilo linalotutia moyo. Maombi yangu ni kwamba tuufanye upendo kuwa utamaduni wetu, ushindi wa aina hii utakuwa mkubwa zaidi kuliko kushinda hata Uchaguzi.
Pia , Mama Samia ametoa pole kwa internet kukatika ktk zile siku za maandamano wkt wa uchafuzi. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
"Mheshimiwa umeambiwa kwamba naomba huruma ya Mahakama. Mimi siombi huruma ya Mahakama. Siombi, sijaomba na sitaomba.Ninachotaka, utaratibu wa Mahakama usichezewe. Mawakili wa Serikali na DPP wanachezea utaratibu wa Mahakama. Mimi siyo aina ya watu ambao wataomba huruma ya Mahakama, kwa sababu nasimamia ninachoamini kuwa ni kweli. Wanaomba huruma ya Mahakama ni wenye hatia."
Tundu Antiphas Mughwai Lissu -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
JOHN MNYIKA NA GODBLESS LEMA WAWAKA MKUTANO WA HADHARA CHADEMA SHINYANG... youtu.be/c79h6cZsWGM via @YouTube
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
LIVE: MASWA -SIMIYU IMEITIKA- JOHN MNYIKA, LEMA, NGOTO NA ASKOFU MWAMAK... www.youtube.com/live/Vk92njQdgfI via @YouTube
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
LIVE: ITILIMA-SIMIYU IMEITIKA- JOHN MNYIKA, LEMA, NGOTO NA ASKOFU MWAMA... www.youtube.com/live/4D6xr0diMEo via @YouTube
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
BARIADI IMEITIKA PAMOJA NA USUMBUFU MKUBWA WA KUPATA VIWANJA.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
LIVE: BARIADI IMEITIKA- JOHN MNYIKA, LEMA, NGOTO NA ASKOFU MWAMAKULA WAN... www.youtube.com/live/1i-qN09i9xo via @YouTube
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
LIVE: LAMADI IMEITIKA- JOHN MNYIKA, LEMA, NGOTO NA ASKOFU MWAMAKULA WANA... www.youtube.com/live/bgpOB9DGh6Y via @YouTube
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Bunda Mjini
LIVE: MNYIKA, GODBLESS LEMA, NGOTO NA ASKOFU MWAMAKULA WANAUWASHA MOTO M... www.youtube.com/live/V5JKNEUTel0 via @YouTube -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
#live: Mnyika Godbless Lema, Askofu Mwamakula Wanaihubiri No Reform No E... www.youtube.com/live/EdlV9Zx01Ng via @YouTube
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Muda Huu Tukiwa Kiabakari.
LIVE: MNYIKA, GODBLESS LEMA, NGOTO NA ASKOFU MWAMAKULA WANAUWASHA MOTO M... www.youtube.com/live/FBfD_jN_uj4 via @YouTube -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
LIVE: MNYIKA, LEMA, ASKOFU MWAMAKULA NA NGOTO WANAUWASHA MOTO MUDA HUU T... www.youtube.com/live/U58R0I81aCE via @YouTube
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
LIVE: MNYIKA, LEMA WANAUWASHA MOTO MUDA HUU KIHESA www.youtube.com/live/5Q3y7ycPZJI via @YouTube
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
🅻🅸🆅🅴 HECHE, MNYIKA, LEMA NA DKT. SLAA WANAUNGURUMA BUKOBA MJINI - YouTube www.youtube.com/watch?v=9xNeGPa1sXA
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Bunge La EU Linaendelea Na Kesi Ya Tundu Lissu www.youtube.com/live/9jS4bRPGQjE
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Tone Tone Iendelee CHADEMA HQ MPESA NAMBA 0744446969.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Sasa Pengine Tunaweza Kujua Mdude Yuko Wapi Na RCO Mbeya Anaweza Kusaidia Taifa Kutambua Ukweli Huu.
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
The most dangerous anger comes from someone with a good heart. They hold it in, stay calm, and forgive, until one day, they can't anymore. Don't push a good person too far.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Huko wapi Hilda ? Mwenyezi Mungu Nakuomba Huyu Mdogo Wetu Apatikane Sasa Akiwa Hai.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Mh Rais Nakusalimu. Tumetoka Mwananyamala Hospital , Majeruhi Rafiki Zetu Na Viongozi Wenzetu Ambao Tumewakuta Wako Tisa (9) Waliokamatwa Leo Mahakamani , Lakini Yuko Mtu Mmoja Tumeambiwa Alipigwa Sana Na Tunaambiwa Amekufa, Tumefika Mochwari Tukakuta Polisi Wanataka Kushusha Maiti. Tulikaa Pembeni Ili Wamalize Kazi Yao , Badala ya Mwili Kushushwa Ili Tuweze Kuitambua Hiyo Maiti, Badala Yake Gari Ya Polisi Ilikimbia Na Kuondoka na Mwili Wa Marehemu Wkt Tulikuta Marehemu Alikuwa Amekwisha Andikishwa Kuingia Mochwari. Nimesema Nikupe Taarifa Na Pia Nikutakia Kazi Njema Sana Na Mungu Akulinde Wewe Na Familia Yako. DAMU ITANENA.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Nimefika Mahakama ya Kisutu Kesi ya Mh Mwenyekiti Tundu Lissu hataletwa Mahakamani badala yake kesi hii imeamriwa isikilizwe kwa njia ya mtandao.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Dar es Salaam Inayoketi Kisutu Shauri la Jinai namba 202504102000008606 Jamhuri dhidi ya Tundu Antipace Lissu mbele ya Mhe. Geofrey Mhini, Hakimu Mkazi Mwandamizi.
Tafadhali tumia kiungo (link) kifuatacho virtualcourt.judiciary.go.tz/kisutu kuendelea na shauri kwa njia ya mtandao. Shauri limepagwa kwa usikilizaji wa awali leo 24/04/2025 saa tatu asubuhi.
Hii ya Uchochezi.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Dar es Salaam Inayoketi Kisutu Shauri la Jinai namba 202504102000008607 Jamhuri dhidi ya Tundu Antipace Lissu mbele ya Mhe. Franco Kiswaga.
Tafadhali tumia kiungo (link) kifuatacho virtualcourt.judiciary.go.tz/kisutu kuendelea na shauri kwa njia ya mtandao. Shauri limepagwa kwa kutajwa leo 24/04/2025 saa tano asubuhi.
Hii ya Uhaini.
Tafadhali kila mtu aingie kusikiliza wakati huu. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Makamu Mwenyekiti CHADEMA akamatwa na Polisi. CHADEMA ilikuwa ifanye mkutano leo KARIAKOO , TAARIFA ya Mkutano ilipekekwa Wiki Moja Iliyopita na Mkutano ulianza kutangazwa. Leo Mchana Polisi wameleta barua kuzuia mkutano kufanyika Kariakoo. Makamu Mwenyekiti Kamanda John Heche alienda eneo la mkutano kuendelea na mkutano, alipofika Polisi walimzuia na wamemkamata na kwenda naye pasipo julikana, tunafuatilia , habari zaidi tutawaleteeni muda sio mrefu.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
MASASI nyie ni watu WEMA sana. Mungu awabariki sana. Tafadhali endeleeni kuchanga Tone Tone. Mpesa CHADEMA HQ 0744446969
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Gazeti la Mwanachi na nyie mko kwenye huu mradi ? Ikiwa ni Muhimu basi Tutauelekeza umma kitu cha kufanya dhidi yenu , kwa muda sasa tunawatazama kwa umakini na tunagundua jambo hili.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Siku moja nilikutana na Mzee Wasira kwenye mkutano mmoja Serena Hotel , nikamwambia Mzee huoni kuwa hali ni mbaya Nchini ? Akaniambia naona lakini nitasema kama utanifundisha namna ya kutoroka Nchini bila kukamatwa !!!
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Tuendelee kuchangia chama chetu.
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Tukio letu la Leo Litaanza Saa Moja Usiku Hapa Makao Makuu ya Chama na Itakapofika Saa Tatu Usiku Tutakuwa LIVE ITV na RADIO ONE kuanzia Saa 3 Usiku Mpaka Saa Tano Usiku.Vile Vile Fuatilia Ktk Mitandao ya Kijamii Kuanzia Saa Moja Usiku. Club house , X , Youtube , Instagram , Facebook.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Makao Makuu maandalizi yanaendelea kwa kasi ya 7G . Defeat can never be our option.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Kuna Masuala ya UFUNDI Yalitokea Kwa Jamaa Yetu NIMO ,Tiyari NIMO Amerekebisha , Sasa Unaweza Kuwemo. Sasa Andika NIMO Kwenda Namba 0744446969. NIMO Anaomba Radhi Kwa Usumbufu Uliojitokeza.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Changia ku-support harakati CHADEMA.Jina litasema M-Pesa CHADEMA HQ: 0744-446969
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Ingewezekana Mkutano Mkuu wa Chama chetu utakaofanyika Mwezi January utoke na jina la Mgombea Urais na pia utoe mamlaka kwa Kamati Kuu/Baraza Kuu kutafuta mgombea mwenza na kumthibitisha kwa niaba ya mkutano mkuu ili chama kitoke na jina la mgombea sambamba na viongozi wakuu wa Chama. Jambo hili ni muhimu kwa ajili ya branding ya mgombea Urais na masuala ya uratibu wa masuala ya kampeni na raslimali fedha kwa mgombea. Pengine wazo hili likifanyiwa kazi bila Shaka tunaweza kumaliza salama zaidi na kupunguza kelele nyingi zisizokuwa na maana.Kamati Kuu inaweza kufikiri hivi.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
CCM wanatufuatilia sana, wana hifadhi kila kauli zetu juu ya wagombea wetu wote ktk mchakato wa uchaguzi wa Chama wa viongozi wakuu Mwezi January , bila shaka watazitumia kauli hizi Mwaka 2025 kama tutashiriki na kutakuwepo na uchaguzi huru. Lakini pia wananchi wana share kila habari inayoleta fitina na uchungu miongoni mwetu. Hii ni hatari. Chama cha siasa za upinzani na harakati za kutafuta utawala bora zinaongozwa na inner purpose na passion , kusudi likifa Chama kinakufa kwa sababu 99% ya viongozi na wanachama wanafanya wajibu wa kazi za Chama kwa kujitolea , sasa watawezaje kujitolea kama hakuna purpose ? Moral inajengwa na nidhamu . Kwa hali ilivyo sasa tuna uchungu sisi kwa sisi kuliko tulivyo na uchungu dhidi ya CCM , kampeni ya sasa ya dhihaka na matusi kwa viongozi na wananchi ambao hatuwaungi mkono imekuwa kali kuliko kampeni ya kukomesha mauaji na utekaji Nchini. Let’s get back to the purpose na kila mtu aheshimiwe na kuthaminiwa kwa upande aliouchagua kwa maana ndiyo demokrasi yenyewe.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Ilifikiriwa hili jambo haliwezekani Msumbiji na kumbe ni habari ya watu kufika mwisho wa kuvumilia ( Tipping Point ) , ndani ya siku 3 watu 125 wameuwawa na serikali na bado watu wanasonga na maandamano. Tanzania inaona haya hayawezi kutokea ndio maana viongozi wanaendesha Nchi kwa namna wanavyojisikia.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Huu uhuni mkubwa.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Hiki ni kituo cha uandikishaji karibu na nyumbani kwangu, hawa ni wanafunzi wanaandikishwa na msimamizi wa uchaguzi.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Wananchi msikate tamaa kwenda kujiandikisha kwa sababu ya figisu figusu na ukiukwaji wa sheria unaoendelea ktk uandishi daftari ktk uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Ni bora mkajiandikisha mkapiga kura wakaiba kuliko mkaacha kujiandikisha halafu wakashinda uchaguzi. Wakiiba watakuja kuvuna mshahara wa dhambi , ni muhimu pia kuwaandalia mshahara huu. Nyie mkikata tamaa sisi tunaopita mbele yenu tutakuwa wapweke sana ktk wajibu huu muhimu ktk kupigania ustawi wa Nchi yetu. Nendeni mkajiandikishe pia mchukue na rafiki yako, mchumba, mama , mke , mume baba, babu na shawishi kila mtu. Kazi hii inakuhusu wewe na mimi. Don’t Give Up. Tutavuka tukiwa na nguvu siku moja japo kuwa tunapita ktk bonde la uvuli wa mauti.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Huna Baba wala Mama. YATIMA ambaye huko very focused ktk HAKI na KWELI. Naujua moyo wako na mawazo yako juu ya haki na kweli , you are a very good boy , thinking about others all the time. Nimeamka kusali kwa ajili yenu wote mnaopita ktk mateso na huzuni kwa ajili ya wengine na Nchi yenu. Haitakuwa rahisi kabisa kwao na familia zao wote wanaohusika na mateso kwa wengine. God can not be mocked zaidi.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
This is Lack of quality THINKING. Hata kama mlikuwa mmekusudia eneo hili la COCO Beach kufanyike biashara basi ni dhahiri kwamba standard ya biashara yenyewe hazikupaswa kuwa za aina hii.Huu ni ufukwe mrefu kabisa ktk eneo Posh la Jiji,lakini mmeshindwa ku regulate quality na standard.Mmeua ajira nyingi zaidi kwa kushindwa ku apply tu a proper THINKING ktk eneo hili.Kama fikra zako hazijali ktk kuzingatia ubora na classy basi uwezi kuwa na utamaduni wa raia wako kuwa na quality Thinking.Hii ni hatari maana maisha bora yanajengwa na mawazo na sio rasilimali.
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Haki za Vyama vya Siasa ziheshimiwe.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Hamjui hata propaganda.BAVICHA tena ? 😀😀😀😀
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
KATAA DHARAU - Unaweza kuishi bila kazi ya Serikali,una umri wa kutetea principle kuliko chakula. Kwanza kwa umri wako ni lazima utakuwa na masharti ya kula.Kwa hiyo mboga za majani na matango huwezi shindwa.Mtazame Jenerali Ulimwengu/Prof Assad.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Ataondoka nyumbani akifika miaka 18 .Nahesabu ...bado miaka mitatu.
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Jambo moja nina uhakika nalo ni kuwa HAKI ITASHINDA DHIDI YA DHULUMA
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
MillardAyo ana post sana matukio mabaya ya Polisi Kenya. TZ matukio kama haya huwa haoni,anafikiri yuko salama,kila anaye fumbia macho uhalifu dhidi ya ubinadamu ajue atavuna.Inatubidi tutathimini vyombo vya habari vinavyo fumbia macho haki na kuanza Kampeni negative dhidi yake
-
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema
Kama @ChademaMdude kavunja sheria,ni muhimu sheria halali zikafuata mkondo,tabia ya kutekana/kutesana inaharibu Nchi,mna lazimisha watu kufikiri visasi,tukiingia ktk hatua hii,familia za watekaji na watekwaji hazitakuwa salama,kwa kutowaza vizuri mnaona mambo haya hayawezekani






































































































































































































































































































































































































































































































































































































