MWIGULU AMPONGEZA NDEJEMBI, AMSIFU RAIS SAMIA KWA KUMCHAGUA MTU MAHIRI NA MCHAPAKAZI
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, amempongeza Mhe. Deogratius John Ndejembi kwa kuaminiwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Kamati Kuu ya CCM na Halmashauri Kuu ya CCM na kuteuliwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Dkt. Mwigulu ameitumia nafasi hiyo pia kumpongeza Rais Samia kwa kile alichokiita uwezo wa kumuona Ndejembi na kutambua sifa zake za uongozi, akieleza kuwa kiongozi huyo anazo sifa zinazomfanya astahili kupewa dhamana hiyo kubwa ya kitaifa.
Akizungumza leo Alhamisi, Agosti 27, 2026, Bungeni jijini Dodoma wakati wa kipindi cha maswali na majibu kwa Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu amesema Ndejembi ni kiongozi mahiri, makini na mchapakazi anayefanya kazi bila kuchoka kwa ajili ya kuhakikisha Watanzania wanapata manufaa.
"Mhe. Spika, Deogratius Ndejembi kama kiongozi ni kiongozi mahiri sana, ni kiongozi makini, kiongozi mchapakazi anayefanya kazi bila kuchoka ili Watanzania waweze kupata manufaa." Amesema Dkt. Mwigulu.
Waziri Mkuu amesema pamoja na uwezo wa kufanya kazi, Ndejembi pia ana sifa za unyenyekevu na upole, akimtaja kuwa mtu rahimu na asiye na hiana ndani yake.
Kwa upande mwingine, Dkt. Mwigulu amemhakikishia Ndejembi kuwa yeye pamoja na mawaziri wenzake wako tayari kushirikiana naye katika kutekeleza majukumu yake mapya, ikiwa ni pamoja na kupokea na kutekeleza maelekezo yatakayosaidia kufanikisha maagizo ya Rais Samia katika kuijenga Tanzania.
Kauli hiyo ya Waziri Mkuu inaweka wazi kuwa uteuzi wa Ndejembi haukuangalia nafasi pekee, bali ulizingatia pia sifa za kiuongozi ambazo amekuwa akizionesha katika utekelezaji wa majukumu yake.
Mwigulu Nchemba
Mwigulu Lameck Nchemba (born 7 January 1975) is a Tanzanian economist and CCM politician, who has served as the elected Member of Parliament for Iramba West Constituency since 2010. On 13 November 2025, President Samia Suluhu Hassan appointed him as the Prime Minister of Tanzania, succeeding Kassim Majaliwa. Before his current appointment, he served as the Minister of Finance in the Tanzanian Cabinet, since March 2021. More on Wikipedia
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
MR BEN
@Eric__Bernard
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Veriafya
@Veriafya
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Mei 4, 2026, amesema hadi sasa Tanzania haina Mgonjwa wa Ebola na Serikali imechukua hatua zote kujilinda, ikiwemo kutoa elimu sahihi kwa Wananchi.
Amesisitiza umuhimu wa kutoa taarifa kwa haraka pindi wananchi wanapohisi uwepo wa Viashiria vya Ugonjwa huoThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
𝐃𝐫.𝐙𝐚𝐜𝐤™🇹🇿
@_zack255
RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN ATOA SH. MILIONI 500 KWA SERENGETI BOYS, ATUMA NDEGE MAALUM KUWAREJESHA NCHINI
WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Serikali imetoa zawadi ya sh. milioni 500 kwa Timu ya Taifa ya Tanzania ya vijana chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) kwa kufanikiwa kutinga hatua ya fainali ya mashindano hayo na kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania kimataifa.
Dkt. Mwigulu amesema hayo leo (Ijumaa, Mei 29, 2026) ofisini kwake Mlimwa, Dodoma wakati akitoa salamu za pongezi kwa timu hiyo kufuzu hatua ya fainali kwa niaba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Amesema Rais Samia amewapongeza wachezaji, benchi la ufundi na viongozi wote wa timu kwa mafanikio hayo makubwa ambayo yameendelea kuandika historia mpya katika sekta ya michezo nchini.
“Mheshimiwa Rais amenielekeza nitoe pongezi hizi kwa vijana wetu wa Serengeti Boys kutokana na mafanikio makubwa ya kutinga fainali na kuiwakilisha vema Tanzania katika mashindano hayo,” amesema Dkt. Mwigulu.
Waziri Mkuu amesema Serikali itatuma ndege maalum kwa ajili ya kuwafuata vijana hao watakapomaliza mashindano hayo ili kurejea nchini pamoja na kombe endapo watafanikiwa kutwaa ubingwa. “Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa ndege kwa ajili ya kuwafuata vijana wetu watakapokuwa wamemaliza mashindano hayo na kurejea nao nyumbani,” amesema.
“Tunaamini huu ni mwanzo tu wa pongezi ambazo Mheshimiwa Rais ameanza kuzitoa. Tunaamini kwamba wakirejea na kombe hilo, kutakuwa na sababu zaidi ya kuwapongeza kwa mafanikio hayo makubwa.”
Waziri Mkuu amemwelekeza Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Paul Makonda na wadau wanaohusika, waendelee na uratibu wa wa safari kwa watu watakaokwenda kuwaunga mkono vijana wetu.
Katika hatua nyingine, Dkt. Mwigulu amesema endapo Serengeti Boys watatwaa ubingwa, Serikali itawapatia kila mchezaji kiwanja kimoja katika Mji wa Suluhu New City uliopo mkoani Morogoro ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wao katika kuitangaza Tanzania kupitia michezo.
Waziri Mkuu pia amewahamasisha Watanzania, taasisi, mashirika na wadau mbalimbali wa michezo kuendelea kutoa msaada na motisha kwa timu hiyo kuelekea mchezo wa fainali.
“Shime shime vijana wetu, inawezekana. Tuleteeni kikombe kile, mleteeni Dkt. Samia Suluhu Hassan kikombe, tuleteeni Watanzania ushindi huo. Kwa kiwango mlichokionesha, tunaamini mna uwezo wa kutwaa ubingwa huo,” amesema.
Sambamba na hilo, Waziri Mkuu amempongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwa kinara wa maendeleo ya michezo nchini na kuchochea mafanikio yanayoendelea kupatikana katika sekta hiyo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Thomas J. Kibwana
@thomasjkibwana
Tanzania inawakilishwa na Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, katika Mkutano wa 61 wa Mwaka wa Bodi ya Magavana wa African Development Bank unaofanyika mjini Brazzaville, Jamhuri ya Congo, kuanzia tarehe 25 hadi 29 Mei 2026 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Kintélé.
Mkutano huo unafanyika sambamba na Mkutano wa 52 wa Mwaka wa Bodi ya Magavana wa African Development Fund.
Maeneo makuu ya majadiliano katika mikutano hiyo ni pamoja na:
• Uhamasishaji wa rasilimali kwa ajili ya maendeleo ya Afrika
• Ufadhili wa miundombinu
• Fedha za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kukuza uchumi wa kijani
• Uendelezaji wa viwanda na biashara
• Mageuzi ya mifumo ya kifedha
• Mabadiliko ya vijana na demografia
• Uimara wa uchumi wa Afrika katika mazingira ya uchumi wa dunia uliogawanyika na wenye misukosuko
Mikutano hiyo inatarajiwa kutoa mwelekeo mpya wa namna Afrika itakavyoweza kujitegemea zaidi katika kugharamia maendeleo yake na kuimarisha ustahimilivu wa uchumi wa bara hilo. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
𝐃𝐫.𝐙𝐚𝐜𝐤™🇹🇿
@_zack255
WAZIRI MKUU ATETA NA RAIS WA BENKI YA AfDB
WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba amefanya mazungumzo na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Dkt. Sidi Ould Tah kando ya Mkutano wa 61 wa Mwaka wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Afrika unaofanyika leo Jumanne Mei 26, 2026 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Kintele (Kintele Congress Centre) jijini Brazzaville, Jamhuri ya Kongo.
Mazungumzo hayo yalijikita katika masuala mbalimbali ya maendeleo pamoja na ushirikiano wa kiuchumi kati ya Tanzania na taasisi hiyo.
Dkt. Mwigulu anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mkutano huo unaowakutanisha viongozi mbalimbali wa Afrika pamoja na wadau wa maendeleo kujadili masuala ya uchumi, uwekezaji na maendeleo ya bara la Afrika. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
MINISTRY OF WATER AND ENVIRONMENT 🇺🇬
@min_waterUg
#mweworks: The @min_waterUg Permanent Secretary; Dr. @okidi64 received the prestigious Regional Award from the Prime Minister of the United Republic of Tanzania; Dr. @mwigulunchemba1 in Nane Nane, Mwanza, Tanzania for pioneering Lake Victoria rescue.
@UgandaMediaCent -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Dodoma_Zone
@Dodoma_Zone_
TANZANIA YAPIGIWA MFANO MAGEUZI YA KISERA, USIMAMIZI WA KODI
✔️Ni katika mdahalo maalum kwenye Mkutano wa Mwaka wa AfDB
WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba ameshiriki mdahalo maalum wa uzinduzi wa taarifa ya African Economic Outlook 2026 ambapo ametoa taswira ya jinsi Tanzania ilivyofanikiwa kuimarisha usimamizi wa fedha za umma na mageuzi katika sekta ya fedha.
Akizungumza katika mdahalo huo jana jioni (Jumanne, Mei 26, 2026) katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Kintele (Kintele International Conference Centre), jijini Brazzaville, Jamhuri ya Kongo, Waziri Mkuu alisema Tanzania imeendelea kuchukua hatua za kuimarisha sekta binafsi na kuongeza vyanzo vya mapato ya ndani katika kuimarisha uhamasishaji wa rasilimali za ndani.
“Hatua hizo zinaenda sambamba na uamuzi wa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan wa kuunda tume ya kupitia mifumo ya kodi, usimamizi wa kodi, pamoja na viwango vya kodi, kwa lengo la kufanya mfumo wa ukusanyaji kuwa rafiki zaidi na kuongeza wigo wa mapato ya Serikali.”
Waziri Mkuu alikuwa akijibu swali la mwezeshaji wa mdahalo huo, Dkt. Joy Kategekwa ambaye pia ni Mkurugenzi wa Uratibu na Ushirikiano wa Kikanda wa Benki ya AfDB ambaye alimtaka Waziri Mkuu aeleze uzoefu wa Tanzania katika usimamizi wa fedha za umma na jinsi ambavyo imefanikiwa kufikia bajeti ya nchi inatumia asimilia 70 ya mapato ya ndani.
Akitoa ufafanuzi zaidi, Dkt. Mwigulu alisema Tanzania iliamua kuimarisha ukusanyaji wa mapato kwa kuiongezea ufanisi Mamlaka ya Mapato ikiwemo kuweka mifumo ya ukusanyaji kwa kutumia njia za kidijitali kama vile mashine za EFD na kufanya malipo kwa njia za mitandao ya simu.
“Mamlaka za Serikali za Mitaa ziliimarishwa kwa kuruhusiwa kukusanya mapato yasiyo ya kikodi na tukahakikisha kuwa kunakuwa na nidhamu ya matumizi ya fedha kwa kila senti inayokusanywa (prudency) na wananchi waliona fedha zao zinatumika katika miradi hiyo,” alisema na kuongeza:
“Tanzania ni miongoni mwa wanufaika wa ushirikiano na Benki ya Maendeleo ya Afrika na tumepata nafasi ya kushirikisha uzoefu wetu kuhusu utekelezaji wa miradi mbalimbali kwa kutumia vyanzo vya ndani vya fedha ikiwemo ujenzi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere, miradi ya huduma za jamii, u -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Dr. Deo Mwapinga
@dmwaps
Honoured to meet with the Prime Minister of the United Republic of Tanzania, @mwigulunchemba1 , in Brazzaville-Rep of Congo today for a constructive courtesy call and strategic engagement.
We discussed the continued role of regional parliamentary diplomacy and the importance of multi-sectoral collaboration in advancing peace, development, and women’s leadership across the Great Lakes Region.
I also had the opportunity to brief the Prime Minister on the upcoming @FPCIRGL Women’s Platform Conference scheduled for November 2026 in Tanzania, a strategic platform expected to convene Women parliamentarians, speakers, civil society, and regional stakeholders to strengthen cooperation and amplify Africa’s soft power and inclusive leadership agenda.
Grateful for the warm reception, encouragement, and continued support from the Government of Tanzania. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
mbelwa Kairuki
@MbelwaK
Modern wars don’t respect borders. African countries need Iran peace talks to succeed www.cnbcafrica.com/2026/modern-wars-dont-respect-borders-…
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Tanzania High Commission I United Kingdom
@UbaloziUK
Modern wars don’t respect borders. African countries need Iran peace talks to succeed www.cnbcafrica.com/2026/modern-wars-dont-respect-borders-…
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
The New Vision
@newvisionwire
Tanzanian Prime Minister Mwigulu Nchemba on Thursday called on East African Community (EAC) member states to strengthen cooperation in protecting and conserving Lake Victoria, saying it is a vital shared resource that supports the livelihoods and economies of millions of people in the region.
DETAILS👇🏽#visionupdates
www.newvision.co.ug/category/agriculture/tanzanian-pm-cal… -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Thomas J. Kibwana
@thomasjkibwana
@cnbcafrica imechapisha makala ambayo Waziri Mkuu Mwigulu Nchemba amezungumzia kuhusu usalama wa nishati katika muktadha wa Afrika, pamoja na juhudi za Tanzania katika kuhakikisha ustahimilivu wa nishati.
www.cnbcafrica.com/2026/modern-wars-dont-respect-borders-… -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Nishati
@Nishati2017
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba amesema kuwa utekelezaji wa Mradi wa Gridi Imara utakuwa suluhu ya upatikanaji wa umeme wa uhakika utakaokidhi ongezeko kubwa la matumizi ya umeme kufuatia upanuzi wa huduma hiyo vijijini, vitongojini,
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Dr. Akinwumi A. Adesina, CON, CGH
@akin_adesina
President @SuluhuSamia’s pro-investment stance and Aliko Dangote’s big drive for industrialization are exactly what Africa needs. Africa will develop faster through investment to unlock its vast sovereign assets. Tanzania is a great place for this. @AlikoDangote
Samia Suluhu
@SuluhuSamia
Ikulu, Dar es Salaam, 16 Mei, 2026.
Nimekutana na kufanya mazungumzo na Mwanzilishi na Mmiliki wa Dangote Group, Alhaji Aliko Dangote pamoja na ujumbe wake.
Alhaji Dangote ni mmoja wa wawekezaji wakubwa Tanzania ambapo kiwanda chake cha saruji (Dangote Cement) mkoani Mtwara kinakuza uchumi wetu kupitia biashara ya saruji, ajira kwa Watanzania na kukuza sekta fungamanishi. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Samia Suluhu
@SuluhuSamia
Ikulu, Dar es Salaam, 16 Mei, 2026.
Nimekutana na kufanya mazungumzo na Mwanzilishi na Mmiliki wa Dangote Group, Alhaji Aliko Dangote pamoja na ujumbe wake.
Alhaji Dangote ni mmoja wa wawekezaji wakubwa Tanzania ambapo kiwanda chake cha saruji (Dangote Cement) mkoani Mtwara kinakuza uchumi wetu kupitia biashara ya saruji, ajira kwa Watanzania na kukuza sekta fungamanishi. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
𝐃𝐫.𝐙𝐚𝐜𝐤™🇹🇿
@_zack255
MSIZUIE WANAFUNZI KUFANYA MITIHANI-DKT. MWIGULU
Asema Serikali itaendelea kuongeza fedha za mikopo ya elimu ya juu
WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba amezitaka taasisi za elimu nchini kutowazuia wanafunzi kufanya mitihani ya masomo yao kwa kushindwa kulipa ada.
Pia, Waziri Mkuu amesema Serikali itaendelea kuongeza fedha za mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu na vyuo vya kati ili wanafunzi wengi zaidi wanufaike na mikopo hiyo.
Mheshimiwa Dkt. Mwigulu ametoa maelekezo hayo leo (Alhamisi Mei 14, 2026) Bungeni jijini Dodoma katika kipindi cha Maswali kwa Waziri Mkuu wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Latifa Khamis Juwakali aliyetaka kujua mkakati wa Serikali kiuhusu wanafunzi wanaozuiwa kufanya mitihani kwa kutokulipa ada. #tumeyajajichande
#tumeyauchunguzireport
Umoja Na Amani -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Alvaro Lario
@IFADPresident
At the #africaforward Summit in Nairobi, I held productive bilateral discussions with African leaders on strengthening partnerships with @IFAD and advancing investment in rural economies through #ifad14.
In the bilateral with His Majesty King Letsie III of Lesotho, we discussed the country’s priorities around nutrition, resilience and private-sector-led rural transformation. IFAD’s partnership with Lesotho continues to expand through investments in horticulture, financial inclusion and rural entrepreneurship, while mobilizing strong co-financing support from partners including @WorldBankGroup, @TheOPECFund and the @theGEF.
My meeting with President @duma_boko of #botswana focused on the catalytic effect of collaborating with national development banks and the private sector, including commercial banks and local SMEs, aligned with national priorities. With our investment in Bank Gaborone for example we are complementing our sovereign investments by crowding in private capital to enhancing finance for rural entrepreneurs and farmers toward sustainable food systems. We further discussed the impact of recent floods and the importance of climate smart farming and resilient infrastructure.
With President @julius_maadabio of #sierraleone, discussions centred on food security, resilience and strengthening integrated, climate-resilient food systems. Through major programmes supporting livestock, agricultural value chains and rural finance, IFAD’s partnership in Sierra Leone now spans 10 projects with total financing of US$473 million, demonstrating the scale of long-term investment and co-financing being mobilized around rural transformation.
I also met with Prime Minister @mwigulunchemba1 of #tanzania to discuss strengthening cooperation with IFAD and advancing investment in youth employment, climate-smart agriculture and rural economic opportunity. Tanzania is now one of IFAD’s largest portfolios in Africa, with more than US$3.3 billion in total financing mobilized since 1978, including new efforts to structure blended investment around the BBT-Coffee Programme and Tanzania’s wider rural transformation agenda.
Across all discussions, there was strong recognition that investing in the first mile is critical not only for food security, but for economic resilience, stability and long-term growth across the continent.
#financingthefirstmile #ifadimpact -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Maelezo News
@maelezonews
WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba ametoa wito kwa wadau wa maendeleo kuoanisha malengo yao na Bara la Afrika ili kuchochea maendeleo endelevu.
Amesema hayo aliposhiriki katika mjadala kuhusu maendeleo ya sekta ya kilimo wakati wa Ushirikiano kati ya Afrika na Ufaransa uliofanyika Mei 11 hadi 12, 2026 jijini Nairobi, Kenya.
“Tumekaa muda mrefu tukizungumzia kujenga uwezo badala ya kujenga miundombinu itakayowezesha bara letu na nchi zetu kuendesha ajenda zao ipasavyo,” amesema.
Aidha, Waziri Mkuu alisisitiza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano katika uhamishaji wa teknolojia na matumizi ya mifumo ya kisasa ya kilimo.
“Tunatarajia ushirikiano katika uhamishaji wa teknolojia ikiwa ni pamoja na uendelezaji wa matumizi ya zana za kisasa za kilimo, utekelezaji wa huduma za ugani na mifumo ya kidijitali. Si muda sasa wa kusafirisha malighafi nje ya nchi, tunataka mwelekeo wetu uwe kwenye kuongeza thamani,” amesema.
Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba alimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika Mkutano wa Ushirikiano kati ya Afrika na Ufaransa uliofanyika Mei 11 hadi 12, 2026 jijini Nairobi, Kenya.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Dodoma_Zone
@Dodoma_Zone_
WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba akisalimiana na Rais wa Kenya Dkt. William Ruto wakati wa hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa Ushirikiano kati ya Afrika na Ufaransa (Africa Forward Summit: Africa-France Perternship for Innovation and Growth) unaofanyika jijini Nairobi Kenya, leo Mei 12, 2026.Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu amemuwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mkutano huo
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
URT Updates
@urtupdates
🇹🇿 Prime Minister Dr. @mwigulunchemba1 joined President H.E. @EmmanuelMacron, President H.E. @WilliamsRuto, and First Lady @MamaRachelRuto at a State Dinner held for Heads of State and Government attending the Africa Forward Summit in 🇰🇪, focused on strengthening Africa–France.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
The Rapid Response Africa
@Africans24
JUST IN: Tanzania’s Prime Minister Dr. Mwigulu Nchemba has met IFAD President Alvaro Lario at the ongoing Africa Forward Summit in Nairobi as Tanzania accelerates its agricultural transformation agenda.
Tanzania is set to implement a 1.1 Trillion agriculture budget for FY2026/27 aimed at raising the sector’s contribution to GDP to 36.3% by 2030, alongside plans to commercialize and fully equip 2.4 million acres with irrigation infrastructures. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Haki Ngowi
@Hakingowi
📍Kenya
▪️WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU AKUTANA NA RAIS WA IFAD, NAIROBI
▪️Wajadili Kilimo himilivu na uendelezaji wa Kilimo Biashara
WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Mei 11, 2026 amekutana na Rais wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo ya Kilimo (IFAD), Alvaro Lario, jijini Nairobi, Kenya, ambapo wamejadili maeneo mbalimbali ya ushirikiano katika sekta ya kilimo na uwezeshaji wa wananchi kiuchumi.
Katika mazungumzo hayo, Dkt. Mwigulu amesema Tanzania itaendelea kushirikiana na IFAD katika maeneo mbalimbali ikiwemo kilimo himilivu cha tabianchi, maendeleo ya kilimo biashara, mapinduzi ya kidijitali katika sekta ya kilimo pamoja na uwezeshaji wa vijana na wanawake kiuchumi.
Aidha, Waziri Mkuu amesema Tanzania inatarajia kuendelea kushirikiana na IFAD katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ya kilimo ikiwemo mpango wa kuongeza uzalishaji wa alizeti ili kusaidia kuongeza upatikanaji wa mafuta ya kula nchini.
“Kimekuwa ni kikao kizuri kwa sababu tumekuwa na ushirikiano nao kwa muda mrefu, ambapo katika kipindi kilichopita tumeshirikiana nao katika miradi mbalimbali, na hasa miradi katika sekta za uzalishaji”.
“Lakini pia tumedhamiria kuendelea kushirikiana katika kuendeleza mazao ya mchanganyiko ambayo katika miaka ya nyuma ilikuwa inachukuliwa kuwa ni mazao ya chakula peke yake, kwasasa mazao haya niya biashara na tunayafanya sehemu ya kukuza biashara ambayo Tanzania inafanya na nchi nyingine”
Ameongeza kuwa Tanzania inatarajia kuendelea kushirikiana na IFAD katika sekta ya mifugo na mazao ya baharini kwa upande wa Zanzibar.
“Sambamba na hayo, tunategemea kushirikiana nao katika utekelezaji wa kilimo endelevu ambacho kinasaidia kampeni yetu ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi nchi”. Amesisitiza Dkt. Mwigulu
Kwa upande wa Rais wa IFAD Alvaro Lario, amesema kuwa wataendelea kuhakikisha mipango na utekelezaji wa IFAD vinaendana na malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo ya Tanzania 2050
“Kwasasa tunasubiri kusikia vipaumbele ya Tanzania ili tujue namna gani tunaweza kusaidia katika maeneo vya utoshelevu na usalama wa chakula pamoja na uongezaji thamani wa mazao” -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
The Rapid Response Africa
@Africans24
JUST IN: Tanzania is set to participate in the Africa Forward Summit in Nairobi, an event expected to be attended by Emmanuel Macron.
The Tanzanian delegation will be led by Dr. Mwigulu Nchemba, Prime Minister of Tanzania, an economist with a PhD in Economics and a former Finance and Planning Minister.
The summit follows the 15 May 2024 meeting between President Samia Suluhu Hassan and President Macron, where both leaders signed a clean and safe energy cooperation pact aimed at advancing Africa’s energy transition by 2030 — an agenda Tanzania is expected to further champion at the summit in Nairobi. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
The Rapid Response Africa
@Africans24
UPDATE: As AFCON 2027 approaches, Tanzania is preparing a major hospitality investment push, with plans to introduce nearly 30 tax incentives targeting hotel development/Investment.
The country already offers strategic investors reduced import duties of 0–5% alongside tailor-made tax arrangements under its Strategic Investment framework.
Yesterday, Prime Minister Dr. Mwigulu Nchemba inaugurated the $13 million Mikumi Wildlife Lodge a luxury facility positioned inside Mikumi National Park, one of Africa’s most scenic safari destinations, featuring licensed airstrip access and premium 5-star hospitality standards. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Royaltourtv
@royaltourtzinfo
PM Dr. Mwigulu Nchemba launched the new Mikumi Wildlife Lodge TODAY inside the park.
His message: "This is world-class. Private investors, we're ready for you."
The $13M+ upgrade includes new airports, roads, and 5-star lodges ahead of AFCON 2027.
#breakingnews #afcon2027 -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Haki Ngowi
@Hakingowi
📍IKULU, Chamwino
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri Mkuu Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, Spika wa Bunge Mhe. Mussa Azzan Zungu, Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi Dkt. Moses Kusiluka, Kamishna wa Maadili Mhe. Jaji Sivangilwa Mwangesi katika picha na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi Ajira na Mahusiano) Dkt. Evaline Wilbard Munisi, Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma tarehe 06 Mei, 2026. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Haki Ngowi
@Hakingowi
📍Bungeni, Dodoma
Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba akifurahia jambo na mwanafunzi wa darasa la 6 Jenipher Mwita Chaha, wa Chemchemi Nursery and Primary School iliyopo Nkuhungu Dodoma, katika viwanja via Bunge, jijini Dodoma, Mei 6, 2026. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
The Chanzo
@TheChanzo
Waziri Mkuu Mwigulu Nchemba: Kama Mlipokea Tofali kwa Nini Hamjawalipa Wananchi?
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Umekuwa wakati wenye tija na manufaa makubwa kwa nchi zetu mbili wakati wa ziara yako nchini, Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Kenya, Dkt. William Samoei Ruto.
Hotuba zenu Ikulu, Dar es Salaam, yako pamoja na ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mei 4, 2026, pamoja na mazungumzo yaliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), zimeonesha dhamira ya dhati ya kuimarisha ushirikiano wa kihistoria kati ya Tanzania na Kenya, sambamba na kuendeleza maono ya waasisi wetu, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Hayati Mzee Jomo Kenyatta.
Aidha, hotuba yako mbele ya Bunge imeakisi kwa dhahiri msimamo wa uongozi unaoamini katika mshikamano wa bara la Afrika na umuhimu wa ushirikiano wa kikanda kama nguzo ya kujenga uchumi imara na kujitegemea.
Kama ilivyoelezwa na Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaendelea kuthamini na kuunga mkono juhudi hizi kwa lengo la kuimarisha uhusiano wa kindugu na kukuza ustawi wa wananchi wa nchi zetu mbili pamoja na ukanda mzima wa Afrika Mashariki.
Karibu sana, na karibu tena Tanzania, Mheshimiwa Rais Dkt. William Samoei Ruto. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
EastAfricaTV
@eastafricatv
#video Akizungumza na wananchi katika eneo la Idofi, Makambako mkoani Njombe leo Mei 2, 2026, Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba amesema: “Hiyo barua waliyomuandikia kama mnayo hapo ichaneni hapa nikiwa naiona.” Kauli hiyo ilitolewa baada ya kupokea kero moja kwa moja kutoka kwa mwananchi mmoja aliyekutana naye wakati wa mazungumzo ya hadhara.
Katika maongezi hayo pia, waziri mkuu ameonya juu ya migogoro ya ardhi inayosababishwa na watumishi wa serikali huku akiagiza wanaohusika wachukuliwe hatua.
#eastafricatvThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
𝐃𝐫.𝐙𝐚𝐜𝐤™🇹🇿
@_zack255
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiteta jambo na Waziri Mkuu Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi 2026), ambayo Kitaifa yamefanyika Mkoani Njombe, tarehe 01 Mei, 2026.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Haki Ngowi
@Hakingowi
📍Dodoma
Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba akizungumza na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mussa Zungu walipokutana katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, wakielekea Dodoma, leo tarehe 30 Aprili, 2026. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
The Rapid Response Africa
@Africans24
Yesterday, The Prime Minister of the United Republic of Tanzania, Hon. Mwigulu Nchemba, met with the Minister for Foreign Affairs of the Republic of Belarus, Hon. Maxim Ryzhenkov, for discussions aimed at strengthening economic and diplomatic ties between Tanzania and Belarus. The meeting took place at the Prime Minister’s Office (Magogoni) in Dar es Salaam.
Both parties explored opportunities for cooperation in agriculture, fisheries, education, health, and the pharmaceutical industry, focusing on increasing investment, promoting knowledge and technology transfer, and adding value to boost economic growth. During the meeting, Hon. Ryzhenkov was accompanied by the Minister for Foreign Affairs and East African Cooperation, Amb. Mahmoud Thabit Kombo (MP).
Hon. Ryzhenkov is in Tanzania on an official working visit until April 30, 2026, as part of efforts to further strengthen strategic cooperation between Tanzania and Belarus. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Swahili Times
@swahilitimes
Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, amezitaka mamlaka husika kuachia vyombo vya moto vya biashara vilivyokamatwa kwa makosa madogo yanayohusiana na faini.
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Embassy of Belarus in Kenya
@EmbKenya
#belarus FM Maksim Ryzhenkov met with #tanzania’s PM Mwigulu Nchemba today.High-level political ties to boost trade & econ cooperation in agriculture, industry, pharma, education. Letter from President Lukashenko invites Tanzanian President to Belarus. Mutual visits ahead!
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Belarus MFA 🇧🇾
@BelarusMFA
🇧🇾🇹🇿 Deepening the #belarus-#tanzania partnership.
FM Maxim Ryzhenkov met with PM @mwigulunchemba1. On today's meeting agenda: turning strong political ties into economic results 🤝✨The Belarusian FM also delivered a message from President Aleksandr Lukashenko to President @SuluhuSamia, including an invitation to visit #belarus -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Haki Ngowi
@Hakingowi
📍Dar es Salaam
Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba amefanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali Madini, Mafuta na Gesi Asilia (TEITI) Balozi Wilson Kajumula Ofisi ndogo ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es Salaam, Aprili 27, 2026 -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Hujambo ndugu, nimepokea swali lako. Tafadhali nipatie mawasiliano yako ili niweze kupata ufafanuzi zaidi na kulifuatilia ipasavyo.
Hancy Machemba
@hancymachemba
Mh waziri mkuu @mwigulunchemba1 mchumi na msomi hasa. Naomba kujua kwann serikali inapambana sana kuinua wananchi wake na wakati huo huo Kuna baadhi ya taasisi za serikali zinauwa uchumi wa watu hao hao?
Unakuta supplier anadai tasisi kwa miaka pengine mtaji kakopa bank. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ben Mwanantala Mzalendo
@ben_mwanantala
"MWIGULU-WATU WANASEMA NASHUGHULIKA NA VITU VIDOGOVIDOGO."
Waziri Mkuu amewahakikishia watanzania kwamba hakuna mwananchi ambaye hatasikilizwa Kero yake.
Kwakua kila mwananchi ana haki ya kusikilizwa.
@mwigulunchemba
@gersonmsigwa
@jokatemwegelo
@owm_tz
@ikulu_mawasiliano -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Dodoma_Zone
@Dodoma_Zone_
Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba akiteta na Elina Mwandu (mwenye Mahitaji Maalum) baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara na kusikiliza kero za wananchi katika uwanja wa Shule ya Msingi Msanga wilayani Chamwino Dodoma, Aprili 19, 2026.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Nipashe Tanzania
@Nipashetz
Waziri Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba jana Aprili 20, 2026 amemkabidhi kitimwendo Helena Joseph Mwandu (mwenye mahitaji maalum), Ofisini kwa Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma.
Waziri Mkuu aliahidi kumpatia Helena kiti hicho katika mazungumzo waliyoyafanya baada ya mkutano wa hadhara aliouhutubia kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Msanga wilayani Chamwino Dodoma, Aprili 19, 2026.
Akizungumza baada ya kupatiwa kiti hicho, Helena alimshukuru Waziri Mkuu Dk. Mwigulu kwa kumpatia kitimwendo hicho kwani kitamsaidia katika shughuli zake.
Imeandikwa| Mwandishi Wetu
Tembelea epaper.ippmedia.com kusoma Habari hii ndani ya gazeti lako au wasiliana nasi 📞+255 745 -700 710 au 0677- 020 701 kwa maelezo zaidi.
#nipashedigital #nipashemwangawajamii #miaka30yakupashahabariThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Haki Ngowi
@Hakingowi
📍Dodoma
▪️WAZIRI MKUU ATIMIZA AHADI YA KUMPATIA KITIMWENDO HELENA JOSEPH
Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba leo (Aprili 20, 2026) amemkabidhi kitimwendo Helena Joseph Mwandu (mwenye mahitaji maalum), Ofisini kwa Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma.
Waziri Mkuu aliahidi kumpatia Helena kiti hicho katika mazungumzo waliyoyafanya baada ya mkutano wa hadhara aliouhutubia kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Msanga wilayani Chamwino Dodoma, jana (Aprili 19, 2026).
Akizungumza baada ya kupatiwa kiti hicho, Helena amemshukuru Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu kwa kumpatia kitimwendo hicho kwani kitamsaidia katika shughuli zake. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Bunge la Tanzania
@bunge_tz
Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba amewaongoza waombolezaji katika kuaga mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) Marehemu William Vangimembe Lukuvi leo Machi 27, 2026 katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ofisi ya Waziri Mkuu
@TZWaziriMkuu
WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba ameagiza mamlaka zinazohusika kuchukua hatua kali dhidi ya muuguzi mmoja mkoani Tabora anayedaiwa kufanya upasuaji wa mgonjwa nyumbani kwake kinyume na maadili ya taaluma ya afya.
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ofisi ya Waziri Mkuu
@TZWaziriMkuu
Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba amemuagiza Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Geita kufanya uchunguzi kuhusu madai ya ubadhirifu wa fedha katika mradi wa ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) Nyang’wale.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Haki Ngowi
@Hakingowi
📍 Tanga
▪️WAZIRI MKUU AMALIZA ZIARA TANGA, AAGIZA FAGIO LIPITE MUHEZA
▪️Ahimiza Wakuu wa Wilaya wakasikilize wananchi na kutatua kero zao
WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba amemwagiza Waziri wa Nchi (OWM – TAMISEMI), Prof. Riziki Shemdoe arudi Halmashauri ya Muheza na kusafisha watumishi wote waliohusika na ubadhirifu wa fedha za mradi wa jengo la ofisi.
Ametoa agizo hilo jana (Jumanne, Februari 17, 2026) wakati akizungumza na viongozi na watumishi wa Mkoa wa Tanga katika kikao cha majumuisho ya ziara yake ya siku tano mkoani humo yaliyofanyika kwenye Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA).
“Muheza ndiyo wilaya iliyonidisappoint sana kwa sababu huku kwingine nimekuta upungufu bali kule Muheza ni uharibifu. Mheshimiwa Waziri kesho rudi Muheza, nenda kachukue hatua. Shirikiana na Waziri wa Utumishi, mchukue hatua,” alisisitiza.
Dkt. Mwigulu amesema kuna baadhi ya vifaa vilinunuliwa lakini havikufika site (eneo la mradi). “Nondo zenye thamani ya shilingi milioni 9.2 zililipwa kwa mzabuni Saifi Store wa Tanga lakini hazikufikishwa site, maana yake zimechepushwa.”
“Kuna marine boards vipande 192 vyenye thamani ya shilingi milioni 7.8 havikufika site. Wanaohusika ni Mhasibu, Rajab Mushi na Mhandisi Abdalla Jaha na Afisa anayehusika kupokea vifaa.”
Alisema mbali ya hivyo, kuna malipo mengine ya sh. milioni 4.4 yalifanywa ili kulipia mifuko 3,800 ya saruji lakini mifuko 300 haikufika kwenye eneo la ujenzi. “Afisa manunuzi na Afisa utumishi ambaye alikuwa ni mwenyekiti wa kamati ya mapokezi ya vifaa vya mradi watafutwe hawa pamoja na Mkurugenzi wa Mwanambonde General Enterprises.”
Waziri Mkuu alisema kuna ukiukwaji wa taratibu za serikali ambao ulifanyika ikiwemo kumlipa mshauri mwelekezi bila ya kuwa na mkataba wowote. “Kuna huyu AG Engineering amelipwa shilingi milioni 98.7 bila kuwa na mkataba. Huyu kalipwa za nini? Kuna mshauri mwelekezi kalipwa shilingi milioni 11.9 bila mkataba.”
“Kibaya zaidi, shilingi milioni 343 zimetumika nje ya mradi kwa kulipana posho. Mheshimiwa Waziri nenda kasafishe wote pale. Safisha wote pale hii wilaya ianze upya. Ongea na Waziri wa Utumishi kila mmoja apate adhabu anayostahili,” alisisitiza.
Kwa ujumla, Waziri Mkuu aliwataka viongozi wa mkoa huo wakamilishe hoja za sekta mbalimbali zilizoibuliwa na wananchi kwenye wilaya na Halmashauri zote alizopita. “Wakuu wa Wilaya wafanye ziara katika kata na kusikiliza kero za wananchi. Wao wanataka kusikia majibu ya serikali. Wanataka jambo lao litatuliwe na serikali.”
Mapema, Mkuu wa Mkoa Tanga, Dkt. Batilda Burian alimshukuru Waziri Mkuu kwa kufanya ziara kwenye wilaya zote saba za mkoa huo, Halmashauri 11 na majimbo 12 ambako alikagua na kuzindua miradi yenye thamani ya sh. bilioni 751.
“Ziara yako ni darasa ambalo limetupa namna mpya ya kuwatumikia wananchi. Sisi tunabaki na kauli yako kwamba tusizoee matatizo ya wananchi, tutaifanyia kazi kwa kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi,” alisema. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
millardayo
@millardayo
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mwigulu Nchemba amemuagiza Mkurugenzi wa Wilaya ya Same pamoja na Watumishi wa Halmashauri hiyo wamlipe papohapo Fundi ujenzi kiasi cha shilingi 2,850,000 ambazo hajalipwa tangu mwaka 2022 alipojenga matundu ya choo cha Shule ya Sekondari ya Gonja.
Dk. Nchemba ametoa Uamuzi huo hii leo Februari 18, 2026 wakati akisikiliza kero za Wananchi wa Ndungu, Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro ambapo Fundi huyo aliwasilisha kero hiyo na kisha Waziri Mkuu kutoa agizo “ninataka huyu Mwananchi alipwe hapahapa, sasa hapo mlipo nataka kila Mtu atoe hela yake mfukoni mchange mumlipe”
#millardayoupdatesThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Dodoma_Zone
@Dodoma_Zone_
Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba alivyoshuka jukwaani kumsikiliza Mlemavu wa Miguu ndugu shabani Sabuni.
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Hongera Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uongozi thabiti unaoimarisha ulipaji wa kodi kwa haki na usawa. TRA imeandika historia kwa kukusanya TZS Trilioni 4.13 mwezi Desemba 2025. Pongezi kwa TRA kwa weledi na uwajibikaji kwa maslahi ya Taifa.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ofisi ya Waziri Mkuu
@TZWaziriMkuu
Heri ya Mwaka Mpya 2026.
-
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Tunauanza mwaka mpya kwa imani na matumaini, tukijua Mungu anafanya jambo jipya kwa kila mmoja wetu (Isaya 43:19).
Heri ya Mwaka Mpya wenye baraka. -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Asanteni wananchi wa Mikoa ya Songwe na Mbeya. Amani yetu ndiyo maendeleo yetu, tuilinde kwa maslahi ya Taifa.
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Kesho wananchi wote wa Singida tunawatumia salamu wasiolitakia mema Taifa letu, tutapiga kura za kishindo kwa Dkt Samia na wagombea wote wa CCM.
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Kesho mapema tunatiki ✅ kwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Wabunge na Madiwani wa CCM — kwa ajili ya Maendeleo Endelevu, Amani na Mshikamano.
Kwa kuelekea ushindi wa kishindo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM). Tunasema: Kazi Iendelee, Utu Udumishwe. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Swahili Times
@swahilitimes
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Iramba Magharibi, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema serikali ya Rais Samia Suluhu imetengeneza fursa nyingi za ajira kwa vijana kuliko awamu zote.
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Mgombea wa nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Iramba Magharibi Mkoani Singida kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, amesema katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Serikali ya Awamu ya Sita imeweka rekodi ya kuajiri vijana wengi zaidi na kutengeneza fursa nyingi za ajira kwa Watanzania katika sekta mbalimbali kuliko kipindi chochote kilichopita.
Akizungumza leo Jumapili Oktoba 19, 2025, katika Mkutano wa Kampeni za Mgombea wa Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Samia Suluhu Hassan uliofanyika Viwanja vya Kizwite, Sumbawanga Mjini mkoani Rukwa, Dkt. Mwigulu amesema hatua hiyo inaonesha dhamira ya Rais Samia katika kujenga uchumi jumuishi unaowanufaisha wananchi wa makundi yote.
Amesema Dkt. Samia ni kiongozi mwenye upendo, anayeguswa na matatizo ya wananchi wake na anayechukua hatua za vitendo katika kuyatatua. Ametolea mfano namna alivyosikia malalamiko kuhusu tozo, kodi nyingi na ukosefu wa urasimu rafiki kati ya wafanyabiashara na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), na kuchukua hatua ya kuondoa zaidi ya kodi na tozo 250 zilizokuwa kero kwa wananchi.
Aidha, Dkt. Mwigulu amesema Rais Samia alihakikisha madeni makubwa yaliyokuwa yakidaiwa na Serikali yanalipwa, hatua iliyopunguza mzigo kwa wananchi na kuongeza ufanisi wa taasisi za umma, huku akiboresha huduma za afya kwa kujenga hospitali na kununua vifaa tiba vya kisasa ikiwemo mashine za CT-Scan katika hospitali mbalimbali nchini.
Ameongeza kuwa mafanikio hayo yameendelea kutambuliwa kimataifa na taasisi kubwa kama Benki ya Dunia, ambazo zimeitaja Tanzania kuwa miongoni mwa nchi kinara katika sekta za maji, elimu na afya kwa kutimiza malengo ya maendeleo endelevu (SDGs).
Dkt. Mwigulu amewataka Watanzania kuendelea kumuamini Dkt. Samia, akisema wanaoikosoa Serikali ya Awamu ya Sita hawana nia njema, bali wanataka kudhoofisha maendeleo yanayowanufaisha wananchi wengi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Habari Muhimu
@HabariMuhimu
Dkt. Mwigulu: Wapuuzeni waozusha tunachaposha hela
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Swahili Times
@swahilitimes
Mgombea Ubunge Jimbo la Iramba, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema hakuna nchi yenye mtambo wa kuchapisha fedha zake, hivyo wanaosema nchi inachapisha fedha kwa ajili ya uchaguzi wanapotosha.
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
ROYAL TELEVISION PLUS
@Royaltv_plus
Mgombea wa nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Iramba Magharibi Mkoani Singida kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba amesema katika Miaka minne ya Uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, serikali yake ya awamu ya sita imeweka rekodi ya kuajiri Vijana wengi zaidi na kutengeneza fursa za ajira kwa Watanzania wengi zaidi katika sekta mbalimbali kupita wakati mwingine wowote.
Mwigulu ametaja takwimu hizo leo Jumapili Oktoba 19, 2025 wakati wa Mkutano wa kampeni za Mgombea wa nafasi ya Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Dkt. Samia Suluhu Hassan, Sumbawanga Mjini kwenye Viwanja vya Kizwite Mkoani Rukwa, akimtaja Dkt. Samia kama kinara pia wa utekelezaji wa miradi mingi ya maendeleo na mwenye upendo mkubwa kwa watu wake.
Amemtaja Dkt. Samia pia kama kiongozi mwenye kuguswa na kuyatafutia suluhu matatizo ya wananchi wake, akieleza namna ambavyo pia alisikia na kuondoa misururu ya kodi, ubambikizaji wa tozo na kodi pamoja na mahusiano mabaya ya mamlaka ya mapato TRA katika ukadiriaji wa kodi kwa wafanyabiashara.
"Mhe. Mgombea mara baada ya kupata manung'uniko hayo kodi na tozo zaidi ya 250 alizifuta ili kuwapa nafuu watanzania. Alikuta pia madeni mengi serikali ikidaiwa, nayo alilipa yote ili kuwapa nafuu Watanzania, Amejenga hospitali, amenunua mashine za CT- Scan na mambo mengine mengi kila kona ya Tanzania." Amesema Mwigulu.
Dkt. Mwigulu Nchemba pia amesema mambo hayo aliyoyafanya Dkt. Samia kwa kipindi kifupi yametambulika pia kimataifa kwa Taasisi zote kubwa zinazopima maendeleo bora ya kiuchumi na ustawi wa jamii, akisema chini ya Dkt. Samia Tanzania imetajwa na Benki ya dunia mara kadhaa kama kinara katika sekta za maji, elimu na afya kwa kutimiza malengo ya milenia, akiwasihi watanzania kuwakataa wale wote wanaomshambulia Dkt. Samia kwani dhamira ya watu hao ni kudhohofisha maendeleo ya wananchi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
I have received with deep sorrow the news of the passing of our icon, Raila Amollo Odinga.
May the Almighty God grant him eternal rest and peace, and may He comfort his family and loved ones during this difficult time. Amen. 🕊️ -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Asante sana Mheshimiwa Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, Mgombea Mwenza wa Urais wa Chama chetu, na karibu tena Iramba!
October tunatiki kwa kishindo na kuvunja rekodi.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Haki Ngowi
@Hakingowi
📍 Iramba
▪️IRAMBA OKTOBA 29 TUNATIKI SAMIA ✅️
📸 MATUKIO mbalimbali katika mkutano wa hadhara wa Kampeni wa Mgombea Mwenza, Dk. Emmanuel Nchimbi, uliofanyika Kijiji cha Ishenga, Jimbo la Iramba Mashariki, mkoani Singida, tarehe 14 Oktoba, 2025.
#oktoba29tunatikisamia -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Miaka 26 ya Kumbukizi ya Kifo cha Baba wa Taifa.
🕊️🇹🇿
Naungana nanyi wote kukumbuka na kutafakari maisha na mafunzo ya mpendwa wetu, Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Kwangu, ataendelea kuwa Mwalimu wa vizazi vyote, mwanga usiozimika. -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
KARIBU SANA MKOANI SINGIDA
Mheshimiwa Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, Mgombea Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM). -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Haki Ngowi
@Hakingowi
📍 Iramba, Singida
▪️DKT. MWIGULU NCHEMBA AUNGA MKONO UNUNUZI WA JEZI HALISI (ORIGINAL)
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba ameunga mkono kampeni ya kununua jezi halisi (original) za timu ya Simba SC, akitoa rai kwa wapenda soka wote kuepuka jezi bandia (feki).
Amesema jezi feki zinaikosesha timu mapato muhimu kwa ajili ya usajili wa wachezaji bora, na pia zinaikosesha serikali mapato ya kodi.
Ameyasema hayo nyumbani kwake Misigiri Iramba Mkoani Singida, alipotembelewa na ugeni wa timu ya mauzo ya simba ukiongozwa na Msemaji wa Timu hiyo Ahmed Ally. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Simba Sports Club
@SimbaSCTanzania
Waziri wa Fedha na mdau wa michezo nchini, Dkt. Mwigulu Nchemba akielezea madhara ya mashabiki kununua jezi feki kwa klabu na kwa serikali. #nguvumoja
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Simba Sports Club
@SimbaSCTanzania
Licha ya kununua jezi hizo lakini pia Dkt. Nchemba amewataka mashabiki kununua bidhaa za klabu kwani kwa kufanya hivyo wanasaidia kuinua uwezo wa kifedha wa klabu jambo ambalo linaisaidia taasisi kujiendesha kikamilifu. #nguvumoja
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Simba Sports Club
@SimbaSCTanzania
Waziri wa Fedha na Mipango na mdau wa michezo nchini, Dkt. Mwigulu Nchemba ameunga mkono kampeni ya kuhamasisha mashabiki kukataa jezi feki na kununua orijino kwa kununua jezi 200. #nguvumoja
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Haki Ngowi
@Hakingowi
📍 Ikungi, Singida
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Dkt. Tulia Ackson, akiwasili katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Sepuka, Kata ya Sepuka, Ikungi mkoani Singida leo tarehe 17 Septemba, 2025.
Dkt. Tulia anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi katika uzinduzi wa kampeni za Ubunge katika Jimbo la Ikungi Magharibi kupitia CCM ambapo chama hicho kimemteua Ndg. Elibariki Immanuel Kingu kuwania nafasi hiyo. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Safari ya CCM
@SafariyaCcm
SEKTA YA MADINI IRAMBA TUMETEKELEZA
@ccm_tanzania
#safariyaccm
#safariyaushindi
#octobatunatiki
#kazinaututunasongambele -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Samia Did
@Samia_Did
Serikali kuendelea kujenga barabara kwa kiwango cha lami Iramba zinazokwenda kukuza uchumi.
#oktobatunatikisamia -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Jansen 97
@Jansen_2019
WANA IRAMBA-SINGIDA MPENI DKT SAMIA SULUHU HASSAN AKATIMIZE AHADI HIZI ZA IRANI YA CCM 2025-2030 KWA VITENDO.
Chagua CCM ✅️
Chagua Dkt Samia Suluhu Hassan✅️ #kazinautu
#tunasongambele -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Chama Cha Mapinduzi
@ccm_tanzania
✅ 𝗜𝗥𝗔𝗠𝗕𝗔 𝗧𝗨𝗡𝗔𝗠𝗧𝗔𝗞𝗔 𝗦𝗔𝗠𝗜𝗔, 𝗜𝗪𝗘 𝗠𝗩𝗨𝗔 𝗜𝗪𝗘 𝗝𝗨𝗔, 𝗧𝗨𝗡𝗔𝗠𝗩𝗨𝗦𝗛𝗔 𝗢𝗞𝗧𝗢𝗕𝗔 29
Mgombea wa Nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi wa Iramba katika muendelezo wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu kwa Chama hicho mkoani Singida tarehe 10 Septemba, 2025.
#kazinautu
#chaguasamia
#chaguaccm -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Swahili Times
@swahilitimes
"Tangu uingie uongozi wako [Rais Samia Suluhu], fedha zimekwenda mikoani kwa wingi ambao haujawahi kutokea tangu nchi hii ipate uhuru. Hicho ni kipimo kwamba nchi inaongozwa na kiongozi mwadilifu ambaye anatumia vyema rasilimali za taifa hili." - Dkt. Mwigulu Nchemba, Mgombea Ubunge Jimbo la Iramba Magharibi mkoani Singida
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
JamalKita255
@JamalKita255
NONDO ZA MWIGULU NCHEMBA KWENYE KAMPENI IRAMBA, SINGIDA
Wananchi wamesema Oktoba watajitokeza Kumpigia kura Dkt. Samia Suluhu Hassan kwasababu ametekeleza ahadi za Ilani ya CCM
#dirayasamia #kazinautu2025 #samiahadi2030This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
𝐃𝐫.𝐙𝐚𝐜𝐤™🇹🇿
@_zack255
Iramba Mmetisha.
OKTOBA TUNATIKI ✅️ -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
IRAMBA KUMECHANGAMKA.
-
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Mama ametusikiliza na sisi kazi yetu ni kutiki October 29.
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
cousin 420
@420Cousin
Asanteni sana Iramba.
Uelekeo ni Igunga now Kilometa 137 za kwenda kuinadi Ilani Igunga.
Kwaherini Singida. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
SemeniTena
@SemeniTena
Utekelezaji wa miradi ya maji kuendelea ili wananchi wote waweze kupata huduma ya maji safi na salama Iramba.
#oktobatunatikisamia -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Dira Ya Samia
@DiraYaSamia
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Dkt. @SuluhuSamia, leo tarehe 10 Septemba 2025 ameendelea na mikutano ya kampeni mkoani Singida, katika Jimbo la Iramba.
Akiwahutubia wananchi, ameeleza kuwa CCM ina mipango mikubwa ya kuchochea maendeleo ya Taifa na kuwataka Watanzania kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura tarehe 29 Oktoba 2025 ili kukichagua Chama Cha Mapinduzi.
Aidha, amewashukuru wananchi wa Singida kwa kujitokeza kwa wingi kwenye mkutano huo, jambo linaloonesha imani kubwa waliyonayo kwa CCM na dhamira yake ya kuendeleza maendeleo ya nchi.
#haijapatakutokea #dirayasamia #kazinautu2025 #samiahadi2030 @ccm_tanzaniaThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
.
@Mwanahalisitz
Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 10 Septemba 2025, ameendelea na kampeni zake wilayani Iramba, mkoani Singida, ambapo amesisitiza dhamira ya Serikali kuendelea kuinua sekta ya madini na kuimarisha ajira kwa vijana.
Akizungumza mbele ya wananchi wa Iramba, Samia ameeleza kuwa soko la madini Shelui limekuwa na mchango mkubwa kwa wachimbaji wadogo, likiwa tayari limeuza madini yenye thamani kubwa.
“Tuahidi kuanzisha soko la madini, soko limeanzishwa Shelui wilaya ya Iramba ambapo zaidi ya gramu milioni 1.5 zimeuzwa kwa thamani ya Bilioni 192. Bilioni 192 zimeingia mikononi kwa wachimbaji ndugu zangu ndani ya Wilaya hii ya Iramba, lakini soko lile linaendelea kutoa huduma. Niwaombe sana wachimbaji, tumeweka soko lile ili dhahabu inayochimbwa, vito vinavyopatikana, vikauzwe ndani ya soko lile badala ya kuichepusha na kuipeleka nje bila kuuza ndani ya nchi,” amesema.
Aidha, amebainisha hatua zilizochukuliwa na Serikali kuhakikisha wachimbaji wadogo wanapata fursa.
“Vilevile tumeahidi kutoa kipaumbele kwa ajili ya wachimbaji wadogo. Nadhani mmeshuhudia, tayari kulikuwa na maeneo yamehodhiwa na watu ambao hawayatumii, tukafuta leseni zao na tukagawa upya. Tumetoa leseni thelathini na mbili (32) kwa vikundi 9 ndani ya wilaya ya Iramba na wachimbaji wadogo wa madini, na leseni nane (8) za uchenjuaji madini ya dhahabu katika eneo la Sekenke. Hiyo yote ni kuhakikisha vijana wetu wanapata ajira za kutosha iwe kwenye kilimo, miradi au madini kokote kule,” ameongeza.
Kuhusu miradi ya nishati, Samia ametaja hatua za utafiti wa mafuta na gesi unaoendelea, akisema unalenga kuongeza fursa za ajira na uwekezaji zaidi mkoani Singida na kwingineko.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Alafa Minja
@alafa_lalaby
AHADI YA MGOMBEA URAIS NDG. SAMIA SULUHU KWA WANA IRAMBA
Ameahidi ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami kati ya wilaya ya Iramba na wilaya ya Mkalama ili kuimarisha mahusiano na kukuza uchumi kwa wananchi.
#oktobatunatikisamia -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Gwax
@Gwax197393Gwax
#oktobatunatikisamia amerahisisha shughuli za uchimbaji kwa wachimbaji wadogo Iramba kwa kuwafikishia umeme.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Dira Ya Samia
@DiraYaSamia
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Dkt. @SuluhuSamia, akiendelea na kampeni zake mkoani Singida, Jimbo la Iramba, ameeleza kuwa serikali inaendelea na utafiti wa mafuta na gesi katika Kitalu cha Eyasi Wembere.
Amesema kuwa, mradi huo utaleta manufaa makubwa kwa wananchi, kuvutia uwekezaji zaidi katika maeneo ya Iramba, Igunga na Meatu, na kufungua fursa mpya za ajira endapo utafiti utakamilika kwa mafanikio.
Aidha, amewataka vijana wa Iramba kuchangamkia fursa hizo mapema ili wasiachie vijana kutoka mikoa mingine kuzitumia na wao kubaki watazamaji.
Kwa upande mwingine, Mhe. Dkt. Samia ametangaza kuwa katika Iramba Mashariki serikali itakamilisha ujenzi wa skimu kubwa ya umwagiliaji katika Kijiji cha Ishishi, Kata ya Msingi, kwa gharama ya shilingi bilioni 34. Mradi huo unalenga kuwawezesha wakulima kulima mara mbili kwa mwaka na kuongeza uzalishaji.
#haijapatakutokea #dirayasamia #kazinautu2025 #samiahadi2030This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Dira ya Tanzania
@DirayaTanzania
"Kule Iramba Mashariki tutakamilisha mradi mkubwa wa kilimo cha umwagiliaji katika Kijiji cha Ishishi kwa gharama ya shilingi bilioni 34, lengo ni kuwafanya wakulima walime na kuvuna mara mbili kwa mwaka.”- Ndg. Rais Samia Suluhu, Mgombea Urais CCM
#oktobatunatikisamia -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
GreenArmy 2025
Sehemu ya hotuba ya Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Dkt. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akizungumza na wananchi wa Iramba leo Septemba 10, 2025.
#greenarmyoktobatunatiki✅
#kazinaututunasongambele
#rundikakurakwadktsamia20254 media couldn't be displayed. See them on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
MR BEN
@Eric__Bernard
SAMIA AWAHAKIKISHIA IRAMBA: AFYA, ELIMU NA MAJI
Mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan ameendelea na kampeni zake za Uchaguzi Mkuu 2025 kwa kuzungumza na wananchi wa Wilaya ya Iramba, Mkoa wa Singida, akiahidi kuendeleza miradi mikubwa inayolenga kuinua ustawi wa wananchi.
Katika sekta ya afya, Dkt. Samia amesema Serikali itakamilisha ujenzi wa vituo vitatu vipya vya afya katika maeneo ya Mtoa, Mwandegembe na Irungu, hatua ambayo itaboresha upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi wa Iramba.
Akizungumzia elimu, ameeleza kuwa Serikali imekamilisha ujenzi wa shule mpya ya Amali pamoja na Shule ya Sekondari ya Mbelekese, ili kuongeza nafasi za wanafunzi kuendelea na masomo kwa mazingira bora na yenye hadhi.
Kwa upande wa maji, Dkt. Samia amesema Serikali imetekeleza ujenzi wa tenki kubwa la maji Kizonzo lenye ujazo wa lita 300,000, na pia itaendeleza utekelezaji wa mradi mkubwa wa maji kutoka Ziwa Victoria, ili kuhakikisha wananchi wa Iramba wanapata maji safi na salama kwa uhakika.
Vilevile, kupitia sekta ya madini, Serikali imeanzisha soko la uuzaji wa dhahabu, litakalowawezesha wachimbaji wadogo kupata masoko yenye uhakika na kuongeza kipato cha wananchi. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Kigogo Media
@kigogo2014
(Day 13/60 ya kampeni za CCM)
IRAMBA LEO ..
Umati wa wananchi wa Wilaya ya Iramba umejitokeza kwa wingi katika mkutano wa kampeni za mgombea urais kupitia CCM Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan katika uwanja wa CCM Lulumba Kiomboi leo Septemba 10, 2025 ikiwa ni muendelezo wa Chama hicho kuomba ridhaa ya kuchaguliwa tena kuingoza Tanzania kwa miaka mitano ijayo 2025- 2030.
#kigogomediaupdates -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
MR BEN
@Eric__Bernard
Wana Iramba wamempokea Mgombea Urais wa CCM kwa Tabasamu Kubwa sana, nyuso zenye bashasha, wakiwa na matumaini ya maendeleo na Mioyo yao imejaa Shukrani kwa Makubwa yamefanyiwa na Chama Tawala kwenye Maeneo yao!! Hawa Wote Oktoba wanatiki ✅
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Taifa Daily
@TaifaDaily
📍Singida
Crowds of residents in Iramba, Singida Region gathered to welcome and listen to CCM presidential candidate, President Samia Suluhu Hassan. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Swahili Times
@swahilitimes
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba amesema wakati wa janga la UVIKO-19 Rais Samia Suluhu alitumia fedha za kujikimu na janga hilo kufanya miradi mbalimbali ya maendeleo.
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
MR BEN
@Eric__Bernard
UMATI WA WANANCHI IRAMBA WAMPOKEA DKT. SAMIA
Umati wa Wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu za Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Iramba, mkoani Singida Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Jumatano tarehe 10 Septemba, 2025. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Chama Cha Mapinduzi
@ccm_tanzania
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Chama Cha Mapinduzi
@ccm_tanzania
✅ 𝗜𝗥𝗔𝗠𝗕𝗔 𝗜𝗠𝗘𝗖𝗛𝗔𝗥𝗨𝗞𝗔, 𝗛𝗔𝗣𝗔 𝗛𝗔𝗪𝗔𝗖𝗛𝗘𝗞𝗘𝗦𝗛𝗜 𝗪𝗔𝗟𝗔 𝗛𝗔𝗪𝗔𝗬𝗨𝗠𝗕𝗜𝗦𝗛𝗪𝗜, 𝗖𝗛𝗔𝗚𝗨𝗢 𝗟𝗔𝗢 𝗡𝗜 𝗦𝗔𝗠𝗜𝗔
Tazama umati wa maelfu ya wananchi wa Iramba mkoani Singida waliojitokeza kwa wingi katika uwanja wa Lulumba katika kumpokea na kumsikiliza Mgombea wa Nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya CCM, Rais Dkt. 𝗦𝗮𝗺𝗶𝗮 𝗦𝘂𝗹𝘂𝗵𝘂 𝗛𝗮𝘀𝘀𝗮𝗻 leo tarehe 10 Septemba 2025.
Rais Dkt. Samia yumo mkoani Singida ikiwa ni muendelezo wa mikutano ya kampeni za Urais kupitia CCM.
𝙆𝙬𝙖 𝙄𝙧𝙖𝙢𝙗𝙖 𝙝𝙞𝙞 𝙝𝙖𝙩𝙪𝙙𝙝𝙖𝙣𝙞 𝙠𝙖𝙢𝙖 𝙬𝙖𝙩𝙖𝙬𝙚𝙯𝙖 𝙠𝙬𝙚𝙡𝙞 𝙠𝙪𝙨𝙝𝙞𝙣𝙙𝙖𝙣𝙖 𝙣𝙖 𝘾𝘾𝙈
#kazinautu
#chaguasamia
#chaguaccm -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
-
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Anasubiriwa Mama Iramba.
2 media couldn't be displayed. See them on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Mkataba wetu na Dkt. Samia Suluhu Hassan ulikuwa ni kazi, na kazi hiyo ameifanya kwa ufanisi mkubwa sana. Tusidanganywe na wapiga kelele maana wameshapoteza muelekeo na hawana ajenda.
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Dodoma_Zone
@Dodoma_Zone_
Matukio mbalimbali katika mkutano wa hadhara wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) uliofanyika Manyoni mkoani Singida tarehe 09 Septemba, 2025.
-
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Tukutane kesho asubuhi saa 1 kumpokea Mama yetu kipenzi Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan katika uwanja wa CCM LULUMBA KIOMBOI.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
𝐃𝐫.𝐙𝐚𝐜𝐤™🇹🇿
@_zack255
Kazi Na Utu Tunasonga Mbele 💪
-
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Mama karibu sana mkoa wa Singida, kura zote za mkoa huu ni zako.
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
JIMBO LA IRAMBA MAGHARIBI
@jimbolairamba
PICHA RASMI YA KAMPENI KWA MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA IRAMBA MAGHARIBI - DKT MWIGULU LAMECK NCHEMBA MADELU.
KAZI NA UTU, TUNASONGA MBELE
OKTOBA TUNATIKI ✅ -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
IRAMBA KUMEKUCHA, KARIBUNI WATANZANIA WOTE.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
MR BEN
@Eric__Bernard
TANZANIA KUWA YA UCHUMI JUMUISHI NA YENYE USTAWI KWA WOTE- DKT. SAMIA
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi Dkt. Samia Suluhu Hassan amesisitiza adhma yake ya kuendelea kuijenga Tanzania yenye uchumi Jumuishi na ustawi kwa wote ikiwa atachaguliwa tena kuiongoza Tanzania kwa miaka mitano ijayo, akitaja nia yake pia ya kuendelea kuimarisha Vyama vya ushirika na ushirika nchini ili kuwafanya wakulima kufaidi nguvu na jitihada zao katika Kilimo.
Mbele ya maelfu ya wananchi wa Mji wa Iringa leo Jumapili Septemba 07, 2025 kwenye uwanja wa michezo Samora Mkoani Iringa. Dkt. Samia ambaye amehitimisha ziara yake ya siku mbili Mkoani humo kwaajili ya kujinadi kuelekea uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, Dkt. Samia ameeleza kuwa katika kutekeleza hilo, amejipanga pia kuhimiza matumizi ya TEHAMA kwenye Sekta za kilimo nchini ikiwemo kwenye Ushirika ili kuendana na mahitaji halisi yaliyopo duniani.
Dkt. Samia amebainisha kuwa ataendelea pia kulea na kukuza vyama vya ushirika nchini ili viweze kusimama vyenyewe, kuwa na uwezo wa kutafuta mikopo, kusambaza pembejeo kwa wanachama na baadae kununua mazao, kutafuta masoko ndani na nje ya nchi pamoja na kuwa na uwezo wa kujenga maghala ya kuhifadhia mazao ya kilimo.
"Nataka niwahakikishie kwamba tumejipanga vyema kuvilea vyama vya ushirika na ushirika ndani ya nchi yetu na lengo ni kumuwezesha mkulima kufaidi nguvu na jasho lake na huku ndiko kumuinua Mkulima. Niwaambie pia kwamba la muhimu katika vyama vya ushirika ambalo tunalifanyia kazi ni kuhakikisha tuna watu mahiri kwenye kuelewa kuendesha ushirika lakini pia matumizi ya tehama ili kuongeza uwazi kwenye mapato na matumizi ya ushirika, huko ndiko kwenye kuleta vurugu mpaka ushirika unavunjika." Amesisitiza Dkt. Samia.
Akizungumzia jitihada ambazo tayari zimechukuliwa katika awamu yake ya kwanza Dkt. Samia amesema serikali yake ilichukua hatua kadhaa za makusudi ikiwa ni pamoja na kuanzisha benki ya ushirika nchini pamoja na kuimarisha usimamizi wa Ushirika kupitia Tume ya maendeleo ya ushirika ili kuwezesha Vyama vya ushirika kupata mahitaji na mitaji nafuu katika kuwawezesha kujitegemea na kujiendesha. -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
OKTOBA TUNATIKI, WANAIRAMBA TUKUTANE KWA WINGI VIWANJA VYA CCM LULUMBA TAREHE 10/09/2025.
-
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
KARIBU SANA MAMA WILAYANI IRAMBA
Wananchi wote tukutane kwa shangwe na nderemo viwanja vya CCM Lulumba tarehe 10/09/2025 kumpokea Mama yetu kipenzi, kumshukuru kwa maendeleo makubwa aliyotuletea na kumkabidhi tano tena.
Kazi na Utu tunasonga Mbele. -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Watanzania wanakanyagana kumsikiliza Mama, kila rika linamkimbilia.
-
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Kazi, maendeleo na matokeo yameeleweka kote nchini, mafuriko haya ndiyo SAMIA EFFECT.
-
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
VERIFIED, ✅ Dkt. Samia & Dkt. Nchimbi.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Daily News Tanzania
@dailynewstz
SINGIDA: THE government is set to deploy a hightech specialised aircraft to survey six mineral-rich blocks covering over 100,000 square kilometres, equivalent to 18 per cent of the country’s land area.
The aerial survey project is scheduled to begin in the 2025/26 financial year, aiming to unlock untapped mineral potential across key regions.
Read more: dailynews.co.tz/aerial-tech-to-aid-exploration/ -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Nimesikitishwa sana na taarifa za kifo cha Mheshimiwa Job Ndugai. Naiombea familia yake faraja, na Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Haki Ngowi
@Hakingowi
📍Iramba
▪️DKT MWIGULU NCHEMBA AONGOZA KURA ZA MAONI JIMBO LA IRAMBA MAGHARIBI
Dkt. Mwigulu Nchemba ameibuka mshindi katika kura za maoni kwa nafasi ya ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Jimbo la Iramba Magharibi.
Dkt. Mwigulu amepata kura 10,604 kati ya jumla ya kura halali 12,429 zilizopigwa, ikiwa ni sawa na asilimia 85.31 ya kura zote. Ushindi huu unamfanya kuwa mshindi dhidi ya wenzake watatu waliokuwa wakichuana naye. -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Asanteni sana, Kazi Inaendelea.
-
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Kazi na Utu tunasonga Mbele, Iramba Kazi Inaendelea.
-
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Natoa shukrani za dhati kwa Mwenyekiti wa CCM Taifa, Mhe Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Kamati Kuu ya CCM kwa heshima na imani yao ya kuniteua mmoja wa wagombea wa kutafuta ridhaa ya Chama chetu kwa nafasi ya mgombea Ubunge wa 2025 - 2030 Jimbo la Iramba Magharibi. Asanteni Sana.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Haki Ngowi
@Hakingowi
📍Iramba
▪️MWENGE WA UHURU WALETA NEEMA SINGIDA, DKT. MWIGULU NCHEMBA ATOA WITO WA UMOJA NA KUIUNGA MKONO SERIKALI
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Ndg. Ismail Ally Ussi, amempongeza Waziri wa Fedha na Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), kwa usimamizi madhubuti wa utoaji wa fedha katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Singida na nchini kote.
Akizungumza wakati wa ukaguzi na uwekaji wa jiwe la msingi kwenye ujenzi wa daraja la Konkilangi pamoja na barabara ya changalawe yenye urefu wa kilomita 1.5 katika Wilaya ya Iramba, Ndg. Ussi alisema:
“Kufuatia usimamizi mzuri wa fedha za maendeleo zinazotolewa na Serikali, tumeona matokeo chanya hususani katika miradi ya miundombinu, maji, afya, elimu, umeme na huduma nyingine muhimu zinazokuza ustawi wa jamii kiuchumi. Hongera sana Dkt. Nchemba kwa kazi kubwa unayoifanya ya kumsaidia Mheshimiwa Rais katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma stahiki.”
Kwa upande wake, Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), alisisitiza dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ya kuhakikisha huduma muhimu zinawafikia wananchi kote nchini kwa mujibu wa Ilani ya CCM 2020–2025.
“Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameonyesha uongozi thabiti katika kutatua changamoto zinazowakabili wananchi kwa kuboresha mazingira ya huduma za kijamii na kiuchumi kwa manufaa ya Taifa,” alisema Dkt. Nchemba.
Aidha, Dkt. Nchemba alitoa wito kwa wananchi kuendelea kuiunga mkono Serikali katika jitihada zake za kuwaletea maendeleo na akalaani vikali vitendo vya uchochezi vinavyolenga kuvuruga umoja wa kitaifa.
Katika mbio hizo wilayani Iramba, Mwenge wa Uhuru ulikagua, kuweka mawe ya msingi na kuzindua miradi saba ya maendeleo yenye thamani ya shilingi bilioni 7.8, ikiwa ni ishara ya mafanikio ya juhudi za Serikali kuwaletea wananchi maendeleo ya kweli.
Miongoni mwa miradi iliyogusa maisha ya wananchi moja kwa moja ni mradi wa maji uliopo kijijini Nsusu, uliotembelewa na Mwenge wa Uhuru. Mradi huo unatarajiwa kuhudumia zaidi ya wakazi 4,000 waliokuwa wakikabiliwa na changamoto ya muda mrefu ya ukosefu wa maji safi na salama.
Wakazi wa kijiji hicho wameishukuru Serikali kwa kuwafutia machozi na kusema kuwa sasa matumaini yamerudi.
Kaulimbiu ya Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2025 ni:
“Jitokeze, Shiriki Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 kwa Amani na Utulivu”, ikisisitiza umuhimu wa mshikamano, ushiriki wa wananchi na kuenzi amani iliyoasisiwa na waasisi wa Taifa. -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Hongera sana Mhe. Rais @SuluhuSamia kwa uongozi mahiri na wa maono uliofanikisha mchakato wa kihistoria wa upatikanaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050. Uongozi wako shirikishi umeweka msingi thabiti wa kujenga Taifa jumuishi, lenye ustawi na haki kwa wote. Hii ni hatua kubwa kuelekea Tanzania tunayoitaka.
Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 ni mwongozo wa kimkakati wa muda mrefu unaolenga kuielekeza Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati wa juu, yenye maendeleo jumuishi, haki, na ustawi kwa wote ifikapo mwaka 2050.
Ni dira ya Watanzania wote, kwa vizazi vya sasa na vijavyo.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Haki Ngowi
@Hakingowi
▪️DKT. NCHEMBA AMEFANYA MAZUNGUMZO NA UJUMBE WA KAMPUNI YA MINARA
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, amekutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe kutoka Kampuni ya Minara Tanzania, ulioongozwa na Makamu wa Rais wa Kampuni hiyo, Bw. Richard Cane, ambapo pamoja na mambo mengine, wamejadili namna ya kuendeleza ushirikiano katika kukuza Sekta ya Mawasiliano nchini.
Mkutano huo umehudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Makamu wa Rais wa Kampuni ya Minara anayesimamia nchi za Afrika na Asia, Bw. Nicholous Vane, pamoja na wajumbe wengine kutoka Wizara ya Fedha na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na Kampuni ya Minara Tanzania.
📸:W/Fedha -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Mapema leo, nimekutana na kufanya mazungumzo na Uwakilishi wa Uongozi wa Minara Tanzania Ltd. Mazungumzo yetu yamegusa maeneo mbalimbali ya ushirikiano katika kukuza sekta ya mawasiliano na mchango wake katika uchumi wa Taifa.
-
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Leo katika Uwanja wa Jamhuri, Dodoma, nimeungana na Mwamnyeto Foundation kushiriki mechi ya hisani ya kurudisha kwa jamii kati ya Team Mwamnyeto na Dodoma Combine.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ally Mkimo📝
@ally_mkimo
Been reading this thing.
Iko "Well Written" kudos kwa @BankOfTanzania na @mofURT kwa ujumla👏 -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Haki Ngowi
@Hakingowi
📍Arusha
▪️DKT. NCHEMBA AIPONGEZA TRA KWA UFANISI
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, amesema kuwa kuna ongezeko kubwa la makusanyo ya kodi mara tu baada ya Serikali ya Awamu ya Sita kuingia madarakani ambapo kwa mwaka wa fedha 2021/22, TRA ilikusanya shilingi trilioni 22.2; mwaka wa fedha 2022/23 ilikusanya shilingi trilioni 24.1; mwaka wa fedha 2023/24, ilikusanya shilingi trilioni 27.6 na kwa mwaka wa fedha ulioishia tarehe 30 June 2024/25 imeshuhudiwa kiasi cha shilingi trilioni 32.26 sawa na ufanisi wa asilimia 103.9 kutoka lengo la kukusanya kiasi cha shilingi trilioni 31.05.
Mhe. Dkt. Nchemba, ameyasema hayo wakati akimkaribisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, kufungua rasmi Kikao Kazi cha Tathimini ya Utendaji kazi cha Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), katika Mwaka wa Fedha 2024/2025, kinachofanyika kwa siku tano katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC), jijini Arusha.
Alibainisha kuwa makusanyo hayo yamewezesha kufadhili miradi mbalimbali ya kimkakati ya maendeleo na akatumia fursa hiyo kuipongeza Menejimenti na watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa kujituma na kufanya kazi kwa weledi, uaminifu na uwajibikaji mkubwa waliouonesha katika kufanikisha malengo hayo.
Aliwataka watumie kikao kazi hicho kuweka mikakati thabiti ya utendaji kazi ili kuongeza ufanisi na tija katika kufikia malengo zaidi ili kuendelea kuchangia maendeleo kwa masilahi mapana ya ujenzi wa Taifa.
📸:W/Fedha -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Dirisha la usajili bado liko wazi?
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
-
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Hivi ndivyo ninavyojiandaa kwa ajili ya uchaguzi wa amani.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
JIMBO LA IRAMBA MAGHARIBI
@jimbolairamba
KARIBU MWENGE WA UHURU WILAYANI IRAMBA JULAI 21,2025
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
JIMBO LA IRAMBA MAGHARIBI
@jimbolairamba
Songeli zigizigi
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Haki Ngowi
@Hakingowi
📍Dodoma
1:Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akisalimiana na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, alipowasili kwa ajili ya kuhudhuria katika kikao cha wafanyakazi wa Wizara yake kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jiji la Dodoma uliopo Mji wa Serikali, Mtumba.
2:Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Huduma za Hazina, Bi. Jenifa Christian Omolo, alipowasili kwa ajili ya kuhudhuria katika kikao cha wafanyakazi wa Wizara yake kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jiji la Dodoma uliopo Mji wa Serikali, Mtumba. Anayeshuhudia ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha- Usimamizi wa Fedha za Umma, Bi. Amina Shaaban (kulia).
3:Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiteta jambo na Mhasibu Mkuu wa Serikali CPA (T), Leonard Mkude, baada ya kumalizika kwa Kikao cha Watumishi wa Wizara hiyo kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jiji la Dodoma uliopo Mji wa Serikali, Mtumba.
4:Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiteta jambo na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, wakati wa kikao cha watumishi kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jiji la Dodoma uliopo Mji wa Serikali, Mtumba, ambacho kilitoa fursa kwa watumishi kukutana kwa pamoja, kukumbushana na kubadilishana uzoefu, taarifa na uelewa kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu utekelezaji wa majukumu ya Wizara na Serikali kwa ujumla.
📸:W/Fedha -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Gilly Bonny Tv
@GillyBonnyTv
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, amewaagiza viongozi na watumishi wa Wizara hiyo kuendelea kufanya kazi kwa bidii, weledi na uaminifu ili kuendelea kusimamia uchumi wa nchi.
Ametoa agizo hilo wakati wa Kikao cha watumishi wa Wizara hiyo ambacho kinatoa fursa kwa watumishi kukutana kwa pamoja, kukumbushana na kubadilishana uzoefu, taarifa na uelewa kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu utekelezaji wa majukumu ya Wizara na Serikali kwa ujumla.
Dkt. Nchemba aliwakumbusha watumishi hao kutambua kuwa Wizara ya Fedha ni moyo wa Serikali hivyo ikiyumba tu nchi itayumba na kuleta madhara kijamii na kiuchumi. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Thomas J. Kibwana
@thomasjkibwana
📊 MAKUSANYO YA KODI NCHINI TANZANIA: (2015/16–2024/25)
Kwa mujibu wa takwimu kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), makusanyo ya kodi yamekuwa yakiongezeka kwa utaratibu katika kipindi cha miaka kumi iliyopita — na kufikia kiwango cha juu zaidi cha TSh trilioni 32.3 kwa mwaka wa fedha 2024/25.
Takwimu Muhimu:
• 2015/16: TSh trilioni 13.4
• 2020/21: TSh trilioni 18.1
• 2024/25: TSh trilioni 32.3
Katika mwaka wa fedha 2024/25, TRA ilivuka malengo ya makusanyo kwa kila mwezi kwa mara ya kwanza katika historia yake, na kufikia asilimia 103 ya lengo la mwaka.
📈 Mambo yanayoweza kuchangia ukuaji huu ni pamoja na:
• Ukuaji wa uchumi na mfumuko wa bei
• Maboresho ya mifumo ya ukusanyaji na utii wa walipa kodi
• Mageuzi ya kiutawala na matumizi ya teknolojia
• Mwelekeo wa sera za kifedha na kiuchumi
🪜Kupanda kwa kasi kuanzia mwaka 2021/22 kunaashiria mabadiliko ya msingi katika mwenendo wa makusanyo na kunastahili kuchunguzwa kwa kina — hususan kuhusu nafasi ya sera, uongozi na usimamizi wa taasisi.
🔍 Uendelevu wa mwenendo huu utategemea uimara wa taasisi za kifedha, sera thabiti, na uthabiti wa uchumi kwa ujumla. -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Songeli zigizigi.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Haki Ngowi
@Hakingowi
📍Singida
▪️MHE. DKT. NCHEMBA ASHIRIKI HARAMBE KUU KANISA LA KKKT KANDA YA KATI
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, ameshiriki Harambee Kuu ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Dayosisi ya Kati na kufanikisha kukusanya fedha zaidi ya shilingi bilioni moja zitakazotumika kujenga Hospitali.
Harambee hiyo iliyofanyika leo tarehe 29 Juni, 2025 akiwa Mgeni Rasmi katika Ibada iliyoongozwa na Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Dkt. Alex Gehaz Malasusa,) kwa kushirikisha na waumini mbalimbali kutoka ndani na nje ya Dayosisi hiyo.
Mhe. Dkt. Nchemba, amewashukuru Waumini wote walioshiriki katika harambee hiyo muhimu kwa Dayosisi na kuwasihi kuendelea kumtumaini Mungu kupitia matoleo yao katika kufanikisha shughuli za Kijamii kusonga mbele huku akiwasihi Waumini wa dhehebu hilo na madhehebu mengine nchini kuendelea kudumisha amani na mshikamano uliopo katika Taifa linapoelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba 2025.
Kwa upande wake Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Dkt. Alex Gehaz Malasusa, wakati wa muhubiri yake amesema Imani waliyonayo Watanzania kwa Serikali yao katika kulinda umoja, upendo na mshikamano uliopo ni kubwa hivyo Taifa liendeleze mshikamano huo kwa nguvu zote.
Ameongeza kuwa Kanisa lina mchango mkubwa katika kudumisha amani na kujenga nyumba za Ibada zinazotumika kutoa huduma muhimu kwa Wananchi ikiwemo Vituo vya kulelea Watoto, Hospitali na kuwalea kiroho waumini wake wakati wote.
Pia amemshukuru Mhe. Dkt. Nchemba kwa kujitolea katika shughuli mbalimbali za Kidini zinazofanyika na kuhakikisha huduma hiyo inaboreshwa katika maeneo mbalimbali hapa Nchini.
Harambee hiyo ilihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Halima Dendego, Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhe. Godwin Gondwe Waimbaji wa nyimbo za Injili na Viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali
📸:W/Fedha -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Patricia Laverley
@PatLaverley
The African Development Bank Group recently concluded a pivotal visit to Tanzania, underscoring its profound commitment to the nation's development agenda. On June 14th, President Dr. Akinwumi Adesina experienced Tanzania's state-of-the-art Standard Gauge Railway (SGR) firsthand. This journey vividly demonstrated the transformative power of infrastructure in integrating our continent and connecting communities.
Beyond the SGR, President @akin_adesina also visited other crucial @AfDB_Group supported development projects, including the significant Msalato International Airport and Dodoma City Outer Ring Road project. These visits reaffirmed the tangible impact of our collective efforts. In a profound gesture recognizing his impactful leadership, Her Excellency @SuluhuSamia, President of the United Republic of Tanzania, officially renamed the Dodoma City Outer Ring Road after President Adesina. This renaming symbolizes the deep appreciation for the Bank’s contributions to the continent under his 10-year tenure. The African Development Bank Group has delivered an unprecedented scaling up of support in Tanzania, channelling over $4.73 billion in the last decade alone. This represents 53% of the Bank's total cumulative funding in the country since its operations began, driving monumental progress in vital sectors like infrastructure, agriculture, and human capital development, directly improving livelihoods and fostering sustainable economic growth across the nation.
We are steadfast in our dedication to this enduring partnership, poised for even greater shared achievements with Tanzania. @mofURT @ikulumawasliano @tanroadshq @mwigulunchemba1
official Speech: www.afdb.org/en/news-and-events/speeches/remarks-dr-akinw… -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
ASANTENI SANA WANANCHI WA KIJIJI NSELEMBWE, KATA YA SHELUI.
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Uzinduzi wa Kituo cha Afya cha Shelui, karibuni wote.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Haki Ngowi
@Hakingowi
📍Iramba, Singida
▪️DC MWENDA AONGOZA HAFLA MAALUM YA KUWAAGA WAHESHIMIWA MADIWANI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA IRAMBA WALIOHITIMISHA KIPINDI CHA MIAKA MITANO
Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Mkoani Singida, Mhe. Suleiman Yusuph Mwenda, ameongoza hafla maalum ya kuwaaga Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba waliomaliza kipindi cha miaka mitano madarakani tangu uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.
Hafla hiyo imefanyika Juni 18, 2025, katika viwanja vya ofisi ya Halmashauri ya Iramba, ambapo DC Mwenda aliwapongeza madiwani kwa mchango wao mkubwa katika maendeleo ya wilaya hiyo. -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ukiongozwa na Gavana wa Benki hiyo, Bw. Emmanuel Tutuba, ambapo umeangazia mafanikio ya Benki hiyo katika kuendelea kuimarisha uchumi.
Akizungumza katika mkutano huo uliofanyika katika Ofisi za Wizara ya Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma, Dkt. Nchemba aliitaka Bodi hiyo ya Benki Kuu ya Tanzania kuendelea kusimamia misingi iliyoanzisha Bodi hiyo.
Alisema kuwa Wizara ya Fedha itaendendelea kutoa ushirikiano kwa Bodi hiyo ili kuendelea kuimarisha uchumi kwa manufaa ya wananchi na Taifa kwa ujumla.
Kwa upande wake Gavaa wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba, alisema kuwa Benki Kuu imeendelea kufanya vizuri katika kuimarisha uchumi na hilo linadhihirika baada ya nchi kupitia vipindi tofauti vya msukosuko wa uchumi uliozikumba pia nchi nyingi Duniani.
@BankOfTanzania -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Kigongo–Busisi: fahari ya Kanda ya Ziwa, Mama aliahidi na ametenda.
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Kwa kazi alizofanya, kwa dira aliyoitoa, na kwa matumaini aliyojenga, Oktoba tunatiki kwa Mama bila kusita.
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Haki Ngowi
@Hakingowi
📍Dodoma
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (Mb.), leo ameongoza kikao cha pili cha Tume ya Taifa ya HABARI PICHA- Mipango Jijini Dodoma. Prof. Mkumbo ameongoza kikao hicho kilichojadili Mandalizi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 na Mpango Elekezi wa Maendeleo wa Mmuda Mrefu (LTPP) kwa niaba ya Mwenyekiti wa Tume hiyo, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
📸:O/Rais Mipango na Uwekezaji -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Dr. Akinwumi A. Adesina, CON, CGH
@akin_adesina
Thank you very much Your Excellency @SuluhuSamia, President of the United Republic of Tanzania! Asante Sana! 🙏🏽❤️🙏🏽
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Bank of Tanzania
@BankOfTanzania
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Yericko Nyerere
@YerickoNyerereT
Moja ya jambo muhimu sana kwa nchi yetu ni hili liliotokea Ufaransa juzi ambapo Tanzania imeondolewa kwenye orodha ya nchi zenye mapungufu ya kimkakati katika udhibiti wa utakatishaji fedha haramu, ufadhili wa ugaidi na silaha za maangamizi, maarufu kama “grey list”, baada ya kikao cha mwisho cha Kikosi Kazi cha Kifedha cha Kimataifa (FATF) kilichofanyika mjini Strasbourg, Ufaransa. Tangazo hilo lilitolewa na Rais wa FATF, Bi. Elisa de Anda Madrazois, baada ya tathmini iliyobaini kuwa Tanzania imekamilisha kikamilifu hatua zote za kimageuzi ilizoelekezwa tangu ilipoorodheshwa mwaka 2022.
Kwa msiojua madhara ya jambo hilo ni kwamba sisi tunaofanya biashara za kimataifa tulikuwa kwenye kizuizi kikubwa na kukwamisha biadhara zetu huko duniani, Miamala ya kibenki ya kimataifa ilikuwa katika kizuizi kikubwa kwa muda mrefu, Mfano Amazo, Google, nk walikuwa hawaruhusu bank za kitanzania katika mifumo yao, Royalties za kibiashara kati yangu na makampuni hayo zilikuwa haziwezi kwenda moja kwa moja katika akaunti yangu ya benk kwa hapa Tanzania hadi wakuandikie ectronic cheque ambayo nayo ilikuwa haipokelewi na benk za bongo, Ilifikia wakati ili ufanye biashara za kimataifa bila usumbufu tunakwenda kufungua akaunti Uingereza, Marekani au Afrika Kusini kwakuwa Tz tuko gizani kabisa, benk zetu zinaishia vingunguti tu! Kwaupande wa nchi ilikuwa blacklisted na mifumo ya fedha ya kimataifa na hivyo wawekezaji wa kubwa duniani hawakuthubutu kuingiza mitaji yao Tanzania. Naaam sasa kwa tangazo hili tumeunganishwa na dunia upya.
Nawapongeza Ujumbe wa Tanzania katika kikao hicho, ukiongozwa na Naibu Gavana wa Benki Kuu, Bi. Sauda Msemo, na Kamishna wa Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu (FIU), Bw. Majaba Magana, ambapo ujumbe huo uliwahakikishia washirika wa kimataifa kuwa serikali itaendelea kuimarisha mifumo ya udhibiti wa fedha na kuhakikisha uwazi, uwajibikaji na utawala bora vinazingatiwa.
Nichukue nafasi hii kupongeza Wizara ya Mashauri ya Fedha na Uchumi chini ya @mwigulunchemba kwa kufanikisha hilo, Pia nipongeze Wizara ya Mashauri ya Kigeni chini ya Mahamud Kombo, Hii ni hatua kubwa sana katika Ujasusi wa Kiuchumi kwa nchi yetu.
Na Yericko Nyerere -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Nguvu ya Umma imeongea, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ndiye kipenzi halisi cha Watanzania, na mapenzi haya yanatoka kwenye vilindi vya nyoyo zao.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Haki Ngowi
@Hakingowi
📍Dar es Salaam
▪️DKT. NCHEMBA: RAIS WA AfDB DKT. AKINWUMI ADESINA NI MWANA THABITI WA AFRIKA
Waziri wa Fedha,Dkt. Mwigulu Nchemba, ameshuhudia tukio la kumtunuku Dkt. Akinwumi Adesina, Rais anayeondoka wa Benki ya Maendeleo ya Afrika, Shahada ya Heshima ya Uzamivu (Honoris Causa), iliyotolewa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam tarehe 13 Juni 2025, kwa kutambua mchango wake mkubwa katika maendeleo ya Afrika katika zama za sasa.
Mhe. Dkt. Nchemba alisema kuwa heshima hiyo ni uthibitisho wa yale ambayo wengi barani Afrika na duniani wanayajua tayari kwamba Dkt. Adesina ni kiongozi mwenye maono, bingwa wa maendeleo, na mwana wa kweli wa Afrika aliyejitolea kubadili simulizi la bara hili na kwamba Tanzania inajivunia kuwa miongoni mwa mataifa yanayosherehekea mafanikio na urithi wake wa kipekee.
Alisema kuwa kupitia mpango wa Building a Better Tomorrow (BBT), Vijana katika Kilimo Biashara, Benki ya Maendeleo ya Afrika chini ya uongozi wa Dkt. Adesina imewezesha zaidi ya vijana 11,000 wa Kitanzania kuwa wajasiriamali wa kilimo. Kwa kuwapatia ardhi, pembejeo, na mikopo, mpango huu haukuwa tu ajira kwa vijana bali umeleta matumaini mapya vijijini kuwa ustawi unawezekana.
“Dhamira ya Dkt. Adesina kwa Tanzania pia ilidhihirika wakati wa janga la COVID-19, moja ya nyakati ngumu zaidi kwa dunia nzima, Chini ya uongozi wake, Benki ilitoa msaada wa kifedha wa takribani dola za Marekani milioni 50, uliosaidia serikali yetu kushughulikia dharura ya afya, kuendeleza uchumi, na kuwalinda wanyonge” alisema Mhe. Dkt. Nchemba
Alieleza kuwa athari za Dkt. Adesina hazikuishia Tanzania pekee bali aliongoza ajenda mpya ya maendeleo Afrika. Pamoja na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Benki ya Dunia, Bw. Ajay Banga, aliasisi Mkutano wa Nishati Afrika na kuanzisha Mission 300, lengo la kuhakikisha upatikanaji wa nishati kwa Waafrika milioni 300 ifikapo mwaka 2030.
“Katika majukwaa ya kimataifa, Dkt. Adesina amekuwa sauti ya kuaminika ya Afrika, akitetea upatikanaji wa fedha kwa mabadiliko ya tabianchi, usalama wa chakula, na usawa katika ushirikiano wa kiuchumi unaozingatia matarajio ya mataifa ya Afrika” alisisitiza Dkt. Nchemba
Alisema kuwa chini ya uongozi wake, Benki ya Maendeleo ya Afrika ilileta mtazamo mpya wa kugharamia miradi mikubwa yenye athari za moja kwa moja. Kinyume na mikopo ya awali iliyokuwa ikigusa maeneo mengi bila athari kubwa kwa watu, ambapo Dkt. Adesina alihakikisha miradi yenye tija inapata msukumo.
Dkt. Nchemba alitaja baadhi ya miradi inayofadhiliwa na AfDB hapa nchini kuwa ni pamoja na
* Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Msalato, Dodoma
* Barabara ya Iringa – Dodoma – Babati
* Barabara ya mzunguko wa mji wa Dodoma
* Mradi wa Maji safi na Usafi wa Mazingira (AUWSA – Arusha) uliowafikia zaidi ya wakazi 600,000 wa Arusha na Viunga vyake.
* Katika sekta ya nishati, kuna miradi kadhaa ikiwemo Mradi wa Gridi ya Kaskazini Magharibi – (msongo wa kilovolti 400 kutoka Nyakanazi hadi Kigoma), ambao umeongeza uwezo wa gridi ya taifa katika mikoa ya Kigoma na Kagera.
* Na zaidi ya yote, usaidizi katika reli ya SGR – Lot 6 (Tabora–Kigoma), na Lot 7 (Uvinza–Musongati, Burundi hadi DRC).
“Dkt. Adesina, urithi wako unaacha funzo kwa taasisi zote za kimataifa – kuwa msaada kwa Afrika lazima uambatane na mipango ya kitaifa, usiwe wa masharti yasiyokubalika, na uzingatie miradi ya kimkakati yenye uwezo wa kubadilisha maisha ya watu. Sio mikopo ya “chapati na mandazi” inayoongeza madeni bila kuleta mabadiliko” aliongeza Dkt. Nchemba
Alisema kuwa ni jambo la heshima kubwa kuona Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, taasisi ya elimu ya juu ya muda mrefu na inayoheshimika sana, kumtunuku shahada hiyo ya heshima ambayo ni ishara ya heshima ya kitaaluma, na shukrani kwa ubora, mshikamano wa Kiafrika, na uongozi wa kweli.
📸:W/Fedha -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Haki Ngowi
@Hakingowi
📍Dodoma
▪️DKT. NCHEMBA AMUAGA DKT. ADESINA
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu ((Mb), ameungana na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, kumuaga Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Dkt. Akinwumi Adesina, katika Uwanja wa Ndege wa Dodoma, baada ya kukamilisha ziara yake ya siku mbili nchini, ambapo alitunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kutambua mchango wake katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika Bara la Afrika ikiwemo Tanzania kupitia uongozi wake na baadae aliungana na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kutembelea na kukagua miradi miwili ya kimkakati inayofadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) ukiwemo ujenzi wa barabara ya mzunguko wa nje ya Jiji la Dodoma (Dodoma outer ring road) yenye urefu wa kilomita 112.3, katika eneo la Mtumba, Jijini Dodoma, pamoja na Mradi wa Ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato Jijini Dodoma, unaohusisha njia ya kuruka na kutua ndege (runway) jengo la abiria, jengo la kuongozea ndege pamoja na Miundombinu mengine.
📸:W/Fedha -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Haki Ngowi
@Hakingowi
📍Dodoma
▪️TANZANIA YATOKA RASMI KWENYE ORODHA YA NCHI ZENYE MAPUNGUFU YA KIMKAKATI KATIKA MIFUMO YA UDHIBITI UTAKATISHAJI FEDHA HARAMU, UFADHILI WA UGAIDI, NA UFADHILI WA SILAHA ZA MAANGAMIZI (GREY LIST)
Na Benny Mwaipaja, Dodoma
Tanzania imeondolewa kwenye Orodha ya nchi zenye mapungufu ya kimkakati katika mifumo ya udhibiti utakatishaji fedha haramu, ufadhili wa ugaidi, na ufadhili wa silaha za maangamizi (Grey List).
Uamuzi huo umetangazwa na Rais wa Kikosi Kazi cha Kifedha cha Kimataifa (FATF) Bi Elisa de Anda Madrazois, mwishoni mwa Mkutano Mkuu wa FATF uliofanyika katika Mji wa Strasbourg nchini Ufaransa kuanzia tarehe 10 hadi 13 Juni 2025.
Ikumbukwe kwamba Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliorodheshwa kwenye orodha ya nchi zenye mapungufu ya kimkakati katika mifumo ya udhibiti utakatishaji fedha haramu, ufadhili wa ugaidi na ufadhili wa silaha za maangamizi (Grey list) mnamo mwezi Oktoba, 2022.
Wakizungumza kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa Mkutano wa FATF, Ujumbe wa Tanzania, ukiongozwa na Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Wataalamu ya Kuzuia Utakatishaji Fedha Haramu, Bi. Sauda Msemo na Kamishna wa Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu (FIU) Bw. Majaba Magana, umeihakikishia FATF na mtandao wa kimataifa kuwa Tanzania ina dhamira ya dhati ya kuhakikisha mifumo yake ya udhibiti inabaki kuwa imara.
“Serikali iatendeleza ushirikiano wa kimataifa; na kusimamia maadili ya uwazi, uwajibikaji na utawala bora kwenye mfumo wa kifedha, ambavyo vitachangia kuimarisha usalama wa nchi, kanda, na mtandao mzima wa kifedha kimataifa” alisema Bi. Msemo.
Akizungumzia kuhusu tukio hilo akiwa Dodoma, Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) aliishukuru Kamati Ndogo ya Kundi la Afrika kwa ushirikiano katika mchakato mzima, Sekretarieti ya FATF na Kikundi cha Kupambana na Utakatishaji Fedha Haramu Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAAMLG) kwa jitihada kubwa zilizoiwezesha nchi kuondolewa katika grey list na kwamba anatambua na kuthamini msaada wa kitaalam na kifedha kutoka kwa washirika wa maendeleo katika jitihada hizo.
“Tunapenda kuuhakikishia Umma na Jumuiya ya Kimataifa kuwa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, amedhamiria kuhakikisha kuwa nchi yetu inabakia kuwa salama dhidi ya vitendo vya uhalifu katika mfumo wa kifedha.” Alisema Mhe. Dkt. Nchemba.
Alisema kwamba nchi itadumisha matokeo mazuri ambayo Tanzania imeyapata na kuendelea kushirikiana na wadau wa ndani na nje ya nchi katika mapambano dhidi ya utakatishaji fedha haramu, ufadhili wa ugaidi na ufadhili wa silaha za maangamizi; ili kuhakikisha kuwa Tanzania inabaki kuwa kinara wa uadilifu na uwazi katika mifumo ya kifedha, yenye kujipambanua kwa maendeleo endelevu na ustawi.
Mhe. Dkt. Nchemba ameitangazia jumuiya za kimataifa kuwa Tanzania ni Mamlaka inayoheshimika na yenye mazingira salama kwa uwekezaji, na fursa kubwa kwa washirikia wa ndani na nje ya nchi katika masuala ya kifedha na kiuchumi kwa ujumla na kuwahimiza wachangamkie fursa hiyo. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
African Development Bank Group
@AfDB_Group
Today, @AfDB_Group Pres @akin_adesina was awarded an Honorary Doctorate by @UdsmOfficial for his contribution to the continent’s growth. The doctorate was conferred by the University’s Chancellor & Former Pres @jmkikwete at the 55th Graduation Ceremony held in Tanzania.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
African Development Bank Group
@AfDB_Group
"Tanzania is proud to stand among the nations celebrating this journey and enduring legacy. Through the ‘Building a Better Tomorrow’ program, youth in Tanzania have hope, because of the visionary leadership of the @AfDB_Group. The program has enabled over 11,000 young Tanzanians to become agricultural entrepreneurs by providing land, inputs, and financing." - @mofURT, @mwigulunchemba1
-
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
My bro Zitto, you are wrong. WHT on retained earnings is not double taxation on the same income. It is an anti avoidance rule aimed at addressing the equity principle of taxation whereby dividends are taxed, while retained earnings are not.
Zitto MwamiRuyagwa Kabwe
@zittokabwe
Mr @mwigulunchemba1 Finance Minister, this is WRONG. It is a double taxation on the same income.
When the company makes profit, the government charges a corporate rate of 30% and company retains 70% of the declared profit. Then the latter can either pay it to the shareholders as DIVIDEND or retain within the company (retained earnings). Taxing the retained earning, is double taxation. It has huge consequences on capitalizing the companies.
Please SCRAP this proposal -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Leo nimewasilisha Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2025/26.
Ni bajeti ya kazi, maendeleo na mafanikio chini ya uongozi wa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Tanzania inawekeza kwa wananchi wake kwa uchumi wa sasa na vizazi vijavyo.
Tumuombee, tumuunge mkono.
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
-
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
LEO nitawasilisha mbele ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2025/2026.
📍 Bungeni, Dodoma
🕓 Saa 10:00 jioni
#bajetiyamaendeleo
#bajetikuuyawananchi -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Tarehe 12 Juni 2025, nitawasilisha Bungeni Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026.
-
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Wengine hatuna familia nje ya nchi, watoto na wazazi wetu wako hapa nchini, mashamba yetu yako hapa, hatuna pa kukimbilia, tutailinda nchi yetu kwa wivu mkubwa sana, TUSICHEZEANE KABISA.
-
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
JIMBO LA IRAMBA MAGHARIBI
@jimbolairamba
Eid Mubarak
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
CharlieBihemo
@CharlieBihemo
Mbunge wa Jimbo la iramba Magharibi @jimbolairamba Mhe @mwigulunchemba1 anawatakia Watanzania Wote
Eid Mubarak -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Honored to strengthen the strategic partnership between Tanzania and Norway.
We deeply value Norway’s unwavering commitment to our national development agenda, grounded in inclusive growth, sustainability, and long-term resilience.
Ambassador Tone Tinnes
@NorAmbTZ
Today I met with Hon. Mwigulu Nchemba to discuss Norway–Tanzania cooperation in rural energy, women in engineering, tax reform & poverty reduction through TASAF.
Norway has contributed TZS 188+ billion to support inclusive development led by the Government of Tanzania.
🇳🇴🤝🇹🇿 -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ambassador Tone Tinnes
@NorAmbTZ
Today I met with Hon. Mwigulu Nchemba to discuss Norway–Tanzania cooperation in rural energy, women in engineering, tax reform & poverty reduction through TASAF.
Norway has contributed TZS 188+ billion to support inclusive development led by the Government of Tanzania.
🇳🇴🤝🇹🇿 -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Tanzania Bankers Association
@tba_forbankers
On 2nd and 3rd June 2025, TBA, represented by Ms Tuse M. Joune, our Executive Director, joined the National Tax Think Tank convened in Dodoma, Tanzania.
#tbaforbankers #tba30yearsanniversary #umojawamabenkitz #advocacyinaction #thevoiceofthebankingsector -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Bank of Tanzania
@BankOfTanzania
Katika juhudi za kulinda watumiaji wa huduma za fedha dhidi ya manyanyaso ya kifedha na kuhakikisha haki na usawa katika sekta ya fedha, Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, amezindua mfumo mpya wa kushughulikia malalamiko ya wateja uitwao SEMA NA BOT pamoja na
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ayeem Ndimbo
@ally_ndimbo
A Bold Step Forward for Fintech in Tanzania congratulations to @mwigulunchemba1 and @BankOfTanzania for launching two MAJOR systems:
Fintech Regulatory Sandbox
Customer Complaint Platform – Sema na BoT
This is the kind of bold move we desperately need in our financial ecosystem -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Dcirambaofficial
@DCIRAMBA
Twiga akivuka barabara eneo la Mingela akitoka katika msitu wa Sekenke Tulya akielekea ziwa Kitangiri 1987.
Kutokana na uharibifu wa mazingira wanyama hao wamehama na hawapo tena katika msitu huo.
Juhudi ya Serikali kwasasa ni kulinda msitu huo.
#irambankulu -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
MR BEN
@Eric__Bernard
UFAFANUZI WA KITAALAMU: BAJETI YA WIZARA YA FEDHA
Kati ya TSh trilioni 20.19 zilizowasilishwa na kuidhinishwa kwa Bajeti ya Wizara ya Fedha 2025/26:
Takribani TSh trilioni 18.33 ni kwa ajili ya huduma za kifedha kwa taifa – ikijumuisha ugharamiaji wa deni la serikali, kulipa riba, na kudhibiti hatari za kifedha, si "matumizi ya kawaida" tu kama inavyodhaniwa.
TSh trilioni 1.10 ni mishahara kwa watumishi walio chini ya mafungu 8 ya Wizara hiyo (kama vile Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali, Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu, NAOT nk) – kazi hizi ni uti wa mgongo wa usimamizi wa fedha za umma.
TSh bilioni 757.79 ni kwa miradi ya maendeleo ya moja kwa moja ndani ya Wizara ya Fedha. Hii haina maana kuwa miradi mingine ya taifa haifanyiki – bali hiyo inatoka kwenye Bajeti Kuu (General Budget) ambayo ni zaidi ya TSh trilioni 49.35.
Kwa mantiki hiyo, hoja kwamba “3.5% ndiyo fedha ya maendeleo” ni upotoshaji kwa sababu:
Bajeti ya maendeleo ya Wizara ya Fedha pekee haipaswi kuchukuliwa kama bajeti ya maendeleo ya serikali nzima. Zipo bajeti za maendeleo za Wizara ya Ujenzi, Afya, Elimu, Nishati nk – kila moja ikiwa na miradi ya maendeleo inayosimamiwa na fedha nyingi zaidi.
Wizara ya Fedha si Wizara ya ujenzi wa barabara au shule – bali ni wizara ya kuhakikisha fedha zipo, zinasimamiwa kwa nidhamu, na kila taasisi inalipwa kwa wakati. Hii ni kazi ya maendeleo ya mfumo mzima wa kiuchumi. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Dira Ya Samia
@DiraYaSamia
🎥BUNGENI: Waziri wa Fedha, Dkt. @mwigulunchemba1, amebainisha kuwa Serikali imeendelea kutekeleza kwa ufanisi mpango wake wa kuhudumia deni la Taifa kwa kuhakikisha malipo yote muhimu yanafanyika kwa wakati.
Akizungumza leo tarehe 4 Juni 2025 bungeni jijini Dodoma wakati wa kuwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Fedha kwa mwaka wa fedha 2025/2026, Dkt. Mwigulu amesema hadi kufikia Aprili 2025, Serikali imelipa jumla ya shilingi trilioni 10.19 kwa ajili ya deni lililofikia muda wa kulipwa. Hili ni sawa na asilimia 84.8 ya lengo la mwaka.
Dkt. Mwigulu amesisitiza kuwa Serikali itaendelea kusimamia kwa umakini deni la Taifa ili liendelee kuwa himilivu na lisilete mzigo.
@SuluhuSamia @ikulumawasliano
#dirayasamia #kazinautu2025 #kazinaututunasongambeleThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
BADO SIKU 1📌
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Haki Ngowi
@Hakingowi
📍Bungeni,Dodoma
▪️SERA ZA WAHISANI HAZINA ATHARI ZA MOJA KWA MOJA ZA KIBAJETI
Serikali imesema kuwa hakuna athari za moja kwa moja za kibajeti kutokana na amri za kimamlaka alizotoa Rais wa Marekani, Dornald Trump za kusitisha misaada kwa Tanzania.
Hayo yalisemwa bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Moshi Vijijini, Mhe. Prof. Patrick Alois Ndakidemi, aliyetaka kujua ni kwa kiasi gani amri za kimamlaka alizotoa Rais Dornald Trump wa Marekani za kusitisha misaada Tanzania, zilivyoathiri miradi iliyokuwa inaendelea nchini.
Dkt. Nchemba alisema kuwa Serikali ya Tanzania haikuwa na ushirikiano wa Serikali kwa Serikali kwa masuala ya fedha za miradi ya maendeleo na Serikali ya Marekani kwa kuwa ilikuwa inatumia taasisi zake ambazo zilikuwa zinashirikiana na taasisi za Tanzania.
“Kwa upande wa taasisi zilizokuwa zinapokea fedha kutoka taasisi za Marekani, tayari Serikali imefanya tathmini si tu kwa tamko la Marekani bali kwa mwenendo wote unaohusisha fedha zinazotoka kwa washirika wa maendeleo na tayari hatua zimeanza kuchukuliwa”, alisema Dkt. Nchemba
Alisema kuwa huko nyuma kulikuwa na fedha za misaada zilizokuwa zinaenda kwenye bajeti kwa ajili ya miradi ya maendeleo lakini kwa sasa Serikali inatekeleza miradi ya maendeleo kupitia fedha za ndani kufidia pengo la miradi ambayo bajeti yake ilikuwa inatoka kwa nchi wahisani.
Dkt. Nchemba alisema kuwa kutokana na yaliyotokea hivi karibuni kuhusu Sera za nje kutoka kwa Wahisani tayari Serikali imepangilia upya matumizi yake kwa bajeti inayoendelea na kupata zaidi ya shilingi bilioni 220 zilizokuwa zinahitajika hasa kwenye maeneo yaliyoonekana kuathirika hususani sekta ya afya ambayo zimepelekwa zaidi ya shilingi bilioni 88 kuendelea na utekelezaji wa miradi.
Alisema kuwa kupitia tathmini iliyofanywa, Serikali itaendelea kutekeleza miradi ya maendeleo ambayo ilikuwa inapata fedha kutoka kwa washirika wa maendeleo ili kuhakikisha miradi ya maendeleo na maisha ya watanzania hayaathiriki kutokana na mabadiliko ya kisera kutoka kwa mbia yeyote wa maendeleo
Akijibu swali la msingi kuhusu namna Serikali ilivyojiandaa kukabiliana na mabadiliko ya Sera za baadhi ya nchi tajiri kulisaidia Taifa kukuza uchumi, Mhe. Dkt. Nchemba alisema Serikali inaendelea na jitihada mbalimbali za kuongeza mapato ya ndani ili kuhakikisha kuwa sehemu kubwa ya bajeti inagharamiwa kwa kutumia mapato ya ndani.
Alisema kuwa kwa kutambua umuhimu wa mahitaji ya kibajeti ikiwemo ugharamiaji wa miradi ya maendeleo, Serikali itaendelea kuvutia ushiriki wa sekta binafsi katika ugharamiaji wa miradi ya maendeleo kwa kutumia njia mbadala ikiwemo ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi.
Dkt. Nchemba alisema kuwa hatua hiyo itasaidia kuipunguzia Serikali mzigo wa kukopa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kupunguza utegemezi wa kibajeti kutoka kwa Washirika wa Maendeleo.
📸:W/Fedha -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Neno kutoka kwa Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb).
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
BADO SIKU 2
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Swahili Times
@swahilitimes
Serikali imesema itaendelea kutekeleza miradi ya maendeleo ambayo ilikuwa ikipata ufadhili wa kifedha kupitia taasisi za Marekani baada ya tamko la usitishaji wa misaada lililotolewa na Rais Donald Trump.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Michuzi Blog
@michuziblog
#michuzitv_updates:-WAZIRI wa Fedha,Mwigulu Nchemba amesema Serikali itaendelea kuvutia ushiriki wa sekta binafsi katika ugharamiaji wa miradi ya maendeleo kwa kutumia njia mbadala ikiwemo ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi. @mwigulunchemba1
👇
www.instagram.com/p/DKY7HWRN2lr/ -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Haki Ngowi
@Hakingowi
📍Abidjan,Côte d’Ivoire.
▪️DKT. NCHEMBA AIPA KONGOLE AfDB KWA KUCHANGIA MAENDELEO YA TANZANIA
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) amesema kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatambua kwa dhati na kuthamini ushirikiano wa karibu na wa kimkakati na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) uliochangia utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo ya miundombinu, nishati, maji, kilimo, na ustawi wa kijamii.
Mhe. Dkt. Nchemba amesema hayo wakati akitoa majumuisho ya uwakilishi wa Tanzania katika Mkutano wa 60 wa Baraza la Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na Mkutano wa 51 wa Baraza la Magavana wa Mfuko wa Maendeleo wa Benki hiyo (ADF), iliyofanyika katika Hoteli ya Sofitel Ivoire, Abidjan, nchini Côte d’Ivoire.
Alisema kuwa katika miaka ya hivi karibuni, Tanzania imekuwa na ongezeko kubwa la ushirikiano na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), ambapo hivi sasa Serikali inatekeleza miradi ya maendeleo ya kimkakati 25 ikiwemo 21 ya Serikali (Tanzania Bara na Zanzibar) na miradi 4 ni ya sekta binafsi katika sekta za miundombinu, nishati, usafirishaji, maji, usafi wa mazingira, pamoja na kilimo, yote kwa pamoja ikiwa na thamani ya dola za Marekani bilioni 3.54.
Mhe. Dkt. Nchemba aliitaja baadhi ya miradi hiyo kuwa ni pamoja na Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR), Ujenzi wa Barabara za Mzungumko jijini Dodoma, ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Msalato mkoani Dodoma. ambayo kukamilika kwake kutaleta mageuzi makubwa ya kiuchumi nchini Tanzania.
“Kwa kuwa miradi hii inaendana na vipaumbele vya kitaifa na Ajenda ya Maendeleo ya 2063 ya Umoja wa Afrika pamoja na Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs), Tanzania inatarajia kuendelea kushirikiana na AfDB kupitia mikakati ya ADF-17 na vyanzo vingine vya fedha ili kuharakisha maendeleo jumuishi na endelevu kwa taifa na ukanda wa Afrika kwa ujumla” alisema Dkt. Nchemba.
Alisema kuwa chini ya Mfuko wa Maendeleo wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADF) mzunguko wa 17, Tanzania itaendelea kupata rasilimali fedha kwa kutumia mifumo mbalimbali ikiwemo dhamana za mkopo ili kusaidia miradi mikubwa ya miundombinu kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wa Tanzania.
Akizungumzia kuhusu Rais Mteule mpya wa Benki ya Maendeleo ya Afrika, Dkt. Sidi Quld Tah, alisema Rais huyo mpya wa AfDB si mgeni kwa Tanzania ambapo alimpongeza kwa ushindi wake na kwamba Tanzania itashirikiana naye kikamilifu kuhakikisha agenda za nchi za kuharakisha maendeleo yake zinafikiwa kama alivyofanya mtangulizi wake, Dkt. Akinumwi Adesina.
Benki ya Maendeleo ya Afrika, AfDB, imetimiza miaka 60 tangu kuzishwa kwake ikiwa na wanachama 81 zikiwemo nchi 54 za Afrika na imekuwa ikitoa mchango mkubwa wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika nchi hizo, ikiwemo Tanzania.
Mkutano huo wa Mwaka wa AfDB ulihudhuriwa pia na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Kamishna wa Fedha za Nje Wizara ya Fedha, Bw. Rished Bade, Katibu Msaidizi wa Baraza la Mawaziri, Bw. Fidelis Mkatte pamoja na maafisa wengine waandamizi kutoka Serikali ya Tanzania
📸:W/Fedha -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, amefanya mazungumzo na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anayemaliza muda wake Dkt. Akinumwi Adesina, kando ya Mkutano wa Mwaka wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) unaofanyika katika Hoteli ya Sofitel Ivoire Jijini Abidjan nchini Côte D’ivoire, ambapo pia Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), alishiriki Mkutano huo akiwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dennis Londo, Balozi wa Tanzania nchini Côte D’ivoire, mwenye Makazi yake nchini Nigeria Balozi Selestine Kakele, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba pamoja na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar, Dkt. Juma Malik Akil, ambapo pamoja na mambo mengine, walijadiliana namna ya kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Taasisi hiyo ya Fedha.
@vpo_tanzania @AfDB_Group -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), ameishukuru Benki ya Maendeleo ya Afrika Kusini (@DBSA_Bank ), kwa kushiriki katika ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR), mradi ambao ni muhimu kwa uchumi wa Tanzania na nchi jirani zitakazonufaika na mnyororo wa thamani wa mradi huo wa kikanda.
Mhe. Dkt. Nchemba amesema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Bi. Buitumelo Mosako, kando ya Mikutano ya Mwaka ya Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) iliyofanyika, Abidjan nchini Ivory Coast.
“Tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa Benki ya Maendeleo ya Afrika Kusini (DBSA) kwa mchango wenu muhimu katika kufadhili ujenzi wa SGR kipande cha 3 na 4 (Makutupora hadi Isaka) kwa kiasi cha dola za Marekani milioni 100. Zaidi ya hapo, tunatambua na kuthamini msaada wa kifedha wa kiasi cha dola milioni 100 uliotolewa awali kwa ajili ya kujenga kipande cha 2, ambao uliweka msingi imara kwa mradi mzima wa SGR” alisema Dkt. Nchemba
Alisema kuwa kutokana na juhudi hizo za pamoja, maendeleo ya ujenzi yamekuwa makubwa ambapo kipande cha 1 (Dar es Salaam hadi Makutupora) kimekamilika kwa asilimia 99.63 na treni imeanza kufanya kazi rasmi Julai 2024, wakati kipande cha 3 (Makutupora hadi Tabora) ujenzi wake umefikia asilimia 14.53, na kipande cha 4 (Tabora hadi Isaka) kimefikia asilimia 6.48.
“Bi. Boitumelo Mosako, kutokana na umuhimu wa mradi huu, nachukua fursa hii tena kuiomba benki yako iendelee kuunga mkono utekelezaji wa kipande cha 6 na 7 ya Reli ya Kisasa (SGR), ambavyo upatikanaji wake wa fedha za kutekeleza vipande hivyo unasimamiwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB).
Aliongeza kuwa Tanzania imefungua milango ya ushiriki wa sekta binafsi katika kuendesha mradi huo wa kimkakati ikiwemo uwekezaji wa mabewa na vichwa vya treni na kutoa wito kwa wawekezaji kuchangamkia fursa hiyo.
Aidha, Mhe. Dkt. Nchemba aliishukuru Benki hiyo kwa kuonesha utayari wake wa kutaka kuwekeza zaidi katika maendeleo ya Tanzania katika sekta za elimu, maji, afya, ujenzi wa miundombinu pamoja na kilimo.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya DBSA, Bi. Buitumelo Mosako, alisema kuwa milango ya ushirikiano na Tanzania iko wazi na kwamba Benki yake ina subiri kukamilika kwa Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2050 ili waweze kuangalia maeneo ya kushirikiana.
Alisisitiza kuwa Benki yake iko tayari kuwekeza zaidi Tanzania katika kusaidia miradi ya kimkakati na kijamii katika sekta za maji, afya, nishati, uchumi wa kidigitali, ujenzi wa makazi ya gharama nafuu na ujenzi wamiundombinu mbalimbali.
Kikao hicho kimehudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Katibu Msaidizi wa Baraza la Mawaziri, Bw. Fidelis Mkatte, Kamishna wa Fedha za Nje Wizara ya Fedha, Bw. Rished Bade, Kamishna wa Idara ya Usimamizi wa Deni la Serikali, Wizara ya Fedha, Bw. Japhet Justine, pamoja na maafisa wengine waandamizi kutoka Serikali ya Tanzania. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), ameongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa kawaida wa Magavana wa Eneo la Afrika Mashariki la Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) uliofanyika katika Hoteli ya Tiama, Jijini Abidjan nchini Côte d'Ivoire, ambao ni mkutano wa kisheria unaowashirikisha Magavana, Magavana Mbadala, Wawakilishi wa Muda, pamoja na wajumbe maalum (kawaida wajumbe wawili) kutoka kila nchi za Afrika Mashariki, Mkurugenzi Mtendaji pamoja na wafanyakazi wa Ofisi ya Eneo husika.
Eneo la Afrika Mashariki ndani ya Benki ya Maendeleo ya Afrika linajumuisha nchi tisa (9), ambazo ni: Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Ethiopia, Somalia, Sudan Kusini, Eritrea, na Shelisheli.
Kwa sasa, Eneo hili linawakilishwa kwenye Bodi ya Wakurugenzi na Mkurugenzi Mtendaji Bw. Jonathan Nzayikorera kutoka nchini Rwanda. Mwenyekiti wa Eneo hilo aliyemaliza muda wake wa miaka mitatu ni Mhe. Dkt. Uzziel Ndagijimana, ambaye pia ni Gavana (Waziri wa Fedha) wa Rwanda.
Mkutano huo ulihudhuriwa pia na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali, ambaye pia ni Gavana Mbadala (Alternating Governor) wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB), Dkt. Natu El-maamry Mwamba na Kamishna wa Idara ya Fedha za Nje Wizara ya Fedha ambaye pia kwa sasa ni Mkurugenzi Mtendaji Mbadala wa AfDB, Bw. Rished Bade.
@AfDB_Group -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Haki Ngowi
@Hakingowi
📍Abidjan, Côte d’Ivoire
▪️DKT. NCHEMBA AKUTANA NA RAIS WA AFDB ANAYEMALIZA MUDA WAKE DKT. AKWINUMI ADESINA-ABIDJAN
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb), kushoto, akifurahia jambo na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anayemaliza muda wake, Dkt. Akwinumi Adesina, walipokuta katika Hoteli ya Sofitel Ivoire, Abidjan, Côte d’Ivoire, mahali ambapo unafanyika Mkutano Mkuu wa mwaka 2025, ambao utakuwa wa 60 wa Bodi ya Magavana wa AfDB na wa 51 kwa Mfuko wa Maendeleo wa Benki hiyo (ADF), ulioanza jana tarehe 26 hadi 30 Mei 2025, na utajumuisha uchaguzi wa Rais mpya wa Benki hiyo atakayemrithi Dkt. Adesina ambaye ni raia wa Nigeria na pia utafanyika uchaguzi wa Wakurugenzi Watendaji wa Taasisi hiyo kubwa ya fedha barani Afrika.
Zaidi ya wajumbe 6,000 wanatarajiwa kuhudhuria, wakiwemo Marais na Wakuu wa Serikali za Afrika, Mawaziri wa Fedha, Magavana wa Mabenki Kuu, washirika wa maendeleo, wawakilishi wa sekta binafsi, viongozi wa asasi za kiraia, wasomi, taasisi za utafiti, NGOs, na wadau wengine. Ukiwa na Kaulimbiu "Kufanya Rasilimali za Afrika Kufanya Kazi kwa Maendeleo ya Afrika".
Mhe. Dkt. Nchemba anamtaja Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB anayemaliza mhula wake, Dkt. Akwinumi Adesina, kuwa ni kiongozi mahili na mtu muhimu katika maendeleo ya Tanzania tangu alipochukua uongozi wa Taasisi hiyo ambapo kupitia ufadhili wa miradi ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii, Tanzania imepiga hatua kubwa kimaendeleo.
📸:W/Fedha -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), kushoto, akifurahia jambo na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (@AfDB_Group ) anayemaliza muda wake, Dkt. @akin_adesina , walipokuta katika Hoteli ya Sofitel Ivoire, Abidjan, Côte d’Ivoire, mahali ambapo unafanyika Mkutano Mkuu wa mwaka 2025, ambao utakuwa wa 60 wa Bodi ya Magavana wa AfDB na wa 51 kwa Mfuko wa Maendeleo wa Benki hiyo (ADF), ulioanza jana tarehe 26 hadi 30 Mei 2025, na utajumuisha uchaguzi wa Rais mpya wa Benki hiyo atakayemrithi Dkt. Adesina ambaye ni raia wa Nigeria na pia utafanyika uchaguzi wa Wakurugenzi Watendaji wa Taasisi hiyo kubwa ya fedha barani Afrika.
Zaidi ya wajumbe 6,000 wanatarajiwa kuhudhuria, wakiwemo Marais na Wakuu wa Serikali za Afrika, Mawaziri wa Fedha, Magavana wa Mabenki Kuu, washirika wa maendeleo, wawakilishi wa sekta binafsi, viongozi wa asasi za kiraia, wasomi, taasisi za utafiti, NGOs, na wadau wengine. Ukiwa na Kaulimbiu "Kufanya Rasilimali za Afrika Kufanya Kazi kwa Maendeleo ya Afrika".
Mhe. Dkt. Nchemba anamtaja Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB anayemaliza mhula wake, Dkt. Akwinumi Adesina, kuwa ni kiongozi mahili na mtu muhimu katika maendeleo ya Tanzania tangu alipochukua uongozi wa Taasisi hiyo ambapo kupitia ufadhili wa miradi ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii, Tanzania imepiga hatua kubwa kimaendeleo. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, akizungumza jambo na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), kando ya Mkutano Mkuu wa mwaka 2025 ambao utakuwa wa 60 wa Bodi ya Magavana wa ADB na wa 51 kwa ADF, unaoanza leo tarehe 26 hadi 30 Mei 2025 katika Hoteli ya Sofitel Ivoire, Abidjan, Côte d’Ivoire, na utajumuisha uchaguzi wa Rais na Wakurugenzi Watendaji wa Taasisi hiyo baada ya Rais wake wa sasa, Dkt. Akwinumi Adesina, kumaliza muda wake.
Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, anaongoza ujumbe wa Tanzania katika Mikutano ya Mwaka ya AfDB ambayo ni tukio muhimu zaidi la Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB). Hutoa fursa kwa Kundi la Benki – likijumuisha Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB), Mfuko wa Maendeleo ya Afrika (ADF), na Mfuko Maalum wa Nigeria – kufanya tathmini ya maendeleo ya mwaka uliopita pamoja na wanahisa. Pia ni jukwaa mahsusi kwa viongozi wa serikali na washiriki wengine, wakiwemo waandishi wa habari, kujadili masuala muhimu ya maendeleo ya Afrika.
Zaidi ya wajumbe 6,000 wanatarajiwa kuhudhuria, wakiwemo Marais na Wakuu wa Serikali za Afrika, Mawaziri wa Fedha, Magavana wa Mabenki Kuu, washirika wa maendeleo, wawakilishi wa sekta binafsi, viongozi wa asasi za kiraia, wasomi, taasisi za utafiti, NGOs, na wadau wengine.
Kaulimbiu ya mwaka huu ni "Kufanya Rasilimali za Afrika Kufanya Kazi kwa Maendeleo ya Afrika". Lengo ni kutambua na kutumia rasilimali mbalimbali za Afrika – watu, maliasili, fedha, na biashara – kwa ajili ya mabadiliko ya kimuundo ya bara hili. Malengo ni kukuza uchumi jumuishi, wa kijani na wenye ustahimilivu, huku yakihamasisha ushirikiano wa kimataifa wa kifedha.
Mkutano pia utajadili masuala mtambuka kama mageuzi ya kidijitali, uimarishaji wa taasisi na utawala bora. Haya yote yanalingana na utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs), Mkataba wa Paris wa Mabadiliko ya Tabianchi, Ajenda 2063 ya Umoja wa Afrika, na Mikakati Kuu Mitano ya Benki ya Maendeleo ya Afrika (High 5s).
Mbali na mikutano rasmi ya Bodi ya Magavana, kutakuwa na matukio ya maarifa yaliyoandaliwa na Benki pamoja na nchi mwenyeji, Côte d’Ivoire.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba na Katibu Mkuu ambaye pia ni Mlipaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania, Dkt. Natu Elmaamry Mwamba, ni miongoni mwa Magavana na Magavana Mbadala wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), mtawalia.
@AfDB_Group @vpo_tanzania -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
MR BEN
@Eric__Bernard
Dodoma Imeitikaaaaaaa
Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa!!!!This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Lemutuz TV
@lemutuztv
Waziri wa Fedha @mwigulunchemba1 ambaye ni Mjumbe ndani ya Klabu ya Yanga anga SC amewataka Watanzania Wote kuweka tofauti zao pembeni kwa leo na kuiombea Klabu ya Simba SC ushindi katika Mchezo wa leo dhidi ya RS Berkane Fainali ya pili kombe la Shirikisho Afrika, kwani Simba wakishinda Ubingwa heshima inabaki Tanzania na Sio Simba pekee.
#lemutuzupdates -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
PAN-AFRICANISM.
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Haki Ngowi
@Hakingowi
▪️MAMBO YA KIHISTORIA YALIYOFANYWA NA RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN MPAKA SASA
▪️Amekuza Demokrasia
▪️Amekuza Mahusiano Kimataifa
▪️Amekuza Uchumi
▪️Ameanzisha Miradi Mipya
▪️Amemalizia Miradi Aliyoikuta
▪️Matibabu Bure Wazee na Watoto
▪️Amekuza Sekta ya Madini
▪️Ameongeza Bajeti ya Kilimo
▪️Amepeleka Umeme kila Kijiji
▪️Amejenga Madarasa kila Shule
▪️Amevutia Wawekezaji
▪️Analinda Amani ya Tanzania
▪️Ameajiri Watumishi Wengi
▪️Amewapa Mikopo Wasanii
▪️Amekuza Utalii
▪️Amejenga Mtandao Mkubwa wa Barabara -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
PAN-AFRICANISM.
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Haki Ngowi
@Hakingowi
📍Arusha
▪️DKT. NCHEMBA AHIMIZA USHIRIKIANO WA NCHI ZA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), ameongoza ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano wa 17 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wanaosimamia masuala ya fedha na uchumi la Jumuiya ya Afrika Mashariki (17th SCFEA), uliofanyika Makao Makuu ya Jumuiya hiyo Jijini Arusha, leo tarehe 20 Mei, 2025, ambapo amehimiza nchi wanachama kuimarisha zaidi utengamano wa kikanda ili kuharakisha maendeleo ya nchi hizo.
Mkutano huo, pamoja na masuala mengine, umejadili taarifa ya mashauriano ya kibajeti kuhusu viwango vya pamoja vya Ushuru wa Forodha vya Afrika Mashariki kwa mwaka 2025/26; kupokea na kujadili Taarifa ya Utekelezaji wa Maamuzi ya Mkutano wa 16 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wanaosimamia masuala ya Fedha na Uchumi (16th SCFEA); na kupokea na kujadili Taarifa ya Mkutano wa Kamati ya Kikanda ya Ufuatiliaji wa Utekelezaji wa Umoja wa Fedha wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Aidha, agenda nyingine ilikuwa kupokea na kujadili taarifa ya mkutano wa pamoja wa Kamati ya Kisekta ya Masuala ya Bajeti na Kamati Ndogo ya masuala ya Fedha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki; kupokea na kujadili taarifa ya Warsha ya 11 ya kikanda ya Masuala ya Usimamizi wa Fedha na Bajeti na kupokea na kujadili taarifa ya Mkutano wa 28 wa Kamati ya Masuala ya Fedha (MAC).
Vile vile, mkutano umepokea wasilisho la nchi wanachama kuhusu mwenendo wa viashiria vya uchumi jumla, hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa vigezo vya uchumi jumla vya mtangamano wa kikanda na vipaumbele vya bajeti kwa mwaka 2025/26 kutoka kwa nchi wanachama; kujadili dhima za bajeti za nchi wanachama kwa mwaka 2025/26; pamoja na kubuni kauli mbiu moja ya bajeti ya EAC.
📸:W/Fedha -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), ameongoza ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano wa 17 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wanaosimamia masuala ya fedha na uchumi la Jumuiya ya Afrika Mashariki (17th SCFEA), uliofanyika Makao Makuu ya Jumuiya hiyo Jijini Arusha, leo tarehe 20 Mei, 2025, ambapo amehimiza nchi wanachama kuimarisha zaidi utengamano wa kikanda ili kuharakisha maendeleo ya nchi hizo.
Mkutano huo, pamoja na masuala mengine, umejadili taarifa ya mashauriano ya kibajeti kuhusu viwango vya pamoja vya Ushuru wa Forodha vya Afrika Mashariki kwa mwaka 2025/26; kupokea na kujadili Taarifa ya Utekelezaji wa Maamuzi ya Mkutano wa 16 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wanaosimamia masuala ya Fedha na Uchumi (16th SCFEA); na kupokea na kujadili Taarifa ya Mkutano wa Kamati ya Kikanda ya Ufuatiliaji wa Utekelezaji wa Umoja wa Fedha wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Aidha, agenda nyingine ilikuwa kupokea na kujadili taarifa ya mkutano wa pamoja wa Kamati ya Kisekta ya Masuala ya Bajeti na Kamati Ndogo ya masuala ya Fedha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki; kupokea na kujadili taarifa ya Warsha ya 11 ya kikanda ya Masuala ya Usimamizi wa Fedha na Bajeti na kupokea na kujadili taarifa ya Mkutano wa 28 wa Kamati ya Masuala ya Fedha (MAC).
Vile vile, mkutano umepokea wasilisho la nchi wanachama kuhusu mwenendo wa viashiria vya uchumi jumla, hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa vigezo vya uchumi jumla vya mtangamano wa kikanda na vipaumbele vya bajeti kwa mwaka 2025/26 kutoka kwa nchi wanachama; kujadili dhima za bajeti za nchi wanachama kwa mwaka 2025/26; pamoja na kubuni kauli mbiu moja ya bajeti ya EAC. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
East African Community
@jumuiya
📍JUST IN
✍️ 17th Meeting of the Sectoral Council on Finance and Economic Affairs - #ministerialsession
17th Meeting of the Sectoral Council on Finance and Economic Affairs #scfea concluded successfully today in Arusha, Tanzania, bringing together Finance and Economic Affairs Ministers from across the region to discuss pressing issues and collaborative strategies for sustainable economic growth.
➡️ Key highlights from the meeting included consideration of the reports on ;
🔹Monetary Affairs Committee & the status of the East African Monetary Union -#eamu Roadmap
🔹 Implementation of the Customs Union and Common Market Protocols
🔹 Establishment of the East African Monetary Institute (EAMI) and other #eamu Institutions
🔹 Harmonization of Payment and Settlement Systems &
🔹 Contributions of the EAC Partner States to the EAC Main Budget
@SMannette1 -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
TUTAILINDA NCHI YETU KWA WIVU MKUBWA, TUSICHEZEANE.
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
HONGERA PROF. JANABI UMETUFUTA MACHOZI.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Wizara ya Afya Tanzania 🇹🇿
@wizara_afyatz
Hongera Prof. Mohammed Janabi kwa kuchaguliwa kuwa Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Afrika
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
JIMBO LA IRAMBA MAGHARIBI
@jimbolairamba
Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi na Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 akionyesha kadi yake ya mpiga kura mara baada ya kushiriki zoezi la uboreshaji wa taarifa zake katika Daftari la Kudumu la Mpiga Kura Mei 17, 2025 katika Ofisi ya Kijiji Misigiri, Wilayani Iramba
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), leo ameongoza kwa vitendo katika kutekeleza haki yake ya msingi ya kidemokrasia kwa kuboresha taarifa zake za Mpiga Kura katika Kituo cha Ofisi ya Mtendaji wa Kijiji cha Misigiri, Wilaya ya Iramba, Mkoa wa Singida.
Uboreshaji huu ni sehemu ya Awamu ya Pili ya zoezi la kitaifa la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na Uwekaji Wazi wa Daftari la Awali, linaloendelea kote nchini kuanzia tarehe 16 hadi 22 Mei 2025, Tanzania Bara na Zanzibar. Vituo vyote vinapokea wananchi kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni kila siku.
Mhe. Dkt. Nchemba amesisitiza umuhimu wa kila Mtanzania kutumia haki na wajibu huu wa kikatiba kwa kujitokeza kuboresha taarifa zao, kuhakiki usahihi wa taarifa, na kuhakikisha kuwa wako tayari kushiriki kikamilifu katika uchaguzi Mkuu ujao. Amesema: “Uchaguzi ni haki, ni wajibu, na ni chombo cha kulinda amani, maendeleo na usalama wa Taifa letu. Tujitokeze wote.”
Wananchi wote wanaohitaji kuboresha taarifa zao, kujiandikisha kwa mara ya kwanza au kuthibitisha majina yao katika daftari, wanakumbushwa kujitokeza kwa wakati kwenye vituo vyao. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), amekutana nakufanya mazungumzo na Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe. Chen Mingjian, katika ofisi yake jijini Dodoma, ambapo wamejadiliana namna ya kushirikiana zaidi katika masuala ya kiuchumi kwa ajili ya faida ya wananchi wa pande hizo mbili, mazungumzo yaliyofanyika baada ya kushiriki hafla ya kusaini mikataba miwili ya msaada wa jumla ya Yuan za China milioni 500, sawa na shilingi bilioni 185 kwa ajili ya mradi wa upanuzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete pamoja na kusaidia program ya ushirikiano wa kiuchumi na kitaalamu.
@ChineseEmbTZ -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China zimetia Saini mikataba miwili ya msaada wa jumla ya Yuan za China milioni 500, sawa na shilingi bilioni 185 kwa ajili ya mradi wa upanuzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete pamoja na kusaidia program ya ushirikiano wa kiuchumi na kitaalamu.
Mikataba hiyo imesainiwa Ofisi za Wizara ya Fedha (Treasury Square) na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb) kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe. Chen Mingjian.
Akizungumza baada ya kusainiwa kwa mikataba hiyo, Dkt. Nchemba, alisema kuwa Mkataba wa kwanza ni wa Ushirikiano wa Kiuchumi na Kitaalam wenye thamani ya Yuan za China milioni 200 sawa na shilingi bilioni 74.2 na Mkataba wa pili kwa ajili ya mradi wa Upanuzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete kuwa Kituo cha Umahiri cha matibabu na upasuaji wa moyo Afrika Mashariki na Kati wenye thamani ya Yuan za China milioni 300, sawa na shilingi bilioni 111.2.
“Lengo la misaada hii ni kuwezesha utekelezaji wa miradi itakayochaguliwa na kukubalika kwa pamoja na Serikali za Tanzania na China, na mkataba wa pili una lengo la kujenga Kituo cha Umahiri cha Matibabu ya Magonjwa ya Moyo ya Watoto kwa ajili ya Tanzania na nchi za Afrika Mashariki na Kati”, alieleza Dkt. Nchemba.
.
Dkt. Nchemba alisema kuwa, msaada wa Ushirikiano wa kiuchumi na Kitaalamu ni ahadi aliyoitoa Mhe. Xi Jinping, Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, wakati wa kikao chake na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati wa Mkutano wa Jukwaa la Tisa la Kilele la Ushirikiano wa China na Afrika la mwaka 2024, uliofanyika jijini Beijing.
Alisema kuwa msaada wa ujenzi wa hospitali ya magonjwa ya moyo kwa watoto Mloganzila - unatarajiwa kuleta manufaa makubwa kama vile upatikanaji wa huduma bora za afya, kukuza uchumi kupitia kuongeza ajira na kuchochea biashara kwa wananchi ili kuboresha maisha yao, kukuza utafiti katika masuala ya afya na elimu na kuendeleza miundombinu.
Alisema kuwa misaada hiyo inadhihirisha kwamba Jamhuri ya Watu wa China inabaki kuwa rafiki wa kweli na wa kutumainiwa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuahidi kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kimaendeleo na kuendelea kudumisha urafiki wa muda mrefu kwa manufaa ya pande hizo mbili.
Aidha amemhakikishia Balozi huyo wa China utayari wa Serikali ya Tanzania chini ya uongozi wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuendelea kuimarisha ushirikiano na Serikali ya China.
Kwa upande wa Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe.Chen Mingjian, alisema kuwa nchi yake itaendelea kushirikiana na Tanzania kutokana na ushirikiano wa kihistoria wa muda mrefu na pia imani ya Tanzania kwa nchi hiyo katika kukuza maendeleo ya wananchi.
Aidha alisema kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi kinara yenye ushirikiano bora wa kiuchumi na kijamii na imeshirikiana na Tanzania katika nyanja mbalimbali za maendeleo ikiwemo ujenzi wa reli ya TAZARA, mradi ambao umekuwa wa kielelezo cha uhusiano huo.
Alisema kuwa msaada wa sekta ya afya kupitia Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete ambao umelenga kunusuru maisha ya watoto wanaougua maradhi ya moyo, pia utakuza ajira na kuwa sehemu ya utalii wa kimatibabu watakaokuja nchini kutoka mataifa mengine.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Dkt. Peter Kisenge, aliishukuru China kwa ufadhili huo utakao kuwa mkombozi mkubwa wa matibabu ya moyo kwa watoto kupitia ujenzi wa Kituo hicho cha Umahiri kitakachojengwa katika Hospitali ya Mloganzila.
Alisema kuwa changamoto ya kiafya kwa watoto inayosababishwa na maradhi ya moyo ni kubwa ambapo takwimu zinaonesha kuwa kati ya Watoto 200 wanaozaliwa, Watoto wawili wanazaliwa wakiwa na matatizo ya moyo na kwamba ujenzi wa Kituo hicho cha umahiri utaondoa changamoto ya matibabu.
Hafla hiyo ilihudhuriwa pia na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Mhe. Ismail Rumatila, ambaye aliahidi kuwa Serikali itasimamia utekelezaji wa mradi huo kama ilivyokusudiwa ili kuleta tija na kuboresha upatikanaji wa huduma na matibabu ya magonjwa ya moyo nchini. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Haki Ngowi
@Hakingowi
📍Dodoma
🇹🇿🇨🇳
▪️TANZANIA YAPOKEA MSAADA WA SH. BILIONI 185 KUTOKA CHINA
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China zimetia Saini mikataba miwili ya msaada wa jumla ya Yuan za China milioni 500, sawa na shilingi bilioni 185 kwa ajili ya mradi wa upanuzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete pamoja na kusaidia program ya ushirikiano wa kiuchumi na kitaalamu.
Mikataba hiyo imesainiwa Ofisi za Wizara ya Fedha (Treasury Square) na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe. Chen Mingjian.
Akizungumza baada ya kusainiwa kwa mikataba hiyo, Dkt. Nchemba, alisema kuwa Mkataba wa kwanza ni wa Ushirikiano wa Kiuchumi na Kitaalam wenye thamani ya Yuan za China milioni 200 sawa na shilingi bilioni 74.2 na Mkataba wa pili kwa ajili ya mradi wa Upanuzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete kuwa Kituo cha Umahiri cha matibabu na upasuaji wa moyo Afrika Mashariki na Kati wenye thamani ya Yuan za China milioni 300, sawa na shilingi bilioni 111.2.
“Lengo la misaada hii ni kuwezesha utekelezaji wa miradi itakayochaguliwa na kukubalika kwa pamoja na Serikali za Tanzania na China, na mkataba wa pili una lengo la kujenga Kituo cha Umahiri cha Matibabu ya Magonjwa ya Moyo ya Watoto kwa ajili ya Tanzania na nchi za Afrika Mashariki na Kati”, alieleza Dkt. Nchemba.
.
Dkt. Nchemba alisema kuwa, msaada wa Ushirikiano wa kiuchumi na Kitaalamu ni ahadi aliyoitoa Mhe. Xi Jinping, Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, wakati wa kikao chake na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati wa Mkutano wa Jukwaa la Tisa la Kilele la Ushirikiano wa China na Afrika la mwaka 2024, uliofanyika jijini Beijing.
Alisema kuwa msaada wa ujenzi wa hospitali ya magonjwa ya moyo kwa watoto Mloganzila - unatarajiwa kuleta manufaa makubwa kama vile upatikanaji wa huduma bora za afya, kukuza uchumi kupitia kuongeza ajira na kuchochea biashara kwa wananchi ili kuboresha maisha yao, kukuza utafiti katika masuala ya afya na elimu na kuendeleza miundombinu.
Alisema kuwa misaada hiyo inadhihirisha kwamba Jamhuri ya Watu wa China inabaki kuwa rafiki wa kweli na wa kutumainiwa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuahidi kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kimaendeleo na kuendelea kudumisha urafiki wa muda mrefu kwa manufaa ya pande hizo mbili.
Aidha amemhakikishia Balozi huyo wa China utayari wa Serikali ya Tanzania chini ya uongozi wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuendelea kuimarisha ushirikiano na Serikali ya China.
Kwa upande wa Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe.Chen Mingjian, alisema kuwa nchi yake itaendelea kushirikiana na Tanzania kutokana na ushirikiano wa kihistoria wa muda mrefu na pia imani ya Tanzania kwa nchi hiyo katika kukuza maendeleo ya wananchi.
Aidha alisema kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi kinara yenye ushirikiano bora wa kiuchumi na kijamii na imeshirikiana na Tanzania katika nyanja mbalimbali za maendeleo ikiwemo ujenzi wa reli ya TAZARA, mradi ambao umekuwa wa kielelezo cha uhusiano huo.
Alisema kuwa msaada wa sekta ya afya kupitia Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete ambao umelenga kunusuru maisha ya watoto wanaougua maradhi ya moyo, pia utakuza ajira na kuwa sehemu ya utalii wa kimatibabu watakaokuja nchini kutoka mataifa mengine.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Dkt. Peter Kisenge, aliishukuru China kwa ufadhili huo utakao kuwa mkombozi mkubwa wa matibabu ya moyo kwa watoto kupitia ujenzi wa Kituo hicho cha Umahiri kitakachojengwa katika Hospitali ya Mloganzila.
Alisema kuwa changamoto ya kiafya kwa watoto inayosababishwa na maradhi ya moyo ni kubwa ambapo takwimu zinaonesha kuwa kati ya Watoto 200 wanaozaliwa, Watoto wawili wanazaliwa wakiwa na matatizo ya moyo na kwamba ujenzi wa Kituo hicho cha umahiri utaondoa changamoto ya matibabu.
📸:W/Fedha -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Kwame Kivaisi
@kwamekivaisi
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Taasisi ya Moyo-JKCI
@TaasisiMoyoJKCI
Tanzania na China zimesaini Mkataba wa Msaada wa Shilingi Bilioni 111.2 kwa ajili ya mradi wa upanuzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete eneo la Mloganzila kuwa Kituo cha Umahiri cha matibabu ya moyo kwa watoto Afrika Mashariki na Kati
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
JIMBO LA IRAMBA MAGHARIBI
@jimbolairamba
Ewe mwana Iramba usipoteze nafasi hii muhimu tumia siku Saba kuanzia Mei 16 -22,2025 kuboresha Taarifa zako na wale ambao hawakupata fursa kwenye zoezi lililopita kujitokeza kujiandikisha
Usipoteze fursa hii ujanja ni kujiandikisha.Mimi Nitashiriki wewe je ?
@mwigulunchemba1 -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Nicol Adamcova
@CZAmb_Nairobi
Signing the Double Taxation Avoidance Agreement between #czechia and #tanzania. In Dar es Salaam, with @mwigulunchemba1, Hon. Minister of Finance. Important milestone promoting trade & investment. Follow-up of the meeting of Foreign Ministers @JanLipavsky & @mahmoudkombo.
🇨🇿🤝🇹🇿
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
🇹🇿🇨🇿
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Czech zimetia saini Mkataba wa Kuondoa Utozaji Kodi ya Mapato Mara Mbili na Kuzuia Ukwepaji Kodi, hatua itakayosaidia kufungua uchumi wa nchi kwa kuvutia uwekezaji wa kimataifa na utawezesha wawekezaji na wafanyabiashara wanaofanya shughuli kati ya Tanzania na Czech.
Mkataba huo ujulikanao kama Agreement on the Avoidance of Double Taxation and Prevention of Fiscal Avoidance and Evasion in Respect to Tax on Income, umesainiwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), kwa niaba ya Tanzania, na Balozi wa Jamhuri ya Czech nchini Tanzania mwenye makazi yake ya kudumu nchini Kenya, Mhe. Nicol Adamcová ( @CZAmb_Nairobi ), kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Czech, katika hafla iliyofanyika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza baada ya kusaini mkataba huo, Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), alisema kuwa mkataba huo utasaidia kuondoa hatari ya kipato kilekile kutozwa kodi mara mbili katika nchi mbili tofauti, kuhamasisha sera za haki za kikodi, na kuimarisha imani ya wawekezaji.
“Mkataba huu ni hatua muhimu katika jitihada za Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kufungua uchumi wa nchi kwa kuvutia uwekezaji wa kimataifa na utawezesha wawekezaji na wafanyabiashara wanaofanya shughuli kati ya Tanzania na Czech” alisema Dkt. Nchemba.
Aliongeza kuwa Takwimu za Shirika la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo (OECD) zinaonesha kuwa nchi zilizo na mikataba madhubuti ya kuepusha kodi ya maradufu huvutia hadi asilimia 30 zaidi ya uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje, ikilinganishwa na zile zisizo na mikataba hiyo.
“kupitia Mkataba huu tunatarajia kuvutia mitaji mikubwa kutoka Czech kuja kuwekeza Tanzania, hususan katika sekta za kutengeneza magari na ndege, vifaa vya umeme, mitambo na mashine mbalimbali na kupitia uwekezaji huo, Tanzania inatarajia kunufaika na ukuaji wa sekta za uzalishaji, maendeleo ya viwanda, na kuongezeka kwa ajira kwa wananchi” alisema Mhe. Dkt. Nchemba.
Kwa upande wake Balozi wa Jamhuri ya Czech nchini Tanzania mwenye makazi yake nchini Kenya, Mhe. Nicol Adamcová, alisema kuwa ushirikiano kati ya Tanzania na Czech ni wa muda mrefu na wenye tija, hivyo kusainiwa kwa mkataba huo utawapa fursa kwa wawekezaji wa Kitanzania kuwekeza nchini Czech bila vizuizi vya kikodi.
“Nina furaha kubwa kuwa tumetia saini mkataba huu na ni jambo muhimu, ni kipengele cha msingi kinachoonyesha kuwa kuna kiwango cha juu cha kuaminiana kati ya nchi zetu mbili, kama isingekuwa hivyo, tusingetumia muda na nguvu kujadiliana kuhusu” alisema Mhe. Adamcová.
Aliongeza kuwa makubaliano hayo ni muhimu na ni ushahidi muhimu wa utulivu wa mazingira na hali ya biashara katika nchi hizi mbili.
Kwa mujibu wa takwimu za UN COMTRADE, mwaka 2022 biashara baina ya Tanzania na Czech ilifikia takribani dola milioni 16.2 za Kimarekani, hasa katika sekta za mitambo, vifaa vya umeme, teknolojia za usafirishaji, na bidhaa za kilimo. Mkataba huu unatarajiwa kuongeza zaidi kiwango cha biashara na uwekezaji kati ya pande hizo mbili. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Dcirambaofficial
@DCIRAMBA
Ewe mwana Iramba usipoteze nafasi hii muhimu tumia siku Saba kuanzia Mei 16 -22,2025 kuboresha Taarifa zako na wale ambao hawakupata fursa kwenye zoezi lililopita kujitokeza kujiandikisha
Usipoteze fursa hii ujanja ni kujiandikisha.Mimi Nitashiriki wewe je ?
@mwigulunchemba1 -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Haki Ngowi
@Hakingowi
📍Dar es Salaam
1-2:Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) na Balozi wa Jamhuri ya Czech nchini Tanzania mwenye makazi yake ya kudumu Nairobi-Kenya, Mhe. Nicol Adamcova, wakitia saini Mkataba wa Kuondoa Utozaji Kodi ya Mapato Mara Mbili na Kuzuia Ukwepaji Kodi (Agreement for the Elimination of Double Taxation with Respect to Taxes on Income and for the Prevention of Tax Evasion and Avoidance), katika ukumbi wa Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam, ambapo mkataba huo utawezesha wawekezaji na wafanyabiashara wanaofanya shughuli kati ya Tanzania na Czech kutozwa kodi mara moja pekee, badala ya mara mbili kwa mapato ya aina moja.
3:Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) na Balozi wa Jamhuri ya Czech nchini Tanzania mwenye makazi yake ya kudumu Nairobi-Kenya, Mhe. Nicol Adamcova, wakibadilishana Mkataba wa Kuondoa Utozaji Kodi ya Mapato Mara Mbili na Kuzuia Ukwepaji Kodi (Agreement for the Elimination of Double Taxation with Respect to Taxes on Income and for the Prevention of Tax Evasion and Avoidance), katika ukumbi wa Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam, ambapo mkataba huo utawezesha wawekezaji na wafanyabiashara wanaofanya shughuli kati ya Tanzania na Czech kutozwa kodi mara moja pekee, badala ya mara mbili kwa mapato ya aina moja.
4:Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) na Balozi wa Jamhuri ya Czech nchini Tanzania mwenye makazi yake ya kudumu Nairobi-Kenya, Mhe. Nicol Adamcova, wakionesha Mkataba wa Kuondoa Utozaji Kodi ya Mapato Mara Mbili na Kuzuia Ukwepaji Kodi (Agreement for the Elimination of Double Taxation with Respect to Taxes on Income and for the Prevention of Tax Evasion and Avoidance), katika ukumbi wa Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam, ambapo mkataba huo utawezesha wawekezaji na wafanyabiashara wanaofanya shughuli kati ya Tanzania na Czech kutozwa kodi mara moja pekee, badala ya mara mbili kwa mapato ya aina moja.
📸:W/Fedha
📃:W/Fedha
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Czech zimetia saini Mkataba wa Kuondoa Utozaji Kodi ya Mapato Mara Mbili na Kuzuia Ukwepaji Kodi, hatua itakayosaidia kufungua uchumi wa nchi kwa kuvutia uwekezaji wa kimataifa na utawezesha wawekezaji na wafanyabiashara wanaofanya shughuli kati ya Tanzania na Czech.
Mkataba huo ujulikanao kama Agreement on the Avoidance of Double Taxation and Prevention of Fiscal Avoidance and Evasion in Respect to Tax on Income, umesainiwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), kwa niaba ya Tanzania, na Balozi wa Jamhuri ya Czech nchini Tanzania mwenye makazi yake ya kudumu nchini Kenya, Mhe. Nicol Adamcová, kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Czech, katika hafla iliyofanyika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza baada ya kusaini mkataba huo, Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), alisema kuwa mkataba huo utasaidia kuondoa hatari ya kipato kilekile kutozwa kodi mara mbili katika nchi mbili tofauti, kuhamasisha sera za haki za kikodi, na kuimarisha imani ya wawekezaji.
“Mkataba huu ni hatua muhimu katika jitihada za Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kufungua uchumi wa nchi kwa kuvutia uwekezaji wa kimataifa na utawezesha wawekezaji na wafanyabiashara wanaofanya shughuli kati ya Tanzania na Czech” alisema Dkt. Nchemba.
Aliongeza kuwa Takwimu za Shirika la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo (OECD) zinaonesha kuwa nchi zilizo na mikataba madhubuti ya kuepusha kodi ya maradufu huvutia hadi asilimia 30 zaidi ya uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje, ikilinganishwa na zile zisizo na mikataba hiyo.
onyesha kuwa kuna kiwango cha juu cha kuaminiana kati ya nchi zetu mbili, kama isingekuwa hivyo, tusingetumia muda na nguvu kujadiliana kuhusu” alisema Mhe. Adamcová.
Aliongeza kuwa makubaliano hayo ni muhimu na ni ushahidi muhimu wa utulivu wa mazingira na hali ya biashara katika nchi hizi mbili. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
🇹🇿🇨🇿
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Czech zimetia saini Mkataba wa Kuondoa Utozaji Kodi ya Mapato Mara Mbili na Kuzuia Ukwepaji Kodi, hatua itakayosaidia kufungua uchumi wa nchi kwa kuvutia uwekezaji wa kimataifa na utawezesha wawekezaji na wafanyabiashara wanaofanya shughuli kati ya Tanzania na Czech.
Mkataba huo ujulikanao kama Agreement on the Avoidance of Double Taxation and Prevention of Fiscal Avoidance and Evasion in Respect to Tax on Income, umesainiwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), kwa niaba ya Tanzania, na Balozi wa Jamhuri ya Czech nchini Tanzania mwenye makazi yake ya kudumu nchini Kenya, Mhe. Nicol Adamcová ( @CZAmb_Nairobi ), kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Czech, katika hafla iliyofanyika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza baada ya kusaini mkataba huo, Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), alisema kuwa mkataba huo utasaidia kuondoa hatari ya kipato kilekile kutozwa kodi mara mbili katika nchi mbili tofauti, kuhamasisha sera za haki za kikodi, na kuimarisha imani ya wawekezaji.
“Mkataba huu ni hatua muhimu katika jitihada za Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kufungua uchumi wa nchi kwa kuvutia uwekezaji wa kimataifa na utawezesha wawekezaji na wafanyabiashara wanaofanya shughuli kati ya Tanzania na Czech” alisema Dkt. Nchemba.
Aliongeza kuwa Takwimu za Shirika la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo (OECD) zinaonesha kuwa nchi zilizo na mikataba madhubuti ya kuepusha kodi ya maradufu huvutia hadi asilimia 30 zaidi ya uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje, ikilinganishwa na zile zisizo na mikataba hiyo.
“kupitia Mkataba huu tunatarajia kuvutia mitaji mikubwa kutoka Czech kuja kuwekeza Tanzania, hususan katika sekta za kutengeneza magari na ndege, vifaa vya umeme, mitambo na mashine mbalimbali na kupitia uwekezaji huo, Tanzania inatarajia kunufaika na ukuaji wa sekta za uzalishaji, maendeleo ya viwanda, na kuongezeka kwa ajira kwa wananchi” alisema Mhe. Dkt. Nchemba.
Kwa upande wake Balozi wa Jamhuri ya Czech nchini Tanzania mwenye makazi yake nchini Kenya, Mhe. Nicol Adamcová, alisema kuwa ushirikiano kati ya Tanzania na Czech ni wa muda mrefu na wenye tija, hivyo kusainiwa kwa mkataba huo utawapa fursa kwa wawekezaji wa Kitanzania kuwekeza nchini Czech bila vizuizi vya kikodi.
“Nina furaha kubwa kuwa tumetia saini mkataba huu na ni jambo muhimu, ni kipengele cha msingi kinachoonyesha kuwa kuna kiwango cha juu cha kuaminiana kati ya nchi zetu mbili, kama isingekuwa hivyo, tusingetumia muda na nguvu kujadiliana kuhusu” alisema Mhe. Adamcová.
Aliongeza kuwa makubaliano hayo ni muhimu na ni ushahidi muhimu wa utulivu wa mazingira na hali ya biashara katika nchi hizi mbili.
Kwa mujibu wa takwimu za UN COMTRADE, mwaka 2022 biashara baina ya Tanzania na Czech ilifikia takribani dola milioni 16.2 za Kimarekani, hasa katika sekta za mitambo, vifaa vya umeme, teknolojia za usafirishaji, na bidhaa za kilimo. Mkataba huu unatarajiwa kuongeza zaidi kiwango cha biashara na uwekezaji kati ya pande hizo mbili. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
TRA Tanzania
@TRATanzania
#ubunifu Kama una wazo lako la ubunifu kuhusu namna ya kuongeza wigo wa kodi, tumia nafasi yako kujaribu bahati yako na ushinde! Tembelea Tovuti ya TRA (www.tra.go.tz) ujaze fomu maalum na kuwasilisha wazo lako.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
TRA Tanzania
@TRATanzania
#zawadi Hizi ndiyo zawadi kwa Wabunifu wa tuzo za ubunifu wa kuongeza wigo wa kodi. Changamkia fursa!.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
TRA Tanzania
@TRATanzania
#rewards These are the rewards for the innovators of the tax base increase awards. Seize the opportunity!
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
JIMBO LA IRAMBA MAGHARIBI
@jimbolairamba
ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU YA PILI MEI 16 - 22,2025
-
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Happy Mother’s Day to all. You are our wonderful moms, we celebrate you today and always.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Samia Suluhu
@SuluhuSamia
Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Bw. Charles Hilary, Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano Ikulu Zanzibar kilichotokea leo Mei 11, 2025.
Ninatoa pole kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Mwinyi, familia, ndugu, jamaa na marafiki na wadau wote wa sekta ya habari nchini kwa msiba huu.
Ndugu Charles Hilary atakumbukwa kwa mchango wake adhimu wa zaidi ya miaka 40 katika kukuza sekta ya habari nchini tangu akiwa redioni hadi kwenye televisheni, pamoja na unasihi kwa wanahabari wachanga.
Namuomba Mwenyezi Mungu aijaalie familia yake uvumilivu na subra katika kipindi hiki kigumu, na ailaze roho ya mpendwa wetu mahala pema.
Hakika sote ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake tutarejea. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Dcirambaofficial
@DCIRAMBA
MIAKA MINNE YA UONGOZI WA SERIKALI YA AWAMU YA SITA WILAYANI IRAMBA
Upatikanaji wa Maji safi na salama
@mwigulunchemba1
@ikulumawasliano
@Hakingowi -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), amewataka Watumishi wa Wizara ya Fedha, kutekeleza majukumu yao ya kila siku kwa kuzingatia misingi ya kazi na utawala bora ili kuepusha malalamiko yasiyo na lazima kutoka kwa wadau wake wakiwemo wananchi.
Mhe. Dkt. Nchemba alisema hayo wakati akifungua Mkutano wa 38 wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara ya Fedha, lililofanyika katika katika Kituo cha Mikutano cha APC, kilichoko Bunju mkoani Dar es Salaam.
Aidha, Mhe. Dkt. Nchemba aliutaka Uongozi wa Wizara kumchukulia hatua stahiki kwa mujibu wa taratibu mtumishi yeyote atakayebainika na kuthibitika kwenda kinyume na misingi ya maadili katika utendaji kazi ili kulinda heshima ya Wizara.
‘’Ninatambua kwamba mnafahamu misingi ya utendaji kazi katika utumishi wa umma, hivyo, si jambo jema kusikia mtumishi yeyote wa Wizara ya Fedha anakiuka misingi ya utawala bora katika utumishi wa umma’’, alisema Mhe. Dkt. Nchemba.
Pia, Mhe. Dkt. Nchemba aliwapongeza watumishi wote wa Wizara hiyo kwa kazi na mchango wao moubwa uliofanikisha majukumu yake ya kuismamia uchimi wa nchi na kuwezesha upatikanaji wa Fedha zinazotumika kutekeleza miradi mbalimbali ya kiuchumi na kijamii.
Aliwataka Watumishi wa Wizara kuendelea kufanyakazi kwa ushirikiano kati ya Watumishi ndani ya Idara, Wizara na Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Fedha, na kuzielekeza Taasisi kutekeleza majukumu yao ya msingi kama inavyoratajiwa na Serikali pamoja na wadau wengine.
Mhe. Dkt. Nchemba aliongeza kuwa kutokana na Uwekezaji mkubwa uliofanywa na Wizara katika kuwapatia mafunzo Watumishi wake, hivyo ni lazima matokeo ya mafunzo hayo yaonekane kwa vitendo kupitia utendaji wa kila mtumishi, na kusisitiza umuhimu wa Watumishi kuendelea kupatiwa mafunzo ya mara kwa mara ili kuboresha utendaji na kuendana na kasi ya mabadiliko ya teknolojia.
Awali, akimkaribisha Mgeni Rasmi, Mwenyekiti wa Baraza hilo la Watanyakazi ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, alisema kuwa lengo kuu la Baraza la Wafanyakazi ni kuwashirikisha Wafanyakazi katika utekelezaji wa shughuli za Wizara kwa kushirikiana na Uongozi ikiwa ni pamoja na kuishauri Wizara juu ya ufanisi wa kazi na hatua zinazofaa kuchukuliwa ili huduma zinazotolewa na Wizara zikidhi matarajo ya wateja.
Dkt. Mwamba aliongeza kuwa katika utekelezaji wa majukumu ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2024/25, Wizara imepata mafanikio mbalimbali yakiwezo kupandishwa vyeo kwa Watumishi 484 wa kada mbalimbali na kulipa jumla ya shilingi 521,980,765/= yakiwa ni malimbikizo ya mishahara kwa Watumishi wa Wizara.
"Aidha, katika mwaka wa fedha 2024/25 Serikali imeshatoa kibali ili watumishi wenye sifa waweze kupandishwa vyeo. Uchambuzi wa awali umebaini kwamba watumishi 313 wana sifa za kupandishwa vyeo’’ alisema Dkt. Mwamba.
Dkt. Mwamba aliongeza kuwa Mkutano wa 38 wa Baraza la Wafanyakazi ni mwendelezo wa mikutano mingine ambayo imekuwa ikifanyika kila mwaka ambapo kupitia mikutano hiyo wajumbe wamekuwa wakitoa maoni na mapendekezo ambayo yamesaidia kwa kiasi kikubwa kuboresha maslahi ya watumishi na utendaji kazi wa Wizara.
Mkutano wa 38 wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha, umekutanisha Wajumbe kutoka Makao Makuu ya Wizara, Wakuu wa Hazina Ndogo na Wahakikimali kutoka Mikoa yote ya Tanzania Bara. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Haki Ngowi
@Hakingowi
📍Dar es Salaam
▪️MHE. DKT. NCHEMBA AHANI MSIBA WA HAYATI CLEOPA MSUYA
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amefika kuhani msiba wa aliyekuwa Makamu wa Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Waziri Mkuu Mstaafu, na ambaye pia aliwahi kuwa Waziri wa Fedha na Mipango (1973–1975) na Waziri wa Fedha na Uchumi (1986–1989), Hayati David Cleopa Msuya, nyumbani kwake Upanga Jijini Dar es salaam.
Akizungumza na familia ya Hayati Msuya, Mhe. Dkt. Nchemba alisema kuwa, Hayati David Cleopa Msuya atakumbukwa kwa mchango mkubwa alioutoa katika uongozi wake wakati wa uhai wake ikiwemo kuweka misingi imara ya usimamizi wa uchumi wa nchi akiwa Waziri wa Fedha na nafasi nyingine alizozishika na kwamba wataenzi mchango wake huo kwa kuhakikisha kuwa uchumi unazidi kuimarika kwa manufaa ya wananchi.
📸:W/Fedha -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), amefika kuhani msiba wa aliyekuwa Makamu wa Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Waziri Mkuu Mstaafu, na ambaye pia aliwahi kuwa Waziri wa Fedha na Mipango (1973–1975) na Waziri wa Fedha na Uchumi (1986–1989), Hayati David Cleopa Msuya, nyumbani kwake Upanga Jijini Dar es salaam.
Akizungumza na familia ya Hayati Msuya, Mhe. Dkt. Nchemba alisema kuwa, Hayati David Cleopa Msuya atakumbukwa kwa mchango mkubwa alioutoa katika uongozi wake wakati wa uhai wake ikiwemo kuweka misingi imara ya usimamizi wa uchumi wa nchi akiwa Waziri wa Fedha na nafasi nyingine alizozishika na kwamba wataenzi mchango wake huo kwa kuhakikisha kuwa uchumi unazidi kuimarika kwa manufaa ya wananchi. -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Habemus Papam.
Viva il Papa. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
clickHabari
@clickHabari
Waziri wa Fedha Tanzania, Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba na Waziri wa Uchumi Msumbiji, Mhe. Basilio Zefanias Muhate wakitia saini Hati ya Makubaliano (Memorandum of Understanding) kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Msumbiji kuhusu Uanzishaji na Utekelezaji wa Kituo cha Pamoja cha Forodha (One Stop Border Post - OSBP) katika eneo la Mtambaswala/Negomano.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Taifa Daily
@TaifaDaily
The Minister of Finance of Tanzania, Hon. Mwigulu Lameck Nchemba, and the Minister of Economy of Mozambique, Hon. Basilio Zefanias Muhate, signed a Memorandum of Understanding (MoU) between the United Republic of Tanzania and the Republic of Mozambique on the Establishment and Implementation of a One Stop Border Post (OSBP) at the Mtambaswala/Negomano border area.
#taifadaily -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
The Citizen Tanzania
@TheCitizenTz
Tanzania boosts sports budget by 67 percent ahead of 2027 Afcon www.thecitizen.co.tz/tanzania/sports/tanzania-boosts-spor…
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Tanzania Agricultural Development Bank
@tadbtz
On 23 April 2025, TADB joined a key meeting with Hon. Dr. Mwigulu Nchemba Minister of Finance, IFAD President Alvaro Lario and team to strengthen ongoing cooperation. TADB is proud to be a beneficiary of IFAD’s AFDP and C-SDTP projects.
#tadb #ifad #afdp #csdtp -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Tanzia🕯️
-
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Nimesikitishwa sana na kifo cha Mzee Cleopa David Msuya, Makamu wa Kwanza wa Rais, Waziri Mkuu Mstaafu, na Waziri wa Fedha wa zamani. Atakumbukwa kwa uadilifu na mchango wake mkubwa kwa Taifa letu. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Samia Suluhu
@SuluhuSamia
Taarifa ya kifo cha Makamu wa Kwanza wa Rais na Waziri Mkuu Mstaafu, Mheshimiwa David Cleopa Msuya, kilichotokea leo katika Hospitali ya Kumbukumbu ya Emilio Mzena, Dar es Salaam.
Ninatoa pole kwa ndugu, jamaa, marafiki na Watanzania wote.
Apumzike kwa Amani.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Bank of Tanzania
@BankOfTanzania
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Dcirambaofficial
@DCIRAMBA
ZIARA YA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO WILAYA YA IRAMBA
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ahmad Issa Michuzi
@MichuziJr
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Mhe. Abdullah Bin Zayed Al Nahyan, wakishuhudia utiaji saini wa Hati ya Makubaliano baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kuhusu ushirikiano katika uwekezaji kwenye sekta ya madini, tarehe 05 Mei, 2025 Ikulu jijini Dar es Salaam. @ikulumawasliano @SuluhuSamia @mwigulunchemba1
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Samia Suluhu
@SuluhuSamia
Kheri ya Siku ya Kimataifa ya Uhuru wa Vyombo vya Habari.
Ninafarijika kuona tumepiga hatua kubwa katika kuimarisha uhuru wa vyombo vya habari na kujieleza, ambapo mwaka 2025 tumepanda zaidi katika viwango vya uhuru wa vyombo vya habari duniani. Haya ni matokeo ya kazi kubwa iliyofanywa na kila mdau kwenye sekta hii muhimu.
Ninaendelea kuvisihi vyombo vya habari kutumia weledi katika kazi zenu ili kuendelea kujenga na kuimarisha amani, utulivu na umoja wa kitaifa, hasa kipindi hiki tunapoelekea kwenye Uchaguzi Mkuu. Ninyi ni wadau na washiriki muhimu si tu kwa shughuli za Serikali, bali pia kwa uhai wa Taifa letu. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Bank of Tanzania
@BankOfTanzania
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Heri ya Siku ya Wafanyakazi - MEI MOSI
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), akiwa katika Ubalozi wa Tanzania Jijini NewYork nchini Marekani ambapo aliongoza Ujumbe wa Tanzania kushiriki Jukwaa la Ufadhili wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa kwa mwaka 2025 (ECOSOC Forum on Financing for Development Follow-Up (FfD Forum), lililowahusisha mawaziri wa Fedha, Mipango, Mambo ya Nje na sekta nyingine pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo yakiwemo mashirika ya Fedha ya Kimataifa kwa ajili ya kufanya tathmini ya utekelezaji wa Maazimio ya Umoja wa Mataifa kuhusu Ufadhili wa Maendeleo, uliofanyika Makao Makuu yabImojanwa Mataifa, Jijini New York.
Mhe. Dkt. Nchemba, ambaye aliambatana na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban, na Maafisa wengine waandamizi wa Wizara na Mambo ya Nje, alipokelewa na Mkuu wa masualanya Utawala wa Ubalozi huo, Bw. Joachim Otaru.
@mfa_tanzania -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Haki Ngowi
@Hakingowi
📍New York
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), akiwa katika Ubalozi wa Tanzania Jijini New York nchini Marekani ambapo aliongoza Ujumbe wa Tanzania kushiriki Jukwaa la Ufadhili wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa kwa mwaka 2025 (ECOSOC Forum on Financing for Development Follow-Up (FfD Forum), lililowahusisha mawaziri wa Fedha, Mipango, Mambo ya Nje na sekta nyingine pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo yakiwemo mashirika ya Fedha ya Kimataifa kwa ajili ya kufanya tathmini ya utekelezaji wa Maazimio ya Umoja wa Mataifa kuhusu Ufadhili wa Maendeleo, uliofanyika Makao Makuu yabImojanwa Mataifa, Jijini New York.
Mhe. Dkt. Nchemba, ambaye aliambatana na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban, na Maafisa wengine waandamizi wa Wizara na Mambo ya Nje, alipokelewa na Mkuu wa masualanya Utawala wa Ubalozi huo, Bw. Joachim Otaru.
📸:W/Fedha -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), akiangalia bendera ya Tanzania katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa (UN), Jijini New York, nchini Marekani, alipohudhuria Jukwaa la Ufadhili wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa kwa mwaka 2025 (ECOSOC Forum on Financing for Development Follow-Up (FfD Forum), lililowahusisha mawaziri wa Fedha, Mipango, Mambo ya Nje na sekta nyingine pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo yakiwemo mashirika ya Fedha ya Kimataifa kwa ajili ya kufanya tathmini ya utekelezaji wa Maazimio ya Umoja wa Mataifa kuhusu Ufadhili wa Maendeleo.
-
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Karibu Mama, SINGIDA NI KWAKO.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
The Citizen Tanzania
@TheCitizenTz
Finance Minister Dr Mwigulu Lameck Nchemba has urged African countries to embrace strategic intra-continental investment and trade as a means to navigate the shifting tides of global economic policies.
www.thecitizen.co.tz/tanzania/news/national/tanzania-s-fi… -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Dickson Mathias Muze
@dickmuze
Hii picha nilipiga na Mhe.Mwigulu uchaguzi miaka kadhaa iliyopita, jamaa namkubali sana, very humble na mtu wa watu.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), amesema kuwa Tanzania iko tayari kushirikiana na wadau mbalimbali zikiwemo serikali, mashirika ya kimataifa, sekta binafsi na asasi za kiraia ili kutafsiri kwa vitendo ahadi za Beijing+30 kuelekea Mkutano wa Nne wa Kimataifa kuhusu Ufadhili wa Maendeleo (FFD4), utakaofanyika kuanzia tarehe 30 Juni hadi 3 Julai 2025, Sevilla nchini Uhispania.
Dkt. Nchemba ameyasema hayo Jijini NewYork nchini Marekani, aliposhiriki mjadala ulioandaliwa na Taasisi ya Kimataifa inayojihusisha na masuala ya usawa wa kijinsia (UN Women), uliojikita kujadili namna ya kupata fedha kwa ajili ya kupunguza na kuondoa kabisa pengo la kijinsia katika uchumi na kuwawezesha wanawake kujikwamua kiuchumi wenye kauli mbiu isemayo “Kutoka Beijing hadi FfD4: Kuunganisha Ahadi Kupitia Ushirikiano wa Wadau kwa Usawa wa Kijinsia, Uwezeshaji wa Kiuchumi wa Wanawake na Maendeleo Endelevu”.
Alizitaja baadhi ya hatua zilizochukuliwa na Serikali katika kuwawezesha wananwake na makundi mengine kiuchumi kuwa ni pamoja na kuwekeza katika elimu bora kwa wasichana hasa wa maeneo ya vijijini, kuwezesha upatikanaji wa huduma za kifedha kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake (WDF) na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana (YDF).
Dkt. Nchemba kuwa Serikali inatoa msaada wa kisheria bure kupitia kampeni kama Mama Samia Legal Aid Campaign ambayo hadi Februari 2025 ilikuwa imetoa msaada wa kisheria kwa wanawake 681,326.
“Tunatoa mafunzo ya elimu ya kifedha na ya kidijitali kwa wanawake na vijana kupitia huduma za uendelezaji wa biashara, tunatoa mikopo yenye masharti nafuu kwa wanawake, vijana, na watu wenye ulemavu na kukuza bajeti jumuishi kijinsia na kuhakikisha uchambuzi wa kijinsia unajumuishwa katika upangaji na utekelezaji wa bajeti ya umma” alisema Dkt. Nchemba.
Alisema kuwa pamoja na mafanikio hayo, bado kuna vikwazo vya kimfumo vinavyozuia wanawake kufikia uwezo wao kamili wa kiuchumi na kubainisha kuwa mchakato wa FfD4 ni fursa muhimu ya kuhakikisha upatikanaji wa rasilimali za kifedha, sera jumuishi, na ushirikiano wa kibunifu unaoipa kipaumbele usawa wa kijinsia, kwa ajili ya kasi zaidi ya maendeleo.
“Tanzania inaipongeza UN Women kwa kuandaa nyaraka ya rasilimali (resource paper) inayotoa mwongozo wa kisera wa kifedha kwa mtazamo wa kijinsia. ambayo ni nyenzo muhimu itakayosaidia kuhakikisha kuwa uwezeshaji wa kiuchumi wa wanawake unakuwa kiini cha majadiliano na matokeo ya FfD4”. Aliongeza Dkt. Nchemba
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Sera, Programu, Divisheni ya ushirikiano wa Kimataifa wa UN Women, Bi. @sarah_hendriks , alisema kuwa suala la kuwawezesha wanawake kiuchumi linapaswa kuwa agenda ya kudumu ya mataifa mbalimbali hususan ya kiafrika ili kujenga jamii yenye nguvu ya kiuchumi kupitia uwekezaji wa mitaji, elimu, biashara na kuwawezesha kufikia masoko kwa njia ya kidigiti.
Mkurano huo ulihudhuriwa pia na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban na uliwashirikisha wadau kutoka sekta mbalimbali duniani, wanaokutana Jijini, NewYork nchini Marekani. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Haki Ngowi
@Hakingowi
📍 New York
DKT. NCHEMBA: SERIKALI IKO TAYARI KUSHIRIKIANA NA WADAU KUIMARISHA USAWA WA KIJINSIA
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amesema kuwa Tanzania iko tayari kushirikiana na wadau mbalimbali zikiwemo serikali, mashirika ya kimataifa, sekta binafsi na asasi za kiraia ili kutafsiri kwa vitendo ahadi za Beijing+30 kuelekea Mkutano wa Nne wa Kimataifa kuhusu Ufadhili wa Maendeleo (FFD4), utakaofanyika kuanzia tarehe 30 Juni hadi 3 Julai 2025, Sevilla nchini Uhispania.
Dkt.Nchemba ameyasema hayo Jijini NewYork nchini Marekani, aliposhiriki mjadala ulioandaliwa na Taasisi ya Kimataifa inayojihusisha na masuala ya usawa wa kijinsia (UN Women), uliojikita kujadili namna ya kupata fedha kwa ajili ya kupunguza na kuondoa kabisa pengo la kijinsia katika uchumi na kuwawezesha wanawake kujikwamua kiuchumi wenye kauli mbiu isemayo “Kutoka Beijing hadi FfD4: Kuunganisha Ahadi Kupitia Ushirikiano wa Wadau kwa Usawa wa Kijinsia, Uwezeshaji wa Kiuchumi wa Wanawake na Maendeleo Endelevu”.
Alizitaja baadhi ya hatua zilizochukuliwa na Serikali katika kuwawezesha wananwake na makundi mengine kiuchumi kuwa ni pamoja na kuwekeza katika elimu bora kwa wasichana hasa wa maeneo ya vijijini, kuwezesha upatikanaji wa huduma za kifedha kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake (WDF) na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana (YDF).
Dkt. Nchemba kuwa Serikali inatoa msaada wa kisheria bure kupitia kampeni kama Mama Samia Legal Aid Campaign ambayo hadi Februari 2025 ilikuwa imetoa msaada wa kisheria kwa wanawake 681,326.
“Tunatoa mafunzo ya elimu ya kifedha na ya kidijitali kwa wanawake na vijana kupitia huduma za uendelezaji wa biashara, tunatoa mikopo yenye masharti nafuu kwa wanawake, vijana, na watu wenye ulemavu na kukuza bajeti jumuishi kijinsia na kuhakikisha uchambuzi wa kijinsia unajumuishwa katika upangaji na utekelezaji wa bajeti ya umma” alisema Dkt. Nchemba.
Alisema kuwa pamoja na mafanikio hayo, bado kuna vikwazo vya kimfumo vinavyozuia wanawake kufikia uwezo wao kamili wa kiuchumi na kubainisha kuwa mchakato wa FfD4 ni fursa muhimu ya kuhakikisha upatikanaji wa rasilimali za kifedha, sera jumuishi, na ushirikiano wa kibunifu unaoipa kipaumbele usawa wa kijinsia, kwa ajili ya kasi zaidi ya maendeleo.
“Tanzania inaipongeza UN Women kwa kuandaa nyaraka ya rasilimali (resource paper) inayotoa mwongozo wa kisera wa kifedha kwa mtazamo wa kijinsia. ambayo ni nyenzo muhimu itakayosaidia kuhakikisha kuwa uwezeshaji wa kiuchumi wa wanawake unakuwa kiini cha majadiliano na matokeo ya FfD4”. Aliongeza Dkt. Nchemba
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Sera, Programu, Divisheni ya ushirikiano wa Kimataifa wa UN Women, Bi. Sarah Hendriks, alisema kuwa suala la kuwawezesha wanawake kiuchumi linapaswa kuwa agenda ya kudumu ya mataifa mbalimbali hususan ya kiafrika ili kujenga jamii yenye nguvu ya kiuchumi kupitia uwekezaji wa mitaji, elimu, biashara na kuwawezesha kufikia masoko kwa njia ya kidigiti.
Mkutano huo ulihudhuriwa pia na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban na uliwashirikisha wadau kutoka sekta mbalimbali
📸:W/Fedha -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Dcirambaofficial
@DCIRAMBA
KAMBI MAALUMU YA MADAKTARI BINGWA WA RAIS SAMIA HOSPITALI YA WILAYA YA IRAMBA
@Hakingowi
@mwigulunchemba1
@jimbolairamba -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), ametoa rai kwa nchi zilizoendelea kupunguza gharama za mikopo na kutoa muda mrefu wa kulipa madeni ili kuziwezesha nchi zinazoendelea zikiwemo za Afrika kutekeleza miradi ya maendeleo itakayochochea ukuaji wa uchumi na maisha ya wananchi kwa ujumla.
Mhe. Dkt. Nchemba ametoa rai hiyo jijini NewYork nchini Marekani, wakati akichangia mada katika Jukwaa la Ufadhili wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa kwa mwaka 2025 (ECOSOC Forum on Financing for Development Follow-Up (FfD Forum), linalofanyika Makao Makuu ya Umoja huo, Jijini NewYork nchini humo.
Alisema kuwa Mbinu za utoaji wa viwango vya mikopo zinapaswa kubadilika ili kuakisi kwa usahihi uwezo wa kweli wa nchi zinazoendelea kulipa madeni na kuhimiza matumizi zaidi ya fedha mchanganyiko (blended finance), upanuzi wa dhamana za hatari kutoka kwa Benki za Maendeleo ya Kielelezo (MDBs), na utekelezaji wa mipango ya uwazi wa madeni ili kusaidia kupunguza gharama za hatari zinazoonekana.
Dkt. Nchemba alipongeza juhudi zinazofanywa na mataifa pamoja na taasisi za fedha zinazokopesha kwa kuboresha upatikanaji wa mikopo nafuu lakini kwa nchi nyingi zinazoendelea, ikiwemo Tanzania, inakwazwa na viwango vikubwa vya gharama za mikopo na ulipaji wa madeni husika unaoathiri bajeti za nchi hizo.
Alipendekeza masuala matatu ya kufanyiwa kazi ikiwemo upatikanaji wa mikopo nafuu, kuongeza kasi ya kurekebisha muundo wa ulipaji madeni, kuwezesha upatikanaji wa mikopo mchanganyiko (blended finance) inayozingatia mahitaji pamoja na kuzisaidia nchi zinazoendelea kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Akizungumzia umuhimu wa sekta binafsi katika kukuza uchumi, Dkt. Nchemba alisema kuwa uwekezaji wa sekta binafsi ni muhimu ili kutimiza malengo ya maendeleo ya milenia kwa kujenga uchumi himilivu, jumuishi na kuhakikisha hakuna mtu anayeachwa nyuma kimaendeleo.
Alishauri kuimarisha majukwaa ya kuwezesha uwekezaji ambayo yanaunganisha fursa na mitaji ya kimataifa, kuchochea athari chanya, na kuhakikisha hakuna anayeachwa nyuma na kwamba Tanzania iko tayari kushirikiana na washirika wote kufungua uwekezaji binafsi kwa maendeleo jumuishi na endelevu.
Dkt. Nchemba alisema kuwa Tanzania, chini ya uongozi mahili wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imefanya mageuzi makubwa ya kisera ya upatikanaji wa fedha, kuweka uwazi wa matumizi na kutanua wigo wa upatikanaji wa mikopo nafuu kwa wanawake, vijana na watu wenye mahitaji maalum.
“Tunaendeleza ujumuishaji wa kifedha kupitia majukwaa ya kidijitali na kufanikisha urasimishaji wa sekta isiyo rasmi ili kuongeza upatikanaji wa masoko na fedha. Kwa ngazi ya kimataifa, tunatoa wito wa kuoanisha kwa kiwango kikubwa zaidi uwekezaji binafsi na vipaumbele vya kitaifa, kuimarisha ushirikiano wa kimataifa, na kuanzisha taasisi za msaada kama Kituo cha Kimataifa cha Msaada wa Uwekezaji kwa Nchi Zenye Maendeleo Duni (LDCs)” alisema Dkt. Nchemba.
Alisema kuwa Kitaifa, Tanzania inatengeneza mikakati ya fedha endelevu, dhamana zenye mwelekeo mahsusi (thematic bonds), na inatumia ubunifu wa kidijitali ili kuvutia rasilimali. kuanzisha mifumo ya uwekezaji kutoka kwa diaspora na kuhamasisha uwekezaji katika miundombinu endelevu na inayostahimili mabadiliko ya tabianchi.
Alishauri kuimarisha majukwaa ya kuwezesha uwekezaji ambayo yanaunganisha fursa na mitaji ya kimataifa, kuchochea athari chanya, na kuhakikisha hakuna anayeachwa nyuma na kwamba Tanzania iko tayari kushirikiana na washirika wote kufungua uwekezaji binafsi kwa maendeleo jumuishi na endelevu.
Jukwaa la Ufadhili wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa linawahusisha mawaziri wa Fedha, Mipango, Mambo ya Nje na sekta nyingine pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo yakiwemo mashirika ya Fedha ya Kimataifa kwa ajili ya kufanya tathmini ya utekelezaji wa Maazimio ya Umoja wa Mataifa kuhusu Ufadhili wa Maendeleo. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
HabariLeo
@HabariLeo
WASHINGTON — Waziri wa Fedha, Dk. @mwigulunchemba1, akizungumza na Waziri wa Fedha wa Malawi, Simplex Chithyola Banda, ndani ya Jengo la Makao Makuu ya Benki ya Dunia, Jijini Washington D.C, wakati wa mikutano ya mwaka 2025 ya majira ya Kipupwe ya Shirika la Fedha Duniani (IMF) na Benki ya Dunia.
#habarileoupdates -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb)(kulia), akizungumza na Waziri wa Fedha wa Malawi, Mhe. Simplex Chithyola Banda, ndani ya Jengo la Makao Makuu ya Benki ya Dunia, Jijini Washington D.C, wakati wa mikutano ya mwaka 2025 ya majira ya Kipupwe ya Shirika la Fedha Duniani (IMF) na Benki ya Dunia.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Haki Ngowi
@Hakingowi
📍Washington D.C, Marekani
▪️BENKI YA DUNIA YAIMWAGIA SIFA TANZANIA KWA KUSIMAMIA VIZURI UCHUMI WAKE
BENKI ya Dunia imeimwagia sifa Tanzania kwa usimamizi mzuri wa uchumi wa nchi na kuwa nchi ya kupigiwa mfano barani Afrika licha ya misukosuko mbalimbali ya kiuchumi inayoikabili dunia.
Pongezi hizo zimetolewa na Makamu mpya wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini, Dkt. Ndiamé Diop, alipokutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa Tanzania, unaoongozwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, kwenye Mikutano ya Majira ya Kipupwe ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia, Jijini Washington D.C, nchini Marekani.
Dkt Diop alisema kuwa Tanzania ni nchi ya mfano katika usimamizi wa sera za uchumi na fedha ambapo licha ya changamoto za UVIKO 19 na mizozo ya kisiasa inayoendelea sehemu mbalimbali duniani, tathimini ya Benki hiyo inaonesha kuwa uchumi wa Tanzania uko imara ikilinganishwa na nchi nyingine nyingi za Afrika.
Alisifu pia mikakati iliyowekwa na Serikali kwa ajili ya kukabiliana na changamoto ya Sera za nje za Marekani na duniani kwa ujumla za kupunguza misaada na kuondoa ufadhili katika miradi mbalimbali ikiwemo sekta ya afya, kwa kutumia fedha zake za ndani.
Aidha, alipongeza uhusiano imara uliopo kati ya Tanzania na Benki ya Dunia na kuahidi kuwa Benki yake itaendelea kuisaidia Tanzania katika jitihada zake za kukuza uchumi na kuwaondolea umasikini wananchi wake kwa kusaidia fedha zitakazotumika kutekeleza miradi mbalimbali ya kiuchumi na kijamii pamoja na kutoa misaada ya kiufundi itakayochochea ukuaji wa uchumi.
Kwa upande wake, Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba alimweleza Makamu mpya wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini, Dkt. Ndiamé Diop, aliyechukua nafasi ya Bi. Victoria Kwakwa, aliyemaliza muda wake, kwamba Benki ya Dunia ni mdau mkubwa wa maendeleo wa Tanzania.
Alisema kuwa, usimamizi mzuri wa uchumi unatokana na mwongozo na maono makubwa ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muunganio wa Tanzania, ambaye ameelekeza fedha nyingi katika sekta za uzalishaji na maendeleo ya jamii lakini pia ujenzi wa miundombinu inayochochea ukuaji wa uchumi.
Aliongeza kuwa Serikali imejipanga kuendelea kusimamia uchumi kwa kuimarisha sera za uchumi na fedha pamoja na kuishirikisha kikamilifu sekta binafsi katika kujenga uchumi wa nchi pamoja na kukabiliana na changamoto zinazotokana na mabadiliko ya mwelekeo ya kisera yanazotokea duniani ambayo kwa namna moja ama nyingine yameziathiri nchi nyingi za Afrika.
Uwekezaji wa Benki ya Dunia katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kiuchumi na kijamii nchini Tanzania umefikia dola za Marekani bilioni 10.9 ambapo miradi 38 ya maendeleo inatekelezwa katika sekta mbalimbali ikiwemo afya, maji, elimu, nishati, ujenzi wa miundombinu ya Barabara, ujenzi wa masoko na miradi ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
📸:W/Fedha -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
ikulu_Tanzania
@ikulumawasliano
Repost from @SuluhuSamia
•
Pongezi za dhati kwa Klabu ya Simba kwa ushindi katika mchezo wa Mashindano ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF Confederation Cup), na kuandika historia ya kufika fainali ya mashindano haya. Mmeipa nchi yetu heshima kubwa. Nawatakia kila kheri. Mnayo hamasa yangu wakati wote. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Samia Suluhu
@SuluhuSamia
Pongezi za dhati kwa Klabu ya Simba kwa ushindi katika mchezo wa Mashindano ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF Confederation Cup), na kuandika historia ya kufika fainali ya mashindano haya. Mmeipa nchi yetu heshima kubwa. Nawatakia kila kheri. Mnayo hamasa yangu wakati wote.
-
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Hongera Mnyama, Super sana. Kimataifa tuko pamoja, Tanzania kwanza. Mmewakilisha vyema nchi yetu.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
BENKI ya Dunia imeimwagia sifa Tanzania kwa usimamizi mzuri wa uchumi wa nchi na kuwa nchi ya kupigiwa mfano barani Afrika licha ya misukosuko mbalimbali ya kiuchumi inayoikabili dunia.
Pongezi hizo zimetolewa na Makamu mpya wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini, Dkt. Ndiamé Diop, alipokutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa Tanzania, unaoongozwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 , kwenye Mikutano ya Majira ya Kipupwe ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia, Jijini Washington D.C, nchini Marekani.
Dkt Diop alisema kuwa Tanzania ni nchi ya mfano katika usimamizi wa sera za uchumi na fedha ambapo licha ya changamoto za UVIKO 19 na mizozo ya kisiasa inayoendelea sehemu mbalimbali duniani, tathimini ya Benki hiyo inaonesha kuwa uchumi wa Tanzania uko imara ikilinganishwa na nchi nyingine nyingi za Afrika.
Alisifu pia mikakati iliyowekwa na Serikali kwa ajili ya kukabiliana na changamoto ya Sera za nje za Marekani na duniani kwa ujumla za kupunguza misaada na kuondoa ufadhili katika miradi mbalimbali ikiwemo sekta ya afya, kwa kutumia fedha zake za ndani.
Aidha, alipongeza uhusiano imara uliopo kati ya Tanzania na Benki ya Dunia na kuahidi kuwa Benki yake itaendelea kuisaidia Tanzania katika jitihada zake za kukuza uchumi na kuwaondolea umasikini wananchi wake kwa kusaidia fedha zitakazotumika kutekeleza miradi mbalimbali ya kiuchumi na kijamii pamoja na kutoa misaada ya kiufundi itakayochochea ukuaji wa uchumi.
Kwa upande wake, Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba alimweleza Makamu mpya wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini, Dkt. Ndiamé Diop, aliyechukua nafasi ya Bi. Victoria Kwakwa, aliyemaliza muda wake, kwamba Benki ya Dunia ni mdau mkubwa wa maendeleo wa Tanzania.
Alisema kuwa, usimamizi mzuri wa uchumi unatokana na mwongozo na maono makubwa ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muunganio wa Tanzania, ambaye ameelekeza fedha nyingi katika sekta za uzalishaji na maendeleo ya jamii lakini pia ujenzi wa miundombinu inayochochea ukuaji wa uchumi.
Aliongeza kuwa Serikali imejipanga kuendelea kusimamia uchumi kwa kuimarisha sera za uchumi na fedha pamoja na kuishirikisha kikamilifu sekta binafsi katika kujenga uchumi wa nchi pamoja na kukabiliana na changamoto zinazotokana na mabadiliko ya mwelekeo ya kisera yanazotokea duniani ambayo kwa namna moja ama nyingine yameziathiri nchi nyingi za Afrika.
Uwekezaji wa Benki ya Dunia katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kiuchumi na kijamii nchini Tanzania umefikia dola za Marekani bilioni 10.9 ambapo miradi 38 ya maendeleo inatekelezwa katika sekta mbalimbali ikiwemo afya, maji, elimu, nishati, ujenzi wa miundombinu ya Barabara, ujenzi wa masoko na miradi ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
@WBTanzania @WorldBank -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Heri ya miaka 61 ya Muungano wa Tanzania
-
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Requiescat in Pace, Sancte Pater.
Thank you for guiding us in faith and humility. May the angels lead you into paradise.
Amen. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
TRA Tanzania
@TRATanzania
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
TRA Tanzania
@TRATanzania
#muungano Miaka 61 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
TRA Tanzania
@TRATanzania
#muungano Miaka 61 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
ikulu_Tanzania
@ikulumawasliano
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
TRA Tanzania
@TRATanzania
#muungano Miaka 61 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Bank of Tanzania
@BankOfTanzania
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Samia Suluhu
@SuluhuSamia
Hotuba yangu kwa Taifa hii leo kuelekea Miaka 61 ya Muungano.
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia, anayesimamia Kundi la Kwanza la nchi za Kanda ya Afrika (Africa Group 1 Constituency), Dkt. Zarau Wendeline Kibwe, Makao Makuu ya Benki hiyo Jijini Washington D.C, nchini Marekani, ambapo walizungumzia kuhusu ushirikiano kati ya Tanzania na Benki hiyo.
Pamoja na kuishukuru Benki ya Dunia kwa kuendelea kutoa fedha zinazotumika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo na kuonesha utayari wake wa kusaidia ujenzi wa mradi wa kimkakati wa Reli ya Kisasa (SGR), Mhe. Dkt. Nchemba alimkumbusha Dkt. Kibwe, kuhusu maombi ya Tazania ya kutaka Kiswahili kiwe sehemu ya lugha rasmi za mawasiliano katika mikutano ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia kutokana na umuhimu wake katika maendeleo ya Bara la Afrika na Dunia kwa ujumla.
Katika kikao hicho pia alishiriki Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Mhe. Stanslaus Nyongo, aliyezungumzia kuhusu kuanza kwa utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050 itakayosaidia kuchochea maendeleo ya watu na kukuza uchumi wa nchi, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Zanzibar, Dkt. Juma Malik Akil, alkyezungumzia kuhusu mafanikio ya Serikali ya Zanzibar kupitia misaada na mikopo nafuu inayotolewa na Benki ya Dunia na kuinufaisha Zanzibar moja kwa moja, Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Dkt. Fred Msemwa, Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Dkt. Elsie Kanza, Kamishna Msaidizi wa Fedha za Nje, Wizara ya Fedha, Bw. Robert Mtengule, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Sheria, Wizara ya Fedha, Bi. Zawadi Maginga na Viongozi wengine kutoka Wizara ya Fedha na Benki ya Dunia. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), amezishauri nchi za Afrika kuweka mikakati ya kufanya uwekezaji na biashara ndani ya Bara la Afrika ili kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya sera za kiuchumi zinazojitokeza hivi sasa duniani.
Mhe. Dkt. Nchemba ametoa ushauri huo jijini Washington D.C, nchini Marekani, wakati akichangia taarifa ya Mwaka ya utekelezaji ya majukumu ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), wakati wa Mkutano wa Majira ya Kipupwe (Spring Meetings) wa Magavana wa Shirika hilo wa Nchi za Afrika Kundi la Kwanza (Africa Group I Constituency – IMF).
Alisema kuwa mabadiliko ya kisera yanayojitokeza hivi sasa duniani ikiwemo vikwazo vya kibiashara vinavyotolewa na mataifa makubwa kwa kuongeza ushuru na tozo mbalimbali, iwe ni chachu kwa nchi za Afrika kutafuta njia za kujiimarisha kiuchumi kwa kuweka mipango madhubuti katika bajeti za nchi na kuuziana bidhaa.
Dkt. Nchemba alisisitiza kuwa hali ilivyo sasa inaonesha nchi za Afrika zinakuwa washindani wa kibiashara badala ya kuwa washirika hali inayotishia mustakabali wa kiuchumi wa nchi hizo.
Alisisitiza umuhimu wa nchi za Afrika kuangalia maeneo ya uwekezaji katika miundombinu mbalimbali ndani ya Bara hilo ikiwemo ujenzi wa viwanda vya kutengeneza dawa muhimu za binadamu na sekta nyingine zitakazochangia kukuza ajira kwa wananchi wao pamoja na kuimarisha uchumi wa nchi hizo.
Mhe. Dkt. Nchemba alisema kuwa ufinyu wa ufadhili wa kimataifa, unaochochewa na kupanda kwa viwango vya riba katika nchi zilizoendelea kiuchumi na kuhama kutoka kutoa misaada na ukopeshaji wa masharti nafuu, kumezuia zaidi nafasi ndogo ya kifedha katika nchi hizi kujiletea maendeleo.
Aliongeza kuwa matokeo yake, kuyumba kwa uchumi mkuu kumeongezeka, uwezo wa kitaasisi umemomonyoka, na upatikanaji wa ufadhili wa masharti nafuu na wa soko umezidi kuwa na vikwazo, na kudhoofisha matarajio ya kufikia maendeleo yanayotarajiwa.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Mkutano huo ambaye ni Gavana wa Benki Kuu ya Botswana, Bw. Cornelius Dekop, aliunga mkono ushauri wa Tanzania na kusisitiza kuwa uchakataji wa bidhaa ndani ya nchi za Afrika pamoja na ushirikiano wa kibiashara, utakuwa na tija kubwa kuliko utegemezi wa biashara nje ya mipaka ya Afrika.
Alisisitiza kuwa changamoto za kibiashara zilizopo hivi sasa katika dunia itumike kama fursa ya kuliamsha Bara la Afrika kutafuta njia za kujiimarisha kiuchumi kwa kuwa katika Bara hilo kuna soko kubwa na pia fursa za uwekezaji na biashara kwa ujumla. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb)(kushoto), akisalimiana na Waziri wa Fedha wa Afrika Kusini, Mhe. Enoch Godongwana, Nje ya Jengo la Makao Makuu ya Benki ya Dunia, Jijini Washington D.C, ambako inafanyika mikutano mwaka 2025 ya majira ya Kipupwe ya Shirika la Fedha Duniani (IMF) na Benki ya Dunia.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb)(kushoto), akisalimiana na Waziri wa Fedha wa Zambia, Mhe. @S_Musokotwane , kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Mawaziri wa Fedha wa nchi za Afrika, wanachama wa Shirika la la Fedha la Kimataifa IMF na Benki ya Dunia, ulioongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa IMF, Bi. Kristalina Georgieve, ikiwa ni sehemu ya mikutano ya majira ya Kipupwe ya Shirika la Fedha Duniani (IMF) na Benki ya Dunia, inayoendelea jijini Washington D.C, nchini Marekani.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb)(kushoto), akisalimiana na Waziri wa Fedha wa Rwanda, Mhe. Yusuf Murangwa, Nje ya Jengo la Makao Makuu ya Benki ya Dunia, Jijini Washington D.C, ambako inafanyika mikutano mwaka 2025 ya majira ya Kipupwe ya Shirika la Fedha Duniani (IMF) na Benki ya Dunia.
@RwandaFinance -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb) amesema kuwa Tanzania imejipanga kukabiliana na mabadiliko ya sera za nje za Marekani kuhusu misaada kwa nchi za Afrika kwa kutumia rasilimali zake ndani kupitia Bajeti Kuu ya Serikali.
Mhe. Dkt. Nchemba amesema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kundi la Kwanza la Nchi za Afrika wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Bw. Adran Ubisse, kando ya Mikutano ya Majira ya Kipupwe ya IMF na Benki ya Dunia, inayofanyika Jijini Washington D.C, nchini Marekani.
Dkt. Nchemba alikuwa akijibu swali la Bw. Ubisse, aliyetaka kufahamu mipango ya Serikali ya kukabiliana na uamuzi wa Marekani wa kusitisha misaada yake kwa Bara la Afrika ikiwemo sekta ya afya pamoja na kuweka ushuru wa bidhaa zinazoingizwa nchini humo kutoka mataifa hayo na mengine duniani kote.
Alisema kuwa Serikali imetenga fedha na kuongeza mafungu ya matumizi kupitia Bajeti Kuu ya Serikali ya Mwaka wa Fedha 2025/2026, kwa ajili ya kugharamia sekta mbalimbali zinazoathiriwa moja kwa moja na uamuzi huo wa Marekani, ikiwemo sekta ya afya.
Dkt. Nchemba alifafanua kuwa Serikali imejipanga kubana matumizi yake ya kawaida na kuelekeza fedha nyingi katika maeneo ya huduma za jamii na sekta za uzalishaji ili kulinda uchumi wa nchi unaokua kwa kasi lakini pia kuhakikisha kuwa wananchi wanapata huduma muhimu za kijamii.
“Nchi zetu za Afrika, Tanzania ikiwemo, hatuwezi kuruhusu dira yetu ya maendeleo ikakwazwa na mabadiliko ya kisera ya mataifa mengine, tutachukua hatua Madhubuti za kutenga fedha kwa ajili ya huduma za jamii, kukuza uzalishaji pamoja na ujenzi wa miundombinu ambapo tutapitia upya eneo la matumizi na mapato ya serikali” alisema Dkt. Nchemba.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Mhe. Stanslaus Nyongo, alisema kuwa Serikali imekamilisha Dira Mpya ya Taifa ya Maendeleo ya 2050, ambayo imeweka misingi ya kukuza uwezo wa nchi kujitegemea kwa kuimarisha sekta muhimu za uzalishaji, ikiwemo kilimo, matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano, hatua itakayokuza kipato cha mtu mmoja mmoja na uchumi wa taifa kwa ujumla.
Alisema kuwa kupitia Dira hiyo itakayoanza kutumika kuanzia mwaka wa fedha 2025/2026, ambayo hivi sasa inaandaliwa mpango wa utekelezaji wa mwaka mmoja mmoja, utaongeza uwezo wa kipato cha Mtanzania, kwa mwaka, kutoka dola za Marekani 1,250 za sasa hadi kufikia dola 4,700 ifikapo mwaka 2050.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Kundi la Kwanza la Nchi za Afrika wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Bw. Adran Ubisse, aliipongeza Tanzania kwa kuchukua hatua hizo madhubuti za kusimamia uchumi na kuhakikisha kuwa sera za nje za misaada za mataifa mengine haziathiri mustakabali wa maendeleo ya nchi na huduma za kijamii kwa ujumla.
Alisema kuwa IMF inakuna kichwa namna ya kuyasaidia mataifa mbalimbali ya Afrika kuwa na sera na uwezo wa kuhimili mikikimikiki hiyo kupitia program mbalimbali zinazosimamiwa na Shirika lake ikiwemo kujiandaa na maombi mengi ya fedha yanayotarajiwa kuwasilishwa na nchi mbalimbali ili yawe na uwezo wa kujiimarisha kiuchumi.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, ambaye ni miongozi mwa Magavana wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia yam waka 2025,, Taasisi ambazo Tanzania inamiliki hisa, anaongoza Ujumbe wa Tanzania katika Mikutano hiyo ya Majira ya Kipupwe (The IMF and World Bank Spring Meetings 2025).
Viongozi wengine alioambatana nao ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Mhe. Stanslaus Nyongo (Mb), Magavana Mbadala wa IMF na Benki ya Dunia, ambao ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Emmanuel Tutuba, Katibu wa Baraza la Mawaziri, Bw. Nsubili Joshua na Mshauri wa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan wa masuala ya uchumi, Dkt. Blandina Kilama
Wengine ni Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango-Zanzibar, Dkt. Juma Malik Akil, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban, Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Dkt. Fred Msemwa na baadhi ya Wakuu wengine wa Taasisi za Serikali. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), amekutana na kufanya Mazungumzo na Mkurugenzi wa Shirika la Fedha la Kimataifa -IMF anayesimamia Kanda ya Afrika, Bw. Abebe Selassie, kando ya Mikutano ya Majira ya Kipupwe ya IMF na Benki ya Dunia, inayofanyika Jijini Washington D.C, nchini Marekani, ambapo wamejadiliana masuala mbalimbali ya ushirikiano ikiwemo utekelezaji wa programu ya Extended Credit Facility-(ECF), inayohusisha upatikanaji wa mkopo nafuu kwa ajili ya kuimarisha uchumi wa nchi kupitia sekta za uzalishaji na huduma za jamii pamoja na ufadhili wa kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi kupitia dirisha la Resilient and Sustainable Fund (RSF) kutoka Shirika hilo.
Kikao hicho kimehudhuriwa na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Mhe. Stanslaus Nyongo (Mb), Magavana Mbadala wa IMF na Benki ya Dunia, ambao ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Emmanuel Tutuba, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango-Zanzibar, Dkt. Juma Malik Akil, Naibu Gavana Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dkt. Yamungu Kayandabila, na maafisa wengine waandamizi wa Serikali na IMF.
@IMFNews -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Rais Mstaafu wa Serikali ya ya Awamu ya Nne, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb) pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Dkt. Elsie Kanza, kando ya Mikutano ya Mwaka ya Majira ya Kipupwe ya Mwaka 2025, inayoendelea Jijini Washington D.C, nchini Marekani.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Haki Ngowi
@Hakingowi
📍Washington D.C
Rais Mstaafu wa Serikali ya ya Awamu ya Nne, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb) pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Dkt. Elsie Kanza, kando ya Mikutano ya Mwaka ya Majira ya Kipupwe ya Mwaka 2025, inayoendelea Jijini Washington D.C, nchini Marekani.
📸:W/Fedha -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), amekutana na kufanya Mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Masuala ya Utawala na Uendeshaji wa Benki ya Dunia, Bi. @bjerde_anna , kando ya Mikutano ya Majira ya Kipupwe ya IMF na Benki ya Dunia, inayofanyika Jijini Washington D.C, nchini Marekani, ambapo pamoja na mambo mengine, Dkt. Nchemba aliishukuru Benki hiyo kwa mchango mkubwa wa maendeleo ya Tanzania kupitia miradi mbalimbali inayopata fedha kutoka Taasisi hiyo pamoja na kuonesha nia ya kusaidia ujenzi wa Mradi wa Reli ya kisasa (SGR)
Aidha, katika kikao hicho, alitambulishwa Makamu wa Rais Mpya wa Benki ya Dunia anayesimamia Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini, Bw. Ndiamé Diop, ambaye ameteuliwa hivi karibuni baada ya Bi. Victoria Kwakwa kumaliza muda wake.
Kikao hicho kimehudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Dkt. Elsie Kanza, Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Dkt. Fred Msemwa, Kamishna wa Idara ya Usimamizi wa Deni la Serikali, Wizara ya Fedha, Bw. Japhet Justine, Kamishna Msaidizi kutoka Idara ya Fedha za Nje, Wizara ya Fedha, Bw. Robert Mtengule, Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania, Bw. Nathan Belete na viongozi wengine waandamizi wa Serikali na Benki ya Dunia. -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Heri ya Pasaka wote.
Yesu Kristo amefufuka, Hakika amefufuka.
Tunamshukuru Mungu kwa neema ya wokovu kupitia mateso, kifo, na ufufuo wa Bwana wetu Yesu Kristo. Pasaka ni kumbukumbu ya ushindi wa uzima dhidi ya mauti, na ahadi ya tumaini jipya kwa wote tunaomwamini.
Tuendelee kuishi kwa upendo, msamaha, na kumtumikia Mungu kwa moyo wa unyenyekevu.
Heri na baraka tele katika Sikukuu hii ya Ufufuo. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Bank of Tanzania
@BankOfTanzania
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba, ameshiriki katika kikao cha hitimisho la majadiliano kati ya Serikali ya Tanzania na timu ya wataalam kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF). Kikao hicho kilifanyika tarehe 17 Aprili 2025 katika ofisi za BoT, jijini
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), amelihakikishia Shirika la Fedha la Kimataifa ( @IMFNews ) kwamba, Serikali itaendelea kufanya maboresho ya sera na mipango yake kwa kuhakikisha sekta mbalimbali za kiuchumi na kijamii pamoja na kuimarisha sekta binafsi zinapewa kipaumbele.
Dkt. Nchemba amesema hayo wakati akifunga vikao vya majadiliano kati ya Serikali na Timu ya Wataalam kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), baada ya kukamilisha tathimini ya awamu ya tano ya utekelezaji wa program ya Extended Credit Facility-(ECF), inayohusisha mkopo nafuu kwa ajili ya kuimarisha uchumi wa nchi kupitia sekta za uzalishaji na huduma za jamii pamoja na awamu ya pili ya utekelezaji wa program ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi kupitia dirisha la Resilient and Sustainable Fund (RSF) kutoka Shirika hilo.
Akifunga vikao hivyo katika Kikao cha majumuisho kilichofanyika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Jijini Dar es Salaam, Dkt. Nchemba, alieleza kufurahishwa kwake na taarifa iliyowasilishwa na Kiongozi wa Timu hiyo Bw. Nicolas Blancher, inayoonesha kuwa Tanzania imetekeleza ipasavyo vigezo vilivyowekwa na Shirika hilo katika mipango hiyo ya ECF na RSF.
Aliahidi kuwa Serikali itaendelea kusimamia ipasavyo utekelezaji wa programu hizo mbili zenye thamani ya dola za Kimarekani bilioni 1.832, ambapo kiasi cha dola bilioni 1.1 ni kwa ajili ya Mpango wa kuimarisha Uchumi wa nchi kupitia sekta za uzalishaji na kiasi cha dola milioni 786 ni kwa ajili ya Mpango wa nchi kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi, ambapo program hizo mbili zinatekelezwa katika kipindi cha miaka minne kuanzia mwaka 2022/2023 hadi 2025/2026.
Kwa upande wake, Kiongozi wa Timu ya Wataalam kutoka IMF waliofanya tathimini hiyo, Bw. Nicolas Blancher, alisema kuwa tathimini yao ya awamu ya tano imeonesha kuwa Tanzania imetekeleza vizuri mpango wa ECF na RSF na kushauri hatua kadhaa zinazotakiwa kuendelea kuchukuliwa ikiwemo kuimarisha zaidi huduma za jamii na kuendelea kuimarisha mazingira bora ya kufanyabiashara na uwekezaji.
“Matarajio ya uchumi wa Tanzania ni mazuri kwakuwa utaendelea kukua kwa kasi, huku mfumuko wa bei ukiendelea kuwa chini, nakisi ya mauzo na manunuzi ya bidhaa na huduma nje ya nchi ikipungua, na upatikanaji wa fedha za kigeni ukiongezeka” alisema Bw. Blancher.
Aliongeza kuwa hatua za kuwianisha vizuri mapato na matumizi ya serikali katika mwaka wa fedha wa 2025/26, zitasaidia kuhifadhi uhimilivu wa deni la serikali, huku zikilinda matumizi yenye kipaumbele katika huduma za kijamii.
Bw. Blancher alisema kuwa kuendelea kutekeleza sera za kukabiliana na athari na changamoto za mabadiliko ya tabianchi, zinazoungwa mkono na mpango wa RSF, kutasaidia kujenga ustahimilivu katika kushughulikia madhara ya mabadiliko ya tabianchi.
Alisema kuwa mapendekezo ya tathimini hiyo yatapelekwa mbele ya Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na kwamba uamuzi utakaotolewa na Bodi utaiwezesha Tanzania kupokea ufadhili wa dola za Marekani milioni 441.
Tanzania imefanyiwa Tathimini ya Awamu ya Tano ili iweze kupata fedha kutoka IMF kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya kiuchumi na kijamii ambapo hadi sasa Program ya ECF imepokea kiasi cha dola za Marekani milioni 754.3 kati ya dola za Marekani bilioni 1.1 na kiasi kingine cha dola za Marekani milioni 55 zimepokelewa kupitia dirisha la RSF, mradi wenye thamani ya dola za Marekani milioni 786.
Kikao hicho kilihudhuriwa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-Maamry Mwamba, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba, na Manaibu Gavana, pamoja na Maafisa Waandamizi wa Serikali na wajumbe wa Timu ya Tathimini kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya Usawa wa Jinsia ( @unwomentanzania ), Bi. Hodan Addou, Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam, ambapo wamejadili masuala ya ushirikiano kati ya Shirika hilo na Tanzania hususan katika kuwawezesha wanawake kupitia Bajeti Kuu ya Serikali.
Kikao hicho kimehudhuriwa pia na Kamisha wa Idara ya Sera Wizara ya Fedha, Dkt. Johnson Nyella, Kamishna Msaidizi kutoka Idara ya Fedha za Nje, Wizara ya Fedha, Bw. Robert Mtengule na maafisa wengine waandamizi wa Serikali na Shirika hilo la UN Women. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
UN Women Tanzania
@unwomentanzania
Today, UN Women Rep. Hodan Addou met with Minister of Finance, Hon. Dr. Mwigulu Nchemba @mwigulunchemba1.
Discussions focused on strengthening collaboration to advance gender equality in Tanzania—particularly through gender-responsive budgeting.
#genderequality #grb -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Serikali imesema kuwa fedha ambazo hazijatumika hadi mwisho wa mwaka hurudi Mfuko Mkuu wa Serikali ikiwa ni utaratibu wa kusimamia uwajibikaji na uwazi katika matumizi ya fedha zilizotengwa katika bajeti.
Hayo yameelezwa bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Tandahimba Mhe. Katani Ahmad Katani, aliyetaka kujua lini Serikali itarejesha fedha za miradi zilizochukuliwa na Hazina.
Mhe. Dkt. Nchemba, alifafanua kuwa kwa mujibu wa kifungu cha 29 cha Sheria ya Bajeti SURA 439, fedha ambazo hazijatumika hadi mwisho wa mwaka zinakoma matumizi yake na kurudishwa Mfuko Mkuu wa Serikali.
Aliongeza kuwa iwapo kuna miradi au shughuli ambazo hazijakamilika, Fungu husika linatakiwa kutenga bajeti na kuwasilisha maombi kwa kuambatisha hati za madai au nyaraka za utekelezaji wa miradi hiyo.
Mhe. Dkt. Nchemba alisema kuwa azma ya Serikali ni kuhakikisha kuwa miradi yote inatekelezwa ili kuleta maendeleo kwa wananchi. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Haki Ngowi
@Hakingowi
📍Bungeni, Dodoma
▪️FEDHA ZISIZOTUMIKA HADI MWISHO WA MWAKA KURUDI MFUKO MKUU WA SERIKALI
Serikali imesema kuwa fedha ambazo hazijatumika hadi mwisho wa mwaka hurudi Mfuko Mkuu wa Serikali ikiwa ni utaratibu wa kusimamia uwajibikaji na uwazi katika matumizi ya fedha zilizotengwa katika bajeti.
Hayo yameelezwa bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Tandahimba Mhe. Katani Ahmad Katani, aliyetaka kujua lini Serikali itarejesha fedha za miradi zilizochukuliwa na Hazina.
Mhe. Dkt. Nchemba, alifafanua kuwa kwa mujibu wa kifungu cha 29 cha Sheria ya Bajeti SURA 439, fedha ambazo hazijatumika hadi mwisho wa mwaka zinakoma matumizi yake na kurudishwa Mfuko Mkuu wa Serikali.
Aliongeza kuwa iwapo kuna miradi au shughuli ambazo hazijakamilika, Fungu husika linatakiwa kutenga bajeti na kuwasilisha maombi kwa kuambatisha hati za madai au nyaraka za utekelezaji wa miradi hiyo.
Mhe. Dkt. Nchemba alisema kuwa azma ya Serikali ni kuhakikisha kuwa miradi yote inatekelezwa ili kuleta maendeleo kwa wananchi.
📸:W/Fedha -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
tanzanialeotz
@tanzanialeotz
Mwigulu: Samia ameivusha nchi
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisalimiana na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande, alipowasili katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), Dar es salaam, kwa ajili ya kufungua Kongamano la Kodi na Uwekezaji la Mwaka 2025, ambapo katika hafla hiyo Dkt. Mpango, aliwataka washiriki kutumia kongamano hilo kama sehemu ya kuwasilisha na kujadiliana kuhusu mambo muhimu yatakayosaidia Serikali kujitegemea kwa kutumia mapato yake ya ndani yanayotokana na kodi pamoja na kuboresha mazingira ya kufanyakazi na uwekezaji nchini.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, ni miongozi mwa Viongozi wa Serikali walioshiriki Mapokezi ya Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Bank of Tanzania
@BankOfTanzania
TUTAENDELEA KUDHIBITI UHALIFU WA KIFEDHA-MAJALIWA
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa, amesema kuwa Tanzania itaendelea kushiriki kikamilifu na kutekeleza matakwa ya kimataifa katika kupambana na kudhibiti uhalifu wa kifedha, ikiwa ni sehemu ya -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
NewTimesTanzania
@NewTimesTZ
SERIKALI YAFIDIA FEDHA ZA NDANI BAADA YA MAREKANI KUSITISHA UFADHILI
Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Serikali imekamilisha tathmini ya athari zitakazojitokeza kwa miradi ambayo ilikuwa ikipata ufadhili kupitia Serikali ya Marekani ambapo maeneo yaliyoathirika kwa kiasi kikubwa yanajumuisha sekta ya afya.
Dkt. Nchemba ameyasema hayo leo Aprili 15,2025 Bungeni Jijini Dodoma wakatia akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Kagera Neema Lugangira aliyehoji Serikali imechukua hatua gani ili kupunguza makali ya mabadiliko ya Sera za nje katika masuala ya fedha za Maendeleo Kimataifa kwa Mataifa yaliyoendelea.
“Miradi mikubwa iliyokuwa inagharamiwa kupitia mshirika huyo imetengewa bajeti kupitia fedha za ndani,” amesema.
Ameongeza kuwa Serikali inaendelea na tathmini kwa maeneo mengine yanayoweza kuathirika kwa kiasi kikubwa kutokana na mabadiliko ya sera hizo za nje katika masuala ya fedha kwa kuangalia na washirika wengine wa Maendeleo ambao Serikali ya Marekani imekuwa ikitoa mchango wao.
Aidha, akiuliza swali la nyongeza kwa Waziri huyo kama serikali haioni haja ya kuondoa gharama zisizo za lazima ili kuokoa fedha ambazo zinaweza kuelekezwa kuokoa mianya hiyo Dkt. Nchemba amesema tiyari suala hilo wameanza kulifanyia kazi ambapo iliunda timu iliyokuwa chini ya ofisi ya Waziri Mkuu ili kupitia sekta zote na eneo la afya ndilo lilionekana kuhitaji kuchua hatua za haraka.
#nttupdates -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Haki Ngowi
@Hakingowi
📍Bungeni, Dodoma
▪️DKT. NCHEMBA: HAKUNA SEKTA ITAKAYOKOSA FEDHA KUTOKANA NA MABALILIKO YA SERA
Serikali imewahakikishia Watanzania kuwa hakutakuwa na sekta itakayokosa fedha kwa sababu ya mabadiliko ya sera ya baadhi ya mataifa zinazolenga kupunguza kuyasaidia mataifa yanayoendelea ikiwemo Tanzania.
Hayo yamebainishwa bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), wakati akijibu hoja za wabunge zilizojitokeza katika Bunge la Kumi na mbili, mkutano wa 19 katika kikao cha sita.
Alisema Serikali imefanya tathmini katika sekta zote kupitia Timu iliyochini ya Waziri Mkuu na kuanza kuchukua hatua baada ya baadhi ya mataifa kubadili sera zao ili kupunguza fedha kwa nchi zinazoendelea kama Tanzania.
“Tulikuwa na mahitaji ya takribani shilingi bilioni 220 kwenye sekta ya Afya ili kuziba pengo la fedha ambazo tulikuwa tunazitarajia kutoka kwa wadau wa maendeleo, Serikali tayari imetoa kiasi cha shilingi bilioni 98 kwenda kwenye sekta ya afya ili kufidia pengo lililojitokeza na tathmini hiyo inaendelea katika maeneo mengine na utoaji wa fedha utaendelea katika maeneo mengine ambayo yanahitaji fedha”, alisema Dkt. Nchemba.
Aidha, Dkt. Nchemba alimpongeza Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kazi kubwa anayoifanya kwa kuwa ameweza kuivusha nchi kipindi ambacho dunia nzima imekuwa ikipita kwenye msukosuko ya kiuchumi ambayo imekuwa ikitokea mfululizo kwa kipindi cha miaka minne.
Alisema kuwa kulitokea changamoto ya Uviko 19, uhaba wa fedha za kigeni na sasa sera za nje za baadhi ya mataifa ambazo tayari Serikali imeanza kuchukua hatua na kama taifa linaamini litavuka.
Dkt. Nchemba alisema kuwa sekta ya Afya ndiyo iliyoguswa zaidi ambapo Serikali itaendelea kuchukua hatua zaidi ikiwemo kuwekeza fedha kwenye uzalishaji ndani ya nchi wa madawa na vifaa tiba vilivyokuwa vinapatikana kupitia wabia.
Alisema kuwa Mpango wa Maendeleo na Bajeti itakayosomwa katika Bunge linaloendelea, sehemu ya fedha itaelekezwa kwenye viwanda vinavyozalisha madawa ndani ya nchi ili kuweza kujitegemea kama nchi katika eneo hilo.
“Nchi yetu na umri wake na uwezo wake na uwekezaji uliofanyika kwenye sekta ya afya tunaweza kujitegemea kumaliza ugonjwa wa Malaria, magonjwa ya TB, vitenganishi na madawa mengine”, alieleza Dkt. Nchemba.
Alisema kuwa fedha zingine zitaelekezwa kwenye Bima ya Afya kwa wote kama ambavyo Mhe. Rais alivyotoa maelekezo.
Dkt. Nchemba alisema Serikali itatengeneza mkakati wa kubana matumizi kwenye maeneo yenye uhitaji mdogo na kupeleka fedha kwenye maeneo yenye uhitaji mkubwa na ya lazima kama miundombinu, afya, elimu, maji, umeme na sekta zingine za uzalishaji.
Aidha, alibainisha kuwa Tanzania imeingia kwenye kumbukumbu ya kupanga jambo kubwa na kulitekeleza kama mradi wa umeme wa Mwalimu Nyerere, Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) ambao hata baadhi ya mataifa makubwa hawana mradi kama huo ambao kwa sasa zaidi ya kilomita 722 zinaonekana na sehemu kubwa imeanza kufanya kazi hususani kipande cha Dar es Salaam hadi Dodoma.
Alisema vipande vilivyosalia tayari vina Wakandarasi na upatikanaji wa fedha upo katika hatua za mwisho ambapo kuanzia mwaka wa fedha huu fedha katika vipande hivyo itapatikana ili kuhakikisha miradi hiyo inakamilika.
Aliitaja miradi mingine kuwa ni pamoja na Mradi wa Daraja la Kigongo Busisi ambao umekamilika na sasa upo tayari kwa matumizi na mradi wa bomba la mafuta kutoka Hoima hadi Tanga ambapo Tanzania imetekeleza wajibu wake kwa kiasi kikubwa.
Vilevile alisema kuwa tayari amefanya mazungumzo na mawaziri wa kisekta kwenye eneo la barabara, maji, kilimo na sekta nyingine na tayari fedha zimetolewa na na zitaendelea kutolewa
Amesema mambo yote hayo yanahitaji kuongeza mapato, hivyo Serikali imekubaliana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuongeza elimu kwa mlipa kodi ili kuweza kulipa kodi kwa hiari kama Mhe. Rais alivyoelekeza ambapo elimu itatolewa kwenye michezo, mashuleni na maeneo mengine.
📸:W/Fedha -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Baadhi ya wadau wakifuatilia mada ya kwanza kuhusu Kuimarisha Sera za Ushirikishwaji wa Wananchi kwa Lengo la Kuongeza Mapato ya Kodi: Mpango Mkakati wa Ugawaji wa Rasilimali, wakati wa Kongamano la Kodi na Uwekezaji 2025, lenye kaulimbiu ya “Kuongeza ukuzaji wa Rasilimali za ndani kupitia kustawisha fursa za wananchi”.
Mjadala wa mada hiyo umeongozwa na Mkurugenzi wa Chama cha Wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TWCC), Bi. Mwajuma Hamza, na kujadiliwa na jopo la wazungumzaji kama Mwenyekiti, Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF, Bi. Angelina Ngalula, Mkurugenzi Mkuu wa Clouds Media Group, Bw. Joseph Kusaga, Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la KKKT, Usharika wa Kijitonyama, Dkt. Eliona Kimaro na Afisa Mkuu wa Uendeshaji wa Benki ya CRDB, Bw. Bruce Mwile Mwasenga. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Haki Ngowi
@Hakingowi
📍Dar es Salaam
Waziri wa Fedha, Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), akihutubia katika hafla ya Ufunguzi wa Kikao cha ngazi ya Juu cha Kikosi Kazi cha Kimataifa cha Kudhibiti Fedha Haramu (The Financial Action Task Force (FATF) Africa Joint Group), kikao kilichofunguliwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, katika Ukumbi wa Mikutano wa Kilimanjaro wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), jijini Dar es Salaam
Akizungumza wakati akimkaribisha Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa kuhutubia, Mhe. Dkt. Nchemba alisema kuwa Tanzania imeweka mifumo madhubuti ya kukabiliana na vitendo vya utakasishaji fedha haramu na udhibiti wa vitendo vya ufadhili wa ugaidi na kwamba iko tayari kushirikiana na Kikosi kazi hicho kinachoongozwa na Bi. Yonesha Sahye, ambacho kiko nchini kwa ajili ya kufanya tathimini ya nchi ilivyojipanga kukabiliana na vitendo hivyo vya utakasishaji fedha haramu, ufadhili wa ugaidi na udhibiti wa usambazaji wa silaha za maangamizi kwa viwango vya kimataifa.
Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar, Mh. Dkt. Saada Mkuya Salum, Mh. Innocent Bashungwa [Waziri wa Mambo ya Ndani - JMT], Mh. Dkt. Doroth Gwajima [Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake, na Makundi Maalum], Eng. Zena Said [Katibu Mkuu Kiongozi - SMZ], Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Bw. Eliakim Chacha Maswi (Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria), Bw. Emmanuel Tutuba [Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania], Bi. Sauda Msemo [Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania na Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Wataalamu Mbalimbali dhidi ya Utakatishaji Fedha Haramu] na Bw. Majaba Magana [Kamishna wa Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu] na Viongozi wengine wa Serikali.
📸:W/Fedha -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Serikali imewahakikishia Watanzania kuwa hakutakuwa na sekta itakayokosa fedha kwa sababu ya mabadiliko ya sera ya baadhi ya mataifa zinazolenga kupunguza kuyasaidia mataifa yanayoendelea ikiwemo Tanzania.
Hayo yamebainishwa bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), wakati akijibu hoja za wabunge zilizojitokeza katika Bunge la Kumi na mbili, mkutano wa 19 katika kikao cha sita.
Alisema Serikali imefanya tathmini katika sekta zote kupitia Timu iliyochini ya Waziri Mkuu na kuanza kuchukua hatua baada ya baadhi ya mataifa kubadili sera zao ili kupunguza fedha kwa nchi zinazoendelea kama Tanzania.
“Tulikuwa na mahitaji ya takribani shilingi bilioni 220 kwenye sekta ya Afya ili kuziba pengo la fedha ambazo tulikuwa tunazitarajia kutoka kwa wadau wa maendeleo, Serikali tayari imetoa kiasi cha shilingi bilioni 98 kwenda kwenye sekta ya afya ili kufidia pengo lililojitokeza na tathmini hiyo inaendelea katika maeneo mengine na utoaji wa fedha utaendelea katika maeneo mengine ambayo yanahitaji fedha”, alisema Dkt. Nchemba.
Aidha, Dkt. Nchemba alimpongeza Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kazi kubwa anayoifanya kwa kuwa ameweza kuivusha nchi kipindi ambacho dunia nzima imekuwa ikipita kwenye msukosuko ya kiuchumi ambayo imekuwa ikitokea mfululizo kwa kipindi cha miaka minne.
Alisema kuwa kulitokea changamoto ya Uviko 19, uhaba wa fedha za kigeni na sasa sera za nje za baadhi ya mataifa ambazo tayari Serikali imeanza kuchukua hatua na kama taifa linaamini litavuka.
Dkt. Nchemba alisema kuwa sekta ya Afya ndiyo iliyoguswa zaidi ambapo Serikali itaendelea kuchukua hatua zaidi ikiwemo kuwekeza fedha kwenye uzalishaji ndani ya nchi wa madawa na vifaa tiba vilivyokuwa vinapatikana kupitia wabia.
Alisema kuwa Mpango wa Maendeleo na Bajeti itakayosomwa katika Bunge linaloendelea, sehemu ya fedha itaelekezwa kwenye viwanda vinavyozalisha madawa ndani ya nchi ili kuweza kujitegemea kama nchi katika eneo hilo.
“Nchi yetu na umri wake na uwezo wake na uwekezaji uliofanyika kwenye sekta ya afya tunaweza kujitegemea kumaliza ugonjwa wa Malaria, magonjwa ya TB, vitenganishi na madawa mengine”, alieleza Dkt. Nchemba.
Alisema kuwa fedha zingine zitaelekezwa kwenye Bima ya Afya kwa wote kama ambavyo Mhe. Rais alivyotoa maelekezo.
Dkt. Nchemba alisema Serikali itatengeneza mkakati wa kubana matumizi kwenye maeneo yenye uhitaji mdogo na kupeleka fedha kwenye maeneo yenye uhitaji mkubwa na ya lazima kama miundombinu, afya, elimu, maji, umeme na sekta zingine za uzalishaji.
Aidha, alibainisha kuwa Tanzania imeingia kwenye kumbukumbu ya kupanga jambo kubwa na kulitekeleza kama mradi wa umeme wa Mwalimu Nyerere, Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) ambao hata baadhi ya mataifa makubwa hawana mradi kama huo ambao kwa sasa zaidi ya kilomita 722 zinaonekana na sehemu kubwa imeanza kufanya kazi hususani kipande cha Dar es Salaam hadi Dodoma.
Alisema vipande vilivyosalia tayari vina Wakandarasi na upatikanaji wa fedha upo katika hatua za mwisho ambapo kuanzia mwaka wa fedha huu fedha katika vipande hivyo itapatikana ili kuhakikisha miradi hiyo inakamilika.
Aliitaja miradi mingine kuwa ni pamoja na Mradi wa Daraja la Kigongo Busisi ambao umekamilika na sasa upo tayari kwa matumizi na mradi wa bomba la mafuta kutoka Hoima hadi Tanga ambapo Tanzania imetekeleza wajibu wake kwa kiasi kikubwa.
Vilevile alisema kuwa tayari amefanya mazungumzo na mawaziri wa kisekta kwenye eneo la barabara, maji, kilimo na sekta nyingine na tayari fedha zimetolewa na na zitaendelea kutolewa.
Amesema mambo yote hayo yanahitaji kuongeza mapato, hivyo Serikali imekubaliana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuongeza elimu kwa mlipa kodi ili kuweza kulipa kodi kwa hiari kama Mhe. Rais alivyoelekeza ambapo elimu itatolewa kwenye michezo, mashuleni na maeneo mengine. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. @mwigulunchemba1 (Mb), ameshiriki hafla ya Ufunguzi wa Kikao cha ngazi ya Juu cha Kikosi Kazi cha Kimataifa cha Kudhibiti Fedha Haramu (The Financial Action Task Force (FATF) Africa Joint Group), kikao kilichofunguliwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, katika Ukumbi wa Mikutano wa Kilimanjaro wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), jijini Dar es Salaam.
Akizungumza wakati akimkaribisha Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa kuhutubia, Mhe. Dkt. Nchemba alisema kuwa Tanzania imeweka mifumo madhubuti ya kukabiliana na vitendo vya utakasishaji fedha haramu na udhibiti wa vitendo vya ufadhili wa ugaidi na kwamba iko tayari kushirikiana na Kikosi kazi hicho kinachoongozwa na Bi. Yonesha Sahye, ambacho kiko nchini kwa ajili ya kufanya tathimini ya nchi ilivyojipanga kukabiliana na vitendo hivyo vya utakasishaji fedha haramu, ufadhili wa ugaidi na udhibiti wa usambazaji wa silaha za maangamizi kwa viwango vya kimataifa.
Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar, Mh. Dkt. Saada Mkuya Salum, Mh. Innocent Bashungwa [Waziri wa Mambo ya Ndani - JMT], Mh. Dkt. Doroth Gwajima [Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake, na Makundi Maalum], Eng. Zena Said [Katibu Mkuu Kiongozi - SMZ], Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Bw. Eliakim Chacha Maswi (Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria), Bw. Emmanuel Tutuba [Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania], Bi. Sauda Msemo [Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania na Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Wataalamu Mbalimbali dhidi ya Utakatishaji Fedha Haramu] na Bw. Majaba Magana [Kamishna wa Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu] na Viongozi wengine wa Serikali. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
URT Updates
@urtupdates
TUTAENDELEA KUDHIBITI UHALIFU WA KIFEDHA-MAJALIWA
WAZIRI MKUU, @KassimMajaliwa_ amesema kuwa Tanzania itaendelea kushiriki na kutimiza matakwa ya kimataifa katika kupambana na kudhibiti uhalifu wa kifedha.
Amesema kuwa Tanzania inatambua changamato za uhalifu wa kifedha na imejidhatiti katika kudhibiti hali hiyo kwa viwango vya kimataifa vilivyopo.
Amesema hayo leo Jumatatu (Aprili 14, 2025) wakati Ufunguzi wa Mkutano kati ya Ujumbe wa Tanzania na Kikosi Kazi cha Kimataifa cha Kudhibiti Fedha Haramu, kwenye ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania @BankOfTanzania jijini Dar es Salaam.
Amesema kuwa kufuatia tathmini zilizofanywa na taasisi za Kuthibiti Uhalifu wa Kifedha Kusini Mashariki mwa Afrika mwaka 2021 na Kikosi cha Kimataifa cha Ushirikiano na Tathmini ya mwaka 2022, Tanzania imeimarisha mifumo ya kupambana na fedha haramu ikiwemo kujengea uwezo wa rasilimali watu na vifaa taasisi zinazohusika katika mapambano hayo.
Waziri Mkuu ameyataja maeneo yaliyofanyiwa kazi kuwa ni mabadiliko ya sheria na sera, matumizi ya takwimu na teknolojia, kuimarisha sekta nyumba na ardhi, kuwajengea uwezo wadau na kuimarisha usimamizi wa Taasisi za za kifedha.
Kwa upande wake, Waziri wa Fedha Dkt. @mwigulunchemba1 amesema kuwa Tanzania baada ya kupokea mpango kazi kutoka Kikosi Kazi cha Kimataifa cha Kupambana na Fedha Haramu ilifanya maamuzi ya ngazi ya juu ya kuimarisha usimamizi uhalifu wa kifedha nchini hali ambayo imeonesha mafanikio makubwa. -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
-
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Huyu ni Prof Michael Ndanshau, Mhadhiri Mwandamizi wa Uchumi wa muda mrefu wa UDSM, Amenifundisha mimi, amemfundisha Zitto Kabwe na wanafunzi wote waliowahikusoma Econ na wa BCOM, na amefundisha vyuo mbalimbali ikiwepo Mkwawa, Sio KAILIMA wala hajawahifanya kazi Tume ya Uchaguzi. Wapuuzeni wazushi hawa, Hawana aibu wala hawamwogopi Mungu. Hawana uchungu na Taifa hili, Ni jitihada za kupandikiza Chuki.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Foreign Affairs 🇵🇱
@PolandMFA
🇵🇱🇹🇿 relations, encouraging 🇵🇱 businesses to invest in Tanzania, and development cooperation between the two countries were the main topics of yesterday’s meeting between Deputy FM @RadwanAnia and Tanzania’s Minister for Finance @mwigulunchemba1.
www.gov.pl/web/diplomacy/deputy-minister-anna-radwan-rhre… -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), ameishukuru Serikali ya Poland kupitia Shirika lake la Bima (KUKE), kwa kuonesha nia ya kudhamini upatikanaji wa fedha kwa ajili ya Ujenzi wa kipande cha 3 na cha 4 cha Mradi wa Reli ya Kisasa wa SGR kuanzia Makutupora hadi Tabora na kinachoanzia Tabora hadi Isaka.
Dkt. Nchemba alitoa shukrani hizo Mjini Warsaw nchini Poland, alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Poland (KUKE), Bw. Janusz Wladyczak, alipokuwa akihitimisha ziara yake ya kikazi katika nchi za Italy, Ufaransa na Poland, iliyolenga kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi kati ya Tanzania na nchi hizo.
Alisema kuwa upatikanaji wa fedha hizo utawezesha ukamilishaji kipande cha 3 (lot 3) cha reli chenye urefu wa km 294, kutoka Makututupora ya mkoani Singida hadi Tabora na kipande kingine cha 4 (lot 4) chenye urefu wa kilometa 130, kutoka Tabora hadi Isaka.
“Mradi huu wa kimkakati ni daraja litakalo ifungua nchi yetu kibiashara na nchi tunazopakana nazo zinazotumia Bandari ya Dar es salaam, kwa kuziba pengo la uhaba wa usafiri wa njia ya reli kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza na kukuza soko la bidhaa katika nchi za ukanda wa Afrika Mashariki na Maziwa Makuu, ikiwemo Uganda, Burundi na DRC Congo” alisema Dkt. Nchemba.
Alifafanua kuwa Ujenzi wa kipande cha 1 na cha 2 cha SGR (Dare Salaam-Morogoro-Dodoma – Makutupora) uliogharimu dola za Marekani bilioni 3.14 umekamilika na huduma za reli zimeanza kutolewa tangu Julai mwaka jana (2024), huku kipande cha 3 hadi 7 cha Reli hiyo kuelekea mkoani Mwanza kitakachogharibu dola za Marekani bilioni 8.6 uko katika hatua mbalimbali za utekelezaji.
Dkt. Nchemba alisema kuwa Serikali inatafuta fedha kutoka vyanzo mbalimbali ili kuwezesha kukamilisha mradi huo mkubwa wa kimkakati na kuishukuru Poland, Kupitia Shirika lake la Bima (KUKE) kwa kuitafutia Serikali fedha za kukamilisha mradi huo utakaochangia kukuza biashara, ajira na hatimaye uchumi wa wananchi na nchi husika zinazoguswa na miundombinu ya Reli hiyo.
Aidha, katika kikao chao, aliliomba Shirika hilo kuwashawishi wawekezaji kutoka Poland kushirikiana na Serikali pamoja na Sekta Binafsi ya Tanzania kuwekeza katika miradi mingine yenye tija hususan katika sekta za kilimo, nishati, maji, afya, utalii na ujenzi wa miundombinu mingine ya viwanda vya uzalishaji bidhaa kwa faida ya nchi hizo mbili kiuchumi na kijamii.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Poland (KUKE), Bw. Janusz Wladyczak, alibainisha kuwa Poland iko tayari kushiriki katika Ujenzi wa Reli ya Kisasa ya SGR kutokana na umuhimu wake kiuchumi kwa Tanzania na nchi Jirani na kuahidi kuwa Poland iko tayari pia kushirikiana na Tanzania kwenye miradi mingine ya maendeleo kupitia Serikali kwa Serikali na wawekezaji binafsi.
Alisema kuwa nchi yake imebobea katika kilimo, uzalishaji wa bidhaa za mifugo, teknolojia ya nishati, madini na bidhaa nyingine kadha wa kadha zinazozalishwa kwa gharama nafuu na ubora wa hali ya juu na kwamba wawekezaji kutoka nchini humo wako tayari kuwekeza Tanzania.
Naye alitoa rai kwa kampuni za Kitanzania, kuwekeza nchini Poland ambapo utaratibu wao ni kwamba kampuni itakayowekeza nchini humo itapewa hadhi ya kuwa Kampuni ya Kipoland na kupewa fursa ya kufaidi soko kubwa la bidhaa la nchi za Jumuiya ya Ulaya. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Miaka 53 ya Kumbukizi ya Kifo cha Hayati Abeid Amani Karume. Tutamuenzi Daima
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa Shirika la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo ( @OECD ), Bw. @MathiasCormann , Makao Makuu ya Shirika hilo yaliyopo Jijini Paris nchini Ufaransa, ambapo pamoja na mambo mengine wamejadiliana namna Tanzania na Shirika hilo wanavyoweza kushirikiana katika kuimarisha usimamizi wa sera za kodi, usimamizi wa fedha za umma, mageuzi ya taasisi za kifedha na kuimarisha masuala ya uwekezaji nchini Tanzania.
Mhe. Dkt. Nchemba ilieleza dhamira ya Serikali ya kuimarisha uwezo wa taasisi zake za kifedha kwa kupokea usaidizi wa kitaalamu kutoka OECD katika maeneo hayo, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuongeza mapato ya ndani, kuvutia uwekezaji na kuboresha mazingira ya biashara
Dkt. Nchemba alisema kuwa Tanzania ipo tayari kushirikiana na Shirika hilo kwa kupokea utaalam katika kuimarisha vyanzo vya mapato ya ndani, kuimarisha uwekezaji na kukuza uchumi jumuishi utakaochangia kuimarisha mapato yake ya ndani, kuboresha zaidi mazingira ya uwekezaji na ufanyaji biashara na hatimaye kukuza uchumi na maendeleo ya wananchi kwa ujumla.
Dkt. Nchemba alisema kuwa Tanzania inakubaliana na utozaji wa kodi wenye usawa katika uwekezaji hususani katika uchumi wa kidigitali hivyo Tanzania inaendelea kuliomba Shirika la OECD kutoa mafunzo ya kiufundi katika eneo hilo.
“Tanzania itaweza kuimarisha usimamizi wa fedha za umma, kuongeza uwazi, na kuvutia mitaji ya kimataifa inayohitajika kwa utekelezaji wa Ajenda ya Maendeleo Endelevu ya 2030” alisema Mhe. Dkt. Nchemba.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Shirika la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo (OECD), Bw. Mathias Cormann alisema kuwa Shirika lake liko tayari kushirikiana na Tanzania katika masuala ya usimamizi wa sera za kodi na uwekezaji ili kukuza Uchumi wa nchi kwa kuvutia zaidi mitaji kutoka nje ya nchi.
Ameipongeza Tanzania kwa juhudi zake katika kuhakikisha kunakuwa na kodi zenye usawa hususani katika mazingira yaliyopo sasa ya uchumi wa kidigitali na kuishauri walishauri Tanzania ijiunge na Kituo cha Maendeleo cha OECD, ambacho kwa sasa kina nchi wanachama 12 kutoka Afrika.
Bw. Cormann alizitaja faida za kuwa mwanachama wa kituo hicho ni pamoja na kuchapishwa kwa takwimu za mapato ya kodi (Revenue Statistics), ambazo hutoa uwazi kwa wawekezaji na wadau wa maendeleo, na kusaidia nchi kuonyesha uwezo wake wa kifedha kwa taasisi za fedha za kimataifa na wawekezaji binafsi.
Aidha, aliialika Tanzania kushiriki katika Mkutano wa Jukwaa la Misaada kwa Maendeleo Endelevu, utakaofanyika mwezi Mei mwaka huu, mkutano ambao utatoa nafasi kwa Tanzania kuwasilisha vipaumbele vyake vya maendeleo, kujifunza kutoka kwa wengine, na kuanzisha ushirikiano mpya katika sekta za mazingira, mabadiliko ya tabianchi na uchumi jumuishi. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Haki Ngowi
@Hakingowi
📍Paris,Ufaransa
▪️DKT. NCHEMBA NA SHIRIKA LA OECD LA UFARANSA WAZUNGUMZIA SERA ZA KODI NA UWEKEZAJI UFARANSA
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa Shirika la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo (OECD), Bw. Mathias Cormann, Makao Makuu ya Shirika hilo yaliyopo Jijini Paris nchini Ufaransa, ambapo pamoja na mambo mengine wamejadiliana namna Tanzania na Shirika hilo wanavyoweza kushirikiana katika kuimarisha usimamizi wa sera za kodi, usimamizi wa fedha za umma, mageuzi ya taasisi za kifedha na kuimarisha masuala ya uwekezaji nchini Tanzania.
📸:Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha-Paris
- -
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa Shirika la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo (OECD), Bw. Mathias Cormann, Makao Makuu ya Shirika hilo yaliyopo Jijini Paris nchini Ufaransa, ambapo pamoja na mambo mengine wamejadiliana namna Tanzania na Shirika hilo wanavyoweza kushirikiana katika kuimarisha usimamizi wa sera za kodi, usimamizi wa fedha za umma, mageuzi ya taasisi za kifedha na kuimarisha masuala ya uwekezaji nchini Tanzania.
Mhe. Dkt. Nchemba ilieleza dhamira ya Serikali ya kuimarisha uwezo wa taasisi zake za kifedha kwa kupokea usaidizi wa kitaalamu kutoka OECD katika maeneo hayo, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuongeza mapato ya ndani, kuvutia uwekezaji na kuboresha mazingira ya biashara
Dkt. Nchemba alisema kuwa Tanzania ipo tayari kushirikiana na Shirika hilo kwa kupokea utaalam katika kuimarisha vyanzo vya mapato ya ndani, kuimarisha uwekezaji na kukuza uchumi jumuishi utakaochangia kuimarisha mapato yake ya ndani, kuboresha zaidi mazingira ya uwekezaji na ufanyaji biashara na hatimaye kukuza uchumi na maendeleo ya wananchi kwa ujumla.
Dkt. Nchemba alisema kuwa Tanzania inakubaliana na utozaji wa kodi wenye usawa katika uwekezaji hususani katika uchumi wa kidigitali hivyo Tanzania inaendelea kuliomba Shirika la OECD kutoa mafunzo ya kiufundi katika eneo hilo.
“Tanzania itaweza kuimarisha usimamizi wa fedha za umma, kuongeza uwazi, na kuvutia mitaji ya kimataifa inayohitajika kwa utekelezaji wa Ajenda ya Maendeleo Endelevu ya 2030” alisema Mhe. Dkt. Nchemba.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Shirika la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo (OECD), Bw. Mathias Cormann alisema kuwa Shirika lake liko tayari kushirikiana na Tanzania katika masuala ya usimamizi wa sera za kodi na uwekezaji ili kukuza Uchumi wa nchi kwa kuvutia zaidi mitaji kutoka nje ya nchi.
Ameipongeza Tanzania kwa juhudi zake katika kuhakikisha kunakuwa na kodi zenye usawa hususani katika mazingira yaliyopo sasa ya uchumi wa kidigitali na kuishauri walishauri Tanzania ijiunge na Kituo cha Maendeleo cha OECD, ambacho kwa sasa kina nchi wanachama 12 kutoka Afrika.
Bw. Cormann alizitaja faida za kuwa mwanachama wa kituo hicho ni pamoja na kuchapishwa kwa takwimu za mapato ya kodi (Revenue Statistics), ambazo hutoa uwazi kwa wawekezaji na wadau wa maendeleo, na kusaidia nchi kuonyesha uwezo wake wa kifedha kwa taasisi za fedha za kimataifa na wawekezaji binafsi.
Aidha, aliialika Tanzania kushiriki katika Mkutano wa Jukwaa la Misaada kwa Maendeleo Endelevu, utakaofanyika mwezi Mei mwaka huu, mkutano ambao utatoa nafasi kwa Tanzania kuwasilisha vipaumbele vyake vya maendeleo, kujifunza kutoka kwa wengine, na kuanzisha ushirikiano mpya katika sekta za mazingira, mabadiliko ya tabianchi na uchumi jumuishi.
@MathiasCormann -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), amesema kuwa mradi wa treni ya kisasa, SGR, utainufaisha nchi ya Tanzania na nchi nyingine zinazotumia Bandari ya Dar es Salaam kiuchumi na kijamii kwa kukuza biashara na uchumi katika Ukanda wa Maziwa Makuu na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC).
Dkt. Nchemba amesema hayo Jijini Paris nchini Ufaransa, alipokutana na kufanya mazungumzo na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Kimataifa ya Societe Generale, Bw. Pierre Palmieri, iliyoshiriki kugharamia mradi wa SGR kipande cha 2 na ununuzi wa mabehewa na vichwa vya treni vya SGR.
Aliishukuru benki hiyo kwa kushiriki katika mradi huo wa kikanda ambao ni wa kimkakati katika kukuza biashara na pia kuonesha nia ya kuendelea kusaidia ujenzi wa SGR unaoendelea ambao kukamilika kwake kutafungua fursa mbalimbali za kiuchumi.
Dkt. Nchemba aliishauri benki hiyo kuangalia maeneo mengine ya kuwekeza nchi Tanzania katika sekta za viwanda, kilimo, nishati, ujenzi wa miundombinu, elimu, afya na pia kushirikiana na sekta binafsi zikiwemo benki za ndani.
Alirejea wito wake kwa Jumuiya ya kimataifa kushirikiana na Tanzania kwa kuwekeza katika mradi huo wa SGR kwa kutoa huduma za uendeshaji ikiwemo miundombinu ya mabehewa na vichwa vya treni ili kunufaika na soko kubwa la biashara ya treni katika ukanda huo zikiwemo nchi ambazo zinategemea Bandari ya Dar es Salaam, ambazo nchi zao hazipakani na Bahari.
Kwa upande wake, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Asociete Generale, Bw. Pierre Palmieri, alisema kuwa benki yake inajivunia kutoa mchango wake katika kuhakikisha kuwa fedha zinapatikana kwa ajili ya mradi huo mkubwa na wa kimkakati kwa nchi ya Tanzania na Ukanda wote wa Afrika.
Bw. Palmieri aliahidi kuwa benki yake itaendelea kuendelea kushirikiana na Tanzania katika maeneo mengine katika nyanja mbalimbali za kiuchumi na kijamii ikiwemo sekta ya madini pamoja na ushauri wa kitaalamu katika sekta ya masoko ya mitaji. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
JIMBO LA IRAMBA MAGHARIBI
@jimbolairamba
UFARANSA YAKARIBISHWA KUWEKEZA KWENYE VIWANDA VYA KUTENGENEZA DAWA MUHIMU NCHINI TANZANIA www.mwigulunchemba.com/2025/04/04/ufaransa-yakaribishwa-k…
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), ametembelea Ubalozi wa Tanzania, Mjini Paris, nchini Ufaransa, akiwa katika ziara ya kikazi nchini humo na kuzungumza na Balozi wa Tanzania, Mhe. Ali Jabir Mwadini, ambapo pamoja na mazungumzo mengine, alimpongeza yeye binafsi na wafanyakazi wote wa Ubalozi huo kwa kazi nzuri ya kuiwakilisha nchi na kusimamia diplomasia ya uchumi katika Taifa hilo, baada ya kupokea taarifa fupi ya utekelezaji wa majukumu ya Ubalozi huo.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Bank of Tanzania
@BankOfTanzania
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Haki Ngowi
@Hakingowi
📍Paris ,Ufaransa
▪️UFARANSA YAKARIBISHWA KUWEKEZA KWENYE VIWANDA VYA KUTENGENEZA DAWA MUHIMU NCHINI TANZANIA
Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), ametoa wito kwa wawekezaji kutoka Ufaransa kuwekeza nchini Tanzania katika Sekta ya viwanda vya kuzalisha dawa za binadamu ili kukabiliana na upungufu wa dawa muhimu za binadamu hali inayosababishwa na mabadiliko sera za nchi mbalimbali duniani.
Dkt. Nchemba ametoa rai hiyo jijini Paris nchini Ufaransa, alipokutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD), ukiongozwa na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Bw. Bertrand Walckenaer.
Alisema Serikali ya Tanzania chini ya Uongozi wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inajipanga kutekeleza miradi ya ujenzi wa viwanda vitakavyozalisha dawa muhimu zikiwemo za malaria, kifua kikuu na dawa za kufubaza virusi vya ukimwi (ARVs) ili kulinda maisha ya watu.
Dkt. Nchemba alikuwa akijibu hoja ya Kiongozi huyo wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) Bw. Walckenaer, aliyetaka kufahamu mipango ya Serikali ya kukabiliana na mabadiliko ya Sera za Serikali ya Marekani ambayo imesitisha utoaji misaada kwenye sekta mbalimbali ikwemo ya Afya.
Aliishauri AFD kuiunga mkono Tanzania katika kutekeleza azma ya kujenga miundombinu ya viwanda vya uzalishaji wa bidhaa hizo ili kunusuru maisha ya mamia ya wananchi waliokuwa wakitegemea misaada ya dawa kutoka nje ya nchi na kwamba wawekezaji watanufaika na soko kubwa la bidhaa na huduma katika eneo lote la Maziwa Makuu na nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
“Tunaikaribisha AFD kushirikiana na Serikali ya Tanzania pamoja na Sekta binafsi katika uzalishaji wa dawa na vifaa tiba ili nchi iweze kujitegemea katika eneo muhimu la Afya”, alieleza Dkt. Nchemba.
Aidha, alisema kuwa Serikali ya Ufaransa imekuwa ikiisaidia Tanzania katika agenda za maendeleo kuanzia mwaka 1980, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Dar es Salaam, maendeleo ya sekta ya nishati, maji na kilimo, miradi ambayo imekuwa na manufaa makubwa kwa wananchi.
Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD), Bw. Bertrand Walckenaer, alisema kuwa suala la nchi za Afrika ikiwemo Tanzania kuwa na viwanda vyake vya kuzalisha dawa ni muhimu kwa ajili ya mustakabali wa maisha ya wananchi wake.
Alibainisha kuwa hatua ya Marekani ya kufuta misaafa ya sekta ya afya na misaada ya kibinadamu zilizokuwa zikisaidia mataifa mbalimbali duniani kupitia Shirika lake la Misaada (USAID), zinasababisha kuwe na ulazima wa nchi zinazoendelea zilizokuwa zinanufaika na misaada hiyo kutafuta namna ya kukabiliana na hali hiyo.
Aliahidi kuishawishi sekta binafsi kutoka Ufaransa kuwekeza nchini Tanzania katika sekta ya afya kwa kujenga viwanda vya kutengeneza dawa ili kutimiza lengo na matarajio ya nchi katika kuwahudumia wananchi.
Alisifu mazingira ya uwekezaji nchini Tanzania, pamoja na usimamizi mzuri wa uchumi wa nchi na mazingira mazuri ya uwekezaji unaopaswa kupigiwa mfano na mataifa mengine ya Afrika.
Bw. Bw. Bertrand Walckenaer, alisema Shirika la Maendeleo la Ufaransa limewekeza kiasi cha Euro bilioni 1.3 kwa miradi mbalimbali nchini Tanzania kutokana na utulivu wa sera na uchumi wake na kwamba wataendelea kushirikiana na Tanzania katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwa manufaa ya nchi hizo mbili.
Fedha hizi zimeelekezwa kwenye miradi ya sekta za; Maji, Nishati, Miundombinu ya Usafirishaji, Kilimo na Maliasili na Utalii.
📸:W/Fedha -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), ametoa wito kwa wawekezaji kutoka Ufaransa kuwekeza nchini Tanzania katika Sekta ya viwanda vya kuzalisha dawa za binadamu ili kukabiliana na upungufu wa dawa muhimu za binadamu hali inayosababishwa na mabadiliko sera za nchi mbalimbali duniani.
Dkt. Nchemba ametoa rai hiyo jijini Paris nchini Ufaransa, alipokutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa ( @AFD_en ), ukiongozwa na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Bw. Bertrand Walckenaer.
Alisema Serikali ya Tanzania chini ya Uongozi wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inajipanga kutekeleza miradi ya ujenzi wa viwanda vitakavyozalisha dawa muhimu zikiwemo za malaria, kifua kikuu na dawa za kufubaza virusi vya ukimwi (ARVs) ili kulinda maisha ya watu.
Dkt. Nchemba alikuwa akijibu hoja ya Kiongozi huyo wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) Bw. Walckenaer, aliyetaka kufahamu mipango ya Serikali ya kukabiliana na mabadiliko ya Sera za Serikali ya Marekani ambayo imesitisha utoaji misaada kwenye sekta mbalimbali ikwemo ya Afya.
Aliishauri AFD kuiunga mkono Tanzania katika kutekeleza azma ya kujenga miundombinu ya viwanda vya uzalishaji wa bidhaa hizo ili kunusuru maisha ya mamia ya wananchi waliokuwa wakitegemea misaada ya dawa kutoka nje ya nchi na kwamba wawekezaji watanufaika na soko kubwa la bidhaa na huduma katika eneo lote la Maziwa Makuu na nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
“Tunaikaribisha AFD kushirikiana na Serikali ya Tanzania pamoja na Sekta binafsi katika uzalishaji wa dawa na vifaa tiba ili nchi iweze kujitegemea katika eneo muhimu la Afya”, alieleza Dkt. Nchemba.
Aidha, alisema kuwa Serikali ya Ufaransa imekuwa ikiisaidia Tanzania katika agenda za maendeleo kuanzia mwaka 1980, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Dar es Salaam, maendeleo ya sekta ya nishati, maji na kilimo, miradi ambayo imekuwa na manufaa makubwa kwa wananchi.
Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD), Bw. Bertrand Walckenaer, alisema kuwa suala la nchi za Afrika ikiwemo Tanzania kuwa na viwanda vyake vya kuzalisha dawa ni muhimu kwa ajili ya mustakabali wa maisha ya wananchi wake.
Alibainisha kuwa hatua ya Marekani ya kufuta misaafa ya sekta ya afya na misaada ya kibinadamu zilizokuwa zikisaidia mataifa mbalimbali duniani kupitia Shirika lake la Misaada (USAID), zinasababisha kuwe na ulazima wa nchi zinazoendelea zilizokuwa zinanufaika na misaada hiyo kutafuta namna ya kukabiliana na hali hiyo.
Aliahidi kuishawishi sekta binafsi kutoka Ufaransa kuwekeza nchini Tanzania katika sekta ya afya kwa kujenga viwanda vya kutengeneza dawa ili kutimiza lengo na matarajio ya nchi katika kuwahudumia wananchi.
Alisifu mazingira ya uwekezaji nchini Tanzania, pamoja na usimamizi mzuri wa uchumi wa nchi na mazingira mazuri ya uwekezaji unaopaswa kupigiwa mfano na mataifa mengine ya Afrika.
Bw. Bw. Bertrand Walckenaer, alisema Shirika la Maendeleo la Ufaransa limewekeza kiasi cha Euro bilioni 1.3 kwa miradi mbalimbali nchini Tanzania kutokana na utulivu wa sera na uchumi wake na kwamba wataendelea kushirikiana na Tanzania katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwa manufaa ya nchi hizo mbili.
Fedha hizi zimeelekezwa kwenye miradi ya sekta za; Maji, Nishati, Miundombinu ya Usafirishaji, Kilimo na Maliasili na Utalii. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
JIMBO LA IRAMBA MAGHARIBI
@jimbolairamba
𝐃𝐊𝐓 . 𝐍𝐂𝐇𝐄𝐌𝐁𝐀 𝐀𝐙𝐔𝐑𝐔 𝐔𝐁𝐀𝐋𝐎𝐙𝐈 𝐖𝐀 𝐓𝐀𝐍𝐙𝐀𝐍𝐈𝐀 𝐍𝐂𝐇𝐈𝐍𝐈 𝐈𝐓𝐀𝐋𝐘
www.mwigulunchemba.com/2025/04/03/dkt-nchemba-azuru-ubalo… -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
JIMBO LA IRAMBA MAGHARIBI
@jimbolairamba
𝐃𝐊𝐓. 𝐍𝐂𝐇𝐄𝐌𝐁𝐀 𝐀𝐊𝐔𝐓𝐀𝐍𝐀 𝐍𝐀 𝐔𝐉𝐔𝐌𝐁𝐄 𝐖𝐀 𝐁𝐄𝐍𝐊𝐈 𝐘𝐀 𝐌𝐀𝐄𝐍𝐃𝐄𝐋𝐄𝐎 𝐘𝐀 𝐈𝐓𝐀𝐋𝐘
www.mwigulunchemba.com/2025/04/03/dkt-nchemba-akutana-na-… -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Haki Ngowi
@Hakingowi
📍Rome,Italy
▪️DKT. NCHEMBA AKUTANA NA UJUMBE WA BENKI YA MENDELEO YA ITALY
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe wa Benki ya Maendeleo ya Italia (CDP International Development Cooperation), ukiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Bw. Dario Scannapieco, Mjini Rome Italia, ambapo pamoja na mambo mengine, walijadiliana kuhusu namna Tanzania na Benki hiyo, zitakavyoshirikiana katika utekelezaji wa miradi ya kiuchumi na kijamii ikiwemo kilimo (usalama wa chakula), kukuza uzalishaji viwandani, usalama wa nishati na miundombinu endelevu, sekta ya maji, afya, elimu na mafunzo pamoja na kuiwezesha sekta binafsi kushiriki katika shughuli za kukuza uchumi wa nchi.
Miongoni mwa maeneo ambayo Taasisi hiyo inaisaidia Tanzania ni pamoja na sekta ya elimu ambapo imetoa ufadhili wa ujenzi wa vyuo vya ufundi vya elimu ya juu ikiwemo Karume Institute of Science and Technology, Arusha Technical College, Mbeya University of Science and Technology na Dar es Salaam Institute of Technology, ambavyo vinatarajia kutoa usaidizi wa kukuza ujuzi na ajira hususan kwa vijana
📸:W/Fedha -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
TheGuardianTzOnline
@TheGuardianTzO1
#photo Finance Minister Dr Mwigulu Nchemba (L) pictured in Rome, Italy, yesterday exchanging greetings with Italian Credit Insurance Agency CEO Alessandra Ricci. He commended Italy for having pledged a loan guarantee in support of the subsequent implementation of...
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe wa Benki ya Maendeleo ya Italia (CDP International Development Cooperation), ukiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Bw. Dario Scannapieco, Mjini Rome Italia, ambapo pamoja na mambo mengine, walijadiliana kuhusu namna Tanzania na Benki hiyo, zitakavyoshirikiana katika utekelezaji wa miradi ya kiuchumi na kijamii ikiwemo kilimo (usalama wa chakula), kukuza uzalishaji viwandani, usalama wa nishati na miundombinu endelevu, sekta ya maji, afya, elimu na mafunzo pamoja na kuiwezesha sekta binafsi kushiriki katika shughuli za kukuza uchumi wa nchi.
Miongoni mwa maeneo ambayo Taasisi hiyo inaisaidia Tanzania ni pamoja na sekta ya elimu ambapo imetoa ufadhili wa ujenzi wa vyuo vya ufundi vya elimu ya juu ikiwemo Karume Institute of Science and Technology, Arusha Technical College, Mbeya University of Science and Technology na Dar es Salaam Institute of Technology, ambavyo vinatarajia kutoa usaidizi wa kukuza ujuzi na ajira hususan kwa vijana. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Bank of Tanzania
@BankOfTanzania
Zoezi la ubadilishwaji wa noti za zamani lililoanza tarehe 06 Januari 2025 linatarajiwa kumalizika tarehe 05 Aprili 2025 ambapo matumizi ya noti hizo yatafikia ukomo wa kuwa fedha halali za Tanzania.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), ametembelea Ubalozi wa Tanzania mjini Rome nchini Italia akiwa katika ziara ya kikazi nchini humo na kuzungumza na wafanyakazi wa Ubalozi huo ambapo aliwapongeza kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kuiwakilisha nchi kupitia diplomasia ya uchumi katika Taifa hilo baada ya kupokea taarifa fupi ya utekelezaji wa majukumu ya Ubalozi huo kutoka kwa Kaimu Mkuu wa Kituo cha Ubalozi wa Tanzania nchini Italia, Bi. Eva Kaluwa.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
JIMBO LA IRAMBA MAGHARIBI
@jimbolairamba
DKT. NCHEMBA ATETA NA MKURUGENZI MTENDAJI WA SACE NCHINI ITALIA
www.mwigulunchemba.com/2025/04/02/dkt-nchemba-ateta-na-mk… -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Haki Ngowi
@Hakingowi
📍Rome
▪️DKT. NCHEMBA ATETA NA MKURUGENZI MTENDAJI WA SACE NCHINI ITALIA
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) ameishukuru Italia kwa kutoa dhamana ya mkopo wa kujenga Reli ya Kisasa (SGR), kipande cha Kwanza na cha pili kuanzia Dar es Salaam, Morogoro, Dodoma hadi Makutupora mkoani Singida, ambavyo ujenzi wake umekamilika na treni imeanza kutoa huduma kuanzia Dar es salaam hadi Dodoma.
Mhe. Dkt. Nchemba ametoa shukrani hizo mjini Rome nchini Italia, alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Italia (SACE), Bi. Alessandra Ricci.
Alieleza kuwa kutokana na mchango huo, SGR imeanza kutoa huduma ya kubeba abiria kuanzia Julai mwaka 2024, ikiwa ni mafanikio makubwa katika historia ya usafiri nchini, ambapo muda wa safari kati ya Dar es Salaam na Dodoma umepungua kutoka saa nane hadi takriban saa tatu.
Aidha, Mhe. Waziri Nchemba alieleza kuwa Serikali inatambua na kuthamini nia njema ya SACE kuendelea kudhamini ujenzi wa reli toka Dodoma hadi Isaka
Aidha, Dkt. Nchemba aliwaalika wawekezaji kutoka Italia kwenda kuwekeza nchini Tanzania katika sekta mbalimbali ikiwemo uendeshaji wa miundombinu ya reli pamoja na ujenzi wa viwanda vitakavyosaidia kukuza ajira na kukuza uchumi wa nchi wa pande hizo mbili.
Alisema kuwa Tanzania iko katika eneo zuri la kimkakati kijiografia kwa kupakana na nchi 6 zisizopakana na Bahari na zinazotegemea Bandari ya Dar Es Salaam, hatua ambayo inalifanya eneo lote la nchi na nchi jirani kuwa soko zuri na la ukakika la bidhaa na huduma na kuishauri sekta binafsi ya nchi hiyo kuchangamkia fursa hizo.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Italia, SACE, Bi. Alessandra Ricci, alisema kuwa Italia imeichagua Tanzania kuwa miongoni mwa nchi 14 za Afrika zitakazonufaika na usadizi wa kifedha kutoka nchi hiyo kutokana na uhusiano mzuri wa kiuchumi uliopo kati ya nchi hizo mbili kupitia Mpango wake wa Ushhirikiano kati ya Italia na nchi za Afrika ujulikanao kama Piano Mattei.
Bi. Ricci aliahidi kuwa Shirika lake liko tayari kuendelea kushirikiana na Tanzania katika kugharamia mradi wa SGR kipande cha 3 na 4. kinachoanzia Makutupora mkoani Singida -Tabora hadi Isaka, kutokana na umuhimu wa mradi huo katika kukuza biashara katika ukanda wa Afrika Mashariki na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
📸:W/Fedha -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb) ameishukuru Italia kwa kutoa dhamana ya mkopo wa kujenga Reli ya Kisasa (SGR), kipande cha Kwanza na cha pili kuanzia Dar es Salaam, Morogoro, Dodoma hadi Makutupora mkoani Singida, ambavyo ujenzi wake umekamilika na treni imeanza kutoa huduma kuanzia Dar es salaam hadi Dodoma.
Mhe. Dkt. Nchemba ametoa shukrani hizo mjini Rome nchini Italia, alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Italia ( @sacesimest ), Bi. Alessandra Ricci.
Alieleza kuwa kutokana na mchango huo, SGR imeanza kutoa huduma ya kubeba abiria kuanzia Julai mwaka 2024, ikiwa ni mafanikio makubwa katika historia ya usafiri nchini, ambapo muda wa safari kati ya Dar es Salaam na Dodoma umepungua kutoka saa nane hadi takriban saa tatu.
Aidha, Mhe. Waziri Nchemba alieleza kuwa Serikali inatambua na kuthamini nia njema ya SACE kuendelea kudhamini ujenzi wa reli toka Dodoma hadi Isaka
Aidha, Dkt. Nchemba aliwaalika wawekezaji kutoka Italia kwenda kuwekeza nchini Tanzania katika sekta mbalimbali ikiwemo uendeshaji wa miundombinu ya reli pamoja na ujenzi wa viwanda vitakavyosaidia kukuza ajira na kukuza uchumi wa nchi wa pande hizo mbili.
Alisema kuwa Tanzania iko katika eneo zuri la kimkakati kijiografia kwa kupakana na nchi 6 zisizopakana na Bahari na zinazotegemea Bandari ya Dar Es Salaam, hatua ambayo inalifanya eneo lote la nchi na nchi jirani kuwa soko zuri na la ukakika la bidhaa na huduma na kuishauri sekta binafsi ya nchi hiyo kuchangamkia fursa hizo.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Italia, SACE, Bi. Alessandra Ricci, alisema kuwa Italia imeichagua Tanzania kuwa miongoni mwa nchi 14 za Afrika zitakazonufaika na usadizi wa kifedha kutoka nchi hiyo kutokana na uhusiano mzuri wa kiuchumi uliopo kati ya nchi hizo mbili kupitia Mpango wake wa Ushhirikiano kati ya Italia na nchi za Afrika ujulikanao kama Piano Mattei.
Bi. Ricci aliahidi kuwa Shirika lake liko tayari kuendelea kushirikiana na Tanzania katika kugharamia mradi wa SGR kipande cha 3 na 4. kinachoanzia Makutupora mkoani Singida -Tabora hadi Isaka, kutokana na umuhimu wa mradi huo katika kukuza biashara katika ukanda wa Afrika Mashariki na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC). -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
JIMBO LA IRAMBA MAGHARIBI
@jimbolairamba
𝐄𝐈𝐃 𝐌𝐔𝐁𝐀𝐑𝐀𝐊
-
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Mabala
@Mabala84
Mwigulu asimulia alivyo Mchumbia Mkewe 😘
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Bank of Tanzania
@BankOfTanzania
-
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Asante sana Kaka yangu Kibanda.
Absalom Kibanda
@absakibanda
Keep the faith brother. Mungu awafute machozi. Mpe pole shemeji yetu mcha Mungu
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
HABARIMPYA TV
@HabarimpyaTv
Dar es Salaam, 24 Machi 2025 – Ibada ya maombolezo ya Marehemu Wilfred Joachim Ngure, Mkwe wa Waziri wa Fedha, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Nchemba, imefanyika jana usiku jijini Dar es Salaam.
Ibada hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali akiwemo Waziri wa Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha anayesimamia Uchumi, Ndugu Elijah Mwandumbya, pamoja na maafisa waandamizi wa wizara hiyo wakiwemo Kamishna wa Idara ya Fedha za Nje, Ndugu Rished Bade, Kamishna wa Idara ya Sera, Ndugu Johnson Nyela, na Kamishna wa Deni la Taifa, Ndugu Japhet Sayi. Ibada hiyo iliongozwa na Mchungaji Daniel Sendoro.
Mwili wa Marehemu unatarajiwa kuwasili nchini leo mchana na utapelekwa Hospitali ya Jeshi ya Lugalo kwa maandalizi ya mwisho kabla ya kuagwa kesho nyumbani kwake, Boko DAWASA. Baada ya shughuli hiyo, mwili wa Marehemu utasafirishwa hadi Shia, Old Moshi, mkoani Kilimanjaro, ambako maziko yatafanyika Jumatano, tarehe 26 Machi 2025.
Tunaendelea kuwaombea faraja familia, ndugu na marafiki wa Marehemu katika kipindi hiki kigumu. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi. -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Asante sana ndugu yangu.
CharlieBihemo
@CharlieBihemo
Pole Sana Kiongozi Waziri wa Fedha Mhe @mwigulunchemba1 Kwa Msiba Mzito wa Baba mkwe wako
MUNGU awatie nguvu kwenye kipindi hiki kigumu cha kumpoteza Mzee Ngure
Mzee huyu ambae amalitumikia taifa hili akiwa Mtumishi wa Jeshi la Magereza
Mungu amlaze mahari Pema peponi amina -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Asante sana Comrade.
Peter Madeleka
@PMadeleka
POLE SANA Mheshimiwa @mwigulunchemba1 kwa KUFIWA na BABA MKWE wako. MUNGU akawe FARAJA kwenu kwenye kipindi hiki cha HUZUNI na MAOMBOLEZO. Bwana alitoa, na Bwana AMETWAA, jina lake LIHIMIDIWE.
-
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Asante sana Mashibe.
BANTU MEDIA
@BantuMTZ
Pole sana @mwigulunchemba1 na Neema Mwigulu kwa Msiba mzito, Mwenyezi Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya Marehemu. Amen.
-
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Asante sana ndugu yangu.
Michael Bwoma
@MichaelBwoma
Sorry for your Loss mzee wangu @mwigulunchemba1, Mungu amuweke mahala pema peponi, Amen. Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lihimidiwe
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
TRA Tanzania
@TRATanzania
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Bank of Tanzania
@BankOfTanzania
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Bank of Tanzania
@BankOfTanzania
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Bank of Tanzania
@BankOfTanzania
UCHUMI WA TANZANIA WAZIDI KUIMARIKA – GAVANA TUTUBA
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Emmanuel Tutuba, ameeleza kuwa hali ya uchumi wa nchi inaendelea kuimarika, huku sekta ya fedha ikionyesha uimara na ukuaji thabiti. -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Hatua nyingine kubwa katika kutekeleza ahadi ya Mhe. Rais Dkt. @SuluhuSamia ya kumtua mama ndoo kichwani. Tumeanza utekelezaji wa Ujenzi wa Mradi wa Maji safi na salama wa Tunduma-Vwawa Mkoani Songwe, wenye thamani ya TZS Bilioni 119.9. Mradi huu utawahudumia wananchi 219,309.
Post not available here, view on X
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
HABARIMPYA TV
@HabarimpyaTv
Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba @mwigulunchemba1 ni miongoni mwa Viongozi wanaotambua mchango mkubwa wa Waziri wa Maji Jumaa Aweso Jumaa Aweso katika sekta ya maji na usimamizi wa kampeni ya Rais Samia @SuluhuSamia ya kumtua mama ndoo kichwani,.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), ameshuhudia utiwaji saini wa Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji wa Tunduma,- Vwawa, Kati ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Eng. Mwajuma Waziri, kwa niaba ya Serikali na Meneja Mradi wa Kampuni ya Ukandarasi ya China (China Civil Engineering Construction Corporation-CCECC), Bw. Ning Yunfeng, utakaogharimu shilingi bilioni 119.9 za Tanzania, kutoka chanzo cha maji ya Mto Momba, ulioko Wilayani Momba, mkoani Songwe.
Mradi huo utahusisha ujenzi wa chanzo cha maji (Intake) chenye uwezo wa kuhifadhi lita milioni 21.5, ujenzi wa Kituo cha kuchakata na kutibu maji chenye uwezo wa kuzalisha lita 20m kwa siku, ujenzi wa mtandao wa mabomba ya kusafirisha maji yenye kipenyo cha 100mm yenye urefu wa kilometa 96, ujenzi wa matenki ya maji yenye uwezo wa kuhifadhi ujazo wa lita 5m litakalojengwa katika Mtaa wa Uwanjani/Uhuru, Hakmashauri ya Mji-Tunduma, tenki la lita 3m litakalojengwa katika Kijiji cha Ikana na tenki lenye ujazo wa lita 2m litakalojengwa katika Kijiji cha Nkangamo, Ununuzi wa pampu, Ujenzi wa Ofisi na Vitendeakazi vingine.
Akihutubia mamia ya wakazi wa Mkoa wa Songwe waliojitikeza kushuhudia tukio hilo katika Viwanja vya Uwanjani, mjini Tunduma, Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, aliwahakikishia wananchi hao kuwa Serikali itatoa fedha zote za kutekeleza mradi huo ambao ni ahadi ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya kumtua mama ndoo kichwani.
Kwa upande wake, Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso, alimpongeza Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kutoa kiasi hicho cha fedha takriben sh. bilioni 120, ambazo ni fedha za ndani, kwa ajili ya kuwaondolea adha ya maji wananchi wa Tunduma, Vwawa na Mlowo, watakaofikiwa na mradi huo.
Mradi huo unatarajia kuwanufaisha wakazi 219,309 katika miji hiyo ya Tunduma, Vwawa na Mlowo, ambapo ujenzi wake utachukua miezi 18 kukamilika na kuanza kutoa maji safi na salama. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
URT Updates
@urtupdates
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), ameshuhudia utiwaji saini wa Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji wa Tunduma,- Vwawa, Kati ya Katibu Mkuu @maji_mowi, Eng. Mwajuma Waziri, kwa niaba ya Serikali na Meneja Mradi wa Kampuni ya Ukandarasi ya China (China Civil Engineering Construction Corporation-@CCECC8), Bw. Ning Yunfeng, utakaogharimu Tsh. bilioni 119.9 kutoka chanzo cha maji ya Mto Momba, ulioko Wilayani Momba, mkoani Songwe.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Miaka minne ya Mhe. Dkt. @SuluhuSamia , Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
-
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Hongera Mheshimiwa Rais @SuluhuSamia kwa kutimiza miaka 4 ya uongozi wako thabiti na wenye dira. Katika kipindi hiki, Tanzania imepiga hatua kubwa kiuchumi kwa kuimarisha ukusanyaji wa mapato, kudhibiti mfumuko wa bei, kukuza uwekezaji, kukamilisha miradi ya kimkakati na kuimarisha sekta za kimkakati kama nishati, miundombinu, na kilimo. Uongozi wako umeleta mageuzi ya kweli na kuimarisha ustawi wa Taifa kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho. 🇹🇿💚
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Victoria Kwakwa
@VictoriaKwakwa
Nimefurahi sana kukutana tena na Mheshimiwa Dkt. @mwigulunchemba1. Nimetoa shukrani zetu za dhati kwa #tanzania kwa mafanikio ya Mkutano wake wa Nishati uliofanyika Januari na kupongeza ushirikiano wetu uliodumu kwa zaidi ya miaka 63. #poweringafrica
-
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
It was a pleasure meeting you once again, @VictoriaKwakwa. Tanzania sincerely appreciates your leadership and commitment to strengthening our enduring partnership with the @WorldBank. Your contributions have been pivotal in advancing key economic and social initiatives, including energy, infrastructure, and financial reforms.
As you complete your tenure, we reaffirm our commitment to deepening this collaboration and look forward to working closely with your successor to drive Tanzania’s development agenda forward. Wishing you continued success in your next endeavors.
#poweringtanzania
#poweringafrica
Victoria Kwakwa
@VictoriaKwakwa
It was a pleasure to meet Hon. Dr. @mwigulunchemba1 once again. I conveyed our deep appreciation for #tanzania’s successful Energy Summit in January and reaffirmed our enduring partnership—63 years and counting. #poweringafrica
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Victoria Kwakwa
@VictoriaKwakwa
Nimefurahi kukutana na Mheshimiwa Rais @SuluhuSamia na kuipongeza #tanzania kwa uongozi wake katika rasilimali watu na upatikanaji wa nishati. Nilimpongeza kwa Mkataba wa Kitaifa wa Nishati wenye lengo la kuunganisha kaya milioni 8.3 na kufikia asilimia 75 ya umeme ifikapo 2030.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Victoria Kwakwa
@VictoriaKwakwa
It was a pleasure to meet Hon. Dr. @mwigulunchemba1 once again. I conveyed our deep appreciation for #tanzania’s successful Energy Summit in January and reaffirmed our enduring partnership—63 years and counting. #poweringafrica
-
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Pumzika Pema JPM.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha. Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), ameagana na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia Kanda Afrika Mashariki na Kusini, Bi. @VictoriaKwakwa , anayekaribia kumaliza muda wake, wakati wa Chakula cha Jioni alichomwandalia Jijiji Dar es Salaam, na kumshukuru kwa jitihada zake za kusimamia maslahi ya Tanzania kwa upendo wa hali ya juu katika kipindi chote alichoitumikia Taasisi hiyo kubwa ya Fedha Duniani.
Kwa Upande wake, Bi. Victoria Kwakwa, alisifu ushirikiano alioupata kutoka kwa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, na kwamba anajivunia mafanikio makubwa ambayo Tanzania imeyafikia katika nyanja za kiuchumi na kijamii, kwa kuwa na uchumi imara, ikilinganishwa na nchi nyingi za Afrika.
Alisema kuwa anastaafu kazi lakini ana uhakika Makamu Mpya wa Rais wa Benki ya Dunia atakaye chukua nafasi yake (Jina linahifadhiwa) kuzisimamia nchi za Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika, atatoa ushirikiano mkubwa kwa Tanzania ili nchi iweze kufikia malengo iliyokusudiwa kupitia Benki ya Dunia.
Tukio hilo la kumuaga Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia, Bi. Victoria Kwakwa, imehudhuriwa pia na Naibu Waziri wa Uchukuzi, Mhe. David Mwakiposa Kihenzile, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban, Mkurugenzi wa Biashara ya Kimataifa na Diplomasia ya Uchumi, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi John Ulanga, Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia, Bw. Nathan Belete, Kamishna wa Idara ya Fedha za Nje, Wizara ya Fedha, Bw. Rished Bade, na Maafisa wengine waandamizi wa Wizara ya Fedha na Benki ya Dunia.
@WBTanzania @WorldBank @WorldBankAfrica @BeleteNathan -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), amerejea salama nchini baada ya kushiriki Mkutano wa 50 wa Bodi ya Wadhamini (Governing Council) ya Benki ya Maendeleo ya Afrika Mashariki (EADB), pamoja na Mawaziri wenzake wa Fedha, Mhe. Matia Kasaija (Uganda), Mhe. Ng’ongo John Mbadi (Kenya) na Mhe. Yusuf Murangwa (Rwanda) uliofanyika, katika Hoteli ya Serena, Kampala-Uganda.
Tanzania ni mwanahisa wa Benki hiyo ya Maendeleo ya Afrika Mashariki yenye ukwasi mkubwa na imekuwa ikiipatia Serikali mikopo nafuu inayotumika kuchagiza maendeleo ya nchi, pamoja na kuiwezesha Sekta Binafsi katika nchi wanachama kutekeleza miradi ya maendeleo.
Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebe, Mhe. Dkt. Nchemba, aliagwa na Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Mhe. Meja Jenerali Paul Simuli. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), ametembelea Ofisi za Ubalozi wa Tanzania ziizopo Kampala nchini Uganda, baada ya kuhitimisha Mkutano wa 50 wa Benki ya Maendeleo Afrika Mashariki (EADB) na kumpongeza Mhe. Balozi wa Tanzania nchini humo, Meja Jenerali Paul Simuli na watumishi wa Ubalozi huo kwa kazi nzuri wanayofanya.
Alisisitiza umuhimu wa kuendelea kuimarisha diplomasia ya uchumi na kuzitumia fursa mbalimbali za ukuzaji biashara kwa manufaa ya nchi hizo mbili ikizingatiwa kuwa Tanzania na Uganda ni nchi rafiki na zina historia kubwa na ya kujivunia.
Katika ziara hiyo, Mhe. Dkt. Nchemba aliambatana na Kamishna wa Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Dkt. Charles Mwamwaja na Maafisa wengine wa Serikali. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
UNAFRI
@UNAFRI21
On Friday, 14th March 2025, the Honorable Dr. Mwigulu Lameck Nchemba Madalu (MP) @mwigulunchemba1 , Minister for Finance of Tanzania @mofURT , engaged in a meeting with Mr. Munanura Andrew Karokora @KarokoraAndrew , Deputy Director General of the United Nations African Institute for the Prevention of Crime and the Treatment of Offenders (UNAFRI), in Kampala, Uganda. During the meeting, Mr. Karokora provided a comprehensive overview of UNAFRI's operations and its pivotal role in enhancing crime prevention and criminal justice systems across Africa. He extended his appreciation to Tanzania for its continued financial support and active participation in the institute's programs. The meeting was also attended by Dr. Ahmed Linga, Director of Training and Programmes at UNAFRI, and Dr. Charles Mwamwaja @Dr_C_Mwamwaja , Commissioner of Financial Sector Development at the Ministry of Finance, Tanzania.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Uwakilishi kutoka Shirika la Kikanda la Umoja wa Mataifa lijulikanalo kama United Nations African Institute for the Prevention of Crime and the Treatment of Offenders ( @UNAFRI21 ), lenye Makao Makuu yake Kampala, Uganda, ukiongozwa na Naibu Mkurugenzi wake Mkuu, Bw. Munanura Andrew Karokora, kando ya Mkutano wa 50 wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Mashariki (EADB), ambapo walijadili masuala ya ushirikiano kati ya Tanzania na Taasisi hiyo katika wajibu wa kifedha (financial obligations).
Pamoja na hayo, walijadili pia uwezekano wa ushirikiano wa UNAFRI na Wizara katika kuratibu programu za mafunzo na tafiti kwa taasisi za Wizara pamoja na taasisi nyingine za kifedha hususani katika masuala ya uzuiaji uhalifu wa kifedha (financial crime prevention).
Kikao hicho kifupi kiliwashirikisha pia Kamishna wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Dkt. Charles Mwamwaja na Dkt. Ahmed Linga ambaye ni Mkurugenzi wa Mafunzo na Programu wa UNAFRI. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Bank of Tanzania
@BankOfTanzania
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), amekutana na kufanya Mazungumzo na Waziri wa Uchukuzi wa Uganda, Jenerali Edward Katumba Wamala, Kando ya Mkutano wa 50 wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Mashariki (EADB), jijini Kampala-Uganda, ambapo wamejadiliana kuhusu namna Reli ya Kisasa ya SGR, inaweza kusisimua biashara kati ya nchi hizo mbili kwa kutumia Kituo cha Mwanza ambapo mpango uliopo ni kuifanya mizigo inayotoka Bandari ya Dar es Salaam kuelekea Uganda, ivushwe kwa njia ya vivuko maalum kupitia Ziwa Victoria.
Dkt. Nchemba alisema kuwa Mradi huo wa SGR umefikia zaidi ya asilimia 60 na kushauri Mamlaka za Tanzania na Uganda kupitia Timu za Wataalamu zianze kufikiria kutumia fursa hiyo kurahisisha usafirishaji wa mizigo kati ya nchi hizo mbili, pendekezo ambalo liliungwa mkono na Jenerali Edward Katumba Wamalwa.
Katika kikao hicho, Mhe. Dkt. Nchemba aliambatana na Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Meja Jenerali Paul Simuli na Kamishna wa Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Dkt. Charles Mwamwaja. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Pakua sasa Jarida la Hazina Yetu Toleo la Pili Mwaka 2024/25 kupitia Tovuti yetu: www.mof.go.tz/publications/newsletters
ujisomee habari mbalimbali kutoka Wizara ya Fedha. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
LIMETOKAAAAA!!
Pakua sasa Jarida la Hazina Yetu Toleo la Pili Mwaka 2024/25 kupitia Tovuti yetu: www.mof.go.tz/publications/newsletters
ujisomee habari mbalimbali kutoka Wizara ya Fedha. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), na Mawaziri wenzake wa Fedha, Mhe. Matia Kasaija (Uganda), Mhe. Ng’ongo John Mbadi (Kenya) na Mhe. Yusuf Murangwa (Rwanda) wameshiriki Mkutano wa 50 wa Bodi ya Wadhamini (Governing Council) ya Benki ya Maendeleo ya Afrika Mashariki (EADB), unaofanyika leo tarehe 13 Machi 2025, katika Hoteli ya Serena, Kampala-Uganda.
Tanzania ikiwa moja wa nchi Wanahisa wa Benki hiyo na inanufaika kwa ufadhili wa miradi ya kimkakati na ya kijamii ikiwemo Mradi wa Reli ya Kisasa SGR pamoja na Benki hiyo kuiwezesha Sekta Binafsi ya Tanzania kupata mikopo yenye riba nafuu.
Mkutano huo umewashirikisha Wadhamini na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki hiyo wakiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ambaye pia ni Kamishna wa Idara ya Maendeleo ya Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Dkt. Charles Mwamwaja na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Bw. Benard Mono. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), amewasili Jijini Kampala nchini Uganda jana usiku, kushiriki Mkutano wa 50 wa Bodi ya Wadhamini (Governing Council) ya Benki ya Maendeleo ya Afrika Mashariki (EADB), utakaofanyika leo tarehe 13 Machi 2025 katika Hoteli ya Serena, Jijini Kampala na kulakiwa na Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Mhe. Meja Jenerali Paul Simuli na Viongozi wengine Wakuu wa Benki hiyo, akiwemo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya EADB, ambaye pia ni Kamishna wa Idara ya Maendeleo ya Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Dkt. Charles Mwamwaja na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Bw. Benard Mono.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe kutoka Kampuni ya Ujezi wa Reli ya CRCC ya China, ikiongozwa na Makamu wa Rais wa Kampuni hiyo Bw. Zhao DianLong, iliyotia nia ya kuwekeza kwenye Ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA), katika Ukumbi wa Mikutano wa Waziri wa Fedha, Treasury Square, Jijini Dodoma, ambapo Mhe. Dkt. Nchemba, aliiahidi Kampuni hiyo utayari wa Serikali wa kushirikiana nayo kuboresha miundombinu ya mradi huo wa kihistoria ili kukuza biashara na uchumi kati ya Tanzania na Zambia katika sekta ya usafirishaji.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb) na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo, wamewasilisha Mapendekezo ya Mpango na Kiwango cha Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2025/2026 mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, jijini Dodoma, ambapo Serikali imependekeza kukusanya na kutumia jumla ya shilingi trilioni 57.04 kwa mwaka wa Fedha 2025/26, sawa na ongezeko la asilimia 13.4 ikilinganishwa na Bajeti ya mwaka wa Fedha 2024/25 ya shilingi trilionin 50.29.
@kitilam -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), amewasilisha Mapendekezo ya Mfumo na Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2025/26, kwenye Kamati ya Bunge zima, katika Ukumbi wa Pius Msekwa, Bungeni jijini Dodoma, ambapo Serikali imependekeza kukusanya na kutumia jumla ya shilingi trilioni 57.04 kwa mwaka 2025/26, sawa na ongezeko la asilimia 13.4 ikilinganishwa na Bajeti ya Mwaka wa Fedha, 2024/25 ya shilingi trilioni 50.29.
Hafla hiyo imeongozwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa na kuhudhuriwa pia na Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Mussa Azan Zungu, na viongozi waandamizi wa Serikali. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Uwasilishaji wa Mapendekezo ya Mpango na Kiwango cha Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2025/26.
-
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Kuelekea week end, Mwalimu wa Hesabu nipo 📚✏️. Hapa tunakata pindi la Probability. Karibu, lakini umechelewa kidogo—tumeshamaliza Algebra, Logarithm, Functions, Sequence & Series 🤗🤗📖.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Bank of Tanzania
@BankOfTanzania
Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba, amesema Serikali inaendeleza jitihada ya kukuza matumizi ya fedha kidijitali badala ya pesa taslimu ili kuendana na madadiliko ya kiteknolojia yanayoendelea hivi sasa. Dkt. Mwigulu ameyasema hayo tarehe 6 Machi Benki Kuu jijini
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), amefungua Mhadhara wa 9 wa Kumbukumbu ya aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Marehemu Gilman Rutihinda (1988-1993), uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kilimanjaro, Benki Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam, uliobeba kaulimbiu ya “Kuongoza Mageuzi ya Uchumi wa Kidigitali: Fursa za Ubunifu wa Kifedha na Ujumuishaji”, ambapo Dkt. Nchemba, alitoa wito kwa watanzania kufanya miamala kwa njia za kidigitali badala ya kutumia fedha taslimu kwa kuwa Serikali imewekeza kwa kiasi kikubwa katika mifumo ya kidigitali inayowezesha kufanya matumizi kwa njia hizo kupitia mitandao ya simu, benki na njia nyingine.
Mhadhara huo, umehudhuriwa na familia ya Marehemu Rutihinda, ikiongozwa na Mjane wa Marehemu, Bi. Josephine Rutihinda, pamoja na wadau mbalimbali wa masuala ya uchumi na fedha kutoka ndani na nje ya nchi, ikiwa ni sehemu ya kumuenzi Gavana Gilman Rutihinda, aliyefariki dunia akiwa madarakani mnamo mwaka 1993 baada ya kufanya mageuzi makubwa katika sera za uchumi na fedha kwa kuhimiza ubunifu na matumizi ya kidigitali katika kuendesha uchumi wa nchi.
@BankOfTanzania -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe kutoka Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi wa Afrika Mashariki ( @EACOP_ ), ukiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mradi huo, Bw. Philippe Groueix, Kando ya Mkutano wa 11 wa Mafuta na Gesi unaozihusisha nchi za Afrika Mashariki unaoendelea katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere, JNICC, Jijini Dar es Salaam, ambapo wamejadiliana kuhusu maendeleo ya ujenzi wa mradi huo.
Kikao hicho kifupi kiliwashirikisha pia Kamishna wa Idara ya Sera, Wizara ya Fedha, Dkt. Johnson Nyella, Afisa Mwandamizi kutoka Idara ya Sera, Wizara ya Fedha, Bw. Justine Mlewa, Mkurugenzi Mtendaji wa EACOP, Bw. Guillaume Dulout, Mkuu wa masuala ya Utawala na Rasilimali Watu wa EACOP, Bw. Geofrey Mponda na Meneja Uhusiano wa Serikali wa Mradi huo Bi. Evelyne Amasi. -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Tunapoanza kipindi hiki cha Kwaresma, na iwe wakati wa tafakari, toba, na kuimarisha imani. Mungu atujaze neema na baraka katika safari hii ya kiroho.
Kwaresma Njema. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
German Embassy Dar es Salaam
@GermanyTanzania
🇩🇪 inaunga mkono kikamilifu Dira ya 🇹🇿2050 & inasaidia lengo lake la kuharakisha uthabiti & maendeleo jumuishi. Katika Mazungumzo ya Kistratejia ya Ngazi ya Juu Ijumaa, 28 Februari huko Dodoma, tumekuwa na majadiliano kuhusu changamoto ya kupungua kwa misaada rasmi ya maendeleo.
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), amesema kuwa Serikali inaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji na ukuaji wa uchumi nchini.
Dkt. Nchemba alisema hayo jijini Dodoma wakati akifungua Mkutano wa Majadiliano ya Kimkakati kati ya Serikali na Washirika wa Maendeleo Ngazi ya Juu, ambao unalenga kubadilishana maarifa, taarifa, na uzoefu kuhusu sera na mikakati ya maendeleo ya nchi.
Alisema Serikali imewasilisha bungeni Muswada wa Sheria ya Uwekezaji Tanzania (Tanzania Investment Act, 2024) na kuanzisha Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi (Tanzania Investment and Special Economic Zones Authority) ili kuboresha mazingira ya uwekezaji.
“Serikali kupitia Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) na Kituo cha Uwekezaji kati ya Sekta Binafsi na Umma (CPPP) imeendeleza majadiliano kati ya sekta ya umma na sekta binafsi ili kuongeza ushiriki wa sekta binafsi katika maamuzi”, aliongeza Mhe. Dkt. Nchemba.
Mhe. Dkt. Nchemba ambaye ni Mwenyekiti wa Mkutano huo, alisema Serikali pia inaandaa Mkakati wa Kitaifa wa Uendelezaji wa Uwekezaji (2025/2026 – 2034/2035) ambao utakuwa na mpango wa utekelezaji, ufuatiliaji na tathmini, unaoeleza majukumu ya kila mdau na viashiria vya kupima maendeleo.
Dkt. Nchemba alibanisha kuwa katika kipindi cha mwezi Julai 2024 hadi Desemba 2024, Serikali imeongeza uwezo wa uzalishaji umeme kwa asilimia 30.3, hasa kupitia Mradi wa Umeme wa Maji wa Julius Nyerere (JNHPP) ili kupunguza gharama za biashara.
“Kupitia Sheria ya Fedha ya mwaka 2024, Serikali imepunguza au kuondoa ada na tozo mbalimbali ili kuboresha mazingira ya biashara”, aliongeza Mhe. Nchemba.
Dkt. Nchemba alisema Serikali pia imepata mafaniko makubwa katika ukuaji wa uchumi jumuishi ambapo idadi ya shule na wanafunzi imeongezeka, vituo vya afya vimeongezeka na huduma zimeboreshwa, huduma za maji zimeongezeka katika maeneo yote nchini pamoja na ongezeko la ajira.
Aidha, alitoa rai kwa wadau wote kushirikiana kwa karibu na Serikali ili kufanikisha utekelezaji wa Mwongozo wa Ushirikiano wa Maendeleo (DCF) ambao umetilia mkazo utaratibu wa ufadhili wa miradi ya mabadiliko ya tabianchi (climate financing modality) na kuimarisha Ushirikiano kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) kama njia mbadala za ufadhili.
Kwa upande wake Mwenyekiti Mwenza wa Kundi la Washirika wa Maendeleo na Balozi wa Ireland nchini, Mhe. Nicola Brennan aliishauri Serikali kuendelea kuboresha mazingira ya biashara kwa kuondoa vikwazo vinavyozuia uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni.
Alisema hii itaongeza mchango wa sekta binafsi katika kuleta uwekezaji, ajira, uvumbuzi, na suluhisho kwa changamoto mbalimbali ili kujenga uchumi imara.
“Wadau wa Maendeleo tayari tumekuwa na majadiliano mazuri kuhusu hili, na tunapongeza utayari wa Serikali kushirikiana nasi kuona jinsi bora ya kuondoa vikwazo na kuvutia uwekezaji zaidi wa moja kwa moja wa kigeni (FDI) nchini Tanzania, pamoja na kuimarisha sekta ya biashara ya ndani”, aliongeza.
Mhe. Brennan alisema Washirika wa Maendeleo watahakikisha kuwa Dira ya Maendeleo ya Mwaka 2050 inapata ufadhili wa uhakika na endelevu, hasa katika sekta za afya, elimu na sekta ya kijamii kwa ujumla.
“Tunapopanga vipaumbele katika matumizi ya rasilimali finyu za Msaada wa Maendeleo (ODA), ni muhimu pia kuelewa vyema vyanzo vingine vya ufadhili vinavyopatikana kwa nchi zenye kipato cha kati nje ya ODA, pamoja na mchango ambao sisi kama Wadau wa Maendeleo tunaweza kutoa kusaidia Tanzania kuzifikia na kuzitumia fursa hizo ipasavyo. Tunatazamia kujadili zaidi suala hili kwa kina.”
Aliahidi kuwa Washirika hao wataendelea kushirikiana na Tanzania kuhakikisha maendeleo yanapatikana na kustawisha jamii. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
NBCTanzania
@NBCTanzania
"Niwapongeze NBC kwa ufadhili wao wanaoufanya kwenye sekta ya michezo. Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni amesema kwamba timu yake imepata ufadhili wa bus hata kule Singida Mheshimiwa Mgeni Rasmi lile bus zuri wanalolitumia timu bora ya Singida imetoka NBC kwa makubaliano kama yale
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Uongozi wa Benki ya @myaccessbank ukiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki hiyo, Bw. Protase Ishengoma, baada ya kufanya ziara fupi ya kutambulisha shughuli za Benki hiyo, katika Ofisi Ndogo ya Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam, na kujadiliana kuhusu fursa za ushirikiano kati yake na Serikali katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo.
Katika Kikao hicho kilihohudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha ambaye pia ni Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Natu El-maamry Mwamba na Viongozi wengine waandamizi wa Wizara ya Fedha na Benki hiyo, Mhe. Dkt. Nchemba, alitoa wito kwa Taasisi za Fedha nchini, kuiwezesha sekta binafsi kupata mitaji ili iweze kuchangia kwa kiwango kikubwa ukuaji wa Uchumi, kukuza ajira na maendeleo ya nchi kwa ujumla.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Access Bank, Bw. Protase Ishengoma, aliipongeza Serikali kwa kutekeleza miradi mikubwa ya kijamii ikiwemo ile ya kimkakati na kuahidi kuwa Benki yake ambayo ina misuli ya kifedha, iko tayari kushiriki katika ujenzi wa miradi mbalimbali nchini ikiwemo pia kuwa miongoni mwa Taasisi zinazoweza kufanya majukumu ya kuitafutia Serikali fedha za kutekeleza miradi hiyo. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi Mpya wa Uswisi hapa nchini, Mhe. Nicole Providoli, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam ambaye alifika kujitambulisha. Katika kikao hicho walijadili masuala kadhaa ya ushirikiano wa kiuchumi kati ya Tanzania na Switzerland, kupitia miradi mbalimbali ya maendeleo inayofadhiliwa na nchi hiyo, ukiwemo mradi wa kusaidia kaya maskini kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), ambapo tangu mwaka 2023, Uswisi imechangia shilingi bilioni 88.1 katika Mfuko huo.
Mkutano huo umehudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha ambaye pia ni Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Kamishna Msaidizi wa Idara ya Fedha za Nje, Bw. Melkzedeck Mbise, Afisa Program-Utawala - kutoka Ubalozi wa Uswisi, Bi. Jacquiline Ngoma, na Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Lisa Kilua. -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Kuelekea "DERBY YA KARIAKOO" 🔥⚽️ Tunakaa na Masela nasi kufanya uchambuzi wa mpambano huu wa kihistoria! 🔥🙌 Je, nani ataibuka kidedea?
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
ikulu_Tanzania
@ikulumawasliano
Watoto yatima pamoja na watoto wenye mahitaji maalum wakiwa kwenye Iftar iliyoandaliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Ikulu Jijini Dar es Salaam 03 Machi, 2025.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), ameshiriki uzinduzi wa huduma za kidigitali za Benki ya NBC (NBC Kiganjani App) inayomwezesha mteja kupata huduma za kibenki kigigitali kwa kutumia simu za mkononi. tukio ambalo, Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa alikuwa Mgeni Rasmi, lililofanyika katika Ukumbi wa The Super Dome, Masaki, Jijini Dar es Salaam.
Akimkaribisha, Mhe. Waziri Mkuu kuzungumza na kuzindua NBC Kiganjani App, Mhe. Dkt. Nchemba aliipongeza NBC kwa ubunifu walioufanya na kwamba hatua hiyo si tu kwamba inaimarisha maendeleo ya sekta ya benki, bali pia inaendana na dhamira ya serikali ya Awamu ya Sita, inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya kujenga uchumi jumuishi unaowezesha upatikanaji wa huduma za kifedha kwa wananchi wote.
Aidha, Mhe. Dkt. Nchemba, aliipongeza Benki hiyo kwa kudhamini Ligi Kuu ya Tanzania Bara (NBCPL) ambayo kupitia udhamini wao imekuwa na msisimko mkubwa na kuiwezesha Tanzania kupanda viwango na kuwa ligi namba 4 kwa Ubora barani Afrika. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo mafupi na Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Mhe. Charlotta Ozaki Macias, kando ya Mkutano wa Majadiliano ya Ngazi ya Juu kati ya Serikali na Washirika wa Maendeleo, Ofisini kwake, Treasury Square jijini Dodoma, ambapo wamejadiliana kuhusu maendeleo ya Ujenzi wa Reli ya Kisasa - SGR, Mradi ambao nchi yake inafadhili sehemu ya mradi huo.
Kikao hicho kiliwashirikisha Kamishna wa Idara ya Madeni-Wizara ya Fedha, Bw. Japhet Justine na Msaidizi wa Balozi huyo, Bi. Sandra Diesel.
@SwedeninTZ -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), akiwa katika Treni ya Kisasa (SGR) na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia, Bw. @BeleteNathan na abiria wengine kutoka Dar es Salaam kuelekea Jijini Dodoma. Mradi wa SGR ambao kipande cha kuanzia Dar es Salaam hadi Dodoma kimekamikika, ni miongoni mwa miradi ya Kimkakati inayotekelezwa na Serikali na umepata uungwaji mkono na wadau mbalimbali wa maendeleo ikiwemo Benki ya Dunia na umekuwa Mradi maarufu unaotumiwa na watu mbalimbali wakiwemo Viongozi wa Serikali.
youtu.be/NYud6aIZPfYThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Bank of Tanzania
@BankOfTanzania
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), akiagana na aliyekuwa Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Dkt. Albina Chuwa, Katika Ofisi ya Waziri wa Fedha, Treasury Square, Jijini Dodoma, ambapo pamoja na mambo mengine, alimpongeza Dkt. Chuwa kwa kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi mkubwa na kumtakia kila la kheri katika majukumu yake mengine baada ya kustaafu, Dkt. Chuwa kwa upande wake alimshukuru Mhe. Dkt. Nchemba, kwa miongozo na usimamizi mahiri wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, hatua iliyoifanya Taasisi hiyo kuwa moja ya Taasisi inayoheshimika duniani.
Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, alimteua Dkt. Amina Msengwa, kuchukua nafasi ya Dkt. Albina Chuwa, ambaye amestaafu rasmi baada ya kuongezewa vipindi viwili vya mikataba baada ya kustaafu miaka michache iliyopita kutokana na umahiri wake katika kusimamia masuala ya takwimu nchini ikiwemo Sensa za Watu na Makazi zilizofanyika chini ya usimamizi wake. -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Ndugu zangu Waislamu, tunaanza mwezi Mtukufu wa Ramadhani tukitekeleza moja ya nguzo kuu za Uislamu. Huu ni mwezi wa rehema, msamaha, na ibada. Nawatakia Waislamu wote mfungo mwema wenye baraka na amani.
Ramadhan Kareem. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), amesema kuwa Serikali inaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji na ukuaji wa uchumi nchini.
Dkt. Nchemba alisema hayo jijini Dodoma wakati akifungua Mkutano wa Majadiliano ya Kimkakati kati ya Serikali na Washirika wa Maendeleo Ngazi ya Juu, ambao unalenga kubadilishana maarifa, taarifa, na uzoefu kuhusu sera na mikakati ya maendeleo ya nchi.
Alisema Serikali imewasilisha bungeni Muswada wa Sheria ya Uwekezaji Tanzania (Tanzania Investment Act, 2024) na kuanzisha Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi (Tanzania Investment and Special Economic Zones Authority) ili kuboresha mazingira ya uwekezaji.
“Serikali kupitia Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) na Kituo cha Uwekezaji kati ya Sekta Binafsi na Umma (CPPP) imeendeleza majadiliano kati ya sekta ya umma na sekta binafsi ili kuongeza ushiriki wa sekta binafsi katika maamuzi”, aliongeza Mhe. Dkt. Nchemba.
Mhe. Dkt. Nchemba ambaye ni Mwenyekiti wa Mkutano huo, alisema Serikali pia inaandaa Mkakati wa Kitaifa wa Uendelezaji wa Uwekezaji (2025/2026 – 2034/2035) ambao utakuwa na mpango wa utekelezaji, ufuatiliaji na tathmini, unaoeleza majukumu ya kila mdau na viashiria vya kupima maendeleo.
Dkt. Nchemba alibanisha kuwa katika kipindi cha mwezi Julai 2024 hadi Desemba 2024, Serikali imeongeza uwezo wa uzalishaji umeme kwa asilimia 30.3, hasa kupitia Mradi wa Umeme wa Maji wa Julius Nyerere (JNHPP) ili kupunguza gharama za biashara.
“Kupitia Sheria ya Fedha ya mwaka 2024, Serikali imepunguza au kuondoa ada na tozo mbalimbali ili kuboresha mazingira ya biashara”, aliongeza Mhe. Nchemba.
Dkt. Nchemba alisema Serikali pia imepata mafaniko makubwa katika ukuaji wa uchumi jumuishi ambapo idadi ya shule na wanafunzi imeongezeka, vituo vya afya vimeongezeka na huduma zimeboreshwa, huduma za maji zimeongezeka katika maeneo yote nchini pamoja na ongezeko la ajira.
Aidha, alitoa rai kwa wadau wote kushirikiana kwa karibu na Serikali ili kufanikisha utekelezaji wa Mwongozo wa Ushirikiano wa Maendeleo (DCF) ambao umetilia mkazo utaratibu wa ufadhili wa miradi ya mabadiliko ya tabianchi (climate financing modality) na kuimarisha Ushirikiano kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) kama njia mbadala za ufadhili.
Kwa upande wake Mwenyekiti Mwenza wa Kundi la Washirika wa Maendeleo na Balozi wa Ireland nchini, Mhe. Nicola Brennan aliishauri Serikali kuendelea kuboresha mazingira ya biashara kwa kuondoa vikwazo vinavyozuia uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni.
Alisema hii itaongeza mchango wa sekta binafsi katika kuleta uwekezaji, ajira, uvumbuzi, na suluhisho kwa changamoto mbalimbali ili kujenga uchumi imara.
“Wadau wa Maendeleo tayari tumekuwa na majadiliano mazuri kuhusu hili, na tunapongeza utayari wa Serikali kushirikiana nasi kuona jinsi bora ya kuondoa vikwazo na kuvutia uwekezaji zaidi wa moja kwa moja wa kigeni (FDI) nchini Tanzania, pamoja na kuimarisha sekta ya biashara ya ndani”, aliongeza.
Mhe. Brennan alisema Washirika wa Maendeleo watahakikisha kuwa Dira ya Maendeleo ya Mwaka 2050 inapata ufadhili wa uhakika na endelevu, hasa katika sekta za afya, elimu na sekta ya kijamii kwa ujumla.
“Tunapopanga vipaumbele katika matumizi ya rasilimali finyu za Msaada wa Maendeleo (ODA), ni muhimu pia kuelewa vyema vyanzo vingine vya ufadhili vinavyopatikana kwa nchi zenye kipato cha kati nje ya ODA, pamoja na mchango ambao sisi kama Wadau wa Maendeleo tunaweza kutoa kusaidia Tanzania kuzifikia na kuzitumia fursa hizo ipasavyo. Tunatazamia kujadili zaidi suala hili kwa kina.”
Aliahidi kuwa Washirika hao wataendelea kushirikiana na Tanzania kuhakikisha maendeleo yanapatikana na kustawisha jamii. -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
ASANTENI TANGA.
2 media couldn't be displayed. See them on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
TAMISEMI
@tamisemi_tz
UPDATES: RUFIJI
Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya Mawaziri kwenye Dua maalumu ya kumuomba marehemu Alhaji Omary Mchengerwa baba mzazi wa Mhe. Mohamed Mchengerwa , Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - TAMISEMI. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb) na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. @kitilam , wamekutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe kutoka Benki ya Dunia ukiongozwa na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia, anayeziwakilisha pia nchi za Malawi, Zambia na Zimbabwe, Bw. @BeleteNathan , katika Ofisi za Wizara ya Fedha (Treasury Square), jijini Dodoma, ambapo pamoja na mambo mengine wamejadiliana namna ya kuongeza ushirikiano katika kuendeleza biashara na uwekezaji kwa kushirikiana na Sekta Binafsi.
Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban, Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Dkt. Mursali Milanzi, Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, anayeshughulikia Utendaji na Tathmini, Dkt. Linda Ezekiel na Viongozi wengine waandamizi wa Wizara ya Fedha, Tume ya Mipango na Maafisa wengine waandamizi kutoka serikalini.
@OR_MU1 @WBTanzania -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), akiwa katika Treni ya Kisasa (SGR) na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia ambaye pia anaziwakilisha nchi za Zambia, Malawi na Zimbabwe, Bw. @BeleteNathan , wakiwahi kushiriki Mkutano wa Majadiliano ya Kimkakati wa Ngazi ya Juu kati ya Serikali na Washirika wa Maendeleo unaotarajiwa kufanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kambarage, Treasury Square, Jijini Dodoma.
Mradi wa SGR ambao kipande cha kuanzia Dar es Salaam hadi Dodoma kimekamikika, ni miongoni mwa miradi ya Kimkakati inayotekelezwa na Serikali na umepata uungwaji mkono na wadau mbalimbali wa maendeleo ikiwemo Benki ya Dunia na umekuwa Mradi maarufu unatumiwa na watu mbalimbali wakiwemo Viongozi wa Serikali. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), ameongoza kikao cha Serikali na Ujumbe kutoka Kampuni ya Leonardo ya nchini Italia, ukiongozwa na Makamu wa Rais wa Kampuni hiyo anayesimamia Kanda ya Afrika, Bw. Claudio Sabatino, ambapo wamejadili namna Kampuni hiyo inavyoweza kushirikiana na Tanzania katika masuala mbalimbali ya maendeleo.
Kikao hicho kilichofanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha Jijini Dar es Salaam, kimehudhuriwa pia na Katibu Mkuu na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Kamishna Msaidizi wa Idara ya Madeni, Bw. Omary Khama, Kamishna Msaidizi wa Idara ya Fedha za Nje, Bw. Robert Mtengule na maafisa wengine wa Serikali na Kampuni ya Leonardo. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Bank of Tanzania
@BankOfTanzania
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), amekutana na kufanya majadiliano na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Profesa Palamagamba Kabudi, kuhusu maendeleo na changamoto zinazoikabili sekta ya michezo hususan mpira wa miguu nchini, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam.
Katika majadiliano hayo, Serikali imeipongeza TFF na Bodi yake ya Ligi, kwa kusimamia kwa weledi masuala ya maendeleo ya soka na kuliletea Taifa heshima kubwa barani Afrika na kupewa jukumu la kuandaa mashindano ya CHAN na AFCON, na kukubaliana pia namna tasinia ya utamaduni, sanaa na michezo inavyoweza kutumika kuhamasisha uzalendo wa kulipa kodi kwa hiari, kupitia kampeni ya kudai na kutoa risiti kwa ajili ya maendeleo ya nchi.
Majadiliano hayo yaliwashirikisha viongozi wa juu wa Wizara ya Fedha wakiongozwa na akiwemo Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-Maamry Mwamba, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya, Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, Bw.Yusuph Mwenda, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania- TFF, Bw. Wallace Karia, viongozi waandamizi wa Wizara ya Fedha, pamoja na Taasisi zinazosimamia michezo nchini.
@Tanfootball @TRATanzania -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), akiwa na Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe na Naibu wake Mhe. David Silinde, wakati wa Kongamano la Tatu la Kahawa Barani Afrika, lililofungwa rasmi leo na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam-JNICC, ambapo msisitizo mkubwa kwa nchi 25 za Afrika zinazozalisha kahawa ni kuongeza thamani ya zao hilo ili kuongeza mnyororo wa thamani ili liweze kuchangia zaidi ukuaji wa uchumi wa nchi hizo pamoja na kukuza ajira hususan kundi la Vijana.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), akiteta jambo na Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda, wakati wa Kongamano la Tatu la Kahawa Barani Afrika, lililofungwa rasmi leo na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam-JNICC, ambapo msisitizo mkubwa kwa nchi 25 za Afrika zinazozalisha kahawa ni kuongeza thamani ya zao hilo ili kuongeza mnyororo wa thamani ili liweze kuchangia zaidi ukuaji wa uchumi wa nchi hizo pamoja na kukuza ajira hususan kundi la vijana.
Taarifa zilizopo zinaonesha kuwa Nchi za Afrika kwa pamoja zinapata wastani wa dola bilioni 2.5 kila mwaka kutokana na mauzo ya kahawa nje ya nchi wakati biashara ya kahawa duniani ina thamani ya dola bilioni 500, mapato hayo madogo ni kutokana na kuwa zaidi ya asilimia 90 ya kahawa ya Afrika inasafirishwa kama malighafi. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), ameshiriki Kongamano la Tatu la Kahawa Barani Afrika, lililofungwa rasmi leo na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam-JNICC, ambapo msisitizo mkubwa kwa nchi 25 za Afrika zinazozalisha kahawa ni kuongeza thamani ya zao hilo ili kuongeza mnyororo wa thamani ili liweze kuchangia zaidi ukuaji wa uchumi wa nchi hizo pamoja na kukuza ajira hususan kundi la vijana.
Taarifa zilizopo zinaonesha kuwa Nchi za Afrika kwa pamoja zinapata wastani wa dola bilioni 2.5 kila mwaka kutokana na mauzo ya kahawa nje ya nchi wakati biashara ya kahawa duniani ina thamani ya dola bilioni 500, mapato hayo madogo ni kutokana na kuwa zaidi ya asilimia 90 ya kahawa ya Afrika inasafirishwa kama malighafi. -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Home sweet home.
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Hon.Ambassador Dr. Pindi Chana
@dr_pindi
Leo nimeshiriki katika kikao kuhusu Mradi wa Kuimarisha Usimamizi wa Mazingira Kanda ya Kusini kilichoongozwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), kilichofanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam leo.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), akiongoza kikao, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam, kilichomshirikisha Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana, na Ujumbe kutoka Wizara ya Maji, ambapo wamejadili kuhusu namna ya uboreshaji wa Sekta ya Utalii na Huduma za Jamii katika Ukanda wa Kusini. Kikao hicho pia kimemshikirisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi, na Maafisa kutoka Wizara ya Fedha.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Magogoni Daily
@magogonidaily
Mama na Wananchi wake. Mtumishi Namba 1 wa Watanzania.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Abdul
@AbdulAmeir
“Hatua ya kwanza ya kujifunza ni kutulia na kukaa kimya. Hatua ya pili ni kutazama na kusikiliza.” - @SuluhuSamia
-
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Baada ya kuhitimisha shughuli za Bunge, sasa tunaendelea na kazi za wananchi jimboni! Huduma kwa wananchi ni kipaumbele chetu daima.
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Dr. Akinwumi A. Adesina, CON, CGH
@akin_adesina
With my dear sister President @SuluhuSamia of the United Republic of Tanzania, at the African Union Summit in Addis Ababa. I applaud and congratulate you on the endorsement of your clean cooking plan for Africa by the Heads of State. You are an amazing leader!
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia, anayeziwakilisha pia nchi za Malawi, Zambia na Zimbabwe, Bw. @BeleteNathan , katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha Jijini Dar es Salaam, ambapo wamejadili kuhusu utekelezaji wa baadhi ya miradi ya kiuchumi na kijamii inayokusudiwa kufadhiliwa na Benki hiyo ikiwemo ujenzi wa Reli ya Kisasa-SGR.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Serikali imeeleza kuwa masaa yanayotumiwa na Wabunge wenye sifa ya Mhasibu wa Umma aliyeidhinishwa (CPA), katika ushiriki wa vikao vya Kamati za Kudumu za Bunge za Hesabu za Serikali (PAC), Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), Mitaji ya Umma (PIC) pamoja na uchambuzi wa Bajeti ya Serikali yanatambuliwa kama ni mafunzo endelevu (CPD hours).
Hayo yameelezwa bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Kilindi, Mhe. Omari Mohamed Kigua, alietaka kujua wakati ambao wabunge wenye sifa ya CPA Ushiriki wao kwenye Kamati za LAAC, PIC, PAC na Bajeti utachukuliwa kama CPD hours.
Alisema mafunzo endelevu rasmi (yaani uso kwa uso, au ya kielectroniki) na mafunzo endelevu yasiyo rasmi ikiwa ni pamoja na kushiriki mikutano ya kiufundi katika tasnia ya Uhasibu na Ukaguzi yanatambulika katika Mwongozo wa Mafunzo Endelevu ya Kihasibu Tanzania (Continued Professional Development- CPD Guideline), ulioidhinishwa na Bodi ya Wakurugenzi ya NBAA na kuanza kutumika rasmi Julai 01, 2020.
“Kwa kufuata mwongozo huo, na kwa kuzingatia muda unaotumiwa na Waheshimiwa wabunge wakati wa ushiriki wa mikutano ya Kamati za Bunge, hasa zile zinazohusu masuala ya uhasibu au ukaguzi kama LAAC, PIC, PAC na uchambuzi wa Bajeti ya Serikali, masaa wanayotumia wabunge wenye CPA yanatambuliwa kama ni mafunzo endelevu (CPD hours)”, alibainisha Mhe. Nchemba.
Aliongeza kuwa Mheshimiwa Mbunge ambaye ni Mwanachama wa NBAA ataingia kwenye akaunti yake, atapandisha ratiba ya kikao husika na uthibitisho wa mahudhurio katika mkutano husika ili masaa yake yahesabiwe.
Mhe. Dkt. Nchemba alifafanua kuwa ni jukumu la mwanachama mwenyewe kuingia kwenye mfumo, na siyo mtu mwingine (third party) na kutoa uthibitisho huo kwenye mfumo wa NBAA. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), akiwasilisha Bungeni ombi la nyongeza ya mapato na matumizi ya jumla ya shilingi bilioni 945.7 kwa ajili ya kuongeza kwenye Bajeti ya Serikali ya mwaka 2024/25 kutoka shilingi trilioni 49.346 iliyoidhinishwa awali hadi shilingi trilioni 50.291, ambapo ameeleza kuwa fedha hizo zitakazotekeleza shughuli za sekta za elimu, afya utalii na program mbalimbali za kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia ya nchi, zimepatikana kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF).
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Bunge limepitisha nyongeza ya mapato na matumizi ya jumla ya shilingi bilioni 945.7 kwa ajili ya kuongeza kwenye Bajeti ya Serikali ya mwaka 2024/25 kutoka shilingi trilioni 49.346 iliyoidhinishwa awali hadi shilingi trilioni 50.291.
Nyongeza hiyo imewasilishwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), ambaye ameeleza kuwa fedha hizo zitakazotekeleza shughuli za sekta za elimu, afya utalii na program mbalimbali za kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia ya nchi, zimepatikana kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF).
Alisema shilingi bilioni 325.9 zimetengewa Wizara ya Fedha, kwa ajili ya matumizi ya kitaifa, kugharamia malipo ya madeni ya watumishi, wakandarasi na wazabuni wa ndani pamoja na ujenzi wa miundombinu ya Serikali katika Mji wa Serikali Mtumba.
Mhe. Nchemba aliongeza kuwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imetengewa shilingi bilioni 131.4 kwa ajili ya kugharamia mahitaji ya Mtaala mpya wa sekta ya elimu ikiwemo ujenzi wa shule za sekondari za amali, upatikanaji wa vifaa na walimu.
“Fedha hizo zitagharamia ukamilishaji wa ujenzi wa vyuo vya VETA, ujenzi wa maktaba ya Chuo Kishiriki cha Elimu Mkwawa (MUCE), ujenzi wa miundombinu ya Chuo cha Nelson Mandela-Arusha, ujenzi wa majengo ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima pamoja na ujenzi wa Jengo la Maktaba Mwanza”, alibainisha Mhe. Dkt. Nchemba.
Aliongeza kuwa Wizara ya Afya imeongezewa shilingi bilioni 53.7 kwa ajili ya kugharamia dawa, vifaa tiba na vitendanishi.
Mhe. Dkt. Nchemba alisema Ofisi ya Rais – TAMISEMI imeongezewa shilingi bilioni 173.7 kwa ajili ya sekta ya elimu, afya na kuiwezesha TARURA kukarabati miundombinu ya barabara na madaraja iliyoathirika na mvua za masika ili iweze kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Alisema shilingi bilioni 260.7 zimetengwa kwa ajili ya Wizara ya Maliasili na Utalii ili kugharamia uendeshaji na ukarabati wa miundombinu ya barabara katika Hifadhi za Taasisi za Utalii za Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) na Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA.)
Aidha, Mhe. Dkt. Nchemba alisema mgawanyo huo umezingatia maono ya Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuwa na nguvu kazi yenye ujuzi wa kuhakikisha utekelezaji wa elimu ya amali ni unafanyika kwa vitendo. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
HabariLeo
@HabariLeo
DODOMA: WAZIRI wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba, amewasilisha bungeni pendekezo la kuomba nyongeza ya bajeti ya serikali ya mwaka 2025/2026 ya Shilingi bilioni 945.7.
Amesema nyongeza hii itatekeleza miradi katika sekta za elimu, afya, taasisi za utalii, na kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.
Dk. Mwigulu alisisitiza kuwa mgawanyo wa fedha hizo utafuata maono ya Rais Samia Suluhu Hassan, akilenga kuimarisha nguvu kazi yenye ujuzi kwa utekelezaji wa mitaala mipya ya elimu.
Akaongeza kuwa fedha hizi zitazingatia mapendekezo ya sekta tajwa na ushauri wa kamati ya kudumu ya bunge, kuhakikisha utekelezaji wa mipango unafanikiwa kwa ufanisi.
Imeandaliwa: Kulthum Ally -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Mchango wangu wa leo katika Mjadala wa Taarifa ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC).
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Chakula Duniani ( @WFP_Tanzania ), Bw. Ronald Tran Ba Huy, Jijini Dodoma, ambapo wamekubaliana kuendeleza ushirikiano wa kimaendeleo katika kukuza uchumi jumuishi katika nyanja mbalimbali ikiwemo kushiriki katika utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, inayolenga, pamoja ma mambo mengine, kukuza, ajira, kupambana na umasikini, kukuza mauzo ya budhaa nje ya nchi na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kupitia za upatikanaji wa nishati safi ya kupikia.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Brand Tanzania
@Brand_Tanzania1
In this fiscal year so far, Tanzania government via Ministry of Water has achieved the following:
(i) Completed the implementation of 286 water projects across the country, of which 68 are urban projects and 218 are rural projects.
(ii) Increased water production from 7,779,712,732.4 cubic meters in December 2023 to 8,439,342,171.4 cubic meters in December 2024 for both urban and rural areas.
(iii) Improved access to clean and safe water in rural areas from 79.6% in December 2023 to 83% in December 2024, and in urban areas from 90% in December 2023 to 91.6% in December 2024.
Some bold moves. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Brand Tanzania
@Brand_Tanzania1
Tanzania’s agricultural budget has increased from 294 billion shillings in the fiscal year 2021/22 to 1.24 trillion shillings in 2023/24.
This increase has contributed to the following areas:
i. The growth rate of the agricultural sector has risen from 2.7% in 2020 to 3.9% in 2023;
ii. Exports of agricultural products have increased from 1.2 billion US dollars to 2.3 billion US dollars, representing a growth of 99.67%;
iii. Food self-sufficiency in the country has increased from 114% in the fiscal year 2021/22 to 140% in 2023/24.
Some iron-marks the 6th phase Government is cementing. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), akiteta jambo na Mbunge wa Viti Maalum, na Mwenyekiti wa Chama cha Wabunge cha Kutokomeza Malaria Tanzania (TAPAMA), Mhe. Riziki Lulida, nje ya Jengo la Hazina, Jijini Dodoma, baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe wa Asasi ya Kiraia inayojihusisha na masuala ya watu Wenye Ulemavu (SWAUTA), ambapo pamoja na mambo mengine, Mhe. Dkt. Nchemba aliwahakikishia utayari wa Serikali kuendelea kuyasaidia Makundi Maalumu kufikia ndoto yao ya kujikwamua kiuchumi kupitia mipango na ruzuku inayotolewa na Serikali kupitia Bajetu Kuu.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akimsaidia Mbunge wa Viti Maalum, na Mwenyekiti wa Chama cha Wabunge cha Kutokomeza Malaria Tanzania (TAPAMA), Mhe. Riziki Lulida, nje ya Jengo la Hazina, Jijini Dodoma, baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe wa Asasi ya Kiraia inayojihusisha na masuala ya watu Wenye Ulemavu (SWAUTA), ambapo pamoja na mambo mengine, Mhe. Dkt. Nchemba aliwahakikishia utayari wa Serikali kuendelea kuyasaidia Makundi Maalumu kufikia ndoto yao ya kujikwamua kiuchumi kupitia mipango na ruzuku inayotolewa na Serikali kupitia Bajetu Kuu. -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Leo nimekutana na kufanya kikao na Wawakilishi wa NGOs za Watu Wenye Ulemavu (WWU) wakiongozwa na Mhe. Riziki Lulida, Mwenyekiti wa TAPAMA na Mbunge wa Viti Maalum.
Tumejadili ushirikiano kati ya kundi hili na Serikali, na nimewahakikishia kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea kuboresha mazingira ya watu wenye Makundi Maalumu ili kuwawezesha kujikwamua kiuchumi kupitia program mbalimbali ikiwemo ruzuku inayotolewa kupitia Bajeti Kuu ya Serikali. -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Mchango wangu wa leo katika Mjadala wa Taarifa ya Kamati ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa pamoja na Kamati ya Elimu, Utamaduni na Michezo.
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Serikali imesema kuwa asilimia 20 ya mapato ya kodi zitarejeshwa katika halmashauri husika baada ya Mkataba wa Makubaliano (MoU) kati ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Ofisi ya Rais – TAMISEMI kuhusu kuboresha usimamizi na ukusanyaji wa kodi hiyo utakapo kamilika.
Hayo yameelezwa bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb) alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Mtwara Mjini, Mhe. Hassan Seleman Mtenga wakati ambao Serikali itarejesha makusanyo ya Kodi ya Ardhi ya asilimia 20 kwa Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara Mikindani.
Mhe. Dkt. Nchemba alisema Serikali kupitia Sheria ya Fedha ya mwaka 2023/24 ilifanya marekebisho ya Sheria ya Fedha ya Serikali za Mitaa, Sura 290 kwa kuzitaka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Ofisi ya Rais – TAMISEMI kuingia Mkataba wa Makubaliano ya Ushirikiano (MoU) katika usimamizi na ukusanyaji wa kodi ya pango la ardhi na kuweka utaratibu wa urejeshaji wa asilimia 20 ya mapato kwa halmashauri ili kuziwezesha katika ufuatiliaji na ukusanyaji wa mapato hayo.
"Serikali iliweka utaratibu huo ikiwa na lengo la kuhakikisha kuwa kuna tija katika ukusanyaji wa mapato yatokanayo na pango la ardhi inaongezeka na kuondoa kero zilizokuwa zinawakabili walipa kodi kwenye maeneo husika", alibanisha Dkt. Nchemba.
Alilihakikishia Bunge kuwa Mkataba huo utakapokamilika na kuwasilishwa Wizara ya Fedha, fedha hizo zitarejeshwa kama utaratibu unavyotaka. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Chama Cha Mapinduzi
@ccm_tanzania
BALOZI NCHIMBI ACHANGISHA SH. 1.7B UJENZI OFISI YA CCM MKOA WA SINGIDA
Matukio mbalimbali katika picha wakati wa hafla ya chakula cha jioni iliyoenda sambamba na harambee ya uchangishaji wa fedha na vitu vingine, kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida, ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi. Jumla ya kiasi cha fedha takriban shilingi bilioni 1.7 zilipatikana. Hafla hiyo iliyowahusisha viongozi, wanachama, wafuasi wa CCM na wananchi wa kada mbalimbali, ilifanyika Ukumbi wa Jenerali Venance Mabeyo, jijini Dodoma, tarehe 9 Februari 2025. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Rémy Rioux
@RiouxRemy
Very positive discussions with Deputy-PM @DBiteko & Finance Minister @mwigulunchemba1 about @AFD_France activities in Tanzania🇹🇿 (energy, water, transport, financial sector) with @Proparco & @expertisefrance. Thank you Ambassador @annesophieave & team led by @CelineRobertAFD💪🏼🙏🏼
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
TRA Tanzania
@TRATanzania
#ajiratra Bofya link hii kuomba
recruitment.tra.go.tz/tra_careers/login.aspx -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
TRA Tanzania
@TRATanzania
-
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Happy birthday @ccm_tanzania.
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), amesema Serikali imechukua hatua madhubuti kudhibiti mianya ya ukwepaji kodi unaosababishwa na mabadiliko ya majina ya kampuni za kigeni kwa kuhakikisha Namba ya Utambulisho wa Kodi (TIN) inabaki ile ile hata kama kampuni itabadilisha jina.
Hayo ameyasema bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Tarime Mjini, Mhe. Michael Mwita Kembaki, aliyetaka kujua hatua zinazochukuliwa na Serikali kwa wawekezaji wa nje ambao kila baada ya miaka kadhaa hubadili majina ya Kampuni kwa lengo la kukwepa kodi.
Mhe. Dkt. Nchemba alisema kuwa Serikali imechukua hatua mbalimbali ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa Sheria ya Kampuni, Sura 212, ambayo inawataka wawekezaji kutoa taarifa kwa Msajili wa Kampuni (BRELA) wanapobadilisha jina la kampuni.
“Historia ya mabadiliko yote ya majina ya kampuni huhifadhiwa kwenye kumbukumbu rasmi ili kuhakikisha majina mapya hayawezi kutumika kuficha madeni ya kodi au kushiriki katika shughuli zisizo halali”, alisema Dkt. Nchemba.
Alisema kuwa kupitia Sheria ya Usimamizi wa Kodi, Sura 438, Serikali pia imeweka sharti kwamba Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuhakikisha Namba ya Utambulisho wa Kodi (TIN) inabaki ile ile hata kama kampuni itabadilisha jina kwa kuwa TIN hutumika kufuatilia historia ya ulipaji kodi wa kampuni, hivyo mabadiliko ya jina hayaondoi wala kufuta wajibu wa kodi.
Aidha, akieleza kuhusu kodi zinazotozwa wakati wa kubadili jina la Kampuni kwa watanzania na wageni, Dkt. Nchemba alisema kuwa kubadili jina la Kampuni haiathiri wala haihusiani na masuala ya kikodi.
Alisema kuwa kinachosababisha kuwepo na kodi au ukwepaji wa kodi ni mabadiliko ya umiliki kwa kuuza Hisa ambazo zitaleta kipato cha ziada ambacho kinatakiwa kulipiwa kodi kutokana na faida iliyopatikana.
“Kama mmiliki ni yuleyule ameamua kubadilisha jina la Kampuni kwa ajili ya matangazo ya kibiashara na Namba ya Mlipa Kodi ni ileile, haileti badiliko lolote kwenye kodi”, alifafanua Dkt. Nchemba.
Alisema kuna kampuni za nje ambazo zinamiliki sehemu ya kampuni nchini na hazina shughuli zaidi ya zinazofanyika Tanzania, ikitokea wamebadilishana umiliki unaozidi asilimia 50, hapo kuna kodi ambayo ni lazima ikusanywe.
Alisema Serikali imefanyia kazi kwa kiasi kikubwa suala hilo lililokuwa likijitokeza katika maeneo ya mawasiliano, madini na mengine na amewatoa hofu wabunge kuwa Serikali imeweka kwenye Sheria na inafuatilia kwa umakini panapotokea jambo hilo na kodi stahiki ya Serikali inakusanywa. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Jambo TV
@Jambotv_
Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba @mwigulunchemba1 , amesema Serikali imechukua hatua madhubuti kudhibiti mianya ya ukwepaji kodi unaosababishwa na mabadiliko ya majina ya kampuni za kigeni kwa kuhakikisha Namba ya Utambulisho wa Kodi (TIN) inabaki ile ile hata kama kampuni itabadilisha jina.
Hayo ameyasema bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Tarime Mjini, Michael Mwita Kembaki, aliyetaka kujua hatua zinazochukuliwa na Serikali kwa wawekezaji wa nje ambao kila baada ya miaka kadhaa hubadili majina ya kampuni kwa lengo la kukwepa kodi.
Dkt. Nchemba amesema kuwa Serikali imechukua hatua mbalimbali ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa Sheria ya Kampuni, Sura 212, ambayo inawataka wawekezaji kutoa taarifa kwa Msajili wa Kampuni (BRELA) wanapobadilisha jina la kampuni.
“Historia ya mabadiliko yote ya majina ya kampuni huhifadhiwa kwenye kumbukumbu rasmi ili kuhakikisha majina mapya hayawezi kutumika kuficha madeni ya kodi au kushiriki katika shughuli zisizo halali”, amesema Dkt. Nchemba.
Amesema kuwa kupitia Sheria ya Usimamizi wa Kodi, Sura 438, Serikali pia imeweka sharti kwamba Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuhakikisha Namba ya Utambulisho wa Kodi (TIN) inabaki ileile hata kama kampuni itabadilisha jina kwa kuwa TIN hutumika kufuatilia historia ya ulipaji kodi wa kampuni, hivyo mabadiliko ya jina hayaondoi wala kufuta wajibu wa kodi.
Aidha, akieleza kuhusu kodi zinazotozwa wakati wa kubadili jina la kampuni kwa Watanzania na wageni, Dkt. Nchemba amesema kuwa kubadili jina la Kampuni haiathiri wala haihusiani na masuala ya kikodi.
Amesema kuwa kinachosababisha kuwepo na kodi au ukwepaji wa kodi ni mabadiliko ya umiliki kwa kuuza hisa ambazo zitaleta kipato cha ziada ambacho kinatakiwa kulipiwa kodi kutokana na faida iliyopatikana.
“Kama mmiliki ni yuleyule ameamua kubadilisha jina la kampuni kwa ajili ya matangazo ya kibiashara na Namba ya Mlipa Kodi ni ileile, haileti badiliko lolote kwenye kodi”, amefafanua Dkt. Nchemba.
Amesema kuna kampuni za nje ambazo zinamiliki sehemu ya kampuni nchini na hazina shughuli zaidi ya zinazofanyika Tanzania, ikitokea wamebadilishana umiliki unaozidi asilimia 50, hapo kuna kodi ambayo ni lazima ikusanywe.
Amesema Serikali imefanyia kazi kwa kiasi kikubwa suala hilo lililokuwa likijitokeza katika maeneo ya mawasiliano, madini na mengine na amewatoa hofu wabunge kuwa Serikali imeweka kwenye Sheria na inafuatilia kwa umakini panapotokea jambo hilo na kodi stahiki ya Serikali inakusanywa. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Dr. Akinwumi A. Adesina, CON, CGH
@akin_adesina
Many thanks to a great African leader! My wife Grace and I, with our dearest sister and friend, President @SuluhuSamia of Tanzania. Thank you for your great leadership and incredible and generous hospitality in hosting us for the landmark Africa Energy Summit. Asante Sana!
-
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Nuru ya Taifa, Dkt. Samia Suluhu Hassan.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. @mwigulunchemba1 (Mb), amesema kuwa Serikali ipo katika hatua za mwisho za kuanza zoezi la kutoa fedha kwa ajili ya vituo vya afya vya kimkakati katika majimbo na ukamilishaji wa maboma yaliyojengwa na wananchi.
Mhe. Dkt. Nchemba ametoa kauli hiyo bungeni jijini Dodoma wakati akitoa majibu ya nyongeza baada ya maswali ya wabunge kuhusu fedha za ujenzi wa vituo vya afya na ukamilishaji wa maboma ambayo yamejengwa kwa nguvu za wananchi katika sekta ya afya na elimu.
“Tuko katika hatua ya mwisho kuanza utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa miundombinu ya kimkakati ya elimu na vituo vya afya msingi itakayokwenda sambamba na ukamilishaji wa maboma ambayo yamejengwa kwa nguvu ya wananchi”, alisema Dkt. Nchemba.
Awali Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe. Zainab Katimba, alilieleza Bunge kuwa Serikali itatoa kiasi cha shilingi milioni 250 kwa kila jimbo kwa ajili ya kuendeleza miundombinu ya kutolea huduma za afya msingi, zikiwemo Zahanati.
Alisema kuwa Wabunge walijaza fomu za kuainisha maeneo ya kimkakati katika majimbo yao ili kujenga vituo vya afya kupitia fedha kutoka Serikali Kuu na mapato ya ndani kutoka Halmashauri.
Aidha, alizihimiza Halmashauri kupitia mapato ya ndani kutenga fedha kwa ajili ya kujenga miundombinu hiyo muhimu ya afya msingi. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Dr Charles Mwamwaja
@Dr_C_Mwamwaja
Wamaasai na Elimu ya Fedha; Badala ya kuhifadhi fedha nyumbani baada ya kuuza mifugo, Wamaasai wa Ngorongoro wanahamasishwa kutumia benki kwa usalama na faida zaidi.
Kutunza pesa nyumbani kunawaweka kwenye hatari ya wizi na hasara.
✅ Benki inasaidia kuhifadhi, kuwekeza, na kupata mikopo salama kwa maendeleo yao!
#elimuyafedha
@mwigulunchemba1
@mofURT -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
TBC DIGITAL
@TBConlineTZ
Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema wapo katika hatua za mwisho za kupata fedha za kuendeleza ujenzi wa Reli ya Kisasa ya SGR kwenye vipande vilivyobaki vya Dodoma - Tabora - Kigoma - Mwanza na makubaliano ya kupata fedha hizo yameshafanyika na ujenzi huo utaendelea
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
FLORY OKANDJU OKONGE, PhD
@FloryOKANDJU
Today in Dar es Salaam, I witnessed another key milestone for the Central Corridor SGR project, the signing of a Works Contract for the 282 km railway from Uvinza (Tanzania) to Musongati (Burundi). This strategic cross-border infrastructure will boost regional connectivity, trade, and integration.
I reaffirmed @ccttfaorg's commitment to coordinating the planning and implementation of this transformative Central Corridor SGR project, ensuring alignment with the vision of our Heads of State and support from key development partners. @tzrailways @MielsBurundi @WizarayaUC @AfDB_Group -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), ameshuhudia utiwani saini wa Mikataba ya Ujenzi wa Reli wa Kipande cha Reli namba 7 na 8, kuanzia Uvinza (Tanzania) hadi Msongati (Burundi) kati ya Tanzania, Burundi na Kampuni za ukandarasi za CREGC na CREDC za nchini China, utakaogharimu dola za Marekani bilioni 2.134 sawa na shilingi za Tanzania trilioni 5.38, tukio lililofanyika Stesheni Kuu ya Shirika la Reli Tanzania-TRC, Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Dkt. Nchemba alisema kuwa fedha za kukamilisha ujenzi wa mradi huo zipo na zimetolewa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), na kutoa wito kwa Taasisi nyingine za Fedha za Kimataifa kuiga mfano wa Benki hiyo kwa kutoa fedha zitakazo chagiza maendeleo ya nchi za Afrika badala ya kung’ang’ania kutoa fedha za kugharamia semina na kujengeana uwezo, kula chapati na maandazi, mambo ambayo amesema hayana tija kubwa ya kuwakwamua Wananchi kiuchumi. -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Nimemuaga Rais wa Benki ya Dunia, Bw. Ajay Banga, baada ya hitimisho la Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa Nchi na Serikali za Afrika uliofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC).
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Haki Ngowi
@Hakingowi
📍Dar es Salaam
🇹🇿🇰🇲
▪️TANZANIA NA COMORO KUENDELEZA USHIRIKIANO WA KIUCHUMI.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha wa Visiwa vya Comoro, Mhe. Ibrahim Mohamed Abdourazak, Kando ya Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa Nchi na Serikali, uliohitimishwa tarehe 28 Januari 2025, katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam, ambapo pamoja na mambo mengine, wamejadili namna ya kuongeza ushirikiano kupitia biashara na uwekezaji.
Kwa upande wake, Waziri wa Fedha wa Comoro, Mhe. Ibrahim Mohamed Abdourazak, alisema kuwa nchi yake inajivunia uhusiano na ushirikiano wa kihistoria uliopo kati ya nchi hizo mbili na kumwomba Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Nchemba kuzihamasisha Taasisi za Fedha za Tanzania kufungua huduma zao nchini Comoro ili kurahisisha biashara na uwekezaji ili kukuza uchumi, kwa faida ya nchi hizo mbili.
Mkutano huo ulihudhuriwa pia na Balozi wa Tanzania nchini Comoro, Mhe. Said Yacoub, Kamishna wa Idara ya Madeni, Wizara ya Fedha, Bw. Japhet Justine, Kamishna Msaidizi wa Idara ya Fedha za Nje, Wizara ya Fedha, Bw. Robert Mtengule, na Maafisa wengine kutoka Wizara ya Fedha na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki pamoja na ujumbe kutoka Wizara ya Fedha ya Comoro.
📸:W/Fedha -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha wa Libya, Mhe. Dkt. Khalid Al Mabrouk Abdalla, Kando ya Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa Nchi na Serikali, uliohitimishwa tarehe 28 Januari 2025, katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam, ambapo pamoja na mambo mengine, wamejadili namna ya kuongeza ushirikiano kupitia Sekta mbalimbali za uzalishaji.
Mkutano huo ulihudhuriwa pia na Kamishna wa Idara ya Madeni, Wizara ya Fedha, Bw. Japhet Justine, Kamishna Msaidizi wa Idara ya Fedha za Nje, Wizara ya Fedha, Bw. Robert Mtengule, na Maafisa wengine kutoka Wizara ya Fedha na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki pamoja na ujumbe kutoka Wizara ya Fedha ya Libya. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
AIIB
@AIIB_Official
Attending the @AfDB_Group-@WorldBank #mission300 Africa Energy Summit alongside senior government officials from AIIB Members and leaders from public and private development actors, President Jin reaffirmed AIIB’s commitment to support 🌍Africa's ⚡️development.
📍🇹🇿Dar es Salaam -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Rais na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara na Maendeleo (Trade and Development Bank Group- @TdbGroup ), Bw. @AdmassuTadesse , Kando ya Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa Nchi na Serikali, unaofikia kilele leo (28.01.2025), katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano (JNICC), Jijini Dar es Salaam, ambapo pamoja na mambo mengine, Mhe. Dkt. Nchemba aliishukuru Benki hiyo kwa kuchangia maendeleo ya nchi kwa kutoa fedha za kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ya kiuchumi ikiwemo ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR kipande cha 2 kinachoanzia Morogoro hadi Dodoma, ambayo ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 100.
Ameiomba Benki hiyo kushiriki pia katika ujenzi wa Reli ya Kisasa SGR kwa kipande (Lot 6, kuanzia Tabora hadi Kigoma na kipande cha 7, ninachoanzia Uvinza hadi Msongati, ambavyo utafutaji fedha wake unaratibiwa na Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB), kwa niaba ya Serikali.
Kwa upande wake, Rais na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara na Maendeleo (Trade and Development Bank Group-TDB), Bw. Admassu Tadesse, ameipongeza Tanzania kwa hatua kubwa iliyopiga kimaendeleo na kuahidi kuwa Benki yake itaendelea kutoa ushirikiano kwa kutoa fedha za ujenzi na upanuzi wa Bandari ya Dar es Salaam (ujenzi wa gati namba 8 hadi 11 na kuahidi kuwa iko tayari pia kutoa fedha za ujenzi wa SGR kwa kipande cha 6 na cha 7.
Kikao hicho kiliwashirikisha pia, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba na Naibu wake, Bi. Amina Khamis Shaaban, Kamishna Idara ya Fedha za Nje, Wizara ya Fedha Bw. Rished Bade, Kamishna wa Idara ya Madeni Wizara ya Fedha, Bw. Japhet Justine, na Viongozi wengine waandamizi wa Wizara ya Fedha na TDB. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Sweden in Tanzania
@SwedeninTZ
At the #mission300 Energy Summit, we discussed deepening Sweden and Tanzania’s collaboration in energy, transport, and health sectors. Together, we’re accelerating development and fostering innovation for a sustainable future. #swedenintanzania🇸🇪🇹🇿
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), akizungumza jambo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni, Kando ya Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa Nchi na Serikali, unaofikia kilele leo (28.01.2025), katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano (JNICC), Jijini Dar es Salaam.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Bundesentwicklungsministerium
@BMZ_Bund
„We don’t feel like donors. We feel like partners working on a joint mission. Together we can give 300 Million people access to energy.“ State Secretary Jochen Flasbarth at the Africa Energy Summit in Tanzania, meeting Finance Minister @mwigulunchemba1 #mission300 #poweringafrica
-
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
"The time to act is now, We have to act now".
#poweringtanzania
#poweringafrica
#mission300africaenergysummitThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb) (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa Serikali ya Liberia, ukiongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango wa Liberia, Bw. @KpeheNgafuan , siku ya kwanza ya Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa Nchi na Serikali, unaofanyika kwa siku mbili katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa (JNICC), Jijini Dar es Salaam (27&28 Januari, 2025).
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ( @DBiteko ), akizungumza na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), pamoja na ujumbe wake pamoja na Wizara ya Nishati, walipofanya vikao katika Ofisi yake Ndogo iliyopo katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam, ambapo Mhe. Naibu Waziri Mkuu, kwa nyakati tofauti, aliongoza Vikao na Shirika la Maedeleo la Ufaransa (@AFD_en ), Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania (@SwedeninTZ ), ambapo walijadili namna Tanzania, Ufaransa na Sweden zitaendeleza ushirikiano wa kimkakati ili kuharakisha maendeleo.
Mkutano huo umefanyika Kando ya Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa Nchi na Serikali, unaofanyika kwa siku mbili katika Kituo hicho cha Mikutano, tarehe 27-28 Januari, 2025. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
The BizLens
@thebizlens
Access to reliable electricity is pivotal for economic transformation in Africa, creating jobs, empowering communities, and improving living standards, Tanzanian Finance Minister Dr Mwigulu Nchemba has said.
thebizlens.co.tz/2025/01/27/dr-nchemba-reliable-electrici… -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
The Citizen Tanzania
@TheCitizenTz
The Minister for Finance Mwigulu Nchemba on Monday urged African countries to collaborate with development partners, commercial banks and impact investors as one of the strategies to address electricity challenges in the continent. www.thecitizen.co.tz/tanzania/news/national/finance-minis…
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
TBC DIGITAL
@TBConlineTZ
Waziri wa Fedha wa Tanzania Dkt. Mwigulu Nchemba ametoa wito kwa taasisi za kifedha za ndani na za Kimataifa kuwa mstari wa mbele katika kutoa mitaji ili kufanikisha malengo yaliyowekwa kwenye ajenda ya ‘Mission 300’, ya kufikisha nishati ya umeme kwa waafrika milioni 300
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), ameiambia Jumuiya ya Kimataifa kwamba Serikali ya Tanzania imeendelea kutenga na kuongeza bajeti kila mwaka ya kujenga miundombinu ya uzalishaji nishati likiwemo Bwawa la Mwalimu Nyerere lenye uwezo wa kuzalisha MW 2,115 za umeme pamoja na njia yake ya kusambaza umeme, uliogharimu shilingi za Tanzania trilioni 6.6 na dola za Marekani milioni 133.7, kutokana na umuhimu wake katika kuchochea maendeleo na ustawi wa wananchi kiuchumi na kijamii.
Mhe. Dkt. Nchemba alisema hayo wakati akitoa neno wakati wa uwasilishaji wa Mpango Mahsusi wa Serikali ya Tanzania wa Nishati (Compact) wa kuboresha masuala ya Nishati, uliofanyika kando ya Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa Nchi na Serikali, unaofanyika kwa siku mbili Jijini Dar es Salaam (27 na 28 Januari, 2025), na kusisitiza kuwa Nchi imejipanga kuhakikisha kuwa inafikia lengo la uunganishaji umeme kwa asilimia 75 na kufikia asilimia 100 ya upatikanaji wa umeme lakini pia kufikisha asilimia 75 ya upatikanaji wa nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2030.
Mgeni Rasmi katika uwasilishaji wa Mpango huo (Compact), alikuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko na kuhudhuriwa na Viongozi wakuu wa Taasisi za Fedha Duniani akiwemo Bw. Ajay Banga, Rais wa Benki ya Dunia na Dkt. Akinwumi Adesina, Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB). -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Agence Française de #Développement (AFD) 🇫🇷 🇪🇺
@AFD_France
#mission300
⚡️ Lors de sa rencontre avec le vice-premier ministre 🇹🇿, Dr. Doto Biteko et le ministre des finances @mwigulunchemba1 , @RiouxRemy a affirmé notre engagement à financer un plan de transition énergétique équitable, juste, sûr et abordable pour la Tanzanie, avec le soutien de l'@IEA. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
AFD_en 🇫🇷 🇪🇺
@AFD_en
#mission300
⚡️Meeting with 🇹🇿 Deputy Prime Minister, Dr. Doto Biteko and Minister for Finance @mwigulunchemba1, @RiouxRemy asserted our commitment to financing a fair, just, secure & affordable Energy Transition Plan for Tanzania, with the backing of the @IEA.
@ONWM_Tanzania @mofURT -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe kutoka Taasisi ya Uwekezaji ya Ufaransa- @Meridiam , ukiongozwa na Afisa Mikakati Mkuu, Bi. Marie Lam-Frendo, kando ya Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Afrika, ulioanza leo (27.01.2025), katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Cha Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam, ambapo walijadiliana kuhusu uwekezaji nchini kupitia njia ya Ubia kati ya Serikali na Sekta Binafsi – PPP, hususan Mradi wa Mabasi yaendayo haraka - UDART.
Kikao hicho kiliwashirikisha pia, Kamishna wa Idara ya Madeni Wizara ya Fedha, Bw. Japhet Justine, Kamishna Msaidizi Idara ya Fedha za Nje, Wizara ya Fedha Bw. Robert Mtengule na Viongozi wengine waandamizi wa Wizara ya Fedha na Meridiam. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), amehutubia wakati wa Mjadala kuhusu mchango wa Washiriika wa Maendeleo wa Kimataifa, katika kuchangia nchi za Afrika kukabiliana na changamoto ya upatikanaji wa nishati ya uhakika, kuelekea Kilele cha Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali unaotarajiwa kufanyika kesho (28.01.2025), katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam, ambapo ametoa wito wa nchi za Afrika kwa kushirikiana na Taasisi za fedha za Kimataifa na Sekta binafsi kutoa fedha kwa ajili ya kuimarisha Sekta ya nishati Barani Afrika itakayochangia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa maendeleo endelevu yatakayosaidia kukuza ajira, uchumi endelevu na kuboresha maisha ya watu.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
The Chanzo
@TheChanzo
Mwigulu stresses the importance of Development Partners in Africa's energy transformation.
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Tanzania Business Insight
@TanzaniaInsight
𝗠𝘄𝗶𝗴𝘂𝗹𝘂 𝗰𝗮𝗹𝗹𝘀 𝗳𝗼𝗿 𝗻𝗲𝘄 𝗳𝘂𝗻𝗱𝗶𝗻𝗴 𝗰𝗼𝗺𝗺𝗶𝘁𝗺𝗲𝗻𝘁 𝘁𝗼 𝗲𝗹𝗲𝗰𝘁𝗿𝗶𝗳𝘆 𝗔𝗳𝗿𝗶𝗰𝗮
"Allow me to take this opportunity to encourage our development partners to straightforward and announce a new funding commitment and technical support initiative that will drive Africa's energy transformation forward and reach the objective of our Mission 300. Development partners' contribution, both multilateral and bilateral, are essential in helping us achieve our goals of universal energy access by 2030,. economic prosperity and environmental sustainability" Tanzania's Finance Minister Mwigulu Nchemba.
#africaenergysummit
#mission300africaenergysummit
#mission300africaenergy
#mission300
#poweringafrica -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb) (Kushoto), akisalimiana na Rais wa Benki ya Dunia, Bw. Ajay Banga, kando ya Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Afrika, ulioanza tarehe 27 Januari 2025 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Cha Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam. Mkutano huo unaotarajiwa kutamatika tarehe 28 Januari 2025 utawakutanisha Wakuu wa Nchi za Afrika na wadau muhimu wa sekta ya nishati ili kujadili mikakati ya kuhakikisha upatikanaji wa nishati ya uhakika, nafuu, na endelevu kwa maendeleo ya Bara la Afrika.
@WorldBank -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu wa Nchi Wizara ya Ushirikiano wa Uchumi na Maendeleo wa Serikali ya Shirikisho ya Ujerumani, Mhe. Jochen Flasbarth, kando ya Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Afrika, ulioanza leo katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Cha Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam, ambapo katika mazungumzo yao, walikubaliana kuendeleza ushirikiano wa kiuchumi kati ya Tanzania na Serikali ya Shirikisho la Ujerumani.
Kikao hicho kiliwashirikisha pia Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba na Naibu wake, Bi. Amina Khamis Shaaban na Viongozi wengine waandamizi wa Wizara ya Fedha na Wizara ya Ushirikiano wa Uchumi na Maendeleo wa Serikali ya Shirikisho ya Ujerumani.
@BMZ_Bund -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Swahili Times
@swahilitimes
“Nishati ni msingi muhimu kwa uchumi na jamii zetu. Tunaweza kudhani ni jambo la kawaida. Fikiria maisha bila nishati kwa siku moja, mwezi mmoja, au mwaka mmoja. Kwa baadhi ya jamii, hali hii haiwezi kufikirika. Upatikanaji wa nishati ya uhakika na nafuu unaweza kuchochea ukuaji wa uchumi, kuunda ajira, na kuwawezesha wananchi wetu.” - Dkt. Mwigulu Nchemba, Waziri wa Fedha katika mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika, Jijini Dar es Salaam
-
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Mapema leo, kando ya Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa Nchi za Afrika – (Mission 300) unaoendelea katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam, nimekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait ( @kuwaitfund ), Bw. Albahar Waleed. Mazungumzo yetu yamejikita katika kuimarisha ushirikiano wa kimaendeleo kati ya nchi zetu.
#poweringafrica
#poweringtanzania
#mission300africaenergysummitThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Tanzania Business Insight
@TanzaniaInsight
𝗧𝗮𝗻𝘇𝗮𝗻𝗶𝗮 𝗮𝗻 𝗔𝗳𝗿𝗶𝗰𝗮𝗻 𝗯𝗲𝗮𝗰𝗼𝗻 𝗳𝗼𝗿 𝗮𝗰𝗰𝗲𝘀𝘀 𝘁𝗼 𝗲𝗹𝗲𝗰𝘁𝗿𝗶𝗰𝗶𝘁𝘆 - 𝗪𝗼𝗿𝗹𝗱 𝗕𝗮𝗻𝗸 𝗰𝗵𝗶𝗲𝗳
"Let me add my thanks to the government of Tanzania, not only for hosting us but also in the manner in which they have been executing access to electricity increase in their own country over the past few years. They've made enormous progress and that's kind of a lighthouse and a beacon for others to follow as well although they have ambitions to do even more in the coming period, so congratulations (to Tanzania)'" World Bank President Ajay Banga.
#africaenergysummit
#mission300africaenergysummit
#mission300africaenergy
#mission300
#poweringafrica -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Mission 300 Africa Energy Summit: Ministerial & Partnerships Day (Day 1).
#poweringafrica
#poweringtanzania -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait (Kuwait Fund for Arab Economic Development @KuwaitFund ), Bw. Albahar Waleed, Kando ya Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Afrika, ulioanza leo katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Cha Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam, ambapo katika mazungumzo yao, walikubaliana kuendeleza ushirikiano kati ya Serikali na Mfuko huo kupitia ufadhili wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta za maji, umaendeleo ya miundombinu, na huduma jumuishi za kijamii.
Kikao hicho kiliwashirikisha pia Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu Elmaamry Mwamba na Naibu wake, Bi. Amina Hamisi Shaaban, Mkuuwa Idara ya Mashariki ya Kati, Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika, Mhe. Balozi Abdalah Kilima, Viongozi wengine waandamizi wa Wizara ya Fedha na Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait. -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Hongera na baraka tele katika siku yako ya kuzaliwa, Mheshimiwa Rais Dkt. @SuluhuSamia Mungu akujalie afya na siha njema, hekima na mafanikio katika uongozi wako. Happy Birthday MAMA.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Anna Bjerde
@bjerde_anna
Grateful to Tanzania for hosting the Mission 300 Africa Energy Summit.
With Minister @mwigulunchemba1, we discussed building on Tanzania’s success in increasing access to electricity through renewables, regional interconnectivity & public-private partnerships.
#poweringafrica
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia Kanda ya Afrika Mashariki, Bi. @VictoriaKwakwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo anaye simamia masuala ya Utawala, Bi. @bjerde_anna , Jijini Dar es Salaam, Kando ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika unaohusu nishati, ambapo pamoja na mambo mengine, Mhe. Dkt. Nchemba aliwaeleza wageni wake kuwa Tanzania inahitaji zaidi ya dola za Marekani bilioni 12.9 zikiwemo dola za Marekani bilioni 4.04 kutoka Sekta Binafsi kwa ajili ya kuwekeza kwenye eneo la uzalishaji nishati nchini.
Katika kikao hicho kilichomhusisha pia Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba na Naibu wake, Bi. Amina Hamisi Shaaban, Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Dkt. Elsie Kanza na Viongozi wengine waandamizi wa Wizara ya Fedha, Dkt. Nchemba alieleza kuwa kiwango hicho cha fedha kitaiwezesha Tanzania kufikia uzalishaji wa nishati kwa asilimia 75 ifikapo Mwaka 2030 na kiwango cha asilimia 80 cha matumizi ya nishati safi ya kupikia ifikapo Mwaka 2034 na kutimiza lengo la kufikisha asilimia 65 ya nishati mchanganyiko itakayowezesha nchi kuzalisha Megawati 1,800 za umeme kwa njia ya umeme jua, upepo, joto ardhi na umeme wa kutumia nguvu ya maji. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Dkt. @akin_adesina , kando ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Nishati ujulikanao kama “Mission 300”, utakaofanyika tarehe 27 hadi 28 Januari 2025 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam. Katika kikao chao walijadiliana masuala mbalimbali ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Benki hiyo.
Katika kikao chao kilichohudhuriwa na Viongozi waandamizi wa AfDB na Wizara ya Fedha, Dkt. Adesina ameahidi kuwa Benki yake itaendelea kushirikiana na Tanzania ili kuhakikisha kuwa agenda zake za kupiga hatua kiuchumi na kuwahudumia wananchi wake inafikiwa. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Nishati
@Nishati2017
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Nishati
@Nishati2017
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia Kanda ya Afrika Mashariki, Bi. @VictoriaKwakwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo anaye simamia masuala ya Utawala, Bi. @bjerde_anna , Jijini Dar es Salaam, Kando ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika unaohusu nishati, ambapo pamoja na mambo mengine, Mhe. Dkt. Nchemba aliwaeleza wageni wake kuwa Tanzania inahitaji zaidi ya dola za Marekani bilioni 12.9 zikiwemo dola za Marekani bilioni 4.04 kutoka Sekta Binafsi kwa ajili ya kuwekeza kwenye eneo la uzalishaji nishati nchini.
Katika kikao hicho kilichomhusisha pia Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba na Naibu wake, Bi. Amina Hamisi Shaaban, Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Dkt. Elsie Kanza na Viongozi wengine waandamizi wa Wizara ya Fedha, Dkt. Nchemba alieleza kuwa kiwango hicho cha fedha kitaiwezesha Tanzania kufikia uzalishaji wa nishati kwa asilimia 75 ifikapo Mwaka 2030 na kiwango cha asilimia 80 cha matumizi ya nishati safi ya kupikia ifikapo Mwaka 2034 na kutimiza lengo la kufikisha asilimia 65 ya nishati mchanganyiko itakayowezesha nchi kuzalisha Megawati 1,800 za umeme kwa njia ya umeme jua, upepo, joto ardhi na umeme wa kutumia nguvu ya maji. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Rais wa Benki ya Dunia (@WorldBank ), Bw. Ajay Banga amewasili nchini mchana wa leo tarehe 26 Januari 2025, Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es Salaam, kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Nishati ujulikanao kama “Mission 300”, utakaofanyika tarehe 27 hadi 28 Januari 2025 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam Bw. Banga amepokelewa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Cosato Chumi kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe.Dkt. Elsie Kanza, Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini Bw. Nathan Belete, Kamishna wa Idara ya Fedha za Nje, Wizara ya Fedha, Bw. Rished Bade na Viongozi wengine waandamizi wa Serikali.
Mkutano huo unatarajiwa kuwa utahudhuriwa na Wakuu wa Nchi 25 na Makamu wa Rais, Mawaziri Wakuu na Naibu Mawaziri Wakuu 10 inafanya idadi ya viongozi wa ngazi ya juu kufikia 35 na utajadili namna ya upatikanaji wa nishati ya uhakika, nafuu, na endelevu kwa watu milioni 300 barani Afrika ifikapo mwaka 2030.
#mission300
#poweringafrica
#poweringtanzania -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
MFA Tanzania
@mfa_tanzania
The President of the African Development Bank (AfDB), Dr. @akin_adesina, has arrived in Tanzania to attend the African Heads of State Summit on Energy, scheduled to take place from 27th to 28th January 2025 at the Julius Nyerere International Convention Centre in Dar es Salaam.
Dr. Adesina was welcomed by Minister for Finance Hon. Dr. Mwigulu Nchemba Dar es Salaam Regional Commissioner Hon. Albert Chalamila and Deputy Minister for Foreign Affairs and East African Cooperation Hon. Cosato Chumi at @jnintairport .
The Heads of State Summit will bring together African leaders and energy key stakeholders to discuss strategies for ensuring reliable, affordable, and sustainable energy for the African continent’s development. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
MFA Tanzania
@mfa_tanzania
WORLD BANK PRESIDENT ARRIVES IN DAR ES SALAAM
The President @WorldBank Mr. Ajay Banga has arrived in Dar es Salaam, Tanzania to participate in the African Heads of State Energy Summit, which will take place from January 27-28, 2025, at the Julius Nyerere International Conference Centre (JNICC) in Dar es Salaam.
@jnintairport, Mr. Banga was received by Deputy Minister for Foreign Affairs and East African Cooperation, Hon. Cosato Chumi, on behalf of the Minister of Foreign Affairs and East African Cooperation, Dr. Natu Mwamba, the Permanent Secretary @mofURT Dr. Natu Mwamba, Tanzanian Ambassador to the United States, Hon. Dr. Elsie Kanza, the World Bank Country Representative, Mr. Nathan Belete, and other senior government officials.
The summit aims to bring together African heads of state and key stakeholders from the energy and finance sectors to discuss concrete strategies to provide reliable, affordable, and sustainable energy to 300 million people across Africa by 2030.
The World Bank has been a key partner in supporting energy access projects in the country and across Africa in various ways, including funding national grid expansion projects, renewable energy development, mini-grids, policy support, and enabling private sector participation in the energy sector, with a focus on reaching underserved communities.
Among others, the summit is expected to approve and sign the Africa Energy Compact, sign the first phase of the National Energy Compacts for the 2025-2030 period, and adopt the Dar es Salaam Declaration on the Africa Heads of State Energy Summit, which will include 14 countries: Tanzania, the DRC, Ivory Coast, Burkina Faso, Chad, Liberia, Madagascar, Malawi, Mauritania, Mozambique, Niger, Nigeria, Senegal, and Zambia.
Tanzania is one of the leading countries in Africa in the energy sector. As of December 2024, electricity generation in mainland Tanzania had reached 3,169.20 MW, a significant increase from 14% in 2011 to 78.4% in 2020. At the same time, through the Rural Energy Agency (REA), almost all villages in the country have access to electricity. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Dr Charles Mwamwaja
@Dr_C_Mwamwaja
Hongera @NMBTanzania kwa kutenga TZS Bilioni 100 kwa mikopo ya Nishati Safi ya kupikia!
Hatua hii ni suluhisho kwa afya, mazingira, na jamii, ikilenga wasambazaji wa mitungi na majiko ya gesi kwa riba nafuu ya 1% kwa mwezi (6.6% kwa mwaka effective rate). 👏
Kwa kushirikiana na Taifa Gas, NMB itatoa elimu ya Nishati Safi kupitia NMB Kijiji Day kwa vijiji 2,000 ifikapo 2025. Hii ni hatua kubwa kuelekea maendeleo jumuishi!
Hongereni CEO wa NMB @RuthZaipuna kwa uongozi bora.💡 #nishatisafi #nmbinitiative -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Jana tumewapokea Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Dkt. @akin_adesina, na Mkurugenzi Mtendaji wa Utawala wa Banki ya Dunia, Bi. @bjerde_anna, wamewasili nchini tarehe 25 Januari 2025, Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es Salaam, kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Nishati, utakaofanyika tarehe 27 hadi 28 Januari 2025 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
President Dr. Samia Suluhu Hassan warmly welcomes African leaders, delegates, and partners to the Africa Energy Summit 2025, scheduled for January 27–28, 2025, in Dar es Salaam, Tanzania. This pivotal gathering will foster collaboration and innovation to advance sustainable energy solutions across the continent.
#mission300
#poweringafrica
#poweringtanzaniaThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Dkt. @akin_adesina , na Mkurugenzi Mtendaji wa Utawala wa Banki ya Dunia, Bi. @bjerde_anna , wamewasili nchini leo usiku tarehe 25 Januari 2025, Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es Salaam, kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Nishati, utakaofanyika tarehe 27 hadi 28 Januari 2025 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Viongozi hao wamepokelewa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb) Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila, na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Cosato Chumi.
Mkutano wa Wakuu wa Nchi utawakutanisha Wakuu wa Nchi za Afrika na wadau muhimu wa sekta ya nishati ili kujadili mikakati ya kuhakikisha upatikanaji wa nishati ya uhakika, nafuu, na endelevu kwa maendeleo ya Bara la Afrika.
Mkutano huo inatarajiwa kuwa utahudhuriwa na Wakuu wa Nchi 25 na Makamu wa Rais, Mawaziri Wakuu na Naibu Mawaziri Wakuu 10 inafanya idadi ya viongozi wa ngazi ya juu kufukia 35. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (wa pili kulia), Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila (wa pili kushoto) na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Cosato Chumi (Mb) (wa kwanza kulia), wakiongea na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) nchini Tanzania, Bi. Patricia Laverley, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam, wakisubiri kuwapokea Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, Dkt. Akinwumi Adesina, na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayesimamia masuala ya Utawala, Bi. Anna Bjerde, wanaotarajiwa kuwasili nchini usiku wa leo tarehe 25 Januari 2025, kwa ajili ya kushiriki Kilele cha Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa nchi za Afrika, utakaofanyika kuanzia tarehe 27-28 Januari, 2025, Jijini Dar es Salaam.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Cosato Chumi (Mb), katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kuwapokea wageni mbalimbali akiwemo Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, Dkt. Akinwumi Adesina, na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayesimamia masuala ya Utawala, Bi. Anna Bjerde, wanaotarajiwa kuwasili nchini usiku wa leo kwa ajili ya kushiriki Kilele cha Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa nchi za Afrika, utakaofanyika kuanzia tarehe 27-28 Januari, 2025, Jijini Dar es Salaam.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), ameshiriki hafla ya kuzindua mkopo maalumu wa Benki ya @NMBTanzania , wa kuwakopesha wafanyabiashara wadogo na wa kati wa biashara ya nishati safi, shilingi za Kitanzania bilioni 100, katika kipindi cha miaka miwili, mahsusi kwa ajili ya utoaji wa mikopo kwa miradi, na biashara zinazolenga kupeleka Nishati safi ya kupikia kwa Watanzania.
Akitoa salaam zake katika hafka hiyo iliuotanyika katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam, na kuongozwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Doto Biteko, Mhe. Dkt. Nchemba aliipongeza NMB, kwa kutekeleza maono ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, anayesimamia kwa dhati agenda ya kitaifa ya matumizi ya nishati safi ya kupikia ili kuhifadhi mazingira, kulinda afya za watu na kuimarisha uchumi wa nchi. -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Uzinduzi wa Kitabu kiitwacho “The Magnets of Good Fortunes: A concise Guide to Success”, kilichoandikwa na Dkt. Mosses Leonard Mwizarubi, Msaidizi wa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba.
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), amezindua Kitabu kiitwacho “The Magnets of Good Fortunes: A concise Guide to Success”, kilichoandikwa na Dkt. Mosses Leonard Mwizarubi, ambaye ni Msaidizi wa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba, katika Ukumbi wa Hotel ya Hyatt Regency, Jijini Dar es Salaam, ambapo alimpongeza Mwandishi wa Kitabu hicho kinachogusa maeneo mbalimbali ya maisha na kuhamasisha ustawi wa maisha na mafanikio kwa kumiliki mali, na kutoa rai kwa Jamii kujenga utamaduni wa kusoma na kuandika vitabu kwakuwa ni nguzo muhimu ya maendeleo na ustawi wa jamii yoyote ile duniani.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na watu mbalimbali mashuhuri, akiwemo Gavana wa Benki ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba, Manaibu Gavana, Bi. Sauda Mwema na Dkt. Yamungu Kayandabila, Wazazi wa Dkt. Moses Mwizarubi pamoja na mke wake, Wakuu wa Taasisi za Fedha, Uongozi Institute na wanazuoni mbalimbali.
@BankOfTanzania -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Leo nilipata fursa ya kuwa mgeni rasmi katika hafla ya kuorodheshwa rasmi kwa Hati Fungani ya Benki ya Azania ijulikanayo kama Bondi Yangu, katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (
@dsetanzania
), hafla iliyofanyika katika Ofisi za DSE, jijini Dar es Salaam.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
DAR ES SALAAM STOCK EXCHANGE
@dsetanzania
24.01.2025: Benki ya Azania kupitia Soko la Hisa la Dar es Salaam leo imezindua hatifungani yake ya "Bondi Yangu" yenye thamani ya shilingi bilioni 30 (TSH. 30,000,000,000) na uwezekano wa kuchukua ziada ya shilingi bilioni 15 (TSH. 15,000,000,000), ikiwa ni toleo la kwanza la programu ya hatifungani ya Azania yenye thamani ya shilingi za kitanzania BIlioni Mia Moja (TSH. 100,000,000,000).
MATOKEO YA MAUZO YA HATIFUNGANI
Mauzo ya hatifungani ya Azania yalifunguliwa tarehe 04 Novemba 2024 na kufungwa tarehe 06 Desemba 2024, ambapo kiasi cha shilingi 63,267,980,000 kimepatikana ikilinganishwa na shilingi bilioni 30 zilizotarajiwa kukusanywa, sawa na mafanikio ya asilimia 210.9.
Mgeni Rasmi wa tukio hili alikua ni Waziri wa @mofURT Mh. Dk. @mwigulunchemba1 (Mb), akisondikizwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana @cmsatz CPA. Nicodemus Mkama , Afisa Mtendanji Mkuu wa @dsetanzania
Ndg. @PeterNalitolela na Mkurugenzi Mkuu wa @azaniaBank_ltd Ms. Esther Mang'enya. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Serikali imezishauri taasisi mbalimbali nchini kujiorodhesha kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) ili kutoa fursa kwa wananchi kushiriki kukuza uchumi wao binafsi na uchumi wa nchi kwa njia za kidijitali.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), wakati wa hafla ya kuorodhoreshwa rasmi kwa Hati Fungani ya Benki ya Azania ijulikanayo kama Bondi Yangu, katika Soko la Hisa la Dar es Salaam ( @dsetanzania ), hafla iliyofanyika katika Ofisi za DSE, jijini Dar es Salaam.
Mhe. Dkt. Nchemba alisema kuwa Uorodheshwaji wa Hatifungani hiyo utakuza ukwasi kwa wawekezaji kwa kutoa mwanya wa kuuza na kununua kupitia soko hilo na utaleta chachu kubwa katika kukuza Soko la Hisa la Dar es Salaam ambalo limekuwa mstari wa mbele katika kutoa fursa kwa watanzania kushiriki katika sekta rasmi ya fedha.
“Taarifa mbalimbali zilizotolewa zinaonesha mauzo ya Bondi Yangu yamekuwa ya mafanikio makubwa kwa kukusanya jumla ya Shilingi bilioni 63.3 ambayo ni mafanikio ya asilimia 210.9, mafanikio ya namna hii ni nadra kwa mtoaji wa kwanza wa Hatifungani na hii inadhihirisha kuwa Benki ya Azania imeanza na mwanzo mzuri wa utoaji wa Hatifungani yake na malengo yao ni kukusanya zaidi ya TZS 100 bilioni ili kusaidia makundi ya wanawake, vijana na wajasiriamali wadogo kuweza kushirikishwa katika sekta rasmi ya fedha hapa nchini” alisema Dkt. Nchemba.
Dkt. Nchemba aliongeza kuwa Serikali itaendelea kuhakikisha kuboresha mazingira ya kufanya biashara ili taasisi mbalimbali ziendelee kuja na ubunifu wenye tija ili kusaidia utoaji wa mikopo nafuu kwa makundi mbalimbali ya kinamama, vijana na wajasiriamali na kuleta chachu zaidi katika kuwawezesha wale ambao wanakwama kupata huduma rasmi za kibenki kuwezeshwa kiuchumi.
Aidha, Dkt. Nchemba alitoa wito kwa wananchi na wawekezaji kuchangamkia fursa ya awamu ya pili ya Hatifungani pale itakapozinduliwa rasmi ili kuongeza chachu ya maendeleo kwa taifa letu.
“Napenda kuwahakikishia wawekezaji na wananchi kwa ujumla kuwa Serikali yetu chini ya Uongozi mahiri wa Mama yetu, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea kuweka mazingira bora ya uwekezaji katika sekta ya fedha na hasa kwenye masoko ya mitaji na dhamana” aliongeza Dkt. Nchemba.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Azania, Dkt. Esther Mang’enya, alisema kuwa hadi sasa jumla ya wawekezaji 650 wamefungua akaunti za CDS kuwawezesha kushiriki katika mauzo ya Bondi Yangu na shughuli zingine za masoko ya mitaji na dhamana ambapo zaidi ya asilimia 97.3 ya wawekezaji walioshiriki katika “Bondi Yangu” ni wawekezaji mmoja mmoja (retail investors).
Aidha, Afisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa la Dar es Salaam, Bw. Peter Nalitolela, alisema kuwa thamani ya uwekezaji wa hatifungani katika soko hilo imeendelea kuongezeka na sasa imefikia takribani shilingi trilioni 27.6, huku idadi ya wawekezaji ikiwa imefikia 637,137.
Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), CPA Nicodemus Mkama, amepongeza mafanikio hayo, akibainisha kuwa yanatokana na mazingira wezeshi ya uwekezaji yaliyowekwa, ikiwa ni pamoja na kuondolewa kwa kodi ya zuio kwenye faida ya hatifungani za taasisi.
@azaniaBank_ltd -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Leo tunazindua kitabu cha mdogo wangu Mosses Mwizarubi, The Magnets of good fortunes, hongera sana. Karibuni sana.
-
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
ASANTENI WALIPAKODI
Awali ya yote, nichukue fursa hii kumshukuru kwa dhati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kukubali kuwa Mgeni Rasmi katika hafla ya utoaji Tuzo kwa Walipakodi Bora wa mwaka 2023/24.
Tunathamini sana heshima hii na uongozi wako wa kuhamasisha ulipaji kodi kwa maendeleo ya Taifa letu.
Mheshimiwa Rais, tunapokea kwa uzito mkubwa mwelekeo, maelekezo na maagizo uliyotupa. Napenda kukuhakikishia kuwa tayari tumeanza kuyafanyia kazi kwa haraka na kwa weledi, tukiweka msisitizo katika ukusanyaji wa mapato kwa haki—bila dhuluma kwa walipakodi na bila kuruhusu mianya ya ukwepaji kodi kutoka kwa wasio waaminifu.
Kwa heshima kubwa, tunashukuru sana kwa kukubali kuzibeba Tuzo hizi kwa Jina lako, ambapo sasa zitajulikana kama TUZO ZA RAIS kwa Walipakodi Bora. Hatua hii ni ya kihistoria na inatoa msukumo mkubwa kwa walipakodi wote nchini, huku ikihamasisha uwajibikaji na uwazi katika kulipa kodi. Tunaamini kuwa hatua hii itaongeza hadhi ya Tuzo hizi hadi ngazi ya kimataifa.
Pia, nawapongeza kwa dhati Kamishna Mkuu wa TRA na watumishi wote wa Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa maandalizi mazuri na mafanikio ya hafla hii. Kazi haijaisha—sasa ni wakati wa kutekeleza maelekezo na matarajio ya Mheshimiwa Rais kwa bidii na umakini mkubwa.
Kwa Walipakodi wote mlioibuka washindi wa tuzo hizi siku ya jana, hongereni sana! Mmeonesha mfano bora wa uzalendo kwa kulipa kodi kwa uaminifu. Ni rai yangu kwenu kuendelea na moyo huo huo, kwani kupitia kodi zenu, Taifa letu linaweza kujitegemea kiuchumi na kusonga mbele kimaendeleo, kama ambavyo Mheshimiwa Rais ameazimia.
Natoa wito kwa Walipakodi wote nchini kuhakikisha wanalipa kodi stahiki kwa hiari, ili kuepuka migogoro isiyo ya lazima na kusaidia kukuza uchumi wetu kwa manufaa ya wote.
ASANTENI WALIPAKODI, ASANTE MHESHIMIWA RAIS. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
ikulu_Tanzania
@ikulumawasliano
Rais Dkt. Samia akishiriki kwenye hafla ya Tuzo za Mlipakodi Bora wa mwaka 2023/24 katika ukumbi wa The Super Dome, Masaki Jijini Dar es Salaam tarehe 23 Januari, 2025.
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Jambo TV
@Jambotv_
Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba, amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa miongozo yake madhubuti katika ukusanyaji wa kodi bila kutumia mabavu, akisisitiza kuwa mbinu hiyo imezaa matunda makubwa katika kuongeza mapato ya nchi.
Pongezi hizo zimetolewa Januari 23, 2025, wakati wa kilele cha Siku ya Mlipakodi, ambapo Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imewatunuku walipakodi 1,228 kutoka sekta mbalimbali nchini kwa mchango wao wa kikodi ambapo Rais Samia anakabidhi tuzo hizo, ikiwa ni ishara ya shukrani kwa walipakodi.
Dkt. Mwigulu amesema kauli ya Rais Samia ya kuhimiza ukusanyaji wa kodi kwa hiari imechangia kwa kiasi kikubwa kufanikisha makusanyo makubwa ya kodi. Pia ameeleza kuwa Rais amekuwa akifanya mapitio ya sheria za kodi kupitia tume maalum na kuwezesha TRA kujenga mifumo ya kisasa ya ukusanyaji wa kodi.
“Katika kipindi cha uongozi wa Mhe. Rais Samia, fedha nyingi zimeongezwa kwenye sekta za kilimo, huduma za jamii, afya, na miundombinu, ambapo barabara nyingi zimejengwa mijini na vijijini,” amesema Dkt. Mwigulu.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amesema mkoa huo utaimarisha biashara za usiku na mchana ili kuchochea maendeleo. Amebainisha kuwa hatua za kufunga taa na kamera za CCTV zinaendelea kufanyika ili kuboresha usalama, huku vyombo vya dola vikiwa tayari kulinda mazingira ya kibiashara.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya TRA, Bw. Mussa Uledi, amesisitiza umuhimu wa uwepo wa Rais Samia katika utoaji wa tuzo hizo, akisema kuwa uwepo huo unatoa motisha kwa walipakodi.
Bw. Uledi ameongeza kuwa TRA imeanza kutumia mfumo wa TANCIS, ambao unarahisisha shughuli za forodha bandarini, mipakani, na viwanja vya ndege, sambamba na kuhakikisha mifumo ya taasisi nyingine inasomana ili kuongeza ufanisi. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
BONGO NEWS TV
@BongoNewsTV
VIDEO: Waziri wa fedha Dkt Mwigulu Nchemba amesema Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatimiza ahadi zake zote kwa vitendo
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
ikulu_Tanzania
@ikulumawasliano
RAIS DKT. SAMIA AKIHUDHURIA HAFLA YA UTOAJI TUZO KWA WALIPAKODI BORA WA MWAKA 2023/2024 x.com/i/broadcasts/1BdGYEEEaAQGX
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
ikulu_Tanzania
@ikulumawasliano
RAIS DKT. SAMIA AKIHUDHURIA HAFLA YA UTOAJI TUZO KWA WALIPAKODI BORA WA MWAKA 2023/2024 x.com/i/broadcasts/1OdJrXXXOQPKX
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
ikulu_Tanzania
@ikulumawasliano
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Viongozi pamoja na wageni mbalimbali wakiwa kwenye hafla ya Tuzo za Mlipakodi Bora wa mwaka 2023/24 iliyofanyika katika ukumbi wa The Super Dome, Masaki Jijini Dar es Salaam tarehe 23 Januari, 2025.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
ikulu_Tanzania
@ikulumawasliano
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akikabidhi Tuzo za Mlipakodi Bora wa mwaka 2023/24 kwa wafanyabiashara wanaomiliki Makampuni mbalimbali kwenye hafla iliyofanyika katika ukumbi wa The Super Dome, Masaki Jijini Dar es Salaam tarehe 23 Januari, 2025.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
ikulu_Tanzania
@ikulumawasliano
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akikabidhi Tuzo za Mlipakodi Bora wa mwaka 2023/24 Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB Bi. Ruth Zaipuna kwenye hafla iliyofanyika katika ukumbi wa The Super Dome, Masaki Jijini Dar es Salaam tarehe 23 Januari, 2025.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
ikulu_Tanzania
@ikulumawasliano
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akikabidhi Tuzo ya mlipa kodi binafsi mwenye hadhi ya juu, Mmiliki wa Kampuni za Bakhresa Group, Said Salim Bakhresa kwenye hafla iliyofanyika katika ukumbi wa The Super Dome, Masaki Jijini Dar es Salaam tarehe 23 Januari, 2025.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
ikulu_Tanzania
@ikulumawasliano
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza kwenye hafla ya Tuzo za Mlipakodi Bora wa mwaka 2023/24 katika ukumbi wa The Super Dome, Masaki Jijini Dar es Salaam tarehe 23 Januari, 2025.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
ikulu_Tanzania
@ikulumawasliano
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
ikulu_Tanzania
@ikulumawasliano
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea Tuzo kutoka kwa Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba kwenye hafla ya Tuzo za Mlipakodi Bora wa mwaka 2023/24 katika ukumbi wa The Super Dome, Masaki Jijini Dar es Salaam tarehe 23 Januari, 2025.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), akiteta jambo na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, wakati wa usiku wa hafla ya utoaji tuzo kwa walipakodi waliofanya vizuri kwa mwaka wa fedha 2023/24, tukio lililofanyika katika ukumbi wa The Super Dome, Masaki, jijini Dar es Salaam.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akipokea Tuzo maalum ya kutambua mchango wake wa kuhamasisha ulipaji wa kodi kwa hiari kutoka kwa Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), wakati wa usiku wa hafla ya utoaji tuzo kwa walipakodi waliofanya vizuri kwa mwaka wa fedha 2023/24, tukio lililofanyika katika ukumbi wa The Super Dome, Masaki, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Yusuph Mwenda na Wapili Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka hiyo, Bw. Mussa Uledi.
@SuluhuSamia @ikulumawasliano @TRATanzania -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), akitoa hotuba yake fupi katika hafla ya utoaji tuzo kwa walipakodi waliofanya vizuri kwa mwaka wa fedha 2023/24, ambapo amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa miongozo anayoitoa katika ukusanyaji wa Kodi bila kutumia mabavu.
Amesema kauli ya Mhe. Rais kutaka Kodi ikusanywe kwa hiari imezaa matunda kwa kupatikana kwa makusanyo makubwa ya Kodi, pia Mhe. Rais ameunda Tume ya kufanya mapitio ya Sheria za Kodi na kuiwezesha TRA kujenga mifumo inayoweza kuleta tija kwenye makusanyo.
Dkt. Mwigulu amesema katika kipindi hiki cha Uongozi wa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameongeza kwa kiasi kikubwa fedha katika sekta ya Kilimo, huduma za jamii, sekta ya Afya na katika Miundombinu ambapo barabara zinajengwa mijini na vijijini. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Meza Kuu wakiongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakiimba wimbo wa Taifa na wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, wakati wa usiku wa utoaji tuzo kwa wafanyabiashara waliofanya vizuri kwa mwaka wa fedha 2023/24.
Hafla hiyo imehudhuriwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson, Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Bw. Emmanuel Tutuba, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (@TRATanzania ) Bw. Yusuph Juma Mwenda, viongozi wengine waandamizi wa Serikali na dini, katika ukumbi wa The Super Dome, Masaki, jijini Dar es Salaam ambapo taasisi na wafanyabiashara zaidi ya 100 wanatunukiwa tuzo mbalimbali. -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Leo ni siku ya Shukrani kwa Mlipakodi 2025, Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan atakuwa Mgeni Rasmi, Ukumbi wa The Super Dome, Dar es Salaam.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akipokea taarifa ya maandalizi ya tukio la utoaji tuzo kwa wafanyabiashara katika kilele cha Siku ya Mlipa Kodi, kutoka kwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Yusuph Mwenda, hafla inayotarajiwa kufanyika leo usiku tarehe 23 Januari 2025 katika ukumbi wa The Super Dome, Masaki, jijini Dar es Salaam, ambapo Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi.
Kikao hicho kimehudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Mcha Hassan Mcha na viongozi wengine wa Wizara ya Fedha na TRA. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), ameshiriki mjadala ulioandaliwa na Shirika la Fedha la Kimataifa ( @IMFNews ) ukiwashirikisha wawakilishi kutoka nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara, unaofanyika Jijini Dar es Salaam, ambapo ametumia fursa hiyo kuzitaka Taasisi za Fedha za Kimataifa kuzisaidia nchi zinazoendelea kwa kuweka mifumo rafiki ya kutoa mikopo yenye riba nafuu zaidi ili ziweze kutekeleza miradi na program mbalimbali zitakazochochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Dkt. Nchemba alisema kuwa changamoto za mizozo ya kivita baina ya Urusi na Ukraine na maeneo mengine pamoja na UVIKO 19, vimesababisha nchi zinazoendelea kuyumba kiuchumi hivyo zinahitajika jitihada za makusudi kutoka Taasisi za Fedha za Kimataifa, ikiwemo IMF, kuingilia kati kunusuru mtanziko huo wa kiuchumi na kuziwezesha nchi hizo kuwahudumia wananchi wake kikamilifu.
Mjadala huo ulisimamiwa na Mkurugenzi wa Shirika la Fedha la Kimataifa anayesimamia Kanda ya Afrika, Bw. Abebe Sellasie, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba, Mwakilishi Mkazi wa IMF, Bw. Sebastian Acevedo na waalikwa mbalimbali kutoka nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara, na umefanyika katika Hotel ya Sea Cliff, Jijini Dar es Salaam. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), amepokea Noti Mpya kifani za shilingi elfu kumi, elfu Tano, elfu Mbili na shilingi elfu moja, kutoka kwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam, Noti ambazo zitaanza kutumika sambamba na Noti zilizopo hivi sasa, kuanzia tarehe Mosi Februari, 2025.
@BankOfTanzaniaThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba amesema kuwa Noti Mpya za Tanzania zenye Saini ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb) na yeye mwenyewe, za toleo la mwaka 2010, zitaingia kwenye mzunguko kuanzia tarehe mosi Februari mwaka huu.
Gavana Tutuba amesema hayo wakati akimkabidhi Mhe. Dkt. Nchemba, Noti kifani za shilingi elfu kumi, elfu Tano, Elfu Mbili na Shilingi Elfu moja, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam, kwa mujibu wa Sheria na Taratibu zinazosimamia masuala ya fedha nchini.
“Mheshimiwa Waziri, ninayofuraha kukujulisha kuwa zoezi letu la uchapaji upya wa Noti kwa marejeo ya toleo la mwaka 2010, limekamilika na tayari tumewajulisha wananchi kupitia taarifa niliyoitoa kupitia Gazeti la Serikali” alisema Bw. Tutuba.
Gavana Tutuba alifafanua kuwa Noti hizo zitatumika sambamba na Noti zilizopo hivi sasa, zinamwonekano wa Noti zinazotumika hivi sasa zilizotolewa Mwaka 2010, ikiwemo alama za usalama, ukubwa, rangi na mambo mengine, isipokuwa ina marekebisho kwenye saini ya Waziri wa Fedha, na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania.
“Saini ya aliyekuwa Waziri wa Fedha ambaye hivi sasa ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango imebadilishwa na kuwekwa Saini yako Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba na Saini ya aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania aliyestaafu, Prof. Florens Luoga, imebadilishwa na kuwekwa Saini ya Gavana wa Benki Kuu wa sasa, Bw. Emmanuel Tutuba” aliongeza Bw. Tutuba.
Akizungumza baada ya kupokea sampuli za Noti hizo mpya, Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, alimshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuruhusu jambo hilo kufanyika na kumpongeza Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba, kwa kusimamia mchakato wa uchapaji wa Noti hizo kwa weledi na uadilifu mkubwa.
“Mpaka kufikia hatua hii ni heshima kubwa kwa Taifa letu na inaendeleza heshima ya wataalam wetu mnavyoweza kusimamia kwa umakini mambo yenye maslahi mapana kwa nchi yetu” Alisema Dkt. Nchemba.
Mhe. Dkt. Nchemba aliridhia Noti hizo ziingizwe kwenye mzunguko na kuanza kutumika kama ilivyopangwa tarehe moja Februari mwaka huu.
@BankOfTanzania -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Mama Yuko Kazini
@mamayukokazini
𝐌𝐀𝐊𝐔𝐒𝐀𝐍𝐘𝐎 𝐘𝐀 𝐊𝐎𝐃𝐈 𝐎𝐊𝐓𝐎𝐁𝐀-𝐃𝐄𝐒𝐄𝐌𝐁𝐀 𝐘𝐀𝐏𝐀𝐀
Elimu ya kutosha kwa walipa kodi, usimamizi imara pamoja na mazingira salama na rafiki ya kufanya biashara nchini yanawahamasisha watanzania kulipa kodi ili kuijenga nchi yao.
#mamayukokazini -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), ameshiriki Maadhimisho ya Miaka 60 ya kuanzishwa kwa Chuo cha Biashara Tanzania (CBE) pamoja na uzinduzi wa Dira ya Miaka 50 ijayo ya Chuo hicho, yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam, na kuahidi kuwa Serikali itaendelea kuboresha vyuo vyake mbalimbali nchini, ikiwa ni dhamira ya dhati ya Serikali ya Awamu ya Sita, inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya kuhakikisha sekta ya elimu ikiwemo elimu ya biashara inakuwa na mchango mkubwa katika kukuza ajira, uwekezaji na uchumi wa nchi kwa ujumla.
Maadhimisho hayo yaliongozwa na Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko, na kuhudhuriwa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani Jafo (Mb), ambaye Wizara yake inakisimamia Chuo hicho, Bodi ya Wakurugenzi, Uongozi wa Chuo, Wanafunzi, Viongozi wastaafu waliofanya kazi katika Chuo hicho kwa nyakati tofauti ambao walipewa tuzo pamoja na wadau wengine mbalimbali. -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
𝐒𝐀𝐅𝐔 𝐘𝐀 𝐂𝐇𝐀𝐌𝐀 𝐂𝐇𝐀 𝐌𝐀𝐏𝐈𝐍𝐃𝐔𝐙𝐈 𝐈𝐌𝐄𝐓𝐈𝐌𝐈𝐀
𝐀𝐒𝐀𝐍𝐓𝐄𝐍𝐈 𝐖𝐀𝐉𝐔𝐌𝐁𝐄, 𝐊𝐀𝐙𝐈 𝐈𝐄𝐍𝐃𝐄𝐋𝐄𝐄. -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Hongera Sana my Brother Balozi Dr Emanuel Nchimbi, Timu ya Ushindi 2025 imekamilika. “USHINDI WA CCM 2025 NI UHAKIKA”.
-
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Wajumbe tumeamua kwa Sauti Moja, na Sauti ya wengi ni sauti ya Mungu.
Ni Dkt. Samia Suluhu Hassan na Dkt Hussein Ally Mwinyi tena 2025. -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Tunaendelea na Mkutano Mkuu.
-
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Hongera sana Mheshimiwa Stephen Masato Wasira kwa kuchaguliwa kwa kishindo kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara. Ushindi huu ni uthibitisho wa uongozi wako imara, uzoefu wa muda mrefu, na mchango wako muhimu kwa Chama na Taifa.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Serikali imesema kuwa itaendelea kushirikiana na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), na kuhakikisha Fedha zote za maendeleo zinazotolewa na Shirika hilo zinatumika kukamilisha azma ya kukuza uchumi wa nchi.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), jijini Dodoma wakati akimuaga Kiongozi wa Timu ya Wataalam ya Shirika la Fedha la Kimataifa ( @IMFNews ) kwa Tanzania, Bw. Charalambos Tsangarides, aliyemaliza muda wake baada ya kuhudumu kwa zaidi ya miaka mitatu na nusu.
Alisema Serikali itaendelea kutekeleza dhamira yake ya kuwaletea wananchi maendeleo na kukuza uchumi kwa ujumla kupitia juhudi mbalimbali inazofanya ikiwemo kutafuta fedha za kutekeleza miradi mbalimbali ya kimkakati.
‘Kwa niaba ya Serikali ya Tanzania, napenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa kujitolea kwako katika kusaidia safari ya maendeleo ya kiuchumi ya nchi yetu, ninawahakikishia kwamba Timu yangu itawapa ushirikiano wote unaohitajika, kwa upande mwingine, nina furaha kuwajulisha kwamba tunaendelea vyema na hatua zetu za mageuzi chini ya program mpya ya Serikali ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi kupitia dirisha la Resilient and Sustainable Fund (RSF),’’ alisema Dkt. Nchemba.
Dkt. Nchemba, mbali na kumuaga Kiongozi huyo wa IMF nchini, alitumia fursa hiyo kumkaribisha Kiongozi mpya anayechukua nafasi hiyo Bw. Nicolas Blancher, huku akimuahidi ushirikiano kutoka Serikali ya Tanzania.
‘’Napenda kuchukua fursa hii kumkaribisha rasmi Bw. Nicolas Blancher, kama Kiongozi wetu mpya wa “Mission” kwa Tanzania na tunafurahi kupata nafasi ya kushuhudia mwongozo kutoka kwa mtaalamu mwingine kama tulivyofanya na Kiongozi wa “Mission”anayemaliza muda wake katika kufanikisha maendeleo yetu endelevu ya kiuchumi’’ alisema Dkt. Nchemba.
Kwa upande wake Kiongozi wa Timu ya Wataalam ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) kwa Tanzania, anayemaliza muda wake, Bw. Charalambos Tsangarides, ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano mkubwa alioupata wakati akitekeleza majukumu yake nchini.
Aidha, ameipongeza Serikali kwa juhudi za kusimamia maendeleo ya kiuchumi na kuahidi kuendelea kushirikiana na Tanzania katika kuimarisha ustawi wa wananchi wake hata baada ya kumaliza muda wake wa kuhudumu.
Naye Kiongozi Mpya wa Timu ya Wataalam ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Bw. Nicolas Blancher, ameahidi kushirikiana kikamilifu na Serikali ya Tanzania na kumhakikishia Dkt. Nchemba kuwa ataendeleza ushirikiano na kazi zilizofanywa na mtangulizi wake huku akisisitiza dhamira ya kuhakikisha malengo yaliyowekwa yanatimia. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Shirika la Maendeleo la Japan ( @jica_direct_en ), Bi. Katsura Miyakazi , jijini Dar es Salaam ambapo wamejadiliana masuala mbalimbali ya namna kuimarisha zaidi ushirikiano wa kiuchumi na kimaendeleo kati ya Tanzania na Japan kupitia JICA.
Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa pia na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Chriastian Omolo na Mkurugenzi Mkazi wa JICA Bw. Hitoshi Ara, Mhe. Dkt.Nchemba aliishukuru Japan kwa kuchangia maendeleo ya nchi kupitia ufadhili wa miradi mbalimbali ya kijamii na kiuchumi katika sekta za nishati, afya, kilimo, elimu na miundombinu ya usafiri na usafirishaji, ambapo alisema Japan kupitia JICA, imeipatia Tanzania mikopo yenye masharti nafuu yenye thamani ya dola za Marekani bilioni 1, misaada ya fedha yenye thamani ya dola za Marekani bilioni 1.2 na misaada ya kiufundi yenye thaman ya dola za Marekani bilioni 0.9, pamoja na kuwapatia mafunzo mbalimbali ya kitaalam zaidi ya wataalam 22,000 nchini Japan. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Japan zimetia Saini Hati za Mkataba wa Yen za Japan bilioni 22.742 sawa na takribani shilingi bilioni 354.45 za kitanzania kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa Uendelezaji wa kilimo vijijini unaojulikana kama “Agriculture and Rural Development Two Step Loan Project”.
Mkataba huo umetiwa saini Jijini Dar es Salaam kati ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), na Makamu wa Rais wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan ( @jica_direct_en ), Bi. Miyazaki Katsura na kushuhudiwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan, Mhe. Fujii Hisayuki, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Cosato Chumi, Balozi wa Japan nchini anayemaliza muda wake, Mhe. Yasushi Misawa, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Omolo, na viongozi wengine waandamizi wa Serikali.
Akizungumza baada ya kusaini Hati hizo za Mikataba ya mkopo huo wenye masharti nafuu, Dkt. Nchemba alisema kuwa, utekelezaji wa mradi huo utachochea ukuaji wa sekta ya kilimo kwa kuongeza uzalishaji kwa wakulima kupitia upatikanaji wa mitaji nafuu na pia itasaidia utoaji wa mikopo ya muda wa kati na mrefu kwa wakulima, vikundi vya uzalishaji, na taasisi zinazojihusisha na kilimo kwa kuziwezesha kuwekeza katika kilimo cha kisasa, kupata pembejeo bora na teknolojia ya juu ya kilimo.
Aliongeza kuwa Upatikanaji wa mitaji ya kilimo kupitia mradi huo utawawezesha pia wakulima kulima mazao mchanganyiko, na kuwa na kilimo kinachostahimili mabadiliko ya tabia nchi, ambako kutachangia usalama wa chakula, maendeleo vijijini na uimara wa uchumi kwa ujumla.
“Mradi huu unaendana na Mpango wetu wa Maendeleo wa Miaka Mitano ambao una maudhui ya kufikia ushindani na Uchumi wa viwanda kwa maendeleo ya watu ili kuongeza tija na uzalishaji kwa kutumia rasilimali zilizopo na pia unaendana na Mpango wa Pili wa Maendeleo ya Sekta ya Kilimo ambao unalenga kuimarisha na kuchochea matumizi ya zana za kisasa za kilimo, usalama wa chakula na lishe, kuwezesha upatikanaji wa masoko, na kuwezesha uongezaji wa thamani” alisema Dkt. Nchemba.
Aidha Dkt. Nchemba, alisema kuwa Tanzania imenufaika na ufadhili wa Japan kwa miaka zaidi ya 60 hasa kwenye sekta za kilimo, maji, Afya, Nishati, usafirishaji na elimu kupitia kujengewa uwezo kupitia mashirika makubwa ya kimataifa ambako Serikali ya Japan inachangia kwa ajili ya miradi mingine ya kijamii na kiuchumi.
“Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatambua na kushukuru kwa ufadhili ambao umekuwa ukitolewa na Serikali ya Japan ambao hutekelezwa na JICA, Uhusiano huu wa muda mrefu umechangia kwa kiasi kikubwa katika kuchochea ukuaji endelevu wa uchumi na kuboresha maisha ya Watanzania” alisema Dkt. Nchemba.
Kwa upande wake Makamu wa Rais wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA), Bi. Miyazaki Katsura, alisema kuwa Mradi huo unalenga kuboresha uzalishaji wa kilimo na mapato ya wakulima katika mnyororo wa thamani wa mazao manne yaliyopewa kipaumbele katika Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano wa Serikali ya Tanzania, (FYDP III), ambayo ni Mpunga, Mahindi, Ngano, na Alizeti, na kuimarisha usalama wa chakula nchini.
Bi. Katsura aliongeza kuwa, JICA imekuwa ikiweka kipaumbele katika Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (FYDP III) pamoja na Mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili (ASDP2) katika shughuli zake na itaendelea kushirikiana na Tanzania ili kuendana na Dira ya Maendeleo ya Tanzania 2025.
@tadbtz -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), amesema kuwa dola za Marekani bilioni 2.5 zilizoahidiwa kutolewa na Jamhuri ya Korea Kusini kwa Tanzania hivi karibuni, zitasaidia kutekeleza miradi muhimu ya maendeleo itakayochangia kusisimua ukuaji wa uchumi wa nchi na maisha ya Watanzania kwa ujumla.
Dkt. Nchemba amesema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Korea Kusini nchini Tanzania, Mhe. Eunju Ahn, ambapo pamoja na mambo mengine, walijadili namna ya kuimarisha zaidi ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kati ya nchi hizo mbili.
“Nchi yetu inasubiri kwa hamu kubwa utekelezaji wa miradi inayotokana na fedha hizo na hata katika Hotuba yake ya Mwisho wa Mwaka 2024, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, alielezea kwa kina namna fedha hizo zitakavyotumika kupitia utekelezaji wa miradi mbalimbali yenye lengo la kutimiza ajenda ya kitaifa ya kuwaletea watanzania Maendeleo” Alisema Dkt. Nchemba.
Alieleza kuwa makubaliano ya miradi itakayotumia fedha hizo iko katika sekta muhimu za maendeleo itakayochangia kukuza ajira, uchumi na maendeleo ya teknolojia ya Habari na Mawasiliano.
Dkt. Nchemba aliahidi kuwa Tanzania iko tayari kuongeza kasi ya ushirikiano kati ya nchi hizo ili kufanikisha malengo ya uhusiano uliodumu kwa miaka mingi kati yake na Korea kwa faida ya wananchi wa pande hizo mbili.
Kwa upande wake, Balozi wa Korea Kusini hapa nchini, Mhe. Eunje Ahn, alisema kuwa Korea inaitazama Tanzania kama mdau wake mkubwa wa maendeleo ambapo haijawahi kushuhudiwa nchi yoyote Barani Afrika ikipewa fedha nyingi kiasi cha dola za Marekani bilioni 2.5, kwa wakati mmoja kama ilivyofanyika kwa Tanzania.
Mhe. Ahn aliseza kuwa kupitia fedha hizo, Korea itaisaidia Tanzania kutekeleza miradi 12 ya kimkakati iliyowasilishwa na Serikali, ambayo inatarajiwa kukuza uchumi wa nchi kupitia miradi mbalimbali itakayotekelezwa na Serikali pamoja na Sekta Binafsi.
Alisema kuwa Korea inaiona Tanzania kuwa nchi yenye maendeleo makubwa ya kiuchumi na kijamii na kwamba muda mfupi ujao itafikia viwango vya juu vya ukuaji wa Uchumi kutokana na umahili wa usimamizi wa shughuli zake za kiuchumi ikilinganishwa na mataifa mengi ya kiafrika na ulimwengini kwa ujumla
Katika kikao chao, Mhe. Dkt. Nchemba na Balozi wa Korea Kusini nchini Tanzania, Mhe. Eunje Ahn, walijadiliana kuhusu fedha, dola bilioni 2.5 ambazo mkataba wake ulisainiwa tarehe 2 Juni, 2024 nchini Korea na kushuhudiwa na Marais wa nchi hizo mbili pamoja na kuondoa changamoto ya utozaji kodi mara mbili na ukwepaji kodi kwa kampuni zinazowekeza katika nchi hizo mbili pamoja na kuvutia uwekezaji. -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
-
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Jana nimefungua Kikao Kazi cha siku 5 kinacho Tathmini Utendaji kazi wa Nusu Mwaka wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025, kinachofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano Arusha (AICC), Jijini Arusha.
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Asante sana Comrade.
FESTO RICHARD SANGA
@festosangatz
Happy Birthday Mwalimu wangu @mwigulunchemba1 , nakuombea saana uwe na afya njema,mafanikio zaidi na kufika ndoto zako kadri mwenyezi Mungu atakavyo ruhusu.
(Photo: Was taken at Namibia State House April 2014 after the Inaguration ceremony of the late President Hon. Hage Gottfried Geingob -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Asante sana Madenge.
Ayubu Madenge
@ayubu_madenge
Sekondari alisoma Ilboru na Mazengo, Chuo akaenda UDSM akasoma Degree, Masters na PhD hapo hapo UDSM akawa mpaka Best Student wa Uchumi. Akafanya kazi Benki Kuu (BOT) kisha akaingia kwenye siasa akawa Mbunge na Waziri. Mwigulu Nchemba, Waziri wa Fedha ametimiza umri wa miaka 50.
-
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Asante sana ndugu yangu.
Gabriel Mwang'onda🇹🇿
@GMwangonda
@mwigulunchemba1 Happy Birthday Kiongozi.
-
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Asanteni sana wanachiiii
#gusaachiatwendekwao
Young Africans SC
@YoungAfricansSC
Kheri ya siku ya kuzaliwa Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba Waziri wa Fedha na Mjumbe wa Baraza la Wadhamini Young Africans SC
#timuyawananchi
#daimambelenyumamwiko -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Enock Kiswaga
@TheRealEkiswaga
Mtu mwenye humility ya hali ya juu na alie kua kisiasa sana Happy birthday @mwigulunchemba1 Mungu aendeleee kukulinda...Endeleaa kushusha dola mpaka ifike buku😀😀😀. Enjoy your birthday Mamba mwenyewe💪🏿💪🏿💪🏿 Endeleaa kumtumainia Mungu. Mbele ipo Sawa🌚🟢 Kikubwa hatujakutana Bara barani😀😀😀
-
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Namshukuru Mungu kwa Afya na kwa kuongeza mwaka mwingine wa kuendelea kuishi ili nilitimize kusudi lake la kunileta duniani na kulitumikia Taifa langu.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mheshimiwa Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), ameipongeza Mamlaka ya Mapato Tanzania @TRATanzania kwa kuongeza makusanyo ya kodi kutoka sh. trilioni 22.2 mwaka wa fedha 2021/22 hadi kufikia sh. tril. 27.6 mwaka wa fedha 2023/2024 na kuvunja rekodi ya kukusanya sh. trilioni 16.528 katika kipindi cha Nusu Mwaka wa Fedha 2024/2025 kinachoanzia Julai hadi Desemba Mwaka 2024.
Dkt. Nchemba alitoa pongezi hizo, wakati akifungua Kikao Kazi cha siku 5 kinacho Tathmini Utendaji kazi wa Nusu Mwaka wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025, kinachofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano Arusha (AICC), Jijini Arusha.
Alisema kuwa fedha hizo zimeisaidia Serikali kutekeleza miradi ya kimkakati inayolenga kuboresha huduma za jamii kama vile Bwawa la Kuzalisha Umeme la Julius Nyerere, Mradi wa Treni iendayo kasi (SGR), miundombinu ya barabara, huduma za jamii na mingine mengi
Dkt. Nchemba aliitaka TRA kuimarisha zaidi mifumo ya kisasa ya kielektroniki ya kukusanya mapato ya Serikali ili kuongeza uwazi, tija na ufanisi kwa kukusanya mapato pamoja na kuziba mianya ya maafisa wa TRA kukutana uso kwa uso na walipakodi.
Aidha, Dkt. Nchemba alirejea wito wake kwa Mamlaka hiyo kutofunga biashara za watu wanaowadai kodi badala yake waweke utaratibu wa kuzilea biashara hizo huku wakihakikisha kodi stahiki zinalipwa na wahusika kwa kuwa vitendo vya kufunga biashara vinaathiri uchumi wa nchi pamoja na kuvuruga mfumo wa biashara husika na kuwasababishia watu umasikini na kuwakosesha wananchi ajira.
Dkt. Nchemba alitumia wasaa huo pia kuwataka wafanyabiashara kuacha tabia ya kukwepa kulipa kodi, kutumia ipasavyo mashine za kukusanya mapato ya Serikali (EFDs) na kuwahimiza watoe risiti halali zinazoendana na thamani ya manunuzi yaliyofanyika huku wananchi kwa upande wao wakihimizwa kudai risiti halali wanaponunua bidhaa na huduma mbalimbali.
Kwa upande wake, Kamisha Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, Bw. Yusuph Juma Mwenda, alisema kuwa Kikao kazi hicho, pamoja na mambo mengine, kilikuwa na malengo kadhaa ya kuimarisha ukusanyaji wa kodi ili kufikia malengo waliyowekewa na Serikali ya kukusanya shilingi trilioni 30.449 katika Mwaka wa Fedha 2024/2025.
Alimhakikishia Mhe. Waziri wa Fedha, kwamba Mamlaka hiyo itafikia malengo hayo na pengine kuzidi kidogo kutokana na viashiria vya ukusanyaji mapato katika kipindi cha Nusu Mwaka wa Fedha 2024/2025 ambapo hadi kufikia Desemba mwaka 2024, TRA imekusanya sh. trilioni 16.528, ikilinganishwa na makusanyo ya sh. trilioni 9.242, ya kipindi kama hicho Mwaka 2020/2021, ikiwa ni ongezeko la asilimia 78.78.
Bw. Mwenda alisema kuwa mafanikio hayo yanatokana na TRA kuendelea kuhamasisha ulipaji kodi wa hiari, kuwasikiliza walipakodi na kutatua changamoto zao hatua iliyochangia kukua kwa uhusiano kati ya Mamlaka na walipakodi hususan kupitia viongozi wa vyama vya wafanyabiashara wote nchini wanaoendelea kuunga mkono kwa vitendo juhudi zinazofanywa na Serikali baada ya maelekezo ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuboresha mazingira ya biashara na ulipajikodi nchini.
Aliwahimiza watumishi wa TRA kuendelea kufanyakazi kwa bidii, juhudi na maarifa ili kufanikisha malengo ya Serikali ya kukusanya mapato yake kupitia kodi mbalimbali pamoja na kuzingatia weledi wanapotekeleza majukumu yao wakati Serikali kwa upande wake ikiendelea kuwajengea mazingira mazuri ya kufanya kazi. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), ameshiriki mkutano wa Kamati ya Barabara ya Mkoa wa Arusha na kuahidi kuwa Serikali itaongeza kasi ya mtiririko wa utoaji fedha kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya miundombinu ya Barabara nchini ukiwemo mkoa wa Arusha hususan kwenye miradi ambayo iko katika hatua mbalimbali za ukamilishwaji ili kuchochea kasi ya uchukuzi wa bidhaa na watu, hatua ambayo amesema itachangia ukuaji wa kipato kwa wananchi na uchumi wa nchi kwa ujumla.
Ahadi hiyo inafuatia maombi maalumu yaliyowasilishwa katika Mkutano huo na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Paul Makonda, ambaye alisisitiza umuhimu wa Serikali kuupa mkoa huo kipaumbele katika kuboresha miundombinu yake ya Barabara kutokana na umuhimu wake katika kuchangia mapato ya Serikali hususan katika sekta ya utalii. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), akiambatana na Waziri wa Ujenzi, Mhe. Abdallah Ulega, wakiwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Paul Makonda, walipomtembelea Ofisini kwake jijini Arusha, walipofanya ziara ya kikazi mkoani humo.
Katika ziara hiyo, Mhe. Dkt. Nchemba na Mhe. Ulega, walishiriki mkutano maalum wa Kamati ya Barabara ya Mkoa wa Arusha uliowashirikisha wadau wengine mbalimbali wakiwemo wabunge wa mkoa huo, ambapo walijadili namna va upatikanaji wa fedha kwa ajili ya kuimarisha miundombinu ya Barabara mkoani Arusha ambao ni mkoa wa kitalii na unachangia wa kiasi kikubwa uchumi wa nchi kutokana na mapato yanayotokana na sekta mbalimbali za uzalishaji hususan utalii.
@WizarayaUJ -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Nawatakia nyote heri ya Mwaka Mpya 2025.
-
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Heri ya Sikukuu ya Krismasi kwenu nyote. Tusherehekee kwa amani na utulivu, tukishirikiana kile tulichonacho na kuwasaidia wasiojiweza.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Bank of Tanzania
@BankOfTanzania
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), ameikaribisha Saudi Arabia kuwekeza Tanzania katika fursa mbalimbali zikiwemo utalii, kilimo, madini, uendelezaji wa miundombinu pamoja na uchumi wa buluu.
Dkt. Nchemba alitoa mwaliko huo alipokutana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri wa Wizara ya Uchumi na Mipango wa Saudi Arabia, Eng. Ammar Naqadi, Kando ya Mkutano wa Jukwaa la Biashara na Uwekezaji, lililoandaliwa na Ubalozi wa Tanzania, kwa kushirikiana na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na Shirika la Kuendeleza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA), lililofanyika hivi karibuni Mjini Riyadh nchini Saudi Arabia.
Alibainisha kuwa Tanzania inaendelea na mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) ambapo imeshakamilika kipande kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma na ujenzi unaendelea kwa vipande vinavyoelekea Mwanza na DRC kupitia Burundi hivyo ni fursa kwa Saudi Arabia kuwekeza katika miundombinu hiyo ambayo itachochea ukuaji wa bishara kati ya Saudi Arabia, Tanzania na nchi za Afrika Mashariki.
‘‘Bado tunakusanya rasilimali tunatamani wewe na taasisi yako kuona namna ambavyo tunaweza kushirikiana katika ujenzi na uendeshaji wa mradi huu wa reli ya kisasa ambao utahusisha na sekta binafsi ikiwemo katika usafirishaji wa mizigo na safari za kila siku’’, alieleza Dkt. Nchemba.
Aidha, Dkt. Nchemba alieleza kuwa Tanzania ina fursa katika sekta ya kilimo ambapo ina ardhi ya kutosha na yenye rutuba kuweza kuzalisha mazao ya aina mbalimbali kwa wingi hivyo ni vema Saudi Arabia ikatazama fursa katika sekta hiyo muhimu.
‘’Tunaweza kushirikiana katika kilimo ikiwemo usalishaji wa ngano, mafuta ya kupikia pia tuna ranchi ambazo zinaweza kutumika kuzalisha nyama za kutosha na hivyo kupata mazao na bidhaa za kusafirisha nje ya nchi jambo litakalotunafaisha sisi pamoja na ninyi pia’’, alifafanua Dkt. Nchemba.
Aliongeza kuwa Tanzania pia ina aina ya madini ambayo yanapatikana Tanzania tu hivyo hiyo ni fursa muhimu kwa Saudi Arabia kuweza kushirikiana na Tanzania kuwekeza katika sekta hiyo kwa kujenga viwanda vya kuchakata madini ili kuyaongezea thamani.
Uwekezaji huo utawezesha kubadilishana uzoefu na Saudi Arabia wa rasilimali watu pamoja na teknolojia itakayoisaidia Tanzania katika kupiga hatua ya maendeleo ya kiuchumi haraka zaidi.
Naye Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Zanzibar, Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum, alisema kuwa Zanzibar ina fursa zinazoweza kutumiwa na Saudi Arabia ikiwemo sekta ya utalii wa fukwe za asili zilizopo Zanzibar, fursa ya uvuvi wa kina kirefu na uchakataji wa mazao ya uvuvi pamoja na uwepo wa vyanzo vya gesi na mafuta vilivyogunduliwa ni fursa muhimu kwa Saudi Arabia kutokana na uzoefu wake katika sekta hiyo.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Uchumi na Mipango wa Saudi Arabia, Eng. Ammar Naqadi, alisema kuwa Saudi Arabia iko tayari kushirikiana na Tanzania katika uendelezaji wa miundombinu ya reli ili kurahisha usafirishaji wa watu, mazao na mizigo ili kuchochochea ukuaji wa biashara ambapo ushiriki wa sekta binafsi ni muhimu katika kufanikisha biashara kati ya nchi hizo mbili.
Alisema nchi hiyo iko tayari kushirikiano na Tanzania katika fursa za kuendeleza sekta ya madini, kilimo, mafuta na gesi, utalii, uchakataji wa mazo ya bahari miundombinu pamoja na utalii ambapo wataandaa timu ya wataalamu kwa kushirikiana na Sekta binafsi kutembelea Tanzania kujionea fursa za uwekezaji katika sekta hizo ili kujiridhisha na mazingira ya fursa za Tanzania ili kuweza kuwekeza.
Alisisitiza kuwa katika kufanikisha ukuaji wa biashara baina ya Tanzania na Saudi Arabia suala la utozaji kodi mara mbili ni muhimu kufanyiwa kazi ili kuwawezesha wafanyabiashara kutopata changamoto wafanyapo biashara kati ya pande hizo.
Katika kikao hicho Dkt. Nchemba aliambatana na Mawaziri wenzake wawili, akiwemo Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani Jafo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Zanzibar, Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, Mhe. Dkt. Moh’d Juma Abdalla. -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Nimefanya ziara ya kikazi nchini Oman na Saudi Arabia, ambako tumefanya mazungumzo na viongozi waandamizi wa nchi hizo kuhusu kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kimaendeleo.
Nchini Oman, tumesaini Mkataba wa Kuondoa Utozaji Kodi ya Mapato Mara Mbili, hatua hiyo inalenga kuboresha na kurahisisha shughuli za kibiashara, kuvutia uwekezaji kati ya Tanzania na Oman na kupanua fursa za kiuchumi hasa katika sekta za viwanda na uzalishaji. Kusainiwa kwa mkataba huu ni hatua muhimu katika jitihada za Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, za kufungua uchumi wa nchi kwa kuvutia uwekezaji wa kimataifa.
Nchini Saudi Arabia, nimeshiriki katika Jukwaa la Biashara na Uwekezaji lililoandaliwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia kwa kushirikiana na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na Kituo cha Kuendeleza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA), lilichofanyika makao makuu ya Chemba ya Wafanyabiashara ya Riyadh. Vilevile, tumefanya mazungumzo na viongozi waandamizi wa Saudi Arabia kuhusu kuimarisha ushirikiano katika sekta za maji, afya, nishati, na miundombinu.
Ziara hii ni hatua muhimu katika kufungua fursa za kiuchumi na kukuza ushirikiano wa kimaendeleo kati ya Tanzania na mataifa hayo mawili.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), ameongoza ujumbe wa Mawaziri wenzake akiwemo Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe., Dkt. Selemani Jafo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Zanzibar, Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum, kutembelea Mfuko wa Maendeleo wa Saudi Arabia ( @SaudiFund_Dev -SFD), Mjini Riyadh nchini Saudi Arabia, ambapo walizungumza na Mwenyeji wao, Mkurugenzi Mtendaji wa Saudi Fund, Bw. Sultan Al-Marshad, na kujadili kwa kina masuala ya ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kati ya Mfuko huo na Tanzania.
Mhe. Dkt. Nchemba, aliishukuru Saudi Arabia kupitia Mfuko huo kwa kuchangia maendeleo ya Tanzania katika sekta za maji, afya, nishati na ujenzi wa miundombinu ya barabara, ikiwemo ukarabati wa Mradi wa Maji mkoani Mara (USD 15m), Ujenzi wa Mradi wa Maji wa Same-Mwanga-Korogwe (USD 25m), ujenzi wa Barabara za Vijijini Awamu ya Pili-Zanzibar (USD 11.4m), Ukarabati na Upanuzi wa Hospitali ya Mnazi Mmoja-Zanzibar (USD 15m) na kushirikiana na wadu wengine kufadhili Mradi wa Ujenzi wa Njia ya Umeme wa msongo wa 220kV kuanzia Benako mkoani Kagera hadi Kyaka (USD 105.4m).
Mazungumzo hayo pia yalishuhudiwa na Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, Mhe. Moh’d Juma Abdalla, Mkuu wa Idara Mashariki na Kati Mhe. Balozi Abdalah Abasi Kilima, Kamishna wa Idara ya Madeni-Wizara ya Fedha, Bw. Japhet Justine na Kaimu Kamishna wa Idara ya Fedha za Nje, Bw. Robert Mtengule. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
الصندوق السعودي للتنمية
@SaudiFund_Dev
#الرياض | استقبل سعادة الرئيس التنفيذي لـ #الصندوق_السعودي_للتنمية أ.سلطان المرشد، في مقر الصندوق اليوم؛ معالي وزير المالية في جمهورية تنزانيا الاتحادية، د.مويجولو لاميك نتشيمبا، والوفد المرافق من أصحاب المعالي والسعادة. وجرى خلال اللقاء؛ مناقشة سبل تعزيز التعاون التنموي لتمويل القطاعات الحيوية في #تنزانيا.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Japhet Justine
@JaphetSayi
“… Economic growth has gained momentum, with real GDP growth picking up to 5.4 percent
(year-on-year) in the first half of 2024, from 5.1 percent in 2023. Inflation remains within the
central bank’s target and a growth-friendly fiscal consolidation is underway. The current
account deficit narrowed in FY2023/24, driven by strong exports of services and a slowdown
in imports. Pressures in the foreign exchange market have eased, reflecting seasonal current
account flows, a tight monetary policy stance, and exchange rate flexibility ….” 👏🏽👏🏽👏🏽 -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Japhet Justine
@JaphetSayi
Just Published - IMF Staff Report on Tanzania dated 13 Dec, 2024
Enjoy
www.imf.org/-/media/Files/Publications/CR/2024/English/1t… -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
الصندوق السعودي للتنمية
@SaudiFund_Dev
#riyadh | #sfd CEO Mr. Sultan Al-Marshad, received today the Minister of Finance of the United Republic of Tanzania, H.E Dr. @mwigulunchemba1 and his accompanying delegation. During their meeting, ways to enhance development cooperation to support vital sectors in Tanzania were discussed.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), akiwa miongoni mwa Mawaziri wa Kisekta walioshiriki Jukwaa la Biashara na Uwekezaji lililoandaliwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia kwa kushirikiana na Kituo cha Uwekezaji Tanzania TIC na Kituo cha kuendeleza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA), lililofanyika makao Makuu ya Chemba ya Wafanyabiashara yalipo Riyadh nchini Saudi Arabia, ambapo Mgeni Rasmi katika ufunguzi wa Jukwaa hilo alikuwa waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo.
Jukwaa hilo limewaleta pamoja wafanyabiashara wa Tanzania na Saudi Arabia, ambapo kwa siku kadhaa, watapata nafasi ya kujadiliana kuhusu fursa za uwekezaji zinazopatikana katika nchi hizo mbili ili kukuza biashara na uwekezaji, hatua ambayo lengo lake ni kuinua na kukuza zaidi uchumi wa nchi hizo mbili.
Akifungua Jukwaa hilo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo, alisema kuwa licha ya ushirikiano na uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo kudumu kwa zaidi ya miaka 40, kiwango cha biashara (mauzo) kati ya Tanzania na Saudi Arabia kiko chini na kimekuwa kikiunufaisha upande mmoja wa Saudi Arabia, ambapo wakati mauzo ya nje ya Saudi Arabia nchini Tanzania yakifikia dola za marekani bilioni 52.3, Tanzania imeiuzia nchi hiyo bidhaa zenye thamani ya dola milioni 12.3 pekee.
Alitoa wito kwa kampuni za Saudi Arabia kwa kushirikiana na wenzao wa Tanzania, kuongeza uwekezaji na kiwango cha biashara kati ya nchi hizo mbili kwa kutumia fursa za kiuchumi na mazingira bora ya uwekezaji yaliyopo hivi sasa nchini Tanzania kuwekeza mitaji ili kunufaika na soko kubwa linalipatikana nchini Tanzania na nchi jirani hususan katika sekta za kilimo, usindikaji bidhaa za kilimo, nishati ya kijani, uchumi wa buluu, madini, mafuta na gesi pamoja na masuala ya kidigitali. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), akipokea zawadi kutoka kwa Makamu Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara, Riyadh, nchini Saudi Arabia, Bw. Ajian Saad Al-jlan, kwa kutambua mchango wake katika kukuza biashara na masuala ya uwekezaji nchini Tanzania, kupitia wadhifa wake wa Waziri wa Fedha. Tukio hilo limefanyika wakati wa ufunguzi wa Jukwaa la Biashara na Uwekezaji na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, Jukwaa lililoandaliwa na Serikali kupitia Ubalozi wa Tanzania nchini humo, likiwa na lengo la kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo Tanzania kwa jumuiya ya wafanyabiashara wa Saudi Arabia ili kuvutia mitaji na teknolojia vitakavyochochea ukuaji wa uchumi na kukuza kipato kwa wananchi na taifa kwa ujumla.
Mawaziri wengine waliotunukiwa zawadi hizo ni Prof. Kitila Mkumbo, Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Suleiman Jafo, Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde, Waziri wa Nchi Ofisi ya rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji-Zanzibar, Mhe. Shariff Ali Shariff na Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Fatma Rajab
@FatmaRajab13
I witnessed the signing ceremony of the Double Taxation Treaty (DTA) 🇹🇿 and 🇴🇲 held in Muscat at Oman Tax Authority Office on 15th December 2024. Hon. Mwigulu Nchemba Min. Of Finance from 🇹🇿 and H.E Nasser Khamis Al Jamshi Chairman of Oman Tax Authority exchanged the documents.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), amehitimisha ziara yake ya siku mbili nchini Oman ambapo akiwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Muscat – Oman, akielekea nchini Saudi Arabia ambako atakuwa na ziara nyingine ya kikazi, aliagwa na Mhe. Balozi wa Tanzania nchini humo, Mhe. Fatma Rajab.
Akiwa nchini Oman, pamoja na mambo mengine, Mhe. Dkt. Nchemba alitia saini Mkataba wa Kuondoa Utozaji Kodi ya Mapato Mara Mbili na Kuzuia Ukwepaji Kodi, ujulikanao kama An Agreement for the Elimination of Double Taxation with Respect to Taxes on Income and Prevention of Tax Avoidance and Evasion, wenye lengo la kukuza biashara na uwekezaji kati ya nchi hizo mbili.
Aidha, Mhe. Dkt. Nchemba, amewasili nchini Saudi Arabia kwa ajili ya kushiriki katika Jukwaa la Biashara na Uwekezaji, linalotarajiwa kufanyika katika Makao Makuu ya Chemba ya Biashara Riyadh, Saudi Arabia. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
جهاز الضرائب - سلطنة عُمان
@omantax
وقّعت سلطنة عُمان وجمهورية تنزانيا المتحدة في مسقط اليوم اتفاقية "إزالة الازدواج الضريبي بالنسبة للضرائب على الدخل ومنع التهرب من الضرائب" وذلك بهدف توفير بيئة استثمارية جاذبة، وحماية المستثمرين من فرض ضرائب مزدوجة، وتعزيز الشفافية في المعاملات المالية بين البلدين
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
جهاز الضرائب - سلطنة عُمان
@omantax
The Sultanate of Oman and United Republic of Tanzania signed an agreement on "the Avoidance of Double Taxation and the Prevention of Fiscal Evasion with respect to Taxes on Income" today in Muscat
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
صحيفة وهج الخليج
@wagulf
#وهج_الخليج | سلطنة #عُمان وجمهورية #تنزانيا توقعان على اتفاقية إزالة الازدواج الضريبي
@omantax
www.wa-gulf.com/1121713 -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Kisultan ya Oman, zimetia saini Mkataba wa Kuondoa Utozaji Kodi ya Mapato Mara Mbili na Kuzuia Ukwepaji Kodi, ujulikanao kama Agreement for the Elimination of Double Taxation with Respect to Taxes on Income and Prevention of Tax Avoidance and Evasion.
Mkataba huo umesainiwa Mjini Mascut nchini Oman na Waziri wa Fedha wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), na Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mapato ya Oman, Bw. Nasser Al-Jashmi.
Mhe. Dkt. Nchemba amesema kuwa kusainiwa kwa mkataba huo ni hatua muhimu katika jitihada za Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, za kufungua uchumi wa nchi kwa kuvutia uwekezaji wa kimataifa.
Ameongeza kuwa Mkataba huo utawezesha wawekezaji na wafanyabiashara wanaofanya shughuli kati ya Tanzania na Oman kutozwa kodi mara moja pekee, badala ya kutozwa mara mbili kwa mapato ya aina moja, hali ambayo awali ilikuwa ikikwaza ustawi wa biashara kwa pande zote mbili.
Mkataba huo pia unalenga kuvutia mitaji mikubwa kutoka Oman kuja kuwekeza Tanzania, hususan kupitia kampuni kubwa zinazomilikiwa na familia za kifalme, sambamba na wawekezaji binafsi ambapo kupitia uwekezaji huo, Tanzania inatarajia kunufaika na ukuaji wa sekta za uzalishaji, maendeleo ya viwanda, na kuongezeka kwa ajira kwa wananchi.
Aidha, wawekezaji wa Kitanzania sasa wataweza kuwekeza Oman bila vizuizi vya kikodi, huku wakilindwa na mkataba huo ili kuepusha kulipishwa kodi mara mbili.
Hatua hiyo pia inatoa fursa kwa wafanyabiashara wa Tanzania kupanua shughuli zao katika masoko ya kimataifa, hasa katika ukanda wa Ghuba.
Kwa ujumla, Mheshimiwa Dkt. Nchemba amesema kuwa mkataba huo unatarajiwa kufungua ukurasa mpya wa ushirikiano wa kiuchumi kati ya Tanzania na Oman, huku Oman ikivutiwa zaidi na fursa za uwekezaji nchini Tanzania kutokana na jiografia yake ya kimkakati, vivutio vyake vya kiuchumi, na mazingira bora ya uwekezaji ikilinganishwa na nchi nyingine za Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb) akizungumza na watumishi wa Ubalozi wa Tanzania Muscat- Oman na wadau wengine katika Makazi ya Balozi wa Tanzania nchini Oman, Mhe. Fatma Rajab, ambapo Mhe. Dkt. Nchemba yuko nchini humo kwa ziara ya kikazi. Amempongeza Mhe. Balozi Fatma Rajab kwa kazi kubwa na njema ya kueneza diplomasia ya kiuchumi nchini humo kwa mafanikio makubwa.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), akizungumza katika kikao kifupi na Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mapato ya Oman, Bw. Nasser Khamis Al-Jashmir, kuhusu namna ya kuimarisha ushirikiano kati ya Oman na Tanzania katika eneo la kodi ili kurahisisha ufanyaji biashara kwa faida ya nchi hizo mbili. Mhe. Dkt. Nchemba yuko katika ziara ya kikazi Muscat nchini Oman. Mazungumzo hayo yalimshirikisha pia Balozi wa Tanzania nchini Oman, Mhe. Fatma Rajab na Mkurugenzi Mtendaji wa Mipango na Sera za Kodi katika Mamlaka ya Kodi-Oman, Bw. Hamed Al-Hashmi.
-
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Sincere gratitude goes to Her Excellency, Dr. Samia Suluhu Hassan, for her steadfast leadership, providing clear guidance and direction that has made these achievements possible.
Pope Mwita I
@EJ_Mwita
Congratulations! We are incredibly proud of you. Your friend @mwigulunchemba1 has made remarkable strides in stabilizing the Tanzanian Shilling, successfully reducing the national debt by TZS 6 trillion.
This impressive feat saw the exchange rate improve from 2800 to 2300 in just four months, showcasing exemplary leadership and economic acumen. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Haki Ngowi
@Hakingowi
📍Dar es Salaam
▪️BENKI YA DUNIA YAIPONGEZA TANZANIA MRADI WA SGR
Benki ya Dunia imeshangazwa na hatua kubwa iliyofikiwa na Serikali katika kutekeleza Mradi wa Kimkakati wa Reli ya Kisasa wa SGR, na kuahidi kuwa itaweka mkono wake kusaidia ujenzi wa Reli hiyo muhimu kwa kukuza biashara na ukuaji wa uchumi wa nchi.
Kauli hiyo imetolewa Jijini Dar es Salaam, na Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika wa Benki ya Dunia anayesimamia Ujenzi wa Miundombinu, Bi. Wendy Hughes, aliyepo nchini kwa ziara ya kikazi, alipokutana na kufanya mazungumzo na Mawaziri watatu wa Kisekta, wakiongozwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa na Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. Abdallah Ulega.
Bi. Hughes aliyeambatana na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia, Bw. Nathan Belete na Viongozi wengine waandamizi wa Benki hiyo, alisema kuwa amesafiri kwa kutumia reli hiyo kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma na kushangazwa na kiwango cha ubora wake wa viwango vya kimataifa.
Alisema kuwa Benki ya Dunia inaendelea kuchakata maombi yaliyowasilishwa na Serikali katika Benki hiyo, na kwamba iko tayari kusaidia ujenzi wa Reli hiyo ya Kimkakati na kushauri pia sekta binafsi ishirikishwe kikamilifu kuhakikisha kuwa malengo ya kuanzishwa kwa mradi huo yanafikiwa kwa ufanisi mkubwa.
Wakizungumza katika kikao hicho kuhusu Mradi wa SGR, Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, na Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Profesa Makame Mbarawa, waliishukuru Benki ya Dunia kwa kuamua kutoa fedha za kujenga mradi huo ambao umefikia hatua mbalimbali za ujenzi na ni mfano Barani Afrika na Duniani kwa ujumla
Walieleza kuwa Mradi wa SGR unaogharimu zaidi ya shilingi trilioni 10 za Tanzania, ni muhimu katika kuimarisha biashara na usafirishaji wa abiria na mizigo si tu kwa Tanzania, bali katika nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu, ambapo biashara kati ya nchi hizo inatarajiwa kuongezeka na kusaidia kutatua tatizo la ajira kwa wananchi.
Mkutano huo uliowashirikisha Wakuu wa Taasisi katika Sekta ya Usafirishaji na Ujenzi, ulikuwa na ajenda tatu ikiwemo ujenzi wa Mradi wa Mabasi yaendayo haraka Jijini Dar es Salaam-BRT, Mradi wa Reli kwa Kiwango cha Kimataifa-SGR na namna ya kuimarisha ushirikiano katika kutekeleza miradi kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi-PPP.
📃:Wizara ya Fedha
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, akilakiana na Mkurugenzi wa benki ya Dunia, anayesimamia Miundombinu, Bi. Wendy Hughes, alipofanya ziara ya kikazi nchini, ambapo Mkurugenzi huyo alikutana na kufanya mazungumzo na Mawaziri watatu wa Kisekta, akiwemo Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa na Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. Abdallah Ulega, ambapo walijadili kuhusu Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka-BRT, Ujenzi wa Mradi wa Treni ya Mwendo Kasi (SGR), na namna ya kuiwezesha sekta binafsi kwa kushirikiana na Sekta ya Umma kushiriki katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
📸:Wizara ya Fedha -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Serikali ya Tanzania na Benki ya Dunia (WB) wamesaini mikataba miwili (2) yenye thamani ya dola za Marekani milioni 104, sawa na takriban shilingi bilioni 248, kwa ajili ya kusaidia utekelezaji wa Mradi wa Kukuza Usawa wa Kijinsia nchini Tanzania, maarufu kama “PAMOJA”.
Hafla ya utiaji saini wa mikataba hiyo imefanyika jijini Dar es Salam kati ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) kwa niaba ya Serikali na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia, Bw. Nathan Belete.
Akifafanua kuhusu mikataba hiyo, Mhe. Dkt. Nchemba alisema kuwa mkataba wa dola za Marekani milioni 4, sawa na zaidi ya shilingi bilioni 9.5 ni msaada na Mkataba wa dola za Marekani milioni 100, sawa na zaidi ya shilingi bilioni 238 ni mkopo wenye masharti nafuu.
Alisema mradi wa PAMOJA uliosainiwa utasaidia kuongeza upatikanaji wa fursa za kiuchumi kwa wanawake pamoja na huduma za kuzuia na kukabiliana na ukatili wa kijinsia Tanzania Bara na Zanzibar.
‘’Hili litatimizwa kupitia uimarishaji vikundi vya wanawake kwa kuwajengea ujuzi wa biashara na kuwaunganisha na fursa za masoko, kuongeza fursa za mikopo nafuu kwa vikundi vya wanawake, kuwaongezea upatikanaji wa huduma za kifedha kupitia mifumo rasmi ya kifedha pamoja na kuimarisha huduma za kukabiliana na ukatili wa kijinsia”, alifafanua Mhe. Dkt. Nchemba,
Alisema mradi huo utawanufaisha moja kwa moja wanawake wapatao 319,850 na walengwa wengine 399,000, wakiwemo wanafamilia za wanufaika.
Alisistiza kuwa kukuza usawa wa kijinsia si suala la wanawake pekee bali ni msingi wa Taifa la kidemokrasia, lenye haki na linalostawi na kuongeza kuwa kuondoa tofauti za kijinsia kunaboresha uzalishaji na kuimarisha uhimilivu wa kiuchumi.
“Mradi wa PAMOJA ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango wa Tatu wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano wa Taifa 2021/22 - 2025/26, Rasimu ya Dira ya Maendeleo ya 2050 na pia ni sehemu ya ajenda kuu ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye amelipa kipaumbele suala la usawa wa kijinsia”, alisema Mhe. Dkt. Nchemba.
Alisema utekelezaji wa mradi huo ni ushahidi wa dhamira ya Serikaliya kufanikisha Malengo ya Maendeleo Endelevu (hususan Lengo la 5) na kuonesha nia thabiti ya kufanikisha ukuaji wa uchumi unaowajumuisha wote.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania, Bw. Nathan Belete, alisema kuwa mradi huo utatatua changamoto za kijinsia za kijamii na kiuchumi kwa kuwawezesha wanawake kiuchumi na kubainisha mila potofu ili kukabiliana na ukatili wa kijinsia.
Aliiomba Serikali kuzikutanisha pamoja Wizara zote za kisekta zinazohusika katika utekelezaji wa mradi huo kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazowakabili wanawake na Watoto.
Alisema wanatarajia mradi huo utaanza kutekelezwa mapema na kuona matokeo ya utekelezaji pamoja na faida watakazo zipata walengwa wa mradi huo.
Kwa upande wa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima (Mb), alimpongeza Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa jitihada mbalimbali anazofanya kuwainua wanawake kiuchumi ikiwemo kuwezesha upatikanaji wa fedha kwa ajili ya mradi wa PAMOJA.
Alisema katika hatua za awali za utekelezaji wa mradi huo, Wizara yake imeshazindua Sera ya Taifa ya Jinsia na Maendeleo ya Wanawake pamoja na Mkakati wake ambao uwezeshaji wanawake kiuchumi ni miongoni mwa malengo yake.
Alisema mradi huo umekusudia kujenga nyumba salama 10 kwa ajili ya kuwahifadhi Watoto wanaokumbana na ukatili wa kijinsia pamoja na kujenga vituo 200 vya malezi salama na makuzi ambapo vituo 184 vitakuwa Tanzania Bara na 16 vitajengwa Zanziber.
“Afisa Ustawi wa Jamii na Maendeleo ya Jamii wamekuwa wakihangaika kupata ofisi za kufanyiakazi na kutoa huduma pamoja na vifaa kazi ikiwemo usafiri, sasa kwa kutumia fedha hizi watapata Ofisi 40 za maafisa Maendeleo ya Jamii na Ofisi 40 za Maafisa Ustawi wa Jamii”, alifafanua Mhe. Dkt. Ngwajima.
Alisema fedha hizo zitasaidia kuwachangamsha wanawake kiuchumi, kupata elimu ya kibiashara, mitaji pamoja na kufanya biashara wakiwa na uelewa mpana kwa sababu wataalam wamewezeshwa kuwafikia popote walipo.
Aliahidi kuhakikisha fedha hizo zitatumika kikamilifu kwenye mradi iliyokusudiwa na kuleta matokeo Chanya. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII
@maendeleoyajami
#matukiokatikapicha
Zoezi la utiaji saini wa mkopo kati ya Serikali ya Tanzania na Benki ya Dunia @WorldBank @WBTanzania wenye thamani ya Dola za Kimarekani Milioni 100 na Msaada Dola za Kimarekani Milioni 4 ili kutekeleza Mradi unaojulikana kwa jina la PAMOJA unaolenga kuwawezesha Wanawake Kiuchumi na kutokomeza Ukatili wa Kijinsia lililofanyika Desemba 12, 2024 jijini Dar Es Salaam.
Waziri wa @mofURT Mhe. @mwigulunchemba1 ametia saini mkopo huo kwa niaba ya Serikali na kushuhudiwa na Waziri wa @maendeleoyajami Mhe. @Dr_DGwajima na Viongozi wengine kutoka Wizara ya @maendeleoyajami na Wizara ya @mofURT na Wawakilishi kutoka @WBTanzania -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb) na Viongozi wengine waandamizi wa Serikali wameshiriki hafla ya uzinduzi wa Rasimu ya Kwanza ya Dira ya Taifa ya Maendeleo iliyofanyika Visiwani, Zanzibar, leo tarehe 11 Desemba 2024.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Kenny Mmari Snr.
@KennedyMmari
USD haijaanguka, TZS ndiyo inaimarika. Nimesisitiza hili kuwa sarafu nyingi tu duniani zinaendelea kuanguka dhidi ya USD ikiwamo Euro, Rupee, Ruble, RMB na kadhalika.
Mafuta yameshuka bei kufikia dola 72 kwa pipa moja kwenye soko la dunia, na pengine yatashuka zaidi katika bei ya rejareja kwenye miezi michache ijayo. Mafuta yakishuka, mara nyingi huakisi kwenye bei ya bidhaa hivyo mfumuko wa bei huimarika. Hata hivyo, takwimu zinaonesha mfumuko wa bei kwa Tanzania upo imara, chini ya asilimia 4 kwa kipindi kirefu sasa.
𝗠𝗧𝗔𝗔𝗟𝗔𝗠𝗨🌐
@LudoFredrick
Ndugu mchambuzi @KennedyMmari je, anguko hili la USD tutarajie kushuka kwa bei ya mafuta na bidhaa nyingine?
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Kenny Mmari Snr.
@KennedyMmari
The Tanzanian shilling is bouncing back hard against the US dollar.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), amezindua Jukwaa la kwanza la Wadau wa Sekta ya Fedha kwa mwaka 2024, katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam, Jukwaa litakalotumiwa na wadau kujadili fursa na hatua mbalimbali za kuboresha Sekta ya Fedha ikiwa ni pamoja na huduma ujumuishaji na endelevu za kifedha kwa njia ya kidigitali pamoja na kushirikishana namna bora ya kukuza matumizi ya teknolojia na uvumbuzi ili kukuza na kuimarisha Sekta ya Fedha nchini.
Jukwaa hilo limewakutanisha wadau mbalimbali wa Sekta ya Fedha kutoka Sekta za Umma na Binafsi wakiwemo kutoka benki na taasisi za fedha, kampuni za bima, vyama mwavuli vya sekta ya fedha, vyama vya ushirika wa akiba na mikopo, vikundi vya kijamii vya huduma ndogo za fedha.
Jukwaa hilo limehudhuriwa pia na Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Adolf Mkenda, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bi. Sauda Msemo na Mkurugenzi wa Hifadhi ya Jamii kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Bw. Festo Fute.
Akizungumza katika Hafla hiyo, Mhe. Dkt. Nchemba aliwahimiza wafanyabiashara na Wananchi kwa ujumla kuweka fedha zao Benki na kwamba Mamlaka ya Mapato Tanzania imeelekezwa na Mhe. Rais kutofunga akaunti za wateja wanaowadai kodi, jambo ambalo TRA, wameanza kulitekeleza.
Ameahidi pia kuwa Wizara ya Fedha, kwa kushirikiana na Taasisi zake itaendelea kuzichukulia hatua kali Taasisi zinazotoa mikopo yenye riba kubwa (mikopo kausha damu) kwa kuwa zinatweza utu wa wakopaji wanaonyang’anywa mali zao kwa kushindwa kulipa mikopo waliyokopa kwenye Taasisi hizo.
Naye Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Adolf Mkenda, aliipongeza Wizara Fedha kwa kuandaa Jukwaa hilo na kwamba Wizara yake imetambua umuhimu wa masuala ya uchumi na fedha na imeandaa Mtaala Mpya wa Elimu utakao wawezesha wanafunzi kupata elimu ya ujasiriamali pamoja na biashara ili kuwajengea maarifa ya kujikwamua kiuchumi.
Kwa upande mwingine aliwataka wakopaji kutumia fedha wanazokopa kwa ajili ya kutekeleza miradi itakayowaongezea fedha ili wapate tija ya mikopo yao badala ya kuzitumia fedha za mikopo kwa malengo yasiyokusudiwa.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba alisema Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na wadau wa Sekta ya Fedha nchini imeandaa Jukwaa la wadau wa Sekta ya Fedha ili kubadilishana mawazo na uzoefu, kupeana taarifa, kujengeana uwezo, kushirikishana katika mafanikio na changamoto na kutafuta suluhu ya pamoja kwa changamoto zinazoikabili sekta ya fedha nchini.
Alisema malengo ya Jukwaa la Wadau wa Sekta ya Fedha kwa mwaka 2024 ni pamoja na kutoa taarifa kuhusu utekelezaji wa Mpango Mkuu wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha kwa kipindi cha miaka mitatu (2020/21-2023/24) na kushirikishana mbinu bora za kiutendaji na uzoefu katika Sekta ya Fedha.
Katika Halfa hiyo Nyaraka zilizozindulia ni Mkakati wa Upatikanaji wa Fedha kwa Wajasiriamali Wadogo na Wa kati wa Mwaka 2023/24 – 2028/29, Mwongozo wa Mitaji halaiki (Crowdfinancing) pamoja na Mwongozo wa Utoaji Hatifungani za kwa kutumia mfumo wa Sheria (Sukuk) kwa Kampuni na Taasisi za Umma wa Mwaka 2023. -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Leo tumezindua Jukwaa la Kwanza la Wadau wa Sekta ya Fedha kwa mwaka 2024, jukwaa hili litajadili fursa na hatua mbalimbali za kuboresha Sekta ya Fedha ikiwa ni pamoja na huduma ujumuishaji na endelevu za kifedha kwa njia ya kidijitali pamoja na kushirikishana namna bora ya kukuza matumizi ya teknolojia na uvumbuzi ili kukuza na kuimarisha Sekta ya Fedha nchini. Ushirikiano kati ya Sekta ya Umma na Binafsi ni msingi wa maendeleo yetu. Pamoja tunaweza.
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Thomas J. Kibwana
@thomasjkibwana
Kumbe USD 1 ishashuka hadi TZS 2,490?
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe, Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), akiwa na Walimu wake waliomfundisha Masuala ya Uchumi na Fedha katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Adolf Mkenda na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, walipokutana ana kwa ana wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Kwanza la Wadau wa Sekta ya Fedha kwa mwaka 2024, katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Bado Siku 1 Kuelekea Jukwaa la Wadau wa Sekta ya Fedha mwaka 2024, katika Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam.
#jukwaalawadausektayafedha -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki @mfa_tanzania , Mhe. Balozi Mahmood Thabit Kombo (Mb.) wameshiriki Mkutano wa Dharura wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), uliofanyika tarehe 9 Desemba, 2024 kwa njia ya mtandao kutokea Ofisi Ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje, Jijini Dar es Salaam, ambapo ajenda kuu ilikuwa kujajili ulinzi wa amani.
Mkutano huo pia umewashirikisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo na Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa, Dkt. Faraji Mnyepe na Viongozi wengine waandamizi kutoka Wizara ya Fedha, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, na Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
JIMBO LA IRAMBA MAGHARIBI
@jimbolairamba
𝐇𝐄𝐑𝐈 𝐘𝐀 𝐌𝐀𝐀𝐃𝐇𝐈𝐌𝐈𝐒𝐇𝐎 𝐘𝐀 𝐌𝐈𝐀𝐊𝐀 63 𝐘𝐀 𝐔𝐇𝐔𝐑𝐔
-
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
TRA Tanzania
@TRATanzania
Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba amewataka watanzania kukemea na kulaani vitendo vya baadhi ya watu kujichukulia sheria mkononi. Ameyasema hayo wakati akiongoza waombolezaji kuaga mwili wa aliyekuwa mtumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Amani Kamuguna Simbayao
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), ameahidi kuwahudumia kimahitaji watoto wawili wa marehemu, Amani Kamguna Simbayao, aliyekuwa mtumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania- @TRATanzania , aliyefariki Dunia katika Hospitali ya Taifa ya Mifupa Muhimbili-Moi-Dar es salaam, aliyefariki dunia kwa kushambuliwa na watu katika eneo la Tegeta kwa Ndevu, jijini Dar es Salaam, tarehe 6 Disemba, 2024.
Dkt. Nchemba ametoa ahadi hiyo wakati akiongoza waombolezaji kuuaga mwili wa marehemu katika Viwanja vya Michezo vya TRA, Kurasini Jijini Dar es Salaam.
Aidha, Mhe. Dkt. Nchemba. Amemwagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maanry Mwamba, ambaye aliwakilishwa na Naibu Katibu Mkuu, Bw. Elijah Mwandumbya, katika tukio hilo, na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, Bw. Yusuf Juma Mwenda, kuhakikisha kuwa kiasi cha shilingi milioni 200 kinatafutwa kwa ajili ya kuanzisha Mfuko Maalum utakao tumika kuwanunulia watoto hao (Najimu Amani Sumbayao (8) na Badria Amani Simbayao (3), pamoja na mama yao, Bi. Arafat Abdalla Ukomo, Hati Fungani za Benki Kuu ya Tanzania, kwa ajili ya uhakika wa kupata huduma stahiki kama vile elimu na mambo mengine.
Maelekezo hayo yanafuatia maombi yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila, wakati alitoa salam za Mkoa wake, ambapo alipendekeza uwepo mpango mahsusi wa kuisaidia familia hiyo kimaisha ili iwe motisha kwa familia hiyo iliyopoteza shujaa aliyemwaga damu yake wakati akilitumikia Taifa.
Marehemu Amani Simbayao, alikuwa Afisa Usafirishaji (dereva) wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, ambaye alipigwa na kuumizwa vibaya na watu akiwa kazini na wafanyakazi wenzake wengine wawili katika eneo la Tegeta Kwa Ndevu, Jijini Dar es Salaam. wakati walipokuwa wakilifuatilia gari moja lililokuwa linashukiwa kukiuka masuala ya kiforodha.
Katika tukio hilo la kuuaga mwili wa marehemu, Mhe. Dkt. Nchemba, alilaani vikali tukio hilo la watu kujichukulia Sheria mkononi na kumuua Mtumishi asiye na hatia hata baada ya kujitambulisha kuwa ni Mtumishi wa TRA, na ametoa wito kwa vyombo vya dola kuwachukulia hatua kali za kisheria wale wote waliohusika na tukio hilo baya ili liwe fundisho kwa watu wengine.
Aliwatia moyo wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), wasikatishwe tamaa na tukio hilo, bali waendelee kuchapakazi kwa bidii kwa manufaa ya Taifa. -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Leo tumetoa heshima za mwisho kwa Mtumishi wa TRA, Bwana Amani Kamguna Simbayao, aliyefariki akiwa kazini akihudumia Taifa. Sina maneno ya kutosha kubeba uzito wa simanzi zangu. Nimetoa pole kwa familia yake, ndugu, jamaa, na watumishi wa TRA. Mungu awape faraja na ustahimilivu katika kipindi hiki kigumu, na roho ya marehemu ipumzike mahali pema peponi.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Haki Ngowi
@Hakingowi
📍Dar es Salaam
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), ameongoza ujumbe wa Tanzania katika kikao kati ya Serikali na Ujumbe wa Wataalam kutoka Benki ya Dunia, ukiongozwa na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia, Bw. Nathan Belete, kilichojadili vipaumbele vya miradi ya nchi itakayotekelezwa kupitia Dirisha Jipya la IDA21, kikao kilichofanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam. Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Kamishna wa Idara ya Fedha za Nje, Wizara ya Fedha, Bw. Rished Bade na Viongozi wengine waandamizi wa Serikali kutoka Wizara ya Fedha na Benki ya Dunia.
📸:W/Fedha -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Bado Siku 3 Kuelekea Jukwaa la Wadau wa Sekta ya Fedha mwaka 2024, katika Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam.
#jukwaalawadausektayafedha -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), ameongoza ujumbe wa Tanzania katika kikao kati ya Serikali na Ujumbe wa Wataalam kutoka Benki ya Dunia, ukiongozwa na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia, Bw. @BeleteNathan , kilichojadili vipaumbele vya miradi ya nchi itakayotekelezwa kupitia Dirisha Jipya la IDA21, kikao kilichofanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam. Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Kamishna wa Idara ya Fedha za Nje, Wizara ya Fedha, Bw. Rished Bade na Viongozi wengine waandamizi wa Serikali kutoka Wizara ya Fedha na Benki ya Dunia.
@WBTanzania -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Serikali ya Tanzania na Shirika la Maendeleo La Ufaransa (AFD) wamesaini mikataba minne (4) yenye jumla ya euro milioni 118.8 sawa na takriben shilingi bilioni 323.4 kwa ajili kutekeleza miradi mbalimbali nchini ikiwemo Awamu ya Pili ya mradi wa nishati jua wa Kishapu Mkoani Shinyanga, pamoja na uendelezaji wa misitu na utunzaji wa hifadhi ya misitu ya mikoko.
Hafla ya utiaji saini wa Mikataba hiyo imefanyika jijini Dar es Salam kati ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), kwa upande wa Serikali na Naibu Balozi wa Ufaransa nhini Tanzania, Mhe. Axel-David Guuillon pamoja na Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa (@AFD_en ), Bi. @CelineRobertAFD
Akizungumza baada ya kusaini Mikataba hiyo, Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba alisema katika Mikataba hiyo iliyosainiwa euro milioni 75.9 ni kwa ajili ya utekelezaji wa Awamu ya Pili ya Mradi wa Nishati ya jua unaotekelezwa Kishapu Mkoani Shinyanga.
Alisema kuwa mradi huo utazalisha Megawati 150 ambapo Awamu ya Kwanza upo katika hatua za utekelezaji na unatarajiwa kuzalisha Megawati 50 na Awamu ya Pili ambayo mkataba wake umesainiwa inatarajiwa kuzalisha Megawati 100 na kufanya jumla ya Megawati zitakazozalishwa kuwa 150.
"Kuingiza Megawati 150 kwenye gridi ya Taifa, kutapunguza utegemezi wa nishati ya nguvu za maji ambayo inaathirika kwa kiasi kikubwa kutokana na mabadiliko ya tabianchi. Mradi huu utaongeza upatikanaji wa nishati ya uhakika katika Mkoa wa Shinyanga ambao una umuhimu wa kimkakati wa kiuchumi na kijamii kutokana na kuwepo kwa shuhguli kubwa na ndogondogo za uchimbaji madini" alibainisha Mhe. Dkt. Nchemba.
Alisema Mkataba wa pili wa Euro milioni 39.9 ni kwa ajili ya uendelezaji wa mashamba ya misitu na utunzaji wa hifadhi ya mikoko ili kuongeza wigo wa upandaji miti, kuboresha ubora na wingi wa mbegu za miti na kuboresha usimamizi wa mbegu hizo.
Alisema mradi huo utaimarisha vituo vya kukusanya mbegu za miti na kuanzisha vitalu vya kisasa vya miti ikiwa ni pamoja na kutaboresha utunzaji wa hifadhi ya misitu ya mikoko, kuboresha uhifadhi wa uhasilia wa mazingira na kuchangia kuinua utalii na kuboresha Maisha ya jamii.
Dkt. Nchemba alisema mikataba ya euro milioni 2 ni kwa ajili ya utunzaji wa hifadhi ya mikoko na euro milioni 1 ni kwa ajili ya kufadhili Mpangokazi wa Jinsia unaotekelezwa na Shirika la Ugavi wa Umeme nchini (TANESCO), chini ya mradi wa uendelezaji wa nishati ya Jua.
“Huu ni mwendelezo wa ushirikiano wetu mzuri ambao umeshuhudiwa kwa kuwepo kwa miradi mbalimbali ambayo inafadhiliwa kwa mikopo nafuu kutoka Serikali ya Ufaransa kupitia AFD”, alisema Mhe. Dkt. Nchemba.
Alisema kuwa Serikali ya Ufaransa kupitia AFD imefadhili miradi mbalimbali kupitia mikopo nafuu katika sekta za Nishati, Maji, Usafirishaji na Kilimo ambayo mingine inaendelea na mingine imekamilika.
Naye Kaimu Balozi wa Ufaransa hapa nchini, Mhe. Axel-David Guuillon alisema miradi itakayotekelezwa kupitia mikataba hiyo ni muhimu kwa maendeleo ya nchi kwa kuwa itasaidia kupunguza gharama za kuagiza mafuta pamoja na kuhifadhi mazingira.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD), Bi. Celine Robert, alisema kuwa mikataba hiyo ni mwendelezo wa uhusiano uliopo kati ya Tanzania na Shirika hilo.
Alisema mkataba wa kuendeleza misitu nchini utaiwezesha Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), kujumuisha ukuaji wa uchumi, ushirikishwaji wa jamii na utunzaji endelevu wa mazingira.
Bi. Robert alisema mkataba wa Awamu ya Pili ya mradi wa nishati ya jua Kishapu Mkoani Shinyanga, utaiwezesha nchi kukabiliana na changamoto za umeme kwa kuwa Tanzania itakuwa na vyanzo tofauti tofauti vya umeme.
“Mabadiliko ya hali ya hewa yapo na yanaathari nyingi siku za usoni, mradi huu wa umeme utaiwezesha Tanzania kukabiliana na tatizo la umeme hususani yanayotokana na mabadiliko ya hali ya hewa pamoja na kutunza mazingira” alisema. Bi. Robert.
Kwa upande wa Manaibu Mawaziri wa Sekta ambazo zitatekeleza miradi hiyo walisema watasimamia kikamilifu miradi hiyo ili kuhakikisha inafikia malengo kusudiwa ambapo Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga alisema mkataba wa Awamu ya Pili ya mradi wa nishati ya jua Kishapu Mkoani Shinyanga ni mradi muhimu ambao unaenda kuchagiza miradi mingine ambayo inazalisha nishati jadidifu ambazo zinapunguza athari za mazingira.
Naye Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dunstan Kitandula, alisema fedha hizo zilizosainiwa katika mikataba hiyo zitatumika kupanda miti na kusimamia misitu ya mikoko.
Alisema mikataba hiyo itaiwezesha nchi kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi pamoja na kuongeza uwezo wa kuvuna mazao yanayotokana na misitu -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Nimesikitishwa na tukio la kushambuliwa kwa watumishi watatu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na gari lao (STL 9923) walipokuwa wakitekeleza majukumu yao ya kisheria ya kudhibiti magendo na magari yaliyoingizwa nchini kinyume cha sheria, usiku wa tarehe 5 Desemba 2024, katika eneo la Tegeta kwa Ndevu, Dar es Salaam.
Watumishi hao walikuwa wakifuatilia gari namba T229 DHZ (BMW X6) lililoingizwa nchini bila kulipa kodi stahiki. Natoa pole kwa wote waliojeruhiwa na kuwaombea wapate nafuu haraka.
Wizara ya Fedha inalaani vikali tukio hili na kuahidi kuwa hatua kali zitachukuliwa dhidi ya wahusika wa uhalifu huu. Aidha, TRA itaendelea kutekeleza majukumu yake kwa weledi na kwa mujibu wa sheria.
Tunatoa wito kwa wananchi wote kushirikiana na Serikali kuhakikisha kuwa sheria za kodi zinatekelezwa ipasavyo kwa Maendeleo ya Taifa letu. Tukumbuke, "Kodi Zetu ndiyo Maendeleo Yetu". -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Benki ya Dunia imeahidi kutoa kiasi cha takribani Dola za Marekani milioni 300 kwa ajili ya kusaidia Awamu ya Tatu ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini nchini chini ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania (TASAF) ambayo inatajiwa kutekelezwa baada ya kukamilika kwa Awamu ya Pili ya Mpango huo mwakani.
Hayo yameelezwa jijini Dar es Salaam na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini, Bw. Nathan Belete katika Mjadiliano ya Ngazi ya Juu kati ya Serikali na wadau wa maendeleo kuhusu mustakabali wa Awamu ya Tatu ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini chini ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania (TASAF).
Bw. Belete alisema wameamua kutoa fedha hizo kwakuwa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unatekelezwa na TASAF ni mfano wa kuigwa duniani kwasababu umechangia kukabiliana na umaskini na kuonesha matokeo chanya .
Aliipongeza Serikali kwa mafanikio mbalimbali iliyoyapata kupitia Awamu ya Kwanza na ya Pili ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini chini ya TASAF na kuahidi kuwa benki hiyo kwa kushirikiana na washirika wengine wa maendeleo wataendelea kushirikiana na Serikali kuhakikisha inafikia malengo yake hususan ya kuwawezesha wananchi kukabiliana na umaskini.
Naye Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), ambaye aliongoza majadiliano hayo, alisema Awamu ya Tatu ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini itakuwa na mpango jumuishi utakao endana na Dira ya Maendeleo ya Taifa inayoandaliwa ya 2025 -2050.
Alisema utakuwa mpango jumuishi kwa kuwa hatuo acha mtu yoyote nyuma kwa kuhakikisha kuwa unawezesha wananchi wa hali ya chini kujumuishwa katika mpango mkuu kwa kushiriki katika miradi mbalimbali inayoendelea nchini.
“Uandaaji wa Mpango wa Tatu wa TASAF utahusisha shughuli za uzalishaji ambazo hazita bagua sehemu ya jamii yetu, makundi yote yatahusishwa katika shughuli za maendeleo na mgawanyo wa bajeti kwa ajili ya maendeleo hayo ”, alisema Dkt. Nchemba.
Alisema Awamu ya Tatu ya Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini inaandaliwa baada ya mafanikio makubwa yaliyopatikana katika Mpango wa Kwanza na Wapili ambapo kumekuwa na shuhuda mbalimbali kutoka kwa wanufaika ambao vipato vyao vimeongezeka kutoka hatua moja kwenda nyengine kwa kuoonesha shughuli walizo fanikiwa kuzifanya kutokana na mradi huo.
Akizungumzia uchumi wa nchi, Dkt. Nchemba alisema uchumi unatarajiwa kukua kwa asilimia 5.4 mwaka 2024 kutoka asilimia 5.1 mwaka 2023 na kubainisha kuwa utendaji wa uchumi wa Tanzania kuanzia 2020 hadi 2024 unaonesha kuimarika.
Alisema kukua na kuimarika huko kwa uchumi wa nchi kunatona na mabadiliko ya sera za Serikali na jitihada za kukabiliana na changamoto za kitaifa na kimataifa ambazo ni zimekuwa kikwazo cha shughuli mbalimbali za kiuchumi.
Kwa upande wake, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwan Kikwete alisema majadiliano hayo yamefanyika kwa kuwa Mpango wa Pili wa Kunusuru Kaya Maskini unatarajia kumaliza muda wake mwakani hivyo ilikuwa ni muhimu Serikali na wadau kukutana kuangalia namna bora ya kuanzisha Mpango mwengine ambao utakuwa na manufaa kwa Taifa.
Alisema katika majadiliano hayo wadau wote muhimu wameonesha nia ya kuendelea kushirikiana na Serikali katika Mpango wa Tatu wa Kunusuru Kaya Maskini.
Naye Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Fedha na Mipango - Zanzibar, Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salim alisema ni muhimu Awamu mpya ya Kunusuru Kaya Masikini ifungamanishwe na masuala ya kidigitali ambayo yatawezesha wanufaika kupokea fedha kidigitali ili kuongeza usalama na kuhamasisha uwekaji akiba.
Alisema Zanzibar pia ni wanufaika wa Mfuko TASAF ambapo wananchi wengi wanaoishi katika kaya maskini wamekuwa wakipatiwa misaada mbalimbali kupitia miradi ya Kunusuru Kaya Maskini.
Aliongeza kuwa licha ya miradi ya TASAF kusaidia kaya maskini kujiinua kiuchumi visiwani Zanzibar pia imesaidia kujenga shule na vituo vya afya.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa TASAF, Bw. Shedrack Mziray alisema kuwa Mpango wa Tatu wa Kunusuru Kaya Maskini unatarajia kugharimu takribani Dola za Marekani milioni 500 na kuhususha wanufaika wapya na baadhi ya wanufaika wa Awamu ya Pili ambao bado wahitaji msaada wakiwemo wazee wasiojiweza, wajane na wote watakao bainika kuwa halizao zinahitaji haziridhishi.
Majadiliano hayo yalihusisha Mawaziri mbalimbali wa kisekta kutoka Tanzania Bara na Visiwani, Benki ya Dunia na wadau wa maendeleo nchini. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Samuel Munzele Maimbo
@SamMMaimbo
It was a privilege to meet with Hon. Mwigulu Nchemba (@mwigulunchemba1), Minister of Finance of Tanzania, and Hon. Mahmoud Thabit Kombo, Minister of Foreign Affairs and EAC Cooperation, to discuss collaborative strategies for a stronger, more resilient Africa.
Tanzania, like many African nations, possesses a wealth of young talent, abundant natural resources, and a vibrant entrepreneurial spirit.
With the shared belief that accelerating development in Africa is a collective effort, I extend my deepest thanks to President Samia Hassan (@SuluhuSamia), whose government I am honored to partner on this mission.
• • •
Ce fut un privilège de rencontrer Son Excellence Mwigulu Nchemba , ministre des Finances de la Tanzanie, et Son Excellence Mahmoud Thabit Kombo, ministre des Affaires étrangères et de la Coopération de la Communauté d’Afrique de l’Est (CAE), afin de discuter de stratégies collaboratives pour une Afrique plus forte et plus résiliente.
La Tanzanie, comme de nombreux pays africains, regorge de jeunes talents, de ressources naturelles abondantes et d’un esprit entrepreneurial dynamique.
J’ai l’intime conviction que l’accélération du développement en Afrique passe nécessairement par un effort collectif. J’adresse, à cet égard, mes plus sincères remerciements à la présidente Samia Hassan, dont le gouvernement est un partenaire inestimable dans cette mission.
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb) (kushoto), akizungumza jambo na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia masuala ya bajeti na Mipango ya Kimkakati, Dkt. Samuel Maimbo, ambaye pia amepitishwa na Wakuu wa nchi za Afrika Mashariki kugombea nafasi ya Urais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) katika uchaguzi unaotarajiwa kufanya hivi karibuni.
Mazungumzo yao yamefanyika wakati wa siku ya kwanza ya ufunguzi wa Mkutano wa Pili wa Jumuiya ya Wahasibu Wakuu wa Serikali wa Nchi za Afrika unaofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC).
@AAAG_Africa -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb) (kulia), akipokea zawadi ya picha inayoonesha taswira za wanyamapori watano wakubwa wanaopatikana katika Hifadhi za Taifa za Tanzania kutoka kwa Waziri wa Ujenzi , Mhe. Innocent Bashungwa, aliyemwakilisha Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ikiwa ni alama ya mchango wake katika kusimamia sekta ya uhasibu nchini, sekta ambayo inapigiwa mfano na mataifa mengine ya Afrika kutokana na kuwa na mifumo imara ya uhasibu.
Aidha, Naibu Katibu Mkuu, CPA. Elijah Mwandumbya akipokea zawadi kama hiyo kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, kwa kutambua mchango wake pia katika kusimamia sekta ya uhasibu nchini, wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Pili wa Jumuiya ya Wahasibu Wakuu wa Serikali wa Nchi za Afrika, unaofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano-Arusha (AICC) kuanzia tarehe 2 hadi 5 Disemba, 2024.
@AAAG_Africa @SuluhuSamia @KassimMajaliwa_ @innobash -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), akiteta jambo na Balozi wa Italia nchini Tanzania, Mhe. Giuseppe Coppola, Kando ya Kilele cha Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki, unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa-Arusha (AICC) leo tarehe 30 Novemba, 2024
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Paul Makonda, Kando ya Kilele cha Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki, unaofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano-Arusha (AICC) leo tarehe 30 Novemba, 2024.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), akizungumza na Viongozi wa dini wa Mkoa wa Arusha akiwemo Sheikh Shaaban Juma Abdallah Mkoa wa Arusha (BAKWATA), Askofu Dkt. Israel Maasa Ole Gabriel, wa Kanisa la International Evangelism, Askofu Ayubu Munna wa Kanisa la FPCT Jimbo la Arusha, wakati wa Kilele cha Mkutano wa Kawaida wa 24 wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, unaofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano-Arusha (AICC), leo tarehe 30 Novemba, 2024.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), ameungana na baadhi ya Mawaziri na Viongozi wengine Serikalini, kushiriki Kilele cha Mkutano wa 24 wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, unaofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano-Arusha (AICC), leo tarehe 30 Novemba, 2024.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), akipitia nyaraka kabla ya kuanza kwa Mkutano wa 46 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki unaofanyika Makao Makuu ya Jumuiya hiyo, Jijini Arusha, ambapo mawaziri watajadiliana kuhusu utengamano wa kiuchumi na kibiashara miongoni mwa nchi wanachama wa jumuiya hiyo.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Haki Ngowi
@Hakingowi
📍Iramba
▪️DKT. NCHEMBA APIGA KURA IRAMBA
Waziri wa Fedha na Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), leo Novemba 27, 2024, ameungana na wananchi wa jimbo lake katika zoezi la kupiga kura kuwachagua viongozi wa Serikali za Mitaa, Vitongoji na Vijiji.
Dkt. Nchemba amepiga kura katika Kituo cha Ofisi ya Mtendaji wa Kijiji cha Misigiri, Kata ya Ulemo, Wilaya ya Iramba, mkoani Singida.
Akizungumza mara baada ya kupiga kura, aliwasihi wananchi kuhakikisha wanatumia haki yao ya msingi ya Kikatiba kushiriki kikamilifu katika uchaguzi huo.
"Uchaguzi huu ni wa haki na demokrasia. Tumeshuhudia zoezi likiendeshwa kwa uhuru kabisa. Naomba wananchi wote ambao bado hawajapiga kura wajitokeze kwa wingi kufanya hivyo, kwani ni haki yao ya msingi," alisema Dkt. Nchemba.
Aliongeza kuwa uchaguzi ni fursa muhimu ya kuchagua viongozi wenye maono ya maendeleo na uwezo wa kusikiliza na kutatua changamoto za wananchi.
"Nimetimiza wajibu wangu wa kupiga kura, na niwaombe wananchi kote nchini kufanya hivyo kwa maslahi makubwa ya Taifa letu," alisisitiza.
Dkt. Nchemba aliambatana na Mkewe Bi. Neema Ngure katika zoezi hilo la upigaji kura. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Lemutuz TV
@lemutuztv
DKT. NCHEMBA APIGA KURA IRAMBA
Waziri wa Fedha na Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), leo Novemba 27, 2024, ameungana na wananchi wa jimbo lake katika zoezi la kupiga kura kuwachagua viongozi wa Serikali za Mitaa, Vitongoji na Vijiji.
Dkt. Nchemba amepiga kura katika Kituo cha Ofisi ya Mtendaji wa Kijiji cha Misigiri, Kata ya Ulemo, Wilaya ya Iramba, mkoani Singida.
Akizungumza mara baada ya kupiga kura, aliwasihi wananchi kuhakikisha wanatumia haki yao ya msingi ya Kikatiba kushiriki kikamilifu katika uchaguzi huo.
"Uchaguzi huu ni wa haki na demokrasia. Tumeshuhudia zoezi likiendeshwa kwa uhuru kabisa. Naomba wananchi wote ambao bado hawajapiga kura wajitokeze kwa wingi kufanya hivyo, kwani ni haki yao ya msingi," alisema Dkt. Nchemba.
Aliongeza kuwa uchaguzi ni fursa muhimu ya kuchagua viongozi wenye maono ya maendeleo na uwezo wa kusikiliza na kutatua changamoto za wananchi.
"Nimetimiza wajibu wangu wa kupiga kura, na niwaombe wananchi kote nchini kufanya hivyo kwa maslahi makubwa ya Taifa letu," alisisitiza.
Dkt. Nchemba aliambatana na Mkewe Bi. Neema Ngure katika zoezi hilo la upigaji kura. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
The 2nd African Association of Accountants General (AAAG) conference will be held from December 2-5, 2024, in Arusha, Tanzania.
Theme: Building Public Trust in Public Financial Management (PFM) Systems for Sustainable Growth.
Register now at conference.aaag.org.zm -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha na Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), leo Novemba 27, 2024, ameungana na wananchi wa jimbo lake katika zoezi la kupiga kura kuwachagua viongozi wa Serikali za Mitaa, Vitongoji na Vijiji.
Dkt. Nchemba amepiga kura katika Kituo cha Ofisi ya Mtendaji wa Kijiji cha Misigiri, Kata ya Ulemo, Wilaya ya Iramba, mkoani Singida.
Akizungumza mara baada ya kupiga kura, aliwasihi wananchi kuhakikisha wanatumia haki yao ya msingi ya Kikatiba kushiriki kikamilifu katika uchaguzi huo.
"Uchaguzi huu ni wa haki na demokrasia. Tumeshuhudia zoezi likiendeshwa kwa uhuru kabisa. Naomba wananchi wote ambao bado hawajapiga kura wajitokeze kwa wingi kufanya hivyo, kwani ni haki yao ya msingi," alisema Dkt. Nchemba.
Aliongeza kuwa uchaguzi ni fursa muhimu ya kuchagua viongozi wenye maono ya maendeleo na uwezo wa kusikiliza na kutatua changamoto za wananchi.
"Nimetimiza wajibu wangu wa kupiga kura, na niwaombe wananchi kote nchini kufanya hivyo kwa maslahi makubwa ya Taifa letu," alisisitiza.
Dkt. Nchemba aliambatana na Mkewe Bi. Neema Ngure katika zoezi hilo la upigaji kura. -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Pumzika kwa amani kaka yangu 😭😭.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Waziri wa Fedha, na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM @ccm_tanzania Taifa, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba @mwigulunchemba1 , amewahimiza wananchi wa Mkoa wa Singida kushiriki kikamilifu katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika, Novemba 27, 2024.
Akizungumza katika Mkutano wa kufunga kampeni za uchaguzi uliofanyika, Novemba 26, 2024, katika Kata ya Puma, Wilaya ya Ikungi, Dkt. Nchemba amewasihi wananchi kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani na utulivu, huku akisisitiza umuhimu wa kuchagua viongozi wa vitongoji, mitaa na vijiji wanaotokana na CCM kwa maendeleo ya jamii.
Amewahimiza wananchi kutunza mshikamano na kudumisha umoja kwa kuhakikisha uchaguzi unakuwa wa haki na usio na migogoro, kwa maslahi ya taifa zima.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Leo tumehitimisha Kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mkoani Singida.
Nimewasisitiza wananchi kuhusu umuhimu wa uchaguzi huu kama nyenzo ya kuimarisha uwakilishi na kuboresha huduma za kijamii katika maeneo yetu. Pia, nimewaombea kura wagombea wa CCM ili waendelea kusimamia maendeleo na ustawi wa wananchi.
Nawatakia Watanzania wote uchaguzi wa haki, amani, na utulivu kwa manufaa ya Taifa letu.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Wembe ni ule ule, Ushindi kwa Chama Cha Mapinduzi.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), ameshuhudia utiaji saini wa makabidhiano ya kuanza kwa utekelezaji wa mradi mkubwa wa ukarabati wa Skimu ya Umwagiliaji Masimba katika Wilaya ya Iramba, Mkoa wa Singida, wenye thamani ya shilingi bilioni 10.5.
Mradi huo, unaotekelezwa na Serikali kupitia Wizara ya Kilimo kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, unalenga kuongeza tija ya kilimo kwa wakulima wa eneo hilo na kuboresha maisha ya zaidi ya watu 24,000 kutoka vijiji vya Masimba, Urughu, Mlandala, Mang’ole, na Ujungu.
Akizungumza katika Hafla ya kukabidhi eneo la mradi kwa mkandarasi iliyofanyika katika Kata ya Urughu, Waziri wa Fedha na Mbunge wa Iramba Magharibi, Dkt. Mwigulu Nchemba, alisisitiza kuwa hatua zinazochukuliwa na Wizara ya Kilimo, chini ya uongozi wa Waziri Hussein Bashe, zinaimarisha kilimo cha kisasa na kuleta mapinduzi katika sekta hiyo, ambayo ni mhimili wa uchumi wa wananchi wengi nchini.
Dkt. Nchemba, aliongeza kuwa mradi huo ni mfano wa jinsi serikali inavyotekeleza dira ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuboresha sekta ya kilimo, na hasa kilimo cha umwagiliaji, ili kuhakikisha uzalishaji endelevu na maendeleo ya jamii za vijijini.
Akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Mkurugenzi Idara ya Uendelezaji Miundombinu, Ndugu. Raphael Laizer, alifafanua vipengele vya mradi, ambavyo ni pamoja na: Ukarabati wa bwawa na sehemu ya utoro wa maji, Kuondoa mchanga na tope ndani ya bwawa ili kuongeza ujazo wake kwa mita za ujazo 250,000, Ujenzi wa mfereji mkuu wa mita 200 kwa kiwango cha zege, Ujenzi wa mifereji ya upili yenye urefu wa mita 9,254 kwa kiwango cha zege.
Nae Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Mhe. Suleiman Mwenda, alisema mradi huu ni hatua kubwa inayojibu kilio cha muda mrefu cha wakulima wa eneo hilo kwa kutatua changamoto za upatikanaji wa maji ya uhakika kwa kilimo.
Skimu hiyo itakuwa na eneo la ekari 1,800 za umwagiliaji, ambapo wakulima watazalisha mazao ya mpunga na mbogamboga kwa wingi, hatua inayotarajiwa kuongeza mapato na kuboresha hali ya maisha.
Mradi huo ni sehemu ya juhudi za serikali kuhakikisha kuwa sekta ya kilimo inakuwa kichocheo kikubwa cha ukuaji wa uchumi na ustawi wa wananchi. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Haki Ngowi
@Hakingowi
📍Iramba,Singida.
▪️ZAIDI YA BILIONI 10 SKIMU YA UMWAGILIAJI MASIMBA KUNUFAISHA WAKULIMA 24,000 MKOANI SINGIDA*
Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba ambaye ni mbunge wa Iramba Magharibi ameipongeza Wizara ya Kilimo kwa kuendelea kuboresha sekta ya kilimo nchini kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kwani hatua zinazochukuliwa zitaboresha maisha ya Watanzania hasa wakulima.
Amesema Waziri wa. Kilimo Hussein Bashe anaitendea haki sekta ya kilimo na hakuna miujiza katika uchumi zaidi ya mapinduzi yanayofanywa sekta hiyo inayogusa watu wengi kupitia Umwagiliaji
Dkt. Mwigulu ametoa kauli hiyo wakati wa hafla ya kukabidhi eneo la mradi wa ujenzi skimu ya umwagiliaji Masimba kwa mkandarasi iliyopo kata ya Urughu wilaya ya Iramba mkoani Singida.
Amesema serikali kupitia Wizara ya Kilimo inatekeleza dira ya Rais kwa kuwahakikishia Watanzania kuwa na kilimo cha kisasa na kufanya mapinduzi ya kilimo kupitia sekta ya kilimo cha umwagiliaji.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Iramba Magaharibi Mhe. Suleiman Mwenda amesema ni kilio cha muda mrefu kwa wakulima wa eneo hilo kuhitaji kuwa na kilimo cha umwagiliaji cha uhakika.
Amesema awali halmashauri ya wilaya ya Iramba Magharibi iliweka makadirio ya gharama za ukarabati wa bwawa la umwagiliaji katika skimu hiyo ambayo ni kiasi cha Shilingi bilioni 2.
Akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Mkurugenzi Idara ya Uendelezaji Miundombinu Mha. Raphael Laizer amesema mradi huo unagharimu kiasi cha Shilingi bilioni 10,496,185,520 ambapo utajumuisha ukarabati wa bwawa na sehemu ya utoro wa maji, Kuchimba mchanga na tope ndani ya bwawa ili kuongeza ujazo wa bwawa mita za ujazo 250,000, Ujenzi wa mfereji mkuu mita 200 kwa kiwango cha zege na Ujenzi wa mfereji wa upili mita 9,254 kwa kiwango cha zege.
Kukamilika ka ukarabati skimu ya umwagiliaji Masimba utanufaisha wakazi 24,000 wa Vijiji vitano ambavyo ni Masimba, Urughu, Mlandala, Mang’ole na Ujungu huku zao litakalolimwa ni mpunga pamoja na mbogamboga.
📸:NIRC -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Tunaendelea na Kampeni ya Mtu kwa Mtu, Nyumba kwa Nyumba, Kijiwe kwa Kijiwe.
Post not available here, view on X
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Dcirambaofficial
@DCIRAMBA
HAFLA YA KUMKABIDHI MKANDARASI ENEO LA MRADI UJENZI WA SKIMU YA UMWAGILIAJI MASIMBA ILIYOPO KATA YA URUGHU WILAYANI IRAMBA
@mwigulunchemba1
@nirc_tz
@Hakingowi
@HusseinBashe -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Bank of Tanzania
@BankOfTanzania
-
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Uzinduzi wa kampeni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa Kata ya Kidaru, Iramba.
Post not available here, view on X
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
-
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Congratulations, President @SuluhuSamia, For your historic and trailblazing address at the G20 Summit. Your eloquent advocacy for Africa's prosperity and resolute call for global cooperation in overcoming systematic poverty exemplify unparalleled leadership, patriotism and Vision.
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Hongera Mhe Rais, Hongera Tanzania, Hongera Taifa Stars.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), akifurahia jambo na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (@AfDB_Group ) Dkt. @akin_adesina , katika Viwanja vya Michezo vya Olimpiki, Baku, nchini Azerbaijan, unapofanyika Mkutano wa 29 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP-29).
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Dr. Akinwumi A. Adesina, CON, CGH
@akin_adesina
It was good to see Tanzania’s Minister of Finance Dr. @mwigulunchemba1 at Cop 29 in Baku. Tanzania can always count on my strong support and that of the African Development Bank Group.
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), akifurahia jambo na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (@AfDB_Group ) Dkt. @akin_adesina , katika Viwanja vya Michezo vya Olimpiki, Baku, nchini Azerbaijan, unapofanyika Mkutano wa 29 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP-29).
-
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Karibu sana Iramba Mlezi wa CCM Mkoa wa Singida na Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Zubeir Ali Maulid.
-
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
C'était une très bonne rencontre avec mon frère qui est fier de lui.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), akisisitiza umuhimu wa kuongeza fursa za uwekezaji katika uchumi wa buluu na maji ya bahari kwa ajili ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi hususan katika eneo la kodi na kukuza ajira, wakati akimkaribisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dkt. Ashatu Kijaji Kachwamba, kufungua mkutano wa kunadi fursa za uwekezaji katika sekta ya uchumi wa buluu zilizopo Tanzania, kwa niaba ya Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, pembezoni mwa Mkutano wa 29 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP-29) unaofanyika kuanzia tarehe 11 hadi 22, Vovemba 2024, katika Mji wa Baku, nchini Azerbaijan.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 , ametoa wito kwa Serikali, Sekta Binafsi na Washirika wa maendeleo kuunga mkono agenda ya kuhimiza matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa manufaa ya watu waishio Barani Afrika.
Dkt. Nchemba ametoa wito huo wakati akifunga mkutano uliojadili umuhimu wa matumizi ya nishati safi ya kupikia, kwa niaba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, pembezoni mwa Mkutano wa 29 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko yaTabianchi (COP-29) unaofanyika katika Mji wa Baku nchini Azerbaijan.
Alisema kuwa ni muhimu kwa nchi za Afrika kutekeleza sera zinazochochea kasi ya matumizi ya teknolojia za nishati safi ya kupikia na kutenga fedha za kutosha kuisadia jamii hususan iliyoathirika zaidi na athari hasi ya mabadiliko ya tabianchi.
“Ni muhimu kujenga ushirikiano unaolenga kuongeza ujuzi na utaalam ili kuhakikisha kuwa suluhisho la changamoto ya matumizi duni ya teknolojia ya kuwezesha matumizi ya nishati safi ya kupikia inapatiwa ufumbuzi wa kudumu” alisema Dkt. Nchemba kwa niaba ya Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Mpango
Dkt. Nchemba alilisisitiza umuhimu wa wadau wote kushirikiana ili kuweka mazingira wezeshi ya mipango ya matumizi ya nishati safi ya kupikia ili kujenga mustakabari na kesho iliyobora kote Barani Afrika.
Mkutano huo wa nishati safi ya kupikia uliandaliwa na Tanzania kwa kushirikiana na Umoja wa Afrika (AU) pamoja na Tume ya Nishati Afrika (AFREC) uliyofanyika pembezoni mwa Mkutano wa 29 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP-29) unaofanyika katika Mji wa Baku nchini Azerbaijan.
Zaidi wa watu elfu 50, wakiwemo wanadiplomasia kutoka zaidi ya nchi 200 wanachama wa Umoja wa Mataifa, wanakutana katika Jiji la Baku, nchini Azerbaijan wakijadili namna ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi kwa kutafuta vyanzo vya fedha za uhakika za kutekeleza miradi mbalimbali ya kimkakati ya kukabiliana na changamoto hizo, ikiwemo kuhimiza matumizi ya nishati safi ya kupikia. -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Natoa pole kwa Ndugu, Jamaa na Marafiki kufuatia ajali ya kuporomoka kwa jengo la ghorofa katika Kata ya Kariakoo, Wilaya ya Ilala, Mkoa wa Dar es Salaam.
Mwenyezi Mungu awaponye majeruhi haraka na kuwapa faraja wote walioathirika. Tuendelee kuwaombea subira na utulivu wenzetu katika kipindi hiki kigumu. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 , amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa Mataifa anayesimamia Kamisheni ya Uchumi Kanda ya Afrika, Bw. Claver Gatete, pembezoni mwa Mkutano wa 29 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP-29) unaofanyika katika Mji wa Baku nchini Azerbaijan. Katika mazungumzo yao walijadiliana namna ya kuongeza ushirikiano kati ya Tanzania na Umoja wa Mataifa, hususan katika kutafuta vyanzo mbadala vya fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo na kuboresha sera za uchumi ili kuchochea maendeleo ya nchi.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 , ametoa wito kwa Serikali, Sekta Binafsi na Washirika wa maendeleo kuunga mkono agenda ya kuhimiza matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa manufaa ya watu waishio Barani Afrika.
Dkt. Nchemba ametoa wito huo wakati akifunga mkutano uliojadili umuhimu wa matumizi ya nishati safi ya kupikia, kwa niaba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, pembezoni mwa Mkutano wa 29 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko yaTabianchi (COP-29) unaofanyika katika Mji wa Baku nchini Azerbaijan.
Alisema kuwa ni muhimu kwa nchi za Afrika kutekeleza sera zinazochochea kasi ya matumizi ya teknolojia za nishati safi ya kupikia na kutenga fedha za kutosha kuisadia jamii hususan iliyoathirika zaidi na athari hasi ya mabadiliko ya tabianchi.
“Ni muhiu kujenga ushirikiano unaolenga kuongeza ujuzi na utaalam ili kuhakikisha kuwa suluhisho la changamoto ya matumizi duni ya teknolojia ya kuwezesha matumizi ya nishati safi ya kupikia inapatiwa ufumbuzi wa kudumu” alisema Dkt. Nchemba kwa niaba ya Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Mpango
Dkt. Nchemba alilisisitiza umuhimu wa wadau wote kushirikiana ili kuweka mazingira wezeshi ya mipango ya matumizi ya nishati safi ya kupikia ili kujenga mustakabari na kesho iliyobora kote Barani Afrika.
Mkutano huo wa nishati safi ya kupikia uliandaliwa na Tanzania kwa kushirikiana na Umoja wa Afrika (AU) pamoja na Tume ya Nishati Afrika (AFREC) uliyofanyika pembezoni mwa Mkutano wa 29 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP-29) unaofanyika katika Mji wa Baku nchini Azerbaijan.
Zaidi wa watu elfu 50, wakiwemo wanadiplomasia kutoka zaidi ya nchi 200 wanachama wa Umoja wa Mataifa, wanakutana katika Jiji la Baku, nchini Azerbaijan wakijadili namna ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi kwa kutafuta vyanzo vya fedha za uhakika za kutekeleza miradi mbalimbali ya kimkakati ya kukabiliana na changamoto hizo, ikiwemo kuhimiza matumizi ya nishati safi ya kupikia. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 , amezitaka nchi zilizoendelea kutimiza ahadi yao ya kutoa dola za marekani bilioni 500, sawa na dola bilioni 100 kila mwaka kwa ajili ya kuzisaidia nchi zinazoendelea kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi katika kipindi cha miaka mitano, kuanzia mwaka 2020 hadi mwaka 2025.
Mhe. Dkt. Nchemba (Mb), ametoa kauli hiyo wakati akichangia hoja katika Mkutano wa Ngazi ya Juu wa Mawaziri uliojadili namna ya kupata fedha kwa ajili ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, pembezoni mwa Mkutano wa 29 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP-29) unaofanyika katika Mji wa Baku, nchini Azerbaijan
Alisema kuwa ripoti ya Mkutano wa COP28, uliofanyika Dubai mwaka jana, inaonesha kwamba kuna kasi ndogo katika kutimiza ahadi ya Mkataba wa Paris katika kuhamasisha upatikanaji ama uchangiaji wa dola 100 bilioni ambapo kuna pengo la takribani dola bilioni 60 kila mwaka hali inayo ziathiri nchi zinazoendelea katika kupanga mipango ya maendeleo.
Aidha, Dkt. Nchemba alisema kuwa Tanzania inataka kuwe na uwazi katika namna fedha hizo dola bilioni 100 zinazotakiwa kutolewa kila mwaka kwa nchi zinzoendelea ili kuweka uwajibikaji kulingana na Mkataba wa Paris kuhusu suala hilo la kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Alisema kuwa mabadiliko ya Tabianchi ni janga linalobomoa Uchumi wan chi zinazoendelea na kushauri matamanio na ahadi zinazotolewa na mataifa makubwa yawekwe katika vitendo ili kuzinusuru nchi zinazoendelea kutokana na madhara yanayosababishwa na mabadiliko hayo ya tabianchi.
Dkt. Nchemba alisema kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazoendelea iliyoathirika na matokeo hasi ya mabadiliko ya tabianchi na inajitahidi kutumia rasilimali zake kukabiliana na athari hizo ikiwemo kurejesha miundombinu iliyoharibiwa na mafuriko lakini fedha hizo za ndani hazitoshelezi mahitaji.
“Pia tunatoa wito wa kupitia upya usanifu wa kifedha wa kimataifa na utaratibu wa ufadhili chini ya mkataba ili kusaidia uhamasishaji wa fedha thabiti na za muda mrefu kwa kiwango cha uwekezaji unaohitajika na nchi zinazoendelea kupambana na shida ya mabadiliko ya tabianchi” alisema Dkt. Nchemba” Alisisitiza Dkt. Nchemba..
Zaidi wa watu elfu 50, wakiwemo wanadiplomasia kutoka zaidi ya nchi 200 wanachama wa Umoja wa Mataifa, wanakutana katika Jiji la Baku, nchini Azerbaijan wakijadili namna ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi kwa kutafuta vyanzo vya fedha za uhakika za kutekeleza miradi mbalimbali ya kimkakati ya kukabiliana na changamoto hizo, ikiwemo kuhimiza matumizi ya nishati safi ya kupikia. -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
An honor engaging with @claverGatete, Our discussion of subtle macroeconomic methods, alternative capital mobilisation, and infrastructure fortification points to transformative possibilities. Looking forward to observable advancements.
#cop29baku
ECA
@ECA_OFFICIAL
Delighted to meet my brother @mwigulunchemba1, Finance Minister of #tanzania. We discussed collaboration on access to alternative finance sources, infrastructure development, and effective macroeconomic management to prioritize development needs - @ClaverGatete at #cop29baku
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, akiteta jambo na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), katika Banda la Maonesho la Tanzania, lilipo katika Uwanja wa Michezo wa Baku, unapofanyika Mkutano wa 29 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP-29), Jijini Baku nchini Azerbaijan, ambapo Mhe. Makamu wa Rais anaongoza Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huo akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
The Citizen Tanzania
@TheCitizenTz
Hope as dollar becomes widely available again, this along with a range of local and international news, exclusive stories and business insights, only in The Citizen this Tuesday, November 12, 2024.
Get your copy at your nearest newsstand or read online via Mwanaclick.
For Android users:
play.google.com/store/apps/details?id=com.mcl.mwanaclick
For iOS users:
apps.apple.com/tz/app/mwanaclick/id6483937075
website : www.thecitizen.co.tz
#empoweringthenation -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Bank of Tanzania
@BankOfTanzania
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Tanzania (DCEA), Aretas Lyimo, ambapo wamejadili masuala mbalimbali ya maendeleo ya Mamlaka hiyo, katika Ofisi ya Waziri wa Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma.
Kikao hicho kimehudhuriwa pia na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Kamishna Msaidizi wa Idara ya Usimamizi wa Bajeti, Bw. Andambike Mololo wa Wizara hiyo, Kamishna wa Utawala DCEA, Shaaban Khatib Baraza na Kamishna Msaidizi Mipango na Bajeti DCEA, Lusajo Gilbert . -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Kwa huzuni kubwa, nimesikitishwa na kifo cha Bw. Lawrence Nyasebwa Mafuru, Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, kilichotokea leo, tarehe 09 Novemba 2024, nchini India. Kabla ya uteuzi wake Tume ya Mipango, Marehemu alishika nafasi mbalimbali ikiwemo Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango. Pole kwa familia yake, Mhe Prof. Kitila Mkumbo Waziri wa Nchi (Mipango na Uwekezaji), Watumishi wa Tume ya Mipango, na wote walioguswa na msiba huu. Tutamkumbuka kwa mchango wake mkubwa na utumishi wa kujitolea. Bwana Ametoa na Bwana Ametwaa Jina lake lihimidiwe, Amina.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb) pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Mhe. Prof. @kitilam (Mb) na Waziri wa Madini Mhe. Antony Mavunde (Mb), wamekutana na kufanya mazungumzo jijini Dodoma kuhusu maendeleo ya Sekta ya madini na uwekezaji ili kuendelea kukuza Uchumi wa nchi.
Mkutano huo pia ulihudhuriwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Hamza Johari, Kamishna wa Idara ya Usimamizi wa Madeni Wizara ya Fedha, Bw. Japhet Justine na wajumbe wengine kutoka Wizara hizo tatu. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa Kampuni ya Black Rock Mining Limited, inayomiliki Kampuni Tanzu ya Faru Graphite, ukiongozwa na Mwenyeki wa Kampuni hiyo yenye Makao yake Makuu nchini Australia, Bw. Richard Crookes.
Mazungumzo hayo yalihusisha masuala ya utekelezaji wa Mradi wa Madini wa Mahenge Graphite uliopo mkoani Morogoro, ambapo Mhe. Dkt. Nchemba alieleza umuhimu wa mradi huo katika maendeleo ya nchi kiuchumi na kijamii na kwamba Serikali itahakikisha kuwa mradi huo unafanyakazi kama ulivyokusudiwa.
Mkutano huo ulihudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Mwenyekiti wa Kampuni Tanzu ya Faru Graphite, Bw. Ian Murray, Mkuu wa Masuala ya Fedha wa Kampuni ya Black Rock Mining Limited, Bw. Paul Sims, Meneja Uhusiano wa Kampuni Tanzu ya Faru, Bw. Alimiya Osman na wajumbe wengine kutoka Wizara ya Fedha na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), amewasilisha bungeni, Jijini Dodoma, Mapendekezo ya Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), amezindua rasmi utoaji wa Hati Fungani ijulikanayo kama "Bondi Yangu" ya Benki ya @azaniaBank_ltd , inayotarajia kukusanya jumla ya shilingi bilioni 100 kupitia soko la mitaji, hatua ambayo amesema ni kielelezo tosha cha umuhimu uliowekwa na Benki hiyo katika kukuza Sekta ya Fedha nchini. Tukio hilo limefanyika katika Hoteli ya Best Western, Jijini Dodoma.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Serikali imesema kuwa Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani imetoa msamaha wa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwenye uingizwaji wa vyakula vya mifugo ikiwemo vyakula vya Samaki vinavyotambulika kwa HS Code 23.09 chini ya utaratibu wa utozaji ushuru wa pamoja wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Hayo yameelezwa bungeni, jijini Dodoma na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Mheshimiwa Jacqueline Ngonyani Msongozi, aliyetaka kujua mpango wa Serikali wa kupunguza kodi ya uingizaji wa vyakula vya samaki nchini.
‘’Vifaa vinavyoagizwa kutoka nje na watu wanaojihusisha na ufugaji wa samaki na kilimo ambavyo Kamishna ameridhika kuwa ni kwa matumizi katika sekta ya ufugaji wa samaki vimeondolewa Ushuru wa Forodha kwa mujibu wa Kifungu cha 15(a) cha Sehemu B ya Jedwali la Tano ya Sheria ya Usimamizi wa Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, alisema Mhe. Nchemba.
Dkt. Nchemba alifafanua kuwa Serikali inaendela kuongea na sekta ili kuona maeneo ambayo yanastahili kupata ruzuku na tayari baadhi ya maeneo Serikali inatoa ruzuku na itaendelea kutoa ruzuku katika maeneo mbalimbali kwa kuzingatia upatikanaji wa fedha.
Aliongeza kuwa Serikali inaweka vivutio kwenye uzalishaji wa bidhaa ili kujitosheleza ndani ya nchi ili kupunguza uagizaji wa bidhaa kutoka nje na kuwa itaangalia maeneo ya maboresho katika bajeti ijayo kufanikisha kuongeza uzalishaji wa ndani. -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Jimbo la Iramba Magharibi tumepokea kwa Mshituko Mkubwa Sana taarifa za Kifo cha ndugu yetu, Mheshimiwa Kipenka Msemembo Mussa, Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Natoa pole kwa wote walioguswa na kifo chake. Alikuwa kiongozi wa mfano, na mchango wake katika sekta ya Sheria utakumbukwa daima. SUPIA NI MATILIGA TATA😭
Amina. -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Nchini Marekani, nimeshuhudia utiaji saini wa makubaliano ya ufadhili wa dola za Marekani milioni 225 kati ya CRDB Bank PLC na @mufgbk_official ya Japan, kwa ajili ya miradi ya kuhifadhi mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Pia, nimeshiriki mjadala wa kuiwezesha Afrika kuwa na nishati ya uhakika, ulioandaliwa na Mission 300, ambapo nimesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya nchi za Afrika, Taasisi za Fedha za Kimataifa, na Sekta Binafsi katika kuhakikisha uwekezaji wa nishati nafuu na endelevu kwa maendeleo ya kiuchumi na fursa za ajira barani Afrika.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
The 2nd African Association of Accountants General (AAAG) will be held from December 2-5, 2024, in Arusha, Tanzania.
Register now at conference.aaag.org.zm.
Don't miss it!
@AfricanAGs -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), akiteta jambo na Mkurugenzi Mkaazi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania, Bw. @BeleteNathan , Makao Makuu ya Benki ya Dunia jijini Washington D.C nchini Marekani ambapo Dkt. Nchemba anaongoza ujumbe wa Tanzania katika Mikutano ya Mwaka ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF). Bw. Belete ndiye msimamizi wa sera na mipango mbalimbali ya Benki ya Dunia nchini Tanzania na amekuwa kiungo muhimu kati ya Serikali na Benki hiyo.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), ameshuhudia utiaji saini wa makubalino ya ufadhili wa dola za Marekani milioni 225 kati ya @CRDBBankPlc na Benki ya @mufgbk_official ya Japan, kwa ajili ya kuwezesha utekelezaji wa miradi yenye mlengo wa kuhifadhi mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi. Benki ya CRDB imewakilishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Bw. Abdulmajid Nsekela na kwa upande wa MUFG Bank, mkataba huo umesainiwa na Mkurugenzi Mtendaji anayesimamia Masoko, Bw. Christopher Marks.
Tukio hilo limefanyika katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania Jijini Washington D.C nchini Marekani, Kando ya Mikutano ya Mwaka ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), ambapo Mhe. Dkt. Nchemba anaongoza ujumbe wa Tanzania katika mikutano hiyo na kushuhudiwa pia na Waziri wa Nchi, Fedha na Mipango-Zanzibar, Dkt. Saada Mkuya Salum, Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Dkt. Elsie Kanza, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba, na viongozi wengine waandamizi wa Serikali na Benki ya CRDB -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Tumekamilisha kwa mafanikio makubwa Mikutano ya Mwaka ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) iliyofanyika jijini Washington D.C., Marekani. Ujumbe wa Tanzania ulijikita katika mijadala ya kisekta, ikilenga kuimarisha diplomasia ya kiuchumi na ushirikiano na Taasisi za kifedha za kimataifa kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), amerejea wito wa Tanzania kwa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), kukifanya Kiswahili kuwa miongozi mwa lugha rasmi za mawasiliano katika mikutano ya Taasisi hizo kubwa za Fedha Duniani.
Dkt. Nchemba ametoa rai hiyo alipoongoza Ujumbe wa Tanzania katika mazungumzo na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika, Bi. @VictoriaKwakwa , Jijini Washington D.C, nchini Marekani, ambako Mikutano ya Mwaka ya Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF na Benki ya Dunia inafanyika.
Amesisitiza kuwa Kiswahili ni lugha ya Afrika na pia ni lugha rasmi inayotumika katika Mikutano ya Umoja wa Afrika hivyo imefika wakati kwa Taasisi hizo kubwa za Fedha Duniani kukifanya Kiswahili kuwa miongoni mwa lugha zinazotambulika rasmi na kutumika katika Mikutano ya Benki ya Dunia na IMF.
Katika hatua nyingine, Dkt. Nchemba ameishukuru pia Benki ya Dunia kwa kuahidi kusaidia ujenzi wa mradi mkubwa wa Reli ya Kisasa SGR, unaoendelea nchini Tanzania kwa kuwa mradi huo ni miongozi mwa miradi ya kipaumbele ya kitaifa kutokana na umuhimu wake katika kukuza biashara na uchumi wa nchi na mataifa mengine yatakayounganishwa na Reli hiyo.
Aidha, Dkt. Nchemba, ametoa shukrani kwa uamuzi wa Benki ya Dunia, kubeba ajenda ya kuwawezesha na kuwajengea uwezo wakandarasi wa ndani ili waweze kushiriki katika utekelezaji wa miradi mbalimbali inayotekelezwa nchini Tanzania kupitia ufadhili wa Benki ya Dunia na IMF badala ya mfumo wa sasa unaowanufaisha zaidi wakandarasi wa kigeni.
Kwa upande wake, Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia Kanda ya Afrika Mashariki, Bi. Victoria Kwakwa, aliahidi kuwa Benki ya Dunia itaendelea kushirikiana na Tanzania kwa kuiwezesha kutimiza malengo yake ya kimaendeleo na kiuchumi kupitia misaada ya kiufundi na kifedha.
Bi. Kwakwa ameeleza kuwa mradi wa Reli ya Kisasa wa SG, mradi wa kusambaza nishati ya umeme hususan vijijini, kuwawezesha wakandarasi kupata zabuni za miradi na mradi wa kuboresha elimu ni miongoni mwa mipango itakayopewa kipaumbele ili kuharakisha maendeleo ya watu na kuimarisha uchumi wa Tanzania.
Ameipongeza Tanzania kwa kukubali kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika wa Kilele cha Nishati utakaofanyika Jijini Dar es Salaam mwishoni mwa mwezi Januari mwakani (2025), ambapo itasainiwa mikataba ya ufadhili wa usambazaji wa nishati kwa nchi 15 za kwanza zilizoteuliwa kunufaika na mpango huo ikiwemo Tanzania, ambapo lengo la mkakati huo ni kuwafikia zaidi ya watu milioni 300 Barani Afrika kwa kuwaunganisha na umeme ifikapo mwaka 2030. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 , Mb), akishiriki Kilele cha Mkutano wa Mwaka wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), uliofanyika katika Ukumbi wa DAR Constitution, Jijini Washington D.C, nchini Marekani na kuhutubiwa na Viongozi Wakuu wa Taasisi hizo, Rais wa Benki ya Dunia, Bw. Ajay Banga na Mkurugezi Mtendaji wa Shirika la Fedha na Kimataifa, Bi. Kristalina Georgieva. Wanaoonekana katika picha ni Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba (nyuma) na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya (kushoto)
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Taasisi ya Benki ya Dunia inayojihusisha na utoaji mikopo na misaada kwenye sekta binafsi (International Finance Corporation ( @IFC_org ), Bw. Sergio Pimenta, ambapo walijadili mipango ya uendelezaji sekta binafsi na uwekezaji nchini Tanzania, mkutano uliofanyika kando ya Mikutano ya Mwaka ya Benki ya Dunia iliyoandaliwa na Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Jijini Washington D.C, Marekani.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), ameongoza Ujumbe wa Tanzania katika mkutano na Mkurugenzi Mtendaji wa Masuala ya Utawala na Uendeshaji wa Benki ya Dunia, Bi. @bjerde_anna , uliofanyika Jijini Washington D.C, nchini Marekani, ambapo masuala mtambuka ya ushirikiano kati ya Benki ya Dunia na Tanzania yalijadiliwa, ikiwemo maandalizi ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Nishati, utakaofanyika Jijini Dar es Salaam, mwezi Januari mwaka 2025.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Abertus Paschal 🇹🇿𝕏
@rutaraka
📍 Washington D.C
🇹🇿🇺🇸
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), amerejea wito wa Tanzania kwa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), kukifanya Kiswahili kuwa miongozi mwa lugha rasmi za mawasiliano katika mikutano ya Taasisi hizo kubwa za Fedha Duniani.
Dkt. Nchemba ametoa rai hiyo alipoongoza Ujumbe wa Tanzania katika mazungumzo na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika, Bi. @VictoriaKwakwa Jijini Washington D.C, nchini Marekani, ambako Mikutano ya Mwaka ya Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF na Benki ya Dunia inafanyika.
Amesisitiza kuwa Kiswahili ni lugha ya Afrika na pia ni lugha rasmi inayotumika katika Mikutano ya Umoja wa Afrika hivyo imefika wakati kwa Taasisi hizo kubwa za Fedha Duniani kukifanya Kiswahili kuwa miongoni mwa lugha zinazotambulika rasmi na kutumika katika Mikutano ya Benki ya Dunia na IMF.
Katika hatua nyingine, Dkt. Nchemba ameishukuru pia Benki ya Dunia kwa kuahidi kusaidia ujenzi wa mradi mkubwa wa Reli ya Kisasa SGR, unaoendelea nchini Tanzania kwa kuwa mradi huo ni miongozi mwa miradi ya kipaumbele ya kitaifa kutokana na umuhimu wake katika kukuza biashara na uchumi wa nchi na mataifa mengine yatakayounganishwa na Reli hiyo.
Aidha, Dkt. Nchemba, ametoa shukrani kwa uamuzi wa Benki ya Dunia, kubeba ajenda ya kuwawezesha na kuwajengea uwezo wakandarasi wa ndani ili waweze kushiriki katika utekelezaji wa miradi mbalimbali inayotekelezwa nchini Tanzania kupitia ufadhili wa Benki ya Dunia na IMF badala ya mfumo wa sasa unaowanufaisha zaidi wakandarasi wa kigeni.
Kwa upande wake, Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia Kanda ya Afrika Mashariki, Bi. Victoria Kwakwa, aliahidi kuwa Benki ya Dunia itaendelea kushirikiana na Tanzania kwa kuiwezesha kutimiza malengo yake ya kimaendeleo na kiuchumi kupitia misaada ya kiufundi na kifedha.
Bi. Kwakwa ameeleza kuwa mradi wa Reli ya Kisasa wa SG, mradi wa kusambaza nishati ya umeme hususan vijijini, kuwawezesha wakandarasi kupata zabuni za miradi na mradi wa kuboresha elimu ni miongoni mwa mipango itakayopewa kipaumbele ili kuharakisha maendeleo ya watu na kuimarisha uchumi wa Tanzania.
Ameipongeza Tanzania kwa kukubali kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika wa Kilele cha Nishati utakaofanyika Jijini Dar es Salaam mwishoni mwa mwezi Januari mwakani (2025), ambapo itasainiwa mikataba ya ufadhili wa usambazaji wa nishati kwa nchi 15 za kwanza zilizoteuliwa kunufaika na mpango huo ikiwemo Tanzania, ambapo lengo la mkakati huo ni kuwafikia zaidi ya watu milioni 300 Barani Afrika kwa kuwaunganisha na umeme ifikapo mwaka 2030.
📸: W/Fedha -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa rais wa benki ya Dunia anayesimamia Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini, Bw. @VictoriaKwakwa , Jijini Washington D.C, nchini Marekani, ambapo mazungumzo hayo yalilenga namna kuimarisha ushirikiano wa muda mrefu uliopo kati ya Tanzania na Benki hiyo. Benki ya Dunia imeahidi kuendelea kushirikiana na Tanzania katika kuimarisha sera za kiuchumi na kifedha pamoja kusaidia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kiuchumi na kijamii ili kuharakisha zaidi maendeleo ya nchi.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha wa Burundi, Mhe. Audace Niyonzima, Jijini Washington D.C, nchini Marekani, ambapo mazungumzo yao yalilenga namna ya kupata fedha kutoka Benki ya Dunia na IMF, kwa ajili ya kujenga Reli ya Kisasa ya SGR itakayounganisha nchi hizo mbili kuanzia Uvinza- Msongati-Gitega - Uvira hadi Kindu nchini Burundi.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia, anayesimamia Kundi la Kwanza la nchi za Kanda ya Afrika (Africa Group 1 Constituency), Dkt. Floribert Ngaruko, Makao Makuu ya Benki hiyo Jijini Washington D.C, nchini Marekani, ambapo walizungumzia kuhusu ushirikiano kati ya Tanzania na Benki hiyo. Tazania ilisisitiza maombi yake ya kutaka Kiswahili kiwe sehemu ya lugha rasmi za mawasiliano katika mikutano ya Benki ya Dunia kutokana na umuhimu wake katika maendeleo ya Bara la Afrika na Duniani kwa ujumla. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango - Zanzibar, Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum, alikuwepo katika mazungumzo hayo.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Mary Porter Peschka
@MPPeschka
IFC is increasing its presence in Tanzania and increasing support for the private sector. Excellent meeting with @mofURT’s @mwigulunchemba1 at #wbmeetings.
Sergio Pimenta
@SergioPimenta_
In #tanzania, @IFC_org is focused on affordable #housing, access to finance, and women's economic empowerment, among others. I discussed these priorities and more with the Tanzanian delegation led by Finance Minister, H.E. Mwigulu Nchemba, at the #wbgmeetings.
#ifcinafrica -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Asante sana, Sergio Pimenta @SPimentaIFC, na @IFC_org kwa kujitolea kuunga mkono ajenda za maendeleo ya kiuchumi ya Tanzania. Tunaamini kuwa uwekezaji wenu katika nyumba nafuu, upatikanaji wa fedha, na uwezeshaji wa wanawake utakuwa na mchango mkubwa katika kuboresha maisha ya Watanzania. Ushirikiano wetu ni hatua muhimu kuelekea mustakabali thabiti wa Taifa letu.
Sergio Pimenta
@SergioPimenta_
In #tanzania, @IFC_org is focused on affordable #housing, access to finance, and women's economic empowerment, among others. I discussed these priorities and more with the Tanzanian delegation led by Finance Minister, H.E. Mwigulu Nchemba, at the #wbgmeetings.
#ifcinafrica -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Ilikuwa kikao kizuri sana, @DFC_CEO @DFCgov. Tunashukuru kwa dhamira yenu ya kuunga mkono maendeleo ya kiuchumi ya Tanzania. Ushirikiano wetu utakuwa kichocheo muhimu kwa sekta binafsi.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Marekani (International Development Finance Corporation), Bw. Scott Nathan, ambapo wamejadili kuhusu ushirikianao kati ya Tanzania na Shirika hilo katika sekta mbalimbali za uzalishaji ikiwemo madini, ukuzaji biashara ndogondogo na kuisaidia sekta binafsi ili kuharakisha maendeleo ya nchi. Mkutano huo umefanyika kando ya Mikutano ya Mwaka ya Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF na Benki ya Dunia inayoendelea Jijini Washington D.C, nchini Marekani.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Jambo TV
@Jambotv_
Benki ya Dunia, imemchagua Mtanzania, Dkt. Zarau Wendeline Kibwe, kuwa Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Benki ya Dunia atakayesimamia Kanda Namba Moja ya Afrika inayojumuisha nchi 22 ikiwemo Tanzania, nafasi ambayo Tanzania imewahi kuihudumu miaka 54 iliyopita.
Uamuzi wa Dkt. Kibwe kuikwaa nafasi hiyo nyeti katika taasisi hiyo kubwa ya Fedha Duniani, umetangazwa katika Mkutano wa Mwaka wa Kundi la Kwanza la Nchi za Afrika wa Benki ya Dunia, uliofanyika Jijini Washington D.C, nchini Marekani ambapo Mikutano ya Mwaka ya Shirika la Fedha Duniani (IMF) na Benki ya Dunia inafanyika.
Kabla ya kuchaguliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Benki hiyo atakayesimamia Kanda Namba Moja ya Afrika, Dkt. Kibwe alihudumu katika ofisi hiyo ya bodi kama Naibu Mkurugenzi Mtendaji, Mshauri na Mshauri Mwandamizi kwa zaidi ya miaka saba, tangu mwaka 2017.
Akizungumza Jijini Washington D.C, baada ya kutangazwa kuchukua nafasi hiyo, Dkt. Zarau Wendeline Kibwe amesema kuwa ataitumia nafasi hiyo kusimamia uendeshaji wa benki na taasisi zake pamoja na kutetea maslahi ya nchi katika Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Dunia pamoja na maslahi ya Kanda ya Afrika anayoisimamia ili kukuza maendeleo na uchumi wa nchi hizo.
Akizungumza kwa niaba ya Serikali katika Mkutano huo uliomtangaza Dk. Kibwe kuchukua nafasi hiyo, Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, anayeongoza Ujumbe wa Tanzania katika mikutano hiyo ya mwaka ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia, amesema kuwa hayo ni matokeo ya juhudi za Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, anavyoifungua nchi na kukuza Diplomasia ya Kimataifa.
Dkt. Nchemba amempongeza Dkt. Kibwe kwa kupata nafasi hiyo na kwamba kutokana na umahiri wake katika masuala ya uchumi na fedha, pamoja na uzoefu wake wa muda mrefu katika ofisi hiyo, anaamini kuwa maslahi ya nchi yataendelea kulindwa ipasavyo kwa manufaa ya Watanzania.
Dkt. Zarau Wendeline Kibwe ni mchumi wa Kitanzania ambaye hivi karibuni amechaguliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia kwa Kanda Namba Moja ya Afrika inayojumuisha nchi za Botswana, Burundi, Eritrea, Eswatini, Ethiopia, Gambia, Kenya, Lesotho, Liberia, Malawi, Msumbiji, Namibia, Rwanda, Shelisheli, Sierra Leone, Somalia, Sudan Kusini, Sudan, Tanzania, Uganda, Zambia, na Zimbabwe.
Kabla ya kujiunga na Ofisi ya Bodi, Dkt Kibwe alihudumu kama Mchumi wa Benki ya Dunia kwa Tanzania ambapo katika kipindi cha miaka 15 ya kazi yake, Dkt. Kibwe amehudumu katika Serikali ya Jamhuri wa Muungano katika nafasi mbalimbali ikiwemo ya Mchambuzi Mwanadamizi wa Sera (Ofisi ya Rais – Tume ya Mipango), Mhadhiri Msaidizi (Chuo Kikuu Dodoma), Afisa Forodha Msaidizi (Mamlaka ya Mapato Tanzania), na Mhadhiri Msaidizi (Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere).
Dkt. Kibwe ana Shahada ya Uzamivu (Ph.D.) katika Uchumi wa Maendeleo, Shahada ya Uzamili (MA) katika Uchumi wa Maendeleo, na Shahada ya Umahiri katika Sera za Umma, zote kutoka Taasisi ya Taifa ya Mafunzo ya Sera (GRIPS) huko Tokyo, Japan.
Alipata Shahada yake ya Kwanza ya Sayansi katika Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe kilichopo Morogoro, Tanzania. -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Hongera sana Dkt. Zarau Wendeline Kibwe @zaweki kwa kuchaguliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Benki ya Dunia atakayesimamia Kanda Namba Moja ya Afrika inayojumuisha nchi 22 ikiwemo Tanzania, nafasi ambayo Tanzania imewahi kuihudumu miaka 54 iliyopita. Nafasi hii ni ushuhuda wa umahiri na juhudi kubwa za Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika diplomasia ya kimataifa. Tanzania imeandika historia tena.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Benki ya Dunia, imemchagua Mtanzania, Dkt. Zarau Wendeline Kibwe, kuwa Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Benki hiyo atakayesimamia Kanda Namba Moja ya Afrika inayojumuisha nchi 22 ikiwemo Tanzania, nafasi ambayo Tanzania imewahi kuihudumu miaka 54 iliyopita.
Uamuzi wa Dkt. Kibwe kuikwaa nafasi hiyo nyeti katika Taasisi hiyo kubwa ya Fedha Duniani, umetangazwa katika Mkutano wa Mwaka wa Kundi la Kwanza la Nchi za Afrika wa Benki ya Dunia, uliofanyika Jijini Washington D.C, nchini Marekani ambapo Mikutano ya Mwaka ya Shirika la Fedha Duniani IMF na Benki ya Dunia inafanyika.
Kabla ya kuchaguliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Benki hiyo atakayesimamia Kanda Namba Moja ya Afrika, Dkt. Kibwe alihudumu katika Ofisi hiyo ya Bodi kama Naibu Mkurugenzi Mtendaji, Mshauri na Mshauri Mwandamizi kwa zaidi ya miaka saba, tangu mwaka 2017.
Akizungumza Jijini Washington D.C, baada ya kutangazwa kuchukua nafasi hiyo, Dkt. Zarau Wendeline Kibwe amesema kuwa ataitumia nafasi hiyo kusimamia uendeshaji wa Benki na Taasisi zake Pamoja na kutetea Maslahi ya nchi katika Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Dunia pamoja na maslahi ya Kanda ya Afrika anayoisimamia ili kukuza maendeleo na uchumi wa nchi hizo.
Akizungumza kwa niaba ya Serikali katika Mkutano huo uliomtangaza Dkt. Kibwe kuchukua nafasi hiyo, Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 , anayeongoza Ujumbe wa Tanzania katika Mikutano hiyo ya Mwaka ya Shirika la Fedha la Kimataifa – IMF na Benki ya Dunia, amesema kuwa hayo ni matokeo ya juhudi za Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, anavyoifungua nchi na kukuza Diplomasia ya Kimataifa.
Dkt. Nchemba amempongeza Dkt. Kibwe kwa kupata nafasi hiyo na kwamba kutokana na umahili wake katika masuala ya uchumi na fedha, pamoja na uzoefu wake wa muda mrefu katika Ofisi hiyo, anaamini kuwa maslahi ya nchi yataendelea kulindwa ipasavyo kwa manufaa ya watanzania.
Dkt. Zarau Wendeline Kibwe ni mchumi wa kitanzania ambaye hivi karibuni amechaguliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia kwa Kanda Namba Moja ya Afrika inayojumuisha nchi za Botswana, Burundi, Eritrea, Eswatini, Ethiopia, Gambia, Kenya, Lesotho, Liberia, Malawi, Msumbiji, Namibia, Rwanda, Shelisheli, Sierra Leone, Somalia, Sudan Kusini, Sudan, Tanzania, Uganda, Zambia, na Zimbabwe.
Kabla ya kujiunga na Ofisi ya Bodi, Dkt Kibwe alihudumu kama Mchumi wa Benki ya Dunia kwa Tanzania ambapo katika kipindi cha miaka 15 ya kazi yake, Dkt. Kibwe amehudumu katika Serikali ya Jamhuri wa Muungano katika nafasi mbalimbali ikiwemo ya Mchambuzi Mwanadamizi wa Sera (Ofisi ya Rais – Tume ya Mipango), Mhadhiri Msaidizi (Chuo Kikuu Dodoma), Afisa Forodha Msaidizi (Mamlaka ya Mapato Tanzania), na Mhadhiri Msaidizi (Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere).
Dkt. Kibwe ana Shahada ya Uzamivu (Ph.D.) katika Uchumi wa Maendeleo, Shahada ya Uzamili (MA) katika Uchumi wa Maendeleo, na Shahada ya Umahiri katika Sera za Umma, zote kutoka Taasisi ya Taifa ya Mafunzo ya Sera (GRIPS) huko Tokyo, Japani.
Alipata Shahada yake ya Kwanza ya Sayansi katika Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe kilichopo Morogoro, Tanzania. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), ameongoza Ujumbe wa Tanzania, katika Mkutano wa Shirika la Fedha la Kimataifa (@IMFNews ) wa Mawaziri wa Fedha na Magavana wa Benki Kuu wa Kundi la Kwanza la Nchi za Afrika (Africa Group I Constituency) uliofanyika Makao Makuu ya Shirika hilo Jijini Washington D.C nchini Marekani, ambapo pamoja na mambo mengine, Mkutano huo ulijadili masuala ya kiutawala na namna ya nchi wanachama za Ukanda huo wa Afrika zinavyoweza kukabiliana na changamoto za athari hasi za mabadiliko ya tabianchi na kukuza Uchumi kwa kushirikiana na Taasisi hiyo kubwa ya Fedha Duniani.
Ujumbe wa Tanzania umewahusisha Viongozi mbalimbali wakiwemo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango-Zanzibar, Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya, Gavana wa Banki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba, Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, anayesimamia Sera za Fedha na Uchumi Dkt. Yamungu Kayandabila, na Viongozi wengine waandimizi wa Serikali. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), ameongoza Ujumbe wa Tanzania, kukutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji na Rais wa Mfuko wa Bezos Earth (Bezos Earth Fund), Dkt. Andrew Steer, ambapo walijadili kuhusu fursa za Taasisi hiyo kuwekeza nchini Tanzania katika sekta mbalimbali za kiuchumi na kijamii.
Tukio hilo limefanyika katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania, Jijini Washington D.C, nchini Marekani, kando ya Mikutano ya Mwaka ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia, ambapo katika Mkutano huo alikuwepo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Zanzibar, Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Dkt. Elsie Sia Kanza, na maafisa wengine waandamizi wa Serikali na Mfuko huo (Bezos Earth Fund).
Bezos Earth Fund ni Mfuko unaoshughulika na kusaidia nchi mbalimbali kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwa kuwekeza, pamoja na mambo mengine, kwenye sekta ya hifadhi ya mazingira, kilimo endelevu, nishati jadidifu, viwanda na kusaidia upatikanaji na matumizi ya teknolojia za kuhifadhi na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
@BezosEarthFund -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Jambo TV
@Jambotv_
Licha ya changamoto kubwa zinazokumba uchumi wa dunia, Tanzania imefanikiwa kujiimarisha kiuchumi na kuingia kwenye orodha ya nchi kumi bora barani Afrika kwa Pato la Taifa (GDP) kwa mwaka 2024 ikishika nafasi ya 10, hiyo ni kulingana na ripoti mpya ya Mtazamo wa Uchumi wa Dunia (WEO) iliyotolewa na Shirika la Fedha Duniani (IMF) mwezi Oktoba, 2024.
Katika mkutano wa mwaka wa IMF uliofanyika Washington, Marekani, uchumi wa Tanzania unatarajiwa kufikia dola za Kimarekani bilioni 79.87 ifikapo mwisho wa mwaka 2024.
Ukuaji huu umeelezwa kuwa ishara ya mafanikio ya sera bora na uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, ambaye ameendelea kusisitiza umuhimu wa maendeleo shirikishi katika sekta muhimu za kilimo, utalii, na viwanda.
Ukuaji wa uchumi wa Tanzania umeonekana kuwa endelevu na unaonyesha matumaini makubwa kwa miaka ijayo. Kulingana na makadirio ya IMF, ukuaji wa Pato la Taifa (GDP) wa Tanzania ulifikia asilimia 5.1 mwaka 2023 na unatarajiwa kuongezeka hadi asilimia 5.4 mwaka 2024, huku ikikadiriwa kufikia asilimia 6.0 mwaka 2025. Ukuaji huu unadhihirisha kuwa Tanzania inaimarisha misingi ya uchumi imara, licha ya changamoto za kimataifa kama vile mabadiliko ya tabianchi, bei za mafuta, na migogoro ya kikanda.
Kulingana na taarifa hiyo, Afrika Kusini inaongoza ikiwa na ukuaji wa uchumi wa Dola bilioni 403, ikifuatiwa na Misri (Dola Bil. 380). Kwa mataifa ya Afrika Mashariki katika orodha hiyo ukiachana na Tanzania, ni nchi ya Kenya ambayo ipo nafasi ya saba ikiwa na Dola bil. 116.3.
Kiujumla, Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) kupitia kwa Mkurugenzi mkuu wa shirika hilo, Kristalina Georgieva linatabiri ukuaji wa asilimia 4.2 kwa Afrika ifikapo mwaka 2025, huku likiona ukuaji thabiti lakini wa polepole barani humo.
“Eneo la Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara linaonyesha viwango vya ukuaji ambavyo viko thabiti mwaka huu ikilinganishwa na mwaka uliopita, takriban asilimia 3.6, na tunatarajia kuongezeka hadi takriban asilimia 4.2 mwakani,” alisema Pierre-Olivier Gourinchas, Mchumi Mkuu wa IMF.
Kulingana na takwimu za IMF kuhusu uchumi wa nchi zinazoendelea na masoko yanayokua, Tanzania imeweza kudhibiti viwango vya mfumuko wa bei ukilinganisha na baadhi ya nchi jirani. Kwa mfano, mwaka 2024, nchi nyingi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara zinatarajia mfumuko wa bei wa juu zaidi, kama vile Angola (asilimia 18.1) na Ghana (asilimia 19.5), wakati Tanzania inaendelea kusimama imara na viwango vya wastani vya mfumuko wa bei.
“Mfumuko wa bei unadhibitiwa katika baadhi ya nchi... na kufikia viwango karibu na malengo, lakini nusu ya nchi bado ziko mbali sana na malengo hayo, na theluthi moja bado zinakabiliwa na mfumuko wa bei wa tarakimu mbili,” alisema Jean-Marc Natal, Mkuu wa Idara ya Utafiti, IMF.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo ya IMF, ukuaji wa uchumi katika nchi za Afrika hasa Kusini mwa Jangwa la Sahara umekuwa wa polepole lakini endelevu. Ukuaji huo unakadiriwa kufikia asilimia 4.2 ifikapo mwaka 2025, kutoka asilimia 3.6 mwaka 2024. Ripoti hiyo inaeleza kuwa ukanda huu umekumbwa na changamoto mbalimbali kama vile mabadiliko ya tabianchi na migogoro, hali inayofanya ukuaji wa uchumi kuwa wa kusuasua katika baadhi ya nchi. Hata hivyo, Tanzania imeweza kuvuka vikwazo hivyo na kuendelea kujenga uchumi wa kisasa unaojumuisha sekta mbalimbali muhimu kama kilimo, viwanda, na utalii. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb) akiteta jambo na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini, Bi. @VictoriaKwakwa baada ya kukamilika kwa mjadala uliohusu kuiwezesha Afrika kuwa na nishati ya uhakika, ulioandaliwa na Taasisi ya Mission 300, Kando ya Mikutano ya Mwaka ya Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF na Benki ya Dunia. Jijini Washington D.C nchini Marekani, ambapo Dkt. Nchemba alikuwa mtoa mada katika mjadala huo.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb) na Rais wa Benki ya Dunia, Bw. Ajay Banga wakiteta jambo kabla ya Mkutano wa Mawaziri wa Fedha na Magavana wa Benki Kuu za nchi za Afrika (African Caucus - WB) Jijini Washington D.C, nchini Marekani, ambako Dkt. Nchemba, anaongoza Ujumbe wa Tanzania katika Mikutano ya Mwaka ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Jambo TV
@Jambotv_
Waziri wa Fedha wa Tanzania Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu ameshiriki Mkutano wa Mawaziri wa Fedha na Magavana wa Benki Kuu za nchi za Afrika (African Caucus - WB) uliomshirikisha Rais wa Benki ya Dunia, Bw. Ajay Banga, Jijini Washington D.C, nchini Marekani, ambako Dkt. Nchemba, anaongoza Ujumbe wa Tanzania katika Mikutano ya Mwaka ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia.
Mkutano huo uliwapa fursa Mawaziri wa Fedha na Magavana wa Benki Kuu za Afrika kuwasilisha vipaumbele na changamoto zinazoathiri maendeleo barani Afrika kwa Rais wa Benki ya Dunia Bw. Ajay Banga, ili kuzingatiwa katika mipango na mikakati ya ushirikiano kati ya Benki ya Dunia na nchi za Afrika.
Baadhi ya changamoto zilizoainishwa ni pamoja na fursa chache za ajira kwa vijana, miundombinu hafifu ya umeme, barabara na tehama, uzalishaji mdogo wa chakula, tishio katika uhimilivu wa madeni, na ongezeko la gharama za upatikanaji wa mikopo.
Bw. Banga alikubaliana na umuhimu wa upatikanaji wa umeme wa uhakika na wa kutosha katika kuchochea shughuli za uchumi na namna unavyoweza kuathiri uzalishaji wa mbolea na chakula.
Amebainisha kuwa Benki ya Dunia ipo tayari kusaidia utekelezaji wa miradi ya umeme ambayo inahusisha matumizi ya nishati rafiki kwa mazingira na kuhimiza matumizi ya TEHAMA hususan kwa kundi kubwa la vijana kwa kuwa ni chanzo moja wapo kikubwa cha ajira. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Abertus Paschal 🇹🇿𝕏
@rutaraka
📍Washington DC, Marekani
🇹🇿🇺🇸
▪️IMF YAIMWAGIA SIFA TANZANIA USIMAMIZI WA SERA ZA UCHUMI
Shirika la Fedha la Kimataifa - IMF, limeimwagia sifa Tanzania kwa namna inavyosimamia sera zake za uchumi na fedha ikiwemo kudhibiti kasi ya mfumuko wa bei ikilinganishwa na nchi nyingi za Afrika.
Pongezi hizo zimetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa IMF anayesimamia Kundi la Kwanza la Nchi za Afrika, Bw. Willie Nakunyanda, alipokutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa Tanzania unaoshiriki Mikutano ya Mwaka ya Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF na Benki ya Dunia, ukiongozwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb.), Makao Makuu ya Taasisi hiyo, Jijini Washington D.C, nchini Marekani.
Kiongozi huyo amesema kuwa nchi nyingine za Afrika zinalo la kujifunza kuhusu usimamizi wa uchumi na sera za fedha kutoka Tanzania kutokana na umahili wake katika eneo hilo ambapo nchi imekuwa imara kiuchumi licha ya misukosuko mingi ya kiuchumi na kijamii inayojitokeza duniani.
📸: W/Fedha -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Shirika la Fedha la Kimataifa - IMF, limeimwagia sifa Tanzania kwa namna inavyosimamia sera zake za uchumi na fedha ikiwemo kudhibiti kasi ya mfumuko wa bei ikilinganishwa na nchi nyingi za Afrika.
Pongezi hizo zimetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa IMF anayesimamia Kundi la Kwanza la Nchi za Afrika, Bw. Willie Nakunyanda, alipokutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa Tanzania unaoshiriki Mikutano ya Mwaka ya Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF na Benki ya Dunia, ukiongozwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 , Makao Makuu ya Taasisi hiyo, Jijini Washington D.C, nchini Marekani.
Kiongozi huyo amesema kuwa nchi nyingine za Afrika zinalo la kujifunza kuhusu usimamizi wa uchumi na sera za fedha kutoka Tanzania kutokana na umahili wake katika eneo hilo ambapo nchi imekuwa imara kiuchumi licha ya misukosuko mingi ya kiuchumi na kijamii inayojitokeza duniani. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 , ameshiriki mjadala kuhusu kuiwezesha Afrika kuwa na nishati ya uhakika, ulioandaliwa na Taasisi ya Mission 300, Kando ya Mikutano ya Mwaka ya Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF na Benki ya Dunia. Jijini Washington D.C nchini Marekani, na kuzihimiza nchi za Afrika kwa kushirikiana na Taasisi za Fedha Duniani pamoja na Sekta Binafsi, kuhakikisha kuwa zinawekeza kwenye uzalishaji wa nishati ya uhakika na yenye gharama nafuu ili kutimiza malengo ya kujiimarisha kiuchumi, kuchochea uwekezaji, uzalishaji wa bidhaa na huduma na kukuza ajira.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), ameshiriki Mkutano wa Mawaziri wa Fedha na Magavana wa Benki Kuu za nchi za Afrika (African Caucus - WB) uliomshirikisha Rais wa Benki ya Dunia, Bw. Ajay Banga, Jijini Washington D.C, nchini Marekani, ambako Dkt. Nchemba, anaongoza Ujumbe wa Tanzania katika Mikutano ya Mwaka ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia.
Mkutano huo uliwapa fursa Mawaziri wa Fedha na Magavana wa Benki Kuu za Afrika kuwasilisha vipaumbele na changamoto zinazoathiri maendeleo barani Afrika kwa Rais wa Benki ya Dunia Bw. Ajay Banga, ili kuzingatiwa katika mipango na mikakati ya ushirikiano kati ya Benki ya Dunia na nchi za Afrika. Baadhi ya changamoto zilizoainishwa ni pamoja na: fursa chache za ajira kwa vijana; miundombinu hafifu ya umeme, barabara na tehama; uzalishaji mdogo wa chakula; tishio katika uhimilivu wa madeni; na ongezeko la gharama za upatikanaji wa mikopo.
Bw. Banga alikubaliana na umuhimu wa upatikanaji wa umeme wa uhakika na wakutosha katika kuchochea shughuli za uchumi na namna unavyoweza kuathiri uzalishaji wa mbolea na chakula. Hivyo alibainisha kuwa Benki ya Dunia ipo tayari kusaidia utekelezaji wa miradi ya umeme ambayo inahusisha matumizi ya nishati rafiki kwa mazingira na kuhimiza matumizi ya TEHAMA hususan kwa kundi kubwa la vijana kwa kuwa ni chanzo moja wapo kikubwa cha ajira.
@WorldBank -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Abertus Paschal 🇹🇿𝕏
@rutaraka
📍Washington DC, Marekani
🇹🇿🇺🇸
Ujumbe wa Tanzania, ukiongozwa na Waziri wa Fedha Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb.) umekutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha Duniani (IMF), anayesimamia Kundi la Kwanza la Nchi za Afrika (Africa Group 1 Constituency), Bw. Willie Nakuyanda.
Katika kikao hicho, Bw. Nakuyanda aliipongeza Tanzania kwa usimamizi bora wa uchumi, akisisitiza mafanikio ya programu ya "Extended Credit Facility" ambayo inanufaika nayo kupitia IMF.
Vilevile, alielezea kuridhishwa na jinsi Benki Kuu ya Tanzania inavyotekeleza Sera ya Fedha kwa ufanisi, na kupelekea kuwa na mfumuko mdogo wa bei wa takriban asilimia 3 kwa mwaka 2024, pamoja na kuongezeka kwa upatikanaji wa fedha za kigeni nchini.
Hayo yamejiri katika mikutano ya mwaka ya IMF na WB inayoendelea Washington DC, nchini Marekani.
📸: Benki Kuu - BOT -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Bank of Tanzania
@BankOfTanzania
Ujumbe wa Tanzania, ukiongozwa na Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba, umekutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha Duniani (IMF), anayesimamia Kundi la Kwanza la Nchi za Afrika (Africa Group 1 Constituency), Bw. Willie Nakuyanda.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Haki Ngowi
@Hakingowi
📍Washington D.C
🇹🇿🇺🇸
▪️DKT. NCHEMBA AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA MIKUTANO YA MWAKA YA BENKI YA DUNIA NA IMF WASHINGTON D.C MAREKANI
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), amewasili Washington D.C nchini Marekani, ambapo ameongoza ujumbe wa Tanzania unaohudhuria Mikutano ya Mwaka (Annual Meetings) ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa(IMF), yenye kaulimbiu ya “Vision to Impact”.
Akiwa katika Ubalozi wa Tanzania, Mhe. Dkt. Nchemba alipokea Taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya ubalozi kutoka kwa Mhe. Balozi Dkt. Elsie Sia Kanza, ambapo amempongeza Balozi na timu yake kwa kazi kubwa ya kuiwakilisha nchi.
Ujumbe wa Tanzania umewahusisha Viongozi mbalimbali wakiwemo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango-Zanzibar, Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya, Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango-Zanzibar, Nd. Aboud Hassan Mwinyi, Gavana wa Banki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba, Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, anayesimamia Sera za Fedha na Uchumi Dkt. Yamungu Kayandabila, Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Mcha Hassan Mcha na Viongozi wengine waandimizi wa Serikali.
📸:W/Fedha -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), amewasili Washington D.C nchini Marekani, ambapo ameongoza ujumbe wa Tanzania unaohudhuria Mikutano ya Mwaka (Annual Meetings) ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa(IMF), yenye kaulimbiu ya “Vision to Impact”.
Akiwa katika Ubalozi wa Tanzania, Mhe. Dkt. Nchemba alipokea Taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya ubalozi kutoka kwa Mhe. Balozi Dkt. Elsie Sia Kanza, ambapo amempongeza Balozi na timu yake kwa kazi kubwa ya kuiwakilisha nchi.
Ujumbe wa Tanzania umewahusisha Viongozi mbalimbali wakiwemo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango-Zanzibar, Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya, Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango-Zanzibar, Nd. Aboud Hassan Mwinyi, Gavana wa Banki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba, Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, anayesimamia Sera za Fedha na Uchumi Dkt. Yamungu Kayandabila, Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Mcha Hassan Mcha na Viongozi wengine waandimizi wa Serikali. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), ameshiriki kikao cha Ujumbe wa Tanzania uliowahusisha Mawaziri na Makatibu Wakuu na Ujumbe wa Shirika la Marekani la Changamoto za Milenia (@MCCgov ), ulioongozwa na Mkurugenzi Mtendaji anayesimamia utendaji wa Sera, Bw. Dan Barnes, kilichofanyika katika ukumbi wa Kambarage, Treasury Square, jijini Dodoma, ambapo wamezungumza masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Shirika hilo.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), ameongoza ujumbe wa Tanzania katika kikao cha kuhitimisha tathmini kati ya Serikali na Ujumbe kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa ( @IMFNews ) ulioongozwa na Bw. Charalambos Tsangarides, kwa njia ya mtandao, akiwa jijini Dodoma.
Timu hiyo ya wataalamu kutoka IMF imekuwa nchini kwa majuma kadhaa ikifanya Tathmini ya Awamu ya Nne ya utekelezaji wa Program ya Extended Credit Facility-(ECF), inayohusisha upatikanaji wa mkopo nafuu kwa ajili ya kuimarisha uchumi wa nchi kupitia sekta za uzalishaji na huduma za jamii pamoja na kufanya mapitio na tathmini ya kwanza (1st Review) ya Program mpya ya Serikali ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi kupitia Dirisha la Resilient and Sustainable Fund (RSF).
Kikao hicho kilihudhuriwa na Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba, Manaibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bi. Sauda Msemo na Dkt. Yamungu Kayandabila, na Maafisa wengine waandamizi wa Serikali ambao walishiriki Mkutano huo wa kuhitimisha tathimini wakiwa Ukumbi wa Mikutano wa Mount Meru wa Benki Kuu ya Tanzania, Jijini Dar es Salaam. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Haki Ngowi
@Hakingowi
📍Misigiri,Iramba
▪️DKT NCHEMBA AHIMIZA WANANCHI WAJIANDIKISHE
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) amejiandikisha katika daftari la wapiga kura wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Kituo cha Ofisi ya Mtendaji wa Kijiji cha Misigiri kilichopo Kata ya Ulemo wilayani Iramba, mkoani Singida.
Baada ya zoezi hilo Dkt. Nchemba amezungumza na wananchi kadhaa wa eneo hilo waliojitokeza kujiandikisha na kuwaelimisha umuhimu wa kujiandikisha katika daftari hilo la uchaguzi wa Serikali za mitaa.
Akizungumza na wananchi hao ametoa rai kwa wananchi kutambua kuwa uandikishaji wa daftari la kudumu la uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi Septemba mwaka huu, haumpi sifa mwananchi kushiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa isipokuwa hadi ajiandikishe kwenye daftari litakalomwezesha kuwachagua viongozi anaowataka katika ngazi ya Serikali za Mitaa.
Aidha, ametoa wito kwa wananchi kwenda kujiandikisha katika daftari la uchaguzi wa Serikali za Mitaa lililozinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan, tarehe 11 Oktoba mwaka huu hadi tarehe 20 Oktoba ili kumchagua kiongozi atakayeungana na Serikali kuwaletea maendeleo.
“Napenda kutoa wito kwa wananchi kuwa mjitokeze kujiandikisha kwani zoezi halitumii muda mrefu, ndani ya dakika moja unakuwa umemaliza kujiandikisha,” amesema Dkt. Nchemba.
Dkt. Nchemba aliambatana na Mkewe Bi. Neema Ngure katika zoezi hilo ambalo linalenga kuandikisha wananchi 141,000 katika Wilaya hiyo. -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Leo nimejiandikisha katika Daftari la Wapiga Kura wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Kituo cha Ofisi ya Mtendaji wa Kijiji cha Misigiri, natoa rai kwa wananchi wote mjitokeze kwa wingi kujiandikisha, uchaguzi wa Serikali za Mitaa ni msingi wa maendeleo yetu.
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb) leo tarehe 15.10.2024 amejiandikisha katika daftari la wapiga kura wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Kituo cha Ofisi ya Mtendaji wa Kijiji cha Misigiri kilichopo Kata ya Ulemo wilayani Iramba, mkoani Singida.
Baada ya zoezi hilo Dkt. Nchemba amezungumza na wananchi kadhaa wa eneo hilo waliojitokeza kujiandikisha na kuwaelimisha umuhimu wa kujiandikisha katika daftari hilo la uchaguzi wa Serikali za mitaa.
Akizungumza na wananchi hao ametoa rai kwa wananchi kutambua kuwa uandikishaji wa daftari la kudumu la uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi Septemba mwaka huu, haumpi sifa mwananchi kushiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa isipokuwa hadi ajiandikishe kwenye daftari litakalomwezesha kuwachagua viongozi anaowataka katika ngazi ya Serikali za Mitaa.
Aidha, ametoa wito kwa wananchi kwenda kujiandikisha katika daftari la uchaguzi wa Serikali za Mitaa lililozinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan, tarehe 11 Oktoba mwaka huu hadi tarehe 20 Oktoba ili kumchagua kiongozi atakayeungana na Serikali kuwaletea maendeleo.
“Napenda kutoa wito kwa wananchi kuwa mjitokeze kujiandikisha kwani zoezi halitumii muda mrefu, ndani ya dakika moja unakuwa umemaliza kujiandikisha,” amesema Dkt. Nchemba.
Dkt. Nchemba aliambatana na Mkewe Bi. Neema Ngure katika zoezi hilo ambalo linalenga kuandikisha wananchi 141,000 katika Wilaya hiyo. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Bank of Tanzania
@BankOfTanzania
-
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Chaguo la Watu, Kipenzi cha Taifa.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), ameshiriki uzinduzi wa Tawi la Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ), lililopo Wilaya ya Nyamagana, Mwanza, tarehe 13.10.2024.
Mgeni Rasmi katika hafla hiyo alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi. -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Chen Mingjian 陈明健
@ChenMingjian_CN
So pleased to talk with Hon. Minister @mwigulunchemba1 at Dar es Salaam. Let us work together to facilitate cooperation between two countries.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Shirika la Fedha la Kimataifa ( @IMFNews ) na Benki ya Dunia (@WorldBank ), zimeitangaza Tanzania kuwa nchi ya pili, baada ya Madagascar, kunufaika na Mfumo wa Ushirikiano wa Kuimarisha Hali ya Hewa kwa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na athari mbaya za uharibifu wa mazingira.
Kupitia Mfumo huo, IMF na WBG watafanya kazi kwa karibu na washirika wengine wa maendeleo, kuratibu juhudi zao za kuunga mkono ajenda ya mageuzi ya sera ya Tanzania ili kukabiliana na vihatarishi na changamoto zinazohusiana na mabadiliko hayo ya tabianchi na kuimarisha ustahimilivu wa uchumi wa Tanzania.
Akizungumza Jijini Dar es Salaam, Kiongozi wa Timu ya Wataalam kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa, Bw. Charalambos Tsangarides, alisema kuwa kupitia mpango huo, IMF itaunga mkono kuanzishwa kwa kanuni za uwekezaji wa umma zinazohimili mabadiliko ya tabianchi na utoaji taarifa, huku Benki ya Dunia itajikita katika kusaidia kutekeleza miradi katika sekta zitakazoimarisha uwezo wa Tanzania kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kama vile nishati, maji, hifadhi ya jamii na kilimo.
Taasisi hizo mbili pia zitasaidia uboreshaji na utekelezaji wa sera ya Tanzania ya usimamizi wa hatari za maafa, ikiwa ni pamoja na kufadhili mfumo wa kukabiliana na hatari hizo na uimarishaji wa mtandao wa usalama wa kijamii ili kukabiliana na majanga ya hali ya hewa.
IMF na Benki ya Dunia pia zitasaidia sera za kuboresha usimamizi wa rasilimali za maji, kupanua upangaji na usimamizi wa matumizi bora ya ardhi ya vijiji, kusimamia vihatarishi vya hali ya hewa katika uchumi na fedha na kutoa msaada wa kiufundi na kifedha kwa kuishirikisha pia sekta binafsi.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia, Bw. Nathan Belete, akizungumza kwa njia ya mtandao kutoka Washington D.C, nchini Marekani, alisema kuwa Tanzania itanufaika na msaada wa kiufundi na kifedha kutoka taasisi hizo mbili katika kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa miundombinu itakayokuza uzalishaji, kuhifadhi mazingira na kuwa na mchango mkubwa katika kuinua uchumi wa nchi.
Kwa upande wake, Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1, amezishukuru Taasisi hizo kubwa za Fedha Duniani (IMF na Benki ya Dunia) kwa kuiteua Tanzania kuwa nchi za mwanzo duniani, zitakazo nufaika na mpango huo kwa kuunga mkono juhudi za Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye ni kinara wa mapambano ya kukabiliana na athari mbaya za mabadiliko ya tabianchi.
@SuluhuSamia @ikulumawasliano @dr_mpango @KassimMajaliwa_ @DBiteko -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Victoria Kwakwa
@VictoriaKwakwa
The addition of freight services will be important for long-term financial sustainability. @WorldBank is committed to supporting Tanzania’s ambitious rail modernization program as part of an integrated multimodal connectivity strategy to boost trade and growth.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Victoria Kwakwa
@VictoriaKwakwa
Very pleasant ride on Tanzania's new SGR from Dar es Salaam to Dodoma. The SGR has cut travel time close to 50%, bringing huge efficiency and climate mitigation gains. Warm congratulations to the Government of #tanzania on this impressive achievement.
-
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Tujitokeze sote kujiandikisha na kushiriki Uchaguzi huu muhimu.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Masuala ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Kampuni ya vinywaji vya @Heineken , Bw. Frank Ford, aliyemtembelea Ofisini kwake, Jengo la Treasury Square, jijini Dodoma, akiambatana na Afisa Masoko wa Kampuni hiyo. Bi. Lilian Pascal, ambapo walijadili kuhusu maendeleo ya kampuni hiyo iliyowekeza hapa nchini na namna inavyochangia katika pato la Taifa na Uchumi wa nchi kwa ujumla.
Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha anayesimamia Sera za Uchumi, Bw. Elijah Mwandumbya na Kamishna Msaidizi, Idara ya Sera, Bw. William Mhoja, pamoja na Maafisa wengine waandamizi wa Wizara ya Fedha. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Umoja wa Mabenki Tanzania (TBA), jijini Dodoma, ambapo walijadili kuhusu mchango wa Sekta ya Benki katika uchumi wa nchi kupitia huduma jumuishi za kifedha.
Kikao hicho kilihudhuriwa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, (BoT), Bw. Emmanuel Tutuba, wakati ujumbe wa TBA uliongozwa Mwenyekiti wake, Bw. Theobald Sabi. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Haki Ngowi
@Hakingowi
📍Dar es Salaam - 📍Dodoma
▪️Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini, Bi. Victoria Kwakwa aipongeza Tanzania kwa uwekezaji mkubwa wa mradi huo wa SGR
Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini, Bi. Victoria Kwakwa, amesafiri kwa njia ya Treni ya Kisasa-SGR kuanzia Dar es Salaam hadi Dodoma ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku 3 nchini Tanzania kwa lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Benki ya Dunia.
Katika ziara hiyo, amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), na Mawaziri wengine wa Kisekta kuhusu ufadhili wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini Tanzania ikiwa ni pamoja na uwezekano wa Benki hiyo kushiriki katika ufadhili wa vipande vya SGR vilivyosalia.
Bi Kwakwa alitumia fursa hiyo kuipongeza Tanzania kwa uwekezaji mkubwa wa mradi huo wa SGR ambao amesema utakuwa kichocheo kikubwa cha usafirishaji wa abiria na mizigo na kuchangia ukuaji wa uchumi si tu kwa Tanzania bali kwa nchi zote za Ukanda wa Maziwa Makuu.
📹:W/FedhaThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Tujitokeze Kujiandikisha. Asante Mhe Rais kwa kuongoza kwa mfano.
-
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Karibu sana Dodoma, Tanzania @VictoriaKwakwa Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia kwa Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini, ni furaha yetu kuona umesafiri kwa Treni ya Kisasa-SGR kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma. Uwekezaji huu mkubwa kwenye SGR utachochea ukuaji wa uchumi na kuboresha usafirishaji kwa Tanzania na nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu. Tunafurahi kuendelea kushirikiana na @WorldBank kwa manufaa ya maendeleo yetu.
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini, Bi. @VictoriaKwakwa , amesafiri kwa njia ya Treni ya Kisasa-SGR kuanzia Dar es Salaam hadi Dodoma ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku 3 nchini Tanzania kwa lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Benki ya Dunia. Katika ziara hiyo, anatarajia kukutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), kuhusu ufadhili wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini Tanzania ikiwa ni pamoja na uwezekano wa Benki hiyo kushiriki katika ufadhili wa vipande vya SGR vilivyosalia.
Bi Kwakwa alitumia fursa hiyo kuipongeza Tanzania kwa uwekezaji mkubwa wa mradi huo wa SGR ambao amesema utakuwa kichocheo kikubwa cha usafirishaji wa abiria na mizigo na kuchangia ukuaji wa uchumi si tu kwa Tanzania bali kwa nchi zote za Ukanda wa Maziwa Makuu.
Katika safari hiyo Bi. Kwakwa aliambatana na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania Bw. @BeleteNathan , na Maafisa Waandamizi wa Benki hiyo Bw. Nicholas Soikan na Bi. Makiko Watanabe.
@WorldBank @WBTanzania -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini, Bi. @VictoriaKwakwa , amesafiri kwa njia ya Treni ya Kisasa-SGR kuanzia Dar es Salaam hadi Dodoma ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku 3 nchini Tanzania kwa lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Benki ya Dunia. Katika ziara hiyo, anatarajia kukutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), kuhusu ufadhili wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini Tanzania ikiwa ni pamoja na uwezekano wa Benki hiyo kushiriki katika ufadhili wa vipande vya SGR vilivyosalia.
Bi Kwakwa alitumia fursa hiyo kuipongeza Tanzania kwa uwekezaji mkubwa wa mradi huo wa SGR ambao amesema utakuwa kichocheo kikubwa cha usafirishaji wa abiria na mizigo na kuchangia ukuaji wa uchumi si tu kwa Tanzania bali kwa nchi zote za Ukanda wa Maziwa Makuu.
Katika safari hiyo Bi. Kwakwa aliambatana na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania Bw. @BeleteNathan , na Maafisa Waandamizi wa Benki hiyo Bw. Nicholas Soikan na Bi. Makiko Watanabe.
@WorldBank @WBTanzania -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Nimekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa China hapa nchini, Mheshimiwa @ChenMingjian_CN , Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha Jijini Dar es Salaam, tumejadili masuala muhimu ya ushirikiano kati ya China na Tanzania uliodumu kwa miaka 60 sasa.
Miongoni mwa masuala hayo ni ufadhili wa ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR unaoendelea hivi sasa kwa kipande cha tano cha kuanzia Mwanza hadi Isaka na kipande cha sita kinachoanzia Tabora hadi Kigoma.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
🇹🇿🇴🇲
Tanzania na Oman zimekubaliana kuendeleza ushirikiano katika nyanja mbalimbali za maendeleo ikiwemo Sekta ya Nishati na Madini, kutengeneza mazingira bora ya uwekezaji, kubadilishana uzoefu na mafunzo katika masuala ya kodi pamoja na kuondoa utozaji kodi mara mbili kwa wawekezaji na wafanyabiashara watakaofanya shughuli zao kati ya nchi hizo mbili.
Hayo yamesemwa wakati wa kikao cha Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb) alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Oman nchini Tanzania, Mhe. Saud Al-Shidhani, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha Jijini Dar es Salaam.
Mhe. Dkt. Nchemba, alisema kuwa ajenda kubwa ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ni kuhakikisha inawezesha sekta binafsi kuwa na nguvu, sambamba na uboreshaji wa mazingira ya biashara na uwekezaji, hivyo ushirikiano kati ya nchi hizo utaendelea kunufaisha sekta binafsi na wawekezaji kwa kiasi kikubwa.
“Serikali zetu mbili zimeanzisha Tume ya Kudumu ya Pamoja inayosimamia maeneo ya ushirikiano kati ya nchi zetu mbili, ikiwemo biashara na uwekezaji, hivyo natarajia kutakuwa na fursa ya kupanua zaidi ushirikiano wetu wa maendeleo kwa manufaa ya watu wetu” alisema Dkt. Nchemba
Alikubali maombi ya Balozi wa Oman ambaye alisisitiza umuhimu wan chi yake kujifunza zaidi kuhusu mifumo ya kodi kutoka Tanzania kwa kuwa Mamlaka ya Mapato Tanzania ina uzoefu mkubwa katika aneo hilo na kwamba nchi yake imeanza kutoza kodi hivi karibuni.
“Tunatazamia Ushirikiano wa mafunzo hasa kwenye masuala ya kodi, na sehemu ambazo nchi zetu hizi mbili zina utaalamu mahsusi, lengo ni kujengeana uwezo pamoja ili tuweze kunufaika zaidi” alisema Dkt. Nchemba.
Naye Balozi wa Oman nchini Tanzania, Mhe. Saud Al-Shidhani, ameipongeza Tanzania kwa kupiga hatua katika masuala ya kodi na ameona fursa ya kubadilishana uwezo katika masuala ya kodi ikiwa ni moja ya ajenda kubwa ya ushirikiano kati ya nchi hizo.
Mhe. Balozi Al-Shidhani, alisema kuwa biashara kati ya nchi hizi mbili umeongezeka kwa kiasi kikubwa na kuna tija kubwa ya kuondoa utozaji kodi mara mbili kwa wawekezaji na wafanyabiashara wanaofanya shughuli zao kati ya nchi hizo mbili.
“Tunapenda kusema kuwa Oman tunataka kujifunza namna ya kushughulikia masuala ya ukusanyaji wa mapato kwa Kuwa Tanzania tayari imepiga hatua katika masuala hayo na sisi tumeanza miaka ya karibuni, kwa hiyo tuna mengi ya kujifunza” alisema balozi huyo.
Kikao hicho kilihudhuriwa na Kamishna Msaidizi Idara ya Fedha za Nje Bw. Melckzedeck Mbise, Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Sheria Wizara ya Fedha, Bi. Mwantumu Sultan na Maafisa wengine waandamizi wa Serikali. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
🇹🇿🇨🇳
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), ameishukuru China kwa kufikia hatua za mwisho za kufadhili ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR unaendelea hivi sasa kwa kipande cha tano cha kuanzia Mwanza hadi Isaka na kuahidi kuyafanyiakazi maombi mengine ya kipande cha sita kinachoanzia Tabora hadi Kigoma.
Dkt. Nchemba ameyasema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa China hapa nchini, Mheshimiwa Chen Mingjian, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha Jijini Dar es Salaam, ambapo walijadili masuala muhimu ya ushirikiano kati ya China na Tanzania uliodumu kwa miaka 60 sasa.
Dkt. Nchemba alisema kuwa Mradi wa Reli ya Kisasa ni muhimu kwa uchumi na maendeleo ya Watanzania na kwamba ujumbe wa Mheshimiwa Balozi Chen kwamba China kupitia taasisi zake inakamilisha taratibu za ndani za kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa reli hiyo umepokelewa kwa mikono miwili na Serikali.
Kwa upande wake, Balozi wa China hapa nchini, Mheshimiwa Chen Mingjian, amesema kuwa nchi yake inauchukulia uhusiano wake na Tanzania kuwa ni wa kipekee na kwamba maelekezo ya Kiongozi wa nchi hiyo Mheshimiwa XI Jinping ni kwamba anataka uhusiano huo uwe wa mfano na kielelezo barani Afrika.
Alisisitiza kuwa maombi ya Tanzania ya kupata fedha kwa ajili ya kipande cha tano na mengine ya kutaka ufadhili wa ujenzi wa kipande cha 6 yamepokelewa na kwamba uamuzi wake utatolewa hivi karibu baada ya mambo machache yanayofanyiwakazi kukamilika.
Aidha, alieleza kuwa mpango wa miaka mitatu wa China wa ushirikiano kati yake na nchi za Afrika (FOCAC), umeitengea Tanzania kiasi kikubwa cha fedha ambazo zitaelekezwa katika miradi inayogusa masuala ya uchumi wa kijani, biashara na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT). -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Nimekutana na Balozi wa Oman hapa nchini Mhe. Saud Al Shidhani, tumejadiliana masuala mbalimbali ya mashirikiano ikiwemo kubadilisha uzoefu katika sekta ya Mafunzo ya Nishati, Gesi, Madini na Kodi. Aidha, kutumia fursa ya Uboreshajwaji wa Mazingira ya Uwekezaji, Ushirikiano wa pamoja na kuangalia namna ya utekelezaji wa mkataba wa kuondoa utozwaji wa Kodi mara mbili katika sekta ya biashara kati ya nchi hizi mbili.
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), amekutana na kufanya mazungunzo na Mkurugenzi Mtendaji wa United Bank of Africa (@UBAGroup ), Bw. Gbenga Makinde, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha Jijini Dar es Salaam, ambapo ameishukuru Benki hiyo kwa kuwa tayari kushirikiana na Serikali katika kufadhili miradi mbalimbali ya maendeleo.
Kwa upande wake, Bw. Makinde, ameeleza kuwa Benki yake imekuwa ikishirikiana na Tanzania katika kutekeleza baadhi ya miradi yake ya kimkakati ikiwemo Bwawa la Kuzalisha Umeme la Julius Nyerere, kwa kuwawezesha kifedha wakandarasi wanaojenga mradi huo na kwamba hivi sasa Benki hiyo iko tayari kushirikiana moja kwa moja na Serikali kwa kutoa fedha za kutekeleza miradi husika. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
🇹🇿🇮🇹
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), ametoa wito kwa wawekezaji kutoka nchini Italia kutumia mazingira mazuri ya uwekezaji yaliyopo hapa nchini kuwekeza mitaji yao katika miradi mbalimbali ya kiuchumi na kijamii ili kukuza uchumi wa pande hizo mbili.
Dkt. Nchemba ametoa wito huo alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Italia hapa nchini Mhe. Giussepe Sean Coppola, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam.
Alisema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita, inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imeweka vivutio mbalimbali vya uwekezaji na kuialika sekta binafsi ya Italia, kushirikiana na Serikali kwa kuwekeza katika ujenzi na uendeshaji wa miradi mbalimbali hapa nchini ukiwemo mradi wa Reli ya Kisasa wa SGR.
Kwa upande wake, Balozi wa Italia hapa nchini Mhe. Giussepe Sean Coppola, alimwagia sifa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kusimamia vizuri uchumi na maendeleo ya nchi ikiwemo kuunda tume ya kushughulikia changamoto za kikodi nchini.
Alisema kuwa anaamini matokeo ya Tume hiyo yataongeza chachu ya kufanyabiashara na uwekezaji hapa nchini hatua itakayochochea ajira, ukuaji wa uchumi na kuongeza ushiriki wa sekta binafsi katika kuchochea maendeleo ya nchi.
Aliahidi kuwa nchi yake itaendelea kushirikiana na Tanzania katika Nyanja mbalimbali za kiuchumi na kijamii kwa kuchangia utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwemo sekta ya kilimo kwa kuendeleza mnyororo wa thamani wa zao la kahawa chini.
Italia imekuwa mdau mkubwa wa maendeleo wa Tanzania kwa kufadhili miradi mbalimbali kupitia bajeti kuu ya Serikali, ikiwemo miradi ya maji, afya, mafunzo ya ufundi stadi na huduma katika sekta za utalii na hoteli, uchumi wa buluu na usawa wa kijinsia. -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Nimefanya mazungumzo na Balozi wa Italia nchini Tanzania Mhe. Giuseppe Sean Coppola, Jijini Dar es Salaam, tumejaadili maeneo mengi ya mashirikiano ambayo yataimarisha ushiriakiano kati ya Tanzania na italia zikiwemo fursa mbalimbali za uwekezaji nchini na kwa manufaa ya nchi zetu.
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Bank of Tanzania
@BankOfTanzania
-
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Leo nyumbani nilitembelewa na watoto wa kituo cha watoto yatima (Watoto Kwanza), nimekubali kuwa Mlezi wao.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
🇹🇿🇭🇺
Balozi wa Hungary hapa nchini mwenye Makazi yake Jijini Nairobi nchini Kenya, Mhe. Zsolt Mészáros, ameipongeza Tanzania kwa kusimamia vema sera zake za fedha na uchumi, hatua iliyoifanya iendelee kuimarika kiuchumi na kuahidi kuwa nchi yake itaongeza ushirikiano kwa faida ya nchi hizo mbili.
Mhe. Mészáros ameyasema hayo, alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), Katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam.
Alisema kuwa nchi yake imekuwa ikifuatilia kwa karibu maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya Tanzania ikiwemo hatua kubwa inazochukua kuvutia uwekezaji wakiwemo wanaotoka nchini mwake.
Aliahidi kuwa nchi yake iko tayari kushirikiana na Tanzania katika kuchangia maendeleo yake hususan katika sekta za huduma za jamii kama vile maji kupitia mpango wake maalumu wa kushirikiana na Serikali ujulikanao kama Tied Aid Facility.
Akizungumza na Balozi huyo wa Hungary, Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb) amesema kuwa uchumi wa Tanzania umeimarika ambapo katika robo ya kwanza ya mwaka huu wa fedha, uchumi umekua kwa wastani wa asilimia 5.6 ikilinganishwa na ukuaji wa wastani wa asilimia 5 katika kipindi kama hicho mwaka jana.
Alisema kuwa makadirio ya ukuaji wa uchumi katika kipindi cha mwaka 2024/2025 ni wastani wa asilimia 5.4 na asilimia 5.8 mtawalia, kufuatia miongozo na usimamizi mzuri wa uchumi, wa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
“Takwimu zilizotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) mwezi Agosti mwaka 2024, zinaonesha kuwa uchumi wetu umeimarika licha ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali huku ukuaji huo ukichangiwa kwa kiasi kikubwa na sekta za ujenzi, kilimo, fedha na sekta ya bima” alisema Dkt. Nchemba.
Aidha, Dkt. Nchemba amemweleza Balozi huyo kuwa kasi ya mfumuko wa bei imedhibitiwa na kuwa katika kiwango wa tarakimu moja cha asilimia 3.1, kiwango ambacho kimekubaliwa pia katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) zilizoweka ukomo wa asilimia 8 na kiwango cha nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika (SADC) cha asilimia 3 hadi 7.
Amesema kuwa uimara wa uchumi wa Tanzania umethibitishwa pia na mashirika yanayofanya tathimni ya uwezo wa nchi kukopesheka duniani, ikiwemo Taasisi ya Moody’s ambayo hivi karibuni, iliipandisha Daraja Tanzania kutoka Daraja B2 kwenda Daraja B1 pamoja na Taasisi ya Fitch ambayo imeipa Tanzania Daraja B+ yenye Mtazamo Chanya (positive Outlook).
Dkt. Nchemba amesema kuwa hatua hiyo imeifanya Tanzania na sekta binafsi kuaminiwa zaidi na taasisi za fedha za kimataifa kwamba zinaweza kuyafikia masoko ya fedha ya kimataifa na kuvutia uwekezaji wa mitaji na teknolojia kutoka maeneo mbalimbali duniani.
Alitoa wito kwa wawekezaji kutoka Hungary kuja kuwekeza nchini katika maeneo mbalimbali watakayo ona yanawafaa kutokana na Serikali kuweka mazingira bora yanayovutia uwekezaji. -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Hongera sana Mhe Rais kwa hatua hii ya kimapinduzi kwenye ukusanyaji wa kodi nchini.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Bank of Tanzania
@BankOfTanzania
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Bank of Tanzania
@BankOfTanzania
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Bank of Tanzania
@BankOfTanzania
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba, akisoma taarifa ya Kamati ya Sera ya Fedha (MPC) ya Bodi ya Wakurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania, iliyokutana tarehe 2 Oktoba 2024.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Bank of Tanzania
@BankOfTanzania
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, CGP Jeremiah Yoram Katungu, ambaye amefika ofisini kwake kujitambulisha, akiwa ameambatana na Maafisa wengine wa ngazi ya juu wa Jeshi hilo, ambapo wamejadili masuala mtambuka ya namna ya kushirikiana ili kuhakikisha kuwa majukumu ya Jeshi hilo yanatekelezwa kwa ufanisi.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Haki Ngowi
@Hakingowi
📍Dar es Salaam
▪️MHE. DKT. NCHEMBA APOKEA TAARIFA YA UTEKELEZAJI YA MWAKA YA PPRA
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), amepokea Taarifa ya Tathmini ya Utendaji Kazi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), kwa mwaka wa fedha 2023/2024, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha Jijini Dar es Salaam, 28 Septemba, 2024, na kuiagiza Menejimenti na Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka hiyo kuhakikisha kuwa watoa huduma wanaopata zabuni kupitia Mfumo wa Ununuzi wa Kieletroniki wa NeST, wanatumia malighafi na bidhaa zinazozalishwa ndani ya nchi isipokuwa kwa bidhaa ambazo ni lazima ziagizwe nje ya nchi kutokana na kutopatikana hapa nchini, hatua ambayo amesema itakuza uzalishaji wa bidhaa na huduma za ndani, kukuza ajira, kuongeza wigo wa kodi na kuchangia maendeleo ya nchi kupitia utekelezaji wa miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali.
Ripoti hiyo imekabidhiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya PPRA, Dkt. Leonada Mwagike na kushuhudiwa na Naibu Makatibu Wakuu wa Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo na Bi. Amina Khamis Shaaban, Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya PPRA, baadhi ya Menejimenti ya Wizara ya Fedha, wafanyakazi wa PPRA na wageni wengine waalikwa.
Aidha, Dkt. Nchemba amezitaka Taasisi za umma nchini kuhakikisha zinatumia Mfumo wa Ununuzi wa Umma wa Kielektroniki (NeST) kwakuwa hakuna mbadala wake ili kuongeza uwazi na uwajibikaji na udhibiti wa ndani wa Taasisi nunuzi, na hivyo kuendana na maelekezo ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, aliyeitaka Wizara ya Fedha kudhibiti matumizi ya fedha za Serikali hasa kwenye utekelezaji wa miradi ili iendane na thamani ya fedha inayotumika kutekeleza miradi husika.
📸:W/Fedha -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Eng Yuda Kemincha
@yudakemincha84
Hii haijawahi kutokea, 2025 ni ushindi wa Sunami! @SuluhuSamia
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
The Voices of Tanzanians.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Malima Chacha
@ChachaMalima
Ruvuma imezungumza kwa sauti kuu, full house Majimaji huwa ni 30k. Majimaji imetapika na 60k ya Lupaso
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
The Voices of Tanzanians.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
MHE. DKT. NCHEMBA APOKEA TAARIFA YA UTEKELEZAJI YA MWAKA YA PPRA
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), amepokea Taarifa ya Tathmini ya Utendaji Kazi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), kwa mwaka wa fedha 2023/2024, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha Jijini Dar es Salaam, 28 Septemba, 2024, na kuiagiza Menejimenti na Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka hiyo kuhakikisha kuwa watoa huduma wanaopata zabuni kupitia Mfumo wa Ununuzi wa Kieletroniki wa NeST, wanatumia malighafi na bidhaa zinazozalishwa ndani ya nchi isipokuwa kwa bidhaa ambazo ni lazima ziagizwe nje ya nchi kutokana na kutopatikana hapa nchini, hatua ambayo amesema itakuza uzalishaji wa bidhaa na huduma za ndani, kukuza ajira, kuongeza wigo wa kodi na kuchangia maendeleo ya nchi kupitia utekelezaji wa miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali.
Ripoti hiyo imekabidhiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya PPRA, Dkt. Leonada Mwagike na kushuhudiwa na Naibu Makatibu Wakuu wa Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo na Bi. Amina Khamis Shaaban, Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya PPRA, baadhi ya Menejimenti ya Wizara ya Fedha, wafanyakazi wa PPRA na wageni wengine waalikwa.
Aidha, Dkt. Nchemba amezitaka Taasisi za umma nchini kuhakikisha zinatumia Mfumo wa Ununuzi wa Umma wa Kielektroniki (NeST) kwakuwa hakuna mbadala wake ili kuongeza uwazi na uwajibikaji na udhibiti wa ndani wa Taasisi nunuzi, na hivyo kuendana na maelekezo ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, aliyeitaka Wizara ya Fedha kudhibiti matumizi ya fedha za Serikali hasa kwenye utekelezaji wa miradi ili iendane na thamani ya fedha inayotumika kutekeleza miradi husika. -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
The Voices of Tanzanians.
-
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Kipenzi cha Watanzania.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Bank of Tanzania
@BankOfTanzania
-
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
IPUUZWE, NI FEKI.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Haki Ngowi
@Hakingowi
📍 Antananarivo, Madagascar
🇹🇿🇲🇬
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Taasisi ya Africa50, ambaye pia ni Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika, Dkt. Akinwumi Adesina, baada ya kuhitimishwa kwa Mkutano wa Mwaka wa Wanahisa wa Taasisi ya Africa50 (General Shareholders Meeting - GSM) na Jukwaa la Miundombinu la Afrika (Infra for Africa Forum meeting) Taasisi ambayo Tanzania ni mwanachama, uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Ivato, Mjini Antananarivo, nchini Madagascar.
Mhe. Dkt. Nchemba, alimwakilisha Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika Mkutano huo ulioangazia masuala ya ujenzi wa miundombinu inayochochea ukuaji wa uchumi Barani Afrika, pamoja na kupigia chapuo matumizi ya nishati safi ya kupikia ili kuimarisha uchumi wa nchi hizo na watu wake na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi yanayotokana na athari za uharibifu wa mazingira.
📸:W/Fedha -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), ameshiriki mjadala kuhusu umuhimu wa matumizi ya Nishati safi ya kupikia, akimwakilisha Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika Mkutano wa Mwaka wa Wanahisa wa Taasisi ya Africa50 (General Shareholders Meeting - GSM) na Jukwaa la Miundombinu la Afrika (Infra for Africa Forum meeting) Taasisi ambayo Tanzania ni mwanachama, uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Ivato, Mjini Antananarivo, nchini Madagascar.
@SuluhuSamia @ikulumawasliano -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Taasisi ya Africa50, ambaye pia ni Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika, Dkt. @akin_adesina , baada ya kuhitimishwa kwa Mkutano wa Mwaka wa Wanahisa wa Taasisi ya Africa50 (General Shareholders Meeting - GSM) na Jukwaa la Miundombinu la Afrika (Infra for Africa Forum meeting) Taasisi ambayo Tanzania ni mwanachama, uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Ivato, Mjini Antananarivo, nchini Madagascar. Mhe. Dkt. Nchemba, alimwakilisha Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika Mkutano huo ulioangazia masuala ya ujenzi wa miundombinu inayochochea ukuaji wa uchumi Barani Afrika, pamoja na kupigia chapuo matumizi ya nishati safi ya kupikia ili kuimarisha uchumi wa nchi hizo na watu wake na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi yanayotokana na athari za uharibifu wa mazingira.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), ametoa wito kwa nchi za Afrika kutafuta njia na mikakati ya kuboresha uchumi na maisha ya wananchi wake kwa kutumia nishati safi ya kupikia ikiwa ni hatua pia ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya Tabianchi yanayochangiwa na uharibifu wa mazingira.
Dkt. Nchemba ametoa wito huo mjini Antananarivo nchini Madagascar kwa niaba ya Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati akihutubia katika Mkutano wa Mwaka wa Wanahisa wa Taasisi ya Africa50 (General Shareholders Meeting - GSM) na Jukwaa la Miundombinu la Afrika (Infra for Africa Forum meeting) Taasisi ambayo Tanzania ni mwanachama, uliofanyika leo tarehe 19 Septemba, 2024, katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Ivato, na kufunguliwa na Rais wa Nchi hiyo, Mhe. Andry Rajoelina.
Aidha, Dkt. Nchemba alizishauri nchi hizo kuwekeza katika kutoa elimu kwa umma kuhusu umuhimu wa wananchi wao kutumia nishati safi ya kupikia pamoja na faida zinazoambatana na utunzaji wa mazingira kiuchumi na kijamii.
Dkt. Nchemba pia ametoa wito kwa taasisi za fedha na sekta binafsi kushiriki katika kampeni ya matumizi ya nishati safi ya kuopikia ikiwemo gesi iliyosindwa, nishati ya jua, umeme wa joto ardhi, biogas, kwa kuwezesha upatikanaji wa fedha na pia kuzalisha vifaa ama majiko yanayotumia nishati hiyo.
Katika msafara huo, Mhe. Dkt. Nchemba ameambatana na Naibu Katibu Mkuu anayesimamia Fedha za Umma (Public Finance Management) Bi. Amina Khamis Shaaban na Balozi wa Tanzania nchini Madagascar, Mhe. Faustine Kasike.
Mkutano wa Wanahisa wa Africa50, unatarajiwa kuwakutanisha wadau mbalimbali kutoka Bara la Afrika na duniani kwa ujumla wakiwemo Wawekezaji kutoka Taasisi za Umma na Sekta Binafsi, wakopeshaji, wataalam wa ujenzi wa miundombinu na kuwawezesha kutafuta suluhisho la changamoto za miundombinu katika Bara la Afrika pamoja na kukabikliana na athari za mabadiliko ya tabianchi na watahimizana kuhusu matumizi ya nishati safai ili kuchochea uchumi na maendeleo ya nchi hizo. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), amewasili Jijini Antananarivo nchini Madagascar, ambapo ameongoza Ujumbe wa Tanzania, akimwakilisha Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika Mkutano wa Mwaka wa Wanahisa wa Taasisi ya Africa50 (General Shareholders Meeting - GSM) na Jukwaa la Miundombinu la Afrika (Infra for Africa Forum meeting) Taasisi ambayo Tanzania ni mwanachama, itakayofanyika tarehe 19 Septemba, 2024, katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Ivato, na utafunguliwa na Rais wa Nchi hiyo, Mhe. Andry Rajoelina.
Alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Antananarivo, Mhe. Dkt. Nchemba alilakiwa na Balozi wa Tanzania nchini Madagascar, Mhe. Faustine Kasike na Maafisa waandamizi wa Taasisi ya Africa50, akiwemo Bw. Youssef Abdourabbih, anayehusika na masuala ya Utawala.
Katika msafara huo, Mhe. Dkt. Nchemba ameambatana na Naibu Katibu Mkuu anayesimamia Fedha za Umma (Public Finance Management) Bi. Amina Khamis Shaaban.
Mkutano wa Wanahisa wa Africa50, unatarajiwa kuwakutanisha wadau mbalimbali kutoka Bara la Afrika na duniani kwa ujumla wakiwemo Wawekezaji kutoka Taasisi za Umma na Sekta Binafsi, wakopeshaji, wataalam wa ujenzi wa miundombinu na kuwawezesha kutafuta suluhisho la changamoto za miundombinu katika Bara la Afrika pamoja na kukabikliana na athari za mabadiliko ya tabianchi na watahimizana kuhusu matumizi ya nishati safai ili kuchochea uchumi na maendeleo ya nchi hizo.
Africa50 ni Taasisi ya Kifedha yenye Makao Makuu yake Casablanca, Morocco, ambayo imejikita katika nyanja mbili za uwekezaji ambazo ni; Maendeleo ya Miradi na Fedha za Mradi (Project Development and Project Finance) ikiwa na lengo la kuchagiza maendeleo ya miundombinu barani Afrika kwa kuzingatia umuhimu na mchango wa miradi husika kitaifa na kikanda. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), ametembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Soko Kuu la Jiji la Mwanza, wenye thamani ya shilingi bilioni 23.4, Mradi ambão utakapo kamilika, utawezesha wafanyabiashara wapatao 1,400 kupata maeneo mazuri ya kufanyia biashara.
Aidha, mradi huo utakuwa na Maduka 514 (madogo, ya kati na makubwa) ndani na nje ya jengo, Vizimba 332 vya matunda na mbogamboga, Vizimba 372 vya nafaka, Mama lishe maeneo 12, eneo kwa ajili ya Wafanyabiashara ndogondogo (Machinga 167), ofisi 5, eneo moja la kukusanyia taka, eneo la maegesho ya Magari madogo 192 chini ya usawa wa Ardhi (basement) na vyoo.
Dkt. Nchemba alielezwa kuwa, mradi huu utasaidia kuongeza mapato ya Halmashauri ya Jiji ambapo jumla ya Shillingi Billion 3.5 zinatarajiwa kukusanywa kwa mwaka, kupendezesha Jiji la Mwanza na kulifanya kuwa la Kisasa zaidi. Pia mradi huo utasaidia kukua kwa biashara nyingine kutoka kwa Wafanyabiashara wa ndani, mikoa ya jirani na nje ya nchi. Mradi huu umetoa ajira kwa vijana wapatao 175 ambao walikuwa wakiendelea na kazi mbalimbali za ujenzi.
Mhe. Dkt. Nchemba, yuko katika ziara ya siku 7 ya kikazi mkoani Mwanza, ambapo naungana na Mawaziri wenzake wa sekta mbalimbali wanaotembelea maeneo mbalimbali ya nchi, kutembelea, kukagua, kuweka mawe ya msingi na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa katika mikoa hiyo kwa manufaa ya wananchi kufuatia juhudi kubwa zilizofanywa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupeleka fedha nyingi za miradi katika mikoa yote nchini, katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wake. -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Asante sana Mhe Rais, Nchi yetu ni Tanzania, hatuna Nchi nyingine.
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Jambo TV
@Jambotv_
HABARI PICHA:
Matukio katika picha wakati Waziri wa Fedha na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Dkt Mwigulu Lameck Nchemba Madeluakihutubia maelfu ya wananchi wa wilaya ya Misungwi katika Viwanja vya Amani, katika mkutano ulioandaliwa na Mbunge wa jimbo hilo ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Alexandar Pastory Mnyeti.
Akizungumza katika mkutano huo, Dkt. Nchemba amewaomba Watanzania kuendelea kumwombea kwa Mwenyezimungu, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili awe na afya njema anapotekeleza majukumu yake ya kuwahudumia Watanzania kwa upendo na ari kubwa.
Amesema serikali imeendelea kutoa fedha nyingi wakati huu kuliko wakati wowote ule ambapo kila mahali nchini, inatekelezwa miradi ya maendeleo inayogharimu fedha nyingi, ikiwamo miradi ya kimkakati kama SGR, umeme wa Bwawa la Julius Nyerere, Ujenzi wa Daraja la Kigongo-Busisi na mingine mingi katika sekta za uzalishaji, afya, maji, elimu na miundombinu. -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Asanteni sana wananchi wa Misungwi kwa mapokezi yenu makubwa.
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Jambo TV
@Jambotv_
Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu amewasili wilayani Misungwi, mkoani Mwanza kwa ziara rasmi ya kikazi na kupokelewa na viongozi na wananchi wa wilaya hiyo.
Katika ziara hiyo Dkt. Nchemba atakagua maendeleo ya ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Tanzania (TIA) Kampasi ya Mwanza na kisha atazungumza na wananchi wa Misungwi katika mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Mbunge wa Jimbo hilo ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Alexander Mnyeti katika uwanja wa Amani, Misungwi Mjini.
Dkt. Nchemba yuko mkoani Mwanza kwa ziara ya kikazi ambayo imelenga kutembelea na kukagua, kuzindua na kuweka mawe ya msingi katika miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali mkoani humo. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Haki Ngowi
@Hakingowi
📍Mwanza
▪️DKT. NCHEMBA ATEMBELEA NA KUKAGUA UJENZI WA CHUO HA UHASIBU KAMPASI YA MWANZA
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), ametembelea na kukagua ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Tanzania, Kampasi ya Mwanza, inayojengwa na Serikali kupitia Wizara ya Fedha, kwa gharama ya shilingi bilioni 7.8, kitakachokuwa na uwezo wa kuhudumia wanafunzi zaidi ya 5,000 kwa wakati mmoja, na kuahidi kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuwekeza rasilimali fedha katika sekta mbalimbali za maendeleo ikiwemo sekta ya elimu.
Mkuu wa Chuo hicho Profesa William Pallangyo, alieleza kuwa katika kipindi cha miaka mitatu, Serikali kupitia Wizara ya Fedha, imekipatia Chuo hicho shilingi bilioni 58.1 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya ujenzi wa miundombinu ya kujifunzia na kufundishia katika Kampasi zake nane za Mtwara (bil. 6.1). Mbeya (Bil 3.2), Mwanza (bilioni 7.8), Kigoma (bilioni 11) na Zanzibar (sh. bilioni 30).
Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) yuko katika ziara ya kikazi ya siku 7 mkoani Mwanza, ambapo atafanya shughui za kukagua, kutembelea, kuzindua na kuweka mawe ya msingi katika miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa mkoani Mwanza.
📸:W/Fedha -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Lemutuz TV
@lemutuztv
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu amewasili Misungwi - Mwanza kwa ziara rasmi ya kikazi na kupokelewa na Viongozi na wananchi wa wilaya hiyo.
Ziara hiyo imelenga kutembelea na kukagua, kuzindua na Kuweka mawe ya msingi katika Miradi ya Maendeleo. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), ametembelea na kukagua ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Tanzania (TIA), Kampasi ya Mwanza, inayojengwa na Serikali kupitia Wizara ya Fedha, kwa gharama ya shilingi bilioni 7.8, kitakachokuwa na uwezo wa kuhudumia wanafunzi zaidi ya 5,000 kwa wakati mmoja, na kuahidi kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuwekeza rasilimali fedha katika sekta mbalimbali za maendeleo ikiwemo sekta ya elimu.
Mkuu wa Chuo hicho Profesa William Pallangyo, alieleza kuwa katika kipindi cha miaka mitatu, Serikali kupitia Wizara ya Fedha, imekipatia Chuo hicho shilingi bilioni 58.1 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya ujenzi wa miundombinu ya kujifunzia na kufundishia katika Kampasi zake nane za Mtwara (bil. 6.1). Mbeya (Bil 3.2), Mwanza (bilioni 7.8), Kigoma (bilioni 11) na Zanzibar (sh. bilioni 30).
Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) yuko katika ziara ya kikazi ya siku 7 mkoani Mwanza, ambapo atafanya shughui za kukagua, kutembelea, kuzindua na kuweka mawe ya msingi katika miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa mkoani Mwanza. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Haki Ngowi
@Hakingowi
📍Misungwi,Mwanza
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), amewasili wilayani Misungwi, Mkoani Mwanza kwa ziara rasmi ya kikazi na kupokelewa na Viongozi na wananchi wa wilaya hiyo. Katika ziara hiyo Mhe Dkt. Nchemba atakagua maendeleo ya ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Tanzania (TIA) Kampasi ya Mwanza na kisha atazungumza na wananchi wa Misungwi katika mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Mbunge wa Jimbo hilo ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Alexander Mnyeti Katika uwanja wa Amani, Misungwi Mjini.
Mhe. Dkt. Nchemba yuko mkoani Mwanza kwa ziara ya kikazi ambayo imelenga kutembelea na kukagua, kuzindua na Kuweka mawe ya msingi katika Miradi ya Maendeleo inayotekelezwa na Serikali mkoani humo.
📸:W/Fedha -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Mkuu wa Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza, Mhe. Mheshimiwa Johari Samizi, ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita, inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kuipatia Wilaya yake, zaidi ya shilingi bilioni 39 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika Wilaya hiyo katika kipindi cha miaka mitatu ambazo zimeelekezwa kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo sekta za afya, elimu, maji na mingine mingi.
Mhe. Samizi, ametoa shukrani hizo wakati alitoa salaam za Wilaya na Mkoa wa Mwanza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Said Mtanda, wakati wa Mapokezi ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), aliyeanza ziara ya kikazi ya siku 7 mkoani Mwanza ambapo anatarajia kutembelea, kukagua, kuweka mawe ya msingi na kuzindua miradi ya maendeleo katika Wilaya zote za mkoa wa Mwanza. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), ameshiriki kwenye Kilele cha Maonesho ya Saba ya Mifuko na Programu za Uwezeshaji kwa Mwaka 2024 leo Septemba 14, 2024 mkoani Singida, ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Dotto Biteko, aliyemwakilisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa.
Maonesho hayo yalibeba ujumbe na kauli mbiu ya “Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Unufaike na Fursa za Uwezeshaji. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb) ametoa pole kwa Familia ya Marehemu Askofu Chediel Sendoro aliyekuwa Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT)- Dayosisi ya Mwanga, Mkoani Kilimanjaro, aliyefariki kwa ajali ya gari iliyotokea tarehe 09 Septemba, 2024.
Dkt Nchemba aliambatana na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Nurdin Babu na kupokelewa na Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Karagwe, Dkt. Benson Bagonza. -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Natoa pole zangu za dhati kwa familia ya marehemu Askofu Chediel Sendoro wa KKKT – Dayosisi ya Mwanga, Kilimanjaro, aliyeaga dunia kufuatia ajali ya gari iliyotokea hivi karibuni. Tunamuombea marehemu apumzike kwa amani na Mungu aipe familia yake, ndugu, jamaa na marafiki, faraja katika kipindi hiki kigumu.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), kwa niaba ya Waziri Mkuu, Mhe. Kasim Majaliwa Majaliwa, amefunga rasmi Jukwaa la 16 la Ununuzi wa Umma la Nchi za Afrika, Jijini Arusha na kuzishauri nchi hizo za Jumuiya ya Afrika Mashariki kutumia Mifumo wa Ununuzi ya Kidijitali katika nchi zao kama ilivyo kwa Tanzania, ambayo imezindua Mfumo wake wa Ununuzi wa NeST, ambao lengo lake ni kuongeza ufanisi na uwazi katika Sekta ya Ununuzi.
-
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Leo, kwa heshima kubwa, nilipata fursa ya kumwakilisha Waziri Mkuu, Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa, kufunga Jukwaa la 16 la Ununuzi wa Umma kwa Nchi za Afrika Mashariki, lililofanyika Jijini Arusha.
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Ziara ya Waziri wa Fedha, Mhe. @mwigulunchemba1 (Mb), Mkoani, Mwanza.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
UK in Tanzania
@UKinTanzania
Last week, Balozi @MYoungFCDO met Hon. Dr. Mwigulu Nchemba @mwigulunchemba1, Minister of Finance @mofURT.
They discussed strengthening 🇬🇧🤝🇹🇿 collaborations in education, health, anti-corruption & the Mutual Prosperity Partnership.
💫Working together towards shared prosperity! -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Lemutuz TV
@lemutuztv
Anaandika Waziri wa Fedha - @mwigulunchemba1
"Mwanangu buana, Ulifunga goli la muhimu sana katika mechi muhimu sana Jana. Anyway hii ni kawaida yako, ndivyo ulifanya ukiwa mitaa ya Jangwani, ndivyo unaendelea kufanya mitaa ya Chamazi. Ulishafanya makubwa Jangwani na Chamazi,.. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Samia Suluhu
@SuluhuSamia
Hongera kwa vijana wetu Taifa Stars kwa ushindi wenu dhidi ya Guinea katika hatua ya makundi kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025. Tunawaunga mkono na kuendelea kuwatakia kila la kheri katika hatua hii muhimu.
-
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Taifa Stars leo mmenipa raha. Ushindi mmoja, ndio mwanzo wa ushindi mwingine. Kila la kheri.
-
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Nimehuzunishwa sana na taarifa za kifo cha Baba yetu Askofu Chediel Sendoro - KKKT Mwanga. Tumempoteza kiongozi aliyekuwa na mchango mkubwa sana kwa jamii yetu, So Sad, Bwana ametoa, Bwana ametwaa, Jina lake lihimidiwe.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Serikali imesema inaendelea kuweka mikakati na mbinu mbalimbali za muda mfupi, wa kati na mrefu katika kushughulikia changamoto ya uhaba wa Fedha za Kigeni (Forex), ikiwemo kuainisha baadhi ya sekta ambazo zinaweza kuleta mapato zaidi ambayo yatatoa suluhisho la kudumu la uhaba wa fedha za kigeni.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi mpya wa Uingereza nchini Tanzania, Mhe. Marrianne Young (@MYoungFCDO ) aliyefika Ofisini kwake Jijini Dodoma kwa ajili ya kujitambulisha.
Mhe. Dkt. Nchemba amesema kuwa, katika bajeti inayoendelea, Serikali imeweka vipaumbele kwa baadhi ya sekta ambazo ni za kuongeza mapato ya fedha za kigeni japokuwa kama nchi kuna hali tofauti na baadhi ya nchi nyingine zinazoizunguka Tanzania kwakuwa inatekeleza miradi mikubwa ya kimkakati.
Aliongeza kuwa, hali hiyo imesababishwa na kutokuwa na uwiano katika uingizaji wa bidhaa nchini na uuzaji wa bidhaa nje ya nchi, lakini pia imetokana na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kimkakati kama mradi wa kuzalisha umeme wa Bwawa la Nyerere, mradi wa Reli ya Kisasa (SGR) na Daraja la Busisi.
“Ni wazi kwamba kila unapokuwa na tofauti yoyote kati ya kile unachouza nje na kile unachoagiza kutoka nje, kutakuwa na shinikizo kwenye fedha za kigeni, na hicho ndicho kinachotokea na pia mikakati na hatua zinazochukuliwa zitasaidia kupata suluhisho la kudumu siku za karibuni” alisema Mhe. Dkt. Nchemba.
Aidha Mhe. Dkt. Nchemba alitumia fursa hiyo kumpongeza Balozi huyo kwa kuteuliwa kuwa Balozi wa Uingereza nchini na kuahidi kuendelea kufanya kazi pamoja ili kuendeleza ushirikiano kati ya Tanzania na Uingereza katika kuhakikisha maendeleo endelevu ya kiuchumi.
“Dhamira ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuendelea kushirikiana na Serikali ya Uingereza ili kuimarisha ushirikiano muhimu wa maendeleo” alisema Dkt. Nchemba.
Mhe. Dkt. Nchemba aliongeza kuwa, Uingereza ni mdau muhimu wa maendeleo kwa kuendelea kutekeleza ajenda ya Maendeleo ya Kitaifa kama ilivyoainishwa chini ya Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025 na Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/22–2025/26 (FYDP III).
“Tunashukuru sana kwa msaada thabiti ambao Serikali ya Uingereza imekuwa ikitoa kwa Tanzania, hususan katika maeneo ya ulinzi wa kijamii kupitia Mpango wa TASAF awamu ya II, Sekta ya Elimu, Afya kupitia Mfuko wa Pamoja wa Afya na Msaada wa Mpango wa Kupambana na Rushwa ambao umechangia kwa kiasi kikubwa maendeleo endelevu ya kiuchumi nchini Tanzania” alisema Dkt. Nchemba.
Kwa Upande wake, Balozi huyo mpya wa Uingereza nchini, Mhe. Marrianne Young, amemshukuru Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu kwa kumkaribisha na kuahidi kuendeleza ushirikiano kati yao katika kusukumu gurudumu la maendeleo ya kiuchumi kwa Tanzania.
“Ningependa kuwapongeza kwa sera imara za uchumi wa jumla na maendeleo, Ninaelewa kwamba tumekuwa na msaada wa muda mrefu kutoka Mamlaka ya Mapato na Forodha ya Uingereza (HMRC) katika eneo hili na tunafanya kazi zaidi ili kusaidia juhudi za Serikali ya Tanzania za kuongeza wigo wa mapato”
Kikao hicho kimehudhuriwa na Kamishna wa Idara ya Usimamizi wa Madeni Wizara ya Fedha, Bw. Japhet Justine, viongozi wandamizi wa Wizara ya Fedha na Maafisa kutoka Ubalozi wa Uingereza.
@UKinTanzania -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
DKT. NCHEMBA AKUTANA NA WALIMU WAKE WA SEKONDARI YA ILBORU
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), amekutana na walimu wake waliomfundisha katika Shule ya Sekondari Ilboru iliyopo Mkoani Arusha.
Walimu hao ambao wengi ni wastaafu waliambatana na walimu waliopo sasa wa shule hiyo. Mhe. Dkt. Nchemba alifanya nao mazungumzo baada ya ziara yao ya kutembelea Bunge, jijini Dodoma, ambapo amewashukuru na kuwapongeza kwa kazi kubwa ya kuwafundisha wanafunzi ambao mchango wao umekuwa mkubwa katika ujenzi wa Taifa. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
DAR ES SALAAM STOCK EXCHANGE
@dsetanzania
Strengthening partnerships for economic growth.
The @dsetanzania CEO, Mr. @PeterNalitolela (L), pays a courtesy visit to the @mofURT of the Republic of Tanzania, Hon. Dr. @mwigulunchemba1 (R), at his office in Dodoma to discuss key initiatives in advancing Tanzania's financial markets through financial literacy & awareness; attractive & accomodative regulations for investment for individuals and businesses - both domestic and foreign.
#leadership #finance #economicdevelopment #tanzania -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Afisa Mtendaji Mkuu Mpya wa Soko la Hisa la Dar es Salam (@dsetanzania ), Bw. Peter Nalitolela, aliyefika kujitambulisha akiwa ameambatana na baadhi ya watendaji wa Soko la Hisa la Dar es Salaam katika Ofisi ya Waziri wa Fedha, jijini Dodoma, ambapo Mhe. Dkt. Nchemba, amemtakia yeye na Menejimenti yake afya njema wanapotekeleza majukumu yao ya kila siku.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb) ameshiriki katika ufunguzi wa Mkutano wa 35 wa Kamati ya Kudumu ya Fedha ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Haki Ngowi
@Hakingowi
📍Arusha
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) ameshiriki katika ufunguzi wa Mkutano wa 35 wa Kamati ya Kudumu ya Fedha ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango.
📸:W/Fedha -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), akipongezwa na viongozi mbalimbali baada ya kutamatika kwa Mkutano wa kuwajengea uwezo Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Waganga Wakuu wa Mikoa na Waganga Wakuu wa Wilaya, kuhusu Sheria ya Ununuzi wa Umma na Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi na Matumizi Sahihi ya Takwimu, tukio lililofanyika katika ukumbi wa Jiji, uliopo mji wa Magufuli-Mtumba, jijini Dodoma.
-
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Nimekuwa na wakati mzuri wa kufungua mkutano wa kuwajengea uwezo Viongozi wenzangu kuhusu Sheria ya ununuzi wa Umma na Sheria ya Ubia kati ya Sekta za Umma na Sekta binafsi na matumizi sahihi ya Takwimu kwa Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri na Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya, katika ukumbi wa Mikutano wa Jiji la Dodoma uliopo katika eneo la Mji wa Serikali, Mtumba, Dodoma, leo tarehe 31 Agosti 2024.
Niendelee kuwasisitiza Viongozi wa Taasisi za Serikali na Binafsi kuhakikisha wanatumia vizuri mifumo ya Kidigitali katika shughuli za Ununuzi ili ziweze kuleta tija kwa watanzania na Serikali kwa ujumla katika kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika kukuza Uchumi wa Nchi kwa njia mbalimbali ikiwemo njia ya Kidigitali.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Haki Ngowi
@Hakingowi
📍Dodoma
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akizungumza wakati akifungua Mkutano wa kuwajengea uwezo Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Waganga Wakuu wa Mikoa na Waganga Wakuu wa Wilaya, kuhusu Sheria ya Ununuzi wa Umma na Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi na Matumizi Sahihi ya Takwimu, tukio lililofanyika ukumbi wa Jiji, uliopo mji wa Magufuli-Mtumba, jijini Dodoma, ambapo amewasihi viongozi hao kutumia vyema mafunzo hayo katika kutekeleza majukumu mbalimbali katika ununuzi wa vifaa na utekelezaji wa miradi kupitia Mfumo wa Ununuzi wa umma (Nest) na fursa ya kutekeleza miradi kwa njia ya Ubia.
📸:W/Fedha -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
MAMLAKA ZA SERIKALI NA SEKTA BINAFSI ZATAKIWA KUTUMIA FURSA ZILIZOPO KATIKA SHERIA YA PPP
Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb) ametoa rai kwa Mamlaka za Serikali pamoja na wawekezaji kutoka Sekta binafsi kutumia fursa zilizopo katika Sheria ya Ubia kati ya Sekta Binafsi na Sekta ya Umma (PPP) kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo ili kupata faida na kuipunguzia Serikali mzigo wa kibajeti.
Mhe. Dkt. Nchemba ametoa rai hiyo Mjini Dodoma, wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Waganga Wakuu wa Mikoa na Waganga Wakuu wa Wilaya, kuhusu Sheria ya Ununuzi wa Umma, sura Na. 410, Sheria ya Ubia kati ya sekta ya Umma na Binafsi, Sura Na. 103 na mafunzo ya matumizi ya takwimu zinazozalishwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu, katika Ukumbi wa Mikutano wa Jiji la Dodoma, uliopo Mji wa Serikali Mtumba.
Aliwahimiza Maafisa Masuuli wote kuzingatia maelekezo ya Waraka wa Hazina namba 7 wa mwaka 2020/21 unaotoa maelekezo na mwongozo katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa utaratibu wa PPP.
Alisema kuwa Sheria ya PPP Sura 103 imefanyiwa marekebisho kwa kuweka mazingira wezeshi ili kuimarisha ushiriki wa sekta binafsi katika kutekeleza miradi ya ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi, Sheria hiyo inaruhusu wawekezaji katika miradi ya ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi kunufaika na vivutio vya kikodi na visivyokuwa vya kikodi, sawa na wale wanaopata vivutio chini ya Sheria ya Uwekezaji Tanzania, Sura ya 38.
“Sheria ya PPP inaruhusu taasisi za umma kununua mbia anayekidhi vigezo moja kwa moja kwa miradi isiyohitaji ushindani ili kupunguza muda wa hatua za ununuzi na pia imetoa fursa kwa wawekezaji wa kigeni kushirikisha wazawa katika miradi ya PPP ili kuwawezesha kiuchumi na kuendeleza wataalamu wa ndani”, alisema Dkt. Nchemba.
Akizungumzia suala la matumizi sahihi ya Takwimu Dkt. Nchemba alisema kuwa maendeleo ya Taifa lolote ulimwenguni yanatokana na matumizi sahihi ya takwimu zilizozalishwa na vyombo vyenye jukumu hilo katika kupanga mikakati mbalimbali ya maendeleo.
Alisema kuwa utekelezwaji wa mipango yote ya mendeleo nchini Tanzania umekuwa ukifanywa kwa kuzingatia takwimu zilizoandaliwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu ambayo ilianzishwa kwa Sheria ya Takwimu ya Mwaka 2015 ambayo imeipa mamlaka ya kuandaa na kuchapisha takwimu mbalimbali zinazohitajika kwa matumizi ya kimaendeleo ikiwemo kiuchumi, kijamii na kisiasa.
Dkt. Nchemba alisema pamoja na kuwepo kwa Ofisi ya Taifa ya Takwimu inayofanya kazi nzuri ya kutoa takwimu mbalimbali, bado matumizi ya takwimu hizo katika upangaji na utekelezaji wa mipango hauridhishi, kwa kuwa mara kadhaa imetiliwa mashaka kama ilitumia takwimu sahihi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu.
“Mipango yenye mashaka inatupotezea muda lakini pia imekuwa ni chanzo cha kutofanikishwa kwa malengo mbalimbali hususani malengo ya kutoa huduma bora kwa wananchi, natoa rai kwa taasisi zote za umma hapa nchini kuhakikisha zinazingatia na kuongeza matumizi ya takwimu zinazozalishwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu katika kuandaa mipango yote muhimu kwa kadri inavyowezekana”, alisisitiza Dkt. Nchemba.
Kwa upande wake Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe. Dkt. Festo Dugange, alisema kuwa katika historia ya nchi ya Tanzania hakuna kipindi ambacho Mamlaka za Serikali za Mitaa na Mikoa zimetekeleza miradi mingi kama kipindi cha Serikali ya Awamu ya Sita.
Amesema bajeti kubwa ya Serikali inaenda TAMISEMI na kwa kiasi kikubwa inatumika kwenye ununuzi katika utekelezaji wa miradi lakini pia shughili mbalimbali za kiofisi.
Alisema kuwa katika taarifa nyingi za Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kumekuwa na changamoto kubwa kwenye eneo la ununuzi, hivyo mafunzo hayo ni fursa muhimu kwa watendaji walioshiriki ili kuweza kutekeleza shughuli zao hususani za ununuzi lakini kutumia takwimu sahihi kupanga mipango ya maendeleo
Akizungumza kwa niaba ya Wakuu wa Mikoa walioshiriki Mafunzo hayo, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Bw. Martin Shigella, alisema kuwa wanapopata majukwaa ya mafunzo kama hayo yanasaidia kujua jambo gani la kufanya ili kusukuma jambo ambalo limekwama katika mkoa husika.
Aidha alimshukuru Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Nchemba kwa kuwaalika na wapo tayari kufanyia kazi yale yote yatakayowasilishwa kupitia mada mbalimbali katika kusukuma gurudumu la maendeleo.
Mkutano huo umewashirikisha Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Waganga Wakuu wa Mikoa na Waganga Wakuu wa Wilaya. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe (Mb) aliyeambatana na wataalamu kutoka Wizara ya Kilimo katika Ofisi za Wizara ya Fedha, jijini Dodoma, ambapo wamejadiliana masuala mbalimbali yanayolenga kuboresha na kukuza Sekta ya Kilimo nchini.
Kikao hicho kimehudhuriwa pia na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo pamoja na Viongozi wengine waandamizi wa Wizara ya Fedha. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), alipokuwa anawasili katika ukumbi wa Jiji, uliopo mji wa Magufuli-Mtumba, jijini Dodoma, kwa ajili ya kufungua Mkutano wa kuwajengea uwezo Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Waganga Wakuu wa Mikoa na Waganga Wakuu wa Wilaya, kuhusu Sheria ya Ununuzi wa Umma na Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi na Matumizi Sahihi ya Takwimu, katika ukumbi wa Jiji kwenye Sekta ya Ununuzi na ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), akiongoza viongozi mbalimbali kuimba Wimbo wa Taifa na Wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Kabla ya kuanza kwa Mkutano wa kuwajengea uwezo Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Waganga Wakuu wa Mikoa na Waganga Wakuu wa Wilaya, kuhusu Sheria ya Ununuzi wa Umma na Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi na Matumizi Sahihi ya Takwimu, tukio lililofanyika katika ukumbi wa Jiji, uliopo mji wa Magufuli-Mtumba, jijini Dodoma.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), akiwa katika kikao kifupi na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Dkt. Festo Dugange, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bi, Jenifa Christian Omolo, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Bw. Dennis Simba na wataalamu kutoka PPRA, Kabla ya kufungua Mkutano wa kuwajengea uwezo Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Waganga Wakuu wa Mikoa na Waganga Wakuu wa Wilaya, kuhusu Sheria ya Ununuzi wa Umma na Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi na Matumizi Sahihi ya Takwimu, katika ukumbi wa Jiji, uliopo mji wa Magufuli-Mtumba, jijini Dodoma.
-
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Congratulations my Daddy.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Chuo cha Uongozi cha ESAMI, Dkt. Peter Kiuluku, alieambatana na Meneja Mkazi wa Chuo hicho, Bw. Uli Mtebe, katika ofisi ya Waziri wa Fedha, jijini Dodoma, ambapo wamwejadiliana masuala mbalimbali ya ushikiriano kati ya Wiazara na Chuo hicho hususan mafunzo ya watumishi wa Wizara katika Chuo hicho ndani na nje ya nchi.
Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo, Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu, Bw. Lusius Mwenda na Mkurugenzi Idara ya Mipango, Bw. Moses Dulle. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Serikali imeeleza kuwa katika bajeti ya mwaka 2023/24, ilitenga jumla ya shilingi bilioni 600 kwa ajili ya kulipa madeni ya wazabuni, wakandarasi, watumishi na watoa huduma mbalimbali ili kupunguza mzigo wa madeni na kuimarisha utendaji wa miradi ya Serikali.
Hayo yameelezwa bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), alipokuwa akijibu swali la Mheshimiwa Bupe Nelson Mwakang’ata, Mbunge wa Viti Maalum, aliyetaka kujua ni lini Serikali itawalipa wazabuni na wakandarasi waliotoa huduma mbalimbali katika Mkoa wa Rukwa, ambao hawajalipwa kwa kipindi cha miaka mitano.
Mhe. Chande alisema kuwa Serikali itawalipa wazabuni na wakandarasi waliotoa huduma mbalimbali na kueleza kuwa hadi kufikia Juni 2024, jumla ya shilingi 491,254,100,645.65 zimetolewa kwa ajili ya kulipa madeni ya wazabuni na wakandarasi nchini kote.
“Kati ya kiasi cha shilingi 88,629,271.20 zilitolewa kulipa wazabuni na wakandarasi wa Mkoa wa Rukwa. Hata hivyo, kiwango hiki bado kimeonekana kuwa kidogo ukilinganisha na mahitaji ya malipo katika mkoa huo, jambo ambalo katika mwendelezo wa utekelezaji wa miradi muhimu ya maendeleo” alifafanua Mhe. Chande.
Vile vile, Mhe. Chande amejibu swali la Mheshimiwa Constantine John Kanyasu, Mbunge wa Geita Mjini, aliyetaka kujua kuhusu malipo ya posho za nyumba na majukumu kwa watumishi wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (CKHT) ni lini serikali itawalipa watumishi hao ambao hawajalipwa tangu mwaka 2020.
Mhe. Chande alisema kuwa Wizara ya Fedha imepokea na kuhakiki madeni ya watumishi wa CKHT yenye thamani ya shilingi 5,430,613,831 na kuwa taratibu za kushughulikia malipo ya madeni hayo zinaendelea, na ahadi ilitolewa kuwa malipo yatatekelezwa katika mpango wa bajeti wa mwaka 2024/25.
“Serikali imejipanga kikamilifu kushughulikia suala hilo na kwamba malipo hayo yatatekelezwa ndani ya muda uliopangwa na kutambua umuhimu wa motisha kwa watumishi na itaendelea kuhakikisha kuwa haki zao zinaheshimiwa na kulindwa, na kwamba ucheleweshaji wa malipo hautajirudia tena katika siku zijazo”. Alisema Mhe. Chande
Aliongeza kuwa serikali imeweka mipango madhubuti ya usimamizi wa fedha, kuhakikisha uwazi katika usimamizi wa posho na madeni, na kuongeza ufuatiliaji wa karibu kuhusu utekelezaji wa bajeti ili kuepusha ucheleweshaji wa malipo. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Bado Siku 2📌
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Wizara inawakaribisha kushiriki mkutano huu unaohusu utekelezaji wa Sheria ya Ununuzi wa Umma, Sura 410 na Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, Sura 103 pamoja na matumizi sahihi ya takwimu.
-
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Hongera sana Dkt. Faustine Ndugulile @DocFaustine ,Proud of you Madam President kwa kuunga mkono watanzania washike nafasi muhimu za kimataifa.
-
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Vote for Dr. Faustine Ndugulile @DocFaustine for WHO AFRO Director!
His experience and commitment to health matters make him the right choice for Africa’s Future.
#ndugulile4whoafro -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Clouds Media
@CloudsMediaLive
Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba (Baba Izack) akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda (Baba Keagan) walipokutana Kizimkazi kwenye kilele cha Kizimkazi Festival.
Unafikiri walipokutana wamezungumza nini?
#kizimkazifestival -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), alikuwa Mgeni Rasmi katika Jubilee ya kutimiza miaka 25 ya Upadre ya Mhashamu Askofu Antony Gasper Lagwen, wa Jimbo Katoliki Mbulu iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Bikira Maria Mpalizwa Mbinguni, Mjini Mbulu Mkoani Manyara, ambapo ameahidi kuwa Serikali itatoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa Barabara yenye urefu wa kilometa 50 itakayojengwa kwa kiwango lami kutoka Hydom – Labay hadi Garbabi kuanzia robo ya kwanza ya mwaka huu wa fedha (2024/2025).
Barabara hiyo inatajiwa kugharimu shilingi bilioni 12 na itakapokamilika itarahisisha shughuli za usafiri na usafirishaji wa abiria na mizigo kwa wakazi wa wilaya hiyo na mkoa wa Manyara kwa ujumla.
Mhashamu Askofu Antony Gasper Lagwen, alizaliwa wilayani Mbulu Mkoani Manyara Mwaka 1967 na alipata Upadre mnamo mwaka 1999 na baadae kuwa Askofu mwaka 2018. -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Ujenzi wa Kampasi ya Babati ya Chuo cha Uhasibu Arusha, naupongeza Uongozi wa Chuo kwa ufanisi mkubwa wa utekelezaji wa mradi huu kwa utaratibu wa force account.
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb) ameweka jiwe la msingi kwa awamu ya kwanza kati ya awamu tatu za ujenzi wa Kampasi ya Babati ya Chuo cha Uhasibu Arusha na kuupongeza Uongozi wa Chuo hicho kwa ufanisi mkubwa wa utekelezaji wa mradi huo kwa utaratibu wa force account.
Awamu hiyo ya kwanza ya mradi inajumuisha ujenzi wa jengo la taaluma (departmental building), mabweni (hostels) na bwalo la chakula (cafeteria), ambapo ujenzi huo umegharimu shilingi bilioni 10, kati ya fedha hizo, shilingi bilioni 6 zinatokana na mapato ya ndani ya Chuo hicho na kiasi cha shilingi bilioni 4 kimetolewa na Serikali (Wizara ya Fedha), ambayo ni mmiliki wa Chuo hicho.
Jengo la taaluma lenye ghorofa tano katika awamu wa kwanza ya mradi huo limefikia asilimia 95 mpaka sasa, likiwa na vyumba vya madarasa, kumbi za mihadhara, vyumba vya Semina, maabara za kompyuta, maktaba, ukumbi wa mikutano na ofisi za wafanyakazi.
Aidha, kwa upande wa mabweni (hostels) yanayojengwa yatakapokamilika yatakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 1,456 kwa wakati mmoja na Bwalo la chakula (cafeteria) litakuwa na uwezo wa kuchukua watu 200 kwa wakati mmoja.
Tukio hilo la uwekaji Jiwe la Msingi limehudhurudhiriwa na Viongozi na wadau mbalimbali wa akiwemo, Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mhe. Queen Sendiga. -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Nimeweka jiwe la Msingi katika ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) Tawi la Babati mkoani Manyara. Naupongeza sana uongozi wa Chuo kwa kupanua wigo wa upatikanaji wa huduma ya elimu karibu na Jamii.
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Jambo TV
@Jambotv_
Waziri wa Fedha Dkt. @mwigulunchemba1 ameungana na abiria wengine kutumia usafiri wa treni ya mwendo kasi (SGR), kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma na kuonja ladha ya usafiri huo ambao umekuwa ukifanyiwa kila jitihada ili ufike nchini kote na kuchochea biashara katika ukanda wa Maziwa Makuu.
Aliyekaa pembeni yake ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Mhandisi Ismail Hassan Rumatila. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Daily News Tanzania
@dailynewstz
TANZANIA: THE Minister for Finance, Dr Mwigulu Nchemba, has called for comprehensive reforms in the international financial system to make it more inclusive and responsive to the needs of developing countries.
Read more:-dailynews.co.tz?p=66224 -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), ameungana na abiria wengine kutumia usafiri wa treni ya mwendo kasi (SGR), kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma na kuonja ladha ya usafiri huo ambao Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, anafanya kila jitihada kuhakikisha kuwa mradi huo wa kimkakati unakamilika na kuchangia kuchochea biashara katika ukanda wa Maziwa Makuu. Aliyekaa karibu naye ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Afya, Mhandisi Ismail Hassan Rumatila,
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Jambo TV
@Jambotv_
Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba ameihakikishia Jumuiya ya Kimataifa na Watanzania kwa ujumla kwamba Serikali inaendelea kuweka na kuboresha mazingira ya uwekezaji ikiwamo kuboresha mifumo yake ya kodi.
Dkt. Nchemba ameyasema hayo katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha Jijini Dar es Salaam wakati akiagana na Balozi wa Uswizi aliyemaliza muda wake wa ubalozi nchini Tanzania Didier Chassot.
Amesema kuwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameunda timu ya wataalamu ya kupitia na kuja na mapendekezo yatakayosaidia kuboresha mifumo yake ya kodi ili kuvutia zaidi biashara na uwekezaji nchini.
Dkt. Nchemba amefafanua kuwa pamoja na kuundwa kwa timu hiyo, Serikali pia imechukua hatua kadhaa za kuboresha ya kielektroniki ya ukusanyaji kodi inayosaidia kukusanya mapato yake kwa ufanisi na kuondoa usumbufu kwa walipakodi.
Amesema kuwa lengo la kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji pamoja na kuimarisha mifumo ya kodi ni kuhakikisha kuwa idadi ya walipakodi inaongezeka hatua itakayosaidia pia kuiwezesha serikali kupunguza viwango vya kodi ya ongezeko la thamani siku za usoni kwa sababu walipakodi watakuwa wengi.
Kwa upande wake Balozi wa Uswizi aliyemaliza muda wake nchini Didier Chassot, ameipongeza Serikali kwa uamuzi huo wa kupitia mifumo ya kodi na kwamba anaamini mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao nchini watapata pia nafasi ya kuzungumza na kujadiliana na serikali kuhusu masuala hayo kama walivyoomba.
Balozi Chassot ametumia fursa hiyo ya kuagana na Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba kuipongeza Serikali ya Awamu ya Sita kwa hatua kubwa iliyopiga kimaendeleo katika kipindi kifupi.
Ameahidi kuwa Uswisi inaandaa mpango mpya wa ushirikiano wa kimaendeleo na Tanzania, utakaojielekeza katika kufanikisha ajenda mbalimbali za maendeleo ya nchi kupitia programu zake mbalimbali ikiwamo kusaidia mfuko wa maendeleo ya jamii-TASAF, usimamizi wa fedha za umma, biashara na uwekezaji kupitia asasi za kiraia na sekta binafsi.
Didier Chassot ameitumikia nafasi hiyo ya ubalozi akiwa nchini kwa kipindi cha miaka minne na ameahidi kuendelea kuwa Balozi mzuri wa Tanzania atakaporejea nchini kwake kuendelea na majukumu yake mengine. -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
#kizimkazifestival #kizimkaziimeitika
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), ameihakikishia Jumuiya ya Kimataifa na Watanzania kwa ujumla kwamba Serikali inaendelea kuweka na kuboresha mazingira ya uwekezaji ikiwemo kuboresha mifumo yake ya kodi.
Dkt. Nchemba ameyasema hayo katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam, wakati akiagana na Balozi wa Uswisi aliyemaliza muda wake wa ubalozi hapa nchini, Mhe. Didier Chassot.
Alisema kuwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ameunda timu ya wataalam ya kupitia na kuja na mapendekezo yatakayosaidia kuboresha mifumo yake ya kodi ili kuvutia zaidi biashara na uwekezaji nchini.
Mhe. Dkt. Nchemba alifafanua kuwa pamoja na kuundwa kwa timu hiyo, Serikali pia imechukua hatua kadhaa za kuboresha ya kielektroniki ya ukusanyaji kodi inayosaidia kukusanya mapato yake kwa ufanisi na kuondoa usumbufu kwa walipa kodi.
Alisema kuwa lengo la kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji pamoja na kuimarisha mifumo ya kodi ni kuhakikisha kuwa idadi ya walipakodi inaongezeka hatua itakayosaidia pia kuiwezesha Serikali kupunguza viwango vya kodi ya ongezeko la thamani siku za usoni kwa sababi walipakodi watakuwa wengi.
Kwa upande wake Balozi wa Uswisi aliyemaliza muda wake hapa nchini, Mhe. Didier Chassot, aliipongeza Serikali kwa uamuzi huo wa kupitia mifumo ya kodi na kwamba anaamini Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini watapata pia nafasi ya kuzungumza na kujadiliana na Serikali kuhusu masuala hayo kama walivyoomba.
Balozi Chassot alitumia fursa hiyo ya kuagana na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, kuipongeza Serikali ya Awamu ya Sita kwa hatua kubwa iliyopiga kimaendeleo katika kipindi kifupi.
Aliahidi kuwa Uswisi inaandaa mpango mpya wa ushirikiano wa kimaendeleo na Tanzania, utakaojielekeza katika kufanikisha agenda mbalimbali za maendeleo ya nchi kupitia program zake mbalimbali ikiwemo kusaidia mfuko wa maendeleo ya jamii-TASAF, usimamizi wa fedha za umma, biashara na uwekezaji kupitia asasi za kiraina sekta binafsi.
Mhe. Didier Chassot, ameitumikia nafasi hiyo ya ubalozi akiwa hapa nchini kwa kipindi cha miaka minne na ameahidi kuendelea kuwa Balozi mzuri wa Tanzania atakaporejea nchini kwake kuendelea na majukumu yake mengine.
@SwissMFA -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Hongera sana Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-Organ Troika). Uteuzi huu unaakisi imani kubwa ya viongozi wenzako duniani katika uongozi wako mahiri na ni ushuhuda wa uongozi wako thabiti na kujitolea kwa maendeleo ya Jumuiya yetu.
-
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Haki Ngowi
@Hakingowi
📍Geita
VIDEO:
Waziri wa Fedha Dkt Mwigulu Nchemba alipomuwakilisha Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe . Dkt Dotto Biteko katika Jubilei ya miaka 25 ya Updre ya Askofu Flavian Matindi Kassala,iliyofanyika katika kanisa kuu la bikira Maria Malkia wa Amani,mkoani Geita Jumapili 11-08-2024
📹:W/Fedha -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb) na Viongozi mbalimbali wa Serikali na Taasisi wameshiriki tukio la uzinduzi wa Tawi la Benki ya KCB wilayani Geita, mkoani Geita, ambapo Mgeni Rasmi katika hafla hiyo alikuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb) leo tarehe 12 Agosti, 2024 amezuru kaburi la aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya tano, Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Wilayani Chato Mkoani Geita.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe Dkt.@mwigulunchemba1 (Mb), ametoa rai kwa viongozi wa dini kuendelea kuliombea Taifa ili liendelee kuwa na umoja wa kitaifa ulioletwa na falsafa za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Mhe. Dkt. Nchemba ametoa rai hiyo wakati akiwahutubia waumini wa Kanisa la Kikatoliki Jimbo la Geita, alipohudhuria Jubilei ya Miaka 25 ya upadre ya Askofu Flavian Matindi Kassala, yaliyofanyika Kanisa Kuu Bikira Maria Malkia wa Amani, Mkoani Geita.
"Ni vyema kutambua kwamba tunahitaji kushindanisha sera na falsafa zinazolenga kuendeleza na kuunganisha Taifa letu na sio kuleta mgawanyiko na kubaguana"
Aidha, Dkt. Nchemba amewaomba viongozi wa dini kuendelea kushirikiana na Serikali kutoa elimu na kukemea masuala ya ukatili wa watoto na kijinsia yanayofanywa katika jamii. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), amewaasa wananchi kuacha kugombana kwa sababu za siasa kwani kitendo hicho kinasababisha maafa, yatima, wajane na kukosekana kwa amani.
Dkt. Nchemba ameyasema hayo kwenye kilele cha Makambi alipokuwa akizungumza na waumini wa Kanisa la Waadventista (Wasababato) Mjini Katoro, Mkoani Geita.
Dkt. Nchemba, amewaasa waumini hao kuepuka kujihusisha na siasa za fujo na vurugu kwasababu zinaleta madhara makubwa kwa familia moja moja na nchi kwa ujumla hivyo kuathiri uchumi, umoja na mshikamano wa Taifa.
Aidha, Dkt Nchemba amewataka waumini hao kuendelea kumwombea Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ili aendeleze kudumisha maelewano, mshikamano na kusikilizana ambazo ndio zimekuwa falsafa zake tangu aingie madarakani. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Clouds Media
@CloudsMediaLive
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), amewaasa wananchi kuacha kugombana kwa sababu za siasa kwani kitendo hicho kinasababisha maafa, yatima, wajane na kukosekana kwa amani.
Dkt Nchemba ameyasema hayo kwenye kilele cha Makambi alipokuwa akizungumza na waumini wa Kanisa la Waadventista (Wasababato) Mjini Katoro, Mkoani Geita.
Dkt Nchemba, amewaasa waumini hao kuepuka kujihusisha na siasa za fujo na vurugu kwasababu zinaleta madhara makubwa kwa familia moja moja na nchi kwa ujumla hivyo kuathiri uchumi, umoja na mshikamano wa Taifa.
Aidha, Dkt Nchemba amewataka waumini hao kuendelea kumwombea Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ili aendeleze kudumisha maelewano, mshikamano na kusikilizana ambazo ndio zimekuwa falsafa zake tangu aingie madarakani.
#cloudsdigitalupdates -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Haki Ngowi
@Hakingowi
📍Katoro,Geita
▪️NI USHAMBA KUGOMBANA KISA UCHAGUZI.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), amewaasa wananchi kuacha kugombana kwa sababu za siasa kwani kitendo hicho kinasababisha maafa, yatima, wajane na kukosekana kwa amani.
Dkt Nchemba ameyasema hayo kwenye kilele cha Makambi alipokuwa akizungumza na waumini wa Kanisa la Waadventista (Wasababato) Mjini Katoro, Mkoani Geita.
Dkt Nchemba, amewaasa waumini hao kuepuka kujihusisha na siasa za fujo na vurugu kwasababu zinaleta madhara makubwa kwa familia moja moja na nchi kwa ujumla hivyo kuathiri uchumi, umoja na mshikamano wa Taifa.
Aidha, Dkt Nchemba amewataka waumini hao kuendelea kumwombea Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ili aendeleze kudumisha maelewano, mshikamano na kusikilizana ambazo ndio zimekuwa falsafa zake tangu aingie madarakani.
📸:W/Fedha -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
TRA Tanzania
@TRATanzania
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, Bw. Yusuf Mwenda, Katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha Jijini Dar es salaam, ambapo wamejadili masuala mbalimbali ya kuimarisha utendaji kazi wa Taasisi hiyo muhimu huku jambo kubwa likiwa ni kuweka mikakati ya kutekeleza maelekezo ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ili kuboresha ukusanyaji kodi kwa ajili ya maendeleo ya nchi.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
African Medical Centre of Excellence
@amceafrica
We were honoured to host Tanzanian Minister of Finance Dr. Mwigulu Nchemba, Permanent Secretary Dr. Natu Mwamba, and Acting High Commissioner Ms. Judica Nagunwa at our Abuja site. Their visit underscores vital healthcare collaboration. #amce #afreximbank #kcl
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Heri ya Siku ya Wakulima - NANE NANE
#kilimokinalipa -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Bank of Tanzania
@BankOfTanzania
Waziri wa Fedha, Mhe. Dk. Mwigulu Nchemba (Mb), ameongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa Kamati ya Mawaziri wa Fedha na Uwekezaji wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika unaofanyika kwa njia ya mtandao kwa siku mbili (tarehe 6-7 Agosti, 2024).
-
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
-
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
IMANI HUZAA IMANI, WATANZANIA WANAONGEA KWA VITENDO IMANI YAO KWAKO.
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
MAMA WA TAIFA, WANANCHI WA MOROGORO WAMEKUBALI KAZI YAKO.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), ameongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa Kamati ya Mawaziri wa Fedha na Uwekezaji wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika ( @SADC_News ) unaofanyika kwa njia ya mtandao kwa siku mbili (tarehe 6-7 Agosti, 2024) kutokea Ukumbi wa Mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania, Jijini Dares Salaam. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango-Zanzibar, Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum (Mb), Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban, Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bi. Saada Kassim Msemo, na Maafisa wengine waandamizi wa Serikali wanashiriki mkutano huo.
Mkutano huo unajadili masuala ya utangamano wa Jumuiya hiyo, ikiwemo hali ya kiuchumi katika nchi wanachama pamoja na kuanzishwa kwa Mfuko wa Maendeleo wa Kikanda wa SADC utakaotumika kutatua changamoto mbalimbali za upatikanaji wa fedha kwa ajili ya kutekeleza mipango na miradi mbalimbali ya kiuchumi na kijamii katika nchi hizo. -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
TAZAMA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN ALIVYOKARIBISHWA NA BENDERA YA CHAMA RAFIKI (CHADEMA) KWENYE MKUTANO WAKE.
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
TANZANIA KUJENGA KITUO CHA UMAHILI CHA HUDUMA YA MATIBABU
Tanzania inatarajiwa kuwa miongoni mwa nchi tano za Afrika zitakazonufaika na ujenzi wa mradi mkubwa wa Hospitali itakayokuwa na viwango vya dunia vya utoaji huduma za matibabu (African Medical Center of Excellence (AMCE), kupitia mradi unaotekelezwa na African Export-Import Bank (Afreximbank) kwa kushirikiana na Hospitali ya Chuo Kikuu cha King, iliyoko London nchini Uingereza.
Hayo yameelezwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kituo cha Umahili cha Kimatibabu, Abuja, Bw. Brian Deaver, wakati Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), alipoongoza ujumbe wa Tanzania kutembelea ujenzi wa mradi wa aina hiyo, nje kidogo ya mji wa Abuja, nchini Nigeria.
Bw. Deaver alieleza kuwa Hospitali hiyo itakayokuwa na uwezo wa kulaza wagonjwa 500 kwa wakati mmoja, itatumia teknolojia ya kisasa ambayo haijawahi kutumika katika Bara la Afrika kwa ajili ya kutibu magonjwa ya kansa ya damu na sickle cell.
Alifafanua kuwa Hospitali hiyo pamoja na hospitali nyingine zitakazojengwa nchini Ghana, Kenya na Tanzania, zitatoa huduma mtambuka ikiwemo uchunguzi, matibabu, tiba kwa anjia ya nyuklia, upasuaji, huduma baada ya upasuaji na huduma nyingine zinazojulikana kitaalam kama oncology, haematology na magonjwa ya moyo.
“Tunapotekeleza mradi huu tunalenga kutoa huduma bora za afya, kutoa mafunzo kwa wataalam wa afya, kufanya utafiti, kutoa ajira, kudhibiti mahitaji ya matumizi ya fedha za kigeni hususan dola na kukuza utalii wa kimatibabu kwa nchi za Afrika” aliongeza Bw. Deaver
Wakizungumza baada ya kutembelea mradi huo unaotarajiwa kugharimu zaidi ya dola za Marekani milioni 260, Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu Elmaanry Mwamba, walisema kuwa mradi huo wa mfano si tu kwamba utasaidia huduma za kimatibabu kwa wananchi, bali pia itakuwa sehemu ya utalii wa kimatibabu kwa watu kutembelea na kupata huduma hizo kutoka nje ya Tanzania.
Kwa upande wake, Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Nigeria, Bi. Judica Nagunwa, alisema kuwa jitihada zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika sekta ya uchumi na matibabu, umelenga kuimarisha afya za watanzania na kwamba ubalozi wake utatumia kila fursa kuhakikisha kuwa mradi huo unatekelezwa kwa manufaa ya watanzania.
Afreximbank ni Taasisi ya fedha ya kimajumui ya kimataifa (Pan-African multilateral financial institution) yenye majukumu ya kutoa fedha na kuendeleza biashara kwenye nchi za Afrika.
Dkt. Nchemba, ameongoza ujumbe wa Tanzaniaakiwa na Ujumbe wa Tanzania, akiwemo Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Natu El-maamry Mwamba na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Fedha na Mipango-Zanzibar, Bw. Aboud Hassan Mwinyi, wanashiriki Mikutano ya Nchi za Afrika (African Caucus Meetings), uliowashirikisha Mawaziri wa Fedha na Magavana wa Benki Kuu kutoka nchi wanachama wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF). -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
ZIARA YA MHE RAIS DKT SAMIA SULUHU HASSAN MKOA WA MOROGORO.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Haki Ngowi
@Hakingowi
📍Abuja, Nigeria
▪️TANZANIA KUJENGA KITUO CHA UMAHILI CHA HUDUMA YA MATIBABU
Tanzania inatarajiwa kuwa miongoni mwa nchi tano za Afrika zitakazonufaika na ujenzi wa mradi mkubwa wa Hospitali itakayokuwa na viwango vya dunia vya utoaji huduma za matibabu (African Medical Center of Excellence (AMCE), kupitia mradi unaotekelezwa na African Export-Import Bank (Afreximbank) kwa kushirikiana na Hospitali ya Chuo Kikuu cha King, iliyoko London nchini Uingereza.
Hayo yameelezwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kituo cha Umahili cha Kimatibabu, Abuja, Bw. Brian Deaver, wakati Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, alipoongoza ujumbe wa Tanzania kutembelea ujenzi wa mradi wa aina hiyo, nje kidogo ya mji wa Abuja, nchini Nigeria.
Bw. Deaver alieleza kuwa Hospitali hiyo itakayokuwa na uwezo wa kulaza wagonjwa 500 kwa wakati mmoja, itatumia teknolojia ya kisasa ambayo haijawahi kutumika katika Bara la Afrika kwa ajili ya kutibu magonjwa ya kansa ya damu na sickle cell.
Alifafanua kuwa Hospitali hiyo pamoja na hospitali nyingine zitakazojengwa nchini Ghana, Kenya na Tanzania, zitatoa huduma mtambuka ikiwemo uchunguzi, matibabu, tiba kwa anjia ya nyuklia, upasuaji, huduma baada ya upasuaji na huduma nyingine zinazojulikana kitaalam kama oncology, haematology na magonjwa ya moyo.
“Tunapotekeleza mradi huu tunalenga kutoa huduma bora za afya, kutoa mafunzo kwa wataalam wa afya, kufanya utafiti, kutoa ajira, kudhibiti mahitaji ya matumizi ya fedha za kigeni hususan dola na kukuza utalii wa kimatibabu kwa nchi za Afrika” aliongeza Bw. Deaver
Wakizungumza baada ya kutembelea mradi huo unaotarajiwa kugharimu zaidi ya dola za Marekani milioni 260, Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu Elmaanry Mwamba, walisema kuwa mradi huo wa mfano si tu kwamba utasaidia huduma za kimatibabu kwa wananchi, bali pia itakuwa sehemu ya utalii wa kimatibabu kwa watu kutembelea na kupata huduma hizo kutoka nje ya Tanzania.
Kwa upande wake, Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Nigeria, Bi. Judica Nagunwa, alisema kuwa jitihada zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika sekta ya uchumi na matibabu, umelenga kuimarisha afya za watanzania na kwamba ubalozi wake utatumia kila fursa kuhakikisha kuwa mradi huo unatekelezwa kwa manufaa ya watanzania.
Afreximbank ni Taasisi ya fedha ya kimajumui ya kimataifa (Pan-African multilateral financial institution) yenye majukumu ya kutoa fedha na kuendeleza biashara kwenye nchi za Afrika.
Dkt. Nchemba, ameongoza ujumbe wa Tanzaniaakiwa na Ujumbe wa Tanzania, akiwemo Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Natu El-maamry Mwamba na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Fedha na Mipango-Zanzibar, Bw. Aboud Hassan Mwinyi, wanashiriki Mikutano ya Nchi za Afrika (African Caucus Meetings), uliowashirikisha Mawaziri wa Fedha na Magavana wa Benki Kuu kutoka nchi wanachama wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF).
📸:W/Fedha -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Clouds Media
@CloudsMediaLive
Benki ya Dunia imeipongeza Tanzania kwa hatua kubwa iliyopiga katika kutekeleza mradi wa kimkakati wa Reli ya Kisasa-SGR kwa kuwa ni miongoni mwa miradi itakayochochea ukuaji wa uchumi wa nchi pamoja na kuboresha huduma ya usafiri na usafirishaji kwa wananchi.
Pongezi hizo zimetolewa mjini Abuja nchini Nigeria na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia nchi za Ukanda wa Mashariki na Kusini mwa Afrika, Bi. Victoria Kwakwa, alipokutana na ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, Kando ya Mikutano wa Mawaziri wa Fedha na Magavana wa Benki Kuu za Nchi za Afrika, ambazo ni wanachama wa Benki ya Dunia na Shiruka la Fedha la Kimataifa-IMF.
Dkt. Victoria Kwakwa, amesema kuwa si rahisi kwa nchi nyingi za Afrika kujenga mradi mkubwa wa reli kama ilivyofanya Tanzania kwa kuwa ina gharama kubwa lakini kukamilika kwake kutachochea biashara katika eneo la Maziwa Makuu huku akimmwagia sifa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuzindua rasmi safari za treni hiyo kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma.
Kwa Upande wao, Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na Katibu Mkuu na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Natu El-maamry Mwamba, walipokea pongezi hizo kwa niaba ya Serikali na kueleza kuwa lengo la mradi huo ni kuunganisha baadhi ya nchi za Ukanda wa Afrika Mashariki ili kufungua milango ya biashara.
#cloudsdigitalupdates -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), ameongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa 24 wa Mawaziri wa Fedha na Magavana wa Benki Kuu za nchi za Afrika ambazo ni Wanachama wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la KImataifa (@IMFNews ) (Africa Caucus Meetings) unaofanyika katika Hoteli ya Transcorp Hilton, mjini Abuja Nchini Nigeria. Mkutano huo umefunguliwa rasmi tarehe 2 Agosti, 2024 na Makamu wa Rais wa Nigeria, Mhe. Kashim Shettima.
Mkutano huo unajadili namna ya kuboresha biashara katika nchi za Afrika kwa kuweka mazingira mazuri ya kusisimua biashara kwa kujenga miundombinu itakayowezesha kukuza biashara miongoni mwa nchi za Afrika na wataweka msimamo wa pamoja na kupeleka agenda ya namna Taasisi za Fedha za Kimataifa ikiwemo Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF, zinatakiwa kuziwezesha nchi hizo kifedha na kiutaalam ili zifikie malengo husika. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia nchi za ukanda wa Mashariki na Kusini mwa Afrika, Bi. @VictoriaKwakwa , mjini Abuja Nchini Nigeria, ambapo katika mazungumzo yao, Bi. Kwakwa aliipongeza Tanzania kwa hatua kubwa iliyofikia katika utekelezaji wa mradi wa kimkakati wa Reli ya Kisasa (SGR) ambayo imeanza kutoa huduma kati ya Dar es Salaam, Morogoro hadi Dodoma, na safari zake kuzinduliwa rasmi na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, juzi.
Mkutano huo uliofanyika kando ya Mkutano ya 24 wa Mawaziri wa Fedha na Magavana wa Benki Kuu za nchi za Afrika, ambazo ni wanachama wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF umehudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba na Kamishna Msaidizi wa Idara ya Fedha za Nje, Wizara ya Fedha, Bw. Robert Mtengule, katika Hoteli ya Transcorp Hilton. -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
HAPPY SIMBA DAY
Mnajua mimi sio mwanasimba; Lakini buana,
1) Simba wameasisi hii mambo ya Matamasha ya Vilabu- hili ni jambo zuri.
2) Wameset viwango vya mechi na mafanikio Kimataifa na Mimi ni Shabiki wa SIMBA ya Kimataifa.
3) Simba haipati tabu kujaza uwanja iwe tamasha au mechi ya kimataifa.
USIMCHUKIE MTU KWA KUFANIKIWA.
SIMBA NGUVU MOYA!!!!! -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Benki ya Dunia, na Baadhi ya Mawaziri wa Fedha wa nchi za Afrika, wakati wa Mikutano ya Mawaziri wa Fedha na Magavana wa Benki Kuu kutoka nchi za Afrika (Africa Caucus Meetings), Nchi wanachama wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF, unaofanyika katika Hoteli ya Transcorp Hilton, mjini Abuja Nchini Naigeria.
Miongoni mwa Viongozi hao ni Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika, Bi. Viktoria Kwakwa, na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayesimamia Kundi la Kwanza la nchi za Kanda ya Afrika (Africa Group 1 Constituency), Dkt. Floribert Ngaruko.
Wegine ni Waziri wa Fedha na Mipango wa Sudan, Mhe. Dkt. Gabriel Ibrahim Mohamed na Waziri wa Fedha na Maendeleo ya Kiuchumi wa Uganda, Bw. Amos Lugoloobi na pia aliteta jambon a Katibu Mkuu ambaye pia Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Natu El-maamry Mwamba.
@WorldBank -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), akiwa na Ujumbe wa Tanzania katika Ubalozi wa Tanzania, uliopo Abuja nchini Nigeria, ambapo yeye na ujumbe wake, akiwemo Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Natu El-maamry Mwamba na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Fedha na Mipango-Zanzibar, Bw. Aboud Hassan Mwinyi, wanashiriki Mikutano ya Nchi za Afrika (African Caucus Meetings), ukiwashirikisha Mawaziri wa Fedha na Magavana wa Benki Kuu kutoka nchi wanachama wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF).
Mhe. Dkt. Nchemba na ujumbe wake walipowasili katika Ubalozi huo, walilakiwa na Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Nigeria, Bi. Judica Nagunwa akiambatana na Mwambata Jeshi wa Ubalozi Brigedia Jenerali Julius Kadawi na Maafisa wengine waandamizi.
Akizungumza na Watumishi wa Ubalozi, Mhe. Dkt. Nchemba, aliupongeza Ubalozi huo kwa kusimamia vema Diplomasia ya kiuchumi na kuvutia uwekezaji na mitaji kutoka katika Taifa hilo kubwa barani Afrika.
Alitoa wito kwa Ubalozi huo kufanya utafiti namna lugha ya kiswahili inaweza kunadiwa katika Mataifa kadhaa ya kiafrika wanayoyasimamia kutokana na umuhimu wa lugha hiyo katika kuunganisha Bara hilo.
Alisema kuwa kiswahili ni bidhaa ambayo ikienea na kutumiwa na Mataifa mengi duniani itakuza ajira kwa walimu wa kitanzania watakaotumika kufundisha lugha hiyo lakini pia kuharakisha maendeleo katika nchi zitakazozungumza lugha hiyo.
Kwa upande wake, Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Nigeria, Bi. Judica Nagunwa, alisema watalifanyia kazi suala la kukuza matumizi ya kiswahili katika nchi wanazoiwakilisha nchi na kwamba tayari kuna Ushirikiano na makubaliano ya kitaasisi kati ya Tanzania na Nigeria katika kueneza lugha ya kiswahili kupitia vyuo vikuu vya Tanzania na Nigeria lakini pia kupitia Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC).
Aidha, Bi. Nagunwa alisema kuwa Nigeria ni nchi kubwa kiuchumi na kwamba Tanzania imenufaika na uwekezaji wake nchini Tanzania, kikiwemo Kiwanda cha Saruji cha Dangote na Benki ya UBA -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Hongera sana Mhe Rais kwa uthubutu na usimamizi wako. Reli hii itaboresha huduma ya usafiri na kurahisisha biashara, hivyo kuchochea maendeleo ya kiuchumi nchini.
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Dr. Ouma Duncan
@OumaDun
It was a great conversation with the Honorable Minister, his team and other stakeholders!
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), amezindua rasmi Ripoti ya Mapitio ya Hali ya Mwenendo wa Uchumi wa Tanzania kwa mwaka 2024, iliyoandaliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (@AfDB_Group ), yenye kauli mbiu isemayo “Driving Tanzania’s Transformation - The Reform of the Global Financial Architecture”.
Mhe. Dkt. Nchemba, amezindua Ripoti hiyo kwa njia ya mtandao akiwa Abuja nchini Nigeria, ambako anaongoza ujumbe wa Tanzania kushiriki Mikutano ya Nchi za Afrika (African Caucus Meetings), wanachama wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF).
Ripoti hiyo inaonesha kuwa Tanzania imepiga hatua kubwa kiuchumi na kijamii na kuwa kinara miongoni mwa nchi za Afrika Mashariki, licha ya changamoto zinazoikabili Dunia ikiwemo athari za UVIKO-19, mabadiliko ya tabianchi na mizozo ya vita inayoendelea maeneo mbalimbali duniani.
Dkt. Nchemba amebainisha kuwa Tanzania itaendelea kuimarisha Uchumi wake kupitia Mpango wake wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (FYDP III), wenye lengo la kujenga uchumi imara, shirikishi na wenye ushindani kupitia sekta za uzalishaji, ikiwemo kilimo, uzalishaji viwandani, kuongeza thamani ya bidhaa, uwekezaji na biashara pamoja na kukuza ajira kwa wananchi hususan vijana.
Amezitaka Taasisi za Fedha za Kimataifa, ikiwemo Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), kuweka mazingira ya upatikanaji wa fedha zenye masharti nafuu ili kuziwezesha nchi za Afrika kuwa na uwezo endelevu wa kutekeleza mipango ya maendeleo kwa ajili ya nchi zao.
Dkt. Nchemba alitaja eneo linalokwamisha maendeleo ya nchi hizo za Kiafrika ikiwemo Tanzania kuwa ni pamoja na athari za mabadiliko ya tabianchi ambapo kila mwaka Tanzania inahitaji dola za Marekani bilioni 6.3 za kukabiliana na hali hiyo zikiwemo athari za papo kwa papo zinazotokana na mabadiliko ya hali ya hewa.
Ripoti hiyo ya Mwenendo wa Uchumi wa Tanzania iliyowasilishwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika inaonesha kuwa uchumi wa Tanzania umezidi kuimarika na unatarajia kupanda kutoka asilimia 5.1 mwaka 2023, hadi asilimia 5.7 mwaka 2024, na utafika asilimia 6 mwaka 2025.
Tanzania imesifiwa pia kwa kufanikiwa kudhibiti mfumuko wa bei na kubaki katika wigo wa chini ya asilimia 3.3 kutokana na sera bora za kiuchumi zinazochukuliwa na Serikali ya Awamu ya Sita.
Ripoti hiyo imezitaja sekta zilizochangia ukuaji huo wa uchumi kuwa ni pamoja na sekta ya fedha, huduma, kilimo, kuimarika kwa mazingira ya uwekezaji, biashara, na sekta ya madini.
Benki ya Maendeleo ya Afrika imeishauri Tanzania kuendelea kusimamia vizuri sera zake za fedha na uchumi, kwa kuendelea kuwekeza zaidi kwenye sekta za uzalishaji, kilimo, nishati na kuboresha zaidi mazingira ya uwekezaji pamoja na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.
Uzinduzi huo wa Hali ya Uchumi wa Tanzania, umehudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Viongozi waandamizi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika, AfDB, Wachambuzi wa masuala ya uchumi wa ndani na nje ya nchi pamoja na wawasilisha mada. -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
All the best team, This will open a new chapter in our tax administration and bring forth voluntary compliance. Hongera Mhe Rais.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
ikulu_Tanzania
@ikulumawasliano
UTEUZI
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), amezindua rasmi Ripoti ya Mapitio ya Hali ya Mwenendo wa Uchumi wa Tanzania kwa mwaka 2024, iliyoandaliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (@AfDB_Group ), yenye kauli mbiu isemayo “Driving Tanzania’s Transformation - The Reform of the Global Financial Architecture”.
Mhe. Dkt. Nchemba, amezindua Ripoti hiyo kwa njia ya mtandao akiwa Abuja nchini Nigeria, ambako anaongoza ujumbe wa Tanzania kushiriki Mikutano ya Nchi za Afrika (African Caucus Meetings), wanachama wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF).
Ripoti hiyo inaonesha kuwa Tanzania imepiga hatua kubwa kiuchumi na kijamii na kuwa kinara miongoni mwa nchi za Afrika Mashariki, licha ya changamoto zinazoikabili Dunia ikiwemo athari za UVIKO-19, mabadiliko ya tabianchi na mizozo ya vita inayoendelea maeneo mbalimbali duniani.
Dkt. Nchemba amebainisha kuwa Tanzania itaendelea kuimarisha Uchumi wake kupitia Mpango wake wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (FYDP III), wenye lengo la kujenga uchumi imara, shirikishi na wenye ushindani kupitia sekta za uzalishaji, ikiwemo kilimo, uzalishaji viwandani, kuongeza thamani ya bidhaa, uwekezaji na biashara pamoja na kukuza ajira kwa wananchi hususan vijana.
Amezitaka Taasisi za Fedha za Kimataifa, ikiwemo Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), kuweka mazingira ya upatikanaji wa fedha zenye masharti nafuu ili kuziwezesha nchi za Afrika kuwa na uwezo endelevu wa kutekeleza mipango ya maendeleo kwa ajili ya nchi zao.
Dkt. Nchemba alitaja eneo linalokwamisha maendeleo ya nchi hizo za Kiafrika ikiwemo Tanzania kuwa ni pamoja na athari za mabadiliko ya tabianchi ambapo kila mwaka Tanzania inahitaji dola za Marekani bilioni 6.3 za kukabiliana na hali hiyo zikiwemo athari za papo kwa papo zinazotokana na mabadiliko ya hali ya hewa.
Ripoti hiyo ya Mwenendo wa Uchumi wa Tanzania iliyowasilishwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika inaonesha kuwa uchumi wa Tanzania umezidi kuimarika na unatarajia kupanda kutoka asilimia 5.1 mwaka 2023, hadi asilimia 5.7 mwaka 2024, na utafika asilimia 6 mwaka 2025.
Tanzania imesifiwa pia kwa kufanikiwa kudhibiti mfumuko wa bei na kubaki katika wigo wa chini ya asilimia 3.3 kutokana na sera bora za kiuchumi zinazochukuliwa na Serikali ya Awamu ya Sita.
Ripoti hiyo imezitaja sekta zilizochangia ukuaji huo wa uchumi kuwa ni pamoja na sekta ya fedha, huduma, kilimo, kuimarika kwa mazingira ya uwekezaji, biashara, na sekta ya madini.
Benki ya Maendeleo ya Afrika imeishauri Tanzania kuendelea kusimamia vizuri sera zake za fedha na uchumi, kwa kuendelea kuwekeza zaidi kwenye sekta za uzalishaji, kilimo, nishati na kuboresha zaidi mazingira ya uwekezaji pamoja na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.
Uzinduzi huo wa Hali ya Uchumi wa Tanzania, umehudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Viongozi waandamizi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika, AfDB, Wachambuzi wa masuala ya uchumi wa ndani na nje ya nchi pamoja na wawasilisha mada. -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
John, unatutangazia ambavyo bado uko karne ya zamani hivyo? Dunia haitusubiri, nikufundishe kidogo, watu wanatembea na Credit Card, Viza Card, Debt Card, walishatoka kutembea na Cash. Ukiwa Nchi yeyote unachanja kwa card. Hata ndani ya Nchi tunahamasisha watu tuhame kutoka kutumia Cash twende Cashless. Unabeba macash ya nini? Wakati wewe unanishangaa mimi, Dunia nzima inakushangaa wewe, unaweza kuwa na PASSPORT BUT huna uelewa wa Cashless economy. Kwa hiyo kila Nchi ukienda unakwenda kuibadili TZS? Siasa buana inaruhusu utukanwe hata na asiye na upeo na jambo husika👏👏👏👏.
John Pambalu
@John_Pambalu
Huyu jamaa hafai duniani wala mbinguni. Nilishinda njaa uwanja wa kimataifa wa Amsterdam-Uholanzi na hela ninayo. Ilikuwa hivi 19.07.2024 nimeondoka nchini kuja Marekani. Nikachukua cash nafika Airport bureau zote hawana hata Dollar 1 ya mfano. Nikaondoka nafika Amsterdam nikataka kubadilisha Tsh. Wakasema haitambuliki labda Ksh. Nikasema nani kairoga nchi yangu😭😭😭?.
-
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Nimeona bango hili likizunguka mitandaoni. Pamoja na uhuru wa kuabudu tulionao, tujiepushe kuhusishana kwenye jambo ambalo hatujapanga pamoja. Kuna walioniuliza kama nalifahamu jambo hili, kiukweli SILIFAHAMU.
Tuendele kuiombea nchi yetu, viongozi wetu wakuu, viongozi wengine wote na Watanzania kwa ujumla. Binafsi niombeni niendelee kutimiza kikamilifu jukumu hili nililopewa kwa sasa. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Bank of Tanzania
@BankOfTanzania
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Elikunda Materu
@materuni
Waziri @mwigulunchemba1 amefafanua hapa youtu.be/XLDGcz7Hon8
-
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
PUUZENI TAARIFA YA NIPASHE, HAKUNA UCHOTAJI FEDHA BOT, HUU NI MWENDELEZO WA KUZUA TAHARUKI KWA MAKUSUDI, BOT INASIMAMIA KWA UMAKINI SANA SHERIA ZA NCHI NA MIIKO YA BENKI KUU ZOTE DUNIANI.
Nimesoma taarifa hiyo ambayo inatokana na uchambuzi wa NGO iitwayo WAJIBU inayoongozwa na Mzee Ludovic Uttoh, CAG Mstaafu. Kwa ujumla maelezo ya taarifa hiyo yanaeleweka na hayana utata wowote, hivyo sijui kwa nini mwandishi wa Nipashe ameeleza kuwa KUNA UTATA BoT.
Taarifa imeelezea suala ambalo ni la kawaida na huwa linafanyika kila mwaka kutokana na Sheria ya BoT inayoruhusu kutoa advances or Short Term Loans kwa Serikali ili kukidhi mahitaji ya matumizi ambayo yanakuwa hayajapata mapato. Kwa mujibu wa kifungu cha 34 hadi 37 cha BoT Act, Serikali inaruhusiwa kukopa hadi 18% ya makusanyo halisi ya ndani ya mwaka uliopita. HILI LIMEKUWA LIKIFANYIKA HIVYO TANGU BOT IANZISHWE, BOT NI BENKI YA SERIKALI, SERIKALI UCHUKUA ADVANCE KWA MUJIBU WA SHERIA BADALA YA KUKOPA KWA RIBA KUBWA KUTOKA BENKI ZA KIBIASHARA.
Hivyo, kwa mwaka 2022/23, Serikali ilikuwa inaweza kukopa BoT kiasi kinachofikia TZS. 4.5 trillion. Hivyo, taarifa ya kuwepo kwa mkopo wa TZS. 1.7 trilioni ni suala ambalo liko ndani ya wigo unaokubalika kisheria. Kiasi hicho kilipofika mwisho wa Mwaka kilijumuishwa kwenye Treasury Bonds za Mwaka husika ambazo zinaendelea kulipia riba kama sehemu ya mikopo ya ndani.
Utaratibu huo ni wa kawaida na ufanyika kwa Benki Kuu za nchi nyingi duniani, pindi Serikali inapohitaji Fedha za kugharamia Bajeti wakati bado inaendelea kujipanga na kukusanya mapato kutoka katika vyanzo mbalimbali. Ndio maana hata IMF waliridhika kuwa BoT na Serikali wamezingatia Sheria na taratibu za kimataifa kama inavyotakiwa. Kutokana na uzingatiwaji wa Sheria hizo, Bodi ya IMF waliridhia kutoa USD. 300 milioni kwa mwaka 2023/24 na Benki ya Dunia waliridhia kutoa USD. 750 milioni kwa mwaka 2023/24 kwa kuwa tathmini ya Pili ya program ya IMF iliyofanyika Desemba 2023 iliangalia masuala mbalimbali yakiwemo ya mapato, matumizi, madeni, uzingatiwaji wa Sheria ya BoT, ukuaji wa uchumi, mfumuko wa bei, urari wa biashara, thamani ya shilingi na usimamizi wa masoko ya fedha nchini.
Kutokana na maelezo haya, nadhani mwandishi wa gazeti la Nipashe hakupaswa kusema kuwa kuna utata BOT tena bila hata kuulizia au kuomba ufafanuzi kutoka BoT. Inawezekana aliandika kwa nia ovu ya kuupotosha umma, kuidhalilisha BoT na kusababisha taharuki kwa jamii. Aidha, inawezekana mwandishi ameandika kwa kutojua Sheria suala ambalo angeuliza angepewa ufafanuzi unaotakiwa.
Kutokana na maelezo hayo, BoT itaandaa taarifa kwa umma na kukanusha na kutoa elimu kuwa hakuna utata wowote uliopo kutokana na taarifa hizo bali ni suala la kawaida ambalo Serikali inaruhusiwa kukopa kwa kuzingatia ukomo wa 18% ya mapato halisi ya mwaka uliopita, kama ilivyo kwa Sheria za nchi nyingine duniani. Hata ukomo huu upo kwenye viwango karibiana kati ya Nchi zote za EAC. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Mjinifm
@mjinifm
Waziri wa Fedha, Mh. Dkt. @mwigulunchemba1 "Mb" amekuwa mgeni rasmi katika mechi ya Hisani ya Ufunguzi wa mashindano ya '’PBZ YAMLE YAMLE CUP 2024'’ Msimu wa 6, Iliyowakutanisha Mazombi FC dhidi ya Mboriborini FC, DIMBA la Amaan Stadium, Zanzibar.
✍🏾 @Justinekesy
@mjinifm 92.5 -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Waziri wa Fedha, Mhe Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb) amekuwa mgeni rasmi katika Mechi ya Hisani ya Ufunguzi wa mashindano ya '’PBZ YAMLE YAMLE CUP 2024'’ Msimu wa 6, Iliyowakutanisha Mazombi Fc dhidi ya Mboriborini Fc Katika uwanja wa Amaan Stadium, Visiwani Zanzibar, ambapo timu ya Mazombi FC imeibuka kidedea kwa kushinda kwa mikwaju ya penati 4 dhidi ya 2.
Akizungumza katika Mchezo huo Dkt Nchemba amezipongeza timu zote mbili kwa kuonesha mchezo wa kiwango kikubwa na ameahidi Serikali itaongeza nguvu katika mashindano hayo. -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Puuzeni taarifa ya “Tanzanialeaks” Serikali haijafilisika, Ameandika hatujalipa Bwawa - Uongo mtupu, Bwawa la Mwl Nyerere hatudaiwi hata Invoice Moja na Wiki jana tumewasha na mtambo wa 7, ( Sasa tumeshawasha 7, 8 & 9 kila mmoja 235MW). Ameandika kuhusu Yapi, hawa walikuwa na matatizo madogo kama kampuni nayo yanaendelea kutatuliwa, Malipo yameendelea kulipwa kwenye Sekta zote na mengine yapo kwenye hatua za mwisho za malipo. Waongo buana amesahau kwamba ndio tuko wiki ya pili ya mwaka mpya wa Fedha. Puuzeni ni wale wale wenye wenye kututakia mabaya.
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Jambo TV
@Jambotv_
VIDEO:
Kikao kazi kilichohusisha Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na viongozi wa wafanyabiashara chini ya uratibu wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) kilichofanyika leo, Alhamisi Julai 18.2024 Johari Rotana Hotel, jijini Dar es Salaam pamoja na mambo mengine kimeadhimia pande hizo mbili kukutana kila baada ya miezi mitatu (3) ili kujadili changamoto za kikodi zinazowakwamisha wafanyabishara na kutafuta majawabu ya pamoja ili waweze kufanya biashara zao na walipe kodi stahiki
Hayo yameelezwa na Kamishna Mkuu wa TRA Yusuph Mwenda mbele ya wanahabari ikiwa ni muda mfupi baada ya kukamilika kwa kikao kazi hichoThis media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
KODI NI MAENDELEO YA NCHI YETU.
HONGERA MZALENDO NAMBA 1 WA TAIFA LETU.This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Wameona na wanashuhudia Miradi yote ya kimkakati umeitekeleza imekamilika, na unaendeleza ambayo haijakamilika, Fedha za huduma za jamii zinawafikia kwa wingi kuliko kipindi chochote tangu uhuru, uongozi wako ni bora, mwadilifu, unawapenda kwa kutoa ruzuku, elimu bure na kujenga miradi ya umwagiliaji. Unakuza Sekta binafsi ambayo ndio maisha yao. Pokea Maua yako Mama.
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
The Chanzo
@TheChanzo
TRA yafanya maamuzi haya magumu kumaliza kero za wafanyabiashara Tanzania.
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Ilikuwa furaha kujumuika nyumbani mwa Bwana na washarika wa Mundarara, Longido.
This media couldn't be displayed. See it on the original post. -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
TRA Tanzania
@TRATanzania
-
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Ministry of Finance Tanzania
@mofURT
Tazama Youtube: Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), akihitimisha Kikao cha Tathmini ya Utendaji Kazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (@TRATanzania ), kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024, kilichofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano Arusha (AICC).
www.youtube.com/watch?v=F4fKw-jFHLg
#hazinatv -
Mwigulu Nchemba, PhD reposted
Jambo TV
@Jambotv_
Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba @mwigulunchemba1 amemwagiza Kamishna Mkuu mpya wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Yusuph Juma Mwenda kuwachukulia hatua kali za kisheria na kinidhamu ikiwamo kuwafukuza kazi baadhi ya watumishi wa mamlaka hiyo wanaokiuka maadili ya kazi zao kama kudai na kupokea rushwa, kwa kuwa vitendo hivyo vinaitia doa TRA na kuikosesha Serikali mapato.
Dkt. Nchemba amesema hayo wakati akihitimisha Kikao cha Tathmini ya Utendaji Kazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 kilichofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano Arusha (AICC).
Aidha Dkt. Nchemba amemwagiza Kamishna huyo kuwachukulia hatua kali wafanyabiashara wasiowasilisha ritani za Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwa kuwa fedha hizo zinatakiwa kuwasilishwa serikalini kupitia TRA ikizingatiwa kuwa wafanyabiashara ni Mawakala wa Serikali wa kukusanya kodi hiyo, na hazitakiwi kufanywa kama sehemu ya mapato yao.
Halikadhalika Dkt. Nchemba amewataka watumishi wa TRA kuongeza ubunifu, umahiri na kuhakikisha wanatenda haki wakati wa kukusanya mapato ya Serikali ili kutimiza matarajio ya Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuwaletea Watanzania maendeleo ya uhakika.
Pia Dkt. Nchemba ametumia fursa hiyo kuwapongeza TRA kwa utendaji kazi mahiri kwa mwaka wa fedha ulioisha wa 2023/24, ambapo walikusanya kiasi cha Shilingi trilioni 27.64, ambayo ni sawa na ufanisi wa asilimia 97.67 ya lengo la kukusanya Shilingi trilioni 28.30 ambayo ni sawa na ongezeko la asilimia 14.50, ikilinganishwa na makusanyo ya Shilingi trilioni 24.14 katika mwaka wa fedha uliopita 2022/23.
Katika hafla hiyo Dkt. Nchemba aliambatana na Naibu Waziri wa Fedha Hamad Hassan Chande, Kamishna Msaidizi wa Idara ya Sera Wizara ya Fedha William Mhoja, na maafisa wengine waandamizi wa Wizara ya Fedha. -
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Ufafanuzi wa hoja kushusha Kodi ya ongezeko la thamani (VAT) toka 18% kwenda 12%.
-
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
TAARIFA
-
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
-
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Mauji#Mbande CRDB,Tumepoteza askari 4 wapambanaji.Nimefika usiku huu eneo la tukio,hatutaishia kulaani,wajisalimishe
-
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
#hatua ya kuboresha makazi ya polisi na idara zake ni kipaumbele chetu.Vifaa vya kazi na maslai yao tunayazingatia.
-
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
#asante Mh.Rais J.P.Magufuli kwa kuendelea kuniamini na kunipa dhamana ya kuongoza wizara ya mambo ya ndani ya nchi.
-
Mwigulu Nchemba, PhD
@mwigulunchemba1
Fuatilia mahojiano yangu ndani ya DAKIKA 45 Usiku huu kuanzia saa 3 Kamili ITV. instagram.com/p/1tIbOcCeFC/










































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































